Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Additional Answers from Prime Minister to Hon. Kassim Majaliwa Majaliwa (45 total)

MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru sana kwa majibu mazuri ambayo ninaamini yamekidhi kiu ya Watanzania wengi wanyonge, hususan Watanzania ambao wamekuwa wakikosa maendeleo, hususan wa Jimbo langu ya Rufiji. Ninaamini sasa Sheria hii itaweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo kwa Jimbo langu la Rufiji, hususan ujenzi wa Barabara ya Nyamwage – Utete. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ufafanuzi tu kuhusiana na hilo, labda ni kama ombi tu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu majibu ni mazuri, ni lini sasa Serikali itaamua mambo haya ya maadili yaingie katika Mitaala ya Shule za Sekondari na Shule za Msingi ili vijana wetu wawe na maadili? Msingi wa maadili uanzie Shule za Msingi na Sekondari.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napokea ombi lako na ni ombi zuri kwamba, ili tujenge maadili mema tunatakiwa tuanze kutoka ngazi za chini, lakini njia ambayo tumeitumia ni kwamba, watumishi wetu hawa ambao pia wameapa kuwa watumishi wenye maadili mema, wakiwemo Walimu ambao wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa, ndio ngazi ya awali ambayo wanasimamia vizuri vijana wetu kutoka ngazi ya shule, wanawalea watoto wetu, wanawasimamia kuwa na nidhamu, kuwa waadilifu, lakini pia, wanadhibiti vitendo vya wizi miongozi mwao ni sehemu ya mafunzo tosha ikiwa ni sehemu ya malezi ambayo yanatolewa na ngazi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutaendelea kuimarisha mabadiliko ya mitaala yetu kwa kuingiza maeneo haya ya utumishi bora, maadili mema ili tupate Watanzania wengi wenye maadili na hatimaye huko mbele tuweze kujihakikishia na shughuli zote za maendeleo nchini tukiamini kwamba kila mmoja atakuwa amelelewa vizuri kwenye familia yake anapokwenda shuleni na pia hata kwenye utumishi kufuata pia Sheria na Kanuni ili kuleta matokeo mazuri. Ahsante sana.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii, nami niweze kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali ambalo nimeona kuna umuhimu wa kuliuliza kwa sababu jana nilisikia ufafanuzi kutoka kwa Mheshimiwa Rais, lakini bado nimeendelea kupokea message kutoka kwa watu mbalimbali wakiuliza kuhusu swali hilo. Suala hilo ni kwamba, kumekuwepo na taarifa katika mitandao ya kijamii na mitaani kwamba Serikali imefuta ajira hali ambayo imesababisha tahamaki na taharuki miongozi mwa wahitimu mbalimbali waliokuwa wanatarajia kuajiriwa na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, taarifa hizo za mitandaoni na mitaani zinasema pia kwamba Serikali haitafanya tena promotion wala kupandisha madaraja, hali ambayo pia inawafanya Watumishi wa Umma kwa namna fulani morali yao kushuka.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa napenda kusikia ukweli halisi ni upi katika suala hili. Je, ni kweli kwamba Serikali haitaajiri tena? Ni kweli haitapandisha madaraja tena? Nakushukuru.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cosato Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimejibu swali la Mheshimiwa Mbogo, ni kwamba sasa hivi kuna watu wengi hupenda kusema maneno ambayo siyo sahihi na hili pia napenda nikanushe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati nzuri sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jana kwenye hotuba yake ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Benki Kuu, ametoa ufafanuzi mzuri sana. Nami nataka nitumie nafasi hii kurudia tu yale ambayo Mheshimiwa Rais ameyasema kwa kuwahakikishia Watumishi wa Umma na wale ambao wanatarajia kuajiriwa kwamba Serikali haijasitisha ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imesimamisha kwa muda kuajiri kwa sababu tunaendelea na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa. Kazi hii ilishaanza, sasa hivi tunaikamilisha. Katika ukamilishaji huu, tunataka tujue sasa watumishi hewa ni akina nani kwa kila idara na kila sekta na watumishi walioko sasa kazini ni akina nani; ili tuweze kujua idadi ya watumishi waliobaki na pengo yaliyopo ndipo sasa tuweze kuajiri kwa ajili ya kusheheneza mahitaji ya watumishi kwenye maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali inafanya mapitio ya Miundo ya Utumishi kwa lengo la kuboresha. Tunaposema kuboresha, maana yake sasa tunataka tupate tija zaidi kwa watumishi. Kwa hiyo, naomba niwasihi Watumishi wote wa Umma kwamba zoezi hili halilengi kuwakandamiza watumishi; kazi hii hailengi kuathiri utumishi wao na madaraja yao, bali kuboresha watumishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwahakikishie Watumishi wa Umma kwamba Serikali hii inawapenda sana na inajali mchango mkubwa ambao watumishi mnautoa kwa Serikali hii. Ili tuweze kufanya kazi kwa motisha, Serikali hii imeona ni muhimu sasa kuboresha zaidi miundo mbalimbali na maslahi mbalimbali, lakini pia kuona idadi ya watumshi tuweze kutumia fedha inayotakiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka muwe na amani kwamba kazi hii inayoendelea ni ya muda mfupi sana. Itakapokamilika, ajira zote ikiwemo na elimu, afya, majeshi, ambazo pia zilikuwa tayari zianze karibuni, zote zitarudishwa na watu watapelekwa kwenye vituo vya kazi kwenda kuanza kazi zao na madaraja mapya yatakuwa yameshatolewa.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri, lakini nilikuwa naomba ile sehemu kwa umuhimu uliopo, kwa kuwa wenzetu wanaweza kuja siku moja pale, kwa ajili ya kutaka kujua walipoishi; kwa kuwa ni sehemu ambayo ina kumbukumbu muhimu na viongozi wengi wakubwa walikaa, basi angalau Serikali ifikirie kujenga kitu kingine mbadala kwa ajili ya kuwaenzi na kuwakumbuka wale wenzetu wa Afrika Kusini. Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ametoa ombi kwamba kwa kuwa eneo hilo la Kilolo lina umuhimu wa kuwa na shule nyingi za sekondari, ifikiriwe kuwa eneo hilo libadilishwe badala ya Magereza liwe elimu. Ni wazo zuri na ni ombi, tunaweza kuangalia ndani ya Serikali, lakini bado nilipokuwa najibu swali la msingi, nilisema eneo hilo la Kilolo linahitaji kuwa na taasisi za shule nyingi kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, bado Halmashauri na wananchi wanahitajika kuweka mikakati ya ujenzi wa shule nyingine, huku Serikali ikiangalia umuhimu na uwezekano wa kubadilisha hilo Gereza kuwa elimu; lakini bado Magereza ni eneo muhimu na ni jambo la msingi pia kuwa na Gereza kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kadiri ambavyo Serikali tutafanya mapitio, tutawezakuwapa taarifa wananchi wote wa Kilolo.
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa majibu yake mazuri, lakini ningependa kujua sasa, eneo hili la watumishi kupitia Halmashauri zetu, wamejipangaje kwa suala zima la mapokeo haya ya mabadiliko ya kuendelea kutaka kuleta maendeleo zaidi? Kwa sababu kuna maeneo mengine tuna Makaimu Wakurugenzi na Makaimu Watendaji mbalimbali. Sasa napenda kujua Serikali imejipanga vipi katika eneo hili la Watendaji wetu? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa namna gani tumejipanga kuhakikisha fedha hizi zinapokelewa na watu stahiki, kwa maana wenye mamlaka kamili; kama ambavyo mnajua, Mheshimiwa Rais anaendelea kuunda Serikali kwa kuteua watumishi mbalimbali katika kada mbalimbali. Najua hatua iliyobaki sasa ni ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wenye dhamana. Wakurugenzi watashirikiana na Wakuu wa Idara na watumishi wote kwenye Halmashauri zetu.
Kwa hiyo, moja kati ya mikakati ya kuhakikisha kwamba tunapeleka fedha kwa wahusika ni kwa kukamilisha uundaji wa Serikali kwenye ngazi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya jambo ambalo litatokea pindi Mheshimiwa Rais atakapofanya maamuzi ya kusoma orodha ya Wakuu wa Wilaya na Wakarugenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, muhimu zaidi, ni kwamba mtumishi yeyote atakayekuwa kwenye eneo hilo na fedha zimefika na anawajibika kuzipokea ili aende kuzisimamia, anao wajibu wa kuzisimamia. Kwa sababu jukumu hili la kila mtumishi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa, inaweza kuwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara na Mkuu wa Idara huyo kwa idara yake, anawajibika kupeleka fedha kwenye ngazi ya vijiji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi anawajibika kufanya hilo na Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote ambaye atahusika kwa ubadhirifu wa fedha ambazo tutazipeleka kwenye shughuli za maendeleo kwenye ngazi zetu za Vijiji na Kata.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Nakushukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yako, lakini ningependa kuuliza maswali ya ziada kama ifuatavyo:-
Kauli yako Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba katika Jimbo lako la uchaguzi mmekubaliana muache siasa mfanye kazi, niliomba tu utambue kwamba siasa vilevile ni kazi. Vilevile kwa sababu kauli ya Waziri Mkuu ni agizo bila kujali umeitolea Jimboni kwako ama nyumbani kwako Mheshimiwa Waziri Mkuu, kauli yako unapoitoa mahali popote kama Kiongozi Mkuu ni agizo. Sasa kwa sababu Mahakama Kuu Mwanza wakati ikisikiliza kesi ya Alphonce Mawazo ilitoa hukumu kwamba Jeshi la Polisi halina mamlaka ya kisheria ya kuzuia mikutano ya Vyama vya Siasa yakiwemo maandamano kwa kisingizio cha...
Mheshimiwa Spika, narudia hapo kwa kisingizio cha wana taarifa za kiintelijensia na Mahakama Kuu ikaagiza Jeshi la Polisi kama mna taarifa za kiintelijensia ina maana mna msingi mzuri wa kulinda usalama. (Makofi)
Kwa hiyo solution siyo katazo, solution ni Jeshi la Polisi kuwasiliana na wahusika ili waweze kuwalinda vizuri kwa sababu tayari wana taarifa za uvunjifu wa amani.
Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu uko tayari sasa kutoa tamko kwa Taifa na kwa kupitia Bunge hili, kwamba lile katazo la mikutano ya siasa ya vyama vya siasa, sasa unalisitisha rasmi?
La pili hapo hapo, je, kwa kutoa tamko lile vilevile uko tayari tena kulieleza Jeshi la Polisi, liheshimu mhimili wa tatu ambao ni Mahakama ambayo ime-declare kwamba hawana mamlaka ya kutoa katazo wakati wanapopata taarifa za kiintelijensia?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya nyongeza ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Mheshimiwa Mbowe. Kama ambavyo nimeeleza awali kwamba Katiba inaeleza, lakini Sheria ndiyo inayoongoza nchi hii kuweka miongozo ya utaratibu. Siasa nchi hii haijaanza leo, upo utaratibu na zipo taratibu za kimsingi, kama chama kinahitaji kufanya mikutano lazima wafuate utaratibu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, suala la Mahakama kuzuia Jeshi la Polisi kufanya kazi, hii ni mihimili miwili tofauti, Mahakama siwezi kuzungumzia habari za mhimili mwingine na kuutolea kauli.
MHE. MUSSA AZZAN ZUNGU: Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru kwa jibu lako, lakini bado niko hapo hapo.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, nchi jirani moja hapa katika hizi za Afrika Mashariki, informal sector watu hawa wa madaladala, vinyozi, welders na kazi za kawaida ambazo siyo rasmi, wamewekwa katika viwango hivyo na wameweza kuchangia kwenye pato la Serikali trilioni nane mwaka 2009.
Hoja yangu ni kwamba, najua changamoto ambazo zipo kwenye Idara za TRA na zingine, basi Serikali ijaribu tu kulipitia na kutazama kwa sababu trilioni nane, kwa informal sector ni sawasawa na kiwango ambacho TRA ndiyo ilikuwa inakusanya miaka minne, mitano iliyopita.
Kwa hiyo, naomba tu Mheshimiwa Waziri Mkuu, mlitazame na mlifikirie kwa siku zinazokuja kama Serikali itaona upo umuhimu wa kuongeza mapato yake, informal sector nayo iweze kulipa VAT na Serikali ipate mapato yake. Nakushukuru.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Azzan Zungu Mbunge wa Ilala, kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa ametoa ombi na kwenye jibu langu la msingi nimesema, bado tunaendelea kukaa pamoja na wadau wetu; ambao ni wafanyabiashara wakiwemo na hao wa informal sector. Kwa hiyo, kadri tutakavyokuwa tunakutana, tunabadilishana mawazo, tunaweza pia kuboresha mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato, tukitambua pia kwamba, sekta hiyo nayo ina mchango mkubwa sana kwenye pato la Serikali.
MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru. Swali langu la nyongeza ni je, wale wakulima ambao korosho zao zimepotea zikiwa ghalani na Serikali ndiyo ilifanya uzembe kwa kuweka dhamana ndogo kwa mwendesha ghala, Serikali iko tayari sasa kuwalipa wakulima wale ambao pesa zao bado wanawadai?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Katani, Mbunge wa Tandahimba kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ni kweli uko uendeshaji wa hovyo wa Vyama vya Msingi, pamoja na Vyama Vikuu, vinavyosimamia korosho na ndiyo sababu Serikali imesimamia kidete kwenye mazao yote; korosho, pamoja na mazao mengine, kuweka usimamizi wa dhati wa kuhakikisha kwamba wakulima sasa wanapata tija kwenye masoko ambayo wanapeleka mazao yao ili waanze kunufaika na mazao waliyonayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Katani anataka kujua wale waliopoteza korosho. Mifumo inayotumika pale, mara nyingi haisimamiwi na Serikali bali na Vyama vyao wenyewe vya Ushirika ambapo wao wenyewe wamechagua ushirika wao, ukisimamiwa na Mrajisi ambaye ndiye pia tumemtaka asimamie kwa dhati namna ya kuuza mazao hayo, pamoja na kutafuta masoko yake ili
wakulima waweze kupata fedha. Sasa wakulima wote ambao wamepoteza korosho, wajibu wao wa kwanza ni kuwauliza viongozi wao wa Chama cha Msingi na Chama Kikuu, kupitia mikutano yao. Wanayo mikutano yao ya haki kabisa na ya msingi na wanayo nafasi ya kuwahoji viongozi wao wa ushirika wa Chama cha Msingi AMCOS pamoja na Chama Kikuu, kwa vyama vile vikuu vinavyoongoza zao hilo la korosho.
Mheshimiwa Spika, pale itakapoonekana hawajaridhika na majibu hayo, wanachama wenyewe wanao uwezo wa kuwapeleka Mahakamani ili Sheria iweze kufuata mkondo wake. Mahakama maamuzi yake yatakayotolewa, ndiyo yale ambayo yataweza kuwawajibisha viongozi wa hovyo, ambao pia wanawasababishia wakulima kupoteza mazao yao. Hii sasa siyo kwa korosho tu; kwa mazao kama pamba, tumbaku, kahawa; yote haya ni mazao ambayo yanauzwa kwa utaratibu ambao sasa tunataka tuusimamie, tuhakikishe kwamba wakulima wanapata tija. Mazao haya ndiyo yanaipatia pato Serikali, lakini wakulima ndiyo wanategemea sana katika kuendesha shughuli zao.
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni lini atakuwa tayari kutembea Tabora ili nako ajionee migogoro hasa katika Wilaya ya Sikonge?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu kwamba, nimeamua kufanya ziara katika Mkoa wa Tabora baada tu ya Bunge hili kwa sababu mbili. Moja, kufanya hilo, lakini pili nakuja kuongea na wadau wa zao la tumbaku; nakuja kufanya mapitio ya zao la tumbaku ambalo limekuwa kero kubwa. Nakuja kuongea na wakulima wenyewe, Viongozi wa Vyama vyao vya Msingi, kuongea na wafanyabiashara na wenye viwanda ili tubaini tatizo liko wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mkakati ambao tumeufanya kwenye zao la korosho, tunahamia kwenye tumbaku na baadaye tunakwenda kwenye pamba, tutakwenda na kwenye kahawa vile vile, kwa lengo la kuwapa tija wananchi waone kabisa kwamba sasa ni wakati wao wa kupata tija ya mazao wanayoyalima ili waweze kupata manufaa.
MHE. DKT. ELLY M. MACHA: Mheshimiwa Spika, swali moja dogo la nyongeza. Mheshimiwa Waziri Mkuu ahsante kwa majibu yako mazuri. Nafikiri huo mkataba una tija ndiyo maana Serikali yetu ulisharidhia. Naomba kuuliza, ni lini sasa hiyo ripoti itaandikwa na kupelekwa kwenye ile Committee?
Mbunge, kwa kuwa sasa tuna Waziri mwenye dhamana na anayeshugulikia jambo hili au watu wenye mahitaji maalum na ameshaanza kazi ya kupitia shughuli mbalimbali na mahitaji yao na kuingiza kwenye mipango; na kwa kuwa pia mmesharidhia hata kwenye bajeti yetu, basi wakati wowote na wewe ukiwa
mmoja kati ya Wabunge hapa na Mheshimiwa Waziri yupo hapa, tunaamini unaweza kuwa mshiriki wa kwanza kati ya washiriki ambao tunataka tuwaingize kwenye orodha ya watakaokuwa wanafanya mapitio haya ili tuweze kuona kama jambo hilo sasa litakamilika wakati gani.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni wakati wowote kuanzia sasa. Kwa kuwa Mheshimiwa Dkt. Possi yupo, mtashirikiana naye katika hili na amelisikia, nimtake tu sasa aanze mchakato huo mara moja kuwakusanya wadau wote ili tuanze kupitia mahitaji yale ili yaweze kutekelezwa katika kusaini mikataba yetu kama ambavyo tumekubaliana.
MHE. HASSAN E. MASALA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ambayo imenadiwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli mwaka 2015; moja ya ahadi kubwa ambayo ilitolewa kwa Watanzania ni ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Naomba kufahamu kupitia Serikali yetu, imejipanga vipi katika kutekeleza ahadi hii ambayo kimsingi inasubiriwa na Watanzania walio wengi?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Masala, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mkoani Lindi, kama ifuatavyo:-
Kwanza, nataka niwaambie Watanzania kwamba Chama cha Mapinduzi kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2015 imefafanua mambo mengi ambayo tumeamua tuyatekeleze katika kipindi cha miaka mitano. Jambo ambalo Mheshimiwa Mbunge ametaka kujua utekelezaji wake ni lini, nataka nimhakikishie kwamba ahadi zetu zote zilizoahidiwa na Chama cha Mapinduzi zitatekelezwa kama ambavyo zimeahidiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumedhamiria kujenga barabara zetu kwa kiwango cha lami na tumeanza na mkakati wa kuunganisha barabara za ngazi za Mikoa, zinazounganisha Mikoa kwa Mikoa; tukishakamilisha hizo, tunaingia kwenye barabara zinazounganisha ngazi za Wilaya na barabara zote ambazo zimeainishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa awamu hii ni barabara ambazo zitakamilishwa kupitia bajeti ambayo sasa mnaipitisha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi itakapokuja hapa, naomba niwashawishi Waheshimiwa Wabunge kuweza kuipitisha ili tuanze kazi ya kukamilisha barabara ambazo nimezitaja. Pale ambapo barabara za Mikoa hazijakamilika, tunataka tuzikamilishe. Tukishakamilisha hizo zote, tunaanza ngazi za Wilaya ili tuendelee.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niwahakikishie Watanzania wote kwamba ahadi zote zilizotolewa na Mheshimiwa Rais kwa kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 zitakamilishwa kama zilivyoahidiwa. Ahsante sana.
MHE. ABDALLAH A. MTOLEA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru kwa majibu yako mazuri, lakini pamoja na hayo, hizi tozo zinazotokana na ardhi kwa maana ya Property Tax na Service Levy, it‟s just a peanut kwenye uwekezaji ambao umekuwa ukifanyika. Kwa mfano, katika uwekezaji wa EPZA ambao unafanyika katika Kata ya Kurasini kwenye Halmashauri ya Temeke; ardhi ambayo Halmashauri tumeitoa, kwa sasa ina thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 100. Unatoa ardhi ya shilingi bilioni 100 halafu uende ukasubiri mrejesho kwa kupitia Property Tax na Service Levy vinakuwa havifanani. Hivi kweli Ofisi yako haioni umuhimu wa kuifanya Halmashauri ya Temeke kupata angalau hisa 10 katika uwekezaji huu?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtolea Mbunge wa Temeke kama ifuatavyo:-
Wakati huu tukiwa tunafanya mabadiliko makubwa na mapitio makubwa kwenye uwekezaji katika maeneo yote, tunaanza kugundua baadhi ya changamoto ambazo zinajitokeza, lakini pia usimamizi wa maeneo hayo pia tumeanza kuona kwamba upo umuhimu wa mamlaka yenyewe kuwa inaweza kuweka mipango yake ili iweze kupata manufaa ya uwekezaji uliopo. Moja kati ya mifano niliyonayo kwenye Halmashauri ya Temeke ni pale Temeke mwisho eneo ambalo mmebomoa majengo na sasa mmepata mwekezaji wa kampuni moja ya Kichina.
Mheshimiwa Spika, Halmashauri ndiyo inafanya maamuzi ya uwekezaji ule na ndiyo aina nyingine ya uwekezaji nilioutaja kwamba Halmashauri inaweza kunufaika zaidi. Sasa hivi mpo kwenye mjadala wa manufaa yenyewe na tozo ambazo mtazipata kutoka kwenye kampuni ile. Kwa hiyo, utaratibu ule pamoja na usimamizi wa Halmashauri yenyewe, lakini bado Serikali sasa tunataka tuipeleke ili iweze kuona kwamba je, Halmashauri yetu inaweza kunufaika?
Mheshimiwa Spika, ninachoweza kusema sasa ni kwamba, Serikali inaandaa utaratibu wa kusimamia uwekezaji wa namna hii ili Halmashauri zetu za Wilaya, Manispaa ziweze kupata tija kwenye uwekezaji ambao sasa tumefungua milango kwa wingi na watu wengi wanaingia kwa ajili ya uwekezaji ili Halmashauri zetu zisiweze kukosea.
Mheshimiwa Spika, wito wangu kwa Halmashauri zote nchini na Waheshimiwa Wabunge ni Wajumbe wa Mabaraza ya Madiwani, tuzingatie sana kwamba uwekezaji huu unaofanyWa kwenye maeneo yetu unaleta tija kwenye Halmashauri zetu na lazima tusimamie hilo kwa pamoja na Serikali itaanza kufanya ufuatiliaji wa kina kuona kuwa uwekezaji ule kwenye Halmashauri zile za Wilaya unawaletea tija Wanahalmashauri hiyo wakiwemo Baraza la Madiwani ambao ndiyo wasimamizi wakuu. Kwa hiyo, tutaendelea kufuatilia uwekezaji huu tuone tija ambayo inaweza kupata pia Halmashauri zetu kote nchini.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa na mimi nimwulize Waziri Mkuu swali.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni dhahiri kwamba wanafunzi hawatakiwi kufanya siasa Vyuoni, lakini kumekuwepo na ama mkakati au maelekezo ambapo Menejimenti ya Vyuo inawanyanyasa wanafunzi wanaokuwa hawapendezwi na siasa ya Chama cha Mapinduzi. Je, ni kweli kwamba kuna hayo maelekezo? Kama hakuna maelekezo, Serikali inazieleza nini sasa Menejimenti za Vyuo kuhusu hii tabia ambayo imejengeka ya kuwanyanyasa vijana na hata kuthubutu kuingilia Uongozi wa Serikali za Wanafunzi? Mojawapo ya Chuo ambacho kimekithiri ni Chuo Kikuu cha Dodoma.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Tarime, kama ifuatavyo:-
Kwanza nataka nikanushe kwamba siyo kweli kwamba kuna maelekezo kwenye Vyuo vyote vya Elimu ya Juu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, hakuna unyanyasaji wowote unaofanywa kwenye Vyuo kwa wanafunzi ambao... (Makofi/Kelele)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, Watanzania wote wanao uhuru wa kujiunga na vyama vyovyote wanavyovitaka, lakini kila eneo limeweka utaratibu wake. Hakuna zuio la wafanyakazi kujiunga na vyama vyovyote lakini liko zuio la mtumishi anapokuwa kazini kuendesha siasa. Hakuna zuio la mwanafunzi yeyote kama Mtanzania kujiunga na Chama anachokitaka yeye, lakini zuio ni kwamba hutakiwi kufanya siasa wakati wa masomo ili u-concentrate na masomo yako. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, inaweza kutokea labda vijana wawili wenye itikadi tofauti huko wakafanya mambo yao, wakatofautiana huko, huo siyo utaratibu wa Serikali, ni utaratibu wao wao wenyewe. Kwa hiyo, nawaomba sana niwasihi Viongozi wa Vyama vya Siasa, tusilione hili kama ni msimamo wa Serikali, badala yake tulione hili kama ni mapenzi ya watu wengine, kama ambavyo vijana wafanyabiashara huko wanavyoweza kukorofishana mahali pao, lakini haina maana kwamba yule wa Chama Tawala anapokorofishana na mtu mwingine wa Chama cha Upinzani huko kwenye biashara zao tukasema labda soko lile, Chama Tawala kimepeleka watu wake kuzuia watu wa Vyama vingine wafanye vurugu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho, niwasihi Watanzania wote; Tanzania hii ni yetu sote na tunahitaji maendeleo ya Watanzania wote. Kila mmoja anao uhuru wa kupenda Chama anachokitaka. Kama kuna maeneo yanabana kisheria na kwa utaratibu wa matumizi au matakwa hayo kuyapeleka maeneo hayo, lazima yazingatiwe. Serikali hii itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali Vyama vyao; tutaendelea kuwahudumia Watanzania wote bila kujali Vyama vyao; pia tutatoa elimu kutoka ngazi ya awali mpaka elimu ya juu bila kujali mapenzi ya Chama chako. (Makofi)
Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikusihi tu uamini bado kwamba Serikali hii haina jambo hilo wala haina maagizo hayo mahali pa kazi na uwe na amani. Nami nasema Watanzania hawa ni ndugu, wanaishi pamoja na bado tunapenda washiriki kikamilifu katika masomo yao. Ahsante sana.
Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru kwa jibu lako, lakini bado niko hapo hapo.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, nchi jirani moja hapa katika hizi za Afrika Mashariki, informal sector watu hawa wa madaladala, vinyozi, welders na kazi za kawaida ambazo siyo rasmi, wamewekwa katika viwango hivyo na wameweza kuchangia kwenye pato la Serikali trilioni nane mwaka 2009.
Hoja yangu ni kwamba, najua changamoto ambazo zipo kwenye Idara za TRA na zingine, basi Serikali ijaribu tu kulipitia na kutazama kwa sababu trilioni nane, kwa informal sector ni sawasawa na kiwango ambacho TRA ndiyo ilikuwa inakusanya miaka minne, mitano iliyopita.
Kwa hiyo, naomba tu Mheshimiwa Waziri Mkuu, mlitazame na mlifikirie kwa siku zinazokuja kama Serikali itaona upo umuhimu wa kuongeza mapato yake, informal sector nayo iweze kulipa VAT na Serikali ipate mapato yake. Nakushukuru.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Azzan Zungu Mbunge wa Ilala, kama ifuatavyo:-
Kwa kuwa ametoa ombi na kwenye jibu langu la msingi nimesema, bado tunaendelea kukaa pamoja na wadau wetu; ambao ni wafanyabiashara wakiwemo na hao wa informal sector. Kwa hiyo, kadri tutakavyokuwa tunakutana, tunabadilishana mawazo, tunaweza pia kuboresha mfumo mzuri wa ukusanyaji wa mapato, tukitambua pia kwamba, sekta hiyo nayo ina mchango mkubwa sana kwenye pato la Serikali.
MHE. FREEMAN A. MBOWE:
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru kwa ajibu yako na ninaomba nikuulize maswali mengine machache ya ziada.
Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na nia njema sana ya kulinda viwanda
vya ndani ni dhahiri kwamba maamuzi yote ya kiutawala lazima yafanyiwe kwanza utafiti. Na tunapozungumza ninahakika Serikali yako inatambua kwamba kuna mradi mkubwa wa uwekezaji wa kiwanda cha sukari uliokuwa umependekezwa katika eneo la Bagamoyo uliouzungumza ambao umeanza kuratibiwa tangu mwaka 2006 wenye capacity ya kuzalisha sukari tani 125,000 kwa mwaka, lakini Serikali mpaka dakika hii tunapozungumza urasimu unasababisha mradi huu haujapewa kibali cha kuanza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu, pamoja na kwamba ulisema kuna bei ya
elekezi sukari ambayo ingehitaji soko la sukari liweze kuwa controlled na Serikali, jambo ambalo linaonekana kushindikana. Unatupa kauli gani Watanzania kuhusiana sasa na hatima ya hayo mambo niliyokuuliza?
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali pana la Mheshimiwa Mbowe, Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kama ifuatavyo:-
Kwanza tuna hilo shamba la Bagamoyo ambalo umelisema ambalo
umesema kumekuwa na urasimu wa muda mrefu. Nataka nijibu hili vizuri kwa sababu pia Wabunge tumeshirikiana nao sana katika kufanya maamuzi ya shamba lile. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, shamba la Bagamoyo kwa ukubwa wake na
mategemeo yake kwa mipango ya kuzalisha sukari inategemea sana Mto Wami. Mpakani mwa Mto Wami tumepakana na Mbuga ya Saadani, Mbuga ya Saadani uwepo wake na sifa iliyonayo inategemea sana wanyama wale kunywa maji Mto Wami. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, uwekezaji wa shamba la sukari unahitaji maji mengi nayo yanatakiwa yatoke Mto Wami. Bado kuna mgongano kidogo wa mpaka kati ya shamba letu hilo la sukari linalotegemewa kulima miwa na Mbuga ya Saadani. Kamati ya Kudumu ya Bunge imefanya ziara na imeishauri Serikali kuangalia vinginevyo na mimi nimepokea ushauri wao vizuri kwa sababu una mantiki. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Kamati ya Bunge imeishauri Serikali kwamba ni vyema
tukahifadhi mbuga, tukatafuta maeneo mengine ya kilimo cha sukari ili kulinda Mto Wami ambao unatumiwa na wanyama wetu kwenye Mbuga ya Saadani kuliko kupeleka shamba tukatumia maji yale tukafukuza wanyama hakutakuwa na mbuga tena.
Mheshimiwa Spika, sisi bado tuna nafasi kubwa ya maeneo mengi ambayo yamefanyiwa utafiti ya kulima sukari, mbali ya eneo la Morogoro na kule Kigoma, lakini tuna eneo la shamba lililokuwa linamilikiwa na Bodi ya Sukari kule Kilombero, nalo pia lina nafasi nzuri tu tunaweza kuzungumza na wakulima wanaolima mashamba ya kawaida watuachie tuweze kuwekeza.
Mheshimiwa Spika, lakini tuna Mto Rufiji tuna bonde kubwa sana uliokuwa
unamilikiwa na watu wa Bonde la Rubada, wana eneo kubwa sana. Kwa hiyo, tuna maeneo hayo mengi, tutakapopata wawekezaji wengi tutaanza kupima viwanda vilivyopo na uzalishaji wake. Makubaliano ya kiwanda kipya na uzalishaji wake tukigundua kwamba, uzalishaji wake unatosha mahitaji ya nchi.
Tutaanza kuwakabidha Kigoma, tutawepeleka Morogoro kule Kilosa, tutawapeleka hapa Ngerengere na Bagamoyo iwe sehemu ya mwisho baada ya kuwa Kamati ya Bunge imetushauri vizuri juu ya kulinda Mbuga yetu ya Saadani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, eneo la pili, ambalo umelitaja ni hili la bei elekezi, kwa
