Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Anastazia James Wambura

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwa maandishi. Kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mwijage na Naibu Waziri wake Mheshimiwa Manyanya, pamoja na timu yao ya watendaji wa Wizara kwa jinsi wanavyosimamia vizuri Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri, ili viwanda vyetu viweze kufanya kazi kwa tija ni lazima kuhakikisha ipo malighafi ya kutosha. Katika mikoa inayolima korosho, msimu huwa unaisha mwezi Desemba, inashangaza sana kuona kwamba wateja wa korosho iliyobanguliwa wanapoagiza bidhaa hii tena tani 50 tu kwa mwezi. Inakosekana kwa madai kwamba hakuna malighafi wakati ambapo mahitaji yenyewe yametoka mwezi wa pili. Hii inamaanisha kwamba uzalishaji katika viwanda vyetu huwa ni kwa kipindi cha miezi mitatu tu (Novemba, Desemba na Januari).

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba jitihada ifanyike kufuatilia tatizo ni nini. Je, ni ukosefu wa mitaji ya kununua malighafi ya kutosha au ni kukosa mgao wa kutosha ikiwa na maana ya kibali cha ununuzi kimewabana wenye viwanda? Kaeni na wenye viwanda vya korosho na Wizara ya Kilimo ili kujadili namna bora ya kuwezesha upatikanaji wa korosho kwa viwanda vyetu katika kipindi cha mwaka mzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vyetu vidogo bado vina changamoto kubwa ya kukatikakatika umeme hovyo na ukosefu wa maji na hivyo kuathiri uzalishaji kwa ufanisi na tija. Wizara ya Viwanda ikae na Wizara ya Maji na Wizara ya Nishati ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu itolewe kwa wajasiriamali kuhusu namna ya kuanzisha viwanda vidogo. Naunga mkono hoja.