Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

Hon. Joseph Osmund Mbilinyi

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Mbeya Mjini

Contributions

nil

Answers

nil

Commettees

0

Ministries

nil

Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi. Katika kujadili mpango naomba kwanza Dkt. Mpango aniambie toka Awamu ya Tano imeingia kuna FDIs ngapi zimeshakuja nchini, naomba anipe takwimu, FDIs ni Foreign Direct Investiments. Naomba kujua ni ngapi toka Awamu ya Tano iingie madarakani, zimeshakuja nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia napenda nijue toka Awamu ya Tano kwenye Arbitration Courts, kwenye Mahakama za nje kuna migogoro na kesi ngapi dhidi yetu? Maana tunasikia tu ACACIA wameenda Mahakamani, mara Pan African Energy wako Mahakamani kutudai kwa hiyo, tunaomba tujue pamoja na gharama ya fedha ambazo wanataka tuwalipe kupitia hizo mahakama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu katika haya mambo no one is perferct. Na sisi kazi yetu kushauri humu ndani na ninyi huko mnatakiwa Mawaziri mnatakiwa mumshauri Rais msimuogope, tunarudia kusema hiki kitu. Na ndio maana kwa sababu, hakuna mtu perfect, even the President can not be perfect every time na ndio maana pamoja na mbwembwe zote tukasubiri Baraza la Mawaziri kachukua time sana kutangaza Baraza la Mawaziri, lakini mpaka leo bado ameshatumbua Mawaziri 11. Kwa hiyo, kama angekuwa perfect wale aliochelewa kuwateuwa ina maana wangekuwa sawasawa na angeenda nao mpaka leo, lakini mpaka sasa hivi 11 wameshatumbuliwa, hii inamaanisha kwamba no one is perfect na muendelee kumshauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana nimuunge mkono my friend, Mheshimiwa Lusinde katika Bunge lililopita 2010/2015 alikuwa na hoja yake anapenda sana kuisema Bungeni kwamba, viongozi tupimwe afya ya akili. Hili alilisema sana Mheshimiwa Lusinde wakati ule sikumuelewa, lakini kwa trend ya mambo yanavyokwenda sasa hivi katika hii nchi kwa kweli, naomba ni … halafu nimuunge mkono Mheshimiwa Lusinde ile hoja yake kwamba kuanzia sasa viongozi wote kuanzia chini Serikali ya Mtaa, Diwani, Mbunge, Rais, hakuna kuchaguliwa kama hajaenda kupimwa afya ya akili kwa sababu mambo yanavyokwenda sio sawasawa kabisa, angalia wanachofanya ma-DC…

KUHUSU UTARATIBU . . .

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Kanuni haiwezi kuzidi Katiba. Mambo mengine ni matakwa ya kikatiba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu sikum-cite mtu, individual, nimezungumzia mfumo wa uteuzi. Ndio kitu nilichozungumzia hapa, mfumo wa uteuzi kwamba, tunavyoteuwa kuanzia Diwani, Mbunge kwenda juu, pengine hata Mwenyekiti wa Kiti na Spika nao inabidi wapite katika huo mchakato, lakini ninyi kwa sababu mtakuwa mmeshachekiwa kama Wabunge kwa hiyo, mtakuwa safe kukaa kwenye hicho kiti kwa hiyo, it is not personal.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natumaini unanitunzia dakika zangu ili nifanye kazi yangu ya Kibunge kwa sababu hii nchi tunafika hapa, tunafunganafungana hovyo, tunapiganapigana risasi hovyo kwa sababu ya unafiki, watu hawataki kusema ukweli. Angalia walichokifanya wale Maprofesa wa Chuo Kikuu juzi pale Mlimani, Nkrumah Hall ni sehemu ya tafakuri ya Taifa. Hayati Mwalimu Nyerere alikuwa anaenda pale kukutana na wasomi ku-discuss mustakabali wa nchi, leo hii maprofesa watu wazima kabisa wanamuita pale kiongozi wanaanza kumsifia, sio vibaya kusifia, lakini wange-balance wamwambie na mapungufu yake kwa maslahi ya nchi hii, hicho ndio tulichotakiwa kufanya, hakuna anayemwambia ukweli kiongozi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa nje watu wanalia, na mimi najua, Mheshimiwa Msigwa anajua, Mhesimiwa Jesca anajua, Mheshimiwa Mhagama unajua, AG unajua, Waziri Mkuu unajua, nje watu wanalia we are not happy, the nation is in sombre … the nation is not happy. Tuambiane ukweli, ili tusonge mbele. Unaona sisi mnatufunga tunatoka tunatabasamu ni kwa sababu ya Taifa hili. Kwa sababu ya mslahi ya Taifa hili na si vinginevyo, lakini tungetoka tumenuna tungezidi…

T A A R I F A . . .