nini tunatoa bei elekezi.
Mheshimiwa Spika, mara nyingi tunakaa sana na wazalishaji wa viwanda
wa sukari na kufanya mapitio na kwa mara ya mwisho tumekutana hata wale waagizaji wa muda mrefu na sasa tunajua kupitia mitandao tunajua bei wanayonunulia sukari huko ughaibuni. Brazil na kule Uarabuni tumeshafanya calculation za pamoja mpaka sukari inaingia nchini na kulipa kodi zake.
Mheshimiwa Spika, usafirishaji kutoka Dar es Salaam na kuipeleka mpaka
mkoa wa mwisho Kagera, Lindi, Ngara, tunajua kule Ngara itauzwa bei gani.
Kwa hiyo, wajibu wa Serikali kutoa bei dira ni kumlinda sasa mwananchi wa kawaida asije auziwe kwa gharama kubwa kwa kisingizio cha usafirishaji huku tukiwa tunajua usafirishaji kutoka Brazil mpaka Dar es Salaam, Dar es Salaam mpaka Ngara na mwananchi wa Ngara atanunua sukari kwa kiasi gani.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo suala la bei elekezi litategemea linaweza
likabadilika kutegemea na gharama ya usafirishaji ambayo na sisi pia tunafuatilia kwa karibu kupitia Bodi yetu ya Sukari. Kwa hiyo, suala bei dira linaweza kubadilika na sisi tunatoa kauli kutegemea na uagizaji lakini lazima wananchi waamini kwamba Serikali hii inawalinda walaji wadogo ili wasinunue sukari kwa bei ya juu.
Mheshimiwa Spika, nishukuru kupata nafasi ya kuuliza swali la moja kwa moja kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwanza tunafahamu kwamba maji ni uhai na Sera ya Taifa ya Maji inahitaji kila mwananchi kuweza kuyafikia maji ndani ya umbali wa mita 25. Je, Serikali ya Awamu ya Tano imejipangaje kuhakikisha maji haya yanawafikia wananchi especially
wananchi wa Mkoa wa Lindi ambao wanatatizo kubwa sana la maji?
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini kama ifuatavyo:-
Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Kaunje, amekuwa anafuatilia sana
mwenendo wa maji na hasa alipoweka kule mwishoni hasa wananchi wa Mkoa wa Lindi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Sera ya Maji nchini imetamka wazi kwamba Serikali itasambaza maji kwa wananchi wake kote nchini mpaka ngazi za vijiji tena kwa umbali usiozidi mita 400 hiyo ndiyo sera na wakati wowote Wizara ya Maji inapofanya kazi yake inafanya kazi kuhakikisha kwamba sera hiyo inakamilika. Iko mipango mbalimbali na nadhani Wizara ya Maji itakuja na bajeti hapa ikiomba ridhaa yenu muipitishe Waheshimiwa Wabunge ili tukaendelee kutekeleza hiyo sera ya kusambaza maji, na mikakati yetu sisi, maji lazima yawe yamefika kwenye ngazi za vijiji kwa asilimia mia moja ifikapo mwaka 2025 na ikiwezekana kufikia mwaka 2020 hapa kwa zaidi ya asilimia tisini huo ndiyo mkakati wetu. Mkakati huu utatokana tu kama tutaendelea kupata
fedha nyingi Serikalini na kuzipeleka Wizara ya Maji ili Wizara ya Maji waendelee na mkakati ambao wanao. Kwa hiyo, niseme tu kwamba kwa malengo haya tunakusudia kusambaza maji kwenye maeneo yote ya vijiji na maeneo ya miji ili wananchi wetu waweze kupata tija ya maji kwenye maeneo haya. Kwa miradi ambayo ipo, ambayo imeelezwa kwamba ipo inaendelea kutekelezwa, tunaamini
miradi hiyo kwa watu wote ambao tumewapa kazi hiyo wataendelea kutekeleza kadri ambavyo tunawalipa fedha zao ili waweze kukamilisha.
Waliokamilisha wakamilishe miradi ambao hawajakamilisha tunaendelea kuwapelekea fedha ili waweze kukamilisha ili maji yaweze kutolewa na kila mwananchi aweze kunufaika na sera hiyo ya Serikali.
MHE. HASSAN S. KAUNJE:
Mheshimiwa spika, ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu, sababu zinazosababisha muda mwingine kutokupatikana maji ni pamoja na wakandarasi ambao wanakuwa wamelipwa lakini wanashindwa
kukamilisha miradi ya maji kwa wakati na sababu hizo ni pamoja na mradi wa Ng‟apa ambao uko Lindi. Je, ni hatua gani zinachukuliwa na Serikali dhidi ya wakandarasi wa aina hii ili maji yaweze kuwafikia wananchi?
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la
Mheshimiwa Kaunje, Mbunge wa Lindi Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu langu la
msingi, suala la wakandarasi wetu kwa sababu malengo ya Serikali tunawapa hizi kazi ili waweze kuzimaliza katika kipindi kifupi sasa kama inatokea mkandarasi hawezi kamaliza kazi kwa kipindi kifupi, ziko sababu mbalimbali ambazo pia tumezizoea maeneo mengine, malipo kutoka kwa kuchelewa nako kutokana na tatizo la fedha inawezekana mkandarasi hajamaliza. Lakini malengo yetu kama mkandarasi analipwa vizuri na kwahiyo basi anatakiwa akamilishe mradi huo kwa wakati uliokubalika. Lakini ikitokea mkandarasi
hajamaliza kama kuna tatizo la fedha hilo ni juu ya Serikali kupitia Wizara ya Fedha kukamilisha kulipa madeni ili mradi ukamilike. Kama mkandarasi amelipwa fedha zote au zaidi ya asilimia 90 na hajakamilisha kwa kipindi kinachotakiwa, zipo taratibu za kisheria za kufanya kwa sababu ameingia zabuni kisheria na kwa hiyo, tunaweza tukatumia utaratibu wa kisheria pia kwa kuadhibu mkandarasi ambaye hajamaliza kazi lakini pia amelipwa fedha.
Sasa sina uhakika na mradi wa Lindi uko katika sura gani na kama
ingekuwa session hii inaweza kumpa Waziri Mkuu nafasi ya kupata majibu sahihi ningweza kukupa jibu sahihi la mradi huo wa Ng‟apa.
MHE. LUCY S. MAGERELI:
Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, nilichotamani kusikia kutoka kwako ni tamko lako kama Serikali kuziagiza Halmashauri kutoa ushirikiano kwa
GS1 lakini TFDA, TBS na washirika wengine ikiwemo Wasajili wa Viwanda wa Makampuni kwa sababu hiyo ni timu inayofanya kazi pamoja. Changamoto hiyo imekuwa kubwa kwa sababu ya kupata
resistance kutoka kwa Halmashauri, lengo mlilolianzisha lilikuwa jema lakini Halmashauri hazitoi ushirikiano na kutotoa ushirikiano zinawanyima fursa wazalishaji na wafungashaji wadogo kupata fursa hiyo.
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, nimekusikia kwa namna ambavyo ume-experience
huko ambako umeona kwamba Halmashauri zetu hazitekelezi maagizo yetu ambayo tunayatoa na inawezekana siyo Halmashauri tu ziko pia nyingine ambazo pia zinafanya jambo hilo hilo. Kwa hiyo, nilichukue jambo lako baada ya kikao hiki nitawasiliana na Waziri wa TAMISEMI kuhakikisha kwamba maagizo yetu ya Serikali yanatekelezwa na wazalishaji wetu wadogo wanapata nafasi.
Lakini pia Wizara ya Kilimo nayo pia ilichukue hili kwa sababu tunayo
Maonesho ya Kilimo ambayo sasa tumeyaanzisha katika kanda mbalimbali, hawa wajasiriamali wadogo wapate nafasi za kwenda kuonyesha bidhaa zao kwenye maonyesho yale ili pia waweze kutangaza soko lao, waonyeshe ubora wao na sasa Halmashauri zisimamie wajasiriamali wadogo hao kwenda kwenye maonyesho hayo ili uonyesha kazi zao ziweze kuleta tija zaidi huo ndiyo msisitizo wa Serikali.
(Makofi)
MHE. VENANCE M. MWAMOTO:
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri, lakini nilikuwa naomba ile sehemu kwa umuhimu uliopo, kwa kuwa wenzetu wanaweza kuja siku moja pale, kwa ajili ya
kutaka kujua walipoishi; kwa kuwa ni sehemu ambayo ina kumbukumbu
muhimu na viongozi wengi wakubwa walikaa, basi angalau Serikali ifikirie kujenga kitu kingine mbadala kwa ajili ya kuwaenzi na kuwakumbuka wale wenzetu wa Afrika Kusini. Ahsante.
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ametoa ombi kwamba kwa kuwa eneo hilo la Kilolo lina umuhimu wa kuwa na shule nyingi za sekondari, ifikiriwe kuwa eneo hilo libadilishwe badala ya Magereza
liwe elimu. Ni wazo zuri na ni ombi, tunaweza kuangalia ndani ya Serikali, lakini bado nilipokuwa najibu swali la msingi, nilisema eneo hilo la Kilolo linahitaji kuwa na taasisi za shule nyingi kulingana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo.
Mheshimiwa Naibu Spika, bado Halmashauri na wananchi wanahitajika
kuweka mikakati ya ujenzi wa shule nyingine, huku Serikali ikiangalia umuhimu na uwezekano wa kubadilisha hilo Gereza kuwa elimu; lakini bado Magereza ni eneo muhimu na ni jambo la msingi pia kuwa na Gereza kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kadiri ambavyo Serikali tutafanya mapitio,
tutaweza kuwapa taarifa wananchi wote wa Kilolo .
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH:
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa majibu yake mazuri, lakini ningependa kujua sasa, eneo hili la watumishi kupitia Halmashauri zetu, wamejipangaje kwa suala zima la mapo
keo haya ya mabadiliko ya kuendelea kutaka kuleta maendeleo zaidi? Kwa sababu kuna maeneo mengine tuna Makaimu Wakurugenzi na Makaimu Watendaji mbalimbali. Sasa napenda kujua Serikali imejipanga vipi katika eneo hili la Watendaji wetu? Ahsante.
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa namna gani tumejipanga kuhakikisha fedha hizi zinapokelewa na watu stahiki, kwa maana wenye
mamlaka kamili; kama ambavyo mnajua, Mheshimiwa Rais anaendelea kuunda Serikali kwa kuteua watumishi mbalimbali katika kada mbalimbali.
Najua hatua iliyobaki sasa ni ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wenye dhamana. Wakurugenzi watashirikiana na Wakuu wa Idara na watumishi wote kwenye Halmashauri zetu.
Kwa hiyo, moja kati ya mikakati ya kuhakikisha kwamba tunapeleka
fedha kwa wahusika ni kwa kukamilisha uundaji wa Serikali kwenye ngazi ya mamlaka ya Serikali za Mitaa na Halmashauri za Wilaya jambo ambalo litatokea pindi Mheshimiwa Rais atakapofanya maamuzi ya kusoma orodha ya Wakuu wa Wilaya na Wakarugenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, muhimu zaidi, ni kwamba mtumishi yeyote
atakayekuwa kwenye eneo hilo na fedha zimefika na anawajibika kuzipokea ili aende kuzisimamia, anao wajibu wa kuzisimamia. Kwa sababu jukumu hili la kila mtumishi wa mamlaka ya Serikali za Mitaa, inaweza kuwa Mkurugenzi au Mkuu wa Idara na Mkuu wa Idara huyo kwa idara yake, anawajibika kupeleka fedha kwenye ngazi ya vijiji kwa ajili ya utekelezaji wa miradi anawajibika kufanya hilo na Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote ambaye atahusika kwa ubadhirifu wa fedha ambazo tutazipeleka kwenye shughuli za maendeleo kwenye ngazi zetu za Vijiji na Kata.
MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA:
Mheshimiwa Naibu Spika,
Mheshimiwa Waziri Mkuu nakushukuru sana kwa majibu mazuri ambayo ninaamini yamekidhi kiu ya Watanzania wengi wanyonge, hususan Watanzania ambao wamekuwa wakikosa maendeleo, hususan wa Jimbo langu ya Rufiji.
Ninaamini sasa Sheria hii itaweza kusaidia upatikanaji wa maendeleo kwa Jimbo langu la Rufiji, hususan ujenzi wa Barabara ya Nyamwage –
Utete.
Mheshimiwa Naibu Spika, ufafanuzi tu kuhusiana na hilo, labda ni kama ombi tu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu majibu ni mazuri, ni lini sasa Serikali itaamua mambo haya ya maadili yaingie katika Mitaala ya Shule za Sekondari na Shule za Msingi ili vijana wetu wawe na maadili? Msingi wa maadili uanzie Shule za Msingi na Sekondari.
WAZIRI MKUU:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza
la Mheshimiwa Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napokea ombi lako na ni ombi zuri kwamba, ili
tujenge maadili mema tunatakiwa tuanze kutoka ngazi za chini, lakini njia ambayo tumeitumia ni kwamba, watumishi wetu hawa ambao pia wameapa kuwa watumishi wenye maadili mema, wakiwemo Walimu ambao wanafanya kazi yao kwa weledi mkubwa, ndio ngazi ya awali ambayo wanasimamia vizuri vijana wetu kutoka ngazi ya shule, wanawalea watoto wetu, wanawasimamia kuwa na nidhamu, kuwa waadilifu, lakini pia, wanadhibiti vitendo vya wizi miongozi mwao ni sehemu ya mafunzo tosha ikiwa ni sehemu ya malezi ambayo yanatolewa na ngazi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutaendelea kuimarisha mabadiliko
ya mitaala yetu kwa kuingiza maeneo haya ya utumishi bora, maadili mema ili tupate Watanzania wengi wenye maadili na hatimaye huko mbele tuweze kujihakikishia na shughuli zote za maendeleo nchini tukiamini kwamba kila mmoja atakuwa amelelewa vizuri kwenye familia yake anapokwenda shuleni na pia hata kwenye utumishi kufuata pia Sheria na Kanuni ili kuleta matokeo mazuri. Ahsante sana.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, haihitaji utafiti wa ziada kujua uchumi umeshuka. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini tunatambua kwamba Benki Kuu ndiyo taasisi muhimu katika Taifa ambayo mara kwa mara kila baada miezi mitatu ina-release data fulani fulani kuonesha hali ya uchumi katika Taifa, na tayari hali ya uchumi katika Taifa imeshaelezwa kwenye Ripoti ya Benki Kuu ambayo inatoka quarterly, kila baada ya miezi mitatu kwamba kuna kushuka kwa hali ya juu katika importation, kuna kushuka katika exportation, kuna kushuka katika construction industry, kuna kushuka katika circulation ya fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi majuzi tulimsikia Mheshimiwa Rais akisema kwamba watu wanaweka fedha nyumbani, wanahifadhi fedha na ndiyo sababu mzunguko wa fedha umepungua katika circulation, kitu ambacho mimi binafsi naamini si kweli, na sijui vyanzo vya Mheshimiwa Rais ni nini kama Serikali ilikuwa haijafanya utafiti wa kina kujua kweli hali hiyo ipo. Mheshimiwa Spika, sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kamati ya Bunge ya Biashara na Uwekezaji ilikwenda Bandarini na ilitoa ripoti ambayo ni dhahiri, ni Kamati ya Bunge imedhihirisha hilo. Hao wadau mnaosema mtawashirikisha tayari wanalalamika. TATOA wanalalamika kuhusu mizigo yao, mahoteli yanafungwa, makampuni yanafungwa, watalii wamepungua, utafiti gani bado mnahitaji mjue kwamba uchumi umeanguka? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilitegemea leo Waziri Mkuu ujue kabisa waziwazi kwamba uchumi unaanguka na uchumi umeanguka na utueleze measures ambazo mnachukua kurekebisha hali hii. Lakini it seems like the government haina uhakika ni nini kinaendelea. Waziri Mkuu unaonaje katika mazingira hayo, mka-declare kwamba mmeshindwa kuendesha Serikali hii? (Makofi)
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbowe, Mbunge na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwa kuanza kusema kwamba Serikali hiihaijashindwa kuongoza nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote, tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa sana kwenye sekta zote. Kazi hiyo imeanza kwa kufanya marekebisho makubwa ya maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa vilevile. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani umeeleza hasa juu ya bandari. Kwanza nieleze kwamba Serikali imekuwa ikifanya mawasiliano na mataifa mengine yanayoendesha shughuli za bandari. Mwezi mmoja uliopita nilipokea timu ya wafanyabiashara maarufu duniani kutoka Singapore akiwemo mfanyabiashara anayefanya biashara za meli duniani. Alinieleza kwamba suala la mdororo wa usafirishaji wa mizigo kwa njia ya meli imeshuka duniani kote.
Mheshimiwa Spika, suala la kupungua kwa mizigo maeneo yote ni kwa sababu ya hali ya kiuchumi duniani iliyotokana na kuporomoka kwa bei ya gesi na mafuta duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukanda huu wa kwetu wa Afrika Mashariki ambako bandari yetu inatumika sana, nataka nikuhakikishie, Tanzania kupitia bandari zetu tunategemea sana mizigo kutoka Congo, Rwanda, Burundi kidogo lakini pia na Zambia; na wote mnajua kwamba Congo na Zambia ni nchi ambazo zilikuwa zinaelekea kwenye uchaguzi na kulikuwa na migongano mingi ndani ya nchi na wafanyabiashara wengi walisimama kidogo kufanya biashara zao; na hiyo ikasababisha kupungua hata kwa kiasi cha mizigo. Sio tu kwa Bandari ya Dar es Salaam pia hata usafirishaji kwenda kwenye bandari nyingine kutoka kwenye nchi hizo ambazo nimezitaja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini nataka nikupe faraja kwamba wiki moja iliyopita tumepata barua kutoka kwa timu ya wafanyabiashara wa Congo. Kutokana na hali iliyokuwepo awali na stabilization iliyopo sasa wametuhakikishia kwamba sasa usafirishaji wa mizigo yao yote utafanyika kupitia Bandari ya Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Rwanda wametuandikia barua kutuhakikishia kwamba kutokana na mdororo uliokuwepo awali wafanyabiashara wengine kuamua kupeleka maeneo mengine kwa sababu ya hali ya kiuchumi lakini sasa wameamua mizigo yote itapitia Bandari ya Dar es Salaam, hasa kwa mkakati wetu wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayotoka Dar es Salaam - Tabora mpaka Bandari kavu ya Isaka, lakini tunaunganisha pia na reli hiyo standard gauge kwenda nchini Rwanda na kwa hiyo jitihada za kusafirisha mizigo sasa zitaimarishwa ili kuleta motisha ya ujenzi wa reli hiyo ili iendelee kusafirisha mizigo hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge nataka nikuhakikishie, ni kwamba haya yote uliyoyaeleza kama kuna jambo ambalo tunahitaji kukaa pamoja ni jambo la uchumi na hili ni jambo endelevu na nataka nikuhakikishie kwamba tutalifanyia kazi kwa kiasi kikubwa ili sasa tujiridhishe kila eneo na yale ambayo yanatakiwa na kama kufanya kampeni zaidi ya kupata wafanyabiashara zaidi, Serikali itafanya hilo kwa lengo lile lile la kuhakikisha kwamba uchumi wa nchi yetu hauporomoki na wala hauwezi kuathiri mahusiano na nchi nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hiyo ndiyo commitment ambayo naweza kukupatia kwa ajii ya maeneo haya. (Makofi)
MHE. JAKU HASHIM AYOUB: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na mimi niendelee kumshukuru Waziri Mkuu kwa umakini wake wa hali ya juu kujibu suala hili nililomuuliza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu hii imekuwa kama miongo ya mvua za masika. Ni sababu gani hasa Serikali kuwa haijajipanga kuonekana tatizo hili likafika pahala likamaliza kabisa suala la sukari?
Baada ya miezi mitatu, sita atakuja kiongozi mwingine atasahau kuhusu suala hili, kwa hiyo, Serikali ikajipange na suala hili, wananchi ndio muhimu na mlikuwa mkipiga kelele kuwa mtawajali wananchi, Serikali haiogopi hasara kwa ajili ya wananchi wake ni hilo tu Mheshimiwa.
SPIKA: Mimi naona kilichotolewa ni ushauri tu, lakini kwamba haijajipanga tusubiri ripoti ni ushauri tu.
MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi binafsi na Watanzania wote wana imani na Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Waziri Mkuu wetu na tuna imani haya yote aliyoyasema hapa kwa Serikali hii ya Awamu ya Tano yatatekelezeka.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimuulize swali dogo tu la nyongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu. Atakuwa tayari sasa kuzifuatilia Halmashauri zote ziwe zinapokea pesa kwa kutumia mashine za kielektroniki?
yote, tumeendelea kuwaagiza Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na watendaji wa Halmashauri wakiwemo Wakurugenzi kuhakikisha kwamba moja ya majukumu yao waliyonayo ni kuhakikisha na kujiridhisha kwamba kila eneo la makusanyo, vifaa vya kielektroniki vinatumika na kwa hiyo, wajibu wangu ni kusimamia kuona kwamba matumizi ya vifaa hivi yanafanyika na yanaendelea. Ahsante sana.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwanza niseme tu kwamba majibu ya Mheshimiwa Waziri Mkuu yamenishtua; amesema fedha inatolewa mara moja kwa mwaka na wengine wanasema ni mara mbili kwa mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu nijue, mimi ni Mbunge wa Jimbo la Ukonga; niliposoma sheria inasema unapogawanya zile fedha inabidi kuangalia population na mazingira ya Jimbo. Kwa mfano, Jimbo la Ukonga na Jimbo la Segerea, mwenzangu anapokea shilingi milioni 33, mimi napokea shilingi milioni 16. Ni kama mara mbili yangu, lakini wananchi wa Segerea ni karibu 600,000; mimi watu wa Jimbo langu tumezidiana kama watu 50,000 hivi.
Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu upo tayari kusimamia Serikali yako ili kuangalia hali halisi ya majimbo yetu yalivyo. Mtu mwenye mazingira magumu ya Jimbo lake apate fedha nyingi zaidi kwa sababu hata mahitaji ya miundombinu ni mingi zaidi kuliko Majimbo mengine? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kumejitokeza matatizo kidogo kwenye Halmashauri zenye Jimbo zaidi ya moja na hasa Majimbo yale ambayo yameanzishwa kipindi hiki cha karibuni. Jukumu la Serikali kupitia Wizara husika ni kuendelea kufanya sensa kabla hatujaanza kuzipeleka fedha ya kutambua idadi ya wananchi walioko kwenye Jimbo husika baada ya kuwa Halmashauri yote kuwa ina Majimbo zaidi ya moja; tuweze kujua kila Jimbo lina wananchi wangapi ili sasa tunapopeleka fedha, tupeleke tukiwa tuna maelekezo hasa kwenye Halmashauri zenye Majimbo zaidi ya moja, kwamba kila Jimbo sasa lipate mgao kiasi gani?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mwita niseme, tatizo lililoko Ukonga na eneo la Segerea litakwisha kwa sababu kazi hiyo inafanyika ndani ya Wizara kabla hatujaanza kupelekka fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaamini kama Jimbo lako lina idadi kubwa ndilo ambalo litapata fedha nyingi kulinganisha na Jimbo lingine ambalo lina idadi ndogo ya wananchi ili sasa kila Mbunge kwenye eneo lake aweze kupanga mipango ya maendeleo kwa fedha ambayo imekuja inayolingana na idadi ya wakazi kwenye eneo hilo.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu ya Waziri Mkuu kuonesha kwamba hiyo sera bado ipo. Kwa uzoefu wangu, utekelezaji wa sera hiyo haupo. Nina mifano, nchi za jirani anapokuja mwekezaji kuwekeza katika nchi hiyo huwa anaruhusiwa kuja na watu watano tu kutoka nchini kwake, tofauti na ilivyo hapa nchini kwetu. Wawekezaji wa kwetu hawana hiyo sera; hawana limit ya kuweka wafanyakazi kutoka nchini kwao. Ndiyo hiyo inayosababisha sasa hivi viwanda vingi vinaendeshwa na wageni wakati sisi wenyewe Watanzania tunapoteza ajira.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushahidi huo ninao kwa sababu nimefanya kazi kwenye sekta ya watu binafsi siyo chini ya miaka 30 mpaka naingia hapa Bungeni. Tumeshaona wafanyakazi wengi wako zaidi ya miaka 20 wafanyakazi wa nchi za nje. Ukiwauliza vibali vyao havieleweki na wengine kama wanakuja Wakaguzi, wanafungiwa kwenye ma-godown, huo ushahidi ninao.
Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, nipe kauli yako, ni lini Serikali yetu itaweza kufuatilia hili suala ili kuzalisha ajira kwa watu wetu? Lini itaweka sheria kwa wawekezaji kwamba wanahitajika walete wafanyakazi wangapi kutoka kwenye nchi wanazotoka?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nimhakikishie kwamba jambo hili tunalisimamia tena kwa ukaribu zaidi. Sera aliyoitaja ya nchi za nje ndiyo sera yetu nchini kwamba mwekezaji yeyote anayekuja kuwekeza nchini iwe ni kiwanda au sekta ambayo inahitaji utalaam, tumeruhusu watumishi watano, ndio ambao wanaruhusiwa kuingia kufanya kazi nchini. Sekta zote ambazo zinaweza kufanywa na Watanzania, tumeweka utaratibu na tunasimamia kwamba sekta zote hizo zitafanya kazi na Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna eneo ambalo linalalamikiwa, basi Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane, kwa sababu sekta ya kazi iko ofisi kwangu. Nina Naibu Waziri anayeshughulikia ajira na kazi na nina Katibu Mkuu. Kwa hiyo, ni rahisi pia kufuatilia maeneo hayo ili tuone kwamba tunafungua nafasi hizo kwa Watanzania badala ya kuwa tunajaza raia kutoka nje ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, bado Serikali hii haizuii mashirika ya nje au wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza nchini, lakini lazima wanapofika Tanzania wataendelea kufuata sheria na sisi Serikali tutasimamia sheria hiyo kuwa inatumika ili kufungua nafasi kwa Watanzania.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Napenda vilevile nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hatua ambazo Serikali imechukua kuhakikisha kuwa wakulima wetu wanapata pembejeo za ruzuku. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, napenda niulize swali dogo tu la nyongeza. Pamoja na hizo pembejeo za ruzuku, Ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi tuliahadi kupunguza bei za pembejeo kwa msimu huu. Je, Serikali imechukua hatua gani au mkakati gani kuhakikisha kuwa kwa msimu huu pembejeo zote zinakuwa na nafuu kwa wakulima wetu? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli azma yetu Serikali ni kuhakikisha kwamba mkulima anapata pembejeo kwa gharama nafuu, lakini pia kwa wakati ili aweze kulima mazao mengi zaidi ili pia tuondokane na shida ya chakula nchini, lakini pia aweze kuuza mazao hayo pale ambako wanahitaji kuuza kwa ajili ya kuongeza uwezo wa kifedha ndani ya familia yake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumesema kwamba Serikali inatoa pembejeo kwa asilimia 25 ya mahitaji ya pembejeo na asilimia zilizobaki mkulima mwenyewe huwa anaweza kuendelea kuongeza ili kuweza kupata pembejeo; hii ni gharama nafuu, lakini tutaendelea kuangalia unafuu zaidi ili kumwezesha mkulima kupata pembejeo kwa gharama nafuu aweze kulima kilimo chenye tija kwa gharama nafuu vile vile.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nichukue jambo lako na tuendelee kuingia kwenye Serikali tuone utaratibu wa kuweza kupunguza gharama hizi ili wakulima wetu waweze kulipa fedha kidogo zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
MHE. SULEIMAN A. SADDIQ: Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakushukuru sana kwa majibu hayo. Kwa kuwa viwanda vya ndani vimejipanga, na kiwanda cha sukari Mtibwa ambacho kiko katika Jimbo la Mvomero na Wilaya ya Mvomero kimejipanga vizuri sana. Je, Serikali iko tayari kuvisaidia sasa viwanda hivi vya ndani ili viweze kukamilisha lengo la Taifa?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saddiq kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, wakati wote tumekuwa tukiendesha mazungumzo kati ya viwanda vyote vya ndani ikiwemo vya sukari, namna bora ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao na bidhaa zenye ubora kwa namna ambayo Serikali inaweza na utayari wake iliyonao, kuvisaidia viwanda hivi kuweza kuzalisha zaidi. Kama ambavyo nimesema kwenye jibu la msingi, Serikali imekaa mara nyingi na wazalishaji wa sukari, kuona mwenendo wa uendeshaji wa viwanda vyao na uzalishaji wake, kupata changamoto zinazowakabili kwenye uzalishaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imedhamiria kulinda viwanda vya ndani na kusaidia uzalishaji mpana, tunao mpango na tumeandaa pia njia nzuri ya viwanda hivi kupata msaada wa kuendelea kuzalisha ikiwemo kupata mitaji, kupitia mabenki tuliyonayo na pia kuhamasisha wakulima wanaolima jirani ili waweze kuzalisha mazao yanayofanana na yale ili kuongeza uzalishaji. Kwa hiyo, Serikali itaendelea kuwa pamoja na wazalishaji ili kuweza kuzalisha zaidi zao la sukari.
MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumshukuru sana Waziri Mkuu kwa ufafanuzi mzuri na ambao kweli ulitolewa na Waziri wa chakula. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu tunayo makundi mawili, kundi ambalo lina uwezo wa kifedha lakini bei iko juu na utaratibu wa Serikali ni kuwapelekea ili kwenda kupunguza mfumuko wa bei, lakini tunalo kundi pia ambalo lilitajwa na Waziri wa Kilimo, kaya kama 3,000 hivi ambazo zina hali mbaya na hazina uwezo hata wa kununua chakula. Je, Serikali sasa ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba jambo hili linaenda kuwasidia wananchi wake?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la uwezo mkubwa, mdogo au wa kati wa kifedha ni jambo pana ambalo kila mmoja na katika kila familia inayo utaratibu wa kujiongezea uchumi kwenye maeneo yao badala ya Serikali kuwaahidi kwamba tutawapelekea fedha ili kuwaongezea fedha; na kwa kuwa tumesema chakula sasa kinapanda kwenye masoko, ni kweli, lakini ni kwa sababu ya hofu ya hali ya hewa ambayo tunayo ya msimu huu wa kilimo, watu wengi wameweka chakula ndani wakidhani, kutumia nafasi hiyo wanaweza kujipatia fedha nyingi. Jambo hili halikubaliki kimsingi kwa sababu tunawaumiza wale ambao wana kipato cha chini kwa ujumla wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata kama hali ya chakula inakuwa nzuri, bado tuna kundi la watu ambao hawana uwezo wa kifedha. Muhimu zaidi watanzania wote tutambue umuhimu wa kila mmoja kuwa lazima apate chakula, aweze kupata mavazi, aweze kupata malazi kwa kile kidogo alichonacho.
Kwa hiyo, wafanyabiashara wetu nawasihi sana, tusijenge tabia ya kupandisha bei vyakula au bidhaa zetu bila sababu yoyote ile ili iweze kuwawezesha wale wote ambao wamezoea kuishi katika maisha ya kawaida, maisha ya kati na wale wapate chakula, waweze kupata huduma nyingine ili pia waweze kuendesha maisha yao. Huo ndiyo msingi imara wa jambo hilo.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kukiri kwamba Taifa letu lina historia ya watu kuheshimiana, ni jambo jema na ni kweli tumekuwa na historia hiyo na hofu ninayoizungumza ndiyo hiyo hiyo kwamba ustaarabu na utamaduni huo unaonekana kupotea kwa kasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na Serikali kututaka tuiamini, tuipe muda lakini hapa tunazungumzia kifo au kupotea kwa mtu. Jambo hili linazua hofu kwa familia na kwa Watanzania wote katika ujumla wake. Nina hakika mtu yeyote mwenye mapenzi mema na nchi yetu anaona jambo hili linataharuki kubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ni utamaduni wa nchi yetu kushirikiana na mataifa mbalimbali katika maeneo


