Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Juma Othman Hija

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tumbatu

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi kwa kunipa fursa hii ya kuchangia katika hotuba hii ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Pili, nampongeza Waziri na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwakilisha ripoti hii kwa umakini mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali yetu kwa kutangaza na kuweka azma ya kuifanya nchi yetu kuwa nchi ya viwanda. Jambo hili ni jema lakini linahitaji matayarisho makubwa ili kufikia lengo. Lazima tuwe na rasilimali za aina zote hasa rasilimali watu na vifaa (Human Resource and Materials).

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ushauri wangu kwenye kutayarisha rasilimali watu lazima tuwatayarishe vijana wetu kwa kuwapatia taaluma inayohusu viwanda. Haitakuwa vizuri leo tuna vijana waliomaliza vyuo wengi, tukatumia wataalam wa kigeni badala ya vijana wetu kwa ukosefu wa ujuzi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutayarisha rasilimali vifaa ni lazima Serikali itilie mkazo kwenye sekta ya kilimo. Kilimo ndiyo msingi wa kila jambo pamoja na viwanda. Hivyo, Serikali ni lazima kuiwezesha kwa maeneo yote sekta ya kilimo kwa kuipatia vitendea kazi na ruhusa zote zitakazo fanikisha azma hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.