Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Cecil David Mwambe (65 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa Mwaka wa Fedha wa 2016/2017.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi ya kuchangia, lakini hata hivyo niende moja kwa moja kujikita kwenye hoja za msingi.
Kwanza kabisa nataka nimshauri Waziri kwamba sasa hivi tuna makampuni makubwa mawili yanayotoa huduma za ndege Tanzania, FastJet pamoja na Precision. Waheshimiwa wengine walichangia wakikueleza kwamba wale watu wameamua kuwa wezi moja kwa moja; mimi nina mfano moja kwa moja wa Precision Air, ndiyo ndege peke inayokwenda Mtwara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na uwanja wa Mtwara kutokukarabatiwa kwa miaka mingi, lakini Precision Air wamekubali kwenda pale na kutoa huduma kwa ajili ya watu wa Mtwara. Adha ya kwanza tunayoipata Precision Air, reporting time Dar es Salaam ni saa 10.00 usiku kama vile unakwenda nchi za nje. Lakini hata hivyo, kule Mtwara tunatakiwa turipoti saa 11.00 asubuhi kila siku katika siku zote 365 katika mwaka. Sasa kwa sisi tunaotokea mbali na Mtwara Mjini tunalazimika kutoka majumbani kwetu saa 9.00 usiku, wengine saa 8.00 usiku kama akina Mheshimiwa Mkuchika na wengine wanaotokea Newala. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme wazi pia kwamba, hawa watu nauli zao zimekuwa kubwa sana hazifanani na hali halisi na uchumi wa watu wa Mtwara. Precision Air tiketi ya kwenda na kurudi Mtwara sasa hivi imefikia shilingi 850,000, hakuna jinsi ya kuweza kubadilisha. Lakini hawa FastJet unapokwenda Arusha au Moshi ukiwa unaelekea huko, ukitaka kubadilisha safari yako tiketi uliyokata Dar es Salaam kwa shilingi 200,000 unaambiwa kule uongezee shilingi 200,000 ili waweze kukupangia tarehe nyingine uweze kusafiri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Waziri mambo hayo ayaangalie kwa jicho la karibu sana kwa sababu tunatamani kupata huduma hizi za ndege kwenda majumbani kwetu, lakini kwa bahati mbaya kabisa gharama hizi zimekuwa kubwa sana. Ni bora kwenda Afrika ya Kusini au sehemu nyingine kuliko kusafiri kwenda Mtwara kwa sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye masuala ya barabara; tumeona hapa vizuri kabisa mmetenga, utaanza kufanyika upembuzi yakinifu kwa ajili ya barabara ya Nanganga - Ruangwa - Nachingwea ambako ni nyumbani kwa Waziri Mkuu, ni jambo nzuri kufikiria haya mambo. Lakini sisi tulisema kwamba, hizi barabara ni ring roads, utakapomfikisha Waziri Mkuu katika barabara nzuri kabisa nyumbani kwake, akitaka kutoka pale kuelekea Nachingwea atakwenda vizuri, lakini atashindwa kufika Masasi ambako nako ni central business, anatakiwa akafanye shughuli zake nyingine kule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona pia katika barabara ya kutokea Mtwara kwenda Newala kurudi mpaka Masasi, zimetengwa sasa hivi pesa kwa ajili ya kufanya kazi katika kilometa 50 tu. Tunasema wazi kwamba hizi hazitoshi, kwa sababu barabara ile toka nchi hii haijapata uhuru iko vile na mliahidi kwamba, mtaweka pale ndani wakandarasi wasiopungua wanne kwa kuwapa vipande vidogo vidogo, ili iweze kukamilika kwa wakati. Hatujaona Serikali hii inafanya jambo hili na sisi tunasema tunaomba mara moja tupewe taarifa hii. Lakini pia barabara ya Lukuledi kwenda Nachingwea hatujaona sehemu yoyote serious inayoonesha kwamba kuna pesa zozote zimetengwa pale kufanya chochote ikiwemo fidia kwa ajili ya watu wa Lukuledi na maeneo mengine.
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kuhusu vijiji vya Chipite, Chikindi zahanati, Mbamba, Mbaju, Rahaho, Nanajani pamoja na Mlingura. Vijiji hivi vimepitiwa na waya wa umeme za KVA 33, kuelekea maeneo ya mbele. Nini mpango wa Serikali katika kuhakikisha vijiji hivi vinashushiwa umeme wakati wananchi waliharibu mazao yao mikorosho, miembe na mengineyo?
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia katika Kijiji cha Chikindi kuna zahanati pale umeme umepita karibu wanaambiwa walete nguzo kwa shilingi milioni moja. Serikali haioni kama ni muhimu sana kuweka umeme katika maeneo hayo?
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Nanajani kuna gereza pale, hadi leo wanafuata maji mbali kwa ajili tu ya kukosa umeme. Mitambo ya umeme katika eneo la Masasi ni duni sana. Ningeomba kufahamu mipango ya Serikali katika eneo hilo.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Katika dakika zangu tano nitatumia dakika mbili na nusu na mbili na nusu ntampatia Mheshimiwa Sugu. Mheshimiwa Mwenyekiti, kifupi tu nimwambie kaka yangu pale Mheshimiwa Bilakwate kwamba kwa kumtetea Makonda, Makonda siyo mamlaka ya uteuzi. Kwa hiyo, anatwanga maji kwenye kinu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi nataka kuona Bunge hili linavyoweza kushauri Serikali hasa kwenye mamlaka ya uteuzi. Tumeshuhudia sasa hivi kama tulivyosikia Wakuu wa Mikoa wanaamua tu kukurupuka na kutoa maagizo, kama alivyotoka kusema Ndugu yangu Mheshimiwa Mlinga hapa. Tumesikia pia Mkuu wa Mkoa wa Mtwara naye na nimeona mimi mwenyewe meseji jana, naye anaanza kuwaambia watu kama wanafahamu watu wanaoshughulika na madawa ya kulevya basi wamtaarifu ili na yeye apate kiki kwenye vyombo vya habari kama ilivyofanyika maeneo mengine. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kifupi huu ni uvunjifu wa maadili ya viongozi. Tumeona hapa Bunge likiwa haliheshimiwi, Wabunge wanakamatwa muda wowote, mimi mwenyewe ni mwathirika. Mkuu wetu wa Mkoa wa Mtwara alitoa taarifa kwa kuagiza Kamati ya Ulinzi na Usalama Wabunge watatu wa Wilaya ya Masasi tukamatwe kwa sababu hatukutaka kuhudhuria mkutano wake aliokuwa anataka kujadili mambo ambayo Waziri Mkuu tayari alikuwa anayafanyia kazi. Bahati nzuri viongozi walituheshimu wakakataa kutekeleza maagizo yake. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kifupi tuone Bunge sasa linasimamia misingi yake. Tusipoweza kuishauri vyema Serikali hasa mamlaka ya uteuzi, tumwachie pia Waziri wa Mambo ya Ndani afanye kazi zake na Mawaziri wote wafanye kazi zao. Wateule wa Rais wameonesha kama wao ndiyo watu muhimu sana kwenye Taifa hili kuliko hata Mawaziri ambao wana mamlaka makubwa kimsingi kuliko Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na wengine. Mheshimiwa Mwenyekiti, napata hofu kwa sababu vurugu kubwa zaidi zitatokea kuanzia mwakani. Hawa wote walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni walewale ambao walikuwa makada na wanataka kwenda kugombea nafasi mbalimbali katika majimbo yao hasa zaidi Ubunge. Kwa hiyo, tutafika wakati misuguano au mivutano itakuwa mikubwa sana katika maeneo yetu, tuliangalie hili jambo kwa wema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi ya kuweza kuchangia kwenye Wizara ambayo iko mbele yetu sasa hivi. Kabla sijaenda mbali sana nilitaka niongee mambo mawili kimsingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kabisa ni kuishauri Wizara ya Miundombinu kwamba waangalie ni namna gani wanaweza wakawashauri wahusika wa bandari, kwa sababu ninafahamu Kisheria, watu wa bandarini wanaruhusiwa kuuza mali mbalimbali zilizoko bandarini ambazo wahusika wameshindwa kulipia ushuru ikiwemo pamoja na magari na vitu vingine. Bahati mbaya kabisa kuna wananchi Watanznaia zaidi ya 2,000 ambao wamenunua magari kwa njia za mnada bandarini lakini bado wanalazimishwa kulipa port charges pamoja na other charges za bandari. Sasa Watanzania wanatamani kutaka kufahamu kwamba kimsingi unaponunua chombo chochote kama gari bandarini kupitia kwenye mnada unalazimika kulipia tena na other charges? Kwa nini wanaruhusu kufanya mnada kama bado mtu haambiwi hali halisi au gharama halisi za ununuzi wa vyombo vile ambavyo wananchi wameshindwa kuvilipia bandarini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili nililotaka nichangie ni kuhusiana na suala la barabara. Sisi wakazi wa Mtwara kwa kipindi kirefu kama wengi mnavyofahamu katika hata Mabunge yaliyopita walitokea wazee wetu ambao walikuwa Wabunge wa Mtwara, walikuwa wanatamani upande wa Mtwara uunganishwe na upande wa Mozambique kwa sababu ya shida kubwa ya barabara ambazo tulikuwa tunazipata. Miaka ya karibuni Serikali imeamua kujenga barabara na ndiyo sasa hivi tunaweza kufika Mtwara kwa wakati.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini bado tuna tatizo moja kubwa sana. Tunapoongelea suala la uchumi wa Mtwara tunaongelea kuhusu ring roads za barabara zetu ambazo zinaunganisha mkoa wa Mtwara pamoja na Lindi. Ukienda kwenye Kitabu cha Mheshimiwa Waziri, taarifa aliyotoa hapa ukurasa wa 165, utakuta hapa anaongea kuhusu barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay. Sina uhakika kama yamefanyika makosa kwenye ku-record lakini pesa inayoonekana imetengwa hapa wanaongea habari za shilingi 64,514,000.144. Sasa labda kama ni bilioni basi mje kutuambia; lakini hata kama mtasema ni bilioni, hizo barabara tunazoziongelea kwa kutumia hiyo bilioni 64, tunaanza kuongea kuanzia barabara ya Masasi - Songea kuelekea Mbamba Bay. Lakini pia barabara hii inajumuisha pamoja na kulipa gharama mbalimbali za wakandarasi waliofanya kazi kwenye barabara ya Masasi kuelekea Songea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna kilometa 70 za Mangaka – Nakapanya ziko ndani ya hii shilingi bilioni 64 kama si milioni. Kuna kilometa nyingine 66 ziko ndani ya hii shilingi bilioni 64, kuna kilometa nyingine 65 Mangaka – Mtambaswala ziko ndani ya hizo hizo pesa; kuna kilometa zingine 59 Tunduru na Matemanga zinaongea kuhusu hizo shilingi bilioni 64. Kuna kilometa 60 za Kilimasera – Matemanga. Mwisho kabisa wanasema, barabara za Masasi
– Newala (Mtwara), sehemu ya Mtwara – Navira kilometa 50 na kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Mbinga – Mbamba Bay kilometa 66, Masasi – Nachingwea – Nanganga kilometa 91.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa masikitiko kabisa ninataka kusema bado tunarudi na lile lile wazo letu la zamani kwamba kama Serikali haina mapenzi mema na watu wa Kusini mtupe hii taarifa tuamue kujitenga wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ngombale ametoka kuchangia hapa karibuni, mmesikia kuhusu matatizo makubwa ya barabara inayoanzia Nangurukuru kuelekea Liwale. Watu hawa hawa wa Liwale wanatumia masaa sita kutokea Nachingwea mjini kuelekea Liwale kipindi hiki ambacho hakuna mvua, lakini wakati wa mvua wanakwenda kwa masaa tisa mpaka 12 umbali wa kilometa 95 Nachingwea – Liwale. Sijui katika hii mika zaidi ya 50 ya uhuru mnataka kutuambia nini.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kule ndani unakuja kukuta bado kuna shida. Sasa hivi Serikali imeamua kuhamisha makao makuu ya nchi kuja kuyaweka Dodoma. Sisi wakazi wa Mikoa ya Kusini; Mtwara, Lindi pamoja na Ruvuma ili tuweze kufika Dodoma tunalazimika kupita tena Dar es Salaam. Tulikuwa tunakwenda Dar es Salaam kwa sababu ndiko ambako yalikuwa yanajulikana kama makao ya nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri kwenye kitabu chake alichokitoa hapa leo, sijaona kama Serikali ina mpango wowote wa kutaka kuunganisha mikoa ya Kusini kupitia Masasi, Nachingwea, Liwale hadi Morogoro kwa sababu ndiyo njia fupi sana ya kutuwezesha sisi kuweza kufika Dodoma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Waziri ni mtu anayetokea Jimbo la Namtumbo ambalo ni karibu tu na haya maeneo niliyoyataja, lakini yeye akiwa bado Wizarani hajaona kama kuna namna au kuna haja kweli ya ndugu zake wa Namtumbo kuhakikisha anawapitisha njia fupi ya kufika Dodoma pamoja na Wabunge wote na watu wote wanaotakiwa kufika Dodoma kwa wakati. (Makofi)
Kwa hiyo, niiombe Serikali ifikirie sasa ione namna ya kuunganisha Mkoa wa Lindi, Mkoa wa Mtwara, Mkoa wa Ruvuma kutokea Masasi, Nachingwea kupitia Liwale mpaka kufika Mahenge – Morogoro na kutoka Mahenge kuja Ifakara na maeneo mengine ni njia fupi sana ya kuweza kutufikisha Dodoma badala ya kung’ang’ana na ile njia ya zamani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la pili nakuja suala la reli. Mheshimiwa Naibu Spika kwa taarifa yako labda kama umesoma vizuri historia ya Tanzania, na nataka niwakumbushe pia na Waheshimiwa Mawaziri, mwaka 1949 ilizinduliwa reli ya kwanza ya Kusini, ilikuwa inatokea Mtwara inapita Mkwaya, Mnazi mmoja na vijiji vingi, Lukuledi kuelekea Nachingwea. Siku moja Mheshimiwa Nape hapa aliuliza na Serikali miaka miwili, mitatu iliyopita ilisema wana mpango wa kufufua reli ile.
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona hapa kuna crisis, kuna watu wengi ambao walikuwa wanatamani kuwekeza kwenye reli ya kati ambayo sasa inakwenda kwenye standard gauge. Sasa niwaombe, watu wale ambao wameshindwa kuwekeza kwenye reli ya kati tuwaombe waje kuwekeza kwenye reli hii ya Kusini ambayo inakwenda Mchuchuma, Liganga itapita Tunduru, itakwenda Songea itaweza sasa kuboresha na kuongeza mapato ya Taifa kwa ajili ya bandari ya Mtwara ambayo ni bandari inayozalisha gesi. (Makofi)
Kwa hiyo tuwaombe Serikali jambo hili mlifikirie kwa ajili ya kuongeza uchumi lakini pia kurahisisha usafiri. Barabara zetu hizi ambazo tumezilalia kwa muda mrefu toka wakati wa uhuru mpaka miaka mitatu iliyopita zinakwenda kuharibika kwa kupitisha magari yenye uzito mkubwa tofauti na stahiki zake. Magari yanayobeba makaa kutoka Mchuchuma na maeneo mengine, magari yanayobeba makaa ya mawe ambayo yanatakiwa yalete Bandarini Mtwara. Kwa hiyo, tuiombe Serikali kwa namna ya kipekee watueleze; kama itashindikana basi tutaishia kutoa shilingi; wana mpango gani na reli ya Kusini, hilo tunataka tulifahamu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la tatu ni suala la ndege. Si maeneo mengi sana yanayotumia ndege katika maeneo yetu lakini wachache wanatamani kutumia ndege. Tumeona sasa Serikali hata kama walifanya nje ya bajeti ya kawaida kabisa lakini wameamua kuzileta ndege. Sasa hivi kwenda Mtwara, one way ticket ni shilingi 631,000 kutoka Precision Air. Ukiwahi kukata mapema utapata hiyo ticket kwa shilingi 410,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, mambo haya yanatokea maeneo mengi, tumeona Serikali sasa inataka kuleta ndege maeneo yale na wanatangaza kwamba itakuwa ni yenye gharama nafuu; lakini tuwaombe ndege ile isiishie Mtwara Mjini. Watu wa Masasi wanatamani kutumia ndege, watu wa Ndanda wanatamani kutumia ndege ambazo ni kilometa 200, pamoja na watu wa Nachingwea. Maeneo yote haya yana viwanja vya ndege tena vikubwa vya siku nyingi.
Kiwanja cha Nachingwea kilikuwa kinatumika wakati wa vita za ukombozi Kusini mwa Afrika kila mtu anatambua, kiwanja cha Nachingwea pale kuna kambi kubwa ya jeshi ambao wanahitaji ndege kutua pale. Viwanja hivi sasa viboreshwe viweze ku-accommodate kwa ajili ya kutua ndege za Serikali ambazo tunaamini pamoja na kuwa commercial lakini nia yake hasa ni kutoa huduma kwa ajili ya jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tuwaombe, kama hamna mpango, kwa sababu sijaona kwenye vitabu vyenu, wa kuboresha viwanja vya ndege vya Masasi na Nachingwea, watu wale wanaozunguka viwanja vile vya ndege ni bora tukawaeleza ili waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida za uchumi, kufuga pale Mbuzi na vitu vingine kwasababu nyumba zao zilichorwa “X” na lile eneo sasa hivi limekuwa vichaka, linafaa kabisa kuwa malisho ya mifugo. Kama mnapata nafasi Mheshimiwa Waziri nikuombe twende pamoja ukalione hili, kimsingi niunge mkono hoja…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. CECIL D. MWAMBE: …hoja ya upinzani.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa mara ya pili nawashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Ndanda baada ya kuamua kuondokana na boya wa Chama cha Mapinduzi walisema nije kuwawakilisha hapa ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ningependa nichangie katika huu mpango, kwanza kabisa kwa kumpa pole Mheshimiwa Magufuli kwa sababu amepokea Serikali iliyorithi matatizo mengi sana katika mfumo wetu wa uongozi, lakini hata hivyo namwamini kwa sababu naamini ataweza kutatua mgogoro wa UDA, lakini pia hapa ndani tunategemea kusikia mgogoro wa Home Shopping Center umetatuliwa, lakini pia tutasikia issue ya makontena nayo imekamilika na waliohusika katika hujuma hizo wanachukuliwa hatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite moja kwa moja katika hoja, lakini pia nikiwapa pole familia mbili za ma-suppliers ambao wamefariki katika eneo langu, kuna mmoja anaitwa Muwa Gereji na mwingine Ndelemule, hawa watu walikuwa wanaidai Serikali kwa ajili ya kutoa huduma katika Chuo cha Wauguzi cha Masasi mpaka wamefariki Serikali haijaweza kuwalipa fedha zao na kilichowaua ni presha baada ya kuambiwa mali zao zinauzwa walizokuwa wamewekea bondi wakati huo. Tunaomba sasa Mpango huu uoneshe wazi mpango wa waziwazi kabisa wa kutaka kusaidia kuwalipa Suppliers pamoja na Wakandarasi wengine katika maeneo mbalimbali tusije tukawaletea matatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara tunaomba kama ingewezekana basi ungeingizwa ikawa ni ajabu nane katika yale maajabu ya dunia. Kwa sababu Mtwara ndiko ambako sisi kwa kipindi kirefu wakati huo nilikuwa naona hapa akina Mzee Nandonde na wengine wakiwakilisha Mikoa ya Mtwara mengi walikuwa wanayasema lakini yalikuwa hayatekelezwi. Siku za hivi karibuni pamegundulika gesi kule pamoja na vitu vingine, Serikali iliyopita ikaamua kuondoa gesi ile tena kwa gharama kubwa sana na kuipeleka kwenda kuzalishia umeme maeneo ya Kinyereze megawati 150 bila kuangalia kwamba tunategemea lini kurudisha ghrama za uzalishaji ule ili wananchi waweze kunufaika nayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lLakini pia Mkoa wa Mtwara ndiyo Mkoa pekee ambao una chanzo kikubwa cha uzalishaji wa umeme lakini maeneo mengi ya Mkoa ule hakuna hata umeme. Hata yale maeneo ambayo yamepitiwa na umeme kwa nguzo juu ya maeneo yale, kwa mfano ukienda Kijiji cha Chipite, ukipita Kijiji cha Mumbulu, ukipita Kijiji cha Liputu na Majani, lakini pia ukienda katika Kijiji cha Rahaleo pamoja na Liloya, maeneo haya nguzo zinapita juu ya vichwa vya watu. Watu wale waliambiwa wakate mikorosho yao, watu wale waliambiwa wakate miembe katika maeneo yale wakiamini kwamba siku moja watapata umeme lakini hata hivyo watu wale hawana umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Waziri wa Nishati na Madini, asipoviingiza vijiji hivi katika Mpango wa kupatia umeme nitakuwa wa kwanza kushika fungu ili bajeti yake isipite katika Bunge lijalo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme wazi, kule kwetu kuna utaratibu wa kitu kinaitwa stakabadhi ghalani. Ule utaratibu siyo mzuri sana kwa mwanzo, lakini kwa sababu upo na upo pale kisheria ninawashauri watu wa Mtwara tuendelee kuutumia, isipokuwa tunataka marekebisho makubwa sana katika utaratibu ule. Wanakijiji wa Kijiji cha Ujamaa Nagoo, walipotelewa Korosho zao tani 103 mwaka jana, lakini sheria ya stakabadhi ghalani inasema wazi na nitaomba nii-qoute hapa, kwenye section 18 sub-section (d), lakini pia ukienda kwenye section 22 sub-section 3 inamtaka mmliki wa ghala, utakapotokea upotevu wa mali yeyote ya mtu aliyetunza katika ghala lake ndani ya siku kumi aweze kulipa na kufidia vile vitu vilivyopotea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo sasa hivi lina mwaka mmoja, waliyosababisha ule upotevu wanajulikana, akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho ambaye tunamwambia kabisa Waziri wa Kilimo kwamba atakapokuja kwetu Mwenyekiti huyo akiendelea kumuacha hatutampa ushirikiano kwa sababu siyo mtu anayetaka kutusaidia kuliendeleza zao la korosho, isipokuwa amekwenda pale kwa ajili ya hujuma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nikueleze wazi, Masasi ndiko ambako kulikuwa kuna viwanda vikubwa vya korosho, viwanda vile sasa hivi vimegeuzwa kuwa maghala ya kutunzia choroko na mbaazi, havifanyi kazi iliyokusudiwa ya awali. Tunasema hatutaki, mtakapokuwa mnapanga mpango wenu, mkiamua kifikiria viwanda katika maeneo yetu basi tungependa sana muanzie katika viwanda vile ambavyo sisi tulivizoea, msituletee viwanda vya ajabu, halafu mkaja kutujazia watu kutoka maeneo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatamani kwanza tushughulike na korosho yetu kwa kuanzia, baadaye mtutafutie viwanda vingine vitakavyokuwa na tija, lakini tunafahamu ujenzi wa viwanda vipya ni wa muda mrefu tena wenye gharama kubwa, kwa hiyo kwanza mturudishie vile viwanda vyetu vya asili ambavyo ni Viwanda vya Korosho katika eneo letu visitumike kama maghala kama ilivyo sasa hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nikuambie, Msimamizi Mkuu wa Bodi ya leseni za maghala, amekua akihusika kwa kiasi kikubwa kwa kupokea rushwa lakini pia kuto kutenda haki kwenye utoaji wa leseni za maghala. Namtaka pia Waziri wa Kilimo atakapokuja hapa na mpango wake naye atueleze anataka kufanya nini katika eneo hili, kwa sababu sasa hivi kupata leseni za maghala kule kwetu ni sawa na mbingu na dunia kitu ambacho tunasema hatutataka kiendelee na tusingependa iendelee kufanyika hivi, utuondolee yule Mkurugenzi katika eneo lile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nirudi katika eneo lingine katika huu utaratibu wa korosho kuna mchango kule unaitwa export levy, madhumuni ya awali kabisa ya export levy ni kwa ajili ya kuwagharamia wakulima kuweza kupata pembejeo lakini pamoja na mafunzo. Hizi fedha zinaishia Dar es Salaam ambako hakuna mikorosho, sisi kule tunaoishi na mikorosho fedha hizi hatuzioni. Hata hivyo pembejeo zile hazifiki kwa wakati, tunashauri sasa export levy ikishakusanywa ile fedha ipelekwe katika kila Halmashauri na Halmashauri zile zitaamua zenyewe kwa sababu Halmashari zote zinazolima korosho zinatofautiana katika misimu ya ulimaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri asituletee sisi pembejeo Masasi akatufananisha sisi na watu wa Mkuranga kwa sababu misimu yetu inakuwa tofauti katika maeneo haya. Kwa hiyo, nishauri kabisa export levy iende moja kwa moja kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kupanga mikakati na wakulima wake waweze kununua pembejeo kwa wakati ziweze kuwafikia wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimepitia pia kitabu cha Mpango, Mpango mzuri sana mmeweka humu ndani, lakini niseme, nina maslahi katika eneo hili. Tuje kwenye suala la usafiri na usafirishaji. Imeguswa hapa katika eneo moja kuhusu reli ya kati, niwapongeze sana Wabunge wanaotoka katika reli ya kati na naiomba Serikali ihakikishe inatekeleza hili kwa sababu reli ya kati ni sehemu kubwa sana ya uchumi wetu sisi wote Tanzania hakuna asiyetambua hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia niunganishe, mwaka huu naona hapa tuna bahati tumechajiwa kuhusu reli pia ya Mtwara kwenda Mbambabay imetajwa humu kwenye huu mpango. Tusipoiona katika utekelezaji nitakuwa wa kwanza kushika kifungu ili kwanza hili litekelezwe kwa ajili ya maslahi ya watu wa Mtwara na watu wa Kusini kwa ujumla ndipo tuangalie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ningetaka kuwaangaliza jambo moja, unapokuja Mtwara, unaposema unakwenda kwenye barabara ya uchumi, ile barabara ni ndefu sana inaanzia Mtwara Mjini inakwenda mpaka Newala lakini pia inatokea mpaka Masasi. Inaendelea Mpaka Nachingwea, Liwale, Ruangwa anakotokea Waziri Mkuu ambako leo nimepata taarifa kwa sababu na mimi ndugu zangu wanaishi kule kwamba ukitaka kwenda kijijini kwa Waziri Mkuu hakupitiki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tuseme na yeye anahitaji kupata barabara, ile barabara inakuja kutokea Nanganga, nimeona pale kuna daraja limetajwa na Nanganga Two, ningependa siku moja na Waziri tufuatane tukaangalie vizuri huu mpango tuone kama kweli unatekelezeka hasa maeneo ya Kata za Lukuledi na Kata nyingine hapa katikati watu wengi walichorewa nyumba zao X, sasa waliniagiza nije kuuliza lakini pia kutoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi na Miundombinu kwamba X zile kama hamna matumizi nazo basi tunaomba tukazifute, tutatafuta wenyewe rangi ya kufutia kwa sababu zinawapa watu presha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wengi waliyo na X katika maeneo ya Dar es Salaam wamekuwa wakivunjiwa nyumba zao. Kule kwetu sisi kuna X, hatuambiwi kama barabara ya Masasi kwenda Nachingwea - Liwale, kwenda Ruangwa mpaka Nanganga itajengwa lini? Haya maneno ya upembuzi yakinifu ninaomba mtakapokuwa mnataja miradi yote inayohusika katika eneo langu lisitumike kwa sababu nitakuja niondoe kifungu, nataka mnipe tarehe mahsusi tutaanza siku fulani, tutamaliza siku fulani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifu nimesikia hili neno toka nikiwa mdogo na maeneo mengi yaliyokuwa yanatumika eneo hili vile vitu pale havitekelezwi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa namna ya pekee niseme kule kwetu tuna madhila mengi sana, ukija kwenye masuala ya kiafya sasa hivi kuna mgogoro mkubwa sana unaendelea katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi, ningemtaka Waziri tukutane halafu baada ya hapo nimwelekeze nini pale kinaendelea kwa sababu wakubwa waliopo pale hawataki kuambiwa ukweli na watu walioko chini yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Daktari mmoja pale anafanyiwa figisu, anataka kufukuzwa na hii inashirikisha Mkurugenzi wa Wilaya pamoja na Daktari Mfawidhi wa pale, amekuwa akiwanyanyasa wafanyakazi wale kimapenzi, kwa hiyo, naomba Waziri nikuletee taarifa hii rasmi na nitaomba nikae na wewe ili tuliweke hili sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Waziri wa Ardhi sasa hivi Wilaya ya Masasi imeanza kuwa na migogoro mikubwa ya ardhi kuhusu upimaji na mambo mengine, Mheshimiwa Lukuvi hili tutaliongea na bahati nzuri uliniambia ulishawahi kuishi maeneo yale sasa umetaka kuanza kutugombanisha kwa ajili ya udongo wetu hasa zaidi katika Kijiji cha Mtandi na hivi ninavyokwambia hapa ninaomba tafadhali tukae nikufahamishe zaidi nayafahamu matatizo ya lile eneo kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mwisho kabisa niseme kwamba, Tanzania ni nchi kubwa sana tena ni nchi pana, kwa hiyo tunatamani patakapokuwa panafanyika mikakati na mipango ya maendeleo basi mipango hii ingekuwa inagawanywa kwa mtambuka ili kila eneo angalau kidogo watu waguswe nalo, lakini siyo maeneo mengine yanasahaulika moja kwa moja yatakuja kutuletea shida katika utekelezaji wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia kwamba katika maeneo haya kuna shida kubwa sana ya maji, lakini cha kushangaza kuna bomba kubwa la maji linaloelekea katika Wilaya ya Nachingwea likitokea Ndanda kupitia pale Mwinji. Sasa niseme wazi tunaomba utueleze na mpango wako uje utuambie wananchi wanaokaa juu ya bomba lile kuna mpango gani wa kuwapatia maji katika maeneo yao, kama hili halitafanyika nitawahamasisha tutoboe na tuanze kunywa pale katika eneo letu. Hata hivyo, siungi mkono pale nitakapopatiwa maelezo mazuri kuhusu maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi kwa ajili ya kuchangia kwenye hotuba ya Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze tu kwa kumweleza kwamba mwishoni sitakuwa tayari kuunga mkono hoja ya Wizara yake na mambo yakienda hivi, basi nitaishia kushika shilingi kwa sababu kuna mambo ya msingi, sisi kama wakulima wa korosho tungehitaji kuyasikia na yanapata suluhisho katika Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi kirefu sana korosho tumekuwa tukiisifu kila mara kwamba ni moja kati ya mazao makubwa kabisa ya biashara kwa ajili ya Tanzania. Kwa mwaka huu peke yake asilimia 90 ya zao la korosho imekuwa exported kupelekwa katika nchi ya India. Ukiangalia kwa kina, watumiaji wakubwa kabisa wa korosho wapo katika nchi za Ulaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tulikuwa tukijiuliza kila mara, inakuwaje sasa Wahindi ndio wawe wanunuaji wakubwa wa mazao yetu badala ya kuwatafuta wale final consumers tukawashauri wao waje kutuwekea viwanda katika maeneo yetu?
Kwa hiyo, kimsingi tunaomba viwanda vyetu vile ambavyo vilikuwa vinazalisha korosho vifufuliwe kwa kutafuta watu kutoka Europe ambao na wenyewe wananunua korosho kwa madalali kutoka India. Naomba hili lifanyiwe kazi.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumshukuru kidogo Mheshimiwa Waziri Mkuu…
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika kipindi kilichopita amejitahidi na ameondoa tozo mbalimbali ambazo zilikuwa kero kwa ajili ya wakulima wa korosho lakini bado kuna mambo ya msingi ameacha.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Tunafahamu kabisa Serikali iliamua waziwazi kuondoa na kupunguza kodi ya magunia...
MHE. CECIL D. MWAMBE: …zilitumika kwa ajili ya wanachama wa vyama mbalimbali vya Ushirika katika Vyama Vikuu vya Mkoa wa Mtwara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yako, nikueleze kwamba kumefanyika ubadhirifu mkubwa sana katika biashara ya magunia na nashukuru Mheshimiwa aliyetoka hapa kuongea, anaitwa Mheshimiwa Kaunje alikuwa Mwenyekiti kwa kipindi kilichopita, sasa hivi tupo naye hapa Bungeni, anaweza akaisaidia Wizara yako kutueleza kimsingi. Wakulima wa korosho Mtwara wanakatwa shilingi 56 katika kilo moja kwa maana kwamba wanakatwa shilingi 5,600 ili kuweza kujaza gunia moja, kugharamia gharama za magunia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda sokoni sasa hivi unaweza kununua gharama ya gunia moja kwa shilingi 4,000. Kitu ambacho tunajiuliza, magunia haya ambayo tunaambiwa yamesamehewa Kodi ya Ongezeko ya Thamani lakini mkulima anapata gunia hili kwa shilingi 5,600, tunaomba kufahamu hii biashara inakuwaje? Nani ana maslahi na hii biashara na tungependa tupate majibu yako hapa karibuni, kwa sababu kama nilivyoeleza, kesho naweza nikashika shilingi yako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunataka tufahamu, kwa sababu kwa kipindi kirefu, tulikuwa tukiona wakulima wa korosho wanashindwa kulipwa pesa zao kwa wakati; imetokea sasa hivi na tushukuru uongozi wa Serikali ya Mkoa, kwa kupitia Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, ametueleza wazi kabisa kwamba vyama 49 vya msingi vya Tandahimba vimeshindwa kuwalipa wakulima shilingi bilioni 1.4. Tunataka tujue wazi kabisa kwamba wakulima hawa watapewa lina pesa zao kabla Mheshimiwa hujahitimisha hotuba yako?
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia imekuja kutokea na jambo linguine, vyama 36 vilivyopo chini ya Ushirika wa MAMKU kutokea Wilaya ya Masasi na vyenyewe vimeshindwa kuwalipa wakulima hawa four billion katika msimu huu tu mmoja; hivi ndiyo vitu ambavyo vimewasilishwa kwetu. Tumshukuru Mheshimiwa Mrajisi, alikuja pia kule, ameongea na wakulima, wana mambo mengi Mheshimiwa ya kukueleza, lakini kwa bahati mbaya sana kila mara tulipojaribu kutaka kukueleza jambo hili ulikuwa ukikosa nafasi, machache uliyasikia, lakini ukitaka kusikia mengi zaidi uje kule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kabisa tunasema kwamba haturidhiki na utendaji wa bodi. Bodi ya Korosho imekuwa ikiyafahamu matatizo haya kwa kipindi kirefu sana, lakini imekuwa ikitumika kisiasa. Ukitaka kupata kazi kwenye Bodi ya Korosho, basi kwanza lazima uwe mstaafu wa siasa. Ndugu zetu wa Vietnam wameweka pale watu ambao ni creative, vijana wenye nguvu, wenye uwezo wa kuleta mawazo mbadala kwa ajili ya kuboresha korosho zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu wazi kwamba Vietnam walikuja kuchukua mbegu za korosho Mkoa wa Mtwara, tena walikwenda kuchukua katika kijiji ambacho kipo Jimboni kwangu, kinaitwa Kijiji cha Lukuledi. Wale wenzetu wamekuwa wakitumia zao la korosho kama zao kuu la uchumi kule kwao. Sisi sasa hivi tunaweka watu ambao ni wazee katika bodi, waliostaafu kwenye active politics, tunataka wao wawe creative. Tumeona hawawezi kutufanyia chochote. Wameshindwa kutatua kero mbalimbali za wakulima! Hii ipo katika bodi nyingi. Bodi nyingi sasa hivi zinatumika kisiasa, tunaomba ziwe dissolved, wawekwe pale watu ambao ni creative kwa ajili ya kusaidia Taifa na wakulima wa mazao mbalimbali katika maeneo yao. (Makofi)
Mheshimiwa Waziri, suala hili tulikupa taarifa mapema sana, lakini tunaona mpaka sasa hivi halijachukuliwa hatua. Naomba niliongee hapa na nitaomba Wabunge wanaotoka Mtwara na Wabunge wote walio na maslahi na masuala ya korosho watani-support kuhakikisha tunashika shilingi yako kama hautatueleza hatua gani za msingi utazichukua kwa ajili ya kuhakikisha watu hawa wanachukuliwa hatua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wale waliopoteza pesa ya ukulima ambayo ni five billion katika msimu huu, lakini pia tunataka tuone bodi ilichukua hatua gani? Kama ilishindwa kuchukua hatua kwa wakati, basi bodi na yenyewe sasa hivi ichukuliwe hatua kwa sababu imeshindwa kufanya kazi zake za msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikueleze wazi, makato ya korosho yalifikia mpaka shilingi 264 katika msimu uliopita, lakini ukiangalia katika hizi shilingi 264, bahati nzuri Mheshimiwa Waziri Mkuu amepunguza baadhi ya tozo, lakini bado kuna tozo pale ndani ambazo ni kero kubwa kwa wakulima, tunataka sasa tukae ili wakulima watakapokuwa wanaanza kutayarisha mashamba yao basi wajue wazi bei ya korosho itakuwa ni kiasi gani? Kwa sababu sasa hivi watu wamekuwa wakilima kwa mazoea zao la korosho zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna hata mwaka mmoja ambao mkulima anaweza aka-realize kwamba sasa hivi nimepata faida, kwa sababu anatumia gharama kubwa kutayarisha mashamba, lakini pesa anayokuja kuipata mwishoni ni ndogo sana na ukichanganya na huu utitiri wa nvyama lakini pia pamoja na watu wasiokuwa waaminifu wanaodhulumu pesa zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ni wazi kabisa tuseme haturidhiki na hali ilivyo katika zao la korosho katika Mikoa ya Mtwara na Lindi na maeneo mengine yote ambako wanalima korosho. Tuseme wazi, tunataka mabadiliko makubwa yafanyike kabla ya msimu ujao wa korosho haujaanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kwetu kuna kitu kinaitwa CDTIF. Wale watu lengo lao la msingi ilikuwa ni kwa ajili ya kusaidia kufanya utafiti, kuendeleza zao la korosho, kusaidia wakulima wadogo wadogo kuwapa mbegu, kuwasaidia kupata mikopo ili kudumisha na kuendeleza zao la korosho. Jambo hili halifanyiki na wale watu. Sasa hivi wamegeuka na kuamua kuwa wafanyabiashara. Wanajihusiasha na biashara ya magunia kwa sababu ndicho kitu kinachowapa wao fadia. Wamejihusisha na biashara ya pembejeo, pembejeo hizi haziwafikii wakulima kwa wakati, mpaka sasa hivi imefika wakati uzalishaji unapungua kwa sababu hawapati pembejeo kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile wanashindwa kufanya research. Kuna wataalam walikuja kule kutoka SUA, wamekuja na utaratibu mpya sasa hivi, wana madawa ambayo yanaitwa GI Grow. Tunaomba sasa nalo liingizwe katika ruzuku kwa sababu tusiangalie tu kuondoa au kutumia sulfur ya maji lakini pia tuangalie jinsi ya kuwaongezea tija wakulima katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nikueleze kwamba watu wa Mtwara wanakusubiri sana wakakueleze kero zao. Bahati mbaya sana viongozi mnapokuja mnakuwa na utaratibu wa kutaka kukutana na viongozi wa Vyama vya Ushirika, kukutana na viongozi wa Bodi. Wale sio watu wenye kero, watu wanaokerwa kule ni wale wakulima wa chini kabisa ndio ambao wanahitaji wakuone wewe. Mkifika pale, achaneni na haya mambo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wakulima ambao wanadhulumiwa, Mheshimiwa Katani hapa kaongea kwa kirefu kidogo, lakini nami naomba nichangie hapa. Kwenye Jimbo langu kuna kijiji kimoja peke yake kimepoteza tani zake 103 za korosho. Sasa hivi ni mwaka wa nne hawajapewa fidia kuhusu korosho zao, Bodi ya Leseni ipo pale, inashindwa kuwasaidia chochote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba tukuelekeze majipu ya msingi ambayo tulitamani tuyaone yanatumbuliwa katika kipindi hiki tunachoelekea. Bodi ya Korosho tumesema sisi kama Wabunge tunaotokea Mtwara, hatuoni uwezo wao wa kufanya kazi, bodi ile imezeeka, tunataka wabadilishwe wawekwe watu ambao ni creative kwa ajili ya kuendesha zao la korosho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wasimamizi wa Mfuko wa Leseni za Maghala na wenyewe hatuwahitaji wakae pale, wawekwe watu ambao nafikiri wanaweza kweli wakawasaidia watu wa maghala pamoja na wakulima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nikueleze, ule Mfuko wa CDTIF ambao Mheshimiwa Bwanausi kama ulimsikia pale akisema, wanafanya kazi zao kwa siri kubwa sana. Hatujui wanapata shilingi ngapi na wanazitumia kufanyia nini, lakini kiasi kikubwa cha pesa wanazozikusanya zinakwenda kufanya shughuli za utawala badala ya kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine kubwa linatukera linaitwa export levy. Tunaomba hii pesa inapokusanywa, ipelekwe moja kwa moja katika Halmashauri husika na isibaki na hawa watu kwa sababu wanaitumia vibaya. Haiwasaidii wakulima, inawasaidia wao wanaokaa maofisini, wakulima wanaendelea kuwa maskini, wao wakijilipa mishahara mikubwa katika maeneo yao. (Makofi)
Kwa hiyo, Mheshimiwa nikueleze wazi, utakapokuwa unahitimisha hotuba yako, tunaomba tupate majibu kuhusu masuala yetu haya na usipofanya hivyo, sisi tutashirikiana kwa umoja wetu, tutahakikisha tunashika shilingi yako mpaka pale utakapotupa suluhisho la matatizo tuliyonayo. Ahsante, siungi mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na historia ndefu ya elimu ya Wilaya ya Masasi, naomba kiambatanisho namba 1 na 2 vipokelewe kama mchango wangu wa maandishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kudidimia kwa elimu Wilaya ya Masasi. Wakati Tanganyika tunapata uhuru mwaka 1961, kiwango cha elimu literacy rate katika Wilaya ya Masasi kilikuwa asilimia 85. Kiwango cha juu kabisa kuliko Wilaya zote za wakati ule; hii haikuwa kwa bahati tu bali ilitokana na juhudi za dhati za wamisionari (wazungu) wa Kanisa Anglikana kwa kiwango kikubwa tangu mwaka 1876 na wale wa Kikatoliki kuanzia mwanzo wa karne ya 1900. Vijiji vyote vikubwa vilikuwa na kanisa (mtaa – Kianglikana au Paroko Kikatoliki). Na vitongoji vilikuwa na makanisa madogo (Anglikana) au vigango (Kikatoliki) vilivyosimamiwa na walimu au Makatekisti.
Vijiji hivi vyote na baadhi ya vitongoji palikuwa na shule za Wamisionari. Shule za Serikali kwa maana ya shule za Serikali ya Mitaa (district council/native authority) zilikuwa mbili tu Wilayani, middle schools nazo zilianzishwa miaka ya mwanzo mwa 1950 Chiungutwa na Mbemba. Shule hizi zote za vijijini za misheni zilipokea wanafuzi wa dini zote mbili kuu, kikristo na kiislamu. Hivyo ni dhahiri mtandao wa shule hizi za misheni ulikuwa mkubwa Wilayani Masasi, kiasi cha kuwezesha kufikisha asilimia hii kubwa ya 85 wakati tunapata uhuru. Ukaguzi wa hizi shule ulikuwa wa makini na ukifanywa na wamisheni wenyewe (wazungu) na hivyo elimu kuwa bora.
Vivyo hivyo, shule za sekondari na za ualimu katika Wilaya ya Masasi zilikuwa za misheni, sekondari ya Chidya ya Anglikana na Ndanda ya Katoliki pia Chuo cha Walimu wa kike pekee Ndwika na vyuo vya wakunga Lulindi cha Anglikana na Ndanda cha Katoliki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu masomo ya juu, wanafunzi waliotakiwa waendelee na masomo zaidi walitoka katika shule hizi mbili za misheni kwenda katika shule kuu mbili za misheni za Minaki (Anglikana) na Pugu (Katoliki). Pia waliweza kwenda shule za Serikali za Tabora, Tanga na kadhalika na baadaye Makerere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwango vya juu vya nidhamu, uadilifu na uwajibikaji (commitment) ndiyo ishara kuu na misingi ya uendeshaji wa shule hizi za misheni kufuatana na maadili ya kidini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio, Makatibu Wakuu, viongozi Ikulu wawili wa kwanza baada ya kupata uhuru, Dunstan Omari na Joseph Namatta walisoma Chidya hata baadae kufika Makerere wakitokea Minaki. Pia enzi za ukoloni Dunstan Omari alikuwa District Officer wa kwanza Mwafrika. Rais Mstaafu Benjamin Mkapa pia ni zao la shule ya misheni ya Ndanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya wengine waliofanikiwa kupata uongozi wa juu katika Awamu ya Kwanza kutoka shule za Chidya, Ndada na Ndwika ni kama ifuatavyo:-
1. Mzee Fredrick Mchauru – Katibu Mkuu Wizara mbalimbali na Mshauri wa Rais
2. Nangwanda Lawi Sijaona – Waziri
3. Mama Thecla Mcharoru – Katibu Mkuu UWT
4. Yona Kazibure MSc (Physics) wa kwanza Makerere – Chief Engineer Radio Tanzania.
5. Mama Anna Abdallah – Mwenyekiti UWT
6. Beda Amuli – Architect Mwafrika wa Kwanza Tanzania
7. Mama Kate Kamba - Katibu Mkuu UWT
8. Yuda Carmichael Mpupua – Naibu Katibu Mkuu na Chief Agricultural Officer
9. Dkt. Isaya Mpelumbe – Director of Veterinary Service na Kamishina wa Kilimo na Mifugo
10. Alex Khalid – Katibu Mkuu
11. Major Gen. Rowland Makunda – Mkuu wa Navy kuanzia vita vya Idi Amin
12. Philip Magani – Chairman/Managing Director CRDB
13. Paul Mkanga – Katibu Mkuu
14. Dkt. John Omari – Fellow of the Royal 1 Surgeons wa kwanza Tanzania
15. John J. Kambona – Director of Fisheries Tanzania na FAO Headquarters Rome.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia walimu wa kwanza kutoka Makerere walifundisha shule maarufu za Serikali za sekondari tangu ukoloni kama vile Tabora, Old Moshi, Tanga ni Curtius Msigala, Joseph Banali, Peter Nampanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya siasa na hatima. Tangu shule zile za misheni kuwa chini ya Serikali mbali na nyingine nyingi kujengwa, kwa jumla kiwango cha elimu Wilayani Masasi kimezidi kuporomoka. Ufaulu katika shule zote za awali na sekondari umezidi kushuka. Ufaulu wa shule za awali kuingia sekondari umekuwa mdogo na Wilaya kuwa mojawapo ya zile za chini kabisa nchini inashangaza hata shule maarufu kongwe (tangu mwaka 1923) ya Chidya haijapata hadhi ya kuwa high school hadi leo, kuna nini? Hili ni jambo lisilokubalika na viongozi, Wabunge, Madiwani na watawala wanawajibika kuelewa awareness na kuhimiza kulifanyia kazi kwa nguvu zao zote wakishirikiana na wananchi kurekebisha hali hii mbaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mwanaharakati aliyeandika kitabu How Europe Underdeveloped Africa, si vizuri mwingine akaandika kingine. How Tanzania Underdeveloped Masasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Wizara hii ya Nishati na Madini. Moja kwa moja nielekeze kwanza mchango wangu katika Shirika la Umeme la TANESCO. Mpaka sasa hivi tunafahamu TANESCO wana deni kubwa sana kutoka kwa wazabuni, lakini pia kutoka kwa watu mbalimbali. Namwomba Mheshimiwa Waziri watakapokuwa wanaleta majumuisho yao watueleze wazi wazi, kama kuna mpango wowote wa kukiongezea nguvu Kitengo cha Masoko cha Shirika la Umeme Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, watu wale wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea. Nafikiri kama wanaamua kufanya kazi kibiashara, basi angalau wangekuwa wanazungukia kwenye maeneo ambako kuna ujenzi mpya unaendelea na wao kutafuta wateja badala ya wateja kuanza kuhangaika kwenda kwenye Ofisi za TANESCO kuomba wakaandikishwe. Hata hivyo, watu hao wanaokwenda Ofisi za TANESCO wakishalipa pesa yao kwa ajili ya gharama za kuunganishia umeme, hili zoezi linakuwa refu sana, wamekuwa wenye urasimu mkubwa sana watu hawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii tunaiona zaidi katika maeneo yetu, ukifika maeneo ya Masasi, ukifika maeneo ya Ndanda, hasa zaidi maeneo ya sokoni, kuna watu wengi sana wamejiandikisha pale kupata huduma ya umeme, lakini sasa hivi ni miezi mitatu, miezi minne watu wale wanashindwa kupelekewa umeme ambao tayari wameshaulipia. Sasa TANESCO watueleze kama walikuwa tu wanatumia kiujanja ujanja kutaka kukopa pesa kwa hawa watu wanaotaka kuunganishiwa umeme na hawawekewi umeme kwa muda, wakati masharti ni kuwapelekea. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia niseme, kwenye biashara ya mafuta, EWURA pamoja na tozo mbalimbali zilizopo kwenye biashara ya mafuta. Mfanyabiashara wa mafuta ni mtu amekuwa wa kuonewa sana kwa kipindi kirefu. Ukiangalia gharama za mafuta sasa hivi japokuwa zimeshuka kufikia sh. 1,600/=, lakini nyingi katika hii pesa inakwenda kwenye upande wa Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, tozo za mafuta zinakadiriwa kufikia sh. 500/= mpaka sasa hivi na mfanyabiashara wa mafuta anapata tu pale sh. 200/=. Kwa hiyo, sh. 900/= ni gharama halisi ya mafuta. Kwa nini Serikali isione kuna haja ya kupunguza kodi mbalimbali zilizoko kule ndani ya mafuta hasa zaidi hizi tozo ili mwananchi aweze kununua mafuta kwa gharama nafuu zaidi tofauti na gharama iliyopo sasa hivi? Naamini kwa sababu umekuwa ukipata sifa nyingi na hili jambo unaweza kulichukulia hatua. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kusikitika kabisa niwaambie kwamba, katika eneo letu la Wilaya ya Masasi, suala la kukatikiwa umeme sasa hivi limekuwa kama fashion. Haipiti siku mbili, siku tatu, lazima umeme utakatika. Ukipiga simu TANESCO kutaka kufahamu kwa nini imekuwa hivyo, hata wenyewe wakati mwingine wanashindwa kujua sababu za msingi. Mara utaambiwa mikorosho imedondokea nguzo, mara utaambiwa miundombinu duni katika eneo hili kwa sababu iliwekwa kwenye miaka ya 1990.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sasa tufahamu wazi kabisa Serikali ina mpango gani kuweza kutubadilishia miundombinu katika eneo letu la Wilaya ya Masasi ili tuweze kupata umeme wa uhakika kwa sababu umeme huu unazalishwa katika maeneo yetu ya Mtwara na tumeambiwa kwamba unatumia umeme wa gesi lakini tuseme kweli, sisi hatufaidi umeme ule kwa sababu tunaupata kwa matatizo makubwa sana katika Wilaya zote zinazozunguka maeneo ya Masasi ikiwa ni pamoja na Nanyumbu na maeneo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Ndanda ndiyo kuna vichekesho, kwa sababu katika maeneo haya ndiko unakopita umeme unaokwenda kutumika maeneo ya Masasi, maeneo ya Nachingwea na maeneo mengine. Hata huko Ruangwa maeneo ya kwa Waziri Mkuu umeme wake unakatiza katika maeneo ya Jimbo langu. Wazee na vijana, watu mbalimbali katika maeneo yale walishawishiwa wadondoshe mikorosho yao, wengine wakate miembe ili zipite pale nguzo kwa ajili ya kuwaletea wao huduma za umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kumweleza mara nyingi tu hapo Mheshimiwa Waziri katika suala hili, lakini ni ajabu kabisa mpaka sasa hivi tunaingia katika hili Bunge la Bajeti, hakuna hatua zilizochukuliwa za moja kwa moja katika vijiji ambako nguzo za umeme zinapita katika maeneo hayo. Tunaomba tupewe taarifa ya vijiji vile. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda katika Vijiji vya Chipite, Mkwera, Nanganga na maeneo mengine, umeme unapita juu ya vichwa vyao, lakini pale chini watu wale hawana umeme. Kuna wakati ulifika katika Kijiji cha Liputu, Mzee wangu mmoja pale alikuwa haoni umuhimu wa kuwa na zile nguzo shambani kwake, aliamua kuchoma nguzo moja moto. Bahati nzuri wakati huo alifikishwa Polisi, wakati ule Mheshimiwa Mkuu wa Kituo ana busara, kabla hajaamua kujiingiza kwenye siasa, walimaliza lile jambo amicably lakini yule mzee alikuwa haoni umuhimu wa kuwa na nguzo inayopita shambani kwake. Yeye alikuwa anatamani lile eneo alitumie kwa ajili ya kilimo na siyo kupitisha nguzo ambazo zinakwenda kunufaisha watu mwishoni mwa lile eneo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuweza kupunguza gharama, nafikiri wakati mwingine TANESCO ifikirie kuwa na njia mbadala. Kusingekuwa na haja ya kupitisha umeme maporini, badala ya umeme ule kuupitisha kwenye vijiji ambako wanakaa watu, vikakona vikaenda kule. Sisi tumeamua sasa hivi kufuata njia kuu moja kwa moja. Kusingekuwa na haja ya kupitisha umeme katika Kijiji cha Chigulungulu ambapo umeme ule sasa hivi unatakiwa uzunguke Namalembo ili kufika mpaka Msikisi wakati tayari kulikuwa kuna shortcut inayopitia katika Vijiji vya Chiroro na vijiji vingine katika Kata ya Msikisi ili kuweza kupata umeme katika maeneo yale. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunashindwa pia kuelewa, pale TANESCO wanapokuja kutaka kuunganishia umeme nyumbani kwako, wao walikuwa na jukumu la awali la kuweka miundombinu iwakaribie watu katika maeneo yao ambako ujenzi unaendelea. Sasa hivi kunaonekana kuna mtindo wa TANESCO kuweka nguzo tu katika maeneo ya barabara. Utakapotaka wewe kuomba umeme ambaye ujenzi wako umemaliza, kiwanja cha tano kwenye mtaa wako, unaambiwa ulipie zile nguzo zote ambazo ziko pale barabarani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaomba kupata jibu, nguzo hizi mwishoni zinakuwa mali ya nani? Gharama zile nilizolipia mimi kuwekeza kwenye nguzo zile mwanzoni: Je, naweza nikarudishiwa na hili shirika baadaye watu wa hapa katikati ili kufika nyumbani kwangu wakishakuwa wamejenga katika maeneo yao? Tunaomba hili tupate jibu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia nilitoa taarifa katika Kijiji cha Chikundi, kuna Zahanati pale inatoa huduma nzuri sana kwa ajili ya akinamama kujifungua ili kuweza kupunguza mzigo wa akinamama wanaokwenda kujifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda. Sasa hivi wana miaka mitatu, miaka minne inakadiriwa panatakiwa kupatikana nguzo kama kumi, kumi na moja; lakini wale Wamisionari wa Ndanda wamepelekewa quotation ya shilingi milioni 11 ili kuweza kuweka umeme katika ile Zahanati ya Chikundi ambako yule mama pale, Mkunga anajitahidi kuwasaidia akinamama kujifungua akiwamulika kwa tochi. Tunaomba sasa hapa tupate majibu moja kwa moja, mnaweza mkatusaidia vipi katika maeneo yale? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kinachochekesha zaidi, mimi napakana na Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Jimbo lake na baadhi ya maeneo fulani. Wanakijiji wengine wanatoka vijijini ambako ni mbali kabisa kufika kule kwa Waziri Mkuu, wanategemea kupata umeme kutokea katika upande wa Jimbo la Ndanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, Vijiji vya Chinongwe, Mandanga, Likwachu pamoja na Vijiji vya Mbecha, wale watu siku za Jumamosi wanafanya maandamano ya kuja upande wa Ndanda kununua ice cream, kwa sababu kule kwao wanakosa hata ice cream. Tumwonee Mheshimiwa huruma, tuhakikishe tunapeleka umeme katika haya maeneo ili watu waweze kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Ngamadani, pale pana gereza kubwa sana, lakini nako penyewe umeme unapita juu ya vichwa vyao. Pana wafungwa pale, pana Askari Magereza pale, siku wakija kupotea msiwalaumu lakini wanaishi kwenye mazingira magumu! Wanashindwa kuvuta maji kwa ajili ya kupeleka kwa matumizi ya wale Maafisa Magereza pamoja na wafungwa wao waliopo katika eneo lile kwa sababu ule mkusanyiko ni mkubwa sana. Tunaomba mtusaidie katika maeneo yetu, hatufahamu sisi tumewakosea nini nyinyi, lakini tunasema. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Chingulungulu na kwenyewe umeme unakatiza juu ya vichwa vya watu. Mnashindwa tu kupeleka transformer ndogo ikashusha umeme kwa ajili ya kuhudumia watu pale. Tungepata angalau transformers chache za KV 50 zingeweza kusaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, niliongea na Meneja wa TANESCO siyo muda mrefu, aliniambia makadirio ya nguzo 1,200, pamoja na transformer 30 litaweza kumaliza tatizo la umeme katika eneo letu; lakini mimi nishushe zaidi, hata mkitupa nusu ya hii tutawaelekeza sisi alternative route za kuweza kuwafikia watu kwa kutumia transformer moja katika vijiji viwili au vijiji vitatu ikiwezekana kwa sababu njia za mikato za kuelekea hayo maeneo sisi tunazitambua. Tulikuwa tukifanya kampeni katika hayo maeneo, kwa hiyo, tunajua vizuri. Hii pia itasaidia TANESCO kuweza kupunguza gharama.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Chigugu, Vijiji vya Mbemba pale kuna zahanati kubwa sana, iko pale toka enzi za ukoloni, lakini mpaka sasa hivi hawana umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha. Ahsante. Nasubiri majibu ya Mheshimiwa Waziri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kufahamu ni mita ngapi toka katikati ya hifadhi ya barabara mpaka kwenye barabara kuu? Je, wananchi wa Lukuledi, Naditi, Chikunja watalipwa fidia ya nyumba zao zilizowekwa alama ya “X”?
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa nafasi uliyonipa kuchangia. Naomba moja kwa moja niende kwenye hoja. Kwanza naanza kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kutimiza wajibu wake kwa kuivunja Bodi ya Korosho na sasa hivi tunaona wakulima na wananchi wa Mtwara wakiwa wanafurahi kwa sababu korosho yetu imefikia kuuzwa kwa sh. 3,800. Hata hivyo, Mheshimiwa Mpango pamoja na Mheshimiwa Waziri wa Kilimo sijaona vema katika mpango wenu juu ya maendelezo au mwendelezo wa viwanda tulivyonavyo Mtwara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulisema toka mwanzo kwamba Mtwara hatuhitaji viwanda vipya kabisa, tunahitaji tu maboresho kwenye viwanda vyetu vya korosho na tunataka kufanya sasa tathmini ya vile viwanda kwa sababu majengo tulikuwa nayo, lakini yaliuzwa kwa watu ambao hawajulikani au wanajulikana kwa bei chee kabisa na wanawatumia kufanyia shughuli nyingine hasa zaidi wamegeuza kuwa maghala badala ya kufanya sehemu za kuzalisha korosho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa tathmini ifanyike, mpitie pamoja na mikataba waliyouzia maghala yale ikiwezekana sasa mle ndani viwekwe viwanda vidogovidogo na wazalishaji waendelee kubangua korosho zao kama ambavyo inafanyika kwenye kiwanda kwa Mheshimiwa Nape katika Jimbo la Mtama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakumbuka miaka ya 80, Tanzania ilikopa shilingi bilioni 20 kutoka kwa Wajapan pamoja na Serikali ya Italia, sasa tunataka hizi pesa kweli zilete manufaa kwa wananchi. Pamoja na manufaa ya wananchi wanayoyapata kutoka kwenye korosho, sasa hivi pamekuwa kidogo na ucheleweshaji wa malipo. Tunaomba na hili Waziri wa Kilimo alifuatilie tuone hawa wananchi wanalipwa kwa wakati kwa sababu sasa hivi ni mnada wa tatu kufanyika lakini bado wananchi hawajapata posho zao kwa uhakika na hawajui watamalizia lini kulipwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie Waziri wa Kilimo pamoja na mazuri yote yanayofanyika, kuna hii karatasi ipo hapa mbele yangu. Kuna Kampuni moja inaitwa HAMAS iko kule Mtwara, hawa watu wali-supply sulphur kwa ajili ya wakulima wa korosho mwaka jana na mwaka juzi, matokeo yake waliishia kufikishana Mahakamani na kampuni hii ililipwa shilingi milioni 953.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naileta kwenu kwa sababu sisi wananchi wa Mtwara tusingependa Kampuni hii tena ikapewa tenda ya ku-supply sulphur kwa sababu wanaleta ujanja ujanja na mwishoni wanapeleka Mahakamani wanaishia kulipwa pesa ambayo hawajaifanyia kazi. Nitaomba nafasi na Waziri Mkuu ikiwezekana tulijadili jambo hili kwa kina kwa sababu kuna taarifa za kutosha, achilia mbali hii karatasi niliyoshika hapa mbele yangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye kitabu cha Mheshimiwa Waziri cha Mpango kwenye ukurasa wa 22, tumeongelea pale ndani kwamba kuna samaki wanaoingizwa nchini wanaagizwa kutoka nje. Tungependa sasa kufahamu kwa nini viwanda vyetu au maziwa yetu yasitumike watu wale wakawezeshwa wakaanza kuzalisha samaki hapa nchini baada ya kuamua wao kuvua na tunaleta sisi samaki kutoka nje. Kwa hiyo, kwa vyovyote lazima sasa tuamue tuwawezeshe watu wetu wao wajitosheleze kwanza soko la ndani, kama tuna soko la kutosha kabisa la ndani kwa nini sasa tuanze kuagiza samaki kutoka nje? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye ukurasa wa 34 inaonesha pale ndani kuna tafiti mbalimbali zimefanyika za masuala ya kilimo. Mimi bado nirudi tena kwa wakulima wa korosho, niseme kuna tafiti nyingi kweli zimefanyika na Serikali imewekeza pesa nyingi sana pale ndani ikiwemo utafiti wa mabibo ambao unaonyesha una asilimia mara tano zaidi kutoa vitamin ‘C’ tofauti ilivyokuwa tunda la chungwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunataka sasa zile tafiti zianze kufanyiwa kazi, tusiendelee tu kukaa na mavitabu tukaanza tena kuwekeza kwenye pesa kwa ajili ya tafiti, twende tukawasaidie wale wakulima wa korosho kwa sababu kwa kufanya hizi tafiti vile viwanda vikianza kutengeneza basi kutaongeza mapato kwa wakulima wa korosho kwa sababu, sasa hivi hata bibo tunatamani lianze kununuliwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa badala ya kuendeleza kufanya taafiti mbalimbali, tafiti ambazo tayari zilishafanyika kutoka kwenye korosho, basi zitekelezwe ili kuwaongezea wakulima kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye ukurasa wa 38, tunakuta pale ndani Mheshimiwa Waziri wanasema tunataka kuwa-encourage investors waje kuwekeza nchini kwenye masuala ya viwanda. Naomba niongelee kwa masikitiko sana Kiwanda cha Dangote. Dangote walipokuja kuweka kiwanda Mtwara walisema kwamba watapewa umeme wa kutumia gesi ili waweze kuzalisha kwa gharama nafuu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshukuru kidogo bei ya cement imeshuka katika maeneo yetu imefikia shilingi 11,000, Mwekezaji huyu ana matatizo makubwa sana, mpaka sasa hivi hajapelekewa gesi pale kiwandani, amelazimishwa akanunue makaa ya mawe kutoka Mchuchuma na utafiti unaonesha kwamba gharama za kutoa makaa wa mawe Mchuchuma zimeongezeka kwa asilimia 20 zaidi tofauti na ambavyo angeweza kuleta makaa ya mawe au ambavyo alikuwa analeta kutoka South Africa. Kwa hiyo, tumsaidie yule Mwekezaji aendelee kuzalisha cement katika eneo lile ili simenti iweze kushuka, tuachane sasa na biashara ya zamani ya biashara ya matope wananchi watumie tofali za cement kujenga nyumba bora. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaomba sasa hivi bandari ya Mtwara ndiyo iwe bandari kuu itakayotumika kusafirisha mazao yetu ikiwemo pamoja na korosho. Tulipata pale taarifa wakati fulani kwamba Dangote na tunafahamu Dangote wanaleta cement Dar es Salaam kwa kutumia barabara. Barabara ile tumelalamikia kwa miaka 54 iliyopita ni miaka mitatu, minne iliyopita ndiyo barabara ya Mtwara imejengwa, sasa badala ya kusafirisha cement ya Dangote kwa kutumia bandari ya Mtwara bado cement inakuja Dar es Salaam kwa kutumia barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ile ikiharibika Serikali hii haitaweza tena kujenga barabara, tunaomba tafadhali utaratibu ufanyike cement ya Dangote isafirishwe kwa kutumia Bandari ya Mtwara na siyo kupeleka kwa barabara, barabara itumike kwa matumizi mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu hizi kampuni zinazosafirisha cement ni Kampuni za wakubwa wanasingizia kuna kipande fulani cha barabara panaitwa Mikindani kwamba tuta lile litaharibika, kuharibu tuta dogo la kilometa 10 ni nafuu zaidi kuliko kuharibu barabara nzima ya kilometa 300 hadi 400 kufika Dar es Salaam, mtaturudisha kule tulikotutoa siku za mwanzo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona sasa hivi katika maeneo mengi ya Kusini kuna uchimbaji wa madini unafanyika katika maeneo madogo madogo (small scale). Tunataka kupata taarifa sahihi kule kunakochimbwa madini ni nini kinapatikana, madini gani yapo tuwaeleze wananchi wa Mtwara ili waweze sasa wao kuangalia nafasi ya kutumia fursa walizonazo katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zamani walikuwa wanasema Mikoa ya Kusini iko nyuma hasa zaidi Mtwara na Lindi, sasa hivi fursa tunazo za kutosha, tunachoomba tu sasa kutengenezewa mazingira wezeshi tuweze kufanya shughuli zetu wenyewe za kujizalishia kipato badala ya kila kitu tulichonacho ninyi mnataka kukiondoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sikuona sababu za msingi za kutengeneza ule mtambo wa kuzalisha umeme wa Kinyerezi badala ule mtambo ungetengenezwa kule kwetu, ungeweza kutoa ajira kwa vijana wetu, kidogo tunachokipata mkiache tukitumie baadaye kinachobaki mkipeleke kwa wengine nao wakakitumie. Tulikuwa nyuma kwa muda mrefu sana, tunaomba sasa resources zilizoko Mtwara zitumike kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Mtwara na kwa Taifa zima kwa ujumla ili vijana wetu waweze kupata ajira ya kutosha katika maeneo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuendelee bado katika lile jambo ambalo tulisema pale awali. Mtwara pia tunategemea sana uvuvi. Tuna eneo kubwa ambalo linaweza kufanyika shughuli za uvuvi. Tuiombe Serikali sasa iamue wazi kutuwekea hata kiwanda sasa cha uvuvi. Kama nilivyosema majengo ya kuweka hivi vitu tunayo lakini watu waliyageuza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda aamue sasa mara moja aka-review mikataba iliyowapa watu uendeshaji wa maghala kule Mtwara badala ya kufanya viwanda na wanaendelea kuhifadhia mazao wakijipatia pesa kwa sababu si kitu ambacho walikubaliana. Tunataka sasa viwanda vile vianze uzalishaji wa korosho ili kuongeza tija kwenye mazao ya korosho na wakulima waweze kupata kipato cha kutosha pamoja na kuongeza mzunguko wa pesa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa nafasi uliyonipatia, nitakapopata tena wakati nitatoa maelezo zaidi. Ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuweza kuchangia kwenye hoja iliyoko mbele yetu taarifa ya Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Bajeti kuhusu utekezaji wa shughuli zake katika kipindi kuanzia mwezi Januari, 2016 mpaka Januari, 2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza mimi ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya Bajeti na kwa kipindi hiki chote tulikuwa tukifanya kazi pamoja kuhakikisha bajeti yetu inakwenda vizuri hasa zaidi katika jukumu letu la kutaka kuisimamia Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwanza kabisa Kamati yetu imekutana na changamoto nyingi sana; na Mheshimiwa Mwenyekiti wakati anawasilisha taarifa yake tumeona na karibu Kamati zote zilizokuwa zinatoa hapa taarifa zake wamekuwa wakilalamikia kuhusu jambo hili, kukosekana kwa mafunzo kwa visingizio kwamba hatuna bajeti ya kutosha kwenye kufanya shughuli hizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali ya kushangaza kabisa, Kamati ya Bajeti kama ulivyosema ndio kubwa hasa na inayosimamia mustakabali mzima wa nchi yetu hasa zaidi kwenye mapato na matumizi, lakini tunakosa mafunzo ya kutosha, Ofisi ya Katibu, pia Ofisi ya Spika haijaipa Kamati hii kipaumbele kuhakikisha kwamba tunajua majukumu yetu ya msingi, kwa kuwa exposed kwenye maeneo mbalimbali na ukizingatia tulio wengi kule ndani ni wageni ambao tunahitaji hasa na sisi siyo wataalam wa mahesabu katika hali kubwa. Kwa hiyo, Bunge hili lione sasa kuna haja ya lazima kabisa ya kuhakikisha Wajumbe wa hii Kamati wanapata mafunzo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tuna changamoto kubwa sana kutoka kwenye Wizara mbalimbali hata Wizara ya Fedha yenyewe, kumekuwa na usiri mkubwa sana wa kupatiwa hizi taarifa. Utakuta tunakwenda kwenye vikao, tumebakisha muda mchache kuanza vikao vyetu ndipo taarifa zinapokuja ambazo wanataka sisi tuweze kuchangia na kutoa mapendekezo kwa Serikali. Kwa hiyo, tuombe tuwe tunapata taarifa kwa wakati ili tuweze na sisi kuzipitia vizuri tuweze kutoa mapendekezo yetu kwa Serikali. Kama unavyofahamu jukumu letu ni pamoja na kusimamia suala zima la Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hapa inajadiliwa kwamba kuna ukuaji mkubwa sana wa Deni la Taifa. Siyo siri kwamba Deni la Taifa linakuwa na hasa zaidi deni la ndani limekuwa likikuwa kila mara, hii inadhoofisha sana sekta binafsi kwenye kupata mikopo. Kwa sababu Serikali nayo sasa imekuwa ikishindana na wafanyabiashara wadogo wadogo, Serikali imekuwa ikishindana na wamachinga na watu wengine kuweza kupata mikopo katika mabenki yetu ya kibiashara. Kwa sababu Serikali wana nguvu kubwa sana, wao ndiyo hasa wanaopendelewa na inaonekana hili jambo linafanywa kama maagizo maalum kwamba Serikali ipewe kipaumbele cha kukopeshwa.
Hivyo, tunazuia mzunguko wa pesa wa kawaida kabisa hapa ndani kwetu na ndiyo maana sasa tunaanza kuona inflation zinapanda. Wafanyabishara wanashindwa kulipa madeni yao, kwa sababu sasa hivi hawakopeshwi tena. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi tunaona wanafilisiwa kama tulivyosikia kuna wafanyabiashara wazabuni wa Serikali, kuna Wazabuni ambao walikuwa wamekopa na wanafanya shughuli na majeshi, tunaona watu hawa wanashindwa kulipa madeni yao kimsingi na hawawezi kukopesheka tena. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeacha jukumu lake, Serikali ni jambo kubwa sana, ilitakiwa itoe mikopo yao nje ya nchi kuja kuleta Tanzania, kuja kuongeza mzunguko wa pesa katika nchi yetu na katika mzunguko wetu wa kawaida kabisa wa pesa. Sasa hivi tumeona nao kwa sababu ya kutokutekeleza majukumu yao ya msingi, kutokufuata masuala ya utawala bora na sheria wameamua nao wawe wanakopa hapa ndani, kiasi kwamba wanazuia mzunguko wa pesa, na kufanya pesa iwe na mzunguko mdogo (circulation of money).
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaona wanakwenda kukopa au kuchukua pesa kwenye mifuko, kiasi kwamba wastaafu wanashindwa kulipwa pesa zao kwa wakati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wamekuwa wakizungushwa, tunafahamu hapa katikati kuna ma- DAS, kuna ma-DED ambao kabisa ni Watumishi wa Serikali wanashindwa kupata pension zao. Mifuko ya PPF, NSSF tumeanza kuona sasa wanashindwa kuwalipa watumishi kwa sababu tu pesa nyingi zimechukuliwa tena na Serikali, Serikali inashindwa kuzirudisha pesa zile kwenye mzunguko, matokeo yake wanakwenda kugharamia vitu ambavyo viko nje ya bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi pesa hazitoki mfukoni kwa mtu mmoja, hazitoki mfukoni kwa Mheshimiwa Rais, hizi pesa ni zile ambazo sisi tunazikusanya, badala ya kwenda kufanya majukumu tuliyoyapangia kibajeti, zinakwenda kufanya kadri ya mahitaji ya Mheshimiwa Rais, na kwenda kufanya kadri ya mahitaji wa viongozi mbalimbali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuziachie pesa zizunguke, watu waliostaafu wapewe sasa haki yao, kwa sababu tunajua baada ya kustaafu watu wana muda mfupi tu wa kuweza kuishi hapa duniani, basi wapewe pesa zao kwa wakati wazitumie wanavyotaka wao, badala ya kwenda kugharamia miradi ambayo siyo ya kibajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona pia kuna madeni ya majeshi, watumishi wa jeshi tuliondoa hapa masuala ya kodi kwenye vifaa mbalimbali wanavyotumia kwenye maduka ya majeshi, lakini wakasema pesa hizo wataongezewa kwenye masurufu yao, pesa hizo wataongezewa kwenye mishahara yao. Sina uhakika mpaka kufikia leo ni shilingi ngapi zimepelekwa kwenye majeshi kwa ajili ya ku-subsidize ile kodi ambayo ilikuwepo walikuwa wanalipiwa mwanzo na Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mwenyekiti wa Kamati anatoa taarifa hapa na wote tunafahamu kwamba Serikali iliamua kujikita kutoa asilimia 40 yote iende kwenye shughuli za maendeleo, lakini hapa tumesikia katika ripoti na hii kila mtu anaifahamu, hakuna reflection hauwezi kuona hali halisi ya kilichofanyika sasa hivi. Hakuna tofauti wakati huo asilimia 40 ya maendeleo iliyopo sasa hivi na asilimia zile ndogo ambazo zilikuwepo siku za nyuma. Pesa za maendeleo hazifiki kwa wakati kwenye maeneo yanakotakiwa kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunashindwa kuelewa tunajitangazia kwamba tunakusanya pesa nyingi sana kwa ajili ya shughuli za maendeleo, nchi yetu iweze kufanikiwa kuvunja hapa rekodi, ukiangalia hapa kwenye baadhi ya kurasa inaonyesha kabisa wazi kwamba zimekusanywa pesa nyingi sana, lakini kimsingi pesa hizi haziendi ku-reflect maisha halisi ya wananchi wanayoyaishi mitaani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaanza kuhisi kwamba hata inflation inapanda mzunguko wa pesa umekuwa mdogo. Serikali inasema inapeleka pesa za maendeleo, maendeleo hayo kwa sasa hivi kwa kweli hatuyaoni. Halmashauri zimekuwa zikilia njaa, hakuna mtu anayeweza kutekeleza wajibu wake, miradi mingi imesimama, pesa nyingi ndiyo tunatambua inakwenda kulipa madeni mbalimbali lakini kimsingi mzunguko wa pesa umeondoka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye ukurasa wa 43 wa hii taarifa tuliyonayo hapa, mpaka leo Serikali bado inang‟ang‟ana na vyanzo vilevile vya mapato vya asili wakati ilifanyika tafiti na Mheshimiwa Chenge wewe ndiye ulikuwa Mwenyekiti wa tafiti hizo, ukapendekeza vyanzo vipya vya mapato Serikalini, lakini Serikali hii tunayoiita sikivu mpaka sasa hivi bado imeshindwa kutumia vyanzo vipya vya mapato. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunategemea tuendeshe nchi yetu kwa kulipia kodi au kuongeza kodi za sigara kila mara, si ajabu utakuja kuona bajeti ijayo sigara inapandishwa tena bei, soda, bia zinakwenda kupandishwa bei na vinywaji vingine lakini huu siyo msingi wa kweli, kama nchi inataka kusimama, kama nchi kweli inataka kuendelea tutegemee vyanzo hivi kila mara. Kulikuwa kuna mapendekezo mazuri kabisa ya vyanzo vipya vya mapato, lakini Serikali imeendelea kudharau.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulifikiri sasa Serikali hii itaamua kuchukua vile vyanzo na kuamua kuvifanyia kazi, lakini tunaona hapa Kamati inaleta taarifa yao. Tunatakiwa sasa kukamilisha tathmini ya ukusanyaji wa mapato kupitia Bahari Kuu, hiki chanzo ni kizuri sana cha mapato lakini hakijaanza kutumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu kabisa tunatakiwa tuanze sasa hivi kuongeza vyanzo vipya vya mapato. Tuseme kwamba Shirika la Umeme halizalishi vizuri umeme wake, kwa hiyo tuende tuanze kuipa nguvu zile sehemu mbalimbali ambazo zinataka kuzalisha umeme. Kwa mfano, watu geothermal, kuna umeme wa upepo, kuna watu wanataka kutumia hizi solar energies, tuanze kuona sasa hivi viwe vyanzo vingine vya kuweza kuongezea Serikali mapato na TANESCO iende kulipa deni lake sasa ili kimsingi watu uzalishaji uongezeke.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona tatizo kubwa sana la umeme hapa Mkoa wa Mtwara sasa hivi linatokea na hili jambo linatokea ni kwa sababu ya kung‟ang‟ania chanzo kimoja cha umeme. Wilaya nzima au Mkoa zima wa Mtwara kuna tatizo kubwa sana la umeme tuwaongezee wale watu nguvu ili waweze kuzalisha sasa na waweze kuchangia vizuri kwenye pato la Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa sana niseme tu kwamba pamoja na Kamati kuleta taarifa zake hapa mbele, lakini siyo kila mara Kamati hii haionekani kuwa ni kipaumbele, wakati ina jukumu kubwa la kusimamia mchakato mzima wa bajeti toka mwanzo wake mpaka pale tutakapomalizia. Kwa hiyo, kifupi niseme tunaomba tafdhali kwamba sasa hivi mependekezo yale yaliyotolewa na Kamati ya Chenge, vyanzo mbalimbali vya mapato vianze kuwa adopted. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hapa karibuni kuna utaratibu umeanza wa kukata pesa kwenye miamala, hili jambo linaumiza sana Watanzania, hili jambo linaumiza wananchi wote tulifikirie tena upya ili kuwe kuna thamani halisi ya matumizi ya zile pesa shilingi 1,000 basi ipate thamani yake, shilingi 500 basi ipate thamani yake. Lakini tunakwenda kwenye miamala ya kibenki tuona gharama zimeongezeka, tunakwenda kwenye miamala ya simu, tunaona kule gharama zimeongezeka, hivi vitu vyote havileti picha nzuri kwa wananchi. Kwa hiyo, tufikirie vyanzo vingine vya mapato, kwa sababu vyanzo vya kawaida hivi vya kodi vimeshindwa kabisa na vimekuwa kama ni traditional sources of income to the government. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona sasa hivi mpaka polisi tunaanza kuwaingiza na wenyewe ili waanze nao kuwa ni source of income ya Serikali, hili jambo siyo jema tufikirie vyanzo vile ambavyo Mheshimiwa Chenge wewe kwa nafasi yako ulishauri kabisa Serikali. Kama walikuwa hawana haja ya kutaka kulisikia kusingekuwa na haja ya kutumia pesa nyingi kuipa ile Kamati iliyoanza kufikiri kuhusu hivi vyanzo. Asante kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba ya Wizara ya Viwanda na Biashara. Mheshimiwa Mwijage ni kaka yangu na mara nyingi tumekuwa tukiwasiliana na leo nataka nimkumbushe tu mambo machache ambayo tungependa Mheshimiwa Rais lakini pamoja na Taifa liyafahamu. Kwanza kabisa nimfahamishe kwamba mwaka wa jana wakati fulani Mheshimiwa Waitara alichangia akimtaka CAG kwenda kufanya ukaguzi maalum Chuo cha Elimu ya Biashara, Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, CAG amekwenda kukagua amekiri lakini bahati mbaya sana ukaguzi huu umefanyika Chuo cha Dodoma pamoja na Chuo cha Mwanza, Dar es Salaam ambako ndiko kwenye upotevu wa zaidi wa Sh.400,000,000 ukaguzi haujafanyika. Taarifa za CAG ni hizi hapa, naomba apatiwe copy.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimkumbushe Mheshimiwa Waziri mambo machache. Tunatamani sana kuwa na viwanda Tanzania, lakini Sera yetu bado haijabadilika. Ukiangalia kimtazamo, wawekezaji wengi wanashindwa kuja Tanzania kwa sababu ya kodi. Kodi nyingi zinatozwa kabla mtu hajawekeza hata kitu kimoja; atakutana na watu wa ardhi, watataka pesa kutoka kwake, atakutana na watu wa NEMC, atataka pesa kutoka kwake. Sasa tunawavutiaje wawekezaji kama vyanzo au vivutio vya uwekezaji ni vichache au vilivyokuwa na misongo misongo? Kwa hiyo, tuangalie namna bora ya kufanya, NEMC pamoja na watu wa ardhi waone namna ya kutoza kodi ikiwezekana baada ya mtu kuwekeza katika mazingira fulani.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, nataka nimkumbushe lakini pia tumsaidie Mheshimiwa Waziri kumkumbusha Mheshimiwa Rais; alipokuja Mtwara wakati anaomba kura, alisema atahakikisha viwanda vya korosho vinafanya kazi. Sasa hivi tuna mwaka mmoja takriban na nusu viwanda vile havijaanza kufanya kazi na hatujaona juhudi zozote zinafanyika angalau kuwatafuta wale watu ambao walipewa viwanda na Serikali ili waviendeleze. Vile viwanda sasa vimegeuka kuwa maghala. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tafiti mbalimbali zimefanyika ambazo zinaonesha kabisa kwa kutumia tu korosho iliyoko Mtwara sisi tunaweza tusiwe watu tunaohitaji viwanda vingine vyovyote. Korosho yetu ina uwezo wa kututoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina hii paper hapa mbele yangu inasema; justification for cashew value addition in Tanzania. Hii karatasi nitaileta kwako lakini ina mambo mengi sana humu ndani ikiwa ni pamoja na kuonesha faida mbalimbali zinazoweza kupatikana baada ya kuwa na kiwanda cha korosho; kwa sababu unapozalisha korosho zile cashewnut kernels, zile korosho za ndani ni asilimia 25 ndiyo ambayo inatumika na inasafirishwa kwenda nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kule inakokwenda wanapata maganda ya korosho ambayo ni asilimia 50 – 60 na saa zingine inafikia 70 – 80 ya maganda ya korosho. Sasa faida za maganda ya korosho. Sasa, faida ya kwanza kabisa maganda yanaweza yakatumika kutengeneza break lining kwa ajili ya magari. Maganda ya korosho yanaweza yakatumika kutengeneza vilainishi vinavyotumika kwenye nchi zenye joto kali, maganda ya korosho yanaweza yakatumika kutengeneza vipodozi (cosmetics). Nadhani ukiangalia watu wa Mtwara wengi utaona wamejichora alama fulani za korosho, maana yake kwamba inaweza kubadilisha ngozi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tukiangalia maganda haya haya ya korosho (sina hakika sana) lakini ilikuwa inasadikika Mheshimiwa Rais alifanya research yake kwa kutumia maganda ya korosho akisema kwamba maganda ya korosho ni dawa nzuri sana ya kuua vidudu kuliko hizi dawa mnazoziingiza kutoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia maganda ya korosho yanaweza kutengeneza ceiling board. Sasa niombe Wizara wafufue viwanda vilivyoko Mtwara; hii sehemu waliyoitaja ndiyo inayoingiza pesa nyingi kwenye korosho kuliko hizi korosho chache wanazozitegemea ambazo ni asilimia 20 – 25. Kwa hiyo, waone namna watakavyofanya kuhakikisha viwanda vile vya korosho Mtwara vinafufuliwa kwa ajili ya kuongezea pesa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa taarifa yako tu mwaka huu Tanzania au korosho ya Tanzania ndiyo limekuwa zao la kwanza lililoingizia mapato makubwa Taifa hili. Sasa tuone hicho tunachokipata ni asilimia 25 tu ya hali halisi. Tulete viwanda, tuwatafute wawekezaji waje kuwekeza ili waweze kuzalisha tupate hivi vitu vingine. Hizo break lining zinazotoka India, China nyingine zinatengenezwa kwa kutumia maganda ya korosho.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Tanzania miaka ya 60 na 70 tulikuwa na viwanda vya kutosha tu maeneo ya Mtwara, Lindi, Ruvuma pamoja na Pwani, bahati mbaya vile viwanda viliuzwa na watu wanavifanya maghala. Sasa tunaamua kuondoa korosho zetu tunaziuza tunapeleka nchi za nje. Kule wenzetu wanakwenda kutengeneza hivi vitu ambavyo wanarudisha kwetu kuviuza. Faida ya korosho si kwenye ubanguaji ni mazao yanayotokana na ile korosho baadaye. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwongezee Mheshimiwa Waziri kitu kingine ambacho Watanzania wengi hawakifahamu na Mheshimiwa Waziri naomba achukue hili very serious. Kuna pombe inazalishwa kutokana na mazao ya korosho (bibo), ile pombe jina lake halisi inaitwa nipa. Watanzania walio wengi wanatumia hii pombe, inafahamika kwa majina mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye Sheria hii inaitwa Intoxication Liquors Act 1968, ilitambua pombe mbalimbali za kienyeji katika maeneo yao. Sasa sisi kule kwetu tunatengneneza pombe inaitwa nipa kama nilivyoeleza, lakini inatambulika kama pombe ya Moshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tafsiri yake inasema hivi – Moshi means the distilled liquor commonly known as Moshi, Kitaifa, lakini pia watu wa Mtwara pamoja na Lindi tunaita nipa or piwa – watu wa Moshi. Sasa nimwombe; hii haijawahi kuharamishwa hata siku moja na hakuna Sheria yoyote iliyobadilishwa na kuharamisha hii pombe ya nipa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naongea hivyo kwa sababu kuna faida kubwa inayopatikana kwenye mabibo. Kwa mfano tu mwaka huu mabibo zaidi ya tani milioni moja na laki tatu yamezalishwa, lakini yametumika kiasi kidogo sana, watu wanakula wanatupa. Sasa tukiamua kuchukua hatua tukaenda mbele, tunaweza kupata wine, tunaweza kupata pale ndani hizo whisky na vitu vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, si hivyo tu, hii nipa ikiwa distilled, kwa sababu jukumu la Mheshimiwa Waziri kadri ya Sheria iliyoko hapa mbele ni wewe unatakiwa kutoa leseni kwa wapika nipa, si wapika gongo, wanaopika nipa inayotokana na mazao ya shambani; kama ambavyo iko kwa watu wanaopika nipa hiyo hiyo jina lingine tuseme Moshi wanaita piwa wanawauzia kiwanda cha K-Vant wanatoa pale ndani spirit. Ile spirit inatumika hospitalini kwa shughuli mbalimbali. Kwa hiyo inakuwa distilled vizuri, inakwenda kutumika vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kule kwetu tunatambua, watu wengi wanafahamu, sisi tunauza ile nipa kwa chupa moja ya fanta Sh.500, ile chupa ya bia Sh.1,000. Wakiamua sasa kuigeuza ikawa zao la biashara wananchi wakapewa leseni, wataipika vizuri si mafichoni kule ambako inatoka ikiwa chafu kwa sababu hawatumii vifaa vizuri. Itakapokuja hapa mbele itapata bei nzuri, hawatakunywa wale watu, hawataweza kununua, lakini itakwenda kutumika kuongeza na kukuza kipato cha wakulima. Pia wakati huo huo itasaidia kwenye hospitali zetu, sisi tunafanya importation ya spirit kutoka maeneo mbalimbali, spirit hii inapatikana kwenye nipa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria hizi hapa. Mara ya kwanza kabisa lilijadiliwa jambo hilo la ilisainiwa hii hapa na marehemu Mheshimiwa Mzee Kawawa. Mara ya pili imejadiliwa tena hii Imesaini na wakati huo Katibu wa hili Bunge ambaye alikuwa Mzee Msekwa. Baadaye Mheshimiwa hayati Nyerere Baba wa Taifa naye alisaini, hawakuharamisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, ilipoanza kuharamishwa hii ni pale ambapo mlianza kuiita, kuna jina waliita wataalam, unajua wanasema ukitaka kumpiga mbwa, mpe jina baya. Wakaanza kuita inaitwa illegal illicit alcohol, hii sasa ndiyo gongo. Hata hivyo, sisi kwetu hatutengenezi gongo, tunatengeneza nipa pure, inatokana na mazao ya shambani. Tuwaruhusu wale watu wajiongezee kipato, kwa sababu ni kweli inafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mwijage akija kule nyumbani hata mimi nitamtafutia kichupa kidogo cha nipa aonje ladha yake ambayo inafanana na whisky, hizi tunazo import kutoka nchi mbalimbali, tunazileta Tanzania tunazitoza kodi wakati tunapoteza mapato kule kwa wakulima, lakini pia pamoja na kuwaongezea kipato wakulima wetu. Kwa hiyo, kuna hii research nimeweka hapa kwako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hilo hilo bibo ni zuri zaidi kuliko ilivyokuwa pamoja na hizi citrus fruits, ina vitamin c mara tano zaidi. Sasa kwa nini tusiache wale wananchi wakajipatia kipato kutokana na hivi vitu? Sheria iko wazi, ikiwezekana Mheshimiwa akija hapa awaombe radhi Watanzania waliofungwa kwa kutumia mazao yao ya shambani kutengeneza pombe ambayo inaitwa haramu wakati pombe hiyo haijawahi kuharamishwa, ni sehemu ya kuongezea kipato wakulima. Kwa hiyo, naona unamwonesha Mheshimiwa Mwigulu hapo awataarifu polisi wake, lakini na Mheshimiwa Waziri wa Viwanda ana jukumu la kutoa leseni kwa watengenezaji wadogo wadogo ili waweze kufanya vizuri, wakauzie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utafiti umekamilika Chuo cha Kilimo Naliendele, wanasubiri tu sasa kununua hivi vitu kutoka kwa wakulima wa korosho. Bei ya korosho inaweza ikashuka muda wowote na faida ya korosho inapatikana kwenye mazao mbadala. Mwaka huu tumefanikiwa kuuza mpaka Sh.4,000 lakini niseme tukiamua sasa kuwaachia wakulima wakawa huru wakafanya jambo hili kwa Mheshimiwa Waziri kuwapa leseni, kilo moja ya korosho na mazao yake wanaweza kupata mpaka Sh.6,000 au 7,000 na haitashuka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nia yangu hasa ni kuonesha economic importance of cashewnuts na chain nzima ya korosho. Naomba Mheshimiwa Waziri alichukulie hili very serious na nitakwenda ofisini tuweze kulijadili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naunga hoja ya Upinzani.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hotuba iliyoko mbele yetu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji. Nianze moja kwa moja kwa kumshauri Mheshimiwa Waziri kwamba aliyetufikisha hapa ni yeye mwenyewe Waziri kwa sababu mara nyingi anapoongea na kutaka kuli-address Bunge au hata ku- address Taifa amekuwa akitumia neno moja anasema mimi ni mzee wa sound. Hili jambo linamharibia yeye, lakini pia linatuharibia na sisi kama nchi. Hata hivyo wanaotakiwa kumsaidia nao wanapata akili ile ile kwamba tunatakiwa tupige sound ili tuweze kufika mahali fulani, sasa athari zake ndiyo hizo ambazo tunaziona leo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa tu mifano michache, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara lakini pia ni Waziri Kivuli kutoka kwenye Serikali yetu ambayo tunategemea Mungu akitujaalia tutakuja kuiongoza hii nchi, nitakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara na sitegemei kama nitafanya kama ambavyo kaka yangu Mheshimiwa Waziri hapa anafanya kwa sababu kwa vyovyote vile tunataka kulisogeza hili Taifa letu mbele. Ndiyo maana juzi wakati ninatoa mchango wangu nilijaribu kuwakumbusha ndugu zangu Wabunge kwamba lazima tuangalie kwanza uzalendo na kulitetea Taifa letu ili tuweze kujua tunakwenda wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Chama cha Mapinduzi ndiyo ambayo sasa hivi kaulimbiu yake ni masuala ya viwanda kwamba tutakapofika mwaka 2020/2025, basi nchi yetu iwe ya viwanda. Lakini nimwambie tu Mheshimiwa Waziri kwamba ameanza vibaya jukumu hili. Tukiwa kwenye Kamati tuliletewa taarifa kwamba mpaka sasa Tanzania kuna viwanda 53,050 viwanda hivyo ambavyo Tanzania tunavyo mpaka sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Jimboni kwangu sina kiwanda kile ambacho kipo wananchi wanakifahamu kwamba hiki ni kiwanda na ile tafsiri ya viwanda iliyozoeleka kwenye mitaa yetu, lakini tumeona wamezidi kuwapa jukumu pia sasa hivi kutoka TAMISEMI wamekwenda kuwapa majukumu Wakuu wa Mikoa na wengine kwamba kila Mkoa lazima wamhakikishe wamepata viwanda 100. Wanachokifanya sasa hivi ni kwamba Mkuu wa Mkoa anaamua, anatafuta watu 25 wenye uwezo wa kuwa na cherehani nne, nne halafu analeta taaifa kwamba tumefanikiwa kupata viwanda 100. Sasa hii hatuwezi kwenda vizuri. Tunachojaribu sisi kuangalia ni vile viwanda vya kimkakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuomba ile taarifa kwamba nchi yetu ina viwanda 53,000 na mimi nilitamani nivijue ili kama inawezekana basi niweze kufahamu Jimboni kwangu kuna viwanda vingapi, lakini bahati mbaya kabisa na Mheshimiwa Naibu Waziri nilimkumbusha kwenye kikao chetu cha mwisho cha Kamati mpaka tunaingia hapa hiyo taarifa sijaipata, sijui kama wajumbe wenzangu, Mwenyekiti au Makatibu wa Kamati kama walipata hiyo taarifa inayoonesha Tanzania tuna viwanda 53,000 kwa sababu nilitaka tuvifahamu kwa majina ili tuweze kuwasaidia ndugu zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba tena sasa kiti chako watuambie hizo taarifa, walisema ni document kubwa sana tukaomba basi tupate in software ili iweze kutusaidia kuvitambua hivyo viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wanapoongelea habari ya viwanda, ukienda kwenye kitabu chao cha hotuba, ukienda ukurasa wa 13 kwenye taarifa ya Mheshimiwa hapa waziri anasema miradi mipya ya viwanda, sasa sehemu ambayo sijaielewa na nitaisoma kidogo kama alivyoelezea

