Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Rev. Peter Simon Msigwa

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Iringa Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uzima tena tumerudi mahali hapa kama kawaida. Bila kusahau, nampongeze Msemaji wa Kambi ya Upinzani, Mheshimiwa Halima Mdee kwa hotuba iliyosheheni mawazo pevu ambayo naamini Mheshimiwa Dkt. Mpango atayafanyia kazi. Sisi kama Wapinzani tumekuwa tukitoa ushauri mwingi, kwa manufaa ya Taifa hili na Serikali hii namshauri Waziri apitie kitabu cha Sera Mbadala za CHADEMA zitamsaidia katika kuandaa mpango kwa sababu tunapenda kulisaidia Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema haya, tumekuwa tukitoa mpango wa mwaka mmoja mmoja kutoka kwenye mpango wa miaka mitano. Kwa experience ambayo imeonekana sasa hivi, hasa hii miaka miwili ya karibuni, kuna miradi mingi imeingizwa ambayo haikuwepo kwenye mpango wa miaka mitano, jambo ambalo linatufanya tuonekane kama Taifa hatujui tunakotaka kwenda lakini ni wakati muafaka wa kujitafakari kama Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mdee katika hotuba amezungumzia sana kuhusiana na suala la Katiba, kwamba ni kipaumbele na kilio cha wananchi na amesema kwamba mipango yote mizuri hii kama hatutaangalia kilio cha wananchi itakuwa haina maana. Kwa kuongezea hapo, Mheshimiwa Dkt. Mpango nataka tujiulize maswali kama manne kama Taifa tunapoendelea na mipango hii, vinginevyo tutakuwa tunapoteza muda na tunapoteza kodi za wananchi. Hebu tujiulize kama Taifa, tunapopanga mpango huu nchi yetu kidiplomasia ikoje as we speak? Mahusiano yetu na mataifa mengine yakoje? Wanatuonaje kama Taifa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mkapa aliwahi kusema, Tanzania inauhitaji ulimwengu kuliko ulimwengu unavyoihitaji Tanzania. Ni maneno ya hekima ambayo tunatakiwa tuyatafakari, watu wanatuonaje kwa sasa? Katika historia haijawahi kutokea, tunamkuta hata Balozi wa EU anaitwa kujadili mahusiano na Taifa letu, kuna nini? Tunatakiwa tujiulize, tunazungumza masuala ya kujipanga, lazima tujue Taifa letu limekaaje Kimataifa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tujiulize foreign investors wanaionaje nchi yetu, are they comfortable kufanya biashara katika nchi yetu? Hatuwezi kukaa kimya tukajipongeza hapa tukawa na sifa nyingi na pambio lakini hatujiulizi haya maswali. Wawekezaji wanajionaje kuwepo katika nchi hii? Wako salama, wanaweza wakafanya biashara zao? Takwimu zinaonesha kwamba foreign investors wanafunga virago wanaondoka katika nchi yetu kwa sababu wanaona hawako salama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, wawekezaji wa ndani wako salama? Hiyo purchasing power kwa watu wetu ipo? Haiingii akilini matajiri wa nchi hii wote hawana raha. Kama tajiri mkubwa, bilionea, anaweza akakamatwa katika nchi hii, akatekwa, akafichwa, akarudishwa, mambo yakaendelea kama yalivyo, nani atakuwa na raha ya kutaka kuleta hela katika nchi hii akafanya biashara? Serikali haisemi chochote, hatujui nani amemkamata, amerudishwa, alivyokamatwa hajapewa hata nafasi ya kusema alikuwa wapi, nani atakuja kuweka biashara hapa ndani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo hatuwezi kufumba macho kwamba hayapo katika nchi. Bado mnataka tukuze uchumi, haya ni masuala ambayo kama Wabunge lazima tujadili. Serikali lazima iwe accountable, usalama wa wafanyabiashara wetu ukoje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezungumza mambo ya kidiplomasia. Kuna clip moja ilikuwa inatembea, kuna Wanaigeria wawili walikuja hapa nchini wameitangaza dunia nzima jinsi ambavyo hatuko friendly kwa wageni. Kuna clip moja inamwonesha mtu wa Denmark/Danish alikuja kuwekeza, anamwomba Rais aingilie kati, hatuko friendly kwa hawa wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Mheshimiwa Dkt. Mpango Serikali haieleweki inaendesha uchumi wa aina gani? Ni uchumi wa ujamaa na kujitegemea hundred percent ambao Mwalimu Nyerere alishindwa wakati ule au ni uchumi wa aina gani, tufafanuliwe. Kama ni uchumi tufafanuliwe watu wanakuja