Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Anatropia Lwehikila Theonest (59 total)

Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa fursa hii. Na mimi kwa vile nachangia kwa mara ya kwanza, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata hii fursa, nakishukuru chama changu cha CHADEMA kwa kuniamini na kunipa fursa na nawashukuru wananchi wa Jimbo la Segerea walionipigia kura zaidi ya 49,000. Kwa bahati mbaya sana, nikiwa nimejitoa katika Tume ya Uchaguzi na nimetimiza masharti yote lakini kwa yale yale tunayoyasema kukosa utawala bora, within a deadline, jina langu likarudi nikapigiwa kura zote. Nawashukuru kwa kutupa Madiwani 13 wa UKAWA na tukiwa tumeshinda kwa kura nyingi sana kwa wagombea wote wawili na nawaahidi nitawatumikia, gamba kwetu halina nafasi. (Makofi)
Ndugu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwenyekiti, kumradhi, mimi ni Mbunge mgeni kwa hiyo nitahitaji sana kujifunza. Nimepitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 63(2) kinataja wajibu wa Mbunge kwamba ni kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla sijaja mahali hapa nilishangaa sana. Je, Wabunge wa CCM kweli huwa wanasoma Katiba? Nini wajibu wetu kama Wabunge? Sisi ni mhimili, kama ulivyo mhimili wa Serikali, kazi yetu ni kuishauri Serikali, kuwaambia tunataka wafanye moja, mbili…
MWENYEKITI: Mimi nawasihi sana Waheshimiwa Wabunge, maana ukisema kwamba huna uhakika na Wabunge wa CCM kama wanasoma Katiba na wewe ni mgeni, sasa umepata uzoefu wapi? (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nimepata uzoefu kwa kuangalia kwenye television kwamba hatutimizi kazi yetu ya msingi ambayo ni kuishauri Serikali. Mimi ndiyo nachoenda kufanya, kuishauri Serikali. Sipo hapa kwa kazi ya kuisifia Serikali, sipo kwa kazi ya kumsifia Magufuli kwa sababu aliomba kura mpaka kwa kupiga push-up, kwa sababu alijua jukumu analoenda kufanya. (Makofi)
Tumekuwa na changamoto ya ardhi. Nimepitia Mpango na mnaonyesha takwimu zenu kwamba kwa nchi ya Tanzania, mmeweza kupima 10% tu ya ardhi ya Tanzania. Natokea katika Jiji la Dar es Salaam ambalo limekuwa na migogoro mikubwa ya ardhi. Wananchi zaidi ya kaya 16,000 zimewekewa alama ya “X” kwamba wanaishi kwenye mabonde, wanaenda kubomolewa majumba yao. Zaidi ya watu 99,000 watakuwa ni watu wasio na makazi. Changamoto ni kwamba Serikali ilikuwepo, watendaji walikuwepo, Waziri Lukuvi ambaye ni Waziri sasa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alifanya nini wakati wote ambapo wananchi wameishi katika maeneo hayo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka mwaka 1998 yalitengwa maeneo ya Tegeta ili wananchi waliokuwa wanaishi mabondeni wahamie hali kadhalika mwaka 2011 akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wananchi wa Jimbo la Segerea, wananchi wa Ilala, wanataka viwanja vyao kwa sababu wanasema anahusika katika uporaji wa maeneo waliyopewa wananchi waliokuwa wanaishi mabondeni. Kama hiyo haitoshi, tuna changamoto ya migogoro ya ardhi kwa sababu Wizara ya Ardhi haijafanya kazi. Kuna migogoro ya wakulima na wafugaji kwa sababu asilimia kubwa ya maeneo hayajapimwa. Alivyochaguliwa au alivyoteuliwa juzi, pale katika Wizara ya Ardhi kulikuwa na National Council of Professional Surveyors, ni Bodi ya ma-surveyor, ameenda pale akaivunja. Pengine alifanya kitu cha msingi lakini tokea ameingia katika huo wadhifa amefanya nini baada ya kuvunja hiyo Bodi ambayo ilikuwa inashiriki katika kukagua na kudhibiti wanavyofanya kazi ma-surveyors? Tunaendelea kutengeneza migogoro juu ya migogoro. Tunafanya kazi kwa kutafuta sifa. Tumekuwa watu wa hapa kazi tu na tunafanyia kazi kwenye TV. Mawaziri wanashindana nani leo ataonekana kwenye media, hapa tuwashauri mfanye nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine ni ma-celebrity wazuri tu. Katika kitabu cha Ideal State, Plato aliainisha makundi ya aina tatu. Kuna iron, silver na golden. Kuna wengine walipaswa kuwa ma-celebrity leo ndiyo tumewapa Uwaziri na tunawapa dhamana kubwa ya kuongoza Serikali. Tunakosa cha kuwashauri kwa sababu kila mwaka mnakuja na mipango mizuri ambayo haitekelezeki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye suala la miundombinu hususan Jiji la Dar es Salaam. Mmejipanga kwamba mnataka viwanda lakini viwanda tunaviwekaje katika maeneo ambayo hayana barabara? Unasafirishaje hayo material pamoja na vilivyozalishwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine? Ni changamoto ambazo ni za msingi. Segerea hatuna barabara kwani zote ni mbovu na hatuna barabara za mitaa zote ni mbovu. Serikali ipo miaka 54 ya Uhuru na mnataka tuwashauri, tuwashauri nini wakati mmekuwa mnasema kila siku mnashindwa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la lingine ambalo nitalizungumzia ni gap baina ya walikuwa nacho na wasiokuwa nacho. Inaonyesha, tangu mwaka 1992 tulikuwa na umaskini kwa asilimia 39 lakini mpaka mwaka 2007 mmeweza kupunguza kwa asilimia nne tu. Miaka 15 mmepunguza umaskini kwa asilimia nne tu na leo mnasema tuwashauri, tuwashauri nini? Tunachoweza kuwashauri, tokeni, mmeshindwa, tunaomba tuweze kuongoza nchi kwa sababu tunastahili. (Makofi/Kicheko)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nazaliwa Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Kyerwa, nitawasemea. Nimeenda katika Mkoa wa Kagera, Wilaya ya Kyerwa, nilichokikuta, Waziri wa Mambo ya Ndani aende kuona, kuna watu wamejitangazia nchi ndani ya nchi. Kuna watu wanajulikana kama Runyogote, Daniel na mwingine alikuwa Mbunge katika Bunge hili la Jamhuri, wametangaza nchi yao ndani ya nchi. Wana uwezo wa kuamrisha, wakaamrisha Askari wakaenda kukamata watu, wakakata migomba na wakapiga wananchi. Wanaweza kutangaza tunafunga barabara na wakafunga barabara.
MWENYEKITI: Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nichukue fursa hii kuwapongeza akinamama wote waliokuwa wanaadhimisha siku yao jana na kipekee kabisa wanawake wa UKAWA kwa namna tulivyoshikamana dhidi ya dhuluma na dharau yoyote inayoweza kujitokeza kwa mwanamke. Pia, nitoe masikitiko kwa Naibu Spika ambaye ni mwanamke alionekana kindakindaki kutopenda kukemea kilichokuwa kinatokea na hata tulipoomba nafasi ya kuonesha hisia zetu, alionekana kuiminya, nitoe masikitiko sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, na-declare interest, mimi ni Mjumbe katika Kamati ya Viwanda na Biashara, kwa hiyo, nimeshiriki sana katika kipindi hiki cha Ubunge wangu katika Kamati husika. Nimeona kwa vitendo ni namna gani tunamaanisha tukisema tunataka kujenga uchumi wa viwanda na ni namna gani tunawahadaa Watanzania tukitaka kuwaeleza ukweli juu ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe masikitiko yangu kwa sababu watu wengi wamepongeza hotuba, ukiiangalia hotuba kwa maneno tu siyo mbaya, lakini ukienda kwenye money value ya kile wanachokisema kwamba wanaenda kukitekeleza, ni vitu viwili tofauti. Pia, kwenye Kamati nilimwambia Waziri nikasema ni bora tuseme ukweli kuliko kuwahadaa Watanzania kwamba tunaenda kwenye uchumi wa viwanda, ila tuseme siku moja tunaweza kwenda kwenye uchumi wa viwanda. Kwa bajeti ya mwaka huu ambayo ni shilingi bilioni 81 ukiisoma na uki-analyse kipengele kwa kipengele hatuwezi kwenda kwenye uchumi wa viwanda ila tunaweza kuanza kwenda kwenye uchumi wa viwanda pengine miaka 20 au 30 ijayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, je, tofauti yake na bajeti iliyopita ni ipi? Tofauti ya bajeti iliyopita ilikuwa ni shilingi bilioni 87. Kwa masikitiko kabisa bajeti ya maendeleo ilikuwa shilingi bilioni 35, lakini mpaka Machi ilikuwa imetoka shilingi bilioni moja tu ikienda kwenye viwanda. Hao hao ambao tukonao leo wanaosema kazi tu ndiyo walikuwa kwenye madaraka, je, nini kilitokea? Kama bajeti imepangwa kwa 100% ambayo ni shilingi bilioni 35 ya kuendesha viwanda, lakini inapatikana 5% tu ambayo ni shilingi bilioni moja ya kuendesha viwanda, je, tunaweza kwenda tunakotarajia kwenda?
Mheshimiwa Naibu Spika, kama hiyo haitoshi nimesoma Dira na Dhima ya Wizara ya Viwanda, inaongea wazi kwamba inataka kutengeneza mazingira wezeshi ya ukuaji wa biashara. Ikaja kwenye Dhima inasema kutengeneza msingi shindani wa viwanda wenye kuwezesha biashara ulimwenguni na maeneo mengine. Unaona kwamba plainly Wizara imejikita katika kuandaa mazingira. Sasa kama tunaandaa mazingira, tunaandaa mazingira namna gani? Ni kwa kutengeneza sera ambazo ni rafiki kwa wawekezaji, ni kwa kutengeneza sera ambazo zitawezesha ushindani, ni kwa kutengeneza sera ambazo zitaweza kuwa-accommodate wawekezaji kuja kuwekeza katika nchi yetu. Kwa hiyo, sasa ambacho tungekuwanacho hapa ni kujadili sera ambazo zitasaidia kuleta viwanda. Hicho ndicho nilichokiona kwenye bajeti ya Viwanda na Biashara.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama haitoshi sehemu kubwa ya ziara tuliyoifanya kilio kikubwa cha maeneo tuliyoenda ni maeneo ya uwekezaji hususan kupata maeneo ambayo tunaweza tukafanya uwekezaji kwa ajili ya maandalizi sasa ya viwanda. Tulienda EPZA wakatuambia kwamba katika bajeti ya mwaka jana walipaswa kulipa fidia ya shilingi bilioni 60 kwa ajili ya kupata maeneo ya uwekezaji lakini ni shilingi bilioni moja ilitoka na kwa inflation rate tunapaswa kulipa shilingi bilioni 190.9 almost shilingi bilioni 191. Ile iliyokuwa shilingi bilioni 60 mwaka jana inflation rate imeenda mpaka leo tunahitaji kulipa shilingi bilioni 191! Hiyo fidia tu inazidi bajeti ya Wizara ambayo ni shilingi bilioni 81! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaweza kuwahadaa watu tunavyoweza, lakini uhalisia utabaki, tutarudi hapa mwaka kesho tutaanza kuogopa kuangaliana usoni kwa sababu hatuwaambii watu ukweli, ni usanii unaoendelea. Pesa iliyotengwa haiwezi kukidhi haja ya tunachotaka kufanya. Kwa hiyo, nasema ni bora tuseme uhalisia kwamba tuna plan, tunafikiria kutengeneza nchi ya viwanda, lakini bado hatujafika huko kwa sababu ya bajeti tuliyokuwanayo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia nimeangalia ile miradi ambayo itakuwa vichocheo ambapo moja kati ya miradi hiyo ni kilimo. Ukiangalia kilimo na bajeti ya kilimo husika huwezi kuona coloration between kuwa na viwanda na kuwa na bidhaa zitakazosaidia viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilienda mbali zaidi kuangalia kweli nchi yetu iko serious inathamini kilimo? Nikaangalia ajira tu zilizoelekezwa katika sekta ya kilimo ilikuwa ni aibu kwa sababu Waziri, Mheshimiwa Angellah Kairuki alisema kwa mwaka jana kulikuwa na ajira takribani 3,000 ambapo kwenye kilimo ilikuwa ni robo ya ajira hizo 3,000 zilizokuwepo kwa mwaka jana. Kwa hiyo, unaweza ukaona ni kwa namna gani hatujajipanga wala kuwekeza kwenye kilimo ambapo tunataraji kilimo kiwe ni kichocheo kwenye viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kama hiyo haitoshi ukiangalia 80% ya wananchi wetu kwa maana ya Watanzania ni wakulima ambao wanaishi katika absolutely poverty, katika umaskini wa kiwango cha juu. Wakaenda mbali zaidi wanaonesha kwa miaka 15 iliyopita uchumi wa mkulima ambao ni 80% umaskini umepungua kwa 3.4% ambayo ni kidogo sana. Hawa wakulima maskini ndiyo tunawatarajia wawe catalyst katika kuendesha viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Kamati niliuliza, je, tumejiuliza ni kwa nini viwanda vili-fail? Ni kwa nini viwanda vilikufa? Takwimu ziko wazi! Viko viwanda 34 ambavyo vimekufa na vimegeuzwa kuwa maghala. Nilitaraji Waziri aje atuambie ni kwa nini vile vilikufa na tumeandaa mkakati gani kwa ajili ya kufufua tena hivyo viwanda? Mheshimiwa Waziri ameandika kwenye kitabu chake kwamba sababu kubwa ni kwamba watu walikopa pesa wakikopea hivyo viwanda na bahati mbaya vikageuzwa maghala lakini hiyo Serikali ya Hapa Kazi Tu ilikuwepo na hatujaona mkakati mahsusi wa kuzuia kurudi nyuma tulikotoka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitaongelea kidogo hujuma za dhahiri tunazofanya au Serikali inazofanya dhidi ya hata vile viwanda vidogo ambavyo vinajitahidi kuchechemea. Kama Kamati tulitembelea kiwanda cha TANALEC, wale ni wazalishaji wakubwa wa transformer. Hiyo kampuni ya TANALEC Serikali ina hisa ya 30%. Cha kushangaza Serikali imewahi kutoa tenda ndogo sana ya kuzalisha transformer 3,000 ambayo wanadai kwamba ni 10% ya transformer zinazohitajika nchini na tenda zilizokuwa zinabaki wamepewa nchi za nje, India, China na wengine. Hivyo kile kiwanda wanalalamika kwamba kukosa tenda za Serikali wamelazimika kupunguza ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wafanyakazi takribani 55 walilazimika kuacha kazi kwa sababu walishindwa kuwalipa kwa lengo la ku-stabilise, lakini kama haitoshi wameendelea kushindwa kujiendesha. Swali ni je, Serikali inajihujumu yenyewe? Kama sisi Serikali tuna hisa kwenye kiwanda kile kwa nini tunazidi kujihujumu? Moja kati ya hasara tunayopata tunashindwa kupata Pay As You Earn kwa sababu watu wametoka kazini. Tungewaajiri watu kwa sababu kile ni kiwanda chetu tungepata Pay As You Earn lakini pia tungeweza kusaidia familia mbalimbali za watu wale ambao wameajiriwa katika eneo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kikubwa ambacho tulikiona ni mlundikano wa titiri za regulatory authorities. Ningependa Waziri atuambie nini tofauti ya TFDA na TBS? Wanafanya almost the same function! Kinachoonekana pale ni kuongeza mlolongo ili wale wafanyabiashara wakate tamaa. Nataka kujua pia tofauti ya OSHA na Fire! Kwa sababu OSHA wakifika kwenye kiwanda wanaangalia zile fire extinguisher, wale Fire wenyewe wakija wanaangalia fire extinguisher! Kwa hiyo, naishauri Serikali iangalie ni namna gani inaweza ikapunguza mlolongo wa zile regulatory authorities kwa lengo la kuongeza ufanisi kwa wafanyabiashara au wale wenye viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho nimekiona ni changamoto, wale wafanyabiashara wanasema wanavyofika bandarini Serikali au mamlaka imekuwa ikipandisha bei kutegemea wao wanavyojisikia. Wanadhani kama mtu amechukua container la bidhaa fulani kutoka nchi jirani amekuja amepata punguzo kutokana na competition alivyoweza kupata, akifika bandarini wanamwambia kwa uzoefu wetu huwa inauzwa hivi. Kwa hiyo, imekuwa ni changamoto ya kuwapandishia bei wafanyabiashara kutegemeana na mahitaji ya yule anayefanya tathmini. Kama haitoshi vigezo haviko dhahiri ni kwa namna gani hiyo pesa imekuwa inaongezwa katika hizo bidhaa zao ambayo imeendelea kuwa changamoto.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, Dar es Salaam inaweza kuwa kivutio kwa watalii. Tuna eneo la Dar es Salaam Zoo ambalo ni eneo la mtu binafsi, Serikali inaweza pia kuanzisha eneo kama hilo kwa ajili ya kipato hasa maeneo ya Kigamboni, utalii huu utakwenda sambamba na Daraja la Kigamboni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utalii wa majengo ya kale, Bagamoyo, historia ya Bagamoyo ikiwa promoted vizuri itaongeza tija katika cultural tourism; Kaole ilikuwa kivutio sana, kadri tulivyoshindwa kutangaza ndivyo utalii huu umefifia.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nichukue fursa hii kupongeza uamuzi uliouchukua, kiukweli tunaona mambo mengi yanaenda ndivyo sivyo napongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye hotuba yetu ya Kamati, kwanza, na-declare interest ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira, kwa hiyo mambo nitakayoyaongea hapa nayajua hasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taarifa ya Wizara mpaka tunavyoongea tarehe 31 Januari, 2017 tukiwa kwenye robo ya tatu, Wizara imepokea fedha ya maendeleo kutoka kwenye bajeti ya bilioni 42, imepokea bilioni 7.6 sawa na asilimia 18.6. Naongea hayo tukiwa tumebakiza theluthi moja tu ya kumaliza mwaka, Wizara imepokea pesa ya maendeleo shilingi bilioni 7.6 nimesema hapa nimemwambia Waziri wa Viwanda mimi leo nitakutetea, una haki ya kuwa unapiga propaganda kwa sababu kiukweli hakuna chochote unachoweza kufanya bila kuwa na pesa, hakuna chochote unaweza kukifanya kwenye Wizara yako, kwenye idara zako bila kuwa na fund.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongea nini kama tunakuja hapa tena na bajeti ambayo imekuwa na ongezeko la asilimia 16. Kipindi cha mwaka 2015/2016 pesa ya maendeleo ilikuwa ni bilioni 35, Watu mmekuja hapa mnajinasibu kwa Serikali iliyopita ilikuwa imelala, sasa tunaongeza bajeti, mmeongeza bajeti kwa asilimia 16, tumeenda kwenye bilioni 42, lakini tunavyoongea leo katika robo ya tatu ni bilioni 7.6 tu zimepelekwa kwenye Wizara kama fedha za maendeleo. Swali najiuliza, Are we still on the track? Bado tupo kwenye mpango wetu wa kuleta maendeleo?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu mtashangaa nitakachowaambia hiki. Mtukufu alivyokuwa katika ziara zake anahamasisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Hostel ambayo tunapongeza sana, alitoa ahadi kwamba atatoa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa hostel za wanafunzi wa vyuo. Hatukatai, lakini tunarudi katika swali la msingi; hicho ndiyo tulichokuja Bungeni na kubajeti kwamba tunataka kufanya kama kipaumbele cha Taifa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo hostel ambazo Mtukufu ameenda ametoa bilioni 10 kwa nyakati ambazo aliona zinafaa, lakini tupo tunaongelea Serikali ya viwanda, tunaongelea uchumi wa viwanda, bado wana bilioni 7.6 katika theluthi ya tatu. Tutamlaumu Waziri maskini ya Mungu, tutamsema sana lakini atafanya nini? Atasema nini? Turudi tuiulize Serikali bado tupo kwenye track? Bado tunataka kuendesha uchumi wa viwanda au zilikuwa ni story tu ambazo tulikuwa tunajinasibu kwa sababu ilikuwa Serikali mpya kwa hiyo tulitaka kuja na kitu kipya? Na kiukweli ndiyo hicho ninachokiona. Tulitaka kuja na kauli mbiu mpya japo kitu kilikuwa kile kile, business as usual na inaonekana katika money value. Tunaongelea mabadiliko yoyote, tunaongelea kutoka stage moja kwenda sehemu nyingine sasa tuko wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo viwanda ambavyo Mheshimiwa Waziri anakuwa anafungua kila siku bahati mbaya sisi Kamati hatujui, ila kubwa zaidi ninachojua anafungua viwanda vya watu, viwanda vidogo vidogo vya watu binafsi kitu ambacho pia sio kibaya, lakini turudi kama Serikali yake sasa, Serikali inataka kufanya nini kama mkakati wa kuanzisha viwanda katika nchi yetu? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu alikuja kwenye kamati yetu anaeleza kile kilichoitwa mkakati wa kufufua viwanda. Akatueleza katika kipindi cha mwaka mmoja mwaka ambao tupo sasa 2017...
NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: kuhusu utaratibu, Kanuni ya 68...
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nitakariri vizuri, Mtukufu Rais wakati anazindua majengo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam aliahidi atatoa bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa chuo. Sasa swali linakuja? Track na mchezo wetu na wimbo wetu hapa Bungeni ilikuwa ni viwanda lakini katika theluthi ya tatu ya viwanda yenyewe, Wizara husika imepewa tu, bilioni 7.6 ikiwa chini ya pesa alizotoa Mtukufu Rais alivyoshawishiwa na maendeleo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitapenda Waziri anikumbushe vizuri, kama bado tuko kwenye wimbo ule ule au tumebadilisha kauli na sasa tuko kwenye kitu kingine kama sera yetu ya Awamu ya Tano. Nimekwenda kwenye mkakati wa viwanda aliowasilisha Katibu Mkuu kwenye Wizara yetu ni kwamba; kwa Mwaka huu wa Fedha na pesa waliyoipata wameweza kufufua kiwanda kimoja tu, kwa mwaka mmoja. Kwa hiyo, kwa vile bado miaka minne, tutarajie kwa pace iliyopo tutaweza kuwa na viwanda vitano tu! Hii tunasema ni Serikali ya viwanda, sasa swali, je, kauli mbiu tulizokuwa tunaziimba za nchi ya viwanda zilikuwa sahihi au tulikuwa tunawahadaa Watanzania?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, tumeuliza juu ya Sera, ni Sera gani tuliyonayo kama nchi? Bado tuko kwenye Sera ya Ujamaa na Kujitegemea, tuko kwenye Sera ya Ubepari? Bado hata sisi wenyewe hata kauli mbiu ya nchi yetu hatuelewi tuko sehemu gani. Hilo swali tumeliuliza katika Kamati yetu. Tunakuja hapa tunasema sisi kama Serikali tunaenda kuwekeza kwenye viwanda, sisi kama Serikali tuna uwezo wa kuwekeza kwenye viwanda?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza Mbunge mwenzangu; tumejiuliza ni kwa nini viwanda vyetu vilishindwa katika Awamu zilizopita na bado tunajidanganya kwamba tuna uwezo wa kuwekeza kwenye viwanda. Tukae chini tujiulize, Sera yetu ni nini? Ujamaa na Kujitegemea au tunaacha watu binafsi wawekeze kwenye viwanda. Kama tunataka watu binafsi wawekeze kwenye viwanda tumejiandaa vipi kuondoa kero ambazo zimekuwa zinawasibu na kurudisha viwanda nyuma. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakuja kwenye kero mbalimbali ambazo wafanyabiashara wanapitia. Tumeandaa mazingira gani mazuri ya kuvutia wawekezaji wakati hapa nchini wafanyabiashara na wawekezaji wadogo tunawaona ni wapiga deal tu, leo sasa imekuja kauli mpya, wanaonekana kama ndiyo wanafanya biashara haramu. Sera zetu ni zipi kuhusu wawekezaji, hilo ndilo swali la tatu tunalopaswa kujiuliza juu ya mazingira rafiki. Nitaomba muda wangu ulindwe kwa sababu kuna mtu aliutumia vibaya tena kwa makusudi! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira rafiki ya viwanda. Kuondoa tozo mbalimbali, kuweka one stop center. Nimeongea hapa Bungeni na narudia leo, tuwekeni one stop center na sio one collection center, kitu ambacho tunacho leo ni one collection center. Unaenda pale unawakuta Idara mbalimbali lakini wapo hawawezi kutoa maamuzi. Mtu yupo kama representative na inapokuja kwenye kufanya maamuzi anasema ngoja nimpigie bosi wangu. Sasa tunachokitaka ni one stop center na sio one collection center kama ilivyo leo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama haitoshi; kuna titiri mbalimbali za utozaji wa kodi. Unaenda TBS unaenda, TFDA, unaenda OSHA na vitu vingine ambavyo vinafanya kazi zile zile more or less the same function na tunasema kwenye Kamati tunataka mpango mkakati wa ku-harmonize hizi taasisi, hizi regulatory authority – tuwe na vitu vichache ambavyo vinapunguza kero kwa wafanyabiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kama haitoshi na inayosikitisha zaidi, TBS wanalalamika, TFDA wanalalamika, wanavyotaka kuingiza mashine za maabara wanatozwa pesa nyingi sana kama tozo ya ile mizigo inayoingia nchini na tunaomba sasa tozo zile zitolewe au zipunguzwe ili waweze kuingiza mashine za kutosha kwa ajili ya kuleta ufanisi ili kupunguza pia gharama za kupima vile vitu ambavyo wanapima kama whatever!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni miradi ya kuchochea maendeleo. Tangu nikiwa mwanafunzi wa shule nasikia mnaongelea Liganga na Mchuchuma. Nataka Waziri atuambie, hiyo story mwisho lini? Hii Serikali inayotuongopea na Hapa Kazi Tu ina mipango mikakati gani ya kumaliza ujenzi wa viwanda vya Liganga na Mchuchuma kama vichochezi vya kiuchumi wa miradi mingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokiona leo ni Mtukufu Rais kama mlivyosema akifanya ziara sehemu fulani akaona kuna changamoto ya barabara anaagiza barabara fulani itengenezwe kitu ambacho sisemi kama ni kibaya, lakini lazima tujikite katika kujenga miundombinu ambayo ita-link viwanda, maeneo ya uwekezaji na itawezesha ufanyaji wa biashara na mazingira mazuri kwa maana ya miundombinu katika eneo husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni kuongezeka kwa riba ya yale maeneo ambayo yalikuwa yametengwa kama maeneo ya uwekezaji, EPZA. Tunavyozidi kuchelewa kulipa fidia ya maeneo hayo ndiyo gharama ya haya maeneo yanavyozidi kupanda. Amesema Mwenyekiti wa Kamati ilianza ikiwa bilioni 60, mwaka jana ilikuwa bilioni 191 na yeye amemalizia kusema hajui mwaka huu tutaambia ni bilioni ngapi, who knows pengine itakuja bilioni 300! Swali ni je, bado tuko kwenye the same track ya kutaka kuwekeza? Nini vipaumbele na mawazo yetu juu ya kuwekeza?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Katibu Mkuu anasema wanataka waanzishe EPZA, maeneo maalum ya uwekezaji. Sasa maeneo maalum ya uwekezaji yanazidi kubaki kuwa ndotoni kwa sababu uhalisia haupo, maeneo hayajalipiwa fidia, hakuna hata ndoto ya kupata pesa ya kulipia fidia halafu tunakuja hapa tunasema Serikali ya viwanda. Ni lazima tujipange upya na tuamue tunataka kufanya nini kama Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama sisi hatuwezi kuwekeza kwenye viwanda, tuandae Sera, mazingira, mazuri ya watu wengine kuwekeza. Kuna watu wanaosaidia kuleta ushindani katika kuwekeza, mfano fair competition kuna taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Fair Competition Commission. Wanakuja kutuambia wana wafanyakazi 53 tu na sio hao tu kuna TBS, kuna wafanyakazi, kuna idadi chache sana ya wafanyakazi na wale wanapaswa kufanya kazi nchi nzima. Tunategemea wale watu wafanye kazi kwa miujiza na wanachodai ni kwamba hawapati vibali vya kuajiri…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: AhsanteMheshimiwa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwepo na utaratibu wa kurudisha vyeti vya vyuo kwa wale wanaopotelewa vyeti vya NECTA pale aliyepotelewa akiwa na ushahidi usiotia shaka wa kupotelewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ada elekezi za shule hazitekelezeki labda vitu kama michango ya majengo kwa shule binafsi yapigwe marufuku. Private investiment inawahusu vipi wazazi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kuanzishwe Bodi ya Elimu na Walimu wasajiliwe na wawe responsible nayo hasa mambo yanayohusu maadili. Vyuo Vikuu viwe categorized kwa level zake lakini viwe na specialize hata kama kutakuwepo na kozi nyingine zaidi, lakini chuo kijulikane kwa specialization moja au mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Sera ya Elimu iangaliwe upya, kwani jamii tuliyonayo leo ya vijana kutopenda kazi, kusema uongo na unafiki ni zao la sera isiyokuwa na dira ya wapi tunaenda na nini tunataka ku-achieve.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwango kisichoridhisha cha mshahara wa shilingi 570,000/= haiwezi kukidhi maisha ya mtu, lazima Serikali ibuni njia nyingine za kuwasaidia Walimu vitu kama Transport Allowance, Accommodation Allowance na Teaching Allowance.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upandishwaji wa madaraja kwa Walimu unachukua muda mrefu sambamba na malipo ya vyeo hivyo vipya.
Vile vile nashauri kuwepo na chombo cha kusikiliza rufaa za wanafunzi ambao huwa wanakata pale wanapokuwa hawajaridhishwa na usahihishaji wa NECTA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima Wizara ibuni namna nyingine ya kutambua uwezo wa wanafunzi kwani njia moja tu ya mtihani siyo sahihi. Pia kuna uwezo na vipawa mbalimbali nje na kukariri majibu ya mtihani, kila mtu awe awarded kwa uwezo wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Walimu wa Nursery School wasajiliwe na watambuliwe rasmi katika mfumo wa Walimu. Jiji la Tanga ni kati ya mikoa iliyosahaulika na kuwa na vyuo vichache vya Serikali.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, umeme kukatiza maeneo machache tu ya mjini (REA) huku vijiji vingi vikibaki bila umeme.
Mheshimiwa Spika, nguzo za REA/umeme zimewekwawekwa tu bila kufuata barabara na mara nyingi zinakatiza katika viwanja vya watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, fluctuation ya umeme kitu kinachoshusha rate/quality za uzalishaji viwandani.
Mheshimiwa Naibu Spika, nguvu ndogo na bajeti ndogo kuwekwa katika joto ardhi, nishati inayoonekana ni ya gharama nafuu.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa mapendekezo kwa Serikali juu ya hitaji la msingi la kutumia transformer za TANELEC kwa lengo la kupunguza gharama ambazo Serikali inaingia kwa kununua transformer za China/India wakati Tanzania ina hisa kwenye hiyo kampuni.
Mheshimiwa Naibu Spika, pesa nyingi imetoka kwa mwaka 2015/2016, lakini bado changamoto za umeme ziko dhahiri. Hivyo, ama usimamizi ni mbovu au miundombinu hii haiwagusi watu moja kwa moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, napendekuza kushushwa nishati ya gesi kwa lengo la kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi wanaoitumia.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ANATROPIA L. THEOPIST: Mheshimiwa Naibu Spika, Kuondoa Milolongo ya Vikwazo Katika Uwekezaji; mlolongo wa utaratibu wa kumiliki ardhi ni gharama kubwa ya upimaji na umiliki wake. Wingi wa Tozo mbalimbali, kodi na ushuru katika biashara na huduma ziwe harmonized na zipunguzwe ili kuvutia zaidi uwekezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuandaliwe vipaumbele vichache vyenye kuandaa mazingira ya uchumi wa viwanda na kuhakikisha vinatekelezwa. Kwa mfano mpango ujao uhakikishe fidia zinalipwa kwa ajili ya EPZA kwa angalau asilimia 60 na Miradi ya Chuma na Umeme tu, tofauti na mpango unaoonesha vipaumbele zaidi ya 16, katika nchi yenye uchumi mdogo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipaumbele kingine kuelekezwa iwe katika kilimo ambayo ndiyo sekta inayoajiri watu wengi. Hii iende sambamba na uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo vya kuhudumia au kuongeza thamani katika mazao yao. Hii iende sambamba na kuongeza pesa katika taasisi zinazounda viwanda hivi kama TEMDO, COSTECH, TIRDO etc.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuongeza ushirikishaji wa sekta binafsi kati maandalizi ya sera, kodi na tozo mbalimbali. Kwa mfano, kuanza kutoza asilimia 18 kwenye auxiliary services za bandari na katika sekta ya utalii imepelekea anguko kubwa la kibiashara kwani wahusika hawakuwa wamejiandaa kwa mabadiliko husika, hali kadhalika wasafirishaji, TATOA, TAFFA na wadau wengine wanaohusika na upandishaji wa tozo hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ubunifu Katika Kuibua Vyanzo Vipya vya Mapato. Kumekuwepo na changamoto ya kodi mpaka kuwa kero. Ubambikaji wa kodi toka kwa maafisa wa TRA kwa lengo la kuongeza pato la ndani, ikienda sambamba na focus kwa makosa ya barabarani ni mzigo unaobebwa na watu wachache tu. Wizara na Serikali iwaze vyanzo vipya vya kodi ili kodi isambae na isiwe mzigo kwa watu wachache kama ilivyo sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuwe na mpango wa kuoanisha elimu na uchumi wa viwanda tunaouendea, kuandaa wanafunzi sambamba na tunakotaka kwenda, tofauti na ilivyo sasa ambapo wanafunzi hata wakimaliza vyuo hawana ujuzi wa kile kinachohitajika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kusambaza Uchumi; Mipango ioneshe dhahiri yale maeneo yaliyosahaulika kama vile Mikoa ya Kagera, Mwanza, Kusini na mengineyo inayosadikiwa kuwa maskini ili ipewe kipaumbele katika miradi ya maendeleo. Hatutarajii kuona mchanga unaongezwa kwenye kichuguu, Priority has to be to less developing regions
Mheshimiwa Naibu Spika, kuwe na mkakati thabiti wa kutekeleza bajeti ambazo tumekuwa tukiziandaa kila mara. Kwa mfano, bajeti zimekuwa zikiletwa Bungeni lakini mpaka mwisho wa mwaka pesa zinakuwa hazijapelekwa. Tunatarajia kuona namna ambayo pesa zitapatikana na si tozo na kodi kero tunazoziona kwa sasa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake pamoja na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nitaanza kwa kum-quote mwanasayansi mmoja anaitwa Albert Einstein aliwahi kusema; “Dunia ni mahali hatari pa kuishi siyo kwa sababu ya watu ambao ni wabaya, bali ni kwa sababu ya watu ambao hawafanyi lolote dhidi ya uovu.” Nitarudia, dunia ni mahali hatari pa kuishi siyo kwa
sababu ya watu waovu bali kwa sababu ya watu wema ambao hawawezi kukemea uovu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini nasema haya? Tangu asubuhi leo tunaongelea kupotea kwa mwananchi wa Tanzania anayeitwa Ben Saanane. Wanahesabika ni watu wangapi wanasema Ben Saanane kapotea na wanaoonekana kuongelea kupotea Ben Saanane wamekaa upande fulani, lakini Ben Saanane ni mwananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ana haki ya kuishi na ambaye kwa kupitia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaipa Serikali mamlaka ya kulinda uhai na usalama wa raia wake kwa mujibu wa Katiba hii. Tunapoongea kila siku hapa hatupewi jibu kutoka kwenye vyombo husika na kwa Waziri husika, huko ni kuonesha tunashindwa kutimiza wajibu wetu na ndiyo tunarudi kwenye kauli kwamba watu wema tunavyozidi kunyamaza kimya tunafanya dunia iwe siyo mahali salama pa kuishi, hilo ni jambo la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nitarudi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nirudi kwenye majukumu yetu kama Wabunge hasa tukiwa kwenye Bunge la Bajeti hasa tukiwa na wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali. Siku za hivi karibuni nimeona mara nyingi mtu ukiongea
unaambiwa umemwongelea Rais badilisha hotuba au umemtaja Rais, nataka kujua ni lini Bunge kama Bunge inaruhusiwa kuisema au kuisimamia Serikali?
Mheshimiwa Naibu Spika, nitasoma kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Toleo la mwaka 1977 ibara ya 4(2) inaipa mamlaka Bunge na inasema; “...na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni
Bunge na Baraza la Wawakilishi.”
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Bunge tunapewa mamlaka ya kuisimamia Serikali, kusimamia utendaji wa kazi zake za umma na tunafanya hivyo kwa niaba ya wananchi ambao ni umma. Tunapokuwa tunakuja hapa tunasema Serikali haijafanya moja, mbili, Rais katoa tamko moja, mbili na tunaambiwa tufute nini wajibu wetu kama Wabunge?
Mheshimiwa Naibu Spika, naenda mbali zaidi kifungu cha 63(2) nitasoma kinasema; “...kwa niaba ya wananchi, kuisimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Katiba hii.”
Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge humu ndani kila mtu aliapa kuilinda Katiba hii, tunapofika hapa tunaambiwa tusiseme, tusiielekeze Serikali, tusiikosoe Serikali tuliapa nini hapa kama siyo unafiki? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Katiba hiyo hiyo tuliyoapa kuilinda na kuitekeleza inakuja Ibara ya 100 kama Bunge inaongelea Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Ibara ya 100(1) na (2) “Kutakuwa na uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge…” Pia kifungu cha 46A kinaongelea ni namna gani Bunge kama muhimili linavyoweza kumshtaki na kumwajibisha Rais. Kama tunakuja hapa Bungeni tunaambiwa usimseme mtukufu ukimsema umevunja Katiba ni lini kama Bunge likiamua sijasema lifanye hivyo, lini kama Bunge likiona inafaa linaweza kumjadili na hata kumwondoa Rais madarakani kama tunaogopa hata kusema utendaji wa Rais. (Makofi)
Waheshimiwa Wabunge wenzangu tusikwepe madaraka yetu, hii nchi imeridhia utawala bora, kuna checks and balances. Kama Bunge tunawajibu wa ku-oversee Serikali inafanya nini, kama Bunge tunapaswa kuiambia Serikali ulivyofanya hivi ni sahihi au siyo sahihi. Iweje kila siku mnasema msitamke hilo neno huyo ni mtukufu, huyu ni nani, naona sasa tunavuka mipaka. Tunaendelea kupunguza uhuru wetu bila kujua kwamba kuendelea kujinyima uhuru hatuwatendei haki watu tunaowawakilisha. Tunasahau tunavyoendelea kujinyima uhuru tunashindwa kuhoji mambo kadha wa kadha ambayo yanatuhusu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu bajeti. Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi na msimamizi wa Serikali Bungeni, tunaongelea Serikali unayoisimamia kwa mwaka unaoisha wa fedha 2016/2017 Serikali yako tukufu ikiwa imepanga bajeti ya shilingi trilioni 11 imeweza tu kukusanya trilioni tatu sawa na asilimia 26 kama mapato ya ndani, ikaweza kupata shilingi bilioni 871 ambazo ni fedha za wahisani. Kwa hiyo, jumla ya bajeti kwa fedha tuliyonayo ya
maendeleo tunaona tuna shilingi bilioni 33 ambayo ni asilimia 33 ya bajeti nzima mnayoileta tuiongelee.(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini ninayasema haya? nasema haya kwa sababu ukisoma kwenye takwimu unaambiwa uchumi unapaa, uchumi haupai tu, uchumi ni matokeo ya fedha zilizopekewa kwenye Halmashauri. Uchumi kukua mabadiliko ya maisha ya watu ni matokeo ya fedha tulizoweza kukusanya, takwimu za TRA zinasema kwamba uchumi umeendelea kupaa na wamekusanya fedha nyingi. Wanaonesha mpaka Machi, 2017 wameweza kukusanya
shilingi trilioni 1.34; ukilinganisha na mwezi wa Machi 2016 ambako walikusanya shilingi trilioni 1.31 ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.23. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kwa mwaka huu tumekuwa na turn over ndogo ya fedha za maendeleo kuliko wakati mwingine wowote. Nataka nijue kama uchumi unakua kwa TRA mbona fedha ya maendeleo haiendi? Mimi ni mtu wa Dar es Salaama kwa takwimu za mwezi Oktoba 2016, kulikuwa na biashara 1,741 ambazo zimefungwa katika Jiji la Dar es Salaam ambayo inaonesha ni sawa na biashara 580 sawa na biashara 19 kwa siku zinafungwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hapo naona contradiction TRA mapato yanapanda na biashara
zinashuka, lakini bajeti ya maendeleo inazidi kushuka kabisa, hapo kuna kitu hakipo straight Waziri Mkuu, msimamizi wa kazi za Serikali Bungeni tunaomba utuambie mbona contradiction? Mapato yamepanda, biashara zinafungwa na fedha ya maendeleo haiongezeki ni lazima tuangalie. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana nimewasomea Waheshimiwa Wabunge kwamba abunge tuna jukumu la kuisimamia Serikali, Serikali ituambie kama uchumi unakua mbona hatuoni fedha za maendeleo kwenye maeneo yetu? Mmechukua hata hela yetu ambayo ni kodi
ya majengo, mmeiongeza kwenye hiyo fedha ya maendeleo, kule kwetu kumedorora kule. Mimi nadhani ni heri zile fedha za kodi ya majengo tuziache kwenye Halmashauri ili kwenu yakibuma walau kwenye Halmashauri zetu mambo yanaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais aliwaomba wananchi kwamba wampe muda kitambo ana hakiki watumishi hewa, aliomba miezi miwili leo tunaingia mwaka wa pili, watu wamemaliza elimu zao, watu wamepata mikopo wamesoma huu ni mwaka wa pili hawajui wataajiriwa lini, tunataka kujua hawa watu wataajiriwa lini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho kabisa ambalo lipo kwenye Ofisi ya Spika ni kwamba tuliambiwa fedha zilibaki kwenye Mfuko wa Bunge takribani shilingi bilioni sita zikarudishwa Ikulu lakini hapa Wabunge wanalia wanasema hawana Ofisi, Ofisi hazina furniture, tumekuwa tunajibana lakini kumbe watu wanapeleka fedha Ikulu. Tuangalie kipi kipaumbele tunaweza kufanya kama taasisi ya Bunge ni kuwapendezesha waliopo Ikulu au ni kufanya kazi kama muhimili na kujenga ofisi kwenye maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaweza kuamua tunataka kufanya nini, tunataka kufanya kama Wabunge au tunataka kufanya kama vivuli vya Serikali Dodoma? Tuamue tunaweza kufanya vipaumbele tukaamua kwamba tunataka tuisimamie Serikali, tunataka kuishauri Serikali na tunataka kuihoji Serikali ni kwa nini fedha za maendeleo hazijaja, kwa nini fedha za wahisani haziletwi? Ni kwa sababu tumeamua sisi kama Wabunge na pengine Wabunge waliokuwa wengi wameamua kunyamaza kimya. Pengine Wabunge walio wengi wanaoamua kusema wanaonekana wanasema sana na hawapaswi kusema, tuangalie tunawatendea haki Watanzania au hatuwatendei haki? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaitendea haki mioyo yetu na ninarudi kwenye kauli ya Albert Einstein anasema; “Dunia ni mahali hatari pa kuishi si kwa sababu ya watu ambao ni wabaya, bali ni kwa sababu ya watu ambao hawafanyi lolote dhidi ya uovu.” Ujiulize upo kwenye upande upi wa shilingi, umeamua kunyamaza na kuacha mabaya yatamalaki au umeamua kukemea uovu ili mambo mema yatamalaki. Tukifuata kauli ya maneno hayo tutaweza kuwa Wawakilishi na Wabunge wema wenye kuisimamia Serikali na Serikali haiwezi kuleta tena asilimia 35 ya bajeti, itahakikisha itamiza hata asilimia 70 kwa sababu inajua wakija Bungeni bajeti haitapita, wakija Bungeni wataulizwa maswali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunachokiona hapa hata ikija asilimia tatu wanaoafiki tusemeje wanakuwa wengi inapita, lakini maendeleo hayaendi, Tanzania ya viwanda tunaweza kuisubiri na tukakesha inaweza isionekane kesho wala keshokutwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushuruku kwa nafasi hii. Nichukue nafasi hii kutoa masikitiko yangu kwa niaba ya Kambi yetu kwamba hatujaridhishwa na mambo mengi. Napenda kutoa hayo masikitiko yangu.

