Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tumbatu
Contributions
nil
Answers
nil
Commettees
1
Ministries
nil
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia katika hotuba ya Waziri wa Kilimo. Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Kilimo pamoja na watendaji wake wote kwa kuandika na kuiwakilisha hotuba hii kwa ufanisi mkubwa. Katika kuchangia hotuba hii ya kilimo, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuipongeza Wizara kwa juhudi zake inayochukua kuimarisha na kuhamasisha wakulima wa nchi hii. Wakulima wa nchi hii wameendelea kuonesha juhudi zao katika kilimo cha mazao tofauti hasa yale mazao ya biashara. Juhudi hizi zimeonekana kudorora kutokana na upatikanaji wa masoko ya kuuza mazao hayo. Wakulima wamekuwa wakilundika mazao yao katika maghala kwa muda mrefu jambo linalopelekea kuvunja moyo kwa kiasi fulani. Hivyo nachukua fursa hii kuiomba Serikali kupitia Wizara hii kulichukulia suala hili la kuwatafutia masoko ya uhakika wakulima wetu ili wawe na uhakika wa kuuza mazao yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali yetu kupitia Wizara ya Kilimo inachukua juhudi ya kutafuta namna ya kuboresha kilimo kwa kuwatafutia wakulima wetu zana za kilimo. Nachukua nafasi hii kuipongeza Wizara kwa jambo hili zuri. Imeonekana kuwa jambo hili lina tatizo la wakulima wetu kutomudu kununua zana hizo za kilimo hasa matrekta. Hii ni kutokana na bei kubwa ya ununuzi wa matrekta. Wakulima wa nchi hii, idadi kubwa ni wakulima wa kipato cha chini/kati kiasi ambacho uwezo wao ni mdogo sana. Hivyo naiomba Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuangalia utaratibu mzuri wa kuwawezesha wakulima kupata zana hizi kwa kuwapunguzia bei au kuwakopesha kwa masharti nafuu wakulima wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.