Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Ummy Ally Mwalimu (1 total)

MHE. UMMY A. MWALIMU aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwaunganishia umeme wa gharama nafuu wananchi wa maeneo ya pembezoni yenye sifa za Vijiji, Tanga?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kurahisisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa bei nafuu kwa maeneo ya pembezoni mwa Jimbo la Tanga Mjini, Serikali kupitia REA, inaendelea kutekeleza Mradi wa Peri-Urban III ambapo Mkandarasi aitwaye OK Electrical anaendelea na zoezi la kuunga wateja kwa baadhi ya mitaa kwa gharama ya shilingi 27,000 ambapo mpaka sasa jumla ya wateja 1,302 wameshaunganishiwa huduma ya umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, maeneo yaliyosalia yapo kwenye mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 vya kila Mbunge, ambapo Jimbo la Tanga Mjini litapelekewa umeme kwenye mitaa 15. Serikali inaendelea kuwahimiza wananchi kuunganisha umeme wakati ambapo ujenzi wa miradi unaendelea. Ahsante.