Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Emmanuel Papian John (29 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri na kazi nzuri, ambayo inaifanya baada ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais. Napenda kushauri mambo machache yafuatayo:
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona kwenye elimu Serikali imefanya mambo mengi, lakini na mengi yamezungumzwa humu ndani ambayo yanaelekeza ni jinsi gani ambavyo elimu inaweza kwenda na jinsi gani iwe na watu wote wametoa ushauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kumshauri Mheshimiwa Waziri kwamba aanze na Primary Schools. Ile mitaala ya Primary Schools ya zamani tuliyoizoea airudishie ule mfumo kwamba ukikuta Kitabu cha Darasa la Kwanza anachokisoma Mwanafunzi aliyeko Nkasi Tanzania, kule Rukwa, Sumbawanga, kitabu hicho hicho tukikute Lindi cha Darasa la Kwanza, kinachofanana na kinachosomeka vile vile. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Mheshimiwa Waziri a-plan Primary Schools kwanza, asiende haraka! Sekondari pumzika, Vyuo pumzika, taratibu tu, kule kunakwenda kuna Makamishina, kuna watu wanafanya, wewe nenda na Primary Schools, jenga misingi; hakikisha Walimu wanafundisha, hakikisha shule zinakaguliwa, hakikisha kuna utaratibu wa elimu kwa zile ambazo ni Sekondari, za Kiingereza Primary Schools wawe na mitaala inayofanana. Zile za Kiswahili zirudi vile vile kama zamani. Sayansikimu; mtoto afundishwe kutengeneza mwiko, chungu, afundishwe kupika, kulima; tunataka hiyo ianze Primary School bila haraka kwa mwaka huu. (Makofi)
Mwaka kesho wewe nenda Secondary School, Form One mpaka Form Six, panga mambo vizuri, usiwe na haraka, pesa hazitoshi na sisi ndiyo wakusanyaji, hazipo! Hicho kidogo kinachopatikana, mwaka kesho plan for Secondary School, Form One mpaka Form Six. Mwaka unaofuata, plan kwa ajili ya vyuo, nenda tena mpaka Vyuo Vikuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri awatafute wale Walimu wa zamani waliokuwa wanafundisha zile shule za primary; kaa nao, zungumza nao wakupe tactics na the way kuingia katika huu mfumo wa kutengeneza elimu bora kama ile ya zamani ambayo tunahitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Waziri akae na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Tunao Mabalozi nje, wafanye kazi ya kutafuta scholarships kwa ajili ya wanafunzi wetu waende wakasome nje. Kila mwaka Balozi yeyote kwenye nchi aliyomo ambayo ina uwezo, aweze kuita na kutafuta wafadhili wasaidie watoto wetu wakasome nje. Lengo kuu la kusomesha watoto wetu nje, Watanzania wamejifunga; Watanzania wako magereza, wamefungwa; hawatoki nje! Wanafikiri hapa panaweza. Waende nje wakapigwe, wapigwe baridi, wapate shida, walale njaa, wakirudi Tanzania watashughulika na uwekezaji. Mheshimiwa Waziri, hebu jitahidi zungumza na hao watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, hawa wawekezaji mnaowaona ni kwa sababu wameona fursa huku, tupeleke watoto wetu kule. Wale watoto ukikaa nao ukiwaambia nenda kasome au nenda Netherlands, ukimaliza degree shawishi mfadhili ndugu yako mwingine apate nafasi umlete huko huko. Mkibaki huko, sawa; mkirudi Tanzania, sawa. Tutakuwa tumetengeneza Watanzania kwenye exposure ya dunia hii nao watoke nje wakaone vilivyoko huko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mkaguzi mmoja Kiteto alikuja ametoka kwenye kanda, ana gari, hana mafuta, hana nini. Nikamuuliza, sasa vipi? Anasema sasa nitakagua nini? Anataka kukagua na anayeombwa mafuta ni Mkurugenzi na akienda kuomba Mkurugenzi mafuta Mkurugenzi haiwezekani akamnyima mafuta kwa sababu anakwenda kumkagua; akimkagua anamletea madudu; akimletea madudu, hawataelewana. Matokeo yake anakosa mafuta, anakaa mezani analipwa mshahara bure. Hii ndiyo mishahara hewa ambayo tunazungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hawa Wakaguzi waanze na Primary School wakutengenezee kitabu, wakuletee ujue matatizo ya Primary School kwa nchi nzima kwa mwaka huu ili ujue sasa shida za ku-tackle matatizo ya Primary School yanaanzia wapi na yanakwenda wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto tuna shule za mabweni chache, lakini watoto wetu kwa sababu ya maeneo ya kifugaji, ni mbali. Shule nyingine ni kilometa 14, shule nyingine 15, sasa watoto kwenda shuleni ni ngumu.
Nakuomba, kuna shule za Dongo za sekondari, tunaomba hizi shule za bweni, za kifugaji basi mtusaidie waweze kusoma kwa maana ya kupata hela ya chakula ili wale watoto tuweze kuwa-accommodate kule kwa sababu wakirudi majumbani mwisho wa siku wanaolewa. Kule kuna ndoa ambayo Mkuu wa Shule akipewa ng‟ombe mmoja anaachia mtoto anakwenda anaolewa na anaolewa underage. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba zile shule zangu za Dongo, kuna Engusero, kuna Resoit Secondary School, kuna Rarakin Primary School. Hizi shule tunaomba zipate msaada wa kupata hela ya chakula ili watoto waweze kulala bwenini na wote tuwabebe wakae huko wasiweze kutoka kwenda kuolewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunamshukuru Mheshimiwa Rais, ali-plan na sasa tumefikia, changamoto zipo, ni nyingi, lakini tuna hakika kwa kushirikiana tutaweza. Naomba niseme, Bunge hili lilikwenda likazuia kidogo fimbo za makalio kidogo na kwenye mikono, hebu turudishe fimbo watoto wajue kwamba jamani kuna malezi. Turudishe bakora kidogo kwenye mikono; Walimu wanadharaulika! Wakisema, hawasikiki! Hebu turudishe huo utaratibu jamani, turudi tulikotoka. Sisi ni Waafrika. Ni lazima kuwa na nyenzo kidogo twende, hatutafika!
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hebu ajitahidi aangalie namna ya kuliweka hili, fimbo zirudi kidogo. Aombe huko juu fimbo zirudi halafu watoto waanze kuogopa, hata wawahi shuleni wakasome wakiambiwa wasome; wakikemewa wakimbie, wakiitwa waje wanakimbia. Discipline iwepo. Walimu wanatukanwa shuleni na mtoto wa Darasa la Tano na wazazi twende tukaseme. Waheshimiwa Wabunge nanyi semeni huko tushinikize hili tuondoe tabia utovu wa nidhamu, halafu watoto warudishiwe fimbo kidogo halafu mambo yasonge mbele.
Mheshimiwa Waziri, naomba kusema kwamba nakushukuru lakini anza na primary mwaka huu, umalize matatizo ya primary; mwaka kesho sekondari, mwaka kesho kutwa vyuo vikuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha, naunga mkono hoja. Ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naunga mkono hatuba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Madini kwa asilimia mia moja. Tatizo kubwa la umeme Kiteto ni umeme wa REA katika Kata ya Kijungu, Kata ya Songambele, Kata ya Magungu, Kata ya Dongo na Kata ya Sunya. Kata hizi zote zilikuwa za REA II, sasa tunaomba majibu ni lini Kata hizi zitapatiwa umeme, maana sasa tumeingia REA Awamu ya III haya maeneo yakiwa bado?
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.
Hali ya Uchumi wa Taifa Kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo ya Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nimpongeze Rais kwa maamuzi mazuri anayofanya kwa ajili ya nchi yetu.

Jambo la kwanza ninaloshukuru, nashukuru kwamba wale wenzetu wataalam Wakurugenzi wa Acacia wamekuja kuona ni jinsi gani wanaweza ku-negotiate na Serikali kulipa deni lao. Naomba niseme jambo, wakati mnakwenda kwenye negotiation hiyo, naomba wale mabwana walipe kwanza trilioni 35 mezani ili muweze kuanza mazungumzo. (Makofi)

Mhesimiwa Mwenyekiti, kabla ya mazungumzo yoyote yale walipe trilioni 35 kwanza zikae mezani halafu muanze kuchakata maneno, mengine mtazungumza na mtaendelea mbele kujua ni namna gani wanatakiwa kulipa lakini heshima ya nchi yetu kwanza, bajeti yetu ya Tanzania kwa mwaka mzima wailipe mezani down payment kuonyesha kwamba ni commitment fee kwa ajili ya kuilipa nchi yetu gharama zao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, niombe wale wataalam wetu waweze kwenda Ghana wajifunze ni namna gani wao kwenye madini walifanikiwa. Watengeneze ile ripoti waangalie ni namna gani wao wamefanikiwa vipi halafu sasa watakapokaa na hao wenzetu wajue ni techniques zipi za kuwatega na kutengeneza hili jambo likae vizuri ili siku nyingine lisijitokeze na nchi yetu iache kupoteza kwenye suala la madini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Rais kwa kuonyesha jinsi gani ameji-commit katika hili, Rais kutoka nje kwenda Ulaya kila wakati sio zuri, hawa weupe na wao waje hapa wainame pale Ikulu wa-bend kwa Rais wetu, ametujengea heshima. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha kwamba hawa watu na wao tunaweza kuwamudu, hawa watu kila siku ukienda kuwainamia wanafikiri sisi ni wajinga kwa sababu weusi. Sasa safari hii Rais ametujenga heshima, Bunge hili tumuunge mkono na tuhakikishe kwamba anatutetea kwa jinsi ilivyo, wawe wanakuja wanainama Ikulu, wana-bend wakimaliza wanapanda ndege zao wanaondoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais ameshamaliza kazi, sasa Bunge hili pekee ndiyo chombo pekee kinachoweza kumaliza migogoro iliyobaki. Tukubali tuungane tuwe wamoja tujenge nchi tukiwa serious, nje tucheke lakini ndani we need to be serious ili Tanzania ifike mahali inapotakiwa kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna malipo yanayotakiwa kupatikana kwenye zile Halmashauri ambapo ile mikodi imekuwepo, wamechimba wananchi wetu wameendelea kuteseka, levy hawapati wanadai wenzao wanatimua vumbi. Kabla ya wataalam wetu kukaa kujadiliana na hawa watu wawe wameshalipa zile service levy kule kwenye yale maeneo, wakimaliza ndiyo warudi mezani ili waweze kuanza sasa mazungumzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 93 wa kitabu hiki kuna Ranchi za Taifa. Ranchi hizi za Taifa zimekuwa zinasakamwa sana lakini naomba niseme National Ranching Company ni eneo pekee ambalo leo watafiti wetu wa Ph.D Program kwenye agriculture na mifugo wanafanyia hapo, moja. Mbili, vijana wetu wa field diploma na certificates wanafanyia field hapo ndiyo jicho pekee unaloweza kutafiti na kuona ukaandikia mwanafunzi alama za field aliyoifanya kwenye maeneo yake vyuoni. Sasa tunaomba NARCO iongezewe fedha kutoka shilingi milioni 126 kwenda shilingi milioni 250 ili iweze kufanya mambo yafuatayo:-

(i) Kuhakikisha kwamba wana-develop production ya mifugo mitamba kwa ajili ya maziwa hapa nchi.

(ii) Kukarabati maeneo ya majengo yao kwa sababu mengi yamechakaa kwenye ranchi zetu zote, ukiangalie zile headquarters, ukiangalia maeneo ya malisho, ukiangalia zile paddocks, kote kumechakaa. Tunaomba Serikali ilione hili lakini itambue haya maeneo kwa beacons kupunguza invasion ya vijiji na watu wanao-cross kutoka maeneo mablimbali ili haya maeneo yawe earmarked yalindwe kwa sababu ya training institutions kwa ajili ya nchi yetu. (Makofi)

(iii) Kuna kiwanda kile cha Ruvu, tunazungumza habari ya mifugo kuwa mingi, tunazungumza habari ya kuvuna mifugo, lakini hakuna meat industry ambayo inaweza kupeleka wale watu wakauza mifugo yao pale. Tunaomba hicho kiwanda kijengwe haraka ili hiyo mifugo ipate mahali pa kuweza kuvunwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la hii barabara yetu ya kutoka Handeni – Kibirashi – Kibaya – Singida; hii ni barabara ambayo inafungua fursa za kiuchumi kwenye ripoti ya kitabu chako hiki. Niombe barabara ya Iringa – Dodoma iko kwenye final touches mnamalizia, barabara ya Dodoma – Babati mko kwenye final touches mnamalizia, tunaomba priority iwe barabara hii kwa sababu zifuatazo:-

(i) Tunakwenda kujenga bomba la mafuta tumefanikiwa jitihada zimefanyika za Serikali, along hiyo barabara tunaomba basi hii barabara wakati bomba linajengwa sambamba na hii barabara ijengwe kiwango cha lami ili kuruhusu mizigo kuweza kupitika kwa urahisi lakini hizo fursa tuzifungue. (Makofi)

(ii) Hiyo barabara peke yake inafungua ile Bandari ya Tanga kuweza kupitisha mizigo inayokwenda Rwanda, Burudi na Kongo. Ile barabara itapunguza msongamano wa Bandari ya Dar es Salaam ili Bandari ya Da es Salaam ipunguze congestion magari yatembee kupita kule ili yaweze kutoka na kwa haraka zaidi na kupunguza mizigo na nchi yetu ipate mapato kwa sababu ya kupunguza msongamano. (Makofi)

(iii) Ikitokea tukawa na production ya kutosha njia pekee inayoweza kupeleka mazao nje kwa maana ya Kenya wakiwa na demand ni njia ya Mombasa, lakini kwa sababu area ya production ni Singida, Dodoma, Manyara na Tanga, njia pekee ni hiyo ambayo itapitisha yale mazao. Tunaomba hii barabara ifunguke kwa lami ili njia hizo ziweze kupitisha mazao magari yaende Mombasa kwa haraka na kuhakikisha kwamba hiyo barabara na gharama za nafuu kwa mkulima na mazao yetu wakulima wetu wakapate faida kutokea Mombasa, nchi jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna benki zetu za biashara. Mheshimiwa Waziri tunaomba ufumbe macho hizi benki kuna mahali zilikosea mmeziadhibu vya kutosha, tunaomba ufumbe macho uwasamehe; Benki za CRDB ziko zina shake, NMB ziko zina shake na hizi benki nyingine za biashara, tunaomba tunazidi kusisitiza wafungulieni nafasi wafanye kazi watu wetu waweze kukopa wafanye kazi, ili watu wetu waweze kulipa kodi na sisi tupate mapato kwa maana ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo muhimu la zaidi ninachoomba, Benki ya Kilimo hii ndio njia pekee tunayoweza ku-access wakulima 85% ya Watanzania, wakulima na wafugaji wanaofanya kazi, njia pekee ya kuwafikia ni njia ya Benki hii ya Kilimo, hii benki tunaomba ipewe mtaji. Hawa jamaa katika hizo shilingi trilioni 35 nilizozungumza atakazoweka down payment mezani trilioni tano peleka Benki ya Kilimo, ikae huko ndio wakulima wetu wakafutie jasho kwa kukopa hizo pesa wakafanye kazi za uzalishaji wakaweze kuinua kipato chao cha maisha kwa maana ya benki hii, kupitia hii benki. Hii benki ndio itakuwa njia pekee na mkobozi kwa ajili ya watu wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tuko kwenye kanda kame, Mkoa wa Dodoma, Mkoa wa Manyara, Mkoa wa Shinyanga na Mkoa wa Simiyu, haya ni maeneo kame sana kwa nchi yetu. Priority iwe ni kuangalia ni namna gani ya kuhakikisha kwamba haya maeneo uanapata maji. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, issue kubwa ya maeneo haya ni uwezo wa kupatikana mabwawa makubwa mapana yenye uwezo wa ku-support watu na mifugo yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe tunalo Bwawa kubwa la Dongwa ambalo limeingizwa kweye programu ya mwaka 2017/2018, niombe hili bwawa litakapochimbwa lina worth ya shilingi bilioni 24; tunaomba mtusaidie hili bwawa lichimbwe kwa sababu hili bwawa linapeleka maji Wilaya ya Gairo, hili bwawa linapeleka maji Kongwa kwa maana ya Mkoa wa Dodoma, hili bwawa linapeleka maji Kiteto kwa maana ya Mkoa wa Manyara. Kwa sababu hili bwawa litakuwa kubwa sana mkilichimba mtakuwa mmeokoa wilaya tatu kwa wakati mmoja, lakini watu wengi wataweza kuondoka kwenye hiyo shida kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nikuombe. Nasisitiza nakuomba ile milioni 50 ya kila kijiji, niombe utume wataalam wako wawili/watatu waje pale Kiteto waone tulivyo- strategize namna gani ya kuweza kutumia pesa kwenye VICOBA. Ile timu yako itakapoona inaweza kujua ni wapi pa kuingilia na zile pesa zikaweza kufanya kazi vizuri.

