Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

Hon. Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

MHE. KANGI A. N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami niungane kuunga mkono Azimio hili la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli. Watanzania tulimwomba Mungu atuletee Rais ambaye ni jasiri, Rais ambaye ana uthubutu, Rais ambaye atakuwa mlinzi wa rasilimali za nchi yetu na Mungu akasikia kilio chetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya watu ambao wanasimamia kauli zao ni Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Mheshimiwa John Pombe Magufuli kabla hata hajawa Rais wa nchi hii, alitoa kauli kwamba atakapokuwa Rais atahakikisha mchanga wa dhahabu hautasafirishwa tena kwenda nchi za nje. Mheshimiwa Magufuli kabla hajawa Rais alisema, ole wao Watanzania watalimia meno endapo atakuwa Rais wa nchi hii. Leo tunashuhudia Watanzania aliowalenga kulimia meno ni mafisadi wanaoiba rasilimali za nchi hii na sasa wanaanza kulimia meno. Namwomba Rais wetu hata wale wanaoshabikia na kuunga mkono mafisadi na wenyewe awaweke katika kulimia meno kwa sababu na wao wanashabikia kuibiwa rasilimali zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika nchi zote duniani huwezi ukampata mtu wa aina ya Magufuli ambaye amezaliwa kila wakati, ambaye anazaliwa kila mahali na ndiyo maana hata nchi zingine wanaanza kumlilia kwamba huenda na sisi tungekuwa na mtu kama huyu mtu ambaye ana uchungu na watu wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais wetu wakati anapokea Ripoti ya Makinikia alitaka kulia, nilimwona ameshika shavu la kushoto, anasema kama na yeye ana damu Rais wetu analia na rasilimali za Watanzania. Leo kuna watu hawataki tumpongeze Rais wetu wakati amejitoa mhanga, kuna watu wanajitoa mhanga kulipua ndege, kuna watu wanajitoa mhanga kulipua hata Mabunge leo Rais anajitoa mhanga kufa kwa ajili ya rasilimali za Watanzania kwa nini tusimuunge mkono mtu kama huyu? Ndiyo maana ukisoma Isaya 54:17 unasema, kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu hauta… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)