Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nashukuru sana kwa kupata nafasi ya kuchangia hoja hii muhimu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napenda sana kuusifu uongozi wa Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Profesa Mbarawa na wasaidizi wake wote, kwa sababu Wizara hii ni Wizara mojawapo ambayo imeonesha kwa kweli ni kitu gani Awamu ya Tano inataka. Miradi mikubwa mingi sana imeanza kutekelezwa, tukianzia kwenye barabara, SGR, madaraja, bomba la mafuta la Tanga, flyovers, vivuko na mengineyo mengi. Hata hivyo nimefurahishwa sana na hotuba ya Mheshimiwa Waziri hasa hasa kwenye miradi hii mikubwa. Isipokuwa nimesikitika sana baada ya kuona kwamba reli ya Tanga imeachwa kabisa. Nimeangalia nimesoma kwa haraka haraka, lakini sijaona reli ya Tanga ikizungumziwa. Najua upembuzi yakinifu umemalizika kati ya Tanga mpaka Arusha na sasa hivi unafanyika upembuzi yakinifu wa Arusha mpaka Musoma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ningeshauri kwamba hii reli ya Tanga ambayo upembuzi yakinifu umeshafanyika wa Arusha mpaka Tanga basi ingeanza kutangazwa kwa njia ya PPP ili wawekezaji waanze kufanya kazi hiyo. Naamini kabisa wawekezaji wa PPP watakapoarifiwa mradi huu unaweza kuanza mara moja. Nafahamu wapo na wanategemea Serikali itaanza kuutanga hivi karibuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo tunategemea bandari. Nimeona kwenye ratiba hapa Bandari ya Tanga ambayo ni bandari kubwa na sasa hivi kutokana na bomba la mafuta ambalo linategemewa kuanza tunategemea kwamba kazi itaanza. Mwaka uliopita ilitengewa fedha lakini naona kazi inakwenda kwa kusuasua, sasa nategemea kwamba basi wakati huu itatengenezwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nakuja kwenye jimbo. Barabara yangu ya Amani - Muheza kilometa 36 mwaka 2017 tulitengewa shilingi bilioni tatu. Nilitegemea kwamba kazi ingeanza lakini naona kwenye maandiko ya Mheshimiwa Waziri kwamba anatafutwa mkandarasi na kila nikimuuliza Meneja wa TANROADS Tanga vipi umefikia wapi ananiambia tunashughulikia. Sasa tutashughulikia huyu mkandarasi sijui atapatikana lini na fedha hizi zinaweza kurudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kwamba nimetengewa tena shilingi bilioni tano, sasa naamini kabisa shilingi bilioni tatu zangu zile na shilingi bilioni tano hizi nikijumulisha pamoja ni shilingi bilioni nane naamini nitapata karibu kilometa 20.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri nakuomba sana fedha hizi zije ili hii kazi iweze kuanza. Nashukuru sana kwamba barabara ya Tanga mpaka Pangani mtaanza kuitengeneza na nimeona hapa mmeitengea hela kwa hiyo, nakushukuru sana na nategemea kwamba barabara hiyo yenyewe itaanza kutengenezwa kwa sababu barabara hiyo inapita pia kwenye jimbo langu. Namshukuru sana Mheshimiwa Elias Kwandikwa, alikuja na aliiona barabara hii na aliona matatizo yake. Kwa hiyo, naamini kabisa kwamba kazi itaanza mara kwa sababu waliwapa matumaini wanachi wa Amani kwamba kazi hii itafanyika na sasa hivi wanategemea kwamba kazi hiyo itaanza kufanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mawasiliano ya eneo hilo hilo la Amani, tuna tatizo kubwa sana la mawasialiano. Nafikiri sasa hivi imefika wakati kwamba kukimbilia kwenye mapaa ya nyumba au kupanda kwenye miti kwa ajili ya mawasiliano iwe imekwisha. Sasa naamini kwamba nimempa list Naibu Waziri ambaye aliuliza maeneo ambayo mawasiliano hakuna; na nimempa list ya Tarafa yote ya Amani, Muheza; Tarafa yote ya Bwembwera ambako mawasiliano yanakuwa ni tabu sana kwenye baadhi ya vijiji. Kwa hiyo, nategemea kwamba katika kipindi hiki basi atazituma hizi kampuni za simu kuja kusaidia kwenye haya mawasiliano, vinginevyo suala la TARURA bado hatujaona matunda yake. Muheza hawajaletewa hela kabisa na hii TARURA, hata shilingi moja; sasa inakuwa taabu na kuwa- control hawa TARURA, najua ni TAMISEMI lakini inakuwa taabu sana kwa sisi kuweza kupata mawasiliano ya kujua kama wamepewa hela au hawakupewa hela, wao wapo wapo tu. Sasa naomba wapewe hela ili waweze kuonesha hiyo kazi ambayo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)