Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

Hon. Lucy Fidelis Owenya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadilio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Maliasili na Utalii

MHE. LUCY F. OWENYA: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru. Utalii unachangia asilimia 17.5 kwenye Pato la Taifa, lakini utalii ungeweza kuchangia zaidi kama tungeweza kuwekeza katika kuiwezesha TTB iweze kutangaza utalii zaidi.

Mheshimiwa Spika, ni jambo la kusikitisha TTB inapewa 2.4 billion kwa ajili ya matangazo, watatangaza nini? Kutangaza CNN tangazo moja tu ni shilingi bilioni 1.2, wakienda kwenye maonesho/exhibition, mfano wameenda Ujerumani ITD, pavilion moja ni zaidi ya shilingi milioni mia nne, sasa watatangazaje utalii wa Tanzania?

Mheshimiwa Spika, uki-compare na nchi za jirani, mfano nchi kama Kenya, imetenga shilingi bilioni ishirini na sita kwa ajili ya Kenya Tourist Board, South Africa imetenga shilingi bilioni 60, Namibia wametenga shilingi bilion 20, Uganda yenyewe, nchi ndogo kama Uganda imetenga shilingi bilioni nane kwa ajili ya kutangaza utalii. Sasa hapa kwetu tutautangazaje utalii bila kuiwezesha TTB?

Mheshimiwa Spika, 2.8 billion Mheshimiwa Spika, tunazungumzia watalii kuwa wengi, Mheshimiwa Waziri amesema watalii wa Tanzania wamefika 1.3 million ambao wamekuja kuitembelea Tanzania. Lakini, Kenya pamoja na matatizo na waliiondoa VAT lakini watalii wa Kenya wamekuwa ni wengi kuliko Tanzania, walikuwa milioni milioni na laki nne.

Mheshimiwa Spika, sasa kama ni mambo yale unayosema ya VAT haiku-affect Tanzania naomba mkakae mfanye tathmini upya, muangalie kweli kama VAT haiku- affect utalii wa Tanzania kwa sababu ile VAT iliyoongezeka ukiangalia zile fedha za mwaka juzi hiyo piece iliyoongezeka ni ile VAT 18% iliyoongezeka, kwa hiyo mapato hayajaongezeka. Kwa hiyo, naomba mlitathmini upya suala zima la VAT katika utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine kwenye masuala ya wafanyabiashara wa utalii ni hizi tozo, mlolongo wa tozo. Unakwenda kwenye ofisi ya mtu unakuta imepambwa na certificate nyingi tu, wafanyabiashara hawakatai kulipa kodi lakini tunaomba mfanye basi iwe dirisha moja, maana time is money huwezi kumchukua mfanyabiashara anatoka ofisi hii anaenda ofisi hii, mnampotezea muda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ikiwa ni kwenye dirisha moja, watalipa hizo kodi. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri tunaomba sana mfanye iwe ni kwenye dirisha moja na wafanyabiashara watalipa hizo tozo kwenye dirisha moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna kitu nimekuwa nikizungumzia hapa mara nyingi kuhusu volunteers. Kuna hawa wanafunzi wanatoka nje, they are just 16/14 years old, wanakuja wazazi wao wanakusanya pesa kule kwenye nchi za nje wanakuja wanafanya community work, wanajenga mashule, wanajenga madarasa, mabwalo na kila kitu. Kazi ya hawa wanafunzi wanakuja kama wiki mbili, wanakuja wanapiga rangi, wanajenga madarasa lakini wanatumia mafundi watanzania wao wanataka tu ile adventure. Lakini unakuta Serikali naomba na Wizara ya Mambo ya Ndani mnawa-charge dola 500 za kufanya kazi pamoja na dola 50 za tourist visa, lakini wale watoto hawafanyi kazi wakija Tanzania wanafanya hiyo community work kwa siku saba lakini wanaenda kupanda Mlima Kilimanjaro, wanaenda Ngorongoro wanaenda Serengeti mpaka Zanzibar. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hii, kazi hiyo wanaofanya ni part of tourism sasa badala ya kuwa-encourage kwamba waendelee na hiyo part of tourism ambayo tumeianzisha, sasa mnawafanya wanaacha wengine wamehamia Mombasa kwa sasa hivi. Kwa hiyo, Mombasa wamewapokea na wanafanya hizo community work kule, kule Moshi wamejenga shule nyingi tu lakini sasa hivi wame- cancel zile booking wanaenda Mombasa.

Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba uliangalie hilo ili muweze kuwafanya hawa wafanyakazi warudi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoongelea Mlima Kilimanjaro kila siku tunaonga hapa kuhusu Mlima Kilimanjaro. Mlima Kilimanjaro unaiingizia mapato Serikali mapato mengi sana, lakini bado tumeshauri mara nyingi ili kulinda mazingira kwa kuanzia tu, tunaomba ile njia ya Machame route mjenge mahema kwa ajili ya kulia mess tents, nataka nijue pamoja na vile vyoo kutoka Ujerumani vilikuwa vya majaribio chemical toilets vimefikia wapi.