mbalimbali na kwa sababu mataifa yanatofautiana katika uwezo wa kufanya tafiti, uwezo wa kufanya uchunguzi na kipekee nikizungumza Uingereza ambayo tuna mahusiano mazuri nao wametumika maeneo mbalimbali duniani pale ambapo panaonekana pana uzito wa kiuchunguzi, taasisi yao ya Scotland Yard ina uwezo wa kusadia. Kama ambapo ilifanyika Kenya wakati amepotea na ameuwawa katika mazingira ya kutatanisha Robert Ouko aliyekuwa Kiongozi katika Jamhuri ya Kenya watu wakaomba Serikali kama imeshindwa kuchunguza iombe Scotland Yard watoe msaada na wana utaalam mkubwa katika forensic investigation na waliweza kufanya hivyo na wakatoa taarifa yao iliyokuwa sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na mazingira hayo basi kwa nini Serikali isitoe kauli kwa sababu miezi sita ni mingi na hofu inazidi kuwa kubwa, kwa nini Serikali isione umuhimu wa ku-engage Scotland Yard iweze kuja kusaidiana na jeshi letu na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ili kuonyesha ile nia njema kujaribu kuchunguza jambo hili kwa haraka kwa sababu wenzetu tukiri wana teknolojia ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile Waziri Mkuu atakumbuka katika uhuru na haki niliyoizungumzia hapa hajatoa kauli yoyote kuhusu kurushwa kwa Bunge live. Hebu tupe kauli ya Serikali basi turejee utamaduni wetu wa Kitanzania Bunge hili lisikike kwa wananchi ambao wametutuma hapa ndani. Tunaomba kauli ya Serikali kwenye hilo vilevile.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, najua kuna maswali mawili, la kwanza ni lile la kwa nini Serikali isishirikiane na mataifa mengine katika kufanya uchunguzi wa matukio kadhaa ndani ya nchi. Kwanza, nataka nikuthibitishie kwamba Taifa letu linayo mahusiano na mataifa kadhaa ambayo tunashirikiana kwenye mambo mbalimbali ikiwemo na mambo ya kiulinzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na matukio haya yanayojitokeza huku ndani, nikuhakikishie pia Taifa letu lina uwezo wa ndani wa kufanya ufuatiliaji wa kutambua matukio haya ya awali ya mtu kufariki au kutoweka mahali. Baada ya familia husika kutoa taarifa tunaweza tukafanya uchunguzi huo na baadaye tukaweza kubaini vyanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana nimesema yote haya lazima mtuamini Serikali kwamba tunayo nia njema kabisa ya kutambua vyanzo na namna ya kudhibiti uendelezaji wa matukio yote ambayo yamejitokeza nchini.
Mheshimiwa Spika, ni kwamba Serikali haina kikomo cha uchunguzi kutegemea na nature ya tatizo lenyewe. Familia ya mtajwa aliyetangulia mbele za haki au vinginevyo hata sina uhakika, tunaweza kusema kwamba uchunguzi huu utakapokamilika taarifa itatolewa. Ingawa umesema kwamba ni miezi sita lakini kama ambavyo nimesema kwenye jibu la msingi kwamba itategemea kama vyombo vyetu vinapata msaada kutoka kwenye jamii na vyanzo vingine