yeye; kuanzia Julai, 2017 mpaka Machi, 2018 jumla ya miradi 243 yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 4,169.11 inatarajiwa kuajiri watu 49 ilikuwa imesajiliwa, wanaiongeza hiyo wanasema kwenye miradi mipya ya viwanda. Mimi nilitegemea kama Bunge au kama sisi Watanzania tulikuwa tuna interest ya kusikia bada ya kusajili nini kimefanyika, usajili tu peke yake haitusaidii, kwa hiyo, tumeleta hapa habari ndefu sana lakini kimsingi tunataka tusikie mwishoni nini kimefanyika baada ya usajili huu. Hii ndiyo maana tunasema tunakwenda mbele na tunarudi nyuma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kuangalia pia kwenye kitabu chao hiki hiki, tunajaribu kuongelea hapa wanasema viwanda mama na miradi ya kielelezo. Tumeona hapa wabunge wengi sana wanaongea habari ya Mchuchuma karibia asilimia 50 ya Wabunge walioongea kuchangia kwenye hii Wizara wanaongea habari ya Mchuchuma. Huko Mchuchuma tunakoongea sasa hivi pesa ya Mchuchuma na Liganga pesa iliyotengwa ni karibia shilingi bilioni 10 ambayo inakwenda kufanya nini kimsingi bado haijasemwa moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania hii ni nchi ambayo kwa vyovyote ili tuweze kwenda sawa sawa lazima tuangalie wenzetu walivyopita waliopita walikuwa wanafanya nini kama ambavyo Mheshimiwa Mariam Ditopile pale alijaribu kushauri kwa sababu hizi regime lazima zipokee kijiti kutoka kwenye regime iliyopita. Tumeona sasa hivi kulikuwa kuna utaratibu wa Mtwara corridor, Serikali ya Awamu hii ya Tano imesahau kabisa habari ya Mtwara corridor na hii inajithibitisha wazi wazi tunapokwenda kuongea habari ya Mchuchuma, tunakuja hapa tunaita Mradi wa Mchuchuma na Liganga ambao ni mradi mama na mradi kielelezo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka kwenda kuchimba chuma, nchi za Ulaya pamoja na china walipofanya mapinduzi ya kiviwanda wao walitegemea sana chuma. Chuma ndio kiwanda mama ili uweze kujenga kitu kingine chochote unahitaji kupata chuma. Unaambiwa pale
Mchuchuma na Liganga tukiamua ile kuchuma chuma yetu tuna uwezo wa kujitosheleza chuma kama sisi wenyewe kama nchi, lakini pia tuna uwezo wa kuichukua hii chuma tukaipeleka nchi za nje kwenda kuuza tukajiingilia sisi forex matokeo yake sasa hivi pesa nyingi za kigeni Serikali hii imeamua kuzitumia kwenda kununa chuma nje kwa ajili ya kuja kufanya miradi mikubwa hapa kwetu badala ya kuwekeza kwetu baada ya miaka mitano au 10 mbele tukahakikisha na sisi tunapata chuma hapahapa nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kuisikitisha kabisa ni kwamba ili chuma iweze kufika bandarini na tunategemea bandari itakayosafirisha chuma ni Bandari ya Mtwara hakuna mpango mkakati mzuri unaoonesha namna ya kusafirisha chuma hii. Bado tunataka turudi miaka ya 40 kwa kusafirisha chuma kutoka Mchuchuma na Liganga kuleta kuileta Bandari ya Mtwara kwa kutumia barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara za Mtwara, Songea tumezipata kwa shida kubwa sana, leo hii tunataka kurudi kulekule badala ya kufikiria kujenga Reli, ambao mkakati wake hauonekani. Sasa hivi karibia mwaka wa 20 kule kuna watu walioekewa X kuonyesha kwamba kunatakiwa kupita reli inayotoka Linganga na Mchuchuma hiyo Reli inakwenda mpaka bandarini Mtwara imepita Jimbo la Mtama, imepita baadhi ya maeneo la Jimbo Ndanda, imepita Songea, Tunduru na kuelekea kote mpaka kufika Liganga na huko Mchuchuma lakini Serikali haijaonesha kwa namna yoyote jinsi gani inataka kufanya kazi kwenye hii Reli ya Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hii Reli ya Kusini kihistoria ilikuwepo toka mwaka 1949 lakini mara tu baada ya uhuru Reli ya Kusini iling’olewa. Tulitegemea leo tunakwenda kuendeleza ile Reli ya Kusini ili iweze wale wananchi pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye kitabu cha Kamati hapa, matatizo yaliyopo kwenye hii na ninaomba Mheshimiwa Waziri akasome ili kuboresha kwenye majibu yake atakapokuja hapa. Wenyewe wanasema kwenye ukurasa wa sita na Kamati inaishauri Wizara. Inasema hivi, upatikanaji wa fedha kutoka Hazina kwa kiwango kikubwa unaonyesha kuwa Serikali inapanga matumizi makubwa yasioakisi uhalisia wa vyanzo vya mapato, hali hii imeathiri kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu ni ushauri wa Kamati, na Mheshimiwa Mwijage naomba hii uingalie sana, ndugu zetu wa Wizara ya Fedha hawana nia njema na wewe. Hawana nia njema na Naibu wako Waziri kwa sababu ndio wanaokwamisha. Haiwezekani bajeti iliyopitishwa kwenye pesa za maendeleo wawape nyinyi asilimia tisa tu, na wakati mwaka uliopita 2015/16 waliwapa asilimia tano na bado tunasema nchi yetu tunataka kuisogeza kwenda kuwa nchi ya viwanda. Nchi ya viwanda inapewa pesa za maendeleo, Wizara inayosimamia masuala haya asilimia tisa Wizara inayosimamia maswala haya asilimia tano. Kwa hiyo, katika hii miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Tano pesa pekee ambayo imepata kwa ajili ya maendeleoe kwenye Wizara yako ni asilimia 14 pekee. Ni kweli tuna nia ya kutekeleza hiyo Ahadi ya viwanda kwa wananchi? Na lazima watu tuwaambie ukweli kwa sababu tusipofanya hivyo hatutaweza kufika kokote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati imeendelea kwenda mbele, kwenye changamoto zilizopo wanasema hivi kumekuwa na ucheleweshwaji wa fedha za maendeleo, jambo linalokwamisha utekelezaji wa miradi hiyo kwa wakati na hatimaye kupanda kwa gharama hizo mwaka hadi mwaka. Hayo ndio matataizo na umeangalia hapa Wizara zote wamejaribu kuongelea suala hilo hilo. Ukienda Wizara ya Maji kuna matatizo ya ucheleweshwaji wa pesa, ukienda Wizara ya Nishati na Madini yaani ni kote kuna matatizo ya ucheleweshwaji wa pesa unaofanywa labda kwa makusudi kabisa na Waziri kwa maana ya kutokutaka kuwasaidia wenzie ili ikiwezekana yeye ndio aonekane anafanya vizuri kuliko Mawaziri wote, jambo hili msipolikemea haraka katika vikao vyenu vya Baraza la Mawaziri niwaambie Hazina Wizara ya Fedha inawaangusha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninavyofahamu kwa uelewa wangu mdogo tuu wa masuala ya mahesabu mimi ni mtaalam wa hesabu pia, kwamba mara baada ya kupitisha bajeti kinachofata kunakuwa kuna cash flow hazina wanatakiwa watoe pesa kutokana kwenye cash flow kwenye matukio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 10 wanatakiwa wawe wamepata shilingi milioni mbili kwa ajili ya kugharamia shughuri fulani. Lakini sasa hivi kuna utaratibu mpya hata sijui hata unapotokea. Bunge likishapitisha hapa kuna watu wengine nawasikia hapa kwenye taarifa wanasema kutoka juu ya Mheshimiwa Waziri mwenyewe hapa kuna sehemu ameandika wakati anajadili hilo suala la Liganga na Mchuchuma yaani ni robo tu ya ukurasa kwenye kitabu chake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mwishoni kabisa anamalizia kwamba huu Mradi wa Liganga na Mchuchuma unakwenda vizuri anasema; taarifa ya awali ambayo inatakiwa kutolewa maamuzi na mamlaka husika. Sasa mamlaka anayopewa Waziri na Bunge hili halafu naye anatafuta mamlaka nyengine husika kwa nini hiyo sasa isije hapa ikajibu maswali ya Wabunge kwamba Mchuchuma na Liganga itaanza kufanya lini shughuli zake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nikuombe jambo moja, mama yetu Mheshimiwa Lulida hapa ameongea kuhusu viwanda vya korosho kule Mtwara ambavyo sisi tumeshakata tamaa moja kwa moja wa sababu hatuoni juhudi yoyote ile ikifanywa ili kuweza kufanya, kwa hiyo tunakuomba sana ujitahidi ili vile viwanda ziweze kuanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine jaribu kufungamaana na Wizara ya Kilimo, kwa sababu ili uweze kufanya kazi vizuri lazima ushirikiane na Wizara.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji. Kwanza nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi bilioni sita point nane kwa ajili ya Miradi ya Maji iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Niseme wazi kwamba kwa kipindi kirefu fedha zilikuwa zikitengwa kwa ajili ya kuongeza na kupanua miundombinu katika shirika letu linalogawa maji kule kwetu ambao ni MANAWASA.
lakini kwa bahati mbaya sana hazikufika. Mwaka huu tena tunaona wametengewa pale shilingi bilioni moja, sasa tunaomba hizi fedha zifike ili waweze kupeleka maji katika Vijiji vya Mpohora, Nangoo, Mbemba, Mbaju, Chigugu, Chikundi, Liloya na Makongwa pamoja na Njenga maeneo ambayo yanapitiwa na bomba kubwa kabisa la maji yanayotokea Mto Mbwinji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wa Ndanda tuna neema kubwa sana ya maji na maji mengine sisi tunayauza, maana yake kwamba yanatutosha. Tatizo kubwa tulilonalo ni miundombinu katika maeneo yetu, tukiweza kusaidiwa fedha za kuweza kuweka miundombinu maji haya tutahakisha yanafika katika Vijiji vya Lilala, kwa sababu kuna mradi unaoishia pale unaoelekea Vijiji vya Chiwale. Lakini tuna maji mengi sana maeneo ya Namajani ambayo yanatumiwa na askari magereza pale, tatizo tu pale ni kupata umeme ili transfoma ishushwe pale waweze kupampu maji yale yatumike maeneo ya Kata ya Namajani, yanaweza kufika pia Kata ya Mlingula pamoja na Chilolo kwa sababu eneo hili pia kuna wakazi wengi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipata msaada wa JICA kwa ajili ya utengenezaji wa kisima katika Kijiji cha Nambaya, lakini kwa bahati mbaya sana kisima kile hakijamaliziwa na wananchi wanahitaji yale maji. Tunaomba waangalie ni jinsi gani wanaweza kutusaidia kumalizia kile kisima ili wananchi waweze kupata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tuseme tunatamani sana kuona watu wa MANAWASA wanapewa fedha ya kutosha kwa sababu sasa hivi pamoja na kudai fedha nyingi katika Idara mbalimbali za Serikali, lakini wamekuwa hawana fedha za kutosha kwa ajili ya kuweza kujipanua kufikia maeneo mengi sana waweze kuendesha miradi yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaamini wakiwawezesha MANAWASA kutakuwa hamna shida ya maji katika maeneo yetu na tutaacha kufanya kampeni kwa kutumia shida za wananchi hasa zaidi maji kwa sababu watu hawa wote wana uwezo wa kupata maji katika maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimwombe Mheshimiwa Waziri, atakapokuja kuhitimisha hapa atatuambia ni jinsi gani anataka kuwapa nguvu MANAWASA pamoja na Mheshimiwa Meneja yule ili sasa aache kuaibika kwa sababu anashindwa kupeleka maji katika vijiji vilivyopo karibu sana na eneo lake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, hasa zaidi ukiangalia Kijiji cha Chikunja na Kijiji cha Lukuledi ambako hivi karibuni tulikuwa na mradi wetu wa maji lakini ulikuwa unaendeshwa kifisadi, tuliurudisha mikononi mwa wananchi tunaomba pia nao mtusaidie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, japokuwa wale watu wanafikiri kuna fidia watakuja kupata, lakini hata hivyo kwa sababu hawakusoma ripoti ya mapato na matumizi hakuna fidia yoyote tunawaambia watakayoweza kupata pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipata msaada sisi kutoka TASAF, lakini kumefanyika ubadhirifu wa fedha shilingi milioni 378. Waliofanya ubadhirifu huu tunawafahamu, tumejaribu kufuatilia hili jambo polisi kwa muda mrefu sana limekuwa likisumbua lakini tusingepata shida ya maji katika baadhi ya vijiji kwa sababu tayari kulikuwa kumeshatengwa fedha ya kuchimbwa mabwawa katika Vijiji vya Masonga, Mraushi na vijiji vingine vinavyozunguka ambavyo vingeweza kuhudumia Kata tano katika maeneo yale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaomba Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya TAMISEMI japokuwa Waziri nimempa taarifa kuhusu jambo hili amesema analishughulikia kwa ukaribu sana. Hivyo, tunataka atakapokuja hapa kuhitimisha, basi atuambie wazi jinsi gani anaweza akasaidia watu wa Wilaya ya Masasi kuweza kupata maji kiurahisi kwa sababu maji ni mengi, tatizo kubwa tulilonalo ni miundombinu ili iweze kuwafikia watu mbalimbali katika maeneo yale. Vile vile na kuwaongezea nguvu MANAWASA ili waweze kugawanya maji haya kwa uhakika zaidi katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukifanya hivi tutakuwa tumemaliza tatizo la maji katika maeneo yetu kwa sababu maji tunayo ya kutosha, shida kubwa tuliyonayo sisi ni miundombinu, kiasi watu wale wanaopitiwa na bomba kubwa la Mto Mbwinju wanashindwa kupata maji ya kutosha na maji yale ni safi na salama yanayokwenda Nachingwea. Kwa hiyo tunaomba atakapokuja …
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia hoja iliyoko mezani leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna changamoto nyingi sana kwenye Wizara ya Afya na kila mara imekuwa ikipangiwa bajeti ndogo sana kulinganisha na mahitaji. Sasa hivi kumekuwa na mkanganyiko mkubwa sana kati ya Wizara ya Afya na TAMISEMI. Kwa nini Serikali iliamua kuchanganya kazi za Wizara hizi mbili? Kwa mfano, inapofikia suala la majengo ni jukumu la TAMISEMI, halafu watumishi ni wa Wizara ya Afya. Ningependekeza masuala haya yote ya ajira na majengo yangetakiwa kuwa chini ya Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine linahusu Jimbo moja kwa moja; wakati wa ziara ya Waziri Mkuu aliahidi kuleta gari la wagonjwa kwenye Zahanati ya Chiwale, napenda kufahamu ahadi kama imekufikia na utekelezaji wake utafanyika lini ukizingatia kwamba Jimbo la Ndanda lina kituo cha afya kimoja tu, kati ya Kata 16, hili lifanyike kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni juu ya majengo; pamekuwa na sintofahamu kubwa sana juu ya aina ya majengo yanatotakiwa. Wananchi wanahitaji majengo ya kuweza kupatiwa huduma, lakini Serikali imetengeneza ramani ambazo kwa hali ya wananchi wetu ambao tumewataka weweze kukamilisha majengo haya mpaka hatua ya lenta ndipo Serikali itayapokea, lakini suala hili limekuwa gumu sana kutekelezwa kwa sababu ya uwezo mdogo wa wananchi pamoja na kukatishwa tamaa na hali ya kutokukamilishwa kwa majengo ambayo wananchi tayari wameshakamilisha majengo hayo. Pamoja na kuangalia miaka ya mbele, basi Serikali sasa ikubali angalau kukamilisha majengo ya zamani (maboma).
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2017 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nianze na kuwakumbusha Watanzania wote Waislam kwa Wakristo tusome Luka 8:18. Luka 8:18 inaelezea juu ya mambo ya mali, aliyenacho ataongezewa na yule asiyekuwa nacho hata kile kidogo ambacho anahisi anacho na chenyewe atanyang’anywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maana sana kusema maneno haya ya utangulizi wa kwenye Biblia kwa sababu ni wazi kabisa sasa hivi Serikali ya Chama cha Mapinduzi ambayo ndiyo inaongoza nchi hii imeamua kusimama kwenye huu mstari Luka 8:18 na nina mifano ya kuhalalisha kwa nini nimeamua kusema hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia bajeti ya Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mpango kule ndani hakuna sehemu ambako amekwenda kuonesha kwamba watumishi wote wa kada zote watakwenda kuongezewa mishahara yao. Pamoja na kukamilisha masuala ya uhakiki na walisema kwamba baada ya uhakiki mara moja watakwenda kuboresha mishahara. Juzi hapa Mheshimiwa Waziri Mkuu amesimama anasema suala la nyongeza ya mishahara itabaki kuwa siri, itafanywa kimya kimya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tujiulize bei za mazao na bidhaa nyingine zinapanda, tumeona kabisa kwamba hata kwenye shule ada zinapanda, lakini watumishi wao hawaongezewi mishahara wakiwemo na watumishi wa Bunge wanaotusaidia hapa ndani mishahara yao haipandishwi sasa hivi kwa mwaka wa pili au wa tatu kwa kisingizo cha uhakiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya kabisa wale wachache ambao walikuwa wanatakiwa kupandishiwa mishahara yao walipewa barua za kupandishiwa madaraja wakiwemo Polisi na Wanajeshi. Ukienda Jeshi la Zima Moto ni kilio, wamenyanga’anywa ile mikataba yao ya mwanzo, wiki mbili tatu zilizopita wakati tunakuja kwenye Bunge la Bajeti wamepewa barua nyingine wanaambiwa vile vyeo vyao vya awali vimesahaulika wanaanza kuhesabiwa toka juzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Rais anashangaa, anamwambia hapa Mama Jenista Mhagama kwamba eti anahisi anaajiri vilaza ndiyo maana watu hawafanyi kazi vizuri huko mtaani, hapana na sidhani kama alimjibu. Nataka leo nimwelekeze amwambie Rais hawa watu wamekuwa demotivated kwa sababu hawapati stahiki na mishahara yao, hawafanyi kazi kwa moyo kama ambavyo ikuwa zamani, hili ndiyo tatizo pekee lililopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Mheshimiwa mama Jenista kama inawezekana awasiliane na Rais amweleze kwamba hawa watu wamekuwa demotivated wanataka wapandishwe vyeo na mishahara ili waweze kufanya vizuri. Kuna watumishi wa umma wengi wamebaki kwenye vilio sasa, Walimu na wengi waliobakia wanasikiliza Bunge ili tuweze kuwasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu yetu ya awali kama Wabunge yalikuwa ni kuisimamia, kuielekeza na kuishauri Serikali, lakini hapa tumeona sasa hivi mtindo huku ndani na hasa zaidi ndugu zetu wa Chama cha Mapinduzi wanavunja sana Kanuni ya 154. Hii kanuni ya 154 inaruhusu kabisa kutoa pongezi za aina yoyote, anayetakiwa kufanya jambo hili kwa niaba ya wote Wabunge ni Mheshimiwa anayekuwepo kwenye Kiti siku hiyo pale. Sasa imekuwa kama utamaduni ili uweze kuonekana utaanza kumsifia Waziri Mheshimiwa Dkt. Mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zamani wakati sijawa Mbunge nilifikiri hili jambo linakwendaje; unanisifia wee halafu mwishoni unaanza kumwambia lakini hata hivyo rekebisha hii. Twendeni kwenye point tuisimamie na tuishauri Serikali na ndiyo liwe lengo letu wote. Wote tunatamani kupongeza lakini wasiopongeza wanaonekana wabaya kwa sababu wengine wanapongeza na ndiyo tumefikia hapo, hii ni double standard. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa pia niongee leo ni masuala machache kwa ajili tu ya kuishauri kama ambavyo nimeanza toka mwanzo. Nimenukuu hapa Luka 8:18 na ndiko walikosimama Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Twende kwenye gesi Mtwara, mpaka sasa hivi gesi ya Mtwara inatumika kwa asilimia saba tu, wale Wawekezaji wa Maurel and Prom wamekuja kulalamika kwamba wao wanashindwa hata kurudisha mtaji wao kwa sababu gesi ile haitumiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha ajabu Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeruka imeachana na gesi ambayo ingekwenda kuwanufaisha watu wa Mtwara, wamekimbilia kufanya mradi wa Stiegler’s Gorge ambao thamani yake halisi mpaka utakapokuja kukamilika haifahamiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuna nia ya kupinga huu mradi lakini kwa nini tusikamilishe miradi iliyopo mwanzoni ya kimaendeleo inayoweza kusaidia ili mambo mengine yafanyike. Hiyo pesa inayokwenda Stiegler’s Gorge ingekwenda kutumika kusaidia kwenye miradi ya maji, kujenga zahanati na kufanya shughuli zingine tukaokoa maisha ya watu wetu tukaongeza life span. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la reli (Standard Gauge). Reli ya Tanzania kulikuwa kuna reli inaitwa Reli ya Kusini ilikuwa inaanzia Mtwara inapita Newala, inakwenda Masasi inanyooka kwenda kule chini. Hii reli ingekuwepo mpaka sasa hivi ingetusaidia kudumisha au

kupata chuma cha kujenga hiyo reli ya standard gauge hapo katikati, kwa sababu Mchuchuma na Liganga uwekezaji wake sasa hivi ungekuwa umeshakwenda mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeachana na hiyo, tunatumia forex nyingi kununua chuma kwa ajili ya kutengeneza reli na tunasema hapo tuna miradi mingine ya kimkakati, huko Stiegler’s Gorge tunakoongelea inatakiwa na kwenyewe ipelekwe chuma, kwa nini Serikali isifikirie kutengeneza Mchuchuma kwanza kwa hizo pesa zote tena kwa haraka tupate chuma yetu wenyewe, nyingine tuiuze nje na nyingine tutumie kwenye miradi yetu ya kipaumbele. Matokeo yake wao wanaamua kuingiza tu (import) ndiyo maana shilingi inashuka kila siku, hii ni biashara ya kawaida kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine hapa ambalo kwa kweli hili kwetu ndiyo lenyewe. Hapa nina makaratasi mengi tu na Mheshimiwa Omary Mgumba nimwombe kabisa atuombe radhi watu wa Mtwara kwa sababu Mgumba kilichomleta Mtwara ilikuwa ni biashara ya korosho, walikuwa wanafanya kazi na kampuni moja inaitwa Olam Tanzania Limited, hawa ndiyo walikuwa watu wanaowafanya watu wa Mtwara waendelee kubaki vile wanavyobaki kwenye korosho kwa sababu walikuwa wanajua wananufaika na nini. Ndiyo maana anakuja kutetea, anawatetea ambao walikuwa waajiri wake na hao ndiyo waliotufikisha hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia ya export levy ipo hapa ndani, karatasi hizi ninazo na hizi karatasi nitaku…

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini muda wangu umeutunza. Nataka tu nikwambie wakati tukiwa Wabunge wageni kabisa mwaka juzi, Mheshimiwa alinikutanisha na Meneja Mkuu wa Olam duniani, sijui alimtoa wapi tukakutana hapo nje, sasa ndiyo anaoendelea kuwatetea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia ya export levy ninayo hapa na nitampa pale Waziri, nataka nisome tu mistari michache nikueleze. Wanasema hivi changamoto hii ilipata utatuzi kupitia maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa wadau wa korosho uliofanyika tarehe 12 mpaka 14 Aprili, 1994, Mkoani Mtwara katika Wilaya ya Masasi. Mkutano huu pamoja na mambo mengine uliazimia mambo yafuatayo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza kabisa walisema kuweka mikakati ya kuwa na utafiti endelevu wa zao la korosho. Pia kuwa na usimamizi wa uratibu mzuri wa tasnia ya korosho nchini; kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo ikiwemo kuhakikisha upatikanaji wa mbegu bora na kuendeleza ubanguaji wa korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Serikali inakuja hapa pesa zetu sisi tunadai ili tukafanye mambo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ulikuwa Attorney General, kwa hiyo naamini kabisa unafahamu na ndiyo maana ulisema historia hii unaifahamu. Ahsante sana Mheshimiwa Chenge kwa kunisaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kati ya tafiti ambazo zipo, nilimshauri mwaka jana hapa Waziri wa Viwanda kwamba tunaomba tufanye utafiti na jana tumekaa hapa na wadau wanaozalisha pombe na vitu vingine wanalalamika upatikanaji wa alcohol. Nilikwambia mabaki yanayobaki kwenye korosho na ndiyo maazimio yao pale ikiwemo pamoja na zile kitu kwetu tunaita kochoko inapatikana kule ndani nipah, ukiamua kuitengeneza vizuri unapata ethanol, methanol na vitu vingine mle ndani ili kuwaongezea wakulima wale kipato. Huu utafiti ulikuwa unafanyika Naliendele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, athari za kuondoa hiyo export levy ya kwanza kabisa inasema upotevu mkubwa wa idadi ya mikorosho nchini Tanzania. Hapa karibuni tumeona Serikali inawasisitiza mikoa mingine waanze kulima korosho wakimemo Tumbi, Mkuranga Mkoa wa Pwani, Mkoa wa Dodoma Mpwapwa, Tabora, Singida na mikoa mingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka niwaambie Watanzania hawa ambao wanaingizwa huu mkenge, zao la korosho sisi ndiyo limetufanya wakazi wa Mikoa ya Kusini tuwe maskini, lakini tulikuwa tunavumilia, tukagundua kwamba tunahitaji pesa ili tuweze kuliendeleza. Serikali ya

Chama cha Mapinduzi inakwenda kutoa mtaji wetu wa kuendeleza zao hili, sasa wanataka kuingiza mkenge Watanzania wasiohusika na jambo hili. Hili jambo ni la Wamakonde watuachie wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine hili tunalosema, wazee wetu akina Mzee Nandonde wakati huo walikuwa wanaomba Kusini basi tutengwe na Tanzania iliyobaki ambayo tunafikiri maendeleo yao yanakwenda kwa kasi, tuishie kuna sehemu moja hapo panaitwa Kinyonga, Kilwa. Kule tunajitosheleza, tuna gesi na korosho zetu tutajua wenyewe namna ya kujiendesha pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii pesa ya export levy ilikuwa na mgawanyo wake maalum ambao upo kisheria, asilimia 35 inakwenda Serikalini na asilimia 65 ilikuwa na matumizi yake, karatasi hii hapa inayoonesha matumizi mbalimbali ya pesa hiyo asilimia 65, mpaka sasa hivi Serikali wametoa bilioni 10 katika bilioni 211 tunazoidai Serikali hii. Tunataka Mheshimiwa Dkt. Mpango akija pale atueleze hiyo balance inayobakia yote wamepeleka wapi na kufanyia nini wakati wenyewe tunaumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tunakoelekea sasa ni kubaya na ndiyo maana hapa juzi Mheshimiwa Bwege alisema tunakwenda kuandamana na tunakwenda kuandamana kweli. Nitaongoza maandamano Jimbo la Ndanda la kudai haki na stahiki yetu kwa sababu tunadhulumiwa na tunaonewa. Kila kidogo tunachojaribu kukikusanya kwa nguvu zetu Serikali inakwenda inapora, wanaleta sheria hapa wanataka watudhulumu. Basi kwanza walete pesa tuliyonayo, halafu baada ya hapo wao walete huo utaratibu wao wa kutaka kubadilisha hii sheria ili tuone mwisho wake. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii document nitaipa hapo Kamati yako. Kati ya mambo ambayo yatakwenda kufeli huko mbele ni pamoja na taasisi itapoteza wafanyakazi Watafiti waliobobea kwenye utafiti wa zao la korosho.

Tanzania ambako tunazalisha maeneo mengi, kati ya hao watafiti pale Naliendele Chuoni wameajiriwa wafanyakazi 126 kati ya hao wafanyakazi 71 wameajiriwa kwenye programu ya utafiti wa korosho ambapo mishahara yao inatokana na cashewnut levy. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu hapa Mheshimiwa Mgumba anakuja anasimama anataka kutetea wanaomtuma anataka kutuaminisha kwamba… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali Wizara ya Maji na Umwagiliaji 2018/2019
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kutumia muda huu kuchangia kwenye hotuba iliyoko mbele yetu ambayo ni Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nikitaarifu kiti chako kwa sababu Mheshimiwa Nsanzugwanko hapa ametoka kumalizia anasema kwamba kuna uwezekano mkubwa DAWASA na DAWASCO sasa hivi wanakwenda kuunganishwa, hii ni kwa ajili ya wakazi wa Dar es Salaam lakini naomba tu tuwasaidie jambo moja na kiti chako kifahamu kwamba kuna ubadhirifu mkubwa sana umefanyika ndani ya DAWASCO na wanapokwenda sasa hivi kuunganisha DAWASCO na DAWASA madeni haya yote yatarudi kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, zaidi ya shilingi bilioni 800 na kuna madeni makubwa sana pale ndani, kwa hiyo tunaomba tufahamu, kuna madeni ya umeme ambayo ni shilingi bilioni 3.5; kuna madeni ya NSSF pamoja na PSPF karibu shilingi bilioni 12; kuna madeni pale ya TRA na madeni mengine mengi kiasi wale wafanyakazi wa DAWASCO na wafanyakazi wa DAWASA wao hawaelewi wanasimama upande gani kwenye kulikamilisha hili jambo lao. Kwa hiyo, tunamuomba Waziri na ikiwezekana uagize kiti chake kifanye Special Audit kabla ya hizi taasisi mbili hazijaunganishwa kutokana na madeni yaliyoko kule ndani, otherwise tunakwenda kuwasababishia matatizo makubwa sana watumishi wanaobaki na wale wengine watakaohama pale.

Mheshimiwa Spika, kama tulivyosema toka mwanzo Wizara hii ni Wizara nyeti sana inagusa maeneo yote ya Tanzania na kilio kimekuwa kikubwa sana kwa Wabunge wote na wewe mwenyewe pia umeshuhudia kinachotokea hapa. Naomba nitumie nafasi yangu kuwakumbusha pia Wabunge wenzangu majukumu yetu kimsingi.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa niseme tunatakiwa tuwe wazalendo kwa ajili ya Taifa letu. Jambo la pili tuhakikishe tunasimama mguu mmoja na wapiga kura wetu lazima tuone maslahi ya wapiga kura wetu yanasimamiwa na jambo la tatu lazima tuwe na uhakika kwamba tunavitetea na kuvilinda vyama vyetu kwa uchache wake lakini ni jambo la tatu; na mwisho kabisa tuangalie nafsi zetu wenyewe.

Mheshimiwa Spika, Bunge lako na ninavyoona mimi nilivyojifunza kwa hizi siku chache nilizoko hapa ndani kwamba sasa hivi linaanza kuegemea upande mmoja tu, tunaangalia sana maslahi ya chama, tunasahau wapiga kura wetu, tunasahau uzalendo juu ya nchi yetu, lakini pia tunasahau kuhusu nafsi zetu wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumepokea hizi taarifa zote mbili kutoka kwa Kamati, lakini pia tumepokea taarifa ya Waziri mwenyewe kwenye kitabu chake. Vitabu hivi ukiviangalia kwa pamoja vinatofautiana sana kwenye baadhi ya maeneo. Tukianza moja kwa moja kwenye suala la umwagiliaji. Ukienda kwenye kitabu cha Waziri, suala la umwagiliaji ukurasa wa 11 wanasema hivi; “Mheshimiwa Spika, nchi yetu ina eneo la hekta 29.4 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, ambapo hekta 2.3 zina uwezekano mkubwa wa kumwagiliwa, hekta 4.8 uwezekano wa kati na hekta 22.3 zina uwezekano mdogo wa kumwagiliwa.” Anaendelea kusema kwamba; “Serikali ina nia ya kujenga miundombinu yenye jumla ya hekta milioni moja kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo. Hadi mwezi Machi, 2018 jumla ya hekta 475,000 zinamwagiliwa sawa na asilimia 47.44 ya lengo la asilimia 1.6 eneo linalofaa kumwagiliwa”

Mheshimiwa Spika, wasiwasi wangu taarifa hizi zote walizotupatia huku juu zilikuwa irrelevant. Taarifa hapa ya muhimu walikuwa watuonyeshe namna hii heka milioni moja ambavyo wao wanakwenda kuitumia, matokeo yake wanatuletea taarifa zenye kuvutia, zinazoongea habari za heka milioni 29.4 mwisho kabisa wanakwenda kumalizia kwa kuongelea tu hekta milioni moja ambazo nazo hatujafanikiwa wanakwenda kusema tunakwenda kufanya asilimia 47.44.

Mheshimiwa Spika, tunasema tunataka kwenda kuwa nchi ya viwanda. Sasa tujiulize tunakwenda kwenye viwanda vya aina gani, kwa sababu tunapoenda kung’ang’ana bila kuwasaidia wakulima wa nchi hii maeneo mengi yanafaa kabisa kwa kilimo na yapo yanaonekana tunakwenda kuoanisha vipi kati ya viwanda hivi na sekta ya kilimo. Kwa nini tusitumie nguvu nyingi kuwaongezea nguvu wakulima, tukawaongeza asilimia kidogo pale kwenye suala la umwagiliaji tukaenda kuwasaidia badala ya sasa hivi kujikita kwenye viwanda vya uzalishaji mali. Kwa mfano, tunasema tunakwenda kutengeneza nondo na vitu vingine. Tunawasaidiaje wakulima ambao ni asilimia 85 ya wananchi wetu hapa Tanzania ili wao waweze kujikwamua kiuchumi tuweze kusogea mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wameongelea hapa kwenye Fungu Na. 49 kwenye suala la pesa za maendeleo. Ukienda kwenye kitabu cha Kamati wanasema wenyewe hapa kwamba So far…kwenye Kitabu hiki cha Waziri wanasema wamepata pesa walizozipokea mpaka sasa hivi walizokuwa wametengewa ni shilingi bilioni 648 lakini wao mpaka sasa wamepokea shilingi bilioni 347. Kamati inatuambia wamepokea shilingi bilioni 135 sasa tumuelewe nani? Ndiyo maana Wabunge wengine wamependekeza hili sasa suala la kuwakalisha Kamati na Wizara watuambie pesa walizozipata mpaka sasa hivi kiasi gani ili tuweze kuwaeleza Watanzania kwamba Mheshimiwa Waziri wa Maji pamoja na juhudi zake zote anashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu hana ushirikiano mzuri au watu wa Wizara ya Fedha wanataka kumuangusha kwa makusudi. Haiwezekani watengewe bajeti yote hii halafu waende kupata tu pesa kiasi kidogo wakati wenyewe tunasema tuna nia ya kutaka kumtua Mama ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda hata kwenye hiki kitabu chao labda ndiyo maana iko hivi, Mheshimiwa hapa anaonekana Mheshimiwa Makamu wa Rais akimtwisha Mama ndoo kichwani. Kwa hiyo, tafsiri yake ni kwamba Serikali haitaki kuwatua ndoo akina mama halafu tunakuja kuitetea hii Wizara kwamba ipate pesa ya kutosha kwa ajili ya kwenda kuwatua ndoo akina mama na ndiyo maana basi utakuta Wizara ya Fedha haipeleki pesa ya kutosha kuhakikisha miradi ya maji maeneo mbalimbali inakamilika. Kwa hiyo, kwa namna ya pekee kabisa tuwaombe Wizara ya Fedha wahakikishe pesa za maji kila mara zinafika pale kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kuna mradi hapa umetajwa sana wa Stiglers’ Gorge.

Tunaongelea hapa kuhusu mradi wa Stiglers’ Gorge. Huu mradi nia yake ilikuwa ni kuongeza uzalishaji wa umeme ili twende kwenye nchi ya viwanda. Sasa tunasema kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa ni nchi ya viwanda, lakini tukumbuke Bunge hili liliazimia kwamba miradi hii ya kimkakati na ndiyo kisa cha kwenda kuwekeza kwenye miradi ya gesi. Inakuwaje tunakwenda kwenye gesi, gesi inayosemwa inatumika kwa asilimia saba tu, leo tunaacha hii pesa ingekwenda kutumika kuwasaidia akina mama kupata maji tunakwenda kuwekeza Stiglers’ Gorge wakati Mto Rufiji sasa hivi hata yale makingio yake ya maji yameanza kupungua. Mwanzoni Mto Rufiji ulikuwa unapokea maji kutoka mito midogo midogo 29. Sasa hivi Mto Rufiji unapokea maji kutoka kwenye mito mitano tu, kwa hiyo kwa vyovyote huu mto baada ya muda fulani unaweza ukashangaa unakauka.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, naomba nikuambie kwamba kutokana na haya mambo yanayotokea kama hivi unavyoona hii michango na vitu vingine tunashindwa hasa kusimamia uzalendo ule tunaouhitaji wa kuweza kwenda kumtua mama sasa ndoo kichwani. Tumebakisha tu kwenda kusifia tunafikiri hii ndiyo sifa ya msingi ya Ubunge badala ya kuisimamia na kuishauri Serikali. Tumebakisha kupongeza badala ya kwenda kutoa michango yetu ili iweze ku-improve hizi ripoti zilizoko pale.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo yanayohusiana na Taifa kwa ujumla sasa nirudi Jimboni kwangu. Tuna vijiji kule kwetu vingi sana, ukienda Kata ya Mlingura, ukienda Kata ya Namajani, ukienda Kata ya Msikisi pamoja na Malembo, Chingulungulu, Nanganga pamoja na Liputo haya maeneo yote ndiko ambako linapita bomba la Mbwinji linalopeleka maji Wilaya ya Nachingwea, lakini pia linapeleka maji Wilaya ya Ruangwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali hapa mwaka jana ilituambia vijiji vyote ambavyo viko kwenye radius ya kilometa kumi kutoka kwenye bomba kubwa vitapatiwa maji. Mimi nilisema hapa na nikatoa ushauri mnataka tusichimbe visima virefu kwa sababu tunafahamu lile bomba liko mita tano tu toka usawa wa ardhi, tutakwenda sasa kutoboa ili wananchi wapate yale maji kirahisi kama Serikali haitaamua kuyapeleka yale maji vijijini moja kwa moja.

Mheshimiwa Spika, kule kwetu kuna chombo kinaitwa MANAWASA ndiyo kinachotusababishia maji watu wa Masasi pamoja na watu wa Nachingwea. Mara nyingi wamekuwa wakiahidiwa kupata pesa, ukiongea na Mkurugenzi wa MANAWASA anasema chombo kile kikiongezewa nguvu kina uwezo wa kutatua tatizo la maji Kanda ya Kusini kuanzia Nachingwea mpaka Kilwa, wanahitaji tu kupewa pesa kidogo. Lakini kuna sintofahamu inayoendelea, kuna miradi ya mabwawa inaendelea kwenye maeneo haya na mtakumbuka hapa Waziri wa TAMISEMI alituambia kwamba wanataka kwenda kutengeneza Bwawa Lukuledi kwa kutumia pesa shilingi milioni 60 kufanya upembuzi yakinifu. Wakati tayari tulifanikiwa kupeleka maji Kijiji cha Chikunja kwa kutumia shilingi milioni 70, sasa hatuoni faida kubwa sana ya mabwawa haya badala ya kuwekeza kwenda kupata maji safi na salama. Muwashirikishe wenyeji wa maeneo husika ili kuweza kujua miradi ya kipaumbele kwenye maeneo yao, vinginevyo tutakuwa tunatumia nguvu kubwa kwenye eneo lisilohusika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna mradi wa maji unaoanzia Kata ya Mwena, Chikundi, Chigugu, Chikukwe na Vijiji vya Maparagwe pamoja na Mbemba. Mradi huu tunashukuru unaendelea vizuri lakini kuna tatizo moja, mkandarasi analalamika halipwi pesa zake kwa wakati mradi unasuasua.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi na usipate hofu. Bahati mbaya sana kila mara tunapopewa nafasi tunapojaribu kuishauri Serikali kwa sababu wametubandika jina wanaita vyama vya upinzani badala ya kuita vyama rafiki vya vyama tawala, basi kile tunachokisema mara nyingi wao wanafikiri kwamba tunakuja kupinga. Hata hivyo, kila mara tukija humu ndani tuna mawazo mazuri kabisa, tumeona hotuba yetu ya Kambi ilivyosema, bahati mbaya sana wakati wa bajeti hatukupata nafasi ya kutoa hizi hotuba lakini leo tumewaeleza hapo kuhusiana na huu mpango uliko hapo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma hiki kitabu cha mpango wa mwaka mmoja ambao Mheshimiwa Dkt. Mpango ametuletea hapa, sisi kama Wabunge kazi yetu ya kwanza kabisa ni pamoja na kuishauri Serikali. Tumejaribu kushauri mara nyingi lakini Mheshimiwa Dkt. Mpango alikuwa anafikiri kama tunampinga na kubeza, kile tunachokiwaza sisi na mawazo yetu mengi yalikuwa hayachukuliwi ili kuboresha na kulifanya Taifa letu liende pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kwenye hotuba yake kama ambavyo iko mbele yetu kwenye ukurasa wa 34, maeneo mengi yanaonesha ni namna gani mipango mingi iliyokuwa imepangwa itekelezwa mwaka jana haikutekelezeka. Nitatoa tu mfano wa masuala machache. Anasema kutofikiwa kwa lengo la kodi zinazotokana na ajira (Pay As You Earn), anatoa na sababu, kulikosababishwa na kutofikiwa kwa malengo ya ajira mpya na kutoongezeka kwa mishahara. Sasa ni mara ngapi humu ndani tumesimama tunajaribu kuishauri Serikali iongeze mishahara kwa watumishi ili haya mambo yaweze kufuatiliwa pale? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. Mpango kwa kweli kabisa kutoka moyoni na ningetamani sana kabla ya ule mdahalo ambao ulifanyika chuo kikuu usingefanyika kwanza mpaka Mheshimiwa Dkt. Mpango alete huu mpango wake na kulieleza Taifa ni nini kinatokea. Maprofesa walismama pale wakaishia tu kusifu, kutukuza na kupongeza, muda wote ndiyo kazi ambayo waliifanya lakini hawakushauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Mheshimiwa Dkt. Mpango anakuja tena ndani ya Bunge anatueleza mwenyewe ni namna gani mambo huko nje hayaendi. Hili ni jambo la sisi wote kumpongeza badala ya kuishia tu kusifia yale mazuri au kusifia yale mengine tunayofikiri kwamba ni ya kujenga lakini kimsingi Mheshimiwa Dkt. Mpango mwenyewe anakiri kwamba mambo hayaendi, uchumi umeporomoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukieda kwenye point yake namba tatu anasema, kushuka kwa biashara za kimataifa kulikopelekea kutofikia malengo ya uingizwaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi kama ambavyo ilitarajiwa. Anaendelea kusema kwamba, kuendelea kuwepo kwa madai mbalimbali yakiwemo ya wakandarasi, watoa huduma, wazabuni na watumishi wa umma. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ndani kila siku tunakuja na neno uhakiki ili tuweze kuwalipa watumishi wa umma lakini bado wanakiri madai hayo yapo, wakandarasi wa ndani hawalipwi, kwa hiyo, maana yake pesa haizunguki. Hawa wakandarasi wa ndani ndiyo watu ambao wanaendesha uchumi wa nchi yetu, wao ndiyo wanaokwenda kununua kwenye maduka yetu madogomadogo na kufanya uchumi uweze kuzunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini mimi nimwambie kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango, kwamba sisi Chama cha Demokrasia na Maendeleo tumekuja na Sera Mbadala na naomba nikupe hii copy kama zawadi ukaisome na jioni nitakuletea copy nyingine ikiwezekana umfikishie Mheshimiwa Rais naye asome aone mawazo yetu, alinganishe na hayo ya kwenu muweze kuboresha. Haya yote uliyoyasema hapa ndani na kuyaandika hapo mimi nataka tu nikupeleke katika baadhi ya pages kwenye sera yetu halafu wewe utakwenda kusoma zaidi uweze kudadavua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija kwenye Sera ya CHADEMA ukurasa wa 17, hapa tumeweka wazi Mheshimiwa Dkt. Mpango na naomba ukasome vizuri tu, tunaongelea kuhusu mikakati jumuishi ya uchumi wa Taifa. Tunasema hivi, kuimarisha uchumi, kukabiliana na changamoto za ajira na bei ya bidhaa, ndiyo ambayo umeyalalamikia huku, sisi tumepata suluhisho, utakwenda kuisoma mwenyewe vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili tunasema, kuwa na mfumo wa kodi unaotabirika. Mheshimiwa Zungu hapa ametoka kuchangia sasa hivi anakueleza masuala ya kodi yasiyotabirika (unrealistic taxes). Tunakwenda kutoza watu kodi, watu wanalalamika VAT hazirudishwi, kodi ya sukari ghafi kwenye viwanda hazirudishwi. Kwa hiyo, tunaomba kuwe kuna mfumo wa kodi unaotabirika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tunasema hivi, kuhakikisha kuwa kuna uwiano kati ya mauzo ya nje na kuagiza bidhaa za chini. Hii inakwenda sambamba kabisa na unapokuja hapa, sisi tumeanza kutengeneza reli na tulimshauri wakati fulani, tunakwenda kutengeneza ReIi ya Kati (Standard Gauge), tunanunua chuma nje, wataalam nao wanatoka nje, hivi kwa nini tusifikirie kwanza tukaanza kutengeneza kiwanda mama cha chuma kule Mchuchuma pamoja na kuboresha na kutengeneza Reli ya Kusini ili kwamba chuma yetu ya Mchuchuma tuilete Bandari ya Mtwara ikifika pale Mtwara itaondoka, nyingine itakwenda kuuzwa nje, nyingine itakuja kutengeneza Reli yetu ya Kati.