Sisi tunaamini na ninakuahidi na mimi ndio nitakuwa msimamizi na mimi ndio nitakuwa mdaiwa wa kwanza na ninaomba nisaini nikishindwa kurejesha hizo pesa nisigombee Ubunge mwakani na kadi yangu ya chama nirejeshe kwa ajili ya wale wananchi wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nimeji- commit kwamba hizo pesa nitazirejesha kwa sababu nina uhakika kwa nature ya mazingira tuliyotengeneza ya VICOBA pesa ya Serikali haitapotea, wananchi kiuchumi watanyanyuka na sisi tuna uhakika wa kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Maana nimekaa muda mrefu naona wanaongea mara mbili mara tatu mimi nakosa nafasi, lakini nashukuru kwa kupata hiyo nafasi.
Kwanza niwapongeze wananchi wa Kiteto kwa kunichagua, wale wananchi wamenipa kura nyingi, wameniamini. Wananchi wa Kiteto nawashukuru sana na naendelea kuwaombea na naahidi kwamba nitawatumikia kama ambavyo wameniamini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia upande wa kilimo kwa sababu kwanza ni bwana shamba, ni mkulima, ni mfugaji, nina uzoefu kwenye kilimo zaidi ya miaka 25. Kilimo cha nchi hii kimeshindikana, lakini nadhani kuna mahali ambapo yawezekana tumejichanganya, hebu tufikirie ni wapi tumekosea. Nchi hii sasa hivi tuna- import zaidi ya asilimia 60 ya mbegu za mahindi na mbegu za aina nyingine. Tunapolalamika, tumejiuliza kwamba sasahivi tumejiuliza habari ya pembejeo, lakini hata huyo msambazaji wa pembejeo atapata wapi hizo pembejeo. Nchi nzima hakuna mbegu asilimia 60, tunayo ardhi ya kutosha, tunao wataalamu, tunazo benki kwa nini watu wetu hawawezi ku-invest kwenye kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Serikali haijachukua jukumu la kuwabinafsishia watu maeneo wakaweza kuendesha kilimo cha kuzalisha mbegu kiasi kwamba mbegu zikatosha na usumbufu ukapungua kwa wakulima wetu. Kuna Kanda ya Ziwa ukiangalia Kigoma, ukaangalia Kagera, ukaangalia ile kanda ya Kibondo nzima, mvua zinatosha, tungeweza kutenga maeneo, ule ukanda wote tukaweza kuzalisha mbegu, zikaweza kusaidia nchi yetu kwa maana ya kilimo, hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Benki ya Kilimo imeanzishwa, ukiangalia mtaji wa Benki ya Kilimo, ukikopesha watu utakopesha watu ambao hawazidi 10, 20 hii benki na jinsi ambavyo tunawakulima na asilimia kubwa ya watu wetu ni wakulima na wafugaji hebu niambie kwa mtaji huu tunakwenda wapi!
Mheshimiwa Mwenyekiti, hamisheni pesa zilizoko kwenye ile Benki ya TIB, zipelekwe kwenye Benki ya Kilimo, kopeni pesa ingiza kwenye ule Mfuko, ruhusu wananchi wetu wakakope waweze kufanya kazi. Hata tutakapokwenda kutoza kodi, kuna kitu cha maana cha kutoza kwa sababu watu watakuwa wamezalisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, benki nyingi za kibiashara zimeweza kukopesha wakulima na wakulima wengi wamefeli kwa sababu ya riba kuwa juu. Hata hivyo, jambo kubwa na shida kubwa hapa inaonekana ni kwa sababu hizi benki, Benki Kuu imekuwa inakopa, inaweka government guarantee na bado hazilipi zile benki na zile benki kwa sababu zinaogopa kufilisika haziwezi kushusha interest, mkulima na mfugaji wataponea wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Benki Kuu haiwezi ku-gurantee, iki-guarantee hailipi zile benki, hicho kilimo kitaenda wapi, watapunguza riba waende wapi na wanapesa za watu! Naomba kushauri, Benki ya Kilimo iimarishwe, mitaji ihamie huko, watu wakakope huko, wakachape kazi. Ukimaliza unawaandikisha VAT na TIN halafu wanalipa kodi kwa raha zao, wanaendelea kutambaa kwenye nchi yao kwa neema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto tunazalisha mahindi kwa maana ya kulisha central zone including Dar es Salaam, Morogoro, Arusha na Manyara. Awamu iliyopita, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete alizungumza suala la kutujengea lami kutoka NARCO kwenda Kiteto ili mazao yaweze kutoka kwa salama. Mpaka leo hii barabara tumeimba, tumeomba, nimemwambia Ndugai, Ndugai amelia Bungeni, imeshindikana barabara, hebu niambieni hii barabara inajengwa lini niende kuwaambia wananchi. Maana Magari yanaanguka sasa hivi madaraja yemekwisha, magari yameanguka, chakula cha msaada kimeshindwa kwenda, watu watakufa njaa, barabara imekufa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa mniambie leo, mimi sijui cha kuwaambia. Maana wananchi watakuja wenyewe hapa hapa maana Kiteto ni karibu hapo, wakiamua saa nne wako hapa, sasa mniambie niwaambie nini, hii barabara kwa nini haijengwi na sisi tunalisha watu? 90 percent ya mazao yanayokuja NFRA hapa yanatoka Kiteto, lakini Kiteto imegeuka vumbi, sisi hatuna benefit yoyote kwa sababu hata wananchi wetu hizi barabara wamezikosa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu amani; Kiteto ni Darfur ndogo. Bunge lililopita wame-debate, mapigano ya wakulima na wafugaji watu wamekwisha. Nataka kuiuliza Serikali iniambie leo tunafanya nini ili kuhakikisha kwamba amani inatengemaa Kiteto, wakulima na wafugaji waweze kubaki salama?
MWENYEKITI: Mheshimiwa Emmanuel hebu tulia kidogo. Tafadhali usiite Kiteto ni Darfur ndogo, wote tunajua nini kinaendelea Darfur, tafuta mfano mwingine tafadhali.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Haya nimefuta, lakini si zilipigwa na wewe unajua? (Kicheko)
MWENYEKITI: Mheshimiwa ukishafuta usiendelee tena na maneno mengine, futa uendelee kutoa hoja yako.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Haya nimefuta.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto watu wameumizana, lakini katika mambo ambayo yamesababisha ile Kiteto watu waumizane ni pamoja na viongozi, watendaji wa Serikali kushindwa kufanya kazi. Katikati ya mgogoro wa wakulima na wafugaji kuna watu wana-benefits ndani ya haya. Wanashindwa kufanya kazi za sehemu zao ili amani iweze kupatikana na kusema ukweli na kuusimamia. Hapa watendaji wa Serikali tuamini, tuseme waliteleza na walishindwa Serikali kuchukua hatua kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kuhusu NGOs. Kiteto kuna NGOs zinapenyeza penyeza zinakuja, wanazungumza, mara tunataka hifadhi ya nyuki, mara pingos, mara nini, kila siku wamo, wanazunguka, wanaita makundi machache, wanafanya vikao, wanalipana posho. Mmoja akiulizwa Mbunge wenu yuko wapi, wanasema, Mbunge tumechelewa kumpa taarifa kwa sababu ilikuwa ni haraka haraka. Mipango na haya mambo yanayopangwa ndani ya ile Wilaya, ndiyo matokeo ya kumaliza watu yanayoendelea sasa hivi.
Niombe Serikali iliangalie hili, Serikali ifungue macho ione lakini ichukue hatua za haraka na za makusudi kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni wanasiasa. Siasa zinazochezwa Kiteto zimekuwa ni za kihuni, sasa hivi tuko salama. Sasa niombe Serikali inisaidie, wale wanasiasa uchwara wanaokuja kutembeza siasa pale, tupige siasa wakati wa siasa, lakini wakati wa kazi, tuchape kazi badala ya kugombanisha wakulima na wafugaji. Wewe ukitafuta siasa, njoo wakati wa siasa tupige, tukimaliza tuhimize amani, tuhakikishe kwamba watu wote wana uwezo wa kufanya kazi, mkulima aende shambani, mfugaji aende shambani. Niombe Serikali inisaidie kupima ardhi ya Kiteto vizuri, iipime yote, mkulima ajue anaishia wapi na mfugaji ajue anaishia wapi, mwisho wa siku sisi tuijenge amani na Serikali isimame katikati kutekeleza hilo, huu muda wenyewe ni mdogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nizungumzie afya, hospitali ya Kiteto, tumeomba pesa, tumeahidiwa, tumeambiwa, sasa tumechoka. Tunaomba jamani ile hospitali ikarabatiwe maana sasa hospitali itakuwa chanzo cha magonjwa ya mlipuko pale. Wodi ya wanaume iliyoko pale imechanganya na wale wagonjwa wa TB (Tuberculosis), wote wanachanganyika humo humo, sasa wale watu wataponea wapi? Aliyejeruhiwa ameanguka na pikipiki humo humo, aliye kwenye dozi ya TB yumo humo humo. Sasa tutajengewa lini hii wodi za wanaume zitenganishe hawa watu ili wananchi wasiweze kuambukizana magonjwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, niiombe Serikali inisaidie na Waziri wa afya, hakikisheni kwamba mnaweza kunitatulia huu mgogoro na ile hospitali ikarabatiwe maana sasa imefika mahali tunafanya repair tunazibaziba wenyewe, tunakwenda huko tunakarabati mahali, tunasogezasogeza ili lile jengo lisije likaangukia wagonjwa halafu tukaongeza wengine tena wodini, tukaongezea yale magonjwa wanayoumwa, halafu tunaongezea mengine tena ya jengo kuwaangukia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine tulilonalo Kiteto ni la maji. Kata za Dongo, Songambele, tumechimba visima, ile nchi ni kame. Hebu Serikali iangalie mfumo mpya wa kutusaidia, ile nchi ni kame, wamechimba visima havifiki. Visima vilivyochimbwa vikipatikana maji havifungwi mapampu ili watu waweze kupata maji. Niombe Serikali iweze kuliona hili kwamba kama inawezekana, tuchimbiwe mabwawa ya kutosha, watu watatumia maji na mifugo itatumia maji hayo hayo ili angalau tuweze kuokoa maisha ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, maji ndani ya Mji wa Kibaya; ule mji Rais ametuahidi visima kumi, ametuahidi pesa, vile visima vimeshindikana. Sasa ule Mji wa Kibaya mnataka watu waende wapi, imeshindikana, watu hawapati maji na tumeahidiwa maji muda mrefu sana. Naomba Serikali iweze kuliona hili ule Mji wa Kibaya uweze kuokolewa maana watu wameongezeka, maji hatuna, tuna visima viwili, maji hayatoshi, watu wanabeba ndoo, akinamama wameota vipara. Na mimi niliwaahidi akinamama nikiwa Mbunge mtaota nywele mwanzo mwisho. Naomba Serikali ichukue jukumu la kuhakikisha kwamba hawa akinamama wanaota nywele kichwani. (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, muda wako umekwisha. Sasa atafuata Mheshimiwa Jamal Kassim Ali.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nianze kwa kushukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba nzuri ambayo imejaa mambo mengi ambapo yote yanakidhi matarajio ya Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala la kilimo. Wizara ya Kilimo nilidhani ingeweza kutusaidia kwa maana kwamba Benki ya Kilimo ingeweza kubeba zile pesa ambazo ziko TIB ili kuongezea mtaji ambao ni ile shilingi bilioni 60 inayotajwa kwenye hotuba ya Waziri Mkuu. Fedha nyingine nilizotaka ziweze kuhama ni zile za Mfuko wa Pembejeo wa Kilimo ambazo ziko Exim Bank. Zile pesa kama zingehama zingeweza kuongezea capital kwenye ile bilioni 60 ili wananchi waweze kukopa kwa urahisi kwa sababu itakapokuwa fedha zote ziko mahali pamoja itatusaidia kuweza kukopa na wananchi wetu wengi ambao ni asilimia 80 wako vijijini wangeweza kukopa pesa hizo, hilo ni jambo la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili NFRA wamesema watanunua tani laki moja. Tani laki moja ni kiasi kidogo cha chakula, naomba Serikali iweze kununua chakula karibu tani laki mbili ili itakapotokea shortage tuweze kukabiliana na uhaba wa chakula. Hata hivyo, tutakapokuwa na excess wana uwezo wa kuuza nje kwa maana kwamba kurudisha pesa ili waweze kwenda kwenye season nyingine ya ununuzi wa chakula.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pembejeo za kilimo. Hebu tuangalie ni njia ipi ambayo inaweza kutusaidia. Kwenye kilimo ningeshauri tuangalie ni namna gani ya kuweza kuzalisha mbegu zetu wenyewe kuliko importation ya mbegu ambapo tunatumia foreign currency kuziingiza hapa nchini, ni gharama kubwa. Pia Serikali iangalie ni namna gani ya ku-invest kwenye kilimo cha mbegu ili tuweze kuzalisha mbegu wenyewe nchini na kupunguza hali ya kutegemea mbegu za nje ambazo mara nyingine ni hatarishi kwa maana ya kilimo chetu hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni dawa za ruzuku za mifugo. Ukiangalia dawa za ruzuku za kuogesha mifugo hapa nchini zinasumbua, haziui isipokuwa kwenye ile zero grazing (ng’ombe wale wa majumbani) lakini ukienda kwenye wale ambao wanafuga nje mifugo mingi kupe hawafi. Nashauri na kuiomba Serikali iangalie importation ya dawa hizi au wale watengenezaji basi waangalie mara mbili kwa sababu kupe hawafi, ng’ombe wanazidi kuumwa na hii inachangia sana kusababisha mifugo yetu kutokuwa na afya na mwisho wa siku tunakuwa na mifugo ambayo haiko kwenye kiwango kwa sababu ya dawa ambazo hazikidhi kiwango cha kuweza kutibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuomba ujenzi wa Kiwanda cha Nyama pale Ruvu. Naomba Serikali ijikite kuangalia namna gani ya kujenga Kiwanda cha Nyama ili mifugo yote inayoweza kuingia Pugu iishie pale Ruvu ikachakatwa, nyama zikaingia kwenye supermarkets na masoko yetu tukawa na nyama bora. Hii itasaidia kuwa na nyama ambazo zimepimwa na ziko kwenye viwango. Pia tutaweza kujua ni mifugo kiasi gani tumechinja lakini hata ili revenue yetu haiwezi kupotea kuliko kwenda kushindana pale Pugu. Hilo ni jambo ambalo ningeomba Serikali ijikite kulishughulikia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine naomba soko la mazao Kiteto, sisi tunazalisha mazao mengi sana. Ukiangalia central zone nzima inategemea mazao ya Kiteto, Dar es Salaam inategemea Kiteto, Tandale nzima inategemea Kiteto kwa asilimia karibu 50 lakini hatuna soko.
Naomba Serikali ilione hili itujengee soko ndani ya Wilaya yetu hata kama kuna soko la Kibaigwa lakini tuwe na soko letu la ndani. Mheshimiwa Waziri wa Viwanda alione hili, tuwe na soko letu la ndani tuweze kuwa na internal collection yetu, tuweze kuona ni namna gani na sisi tunaweza kuvuka huko mbele tunakokwenda ili tuweze kupata namna gani ya kuweza kuingiza mapato lakini na watu wetu waweze kufaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiachana na hilo, lile soko pamoja na NFRA kwa mfano inanunua mazao Kiteto zaidi ya tani labda 10,000 au 15,000 ile transportation cost ya kuja NFRA tungependa wapewe wananchi wetu wenye magari wasafirishe kile chakula kuliko kumpa zabuni mtu akasafirisha kile chakula na wananchi wakabaki pale. Ni mojawapo ya creation employment kwa vijana wetu. Watu wetu waweze kufaidi hata hii asilimia ndogo ya kusafirisha hicho chakula kwa sababu na wao magari wanayo. Hii inaweza kusaidia kwa sababu tenderer anaweza kusafirisha kwa gharama kubwa wakati wale wananchi wanaweza kusafirisha kwa gharama ndogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu shilingi milioni 50 kila kijiji, plan yake vyovyote vile itakavyokuwa kwa Kiteto tumejitahidi kufungua VICOBA, SACCOS na vikundi mbalimbali lakini ningeomba nitengeneze commitment. Hebu twende tuangalie kwenye maeneo hizi pesa zikienda, je, kwa mfano Kiteto tunaweza kutengeneza commitment yetu ya kutumia pesa hizi, tukazalisha, zikazunguka kwa wananchi, tukazisimamia wenyewe, kukaja returns kwa kufikiria muundo wetu wa namna gani ziweze kuzunguka zikafikia watu. Maana tukienda kwa maana kwamba kuna watu wale ambao watakuwa ni wajasiriamali ndiyo wapate hizo pesa then wale ambao siyo wajasiriamali katika ile routine ya mzunguko wa zile pesa wao watakuwa wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri sisi Wilaya ya Kiteto tulete plan yetu mkiona inafaa basi tu-guarantee, tu-sign contract, mtupe hizo pesa tuzizungushe kwa maana ya wananchi wetu katika zile SACCOS and then tuzalishe ile riba na bado tuoneshe ile flow ya matumizi ya zile pesa na jinsi ambavyo zinavyoweza kurudi Serikalini ili ziwasaidie wengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hiyo trend ni kwamba tutakapokuwa tumeweza kuwapa watu wengine wale wazee ambao hawawezi kupata hizo pesa basi watakwenda kwenye ile role ya TASAF. Ile asilimia 10 ya vijana na wanawake ambayo itakusanywa kutokana na ile collection ya Halmashauri basi itasaidia vijana. Lengo letu ni ku-make sure kwamba tunaweza ku-monitor wenyewe, tukajua ni watu gani wanaweza kupata pesa hizo na nani hana, nani anastahili na nini kifanyike ili mradi ile community nzima iweze ku-benefit kutokana na hiyo collection na zile generation ya income ambazo tutakuwa tumezipata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nizungumzie kuhusu mapato. Tumekubaliana ndani ya Serikali zile electronic machines zitatumika kukusanya mapato. Kuliko sasa hivi kwenda kwenye ku-tender, sijui tenderer amepata pesa, nashauri kwamba Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Halmashauri wasimamie kwa kutumia electronic machines tukusanye mapato wenyewe. Hii ni creation of employment, tujue tumepata nini, Halmashauri zetu zinaweza kukusanya zaidi kuliko tenderer ambaye anaweza ku-benefit zaidi kuliko Halmashauri zetu ambazo zingeweza kusimamia zenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kuna barabara ambayo inatoka NARCO hapa njiapanda kwenda Kiteto. Hii barabara wakulima wengi wanaitumia, tunaomba Serikali ituone. Ni ahadi ya Serikali tangu mwaka juzi, Mheshimiwa Jakaya Kikwete alituahidi kwamba angeweza kuitengeneza barabara hii. Tunaomba Serikali ya awamu hii kupitia mpango wake wa fedha hebu tuoneeni huruma, hii barabara haina shida kabisa, ina madaraja mawili tu au matatu. Mheshimiwa Waziri Mkuu uko hapa, tuokoe kidogo angalau na sisi tupitishe mazao yakafikie walaji kwa gharama nafuu lakini na mkulima aweze ku-benefit kale ka-profit kwa sababu transportation cost zitashuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna barabara ya Handeni – Kilindi – Kiteto – Chemba – Singida. Barabara hii inafungua mikoa mitano, inafungua Tanga, Manyara, Dodoma na Singida. Ile pipeline ya mafuta wanayosema ya kutoka Uganda itapita pale. Hebu Serikali tuoneni huruma, tunaomba hii barabara muiweke kwenye mpango. Barabara hii itakapofungua mikoa hii itapunguza hata msongamano wa hii barabara ya Dar es Salaam ili watu wengine wapitie kule lakini tutakuwa tumefungua mikoa kwa maana ya programu ya kufungua mikoa yote kwa barabara za lami na watu wote waweze kupita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu CDA naomba Serikali ijaribu kuona ni namna gani inaweza kutengeneza plan ya EPZ zone kubwa hapa Dodoma ili vitu vingi na investors wengi waje Dodoma wakuze mji wetu na ivutie watu ili tupunguze msongamano Dar es Salaam. Hilo la msongamano linaweza kuhamia Dodoma, tukaweka kijiji kingine ambacho ni business city center ndani ya mji wetu wa Dodoma na ikapanua mji na kuongeza ajira na watu wakaongezeka Dodoma na sisi tukaendelea ku-benefit. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, muda wangu ni mchache naona umekwisha, naomba kuishukuru Serikali. Nimpongeze Rais Magufuli kwa kazi anayoichapa, wote tumuunge mkono. Tulimuomba Mungu atupe Rais ambaye anatufaa Watanzania kwa sasa. Hebu tumuunge mkono, tukubaliane naye, maamuzi anayoyafanya tumuunge mkono, tusibaguane kwa itikadi za vyama, tuhakikishe kwamba tunamuunga mkono, tumpe full support ili aweze kulisukuma gurudumu la maendeleo ya Watanzania kule tunakotakiwa kwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumuunge mkono Mheshimiwa Waziri Mkuu, anachapa kazi, yuko makini, hana mjadala, kazi lazima iende, tusiwakatishe tamaa viongozi wetu. Tunawaunga mkono Mawaziri wetu, chapa kazi tuko nyuma yenu, fungulieni speed zote, fanana kama gari linaloshuka mlima halina break tusonge mbele, huko tutakakoishia Watanzania wote tutakuwa tumekubaliana kwamba lazima maendeleo yapatikane. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika naomba kuchangia kwa kushauri mambo yafuatayo:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, Serikali isaidie ujenzi wa ofisi ya Tume ya Maadili, wasaidiwe vyombo vya usafiri angalau gari moja kila mwaka, ikibidi wakope kwenye Mifuko wajenge na Serikali ilipe polepole ili waache kupanga kama sehemu ya kupunguza gharama kwa Serikali pia kama sehemu ya kutunza siri na ulinzi wa kutosha kwenye ofisi zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, ni kuhusu Ofisi ya Nyaraka za Serikali. Hiki ni kitengo muhimu sana naomba wapewe fedha kwa awamu, pia wajenge na kwa sababu wana maeneo wasaidiwe. Watumishi kwenye Wilaya na Mikoa huonesha uzembe mkubwa katika utunzaji wa nyaraka katika maeneo yao, nashauri watumishi wazembe kupitia DED watambuliwe na kupewa onyo kali.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hata kama ni dakika kidogo. Nakushukuru sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ninalotaka kuzungumzia, nimekuwa nashauri sana juu ya Benki ya Kilimo. Nimeomba mara nyingi sana kwamba hii Benki ya Kilimo ina mtaji mdogo, nimeomba zile pesa za TIB zihamie Benki ya Kilimo; nimeomba zile pesa za Mfuko zilizoko Exim zihamie Benki ya Kilimo ili benki yetu iwe na mtaji wakulima na wafugaji wetu waweze kukopa kwenye benki moja ili waende kwenye chombo kimoja, wapate huduma mahali pamoja, warejeshe malipo yao mahali pamoja.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hii benki ihamie Dodoma. Kwa nini benki ikae Da es Salaam kwenye yale majengo maghorofa yanayolipa gharama kubwa! Majengo yapo Dodoma katikati ya nchi, anayetoka kusini aingie, anayetoka Kaskazini aje, anayetoka Magharibi aje lakini naomba hii Benki ihamie Dodoma. Hilo ni jambo la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili nililotaka kuzungumza ni hili suala la migogoro ya wakulima na wafugaji. Migogoro ya wakulima na wafugaji mara nyingi ukikuta mahali kuna mgogoro, wakulima na wafugaji wanapigana, mwanasiasa anafaidika na ule mgogoro. Watendaji wa Serikali wanafaidika na ule mgogoro!
Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Serikali iangalie ni namna ipi tunaweza kufanya ili kuhakikisha kwamba mgogoro unapotokea mahali, unakabiliwa kwa wakati, wale Watendaji wa Serikali, Mwanasiasa anayeshiriki katika hilo, achukuliwe hatua haraka na Serikali ijulishwe na wananchi wajue ili kuweza kuhakikisha kwamba tunakabiliana na migogoro inayotokea baina ya wananchi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nizungumzie NARCO. Ukitaka kuitafuta Wizara ya Mifugo, lazima utaitafuta NARCO; ukitaka kuzungumzia mifugo nchini, lazima uitafute NARCO. Wabunge wengi wamezungumza habari ya mashamba yaliyoko huko Kalambo, Kagera, Arusha, Tanga; NARCO ndiyo yenye maeneo makubwa, lakini NARCO haipewi mtaji. Kwa nini haipewi mtaji? Nilishaomba nikasema, NARCO iombewe pesa za nje zenye riba nafuu ikopeshwe, mashamba yajazwe mifugo, tuajiri wataalam waingie pale, tuwasainishe mikataba, wakishindwa, ni Magereza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mashamba yako wazi, wafugaji pembeni wanayavamia, mwisho wa siku inaleta migogoro. Ndiyo maana inafika mahali watu wengine wanasema haya mashamba yachukuliwe, yanyang‟anywe. Haya mashamba yanakwenda wapi na ndiyo jicho la Wizara! Hakuna mahali pengine unaweza kuiona mifugo au kufanya researches? Watu wengi, sasa hivi wataalam wetu na vijana wengi wanaofanya Ph.D, Masters, kwenye fields wanakwenda kwenye hayo maeneo.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba na kuishauri Serikali kwamba iombe pesa za nje kwa ajili ya NARCO, i-inject pesa za kutosha, iongeze wataalam tuweze kusimamia hayo maeneo na tuweze kufanya kazi kwa kuingiza mapato kwa maana nzima ya hiki Kitengo chetu cha Mifugo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikiwa kwenye Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa, mikoa ilipokuja juzi Dar es Salaam, nilikuwa nawaambia kila mkoa ujaribu kuainisha ni mazao gani yanaweza kustawi lakini ambayo ni commercial. Tusi-base kwenye mahindi, mwisho wa siku tukivuna, yanakuwa mengi, hayana soko. Mikoa ikiweza kuainisha yale mazao kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, yale mazao ya biashara; ufuta, alizeti na kadhalika yanaweza kusaidia mazao yakatoka nje tukaingiza foreign currency badala ya ku-depend on haya mazao ambayo asubuhi na jioni hatuna bei, bei imepatikana, haipo na internal collection bado haipo.
