Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kuwapongeza Waziri wa Habari, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu, watendaji wote walio chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa kazi nzuri waliyoifanya katika kuhakikisha sekta zilizoko katika Wizara hiyo zinasonga mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo kuna changamoto kadhaa ambazo zinatakiwa kufanyiwa maboresho. Changamoto hizo ni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi cha karibu miaka 30 iliyopita kumekuwa na ulegevu kwa kiasi fulani kwa Serikali yetu kwa kutokuwa karibu na vijana (rika la miaka 12-35), kundi ambalo linahitaji kuelewa, kuelimishwa na kuthaminiwa kwa kuwa vijana ndio nguvu kazi ya nchi yoyote duniani hususan Tanzania. Kwa kuwatumia vizuri vijana wetu watasaidia kuongeza uchumi wa nchi na pia watajiajiri wao wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wasanii wetu wanahitaji elimu ya ujana, mila zetu, utamaduni wa Mtanzania, staha, heshima, nidhamu, utu, utaifa na uzalendo kwa nchi yetu. Haya yote yanahitaji fedha za bajeti katika Baraza la Michezo (BASATA) ili zitumike kwa kuwapatia elimu, mafunzo, warsha, semina, hamasa, matangazo mbalimbali ambayo yatasaidia kuwaelimisha wasanii/vijana wa Kitanzania kuelewa na kujiheshimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ijipange upya katika kutambua na kusimamia vijana wasanii wa aina mbalimbali yaani music, ngoma za jadi, wachoraji, waimbaji injili, muziki wa dansi, waigizaji, wanamichezo na wengine wanaojihusisha na sanaa. Kwani wasanii wana mchango mkubwa katika ustawi wa nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu enzi ya kutafuta uhuru wa nchi yetu ya Tanzania. Kwani wasanii wetu walikuwa bega kwa bega katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika kwa kuimba na kucheza ngoma za kudai uhuru wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba tena Serikali kutoa fedha za bajeti za kutosha kwa ajili ya kuelimisha wasanii kwani mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Tukiri eneo hili tulilisahau likajilea lenyewe. Tukumbuke vijana ni kundi lenye nguvu na pia wana muda mwingi wa kuishi hapa duniani, tulilee na kulielekeza vema. Msanii Diamond anaiwakilisha Tanzania anahitaji kuelimishwa na kulelewa vema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga hoja mkono kwa asilimia mia moja.