Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

Hon. Amb. Adadi Mohamed Rajabu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini

MHE. BALOZI ADADI M. RAJAB: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja na napenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza juhudi zote Serikali inazochukua za kudhibiti utoroshaji wa madini yetu kama uimarishaji wa mifumo ya ulinzi sehemu mbalimbali zenye madini; uboreshaji wa mikataba mbalimbali ya madini na sheria; na uboreshaji na kuinua biashara ya madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi kwa ukuta wa Mererani ambao umesaidia kudhibiti madini ya tanzanite, ila CCTV cameras ijengwe kuanzia sehemu ya ulipuaji; kituo kimoja kitakachokidhi mambo yote kwa pamoja kijengwe hapohapo karibu na mlango wa kutokea, pawepo na benki na sekta zote muhimu. Aidha, mnada wa tanzanite uboreshwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa kiwanda cha kusafisha/kuchakata madini ufanywe kwa haraka ili kuongeza thamani ya madini yetu badala ya kupeleka India.

Mheshimiwa Naibu Spika, Muheza maeneo ya Amani – Sakale, Kata ya Mbomole kuna madini ya dhahabu na wananchi kila mara wanakamatwakamatwa na kufukuzwa. Nimemuomba Naibu Waziri, Mheshimiwa Doto, wiki iliyopita anitumie wataalam tujue tuna madini kiasi gani, je, yapo Milima ya Sakale? Je, yapo katika Mto Kihara? Kama ni hivyo tutengeneze utaratibu mzuri wananchi wa Muheza waanze kuchimba huko Mlimani Sakale.