Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Dr. Christine Gabriel Ishengoma (76 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii. Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenifanya niweze kusimama hapa mbele yenu leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, naomba kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge pomoja na viongozi wa Bunge kwa kuweza kunifariji kwenye msiba ulionipata wa kuondokewa na mama yangu mzazi. Nawashukuru sana, Mwenyezi Mungu awabariki. MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, naomba pia, kumpa pongezi Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya. Pongezi pia kwa Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa kazi anayoifanya pamoja na Naibu na watendaji wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kuchangia kwenye bajeti. Ni kweli kabisa wote mnaamini kuwa pesa tunazopitisha sizo zinazotolewa. Naomba sana kama kweli tunakipa kipaumbele kilimo, pesa tunazozipitisha ziweze kutolewa zote. Kila mmoja anajua kilimo, mifugo pamoja na uvuvi ndiyo uhai wa mwanadamu, kwa hiyo, naomba sana kitiliwe mkazo kwa upande huu wa bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kilimo ni sayansi. Kwa hiyo, naomba sana kwenye upande wa utafiti hela zinazotengwa ziweze kuongezwa. Tuna vyuo vikuu, kwa mfano Chuo Kikuu cha Sokoine wanafanya utafiti, tunazo research centres mbalimbali, Ilonga, Uyole, Ukiliguru, Maruku, zote zinafanya utafiti pamoja na vyuo vingine vya uvuvi. Naomba sana hela ziweze kutolewa kwa watafiti wetu. Pia pamoja na utafiti unaofanyika tuweze kupata mrejesho kwa wakulima wetu kusudi waweze kuutumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Benki ya Kilimo imeanza kazi, ni kweli, lakini mpaka sasa hivi bado iko Dar es Salaam. Kwa mfano, kwa Mkoa wangu wa Morogoro ni wakulima wazuri sana, mikoa mingine iko mbali sana kama Ruvuma, Kagera, kwa hiyo, kama Mheshimiwa Waziri alivyosema ningeomba sana matawi yaweze kufunguliwa haraka iwezekanavyo kwa mikoa hii yote kusudi waweze kutumia hii Benki ya Kilimo kwa mikopo kama ilivyopangwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye pembejeo na hasa naongelea kuhusu mbegu. Inaonekana kuwa asilimia kubwa ya mbegu zinatoka nje na hazitozwi kodi, narudia tena hazitozwi kodi lakini mbegu zinazozalishwa hapa nchini zinatozwa kodi. Naomba ufafanuzi kama nimeeleweka. (Makofi)
Jambo lingine ni kuhusu viwanda vya mbolea na vyenyewe inaonekana kuwa mbolea inayotoka nje inafikiriwa zaidi kuliko mbolea inayotoka hapa nchini. Kwa mfano, tunacho Kiwanda cha Minjingu, naomba sana viwanda ambavyo vipo hapa nchini viweze kupewa kipaumbele na ruzuku yake iweze kutolewa vizuri iwezekanavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu na inawezekana, kama tunaweza mambo mengine kwa nini hiki kisiwezekane? Mheshimiwa Waziri naomba tujitahidi sana kuzalisha mbegu hapa nchini Tanzania kwa sababu kwanza kabisa mbegu inayozalishwa hapa inaendana na hali ya hewa ya hapa lakini ukitoa mbegu za nje ndiyo maana unapata viotea na vibua. Kwa hiyo, naomba sana tujitahidi kuzalisha mbegu zetu hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine naomba kuongelea utaratibu au mfumo mzima wa ruzuku. Namshukuru Mheshimiwa Waziri anaendelea kusema kuwa mfumo huu utabadilishwa, utabadilishwa lini? Serikali mnafanya vizuri, naomba sana huu mfumo wa voucher uweze kubadilishwa kusudi iwepo system ambapo mkulima yeyote yule mdogo na mkubwa unakwenda dukani unapata mbolea na mbegu wakati wowote kama unavyokwenda dukani kununua majani ya chai.
Mheshimiwa Mwenyekiti, masoko. Ni kweli mazao mengine hayana masoko lakini hatutamaliza tatizo hili la masoko mpaka tuwe na viwanda, mnyororo wa kuthamanisha mazao. Kwa hiyo, naomba Wizara ya Kilimo iweze kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara kuanzisha viwanda ili kusudi hizi malighafi ya kilimo ziweze kutumika kwenye viwanda hivi.
Ni kweli Afisa Ugani hawatoshi lakini mimi naamini Vyuo vya Kilimo kila siku, kila mwaka vinazalisha wataalam hawa. Naomba Serikali ione jinsi ya kuwaajiri Maafisa Ugani hawa wote. Kama kweli kilimo, uvuvi na mifugo tunakipa kipaumbele na wenyewe waweze kuajiriwa mara moja mara wanapomaliza masomo yao maana wako wengi.
Jambo lingine ambalo naweza kuongelea hapa ni kilimo cha mkataba. Kilimo cha mkataba ni kizuri kwa sababu kinakupa pembejeo zote na kinatoa service za Afisa Ugani kwa kila jambo. Kwa hiyo, naomba kiweze kufikiriwa kiendane pamoja na uwekezaji. Wawekezaji na wenyewe tuweze kuwakaribisha waweze kuwekeza kwenye upande wa kilimo, uvuvi na mifugo kusudi tuweze kutatua jambo hili la masoko kwa kuwekeza kwenye viwanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha mboga na matunda. Naomba kuwataarifu kuwa Mkoa wangu wa Morogoro ni moja ya mikoa ambayo inalima sana mboga na matunda pamoja na mikoa mingine kama Tanga. Kwa hiyo, naomba sana tuone jinsi ya kuthaminisha mazao haya ya mboga pamoja na matunda kusudi yaweze kupata thamani kwa sababu karibu asilimia 32 zinapotea hivihivi. Kwa hiyo, naomba tuliangalie sauala hili. Hata hivyo, hapohapo tujikite na tuwe na mkakati wa kuwasaidia vijana na wanawake kwenye kilimo cha mboga na matunda. Kwa kulima mboga na matunda unaweza ukapata kipato kwa muda mfupi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha miwa Mkulazi. Eneo limetengwa lakini kwenye kitabu Mheshimiwa Waziri sikuweza kuona vizuri kama limezungumziwa. Kama lipo, ningeomba kupata ufafanuzi kwa sababu wakulima wa Mkulazi, Morogoro tayari wamejitayarisha, wametenga eneo lao kwa hiyo naomba liweze kutumika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongelea mbegu za mafuta kwa mfano, ufuta, alizeti, pamoja na karanga. Naomba sana zipewe kipaumbele, Serikali tuangalie namna ya kupunguza kuingiza mafuta hapa nchini kusudi tuweze kutumia mafuta tunayotengeneza wenyewe. Haya mafuta ya alizeti yanayosambaa barabarani yanakwenda under rancidity yaani yanaharibika. Kwa hiyo, naomba sana na haya mafuta tunayotengeneza hapa nchini yaweze kuwekwa vizuri kusudi wananchi waweze kupenda kuyatumia. Naomba Wizara ya Viwanda iweze kushirikiana pamoja na Wizara ya Kilimo kwenye mambo mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukuzaji wa viumbe majini, mabwawa ya samaki ni jambo zuri sana, unakwenda hapo unatoa samaki wako, unaingia ndani unapika unapata lishe. Kwa hiyo, naomba sana kama Mheshimiwa Waziri alivyosema tukazanie huu uzalishaji wa viumbe vya majini ili tuweze kupata lishe pamoja na kipato kwa kutumia bahari na mito yetu. Nimefurahi sana kuona kuwa watatoa ruzuku kwa wavuvi wadogo wadogo, hicho ni kitu kizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijamaliza, naomba sana kuongelea kuhusu mifugo. Wafugaji na wenyewe tuwaangalie kwenye kuwawekea miundombinu.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumuuliza Waziri, viwanda vya mbolea vya Kilwa, Lindi, Mtwara na Kibaha ni lini vitaanza kujenga, kukamilika na kutoa mbolea. Namna hii tutapunguza tatizo la mbolea Tanzania.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia kwenye bajeti ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama hapa. Pili, nawashukuru wanawake wa Morogoro kwa kunileta tena humu Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nampongeza Mheshimiwa Waziri Charles Mwijage kwa mipango yake mizuri yote aliyoitoa kwenye kitabu chake cha bajeti. Mheshimiwa Waziri unaweza, nakuamini, naomba ufanye kazi, yale yote uliyoyaandika kwenye kitabu na Kamati yako na Wizara yako muweze kuyatekeleza kama yalivyopangwa pamoja na Wizara yako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa yote, hata wewe mwenyewe unavyoendesha Bunge lako hili Tukufu. Nianze kabisa na wafanyabiashara. Hapa naanza na sekta hii kwa sababu ya wafanyabiashara wadogo wadogo na hasa akina mama na vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mmoja ni shuhuda kuwa sekta hii kwa upande wa biashara, akina mama wengi sasa hivi, hakuna mama anayelala, kila mama anafanya biashara; na biashara nyingi wanazozifanya kama tulivyosema kuwa viwanda sana sana ni usindikaji kutokana na malighafi ya kutoka kwenye kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasindika, lakini Mheshimiwa Waziri tatizo wanalolipata hawa akina mama, jambo la kwanza ni tatizo la kupata kibali cha TBS. Wanahangaika sana, mikoa yote. Watu wengi wanahangaika sana, hasa akina mama, kupata mambo ya TBS. Wanafanya usindikaji mzuri, usindikija wa mvinyo, usindikaji wa achali na mambo mengine. Kwa hiyo, naomba sana waelekezwe jinsi ya kupata TBS na minyororo yote ya kupata TBS iweze kufupishwa kusudi wapate TBS kwa urahisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kwa wafanyabiashara hawa wadogo wadogo, naomba waweze kujengewa mazingira mazuri hasa kwa kupata mikopo ambayo kuwawezesha kufanya hii biashara yao kwa urahisi, kwa sababu wakifanya biashara ndiyo hapo hapo wanainua pato lao na pato la nchi kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, ni kweli Serikali haifanyi biashara, lakini tunatafuta wawekezaji. Naomba sana wawekezaji wanapopatikana, jaribuni kuwasambaza kwenye mikoa yote ya Tanzania. Kuna mikoa ambayo haijafaidika na viwanda hivi. Mikoa ya pembezoni bado haijafaidika sana na viwanda. Kwa hiyo, naomba uiangalie vizuri na yenyewe iweze kupata wawekezaji ilimradi cha msingi wawekezaji waweze kupewa miundombinu. Sana sana ni land bank, ili iweze kutiliwa maanani. Kwa sababu unampeleka mwekezaji, kwa mfano, unampeleka Morogoro, Iringa, Kagera au Pwani, lakini unakuta huko hakuna area ambapo anaweza akafanyia. Huyo mwekezaji anahangaika, mwisho anarudi na inaonekana hana pa kufanyia biashara na mwisho wake anahama anakwenda kwenye nchi nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu viwanda. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais, amesema kuwa nchi yetu inabidi iwe nchi ya uchumi wa viwanda. Ni kweli inawezekana sisi wenyewe tukijituma. Tukijituma inawezekana. Namwomba sana Mheshimiwa Waziri aangalie viwanda vilivyokuwepo, hasa miaka ya 1980, nchi yetu ilikuwa na viwanda vingi sana. Kwa mfano, nikianza na Mkoa wangu wa Morogoro, tulikuwa na viwanda vingi. Nianze na Kiwanda cha Juisi ambacho huwa nakisemea mara kwa mara kwa sababu mimi mwenyewe napenda sana juisi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanda cha Juisi cha Morogoro na mikoa mingine iliyo karibu kwa mfano tumesema Mkoa wa Tanga, Muheza, Lushoto, Iringa na mikoa mingine wanalima sana matunda na mboga mboga. Kwa upande wa juisi naomba sana kiwanda hiki kiweze kuangaliwa. Mheshimiwa Waziri nakuomba sana kiweze kufanya kazi. Ni kweli ni aibu kuona watu wananunua juisi kutoka Saudi Arabia ambao kweli nchi yao siyo fertile kama nchi yetu. Kwa hiyo, naomba sana hili tuliangalie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili siku moja niliongea lakini ikaonekana kuwa hivi viwanda, pamoja na Kiwanda cha Azam nikiunganisha pamoja, wanaleta sana sana concentrate ambayo siyo nzuri. Nchi yetu ni nzuri ambapo tunalima matunda. Kama kuna tatizo la ubora wa matunda, tulifanyie kazi. Tuna watafiti wetu, waweze kufanya kazi, huu ubora unaweza ukawaje ukatoa juisi ambayo haiwezi kuchacha mara moja. Tuifanyie kazi pamoja na maabara ziweze kuwepo za ku-test shelf life ya hii juisi iweze kuendelea kwa muda mrefu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu bado niko hapo hapo, niongelee kiwanda cha ngozi. Tulikuwa na Kiwanda cha Ngozi - Morogoro ambacho sidhani kama kinafanya kazi. Kilikuwa kinatoa bidhaa ya ngozi, lakini sasa haipo. Kuna Kiwanda cha Kioo, tulikuwa tunapata sahani na vikombe lakini hakuna.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa upande wa kiwanda cha 21st Century hicho kinafanya kazi vizuri, lakini Mheshimiwa Waziri naomba ukiangalie mazingira yake kusudi kiweze kuzalisha kwa wingi na kitumie mazingira ambayo ni rafiki kwa mazingira, kiache kuharibu mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Mheshimiwa Waziri hivi viwanda viweze kusambaa mijini pamoja na vijijini, hasa mahali pale penye umeme. Naomba ushirikiane na Wizara nyingine kama Wizara inayoshughulika na mambo ya Nishati na Madini pamoja na Wizara ya Maji pamoja na Wizara ya Kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda kingine ni Kiwanda cha Magunia. Tulikuwa na Kiwanda cha Magunia Morogoro, tulikuwa na viwanda vingi Morogoro, Morogoro ulikuwa ni Mkoa wa viwanda, lakini sasa hivi viwanda vyote kwa wastani havifanyi kazi. Siyo Morogoro tu, tulikuwa na Tanganyika Packers ya Dar es Salaam, tulikuwa tunakula nyama za makopo na samaki za makopo na kila kitu, lakini sasa hivi tuna-import vitu hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia kwa Mheshimiwa Waziri ambaye namuamini kuwa atafanya kazi hii, naamini kuwa viwanda vyote, kama alivyosema kwenye hotuba yake, viwanda vyote vilivyokufa atavifufua, naomba kweli vifufuliwe kusudi tuweze kupata ajira kwa vijana wetu, tuweze kupata ajira kwa akina mama, tuweze kupata masoko ya mazao ya kilimo ambayo wakulima wengi wanalima, lakini mpaka sasa hivi hawapati soko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna viwanda vya korosho. Kwa mfano, Kiwanda cha Korosho Kibaha (TANITA), hakifanyi kazi. Najua hakifanyi kazi lakini na wewe Mheshimiwa Waziri unaelewa kwa nini hakifanyi kazi, naomba kifanye kazi ili wananchi wa Mkoa wa Pwani waweze kukitumia kwa kuuza korosho zao kupitia kwenye kiwanda hicho. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi wenyewe naomba tuhamasishe wananchi waweze kufungua na kuanzisha viwanda vidogo vidogo hasa huku vijijini mahali ambapo kuna umeme. Tunashukuru sana kwa sababu sasa hivi vijiji angalau vingi vingi vina umeme wa REA…
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa hayo machache ambayo nimechangia. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia kwenye hotuba ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kutoa pongezi. Kwa kweli ni furaha sana kuchangia kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu mambo mengi mazuri sana yamefanyika. Nampa pongezi Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mwenyezi Mungu azidi kumbariki.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpa pongezi pia Mheshimiwa Rais kwa kufanya mambo mengi mazuri. Tunampongeza sana na tunamwombea mbele ya Mwenyezi Mungu, tunaamini kuwa utapita bila kupingwa, hakuna Mpinzani mbele yako. Nikirudi kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu amefanya mambo mazuri sana kumsaidia Mheshimiwa Rais na wewe Ruangwa watakupa kura za kutosha utapita bila kupingwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Jenista kwa kumsaidia mambo mengi Mheshimiwa Waziri Mkuu. Vilevile niwapongeze Mheshimiwa Kairuki kwa mambo yote anayosaidia; Mheshimiwa Mavunde na Mheshimiwa Stella Ikupa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wewe mwenyewe umefanya mambo mazuri sana. Tunajidai kwenye Bunge hili kwa kuwa na Bunge mtandao. Mwenyezi Mungu akubariki na umeacha alama, kila mmoja atakuwa anajua kuwa wewe ndiyo ulianzisha Bunge mtandao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tunakushukuru sana na tunakupongeza sana pamoja na Naibu wako pamoja na Wenyeviti wote kwa kutuongoza kwa muda wa miaka mitano kwenye Bunge hili. Tunawashukuru na Mwenyezi Mungu awabariki nyote.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mafanikio ni mengi ambayo yote yameandikwa kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na kila mmoja anayaona kama anajidai haoni sijui yeye yuko wapi. Reli tumeiona, elimu tumeiona, hospitali tunaziona, maji tunaona, kila kitu tunaona. Kwa kweli Serikali yetu ya Awamu ya Tano tunaipongeza, Tanzania tunajivunia na tunafurahi kuishi kwenye nchi yetu, inapendeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze kuongelea kuhusu miundombinu. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais, kwa kweli wamejitahidi pamoja na Mheshimiwa Waziri Mkuu, mmefanya mambo mazuri sana. Nianze na barabara. Barabara za lami zimejengwa, tumeunganishwa. Naweza nikatoka hapa nikaenda Ruvuma siku hiyo hiyo; nikaenda Mtwara siku hiyo hiyo nikafika; nikaenda Lindi siku hiyo hiyo nikafika; nikaenda Kagera nikafika siku hiyo hiyo; nikaenda Mara siku hiyo hiyo nikafika. Kwa hiyo, nashukuru sana kwa mambo hayo ambayo mmeyafanya kwa kuunganisha barabara za lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nashukuru kwa upande wa barabara za vijijini, zilikuwa zimejengwa kweli siyo uongo, lakini mambo ya tabianchi hatuwezi kuyabadilisha. Ni kweli tumepata mafuriko, yametokea na tumeyaona, Ila nawashukuru sana, tena sana kwa sababu ingawa yametokea kwa mfano kwenye Daraja letu la Kiegea ambalo linaunganisha barabara na usafiri wa kwenda mpaka nchi za nje, Mheshimiwa Rais alifika, Mheshimiwa Waziri Mkuu amefika, Mheshimiwa Waziri, Eng. Kamwelwe amefika na Waheshimiwa wamefika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru kuwa licha ya kuondolewa hayo madaraja, lakini Serikali inachukua tahadhari haraka sana na kurudisha usafiri na sasa hivi magari yanapita kwenye Daraja letu la Kiegeya ambalo liko kwenye Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande huo huo, naomba tena sana, kwa sababu barabara za vijijini kutokana na mabadiliko ya tabianchi na mafuriko yaliyotokea barabara nyingi za vijijini zimeharibika. Kwa sababu barabara nyingi za vijijini ziko chini ya TARURA, nami naungana na watu wanaosema kuwa TARURA waongezewe fedha za bajeti kwa sababu ya kutengeneza hizo barabara. Madaraja mengi ya vijijini yameharibika, siyo Morogoro tu, ni mikoa mingi imepata dharura hiyo. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri Mkuu iwe dharura, iweze kuchukuliwa ili hayo madaraja yaweze kutengenezwa na tuweze kupata usafiri hasa kwa mazao pamoja na wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa afya, kwa kweli tunashukuru sana kwa ujenzi wa Vituo vya Afya, ujenzi wa Zahanati, ujenzi wa mahospitali na hata Mkoa wangu wa Morogoro yamejengwa, tunakushukuru sana. Naomba kutoa ushauri kuwa mpaka sasa hivi unakuta Vituo vya Afya vingine na zahanati nyingine kuwa wataalam hawatoshi. Kwa hiyo, naomba huo mgawanyo wa wataalam; manesi, madaktari bingwa, wataalam wa maabara, uweze kuangaliwa ili tuweze kupata mgawanyo vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunajivunia hata hospitali zetu za kanda, sasa hivi kwa kweli zinafanya vizuri. Ukiona Benjamin Mkapa inafanya kazi vizuri, Muhimbili inafanya kazi vizuri hata za Kitaifa. Kwa hiyo, sasa hivi tumepunguza hata wagonjwa kwenda nchi za nje na hasa ukiangalia na ugonjwa huu wa Corona. Kwa hiyo, tunamshukuru Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Corona nami naomba kuongelea Corona; kwa kweli ni ugonjwa ambao unaumiza sana. Nilikuwa naangalia kwenye mtandao, unaona unawashika hata watoto wadogo, wanatenganishwa na wazazi wao. Kwa hiyo, ninachokiomba kwa Ugonjwa kwa ugonjwa wa Corona, tuuangalie kwa makini. Pia nawashauri wazazi waweze kuchukua ushauri ambao tunapewa pamoja na Mawaziri wetu, Rais wetu na Waziri Mkuu ili tuweze kuwalinda hata watoto wetu ambapo wewe mzazi unaweza ukapona lakini mtoto wako akachukuliwa akawekwa kwenye karantini. Kwa hiyo, inasikitisha sana.