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushukuru, naunga mkono hoja. Ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napongeza Serikali kwa jitihada ambazo imezifanya kutupa huduma pale Kiteto kwa kutujengea kituo cha afya pale Sunya, wanajenga barabara ya zaidi ya bilioni 6.3 kwa kupitia fedha za USAID, niipongeze sana Serikali. Naipongeza Serikali kwa jitihada ambazo zimetupa kwa kujenga shule zetu za sekondari zaidi ya milioni
215 imetuletea na shule inaendelea kupauliwa na sasa vijana wetu wataendelea kupata elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali yetu ya Wilaya ya Kiteto ilikuwa ni kituo cha afya na baadaye wakaamua kiwe hospitali ya Wilaya. Sasa nataka kuomba Serikali itusaidie ikiweza kututengea milioni 500 tukaongeza majengo kwenye ile jengo, hospitali yetu ya Wilaya itakuwa imekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tuna jengo la boma la halmashauri ambalo linaendelea kujengwa na hili jengo tumefikia mahali ambapo sasa tuko kwenye hatua za mwisho. Hata hivyo, kwa mwaka huu haikutengewa pesa zozote kwa mwaka wa 2018/2019, hili jambo limetusikitisha sana, tunaomba Serikali iliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe, kuna maeneo ambayo yametengewa pesa kwa ajili ya majengo halmashauri zao hawajenga, hawana viwanja, wanatafuta maeneo, wako kwenye michakato. Pesa zimekaa zaidi ya miaka miwili, lakini kwa halmashauri ambayo ni kama ya Kiteto jengo liko kwenye finishing haliwezi kupata pesa. Niombe Mheshimiwa Waziri Jafo hili suala analifahamu hili jengo amelitembelea afanye jitihada atutengee pesa tumalizie jengo sisi tuendelee kuchapa kazi pale Kiteto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuomba kuna hili suala la TARURA, barabara vijijini. Niishauri Serikali iangalie upya, hawa ma-engineer hebu wapeni training. Usimamizi wa hizi barabara unatupa mashaka, Mheshimiwa Waziri Jafo ameshiriki kuona ile barabara ya Sunya Namelock na jinsi ambavyo madaraja yamejengwa, tuna Mkandarasi Mshauri Mtanzania amepewa kazi. Madaraja hayawezekani kupitika tu peke yake na hata tu kupitisha maji kwa sababu yale ambayo yamekwishajengwa, Engineers wapo, wataalam wapo, Engineer wa Wilaya yupo, tumehangaika angalia barabara haiwezi kupitika ambayo ina-spend over 6.3 billion, hivi kweli hawa ma-engineer ni Watanzania na wazalendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kwenye hili, hii barabara ya Sunya Kiteto Sunya Namelock hii barabara isipopitika, imetumia bilioni 6.3, hawa ma-engineer mshauri wa madaraja, hawa watu naomba Serikali iwashughulikie, kabla ya hapo wasipofanya hivyo, hii barabara isipopitika miaka mitatu ijayo mimi Rais akikanyaga Kiteto ni wa kwanza kushika maiki kutaja hii kampuni ya kitapeli iliyo tapeli Wilaya yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala bora, hebu tusaidieni jamani watu wa utawala bora, hebu kaeni na watendaji wa Serikali wafundisheni zile ethics za zamani tulizokuwa nazo, watu wajue namna gani ya kufanya kazi kwenye maeneo yao. Migogoro mingi inayoibuka kwenye maeneo yetu ni kwa sababu watu wameshindwa kui- manage kabisa na hawahangaki nayo. Niombe utawala bora Wizara ya Mheshimiwa Mkuchika isimame iliangalie hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili liende sambamba na kutoa watumishi. Leo tunajenga vituo nchi nzima vya afya watendaji wako wapi, leo Kiteto pale ina zahanati haina mtumishi dawa wananchi watakunywa wapi, niombe nahitaji watumishi wa afya watumishi waliondoka wote na watumishi wamehamishwa, Wizara ya TAMISEMI imesema mtumishi anapoomba uhamisho apewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa watumishi Kiteto wamehama 30, nina deficit ya 30, nipeni watumishi wangu niendelee kubaki na deficit lakini nikibaki na walewale wa 30. Mmewaruhusu na hamkunipa wengine, sasa watumishi watafanyaje kazi. Niombe Serikali nahitaji watumishi wa Wizara ya Afya, vituo vimefungwa, vimesimama, hakuna mtu mwenye uwezo wa kutoa dawa, wananchi wanakuja vituoni, lakini hawapati huduma. Sasa naomba Serikali iliangalie hili haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeomba ambulance zaidi ya miaka mitatu tangu nikanyage hapa Bungeni. Ambulance inayotumika pale Kiteto ni gari ya CCM ambayo nai-service mimi na naweka mafuta na kadhalika. Sasa niambieni hii gari inaenda kuchakaa, sasa kwa nini isipewe gari ya ambulance wakati mnajua maeneo makubwa coverage umasaini pale Makame, Ndedo, Loolera clinic sasa akinamama hawawezi kwenda? Kwa nini akinamama hawawezi kwenda clinic na Wabunge wa Viti Maalum naomba humu ndani mkinyanyuka wa Manyara, mdai gari ya ambulace pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa mpole sana sasa I am too tired! Sasa nasema, ifikapo mwezi wa Nane hamjanipa gari nawapa gari ya Ubunge iende kuchapa kazi kule, mimi nitatembea na daladala. Siwezi ku-tolerate this level kwa sababu wananchi wanajifungulia kwenye magari, wanajifungulia kwenye lori, wanajifungulia barabarani, tunaegesha malori yanashusha kuni wanawake wanajifungua tunawapakia humu, tunaelekea wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto coverage kwenye zile rural areas hatuwezi kutembea watakwenda wapi nimekuwa mpole sana sasa imefika mahali I am too tired, nahitaji gari immediately. I am too tired, nahitaji gari la ambulance siyo ya kwangu, nimeomba Ofisi ya Waziri Mkuu, nikamwambia kama kuna gari imeanguka kwake Ofisini wanipe hilo gari nishirikiane na Mkurugenzi tukarabati litembee hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nikamwambia Mheshimiwa Jafo nipeni gari lililoanguka hapo nishirikiane na Mkurugenzi tutengeneze, hakuna. Sasa nifanye nini? Nataka gari I am tired, nataka gari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mikopo ya vijana, vijana, vijana wamefungua SACCOS tumehangaika, Mkurugenzi wa Halmashauri amekusanya ile 10 percent, ameingiza 10 million amehangaika, tumehangaika tumechangishana, vijana wameanza kukopa, nimeomba pesa jamani tusaidieni kwenye hii mifuko ya vijana hii mnayoitaja kila siku, haya mabilioni mnayosema, mbona hatuyaoni kule kwa wananchi? Wameomba document tumeleta hapa, SACCOS iko very straight, vijana wapo, wanalima, wanafuga, wanahangaika barabarani, kwa nini hamtupi hata fedha kidogo wale vijana wakafanya kazi, kwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii mifuko wanayoitaja ni ya nini? Combine hii mifuko yote, hii mifuko waliyoitaja ya vijana wakusanye kwenye mfuko mmoja, waweke mahali pamoja, waonyeshe data kwamba tumetoa hapa, tumepeleka hapa otherwise hakuna kilichofanyika na mwisho wa siku watakuwa wanasoma takwimu ambazo siyo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe SACCOS yangu ya vijana na wanawake wamefungua pale, Mkurugenzi amehangaika nina Mkurugenzi mzuri sana, hizi 10 percent anahangaika nazo, anatoka Ofisini saa saba, saa nane, anakusanya pesa anaingiza kwenye ile mifuko, vijana wanakopa, naomba Serikali im-support, imuunge mkono Mkurugenzi otherwise watakuwa wanamsulubu na vijana wetu hawawezi kufanya kazi, mwisho wa siku tutakuwa na vijana wahuni mtaani tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kushauri, ukiwa unajenga majengo mengi, una-project kwenda kutoa huduma, nenda sambamba na watumishi. Niombe Serikali iwarudishe wale vijana wa Rural Medical Aids, zamani walikuwa wanabeba kits, anakwenda hospitali, zahanati, anakaa hapo, anasubiri mgonjwa, anamtibu, anaendelea sasa rudisheni hawa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa vijana mnawalipa mishahara midogo, mshahara kidogo, kesho anakwenda Medical Assistant, atakwenda RMO eshokutwa atakwenda degree, mwisho wa siku unampandisha polepole na Serikali through the budget itakuwa inakwenda inapanda polepole kuendelea kuwa-accommodate hawa watu, lakini tuwe na watumishi kwenye rural areas ili zile zahanati zetu ziweze kufanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hawa watumishi warudisheni ili hivi vyuo virudi kufanya training kwa sababu ni vijana ambao walikuwa wana-rescue situation, sambamba na enzi zile mnakumbuka UPE tulikuwa na Walimu wa darasa la saba wanafundisha, leo tumewa-phase out tumemaliza lakini ni we need Teachers. Lazima tuwe na alternative as a Government, lazima tuwe na alternative na options kwenda sambamba, tunajenga shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maboma mengi kule Kiteto, mengine siyasemi hapa, siwezi kuyasema hapa ni ya kwangu na kifua changu, siwezi kuyasema hapa, lakini niombe; nipeni special funds kidogo nimalizie yale maboma na nyumba za Walimu. Kuna mahali Kiteto ukipeleka Mwalimu anang’ang’ania suruali ya Mkurugenzi na gari aliyoshuka nayo ni porini, hakubali kukaa na hana nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba moja walimu saba, maboma yameshindikana kukamilika, hatuna nyumba za Walimu, wananchi wamechanga wamefikisha mahali haiwezekani, nipeni special funds. Rural areas kama ya Kiteto ni special na watumishi wengi hawakubali kwenda wanaogopa, wengi wameolewa, wameondoka. Sasa tupeni watumishi na tujengeeni yale maboma ya nyumba za Walimu, Walimu wakubali kukaa, inafika mahali wanaogopa, ikifika jioni anaogopa, shule nyingi zipo porini, sasa zile shule zilizopo porini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napongeza Serikali kwa jitihada ambazo imezifanya kutupa huduma pale Kiteto kwa kutujengea kituo cha afya pale Sunya, wanajenga barabara ya zaidi ya bilioni 6.3 kwa kupitia fedha za USAID, niipongeze sana Serikali. Naipongeza Serikali kwa jitihada ambazo zimetupa kwa kujenga shule zetu za sekondari zaidi ya milioni 215 imetuletea na shule inaendelea kupauliwa na sasa vijana wetu wataendelea kupata elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali yetu ya Wilaya ya Kiteto ilikuwa ni kituo cha afya na baadaye wakaamua kiwe hospitali ya Wilaya. Sasa nataka kuomba Serikali itusaidie ikiweza kututengea milioni 500 tukaongeza majengo kwenye ile jengo, hospitali yetu ya Wilaya itakuwa imekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tuna jengo la boma la halmashauri ambalo linaendelea kujengwa na hili jengo tumefikia mahali ambapo sasa tuko kwenye hatua za mwisho. Hata hivyo, kwa mwaka huu haikutengewa pesa zozote kwa mwaka wa 2018/2019, hili jambo limetusikitisha sana, tunaomba Serikali iliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe, kuna maeneo ambayo yametengewa pesa kwa ajili ya majengo halmashauri zao hawajenga, hawana viwanja, wanatafuta maeneo, wako kwenye michakato. Pesa zimekaa zaidi ya miaka miwili, lakini kwa halmashauri ambayo ni kama ya Kiteto jengo liko kwenye finishing haliwezi kupata pesa. Niombe Mheshimiwa Waziri Jafo hili suala analifahamu hili jengo amelitembelea afanye jitihada atutengee pesa tumalizie jengo sisi tuendelee kuchapa kazi pale Kiteto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuomba kuna hili suala la TARURA, barabara vijijini. Niishauri Serikali iangalie upya, hawa ma-engineer hebu wapeni training. Usimamizi wa hizi barabara unatupa mashaka, Mheshimiwa Waziri Jafo ameshiriki kuona ile barabara ya Sunya Namelock na jinsi ambavyo madaraja yamejengwa, tuna Mkandarasi Mshauri Mtanzania amepewa kazi. Madaraja hayawezekani kupitika tu peke yake na hata tu kupitisha maji kwa sababu yale ambayo yamekwishajengwa, Engineers wapo, wataalam wapo, Engineer wa Wilaya yupo, tumehangaika angalia barabara haiwezi kupitika ambayo ina-spend over 6.3 billion, hivi kweli hawa ma-engineer ni Watanzania na wazalendo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe kwenye hili, hii barabara ya Sunya Kiteto Sunya Namelock hii barabara isipopitika, imetumia bilioni 6.3, hawa ma-engineer mshauri wa madaraja, hawa watu naomba Serikali iwashughulikie, kabla ya hapo wasipofanya hivyo, hii barabara isipopitika miaka mitatu ijayo mimi Rais akikanyaga Kiteto ni wa kwanza kushika maiki kutaja hii kampuni ya kitapeli iliyo tapeli Wilaya yangu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala bora, hebu tusaidieni jamani watu wa utawala bora, hebu kaeni na watendaji wa Serikali wafundisheni zile ethics za zamani tulizokuwa nazo, watu wajue namna gani ya kufanya kazi kwenye maeneo yao. Migogoro mingi inayoibuka kwenye maeneo yetu ni kwa sababu watu wameshindwa kui- manage kabisa na hawahangaki nayo. Niombe utawala bora Wizara ya Mheshimiwa Mkuchika isimame iliangalie hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili liende sambamba na kutoa watumishi. Leo tunajenga vituo nchi nzima vya afya watendaji wako wapi, leo Kiteto pale ina zahanati haina mtumishi dawa wananchi watakunywa wapi, niombe nahitaji watumishi wa afya watumishi waliondoka wote na watumishi wamehamishwa, Wizara ya TAMISEMI imesema mtumishi anapoomba uhamisho apewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa watumishi Kiteto wamehama 30, nina deficit ya 30, nipeni watumishi wangu niendelee kubaki na deficit lakini nikibaki na walewale wa 30. Mmewaruhusu na hamkunipa wengine, sasa watumishi watafanyaje kazi. Niombe Serikali nahitaji watumishi wa Wizara ya Afya, vituo vimefungwa, vimesimama, hakuna mtu mwenye uwezo wa kutoa dawa, wananchi wanakuja vituoni, lakini hawapati huduma. Sasa naomba Serikali iliangalie hili haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeomba ambulance zaidi ya miaka mitatu tangu nikanyage hapa Bungeni. Ambulance inayotumika pale Kiteto ni gari ya CCM ambayo nai-service mimi na naweka mafuta na kadhalika. Sasa niambieni hii gari inaenda kuchakaa, sasa kwa nini isipewe gari ya ambulance wakati mnajua maeneo makubwa coverage umasaini pale Makame, Ndedo, Loolera clinic sasa akinamama hawawezi kwenda? Kwa nini akinamama hawawezi kwenda clinic na Wabunge wa Viti Maalum naomba humu ndani mkinyanyuka wa Manyara, mdai gari ya ambulace pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa mpole sana sasa I am too tired! Sasa nasema, ifikapo mwezi wa Nane hamjanipa gari nawapa gari ya Ubunge iende kuchapa kazi kule, mimi nitatembea na daladala. Siwezi ku-tolerate this level kwa sababu wananchi wanajifungulia kwenye magari, wanajifungulia kwenye lori, wanajifungulia barabarani, tunaegesha malori yanashusha kuni wanawake wanajifungua tunawapakia humu, tunaelekea wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto coverage kwenye zile rural areas hatuwezi kutembea watakwenda wapi nimekuwa mpole sana sasa imefika mahali I am too tired, nahitaji gari immediately. I am too tired, nahitaji gari la ambulance siyo ya kwangu, nimeomba Ofisi ya Waziri Mkuu, nikamwambia kama kuna gari imeanguka kwake Ofisini wanipe hilo gari nishirikiane na Mkurugenzi tukarabati litembee hakuna.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nikamwambia Mheshimiwa Jafo nipeni gari lililoanguka hapo nishirikiane na Mkurugenzi tutengeneze, hakuna. Sasa nifanye nini? Nataka gari I am tired, nataka gari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mikopo ya vijana, vijana, vijana wamefungua SACCOS tumehangaika, Mkurugenzi wa Halmashauri amekusanya ile 10 percent, ameingiza 10 million amehangaika, tumehangaika tumechangishana, vijana wameanza kukopa, nimeomba pesa jamani tusaidieni kwenye hii mifuko ya vijana hii mnayoitaja kila siku, haya mabilioni mnayosema, mbona hatuyaoni kule kwa wananchi? Wameomba document tumeleta hapa, SACCOS iko very straight, vijana wapo, wanalima, wanafuga, wanahangaika barabarani, kwa nini hamtupi hata fedha kidogo wale vijana wakafanya kazi, kwa nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii mifuko wanayoitaja ni ya nini? Combine hii mifuko yote, hii mifuko waliyoitaja ya vijana wakusanye kwenye mfuko mmoja, waweke mahali pamoja, waonyeshe data kwamba tumetoa hapa, tumepeleka hapa otherwise hakuna kilichofanyika na mwisho wa siku watakuwa wanasoma takwimu ambazo siyo kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe SACCOS yangu ya vijana na wanawake wamefungua pale, Mkurugenzi amehangaika nina Mkurugenzi mzuri sana, hizi 10 percent anahangaika nazo, anatoka Ofisini saa saba, saa nane, anakusanya pesa anaingiza kwenye ile mifuko, vijana wanakopa, naomba Serikali im-support, imuunge mkono Mkurugenzi otherwise watakuwa wanamsulubu na vijana wetu hawawezi kufanya kazi, mwisho wa siku tutakuwa na vijana wahuni mtaani tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kushauri, ukiwa unajenga majengo mengi, una-project kwenda kutoa huduma, nenda sambamba na watumishi. Niombe Serikali iwarudishe wale vijana wa Rural Medical Aids, zamani walikuwa wanabeba kits, anakwenda hospitali, zahanati, anakaa hapo, anasubiri mgonjwa, anamtibu, anaendelea sasa rudisheni hawa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa vijana mnawalipa mishahara midogo, mshahara kidogo, kesho anakwenda Medical Assistant, atakwenda RMO eshokutwa atakwenda degree, mwisho wa siku unampandisha polepole na Serikali through the budget itakuwa inakwenda inapanda polepole kuendelea kuwa-accommodate hawa watu, lakini tuwe na watumishi kwenye rural areas ili zile zahanati zetu ziweze kufanyakazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hawa watumishi warudisheni ili hivi vyuo virudi kufanya training kwa sababu ni vijana ambao walikuwa wana-rescue situation, sambamba na enzi zile mnakumbuka UPE tulikuwa na Walimu wa darasa la saba wanafundisha, leo tumewa-phase out tumemaliza lakini ni we need Teachers. Lazima tuwe na alternative as a Government, lazima tuwe na alternative na options kwenda sambamba, tunajenga shule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maboma mengi kule Kiteto, mengine siyasemi hapa, siwezi kuyasema hapa ni ya kwangu na kifua changu, siwezi kuyasema hapa, lakini niombe; nipeni special funds kidogo nimalizie yale maboma na nyumba za Walimu. Kuna mahali Kiteto ukipeleka Mwalimu anang’ang’ania suruali ya Mkurugenzi na gari aliyoshuka nayo ni porini, hakubali kukaa na hana nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyumba moja walimu saba, maboma yameshindikana kukamilika, hatuna nyumba za Walimu, wananchi wamechanga wamefikisha mahali haiwezekani, nipeni special funds. Rural areas kama ya Kiteto ni special na watumishi wengi hawakubali kwenda wanaogopa, wengi wameolewa, wameondoka. Sasa tupeni watumishi na tujengeeni yale maboma ya nyumba za Walimu, Walimu wakubali kukaa, inafika mahali wanaogopa, ikifika jioni anaogopa, shule nyingi zipo porini, sasa zile shule zilizopo porini…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naipongeza Serikali kwa kazi zote inazozifanya na jinsi mpango huu ulivyotengenezwa na unavyotupa direction ya wapi tunapokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema jambo moja kwamba kwenye mpango huu sijaona ule mradi wa umeme wa Kakono ambao unazalisha megawatts 78. Benki ya Maendeleo ya Afrika ilishamaliza kazi yake na kuna vitu vilikuwa vinaendelea lakini siuoni kwenye mpango hapa. Waziri atakapokuja atuambie huu mpango umefikia wapi kwa sababu megawatts 78 siyo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la maji linaonekana kwa nchi ni tatizo kubwa sana. Nashauri tuongeze Sh.50 kwenye mambo ya simu, tulete hizi pesa kwenye maji baada ya miaka miwili tutakuwa hatuna madeni lakini miradi mingi ya maji nchini itakuwa imemalizika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kilimo nataka kushauri kwamba tunaweza kuigawa nchi yetu kwa zone, nimeona kwenye mpango hapa ukionyesha mikoa tofauti tofauti, tuigawe nchi yetu kwenye zone lakini tunapofanya zoning tutengeneze zile agro-processing centers huko huko ambazo zitaweza kuwa-managed na Watanzania na foreigners watakaokuja ku-invest pesa zao wakae na Watanzania huko huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri hawa investors watakaokuja kwenye hizo agro-processing plant katika maeneo hayo washirikiane na Watanzania. Kama Mtanzania anaweza kuingiza 30% aendelee yule mwekezaji akija na 50% aendelee, 20% iwe ni ya wale outgrowers wadogo wadogo waweze ku-manage uchumi kwenye vile viwanda vitakavyokuwa kwenye maeneo hayo ili growth ya economy iende sambamba na uhalisia wa maisha ya watu wetu tunaowaona kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kufanya hivi ita-protect wale wakulima wadogo kwa sababu tulipobinafsisha hivi viwanda vya chai anazalisha ile chai yake akimaliza ana- determine chai price ya yule mkulima ambaye ni outgrowers. Kwa hiyo, mwisho wa siku yeye akisema anapunguza bei anapunguza kwa sababu already ana mashamba. Suala hili naomba Serikali iliangalie sana kwamba anakuwa na kiwanda, hana involvement na shareholders wadogo mwisho wa siku lazima awanyonye na awaamulie anavyotaka, atawamaliza na mwisho wataning’inia bila mazao yao kununuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili litasaidia jambo lingine kwamba hata kama atakuwa na hicho kiwanda atazalisha mwisho wa siku atakachofanya chochote kile kwa sababu outgrowers wetu na wao wana share pale ni wanufaika wa ile income atakayopata. Kwa maana hiyo, itatusaidia hata ku-protect price ya wale wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine hawa foreigners watakapokuja nao watatusaidia ku-oversee masoko ya nje ya haya mazao tunayozalisha. Leo tumepata shida ya mbaazi kwa sababu hatuna watu nje. Leo tunapata shida ya korosho ni kwa sababu hatuna watu nje lakini ingekuwa tunabangua korosho hizi siasa uchwara usingezisikia Mtwara, usingesikia udalali, usingesikia kelele pale Mtwara kwenye korosho kwa sababu wale wakulima wenyewe wangekuwa ni shareholders kwenye zile agro- processing plants ambapo ni beneficiary, nani angezalisha siasa pale?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Uganda inakwenda kuwa nchi ya kwanza Afrika kwenye uzalishwaji wa maziwa na teknolojia wameichukua Tanzania ten years back. Niombe Mheshimiwa Waziri hebu tafuta timu ya watu kutoka Ofisi yako ya Mipango, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TIC, Benki ya Kilimo na Benki Kuu, team up hawa watu waangalie ni mbinu gani tunaweza kuzitumia kuhakikisha kwamba Tanzania inaweza kuwa the biggest producer of milk Barani Afrika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uganda leo wana-export zaidi maziwa na kwenye contribution ya uchumi wao sasa hivi maziwa yanaenda kuiondoa kahawa na chai, kahawa inaenda kuwa ya tatu, chai inakuwa ya pili na maziwa yanakuwa ya kwanza. Ukiangalia ecological area na environment yetu sisi tuna maeneo makubwa lakini yenye weather sawa na Uganda, kwa nini hatujafanikiwa kwenye sekta hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mheshimiwa Dkt. Mpango asije kusema tunahitaji big investment kwenye hili, hakuna pesa nyingi. Shida tunayoipata ni kwamba hatuna access ya grants kwenye agro-business na kwa wakulima wetu. East Africa Tanzania ni ya mwisho ku-access grants, Ulaya watu wanashusha grants Kenya na kwenye nchi nyingine, wanaweka miundombinu na vitu vyote wakimaliza wanakwambia wewe fanya kazi, maisha ya raia wao wanakuwa vizuri wewe unakusanya kodi. Mheshimiwa Dkt. Mpango hapa usije kutuambia unahitaji hela, hakuna hela, wale watu wana uwezo wa kua-access grants. Team up your people waende wakafanye kazi hizo na sisi wakulima wetu wa-access grants waweze kufanya kazi na sisi tupate msaada. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, Mheshimiwa Dkt. Mpango wala usije ukatuambia chochote nenda katafute washauri Marekani hata wapi waje wakushauri wakuambie ni mipango gani inatufaa. Wewe usitusikilize sisi wanasiasa, panga pangua, panga vitu vyako sisi tunataka kuondoka kwenye umaskini na hizi shida tulizonazo. (Makofi)

