Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza niungane na Bajeti Mbadala ya Kambi ya Upinzani na pia ni- endorse statement ya KUB, Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe kwamba Awamu hii ya Tano imekuwa na bajeti hewa endelevu ikiwemo bajeti hii. Bajeti hii ni hewa kwa sababu haifikii malengo.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2016/2017 malengo yalikuwa trilioni 29 zilipangwa, lakini only trilioni 20 zilitoka. 2017/2018, trilioni 31 lakini only trilioni 21 zilitoka. Makisio wanaweka makubwa kuliko uhalisia wa vyanzo vya mapato, kwa hiyo wanaleta makisio hewa na wanajua kabisa kwamba ni hewa kwa sababu haliwezi gap lile likawa linajirudia kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii inafanya matumizi nje ya bajeti iliyopitishwa na Bunge lako. Kwa mfano ujenzi wa ukuta Mererani, hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ujenzi wa airport Chato, suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma, haya yote yanaweza yakawa mambo mazuri, lakini ili yakamilike katika uendeshaji wa nchi yalitakiwa lazima yapite kwenye Bunge lako Tukufu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata Sera ya Viwanda ni hewa kwa sababu kila siku tunaskia mnazindua viwanda vipya na kuhesabu idadi imeongezeka, mara viwanda 3,000 tayari siku mbili unasikia kuna viwanda 4,000, hatuoneshwi ujenzi tunaoneshwa uzinduzi. Hii maana yake ni nini; maana yake ni kwamba hawa jamaa wanazindua viwanda ambavyo vipo toka zamani. Kwa mfano kulikuwa na kiwanda kimoja Mwanza, sitaki kukitaja, kilishazinduliwa toka mwaka 2013 huko na marehemu Kigoda, Waziri wa Viwanda, lakini juzi naangalia kwenye taarifa ya habari naona Waziri Mkuu anakwenda kuzindua tena kiwanda kile kile ambacho mimi taarifa zake za uzinduzi nilikuwa nazo. Kwa hiyo tunakwenda na vitu hewa.

Mheshimiwa Spika, sasa mimi nabaki najiuliza; huyu Mheshimiwa Dkt. Mpango alikuwa ametoka, alikuwa ni Katibu wa Tume ya Mipango kwenye Awamu ya Nne chini ya Dkt. JK na nchi ilikuwa inakwenda, sasa hivi wamemweka juu zaidi, ni Waziri kwenye Awamu ya Tano, lakini mambo hayaendi kiasi kwamba najiuliza kweli hii mipango ni ya kwake au kuna mtu anapanga wana-impose tu kwenye makabrasha yake aje kusema humu Bungeni? Hivyo ndivyo vitu ninavyojiuliza, nina uhakika kabisa mipango hii siyo ya Mheshimiwa Dkt. Mpango, kuna mtu anapanga hii mipango sasa sijui anatumia vigezo gani.

Mheshimiwa Spika, sababu zinajulikana, otherwise Wabunge wa CCM hususani wamejaa unafiki. Asilimia 98/99 ya Wabunge wa CCM wanalalamika pamoja na sisi mambo yanavyokwenda, hawaridhiki na hali inavyokwenda katika Awamu hii ya Tano lakini hawasemi hadharani. Sasa sisi tukisema nje wanatulaumu, wanasema sasa ninyi tunawaambia halafu mkifika ndani… (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mbilinyi, ukisema Wabunge wa CCM ni wanafiki unajua unamsema na Spika pia?

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Hapana, wewe uko exempted kwa sababu hata sasa hivi umeonesha kidogo unanyoosha Kiti kusema ukweli, kwa hiyo tunakupa tano zako. Wakifanya vizuri tunawasifia, wakikosea tunakosoa na tunapokosoa hatuna chuki, no personal vendetta against anybody. Tunapochangia na kukosoa, yote ni kwa ajili ya Taifa hili tukiamini kwamba Taifa hili ni letu sote.

Mheshimiwa Spika, sasa hawa wenzetu wanalalamika nje; kwenye korido huko, kwenye chai na ukisema wanasema kwamba ninyi tunawaambia mkifika ndani tena mnatutoa nishai. Of course lazima tuseme ili nchi iende, wanataka tukae navyo sisi moyoni na sisi tupate presha, presha bakini nazo ninyi wenyewe.

Mheshimiwa Spika, hawa watu wanaokaa kimya ni hatari zaidi kuliko sisi tunaosema. Niseme, mtu kama Mheshimiwa Bashe, Mheshimiwa Nape, Mheshimiwa Alhaji Bulembo hawa siyo tatizo ndani ya CCM kwa sababu hawa angalau wanaongea, tatizo ni ninyi msiosema halafu mnalalamika kwenye makorido (corridors). (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunatakiwa tujue kitu kimoja; katika Taifa la watu almost 55,000,000, sisi tuliomo humu 300 plus, sisi tuko privileged to serve, sasa tusije tukatumia hii privilege to serve kusaliti wananchi; huku unasema hivi huku unasema vile. Halafu kitu kimoja nimefanya utafiti nimegundua, you guys don’t love President Dr. Magufuli, ninyi CCM hamumpendi Dkt. Magufuli. Hamumpendi Rais wetu wala hamlipendi hili Taifa kwa sababu mtu unayempenda lazima umwambie ukweli mambo yanapokuwa hayajakaa sawasawa na hili tunalisema kila siku.