Mheshimiwa Spika, lakini tuna mchango kutoka kwenye hotuba ya Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambao nimeambiwa tumepewa humu ndani na nitaeleza. Sisi kama Kambi ya Upinzani au kama CHADEMA hatujaridhishwa na mwenendo wa Tume ya Uchaguzi ambavyo imekuwa ikifanya kazi zake. Kumekuwa na upungufu mkubwa sana katika Tume ya Uchaguzi ambayo kimsingi tunaiona kwamba Tume haiko huru. Inasikitisha kwamba tuko kwenye nchi ya kidemokrasia, tuna referee ambaye anapaswa kuwa Tume huru ya Uchaguzi na badala yake siyo Tume huru ya Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, tuna Tume ambayo Mwenyekiti wake ni mteule wa Rais ambaye ni Mwenyekiti wa chama fulani. Tunajiuliza, je, wengine wanafanyaje? Ni kwa nini yule ambaye ni Mwenyekiti wa chama ndiyo anatuchagulia refa ambapo sisi wengine hatuko kwenye chama chake? Kama hiyo haitoshi kwa maana ya muundo wa Tume, uongozi wake, Mwenyekiti wake, wasaidizi wake, Makamishna wanajikuta ni wateule wa Mwenyekiti wa chama fulani, automatic wanapoteza kile kinachoitwa kuwa huru katika kusimamia mchakato wa uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, sisi wote hapa tumekuwa tunashangilia ukitaja Simba au Yanga, ukimwambia referee ana maslahi na Yanga na aende kuchezesha mechi ya Simba watu wataandamana usiku kucha. Ni kwa nini sisi tuone ni fair tunakuwa na Mwenyekiti ambaye anaenda kupiga kipenga, ambaye anapaswa kusimama katika lakini ni mteule wa chama fulani.

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi, tuna wasimamizi wasaidizi…

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Taarifa Mheshimiwa Waziri wa Nchi.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, naomba tu kumpa taarifa mchangiaji kwamba Tume hii ya Uchaguzi na uteuzi wa viongozi wote waandamizi wa Tume iko kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tume hii kwa uhalali huo huo iliweza pia kumtangaza hata yeye Mheshimiwa Anatropia kuwa Mbunge na yuko ndani ya Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waheshimiwa Wabunge wote ambao wako ndani ya Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niendelee tu kumkumbusha Mheshimiwa Anatropia anapodai kwamba Tume hii siyo huru ina maana basi hata Ubunge wake yeye sio halali. Kama Ubunge wake ni halali na yuko ndani ya Bunge basi Tume hii imeendelea kufanya kazi yake kwa maadili na kwa kuzingatia Katiba na kwa sababu hawa viongozi wote wako kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Theonest pokea hiyo.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nadhani siyo lazima niipokee, kuna msemo wanasema the means justify the end na mimi ndiyo nachoeleza leo na kwenye Kambi yetu tumeshauri tulete hapa mabadiliko ya sheria husika tuwe na Tume huru. The means justify the end. Kama unavyonileta hapa Mbunge wa CHADEMA unategemea nitakaa kutetea CCM? Amekuja hapa Msajili wa Vyama vya Siasa ameshangiliwa sana na kuna mtu mmoja aka-post sitamtaja jina akasema wale ambao hamshangilii shauri yenu, hiyo inaonesha to what extent ile level ya independence ipo questionable, the means justify the end. (Makofi)

SPIKA: Kwa hiyo, angekuwa ni huyo ambaye wewe unasema awe angeshangiliwa ingekuwa ni mbaya? Sioni uhusiano wa kumshangilia mtu na role yake, endelea tu.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pili, tuna Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kwa maana ya Wakurugenzi wa Halmashauri kwenye Wilaya zetu. Ukiangalia composition ya watu wengi majority tunaweza kutaja hata majina wameshiriki kwenye kura za maoni za Chama cha Mapinduzi, baada ya kuachwa ndiyo wameenda kuteuliwa kuwa Wakurugenzi, to what extent wale watu wanaweza kuwa so independent? Hiyo yote inaleta questionability ya Tume whether ni huru au siyo huru.

Mheshimiwa Spika, kama hiyo haitoshi kuna funding yenyewe ya Tume, tuna Tume ambayo inategemea busara za Mwenyekiti kwa maana ya Mheshimiwa Rais hatuna namna ambayo tunaweza ku-finance Tume yetu zaidi ya kutegemea …

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Ruksa Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, tukiendelea kuacha haya maneno yatakuwa yanachukuliwa kama ni maneno sahihi lakini si kweli. Kwenye hotuba hii ya bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu tunayo Vote maalum kwa ajili ya Tume ya Uchaguzi na inatengewa bajeti na Bunge lako kila mwaka.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya Uchaguzi inapofika kwenye suala la uchaguzi, kisheria na Kikatiba fedha za uchaguzi zinatolewa na Mfuko Mkuu wa Serikali. Kwa hiyo, ni lazima atenganishe hayo mambo mawili, tusiendelee kuacha watu wanazungumza tu vitu ambavyo wakati mwingine siyo vya kweli. Vinginevyo nitakuja kuomba kanuni ya utaratibu na mwongozo ili Mheshimiwa Anatropia athibitishe kama Tume hii inapewa fedha kwa hisani. Tuna Vote hapa tutaipitisha na fedha za uchaguzi kwa mujibu wa Sheria na Katiba zinatengwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, taarifa nimeipokea lakini amount inayokuwa allocated kwenye Vote inaamuliwa na nani? Tutakuja hapa tutaongea, inaamuliwa na nani?

Mheshimiwa Spika, tunakuja kwenye uandikishaji wa BVR. Kumekuwepo na changamoto ya uandikishaji wa BVR tunakumbuka 2015 lakini hebu tuangalie tangu 2015 ni mara ngapi imekuwa updated na tumekuwa na chaguzi ngapi zilizofanyika hapa katikati. Ina maana assumption ni kwamba wale waliojiandikisha 2015 ndiyo bado wana exist kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ni kwa nini haiwi updated na kwa nini tunaendelea ku-maintain kwamba wale watu bado wako wote lakini wale ambao hawapo kwa nini hawatolewi na waliofikisha miaka 18 wako eligible ku-vote kwa nini wanakuwa hawaingizwi kwa wakati. Hiyo pia inatilia shaka uhuru wa Tume huru ya Uchaguzi.

Mheshimiwa Spika, tuje kwenye suala lingine, Tume imeendesha chaguzi kadha wa kadha na nyingine zimekuja hizi mpya za voda faster ambazo hazioneshi uhalisia. Uhalisia wa uchaguzi unauona kwenye mchakato husika. Mchakato wa kwanza ni pamoja na watu kuchukua na kurudisha fomu, tuna wagombea niongelee Korogwe, mgombea amepiga kambi kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Uchaguzi siku nzima, Mkurugenzi hatokei na deadline imefika na unaambiwa amekosa vigezo kwa sababu hajarudisha kwa wakati. Unaweza ukaona ni michakato ambayo inakuwa manipulated makusudi sijui ni kwa nia gani kwa sababu nchi inayoamini kwenye demokrasia nikiingia kwenye uchaguzi naamini nitashinda au utashindwa lakini ikifikia wakati mna mifumo ambayo haipo independent…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Unajua Mheshimiwa Anatropia unajiweka kwenye eneo ambalo nashindwa hata kukulinda lakini umechagua mwenyewe kujiweka kwenye eneo hilo ndiyo linakupa shida kidogo. Duniani hapa kama huyo mgombea wenu alipata matatizo fulani si alikuwa aende Mahakamani tu. Sasa ukituambia sisi Bunge hapa tufanye nini? Kama alifanyiwa jambo ambalo siyo sawa angeenda tu Mahakamani. Hizi taarifa unayosikia na nini wala yasingejitokeza. Endelea tu kuchangia muda bado ni wako, mtunzieni muda wake.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, ushiriki wa vyombo vya dola na kwa kiwango kikubwa katika mchakato mzima wa uchaguzi, tukianzia kupiga kura na kutangaza matokeo. Unaona nguvu kubwa inatumika lakini kama haitoshi kuna incidence ambapo Polisi wamekimbia na maboksi ya kupigia kura, imetokea Kinondoni. Nayaongea haya kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu yeye ndiyo msimamizi anapaswa kukumbusha watu wajibu wao, anapaswa kuangalia, je, taratibu zinafuatwa na kama hazifuatwi yeye ndiyo anasimamia. Ninaongea kwenye hotuba yake kwa sababu yeye ndiyo mtu anayehusika katika suala hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na mauaji na ugomvi mbalimbali, tuna Katibu wetu wa Kata ya Hananasifu aliuawa katika uchaguzi wa Kinondoni mpaka leo hatupewi taarifa uchunguzi umefikia wapi na aliuawa kwa nini? Hayo ni maswali ya kujiuliza, kama tuliamua ku-embrace demokrasia na tumeamua kuiweka pembeni na kucheza na mifumo tuliyonayo kwa ajili ya kupata matokeo, tunaiweka nchi yetu katika mazingira ambayo siyo sahihi. Tunaiweka nchi yetu katika mazingira ambayo sisi wenyewe tunai-push ambako wengine hawataki kwenda.

Mheshimiwa Spika, kugoma kutoa viapo vya Mawakala, huo ni mchakato wa kawaida wa uchaguzi, inakuwaje Wasimamizi Wasaidizi, Maafisa Watendaji wasitoe viapo kwa wakati? Kwa nini chama kimoja kipewe na kingine kisipewe? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naweza kuongea mengi, lakini mnapaswa kujua, kama tunaingia kwenye mchezo, naamini mnajinasibu kwamba Serikali yenu inafanya vizuri, imepeleka miradi, imepeleka maji, imepeleka shule, hebu twende kwenye uwanja sawa wa uchaguzi, tuwaache Watanzania wachague kati ya mliyoyatenda na sera zetu. Kati ya mlichowapelekea na sisi tutakachokuwa tunawaambia, kuliko kubaki nyuma kutumia vyombo vya dola vilivyopo, kucheza na Tume, kucheza na mfumo kwa ajili ya kupata matokeo. Tuacheni, naamini mmefanya mazuri, twendeni tukapige jaramba, wananchi wenyewe wataamua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakuja kwenye hoja yangu ya pili, naongelea uminywaji au mifumo ya utoaji haki isiyoridhisha. Leo kupewa dhamana katika Kituo cha Polisi au Mahakamani nimekuwa ni hisani siyo tena haki. Nitatoa mfano wa kilichomtokea Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Aikaeli Mbowe. Sitaeleza chote kilichotokea, lakini Jaji Rumanyika alisema, kilichofanyika katika shauri hili ni sawa na kuchukua mzigo ukaufunga mbele ya mkokoteni, kwa maana ni mambo ambayo ni ya aibu. Akasema, masharti ya kufuta dhamana yanapaswa kuwa magumu kuliko masharti ya kutoa dhamana. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Theonest, unajua unachojadili ni mambo ya Mahakamani ambayo tena kesi yenyewe bado inaendelea na pia, Jaji wa Mahakama ya juu anakosoa vitendo vya Mahakama ya chini yake. Sasa unataka Bunge tuingiliaje? Endelea tu Mheshimiwa Theonest, naona leo kidogo haujajipanga vizuri.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, natoa mfano wa kinachopaswa kusimamiwa. Ninaeleza kilichotokea, ninaeleza wajibu wetu kama watunga sheria. Ninaeleza umuhimu wa kutoa haki kwamba, ukienda Magerezani wamejaa watu ambao wangeweza hata kupatiwa dhamana tuka-save fedha nyingi za Serikali kuliko kuendelea kuweka watu ndani.

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo kupandikiza kesi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Naambiwa ni kengele ya pili, lakini kwa kuwa ulikatizwa katizwa sana, nakuongeza dakika tatu.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kumekuwepo tatizo la Polisi kubambikiza kesi kwa wananchi likiwepo suala zima la money laundering. Sasa hivi ndiyo umekuwa mtindo wa kisasa. Ukitaka kupigwa kule ndani na usitoke, kesi unayobambikizwa ni ya money laundering ambayo upelelezi wake unachukua muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, ni lazima tuangalie hata vyombo vyetu vinavyofanya kazi. Nadhani ni kama wiki mbili au tatu zimepita tumepata taarifa ya mtu aliyebambikizwa kesi na Askari, lakini upelelezi ulivyokuja kujulikana ikaonekana alibambikizwa kesi na katika mazingira ambayo imeonekana siyo fair. Ni lazima tuangalie mifumo yetu, ni lazima tuangalie, nasi tunatoa rai kwa mujibu wa sera za chama chetu kwamba, kupatiwa haki haitakuwa tena hisani, haki ni lazima ipatikane na ipatikane kwa wakati. Siyo tu kupatikana kwa wakati, ni lazima ionekane inatendeka.

Mheshimiwa Spika, ninamaliza kwa kusema, sisi kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo, tunaamini amani na utulivu wa nchi yetu utapatikana katika mifumo iliyopo ikiwa inasimiwa kwa amani. Nimetoa mfano mkubwa wa Tume ya Uchaguzi, kama tuki-temper na Tume ya Uchaguzi; kwa mfano, tunaenda kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa, tuki-maneuver na chaguzi za Serikali za Mitaa tunaenda kuwasha moto ambao hatuujui.

Mheshimiwa Spika, wananchi hawako tayari kuzidi kuonewa kwa sababu ukweli wanaujua, haki zao wanazijua na ukweli wanaujua.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru nianze kwa kueleza changamoto ambayo wakulima wa Mkoa wa Kagera hususan Wilaya ya Karagwe waliipata, Karagwe na Kyerwa katika zao lao la kahawa. Nataka tunavyopanga Mipango tuone ni namna gani tunaweza ku-rescue changamoto wanazopitia hawa wakulima ambao wamekuwa miaka yote kahawa ni kipato chao ni uchumi wao wa muda mrefu, kahawa kwao ndiyo dhahabu na ndiyo diamond. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunavyoongea, uchumi wa Mkoa wa Kagera, uchumi wa Wilaya za Karagwe na Kyerwa umeanguka kabisa. Kipato kidogo walichokuwa wanakipata husomesha watoto, kujenga, kutunza familia zao, kujenga nyumba kiliparaganyika. Soko la kahawa lilianguka lakini kama haitoshi, Serikali ikaanza kununua Kahawa kupitia Vyama vya Ushirika KDCU, changamoto ndiyo ilikoanzia, kabla ya hapo tulikuwa na wafanyabiashara kwa maana ya Makampuni yananunua kahawa, tumeona mikoa tofauti tofauti tukiangalia korosho, Makampuni yananunua korosho, tukiangalia pamba, Makampuni yananunua pamba, tukiangalia mazao mengine alizeti, Makampuni yananunua alizeti, lakini ikija katika Mkoa wa Kagera mnaambiwa Makampuni yasinunue na badala yake ni Vyama vya Ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyama vya Ushirika vinatupa bei gani? Msimu uliopita kilo moja ya kahawa inanunuliwa kwa shilingi 1,100. Mkulima ambaye alitarajia kujikwamua analea Kahawa kwa miezi sita anakuja kupewa shilingi 1,100 watu wamerudi kwenye umaskini, maisha yamekuwa magumu na takwimu ziko wazi. Takwimu za Mkoa wa Kagera miaka yote inaelekea kwamba ni mkoa unaozidi kurudi nyuma, zinatajwa Wilaya kama Ngara, zinaonekana ni kati ya wilaya tano za mwisho, tatizo ni nini? Watu wanalima, ardhi ina rutuba, tuna msimu wa kutosha, lakini mazao yetu yakifikia kuuzwa, Serikali inasema msiuze kuna bei elekezi, kuna shilingi 1,100. Tatizo ni nini? Kama korosho zinaweza kuruhusiwa makampuni kununua ni kwa nini kahawa zisiruhusiwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka uliopita 2017/2018 kahawa ilienda mpaka kilo moja kwa shilingi 2,000. Tunavyoongea leo 2018/2019 kahawa ni shilingi 1,100 kama nilivyokwishasema, changamoto imekuwa nini, ni kwa nini Serikali haijawasaidia wakulima hawa? Tulisikia tamko la Mheshimiwa Rais kupitia Vyombo vya habari kwamba kahawa isinunuliwe chini ya shilingi 1,400 lakini nimwambie Mheshimiwa Waziri, hakuna mkulima aliyeweza kuuza kilo kwa shilingi 1,400, tatizo ni nini? Tunaambiwa kuna tozo, ni tozo gani sisi hatuzifahamu na kwa nini tuumizwe wakulima? Kama uchumi wetu, uti wa mgongo wa wakulima wa Mkoa wa Kagera ni kahawa, kwa nini zao hili likianguka Serikali haiwazi namna ya kuwapa ruzuku? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tangazo la Serikali nimelinukuu hapa, ambalo lilionesha kwamba wangepewa ruzuku ya Sh.100 kwa mwaka uliopita, kwa kila kilo iliyouzwa, lakini ninavyoongea hapa, hakuna hata mkulima mmoja aliyewahi kupewa ruzuku hata ya senti kwenye kahawa alizouza, ni kwa nini tunafanyiwa haya, wakulima sisi wa Mkoa wa Kagera. Ni kwa nini watu wanakatishwa tama? Ni kwa nini mnaamua kuturudisha kwenye umaskini, wakati Mungu ametupa ardhi, Mungu ametupa rutuba, Mungu ametuwezesha, ni kwa nini? Nataka nipewe majibu ni Mpango gani uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukivuka kwetu, ukisema Mlongo ni mpakani mwa kama kilomita mbili, ukitoka upande wa Tanzania ukaingia upande wa Uganda, nimekuwa surprised hata ya leo, kilo ya kahawa ninavyoongea inanunuliwa kwa zaidi ya Sh.3,000, lakini upande wa Tanzania ambao ni just kilomita moja au mbili inanunuliwa kwa shilingi 1,100 tatizo ni nini? Sisi wakulima tunasema minada imekuwa inaendeshwa Kilimanjaro, ndiyo kuna minada ya kahawa ambayo inapelekewa kwenye Soko la Dunia, ni kwa nini hiyo minada haifanyiki kwetu ambako sisi tunazalisha sana kahawa? Ni kwa nini wakulima wa Mkoa wa Kagera wanaonekana ni kama second class? Ni kwa nini wakulima wa Mkoa wa Kagera hawawezi kuonyeshwa thamani ya biashara ya zao lao la kilimo ambalo wamelitegemea muda wote? Nataka Serikali iniambie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nime-google nikaona hata prices za dunia, nikaona kwamba iko around, mfano kama arabica coffee ni dola 2.85 ambayo ni equivalent na shilingi 4,835, ukija robusta inakuja kama dola 1.75 ambayo inaweza kuja mpaka shilingi 3,000, lakini sisi kwetu, soko halipandi na hatujui hiyo KDCU inashindanishwa na nani? Ukitaka kuleta monopoly kwenye soko ujue utawaumiza wale wakulima. Unavyoamua KDCU ndiyo wanaamua kununua zao la kahawa, unaua kabisa soko, yeye atakachoamua ndiyo kitakachofanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachosikitisha, hawa wakulima hizo fedha wanalipwa kwenye akaunti, wanalipiwa kwenye akaunti benki, wanakopesha Chama, wanasubiri wiki nzima, wao wakishakusanya fedha watumiwe kwenye meseji waende wakachukue fedha. it is not fair haiwezekani, sisi watu wa Mkoa wa Kagera hatutaki, hili ni zao letu, tunataka litukomboe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi, nimepitia bajeti ya kilimo, katika miaka mitatu consecutively nikaona ambavyo kilimo kimeenda kinashuka lakini na ukiangalia mchango wa kilimo katika Pato la Taifa unaona ni mdogo sana, inaoneshwa hapa kwenye taarifa ukurasa wa tano, kwamba mwaka 2016/2017, kilimo kimekua kwa asilimia 7.6. Mwaka unaofuata imekuwa asilimia 5.6, uliofuata ni asilimia 5.3. Kama hatuwekezi fedha ya kutosha kwenye sekta inayowaajiri watu wengi maana yake we are likely kuwa-starve. Ni sawa, tunaweza kuona tunafanya miradi mikubwa, lakini miradi hiyo mikubwa kama haigusi watu wengi, ni kupoteza muda na wananchi wanaendelea kuwa maskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naingia kwenye hoja yangu ya mwisho, naombeni Mipango wanayoenda kupanga iguse watu wengi na siyo watu wachache. Wapange Mipango inayotekelezeka, waache ku-bust bajeti wakati bajeti haitekelezeki, roughly kwa miaka mitatu, bajeti ukifanya estimate imetekelezwa kwa asilimia 36 tu, kwa miaka mitatu ya bajeti ya maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa narudi kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Nataka kuwaambia hivi tunachokitengeneza leo kwa kuona Vyama vya Upinzani katika nchi ni second class citizen, tunavyotaka kuona kwamba kuna watu ni wazalendo wakiwa kwenye Chama Tawala, basi wao ni wazalendo, lakini sisi wengine siyo wazalendo, maneno kama kuunda jukwaa la wazalendo, Walimu wazalendo, tunataka kutengeneza kinachotokea South Africa, tunataka ku-turn this country into a zone of phobic country. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, South Africa unaona wanauana leo walianza kidogo kidogo kwamba huyu, huyu ni Mkaburu, sawa alikuwa na rangi yake, lakini leo nawaona hao hao weusi wanaanza kuuana wao kwa wao na sisi tunakotaka kwenda mtu ukionekana unaji-associate na Vyama vya Upinzani kama ni kazi utapoteza, kama ni promotion utakosa, kama ni kuhamishwa utahamishwa, tunachokitengeneza ni nini? Tunataka ku-burn down hii nchi kwa sababu ya madaraka na nataka kuwaambia hakuna hali ya kudumu, there is no situation which is permanent, unaweza ukajiona leo wewe uko viti vya juu lakini kesho tutakutana benchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mifano ya kudumu, tuna mifano halisia, kuna watu walikuwa Mawaziri Wakuu katika nchi hii, leo tuko nao tunalalamika, msijione leo mmekalia viti vyekundu mkadhani mtadumu kuwa hivyo, tusiangalie maslahi ya tumbo letu katika gharama ya nchi yetu, no please. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie ni namna gani tunaweza kuwaunganisha Watanzania, tuangalie namna gani siasa zinaweza kutusaidia kuipeleka nchi yetu mbele, tupishane kwa hoja tusipishane kwa Vyama vyetu, tupishane kwa miono, tusipishane kwa maslahi, mimi ninachokiona hapa ni maslahi nani atabaki kwenye nafasi gani, nani atabaki azidi kuwa katika nafasi fulani na aonekane zaidi. Hayo mambo hayatujengi na hayo mambo hayataisaidia nchi, we can torn this country into pieces kama hatutobadilika, nataka niwaambie wanasiasa wenzangu tunaweza tukaamua ni aina gani ya nchi tunataka kuijenga, aliyoiacha Mwalimu Nyerere ambayo tunaonana sisi wote ni ndugu, sisi wote ni marafiki au nchi mpya ambayo South Africa leo wanalia, au nchi mpya ambayo Rwanda imewa-cost.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusema, Mipango siyo tatizo, Mipango ni matumizi, tutakuja hapa tutaongea, tutapewa posho, tutarudi Majimboni, lakini tukirudi bajeti imetekelezwa kwa asilimia 20, Bajeti imetekelezwa kwa asilimia nne. Nitoe mifano tena halisi kabisa kama muda utaniruhusu, katika mwaka wa fedha 2016/2017, Wizara ya Kilimo, katika fungu la maendeleo ilitengewa bilioni 100, ni bilioni mbili tu ziliweza kutolewa, imagine tumekaa Bunge zima hapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Nami nisiwe mbali na wasemaji wengi kuongelea juu ya janga la Corona. Kusema ukweli sisi kama Serikali Kivuli hatujaona initiative za kutosha, siwezi kusema hakuna ambacho kinafanyika lakini initiativezilizopo bado zinatutia mashaka iwapo changamoto itakuwa kubwa, kama nchi za wenzetu, je, sisi tutasalimika? Kama Italia, Hispania wanalia na China wameumia sisi tutasalimika?

Mheshimiwa Spika, tunaamini bado kuna njia ambazo zinapaswa kuwa za nguvu zaidi. Siyo kwamba watu wapigwe, walazimishwe kuingizwa ndani, walazimishwe kufungwa lakini bado kuna mechanism ambapo Serikali inaweza ikasaidia kama ambavyo wanafanya Rwanda. Unaweza ukasema Rwanda ni mfano mdogo mzuri wa initiative zinazofanyika.

Mheshimiwa Spika,naamini bado tuna nafasi ya kufanya kitu kabla janga hili halijawa kubwa unless tuendelee kuamini kwamba hamna kitakachotokea. Lazima twende na global trend, kama tunaona challenge ni kubwa sisi tunajiandaaje? Waswahili wanasema ni afadhali ujue Mungu yupo uishi vizuri kuliko uishi vibaya halafu ugundue yupo utakosa pa kukimbilia. Huo ndiyo wito wangu kwenu.

SPIKA: Huko Rwanda kuna nini kizuri kinafanyika?

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Rwanda unaweza ukaona wametagaza total lock down, lakini kama haitoshi, wamewagawia vyakula watu ambao wana changamoto ya maisha.

SPIKA: Haya, basi nimekuelewa. Endelea na mchango wako, kumbe ni total lock down.

MBUNGE FULANI: Endelea.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Ndiyo, nimekusikia Mheshimiwa Goodluck.

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, nataka nimpe taarifa mzungumzaji anayezungumza kuwa Serikali hatua ambazo imechukua, siyo zote ambazo imezitangaza. Nataka nimpe mfano mmoja tu; agizo la Waziri Mkuu kwa Wakuu wa Mikoa wote, likaenda mpaka kwa Wakuu wa Wilaya, kila Wilaya katika Hospitali ya Wilaya imetengeneza withholding rooms na treatment unit. Hiyo treatment unit imegawanyika katika sehemu mbili; high risks na low risk.

Mheshimiwa Spika, vile vile kila wilaya ambayo iko mpakani, kuna sehemu maalum wametenga kwa wale wageni wanaoingia. Kwa mfano, Tunduma kuna wageni 84 mpaka sasa hivi wameifadhiwa mpaka zipite siku 14 ndiyo wataingia. Kwa hiyo, vitu vingine vizito siyo vya kuzungumzwa hadharani. Ahsante sana.

SPIKA: Taarifa hiyo Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, naendelea. Kwa sababu kama mambo hayazungumzwi hadharani, yatajulikanaje sasa? Si lazima yazungumzwe ili watu waweze kuchukua hatua! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niongelee changamoto ya zao la kahawa. Zao la kahawa linachangia katika pato la Taifa zaidi ya asilimia tano, lakini ni moja kati ya mazao ambayo siyo tu yamesahaulika bali kuna mkakati unaonekana kama linataka kusukumwa pembeni. Changamoto ambazo wakulima wanapitia na hususan wakulima wa Mkoa wa Kagera, specifically Wilaya ya Kyerwa na Karagwe, yale ndiyo maeneo ambayo tunazalisha kahawa sana; na inaajiri karibia kila kaya. Almost kila kaya ni wakulima wa kahawa. Kipato chao kila siku ni kahawa.

Mheshimiwa Spika, changamoto ambayo imewakuta wakulima ni kwamba soko limekuwa gumu. Wanalima bila kujua wanauza wapi? Wanalima bila Serikali kuonyesha initiative ni kiasi itaweza kusaidia ili waweze kuzalisha zaidi?

Mheshimiwa Spika, nimeipitia Report ya Agricultural Non-State Actors Forum, inaonyesha ni kiwango gani licha ya research kufanyika na kuainisha changamoto za kimfumo zinazowakuta wakulima wa zao la kahawa, bado changamoto hizo hazijatatuliwa ikiwa ni pamoja na Bodi ya Kahawa kuiwezesha kuwa msimamizi wa zao la kahawa.

Mheshimiwa Spika, pia Shirika la TaCRI ambalo linajihusisha na kufanya utafiti wa magonjwa yanayosumbua kahawa, kuzalisha kahawa mpya na mbinu za uzalishaji bora, limekuwa halipewi fedha au fedha za kutosha kwa ajili ya kufanya hiyo kazi. Utaona kwamba ni juhudi za makusudi za kuhakikisha zao la kahawa mbali na kukosa soko, linazidi kudidimia.

Mheshimiwa Spika, pili, changamoto kubwa ambayo wananchi wamezidi kuiona, sijui ni kuzuia au nini kimefanyika mpaka Vyama vya Ushirika ndiyo vinaonekana kuwa mnunuzi pekee wa zao la kahawa. Mheshimiwa Waziri Mkuu ameenda Wilaya ya Karagwe na Kyerwa mara kadhaa, lakini sasa ametusaidiaje kutatua changamoto ambayo tunaona chama cha msingi hakijawezesha wananchi kuuza mazao yao kwa thamani ambayo waliitarajia? Msimu uliopita walikuwa wananunua kilo moja kwa shilingi 1,100/=. Msimu huu ambao ni msimu mdogo, tunaita Ndagasa, walipaswa kununua kwa shilingi 700/= lakini vile vile hawajanunua.

Mheshimiwa Spika, watu wana mazao, hawawezi kuuza kokote, mashirika au makampuni binafsi hayawezi kununua, watu wako stranded, watu wanapaswa kupata fedha ya kupeleka watoto shule, wanapaswa kujiendeleza katika maisha yao, hayo mambo yote yamekuwa ni magumu. Changamoto ni kwamba watu wamezidi kuwa masikini na kuna msemo unasema, watu wa huku wanajikuta wanabaki kuwa masikini, masikini na wa mwisho katika trend ya ranks za maendeleo yamekuwa Tanzania Bara.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sasa tunaweza kuona ni Serikali inafanya deliberatively kuhakikisha tunazidi kuwa masikini licha ya kwamba tuna nyenzo ya kujikwamua kama wakazi au kama wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Spika, nimepitia bajeti ya Chama cha Ushirika kwa estimates zao za mwaka 2020/2021…

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia, umesema Serikali inafanya makusudi!

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushindwa kubadilisha mifumo ambayo inaendelea kukandamiza wakulima wa kahawa ni sawasawa na kufanya makusudi ili wananchi wazidi kuwa masikini. Hakuna namna nyingine nitakayoitumia kwa sababu kama tutaondoa vikwazo, kama tutajaribu ku-encourage…

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Unapewa taarifa Mheshimiwa Anatropia. Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, tafadhali.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mzungumzaji kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza zao a kahawa, ni kweli kabisa wakulima wa Kagera wanalima vizuri sana na wanajitahidi sana kulima, Serikali kwa kuona changamoto za masoko ilichukua hatua za dhati kabisa za kuimarisha Vyama vya Ushirika ikiwa ni pamoja na kuwapatia fedha Vyama vya Ushirika ili viweze kununua kwa wakulima na kuhakikisha wanapata bei nzuri. Hii imefanyika vizuri sana na vyama vingi vimefanikiwa katika hilo eneo.

Mheshimiwa Spika, pia tuliweza kuhakikisha kwamba tunazuia wale walanguzi ambao walikuwa wanachukua kahawa na kwenda kuipeleka nchi jirani. Zaidi ya hapo, tumeiwezesha Bodi ya Kahawa kuisimamia vizuri sana na ndiyo maana uzalishaji umeongezeka na bei imeimarika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, haya anayoyasema kwamba Bodi ya Kahawa imesahaulika, Vyama vya Ushirika havijasaidiwa, havina uwezo, labda atuambie ni chama gani ambacho hakina uwezo? Kwa sababu kwa takwimu za Serikali ni kwamba tumeviwezesha vya kutosha na kuna mchango mzuri sana ambao unaendelea.

Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba kumpa hiyo taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia unapokea taarifa hiyo?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu ya ripoti niliyoisoma ambayo ukitaka nitakupatia na iko online inasema...

SPIKA: Ripoti hiyo kutoka wapi yaani? Ili tuweze kufuatilia wote maana hii ni ya Serikali. Hiyo yako ni ya kutoka wapi?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, ni ANSAF ambao ni wadau.

SPIKA: ANSAF ndio…

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, wanaita Agriculture Non Sector Actors Forum.

SPIKA: Sasa forums hizo, yaani wewe una...

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, wamefanya utafiti, wana data…

SPIKA: Sasa upande huu umepewa taarifa halisi za Kiserikali.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nami ndiyo nataka niseme, utafiti walioufanya umeonyesha kwanza vyama vyenyewe vimekuwa havina wataalam hata wa kukidhi mahitaji ya vyama husika. Hiyo nitasema. Nilitaka niunganishe na taarifa ambayo niliyosoma estimate ya Chama cha Ushirika.

SPIKA: Huo utafiti umekuwa vetted na TBS? Bureau of Statistics?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, imekuwa published. Kwa hiyo, kama iko published, assumption ni kwamba imekuwa satisfied. (Makofi)

SPIKA: Haya bwana, kama hao ANSAF unawaamini, endelea tu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ni kengele ya kwanza eeh!

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Ni kengele ya kwanza.

SPIKA: Ni ya kwanza.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nilitaka nimjibu, wameonyesha changamoto iliyopo kwenye management halisi ya Vyama vya Ushirika, lakini hiyo imeonekana hata kwenye bajeti husika. Bajeti ya Chama cha Ushirika ambayo inaonekana estimate zaidi ya shilingi bilioni 1.5 itaenda kwenye Managerial Activities kulipa fidia, kuhamisha kutoka eneo moja kwenda lingine na hii naweza nikakupatia, ambayo inaonekana fedha nyingi inatumika kwenye Managerial Activities na siyo kulipa wale wakulima wenyewe.

Mheshimiwa Spika, hii inaonyesha kwamba activities za ku-run au activities za kuandaa zao la kahawa, cost moja ya kilo itakuwa ni zaidi ya shilingi 1,700/= wakati wakulima wanaweza kuuza kwa shilingi 1,300/=. You can imagine kwamba anayelima kwa zaidi ya miaka mitano...

SPIKA: Hiyo ni bajeti ya Chama cha Ushirika cha Kagera ambako na wewe unatoka.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Ndiyo.

SPIKA: Nanyi ndio wanachama wa hicho Chama cha Ushirika.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Ndiyo, ndiyo, ndiyo.

SPIKA: Sasa unamlaumu nini Waziri wa Kilimo katika hilo kwa mfano?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika ninaiambia Serikali na huo ndiyo wito ninaoenda kuutoa kabla sijamaliza. Serikali ni lazima ifanye study kuona ni namna gani inaweza ikasaidia kwenye kuimarisha zao la kahawa badala ya mbinu tulizonazo leo za kutumia Vyama vya Ushirika ambavyo vimekuwa havina uwezo na uzoefu. Hiyo ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ya pili, tunaposubiri madalali, middle men watoke Ulaya au wapatikane hapa katikati waende Ulaya watutafutie soko ili sisi tuuze, ni lazima Serikali iangalie, tunawezaje ku-penetrate kwenye soko husuka ili tuweze kuuza; Mheshimiwa Rais anasema win win situation. Kwa nini win win situation tunazitaka kwenye madini; tunazitaka kwenye dhahabu; hatuzitaki kwenye kahawa? Sasa ni lazima tutengeneze mkakati hata wakulima wetu wafaidike kama ambavyo tunataka wafaidike kwenye mazao mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wito wangu mwingine, kwa nini minada ifanyike kwenye Mikoa ya Kilimanjaro? Hii nairudia kwa mara nyingine. Hii ikifanyika kwenye mkoa husika kama Kagera, itasaidia kuondoa gharama za usafirishaji zinazohusika kwa ajili ya kufuata mnada wa Kilimanjaro.

MHE: INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Unapewa taarifa na Mchungaji.

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nimpe taarifa mchangiaji anayechangia kwamba kuna jambo ambalo amesema kuwa Vyama vya Ushirika ndiyo wanunuzi wa kahawa. Vyama vya Ushirika siyo wanunuzi wa kahawa, ni wasimamizi; na suala la mnada limekuwa likifanyika Mkoa wa Kagera. Mwaka 2019 limefanyika na wanunuzi wote waliwatangazia wenye bei nzuri wakanunue. Pamoja na hizo changamoto zilizopo kwenye kahawa, lakini minada imefanyika Kagera, lakini Vyama vya Ushirika siyo wanunuzi, ni wasimamizi.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nadhani anaji-contradict.

SPIKA: Anakwambia Jimbo limejaa. (Kicheko)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nami nataka kukwambia hii ni pressure ya Jimbo na nimelikalia hasa! (Makofi/Kicheko)

Hiyo ni pressure ya Jimbo na ninalikalia hasa!