T A A R I F A . . .

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimesema wanasiasa siyo Wabunge, maana hata kule mtaani tuna wanasiasa kwani wanasiasa ni sisi peke yetu tuliomo humu ndani? Hatuna waandishi wa habari wanaamka asubuhi wanatangaza ya kwao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa namshauri Waziri wangu, mambo mengine usiwe unatuaga, wewe nenda kachape kazi tunatafuta maendeleo, hapa tunakuja kuku- support mambo mengine tu. Wewe unatuaga kufanya nini?

Tafuta pesa na wataalam huko watusaidie, Tanzania hatuwezi kuifunga, hii siyo kisiwa, nchi imeshakwenda na duniani nyingine, Watanzania wanatakiwa watoke na wapate ajira. Tafuta technical persons watusaidie, sisi siyo kisiwa, siyo kwamba ni wajinga lakini kupata ushauri na akili ni kuhemea brain, unaingiza hapa tunapata maisha, watu wanahitaji kubadilika, wewe tusaidie. Mtu mwingine akija kwako analeta siasa unamsikiliza, nunua ream za karatasi mwambie nenda kaniandike ya kwako kwenye makaratasi akupe nafasi ya kufanya kazi uweze kupumua. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kushauri jambo lingine la mwisho kwamba Watanzania hawafanyi kazi. Nchi nyingine they are working over night, kadiri wanavyofanya kazi usiku na mchana ndivyo zile mashine zinatema kodi. Saa nne tumelala, saa mbili tayari, Dar es Salaam saa tatu wako barazani wanazungumza habari ya wanawake, mama ana tako, mama ni mnene, utafanya lini hiyo biashara, utapata kodi saa ngapi? (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe na Bunge hili mnikubalie nchi hii ifanye kazi usiku na mchana. Watu waondoke kwenye ufuska na kufikiria mawazo mabaya na kutukanana hovyo hovyo, tufanye kazi, watu wafanye kazi mchana na usiku. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua Kariakoo nzima leo, ukaamua maduka yote fungueni mchana na usiku, you are creating employment to our graduates ambao wako mtaani wanacheza na simu. Vilevile una-create employment kwa watu ambao ni jobless wanafanya kazi mchana wengine wanafanya kazi usiku, tunaongeza ajira, shift zinakuwa mchana na usiku halafu kodi inaendelea kukusanywa. Kwani saa nane usiku mashine ya EFD haitoi risiti, inatoa. Je, wewe Mheshimiwa Dkt. Mpango haupati fedha? Nashauri tuanze biashara usiku na mchana. (Makofi/ Kicheko)


Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kushauri jambo lingine kwamba huu mpango wetu sisi twende kushauri Serikali lakini tusibeze yale yanayofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho nashauri kwamba Benki ya Kilimo TADB, niungane na Mheshimiwa Saada, Mheshimiwa Dkt. Mpango angalia ni namna gani unaweza kufanya isiwe kama commecial bank iendane na hali halisi ya mazingira ya Watanzania, waweze kukopesheka vinginevyo zile pesa zitakaa pale, utalaumu watendaji, utawafukuza, utaajiri wengine na pesa hazitatoka. Mheshimiwa Waziri angalia ni namna gani ya kushusha zile pesa katika mfumo ambao ni reasonable. Utamwambia aandike business plan na yeye ana heka zake mia mbili anataka akakope trekta na TADB inatakiwa impe hela PASS im-garantee atatokea wapi? Punguzeni masharti, angalieni ni namna gani ya kui-handle ile benki ili iweze kwenda sambamba na life brain na stahili za wakulima wetu kule kwenye grassroot. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwanza kwa kunipa nafasi na napongeza Bajeti ya Wizara ya Fedha kwa maana ya namna ambavyo imekuja na inavyokidhi mahitaji yetu na kwa namna ambavyo mapunguzo mengi ya kodi na utitiri wa kodi nyingi kwa Watanzania ambavyo zimeondolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kusema juu ya viwanda, lakini niongezee pale kwa Mheshimiwa Selasini kwamba wakati tunafikiria kuchukua hivi viwanda kuvitaifisha, zipo benki zetu zilikopesha hivi viwanda kwa miaka kadhaa na zile pesa ziko huko na ni za Watanzania ambao wali-inject pesa zao kwenye zile benki zikatunzwa. Tutakapokwenda kutaifisha hivyo viwanda kwa ule utaratibu mzima wa kuondoka na watu wa Biashara na Viwanda watu wa Wizara ya Fedha, watu wa TAMISEMI na ule mnyororo mzima wa kwenda kuhakikisha kwamba vile viwanda vinarudi Serikalini, basi mimi nataka tuongezee kwamba tuondoke na wale watu wa benki zetu wanaokopesha wakae chini na document zao, wahakikishe wanaona chao kiko wapi na mwisho wa siku Serikali itakapochukua mamlaka ya kuvitaifisha basi na zile benki zetu ziweze kuokolewa kwa sababu tukivitaifisha na pesa za benki zilizokopesha pale ziko kule tayari ni kwamba tumesababisha benki zetu kuanguka. (Makofi)

Sasa naomba nifikirie wakati mnakwenda muongozane na hizo benki zilizokopesha ili kuweza kuokoa chao kwa sababu tayari kama mtu ameshakufa ni lazima tujue nani anadaiwa na nani alikuwa anadai ili marehemu aondoke salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kusema juu ya hivyo viwanda, leo tunajenga viwanda Tanzania lakini kuna jambo moja nimeanza kuligundua kwamba inawezekana ikatufikisha pagumu. Naomba Serikali ifanye jambo moja la utafiti wa kina na ijiridhishe kwamba kuna nchi ndani ya East Africa sasa baada ya kuona Tanzania inajenga viwanda ikifika saa 5 usiku inashusha half price ya umeme ili viwanda viweze ku-produce na ile raw material na zile product zote ziweze ku-compete na bidhaa za viwanda vyetu hapa Tanzania. Serikali ilichunguze, ilifanyie kazi kwa haraka, ipunguze michakato, isijadili mara nyingi ili kuokoa viwanda vyetu tunavyovijenga sasa ili viweze kubaki salama. Vinginevyo zile products za hivyo viwanda zikiingia hapa yeye atakachofanya ataondolewa kodi, atapunguza kodi, ata- compete na viwanda vya hapa, under that competition management ya ku-manage hilo soko itakuwa kwenye competitive na hizo nchi hatutakuwa tuna-benefit kitu na mwisho wa siku viwanda vyetu vinaweza ku-collapse. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nizungumze juu ya ardhi; kodi ya ardhi mimi naona kama inakuwa kubwa. Kodi ya ardhi kwenye investment za mashamba makubwa, ranches, industrial areas, mambo mengi, naona kama kodi ya ardhi inakuwa kubwa. Naomba Serikali mliangalie hili na kwa accumulation ya madeni makubwa yaliyopo hebu ondoeni penalty na interest muone ni namna gani watu wanaweza ku-afford kulipa hizi accumulated madeni mengi ili watu waweze kukusanya na hiyo pesa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Rais amekuwa anaonesha mara nyingi, waive interest, waive penalty kwenye benki, waive kwenye kodi za Serikali, punguza haya mambo ili watu waweze kufanya kazi otherwise utakuwa unahesabu mabilioni ya pesa makubwa yaliyowekwa kwa wananchi ambayo ni unaffordable watu kulipa na badala yake mnaishia kuhesabu mabilioni ambayo hayawezi kulipika na mwisho wa siku mnaishia migogorio. Waive hii ku-simplify maisha ya watu, punguzeni hii ili watu waone namna gani ya kuweza kusonga mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna miradi ya kimkakati kwenye Halmashauri zetu ambazo watu wamekuwa wana- apply wanatengeneza miradi ya kimkakati ambayo ni ya kuona ni namna gani hizo Halmashauri zetu zinaweza kujitegemea.