na teknolojia ambayo tunaitumia kuweza kufikia hatua ya kupata majibu ya uchunguzi ambao tunautoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, bado naendelea kutoa kauli ya kuwaomba Watanzania kuwa watulivu na kuamini jeshi letu kwamba linafanya kazi. Vilevile sisi Serikali jambo hili ni letu, Watanzania watupe ushirikiano wa kutuhabarisha vyanzo vya matukio haya ili tuweze kufikia hatua muhimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge alitaka pia kupata ufafanuzi wa jambo la pili ambalo lilishazungumzwa na Bunge lililopita na maamuzi yalishatolewa ya kwamba Bunge letu litakuwa limeweka utaratibu wa namna ya kuwafikishia matangazo Watanzania. Utaratibu huo unaendelea na Watanzania wanapata matangazo kupitia utaratibu ambao tumeuandaa. Kwa hiyo, tutaendelea kuboresha kadiri ambavyo tunaona inafaa ili kuweza kuwafikishia ujumbe Watanzania. Ahsante sana.
MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu yake mazuri Waziri Mkuu naomba nimuulize swali la nyongeza. Haijalishi kwamba ni kiasi gani cha pesa kilichochukuliwa, ufahamu wangu ulikuwa ni hizo lakini nimepata majibu kwamba ni bilioni 6. Sasa hizi shilingi bilioni 6 kwa sababu hii ni haki ya wananchi, je, wanchi hawa wanazipataje?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Salma Kikwete kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, stahili ya msingi hapa ni wakulima kupata haki yao ya msingi lakini kwa kuwa tulianzisha huo uchunguzi na tulihusisha vyombo vyetu na vina utaratibu kwa hiyo vitakapokamilisha kabisa uchunguzi hatua kali zitachukuliwa. Inawezekana pia moja kati ya hukumu itakayotolewa ni pamoja na kurejesha fedha kwa wale wote waliothibitika kwamba fedha hizo wamezipoteza na hiyo ndiyo njia sahihi ambayo tunatarajia vyombo vyetu vinaweza vikatoa maamuzi hayo ili wakulima waweze kupata stahiki yao ili waendelee pia kuboresha kilimo kwa msimu ujao. Tutaendelea kufanya hilo kwa mazao yote ambayo fedha hii inapotea, tutawasiliana kuona sheria zinazotumika lakini ni vyema tukaona kabisa kwamba sheria inayowataka wakulima warejeshewe fedha inaweza kuwa nzuri zaidi ili haki yao isiweze kupotea kabisa. Serikali itasimamia jambo hilo pia.
MHE. GODBLESS J. LEMA: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yake. Kwa sababu TRA ina sheria zake na kwa sababu amekiri kwamba hii task force inakuwa-engaged kwa wale wafanyabiashara ambao ni wadeni sugu wa TRA. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa vile kuna sheria zinazoendesha shirika hili la kodi, ni kwa nini sheria hizo zisitekelezwe kwa kina na kwa uthabiti kuliko kutumia task force ya Jeshi la Polisi, TAKUKURU pamoja na Usalama wa Taifa kitu ambacho kinatia hofu sana wafanyabiashara hao.
Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba TAKUKURU, Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi hawafahamu mambo yanayohusu kodi. Sasa hata kama ni task force kwa nini isiwe inahusisha TRA wenyewe pamoja na sheria zao za kodi ambazo zinajulikana nini kitafanyika iwapo mfanyabiashara ataendelea kukaidi kulipa kodi katika Taifa hili?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Godbless Lema kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema task force ni kwa ajili ya wale ambao kwa makusudi hawataki kutekeleza sheria ya ulipaji wa kodi kwa kuwatembelea kwenye maeneo yao, siyo wote ni wachache wale sugu. Nimeeleza kwamba task force hii imejengwa na TRA wenyewe Polisi na TAKUKURU na hapa kila mmoja ana wajibu wake. Kama mlipa kodi anaamua kulipa mpaka afuatwe na kwa sababu wanakusanya fedha Polisi yeye yuko pale kwa ajili ya ulinzi wa fedha ambayo inakusanywa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, TAKUKURU yuko pale kuona kwamba hakuna nafasi ya rushwa kutokea. Kwa sababu pale inakwenda kumuuliza na wakati mwingine mlipa kodi sugu anaweza kudhani kwamba anadaiwa fedha nyingi akatamani kufanya makubaliano na Afisa wa TRA kwa lengo la kutoa rushwa. Kwa hiyo, mtu wa TAKUKURU yuko pale kuhakikisha kwamba hakuna jambo lolote linalohusiana na rushwa linalofanywa kati ya mdaiwa sugu ambaye hakutaka kulipa yeye mwenyewe labda angeweza kushawishi alipe kidogo ili jambo lake liweze kuisha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kila mmoja ana wajibu wake lakini mwenye dhamana kubwa pale ni TRA kukumbushia sheria, kuonyesha kipindi ambacho amekaa bila kulipa na kwamba sasa anatakiwa kulipa kodi na kwa kuwa ni mdaiwa sugu basi pale inaonekana kwamba hataki kuchukua hatua hiyo wanatakiwa kumpeleka Polisi hata kama itakuwa alikuwa hana notisi. Kwa hiyo, timu ile inalenga zaidi kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vya uovu vinavyoendelea kwenye uendeshaji wa zoezi lile lakini halilengi kumtisha mfanyabiashara. Polisi hawajibiki kumtisha wala TAKUKURU hausiki na mfanyabishara isipokuwa ni TRA mwenyewe kama ambavyo nimeeleza.
Mheshimiwa Spika, kwa hili nataka niwahakikishie wafanyabiashara, pamoja na haya yote yanayoendelea kwamba task force inapita kwenye maeneo haya haina nia mbaya kabisa na wafanyabiashara wetu na wawe na amani. Cha msingi zaidi kila mmoja sasa aone umuhimu wa kulipa kodi bila shuruti ili shughuli zetu ziweze kwenda kama ambavyo tumekubaliana.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Spika, nishukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, swali langu la nyongeza; kwa kuwa mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa hiyo ni nyingi na zimeharibu miundombinu. Serikali ina mpango upi wa dharura kuhakikisha mikoa hii inapata huduma ili katika kipindi inapojipanga waweze kupeleka huduma itakayosaidia kutatua matatizo ya barabara ambazo zimeharibika sana?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Kakoso, ni shahidi kwamba juzi tulipata taarifa kutoka Katavi, kwamba barabara zetu kule zimekatika kutokana na mvua nyingi. Hakuna mawasiliano sasa ya kutoka Mpanda, kwenda Tabora kupitia Sikonge, hakuna mawasiliano kutoka Mpanda kwenda Kigoma kupitia Uvinza, hata tuta la reli nalo limetetereka.
Mheshimiwa Spika, tulichofanya juzi tumechukua hatua za haraka na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amefanya kazi hiyo vizuri, amepeleka Wataalam, hapa ninapozungumza wataalam wapo pale wanaimarisha barabara ile, ili kuweza kurudisha mawasiliano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuwa mvua zinaendelea tumeamua tutafute njia nzuri, ambayo itakuwa na uhakika wa kuunganisha mawasiliano kati ya Mpanda na mikoa ile pamoja na Tabora kwa kurudisha reli, njia ya treni kutoka Dodoma itakwenda Tabora - Kaliua ili iweze kwenda Mpanda. Ile sehemu ya tuta ambalo lilikuwa limeharibika tumeshakamilisha na tayari tumeliambia Shirika la Reli, wauze tiketi Dar es Salaam, abiria wote wanaokwenda Mpanda wapewe mabasi waletwe Dodoma kupanda treni inayokwenda Mpanda.
Mheshimiwa Spika, hiyo ndio njia ambayo tumeamua tuitumie sasa ili kuimarisha usafiri wa kwenda Mpanda; huku Tanroad wakiendelea na ukarabati wa barabara zote ambazo zimekatika na malengo yetu barabara hizo tuziimarishe ili ziweze kupitika wakati wote.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yake, ni ukweli usiopingika kwamba pale muda unapotumika au unapopita sana bila majibu hata status kutolewa katika Bunge, hoja hiyo huonekana kwamba imefifia umuhimu na ulazima wake.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na kwamba umetoa ahadi ya kwamba Wizara zitashughulikia, unaweza ukatoa a firm commitment kwamba katika Bunge hili, kabla Bunge hili la Bajeti halijaisha, Serikali itapitia Hansard na kumbukumbu zote zinazohusiana na Maazimio yaliyopita ya Bunge halafu Serikali itoe status report na naomba itambulike hapa kwamba status report siyo lazima ndiyo iwe ripoti ya uchunguzi ya mwisho, angalau ituambie jambo hili limefikia hapa, limefanyiwa kazi moja, mbili, tatu, bado tutaletewa katika hatua ya baadae.