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepokea Taarifa ya Mheshimiwa Bwege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa lina uwoga ndugu zangu, Taifa lina woga, sasa hatuwezi kujadili maendeleo kwenye uwoga.

T A A R I F A . . .

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu naye ndio anasababisha hoja yangu kwamba nobody is perfect kwamba hata wale waliochaguliwa kwa mbwembwe wametumbuliwa, huyu ni mmoja wa waliotumbuliwa katika wale 11, unaona. Huyu ni mmoja wa waliotumbuliwa katika wale 11. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo we are serious here. Hapa ndugu zangu tuko serious, we love this country. Sisi wengine mnavyotuona tumetokea mtaani mpaka hapa tulipofika tunaona Mheshimiwa Kikwete alipotufikisha na mapungufu yake yote alipotufikisha, lakini at least tulikuwa tunaona mwanga, sasa mnatuingizaje kwenye giza na mmekaa tu hapa jamani mnasema tujadili mipango? Tunajadilije mipango polisi wanauwa watu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, polisi wanatuhumiwa kuuwa watu kila kona. Tukisema kwamba uchunguzi ufanyike mnatukamata badala ya kutuomba ushirikiano tuwape information. Jijini Mbeya kwangu mimi, watoto wawili, vijana wawili wamekufa mikononi mwa polisi, Allen Mapunda wa Kata ya Ihyela amekufa mikononi mwa polisi, Kijana Kapange mpaka leo maiti yake iko mortuary kwa zaidi ya siku 160 kwa sababu familia imegoma inasema tunataka uchunguzi huru, sio polisi wajichunguze, tunataka uchunguzi huru. Mpaka leo maiti ya kijana siku 160 iko imelala mortuary, hili Taifa gani? Halafu mnasema kwamba watu wanafuraha katika Taifa kama hili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawana furaha ndugu zangu. Polisi wanatuhumiwa kuuwa watu with impunity, hakuna mtu anayeingia, hakuna tunachofanya, angalia afya, nilikuwa namuuguza mama pale Hospitali ya Taifa…

K U H U S U U T A R A T I B U. . .

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kangi is my friend, my brother. Yeye mwenyewe ni mhanga wa sintofahamu za Awamu ya Tano, alipigwa kesi ya rushwa sijui iliishia wapi? (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alipigwa kesi, hawa ndio walikuwa ni wahanga wa mwanzo kabisa wa vurugu match. Alipigwa kesi ya rushwa sijui imeishia wapi, kwa hiyo Waheshimiwa... (Kicheko)
Hapa tunaongea masuala ya afya, tunaongea masuala ya mpango wa nchi, lakini mambo hayaendi, kwenye afya tumekazana kujenga majengo, wataalam hatuna, nilikuwa pale Muhimbili, mama anahitaji huduma moja inaitwa vascular surgery naambiwa daktari yuko mmoja tu halafu hayupo ameenda Hijja. Hijja ni kitu kizuri huwezi kumzuia yeye kwenda Hijja, lakini jukumu lenu ni ninyi kuhakikisha kuwa kuna watalaam wa kutosha kwa sababu hilo hitaji ni kaja kugundua ni wagonjwa wengi sana wako lined up na wanapoteza maisha na vile na kila kitu kwa sababu ya kukosa wataalam.

Sasa wewe mtaalam wa vascular surgery Taifa kama hili yuko mmoja, halafu mnasema tunaenda vizuri afya, tunaenda nini tunafanya vipi mnakazana kusema kwamba bajeti ya dawa imeongezeka iko bilioni mbili.

Mimi nitasikia raha mkiniambia bajeti ya dawa imepungua na hiyo bilioni 200, 300 pelekeni kwenye maji na vyanzo vingine sehemu nyingine ambazo ni chanzo cha magonjwa ili bajeti ya dawa ipungue na sio kuongeza bajeti ya dawa halafu kudhani kama ni sifa. Mnasema sasa hivi ni bilioni 200 mwakani mtasema bilioni 400, mwaka unaofuata mtasema bilioni 600 kwenye madawa sio sifa, sifa ni kupunguza bajeti ya madawa maana yake kwamba Taifa lina afya watu hawaugui na si vinginevyo ndugu zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kiongozi unatakiwa kuishi kwa mfano, wewe umetajwa kabla watu hawajatajwa, leo hii wenzako wanatajwa mwaka mmoja, miaka miwili baadae halafu unaanza kuwa-harass na kuwafanya hivi wakati... (Makofi/Kicheko)