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema tena, Waziri wa Fedha, hebu tufanye kazi kwa kufanya analysis kama una Halmashauri 50 au 100 zina application ofisini kwako, zimekuja zinaonesha miradi ya kimkakati, turnover ya mradi katika Halmashauri fulani inaonesha miaka mitano au kumi, lakini kuna Halmashauri uki-implement huo mradi turnover yake ku-manage huo mradi na kuleta income na kupunguza mzigo mkubwa kwa Serikali ndani ya mwaka mmoja, upi wa kuanza? Tengeneza kufata track hivi vitu kwa kuona namna gani quick return of investment uitumie hiyo itusaidie ku-support miradi hii. Leo Kiteto tuna mradi wa gulio, soko la mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, Waziri akitupa sisi zile pesa ambazo tumeomba kwenye soko letu la mradi ni kwamba sisi baada ya misimu mitatu tuna uwezo wa kuwa tunajitegemea kwenye Halmashauri yetu ambayo tunaweza kujitegemea hata kwa asilimia 80. Tukikupunguzia kukudai pesa za kutusaidia kama ruzuku kwa asilimia 80 ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto tumeokoa kitu kikubwa sana. Tusaidie tujenge, tutumie huo mud amfupi kurudisha hiyo pesa ambayo sisi tunajitegemea wenyewe ile pesa uliyokuwa unatuletea upeleke kwenye Halmashauri nyingine ambazo hazina miradi ya ku-survive na ku-sustain zenyewe, tutakuwa tumepunguza burden kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo majengo kwenye Halmashauri zetu tunajenga. Mimi nimeona tunajenga majengo makubwa sana kwenye Halmashauri zetu. Hivi kwenye hizi Halmashauri zetu tuna haja gani ya kujenga Ofisi ya Mbunge kama haya majengo makubwa ya Halmashauri yapo! Mbunge mpe vyumba viwili aweke bendera yake pale, asonge mbele na wananchi wake, tupunguze kujenga, hizi pesa tuzipeleke kwenye shughuli nyingine ambazo zinaweza kusaidia kujenga madarasa yetu. Huo ni ushauri wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niende kwenye mikopo ya kilimo, mifugo na uvuvi; nataka kuiomba Serikali iangalie hivi sisi tunaona kwenye nchi nyingine wanakuwa na grants kubwa zinazo-support miradi mingi kwa wananchi na mwisho wa siku hii miradi inapofanyika kwa mfano miradi ya maziwa, kuboresha wakulima, kufanya mambo ya kahawa, kuwapa mbegu za miche, korosho na kadhalika kuna a lot of grants, kwa nini Tanzania haziji? Hawa donor friends/countries wanao-inject hizi pesa na hii miradi mikubwa na kampuni kubwa zinazo-support hii kwa nini Tanzania hatuwaoni? Hebu jitahidini muwaone. Kama mnaona kwamba wachunguzeni muwaone, hizi grants zinapokuja zinasaidia wale wakulima wetu, wavuvi wetu, wafugaji wetu kufanya namna ambavyo inawezekana waweze ku-survive then wanapokuwa wana-grow ndipo unapoweza ku- introduce kiwanda kikapata raw materials, ndipo utakapokwenda ku-introduce kiwanda kikapata wanafanyakazi wengi, ndipo vijana wetu wasomi walioko mtaani watakapokimbilia. Ndiko Serikali itakapokwenda kukusanya kodi kesho kutwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, we are joking! Hapa tunafanya utani Tanzania kwenye kilimo, mifugo na uvuvi, mfugaji ukimpa ng’ombe wawili wa maziwa au ng’ombe mmoja mwisho wa mwaka ukamwambia wewe nenda TRA kalipe kodi ya shilingi 100,000 hawezi ku-feel kama alikuwa analipa kodi, it’s just a peanuts, lakini kwa nchi tunakuwa tumekusanya kitu kikubwa ambacho mwisho wa siku Serikali inapata.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nishauri, hebu angalieni hizi grants ziende kwa wananchi, zi-supprort ku-uproot poverty iliyopo, lakini pia iwe kama chachu na ku- boost vijana wetu wasomi wanaokimbia SUA wanaenda mtaani, mwisho wa siku wanaanza kusoma kompyuta, amesoma animal science, anaanza kusoma kompyuta, sijui accounts huku amesoma kilimo (agri-business), hiyo biashara ya nini? Hebu jaribu kuona namna gani tunaweza ku-trigger vijana wetu wakaenda kwenye grassroots kwenye sekta ya kilimo na mwisho wa siku tunapo-push hii inafanya benki zetu zianze kupunguza risk ya kukopesha hawa watu kwa sababu tayari mazingira yameshaandaliwa. Kwa hiyo unapomkopesha na anaona end product ya kiwanda ipo, benki haiwezi kusita kujadili mkopo aliyeomba kwa mwananchi mkulima au mfugaji ili aweze kutoa hizo pesa na akaweza kufanya biashara wakati huo tukiendelea kukusanya kodi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naomba niombe mwisho tunayo mazao makubw ya biashara kama kahawa, korosho, chai, pamba na kadhalika, leo tunahangaika kila ukifanya hivi inagoma, ukifanya hivi tunasumbuka wakati tuanfikiria kucheza na haya mazao dunia nzima inatuangalia sio sisi tunaolima haya mazao peke yake. Niombe kuwe kuna uwezo wa kufikiri na kuamua haraka. Uwezo wa kufikiri na kuamua kwa muda ili tuweze kwenda na wakati kwenye haya mazao. The more you delay one month, kahawa imeshuka bei, korosho imepigwa chini, pamba hainunuliki, soko limeanguka, nchi ina-shake, naomba Serikali delayment ya vikao vya michakato ya kutomaliza kwa wakati na kuamua jambo, Serikali iliangalie sana. Wakulima wetu watakufa, watateseka, watapoteza na hatutapata income. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe inapotokea of anything katika business trend yoyote ile umeona kwamba soko la korosho katika mfumo wa kulinunua ime-shake hivi twist immediately, hamisha mzigo wa watu, lipa wakulima pumzika. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata nafasi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ninalopenda kuzungumzia ni juu ya reli hii ambayo imepangwa kujengwa lakini napenda kushauri kwamba ujenzi wa reli hii uwe kwa awamu kwa sababu kila anayesimama anazungumzia reli, lakini reli haiwezi kujengwa kwa wakati mmoja, nafikiri tujenge reli kwa awamu kama ni Dar es Salaam - Tabora, kama ni Dar es Salaam – Mwanza. Hilo ni jambo la kwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kuna barabara ya kutoka Handeni - Kibirashi - Kijungu - Kibaya - Njoro nimeiona kwenye mpango. Barabara hizi kuzijenga ni gharama kubwa kwa Serikali na ukiangalia gharama na jinsi zinavyotakiwa kwa maana kwamba kila mtu anaomba barabara, ningeshauri mambo yafuatayo:-
Naomba Mheshimiwa Waziri safari hii ajenge barabara kutoka Handeni - Kibirashi aishie hapo, mwakani ajenge Kibirashi – Kibaya - Kiteto aishie hapo, mwaka unaofuata ajenge Kibaya - Chemba aishie hapo, mwaka unaofuata ajenge Chemba – Singida, ndiyo njia pekee inayoweza kusaidia barabara hizi kuisha. Hizi barabara unaweka upembuzi, pesa inaingia, feasibility study baada ya muda fedha zikikosekana mnaanza upya tena, hizi zote ni gharama kwa Serikali na tunapata hasara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba kushauri barabara zijengwe kipande kidogo kidogo na kwa awamu. Barabara itakayopata mfadhili wa nje kama ni kilometa 400, 500 akiianza amalize yeye mwenyewe lakini kama ni fedha za ndani tujenge kidogo kidogo ili na maeneo mengine yapate na fedha nyingine zitumike kujenga barabara hizi za vumbi na changarawe katika maeneo mengi ikiwa ni sehemu ya kufungua barabara zetu za vijijini. Hilo ni jambo la pili.
Mheshimiwa Mwenyekiti jambo la tatu, naomba kushauri kama inawezekana tubadilishe mfumo wa manunuzi itusaidie kwenye mambo haya yafuatayo; hizi fedha zinazotengwa kwenda kwenye halmashauri zetu kwa ajili ya barabara hebu toeni asilimia 20 tukopesheni vifaa kwa ajili ya barabara. Mkoa mzima wa Manyara kama umetengewa shilingi bilioni tatu au shilingi bilioni nne, asilimia 20 Serikali tukopesheni vifaa, weka government guarantee tupate katapila na vifaa vingine vya ujenzi wa barabara, sisi wenyewe tu-fuel halmashauri zetu kutokana na collection za ndani, tutumie gharama nafuu kutengeneza barabara zetu za halmashauri vinginevyo ni gharama kubwa kwa Serikali. Tusipobadilisha hii sheria hatuwezi kupata hiyo guarantee na kuweza kununua vifaa vyetu. Najua hii inaokoa fedha nyingi za Serikali lakini kama kuna mikono ya watu wanaotafuna haiwezi kupita. Naomba Wabunge mniunge mkono kwa hili tuweze kuwa na vyombo vyetu vya kutengeneza barabara zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Arusha – Kibaya - NARCO, nimekuwa namwambia Mheshimiwa Spika barabara ya NARCO - Kiteto mbona huizungumzii anasema nimebanwa. Sasa Mheshimiwa Waziri useme leo umembanaje Spika, kwa nini hutengenezi barabara hii? Barabara hii ni ahadi ya Serikali, ni ahadi ya Mheshimiwa Kikwete mwaka 2013 mpaka leo imeshindikana. Nikuombe Mheshimiwa Waziri, jenga barabara ya NARCO – Kongwa na NARCO - Dosidosi tu. Jenga Kongwa kwa mwaka huu mwaka unaofuta jenga Dosidosi mpaka Kibaya kilometa 39, kidogo kidogo mwisho wa siku utafika Oljoro, Arusha. Mimi naomba tujenge barabara kwa awamu ili hii barabara itengenezeke, lengo ni kufungua barabara hii ili mazao yaweze kutoka. Kiteto ndiyo inayolisha Tanzania kwa maana ya Dar es Salaam, ndiyo inayolisha Kanda ya Kati, kwa nini hamfungui barabara hii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwezi wa pili ndani ya barabara ile zimeanguka gari saba kwa siku moja zikipeleka chakula cha msaada. Sasa kwa nini msifungue hii barabara tukaweza kupita, ni zaidi ya kilometa 91 tu. Nadhani jitihada za makusudi hazijachukuliwa kukamilisha ujenzi wa barabara hii. Barabara ya Oljoro - NARCO iliwahi kutengewa shilingi milioni 900 mwaka 2013 za upembuzi mpaka leo hatujui zilienda wapi. Tunaomba hii barabara iangaliwe na itengenezeke, tutaamini kama Thomas tutakapoona wakandarasi wako site. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanja vya ndege, ndege tunazihitaji, tunahitaji Watanzania watembee lakini kuna jambo nataka kushauri. Viwanja vyote vya ndege ambavyo sasa vina vumbi, vimekwanguliwa hebu suburini kwanza, jengeni hivi viwanja vyote ambavyo mmeanza vya Dar es Salaam, Arusha, KIA, Mwanza ili vimalizike, tujenge kwa awamu na tutakapomaliza tuanze kiwanja kimoja kimoja kwani kushika miradi mingi kunatupotezea mambo mengi. Bajeti ya nchi ni ndogo, fedha zinazokusanywa ni kidogo, tufanye jambo liishe tukirudi hapa tuseme liliisha. Kila siku unazungumzia habari ya kiwanja cha Mwanza, miaka 10 unahangaika na nini kama kimetushinda kiacheni! Jenga Dar es Salaam ukimaliza hamia Arusha, ukimaliza hamia Mwanza, ukimaliza hamia Kigoma, ukimaliza hamia Kagera, maliza kwanza kimoja ujue kwamba kiliisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndege. Rwanda ina ndege mpya 14 na ni nchi ndogo, ATC imebaki alama, kwa nini? Mmeonyesha mpango wa kununua ndege lakini kama tunanunua ndege, niwashauri Wabunge wenzangu tukubaliane tutafute CEO wa kampuni au shirika hilo kutoka nje, siyo Mtanzania watalifuta, litaliwa! Watafunaji ni wengi na kwa sababu hakuna anayeiunga mkono Serikali, leo tunalalamika ndege, ndege, tumeuwa wenyewe, tunatafuna wenyewe, kilichoko kinaliwa, mashirika kutoka nje yanatutafuna, tuna-sign wenyewe, mnahangaika na nini? Tu-import wataalam watufanyie kazi tuwalipe ili tuokoe vinavyowezekana. Naomba kushauri hizi ndege zitakazonunuliwa punguzeni watumishi wote wa ATC bakiza wachache, zitembee ndege chache, zifanye kazi, wakope wanunue nyingine ziweze kutembea ndani ya nchi yetu at least kwa hesabu tukijua kwamba wamekopa watalipa, wakishindwa magereza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Mbunge mmoja amesema barabara za lami wanabandua wanabandika, ndiyo! Kitaalam lami life span yake ni miaka 15, ikiisha biashara imekwisha lazima ubandue. Ukiona imedemadema mkandarasi alikuwa mzuri, unashukuru Mungu. Leo hii reli ya kati life span yake ilishaisha, ukiona inademadema Mungu ametusaidia. Mimi naomba watu wazungumze kwa data, tuone ni jinsi gani tunatakiwa tutoke hapa, hizi barabara nyingi kushindikana kwake ni kwa sababu hata wakandarasi wetu wengi wamekuwa wachakachuaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nishauri leo, kama leo Dangote Mtwara simenti inaweza kuwa shilingi 8,000; kwa nini tusijenge barabara za zege? Kama tunaweza kupasua mawe, tukachukua simenti ya gharama nafuu, mwaga zege barabara toka Mtwara kwenda Songea, kwenda Ruvuma pasua huko kote, una haja gani ya kuhangaika? Kama tuna kiwanda Tanga, jenga barabara ya zege kutoka Handeni njoo mpaka Singida watu watambae huko. Una haja gani ya kuagiza lami Ulaya ambayo tunatoa pesa za nje wakati pesa hizo hatuna? Internal collection yetu, simenti ni yetu, mawe ni yetu, mwaga zege barabarani wakandarasi tunao ili barabara ziweze kupitika kwa muda ambao sisi tumekusudia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kushukuru na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri na kwa kazi anayoifanya kwenye Wizara yake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza naomba kumshukuru Waziri kwa kunipa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Kiteto. Tumekuwa na migogoro mingi kwa muda mrefu Kiteto lakini sasa ameshatupa Baraza la Ardhi, tunakushukuru sana na tunakupongeza sana. Tunakuomba meza na vifaa vingine vya ofisini halafu uje ulifungue lianze kuchapa kazi, hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ardhi wamefanya kazi kubwa sana. Mpaka leo Kiteto hali ya amani inayoendelea ni kwa sababu waliweza kupima baadhi ya vijiji, mipaka ikabainishwa na watu wakaweza kuishi kwa amani kwa kipindi hiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi iliyobaki Kiteto si kubwa sana. Namuomba Waziri aje na wataalam wake atusaidie kupima ardhi yote ili finally migogoro yote iweze kufika mwisho. Wafugaji wapate pa kukaa, wakulima wapate pa kukaa, kila mtu ajue kipande chake cha ardhi, mwisho wa siku itapunguza muingiliano ambao kwa sasa umekuwa unatuletea migongano ya kila wakati. Najua ni gharama kubwa, lakini kwa mazingira na hali iliyojitokeza kiteto tunaomba tupewe priority ili tusirudi huko tulikokwishatoka, hilo ni jambo la tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ile Tume ya Waziri Mkuu ya Askofu Mhagachi, ilifanya kazi Kiteto ikamaliza, ripoti imekaa. Tunaomba mumshauri Waziri Mkuu ile ripoti ije, Waziri Mkuu afike, tumalize ule mgogoro, watu wajue nini kilitokea katika ripoti ile na hatimaye watu waweze kujua wapi wanatakiwa wasimamie na nini kifanyike kwa watu wote na atakayeyasababisha matukio mengine basi aweze kushughulikiwa kulingana na ile document itakavyokuwa inaeleza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Kiteto kuna NGOs nyingi ambazo zinanitia mashaka. Siku nyingine tutakuja kukuta Tanzania ilishauzwa hatujui na hivi vibali vinatolewa Serikalini. Kwa kweli NGOs ni nyingi, unashtukia NGO imezaliwa asubuhi watu wanafukuzwa asubuhi wanasema ni CBOs, jioni ni WMAs na hifadhi, sasa tumeshindwa kuelewa kipi ni kipi. Watu wameshalima mashamba, wamejenga, ni vijiji asubuhi wanakuambia hii ni hifadhi au ni WMA, hawa watu tutawapeleka wapi? Asubuhi watu wanaanza kushikiana mikuki na mapanga. Haya siyahitaji Kiteto, naomba Waziri aje hizo NGOs nyingine azipunguze, zifutwe na zijulikane zinafanya nini. Kwa sababu NGOs hizi zinafanya chokochoko za chini na ndizo zinazoibua migogoro ya wakulima na wafugaji Kiteto na kupelekea watu kupigana wakaisha. Tunaomba zifanyiwe kazi zile ambazo hazifanyi kazi vizuri zifutwe na zile zinazofanya kazi vizuri basi ziendelee na ziratibiwe kwa nini zinafanya kazi hizo na vyanzo vyao vya mapato vinatoka wapi ili tuweze kujua hawa watu wanakwendaje na wanatoka wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni hati miliki za kimila. Tunataka tujue, hizi hati miliki za kimila wananchi wetu wamepewa, wanajua mipaka ya maeneo na ni title, benki haziwakopeshi watu hawa, hazizikubali hizi title. Tunaomba Waziri mwenye dhamana azibane benki zinazokataa hizi title, azidhibiti, iende Serikalini, itungwe sheria, wasipewe vibali vya kufungua matawi mengine kama wanakataa hizi title. Tunahitaji watu wetu wapewe mikopo kutokana na title walizonazo kwa sababu ardhi ni yao, wana hati miliki kwa nini wasipewe mikopo kwa kutumia hizo documents zao kwa sababu wana haki nazo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimshukuru Waziri amejitahidi katika kunyang‟anya watu ardhi ambao hawaitumii, kutatua migogoro kwenye maeneo mbalimbali, kwa kweli Mheshimiwa Waziri Lukuvi amethubutu lakini naomba niishauri Serikali, Mheshimiwa Lukuvi apewe ulinzi. Akienda na kasi hii Mheshimiwa Lukuvi watampiga mshale, haki ya Mungu, mshale hauna leseni, mshale haulipiwi kodi, anaweza kutembea huko maporini Kiteto na sehemu nyingine ambako watu wana hasira wakampiga mshale kwa sababu anachapa kazi, hongera sana, amethubutu kufanya hayo. Tuombe Mawaziri na viongozi wengine na Wabunge hebu tumuunge mkono Mheshimiwa Lukuvi, tumsaidie kumtatulia migogoro na sisi, kule tuliko na sisi tufanye, tusiwe ni part ya complain. Viongozi wengi wanalalamika sana, tuko kwa wananchi, migogoro mingine inamalizwa na Wabunge. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiteto leo iko stable kwa sababu niko pale, hata kama kuna differences zozote zile lazima iwe stable, lazima itulie, wameniamini lazima watii kwa mamlaka na sheria za nchi. Wabunge twende kwa wananchi tukachape kazi, migogoro mingine ni differences tu za makabila, tabaka, uchumi, tumezidiana, amelima pakubwa, amelima padogo, ana ng‟ombe wengi, unakaa chini, mnavuta tumbaku, mnakunywa pombe, msivute ile sigara nyingine kubwa, tatua migogoro ya wananchi kabla haijaenda kwa Waziri, kabla haijaenda kwa Mkuu wa Mkoa, kabla haijaenda huko juu kwa Waziri Mkuu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumzia National Housing. Nashukuru sana kuna mchangiaji mmoja amesema National Housing ina kodi kubwa, ina vitu vingi inavyolipa lakini naomba ni-create awareness, National Housing kuna siku moja inaweza kuanguka, ikashindwa kulipa mikopo. Tuwapongeze wamechapa kazi, lakini naomba ni-create awareness kwa Serikali, Marekani iliwahi kuanguka benki zikatingishika ika-shake mpaka dunia nzima na Afrika tukapata shida. Napenda kuwaambia leo wana-flow ya mikopo mikubwa, wana hizi riba na kodi wanazotakiwa kulipa, nimshukuru Waziri mwenye dhamana alishaona na amewasimamisha kuendelea na development, wajenge hizo walizonazo wakae chini, wa-plan upya kwa maana kwamba watengeneze vision wakijua kabisa kwamba wana mikopo ya kulipa, waone capability yao ya kuilipa bila baadae kuja kuitegemea Serikali na kuwa mzigo. Mheshimiwa Lukuvi naomba ulisimamie hilo na uliangalie sana kwa sababu inaweza kutokea ukawa mzigo kwa Serikali, leo ni safi, kesho shimo. Naomba muangalie sana kwa sababu wana amana za mabenki wanaweza kusababisha yakaanguka, huo ni ushauri mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine naomba nishauri Mheshimiwa Waziri, migogoro mingi ya ardhi imekuwepo lakini tukubaliane kwamba katika maeneo mengi watendaji wa Serikali wanaolipwa mishahara, Maafisa Ardhi wanahamisha beacon. Kiteto watu wamekwisha kwa sababu wali-divert beacons za hifadhi wakasababisha watu kuendelea kugombana. Maeneo ya wakulima yakasogea ndani watu wakaanza kupambana, huyu anasema ni hifadhi huyu anasema ni mashamba, mwisho wa siku watu wakamalizana. Hawa Maafisa Ardhi wako wahuni tunaomba uwaondoe wakae pembeni, ajiri vijana wapya, wako mtaani wana vyeti kwapani, tunaomba uwasaidie hao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba nishukuru, nimuombe Mheshimiwa Angeline Mabula, Naibu Waziri, amsaidie Mheshimiwa Lukuvi, kwa kazi namjua akiwa Muleba alikuwa anachapa kazi, kulikuwa na migogoro mingi Kagoma alisimama kidete akaeleza ukweli hadharani wananchi wanakukumbuka sasa chapa kazi kwa Tanzania nzima. Pia kuna Dkt. Yamungu, Katibu Mkuu wa Wizara, ni mchapakazi, chini yake kuna Makamishna tunawapongeza, chapa kazi nchi isonge mbele migogoro ipungue hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kushukuru na kuwasilisha, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nampongeza Waziri mwenye dhamana na Mambo ya Nchi za Nje, Mheshimiwa Mahiga kwa kazi nzuri anayoifanya. Pia nawapongeza Mabalozi wetu kwa kazi nzuri wanazofanya huko nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ya kwangu machache ni ushauri tu. Napenda kushauri Wizara ya Mambo ya Nje wakae na Mifuko ya Jamii. Vile viwanja vyetu vilivyoko nje ambavyo vinahitaji kujengwa wakae na Mifuko ya Jamii wapate pesa wajenge zile nyumba halafu zile pesa wanazolipa kwa maana ya zile nyumba wanazokodi waweze kulipa hiyo Mifuko na kurejesha ili tuweze kuwa na nyumba zetu kwenye Balozi zetu kote duniani ambapo tuna Balozi. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo la pili naomba Mheshimiwa Mahiga ajaribu kuhakikisha kwamba Mabalozi wetu tulionao nje ambao wanatusemea sisi wajitahidi kutafuta nafasi kwa ajili ya vijana wetu watoke nje waende kusoma, kutafuta washirika, misaada, matajiri walioko nje waweze kutu-support kusomesha watoto wetu katika vyuo vikuu vya nje ili waweze kutusaidia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu nataka kuzungumzia Chuo cha Diplomasia, napenda kushauri Wizara ijitahidi kuona ni namna gani inaweza kufanya training kwa ajili ya viongozi wetu hata wale wa kisiasa ambao tuko humu Bungeni. Watuletee wataalam tuelimishwe tujue namna gani ya kuishi kwenye mazingira haya ya kidiplomasia kwa maana tujue namna gani ku-behave kwenye community nje ya hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine nataka kushauri Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, soko letu la East Africa ni kubwa sana, lakini naomba niseme kuna challenge kubwa sana kwenye East Africa ambayo Tanzania haiendani na nchi nyingine. Ukiangalia kwa mfano Kiwanda cha Maziwa Musoma kilikuwa kinapeleka maziwa Kenya, kilipigwa mizengwe mpaka kikafa lakini leo Kenya ina-import maziwa Tanzania na tunakunywa. Unaweza ku-imagine ni namna gani nchi nyingine ndani ya East Africa zinajaribu kuhakikisha kwamba wawekezaji wao, biashara zao, sisi Tanzania ni market kwao lakini sisi kupeleka kwao inakuwa ni ngumu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, leo ukipeleka mahindi Kenya lazima upitishe kwa mtu mmoja anunue hayo mahindi hakuna mtu mwingine mpaka yeye anunue. Mkenya akitoka Kenya kuja hapa lazima aingie Kiteto anunue kwa mkulima aende Hanang, Simanjiro, Iringa hakuna control, it means wao wako aware.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuishauri Wizara hii ijaribu ku-create watu ambao ni business attaché kwenye hizo embassies, wawe aware, waangalie ni namna gani ya ku-control wale watu wanaokuja lakini na wale watu ambao wako kule ili wananchi wetu waweze kupeleka biashara huko na sisi bidhaa zetu ziuzike huko kama ambavyo bidhaa zao zinavyoweza kuuzika hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa Wizara hii wanafanya lakini liko jambo moja nimejiuliza nikashindwa kupata majibu. Kama miaka miwili iliyopita magari yetu mengi yalikuwa yanapeleka mizigo Congo, Rwanda na Burundi. Leo naomba niwape swali moja jepesi, ukitoka Dar es Salaam kukanyaga Dodoma unakutana na magari ya Rwanda zaidi ya mia, nimejiuliza ni kwa nini? Sisi wakati tunapeleka ile mizigo madereva wetu walikuwa wana kazi, turnboy kazi, magari yetu yanakunywa mafuta hapa, creation ya employment ipo, sasa leo kwa sababu ya kushindwa kukabiliana na uwezo wa kupeleka mizigo, kuleta mizengwe mizengwe hapa katikati tumesababisha na kuwaamsha wale sasa wako kikazi zaidi. Hebu jiulizeni tumepoteza shilingi ngapi kwenye nchi yetu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe na kuwashauri mjaribu kuwa watu wa kukabiliana na hali ya soko, tuko kwenye East Africa, soko linatosha, opportunities zilizopo nyie ndiyo mnatakiwa mtuambie kuna hili, fanyeni hili ili Watanzania wetu waweze ku-benefit kwenye hizi nchi ambazo sisi ni Wanajumuiya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kushauri jambo lingine. Huko nje Mabalozi wetu wanazo kazi lakini kazi kubwa ambayo wanatakiwa kuifanya sasa ni ya ku-market Tanzania kwa maana ya uwekezaji, kwa maana ya kututafutia mashirika makubwa na ku-monitor pesa zao zinakuja kufanya nini hapa. Hawa watu wanaokuja kwa kujipenyeza tutashtukia siku nyingine watu wanaingiza pesa hapa, wananyonya uchumi wetu na hatujui na wanajiita wawekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, laundry money zitatembea hapa, uchumi na shilingi yetu itashuka, Watanzania tutabaki maskini wenzetu wakichakachua pesa. Niombe Waziri mwenye dhamana na Mabalozi wetu wajaribu kusimamia hili, waliangalie kwa ukaribu na wajitahidi kuhakikisha kwamba nchi yetu haipotezi na sisi tuna-benefit kutokana na hizo nchi ambazo wao wanaziwakilisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, niwashukuru sana, niwaombe kwa jinsi wanavyoweza wajitahidi kufanya kazi hiyo. Watu wanabeza kwamba Tanzania haijafanya kitu, hatuwezi ushirikiano, hatuwezi umoja, hebu angalieni siku ya kukumbuka Uhuru wetu wageni wa kimataifa wanaokuja kushangilia nchi yetu. Hii ni indication kwamba Tanzania ina heshima ndani ya Afrika, ina heshima ndani ya dunia, kubali usikubali Tanzania kuna kitu imefanya katika investment ya umoja na diplomacy ndani ya dunia hii. Niwaombe mnaotubeza na nyie njooni na njia mbadala ya kutuambia tutoke hapa twende vipi badala ya kubeza yale ambayo tumekwishayafanya, hongereni sana kama Wizara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kushukuru sana na naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nampongeza Waziri wa Fedha kwa hotuba nzuri ya bajeti ambayo inatupa matumaini ya huko tunakokwenda kwa kipindi hiki. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la kwanza ninalotaka kuzungumzia ni kushukuru kwa bajeti hii kwa sababu hii bajeti itafanya Watanzania waweze kufanya kazi. Naomba na kushauri sana wabane, watafute vyanzo vingine, hata hivi ni kidogo, pesa zishindikane kupatikana Watanzania waanze kufanya kazi kwa sababu hawataki kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeona speech ya Rais akizungumza juu ya vijana ambao wanazunguka, watu hawataki kufanya kazi. Naomba Mheshimiwa Waziri Mpango na Naibu Waziri wajitahidi wahangaike kiasi kwamba pesa iwe ngumu ili watu waamke wanatafuta pesa badala ya kufikiri kuangalia runinga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna msamaha wa kodi kwenye makanisa na mashirika ambayo yanatakiwa kusamehewa kodi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipindi hiki ni kipindi ambacho watu wengi wamekuwa wana diverge kodi wanakwepa kwa sababu siyo waaminifu kama zamani. Mtu anaweza kuleta kontena nne anasema hii tunajenga kanisa, ni tiles, ni vioo, kontena moja ndio inayofanya kazi, kontena tatu zinapigwa mtaani, halafu mkimaliza mnasema tunakwenda kusali kumbe kodi imepotea. Hiyo usibadilishe yeyote anayesema kodi ilipwe kwanza, watakapomaliza kulipa kodi atakaporejesha zile risiti kwamba hivi vitu vimetumika, basi wewe mrudishie kilicho chake lakini msamaha usiondoe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo na mifugo. Na-declare interest kwamba, mimi ni mkulima na ni mfugaji, si mdogo ni mkubwa. Naomba na kuzidi kusisitiza ili Watanzania watoke kwenye huu umaskini waende kufanya kazi, wafanye kazi kwa bidii watafute maisha ni lazima Benki ya Kilimo iongezewe mtaji ili tuweze kuondoa wale watu wanaosongana mijini, wanashinda vijana wenye vifua wanatembeza nguo za akinamama za elfu mbili mbili. Ili warudi vijijini ni lazima hii benki iweze kufanya kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la matrekta. Hebu tuingizieni matrekta ya kutosha watu wetu wakope waende mashambani maana hawatalima Dar es Salaam. Tusaidieni ruzuku za pembejeo, hakikisha kwamba tunainua mashamba yote ya kilimo ambayo yanaweza kuzalisha mbegu ili mbegu tunayo-import zaidi ya asilimia 80, zaidi ya bilioni kadhaa zinazotoka nje zibaki hapa ndani ili kuwe na creation ya employment na watu wao watafanya kazi mashambani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tulikuwa na kitengo cha kilimo-anga. Zamani tulikuwa na wataalam wazuri wa kilimo-anga ambao ma-pilot wetu ndio wa kwanza East Africa na Central kwa kuendesha ndege za kumwaga madawa, lakini leo hatuna pilots, hatuna ndege, na kesho kutwa mwezi wa tisa Kondoa inaomba chakula cha msaada. Naomba msikie hapa, tukirudi Bungeni Waziri wa chakula ataombwa chakula kupeleka Kondoa, ndege wamemaliza chakula. Niwaombe, kwenye bajeti yao wafikirie kununua ndege ya kilimo, wapelekeni vijana wetu wakasomee kuendesha ndege za kumwaga madawa Uingeza badala ya kukodi wataalam wa kuja kumwaga dawa hapa, huo ndio ushauri wangu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ATC. Tunanunua ndege tunapongeza kwa mpango huo ndege na zije Watanzania wafanye kazi na shirika lifanye kazi. Naomba kushauri tangazeni nafasi ya Chief Executive Officer wa ATC ambaye atasimamia. Atoke nje hatutaki ubabaishaji kwenye hili shirika tena. Madeni yote yanayodaiwa weka pembeni wataendelea kudaiana na Serikali, wataendelea kudai mishahara huko huko shirika lianze upya, akaunti mpya, CO mpya, watendaji wapya, tusonge mbele. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Hifadhi ya Mazingira. Nchi ya Tanzania ni chafu sana. Niombe kushauri wametenga pesa kwa ajili ya kupanda miti milioni kadhaa nchi nzima. Kwa nini wasifikirie ni namna gani tunaweza kufuta mifuko ya plastic nchi nzima ili tuokoe kwanza udongo, tuokoe ardhi, tuondoe uchafu, tuokoe magonjwa, tuokoe uhai kabla ya kupanda miti? Maana hizi plastic bag zimesambaa na ni nyingi sana madhara yake ni makubwa hatuwezi kuyaona leo lakini ukiangalia nchi yetu kwa uchafu huu ni mara mia tutumie disposable paper ambayo inaweza kwisha na udongo wetu ukabaki salama, huo ndio ushauri wangu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, CAG tunaomba aongezewe pesa, ndilo jicho letu, ndilo jicho la Mheshimiwa Rais, ndilo jicho la Mheshimiwa Waziri Mkuu, ndilo jicho la Mheshimiwa Waziri wa Fedha; hiki kitengo kipewe pesa. Lakini naomba kushauri jambo, kumekuwa na mrundikano wa madeni; mara tunaangalia yalienda wapi, yakaenda wapi miaka kumi bado CAG anakagua haviishi vilipanda vilishuka. Hebu mshaurini CAG afute haya matakataka yaliyoliwa huko nyuma, maana yameliwa na Watanzania hawa hawa wamemaliza, ayafute ili hiki kitengo kiweze kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi. Ni kwamba kipunguziwe mzigo wa ku-audit. Ana-audit miaka kumi ishirini iliyopita huku mbele vinaliwa, huku nyuma ameshindwa kuzuia sasa afanye nini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hebu wafute hivi vitu, Mheshimiwa Waziri afute haya matakataka yote haya yaishe tuanze upya mafaili mapya, tukamatane kwa upya, CAG aweze kufanya kazi kwa ukaribu vinginevyo unamfanya ana-audit vitu wiki mbili tatu hawezi ku-cover nchi kumbe ana audit vitu vya 2013, 2012 huko, badala yake tungekuwa tunakwenda mbele ili aweze kukabiliana na uovu ambao umetokea kwa wakati huo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ambalo nataka kushauri, hawa auditors wa CAG wangeweza hata kukabiliana na watendaji wetu wahalifu kwa wakati. Sasa otherwise ni kwamba anapokwenda ku-audit anakuta mtumishi alihama aliiba, akapandishwa cheo, akaua zaidi badala ya kuokoa pale. Watu wakamatwe kwa wakati kwa sababu tunahitaji hawa watu tuweze kuwakamata kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, TRA. Tunaomba isaidiwe watumishi wengi wa TRA wanapata vitisho kutokana na walipa kodi, kudai kodi siyo kazi rahisi wamefunga roho. Hawa watumishi wetu wa TRA wasaidieni ili waweze kulindwa na usalama wao, otherwise wanaweza kuyumbishwa na wafanyabiashara na viongozi wanasiasa watendaji, mwisho wa siku wakafanya uhalifu wa kuhujumu nchi bila wao kutaka. Naomba wasaidiwe maana wanakutana na shida nyingi na maamuzi mengine wanayafanya bila wao kutaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, watakapofanya hivyo itatusaidia sisi kujua na kukagua vitu vyetu ambavyo vyote vinawezekana na makusanyo mengi yatakuwa makubwa kiasi kwamba, tutakuwa tumeweza kukusanya kiasi ambacho sisi tulikuwa tunakitarajia. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, zahanati. Kiteto tumepewa zahanati tatu, sasa wale Wamasai wangu wa kule porini naenda kilomita 150 watakutana lini na dawa? Simangilo zahanati moja watakutana lini na dawa, clinic watakutana nayo wapi, sasa Mheshimiwa Waziri tunaomba hili suala mliangalie…
Mheshimiwa Naibu Spika, muda umekwisha? Yesu wangu! Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza, naunga mkono hoja. Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayofanya na jinsi anavyosukuma gurudumu la maendeleo kwenye nchi yetu. Siku zilizopita kwenye mwaka 2010 - 2015 wenzetu wa Kambi ya Upinzani walikuwa wanasifia sana utendaji wa Kagame. Walikuwa wanasifia sana jinsi anavyochapa kazi na jinsi ambavyo amenyanyua Shirika la Ndege; na ATC yetu imekufa wakiwa wanalaani pamoja na Rais wetu Mstaafu JK. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nashangaa leo, Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amenunua ndege za kutosha, leo anapingwa. Jambo lingine ni kwamba, wakati wanasema anashauriwa na Kagame, wakati anajenga barabara Magufuli akiwa Waziri, swali ni
je, alikuwa anashauriwa na Kagame? Wakati anakamata meli zilizokuwa zinatuibia samaki kwenye bahari kuu, alikuwa anashauriwa na Kagame? Nawaomba, mkikumbuka kudanganya siku nyingine mkumbuke pia namna gani ya kujibu hoja zenu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nizungumzie jambo dogo tu la Utawala Bora. Leo Jimboni kwangu Kiteto siyo salama sana. Siyo salama kwa sababu ya utawala bora tu, ambao tuna-miss watu ambao kwenye sehemu zao hawafanyi ipasavyo. Kiteto kulitokea mauaji na sasa baada ya Waziri Mkuu kutoka juzi tu miezi miwili wameshakufa watu wawili. Mashamba yameshachomwa zaidi ya thelathini. Tuna viongozi; tuna Mkoa, tuna Wilaya, tuna OCD tuna Mahakama na tuna Ofisi ya DC. Kwa nini vitendo hivi vinaendelea?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niambiwe kwa nini vitendo hivi vinaendelea na Serikali haijachukua hatua? Suala hili ni uzembe wa Watendaji wetu. Excuse ndiyo nyingi. Unaambiwa wamekamamatwa ugoni, wameshikana wapi, lakina umma uliteketea. Siku za hivi karibuni, hapa Jimbo la Kibajaji waliuawa wananchi watatu. Kile kijiji watu walitawanywa, walikamatwa, waliwekwa ndani na Serikali ilionesha jitihada zake. Kwa nini Kiteto hizi jitihada hazifanyiki ili mauaji yaweze kukoma? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba, Kiteto kuna watu wanafikiri kwamba ile amani ilitengenezwa tu. Hata wakati mauaji yanaendelea, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ilikuwepo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilikuwepo, Watendaji wote wa Serikali walikuwepo. Leo wanatumia camouflage kwamba
wametengeneza. Wakati ule Mbunge alikuwa anaunga mkono hiyo hoja, DC aliyekuwepo alikuwa anaunga mkono, ofisi nzima, ndiyo maana umma uliteketea. Leo amani ipo kwa sababu tumefanya changes za utawala wa pale. Kila anaponyanyuka, nipo. Leo nimetengenezewa zengwe, nashughulikiwa. Nami watakaoshughulikiwa kukamatwa au kuwekwa ndani yawezekana nami nimo. Mimi nitakwenda kama Mandella. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukihisi kwamba naweza kudanganya na kusema uongo, siyo sehemu. Ukihisi kwamba naweza kuulinda uovu, siyo sehemu! Kiteto chama pekee, Kamati ya Siasa ya Wilaya ndiyo iliyookoa na kulaani vitendo viovu na Serikali ilikuwepo. Waziri Mkuu aliunda Tume; tunaomba ile ripoti itoke. Ile ripoti ina mambo mengi ndani yake. Ile ripoti itoke kwa sababu gharama ya Serikali imetumika, lakini kumefanyika heavy investigation juu ya matukio yaliyosababisha ile hali kuwa pale. Inaonesha vitendo vingi ambavyo vimefanywa na baadhi ya Watendaji mle ndani katika ile ripoti. Inaonesha involvement ya wale wanasiasa waliofanya hayo mambo pale ili itusaidie way forward tujue namna gani ya kukabiliana na matatizo yaliyoko pale.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine, Kiteto wanasema imevamiwa sana. Leo wanafukuza watu kule, amani inaanza kupungua. Mtu amekaa miaka 20 au 15, maisha yake yako kule, hajui kwingine kwa kwenda, leo anaambiwa aondoke, anakwenda wapi? Wanasema ni
wavamizi, lakini wanasahau kwamba leo wale tunaowafukuza kule; leo Wilaya yangu nusu ya wafugaji wako Kilindi kwa Mheshimiwa Omari Kigua, naye awafukuze?
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunapozungumza, Kata yangu ya Dosidosi inayopakana na Kongwa, robo tatu ya wakulima wake wanalima Kongwa wakati ni wananchi wa Kiteto. Leo tuwafukuze? Wana zaidi ya miaka 30. Ukikaa unaulizwa, “ehee, leteni document ya shamba; hili shamba lako ulilipata lini?” Mtu ana miaka 30, ameoa, ana wajukuu analima Kongwa; ni mwananchi wa Dosidosi Wilaya ya Kiteto. Leo tufukuze watu kwa miaka 20 waliyokaa pale; kisa ni nini? Kwa sababu kuna mazingira ya rushwa, kwa sababu kuna ukabila. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, leo naomba mkubaliane nami, Bunge hili ikitokea kafa mtu Kiteto, namba msimame tuahirishe Bunge tuendelee na mchakato. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tulishakutana na vitu vigumu sana kwenye yale mazingira. Ukiona mgogoro hauishi, jua kuna watu wanachochoea huo mgogoro. Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Ahsante.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naunga mkono hoja na napongeza jitihada zako ikiwemo upatikanaji wa dawa katika hospitali zetu. Niombe gari la wagojwa katika tarafa ya Matui ambayo ina population kubwa ya watu. Gari hilo likae kituo cha afya Engusero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba daktari wa Anesthesia katika kituo chetu Engusero ili operations ziweze kuendelea. Pia tunaomba madaktari na ma-nurse, Wilaya ina upungufu wa watumishi hao ikiwemo Daktari wa Kinywa na Meno.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba ujenzi wa maabara ya Wilaya maana iliyopo ni chumba kidogo Prime Minister alikiona akashangaa na akaniambia nikuambie.