Mheshimiwa Spika, naomba kuongelea kuhusu elimu. Natoa pongezi kwa Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa mambo mengi inayoyafanya kuhusu elimu na hasa kwa mkopo huu ambao umeidhinishwa wa World Bank wa Dola za Kimarekani milioni 500 ambazo zitasaidia watoto wetu wa sekondari pamoja na kupunguza mimba za utotoni kwa sababu hata mahosteli yataweza kujengwa. Kwa hiyo, nashukuru sana kwa hilo.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali pia kwa kurudisha usafiri wa treni kwa upande wa Dar es Salaam kwenda Moshi na Tanga kwenda Moshi, pamoja na uendelezaji wa ujenzi na ukarabati wa Reli ya Kati pamoja na ujenzi wa Reli ya SGR.

Mheshimiwa Spika, ombi langu na ushauri wangu kwako na Mawaziri wote, naomba sana hizi reli zitakapokamilika, tupunguze malori yanayopita kwenye barabara zetu ili mizigo inayobebwa kwenye malori haya iweze kubebwa kwenye treni hizi, kwa sababu haya malori yanaharibu barabara zetu. Hebu angalia Wabunge wote tunasafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, lakini unakuta mahali pengine barabara zetu siyo rafiki kwa sababu ya haya malori ya mizigo. Pia yanaleta msongamano na yanasababisha ajali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ulinzi na usalama. Nchi yetu imebarikiwa kuwa salama chini ya Jemedari wetu, Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Tunashukuru sana vyombo vya ulinzi na usalama, vinafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, naomba sana wananchi wote wanisikilize kwamba tuzidi kutunza amani na usalama kwenye nchi yetu kusudi tuweze kuendelea vizuri kwani amani hainunuliwi, inatunzwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mambo ya Mfuko wa Taifa wa Vijana, natoa pongezi kwa sababu wamefikiwa vijana wengi, vikundi 586, vijana ambao wamefikiwa tayari ni 4,222, lakini ninaomba licha ya kutoa pongezi, elimu izidi kutolewa kwa vijana wote, waweze kupata elimu jinsi ya kupata huu mkopo na hasa kwenye Halmashauri nyingine ambazo bado hazijafikiwa kwa sababu ni Halmashauri 155 ambapo mpaka sasa hivi wametoa hivi vikundi na wameweza kuwapata hao vijana. Hii mikopo iweze kuwasaidia hata vijana ambao wako kwenye kada zozote zile kuanzia wahitimu wa Vyuo Vikuu mpaka wale wa Darasa la Saba, wote waweze kupata na waweze kujiajiri kwa sababu ajira kama tunavyojua haipo. Ajira ni ya kujiajiri na ajira ni wewe mwenyewe.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni kuhusu nishati. Namshukuru sana Waziri, Mheshimiwa Dkt. Kalemani pamoja na Mheshimiwa Subira kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. Ni nzuri sana. Wamefanya kazi nzuri, tumeona umeme. Watu wengine tulikuwa tumezaliwa na kukulia kwenye vibatari, lakini sasa hivi tunaona umeme. Kwa hiyo, jambo ninaloomba ni moja tu; kama mpango ulivyopangwa kuwa vile vijiji pamoja na Vitongoji vilivyorukwa kwa mpango huu wa REA III viweze kufikika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano pale Morogoro kuna Kitongoji cha Chekereni, hakina umeme, lakini naona kuna kiwanda cha mikunde kinawasha umeme pamoja na pale Mtego wa Simba umeme upo, lakini chenyewe kiko katikati hakina umeme. Kwa hiyo, naomba na chenyewe pamoja na vijiji vingine ambavyo vimekosa umeme vipatiwe umeme.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa ni kuhusu pensheni. Kwa kweli kuna wale wafanyakazi wengine ambao hawakufanya kazi kwenye mfumo wa Serikali, wanalia huko, hawajapata pensheni. Walikuwa wanaomba kama inawezekana, watu wote waweze kupata pensheni waweze kupata hela kidogo kama TASAF inavyofanya angalau kuangalia wale ambao hawana uwezo.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Kwa kweli Tanzania yetu inapendeza, tusonge mbele chini ya Chama cha Mapinduzi na Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu tunawapa pongezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi kuchangia hotuba ya bajeti ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Kwanza kabisa nampa pongezi Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana anayoendelea kuifanya ya Chama chetu cha Mapinduzi akitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba kuongea kuhusu afya. Nianze kwa kutoa pongezi kwa Serikali kwa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hasa kwa kujenga vituo vingi vya afya kwenye Halmashauri zetu na kuboresha Zahanati zetu, Hospitali zetu zote za Rufaa. Ila natoa ushauri kwa sababu unakuta Vituo vya Afya vimejengwa lakini vingine havina watumishi wa afya.

Mheshimiwa Spika, mfano mmoja ni Kituo cha Afya Kisaki ambacho tulipewa hasa na Mheshimiwa Hayati Dkt. Magufuli alipotembelea Bwawa la Nyerere; aliona kuwa kuna umuhimu wa pale Kisaki kuwa na Kituo cha Polisi na Kituo cha Afya. Kituo cha afya kimemalizika, lakini mpaka sasa hivi hakina watumishi. Kwa hiyo, kuna vituo vya namna hiyo. Naomba vituo vya afya vilivyokamilika ambavyo havina watumishi wa afya viweze kupewa watumishi hao.

Mheshimiwa Spika, napongeza sana kuona kuwa bajeti ya dawa imeongezeka. Ni kweli imeongezeka lakini bado wananchi hawajapata dawa. Bado kuna tatizo la dawa. Nilishaongea na Waziri wa Afya, Mheshimiwa Dorothy kuhusu dawa na nilifanya ziara kwenye Mkoa wangu wa Morogoro; na ikiwa ni mojawapo ya mikoa mingine kuwa bado tuna tatizo la madawa. Namshukuru Mheshimiwa Waziri, ameongelea kuhusu mambo hayo, kwa hiyo, naomba waichukulie kwa undani tuweze kupata dawa, waweze kutibiwa watu ambao tunaumwa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni ushauri kuhusu Bima ya Afya. Viongozi wetu walishatuambia kuhusu Bima ya Afya kwa watu wote, naomba nalo walifanyie kazi kusudi liweze kutekelezwa. Jambo lingine ni watumishi wa afya kama nilivyosema.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine naomba kuongelea ni dirisha la wazee. Ni kweli tulisema kuwe na dirisha la wazee, lakini inategemea na Halmashauri na Halmashauri. Wazee wengine wanatibiwa vizuri, wengine bado wanahangaika, wanaambiwa mkanunue dawa na unakuta wazee wengine hawana uwezo. Kwa hiyo, nashauri kuwa nalo liweze kuangaliwa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nashauri ni kuwa na maboma hasa kwenye Zahanati. Kwa ile miradi ambayo haijakamilika hasa maboma ya Zahanati naomba yaweze kukamilika na Vituo vya Afya kusudi tuweze kuendelea na miradi mpya kwa kukamilisha miradi ya zamani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo nimekumbana nalo ni chanjo ya watoto wachanga. Naomba Mheshimiwa Waziri wa Afya aifanyie kazi. Bado kuna matatizo; akina mama wengine wanalalamika kuwa watoto wao hawapati chanjo kadiri inavyostahili ambalo ni tatizo kubwa sana. Kama mtoto hajapata chanjo kadiri inavyostahili, anaweza baadaye akapata ugonjwa ambao ungetibiwa kutokana na chanjo. Hilo ni jambo ambalo nimekutana huko vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, magonjwa yasiyoambukizwa nayo sasa hivi imekuwa ni tatizo. Naomba ifanyiwe utafiti na jinsi ya kuyatibu tuweze kuepukana na magonjwa haya ikiwepo kisukari, kansa, magonjwa ya ini pamoja na magonjwa ya moyo. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri kuwa elimu iweze kutolewa kwa wananchi pamoja na kuona jinsi ya kuepukana na hili, lakini na utafiti uweze kuangaliwa.

Mheshimiwa Spika, nikiwa bado kwenye mambo ya afya; tumeingia kwenye Covid tumesahau kuwa bado UKIMWI upo. Naomba suala la UKIMWI, ingawa tuna Kamati ya UKIMWI, ifanyiwe kazi, elimu izidi kutolewa kwa sababu sasa tumekwenda na Covid, tumesahau UKIMWI bado upo. Kwa hiyo, naomba iangaliwe sana kuwa UKIMWI bado upo. Ndiyo sababu uliunda Kamati ya UKIMWI ukijua kuwa UKIMWI bado upo.

Mheshimiwa Spika, wananiambia ni Kamati ya Mambo ya UKIMWI, siyo Kamati ya UKIMWI. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, nilindie muda wangu, huyu Shangazi ananisumbua. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, elimu; naishukuru Serikali kuwa kwa kweli imefanya vizuri katika mambo ya elimu.

SPIKA: Mheshimiwa Shangazi usimsumbue Mheshimiwa Ishengoma. (Kicheko)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya vizuri kwenye mambo ya elimu, elimu bila malipo hasa kwa upande wa ada, lakini tatizo bado lipo kwenye chakula hasa kwa shule za msingi na sekondari zile za kutwa ambapo hawapati chakula cha mchana. Naomba hilo lisisitizwe kwa sababu bila ya kupata chakula huwezi kuwa na lishe bora na huwezi kufikiria na huwezi kufanya vizuri darasani, kwa hiyo naomba hilo nalo liangaliwe.

Mheshimiwa Spika, tumetembea kwenye shule za pembezoni bado kuna tatizo la Walimu, kwa hiyo naomba nalo liangaliwe ingawaje wataajiriwa wengine, lakini awatoshi bado kuna Walimu ambao wapo tu lakini hawajaajiriwa. Kwa hiyo tunaomba utumishi watoe vibali kusudi Walimu waweze kuajiriwa ambao bado hawajaajiriwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, miundombinu bado mingine ni mizuri lakini mingine bado matatizo. Kwa mfano, madawati nashukuru Mheshimiwa Ummy alisema kuwa atanunua madawati, lakini naomba waliangalie watoto wasikao chini waendelee kukaa kwenye madawati. Pia madarasa na nyumba za walimu bado ni matatizo.

Mheshimiwa Spika, nitoe pongezi kwa ukarabati wa Shule Kongwe kweli shule kongwe zimekarabatiwa hasa za shule za sekondari, lakini nikija kwenye madarasa ya shule za msingi, bado ni matatizo. Kwa hiyo shule za msingi naomba na zenyewe ziangaliwe katika kufanyiwa ukarabati.

Mheshimiwa Spika, nikija kwenye mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu; nashukuru na natoa pongezi ndio, mikopo imeongezeka, lakini bado ni tatizo. Kuna wanafunzi ambao wamefaulu na unakuta wengine ni wasichana ambao hawajapa mikopo, wako vijijini, juzi juzi nimekutana na msichana mmoja analia kabisa, wako wengi vijijini, wako wengi mitaani, wamefaulu lakini wamekosa mikopo. Kwa hiyo, naomba vigezo vya mikopo ya elimu ya juu viangaliwe, hata watoto wa maskini ambao ni hitaji waweze kupata mikopo kwa sababu kweli wengine hawajapata mikopo hiyo. (Makofi)

Mheshimwa Spika, sekta ya utafiti hasa Vyuo Vikuu; naomba uangaliwe, uweze kutengewa fedha za kutosha na hiyo asilimia moja inayotengewa iweze kutolewa kwa wakati. Mafao ya Walimu wakiwemo Wahadhiri naomba yaangaliwe na hapa naongea kwa pia kwa ajili ya wafanyakazi wote. Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye hotuba yake amesema pension inatolewa, nashukuru sana, lakini kuna wengine ambao wanasota hawapati pension kwa muda mrefu, naomba waangaliwe, waweze kupata pension zao. Wengine wanatuambia tuwaombee na ndiyo hivyo hapa nawaombea kuwa waweze kupewa pensions zao kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, siwezi kumaliza bila kuongelea miradi ya kimkakati. Namshukuru sana Hayati Dkt. Magufuli, Rais wetu mpendwa, alale mahali pema peponi. Mheshimiwa mama Samia ambaye ni Rais wetu waliungana kwa pamoja na Serikali yetu wakaona miradi ya kimkakati ambayo ilikuwa imekaa kwa muda kabla ya kufanya kazi, sasa imefufuliwa, reli ya mwendokasi ambayo ni SGR, inaendelea kujengwa vizuri. Mpaka sasa hivi tumeambiwa ni asilimia 90.3 Dar es Salaam mpaka Morogoro.

Mheshimiwa Spika, sasa nauliza ni lini itaanza kazi hasa hiki kipande cha Dar es Salaam mpaka Morogoro au tutasubiri reli nzima imalizike? Wananchi wa Morogoro wanaisubiri kwa hamu. Naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu aniambie kwa sababu inaenda vizuri na nashukuru sana kwa sababu hiyo reli ya mwendokasi ikiisha ambayo ni mradi mkubwa, ambaye haoni aje angalie pale inavyopendeza. Watanzania tunajivunia hii reli ambavyo itapunguza mizigo ambayo inaharibu barabara zetu, pamoja na wasafiri na utalii itakuwa ni kivutio kikubwa na itaongeza ajira kwa vijana wetu na wajasiriamali wote pamoja na kipato kwa Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile naomba kuongelea kuhusu bwawa la Mwalimu Julius Nyerere, bwawa hili ni kubwa kama tulivyoambiwa ambalo litaweza kutoa umeme wa kutosha ambao…