Ile tutakayouza nje tutapata pesa za kigeni, badala ya kwenda kukopa kule nje tutakuja kutengeza reli yetu kwa kutumia pesa zetu sisi wenyewe. Kwa hiyo, haya ni mawazo ambayo sisi tunayo na yapo kwenye sera yetu, utakapopata nafasi Mheshimiwa Waziri nenda kaisome vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pia ukurasa wa 19, nataka nikuongezee madini ili tuweze kuboresha, tuishauri Serikali ili nchi yetu iweze kusonga mbele kwa sababu sasa hivi imesimama. Tunakuja hapa kwenye uchumi wa viwanda vyenye tija, hiyo ndiyo sera yetu sisi inavyosema. Tunasema kwamba, kutekeleza mkakati wa mabadiliko makubwa katika sekta ya viwanda. Mheshimiwa Dkt. Mpango, nadhani unaona hali ilivyo sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara lakini tumejaribu kuomba kwa Waziri wa Viwanda watupeleke kwenye viwanda wanavyoviita vilibinafsishwa, viwanda 155 tuweze kujua viko kwenye status gani ili tuweze kuishauri vizuri Serikali na kuona namna ya kusonga mbele lakini nikueleze kabisa sijui kama Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Naibu wake wana nia njema kabisa ya kuhakikisha wanamsaidia Rais kwenye kupata viwanda. Sisi kama CHADEMA tumekuja na suluhisho utakapopata nafasi utasoma utaona namna ya kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesema tunatamani kufungamanisha uchumi wa ndani na viwanda. Tunaimba kuhusu viwanda, viwanda vinavyofanya kazi ni viwanda vichache vya tiles, vya nondo ambavyo vyote vimekuwa concentrated huu Ukanda wa Pwani kwa maana ya maeneo ya Mkuranga na kwingine. Sasa atakayekwenda kununua nondo ni nani na anakwenda kuzitumia wapi kama mazao yake ya shambani hayapatai bei bora? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiangalia sasa hivi hapa kuna hii sintofahamu ya masuala ya korosho lakini ni kwa sababu tu ya kutokuwa na mpango bora kwenye jambo hili. Wale wanunuzi walilazimishwa kuitikia kwamba watakwenda kununua kwa bei ya Sh.3,000. Kimsingi gharama ya kuitoa korosho sasa hivi kuifikisha India ni zaidi ya Sh.4,000 wakati kule wanauza kwa dola moja na senti tatu sawasawa na Sh.3,800 ya Kitanzaia. Kwa hiyo, tunaiomba Serikali kwanza ikiwezekana warudishe ile Sheria ya export levy, iletwe hapa ndani ifutwe kabisa ili kuweza kunusuru hawa wakulima sasa hivi waweze kupata pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tuwaombe sasa, kwa sababu hiyo bei iliyopangwa siyo realistic na watu wanafikiri kwamba wanaolazimisha hii bei isitokee pale ni watu wa Kangomba. Korosho bei elekezi ni Sh.1,550 ndiyo ambayo ilipangwa pale, mtu anakuja na Sh.2,700 anataka kununua tunamwambia hii bei haijakidhi. Ndiyo ni bei ya chini lakini inategemea na soko. Kitendo cha kuondoa export levy, ile pesa ambayo ilitakiwa irudi kwa wakulima zile pembejeo na vitu vingine ndiyo imeleta hii trickle action, tunaona sasa athari zake zinazopatikana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itapoteza mapato kutokana na mauzo ya korosho na uzalishaji umeshuka. Pia Serikali inaweza ikaleta shida zaidi kwamba hizi korosho mwaka huu zisiishe kwa sababu msimu wa maeneo mengine unaanza, korosho yetu inaweza ikabaki, iko nyingi kwenye maghala. Kwa taarifa yako tu, tunavyoongea hapa sasa hivi leo ilikuwa ufanyike mnada wa Tunduru lakini kimsingi hakuna mnunuzi hata mmoja aliyekwenda Tunduru kwenda ku-bid kwa sababu hawawezi kutimiza yale masharti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado niendelee na kitabu chetu cha sera. Ukienda pia ukurasa wa 22 katika harakati za kuendelea kumshuari Mheshimiwa Dkt. Mpango tunasema hivi, usimamizi madhubuti, endelevu wa sekta ya madini…

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mnaweza mkaingia wanafunzi wawili darasani mnafanya mtihani halafu yule anayedesa akafaulu vizuri kuliko aliyeingia na desa lenyewe kule ndani. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini unaulinda muda wangu, kwa hiyo, anachokifanya Mheshimiwa Innocent sikishangai na hawa ndugu zetu wa Chama cha Mapinduzi wanachokifanya wao wanaongelea kuhusu Ilani, sisi tunaongelea kuhusu sera na sisi tuna mawazo yetu tunataka tuyalete hapo mbele ya safari ili yatumike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi naomba niendelee, nimesikia alichokisema napokea taarifa yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Mheshimiwa Zitto nimeipokea na yenyewe iingie kama sehemu ya mchango wangu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niseme kwamba kuna jambo ambalo linaendelea pale, suala la usimamizi madhubuti na endelevu wa sekta ya madini.
Tunaomba kabisa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye hoja iliyopo mbele yetu. Kwanza, moja kwa moja nimpongeze shangazi yangu, Mheshimiwa Mama Lulida, alichokisema Mheshimiwa Mama Lulida ndiyo kitu ambacho kinatokea Mtwara, lakini pia ndivyo vitu vinavyotokea Lindi. Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi ambayo ndiyo iliingia mikataba ya kuuza maghala ambayo yalikuwa ni viwanda vya korosho Mtwara, Lindi, Newala, kwanza imepoteza ajira kwa watu wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaomba basi tu-review upya ile mikataba kwa sababu tunaamini pamoja na ugumu uliopo kule ndani lakini Rais ana nia ya dhati kabisa ya kuwasaidia watu wa Mtwara ili waweze kupata ajira. Sisi Mtwara hatuna shida ya malighafi, tuna malighafi ya korosho ambayo inategemewa sana India. Malighafi pekee wanayoitegemea wale ni kutoka Mtwara ambayo ni korosho na tumeona mwaka huu korosho imeuzwa mpaka shilingi 3,800. Ili kuweza kuongezea wale wananchi kule kipato, tunataka sasa vile viwanda vifufuliwe korosho hii tubangue kule wenyewe. Kwanza ikibanguliwa kule moja kwa moja itauzwa kwa bei kubwa kwa sababu gharama za usafirishaji na tozo nyingine hazitakuwepo, hii pesa atakwenda kuipata mkulima moja kwa moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumeshuhudia maghala haya ndiyo yamekuwa sehemu ambazo zinakwenda kuwafilisi na kuwaibia wananchi, hawapati haki zao stahiki. Maghala haya kule ndani imeingia mikono ya wakubwa ukitaka kugusa biashara za maghala Mtwara basi unatafuta ugomvi na wakubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri tukuombe, hakikisha unapitia vizuri hii mikataba ukishindwa wewe kuisema tupatie sisi tutasema, mpe pale Mheshimiwa Mama Lulida atasema, nipatie mimi nitasema, lakini kimsingi tunachotaka mwishoni wananchi wa Mtwara, wananchi wa Masasi wawe na viwanda vyao vile vya zamani. Viwanda hivi vilijengwa kwa kukopa pesa nchi za nje, ambapo ninaamini bado Serikali hii inaendelea kulipa pesa wakati viwanda vimeuzwa kwa bei rahisi, kwa hiyo nikuombe kabisa upitie hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema tena kidogo kuhusiana na suala la biashara ya mafuta. Watu wengi, na hapa ndani tumeona wakiwa wanachangia, sasa hivi tunaona bei ya mafuta imepanda sana, hata kama tunasema imepungua, asilimia 42 ya tozo mbalimbali zilizopo kwenye bei za mafuta zinakwenda Serikalini kuendesha vitu mbalimbali, lakini tunawatengenezea ugumu hawa wafanyabiashara wa mafuta. Kwa hiyo, tuone namna gani tunaweza tukawasaidia, tuangalie hizi tozo na kuzi-review. Haiwezekani asilimia 42 yote iwe kama sehemu tu za kodi, mfanyabiashara apate shilingi 120 au 150 sehemu ya kazi anayoifanya pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kimsingi tujaribu kuangalia, tunaposema kwamba watu wa Mtwara sisi tuna shida hatuna shida hasa ya viwanda kama mnavyovisema. Hivi karibuni tu Mheshimiwa Waziri niliongea nawe nikakueleza, tunaweza tukapata juisi kwenye mabibo, tunaweza tukapata nipa kwenye kochoko inayotokana na mabibo, lakini lengo hasa ni kwenda kumuongezea mkulima kipato. Hivi vitu vikiuzwa, hata tukiuza korosho shilingi 3,000, lakini tukauza mabibo yetu yanayokwenda kutengeneza juisi, tukauza zile kochoko zinazokwenda kutengeneza gin, tukaachana na hivi vitu vya ku-import itakwenda kuongezea pia kipato Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hapa tunasema tunataka kupata mapato kwenye Serikali kwa kutumia vileo, ukiangalia asilimia kubwa ya wananchi vijijini ni wanywa gongo, wanywa gongo hawa, na hii gongo tunasema ni pombe haramu haijarasimishwa, lakini ndio wengi wanaokunywa gongo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukiamua sasa kurasimisha ikazalishwa vizuri kwenye vyombo vinavyotakiwa kodi itakwenda kuongezeka kwenye vileo, sawasawa na ilivyo konyagi sawasawa na ilivyo gin sawasawa na ilivyo kwenye K-Vant watu wa Arusha. Kwa hiyo tutoe leseni za watu kuweza kupika gongo ambayo ipikwe kwenye viwanda vinavyotakiwa, ipimwe vizuri, irudi ikaingizie kipato Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakataa bure, asilimia 75 ya Watanzania wanaoishi vijijini wanakunywa gongo, na hii tutambue kama vyanzo vya mapato kwa sababu tutatoza kodi. Tunasikia sifa kutoza kodi kwenye grant’s, tunasikia sifa kutoza kodi kwenye konyagi wakati tunajua wazi wanywaji wa konyagi na grant’s si wengi kama walivyo wanywaji wa gongo. Kwa hiyo tunapoteza mapato, tuangalie namna bora ya kufanya ili tuweze kuzalisha hivi vitu lakini pia itaongeza kipato cha wakulima wetu kama ilivyo kwa wakulima wa miwa. K-Vant inatengenezwa kwa kutumiwa miwa, miwa ni mazao ya wakulima, konyagi inatengenezwa kwa kutumia chemicals nafikiri, lakini pia nipa inatengenezwa kwa kutumia mabibo ambayo inaongezea kipato wakulima kama tutarasimisha na kununua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri nikuombe utakapohitimisha utuambie sisi watu wa Mtwara mna mpango gani na viwanda vyetu vilivyouzwa kiholela holela vya korosho, vinaweza kutoa ajira kwa vijana wetu wote maeneo yale, tunaweza kuongeza tija kwenye korosho. Mheshimiwa Mama Riziki Lulida amesema hapa kwamba hizi ajira zinapelekwa India, tunajisifu tume-export tani laki mbili za korosho kupeleka India, lakini hatufikiri kama tumeondoa ajira za watu zaidi ya 10,000 au watu 20,000 kupeleka India, tunataka kuweka viwanda vya aina gani? Tuwaombe Mtwara tunataka tu viwanda vya kuanzia vya korosho, wala hatuhitaji kutengeneza nondo katika hali hii, korosho yetu isitoke na kwenda nje, iwe processed palepale ili kuweza kuiongeza thamani, muwashawishi wale wawekezaji waliopo kule waje Mtwara kujenga viwanda sio sisi tuwapelekee kwao malighafi, ninaomba ulichukue hili na tafadhali ulifanyie kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru sana kwa kunipa nafasi kwa kuwa mtu wa kwanza kuchangia ili tujaribu sasa kulielekeza Taifa kwenye mambo ya msingi kabisa ambayo sisi tulitamani tuyaone yanafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwanza kwa kuunga mkono, Taarifa ya Kamati ambayo imejaribu kuonesha upungufu mbalimbali ulioko kwenye utekeleza wa azma ya Mheshimiwa Rais inayohusiana na masuala ya viwanda na niishauri meza yako moja kwa moja kabla sijaenda mbali kwamba kwa kweli kwenye suala la viwanda kama ambavyo taarifa yetu ya Kamati imeonesha kuna matatizo makubwa sana, hasa zaidi kwenye utekelezaji wa hili wazo la kuwa na viwanda, lakini pia ukienda kwenye suala la viwanda vilivyobinafsishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo Mheshimiwa Rais aliwaita wawekezaji kwenye sekta ya madini, lakini pia Mheshimiwa Spika naye aliunda hapa tume maalum ya kuchunguza masuala yanayohusiana na madini na makinikia na majibu yaliletwa humu ndani. Sasa nipendekeza kama inawezekana Mheshimiwa Spika naye afikirie kutengeneza tume maalum ya Kibunge ambayo itakwenda kufanya uchunguzi na kuleta majibu yanayohusiana na masuala ya viwanda zaidi ya 150 vilivyobinafsishwa kwa sababu kimsingi hakuna chochote kinachoendelea kwenye hivi viwanda, viwanda pekee vinavyofanya kazi ni viwanda kumi tu kwa hiyo tunamrudisha nyuma sana Rais kwenye wazo lake la viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ukifuatilia kabisa michango inayotolewa na Wabunge, lakini na michango mbalimbali maeneo mengi inaonesha kabisa la Rais la kutaka kuwa na viwanda kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, linakwenda kufeli. Miaka ya 1980 na huko chini kama tunavyoongea hapa tulikuwa na viwanda zaidi ya 150 vya Serikali vilifeli. Sasa sidhani kama kuna utafiti uliofanyika unaoonesha kinaga ubaga ni kwa nini viwanda hivi vilifeli ambavyo Rais anasimama navyo na tumetumia kama ndio sera ya nchi yetu kuhakikisha tunakwenda kuboresha viwanda. Vinginevyo kama hatutafanya haya, vile viwanda vinavyotajwa 3000, viwanda vinavyotajwa 4000 na vyenyewe vitakwenda kufeli kama ambavyo vimefeli hivyo viwanda vingine huko nyuma, tena vilikuwa vichache tu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niombe kushauri kwamba tufanye mabadiliko ya makusudi kabisa ya sera ya viwanda, tufanye mabadiliko makusudi kabisa na utafiti kuona hivi viwanda tunavyovijenga masoko yake yako wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye taarifa ya Kamati ukurasa wa 16 kwenye taarifa ya Kamati hii ambayo iko hapo mbele yako, kwenye ukurasa wa 16 wanaongelea hapa habari ya import duty zaidi sana kwenye sukari ya viwanda. Hawa wenye viwanda wana lalamika kwamba Serikali imekuwa ikiwatoza wao pesa kwa ajili ya kuingiza sukari ya viwanda inayotumika kuzalisha soda na vinywaji vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa bahati mbaya sana kwa miaka mitatu sasa Serikali haijarudisha hii pesa kwao na inaonyesha wazi kabisa na labda Waziri aje kutuambia hapa baadae kwamba Serikali haina mpango wa kurudisha hizi pesa za watu wenye viwanda. Sasa badala ya kuwazungusha kila siku ni bora watuambie moja kwa moja kwamba hizo pesa hazitapatikana kwa sababu hazipo kwenye mfuko wowote na kwa ufupi Serikali haina hiyo pesa ambayo inatakiwa irudishwe kwa watu wenye viwanda kutokana na hii pesa yao. (Makofi)

Kwa hiyo, kwa vyovyote vile mpaka sasa hivi Serikali haina nia ya kufanya hicho kitu na badala yake imeamua kuwazungusha watu walio-deposit kule pesa, kwa hiyo, iamue kuacha au kutokuendelea na kukusanya hii pesa kwa sababu haina uwezo wa kurudisha na tunasababisha viwanda vinakufa, watu wanashindwa kuendeleza na kufanya mambo mengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda ukurasa wa 20 kwenye hili jambo tunalosema Mheshimiwa Rais ana nia njema ya kutaka kuhakikisha Tanzania inakuwa ya viwanda. Lakini soma tu pale, kwamba katika pesa za maendeleo zilizotengwa bilioni 80 zimekwenda bilioni nane tu ambayo ni sawa sawa na asilimia tisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi na ninyi tujiulize kwamba Mheshimiwa Rais anataka Tanzania iwe ya viwanda, lakini pesa za viwanda ambazo zinatakiwa zitolewe na Hazina, pesa za maendeleo haziendi. Kwanza zinakwenda kidogo, tunaambiwa hapa ni asilimia tisa tu. Hata hivyo katika hiyo asilimia tisa na yenyewe haiendi kwa wakati, matokeo yake, watu wanashindwa kufanya shughuli zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeongea hapa habari za SIDO, SIDO ndio tunataka iwe sehemu kubwa ya chachu ya viwanda Tanzania tuwaongezee SIDO nguvu, ili waweze hii sera ya viwanda iweze kutekelezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kimsingi hakuna lolote linalofanyika na awamu hii kuhusiana na masuala ya viwanda kwa sababu hawakujiandaa, wameamua kuja na kitu ambacho utekelezaji wake ni hauwezekani, labda waamue kutafuta namna nyingine ya kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo yanayohusiana na viwanda turudi sasa kwenye viwanda vikuu; na tumejadili hapa mambo mengi, nimeona watu wanajadili masuala ya korosho, Mheshimiwa Waziri pale naye kajibu. Sasa ukiingia upande wa biashara, kwa sababu
tunajadili masuala ya viwanda, pamoja na biashara, kimsingi Mawaziri hawa hawa ambao leo wanatoa maelezo kuhusiana na masuala ya viwanda vya korosho pamopa na bei za korosho kwa ujumla ndio hao ambao walikuja ndani ya Kamati. Juzi hapa Mheshimiwa Hasunga alikuwa anamjibu Mheshimiwa Bobali, anamwambia kwamba uzalishaji wa korosho gharama yake mpaka sasa hivi, kwa hiyo hata wakiuza kwa shilingi 4,180 haina maana kwamba wao wanapata faida kubwa. Ni Waziri huyu huyu na kitabu ni hiki, alipokuja ndani ya Kamati alisema hivi, kwamba mpaka sasa hivi wamepata watu wanaotaka kununua korosho kwa shilingi 3,500 lakini wamewakatalia, kwa sababu gharama za utaratibu wa uendeshaji wa zao la korosho kwa kilo moja mpaka sasa hivi, imefikia shilingi 3,850. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa katika shilingi 3,850 wao wanakwenda kuuza shilingi 4,180. Sasa tunataka watueleze ile gap kati ya shilingi 3,850 au shilingi 3,300 mpaka shilingi 4,180 hii pesa iliyozidi nani anakwenda kupewa? Kwa sababu haioneshi nia ya kutaka kuwarudishia Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini hapa tulisema pia, tunachofanya sisi ni biashara na Serikali imeamua kufanya biashara kupitia benki zake hapa. Wanasema wenyewe kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko Serikali imeamua kufanya biashara ya Korosho sasa wanawazuia. Kilichokuwa kinafanyika mwanzoni, tuseme labda kwenye hili suala la Kangomba ambalo watu wanafikiri ni dhambi kubwa sana, na mimi sioni kama kuna dhambi yoyote inafanyika. Kangomba ni facilitators kama walivyo facilitators kama walivyo facilitators wowote kwenye mazao ya biashara, sawa sawa na watu walivyo kwenye pamba, sawa sawa walivyo watu kwenye mahindi, hata kwenye nyanya, wanasema wafuate mfumo unaotakiwa, hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunajiuliza hivi kutoa nyanya kwa Mkulima na kuipeleka sokoni ni dhambi? Kutoa mahindi kwa mkulima mmoja mwenye uwezo wa kuvuna wa gunia tatu, akaja kuniulizia mimi mwenye uwezo wa kujikimu pesa ya maisha lakini naweza kuvuna hata gunia mia nikazipeleka kwenye maghala makubwa, hii ni dhambi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndicho kinachofanyika kwa wauzaji au Wafanyabiashara wa korosho. Serikali kabla haijapeleka pesa maghala yanafunguliwa kuanzia mwezi wa kumi, korosho inaanza kuvunwa miezi ya nane, mwezi wa saba, wakati huo wote haya yote yanafanyika Serikali haijpeleka pesa. Sasa mtu anapoamua kujikimu kwa kutumia mali yake mwenyewe iliyoko ndani, anachukua korosho anapeleka kwa baba mwenye duka kijijini kwetu anakwenda kubadilishana na unga, anakwenda kubadilishana na sukari, anakwenda kuchukua pesa ili aweze kumtibu mtoto wake, leo Serikali hii sikivu inasimama hapa na kusema hawa watu ni wezi, tuwaombe radhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwaombe radhi wachuuzi wa korosho kwa sababu wao sio wezi, kinachotakiwa kufanyika ni kurasimisha huu mfumo, na yatambulike kwenye mifumo huru. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Serikali inasema inakusanya korosho kupitia Bodi ya Mazao Mchanganyiko, na wanakwenda kuziuza ni lini watakwenda huko chini? Sasa kwa nini tusirasimishe hawa kangomba wakakusanya korosho kidogo kidogo kutoka kwa watu wetu …

T A A R I F A

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakuja hapa kidogo kwenye suala hilo hilo kangomba, naomba niendelee kwamba tafsiri anayoitoa Mheshimiwa Mlinga ninamuomba kwa makusudi kabisa akae na wazee akiwemo Mzee Mkuchika na wengine wote wanaotokea upande huu, ukanda huu unaolima korosho halafu wamwambie kangomba kwa uhalisia ni nini, na si hicho anachokisema yeye. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na kama kangomba ni dhambi wasimame hapa watuambie, kwamba kufanya kangomba ni dhambi na kwamba hairuhusiwi. Vinginevyo kinachotokea ni kwamba Serikali inataka kwenda kufanya dhuluma kwa wafanyabiashara wadogo wadogo wa korosho; na ni kwa nini, korosho …

T A A R I F A

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru kaka yangu Mheshimiwa Zitto kwanza kwa kunikumbusha, na kuiomba Serikali ilete hoja Bungeni ya kurasimisha biashara hii na hawa watu wa katikati ambao wao watakwenda ku-bridge kati ya mkulima pamoja na mnunuzi mkubwa ambaye ni Serikali, kwa sababu wameamua wakafanye hiki kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nitoe tu angalizo kwenye hili jambo ….

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimwia Mwenyekiti, Taarifa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hapa sasa hivi Wakulima wanapewa adhabu…

T A A R I F A

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri kwa kujua tatizo la msingi linalozalisha kangomba Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sasa niiombe Wizara yake ikatoe leseni, ikarasimishe hizo biashara ili wawashauri hao watu walipe kodi, ndilo suluhisho la hili. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu elimu hii hamkuitoa wakati unaotakiwa muitoe niwaombe na Serikali hapa itoe tamko, korosho zote mlizozikusanya mzirudishe badala ya kuwadhulumu kwa sababu hamkwenda kuwaeleza kwamba wanatakiwa kuwa leseni. Kosa hili limeanzishwa na Serikali na mkiliacha litaendelea kujitokeza kwa sababu kangomba ni jina la kilugha la Kimakonde, Kiyao ni mchanganyiko, lakini kiingereza chake hawa watu ndio brokers. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na mlichokifanya Serikali kwa kumwita yule INDO kampuni ambayo mnasema ni ya Kikenya inayomilikiwa na kijana wetu Mtembei ambaye ni muhaya wa Tanzania, anachokifanya yeye ni brokage kwa sababu Serikali imeshindwa kutafuta masoko ya korosho na yeye anakwenda kuziuza hizi korosho nchi za nje, jukumu ambalo lilikuwa lifanywe na Wizara ya Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo mmemruhusu kangomba INDO afanya hiyo kazi muwaruhusu na wale kangomba wengine, lakini kwa kuanzia hakikisheni kwanza korosho zao mlizokusanya mwaka huu mnazirudisha kwa sababu wao si wezi, there is no logic. Nimeona hapa kwene mtandao inasambaa Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Newala amekamata wafanyabiashara na wakulima, wa upande wa Mozambique kuja kuuzia Korosho zao Newala. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhambi gani walikuwa wanafanya kwenye uchumi wetu? Hivi mtu kutoa mali nje na kuzileta hapa ni dhambi? Watu wa kwetu sisi wa mipakani, mpaka wa Mozambique na Tanzania tunatenganishwa na mto Ruvuma, watu wa kwetu wanalima upande wa pili na watu wa huko Mozambique wanasoma upande wa huku, wanaita ng’ambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna asiyejua hapa; Mkuchika na wengine…

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: …babu zake walikuwa wanalima huko, wanakwenda kulima ng’ambo wanarudisha mazao yao pale.

MHE. PASCAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Taarifa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Cecil kaa kidogo. Mheshimiwa Selasini, tulieni, Mheshimiwa Millya.

MHE. JAMES O. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Millya ni mwanasheria.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,...

MWENYEKITI: Mheshimiwa Millya.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Zitto...

MWENYEKITI: Waheshimiwa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

T A A R I F A

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Zitto anatoka Kigoma, hamna korosho, lakini amechangia, sasa sijui hawa watu ambao …. national figure kutoka Kigoma.

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti,...

MHE. SAED A. KUBENEA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge,...

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachojaribu kusema ni kwamba...

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Kubenea kaa chini.

MHE. JAMES K. MILLYA: Taarifa ninayotaka kumpa mzungumzaji…

MWENYEKITI: Kubenea kaa chini.

MHE. JAMES K. MILLYA: ..ni kwamba ….

MWENYEKITI: Waheshimiwa tutaanza kuandika majina.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MHE. JAMES K. MILLYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba mzungumzaji anatetea wauzaji wa Mozambique kuja kuuza korosho kwetu kwa sababu Serikali ya Magufuli imetoa bei nzuri, hao hao ndio wanasema haya makosa yaendelee. Wakati Serikali ya Magufuli inatoa bei nzuri kwa ajili ya wakulima wa korosho Lindi na Mtwara yeye anawatetea wa Msumbiji wakati Rais wetu anawatetea Watanzania, wewe ni mtu wa namna gani? (Makofi)

MBUNGE FULANI: Kweli kabisa.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa Cecil, hebu subiri kwanza.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila utaratibu)

MWENYEKITI: …subiri, kwanza, mimi si ndiye referee hapa? Mheshimiwa Anatropia, Mheshimiwa Magereli, hii ni mara ya mwisho mtatoa sauti zenu bila utaratibu humu ndani, niko very serious.

MBUNGE FULANI: Taarifa Mwenyekiti.

MWENYEKITI: …mjadala ni mzito kwa pande zote mbili. Ukitaka jambo lako Mbunge unasimama kwa mujibu wa Kanuni. Ukifikiri hapa ni kwenye viwanja vya michezo hapa sipo na tunaingia kwenye lala salama, nikikutoa hapa hutarudi mpaka mwaka ujao. Mheshimiwa Cecil! (Makofi/ Kicheko)

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Millya kwa kuliona tatizo linalofanywa na Serikali naipokea taarifa yake …. (Vicheko)

MBUNGE FULANI: Taarifa Mwenyekiti.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ni kwamba hata hiyo Serikali.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyo broker waliyompa kuuza hizo korosho ….

T A A R I F A

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mkuchika.

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA): Mheshimiwa Mwenyekiti, hili Bunge ni jengo linaloheshimika sana, ndiyo maana kabla hatujaanza kazi tunakula kiapo tutafanya kazi, tena tunamalizia Ee Mungu nisaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema uongo katika jengo kama hili, ni jambo la hatari. Mimi ni mkulima wa korosho, nina shamba la korosho. Neno kangomba ni neno la Kimakonde, mimi ni mzee wa Kimakonde, nimesimama hapa nieleze nini maana ya neno kangomba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kangomba ni ununuzi wa korosho kwa kutotumia kapani au kipimo kinachotambulika na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge Wanaopinga Rushwa. Jumamosi iliyopita, acha hii ya jana, tulikuwa na semina pale Dodoma Hotel inayohusu weighs and measures; umuhimu wa vipimo katika biashara ya mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikao kile kililaani kangomba kwa sababu kangomba anasema tu kwamba bakuli hii ni shilingi saba, yule ambaye ana shida anayefanya biashara ya kangomba ni mtu ambaye ananunua korosho kwa mkulima, kwa kipimo ambacho si kidogo, ni kidogo ambacho anamnyonya ili baadae yeye aende apate faida kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sikutegemea mtu anayetoka eneo la korosho, anavyojua wapiga kura wake wanavyoichukia kangomba kule nyumbani, sikutegemea awepo hapa mtu anayetoka eneo la korosho anasema kangomba ni halali; kangomba is corruption, ndiyo maana Serikali inaipiga vita, na tutaendelea kuipiga vita... (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante, Mheshimiwa wameshakuelewa, Mheshimiwa Cecil malizia dakika yako moja.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimwambie tu mzee wangu Mkuchika, namheshimu alisoma na baba yangu, kwamba…

MWENYEKITI: Changia suala ambalo liko kwenye mjadala.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, si najenga hoja.

MWENYEKITI: Haya endelea.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka nimweleze ni kwamba mpaka sasa hivi hiyo Wizara ya Kilimo, wana kesi ngapi Mahakamani za watu waliokwenda kulalamikia kangomba? Na anachokisema mzee si kwamba kangomba haifanyiki, ukimsikiliza kwa nyuma kwa nyuma anachosema irasimishwe ili wakae na mzani wakati wa kununua, ndicho anachokisema pale. (Makofi/Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo na mimi nipokee taarifa yake na nimshukuru na ameliona hili wazo kwamba kinachofanyika watu wanakwenda kununua kwa vipimo visivyo sahihi. Kwa hiyo, ameshauri Serikali kwamba sasa hivi ipeleke mizani kwa wanunuzi wadogo wadogo vijijini ili waweze kuweka hili jambo likae sawa na ndicho kilio chetu, hicho ndicho kilio chetu. Sawa sawa na lile la Mheshimiwa Millya alikuwa analisema pale… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwanza kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye hoja hii iliyopo hapa mbele yetu, hotuba ya Mheshimiwa Waziri kwenye masuala ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali unavyoiona kama ambavyo Mheshimiwa Mnyika alianza kuongea toka mwanzo kwamba kimsingi kuna hali mbaya sana kwenye suala la maji na Wabunge wote waliosimama hapa wamekuwa wakilalamikia suala hili. Niungane na Mheshimiwa Mnyika lakini pia niungane na hotuba yetu ya Kambi Rasmi ya Upinzani kwa kuitaka Serikali irudi na kufanya marejeo kwenye hii miradi yote ya maji kwa ajili ya kupata value for money kwa sababu kuna miradi mingi imesimama na tunaamua kufanya hii kazi kisiasa, tunapeleka pesa kidogo kidogo kwenye maeneo mengi ambayo hayawezi kuleta tija kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kuwashukuru sana wa-missionary wa Ndanda kwa sababu bila wao eneo kubwa sana la Mji wa Masasi pamoja na maeneo ya Ndanda tungekuwa na kiu kuu. Kutokana na uvumbuzi wao uliofanywa miaka ya 1960 na marehemu Bruda Lucas, Mwenyezi Mungu amuweke mahali pema peponi, wametuwezesha kupata maji eneo kubwa, kata nane za mwanzo ambazo ni Ndanda, Mwena, Chikundi mpaka kufikia Kata ya Chigugu pamoja na Kata ya Chikukwe. Tatizo kubwa tulilonalo hapa ni ucheleweshwaji wa uanzishwaji wa mradi huu. Mradi ule umeendelea kutengenezwa pale, tumepokea mabomba tunashukuru lakini pia matenki yameendelea kujengwa kwenye lile eneo pamoja na vizimba kwenye maeneo mengi sana, sasa tatizo mkandarasi anashindwa kuendeleza ile kazi yake kwa sababu hapati pesa kwa wakati kiasi kwamba wananchi wanaanza kukata tamaa na hawajui kwamba maji wataanza kupata lini kwenye eneo hili. Kwa hiyo, bado mpaka sasa hivi wanahangaika na visima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukumbuke sisi watu wa Ndanda tuna maji mengi tu na nilishwahi kusema hapa hata siku ya kwanza kabisa naanza kuchangia nilisema kwamba tatizo kubwa tulinalo watu wa maeneo ya Ndanda kwenye hizo kata nilizozitaja ni miundombinu. Sasa miundombinu imetufikia lakini kazi hii inashindwa kukamilika zaidi ya mwaka wa pili sasa hivi kwa sababu pesa zinapelekwa taratibu. Ni bora hizi pesa zikapelekwa kwa haraka ili ikiwezekana mradi huu ukamilike tuwaondolee kero wale wananchi wa hayo maeneo niliyoyataja ikiwemo pamoja na Maparagwe na Vijiji vya Mbemba na Mbaju. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka niliseme hapa, Jimbo la Ndanda limegawanyika kwenye jiografia mbili; kuna upande wa Mashariki pamoja na upande wa Magharibi. Upande wa Magharibi miaka ya zamani kama mtakumbuka tulikuwa tuna miradi iliyokuwa inafadhiliwa na JICA na DANIDA. Kwa bahati mbaya sana ukienda Kata za Mlingura, Namajani na Msikisi, maeneo haya yote yalikuwa na miradi mikubwa sana ya maji na maji haya yalikuwa yanatokea kwenye Kata ya Namajani. Pale kuna visima, kwenye vile visima vinatakiwa visafishwe na kuboresha miundombinu kwa sababu mpaka pump house ziko pale mpaka sasa hivi, matenki nayo yako pale, kwa hiyo, tunahitaji kuboresha ile miundombinu pamoja na kusafisha visima kwa gharama ya karibia shilingi milioni 300. Nilivyoongea na yule mtaalam wa maji mara ya mwisho alisema hivyo lakini Serikali haijatekeleza jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashangaa hapa wanatuletea mipango mikubwa sana wakati sisi tunahitaji maji kwa haraka tuweze kuwasaidia watu wetu. Serikali inawaza kutengeneza mabwawa na niliongea hapa wakati fulani na Mheshimiwa Waziri na nimeona kwenye kitabu hapa, ukurasa wa 79, wametaja na kijiji pekee ambacho tumepata maji siku za karibuni kwa gharama isiyozidi shilingi milioni 60. Sasa tunawaza kurekebisha mabwawa, kuna Bwawa la Lukuledi na Mihima, tunawaza kutengeneza Mabwawa maeneo ya Chingulungulu, kimsingi maji ya Mbwinji yaliyokwenda Jimbo la Ruangwa, Nachingewa yanatoka Jimbo la Ndanda, Milima ya Nangoo, kwa hiyo, tuna maji mengi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokiomba sisi, badala ya ninyi kufikiria kuhusu kutengeneza mabwawa tupeleke miundombinu ili haya maji yanatopelekwa maeneo hayo niliyoyataja yaweze kufikia eneo kubwa la Jimbo la Ndanda tena kwa gharama nafuu sana tofauti na gharama mnazozifikiria ninyi. Tuwaombe kabisa Serikali kwamba mtakapokuwa mnafanyia kazi miradi hii mtushirikishe sisi wenyeji wa haya maeneo, tunaweza tukawafahamisha, tukawaonyesha vyanzo vizuri zaidi kuliko vile ambavyo nyinyi mnafikiria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine liko kwenye Kata yangu moja ya Chiwata. Kata hii kijiografia iko juu kabisa ya mlima ambako tunapaka kati ya Makonde plateau pamoja na milima ya upande wa Masasi. Bahati mbaya sana Kata ya Chiwata ndiko ambako iko shule kubwa kabisa ya sekondari na sasa hivi imekuwa A-level, shule ya Tiija lakini kuna shida kubwa sana ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna wakati tulifikiri kwa sababu mradi wa madini ulikuwa unaendelea pale na wale wawekezaji walikuwa tayari kusaidia maji kwenye lile eneo, inahitajika kama shilingi milioni 300 mpaka shilingi milioni 400 na Waziri tumeshaliongea jambo hili. Naomba nikusisitize tena, ili tuweze kupata maji safi na salama Chiwata yanayotoka kwenye vyanzo vya maji vya Kambona ambavyo mimi navijua, wewe haujawahi kufika pale, tunahitaji kupata pump, tunahitaji pia kutengeneza tenki kwenye maeneo ya Chibya Sekondari ili tuweze kusambaza kwenye haya maeneo yote na hivi ndivyo inatakiwa ifanyike mtushirikishe. Sasa mnawaza kupeleka pale maji sijui kutoka kwenye source gani wakati kuna chanzo cha gharama nafuu sana cha maji ambacho kitasaidia haya Serikali kuweza kubana matumizi kwenye eneo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango mwingine ni wa kupeleka maji kwenye hizo kata nilizokwambia. Kwa mfano, ukisoma kwenye hii taarifa ambayo iko kwenye ukurasa huu wa 29 nilivyoitaja hapa mwanzoni wanaelezea kuhusu Mradi mkubwa sana wa maji ya Mbwinji lakini naomba tu nikutaarifu kwamba huu Mradi wa Maji ya Mbwinji ulikuwa na andiko lake toka mwanzoni kabisa na walisema wataanza kuhudumia wenyeji wa maeneo husika. Sasa hivi naongea na wewe lakini ukienda kwenye Kata za Nanganga pamoja na mradi ambao ulifanyika kwenye eneo hilo kupeleka maji vijiji vyote, mradi uliofanywa chini ya kiwango na mkandarasi yule bado yupo amefanya ubadhirifu mkubwa lakini amekuwa akilindwa na watu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati mbaya sana hii miradi tumeigeuza kuwa ya kisiasa. Viongozi wa kisiasa kwenye maeneo yetu ndiyo wanaopewa kusimamia miradi hii. Makusanyo yanayopatikana kwenye miradi hii watakapotumia vibaya hakuna mtu anayekwenda kuwahoji hasa wanaotokea kwenye chama tawala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme mradi wa maji uliopo kwenye Kata ya Nanganga haufanyi kazi kwa sabau tu yule mkandarasi alijenga chini ya kiwango, lile chujio la maji pale limeharibika, halijakarabatiwa na mpaka sasa hivi mradi huo haujapokelewa ambapo tunashindwa kupeleka maji kwenye Kata ya Nanganga kwenye vijiji vya Mkwera, Chipite, Nangoo, Lumumburu pamoja na vijiji vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Mawaziri mnapopata nafasi na nakumbuka Mheshimiwa Waziri Kamwele alipokuja alisema kabisa kwamba Bodi ya Maji inayosimami ile ambayo iliundwa na wananchi kwenye hii Kata ya Nanganga ivunjwe kwa sababu imekuwa ikifanya ubadhilifu na watu wanapohoji viongozi wetu wa Serikali za Mitaa na wengine wanawachukulia hatua ambazo sio stahiki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kweli tukIamua kwa mfano Mheshimiwa Mbunge alietoka sasa hivi anaongea habari ya shida ya maji Kwimba. Kwimba ipo karibu na Ziwa la Victoria wala sio mbali kutoka huko, sasa kama mtu aliyeko Kwimba analalamika kuhusu maji sishangai na watu wa Shinyanga na kwingine wakalalamika kwa sababu kidogo wako mbali na hili ziwa. Kwa hiyo, maeneo yenye vyanzo vya maji tuache kufikiria miradi mikubwa sana twende tukaboreshe ile miradi midogo iliyopo kwenye haya maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Lakini tuna tatizo kubwa sana la maji pia kwenye Jimbo letu la Masasi na Masasi ni nyumbani kwangu nina wajibu wa kuwasemea watu wa Masasi. Tuna shida moja tu Masasi wanapewa maji kutoka kwenye watu wa MANAWASA. MANAWASA ndio wanaosimamia chanzo cha maji cha Mbwinji, mpaka sasa hivi ninaongea na wewe ukiangalia kwenye bajeti iliyopangwa huku ndani wanasema watawapelekea maji wote huo mradi unakaribia kukamilika na najua Katibu yuko hapa anasikiliza naweza nikampa maelezo ya ziada baadaye kutokana na muda tulionao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu wazi kwamba mkandarasi ambaye alipelekwa kwenda kufanya tathimini kwa ajili ya kutaka kuanza ule mradi ambao wanasema unakamilika mwezi Juni mwaka huu anashindwa kuendelea na kazi kwa sababu hana pesa ya kufanya hiyo kazi ambayo nyinyi mnasema mlishamfanyia commission ili aweze kuanza. Na hii itasaidia kupata maji safi, hata maji tuliyopeleka huko Nachingwea, Maji tuliyopeleka Rwangwa na ndio maji hayo yanayokwenda Masasi. Lakini yanazidi kuwa machache kwa sababu chujio lile sio zuri tena ni dogo liliwekwa kwa ajili ya kuzalisha maji machache pale, sasa tunahitaji kupata chujio kubwa ili tuweze kupata maji safi na salama Masasi na maeneo mengine yote yanayozunguka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nilisema tuwashukuru sana Wamisionari bila wao huu mtandao mzima wa maji tunaoongelea hili eneo la Kata ya Mwena mpaka kufika Kata ya Chikukwe basi kungekuwa kuna shida kubwa sana. Na maji tunayotumia eneo hili ni safi na salama kwa sababu ndio chanzo cha mwanzo kabisa kabla ya chanzo cha Mbwinji kupeleka maji Masasi, kilikuwa kinatumika chanzo cha Mwena ambako ndiko yanakotoka…ahsante ninaiomba wizara pamoja na kazi nzuri wanayofanya waongeze…

MWENYEKITI: Unga mkono Mheshimiwa, mmh maji yatafikaje kama huungi mkono .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja ya Kambi Rasmi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia kwenye Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, kimsingi, nataka tu niongee mambo matatu, kwanza, ni suala linalohusiana na Reli ya Kusini kwa maana ya Mtwara-Mbambabay. Pili, ni suala linalohusiana na masuala ya barabara ya uchumi ya Mtwara – Newala – Masasi - Nachingwea lakini tunaomba ikiwezekana iongezwe Liwale -Morogoro kwa sababu tunafahamu sasa hivi Makao Makuu ya nchi yetu yamehamishiwa Dodoma. Sisi wakazi wa Mtwara tunakwenda Dar es Salaam kufauata huduma na siyo lazima tufike pale, tungeweza moja kwa moja kutokea huko tunakokutaja tukaja hapa Dodoma straight. Kwa hiyo, tunataka na hii Serikali nayo tuishauri.

Mheshimiwa Spika, suala la mwisho kabisa, nitapenda pia niihoji Serikali kwa sababu mpaka sasa kwenye Wizara hii na idara zake mbalimbali wameshatengewa na pesa zimeshatumika almost trilioni 18 lakini hatujaona kimsingi athari yake kiuchumi ndani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze na suala la barabara hii niliyoitaja ya Mtwara – Mnivata -Newala – Masasi. Ukisoma kwenye hotuba ya Waziri, ukurasa wa 278, kipengele cha tano, wanasema: “Ujenzi wa barabaraya Mtwara –Newala - Masasi”.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ina jumla ya kilometa 221. Kama ambavyo Mheshimiwa Serukamba pale amesema tuangalie value for money. Barabara yenye urefu wa kilometa 221 imetengewa shilingi bilioni 3.4 tu. Kwa wastani wa sasa wa kilometa 1 ya barabara kutengenezwa kwa shilingi bilioni 1, wanatuambia kwamba katika mwaka huu wa fedha watakwenda kujenga barabara hii kwa kilometa 3 tu. Sasa tunampa mkandarasi barabara ya kilometa 221.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameikagua barabara hii akasema tunaomba hii barabara ijengwe kwa haraka sana kwa sababu ni barabara ya uchumi lakini katika hali ya kushangaza Wizara wanatenga shilingi bilioni 3.4 peke yake, wanamkwamisha sana Mheshimiwa Rais. Hawa wasaidizi wake wakati fulani wanashindwa labda kumpa ushauri unaotakiwa.

Mheshimiwa Spika, kimsingi barabara hii ni ya uchumi na ni ndefu, hauwezi kutenga shilingi bilioni 3.4 pekee kwenye barabara yenye urefu wa kilometa 221. Kwa hiyo, tuiombe Wizara ikiwezekana warekebishe fungu hili au waone namna ya kufanya ili kuweza kutekeleza ile ahadi ya Rais.

Mheshimiwa Spika, Rais alipokuja alisema barabara hii atahakikisha wanawekwa wakandarasi watatu mpaka wanne kwa urefu wa kilometa hamsini hamsini kila mmoja. Mpaka sasa barabara inayojengwa ni Mtwara -Mnivata lakini ni asilimia 36 tu ambazo zimeshatekelezwa na sasa ni mwaka wa tatu. Kwa hiyo, tunaiomba Wizara itusaidie, kero ya barabara hii ni kubwa sana na nia yetu sisi ni kusafirisha watu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine hapa, suala la Reli ya Kusini. Kwa muda mrefu sana tumeongea na maeneo mengi watu wanadai fidia ikiwemo maeneo ya Mtama, Ndanda, Masasi na sehemu kubwa sana ya Jimbo la Mtwara Vijijini kwa maana ya kule anapotokea Mheshimiwa Mama Hawa Ghasia.

Mheshimiwa Spika, tatizo lililopo kwenye mradi huu, mpaka sasa haueleweki kwamba ni lini utaanza au Serikali nao wameamua kujiondoa kwenye huu mradi kama walivyofanya miradi ya barabara ya kutoka Dar es Salaam high way mpaka kufikia Chalinze. Kama ni hivyo basi waseme wazi ili wale wananchi waendelee kufanya shughuli zao za kiuchumi kwenye maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika miradi mikubwa ambayo Serikali ilikuwa inaipangilia ni pamoja na mradi wa Liganga na Mchuchuma. Hakuna mwekezaji yeyote atakayekuja hapa kama hatujaboresha hii miuondombinu.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani chuma kisafirishwe kutoka Liganga kuletwa Bandari ya Mtwara kwa kutumia barabara, siyo reliable na hasara ni kubwa na hii mizigo ni mizito. Barabara hizi tuache watumie watu kama ambavyo wengine wamesema lakini hii miradi mikubwa ya kipaumbele itekelezwe tuweze kuona sasa manufaa ya chuma tulichonacho sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tuliishauri Serikali hata kwenye Kamati yetu ya Viwanda Biashara, kwa nini wasifanye uwekezaji mkubwa pale ili kuokoa forex? Pesa ambayo ingepatikana Mchuchuma ingekwenda kujenga hiyo Reli ya Kati ya Standard Gauge. Chuma ambacho kingepatikana Mchuchuma kingekwenda kusaidia kujenga kwenye reli hiyo pia lakini matokeo yake tunaagiza chuma, tuna viwanda vyetu hapa vya nondo vinaweza kutengeneza lakini bidhaa karibia asilimia 90 zinazotumika kwenye standard gauge ni imported. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huko ndiko tunakomalizia pesa zetu za kigeni na tunashindwa kufanya miradi midogo midogo hii ya kuwasaidia wananchi. Tunaona Wizara ya Maji wanalalamika lakini mpaka sasa hivi nguvu kubwa sana inapelekwa kwenye hii miradi mikubwa ambayo utekelezaji wake nao ni wenye kutia shaka kwa sababu hakujafanyika due diligence wala kuonyesha impact assessment kwenye hii miradi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli hii ni muhimu sana kwa watu wa Kusini kama ilivyo kwa watu wa upande wa Magharibi na kwingine kwenye reli hii ya standard gauge. Sasa Serikali ituambie hapa wazi, wana mpango wowote wa kufanya kazi hapa kwa sababu kwenye hivi vitabu hawaonyeshi waziwazi wanataka kwenda kufanya nini. Kwa hiyo, waje watueleze kama kuna mpango huo na kama haupo basi tuwaeleze wananchi wetu waweze kufanya shughuli zao za kiuchumi kwenye maeneo haya. Hii itakuwa ni failure kubwa sana kwa sababu hakuna mwekezaji atakayekuja kufanya kazi Liganga kama miundombinu hii wezeshi hatujaitekeleza na tunajinasibu kwamba sisi ni nchi ya viwanda na mambo mengine. Kwa hiyo, tuanze kwanza na msingi wa usafirishaji kutoka kule Liganga kuja kuleta Bandarini Mtwara ambayo ni Reli ya Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Reli ya Kusini ilijengwa mwaka 1949, mwaka 1963/1964 ilindolewa, kwa vyovyote vile inatakiwa pale kufanyike uwekezaji mkubwa. Ni jambo jema kujenga hii standar gauge railway lakini malengo ya Reli ya Kusini iwe ndiyo ya kipaumbele na malengo yake ni makubwa kwa sababu ni sehemu ambako tutakwenda kuongeza uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, nigusie kidogo suala la barabara, tukitaja barabara inayoishia Masasi. Ukisoma pia kwenye hiki kitabu, barabara inayotokea Masasi kuelekea Nachingwea na yenyewe ina kilometa 45 wametenga shilingi bilioni 1.3 tu. Tuiombe Wizara itueleze, tunapotenga shilingi bilioni 1.3 kwenye barabara yenye urefu wa kilometa 45 tunakwenda kufanya kazi gani na pesa hizi? Pale Masasi sasa hivi kuna ajali nyingi sana kwa sababu kuna round about kubwa, barabara inayounganisha kwenda Songea, Newala, Nachingwea na kurudi Mtwara Mjini, tunaomba pale katikati ikiwezekana ziwekwe taa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili jambo sisi tumelijadili hata kwenye vikao vyetu ya RCC na Road Board kwamba tunahitaji pale kupata taa kwa sabbau ni junction kubwa na watu wengi sana wamekufa akiwemo Afisa Mkuu wa Maji wa Wilaya yetu sisi ya Msasi, alifia pale na ajali nyingi zinatokea, tunaziona. Kwa hiyo, tunaomba pale ziwekwe taa.

Mheshimiwa Spika, hii barabara tunayoitaja inayokwenda Nachingwea pamoja na pesa ndogo mlizozitenga tuishauri sasa Serikali, tunaomba Mkoa wa Mtwara kupitia Wilaya ya Masasi ifunguliwe sasa isiishie Nachingwea peke yake iende mpaka Liwale, ikitoka Liwale iende mpaka upande wa Morogoro, Malinyi. Safari hii ni fupi sana kutoka Masasi mpaka kufika Morogoro, Malinyi siyo zaidi ya kilometa 300 lakini tunalazimika kutembea kilometa 600 kwanza kufika Dar es Salaam ili tuweze kuondoka Dar es Salaam tuje Makao Makuu ya nchi na wakati mwingine unalazimika kusafiri siku mbili mfululizo. Kwa hiyo, niombe Wizara hii wakafanye kazi kwenye barabara hii waone namna ya kuunganisha Wilaya hizi mbili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala lingine niligusia kidogo kuhusiana na uwekezaji mkubwa uliofanyika kwenye Wizara hii. Mpaka sasa hivi Wizara hii na Idara zake wametumia almost 18 trillion kwa maana ya kununua ndege, kutengeneza hivyo viwanja vya ndege na kufanya shughuli mbalimbali zinazohusiana na miundombinu ya hivyo vitu ninavyovisema.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana sisi tulikuja hapa tukasema tunataka tuone manufaa ya moja kwa moja yanayopatikana kwa wananchi kutokana na miradi hii mikubwa inayofanywa na Wizara hii. Sasa utakapokuja Mheshimiwa Waziri tueleze ni namna gani uwekezaji huu mkubwa mlioufanya umenufaisha wakulima wa maeneo yetu wakiwemo wakulima wa korosho na wengine? Ni namna gani uwekezaji huu mkubwa uliofanywa kwenye Wizara hiyo umenufaisha uwekezaji nchini kwetu? Ni namna gani tumewavutia wawekezaji kwa kununua ndege na ni namna gani tumewavutia wawekezaji kwa kufanya huo uwekezaji mkubwa tunaoutaja hapa, Mheshimiwa Waziri uje hapa utueleze. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mtueleze ni namna gani sekta ya kilimo imenufaika na uwekezaji huu mkubwa unaofanywa. Otherwise na yenyewe tutakuwa tunasema bad timing, hatuna proper value for money. Tuiombe Serikali mwisho kabisa ikubali kufanya utafiti wa kina (impact assessment) ili kuweza kujua uwekezaji huu mkubwa uliofanyika pale umenufaisha wananchi kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa tumewekeza…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi jioni ya leo na mimi niweze kuchangia mjadala ulioko mbele yetu, wa Wizara ya Kilimo. Ningependa kujikita kwenye mambo mengi sana lakini kwasababu ya muda ninaomba tu niende sehemu chache lakini nitazitaja zile ambazo ningependa nichangie.

Suala la kwanza ambalo nitalizungumzia ni kuhusiana na mkataba wa Indo na hekaya ya Profesa Kabudi suala la pili ambalo ningependa nizungumzie ni suala la export levy ambalo tulijadili ndani ya Bunge hili hili, suala la tatu ni madeni ya wakulima ya zamani; na Mheshimiwa Waziri nitaomba u- note down wakulima wa korosho walikuwa wanadai pesa ambazo zilifanyiwa auditing tukaambiwa watakuja hapa kutakuwa na kesi vitu vingine havijafanyika pesa ya misimu iliyopita, tunaomba hili ulichukulie.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwambe kabla hujaanza sasa nimeshatoa uamuzi kuhusiana na hilo endelea kuchangia semea, kosoa Serikali.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa.

Kwa hiyo kuna hayo madeni, na nishauri kabisa hapa kwamba sheria ya export levy pale ambapo tuliondoa haimaanishi kwamba zile pesa ambazo Serikali ilikuwa inawajibika kuzirudisha kwa wakulima wa korosho zisiende. Kwa hiyo tunaomba na hizo pesa nazo ziende.

Suala lingine ni suala la mradi wa SAGCOT tunataka hapo mtakapo kuja mje mtupe majibu kabisa kuna taarifa kwamba mradi wa SAGCOT umefutwa kwasababu tumeshinda ku-comply, sasa mtueleze ni kwanini. Pia kukosekana kwa pesa kwenye mradi wa ASDP II ilhali nimeona kwenye vitabu vyenu mnautaja na mkisema kwamba ni mradi wa kimkakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine; nitaomba utueleze Mheshimiwa Waziri, kama ni wewe unahusika au dada yangu pale Mheshimiwa Manyanya ambaye alituambia mbaazi ni mboga. Yeye tunataka mtueleze waziwazi ni shilingi ngapi mpaka sasa hivi imetumika kwa ajili ya kuwalipa wale askari na gharama zima La zoezi la kukusanya zile korosho na je gharama hii itaingia kwenye bei halisi ya kuuzia korosho na ndiyo maana mnashindwa kuziuza hizi korosho? Tunataka sasa mtupe ufafanuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine hapa ni suala la Chuo cha Naliendele. Ningependa kabisa Mheshimiwa Waziri utueleze mna mpango gani hasa mahsusi na Chuo cha Naliendele? Kwasababu tumesema tuna nia ya kutaka kuendeleza hapo. Sisi kwenye kitabu chetu cha Kambi Rasmi ya Upinzani ambayo Waziri wetu alikiweka pale kwenye ukurasa wa 24 kifungu namba 85 ambacho hakikufutwa na Waziri aliyesoma pale hakukisoma kwa wakati ule. Sasa mimi naomba niwasomee na Watanzania wakielewe;

“Katika mazingira ya utatanishi Serikali ilisaini mkataba wa kuuza korosho tani laki moja na Kampuni ya Indo Power ya Kenya mkataba ambao haukutekelezeka licha ya kupigiwa debe na Waziri wa Katiba na Sheria wa wakati huo Mheshimiwa Profesa Palamagamba Kabudi (Mb) na Gavana wa Benki Kuu., Kambi Rasmi Bungeni inataka Serikali kuwawajibisha wahusika wote kwa kulipotosha Taifa na kuliingiza katika hasara kubwa kutokana na mkataba ambao haukufanyiwa upembuzi yakinifu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndio yalikuwa mawazo yetu sisi Kama Kambi Rasmi Bungeni.

KUHUSU UTARATIBU

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru. Nisimame nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Profesa Kabudi kwa kuwalostisha au kuwasababishia hasara wakulima wa korosho Tanzania na kwa kufanya hivyo…(Makofi)

MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwambe, usinifanye kama logic sizifahamu, nimeshaliamulia, kama wewe tusaidie kutoa ushauri ni nini twende mbele.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoshauri…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utaratibu.

MWENYEKITI: Hakuna mtu anayeongea hapa, unampa nani utaratibu, kaa chini, kaa chini.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachoshauri kuna kitu kinaitwa ministerial responsibilities na ninachoshauri kabisa kwa Serikali hii kutokana na ubovu wa mkataba ulioingiwa kati ya kampuni ya Indo Power pamoja na Tanzania, uliosababishia hasara Tanzania na Serikali ya Tanzania nashauri wale Mawaziri wote waliohusika wawajibishwe. Hawa wana haja ya kupisha, kumwacha Mheshimiwa Rais afanye kazi zake vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona hapa Mheshimiwa wetu mama Manyanya pale akishauri anaongea habari za rushwa, sisi kama Kamati tumefanya ziara kwenye ziara mbalimbali tunaambiwa huyu mama ni mpenda rushwa, mpaka wawekezaji wanashindwa kunakuja kuwekeza hapa Tanzania. Sasa leo kinachokuja hapa kutokea yeye anatuambia tunapenda mambo ya rushwa huku anatuambia mbaazi mboga, anakuja hapa mwingine anesema korosho ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume. Wizara hiyo hiyo moja, sisi tunaangalia tu hamuwezi kutudhalilisha hivyo watu wa Mtwara.

MWENYEKITI: Kaa chini. Mheshimiwa Mwambe tuchangie kwa mujibu kwa kuzingatia kanuni za Bunge na kurudisha tena changia hoja yako bila kumtaja Mbunge kwa kumtaja jina.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na control unayojaribu kuifanya ukweli huu utabaki kuwa ukweli. Waheshimiwa hawa Mawaziri tunawalaumu watu wa Wizara ya Kilimo, lakini jambo hili la korosho linahusu watu wa biashara huyu mama yupo pale kwa muda mrefu amekaa na Mawaziri wawili hawezi hiyo kazi ampishe Rais afanye kazi hiyo. (Makofi)

MWENYEKITI: Hakuna mama humu, hakuna mama humu.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa, Mheshimiwa Naibu Waziri yule pale. Tunasema hivyo kwa sababu tuna uhakika sisi tunazunguka kufanya mikutano na wawekezaji wanamlalamikia. Yeye ni mmoja ya watu wanaokwamisha juhudi za watu hata wenye viwanda, anawapa majibu ya hovyo, anakwenda kufanya ziara akiwa na mood, kitu ambacho ni kibaya kabisa. She is out of mood all the time, you see. Kwa hiyo tuombe kabisa waangalie kabisa namna ya kufanya tumsaidie Rais, Rais anawapenda wakulima, wasiowapenda wa kulima na wasiotaka kuwapa hela wakulima ndio walioanzisha haya matatizo, kuanzia waliotayarisha mikataba na sasa hivi hii Wizara inashindwa kuuza korosho. Msmu wa korosho unaanza karibuni, maghala ya korosho yamejaa korosho kule ndani, wakulima wanadai pesa zao, korosho haziondoki baada ya wiki tatu nne zijazo maghala yale korosho tunakwenda kuweka wapi na yenyewe yataharibika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kitu kinaitwa old stock, maana yake ni kwamba zitakapoanza korosho mpya hizi za zamani hazitanunuliwa. Hakuna mtu atakayetaka anunue korosho mbovu ambazo hana uhakika nazo. Kwa hiyo, niombe pamoja na kwamba mnazuia hizi taarifa tuliandika vizuri kabisa kwenye taarifa yetu ya Kambi Rasmi lakini zipo kwenye taarifa yetu hapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine baya kuliko zote, wadau mbalimbali wa korosho hawalipwi pesa zao. Rais ametangaza hata halmashauri hawezi kupewa pesa, halmashauri zetu zitajiendeshaje? Madiwani wanashindwa kulipwa Mheshimiwa Bobali amesema na hiyo sio halmashauri moja. Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ambapo mimi natokea 85% ya mapato yake yanategemea ushuru wa korosho. Leo hii tunaenda kuambiwa pesa hizi hazitapelekwa, halmashauri zitajiendeshaje, tunashindwa kufanya kazi zetu pale kimsingi. Kwa hiyo tunaomba hili jambo liangaliwe kwa makini itumike busara hata kama bei ni mbovu tunafahamu Serikali wanalazimisha kuuza korosho kwa Sh.3,700 ndio ushauri mbovu unaotolewa na hawa watu tunaosema watoke wamuache Rais asadiwe, sisi tuna uwezo, natamani niwe Naibu Waziri Viwanda na Biashara na ndio nafasi yangu upande wa huku kwa sababu hawawezi waliopo pale na sisi ndio kazi yetu. (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine baya kuliko yote tuna Vyama vya Ushirika kule kwetu lakini havipewi pesa zao kwa wakati, tunaomba wamsaidie Mrajisi Mkuu, tunafahamu sasa hivi huyu Mrajisi aliyepo ni wa pili baada ya yule wa kwanza kushindwa kutimiza majukumu yake. Naye hapelekewi pesa imeandikwa kwenye vitabu hapa, Serikali hii ndio haimpelekei pesa, atafanyaje kazi zake, atatimizaje wajibu wake kule chini, tunaua Vyama vya Ushirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, limekuja jambo la kangomba, nishukuru Mheshimiwa pale amesema kwamba kangomba anatambua kwamba ni wajasiriamali lakini tuwaambie kabisa kangomba inazaliwa kutokana na ubovu wa kutekeleza mikakati ya Serikali. Serikali zamani ilikuwa na utaratibu wa kupeka pesa kwenye Vyama vya Ushirika, lakini utaratibu huu umeachwa. Sasa wale wananchi kati ya mwezi wa Tano mpaka wa Nane waniishi kwa kutumia nguvu gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, aibu kabisa, tunazidi kudhalilishwa, Mheshimiwa Waziri anafikiri sisi Mtwara hatuna uwezo wa kuzaana, juzi anaongea na waandishi habari anasema kwamba kuleni korosho kwa wingi zinaongeza nguvu za kiume, sio malengo ya sisi kulima korosho kuongeza nguvu za kiume. Tulikuwa tunalima korosho ili tuweze kupata pesa kigeni, nchi yetu iweze kupata pesa kigeni maendeleo yasonge mbele leo unasimama Waziri ambayo ndio unamsaidia Rais anatuambia kuleni… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. CECIL D. MWAMBE: May your Table be pleased to read my contribution in English as it is research based, it should also be read with Intoxicating Liquour Act. of 1968/ 1966 and 1981.

Justification for cashew value addition in Tanzania. Cashew Apple Processing: In Tanzania, cashew apples are under utilized. In most cashew-growing areas, small quantities of cashew apples are consumed as fruits, though they are not sold in markets as there is no demand for them. A few cashew apples are locally used in production of alcoholic and non alcoholic beverage, but the majority of cashew apples are left to not in the field. Some farmers in Brazil plant cashew primarily for its fruits and the nut is a secondary product which is thrown away, yet they realize a very good profit.

It should be noted that Cashew apple have vitamin C, five times than that in citrus fruits, have high carotene and hence they have good health benefits.

The estimated amount of cashew apple produced in Tanzania is over 1,300,000 tons in major cashew growing areas based on current National cashew production levels. Assuming that only 10% of it (Approximately 130,000 tons) is utilized for production of juice at extraction rate of 70% about 91.1 tons (approximately 91 million liters) of cashew apple juice will be produced. If each liter is sold at a farm-gate price of $o.5,about $45.5 million will be realized in a season.

Equally, if 90% of the remaining cashew apples (Approximately 1,100,000 tons) is used to produce cashew gin (Nipa), farmer could earn even more money than the amount obtained in juice above.

It should be noted that Farmers are already knowledgeable in the production of cashew gin, but they are not aware if there is a law that allows them to distill alcohol as long as they have a valid distilling license from relevant authority. As a result, they produce gin (Nipa) in hiding and once they are caught by Police they face prosecution. This calls the need to create awareness to our farmers. Nipa is called illegal illicit alcohol simply because the producers do not have a licensed to do so. The law is clear that gin (Nipa) can be produced but the producer must have a valid license.

The institute has done a research on cashew apples processing into juice, Jam and Wine. They are in the final stage of commercializing the value addition to juice and wine. Equally the institute has also undertaken research on cashew butter production. They are also in the final stage of studying shelf life of the cashew butter. Broken cashew kernel are sold at Tshs 6,000/kg. Once the 1kg of broken kernels is processed into butter it will produce three jars (each 330 mls) and will be sold at Tsh 6,000 per jar making a total of Tshs18,000.

It should be noted that Cashew kernel is cholesterol free or zero cholesterol therefore it is good for health. These health benefits are the main reason why cashews are quite expensive worldwide. Cashew farmers can double their income if they will add value to cashew kernels, cashew shells and cashew apples.

