Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Hon. Janeth Maurice Massaburi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

1

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu na Watendaji wote walioko katika Wizara hii. Pamoja na pongezi nina machache yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itenge fedha za kutosha kwa Balozi ambazo zinatumika nchi tatu mpaka tano ili Balozi aweze kuzitembelea na kutafuta fursa za kiuchumi kama utalii, viwanda na usalama na uwakilishi uwe wenye manufaa katika nchi hizo. Ofisi za Ubalozi zitengewe fedha za ukarabati wa ofisi za ubalozi na nyumba za watumishi katika Balozi husika ili ziendane na hadhi ya nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, viwanja vya Ubalozi ambavyo havijajengwa vitengewe fedha kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Ubalozi na makazi ya Balozi zetu na watumishi wake. Kwa mfano, kiwanja cha Ubalozi Jijini London kimetelekezwa na kimejaa magugu na mbwa mwitu. Kila ofisi za Ubalozi wetu nje ya nchi ziwe na wataalam wa fani ambazo zitasaidia kuiuza nchi yetu kiutalii, kiutamaduni, lugha ya Kiswahili, kuvutia wawekezaji kuja Tanzania kujenga viwanda, Kujenga hospitali za kitalii kwenye website ya kila Ubalozi kuwe na vivutio vyote vilivyoko katika nchi yetu ili kila mtalii aamue ni eneo gani anapenda kwenda kutalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano, kuna mazoea ya kuona vivutio vichache tu Serengeti National Park, Mlima Kilimanjaro, Ngorongoro Crater, Zanzibar lakini ukiangalia nchi yetu ina vivutio vingi sana kama, Kitulo National Park, Ruaha National Park, Manyara National Park, Mahale National Park, Maporomoko ya Kalambo (Rukwa), Gombe National Park, Saa Nane Island, Arusha National Park, Tarangire National Park, Udzungwa National Park, Kilimanjaro National Park, Serengeti National Park, Selou National Park, Majengo ya Kale Kilwa, Mafia, Bagamoyo, Olduvai George, Nyagoza Mtu wa Kale, Mapango ya Amboni Tanga, Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere – Butiama, Fukwe za Bahari, Utalii wa Water Sports (Bahari na Maziwa Victoria, Tanganyika na Nyasa - Matema Beach). Maeneo ya kale Mtwara Mikindani na Utamaduni wa Ngoma za asili na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vivutio hivyo vyote na vingine ambavyo sikuvitaja viwekwe kwenye matangazo mbalimbali duniani na hasa ziwekwe kwenye website za kila Balozi zetu nje ya nchi. Balozi ziandae maonesho kwa lengo la kuitangaza nchi yetu ya Tanzania, katika sekta za utalii, kiutamaduni na kutumia fursa ya kijiografia ya nchi yetu kupakana na nchi zaidi ya tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.