Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

Hon. Saada Salum Mkuya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019

MHE. SAADA M. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Bajeti ya Serikali. Kwanza kabisa nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango pamoja na Watendaji wote wa Wizara ya Fedha na Mipango kwa kazi nzuri ambayo wameendelea kuifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, truly speaking ni kwamba this time hii bajeti ni very innovative kwa sababu ya measures zake za kodi na naamini kwamba kwa vitendo kabisa tunakwenda kutekeleza ile azma ya East African Community Budget ya Industrilization for job creation na shared prosperity.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maeneo machache ambayo nataka kuchangia. Kwanza ni kuhusiana na madeni ya VAT na Excise ambayo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaidai Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Bahati nzuri leo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesoma Bajeti yake ya Serikali na inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingi trilioni 1.315. Kwa hiyo, kati ya mapato hayo ni pamoja na mapato ya VAT na Excise ambayo yanakusanywa na TRA kupitia TRA ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania upande huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bado kuna deni na Mheshimiwa Waziri nadhani analitambua. Kwa hiyo, tusaidiwe ili kule na kwenyewe maendeleo yaweze kutekelezwa. Kuna shida za maji, barabara; na tunaraji sana wakati tunaingia katika bajeti mpya, bado hizi fedha hazijapelekwa, tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri hili alifanyie uharaka kwa ajili ya kwenda kukamilisha bajeti kwa SMZ. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ni kuhusiana na tozo la VAT kwa upande wa ununuzi wa umeme. Tumezungumza sana na Mheshimiwa Waziri wa Nishati na hili safari hii tumelizungumza lakini limekuwa linakwenda mwaka kwenda mwaka kurudi, limezungumzwa sana na watendaji. Wakati ZECO inanunua umeme kama ni essential supply, kwamba inatozwa na VAT na ZECO anakwenda kuuza Zanzibar mwananchi wa Zanzibar ananunua umeme ukiwa na VAT. Kwa maana hiyo, isingekuwa ZECO kwa sababu tu sasa hivi imesema inasubiri hailipi, hailipi Zanzibar, hailipi Tanzania kwa sababu ya huu mkanganyiko. Hata hivyo ZECO siyo mtumiaji wa mwisho. Kwa hiyo, kutokana na principle ya utozaji wa VAT, mlaji wa mwisho ndio anakwenda kutozwa VAT. Kwa maana hii ni mwananchi wa Zanzibar ambaye anatumia umeme ndiye ambaye analipa VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwananchi wa Zanzibar ndiye ambaye analipa VAT. Sasa inakuwa haiwezekani VAT yenyewe pia ZECO ambaye ananunua umeme kwa ajili ya kwenda ku-supply kule na yenyewe itozwe VAT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Nishati, nimependa siku ambayo anakamilisha bajeti yake, alisema vizuri sana kwamba nishati ama umeme ni siasa; umeme ni uchumi na umeme ni usalama. Amezungumza vizuri sana Mheshimiwa Waziri, lakini sasa hii isi-apply upande mmoja. Tunaomba nishati hii ama huduma hii muhimu iende vile vile isimamiwe kule na wananchi wa kule waweze nao kuendelea na uchumi wao kuweza kusimamia siasa pamoja na usalama uliopo kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana kupitia Finance Bill Mheshimiwa Waziri wa Fedha lirekebishwe, ZECO asinunue umeme TANESCO ikiwa ni pamoja na VAT. Hili ni jambo ambalo linaweza likarekebishwa, maana yake imekuwa tabu miaka nenda, miaka rudi, lakini ni jambo ambalo tunaweza kulirekebisha kupitia Finance Bill. Kwa maana hiyo sasa, badala ya kupunguza hizi kero za Muungano, tunaongeza kero za Muungano kwa sababu tu ya masuala ya administration. Tunaomba na hili lizingatiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kuna baadhi ya taasisi ambazo ni za Muungano ambazo zina-operate Zanzibar, hazilipi umeme ZECO, zinalipa umeme TANESCO. Wanachukua umeme wa ZECO, lakini malipo yanalipwa TANESCO. Nadhani hii haiko sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hili na lenyewe, lile deni ambalo lipo kutokana na huduma hii lilipwe, lakini usimamizi uwe mzuri zaidi. Taasisi za Muungano ambazo zina- operate Zanzibar zilipe umeme Zanzibar, umeme ndiko ambako unakotolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa haraka haraka nimefurahi sana kuona sasa DCF imekamilika na tutakwenda kutekeleza. Nimefurahi kwa sababu Zanzibar wameshiriki kikamilifu katika development mpaka development ya Action Plan ya DCF. Hili napata experience nzuri kwa sababu mimi mwenyewe wakati niko Wizara ya Fedha Zanzibar, nilishiriki katika development ya Joint Assistance Strategy for Tanzania. Utekelezaji wake ulikuwa ulikuwa ni shida kubwa. Shida kubwa ilikuwa inapatikana pale ambapo tupolikuwa tukizungumza hii mikakati miwili, wakati huo kulikuwa kuna MKUKUTA na MKUZA, tuweze ku- harmonize ili twende kwa pamoja tukatafute misaada ya Kibajeti. Haikuwezekana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa hivi hii DCF, tumei-develop vizuri, tume-develop sote, tunashukuru sana kwa ushirikiano uliokuwepo lakini implementation yake iwe ni ya kuweza kuhakikisha kwamba hizi strategies zetu zinakuwa harmonized na kwa maana hiyo tunapokwenda kutafuta misaada iwe tunakwenda pamoja, yaani pamoja na inclusion ya Zanzibar, isiwe tunakwenda separate. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari ya kwenda separate maana yake nini? Maana yake Mheshimiwa Dkt. Mpango tumeweka safari hii GBS kwamba tuna kiasi cha fedha shilingi bilioni 545. Leo Zanzibar wanasoma bajeti yao, wamesema wao hawawezi kuingiza hii GBS kwa sababu hii ni fedha ambayo kwanza haina uhakika. Sasa Mheshimiwa Dkt. Mpango, naomba atakapokuja kujibu hoja aliweke suala la jinsi gani Zanzibar itaweza kushiriki katika ku-mobilize external resources kupitia General Budget Support na DCF ili na yenyewe ipate uhakika wa mapato yake ya kibajeti. Hoja zipo nyingi, lakini tunaomba kwa umuhimu wa pekee hili alipe nafasi aweze kulijibu katika hoja zake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la kiutawala zaidi, Zanzibar leo wakati inasoma bajeti; nadhani sisi Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumesoma tokea Alhamisi, lakini ilivyo Zanzibar, yaani ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tungeweza kusoma bajeti kama vile tulivyokubaliana katika East Africa. Kwa nini hatusomi? Sababu zinaweza zikawa nyingi, lakini ninaloliona ni kwa sababu ya kutokuwa na uhakika wa vyanzo vya mapato kutokana na tax measures ambazo ziko katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili linawezekana. Tax Force ya Tax Reforms tunaomba iwe ina-include Maafisa wa Kodi na wa Wizara ya Fedha ya Zanzibar. Sasa hivi kilichopo, Zanzibar inaalikwa ile siku moja kama ambavyo wanaalikwa wadau wengine wa nje. SMZ ni part ya SMT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba wakati Maafisa wetu wanapoanza kubuni vyanzo vya mapato, wanapoanza ku-develop tax measures za mwaka wa fedha unaokuja from day one, Maafisa wa Kodi wa Zanzibar pamoja na Maafisa wa Sera za kikodi wa Wizara ya Fedha na Mipango ya Zanzibar wawepo katika tax measures. Hii itasaidia sana kuwa na uhakika wa bajeti hata kule upande wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili halihitaji mabadiliko ya sheria wala mabadiliko ya kisera linahitaji uamuzi wa Mheshimiwa Waziri wa Fedha ili hawa watu washiriki tuweze kuondoa huu mgongano wa kikodi na vilevile tutapunguza hizi changamoto za Muungano zinazojitokeza. Pia tutaweza kufanya masuala mbalimbali; kwa mfano, Mheshimiwa Dkt. Mpango safari hii, tumeangalia vizuri, angalau corporate tax imepunguzwa. Maana yake nini? Zanzibar haijapunguza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake nini? Maana yake ni kwamba kama kutakuwa na viwanda vipya vitakuwa attracted sana upande huu ambapo hii corporate tax imepunguzwa kuliko kule. Tungekuwa tumekaa pamoja mwanzo, tukashauriana, tukakubaliana, nadhani hizi tax measures zingekwenda vizuri. Kwa maana hiyo, industraliazation for job creation and shared prosperity ingeweza hata ku-apply kwa upande ule mwingine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tulipo sasa hivi tunapokwenda ndipo tunapoleta mkanganyiko na kwa maana hiyo, baadhi ya kodi haziwezi kutekelezeka, kwa sababu upande mmoja haujawa tayari simpy kwa sababu haujapata muda mrefu wa kuweza ku-mainstream na ku- think about hizi tax measures. Kwa hiyo, hilo ni suala la administration zaidi na naamini kabisa Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa uelewa wake, weledi wake, nia yake njema na nzuri kabisa, hili atalifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi na la umuhimu kabla sijamaliza, tunaomba sana fedha ambayo ilikuwa iende Zanzibar, ipelekwe ifanyie maarifa haraka iende ikasaidie shughuli za kiuchumi Zanzibar. Vile vile masuala ya VAT, tusisubiri consultant kwa sababu ni jambo ambalo linawezekana likarekebishwa kupitia Finance Bill hii ambayo ya mwaka 2018/2019. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, sina zaidi, lakini naendelea kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na Mheshimiwa Naibu wake na Menejimenti nzima ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya jambo hili la leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naunga mkono hoja.