Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono asilimia 120.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuwapongeza viongozi na watendaji wote walioko katika Wizara hii kwa kazi nzuri waliyofanya wakiongozwa na Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Makatibu Wakuu, hakika nawapa pongezi kubwa kwa bidii na uzalendo mlionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo, kuna changamoto kubwa zinatakiwa kupatiwa ufumbuzi/ majibu ili kuleta tija na iweze kupatikana kwa nchi na wananchi kwa ujumla. Changamoto hizo ni kama ifuatavyo; Vyuo vya Ufundi - VETA na uwekezaji mkubwa, Serikali kutumia mitaala kwa lugha ya kiswahili kwa vyuo vya ufundi/VETA kwa ajili ya vijana wanaomaliza darasa la saba, vyuo vya kati kutobadilishwa kuwa vyuo vikuu na elimu ya watu waliyoikosa (elimu ya watu wazima).

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyuo vya Ufundi (VETA) kumekuwa na speed ndogo katika uwekezaji na ujenzi wa vyuo vya ufundi katika nchi yetu na kuzingatia kuwa eneo hili ndilo linalobeba vijana wengi ambao ndiyo nguvu kazi ya Taifa lolote duniani. Kutowekeza katika vyuo vya ufundi
kutasababisha wimbi la vijana kutojishughulisha na kazi na hasa vijana wengi kukimbilia kufanya biashara za kimachinga ambazo ni za kubahatisha na pia kujiunga na makundi ya hovyo/ulevi, kushiriki kwenye mitandao yenye kuharibu maadili yetu ya Kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali iwekeze kwa kiwango kikubwa katika ujenzi wa Vyuo vya Ufundi (VETA) majengo, walimu, vifaa vya kujifunzia, wataalam wa fani ambazo zitakidhi soko la ndani na nchi jirani zinazotuzunguka, mitambo na teknolojia zinazoendana na wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutumia mitaala ya kiswahili kwa Vyuo vya Ufundi (VETA) kwa ajili ya vijana wa darasa la saba kumekuwa na ufanisi mzuri kwa vijana wetu waliomaliza darasa la saba ambao hujishughulisha na kazi ya ufundi kutengeneza magari, mafundi wa umeme wa magari, mafundi welding, mafundi waashi, mafundi mchundo, mafundi wa umeme wa majumbani, mafundi wa computer na kadhalika. Hawa wote kwa asilimia kubwa ni vijana waliomaliza darasa la saba na form form.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuzingatia hayo yote ni vema Serikali ikatumia mitaala ya kiswahili kwa Vyuo vya Ufundi na VETA ili itumike kwa vijana wetu wa standard seven na form four ambao wote hawa ndiyo nguvu kazi kubwa inayojihusisha na fani za aina mbalimbali za ufundi. Kwa mafunzo hayo, vijana wataweza kuongeza tija na ufundi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vyuo vya kati kubadilishwa kuwa vyuo vikuu; kumekuwa na ongezeko la kubadilisha vyuo vya kati na kuwa vyuo vikuu hali hii inadhoofisha vyuo vya kati ambavyo ndivyo vyenye kulenga kutengeneza ajira kwa vijana wengi. Naomba Serikali isitishe suala la kubadilisha vyuo vya kati kuwa vyuo vikuu na badala yake vyuo hivyo viimarishwe kwa kiwango kikubwa na miundombinu ya ufundi, wataalam, wakufunzi na kadhalika, uwekezaji wa vyuo hivyo kwa kuzingatia soko la ndani kama inavyofanyika nchi ya Singapore.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi ya Singapore inawekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya elimu ya ufundi kwa kulenga soko la ajira kwa vijana na kuangalia soko la ndani na nje (nchi jirani). Nchi hiyo inatengeneza vifaa vingi vya kielektroniki kama vifaa vya umeme vya aina zote. Hii imesaidia vijana wengi kwa asilimia 95, vijana wako viwandani wanazalisha bidhaa mbalimbali.