Mheshimiwa Waziri, tunaomba upanuzi wa kituo cha afya cha Sunya maana kinabeba wagonjwa zaidi ya 30,000 tunaomba maabara na upanuzi wa majengo (wodi).
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. EMMANUEL J. PAPIAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napongeza kazi inayofanywa na Wizara na watalaam wake na pili nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi anayoifanya na jitihada nyingi zote za kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ambayo imetengwa hii ya shilingi bilioni 600 ambayo tunalalamika kwamba iende shilingi bilioni 900, mimi ninaona kwamba Wizara imepanga bajeti ambayo ndiyo halisi, kwa sababu hata hii shilingi bilioni 600 yenyewe tukisema leo tuiombe yawezekana hizo fedha zisifike. Fedha ambazo zimetoka ni chini, asilimia 19, ina maana kwamba hata hii tukiiomba yenyewe yawezekana isiwe halisi. Sasa mimi niombe na kushauri kwamba Bunge lako hili likubali tutengeneze ile shilingi 50 iongezeke kwenye mafuta ambayo ndiyo pesa halisi ambayo yawezekana ikawa ni halisi ya kwenda kupeleka kwenye miradi yetu ya maji, angalau ikaongeza Mfuko wa Maji kupata pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watendaji wa wizara wanafanya kazi kwa nguvu kubwa, lakini huku chini kwenye halmashauri zetu watendaji wa Idara za Maji hawafanyi kazi ipasavyo. Idara ya Umwagiliaji Wizarani kuna tatizo la watu kukaimu, watu wengine wamestaafu. Hili suala la umwagiliaji nchini naomba litizamwe kwa kiwango kikubwa, suala la kukaimu linasababisha watu kushindwa kufanya kazi na kufanya maamuzi kwenye maeneo yao. Wale waliostaafu, kama hakuna watu wengine ambao wamewarithi ambao mmekuwa trained na kujua namna ya umwagiliaji nchini basi wale wapewe contract kwa muda wafanye training ya hao wengine ili waweze kusukuma kazi ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo kubwa linalofanya nchi yetu ipoteze fedha nyingi ni tathmini ya miradi ya maji kuwa gharama kubwa sana. Mradi mdogo wa shilingi milioni 20 mtu ana tender shilingi milioni 200, hizi fedha zinavyotoka inalazimisha mradi kuwa nusu nusu na haifiki mwisho na mwisho wa siku miradi mingi ya maji nchini inakuwa viporo na haifiki mahali inapotakiwa.

Kwa hiyo tunaomba tulitazame hili, lakini kwenye tendering documents Wizara iangalie, Serikali iangalie ni namna gani tunaweza kwenda kwenye uhalisia unaoweza kufanya miradi hii iweze kukamilika na fedha za Serikali zisiweze kupotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu wafadhili, miradi mingi ambayo inakuwa supported na wafadhili mimi nadhani hawa wafadhili na wenyewe kuna jinsi wanatupiga chenga. Leo wameleta fedha, kesho wameahidi, keshokutwa wame- cancel, miradi haiwezi kuendelea, hii ni danganya toto. Nchi ijitizame upya ni namna gani tunaweza kutokana na haya masuala ya wafadhili, asubuhi amekushika tai, jioni amekuachia tunakuja Bungeni tunaahidi vitu ambavyo haviwezekani. Tujitizame upya tupunguze hili suala la utegemezi wa wafadhili ambao wanatufikisha mahali ambapo sipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Kiteto wameniomba niiombe Wizara ya Maji, maeneo ya Ndido, Makame, Loolera tupewe bwawa moja angalau kwenye hii tarafa ili basi wale wafugaji wapate maji. Kanda hii ya maeneo ya hizi kata tatu hawahitaji maji safi na salama, wanahitaji ilimradi ni maji, ukinywa usiharishe, usife, ng’ombe wasife, yawe meupe, yawe meusi, yawe blue wao wanahitaji kitu kinachoweza kuitwa maji na Serikali ikawaambia haya ndiyo maji, kwa sababu wamelia miaka mingi hakuna mabwawa, mifugo inakufa, wananchi hawawezi kupata maji ya kutumia. Maji haya yote sisi tunayatumia kwa maana ya binadamu na mifugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi napendekeza na naomba Wizara yako kwamba tupate bwawa moja la maji kwenye tarafa moja kwa mwaka huu, hilo ni jambo la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili tunaomba, kuna mabwawa ambayo wananchi wanachimba wenyewe; ukichukua fedha Wizarani, ukaangalia namna gani ya ku- rescue situation kwa haraka, uka-fund wale watu wanaochimba yale mabwawa kwa mikono yao tunaweza
kuwa na mabwawa madogo madogo kwenye maeneo ambayo wakati Serikali haijapanga ile miradi mikubwa basi wananchi wana mabwawa madogo madogo ambayo wanaweza kuwasaidia maji kwenye maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nishukuru kwa Bwawa la Dongo ambalo limeingizwa kwenye mpango, lakini niiombe Serikali…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nimpongeze Waziri kwa hotuba yake aliyoitoa ambayo inaweza kutusogeza na ikatufikisha mahali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza nataka kusema TRA imefanya kazi nzuri, sasa hivi tunaona kuna mahusiano mazuri kuliko nyuma ambako kulikuwa na maneno mengi, vurugu na wafanyabiashara, mvurugano na kukimbizana, sasa kunaonekana kuna lugha ambayo ni mahusiano mazuri yanayofanya watu kulipa kodi kwa usahihi lakini pia kwa mahusiano mazuri ya lugha na wanafanya vizuri zaidi kuliko kipindi cha nyuma ambacho kulikuwa na mivutano mikali baina ya wafanyabiashara na watoza kodi wetu. Hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, kuna hii Benki ya Kilimo, benki hii tunadhani sasa ndiyo wakati wake, Awamu ya Nne imejitahidi imeanzisha benki hii, lakini tunaomba Serikali basi ione namna gani ya kuiongezea mtaji. Kuna fedha za nje, Nchi kama za China, leo China tunasema ni marafiki zetu wakubwa sana wa kihistoria kwa nchi yetu, kwa nini benki za China Serikali isikope kwa riba nafuu ikaletea pesa Benki yetu ya Maendeleo ya Kilimo ikaipa mtaji wa kutosha ikaisimamia hii benki ikaenda kwa wananchi wetu ambao ndio asilimia 80 ya Watanzania ambao wanajihusisha na shughuli za kutafuta maisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuimarisha benki hii na kuipa mtaji unasaidia watu wengi kuwa kwenye wigo mpana wa kufanya kazi na Watanzania wengi watakapofanya kazi Serikali itaweza kukusanya kodi ya kutosha. Niishauri Serikali ilitazame hili, ilifanyie kazi na ihakikishe kwamba hii benki inapata mtaji kwa kipindi kisicho kirefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hizi benki za biashara, hizi benki sasa hivi zina hali ngumu, zimekopesha watu, watu wameshindwa kurejesha mikopo kwa sababu ya kipindi kigumu, uwezo wa kushindwa kulipa kwa watu umeongezeka, lakini benki hizi zilikuwa na nia njema kwa sababu zimekopesha wakulima ambao hata mahali ambapo kilimo kimeshindikana kwa sababu ya mvua zikajaribu ku-risk zikakopesha hao watu, watu wame-default, sasa benki na zenyewe zinakwenda kuanguka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yawezekana hizi benki za biashara; CRDB, NMB, zina defaulters, mikopo mingi inachechemea. Tunaomba basi Mheshimiwa Waziri na Gavana watazame hili waone huruma mahali ambapo wamekosea, basi warudishe nyuma kidogo, wasamehe kwa sababu wanaoumia ni wengi Watanzania wetu wanaolipa kodi, basi tuone ni namna gani wanaweza kusonga mbele. Vinginevyo, wakiendelea kukandamiza sana kwa hali ilivyo sasa tutapoteza watu wengi kibiashara, tutapoteza kodi kubwa sana lakini pia na nchi itayumba economically. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali ione huruma hivi vyombo vyetu vya fedha mahali vilipokosea basi wawasamehe, wakae chini mezani wawape guidelines za kufanyia kazi, wawape muda, waone ni namna gani wanaweza kusonga mbele, lakini wawalinde kwa sababu na wao walikuwa ni sehemu ya kuchangia uchumi kwenye nchi yetu. Maana hizi defaulting zote zinazoenda ku-appear ni kwamba bado Serikali na yenyewe inaendelea kupoteza mapato. Sasa ili twende pamoja, kwa sababu tunawahitaji, Serikali tunahitaji isipoteze, hizi institutions tunahitaji zisife wala kutetereka kwa sababu nchi inaweza ku-shake. Sasa ili tufikie hapo, basi tunaomba Serikali ishushe mkono, itoe huruma, itoe maelekezo, iangalie ni namna gani hivi vyombo vinaweza kuendelea kufanya kazi bila mvutano wowote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Benki ya TIB ambayo ni benki ya Serikali. Tunaomba Serikali iione na iipe mtaji kama nchi nyingine zinavyokuwa na benki za Serikali ambazo zinapewa fedha na kuzisimamia ili benki hizo zisife.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hili suala la milioni 50 kila kijiji. Kwenye Wilaya yangu tumekaa tukafikiri tukajipangia, tukasema ngoja tuisaidie Serikali. Mimi namsaidia Mheshimiwa Waziri. Wilaya ya Kiteto tuna vijiji 63, hivi vijiji ukitaka kuniletea milioni 50 kila kijiji ataniletea 3,150,000,000, mimi hizi zote asiniletee, sizihitaji kwa sababu Tanzania ni kubwa, Kiteto ni Wilaya katika Wilaya mia moja na kitu za Tanzania, namwomba milioni 500 tu. Hii naomba ifanyike kwa nchi iwe ni pilot study, watu waje wajifunze, waone ni namna gani tutakavyotumia hizi pesa zikaenda kuzunguka kwa watu wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejipangia sisi tuna mpango wa VICOBA Wilaya nzima. Wilaya ya Kiteto inaenda kuwa Wilaya ya kwanza kwenye mfumo wa VICOBA ambapo pesa ya wale wanachama haipotei na mfumo ule haupotezi pesa, watu wanajilinda wenyewe. Akinipa milioni 500 mwezi wa Nane ikaanza kuzunguka kwenye VICOBA katika vijiji kumi tu, nifikapo mwakani mwezi wa Nane nitakuwa nimeshakwenda zaidi ya vijiji 40. Kwa maana ya kwamba zile zitakazokusanywa tunazielekeza kwenye vijiji vingine, kwa maana hiyo pesa itakayozunguka pale tutakapofika 2020 nikisimama kunadi Ilani ya CCM tuliyoiahidi mimi na Mheshimiwa Waziri huko kwa wananchi, nitakuwa nimesha- cover vijiji vyangu vyote 63 kwa hiyo pesa ya milioni 500.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri atakapokuja naomba anipige tafu anipe hiyo ahadi ya milioni 500, anipe mimi na Wilaya nyingine Tanzania zitakwenda kujifunza pale ili tuweze kurudisha pesa. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Waziri mbele yake, hizi pesa akinipa ifikapo 2020 namrudishia 500 ya kwake na wananchi wangu watakuwa wameshapata kazi na Serikali itakusanya kodi kubwa maana hawa wananchi hizi milioni 500 wanapokwenda kufanya kazi, watafanya kazi…..... (Makofi/ Kicheko)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza napongeza kwa Mpango mzuri ambao umeletwa na Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa ajili ya kutengeneza dira ya uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza nalotaka kuzungumza ni kuhusu mazao ya kilimo ambayo ni ya biashara, haya mazao ya tumbuku, chai na kahawa, ni mazao ambayo kwa muda mrefu yameshapoteza masoko hayana bei na wakulima wetu wanateseka. Nilitaka kuishauri Serikali kwamba sasa iangalie namna gani haya mazao ya kibiashara yanaweza yakapata masoko ili Serikali iweze kupata kodi, lakini na wakulima wetu waweze kupata faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine nilitaka kushawishi, hili zao la mahindi nilitaka sasa na lenyewe liingie kwenye Mpango kwamba ni zao la biashara. Mkulima anapolima aweze kupata mazao yake, auze anapotaka aendelee na maisha yake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Rais ameshasema Serikali haina chakula cha kumgawia mtu, wakulima wameshaweka reserve chakula chao, chakula kilichopo hii bumper harvest iliyopo watu waruhusiwe waweze kupeleka mazao yao wanapotaka. Mtu asije na hoja kwamba tuna mikoa ambayo ina upungufu wa chakula, mwaka huu katikati mwezi wa saba na wa nane watu walikuwa wanachukua mahindi Kilindi na Kiteto kupeleka Shinyanga, leo hayo mahindi hayaendi kama kuna deficit Shinyanga kwa nini biashara hii haifanyiki leo? Ruhusuni watu wapeleke mahindi wanapotaka ili waweze kupata faida na waondoke kwenye umaskini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelekea kweye kupanda watu wanahitaji mbolea na pembejeo, wapeni nafasi wakauze mazao yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Zambia wamezalisha mahindi mengi sana na kwa Wilaya za kina Mheshimiwa Kandege mazao yana trespass kwa njia za kawaida za panya yanaingia hapa. Mazao mengine yanapakiwa pale border yanapita yanakwenda upande wa Kenya. Ukiyaangalia yale mahindi ni meupe ni masafi wanapeleka Kenya hatupati kodi. Hivi leo sisi Watanzania wangepakia wakapeleka Kenya nchi yetu ingekusanya kodi. Mheshimwa Mpango unahitaji kukusanya kodi kutoka kwenye haya mahindi yanayokwenda Kenya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gunia la kilo mia Kenya ni 7,500 mpaka 8,000, it means unazungumzia karibia shilingi shilingi 140,000. Mheshimiwa Dkt. Mpango ukikusanya pesa ya kodi pale mpakani Holili na Himo, wewe unahitaji pesa, mkulima amepata faida na barabara zetu hazijachimbwa na magari ya wengine badala ya magari yetu na mkulima wetu ameshapata faida. Turuhusu mazao yaende mkulima ata-debate mwenyewe wapi atapata chakula Rais ameshawaaga kwamba hakuna chakula cha msaada. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la lingine tumekuwa na Kakono Project ambayo mwaka jana tuliiwekea mpango hapa fedha zake zipo, mkopo upo wa African Development Bank, Malagarasi ipo, pelekeni pesa hii miradi ianze ili iweze kuongeza umeme kwenye Gridi ya Taifa tuweze kupata faida. Nilihudhuria kikao kimoja pale Kakono, Mtukula nikakaa pale Misenyi, nikazungumza nikaona wale watu wa African Development Bank baadhi yao ni wa Kenya wanaendelea na project. Nilipokaa nikawaza kama this guy’s wapo kwenye hii project wana uwezo wa kuikwamisha mpaka TANESCO yetu hii miradi isiweze ku-take over ili kupata umeme.

Mheshimiwa Mpango naomba hili uende nalo uliangalie ili tuweze kuona ni wapi imekwamia hii Kakono Project na Malagarasi ili tuweze kuzalisha huu umeme wa maji. Leo ukienda Mtera inazalisha megawati 80 lakini Mtera maji hamna, yamekauka, yatashuka kesho kutwa huwezi kuzalisha hizo megawati lakini ule umeme wa Kakono ni maji ya Nile hayatakatika, hayatashuka megawati zetu 87 zitaingia kwenye Gridi ya Taifa na bado tutaendelea kupata faida, naomba hili liangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine uvuvi bahari kuu. Kuna Mheshimiwa mmoja amezungumza hapa, uvuvi wa bahari kuu sasa hivi Tanzania wanachofuata ni suala la leseni shilingi milioni 30, sijui shilingi milioni 40, ukivua saa mbili ndani ya bahari kuu una meli yako unatengeneza shilingi trilioni moja. Hicho ni chanzo Mheshimiwa Mpango nenda nacho, uje na mpango wa kutuambia tunanunua meli, tunavua bahari kuu, samaki za kwetu tu-export samaki tupate faida. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Kilimo, asilimia 70%, 80% ya Watanzania wanaenda kwenye kilimo, uje na mpango wa kuniambia benki hii inapataje pesa, wewe ndiyo unazo. Hii Benki ya Kilimo leo ndiyo inayokwenda kuokoa watu, benki nyingine sasa hivi zimesha-stuck, haziwezi ku-invest kwenye kilimo kwa sababu ya hali ilivyo na mikopo mingi chechefu sasa hivi ni ile ambayo wali-inject kwenye kilimo hawawezi kwenda zaidi kwa maana hiyo sasa kilimo kitaenda kushuka. Nikuombe Mheshimiwa Mpango, Benki ya China (China Agricultural Bank) ina uwezo wa kutukopesha, itafutie hii benki mtaji iweze kukopesha wakulima wetu ambao ndiyo pesa hiyo itakayozunguka mwisho wa siku utakutana nao kwenye TIN, vioski na mama ntilie, upate watu wa kutoza kodi ambao wameshapata huku kwenye kilimo. Mheshimiwa Mpango hii benki naomba ukija utuambie unaenda kutengeneza shilingi ngapi huko ndani unaichomekea hapo ili iweze kusogea mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, liko suala la afya. Miaka ya 85 kurudi nyuma tulikuwa na vyuo vyetu vya RMAs (Rural Medical Aids), tulikuwa tuna-produce wale watu ambao walikuwa wanakwenda kufanya kazi kwenye zahanati zetu kule vijijini leo zahanati tunazozijenga kwenye mpango wa Wizara ya Afya kwa maana ya afya hazina wataalamu. Tufanye mpango tuwarudishe hawa Rural Medical Aids wakafanye kazi kwenye zile zahanati zetu kwa sababu kuna nurse mmoja atagawa dawa, atazalisha wanawake au atafunga vidonda. Watu hawa wakipatikana kwenye zahanati zinazojengwa nchi nzima afya za watu wetu zinaweza kubaki salama. Nikuombe muangalie ni namna gani mtapanga kurudisha wataalam hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mpango nikushukuru kwanza jambo moja ambalo umeonyesha kwenye Mpango hapa, suala la kujenga barabara ya kutoka Handeni - Kibirashi - Kiteto – Chemba - Kondoa – Singida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikuombe hii barabara sasa kwa sababu imeingia kwenye Mpango ipate pesa iweze kutengenezwa. Wakati hii barabara inatengenezwa tunaomba mtutafutie wafadhili kwenye ukanda huo huo wa kutengeneza viwanda vya kuchambua mchele, kutengeneza unga, kusindika mafuta ya alizeti, kuzalisha juisi ya matunda huko Tanga ili along that road na bomba la mafuta wakati linapita, magari yanapita kupeleka mizigo bandari ya Tanga ili ile mizigo inapopita kuelekea Kanda ya Ziwa, Rwanda, Burundi, Uganda na Kongo basi kuwepo na hivyo viwanda viweze kuzalisha na hayo mazao ya mbegu yaende kwenye hizo nchi ili na sisi wakulima wetu na wananchi kwenye hizo kanda waweze kuwa wamepata faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nikushukuru lakini nikuombe msiwafunge Watanzania waweze kutembea East Africa. Mmeona speech ya Museveni kule kwenye bomba la mafuta Tanga ametukana watu weupe hataki kusikia hii biashara, anasema East Africa tuna population ya one seventy thousand people ambapo tunaweza kuwa ni soko la mazao na kitu chochote tunachozalisha hapa nchini. Watanzania msiwafunge acheni watoke mkiwabana sana they will burst.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naunga mkono hoja na jitihada za Serikali juu ya ujenzi wa barabara nyingi na kwa kiwango cha lami nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maombi yangu ni barabara ya NARCO (Hogoro) – Kibaya – Orkestmet Orjoro (Arusha); tunaomba ijengwe kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni shortcut road ya kwenda Tanga; mbili, kwa sababu Kiteto ni eneo linalozalisha mahindi mengi sana kwa Kanda ya Kati na kulisha Jiji la Dar es Salaam; tatu, maombi yangu tunaomba hizi kilometa 91 NARCO – Kibaya zijengwe kiwango cha lami maana ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara mwaka 2014 alipokuwa ziara Wilaya ya Kongwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Wizara iokoe mazao ya wakulima kuepusha gharama kubwa za usafirishaji wakati wa msimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba mawasiliano kwenye Kata za Raiseri, Loovera pamoja na Kata ya Sunya.