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Tukutane kazini. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Malizia, malizia, bado dakika moja.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

Mheshimiwa Spika, bado kama Serikali mna nafasi ya kuwasaidia wakulima wa Mkoa wa Kagera. Msiwaletee fedha, msiwaletee dhahabu, tusaidieni kwenye zao letu la kahawa, tupatieni soko, lakini ruhusuni biashara huria. Mbona maeneo mengine biashara huria inafanyika? Bodi ya Kahawa itabaki kama refa iangalie nani anacheza rafu; na lengo kubwa ni kuwasaidia wakulima wetu waweze kufaidika kwa mazao yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kupata fursa hii, nimshukuru Mwenyezi Mungu na familia yangu na chama changu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme suala la ardhi kwa Dar es Salaam halijaonekana kupewa kipaumbele kama inavyostahili. Ndugu zangu sote tunajua Dar es Salaam ndiyo Tanzania, wote tunajua changamoto zinazoikuta Dar es Salaam zinasambaa katika mikoa mingine. Dar es Salaam ikiwa mbovu, Dar es Salaam ikiwa ndiyo chanzo cha migogoro, Dar es Salaam ikiwa haitamaniki, tunategemea kwamba sura ya Tanzania itapotea. Ndugu zangu tunavyoongea leo Dar es Salaam ambayo ina population zaidi ya watu milioni nne inatumia master plan ya mwaka 1977. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeendelea kukosa master plan mpya tukitumia master plan ya population iliyokuwepo wakati ule, leo miaka mingi inayofuatia tunatumia plan zile zile. Maeneo yameendelea kuwa machache, watu wamevamia maeneo yote yale yaliyokuwa wazi, maeneo ya mabondeni, maeneo yamekwisha Dar es Saalam imegeuka jiji ambalo siwezi kujua hata nilisemaje. Naona changamoto kubwa zinazotokea hapa ni kutokana na kushindwa kwa Wizara ya Ardhi kusimamia kikamilifu kitovu cha ardhi ambacho ni Dar es Salaam.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina kilio kikubwa cha wananchi wa Msimbazi, mimi ninatokea katika Mkoa wa Ilala, naongelea Ukonga, naongelea Ilala, naongelea Segerea. Tunapita pale mto Msimbazi, mto ule una ukubwa wa hekari takriban 1,900 ume-cover eneo kubwa la makazi na katika Jimbo la Segerea ni Kata sita ambako kuna wakazi takriban 3,000. Mheshimiwa Waziri haya ni majina ya wakazi ambao majina yao yaliwekewa X, hawa wananchi wameishi mabondeni kuanzia miaka ya 1970, wameishi katika bonde la Mto Msimbazi likiwa bado ni bonde dogo. Nasema mto Msimbazi una ukubwa kuanzia Pugu kuja mpaka daraja la Salander, ni eneo kubwa sana takriban ekari 1900 kwa hiyo ni wakaazi wengi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati ule walikuwa wananchi wachache na bonde lilikuwa dogo kwa sababu baada ya muda bonde limeendelea kupanuka, kwa hiyo wakazi wameendelea kuwa wengi, lakini bonde limeendelea kula sehemu kubwa ya makazi ya watu.
Mheshimiwa Mwenyekiti mwaka 1972 Serikali ikaridhia kwamba watu wanaoishi katika mabonde au kwenye squatter areas watambulike kama makazi halali na wananchi wangu katika Jimbo la Segerea na maeneo mbalimbali wakatambuliwa ndiyo maana wengine wakaja kuwa na leseni za makazi. Mheshimiwa Waziri mwaka 1979 eneo lile linakuja kuwa declared kwamba ni hazardous area bila kuangalia kwamba kuna watu walikuwa wanaishi pale ambao wanapaswa kuhamishwa kupelekwa sehemu nyingine. Hiyo compensation na kuwaondoa haikufanyika, wananchi wakaendelea kuishi katika eneo hilo. Kuanzia mwaka 1972 imehalalishwa, mwaka 1979 mnasema ni hazardous area bila kusema watu mnawa-locate wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi tukasikia Waziri wa Mazingira Mheshimiwa January Makamba kupitia NEMC wakaenda wanabomoa, wakaenda wanaweka X katika maeneo ya watu ambao wamekuwa wanaishi pale hawajapewa fidia, bonde limepanuka, ilikuwa ni mita 60 leo watu karibu wote wanajikuta kando kando mwa mto kwa sababu mto umepanuka bila kuwapa fidia. Hawa wananchi, Waziri wanaoteseka na kufukuzwa na kuwekewa X wasijue pa kwenda, ni watu ambao wanalipa kodi kwenye Wizara hii, ni watu ambao Wizara inawatambua kama wakazi halali kwa maana wana leseni za makazi. Sasa tunaomba tujue huo mkanganyiko umekaaje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnadhani ile ni hazardous area na wale ni wananchi halali kwamba wamepewa leseni za makazi tunaomba wapewe fidia. Nimeendesha kesi pamoja na wananchi wangu bahati mbaya kesi yetu imetolewa mahakamani kwa kukosa procedure lakini tunaamini Wizara kupitia kwa Mheshimiwa Waziri haki ya wananchi wanaoishi katika Mto Msimbazi inapaswa kupatikana.
Mheshimiwa Mwenyekiti,Kama tunadhani yale makazi sio halali na sisi pia tunakiri kwamba siyo makazi halali wapewe maeneo mbadala wakajistiri. Kupata ardhi Dar es Salaam ni kazi kubwa sana wote mnajua. Ardhi imepanda thamani lakini pia wanaoishi kule ni watu ambao wana maisha duni. Tunavyowaondoa tunataka waende wapi kama hatuwapi makazi mbadala? Hilo ni la kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili kuna wakazi wa Kipunguni, Kipunguni B na Kipunguni Mashariki, nimefurahi kwamba huo mgogoro umeshafika kwa Waziri na natamani huo mgogoro ufanyiwe kazi kwa sababu umedumu muda mrefu. Huo ni mgogoro kati ya wananchi hawa tangu mwaka 1997 wakipambana na mamlaka ya Airport ambayo ilifanya tathmini ya kiujanja ujanja , ikiwakumbatia watu wachache na kuwapa vihela ambavyo tunaviona kama hongo na kuwahamishia maeneo ya Buyuni ambako walipelekwa na kule hawakupewa viwanja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hapa tuna wananchi wa Kipunguni A na Kipunguni Mashariki ambao wanaishi katika eneo ambalo unaambiwa ni Mamlaka za Airport hawaruhusiwi kuendeleza hayo maeneo, lakini wale wachache ambao wamekuwa reallocated wamepelekwa Buyuni bila kupewa maeneo ina maana wamekuwa dumped pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu mwaka 1997, 1998 watu wanaishi kwenye mahema katika maeneo yale. Wanawake wanateseka, watoto wanateseka na Serikali ipo. Mamlaka nyingi zimejaribu kuingilia akiwepo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ikiwepo mimi Mbunge, wakiwepo Madiwani mbalimbali lakini huo mgogoro umeshindikana na wale wananchi ni wanajeshi wastaafu waliotumikia nchi, lakini bado wameendelea kupigwa danadana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kesi yangu ya tatu naongelea viwanja vya wazi, Dar es salaam viwanja vyote vya wazi vimevamiwa. Waziri Lukuvi amegawa ramani za ardhi katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam, asilimia 80 maeneo ya wazi yamevamiwa na maofisi ya CCM, yamefanywa kuwa pupping place, kama Mheshimiwa Waziri ametoa ramani anatusaidiaje ili hayo maeneo ambayo yamekuwa allocated ni ya wazi yarudishwe kwa umma? Tunataka kufanya maendeleo sisi, tunataka watoto wakapate viwanja vya kuchezea, tunataka kujenga vijana wakafanye ujasiriamali kwenye maeneo husika. Tunaomba maeneo yarudishwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo mengine ya wazi mfano mdogo ni kutolewa kwa eneo la Coco Beach, Mheshimiwa Waziri tunaomba atueleze eneo la Coco Beach limeuzwaje? Wakati Dar es Salaam nzima watu wote tunakwenda kupumzika Coco Beach leo anapewa mwekezaji katika misingi ipi wakati Mheshimiwa Waziri akiwa Waziri. Tutaomba tupewe majibu ya msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kitu cha tatu au cha nne ambacho ni kero kubwa ni utozaji wa gharama inaitwa gharama ya premium katika ku-process hati za ardhi. Hiyo gharama imekuwa ni kubwa ambayo ni seven point five katika kila anaye-process umilikaji wa ardhi anapaswa kulipia. Hiyo gharama inaendelea kuwa kubwa na kuzidi ku-discourage watu kupima maeneo au kurasimisha maeneo na wakishindwa kurasimisha maeneo maana yake Serikali itakosa mapato. Kwa hiyo, ni lazima tuangalie ni akina nani wanakusanya hiyo pesa? Hiyo pesa inakwenda wapi? Naomba Waziri aje na majibu hayo ya kuridhisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni mgogoro wa msitu wa Kazimzumbwi ambao uko katika Jimbo la Ukonga. Huo mgogoro upo tangu mwaka 1994. Watu wakigombania mipaka, wananchi wanagombania mipaka dhidi ya hifadhi ya maliasili, maliasili wanakataa kutambua mipaka ambayo imewekwa na Manispaa pamoja na Wizara kuwa imetambua lakini Maliasili wanakuja leo wanasema hatuwatambui. Uhusiano wa wananchi pamoja na hiyo hifadhi imekuwa ni wa shida sana, wanaotoka kwenda upande wa pili wanawake wanabakwa watu wanapigwa mapanga imekuwa ni changamoto…
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Tunachojadili hapa tatizo letu ni mkataba au ni terms za mkataba? Tukigundua tofauti, kama tunaona terms za mkataba hazitu-favour, tunafanya nini tuwe na terms zinazotu-favour? Tatizo letu ni kukataa au tatizo letu ni ku-argue? Are we arguing or we are complaining? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunachofanya tujitambue kama Taifa, are we in a position to set terms tunazozitaka? Hicho ndicho tunachopaswa kufanya kama Wabunge. Tusitake kukaa hapa kwa vile watu wamekuja, wakatuambia mkataba ni mbovu, basi kila anayesimama anasema mkataba ni mbovu. Let us talk of the issues, mkataba ni mbovu katika lipi? Mkataba ni mzuri katika lipi? Hapo tuta-set tofauti ya kuwa na Mbunge na kuwa shabiki wa kuambiwa sema moja, mbili, tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ya pili tunayopaswa kujua, huu mkataba unasainiwa between blocks; tunaweza kuongea na member states wetu katika block yetu ya East African countries tuka-negotiate the terms. Wanashindwa kukaa kuongea na sisi kwa sababu we always have fear of the unknown. Tuna-fear, tuna-complain, hatuko comfortable hatujielewi. Kenya ikiongea tunajua wanashirikiana na mabepari kwa ajili ya ku-colonize. Taifa lingine likiongea sisi hatuwezi kujisimamia kama nchi? Tutaanza lini kujisimamia? Tuwashawishi sasa member states, the East African blocks twende forward tuwaambie these terms so far are not favourable, we want (a), (b), (c). (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama haitoshi, swali ambalo tunapaswa kuongea leo, tuna bilateral relationship between Kenya, Uganda na nyingine East Afican States, tunakaa humu ndani, tunawa-brand Kenya kama watu wanaotaka watu-colonize halafu Mheshimiwa Rais anaenda kushinda Kenya, anasema those are our brothers and sisters. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, nakumbuka katika hii summit ya East Africa, Museveni aliwaambia, let us not punish the Kenyans simply because they are one inch taller. Tutakuwa tunafanya makosa. Tuongee na Kenya with terms, you guys look here, kwa kusaini huu mkataba, sisi tutapoteza kwa kiwango hiki, mnaonaje? Tunaweza ku-negotiate vipi tu-compensate hii deficit? Instead of arguing, tuna-complain humu ndani. Tujipime upya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kukataa kwa matusi na vijembe, vinahatarisha hata urafiki wetu na Kenya, Uganda, Rwanda na bado hatuna terms tunaleta mezani, tunataka moja, mbili, tatu. Niambieni tunataka nini zaidi ya ku-complain? (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, tukimaliza sasa tujiulize swali, tunagombana na Kenya au tunagombana na Europen Union? Tukikaa sasa kama block ya East Africa ndiyo tutaenda kupambana sasa na European Union between the terms we want to have. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hiyo ndiyo tofauti tunayochangia hapa, tuseme tuna-complain kuhusu mkataba; tunasema tusaini mkataba au tusaini terms? Tusisaini terms; tusisaini mkataba, tusaini terms. Tuwaambie we want (a), (b), (c). Tukizileta hapa, tutasaini na siyo mkataba tunaousema.
Mheshimiwa Spika, nadhani watakuwa wameelewa. Tutofautishe ushabiki na issues. Let us talk of the issues, tusiongelee propaganda.
Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni kwa namna gani mfumo wetu wa elimu unaomuandaa kila mwanafunzi kwenda chuo kikuu, unawaandaa vijana kuingia katika mfumo wa Tanzania ya viwanda kama tunavyojadili Tanzania ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, mhitimu wa chuo kikuu wa Tanzania ni mwanafunzi wa aina gani? Mtu aliyefuzu katika sera ya policy maker ndiyo huyu anaenda kwenye utaalamu wa kuendesha na kusimamia viwanda (uchumi wa viwanda). Nashauri mfumo wa elimu yetu ubadilike kabisa, kuwepo na mjadala wa kitaifa, watu waseme tunahitaji wahitimu wa namna gani. Mfano, tunaweza kuwa na mfumo wa darasa la kwanza mpaka la nane, then miaka miwili au mitatu ya kum-train mtu katika ujuzi fulani (specific areas of interest).

Mheshimiwa Mwenyekiti, mjadala wa kitaifa juu ya hatma ya watoto wanaopata ujauzito na ikabainika hawakujitakia (victims) wapewe nafasi ya kurejea shuleni badala ya kinachoendelea sasa hivi. Tafiti zinaonesha kuwarejesha watoto hawa shuleni (waliozaa) hakujaongezea idadi ya wanaopata mimba shuleni, hili suala badala ya kufanya siasa jamii ipime na kuamua kwa kutumia case studies za nchi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuharakishwa kwa vitabu vya kiada katika ngazi zote ili kutengeneza uelewa wa pamoja, mada za vitabu hivi pia zi-reflect mazingira na mahitaji ya Taifa na utandawazi kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masharti ya usajili wa shule uzingatie huduma muhimu za wanafunzi ukiwemo uwepo wa miundombinu ya maji, vyoo vya uwiano sawa kwa wanafunzi na madarasa, kuliko tunachokiona leo. Asilimia 60 – 70 ya shule hasa za Serikali hukosa miundombinu, hivyo kuwa kero kwa wanafunzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishwaji wa chuo cha ualimu na vyuo vya ufundi katika Wilaya mpya ya Kyerwa, eneo hili lina vijana wengi lakini hakuna chuo chochote wala high school ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubagua wanafunzi wa kupewa mikopo kwa kigezo kuwa ametokea shule nzuri sekondari, wanafunzi hawa hawatendewi haki. Pengine walibahatika kupata mfadhili katika hatua hizo. Kwa kuwa huu ni mkopo hawatendewi haki kunyimwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, madeni ya walimu na wahadhiri. CAG ameainisha kuwa Chuo Kikuu cha Ardhi kinadai malimbikizo ya mishahara ya walimu na marupurupu yao, hii inapunguza morali kwa watumishi hao, Wizara iombe Serikali kulipa madeni hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sera ya elimu bure. Sera ya Elimu Bure haitekelezeki kwa kuwa changamoto ni kubwa sana katika maeneo ya shule hizi, madai ya wasichangie ni mufilisi, pengine kauli mbiu ingebadilika na kuwa changia elimu bure iwe bora, wazazi wangeshiriki kwa chochote kuboresha mazingira ya kufundishia (miundombinu) vyoo, madarasa, vyakula na kadhalika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mchango wangu utajikita katika sekta binafsi ambavyo zimechangia katika uchumi au katika pato la Taifa. Ukiangalia tathmini ya mpango wa pili wa miaka mitano unaokwisha imeeleza bayana kwamba, sekta binafsi haijafanya vizuri kwamba, mchango wako ni chini ya asilimia 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, na ninataka nioneshe masikitiko yangu kwasababu sisi leo sio nchi tena ya ujamaa kwa hiyo, tunahitaji sekta binafsi iweze kuchangia, ili tuweze kuona mabadiliko katika uchumi wa nchi hii. Na ukiongelea sekta binafsi ni pana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukiongelea leo, wengi wakisimama hapa wanaongelea kilimo…

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: …kama kilimo kinafanya vizuri, kilimo ni sekta binafsi.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia Theonest kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Charles Mwijage.

T A A R I F A

MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda nimpe taarifa mzungumzaji. Tanzania ni nchi inayofuata siasa za ujamaa na kujitegemea. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia Theonest nunapokea taarifa hiyo?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Sijui bado kuna nafasi za uteuzi au? (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaelewa mchango wa sekta binafsi kama tukiandaa mazingira mazuri ya watu binafsi, ya wafanyabiashara kufanya kazi katika mazingira wezeshi wataweza kuchangia sana katika uchumi wa nchi yetu. Nimeainisha kuna baadhi ya changamoto nyingi ambazo huwa tunaziongea hapa na zote zinafahamika zinazoikuta sekta binafsi.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mlolongo wa tozo, tozo ni nyingi kila mmoja anajua. Tunakuja usumbufu na mlolongo wa kupata vibali, kila mmoja anajua sitaki kueleza, lakini ambacho nataka nongelee specific ni upatikanaji wa mikopo. Sekta binafsi itawezaje kufanya biashara au kujiendesha bila mikopo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto ya riba kubwa ya mikopo, nilikuwa napitia Taarifa ya BOT katika mwaka wa 2027 walifanya review ya riba za benki na wakawashushia kutoka asilimia walizokuwa wanatoa, leo wako asilimia 12, tisa mpaka asilimia tano kwa mwaka 2020 review ya mikopo ambayo wanapata, lakini ukienda kwenye benki specific wananchi wafanyabiashara wakienda kuchukua mikopo wanachukua kwa shilingi ngapi? Huwezi kupata hata kwa asilimia 11. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe mfano mwingine wa kawaida; wataeleza sababu za kuweka riba kubwa waseme risk ni kubwa. Nimesoma pia kwenye ripoti anasema mikopo chechefu imeanza kupungua imetoka asilimia 11.6 imeenda mpaka asilimia 11.1 japo projection BOT wanasema ifike mpaka asilimia 5. Ni kwa nini tunakuwa na mikopo chechefu?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu riba zinakuwa juu. Watu wanakopa fedha, biashara ni ngumu, automatic wata-default. Niiombe BOT niombe kuangalia au ku-review sera yake ya fedha kuangalia namna ambavyo watawalazimisha mabenki waweze kushusha riba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitatoa mfano mwingine, na-declare interest, ni Mbunge na mnufaika wa mikopo, lakini mfano benki zikiwakopesha Wabunge, Wabunge ambao wana mishahara mikopo yao inakatwa automatic. Yani resk ya ku-default kwa watumishi au watu walioajiriwa ni ndogo kwa nini riba hazishuki? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni lazima hili suala tuliangalie kama tunataka ku-favor sekta binafsi ziweze kufanya vizuri, ziweze ku-access mikopo na ni lazima mikopo iweze kushuka riba. Otherwise watakuwa wanachukua fedha benki wanafanya kazi za kwenda kusaidia benki na sio kuweza kupata kipato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini changamoto nyingine, changamoto ya vitambulisho vya NIDA. Ukienda kama mfano wilaya ninayotokea mimi, kuna mtu aliongeaongea hapa nataka nimpe taarifa; Kyerwa ninyi leo tumepata Rais wa Tanzania Kyerwa walikuwa tayari na Rais mwanamke kwa hiyo, Kyerwa wana Marais wawili wa Tanzania, mmoja Mama Samia mwingine sio mwingine ni mimi na yeye anajua. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Hoyo hoyo!

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nikiongelea changamoto ya vitambulisho vya NIDA naihusianisha…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia, ngoja tuelewane vizuri. Ulikuwa unagombea ubunge ama urais, ili tuelewe ni urais gani unaouzungumzia?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nagombea ubunge. Sasa ubunge ukishafikia level kubwa wanakuita Rais, yaani unakuwa Mbunge Rais. Rais wa jimbo. (Makofi)

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nimeeleza changamoto ya NIDA. Naeleza changamoto ya NIDA…

NAIBU SPIKA: Kuna Taarifa Mheshimiwa Anatropia. Mheshimiwa Innocent Bilakwate.

T A A R I F A

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kunipa nafasi nimpe Taarifa Mchangiaji anayeendelea, Mbunge wa Jimbo la Kyerwa anaitwa Innocent Sebba Bilakwate na Mbunge huyu alimzidi huyo mchangaiji kura 15,943. Kwa hiyo, nampa Taarifa Mbunge anayetambulika ni Innocent Sebba Bilakwate, yeye ni wa kupewa tu. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Aanatropia Theonest unaipokea Taarifa kutoka kwa Mbunge wa Kyerwa?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee. Ukiona mtu anajaribu kuji-justify anajua hajiamini na ha-deserve. (Makofi)

WABUNGE FULANI: Hoyo hoyo hoyo!

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, naongelea changamoto ya NIDA nikihusianisha na vikwazo wanavyopata sekta sekta binafsi. Na nitaongelea specific Kyerwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na nieleze nitakuja hapa nitatumia kanuni kuomba nitoe maelezo binafsi ya Mbunge juu ya changamoto ya watu wa Kyerwa ya ukosefu wa vitambulisho vya NIDA. Hawawezi kupata mikopo kwasababu, ukienda kujaza fomu ni lazima uweke namba ya kitambulisho cha NIDA. Hawawezi kupata bima za afya, wale watu wanafanyaje? Na ile ni mikoa ambayo inapatikana mpakani kila siku unaambiwa wewe ni raia, wewe sio raia; hapo unafanyaje biashara katika mazingira hayo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niombe Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa, ni msimamizi wa jumla aiangalie Kyerwa kwa jicho la upekee hasa suala la vitambulisho vya NIDA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tukitoka hapa nitaeleza kitu kingine. Leo kila mmoja mwenye simu tulioko humu ndani kama kuna server inaweza ikawekwa hapa unaweza ukafanya tathmini ni watu wangapi wanafanya miamala. Leo miamala ya fedha haifanyiki kama luxury, sio starehe, ni biashara. Watu wanafanya biashara, tuko ndani hapa biashara inaendelea, lakini tukirudi kwenye swali bank charges za hiyo miamala ya fedha ni kiasi gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, amekuwa analisemea mara nyingi sana. Kwamba, nikitumia simu yangu nimefanya muamala hapa, sija-consume, sijatumia huduma yoyote ya benki wala mtumishi ni kwa nini nakatwa fedha nyingi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo pia ipo kwenye miamala ya simu. Nimesoma kwenye ripoti ya BOT wamesema hivi, kwenye sera yao wamesema, kuna miamala takribani wamesema milioni 145 ambayo imefanyika katika interval tofauti ikihusisha amount zaidi ya five billion, lakini pia imehusisha watu zaidi ya milioni 22, unaona kwamba, ni idadi kubwa ya watu wanafanya biashara ya mitandao ya simu. Kwa hiyo, niiombe Serikali, nimuombe Waziri Mkuu kuangalia namna gani wanaweza kushusha zile charges za simu ili watu wengi waweze kufanya biashara ili iweze kupunguza gharama ya ufanyaji wa biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa mara nyingi nikiongelea hapa ninasema hivi kama Taifa tumekuwa tukitumia new industrialized nation kama modal. Zile tiger nations kama modal ambazo zimejikwamua kutoka kwenye nchi za ulimwengu wa tatu kuwa ulimwengu wa pili na leo ni nchi zilizoendelea, sisi kama Tanzania tumekuwa tukifanya nini? Miradi mingi ambayo tumekuwa tukiifanya ni kiradi isiyogusa watu wengi, ameeleza Mbunge mmoja hapa, lakini pia modal tunazozitumia ni sahihi?

Mheshimiwa Naibu Spika, humu ndani kulikuwepo na sera wakati fulani wanasema sasa ni kilimo kwanza, wana magari yako branded kila kitu kilimo kwanza, lakini leo tunasema viwanda. Hivi kuna viwanda bila kilimo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani nataraji nione nguvu kubwa ikiwekezwa kwenye kilimo, lakini kwenye taarifa ambayo amewasilisha kwenye mpango aliowasilisha Waziri wa Fedha ameeleza kwamba, kilimo kimeshuka. Tena nimesoma kitu ambacho kimenisikitisha amesema hivi, ameeleza kwamba, kilimo kimeshuka kwasababu sitaweza kuiona kwa haraka, kimeshuka kwasababu watu wamewaza alternative; yaani watu wameamua kuwekeza kwenye vitu vingine, lakini hii nchi leo zaidi ya watu asilimia 80 wana-rely kwenye kilimo. Ina maana kama tunashindwa kuwezesha kilimo na viwanda itakuwa ni mjadala tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nisipoongelea kahawa kwa watu wa Kyerwa hawatanielewa. Hii ni zaidi ya mara 15 na katika mijadala yangu nitaongelea kahawa. Ninaongelea kahawa kwasababu, kuna shida, kungekuwa hakuna tatizo nisingeongelea kahawa; bado kuna changamoto ya soko bado kuna changamoto ya vyama vya ushirika. Na hapa nitamgusa ambaye anahusika na uwekezaji na hiyo niseme ni changamoto nimesoma kwenye bajeti Fungu Namba 11 lililoanzishwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji limetengewa bilioni 7 ambayo wamesema ni asilimia 0.02 kwenye bajeti kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka leo twende kwenye uchumi wa kati sasa, sio kati chini, lakini Wizara au fungu la uwekezaji bado lina bajeti ndogo. Nadhani hata kamati wameeleza, wameeleza vizuri kabisa kwamba, hili fungu liwekewe hata fedha ya maendeleo, hilo fungu liwezeshwe ili liweze kufanya kazi nzuri. Kama tunataka kwenda kwenye uchumi wa kati tunavyofika 2025 basi hayo maneno yawe reflected kwenye vitendo. Kwenye vitendo sio kuongea hap ani fedha iende na ionekane ikiwa inaenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mwisho kabisa japo sio kwa umuhimu ni kuwashukuru ndugu zangu. Mungu awabariki, karibu Kyerwa baba. (Makofi/Kicheko)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru lakini pia nishukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia hotuba ya bajeti. Ninachangia hotuba hii ikiwa inaingia kwenye rekodi. Hotuba ambayo kwa mara ya kwanza tunapata Rais Mwanamke. Nadhani imekuwa ni ndoto ya zaidi ya miaka 50 kwa Taifa letu, kwa wanawake lakini kwa watu wote wanaoamini katika mabadiliko na kwa watu wanaoamini katika 50/50. Kwa hiyo, ninamshukuru Mungu leo ninakuwa sehemu ya historia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mama yetu, ameanza vizuri. Ameanza vizuri nadhani ni kazi yetu Wabunge kumshauri, ni kazi yetu Wabunge kumtia moyo, na ni kazi yetu kumuelekeza pale tukiona mambo hayaendi vizuri. Hiyo, niseme ni moja kati ya commitment yangu mimi pia kama Mwanamke kuelekeza, kutumia mamlaka niliyopewa ya Katiba kama Mbunge kuishauri na kuielekeza Serikali na mimi niseme nitamshauri Mama yangu kama alivyosema kwa staha kuhakikisha anafanya vizuri. Akifanya vizuri, wanawake tutafanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwa kusema malengo tuliyokuwa nayo ya kuwa na Tanzania ya Uchumi wa Kati, malengo tuliyokuwa nayo ya mipango ya miaka mitano, miaka 25 yanaweza yasifikiwe kwa sababu uchumi wetu hauendi kwa namna ambavyo tulikuwa tunatarajia. Uchumi ambao ulitarajiwa katika mwaka 2021 uwe unaenda kwa asilimia Nane mpaka asilimia kumi leo unaenda kwa asilimia Nne (4). Kwa hiyo, matumaini yetu hayawezi kufika kama watu wanavyotaraji. Kama matumaini hayawezi kufika yale ni lazima tuyabadilishe au tuone namna gani tunaweza kubadilika ili tuendane na mabadiliko yaliyoko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na mpango wa kuhakikisha kipato cha Mtanzania kinafikia at least by 2021 dola 1,500 ambayo ni shilingi 3,469 lakini in reality ni kwamba haiwezekani. Leo kipato cha kawaida ni sawa na shilingi 2,557 ambayo ni dola 1,080. Kwa hiyo malengo hayawezi kufikiwa na sababu zimeelezwa ni kutokana na ugonjwa wa corona. Lakini, nitarudi kusema hatuwezi kuwa na mabadiliko ya msingi kama idadi kubwa ambayo tunapaswa kuwaleta on board ambao ni wakulima hawajafikiwa kwa kiwango kikubwa. Wote tutakubaliana idadi kubwa ya Watanzania ni wakulima ambao ni zaidi ya asilimia 64 lakini ni kiwango gani tumewekeza kwenye kilimo? Ukiwasikiliza Wabunge wanaongea mara nyingi na tuseme maeneo mengi wengi tunatokea kwenye mashamba, kwenye vijiji, watalalamikia namna ambavyo kilimo kinaendeshwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna baadhi ya maeneo ambayo tunafanya vizuri kutegemea na asili zetu kwamba tuna mvua za kutosha na kadhalika lakini bado hatufanyi vizuri. Kuna watu wanalalamikia mahindi kukosa soko. Kuna watu wanalalamikia kahawa kukosa soko. Kuna watu wanalalamikia alizeti na mambo mengine. Ni kwa kiwango gani sasa wakati ambapo tunaona uchumi kwa trend ya Dunia hauendi vizuri tumejiandaa katika ku-exhaust kwenye masoko ili at least mazao ya kiuchumi ambayo tuliyonayo, mazao ya kilimo yaweze kufanya vizuri kwenye soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa msemaji mzuri sana katika zao la kahawa na ninaamini kama nchi tukiwekeza vizuri kwenye zao la kahawa tutaweza kufanya vizuri kama kilimo kwenye Pato la Taifa. Leo mchango wa kilimo kwenye Pato la Taifa ni asilimia 27, it’s just a peanuts. Ukiwa na watu wa zaidi ya asilimia 64 wanachangia asilimia 27 kwenye Pato la Taifa then you have failed. Nadhani bado tuna kazi yak uji-stretch ili tuweze kuongeza mapato. Kama tunataka kufanya transformation ya uchumi wa Kati na Watanzania wa-feel kwamba wako kwenye uchumi wa kati tunapaswa kuwekeza kwa watu ambao ni wengi zaidi. Takwimu zinaonesha export ya kilimo ni asilimia 24. Narudia, t’s just a peanut, tunahitaji kufanya vizuri na tuna nafasi ya kufanya vizuri tukiamua kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshaongelea suala la kahawa na niseme leo ninavyoongea leo nimeongea na wakulima wa Kagera wa Kahawa, Uganda kilo ya kahawa ni zaidi ya shilingi 2,500 lakini waliouza kahawa Tanzania kule Kagera wanauza shilingi 1,200, siyo sawa! Ni lazima tuangalie ni namna gani tunaweza ku-trade katika hii biashara ya kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Uganda wanauza wapi ambapo sisi hatupaoni? Nchi nyingine zinauza wapi? Lakini siyo hiyo tu, nimeeleza humu ndani nikasema Uhganda na udogo wa Uganda wanalazisha tani zaidi ya 200,000 kwa mwaka lakini sisi tunazalisha tani 65,000 siyo sahihi! Wakulima wa kahawa wamekuwa frustrated wameacha kulima kahawa kwa sababu ya soko ambalo haliko promising. Lengo hapa ninalolisemea ni namna gani wale waliokuwa wengi wanaweza kuchangia kwenye Pato la Taifa na tutaona mabadiliko drastically kimsingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima wa mahindi wanalalamika, wakulima wa maharage wanalalamika, tunakosea wapi kama Taifa? Kwa hiyo, mimi niiombe Serikali i-exhaust namna ambavyo tunaweza kutumia masoko ya nje, i-exhaust namna ambavyo tunaweza ku-penetrate kwenye soko na nimeeleza mara moja hapa Bungeni, nikasema Duniani au Afrika Kahawa ya Tanzania inashika namba mbili kwa ubora. Kwa hiyo, bado tuna nafasi ya ku-compete kwa sababu tunazalisha kahawa iliyokuwa bora. Wakulima ambao nimeongelea ni zaidi ya asilimia 64 wanapata changamoto gani? Wakulima hawakopesheki kwa sababu ya aina ya kilimo wanachokifanya na hawakopesheki kwa sababu kilimo chenyewe kiko unpredictable, mtu amekopa fedha zake amewekeza kwenye kilimo lakini huwezi kupata soko huwezi kuuza, kwa hiyo automatic uta-default. Kwa hiyo ninafikiria ni lazima tuangalie namna gani tutaweza kuwasaidia wakulima waweze kukopesheka. Mmeanzisha Benki ya Kilimo lakini ni kwa kiwango gani Benki ya Kilimo imewezeshwa? Ni kwa kiwango gani Benki ya Kilimo inaweza kumkopesha hata mkulima wa kawaida? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija wale mnaowasema asilimia 64 ya wakulima lakini unakuta wanaokopesheka ni less than three percent kwa hiyo hatuwezi hata ku-achieve tunachokitaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu ya mikopo na nieleze, mfano kama Kagera, bado tuna fursa ya kufanya biashara. Nimekuwa nikiongelea masoko ya kibiashara ya Mrongo na Nkwenda. Hilo ni eneo jingine ambalo budget na niseme bajeti mwanzoni nilifikiria kwamba inategemea walipa kodi asilimia 20 lakini reality ni walipa kodi asilimia tano. Imagine walipa kodi asilimia tano kutegemeza nchi, ina maana the 95 percent wanaangalia asilimia tano, it’s not fair and the vice versa. Kama tuki-convert the 95 percent ambao ni wakulima na wengine tukawawezesha kufanya biashara kuwapa mikopo wakaweza kuzalisha wakalipa kodi hata mzigo wa wale five percent hautakuwa mkubwa. Kwa hiyo, masoko ya kitega uchumi ambayo yapo Murongo na Nkwenda yakiboreshwa tutaweza kufanya biashara vizuri na watu wa Uganda. Hiyo ni concern nyingine naileta ambayo sasa tunapaswa kuangalia katika sekta ya kilimo ili tuweze kuongeza tija. Hilo ni suala la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wale wakulima wa kawaida tunawasaidiaje waondoke kwenye umaskini? Nimeona takwimu, kuanzia 2016 takwimu za Serikali zinaonesha umaskini ulikuwa asilimia 28 point something na mliahidi kwamba by 2021 tutakuwa tumefika asilimia 16 lakini reality mabadiliko yamekuwa ni asilimia mbili tu, yaani umaskini umepungua kwa asilimia mbili tu. Hatuwezi kupata mabadiliko tunayoyategemea. Tunawezaje kusaidia kupunguza umaskini, mmefanya kazi ya kupeleka umeme vijijini kupitia REA, ni kitu kizuri na ni namna moja ya ku- stimulate uchumi wa vijijini kwa sababu umeme kama umeme bado unakuwa na impact kwa sababu hata wafanyabiashara watafanya mambo mengine ya kipato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nijiulize, ni kwa kiwango gani tumejiandaa miradi ya leo iwe sustainable. Leo tumepeleka umeme kwa kasi vijijini lakini huo umeme utakuwa na cost implication baadaye. Kuna nguzo zitadondoka, kuna mafuriko na vitu vingine. Kwa hiyo, tunavyopeleka umeme ni lazima tuangalie to what extent huo umeme utaendelea kuwepo pale vijijini. Lakini tukijiandaa na emergency zinazotokana na umeme, kunaweza kuwepo na radi zikaharibu miundombinu, lakini kunaweza kuwepo na shoti kutegemea na mazingira ya vijijini. Ni kwa kiwango gani tumejiandaa miradi hii ya umeme hairudi nyuma? Hilo ni swali la pili ambalo kama tutaweza ku-sustain tutakuwa tumeweza kupunguza umaskini katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho Mheshimiwa Waziri umeongea kwenye bajeti yako unafutaje msamaha kwenye vifaa vya umeme vinavyotumia umeme wa jua? Leo ukienda kwenye vijiji miradi ya REA ambayo inaelezwa imeenda vijiji zaidi ya 8,000 wakienda kwenye kijiji kimoja wanafunga umeme katika nyumba 20 tu na nyumba zilizosalia zinatumia umeme wa nishati ya jua - sola. Unavyoenda kuongeza kodi maana yake unawarudisha wale watu kutumia vibatari. Unawarudisha wale watu kununua mafuta ya taa. Unawarudisha kwenye maisha yale ambayo wakati tunazaliwa tuliyaona yako hivyo. Mimi ninashauri
Serikali, hebu tafuteni vyanzo vingine vya mapato hiki cha misamaha ya kodi msikiondoe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi na mimi niongee mawili, matatu kwenye suala zima linahusu watumishi. Tutakubaliana kwamba maendeleo yoyote, iwe ya nchi, iwe ya taasisi, iwe ya familia inategemea nguvu kazi, pale ambapo unakuwa na nguvukazi ambayo si tu hairidhishi lakini pia inakuwa imekatishwa tamaa na kulegalega, hata kwenye familia binafsi huwezi ukapata mafanikio. Tuangalie mfano mdogo wa private companies ni kwa jinsi gani zinaweza zikafanikiwa vis a vis The Government activities au government other things, unajua ni kwa nini? Kwa sababu wanaweza kuwa motivated.

Mheshimiwa Spika, nitaanza kutoa mfano mdogo tu Mheshimiwa Waziri ametuambia kwamba kuna watumishi ambao wanakuwa ni zaidi ya mwaka mmoja wanadai mishahara, tunategemea mtu afanyeje kazi anadai mshahara kwa mwaka mmoja, totally impossible! Mchukue mtu huyo huyo mpeleke kwenye private company au private business anaweza kufanya kazi bila kulipwa? Kwa nini tunapaswa ku-assume kwamba watu wanaweza kufanya kazi za umma wanaweza kufanya kazi Serikalini bila kulipwa na wakaendelea kufanya kazi? Tunaendelea kujidanganya.

Mheshimiwa Spika, nataka niseme Mheshimiwa Waziri na nitataka baadae nitatoa Shilingi atuambie ni kwa namna gani hili suala halitajirudia la Watumishi wa Umma kudai malimbikizo, kudai mishahara wakati huo huo tunategemea walete productivity, hicho kitu hakiwezekani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kabla sijaenda mbali nitataka niseme kwa kifupi kuna suala zima la TASAF. Kila mmoja anelewa umuhimu wa TASAF, na swali langu ninalotaka ku- pause ni kwa kiwango gani TASAF inaweza kuwa endelevu kama inategemea kuwa financed na donors au misaada kwa maana Wizara haitengi fedha kwa ajili ya TASAF? hilo ni swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili ni kwa nini TASAF imekuwa inatumika kama siasa kwenye maeneo yetu, huwa napokea simu nyingi sana wananiambia Mheshimiwa Mbunge nimetishiwa kuondolewa TASAF kwa sababu nimeonyesha nina interest ya Chama fulani. Mimi nadhani haya masuala yafikie mwisho, siyo mara ya kwanza linasemwa hapa Bungeni na siyo mara ya pili na siyo mara ya tatu unless Waziri atuambie kwamba TASAF inatumika kama kiboko kwa ajili ya interest za siasa za Chama Fulani. Nadhani ifikie mwisho na niseme bayana kama itatokea Watendaji wanataka kuwa-punish watu kwa sababu ya interest fulani za vyama na nini kwa kuwanyima TASAF hatutakubali, na tutakaa kuipinga sasa kwa sababu itakuwa haina tija au itabidi itengenezewe jina jingine kwamba hii siyo TASAF bali ni motivation ya kujiunga na itikadi fulani hilo naomba niliweke wazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuje kwenye suala zima la upungufu wa watumishi….

SPIKA: Mheshimiwa Anatriopia nieleweshe vizuri kuhusu jambo hili, kwa sababu niliwaona Wabunge hapa ambao ni wa Chama cha Mapinduzi na walisimama kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri maswali kuhusu TASAF kwamba kuna watu ambao hawamo na wanastahili. (Makofi)

Hii hoja ya kwamba ambao hawamo wanaokutafuta wewe lazima wahusishe hoja ya kutokuwemo na Chama fulani inatokana na nini labda au kwa sababu wewe ni wa Chama kingine kwa hivyo wakikupigia lazima kuna uhusiano na Chama chako. Kwa sababu nimeona nimeyasikiliza maswali hapa na Mheshimiwa Naibu Waziri amejibu maswali mengi sana kuhusu TASAF na hao ni Wabunge wa Chama cha Mapinduzi, hebu nieleweshe mimi ili nijue jambo hili limekaa vipi, Mheshimiwa nakuomba uendelee.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, katika maeneo ambayo tunatoka ukionekana una-element za Upinzani moja kati ya kitu ambacho wanaambiwa tutakutoa TASAF na the next month hapokei fedha, anachopaswa kukifanya ni kwenda kufuatilia mchakato ni wangapi wana uwezo wa kwenda kufuatilia mchakato kama akikubali imeishia hapo, lakini kama ni mtu fighter anasimama firm anapambana mpaka anarudishwa kwenye TASAF.

Mheshimiwa Spika, point ninayotaka ku-make…

SPIKA: Mheshimiwa Waziri nimekuona nitakupa nafasi. Unajua Mheshimiwa Anatropia mimi nisingependa Bunge hili lifikie mahali kwa sababu siku moja niliwahi kusema hapa hatuelekei kufanya maamuzi lakini sasa tunaelekea kufanya maamuzi ukituweka kwa sura hiyo, nimeuliza hivi Wabunge kuna Mbunge mmoja sema sikumbuki ni nani, aliyesema kwake kuna watu ambao wameondolewa kwenye TASAF wakati vigezo bado wanavyo ni nani? Ni Mbunge gani? nadhani Mheshimiwa Sekiboko pale na anatoka Tanga na yeye ni Mbunge wa Viti Maalum. Tanga hakuna Jimbo la Upinzani kule, sasa mimi nawaza kule wale wananchi wa Tanga aliowasemea anatoka Korogwe siyo? Hebu washa kisemeo. Ulisema ni Korogwe au ni wapi?

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Spika, ni Korogwe Mkoa wa Tanga, Korogwe Mjini.

SPIKA: Sasa Korogwe Wabunge wote wawili wa Wilaya ya Korogwe ni wa Chama cha Mapinduzi na kule wapo ambao walikuwepo na sasa wameondolewa kwenye mfumo na ndiyo Wabunge walikuwa wanasema wameondolewa kimakosa kwa sababu vigezo bado wanavyo. Hii hoja ya kwamba wanaokupigia wewe wameonesha alama pengine ama namna fulani kwamba ni wa Chama.

Waheshimiwa Wabunge, nisingependa Bunge lifikie hapo mahali na sababu ni za msingi kabisa, Wabunge wa CCM kama wanaongea na wewe unazungumza hoja yako ni ya msingi, kwamba watu wanostahili wapewe na wasiostahili waondolewe na vigezo vitumike vile vilivyopo, sasa ukiiweka kisiasa kidogo inakuwa mtihani. Hapo ndiyo shida yangu ilipo.

Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na mimi wito wangu ninaotaka kauli ya Mheshimiwa Waziri aseme bayana watu wasionewe au wasipewe kwa sababu iwayo yoyote na kigezo kibaki kilivyo leo. Haya maeneo tumetofautiana uelewa. Korogwe wanaweza kuwa waelewa na eneo jingine vipi maeneo ambayo wengine tunatoka? Ndiyo nataka kauli iwe firm kwamba mtu apewe TASAF kwa sifa ya yeye kuwa na uhitaji wa TASAF full stop, hiyo ndiyo call yangu.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, nadhani hujanielewa vizuri, Mbunge wa jimbo unalotoka wewe ni wa Chama gani? Jimbo unalotoka wewe walimchagua Mbunge wa Chama gani?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, Tume ilimtangaza Mbunge wa CCM.