SPIKA: Ahsante

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tunawashukuru, waendelee iweze kukamilika ili tufaidikea kwa hilo. Nashukuru kwa kunipa nafasi.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenifanya nisimame hapa kwa siku ya leo, pili nawashukuru wananchi hasa wanawake wa Mkoa wa Morogoro walioniwezesha kurudi tena hapa Bungeni. Nampongeza Rais wangu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na Mawaziri wake. Nampongeza pia Waziri wa Fedha kwa mpango mzuri aliouleta mbele yetu, jambo muhimu naomba utekelezwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea kuhusu daraja la Kilombero, nawapa pole wananchi wa Kilombero na Ulanga kwa tatizo hili lililowapata. Kutokana na tatizo hili naomba kwenye mpango wetu huu unaoendelea tuweze kulipatia kipaumbele daraja la Kilombero.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vipaumbele naanza na viwanda; Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa Viwanda, lakini kusema ukweli viwanda vingi vimekufa, imebaki sana Kiwanda cha Tumbaku. Kiwanda cha Tumbaku ni cha watu binafsi, lakini kinafanya kazi nzuri na kimeajiri sana wanawake, kwa hiyo, naomba kiangaliwe vizuri kwa matatizo ambayo yatakuwepo. Kiwanda cha Nguo na chenyewe kinafanya vizuri, kina matatizo madogo madogo kwa sababu mara nyingi huwa kinatumia kuni, kwa hiyo uandaliwe mpango uangaliwe kusudi waweze kutumia nishati bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, viwanda vingi vya Morogoro vimekufa, kwa hiyo naomba wale watu ambao wamechukua hivi viwanda waweze kuvifufua kama hawatavifufua wapewe notice ya kuvirudisha kusudi viweze kufanya kazi. Viwanda hivi tumesema kuwa kwenye mpango viweze kutumia malighafi ambazo zinapatikana hapa nchini na hasa viwanda vya kilimo, uvuvi pamoja na mifugo. Mambo haya yatapendeza kwa sababu yataweza kuinua kipato cha Mtanzania na kitaweza kutoa ajira hasa kwa akinamama pamoja na vijana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa maji, Mkoa wa Morogoro na hasa Manispaa, bado tuna matatizo ya maji. Miradi ipo ya Millennia lakini tatizo la maji bado liko hapa hapo, naomba MORUWASA pamoja na Serikali, Serikali yangu naipenda Mkoa wa Morogoro na hasa Manispaa, waweze kuwapatia maji kama nilivyosema kuwa Manispaa inakua na watu wanaongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro una mito mingi kama ninavyosema, lakini Wilaya nyingi zote, Mji mdogo wa Gairo, Mji mdogo wa Mikumi, Morogoro Vijijini na kwingine kote bado wananchi hawapati maji salama. Wanaoteseka sana ni wanawake, badala ya wanawake hawa ambao ni wazalishaji kutumia huu muda wote kuzalisha, hasa wale ambao ni wakulima wanatumia muda mwingi kutafuta maji. Kwa hiyo, nashauri kwenye mpango huu tuangalie suala la maji na sio Morogoro peke yake ni Tanzania nzima, wanawake wanateseka kutafuta maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira, hapa nasema sana ajira kwa upande wa vijana. Kulikuwepo na Mfuko wa Vijana, naomba kujua unaendeleaje kusudi vijana wanaohitimu kwenye Vyuo vyetu waweze kupata ajira na kutumia vizuri huo Mfuko wa Vijana. Kwa upande wa Morogoro tuna vyuo Vikuu vingi, ambavyo vijana wanahitimu, kwa hiyo naomba huu Mfuko uweze kuwekwa wazi pamoja na sekta zote ambazo zinaweza kutoa mikopo kusudi vijana waweze kuelewa, waweze kujiajiri na kuanzisha Kampuni zao wenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa misitu; nchi yetu ya Tanzania hasa na Mkoa wa Morogoro misitu imekwisha, wanakata miti wanatengeneza mkaa. Naomba kujua nishati mbadala, wananchi waweze kuelewa kuwa watumie nini hasa? Kuna mpango huu wa kata mti panda mti, lakini nafikiri licha ya hivyo haujatiliwa maanani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna sera hii ya agizo la kupanga miti milioni 1,500,000 kwa kila Halmashauri. Ningeomba mkakati uwepo wazi wa kuangalia ni miti mingapi ambayo inaendelea kukua baada ya kupanda, tusiwe tunasema takwimu tu badala ya kufuatilia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mapato; ili nchi yetu iweze kuendelea naomba sana isimamie mapato ya ndani na mapato ya nje ili kusudi tuweze kupata fedha za kutosha kuendeleza nchi yetu. Kwa upande uanzishaji wa Mji wa kilimo (The Agricultural Center) ambayo itakuwa Mkulazi kwa upande Morogoro, naomba mpango huu uangaliwe wananchi hawa wa Morogoro Kusini watafaidikaje na huu mradi wa Agricultural Centre City ambao utakuwa Mkulazi, hasa kwa upande wa Wanawake na Vijana ili kusudi waweze kufaidika kwenye huu Mji wa Kilimo ambao utakuwa pale Mkulazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa reli ya kati; kama ni reli ya kati ya ujenzi naomba kweli iwe reli ya kati. Tunavyoelewa reli ya kati inaanzia Dar es Salaam, Tabora mpaka Mwanza, halafu Tabora mpaka Kigoma na michepuko mingine. Kwa hiyo, reli ya kati iangaliwe kujengwa kwa gauge ambayo imesemwa ili kusudi wananchi waweze kufaidika pamoja na mizigo iweze kupitiwa kwenye reli siyo kwenye barabara, kwa sababu ikipita kwenye barabara hii mizigo mikubwa inaharibu barabara zetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Morogoro, pia tunatumia reli ya TAZARA, naomba iangaliwe kwa sababu kutoka Dar es Salaam kuja Kisaki, mpaka Ifakara, Mlimba, Tanganyika Masagati tunatumia reli hii na Mkoa wa Morogoro ni mkoa wa kilimo, reli hii ya TAZARA inafaa kwa kusafirisha mazao yetu yaweze kuinua Mkoa wetu wa Morogoro.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa nishati; kama unavyojua Morogoro kweli ina vyanzo viwili vya nishati ambavyo ni Kihansi pamoja na Kidatu, lakini mpaka sasa hivi vijiji vingi vya Mkoa wa Morogoro havina umeme. Namshukuru Mheshimiwa Waziri Profesa Muhongo amejitahidi lakini bado hatujapata umeme wa kutosha, kwa hiyo naomba tuweze kuliangalia Mkoa wa morogoro tuweze kupewa umeme.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ardhi; kwa upande wa kupima ardhi pamoja na umilikishaji, pamoja na kutoa hatimiliki. Mheshimiwa Waziri Lukuvi amejitahidi na ameanza vizuri, naomba aendelee kwa sababu upimaji wa ardhi unasaidia sana kupunguza migogoro ya ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukija upande wa Morogoro kwa upande wa wafugaji na wakulima, kwa kweli tuna tatizo kwenye Wilaya zetu za Morogoro hususani Mvemero, pamoja na Kilosa, Morogoro Vijijini na Kilombero wote kwa pamoja, kwa hiyo, naomba tuweze kuiangalia hiyo kusudi tuweze kupima ardhi yote na kuwamilikisha wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo; nikija kwenye upande wa kilimo, Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa kilimo na wanawake ndiyo wakulima kweli, asilimia 70 ya chakula inayotolewa nchini kwetu inazalishwa na wanawake, kwa hiyo, naomba upande wa pembejeo, kwa upande wa Serikali naomba huu mfumo unaotumiwa wa kutoa ruzuku uweze kuangaliwa kusudi uanzishwe mfumo mwingine kama itawezekana wa kuweka pembejeo mwaka mzima lakini kwa kuweka bei elekezi ambayo kila mkulima aweze kuipata kwa wakati wake anaotaka.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Maafisa Ugani; tuna Vyuo vingi vya LITA, vya LITI, Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, wanatoa Maafisa Ugani, ninashauri hawa Maafisa Ugani waweze kuajiriwa mara moja.
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa .
MHE. DKT CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru sana kupata nafasi hii kuchangia angalau kwa maandishi. Nitoe pongezi kwa Waziri na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Naomba kwanza kabisa kuchangia kuhusu umri wa Wahadhiri wa Vyuo Vikuu na hasa Maprofesa wanaofundisha masomo ya science; ni kweli namwomba Mheshimiwa Waziri, Serikali iongeze umri wa kustaafu kwa Wahadhiri wanaofundisha masomo au course za science mpaka miaka 70 au 75 badala ya miaka 60.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa sababu ni tabu kuwapata Walimu hawa wa science katika vyuo vikuu vyetu. Pili, Walimu hawa wanapostaafu kwa mujibu wa Sheria wakiwa na miaka 60 wanakuwa bado wanazo nguvu na afya nzuri na bado wanahitajika katika idara na hata vyuoni mwao. Kiasi wengine wengi kupitia kwenye uhitaji, chuo kinalazimika Mwalimu aendelee kufundisha kwa mkataba wa miaka miwili miwili. Naomba Mheshimiwa Waziri alione hili la kuongeza umri wa kustaafu kutoka miaka 60 mpaka miaka 70, madarasa ya awali yaangaliwe na kusimamiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, msingi wa mwanafunzi kuendelea na kupata elimu nzuri ni darasa la awali, mishahara ya Walimu hawa wa madarasa au shule za awali iangaliwe, Walimu hawa wapate mishahara yao waliyopangiwa kufuatana na daraja lao la ualimu kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. Urudishaji wa hela zilizokopwa na wanafunzi zirudishwe kwa wakati na mara hapo mkopaji na mhitimu wa chuo anapopata kazi, kujiajiri au kuajiriwa kwa mkakati wa wazi na mzuri wa kurudisha hela hizi, kusudi wakopeshe wanafunzi wengine kwani wahitaji ni wengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri somo la ujasiriamali litiliwe mkazo kuanzia secondari hadi vyuo vikuu ili vijana waweze kujiajiri kwenye fani mbalimbali bila matatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwasababu ni dakika tano nitachangia haraka haraka na nitaanza kwa kuchangia mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mazingira yetu yameharibika, na sana sana yameharibika kwasababu ya mkaa pamoja na ukataji wa kuni. Watu wote mnajua kuwa Mkoa wetu wa Morogoro, Mkoa wa Pwani na nchi nzima ya tanzania kwa wastani, mara unapopita utakuta mkaa na utakuta kuni. Kwa hiyo, naomba mikakati iwekwe pamoja na Ofisi ya Makamu wa Rais kuona kuwa itafanyaje ili kuweza kutafuta nishati mbadala badala ya kutumia kuni au kutumia mkaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni karibu asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mkaa na Dar es Salaam tu wanatumia mkaa magunia 200,000 mpaka 300,000. Kwa hiyo, naomba sana hii iweze kupewa kipaumbele kwa kuwa inaleta jangwa, joto, mvua hatupati na tabia nchi inabadilika. Kwa hiyo, naomba itiliwe mkazo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu viwanda. Nashukuru Mheshimiwa Waziri kwa kuwa tutakuwa na kiwanda cha sukari Mkulazi lakini ijulikane kuwa viwanda vingi vya Mkoa wa Morogoro havifanyi kazi. Nilikuwa nakuomba tuone jinsi ya kufufua hivi viwanda viweze kufanya kazi, Mkoa wa Morogoro ulikuwa ni mkoa wa viwanda lakini sasa hivi havifanyi kazi. Ni vizuri tuna Kiwanda cha Maji Udzungwa kinafanya kazi, Kiwanda cha Tumbaku kinafanya kazi lakini viwanda vikifanya kazi tutaweza kupata ajira kwa wakina mama pamoja na vijana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili viwanda viweze kufanya kazi ni lazima uwepo umeme wa uhakika, lazima yawepo maji ya uhakika na ni lazima kuwepo na malighafi na hizi malighafi lazima zitokane na kilimo. Kwa hiyo, inabidi tuangalie hayo mambo na tuangalie mikakati ya kuwa na umeme wa uhakika, maji ya uhakika pamoja na kilimo cha uhakika kinachozalisha malighafi ambazo zitaweza kuendeleza viwanda vyetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa sababu umenipatia nafasi hii na ahsante sana.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru kwa Mungu kwa kuniwezesha kunipatia muda huu wa kuchangia ndani ya Bunge lako Tukufu angalau kwa maandishi. Nipende kumpatia hongera sana Mheshimiwa January Makamba, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwa kazi nzuri anayoifanya, pamoja na Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uharibifu wa mazingira na hasa matumizi ya mkaa. Nchi nzima wananchi karibu asilimia 80 wanatumia mkaa na kuni kama chanzo cha nishati. Pamoja na ukataji wa miti kwa ajili ya kuni na ujenzi Serikali ni vyema isimamie kikamilifu kuhusu uharibifu wa mazingira haya la sivyo nchi itakuwa jangwa. Mheshimiwa Waziri ni vizuri atoe tamko na kukumbusha tena wananchi na viongozi husika, kuhusu kusimamia Sheria ya Mazingira. Ni ukweli miti inapandwa, ambayo, miche 1.5 milioni kila halmashauri inapandwa, tatizo ufuatiliaji wa kuona ni mingapi inaendelea kukua kila mwaka baada ya kupanda ni tatizo, ingekuwa vizuri ufuatiliaji wa miche inapoendelea kukua ukajulikana badala ya kujali kufahamu takwimu za upandaji tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mkaa ni vizuri likaangaliwa kwa undani, ni nini kifanyike kunusuru uharibifu unaojitokeza, ukataji miti kwa kibali uendelee kusimamiwa kwa muda wote na viongozi husika. Elimu kwa wananchi izidi kutolewa kuhusu utunzaji wa mazingira. Bado uharibifu wa vyanzo vya maji unaendelea licha ya mikakati yote ya Serikali ya kukabiliana na tatizo hili, ni vyema Sheria ya Mazingira ifuatwe na kusimamiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, uharibifu wa vyanzo vya maji unasababisha uhaba wa maji, mabadiliko ya tabia nchi, upungufu wa rutuba ya ardhi na matatizo mengi zaidi ya uharibifu wa ardhi. Uharibifu wa vyanzo vya maji na mazingira kuhusu milima ya Uluguru Mkoani Morogoro, wataalam wa SUA wamejitahidi katika mapando ya kuhifadhi milima hiyo lakini tatizo bado lipo pale pale. Kilimo kisichokuwa na tija na ujenzi wa nyumba kama makazi ya wananchi vinaendelea katika milima hiyo, vyanzo vya maji vimekauka kiasi wananchi wa Morogoro Manispaa hawapati maji ya kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Serikali yangu sikivu, iweke mkakati maalum wa kunusuru milima hii ya Uluguru ili hali yake ya uoto, kijani na utiririshaji wa maji (mito) irudie kama ilivyokuwa miaka ya 80. Serikali kuu kwa kushirikiana na Halmashauri ya Manispaa naamini inawezekana kurudisha hali ya milima ya Uluguru ilivyokuwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna uharibifu wa mazingira unaotokana na uchimbaji wa madini na mchanga. Nashauri sheria ndogo katika Halmashauri husika na Sheria ya Mazingira zisimamiwe na kufuatwa, wananchi waendelee kupewa elimu tosha kuhusu utunzaji wa mazingira, wananchi wa pande zote za nchi Bara na Visiwani (Tanzania) wapewe elimu ya faida za mazingira ili kudumisha Muungano wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii, pili namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi nikaongea kwenye Bunge hili kwa leo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri anayoifanya pamoja na Naibu na Wizara nzima kwa ujumla.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa naongelea kuhusu umeme wa REA nampa pongezi Mheshimiwa Waziri pamoja na Wizara nzima kwa upande wa umeme wa REA, kwa sababu umeme wa REA kwa kweli umesambaa kwenye mikao mingi na kwenye vijiji vingi. Umeme wa REA kwanza nashukuru kwa sababu pale ninapokaa nyumbani nashukuru sana Nyakayanja Nyeishonzi tumeweza kupata umeme wa REA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya shukrani hizo Mheshimiwa Waziri nakuomba sana tena sana, Mkoa wa Morogoro umejaliwa sana kuwa na mito mingi, Mkoa wa Morogoro una vyanzo vya umeme ikiwepo Kihansi pamoja na Kidatu lakini Mheshimiwa Waziri bado kuna vijiji vingi ambavyo havina umeme. Kwa hiyo, Phase I ya REA imepita, Phase II bado inaendelea, Phase III naomba mwezi wa saba ukianza naomba uweze kutupatia umeme kwenye vijiji hivi ambavyo havijapata umeme kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro Vijijini, Kilombero pamoja na Mlimba, Ulanga, na Malinyi naomba uwape kipaumbele kwa sababu ndiyo wana vyanzo vikubwa vya umeme. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna nishati mbadala, nimeona kuwa utaipa kipaumbele, naomba sana uzidi kuipa kipaumbele kwa nishati mbadala au jadidi, kwa mfano biogas. Biogas ni rahisi hasa kwa wafugaji, biogas ni kitu rahisi ambacho kila mmoja anaweza akatumia, ni initial costs ambazo ndiyo kazi. Kwa hiyo, biomass pia, umeme wa jua, umeme wa maji, nguvu za maji na upepo kwa mfano Singida pamoja na Makambako ambao tayari ilishaainisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana uviangalie na hasa kwa sababu ukichukulia kuwa kutokana na tabia nchi na uharibifu wa mazingira watu wameanza kukata miti na kutakuwa jangwa. Lakini kama tutatumia hivi vyanzo ambavyo ni rafiki kwa mazingira kwa hiyo watu wataacha kutumia mambo ya mkaa na wataweza kutumia hivi vyanzo vingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Waziri naomba aangalie kuhusu bei ya umeme. Najua amesema inateremka lakini naomba iweze kuteremka zaidi. Pia gesi za kutumia nyumbani na zenyewe ni nishati, bei iko juu, naomba pia iweze kuteremka kwa sababu ikizidi kuteremka wananchi wengi wataweza kutumia hiyo gesi na wataweza kuacha kuharibu mazingira kwa kuchoma mkaa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee mapato hasa mimi naongelea kwa upande wa vituo vya mafuta. Nimefanya utafiti mdogo kuhusu vituo vya mafuta, vituo vya mafuta tumeweka mashine, zile unapoweka mafuta zinakata risiti. Nashukuru kuna zile ambazo zinafanya automatic hata ukiweka lita moja unapata risiti yako, lakini kuna vituo mbalimbali ambavyo hizo mashine hazifanyi kazi na hao wanaouza mafuta wanafanya makusudi wengine hawazitumii hizo mashine na wengine wanatumia vitabu ambavyo mapato yetu hatuyapati kwa urahisi na wengine watu hawajawa na utaratibu wa kuomba hizo risiti kwa hiyo tunazidi kupoteza mapato. Kwa hiyo, naomba elimu itolewe na ufuatiliaji uweze kufuatiwa kusudi tuweze kupata mapato ya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi kwa Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa Profesa Muhongo ambaye nimeshampa hongera, naomba sana wakati pale unajumuisha ingawaje hujatupatia orodha ya vijiji ambavyo vitapatiwa umeme kwenye mikoa yote wakati wa Phase III inayokuja, mimi nakuomba sana uweze kutupatia hiyo orodha ya vijiji ili tuweze kufuatilia na kuona na kuwaambia watu wetu kuwa umeme unakuja kaeni tayari. Hiyo ni nguvu zote na jitihada zote za Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wachimbaji wadogo wadogo, nilikuwa naongelea kuhusu wachimbaji wadogo wadogo. Nakushuru Mheshimiwa Waziri umesema kuwa umewatengea maeneo. Lakini kumbuka kuwa kila mkoa kwa wastani kuna wachimbaji wadogo wadogo, nilikuwa naleta ombi kwako Mheshimiwa Mwenyekiti kuwa Mheshimiwa Waziri aangalie hawa wachimbaji wadogo wadogo waweze kuwapatia elimu. Naelewa kila mkoa au kila kanda kuna ofisi ya madini, hawa maofisa madini wanaweza wakakaa na hawa wachimbaji wadogo wadogo wakaweza kuwapatia elimu na ninaomba na wenyewe waweze kupatiwa ruzuku pamoja waweze kununua vitendea kazi kwa sababu haya madini ukishika hovyo hovyo kwa mikono unaweza ukaungua mikono.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kwa upande wa Mkoa wangu wa Morogoro, Wilaya ya Ulanga ambayo ina madini ambayo hayo madini nashukuru nasikia wanakuja wawekezaji, lakini imeanza mgogoro na hawa wananchi wa Ulanga ambao wanachimba madini yao wanasikia kuwa hawa wawekezaji wataweza kuchukua maeneo yao na hawa wananchi wamekuwa na vitalu vyao vya muda mrefu na wengine ni kurithi.
Kwa hiyo, naomba sana kusudi kukataza hii migogoro isitokee na kuendelea tuweze kuwapa elimu na kuwatengea maeneo yao hao wananchi.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA:Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja na nakushukuru sana.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Mheshimiwa Spika,nakushukuru sana ili niweze kuhitimisha hoja niliyoitoa asubuhi ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu taarifa ya kipindi cha Mwaka mzima ambao umepita.