kuwekeza katika uchumi wa aina gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, tujiulize, mazingira ya civil servants, katika Awamu ya Tano kila mtu amekuwa intimidated, kila mtu ametishwa. Tumezungumzia masuala ya Katiba, Taifa letu kwa sasa haliko united. Tunatakiwa tuwe na kitabu kimoja, tuwe na Katiba ambayo inatu-unite Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati tunapigana Vita ya Uganda, Mwalimu Nyerere alituunganisha wote, tuliona umuhimu wa kupigana Vita ya Uganda, lakini leo vita ya uchumi ni kubwa ambapo wote kwa pamoja tunatakiwa tushikane na kitu kinachoweza kutushikanisha ni Katiba. Hivi tunapozungumza maofisini watu wako timid, wana hofu, culture of impunity imekuwa ya hali ya juu sana, kila mtu anafanya anavyotaka halafu watu hawachukuliwi hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa bahati mbaya sana Mheshimiwa Waziri Mkuu yuko hapa, hasa wateule wa Rais, wanaonekana wanamtii Rais peke yake, hakuna chain of command, kila mtu ni kambale. Utakuta Ma-DC hawaheshimu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa hawaheshimu Mawaziri, kila mtu anafanya anachokitaka. Hii imesababisha kusiwe na discipline katika utendaji kazi katika ofisi za umma. Ni wakati muafaka kama Taifa kuji-unite pamoja, tuwe pamoja; upinzani ndani ya Serikali, watendaji wa umma na watu wote tushikamane pamoja ili tulijenge Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii culture of impunity, mfano mzuri ni bwana mkubwa mmoja hapa kila siku anatoa mambo ya ajabu. Ametoa matamko ambayo tumesikia hata watalii hawataki kuja nchi hii. Utakuzaje utalii kwa namna hii? Halafu Serikali mnasimama mnasema aliyoyasema ni ya kwake yeye, siyo msimamo wa Serikali. Sasa anawezaje mtu kusema mambo yake kwa kutumia instruments za Serikali? Amekaa kwenye ofisi na bendera ya Serikali na Polisi wa Serikali wanamlinda halafu mnasimama mnasema aliyoyasema ni ya kwake mwenyewe. Kama yake mwenyewe mbona hamjamchukulia hatua? Unatumiaje ofisi ya Serikali halafu mnasema ni ya kwake mwenyewe? Hatuwezi kujenga uchumi katika Taifa ambalo liko scattered, Taifa ambalo limetawanyika na halina umoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Utalii naye anasimama bila kuangalia madhara ya vile anavyo-twit; ana- twit, saa hiyo hiyo London nao wanarudi na majibu kwamba tuna-cancel trip na mnajua utalii unachangia fedha ya kigeni asilimia 17. Sasa tutajengaje uchumi wa namna hii Mheshimiwa Mpango na unapimaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapaswa tuweke mambo ya msingi. Tukianza na mambo ya msingi mambo ya juu yatajijenga yenyewe lakini kuna matatizo, wafanyakazi hawako comfortable…

T A A R I F A . . .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, we are in a serious business, tunazungumzia masuala ya uchumi na masuala ya uchumi yakiyumba tutayumba wote hapa. Hizi mbinu ambazo Serikali ya Awamu ya Tano inazitumia ni mbinu ambazo zilitumika karne ya 17 hazifanyi kazi leo. Katika jamii hii watu wanatishwa, hakuna usalama ndani, utajengaje uchumi ambapo hakuna demokrasia, hakuna uhuru wa mawazo na watu hawawezi kujieleza? Humu humu ndani watu tunashindwa kujieleza, tunajengaje uchumi wa hivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona Serikali ya Awamu ya Tano imeleta kongamano kujipima namna ya utendaji kazi. Waliokwenda kwenye kongamano ni hao hao watendaji akina Mheshimiwa Kabudi. Ni hao hao wanaofanya kazi, ni hao hao wanaojipima, ni hao hao wanaojisifu. Hamtaki hata kusikia sisi tunawaonaje? Humu ndani we are not intruders, sisi ni part and parcel ya development ya nchi hii. You don’t want to hear sisi tunawaonaje. Mnafanya kazi wenyewe, mnajipima wenyewe, mnajipongeza wenyewe, halafu mnajitekenya wenyewe. Hiki ni kipimo gani mnachofanya? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo niliyoyasema lazima tujitafakari, mahusiano yetu na Kimataifa yako wapi? Tunahusiana vipi kwa sababu sisi siyo kisiwa. Rais wetu mpendwa mnampa kazi kubwa sana, lakini hamumshauri, ameshindwa kwenda… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)