Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja. Nashukuru na kupongeza sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa namna ilivyotekeleza Ilani ya Uchaguzi na utekelezaji wa maamuzi magumu na yenye tija ya Mheshimiwa Rais katika kuboresha sekta ya uchukuzi kwa vitendo. Niwapongeze pia Waziri mwenye dhamana na Naibu Mawaziri wake kwa kazi kubwa na yenye tija kwa Taifa wanayoifanya kwa ushirikiano mkubwa na watendaji wao. Hongereni sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu katika miradi ya barabara, barabara ya Nyakato – Buswelu – Mhonze kilometa 18, kwa miaka mitatu mfululizo inawekwa kwenye bajeti lakini hadi sasa ni kilometa 1.2 tu imekamilika. Niombe walau kilometa 17 zilizobaki ziingie zote katika bajeti ya 2018/ 2019 ili tuondoe adha hiyo ukizingatia barabara hiyo inapita Makao ya Wilaya. Aidha, mkandarasi JASCO aliyepewa zabuni hiyo hana uwezo, ikiwezekana aondolewe. Katika bajeti imetegewa kilometa moja tu. Ninachelea kusema Awamu ya Tano itakwisha bila kukamilika barabara hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe ukamilishaji wa matengenezo ya kivuko cha Kayenze – Base ambacho kiliwekwa kwenye bajeti ya mwaka 2017/2018 na kinaonekana tena katika bajeti ya mwaka 2018/19. Naomba ukamilishaji wake ili kusaidia wananchi wa Kisiwa cha Base.
Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za Mfuko wa Barabara; matengenezo ya Sabasaba - Busweru road, tayari Halmashauri inaendelea kulipa fidia kwa wananchi. Niombe utekelezaji wake ukamilike kama ulivyopangwa ili kurahisisha mawasiliano na Makao Makuu ya Wilaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara za lami, mzunguko wa barabara za lami katika Manispaa ya Ilemela ni asilimia sita tu. Naomba ukamilishaji wa malengo yaliyowekwa ili hadhi ya Manispaa ilingane lingane na Manispaa zingine nchini.