Mheshimiwa Spika, pili naomba kuwashukuru Mawaziri tayari hoja nyingi wameshazijibu na hasa naomba kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona kwamba Tume ya Mipango amekubali iweze kuanzishwa, tunamshukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Wabunge wengi wamechangia ambao Wabunge 17 wameweza kuchangia hoja yetu ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji lakini kwa sababu ya muda sio lazima niwataje majina kwa sababu mmewaona.

Mheshimiwa Spika, kuna hoja kubwa ambazo zimeweza kuongelewa ikiwepo TAFICO kuwa bajeti ziweze kutolewa kwenye Taasisi mbalimbali ikiwemo TAFICO pamoja na taasisi mbalimbali za Wizara yetu ya Kilimo, Mifugo na Maji ziweze kutolewa fedha.

Mheshimiwa Spika, hoja kutoka kwenye Wizara ya Kilimo, Mheshimiwa Waziri Bashe ameweza kuitolea ufafanuzi na Mheshimiwa Waziri wa Fedha ameweza kuitolea ufafanuzi. Lakini hata hivyo bado Kamati tunasisitiza kuwa mtiririko wa fedha uweze kutolewa kwa wakati. Kwa hiyo, Serikali iweze kufuatilia kwa sababu huwa wananchi wanataka kuona mambo yanatendeka kwa hiyo mtiririko ukifuatiwa pamoja na certificate na nini naamini vitaweza kutolewa na ushauri utaweza kutolewa. Bado Kamati inasisitiza hivyo na muuliza swali ambaye ambaye walikuwa wanataka ufahamu bado tunasisitiza hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfumuko wa bei nao nashukuru kwa sababu tayari umeshafafanuliwa na Waheshimiwa Mawaziri, lakini tunashauri kuwa Serikali iweze kuungalia vizuri sana kusudi wananchi waweze kupata unafuu kwenye huu mfumuko wa bei ambao unaendelea.

Mheshimiwa Spika, suala la mbolea tayari na lenyewe limefafanuliwa na Mheshimiwa Waziri husika Mheshimiwa Hussein Bashe lakini matatizo bado yapo kwa sababu usambazaji bado ni muhimu nao uweze kuangaliwa kwa sababu ili uweze kupata mazao bora ya Kilimo ambayo Wananchi wamehamasika kweli kulima, lazima uweze kutumia pembejeo bora ikiwepo mbolea pamoja na mbegu. Kwa hiyo, Kamati ilivyoshauri pamoja na Waheshimiwa Wabunge, nawashukuru. Jambo hili Serikali mlitilie maanani kama Mheshimiwa Waziri ulivyosema kuanzia Mwezi wa Nane kwa safari ijayo mbolea itakuwa imepatikana, naomba ichukuliwe hatua kama ulivyosema.

Mheshimiwa Spika,kwa upande wa malisho, ni kweli Wafugaji wanapata shida wanahama hama kwa sababu ya kutafuta malisho. Kwa hiyo, tunashauri kuwa Serikali iweze kutoa elimu kuhusu malisho na mbegu za malisho ziweze kupatikana madukani kama mambo mengine yanavyopatikana kusudi wananchi hasa wafugaji waweze kupanda malisho na kulinda malisho na hali ya Wafugaji iweze kubadilika.

Mheshimiwa Spika, jambo kubwa sana lingine lililo ongelewa ni mabadiliko ya tabia ya nchi. Mabadiliko ya Tabia ya Nchi kama Waheshimiwa Wabunge walivyosema, naomba lichukuliwe hatua kwenye uvunaji wa maji, kwenye kulinda vyanzo vya maji. Kwa upande wa Mifugo Serikali iweze kulitilia maanani na kutoa tahadhari ni nini kitatokea kama mambo hayo kusudi kulinda athari ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya Mabadiliko ya Tabia ya Nchi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililotokea ni kuajiri Wafanyakazi wa Sekta hizi tunazo ziwasilisha hasa kwenye taasisi. Ili ufanye kazi vizuri na matokeo ya kazi yaonekane ni lazima ikama ya wafanyakazi iweze kuonekana. Kwa hiyo, vibali viwe vinatolewa viendane na bajeti kusudi wafanyakazi wanaotakiwa waweze kuajiriwa ili kuweza kutoa matokeo mazuri kwenye taasisi na Serikali yetu.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu NARCO au Ranch zimeongelewa. Naomba sana kama Wabunge walivyosema isiwepo mabadiliko ya kusema kubadilisha Ranch kupeleka kwenye mambo mengine kama ya kilimo. Kama ni Ranch imepangwa kwa Mifugo iangaliwe jinsi ya kuboresha kusudi tuweze kupata mifugo ya kutosha kwenye Ranch zetu. Vitalu na vyenyewe viweze kutolewa hasa kwa wananchi waliokaribu na hivyo ili waweze kupata vitalu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kilimo cha umwagiliaji sio tegemezi cha mvua na chenyewe kimeongelewa pamoja na scheme ndogondogo ziweze kufanyika Scheme kubwa. Hata hivyo Mheshimiwa Waziri ameweza kufafanua kuwa Fedha za umwagiliaji zipo na ninaamini kuwa Scheme nyingi zimeanzishwa ziweze kuangaliwa kwa umakini kusudi tuweze kuona kuwa Kilimo cha Umwagiliaji kinafanya kazi na hata kwenye Vituo vya mbegu tuweze kuzalisha mbegu kwa wingi kusudi tuweze kujitegemea. Kwani mpaka sasa hivi kama Wabunge walivyosema na Kamati imeona hivyo hivyo kuwa ni asilimia zaidi ya 60 mpaka sasa hivi ambayo Tanzania hatujitegemei tunapata hizi mbegu kutoka nje.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililoongelewa sana ni Uvuvi haramu, naomba Wizara husika iliangalie ili kukomesha Uvuvi haramu.Tukiendelea na Uvuvi haramu hatuwezi kupata Samaki na sisi Samaki ni lishe, Samaki ni kitoweo na Samaki ni fedha. Kwa hiyo, hilo nalo kama Wabunge walivyosema Wizara inayohusika naomba litilie maanani pamoja na matumizi ya Timba na Makokoro na Taa za Solar nazo zimeongelewa kwa wingi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililosemwa ni mbegu. Je tunaweza tukapata mbegu za mazao mwaka ujao? Mheshimiwa Waziri amelifafanua sina tatizo ya kulisemea kwa sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililoongelewa kwa wingi ni pongezi. Tumetoa pongezi, Kamati imetoa, Waheshimiwa Wabunge wametoa pongezi kwa DAWASA pamoja na Wizara ya Maji jinsi walivyokabiliana na tatizo la maji kule Dar Es Salaam. Kwa hiyo, nazidi kuwapongeza kuwa pongezi hizi zifike na muendelee kufanya hivyohivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine lililoongelewa ni Sekta ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi vituo atamizi kwa ajira ya vijana. Mheshimiwa Waziri ameweza kufafanua kuwa vipo vituo ambavyo vijana wanabidi waweze kuajiriwa na wenyewe Wizara ya Kilimo watume applications kusudi waweze kuajiriwa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni mazao ya bustani nayo yameongelewa, lakini haya mazao ya bustani yanaendana na usafirishaji ambao bado ni tatizo kwa hiyo, tumeshauri na Wabunge wameshauri kuwa Bandari na Viwanja vya Ndege viweze kuwa na green belt maana yake ni nini viwepo vitu vya kupoozea mazao kama haya ya bustani pamoja na uchakataji ambao utakuwa hapo karibu karibu na miundombinu ya usafirishaji iweze kwenda vizuri.

Mheshimiwa Spika, naamini na Serikali imelichukua na ninashauri kuwa Serikali imeji-commit hapa hapa Wizara zote tatu zimesema kuwa ushauri wa Kamati wameuchukua na wataufanyia kazi. Jambo muhimu sana ni kulinda vyanzo vya maji ambavyo tayari Wabunge wamesema sana na Kamati imesema kusudi kutokana na matatizo ya ukosefu wa maji na kuharibu na mambo ya mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mheshimiwa Spika, mtiririko wa fedha tayari nimeshaongelea, tafadhari tunaomba sana hazina pamoja na Wizara mkiwaambia watu kuwa fedha zipo hawaelewi kwa hiyo, tunaomba mkazo uweze kuangaliwa kusudi hatua inayokwenda na hatua inayofuatiwa iweze kufuatiwa kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, Utambuzi wa Mifugo; lilisitishwa jambo hili la utambuzi wa mifugo lakini limejitokeza humu Bungeni na kwenye Kamati kuwa ili tuweze kujua mifugo ni kiasi gani na idadi gani na mifugo hii ni ya nani, jambo la heleni liweze kuangaliwa tena kusudi tuweze kutambua mifugo tuliyonayo.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naweza kugusia ni kuhusu Ushirikiano wa Kiwizara hasa kwenye mambo mnayofanya kwa pamoja. Tumeongelea kuhusu ujenzi wa Mabwawa nalo limechukuliwa naamini Mheshimiwa Waziri Ndaki ametolea ufafanuzi kuwa walishakaa na tunaomba litendeke sio kila Wizara inajifanyia kuona uhai kusudi tuweze kuwa na uhai.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni Sera ambalo na lenyewe limefafanuliwa hapa. Sera ya ushirika Mheshimiwa Simbachawene amelifafanua vizuri.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ulilotaka kujua ni udumavu wa Samaki wa Mtera na uzuri wake kuwa na sisi tunaokula Samaki hao, tunaweza kuwa wadumavu? Kama umeshapitia stage ya udumavu ni kitu kingine lakini kama kuna chemicals nayo ni kitu kingine kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri amesema atalifanyia kazi na tayari amesha wa-assign watu wa TAFICO kulifanyia kazi na utafiti. Tunaomba sana lifanyiwe utafiti haraka sana.

Mheshimiwa Spika, mambo hayo mengi ndio yaliyojitokeza na ninashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kuchangia vizuri hoja yetu ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji. Kwa hiyo, nawashukuru sana na wengi wameunga mikono, nasema ahsante, nahitimisha hoja hii nikisema kuwa natoa hoja na ninaomba Bunge zima liweze kuunga hoja hii kusudi iweze kupita. Ahsante sana nawashukuru. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia katika bajeti hii. Kwanza kabisa, nikupe pongezi kwa kukiendesha vizuri Kiti hicho. Naomba sana kisimamie, endelea na msimamo wako huo huo na Mwenyezi Mungu azidi kukuongoza, kila siku uwe pale pale, nakuombea Mwenyezi Mungu akutangulie katika kukalia Kiti hicho.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, pili, naomba kumpongeza Waziri pamoja na Naibu wake kwa kutuletea bajeti nzuri. Nawapongeza Wizara na Serikali kwa sababu hii bajeti ni nzuri, inajielekeza kutatua kero za wananchi. Pia naipongeza Serikali kwa kutenga asilimia 40 za bajeti nzima kwenda kwenye miradi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo muhimu naomba sana hizi hela zipatikane kwa sababu zikipatikana zitafanya kazi muhimu kama ilivyopangwa. Uzoefu uliokwishajitokeza ni kuwa tunapitisha hela nyingi za kufanya mipango kama ilivyopangwa vizuri sana lakini hela hazipatikani kama tulivyopanga na haziendi maeneo husika kama tulivyopanga na kufanya miradi ya maendeleo kutotekelezwa kama tulivyopanga. Bajeti hii ni nzuri sana kwa sababu ina ongezeko la asilimia 31. Shilingi trilioni 29.5 zikitumika vizuri naamini kuwa kero za wananchi zitaweza kutatuliwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naomba kuliongelea ni kuhusu shilingi milioni 50 ambazo zitapelekwa kwa kila kijiji na kila mtaa. Namwomba Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anajumuisha aweze kufafanua vizuri hizi shilingi milioni 50 zinakwenda kwenye vijiji au mitaa? Kwa sababu kwenye hotuba yake alisema kwenye vijiji lakini kwenye ahadi za Mheshimiwa Rais alisema zinakwenda kwenye vijiji pamoja na mitaa na sisi wananchi wetu tumewaambia kuwa hela zinakuja shilingi milioni 50 kwenye vijiji na kwa kila mtaa. Naomba awaelezee vizuri, kama tunaanza kwenye vijiji sawa, kama tunaendelea na mitaa sawa lakini wananchi wetu waweze kuelewa hizi hela zinakwenda wapi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, nashukuru kwa sababu zinaelekezwa kwa vikundi vya vijana pamoja na vikundi vya akinamama kama mikopo. Ninachoomba iwe revolving fund (hela mzunguko) kusudi watakaorudisha ziweze kukopwa na watu wengine kwenye area hiyo hiyo bila ya kurudishwa Serikalini.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni kuhusu kampeni za Mheshimiwa Rais na kati ya mambo aliyoyasemea ni maji. Alisema wanawake waache kubeba ndoo lakini mpaka sasa hivi wanawake bado wanabeba ndoo. Kwa hiyo, tunaomba hii bajeti ya 2016/2017 iweze kutatua jambo hili la kubeba maji hasa wanawake, waweze kuacha kubeba maji vichwani mwao na wenyewe wachane nywele zao na kufanya kazi nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kamati yetu ya Maji na Kilimo iliongelea kuhusu tozo ya Sh. 50 iweze kuongezeka kwenda kwenye Sh.100 hasa kwenye mafuta kwa kila lita ya diesel na petrol. Hata hivyo, kwenye bajeti ya Mheshimiwa Waziri haipo, naomba sana Mheshimiwa Waziri akubaliane na sisi kusudi huo Mfuko wa Maji uweze kutuna kusudi hela zitakazopatikana ziweze kupeleka maji vijijini pamoja na hela zingine tulikuwa tumesema bilioni 30 ziweze kwenda kwenye kujenga zahanati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ninalopenda kuongelea ni afya. Wewe na Wabunge wenzangu mnakubaliana kuwa ni kweli vituo vya afya vimejengwa katika kila kata na zahanati zimejengwa lakini mpaka sasa hivi nyingi ni maboma. Wilaya ya Ulanga, Mbagamao ina zahanati ambayo bado haijakamilika mpaka sasa hivi. Hivi ninavyoongea sasa hivi kwa mfano kule Morogoro Vijijini, hatuna Hospitali ya Wilaya.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuondoa tatizo la vifo vya akinamama na watoto tunaomba sana hii ahadi iweze kutekelezwa hasa yale maboma ambayo yameshajengwa yaweze kukamilika ili yawe vituo vya afya, zahanati na hospitali. Pia tunaomba sana kwa akinamama, kuna wale wanaopata matatizo ya kujifungua, theatre ziwepo ili waweze kupata msaada wa kujifungua na kufanya operesheni kwenye vituo vya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naweza kuongelea ni kuhusu kilimo. Ili tupate viwanda lazima tuwe na kilimo, umeme na maji. Kilimo chetu bado hakijatengewa bajeti ya kutosha. Maazimio ya Malabo pamoja na Maputo ya kutenga asilimia 10 ya bajeti yote kwenda kwenye kilimo bado hayajatekelezwa. Asilimia 75 ya wananchi wanategemea kilimo na kilimo ndiyo kitaweza kuondoa umaskini wa Mtanzania lakini mpaka sasa hivi naona maazimio haya bado hayajatekelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hata hizo hela chache ambazo zimetengwa kwenye upande wa kilimo ziweze kwenda zote. Kilimo cha umwagiliaji ndiyo mkombozi wetu, tabia nchi mnaiona, nchi yetu inakuwa jangwa, miti inakatwa hovyo, naomba Mheshimiwa Waziri atenge hiyo hela iweze kwenda kwenye kilimo. Naomba sana bajeti inayokuja iweze kukipa kipaumbele kilimo kwa sababu Watanzania wanategemea sana kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa viwanda, viwanda vingi vya Morogoro vimekufa. Kuna mikoa ambayo imetajwa kuwa ni ya viwanda lakini hapo mwanzoni hata Morogoro ilikuwa ni mkoa wa viwanda. Tulikuwa na viwanda 11 mpaka sasa hivi yapata kama viwanda nane vyote vimekufa havifanyi kazi, inakuwaje? Naomba sana hivi viwanda kama alivyosema kwenye bajeti viweze kufufuliwa na viweze kufanya kazi. Kwa mfano, kiwanda cha Moproco, kiwanda cha ngozi na viwanda vingine vyote viweze kufanya kazi kusudi akinamama na vijana waweze kupata kazi ya kuajiriwa kwenye viwanda hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu elimu, hapa kuna ukarabati na ujenzi wa vyuo vikuu, Serikali tunaongeza vyuo ni vizuri sana lakini vyuo vikuu vile vya zamani kama SUA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam viweze kukarabatiwa ili viweze kuendelea vizuri ndiyo na vyuo vikuu vingine viweze kujengwa. Naona zimeanzishwa degree programs, kwa mfano University of Dar es Salaam wameanzisha digrii ya kilimo, je, wana Walimu? Imeanzishwa digrii ya medicine, kuna Muhimbili na Mloganzila imeshajizatiti sawasawa?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali yetu iangalie kwanza vitu vile vilivyokuwepo ndiyo tuweze kuanzisha vingine. Kwa hiyo, naomba hivyo vyuo nilivyovisema viweze kukarabatiwa na miundombinu iweze kuangaliwa. Pia hela za maendeleo hazijapelekwa mpaka hivi ninavyosema…
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana ingawa muda ulikuwa mdogo sana. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Bungeni kwa maandishi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili natoa hongera sana kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara kwa kazi kubwa wanayoifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu misitu. Nashauri uwepo mkakati kabambe wa kutunza misitu yetu. Itungwe sheria ya kuwabana wananchi waache kukata miti hovyo hovyo. Misitu inakatwa kwa matumizi mbalimbali kama nishati (mkaa), ujenzi na pia kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya kata mti panda mti ipo, je, inafuatiliwa? Pia kila Halmashauri kupanda miche ya miti milioni 1.5 kwa mwaka, hivi ni kweli inafuatiliwa sawasawa kuona kuwa miche inayopandwa na ile inayostawi ni asilimia ngapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu asilimia 90 ya Watanzania wanatumia mkaa kama chanzo cha nishati (utafiti umefanyika). Nashauri kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini uangaliwe mkakati kabambe wa kupunguza kutumia mkaa kama chanzo cha nishati badala yake wananchi watumie nishati mbadala na nafuu. Tusipoangalia nchi yetu itakuwa jangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili vyanzo vya maji vitazidi kuharibika na maji yatakauka. Nashauri uwepo mpango kamili wa kunusuru misitu yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, majangili wamezidi kuua wanyama na hasa tembo katika hifadhi zetu na hasa Ruaha, Selous na hata Mikumi. Tembo wanauawa, kilio cha tembo, tembo wachanga wanabaki yatima. Nashauri waajiriwe askari wa kutosha kusudi waweze kunusuru tatizo hili la majangili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba Waziri aweke mikakati kabambe ya kukomesha ujangili huu na hasa ujangili wa tembo. Serikali iangalie sana chanzo cha kuua tembo na kuchukua meno ya tembo hasa ni nini na ni akina nani wapo nyuma ya ujangili huu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, chini ya uongozi wa Awamu ya Tano naomba jambo hili lifanyiwe kazi, atakayebainika yuko nyuma ya biashara hizi achukuliwe hatua kali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu utalii uzidi kutiliwa maanani ili nchi yetu ipate mapato zaidi. Nchi kama Israel uchumi wake unaendelea kuwa mzuri kwa sababu ya utalii, na baadhi ya nchi nyingine. Nchi yetu ni nzuri, inavyo vivutio vingi vya utalii kila kanda na kila mkoa. Ni kwa nini vivutio vya nchi yetu havitangazwi na hasa Kanda ya Kusini, Kanda ya Mashariki na Kanda ya Ziwa? Vyanzo vizidi kutangazwa kama utalii wa Kaskazini unavyotangazwa. Namna hii tutaweza kupata watalii wengi katika nchi yetu na pato la nchi kupitia utalii litazidi kukua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mahoteli katika hifadhi zetu za wanyama zingine hazifanyi kazi, zimeachwa tu. Mheshimiwa Waziri kuna hoteli ambayo ilikuwa nzuri sana kwa muonekano na kwa huduma kwa watalii wa ndani na nje katika Hifadhi ya Wanyama Mikumi, lakini imeachwa kama gofu ndani ya hifadhi. Naomba sana Mheshimiwa Waziri anieleze kuna mkakati gani wa kufufua na kuendeleza hoteli hii ambayo ilikuwa inatoa huduma nzuri kwa watalii?
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara iangalie migogoro inayotokea kati ya wafugaji na wakulima na hasa mifugo kutoka nchi jirani kuingia kwenye misitu inayozunguka Wilaya ya Karagwe. Mheshimiwa Waziri kwa kushirikiana na Wizara husika zingatieni matumizi bora ya ardhi. Migogoro si mizuri katika maisha ya binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia.