Mheshimiwa Naibu Spika, angalau Bunge lipewe status ya Maazimio kadhaa ambayo ni mengi kwa kweli, ambayo yameshaazimiwa na Bunge hili, Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa sababu ya hiyo nia njema ya Serikali, unaweza ukatoa commitment hiyo?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimeeleza awali kwamba masuala yote haya yanagusa maeneo mengi sana ambayo yanatakiwa ufuatiliaji wa kina na baadae nilieleza kwamba kila tukio linagusa Wizara kadhaa, kwa hiyo siwezi kusema kwamba katika Bunge hili nitakuja kuleta taarifa hiyo mpaka pale ambako nitakutana na Wizara, nijue wamefikia hatua gani, pia tutakutana na Mheshimiwa Spika ili tujue utaratibu mzima wa namna ya kupata hizo Hansard na kufanya mapitio. Tukijiridhisha na tukiona kwamba jambo hilo sasa linafaa kuletwa Bungeni na kwa kuwa liliazimiwa na Bunge, basi tutafanya maamuzi ya pamoja ya kuleta Taarifa hiyo Bungeni.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, ahsante kwa majibu yanayotia matumaini, lakini umeainisha kwamba tatizo kubwa tulilonalo ni tatizo la vyanzo vya maji. Je, Serikali haioni sasa imefikia wakati wa kuvuna maji ambayo maji mengi kwa mfano, wakati wa masika kama sasa hivi, maji mengi yanapotea hakuna namna yoyote ya kuvuna hayo maji ili iwe ni chanzo mbadala cha maji?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya mipango ambayo tunayo ni ya uchimbaji wa mabwawa kwenye maeneo ambayo tunadhani tunaona kwamba kuna utiririshaji wa maji hasa msimu wa mvua.