SPIKA: Ndiye aliyechaguliwa. Kwa hiyo, hoja ya kwamba walioko kule wakikupigia wewe ni wa CHADEMA hilo ondoa kabisa, TASAF hata Majimbo ya CCM yameulizwa maswali hapa ndani. Kwa hiyo, iondoe kabisa hiyo sijaelewa ambapo wewe hunielewi ni wapi. Ukiiweka tu kisiasa kwamba kuna mtu hapewi kwa sababu ya siasa humu ndani Wabunge wa CCM wameuliza maswali, ukisema kuna mtu anaondolewa kwa sababu ya kisiasa pia unakuwa hauko sawasawa kwa sababu Wabunge wa CCM wameuliza vivyo hivyo.

Kwa hiyo, wewe changia kwamba kuna hiyo changamoto kwenye TASAF na sote tumeisikia hapa, usiiwekwe kisiasa kwa sababu TASAF kwa maelezo mimi nikikaa hapa mbele nimewasikia na leo uzuri swali lilikuwepo hakuna mtu aliyeuliza swali kwamba kuna mtu alionyesha kadi ya chama fulani ndiyo akapewa au chama fulani ndiyo akanyimwa Hapana! Kwa sababu hata wewe nikikuambia uthibitishe huna uwezo huo. Ama unao Mheshimiwa Theonest ndiyo maana nilikuwa nakuwekea mazingira hayo mchango wako uwe wa jumla kwa changamoto za TASAF na siyo kwamba wenye changamoto wana viashiria vya Chama fulani hapana.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru niendelee. Naomba mchango wangu uwe jumla katika changamoto…

MHE. ROSE V. BUSIGA: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Ngoja kwanza Mheshimiwa Rose lazima uitwe kwanza ndiyo uanze kuzungumza. Mheshimiwa Anatropia kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Rose Busiga. (Kicheko)

TAARIFA

MHE. ROSE V. BUSIGA: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa taarifa Dada yangu kwamba kwa uzoefu nilionao kuhusu TASAF. TASAF wanapochaguliwa ni Kijiji husika, kinakuwa na Mkutano wa hadhara, Mwenyekiti wa Kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji wanapokuwa pale kwenye mkutano wanakijiji wenyewe wanajua maisha ya wenzao ndiyo wanachagua pale. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia Theonest unaipokea taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, naendelea. Kwa sababu wakati mwingine haya mambo huwa yanashamiri sana ikifika wakati wa maneno mengi, nakushukuru sana niendelee.

Mheshimiwa Spika, kuhusu changamoto ya watumishi. Kuna changamoto kubwa na CAG ameainisha dhahiri kwamba kuna upungufu wa asilimia za kutosha, anasema silimia 35 tukiongela kwenye kada nzima ya elimu.

Mheshimiwa Spika, kwa tathmini ambazo kwa projection za kuwa na wanafunzi 50 mwalimu mmoja katika shule ya msingi, lakini mwalimu mmoja wanafunzi 20 kwa shule ya sekondari tumeona bado ni changamoto na hatuoni dalili ya kuifikia kama kuajiri bado kunaendelea kwa kusuasua. Hii hapa imekuwa na impact kubwa, nitatoa mfano. Katika taarifa aliyoitoa kwa mujibu wa ripoti ya CAG inaonyesha wanafunzi asilimia 66 wamepata Division Four mpaka Division Zero na hiyo inatokana na kwamba wanafunzi wengi hawajaweza kupata access ya mwalimu. Walimu hawajaweza kufundisha vya kutosha kwa sababu madarasa yetu ni makubwa na hiki ni kilio nikitoe kwenye eneo langu ambalo ninatokea kwenye Mkoa wangu wa Kagera hususani Wilaya ya Kyerwa, kuna changamoto kubwa ya walimu.

Mheshimiwa Spika, niombe katika uajiri unaoenda kuufanya katika ajira zilizotangazwa tupewe kipaumbele, moja haya ni Majimbo ya Vijijini hii nitoe ni general call, Majimbo ya Vijijini na maeneo mengine lazima yawe na motisha ukilinganisha na maeneo ya Mjini. Kwanza kila mtu anajaribu ku-avoid vijijini, iwapo mishahara ya walimu na watumishi wanaofanya kazi vijijini ikiwa juu pamoja na allowance za posho za kufundisha posho za maeneo inaweza kuvutia kwa wingi haya maeneo kuwa na walimu wa kutosha kinyume na hivyo.

Mheshimiwa Spika, pia tuna changamoto ya walimu wa kike ni maeneo mengi nchini. Walimu wa kike ni muhimu kwa sababu mkumbuke kwamba katika level ya chini wanafunzi wengi pia ni wa kike, wanahitaji assistance ya walimu wa kike lakini wanahitaji role models ya walimu wa kike. Tunawezaje kuwa-motivate walimu wa kike kubaki kwenye maeneo yetu. Moja ni lazima tuwaongezee posho, mbili ni lazima tuwape mazingira ambayo wanaona kwamba ni rafiki, nyumba za watumishi na maeneo.

Mheshimiwa Spika, nataka pia niongelee kukosa motivation kwa watumishi kama nimeeleza tangu awali nikianza na kuwa na malimbikizo makubwa ya mishahara, siyo hiyo tu hata wanaosataafu unatumikia leo una uhakika kwamba hata ukija kustaafu utalipwa posho zako na kiinua mgongo, hiyo michango yenyewe ambayo mamlaka na taasisi mbalimbali zimekuwa haziwasilishi zimekuwa ziki- accrue interest from time-to-time.

Mheshimiwa Spika, nataka nitoe mfano mmoja tu, kwa ajili ya kutopeleka hayo makato Halmashauri kadha wa kadha zimepata faini mfano mmoja Halmashauri ya Muheza ililipa twelve million, Biharamulo six million, Kaliua five million, Mlele five million, kwa ku-sum up zimetumika zaidi ya Billion 260 katika kulipia faini za kutokusanya michango. Sasa leo hatuajiri kwa sababu hatuna fedha lakini hizohizo fedha zinaenda kutumika kwa ajili ya interest za kutopeleka fedha za makato mbalimbali kwenye taasisi husika, na hilo ni swali la jumla ambalo naweza kulitoa hapa, tujiulize sisi kama Serikali mjiulize ninyi kama Wizara mnataka ku-achieve nini? Kusimamia watu kupeleka hayo makato ili msilipe interest na badala yake hiyo pesa ndogo tuitumie kuajiri watumishi? Au tubaki nazo mezani ili kesho tulipe interest? Kupanga ni kuchagua! (Makofi)

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu.

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Spika, nataka tu nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika mambo makubwa na mazuri yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita ni kuongeza motivation kwa watumishi na hasa kupitia haki na stahiki zao.

Mheshimiwa Spika, ninazo taarifa rasmi na ni za uhakika mwaka 2020/2021 Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati anaingia madarakani alikuta bajeti ya Watumishi kupandishwa madaraja ilikuwa ni watumishi 91,000 lakini mpaka Januari mwaka huu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amepandisha madaraja zaidi ya Watumishi 263,555. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakati Dkt. Samia Suluhu Hassan anaingia madarakani alikuta tatizo kubwa la malimbikizo ya mishahara, mpaka mwezi Januari Tarehe 30, alikuwa amekwisha kulipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi zaidi ya 116,000 katika Serikali hii. Kwa hiyo, ninachotaka kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge ni kwamba siyo kweli Serikali haioni umuhimu wa haki na stahiki za watumishi ili kuwapa motivation katika kufanya kazi zao za kila siku. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia unapokea taarifa hiyo?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kitu ambacho napaswa nikiweke wazi mtumishi kupandishwa daraja siyo hisani, ni kwa mujibu wa Kanuni na Utaratibu lakini pia ni increment kwa kazi aliyoifanya. Huwezi kuajiriwa leo ukalipwa sawa sawa na yule aliyekaa miaka Mitano, huo ni wajibu wa Serikali kupandisha madaraja ndiyo tunayaongea hapa.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia kuna taarifa nyingine kutoka kwa Mheshimiwa Halima Mdee.

TAARIFA

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, nilikuwa nampa taarifa Mheshimiwa Anatropia kwamba madai ya Watumishi wa Umma mwaka 2019/2020 ilikuwa Bilioni 334, mwaka 2020/2021 yakaongezeka yakafika Bilioni 429, taarifa ya juzi ya CAG inaonesha madeni ya Watumishi yamefika Bilioni 509, ni taarifa tu nilikuwa nampa Mheshimiwa.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia unaipokea taarifa hiyo?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, naipokea sana, na hilo ndiyo ninalolisema leo. Tunaweza ku- achieve tunachokitaka kama tuna right people on the ground. Ni lazima watumishi wawe motivated kwa kulipwa malimbikizo, kwa kupandishwa madaraja, kwa kulipwa fedha za uhamisho, kwa kulipwa posho kadha wa kadha ambazo zipo kwa mujibu wa utaratibu. Hivyo ndivyo watakavyofanya kazi. Tunakwama wapi? Nilikuwa naangalia clip moja inayoonesha ni namna gani nchi kama Singapore iliweza kufika ilipo. Jibu lilikuwa moja, lazima uwe na watumishi sahihi, ndiyo utaweza ku-achieve hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Seriakli za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nami niongeze machache ambayo Kamati yetu imeweza kuyaona wakati tukipitia hizi ripoti. Nitaanza kwa kuvuta kumbukumbu ya taswira ya Mheshimiwa Rais, siku napokea Ripoti ya CAG nitaenda kunukuu maneno aliyoyasema na kila mmoja aliyasikia na vyombo vyote vya habari viliandika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kusoma, anasema; “Invoice imekuja tunatakiwa kulipa dola milioni 88 unaliza mkataba ulisemaje, hii imetokea wapi? Unaambiwa vifaa vimepanda. Nauliza Mkataba wenu ulisemaje? Mtu anapopokea bila kuuliza, anailetea Serikali ilipe, stupid!”

Mheshimiwa Mwenyekiti, aliendelea kati ya maneno mengine aliyoyasema; “Miradi mingine ambayo tunaifanya inakuwa ni mikubwa ambayo matazamio yake yanajulikana.” Akauliza maneno na akasema; “oneni uchungu na fedha za Serikali, na hivyo vinafanyika kwa sababu kuna watu wanafaidika.” Akaenda mbele zaidi akasema; “Kuna sehemu tumezubaa, pengine kwenye primitive measures, hatuchukui hatua.” Mwisho wa kunukuu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeanza na hayo maneno kwa sababu siku hiyo Mheshimiwa Rais, anawasilisha hotuba niliangalia vizuri na nilimwangalia. Nikaona picha ya mama akionyesha machungu ambavyo anatambua ukubwa, utajiri wa rasilimali zilizopo kwenye nchi lakini zinapigwa na watu wachache. Kamati yetu ya PAC kama ilivyopitia LAAC, tumechukua masaa ya kutosha kukaa, kujadili zile ripoti na baadaye tunajiuliza tuweke nini, tuache nini, kwa sababu ni madudu bandika bandua. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya waliyoyataja wenzetu ni baadhi tu, lakini changamoto yetu kubwa haijawahi kuwa kwenye mifumo, haijawahi kuwa kwenye utaratibu, imekuwa kwenye kitu kimoja ambacho nimekitaja na kukiandika mara tatu, nikasema kutekeleza, kutekeleza kutekeleza. Utaratibu umeandikwa na umeainishwa vizuri, utaratibu wa kuingia, kuhama, kuheshimu na kutimiza matakwa ya Mikataba, tumekuwa hatufanyi hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu umeainisha nini cha kufanya, lakini Watendaji wetu wameacha kufanya yote tunayoyasema. Msemaji mmoja hapa ametueleza kilichotokea katika MSD nitatoa mfano na nitaueleza vizuri. Mtendaji na baadhi ya waliohusika kwenye MSD waliingia kwenye Mkataba na Kampuni moja ya kutoka Misri, ameitaja mwenzangu inaitwa Alhandasia ya kunua vifaa tiba. Ikatanguliza fedha zaidi ya bilioni 3.4 ika-deposit kwenye akaunti, akaunti inajulikana ambayo naweza nikakutajia hapa, ambayo jina la Akaunti inaitwa ASM e-trade, akaunti namba iko hapo 0045609416002 iko kwenye Benki ya Egypt Gulf.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya ku-deposit hizo fedha akijua moja ana-deposit hizo fedha bila ya kuona, ameshinda kandarasi, anapaswa kuonyesha at list uwezo wa ku-perform hizi contract, hajafanya hicho kitu, lakini pia hajafanya utafiti kuja kama ana-exist au ha-exist kwa maana hapati assurance ya benki, lakini ame-deposit zaidi ya bilioni tatu kwenye akaunti ya mtu. Wakasubiri zaidi ya miezi mitatu madawa hayaletwi. Wakaanza kui-consult hiyo kampuni inapatikana wapi, wakamtumia taarifa balozi wetu Misri, akatafuta hiyo kampuni haikujulikana kampuni iko wapi. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo kampuni kwa fedha ambayo wali-deposit ambayo ni bilioni 3.4, tulipaswa kupata aina 75 za madawa tofauti tofauti. Baada ya mkataba kushindikana ikabidi wa-recall kampuni nyingine na hiyo kampuni wakaiambia sasa tusaidie kuchukua hata yale madawa ambayo alipaswa kuleta huyu Alhandasia, tukuongezee kwenye Mkataba uweze ku-delivery akakubali kufanya hivyo. Sasa wakampa mkataba wa bilioni 10, lakini katika ku-delivery akaonyesha katika zile product ambazo alipaswa ku-delivery 75 katika hizo ame-delivery product 29 tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unaweza ukaona nini changamoto ambayo ameieleza mwenzangu. Tulifanya nini, tulifanya due diligence kujihakikishia kwamba hiyo kampuni ina-exist, tulikuwa na assurance performance ya contract na wale watu, hayo ndiyo yanafanyika katika kila item ambayo naigusa hapa. Changamoto ya hii nchi siyo fedha wala siyo uchumi, changamoto ni watendaji ambao wameamua kwa makusudi mazima bila kufuata kanuni na taratibu. Mheshimiwa Rais, akasema tumewanyamazia pengine tuchukue primitive measures, tuweze kuwawajibisha na nataka niulize hapa ni wangapi wamewajibishwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya mabilioni ya fedha yanayoongelewa leo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tukiona kwenye vyombo vya Habari, mtu ameiba zaidi ya bilioni kadhaa, trilioni kadhaa, lakini faini anayokuja kutozwa ni milioni kadhaa na umeshakuwa mtindo wa kawaida tu, iba bilioni utaenda kulipa faini ya milioni, hauwezi kuwa ndiyo mtindo wa maisha na tukaenda, hatutofika kokote kwa mtindo huo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hiyo haitoshi wakagundua chaka lingine na Mheshimiwa Mwenyekiti wa LAAC, ameieleza vizuri, kuna chaka linaitwa TAKUKURU. Sasa siwezi kueleza chochote kwa sababu sijui, lakini kwa mazingira yanayoonekana TAKUKURU ndiyo namna pekee ya watu kuficha madudu yao kwa sababu wanajua tutakagua kwa zaidi ya miaka 10, 15 na baadaye ushahidi utakosa na faili litafungwa na business as usually. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, miradi mingine ambayo imekuwa kwa Watumishi wa Umma ambayo wameisababishia Serikali hasara ni kuhamishwa katika hiyo idara hata haya tunayoyaongelea leo kwenye MSD wamehamishwa kutoka MSD wakapelekwa kwenye idara nyingine, hivi hilo lengo ni nini? kupeleka hasara kwenye maeneo mengine au kuendeleza kutuliza kila sekta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais, anazunguka kila sehemu kutafuta fedha, anahangaika na tozo kila maeneo, lakini kinachofanyika leo ni nini? Ni mifuko yote inavuja asubuhi, mchana na jioni, hatuwezi kwenda namna hiyo. Hivyo naungana na Hotuba ya Kamati zote tatu, pamoja na Kamati yangu hususani juu ya pendekezo la MSD, moja TAKUKURU kukamilisha uchunguzi, lakini pia ni lazima kuwepo na action za kimaadili kama kuna watu wamefanya makosa kwenye Serikali…

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri.

TAARIFA

WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana mchangiaji lakini naomba nimpe taarifa kwamba, wahusika waliohusika na ubadhirifu au uvunjaji wa taratibu za manunuzi chini ya MSD wameondolewa kabisa MSD Tarehe 22 Aprili, 2022. Mheshimiwa Rais aliteua Mkurugenzi mpya na sasa hivi mambo yanaendelea vizuri taratibu zilizobaki ni za kiuchunguzi wa TAKUKURU na vyombo vingine vya uchunguzi. Hatua zimeshachukuliwa tangu Aprili, 2022.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia unaipokea hiyo taarifa?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Bahati mbaya sana kwenye Kamati ambayo Mheshimiwa Spika alinipanga tunaongelea value for money.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukimwondoa katika nafasi yake ume-save shilingi ngapi, nadhani hoja ziwe baada ya ule ubadhirifu alivyovifanya tumeweza kuangalia alikuwa ana kiwango gani ambacho tumekiweka wakati kesi zikishughulikiwa, fedha za walipa kodi ziweze kuwa zimeokolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nadhani hiyo iwe spirit kwa sababu lengo ni kusaidia Taifa na lengo la Mheshimiwa Rais ni kuhakikisha anapata fedha za kuendesha nchi. Pia watu wanauliza alipelekwa wapi, karudishwa Jeshini kuendelea kufanya kazi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee pia suala la KADCO najua muda wangu utakuwa mchache lakini nilikumbushe Bunge lako tarehe 2 Novemba hapa mwaka jana iliongelea suala la KADCO pamoja na kutoa maazimio ambayo maazimio ya KADCO ni pamoja na KADCO kuwa chini ya Mamlaka ya TAA lakini hilo suala mpaka leo halijaweza kufanyiwa kazi, lakini hiyo haitoshi Baraza la Mawaziri lililokaa katika Kikao Namba 15 cha mwaka 2009 liliwahi kutoa maazimio ya kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro kuwa chini ya TAA lakini mpaka leo tunavyoongea miaka 14 baadae hakuna chochote kilichofanyika. Call yetu tunayoitoa ni lazima KADCO sasa iende kwa mujibu wa utaratibu unavyosema kwamba viwanja vya Serikali vitaendeshwa chini ya mamlaka ambazo zimeanzishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niishie hapo kwa hayo machache. Ninaunga mkono maazimio yote yaliyotolewa na Kamati yetu Tukufu. Nakushukuru sana (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nitaanza mchango wangu kwa kum-quote Nelson Mandela, muda wangu ni mchache sana, amesema; I learned that courage was not the absence of fear, but the triumph over it. The brave man is not he who does not feel afraid, but he who conquers that fear. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusemaje; tumefika hapa au tunalazimishwa kufika mnakotaka tufike sio kwa sababu hatuogopi, kwa sababu tunalazimishwa kutokuogopa tena. Humu ndani sisi Wabunge wa Upinzani nakumbuka ndio tulikuwa mstari wa mbele kuwatetea polisi, kutetea makazi yao, kutetea matatizo yao, lakini nini kimetokea; polisi wametufikisha hapa, polisi tulikuwa tunawapenda sana na tunawapenda lakini mnakokwenda baba mmepotea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upolisi ni taaluma na kama walipenda kuwa wanasiasa wangekwenda kugombea kama tulivyofanya sisi. Tunaamini wao ndio wanapaswa kututetea, tunaamini watu ni lazima wajione wako salama mikononi mwa polisi, lakini leo nini kinatokea; ukikamatwa na polisi huna uhakika kama utatoka salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Saguta Heche anakufa akiwa amefungwa pingu mikononi mwa polisi, Akwilina mtoto wa watu akisafiri kwenye daladala, anashutiwa na kufa na polisi na tunakuja kuambiwa hatujaweza kumtambua nani polisi kamuua kwa hiyo faili limefungwa. Mnatupeleka wapi ninyi watu? Tunawapa fedha kutoka kwenye kodi ya nchi hii, polisi tunawapenda lakini mlikotufikisha siko tulikokutamani. Narudia kusema tunaamua kuwa courageous sio kwa sababu sisi sio waoga ila kwa sababu mmetulazimisha kufika hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina case study ya polisi mmoja ambaye alimvamia mtu wangu wa karibu na Mheshimiwa Waziri nilimpigia simu nikakwambia mume wangu amekuwa attacked na polisi anayenifahamu mimi, anaishi kwenye mtaa wangu, yule polisi amemwonea yule baba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimetoa taarifa kwenye kituo kikuu cha polisi, nimekwenda mbali zaidi nimekwenda hata kwa Mnadhimu wa Polisi, bw. Matiko Central, barua ninazo hapa, tangu 2017 hakuna kitu kilichofanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiona, uozo wa polisi wanaouona chini ni kutoka chini mpaka juu. Kama kiongozi mdogo, afisa wa polisi amekosea, unakwenda kwa bosi wake amrekebishe, unakwenda kwa Waziri, Waziri alinipa pole, lakini pole inasaidia nini kama tunawaacha wale vijana wanazidi ku-harass watu wasiokuwa na hatia mtaani kwa sababu tu alikuwa kwenye bodaboda na walikuwa hawajavaa helmets. Ni kazi ya polisi kukamata na kupiga watu kwa sababu hawajavaa helmets? Come on guys! Come on guys! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niambieni kama Polisi wetu hawaelewi miiko na kazi yao kutokana na maandishi yao na vitabu vyao vya PGO’s naomba muwafundishe. Walipotufikisha ndio maana tunaongea haya yote, siyo kwa sababu hatuwapendi, ni kwa sababu wameondoka wenye msingi. Turudi kwenye masuala mazima ya maadili ya Jeshi la Polisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani tunajua tunapokuja hapa tunachopaswa kuongelea ni weledi wa Jeshi la Polisi, ni namna gani linafanya kazi, ni namna gani inatumia kodi tunazowapatia na ni namna gani ina-deal na raia? Those are the things you must be talking here. Hatupaswi kuwasifia, kufanya kazi ni wajibu wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunachokitaka ni kuangalia makandokando yao na namna gani tunaweza kuwarekebisha kwenda mbele. Wamegeuka wanasiasa, wamegeuka wapiga debe wa Chama cha Mapinduzi. Nani hataki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kuwaambia Jeshi la Polisi, sisi tukiingia madarakani, tunawahitaji, tutawatumia wao. Hata hivyo, hatutaki watupe favour sisi dhidi yenu ninyi, tunaka wasimame katika kama referee. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, namalizia kusema, mmomonyoko mkubwa wa maadili ya Jeshi la Poilisi nau- associate na kumhujumu Mheshimiwa Waziri Mwigulu Nchemba. Naamini pengine hawamtaki Mheshimiwa Nchemba. Ni kwa nini tunaona Jeshi la Polisi wanafanya mambo ambayo hatujawahi kuyasikia katika historia ya Taifa hili? Pengine Mheshimiwa Waziri labda ukijiuzulu tunaweza tukapona. Wewe unaonaje? Pengine ukijiuzulu tutaweza kupona. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nam-quote Che Guevara, aliwahi kusema: “If you tremble with indignation at every injustice then your comrade of mine.” Kama dhamira yako Mheshimiwa Waziri inaguswa na matendo ya Jeshi la Polisi na Maafisa wa Jeshi la Polisi, tunataka tukuone ukichua hatua dhidi ya hao maharamia wanaochafua Jeshi la Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Segerea linakabiliwa sana na uharibifu wa miundombinu ya barabara inayosababishwa na kupasuka mabomba ya maji mara kwa mara. Je, ni kwa nini Wizara haisimamii yakanunuliwa mabomba yenye viwango kuepusha hasara ya uharibifu wa miundombinu hiyo? Mfano, barabara ya Mnyamani, Kata ya Vingunguti, Kata ya Kisukuru, Kata ya Tabata barabara ya Mawenzi – Mwananchi, Kata ya Kimanga, barabara ya Twiga, barabara ya Kimanga Liwiti; kupitia mtaa wa Amani, barabara ya Bombom Kijiwe Samri Kata ya Minanzi Mirefu na Kiwalani.

Mheshimiwa Naibu Spika, usafishaji wa mabwawa ya Spenko yanayotumika kuhifadhi maji taka toka viwanda katika eneo la Mnyamani, Mtaa wa Mji Mpya na Kisiwani. Ni lini haya mabwawa yatakumbukwa kwa kuwa yanatoa harufu mbaya kwa wakazi wa eneo hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, kisima cha maji safi kimeendelea kukamilika katika Kata ya Kisukuru, ni ombi letu kwamba vifaa vya usambazaji maji vifike kwa wakati hasa mabomba ya mradi katika eneo hili la shule ya msingi Magoza ambapo pia Naibu Waziri alifika.

Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kusisitiza umuhimu wa kuanzisha kilimo cha umwagiliaji hasa wa mboga mboga katika maeneo ya Chanika ili kuondosha tatizo la wananchi kula mboga zenye sumu zinazolimwa Mto Msimbazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni muhimu Wizara ije na mpango wa namna gani itazidi kudhibiti upotevu wa maji yanayovuja mitaani ilhali maeneo mengine hayapati maji kama vile upotevu wa maji BAWASA wa thamani ya shilingi bilioni 1.5.

Mheshimiwa Naibu Spika, CAG ameainisha kiasi kikubwa cha pesa kinakusanywa kupitia kwa Wakala wa MAXCOM kutowasilishwa kwa wakati licha ya kwamba inakuwa imekusanywa kiwango hicho kwa niaba ya TANESCO, mfano mpaka Juni, 2017 MAXCOM alikusanya shilingi milioni 756 na aliwasilisha shilingi milioni 400 tu. Hii inaathiri utendaji wa DAWASCO na kuendelea kukwamisha juhudi za maji Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, DAWASCO imeelezwa kutumia isivyo fedha zilizotengwa kufanikisha uunganishaji wa maji kwa wateja wapya kwa mujibu wa CAG page 84 report ya ukaguzi wa mashirika ya umma kwa mwaka 2016/2017.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ANATROPIA L. THEONEST, Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, kuna msemo mmoja ni maarufu sana kutoka kwa muhenga mmoja anaitwa Napoleon aliwahi kusema; let China sleep for when the dragon wakes she will shake the world. Alisema Uchina wamesinzia, lakini siku ikiamka dunia itaona. Nataka hilo swali niimuulize ndugu yangu, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara anaiambia nini Tanzania? Wakati na Napoleon akiiona China na kuiambia dunia msione dunia imesinzia ikiaamka itakuwa balaa yeye anatuambia nini? Anatuambia nini wakati tumekuwa tunaongelea changamoto kadha wa kadha za viwanda zikiwa zinajirudia, wakati tunarudia yale yale na kila bajeti inayokuja tuna address yale yale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nitalia na kitu kidogo sana EPZA ninafahamu sisi kama Tanzania tuna copy uchumi wa viwanda kwa lengo nzuri la kwenda kuwa Serikali ya uchumi wa kati au nchi ya uchumi wa kati kwa vision yetu ya 2025 tukiangalia Tiger Nations, tukiangalia Taiwan, Singapore na South Korea, walifanya nini? Wameingia kwenye viwanda ndio, na sisi tunaingia kwenye system viwanda tena kwa wazo la ku-fast track which is good. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tuna - fast truck kuingia kwenye viwanda je tunaangalia wao walifanya nini walijikwaa wapi au kipi walifanya vizuri zaidi ili na sisi tukichukie. Wali-focus kwenye export na mimi ninafurashi kwamba nchi yangu kupitia kwa Waziri Mwijange mnawaza au tunawaza ku-export, lakini ni kwa kiwango gani tume- capitilize kwenye ku-export. Tumekuja na kitu, nimesema nitasemea kitu kinaitwa EPZA, tumefanya nini vya kutosha kuandaa maeneo ya uwekezaji, swali kila wiki swali kila mwezi tunaongelea maeneo ambayo bado madeni ya EPZA lakini pia fedha inayotengwa haitoshi. Nimesoma Fungu 44 katika sera mmeonesha kwamba mmetenga bilioni 1,200,000,000 lakini kwenye kuandaa miundombinu na vitu vingine kadha wa kadha mmeandaa bilioni moja. Nataka mniambie hiyo fedha kidogo itaweza kufanya nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, EPZA ndio msingi mzima wa biashara, msingi mzima wa biashara kama tunateka kwenda 2025 kama nchi ya uchumi wa kati, ni lazima tu-export zaidi. We have to export more, ndio new Tiger’s country walichokifanya. Tuna-export nini? Hilo ni swali la pili, maana nchi hizo za Singapore nchi kama South Korea walikuwa very specific kwamba tunataka tu-capitalize katika moja, mbili, tatu sasa sisi tunataka tu-capitalize katika nini. Tunaweza tukawa na viwanda vingi nchini lakini tunataka dunia itufahamu katika nini? Ukiisema Kenya leo, watakwambia katika Afrika, Kenya ni mzalishaji mzuri wa coffee na tea. Lakini je, Tanzania tuko katika nini? Ni lazima tu-capitalize tunataka kufanya nini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninarudi tena kwenye EPZA, hizo bilioni moja mlizotenga zinatosha kutengeneza miundombinu? Kwenye hotuba yako umeonesha hapa, kwamba tunataka tuweze kutengeneza ukuta wa EPZA ya Benjamini Mkapa umedondoka; tunataka tuweke miundombinu ya maji ya EPZA ya Mkapa kwa sababu haipo. Hivyo ni vitu ambavyo vinaleta ukakasi, ni vitu ambavyo haviwezi kuvutia zaidi wawekezaji. Lakini pia kama haitoshi nimeangalia kwenye the easy of doing business. Watu wanavyokuja kuwekeza fedha zao kutoka duniani kitu cha kwanza wata-google wewe ndio unasema hapo Tanzania, Tanzania ikoje, bado tuna-rank 137 hatujafanya vizuri. Kama tunataka ku-fast track kama tunataka tuwe uchumi wa kati by 2025 hatuko mbali na 2025 guys kama tunadhani tunakaribia huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika report ya CAG ameeleza wawekezaji, niseme sampling aliyoifanya ya viwanda kumi na moja au ya wawekezaji 11 kati ya 57 ambao wamewekeza kwenye EPZA waliahidi wangekuwa na mtaji wa bilioni 131.5 lakini kwa mwaka uliopita wanaonekana wamewekeza only 33% ambayo ni shilingi bilioni 43. Wametudanganya wapi, tumewapokeaje kama wanaleta makaratasi na sio fedha au pengine walikuja na fedha zao wamekutana na vikwazo kadha wa kadha ambavyo tunazidi kuviongelea hapa. Vikwazo kama gharama kubwa ya uzalishaji, gharama ambazo mnatusabibishia leo mnatuambia tunalazimika kununua sukari shilingi 110,000 badala ya shilingi 65,000 kwa lengo la kulinda Viwanda vya ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hatuwezi ku-compete kama hatutashuka chini tukapunguza gharama za uzalishaji tukazalisha bidhaa nzuri tuka-export nje hicho ndio walichokifanya New Tigers Contries, lakini ningeweza kutoa ushauri mdogo wenzangu wamesema, tunaweza kuamua kwamba tunataka ku-focus katika kitu gani, umeonesha kwenye kitabu chako hata hivyo uchumi wa viwanda haujachangia kwa kiwango kikubwa sana. Ukurasa wa 185 haujachangia sana katika pato la Taifa. Tunaona asilimia saba, 6.9% mpaka 5.5% consecutive ambayo ni ya 2017. Ni changamoto kubwa sana tuna hicho kiwango kidogo ambacho kinachangia katika uchumi wa Taifa kama tungeweza kuwekeza katika sekta zinazowa-accommodate watu wengi tungekuwa tunaona mabadiliko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungeweza kuona mabadiliko tena kwa macho, umesema kuna uzalishaji wa pamba nchini na viwanda 11 ambavyo ni processing lakini havifanyi vizuri. Ukurasa wa 22. Ukasema ni asilimia 30 tu ya pamba inayozalishwa nchini inatumika instead 70 percent inakuwa exported tukiamua kuji-reduce tu kutafuta wawekezaji katika viwanda vya nguo ambao ndio kitawa- accommodate watu wengi ambacho ndio kilimo actually ndio walichokifanya nchi ambazo tuna-copy mfano. Ndio walichokifanya hata South Korea tunayoisema. Walianza kuwa na viwanda vya kawaida baadae waka- revolutionaries agriculture yao, sisi bado tuna nafasi nzuri tuna eneo kubwa kwa maana ya ardhi, tuna wakulima, tuna watu wenye hali, tungeweza kuwa tumewafikia watu wengi, tungeweza kubadilisha Tanzania, tungeweza sasa kuingia kwenye a mid ecomonic countries kwa wepesi kushinda nguvu kubwa ambayo tutaenda kuitumia kwa viwanda vya propaganda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kikubwa ambacho ninaomba nisisitize hapa ni tunafangamanisha vipi elimu yetu na uchumi wa viwanda? Katika ku-rank 137 duniani ni wanaangalia na skilis na watu, wale watu wanaoleta viwanda vyao pia wanaangalia hiyo labour force ikoje? Sasa labour force ya vyuo ambao so far wako theoretical na siyo practical itazidi kutu-pull down. Ni lazima tufungamanishe uchumi wetu na viwanda na elimu yetu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, chonde chonde Jeshi letu lisiingizwe kwenye siasa za nchi hii, kazi yao kulinda mipaka na raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ku-define upya mipaka ya majeshi kwani maeneo mengi yamevamiwa na raia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jeshi litumike kujenga uchumi, mashamba maalum, kikosi maalum cha utafiti wa masuala kadha wa kadha ambayo ni changamoto kwa nchi yetu. Jeshi liboreshewe makazi yao wengine wanakaa kwenye majumba yaliyochakaa. Uundaji wa magari ya Nyumbu uliokuwa umekua kwa kiasi kikubwa uliishia wapi? Wanajeshi ndio nguzo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maduka ya jeshi bei rahisi ni ya muhimu sana kupunguza gharama za maisha na kuwafanya wanajeshi kuishi kwa shida.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa dawa za kuua wadudu ni changamoto hasa vijijini, dawa hizi pia zitolewe kama ruzuku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa pembejeo za kilimo kama mbolea katika Wilaya hasa Wilaya ya Kyerwa bado ni changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, power tiller zitolewe wa mkopo katika vikundi na walipe kidogo kidogo kwa wakati tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uimarishaji wa masoko ya mazao ya wakulima hasa yale yanayooza kama nyanya, matunda na kadhalika. Wananchi wamezidi kupata hasara kwa kuwa haya mazao yanakuwa hayatunzwi muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuendeleza zao la maua (hot culture). Hii ndiyo namna kuu tutakayoweza kupata pesa ya kigeni na soko lake liko tayari hasa nchi za Ulaya kama wafanyavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo kubwa la mnyauko katika zao la mgomba (Wilaya ya Kyerwa). Ni kiwango gani Wizara imejipanga kusaidia wakulima hawa kutokomeza tatizo. Sambamba na hilo wananchi wanaokutwa na migomba iliyo nyauka wamekuwa wanatozwa fine. Hii ni sawa na kuweka chumvi kwenye kidonda.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunashindwa kupata soko zuri la ngozi kwa sababu ya ng’ombe kutotunzwa vizuri, kitendo cha kupiga mihuri ng’ombe ni kuzidi kuharibu soko la ngozi nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, kutokomeza na ukomeshaji wa uvuvi haramu uje na mbinu na vifaa mbadala kwa wavuvi kwani hawa watu hiki ndio kimekuwa kipato chao kwa maisha yao yote.

Mheshimiwa Spika, haiingii akilini juu ya faini wanazotozwa hawa watu wanaokamatwa kwa makosa mbalimbali ya uvuvi haramu. Lazima hizi penalty zithibitishwe na sheria ya Bunge kwa kuwa zina sura ya kukomoana, lakini pia na double standards.

Mheshimiwa Spika, Wizara ilipata wapi ujasiri wa kuchoma vifaranga vidogo kiasi kile kutoka Kenya kwa madai ya uingizwaji kiholela? Kwa nini hawakurudishwa Kenya? Huu ni unyama na ni kinyume na haki za wanyama. Wizara ya Mifugo inapaswa pia kulinda haki za wanyama, kweli Wizara yako iliitia doa Serikali hii na kutufanya Watanzania tuonekane watu wa hovyo.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa samaki hawawezi kuzuiwa kutoka eneo moja kwenda na zoezi la uvuvi haramu limewekewa mkazo eneo la Tanzania Serikali/Wizara itueleze ni kwa kiwango gani kampeni hii inafanyika Kenya na Uganda kwa kuwa tunaweza kuwabana wafugaji wetu wakati Kenya na Uganda wanaendelea kuvuna.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaendelea kuona mmomonyoko wa kasi wa kimaadili na wa ghafla wa Jeshi la Polisi na kushamiri kwa kasi vitendo vya uvunjivu wa haki za binadamu. Polisi waliokuwa kimbilio leo wanakimbiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, Mwanza mtoto anafariki kisa mama yupo mahabusu na mtoto hawezi kupewa matibabu; Ndugu Saguta Heche amekamatwa, amefungwa pingu na anauawa; Polisi na bodaboda kana kwamba hawajui sheria, kama mtu hajataka kutii hiyo Sheria ya Usalama Barabarani si anafikishwa mahakamani; na upelelezi unaogusa Afisa wa Jeshi la Polisi haukamiliki au unachukua muda mrefu, liko wapi faili la Akwilina?