Kwanza kabisa nitoe pongezi kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri wanayoifanya kwa kutunza amani. Pili, nashukuru sana na natoa pongezi kwa viongozi wote waliotangulia na waliopo kwa kutunza amani ya nchi yetu kwa sababu nchi ya Tanzania licha ya matatizo mbalimbali yaliyopo lakini bado ina amani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine naomba sana tena sana na nashukuru tuwe na amani na utulivu humu Bungeni mara tunapochangia hoja zetu Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naomba kuchangia ni Wabunge wote tuweze wakati wowote tunapochangia tuweze kufuata Kanuni, Sheria na Taratibu za Bunge. Tukiweza kufuata Kanuni, Sheria na Taratibu za Bunge halitajitokeza tatizo lolote humu Bungeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine lililoongelewa kwenye Kamati nasi wenyewe tunaliongelea hasa Wabunge wote naamini wataafiki ni Wabunge wote kupewa semina kuhusu mambo ya Kanuni, kwa sababu Wabunge wote wakipewa semina kuhusu mambo ya Kanuni Kiti kitakachokuwa kimekaa hapo ulipokaa naamini hakitasumbuliwa kwa sababu wote wataheshimu Kanuni na Taratibu za Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo lilikuwa linasumbua ni Shahidi kuitwa alafu Shahidi haonekani. Ili utunze amani na utulivu na haki ya binadamu unapoitwa kwenye Kamati ya Maadili ni vizuri uheshimu, ufike kwa wakati muafaka ambao unapangiwa, kuliko kuanza kutumiwa Polisi kukamatwa siyo vizuri. Kwa hiyo, naomba kuwa licha ya Wabunge kupewa Semina naamini kuwa tutafuata Kanuni na Taratibu za Bunge kuweza kufika kwa wakati muafaka.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa jinsi unavyoendesha Bunge wewe mwenyewe na Wabunge tukifata, narudia tena tukifata Kanuni na Sheria na Taratibu za Bunge na upendo ukitawala humu Bungeni tutakuwa na amani na utulivu mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niongee hayo, ila kwa kumalizia nirudie kuwashukuru na kuwapa pongezi vyombo vya ulinzi kwani hivi karibuni lilikuwepo wimbi la watoto kupotea kwenye mazingira ya kutatanisha, ila nashukuru sasa hivi naona wimbi hili la watoto kupotea limepungua. Kwa hiyo, hii inadhihirisha kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo machache naunga mkono hoja, namalizia kwa kusema kuwa naomba tufuate Kanuni, Taratibu na Sheria za Bunge tutaendesha vizuri Bunge letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo; na Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) pamoja na Maoni na Mapendekezo yaliyomo katika Taarifa hiyo
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia hii nafasi. Kwanza kabisa nianze kwa kuwapa hongera Kamati zote mbili kwa kazi kubwa waliyoifanya.
Mheshimiwa Naibu Spika, naanza kwa kuchangia juu ya asilimia 10 ya fedha za akinamama pamoja na vijana. Ni kweli Halmashauri nyingi hawapeleki fedha hizi kwa kina mama. Ningeshauri kuwa hizi asilimia ziwe zinapelekwa kwa akinamama kusudi waweze kufanyia biashara zao na vijana pia waweze kufanyia kazi zao kwa sababu hizi fedha zinasaidia katika ajira. Watanzania wote tunafahamu kuwa ajira ni matatizo sasa hivi, kwa hiyo, hizi fedha zingesaidia kwenye ajira ya akinamama pamoja na vijana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri kwa Serikali kuwa walisimamie kusudi hizi fedha ziweze kupelekwa kwa walengwa ambao ni akinamama pamoja na vijana. Pia na mimi naongelea kuhusu hii asilimia 20 ya ruzuku ya Serikali Kuu kutopelekwa kwenye vijiji pamoja na mitaa. Naungana pamoja na Kamati kama inawezekana zipelekwe moja kwa moja kwenye vijiji pamoja na mitaa yetu, kwa sababu hazipelekwi kwenye Halmashauri.
Mheshimiwa Naibu Spika, naongelea kuhusu fedha za maendeleo ambazo kusema ukweli zinachelewa kupelekwa na wakati mwingine hazipelekwi kabisa. Tunawalaumu kweli Wakurugenzi, lakini unakuta kuwa hizi fedha wakati mwingine hazipelekwi kiasi kuwa miradi inasimama.
Mheshimiwa Naibu Spika, akinamama bado wanateka maji kwa sababu miradi ya maji bado haijaendelezwa. Barabara zimesimama huko kwenye Halmashauri zetu kwa sababu fedha hazipo, vituo vya afya pia vimesimama; kiasi vingeweza kuboresha na kupunguza vifo vya akinamama pamoja na watoto; lakini kwa sababu fedha za maendeleo hazipelekwi na wakati mwingine hazipelekwi kwa wakati na wakati mwingine hazipelekwi kabisa. Nashauri Serikali iliangalie jambo hili la kupeleka fedha za maendeleo kwa wakati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee kuhusu Mfumo wa EPICOR. Ni kweli Halmashauri nyingine bado hawajajua vizuri kutumia mfumo huu wa EPICOR kiasi kwamba inaleta hoja kwenye mahesabu. Kwa hiyo, Halmashauri hizi ambazo bado hawajajua kutumia mfumo huu wa EPICOR, naomba sana waweze kupata elimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Ukusanyaji wa Mapato ya Ndani. Mapato ya ndani naomba Halmashauri waweze kusimamia. Imegundulika kwenye Halmashauri nyingi kuwa mapato ya ndani hayakusanywi kama inavyokusudiwa. Kwa hiyo, vyanzo vilivyopo pamoja na vyanzo vipya, Halmashauri waweze kusimamia kusudi iweze kukusanya kama inavyokusudiwa; kusudi miradi ya maendeleo iweze kutimilika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni mafunzo kwa Wakurugenzi. Ni kweli Wakurugenzi wengi wapya kweli hawajajua vizuri kazi zao. Nami naungana na Kamati kuwa waweze kupewa semina ya jinsi ya kufanya kazi zao ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kukaimu; nimekaa huko kwenye mikoa na kweli kukaimu kwa muda hakuna tija. Naomba Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI aliangalie hili, kama mtu ameshakaimu kwa muda mrefu aweze kupitishwa kusudi aweze kushika Idara moja kwa moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mengi yameshaongelewa, kwa hiyo, naomba nimalizie kwa kusema kuhusu Walimu wa sayansi. Imeonekana kuwa Walimu wa sayansi ni tatizo kubwa, hivyo naomba sana liangaliwe, Mheshimiwa Waziri wa Elimu naomba aliangalie suala la Walimu wa sayansi liweze kushughulikiwa kusudi tuweze kupata Walimu hao, no science, no development.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja.
Azimio la Bunge la Kuridhia Ubadilishaji Hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika – Orugundu kuwa Hifadhi za Taifa
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Kwanza kabisa naunga mkono hoja ya azimio iliyopo ya kupandisha hadhi Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika Urugundu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono kwa sababu mapori haya yalikuwa yanaleta matatizo ya wananchi hasa waliozunguka mapori haya. Wakati wanaposafiri lilikuwa ni tatizo kubwa kutokana na ujangili, kutokana na watu wanaobeba silaha yaani ilikuwa ni tatizo kweli. Kwa hiyo naamini kuwa hata vijiji vyote vilivyozunguka mapori haya watakuwa wamefurahi sana, watakuwa na amani, watakuwa kwa kweli wanaona vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, kupandisha haya mapori kuwa Hifadhi ya Taifa kutasaidia kuimarisha na kupandisha utalii kwenye nchi yetu kutokana na mapori haya, kutaimarisha na kupandisha kipato cha nchi pamoja na vijiji vinavyozunguka mapori haya na kutaleta amani kwa wananchi wanaozunguka mapori haya. Kwa kweli ni jambo zuri sana na pia kwa kutumia na kuwepo kiwanja cha Ndege cha Chato kitasaidia sana kuwapeleka Watalii wataokuwa wanakwenda kwenye mapori ya hifadhi hizi kwa sababu hizi Hifadhi za Biharamulo, Burigi, Rumanyika, Ibanda zote zinazunguka Kiwanja cha Ndege cha Chato. Pia kuwepo kwa maziwa ya Victoria, Burigi na Mto Ngono kutasaidia sana watalii na kukuza utalii wa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, nafurahi na sina mengi na naamini kuwa Wabunge wote wataunga mkono na wananchio wote kwa kukuza utalii wa Magharibi na yenyewe itakuwa nzuri sana kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naunga mkono azimio hili. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa kunipatia nafasi hii. Napenda sana kujadili taarifa hizi mbili ya Nishati na Madini pamoja na taarifa ya Miundombinu. Nitaanza kwa kujadili…
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na ninaishukuru Serikali kwa kazi nzuri inayoifanya kwa upande wa Nishati na Madini.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru naomba kuwapa pongezi Wizara ya Nishati na Madini na hasa kwa upande wa umeme. Kwa umeme
wa REA wamefanya mambo mazuri sana, wamesambaza umeme vijijini na nawapongeza sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba vile vijiji ambavyo bado hawajasambaza waweze kuvisambaza, Wizara inasema kuwa kuwa Awamu ya Tatu watasambaza vijiji vyote. Kwa hiyo, naomba kweli waweze kusamba vijiji vyote kwa Awamu hiyo ya Tatu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu umeme wa TANESCO, na wenyewe wanafanya vizuri ila kuna sehemu ambazo bado umeme haujafikiwa vizuri. Kwa hiyo, sehemu ambazo bado hazijafikiwa vizuri kwa mfano Mkoa wangu wa Morogoro, kuna kata pale Manispaa hazijafikiwa
na umeme. Kwa mfano Mindu, pamoja na Kihonda na kata zingine, Kiyegeya naomba sana waangalie waweze kuipatia umeme.
Mheshimiwa Naibu Spika, umeme wa TANESCO, kwa upande wa TANESCO imeonekana kuwa wanadai, na kweli wanadai mashirika mbalimbali kwa mfano magereza, mashule na vitu vingine, kudai sio vizuri. Nilikuwa naomba sana Serikali yetu angalau iweze kupunguza hayo
madeni kwa wakati na ifikie kuwa hayo madeni yamekwisha kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa wachimbaji wadogo wale wa madini, uwekezaji tunaupenda na tunaupenda sana kusudi tuweze kuendelea nchi yetu. Ila nilikuwa naomba kwa wale wachimbaji wadogo wadogo waweze kupewa mahali na wenyewe wawekezaji waweze kuwekeza, waweze kupata mahali pa kuchimba na waweze kupewa ruzuku na hiyo ruzuka iweze kupewa kwa wakati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa bajeti, bajeti inatolewa, bajeti ya Wizara zote tunapanga vizuri, bajeti ya Wizara hii ya Nishati na Madini tumeelezwa kuwa imeandaliwa vizuri, lakini inapokuja kutolewa haitolewi kwa wakati. Kwa hiyo, naomba kuwa mtiririko wa wa fedha
wa Wizara hii uweze kutoka kwa mpangilio kusudi wananchi waweze kupata umeme wa uhakika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema kuwa Tanzania ya viwanda ndio tunayokwenda nayo. Bila ya nishati ya umeme hatuwezi kuwa na viwanda, kwa hiyo, naomba sana hasa huko vijijini umeme uweze kuwepo hata mjini tuwe na umeme wa uhakika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa miundombinu na yenyewe natoa pongezi sana kwa Wizara hii kwa sababu wameweza kutengeneza barabara nyingi za lami, nawapa pongezi, wameweza kuunganisha mikoa mbalimbali kwa barabara za lami, nawapa pongezi.
Ila nawaomba sana kwenye barabara zile ambazo miji ya mikoa haijaunganishwa kwa mfano Kigoma na Kagera na mikoa mingine, naomba sana lami iweze kutumika kusudi watu tuweze kupata usafiri kwa urahisi pamoja na kusafirisha mizigo kwa urahisi na hayo ndio maendeleo.
Serikali yetu inafanya vizuri lakini naomba iweze kufikia na mikoa hiyo ambayo bado haijafikiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa bajeti pia na yenyewe iweze kutolewa kwa wakati. Kwa upande wa makandarasi nafikiri wakiweza kulipwa kwa wakati wataweza kufanya mambo mazuri sana. Kwa hiyo, na wenyewe tuwaangalie kudai madeni ambayo hawalipwi
huwezi kuwa na moyo wa kuendelea na kazi kama hujalipwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kuongelea reli ya kati. Wananchi wengi wanasafiri na reli ya kati, wananchi wengi wanasafirisha mizigo yao na reli ya kati. Kutoharibu barabara inapendekeza hasa kusafiri na reli ya kati, kwa hiyo kujenga reli ya kati kwa standardsgauge Serikali naipa pongezi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naipa pongezi sana kwa kusaini mkataba ambao umesainiwa juzi juzi kusudi Uturuki waanze kujenga ile reli ya kati kwa standardgauge kwa kuanzia Dar es Salaam kuja mpaka Morogoro ikiwa wamu ya kwanza. Na naamini wananchi wengi watasafiri
kwa reli kwa sababu itatumia muda mfupi kama mlivyosikia kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma ni masaa mawili tutamia. Waheshimiwa Wabunge ikiisha naomba wote mtumie hii reli tuweze kuunga mkono Serikali yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mawasiliano, minara ya simu ni muhimu sana. Kuna vijiji vingi hasa Mkoa wangu wa Morogoro ambao bado hawajapata matumizi ya simu kwa sababu hakuna mawasiliano. Kwa hiyo, huo ni mfano tu, ni mikoa mingi, vijiji vingi ambayo minara
hakuna kwa hiyo mawasiliano yanakuwa hafifu. Kwa hiyo, nilikuwa naiomba Serikali, iweze kutimiza ahadi hiyo ya kupeleka mawasiliano hasa vijijini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo cha Ujenzi Morogoro. Chuo cha Ujenzi Morogoro ni kizuri sana na kinatoa wanafunzi wengi lakini hakijasajiliwa. Naomba kisajiliwe kusudi wahitimu waweze kujulikana vizuri sana naungana na Kamati na waweze kuajiriwa kwa sababu bado
tunawahitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, bandari ya Tanga, Bagamoyo na bandari zinginezo kusudi tuende na maendeleo naomba sana tuweze kutimiza na bajeti iweze kutoka ya kumaliza hizi bandari ambazo nimezitaja kwa mfano bandari ya Tanga itasaidia kusafirisha mizigo ya Mikoa ya Kaskazini pamoja na nchi jirani za huko Kenya, Uganda na nchi zinginezo.(Makofi)
Mheshimiwa Niabu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia hii nafasi ya kutoa machache na kuchangia kwenye Kamati hizi nawapa pongezi sana mmefanya kazi nzuri sana, nashukuru na naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii, ya kuongea katika Bunge lako Tukufu. Ninamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kuongea sasa hivi katika Bunge lako.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naanza kwa kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amefanya mambo mengi, mengi kweli. Katika kazi zake muda wake wote huu, ameweza kujenga barabara za lami mahali pote na kwenye majimbo yetu yote na hakuna mtu yeyote anayeuliza mwongozo, hayupo kwenye majimbo yote. Mheshimiwa Rais ameweza kuweka jiwe la msingi la reli na hiyo reli watu wote wataipanda, hakuna mtu atakayeuliza taarifa. Mheshimiwa Rais ameweza kununua ndege ambazo kila mmoja anazipanda, hakuna mtu anayesema mwongozo au taarifa. Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi imefanya mambo mengi sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pale ambapo mambo mazuri yanafanyika ni afadhali upongeze kuliko kubeza kila kitu. Huko Dar es Salam kuna mabasi ya mwendo kasi, kila mmoja anaingia hakuna mtu anayeuliza mwongozo au taarifa au swali la nyongeza, hakuna, kila mmoja anaingia. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais wetu ni kweli anafanya kazi nzuri, ameibadilisha Tanzania kwa muda mfupi, barabara hizi tulikuwa tunaziona Ulaya, flyover zinajengwa aaah, tTunamuombea maisha marefu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kuongelea daraja la mto Kilombero. Wananchi wa Morogoro tunapongeza sana, tuliteseka sana kwa kusafiri kwa kivuko kwenye mto wa Kilombero, kiasi kwamba wengine walipata matatizo. Imekuwa ukombozi kwetu sisi kuona daraja limekamilika. Daraja hili ni kiungo cha Wilaya za Kilombero, Ulanga na Wilaya ya Malinyi. Enzi za kivuko kilikuwa kinafanya kazi kwa saa 12 tu. Kwa hiyo, ukiwa na mgonjwa baada ya saa 12 na ikishindikana kutibiwa kwenye hospitali za Malinyi na Ulanga huyo mgonjwa wako anaweza akafa. Sasa hivi kwa kupata daraja hili mgonjwa anasafirishwa na anakwenda Kilombero kwenye Hospitali ya St. Francis ambayo ndio hospitali kubwa na hasa akina mama wajawazito, na kwa kuwa akina mama wengi wanajifungua usiku, kwa hiyo kuwepo daraja letu la Mto Kilombero kwa kweli ni fahari na imerahisisha usafiri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naongeza tena hapo hapo, wakulima wengi kwa pande zote mbili, upande wa Kilombero/Ifakara na upande wa Ulanga/Minepa na Lupilo; wa Ifakara wanalima mpunga Lupilo na Minepa. Sasa wanawake ndio wanaolima, unaju asilimia 70 ya wanawake ndio wanalima chakula hasa. Kwa hiyo ni ukombozi wa usafirishaji wa vyakula na kwa mwanamke hasa wa mkoa wa Morogoro na mikoa mingine. Kwa sababu Ulanga kuna madini hata watu wengine watatumia daraja hilo la Mto wa Kilombero.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo naomba niongelee reli ya kati, ambapo kilometa 200 tayari Mheshimiwa Rais ameshaweka jiwe la msingi na mkataba umeshasainiwa. Na hiyo reli inaanzia Dar es Saalam kuja Morogoro, wana Morogoro tusime nini? Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa sababu huu ni usafiri mbadala wa barabara, saa moja tu kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro. Naona hata magari yetu tutayaacha tutaanza kusafiri kwa reli. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu mkoa wetu wa Morogoro ni wakulima, wakulima wa mboga, wakulima wa matunda, wa nafaka na kweli watafaidika kwa kusafirisha mazao yao kwa kutumia hii reli. Wananchi wa Morogoro tunampenda sana na tunaishukuru Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi na Mheshimiwa Rais kwa kujenga reli ambayo itatumiwa na watu wote bila kuuliza swali la nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuongelea kuhusu barabara za mkoa wa Morogoro, napenda sana kuongelea barabara ya Dumila mpaka Kilosa. Barabara ya Dumila mpaka Kilosa kilometa 63, kuna sehemu imejengwa kwa kiwango cha lami kutoka Dumila mpaka Ludewa. Kwa kweli barabara hii ilikuwa mbaya sana, sasa hivi unaweza ukatembea usiku na gari lako dogo (saloon) ukafika mpaka Ludewa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kipande cha barabara cha kuanzia Ludewa mpaka Kilosa Mheshimiwa Waziri ambaye na mpongeza na Makatibu wake na Mheshimiwa Naibu Waziri mnafanya kazi nzuri; mmesema kuwa mkandarasi tayali anatafutwa kwa hiyo naomba hiki kipande cha barabara cha kuanzia Ludewa mpaka Kilosa kiweze kujengwa kwa muda muafaka. Kitu ambacho sikuona kwa muendelezo wa barabara hii ya Dumila mpaka Mikumi ni kuanzia Kilosa mpaka Mikumi wananchi wa jimbo la Mikumi wanauliza tutafanyaje mpaka na sisi tuweze kuendana na barabara hii kwa sababu ni wakulima wazuri.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na namshukuru Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nakishukuru sana Chama cha Mapinduzi na nasema naunga hoja asilimia mia moja, ahsante.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nawapongeza Mawaziri wote kwa kazi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naanza na Benki ya Wanawake Morogoro. Naomba kituo cha Benki ya Wanawake Morogoro kama tulivyoongea na Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, hospitali ya Wilaya ya Morogoro ni muda mrefu mimi na Mbunge wa Jimbo tulikuwa tunaongelea hii hospitali ni lini itaanza kujengwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu hospitali ya Ifakara Kibaoni, hospitali ya Ifakara Kibaoni inatumika kama ya Wilaya, lakini kuna watoto njiti (pre mature) ambao hawana chumba cha watoto njiti, wanalazwa pamoja na watoto wengine ambao mama zao wametoka kujifungua, pamoja na wale wanaoumwa. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri aweze kuona kama tunaweza kupata chumba cha watoto hawa njiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Mkoa ya Rufaa ya Morogoro hatuna X-ray, X-ray iliyopo ni mbovu. Hili jambo lilishaongelewa tulikuwa tunaomba X-ray. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kuongelea Hospitali ya Ulanga. Hospitali ya Ulanga wodi zao ni mbovu, kwa hiyo naomba iweze kuangaliwa. Hospitali ya Ulanga tuna X-ray pamoja na Utrasound lakini hatuna wataalam. Mheshimiwa Waziri naomba anisikilize, hatuna wataalam wa Hospitali ya Ulanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu lishe. Kwa upande wa lishe vyuo vikuu na vyuo vingine vinaendelea kutoa elimu ya akinamama lishe (nutrion officers). Naomba hawa nao muwatumie badala ya kutumia tu vidonge vya vitamin A. Wataalam hawa wa lishe nao pia watumieni kwa kuwaajiri kwa kusaidiana pamoja na TAMISEMI mpaka huko wilayani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maendeleo ya Jamii. Ni kweli maendeleo ya jamii yameachwa nyuma, Mheshimiwa Waziri amekazia sana kwenye mambo ya afya lakini Sekta ya Maendeleo ya Jamii ameisahau, naomba aiangalie. Vile vile na wataalam wa maendeleo ya jamii waajiriwe mpaka vijijini kwani wenyewe ndio wanaosukuma maendeleo ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Ndoa; naomba sana hii Sheria ya Ndoa, kama wenzangu walivyosema, iletwe humu Bungeni na kufanyiwa kazi kwa sababu ya kumsaidia mtoto wa kike. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bima ya Afya. Hadi kufikia Marchi ni asilimia 28 tu ndio wanaotumia Bima za Afya kama Mheshimiwa Waziri alivyosoma hotuba yake. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri aje na mkakati atafanyaje kusudi watu wote, wanawake, wanaume na vijana waweze kujiunga na Bima ya Afya kama ilivyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatana na ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi kila kata ni lazima iwe na kituo cha afya na kila kijiji lazima kiwe na zahanati na kila Wilaya lazima iwe na Hospitali. Namwomba Mheshimiwa Waziri tutekeleze hii ahadi ambayo ipo kwenye Ilani ya Chama cha
Mapinduzi kusudi tuweze kutimiza na aanze kutuambia na ni vipi atafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho wa yote naomba kuongelea jukwaa la wanawake. Namshukuru Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuanzisha Jukwaa la Wanawake. Jukwaa la Wanawake la kiuchumi ni jukwaa zuri, ambalo linaunganisha wanawake wote ambapo wanabadilishana mawazo na wanaweza kupata jinsi ya kukopa kutoka kwenye taasisi zote za kukopa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na Mwenyezi Mungu akubariki. Naunga mkono hoja.
TAARIFA YA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE KUHUSU SHAURI LA KUDHARAU NA KUDHALILISHA BUNGE LINALOMKABILI MHE. HALIMA JAMES MDEE (MB)
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naanza kwa kusema kuwa naunga mkono Azimio la Kamati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Halima amekuwa mzoefu mara kwa mara na nianze kusema kwamba Kamati imemuonea huruma kwa kumpatia vipindi viwili. Kama Mwenyekiti alivyoongea ilikuwa iwe zaidi ya hapo ila tumeona kwa sababu tunakaribia mwisho wa Bunge ndiyo akapewa vipindi viwili kwa kulidhalilisha Bunge kwa kusema kuwa ni dhaifu na yeye akiwa ni mmojawapo wa Wabunge. Kwa kweli halileti maana nzuri sana kwani angeweza kutumia njia yoyote ile kulishauri Bunge bila kusema kwenye vyombo vya habari.