Mheshimiwa Spika, hamuwezi kukaa mnalalamika na sisi, mnasema mambo hayaendi lakini mkifika kwenye floor hapa hamsemi ukweli halafu kila mtu akisimama mnam- personalize, mpaka Mheshimiwa Dkt. Mpango anakuja kumfananisha na madikteta wa North Korea kwa ajili ya kupitiliza upambe, yaani unakuwa mpambe mpaka tajiri ananuna, anaona hapa unaharibu, unanifananisha na watu ambao sitaki kufananishwa nao. Kwa hiyo you guys don’t love our president, mngempenda lazima mngemwambia ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niseme, kama nilivyosema, penye ukweli tunapongeza penye tatizo tunasema. Nampongeza sana Rais Magufuli kwa kum-demote, kumtumbua Mkurugenzi Msaidizi wa Usalama wa Taifa TIS, kutoka kuwa Deputy Director mpaka kuwa RAS kwa sababu toka Mheshimiwa Rais amefanya kitendo kile hali ya nchi imetulia kidogo, hatusikii sana mambo ya kuokota watu kwenye viroba, hatusikii watu kupotea toka yule Deputy amekuwa demoted kuwa RAS haya mambo hatuyasikii. Kwa hili nampongeza Rais na aendelee kuchukua mawazo yetu yeye sisi tutampa kwa sababu wao hawataki kutoa mawazo wanafanya unafiki dhidi ya Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nchi hii sasa Mheshimiwa Mbunge kila Taasisi imekuwa kama polisi. Tumetoka kuongea hapo unaona Maafisa wa Wizara wanaanza kutembea na rula kupima samaki, sasa dagaa utapima kwa rula gani, inabidi watutengenezee rula za kupimia dagaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, BASATA nao hawako nyuma kila Taasisi imegeuka kuwa kama polisi, kazi ni kamata, fungia sijui nini. Mimi jana wamefungia nyimbo yangu, inaitwa namba 219, wakati nyimbo hata sijaitoa upambe huo.

Mheshimiwa Spika, na- declare interest mimi ni msanii pia na ni msanii nguli wa hip pop Afrika na duniani na ndiyo nilikotokea na nimetoa mchango mkubwa sana katika sanaa ya muziki wa kizazi kipya, bongo fleva mpaka hapa ilipofikia. Hilo Serikali inatakiwa ilitambue sana na isikilize sana tunapozungumzia masuala ya wasanii na namna inavyotengeneza ajira.

Mheshimiwa Spika, sasa wewe unafungia nyimbo ambayo sijatoa, nyimbo ime-link katika katika industry ya music ku-link kupo, mimi najiandaa kushuti video nyimbo ime- link, BASATA hawajaniita kunihoji, pengine ndiyo nilikuwa nawapelekea hiyo nyimbo waisikilize; wao wanatoa tu statement wanafungia nyimbo ya msanii wakati hawajawahi kuingia studio hata siku moja, hawajui hata mihangaiko ya studio, hawajui hata gharama wanakurupuka tu kufungia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumeijenga hii sanaa miaka mingi mpaka imekuwa ajira, wanataka sisi wote tuimbe mapenzi. Sisi siyo kila mtu lazima aimbe mapenzi, sisi tunaimba masuala ya kijamii…

T A A R I F A . . .

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, kama alivyosema ni kaka yake, kwanza naomba mlinde muda wangu, ningempiga lakini kwa hali dada yangu naomba nimwache, tumsubiri mjomba, sitampiga namheshimu. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ila tu ninachomwambia mimi siyo Roma wala mimi siyo Diamond, naiburuza BASATA Mahakamani kwa suala hili na ndiyo watajua namna gani nchi inatakiwa iendeshwe kwa kufuata utawala bora na sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimeshasema nyimbo imevuja, nyimbo sijaitoa rasmi, wimbo...

(Hapa walijibizana bila kutumia kipaza sauti)

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri Mwakyembe unalielewa suala hili, wimbo umevuja, kwa hiyo BASATA nawasiliana na Mawakili wangu sita ili niwaburuze BASATA Mahakamani, ndiyo watanyooka waache kuchezea kazi za wasanii. Huyo dada yangu Mheshimiwa Shonza mwenyewe hajawahi kuingia hata studio ku-record halafu anakuja anafungia nyimbo za watu kiholela.

Mheshimiwa Spika, nikiacha na hayo ujumbe umeshafika, niombe tu Mheshimiwa Waziri tuondoe siasa kwenye masuala ya uchumi na biashara, nikitangaza interest mimi pia ni mfanyabiashara mchanga ninayeanza.

Mheshimiwa Spika, toka nimeanza kabiashara kangu hawa jamaa wameingiza siasa mara, sijui TRA wamefanya nini, wanakuja wanakuta clear, wanaenda sijui kwenye Taasisi gani wanakuja wanakuta clear, mwisho RSO Afisa Usalama wa Taifa Mkoa anaenda benki iliyonikopesha kuhoji ku-check anakuta kweli mimi nimekopeshwa. Anauliza toka lini mmeanza kukopesha wapinzani? Jamaa akamwambia, Joseph Mbilinyi Mkurugenzi wa kampuni fulani hajaja hapa kama Mbunge, hajaja hapa kama mwanasiasa, amekuja hapa kama mfanyabiashara na mpaka sasa hivi analipa marejesho yake vizuri. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mpango tuache kutumia TRA, tuache kutumia Taasisi zingine ku-discourage wafanyabiashara wachanga kama sisi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.