Pili, tumeendelea kutoa elimu kwa Watanzania kuzitumia mvua na maji ambayo yanatiririka, kuweza kuyaweka pamoja ili yawe akiba yetu ya kuweza kupata maji na kusambaza kwenye vijiji. Mpango huo upo pia hata kwenye bajeti umeona mipango wa uchimbaji mabwawa maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Kuchauka, wewe unatoka Liwale ni jirani yangu na ninapafahamu Liwale, iko miradi mingi sana tu ya kuchimba mabwawa, lakini jambo la kusikitisha ni kwamba juzi nilikuwa nazungumza na Mkurugenzi wako akiripoti kwamba kuna mvua nyingi, mabwawa mengi yameharibiwa, kwa hiyo tuahitaji tena kutenga fedha za kutengeneza mabwawa yako pale, jambo hili nalo tunalifanya karibu maeneo yote ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika nasihi na ninatoa wito kwa Halmashauri zote za Wilaya nchini kuhakikisha kuwa tunatumia vizuri mifereji iliyopo na mvua ambazo sasa zinaisha mwishoni, pia hata msimu ujao wa mvua kuweza kujenga mazingira ya kukusanya maji yanayotiririka, wenye nyumba za bati na nyumba zote watumie mvua hizi kupata maji na kuyaweka mahali ili tuweze kuyatumia kipindi cha ukame, kwa kufanya hilo tutakuwa tumepunguza ugumu wa upatikanaji wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaahidi Waheshimiwa Wabunge na Watanzia wote Serikali itaendelea na mipango yake ya kuhakikisha kwamba tunamtua ndoo Mama ili aweze kufuata maji kwa umbali mfupi na hasa ule umbali ambao tumejiwekea kwenye sera wa usiozidi mita 400. Ahsante
MHE. KUNTI Y. MAJALA: heshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, mkiwa bado kwenye huo mchakato wa kwenda kupitia sheria na mambo kadha wa kadha, hata wewe pia unafahamu kuwa changamoto kubwa iliyopo baina ya wakazi wa Manispaa ya Dodoma na CDA, nini tamko lako kwa CDA kuhusiana na bomoabomoa zinazoendelea bila wananchi hao kulipwa stahiki zao?

Jambo la pili, endapo hamtakamilisha huo mchakato, mnawaambia nini Watanzania wa Manispaa ya Dodoma kwamba ahadi iliyotolewa ilikuwa ya uongo na kuwarubuni Watanzania ili mpate kura then muwapotezee? Kama msipofanya hivyo mnawaambia Watanzania wasiwachague tena kwa sababu mmekuwa na ahadi za uongo zisizotekelezeka? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nimwambie usiwe na mashaka ya utekelezaji wa Ilani zetu na kwamba umeanza kutanguliza majibu ya wananchi msiwachague tena hilo siyo lako, wewe subiri tutekeleze ahadi zetu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachotaka nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote wa Mkoa wa Dodoma wakiwemo na wananchi wa Manispaa, jambo muhimu hapa ni kufanya maboresho ya Mji wa Dodoma ambako ni Makao Makuu ya Serikali. Kama ambavyo nimeeleza kwenye maelezo yangu ya msingi kwamba tayari Tume imeshaundwa wanaendelea kuharakisha zoezi hilo la kuhakikisha kwamba tunaondoka kwenye sheria iliyounda CDA ili kurudi kwenye sheria tuweze kuifanya CDA iweze kufanya kazi zile ambazo zitampa mwananchi haki ya kuweza kumiliki ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lipo swali ambalo limesema wale ambao wanabomolewa na CDA, sasa hili ni lazima tufanye mapitio CDA utaratibu wanaoutumia, wanabomoa kwa ajili ya nini na je, maeneo hayo na wale wanaobomolewa wanatakiwa kupata stahili ya namna gani. Kwa sababu sheria tuliyonayo inamtaka popote ambako unataka kupatumia kwa kuondoa mali ambayo mwananchi amewekeza lazima uilipie fidia.

Kwa hiyo sheria ipo, lazima tuone tufanye mapitio tuone CDA sasa wanaendesha operation wapi na wanalipa au hawalipi ili tuweze kujua kama hawalipi kuna sababu gani za msingi za kutolipa, lakini haki ya kulipwa ipo pale na ninaamini CDA ipo ofisini kwangu, kwa hiyo nitafanyia mapitio halafu nitakupa taarifa.
MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, umekiri kwamba ni kweli Serikali inadaiwa, lakini umesema kwamba kuna dosari ambazo zimejitokeza katika uhakiki wa zoezi hilo na toka mwaka 2014/2015 – 2015/2016 ni muda mrefu. Serikali kwa nini haiwezi kuona kwamba kuna haja sasa ya kuharakisha zoezi hilo kama watu wanastahiki zao wakalipwa kwa maana hivi sasa ninavyozungumza ziko taarifa kwamba kuna baadhi ya mawakala hivi sasa wameuziwa nyumba zao, kuna baadhi ambao hivi sasa wanashindwa kusomesha watoto wao shule na kuna baadhi ya mawakala ambao wamefariki kwa mshituko baada ya kuona nyumba zao zinauzwa na mabenki. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri Mkuu, kazi hii kama hawa watu mmewatambua na wamefanya kazi yao kwa uadilifi. Serikali kwenye hii Kamati ya kuandaa mawakala ilijumuisha Serikali wakiwemo wa TAKUKURU, Polisi, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya. Sioni ni kwa nini uhakiki wa namna hii na ucheleweshaji wa namna hii kwa hawa watu ambao wamefanya kazi yao kwa uadilifu. Mheshimiwa Waziri Mkuu umetoa commitment kwa mawakala hawa kwa siku….

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Devotha Minja muda wako unakwisha naomba uulize swali sasa ili uweze kujibiwa.

MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Waziri Mkuu ulitoa siku 25 kwamba zoezi hili la uhakiki liwe limefanyika Tanzania nzima kwa mawakala zaidi ya 940. Ni kwa nini mpaka sasa kwa miaka hiyo toka mwaka 2014 watu hawa Serikali haitaki kuwalipa haki yao ya msingi?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kupitia mazungumzo yetu kwa pamoja na mawakala wote tulitoa muda ambao tumejipanga kufanya uhakiki wa madeni yaliyobaki ili tuweke utaratibu wa kulipa na tarehe hiyo imeishia jana tarehe 31. Kwa hiyo, sasa nasubiri taarifa kutoka Halmashauri za Wilaya zote zitakazokusanywa kwenye ngazi ya Mikoa na Mikoa itatuletea takwimu na baada ya kupeleka Wizara ya Kilimo ikishapitia watapeleka Wizara ya Fedha na malipo hayo yatalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba baadhi ya mawakala kwa mujibu wa mazungumzo yetu walieleza adha
hiyo ambayo wanaipata, lakini kupitia kauli hii wanasikia pia hata wale wadai kwamba, wale wote ambao watakuwa na madeni sahihi baada ya kuhakikiwa ni watu wema na ndio ambao pia tunajua tunatakiwa tuwalipe. Kwa hiyo, hakuna umuhimu wa kuharakisha kunyang’anya nyumba, na kufanya vitu vingine ni jambo la kuona kwamba taratibu hizi tunazozitumia ni taratibu ambazo zinaleta tija kwa Watanzania, zinaleta tija kwa Serikali kwa sababu tungeweza kupoteza mabilioni ya fedha ambayo yangeweza pia kusaidia kwenye miundombinu nyingine, lakini sasa tumebaini kwamba hayakuwa ya ukweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natumia nafasi hii kutoa wito kwa watumishi wa Serikali wote ambao wamehusika katika hili ambao pia tutawabaini kwamba wao walihusika kwenye wizi, ubadhirifu na udanganyifu huo wote tutawachukulia hatua kali, hilo moja.

Pili, wale wote ambao wameshiriki katika hili, nirudie tena kuwahakikishia kwamba madeni hayo yakishathibitishwa kwamba fulani anadai kiasi fulani tutawalipa kama ambavyo tumetangaza, ahsante sana.
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, vilevile naishukuru sana Serikali yangu inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi, nakushukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri yenye kutia moyo na faraja kwa watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali dogo la nyongeza na swali hili ni kwa mujibu wa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma Wenye Ulemavu ambao katika kifungu cha 3 (12) chenye vipengele vya (a), (b), (c) na (d) vinatambua na vinasisitiza na kusema kwamba, nitanukuu kidogo; “kutambua kuwa ni haki ya watumishi wenye ulemavu kupatiwa mahitaji yao muhimu kama vile vifaa vya kuwaongezea uwezo, fedha kwa ajili ya matibabu na ukarabati wa afya zao (rehabilitation), nyenzo na vifaa hivi vitolewe na waajiri.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninataka kupata kauli yako Mheshimiwa Waziri Mkuu, baadhi ya waajiri hawatekelezi majukumu haya kwa watumishi wa umma wenye ulemavu. Kama baba mwenye dhamana, nini kauli yako kwa waajiri wasiotimiza wajibu wao kama Mwongozo wa Utumishi wa Umma unavyowataka kutekeleza mahitaji hayo kwa watumishi wa umma wenye ulemavu? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo ameeleza kwamba, uko mwongozo wa Serikali juu ya Watumishi wa Umma wanaofanya kazi kwenye taasisi zetu za Serikali, lakini pia sio Serikali tu, hata taasisi zisizokuwa za kiserikali, unawataka waajiri wote wanapowaajiri wenzetu ambao wana mahitaji maalum lazima watekelezewe mahitaji yao ili kuwawezesha kufanya kazi yao vizuri. Kwa maana hiyo, kwa upande wa Serikali Wizara zote ziko hapa, Mawaziri wako hapa, Makatibu Wakuu wanaisikia kauli hii na kwamba lazima sasa watekeleze mahitaji na matakwa ya Serikali ya kuwahudumia hawa watumishi wenye mahitaji maalum kulingana na sekta zao. Kama yeye yuko upande wa ukarani, basi wahakikishe ana vifaa vya kutosha kumwezesha kufanya kazi hiyo vizuri na hivyo kila sekta lazima apate huduma hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatoa wito kwa sekta binafsi kutoa nafasi zaidi za ajira kama ambavyo Serikali tunawaajiri wenye mahitaji maalum. Hakuna sababu ya kukwepa kuwaajiri ati kwa sababu unatakiwa kuwahudumia. Wote ni Watanzania na wote wana uwezo na tumethibitisha uwezo wao, pia hata Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kuthibitisha kwamba sera hii ni yetu ndani ya Serikali ametoa ajira, ameteuwa watumishi ambao wana mahitaji maalum na hawa wote mahali pao pa kazi wanawezeshwa kwa vifaa vitakavyowawezesha kufanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishie tutaendelea kuajiri ndani ya Serikali na ninatoa wito kwa sekta binafsi ziajiri Watanzania wenzetu wenye mahitaji maalum wote ambao tunaajiri, wenye mamlaka ya kuajiri, na
Mwenyekiti wa Tume ya Ajira yuko hapa wa Chama cha Waajiri yuko hapa, asikie ili awaelekeze wenzake kwamba, ni wajibu wa kila muajiri kuwawezesha wenye mahitaji maalum kufanya kazi zao baada tu ya kuajiri, kama ambavyo Sera ya Serikali inahitaji kufanya hivyo. Ahsante.
MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Kwa kuwa tatizo hili la upimaji wa mchanga linaanzia kule ambako ndiko kuna machimbo yenyewe. Ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kule origin source kunawekwa mashine ambazo sasa tatizo hili halitajirudia tena?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, moja kati ya mikakati ambayo tunayo ni kupokea wawekezaji na tumeanza kuona wawekezaji kadhaa wakija kuonesha nia ya kuwekeza kwenye eneo hili. Awali kulikuwa na usiri mkubwa wa namna ya kuwakaribisha wawekezaji hawa kuwekeza kujenga mitambo hii na ndio kwa sababu Serikali imeanza kuchukua hatua za awali kwa vile tunajua kwamba, kuna maeneo ambayo yalikuwa hayaoneshwi wazi ikiwemo na eneo la kuwakaribisha wawekezaji wa kujenga mitambo hii hapa nchini.

Baada ya muda mfupi kama ambavyo mambo yameanza kujitokeza tutaamua kuwekeza, kujenga mashine zetu hapa hapa nchini au kuwakaribisha wawekezaji au kuona uwezo wa Serikali kama tunaweza ili sasa tuweze kutatua tatizo ambalo linatukabili sasa la kupoteza mchanga ambao tunautoa hapa na kupeleka nje kwa ajili ya uyeyushaji na kupata aina mbalimbali za madini. Ahsante.
MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kuna swali dogo tu la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri ambayo kutoka Serikalini.

Swali dogo la tu la nyongeza, kwa kuwa kama ulivyosema kwenye majibu yako ya msingi, kwamba mmegundua kuna watu ambao wameleta madai ambayo si sahihi, lakini naamini pia kuna watu ambao watakuwa madai yao ni sahihi. Sasa nini kauli ya Serikali kwa wale ambao madai yao ni sahihi ambao wamekaa muda mrefu kiasi kwamba imewaongezea gharama kwa maana ya riba sehemu walizokopa, nani atalipa gharama hizi kwa ajili ya usumbufu uliotokea na gharama zilizoongezeka kwenye madeni hayo?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mgumba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu la awali kwamba kwanza tunathamini sana kazi waliyoifanya katika kutoa huduma kwenye sekta zetu. Lakini mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki ambacho sisi tunafanya uhakiki. Baadhi ya wadai nimepata nafasio ya kukutana nao hapa Dodoma wakati huu wa Bunge na kuzungumza nao na kuwaambia kwa nini tumechelewa kuwapa fedha zao, wale ambao kweli wana madai halali.

Mheshimiwa Spika, lakini bado nirudi tena kusema kwamba, hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya uchelewaji huu wa kulipa kwa sababu tuko kwenye zoezi la kuhakiki, ili tujiridhishe. Kama ingekuwa tumechelewa tu, kwamba hatuna kazi yoyote, tumeacha tu hapo kungekuwa na swali ambalo naamini unacholenga kingeweza kupata maelezo. Lakini bado niwahakikishie kwamba taratibu zinakamilika na tulisema tunakamilisha tarehe 30 Juni, yaani kesho tu tarehe 30 Juni, tunatarajia Wizara ya Fedha itapewa taarifa kutoka kwenye Wizara mbalimbali, kwamba madai yetu halali ni haya kwa ajili ya watu hawa kwa huduma waliyoitoa, baada ya hapo tunalipa tu na tutaendelea kuwapa nafasi zaidi ya kutoa huduma.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niwahakikishie kwamba wataendelea kutoa huduma, hasa wale ambao ni waaminifu kwenye awamu ijayo hii ya mwaka wa fedha mpya wa mwaka 2017/2018.
MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ndiyo.

Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana kwa majibu ambayo hakika yameponya nyoyo za watu ambao walikuwa wanaguswa sana na suala hili la CDA. Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa umesema mamlaka haya; na umeeleza vizuri Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma itakavyofanya kazi, naamini na Halmashauri nyingine nchi nzima zitafanya kazi kama ambavyo umetoa maelekezo.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo moja tu, kwamba wanapokwenda kuchukua ardhi kutoka kwa wamiliki au kwa watu ambao wanahodhi zile ardhi zao, wanalipa fidia kwa fedha ndogo sana, lakini wanapokuja kupima na kutaka kuviuza wanauza kwa bei ambayo ni tofauti na ile gharama ambayo walinunulia.

Je, Serikali hapa inaweza pia ikatoa maelekezo kwamba, angalau uwiano wake usipishane sana kwa ajili ya kuwanufaisha hata wale wahusika wa maeneo ambayo yanakuwa yamechukuliwa? Ahsante sana.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mlata, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ziko sheria ambazo zinaongoza fidia na ndizo ambazo tunazifuata. Fidia hizi kuna watu ambao wamepanda mazao kwenye ardhi, lakini wengine hawajapanda chochote. Kwa hiyo, mabadiliko ya bei ama tofauti ya bei inatokana na ambavyo mwenye ardhi alivyoweza kuwekeza kwenye eneo lile. Kama kuna mazao yoyote yanafanyiwa tathmini na tunalipa kwa mujibu wa bei na taratibu zilizopo kisheria.

Kwa hiyo, bado tutasisitiza mamlaka zote za halmashauri zote za Wilaya, Miji na Manispaa na Majiji kufuta sheria zile ambazo zimeelekezwa katika kufanya fidia. Na tumesemea ardhi ya mtu isichukuliwe bila fidia, kwa hiyo, bado hili litaende kuzingatiwa. Na agizo hili naomba wazingatie maeneo yote haya ambayo nachukua ardhi ya mtu, kwamba lazima alipwe kwanza ndipo uweze kuchukua, ili kuondoa migogoro ambayo siyo muhimu kwa sababu sheria ipo na inatuongoza kufanya hivyo, ahsante.
MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, ndiyo.

Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana kwa majibu ambayo hakika yameponya nyoyo za watu ambao walikuwa wanaguswa sana na suala hili la CDA. Lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kuwa umesema mamlaka haya; na umeeleza vizuri Halmashauri ya Manispaa ya



Dodoma itakavyofanya kazi, naamini na Halmashauri nyingine nchi nzima zitafanya kazi kama ambavyo umetoa maelekezo.

Mheshimiwa Spika, kuna tatizo moja tu, kwamba wanapokwenda kuchukua ardhi kutoka kwa wamiliki au kwa watu ambao wanahodhi zile ardhi zao, wanalipa fidia kwa fedha ndogo sana, lakini wanapokuja kupima na kutaka kuviuza wanauza kwa bei ambayo ni tofauti na ile gharama ambayo walinunulia.

Je, Serikali hapa inaweza pia ikatoa maelekezo kwamba, angalau uwiano wake usipishane sana kwa ajili ya kuwanufaisha hata wale wahusika wa maeneo ambayo yanakuwa yamechukuliwa? Ahsante sana.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Mlata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Mheshimiwa Rais alitoa agizo la kuvunja Mamlaka ya CDA na mamlaka hiyo na majukumu yake kuyahamishia Ofisi ya Rais – TAMISEMI, kupitia Manispaa ya Dodoma. Kazi hiyo imeshafanywa na zoezi linaloendelea sasa kwanza wale watumishi wote wa CDA watahamishiwa Manispaa ya Dodoma, lakini tutafanya mchujo kidogo, wale ambao walikuwa na malalamiko, wanalalamikiwa na wananchi wale wote tutawaweka pembeni, kwa sababu tunataka tupate timu mpya ambayo inafanya kazi vizuri.(Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbili, tunaendelea sasa na uhakiki na ukaguzi wa kina kwenye masuala ya fedha na utumishi wenyewe ili tuweze kuanza vizuri, tujue CDA ilipoacha iliacha na fedha kiasi gani na shughuli zake zilifikia hatua gani halafu pia kuweza kuendelea, lakini majukumu yote yanabaki kama yalivyokuwa na CDA yataendelea kufanywa na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma. Kinachobadilika pale ni maandishi, kama kwenye risiti zilikuwa zinasomeka CDA, sasa zitasomeka Manispaa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha utaratibu huu mpango kazi wote utaendelea kama ulivyokuwa. Kama kuna mtu alilipa nusu anataka kumalizia, wataendela kukamilisha malipo yao, kama kuna mtu alishakamiliha hajapata kiwanja, ataenda kukabidhiwa kiwanja chake na namna yoyote ya utendaji wa kawaida utaendelea. Sasa hivi akaunti zote zimefungwa kwa hiyo, huwezi kulipa mpaka hapo tutakapofungua malipo.