Convincing farmers to produce Gin (Nipa) for value addition into Ethanol and Methanol will give them more income. The reason for further processing is due to the fact that Nipa has about 2% methyl alcohol which is not good for health. It makes people blind but it is mainly used in hospitals (popularly) known as methylate spirit). This means adding value to Nipa will make our people more health and equally farmers will tend to sell to get more money.

Naliendele Research Institute is in the process of installing a small scale cashew distilling plants to be specific Fractional Distillation Equipment to separate Nipa into methyl alcohol and ethyl alcohol. The objective is to undertake economic analysis to find out how much more farmer can gain if they sale their Nipa to authorize agent. It is estimated that at moment the Nipa is sold at about Tshs 500 per Fanta bottle which is approximately 330 mls. This means Nipa will be sold at about Tshs 1500 per litre. On the other hand, 100 mls of the methylated sprit (methl alcohol 70% v/v) is sold between Tshs 1,000-2000 in pharmacies.

Naliendele Research want to establish how much can be obtained from the Nipa if it is fractionally distilled. Data from this study will show how much more farmer can get from cashew apples which are sometimes thrown away or under utilize. It is no doubt that they will earn more than selling the Nipa at Tshs 1,500 per litre. Another advantage of adding value to cashew apples in creation of employment in the entire cashew value chain.

Reviving Cashew Processing is Possible; Cashew processors in Tanzania complains that they cannot compete with foreign buyers in buying raw cashewnuts in the warehouse because they hardly get raw cashewnuts when bidding. On the other hand, they also complain that they do not make profit due to high prices. One of the reason why they do not make profit is due to the fact that they depend on only one product when processing and these are the cashew kernel. The cashew shells are not value added. They can produce Cashewnut Shell Liguid(CNSL) and shell cakes to be used as fuel.

The CNSL also can produce several products as follows:-

• Brake linings
• Lubricant is high temperature areas
• Cosmetics
• Insecticides to fumigated buildings
• Ceiling boards for high moisture conditions Cashewnut produce the following:-
• Kernels (20-25% by weight of raw cashewnuts
• Cashew shells (70-80% by weight)
• Cashew shell produce CNSL –(20-25%) of weight of raw cashewnuts
• Cashew shell cake for fuels (50-60%) by weight of raw cashewnuts

It is important for the local processors to be given a high priority in buying cashewnuts in the auction though warehouse receipt system. Arrangement can be done to make sure the local processors do not need go to the auction. They need to be allocate 20-25% of the amount the cashewnuts which was given the highest price during auction.

When a foreign buyer bid and get a certain amount of cashewanuts, 20-25% will be allocated for local processors to buy at the same market price. In this way, farmer will continue getting higher prices while the local processors will have an access to the raw cashewnuts until they satisfied.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi nichangie mchana huu kwa hoja tuliyonayo hapa mbele yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nikiwa ninajijenga sasa ili niweze kuchangia hoja yangu, nilikuwa nataka kwanza nitoe taarifa ndani ya Bunge lako tukufu kwamba kuna magazeti ambayo hatuna uhakika sana, lakini kwa sura ya gazeti hili, inaonekana kama wanatumika kulichafua Bunge lako tukufu, kwa sababu kichwa cha habari cha Gazeti la Tanzanite leo, wanasema njama kukwamisha bajeti yafichuka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huku ndani kuna sura za Wabunge mbalimbali, wakiwepo wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Wabunge wa Opposition, nikiwepo mimi pamoja na Mheshimiwa Msigwa, lakini gazeti hili ukienda ukurasa wa kwanza kuna tangazo, ukurasa wa pili, kuna tangazo la ndege hapa, safari za Bujumbura, Entebbe na ndege yenyewe ni Air Tanzania Corporation. Tunaamini kwamba chombo chochote kilicho makini kwenye kufanya kazi zake, na kama kweli kina nia njema ya kusaidia watu wake ikiwa ni pamoja na kuacha matumizi mabaya ya fedha, hatuwezi kuamini sana kama gazeti hili siyo mali ya Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mwandishi ameendelea, ukienda ukurasa wa tatu anasema, mtandao hatari wa rushwa ndani ya TAKUKURU wabainika. Amewataja hapa na watumishi wengi tu, wanaofanya kazi TAKUKURU akiwatuhumu kuchukua rushwa mbalimbali, ni gazeti ambalo Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ikipeleka matangazo yake kwa maana kwamba wanaliamini na kila kinachofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kuweka kumbukumbu sawa, niomba labda ndugu zetu wasaidizi watusaidie wampatie Waziri wakati anajumuisha atueleze, criteria zilizotumika kuwapa nafasi ya kupata matangazo Gazeti la Tanzanite ambalo hata copy zinazochapwa hazifiki 2000 na kwamba hii tunaamini ni matumizi mabaya ya fedha za Serikali, na gazeti hili linatumika na Chama cha Mapinduzi kama sehemu ya propaganda la kudhoofisha watu wanaotaka kusema na kushauri Bunge lako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hayo machache, mimi nina mambo ambayo ninataka niyazungumzie. La kwanza kabisa linalohusiana na suala la ETS (Electronics Tax Stamps) na namna mabavyo tender hii imepatikana, lakini pia nataka niseme juu ya Pays As You Earn, kodi wanayotozwa watumishi wanyonge wa nchi yetu kutoka kwenye mishahara yao, kutakuwa pia suala la vitambulisho vya wajasiriamali ambavyo tunaaminishana Mheshimiwa Rais amevitoa. Sasa nataka Waziri atuambie, Rais ametoa vitambulisho au anauza vitambulisho! Nitakapojenga hoja tutafika hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa kutakuwa na suala linalohusiana na upungufu wa fedha za kigeni pamoja na mauzo yetu nje ya nchi kutokana na kutokuwa na mwendelezo mzuri wa zao la...

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe kuna taarifa, Mheshimiwa Bashe.

MHE. HUSSEIN M. BASHE: Mheshimiwa Naibu Spika, natakakumpa tu taarifa Mheshimiwa Cecil, kwamba Chama cha Mapinduzi ni chama ambacho kinaamini katika uhuru wa fikra na maoni hakiwezi kutumia gazeti la kihuni, lisilokuwa na ethics za editorial, linaloitwa Tanzanite.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka tu nimpe hiyo taarifa, pamoja na kuwa naungana naye, lakini Chama cha Mapinduzi hakiwezi kutumia Tanzanite kwa sababu ni gazeti la wahuni.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, napokea, na nimshukuru kaka yangu Bashe kwamba ni namna gani tutaona sasa Serikali inayojiita makini inafanya kazi na wahuni ambao wenye Chama cha Mapinduzi hawataki kuipokea, kwa hiyo, mwisho wa siku nitazungumza kwenye haya mambo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nilisema hapa nataka niongee suala la ETS, sisi ndani ya kamati na mimi nimekuwa mhudhuriaji mkubwa kabisa wa kamati ya bajeti. Naomba nitoe kielelezo cha pili kinachoonyesha ubadhirifu mkubwa ikiwa ni pamoja na taarifa za PPRA, Gazeti la The Guardian la Jumanne tarehe 3 Oktoba 2017 wakionya namna ambavyo SIPA ilivyopata tender ya kutengeneza stamp kwa ajili ya kuweka kwenye mambo mbalimbali kama alama ya TRA.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba na hii iingie kwenye taarifa hapo na Mheshimiwa Waziri aje atujibu baadaye atakaporudi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi ninachokisema kama Mheshimiwa Rais Magufuli anasikiatunavyoyasema hapa na yuko tayari kuwasaidia watanzania, hatua ya kwanza ambayo tungependa aichukue ni pamoja na kuichunguza Kampuni ya SIPA inayotengeneza electronic stamps zinazotumika na makapuni mbalimbali kuwataarifu Serikali kwamba ni namna gani ambavyo makampuni hayo yamezalisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kampuni hii ni ya kifisadi, Uganda wamekataa hawataki kufanya nayo kazi, Kenya wamekataa hawataki kufanya nayo kazi, nchi zenye uchumi mkubwa kuliko Tanzania. Wanachokifanya wao kazi yao kubwa ni kuhesabu, kwa mfano, packets za sigara. Packet moja ya sigara gharama yake ni shilingi nane, lakini kwenye packet hiyo hiyo ya sigara, Serikali inapata shilingi tatu! Sasa tunataka kufahamu, kwa nini mtu anayefanya kazi ya kuhesabu anapata fedha nyingi kwenye item moja, tofauti na ambavyo Serikali imekuwa ikikusanya kwenye eneo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za stamps ni kubwa zaidi kuliko na gharama za kodi inayokusanywa na Serikali, lakini, Serikali hii na Mheshimiwa Mpango kama yuko hapo very genuine, leo au kesho atakaposimama kuhitimisha hoja yake siku hiyo, atueleze! Tender ya kuwapa hawa watu kampuni hiyo ya uchapishaji ilipatikanaje? Swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, tunataka atueleze, kwamba hao SIPA ambao wako hapa Tanzania, mkataba wao unasemaje. Kwa sababu taarifa zilizoko mtaani na sisi tunazisikia, kama wawakilishi wa watu ni kwamba mwisho wa siku watakapomaliza mkataba wao wa miaka mitatu, wataondoka na mashine walizozileta ambazo Watanzania wamezitumia! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii haiishii hapo tu, mlisema Rais anataka kuwasaidia wanyonge, lakini tumekuja kugundua kwamba Baraza la Mawaziri linataka kumgombanisha Rais na wanyonge kutokana na maamuzi wanayoyafanya. Kampuni hii ya SIPA inapokwenda kwenye vinywaji baridi, tuchukulie labda mfano wa soda, Coca Cola. Kwenye Coca Cola moja, stamp inawekwa kwa shilingi hizo hizo saba, shilingi nane, Coca Cola hii Serikali wanakwenda kupata labda shilingi moja tu, nilitumia hiyo mifano ya namba kwa sababu mambo ya namba kidogo magumu, kwa hiyo, nitaomba Waziri aje atuelezee. Katika kila stamp moja ni shilingi ngapi na katika kila chupa moja wanakusanya shilingi ngapi na mwisho wa siku, hizi gharama zinakwenda ku-affect wanyonge ambao Mheshimiwa Rais anataka kuwatetea! Hili linahusiana na masuala ya ETS. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo hapa lingine, na sisi Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni leo tulitaka tushauri, pamoja na figisu zilizofanyika lakini tungeomba labda baadhi ya maeneo Serikali iyachukulie maanani. Kwenye ukurasa wa 39, wanaongea kuhusu habari ya Pay As You Earn. Wanyonge hawa, sasa hivi kwa takribani miaka mitatu hawajaongezewa mshahara, mategemeo ya wanyonge wengi, wakiwemo walimu, madaktari na watumishi wa umma kiujumla, kwamba walifikiri basi Serikali hii makini inayowapenda wao kama wanyonge, leo ingekuja hapa ikasimama, ikasema tunapunguza kodi ya mishahara ya wafanyakazi na kupeleka kwenye digit moja kama ambavyo imefanya kwa wafanyabiashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini matokeo yake, nao tunawachukua kama sehemu ya mtaji wetu! Ajira hatutoi, fedha kidogo wanayoipata, inakwenda kule, halafu tunasimama hapa tunakwenda kuambiana na Waziri anasimama akijinasbu, tena Waziri wetu ni mtu wa mahesabu ni mchumi, anasema uchumi wetu unakua kwa asilimia saba, inflation imesimama sijui kwa muda gani hata haieleweki, bei ya sukari wakati mwalimu wa shule ya msingi kima chake cha chini kilikuwa shilingi 350,000, sukari ilikuwa shilingi 1,500. Leo hii Serikali ya Awamu ya Tano haijaongeza mshahara hata shilingi moja, bado bei ya sukari imepanda mpaka shilingi 3,000 lakini kodi ya mshahara imeendelea kumtoza kiasi kilekile, sawasawa na miaka itatu iliyopita, jambo ambalo aliliacha Rais, mzee wetu Jakaya Kikwete. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunajiuliza, tunaposema uchumi umepanda, ni nini sasa hapa kinafanyika na ukiangalia hapa kwenye hiki kitabu ambacho nimesema Waziri akakisome kwa sababu ya muda hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna jambo lingine, sisi tunataka tuelezane hapa ukweli, hivi ni kweli tuna nia ya dhati kabisa ya Muungano kati ya Tanzania na Zanzibar? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wazanzibar wengi najua watasimama watakapopata nafasi, lakini sidhani kama wanaweza wakasema jambo hili. Kwenye kitabu chetu tumesema hivi, toka mwaka 1977 liko kwenye ukurasa wa 34, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijawahi kupeleka gawio lao Wazanzibar ili wakafanye shughuli zao za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, awamu hizi zote zimeongozwa na Chama cha Mapinduzi wala siyo CHADEMA, kule pia hivyo hivyo na wale sisi ni ndugu zetu. Sasa Waziri akisimama atueleze, kama wanataka Kisiwa cha Zanzibar kipotee kwa sababu ya masuala ya kiuchumi, asimame na aseme, kwa nini hawapeleki fedha kwa ajili ya Wazanzibar! (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine, suala la vitambulisho vya wajasiriamali, imekuwa kero sana kwa wananchi na Mbunge yeyote wa Zanzibar atakayesimama akisema anaunga mkono jambo hili, akawe kafara ya wananchi hawa ambao wanadhurumiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshuhudia kwa muda mrefu na mimi naomba...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa namna ya pekee kwa kunipa nafasi ya kuchangia asubuhi hii kwenye Wizara ya Maji kama ambavyo hoja iko mezani.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii pia kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa hotuba nzuri. Naamini imetokea hii kwa sababu ya umahiri wa wasaidizi wake akiwemo Naibu Katibu Mkuu, mama yetu tulimwona hapa mchana na kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwenye utendaji wao wa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia namshukuru sana Mheshimiwa Waziri na nichukue pia nafasi hii kumpongeza Meneja wa MANAWASA Masasi, Ndugu David pamoja na Meneja wa Wilaya wa RUWASA Masasi Eng. Juma kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa sababu ni wasaidizi wake na tunapokuwa na shida wakati fulani tunakwenda kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niyaseme machache kwa maana sasa ya kutaka kuboresha kwenye bajeti ya Mheshimiwa Waziri. Nimesikia hapa unatajwa mradi wa maji wa Ruvuma. Sina uhakika sana kama Mheshimiwa Waziri wewe mwenyewe umefika pale, lakini mradi huu ni ukombozi mkubwa sana hasa zaidi kwa sisi wakazi wa Mtwara kwa maana ya Mkoa, Wilaya ya Masasi na hasa Jimbo la Ndanda, kwa sababu utaenda kuangazia kwenye Kata za Usikisi na Matutwe, Mpanyani pamoja na Majani.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninachokiomba kikubwa kwa Mheshimiwa Waziri, mradi huu utekelezaji wake basi uwe wa haraka kwa sababu shida ya maji anaifahamu na ukiangalia katika statistics katika mikoa karibu yote ya Tanzania, Mkoa wa Mtwara ndiyo uko chini kabisa kwenye upatikanaji wa miradi ya maji. Naye ni shahidi, amekuja kule mara nyingi, tumefanya kikao pamoja naye kama Wabunge wote wa Mtwara kwa ushirikiano wetu ili kuweza kusisitiza kwenye jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee kabisa, naomba pia ukamilishwaji wa miradi inayoendelea kwa sababu nayo isije ikawa chechefu. Kuna mradi wa Liloya, Chikukwe utakaohudumia vijiji 26. Mpaka sasa uko pale kwenye asilimia 75 au 80. Tunaomba Mheshimiwa Waziri utakaposimama basi utueleze ukamilishaji wake utakuwa lini kwa sababu unasaidia eneo kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua nafasi hii pia kushauri kwamba pafanyike maboresho makubwa kwenye mradi wa maji wa Ndanda kwa sababu eneo hilo limekuwa linakua kila siku na linaongezeka. Wananchi wale wanahitaji maji ya kutosha. Kwa hiyo, tuhakikishe na mradi ule nao unaboreshwa na kukamilika kwa kushirikiana na engineer wetu wa RUWASA wa Wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nina jambo moja ambalo pia napenda nimshauri Mheshimiwa Waziri kwa ruhusa yako. Tunajua kwamba kuna mtandao wa umeme wa Taifa ambao unaitwa National Grid, lakini sidhani kama Wizara imeshawahi kufikiria kwamba tunahitaji kuwa na mtandao wa maji na wenyewe wa Kitaifa. Kwa sababu tuna Ziwa Tanganyika Tutakapoamua kulitumia Ziwa Tanganyika, Mto Rufiji, Mto Ruvuma, Lake Nyasa pamoja na Lake Victoria tunaweza tukaapata mtandao mzuri sana wa maji wa Kitaifa badala ya hali iliyoko sasa tunahangaika na small water ports ili iweze kusaidia wananchi katika eneo kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naeleza hapo mwanzoni kwamba Jimbo la Ndanda limegawanyika katika mazingira mawili; upande huu wa Mashariki tatizo la maji siyo kubwa sana kama ambavyo iko upande wa Magharibi. Bahati nzuri pamoja na kwamba nimepata nafasi ya kuchangia, tumekuwa tunakaa na Waziri kila mara kujaribu kushauriana namna ya kusaidia zile Kata nilizozitaja. Nami namwomba kabisa Waziri kwa makini kabisa ahakikishe miradi hii inatekelezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, najua kuna ahadi ya visima, kusuluhisha hili jambo kwa muda mfupi, tumepata visima kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, lakini sasa tunataka tupate maji ya uhakika. Ndiyo maana unapokuja mradi wa Mto Ruvuma tunaufurahia sana kwa sababu tunaamini utakuwa ni suluhisho la kudumu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa kuna tatizo. Sasa hivi tunapata misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali kwa ajili ya visima na wakati mwingine kupata hata network ya usambazaji wa mabomba katika maeneo fulani. Nilikuwa hapa na marafiki zangu, mliwaona asubuhi ambao ni watu wa Relief Partners International kutoka Texas, Marekani na shirika lao lingine la Thirst No More. Kumekuwa na malalamiko kidogo kwamba mara nyingi wanapoleta vifaa Tanzania kwa ajili ya kuja kusaidia watu wenye haja ya maji, vinapofika kwenye maeneo kwa ajili ya kutaka kuvi-clear wanakuwa wanatozwa kodi kubwa sana kana kwamba wao wanakuja pia kufanya biashara wakati purely wanavileta kwa ajili ya msaada kutoka kwenye michango ya wafadhili kule kwao. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri hebu angalia namba ya kurekebisha hizi tozo. Badala ya kuwatoza gharama kubwa sana, pesa hiyo ingeweza kuleta hata visima vingi kwenye maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naweza kutoa tu mfano eneo la Ndanda kama ambavyo nimesema toka mwanzo. Tumefanikiwa kupata visima vitatu kwa wafadhili hawa japokuwa wameahidi kupata vingi zaidi. Ila wanavyojaribu ku-import vitu hapa kwa ajili ya kusaidia; walileta rig hapa, wamelipa kodi karibu dola 60,000. Wanaleta vifaa kwa maana ya pumps, wanasema ukinunua pump tatu Nairobi, gharama ile ni sawa sawa na kununua pump moja Tanzania. Kwa hiyo, gharama zetu sisi ni kubwa zaidi kuliko ambavyo inafanyika Nairobi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa wao mara nyingi wanapenda kwenda kununua Nairobi, halafu waje kutumia Tanzania kwa sababu ya ku-save, lakini bado wanapofika border kuna utaratibu unafanyika wa kujaribu kuthaminisha kwamba kwenye SH kodi fulani ambayo inatumika Tanzania pump hii thamani yake ni shilingi 700,000/=. Kwa hiyo, kodi yake itakuwa hivi. Ila kimsingi, wao hawajanunulia Tanzania, wanaingiza kutoka nchi ya jirani kwa maana ya Nairobi (tutolee mfano) lakini bado wanatakiwa walipe kodi kana kwamba wamenunua Tanzania. Kwa hiyo, kodi zinakuwa juu, wanashindwa kutimiza malengo yao na wale wanapata pesa kutoka kwa wafadhili lakini gharama za miradi zinakuwa kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, jambo lingine kama alivyosema Mheshimiwa Eng. Ezra Chiwelesa katika suala la viunganishi, katika miradi hii ya maji ukiiangalia, sehemu kubwa ambayo inachukua gharama kubwa sana ni kwenye masuala ya viunganishi pamoja na masuala ya mabomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna miradi mingi katika maeneo mbalimbali na nita-cite tena mfano wa Ndanda. Tuna mradi kwenye Kata Nanganga kwa maana ya Kijiji cha Mumburu na maeneo ya Mkwera. Kwa bahati mbaya sana mmeamua ku-centralize suala la manunuzi ambalo linafanywa na watu waliopo Mtwara Mjini ambao hawafahamu kabisa mazingira yaliyopo pale Ndanda, kiasi kwamba tunahamasisha wananchi wachimbe mitaro kwa ajili ya kulaza mabomba lakini mpaka mwishoni, mitaro ile inakuja kufukiwa na maji ya mvua kwa sababu mvua zinaendelea kunyesha maeneo haya na ukiuliza kwa nini? Wanasema mtu wa manunuzi kwa sababu anakaa mbali na eneo hili na anasimamia miradi mingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri ahakikishe Masasi tunapata mtu wa manunuzi ili kuweza ku-fast-track hii miradi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mradi wetu mwingine wa Chiwata. Kwa sababu Chiwata ni Kata ambayo iko nje kidogo pembezoni ya Jimbo la Ndanda, imejitenga na iko juu kabisa ya mlima. Tuna mradi pale wa thamani karibu shilingi milioni 400 utaanza kutekelezwa karibuni, lakini bado tunakaribia kwenda kumaliza mwaka, tumebakiza takribani mwezi mmoja na siku chache hizi zilizobakia, pesa hiyo haijaenda na mradi huo haujaanza kutekelezwa. Tunapata wasiwasi kwamba zitabakia siku chache zaidi halafu mtakuja kutuambia kifungu kile kimefungwa, tusubiri sasa mwaka wa fedha ujao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba kama kuna taratibu za manunuzi zinachelewa zipelekwe hapo mapema, hizo pesa zitoke wananchi wale waweze kupata maji kwa sababu wamekuwa wanasubiri kwa muda mrefu na eneo hili limekuwa na kiu kwa muda mrefu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho kabisa, nampongeza Mheshimiwa Waziri kama nilivyosema mwanzoni na sina mengi ya kusema katika Wizara yake kwa sababu tumekuwa tunawasiliana kila mara. Napongeza pia utendaji wa kazi wa watu wake akiwemo Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu kwa namna wanavyotupa ushirikiano; Engineer wetu wa RUWASA wa Wilaya pamoja na Engineer wa MUNAWASA wa kule Masasi kwa ushirikiano wao. Tumekuwa tunawafanyia vikao vya mara kwa mara pamoja na Madiwani kuhakikisha tunapata suluhisho la kudumu la maji yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana na ninaamini kaka yangu na ndugu yangu hapa Mheshimiwa Aweso atakapokuja kujumuisha, atatueleza mikakati yake mahususi kabisa kwa ajili ya Mkoa wa Mtwara, kwa ajili ya Wilaya ya Masasi, kwa ajili ya Jimbo la Ndanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, naomba nichangie kwa njia ya maandishi kwenye hoja iliyoko mbele yetu.

Mheshimiwa Spika, suala la kwanza kabisa naiomba Serikali ifikirie namna ya kurejesha export levy na ifanye kazi kwa malengo yaliyokusudiwa, asilimia 65 ni ya masuala ya korosho na asilimia 35 iende Serikalini.

Suala la pili ni kuhusu Bodi ya Korosho. Bodi hii haipo kwa muda mrefu kabisa, anaachwa Director General afanye mambo mengi wakati hata uwezo wa kufanya hayo mambo hawezi na badala yake ni kukuza migogoro kati ya watumishi na kujinufaisha zaidi, Director General wa korosho aondolewe, ameshindwa kusimamia tasnia, kazi ni maugomvi na wafanyakazi wenzake na wadau wa tasnia kwa sababu tu za kimaslahi.

Mheshimiwa Spika, pia programu za miche na pembejeo bure kwa wakulima zirudishwe ili kuweza kusadia maeneo mengine ambayo yanalima korosho.

Mheshimiwa Spika, bei ya gunia zipo juu sana hali inayomgharimu mkulima. Hata akichangiwa mnunuzi anapunguza bei ya mkulima, kwenye mjengeko wa bei, pale mnunuzi anapoongezewa gharama maana yake anakata pesa kwa mkulima.

Mheshimiwa Spika, ile sheria iliyofanyiwa marekebisho ni Sheria Na. 18 ya mwaka 2009 na kanuni zake za mwaka 2010. Kwa kubadili kifungu Na 17A ambacho kilikuwa kinaelekeza jinsi ya kukusanya export levy na kuigawa ambapo asilimia 65 ilikuwa inatakiwa ipelekwe kwa ajili ya maendeleo ya tasnia ya korosho na asilimia 35 ipelekwe kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. Baada ya sheria hiyo Na. 18 ya mwaka 2009 kufanyiwa marekebisho mwaka 2017 kwenye kifungu na 17A; ikaelekezwa kwamba fedha zote zipelekwe katika Mfuko Mkuu wa Serikali na tasnia ikiwa na mahitaji itaomba.

Mheshimiwa Spika, ukweli ni kwamba tangu fedha hizo zichukuliwe na Serikali tasnia imedorora, uzalishaji umeshuka kutoka tani 320,000 hadi tani 205,000 mnaweza kuona hasara ambayo Serikali imeisababishia industry ya korosho na imepelekea kukosa mapato kwa wakulima, wadau na Serikali yenyewe. Pia tangu hizo fedha kuzuiliwa Serikali imepeleka kiasi kisichozidi shilingi bilioni 15 kwa ajili ya maendeleo ya tasnia wakati madeni na mahitaji ya kuendeleza tasnia ni zaidi ya bilioni 100. Hivyo turejee kwenye sheria ile ya awali ambayo ilikuwa inapeleka export levy asilimia 65.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kwamba wakati sheria inabadilishwa tayari tasnia ya korosho iikuwa inadai zaidi ya shilingi bilioni 150. Hivyo ni vyema fedha hizo zipelekwe kwenye tasnia ya korosho kwa kuwa sheria ikitungwa hairudi nyuma, bali huenda mbele.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na maneno mengi kuhusu suala la unyaufu, na Serikali bado haijaweka wazi suala hili, kuna haja ya kujibu hoja kwamba je, kuna unyaufu ama laa, Serikali ifanye utafiti wa kutosha kwa sababu katika kila jambo linalotokea huwa linaharibu sana mjengeko wa bei.

Suala lingine ni kuhusu madeni ya wazalishaji wa mbegu ambazo zilisambazwa maeneo mbalimbali nchini, watu hawa hawajalipwa, wengine walikopa kwenye mabenki sasa wanafilisiwa, akina mama waliunda vikundi lakini bado hawajaweza kupata pesa na madeni yako wazi, bado kuna watoa huduma ambao wadai Serikali, kuna walio- supply magunia msimu wa mwaka juzi, nao walikopa.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni yamefanyika mabadiliko katika ngazi mbalimbali za uongozi kwenye vyama vikuu, kumekuwa na utaratibu wa kurithishana madeni, COASCO wakafanye ukaguzi hasa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mtwara na Newala, vinginevyo madeni haya yanabaki kwa wakulima na hasara inakuwa kwao.

Mheshimiwa Spika, irekebishwe sheria pia inayowatambua wakulima wote kama wanachama, kwa sababu pesa zinazokusanywa kwenye faida inayopatikana kwenye mauzo wanakula viongozi, sawa na pesa za maendeleo zinazotokana na makusanyo, hazirudi kwa jamii.

Mheshimiwa Spika, matumizi mabaya ya fedha ya Bodi kutoka kwa DG wa Bodi ya Korosho, zaidi ya shilingi bilioni mbili Wizara ichukue hatua za kinidhamu, rejea ukaguzi wa COASCO.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha kwako Taarifa ya matumizi ya Director General wa korosho Kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani. Wizara ya Kilimo inatakiwa kufanya ukaguzi mara moja ili kuepuka hasara ambayo Serikali inaweza kuipata.

TAARIFA ZA MATUMIZI MABAYA YA OFISI KWA MKURUGENZI MKUU WA BODI YA KOROSHO TANZANIA NDUGU FRANCIS ALFRED KWA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA

A: TAARIFA YA MALIPO YA POSHO YA MAKARIBISHO (ENTERTAINMENT ALLOWANCE) AMBAYO AMELIPWA MKURUGENZI MKUU WA BODI YA KOROSHO BILA MUONGOZO WOWOTE NA BILA KUFANYA MAREJESHO KWA KIPINDI CHA MWAKA SASA

Naleta kwako ushahidi wa malipo, na kwa taarifa zaidi ziko uko Bodi ya Korosho.

1. 4/9/2019 000461 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao Wizara ya Kilimo 500,000 840,000 200,000;

2. 26/8/2019 000444 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao Wizara ya Kilimo 500,000 840,000

3. 28/10/2019 000065 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Mkutano wa Wadau wa Korosho Mkoa wa Pwani 500,000 240,000

4. 13/09/2019 000035 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao Wizara ya Kilimo 500,000 1,080,000

5. 3/12/2019 000216 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Ziara Maeneo Mapya ya Uzalishaji- Dodoma,Tabora,Katavi,Songwe,Mbeya &Njombe 500,000 1,200,000

6. 31/12/2019 000249 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kushughulikia Masuala ya Msimu Rufiji 500,000 360,000

7. 7/1/2020 000262 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao na Wakuu wa Wilaya-Tunduru 500,000 120,000

8. 4/1/2020 000130 Dodoma City Square Restaurant Huduma ya Maji na Chakula Kikao na Mh. Waziri wa Kilimo 1,650,000

9. 6/2/2020 000140 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao na ANSAF -Dodoma 500,000 1,080,000

10. 24/02/2020 000162 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao Wizara ya Kilimo 500,000 1,200,000

11. 27/03/2020 000434 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao na Mkuu wa Mkoa Lindi 500,000 840,000

12. 1/11/2019 000072 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Safari Dsm Kituo cha ITV 500,000 180,000

13. 5/11/2019 000075 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao Dsm - issue ya ACA 500,000 600,000

14. 14/112019 000090 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikazi Kipindi TBC 500,000 360,000

15. 20/11/2019 000099 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao na Clouds 500,000 720,000 150,000

16. 9/1/2020 000272 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kushiriki Ziara ya Waziri Mkuu-Pwani 500,000 480,000

17. 20/01/2020 000295 Francis Alfred Mwakabumbe Entertainment Kikao cha Wizara ya Kilimo 500,000 1,200,000 300,000

Mheshimiwa Spika, taarifa hii nimeitoa kwenye mfumo wa Excel unaweza usieleweke sana, lakini kuna umuhimu wa kupeleka wakaguzi ili taarifa hii iwe vizuri. Jumla 8,000,000 11,340,000 650,000 1,650,000

Mheshimiwa Spika, hakuna muongozo wowote unaompa haki DG ya kulipwa posho ya entertainment, ni maagizo yake tu ya mdomo.

Mheshimiwa Spika, hajafanya marejesho mwaka umepita. Matumizi mabaya ya ofisi na madaraka na ufujaji wa fedha za umma.

Mheshimiwa Spika, issue ni matumizi mabaya ya ofisi kwa kuwa fungu hilo halikuwa kwenye bajeti.

Mheshimiwa Spika, DG ametumia bilioni 1.5 kutoka Mei, 2019 hadi Septemba, 2019 kinyume na bajeti iliyoombea fedha hizo Wizara ya Fedha kupitia Wizara ya Kilimo bila idhini ya mamlaka. (Bajeti iliyoombea fedha hizo imeambatishwa).

Mheshimiwa Spika, DG amefanya addendum ya pembejeo kwa msimu 2019/2020 na kampuni za BAJUTA International Ltd. sulphur tani 11,000 na kampuni ya TFC sulphur tani 8,000 bila idhini ya Kamati ya Zabuni (Tender Board). Ukiukaji wa Sheria ya Manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013 (addendum hizo zimeambatishwa kama vielelezo).

Mheshimiwa Spika, usimamizi mbovu wa mikopo ya pembejeo kwa wakulima hivyo kupelekea zaidi ya shilingi bilioni moja kutolipwa msimu 2019/2020. Fedha hizo zisipopatikana italazimu Serikali itafute fedha za kuwalipa wazabuni ambao waliikopesha CBT pembejeo ili iuze kwa wakulima kisha walipwe fedha.

Mheshimiwa Spika, matumizi mabaya ya ofisi, kwa mfano kutotumia muundo wa bodi uliopo katika kufanya kazi za ofisi mfano aweza kwenye idara akamtuma junior staff bila Mkuu wa Idara kuwa na taarifa hivyo kuleta migongano katika Idara na kazi kwa ujumla. Hiyo imetokea katika Kurugenzi ya Fedha, Idara ya Fedha, Kurugenzi ya Masoko, Kitengo cha Manunuzi na Idara ya Utumishi na Utawala.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mchango wa maneno, naomba pia kuchangia kwa maandishi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2017 nilichangia na kuitaka Serikali ianze kutoa leseni kama sheria inavyotaka ili wananchi waweze kupata fursa ya kuweza kujiongezea kipato, kwa kuuza pombe ya Nipa ambayo ni by product ya mazao ya korosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Nipa tumeweza kupata ethanol, methanol na alcohol ambayo inaweza kutumika viwandani. Haya yanafanyika sana nchi jirani ya Mozambique. Hivyo, Watanzania wanavusha hiyo Nipa na kupeleka nchi jirani ambayo wanatumia kujiingizia pesa za kigeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ni suala la Viwanda vya Korosho Masasi na maeneo mengine. Taarifa ya mwisho inasema kuna kesi Mahakamani, lakini katika hali ya kushangaza, viwanda hivyo sasa hivi vinatumika kama maghala na watu hao wanajipatia kipato wakati Serikali inasubiri kesi Mahakamani. Sasa ni wakati muafaka kesi hizi ziishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho kabisa ni kuhusu stakabadhi ghalani na commodity exchange. Kila mara taratibu hizi huwa zinaanza mikoa ya Kusini. Ni kwa nini? Kwa mfumo wetu wa sasa, commodity exchange kwa Tanzania kwenye mazao ya kilimo ni bado kabisa. Hivi karibuni watu wa TMX wamewaandikia barua wamiliki wa maghala ili waje kukutana nao. Kimsingi watu hawa wanataka kulazimisha wakati maandalizi hayajafanyika. Kwa hiyo,

tunaomba suala la commodity exchange likafanyike kwenye mazao mengine. Sasa naelewa kwa nini Mzee Nandonde (Mbunge wa zamani wa Tandahimba) aliomba Mtwara ijitenge. Kwa nini hakuna mikakati ya uhakika na kuwekeza viwanda?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi tena niweze kuchangia kwenye hii Wizara. Hii ni Wizara nyeti sana kwa sababu asilimia 85 ya wakazi wa Jimbo langu na Tanzania nzima ni wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na muda huu, naomba tu niende moja kwa moja kwenye mambo machache ambayo napenda Wizara ya Kilimo ikayarekebishe ili watakapokuja hapa waweze kutupatia majibu. Kwanza kabisa, nataka niwakumbushe kwamba pamoja na nia njema kabisa ya Serikali ya kutaka wakulima wa korosho walipwe kupitia kwenye bank account lakini zoezi hili limekuwa na usumbufu mkubwa. Kwa hiyo, tunaomba upande wa Serikali waangalie namna bora ya kufanya kuwasaidia hawa wakulima. Wamekuwa wakikesha kwenye benki ukifika pale Masasi, Ndanda kwa kweli imekuwa kero mpaka watu wanajuta kwa nini walikuwa wanalima korosho ili pesa zao wakapatie kule benki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna hujuma nyingine inafanyika kwenye zao la korosho ambayo ni ucheleweshwaji mkubwa wa malipo ya wakulima. Tulipokutana hapa na hata tulipokaa kikao cha wadau wa korosho, tulisema kwamba ndani ya siku saba mnunuzi atakuwa amelipwa malipo yake na ndani ya siku hizo hizo saba tunategemea mpaka mkulima naye atakuwa amepata pesa zake. Kwa hiyo, tunaomba hili nalo likaboreshwe Mheshimiwa Waziri akija hapa aje na majibu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu nikufahamishe kwamba kuna hujuma kubwa sana zinafanyika ndani ya zao la korosho zaidi kwenye ugawaji wa viatilifu. Serikali imepanga na wanasema wataboresha uzalishaji wa zao la korosho. Ni kweli dalili zinaonesha hali nzuri kabisa na kwamba Serikali ina nia njema lakini wasimamizi wa jambo hili hawana nia njema ndiyo ambao wanamwangusha Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2015/2016, korosho zilivunwa tani 155 na hela nyingi tu zilipatikana, tukaendelea kuboresha zao hili. Mwaka 2016/2017, zilivunwa tani 265,000 lakini baadaye 2017/2018 tunaratajia kwenda kupata tani 311,000. Sasa ili tupate tani hizo lazima kuwe na mipango mizuri kutoka hatua za awali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo ambalo mimi limekuwa likinishangaza kila mara. Nilipoanza tu kwa mara ya kwanza kuchangia hapa Bungeni nilitoa taarifa za kampuni moja, mimi naendelea kuiita ya kitapeli mpaka pale nitakapojithibitishia, inaitwa Hammers iko Mkoa wa Mtwara ndiyo ambayo kila mwaka imepata tenda za usambazaji wa viuatilifu vya zao la korosho. Mwaka jana walishindwa ku-deliver tani 700 katika tani 3,000 walizopewa order, na ukienda kwenye ripoti ya CAG anaeleza sababu za msingi kwamba hii kampuni haina uwezo na nina taarifa kwamba hata sasa hivi imepewa kazi ya kusambaza. Wenye kampuni hii wanafahamika, wanafanya hujuma kubwa sana kwenye zao la korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wengi wanashikiliwa kwenye vituo vya polisi kwa kuambiwa wanahujumu uchumi. Huu uhujumu uchumi wa waziwazi tunaowaonesha hapa sasa hivi mkaufanyie kazi. Kuna Jukwaa la Wakulima wa Korosho liko kule Wilayani Masasi na wanafanya vikao vingi sana kwa Mheshimiwa Bwanausi kule Lulindi, tumeazimia Serikali isipochukua hatua juu ya ubadhirifu unaofanywa na kampuni ya Hammers kwa sababu wenyewe wanafahamika, sisi tutakwenda kufungua kesi mahakamani kwa maana ya kutaka kusaidia wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye taarifa ya CAG, anasema kwamba wamegundua Hammers walipopewa tenda ya kupelekea viuatilifu ikiwa ni pamoja na salfa walikuwa wanapunguza kwenye ile mifuko kwa hiyo kumepatikana hasara ya tani 144 sawasawa na thamani ya Sh.837,000,000 sasa hii ni uhujuma kiasi gani? Tunasema Serikali inataka kwenda kuboresha uzalishaji wa korosho, wanaopewa tenda kuleta viuatilifu wamekuwa wakihujumu kila mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini jambo lingine tumeambiwa kwamba nchi yetu inaelekea kuwa nchi ya viwanda hatuoni kabisa mkakati wa wazi unaounganisha Wizara ya Viwanda pamoja na Wizara ya Biashara. Hili zao la korosho ni la moja kwa moja ambalo linatakiwa liwe processed kabla ya kusafirisha ili tuweze kuongeza forex hapa sisi tulipo lakini hakuna mkakati wa moja kwa moja, Wizara hii imekuwa haipewi pesa za kusimamia shughuli zake za maendeleo, Wizara hii imekuwa na yenyewe inalalamika kama ambavyo wananchi wa kawaida kabisa wamekuwa
wakilalamika. Sasa hatuoni juhudi za moja kwa moja za Serikali hasa zaidi za Chama cha Mapinduzi kwa sababu ndiyo kinachoongoza ya kutaka kweli kuwakomboa wakulima hawa ambao tunaambiwa kilimo ni uti wa mgongo wa nchi yetu. Sasa leo tuko karne ya 21 lakini bado tunaambiwa kilimo ni uti wa mgongo na wazee wetu bado wanatumia jembe la kukokota na ng’ombe na wengine jembe la mkono ili kuweza kupata mazao. Tutapata kweli mazao ya kuweza kushindanisha na soko la dunia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la umwagiliaji. Tunatambua kabisa Wizara ya kilimo, wao wanasema hili suala liko upande wa Wizara ya Maji lakini kwa nini hiki Kitengo cha Umwagiliaji kisiwekwe pamoja na kitengo hiki cha Wizara ya Kilimo? Kwa sababu wao ndiyo wanatakiwa kuhakikisha mazao ya kilimo yanapatikana kwa wakati lakini pia kuonesha namna ambavyo watatumia hiyo ardhi yao. Matokeo yake kitengo hiki kimepelekwa kwenye sehemu ambapo wao wanachoangalia ni upatikanaji tu wa maji, nani ataendeleza yale mashamba ambayo yanatakiwa kuwepo pale?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwakawa Fedha 2018/2018 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na nia njema ya Serikali kumekuwa na changamoto nyingi sana kwenye sekta ya kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye zao la korosho kuna maswali ambayo bado hayajapata majibu. Kuna mkakati gani wa Serikali wa kuhakikisha uzalishaji wa korosho unaongezeka? Hivi mwisho kabisa wa matumizi ya sulphur ni nini? Kwa nini utafiti ulifanyika taratibu magonjwa mengine ya korosho tukatumia viatilifu vingine ili kuweza kuongeza uzalishaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa za kampeni za hammers kuhujumu usambazaji wa sulphur liko kila mara, lakini bado hao hao ndio wanapewa tender kila mwaka ya kusambaza viatilifu. Hujuma za msimu uliopita zilitosha kampuni hii isipewe kazi hiyo na wahusika wachukuliwe hatua.

Mheshimiwa Mwwenyekiti, kuhusu suala la malipo ya wakulima, kuna tatizo kubwa sana juu ya malipo ya wakulima juu ya kupokelea pesa zao benki. Bado wananchi hawa wanatakiwa kupewa elimu ya kutosha. Suala lingine ni ucheleweshwaji wa malipo kwa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusimamie sana wanunuzi ili wawalipe wakulima mapema, itasaidia kuepukana na hujuma ya kangamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa ni kuhusu soko na uuzaji wa ufuta. Kuna mkanganyiko mkubwa sana juu ya biashara hii. Tunataka kushauri kwamba suala la ufuta kuingizwa kwenye stakabadhi ghalani litaleta usumbufu mkubwa sana. Unyaufu sio suala la kufumbia macho kabisa litaleta shida kubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ufuta ni zao ambalo lina nyauka kwa haraka sana, suala hili linahitaji utafiti mkubwa sana.
Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uamuzi wake wa Kuendeleza Mji wa Dodoma na Kuupa Hadhi ya Jiji
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia. Kama ambavyo wengine wamesema kwamba nia hii inaweza kuwa njema kabisa, lakini njia za kwenda kufikia kwenye utekelezaji wa hii nia ndiyo ambazo watu wanajaribu kuzisema ili tuweze kurekebisha. Ukienda kwenye Majiji, kati ya vigezo ambavyo vinatakiwa ni pamoja na kuwa na idadi ya watu fulani. Kwa mfano, lazima uwe na watu wasiopungua 500,000 ili uweze kutengeneza jiji kama kigezo. Ukija Jiji la Dodoma hili ambalo sasa hivi tunaenda kuliita jiji ni kati ya Majiji ambayo yanaanza kuongoza kwa vituko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais kwa mara ya kwanza ndio amemchagua Meya wa Jiji la Dodoma, kitu ambacho hata kisheria hakipo. Kwa utaratibu, Meya huwa anachaguliwa na Madiwani wenzie kutokana na Baraza la Madiwani, lakini hapa tumeona. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangaia hata presenter wakati mwenyewe Mheshimiwa anaongea pale, he was not happy, yaani hafurahii kile anachokifanya, ni kama amesukumwa au kuna watu wanamlazimisha kukifanya au kuna kitu wanakitafuta ili kuweza kuwafurahisha watu fulani wakati kimsingi vigezo havijatimia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumemsikiliza vizuri hapa Mheshimiwa Mtulia hapa wakati anachangia, wote tungeelekea kwenye mwelekeo ule wa Mheshimiwa Mtulia ili kuweza kupata Jiji bora la kihistoria na la mfano. Viongozi wanafanya jambo la maana, lakini tunakuja hapa ni kupongezana na kusifiana kwenye vitu ambavyo havijafanywa vizuri. Hili siyo jambo jema sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utafiti ulifanyika, wakasema ili kufanya Dodoma iwe mji au Makao Makuu ya nchi kunatakiwa 40 trillion ili kuliboresha hili jiji na wakashauri kwamba hii transition ifanyike kwa muda wa miaka kumi angalau wafikie milioni nne kutokana na udogo na huu ufinyu wa bajeti yetu.

Sasa ukiangalia sasa hivi hata hawa watumishi…

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo unaona hali iliyoko hapa, hata huyo Meya mwenyewe uteuzi wake ulipitia kwa Mheshimiwa Simbachawene wakati huo ni Waziri wa TAMISEMI. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, utaona ile namna ya kutaka kubebana bado inaendelea wakati utaratibu haujaandaliwa. Anatakiwa kuwa Meya ambaye anatokana na uteuzi kwenye kata. Diwani wa Kata na sio mtu wa kuteuliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona watu wanaoteuliwa, usumbufu wanaotuletea, hata humu ndani ya Bunge, wanaoteuliwa wengi ndiyo ambao wanatuyumbisha kwa sababu wanafanya mambo tofauti na mahitaji ya watu wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii nia inaweza kuwa njema lakini njia tunayotaka kutumia kwenda kutekeleza hii nia siyo nzuri. Tulete hiyo sheria ibadilishwe, zifuatwe taratibu zote za kutangazwa kwa Jiji, vinginevyo kule kote ambako wana nia ya kuwa na Majiji na Serikali hii ndiyo ambayo ilisema tunashindwa kuongoza, tunashindwa kupanua maeneo ya kijiografia kwa sababu ya kubana matumizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tuangalie namna ambavyo sisi tunataka kwenda huko mbele, badala yake sasa yote haya yanayotokea ya kuteuliwa tutalazimisha jambo; sasa hivi ukija kuangalia hapa, hata omba omba wanashindwa kutoka Dar es Salaam kurudi Dodoma kwa sababu hapa hapajakaa vizuri bado kwa ajili ya zile kazi zao. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ukiangalia upande wa pili, Watumishi wa Umma wanatakiwa wahamie hapa, lakini huko kuna migogoro. Pamoja na kwamba wake zetu, wengine waume zao ni watumishi wanatakiwa waje kujiunga nao Dodoma, lakini Dodoma bado hapajakaa kuweza kutangazwa kuwa jiji angalau tu kwa kuanzia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa kuna uhaba wa shule, kuna uhaba wa miundombinu, maji, umeme, vinakatika. Juzi tumetoka kulalamika hapa masuala ya umeme, tunaambiwa transfoma zilizopo haziwezi kuhudumia Dodoma kama Jiji. Haya leo tunataka watumishi wote wa umma wahamie hapa; wale wote wakijazana hapa vyoo vyetu vitaziba. Hali iliyoko Dar es Salaam itakuja kujitokeza na hapa tena. (Kicheko)

Kwa hiyo, kimsingi lazima kwanza tuboreshe, tuhakikishe hapa hakuna haja ya kukimbilia hivi vitu, sisi tunakubali watumie muda mrefu kufanya Dodoma liwe Jiji, ibaki kuwa Makao Makuu ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naombe Serikali irudi tena, Mheshimiwa Simbachawene arudi akatafakari, atafute ule utafiti uliofanyika aipelekee Serikali kwamba jamani hebu boresheni kabla hatujaamua kukurupuka na kwenda kutekeleza hili jambo kabla ya wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda kujidhalilisha tukianza kujilinganisha na Nigeria, mara sijui Somalia na kwingine kote. Tuangalie kwanza mahitaji ya wakati kabla ya hivyo vitu havijaja mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana wewe mwenyewe binafsi kwanza asubuhi ya leo kwa kunipa nafasi ya kwanza kabisa kuchangia majadiliano haya kwenye Wizara ya Viwanda na Biashara, lakini pia nikupongeze kwa kurudi tena hapo mezani na kutuongozea Bunge letu. Pongezi hizi nizipeleke pia kwa Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri, watendaji wote na watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara kwanza kabisa kwa hotuba nzuri kabisa, fupi, inayoeleweka, yenye malengo makubwa ya kimkakati, lakini kwa namna ilivyooanisha kati ya Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano wa Maendeleo na ule wa Mwaka Mmoja amechanganya pia humo ndani na Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa maana ya kutaka kuwatekelezea watu na ndio maana tulisema Ilani hii ni bora ukilinganisha na ilani nyingi zilizoko Barani Afrika kwa sababu ina malengo makuu na yanayotekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nichangie hasa kwenye maeneo matano. Eneo la kwanza kabisa ni utaratibu huu unaotumika sasa na Serikali kwa ajili ya kufanya kuhesabu mali zinazozalishwa kwenye viwanda vya vinywaji, almaarufu kama ETS, ufinyu wa bajeti ya Wizara hii, lakini pia pamoja na masuala ya economic drivers ili tuweze kuisaidia Wizara tuweze pia kuisaidia na nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mkakati ambao nchi yetu imejiwekea tunaweza tukaita ni Wizara mama, na mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara tunafahamu mengi na huwa tunayajadili kule ndani, lakini mwishoni lazima tuyalete hapa ili tuweze kuishauri zaidi Serikali na yaingie kwenye taratibu zetu za Kibunge kwa maana ya Hansard ili kuweza kulisaidia Taifa letu. Malengo ya kuanzisha viwanda ni mazuri sana, lakini namna ya kufikia utekelezaji wa mambo haya ndio sehemu ambayo kidogo inaleta kutokufanya vizuri kwenye mambo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nchi yetu imekubali na imechagua viwanda kuwa kama ni sehemu ya economic drivers. Ni kati ya vile vitu vikubwa ambavyo tunategemea nchi yetu ikasimame ili kupandisha zaidi uchumi wetu, lakini pia kuwasaidia wananchi. Tunafahamu kuna mikakati mikubwa ya Serikali kwenye masuala ua Liganga na Mchuchuma, lakini haya ndio mambo yatakayokwenda kupandisha uchumi wa Kusini, matumizi mazuri ya Bandari ya Mtwara pamoja na kubana matumizi kwenye National Reserve kwa maana ya pesa tutakayotumia nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano tulipoanza kutekeleza mradi wa Standard Gauge Railway kutoka Dar es Salaam kwenda mpaka Kigoma na Tabora mwanzoni kabisa tungefikiria tofauti kwa kuanza kuchimba kile chuma kilichopo Liganga na Mchuchuma ili chuma kile kiweze kutumika kutengeneza reli yetu na kiasi cha pesa kinachobakia kiweze kutumika kufanya mambo mengine kama economic driver, lakini kuchagua ni kuanza. Sasa na sisi tulichagua kuanza kutengeneza SGR, sasa hebu tuone kwa sababu pia kuna mkakati wa kutengeneza reli ya Kusini itakayoanzia Mbamba Bay, itapita Songea, itapita Masasi, itapita maeneo ya Ndanda kuelekea Bandari ya Mtwara ili kuweza kukuza uchumi wa watu wa Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, basi tuone namna sasa ya kuanza kutekeleza mradi huu wa Liganga na Mchuchuma ambao umeanza kutajwa siku nyingi sisi tukiwa wadogo kabisa huko na huu ni uchumi mkubwa kabisa utakaoweza kuendeleza zaidi maeneo ya Kusini ambayo kwa namna fulani yalikuwa yanaonekana kama yametolewa kwenye mkakati wa maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado hapo hapo kwenye suala la economic drivers. Ukiangalia kwenye sekta zinazokua vizuri kuna sekta ya ujenzi inakua kwa asilimia 14 na wote tunakubaliana. Kwa mfano tunapokuwa na barabara bora kwa vyovyote vile tutakuwa na biashara nzuri, tutakuwa na barabara nzuri pia zinazoweza kusafirisha mazao kutoka eneo moja kwenda eneo lingine ikasaidia pia kuwakuza wakulima wetu. Suala la umeme pia limekua kwa asilimia nane, lakini pia kuna suala la usafirishaji na lenyewe karibu asilimia 11.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukienda kwenye mchango kwenye GDP kilimo kinachangia almost asilimia 36 kwenye GDP. Viwanda vinachangia asilimia 24 kwenye GDP, lakini ukija kuangalia kwa ujumla bajeti ya kilimo pamoja na bajeti ya kiwanda ni ndogo sana. Mfano kama ambao nilisema pale toka mwanzo kwamba Mchuchuma na Liganga awamu iliyopita kwa maana ya bajeti iliyopita wamepelekewa shilingi milioni 120 tu halafu leo tunasema tunataka tuone Mchuchuma na Liganga vinakwenda kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, haya majadiliano yanayofanywa na Serikali na hivi vitu vimetajwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi, hebu basi fanyeni hima muone namna sasa ya kukuza uchumi wetu kama ambavyo iko China kwa ajili ya viwanda vya chuma, kwa ajili ya kuboresha ile Bandari ya Mtwara ambako uwekezaji mkubwa kabisa pale umefanyika, lakini hatuoni sasa tija ya kutumia ile bandari kwa sababu kimsingi hatuna mizigo mikubwa ya kuweza kupeleka pale. Tunategemea uzalishaji, mzigo pekee mkubwa unaopelekwa Bandari ya Mtwara ni korosho peke yake, kwa nini sasa tusione na kile chuma tunatakiwa tukilete bandarini kwa ajili ya kukisafirisha kwenda nje, lakini pia tutengeneze na viwanda kwenye maeneo hayo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine ambalo pia Wizara ya Viwanda na Biashara wanatakiwa walione, kubadilisha sheria kidogo hasa zaidi kwenye matumizi ya mazao ya shambani na kila mara nimekuwa najaribu kuwaeleza kwenye hili jambo tufungamanishe Wizara ya Viwanda, Wizara ya Biashara pamoja na TIC au Wizara ya Uwekezaji. Hivi ni karibu sawa vitu vinavyoingiliana, vitu vinavyofanya kazi kwa kushabihiana, wawe na mahusiano mazuri ili tuweze kupata definition ya kila kimoja. Tujue majukumu halisi ya Wizara ya Viwanda na Biashara, wafungamanishe na majukumu halisi ya Wizara ya hawa TIC, lakini pia tuangalie kwenye Wizara ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka tu nitoe mfano hapa na kila mara nimekuwa nasema hapa ndani ya Bunge kuhusiana na mazao yanayobakia shambani hasa zaidi baada ya mavuno ya korosho. Huwa wanatupa kitu fulani kinaitwa kochoko, wenzetu wa Scotland mwaka jana wametengeneza ile pombe yao inaitwa Scotish Whisky wameingiza almost 4.5 billion Euro kwa ajili ya kutengeneza hii pombe. Na sisi tunavyo vifaa vya kutengenezea hivi kwa mfano kochoko. Nia sasa wakulima wale wanunue yale mabibo yanayobakia waweze ku-extract tuweze kupata pesa za kigeni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nilisema nitaliongelea hap ani suala la ETS. Hakuna mgogoro kwamba baada ya Serikali kuamua kutumia mfumo huu wa ETS (Electonic Tax Stamps) kwa ajili ya kuhesabu bidhaa kwenye viwanda ni kweli imeongeza mapato na imepunguza kabisa wizi. Sasa suala lililopo ni kwamba, wafanyabiashara wanalalamikia kwamba, kazi ya ETS ni kuhesabu tu, hii Kampuni ya SIPA, inahesabu chupa moja moja wanaweka pale label na kwenda kuiambia Serikali kwamba kiwanda kwa mfano cha Cocacola kimezalisha chupa 500 tunaomba mkazitoze kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa utakuta kwa mfano juice ya mls 200 kodi inayoipata Serikali ni shilingi 1.08, lakini juice hiyo hiyo ya mls 200 fedha anayoipata SIPA kwa kuhesabu kile kichupa kimoja ni shilingi 23. Sasa mtaona hizi gharama zinakwenda kumuongezea mlaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba sana na Katibu Mkuu wa Wizara Mheshimiwa Dotto James ndio alikuwa ni mmoja wa waasisi wa huu utaratibu na yupo huko kwenu, hebu muangalie kwa nini tusitafute kampuni nyingine itakayoweka hizo stamps, itakayokuwa inahesabu kwa gharama nafuu zaidi ili mapato yake nayo yalingane. Haileti tija akilini kuona eti Serikali inapata shilingi 1.08 alafu yule aliyefanya kazi ya kuhesabu chupa na kuitaarifu Serikali kwamba nimehesabu hizi chupa inapata shilingi 25 katika juice ya mls 200 sawa sawa na ilivyo kwenye soda, kwenye Cocacola au na Pepsi au na nyingine gharama ni kubwa sana ya kuhesabu kuliko ushuru unaokusanywa na Serikali kwa hili nalo tukaliangalie vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti ya maendeleo mwaka jana imepata asilimia 23 tu Wizara hii ni kubwa, lakini sio sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuone pia kuhusu masuala ya viwanda vilivyobinafsishwa Mheshimiwa Waziri umeyataja hapa, ninafikiri umekwenda kuyafanyia kazi tuone kiwanda cha Buko cha Korosho pale Masasi kila siku tukiwauliza mnasema kwamba kuna kesi inayoendelea mahakamani, lakini kuna jambo kubwa ambalo tunakwenda sasa hivi kukutana nalo, kuna biashara za korosho zitaanza hivi karibuni na msimu wa korosho unakenda kufunguliwa na suala kubwa sana Waziri la unyaufu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utakapokuwa unamaliza kutoa hotuba yako na hili utueleze tunaomba sasa kufahamu kinagaubaga na Serikali iseme kwa neno moja je, kuna unyaufu ama la kwenye zao la korosho ili sasa wale wanaokuja kufanya biashara ya korosho, wanaokuja kuhudumia maghala waweze kujua wazi toka wanaanza hii biashara kama ni kweli kuna unyaufu au hakuna kwa sababu imekuwa ikileta mkanganyika mkubwa sana.

Mheshimiwa Waziri niombe pia kukukumbusha suala la blueprint. Imetengenezwa blueprint na Serikali hii na kila siku tunasema kwamba tunaweza tukatumia blueprint ili kuondoa vikwazo vinavyowakuta wafanya biashara kwa hilo nalo ukalifanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi uliyonipatia ahsante kwa muda wako. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana na mimi tena kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu. Lakini wakati naanza kuchangia, nikumbushe kidogo historia yangu labda na historia ya Wilaya yetu ya Masasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nafanya hivyo kwa sababu, tuna tatizo kidogo kwa hiyo, nataka niishauri Serikali, niipongeze kwa kazi nzuri walizozifanya. Lakini pia sasa, tukubaliane kimsingi tunakwenda kufanya nini, ili kuhakikisha Wilaya ya Masasi inapata umeme wa uhakika na vijiji vyake vyote pamoja na Majimbo yote na hasa zaidi Mkoa wa Mtwara wote kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utakumbuka Bunge lililopita, nikiwa natokea huko huko Wilaya ya Masasi na ninapoitaja Wilaya ya Masasi Waheshimiwa Wabunge naomba mkumbuke kwamba, ni kati ya wilaya kongwe sana zilizoko nchini Tanzania ilianzishwa kati ya mwaka 1920 na mwaka 1928. Na Wabunge wengi wamepita pale mbalimbali ndiko alikotokea hata Mheshimiwa Rais wa nchi hii wa Awamu zilizopita, Mheshimiwa Rais Mkapa na mimi nilikuwa kwa mara ya kwanza Mbunge nikitokea kwenye Chama cha upinzani, lakini wananchi wa Masasi walinichagua wa Wilaya ya Masasi na Jimbo la Ndanda hasa ambalo lilikuwa jipya kabisa ili niweze kuwawakilisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini wao walitambua kabisa kwamba, wamenichagua ili nishirikiane nao kuja kuisemea Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ndani ya Bunge lako Tukufu na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi toka wakati huo na kipindi chote, inatambua kwamba na imeahidi kila kijiji kitapata umeme na kila sehemu kwenye zile huduma kubwa za kijamii kama kanisa, misikiti na maeneo mengine yatapata umeme. Sasa, wakati naingia kuliwakilisha Jimbo la Ndanda mwaka 2015 tulikuwa na vijiji 42 ambavyo havina umeme kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini mpaka sasa hivi Wizara hii imefanya kazi nzuri na vijiji vilivyobakia bila kuwa na umeme ni 19 tu. Lakini kwa ahadi hapa ya Mheshimiwa Waziri anatuambia kwa sababu, mambo hayo yapo ndani ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kazi hiyo itakwenda kufanyika ndani ya muda mfupi ujao. Lakini, nataka niwakumbushe na kuwapongeza sana Wizara kwa kazi yao, nipongeze pia uongozi wa Wilaya ya Masasi kwa maana ya Management nzima ya TANESCO Wilaya ya Masasi kwa kazi nzuri wanayoifanya, Mkoa Eng. Fadhili pamoja na Kanda Mzee wetu pale Mzee Makota kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwapongeze pia TANESCO kwamba, tulikuwa tunatamani sana sisi tuliotokea Wilaya ya Masasi kwa sababu miradi ya REA kipindi kilichopita, ilikuwa imekwama sana kutokana na aina ya mkandarasi ambaye walimleta wakati huo. Tumepata mkandarasi bora kabisa ninaamini katika wakandarasi wengi walioko pale ambaye ni Namis Cooperate, amefanya kazi nzuri sana ya umeme vijijini kwenye maeneo mengi na ninaamini sasa amekuja kuwa suluhu ya tatizo la umeme, kwenye Wilaya yetu ya Masasi na Mkoa wa Mtwara, Majimbo ya Ndanda, Masasi pamoja na Lulindi na ninaamini kazi hii ataifanya kwa uhakika mkubwa kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nilikutana na Waziri siku chache na nikamuambia mapendekezo yangu, kuna Kata mbili ambazo hazina umeme kabisa, Kata ya Msikisi na vijiji vyake vyote, vijiji vya Namalembo, Liwale pamoja na Msikisi yenyewe. Kata ya Mpanyani na vijiji vyake vyote, ikiwemo Namalembo, Mpanyani, Muungano pamoja na vijiji vingine vilivyobakia havina umeme kabisa. Kwa hiyo, ninaomba kabisa mkandarasi huyu atakapokuwa anakwenda kufanya shughuli yake ya umeme kule, ambaye tunaambiwa sasa hivi yuko site. Kabla hawajaenda eneo lingine lolote kwenda kufanya kazi ya umeme, waanzie na maeneo haya kwa sababu, watu hawa hawana umeme kabisa bora hata Kata zingine na vijiji vingine wanao umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna tatizo kubwa la usambazaji kwa maana ya kwamba, miradi iliyokuwa imekwenda kwenye maeneo hayo ikianzia maeneo ya Nanganga, maeneo ya Mumbulu ukija maeneo ya Mkwera, ukienda maeneo ya Ndanda Kijiji cha Ndolo, ukienda maeneo ya Mwena Kijiji cha Ndunda, ukija Chikundi Kijiji cha Mkalapa, lakini pamoja na maeneo ya kanisani, ukija Chigugu maeneo ya Mbemba pamoja na Mbaju umeme haujajitosheleza. Kwa hiyo, nimuombe sana Mheshimiwa Waziri huduma ile ya ujazilizi sasa wakati TANESCO wanafanya shughuli zao zingine na umeme unasambazwa kule basi wahakikishe kwa namna ya pekee wanakwenda kufanya ujazilizi kwenye maeneo haya, ili wananchi wa Kata hizi wote kwa pamoja wapate umeme sawa sawa, kwa mujibu wa Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi kwa sababu, ndio iliyosimama na ndiyo inayotekelezeka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina mashaka kidogo na namna ambavyo Wizara hii imejipanga kuhusu kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na hapa nataka niongelee suala la gesi. Mpaka sasa hivi gesi iliyoko Mtwara inatumika kwa wastani wa asilimia 10 tu. Lakini nataka niwakumbushe Wizara kwamba, Serikali ilikopa fedha nyingi sana kuona lile bomba linatolewa kutokea Mtwara na linapelekwa Dar es Salaam kwa ajili ya matumizi hii ni kwa ajili ya kukuza uchumi wa Mtwara na watu wake.

Mheshimiwa Spika, lakini mkumbuke pia kwamba, sehemu kubwa ya uchumi sisi tunategemea kwenye gesi kwa sasa, tunaomba sasa basi miradi hii itekelezwe mapema sana. Kwa sababu, sehemu pekee iliyobakia tunafanya tu kazi za korosho, ndio maana inapofika wakati wa korosho maana wote tunalazimika kusema kwa sababu, ni sehemu ambayo tunategemea kupata fedha kidogo. Lakini miradi ya gesi ikianza hata uzalishaji wa korosho nao utaongezeka na sisi tutakuwa tuna amani kwa sababu, na bandari yetu ya Mtwara pamoja na Mtwara Corridor kwa ujumla, kwa maana ya hii Southern Reli pamoja na bandari ya Mtwara, ambayo Serikali imeweka fedha nyingi na yenyewe itaweza kufanya kazi zake vizuri kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimuombe kabisa Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-windup, atueleze mkakati madhubuti wa kurudi tena kwenye matumizi ya gesi kujenga kile kiwanda kwa ajili ya kuchenjua hii gesi asilia maeneo ya Lindi, kwa maana ya mradi wa NLG na matumizi makubwa ya gesi. Kwa sababu, inashangaza kuona wilaya kama wenzetu Wilaya ya Madaba, ambako anatokea rafiki yangu hapa, Mheshimiwa Muhagama kwamba ni wilaya iliyoanzia mwaka 2015, unailinganisha na Wilaya ya Masasi yenye miaka zaidi ya 50, kwa sababu imeanza miaka 28 kabla ya uhuru wa nchi yetu kwamba, Madaba wao wamejitosheleza kwa umeme na vijiji vyake vyote vimepata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini sisi bado tunaongelea umeme uliobora kwa maana ya kutokukatika katika lakini pia, umeme unaotosha kwenye vijiji vyote. Sasa mtutendee haki wilaya hii ni ya siku nyingi na kama vigezo vya mgawanyo wa mikoa, ilikuwa ni kutokana na umri wa wilaya, Wilaya yetu ya Masasi ingekuwa imeshakuwa mkoa siku nyingi kabisa kabla hata ya wilaya nyingi za Tanzania hii hazijazaliwa. Hata mikoa mingine imeikuta Wilaya ya Masasi ikiendelea ku-exist. Kwa hiyo, niombe sana kazi hii muifanye kwa uhakika kwa sababu, sisi tunatoka kwenye wilaya kongwe kabisa, lakini miundombinu yetu sio mizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa nashauri Serikali kwamba, iangalie uwezekano wa kuwa na line maalum kabisa inayokwenda Masasi kwa sababu, itapita Ndanda kutokana na ukuaji wa eneo hili kwasababu, sasa hivi ni kama business hub. Ni Mji mkubwa kibiashara unaotegemewa sana na Mkoa wa Mtwara, ukiacha Mkoa wa Mtwara wenyewe mjini kwa sababu, sehemu kubwa ya uchumi wao walikuwa wanategemea uchumi wa gesi. Lakini Wilaya ya Masasi sehemu kubwa ya uchumi wao sasa hivi ni masuala ya mazao ya korosho.