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu vyombo vya dola kugeuka wanasiasa, hii inafanyika makusudi kabisa. Tumezoea kuambiwa dola ina mkono mrefu lakini leo ndiyo tumeelewa maana halisi ya neno hilo. Dola ina mkono mrefu dhidi ya wenye mtazamo tofauti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, kuendelea kukamata vijana wadogo wanaoandika tu kwenye mitandao, mbona hawamkamati Musiba? Je, ni kwa kuwa anaongea wanachotaka kukisikia? Mheshimiwa Tundu Lissu kisa kaandika tu meseji kwenye group wanamkamata, akina Mheshimiwa Zitto, Mheshimiwa Mbowe na wengine, ina maana hao Polisi hawajawahi kumsikia Musiba?
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua fursa hii kutoa pole kwa changamoto ambazo viongozi wa kisiasa wa CHADEMA wanapitia. Muda nilionao ni dakika tano, sitaongea mengi, lakini natoa pole sana na ninaamini katika dhana ya utawala bora watu wengi wanaweza kuongea na wanaelewa nini maana ya utawala bora kama tuna viongozi na Wabunge zaidi ya 15 wa Vyama vya Upinzani wanatakiwa kuripoti polisi karibu kila wiki. Salamu zimefika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, nataka nishangae Wizara na utamaduni mpya walioanzisha wa kujibu eti hotuba ya CAG. Nitaongelea TAMISEMI, mfano waliojibu jana na wakatoa taarifa kwamba mapendekezo aliyoyatoa CAG wameyafanyia kazi ikiwa ni pamoja na kufukuza watumishi takribani 4000 na nimei-quote vizuri ambao walituhumiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambie kwa mujibu wa CAG kwenye report aliyoitoa kuna mapendekezo aliyatoa mwaka 2000. Katika kalenda hii ya mwaka 2014/2015 alitoa mapendekezo 15 lakini mpaka mwaka 2017 mapendekezo yenyewe 14 yalikuwa hayajafanyiwa kazi. Kuanzia mwaka 2014/2015 mpaka 2017 aliyoyatoa juzi ndiyo mnaanza kuyajibu kwenye television. Inashangaza sana. Ninachoweza kuwaambia, nendeni mkafanyie kazi mapendekezo aliyoyatoa na siyo kwenda kujibu kwenye television. Mna kazi kubwa ya kufanya, nendeni mkaangalie upungufu aliouainisha kwenye Wizara zenu, kwenye Serikali za Mitaa ili mtuletee majibu sahihi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ni kusikitika kwa kuambiwa makusanyo ya Serikali yanapanda kwa asilimia 90 huku Halmashauri zetu mpaka mwezi wa sita mwaka 2017 zikiwa zimepelekewa asilimia 49 tu ya fedha zilizohitajika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino ina upungufu wa asilimia 68; Halmashauri ya Kibondo upungufu wa asilimia 88 na Halmashauri ya Kigamboni, upungufu wa asilimia 86. Halafu tunakuja humu Wabunge wenzangu wa CCM mnapongeza. Halmashauri zetu zimepelekewa asilimia 49 tu ya fedha za maendeleo. Tutabaki kusifiana hapa, lakini mwisho wa siku tutaona aibu sisi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nitaliongelea ni Wakuu wa Wilaya kukosa instruments. Hii nai- associate na kazi wanayoifanya Wakuu wa Wilaya na Mikoa, wanawakilisha wanaliowatuma. Tumeona mfano mdogo au mfano mkubwa niseme, anachokifanya Mkuu wa Mkoa wa sasa aliyepandishwa, baada ya kutumiwa na CHADEMA kununua Madiwani, akapandishwa kuwa Mkuu wa Mkoa. Sasa ameenda mbali zaidi, anajitangaza hadharani kwamba atawabagua watu wa CHADEMA, atawabagua watu wa upinzani kwa sababu yeye anafanya kazi kwa Ilani ya CCM na hawezi kufanyakazi kwa Ilani ya CHADEMA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami napigia msitari, kwa vile anamwakilisha mtu fulani ambaye ni Rais, kauli ya Mkuu wa Wilaya au kauli ya Mkuu wa Mkoa ni kauli ya Mheshimiwa Rais, kwa hiyo, na sisi tunaweza kusema na hiyo ni kauli ya Rais unless kuwepo na kanusho la kauli aliyoitoa Mnyeti kwamba atazidi kuwabagua wapinzani katika maeneo anayoyaongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa mbalimbali za fedha kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali zimeonesha upungufu mkubwa sana, mfano, Halmashauri ya Bukoba Mjini ilikuwa na takribani shilingi milioni 60 kwenye madaftari, lakini fedha haijapalekwa benki. Halmashauri ya Kigoma-Ujiji ina zaidi ya shilingi milioni 219 katika daftari, lakini fedha hazijapelekwa benki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo inaonesha upungufu mkubwa sana na tunakimbilia kujibu kwenye magazeti, nadhani twende kwenye Halmashauri husika tuone chamgamoto ni ipi? Tufanyie kazi mapendekezo yanayotolewa na CAG, vinginevyo hatuna haja ya ku- allocate fedha kwa CAG kama mapendekezo hatuwezi kuyafanyia kazi, tunakwenda kuwajibu waandishi wa habari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala kubwa kama nitafanikiwa kulimazilia ni kutotengwa kwa asilimia 10 kwa ajili ya wanawake na vijana kwenye Halmashauri. Nimesikia Mheshimiwa Waziri mmoja hapa akisema na zile asilimia 10 zitakuwa hazitolewi riba, lakini kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali anaonesha takribani Halmashauri 164 hazijatenga asilimia hiyo 10 kwenda kwa vijana na akina mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sijui mnavyosema kwamba mnaondoa riba, mnaondoa katika kitu ambacho hakipo? Ni lazima tukae vizuri, tujipange. Kama kweli TAMISEMI iko serious inataka Halmashauri zitenge hiyo fedha, iandae account maalum katika kila kiasi kitakachokusanywa, basi hiyo asilimia ipelekwe.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutopandisha watumishi madaraja licha ya kuwa na sifa stahili mfano kuna watumishi 8,369 katika mamlaka 18 hawajapandishwa kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali mpaka 30 Juni, 2017.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upungufu wa watumishi katika Halmashauri 161 ambao ni takribani 155,013 sawa na 32% ya huhitaji ambao ni takribani 500,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutopelekwa 10% ya own source (mapato ya ndani) katika Halmashauri 143. Ushauri wangu kuwepo na akaunti maalum na hii pesa iwekwe huko kwanza hata kabla ya matumizi ya kawaida mengine kupewa kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakusudia kuja na hoja binafsi kuishawishi Serikali kuleta Muswada wa kuzibana Halmashauri ili pesa hii ipelekwe kwa kundi hili maalum katika jamii yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri kuendelea kupanga bajeti zisizo halisi, ndio maana Halmashauri nyingi zimelazimika kuongeza bajeti zake. Mfano Ilala 10%, Mlele 51% na ya kusikitisha ni Newala 81%, kweli bajeti ina-burst kwa 81%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutopelekwa fedha za maendeleo, hata zile zilipelekwa zimechelewa. Hii inarudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, halmashauri tatu kuendelea kufanya vibaya. Je, watumishi waliopo hawaendelezwi kielimu au ni wezi?
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru, kuna wachumi wa IMF waliwahi kusema, waliandika paper yao moja wakijibu walikuwa wanaulizwa maswali ni fedha kiasi gani nchi inahitaji kukopa; anasema how much a debt is sustainable? Maana tumekuwa na maeneo mengi kuwa deni letu ni himilifu ni toshelevu sasa katika hiyo paper yao ambayo waliandika walijibu kwamba kwa kiswahili wakisema; they don’t know kwamba hawajui ni hela kiasi gani au ni debt kiasi gani ya Taifa ambayo ni sustainable na wakenda mbali zaidi wasema market signals don’t work as should; kwamba zile sign za soko some time hazipo predictable nadhani na hiyo nimwambie Mheshimiwa Dkt. Mpango sometimes market signal haziko predictable.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza kuwa tunajiamini kwamba deni letu ni himilivu, deni la Taifa linalipika hana anayebisha kwa sababu tunaona uchumi unakua kwa mujibu wa takwimu zetu kwa maana ya GDP bado ina tolerate mkopo tuliao nao, lakini swali tunajiuliza kwa nini hii mikopo inakuwa kwa haraka. Sikatai kwamba tunakopa fedha nyingi kwa ajili ya kenudesha miradi yetu mikubwa inayoendelea lakini ushauri wangu nitakao utoa sasa tuangalie hizo fedha tunazozikopa katika miradi tunayoweka, je, itaweza kutupa fedha kwa wakati mfupi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakopa kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi ambayo ni ya muda mrefu hatuna uhakika kama tunaweza kufuna haraka haraka hiyo hiyo naleta kwenye mradi mkubwa tunaouendesha kwenye SGR. Huo mradi mkubwa tunaoendesha ambao sisi humu Bungeni tumekuwa tukipiga kelele kwa ajili ya kufufua mradi mkubwa wa chuma wa Liganga na Mchuchuma nimepitia kwenye kitabu chako mmesema mnakamilisha taarifa za awali, nanihajui kwamba kukamilika kwa mradi mkubwa chuma ndio ungesaidia pakubwa katika mradi mkubwa wa SGR, nani anabisha katika hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha tunazozidi kukopa kwa wahisani au wafadhili tukaiwekeza kwenye kujenga SGR tungeweza kuwekeza kidogo kama tungekuwa tunazalisha sisi chuma hapa nchini. Lakini kama haitoshi tungeweza kupata faida zaidi hata fedha kigeni kwa kuuza chuma lakini badala yake mradi ambao umekuwa kipaumbele 2015/2016 leo inapewa that half a page ndio inazungumziwa na dhani Waziri atupe status leo kuna mwekezaji alijitokeza nadhani anaitwa Szechuan Onda akija na terms zake atuambie amefikia wapi as far as concern kuwekeza katika huu mradi ambao kimsingi ndio mradi wenye kielelezo na unapaswa kuwa kipaumbe kwa nchi yetu kwa nchi yetu kama tunamaanisha tunakata uchumi ukue.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninarudia tena kusema tusijamini sana kusema kama deni letu ni himilivu kama tunaenda kuwekeza katika vitu ambavyo havitaweza kupandisha GDP yetu haraka sana ikiwa ni pamoja na mazao ambayo tutazalisha au uchumi tutakaoweza kuu-nature ukaweza ku-support export ndio itasaidia deni letu lizidi kuwa himilivu. Hao Wakenya leo ambao wanakaribia ku-default na wao walikuwa najinasibu kama tunavyoongea leo kwamba deni lao lilikuwa himilivu na kama haitoshi GDP ya Kenya iko juu kuliko ya kwetu, lakini nini kinatokea ni lazima tujiangalie wanasema ukitaka kuruka ni lazima uagane na nyonga, kwa hiyo sasa tungalie vipaumbele vyetu vya kiuchumi in relation to deni la Taifa hiyo ni ya kwanza, lakini ya pili, nina muda mchache, Serikali...

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzmji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli za wanasiasa zinakua kikwazo katika ustawi wa Mazingira yetu. Sheria ya mita 60 kama ikifanywa kama siasa na kuruhusiwa kuharibu vyanzo vya maji, itakuwa kiama kwa nchi yetu, kwani itaharibu mazingira, kusababisha upotevu wa mvua na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vipi vifungashio vya mikate, ni sehemu ya katazo hilo? Kwa nini tusitoe muda maalum kwa wazalishaji hawa? Naomba ku-declare interest kwamba mimi nazalisha mikate na kutumia mifuko hiyo. Bado hakujawa na mbadala sokoni na wafanyabiashara washanunua mizigo na hata kubadilisha mashines.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ije itusaidie kutengeneza kingo za bonde la Mto Msimbazi kwani bonde linazidi kukua na kutafuna majengo na makaazi ya watu. Tunaomba Wizara itoe kipaumbele kwa mto huu. Tunawaombeni sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishati mbadala kama gesi zishushwe bei hata kupunguza kodi ili wananchi wengi watumie gesi badala ya kuni na mkaa kama ilivyo sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vikundi vya akina mama viwe motivated na Wizara. Wale wanaozalisha mkaa mbadala binafsi, naikaribisha Wizara kutembelea mradi wa akina mama wa Tabata wanaozalisha mkaa mbadala. Karibu mtunishe mfuko wao waweze kupata mashine ya kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Wizara isaidie wabunifu kubuni zaidi mashine za kuzalisha mkaa mbadala.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma katika Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2017
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nitaanza kwa kum-quote anaitwa Authon, aliwahi kusema; “accuracy is the twin brother of honesty,” lakini Edward akasema; “accuracy of the statement is one of the first element of truth” au unazunguka unasema in accuracy is the near keen to falsehood, kwamba usipokuwa accurate you are likely to lie, usipokuwa na taarifa ambazo ziko sahihi, utasema uongo tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina-quote hotuba ya Kamati ambayo mimi ni Mjumbe wake, tumetoa mapendekezo mazuri, akasema ni; “ni muhimu pia ikaangalia kwa makini suala la watumishi wa Wizara na uwezo wao wa kufanya kazi kwa ueledi zaidi.”

Ninarudi kwenye ripoti ya CAG, yeye akasema tulikuwa/tumekuwa na issue kwa muda mrefu ya kutoonekana kwenye vitabu 1.5 trillion; alikuja kwenye kamati yetu na ametoa taarifa yake. Nina-quote sehemu ndogo anasema; however these re-worked totals did not fully reconcile as there where an excess of expenditure over revenue amounting to figure of 290.13 billion. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kumbe alienda kukagua authenticity ya 1.5 trilion akakuta kuna kitu kingine, kuna ongezeko la 290 bilioni. Kwa hiyo kwa jibu simple na alichoenda kuangalia kwamba wapi 1.5 trillion akakuta kuna kingine zaidi ya 1.5 trillion, akakuta kuna ku-spend zaidi kwa bilioni 290. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini tumefika hapa, ni kwa nini tumekuwa na hoja za ukaguzi? Ninarudi kwa watumishi wa Hazina ambao tunawategemea na hawafanyi kazi inayostahiki. Mjumbe yeyote wa Kamati akisimama hapa asiongelee suala la utendaji usioridhisha wa Hazina ambao umeleta hizi auditing queries. Kama tusipo-address hili suala litaendelea kujitokeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali najiuliza, ilikuwa ni bahati mbaya kwamba taarifa hazikuwasilishwa kwa wakati kwa ajili ya kukaguliwa na CAG? Ilikuwa ni bahati mbaya kwa wafanyakazi ambao wapo competent, kwa watu ambao wanajua nini…

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: …deadline ni lini ya kuwasilisha hesabu…

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Goodluck Mlinga.

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia Theonest unaipokea taarifa hiyo?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, sita-deal na watu wanaotafuta umaarufu mdogo mdogo, nakushukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeanza na quote yangu kuonesha weakness kubwa ambayo ipo Hazina ambayo ndio imepelekea kupotea kwa kiwango kikubwa cha fedha ambacho hata leo Mheshimiwa Catherine ametuweka wazi si tena 1.5 trillion bali ni two plus trillion. (Makofi) [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

MHE. KHADIJA NASSIR ALI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Khadija Nassir.

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Khadija.

Mheshimiwa Anatropia Theonest.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nimesema utendaji wa Hazina, siamini kwamba ni wa bahati mbaya, ninaamini kwamba ni utendaji mbovu wa makusudi unaotupeleka au unaotufikisha hapa tulipo leo. Ninaongea kwa masikitiko kutoka kwenye executive summary ya CAG anasema wakati wa kutunza kumbukumbu zao katika…

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa…

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaongelea Hazina ya Taifa inayotumia spread sheet katika kutunza taarifa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, ina maana haya mambo yamefanywa deliberately, haya mambo yamefanywa kimkakati na tupo likely kuendelea kuona hayo mambo, tutakuwa na reconciliation leo, kesho na keshokutwa. Ni Hazina gani haijui lini mwisho wa kuwasilisha taarifa kwa ajili ya ukaguzi wa CAG? Kama haitoshi CAG pia ameanisha kwamba kumekuwepo na mismatch ya hundreds billions of money kutoka kwenye exchequer issue warranty. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano kuna exchequer issue warranty ya bilioni 656.5 ambazo exchequer issue warranty hazi-match na exchequer issue report. Tuna exchequer issue warranty za bilioni 3.45 ambazo zimekuwa cancelled na hakuna taarifa kokote kuonyesha zimekuwa cancelled. Pia kuna exchequer issue warranty ya bilioni 56.07, wameweza ku-verify only 51.3 billion ambayo kuna earning ya bilioni tano na ikaonyesha kwamba Wizara ili-cancel bilioni moja na hapo tunabaki na bilioni 3.29 hazijulikani taarifa zake zipo wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kama haitoshi, kuna exchequer warrant ambazo ni za shilingi bilioni 234. Kwenye Exchequer Release Report hazionekani kokote na wanavyoulizwa, nina-quote hapa, anasema: “The Ministry explained that the fund were released for the previous year transcations which were processed but would not be cleared in The Financial Year 2015/2016.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, CAG akaenda mbali akasema: “The lack of disclosure records of the prior year transaction in the question indicates that the exchequer report was misstated.” (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yako madudu mengi sana ambayo ukiyatazama sisi kama Wanakamati tunaamini kwamba ni lazima mfumo ufanyiwe overhaul. Tusipofanya hivyo, tutakuta fedha nyingi zimeibiwa kuliko ambavyo tunafikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikiongelea kuiba siyo lazima uzipeleke kwenye mfuko wako. Kama fedha zimekuwa planned kufanya kitu A na umefanya na hakuna detail au hakuna viambatanisho, kwa Mhasibu au kwa mtu yeyote anaye-deal na hesabu, hizo fedha zimepotea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakwenda kwenye suala la matumizi ya Fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Kumekuwepo na ununuzi usioridhisha au uwekezaji usiokuwa na tija wa billions and billions of money. Mfano, ardhi iliyonunuliwa katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, ameeleza mwenzangu kwamba plots nne tu. Nimekwenda mbali zaidi, wanasema ni kama ekari 1,000, lakini fedha iliyotumika ni takribani shilingi bilioni 16 point something. Haiingii akilini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakaeleza hata eneo lingine liko Kigoma, Mwandiga, ekari moja kwa shilingi milioni 66. Haiingii akilini! Unaona kwamba kama Serikali ipo, kwa sababu mmeongea leo kana kwamba hii Serikali ndiyo kwanza ina mwaka wa tatu; hii Serikali tuliyonayo leo ina takribani miaka 56 plus madarakani. Kwa hiyo, haya madudu tunayoyaongelea leo yametokea miaka yote ambayo mmekuwa madarakani na ninyi ambao mnapaswa kuisimamia Serikali mnapaswa kuwa answerable. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeongea kwamba kuna fedha, shilingi milioni 888 wamelipwa watu ambao sio Askari Jeshi, sio Polisi, majina yao yapo yameainishwa na Mheshimiwa Waziri anayaona, Waziri ambaye anajitamba kwamba anafanya kazi. Mmeshindwa nini kuwafikisha kwenye vyombo vya dola, kama siyo kwamba tunalea watu na tunaonea watu ambao tunadhani tunaweza tukawaonea? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. In a nutshell nasema, tulichokiona katika Hazina ya Taifa ina-reflect nia yetu kama taifa, ina-reflect kwamba hayo makosa yaliyofanyika katika kuweka takwimu yamefanywa deliberately, kwa lengo la kupoteza au ku- misdirect fedha za walipa kodi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kupata fursa hii kuchangia katika hotuba ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI halikadhalika Utumishi na Utawala Bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaanza kwa mara nyingine kutoa pole kwa viongozi wangu wa chama hususan Kamanda wa anga, tunamwita Kamanda Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe na dada yetu mpendwa Mheshimiwa Esther Matiko kwa kukaa gerezani kwa dhuluma. Huu ni ushahidi mwingine wa uwepo wa hila. Ni ushahidi mwingine wa kutokuwepo au kwa upungufu ya Utawala Bora, watu wanakaa ndani kwa zaidi ya siku 104 kwa sababu ambazo zilionekana ni nyepesi na Mahakama Kuu ilitoa maamuzi inasema Mahakama ya Hakimu Mkazi ilikiuka kanuni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ndiyo tunaanza kuangalia ni kwa kiwango gani katika nchi yetu tunasimamia Utawala Bora? Naendelea kumwambia Mheshimiwa Mbowe tunampenda sana, atabaki kuwa juu, juu, yuko mawinguni. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, kuna mwanazuoni mmoja anaitwa Twain Mark, aliwahi kusema kwamba uzalendo ni kui-support nchi yako, uzalendo ni kuipigania nchi yako kwa kila hali, uzalendo ni kuhakikisha muda wote unaangalia maslahi ya nchi yako na ikiwezekana au ikikuridhisha unaweza kui-support hata Serikali yako.

Mheshimiwa Mwenyekiti, anamaanisha nini? Kwa lugha ya kizungu alisema patriotism is supporting your country all the time and your government if it deserve it. Anasema ui- support nchi yako wakati wote, ui-support nchi yako kwa gharama na damu yoyote, lakini siyo lazima ui-support nchi yako kama hai- deserve hiyo aina ya support inayohitaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema haya? Kumekuwepo na malalamiko mengi ya mambo yanavyoenda ndivyo sivyo yanayofanywa na Serikali. Kumekuwepo na malalamiko mengi hasa kutoka kwa Vyama vya Upinzani, kuonekana tunatendewa ndivyo sivyo. Nikiongea haya, kuna watu hawawezi kunielewa kwa sababu wako tayari kui-support Serikali yao kwa jasho na damu na siyo nchi yao, kwa sababu wanaangalia kipi wanapata kutoka kwenye Serikali na siyo kwenye nchi husika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, TWAWEZA walifanya utafiti na moja kati ya matokeo waliyoyapata wakasema, raia wa Tanzania wanasema hawako huru kukosoa kauli za watawala. Kwamba raia wa Tanzania wanaogopa kusema ukweli kuhusu nchi yao inavyoendeshwa hiyo ni hatari sana kwa mustakabali mzima wa uendeshaji bora wa nchi yetu.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Utawala Bora, kumekuwepo na marufuku mbalimbali, wamesema wenzangu na hasa kuzuia kazi na shughuli za Vyama vya Siasa. Nataka kujua, Mheshimiwa Rais kama anafuata Katiba na Sheria, kama anafuata utawala bora alipata wapi mamlaka ya kuzuia kazi za kisiasa ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya nchi yetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kujua Mheshimiwa Rais alipata wapi mamlaka; alipata wapi moral stand ya kutamka hadharani na kusema watoto wa kike wakipata ujauzito wasiendelee na shule, wakati ni haki yao ya msingi ya kwenda shule regardless ya mambo mengine tunayoyasema. Uthubutu wa kutaja maneno ambayo yanakiuka hata Katiba yenyewe aliyoapa kuilinda anaupata wapi? Hiyo ni swali langu la pili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la tatu, tumekuwa tunalalamika vyombo vya dola kushiriki mambo yanayoonekana ni ya kisiasa, kuonekana vimeegemea kwenye mlango fulani wa chama. Tuliona kwenye vyombo vya habari, mmoja kati ya Polisi Tarime huko akitaja hadharani kidumu Chama cha Mapinduzi na wenzake wakaitikia na hakuchukuliwa hatua zozote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, tumeona kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Ibara ya 74(14) kinachozuia Watendaji wa Tume kuwa wanachama wa Vyama vya Siasa, tumeona wiki iliyopita, somebody Mhagama Katibu wa Mkoa wa CCM anateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri. Hiyo tunaongelea utawala bora upi katika nchi yetu? Tunathamini utawala bora upi? Tunataka tuwasifu Serikali ya Awamu ya Tano kwa lipi? Kwa nini tuwe ma-patriot wa Serikali kama mnafanya mambo ambayo tunayaona yanaenda kinyume na utawala bora tunaousemea? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, tumeona impurity ya vyombo vya dola, impurity ya Polisi. Akwilina alipigwa risasi katika mkutano wa hadhara, yeye akipita kwenye daladala. Tuambiwe leo, uchunguzi umefikia wapi? Tukaambiwa faili limefungwa, huyo Askari specific aliyehusika, alichukuliwa hatua gani? Hiyo ni lazima mtuambie kama tuna-deal na suala linaloitwa utawala bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, kumekuwapo na tuhuma ya vyombo vya dola kuteka, kutesa na wakati mwingine kuua raia wema. Wananchi wamekuwa wakilalamika, watu wamekuwa wakipotea na hatusikii kauli yoyote kutoka Serikalini na hata Wizara inayohusika. Sasa nataka tujue ukweli: Je, ni kweli hao Usalama wa Taifa wanahusika na hayo matendo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo yanatupa maswali kwa kile kilichomkuta Mohamed Dewji. Alitekwa katika filamu ambayo inaonekana haikuchezwa vizuri. Anatekwa katika mazingira yenye CCTV camera, anapelekwa kusikojulikana na anapatikana katika mazingira ambayo hayaeleweki. Hiyo inatupa shaka; je, tuko salama kiwango gani? Kama kweli vyombo vya dola vilifanya au havijafanya, mbona ule mchezo ulifanya wepesi na hatupewi majibu? Kwa nini majibu hayapatikani katika suala zima la kutekwa kwa Mohamed? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi, nini kilitokea kwa Zacharia? Maana yake ilisemekana amekamata watu, amewapiga risasi, lakini inakuja kujulikana ni vyombo vya dola. Mnatushawishi kuamini hilo kwamba tunaowaamini tumewapa madaraka, wanayatumia vibaya. Kama ndivyo ilivyo, tunaiweka hii Serikali au tunaiweka nchi yetu katika mazingira yanayotia shaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaingia kwenye suala zima la uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Natambua mwaka huu tunaenda kuingia kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa. Haijabishwa kokote kwamba Mheshimiwa Rais alitoa kauli kwamba Wakurugenzi watakaowatangaza Wapinzani kushinda uchaguzi kama wataendelea kulipwa mishahara au kupanda magari ya Umma. Haijapingwa kokote baada ya kusikia. Kama ndivyo ilivyo, haijapingwa kokote, tunaamini inabaki imesimama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami natoa wito, Mkurugenzi anayedhani anaweza kupora haki ya mamilioni ya Watanzania watakaokaa kwenye foleni na kupiga kura, mimi namwambia ahakikishe ukoo wake, ndugu zake, jamaa zake hawapo katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni gharama kubwa. Demokrasia ina maumivu makali sana. Watu wanaweka matumaini yao makubwa katika mifumo ya kubadilisha uongozi. Kama kuna mtu mmoja mjinga anaweza kuamua kupora haki kwa maslahi ya tumbo, ninakuhakikishia hapatatosha mwaka huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hilo halitoshi, tumeambiwa kanuni ziko wazi na ninasema kanuni ni lazima ziwe rafiki. Kanuni zisiwepo kwa lengo la kulinda chama kimoja, tumezisoma kanuni na tunaona zinatoa mwanya wa watu wetu kurubuniwa na kununuliwa, zinatoa mwanya wa kubambikiziwa kesi na kama ndivyo ilivyo, mtaelewa nini maana ya nguvu ya Umma. Demokrasia ikishindwa kufanya kazi, mjue kwamba watu watatafuta namna nyingine ya kujitetea na kujilinda. Nawatahadharisha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaenda kwenye suala lingine dogo kabisa wakati namalizia. Naomba tuambiwe, hivyo vitambulisho vya ujasiliamali vilitoka katika mchakato upi? Ni makampuni gani yalishirikishwa na akina nani walipata tenda? Kwa sababu inaonekana kuna kitu kipo nyuma ya pazia hakijulikani. Sisi kama Wabunge watunga sera, hatujui mchakato uliohusika katika kupata Mkandarasi, hivyo vitambulisho vinaendaje? Mpaka sasa kimekusanywa kiasi gani cha fedha kwa vitambulisho vilivyogawiwa? (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Katiba na Sheria
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu umuhimu wa marekebisho ya Katiba kwa ajili ya kupata Tume Huru ya Uchaguzi, kwa nini wanasiasa wanatakiwa kuwa Wakurugenzi wakati ni returning officer wa chaguzi za Jimbo? Mfano, Mhagama aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mlundikano wa maabusu wakati kesi zao zinadhaminika ilihali wanatumia fedha za Umma katika kuwa-sustain, kumekuwepo na ucheleweshwaji mkubwa wa kesi kunakosababishwa na Ofisi ya Taifa ya DPP, Mwendesha Mashtaka, kwani maelezo ya Polisi mara zote yamekuwa, file bado liko kwa DPP.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kurejeshwa haraka kwa mchakato wa Katiba mpya, ufanyike mara moja kwani Katiba zilizopo zinaonesha upungufu mkubwa na imeendelea kupigiwa kelele. Vile vile sheria ya maudhui ya mtandao inaonesha nia mbaya ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutoa maoni na uhuru wa kujieleza licha ya kuwa na vifungu vinavyokiuka mikataba ya Kitaifa. Hivyo ifutwe mara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Serikali kujikita kwenye sensorship ya vyombo vya habari hasa magazeti kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali, hii ni kulitia aibu Taifa na kuonesha ubeberu wa kiutawala.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, kwa nini timu ya hamasa ya kui-support timu ya Taifa iliundwa na Wanasiasa, Mwenyekiti wake akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam? Suala hili linagawa watu kwa kuwa siyo watu wote ni wana CCM. Binafsi sikuunga mkono kwani ilikuwa movement za kisiasa, tuache kuingiza timu zetu katika siasa, uzalendo siyo kampeni ni hiari ya watu kupenda nchi yao. Hii ni aina nyingine ya siasa kwenye Wizara hii, wote tunajua mchakato na sababu za uzalendo.

Mheshimiwa Spika, upungufu katika Sheria ya Huduma za Habari kama ilivyothibitisha Mahakama ya Afrika Mashariki (EAC), sheria hii irudishwe mara moja na kufanyiwa marekebisho.

Mheshimiwa Spika, TBC kuendelea kutumika kama chombo cha propaganda cha CCM. Ni aibu sana kwa Nchi yetu. Rejea vipindi mbalimbali kwenye TBC, swali, je, hii ni TV ya Chama? Mbona kazi za vyama vingine hazionyeshwi? Kuweni wazalendo tuondoe aibu hii kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, ni lini Bunge litaanza kuoneshwa live. Niishauri Wizara kuja na mapendekezo ya kurudisha live broadcasting kwa kuwa ni pesa ya wapigakura. Je, ni sahihi kuwanyima haki ya kujua kinachojadiliwa na kuamuliwa na wawakilishi wao?

Mheshimiwa Spika, maandalizi ya Olympic; nashauri tuwaandae vijana katika michezo mingine kama kurusha tufe, mishale na hata kuruka kwa kuwa tumeshindwa kufanya vizuri katika mpira na kukimbia, hivyo hatuna budi kuangalia nyanja nyingine.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na kauli mpya tata na zenye ukakasi zinazotolewa na Jeshi la Polisi kwa siku za hivi karibuni; mfano, tutawapiga mpaka mchakae – RPC Muroto; tutapiga vipigo vya mbwa koko na nyingine zenye ukakasi kama hizo. Tafsiri ya kauli hizi ni ulevi wa madaraka, ubaguzi na kuwa juu ya sheria.

Mheshimiwa Spika, kauli hizi hazisikiki tu kwa Jeshi la Polisi na hata kwa wanasiasa kama Mkuu wa Mkoa wa Tabora, akimtaka Mungu amshukuru Rais Magufuli na mengine kama haya. Ulevi wa madaraka, lakini kauli hizi zitafsiriwe kama zinaungwa mkono na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa, haiamini tena katika Government of the People for the People by the People.

Mheshimiwa Spika, Fungu Namba 28 – Polisi, limekuwa na upungufu mwingi sana katika matumizi ya fedha na haya yamesemwa na CAG Report 2012/2013 mpaka leo hii. Mfano, zoezi la ujenzi wa vituo vya Polisi vya mfano chini ya mradi wa STACA uliodhaminiwa na Serikali ya Uingereza ukiwa na thamani ya zaidi ya pound milioni tatu (Tsh. 10 billion). Ujenzi wa hivyo vituo ulienda kinyume na MOU.

(1) Budget ya estimates haikuendana na actual implementation. Bajeti ya kukarabati vituo 35 vilikarabatiwa 16 tu ambayo ni asilimia 46 ya kazi.

(2) Ripoti za uwongo, mfano taarifa ya 2012/2013 kukamilika vituo vya Nachingwea, Nyakato na Kondoa.

(3) Ripoti ya 2013/2014 ilionesha hakuna kazi iliyofanyika katika vituo hivyo na walienda site hawakuona chochote.

(4) Mwaka 2014/2015 hakukuwa na ripoti iliyotolewa.

(5) Ujenzi wa vituo vingine bila mikataba na wakandarasi, mfano, M/S Posh-alliance kiasi cha Sh. 515,233,760.

(6) Ufisadi katika ukarabati wa Kituo cha Polisi cha Mfano Makambako (Model Police Station).

(7) Milioni 25 zililipwa kwa mkandarasi kwa ununuzi wa fenicha ambazo hazikununuliwa.

(8) kupotea kwa fedha ya wananchi mikononi mwa Polisi, wanaowekwa mahabusu au zinazokuwa vidhibiti; Tsh. 145,410; Ksh. 25,900 na Euro 800.

(9) Delay in banking revenue collected of Tsh. 93,725,000. Delay in submission of revenue collected na traffic notification of over 24 million.

(10) Kushindwa kukusanya fines zenye thamani ya zaidi ya bilioni 4.4.

(11) Walifanya malipo ya milioni 234, zaidi kwa watoa huduma waliokuwa hawastahili, Time General Supplies.

(12) Malipo kwa watoa huduma ya milioni 103.4 bila kushindanishwa. Single source procurement million 179.4; total of zaidi ya milioni 700 zimekiuka taratibu za manunuzi.

(13) Matumizi ya zaidi ya milioni 345.9 ambazo hazikuidhinishwa na IGP kuanzia 2013 – 2017 na bila vithibitisho kinyume na PGO 121(2).

(14) Matumizi yasiyoeleweka ya kikao cha Viongozi Wakuu kilichofanyika Dodoma tarehe 17 – 19 Aprili, 2017 zaidi ya milioni 156,206,000 zilitumika na hazikuwa na ushahidi out of 246.03 verification ilifanyika kwa milioni 89.8 tu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, je ipi sera ya elimu yetu ya sasa na inalenga kuandaa wahitimu wenye weledi gani?

(i) Ngazi ya elimu ya msingi?

(ii) Ngazi ya kidato cha IV?

(iii) Ngazi ya kidato cha VI?

(iv) Ngazi ya chuo kikuu?

Sera ya nchi yetu inakidhi kweli mahitaji ya soko? Mbona kama kuna ombwe la maandalizi? Rejea idadi kubwa ya wahitimu wasio na ajira katika ngazi zote walizohitimu. Kwa nini tusibadilishe mtizamo wa elimu yetu? Nashauri kuitishwe mjadala wa kitaifa, tupate maoni mbalimbali juu ya mfumo wa elimu uliopo na kama kweli bado unakidhi haja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini tathmini ya Serikali na mfumo wake wa elimu ya 7.4.2? Ukilinganisha na Kenya ya 6.2? Serikali haioni umuhimu wa kupunguza muda mrefu wa vijana kukaa elimu ya msingi wakati haiwapi ujuzi specific?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali ione kuwa huu ni wakati muafaka wa kufufua elimu za kujitegemea shuleni kwa nguvu na kasi ile ile kuondoa changamoto ya kuzalisha watoto wasio ajirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Elimu juu ya mfumo wa mitihani ya mwisho kama kipimo cha ufaulu/daraja la kuvuka hatua nyingine iangaliwe upya. Mfumo utengenezwe vizuri ili kuwe na mfumo wa kutathmini ufaulu kwa kuwa kipimo cha mtihani wa mwisho hakiakisi uelewa wa mtoto/ mwanafunzi; hii ni kwa sababu siku za mtihani zinakuwa fixed/ tension ya mtihani na mambo mengine yanaweza kupelekea mtoto ku-fail wakati amekuwa akifanya vizuri katika kipindi cha kujifunza. Nashauri badala ya final exams tujikite kwenye collective assessment and final exams iwe sehemu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuwepo kwa masomo mengi kwa wanafunzi katika ngazi zote, kuanzia darasa la kwanza hadi la saba. Hii inaweza kuanza kama proposal na ingependeza ikapendeza kufanyika kwenye block yote ya EA.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, service levy imekuwa kero kwa wafanyabiashara iondoshwe haraka, hakuna mkakati mkubwa wa kusaidia kilimo kwa lengo la kufungamanisha uchumi wa viwanda na kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya umeme inaendelea kuwepo kwani, kuna kupungua na kuongezeka umeme hasa eneo la Ukanda wa Pwani kiasi cha kuathiri viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, chuma cha Liganga na Mchuchuma, ndiyo namna pekee ya kuendeleza mradi wa SGR, vinginevyo tutapoteza fedha nyingi kununua chuma, kutoka Japan, Serikali iangalie na kuufanya mradi huu wa kipaumbele kati ya vipaumbele vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutekelezwa Mradi wa Bagamoyo wa SEZ; Serikali lazima ije na kauli moja juu ya hatma ya Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Serikali lazima ione economic impact ya kuanzisha mradi huu mkubwa kwa Taifa. Ni rai yangu Serikali ijifunze na kupembua ni ipi miradi ya mkakati na ianze nayo badala ya miradi mingine, ambayo tija yake inategemea miradi mingine, mfano SGR, inategemea ufanisi wa bandari.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto ya korosho ni rai yetu kuwa wakulima wote watatendewa haki katika kwa malipo stahiki ya mazao yao. Aidha, natoa rai kwa Serikali kuendelea na kuhakikisha mambo haya hayajitokezi tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Nchi ya Uchumi wa Viwanda; haiko clear, ni rai yangu Wizara itakamilisha suala hili haraka. Sera hii ijibu masuala ya PPP mazingira ya kufanyia biashara, elimu za biashara na kadhalika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, ubia wa SUMA JKT na Holley wa kununua hisa za milioni 744 mwaka 2007 na kutengeneza Tanzansino kwa lengo la kuzalisha dawa na bidhaa za madawa. Wabia hawa hawakuelewana, mkataba ukavunjika na kugawana mali na sehemu ya ardhi ya Jeshi ilikuwa sehemu ya mkataba. SUMA JKT wakalazimika kulipa fidia ya fedha kunusuru eneo la Jeshi kuwaangukia mkononi. Swali, ipi ilikuwa nia ya SUMA JKT kuingia ubia wa biashara ya namna hiyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wa SUMA JKT na CAMI ukiitwa CAMISUMA ukiwa na lengo la kuzalisha nguo na kusambaza (CAMISUMA Garments) 2006; SUMA 39% na CAMI 61%. Jeshi lililipa milioni 10 kwa ajili ya umeme na huduma mbalimbali kwenye hivyo viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SUMA JKT na Equator Automatic Co. Ltd; SUMA 30% na Equator 70%. Kuunganisha magari makubwa, basi, mashine za kilimo, magari ya zimamoto etc., mkataba umevunjika na mchakato wa ku-windup unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SUMA JKT na Chenggong Ltd.; Tanzania 80% na Chenggong Ltd. 20%. Lengo ni kukodisha, kuuza vifaa na mitambo mikubwa ya ujenzi, bulldozer, caterpillar etc. Mkataba uliingiwa mwaka 2015 ila upembuzi yakinifu ulifanyika 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wa matrekta ya SUMA JKT (2015) na Kampuni ya Ursus SA kutoka Poland wenye thamani ya bilioni 119.9; lengo kuuza matrekta na vipuri vyake na huduma nyinginezo. Mkataba huu pia haukukamilika, swali, kuna shida gani JKT?

Mheshimiwa Mwenyekiti, manunuzi mbalimbali yamefanyika bila kufuata taratibu au bila kupitishwa na bodi. Manunuzi yenye thamani ya 1,114,565,015 kwa mujibu wa report ya CAG 2015/2016 katika Fungu 39.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanajeshi kupewa bima ya afya; hiki kiwe kipaumbele kwa kuwa huduma ya matibabu kwenye hospitali ya jeshi haijasambaa nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umri wa miaka mitatu hadi sita kabla ya mwanajeshi kuoa ni mrefu mno kiasi cha kupelekea vijana hawa kujiingiza katika uasherati au wanawake kuchelewa sana kupata watoto ukizingatia kuwa umri wa kuzaa huwa unapita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupanda vyeo/ madaraja na mshahara; Jeshi liendelee kuhimiza uzalendo huku Serikali ikitimiza wajibu wake wa nyongeza ya mishahara na madaraja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru kwa nafasi, niipongeze hotuba ya Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni wamesema dhahiri kwamba Jeshi lifanye kazi ya kulinda mipaka ya nchi na ninarudia Jeshi letu tunalipenda sana liendelee kupambana tunapongeza uzalendo wao watulinde. Mambo ya ndani ya nchi kwa maana mambo ya siasa tuwaachie wanasiasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina hoja mbili kwa sababu ya muda, changamoto ya bima ya afya kwa wanajeshi; natambua kwamba wanajeshi wanatibiwa na wanaambiwa watimbiwe kwenye Hospitali ya Jeshi, lakini changamoto inatokea kwamba si kila sehemu ya nchi hii kuna Hospitali ya Jeshi. Wanaopaswa kutibiwa wakati mwingine ni wazazi wa mwanajeshi, ni mwenza wa mwanajeshi na watoto na sio lazima wote wawe wanaishi kwenye eneo la kambi. Nadhani Wizara iangalie na iipe kipaumbele kama ambavyo sisi tunatibiwa na bima za afya na kuchagua ni wapi pa kupata matibabu basi na wananajeshi wazalendo wanaopigania nchi hii wapate haki hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili nitaongelea Fungu Namba 39 ambalo ni JKT natambua JKT kwamba inafanya biashara kwa kupitia Shirika lake la SUMA JKT. Lakini kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye SUMA JKT kiasi kwamba wakati mwingine nakuwa napata wasiwasi CDF wanavyokuwa wa busy anafanyakazi au awaza kufanya kazi ya IGP huku SUMA JKT mbona mambo hayaendi sawa? [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Mwenyekiti, SUMA JKT wamekuwa wanajiingiza kwenye mikataba ambayo si tu haina tija kwa Taifa lakini inahatarisha hata uhai au afya ya usalama wa ndani ya nchi yetu mfano SUMA JKT waliingia mkataba na Shirika/Kampuni ya Kichina la Holley ambayo baadae ikaja kuitwa Tanzansino mwaka 2016. Walitaka kuingia kwenye biashara ya kuzalisha madawa mkataba ukavunjika, lakini sehemu ya ubia ya mkataba ilikuwa ni ardhi ya jeshi, makubliano yakawa katika kuvunja mkataba na ile sehemu ya jeshi ikatolewe ardhi ikatolewa kati China na Tanzania. Walilazimika kutoa fedha kwa ajili ya kunusuru ardhi ya jeshi, you can imagine watu wanaingia mkataba mpaka kukubali eneo ya jeshi liwe sehemu ya makubaliano ya lile eneo ni hatari sana kwa mustakabali wa uhuru wa nchi yetu au mambo ya ndani ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili hawa hawa SUMA JKT waliingia mkataba na Cami katika kiwanda chao cha uzalishaji nguo kinaitwa Cami Suma. Cami Suma walipaswa kuzalisha nguo, walilenga kulisha Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Mkataba umevunjika, hakuna kilichoendelea, lakini kinachosikitisha kati ya Tanzansino na Cami Suma waliendelea kutoa fedha zaidi ya milioni kumi kwa ajili ya ku-service zile mashine, lakini pia na umeme. Unaona kwamba wanaingia kwenye mikataba mibovu, fedha zinatumika na hakuna tija inayopatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio huo tu mkataba waliingia pia SUMA JKT na shirika moja linaitwa Equator Automatic Company ambayo hii nayo ni ya China, lengo lao lilikuwa kuunganisha magari makubwa, magari ya fire, vifaa vikubwa kwa ajili ya ujenzi mkataba huo huo ukasuasua. Mkataba sasa hivi upo kwenye wind up, wakaingia kwenye mkataba mwingine na Kampuni ya Kichina inaitwa Chenggong Limited huo mkataba ambao ni wakuingiza mashine kubwa kubwa kwa ajili ya ujenzi, kukodisha lakini pia na kuuza. Mpaka naongea hapa kumekuwa nakusuasua kwa vibali kwa sababu wakati mwingine mashine zinazoingizwa nchini ni kubwa. Huo ni mfano mdogo tu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, SUMA JKT ambayo inauza haya matrekta ambayo yote tunayajua ali maalufu kama SUMA iliingia mkataba na Kampuni ya URSUS SA kutoka Poland ikiwa ni mkataba wa zaidi ya bilioni 119. Huo mkataba wenyewe masharti hayakutimia mpaka tunavyoongea leo masharti hayakutimia kuna baadhi ya mashine hazikuja na tunavyoongea leo humu ndani kuna zaidi ya Wabunge wanadaiwa milioni 500 hawajalipa, watumishi wa umma wanadaiwa zaidi ya bilioni moja hawajalipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninajiuliza hiyo SUMA JKT ipo kwa ajili ya kusaidia Taifa kwa kupitia biashara au ipo kwa ajili ya kuangamiza Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, na badala namshauri CDF ajikite katika kusaidia hizi taasisi, kwa mujbu wa CAG taarifa ya 2015/2016 kumekuwepo na zaidi ya bilioni 1.14 zimetumika bila kufuata matumizi ya manunuzi ikiwa ni pamoja na bila kupita kwenye Bodi ya Wakurugenzi. Kuna changamoto kumbwa sana ambayo kama Jeshi tunalolitegemea litulize...

MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, kuwekeza katika Utalii katika Jiji la Dar es Salam. Jiji hili bado halijatumika vizuri katika sekta hii, hasa utalii wa mji na maeneo ya kipekee. Mfano nyumba ya makazi ya zamani ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jengo la Salamander, fukwe za bahari nakadhalika. Hii ni muhimu hasa kwa wageni wajapo Jiji la Dar es Salaam kutokea nchi za nje; mfano Jiji la Berlin Ujerumani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutengeneza ramani ndogo na mahsusi kwa maeneo ya kutembelea watalii, kwa mfano ramani mahususi ya Jiji la Dar es Salaam, kuonesha maeno na vivutio vya utalii. Kuongeza na kuboresha vivutio vya utalii Jijini Dar es Salaam, mfano Mto Msimbazi ukitengenezwa vizuri kuruhusu maji kupita wakati wote kwa kuboresha kingo na kuondoa takataka itawezesha matumizi ya boti na watalii wataweza kuzunguka kupita eneo hilo tutapata fedha lakini na mazingira yataboreshwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo yote yanayopita kwenye maeneo ya hifadhi yawe na matuta kwa ajili ya kuwakinga wanyama pori dhidi ya kugongwa na gari, kama inavyoendelea kwa sasa katika barabara ya Morogoro- Mikumi na Kitengule-Karagwe. Sheria na kanuni kali kwa watakaogonga wanyama katika maeneo ya hifadhi ya wanyama. Kuendelea kutangaza vivutio vya Utalii katika vyombo mbalimbali vya kimataifa kama CNN, BBC na hata kudhamini matukio muhimu duniani kama Olympic hata kwa kiwango kidogo kama Rwanda na PL League ya Uingereza.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kwa Mwaka 2019
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, nitoe mchango wangu kwenye Kamati yetu ya PAC ambayo pia ni Mjumbe. Nieleze masikitiko yangu na ya Kamati kwa utendaji usioridhisha wa TRA. Mwenyekiti amewasilisha vizuri sana na mimi nitaeleza pamoja na mambo mengine nitaeleza moja kati ya changamoto ambazo tulielezwa. TRA imekuwa na ufuatiliaji hafifu wa madeni ya kikodi, TRA kutofanyika mapitio ya kina ya miamala ya fedha ya makampuni mbalimbali ya Kimataifa. Na dosari katiika ukusanyaji wa makusanyo ya kodi katika viwanja vya ndege. TRA kutowasilisha kwa wakati mapato inayokusanya kwa niaba ya taasisi nyingine. TRA ina ucheleweshaji usio na tija wa maamuzi ya rufaa ya kikodi, uwepo wa madeni ya muda mrefu yasiyokusanywa. Huo ni mfano wa uozo mwingi ulioko TRA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huo ni mfano wa changamoto TRA inayosababishia watu wengine. TRA inaposhindwa kukusanya kodi inatengeneza msururu wa kuleta changamoto kwa wananchi wadogo wadogo ambao wamekuwa wakiteswa na kukamatwa kwa ajili ya kuchangia michango mbalimbali. Utaambiwa michango ya zahanati, michango ya shule, michango ya shule za kata, shule za misingi, watoto wanakaa chini kwa sababu ya watu wazembe ambao wako TRA. Sina uhakika kama ile bahati mbaya au ni makusudi, kwa sababu kama tunaweza tukaajiri watu ambao tunadhani hawana uwezo maana yake hatutaki kukusanya hela ya kutosha na tunazidi kuwaletea changamoto wananchi wetu wa chini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa katika auditing query za CAG kwa mwaka 2017/2018. Ameonesha kuna zaidi ya bilioni 974 kitengo cha kukusanya kodi za ndani yaani domestic revenue department kulikuwa na dosari alihoji CAG wapi kilipo kiwango cha zaidi ya bilioni 679 na TRA waliweza ku-verify kiasi cha bilioni 56 tu lakini kwa walipa kodi wakubwa (large tax payers) CAG alihoji kiwango cha bilioni 607 ikiwa ni pamoja na $ milioni 24 ambayo ni sawa kama na zaidi ya milioni 500. Hizi ukiziweka pamoja unapata kiwango cha shilingi bilioni 974 kama nilivyokwisha eleza awali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hizo hela zote zimekuwa zinahojiwa kwa mwaka 2017/2018. Hizo hela ungeziweka pamoja kwa kiwango cha kujenga zahanati moja kwa shilingi milioni 244 ingejenga zaidi ya zahanati 3,600. Tutakuwa hapa tunasema wanawake wanakufa kwa kujifungua, watoto wanakaa chini, watoto wanapata mimba kwa kutembea umbali mrefu kufuata elimu katika maeneo kadha wa kadha kumbe tuwasababishia sisi changamoto kwa kuweka watu katika taasisi wasioweza kukusanya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini wakati mwingine najiuliza pengine hawa watu sio kwamba wana uwezo hafifu au inafanywa makusdi.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia kuna taarifa. Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kijaji!

T A A R I F A

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa Taarifa mzungumzaji kwamba afahamu kwamba katika kipindi ambacho TRA imeimarika kiutendaji, kifanisi ni kipindi hiki na ndiyo maana mwezi wa 12, 2019 tumekusanya zaidi ya trilioni 1.976. Kwa hiyo, naomba alifahamu hilo huku akitambua hayo yalioneshwa kwenye Taarifa ya CAG, 2017/2018 ambayo Serikali tumeshaifanyia kazi kwa kiwango kikubwa na ndiyo maana tumeimarisha ukusanyaji wa mapato. Kwa hiyo, wanapojadili aweze tu kusema sasa wapi tuboreshe zaidi kwa sababu madeni mengi tayari tumeshayakusanya mpaka sasa. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Antropia Theonest unapokea Taarifa hiyo?

MHE ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei lakini nasikitika kwamba anakataa hata Taarifa ya CAG. Moja kati ya changamoto ambayo tutapata kama Serikali ni pamoja na kutotaka kushauriwa au kusikiliza watu wengine wanasema nini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni mjumbe wa Kamati…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Anatropia, ngoja tuiweke vizuri kwa sababu Taarifa ambayo Bunge inajadili ni ya 2017/2018 kwa hivyo kwa mujibu wa Kanuni zetu Taarifa uliyokuwa unapewa ni ya kuhusu maboresho yaliyokuja baada ya hiyo Taarifa kutoka. Una uhuru Kikanuni wa kukubali au kukataa lakini sasa sio hoja tena ya Waziri kwamba labda anakataa kupokea unachotoa mapendekezo. Alikuwa anakutaarifu yale ambayo Serikali imeshafanya mpaka sasa. Mheshimiwa Anatropia endelea na mchango wako.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2017/2018 ni bajeti ya kwanza kuwa na deficit ya 19.7 almost asilimia 20 ya kukadiria ambacho hakitekelezeki kwa almost asilimia 20 kwa maana watu wana expectations au wanajua vyanzo vya mapato lakini hawaendi kukusanya fedha. Ni bajeti ya kwanza kuwa na nakisi kubwa ambayo ilikadiriwa bila kukusanywa. Nadhani Waziri ana nafasi ya kujibu na atasaidia ni namna gani hizo changamoto ataweza kuzitatua katika kipindi kinachokuja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ya pili ambayo ililetwa kwenye Kamati ni juu ya kitu kinaitwa immigration. Immigration imeshaongelewa humu ndani zaidi ya mara moja na naiongelea imeletwa kwenye kamati yetu na imesababisha fungu husika kupata hati isiyoridhisha. Mtambo ulionunuliwa kwa ajili ya e-passport haukuwahi kuwa recognized kwamba ulinunuliwa shilingi ngapi, tender ilifanyika wapi? Ulikuwa na gharama gani? Lakini mkataba unahusu nini. Ametumbuliwa juzi Mheshimiwa Kangi Lugola kwa sababu amesaini mkataba ambao haukuletwa Bungeni. Nataka yeyote aniambie hapa, mkataba uliongiwa kwa ajili ya kuleta mtambo wa immigration uliletwa Bungeni? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa Mbunge hapa, uliletwa? Kama tunaamua kufanya haki, tusifanye double standard. Huo mkataba sisi kama Kamati tume-demand uletwe na tuliwafukuza waliokuja kwenye Kamati na jibu walilokuja nalo walisema haya maswali yanahusu usalama, usalama hauwezi kuwa kichaka cha kuingizia hasara Serikali hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu ambacho bado kina-shock, mtambo wenyewe hauko secure, CAG alituambia mtambo hauko secure. Mtu anaweza kuwa nyumbani kwake akawa anachapisha visa, yuko China au kokote anatoa tu Visa sehemu yoyote. Kwa hiyo, sasa ni lazima mjue athari ambayo mnalisababishia Taifa letu kama tunaamua kufichaficha mambo chini ya kapeti. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa. Ahsante sana.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nitaanza namna hii; nasoma Hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati akilifungua Bunge mwaka 2015 alisema: “Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la mchakato wa Katiba, Serikali yangu imepokea kiporo cha mchakato wa Katiba ambao haukuweza kukamilika katika awamu iliyopita. Akaahidi kwamba anatambua na kuthamini kazi kubwa ya kizalendo iliyofanywa na wananchi walioshiriki, hivyo ataiendeleza”.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ni mwaka wa sita, nataka nimwulize au niiulize Serikali, mchakato wa Katiba mpya umefikia wapi? Habari ya Katiba mpya siyo yangu, siyo yako, wala siyo ya Rais, ni ya Watanzania wote ambao walishiriki mchakato mzima. Wimbi la kutaka Katiba mpya lilionekana kabla ya kuanza mchakato mzima ina maana ni hitaji la wananchi ambao wamekuwa wakilitaka muda wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme, demand ni kubwa, hauwezi ku-resist. Unaweza ukawa-suppress watu wasiongee lakini ukweli ni kwamba ahadi aliyoahidi Mheshimiwa Rais kwamba amepokea mchakato wa Katiba, ni lazima aitekeleze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwa nini nimeanza na Katiba? Ni kwa sababu tumeona changamoto kubwa. Mheshimiwa Rais katika hotuba yake ya 2015 na 2020 mara kadhaa ameongelea mchakato wa uchaguzi; ameongelea kushukuru na kuona mchakato ulivyoendelea, lakini mchakato wa Katiba ni mchakato wa wadau. Wadau wa Katiba ni Vyama vya Siasa, ni wananchi, lakini ni Tume. Sasa inafikiaje tunakuja kuona mdau mmoja ndiyo anaona kwamba mchakato ulikuwa ni huru na haki? Ukweli ni kwamba wananchi wanalalamika, wanaona mambo yalienda ndivyo sivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais anaipongeza Tume kwamba imeweza kubakiza fedha kati ya bajeti ya shilingi bilioni 331 iliyotengwa, ilitumia shilingi bilioni 232, kwa hiyo, ilibana matumizi. Tume ilibana matumizi kweli, lakini tuliona kwa vitendo Tume ambavyo haikuweza kufanya kazi sana.

(Hapa kengele ya kwanza ililia)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, muda wangu naona umepunguzwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tume haikuweza kufanya kazi kubwa kama ambavyo ilitarajiwa. Tume ilikabiliwa na changamoto kubwa; huko chini tuliona maafisa au wasaidizi wa Tume wakigeuka na kuvaa nguo ya kijani badala ya kuwa wadau. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeingia katika uchaguzi ambao Tume ya Uchaguzi anapaswa kuwa referee. Hakuna mchezo ambao unakuwa huru na haki ambao player mmoja kama Simba au Yanga ione kwamba haki imetendeka. Siku zote watu wanamwangalia refa, hawana uhakika kama mchezo utachezwa vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niulize swali lingine, siku moja kabla ya uchaguzi tulishuhudia makaratasi mengi yamepigwa kura na kusambazwa mtaani, a day before. Nataka nijue majibu yakija, hizi karatasi zilizokuwa zimepigwa kura, zinasambazwa mtaani, mimi binafsi nilizikamata, zilitoka wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pengine Tume hawakufanya, labda ni Maafisa Wasaidizi waliopewa dhamana. Ndiyo maana tumekuwa tukisema tunahitaji Tume huru ili mshindi atakapokuja ndani hapa kila mmoja aguse kifua aseme, nimeshinda uchaguzi. Siyo tunasema umeshinda uchaguzi, kila mmoja ana wasiwasi kama ameshinda kweli. Hiyo ndiyo aina ya Tume huru tunayoitaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine, tunatamani marekebisho makubwa katika Tume ya Kusimamia Uchaguzi. Wasimamizi Wasaidizi wengi wameonekana sio waaminifu. Hata hivyo, katikati ya mchakato tumeona kubadilishwa kwa Wakurugenzi kinyume na Kanuni za Maadili tulizozisaini, kitu ambacho hakikuwa sahihi. Hiyo ilikuwa ni utangulizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudi kwenye changamoto kubwa ambayo hata Mheshimiwa Rais ameisema. Kuna changamoto kubwa ya maji. Katika hotuba ya 2015 Mheshimiwa Rais aliahidi kumtua mwanamke ndoo. Mwaka 2020 nimesoma kwenye hotuba yake anasema: “Katika maeneo mengine Mheshimiwa Rais ameona watu wanalalamika kukosa maji. Bado kuna changamoto kubwa ya maji.

(Hapa kengele ya pili ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kengele ya pili.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia dakika tano ili niweze kuwasemea wananchi wa Mkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Spika, kimsingi nieleze, nimekuwa mara nyingi nikiongelea changamoto ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Kagera hususan Wilaya za Kyerwa na Karagwe. Nimeuliza maswali mengi nikiongelea barabara na nikihusianisha Wilaya ya Karagwe na Kyerwa na kupakana na nchi ya Rwanda na Burundi. Maelezo yangu yalijikita kuonesha ni potential kiasi gani nchi inaweza kupata kama ikiunganisha Kyerwa na Karagwe na nchi hizi nyingine kwa kupitia lami.

Mheshimiwa Spika, hizi ni wilaya ambazo zinafanya vizuri katika mazao mbalimbali ya kilimo, lakini zinashindwa kufanya biashara na nchi nyingine na Mikoa mingine ya Tanzania Bara au Mikao mingine kwa sababu haina barabara.

Mheshimiwa Spika, nimeeleza mara nyingi sana barabara ya Mgakorongo - Kigarama na Murongo ambayo ina urefu wa kilometa 105. Mheshimiwa Waziri amejibu mara kadhaa, lakini nimesoma hotuba yake ya mwaka 2021, amesema barabara ipo kwenye mchakato, hakusema ipo kwenye upembuzi. Akaenda mbali zaidi, anasema, barabara wanaenda kulipa fidia. Nimesoma leo anasema, sasa ndiyo tunaenda kutangaza zabuni, lakini bado michakato haijafanyika, wananchi wamefanyiwa tathmini hawajalipwa fidia. Sasa je, tunaendaje hatua ya pili kabla bado hatujalipa hizi fidia na watu wameshindwa kuendeleza maeneo yao kwa sababu hawajalipwa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nimekuwa nikiongelea barabara ya Bugene - Nkwenda hadi kwenda Murongo huko huko ambayo ni barabara mbili; ukichukua Wilaya ya Kyerwa inaunganishwa na barabara mbili, ambapo moja unapita Mgakorongo na nyingine unapita Nkwenda. Ina maana hii Wilaya tukiweza kui-link kwa barabara tutaweza ku-tap uchumi ulio kwenye hizi Wilaya.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine, nimeeleza umuhimu wa barabara ya kutoka Benako kuja mpaka Karagwe Bugene. Hii barabara ni muhimu kwa sababu ya ulinzi. Pale ni pori, mara nyingi watu wamekuwa wanapita pale wanatekwa, wanauwawa. Hii barabara kama itaunganishwa, itakuwa ni kichocheo kikubwa cha biashara ya kutoka Karagwe, Kyerwa na Rwanda, na kuna magari mengi yanakwenda Rusumo yanahitaji kutumia hiyo barabara.

Mheshimiwa Spika, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, ni wakati sasa wa Kyerwa na Karagwe kusikika, mmetuacha muda mrefu, hebu fungueni uchumi wa maeneo haya kwa kufungua hizi barabara. Ahadi za muda mrefu, ahadi tamu tamu, maelezo mengi; na kesho nina swali la msingi. Waheshimiwa Wabunge naomba mnisikilize kesho, watakuja watatudanganya vile vile. Sasa ifikie wakati na sisi tupewe hizo barabara ili Wilaya ziweze kuchangia kwenye uchumi wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, nakushukru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru dakika tano ni chache sana niliambiwa nitakuwa na saba nianze kwa kueleza changamoto ya walimu wa wilaya ya Kyerwa, na hii nimepigiwa simu mpaka jana usiku saa tisa walimu walioajiriwa mwaka 2012 hawajawahi kupandishwa madaraja naomba muwafikirie sana na hilo suala lao mlifanyie kazi wanahisi kama wamesahauliwa tafadhali.

Mheshimiwa Spika, lakini pia nongelee changamoto ya stendi kuna shangamoto ya stendi ya mabasi Nkweda, Nkwenda ni mji mdogo na kumekuwa na ajali nyingi kutegemea kwamba mabasi yanageuzia eneo lile dogo, kwa hiyo, kuna changamoto ya ajali nyingi sana naomba hiyo muifanyie kazi.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kwa tathmini fupi naona muda ni mfupi nimepitia miaka tofauti kuangalia bajeti hii ya Wizara ya TAMISEMI na kwa kifupi naweza nikaeleza fedha imekuwa itatengwa lakini haipelekwi.

Mheshimiwa Spika, mwaka mmoja tu ambao ni mwaka jana ndio fedha imeenda kwa asilimia 62 lakini miaka mingine yote inaenda kwa asilimia 54, 52, 50 na hiyo inakuwa reflected kwenye hoja za Wabunge nikulalamikalalamika kwasababu mambo hayafanyiki fedha haiende.

Mheshimiwa Spika, nirudi tena kwenye Wilaya ya Kyerwa tunachangamoto ya huduma za afya tuna hospitali moja ambayo ni hospitali ya Wilaya lakini pia na hospitali ambayo ni ya mission. Lakini tunaambiwa kutakuwa zahanati kwa kila Kijiji tutakuwa na Kituo cha Afya, Kyerwa ina zahanati tatu, kata 24 zina Zahanati 3 ikiwa ni upungufu wa zaidi ya asilimia 80 kwa hiyo, watu wa kerwa hawana huduma za afya kwa asilimia 80.

Mheshimiwa Spika, tunaangalia huduma za afya kwa asilimia 80 tunaangalia zahanati, zahanati zipo 24 tuna vijiji 667 tukiwa na zahanati 23 ambayo ni upungufu wa asilimia 97 kwa hiyo watu asilimia 97 kwenye vijiji hawana huduma za zahanati au za kuweza kupata matibabu wanayostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia watumishi wa umma kwa kada ya afya kuna upungufu wa asilimia 67, tuna watumishi asilimia 24 tu. Kwa hiyo, tunategemea watu wa Kyerwa waishiishi tu, wakiumwa wao wenyewe wanajua itakuwaje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naongea kwa uchungu mkubwa sana, fedha za bajeti zinavyoshindwa kupelekwa kuna maeneo mengine yanafaidika, mengine yanazidi kuwa disadvantaged, moja wapo ni Kyerwa na wilaya zake nyingi za Mkoa wa Kagera; fedha ikiwa haiwezi kwenda haipelekwi kwenye hayao maeneo.

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye habari ya barabara, sitaki kuongelea, muda hautoshi lakini kule hakupitiki. Mimi narudia kusema kilio chao, wale ni Watanzania wanalipa kodi, wanastahili huduma. Kwa mfano, Kituo cha Afya cha Nkwenda nimezaliwa mimi, yaani mimi mama yangu alijifungulia pale Anatropia lakini hakijawahi kufanyiwa ukarabati mpaka leo. Pale kwenye wodi alikolazwa haijawahi kufanyiwa ukarabati mpaka leo mimi nakwenda mama mtu mzima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kituo hicho nachokisema kinahudumia out patients zaidi ya 1,000 kwa mwezi; wanawake wanaojifungua ni 300 mpaka 400 kwa mwezi; operesheni zinazofanyika pale ni zaidi ya 60 mpaka 70 kwa mwezi lakini hicho kituo cha afya kina upungufu wa majengo, hakina hata mashine ya kufulia. Wanawake zaidi ya 400 wanajifungua pale watu wanafua kwa mkono, it is totally unfair. (Makofi)

T A A R I F A

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia ukae chini upewe taarifa. Ndiyo Mchungaji, Mheshimiwa Bilakwate.

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nimpe taarifa. Pamoja na changamoto anazozisema kwenye upande wa afya, zipo, lakini Kituo cha Afya Nkwenda wamejenga maabara kubwa, wameweka jengo la upasuaji, wamepeleka vifaa vya kufulia na vya upasuaji na upasuaji unaendelea. Leo hii kuna jengo kubwa pale la mama na mtoto lina zaidi ya vyumba 24, Serikali inaendelea kuvikamilisha. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, hiyo taarifa waipokee watu wa Kyerwa waone Mbunge wao anavyowatelekeza kwa sababu changamoto anazijua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nieleze, hii siyo siasa, wanaoumia ni wananchi wa Kyerwa, wanaokosa huduma za afya ni watu wa Kyerwa, tusilete drama hapo. Asitafute legitimacy kwa kuumiza watu, tuseme ukweli, pelekeni fedha Kyerwa watu waweze kupata huduma za afya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nimeeleza habari ya changamoto ya watumishi wa afya na wale wachache ambao tuko nao, asilimia 24, wamekuwa wanabaki kwenye maeneo yaleyale madogo. Nitakwenda kutoa suluhisho; Kyerwa bado tuna nafasi ya kuongeza mapato, nimesoma ripoti ya CAG, inaonesha Mkoa wa Kagera ni moja kati ya mikoa ambayo haijafanya vizuri kwenye kupeleka ile asilimia 10 ambayo wanapaswa kurudisha kwa wazee, akina mama na watu wenye ulemavu. Hawapeleki fedha hizo kwa sababu hatuja-exhaust vyanzo vya mapato. Tuna uwezo wa kujenga stendi, tulikuwa na masoko ya kimkakati, yametelekezwa.

Mheshimiwa Spika, tuna uwezo wa kufanya biashara na Waganda, tuna uwezo wa kuwa na masoko tukafanya kazi na halmashauri ikawa na fedha. Tunaomba Kyerwa mtukumbuke kwenye masuala ya miundombinu tuweze kuzalisha vya kutosha, tutaweza kufanya maendeleo.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Muda hauko upande wako Mheshimiwa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kupata hii fursa ya kuchangia katika Wizara ya Elimu. Niungane na maoni ya wasemaji wengi na mmoja wao ameongea mchana akieleza umuhimu wa Wizara ya Elimu kuondosha fedha ya mikopo ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni 500 ambazo zinakuwa zinahesabika kama fedha ya maendeleo. Hiyo fedha inaonyesha kwamba bajeti ya Wizara inakua; bajeti ya Wizara ni kubwa, lakini katika uhalisia wake bajeti inakuwa ni ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano katika mwaka uliokwisha, kati ya miradi 33 ambayo mliahidi kuitekeleza, ni miradi sita tu imetekelezwa ambayo ni sawa na asilimia 18. Sasa hiyo inatosha kuona kwamba bajeti inaonekana iko kubwa, bajeti inajitosheleza lakini fedha inaenda kwenye kukopesha wanafunzi. Hiyo kwa nini haipo kwenye Wizara nyingine? Mbona tunaona hiyo fedha ya mafunzo, fedha ya kufanyia activities nyingine inakuja kama OC, lakini ikija kwenye Wizara ya Elimu, inaonyesha kwamba ni fedha ya maendeleo. Nadhani tusifanye hivyo ili tupate picha halisi, tujue kama fedha haitoshi tupambane ili tuweke fedha za kutosha. Mimi ndiyo wito ninaoutoa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala tumekuwa tukiliongelea humu siyo mara ya kwanza. Kwa hiyo, nitapenda Wizara itueleze, hicho kigugumizi kinatoka wapi? Kwa sababu, hii siyo mara ya kwanza, wala ya pili na aliyeisema hapa alikuwa Mbunge ambaye ni mgeni. Kwa hiyo, ina maana na yeye kwake ni concern na kwetu ni concern. Ina maana Wizara haipati fedha ya kutosha. Tukija hapa tunaona kwamba fedha ya maendeleo ni shilingi bilioni 900, lakini in reality ni kama shilingi bilioni 405 ambayo ni tofauti sasa na fedha ya mikopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapo hapo niungane na waliongea kwamba lazima vyuo vya kati vipewe mikopo, kwa sababu actually wale watu ndio tunaowahitaji kwa sasa. Leo nimesoma taarifa ya CAG kwamba, sokoni kwa maana ya ma-graduate, wanakuja kama 100,000 au 150,000 plus. Katika miaka hii mitano ina maana udahili umeongezeka, tunazidi kutengeneza ma- administrator badala ya kutengeneza watu wanaoenda kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu tuwape wale vijana fedha na tunao wengi kwa sababu ya mfumo wetu wa elimu ambao sijui kama muda wangu utanitosha, lakini ningependa kuongelea mfumo wa elimu tulionao sasa. Hiyo ni ya kwanza, kuondoa kutengeneza fungu special kwa ajili ya hiyo mikopo badala ya kuiacha kwenye kifungu cha maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaenda mbali sana, niongelee changamoto ya Wilaya ya Kyerwa. Mimi ni Diwani katika Halmshauri ya Kyerwa na ninajua Wizara ya Elimu ndiyo ina-deal na kudhibitisha sasa kwamba shule iwe-accredited sasa iweze kuwa-admit wanafunzi na ipate usajili. Kyerwa tuna changamoto ya shule nyingi ambazo hazijawa accredited. Mfano, kuna shule inaitwa Isihoro, ipo Kata ya Mrongo. Hiyo shule wazazi wamechangishana wenyewe. Ina vyumba takribani viwili mpaka tatu na ina vyoo. Ila hiyo shule haijaweza kuanza. Watoto wa maeneo hayo wanatembea zaidi ya kilomita nane kwenda kutafuta elimu, siyo sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sitaki kurudia aliyoyasema Mheshimiwa Spika; wakati wazazi sasa wanaona shule imeanza, wanapata morali ya kuendelea kujenga zaidi, lakini na Serikali itaanza kuweka jicho lake pale, lakini tukiendelea kuyaacha yale yakiwa magofu, tutakuwa tunasaidia nini? Hatupeleki walimu, hatupeleki capitation fee na majengo hayaendelei na juhudi za wananchi zinakuwa hazina maana.

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo ya Isihoro tu, hiyo ipo pia Kashanda. Nimefanya ziara, nimefika kwenye Kata ya Kakanja. Pia kuna shule inaitwa Nyakagera, nimefika. Hiyo shule sasa wamemaliza hadi Darasa la Saba, badala ya kufanyia mtihani pale kwa sababu hajijasajiliwa, wanaenda kufanyia mtihani kwenye Kata ya Kakanja, nadhani siyo sawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tutengeneze utaratibu, ambao at least ameeleza vizuri Mheshimiwa Mwalimu Tunza, kwamba hata tunavyokuwa tunasajili, basi tutengeneze standard kwamba, hii imesajiliwa lakini bado inachangamoto ABC lakini naweza kuruhusiwa kuendelea na kazi nyingine. Hiyo ipo pia huko Kata ya Kichenkura, iko Chakalisa Kata ya Kimuli, iko Kashasha, Kata ya Kibale; Muhulile, Kata ya Nkhwenda; na Chaju Kata ya Mabira. Kwa hiyo, natoa picha mwone sisi Kyerwa kama Halmashauri kama Wilaya tuna changomoto kubwa kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nichomekee hapo hapo, Mheshimiwa Waziri wewe ni mwanamama; unapoenda kugawa hizo sekondari za bweni 26 kwenye mikao mbalimbali, tunaomba Kagera hiyo sekondari ijengwe kule Kyerwa. Ninaomba hayo kwa sababu ukija kuangalia jiografia ya mkoa wetu Kyerwa ni kama imeachwa pembeni. Ni wakati huu tu zile shule za sekondari zimepandishwa hadhi na kuwa high school. Miaka yote hatuna Kidato cha Tano wala cha sita. Kwa hiyo, watoto wa kike wa maeneo yale ni watu ambao kama hawakupewa kipaumbele. Tuna ardhi ya kutosha, tuna eneo la kutosha, hebu tupeni hicho kipaumbele, tutawalipa matokeo ninakuomba sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nirudi pia kwenye ambayo wamesema wenzangu. Tuangalie dira ya elimu vis a vis output, nimepitia kama alivyoongea Mheshimiwa Askofu Gwajima na Mheshimiwa Nusrat. Wamesema Dira ya Elimu inasema ni kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mtazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa. Twende kwenye dhima, kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mfumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya wanafunzi walioelimika. Sitaki kuendelea, lakini Wabunge wengi wameongelea hapa, wanasema Sera yetu ya Elimu ya 2014 ina matatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama kila Mbunge anayesimama anaongea, Serikali inapata kigungumizi gani kurudisha mchakato na wananchi wakashiriki ili tuone aina ya elimu tunayoitaka? Mimi sioni kama sera inaongea vibaya, dhima sioni kama inaongea vibaya, lakini ukiangalia output, kwa nini hai-respond sera inasema nini? Ina maana kuna tatizo somewhere. Aidha ushiriki wa wadau au wameshindwa kuwa compatible, ina maana lazima tutafute solution ya kudumu pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mwingine ambao nitataka kuusemea kwa mfano mfupi tu leo, elimu yetu ya Tanzania tuliyonayo leo ni ya ku-pass mitihani. Ukiangalia humu ndani utaona watu wana ma-degree, watu wana vyeti, watu wana Ph.D, lakini anaelewa nini? Hilo ni swali kubwa ambalo huwezi kulijua.

Mheshimiwa Naibu Spika, mama ni mwalimu; mimi ni mwalimu pia, degree yangu ya kwanza nimesoma Ualimu. Tulifundishwa kwamba elimu ni kile ambacho kinabaki kichwani baada ya vile vyote ulivyofundisha kusahaulika. Sasa sisi tunaoenda kukusanya vyeti, unachokifanya ni kukariri tu; examination, examination and passing the exam. Unapewa cheti, biashara imeishia hapo. Ni lazima tuangalie sera yetu ya 2014, ni lazima tuangalie dira yetu tuweze kuvioainisha hivi vitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaongea kitu kingine. Leo tuna waandishi kadha kadha wa vitabu, lakini mmewahi kuona standard za vitabu vinavyoandikwa? Mmeshaona vitabu wanavyovisoma wanafunzi? Vitabu vingine ni matangopori, yaani matangopori pa pa pa! Nakumbuka tukiwa Advance na O’ Level tulisoma vitabu vya Nyambali Nyangwine, mwalimu anakuja anasema vyote vile mlivyosoma ilikuwa ni OP (out of point). Sasa leo tumeweka censorship ipi ya kuona vitabu wanavyovitumia wanafunzi wetu ni sahihi?

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nitaongelea maeneo matatu kama muda wangu ukiniruhusu. Kwanza, nitaongelea tathmini ya upatikanaji wa fedha lakini na uendelezaji wa habari ya maji. Pili, nitaongelea bajeti iliyoletwa kwenye Halmashauri ya Kyerwa lakini pia na tathimini ya CAG kuhusiana na utendaji lakini na mikataba mbalimbali ambayo imekuwa ikitekelezwa kwenye miradi ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, niseme bajeti imekuwa haiendi na haitoshi. Wabunge kadhaa wamesema utekelezaji wa bajeti ya maendeleo umekuwa ni asilimia 53 ambayo ni ndogo. Nisisahau kusema Mheshimiwa Waziri na Naibu wako mnafanya kazi nzuri sana lakini kazi mnayoifanya isipokuwa na fedha inakuwa ina matunda au tija ndogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mdogo tu ukiangalia kwa takwimu mlizoweka kwenye kitabu chenu mmesema katika mwaka wa wa fedha 2019/2020 mmeweza kuongeza tija katika upatikanaji wa maji vijijini kwa asilimia 2.3 ina maana kutoka kwa asilimia 70.1 hadi asilimia 72 point something ambayo naona kwamba ni tofauti ya asilimia 2 tu. Pia upatikanaji wa maji mjini kutoka asilimia 84 mpaka asilimia 86 unaona kwamba ni asilimia 2 tu. Kwa hiyo, kazi kubwa mnayoifanya ni asilimia 2 tu bado ni ndogo sana. Hata hivyo, mngefanya nini kama hamna fedha au bajeti? Nadhani sasa ni kazi ya Serikali kuhakikisha kwamba inapeleka fedha ya kutosha, hata kama bajeti tunayotenga Bungeni ni ndogo basi iende lakini inavyokwenda kwa asilimia 52, 53 hata kutokee maajabu hakuna kitakachofanyika. Hiyo hoja yangu ya kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ya pili ambayo nataka niongelee, kuna msemo amesema Mhindi mmoja anaitwa Rajendra Singh amesema vita ya tatu ya dunia itatokana na kukosekana kwa maji na wanavyochangia Wabunge hapa inaonyesha Dhahiri. Vita siyo lazima ushike bunduki lakini ukiona kila sehemu kuna changamoto ya maji ujue tayari hiyo ni vita. Kwa hiyo, naomba sana Serikali itoe kipaumbele kuhakikisha kwamba fedha zinakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sio tu fedha kwenda na hiyo ninaingia kwenye sehemu yangu ya tatu, CAG ameainisha changamoto nyingi sana katika miradi ya maji, muda hautoshi ningeweza kuwaeleza. Kwa uchache mikataba haitekelezwi inavyostahili na fedha zinakwenda lakini hakuna usimamizi unaofaa. Naomba Mheshimiwa Waziri utupe majibu ya ripoti ya CAG alivyoeleza changamoto hasa kwenye masuala mazima ya tendering kwamba michakato inakuwa haiendi sawasawa ndiyo maana fedha inapotea na ndiyo maana hatuoni tija katika uwekezaji wa maji. Nitakuomba Mheshimiwa Waziri uweze kuongelea suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sio hiyo tu katika bajeti iliyopita mlipanga kutekeleza miradi 1,116 imetekelezwa miradi takribani 355 ambayo ni sawasawa na asilimia 30 yaani kama tunaogelea pale pale. Hapa nirudi kwenye miradi sasa inayokuja kutekelezwa katika Halmashauri yangu ya Kyerwa. Nimekuwa nikieleza mara nyingi na Mheshimiwa Waziri nimekuwa nikikutumia picha za changamoto za maji za Kyerwa, tuna maji kwa asilimia 50 tu, zaidi ya watu asilimia 50 hawana maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Kyerwa tuna vyanzo vya maji vya kutosha na chanzo kikubwa cha maji ambapo nimewasikia wenzangu wanaongelea huko kwao Rukwa sisi kwetu tuna chanzo kikubwa cha maji ambacho ni Mto Kagera na kata zote zinazozunguka mto huu hazina maji. Nimeona mmeweka kwenye bajeti Kata za Mrongo, Bugomora, Kibale, Businde, Bugara zina changamoto ya maji lakini ni kata zinazopakana na Mto Kagera. Fedha iliyotengwa hapa, muda hautoshi ningeweza kusoma ni ndogo mtakuwa tu mnazibaziba tu viraka. Tunaomba utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji tuweze kutibu changamoto ya maji Wilaya ya Kyerwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini sio hiyo tu watu wa Kyerwa hawatanielewa nisipoongelea changamoto ya Kata ya Kikukuru, kule tangu Uhuru hawajawahi kuona bomba la maji. Kata hiyo ina wakazi zaidi ya 17,000, kwa hiyo, ni kata kubwa sana ambapo lazima Serikali iweze kusikiliza na kupeleka miradi ya maji. Hata kama haina fedha za kutosha basi chimba visima at least kwa wakati huo ambapo tunasubiria miradi mikubwa watu waweze kupata maji. Bajeti ya shilingi bilioni 3 iliyotengwa kwa ajili ya Kyerwa nisema ukweli hiyo ni ndogo sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, muda wangu ni mchache lakini Kata ya Songambele pia ndiyo picha zile nilizokutumia, watu wanakunywa maji na ng’ombe. Kuna Kata ya Rwabwere sehemu inaitwa Mkijugwangoma hawajawahi kuona maji safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari za Mwaka 2016
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha tatu, maana ya maneno, Chombo cha Habari za kielektroniki kunamaanisha na mitandao ya kijamii na njia nyingine zinazoendana na hizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii kwa kusoma itahusisha ma- group ya kwenye mitandao, facebook, messenger na blog na nyingine kama hizo zinazotumika kutoa taarifa kuwa zitaitwa vyombo vya habari na kufuata masharti kama ya vyombo vingine. Ku-include vyombo hivi ni kuminya kwa kiwango kikubwa uhuru wa kupata habari kinyume na Katiba 18(d). Blog hizi na group hizi zinahitaji kupitia process zote kama kupata leseni, Kifungu cha nane (8), hii ni kuendelea kuminya uhuru wa watu kupata taarifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 11; Wajumbe wa Bodi kuteuliwa na Waziri ni kuondoa kabisa uhuru wa Bodi na hii haioneshi nia njema kwa uhuru wa Vyombo vya Habari. Mheshimiwa Waziri ajiondoe kabisa katika uteuzi na badala yake nafasi hii igombewe na Kanuni ziandaliwe, mtu mwenye sifa apatikane kuongoza Bodi na nafasi nyingine zijazwe kwa mtindo huo huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kanuni ya 20(3), inayotaka Mwandishi kuacha kufanya kazi hii atakapopokonywa kitambulisho au kufutwa kwenye orodha ya Waandishi. Mheshimiwa Waziri, huku ni kukariri. Waandishi hawa wamegawanyika katika nyanja mbalimbali; anaweza kukosea katika kuandika akaenda kutangaza. Hii siyo haki kabisa kwa taaluma hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbona Mawaziri wanaweza kuharibu Wizara moja na kupelekwa sehemu nyingine? Tusikomoe watu kwa kuwa tuna mamlaka ya kutunga sheria juu yao. Katika taaluma nyingine kama Udaktari huwa wanafungiwa ili madhara hayo yasijitokeze tena na yanakuwa irreversible, hapa kwenye Uandishi wa Habari hali iko hivyo? Let’s be fair.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 32, mambo yenye kashfa. Tutambue hii ni nchi ya kidemokrasia ya Vyama Vingi na watu wenye mawazo tofauti. Kama tunaamua kufunga watu midomo kwa madai ya kuandika uchochezi tunaenda kuliangamiza Taifa, kwani kuwaza kwamba tunaweza kuwafunga watu midomo, sawa, lakini tutambue haiwezi kuwa wakati wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kifungu cha 50, makosa ya uchochezi, Kifungu cha 51, kutia hofu na uwoga kwa jamii. Vifungu hivi vimelenga kudhibiti nia au kusudi la kutoa maoni tofauti na watawala wanachokifuata.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Niipongeze michango ya Wabunge walio wengi lakini pia mimi nieleze changamoto ya mawasiliano na hasa ya simu kwa Mkoa wetu wa Kagera. Wakati ninyi mnaongelea kijiji kwa kijiji sisi tunaongelea changamoto ya kata kwa kata yaani inafika mahali kata nzima hawana mawasiliano. Changamoto kubwa ya maeneo yale ni kwa sababu yana miinuko, unaweza kuweka eneo moja kwa sababu kuna bonde eneo la pili lipo na changamoto ya mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nimeomba dakika tatu kueleza changamoto kubwa ya mawasiliano hususani kwenye Jimbo la Karagwe na Kyerwa kwa ndugu yangu pale. Jimbo la Kyerwa kama maeneo mengine tuna changamoto pia au tuna fursa ya kupatikana kwenye mipaka ya nchi ya Rwanda na Burundi. Sasa changomoto hiyo ambayo inapaswa kuwa fursa ya kibiashara kwetu imekuwa ni changamoto kwenye suala la mawasiliano.

Mheshimiwa Mwenyekit, kuna changamoto ya kuingiliana kwa mawasiliano upande wa Uganda. Ukiangalia kata nyingi ambazo ziko mpakani ina maana sisi tunakuwa na weak connection muda wote zinakuwa zinaingiliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiagalia kama Kata za kama za Murongo, Bugomora, Kibale, Kibingo ukifika tu unapata meseji ya welcome to Uganda hapo wewe huwezi kufanya mawasiliano ni changamoto kubwa sana. Sio hapo tu ukifika Kata kama za Isingiro, Kaisho na maeneo mengine unaambiwa welcome to Airtel Rwanda, kwa hiyo, tunajikuta muda mrefu sana tuna changamoto ya mawasilisano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo lingine ambalo ni kama bonde na liko mpakani wa Rwanda katika Kata ya Songambele linaitwa Kitega, siku moja nimeenda huko nikasema hivi hii nchi mbona kama hili eneo linaweza likavamiwa likachukuliwa kwa sababu hawana mawasiliano ya aina yoyote na wako jirani sana na Rwanda. Kwa hiyo, naomba nieleze…

T A A R I F A

MHE. ESTER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI. Taarifa.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nataka nimpe taarifa Mheshimiwa Anatropia kwamba kweli kabisa sisi tunaokaa mipakani kwa mfano kule Tarime ukifika mitaa ya Sirari wanakuambia welcome to Kenya unaingia kwenye roaming. Kwa hiyo, wale watu wanaingia gharama kubwa maana wanaoneka kama vile wako nje ya nchi.


Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nataka nimpe hiyo taarifa kwamba hayo matatizo yanawakumba watu ambao wako mipakani. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa naipokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, changamoto ya mawasiliano aliyoyasema Mheshimiwa wa Tarime na maeneo mengine ndiyo kwa kiwango inatukuta Kagera. Niombe sana na sisi Kagera hebu tukumbukeni na oneni Kagera kuna fursa ya biashara. Nimeeleza sisi Kyerwa tunapakana na nchi nyingi, kwa hiyo, tuna fursa nyingi za kibiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mwisho kabisa changamoto ya mawasiliano ya redio, jamani kwa nini mmeamua kutufundisha tuanze kuongea Kinyarwanda na Kiganda tu maana ndiyo redio tunazozisikia kule. Unataka kupata redio za Tanzania mpaka ifike saa kumi na mbili jioni ndiyo utasikia Redio Tanzania wamefungua, nadhani sio sahihi kabisa. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii nami nichangie katika Wizara hii nyeti ambayo inawagusa Watanzania wengi. Niseme natokea kwenye maeneo ambayo pia ni wakulima, Mkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Spika, wakati wengine wakiongelea miradi ya umwagiliaji, Kyerwa, Karagwe na majimbo mengine ya Mkoa wa Kagera hatuongelei miradi ya umwagiliaji. Wakati wengine wanalia na mbolea sisi hatuongelei mbolea, Mungu ametupa rasilimali, mvua ya kutosha, ardhi yenye rutuba na kila kitu, lakini tuna changamoto za kutosha.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kagera tunazalisha kahawa lakini badala ya kahawa kuwa faida imekuwa ni karaha. Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuja Kyerwa wakati fulani, nadhani moja ya kati ya kitu alichowaambia wananchi wale akasema sasa kahawa imekuwa ni ngumu kuuza kwa sababu ya janga la Corona, lakini wale wakulima ambao wanategemea kahawa per se haujaweza kuwapatia masoko, unategemea nini kitatokea? Kwa hiyo, nieleze sisi Mkoa wa Kagera tuna changamoto ya masoko ya kahawa.

Mheshimiwa Spika, nimepitia takwimu, ukiangalia uuzaji au uzalishaji wa kahawa Afrika ya kwanza inakuwa Ethiopia, ya pili ni Uganda, lakini ukiangalia ukubwa wa nchi ya Uganda ukakalinganisha na Kagera au na Tanzania, Uganda ni sawa na Kagera tu, lakini kahawa inazalishwa maeneo mengi Tanzania, Uganda wanatuzidi nini? Ukweli ni kwamba Uganda wanaweza kupata kahawa kutoka Tanzania. Jibu liko very simple kwa sababu wanaweza ku- offer price nzuri. Jana Mheshimiwa Mama Rwamlaza ameeleza hapa na mimi nikaangalia price ya kahawa za maganda bado sisi tuko chini.

Mheshimiwa Spika, pia ukirudi kwenye ranking za nani anazalisha kahawa bora, baada ya Ethiopia Tanzania inakuwa ya pili. Kwenye kuzalisha kahawa kwa wingi Afrika tunajikuta tuko kama wa sita, which means sisi bado tuna- advantage ya kuzalisha kahawa bora na ku-penetrate kwenye soko lakini hatufanyi vizuri.

Mheshimiwa Spika, nini imekuwa changamoto yetu ya msingi? Changamoto ya msingi ni vyama vya ushirika na nimeongea hapa mara nyingi kwamba mfumo tulionao wa vyama vya ushirika haufanyi vizuri, ukweli tuuseme. Hatuwezi kuendelea kung’ang’ania mfumo eti kwa sababu Ilani ya Chama chenu imeongelea ushirika, haiwezekani!

Mheshimiwa Spika, lakini nimepitia kidogo record hapa, nilikuwa napitia audited record za vyama vya ushirika hapa ambayo mmeweka kwenye ripoti yenu. Wanasema kati ya vyama 6,021 vilivyopata hati yenye kuridhisha ni 289, hii ya mwisho anasema hati chafu ni vyama vya ushirika 1,670. Kwa hiyo, sasa na hao watu mnaowang’ang’ania hawawezi hata kuandaa records na ukweli ndio uko hivyo, wanakusanya, hawawezi kulipa kwa sababu hawana fedha, it is obvious wanategemea fedha kutoka benki za biashara, kutoka kwenye Benki ya Kilimo lakini inakuja kwa muda gani? Hawa wakulima wanataka fedha waandae mashamba na waweze kupeleka watoto shule. Imekuwa ni changamoto, mnapata kigugumizi gani kuruhusu mfumo huria ukafanya kazi, ndicho kinachofanyika Uganda. Nimeenda Uganda kwa nauli yangu kwa ajili ya kwenda kuona wao wanafanyaje kuhusiana na zao hili la kahawa kwa sababu Kagera na Uganda ni almost the same, maisha na mazingira ni yaleyale, sisi tumekosea wapi?

Mheshimiwa Spika, mimi niwashauri naomba muache mfumo huria u-take place na badala yake mu-intervene kwenye haya makosa madogomadogo na yapo. Mheshimiwa Waziri umekuwa unaongelea butura, ni kweli butura ipo na inaumiza watu, lakini bado Serikali ina uwezo wa kusimamia na kuzuia hicho kitu kinachoendelea, lakini butura ina tofauti gani na biashara ya benki? Watu wanavyoenda kukopa benki si wanakopa kwa riba? Hata butura watu wanakopa kwa riba, cha msingi ni lazima muone mnaweza ku-regulate vipi ili wakulima wasiumie, hicho ndicho naweza kushauri. Mjue kwamba mnavyozidi kuwabana wakulima mnatengeneza maisha yao yawe magumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini hoja yangu ya pili kwa sababu ya muda niongelee masoko ya kibiashara yale mliyoyajenga Murongo na Nkwenda na maeneo mengine ambayo katika swali la jana nilieleza yamesimama tangu mwaka 2013. Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Kyerwa aliwahi kuuliza swali kuhusu umaliziaji wa haya masoko aliambiwa kwamba zimetengwa shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya kumalizia yale masoko. Swali lilelile akauliza Mheshimiwa Mama Rwamlaza, akaambiwa zimetengwa shilingi 2.5 billion.

Mheshimiwa Spika, nikauliza swali lilelile kwenye Bunge lililopita nikajibiwa uwongo huohuo, nimerudisha hilo swali jana, majibu ninayopewa kwamba, wametenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kwenda sasa kufanya feasibility study kuona yameishia wapi, waanzie wapi kuyajenga, it is not fair Mheshimiwa Waziri. Yale masoko mkiyajenga pale Murongo kwetu ni biashara. Kila kitu kinatoka Uganda upande wa pili kuja Tanzania, wanachokichukua Tanzania ni yale majani tu ya migomba kwa ajili ya kupika sijui wanafanyia na kitu gani kingine. Hii unaiona haiko sahihi. Bado tuna fursa za kufanya biashara, nimewaambia Mikoa ya Kagera hatuhitaji mbolea au irrigation, tunachokitaka ni intervention ya soko basi, mengine tutafanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa hii ya kuchangia katika Wizara hii ambayo kimsingi ndiyo inaakisi uchumi tunaoutaka. Kimsingi ndiyo inaakisi tunataka kwenda kwenye uchumi wa viwanda kwa kiwango gani. Nishati ya umeme ndiyo inahitajika katika kuendesha viwanda lakini je tumewekeza kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, nimepitia Mpango uliopita wa Taifa wa Miaka Mitano ambao ilikuwa 2015 – 2020, tulikuwa na lengo kwamba tunavyofika 2020 tunahitaji kufikisha megawati zaidi ya 4,000 ambayo ni 4,600 plus; kutoka kwenye megawatt 1,500 kuja mpaka megawatt 4,000 plus. Sasa katika hii miaka mitano tumeweza kufika megawatt 1,600 plus ambayo ni ongezeko la megawatt kama 100.2 ambayo sasa ukii quantify kwenye percentage unakuta ni asilimia 2.1 au tumefeli kwa asilimia 97. Kwa hiyo, ni kweli kwamba hatujafanya vizuri kwa sababu kama tunahitaji uchumi wa viwanda ni lazima tuwekeze kwenye nishati ya umeme na hayo ndiyo yalikuwa malengo yetu ya muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia kusaidia viwanda kuweza kutumia gesi asilia, kupitia TPDC tulikuwa tunaona mipango mizuri kwenye makaratasi na kwenye maelezo ya Mawaziri kwamba wanaenda kuunganisha viwanda Dar es Salaam na maeneo mengine ili waweze kutumia gesi asilia na wazo lilikuwa zuri sana. TPDC walikuja na mpango mzuri kabisa wa miaka mitatu na miaka mitano na wakaonyesha kabisa tutapata faida kiasi gani lakini ukweli ni kwamba kazi kubwa haijafanyika. Hata viwanda tu 11 ambavyo walijiwekea kwa Mkoa wa Pwani kwamba vitaunganishiwa nishati ya gesi asilia iweze kutumia hiyo nishati havijafikiwa; viwanda viwili tu wamemaliza kufanya uchambuzi na kila kitu lakini umeme wa gesi haujaanza kutoka. Kwa hiyo, naamini kwamba kama tunahitaji kufanya vizuri ni lazima nguvu iwekezwe TPDC kwa sababu gesi asili inabaki kuwa cheap lakini pia tunayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile kulikuwa na mipango kabambe ya wakazi wa Dar es Salaam na mikoa mingine kuanza kutumia gesi asili majumbani kwamba watatengeneza miundombinu hizo gesi asilia sasa zianze kupatikana kwenye majumba ambapo itasaidia gharama kuwa chini. Waliweka pilot kwamba wataunganisha viwanda 1,000 na makazi 300 leo ni zaidi ya miaka minne hakuna kilichofanyika. Kwa hiyo, nadhani TPDC inahitaji kufanya kazi kubwa kama tunataka tuone mabadiliko kwa macho.

Mheshimiwa Spika, pia walieleza kwamba maeneo ya Kawe, Tegeta na maeneo ya viwanda yataweza kuunganishwa na umeme wa gesi asili lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika. Jambo ambalo limenisikitisha TPDC kuanzisha deposit ya mafuta kwamba wataweza kuwa wana-retain petroleum wakachukua zaidi ya milioni 675 wakakarabati tank Na. 8, walivyoanza kukarabati wakagundua kumbe gharama ya kukarabati ni kubwa kuliko kujenga upya wakaahirisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hata CAG kwenye ripoti yake amesema haya ni matumizi mabaya ya fedha kwa sababu feasibility study ilipaswa kufanyika na kuona kipi kifanyike. Nadhani milioni 675 ni fedha nyingi sana. Hata hivyo, lakini bado lengo liko pale pale, naendelea kuishauri Wizara ni lazima tuimarishe TPDC na ifanye kazi kwa sababu tunaihitaji. Tayari tumewekeza vya kutosha katika gesi asilia hebu tuitende haki tutaona matokeo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nipongeze kwamba kuna kazi imefanyika na inaonekana imefanyika hasa kwenye suala nzima la REA. Mwaka 2015 vijiji vilivyokuwa vimeunganishwa na umeme vilikuwa 2,018 lakini leo tunaongelea vijiji 10,018, ni kazi ya kuigwa. Hata hivyo, hakuna mafanikio yasiyokuwa na changamoto, kuna maeneo mengine kinahesabika kijiji kimeunganishwa umeme lakini ni wakazi 20 tu. Nadhani hapa changamoto inabaki kuwa namna ya kuunganisha umeme.

Nitoe ombi kwa Serikali kama inawezekana, kupeleka umeme vijijini tayari mmetumia gharama ya kutosha, mkandarasi yuko site anapaswa kuunganisha umeme kwenye majumba lakini watu hawako tayari kuunganisha umeme. Nadhani ile gharama ya Sh.27,000 ikiwezekana Serikali iibebe, iwaunganishie watu umeme halafu waanze kukatwa kwenye ankara zao, hapo tutaweza kuona matokeo ya kuunganisha umeme. Otherwise umeme utakuwa unafika kijijini watu hawawezi kuunganisha, ndiyo ushauri naoutoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nije kwenye Halmashauri yangu ya Kyerwa. Sisi Kyerwa tuna vijiji 99, tunaipongeza kabisa Serikali vijiji vyetu 70 vina umeme, lakini bado tuna vijiji 29 havijapata umeme na REA sasa hii Awamu ya Tatu inaonyesha kwamba mtaunganisha vijiji 19, kwa hiyo vinabaki vijiji 10 ambavyo havijui hatima yake. Niombe sana Serikali hebu muiamini Kyerwa muwape umeme, haya ni maeneo ambayo yalibaki pembezoni, ni maeneo ambayo yamekuwa hayana maendeleo kwa mudu mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia ni lazima tuangalie na umeme tunaopata, tumekuwa na changamoto ya kukatika kwa umeme kiasi kwamba mtu anaona bora nisiwashe umeme kwa sababu itaenda kuniaribia kila kitu kwa sababu kila baada ya dakika tano umeme unakatika. Kwa hiyo, naomba nivitaje hivi vijiji, kuna Vijiji vya Rwakabunda, Kagu, Omswekano, Ibale, Muleba, Rwamashaju, Kishanda, Ruita, Kishanda, Rurama, Omkitembe, Ibamba, Ruko, Kitoma, Nshunga, Rushe, Kakerere, Nyamweza, Kitega, Bugara, Mugaba, Businde, Nyakasheni, Nyakatera, Kibale, Kigorogoro, Kijumbura, Mgorogoro na Mkombozi. Hivyo ni vijiji vyetu 29 ambavyo havijafikiwa na nishati ya umeme.

Mheshimiwa Spika, vilevile nimeeleza kwenye muhtasari wangu kwamba bado vijiji vilivyowekewa umeme ni wakazi wachache sana wana umeme. Nikatoa rai kwamba hebu tubebe hii gharama na tuwe tunawakata kwenye ankara kidogokidogo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, hayo ndiyo nilitaka kuongea. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, awali ya yote nianze kwa kukupongeza wewe binafsi kwa kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge. Lakini nijielekeze kwa sababu muda ni mchache. Ni dhahiri kwamba maendeleo ya nchi yoyote yanahitaji umeme, ni dhahiri kama tunahitaji kufikia uchumi wa kati ambao tumekuwa tukiusema, tunahitaji upatikanaji usiosuasua wa nishati ya umeme. Wabunge wenzangu wamekuwa wakichangia mara kadhaa hapa wakiongelea changamoto ya umeme. Nitaiongelea hususan kutokana na taarifa ya Kamati ilivyoieleza hasa suala zima la TANESCO. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, TANESCO ina changamoto kubwa ya fedha, inakabiliwa na madeni makubwa, inadai na inadaiwa. Ukisoma taarifa ya CAG inaeleza si tu kwamba inachangamoto ya fedha lakini pia ina mtaji ambao ni negative yaani working capital ni negative. Ukiangalia uwiano nasoma kwenye taarifa Kamati ya PAC na nianze kwa kumpongeza Mwenyekiti mwana mama amewasilisha vizuri sana. Ahsante sana Mwenyekiti wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukisoma ukurasa wa 26 wanaeleza uchambuzi wa vigezo mbalimbali vya tathmini ya hali fedha TANESCO. Anaeleza uwiano wa mali na madeni ya TANESCO. Anaeleza kwamba uwiano wa mali ambayo kwa kulipa zile fedha ambazo zinaweza kuwa zimeiva current ratio yake, mali ni trilioni 1.4, madeni ni trilioni 2.7. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hiyo ni fedha ambazo zinahitaji kama zikiwiva kwa muda mfupi illipe, kwa hiyo automatic TANESCO haiwezi ku-meet expense zake za mwaka lazima ipeleke mwaka unaofuata au illipe riba au interest. Lakini siyo hiyo uwiano wa ukwasi liquidity. Liquidity ya TANESCO mali za muda mfupi trilioni 1.4, madeni trilioni 2.761 hiyo ni TANESCO.

Mheshimiwa Spika, lakini tunakwenda kwa mtaji working capital, uchukue zile current asset kwamba zile fedha walizonazo fedha zake na mali inakuja ni trilioni 1.27, ije kwenye madeni trilioni 2.76 kwa hiyo, unakuja kupata TANESCO inajiendesha kwa negative trillion 1.296. kwa hiyo tunakata ifanye nini? Tunaweza kuwa na mipango mikubwa ya kuongeza nishati na tumeona juhudi zikifanywa na Serikali lakini shirika ambalo limekasimiwa mamlaka ya kununua na kusambaza umeme kama inajiendesha kwa hasara tujue kwamba changamoto ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, siyo hiyo tu, nimepitia nimeona madeni TANESCO inadaiwa na Songas Capacity Agency zaidi ya bililioni 293 ameeleza hapa Mwenyekiti wa Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini siyo hiyo tu na kwa sababu haijalipa kwa wakati hivyo imepigwa riba ya zaidi ya bilioni 62 hiyo hiyo TANESCO ila cha kushangaza TANESCO hiyo hiyo inaidai taasisi mbalimbali za Serikali zaidi ya bilioni 422. Kwa hiyo, yenyewe ipo ina suffer lakini na wadeni wake ambao hawailipi. Kuna taasisi mbalimbali za Serikali ambazo zimekuwa zikitumia huduma na hazilipi kwa wakati. Nitoe rai kwa Serikali, hebu hizo taasisi kwa sababu zinakuwa zinapewa ruzuku walipe fedha ili TANESCO iweze kujiendesha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama tunataka kuona hayo mabadiliko na mabadiliko chanya ya usambazaji wa umeme tuiwezeshe TANESCO. Tuhakikishe kwamba ina-working capital ya kutosha tuhakikishe kwamba inaweza ku-meet obligation zake za day to day, kwa sababu, mwisho wa siku changamoto kubwa inatokana na riba ambayo imekuwa inapigwa mara kwa mara kwa sababu haiwezi kulipa fedha zake kwa wakati. Hiyo nitaongelea bila kusahau TANESCO na yenyewe imekuwa na madudu yake.

Mheshimiwa Spika, TANESCO iliingia mkataba mwaka, 2007 na Kampuni moja ambayo ni ya Madini ambayo sasa katika huo mkataba TANESCO ilipaswa kuwa inakusanya fedha, kutoka kwenye hiyo Kampuni ya Buzwagi inaweka kwenye a certain account kwa ajili ya kufanya maintenance. Imekuwa haifanyi hivyo for over ten years, ina maana wewe ukaona kwamba mbali na kwamba ina changamoto ya fedha lakini pia, kuna changamoto ya uzembe ambayo TANESCO lazima wasemwe na mamlaka lazima zisimamie kuona inaweza kutimiza vigezo na masharti yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hayo ni machache ambayo naweza kuyasema na kwa sababu ya muda niongelee kidogo issue ya NIDA.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Muda umekwisha nakushukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa hii nafasi ya kuchangia katika Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ukiangalia leo changamoto ya uchumi tuliyonayo pengine tusingekuwa tumefikia kwa kiwango hiki kama tungeweza kuwa tumewekeza vya kutosha katika sekta mbalimbali ambazo ni dhahiri zingeweza kuleta matunda.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaongelea sekta ya mifugo nikiendeleza alikomalizia mwenzangu mama Kaboyoka. Mama Kaboyoka ameongelea takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya ng’ombe na mbuzi na kondoo wameongezeka na mimi nitasema kwa mujibu wa takwimu zenu. Mnasema ng’ombe leo tuna takriban milioni 33, tunakuja mbuzi milioni 25 mpaka 28, tunakuja kondoo na vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo inaonyesha kwamba sekta ya mifugo inakua kama takwimu ni za kweli, lakini ukiangalia ukuaji wa sekta ya mifugo unachangiaje kwenye pato la Taifa wamesema mifugo inachangia kwa 7% mpaka 7.4% kwa miaka miwili mfululizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, unaweza ukaona kwamba hicho ni kiwango kidogo ukilinganisha kwamba ni watu wengi wanaweza kushiriki na kujiajiri katika ufugaji. Ufugaji leo tunaouongelea na kwa kiwango kikubwa katika nchi yetu ni ufugaji wa asili, ufugaji wa asili ambao ungeweza kama ukiwekezwa vizuri kama alivyoeleza mama yangu unaweza ukaleta tija katika nchi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo sisi Tanzania ni wa pili katika mifugo nyuma ya Ethiopia na mmejinasibu kwa takwimu kwamba leo tunaweza kusindika tunapeleka mpaka Uarabuni na maeneo mengine. Hata hivyo, bado hatujafanya vizuri, nguvu kubwa tumeiwekeza kwenye maziwa lakini na bidhaa ya ng’ombe, tumesahau maziwa na nyama. Tumesahau kwamba bado kuna asset kubwa ambayo inatoka kwenye ngozi.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo kila mtu anaenda kununua kitu dukani kama ni bag, kama ni kiatu, kama ni hand bag chochote atatamani kiwe cha ngozi na ataanza kuangalia quality ya ngozi kumbe kuna fursa kubwa sana kwenye ngozi kama tukiwekeza vizuri. Nimepitia takwimu nimeona tunaeleza kwamba tukiwa na mifugo zaidi ya milioni 33 kwa takwimu za mwaka huu zinaonyesha mmeweza kupata piece za ngozi zaidi ya milioni 13. Katika piece zaidi milioni 13 hizo piece zimeweza kuleta zaidi au zikiuzwa zinaweza kuleta zaidi ya bilioni 28. Kwa mwaka uliopita ziko piece milioni 11, lakini katika piece za ngozi milioni 11 inaonekana zilikuwa zimeshauzwa zaidi au chini ya milioni 1.5. Kwa hiyo unaweza ukaona kwamba ngozi ambayo inakusanywa haiuziki na hapo ndiyo nataka nieleze vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya mifugo ya 2006 inaongelea nini kuhusu bidhaa za ngozi? Bidhaa za ngozi duniani na nchi ikishafahamika inatoa ngozi nzuri automatic tutapata bei nzuri. Nchi kama Ethiopia leo nimesoma mnaonyesha kwamba mnauza ngozi Ethiopia lakini kwa nini mnauza ngozi Ethiopia kwa sababu sisi hatuna repetition ya ku-trade ngozi duniani. Repetition ya ngozi yetu ni duni na kwa sababu wanajua ni duni na uduni huo umetokana na kufuga vibaya. Kuna mtu amefanya research anaitwa Mahmood na wenzake, ameeleza kwamba zaidi ya asilimia 60 ya ngozi inaharibikia kwenye machinjio, kwamba ng’ombe anaweza akawa ametunzwa vizuri despite challenges lakini wanavyoingia kwenye machinjio zaidi ya asilimia 60 ya ngozi inakuwa imeharibika. Akaenda mbali zaidi akasema kwa nyama inayokuwa consumed Tanzania ni 10% tu ya nyama ambazo zinachinjwa katika mabucha sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ngozi leo zipo tans and tans na nimesoma taarifa ya wafanyabiashara wanasema wana tani zaidi ya 3,000 tans zipo zimekosa soko kwa sababu hazina ubora na hivyo nitaongelea specific sera ambayo inaendelea leo mtaani kwamba tuweze kuweka alama ng’ombe, Serikali inabandika alama kwenye ng’ombe kwa kutumia hata traditional method ile ngozi inabandikwa na pasi ngozi inaunguzwa kwa hiyo inapoteza value. Kwa hiyo tunarudi kwa Mahmood alivyosema kwamba 60% ya ngozi inaharibikia kwenye mabucha mbali na sababu nyingine yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikasoma taarifa ya Wizara inasema kwamba, wameweza kupeleka visu 100 nadhani something like 116 kwenye mabucha maalum, hivi visu vya uchinjaji 116 vinasaidiaje katika ng’ombe au mabucha au wazalishaji wa nyama katika nchi hii. Which means hatujawekeza vya kutosha na hatuwezi kupata faida ya ngozi ambayo kwa kiwango kikubwa ngozi ndiyo bidhaa nzuri duniani. Wafugaji wanaendelea, viwanda au wawekezaji wa kwenye industry ya lather nchini wanalalamika, mazingira mabovu ya uwekezaji, wanalalamika kukosa incentive, wanalalamikia pia ubovu wa ngozi ambayo tunazalisha nchini. Hapa anaendelea ku-capitalize kwamba ni lazima sera ieleze bayana ni kwa kiwango gani tunaenda kupunguza ubovu wa ngozi inayopatikana ili tuweze kupata fedha za kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, tutajinasibu kwamba tuna ng’ombe wengi tunajinasibu tunazalisha nyama ya kutosha, lakini hebu tu-focus kwenye ngozi pia. Kama tukifanya vizuri kwenye finished product za ngozi na siyo tu viwanda tulivyonavyo leo by the way tulikuwa na viwanda mpaka 11, leo tuna viwanda kama vitatu au vine, lakini siyo tu kwamba vinazalisha finished goods bali vinakuwa na vyenyewe ni kama vina export raw material, vinachakata kidogo halafu vinaenda kuuza kwenye nchi za wenzetu pamoja na Burundi. Hivi leo Burundi ni wa kununua ngozi Tanzania? Leo Burundi ndiyo wanapaswa kuonekana wanazalisha ngozi nafuu ukilinganisha na Tanzania? I think something is wrong somewhere na hiyo ndiyo nataka Ofisi ya Waziri Mkuu itueleze ni mkakati gani mahsusi uliopo kupunguza ubovu wa ngozi ambayo imekuwa ikizalishwa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hiyo tu, tunataka tuambie hiyo sera leo tuliyonayo ya mifugo ya 2006, ni lini itakuwa reviewed ili iendane na wakati nimejipa homework, nikasoma sea ya mifugo ya Kenya, nikasoma sera ya mifugo ya Ethiopia, nikaone wenzetu so far wanajua wanachokifanya kwenye industry. Nadhani Ofisi ya Waziri Mkuu ni wakati umefika tuweze ku-review tuone tunaweza kufanya vizuri kwa kiwango gani zaidi kwenye soko la ngozi duniani.

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo hiyo tu ambayo naweza nikaeleza bidhaa za ngozi ambayo nimekuwa nikizieleza au nimekuwa nikieleza hapa ikikabiliwa na changamoto ya kuwa mbovu bado pia kuna ujanja ujanja hapa katikati, kwamba wanaodili na bidhaa za ngozi wanakuwa na madalali ambao wanalalia hata wao wenyewe wafanyabiashara wanaonunua ngozi, which means tumetengeneza middle men hapa katikati. Wafanyabiashara wa ngozi au wa viwanda vya ngozi wamesema kwamba ngozi yenyewe inayozalishwa ngozi nzima ni chini ya 15% ambayo ni first grade na second grade.

Kwa hiyo, naomba nitoe wito kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo inasimamia sera itusaidie kama ambavyo nguvu kubwa inaelekezwa kwenye maziwa na nyama, tuone mabadiliko kwenye ngozi pia, ndiyo tutaweza kupata tulichokuwa tunataraji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kuongelea changamoto leo ambayo tunapitia ya kupanda kwa bei ya mafuta. Kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na mafuta ya kula yatakuwa na impact kwenye uchumi baadaye…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na mimi kunipa nafasi ya kuchangia machache kati ya yaliokuwa mengi yaliojiri kwenye Kamati yetu. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC. Tumetoa taarifa yetu, hayo ni baadhi ya mengi tuliyoyaona.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kuseme bado kuna changamoto kubwa ya value for money kwenye taasisi mbali mbali ambazo zinapewa fedha na Serikali. Taasisi nyingi au matumizi ya fedha yamekuwa si sahihi kwa sababu ya namna ambavyo haya mafungu, fedha zinavyotoka ina maana fedha kama haitoki kwa wakati, wakati mwingine inachelewesha kazi na hivyo Serikali kulipa riba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nitachangia maeneo mawili, suala la kwanza ni mifuko ya uwekezaji ya wananchi kiuchumi lakini suala la pili, nitaongelea miradi ya maji, usanifu wa miradi ya maji; na hizi ni taarifa ambazo zipo kwenye Ripoti ya CAG.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza ni kuhusu mifuko ya uwekezaji wa wananchi kiuchumi. Katika taarifa ambayo ipo kwenye kishikwambi chetu, Mdhibiti ameonyesha ni kwa kiwango gani fedha zimetumika ndivyo sivyo; na kama hiyo haitoshi imetumika kwa watu wasiokuwa walengwa. Imesema out of 99 bilion ambazo zilitolewa ni zaidi ya bilioni 50.4 zilipigwa kwa maana ziliishia kwenye mikono ambayo haikuwa salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano kulikuwa na mifuko mitatu, mfano, mfuko wa pembejeo ambao ulitengewa bilioni 28, bilioni 20 zilipigwa ina maana kilichoweza kutumika ni bilioni nane tu ambapo ni sawa na zaidi ya asilimia 72 zilitumika ndivyo sivyo. Mfuko wa Kilimo Kwanza ambao ulitengewa bilioni 34, bilioni 28 zilipigwa au kutumika ndivyo sivyo, sawa na asilimia 80. Katika Mfuko wa Self-microfinance out of 34 ni bilioni 3.7 ambazo zilitumika ndivyo sivyo sawa na asilimia saba ya kile kiwango cha fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini ninasema haya, na kwa nini naongelea hizi fedha, ni kwa sababu hizi fedha zimetengwa kwa ajili ya kusaidia wale wafanyabiashara wadogo wadogo, wale watu ambao hawana access na maeneo ya benki.

Mheshimiwa Naibu Spika, takwimu zinaonyesha ni asilimia 28 ya Watanzania hawawezi ku-access fedha za benki, hawawezi ku - access mikopo. Kwa hiyo, hiyo mifuko ililenga asilimia 28 ya lile kundi la kundi la Watanzania ambalo haliwezi ku-access fund, kwa maana ya vikundi vidogo vidogo na watu ambao wana maisha ya chini. Kwa takwimu zetu leo ina maana ni zaidi ya watu milioni 17; na ukilinganisha na nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki, Kenya ni watu asilimia 18 ambao hawawezi ku– access fund, Uganda asilimia 14 na Rwanda asilimia 11. Kwahiyo, unaona kwamba Tanzania tuna asilimia kubwa ya wananchi hawawezi ku-access fund; na Serikali kwa maksudi ilianzisha mifuko na kuweka fedha ili ziweze kuwasaidia hawa watu kujikwamua.

Mhesimiwa Naibu Spika, nini kilichotokea? Kitu cha kwanza kilichotokea, wale ambao walipaswa kusimamia mifuko badala ya fedha hizo kupelekwa kwa wale wajasiriamali na watu wanaohitaji fedha; katika tathmini au katika study walioifanya mwaka 2016 na 2017 zaidi ya 80 percent ya zile fedha zilikuwa zimewekezwa benki au zimekopesha benki badala ya wajasiriamali wadogo wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini si hiyo tu wamesema kwa tathmini ya 2017 mpaka 2021 zaidi ya asilimia 72 fedha zilienda ambako hazikupaswa kwenda. Kwa maana ya wajasiriamali, wale watu wadogo wadogo wakulima akina mama hawakuweza ku-access fund. Kwa hiyo tunaweza kuwa humu ndani tunapiga kelele tunaangalia tutawakwamua vipi wananchi kumbe kuna watu wamepewa mamlaka, watu wanakusanya fedha au watu wamekuwa custodian wa hzio fedha lakini wanazipeleka maeneo yasiyofaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mimi nakumbuka kipindi fulani nikiwa Halmashauri ya Ilala vilikuwa vinatengenezwa vikundi vya mfukoni watu wanaenda wanakusanya fedha wanapiga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na wameeleza na CAG ameeleza ni kwa nini hizo fedha zimepotea. Kwanza, watu walikuwa wanapewa fedha bila kufuata hata vigezo; pili, kulikuwepo na eneo la kuweka dhamana watu walikuwa wanapewa fedha bila hata ya kuweka dhamana, tatu; watu walikua wanakopa fedha bila hata kwenda kufanyia maksudi makubwa waliyoombewa fedha. Ambacho unaweza ukasema kwa kifupi ni kuona kwamba ni conspiracy. Watu waliopaswa kusimamia fedha walishirikiana na baadhi ya watu wakaweza kupoteza hizo hela. Inasikitisha sana, lakini si hiyo tu, walianzisha mifuko mingi; na Kamati yetu imekuja na pendekezo kwamba hiyo mifuko zaidi ya 52 waliyoanzisha kwa kazi ile ile; ningepata muda ningewasomea hii mifuko; mifuko hiyo inatoa mikopo kwa makundi yale yale na mwisho ya mwisho hizo fedha zikapotea. Ndiyo maana tumekuja na pendekezo kwamba mifuko iwe consolidated, iwe michache na iweze kuwa manage. Hayo ni machache (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini katika miradi ya maji, fedha nyingi zinapotea kwa sababu ya miradi ya maji ambayo Mdhibiti na Mkaguzi ameonesha katika ripoti yake ya ufanisi kwamba tatizo kubwa ni kutokuwa na masterplan. Ina maana usanifu wa kina haufanyiki licha ya kwamba sheria…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzumnguzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nami nichangie mawili, matatu kwenye hii Wizara ambayo inawagusa Watanzania walio wengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati nikichangia katika hii Wizara, taarifa na randama na hotuba inaeleza kwamba kilimo kimeshuka toka mwaka 2021 kuja 2022. Mwaka 2021 inaonesha kilimo kilikua kwa asilimia 4.9, leo tunaongelea asilimia 3.9. Vivyo hivyo, kilimo kimeshuka kwa namna ambavyo kimekuwa kikichangia katika Pato la Taifa, kutoka asilimia 27 kuja asilimia 26.3 hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini naongelea haya, unavyoongelea kilimo kushuka maana yake unaathiri sekta ya watu wengi ambayo ameeleza Waziri kwamba ni asilimia 65 wanategemea kilimo. Kilimo kikishuka tunaongelea umaskini, kwamba watu wengi waliokuwa wanategemea kilimo katika kujikomboa katika maisha yao ya kawaida tayari maisha yao yameshapata shaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, kilimo kinavyoshuka kwa sababu kilimo ni mnyororo wa thamani, kilimo kinagusa viwanda, kinagusa sekta mbalimbali za usafirishaji na kwingine, lakini unavyoona kilimo kinashuka ina maana kinakuwa na negative impact kwenye uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyoongelea kilimo, Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali amesema katika eneo dogo tu la uzalishaji wa viwanda vya alizeti, anasema kwamba kati ya viwanda 12 vilivyokuwepo, viwanda vitano vimefungwa. Katika viwanda ambavyo vimebaki kati ya hivyo 12 vinategemea ku-import product kwa asilimia 75. Kwa hiyo, unaona kwamba kilimo kushuka kinakuwa na negative impact ya kwenye uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, Serikali inatumia zaidi ya shilingi bilioni 450 kwa ajili ya kuagiza bidhaa za mafuta kutoka nje. Sasa hiyo tayari inakuwa na multiplier effect kwenye uchumi wa nchi yetu. Sasa ni kwa nini, tunawezaje kuendelea kuongelea changamoto ya kilimo kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru. Ameeleza Waziri hapa, anasema kama nchi tuna ardhi ambayo inafaa kwa kilimo zaidi ya ekari milioni 44, lakini huyohuyo akasema ni ekari milioni 10 tu ambazo zimetumika kwa ajili ya kilimo. Ni takwimu ambazo siyo tu zinakera lakini haziwatendei haki wananchi wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunavyoeleza hapa kuna vinchi vidogovidogo kama Uganda na Rwanda ambavyo bado vinafanya vizuri, licha ya kuwa na ardhi ndogo bado wanaweza kuzalisha vizuri. Swali nauliza, je, Waheshimiwa Mawaziri tunakwama wapi? Hilo ndilo tunapaswa tujiulize. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunakuja na hoja za mbolea, lakini tunaweza kuongelea viwanda vya mbolea miaka 60 baada ya uhuru? Tunakuja na hoja za vita ya Ukraine na Russia, tunapaswa kuongelea hivyo vitu miaka 60 baada ya uhuru? Nadhani kuna kitu hakiko sawa na tukijipanga vizuri tutaweza kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia fedha tu inayotumika kwa ajili ya kuagiza bidhaa za chakula, mmeeleza ngano, sisi hatuzalishi ngano, tunazalisha ngano kidogo, mnatumia US Dollars zaidi ya milioni 221 kuagiza ngano nje badala ya kuwasaidia wakulima wetu tukiwa na ardhi ya kutosha wakazalisha ngano nchini tuka-save hizo US Dollars, tukaweza kuendeleza viwanda au maeneo mengine katika nchi yetu. Kwa hiyo, hapo ni dhahiri kwamba tunakwama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia mmeeleza bayana kwamba kushuka kwa kilimo bado kumekuwa na impact katika uzalishaji. Mmeeleza hivi, katika mwaka uliopita tulizalisha tani milioni 18, kwa mwaka huu unaoisha tumezalisha tani milioni 17, ambapo hapa ukihesabu unaona surplus ni tani milioni mbili. Ukiangalia tani milioni mbili tunaweza ku-export wapi tani milioni mbili? Tunaweza kuingiza fedha za kigeni kiasi gani za kigeni kutoka kwenye kilimo tukiwa na tani milioni mbili tu? Kuna kitu hakiko sawa. Tuna ardhi ya kutosha, tuna vijana wenye nguvu, tuna masoko yametuzunguka, tuna nchi nyingi ambazo zinahitaji chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niliongelea juzi kwamba sisi ni signatory wa Biashara Huru ya Bara la Afrika, tunaenda kufanya nini kama hatujajipanga vizuri kwenye kilimo na tuka- capture na ku-export tukapata fedha za kigeni? Hapo tunalo jambo la kujiuliza na tunapaswa kutoa majibu, Waheshimiwa Mawaziri mmepewa dhamana tuisaidie Serikali tuweze kufikia malengo ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe mfano mwingine. Mmeeleza kwamba kwenye maghala sasa tuna-reserve ya tani 159,000 kama sikosei, lakini ukiangalia tani hizo sisi matumizi yetu kwa mwaka kama nchi tumesema ni tani milioni 15. Ukichukua hiyo milioni 15 ukagawa kwa miezi 12 unapata kwa mwezi nchi inatumia chakula ambacho ni tani milioni moja kama na laki mbili na nusu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukichukua kwa mwezi ukagawa kwa siku unakuta ni tani 41,000 kwa siku. Kwa hiyo, ukichukua zile tani mlizoziweka kwenye reserve ambazo ni tani 159,000 unakuta tuna chakula cha siku tatu tu kuisaidia hii nchi. Yaani kukitokea kama yaliyoikuta Ukraine na Russia, Serikali kwenye National Reserve watu wa nchi hii wata- survive kwa siku tatu tu, itakuwa ni crisis! Kwa hiyo, tuna safari ya kwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo kama hamnunui mazao kuna wananchi wetu wa Kagera. Niliwahi kukwambia Mheshimiwa Waziri, kwamba sisi Kagera, Kyerwa, Karagwe, tunazalisha mahindi. Mahindi kwetu ni kilimo cha biashara. Ukifika wakati wa kuuza mnatuambia tusiuze, lakini ninyi ambao mnapaswa kununua mazao tena kwa bei ya soko, hamnunui. Kwa hiyo wananchi wanabaki kuwa stranded bila kujua cha kufanya. Do you think mnatutendea haki ninyi Mawaziri vijana? Tunakwama wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninalotaka kuongelea ni kilimo cha kahawa. Bado Mkoa wa Kagera tuna changamoto licha ya kuwa leo tumeweza kufanya minada na tunamshukuru Mungu bei ilipanda, tuna changamoto ya mnyauko. Mnyauko uko kwenye kahawa zinaendelea kuharibika tunataka solution.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna changamoto ya mnyauko kwenye migomba (ndizi). Hiyo ni crisis. Leo sisi tunakula ugali kama Wasukuma, siyo sawa. Tunataka majibu ya changamoto ya mnyauko kwenye Mkoa wa Kagera. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeeleza kwamba tunahitaji mbegu za kutosha, miche mipya. Tumekuwa tukilima kwa asili ambayo ni ile miti mikubwa. Tunataka mbegu za kisasa. Nimesoma kwenye takwimu, nikaona hamjatutendea haki, sisi ni wakulima wakubwa wa robusta lakini kwa miche mliyoonesha hapa, licha ya kwamba Mkoa wetu na mikoa mingine inayozalisha robusta ina asilimia kubwa, zaidi ya 40, sisi tumepata miche michache sana, it’s not fair. Nadhani usiwe mkakati mdogo mdogo wa kupunguza nguvu ya robusta kwenye soko please! Tunaomba tupewe miche ya kutosha tuweze ku-compete.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimaliza bila kuongelea masoko ya kibiashara ya Mrongo na Nkwenda sitawatendea haki wananchi wangu wa Kyerwa. Ninataka majibu, kwanza ni fedha kiasi gani ilitumika kujenga yale masoko ambayo mwisho yalitelekezwa, pia sababu ya kuyaanzisha yale masoko ambayo kimkakati yalikuwa mpakani kutusaidia tufanye biashara ya ndizi na kahawa. Je, walioweka huo mkakati walikosea? Kama hawakukosea, sisi tunalima ndizi, ndizi zetu leo zinakuwa smuggled kwenda Uganda, na zinajikuta ziko Marekani na kwingine, kwa nini sisi tusifanye hiyo biashara? (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Anatropia.

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa soko la vanila. Tunaomba mtupe jibu la soko la vanila kwa sababu tupo stranded. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana, muda wako umeisha, nakushukuru sana Mheshimiwa Anatropia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana nami niongee mawili katika hii Wizara ambayo ni moja kati ya Wizara kubwa bahati mbaya sana tunaweza tusiwe tunaona ukubwa wake. Ukubwa wake hauonekani, moja katika bajeti kwa sababu bajeti ina-signify au bajeti inaonesha ni kwa kiwango gani watu mnachukulia serious Wizara husika ambayo mnaisemea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni inapaswa kuwa ndiyo definition halisi ya sura ya nchi lakini leo na bahati mbaya sana wakati ninatafakari nikafikiria pengine Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni tunaichukulia kama Wizara ya Michezo, yaani tunai-qualify kwamba ni mchezo na ndiyo maana tunafanya mchezo na ndiyo maana bajeti yetu inakuja ikiwa ya mchezo mchezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niulize, hivi shilingi bilioni 35 unaweza ukafanya nini, unaongelea fedha ya maendeleo shilingi bilioni 11 imeeleza vizuri Kamati hapa unaweza ukafanya nini? Siyo hiyo tu, tumeona hata bajeti iliyokuwa imetengwa mwaka jana haijaenda kwa asilimia 100. Kwa hiyo ni vitu ambavyo moja ni vichekesho, mbili inatuonesha hata sisi tunaochangia hatuko serious tunafanya sanaa kama Wizara tunavyoiita ya sanaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema siyo sahihi? Moja, mnachopaswa kujua, michezo, utamaduni ni moja kati ya vitu ambavyo tunaweza kupata foreign currency. Ni maeneo ambayo nchi ikiamua kuwekeza vizuri, leo ukiitaja Marekani inajulikana Marekani kwa kucheza rugby. Ukitaja Marekani inaonekana kwa kucheza basket, ukiongelea Kenya wanajulikana kwa kukimbia kwa riadha. Leo ukiitaja India kwa mbali utasikiliza utafikiria Bollywood. Ukiitaja Nigeria utaongelea Nollywood. Sisi tunajulikana kwa lipi? Hatuwezi kukimbiza kuku, hatuwezi kukimbia, hatuwezi kufanya chochote, is it true? Siyo kweli. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vyote tunaweza kuvifanya. Tumekosa utashi wa kufanya hayo yote. (Makofi)

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

TAARIFA

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ramadhan Ramadhan.

MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa mzungumzaji kwamba sisi ukitutaja tunajulikana kama Swahiliwood. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia taarifa unaipokea?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo mbaya hata kuwa Swahiliwood siyo mbaya ni lugha kama ambavyo wengine ni Englishwood ni Indianwood lakini we have to go far, lazima tuende mbali na hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ikabidi niitafute dira, dira ipi inatuongoza kufanya kazi? Dira ipi imekuwa instrument ya Wizara, tena nimesoma ikawa, “Kuwa Wizara inayohakikisha ushiriki wa ushindani katika michezo, sanaa na utamaduni wa kitaifa unaolenga maendeleo ya Taifa.” Nikataka niwaulize ninyi mmeisaidiaje hizi tasnia kuwa washiriki wenye ushindani? Mmesaidiaje michezo kwa maana ya mipira kuwa kwenye ushindani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Yanga niwapongeze watani wangu Yanga mmejaribu baada ya miaka 30 ya Simba leo mmejaribu. Niwapongeze Yanga, mmeona Yanga wamewekeza wakaleta wachezaji wazuri wamepata walichokipata. Vivyo hivo kwenye michezo mingine wanasema numbers don’t lie, eh? Ukiwekeza unapata matokeo, wamewekeza wamepata matokeo. Tunataka tupate matokeo gani kwenye Wizara ya Sanaa na Michezo tukiwa tumewekeza shilingi bilioni 35? Tukiweka hela ya maendeleo ambayo ni shilingi bilioni 11 kwenye bajeti amesema hapa msemaji anasema out of 15 trillion ya fedha za maendeleo, sisi tumeweka shilingi bilioni ngapi, bilioni 11 ambayo ni 0.08 kwenye fedha za maendeleo. Hivi tunataka maajabu kutoka nchi gani tuweze kufanikisha hii sera? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwa nini ninasisitiza umuhimu wa Wizara hii? Moja ni source kubwa ya kupata ajira. Mbili; ni source kubwa ya kupata fedha za kigeni. Tatu; ni source kubwa ya kusaidia hata vipato vya kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma mchango wa Wizara hii katika Pato la Taifa ni 0.03! Siyo sawa, tunaweza kufanya vizuri kama tukiamua. Mimi ningekutana na Mheshimiwa Rais kama ananisikia ni lazima tufanye overhaul. Yaani tufanye a total transformation. Moja; jinsi ambavyo tunaitafsiri michezo katika hii nchi. Hatuwezi kuchukulia michezo kama kitu eti tunataka kufurahisha watu, tumeshaenda zaidi ya kufurahisha watu, tunataka kupata fedha, kupata utajiri kutoka kwenye vipaji vyetu. Kwa hiyo, nitamshauri Mheshimiwa Rais afanye transformation. Pia hii Wizara aipe uzito kama zilivyo Wizara nyingi na kubwa katika nchi hii. Yaani ukiacha Wizara ambayo tunaiona ni kubwa, ya pili inapaswa kuwa Wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa kwa sababu ya umuhimu na ukubwa wake kugusa watu wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafikaje hapo. Moja; ni lazima turudi sasa kwenye tulivyoanza miaka ile, tufungue vyuo mbalimbali vya michezo. Tu-train walimu wa kutosha wa michezo. Ni lazima tu-recruit. Serikali ina maana ni vitu viwili; sera na uwekezaji wa Serikali. Kama sera yetu ikijikita ikaendana sambamba na uwekezaji wa Serikali tutafika tunakokutaka na hapo tunakuja kuongelea mambo ya scouting. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kuna vipaji kadha wa kadha mitaani. Nitatoa mfano Mheshimiwa Waziri. Kuna baadhi ya vijana niliwatoa Kyerwa kuja kuwasaidia kwenye academy mbalimbali kwenye hii nchi. Nataka nikwaambie nimehangaika hata kuwatafutia timu za ku-train mpaka nimechoka. Yaani huwezi hata kupata timu hata kama kijana ana uwezo wa kiasi gani wa kucheza mpira, kupata hata timu ya kuchezea ni changamoto kubwa sana, na hao ni watu ambao at least wanamjua Mbunge, vipi wale ambao hawana hata wa kuwashika mkono? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siyo hiyo tu, walimu uwaandaliwe wa kutosha kwenye vyuo, lakini hivyo vyuo kuna baadhi ya academy leo zina-train michezo. Moja; zipewe ruzuku kidogo lakini zipunguziwe gharama ili ziweze kuwekeza zaidi katika ku-spot na kutengeneza walimu na wanamichezo vilevile. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu; Lazima tutafute partnership. Bahati nzuri wanamichezo tulipata ridhaa ya kwenda Southern Sudan. Tuliona Southern Sudan wanajiandaaje kushika dunia ya michezo. Kila ulikoenda wamefungua academy za basketball, za football, za netball, sisi tunafanya nini hapa? Viwanja vya michezo vilivyokuwepo kwenye maeneo yetu leo vyote vimevamiwa. Maeneo ya wazi yote leo watu wameyafanya mabaa, watu wamejenga na hakuna anayeongelea tena na Wizara hapa sijaona inaelezeaje tunawezaje ku-promote michezo bila kuwa na viwanja vya michezo hususan mpira wa miguu naongelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tuna safari ya kwenda, tuna safari ya kwenda kabla ya kujua tunafikaje kule na hiyo inaanza na total transformation na hiyo inaanza na kubadilisha mindset na hiyo inaanza na political will ambayo sasa hiyo ni bajeti ya Serikali. Nakushukuru. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi niweze kuchangaia katika bajeti iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kwa maombi. Ombi langu la kwanza niliuliza swali siku moja hapa ni kwa kiwango gani Mkoa wa Kagera unachangia kwenye Pato la Taifa, nilijibiwa kwamba tunachangia kwa asilimia 2.3 na swali langu la nyongeza nilisema hatutendewi haki kama Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kagera ina rasilimali za kutosha na inaweza ikachangia sana kwenye Pato la Taifa na sababu kwa nini haichanagii, Moja, hakuna viwanda lakini tunazo rasilimali za viwanda. Ni kazi sasa ya Serikali kuvutia wawekezaji kwa kuweka zile pull factors, kupunguza kodi kadha wa kadha lakini na masharti ya uwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni miundombinu na ndiyo ninachotaka kuongea leo. Ninaiomba Wizara kwa namna ya pekee, tunaomba barabara ambayo inaenda Murongo kutokea Mugakorongo iweze kutengewa na kupatiwa fedha sasa wananchi walipwe fidia na barabara ianze kujengwa. Barabara ya pili ni barabara ya Omurushaka ambayo ni Bugene kuja Nkwenda kuja Kaisho mpaka Murongo. Tuweze kuunganisha hizi barabara mbili tuweze ku – boost uchumi wa Mkoa wa Kagera na sisi tutafurahi kupitia kahawa, kupitia mahindi, kupitia mazao yote ambayo kama Mkoa tunazalisha, tuweze kuchangia hata asilimia 10 kwenye pato la Taifa. Uwezo huo tunao, tuna misimu ya mvua miwili na mambo kadha wa kadha.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nitaongelea. Tunaongelea bajeti leo ambayo ni ya trilioni 44 point something, lakini ukiangalia ile bajeti ya trilioni 44 point something, bajeti ya fedha za maendeleo imeshuka. Ukiangalia bajeti ya trilioni 41 fedha ya maendeleo ilikuwa juu kidogo ilikuwa ni trilioni 15 lakini leo tuna bajeti ya trilioni 44 lakini fedha za maendeleo zinakuja kwenye trilioni 14. Unaona kwamba kuna kushuka, sasa hatuwezi kuji–confine kwenye kutumia ni lazima tuji–confine kwenye kuendeleza vitu tulivyonavyo, kujenga barabara na vitu kadha wa kadha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunchopaswa kufanya ni kuanza kama siyo kufunga mkanda basi ni kuongeza tax base na hilo ndiyo nataka nilitoe. Bajeti ya sasa inaonesha kwamba asilimia 68 itaenda kwenye matumizi, hiyo nadhani haiko sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho wengi wameeleza na mimi nieleze, nimpongeze pia Mheshimiwa Rais amefanya kazi nzuri sana, lakini katika kumpongeza Mheshimiwa Rais ni task kwenu. Alichokifanya Mheshimiwa Rais ndio alichokifanya Yesu siku ya Alhamisi Kuu aliwanawisha miguu Mitume baada ya ya kuwanawisha miguu wakasema nenda fanya na kwa wengine. Rais alivyozindua Royal Tour hakumaanisha yeye aendelee kuandaa Royal Tour na kufanya films. Alitaka ninyi wasaidizi wake nendeni mfanye kama alivyofanya yeye, amefanya mara moja ameweza ku-boost sekta ya utalii zaidi ya asilimia 109 kwa utalii wa ndani, lakini pia na utalii wa nje umekua kwa zaidi ya asilimia 59. Ninyi ambao mmeoneshwa ninyi mitume mmefanya nini? Hilo ni swali kwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ninalolileta kwenu. Bado tuna nafasi ya kufanya kwa ajili ya kuongeza, mimi lengo langu ni tuweze kukusanya zaidi. Nimesikitika Halmashauri zetu zaidi ya 180 kushindwa kukusanya hata trilioni moja. Leo projection imeonesha twende mpaka trilioni moja point something, lakini kwa Halmashauri nyingi tulizonazo kushindwa kukusanya trilioni moja siyo sawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ina maana na ukweli ni kwamba hela inapatikana kwa watu masikini lakini fedha inavuja. Mheshimiwa Waziri umeeleza Mama Samia, Mama yetu hapendi rushwa na ameagiza watu wale waliohusika kwenye ufisadi washughulikiwe. Tunataka taarifa kamili watu wote waliohusika kwenye Halmashauri kutorosha fedha mbichi, kutorosha fedha za hao walipakodi, wameweza kushughulikiwa kwa kiwango gani ili tuweze kupunguza kukopa? Hilo ndilo nalileta kwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri mambo yafuatayo: -

Kwanza; kama Wizara au Serikali lazima m–build trust kwa walipa kodi. Siyo ku–build trust lakini m–prove kwamba kodi mnazokusanya zinatumika sawasawa. Huo ndio ushauri wangu wa kwanza. Kwa kuziba mianya yote ya kodi.

Pili; ni lazima tuwe na mfumo wa ukusanyaji kodi ambao ni rahisi na rafiki kwa kila mtu.

Tatu; ni lazima twende kwenye digital kwenye kukusanya mapato. Tumeongelea suala la TAUSI kwenye Halmasahuri, ni kwa kiwango gani halmashauri zimekuwa zikitumia Mfumo wa TAUSI katika kukusanya mapato. Tumeendelea na mifumo ambayo ni manual inaruhusu watu kuendelea kuchezea mapato ya Serikali, siyo sawa. (Makofi)

Nne; ni lazima tuongeze tax base. Huu mfumo ambao nimekuwa nikieleza mara nyingi wa 28 rules inasababisha watu wakwepe kulipoa kodi. Moja, walipakodi ni wachache na wanapaswa kutoa mzigo mkubwa, kwa hiyo lazima watakwepa. Tutengeneze mfumo ambao katikati walipakodi ni wengi. Walipakodi wawe wengi na kodi zitakuwa nyingi lakini hapo hapo tuondoe mianya ya usumbufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kuna changamoto ya compliance kwa sababu ya ugumu. Tuliongelea blue print hapa kwa nini hamjaleta blue print ili tuweze kupunguza urasimu, usumbufu katika ufanyaji wa biashara hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hayo ni machache nakushukuru, muda ni mchache sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, najua dakika tano ni chache sana nitaongelea mambo mawili. Suala la kwanza ni masoko ya kibiashara ambayo hayo masoko Mheshimiwa Waziri tumekuwa tukieleza sana watu wa Mkoa wa Kagera. Nimeangalia kwenye taarifa ya Waziri sijaona amesema nini. Hayo masoko ndiyo biashara kubwa, hayo masoko ndiyo kiunganishi tunachokitegemea ili tukafanye biashara. Masoko yako Nkwenda, Mrongo na pia Mtukura. Hayo masoko yamejengwa kwa fedha za mikopo, lakini pia na Serikali, sasa kuyatelekeza haina maana ina maana hakuna value for money. Naiomba Wizara hii na Mheshimiwa Waziri ni mchapakazi, hebu aseme neno moja na watu wa Mkoa wa Kagera ili wapone. Kwa hiyo hilo ni suala la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hayo masoko ninayoyaongelea yana uhusiano sana na biashara tunayofanya. Sisi ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya ndizi, leo tunavyoongelea biashara kubwa ya ndizi zinaelekezwa Uganda. Nakumbuka wakati fulani nilimpigia simu Mheshimiwa Waziri nikitaka atatue mgogoro wa wafanyabiashara wa Murongo na wafanyabiashara wa Uganda kuhusu ununuzi wa ndizi. Tulipata solution kwamba ndizi ziweze kuuzwa eneo la wazi pale Mrongo, chafu limechakaa, lakini sasa tukiwa na hayo masoko tutaweza kufanya biashara nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo ndizi ni asset kwa Uganda kwa sababu wanasafirisha nje. Ukienda kwenye Mataifa mbalimbali unakuta ndizi produced from Uganda wakati in reality zinatoka Kagera, ni ndizi za Kagera zinavushwa zinaenda kupandishwa hadhi na kuuzwa nje ya nchi. Kwa hiyo naomba sana hayo masoko yapewe umuhimu ili tuweze kuweka tija katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaongea kama walivyoongea wengine kuhusu zao la kahawa. Nilikuwa nasoma journal moja wamesema ni journal business insider Africa, wanasema baada ya maji na chai kinachofuata kwa kunyweka zaidi ni kahawa. Kwa hiyo kuna fursa nzuri ya biashara tukiwekeza vizuri kwenye kahawa. Nimeangalia nikafanya study tu kwamba tumeweza kuzalisha tani 65,000 it is a peanut, lakini leo tunakuwa na malengo ya kuzalisha tani 72,000, its still small, kwa Mkoa wa Kagera tu ukiangalia wana uwezo wa kuzalisha zaidi ya hekta milioni moja, lakini eneo linalozalisha ni hekta 600,000, lakini siyo hiyo kahawa tu, wanazalisha less than hekta 48,000. Kwa hiyo unaona kwamba maeneo makubwa hayajaweza kuzalisha vya kutosha bado tuna potential ya kuzalisha zaidi kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnadhani kwa nini watu hawapendi kuzalisha kahawa kwa wingi, kuna wakulima takriban 130,000 kwa Mkoa wa Kagera, ni wachache sana kwa sababu eneo la Mkoa wa Kagera linaweza kuzalisha zaidi kwa jinsi nature yake ilivyo. Watu hawazalishi kwa sababu ya rasimu kwenye biashara ya kununua na kuuza kahawa. Niishukuru ofisi yao kupitia Waziri Mkuu, leo wanatangaza biashara ya kahawa itapata uhuru wa kiasi fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri pia ameongelea minada na bado nabaki hapa kwenye swali langu, bado tumejiridhisha kiwango gani kwamba wale wanaokuja kununua kwenye minada hawataweza kuwa na maswali ya price fixing. Kwa sababu hilo pia lipo, wanaweza kuwa wamepanga wakaja watu 10, wameshaweka idadi au kiwango wanachotaka kununua, kwa hiyo automatic mkulima ataumia. Kama hatutapata fedha nzuri ya kuuza kahawa, wasidhani kwamba tutaongeza uzalishaji wa kahawa. Watu watatelekeza kahawa, wamekuja kwetu, namshukuru Naibu Waziri alikuja akagawa miche zaidi ya milioni mbili kwa Mkoa wa Kagera, Kyerwa…

MWENYEKITI: Kuna taarifa.

T A A R I F A

MHE. SAASHISHA. E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa pamoja na mchango wake mzuri na maelezo yake na faida za kahawa, lakini nataka kumpa taarifa kahawa hiyo haijapewa ruzuku.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Anatropia, taarifa hiyo unaipokea?

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa nimeipokea na niongezee hapo hapo. Nimem-quote mkulima mmoja anasema unaweza ukapepeta ukaweka kahawa kwenye magunia, lakini bei inavyokuja hairidhishi. Kwa hiyo automatic kama bei ya kahawa haiwezi kuridhisha, mkulima ata-ignore biashara ya kahawa. Kila siku tutakuja tunatoa mifano mizuri ya Uganda, leo ameeleza Mbunge mmoja hapa, Uganda leo ina rank, the second in Africa kwa kuzalisha kahawa wakati kahawa inatoka Mkoa wa Kagera, siyo sawa, which means kuna shida kwenye soko letu. Tuna shida katika kuendesha masoko na ununuzi mzima wa kahawa kwenye eneo letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazidi kuomba sana kwamba mfumo ambao nimeona na mwongozo wameweka wausimamie vizuri, tuone kama utaleta tija. Kuna madalali wanaumiza sana wakulima, lakini hatuwezi ku-avoid, tutengeneze mfumo madhubuti ambao hawa madalali hawatawaumiza wakulima. Pia walipwe kwa wakati, first come first save. Mkulima anaweza kupima mazao yake leo akaja kulipwa baada ya wiki tatu, yule anayelipwa wa kwanza ni yule anayetoa chochote. Wakiweza kusimamia hiyo mifumo, tunaweza kuleta mabadiliko kwenye soko la kahawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru kwa fursa hii, ninaushukuru Uongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, nawashukuru kwa uwasilishaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni walivyoweza kuudadavua muswada na kabla ya yote nianze kwa salamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe salamu nyingi sana kwa Mkuu wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamanda Sirro kwa kazi anayoifanya hasa baada ya kupitishwa kwa Sheria ya CyberCrime, kupambana vizuri na watu wanaotoa uhuru wa kujieleza. Anaweza kusema anaweza kufanya yote lakini ikiwa ni pamoja na kukamata na kupiga, lakini ajue unaweza kumpiga mtu sana, anaweza kuumia mwanzo lakini akaota sugu na ikawa ni mfumo wa kawaida. Kwa hiyo, apige tu, tutaota sugu, wataota sugu na itakuwa ni sehemu ya kawaida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongeze pale kwamba siyo kila kimiminika kinazima moto, vingine vinachochea moto! Hiyo ni salaamu kwake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeupitia vizuri muswada, mwanzo mpaka mwisho nikajaribu kuaninisha, nikaangalia dhamira hasa ya Serikali tuliyonayo ya Awamu ya Tano inayojinasibu kwa kuchapa kazi, inayojinasibu kwa kuwataka au kwa kuwatetea wanyonge. Mimi natia shaka, nimeiangalia hiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano katika muswada uliokuja, muswada nimeweza kuuchambua katika vipengele vikuu vitatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipengele cha kwanza ni kwamba Muswada ni wa kibaguzi, Muswada ni wa kibaguzi katika Ibara ya Nne. Ibara ya Nne inambagua nani apate taarifa kinyume kabisa na Katiba ya Jamhuri ya Tanzania, kifungu cha 18 Ibara ndogo ya kwanza inayoeleza kila mtu anayeishi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kupata habari lakini huu Muswada unasema anayeishi ndani ya Jamhuri ya Muungano awe raia ndiyo mwenye uwezo wa kupata habari, huo ni ubaguzi wa hali ya juu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ubaguzi mwingine tumeuona mkiibagua Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Masuala ya kisheria ni masuala ya Muungano kwa hiyo sasa muswada unaanza kupoteza uhalali au sheria inapoteza uhalali pale tu inapoamua kubagua kundi fulani dhidi ya kundi lingine. Tunawabagua watu ambao wako ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wengine wana maslahi pia. Tunao wawekezaji, donors, kuna watu wamewekeza pesa zao kama donors ambao wana-deserve kupata taarifa kutoka kwenye Wizara mbalimbali ambako hela yao ndiyo ipo na hapo ndiyo nilipoona dhamira ya Serikali kuuleta huo muswada kwamba watu wanawapa pesa zao, kama donors kama business partners na mnawaambia kupitia sheria au muswada mliouleta hamna uhalali wa kupata habari. Hiyo ni weakness ya kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamshauri Waziri wa Katiba na Sheria kwamba sheria yeyote ambayo inaonesha dhamira ya kubagua watu haina manufaa, tuondoe sasa kuwabagua wote walioko ndani ya Jamhuri kusema raia na badala yake tuseme kila mtu ambaye yuko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kupata taarifa sambamba na hitaji la Katiba ya Jamhuri ya Muungano, hiyo ni ya kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pungufu la pili nililoliona katika huu muswada ni suala zima la kutaka kunyang‟anya haki. Tunakaa upande mmoja wa kutaka kutoa taarifa, lakini upande wa pili tunaeleza ni namna gani ni ngumu kuwapa watu taarifa. Hiyo imejidhihirisha katika namna ambayo watu wanaweza kupata taarifa, mlolongo, bureaucracy na wote tunajua justice delayed, it is justice denied. Kama tunawachelewesha watu kupata taarifa haina tofauti na kuwanyima taarifa, nitakusomea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vifungu mbalimbali ambavyo nitaainisha kabla ya kifungu cha 14 na nianze na kifungu cha 11. Mtu anaomba kupata taarifa kwa mmiliki wa taarifa ambaye ombi lake linatakiwa ndani ya siku 30, unaongelea kutoa taarifa ndani ya siku 30 kwa mujibu wa muswada mliotuletea hapa. Kama haitoshi, yule anayemiliki taarifa anamwambia wa chini yake kwamba atoe taarifa ina maana yule third party atoe taarifa au anatoa taarifa baada ya siku nane na wanaenda mbali zaidi, anayemiliki taarifa atamwambia mtu wa tatu kutoa tarifa haraka inavyowezekana ndani ya siku nane.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Awamu ya Tano inatambua haraka iwezekanavyo ni siku nane, hiyo ni haki kweli? Lakini kama haitoshi kifungu kinaonesha kama mmiliki wa taarifa amepata ombi, kama anaona hatatoa hiyo taarifa inahitajika siku 30 kutoa jibu la taarifa ipo au haipo. Tunaanza kwa siku 30 za kwanza, tunakuja siku 30 za pili ambazo amekata rufaa kwa kutopewa taarifa, lakini pia inafuata siku 30 kwa Waziri ambayo ni ngazi ya tatu kueleza whether atatoa taarifa au hatatoa taarifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu ambao mnasifia muswada tunaongelea siku 90 za raia wa Tanzania kupata taarifa ambayo sasa kwa mawazo ya muswada huu kipengele cha 6(2) kinaongelea mambo ya national Interest. Tumeweka kipengele hiki makusudi kama chaka, kwa sababu tumekuwa tukitumia kwanza neno la national interest tofauti na matarajio ya wengi na ni ngumu ku-set boundaries za national interest. Tumeona kadha wa kadha hili neno likitumika kunyima wanahabari taarifa makusudi kabisa na tunakileta hapa kwenye kipengele cha sita tukiwa na lengo lile lile la kunyima taarifa kwa sababu ya kifungu 6(2)kwamba ni kwa ajili ya national interest.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi adhabu tunazozitoa ambayo ni kipengele changu cha tatu. Nilisema cha kwanza ni ubaguzi, cha pili bureaucracy, lakini cha tatu ni adhabu zinazokuja kutolewa.
Katika organization, katika Wizara kuna watu wamedhihirika kuwa wanafanya kazi bila kuwa na nia njema, lakini mle kwa watu ambao hawana nia njema kuna wenye nia njema ambao wamekuwa wakitoa taarifa na ninyi mnasema wale watakaotupa taarifa kwa mujibu wa kipengele cha 6(6) kinasema mtu yeyote atakayetoa taarifa iliyozuiliwa kinyume na mamlaka anapewa adhabu ya miaka 15 mpaka miaka 20. Ni kwa nini tunaamua kuwaadhibu watu kwa kiwango kikubwa namna ile. Kusudi iko very simple tu tunataka tuwazibe mdomo, hata wale waliokuwa wanafurukuta kwa nia njema waliyokuwa nayo kwa kuona mamlaka iliyokuwepo wanafungwa mdomo.
Mimi kama Mbunge mwenye wajibu wa kuishauri Serikali ni lazima tuangalie upya. Tunawafungaje watu miaka 20? Kwa kosa lipi? Ni lazima tuangalie. Hili kosa lina uhusiano gani na usalama wa nchi? Tujiridhishe. Kwa makosa mengine ya kawaida ambayo mmeainisha kifungo kiwe miaka mitatu mpaka miaka mitano, lakini plus faini au mtu anaweza kutoa either faini au akafungwa kifungo.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza mambo makubwa matatu niliyoyaona katika hii sheria na ninaendelea kushauri kama wenzangu walivyosema, sheria yenye lengo la kubagua watu ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sheria yenye lengo la kushindwa kuwapa watu taarifa kwa sababu ya milolongo na taratibu iliyowekwa na huu muswada, kama hazitaondolewa au kama hazitakuwa addressed otherwise hatuna maana ya kupoteza muda kujadili kitu ambacho kinaenda kuwatesa watu wetu. Tumekuwa muda mwingi tunajadili hapa kwa ushabiki, tumekuwa muda mwingi tunasifia, tunasahau kwamba wajibu wetu ni kuikosoa Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mbunge mwingine amekuja anajaribu kusifia kwamba imeshirikisha wadau, nimejiuliza kwenye suala la wadau, kama tunaongelea habari za kutoa taarifa, tumewaletaje wadau wa habari? Tunasikia wamekuja wa MCT, JUKATA na TEF, are these real stakeholders? Kama tunaongelea Muswada wa Habari then these are the people, lakini kama ndiyo wao tumewa-consult tuna mislead the public. There are stakeholder’s ambao wanaenda kutoa taarifa husika not these ones!
Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa Mwaka 2016
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Awali ya yote nitaomba kutumia muda wangu kuomba ufafanuzi kutoka kwako utatuambia muda utakaoona unafaa; ni muda gani tunaweza kuleta schedule of amendment kwa sababu tumeleta amendment zetu tukaambiwa tumechelewa. Kwa kuwa suala la utungaji wa sheria unahitaji consensus, kwa hiyo tunaomba tujue lini tulete ili kwa pamoja tutunge sheria. Badala ya kubaki wengine na manunguniko kwamba tulikuwa na mapendekezo yetu na hayajaweza kuwa accommodated, naomba hilo ulichukue.
Mheshimiwa Naibu Spika, nikirudi kwenye Muswada, katika nia njema ya kutaka twende pamoja,tuwe na uelewa mmoja, nina mapendekezo kadha wa kadha ambayo Waziri akiona yanafaa, anaweza kuyachukua. Mfano tukianza na kifungu cha 4(2) kinaongelea members wa board, tukienda kwenye schedule yake ambayo iko ukurasa wa 23 anaongelea composition ya board members.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimeshangaa sana ni kwa namna gani Tanganyika Law Society inaweza isiwe mdau katika hii board. Ningependekeza wao kama watu ambao wana mandate au wanalinda maadili au wako concerned na maadili ya hao Wanasheria na Mawakili wawe sehemu ya kikundi hiki au wawe sehemu ya board katika Muswada huu tunaoupendekeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha pili ambacho nimekiona ni cha msingi kipengele cha sita (6) mnaongelea nani awe Registrar; sina wasiwasi na sifa za Registrar kwa sababu inaonekana atatoka atakuwa ni mtu ambaye amekuwa ana-deal na legal affairs sina shida na hiyo. Maana yake atakuwa na background ya kisheria na suala analoenda ku-deal nalo kimsingi lina-deal na mambo ya sheria. Swali langu linakuja kwa assistant registrar ambaye inakuja kipengele cha 8(1) kinaongelea wale ma-assistant registrar watachukuliwa kwenye wilaya na mikoa.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kipengele hiki hakioneshi umuhimu wa kuwa na watu ambao background zao ni za kisheria, naona huu ni upungufu na kama tunaona inafaa tuongeze neno kwamba wachukuliwe watu ambao wamekuwa wana-deal na legal affairs kwenye Ofisi za Wakuu wa Wilaya, kwenye Ofisi za Wakuu wa Mikoa kuna watu wenye background za kisheria tuwatumie hao watu wanaweza ku-play role nzuri na tukapata matokeo tarajiwa zaidi ya kuchukua just anybody. Hayo ndio mapendekezo yangu katika kipengele cha nane (8).
Mheshimiwa Naibu Spika, kama haitoshi nakuja kipengele cha 14, ambacho kinaongelea mamlaka ya rufaa, kwamba mleta maombi sasa maombi yake yasipokubaliwa, Assistant Registrar akikataa maombi yake anaweza ku-appeal kwa Registrar. Registrar akikataa anaweza ku-appeal kwa board, board ikikataa ana-appeal kwa Waziri na huo ndio mwisho wa mamlaka husika, nadhani hii hapa tume-over look Waziri hawezi kuwa final say. Ni rahisi sana unaweza ku-corrupt the whole population ambayo tunayoongelea, lakini siyo rahisi ku-corrupt the High Court.
Mheshimiwa Naibu Spika, napendekeza High Court iwe ndio ya mwisho badala ya kuishia kwa Waziri. Vinginevyo tutakuwa tunaanza kutengeza vitu ambavyo havitakaa vizuri na vitaleta manunguniko; kama mnaona inafaa Mheshimiwa Waziri nashauri tuiongeze hiyo kitu, japo nimeileta nimeona mwenzangu ameleta kwenye schedule of amendment mkiichukua hiyo inaweza ikatuleta matokeo chanya katika kile tunachokitaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha 16 ambacho nimeona ni kizungumkuti, kipengele kidogo cha 3(f) kinamzuia a legal aid provider kutojihusisha na any political activities, kikisomwa sambamba na kipengele cha 43 asijihusishe na mambo ya kisiasa. Tunataka definition, ni mambo yapi ya kisiasa mnayaongelea, tunataka uelewa wa pamoja, mambo yapi ya kisiasa tunayaongelea, kwa sababu ninachoweza kuona nimeona watu wakifanya mambo ya kisheria, wakitoa msaada wa kisheria ni Mawakili nguli na maarufu nchini bado wanafanya mambo ya kisiasa, sasa tunataka uelewa wa pamoja. Isije ikawa ni changa la macho kwamba kuna watu wanabanwa au kuna watu wataanza kuonewa ati wana milengo fulani ya kisiasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, vinginevyo kama hatuwezi kuwa na uelewa wa pamoja katika hilo nitaona tuna lengo la kuonea watu kadha wa kadha au kuna vitu tunajaribu kujificha nyuma yake tukitumia mlengo wa kisiasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha 20, ni special provision paralegals. Hawa paralegals inaelezea ni watu gani, lakini imeenda imejikuta hiki kipengele cha 20 kinatoa vitu viwili ambavyo vina-contradict one another. Mfano kipengele cha 20(2)(c) kinamwelekeza paralegal kutoa msaada wa kuandaa legal document na hiyo kimsingi ndio kazi yake kama msaidizi wa masuala ya kisheria anaandaa document. Sasa ni wakati gani paralegal ataachana na kazi anayofanya advocate. Mmeenda kwenye kipengele cha 3(5) mnasema paralegal asijihusishe na mambo yanayofanywa na advocate mnaona contradiction.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha 2(b) kinamruhusu kuandaa legal document, lakini tunaenda kipengele cha (5) kinasema asijihusishe na mambo yanayofanywa na advocate; ambayo naona there are two contradicting things hapa. Mnamwambia andaa legal document lakini at the same time, mnamwambia asijihusishe na mambo yanayohusiana na mambo ya kisheria. Lazima tuangalie kipi sasa kisimame, kipi kiondoke na nikipishe kingine kuliko kwenda na hivi viwili ambavyo vinatuletea contradiction.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipengele cha 36 kimeeleza vizuri, kutoa msaada wa watu ambao wapo kwenye mahabusu. Mara nyingi tumeona watu ambao wanakuwa wamekamatwa, wapo chini ya polisi watu ambao wanapaswa kuandika maelezo yao, wamekuwa haki zao hazifuatwi, ikiwa ni pamoja na kupewa aidha mwanasheria au legal aid for this matter.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaomba hiki kipengele kiwekwe basi, hata kwenye kesi za mwenendo wa makosa ya jinai, ili wale mawakili au wanasheria au ma-paralegals wawepo wakati mtuhumiwa anahojiwa na polisi. Kitu ambacho hakifanyiki leo, watu wanaku-harass, watu wanatishwa na mawakili wakifanikiwa kuingia mle ndani wanaambulia matusi na kejeli na vitu vingine.
Mheshimiwa Naibu Spika, mifano iko dhahiri, tunakumbuka kilichotokea kwa mawakili kule Arusha kwenye kesi ya Loliondo, it is the same thing, wakili amejitolea kwenda kwa mteja wake kumsikiliza na yeye amewekwa ndani. Kwa hiyo, kama kweli tuna nia ya dhati ya kutoa msaada wa kisheria kwa watu hawa basi hivi vipengele tuvifuate kadiri ambavyo tumeviweka kwenye Miswada yetu au kadri tulivyoandika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia nataka tuongee bayana hata hizi faini ambazo tumewaweka watu, unaona faini zinakuja five milions, ten millions, six months; au faini ya five billions mpaka ten millions au six months tuangalie relationship. Mtu ambaye amechukua pesa, kwa mfano kama huyu paralegal ambaye amechukua fedha kwa mtu anayemsaidia; mnamwambia kama amechukua fedha kwa mtu anayemsaidia faini yake, iwe ni miezi mitatu ngoja nirudi vizuri hapa; nataka tupate uhusiano mzuri kati ya faini, kati ya fedha zinazotozwa na kifungo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tusifanye kwa ajili ya kuwakomoa watu au tusifanye vitu kwa ku-beep watu watakuwa wanaomba pesa kwa wahisani wanaona vifungo au faini ni vidogo, wanapiga pesa nyingi lakini wakijua kwamba wanaenda kulipa kitu kidogo. Nataka tupate uhusiano kati ya faini na makosa yanayofanyika. Nakushukuru, nimemaliza
Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalam ya Walimu Tanzania wa Mwaka 2018
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru. Nampongeza Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuwasilisha vyema, hitaji la walimu siyo utitiri wa taasisi za kudhibiti bali chombo cha kuwasaidia. Walimu kama taasisi wamekuwa na malalamiko siku nyingi. Kada ya walimu imeonekana ni kada iliyodharaulika na kusaulika. Kama haitoshi wale wanaofeli katika hatua mbalimbali wamekuwa wakisokomezwa kwenye ualimu. Sasa tunataka tuone, je, hii taasisi italeta mabadiliko?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Muswada uliyowasilishwa na Serikali, nimepitia vipengele tofauti tofauti, nikianza na composition ya Bodi, muundo wa Bodi unaopendekezwa katika kifungu cha 5 kwa kiwango kikubwa naona unampa Waziri mamlaka mengi sana ya kuteua. Ukisoma Muswada, unaona maeneo mengi sana Waziri anateua. Anaanza kumteua Mwenyekiti wa Bodi, anatoka anawateua wajumbe nane wanaopatikana katika kifungu cha 5(1)(b) katika maeneo tofauti tofauti, anatoka hapo, anakuja kuteua wasaidizi au wasimamizi wa walimu katika Wilaya na Mikoa, hiyo ni kifungu cha 14, wote huo ni uteuzi wa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaona hapa kinachofanyika ni mawazo ya Waziri atakayekuwa anamwona anafaa, tutaenda kuwa na composition ya Bodi ya maoni ya Waziri. Badala yake napendekeza kama ikionekana inafaa, watu wenye vigezo wajitokeze senior professional teachers wagombee hizo nafasi among the contenders ndiyo Waziri aweze kuteua mmojawapo. Sababu kubwa ya kuteua sidhani kama ni bahati mbaya, ni kwa ajili kuteua watu wenye mrengo fulani fulani wanaoutaka watu fulani. Hilo ni pendekezo langu la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, uteuzi mwingine ni appointment of the Registrar ambaye ndiye atakuwa CEO wa Bodi na Deputy Registrar, wote huo ni uteuzi wa Waziri. Huu ni upungufu mkubwa sana kumchukulia Waziri kama Mungu. Hiyo ndiyo tunayoiona leo ya Mheshimiwa Jiwe ambaye anaweza kumteua kila mtu kuanzia juu mpaka chini. Naona tusiendeleze haya mambo ya kumruhusu mtu mmoja atutengenezee anachohisi anaweza kufanya. Badala yake tuwaache walimu wenye uwezo waweze kujitokeza na wateuliwe kushika nafasi katika Bodi yao kwa maana wao ndiyo wana maono ya namna ya kuendesha chombo chao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Muswada sijaona uhusiano wa hii Bodi ya Walimu na Chama cha Walimu kilichokuwepo na badala yake kuna representative kutoka kwenye professional, anasema kuna mwakilishi mmoja kutoka kwenye Chama cha Walimu ambaye naye ni mmoja wa watu watakaoteuliwa na Waziri. Nadhani hiyo tuiangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ambalo nitapenda kuongelea ni ada za usajili. Wote tunatambua kwamba walimu wanalipwa kiwango kidogo cha fedha. Kwa hiyo, tuangalie hata ada ambazo tunaziweka kama sifa mojawapo ya kuwapa usajili ziwe katika minimal stage au ikiwezekana hata isiwepo ili mradi ana vigezo vingine vya msingi siyo lazima alipe, otherwise mtuambie kuanzishwa kwa Bodi husika kunaenda sambamba na kuongeza kipato au mishahara ya walimu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nitapenda nilizungumzie kutoka kwenye huu Muswada linapatikana katika section 23. Masharti yanayoongezeka kwa mwalimu ku-renew license au certificate. Naenda page ya 12 ambapo namwona mwalimu ameshasajiliwa, amepewa leseni lakini katika ku-renew leseni unamwona anahitajika a-submit performance appraisal, a-submit tena kuonyesha amejiendeleza kwa kiwango gani na fedha ya usajili. Hapa nachokiona ni kikwazo kingine cha pili, hii inamaanisha mwalimu anasajiliwa mara mbili. Kwa nini wakati wakati wa ku-renew leseni isiwe ni kupewa tu leseni badala ya kuwa na masharti mengine mapya ambayo naona mnajaribu kuyatengeneza? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu kingine ambacho nimekipitia ni cha 28 kuhusu mtu ambaye siyo Mtanzania kusajiliwa na Bodi. Tuna-assume kwamba nchi nyingine zinazotuzunguka zitakuwa na chombo cha ku-certify walimu. Nadhani ni upungufu, ni lazima kama tunatengeneza Bodi, basi iwe hata na minimum qualification ya kutazama wale watu wanaokuja kufundisha hapa nchini badala ya kutegemea kwamba waje na recommendation kutoka kwenye taasisi za nchini kwao ambazo zimewa-recommend. Nashauri tutengeneze mfumo wa kuwatambua wale walimu na kuwaweka kwenye system waweze kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni code of ethics or code of conduct, nadhani hata Kamati wameisemea. This is general, sitegemei Bodi ikae na kusema hii ni sahihi au hii siyo sahihi. Sitegemei kama wao wana kitu kinaitwa criteria of truth au namna ya kuwa-judge walimu na badala yake uwepo mjadala wa Kitaifa wa ipi miiko sahihi kwa mwalimu? Otherwise viwe vitu ambavyo ni common sana, lakini kutaka kuwawekea kwamba tuna wa-judge kwamba mwalimu akifanya hivi ni tofauti na maadili, akifanya vile ni kinyume na maadili, tunaweza kuwaonea sana walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maeneo mengine ukienda, dressing code ya stahili hii inakubalika lakini kwenye maeneo mengine dressing code ya stahili hii haikubaliki. Kwa maana hiyo, kuwepo na mjadala wa Kitaifa ambapo hata walimu nao waridhie kwamba tuna abide kwamba hii ni sahihi na hii siyo sahihi. Vinginevyo tutawaonea kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika wakati tofauti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ambacho nimekipitia, nashauri kwamba kama kumekuwepo na tuhuma dhidi ya mwalimu, baadaye amekata rufaa kwa Waziri ambapo Kamati imependekeza siku tisini nami naafiki siku hizo tisini badala ya siku thelasini ambazo zinaonekana ni chache, rufaa imeenda tena High Court na mwalimu ameshinda rufaa yake, kuwepo na remedies ambazo mwalimu ataweza kupatiwa. Kama ameshinda kesi yake na ameweza kuwa installed, sasa Bodi husika itoe tamko rasmi kuonesha kwamba walikosea na badala yake wamwondolee zile tuhuma mwalimu aweze kuwa cleared kuendelea na kazi badala ya kuonekana ana makandokando ambayo amekatia rufaa na ameshinda. Kwa hiyo, kwenye marekebisho nitakuja na kipengele cha kupendekeza remedies ambazo mwalimu au mtuhumiwa anapaswa kupewa kama akishinda rufaa yake dhidi ya charges so and so. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hayo machache kwa jinsi nilivyopitia Muswada, naomba niishie hapo.