Mheshimiwa Spika, tutamuagiza Mkurugenzi sasa wa Manispaa, atoe maelezo sahihi kwa Wana Dodoma na kwa Wananchi, Waheshimiwa Wabunge mkiwemo ili kila mmoja aweze kujua, lakini kwa kauli hii ndio usahihi wa taarifa ya CDA kwa namna ambavyo tumeivunja na tumehamishia Mamlaka pale Manispaa ya Dodoma na watumishi wote sasa watawajibika kwa Mkurugenzi wa Manispaa na hakutakuwa na chombo kingine pale.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ambayo tumewaelekeza sasa pale CDA kwenye Idara ya rdhi, kwenye lile jengo lisomeke Idara ya Ardhi - CDA na huko ndani tume- plan sasa Wizara ya Ardhi ipeleke mtu anayeandika Hati. Tunataka pale ndani iwe One Stop Centre. Ukienda kuomba ardhi, ukishapimiwa, ukishalipia, hati unapata humo humo kwenye hilo jengo. Kwa hiyo, tunataka turahisishe upatikanaji wa hati na viwanja kwenye jengo hilohilo moja, ukiingia ndani ukitoka unatoka na hati yako badala tena kwenda mahali pengine. Ahsante.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu, nakubaliana na wewe kwamba maisha ya kila Mtanzania yana thamani kubwa, lakini swali langu lilikuwa specific, sikuzungumza suala la Watanzania wote wanaoathirika kwa matukio mbalimbali. Swali langu lilikuwa very specific ya jambo linaloitwa political persecution, na ningeomba nieleweke hapo.

Mheshimiwa Spika, matukio ya kushambuliwa Mheshimiwa Lissu, lile tukio si la kawaida na naomba tusijaribu kuli-dilute kwa kuchanganya na matukio mengine mengi. Nimeuliza swali specific ambalo ninaomba specific answers. Na uonevu dhidi ya viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani nchini umekuwa ni utamaduni wa kawaida. Vyombo vya dola vinafanya, vinatesa watu na vinaumiza watu.

Mheshimiwa Spika, leo ninavyozungumza hivi ni siku ya tatu tangu Mbunge wangu wa Ndanda, Mheshimiwa Cecil Mwambe akamatwe na polisi Mtwara na yuko chini ya custody sasa hivi ni zaidi ya saa 48, kisa alikuwa anafanya mkutano wa kampeni ya uchaguzi katika kata mojawapo pale Mtwara Mjini, polisi wakamshika. Huyu ni Mbunge na Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini yenye Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, yuko ndani siku ya tatu sasa. Sasa matendo haya ya uonevu yanaendelea na hivi tunavyokwenda kwenye uchaguzi wa marudio katika hizi kata chache, viongozi wetu kadhaa wanakamatwa, wanawekwa ndani, wanapigwa na wanateswa.

Mheshimiwa Spika, sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu ninachouliza, mimi nilikuomba specific utuambie Serikali inaona shida gani? Kwa sababu si mara ya kwanza kwa Serikali hii kuomba msaada wa vyombo vya uchunguzi kutoka nchi za nje. Wakati Benki Kuu ilipoungua Scotland Yard walikuja hapa kufanya uchunguzi kuhusu jambo hili, ni mambo ya kawaida katika jamii ya kimataifa.

Mheshimiwa Spika, na kwa sababu vyombo vya dola tumevi-suspect kwamba either havikuchukua tahadhari ya kulinda viongozi au havikuchukua hatua ya mapema kuzuia uharifu ule aidha kwa kutaka ama kwa kushiriki. Lakini ambacho napenda nikuambie Mheshimiwa Waziri Mkuu, mimi nina imani kabisa vyombo vyetu vya ndani vina uwezo wala sidharau, ila hakuna dhamira ya kuchunguza jambo hili, hapo ndio kwenye tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kwa sababu hakuna dhamira na kwa sababu wanaoonekana wanaumia ni wa upande mmoja tunaitaka Serikali itoe hiyo clearance. Waje watu wafanye investigation kama ni ku-clear kila mtu anaehusika awe cleared ili jambo hili likomeshwe kwa sababu linaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Waziri Mkuu, ni kwa nini sasa usikubali kwa niaba ya Serikali turuhusu vyombo vya uchunguzi vya kimataifa vije vikamilishe jambo hili ili tukate huu mshipa wa fitina?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbowe unaposema jambo hili nilijibu umeliuliza specific, naweza kusema kwamba unapotaka specific basi inabidi sasa vyombo vya usalama vikamilishe kazi yao ndio vije viseme hasa kwa tukio ambao umetaka lizungumzwe. Hakuna mtu yeyote aliyefurahishwa na tendo alilofanyiwa Mbunge mwenzetu. Hakuna mtu yeyote anayefurahishwa na matukio yanayojitokeza huko iwe ya mauaji au ya mashambulio au migongano inayoendelea kwenye jamii yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini vyombo vya dola tumevipa jukumu la kusimamia na kuhakikisha kwamba tunalinda usalama wa raia na mali zao kwa kiwango kinachotakiwa. Na pale ambapo kunatokea tatizo, vyombo vya dola vina majukumu ya kuhakikisha kwamba vinafanya uchunguzi na kuwakamata wale wote ambao wamehusika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nimeeleza hapa kwamba wakati wote watenda makosa ni watu ambao wanafanya matendo yale wakiwa wameshajiandaa pia kuweza uovu wao na kujificha dhidi ya vyombo vya dola. Wanapojificha sio kwamba vyombo vyetu vya dola havina uwezo wa kufanya kazi yake ya uchunguzi. Mimi nimekwambia haya matukio yote, wanayo matukio megi yamejitokeza katika kipindi kifupi, tumeanza hayo kama nilivyoeleza na huwa ninapozungumza Kibiti, Rufiji na Mkuranga sina maana ya kuficha au kulifanya jambo hili lisitambulike, hapana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunachukua mwenendo wa matukio, tunachukua uwezo wa vyombo vyetu na namna vinavyofanya kazi ili kuhakikisha kwamba tunabaini matukio haya na ndiyo sababu wakati wote Watanzania tumeendelea kuwaambia na kuwahamasisha kwamba ni lazima tushirikiane katika kuilinda nchi yetu na kila mmoja ashiriki katika kutoa taarifa. Sisi tunakaribisha mtu yeyote anayejua kama kuna mwelekeo wa jambo hili atusaidie ili
vyombo vya dola viweze kufanya kazi yake kwa urahisi zaidi.
(Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, najua unazungumzia kwa upande wako kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani na yeye Mbunge mwenzetu ambaye ni Mheshimiwa Tundu Lissu anatoka kwenye upande wako, lakini utambue kwamba na sisi pia ni Mbunge mwenzetu na jambo hili ni letu pia, lazima tushirikiane kuhakikisha kwamba jambo hili linapata mwelekeo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nikuhakikishie vyombo vyetu uwezo upo, lakini pale ambapo wataona kama kuna umuhimu huo, vyombo vyenyewe vitafikia hatua vinaweza vikalieleza, lakini mimi siwezi kuhakikishia Taifa kwamba tumekosa uwezo kwa sababu tunaamini vyombo vyetu vinao uwezo wa kufanya uchunguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Kiongozi mwenzangu wa Kambi ya Upinzani naomba uamini kabisa kwamba Serikali yetu inayo nia njema, familia za wale wote walioathirika akiwemo Mbunge mwenzetu, Mheshimiwa Tundu Lissu waamini kwamba Serikali yetu inayo nia njema ya kukamata, lakini pia ya kulinda amani ya nchi hii ili kila mmoja, hata sisi pia tuwe na uhakika wa shughuli tunazozifanya za kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tutaendelea kufanya hilo na tutaendelea kuwasiliana nawe kama kiongozi mwenzetu ili uweze kuona haya na namna ambavyo tunaweza tukatatua matatizo haya ya ndani, juu ya matatizo ambayo yanajitokeza kwenye maeneo yetu, ahsante sana.
MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu unajua vizuri sana, Serikali yako inajua vizuri sana, Watanzania wanajua vizuri sana kwamba vyama vya siasa vya upinzani vimezuiwa kwa miaka minne sasa kufanya kazi zake za siasa za uenezi. Na Mheshimiwa Waziri Mkuu unapotupa maelezo ndani ya Bunge ya kuhalalisha kilichofanyika na ukasema ni utaratibu ambao mmejiwekea mmejiwekea kwa sheria ipi. Najua yote hayo unajua vizuri sana, kwamba Tume ya Uchaguzi unayoiita ni huru kwa sababu imeandikwa kwenye katibu si huru na watendaji wake vilevile wamekuwa ni partisan sana na masuala haya yamejitokeza wazi na yanaonekana.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE.FREEMAN A. MBOWE: Weweee!!!

MHE. ESTER A. BULAYA: Naomba muwe na adabu.

MHE.FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu haya ni majibu mepesi ambayo kuna siku mtakuja kujuta katika nchi hii kwa majibu haya mepesi. Je…

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. ESTER A. BULAYA: Keleleni huko!

MHE.FREEMAN A. MBOWE:… Mheshimiwa Waziri Mkuu, narudia kwa mara nyingine hamuoni ni muda mwafaka sasa Serikali ikaona umuhimu wa wadau mbalimbali ambao wanahusika na masuala ya uchaguzi katika nchi hii kukaa na kutafuta njia bora zaidi ya kwenda kwenye uchaguzi Oktoba kuliko kwenda kibabe kwa namna ambavyo tunataka kwenda?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbowe Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nataka nikanushe kwamba Serikali inaongoza kibabe, haiongozi kibabe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbowe ni kiongozi tunazungumza, tunabadilishana mawazo; sote tunapobadilishana mawazo tunalenga kulifanya Taifa hili liwe na usalama, liwe tulivu ili shughuli zetu ziweze kwenda lakini muhimu zaidi Watanzania wanahijtai maendeleo. Kwa maana hiyo tunapoweka utaratibu wa namna ya kuwafikia wananchi na kupata maendeleo jambo hili si la chama kimoja ni kwa nchi nzima. Hakuna Mbunge wala Diwani aliyezuiliwa kwenye eneo lake kufanya siasa na watu wake. Kunaweza kuwa labda kama kuna tatizo mahali fulani kwa utaratibu ule tunaozungumza tunakutana tuambizane wapi kuna shida. Kama wiki iliyopita Mheshimiwa Sugu alieza kwamba kule Mbeya anazuio na OCD na mimi nilimuita hapa tumezungumza. Mkuu wa Mkoa ameungana naye, Mkuu wa Polisi Mkoa ameungana naye. Shida kama ziko kwenye ngazi ndogondogo huko ni suala kuzungumza kwenye eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani; tunakuheshimu sana, tunatambua una majukumu kwa chama chako lakini Serikali yetu inaendelea kushirikiana na Viongozi wote kwa Mamlaka zao ili kufanya taifa hili liendelee kuwa salama na tulivu, pale ambako kuna shida ya namna hiyo tuendelee kuwasiliana Mheshimiwa Kiongozi wa Kambi za Upinzani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili suala la Tume hii kuonwa kwamba si huru ni mtizamo wa mtu lakini Kikatiba na utendaji wake uiko huru. Pale ambako panaonekana kuna shida basi kwa utaratibu ule paelezwe kwamba hapa kuna shida lakini hatujawahi kuona Rais akiingilia, chama cha siasa kikiinglia ile Tume iko huru na inafanya kazi yake kama ambavyo imetakiwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kukiwa na jambo lolote lile unao uhuru wa kubadilishana mawazo ili tuone wapi tusaidie katika kufanya jambo hilo liweze kwenda sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nakushukuru Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu ni ukweli kabisa kwamba, hawa askari hawapewi hizi sare na hata wakifanya parade utaona uniform zao ziko tofauti-tofauti kwa texture, lakini hata kwa rangi.

Mheshimiwa Spika, nilitaka pia kujua, maana hujajibu swali langu lile jingine, fidia ambazo watarudishiwa gharama ambazo wakati mnaendelea kujiratibu kuhakikisha wanapewa hizi uniform. Je, wataweza kuridishiwa gharama ambazo wamekuwa wakizitumia kujinunulia uniform zao wenyewe?
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu umelieleza hilo na unaonesha unazungumza kama una uhakika wa kwamba, askari wetu wananunua. Na ungependa kujua je, kama askari hao wanaweza kurudishiwa fedha zao kama sera ya kuwapa vifaa bure ipo?

Mheshimiwa Spika, basi naomba nilichukue hilo niwasiliane na Wizara husika, ili tuone msingi wa ununuzi wa vifaa hivyo, halafu tutaweza kuzungumza vizuri na Wizara ya Mambo ya Ndani na tutakupa taarifa Mheshimiwa Mbunge, ahsante. (Makofi)
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Pamoja na kuvunja tume hiyo sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa nini wakulima sasa wasipate wataalam bora kwa ajili ya kilimo hicho cha ili waendane sambamba na huu uvunjaji wa hii tume tupate kilimo chenye tija? Ahsante.
WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Susan Lyimo, Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, utaratibu ambao sasa tunaufanya ni kwamba mbali ya kwamba kuna Tume ya Umwagiliaji, ina maafisa wake lakini tumewashirikisha pia Maafisa Kilimo wa Wilaya, Maafisa Ugani walio kwenye ngazi za vijiji, wote hawa wafanye kazi kama timu moja. kwa hiyo, usimamizi wa kilimo utakuwa ni wa pamoja na kila palipo mradi iwe mradi upo kijijini, tutakuwa na Afisa Ugani wa Kilimo pale kijijini lakini yupo Afisa Ugani kwenye ngazi ya kata, yupo afisa kilimo ngazi ya Wilaya na Afisa Umwagiliaji ngazi ya Wilaya; hawa wote wakifanya kazi kwa pamoja na kwa maelekezo tuliyowapa na kwa sababu pia tulishasambaza maafisa kilimo kwa kuwaamisha kwenye Halmashauri ya Wilaya kuwapeleka vijiji, tuna amini kwa maelekezo yetu chini ya usimamizi makini wa Waziri wetu wa Kilimo na timu yake, tunaweza kufikia hatua nzuri na tuwahakikishie kwamba tutasimamia vizuri Sekta ya Kilimo na hasa kwenye Sekta ya Umwagiliaji. (Makofi)