Mheshimiwa Spika, lakini pale ndipo kuliko na junction ya barabara inayokwenda Songea, inayokwenda Nachingwea, inayokwenda Newala na inayorudi Mtwara Mjini. Kwa hiyo, ni eneo kubwa la kibiashara lakini uchumi wake unazorota kutokana na matatizo ya kukatikakatika umeme mara kwa mara. Kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwa Waziri hakikisha sasa ile line ambayo iko kilometa 120 kutokea Masasi kwenda Mahumbika, mnatupa line pekee ambayo haitakuwa interrupted hapa njiani. Itoke Mahumbika moja kwa moja iende Masasi moja kwa moja kiasi kwamba, likitokea tatizo lolote la umeme njiani ni rahisi kuirekebisha na bajeti yake nadhani imeletwa kwenu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wataalam wa pale wanatuambia, nilikuwa naongea na Engineer Fadhili hapa karibuni kwamba, mkiamua kutumia nguzo za cement itatumika kama bilioni 10, lakini mkiamua kutumia nguzo za miti ni kama bilioni 6 ambayo sio njia ya kudumu sana. sasa hicho ndio kiasi pekee tunachokiomba, hatutamani miradi mikubwa kama ile iliyofanyika kule Namtumbo hapo karibuni. Kama miradi iliyofanyika Madaba, kama ambavyo walisema pale mwanzoni, tunataka mradi ambao utatuhakikishia umeme wa uhakika Masasi ili tuweze kupata umeme ambao utakuwa haukatikikatiki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaposema Masasi ni Wilaya yenye Majimbo matatu matatizo yetu sisi yanafanana, tunatambua hapa Mheshimiwa Waziri Mheshimiwa Geofrey kila mara huwa mnakutana. Kwa hiyo, ona namna na wewe ya kumshauri Waziri mnakuwa wote kwenye cabinet tuweze kupata Masasi umeme wa uhakika. Tuweze kupata Lulindi umeme wa uhakika, tuweze kupata Ndanda umeme wa uhakika kwa sababu Mji huu unakua na ili wawekezaji waweze kuja eneo letu, ni pamoja na kupata uhakika wa umeme pamoja na miundombinu mingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo niendelee kumkumbusha Waziri kwamba, ili kufanikisha vizuri kwenye hii Mtwara Corridor na matumizi ya bandari ya Mtwara basi ihakikishe sasa miradi ile ya gesi inafufuliwa. Kulikuwa kuna ahadi ya Serikali kutengeneza kituo cha uzalishaji wa umeme wa gesi Mtwara, nakumbuka ilikuwa kama KVA 380 hivi au kitu kama hicho, lakini hatuoni chochote kinachoendelea. Sasa ni muda mrefu na tuone kwamba, tutumie advantage iliyopo sasa kufufua miradi yetu ya gesi kwa sababu, si vizuri sana kusema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kutokana na mgogoro ulioko Mozambique bado watu wanatamani kuwekeza Tanzania kwa sababu, ya amani iliyopo, mazingira yetu ni rafiki kabisa kwenye masuala ya uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa nikuombe, kama ambavyo nimesisitiza toka mwanzo mkandarasi ameshafika Masasi ambaye ni Kampuni nzuri sana ya Namis Cooperate, akaanze kazi kwenye Jimbo la Ndanda, kwenye Kata ya Msikisi na Kata ya Mpanyali tu. Akimaliza hapo huko kulikobakia kwingine sisi wenyewe tutakaa tutaongea na kujua nini tunataka tukifanye, lakini naomba kazi hiyo ikafanyike hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nisisitize tu kuhusu usambazaji umeme vijijini, kwenye vijiji nilivyovitaja kwasababu, maeneo haya yanapitiwa na umeme mkubwa unaokwenda Masasi.

Mheshimiwa Spika, nishukuru sana kwa nafasi hii na ninaunga mkono hoja kwa asilimia 100. Naomba haya niliyoshauri Serikali basi ikayafanyie kazi kwa mujibu wa Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi. Ahsante sana kwa kunisikiliza. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee kabisa nishukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia mchana huu kwa lengo mahususi kabisa la kutaka kuishauri Wizara na Serikali katika maboresho ya bajeti zilizowasilishwa pamoja na bajeti hii tunayoijadili wakati huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ya pekee pia nipongeze maamuzi mbalimbali yanayofanywa na mama yetu, Mheshimiwa Samia Suluhu, kwa ajili ya manufaa ya Taifa hili. Na moja kubwa kabisa ni hili suala la Liganga na Mchuchuma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimekuwa Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara kwa muda mrefu sasa. Awamu iliyopita, kipindi changu cha mwisho, nilikuwa Mjumbe hapo na sasa hivi pia nimeendelea kuwa Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la Liganga na Mchuchuma limekuwa likirudi mara nyingi sana, lakini hata hivyo, tulivyojaribu kuwashauri Serikali na wenyewe tulijitahidi sana kuongea humu ndani tukionesha kwamba Liganga na Mchuchuma ni sehemu ambayo inaweza ikatuletea mapato makubwa sana kama nchi. Lakini mama sasa ameamua kuwa jasiri na anataka mradi huu utekelezwe, na tunaomba sana ukatekelezwe kadri ya alivyosema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwakumbushe pia kwamba machimbo haya na miradi hii ya madini mikubwa ndiyo yenye uwezo mkubwa sana wa kuleta mapato mazuri kwenye nchi yetu. Nikumbushe pia kwamba mama kafanya maamuzi mengine magumu sana kwenye Mradi wa Mbunyu uliopo kwenye Jimbo la Ndanda, kwenye Kata ya Chiwata, kwa sababu utekelezaji wake nao umekuwa wa kusuasua lakini utanufaisha Mkoa wa Mtwara, Wilaya ya Newala Vijijini, Wilaya ya Ruangwa pamoja na Wilaya ya Masasi. Kwa hiyo tunaomba kabisa na wenyewe wakauangalie waone namna ya kutaka kwenda kuutekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu pia wakati wa utekelezaji wa Mradi wa Liganga na Mchuchuma kutakuwa na reli pale inayotoka Liganga kuelekea Mtwara kwa maana ya bandarini. Kwa hiyo, matumizi ya bandari yatakwenda kufanyika. Lakini sasa madini hayo ya mbunyu (graphite) yatakayokuwa yanatoka Chiwata, ni rahisi kuyashusha pale Kata ya Chigugu nayo yakapakiwa kwenye reli hii yakaenda bandarini Mtwara na kuweza kusafirishwa kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kufanikiwa kutokana na namna ambavyo Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameleta hii bajeti yetu, na nimuombe Mheshimiwa hapa asiingie kwenye mtego ambao Mawaziri wengine labda waliopita walikuwa wanaingia. Mara nyingi tumekuwa na utaratibu wa kupunguza ama kuongeza kodi, lakini ni mara chache sana tumekuwa tuna utaratibu wa kufikiria kuhusu vyanzo vipya vya mapato kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo moja nilikuwa nalifikiria tu peke yangu, kwamba tuna haja ya kuishauri Serikali ili iweze kupata vyanzo vipya vya mapato, sasa sijui kama Mheshimiwa Waziri ameshawahi kufikiria. Ukiwa bandarini Dar es Salaam na maeneo mengine, utaona magari mengi sana yanakwenda nje ya nchi yamewekwa zile label za IT, zimeandikwa tu kwa marker pen.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sijui kama wasaidizi wako wameshawahi kujiuliza siku moja wakiamua vile vibao viandikwe kwa kutumia vibao halali vya number plates tutakusanya VAT shilingi ngapi na kiasi gani kingekwenda kusaidia kwenye maendeleo ya wananchi wetu. Kwa sababu watu hawa pia wamekuwa wanaharibu barabara. Lakini ukiandika kwa ile marker pen pale unachajiwa shilingi 10,000 tu ambayo inakwenda moja kwa moja kwa mwandikaji na Serikali pale haipati kitu chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona hapa tunaongeza kwenye kodi ya mafuta kwa maana ya road toll ili wananchi wakalipe. Na mpaka sasa Mheshimiwa Waziri ukumbuke Watanzania karibia milioni 2.5 ndio wanaolipa kodi, katika milioni 60. Na tumekuwa na taratibu sasa za kuwabana sana wafanyakazi pamoja na wafanyabiashara. Kwa hiyo, tunawakamua kwa nguvu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tujaribu kuangalia vyanzo vipya vya mapato ili viweze kuwasaidia hawa watu kupokea. Kwa hiyo niombe kabisa hili jambo la number plates mkaliangalie, mkaangalie pia hili wazo la mama kwamba Liganga na Mchuchuma sasa ianze kufanya kazi vizuri. Nia yetu na nia yako kama Waziri iwe ni uboreshwaji wa sera za mapato na matumizi na kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili iweze kusaidia nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, umeongea vizuri sana suala la ETS. Lakini pia umeongea kuhusu suala la industrial sugar, na Jirani yangu hapa, dada yangu Mheshimiwa Hawa naye amelisema, na Waheshimiwa wengine huku nao nimesikia wakiwa wanalisema. Sasa ni vizuri na wewe mwenyewe kwenye taarifa yako umesema umeamua kuondoa kabisa hii tozo ya asilimia 15 kwenye industrial sugar ili iweze kuwasaidia wafanyabiashara kuweza kupata an extra working capital. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukumbuke kwamba Serikali sasa inadaiwa. Ile ambayo mliishikilia zamani mnasema nini kuhusu hii? Kuanza kuwapatia kuanzia sasa na kuendelea wakati huko nyuma zaidi ya miaka kumi hamjawahi kuwa- refund na yenyewe ni ngumu. Na pale umeonesha kidogo kwamba inapunguza mapato ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikukumbushe tena ile ilikuwa ni tozo ambayo mwisho wa siku ilitakiwa iwarudie wenyewe. Haikuwa mapato ya Serikali, Serikali mlikuwa mnaitunza. Sasa mfikirie namna ya kuwarudishia ili waongeze mitaji kwenye uzalishaji wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni sawasawa na VAT. Sijasikia hapo vizuri mkakati wako mahususi wa kuona VAT refunds zinarudi kwa hawa wawekezaji, zinarudi kwa hawa wafanyabiashara ili waweze kukuza mitaji yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine la kuongeza mapato ni suala la ETS. ETS Waheshimiwa Wabunge ni Electronic Tax Stamp ambayo imekuwa inawekwa kwenye vinywaji. Na sisi kwenye Kamati tumeongea mara nyingi. Tunaishauri Serikali kwa mara nyingine, mkataba huu haukuwa bora sana, unasimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara, sasa hatuna uhakika hili jambo linawahusu ninyi moja kwa moja, linawahusu watu wa Viwanda na Biashara, lakini mkakae na kujadiliana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi hii ya kuhesabu chupa moja kwa shilingi 10 wakati Serikali inakwenda kukusanya kodi ya shilingi tatu kwa kuhesabiwa kwa shilingi kumi; tunamnufaisha nani? Kama tunaona kuna uhalali wa kufanya hilo jambo basi niishauri Wizara yako kimkakati kabisa sasa kazi hii ikafanywe na TRA, iwe sehemu ya kuongeza mapato. Kwa sababu hakuna haja ya kutumia gharama kubwa kutayarisha utaratibu wa kukusanya kodi halafu unakwenda kukusanya kodi ndogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, ukipata muda nitakuelewesha kwenye hili kwa sababu wafanyabiashara walikuja kulilalamikia. Kuna kampuni inaitwa SIPA ndiyo inayofanya kazi ya kuhesabu vinywaji tuseme.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano chupa moja ya Coca-Cola inatakiwa ilipiwe kodi ya shilingi tano, anayekwenda kuhesabu chupa na kumwambia TRA kwamba Coca-Cola wamezalisha chupa 20 katika chupa moja analipwa shilingi 10; hii siyo sawa. Muone namna sasa ya kuondoa ili kama inawezekana na kuna ulazima wa kufanya hivyo basi TRA wakafanye hii kazi ili iweze kuwanufaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti ni nzuri kama walivyosema wengi, lakini tuombe sana sasa – na Wabunge wengi hapa wamesema ni kazi nzuri – basi ile shilingi mia iliyotengwa kwenye mafuta lazima tuhakikishe inakwenda kuwa ring fenced na iende huko TARURA kwenda kufanya kazi kwa wakati. Utaratibu wa kupeleka baada ya miezi sita, baada ya mwaka mmoja na wakati mwingine unaambiwa wanapeleka kwa Zimamoto siku za mwisho kabisa za kumalizia bajeti, siyo mzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wana shida kubwa sana ya barabara huko vijijini, wananchi wana shida kubwa ya madaraja pamoja na vivuko. Sasa hela hii ikikusanywa na ukija hapa utueleze kwamba pesa iliyokusanywa kwa ajili ya miradi ya maji na miradi ya barabara awamu iliyopita, kwa maana ya bajeti iliyopita, imekwenda mpaka sasa kiasi gani. Hiyo chenji iliyobakia itapatikana lini ili mkakamilishe… kwa sababu hii ndiyo miradi…

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Shabiby.

T A A R I F A

MHE. AHMED M. SHABIBY: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe taarifa mzungumzaji kwamba haohao SIPA wanaotafuna sasa hivi upande huu ndiyo haohao walikuwa wana tenda ya vinasaba. Kwa hiyo bado wanaendelea kutafuna. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaikubali taarifa hiyo. Na nataka nimuongezee tena hapa Mheshimiwa Waziri kwamba watakapokwenda kufanya review ya hizi kodi mbalimbali wanazoziingiza kwenye mafuta.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo dada yangu pale, Mheshimiwa Paresso, amesema, wakaangalie sasa kwamba mpaka sasa kwenye mafuta kuna kodi zisizopungua 16. Zinakaribia sasa hivi kufikia shilingi 900, tunakaribia kwenda shilingi 1,000. Kwa hiyo kwenye bei ya mafuta ya shilingi 2,5000, shilingi zaidi ya 700 inakwenda kama kodi Serikalini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba sasa mkafanye review tuangalie vyanzo vipya vya mapato, tupunguze hizi kodi mbalimbali ambazo mwisho wa siku zinakwenda kumgandamiza mwananchi. Kwa sababu kwa namna yoyote ile, unapoongeza shilingi 100 kwenye mafuta wasafirishaji nao karibuni utasikia wameongeza gharama za usafirishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nauli kwa mfano kutoka Ndanda kwenda mpaka Masasi badala ya kuwa shilingi 2,500 au 1,500 tuliyoizoea sasa hivi, tunaweza tukaanza kuchajiwa shilingi 3,000 kwa sababu gharama ya mafuta imeongezeka. Na lazima hapa ukumbuke kwamba tunapoongeza hizi gharama za mafuta lazima tuone namna ya ku-balance tutafute sehemu nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipongeze sana bajeti yako, na nikushauri tena kwamba weka malengo katika miaka mitano hii mama ikimpendeza na Mungu ikimpendeza, ukiendelea kuwa hapohapo basi twende kwenye utekelezaji wa budget deficit iwe single digit. Badala ya sasa ambapo tumetekeleza bajeti kwa asilimia 75 mpaka 80, tunatamani siku moja tuambiwe bajeti yetu imetekelezwa kwa asilimia 95 na kuendelea, ili tuwe tuna single digit, ndiyo tutakuja kuona manufaa makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti hii tunapanga hapa tunaomba ikatekelezwe kama tunavyosema. Wakati mwingine inatokea ama mnachelewesha kupeleka pesa, mnataka tena watu kule chini waanze tena kuleta taarifa juu; hili siyo jambo jema. Utakapokuja kwenye mid-year review au quarterly review basi tuone Waziri unapeleka pesa kadri zilivyopangwa hapa na Wabunge ili zikafanye kazi inayokusudiwa na tuone matokeo chanya kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru sana kwa nafasi uliyonipatia. Ahsante kwa muda wako. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuchangia kwenye Wizara tajwa hapo juu. Niishauri Serikali kwamba, iachane na mradi wa Bwawa la Lukuledi na badala yake iongezee nguvu Idara ya Maji ya MANAWASA ili iweze kufikisha maji safi na salama kutoka Masasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la elimu bure. Suala hili liangaliwe kwa umakini, elimu bure imeshindwa kuangalia suala la quality badala yake inaangalia quantity. Kuna haja gani kufurahia idadi kubwa ya wanafunzi, lakini Walimu huna?

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la vituo vya afya na zahanati. Bahati mbaya sana kumekuwa na utata mkubwa juu ya ramani, Serikali iseme wazi kabisa juu ya suala hili, wananchi wanahitaji jengo la kupatia huduma. Pale Serikali itakapopeleka pesa basi ndipo ramani hizo zitumike, wananchi hawawezi kukamilisha na kupata huduma, ndiyo mahitaji. Nishauri kwamba, ramani ziendane na mahitaji ya eneo husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na tatizo kubwa sana la madeni ya wazabuni ambao walitoa vyakula na huduma mbalimbali kwenye shule na vyuo. Watu hawa wengine mpaka wamekufa kwa pressure, tuwalipe wazabuni hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Wilaya ya Masasi. Zimetengwa pesa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya. Nataka kufahamu kazi hii itaanza lini na itafanyika wapi?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia, maalum kabisa ninataka niongee na Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake hasa zaidi waweze kutusaidia sisi wakulima na kipekee kabisa niongee kuhusu wakulima wa korosho.

Mheshimiwa Spika, ukifika Mtwara maeneo yote ambayo utapita wananchi wa kule wanalima korosho, lakini kwa bahati mbaya kabisa ukilinganisha maisha yao halisi na sifa tunazopeana hapa ndani Bungeni kwamba wananchi wa Mtwara na Lindi pengine wa kusini kwa ujumla ni wakulima wa korosho wanaongeza pato kwenye mapato ya nchi yetu hawafanani kabisa na hicho tunachokisema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanaonufaika ni wasimamizi au wa Ushirika au wasimamizi wa Bodi ya Korosho au Wasimamizi wa Vyama Vikuu vya wanaosimamia manunuzi, lakini wakulima kama wakulima hawanufaiki. Mheshimiwa Waziri nilimpa taarifa na nilipeleka mchango wangu pia kwenye maandishi na Mheshimiwa Naibu Waziri pia kwamba kuna ubadhirifu mkubwa sana umefanyika ndani ya Bodi ya Korosho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho ndiyo maana Wabunge wote hapa wanaotokea maeneo hayo wamelalamika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaomba ukafanye ukaguzi pale ndani kuna pesa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zimetumika nje ya utaratibu kabisa na tunamwambia hapa Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anamaliza na ku-windup hapa atueleze hatua anazochukua dhidi ya Mkurugenzi huyu kwa haraka kwa sababu vinginevyo sisi tunakwenda nyumbani kufanya mikutano na wananchi wetu na tutakwenda kuwaeleza kwamba Waziri anamlinda na kumtetea Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho kwa sababu labda ana maslahi binafsi na yeye, lakini sisi hatusaidii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mtu mwingine ni Meneja wa Chama Kikuu cha Msingi cha Mtwara ambaye ni Meneja wa MAMKU Mheshimiwa Naibu Waziri anamfahamu naye ni mmoja wa watu wanaonufaika sana na zao la korosho bila kuwa na shamba hata nusu eka nyumbani kwake na wenyewe tunaomba kabisa na siku ya uchaguzi mkuu pale wakulima walimkataa, wakataka kabisa na kuandamana.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri mwenyewe alihusika kupiga simu akawaambia jambo hili tutahakikisha tunapata suluhisho siku chache zijazo, sasa hivi mwezi mzima umepita hakuna hatua yoyote aliyochukua Mheshimiwa Bashe na yeye tunamuomba kama ana maslahi binafsi na huyu ndugu basi amuondoe Mtwara ampeleke kwao Tabora akasaidie kwenye mazao mengine kwenye Korosho hawezi kufanya kazi. (MakofI)

Mheshimiwa Spika, jambo jingine ni suala la, masuala ya stakabadhi ghalani, Mheshimiwa Mulugo hapa jana aliongea kwa uchungu mkubwa kabisa suala la stakabadhi ghalani akiomba Serikali iondoe mfumo huu. Mheshimiwa Bashe hapa alikuja akaongea mwenyewe ndani ya Bunge hili labda kama alikuwa ameamua kufanya utani na sisi Wabunge kwamba mazao ya maeneo ya Dodoma, Songwe, Katavi wasitumie huu mfumo kwa sababu hawajiandaa kutumia huu mfumo.

Mheshimiwa Spika, lakini sisi kwetu kwenye zao la Korosho mfumo wa stakabadhi ghalani ni sehemu ya ukombozi na uhai, tunachotaka sisi kikubwa mfumo huu uboreshwe na siyo kuondoa kwa sababu umekuwa ukiwasaidia wakulima. Lakini pia, urasimishwe ukipata stakabadhi yako ya ghalani kabla hujalipwa kwenye ghala lako uweze kutumia stakabadhi kwenda nayo hata hospitali na hospitali zikutambue kwa sababu tuna hospitali za Serikali uweze kupata matibabu tuachane na hivyo vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye hotuba yako pia uliyotuwasilishia hapa umeongea kuhusu skimu, lakini mimi naweza kukwambia umeleta utani mkubwa kwenye masuala ya skimu umeitaja skimu ya Ndemba halafu inaonyesha kwamba ina eka moja na hii ni skimu ya Serikali, umeitaja skimu ya Maparagwe yenye eka 450, lakini Kijiji chenyewe cha Maparagwe hakifikii hata eka 30. Mheshimiwa umetaja hapa skimu ya Liputu yenye eka 10 hizi ni skimu za Serikali, umetaja Skimu ya Chingurunguru eka tano ni uongo kwa sababu Chingurunguru hata shida ya maji ya kunywa kule ipo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, waambie watalaam waende hatuna hata maji ya kunywa tuanze sasa kutoa maji mengine ya kumwagilia hicho kitu hakuna. Umetaja skimu ya Ndanda yenye eka 350 eka zinazotumiwa pale hazizidi eka thelathini na wananchi wamekuwa na migogoro kila siku tunataka sasa tujue Serikali kama ilipeleka hapa pesa zimetumika namna gani kwa ajili ya watu hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna suala hapa pia ambalo pia umelitaja na waheshiwa Wabunge wote wamelichangia kuhusiana na suala la pembejeo ambazo zinakwenda kugawiwa sasa na mfumo wa Serikali.

Waheshimiwa Wabunge wameshauri kwamba Serikali itafute pesa na ione namna sasa ya kulipa pembejeo hizi badala yakwenda tena kuwakata wakulima ambao wamekuwa wanakatwa kila wakati na sheria haiwezi kurudi nyuma.

Mheshimiwa Spika, kama mnataka kuanzisha huu utaratibu zile pesa ambazo zilikatwa shilingi bilioni 210 kabla sheria haijabadilishwa ziko wapi? Zilitumika kufanya jambo gani? Kwa nini hizi zisitumike wakati huu na sisi Serikali kuturudishia ili tuendelee kwenda mbele na tuweze kuongeza mavuno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine hapa ni suala la TARI. Wananchi wanakatwa shilingi 25 kwa ajili ya Mfuko wa CBT lakini wananchi pia wanakatwa shilingi 25 kwa ajili ya kupeleka kwenye vyuo vya utafiti. Tunataka Serikali itueleze shilingi ngapi mpaka sasa zimepelekwa kwenye utafiti. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii, nasubiri majibu. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Hesabu za Serikali za Mitaa zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021, na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2021
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia jioni hii kwenye taarifa zilizopo mbele yetu kwa nia ya kutaka kulisaidia Bunge lakini pia kulisaidia Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee sana ninatoa pongezi kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi kikisimamiwa na Mheshimiwa Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan ikiongozwa na Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Majaliwa kwa kazi kubwa zinazofanyika Tanzania na maeneo mbalimbali kwenye Majimbo yetu na kila mtu anaona sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumepewa nafasi kubwa sana ya kuwasaidia Watanzania, kwa wale wapenzi wa mpira wa miguu wanafahamu kuna wakati wanafika wanasema the ball is on our court yaani ukifikia pale nusu ya pili ya kutaka kumaliza mpira na nyinyi ndiyo mnakwenda vizuri mnalazimika kumaliza vizuri. Nipongeze sana taarifa hii iliyoletwa hapa na CAG kwamba yeye ametimiza wajibu wake wote pasipo kuacha nafasi yeyote. Pia Kamati mbalimbali ambazo ripoti zake tunazijadili hapa leo na wenyewe wamefanya kazi yao nzuri sana, sisi wengine sio Wajumbe wa hizi Kamati ambapo ripoti zake tunajadili tunatoka kwenye kamati tofuti. Lakini tupo hapa na mimi nitatoa mchango wangu nikiegemea kwenye taarifa iliyoletwa na Kamati ya PAC.

Mheshimiwa Spika, bila kumung’unya maneno kabisa kwenye Kamati ya PAC kwenye ukurasa wake wa kwanza kwenye maneno yake ya utangulizi paragraph ya pili, wanasema hivi katika taarifa hii Kamati imebainisha maeneo kadhaa ambayo taarifa za CAG zimebainisha uwepo wa changamoto ya matumizi mabaya ya Fedha za Umma. Maeneo hayo ni pamoja na Serikali kupata hasara ya Shilingi ya Billion 68.73 ambayo ni riba zinazosababishwa na Wakala wa Barabara TANROADS, kwa hiyo hapa Kamati wameamua kuimulika wazi kabisa TANROADS na jambo hili lipo kwetu kama Wabunge na wewe ndiye kiongozi wetu.

Mheshimiwa Spika, tunao wajibu sasa wakumsaidia Mheshimiwa Rais, ripoti hii kuisaidia nchi hii pia, ripoti tunayoijadili tunategemea tuache yale mambo kama ambayo yalikuwa yanatokea labda tunaweza tukasema ya business as usual, tumepewa sasa nafasi yakusema wazi na ukweli na wewe kama Spika lazima uache historia ndani ya jengo hili, kwamba wakati wako uliitaka Serikali ilete taarifa ama za kuwawajibisha watu waliosababisha hasara hizi au wewe mwenyewe kuunda Tume Teule za kwenda kuchunguza maeneo haya yanayotajwa sana ndani ya ripoti ya CAG. Hii ndiyo namna pekee ya kuweza kulisaidia Bunge letu na kuweza kulisaidia Taifa letu pia lakuweza kumsaidia Mheshimiwa Rais, nikiangalia nia nzuri kabisa ya watu wa CAG wanataka kuona tunatoka hapa tulipokwama tunakwenda mbele.

Mheshimiwa Spika, kuna wakati fulani taarifa kama hizi zilizo wazi namna hii tulikuwa hatuzipati kila mara lakini leo taariafa inaeleza mapungufu makubwa haya tena tu kwenye baadhi ya maeneo ambayo yeye ameamua kuyataja na kuyakagua. Sasa kama hasara ya namna hii shilingi bilioni 68.73 inapatikana TANROADS peke yake, lakini TANROADS tunaamini wanayo Bodi, TANROADS ina viongozi wake wakiwemo Wakurugenzi Wakuu ambao bado mpaka sasa hivi wanatumikia nasi tuko hapa kama Wabunge, kwa niaba wa wananchi tunaona hasara hizi zinazoletwa na CAG amejaribu kufungua jicho lake na kutuelekeza mambo yanayotokea kwenye maeneo haya. Kwa hiyo, tusitoke hapa mikono mitupu. Hakikisha mambo haya yanakwenda kukomeshwa katika maamuzi yetu tutakayoyafanya ili siku moja tukumbukwe kwamba tulisaidia Taifa hili. (Makofi)

Mheshimiwa SpikaNimetaja tu TANROADS peke yake lakini tunayo MSD, Mheshimiwa Tunza, jana wakati anachangia na yeye namshukuru kwa mchango wake mzuri, alieleza vizuri namna ambavyo MSD wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwenye baadhi ya maeneo. Halmashauri yetu ya Wilaya ya Masasi DC peke yetu tuna karibia Shilingi Billion 180 ya dawa ambazo zinatakiwa zikateketezwe. Waliopeleka dawa hizi Masasi wanafahamika, waliokuwa wanazitunza kwenye bohari zetu wanafahamika. MSD bado ipo, Bodi ya MSD nayo bado ipo.

Mheshimiwa Spika, pia ukiangalia TPA kwenye taarifa ya CAG na pia kwenye taarifa hata hii ya Kamati na wenyewe wametaja, kuna ubadhirifu mkubwa uliofanyika kwenye Bandari ya Mwanza, kuna ubadhiru mkubwa uliofanyika kwenye Bandari ya Kigoma lakini pia na Bandari ya Mtwara kuna harufu za ubadhilifu. Sasa tuko hapa kusaidia kwa hiyo tunaomba wazi na tunaelekea mwishoni sasa kwa hiyo TPA nayo paundwe Tume au Kamati Maalum itayokwenda kufuatilia mambo haya ili tuweze Kwenda mbele kwa sababu kuna sehemu tumekwama. ATCL nayo imetajwa.

Mheshimiwa Spika, KADCO nayo Mheshimiwa Shangai, alichangia vizuri na ameeleza yeye anatoka eneo hili ni mtu anaefahamu vizuri historia nzima ya KADCO na mambo wanayoyafanya. Tuombe sana ili tuweze kusaidia nchi yetu tuondoke hapa tulipo simama.

Mheshimiwa Spika, kuna suala lingine ambalo linasababisha labda wakati fulani hata inflation hii tunayoiyona tunaweza tukasema it’s a created inflation. Kuna suala la madai ya wakandarasi CAG nalo wameliangalia, mwaka 2017/2018 Wandarasi wa ndani walikuwa wanadai almost shilingi trilioni tatu. Mwaka 2018/2019 trilionI 2.7. Sasa hivi 2019/2020 wakandarasi wa ndani wanadai zaidi ya shilingi trilion 3.1. Tunaitaka Serikali ilipe madeni haya yatakwenda kusaidia kupunguza nakisi ya upandaji wa gharama huko nje kwa sababu maisha siyo marahisi tena kama ambavyo tulizoea.

Mheshimiwa Spika, vilevile tukumbuke Wakandarasi hawa na wenyewe wanakopa kwenye mabenki na kuna wanaofilisiwa huko kwenye mabenki wanapokopa ili kuendeleza hii miradi ya Serikli. Sasa kwa nini Serikali haitaki kulipa kwa wakati Wakandarasi wanapofanya kazi, hata kama wengine wameisha raise hizo certificate ili kuweza sasa namna ya kuona kuyafuta hayo madeni kwenye vitabu vya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mambo haya yanakwenda siyo hapo tu. Mpaka sasa CAG anao uwezo wa kukagua Taasisi nyingi za Serikali, lakini nitoe mfano mmoja ambao nasisi tunaona kuna haja au kuongeza wigo, kuna maeneo mengine yanakaguliwa na watu wa COASCO, kwa mfano niseme masuala ya ushirika wanaokagua kwenye hivi Vyama vya Ushirika ni COASCO. Hata hivyo mambo yakiwa mazito sana Serikali huwa inaweka mkono wake na ripoti za COASCO siyo kila mara na sikumbuki kama mara ya mwisho ni lini zililetwa hapa ndani kwa ajili ya kuzijadili.

Mheshimiwa Spika, hapa karibuni tumeona Serikali imekuwa na nia njema sana ikaunda Tume ya Kamati ya pamoja ya manunuzi ya pembejeo, kuna malalamiko makubwa kwamba pembejeo hizi kwa wakulima hasa nitoe mfano kwa wakulima wa korosho hazijawafikia ama kwa wakati lakini wakati mwengine haziwafikia kabisa au zimefika zikiwa chache kiasi wao wanaona ni bora tukarudi kwenye ule mfumo wa zamani Serikali ikitoa pesa basi waende kutumia kwenye ruzuku badala ya kutengeneza hiki kikundi ambacho wanasema ni Kamati maalumu, kumekuwa na ubadhirifu mkubwa sana, sasa tuombe badala ya ukaguzi wao kufanywa na CAG peke yake ikiwezekana ukaguzi maeneo haya ufanywe na Ofisi ya CAG badala ya kuachia hawa COASCO peke yao, ambao siku zote wamekuwa wanakaa na hawa watu wa vyama vya ushirika nakuona mambo wakati mwingine namna wanavyoweza kuyatengeneza ili yaweze kuwanufahisha wao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa namna hii ambavyo tunakwenda na Bunge tunakwenda sasa kuhitimisha nafikiri kesho tutakuwa tunahitimisha hoja zilizopo hapo hapa mbele yetu, niombe sana Kiti chako kiunde Kamati Teule kwenda kuchunguza maeneo haya ambayo Wabunge wote waliyosimama hapa wamechangia na wameyataja, ikiwemo MSD, TPA, TPDC, ATCL, KADCO pamoja na TANROADS tutakuwa tumetenda haki kwa ajili ya nchi yetu pia tutakuwa tumeweza kusaidia nchi yetu kuweza ku-move mbele.

Mheshimiwa Spika, kazi iliyofanywa na Kamati ya PAC, kazi iliyofanywa na LAAC vilevile na kazi iliyofanywa na CAG ni kazi nzuri sana kuacha zikaishia hapa katika sisi tu kuzijadili na hatua zake zisionekane. Aache historia katika Bunge hili na aache historia katika Nchi hii kwa kuelekeza Serikali katika kuhakikisha haya yanayotajwa, hasara zinazopatikana kwenye vyombo mbalimbali vya Serikali pia ubadhirifu unaotajwa waziwazi kwenye maeneo haya ushulikiwe, nasi tuweze kujisifia kwamba kuna wakati tuliweza kuisaidia nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja ambazo zimeletwa hapa mbele yetu pia nisisitize kwa kifupi kwamba kuna haja ya kuunda Kamati Teule kuchunguza maeneo haya ili kuweza kusema ukweli yanayojili ndani kwenye vyombo hivyo.

Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa nafasi hii. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety) pamoja na Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Haki Miliki za Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za Mimea. (Protocal for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights) in The Southern African Development Community – SADC) pamoja na Azimio la Kuridhia Mkataba wa Marrakesh wa mwaka 2013 unaowezesha upatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona, wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma (The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Published Work For Persons Who Are Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled)
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia. Leo nimeamua tu nichangie niweze kuongea na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kwa maana ya kukumbushana majukumu yetu. Ukiangalia trend ya michango yetu sisi wote humu ndani kama Wabunge kuanzia jana pamoja na leo na hotuba zetu sisi za Kambi jana pamoja na leo tumeamua kuunga mkono moja kwa moja Maazimio haya yaliyoletwa mbele hapa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo makusudi ili kuweza kuwakumbusha wenzetu kwamba jukumu letu la Kibunge la kwanza kabisa ni pamoja na kutunga sheria. Suala la pili ambalo ni majukumu yetu pia ni kusimamia na kuishauri Serikali katika kutekeleza mipango mbalimbali. Tukifika kwenye hiyo juncture wote tukajua majukumu yetu kimsingi hatuwezi kuvutana kwenye haya mambo yanayojitokeza humu ndani na kuharibu atmosphere ya Bunge wakati fulani kwa sababu tunakaa na kusikilizana. Kwa hiyo, hali ya hewa inakuwa nzuri kabisa kama ambavyo mmeona imetokea jana na leo pia ilivyotokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nachotaka nikiseme ni kwamba haya Maazimio ambayo yamekuja mbele ya Bunge lako Tukufu, wote tunaungana mkono kusema kwamba yameletwa ndani ya Bunge hili kwa kuchelewa. Yangekuja mapema sana shida tunazozipata huko Majimboni kwetu, kwa mfano, mimi natokea Wilaya ya Masasi ambapo tuna Shule ya Msingi ya Masasi ambapo mimi nilisoma pale darasa la pili mpaka darasa la tano. Pale ndani tuna walemavu wa macho na vijana wenye uoni hafifu, wanavaa miwani lakini bado hawawezi kuona, wanatumia haya maandishi ya nukta nundu. Kipindi cha nyuma walikuwa wanatumia Braille ambazo ziko kama rula, wanachoma kwa vidoti wanaendelea, baadaye waka- improve wakaweka pale mashine, mashine zile kule ndani zimechakaa kabisa na haziwezi kuwasaidia, vijana wapya wanaoingia pale wanashindwa kupata hizi mashine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Ikupa alinisaidia na Mwalimu Kamtande alisema nikushukuru kwa sababu niliweza kupata kwa kufuatilia Serikalini mashine ya kuchapa kwa kutumia nukta nundu. Suala linalokuja na matatizo tunayoyapata, tumempelekea pale mwalimu ambaye ni mwajiriwa kabisa wa Serikali anafundisha shule ya Msingi Chibugu, bahati mbaya sana lakini kutokana na pesa anazozipata hawezi tena kutumia mshahara wake kwa ajili ya kwenda kununua karatasi maalum kwa ajili ya kwenda kuchapa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapoingiza hii teknolojia mpya tunataka sasa nukta nundu zianze kutumika maalum kabisa na Serikali imeiridhia tuone na namna ya kuongeza bajeti. Bahati mbaya sana jambo limekuja baada ya bajeti kuu kupitishwa. Sina uhakika kama Wizara kuna fungu ambalo wamelitenga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo limenipa mshangao, mimi ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na jambo hili limewasilishwa pale na Waziri wangu wa Viwanda na Biashara, hivi kuna mahusiano gani kati ya nukta nundu na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nadhani hili jambo lingekwenda kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kulisimamia vizuri upande unaoshughulika na masuala ya walemavu na wengine, kwa mfano Wizara anayosimamia Mheshimiwa Ikupa hapa lingekuwa na maana zaidi labda na bajeti yake pale ingekwenda vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tumesema tunaunga mkono Azimio hili, hatuna pingamizi lolote. Hata mawazo mazuri yatakayoletwa na Serikali hapa kwa kusikilizana yakianzia kwenye Kamati zetu za mtambuka na baadaye yakaja ndani ya Bunge, wote tukaona tuna nia moja ya kujenga nchi yetu, Taifa letu liweze kuongea kwa lugha moja tunaweza tukafika sehemu nzuri kushauriana kwa kusikilizana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina mengi ya kusema, nilitaka niseme tu hayo machache niwaambie kuna haja ya kuridhiana na kuweza kwenda pamoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nishukuru sana kwanza kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia mchana huu kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Kwanza kabisa nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa namna anavyoipigania nchi yetu na kupambana ili kuweza kuiweka kwenye mstari ulionyooka, hasa kwenye kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati pamoja na kutoa huduma stahiki kwa wananchi, kuboresha masuala ya afya, miundombinu ya elimu pamoja na masuala ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe pia pongezi kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yake nzuri pia kwa namna ambavyo anatusimamia sisi kama Wabunge na anavyotuunganisha na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi hapa ndani wote tuko kama Wabunge na ukitupima kwa madaraja Wabunge sisi wote tunafanana, ni daraja moja kwa sababu tumetokea huko chini kwa wananchi. Wajibu wetu wa kwanza kabisa ni kuismamia Serikali, na wajibu wa pili ni kuishauri Serikali pale tunapoona haifanyi kile ambacho sisi kama Wabunge au wananchi wetu wametuelekeza Serikali ikifanye. Wakati tunafanya mambo haya tunatakiwa kuangalia kuhusu uzalendo wetu na uwajibikaji wetu kwa Taifa kama namba moja lakini kwa wapiga kura na sehemu ya tatu tunatakiwa kuwajibika kwa chama chetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo pamoja na haya yote nitahakikisha kwanza ninalilinda Taifa langu kabla ya chama changu. Nitahakikisha ninawalinda wapiga kura wangu kabla ya chama changu halafu baadaye nitakilinda chama changu dhidi ya haya yote niliyoyataja hapo juu na ndipo nitapata ustawi sahihi na kuweza kuwasimamia na kuwaongoza watu wetu. Nayasema hayo, nataka nishauri Bunge lako na ikiwezekana lishawishike kwamba, kwa kadiri mambo yanavyokwenda tuna haja ya kubadilisha kanuni ili ripoti ya CAG ifanyiwe kazi na Bunge kabla hatujapitisha bajeti nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu zangu za msingi mojawapo kubwa ni kwamba, bajeti hii tunayokwenda kuipitisha ndiyo ile ambayo inalalamikiwa kwamba hapo nyuma pamefanyika ubadhirifu na kuna watu bado wataendelea kupelekewa fedha za Serikali wakiwa bado madarakani. Simaanishi kwamba tuijadili hii bajeti kwa sasa hivi, lakini kwa nia ya kubadilisha kanuni badala ya kusubiri mpaka mwezi wa kumi na moja ambayo itakuwa ni takriban miezi sita toka pesa mpya zilipopelekwa kwenye wizara tofauti ambazo nyingi zinalalamikiwa, watendaji wanalalamikiwa. Tumemsikia Mheshimiwa Rais naye akitaja baadhi ya watu kwamba wanalalamikiwa kwenye haya mambo. Kwa hiyo kimsingi ilitakiwa watu hawa kwanza wawajibike kabla hatujawapelekea pesa zingine ambazo inawezekana wakaenda kuzitumia kwa mtindo ule ule, kwa sababu watajua kwamba itakapofika Mwezi Novemba sisi kama Bunge tutajadili tutaweza kuondoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tubadilishe kidogo mtindo wa ufanyaji wetu wa kazi hasa inapokuja ripoti nzito kama hizi, kwa sababu kuna haja ya kujadili ripoti ya CAG na kuona mapungufu kabla hatujafanya location ya pesa zingine kwenye maeneo yale yale ambayo tayari kuna matobo makubwa ya matumizi mabaya ya pesa za wananchi. Ndio wale tuliosema tunawalinda, tunalinda Taifa lakini baadaye tunajilinda sisi wenyewe na tunataka tuone chama chetu kinaendelea kuongoza nchi hii, lakini haya lazima tuyasimamie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo nilipata nafasi ya kuuliza swali hapa asubuhi; nilikuwa naongea kuhusu barabara ya Nachingwea Masasi. Nakumbuka hapa Waziri wa Fedha alimpa taarifa Mbunge mwenzangu ambaye tunapakana kwenye eneo la mpaka wa Nachingwea. Kwamba mradi wa utekelezaji wa barabara kati ya Masasi na Nachingwea utatekelezwa hivi karibuni. Majibu ya Waziri kama umefatilia vizuri na kuyasikia hapa leo naye amesema upande wao wameshamaliza na taarifa hizi zimekwenda Wizara ya Fedha, ili sasa waweze kutengewa fedha ya utekelezaji wa mradi huu, lakini kimsingi hakuna kinachoendelea mpaka sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi kama watu wa Masasi, Nachingwea na huko hatujaona mobilization inafanyika pale, kwa hiyo tafsiri yake hilo jambo haliwezi kufanyika siku za karibuni. Wilaya ya Nachingwea ni wilaya ambayo inafanana karibia sawasawa kabisa na umri wa uhuru wa nchi yetu, haijawahi kupata barabara ya lami, haijawahi kuunganishwa na sehemu nyingine yoyote yenye lami. Ndiyo maana sisi tunapokaa hapa tunaongea tunashauriana tunaambiana kwamba tunataka Serikali ifanye haya mambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Serikali ipo, majibu haya sisi tunayapokea na hii sio mara ya kwanza basi watueleze kama inashindikana sisi tumezoea kufanya michango kwenye baadhi ya maeneo. Tunachanga ili kujenga madarasa kuisaidia Serikali na sasa hivi nataka watuambie ili tukaweze kufanya michango sisi watu wa Mtwara, Lindi na Nachingwea tuweze kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo pamoja na barabara ya Mtwara, Mnivata-Newala, ambayo nayo ahadi zimekuwa nyingi. Newala- Masasi haijatekelezwa, hatuoni nini pale kinachoendelea pamoja na kwamba hivi karibuni wamelipa fidia lakini hii ya Nachingwea – Masasi ndio tatizo kabisa siku zote tunapewa majibu haya yanayofanana. Kwa hiyo tunaomba Serikali watuambie kama haipo kwenye bajeti yake inashindikana kwa sababu hatujui kilichofata hapo mbele basi sisi kama wananchi wa maeneo haya tuchangishane kwa kukata kwenye mazao yetu ya kilimo pamoja na korosho shilingi 20 ili tukajenge hiyo barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaongelea kipande cha kilometa 42, Masasi-Nachingwea, lakini Wilaya ya Nachingwea ina zaidi ya umri wa miaka 60. Kwa hiyo Serikali kama hata ingeamua kujenga kilometa moja moja toka wakati huo, sasa hivi wangekuwa wameshaenda mbali zaidi ya Nachingwea na wanakaribia kufika Liwale. Kwa hiyo tutakapotoka hapa tutakwenda kuwashauri watu wetu kama inawezekana basi tuchangishane.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kwamba, Mheshimiwa Waziri wakati anawasilisha mpango wake alisema kwamba uchumi wetu unayumbayumba na kwamba inawezekana uchumi ukatoka kwenye asilimia 4.2 kwenda asilimia 3.9. Sababu zinazotajwa katika haya mambo ya kupanda kwa bei za vitu na mengine, ni pamoja na vita ya Ukraine pamoja na Russia pia na yale masuala ya covid. Sasa sisi kama Taifa mpango wetu ni nini? Tunayo miradi yetu mikubwa ya kimkakati tunayo suala la Liganga na Mchuchuma, suala la reli ya kusini, suala la Bandari ya Mtwara, tunayo haya mambo ya gesi ambayo hayatumiki ipasavyo tungeweza kuachana na sababu hizi ndogondogo za kiuchumi kwa sababu kama vita itaendelea kwa miaka 20 manake uchumi wetu bado utaendelea kudorora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine nataka niombe, kwa sababu tuna taarifa za CAG, CAG akakague; na Mheshimiwa Mwenyekiti utaniongoza kuna hili suala la ETS tumelalamikia muda mwingi hapa kwamba ndiyo kati ya vitu ambavyo vinaongeza inflation kwenye bei za bidhaa mbalimbali. CAG sasa akakague na kuona kama tender hii ya ETS bei zilizopo na athari zilizopo kwenye soko atuletee taarifa hapa sisi kama Wabunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka pia CAG akakague na kuangalia Mfuko wa Pembejeo. Ukija Mtwara kwenye zao letu la korosho kuna Mfuko wa Pembejeo wa Pamoja. Mfuko huu umeshafanya kazi zaidi ya miaka mitatu, lakini pia haupo kisheria, ndiyo tunataka CAG akakague atuletee hapa taarifa, kama Mfuko bado unatufaa sisi au kama haufai basi uondolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine tunataka kufanyiwa review kwa export levy, kodi inayotozwa kwenye masuala ya korosho. Pafanyiwe review pia katika tozo mbalimbali ambazo zinatozwa kwenye korosho, hela ya korosho kila mara inaanguka, wakulima wanapata hasara, makampuni yanapata hasara, uchumi wa maeneo yetu unadorora kwa sababu tunategemea zaidi zao la korosho, lakini watu wanashindwa kuja kununua kwa sababu ya tozo zilizopo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepata sisi ziara ya kwenda kwenye nchi wanakozalisha korosho, nchi ambako wanatumia mfumo kama wa kwetu. Sisi Tanzania peke yake ndiyo tuna hizi kodi hapa tunazozitaja. Sasa ni wakati wa kuona kama ni kweli kodi hizi zinastahili ama kodi hizi hazistahili ili tuweze kwenda sawasawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo linaumiza sana wananchi ni masuala ya fidia kwenye maeneo mbalimbali. Kwenye Jimbo la Ndanda tuna mgogoro mkubwa sana na wa siku nyingi wa eneo kati ya Jeshi la Magereza pamoja na wananchi kwenye Kata ya Namajani kwenye Vijiji vya Ngalole pamoja na Chiroro na maeneo hayo. Toka mwaka 2012 Mahakama ilitoa award kwa wananchi na kuwaambia kwamba eneo lile lirudishwe kwa wananchi, Serikali haijafanya hivyo, magereza haijafanya hivyo. Katika bajeti hizi zote sijaona popote ambapo imetengwa fedha ya kwenda kuwapa wale wananchi fidia zao ili waweze kuachia hayo maeneo. Kwa hiyo kama Serikali imeshindwa, tutakapokuwa tunamaliza Bunge na tunakwenda kwenye Wizara ya Ardhi, watueleze ili tukawambie wananchi sasa wakalime kwenye yale maeneo yao, waachane na huu mpango wa Serikali kwa sababu hautaweza kutekelezeka karibuni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la fidia pia. Barabara inayotokaa Nanganga inakwenda Ruangwa nyumbani kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu, inakwenda pia na kuunganisha na Wilaya ya Nachingwea. Palibomolewa pale majumba ya wananchi wa kawaida, palibomolewa misikiti, lakini pamoja na Ofisi yetu ya Chama cha Mapinduzi, hakuna fidia iliyolipwa mpaka sasa hivi na wananchi wanapouliza Serikalini wanasema fungu la fidia lilikuwa halijaandaliwa. Tunaka tutakapokuwa tuna wind-up haya mambo basi tuweze kupata majibu ya pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado nisisitize kwenye yale niliyoyasema kwamba kwa vyovyote vile tunahitaji uchunguzi wa kina wa kuona kama Mfuko huu wa Pembejeo unaosimamia Mikoa ya Mtwara, Lindi na maeneo yote wanayolima korosho bado uko viable na kwamba CAG akaukague tupate taarifa hapa kwa sababu itakuja ndani ya Wizara ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ni kama hayo niliyoyasema, kwa hiyo, naomba nisisitize kufanyike ukaguzi ili wananchi waweze kupata majibu na sisi kama Bunge tubadilishe Kanuni, tujadili taarifa ya CAG kabla hatujatenga pesa kwa bajeti inayofuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi niungane na wengine wote kwanza kukushukuru wewe mwenyewe lakini kwa namna ya pekee kabisa kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa namna ambavyo ameamua kuipa nguvu sasa sekta ya afya. Niwapongeze sana pia Mawaziri, kwa maana ya Mheshimiwa Waziri Ummy pamoja na Naibu Waziri, watendaji wote wa Wizara ya Afya kuanzia wale wa juu kabisa mpaka wa chini ambao tuko nao kule vijijini kwa kazi kubwa wanazozifanya bila kuchoka usiku na mchana.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze kwa namna ya pekee Mawaziri hawa wanavyoshirikiana. Siku zote katika kazi zao ukimkosa Mheshimiwa Ummy ukimpata Mheshimiwa Mollel pale atatatua jambo lako kama ambavyo Mheshimiwa Ummy angeweza kulitatua, kwa hiyo niendelee kuwapongeza kwenye hili. Pamoja na hayo mimi ni mjumbe wa Kamati ya Afya na masuala ya UKIMWI. Tumeongea mengi sana kule ndani na nisingependa niyalete hapa kwa sababu tumeyaleta kwenye taarifa yetu na tulishakubaliana. lakini nina mchongo wangu wa ziada kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue pia nafasi hii kutoa pole sana kwa familia ya Mzee wetu Benard Membe kwa msiba mkubwa uliotokea huko. Wananchi wote wa Jimbo la Mtama, Mbunge wa Mtama pamoja na wananchi wa Chiponda kule Londo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo ambayo ningependa nishauri ili tuweze kuyafanya marekebisho ili Mheshimiwa Waziri waendee kutoa huduma zaidi kama ambavyo sasa hivi wanatoa huduma bora, lakini tunataka huduma bora zaidi kwenye Wizara yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza kabisa, hasa ukiangalia tone za Waheshimiwa Wabunge hapa ndani kuna haja kubwa sana kati ya wizara ya Elimu, Wizara ya Afya pamoja na TAMISEMI mkae na kuanza ku-define upya mipaka yenu ya kazi. Jambo hili limekuwa linatuchanganya sisi pamoja na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana Waheshimiwa Wabunge wenzetu waliopata nafasi wanaongea Habari za zahanati ambazo ni huduma za afya za msingi chini kabisa, kitu ambacho naamini na nyinyi mna-level yenu. Kwa hiyo tunachanganya kati ya majukumu ya TAMISEMI, majukumu ya Wizara ya Afya lakini pamoja na majukumu ya Wizara ya Elimu. Kwa hiyo niombe kabisa tafuta nafasi mtusaidie ku-define hii, na ikiwezekana sasa tuweke mstari ulionyooka.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano ambao uko wazi kabisa, ninyi kwenu mnamiliki CMO, kwa maana Chief Medical Officer, lakini Chief Medical Officer hana mamlaka ya moja kwa moja kwa RMO. RMO naye hana mamlaka ya moja kwa moja kwa DMO. Nafikiri ananielewa Mheshimiwa Waziri; jambo ambalo linaleta mkanganyiko mkubwa, wakati ninyi Wizara ya afya mnatakiwa mfanye kazi kama Jeshi. Amri ikitoka juu kwa maana ya CMO iende mpaka chini kabisa kwa sababu ninyi ndio mnaoshughulikia masuala ya milipuko ya magonjwa pamoja na mengine. kwa hiyo niwaombe mkae na ku-define vizuri jambo hili ili CMO tumpe mamlaka lakini pia CMO awamiliki madaktari wenzie kwenye kada mbalimbali kushuka huko chini badala ya kuacha mfumo kama ambavyo uko sasa hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tulikokuwa kwenye Kamati tulishauri suala la CCBRT pamoja na suala la Ndanda Hospitali; kwa maana ya wale madaktari wa CCBRT kuhakikisha wanapata mishahara yao kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutoa huduma kwa watoto wenye mapungufu lakini pamoja na masuala ya ujumla ya ulemavu ikiwa ni pamoja na huduma za macho. Kwa hiyo wanastahili kupewa mishahara ili kuwapunguzia mzigo na kupunguza gharama kwenye eneo hili. Sawasawa na ilivyokuwa kwa Ndanda Hospitali, sasa hivi wameondolewa basket fund lakini wakati Hospitali yetu ya Kanda ya Mkoa wa Kusini inakua sehemu ambayo tunategemea sana kupata huduma ni Hospitali ya Ndanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tuone namna ambavyo tunaweza tukawarudishia basket fund au kutafuta namna yoyote ya kuwawezesha waweze kugharamia huduma waweze kutoa huduma ya mama na mtoto kwenye eneo hili kwa gharama nafuu kwa sababu sasa hvi yamekuwa malalamiko makubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo jingine ni suala la Mfuko wa Bima ya Afya. Bima ya Afya sasa hivi inasuasua, lakini tukumbuke kwamba hawahawa Bima ya Afya ndio ambao walitoa fedha zao wakapeleka kuchangia kwenye ujenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa pamoja na Muhimbili. Kwa hiyo tuone namna Serikali itakavyolipa madeni haya ili mfuko huu uweze kujiendesha wenyewe kwa sababu sasa hivi hawafanyi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo jingine nakuomba sana Mheshimiwa Waziri ukaangalie taratibu au namna ya kufanya ili mifumo iwe inasomana. Sasa hivi kumekuwa na shida kubwa sana ya huduma za afya. Kwa mfano mgonjwa akitoka Hospitali ya Kanda ya Mtwara akatakiwa kuja kutibiwa Muhimbili Dar es salaam, atakapoleta kadi yake ya afya ikiwa ndani ya masaa 24 itaonekana kwamba imetumika; lakini hata vipimo alivyovifanya Mtwara, Hospitali ya Muhimbili Dar es salaam italazimika kuvirudia tena, kama ilivyo CT scan na vipimo vingine, kitu ambacho kinaongeza gharama kubwa sana. Ni bora hawa watu wenye kadi ya afya wanaweza kujigharamia, lakini watu wanaotumia cash ndani ya muda mfupi anarudia vipimo vilevile mara mbili ama mara tatu kutegemea na hospitali aliyokwenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jambo jingine ambalo nataka kushauri, Tanzania sasa tumeendelea sana kwenye masuala ya afya; tuanzishe kitengo cha medical legal, kwa maana ya kutaka kusimamia taaluma ya madaktari. Siyo siri kwamba maslahi ya madaktari siyo mazuri sana, na ninaomba Wizara yako iboreshe. Kwa mfano sasa hivi wanapata asilimia 40 ya mgonjwa anayemhudumia akitokea kwenye Bima ya Afya, na ndiyo maana madaktari wanakuwa wanaamua wakati mwingine kufanya tiba ambayo si sahihi. Unaweza kukuta mama anauwezo wa ku-push mwenyewe lakini wanajua akiwa hospitalini akimchaji akimwambia kwamba inatakiwa afanyiwe scissor ya milioni moja na laki tano tuseme atapata pale pesa na yeye asilimia 40 ya hiyo pesa ili aweze kujikimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mbaya zaidi kuna madaktari wanaohamisha wagonjwa kutoka kwenye hospitali kubwa na kuwapeleka kwenye hospitali ndogo ambazo haziwezi kutoa huduma nzuri. Na Mheshimiwa Waziri mimi nitakuletea jina la daktari ambaye ninamfahamu amemuumiza ndugu yangu. Alimtoa Hospitali ya Regency akampeleka Hospitali ya Kinondoni, amefanyiwa operation na sasa hivi nakueleza ameridiwa kufanyiwa operation ya appendix kwa mara ya tatu kwa sababu daktari wa kwanza hakufanya majukumu yake sawasawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa watu kama hawa ambao wanaangalia zaidi kuhusu pesa badala ya kutoa huduma ndio ambao tunasema tuunde hii medical legal ili mwisho wa siku huyu naye awe na wajibu wa kushitakiwa kama alivyo mharifu mwingine yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatambua nia ya madaktari ni kutoa huduma, na nia yao hasa ni kuokoa maisha ya mgonjwa; lakini daktari anpofikia kwamba anataka sasa kuanza na kufanya biashara kwenye mwili wa mgonjwa kwa kumtoa hospitali kubwa anampeleka kichochoroni kwenda kumpa huduma ambayo haistahiki na baadaye mgonjwa yule anatolewa akiwa mahututi kwenye hospitali ya kichochoroni na kurudishwa tena kwenye hospitali kubwa, hili jambo halikubaliki. Tuyaangalie, tuwaongezee maslahi yao ili waweze kuacha kitu kingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo jingine, tunazo polyclinics nyingi sana zimezuka sasa hivi. Kunakuwa na emergency zinazotokea mitaani, tunaruhusu watu wa polyclinics waweze kusajiriwa na NHIF ili kuwaza kuzuia ajali kwa kupata huduma hapo wakati mwingine ama vifo vinavyotokea mitaani. Kwa hiyo tuyaone haya na tuone namna ya kuyasaidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kama ambavyo nimesema tangu mwanzo, kwamba mimi ni mjumbe wa Kamati ya Afya, kwa hiyo kwa vyovyote vile mchango wangu sehemu kubwa nilitoa nilipokuwa ndani ya Kamati. Nataka tu kuyasisitiza haya machache, tufanye definition upya ya kuona mstari mzima kutoka Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu pamoja na Wizara ya TAMISEMI.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuangalie pia huo uwezekano wa kuwa na medical legal kwa ajili ya kuwasimamia madkatari ambo wanafanya vitu vya ovyo kwenye fani yao kama ilivyo kwa wengine; na ikiwezekana hata kabla ya kupata leseni nyingine madaktari hawa tukawapa record tracks zao za utendaji wao mzuri huko badala ya kufanya kwa uzoefu tunawapa leseni kila wanapofikia msimu wa ku- renew leseni wakati watu pengine wanayaacha.

Mheshimiwa Naibu Spika, jingine kubwa tuone namna ya kuhakikisha sasa Mfuko wa Bima ya Afya unawezeshwa kwa kulipa madeni yake; madeni yaliyoko Mhimbili, Benjamini Mkapa, na ninaamini pia madeni yaliyoko Bugando; tuhakiishe tunawalipa ili waweze kujiendesha wenyewe, kwa sabau mara nyingi mfuko wa afya tumekuwa tunaona wandaiwa na watu wengi tu huko chini wanashindwa kutoa huduma nzuri na kisingizio kinakuwa kwamba wao hawajapewa hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, Nisisitize kuhusu kuwapa stahiki zao CCBRT, kama ambavyo tumeongea kwenye Kamati. Nirudie tena kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi zake nzuri. Kama ambavyo nimesema, mimi ni mjumbe wa kamati kwa hiyo kwa vyovyote vile mchango wangu nilitoa kule ndani lakini nilitaka nikukumbushe hayo machache.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kwenye majimbo yetu tunaona kuna vituo vya afya. Ukifika Jimbo la Ndanda sasa muda si mrefu tutapata huduma katika maeneo ya Lukuredi, Mpajani, Chilolo, Ndanda yenyewe na Ndanda na maeneo mengi. Kwa hiyo kwa vyovyote vile nikushukuru na kukupongeza, na ninakutakia kila la kheri kwenye utendaji wako. Na nikuhakikishie kwamba kwa sura ninazoziona za Waheshimiwa Wabunge hapa bajeti yako itapita tena kwa kishindo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi niliyopewa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Nishati
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami ninashukuru sana pia kwa kunipa nafasi ya kuchangia jioni ya leo. Niungane na wenzangu wote ambao kwa namna ya pekee kabisa wamempongeza Mheshimiwa Waziri, wamewapongeza Wasaidizi wake wote akiwemo Naibu Waziri, REA na mimi niwapongeze kwa namna ya pekee na niwataarifu kwamba, ule mradi wetu wa kuweka taa kwenye Jimbo la Ndanda wenye thamani ya shilingi milioni 400 tunategemea kuusaini hivi karibuni na Mheshimiwa Waziri umenisaidia sana kwenye hili, sasa Ndanda kwenye Kata zote za eneo la barabara kuu inayoelekea Masasi linakwenda kuwaka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kazi zako nzuri ndizo zinazotufanya leo tusimame na kukupongeza kwa sababu, kwa namna ya pekee kabisa umetugusa kwenye maeneo yetu. Tulipoanza mijadala ya masuala ya REA, mimi binafsi nilikuja ofisini kwako tukiwa na Waheshimiwa Wabunge wenzangu wa Mtwara na nikakuambia pamoja na scope kubwa iliyopo kwenye Jimbo la Ndanda ninaomba concentration tupeleke kwenye maeneo mawili. Ulinikubalia na nimshukuru sana pia, Mkurugenzi wa REA na yeye alinielewa ombi langu na kazi sasa ya kuweka umeme kwenye vijiji vyote vya Kata ya Mpanyani na vijiji vyote vya Kata ya Msikisi inaendelea. Nafikiri kufikia mwezi Julai kwa sababu kuna baadhi ya maeneo wameshaanza kuwasha na mimi nitakwenda kushiriki zoezi hili la uwashaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiyasema haya siyo maana yake kwamba, kazi imekamilika kwa asilimia 100, bado mahitaji ni makubwa ya masuala ya umeme kwenye Jimbo la Ndanda ukiangalia vijiji vya Mbemba, Mbaju na vijiji vingine vingi vinavyozunguka Jimbo la Ndanda tuna mahitaji ya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee naweza nikakuambia Mheshimiwa Rais ameamua ugomvi. Wewe mwenyewe unakumbuka juzi tulipokuja ofisini kwako mimi pamoja na Wabunge wenzangu wa Mkoa wa Mtwara tulikuja kweli tuna kilio kwako kwamba Mtwara tuna tatizo kubwa, umeme umekuwa unakatika kila mara maeneo yote ya Mkoa wa Mtwara, hasa kwenye Wilaya ya Masasi, Wilaya ya Newala, Mtwara Mjini na Wilaya zingine zote, lakini umetuhakikishia ndani ya miezi mitatu ijayo unapeleka turbine yenye uwezo wa kufua umeme megawati 20 ambayo itakuwa kama ni suluhisho la awali la kuhakikisha Mkoa wa Mtwara unapata umeme wa uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, ndiyo maana nasema Mama ametuamulia ugomvi. Wewe mwenyewe umetuelekeza na umetuambia kwamba, pamoja na mradi huu wa REA unaotokea Songea wa Gridi ya Taifa kuleta umeme Masasi umepata pesa nyingine ambayo itatoa sasa umeme Masasi kupeleka Mahumbika. Kwa hiyo, maeneo yote ya Ndanda, Chikukwe, Chigugu na vijiji vyote vya katikati hapa vitakuwa vinapata umeme wa uhakika kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri pamoja na hayo mazuri ambayo wewe unakusudia kwenda kuyafanya nizidi kukupongeza. tumeshuhudia hapa suala la mradi wa LNG na faida zake sisi kama Watanzania wote tunazifahamu. Bado narudia kauli yangu ile ile ya mwazo kwamba, mama ametuamulia ugomvi, Wabunge wa Mkoa wa Mtwara tulikuwa hatueleweki kwa wananchi wote wa Mkoa wa Mtwara kwa sababu, Mkoa wetu miaka kumi iliyopita ulikuwa juu kimaendeleo kwa sababu ya miradi mbalimbali ya gesi. Walikuwa na hamu kubwa ya kusubiri ili waweze kuona sasa utekelezaji wa miradi hii utafanyika lini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndoto kubwa tuliyoisubiri kwa muda mrefu na mimi niwatangazie Wabunge wenzangu, niwatangazie wananchi wa Mtwara na Lindi, sasa inakwenda kutimia, inakwenda kuwa kitu halisi. Kwa namna ya pekee kabisa pia, nimpongeze na Mheshimiwa Hamida kuhakikisha amepambana na wewe Mheshimiwa Waziri kupata pesa za fidia kwa ajili ya wananchi wa eneo la Kikwetu na lile eneo lote ambalo ni kama 5.5 billion wanafidiwa. Hii tafsiri yake ni kwamba, mradi sasa unakwenda kutekelezwa. Haya ni mambo mazuri Mheshimiwa Waziri ambayo tulikuwa tunayasubiri kwa muda mrefu, lakini tunakushauri sasa hakikisha shughuli zinazofuata kutokea sasa za kutiliana saini tuseme, utekelezaji wa miradi, maandalizi yanafanyika kwenye maeneo ya Lindi na Mtwara ili kuweza kusisimua uchumi wa maeneo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, shughuli zitakazofanyika kwenye maeneo haya, badala ya kutumia Uwanja wa Ndege wa Dar-es-Salaam, badala ya kutumia Bandari ya Dar-es-Salaam, hakikisha unawasisitiza hao wawekezaji, ikiwezekana tena kwa mikataba maalum kwamba, mizigo yao, shehena zao zishukie Bandari ya Mtwara, zishukie Bandari ya Lindi kama wataboresha, pamoja na kuondoa mizigo, lakini pamoja na Uwanja wa Ndege wa Lindi ili tuweze kunufaika zaidi. Hayo tu ni baadhi ya mambo ambayo tutakuwa tunayapata pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kikubwa nikusisitize, tumesikia kuhusu miradi mikubwa sana ya kimkakati, ndio maana hawa ndugu zetu wa Ludewa wanalia mpaka leo kuhusiana na suala la Liganga na Mchuchuma. Bado mradi huu umekuwa unatajwa lakini hautekelezwi. Tuiombe Serikali sasa kwa sababu, wawekezaji wameshapatikana jambo hili lifanyike kwa haraka ili sisi tuweze kuanza kuona manufaa haya ikiwezekana kabla hata mwaka huu wa fedha kuisha kazi hizo zianze kufanyika, eneo lile la Lindi lichangamke, maeneo ya Mtwara yote yachamke na wananchi waone kwamba,Serikali yao sikivu inawasaidia kuhakikisha haya yanafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo Mheshimiwa Waziri, nikukumbushe jambo moja, Mheshimiwa Kingu hapa asubuhi aliongea vizuri sana suala la SONGAS. Kwa sasa hivi mahitaji ya umeme ni makubwa, hatujakamilisha bado mradi wa LNG Lindi, ule mradi wa Mtwara wa megawatt 300 haujakamilika na mradi wetu wa Bwawa la Nyerere haujakamilika. Kwa hiyo, ona namna ya kukaa na watu wa SONGAS, boresheni hii mikataba inayotumiwa sasa hivi ili wananchi waweze kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kulikuwa na suala jingine limeongelewa hapa na ukienda kwenye ukurasa wa 36 wa taarifa ya Kamati wanasema kwamba, jukumu la vinasaba ambalo lilikuwa EWURA mwanzoni lilipelekwa TBS, kimsingi inachosema Kamati ni kwamba TBS wameshindwa kufanya hii kazi, kutokuweza kufanya hii kazi maana yake ni kwamba, gharama za mafuta zinaongezeka kwa sababu, sasa hivi wanasema TBS iwezeshwe ili iweze kutengeneza vinasaba, wanataka waanze kutengeneza vinasaba sasa hivi wakati bei ya mafuta inaongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TBS iongezewe watumishi, urasimu wa kupata watumishi unaufahamu na kuna taratibu zake za kupata, tuachane na hawa TBS kwenye hili jambo tuwape watu ambao wana uwezo wa kulifanyia kazi ili twendenao sambamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nilisema pale toka mwanzo kwamba, kutokana na umahiri wako kwenye kazi zako, maeneo yetu sisi yanatofautiana. Kuna maeneo ambako kuna tatizo kweli la umeme, lakini nadhani una nia njema ya kwenda kutekeleza hilo, lakini kuna maeneo ambapo kuna afadhali, sasa tukamilishe haya maeneo yote mawili yaweze kufanana. Mkoa wa Mtwara una vijiji zaidi ya 780 vijiji 800, lakini katika vijiji hivi karibia vijiji 300 havina umeme. Kwa mikakati ambayo umetueleza sisi juzi na ndio maana nakwambia hapa tena kwamba, Mheshimiwa Rais ameamua ugomvi kati yetu sisi Wabunge wa Mkoa wa Mtwara na wewe, lakini kati ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Lindi pamoja na Serikali yao sikivu ya Chama cha Mapinduzi. Tatizo kubwa ambalo lilikuwepo la umeme kwenye Mikoa ya Mtwara na Lindi sasa linakwenda kuisha kwa hatua ulizotueleza za muda mfupi, muda wa kati pamoja na muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasisitiza tu kwamba, hawa watu wanaokuja kuwekeza kwenye masuala ya gesi ninaamini ofisi zao ziko Dar-es-Salaam, ofisi zingine uliniambia wakati ule ziko Arusha na ulisema kwamba, mko kwenye a cell, kwenye contained room ili muweze kufanya majadiliano kwa karibu zaidi. Nikuombe sasa Mheshimiwa Waziri tayari tumeshafikia hatua nzuri na tunakwenda kwenye implementation. Ninaamini na wewe unatamani kufika Lindi kila mara ukaone namna tunavyoishi watu wa Lindi, tunavyoishi watu wa Mtwara, kuwarudisha watu hawa nyumbani tafsiri yake tunakwenda tena kusisimua uchumi wa maeneo yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi kirefu tumekuwa tunategemea korosho tu, lakini sasa tunakwenda kutegemea mazao ya gesi, ikiwa ni pamoja na masuala ya mbolea, lakini pamoja na usafirishaji. Bandari yetu ya Mtwara Serikali imeweka pesa nyingi sana kuhakikisha inatumika. Sasa tunapata bahati nyingine mradi wa Gesi unakwenda kutekelezwa kwenye maeneo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba sana, ninaamini una timu sikivu na jana nilipata taarifa pia, timu yako watu wengine tayari wameshashuka chini kwenda kufanyia kazi haya malalamiko ambayo tulikuletea ofisini kwako. Mheshimiwa Waziri, mimi niungane na wote waliokupongeza, sasa tunataka tuyaone yale uliyotuambia juzi yanakwenda kutekelezwa. Tatizo la kukatikakatika kwa umeme Masasi, Ndanda na maeneo mengine yote ya Mtwara pamoja na Wilaya za Lindi yawe yamekwisha kwenye kipindi tulichokubaliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siku 90 siyo nyingi, tutarudi tena hapa, tutakuja kuulizana kwamba, Mheshimiwa Waziri ulituahidi kwamba, ndani ya siku 90 matatizo haya ya umeme yatakuwa yamekwisha, kwa hiyo tunataka tuone haya mambo unakwenda kuya-implement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze tena sana Mheshimiwa Rais na nitumie ileile kauli yangu ya mwanzo kwamba, Mheshimiwa Rais ametuamulia ugomvi Wabunge wa Mtwara. Ahsante sana kwa nafasi hii, nikupongeze kwa kazi zako, ahsanteni kwa kunisikiliza. (Makofi)
Azimio la Bunge Kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba Baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa Lengo la Kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, na mimi kama Wabunge wengine wote tuliopata nafasi ya kuchangia leo kwanza nikushukuru sana, lakini jambo la pili, kama ambavyo unetuongoza kwamba tuna wajibu sasa wa sisi jambo la kwanza kabisa kuisaidia Serikali yetu kutoa tafsiri sahihi kwa watu wanaofuatilia jambo hili ambalo liko mbele yetu kwa sababu kwa bahati mbaya kabisa lilianza kwenda mitaani ama duniani pasipo sisi Wabunge kupata tafsiri sahihi ama kuelewesha kinachoendelea, na kwa bahati mbaya mikataba hii na hasa zaidi huu mkataba wa makubaliano ulioko mbele yetu kati ya nchi ya Dubai na Tanzania wa kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya kiuchumi ulipata kwenda mtaani kabla sisi wengine hatujauona.

