Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

Hon. Dr. Immaculate Sware Semesi

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo

MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI: Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za maendeleo zinazotolewa na Hazina zimekuwa zikipungua kila mwaka na kusabaisha madhara kwa Watanzania 70% wanaotegemea rasilimali ardhi kwa shughuli za kilimo. Ushauri; Wizara ijipange ili kuhakikisha inatengewa fedha za kutosheleza ili kufanikisha malengo yake. Wizara iunde strategic team ili kufanya tathmini na kuja na mikakati mahususi ya kuiwezesha kutengewa na kupatiwa fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Kilimo haijaweka mikakati ya wazi ya kufungamanisha sekta ya kilimo na sekta ya viwanda, wakati ni dhahiri malighafi (raw materials) nyingi za viwanda husika zinategemea products za kilimo. Ushauri; Wizara ya Kilimo iweke wazi uhusiano wake na sekta ya viwanda, hii pia italeta chachu ya kutengewa bajeti halisia, itasaidia ku-justfy umuhimu wa sekta ya kilimo katika kukuza na kuimarisha viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu pembejeo; kuna changamoto nyingi sana katika eneo hili, maeneo mengi nchini yamekuwa na kilio cha kukosa mbolea ama kutopata kabisa ama kuja kwa kuchelewa sana. Mbolea zimekuwa za ubora hafifu maeneo mengi, hususan ya vijijini kwa sababu za miundombinu mibaya ya barabara mbolea imekuwa ya bei ya juu sana. Sekta hii imekosa mfumo thabiti wa kuuzia pembejeo zisizo na ubora kwenye soko. Mfumo wa sasa wa bulk procurement kwenye mbolea umeongeza changamoto kwenye biashara ya mbolea. Ushauri, Wizara ijitathmini kwa upya na kuja na solution ya kudumu katika kuwezesha/ kuboresha mfumo mzima wa upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika sekta ya kilimo (wataalam na maafisa ugani) ambao wameajiriwa na wachache waliopo wanafanya kazi katika mazingira magumu (ukosefu wa vitendea kazi). Ushauri, Wizara ije na document inayoonesha ni wataalam wangapi wanaohitajika na katika maeneo gani na kufikisha suala hili katika taasisi/Wizara husika ili lipatiwe ufumbuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mapungufu makubwa sana ya udhibiti wa mazao baada ya kuvuna (post harvest losses), hali hii husababishwa na idadi ndogo sana ya maghala nchini, kwa sasa kuna takribani maghala 1,200 wakati kuna vijiji 13,000. Hali na hadhi/teknolojia zinazotumiwa wakati wa kuvuna na kusindika mazao ni duni sana. Hali hii husababisha upotevu mkubwa wa mavuno, takribani 20% ya mazao hupotea baada ya mavuno. Ushauri; Wizara ijipange kimkakati na hata kushirikisha private sector kuhakikisha angalau kila kijiji/kata kinakuwa na ghala la kisasa linaloendana na mazao husika yanayolimwa katika eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni dhahiri kilimo sio kipaumbele kwa Serikali (rejea kitabu cha mpango cha sasa). Basi ni bora Wizara ikajitathmini kwa ujumla wake ili Wizara hii muhimu na nyeti ikawa more visible.