Mheshimiwa Naibu Spika, natanguliza shukrani zangu.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa dakika tano. Kwanza napongeza jitihada nyingi za Serikali ambazo inazifanya kwenye maeneo mbalimbali na kwa namna ambavyo Mawaziri wamejitahidi kufanya kazi kwenye hizi report zao.

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwajali wakulima na wafugaji kwa kupunguza maeneo ya hifadhi ili wakulima wetu na wafugaji wapate maeneo na mahali pa kukaa salama bila ugomvi kwenye maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili nimshukuru Rais kwa kutoa vitambulisho kwa sababu, wajasiriamali wetu sasa wameanza kutambulika na mwisho wa siku watakua, watakuwa ni watu ambao wana uwezo wa kutambulika na watakuwa wakubwa na watakuwa na uwezo wa kukopesheka hapo mbele.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la tatu kuna jambo ambalo nimeliona na Wabunge wengi hawajasema, Rais ameweza kufanya kazi kubwa ya kusaidia kupata matrekta NBC imetoa matrekta, mkulima analipa milioni mbili down payment na leo wakulima wengi wameweza kusambaziwa matrekta nchini.

Mheshimiwa Spika, kwake kuna matrekta 89 yameingia, Wabunge wenzangu mpigieni Makofi Mheshimiwa Spika wetu. Kwa Mheshimiwa Nkamia yameshaingia matrekta 52, kwangu Kiteto yameshaingia matrekta 105. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais ameshafanya kazi kubwa kwa wakulima wetu kwa kuwatambua ili wakapate kufanya kazi kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili suala la TARURA linatupa shida kidogo. Siku za nyuma Madiwani wetu na baraza walikuwa na uwezo wa ku-coordinate zile barabara na kuona wapi pana daraja na wapi pana shida. Sasa hili suala la TARURA kutoleta taarifa kwenye Baraza la Madiwani tunashindwa ku- coordinate na ku-monitor hizi barabara, hata kwa kujua gharama. Hili suala litaendelea kuharibu barabara nyingi, suala la hizi barabara ambazo unakuta wameleta pesa za dharura kwa ajili ya kutengeneza maeneo korofi, huwezi kujua ni kiasi gani, huwezi kujua wanatengeneza wapi, huwezi kudhibiti angalau na kujua kwamba, kilichoingia ni kipi na kilichotoka ni kipi ili kuwabana watendaji wakandarasi kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba kushauri. TARURA, TAMISEMI iweze kutusaidia kuhakikisha kwamba, hawa watu wa TARURA wawe wanaripoti kwenye Baraza, watoe ripoti pesa zilizoingia, viwango vya barabara vinavyojengwa kwa wakati huo, pesa za dharura na kila kitu chote ule mchanganuo upate halafu na sisi Baraza la Madiwani tutoe ripoti na ile ripoti iwe inakuja mpaka mkoani, mkoani iweze kuja kwenye Taifa kwa mazingira ya kila wilaya kuweza ku- monitor barabara zilivyo na uharibifu wake.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine; watendaji wa vijiji na kata mimi napata mshangao. Utumishi wa nchi hii unafanana kama Hati Miliki ya Ndoa ya Kikatoliki kwamba, mpaka ufe au mwenzako afe hamuwezi kuachana. Hii ni shida kubwa unakwenda mahali kijiji kimechanga Sh.2,700,000/=. Juzi nimepigiwa simu hapa, wananchi wanahitaji kupauwa jengo lao, Mtendaji wa Kijiji amechukua pesa, amekwenda amenunua mizigo yake amechakachua, amerudi hapa, haitoshi, hakuna kikao, hakuna kamati, hakuna nini, wanamuuliza anasema hakuna, amekuwa mbabe. Ukienda naye sambamba ni kwamba, mbele wanasema sasa mtumishi ukitaka kumhamisha wanakwambia awe na cheque mkononi, cheque mkononi, unafanyaje?

Mheshimiwa Spika, ukiondoka anakaa hivyo, keshokutwa mchango mwingine, wananchi wanaacha kuchangia maendeleo yao. Lazima TAMISEMI iamue mtumishi mbadhirifu level ya kijiji aidha apewe adhabu ya kuondolewa kazini tuajiri wengine ndio maana tuna wasomi wako mtaani. Tuamue, hii inaweza ku-discipline nchi hii, otherwise ni kwamba, tutaendelea kuwa na debate, Mkurugenzi hawezi ku-manage hawa watu wote, hata akim-manage anamhamisha anakompeleka si kuna Watanzania walewale, si kuna kijiji kilekile, si kuna kata ileile, atachangisha ataharibu. Sasa hii contract ya mtumishi wa Serikali ya Tanzania ambaye hawezi kumeguka akaachwa, eti formular sijui mpaka uajiriwe, ukaulizwe, mupeane adhabu, barua za onyo, hatutafika na wananchi chini wanaumia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naombe kushukuru jitihada nyingi za Serikali zinazofanyika. Napongeza na kuunga mkono hoja. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Waziri kwa hotuba na kwa bajeti yake ambayo ameweza kutuwasilishia. Niombe kumshukuru kwa Bwawa la Dongo ambalo limewekwa kwenye mpango ambapo hili bwawa sasa kwa pesa zilizotengwa japo ni kidogo, lakini naomba hizo pesa zitoke na usanifu uendelee ili wale wananchi wa vijiji vya Dondo na Laiseri viweze kupata maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kiteto ina tatizo kubwa sana la maji kwa kipindi kirefu na kwa maeneo mengi ambayo tumekuwa na tatizo na maji ni kwamba tuliahidiwa kupata mabwawa kwa sababu yale maeneo ni kame. Ninaomba Waziri na Wizara yake waweze kutusaida kukarabati mabwawa yetu upande wa Makame, bwawa ambalo lilichimbwa na wananchi lakini halijakamilika katikati ya Lukiushi na Makame.

Ninaomba pia kukarabatiwa Bwawa la Matui ambalo Mheshimiwa Waziri uliliona, ulilikagua na ukaona kwamba linastahili kukarabatiwa na ni bwawa kubwa ambalo linastahili kukarabatiwa na lipate pesa kwa ajili ya maji ya binadamu, pia umwagiliaji kwa ile kanda ambayo kuna wananchi zaidi ya 20,000 ulijionea mwenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna bwawa la umwagiliaji la Enguselo, hili bwawa limefanyiwa upembuzi yakinifu wananchi walishaachia yale maeneo yao kwa hiari yao na maeneo mengi yameshaachwa kwa muda mrefu na mashamba wameyaacha. Sasa ni lini Wizara itatenga pesa muda wa kufanya uhuishaji kwa kukarabati lile bwawa na kulijenga tayari kwa wanachi kuweza kulitumia kwa ajili ya kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo mabwawa mengi kwa sababu Kiteto ni eneo kame, na jambo la kutusaidia ni mabwawa, kwa mazingira yetu ya wafugaji na wakulima ni lini Serikali itatusadia kupata mabwawa upande wa Makame, Ndido, Rorela, maeneo ambayo ni kame lakini wafugaji wengi hawana mabwawa na mifugo inalazimika kwenda upande wa Simanjiro, upande wa Kilindi na kwenda upande ambako mifugo yetu inalazimika kutafuta maji ikihangaika huku na kule na wafugaji wanapata shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo miradi mingi ya vijiji ambayo haijakamilika, tunaomba Serikali itusaide ni namna gani tunaweza kupata pesa ili hii miradi ya vijiji vya Dosidosi, Ndughu, Nguselo, Lergu, Ndido, Songambele na vijiji vyetu vingi ambavyo sasa vipo kwenye mpango vingine nimevitaja kwenye maandishi baada ya kuwa nimekuandikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba kwa mpango wetu bajeti tuliyotengewa ni ndogo, karibu shilingi bilioni 1.329, sasa Mheshimiwa Waziri kwa pesa hii umepunguza bajeti yetu kwa bajeti ya mwaka jana, kwa bajeti hii miradi yetu ya maji na shida tulizonazo hebu niambie Waziri tunakwenda wapi? Nikuombe Waziri review bajeti yako, fika mahali sasa Kiteto uionee huruma, kwa jinsi ambavyo tuna shida ya maji muda mrefu, katika ilani yetu ya utekelezaji 2015 - 2020 ni mikoa mitano ambayo ipo kwenye plan na ni mikoa kame ambayo ilikuwa na priority. Mkoa wa kwanza ni Simiyu, Mkoa wa pili ni Dodoma, Mkoa wa tatu ni Singida, Mkoa wa nne Shinyanga na Mkoa wa tano ni Manyara.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Manyara leo kwenye bajeti ukiangalia mkoa mzima sisi ni karibu bilioni
7.9 ambayo ni pesa tuliyotengewa. Ukilinganisha na mikoa ambayo bado ina maji na vyanzo vingi vya maji, sasa Mheshimiwa Waziri nikuombe hili nenda nalo, angalia ni namna gani ya kufanya uweze ku-rescue mkoa mzima wa Manyara kwa sababu ya hali nzima kubwa ya upungufu wa maji tulionao kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nmshuruku Mheshimiwa Waziri kwa kututengea pesa kwa ajili ya Mji wa Kibaya, Mji huu ulikuwa ni kame kwa muda mrefu, lakini tuna visima vingi ambavyo vimechimbwa kwa msaada wa jitihada zetu za pesa na ndani kwa maana ya Halmashauri yetu na Mkurugenzi na Baraza letu la Madiwani tumekaa tukapanga tukachimba visima, sasa tunaomba pesa kwa ajli ya ukamilishaji, tunamalizia ili yale maji na zile tenki tulizojenga pale ulipokagua wewe mwenyewe ulivyofika site tuweze kupata namna pesa zinaweza kutusaidia kuhakikisha kwamba zile tanki zinakamlilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, visima vinafungwa pampu maji yanapandishwa pale ulipoona kwenye tanki ili Mji wote wa Kibaya uweze kusambaa maji kwa ajli ya matumizi ya watu wetu kulingana na jinsi ambavyo unaona yale maeneo yetu watu wanaongezeka, ujenzi unaongezeka, lakini na matumizi ya maji yanatakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunayo shida kubwa muda mrefu sana ambayo imetukabili kwa mazingira yetu ya maji, lakini kumekuwa na miradi mingi ambayo imekuwa inahujumiwa na miradi mingi unakuta tunao mradi wa Matui ambo ulijengwa pale Chapakazi zaidi ya milioni 600 zimetumika lakini wananchi hawapati maji, mradi upo nikuombe Mheshimiwa Waziri utakapopata nafasi baada ya maswali na majibu tuongozane, twende Chapakazi uone mradi uliogharimu shilingi milioni 600, kodi za Watanzania na wananchi hawapati maji ili uweze kujiridhisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakuomba kwamba lile eneo la Matuhi unalifahamu, kuna zaidi ya watu 20,000 tumekubaliana kwamba kisima cha Nchimila kifungwe pump, kifungwe umeme ili kiweze kusambaza maji. Tumeshakuletea ile plan na feasibility design nzima imeshakuja, Wizarani tunaomba approval ile design iweze kwenda na tupate pesa ili kuhakikisha kwamba tunatandika mabomba wale wananchi zaidi ya 20,000, ikiwemo vituo vya afya makanisa, misikiti na maeneo yote ya makazi na vituo vidogo zaidi ya 40 zimeshakuwa designed waweze kupata maji kwa sababu kunaweza kutokea mlipuko wa magonjwa kipindi kijacho kwa sababu ya upungufu wa maji na shida kubwa ya maji ya watu ambayo wanapata.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja, ahsanta sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nishukuru na kupongeza Hotuba ya Waziri kwa maneno mazuri na jinsi ambavyo amejipanga na timu yake kwa ajili ya kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pale Kiteto tuna Kituo cha Polisi ambacho kimechakaa na ni muda mrefu, nataka niombe Waziri mwenye dhamana atakapopata muda basi tutembelee pale, tumpitie RPC wetu, twende pale tufanye kikao tuzungumze, tuone lile jambo tunaliwekaje, yawezekana tukafanya marekebisho ya muda wakati tunafikiria kufanya marekebisho ya muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema jambo moja la magereza. Niombe Kamishna wa Magereza, haya magereza mengi yangefanya shughuli za kilimo yangeweza kusaidia sana. Pale Kitengule Karagwe lile gereza kule Kagera kuna mvua ambazo ni za misimu yote miwili. Ningeomba hili gereza liweze kutumika kwa ajili ya kilimo cha kuzalisha mbegu kwa sababu wana mashamba makubwa na ni mazuri na hakuna contamination ya majirani kwa ajili ya kufanya ile pollution ya mbegu ili iweze kutoka mbegu nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe huyu Kamishna wa Magereza azungumze na watu wa ASA hiki kitengo chetu cha mbegu na mimi nitakwenda kama Mjumbe wa Kamati ya Kilimo kama kushauri kwa gharama zangu na timu ya kule ambayo ni ya kilimo ya magereza ili tuweze kukaa chini tuone tuainishe namna gani, hawa watu wanaweza kuzalisha mbegu kwa ajili ya Serikali na wananchi wetu na kwa ajili ya Serikali ili tuweze kupata mapato. Hata hivyo, gereza litapata faida kubwa sana kwa kuzalisha mbegu badala ya kuzalisha yale mahindi 60,000 au 70,000 ambao kwa sasa yawezekana haiwalipi kama magereza pia hailipi kama Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie juu ya suala la Uhamiaji. Uhamiaji wanafanya kazi nzuri na kubwa sana lakini shida kubwa wanayoipata, mimi naona kwenye bajeti hapa Mheshimiwa Waziri atakapokuja aniambie maana nimekusudia kushika shilingi. Hizi pesa alizowapangia ni pesa ndogo sana, hawa watu hawawezi kufanya kazi kwa kiwango ambacho wanafanya na shughuli nyingi walizonazo ambazo ni ku-contol mipaka yetu yote, kulinda ndani, kukamata wahalifu na wahamiaji haramu wakaweza kufanya hili jambo. Kwa bajeti hii hakuna kitu kitakachoendelea unless in between tuangalie ni namna gani Serikali inaweza kuongezea hawa watu bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naweza kutoa mfano mpakani tunao watu wengi ambao wanaingia, hizi nchi jirani ambazo tumepakana nazo kwa kuwa Tanzania tumepakana na nchi nyingi. Kuna malalamiko mengi ambayo watu wanaingia na kumetokea watu; Mheshimiwa Waziri mwenyewe anakumbuka alienda kuchoma silaha pale Kigoma, watu wameingiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, hawa watu wanapoingiza hizi silaha wanakutana na raia wetu wanakaa nao, wanazungumza, wanakula nao, wanahifadhi hizo silaha, leo uhamiaji wanapokwenda kukamata wananchi na baadhi ya Wabunge wanalalamika kwamba wale watu wamewaonea, its quite impossible, lazima Uhamiaji wachape kazi na waendelee wasirudi nyuma na wasikatishwe tamaa na wasonge mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kushauri juu ya jambo la Uhamiaji. Kuna haja ya Uhamiaji kukaa na Wabunge wa Mikoa ya mipakani, Kagera, Kigoma, Tunduma na kwingineko ili kunapotokea zile complains angalau waweze kukaa wakubaliane baadhi ya mambo ambayo technically lazima yafanyike kwa wananchi ili kudhibiti usalama wa wananchi na raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumetokea malalamiko mara nyingi wanasema mtu amekamatwa, amehojiwa, ameshinda kituoni, amefanya nini. Labda niseme hiyo ndio kazi ya Uhamiaji waliosomea ni kukuita na kukuhoji na kukuruhusu urudi nyumbani au ulale ndani, hiyo ndio kazi waliosomea hakuna nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikueleze ukweli hatuna haja ya kukimbia na kuficha haya. Niliwahi kupigwa ile fomu ya kujaza ya uhamiaji, sasa nilipopewa kwanza nikajifikiria nikasema sasa hapa nafanyaje? Fomu ile kama sio raia wa Tanzania, niseme, huwezi kujaza ile fomu. Kama sio raia wa Tanzania halali ile fomu page ya kwanza tu chali, lazima uombe kwenda kukojoa mara mbili. Sasa ndio maana unaona…

T A A R I F A . . .

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu naomba nisiendelee naye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kusema Idara ya Uhamiaji kazi yake ni kuita mtu, ni Mbunge uitwe, ni kiongozi wa dini uitwe, ni Waziri uitwe, wewe ukifika pale chukua fomu yako jaza ukimaliza tawanyika, unahofu nini? Unahofu nini na kulalamika kwamba kwa nini umehojiwa, unahofu nini? Kama una hofu it means wewe sio kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwapongeze Idara ya Uhamiaji, kwanza hii bajeti ni ndogo, ndio maana nasema nakusudia kushika shilingi, waongezewe pesa ili wakamate wengi, wahoji wengi. Maana kuna intervention ya watu wanaingilia kwenye hii mikondo na kutafuta kutengeneza umamluki na uharamia wa kutafuta hawa watu waendelee kupoteza laini, wanasema watu wanakufa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijawa Mbunge pale Dosidosi, Kiteto pale mpakani na Kongwa, nimefika pale Wahabeshi wamepita pale, mmoja kati yao akawa amezidiwa, ameumwa wherever kwenye gari, gari limeharibikia upande wa pili wakaisogeza, mtu wamemwacha porini amekufa na gari iko sealed. Leo unauliza watu wanakufa, wanaokufa ndio hao wanaotoka nje, sio Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana katikati, hapa Kiteto, Kongwa hii hapa, semitrailer imepaki pembeni, watu wameshushwa, ni Wahabeshi wamejaa gari zima wengine wame-faint, wengine wamekufa, hao hao ndio wanaokufa ambao sasa sisi hatuwezi, nchi au Uhamiaji au Polisi haiwezi kulaumiwa kwamba watu wanakufa, wanaokufa ni watu wa nje ambao still Tanzanian…

K U H U S U U T A R A T I B U . . .