Mheshimiwa Naibu spika, mimi naunga mkono na nasema kuwa Kamati kwa kweli imemhurumia la sivyo ukishapata adhabu kubwa hupaswi kupata adhabu ndogo, inabidi upate kubwa zaidi. Naunga mkono kwa vipindi viwili, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kupata muda huu kuweza kuchangia kwa maandishi. Namshukuru Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi sana kwa Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Mheshimiwa Waziri na Makamu wa Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Viumbe Vamizi. Kuhusu hasa gugu la Kongwa ambalo linaharibu malisho ya mifugo ni la muda mrefu sasa ingawaje Serikali inajitahidi kukabiliana nalo, lakini bado ni tatizo. Mheshimiwa Waziri nashauri jitihada zaidi zitumike ili kutokomeza kabisa gugu hili la Kongwa. Naomba maelezo zaidi kwa niaba ya wafugaji na Serikali na hasa kuhusu gugu hili lililoenea katika Ranch ya Kongwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu gugu karoti ambalo linaenea kwa kasi hasa Mikoa ya Kaskazini. Gugu hili ni hatari, Mheshimiwa Waziri anafahamu gugu hili linahatarisha na hasa katika kilimo mazao na malisho. Mheshimiwa Waziri ningependa kujua kwa niaba ya wakulima na wafugaji mikakati inayoendelea ya haraka ili kutokomeza gugu karoti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vyanzo vya maji na upandaji miti rafiki ya vyanzo vya maji. Natoa pongezi za jitihada zinazoendelea kunusuru vyanzo vya maji. Nashauri elimu izidi kutolewa kuhusu vyanzo vya maji na kupanda miti rafiki ili kulinda vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro tuna matatizo ya maji na hasa Halmashauri ya Morogoro Manispaa. Sababu mojawapo ikiwa ni uharibifu wa vyanzo vya maji na ukataji miti katika Milima ya Uluguru. Mheshimiwa Waziri kwa jitihada zake za kulinda mazingira, naomba akaliangalie tatizo hili, ili kunusuru vyanzo vya maji milima ya Uluguru (Morogoro) kwa madhumuni ya upatikanaji wa maji na uhai wa mito kama ilivyokuwa zamani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri kwa kulisimamia suala hili la mifuko ya karatasi. Kama Mheshimiwa Waziri alivyoelekeza kupitia kwenye mkutano (15/04/2019) na kwenye hotuba yake ya bajeti. Nashauri Mheshimiwa Waziri na watalaam wake walisimamie kwa ukamilifu ili tuweze kuondokana na tatizo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la ukataji miti na uchomaji mkaa bado ni tatizo. Elimu zaidi inatakiwa kwa wananchi kuhusu faida na hasara za kutunza mazingira, hasa kwa kupanda miti na kukata miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gunduzi kuhusu nishati mbadala na hasa zinazooneshwa wakati wa maonesho ya Siku ya Wakulima – Nane Nane zipewe kipaumbele kwa kuwaendeleza na kuwawezesha wagunduzi hawa wa nishati mbadala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo la fedha katika ofisi hii ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Nashauri fedha zote zilizoombwa wakati wa bajeti hii zitolewe kwa wakati ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja.
Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nakushukuru na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata muda huu wa kuchangia humu ndani ya Bunge lako Tukufu. Napenda kutoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, Katibu Mkuu na watendaji wa Wizara wote kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi kwa Serikali napenda kuongelea Benki ya Wanawake. Mheshimiwa Waziri uliniahidi kituo cha mikopo na mafunzo ya ujasiriamali, je, Mheshimiwa Waziri ni lini wanawake wa Mkoa wangu wa Morogoro watapata kituo hiki? Nakuomba sana Mheshimiwa Waziri, wanawake hawa hawapatiwe kituo hiki ili waweze kufaidika na mikopo inayotolewa kwa riba nafuu. Naomba tamko lako kwa hili Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya Morogoro, Wilaya hii haina hospitali, je, ni lini hospitali hii itaanza kujengwa kwa ukamilifu? Mheshimiwa Waziri naomba jibu lako wakati utakapokuwa unatoa majibu. Hospitali hii ya Wilaya itaweza kupunguza vifo vya akina mama na watoto na hasa kina mama wajawazito.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Hospitali ya Ifakara au Kibaoni namuomba Mheshimiwa Waziri ashirikiane na Waziri wa TAMISEMI kusudi matakwa ya Hospitali za Wilaya, zahanati na vituo vya afya yatimizwe. Hospitali hii ya Ifakara Kibaoni kuna tatizo ambalo linawahusu watoto ambao wanazaliwa kabla ya wakati yaani watoto njiti, (pre-mature). Hospitali hii haina chumba maalum kwa ajili ya watoto njiti. Watoto hawa njiti wanalazwa wodini pamoja na wale watoto wanaozaliwa kwa wakati (miezi tisa) na wale watoto waliozaliwa kwa ajili ya kuumwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii si nzuri kwani watoto hawa njiti wanatakiwa uangalizi wa hali ya juu. Mheshimiwa Waziri, nakuomba sana chumba cha watoto hawa njiti (pre- mature) kingejengwa haraka iwekanavyo. Pia ingawa hospitali inatumiwa kama hospitali ya Wilaya lakini ina uhaba wa wataalam, dawa na vitendea kazi pia vitendanishi.

