Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
0
Ministries
nil
MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai na kuifanya afya yangu iwe njema mpaka sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kutoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano. Juzi nilikuwa namsikiliza Profesa Patrick Lumumba wa Kenya anampongeza Rais wetu kama Rais na ametoa term mpya ya kiingereza, The Magufulification of Africa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nimpongeze Waziri Mkuu kwa hotuba yake na usimamizi mzuri, lakini niipongeze Serikali kwa ujumla wake kwa jinsi ambavyo inatekekeleza the vision 2025, hasa hii awamu ya pili ya miaka mitano – mitano na utekelezaji wake unaonekana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge elimu tunaona sasa hivi inavyokwenda vizuri. Tunaona jinsi ambavyo barabara zinajengwa, tunaona ujenzi wa reli, tunaona upanuzi wa bandari, tunaona jinsi tunavyoendeleza afya hospitali nyingi au dispensary nyingi katika vijiji vyetu. Vilevile tumeona ndege zinavyonunuliwa kuhakikisha kwamba tunainua uchumi wetu. Ndege siyo tu kwa ajili ya usafiri, lakini wale wenzetu walioko katika sekta ya utalii watakubaliana na mimi jinsi tunavyopata ndege ndivyo tutakavyokuwa na watalii wengi na watakaokuwa wanaleta pesa katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tufanye nini, ili tuweze kuongeza kasi yetu hii ya uchumi. Kwanza kabisa Serikali iangalie upatikanaji wa resource. Resource siyo pesa tu ni pamoja na human resource na time factor. Nilikuwa nikisikiliza mazungumzo yalivyokuwa yanaendelea hapa, I think we are wasting a lot of resource inayoitwa time. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni jambo la kusikitisha tunabishana vitu ambavyo viko obvious ni kwamba wote ni Watanzania na Watanzania wote tushirikiane na tulikubali kuungana. Tuendelee na hilo kwa msimamo huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa zaidi ambacho niweze kukizungumzia ni usimamizi wa resources hizi na shughuli tunazozifanya. Tunaweza tukaona tunafanya vizuri sana katika Serikali Kuu, kwa sababu tuna Wakuu wa Mikoa, tuna Wakuu wa Wilaya, lakini tukienda kwa wenzetu wa TAMISEMI ambao wanaenda chini ambako tunataka tuone maendeleo ya mtu mmoja mmoja hadi vijijini hali yetu siyo nzuri sana. TAMISEMI ukienda pale Wizarani kwa kweli, wanafanya vizuri sana. Nimpongeze sana Katibu Mkuu pamoja na Mawaziri wanafanya kazi nzuri, reaction yao ukipeleka tatizo lako ni instant, lakini ni vipi huku chini tume- fail?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie tu namna ambavyo tunaweza tuka-improve. Wenzetu katika baadhi ya nchi wanasema ili uwe Diwani lazima uwe na elimu ya kiwango fulani, ili uwe Mbunge lazima uwe na elimu ya kiwango fulani, lakini sisi tukifanya hilo tutakuwa tunavunja Katiba yetu, lakini kuna upande mwingine kwa sababu kuna wanasiasa na kuna watendaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watendaji katika Halmashauri zetu, hawa Wakurugenzi tunawapataje? Wenzetu hawa walioko katika Wizara husika Wakurugenzi hawa wanapatikanaje? Au ni hawa wanaotuita sisi kuwa msiwasikilize wanasiasa, wakati Wakurugenzi wengi walikuwa wagombea wakashindwa kupata nafasi, kwa hiyo ni wanasiasa waliokosa nafasi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa sheria hii mpya iliyokuja, ukitoka kwenye utendaji ukaenda kwenye siasa, you will never go back kwenye utendaji, baki huko huko. Umeshindwa umeshindwa, umepata, umepata na ndivyo wenzetu wanavyofanya na lazima hili liwekewe mkazo, ili tuweze kuhakikisha kwamba, tunakuwa na Serikali inayosimamiwa vizuri. Tunakuwa na sera nzuri, lakini usimamizi wake unakuwa na mapungufu. Hilo nadhani tutaliangalia zaidi na wenzetu wakiliangalia vizuri katika area ya monitoring and evaluation. Sasa monitoring and evaluation kwa kiswahili chake kizuri sina uhakika kwa sababu kiswahili kilianzia huko Pwani, kikapita Morogoro wakachakachua, hapa Dodoma wakachakua, kilipofika Mwanza mimi sikumbuki. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie zaidi katika eneo la Watendaji na Madiwani. Madiwani wetu ni watu ambao wamepata Udiwani kwa sababu wana uhuru wa kuweza kutafuta udiwani na wakachaguliwa katika maeneo yao katika Kata zao au kwa kupitia Viti Maalum. Lakini Watendaji hapa kuna issue, na hapa Serikali yetu kupitia kwa Waziri Mkuu lazima tujipange vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kichwa changu na kichwa cha Jenista Mhagama ni vichwa viwili tofauti kabisa na uwezo wetu wa kufikiri uko tofauti kabisa, kwa hiyo ni vema tukapima, tukahakikisha kwamba pale anapofaa Jenista Mhagama aende Jenista Mhagama, pale anapofaa Kitwanga aende Kitwanga, lakini hii ya kubeba jumla jumla na wakati mwingine ndugu zetu ife, siwezi kukubaliana na hilo na bahati nzuri ukiwa msema kweli hata ukikaa pazuri watakuondoa tu. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa unatenda haki kwa kila mtu hata ukikaa Koromije watakuondoa wakupeleke Mtwara. Kwa hiyo, niweze kusema ukweli na iweze kueleweka na ijulikane kabisa hawa wanasiasa katika Halmashauri zetu tuwaacheni wako pale kihalali. Lakini watendaji wetu let us choose the people who are right to every post. Tujipime, tujiangalie, tujitazame. If you are doing the right thing everybody will clap for you. Kama unafanya ubabaishaji wako, watasema huyu naye. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu yetu izungumzwe as a system, isizungumze kama chunk of shule ya msingi, shule ya sekondari, izungumzwe as a system, mfumo mzima and let us produce real na tusijali, wenye akili wapewe resource waweze kuitumikia nchi hii. Wanaozembea zembea wasipewe, after all nchi haiendelezwi na kila mmoja, watu watano wanaweza wakaendeleza nchi. They think, they deliver, they influence others and the country move. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naku-address wewe nilinde tu hawa wasinisumbue. (Kicheko)
Labda niende kwenye Wilaya yangu kwenye Jimbo langu. Kwanza kabisa nianze kwa kuwapongeza TARURA. TARURA wameanza vizuri sana. Wakati tuna Idara ya Ujenzi tu katika Halmashauri zetu tulikuwa na matatizo kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Looh! nilikuwa na mambo mengi lakini sasa sijui nitasemaje. Nizungumzie maji katika maeneo ya Kanyerere, Koromije, Mamae. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba tu nitaomba tena nafasi katika Wizara zinazohusika niweze kuchangia. Tuongeze tena, turudishe tena ziwe dakika kumi na tano jamani. Ahsante sana.