Mheshimiwa Spika, nataka niseme kidogo kwanza kuhusu mimi mwenyewe binafsi. Mimi nilipata nafasi ya kuwa opposition kabla sijarudi tena kwenye chama chetu, chama tawala, Chama cha Mapinduzi na bado niko kwenye ma-group ambayo kuna mchanganyiko wa watu, kuna watu wa Chama cha Mapinduzi, lakini pia kuna watu wa opposition.

Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza na mimi nilipopata kusikia ama kuona kwenye ma-group haya watu wakivutana kuhusiana na masuala haya ya makubaliano kati ya nchi ya Tanzania na Dubai hata mimi nilishtuka kwa sababu nilikuwa sijui nini kinaendelea. Nikajipa nafasi ya kusoma na kujifunza, tukakutana na wataalam wakatuelewesha.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana watu wachache waliamua kuchukua vipengele vinavyowafurahisha wao au vile wanavyoamini kwamba vina controversy na kuvipeleka kwenye public badala ya kusoma tafsiri sahihi ya kila jambo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nitajaribu kusema tu kwenye mambo machache na nitajikita kwenye article 21 ya mkataba huu pamoja na article ya 22; na niwaombe Watanzania wenzangu, hasa tuliopo kwenye yale ma-group tuliyobishania haya mambo na wenyewe wakaangalie halafu baadae tupate tafsiri ya pamoja.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza ambalo nataka niliweke sawa ni hili ambalo limekuwa likipotoshwa mitaani kwamba mkataba huu utatekelezwa kwa kutumia Sheria za Uingereza. Mimi sio mwanasheria, lakini walau Kiingereza ninakifahamu, ukisoma article ya 21 ambayo iko kwenye ukurasa wa 28 kwa Kiingereza na wewe ni mwanasheria, utaniongoza. Inasema hivi;“The governing law of this agreement shall be English Law whereas the governing law of each HGA kwa maana ya Host Government Agreement and the relevant project agreement shall be in the laws of Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo sahihi sana ni kwamba makubaliano haya kati ya nchi ya Tanzania…

SPIKA: Mheshimiwa Mwambe ngoja. Sasa hapo usiseme kwa tafsiri isiyo sahihi, sema kwa tafsiri isiyo rasmi.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo rasmi, nashukuru kwa kunirejebisha.

Mheshimiwa Spika, kwa tafsiri isiyo rasmi sana kipengele hiki kinataka kusema kwamba makubaliano haya yaliyofanywa kati ya nchi ya Dubai na Tanzania yatakuwa kwa kutumia English Law, lakini wanachokisema hapa ni common law kwa sababu Dubai wana sheria zao na Tanzania tuna sheria zetu, kwa hiyo, itatumika common law itakayoweza kuziongoza nchi zote mbili kwenda kutekeleza majukumu waliyokubaliana hapa. Hiyo ni sehemu ya kwanza, kwa hiyo, ule upotishaji, yale maneno kwamba mikataba hii itafanywa kwa kutumia lugha ya Kiingereza, sio sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kipengele hicho hicho tafsiri yake ni kwamba sasa ndio maana pale wanasema kuna Host Government Agreement, tutakapofanya utekelezaji wa vile vipengele vidogovidogo kati ya Bandari ya Tanzania na Bandari ya Dubai au wale waendeshaji kutoka Dubai itatumika Sheria ya Tanzania kwa sababu mwekezaji atakapokuja Tanzania hatua ya kwanza atakayoifanya ni kusajili kampuni yake BRELA. BRELA inatumia sheria za Tanzania kwa hiyo, hili nalo lazima likae sawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo halikuwekwa vizuri sana lilikuwa…

SPIKA: Sasa kwa sababu umesema pia, nikusaidie…

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ndio, naomba unisaidie.

SPIKA: Hicho kifungu chako kiunganishe na kifungu cha tano, ukurasa wa 16. Kifungu cha 5(2) na chenyewe soma.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, Ukurasa wa 16. Kama ulivyoniongoza, article 5 inayosema kuhusu Rights to Develop, Manage or Operate.

Mheshimiwa Spika, kwenye ukurasa wa 16, kifungu kidogo cha pili, kama ulivyoniongoza kinasema hivi, “The State Parties agree the implementation of plans for development of the projects by DPW is subject to the conclusion of definitive Project Agreements, Land Rights and HGAs for each relevant project.” (Makofi)

SPIKA: Sasa mikataba hii ndio inaendana na kile kifungu, itakayoingiwa hapa. Sheria zitakazotumika ni za Tanzania. Haya ahsante. (Makofi)

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kuniongoza.

Mheshimiwa Spika, na jambo la pili ambalo limekuwa linaleta sintofahamu ni kuhusu suala la exclusivity. Kuna wanaodai kwamba DPW wamepewa haki ya kutokuingiliwa milele, yaani kwamba pasitokee mtu mwingine yeyote katikati atakayetaka kufanya kitu chochote.

Mheshimiwa Spika, lakini kwenye mkataba huu kwa uelewa wangu, na ilivyo huku ndani ni kwamba kipindi hiki cha majadiliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai kuhusiana na uwekezaji unaotakiwa ukafanyike bandarini, kipindi cha miezi 12 pasitokee nchi nyingine hapa katikati kutaka kuonesha interest au kutangaza kwamba anaweza akaja na yeye kutaka kuwekeza kwenye eneo hili ambalo ni eneo la phase one. Hii nayo naomba ikae hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na baada ya hapo sasa naomba nitoe ushauri wangu kwa Serikali; kama ambavyo umetuongoza, lakini pia nilisema nitasoma kifungu cha 22, hiki ni cha subsequent amendment, na yenyewe imekuwa inapotoshwa na utaniongoza kwenye mambo ya kisheria, mimi nakwenda tu kwenye mambo ya Kiingereza, kinasema hivi; This agreement may be amended at any time in writing, by the mutual agreement of the State Parties. No amendment to this agreement will have effect without agreement by the signature and the ratification and/or adoption of the appropriate documentation by the State Parties. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hakuna sehemu inayosema mkataba huu ukiingiwa hakutafanyika makubaliano yoyote, makubaliano haya. Kwa hiyo wajibu wetu Bunge kama ulivyosema kutokana na Kanuni zilizopo, tuna wajibu sasa wa kutaka kuishauri Serikali mambo ambayo yakaingiwe kwenye mkataba.

Mheshimiwa Spika, la kwanza kabisa ambalo napenda kushauri ni kuhusiana na suala la muda. Tutakapoletewa mikataba hiyo midogo midogo laizma ku-define muda ili tuweze kupata uhakika wa tunachokifanya, na ninapendekeza kipindi cha mkataba kiwe ni miaka 25, renewable kila baada ya miaka mitano ili kuona sasa kama performance inayopatikana ni nzuri, basi tuendelee kwa vipindi hivyo vitano mfululizo kwa miaka mitano mitano. Isiwe ni open goal.

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei.

TAARIFA

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, huyu mtu anakuja kuwekeza fedha nyingi sana, na fedha zile nazo ziwe recouped kwa muda fulani, payback period itakuwepo, kwa hiyo huwezi kusema ni miaka 25, inaweza ikawa hata miaka 30 kutegemea na aina ya mradi na kutegemea kwamba tija ya uzalishaji faida itakuaje.

SPIKA: Hapo hiyo taarifa inabidi nimlinde. Yeye kwa mawazo yake kasema tunaweza kuanza na miaka 25, ni mawazo yake. Kwa maana ya kwamba Serikali inavyokwenda kuzungumza na huyu mtu hoja ya muda ni muhimu na yeye anapendekeza miaka 25, wewe umetaja 30, labda ni 50, labda ni 10. Kwa hiyo, wote hatujui, tuniambia tu Serikali ikatazame hoja ya muda.

Mheshimiwa Cecil Mwambe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, na ninaamini muda wangu unalindwa.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ninapenda kupendekeza tunapoelekea kwenye hiyo mikataba midogo midogo ya utekelezaji, suala hili la eneo la bandari, ukisoma kwenye haya makubaliano imetaja eneo kubwa sana, na hata ukienda kwenye appendix I na yenyewe imetaja maeneo yaliyopo pale. Sasa wasiwasi uliopo ni kuhusu bandari ambazo zitakwenda kusimamiwa. Kwa hiyo, mimi napendekeza, kwa kuanzia…

SPIKA: Ngoja, eneo kubwa sana ukimaamisha nini?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwenye cover ya huu mkataba hapa inasema concerning, naangalia tu kile kipengele cha mwisho; economic and social partnership to the development…

SPIKA: Unasoma wapi, twende pamoja.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwenye cover ya makubaliano (agreement).

SPIKA: Yaani unasoma jina hapa juu?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ndiyo, chini kabisa sasa, hizo lines mbili za chini.

SPIKA: Sawa, enhe.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, improving performance of sea and lake ports in Tanzania. Sasa unaposema sea and lake ports in Tanzania, linaweza likawa eneo kubwa sana kwa maana…

SPIKA: Hapana, sasa ngoja, ndiyo twende vizuri.

Hili ni jina la mkataba, huku mbele umewekewa hizo appendix I, kama ulivyosema na ukaenda kwenye phase one, ukaenda kwenye phase two; maana yake huu mkataba humu ndani umetaja mambo ambayo yanahusika. Kwa hiyo, hatuwezi kuweka ile namna ambavyo wale watu wameiweka kule nje. Kwa nini, nimesema Bunge la leo lina kazi mbili, hii hapa na kuuelimisha umma kuhusu mkataba huu.

Sasa mkataba huu pamoja na hilo jina la mkataba huku ndani kumetajwa ni mambo gani yanayohusika, na kichwa cha habari cha hiyo appendix I kinaeleza nini hapo Mheshimiwa Mwambe? Kichwa cha habari cha appendix I kinasemaje? Kichwa cha habari tu pale juu. Ukurasa wa 35 hapo juu kabisa, appendix I.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwenye ukurasa wa 35 appendix I inasema; Areas of Cooperation.

SPIKA: Ambayo ndiyo maana nikakupeleka kule.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ndiyo.

SPIKA: Haya yote lazima moja moja wakae mezani wakubaliane, ambalo hawakubaliani linakaa pembeni. Ahsante sana.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.

Kwa hiyo, na mimi nataka kusisitiza kwenye hili, sasa tutakapotoka nje maana yake lazima tuwe specific kwa haya mambo, kwamba kuna areas of cooperation ambazo zipo na zitakubaliwa kutokana na appendix I badala ya ile tunayoambiwa kwamba iko very general, tutakwenda kila bandari ya Tanzania, tutakwenda mitoni, kwenye maziwa na maeneo mengine. Jambo hili siyo sahihi, lakini lilikuwa likitembea huko mitaani, kwa hiyo tukasome hii appendix I tunaweza tukapata uelewa wa pamoja kwa maana ya sasa bandari zitakazokusudiwa, lakini pamoja na area tutakayo-cover.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ninapenda pia kuliweka sawa ni faida zitakazopatikana kwenye utekelezaji wa makubaliano haya kwa maana ya mikataba. Ukisoma taarifa ya Mheshimiwa Mbarawa kwa maana ya Mheshimiwa Waziri kwenye mikataba hii wakati wa utekelezaji kuna mambo mengi tunakwenda kunufaika na sisi kama nchi.

Mheshimiwa Spika, jambo la kwanza kabisa ni kupunguza muda wa meli kukaa bandarini ambayo itakwenda kuongeza efficiency; lakini suala la pili ni la kuongezeka kwa ajira kwa Watanzania kutoka ajira 1,500 lakini tutakwenda mpaka ajira 2,950. Jambo lingine inategemea kuongeza mapato ya Serikali kutoka pesa inayokusanywa sasa hivi bandarini ambayo ni trilioni 7.76 mpaka mwaka 2031 kufikia trilioni 26.70.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, haya ndiyo mambo ambayo sisi kama Watanzania tuna haja ya kuyaweka sawa na ndugu zetu waliopo nje wanaotusikiliza waamini, na Waheshimiwa Wabunge wengi hapa wamekuwa wakielezea kuhusu sisi sasa, wananchi watuamini kwamba hatutaweza kwenda kuwaingiza kwenye kitu ambacho siyo kizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kulikuwa kuna Mkataba wa TICTS ulikuwa unatekelezwa, sasa hivi tunakwenda na wengine kama watakuwa DP World au mtu mwingine atakuwa na interest ya kutaka kuja pale, lakini kimsingi hatuwezi kurudia makosa yaliyofanyika huku nyuma.

Mheshimiwa Spika, nishukuru kwa kunipa nafasi, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia jioni hii kwenye Wizara hii muhimu sana na hotuba ya Waziri wa Nishati. Mwanzo kabisa kwanza ni¬-appreciate mchango wa Mheshimiwa Festo Sanga ambao aliutoa jana, wakati anachangia alikuwa anaeleza vizuri sana kuhusiana na uwezo wa wawekezaji wa ndani kwenye kuzalisha umeme. Alitoa mfano wa Kiwanda cha Kagera Sugar ambao wanatumia malighafi zinazobakia za sukari, yale mabaki ili kuzalisha umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulifanya ziara hapo karibuni na kwenye ziara ile walituonesha mitambo anayosimika sasa hivi yenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 za umeme wakati mahitaji ya Mkoa wa Kagera tuseme kama megawati 10 hivi ukitoa yeye mahitaji yake, lakini mpaka kufikia miaka mitatu, minne ijayo, atakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 60. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri azingatie ule mchango wake na aone namna ya kuondoa hii sheria kandamizi inayowazuia watu wenye uwezo wa kuzalisha umeme kwenye baadhi ya maeneo kuingiza kwenye gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, pamoja na pongezi zangu kwao Mheshimiwa Waziri kwa namna anavyofanya kazi zake na weledi wake kwa kulisaidia Taifa hili na naamini Mheshimiwa Rais, Mama, anamwamini sana kwenye kazi hii. Nafahamu Waziri sasa hivi ndio kiongozi wa majadiliano yanayoendelea kuhusu kukamilika kwa Mradi wa Gesi ya Lindi kwa maana ya LNG wenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 30. Nimwombe sana, mradi huu ni mkubwa na wenye manufaa makubwa sana kwa watu wa Mikoa ya Kusini kwa maana ya Mtwara na Lindi, lakini kwa Taifa lote kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatutegemei mradi huu ni wa muda mfupi, uwekezaji unaofanyika ni wa muda mrefu, utasaidia vizazi na vizazi. Sasa nimwombe Waziri, katika kukamilisha majadiliano ya mkataba huu ahakikishe wanaweka kule ndani clause inayowataka wawekezaji wawe na ulazima wa kutumia Bandari ya Mtwara kwa maana ya kuleta vifaa vitakavyosaidia kwenye uboreshaji wa mradi, lakini pia kutumia Uwanja wa Ndege wa Mtwara pia ambao sasa hivi ni mkubwa sana, umeboreshwa kwa maana ya run way, ina urefu zaidi kidogo ukilinganisha na Uwanja wa Ndege wa Dar-es-Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, sasa hivi pale kuna uwezo wa kutua Antonov yenye uwezo wa kubeba tani nyingi tu ya vifaa. Kwa hiyo, hebu tuwalazimishe hawa watu watumie Uwanja wa Ndege wa Mtwara, watumie pia na Bandari ya Mtwara ili iweze kuchakachua, kuchenjua uchumi wa maeneo haya kwa ajili ya wananchi wa Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nishukuru sana kwa namna wanavyofanya kazi zao na nilimfuata nikamweleza na tulikwenda ofisini kwa Mheshimiwa Waziri mara nyingi tu, Miradi ya REA inatekelezwa kwenye maeneo yetu, lakini kwa bahati mbaya sana scope inakuwa ni ndogo, kwa hiyo, niliomba hapo nyuma katika miaka miwili, mitatu iliyopita, nilikuwa naongea sana kuhusu kata mbili kwa maana ya Kata ya Mpanyani pamoja na Kata ya Msikisi; wakandarasi, mkandarasi wetu Namis Corporate yuko pale na anashirikiana vizuri sana na Meneja wa Wilaya na yeye tumpongeze kwa kazi nzuri anayoifanya, lakini sasa niombe kwa makusudi kabisa kuongeza scope. Watakapokuwa wanatoka kwenye hizi kata wahakikishe vitongoji vyote vya kata hizi vimepata umeme ndipo twende maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu kuna tatizo, sasa hivi ukienda Kata ya Ndanda tunaambiwa kuna umeme, lakini umeme huo haujafika zahanati ya Ndanda na sisi tunasema kwamba, umeme lazima ufike kwenye vituo vya kutolea huduma za kijamii. Umeme pia, haujafika zahanati ya Nasindi, zahanati ya Chihoro, zahanti ya Ngalole, Kituo cha Afya cha Mpanyani, Kituo cha Afya cha Lukuledi, Kituo cha Afya cha Namatutwe, Kanisa Katoliki la Nanganga, pamoja na Kanisa la Chikunja, maeneo haya yote hayajapatiwa umeme, lakini ukisikiliza wanakwambia kata hizi zina umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, historia ndefu kidogo. Kuna kitongoji kimoja kinaitwa Ndolo, kiko kwenye Kata ya Ndanda. Nimwombe sana Mheshimiwa Waziri, atuongezee nguvu kwenye eneo hili, watu hapa wanapata shida sana kwa sababu, miaka mitano, sita iliyopita walikuwa na umeme; walikuwa wanapata umeme kutoka kwa wamisionari wa Ndanda kama msaada, lakini baada ya kuzidiwa mitambo inayozalisha umeme kwenye hiki kitongoji, kwa hiyo, watu wa Ndanda wameamua kuchukua umeme wao, sasa wale watu wamefanya wiring kwenye nyumba zao. Ni kipande kama cha mita 200 tu. Ni suala sasa la kufanya uamuzi ili kuweza kupeleka umeme kwenye kitongoji hicho kwa sababu, watu wale sasa wako gizani wakati miaka mitano iliyopita walikuwa na umeme wa kutosha. Kwa hiyo, niombe sana Waziri tusisitize tufanye kazi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, tulifanya ziara kama nilivyosema kwenye Mkoa wa Kagera, tuliweza kufika kwenye Kiwanda cha Minza wanaozalisha kahawa, lakini kule kwetu Mtwara pia, kuna viwanda vinavyozalisha korosho, kuna viwanda vinavyozalisha pamba. Kuna sheria moja kandamizi inayolazimisha viwanda hivi wakati hawafanyi uzalishaji wachajiwe kitu kinaitwa capacity charge. Capacity charge inachajiwa asilimia 75 ya matumizi ya mwezi uliopita, kwa maana ya previous. Kwa mfano, kama huu ni mwezi Juni nimesimamisha kiwanda kuzalisha, nalazimika kulipa asilimia 75 ya invoice yangu ya umeme ya mwezi uliopita, nisipoendelea kuzalisha bado nitakuwa naendelea kulipa hivyohivyo kwa kuonesha kama ni capacity charge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii ni kandamizi. Sheria ya capacity charge ilitungwa wakati huo ili kuweza kupunguza matumizi ya umeme kwenye viwanda. Nimwombe Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anafanya review ahakikishe sheria hii anaileta tubadilishe ili tuweze kuwasaidia wawekezaji, tuweze kuwavutia wawekezaji. Hata sisi kwenye Kamati yetu ya Viwanda na Biashara na ukiangalia iko mpaka kwenye blue print, haijafikiwa kwenye utekelezaji wake, lakini tunaomba sana capacity charge iondolewe ili wawekezaji wawe na uhuru, asipotumia umeme asiulipie, haina maana ya kumchaji invoice ya umeme na hivi ndio vitu ambavyo tunasema vinaongeza inflation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine kwenye masuala ya gesi haya ambayo niliyasema pale mwanzoni. Tunaomba sana sisi watu wa kusini mijadala hii inayohusiana na masuala ya gesi kwa sababu, sasa hivi wanasema wanaelekea kwenye hatua ya kuwekeana saini, basi baada ya kuwekeana saini mara moja mijadala yote inayohusu masuala ya gesi, matumizi yake na mengine tuyaone yanaletwa kwenye Mikoa ya Mtwara, Lindi na mikoa mingine ya kusini ili iweze kuwachangamsha watu na kuwafanya waone kuna kitu pale kinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii itasaidia kuchangamsha biashara, lakini pia, itawafanya watu wawe aware kwa sababu, wao ndio walinzi wa miundombinu hii. Tusipofanya hivyo kwa sababu kwa miaka karibu takribani kumi, kumi na tano nyuma, shughuli za gesi Mkoa wa Mtwara zilisimama ndio zilizosababisha uchumi wa mkoa wetu sisi kuyumba. Bandari haifanyi kazi vizuri wakati ile bandari ilikuwa inakusudiwa kupeleka vifaa vya gesi pia baada ya Serikali kuongeza kwenye ile berth moja walikuwa wanakusudia pale kutulia vifaa kwa ajili ya kupeleka Mozambique kwenye miradi ya gesi. Sasa miradi ya gesi ya Mozambique haiendi vizuri kutokana na hali ya kiusalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa bahati hii imerudi kwetu, kutoka Bandari ya Mtwara mpaka Lindi ni karibu kilometa 125. Kwa hiyo, tuombe kabisa mizigo itakayokuwa inatakiwa ifike kwa ajili ya uboreshaji wa huu Mradi wa LNG ishuke moja kwa moja Bandari ya Mtwara iweze kupelekwa pale. Ndugu zetu wa Mtwara watachangamka, uchumi wa mkoa wetu utachangamka na utaanza kuona manufaa ya gesi mapema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri asisahau kabisa kuangalia hilo jambo na nimshukuru sana kwa kazi kubwa anazozifanya, sasa hivi Kijiji cha Mumburu kilichopo Jimbo la Ndanda wakandarasi wa REA wako pale. Kijiji cha Nanganga, tunaomba sasa akaongeze nguvu kwa maana ya kupeleka umeme katika Kijiji cha Nanganga A, Kijiji cha Mkwera, Kijiji cha Mumburu kama nilivyosema A na B, isipokuwa baadhi ya vitongoji vinakosa. Tuangalie pia, uwezekano wa kupeleka umeme Kijiji cha Tungani, kuna baadhi ya maeneo yanakosa, lakini pia Kijiji cha Mwongozo pamoja na Mkangu kwenye maeneo yote ya Jimbo la Ndanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri., kama ambavyo nilisema awali kwamba, kazi hizi zinakwenda na tulikutana wakati ule na Mheshimiwa hapa Mkurugenzi wetu wa REA. Yale tuliyoyaongea basi Waziri ataendelea kuyafanyia kazi, lakini kimsingi kazi za umeme Jimbo la Ndanda zinakwenda na naamini hivi karibuni tu watakwenda kuwasha. Nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri na naunga mkono bajeti yake, nimtakie kila la heri katika kutekeleza yale yote aliyoyakusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi jioni hii ili niweze kuchangia na kutoa maoni yangu hasa zaidi kuhusu bajeti iliyopo mbele yetu na kuifanyia maboresho kwa manufaa ya nchi yetu. Kwa namna ya pekee kabisa niwapongeze Mheshimiwa Waziri na Naibu wake Mheshimiwa Chande tumefanya kazi wote pamoja kwenye Kamati ya Viwanda na Biashara, ni mtu makini na hawa wote ni watu makini sana na wasikivu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti iliyopo mbele yetu ni nzuri sana na kwa vyovyote vile imeonesha nia njema kabisa ya Mheshimiwa Rais kutaka kulisongeza Taifa hili mbele. Mimi ni mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara, kwa hiyo nitaongea kidogo kwenye upande wa biashara mambo ya kodi, tozo na mengine kwa maana ya kutaka kuboresha bajeti hii. Kwa namna ya pekee kabisa nimpongeze Mheshimiwa Rais pamoja na Wizara yetu ya Utalii kwa sababu hivi karibuni tumeona Mheshimiwa Rais amesafiri nchi nyingi hapa duniani kwenda kufanya kazi ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii kwenye ile sinema maarufu kabisa inayoitwa Royal Tour. Hata hivyo, jambo ambalo nataka niwakumbushe Waheshimiwa Wabunge kwamba kwenye Bunge lililopita kila mara tulikuwa tunaongea suala la vita ya kibiashara na tulikuwa tunajaribu ku-site namna ambavyo majirani zetu wanajaribu kutumia vivutio vyetu na kuvitangaza kama vivutio hivi ni vya kwao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa vyovyote vile namna mama alivyofanya kazi nzuri kwenye hii sinema ya Royal isingekuwa rahisi majirani zetu kukaa kimya na kuona kwamba sisi sasa tunataka kwenda kuwa sehemu kubwa ya utalii katika Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo lazima tutapigwa madongo kwa kila kona na sisi kama Watanzania lazima tuwe na uwezo wa kuwajibu lakini na kuongeza zaidi vivutio kwa maana ya biashara yetu ya utalii iwe kubwa zaidi kuliko nchi za jirani, kwa sababu sasa hivi tumeamua kueleza sisi wenyewe kwamba sisi kama Watanzania ndio wamiliki wa Mlima wa Kilimanjaro, sisi kama Watanzania ndio wamiliki wa Ngorongoro, sisi kama Watanzania ndio wamiliki wa Loliondo. Kwa hiyo ukishuka Uwanja wa Kimataifa wa Dar es Salaam, ukishuka Uwanja wa Kimataifa wa KIA uliopo Kilimanjaro kwa vyovyote vile utafika Kilimanjaro, utafika Loliondo, lakini pia utafika na Ngorongoro. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, zamani walikuwa wanasema ili ufike Mlima Kilimanjaro unatakiwa ukashuke kwenye uwanja wa nchi za jirani ili iweze kuwa rahisi kutoka kule kurudi hapa. Ninachoomba sasa ni kuboresha miundombinu ili tuweze kwenda sambamba na hizi kelele zinazopigwa na majirani zetu tusizichukulie poa poa kidogo, Mheshimiwa Waziri wa Utalii aongeze juhudi kwenye kuhakikisha sasa vivutio vyetu vya utalii vinatangazwa zaidi duniani kwa ajili ya manufaa ya Watanzania ili tuweze kukuza uchumi wetu tuweze kupelekwa kwenye nchi ya daraja la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona kuna NGOs nyingine na wanaharakati hata Watanzania na wenyewe wamekuwa sehemu ya hujuma zinazofanyika kwa maana ya Ngorongoro lakini pamoja na Loliondo. Kwa hiyo tuwe makini sana tusichanganye mambo haya. Harakati pamoja na haki za binadamuh lakini harakati pamoja na biashara na lazima tutambue kwamba sasa hivi tupo kwenye vita ya kibiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna jambo lingine tumeona sasa hivi nchi yetu kumekuwa na inflation na hii inflation imesababishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa. Ukiangalia vizuri imegawanyika katika namna mbili kuna sababu zetu wenyewe za ndani na kuna sababu za nje. Sababu za nje kila mara tulikuwa tunasema vita lakini pia na upatikanaji wa malighafi za kuzalishia, vitu vingi sisi tulikuwa tuna import.

Mheshimiwa Naibu Spika, niombe sasa na sisi tuwe exports kwa maana tufanye kazi kwa nguvu kabisa tuhakikishe Mradi wetu wa Liganga na Mchuchuma unaanza mara moja ili tuweze ku-export chuma, tuweze kupata fedha za kutosha kufanyia miradi yetu ya ndani. Pia tuangalie, kuna tozo mbalimbali zinazotozwa kwenye bidhaa ambazo zinazalishwa hapa nchini lakini pamoja na bidhaa ambazo zinatoka nje ya nchi, tukiamua kurekebisha tozo hizi kwa vyovyote vile gharama za uzalishaji za ndani zitashuka.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, niwaombe Waziri amemaliza ku-present hii taarifa yake lakini kuna mambo tuyaangalie. Sasa hivi ni zaidi ya miaka minne, mitano, nafikiri toka VAT iliposhushwa kutoka asilimia 20 ikawa hadi 18 hawajagusa tena VAT lakini pia hawajagusa tena corporate tax. Tukiamua kushusha vizuri VAT labda kufikisha asilimia 16, tukashusha corporate tax hadi kufika asilimia 24, kutakuwa na compliance kubwa, watu wengi wataweza kulipa kodi na mauzo yataongezeka na hii itakwenda kuchangia kwenye kuongeza ajira.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwapongeze hapa wakati Waziri anatoa taarifa yake alikubali kabisa kwamba sasa hivi Sheria ya Korosho ambayo ilikuwa ina-hold export levy amekubali sasa kurudisha, lakini tuiboreshe zaidi. Ilipoondolewa wakati ule ilikuwa ni asillimia 65 ambazo asilimia 50 zilikuwa zinarudi Serikali Kuu, lakini 15 zilikuwa zinakwenda kusaidia kwenye vituo vya utafiti na maeneo mengine. Sasa hivi imerudi ni fifty fifty, nimwombe sana Mheshimiwa Waziri tutengeneze kanuni bora kuona namna ya kutumia fedha hii. Sisi tunatamani sana fedha hii ingekwenda kupelekwa kama ruzuku kwenye pembejeo zinazosaidia kuzalisha korosho, lakini fedha imepelekwa Wizarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizarani kuna mazao mengi sana, madhumuni ya fedha hii ilikuwa inakatwa ili ikasaidie wakulima wa korosho pamoja na kwamba sasa hivi wakulima wa korosho wamekuwa mtambuka nchi nzima watu wanahamasishwa kulima korosho, sio jambo baya, lakini ikasaidie tu kuendeleza zao la korosho.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine kuna suala la blueprint. Mheshimiwa Waziri wakati analeta taarifa yake ameongea sana kuhusu suala la blueprint na kwamba kuna kodi zile mbalimbali karibu 15, nafikiri wameamua kuziondoa ili kuweza kuona zinawafanya wawekezaji kuvutiwa kuja nchini kwetu kuwekeza kwa sababu ya kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe kwamba speed inayotumika sasa hivi kwenye kutekeleza mambo mbalimbali yaliyomo ndani ya blueprint ni ndogo sana. Niombe Wizara iongeze speed kwenda kuhakikisha na zile kero zinazotajwa na wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza hapa Tanzania nazo zinaondoka, mojawapo ikiwepo hii ya city levy. city levy inapangwa na halmashauri zetu lakini city levy sheria inataka kuanzia asilimia 0.01 hadi 0.03. Kutokana na kuwa na vyanzo vichache vya mapato Halmashauri nyingi zinaamua kukamua wafanyabiashara. Wengi wanang’ang’ania kutoza asilimia 0.03 wakati ruksa ni kuanzia asilimia 0.01 hadi 0.03.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa karibuni tulifanya ziara Bukoba, tulitembelea viwanda pale na tukaenda kwenye Kiwanda cha AMIMZA kwenda kujionea wenyewe wanaozalisha kahawa lakini pia tulifika kiwanda cha sukari, hii mitaji imekuwa ni kero kubwa sana. Nimwombe Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind up basi atuambie kwamba ni nini, kodi hii lazima iwe ya pamoja,haiwezekani ukienda Mtwara ukute asilimia mbili, ukienda Bukoba ukute asilimia tatu, ukienda maeneo mengine, inakuwa inatofautiana. Kwa hiyo lazima nchi nzima iwe uniform, kama asilimia 0.01 kwa ajili ya city levy iwe hivyo, kama ni asilimia tatu basi iwe hivyo, lakini utofauti unaoletwa kwa kila halmashauri sio mzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la capacity charge. Kuna tozo ambayo ipo kwenye umeme inaitwa capacity charge, kwa kawaida wazalishaji ukienda kwenye kahawa tuseme labda tutumie mfano, lakini ukienda kwenye viwanda vya korosho huwezi kuzalisha kwa mwaka mmoja, kuna kipindi fulani ambacho wanafunga uzalishaji. Sasa unapofunga uzalishaji bado Serikali au kwa maana ya TANESCO wanaendelea kukutoza gharama za umeme kwa asilimia 75 katika mwezi wa kwanza kutokana na previously bili yako. Bili uliyolipa mwezi uliopita tunazota asilimia 75 mwezi huu, halafu ukiacha tena kuzalisha au kutumia umeme, mwezi unaofuata unatozwa asilimia 50. Hii imekuwa kero kubwa sana kwa wafanyabiashara, kwa hiyo tunaomba sasa tuachane na hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine tumeona walifanya marekebisho hapa sasa hivi crude oil, nafikiri itaingia kwa asilimia sifuri, lakini tuangalie na viwanda vya ndani. Unapoamua kuruhusu wafanyabiashara wa nje kuingiza mafuta pasipo kutoza kodi, tafsiri yake unakwenda kusababisha upotevu wa ajira au uzalishaji, lakini tuangalie namna gani hili jambo tunakwenda kulifanya. Kwa vyovyote vile kama sisi Wajumbe wa Kamati ya viwanda na biashara tulikuwa tunajadili ili mara nyingi, utakapomruhusu mwekezaji wa nje aingize ndani mafuta ghafi kwa asilimia sifuri, ndio nia ni njema kutaka kupunguza gharama za mafuta hapa nchini, lakini tuone namna gani tunakwenda kuathiri viwanda vinavyozalisha mafuta hapa nchini kutokea level ya chini, maana yake kwamba wao wananunua alizeti, watakwenda kuzichuja mafuta, watafanya refinery baadaye wanaziingira sokoni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunapoleta crude oil kwa asilimia sifuri, watu wataondoka. Tulikitembelea kiwanda kimoja Dar es Salaam, siwezi kutaja jina, lakini alikuwa analalamika kwamba wanaoleta mafuta toka nje wana-declare kwamba ni crude oil, wanafikia kwenye process, labda katikati ya process nzima ya uzalishaji. Kwa hiyo unaweza ukakuta gharama yake ni chini zaidi kuzalisha na kikubwa anachofanya ni kusafisha na kufanya packaging, lakini wale watu wana watu wanaonunua alizeti mitaani, wana watu wanaosafirisha alizeti kuleta viwandani, lakini pia kuna watu wanaofanya kazi ya kupepeta, kuchekecha hizo alizeti mpaka zinakuwa mafuta. Kwa hiyo tuone namna gani tutavisaidia viwanda vya ndani pamoja na nia njema ya Serikali kutaka kupunguza hizo gharama za uzalishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni suala la kodi kama ambavyo nimesema hapo, tunapoweka kodi nyingi kwenye viwanda, kwa vyovyote vile vitapunguza ajira, tunapoamua kusaidia viwanda kwa kupunguza kodi na sehemu kubwa ndio tunayosema VAT, tumeona hapa Serikali imeamua kufanya VAT refund hapa karibuni, lakini pia tumeiona Serikali inajaribu bado kutaka kuwasaidia wale wawekezaji wa ndani. Mfano, nilioutoa kwenye mafuta unafanana pia mfano huo kwenye viwanda vya bati.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeona sasa hivi kuna viwanda vingi sana vya bati vimeingia Tanzania, lakini wenzetu nitataja kwa jina ALAF, wao ALAF wanachokifanya wananunua rollers zile bar rollers, mara nyingi ukiangalia ukiwa unatoka bandarini unaziona na wao wanaanza process kuanzia ya kwanza kuchukua zile chuma, kuzibonda, kuzi-size, kuzipiga rangi na baadaye kuziweka migongo na kuzikata, lakini kuna viwanda ambavyo wanaingiza hizo material zikiwa tayari karibu na kuwa semi-finished, wakifika hapa Tanzania kazi wanayoifanya ni kupiga rangi na kuweka migongo na kuzikata na kuziingiza sokoni. Kwa hiyo unaweza kuwa na kiwanda cha bati chenye watu 20…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa nafasi na mengine nitayaleta kama mchango wangu kwa maandishi. Ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa namna ya pekee kwa kunipa nafasi ya kuchangia leo. Nimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai kurudi hapa tena leo kwenye Bunge la Kumi na Mbili. Nikishukuru chama changu cha Mapinduzi, Chama ninachokitumikia sasa hivi ambacho ndicho chenye Ilani na walinikabidhi Ilani wakati wa uchaguzi mkuu na nilishinda kwa kishindo Jimbo la Ndanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru sana pia ushirikiano ninaoupata kutoka kwa Wabunge wenzangu wa Chama cha Mapinduzi. Nimesimama hapa nikiwa na furaha kwa sababu kati ya mambo ambayo nilikuwa nayatamani siku zote ni kusimama na kuitetea Ilani ya Chama cha Mapinduzi na mipango mizuri ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwashauri sana ndugu zangu wa upande wa pili, Waheshimiwa Mawaziri pia ikiwezekana tuwagawie wale ndugu zetu Ilani ya Chama cha Mapinduzi kuna mambo mengine wanayabishia kwa sababu hawajayaona, hawajasoma na hawayafahamu vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ya msingi ambayo napenda kuyachangia leo kwenye Mpango huu. Suala la kwanza kabisa ni kuhusu reli ya Kusini. Tunataka hapa Waziri wetu aje kutueleza nini mpango madhubuti wa Serikali kuhusu reli ya Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tumesikia wengi wanaongea, suala la Liganga na Mchuchuma, kama ambavyo nimesema toka mwanzo kwamba liko hata kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Tunaomba sasa likafanyiwe kazi na litekelezwe kwa ajili ya kuongeza uchumi wa watu wa Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia kuna suala la barabara. Barabara ya Mtwara – Newala – Masasi – Nachingwea – Liwale na kipande cha barabara ambacho huwa hakitajwi kinaenda kuunganisha Malinyi ili kuwafanya watu wa Mikoa ya Kusini kwa maana ya Mtwara, Lindi na Ruvuma kufika kirahisi Makao Makuu ya nchi badala ya kupita njia ndefu ya Dar es Salaam. Kuna barabara pia ya Nanganga - Nachingwea – Ruwangwa mpaka Liwale pia na yenyewe tunaomba ifanyiwe kazi na tupate hapa majibu ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la wastaafu, limeongelewa hapa ndani na Wabunge wengi sana, wa ngazi mbalimbali wakiwemo wanajeshi, walimu kuhusu stahiki zao na haki zao za msingi na kumekuwa na ucheleweshwaji mkubwa sana wa malipo yao wakati huu. Kwa hiyo, tunaomba Serikali kwa kina kabisa ije itueleze mikakati yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi nataka nijikite hasa kwenye suala la kilimo. Sisi kule kwetu ni wakulima wa korosho na ni zao la kimkakati la Kitaifa katika yale mazao matano makubwa. Niombe sana Serikali izingatie sasa kuona tunawasaidia hao wakulima wa korosho ili waweze kusaidia kuongeza uchumi katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna matatizo makubwa ambayo huwa yanajitokeza kila mara wakati wa kilimo. Msimu uliopita wa korosho tumeona wakulima wanahangaika sana kupata magunia. Katika karne ya leo kunakuwa na shida ya vifungashio vya korosho yetu tunayotaka kuiuza. Kwa hiyo, niombe sana Serikali iweke msisitizo na Waziri wa Kilimo aje kutueleza hapa mikakati yao ya kuhakikisha magunia na pembejeo kwa maana ya sulphur inapatikana kwa wakati kwa ajili ya wakulima hawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtakumbuka mwaka juzi katika mjadala hapa iliondolewa ile pesa kwa ajili ya tozo ambayo ilikuwa inakwenda kusaidia kufanya utafiti pamoja na kuongeza mambo mengine kwa wakulima. Tuiombe sasa Serikali kutafakari upya kama ambavyo imefanya kwenye kurejesha ile pesa ambayo ilikuwa inakusanywa na TRA kwa ajili ya mabango imekwenda tena kusaidia halmashauri. Kama inawezekana basi, waone namna ya kuwasaidia wakulima, hii pesa ingeweza kurudi kwenda kulipa yale madeni ya zamani ambayo wanadai watu wengi waliotoa huduma kwenye zao hili la korosho na sekta nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia hapa Mbunge mmoja anasema zao la korosho limeshuka kidogo uzalishaji wake, ni kwa sababu ya kukosa utafiti, kukosa dawa kwa wakati na uwezo mdogo wa wasimamiaji. Mazao haya ya kimkakati yanasimamiwa na vyama vya ushirika. Sisi kimsingi tulichoka, pamoja na nia njema ya Serikali kutaka kuboresha, lakini tuone sasa unapatikana mfumo thabiti kabisa utakaokwenda kupata viongozi bora, waadilifu na waaminifu kwenye vyama vyetu vya msingi na kwenye vyama vikuu ili kuweza kuwasaidia wakulima. Tumeona sasa hivi chaguzi mbalimbali zinafanyika ndani ya vyama hivi, lakini kimsingi watu wa COASCO hawajafanya kwa uhakika kabisa mahesabu kwa sababu, wanapobadilishana uongozi kwenye vyama hivi kumekuwa na utaratibu wa kurithishana madeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna madeni makubwa sana ya wakulima sisi tumeyakuta. Tumetoka kwenye Bunge lililopita tumeingia kwenye Bunge hili bado madeni hayo yapo. Kwa hiyo, niiombe Serikali au Waziri wa Kilimo awaagize watu wa COASCO kabla viongozi hawa hawajamaliza kukabidhiana madaraka yao pale, basi kimsingi wahakikishe kabisa wanafanya ukaguzi, ili kuweza kukabidhiana ripoti zilizo safi, lakini tufahamu watu wa kuweza kuwawajibisha pale panapotokea upungufu katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimesema kwamba, kwenye zao la korosho kuna mambo mengi sana, kwa hiyo, tunahitaji kabisa kimsingi, sisi kama wakulima tunaotokea eneo la wakulima wa korosho, tukutane na Mheshimiwa Waziri katika sekta hii ili tuweze kumshauri vizuri kwa sababu, mambo mengi tunayafahamu kule nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja hii kwa mara ya kwanza toka niingie kwenye Bunge hili, kwa sababu huko nyuma nilikuwa siwezi kuunga mkono kwa sababu tulikuwa tuna ilani ambayo tunaitekeleza. Ahsante. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi asubuhi hii, lakini nikupongeze kama alivyotangulia kusema ndugu yangu hapa Mheshimiwa Getere kwamba nafasi uliyonayo ni kubwa sana na naamini dunia inafuatilia Bunge letu la Tanzania na nikuombe sana utengeneze historia kwenye Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, utatutendea haki sana endapo utaelekeza sasa sisi kama Wabunge tukae na kupitia maazimio yote yaliyotolewa na Bunge kwenye Ripoti za CAG kwa miaka mitatu nyuma ili wote waliohusika wawajibishwe ndani ya Bunge letu, kwa sababu hiki ndicho wanachokisubiri wananchi huko nje kuona sisi tumefanya nini.

Mheshimiwa Spika, ukifuatilia kwenye mitandao binafsi unapongezwa sana na Wabunge wengi wanaochangia wanapongezwa sana. Ndugu zetu Mawaziri kwa namna fulani wanalaumiwa na wanakuwa less popular maeneo mengi hasa zaidi wanapotaka kutoa taarifa za kuwa-distract watu kwenye mjadala mzito kama huu unaohusu Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nikuombe pamoja na kwamba kanuni zinaruhusu kufanya hayo mambo Waheshimiwa Mawaziri mtuache tuishauri Serikali, lakini pia tujaribu kuielekeza kwa sababu naamini Bunge hili linafuatiliwa wapi kwenye matobo kwenye maeneo sisi tunakotokea kwa maana ya lutaka kulisaidia taifa letu. Kwa hiyo, mtuache tufanye kazi yetu ya kuishauri Serikali, lakini na kuwashauri na ninyi ili mkachukue hatua mtakaporudi kwenye ofisi zenu.

Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi wameongea na kama ulivyosema hapo kwamba hata muda wenyewe sasa tunapunguza kwa sababu tunaelekea kwenye kuhitimisha. Nimekuja hapa kwa ajili ya kutoa ushauri.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu wa kwanza kuhusu kubadilisha kanuni ili Ripoti ya CAG inapokuja mwezi Machi ikiwezekana Wabunge tukubaliane tuendelee kuijadili kwa kubadilisha kanuni zetu ili tunapokwenda mwezi Julai kwenda kufanya allocation za pesa nyingine kwa ajili ya bajeti inayofuata na haya tuwe tumepata majibu yake, kwa maana ya kwamba taarifa hii tuwe tumeijadili. Kwa hiyo, tuone namna ya kubadilisha kanuni kwenye hilo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine Mheshimiwa Simbachawene jana alijibu kwamba sisi Wabunge ni sehemu ya Kamati za Fedha kwenye Halmashauri zetu. Hakuna Mbunge hapa ambaye hafahamu kwamba ratiba zinatofautiana sana. Sisi tuko hapa Bungeni tunajadili masuala haya, lakini na huko kwenye Halmashauri zetu vikao vya Halmashauri vinaendelea, Kamati za Fedha zinakaa, Mabaraza yanakaa. Kwa hiyo, tuone namna ya kubadilisha kanuni ili tuweze kuhudhuria kwenye hivi vikao na tuweze kuzishauri Halmashauri zetu vizuri namna ya matumizi bora ya hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kumejadiliwa hapa suala la Mfuko wa Usalama wa Raia SACCOS na kwamba taarifa zimekuja kuna upotevu. Mheshimiwa Bulaya jana hapa alisema vizuri tuombe basi kama kweli tuna nia ya kutaka kuwawajibisha hawa watu na Mheshimiwa Naibu Waziri jana alijibu kwamba kuna watu wako mahakamani. Nataka nimkumbushe amemsahau Mheshimiwa Afande Sirro ambaye alikuwa IGP wakati haya mengine yanatokea basi wafanye utaratibu wamrudishe ili naye aunganishwe na hawa watu walioko mahakamani kwa sababu ametwambia kwamba hili jambo liko mahakamani. (Makofi)

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, tukaangalie pia na suala la Mfuko huu wa Kufa na Kuzikana lakini tukaangalie na SACCOS…

SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe kuna tarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ester Bulaya.

TAARIFA

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nampa taarifa, siyo Sirro peke yake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili ametajwa kwenye taarifa baada ya taarifa akapata uteuzi wa Naibu Katibu wa Maliasili na Utalii. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe unaipokea taarifa hiyo?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, naipokea hiyo taarifa nadhani namuongezea Mheshimwa Waziri hapa wigo mpana wa kutimiza wajibu wake.

Mheshimiwa Spika, pia kuna suala la Mfuko huu wa Usalama wa Raia SACCOS, askari wetu wamekuwa na malalamiko makubwa sana, Mheshimiwa Waziri yuko hapa kwamba kila mara wanakatwa, hawapati taarifa zinazohusiana na makato yao, lakini hata hivyo kunakuwa na marejesho ama faida inayopatikana hawajawahi kushirikishwa.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni mishahara imeogezwa, ukiangalia kiasi cha mshahara kilichoongezwa na makato waliyoongezewa polisi kwenye huu mfuko wao havifanani. Kwa hiyo, niwaombe nao wakajaribu kujadiliana na wakubwa wa polisi kwa sababu askari hawa wadogo wanakatwa pesa hizi, lakini wao wanaamini kwa sababu ya utii wanaotakiwa kuwa nao mambo mengine wanashindwa kuyapinga, wanayaleta kwetu sisi kama Wabunge tuseme hapa yasikike ili wakubwa waone namna ya ku-review kwenye haya mambo.

Mheshimiwa Spika, ushauri mwingine lakini hili pia ni ombi na nimemuona hapa rafiki yangu Bwana Ndejembi kwamba tumesoma hizi taarifa zote, tumesikia madudu mengi yanayofanyika kwenye halmashauri zetu. Mimi niko hapa kuomba ukaguzi maalum kwa ajili ya Halmashauri ya Masasi DC. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mchungahela hapa jana wakati anasema, wakati anamalizia kwenye dakika ya tisa alitoa maelekezo kwamba hata kwenye Halmashauri yetu kuna ubadhirifu. Nataka nikuongezee, maeneo ambayo natamani kabisa mkayakague la kwanza kabisa ni eneo ambalo Mheshimiwa Rais alitoa pesa kwa ajili ya madawati, eneo hili halijafanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Spika, eneo la pili ujenzi wa sekondari Shule ya Mpeta, ujenzi ule umekuwa unalalamikiwa sana, lakini pia kuna ujenzi wa ghala letu la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi DC, ujenzi huu umekuwa unalalamikiwa sana. Pia tunayo hospitali yetu Mheshimiwa Rais alitoa pesa nyingi za kwenda kukamilisha Hospitali ya Tarafa ya Chikundi, sasa hivi ni karibu mwaka wa pili, tunaelekea mwaka wa tatu pesa zimekwisha, ujenzi wake haujakamilika.

Mheshimiwa Spika, lakini pia tunalo jengo letu ya Masasi DC ambalo Mheshimiwa Rais alikwenda kulifungua hili jengo mwezi mmoja miezi miwili iliyopita wakatoi wa ziara yake. Wakati Rais anakwenda nataka nikuchekeshe kitu kimoja hapa, palifanyika utaratibu wa kuondoa simenti kwenye Shule ya Sekondari ya Kata ya Chikunja ili kwenda kufanya marekebisho kwenye hili jengo Rais atakapopita aone pale mambo ni safi, naomba mambo yote haya yakakaguliwe na tupate taarifa maalum.

Mheshimiwa Spika, kuna jambo lingine limejitokeza karibuni pesa za likizo za walimu zaidi ya 120 wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi DC nazo zimetumika kwenye matumizi tofauti, walimu hawa hawajalipwa wameshindwa kwenda likizo. Kwa hiyo, nimeombwa na walimu na ili lenyewe nililete hapa niliseme.

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema kwamba mjadala huu umekuwepo hapa kwa siku tatu na sisi tunatokea maeneo hayo, na nakumbuka Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa aje kufanya ziara kwenye Wilaya yetu ya Masasi DC, tulitamani haya mambo yote tumuoneshe tumwambie kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu kuna haya mambo yanayotokea kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo bado niikumbushe Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba sasa waratibu hiyo ziara ya kuja Halmashauri ya Masasi DC, lakini kabla ya hapo ninyi kama watu wa TAMISEMI nendeni mkaangalie haya maeneo niliyowaambia kwa sababu tuna Mkurugenzi mpya, tunae pale DC wetu mpya ambaye ameripoti hivi karibuni, lakini wao wamerithi mambo ambayo wao hawawezi kuyamaliza pale, wameyakuta haya madudu.

Mheshimiwa Spika, pia niishauri Serikali kama inawezekana kila tunapopeleka Mkurugenzi mpya, Mkuu wa Wilaya kwenye maeneo haya ikafanyike kwanza special audit ili wakabidhiwe halmashauri ikiwa clear.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine tunapokaa muda mrefu na hizi taarifa kwa mfano Taarifa ya CAG tunaijadili leo hapa baada ya LAAC kwenda kufanya huko ukaguzi na vitu vingine, kimsingi tumebakisha taarifa mbili, maamuzi ya taarifa zetu tatu za huko nyuma hatujafanyia kazi. Walau sisi tuna historia tulipoingia Bunge la mwaka 2020 lakini tayari haya mambo tulishajadili kati ya 2015 mpaka 2020 tutawaachia kiporo Bunge lijalo kwa sababu tunaacha hivi vitu ambavyo sisi tumeviharibu, tumeshindwa kuviweka sawa sawa tunacha kwa ajili ya Bunge lijalo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niombe taarifa hizi za CAG zikija mwezi Machi tuzijadili kwa sababu kama hapa anatuambia tunapunguza muda wa majadiliano. Taarifa ambayo imekaa miezi sita/saba na sisi leo tunaijadili kwa dakika nane kwa dakika kumi, kwa dakika 15 tunajadili kwa siku tatu kuna mambo mengi ambayo kimsingi tunahitaji kuyachambua.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nisisitize bado tuombe kubadilisha kanuni ili ikiwezekana taarifa hizi zije mapema tuzijadili kwa ajili ya kusaidia Taifa letu, kwa ajili ya kumsaidia Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa nafasi uliyonipatia. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa namna ya pekee kwa kunipa nafasi ya kuchangia leo ambayo ni siku ya pili ya mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nianze kwa kutoa shukrani kwako wewe mwenyewe, Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waheshimiwa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Mtwara wakiongozwa na Mheshimiwa Chikota, viongozi wa chama na Serikali wa Mkoa wa Mtwara, mikoa ya jirani na majimbo Jirani, wananchi wote wa Jimbo la Ndanda na majimbo jirani, kwa namna ya pekee walivyoshiriki kwenye msiba wa mke wangu mpendwa Beatrice na walivyotupa faraja. Ahsanteni sana, nawashukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimerudi hapa kuendelea kufanya kazi zangu nilizotumwa na wananchi wa Jimbo la Ndanda na nimesimama ili nami niweze kuchangia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikiliza vizuri sana Hotuba ya Waziri Mkuu, nami nimeamua kuchagua maeneo manne au matano hivi ambayo ningependa nichangie kwa sababu ndiyo yanagusa Watanzania na wakazi wa Ndanda. Sehemu ya kwanza kabisa ni suala la kilimo; nitatumia hapo muda mrefu kwa sababu nataka kuona wananchi wale, wakazi wa Ndanda na Watanzania ambao ni zaidi ya asilimia 75 wanapata manufaa kutokana na kazi za mikono yao na kazi zao za shambani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameongea suala la umeme, nami nitachangia hapa pia masuala ya afya na masuala ya barabara na mwishoni mambo mengine ya mtambuka kwa ujumla. Kwenye suala la kilimo, nimefanya mazungumzo kwa kina na Naibu Waziri, Mheshimiwa Bashe na kujaribu kumweleza mambo yanayotusibu sisi wakulima na hasa wakulima wa Korosho kwenye sekta hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwakumbushe tu Wabunge wenzangu wote kwa ujumla kwamba, mtakumbuka katika mazao makubwa matato yanayotajwa kimkakati ni pamoja na korosho, lakini kwa masikitiko makubwa sana, mwaka 2020 uzalishaji wa Korosho ulipungua msimu uliopita kutoka msimu ule wa mwanzo. Mwaka 2020 tulipata tani 205 tu, wakati msimu uliofuatia nyuma ulikuwa ni tani 330. Hii imetokana na kutokutimiza wajibu wetu sawa sawa kwenye kuwasaidia wakulima.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ambalo naiomba Serikali ifanye sasa; na tumesikia hapa na kupata majibu kwamba kuna mkakati mzuri kabisa ambapo Serikali inakwenda kununua pembejeo kwa pamoja na kuzigawa kwa wakulima ili ziweze kuwafikia kwa wakati na vile vile tunaamini zitakuwa na ubora unaotegemewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana na nimsisitize sana Mheshimiwa Hussein Bashe, kama mpango huu umepangwa na Serikali, basi utimizwe kama vile ambavyo mmekusudia ili kuweza kuongeza uzalishaji wa korosho. Inasikitisha kuona wafanyabiashara wanajinufaisha sana inapofika misimu ya wakulima kuweza kupata pembejeo pamoja na virutubisho vingine ambavyo vinatumika kwenye mikorosho.

Mheshimiwa Naibu Spika, msimu uliopita na misimu mingine huko nyuma tumeshuhudia sulphur ikiuzwa mpaka kati ya shilingi 35,000/= mpaka shilingi 50,000/= kwenye maeneo mbalimbali, jambo ambalo ni baya sana kiasi kwamba wakulima walikuwa wanashindwa kununua na kuhudumia mikorosho yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tumefurahi kuona nia njema ya Serikali hii ya Awamu ya Tano na Awamu ya Sita kwamba ambapo wanatuahidi kwamba bei za sulphur sasa itapungua mpaka kufikia shilingi 29,000/=, tena zitatolewa kwa wakulima kwa njia ya mkopo ambayo baadaye mnunuzi atachangia kiasi na mkulima naye atakatwa baada ya kuuza korosho zake. Hii itawasaidia sana kwa sababu tutajiondoa kwenye ile mikopo mikubwa iliyoko kwenye mabenki ambayo ilikuwa na tozo kwa riba kubwa kiasi kwamba wakulima walikuwa hawanufaiki na hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba pia Wizara ya Kilimo waboreshe na mifumo ya ununuzi wa Korosho, wasimamie vizuri sana masuala ya ushirika kwa sababu ndiyo yanayoumiza wakulima kila mara. Pia tuboreshe na ule mnyororo mzima wa zao la Korosho, tusiishie tu kununua Korosho; na kila mara nimekuwa nalisema hili jambo ndani ya Bunge hapa, japokuwa wengine hawataki kulielewa sana, kwamba unapovuna Korosho magunia 100 unapata pia na Kochoko au mabaki ya korosho, yale mabibo; na yenyewe unaweza kupata takribani gunia 75 mpaka gunia 100, zinakaribiana. Hizi kule kwetu kila mara nimesema, tunazitumia kupika gongo. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie Waheshimiwa Wabunge, ninachokiomba sasa, Serikali warasimishe na kurekebisha haya mambo, kwa sababu hatuwezi kuyakwepa. Tumeishi namna hiyo, sasa isiwe tena tunasema ni pombe haramu kabla hatujawaeleza ili iweze kuwa halali, nini kifanyike? Nia nzuri ya Wizara iwe ni kuona wakulima wananufaika na mazao yao ya shambani kama wanavyonufaika wakulima wa mazao mengine kwenye maeneo mengine; wakulima wa Kahawa, wakulima wa Miwa na wenyewe wote wananufaika na wanapata mazao makubwa na faida kubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni suala la umeme. Nimemsikia hapa Mheshimiwa Waziri Mkuu anasema, mpaka sasa kuna vijiji takribani 1974 na ninamwomba sana Mheshimiwa Waziri naye tulikuwa tukiongea mara nyingi kwamba kwenye Jimbo Ndanda mpaka sasa kuna vijiji 29 ambavyo havina umeme kabisa na hasa zaidi kuna Kata mbili ambazo na zenyewe hazina umeme kabisa; Kata ya Msikisi pamoja na Kata ya Mpanyani. Naomba mfanye kwa haraka sana kuhakikisha vijiji hivi vinapata umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri; na haya mambo yapo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Kama ambavyo kila mara nimesema, nimefurahi sasa kusimama hapa nikiitetea Ilani ya Chama cha Mapinduzi, achilia mbali sera zetu na mambo mengine, lakini nataka nione ilani hii inatekelezwa na sisi tusimame kwa kifua mbele kwamba ilani yetu imetekelezwa katika eneo letu na watu wa Ndanda nao wajivunie kwamba wamepata sasa msimamizi kwa ilani inayotekelezwa na Serikali hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye masuala ya afya, nawaomba sana Waziri wa afya na Mheshimiwa Waziri Mkuu kwamba tuhakikishe sasa Hospitali ile ya Kanda ya Mtwara inamaliziwa ili wananchi wale waweze kupata huduma. Sasa hivi tunatumia Hospitali ya Ndanda ambayo watu wengi wanailalamikia kwamba ina gharama kubwa sana kwenye kutoa huduma. Nami nataka niwaambie, ukubwa wa gharama huu ni kwa sababu ya uhaba wa Vituo vya Afya vilivyopo kwenye maeneo haya. Kwa mfano, wakazi wa Ndanda walijitahidi sana kujenga boma lao kwa ajili ya Kituo cha Afya, limekamilika mpaka kufika level ya lenta katika Kata ya Mpanyani, Kata ya Mihima na Kata ya Namajani na kwenye maeneo mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba badala ya kuwafanya watu wa Ndanda wakatibiwe kwa gharama kubwa kwenye Hospitali ya Mtakatifu Benedict ya pale Ndanda Mission, basi sasa tukamilishe kujenga kile Kituo cha Afya kilichopo pale ili gharama ziweze kupungua na pia tuwapunguzie adha ya kusafiri safari ndefu ya kwenda Jimbo la Ruangwa huko kwenye Kijiji cha Nandanga kwenda kupata matibabu jambo ambalo siyo zuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine nisisitize pamoja na lile suala la korosho ni suala la barabara. Kwa kipindi kirefu sana tumekuwa na tatizo kubwa sana la barabara. Kuna hii barabara ambayo sijasikia kila mara inatajwa, lakini ni introduction ya barabara inaitwa Cashewnut Ring Road. Barabara hii inaanzia Nangurukuru – Liwale – Ruagwa – Nachingwea – Masasi – Newala – Nanyamba - Mtwara yenye wastani wa kilometa kama 400. Naomba sana, ili bandari yetu iweze kutumika vizuri, basi tuhakikishe hii barabara tunaikamilisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa nafasi uliyonipatia na ninawashukuru sana vijana wa Bunge wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kuchangia kwa maandishi ili kuweza kufafanua baadhi ya mambo kwenye mchango wangu kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la ETS; kazi yake kubwa ni kuhesabu, viwanda vilifunga mashine hizi kwa maelekezo ya Serikali, lakini tija yake haifanani na gharama halisi pamoja na mengine mengi, lakini mkataba wa Kampuni ya SIPA haukuwa wazi sana hasa kwenye suala la bei ya uchapishaji wa stamp hizo. Mkataba huu ulikuwa wa miaka mitano, muda umekwisha, kuna haja sasa ya Serikali kupitia upya mkataba huo ili kuweza kuangalia upya gharama zake.

Hivi sasa kwa mfano gharama ya kuhesabu chupa moja ya juice ya mls 200 ni shilingi 23, wakati Serikali kodi yake ni shilingi 1.8 tu hivyo utaona mwenye kuhesabu anapata pesa nyingi zaidi kuliko Serikali, na hii ni kuongeza tu gharama kwa wazalishaji na hatimaye bei kwa walaji, sawa na vinjwaji baridi na vingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu VAT Refund; kwa nini Serkali hairudishi kwa wawekezaji na wafanyabiashara VAT hasa kwenye viwanda vikubwa, hii pia inachangia sana kukwamisha mitaji na kudorora kwa uzalishaji kwenye viwanda. Serikali inadaiwa sasa walau kiasi cha shilingi bilioni 10 katika VAT, pia kuna suala la industrial sugar, karibu miaka mitano sasa pesa hiyo haijarudi na kusababisha viwanda vingi kuendelea kukosa operating capital, kwa mfano viwanda vya vinywaji baridi, CocaCola na Pepsi, Serikali ibadilishe utaratibu wa kushikilia pesa hi kwa sababu imekuwa mziogo mkubwa sana kwa wenye viwanda.

Kuhusu suala la unyaufu; Serikali kupitia Wizara itoe msimamo ili kuondoa athari zinazoweza kujitokeza wakati wa msimu wa ununuzi wa korosho. Unyaufu umekuwa ni tatizo kubwa na bado mpaka sasa Serikali haijawa na msimamo wa pamoja kuhusu suala hili, mwaka jana wafanyabiashara wa maghala wamepata hasara kwenye uendeshaji wa maghala kwa sababu Serikali imechukua pesa toka kwa wafanyabiashara hao na kuwa hasara kwao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Liganga na Mchuchuma inafaa kuwekewa nguvu zaidi ili kuweza kuendeleza migodi hiyo, pia lazima kuwa na mfumo ulio wazi kwenye jambo hili, lazima sasa Liganga na Mchuchuma zianze uzalishaji ili kuchangamsha uchumi wa Ukanda wa Kusini Bandari ya Mtwara na reli ya Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu biashara ya korosho; katika Ilani ya CCM 2020 - 2025 kuhusu eneo la viawanda vya korosho, ibara ya 34 sehemu ya (c) iliahidi kuanzisha Cooperative Seed Fund, huu ni mfano wa REA, Mfuko wa Maji na Road Fund, kwenye mpango huu CCM ilidhamiria pamoja na mambo mengine kuanzisha viwanda 33 vya kubangua korosho, pamoja na kufufua viwanda vingine vilivyokufa na kufanya ubanguaji kufikia asilimia 50, tani 550,000 kufikia mwaka 2025, vipi bajeti ya Wizara hii imeweza kujibu hii ilani na mkakati uliopo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri sasa jambo hili liwe katika utekelezaji, kuna hasara kubwa sana inapatikana kwenye korosho, hadi sasa korosho ghafi na mazao yake yanauzwa ni pamoja na ajira, nchi inapata hasara kubwa sana, maganda ya korosho ni uchumi, sawa na mabibo, kochoko ndiko ambako wine na mvinyo zinakotokea, kwa mfano Scotland ambako ndiko unakotengenezwa mvinyo wa Scotish Whiscky, wanaliingizia Taifa lao Euro bilioni 4.5 kwa mwaka jana peke yake. Wizara ione namna ya kushirikiana na Wizara ya Katiba na kuamua kubadilisha Sheria ya Vileo (Liquer and Intoxication Act ya 1978) ili wananchi sasa waweze kuzalisha gongo kitaalamu na kuweza kujipatia pesa za kigeni lakini pia ni sehemu ya uchumi kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.
Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara la Afrika
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia. Kama ambavyo mtangulizi wangu amesema Mheshimiwa Eng. Ezra, nami pia ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara. Tumetumia muda hasa kupitia huu Mkataba na mapendekezo yaliyoletwa mbele yetu na Serikali na pia tulipata nafasi ya kuwaona wadau mbalimbali wakiwemo TCCIA na CTI tumesikia pia maoni yao na baadaye tulikutana na maoni ya mwavuli wa watu fulani walioungana, inaitwa Trade Investment Coalition (TIC) juu ya Azimio la Bunge la kuridhia Mkataba na Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Afrika ndiyo ambao tunajadili hapa sasa hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba mchango wao waliouleta kwenye Kamati ungeingia kwenye Hansard kama pia sehemu ya mchango wangu ili kuweza kuboresha zaidi na watu waweze kujifunza baadaye.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawaomba Waheshimiwa Wabunge waridhie huu mkataba lakini lazima tuuridhie kwa tahadhari. Kwa sababu Tanzania tumekuwa na tendency kidogo wakati fulani ya kujilizaliza au kulalamika kwenye mambo ambayo sisi wenyewe labda hatuna nia nzuri ya kuyafanyia utafiti ili tuweze kuona tunakwenda wapi? Naomba radhi sana Waheshimiwa Wabunge waliochangia hapa kwenye hili swali linalohusiana na suala la mahindi na ndugu yangu pale ametumia mfano huo huo, na mimi naomba nitumie mfano huu ili kuweza kujenga hoja yangu vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunasema NFRA wanatakiwa wakanunue mahindi, halafu wayahifadhi na yaende kutumika labda wakati wa majanga. Pia tunatamani wafanyabiashara wa nje nao waje wanunue mahindi yetu Tanzania. Sasa swali ambalo sisi kama Watanzania tuna haja ya kujiuliza, mahindi yetu yana ubora sawa na mahindi yanayolimwa Kenya? Kwa nini Wakenya wasi-saturate kwanza market yao halafu wakaja kuchukua kwetu kiasi kidogo kwenda kujazilizia kwa sababu ya tofauti ya ubora?