Mheshimiwa Waziri, naomba uiangalie hospitali hii ya Ifakara Kibaoni kwa sababu hasa ya watoto hawa njiti ambao hawana chumba maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro tunaomba jengo la mortuary na theatre, x-ray iliyopo haifanyi kazi vizuri na ni ya muda mrefu. Mortuary ni ndogo pia theatre ni ndogo kufuatana na mahitaji, Mheshimiwa Waziri maombi haya ni ya muda mrefu kama hospitali ya rufaa inapaswa kuwa na x-ray inayofanya kazi vizuri, mortuary na theatre.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu elimu ya lishe, miaka ya nyuma elimu ya lishe ilikuwa inatolewa kwenye kliniki na hasa wajawazito na akina mama wanaonyonyesha. Elimu hii ilihusu vyakula vya mtoto na hasa vyakula vya kulikiza na jinsi ya kunyonyesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyuo bado vinatoa watu waliochukua nutrition, naomba tuwatumie kikamilifu licha ya matone ya vitamini A, kuweka virutubisho kwenye unga (fertification), kutoa folic acid etc. Pia Mheshimiwa Waziri tuzidi kuwatumia wataalam hawa kwa upande wa vyakula, kwa namna hii tutapunguza utapiamlo kwa ujumla na vifo vya watoto wachanga na wajawazito. Kwa kusaidiana na Wizara husika waajiriwe kila wilaya/kata mpaka vijijini wapewe vitendea kazi pia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu maendeleo ya jamii, idara hii imesahauliwa, Mheshimiwa Waziri nakuomba jitahidi kuiona na hasa Maafisa Maendeleo ni watu muhimu katika kusukuma maendeleo ya nchi na kwenye makazi yetu. Waajiriwe kimkoa/kiwilaya/kata mpaka Afisa Maendeleo wa Kijiji, namuomba Mheshimiwa Waziri aliangalie vizuri jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Bima ya Afya, mpaka Machi 2017 ni asilimia 28 tu ya Watanzania ndio wanaotuma bima ya afya. Mheshimiwa Waziri ni mkakati gani utumike hasa ili watu wote, wanawake, wanaume na vijana waweze kutumia bima ya afya kikamilifu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kila kijiji kuwe na zahanati, kila kata kuwe na kituo cha afya na kila wilaya kuwe na hospitali kwa mujibu wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Mheshimiwa Waziri naomba useme ni mkakati gani unatumika/utatumia kukamilisha matakwa haya? Naomba na ninashauri jitahidi za kusaidia Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi itimize jambo hili litapunguza vifo vya watoto na kina mama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Sheria ya Ndoa, naumuomba Mheshimiwa Waziri afanye awezavyo iletwe Bungeni. Nimuhimu sana kwa maisha ya watoto wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja .
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Viwanda na Biashara
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza natoa shukrani na sifa kwa Mwenyenzi Mungu kwa kupata nafasi hii kuweza kuchangia kwa maandishi katika Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa hongera na pongezi zangu kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Morogoro miaka ya nyuma ulikuwa mkoa wa viwanda. Hivi ninavyochangia sasa hivi, viwanda vingi vya zamani vilivyokuwa vinafanya kazi, vimekufa, havifanyi kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha hoja yake, wananchi wote hususan wa Mkoa wa Morogoro atueleze hatima ya viwanda hivi ambavyo vimekufa na havifanyi kazi tena kama Kiwanda cha Ngozi, Ceramics na Magunia.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa Serikali kwa kuanza ujenzi wa viwanda nchini Tanzania. Pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa mkakati mkubwa wa ujenzi wa viwanda. Tanzania ya viwanda inawezekana. Viwanda vingi na hasa vidogo na vya kati vimeanza kujengwa katika mikoa yetu yote ya Tanzania. Naamini hata tatizo la soko la mikunde ikiwepo mbaazi, litapatikana hivi karibuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi hizi kwa Serikali, kwani kiwanda cha mikunde/mbazi kimepewa kipaumbele, kimejengwa kiwanda cha kununua na kuchakata mikunde. Kiwanda hiki kimejengwa na wawekezaji kutoka India. Kimejengwa Kata ya Mtego wa Simba, Wilayani Morogoro Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni kuhusu Mradi wa Mchuchuma na chuma cha Liganga. Mradi huu una manufaa sana kwa nchi yetu. Umechukua muda mrefu. Ni miaka wingi sana tangu mradi huu umeanza, mpaka sasa hivi Mheshimiwa Waziri katika hotuba yake anasema, mchakato wa kupitia upya mkataba kati ya NDC na Sichuan Hongda Group unaendelea. Sasa ni muda muafaka mradi huu ufike mwisho, kusudi uweze kuianufaisha nchi yetu, waanze kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, fursa za masoko kwa wajasiliamali wadogo na wa kati, akina mama/wanawake wengi wamejikita sana katika biashara ya usindikaji, nguo na kazi za mikono.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo wanalokumbana nalo ni upatikanaji wa soko/masoko ya uhakika. Mheshimiwa Waziri mkakati wa kuwatafutia masoko kwa uwazi na uhakika ni muhimu ili kuinua uchumi wa familia zao na nchi yetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri jambo hili uliangalie sana ili kuwasidia wananchi wanaojishughulisha wakiwa na nia moja ya kuinua uchumi wa familia zao na uchumi wa nchi yetu kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyenzi Mungu aliyeniwezesha kuchangia leo japo kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri Profesa Maghembe, Naibu Waziri Mheshimiwa Engineer Makani, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote wa Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niongelee kuhusu uharibifu wa mazingira/maliasili. Serikali inajitahidi sana kutoa agizo na usimamizi wa upandaji miti, lakini baada ya kupanda, nani anafuatilia kuona kati ya miti milioni 1.5 iliyopandwa kwa mwaka ni mingapi imekufa na mingapi inaendelea kustawi kwa kila Halmashauri?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini Maafisa Misitu Mikoani na Wilayani wapo. Kwa hiyo, naomba kutoa ushauri kwa Mheshimiwa Waziri kupitia kwa Wakuu wa Mikoa watoe agizo la ufuatiliaji wa miti iliyopandwa kwa mwaka husika na ni mingapi imekufa na mingapi imeendelea kustawi? Namna hii tutaweza kuimarisha ufuatiliaji na kutoa report kwa Waziri. Pia itasaidia uwajibikaji wa upandaji miti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine kama miti yote au asilimia kubwa ya miti inayopandwa itashika na kuendelea kustawi, tutaweza kurudisha uoto na ukijani wa sura ya nchi mahali pengi Mikoani na Wilayani mwetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uharibifu ninaousema ni wa vitendo vya binadamu kwa kukata miti ovyo ovyo bila ya kibali maalum cha kuruhusiwa, ni wapi ukate? Pia kukata tu bila ya kupanda (bila ya kujali sera ya bwana misitu ya kata mti, panda mti) ni kweli wote mnajua kuwa miti nchi nzima inakatwa bila ya mpangilio, hasa katika misitu ya asili. Misitu inakwisha! Naishauri Wizara kuhimiza jambo hili hasa la kutunza miti ya kupanda miti ya asili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sina shaka na Mheshimiwa Waziri, naamini ni mtalaam wa misitu, pamoja na watalaam wake. Tafadhali naomba Mheshimiwa Waziri aokoe nchi kwa kuhimiza utunzaji wa misitu ya Tanzania. Sitaki kurudia faida moja moja ya misitu kwani najua mnajua faida zote za misitu, tatizo ni kuisimamia ili iendelee kustawi na kupunguzwa au kukatwa kwa kibali maalum kutoka Wilayani ambapo Mkuu wa Wilaya ndiye Mwenyekiti wa Kamati husika. Naamini mambo mengine yanaingiliwa na Wizara kwa Wizara tofauti. Shirikianeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miti hiyo inakatwa kwa madhumuni mawili makubwa; kuni na mkaa. Namba ya tatu ya ukataji wa milunda ni kwa sababu ya ujenzi na miti mingine inakatwa bila vibali kwa madhumini ya kutengeneza mbao. Tafadhali tafuta mbadala ya kila kimoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu asilimia 90 ya wananchi (Watanzania) wanatumia kuni na mkaa. Mheshimiwa Waziri, wewe ni mzoefu wa miaka mingi katika tasnia hii; je, tufanyeje kuokoa nchi na kupunguza au kuokoa kilio cha miti? Nashauri chekecheni vichwa watalaam, saidianeni na Katibu Mkuu, Naibu Waziri na Waziri mwenyewe kutafuta nishati mbadala ya kuni na mkaa ambayo itakuwa rafiki na wananchi wengi kama siyo wote kufuatana na aina ya nishati na mahali walipo. Kwa mfano, huu ushauri, ukiambatana na agizo na Sheria Ndogo ya Halmashauri tunaweza kushinda tatizo hili lililo mbele yetu kwa miaka yote. Kwa upande wa familia za wafugaji nashauri waelimishwe kutumia biogas kwani wanayo source.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mbali na wafugaji, pia wananchi wengine wanaofuga ng’ombe wachache au mifugo mingine nao wapewe elimu ya biogas. Wananchi wengine kwa kushirikiana na watalaam husika waelekezwe jinsi ya kutumia joto la jua (solar). Naamini ni kujipanga na kuamua, wananchi wakielekezwa ni nini cha kufanya na kubanwa na utaratibu, sera, sheria ndogo watafuata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia ya wananchi wanaotumia gas asilia ya nyumbani imeongezeka kidogo na hasa ukichanganya na asilimia ndogo sana inayotumia umeme. Tatizo kubwa ni bei. Mtungi wa gesi wa kati sasa ni kati ya shilingi 68,000; shilingi 54,000 mpaka shilingi 52,000 kufuatana na mkoa kwa mkoa. Mtungi huu ukibahatika utachukua wiki mbili au mwezi kwisha (inafuatana na wapishi na matumizi). Hivi kweli kufuatana na mishahara yetu, wangapi Watanzania wataweza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali iingilie kati kushauriana na wafanyabiashara wa gesi ya nyumbani ili bei ipangue watu wengi waweze kumudu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa umeme, sisemi kwani ni ghali zaidi. Shaurianeni na Waziri wa Nishati. Namna hii tutaokoa maliasili yetu hasa misitu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi wakati wa Maonesho ya Nane Nane wavumbuzi wajasiriamali wanaonesha aina mbalimbli za nishati, lakini hakuna anayezitilia maanani, mbali ya kuziona na kuwasifia. Nashauri tujaribu kuziendeleza zinaweza zikawa mkombozi kwa mfano, makaa ya magazeti/karatasi, joto la majiko (banifu), pumba (husks) ya mpunga na kadhalika. Okoa maliasili yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri aangalie utunzaji wa misitu. Huu ndiyo ushauri na ombi la Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kidogo niongelee utalii. Nashauri utalii na hasa vivutio vya kila mkoa vitangazwe kikamilifu kwa pamoja na kuwavutia watalii wengi. Tamaduni za makabila yetu, pia ni utalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa wanafunzi kupata elimu bure kuanzia chekechea mpaka kidato cha nne. Pili, nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na watendaji wote wa Wizara.

Napongeza Bodi ya Mikopo kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu wengi. Kwa upande mwingine kuna wanafunzi ambao wamesoma kwa taabu ya kujilipia au kulipiwa na wazazi wao kwa kusuasua kwa madarasa ya chini, bahati nzuri wanafaulu mpaka Chuo Kikuu lakini kwa bahati mbaya hawapati mikopo kufuatana na vigezo vilivyowekwa. Wanafunzi wengine inabidi waache chuo, kwa sababu ya kukosa malipo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwajali na kuwahurumia wanafunzi hawa wanaokosa masomo kwa sababu hawana fedha za kulipia, nashauri inapowezekana wanafunzi wote wapewe mikopo. Mikopo ni mikopo wapewe kwani mikopo hii watailipa hapo baadae. Mheshimiwa Waziri naomba tuwajali pia watoto hawa wahitaji wa elimu ya juu, hawawezi kulipia elimu yao. Serikali yangu sikivu iwaangalie wanafunzi hawa na wenyewe wapewe mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, motisha kwa wanafunzi wanaofaulu alama za juu na hasa wanafunzi wanaochukua masomo ya sayansi, jambo hili likifanyika kuanzia madarasa ya chini, naamini wanafunzi watajituma kusoma, kufaulu na baadaye kulijenga Taifa letu. Jambo hili pia lielekezwe kwa upande wa walimu. Walimu wanaofanya vizuri katika ufundishaji wapatiwe motisha, hii itawapatia moyo kazini mwao na moyo wa utendaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vitabu nashauri iundwe Kamati ndogo ya kupitia vitabu hivi jambo hili litakuwa zuri, kusudi watoto wetu wapate elimu nzuri, kupitia vitabu vilivyoandikwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi wanohitimu vyuo vya VETA ni pongezi kwa Serikali kwa kuwa na mpango wa kuwa na chuo cha VETA kila Wilaya kwa kuwa vyuo hivi vya VETA vinafundisha kwa vitendo, ni vema kila mtoto anapomaliza mafunzo haya aweze kusaidiwa zana ama vifaa vya kuanzia kazi, angalau kidogo ili waweze kujiajiri wenyewe, nashauri jambo hili liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri pia elimu inayotolewa katika vyuo hivi iwe ya kuhitajika katika eneo husika ambapo chuo kipo. Kwa mfano, kwa wastani kila Wilaya hapa Tanzania hata mijini wananchi wengi hutegemea kilimo, kwa kupata kipato cha familia pamoja na kupata chakula chao, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri nakuomba na kukushauri kuwa kila Chuo cha VETA kuwe na mkondo wa elimu ya kilimo, kwa sababu ya kuinua familia na viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miaka ya nyuma shule hasa za sekondari zilikuwepo zinajulikana kuwa ni shule za kilimo lakini sasa hivi hakuna, nashauri utaratibu huu uanze tena ili kusudi wanafunzi baada ya kupata elimu ya sekondari na kama hakubahatika kwenda elimu ya juu, aweze kujitegemea kwa elimu ya kutosha ya vitendo watakayokuwa nayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vkuhusu Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDCs) naishukuru na kuiomba Serikali kuzidi kuangalia vyuo hivi, kwani wanafunzi wanaomaliza katika vyuo hivi wataendelea kueneza elimu ya vitendo waliyoipata katika maeneo yao. Mheshimiwa Waziri nashauri mabweni yaendelee kujengwa na kuboreshwa katika vyuo hivi ili vyuo hivi watoto wengi waweze kudahiliwa. Namuomba Mheshimiwa Waziri jambo hili aliangalie na kulipa kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia kwa kuongelea walimu wa masomo ya sayansi. Naomba mikakati iongezeke ya kupata walimu wengi wa sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata nafasi hii ili niweze kuchangia kwa maandishi. Kwanza natoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya ndani ya Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, Kuhusu Mradi wa Umeme; Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III). Natoa pongezi kwa jitihada ya Serikali ya malengo ya June 2020 kufikia Vijiji 10,278 na kufikia June 2021 Vijiji vyote vitakuwa na umeme.

Mheshimiwa Spika, vijiji vingi Mkoa wa Morogoro katika Wilaya saba za Morogoro Vijijini, Mvomero, Gairo, Kilombero, Ulanga na Malinyi havijafikiwa na umeme, umeme umefika kwenye centers tu, nazo ni nyumba chache. Naomba umeme Awamu hii ya Tatu vijiji hivi kwenye Wilaya hizi vipatiwe umeme (Mpaka June 2020).

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Kujazilizia Umeme. Kuna Vitongoji vilivyorukwa kama Kimamba D Wilaya ya Kilosa, Vitongoji vya Mtego wa Simba, ikiwemo Chekeleni (karibu na Mikese Fulwe) ambavyo vimerukwa na umeme. Natanguliza shukrani kwa Naibu Waziri kwa sababu ulifika na kuwapatia umeme wananchi wa Kimamba A.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, naomba umeme kwa vitongoji vilivyorukwa vya Kimamba A. Mheshimiwa Naibu Waziri alifika Mtego wa Simba (Morogoro Vijijini), nashukuru umeme wamepata, ila ziliwekwa transformer mbili sasa kwenye Kitongoji cha Zahanati ambapo kuna transformer ya pili na nguzo tayari zipo; ni muda mrefu sasa karibu mwaka mzima umepita.

Mheshimiwa Spika, tunaomba umeme kwa hivyo vitongoji vilivyorukwa (kwenye mradi wa kujazilizia).

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi pia kwa kupeleka gesi asilia majumbani, gesi itakuwa bei ya chini. Mheshimiwa Waziri kuna Mkakati gani wa kufikisha gesi hii kwenye Miji ya Kibaha (Mkoa wa Pwani) na Mji wa Morogoro (Mkoa wa Morogoro)?

Mheshimiwa Spika, Kuhusu Mradi wa Umeme Mto Rufiji. Natoa pongezi kwa Serikali kwa mradi huu, Serikali tusonge mbele kwani tunahitaji umeme mwingi kwa mambo mbalimbali. Jambo lingine muhimu, miundombinu (barabara) za kufikia mradi zitengenezwe kwa wakati. Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoifanya. Pili, naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mwijage, kwa kweli anafanya kazi nzuri sana, ameonyesha umahiri wake kwa kujitahidi kuanzisha hivi viwanda ambavyo ametusomea kwenye hotuba yake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba niongee machache kuhusu Mkoa wangu wa Morogoro. Nianze kwa kupongeza. Naishukuru Serikali yetu kwa jinsi inavyowezesha Mkoa wetu wa Morogoro kwa viwanda ambavyo vinatarajiwa kujengwa. Ni viwanda vingi kiasi. Nikianza na viwanda vya Nyama, Matunda, Kiwanda cha Sukari ambacho kipo Mkulazi watajenga na Kiwanda cha Mbigili Sukari, watajenga; pamoja na Kiwanda cha Sigara ambacho na chenyewe kitajengwa Morogoro; na bila kusahau Morogoro Star City ambapo vitajengwa viwanda mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana hivi viwanda viweze kujengwa kwa wakati ili viweze kuajiri hasa vijana pamoja na wanawake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikimaliza kusema hivyo, kwa Mkoa wangu wa Morogoro kuna viwanda ambavyo vilibinafsishwa na havifanyi kazi. Kwa mfano, Kiwanda cha Canvas, Kiwanda cha Ngozi, Kiwanda cha Ceramic, MOPROCO na Kiwanda cha Juice ambacho kipo Kingorwila. Naomba sana Mheshimiwa Waziri kwenye hotuba yake amesema kuwa viwanda hivi hasa MOPROCO pamoja na Canvas viko karibu kuanza. Naomba viweze kuanza kusudi viweze kutoa ajira hasa kwa vijana pamoja na akinamama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo, naomba kuvipongeza na kuwapongeza wale wawekezaji wa viwanda vya Morogoro ambavyo mpaka sasa hivi vinafanya kazi na vinaajiri sana akinamama na hasa vijana, wasichana na wengine. Nikianza na Kiwanda cha Tumbaku; kiwanda hiki kinaajiri akinamama wengi na kinafanya kazi masaa 24. Kwa hiyo, nawapongeza kwa kazi hiyo nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanda cha Mtibwa Sukari kinafanya kazi, Kiwanda cha Kilombero K1 na K2 vinafanya kazi; Kiwanda cha Maji ya Udzungwa kinafanya kazi vizuri na Kiwanda cha Nguo kinafanya kazi. Bila kusahau Mazava, ingawa Mheshimiwa Waziri amesema hakifanyi kazi, lakini kinafanya kazi ambapo kuna vijana wengi hasa wa kike, wanafanya kazi kwenye kiwanda hicho. Kwa hiyo, nawapongeza kwa sababu wanasaidia vijana, akinababa na akinamama hasa wa Mkoa wa Morogoro kwa kupata ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kilimo hapa, wananchi wengi Tanzania asilimia 75 wanategemea kilimo, lakini viwanda vya mbolea ni matatizo bado. Naomba kuuliza Mheshimiwa Waziri, Kiwanda Mbolea cha Kilwa – Lindi ni lini kitaanzishwa? Pia hapo hapo, Mheshimiwa Waziri alisema kuwa kuna kiwanda cha Pwani, nacho naomba aelezee kidogo kama ni cha mbolea. (Makofi)

