Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii niweze kuchangia katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama katika Bunge lako Tukufu. Pia nampongeza Rais wangu, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya za kujenga Taifa. Nawapongeza pia Mawaziri, Mheshimiwa Profesa Mbarawa na Manaibu wake kwa kazi nzuri wanazozifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nielekee moja kwa moja katika mchango wangu. Kwa kuwa ukarabati unaoendelea wa Barabara ya Nyakanazi – Rusahunga - Rusumo haukidhi viwango kutokana na magari mazito yanayopita pale ya mizigo yanayoelekea nchi jirani za Rwanda, Burundi, Kongo na Uganda. Naomba sana Mheshimiwa Waziri husika na Wizara waweze kuangalia hii barabara itengenezwe kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba waikarabati kwa kiwango kinachokidhi, kwa sababu kila siku kuna viraka vinavyowekwa pale. Mara leo kuna kiraka, mara kesho kuna kiraka, barabara inaendelea kuwa vilevile, bado kuna magari mazito yanayopita pale. Hii ni barabara ambayo ni muhimu sana katika uchumi wa Taifa. Kwa kweli Mheshimiwa Waziri naomba waliangalie hili kwa jicho la huruma na kwa kusaidia wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano kuna watu wana madaladala, wana teksi zinazotoka Ngara mpaka Kahama, kila baada ya mwezi wanabadilisha shock up na hali ilivyokuwa ngumu, kwa kweli inasikitisha sana. Naomba sana Serikali iweze kutuangalia kwa jicho la huruma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba kuongelea huduma za ndege za Dar es Salaam to Bukoba, huduma za Dar es Salaam ni nzuri, abiria wameongezeka sana kutoka Dar es Salaam mpaka Bukoba, lakini trip ya Dar es Salaam to Bukoba ni moja tu. Naomba trips ziongezeke, sisi watu wa Kagera tumezoea sana kutumia ndege kuliko magari, kwa hiyo naomba mtuongezee trips angalau ziwe mbili au tatu, kwa kweli naomba watuangalie sana. Naomba sana sana iwepo trip ya mchana, tuna trip ya alfajiri tu, mtu unaamka saa kumi, saa tisa kuelekea airport, kwa kweli naomba Mheshimiwa Waziri hili waliangalie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hili naomba kama inawezekana kuwepo na trip ya Dar es Salaam – Dodoma - Mwanza kwa sababu Kanda ya Ziwa kuna abiria wengi sana na Dodoma ndiyo Makao Makuu ya Nchi, kwa nini wasituwekee ndege ya kutoka Dar es Salaam – Dodoma - Mwanza? Kama tuko hapa tunahitaji kwenda Mwanza na moja kwa moja inaenda Kagera bila shida, kwa kweli namwomba Mheshimiwa Waziri waweze kutuangalia sana watu wa Kanda ya Ziwa kwa jicho la huruma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakandarasi walio-supply vifaa vya kujenga miundombinu katika Shule za Sekondari Ihungo na Nyakato wakati wa kipindi cha tetemeko bado wanadai pesa zao nyingi. Je, ni lini watalipwa pesa zao? Kwa sababu wame-supply majengo yamekuwa mazuri lakini hawajalipwa pesa zao. Kwa kweli naomba Wizara husika, Mheshimiwa kaka yangu Profesa Mbarawa, naamini ni mtu mzuri sana, hebu atuangalie kwa jicho la huruma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya usikivu wa simu yaliyopo Wilaya ya Ngara, Kata za Nyakisasa, Keza, Kabanga na Rusumo yanaingiliana na Nchi za jirani za Rwanda na Burundi. Nimeshaongelea hili suala zaidi ya mara tatu ndani ya hili Bunge lako Tukufu, lakini sioni kinachoendelea. Wananchi wa Ngara tunapata shida, mtu unapiga simu uko Ngara inaingiliana na mtambo wa Rwanda, inaingiliana na mtambo wa Burundi. Kwa nini wasituangalie waongeze minara, waongeze mitambo ili tuweze kupata communication ambayo ni within Tanzania, kwa nini wasituangalie sana? Nimeshamwomba sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba kuongelea kuna uwanja ambao uko Ngara unaitwa Ruganza Airstrip, ule uwanja umesahaulika kabisa. Tumeutumia sana kipindi cha wakimbizi wakati nafanya kazi UNHCR ndiyo ulikuwa uwanja mkubwa sana na bado kuna madini ya Kabanga nickel, kule Kabanga nickel ndege zinatoka kule zinatumia ule uwanja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, juzi kuna wakimbizi wamepata ajali wakati wanatoka Kigoma wanaelekea Burundi, wanapitia Kigoma – Kasulu – Kibondo – Ngara. Wamefika Ngara wakapata ajali, ule uwanja ndiyo ulitumika na watu wa UN, UN ni shirika kubwa la kimataifa lakini wametua…
(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.