Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa Serikali itueleze viwanda vilivyobinafsishwa mwaka1992, kati ya156 ni vingapi vinavyofanya kazi na visivyofanya kazi ni vingapi na wale waliopelekea hasara hii wamechukuliwa hatua gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi walio wengi zaidi ya asilimia 80 wanaishi vijijini na kule ndiko kilio kilipo, pamoja na Serikali kupeleka umeme vijijini lakini umeme ule ni mdogo sana hata kuwasha taa. Serikali iliahidi kuwekeza katika viwanda vidogo vidogo lakini vimeshindwa kabisa, lazima pawepo na mgongano wa biashara,vyakula viwe process kule kule vijijini na hii itasaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vijana kutokimbilia mjini kutafuta ajira na wengine kuingia katika vitendo viovu. Serikali ije na itueleze nia na mikakati gani ya kuhakikisha mazao yanaongezewa thamani kule kule ili wakulima wapate faida. Hivyo lazima pawepo na viwanda vidogo na vya kati huko vijijini. Wakulima wengi sasa hivi mazao yao yanaozea kwenye maghala kwa kukosa masoko, mfano mahindi na mbaazi wakulima wengi sana wamepoteza mitaji hata ya kuendeleza kilimo chao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mji wa Moshi ulijulikana sana kwa kuwa na viwanda vya misumari, ngozi, makaratasi, viberiti mpaka kiwanda cha dawa lakini sasa hivi kinachofanya kazi tena kwa kuharibu mazingira ya Moshi, harufu mbaya inayochangia afya ya wakazi wa Pasua na Boma Mbuzi ni Kiwanda cha Ngozi. Je, Serikali ina mikakati gani hata ya kufufua Kibo Match, viwanda hivi vilichangia sana kupata ajira kwa vijana wetu lakini cha kusikitisha kwa sasa vingi vimeugezwa kuwa stoo za kuhifadhia vitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda bila kuwa na umeme na maji ya uhakika tutakuwa tunaviongelea viwanda hivi kwenye vitabu na cha zaidi mazingira ya kufanya biashara hapa nchini ni magumu sana, mpaka mfanyabiashara apate kibali cha kufanyia biashara inaweza hata kutumia zaidi ya mwezi. Pia mfumo wa kodi na tozo ni nyingi mno na hii inachangia wafanyabiashara wengi kufanya biashara au kuhama na kwenda kuwekeza kwenye nchi nyingine. Serikali ifanye kazi kwa pamoja kabla TRA haijatoa makisio, basi wawapatie leseni wafanyabiashara wafanye kazi nchini wajue wanawapa makisio ya kiasi gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bei za bidhaa zimekuwa hazipo elekezi Serikali inatoa tu matamko ya kisiasa mfano ilitoa tamko sukari iuzwe shilingi 2,500 kwa kilo lakini sukari inauzwa mpaka shilingi 3,000 kwa kilo sababu hakuna chombo kinachofuatilia bei hizi. Hivi Tume ya Bei (Price Commission) haipo? Pamoja na masoko kuwa huria lakini lazima Serikali iangalie ni jinsi gani wataweka system ya kufuatilia bei za bidhaa kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitafuta mwekezaji kwa ajili ya kiwanda mama cha Machine Tools kilichopo Kilimanjaro. Pamoja na vipuri kupitwa na wakati lakini majengo bado yapo, sasa Serikali imefikia wapi kupata uwekezaji wa kuendeleza kiwanda hiki ambacho kingekuwa mkombozi wa kutengeneza viwanda vidogo na vya kati ili viweze kufanya kazi vijijini?