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichotaka kuzungumzia na huyo aliyenipa taarifa, hao wote wanaokufa mimi nilitarajia yeye atusaidie, aende aiambie polisi kwamba jamani kuna mtu amekufa hapa, ni Mtanzania, jamani fatilieni hili, kwa vyovyote vile atakuwa anawajua, huyu aisaidie polisi. Nataka kuishauri idara yetu hii iendelee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kushauri hawa watu wa NIDA wa vitambulisho. Kwenye hii mikoa ya mipakani watu wanazungumza lugha moja wanazungumza wanaelewana huku na huku, niombe kwamba… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji).
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nipongeze Mawaziri ambao wametuletea bajeti yetu hii, Mawaziri wote wawili kwa ushirikiano mkubwa na bajeti nzuri ambayo imeweza kutusaidia kutupa malengo na mwelekeo wa 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze kwa kazi nzuri na bajeti ambayo mmetutengea Kiteto kwa maana ya TARURA kutupa shilingi bilioni 1.6, secondary school shilingi bilioni 1.4, primary school shilingi bilioni 1.2, Kituo cha Afya cha Engusero shilingi milioni 200 na maboma yanaendelea kumaliziwa. Hongereni sana kwa kazi nzuri ambayo mnaendelea kutusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi hiki ambacho tunaelekea mwishoni mwa bajeti ya 2019 naomba tupate pesa za kumalizia jengo letu la Halmashauri ambalo limesimama muda mrefu. Mheshimiwa Waziri Jafo unajua kabisa hili jengo lipo ukingoni tunahitaji mtutengee pesa kwa haraka ili angalau katika hii miezi miwili mitatu tuweze kufanya kazi ambayo tunadhani kwamba ingeweza kutusaidia kumalizia hilo jengo ili tukafanyie uchaguzi mahali ambapo pako safi na salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunayo miradi hii ya kimkakati ambayo tumeomba pesa na miradi mingi ambayo inaendelea, naomba na kushauri Serikali kwamba kwenye miradi hii ya kimkakati Serikali ingeweza kuainisha maeneo ambayo yanaweza kuwa na miradi ambayo ni highly paying ili iweze kui-fund mapema inaweza kusaidia zile Halmashauri kutengeneza ile internal income yake na kusaidia kupunguza utegemezi Serikali Kuu, jambo hili linaweza kusaidia sana Halmashauri. Zile Halmashauri ambazo hazina miradi mikubwa wala vyanzo vya mapato, inaweza kuhamisha ile pesa ambayo ingeweza kuwa inaenda kwenye zile Halmashauri ikapunguza zile pesa zikaenda kwenye zile Halmashauri na kuhakikisha kwamba tunatengeneza uwiano wa mapato kwenye Halmashauri zetu na kuhakikisha kwamba tunasukuma gurudumu la maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utawala bora. Kwenye utawala bora pale Kiteto tuna nyumba yetu ya TAKUKURU imeharibika na imekwisha. Nilitaka kumwomba Waziri, Mheshimiwa Mkuchika ikikupendeza tuondoke hapa wakati wowote baada ya maswali na majibu ukaangalie hilo jengo, ikikupendeza ukitutengea shilingi milioni 15 tukitumia force account lile jengo tutalikarabati na litakuwa salama. Mimi nikuombe kwa hilo ukubaliane na mimi kabla hujaamua lolote twende kule uone halafu turudi tuweze kuamua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lipo jambo la TASAF. Katika kusaidia kaya maskini tuli-form mfumo ambao uliweza kusaidia watu kukatiwa bima ya afya. Watu wamekuwa wanakatwa pesa zao, bima za afya zinachelewa kuja, watu hawapati matibabu, pesa zinakwenda na mwaka unaisha halafu wanaendelea kupoteza hela zao. Naomba Mheshimiwa Waziri ujitahidi ulione hili na ni namna gani tunaweza kufanya kwa ajili ya kupata bima ya afya basi hizo pesa zinapokatwa bima ya afya iwahi na watu waweze kupata matibabu katika mwaka husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kuzungumza juu ya suala la Madiwani. Madiwani wetu sasa hivi ni viungo muhimu sana na wanafanya kazi sana kwenye maeneo yetu. Madiwani hawa sasa hivi ndiyo wanaoweka pressure ya kusimamia kwenye Baraza la Madiwani na WDC zao kwa ajili ya kusukuma shughuli za maendeleo ya ujenzi wa hivi vituo vya afya vinavyojengwa kote nchini. Madiwani hawa ndiyo tunaowabana kwa ajili ya kujenga maboma na kusimamia pesa kwa kutumia force account ili waweze ku-manage zile fedha vizuri. Madiwani hawa ndio wanaosimamia miradi ya maji, ukusanyaji wa kodi, mapato na ushuru wa Halmashauri kwenye vyanzo vyetu ili kuona ni namna gani ya ku-push maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Serikali na Mheshimiwa Jafo mlione. Nilikuwa naangalia tuna Madiwani zaidi ya 3000 nchi nzima, Madiwani hawa tungewapa pikipiki. Mimi Diwani mmoja anatembea kilomita 120 kwenda na kurudi ni 240, huyo Diwani atakwenda wapi na wapi? Haiwezekani! Nina Diwani ambaye lazima akienda kwenye eneo lake la kijiji fulani lazima alale huko na kesho yake arudi, anapita maporini kuna incidence nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Waziri liangalie suala hili tupate pikipiki kwa sababu tume-afford kuwapa wataalam wa elimu kwenye kata zetu, tuone ni namna gani tunaweza ku-support hawa Madiwani wapate vyombo vya usafiri mafuta watajitegemea lakini tuone namna gani wanaweza kuwa motivated na kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye maeneo yetu na maagizo mengi ambayo Wakurugenzi wetu wanawaagiza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la maboma; Kiteto tuna maboma 92 ya primary schools, secondary schools tumeshamaliza kwa kutumia mapato yetu ya ndani. Niombe tusaidiwe pesa haya maboma yaweze kumalizwa kwa wakati kwa sababu watoto wetu kutoka point moja kwenda nyingine anakwenda kilomita 56; hatuwezi kupeleka wale watoto kwenye hayo maeneo kwa kuanza primary school. Tuna watoto ambao hawawezi kusafiri umbali mrefu na kurudi nyumbani kwa jiografia ya Wilaya yetu maeneo ya kifugaji ya Ndido, Makame, Rolela, Sunya na kuna maeneo mengi ambayo ni makubwa na mapana ambayo watoto hawawezi kwenda shule na kurudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanzisha shule sikizi, zinawasaidia wale watoto kujua kusoma na kuandika, vinginevyo tusipofanya hivyo tuta-create mfumo wa kuwa na watu ambao hawajui kusoma na kuandika na mwisho wa siku wataogopa kwenda shuleni kwa kusubiri hizi shule zikafunguliwe. Niombe review progamme yenu ya kuangalia ni namna gani ya kusajili hizi shule, muangalie madarasa yanayofikiwa, mfumo upi utumike ili watoto wetu waweze kuanza shule na zile shule ziweze kufunguliwa, mpunguze aina ya vigezo ambavyo mnaona kwamba vinaweza kusaidia kuhakikisha kwamba hizi shule zinaanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kumalizia kwa kusema yafuatayo. Nimeona wenzetu watani zetu na wengine wanalalamikia Serikali na Rais kwamba hakuna utawala bora. Watu wanasema kwamba hapatatosha, patachimbika, naomba niwaambie Rais Magufuli ukimwambia kwamba kesho hapatachimbika patatokea fujo, anataka hapohapo. Ogopa Rais ambaye hawezi kurudi nyumba ana-change gear angani kukabiliana na mapambano, huyo ndiyo Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukishaona una kiongozi huyo hapo juu, wewe unachofanya always unakuja mezani mna- debate hoja yako, mnatatua mgogoro mnamaliza, ana-solve matatizo yako akimaliza mnapeana mikono kwaheri. Ukitangaza msuli kwa namna Rais wetu Magufuli alivyo na namna anavyotekeleza shughuli, bora akufyatue mambo mengine mtajadili baadaye. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwape mfano maana tunazungumza kwa mifano, Kibiti hapa juzi walisumbua mbele nyuma, amefyatua mapolisi waliokuwa wanalinda na ule upuuzi uliokuwa unafanyika pale. Amegeuza viongozi pale, amehakikisha amepeleka mtu mmoja tu amecheza vizuri sembuse mahali ambapo panawaka taa. Niwaombe tukae mezani, tuijenge Tanzania kwa kushauriana, tu-debate wote, tutafute solution ya issues zinazoikabili nchi kwa pamoja bila kutishiana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe niwaambie Tanzania ina demokrasia ya kutosha, nchi nyingine zinazotuzunguka, wapinzani na wabishi wote wanazungumzia ughaibuni na nje ya nchi. Unatoka hapa unazungumza mtaani na unarudi nyumbani unalala; unatoka hapo unatukana unarudi unalala, huyo Rais leo East and Central Africa, utampata wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, niwaambieni hapa ndiyo tunaagana, tunatafuta nani anaenda kibra kazaneni na sisi tunakazana, kesho kutwa 2020 mechi uwanjani biashara imekwisha, huko ni CCM, huku ni CCM kazi imeisha. CCM hoyee, Mungu awabariki sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru kwa kunipa nafasi. Nawapongeza Mawaziri ambao wametuletea bajeti hii ambayo inakidhi matarajio ya maeneo mengi kwenye nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipongeze Kamati ambayo na yenyewe imesoma taarifa yake na kuainisha baadhi ya mambo ambayo na sisi tuliyajadili na tukaona kwamba yanafaa kuingia kwenye bajeti hii ya 2019/2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa namna ambavyo imejitahidi kulipa wakandarasi. Mpango wa kulipa wakandarasi unaonekana sasa uko kwenye utaratibu ambao unakwenda vizuri, wakandarasi wengi wanalipwa kwenye maeneo mengi, zaidi ya shilingi bilioni 84 zimetamkwa kwamba zinakwenda kulipa wakandarasi ili waweze kurudi site.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe Wizara iweze kukaa na kuandika barua kwa wakandarasi wote nchini ambao wana miradi vijijini wawe wameripoti kwenye maeneo yao ya kazi kwa sababu wengine wamelipwa na hawajaripoti. Matokeo yake ni kwamba watalipwa watapotea na hizo pesa na mwisho wa siku miradi ya maji haitakamilika. Ili tuweze kudhibiti hali hii tunaomba Wizara iwaandikie barua wawe wameripoti kwa wakati na waweze kufanya kazi na sisi tutarudisha mrejesho kwamba hawa watu sasa watakapo- raise certificates nyingine wawe wame-qualify kwenye kupewa pesa zao nyingine ambazo zitakuwa zinabaki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, naomba Serikali itusaidie juu ya jambo kuongeza shilingi 50 kwenye maji. Hii shilingi 50 tunayoiomba tumeona kwamba ni njia pekee ya kutatua migogoro ya maji nchini mwetu kwenye maeneo mengi. Niombe sasa Serikali ilione hili na Bunge zima tukubaliane kwamba hii shilingi 50 ya maji itakapokuwa shilingi 100 inaonekana miradi mingi vijijini itaweza kukamilika kwa wakati. Kuna miradi mingi na visima vya maji vimesimama, tunadhani kwamba hii shilingi 100 inaweza kusaidia ku-push miradi mengi ya maji vijijini ikaweza kukamilika kwa wakati kabla ya 2021.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hii iende sambamba na vichoteo vya mifugo. Unapotengeneza mradi wa maji unaweza kuweka na kichoteo cha mifugo kwa hiyo maji hayohayo binadamu watatumia upande mmoja na upande mwingine mifugo inapata maji. Kwa hiyo, kwenye vijiji vyetu pale ambapo wakulima na wafugaji wetu wapo wote wata- enjoy mradi uleule ambao uwezo wa pampu ni huohuo, matenki ni yaleyale, ni kiasi cha kuweka tu mbauti kwa ajili ya mifugo na yenyewe ikapata maji ili kupunguza adha ya wanayoipata wafugaji na kusumbuana kwa kwenda kwenye maeneo mengine au kufanya double projects kwenye maeneo wakati sisi tunahitaji pesa ziweze kusaidia maeneo mengi wakati hatuna pesa za kutosha. Kwa hiyo, nadhani hiyo programu inapokuwepo basi kwenye miradi ya maendeleo mikubwa kuwepo na programu ya kutengeneza mbauti kwa ajili ya mifugo halafu miradi yote iende sambamba, binadamu atumie maji lakini na mifugo yetu iweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipongeze kwa Bwawa la Dongo. Muda mrefu tumeahidiwa Bwawa la Dongo kwamba linakwenda kujengwa, mwaka jana kwenye bajeti lilikuwepo na mwaka huu lime-appear tena. Naomba nisaidieni hili bwawa lijengwe, programu ianze, wekeni fund kwa sababu tuna shida kubwa sana katika Vijiji vya Rogoiti, Laiseri, Dongo na vijiji vingi ambapo kanda ile yote ni kame lakini vijiji hivyohivyo vinakwenda mpaka upande wa Dodoma kwa maana ya upande wa Kongwa; vijiji hivyo vinakwenda mpaka upande wa Gairo, Morogoro. Bwawa hilo ni potential kwenye kanda hiyo wa sababu litasaidia maeneo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye bajeti yenu mnaainisha vijiji 19 lakini ni zaidi ya tarafa nne zitakazohudumiwa na bwawa hilo. Zaidi ya vijiji hamsini vitapata maji kutokana na bwawa hilo kwa sababu unaweza kuendelea kufanya extentions kwa kuunga mabomba kwa sababu litakuwa ni bwawa kubwa sana na litatosheleza maeneo hayo. Tunataka tuombe sasa Serikali ichukue initiative ianze kujenga hili bwawa angalau basi miaka miwili, mitatu inayokuja basi bwawa liwe limekamilika ili Gairo, Kiteto na Kongwa wapate maji tuweze kupunguza adha ya maji kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wetu wa Kibaya muda mrefu ni wa ukame lakini maji tunayo chini. Tunaomba Serikali itusaidie jambo moja, tunaomba DDC waje watumie maji kwa sababu tunayo, watuchimbie na yaungwe kwenye tanks ambazo sasa hivi zinajengwa ili tuweze kutosheleza ule Mji wa Kibaya kwa maji tuwe tumepunguza adha ya maji kwenye maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunayo maeneo kame kwa mfano Kata za Makame, Ndido, Rorela, ni maeneo ya wafugaji lakini maeneo yale hayana shida kubwa sana ya maji kwa maana ya maji chini ya ardhi, maji chini ya ardhi yapo, tunachotafuta sisi ni wataalam wa kuweza kuja kuchimba yale maji kwa wakati, mita ni zaidi ya 100, 150 unapata maji. Kwa hiyo, tulitaka surveyors na team work ya Wizara ije kufanya ile survey, ijiridhishe halafu inaweza kutuchimbia kwa awamu angalau na sisi wananchi wetu waweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna tatizo lingine moja la miradi ya maji ambayo haikamiliki na mmeona Rais kila wakati anapotembea analalamikiwa maji, tumekuwa na wakandarasi ambao hawamalizi kazi kwa wakati. Naomba kuishauri Serikali, kama kweli Wizara ya Maji mko serious kumaliza huu mgogoro, tuumalize hivi, wakandarasi wote kwenye kila wilaya ambayo Rais anakanyaga wawe pale waeleze miradi ya maji wamefanya lini, wamemaliza lini, miradi inatoa maji au haitoi, waachane na Rais palepale. Waende kwenye site Rais anapofanya ziara akiuliza miradi ya maji wao wasimame washike microphone waeleze, maji yapo, hayapo aachane nao hukohuko magereza ili tupunguze utapeli wa wakandarasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa wakandarasi wengi inaonekana kwamba ni kifo cha pesa kwa sababu unapotandaza bomba chini kwenye ardhi anakuja anakwambia mimi bomba niliweka, haya, uthibitisho mtachimbua mita 300, 400, mtachimbua kilometa? Sasa kuna uongo na udanganyifu mwingi, anaweza kuwadanganya kwamba aliweka bomba kumbe hakuweka. Sasa mimi naomba ili tumalize ubadhirifu wa pesa za Serikali kwenye miradi ya maji, kila Rais anapokanyaga waende, waseme maji yapo au hayapo waachanie magereza Rais aendelee na safari zake uone kama miradi ya maji kwa wananchi haitapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ndiyo ushauri wangu kwa Serikali, sasa hivi tuamue. Miradi inayoendelea kwenye Wilaya yangu mkandarasi kama hajatoa maji hajapokelewa mimi na yeye tutamalizana mtasikia. Ninyi mmewalea sana na mmesababisha uharibifu mwingi wa maisha ya binadamu na upotevu wa pesa nyingi za Serikali kwenye miradi mingi ambayo inaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mradi wa Matui, Naibu Waziri tulikubaliana kwamba uje Kiteto ukaishia Simanjiro. Njoo Matui uangalie mradi wa shilingi milioni 600 zimeteketea, hakuna maji, watu wanakimbizana, kichoteo ni kimoja, maji hayapatikani. Sasa uje tuamulie pale Matui, tusiache kuzungumza suala hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi sitaki miradi viporo Kiteto, sitaki migogoro, miradi ambayo imeanzishwa kwa sasa hivi ninaisimamia na inatoa maji, ile ya nyuma njoo tumalizane kulekule ueleze wananchi imepotelea wapi, imefia wapi, umeamua nini. Njoo wewe na wakandarasi nikukabidhi wananchi uwahutubie uwaambie kwamba wanapata lini maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba aniahidi ni lini tunakwenda Kiteto, mambo mengine yamekwisha. Naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Waziri na Naibu Waziri pamoja na timu nzima kwa kazi nzuri ya bajeti waliyotuletea.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeahidiwa gari la wagonjwa Kituo cha Afya Engusero. Tunaomba yatakapopatikana basi tupatiwe gari.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa watumishi. Tuna watumishi 296 na upungufu ni watumishi 210, tunaomba tupatiwe watumishi hao kwa ajili ya zahanati, vituo vya afya na hospitali ya wilaya. Vilevile, tunaomba Waziri kutembelea Wilaya ya Kiteto kuzungumza na watumishi na kuangalia uchakavu wa Hospitali ya Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho naunga mkono hoja, Mungu awabariki.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja ya bajeti ya Wizara hii ya Ujenzi na Mawasiliano. Nampongeza Mheshimiwa Waziri na Timu yake kwa hotuba na ripoti nzuri.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kongwa (Hogoro) – Kibaya – Orkesimet – Oljoro – Arusha, ina mpango gani? Tunaomba tujengewe kwa awamu, Kongwa – Kibaya. Sababu ya barabara hii ni kusafirisha mazao toka Chemba, Kiteto, Kilindi na Handeni kwenda Dodoma na Dar es Salaam. Kwa kurahisisha barabara ya Babati – Kibaya – Dar es Salaam, Kondoa – Kibaya – Dar es Salaam, Kilindi – Kibaya – Dar es Salaam, Kilindi – Kibaya – Dodoma, Chemba – Kibaya – Dodoma.

Mheshimiwa Spika, mizigo mingi toka Dar es Salaam kwenda Babati, Simanjiro, Chemba, Kiteto, Kilindi, Kondoa yote inapita hapa. Tusaidieni kwa sababu hii ni too economical.

Mheshimiwa Spika, pia tunaomba kujua barabara ya Handeni – Kiberashi – Kibaya – Chemba – Kondoa – Singida itajengwa lini kwa kiwango cha lami? Umuhimu wa barabara hii ni bomba la mafuta, bandari ya Tanga kwenda Kanda ya Ziwa, kuunganisha Mikoa ya Tanga, Manyara Dodoma na Singida.

Mheshimiwa Spika, naomba Mawasiliano, tupatiwe minara katika Kijiji cha Raiseli, Songambele, Kijunge, Rengatei, Sunya, Dongo, Mangungu na Namelok. Shahidi ni Mheshimiwa Dkt. Kalemani.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza naunga mkono hoja ili nisije nikasahau mwisho.

Mheshimiwa Spika, nipongeze Wizara na Waziri kwa bajeti nzuri ambayo wametuletea, lakini pia nipongeze na Kamati yangu kwa kazi kubwa ambayo tumeifanya inayoongozwa na Mwenyekiti wetu Mheshimiwa Mgimwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo jambo moja ambalo naomba niseme, naipongeza Wizara kwa kazi moja ambayo wameifanya ya kupunguza migogoro ya wafugaji kwenye maeneo ya malisho, wamechukua maeneo makubwa kwenye ranchi za Taifa, wamekodishwa wafugaji, ng’ombe wamehamia mle kwa hiyo kero imepungua kwenye maeneo mengi; Kagera, Ruvu, Kalambo na mikoa mingine ambayo ina ranchi za Taifa ambazo wale wafugaji walikuwa wanazunguka na kuhangaika kwa ajili ya kutafuta malisho. Nawapongeza na nampongeza Mkurugenzi wa NARCO kwa ajili ya kuhakikisha kwamba hili jambo linafanyika na mifugo inapata maeneo ya malisho.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili; niombe kuzungumzia suala la uvuvi haramu na stori nyingi ambazo zimeendelea kwa nchi nzima juu ya uvuvi haramu. Nikushukuru kwa sababu tulikwenda Mwanza kama Kamati, tukakutana na wadau wote; tulikutana na wadau wa viwanda, tukakutana na wavuvi wenyewe na wale madalali ambao wanauza samaki kwenye viwanda.

Mheshimiwa Spika, tulipokuwa kule Mwanza kila mtu tumempa dozi yake; Waziri amepata dozi juu ya watendaji wake ambao hawatimizi wajibu wao sawasawa, lakini na wale madalali tumewapa dozi yao kwa sababu wanafanya udalali kwa kupunguza bei ya wanaokwenda kununua samaki kwa wavuvi na ku-collude pamoja na wenye viwanda. Suala hili ni suala pana, lakini tunaamini sasa tunapokwenda kwa dozi tuliyoacha kule ndiyo maana unaona kidogo sasa hivi hakuna malalamiko kumetulia, isipokuwa yale madogo madogo tunaendelea kuyakamilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati imefanya kazi kubwa, haya mambo mengi yatakwenda yanapungua pole pole na tutafika mahali ambapo tunaitendea Wizara hii haki. Tunalo tatizo kubwa, wavuvi hawasemi ukweli kwenye baadhi ya maeneo mengi na ndiyo maana kuna eneo la uharamu ambao unafanyika. Leo, tunapozungumza Wilaya ya Muleba kwa Mheshimiwa Mwijage pale, uvuvi kwenye vile Visiwa vyote vya Bumbire na wapi kote, leo wana-enjoy samaki wapo, wakienda ziwani wanarudi na samaki wa kutosha ambao wao wanaendelea ku-enjoy.

Mheshimiwa Spika, pia Halmashauri yetu ile ya Muleba nampongeza yule Mkurugenzi alikuwa anakusanya milioni nne kwa mwezi, leo anakusanya milioni 50. Kwa hiyo, Halmashauri inaendelea ku-grow, hiyo ni TAMISEMI ina-earn kutokana na effort za Wizara ya Mifugo. Haya yote twende tunayaona, ukizungumza na wale wavuvi wadogo wadogo wana-enjoy samaki wapo, wamekuwa wanavua kwa muda mfupi na wanapata samaki kuliko kushinda ziwani siku mbili, tatu.

Mheshimiwa Spika, wenye viwanda; wenye viwanda wanakwenda wana-determine price bila kushirikisha Serikali, wanashusha bei, wanadili na madalali wetu, wahuni, matapeli ambao siyo waajiriwa wa Wizara wala siyo watendaji wa Halmashauri. Wanashusha bei ya wavuvi, samaki wao wanawaingiza viwandani, wakishamaliza wale samaki wanawachakata, wakimaliza wanamwambia samaki wako bwana, hawa samaki hawako kwenye size na zile milimita zilizopangwa kwa hiyo ondoka na samaki wako, wameshawachakata mvuvi anapata hasara. Naomba hili suala sasa Wizara iliangalie kwa ukaribu sana na iweze kuona hayo.

Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa inabeba lawama nyingi hizi za uvuvi, lakini on the way mvuvi analeta samaki kwenye kiwanda, anakamatwa na watu wengine na watu wa ushuru ambao ni wa TAMISEMI, Polisi na watu wengine ambao ni Wizara tofauti kabisa na Wizara husika, wanapopigwa faini na kudaiwa ushuru huu mzigo unaenda unatupwa kwenye Wizara husika. Ushauri wangu juu ya hili, tunaomba hizi Wizara ziweze ku-interrupt zione solution ya pamoja juu ya kutatua huu mgogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo jambo la mwisho kwenye uvuvi, tulitengeneza kanuni na sheria hapa juu ya uvuvi, tunaomba hizi sheria na kanuni kandamizi Mheshimiwa Waziri azilete hapa tuzifumue, tupange upya suala la utaratibu wa wavuvi uweze kukaa salama na nchi iweze kubaki salama tupunguze suala la lawama. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lipo suala la viwanda juu ya uzalishaji wa maziwa ya UHT, long life milk. Wameongeza kodi ya maziwa kwa ajili ya ku-reduce importation ya maziwa, lakini wakati huo tumepunguza hiyo, ilikuwa ni ku-promote viwanda vyetu vya ndani, kwa hiyo, viwanda vyetu vinavyozalisha kama Tanga Fresh na Asas wameshafunga mitambo ya UHT, sasa hivi wanajaribu ku-push kuona namna gani wanaweza kupanda wakitegemea wale wazalishaji wa maziwa wadogo, tukitegemea growth yao, Benki ya Kilimo na benki zote (commercial banks) zi-support hawa wakulima waweze ku-grow.

Mheshimiwa Spika, leo Waziri amekuja na suala la kupunguza tozo ya maziwa yanayokuwa imported ya unga, ukipunguza kilo moja ya maziwa ya unga yana-produce lita nane. Ukimpunguzia Azam leo, ukapunguza kwa level hii ya eighty something percent it means unakwenda kusababisha hivi viwanda vya Asas na Tanga Fresh vife asubuhi kwenye hii UHT. Wamekopa kwenye mabenki ya ndani, wana-promote wazalishaji wa maziwa wadogo which means unga unaendelea kuongezeka, maziwa ya unga yanaongezeka, una-import hiyo una impose unapunguza kodi, unasababisha watu wetu kufilisika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nikueleze kwa hili na itatokea na utaiona, kwa hili Mheshimiwa Mpina akae chini atafute cash flow na projections za namna ya importation ya maziwa ku-protect viwanda vyetu vya ndani vya UHT kama programu ilivyokuwa. Hiyo ndiyo inayokwamisha Sekta ya Maziwa nchini kwa sababu investment ya maziwa, mradi kwenye plant ya UHT ni zaidi ya dola milioni nne au tano, sasa anapo-invest amekopa hapa, uka-import hayo ni kwamba hawezi kushindana kwenye soko, mwisho wa siku kinachotokea ni nini? Anaweza kuuza lita ya maziwa Sh.2,600, huyu mwingine ni lazima akiweka zile cost zote vyovyote vile inatozwa 18% lazima atatokea kwenye Sh.3,000. Mwisho wa siku, hakuna uwiano kwenye hili. Niombe Mheshimiwa Waziri aliangalie kwa haraka sana hili ili kuokoa na ku-allow ushindani wa ndani, tuwe kwenye balancing point, asiwepo bora na mwingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende kwenye suala lingine; kwangu kumeanzisha Hifadhi ya Olengapa, nyanda za malisho, lakini kumekuwa na migogoro mingi, watu wanalalamika. Nimefanya ziara, kipofu mmoja akanyoosha mkono anasema mimi shamba langu limekwenda, nilikuwa nalima, ni kipofu, sasa naenda kufa. Alipozungumza kwenye mkutano wenzake wakamwambia ale udongo. Mheshimiwa Waziri aje, tukae tuone hao watu wanaolalamika kwa nini Olengapi wamechukua eneo wasingeacha wale wakulima 300 na eneo lao, ime-incorporate lile eneo ikalichukua ikaacha hawa watu ikiwemo hao vipofu wanaolalamika kwamba wameambiwa na wenzao wakale udongo. Niombe kwamba sasa hilo suala Waziri atakapokuja, basi atusaidie ni namna gani ya kutatua hilo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Emmanuel Papian.

MHE. EMMANUEL P. JOHN: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)