Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

MHE. BALOZI ADADI M. RAJABU: Mheshimiwa
Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja na napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watumishi wote kwa kugeuza Wizara na kuifanya iwe bora. Nawapongeza kwa kuondoa utapeli wa viwanja, migogoro mbalimbali na kuweka nidhamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru kwa kuanzisha mradi wa nyumba ambazo zinajengwa na NHC kule Chatur
- Muheza. Mradi huo umeanza vizuri na Wakandarasi wapo
site.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Muheza hatuna Baraza la Ardhi na malalamiko na migogoro ya ardhi inaongezeka kila siku. Wananchi wa Muheza inabidi waende Tanga. Tafadhali naomba tuangalie uwezekano wa kuanzisha Baraza la Ardhi hapo Mjini Muheza kwa msaada wa Wizara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza miradi mbalimbali ambayo inajengwa na shirika letu la NHC. Miradi hiyo ni mingi, ila bei za nyumba bado ni kubwa. Pendekezo la kuondoa VAT kwa nyumba wanazouziwa wananchi inabidi liendelee kupendekezwa. Kuondolewa huko kutafanya nyumba hizo zinunuliwe kwa wingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Ofisi ya Ardhi Muheza isaidiwe fedha ikarabatiwe, hususan chumba cha kutunza kumbukumbu/takwimu haiendani na vifaa vilivyoletwa. Mheshimiwa Naibu Waziri ameona. Tafadhali naomba liangaliwe, vinginevyo nawapongeza.