Mheshimiwa Naibu Spika, hili liko wazi, tulifanya semina na ndugu yangu Mheshimiwa Engineer Ezra hapa alisema kidogo suala la GMOs; mpaka sasa watu wanaotumia kilimo cha kisasa au kutumia GMO ili kuweza kupata mazao bora, ni wachache sana Tanzania, kitu ambacho kinatusababisha tushindwe kuingia vizuri kwenye soko bora kwa sababu ya ubora wa mbegu hata tunazozalisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, siku moja jaribu kufanya utafiti, chukua mahindi ya Tanzania halafu chukua mahindi ya Zambia, yaweke yote Mezani. Kuna kipimo wanachotumia, ni kama kanyundo fulani kadogo ili kuweza kuangalia ubora wa ile grain. Hindi la Tanzania ukiligonga linatawanyika, lakini ukichukua hindi la Zambia ukiligonga, litakatika vipande vine, vitano au sita. Ndiyo kipimo wanachokitumia, kwa hiyo, mwisho wa siku wanasema mahindi yetu hayana ubora kwa sababu watapata takataka nyingi zaidi kuliko ambavyo unaweza ukapata unga ulio bora.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ninachotaka kusema ni kwamba tunaingia kwenye ushindani wa soko; na katika ushindani huu, pale ndani kuna sheria nyingi. Kwa mfano, Kifungu Na. 39 kinasema kinataka kulinda viwanda vidogo vidogo vya ndani. Sasa unavilinda viwanda vya ndani ambavyo vinatumia malighafi ambazo siyo bora sana ukilinganisha na nje ambako tunategemea ndiyo sehemu utakakokwenda kuuza kama wao wanavyokuja kuuza kwetu, kama ambavyo sasa hivi tumekuwa tukilalamika labda tumevamiwa na soko la China au tunavamiwa labda na soko la jirani hapo Kenya. Kwa hiyo, lazima tuangalie.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa namwomba sana Mheshimiwa Waziri kwamba pamoja na kutaka kuridhia Mkataba huu, lakini lazima tukatoe elimu ya kutosha kwa Watanzania kwamba sasa hivi tunakwenda kwenye mashindano ya kibiashara na tunaongezewa mkataba mwingine mpya. Kwa hiyo, kama hatujaweza kwenda vizuri, kwa mfano, kwenye Mkataba wa Afrika Mashariki, tumekuwa hapa kila mara tunasema tunaona labor mobility, tunaona na masuala ya movement of labor; Wakenya wanapokuja Tanzania kwenye hospitality businesses unafurahia zaidi huduma kuliko ambavyo sisi tunaokwenda kutoa kule kwao.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pamoja na maboresho yote, nakushukuru kwa kunipa nafasi, lakini tuwatake Watanzania tuendelee kujifunza ili tuweze kutoa kilicho bora. Ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia wakati huu wa Mpango. Nimesoma taarifa ya Mheshimiwa Waziri, pia nimesoma na taarifa ya Kamati ya Bajeti, nami niungane nao na niunge mkono taarifa hii iliyopo mbele yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, naomba kukazia baadhi ya maeneo ambayo nilitamani sana Mheshimiwa Waziri atakapokuja ku-wind-up atueleze wanafikiria kufanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma taarifa ya Kamati ya Bajeti, wamesema wazi kwamba pesa ya Mfuko wa Jimbo kwa zaidi ya miaka sita, saba sasa hivi haijaongezwa. Kwa hiyo, fedha tuliyokuwa tunaipata mwaka 2015/2016 ndiyo hiyo hiyo inayopatikana sasa hivi wakati inflation imekuwa inaongezeka kila mwaka. Kwa hiyo, tunaomba ifanyiwe adjustment ili fedha hii iweze kuwa na manufaa yaliyokusudiwa pale mwanzoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningetolea tu mfano wa Jimbo la Ndanda, tunapokea shilingi milioni 42, ambayo ni wastani wa shilingi milioni 2.6 kwa kila Kijiji. Sasa katika vijiji 77 unataka upeleke shilingi milioni 42 ili wale watu uweze kuwagusa wote kwa ajili ya miradi, unaweza ukachagua miradi michache, lakini wengine wanaweza wasielewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine tumeona, na ninaishukuru sana Serikali, imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kwenda kujenga madarasa. Naishauri tena Serikali kwamba madarasa haya yanayokwenda kujengwa takribani 15,000 yaende sambamba na ajira zitakazotolewa. Kwa sababu kama unajenga madarasa 15,000, tafsiri yake unakwenda kuongeza wanafunzi kwenye shule zetu, unakwenda kuongeza na madarasa, lakini kama idadi ya walimu na watumishi itabaki pale pale, basi itakuwa ni tatizo. Hilo ni sawa sawa na jambo ambalo lipo kwenye vituo vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ningependa kuishauri pia Serikali ni kuhusiana na mitambo pamoja na magari yaliyozagaa nchi nzima, kwenye Halmashauri zetu, kwenye hospitali zetu pamoja na kwenye Serikali Kuu. Magari haya yanazidi kuoza na mitambo hii inazidi kuoza. Kama Serikali wana nia njema, ni bora wakauza mapema kwa sababu tayari walishafanya tathmini ya vitu hivi, kwa hiyo, TR atoe kibali mapema yauzwe japo ipatikane fedha kidogo, lakini pia itapunguza kwenye asset badala ya kuonesha Serikali ina magari mengi, ina mitambo mingi ambayo ipo kwenye vitabu vyake, haitumiki, yanabaki kama makuukuu na mengine yanakuwa sasa kama vijumba vya majambazi huko kwenye maeneo yetu. Kwa hiyo, niwaombe sana waiangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, mimi naomba, nawe ni Mwenyekiti wetu, niliona siku moja picha yako umeanza kilimo cha korosho. Sasa utusaidie sana wakulima wa korosho tumekuwa kwenye adha kwa muda mrefu sana kwenye suala la Export Levy. Imefikia mwaka huu hapa ninapoongea nawe mkulima anakatwa takribani shilingi 979/=? Katika hii shilingi 979/= mgawanyo wake uko hivi: Export Levy peke yake inakatwa shilingi 499/=.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sasa sheria hii iletwe ndani ya Bunge na Mheshimiwa Waziri wa Fedha akae na Wizari ya Kilimo wajaribu kuipitia hii sheria na walete mapendekezo ili sheria hii ibadilishwe, kwa sababu imekuwa inakandamiza sana wakulima. Kwa mfano, hiyo Export Levy ni shilingi 499 kwa bei ya mnada huu uliopita. Kwa hiyo, mkulima jumla anakatwa almost shilingi 979. Kati ya hizi, direct deduction ni shilingi 260 au shilingi 270; na kiasi chote kinachobaki huwa kinakatwa indirect kwa kupitia hivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia Sheria hii ya SDF ambayo ilitungwa hapo nyuma kwa ajili ya kutaka kusaidia wakulima, imekuwa kama ni marudio kwa sababu ukiangalia kuna direct deduction ambayo ni pesa ya ushirika shilingi 100, pesa ya CBT shilingi 25, pesa ya TARI shilingi 25, pesa ya Halmashauri shilingi 56, lakini pia kuna pesa ya mchango wa elimu shilingi 30, pesa ya Halmashauri ndiyo sawa na mchango wa elimu, almost, lakini pia ukilinganisha na usafirishaji ni shilingi 50. So in total, unapata karibia shilingi 979.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana tuwashauri hawa ndugu zetu, Wizara ya Kilimo pamoja na Wizara ya Fedha wajaribu kuipitia hii sheria na wailete hapa ndani Bungeni tuibadilishe. Korosho siyo zao la mkoa mmoja au mikoa miwili, mitatu; korosho limekuwa zao la Kitaifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la madeni. Kuna madeni mengi sana ya ndani, mengine yanayotokana na mazao ya kilimo, lakini mengine yametokana na maamuzi ya Serikali. Kwa mfano, ukienda kwenye korosho, madeni ya Bodi pamoja na Vyama vya Ushirika ni takribani shilingi bilioni 40. Tunaomba sana madeni haya yahamishiwe Hazina kwa sababu Bodi haiwezi kuyalipa na vyama vile vya msingi kule kwetu hawawezi kuyalipa, yamekuwa mzigo kwao, yanachafua vitabu vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye Bodi ya Pamba, wanadaiwa zaidi ya shilingi bilioni 60. Pia ni sawa sawa ukienda kwenye tumbaku. Kwa hiyo, tunaomba sasa Mheshimiwa Waziri aridhie madeni haya yachukuliwe na Hazina yaweze kulipwa kwa sababu ni mitaji ya watu waliokuwa wanafanya biashara na Serikali na maeneo mengine kutokana na maelekezo ya Serikali. Kwa hiyo, Wakandarasi wa ndani wanao-supply vitu mbalimbali kwenye huduma za kilimo, kwenye huduma za mashule kwa mfano, Shule ya Sekondari Ndanda, Shule ya Sekondari Chidya watu walipeleka pale chakula, sukari, unga kwa ajili ya wale Watoto na Halmashauri zetu zinaelemewa, hawawezi kulipa tena. Tunaomba Hazina wachukue haya madeni na wayafanyie kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimesema hapo mwanzoni, kuna miradi mikubwa sana ya kimkakati iliyoelekezwa kwa upande wa kusini. Kwa mfano reli ya Kusini hatujui mpaka sasa wamefikia hatua gani na nini kinakwenda kufanyika? Tuna barabara zetu za kiuchumi ambayo ni barabara inayoanzia Mtwara kufika Newala - Masasi - Nachingwea kwenda Liwale kuja kutokea Lupilo kuja kutokea mpaka Morogoro kwa maana ya kutaka kufungua ukanda huu wa kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutamshukuru sana Mheshimiwa Rais, endapo wazi kabisa ataamua sasa kufanya kazi na hii barabara, kwa sababu pia ndiyo barabara inayotokea Songea kupitia Namtumbo kwa sababu tunatamani sisi wakati fulani siyo lazima tufike Dar es Salaam tunapoamua kuja huku, lakini pia ni sehemu ya kufungua ukanda huu wa kusini, tusiwe na barabara moja tu ya kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia utakumbuka kulikuwa na suala hapa la Mtwara Corridor ambayo ilikuwa ni makusudi mazima ya kwenda kuboresha Bandari ya Mtwara. Katika mikakati ya sasa inayotajwa, naona kama habari za Mtwara Corridor zimesahaulika kabisa. Sijasikia ikiwa inatajwa karibuni ndani ya Bunge kwa sababu sisi Wabunge tunaongea kidogo, lakini hata Wizara nayo haijawahi kutuambia habari hii na sijaiona huko.

Kwa hiyo niwaombe sana, kama inawezekana turudishe tena huu utaratibu wa Mtwara Corridor ili kuweza kusaidia Mikoa ya Kusini kwa maana ya Mtwara, Lindi pamoja na Ruvuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la mwisho kabisa niliseme na kwa kusisitiza, tuendelee kuangalia sasa, tumeona hapa Mheshimiwa Rais wameridhia sasa na wameondoa ile withholding tax kwenye mazao mbalimbali. niipongeze sana Serikali kwa hatua hii. Pia tunaomba, sisi hasa tunaotoka kwenye maeneo yanayolima korosho waangalie na uwezekano wa kuja kufanyia maboresho kwenye Sheria ya Export Levy kwa sababu imekuwa yenye maumivu makubwa kwa wakulima na haina tija tena kama ambavyo ilikusudiwa mwanzoni, kwa hiyo sasa hivi ije ikiwa na utaratibu mpya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana na naomba Serikali wazingatie hayo machache kama sehemu ya mchango wangu. (Makofi)
Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi nikupongeze kama mchangiaji aliyepita, na nimekuwa mtu wa pili kupata nafasi ya kuchangia toka uwe Naibu Spika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mambo ambayo ninataka nikukumbushe wewe mwenyewe kwa sababu tulikuwa kwenye Kamati moja na ulihudhuria kikao. Kumetokea malalamiko mengi sana kwenye suala la inflation. Nitatoa mfano mfupi nasi kwenye Kamati tulijadili, kwa mfano sasa hivi tumekuwa tukiongea kuhusu inflation kwenye nondo, kwenye sementi na vifaa vingine vya ujenzi. Examination gloves zimepanda kutoka shilingi 5,000 mpaka shilingi 18,000; paracetamol tablets kichupa chenye kukaa dawa 1,000 kimepanda kutoka shilingi 7,000 mpaka shilingi 22,000; Vitamin B Complex imepanda kutoka shilingi 5,000 mpaka shilingi 32,000. Naomba karatasi hizi nimpatie Mheshimiwa Naibu Waziri kwa sababu yupo hapa meza yako impatie ili waweze kufanyia kazi waone namna ya kuwasaidia wananchi hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo ninataka niliseme hapa leo ni suala kubwa sana ambalo Kamati ya Viwanda na Biashara pia kwa kushirikiana na Kamati ya Bajeti tulileta pamoja mbele ya Mheshimiwa Spika aliyepita ilikuwa ni suala la ETS. Kwa masikitiko makubwa sana na kwa kutaka kuwasaidia Watanzania na sisi wenyewe kama Bunge, Bunge lako limedharauliwa nasi kama Wajumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara hatujaridhika, Serikali iliendelea mbele, wameingia mkataba na Kampuni ya SICPA tofauti na ushauri uliotolewa kwenye Kamati zile na hivi sasa wananchi wamekuwa kwenye sintofahamu kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za uendeshaji wa kampuni hii unazifahamu, katika akili ya kawaida kabisa kwa mfano, wakati huo walikuwa wanatoza mvinyo dola 20, sawa na shilingi 47,700 hata hivyo wanasema wamepunguza kutoka hiyo na sasa hivi wanatoza shilingi 42,000 wao ndiyo wanaliita punguzo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna kampuni ambazo zinaweza zikatoa huduma hiyo hiyo kwa shilingi mbili kwa maana ya dola sawa na shilingi 4,600 ndiyo maana ninakiomba Kiti chako kitoe maelekezo mahsusi kabisa ili tuweze kukaa sisi kama Wabunge tujadili jambo hili katika hatua ya dharura, tuweze kuwasaidia wananchi. Haiwezekani mtu mwenye akili ya kawaida aache kupata huduma kwa shilingi 4,600 ang’ang’anie kwenda kupata huduma ya shilingi 42,000; nini tunaficha nyuma ya mkataba wa SICPA na TRA na Serikali.(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, karatasi ninazo hapa naomba na wewe uzipitie uone kama ninachokisema ni halali na kama hiki ninachokisema ninasingizia nitaomba Bunge lako liniwajibishe kwa sababu tunataka kuwasaidia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, malengo ya kuwa na kampuni hii ilikuwa ni kutaka kuisaidia Serikali kufanya mahesabu ili TRA waweze kutoza kodi stahiki, lakini matokeo yake mzigo huu wote unahamishiwa kwa wanunuzi. Hakuna kitu chochote kinachopatikana kwa Serikali. Nilitoa mfano hapa Bungeni nikasema katika shilingi kumi ambayo inatozwa na mkandarasi anayefanya kazi ya kuhesabu, lakini mkandarasi huyu anailipa Serikali shilingi moja na senti nane kiasi kingine chote cha pesa kinachobakia kinakwenda kwake mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninakuomba uelekeze, Bunge hili linadharauliwa sasa hivi, Kamati yetu ya Viwanda na Biashara imedhauriwa kwa sababu tulitoa ushauri mzuri kwa Serikali hata hivyo TRA wameendelea kuingia mkataba huu, tunataka tufahamu kama Kamati ni nani yupo nyuma ya mkataba SICPA na TRA. Kwa nini tuwapelekee wananchi mzigo mkubwa badala ya kuacha hili jambo likafanyika kama ambavyo Bunge tulishauri. Akili ya kawaida kabisa haiwezi kukubali; unakataa shilingi 4,600 unakimbilia shilingi 42,000 kwa manufaa ya nani? Nchi hii haipati shilingi moja kwa mkataba huu zaidi ya kodi inayotozwa pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, walichokifanya sasa hivi wametumia ujanja karatasi zipo hapa za TRA, wameacha kutoza kwa dola wame-convert zile pesa kwa shilingi halafu zinakwenda bado kutozwa na gharama hizi wale waendeshaji wanazileta tena kwa mlaji ambaye ni mwananchi wa kawaida na ndiyo sababu sasa bidhaa nyingi zinaweza kupata bei kwa sababu mwisho wa siku tozo hizi zinarudi kule. Sukari imepanda bei, chai kwa maana ya juice imepanda bei, soda zimepanda bei huko mtaani kwa sababu kubwa hizi na wenyewe walikuwa wakizileta kila mara.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeanza kuongea hili jambo kwa muda mrefu sana nataka sasa nitoe na mimi unisaidie kabisa, kuona kwa nini Serikali inataka kutuficha, nani yupo nyuma ya mkataba wa SICPA na TRA, kwa nini gharama hizi kubwa tunakwenda kuwahamishia wananchi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba karatasi hizi zikufikie hapo, busara ikuongoze, uende kutusaidia na tunakuomba uje kwenye Kamati yetu ikikupendeza tutakueleza mengi zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hiyo. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nikushukuru pia kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia kwenye Mapendekezo ya Mpango, 2024/2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejipa nafasi ya kusoma hotuba zote mbili za Waheshimiwa Mawaziri ambazo wamewasilisha hapa leo na mimi nikasema basi nijipe nafasi niweze kuchangia kwa maana ya kulishauri Taifa letu. Nilipata nafasi ya kuchangia mwaka 2016 na wakati nachangia nilionesha umuhimu wa chuma kilichopo Mchuchuma ikiunganishwa na bandari yetu ya Mtwara, nashukuru Serikali imefanya maendeleo na sasa hivi tunaambiwa kwamba kule Mchuchuma pamoja na Liganga wameanza kulipa fidia ili wale wananchi waweze kuondoka eneo lile kwa ajili ya kuendeleza huu mradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nishauri kwenye jambo hili kwamba mpango wa sasa wa Serikali ni kuona kwanza tunachimba makaa kadri ya taarifa ambayo iko mbele yetu, wakati ule nachangia mwaka 2016 nakumbuka, nilisema nchi yetu imekuwa inapoteza pesa nyingi sana za kigeni kwa ajili ya ku-export chuma ili kije kuweza kujenga na kufanya matumizi mbalimbali kwa sababu nchi yetu inakuwa kwa kasi, kwa hiyo shughuli nyingi za ujenzi zinafanyika. Kwa hiyo, tuna import nondo nyingi sana lakini pia karibia asilimia 90 au 85 ya chuma chote ambacho kimetumika kwenye ujenzi wa SGR kimekuwa imported.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hii tafsiri yake tumeiondoa forex nyingi sana kupeleka nje. Wakati kimsingi nchi ambazo zinaendelea au zilizoendelea, kabla ya kutekeleza miradi mikubwa ambayo kwa vyovyote vile itapoteza pesa nyingi sana za kigeni wanaanza kuangalia kwanza resources walizonazo wao ndani. Kwa hiyo, kwa ushauri wangu kama nchi tungeanza kwanza ku-extract Chuma cha Liganga ili kiweze kutusaidia kwenye kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo reli hii ya SGR ambayo tunaisema sasa hivi lakini pamoja na ujenzi katika maeneo mbalimbali yanayoendelea ikiwa ni pamoja na majengo ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo bado nasisitiza kwamba tunayo makaa ya mawe maeneo ya Ngapa kule Mbinga na maeneo mengine ambayo kwa sasa hivi yanachimbwa na hatujaweza kufikia hata asilimia kubwa kama ambavyo yanahitakija. Nashangaa kuona sasa Serikali inataka tena kuchimba makaa ya mawe Liganga badala ya kutafuta kwanza mwekezaji wa chuma ambae hatuna kabisa huo mradi hapa Tanzania ili mwisho wa siku chuma hiki ki-support pamoja na kupunguza export ya kwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine sijaona msisitizo mkubwa sana kwenye suala la LNG. Natambua kwamba Lindi tuna mradi ambao unakwenda kutekelezwa karibuni lakini ili kutekeleza huu Mradi wa LNG ambao na wenyewe utakwenda kutusaidia kupunguza matumizi makubwa ya forex kwa ajili ya kuagiza mafuta kutoka nje lakini pia sasa hivi gesi kubwa tunayotumia Tanzania tunaagiza nayo kutoka nje, wakati kimsingi bomba letu la gesi linalotokea Lindi kwa maana ya Mkoa wa Mtwara na Lindi linatumika siyo zaidi ya asilimia 10, tena kwa kuzalisha tu umeme kwenye eneo la Kinyerezi I na II pamoja na kwamba hata sisi Watu wa Mtwara tunashida kubwa sana ya umeme, kwa hiyo tunategemea tuone Serikali inaacha kuagiza sasa gesi pamoja na mafuta kutoka nje na kuweka nguvu kubwa kwenye kuimarisha huu Mradi wa LNG Lindi kupitia Wizara ya Nishati. Kazi ambayo inaendelea sasa hivi lakini utekelezaji wake basi uharakishwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kuhusu suala la Liganga na Mchuchuma linakwenda sambamba na kuikumbusha Serikali, kwamba Serikali hii iko kwenye movement, iko kwenye mwendelezo unaoendelea, sasa hivi tuko kwenye Awamu ya Sita ambayo tuko nayo sasa hivi, lakini mtakumbuka mradi mkubwa wa Mtwara Corridor ulipigiwa sana chepua na Mheshimiwa Hayati Mkapa wakati huo kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu nakumbuka lakini ukija kuangalia yanayotokea sasa hivi kama Mtwara Corridor imekuwa abandoned, yaani utekelezaji wa miradi ile ambayo ilikuwa inakwneda sambamba na maboresho ya Bandari ya Mtwara, maboresho ya Uwanja wa Ndege Mtwara hayawi serious namna hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naishauri Serikali na siku moja hapa Mheshimiwa Bishop Gwajima alishauri kwamba tunapokuwa na nchi kama nchi yetu Tanzania, nchi inayokua lazima tuhakikishe tunapoleta hii mipango inakuwa ni ya muda mrefu, tuseme tunajadili mipango ya miaka 50, kwa hiyo, kila Rais atakayeingia kwenye uongozi wake ahakikishe kwanza anatekeleza yale tuliyokubaliana katika Mpango wa Maendeleo wa Taifa, badala ya kuwa na mpango wa miaka mitano mitano ama mpango wa miaka sita sita kiasi kwamba kila Rais anapokuja basi anakuwa na vipaumbele vya kwake anavyofikiri kwamba ndiyo mambo ya msingi ya kuyafanya.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hali ya kawaida, Bandari ya Mtwara kwa mfano sasa hivi, Serikali imewekeza pale pesa nyingi sana kwa ajili ya kuona ile bandari inakua lakini matumizi makubwa ni kusafirisha makaa ya mawe kwa kiasi kidogo, makaa ya mawe haya yanaletwa na malori yanaleta athari za kuharibu barabara zetu ambapo Serikali hivi karibuni itaingia gharama kubwa ya kufanya marekebisho ya barabara kutoka Songea mpaka Mtwara pia kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tukumbuke kwenye huu Mpango wa Mtwara Corridor kulikuwa kunatajwa habari ya reli ya kusini. Sasa Mheshimiwa wakati unakuja kuhitimisha kwenye jambo hili utueleze, mkakati wa kuwa na reli ya kusini bado upo ama Serikali wameamua kuuacha na unafanya mikakati mingine. Kwa sababu kuna watu wengi ambao ukitokea ukanda wa Mtwara mpaka kufika Songea eneo lile ambako inasemwa reli ya kusini itapita watu waliwekewa “X” mpaka Peramiho nakumbushwa hapa na Mheshimiwa Jenista. Watu waliwekewa “X” kwenye majumba yao, kwa maana ya kwamba nyumba hizi zitavunjwa kwa ajili ya kupitisha reli, ni zaidi ya miaka kumi, zaidi ya miaka 20 sasa hivi mradi huu hautekelezwi tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunataka tuone Serikali itueleze kwamba mkakati ule wa kuwa na reli ya kusini inayoanzia Mchuchuma na Liganga mpaka Bandari ya Mtwara bado upo au Serikali imeuacha? Kama bado upo basi tuuone kwenye vitabu kwa sababu kimsingi tunataka tuone watu wetu ili waweze kuendeleza maeneo yao.

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia tupate matumizi makubwa ya Bandari yetu ya Mtwara kwa sababu sasa hivi…

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwambe kuna taarifa.



TAARIFA

MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka tu nimpige taarifa rafiki yangu na Mbunge makini, katika suala la kuleta mapinduzi huko kusini na kwa Taifa, ujenzi wa barabara ya kiwango cha zege inayotoka Lusitu Kwenda Mawengi ambayo ilikuwa inalenga kwenda Nkomang’ombe kuliko na madini ya makaa ya mawe inaendelea kuhitaji kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo imepangiwa bajeti ya Itoni kuja Lusitu lakini kutoka Nkomang’ombe kuja Liganga kwenda Madaba kwenda Songea ambayo ingetakiwa ijengwe kwa kiwango cha zege kama ilivyoaanza kile kipande cha kwanza, kilometa zilizojengwa ni 50 tu, hatuwezi kwenda kwa kutarajia kufanya mapinduzi kwa kutumia Chuma cha Liganga kwa kwenda kwa kasi ndogo kiasi hicho, vinginevyo mradi huu utaendelea kubaki miaka mingine 20 hadi 30 ijayo.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mwambe taarifa unaipokea?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Senior hapa Mzee wangu kwa taarifa hii nzuri, nami niungane na wewe kwamba hicho unachokisema pia kiwe kama sehemu ya mchango wangu kwa maana ya kutaka kuboresha mchango wangu, taarifa yako nimeipokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, bado nizidi kusisitiza, kwa mfano sasa hivi sisi Wabunge wa Mtwara tunakuwa tunabishana kila mara, kuhusu matumizi sahihi ya Bandari ya Mtwara, badala ya kufikiri kuhusiana na huu mradi wa Mtwara Corridor ambalo ni jambo ambalo lingeweza kuongezea mapato nchi yetu, sisi tumeng’ng’ana na kufikiri kwamba kusafirisha korosho, korosho inayotoka huko Tandahimba, Masasi na maeneo mengine ili kuweza kuboresha bandari yetu kitu ambacho kinafanyika katika msimu wa miezi mitatu mpaka minne tu ambayo haiwezi kusaidia na uwekezaji mkubwa uliofanyika pale na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona hapa katika mpango wanasema wanataka sasa kuweka taa kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara, niendelee kumsisitiza Mheshimiwa Waziri hapa kwamba umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara utaonekana wakati wa utekelezaji wa Mradi wa LNG. Pia, tuangalie na umuhimu wa Bandari ya Mtwara kwa sababu kimsingi barabara ya kutoka Dar es Salaam, Lindi mpaka Mtwara literally imekufa, inahitaji matengenezo makubwa sana. Kwa hiyo, wawekezaji wengi kwa vyovyote watatumia uwanja wa ndege lakini pia watatumia Bandari ya Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hizi zinakufa kwa sababu ya matumizi makubwa ya barabara kwa sababu tunakosa njia nyingine za usafarishaji. Kwa hiyo, tulikuwa tunatumia barabara muda wote kiasi kwamba barabara zetu sasa zimekufa, zinahitaji matengenezo makubwa kwa sababu ya kupitisha malori makubwa ya sementi yaliyokuwa yanatoka Kiwanda cha Dangote na sasa hivi tunashuhudia barabara ya kutoka Songea kupitia Madaba – Tunduru – Masasi - Ndada kuelekea Mtwara na yenyewe imekufa almost, kwa sababu ya kupitisha magari makubwa yanayobeba mkaa kutokea Ngapa, Peramiho na maeneo mengine ambako wanachimba madini haya ya makaa ya mawe. Hii ni pamoja na uchafuzi wa mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kwa vyovyote kama tutakuwa tume-concentrate kwenye ujenzi wa reli ya kusini inayoanzia hayo maeneo niliyoyataja kufika Mtwara bandarani, kwanza tutajitahidi kulinda mazingira yetu kwa sababu reli itakuja moja kwa moja mpaka bandari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mchango wangu nitaleta mchango mwingine wa maandishi ambao uko more detailed lakini ninaomba haya ya sasa myachukue na kuona namna ya kuboresha kwenye taarifa yako. Ahsante sana.
Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi kuweza kuchangia kwenye mjadala uliopo mbele yetu. Nataka nianze na mambo machache, wakati najenga hoja yangu ili kuweza kuonyesha namna gani sisi kama Bunge tumekuwa tukitoka nje ya utaratibu ambao ndio hasa majukumu yetu sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia hata mchangiaji aliyetoka sasa hivi sidhani kati ya mambo makubwa matatu ambayo ni kazi yetu sisi ya kibunge alikuwa analifanya lipi kwa maana ya kuisaidia Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbele yako kuna huu Muswada kama ulivyo hapo unasema the Dodoma Capital City Declaration Act, 2018, lakini huku ndani kuna mambo mawili ambayo yamechanganywa changanywa, jambo la
kwanza kabisa ni tamko la Rais la kutaka kuifanya Dodoma kuwa jiji. Unaendelea sehemu ya pili ni tamko pia la Rais kutaka sasa Dodoma iwe Makao Makuu ya Nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, majukumu ya Bunge na sisi Wabunge ni pamoja na kutunga sheria na kuna watu hapa walikuwa wameshauri toka mwanzo kwamba Rais ameanza hatua ya kwanza ya kutangaza Dodoma kuwa Jiji, kutangaza Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi kabla sheria haijaja hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kimsingi ametupoka sisi kama Wabunge madaraka yetu kimsingi ya kuweza kumshauri kama ambavyo inatakiwa ifanyike. Kwa hiyo, tungepewa kwanza kazi ya kutunga sheria, ndipo tungeendelea kwenye kazi ya kuishauri na kuisimamia Serikali. Hata hivyo, katika mambo yote yaliyopo hapa mbele yetu, hata bajeti ambayo inakuja kufanya hili jambo haieleweki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Simbachawene pale siku ya kwanza kabisa alipoleta lile tamko lake la kutaka tumpongeze Mheshimiwa Rais, kati ya mambo niliyasema wakati nachangia nikamweleza, kwamba utafiti uliofanyika kulifanya Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi, kulifanya Jiji la Dodoma kuwa jiji zinatakiwa pesa takribani shilingi trilioni arobaini kwa ajili ya kufanya hili jambo liweze kukamilika pale. Wataalam wakashauri tufanye utaratibu wa miaka kumi, kumbe hili jambo toka mwaka 1973 Mheshimiwa Halima Mdee hapa kasema utaratibu ndio ulikuwa huo ili kuweza kutenga pesa lazima lifanyike taratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona sasa hivi kuna mambo machache yanaanza kufanyika tunajenga stendi kule nje ya Mji, kuna barabara hapa zinaanza kujengwa hapa Dodoma, haya ndio maandalizi ya kuenda kulifanya Dodoma kuwa Jiji, maandalizi ya kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu, lakini bajeti yake lazima itokane na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tumefika wakati tunaanza kudanganyana tunasema kwamba Jiji la Dodoma lina uwezo wa kufanya hizi kazi zake zote, Jiji la Dodoma ndio linaloongoza kwa mapato Tanzania na kuna Mheshimiwa mmoja hapa anachangia anampongeza kabisa Rais kutangaza Jiji la Dodoma kwamba ndio linaloongoza kwa mapato, lakini anasahau kwamba Madiwani waliopo Dodoma akiwemo Mheshimiwa Bonifance ambaye ni Meya wa Jiji la Ubungo na yeye ni mmoja kati ya watu waliosema kwamba Rais alipotoshwa. Sasa yule anazidi kutaka kuutangazia umma kwamba ile taarifa ya Rais ilikuwa sawa. Kwa hiyo, jukumu letu sisi la kuishauri Serikali tunaachana nalo, tunabaki tuu kazi ya kupongeza kimsingi hii sio kazi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kadri ya kanuni kazi hii ya kupongeza ni ya mtu aliyeko kwenye kiti siku ambayo hoja ile iko pale mbele, tunapoteza muda mwingi kwa ajili ya kupongezana, muda mwingi kwaa ajili ya kusifiana, tunasahau shughuli yetu ya kuisimamia na kuishauri Serikali kimsingi, ndio tunafikishana hapa tulipo sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi yanatokea tuna taarifa kabisa za uhakika kwamba huu Muswada unaokuja hapa lakini ndugu zetu wa Zanzibar ambao ni sehemu ya Muungano hawakushirikishwa vizuri. Huwezi kwenda Zanzibar ukawaandikia tu barua kama ni watoto wadogo eti kwamba tunataka Dodoma kulifanya kuwa jiji na hapo badala Mheshimiwa Rais kutamka kwamba Dodoma ni jiji, ukategemea wao watakujibu wakiwa na roho safi, hawawezi kukubali. Wale sio watoto wadogo, kunakuwa na utaratibu wa ushirikishwaji, Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na Wabunge au Baraza la Mawaziri la Zanzibar pamoja na Baraza la Mawaziri la huku Bara, wakae pamoja kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na Muungano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanakuja hapa na hoja wanasema kwamba Dodoma ni katikati, sasa katikati kutokea wapi? Hili ndio lingekuwa suala la msingi ambalo ningefikiri Waziri angelijibu. Kama hapa Mheshimwa Heche kutoka Mara huko kwao Tarime, mpaka kufika hapa Dodoma naongelea habari za kilomita mia tisa mimi nikiwa natokea masasi mpaka kufika hapa naongelea habari za hizohizo kilomita karibu elfu moja na mia mbili, sasa katikati ni wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwenye bajeti zote zilizopita mpaka bajeti ya mwaka huu Wizara mbalimbali tumezitengea pesa kwa ajili ya kufanya Makao Makuu ya ofisi yao kwenye Mji Mkuu au Makao Makuu ya Nchi. Kwa mfano Wizara ya Viwanda na Biashara ofisi ya TBS imetengwa shilingi bilioni kumi na tisa ili waweze kuijenga Dar es Salaam, na ujenzi ule unaendelea leo hii tunawa-frustrate tunawaambia kwamba Makao Makuu ya Nchi yatakuwa Dodoma ofisi zote zitakuwa zinakuja huku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tunaona na Wizara ya Katiba na zingine zote wanalazimishwa kuja Dodoma lakini hii haishii hapa tu, tunaona maendeleo ya ghafla yanatokea Dodoma kwa sababu kuna wageni wanaohamia. Hawa wageni wanaohamia nikiwemo pamoja na mimi nusu ya maisha yangu, familia yangu iko Dar es Salaam, ndio maana wanasema Serikali hii haieleweki iko barabarani kila siku, iko Dar es Salaam au iko hapa Dodoma kwa sababu muda wote Watumishi wanakuwa kwenye movement.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wamelazimishwa kuhamishiwa Dodoma pasipo kupewa stahiki zao stahili, wote wanavilio, pamoja na wao kuwepo hapa lakini wamekuwa na vilio kwamba pesa waliopata haiwatoshi, pesa waliopata sio stahili yao. Sasa tunalazimisha kufanya haya mambo tumeona sisi Malawi, tumeona Zimbabwe na maeneo mengine wakiwa wanafanya hivyo vitu.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo taarifa siipokei kwa sababu hao watu sisi tunakutana nao na kuongea nao mitaani, walichokifanya Serikali ni kwamba watu hawa wanatakiwa walipwe stahiki zao za uhamisho kadiri ya utaratibu wa Kiserikali, atalipwa perdiem siku ishirini na moja, baada ya pale atalipwa disturbance allowance, atalipwa pesa ya kuhamishiwa mizigo. Tulimsikia Rais akisema hawa watu wahame kwa kutumia malori kwa kutoka Dar es Salaam kuja hapa na treni.

KUHUSU UTARATIBU . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi lakini nikuombe radhi kwanza kabla sijasema nimefundishwa kusema ndio na hapana, lakini ndio na hapana yangu lazima isikilizwe halafu tuweze kufikishana pamoja. Kadri ya taratibu za Bunge na Kibunge anaetakiwa kuthibitisha na imetokea humu ndani mara nyingi ni yule anayefikiri kwamba mimi nimesema uwongo.

Mheshimiwa nafuta kauli, lakini niiambie meza yako pamoja na mimi kufuta kauli ukweli huu bado utaendelea kuishi kwa sababu ndio ukweli uliopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaendelea hapa na kuna watu hapa naona wanapiga kelele kimsingi kwamba hiki kitu kinawaumiza watu wengi, hatujapinga Makao Makuu ya Nchi kuhamishiwa Dodoma, lakini tunasema hili jambo liende na taratibu zake. Watumishi wapewe stahiki zao, bajeti ieleweke kwa mfano mambo ya housing na mengine, miundombinu ya Dodoma haijawa tayari kukaribisha wageni walio wengi kwa hiyo tunataka haya mambo yafanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikwambie tu kwa mfano hawa ndugu zetu wa Malawi waliotoa miji pale Blantyre, lakini pia tuna Lilongwe. Kuna Mji Mkuu na Mji Mkuu wa kibiashara hayo yote tunayakubali. Sasa kama nia sisi kuja Dodoma na kuna Waziri hapa anasema Dar es Salaam sasa hivi hakuna foleni kabisa, jambo ambalo ni la uongo, foleni za Dar es Salaam ziko pale pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni watu wachache sana waliokuja hapa Dodoma wakitokea Dar es Salaam kwa maana ya kuhama nchi kama kweli tumepunguza foleni kwa nini sasa tunajenga daraja linaloanzia hapa Ocean Road kwenda kule Masaki kama wanasema hivyo. Miradi mikubwa hii ndio ambayo ndiyo ingeletwa hapa. Trilioni arobaini ni sawasawa na bajeti yetu ya nchi, tunapoamua tu kufanya kitu kimoja kwa mara moja, shida zake ndio hizi tunazozipata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, yafaa tujifunze wenzetu wa South Africa walianza kujenga mji wao mkuu, lakini baadaye wakatengeneza mji mwingine wa kibiashara sisi tumekuwa na hayo mambo. Tunaongelea hapa habari stahiki za watumishi ambavyo kama hivyo mlivyosema hatuwezi kuthitibsha kwa sababu wale watu hakuna atakayekubali kunipa payroll yake au bank statement itaonekana anaisaliti Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, hili jambo hata watumishi wa umma ambao wamestaafu sasa hivi miaka mitatu, miaka minne wanashindwa kulipwa stahiki zao kwa nini tuamini watumishi wanaohamishiwa Dodoma wanalipwa stahiki zao kwa wakati? Kwa hiyo, hili jambo tuliache kama lilivyo kwa sababu wametaka tufanye hivyo lakini kimsingi linawaumiza Watanzania wengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi jukumu letu kama ambavyo hapa nimesemea mheshimiwa Simbachawene amesimama na Wabunge wengi wa Dodoma, hatupingi moja kwa moja Dodoma kuwa Jiji, Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi yetu, lakini tunachokisema taratibu za kisheria zifuatwe kuhakikisha haya mambo yanakwenda vizuri, Jiji letu litakosa sifa za msingi, capital yetu itakosa sifa za msingi. Kwa hiyo lazima twende na utaratibu tupange bajeti inayoeleweka, tena nashukuru Mheshimiwa Simbachawene sasa hivi ndiyo amekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti labda hapo zamani alikuwa hajui kinachoendelea kule, atuonyeshe ni wapi kuna pesa ya kulipia ….

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, muswada uliopo mbele yetu leo unahusiana na sheria ya masuala ya ubia baina ya sekta binafsi na sekta ya umma. Tumeletewa hapa muswada mbele yetu, lakini ukiangalia historia ya marekebisho ya muswada huu, hii ni mara ya tatu muswada huu umekuwa ukiletwa lakini Bunge hili halijawahi kuelezwa kwa kina ni miradi mingapi sasa hivi inayofanywa kwa ubia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kwenye kitabu cha Kamati ukurasa wa nane, kwenye ukurasa wa nane kwenye kitabu cha Kamati wanaongelea habari za blueprint na nia ya kuleta blueprint ilikuwa ni kuhakikisha wana-sort au wana- solve matatizo yaliyoko kwa hawa wawekezaji wanaokuja kwetu na pamoja na watu wenye viwanda na wengine na hii inasimamiwa na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nia ya blueprint ilikuwa ni kuondoa milolongo mbalimbali ambayo kimsingi ukienda kusoma huu muswada wenyewe mbele yako hapo ukurasa wa sita kifungu cha 2(a) wanasema; “Notwithstanding the sub- section one, the Minister may exempt procurement of unsolicited project from competitive tendering where it meets the following criteria.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye blueprint walikuwa wanataka kuhakikisha tunaondoa kabisa matatizo ambayo hawa wawekezaji wamekuwa wakiyapata pamoja na frustration zao. Lakini wanaleta muswada wanaonesha kama hawataki kutambua vitu ambavyo viko kwenye blueprint. Wanasema kwamba the project shall be of priority to the government at the particular time and broadly consistent with the government strategic objectives. Sasa tunaposema strategies objectives bila kuzi-define moja kwa moja kwamba hizi ni zipi halafu tunataka wawekezaji wawe wanakuja kwa kushirikiana na Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kimsingi kuna sehemu unazidi kwenda hapa chini wanaongeza, wanasema; “the private proponent does not require government guarantee or any form of financial support from the government.” Sasa hii ni kuwachanganya hawa watu, tunaposema ni PPP maana yake ni ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi. Sasa Serikali haiko tayari kutoa pesa kwenye baadhi ya miradi kwa ajili ya uendeshaji wake na leo tunataka tualike hawa watu wakati tulikuwa tukiwa-frustrate kila mara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tujaribu kuangalia hapa tumeuliza swali linalohusiana na suala la reli ya Kusini ambayo ni reli inayoanzia Mtwara Bandarini na kuelekea mpaka Mbambabay, pamoja na Mchuchuma pamoja na Liganga. Hii ndio miradi ya kipaumbele ambayo kama kweli walikuwa na nia njema ya kuhakikisha yanafanywa kwa PPP wangeanza na hiyo miradi. Kwa sababu umuhimu wa hii reli ni kutuwezesha pia sisi kuweza kusafirisha chuma kutoka hayo maeneo kutokea mitaa ya Songea kuileta Mtwara Bandarini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chuma hii tungeweza kuiuza nje tukapata pesa ya kigeni na kugharamia miradi yetu mingine. Lakini matokea yake sasa hivi tumekuwa tukitumia hela nyingi sana tunatumia forex kwa ajili ya kugharamia miradi mikubwa wakati tungeweza kuanza na miradi ya kipaumbele kuwashawishi wawekezaji kuwawekea mazingira bora ya uwekezaji badala ya kutaka kuleta frustration. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mtazamo wangu nadhani nia hasa ya hii ya marekebisho ya sasa hivi yalikuwa yanalenga kifungu cha 47(7), kifungu cha 53(2), kifungu cha 56(1) kifungu cha 7, kifungu cha 57, 61, 62 na wameleta pale kwa makusudi kabisa wanasema Bungeni taarifa ya uhamisho wa fedha, taarifa ya matumizi, taarifa ya utekelezaji, taarifa kuhusu misamaha ya kodi na taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi sita badala ya robo mwaka kama ambavyo ilivyo sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nia yao hasa ni kutaka kuona kwamba tunapata hizi taarifa kila baada ya miezi sita, kwa nini sio baada ya miezi mitatu kama sheria inavyotaka, kwa nini sasa? Waziri atakapokuja aje atueleze kwamba wameamua kuongeza muda lakini sababu yao ya msingi hasa ni nini? Kwa kufanya hivyo tunakwenda kuwavutia wawekezaji au tunakwenda ku-frustrate zaidi industry. Kwa hiyo, marekebisho yanapoenda kufanywa lazima tuone yanakwenda kulenga jambo gani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi sana hapa, tunarudi sasa kule chini kabisa tunasema kwamba mwanzoni ilitangazwa PPP tunatafuta wawekezaji kwa ajili ya barabara ambayo ingeanzia Bandari ya Dar es Salaam
kwenda mpaka Mlandizi kama mchangiaji aliyepita hapa alivyosema, lakini matokeo yake sasa hivi Serikali wameamua kutumia pesa nyingi tena za kwake za ndani kadri wanavyotueleza, kwa sababu mara nyingi tunaona wanataja pesa za ndani halafu mwisho wa siku wanakwenda kukopa ili kugharamia barabara ya Kimara mpaka Kibaha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki ndio kipande ambacho Serikali wangeweza kupata fedha nyingi zaidi na ni sehemu ya kuweza kuweka vivutio. Kwa hiyo, wameachana na ule mradi wa awali wa kupitisha barabara kule Chamazi kuileta pale ambayo ingepunguza kuleta foleni na kinachosababisha haya mambo yote yatokee ni kwa sababu tu Serikali haitaki kufanya mahusiano mazuri na wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji wanakuwa frustrated sera zetu haziko straight kuonesha nini tunataka kiasi wawekezaji wanakuwa wakipata uoga kuja nchini kuwekeza kwa sababu muda wowote yanaweza yakatokea mabadiliko kwa sababu hiki kitu ni kama kitu cha one men show, mtu mmoja anaamua kufanya wakati wowote anaotaka yeye na haya mambo yanatokea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ina-frustrate sana wawekezaji wetu hata kama tutarekebisha hapa sheria mara mia moja, bila kuleta ile Principle Act, tukaona kimsingi nini tunahitaji sisi kukifanya inaweza isiwavutie sana wawekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuhitimisha kabisa na tuelekee pale mbele, sisi kwenye ripoti na taarifa yetu ya Kambi Rasmi ya Upinzani tumeeleza pale wazi kwamba kama Serikali ina nia njema ya kutaka kuona wawekezaji hasa hawa wa kushirikiana public and private sector wanakuja kufanya kazi kwa pamoja cha msingi cha kuangalia kwanza ni kanuni za uwekezaji, mazingira bora ya kuhakikisha hawa wawekezaji wanapokuja wanalindwa na mikataba yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huku ndani tunaongeza sehemu nyingine ukisoma kwenye huu muswada uliopo hapa mbele yetu wanasema hata hizo kesi zitakazofanyika arbitration kama mambo yatakuwa yameshindikana kule ndani zipelekwe mahakama za hapa hapa ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ni mwekezaji gani alete pesa yake nchini kwetu halafu yanapotokea kutokuelewana kati ya mwekezaji pamoja na Serikali na hizi kesi bado zizidi kusikilizwa hapa hapa ndani. Ni kesi ngapi ambazo hazijaenda vizuri tunajua, sheria yetu sasa hivi haijasimama vizuri maeneo mengi. Kwa hiyo, tunawatengenezea mitego kiasi kwamba wawekezaji wetu sisi wanashindwa kuja kwa sababu wanafikiri wanakuja kupoteza pesa zao hapa. Tumeona kwa mfano kuna mradi sasa hivi ukienda jimboni kwangu kuna mradi pale wa kuchimba madini ya graphite.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wawekezaji walikuwa tayari kabisa kuja kuanza ile kazi, lakini wamekuwa frustrated baada ya kuamua sasa kubadilisha ile sheria ya madini, yale masuala yanayohusiana na makinikia ambayo kwa kweli haijafanikiwa kokote, sana sana wale wawekezaji wanapokutana kwenye round table zao kwenye hizo nchi zao wanapojaribu kukusanya mitaji wanaulizana unakwenda kuwekeza nchi gani. Wakiambiwa wanakwenda kuwekeza Tanzania wanakuwa frustrated kwa sababu sheria zetu zimekuwa zikibalika kila mara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inakuja hapa sheria inakuwa vague, mwisho wa siku wanakwenda kuwabana wawekezaji kwa kutumia kanuni ambazo zinakwenda kutengenezwa kwa mamlaka aliyopewa pale Waziri. Kwa hiyo, niombe tu kwa nia njema kabisa kwamba tuangalie namna bora tulete hizo principle act badala ya kufanya amendment vipande vidogo vidogo kila siku kwa sababu watu wanaweza wasio proper correctors wa hivi vitu mwisho wa siku inakuja kuwabana kwenye maeneo ambayo wanashindwa kwenda pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema hizi unsolicited project lazima hapa tuwe wazi kabisa, Serikali inataka kujivutia upande wake tu bila kuangalia hata hawa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekeza wao wananufaika vipi. Hii ni namna ya kuwatisha hawa wawekezaji, tumeona kuna maeneo mengi ambayo wawekezaji wamekuja, lakini mwisho wa siku wameishia ku-withdraw. Tunaambiwa sasa hivi kuna wawekezaji wa viwanda zaidi za 53,000; kuna watu wameenda TIC wameenda kuomba leseni za kutengeneza viwanda lakini tu wakisha-register TIC sisi tunawaita moja kwa moja wawekezaji.

Mheshimwa Mwenyekiti, kwa hiyo hatupeani actual fact, hatupeani figures hasa zinazowahusu hawa wawekezaji, yaani hatupeani takwimu sahihi kabisa kuhusiana na masuala ya wawekezaji. Na hii inawatisha kwa sababu ukienda kwenye mtandao wetu, ukiangalia masuala ya kiuchumi against haya masuala ya uwekezaji utakuta ni vitu viwili tofauti kabisa. Hawa wawekezaji wanapotaka kuja lazima wawe wanaangalia hivi vitu viwili na kufanya mlinganisho kwamba uchumi wa nchi hii ukoje, wawekezaji mazingira yao yakoje. Lakini pamekuwa na milolongo mirefu wawekezaji wengi wanashindwa kuja nchini, ahsante. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuunga mkono hoja maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani.
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Kwanza nataka tu kuweka sawa record ya Bunge lako kwa sababu juzi wakati Waheshimiwa Mawaziri wanajumuisha na Mheshimiwa Attorney General alipewa nafasi ya pia naye ya kutoa mchango wake. Naomba ku-refer sehemu ambayo alikwenda, nina document ambayo ninayo hapa naomba niisome wakati ninajaribu kujenga hoja yangu.

Mheshimiwa Spika, AG alipopewa nafasi ya kutoa maoni yake sina uhakika kama ni makusudi kabisa au kuna mtu alimwagiza aamue kulidanganya Bunge lako. Wakati anatoa taarifa yake, naomba kuisoma, alisema kwamba:

“Pamoja na marekebisho yatakayoletwa na Serikali kuchangia hasa zaidi kwenye hii sheria inayohusiana na masuala ya korosho, kwamba hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu mwaka 2000, Desemba ilisema kwamba, pesa zile ambazo Serikali imekuwa ikikata kwa maana ya export levy, ilikuwa ni mali ya Serikali, mali ya umma”. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, alisoma tu baadhi ya vifungu ambavyo yeye AG kwa malengo yake mwenyewe alikuwa anavitaka, lakini hata hivyo kimsingi ukienda kusoma kwenye ile hukumu ukurasa wa 17 ambayo ninayo hapa na naomba niisome ili kuweka record sawa, tuone ni kwa namna gani AG alikuwa ameamua kulidanga Bunge lako na niliomba hapa mwongozo na bahati mbaya sikupata hiyo nafasi ili kiti chako kiweze kufanya maamuzi juu ya jambo hili. Sehemu ya hukumu inasema hivi:

, “In view of the above were certified that, the trial Judge rightly held that there was no agency relationship between the parties. We are further more certified that since the cashewnuts export levy was not a tax, and the Government or Tax Authority did not legislate for such tax at all. They was also no agency relationship between the Government and the Appellant whatever the case the cashewnut export levy money was not revenue from the taxation so it was not and is not Government revenue. Ordinarily the money would belong to the cashewnut farmers and the right of the above the appeal is lacking the merit we are accordingly dismissed with cost”. (Applause)

Mheshimiwa Spika, sasa Mheshimiwa AG aliposimama, alisema hizo pesa zote ni mali ya Serikali, asilimia 35 na asilimia 65.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo sipokei na nina hiyo kesi hii mbele yako, naiweka hapo kwa maana Serikali ichukue, lakini wakati huo huo fuatilia kwenye Hansard maneno ambayo aliongea AG na niliyoyasema mimi na mimi nilikuwa nataka kusema kuhusu jambo hili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba hiyo nakala ikae mezani kwako, ambayo ndio hukumu hiyo tunayoiongelea sisi. Mheshimiwa Spika, ni Mahakama ya Rufaa, wakati huo naomba uangalie pia muda wangu kwa sababu isije ukatumika vibaya.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza nishukuru sana, taarifa ya Mheshimiwa Zitto naipokea na huko ndiko nilikokuwa naelekea na ndio maana nilisema kwamba Mheshimiwa Attorney General amelidanganya Bunge lako. Sasa kwa sababu Mheshimiwa Zitto amemaliza hili na ameliweka sawa naomba hiyo taarifa yake pia iwe sehemu ya mchango wangu. (Makofi/vicheko)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo machache sasa nataka nirudi, panapokuwa na nia mbaya hata wale walioagizwa kwenye kutekeleza hiyo nia mbaya na wenyewe wana tendency ya kufanya contradictions. Wakati tunachangia humu ndani na Mheshimiwa Attorney General akatoa maelezo yake akasema kwamba hili jambo haliko kisheria hii pesa ilikuwa ya Serikali, lakini hizo hukumu zinaonesha hizi pesa ilikuwa ni mali ya wakulima. Kamati pale Mheshimiwa Mwenyekiti tumesikia naye Mama Ghasia anasema kwamba anaishauri Serikali, anamshauri Waziri waitishe tena kile kikao cha wadau ili waweze kukubaliana namna bora ya kutumia hizi pesa na kuzirudisha kule chini.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, nashukuru, kwa sababu mama naye dhahiri masuala ya korosho anayafahamu, tutajadili wenyewe tutakapokutana nje, lakini natambua tu taarifa ya Kamati na yenyewe inapendekeza kwamba Serikali ikatafakari upya namna hili jambo kwa sababu pia mwisho wa siku kuna haja ya kwenda kukutana na wadau na kufanya majadiliano na kuona namna bora ya kuzitumia pesa hizi. Sasa pale Serikali ilipoamua kutaka kuondoa hili suala mbele ya Bunge lako hapa ukisikiliza taarifa ya Attorney General ni taarifa tofauti kabisa na tuliyopata tukiwa ndani ya Kamati taarifa ambayo ilitolewa na PST.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa huyu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha wakati anatoa taarifa yake anasema kwamba Serikali imeamua ku-control hizi pesa kwa sababu kuna ubadhirifu mkubwa ambao umekuwa ukifanyika hizi pesa zinapopelekwa kule chini, sasa swali linakuja, kwa nini wakulima wote wa korosho waadhibiwe kwa sababu tu ya ubadhirifu wa watu wachache?

Mheshimiwa Spika, vile vile anasema ameagizwa ameagizwa Controller and Auditor General kwenda kufanya ukaguzi wa hesabu za korosho imeonekana kule ndani kuna madudu, amemuagiza zaidi ya mara mbili, zaidi ya mara tatu, sasa Serikali i na mkono mrefu na tulikuwa tukiambiana hapa kila mara, kama kweli Serikali ina mkono mrefu ikachukue hatua.

Mheshimiwa Spika, tumeona mabadiliko ya bodi yamefanyika mara mbili, bodi wamebadilisha mara mbili uongozi, watendaji wa bodi wameondolewa mara mbili lakini Mwenyekiti wa bodi hii anayesimamia masuala haya yote bado yuko pale pale.

T A A R I F A . . .

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, labda ikae kwenye record sawasawa na mtakapofanya vikao vyenu vya chama mwambieni Dkt. Mollel apunguze kujipendekeza kwa sababu anachokifanya hakimpi yeye uhalali wa kuonekana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nataka kusema kwamba nimeondoa taarifa yako nimeondoa taarifa yangu , kwa hiyo nataka niseme kwamba Serikali kaama wana nia ya kuchukua hii pesa basi pafanyike majadiliano, kwa sababu kwenye taarifa ya CAG inaonesha wazi kabisa na anadiriki kusema kuna ubadhirifu ulikuwa ukifanyika ndio maana ndio maana Serikali ikaamua kuchukua huu mfuko. Mheshimiwa Katibu Mkuu amekiri hiyo mbele ya Kamati sasa tunajiuliza sisi kwa nini hatua tu zisichukuliwe kutokana na report ya CAG badala yake Serikali inaamua kufuta Mfuko mzima.

Mheshimiwa Spika, tumeona baadhi ya maeneo kuna kesi hapa 1.5 trilioni imepotea, pesa ya Serikali wanasema kwamba haijulikani namna ilivyotumika, lakini pia tumeona kuna Wizara nyingi zimepata hati chafu mbona hizi Wizara hazifutwi, inakuwaje sasa Mfuko wa Korosho wanasema kuna matumizi mabaya matokeo yake wanafuta Mfuko mzima na wanakwenda kudhoofisha kwa wazalishaji wa korosho.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niombe tu pamoja na Serikali kuamua kufanya ubabe, kung’ang’ania hiyo hoja wanasema wao hawataki kubadilika na ndio inavyoonekana kwa sababu Waziri Mpango mara nyingi hata Mheshimiwa Nape alipotoa hoja yake aliitwa mbele ya Kamati aje kutoa maelezo kwa nini hii pesa haipelekwi, matokeo yake Waziri hakuja pale, hakuna kilichoeleweka na wewe mwenyewe Spika ulitoa hapa maelekezo kwamba watu wakaae na uliongea kwa masikitiko makubwa kabisa kwamba hili jambo linavyofanyika si haki kwa sababu zao limekuwa likikua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na upungufu uliopo sasa tunaomba Serikali ijaribu kufikiria tena upya, hata hivyo hizi sheria sio retrospective sheria hii inaanza tarehe moja ya mwezi wa Saba mwaka huu, mpaka sasa hivi wakulima wa korosho kutokana na sheria wanayokuja kufuata sasa kwa makusudi ili kuhalalisha kuchukua hiyo pesa, bado ile pesa nyingine kule haijapelekwa. Sasa inakuwaje hawataki kulipa deni la zamani, halionekani kwenye bajeti iliyopita, leo wanataka kufuta sheria na kuhalalisha ile pesa iweze kwenda kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, pia ukienda kwenye maombi yangu ya kutaka kubadilisha baadhi ya hizi sheria nimeomba pia kuhusu sheria ya masuala ya mfuko mmoja namba 348. Hata hivyo, yenyewe jinsi ilivyokaa ukiangalia ile sheria ni kwenda kuziua halmashauri zetu. Tunaposema mapato ya halmashauri yaende yakasaidie halmashauri, hii kazi ya D by D imefanyika kwa muda mrefu sana na Serikali hii miaka mitano, miaka 10 yote iliyopita hiyo kazi ilikuwa inafanyika, leo hii Serikali hii adhimu tunayosema inawajali wanyonge, inapenda kugatua madaraka kila mtu aweze kufanya katika sehemu yake, inarudi tena na hii sheria wanataka kuondoa hicho kipengele pesa zote zikusanywe ziende kwenye Mfuko Mkuu.

Mheshimiwa Spika, hii haitaweza kusaidia halmashauri watakapoondoa hizi pesa tafsiri yake shughuli za halmashauri zitakwama na sasa hivi majimbo yameonekana yana pesa nyingi kuliko halmashauri zetu, kwa sababu pesa za majimbo zinakwenda moja kwa moja kwa Wabunge kwa ajili ya kufanya kazi, lakini pesa za halmashauri zina mlolongo mrefu wa kuzipata.

Mheshimiwa Spika, ukirudi huko chini kwenye halmashauri zetu, Wakurugenzi wanalalamika, Wakuu wa Idara wanalalamika, hakuna pesa, lakini bado Serikali hata kile kidogo ambacho kilikuwa kinabakia kule na chenyewe wanakihitaji, wanataka sasa kukiweka kwenye Mfuko wa pamoja, process ya matumizi kwenye Mfuko huu wa pamoja ni ndefu sana, mambo mengi yatakwama.

Mheshimiwa Spika, uzalendo sio kukusanya kila kitu pamoja, kuna sehemu tulisema sisi unapoamua kuwa mzalendo hakikisha unachokifanya leo kitawasaidia na wazalendo wenzio wanaokuja au watu wengine ambao hawana nia njema. Kwa hiyo, niombe tu kuunga mkono hotuba iliyosomwa hapo mbele na Kamati ya Bajeti na kwamba mambo haya yakafanyiwe kazi ili tuweze kwa hakika kabisa kuliboresha Taifa letu, kuweza kuweka mambo mazuri.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
The Finance Bill, 2022
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, na mimi nikushukuru tena kwa kunipa nafasi ya kuchangia na kutoa mawazo yangu kwa nia ya kutaka kuishauri Serikali kufanya marekebisho ya baadhi ya sheria.

Mheshimiwa Spika, la kwanza kabisa nataka tuangalie kwenye ukurasa wa saba.

SPIKA: Ukitutajia kifungu utatusaidia zaidi kuliko ukurasa.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, sawa. Ukurasa wa saba Cap. 203 part 5. Hii ni sheria ya korosho; na nime¬-move schedule of amendment; kwenye sheria hii wanataka kufanya marekebisho lakini wanatumia sheria iliyopita. Sheria iliyopita ilikuwa inataka fedha zinazokatwa au zinazopatikana kutokana na makusanyo ya export levy asilimia 65 ya fedha ile ilikuwa inarudi kwenda kusaidia wakulima.

Mheshimiwa Spika, miaka ya hapo nyuma kidogo fedha hii iliondolewa yote kabisa na ikaenda Serikali Kuu. Juhudi kubwa sana zimefanyika kwa kushirikiana na Serikali na sisi Wabunge wote tunaotokea kwenye maeneo yanayolima korosho na tukapata mafanikio makubwa fedha ile ilirejeshwa. Na mwaka huu ikaanza kutumika kwa maana ya kupeleka ruzuku kwenye pembejeo ambazo zimesababisha wakulima kupewa pembejeo bure.

Mheshimiwa Spika, sasa Wizara ya Fedha inakusudia kufanya mabadiliko, na katika mabadiliko haya wameleta mapendekezo kwenye kifungu a, wanasema asilimia 50 itakuwa remitted to the Ministries responsible for agriculture kwa ajili ya kusaidia kwenye subsides za mazao. Lakini sisi tunataka tuombe zaidi. Hii sheria itamke kabisa kwamba fedha hii inakwenda kutumika kwenye korosho kwa sababu ndiko inakokusanywa. Kwa hiyo, wakubali kuongeza hiki kipengele kama ambavyo iko kwenye schedule of amendment kwamba fedha hii ikatumike kwenye kuboresha au hizo agricultural subsidies kwenye zao la korosho kwa sababu ndiko inakokatwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kipengele cha pili tunaomba kiboreshwe na tunapendekeza iwe kama ifuatavyo. Kwanza tunaridhika kwa makato haya yanayofanyika. Isipokuwa sasa Serikali fedha inayokwenda kwenye Agriculture Development Fund iwe asilimia 15. Maana yake iwe specifically hapa ulifafanua tu wameweka tu asilimia 50 as a block figure kwamba asilimia 50 shall be remitted to the Consolidated Fund.

Mheshimiwa Spika, tunaomba iwe asilimia 15 iende kwenye ADF (Agriculture Development Fund) na asilimia 35 iende kutumika kwenye Consolidated Fund kama ilivyo, kwa maana ya kutaka kuchangia kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, lakini tunapendekeza in the future basi na mazao mengine ambayo yanakuwa exported kutoka Tanzania na wenyewe wawekewe export levy. Kwa sababu makusudi ya hii sheria ilikuwa ni kutaka kuhakikisha badala ya ku-export process za haya mazao yafanyike nchini kwa maana ya kutaka ku-create ajira, kutaka kuzalisha ajira nyingi zaidi. Sasa wakawa wanaweka hizo fedha za export levy kama ni sehemu ya kukatisha tamaa watu wanaotaka ku-export na kuwa-encourage wajenge viwanda nchini kwetu. Lakini sasa hivi inatumika kama mapato na sisi tunakubali na tunanufaika nayo na tunaomba iendelee kama ilivyo kwa maana ya asilimia 50.

Mheshimiwa Spika, lakini iende sasa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kwenda kusaidia na hasa zaidi kwenye zao la korosho kwa sababu mapato haya yametokana na mapato yanayotokana na korosho na siyo mapato ya mazao yote mtambuka. Kwa hiyo, iwe specific na sheria iseme wazi kwamba itasaidia kusaidia kwenye zao la korosho, kwa maana ya mikoa yote waliyoamua kufanya ukulima wa korosho ikawasaidie. Lakini hatutegemei tuone fedha hii inakwenda kusaidia kwenye karanga, inakwenda kusaidia kwenye ufuta sijui, inakwenda kusaidia kwenye mazao mengine. Ni maeneo yale tu iwe specific yanayolima korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na hii sehemu ya pili na yenyewe ikawe waziwazi kabisa, maana hapa wameweka tu asilimia 50 moja kwa moja iende Mfuko Mkuu. Tunatamani hii asilimia 50 iende kwenye kusaidia hizo agricultural inputs za korosho. Hii asilimia 50 igawanywe mara mbili, 15 iende kwenye ADF kwa maana ya sisi wakulima wa korosho tunaamua kwenda kuchangia Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo kwa asilimia 15. Halafu asilimia 35 inayobakia yenyewe iende moja kwa moja kuchangia kwenye Consolidated Fund; kwa maana ya Mfuko Mkuu wa Serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi nzima ili tuweze kukamilisha kule kwetu ujenzi wa barabara Mtwara, Mlivata, Masasi, Nachingwea na huko kwingine kote ili tuweze kupata pale mazao mazuri pamoja na kuboresha bandari yetu.

Mheshimiwa Spika, sheria ya pili ambayo napenda nizungumzie ni sheria hii inayokusudia kuondoa tozo kwenye kuingiza mafuta nchini kwa maana ya ile asilimia 15. Wizara wameleta mapendekezo, wanasema kwamba sasa hivi…

SPIKA: Sasa kwa sababu wewe umetuongoza vizuri, kifungu cha ngapi?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, hii document ni kubwa kidogo nimesahau kuandika hapa kifungu lakini unaweza kunisaidia kama kiko karibu na wewe hapo au Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

SPIKA: Ni sheria gani?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, sheria itakayokuwa inasaidia ku-import crude oil.

SPIKA: Sheria gani?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, mabadiliko ya sheria kwa maana ya inayoondoa kodi kwenye importation ya crude oil.

SPIKA: Haya, endelea na mchango wako.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninachoishauri Serikali. Serikali inapendekeza waweke zero rate, kutoka asilimia 25 iliyokuwa inatozwa mwanzoni kwenye kuingiza crude oil nchini. Wana lengo zuri kabisa ikiwa ni pamoja na kupunguza inflation pamoja na kusaidia kwenye bei ya mafuta ili yasipande, kupunguza inflation kutoka asilimia 25 wameondoa import duty up to zero kwenye crude oil.

Mheshimiwa Spika, lakini nataka niwakumbushe Wizara wafahamu kwamba mafuta mengi tunayotumia hapa nchini kwetu yanatoka nje, na nchi nyingi ambazo tunachukua mafuta kwao hawaruhusu kuondoa crude oil. Kwa sababu wanapoondoa crude oil kule kwao na ku-export tafsiri yake wanapunguza ajira. Kwa hiyo, wanaleta mafuta ambayo yako semi processed.

Mheshimiwa Spika, sasa Tanzania sisi tuna viwanda na tunaipeleka nchi yetu kwenda kuwa nchi ya viwanda. Kuna viwanda vinavyofanya processing za mafuta ya kupikia. Sisi tulipata safari ya tukatembelea kiwanda kimoja Dar es Salaam, Murzah Oil pale. Wao wanachokifanya kikubwa wanaanza kutoka stage za chini kwa kununua alizeti; na tunafahamu wazalishaji wengi wanafanya hivyo; baadaye wanakwenda ku-process alizeti wanapata mashudu, wanauza mashudu na mengine yanakwenda kutumika kwa mifugo na kufanya shughuli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunapoamua kuondoa na kuruhusu watu wayalete mafuta nchini yakiwa semi processed kama ilivyo kwenye viwanda vya bati na vingine tunakuwa tumeondoa sehemu ya ajira, yaani tunapunguza. Hakuna mtu utakayemwambia aendelee ku-maintain wafanyakazi wanaokamua alizeti ilhali anafahamu akiingiza mafuta kutoka nje na kuyaleta hapa yakafikia hapa Tanzania kwa ajili ya kusafisha tu kidogo lakini baadaye kuyafanyia packaging.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, watu wengi watakuwa wanakimbilia kwenye viwanda vya kufanya packaging pamoja na kuyapeleka mafuta sokoni, tutaondoa ajira, tutapoteza ile kodi ya pay as you earn pamoja na kodi nyingine. Kwa hiyo, nikuombe, na niiombe Wizara wazingatie hili. Kwa sababu tukifanya hivi hatutakuwa tena nia ya kulinda viwanda, tutaua viwanda vyetu na pia tutairudisha Tanzania kuwa kama nchi ya wachuuzi; kwa sababu wachuuzi ndiyo wale wanaoleta either processed products au semi processed products.

