Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

Hon. Tundu Antiphas Mughwai Lissu

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Singida Mashariki

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dokta John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua anazochukua kukabiliana na Upotevu wa Mapato ya Serikali katika Sekta ya Madini

MHE. TUNDU A. M. LISSU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Wajibu wa Kikatiba wa Bunge hili ni kuisimamia na kuishauri Serikali, wajibu wa Bunge siyo kuishangilia au kuimba mapambio kwa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema wajibu wa Kikatiba wa Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali siyo kuisifia na kuiimbia mapambio. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili Azimio siyo Azimio la Bunge ni Azimio la wana CCM kumpongeza Mwenyekiti wao wa CCM. Kama sisi siyo wanafiki, kama Wabunge wa Bunge hili siyo wanafiki, basi kwa vile mnataka tumsifu Magufuli kwa kuunda Kamati, tuanze na Rais Benjamin Mkapa aliyeunda Kamati ya Jenerali Mboma, aliyeunda Kamati ya Dkt. Kipokola, aliyeunda Kamati ya Dkt. Bukuku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama sisi siyo wanafiki, twende kwa Kikwete aliyeunda Kamati ya Lau Masha, akaunda Kamati ya Mark Bomani, kama sisi sio wanafiki lakini kwa sababu ni wanafiki hatuko tayari hata kusema kwamba…

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tunavyozungumza, huyo tunayeambiwa amethubutu, mikataba yote ya madini anayoita ya wizi bado ipo, hakuna uliobadilishwa hata mmoja. Hivi tunavyozungumza, sheria zote ambazo zimetungwa miaka yote hii ambazo zimetuleta hapa tulipo, hakuna iliyoguswa hata moja. Hivi tunavyozungumza asilimia 100 ya madini ya dhahabu yanayochimbwa Geita yanasafirishwa kutokea Geita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tunavyozungumza asilimia 100 ya dhahabu inayochimbwa North Mara Tarime inasafirishwa nje kupitia Kiwanja cha Ndege cha Kewanja Tarime. Asilimia 95 ya dhahabu ya Bulyanhulu inasafirishwa nje kutokea kiwanja cha Bulyanhulu. Asilimia 95 ya dhahabu ya Buzwagi inasafirishwa kutoka Buzwagi…

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Taarifa mbili zilizotolewa na Profesa Mruma na Profesa Osoro hazina utaalam wowote, haziwezi zikasimama mahali popote.