Mheshimiwa Spika, tuliona kwenye viwanda vya bati, wakati nilipochangia kama Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara. Tulipata ziara ya kutembelea kwenye viwanda vya mabati, nao walikuwa wanalalamika kwamba kuna viwanda vinavyo export mabati kutoka nchi nyingine ambayo yamebakisha labda process mbili tu; kuyakamilisha ili yaweze kuingia sokoni. Na process mbili ni kuyapiga rangi pamoja na kuyawekea migongo na ya tatu ni kufanya cutting.
Mheshimiwa Spika, na uwezi kulinganisha bei za watu wanaoleta hayo mabati yakiwa tayari. Na nilitoa mfano hapa, ukiwa njiani unaweza ukapishana na yale malori yanayobeba zile rollers zinazokwenda kwenye viwanda. Utakuwa roli zingine zimebeba rollers sita mpaka nane kwenye gari la futi 40. Tafsiri yake ni kwamba wale wanayapeleka kwenye viwanda vya kupiga rangi, kuweka migongo pamoja na kukata. Kwa hiyo, unaweza ukakuta kuna wafanyakazi 10 wanaendesha mashine na bati zikatoka nje zikauzwa.

Mheshimiwa Spika, ukikuta gari imebeba rollers mbili ama tatu zile za futi 40. Tafsiri yake wanapeleka kwenye viwanda ambavyo vinaanza kurekebisha size na mengine.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kwa nafasi hii uliyonipatia na mimi naomba kutoa mchango wangu na Serikali ifanye marekebisho kama nilivyoomba, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mchango wangu kwa njia ya maandishi pamoja na kwamba nimeomba kuchangia lakini napenda kuwasilisha mchango pia kwa sababu ya ufinyu wa muda.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama chetu Chama cha Mapinduzi kwa usimamizi imara kabisa wa ilani, mengi yanayofanyika majibu sisi sote na wananchi ni mashuhuda, jimbo la Ndanda lenye kanda mbili hivi sasa kuna miradi mingi inaendelea tena kwa kasi ambayo haijawahi kutokea, miradi ya maji, zahanati, vituo vya afya na mingine mingi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na mazuri hayo kuna mambo machache ya kurekebisha; kwanza ni suala la Mtwara Corridor; nini msimamo wa Serikali kwenye utekelezaji wa mradi huo mkubwa ambao kimsingi ni mhimili mkubwa sana kwenye ujenzi wa uchumi wa Mikoa ya Kusini, kwani inagusa mradi mkubwa wa Liganga na Mchuchuma, uendelezaji wa bandari ya Mtwara na ustawi wake, reli ya Kusini na maboresho ya barabara Mtwara Mbambabay.

Mheshimiwa Spika, pili, tumeona mambo mengi mazuri ambayo ni kama maono ya binafsi ya Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, hivi ni kwa nini Serikali isifikirie kuona namna ya kuwa na Sheria ya Kilimo kwa ajili ya kulinda mawazo mazuri yote yanayoletwa hapa ndani na Waziri wa Kilimo, kwa sababu siku akibadilishwa inawezakana akaja Waziri mwingine akawa naye na maono yake, lakini mazuri yote kama yatalindwa kisheria basi yatakuwa na tija na muendelezo kwa ajili ya manufaa ya Taifa hili. Tumeona namna alivyohangaika awamu hii Wizara ya Fedha kuhakikisha pesa ya export levy inarejeshwa kwa wakulima na amefanikiwa, sasa ije kwenye Finance Bill na liwe jambo la kudumu badala ya kuwa ni la matakwa ya mtu binafsi.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na udhaifu mkubwa sana kwa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Korosho, tumekuwa na kikao na wewe hivi karibuni, tumeongea suala la matumizi mabaya ya ofisi, naamini pia Mwenyekiti wa Bodi anafanyia kazi mambo ambayo tuliyasema wakati wa mkutano huo, lakini kwa kifupi waangalie namna anavyofanya kazi zake, kuna watu wamekuwa na madai ya muda mrefu ya bonds akiwemo ndugu Kapwapwa kwa jina la Kampuni TF Commodities Ltd. ambaye kwa sasa anadaiwa na benki hivyo naye anakusudia kuishtaki CBT. Nilitoa mapendekezo kama amekuwa Kaimu kwa miaka mitatu au athibitishwe au aondolewe kwani bodi iliyoko sasa ni mpya.

Tatu, kumekuwa na suala la namba za vijiji kwa muda mrefu sasa, vijiji vya Mkalinga, Sululu ya Leo, Chipunda na vingine vingi, hivi kuna ugumu gani kutoa hizo namba za vijiji wakati vitongoji hivyo vimetimiza vigezo vyote, kuna maombi pia ya kata ya Nambawala ili wananchi waweze kujiletea maendeleo yao.

Mheshimiwa Spika, kuna suala pia la mgogoro wa ardhi katika Kata ya Moanyani, umekuwa ni mgogoro wa muda mrefu kama Wizara ya Mambo ya Ndani (Magereza) hawana uwezo wa kulipa fidia wananchi basi watangaze na kuliachia eneo hilo kwani kumekuwa na migogoro kila mara ya maeneo hayo. Bodi pia ina migogoro na wazabuni wa pembejeo kwenye zao la korosho mambo ambayo yanahitaji akili kubwa zaidi kuyatatua kabla hayajaleta migogoro mikubwa uko mbele.

Nne, kuna suala la inflation, Serikali iangalie tena uwezekano wa kulirekebisha suala hilo kwani linaleta mzigo mkubwa sana kwa wananchi sambamba na bei ya mafuta, kwani sehemu karibu nusu ya bei hizo ni tozo, kwa hiyo Serikali iliangalie vyema.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha mchango wangu.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana na mimi kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze moja kwa moja kwa kuipongeza sana hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo imejikita kwenye kuona namna ya kutatua na kusuluhisha matatizo yanayowakabili watanzania, ninaamini tukietekeza hii kama ilivyo tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais pia kwa namna ambavyo tumepata miradi mingi kwenye maeneo mbalimbali kwenye Majimbo yetu. Jimbo la Ndanda sasa limechangamka zaidi ukilinganisha na miaka mitano iliyopita wakati ule hatuna Ilani ambayo tulikuwa tunaisimamia na sasa tupo tunakwenda mstari imara wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, wananchi wamechangamka na bado wanaahidi watakichagua tena Chama cha Mapinduzi ili kuweza kujipatia maendeleo wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo ninapenda kulisema pamoja na pongezi hizo ni kwamba nimpongeze pia Mheshimiwa Waziri wetu wa Kilimo kwa namna ambavyo juzi tu hapa tulikuwa na kikao kwa ajili ya wadau wa korosho kuangalia na kufanya tathmini ya msimu uliopita. Kuna baadhi ya mambo tumeyajadili, kwanza kabisa nimpongeze kwa kuhakikisha export levy kile kiasi cha pesa ambacho kilitengwa kwa ajili ya kusaidia wananchi hasa zaidi kwenye masuala ya pembejeo kimerudi tena na Serikali imeridhia kwamba pesa hiyo itatoa ili kupunguza nakisi ya bei ya pembejeo ili kuwasababishia wakulima waweze kuzalisha kwa gharama nafuu zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nimuombe sasa Waziri wa Fedha ahakikishe jambo hili analileta kwenye Finance Bill, lisiwe tu kwamba ni matakwa ya Waziri walikutana huko wakaonana lakini liwe kisheria kabisa ili kila mwaka sasa hiyo pesa iwe inarudishwa isiwe maamuzi ya kipindi kimoja kimoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine ninaomba pia Mheshimiwa Waziri wa Kilimo yeye mwenyewe alete sheria itakayokuwa inasimamia masuala ya kilimo. Tumesikia hapa juzi wakati wa uzinduzi, wakati wa ugawaji wa pikipiki zile kwa ajili ya wenzetu Maafisa Ugani ameongea mambo mengi sana mazuri kwa ajili ya kuboresha kilimo, hata hivyo mambo haya hayapo kwenye sheria, afanye namna nzuri aweze kuleta sheria hapa tumsaidie kuipitisha ili iweze kuwa kama dira ya shughuli anazotaka kuzifanya kwenye Wizara ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa wa Waziri ya Kilimo, naweza nikakukumbusha mambo machache ambayo tuliyaongea wakati wa kikao chetu cha wadau wa korosho, na nafanya hivyo makusudi ili iingie kwenye Hansard uone na wewe namna ya kuyashughulikia.

Kwanza kabisa tulikushauri kwamba kuna mambo mawili, sasa hivi tunayo Bodi ya Korosho mpya na tunaona inafanya kazi yake vizuri kabisa chini ya Mwenyekiti wetu Mzee wetu Mzee Mwanjile wanafanya kazi nzuri sana, lakini tulikushauri na mimi nilitoa ushauri nikakuambia kwamba tunae Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho ambaye ameshakaa pale ndani zaidi ya miaka mitatu akiwa anakaimu, tukakuomba kama inawezekana fanya mambo mawili ili aweze kufanya kazi zake kwa uhakika, ama umthibitishe kwa sababu amekuwepo Bodi ya Korosho muda mrefu au umuondoe ulete mtu mpya ambaye anaweza akafanya kazi vizuri zaidi ya huyu aliyepo kwa sababu kwa kipindi kirefu hamjamhibitisha, sasa hatuelewi tatizo ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ni kwamba kumekuwa na migogoro mingi ndani ya Bodi ya Korosho na wewe kama Waziri nafahamu labda mingine imekufikia, migogoro ya watumishi, migogoro ya wanunuzi kwa mfano kuna Kampuni moja inaitwa TF Commodities wanadai Bond yao ya Milioni 50 zaidi ya miaka mitatu sana. Tunaomba kwa sababu wale watu wanachajiwa interest kwenye mabenki au warudishiwe au wakatwe hicho kiasi ambacho kinachotakiwa kukatwa balance yake apewe ili aweze kuendesha maisha yake na hii itawapa comfort wanunuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliongea pia suala la usambazaji wa viuatilifu, tunakupongeza sana kwa sababu kiasi fulani kimeshafika kwenye maeneo yanayotakiwa yasambazwe. Hata hivyo tunakuomba kwamba kuna migogoro mingi ya upatikanaji wa tender hizi ambazo zinasimamiwa na bodi ndogo ambayo inaitwa Bodi ya Pembejeo lakini na yenyewe haipo kisheria, kazi wanazozifanya haziwapi amani sana watu wengi wanaosambaza pembejeo kwa sababu imekuwa na aina fulani ya upendeleo, badala ya kuangalia performance wameangalia kama mambo ya kujuanana nayo tunaomba uichunge uone namna ya kusaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba sasa nijikite kwenye mchango wangu rasmi. Nianze kwa kusema kama Wabunge wote tunakubaliana kabisa kimsingi kwamba kuna inflation, kuna ongezeko kubwa sana la bei ya bidhaa mbalimbali. Jana tulimuona Mheshimiwa Waziri wa Fedha akiongea kuhusiana na suala hili la ongezeko la bei, tulimuona pia Waziri wa Viwanda na Biashara nae akiongea kuhusiana na suala la ongezeko la bei. Kwa nafasi zetu kama Wabunge tuna wajibu wa kuishauri Serikali ili iweze kuangalia namna bora tutakavyoweza kupata solution ya kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha uliopo sasa hivi kutokana na ongezeko kubwa la bei ya bidhaa, kuanzia bidhaa za ujenzi mpaka bidhaa za chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana Mheshimiwa Waziri wa Fedha wakati anaongea alisema kwamba anataka kuona namna bora ili kuweza kupunguza bei ya kodi ya sukari. Ameangalia tu element moja ya sukari, lakini nazani suluhisho lingekuwa kuangalia zile tozo mbalimbali zilizoko kwenye mafuta ya magari na kuzipunguza, kwa sababu zaidi ya asilimia 50 ya bei ya mafuta sehemu kubwa ni tozo za Serikali. Kwa hiyo wakaziangalie hizi tozo ili waweze namna ya kuzipunguza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala jingine ambalo tulikuwa tunaliongea kila mara kupitia Waziri wetu wa Viwanda na Bishara lakini Waziri wa Fedha nawe ulifahamu. Kulikuwa na kitu kilikuwa kinaitwa electronic tax stamps (ETS) na chenyewe kilikuwa kinalalamikiwa muda mrefu sana na wafanyabiashara nadhani Kamati yetu ya Viwanda na Bishara kwenye taarifa yake itakuwepo, lakini pia Kamati ya Bajeti na yenyewe taarifa yake itakuwepo. Oneni namna ya kukaa na wafanyabiashara tupate solution ya uhakika kwa sababu ongezeko la shilingi mbili au shilingi tatu kwenye bidhaa yoyote ya kinywaji kwa mfano, soda Coca-Cola itakapoongeza shilingi 30 kwa ajili ya kupitisha hiyo stempu wao hawawezi kuongeza shilingi 30 kwenye kinywaji watakwenda kuongeza kati ya shilingi 50 mpaka shilingi 100, kwa hiyo inaongeza gharama kubwa. (Makofi)

Kwa hiyo, kama tunasema tunataka kuangalia kurekebisha inflation tuangalie vile vitu vidogo vidogo vinavyoongeza gharama kubwa za uzalishaji ili kuweza kuwasaidia wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine kwenye suala la Wizara ya Nishati. Wizara ya Nishati ina mpango wake wa REA ambao kwa Mkoa wa Mtwara sasa hivi kidogo imesuasua na hatufahamu sababu ya msingi ni nini, tutaomba atakapokuja hapa Waziri basi atueleze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nililotaka kusema kubwa ni kwamba Mkoa wa Mtwara na Mkoa wa Lindi ndiko inapozalishwa gesi. Tunashangaa sana watu tunaotokea maeneo haya, gesi ni uchumi wa Kusini kama ambavyo ilikuwa miaka ya huko nyuma na maeneo mengine, lakini kwa kiasi kikubwa mikutano yote inayohusiana na kutaka kufanya mikataba ya LNG, mikataba ya gesi inakwenda kufanyikia eneo la mbali kabisa na maeneo haya. Sasa watu tunaotokea maeneo haya tunanufaika na nini? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatakiwa tuanze kuona tunanufaika tokea mapema. Mikutano inayuhusiana na masuala ya gesi ya LNG pamoja na haya mazao kwa mfano korosho na mengine ifanyike eneo la Mtwara na Lindi ili wafanyabiashara wa kwetu wa maeneo haya waweze kunufaika na mikutano hii. Kwa sababu watu watanunua chakula kwa Mama Lishe, watu watakwenda kulala kwenye lodge hizi zilizopo kwenye maeneo haya ili waanze kuona wananufaika mapema. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa nafasi uliyonipatia, ahsante kwa muda huu. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana na mimi kwa kunipa nafasi kuchangia kwenye hotuba iliyoko mbele yetu na mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Viwanda na Biashara, kwa hiyo, ningependa kushauri Serikali baadhi ya mambo ili tuweze kuona namna ya kuyatatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na jambo la kwanza kabisa, Mheshimiwa Mpakate hapa amechangia vizuri sana kwenye suala la stakabadhi za ghala, lakini yale yote aliyoyasema ili waweze kupata pesa ya kutosha kuna haja ya Sheria ya Stakabadhi za Maghala kuletwa ndani ya Bunge hili ili tuweze kuipitia waongezewe wigo mpana wa kufanya kazi, kwamba maghala yote yasimamiwe na Sheria ya Stakabadhi za Maghala kutoka kwenye bodi ya leseni za maghala. Kwa hiyo, ije sheria, tumuombe Mheshimiwa Waziri hapa ashirikiane na Waziri wa Kilimo na Waziri wa Viwanda na Biashara waone namna ya kuleta sheria sasa maghala yote Tanzania yasimamiwe na Bodi ya Stakabadhi za Ghala. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine liko kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri kwenye ukurasa wa 18; nilikuwa napitia hapa, Mheshimiwa Waziri ameanza vizuri sana anasema; mwenendo wa kupanda bei usipoendana na uhalisia wa soko ni kati ya changamoto zinazokabili sekta yetu ya biashara. Chini ametoa mfano wa bidhaa za kilimo, lakini pia ametoa mfano wa bidhaa za ujenzi; kwa upande wa vifaa vya ujenzi wastani wa bei ya nondo moja ya milimita 12 imepanda kutoka shilingi 20,393 kipindi cha mwezi Machi, 2021 na kufikia shilingi 26,875 mwezi Machi, 2022 maana yake kipindi cha mwaka mmoja kuna ongezeko zaidi ya shilingi 5,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, hiki ndio kinachoongelewa na Wabunge wengi humu ndani na hii ndio maana halisi ya mfumo wa bei na sisi tuko hapa kama Wabunge kuishauri Serikali yetu sikivu ya Chama cha Mapinduzi, lakini pia kutaka kuwasaidia wananchi wote kwamba, tusiambiane hapa kwamba hakuna mfumuko wa bei, mfumuko wa bei upo tena mkubwa na ni real. Lazima sasa sisi kama Wabunge tutafute solution tunatokaje hapa kwenda kudhibiti mfumuko wa bei.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, lakini lazima zifanyike hatua za dharura. Kama Waziri anakiri kuna mfumuko wa bei basi tuweze kujadili hili kwa kina na tutoke hapa na maazimio kwamba, ili kupunguza mfumuko wa bei, kwa sababu kuna upandishaji wa bei kiholela holela kwa wafanyabiashara huko chini pasipo kufuata uhalisia wa soko ama kwenye importation documents zao na hivi vitu vinafanyika makusudi kwa wafanyabiashara wenye tamaa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini utetezi wao mkubwa na Mheshimiwa Waziri hapa anasema kutokana na hili jambo ambalo linaendelea sasahivi, kuna hii vita ya huko Ukraine na maeneo mengine, lakini mambo haya ya kubadilisha- badilisha bei hayajaanza karibuni kwenye nchi yetu. Sasa mimi nataka nishauri kwenye mambo mawili matatu, niishauri Serikali na ione.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesimama hapa leo kama mara ya nne au ya tano ninaongelea suala la ETS kwa sababu tumesema tunatafuta namna ya kuondoa mfumuko wa bei. Ndugu zangu nataka nitoe mfano, ETS ni stamps za kielektroniki zinazotumika na kampuni nyingi, hasa hizi zinazozalisha vinywaji, lakini nimesikia kwamba inawezekana wakaingia mpaka kwenye sukari.

Mheshimiwa Naibu Spika, stamp moja uchapishaji ambayo ni kampuni moja tu pekee sasahivi inaitwa SISPA, anachapisha stamp moja kwa shilingi nane mpaka shilingi kumi; na wale watu wenye viwanda vyao wanapokwenda kulipia zile stamps maana yake watalipa stamps kutokana na bidhaa walizozalisha. Na siku moja nilitoa mfano hata ndani ya Bunge, hata kwenye Kamati kwamba Serikali wanapata kiasi gani kutokana na hizi stamps zinazochapishwa na SISPA?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kushangaza kabisa kwamba Serikali haijataka kujifunza zaidi kwenye hili jambo. Sijaona hatua za waziwazi zilizochukuliwa ili kuweza kuwapunguzia wananchi mzigo wa uzalishaji kwa sababu gharama zote za uzalishaji zinazofanywa na kampuni, kwa mfano kampuni za vinywaji katika kila chupa moja inaweza ikaongezeka kati ya shilingi 10 mpaka shilingi 15 tuseme, lakini mwisho wa siku gharama hizi zinakwenda kwa mlaji wa chini kabisa. Hiyo ni moja ya vitu vinavyoongeza inflation kwenye uzalishaji. (Makofi)

Kwa hiyo, niiombe sana Serikali kabisa na ninafahamu kwamba mkataba mpya wameingia kati ya SISPA na TRA, mkataba ambao haukuwa wazi kwa wawekezaji wengine ambao wangeweza kuzalisha stamps hizi kwa gharama nafuu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaficha nini kwenye jambo hili? Kwa nini hatutaki kuwaondolea wananchi mzigo huu wa kulipia stamps za kielektroniki, jambo ambalo linaweza likafanywa kwa bei rahisi? Kuna wazalishaji wako tayari kuzalisha stamps hizi kwa shilingi mbili, sisi kama Serikali, sisi kama nchi tunang’ang’ania stamp za shilingi kumi kwa nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na katika shilingi kumi hii Serikali inapata 18% tu pesa nyingine yote inayobakia inakwenda kwa yule mtu anayezalisha stamps na kuwauzia watu wenye viwanda. Tuliangalie hili kwa makini na niwaombe sana Wabunge wenzangu tulijadili hili jambo kwa umakini kwa sababu linawaumiza wananchi na sisi tuko hapa tunatafuta namna bora ya kupunguza inflation kwenye bidhaa mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za uzalishaji wa stamps ni kubwa, wenye viwanda wanalalamika, kila siku wanakuja Bungeni mpaka sasa, mwisho wanatuona sisi Wabunge hatuwezi kuwasaidia kwa sababu, hatujatafuta solution, hatujakaa nao, hatujawasikiliza nab ado tunalazimisha mikataba hii izalishwe na wale watu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kuna jambo lingine lipo kwenye vinasaba vya mafuta. TBS sasahivi wanalipa karibu shilingi 16 kwa lita moja, wanalipa kwa SISPA haohao ambao wanazalisha na hizi stamps za kielektroniki. Tunasema tunataka kupunguza gharama, kwa nini tusiangalie tukatafuta vinasaba vya gharama nafuu zaidi vinavyofanya kazi sawasawa na hivi vinavyoletwa na hizi kampuni, ili kupunguza gharama za uingizaji wa mafuta?(Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na malengo ya vinasaba ilikuwa ni kupunguza uchakachuaji. Sasa kama tunataka kupunguza uchakachuaji, tumefanikiwa kwa kiasi gani kwa wakati wote ulipita? Utafiti uko wapi unaoonesha kwamba, kuweka vinasaba kwenye mafuta kumepunguza huu uchakachuaji unaosemwa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatujawahi kuletewa hapa Bungeni sisi tukafanya review. Sana sana tumewaongezea mzigo sasahivi TBS, TBS wanalazimika kulipa kwa SISPA, EWURA nao wamalazimika kulipa kwa SISPA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine kwenye suala la Mtwara Corridor, Bandari ya Mtwara pamoja na Mchuchuma na Liganga. Hivi ni lini Serikali itaamua kwa dhati kabisa kufanya uzalishaji wa makaa ya mawe, lakini pia kufanya uzalishaji wa chuma? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunahangaika hapa kwenye suala la bei ya mafuta. Kwa mfano gesi yetu, sasa hivi ni zaidi ya miaka 20 au miaka 30 tuseme tunaongea kuhusu Mchuchuma, tunaongea kuhusu Liganga, tunaongea kuhusu gesi ya Mtwara. Kama tungekuwa tumeanza kutumia gesi tusingehangaika leo na suala la bei ya mafuta, wako wapi watu wenye kufanya maamuzi? Kwa nini gesi ile ambayo tunajua kabisa iko pale na inatakiwa itumike na wananchi haitumiki? (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia mchana huu na kwa namna ya pekee sana nipongeze Wizara ya Kilimo kwa mitazamo yao chanya, pia nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kukubali kuwasaidia sana Wizara ya Kilimo kwa sababu nimeona hizi siku chache zilizopita Wizara ya Kilimo wamekuwa wakipata fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa BBT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe ushauri kwenye mradi huu wa BBT Mheshimiwa Waziri hakikisha Wizara yako inaungana na Wizara ya Viwanda na Biashara ili kuweza kuona mnyororo mzima wa thamani na kazi zinazofanywa na vijana kwenye hili suala la BBT linaingia sasa masokoni kwa maana ya kuwashirikisha TANTRADE lakini pia na kuwashirikisha watu wa Warehouse Receipts ili kuweza kupata matokeo mazuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ndani ya Bunge hili imetolewa michango mingi sana inayohusiana na kuongeza thamani ya vitu mbalimbali ikiwemo mazao na mwenyewe umekiri kwamba una mikakati ya kutaka kuongeza thamani ya mazao ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wazalishaji wa korosho kwa maana ya wenye viwanda vidogo na viwanda vikubwa na umeomba shilingi zaidi ya bilioni 10 ili kuweza kuwasaidia hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikukumbushe kwa dhati kabisa kama utakumbuka wakati wa kikao chetu cha wadau wa korosho kuna mwenye kiwanda mmoja anayo experience ya kutosha tu alikuwa anatokea Mtwara, Ndugu Mkimi alikuwa na malalamiko yake mengi sana, sasa sina hakika baada ya maelekezo yako kama kuna chochote kimefanyika mpaka sasa hivi. Kwa hiyo, niombe ufuatilie hili ili uweze kuona maelekezo unayoyatoa yanatekelezwa kuweza kuwasaidia watu hawa wenye viwanda tusiwakatishe tamaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri upo hapo lakini nataka ufahamu kwamba wakulima wa nchi hii walikuwa wamekata tamaa kabisa na wengi walikuwa wanataka kuacha shughuli za kilimo lakini baada ya kuja wewe sasa unaonekana kama mkombozi na tunataka tukuongezee machache ili uweze kufanya vizuri zaidi kazi yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwenye Wizara uliyoko ndiko ambako kinafanyika kilimo cha korosho na kilimo cha kahawa na lazima utambue kwamba kuna watoa huduma kwa maana ya wanaopeleka magunia, wanaopeleka viuatilifu pamoja na dawa. Toka mwaka 2017 kuna ambao wanadai nao wanadaiwa na mabenki na wengine wanafilisiwa na mabenki haya kwa sababu mikataba yao ilikuwa ni kwamba watalipa immediately baada ya ku-supply Serikalini. Sasa na wewe wasitake kukuingiza kwenye kichaka hiki cha neno la uhakiki kila mara wanapokwenda kudai madeni yao wanaambiwa uhakiki unafanyika, ama uhakiki haujafanyika lakini ni kama tu utaratibu fulani wa kutaka kuchelewesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ndani ya Bunge lako hili Tukufu palipita azimio hapa baada ya kuletwa Taarifa ya PAC kwamba watoa zabuni hasa wa ndani pamoja na wa nje walipwe fedha zao ili waweze kuhudumia vizuri zaidi wakulima. Kwa hiyo, tukuombe na Mheshimiwa wakati unapokuja hapa ku-windup na hili ndiyo eneo la kuweza kukushikia hata shilingi yako kwa sababu ni jambo la kisera. Hakikisha unatueleza mkakati wako wa kuwalipa wazabuni ili waweze kuwahudumia zaidi wakulima na tuweze kupata tija kwenye kilimo chetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili Mheshimiwa Waziri ni suala la vinywaji. Tunapozalisha korosho asilimia zaidi ya 30 ama 40 ya korosho panapatikana matunda yanaitwa mabibo, yakikaushwa haya yanaitwa kochoko, ukiyapika, kabla haujayapika unapata kinywaji fulani kinaitwa uraka hata uki-google hapo utaona inaitwa urak kwa sababu imeanzia huko kwa wazungu na maeneo ya India imekuja mpaka huku kwetu, kinanywewa, hii inaitwa pombe halali. Ukikausha, ukaloweka, ukachemsha ukapata mvuke inapatikana pombe ya moshi ndiyo hii inayoitwa gongo, lakini Wizara yako wewe mwenyewe na Wizara ya Viwanda na Biashara walipeleka fedha za utafiti Chuo cha Naliendele ili kuweza kuona kama kutokana na gongo hii kinaweza kikafanyika kitu kizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, walikuja kugundua gongo inayopatikana kwenye mabibo inatoa ethanol, inatoa methanol, unapata pale ndani alcohol, unapata chakula cha mifugo lakini pamoja na juice ya mabibo ambayo inaitwa cashew apple. Sasa Serikali imeshawekeza, utafiti umekamilika, kilichobakia sasa ni kufanya implementation. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapoeleza kuhusu mnyororo wa thamani wa zao la korosho pamoja na mambo ya imani na mengine lakini hii ni bishara na ni ajira na nataka nije kusikia unasema nini kuhusu gongo inayopatikana Mikoa ya Mtwara na Lindi na maeneo mengine, ninakumbuka hapa Mheshimiwa Sichalwe juzi wakati anachangia alileta hapa vinywaji vingi sana vinavyozalishwa nje ya nchi lakini vinaletwa Tanzania. Kwa hiyo, tuone sasa Wizara yako ina mkakati gani wa kusaidia kufanya saving kwenye hili jambo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine wakulima wa korosho wametuagiza na mimi wameniagiza nije kwako niseme makato yanayokatwa kwenye zao la korosho ni makubwa sana. Tunaomba kufanya review kwenye zao hili ili kuweza kupata bei bora. Kadri ya makato yanavyokuwa mengi, yawe ya mkulima au yawe ya mnunuzi kwa vyovyote vile mwisho wa siku haya yote yanakwenda kuwekwa kwa mkulima. Hatuwezi kupata bei bora kama haya tunayaacha kama yalivyo. Kwa hiyo tuone namna ambavyo utakuja kuleta hapa hiyo taarifa yako tuweze kukusaidia kuchambua na kupunguza baadhi ya tozo zilizopo kwa mkulima na tozo zingine ambazo ziko kwa mnunuzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunataka tuiombe Serikali kwa sababu ya muda sasa tuishauri kwamba makato kwa ujumla ni shilingi 1,130. Sasa mlete hapa taarifa na mtuchambulie tuone namna ya kuwasaidia lipi liondoke, lipi libaki. Ukienda kwenye kahawa wanakata kama shilingi 200 lakini hiyo ndiyo italipa TARI, italipa kule Bodi yao ya Kahawa, italipa zile union zao, italipa AMCOS, italipa na mambo mengine isipokuwa CESS na hayo yanayobakia. Kwa hiyo, tukuombe Mheshimiwa Waziri ulete hapa tukusaidie kuchambua ili tuweze kuona tozo hizi zinazofanana ziondolewe kwa sababu zimekuwa zinawaumiza sasa wakulima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine tunaomba na tulikuambia wakati wa kikao cha wadau, hebu muombe CAG akatusaidie kukagua Mfuko wa Ununuzi wa Pamoja wa Pembejeo. Wakulima tunaotokea kwenye eneo hilo haturidhiki na namna manunuzi yalivyofanyika kwenye miaka iliyopita hasa zaidi 2019/2020, 2020/2021, 2021/2022 na ndiyo maana unapata ugumu wewe mwenyewe binafsi kuwalipa suppliers walio supply magunia lakini pia pamoja na walio- supply pembejeo kwa sababu ukamilifu wake haukuwa mzuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine Serikali ifute ushuru huu wa shilingi 81 ambao unatozwa kwenye magunia, kwa sababu yale ni vifungashio. Tuwape uhuru wanunuzi wa kuamua watasafirisha mizigo yao kwa kutumia kifungashio cha aina gani. Kuna ambao wanasafirisha kwenye makontena lakini bado utawachaji fedha ya gunia. Kuna ambao wanasafirisha kwa kumwaga kwenye meli kwa maana ya zile bulk supplier lakini bado utaendelea kuwachaji kwenye magunia na hizi gharama zote mwisho wa siku zinarudi kwa wakulima. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Mfuko wa Ununuzi wa Pembejeo wa Pamoja, achia hii kazi ikafanywe na CBT kwa sababu kuna fedha ya Serikali na niombe sasa upeleke kwenda kukagua.

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana pamoja na muda mfupi, lakini naamini mawazo yangu Mheshimiwa Waziri ameyasikia, hata hivyo nimechangia kwa maandishi kwa sababu muda ni mfupi na mambo ya kuishauri Wizara hii tunayo mengi sana. Nikutakie kila la kheri wakati unahitimisha. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, kutokana na suala la muda nalazimika pia kuchangia kwa maandishi na mchango wangu utajikita kwenye zao la korosho pekee kutokana na anguko lililotokea msimu uliopita.

Mheshimiwa Spika, ili kuhami zao la korosho linaloyumba kila mwaka nashauri yafuatayo; kwanza Serikali ikubali kupunguza makato kwa mnunuzi na mkulima (kwa rejea ya msimu uliopita ni wastani wa shilingi 1,130 kwa kilo) ili kuhami bei ya soko.

Pili, Serikali ifute ushuru wa shilingi 110 inayoitwa ya maendeleo ya korosho huku ukweli ukiwa ni fedha za kulipia pembejeo kwani tayari Serikali ile ile iliwatangazia Watanzania kupitia Bunge na sheria ikapitishwa ya kurejesha fedha za export levy asilimia 50 kwa wakulima.

Tatu, Serikali ifute ushuru wa shilingi 81 ya magunia na ieleze ziliko fedha za magunia za misimu ya mwaka 2019/2020, 2020/2021, 2021/2022 ambazo wasambazaji wa magunia ya mwaka 2017 hawajalipwa hadi leo na deni linazidi kuwa kubwa.

Mheshimiwa Spika, nne, Serikali ifute ongezeko la ushuru wa shilingi 20 kwa watunza maghala na kufanya kuwa shilingi 52 hadi itueleze wakulima sababu za msingi za ongezeko hili kubwa la ushuru.

Mheshimiwa Spika, tano, Serikali ipeleke haraka muswada wa sheria kupunguza makato ya export levy kutoka asilimia 15 ya FOB hadi asilimia tisa (single digit) kuhami bei ya soko na Bodi ya Korosho iharakishe mchakato wa kuandaa mapendekezo kwenye kikao kijacho cha wadau kutazama kama bado haya makato yana tija kwa wakulima na ikibainika hayana tija, yafutwe.

Mheshimiwa Spika, sita, Serikali ianzishe mfumo maalum wa ruzuku ya kufidia soko la korosho (subsidies) ili ikitokea soko limeyumba, Serikali iwe na uhakika wa kumuokoa mkulima. Tunaweza kutenga sehemu ya mapato ya export levy kwa ajili hii.

Mheshimiwa Spika, saba ni muda muafaka wa kuanza kutazama upya muundo wa vikao vya wadau wa zao la korosho ambao ndio hupitisha makato kwa wakulima.

Mheshimiwa Spika, mchakato wa kupata wawakilishi kwenye kikao cha wadau upoje na wawakilishi wa wakulima ni asilimia ngapi ya wajumbe wote?

Mheshimiwa Spika, kuhusu pembejeo na kushuka kwa uzalishaji wa korosho; zao la korosho linashuka uzalishaji mwaka hadi mwaka toka tani laki tatu mwaka 2017/2018 hadi tani laki mbili mwaka 2021/2022.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kushuka huku kwa uzalishaji ambako pia kwa mwaka huu makusanyo halisi ni tani laki 1.7; moja ya sababu ya kushuka huku kunatokana pamoja na mambo mengine kama utaratibu usiofaa wa pembejeo, pembejeo zisizozingatia hali ya hewa ya eneo, usambazaji wa pembejeo fake.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwanza utaratibu wa awali wa mkulima kuchangia pembejeo anayoitaka, kwa kiasi anachokitaka urejeshwe huku Serikali ikifidia bei ya ziada kupitia export levy. Hii itasaidia sana mkulima kupata pembejeo aitakayo kutokana na hali ya hewa.

Mheshimiwa Spika, pili, Kamati ya Pamoja ya Ununuzi wa Pembejeo chini ya MAMCU ivunjwe, tuendelee na utaratibu wa zamani kwani kamati hii imetumia fursa hii kujineemesha huku ikiingia mikataba na wazabuni wasio na uwezo, wenye pembejeo fake na pembejeo ambazo hazijawahi kutumika kwenye korosho na zinazoshusha uzalishaji. Kasi ya pembejeo mpya kujaa sokoni ni kiashiria kimojawapo.

Tatu, export levy isitumike kuchangia pembejeo na tuifute shilingi 110 ya maendeeo ya korosho kama tulivyoshauri hapo juu.

Mheshimiwa Spika, nne, Serikali itoke hadharani iseme hatua alizochukuliwa msambazaji wa pembejeo fake zilizokamatwa Masasi, Nachingwea, Tandahimba na Newala ambaye alijinasibu kushirikiana na vigogo wa Serikali huku akikimbizwa China kupisha joto la mijadala na aliporejea hakuna hatua alizochukuliwa.

Mheshimiwa Spika, tano, Serikali ieleze ziliko pembejeo fake ambazo kila mwaka zimekuwa zikikamatwa kila msimu wa korosho unapofika.

Mheshimiwa Spika, mwisho ila sio kwa umuhimu, ni vyema Serikali itoe athari za makisio ya pembejeo vs uzalishaji iliyotolewa na Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho ya tani laki nne na tukaagiza pembejeo kulingana na makisio hayo. Hii bakaa ya tani laki 230 ambayo Serikali inalipa bila mshirika (mnunuzi) tunatoa wapi.

Mheshimiwa Spika, kwa msimu wa mwaka huu wa 2022/2023 indirect charges kwenye kila kilo moja ya korosho ambazo zimeathiri bei ya soko zipo kama ifuatavyo; hizi analipa mnunuzi (mkulima in fact); makato ya maendeleo ya zao la korosho (pembejeo) shilingi 110; ushuru wa watunza maghala shilingi 52; deni la magunia shilingi 81; usafirishaji shilingi 120; export levy ambayo ni sawa na asilimia 15 ya FOB shilingi 380; ICD shilingi 120; Ushuru wa Bandari shilingi 100; vibali shilingi 10; offload shilingi 10; provisional income tax shilingi 70; forwarding charges shilingi 10; na other charges shilingi 50.

Mheshimiwa Spika, kwa vyovyote vile gharama hizi mwisho wake zinarudi kwa wakulima, hivyo nashauri tufanye marejeo ili kuwaongezea morale wakulima na wanunuzi pamoja na kupata mbegu bora. Ahsante kwa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, na mimi nishukuru kwa kupata nafasi hii jioni ya leo. Nikupongeze wewe binafsi kama ambavyo Wabunge wenzangu wamekupongeza, lakini pia nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anazozifanya pamoja na kusimamia Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Nimpongeze pia Mheshimiwa Waziri, Naibu wake, Katibu Mkuu Wizara hii na Katibu Mkuu aliyeondoka, lakini na watendaji wote wa Wizara ya Maji wakiwemo injinia wetu wa mkoa pamoja na injinia wa Wilaya Ndugu Juma. (Makofi).

Mheshimiwa Spika, ukiangalia tone ya Waheshimiwa Wabunge, mimi nimepata nafasi ya kuchangia mwishoni kabisa, tunaelekea mwisho sasa. Ukiangalia tone ya Waheshimiwa Wabunge wote humu ndani sioni kama kuna mashaka kwa Mheshimiwa Waziri kupitishiwa Bajeti yake, tena naamini kwa kishindo kikubwa sana. Kwa sababu ukiangalia tone ya leo na miaka mitatu, minne, mitano iliyopita nyuma Waheshimiwa Wabunge wengi sana wameridhika, na nimeona kila mkoa kuna mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa, ikiwemo pamoja na Mkoa wetu wa Mtwara.

Mheshimiwa Spika, Mzee Mkuchika angepata nafasi ya kusema hapa Bungeni kama wangekuwa wanatoa ruhusa mawaziri kuchangia nafikiri angedondosha machozi kwa furaha. Kwa sababu katika kipindi chake chote cha uongozi alipokuwa anafanya mikutano Newala, huyu Mzee wetu sikumbuki vizuri lakini walikuwa wanamuita kwa kimakonde Nangudyamedi kitu kama hicho, yaani wakiwa na maana kwamba wakati wa mkutano wananchi wasilmuulize swali linalohusiana na mambo ya maji kwa sababu hataweza kulijibu sababu Newala ilikuwa haipatikani maji kabisa. Ndiyo maana Mheshimiwa Hokororo jana hapa alisema kuwa Newala ndiko ambako wananchi walikuwa wanapika chakula kwa kutumia maji ya matiki maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa mradi huu mkubwa unaokwenda kutekelezwa sasa hivi wa Makonde utakaohudumia Wilaya zile nne, ninaamini ni ukombozi mkubwa sana kwa sisi watu wa Mtwara.

Mheshimiwa Spika, nimuombe pia Mheshimiwa Waziri, kwamba mradi huu wa Makonde ni mkubwa sana, utekelezwe kwa wakati, fedha ziende kwa wakati lakini tuangalie na mipango ya muda mrefu. Pamoja na sisi watu wa Ndanda na Masasi, Ruangwa, Nachingwea na wengine wote waliosema, tunajivunia maji ya Mbwinji lakini mradi wa Makonde ungeweza kuleta pia maji maeneo haya, kwa sababu Mto Ruvuma maji yake yamekuwa ya kuhama hama. Pamoja na kwamba mradi unakwenda kutekelezwa lakini chanzo cha maji cha Makonde ni cha uhakika zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna miradi inayotekelezwa Jimbo la Ndanda; kuna mradi wa Chija Chiwata, Chija Mbemba, Ndanda hadi Nangoo, Mradi wa Nanganga Momburu, mradi wa Nambawala ambako mafundi wako wanachimba mitaro sasa hivi, pamoja na mradi wa Namalembo. Niombe sana pesa ziende sasa kwa wakati, kwa maana ya kwamba uangalie cash flow miradi hii itekelezwe ili wananchi waweze kupata maji. Lakini pia tuna maombi. Kuna visima ambavyo vilishachimbwa tayari kwenye vijiji vya Mpanyani, Chilolo, Masiku, Namichi Pamoja Sululu ya leo. Mruhusu Meneja wa Mkoa na Meneja wa Wilaya waweke pale solar pans ili wananchi waweze kuanza kupata maji wakati michakato hiyo ya kutaka miradi hii iwe mikubwa ya kuhudumia eneo kubwa iweze kukamilika.

Mheshimiwa Spika, tuna mradi pia wa Mwena Lihoya, umekuwa unasua sua, lakini tunaziona hatua za kuboresha mradi huu. Mheshimiwa naomba ukafanye marejeo kwenye mradi ule, ili wapelekewe fedha mradi huu ukamilike ili uweze kutoa maji ya uhakika kwenye eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, kuna miradi inayoendelea Jimbo la Tandahimba na Mheshimiwa Katani hujamuona unakumbuka, nafikiri unaamini tone yake ile ya mwaka jana lakini anasema anajipanga kwenye Wizara ya Miundombinu kwa sababu ya barabara zetu kule, mpaka sasa hatuna jibu la uhakika. Wizara ya maji ameamua apumzike kwanza kwa sababu miradi ya maji jimboni kwake inaenda vizuri sana. Vilevile tunangalie cash flow tuweze kuwapelekea maji watu hawa na fedha kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na mazuri yote unayoyafanya, mimi binafsi niombe tumsaidie Meneja wetu wa Wilaya kutekeleza majukumu yake vizuri Eng. Juma kwa kumpatia gari litakalofaa. Tunapokwenda kufanya ziara kwenye Wilaya ya Masasi yenye miradi mikubwa zaidi ya kumi, yenye zaidi ya fedha bilioni 15 ndugu yetu huyu kuna wakati anafika kwenye ziara akiwa kwenye pikipiki kwa sababu gari lake ni bovu, halitengenezeki na liko beyond repair. Tunaomba apatiwe gari jingine ili aweze kusimamia majukumu yake sawasawa na tufanye nae ziara kwa uhakika.

Mheshimiwa Spika, nakumbuka siku moja nimeenda kwenye mkutano wa hadhara na kulikuwa kuna masuala yanayohusiana na masuala yanayohusiana na mambo ya maji Chibya. Tuko katikati ya mkutano namuona Injinia wangu anakuja na pikipiki, bodaboda. maana gari lake imeharibika kwenye milima huko chini, ameshindwa kufika kwenye mkutano kwa wakati, kwa hiyo nikuombe umsaidie.

Mheshimiwa Spika, bado tuna mahitaji makubwa sana ya visima, unafahamu jiografia ya Jimbo la Ndanda kuna eneo la upande wa Magharibi wa jimbo kunashida sana ya maji. Pamoja na mafanikio mazuri hivyo visima alivyovitaja vipo maeneo hayo lakini bado tuna mahitaji ya visima kwenye Vijiji vya Migombani, Pangani, Pachani, Miwale Namatutwe, Natepo, Mihima, Makulani ya Leo pamoja na Chimbo. Niombe sana kwenye Bajeti hii ijayo, tuone watu hawa wanakwenda kupata maji, na kwa kutekeleza miradi hiyo kwa kuchimba visima virefu kwenye maeneo haya, tafsiri yake itakuwa tumemaliza kabisa tatizo la maji kwenye ukanda wa Magharibi wa Jimbo la Ndanda.

Mheshimiwa Spika, na Mheshimiwa Waziri ni msikivu sana. Mara nyingi sisi kama Wabunge wa Mtwara tukwenda kwake tukiwa tuna malalamiko, lakini nadhani safri hii mpaka tunakuja hapa ndani hatuna tena malalamiko yale na wala hatujakaa kikao maalumu na yeye ili aweze kutusaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunachoomba sasa miradi hii ikatekelezwe kwa wakati. Kama unavyofahamu, mwakani kuna uchaguzi mkuu, maeneo haya yamepata shida kwa kipindi kurefu sana, tangu wakati wa uhuru. Newala hawajawahi kuwa na maji ya kutosha, Nanyamba hawajawahi kuwa na maji ya kutosha na Tandahimba hawajawahi kuwa na maji ya kutosha. Ndiyo maana maeneo haya kulikuwa kuna dominance kidogo ya watu wa opposition. Tunakwenda kwenye uchaguzi wa ndani, kwa maana ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, lakini pia tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu. Tunaomba miradi hii ikamilike kwa wakati ili wananchi wapate maji wasije wakatulaumu, tusije tukapoteza maeneo yetu kwa sababu ya kiu kuu inayotamalaki katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nilisema tangu mwanzo, nimesimama hapa, na Waheshimiwa Wabunge wengi wameongea kwa kipindi kirefu wakimpongeza Mheshimiwa Waziri. Nimsisitize tu, kwamba akamilishe miradi hii ili tukae hapa ndani kwa amani kiabisa. Ninaamini mpaka tutakaporudi kwenye bajeti ijayo Mungu akimjalia kuwa hai na sisi kuwa hai basi mambo yatakuwa mazuri. Miradi itakuwa imetekelezwa kwenye Jimbo letu na Ilani ya chama chetu chama tukufu, Chama cha Mapinduzi tutasimama kifua mbele tukikitetea kwa sababu tayari tutakuwa tumepunguza baadhi ya kero kwenye maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo na mimi niungane na wabunge wote waliopita kuunga mkono bajeti hii kwa asilimia 100. Ahsante sana kwa kunisikiliza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa na mimi nafasi ya kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana Wizara ya Kilimo na kama tunavyofahamu kilimo ndiyo uti wa mgongo wa Taifa letu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kazi kubwa sana inayofanywa na Mheshimiwa Bashe na Msaidizi wake Mheshimiwa Mavunde na Wizara yote kwa ujumla na imekuwa yenye tija kubwa kwa wakulima. Nitakuwa na mchango wangu wa maandishi ambao tayari nimeshautuma ukihusu suala la Bodi ya Zabuni inayosimamia masuala ya pembejeo pamoja na magunia, madeni ya wazabuni mbalimbali kwenye Bodi yetu ya Korosho kwa maana ya CBT. Pia nimeleta mchango wangu wa maandishi kuhusu udhaifu wa Menejimenti ya CBT na malalamiko ya watumishi pamoja na viambatisho vyake, nimeleta pia mchango wangu kwa maandishi kuhusu madeni ya Wazabuni mbalimbali hasa madeni ya bond. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pembejeo, tunashukuru maazimio yaliyofanywa na Serikali kuhusu suala la pembejeo lakini ninamuomba sana Mheshimiwa Bashe kwamba mara nyingi pembejeo hizi zinaletwa bure huwa hazitoshelezi kwenye soko lote. Hapo nyumba tulikua na utaratibu wa ruzuku, sasa uone namna ya kusaidia kwa sababu pembejeo zinakwenda chache hazifiki mara nyingi kwa wakati lakini wakulima bado wanalazimika kwenda kununua kwenye maduka ya kawaida ya kibiashara. Sasa wanapofika kwenda kununua ili waweze kuongeza pembejeo ile iliyotolewa na Serikali bure wanakuta pembejeo hiyo ikiwa na gharama kubwa sana. Kwa mfano, mfuko wa sulphur unaweza kufika shilingi 50,000 au shilingi 80,000 ili waweze kujitosheleza. Kwa hiyo, ninakuomba tuangalie sasa na ule utaratibu wa ruzuku. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hilo, jingine ni kuongezee kwamba wakati huu Serikali imeweze kulipia hizi pembejeo zinazoitwa za bure kutokana na fedha ambayo ilikuwa ni ya export levy iliyokuwa inachangiwa na wakulima hapo nyuma, jambo hili halipo kisheria na Mheshimiwa Waziri umelifanya labda kwa sababu mahusiano yako mazuri na Mheshimiwa Waziri wa Fedha, sasa ninaomba wakati wa Finance Bill muilete hiyo, muibadilishe ili fedha hii ya export levy itamkwe kabisa kwamba inakwenda kulipia pembejeo na wakulima wa korosho na wengine wapate pembejeo hizo za bure tunazoziita lakini kwa kutumia fedha hiyo na iwe kabisa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni usambazaji. Mwaka jana tulishuhudia upungufu kidogo kwenye usambazaji hasa zaidi kwenye upande wa magunia, sasa Waziri utakapokuwa unahitimisha pia utueleze Kama umejipanga kiasi gani mwaka huu kuhakikisha hakuna uhaba wa magunia kwenye zao la Korosho kwa sababu ilisumbua sana kwenye misimu iliyopita, kwa hiyo tunaamini wewe pamoja na Wizara yako umejipanga vizuri kwenye hili sambamba na masuala ya Sulphur ili wakulima waweze kupata Sulphur inayojitosheleza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Mheshimiwa Waziri ninakuomba hakikisha sasa unasimamia vizuri ili magunia yaeleweke pamoja na hizi Sulphur mchakato wa usajili wa wakulima, zoezi hili lilianza lakini mpaka sasa hivi halijakamilika na ni muda mrefu sana. Nikukumbushe pia kwa sababu ya muda suala la Bodi. Bodi yetu ni mpya lakini huduma inayotolewa na Bodi….

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Spika, taarifa!

MWENYEKITI: Taarifa Mheshimiwa Cecil Mwambe naomba usubiri; Mheshimiwa Katani.

T A A R I F A

MHE. KATANI A. KATANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimpe taarifa mzungumzaji kuwa Mheshimiwa Waziri tena kwake kule kwenye Tumbaku ameweka mfumo sahihi wa wakulima na hakuna dhuluma ya kwenye pembejeo. Sasa taarifa yangu anapo windup ahakikishe kile alichokifanya kwenye Tumbaku kinakwenda kwenye korosho ili aweze kubaini wakulima sahihi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Cecil Mwambe, unapokea hiyo taarifa?

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea taarifa ya Mheshimiwa Katani na mimi nimuongezee Mheshimiwa Waziri kwamba hata kwenye masuala ya viwanda, tulikuwa tuna viwanda vya korosho Masasi, Lindi, Mtama, Nachingwea pamoja na Newala lakini sasa tunaona Mheshimiwa Waziri anatumia juhudi kubwa sana kufufua Kiwanda cha Tumbaku kilichopo Morogoro cha TLTC labda kwa sababu pia nacho kama anavyoniambia Ndugu Katani kwamba ni mdau wa tumbaku na anatoka Tabora anataka kuwapendelea zaidi watu wa Tabora na sisi watu wa Mtwara kutuacha nyuma kidogo. Kwa hiyo, nimuombe kabisa, mikakati ile iliyofanyika kwenye Tumbaku na mazao mengine ailete sasa kwenye korosho ili tuweze kwenda nae sambamba, tuweze kumshukuru kwa kazi nzuri anazozifanya, tuendelee na tunaamini kwamba haya yote atayafanya katika mwaka huu wa fedha ili tusiwe na malalamiko Wabunge tunaotokea kwenye maeneo yanayozalisha korosho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na hilo waangalie na masuala ya bei. Kuwe na timu ya uhakika kwenye Bodi yetu ya Korosho inayoweza kupata bei za uhakika ili hata wanunuzi wanapokuja kununua kuwe kunafanana kidogo na bei zilizopo kwenye soko la dunia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia mwaka 2021 bei zikidondoka, tunaambiwa matatizo yalikuwa ni UVIKO na mengine. Tunaamini kwa sababu UVIKO sasa umekwisha, bei zitakuwa bora. Miaka miwili mitatu iliyopita korosho iliuzwa mpaka Shilingi 4,000/= lakini mwaka 2021, hapo kati kati tumeshuhudia korosho inauzwa kwa Shilingi 1,500/= mpaka Shilingi 2,000/= kwa wastani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine namwomba Mheshimiwa kuhakikisha tunarasimisha ule utaratibu wa upili. Hata kwenye Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi lipo hili suala. Upili ni Soko la Umoja kwa maana ya ile Primary Market. Hili ni lile soko ambalo linawasaidia wananchi kuweza kutatua matatizo yao kwa mara moja. Huwa linatumika jina la Kangomba, lakini siyo neno jema kwa watu wengine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachotaka sisi ni kwamba mwananchi ambaye ana korosho debe moja ndani ya nyumba yake, baba yake anaumwa, anatakiwa kumpeleka hospitalini, maghala hayajafunguliwa, atazipeleka wapi korosho zake akazibadilishe ziwe fedha aweze kupata huduma? Kwa sababu hawezi kupeleka debe la korosho hospitalini akapata huduma. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mengine nitachangia kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 3) wa Mwaka 2018
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia hoja iliyopo mbele yetu. Niende moja kwa moja kwenye kitabu cha hotuba ya Kamati, Sehemu ya Tano, kipengele cha 3.1.5.

Mheshimiwa Spika, pamoja na uamuzi wa Serikali wa kuondoa hii Sehemu ya Tano kwenye Muswada wao waliouleta hapa mbele, lakini kule ndani kunaonesha kabisa hakukuwa kuna nia njema. Kwa sababu ukiangalia pale ndani, ndiyo maana wachangiaji wengi waliopita wanasema mhimili wako unapokwa madaraka yake. Kabla Serikali haijaleta huu Muswada au wakati inafanya maandalizi ya kuleta huu Muswada mbele yako, tayari wao walikuwa wameshaanza kufanya manunuzi mbalimbali, pamoja na kuamua kutumia hili jina la mobile court. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye kitabu cha hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani, kule ndani utakuta kuna sehemu tumesema, tumefanya utafiti na maeneo yameonekana na kuna ushahidi wa kutosha, kuna magari yanazunguka mitaani yameandikwa mobile court. Sasa tunajiuliza kwamba ni namna gani Attorney General au Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliamua kuanzisha kitengo ambacho wanakuja kukiombea ruhusa ndani ya Bunge lako Tukufu? Hii siyo haki. Ndiyo maana hata tunakuja kuambiwa kwamba mpaka magari yatakayotumika kwa ajili ya kuendeshea hizi Mahakama yalishanunuliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tulikuwa na semina hapa na watu wa TAKUKURU. Wakati Mheshimiwa Rais anachukua nchi, wakati ule anatuhutubia sisi, alisema kati ya mambo atakayopingana nayo makubwa sana ni pamoja na masuala ya rushwa. Ni wazi kabisa kwa kutumia macho ya kawaida, utakuta huu Muswada au utakuta haya marekebisho yanayoletwa hapo walitaka sisi tuwe kama rubber stamp ya kuthibitisha uhalifu mkubwa uliofanyika katika maeneo haya. Nakuomba ikiwezekana pamoja na kwamba Serikali wamaeamua kuondoa jambo hili, hebu tengeneza Tume ndogo ikafuatilie mkataba huu ulioingiwa kati ya Benki ya Dunia na kutusaidia hayo magari, ulikuwa na manufaa gani kwa Watanzania? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya magari yanayotajwa yenye thamani kubwa sana, hayawezi kuingia maeneo mengi ya majimbo yetu kutokana na shida kubwa ya miundombinu iliyoko huko. Kwa mfano, hilo gari wanalosema ni mobile court, linatakiwa likafanye kazi kwenye Jimbo la Ndanda, Kijiji cha Namalembo ambapo hakuna barabara na maeneo mengi ni mabovu, hakuna madaraja, gari ni ndefu zaidi ya mita 35 litafikaje kule chini kabisa maporini? Kwa hiyo, haukufanyika utafiti wa kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiingia hapa kwenye hiki kitabu cha hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati, ni wazi kule ndani anasema kwamba, tungeamua kutumia busara au Mahakama ingeamua kutumia busara, wangewaeleza wale wafadhili watujengee vyumba vya Mahakama kwenye maeneo yetu, kwa sababu hii ndiyo shida halisi ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya masuala ya mobile court yamefanyika nchi nyingi; utafiti unaonyesha yamefanyika India, Pakistan pamoja na Bangladesh. Haya maeneo yana population kubwa, kiasi kwamba kuhamisha watu kwenda eneo lingine, ni suala rahisi. Sisi nchi yetu hatujawa wengi kiasi tunahitaji kupata hizi huduma kule chini kabisa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na nia ya kutaka kuharakakisha mashauri mbalimbali, lakini ndani yake kunaonekana kulikuwa na nia ovu ya watu kutaka kupiga dili katika ununuzi wa haya magari kwa sababu gharama hiyo siyo halisi na uchunguzi ufanyike, kwa sababu watu wa TAKUKURU wapo, walilisikia hili, tunaomba walifanyie uchunguzi waje waeleze. Bunge lako lilitaka kutumika kama rubber stamp kuona watu wanapiga dili kwenye haya mambo ya magari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukueleze tu, kama ambavyo wengine wametoka hapa kuchangia na umekataa kutumia neno fulani la kusema Bunge linaingiliwa. Tukijaribu kugeuza maneno tunajenga tafsiri potofu hata kwa watu wetu wanaotusikiliza. Hili ni neno la kawaida kabisa la Kiswahili. Tunachotaka kumaanisha ni kwamba majukumu ya Bunge sasa kwa namna fulani yanatumika na Serikali kupitishia vitu vyao wanavyovitaja wao, hii ndiyo maana ya taarifa iliyotoka. Kiswahili halisi cha hili neno ni kupokwa madaraka kwa Bunge na mhimili mwingine.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nataka nikupe mifano michache. Kwa mfano, leo asubuhi wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika ulimwagiza Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu wafanye mjadala na watu wa ZECO kuhusiana na masuala ya VAT ambayo inatozwa kule Zanzibar pamoja na hapa. Umesema kwamba watu wale walizuiliwa nje, sasa aliyewazuia nani? Wewe wenyewe unasema siyo wewe uliyetoa amri ya kuwazuia, lakini walizuiwa wasiingie kwenye mhimili wako. Sasa aliyewazuia wale watu ni nani? Ndiyo ninachojaribu kumaanisha.

Mheshimiwa Spika, pamoja muda wangu, nashukuru pia kwa maelezo yako ya kutaka kutuweka sawa, lakini nikuongezee kitu kingine hapa. Hayo magari yalishanunuliwa, sasa tunapata wasiwasi kwamba Bunge hili ndilo linalopitisha bajeti na kwamba hata misaada ya kifedha na isiyo ya kifedha inayopewa nchi hii, maana yake inapita humu ndani na kujadiliwa, pamoja na hayo masuala ya mikataba lakini mambo haya yamefanyika bila ushiriki wako wala ushiriki Bunge lako.

Mheshimiwa Spika, bado tunaona, kwa mfano, Mheshimiwa Rais sasa hivi amekuwa akifanya ziara. Juzi tu ameenda huko Tarime, ukiangalia jumla ya pesa alizozigawa kwenye ziara yake nzima ni karibia shilingi bilioni moja inafika pale. Tunasema siyo jambo baya kufanya jambo lile, kugawa hizo fedha na kufanya kitu kingine na watu wanasema sasa, Mheshimiwa Rais sasa tuanze kumwita Mzee wa Mapesa, hili jina liondolewe kwa Mheshimiwa Cheyo. Sasa tunajiuliza, haya ndiyo matumizi halisi ya hizi bajeti tunazoziweka?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Narudi tena kwenye hoja yetu ya msingi, kama ulivyosema tulipe taarifa Bunge ili liweze kufanyia kazi haya masuala. Naiomba meza yako, lakini pia naliomba Bunge hili lipewe taarifa rasmi na Serikali na huu upande wa Mahakama kwamba ilikuwaje wao wakaanza kufanya purchases ikiwa ni pamoja na kununua haya magari ya Kitengo cha Mobile Court kabla hawajatushirikisha? Kwa sababu tuna shida kubwa sana kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama na tunakumbuka mwaka 2017 Mheshimiwa hapa alitangaza.

Mheshimiwa Spika, naendelea kukuomba tu, najua unaulinda muda wangu. Kwa hiyo, tunaomba sasa Bunge lako lipewe taarifa rasmi na Mheshimiwa Waziri atakapokuja hapa na mwisho wa siku atuambie, kwa sababu wameamua kuondoa hii Sehemu ya Tano kilichokuwa kimesababisha magari hayo yanunuliwe, sasa waje watuambie rasmi, baada ya magari haya kufika, wanakwenda kuyafanyia nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye masuala ya kisheria, siyo mzuri sana lakini tunapata taarifa mbalimbali. Sheria ilirekebishwa mwaka 2010 ambayo inampa Chief Justice mamlaka ya kufanya matumizi yoyote ya kitu ambacho kiko kwake. Sasa tunapata hofu, wanaweza wakaingilia upande wa kanuni, haya magari tukaanza kuyaona yakiwa yanafanya kazi. Kwa hiyo, Bunge lako liambiwe moja kwa moja kwamba jambo hili halitatokea tena, magari haya ikiwezekana huo mkataba usitishwe huko kabla magari hayajafika, hizo fedha zikafanyie shughuli nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna shida ya maji, tuna shida ya vyumba Mahakama, kwa nini walikubali tu kisehemu kidogo cha kununuliwa magari ili kuweza kuwatembeza hao Mahakimu ambayo hayawezi kufika kokote? Humu ndani hatujawahi kupitisha bajeti hata ya matengenezo ya hayo magari? Kwa hiyo, tafsiri yake ni kwamba watakwenda kutumia tena vibaya fedha iliyotengwa na Bunge lako kwa ajili ya shughuli za Kimahakama ambazo kila mara wamekuwa wakilalamika kwamba hizo pesa haziwatoshi. Mbaya kuliko, pamoja na kukiondoa hiki kifungu, ndiyo maana tunasema kulikuwa na nia ovu nyuma yake labda, walikuwa wanasema kwamba hata hizo mobile courts zikienda kufanyika vijijini, yule mshtakiwa haruhusiwi kuwa hata na mwakilishi wa kisheria. Hii ni tofauti na Ibara ya 13 cha Katiba.

Mwenyekiti Spika, kwa hiyo, tunaomba utusaidie.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2019 (Toleo la Kiingereza).
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye hoja hii iliyopo mbele yetu hapa ya Muswada unaohusu masuala ya madini lakini pia zabibu.

Mheshimiwa Spika, nakwenda moja kwa moja kwenye section 5. Kwanza nianze kwa kulikumbusha Bunge lako kwamba kuna wakati tunakuwepo humu ndani kwa nia nzuri kabisa ya kutaka kuishauri Serikali lakini kwa bahati mbaya kabisa kuna watu wanaamua kufanya propaganda badala ya kutekeleza wajibu wetu. Kutokana na hizo propaganda na kushindwa kutekeleza wajibu wetu ndiyo maana leo tupo hapa Siku ya Jumamosi, kinyume kabisa na utaratibu sisi tuliouzoea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka jana wakati tunajadili huu Muswada kuhusiana na sheria hiihii ambayo leo tunakuja hapa kuigeuza, tena kwa speed kubwa sana, baada ya Mheshimiwa Rais kuona kwamba kuna matatizo na wachimbaji hawa wa madini walipokwenda kuongea naye wakamueleza matatizo wanayoyapata kutokana na sheria hii, leo tunakutana hapa tunasema tunataka kubadilisha wenyewe. Tatizo hili tulilianzisha sisi wenyewe kwa sababu tulishindwa kutimiza wajibu wetu wakati huo. Wabunge wengi tu wa Upinzani, tena watu wakaja na reference; hawa watu tumewaona Morena wamekaa na watu ambao wameamua kuwabandika majina sasa wanaitwa mabeberu, wakiwa wanawapa pesa ili kuona sheria hii sasa inakwenda kubadilishwa ili kuweza kuwalinda mabeberu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Mpango tulisoma sisi pale taarifa yetu ya Kambi Rasmi ya Upinzani tukimueleza kwamba unachokwenda kukifanya sasa hivi unakwenda kuonesha au kuwasaidia watu wanaofanya smuggling ya biashara ya madini. Leo hii umeona kwamba hakuna pesa zinazopatikana kutokana na ubovu wa sheria iliyoko kule unaamua kuturudishia hapa ili tuweze kuijadili.

Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya sana tulitumia muda mrefu kuitengeneza sheria hii. Kuna vifungu vingi ambavyo navyo bado ni vibovu vinahitaji kuletwa humu ndani vifanyiwe marekebisho. Muda wa saa moja hautoshi sisi kama Wabunge kuishauri Serikali. Kwa hiyo, tunachokifanya sisi sasa hivi, tumechukua maoni ya wadau lakini tumechukua maoni machache sana ambayo tunakwenda kuyapeleka pale lakini baada ya muda hatutaweza kupata kile ambacho tulikuwa tunakitarajia. Tusifanye nchi yetu kuwa ni nchi ya majaribio kwenye vitu ambavyo vinakwenda kutuangamiza sisi wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukae sisi hapa leo tujiulize, hivi toka tulipopitisha hii sheria mpaka sasa hivi Serikali yetu imepata hasara kiasi gani? Hayo ndiyo maswali ya msingi ya kujiuliza. Pia niwaulize na ninyi wataalam kwamba wakati mnatengeneza hizi sheria, hivi ni kweli mliwa-consult wataalam wanaofahamu mambo haya? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jana kwa bahati mbaya, nasikia baadaye mliamua ku-withdraw, ulivuja mpaka mwongozo wa namna ya kwenda kuzitumia hizi sheria lakini bado kwenye zile kanuni zenu mnakwenda kuleta mambo mengine ya ajabu ambayo hayawezekani. Endeleeni kukaa na wadau muweze kuboresha, mumsaidie Rais kuweza kuwasaidia hawa watu.

Mheshimiwa Spika, mmekwenda huku ndani mnakwenda kuongeza vitu vingine. Sasa hivi mnakuja hapa na issue mnasema kutakuwa na suala la warehouse gems pale, lakini pia kule ndani kutakuwa na masuala ya eti mtu aliyechimba madini huko anakwenda kuya-deposit anapewa stakabadhi, hili suala limeharibu sana kwenye mazao ya korosho. Sisi tuna utaratibu wa stakabadhi ghalani kwenye korosho, mnaleta stakabadhi ya ghala kwenye madini, nani anafahamu quality ya hayo madini, nani atakwenda kupima, nani atakwenda kufanya valuation hiyo siku mnakwenda kufanya vile vitu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashauri waangalie haya mambo kwa makini, wakae na wataalam wawashauri. Hatujaweza kupitia kwa sababu ya huu muda tuliokuwa nao ni mfupi sana, lakini huku ndani kwenye sheria iliyoletwa pamoja na mabadiliko vile vifungu tulivyovipitisha wakati ule vinahitaji kuwa scrutinized zaidi na zaidi ili Sheria yetu ya Madini iweze kuwa bora zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwenye kanuni, wanakwenda kuongeza vitu ambavyo uwezekano wa kuvitekeleza ni mdogo. Serikali hii inadaiwa about 500 billion kwa ajili ya ushuru na kodi mbalimbali zinazolipwa kule, leo tunakwenda tunasema eti kila madini yaliyopo yapelekwe kwenye warehouse. Tunawaambia haiwezekani roli la mchanga kwa sababu nayo ni madini ya ujenzi tuyapeleke kwenye warehouse gems, tutafanyaje hizi kazi? Hivi vitu vingine Serikali wavikubali, tuache, tusiingize vitu visivyowezekana.

Mheshimiwa Spika, niombe muda uongezwe jambo hili lijadiliwe kwa kina. Ahsante sana. (Makofi)