Pia namwomba Mheshimiwa Waziri na Serikali ya Mheshimiwa Rais, pia waweze kupanua wigo kwa upande wa viwanda vya kilimo pamoja na pembejeo kwa sababu asilimia 75 ya wananchi wanategemea kilimo na kwenye kilimo ndiyo tunategemea uchumi wa mwananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukisema viwanda tunamaanisha mambo mengi. Hatuwezi kuwa Tanzania ya viwanda kama hatuna umeme na hatuwezi kuwa Tanzania ya viwanda bila kutegemea kilimo. Ni lazima tuwe na umeme kwa upande wa nishati na kilimo kwa upande wa malighafi. Pia ni lazima tuwe na maji; huwezi kuwa na kiwanda bila ya maji. Vile vile ni lazima tuwe na ardhi na miundombinu muhimu ikiwepo barabara, reli na viwanja vya ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Waziri aweze kushirikiana na hizi sekta kusudi tuweze kuanzisha hivi viwanda na Tanzania iweze kuwa Tanzania ya viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nizungumzie kuhusu fedha za miradi. Kutokana na hotuba ya Mheshimiwa Waziri tumeona kuwa mpaka Machi mwaka huu fedha za maendeleo ilikuwa ni asilimia 18.92. Ikiwa fedha za maendeleo hazitoki, ni shida sana kufanya maendeleo ya viwanda. Kwa hiyo, nashauri kuwa fedha tunazozipitisha hapa Bungeni ikiwezekana ziweze kutoka na kupelekwa kwa wakati kwenye miradi husika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siwezi nikamaliza bila kuongelea wanawake. Wanawake wa Kitanzania wamejitoa sana kwenye biashara. Wanafanya biashara ndogo, za kati na biashara za Kimataifa, matatizo yaliyopo ni masoko. Kwa hiyo, naomba sana Serikali iwajengee mazingira mazuri waweze kupata masoko na kuuza bidhaa zao. Pia hapo hapo, naomba waweze kuunganishwa na TBS pamoja na TFDA kusudi mazao yao na bidhaa zao ziweze kuwa na thamani ya kuweza kuuzwa ndani na nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wangu wa Morogoro bado una ardhi kubwa. Bado tunaomba zaidi na zaidi wawekezaji hasa kwenye viwanda vya maziwa, kwa sababu bado tunazo ng’ombe na kwenye kilimo bado tuna sehemu kubwa ambayo tunaweza kulima matunda, kuendelea kulima mpunga ingawa kuna wawekezaji, lakini hawatoshi. Kwa hiyo, naomba sana tuweze kupata hao wawekezaji na madawa ya kilimo pamoja na mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa SIDO; huwezi kufanya viwanda hasa viwanda vidogo vidogo bila ya SIDO. Kwa hiyo, naomba sana kuwepo mkakati maalum ambao unaweza ukawaunganisha hawa wafanyabiashara pamoja na SIDO.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii na Mwenyezi Mungu akubariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza kwa kuchangia kuhusu bajeti. Bajeti kwa kweli ni ndogo na inashangaza kabisa. Tunasema kuwa maji ni uhai na kila mmoja anajua kuwa maji ni uhai. Maji ni uhai kwa binadamu, maji ni uhai kwa kila kiumbe na maji ni uhai kwa viwanda ambavyo tunasema tunaenda kwenye Tanzania ya Viwanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, bila ya kuwa na maji ya kutosha hatuwezi kuendeleza haya mambo mazuri ambayo tunayopanga. Bajeti ya mwaka huu ni ndogo ukilinganisha na ya mwaka wa jana, nawaomba Waheshimiwa Wabunge kila mmoja atakayesimama aiongelee hii bajeti kusudi tuweze kuiongeza na kufikia angalau ya mwaka wa jana ili tuweze kufikia malengo mazuri ya mwaka 2021 ya kuwa na maji ya kutosha na kuweza kumtua mwanamke ndoo kichwani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni tozo. Mwaka wa jana tuliongelea kwamba tozo kwa ajili ya Mfuko wa Maji iwe sh. 100, lakini haikupitishwa. Sasa hivi nazidi kuongelea zaidi na zaidi na naungana pamoja na Kamati ya Kilimo na Maji kusudi iweze kufikia lita moja ya diesel na lita moja ya mafuta ya petrol kuwa sh. 100. Kwa namna hiyo tutakuwa tumekuza Mfuko wa Maji. Vijijini akinamama wanapata shida sana na hata watoto wa kike ambao ndio wanatumika kuchota maji hawaendi mashuleni kwa sababu ya kutafuta maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 70 ya fedha ambazo zitakuwa zimekusanywa tuzipeleke huko vijijini na asilimia 30 ziweze kupelekwa mijini. Kwa nini nasema hivi, ni kwa sababu mijini kuna miradi mingi ya maji na wafadhili ni wengi ambao wanafadhili mijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukipata maji safi na salama tutaweza kupunguza magonjwa nyemelezi hasa ya tumbo, kwa mfano kipindupindu ambacho kimekithiri kwenye miji yetu pamoja na kuhara kwa tumbo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuongelea juu ya Halmashauri zetu. Kwenye Halmashauri zetu ilikuwepo sheria ndogo ya uvunaji maji, naomba sheria hii irudishwe kwenye hizi Halmashauri zetu. Kama haipo kwenye Halmashauri nyingine itungwe na kama kwenye Halmashauri nyingine ipo isimamiwe vizuri sana kusudi wananchi waweze kuvuna maji kwenye nyumba wanazojenga na pia kwenye mabwawa ambayo watakuwa wameyatengeneza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukipata maji safi na salama tutakuwa tumepunguza mambo mengi. Tutakuwa tumeimarisha afya yetu na familia na wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu fedha za maendeleo. Tunapanga fedha za maendeleo na zinapitishwa vizuri sana, lakini ukiangalia haziji kama tunavyopanga. Kwa mfano mwaka jana fedha za maendeleo ambazo zimetolewa ni aslilimia 19.8 tu kwa upande wa maji na upande wa kilimo cha umwagiliaji ni asilimia 8.4 tu ambazo zimetoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, bila ya kuwa na fedha za maendeleo miradi yetu yote ambayo tutakuwa tunapanga haiwezi kukamilika, ndiyo sababu unakuta tuna miradi mingi viporo. Kwa mfano miradi mingi ya Benki ya Dunia bado haijakamilika kwa sababu fedha tunazotenga hazitoshi na hazitoki.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha zote za ndani hasa ndizo zinazopaswa kutoka kwa sababu fedha za ndani tunakuwa na uhakika nazo. Kwa mfano, mwaka huu, Serikali imetenga asilimia 66 ya fedha za maendeleo za ndani. Kwa hiyo naiomba Serikali, kuwa hizi fedha ambazo zimetengwa tuzisimamie na kwa sababu ni za ndani tunaamini kuwa zitatoka; fedha hizi ziweze kutoka ili zikamilishe miradi yetu ambayo tutakuwa tumetenga.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kilimo cha Umwagiliaji. Hatuwezi kusema kuwa tutaweza kufanikiwa katika kilimo kwa kutegemea mvua na kwa kutegemea jembe la mkono. Kwa hiyo naomba Serikali yetu, kwamba miradi mizuri iliyopangwa ikiwemo ya Mkoa wangu wa Morogoro, kama ile ya Mikula pamoja na miradi mingine, itekelezwe kusudi tuweze kutoka kwenye hekta 468.338 mpaka kwenye hekta milioni moja mwaka 2021. Ukame ulitunyemelea kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi, nyote mnajua. Nchi zote zilizoendelea zinatumia kilimo cha umwagiliaji pamoja na kulima kwa matrekta.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mfumo wa Umwagiliaji. Nashauri; kwa sababu hela tunazotenga hazitoshi na hazitoki kutoka Hazina; kwamba uanzishwe Mfuko wa Umwagiliaji. Tukiwa na Mfuko huu tutakuwa na uhakika kuwa hela tunazotoa kwenye mfuko huo tunaweza kulima na kupata chakula cha kutosha na hivyo tutapata chakula cha uhakika kwa mwaka mzima na tutainua lishe yetu, hasa Mkoa wetu wa Morogoro pamoja na Tanzania kwa ujumla, ambapo sasa hivi tuna utapiamlo unaokaribia asilimia 34 ambayo si nzuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tufanikiwe kwenye kilimo cha umwagiliaji lazima tuwe na watalaam. Hata hivyo, mpaka sasa hivi tuna watalaam wachache; engineers, surveyors ni wachache sana kwa upande wa kilimo cha umwagiliaji. Kwa hiyo, naomba kuiuliza Serikali, je, ina mkakati gani? Kwa sababu tuna vyuo vichache vinavyotoa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kumalizia naomba mradi wangu wa Chalinze namba..

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa muda wako umemalizika

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja, ahsante
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi. Kwanza kabisa nianze kwa kukushukuru wewe na pia kwa kumshukuru Mheshimiwa Rais na tatu kwa kumshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuzungumzia kilimo. Kwa kweli asilimia 65 ya wananchi wa Tanzania wanategemea ajira kutokana na kilimo, wananchi wanategemea chakula kutoka kwenye kilimo na malighafi ya viwanda yanategemewa kutoka kwenye kilimo. Nashauri tena kilimo kiweze kupewa kipaumbele kama inavyotarajiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye upande wa bajeti; bajeti bado ni ndogo. Kuna makubaliano yaliyofanyika kwa nchi husika, makubaliano ya asilimia kumi ya Malabo pamoja na Maputo, lakini mpaka sasa hivi bado hayajatimilika. Kwa mwaka 2016/2017 ni asilimia 4.9 tu ya bajeti nzima ya Serikali ndio imepelekwa kwenye kilimo. Kwa hiyo, kwa kuwa bado Watanzania wengi wanategemea kilimo, kwa hiyo, naomba kizidi kupewa kipaumbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za maendeleo bado zinakwenda kidogo. Tumeona kuwa kwa upande wa kilimo ni asilimia 3.31 tu ndio zimekwenda kwenye fedha za maendeleo na hizo fedha za maendeleo hazitolewi kwa wakati. Kama hatupeleki hizo fedha tunategemea mipango itafanyikaje? Naishauri Serikali iweze kupeleka fedha za maendeleo tuweze kuendelea vizuri na miradi ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili tuweze kuwa na kilimo bora lazima tuweze kufuata kanuni bora za kilimo na baadhi ya kanuni bora za kilimo ni pamoja na kuwa na na maji, mbegu bora, mbolea pamoja na viuatilifu ambavyo vitatuwezesha kupata mazao bora ya kilimo ambayo yatatuwezesha kupunguza utapiamlo ambao umekithiri kwenye nchi yetu; ambao umefikia takribani asilimia 34. Ili kwa pamoja tuweze kuinua kipato cha Mtanzania lazima tuweze kufuata mambo kama haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa mbegu ni asilimia 35 tu ambazo zinazalishwa Tanzania na asilimia 65 zinatoka nje na hizo asilimia 35 tukitaka kuzipeleka zina kodi, zina VAT, lakini zile za nje hazina. Kwa hiyo naomba sana Wizara, mnajitahidi sana nimewapa pongezi, kuna wanaozalisha mbegu, kuna taasisi mbalimbali kama za Magereza, JKT wanazalisha mbegu, kuna utafiti unafanyika kwenye vyuo vya utafiti na taasisi za utafiti, naomba sana tujitahidi tuweze kuzalisha mbegu zetu hapa nchini ili wananchi waache kutumia mbegu ambazo ni za kiasili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitumia mbegu za kiasili huwezi kupata mazao bora ambayo yanahitajika. Tukitumia mbegu bora pamoja na mbolea ndipo tutaweza kuzalisha mazao ambayo yanastahili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa mbolea, naongelea manunuzi ya mbolea kwa pamoja. Mfumo huu tuliusubiri kwa muda mrefu, tulikuwa na mfumo ambao ulikuwa unatumia vocha, mfumo wa kutumia vocha uligubikwa na taswira za rushwa. Lakini sasa hivi tumepata mkombozi, naomba Waheshimiwa Wabunge tuweze kuupitisha mfumo huu na ninaipongeza sana Serikali na Wizara kwa kuja na mfumo huu ambao ni mzuri sana ambao utamnufaisha mwananchi na kila mwananchi ataweza kupata mbolea kwa wakati na itakuwepo kwa wakati wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nawapongeza sana Serikali kwa kuja na Mfumo huu wa Fertilizer Bulk Procurement ambao mwananchi yeyote anaweza kutumia mbolea kwa wakati wowote na ninaamini kuwa bei ya mbolea itapungua. Hata ninyi Waheshimiwa Wabunge mtaweza kutumia mbolea hii kwa sababu ule mfumo wa vocha ulikuwa unawanufaisha wakulima wachache. Kwa hiyo ni mfumo mzuri, mimi naupenda, naomba uweze kuendelea. Naipongeza Serikali kwa kuweza kuufikiria mfumo huu ambao utaanza hivi karibuni.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa tena pongezi sana kwa Serikali kwa kupunguza tozo nyingi sana kwa upande wa kilimo, mifugo na kwa upande wa uvuvi. Hii italeta unafuu sana kwa wakulima, wafugaji na wavuvi ili waweze kuendeleza maisha yao kwa sababu tozo zilizidi na zilizidi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee NFRA ambayo inafanya kazi vizuri, naomba sana iendelee kufanya vizuri. Hata hivyo angalizo, naomba sana hayo maghala ambayo mmesema mtayajenga yaweze kujengwa kwa wakati.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ninashauri mnunue chakula kwa wakati, msisubiri walanguzi waanze kuingia ndipo ninyi muanze kununua na bei elekezi iweze kutolewa mapema, pamoja na mambo mengine ya mizani na magunia yasilete matatizo kwa sababu wakati mwingine huwa yanachelewa kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Halmashauri 55 ambazo zilikuwa na uhaba wa chakula, naomba kujua mpaka sasa hivi ni Halmashauri ngapi ambazo zinahitaji chakula? Kwa sababu najua mvua zimenyesha kwa hiyo Halmashauri nyingine ambazo zilikuwa na uhaba wa chakula sasa hivi zinavuna mazao, sasa tujue kama bado zina uhitaji wa chakula ziweze kupelekewa chakula kuliko chakula kukaa kwenye maghala. Kwa sababu chakula si vizuri kukaa kwenye maghala zaidi ya miaka mitatu, la sivyo kitaharibika, kwa hiyo, naomba sana tuangalie hali hiyo ya chakula na Halmashauri ambazo bado zinahitaji chakula ziweze kupelekewa chakula, naamini mmeanza kupeleka lakini ziweze kupelekewa chakula, nashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, migogoro ya wakulima na wafugaji. Ni kweli tulikuwa na migogoro mikubwa sana ya wakulima na wafugaji, Mkoa wangu wa Morogoro ukiwa unaongoza. Hata hivyo nashukuru kwa sababu ya hii Kamati ambayo tumeambiwa imeleta taarifa, tutaiangalia wakati ukifika. Pia ninaishukuru Serikali kwa sababu Mawaziri mbalimbali walifika huko Morogoro na walifanya kazi nzuri sana. Sasa hivi naamini migogoro imepungua. Lakini kwa nini imepungua, kwa sababu mvua inanyesha, malisho yapo, kwa hiyo inaendelea vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naishauri Serikali iweze kuangalia miundombinu ambayo ni pamoja na majosho na malambo; iangaliwe ili tusije tukarudia kwenye mgogoro huu wa wakulima na wafugaji. Pia naishukuru Serikali kwa sababu imeanza kupima ardhi kwa upande wa Ulanga pamoja na Kilombero. Ukipima ardhi na kutoa hati miliki kila mmoja atakuwa na ardhi yake na hivyo tutaendelea kupunguza migogoro ya wakulima pamoja na wafugaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile naomba elimu ya malisho iendelee kutolewa ili wananchi waweze kujua kujitengenezea majani yao ya kulishia mifugo yao. Nashauri tena elimu ya kuvuna mifugo, yaani tuweze kufanya ufugaji wa kisasa na wenye tija, iendelee kutolewa na hapohapo Mheshimiwa Waziri Mwijage akituletea viwanda vya nyama.

Mhehimiwa Naibu Spika, Afisa Ugani; kuna sera inasema kuwe na Afisa Uganikwa kila kijiji, lakini mpaka sasa hivi bado hatujapata Afisa Uganikwa kila kijiji, ukimuuliza hapa Mbunge mmoja mmoja anaweza akasema hajawahi kumuona Afisa Uganikwenye kijiji chake.

Kwa hiyo, naomba mkakati wa kuendeleza na kuongeza Maafisa Ugani kwa kuomba kibali kwa Waziri mhusika aweze kutoa kibali. Maafisa Ugani wapo… (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, narudia kusema Mwenyezi Mungu akubariki, naunga mkono hoja.
Makadirio ya na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na Wafanyakazi wote wa Wizara hii. Pili, naomba kutoa pongezi kwa kazi wanayoifanya nzuri hasa Mkoa wa Morogoro kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyote mnafahamu kuwa Mkoa wa Morogoro ulikuwa na matatizo sana hasa kwa upande wa wakulima na wafugaji mpaka mapigano na mauaji yakatokea kwa upande wa watu na mifugo. Nashukuru Serikali kwa sababu Mawaziri walifika kwa kusaidiana na uongozi wa Mkoa pamoja na Wilaya waliweza kufanya kazi kadri walivyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa sababu dawa muhimu ya kumaliza hii migogoro ni upimaji wa ardhi. Upimaji wa ardhi ambao sasa hivi umefanyika kwenye Wilaya ya Malinyi, Ulanga pamoja na Kilombero kwa baadhi, nashukuru kwa sababu wametoa hata hati miliki na hiyo ndiyo ingekuwa mkombozi. Tufahamu kuwa hawa wanaopewa hati miliki ni wachache, naomba kwa sababu tumepata ufadhili kutoka Serikali ya Uingereza pamoja na Sweden na Denmark kupitia kwenye mashirika yao ya maendeleo ya DANIDA, DFID pamoja na SIDA nashauri Wizara kama inawezekana waweze hata watu wengine kupimiwa kwa sababu hata registry ambayo ni masjala wameweza kujenga lakini watu wangeweza kumilikishwa wote ingekuwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wa Morogoro ifahamike kuwa ni Wilaya zote zilikuwa na matatizo ya mifugo. Wilaya zote Mvomero nashukuru mmeweza kupima kiasi, Kilosa mmeweza kupima kiasi, lakini mfahamu kuwa watu walikufa Mabwerebwere, watu walipigwa na hasa wanawake ambao walikuwa wanalima mpunga wao, wengi walikimbizwa hawawezi kulima.

Naomba sana tena sana kwa kusaidiana jinsi mlivyoweza kupata ufadhili kutoka kwa mashirika hayo, Mheshimiwa Waziri una wataalam wazuri ambao wanaweza kuandika maandiko ya kuweza kuomba project pamoja na kusaidiana na Halmashauri zetu za Wilaya ya Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro Vijijini hata Manispaa pamoja na kule ambako tayari mmeshaanza kupima tuweze kupata kupimiwa ardhi kwa sababu ni majaribio yaweze kuwa majaribio ya Mkoa mzima watu wote mlikuwa mnajua kuwa Mkoa wa Morogoro ndiyo umeweka historia kwenye migogoro ya wakulima na wafugaji, kuweza kupimiwa ardhi kusudi tupate hatimiliki watu waweze kumiliki pamoja na tuweke historia ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri kuwa kwa Wilaya zingine Mikoa yote ya Tanzania ambayo inajulikana kwa migogoro hii ya wakulima na wafugaji pamoja na migogoro ya ardhi, dawa ni kupima ardhi, kupata hati miliki, hati miliki ambayo inaweza kukusaidia hata kupata mikopo lakini kujua kuwa ni ardhi gani mifugo itaweza kuwa, ni ardhi gani wakulima wataweza kuwa na ni ardhi gani wafugaji wataweza kuwa na hii tutakuwa tumepanga mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua kuwa kwa sababu wataalam ni wachache na kuna vyuo, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Ardhi Morogoro pamoja na Chuo cha Ardhi Tabora, udahili uweze kuongezwa ili kusudi tuweze kupata watumishi wengi wataalam wa ardhi huko kwenye Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa niongelea kuhusu mipango ya miji. Bila ya kupanga miji itakuwa kuna ujenzi holela kama tunaoushuhudia watu wanajenga mpaka milimani na ninyi Wizara mpo, naomba na hilo mliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kushukuru sana nyumba za National Housing zimejengwa pamoja na nyumba za watumishi ardhi hata Mkoa wa Morogoro tumepata lakini tatizo kama wenzangu wanavyosema gharama bado ni kubwa. Naomba muiangalie hiyo gharama ili kusudi hata wale vijana wanaoanza kazi sasa hivi, waweze kupata nyumba zao wakalipia kidogo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kuchangia machache kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchangia jambo moja ambalo sikuweza kulichangia kwa kuongea wakati wa mchango wangu kwa sababu ya muda.

Mheshimiwa Naibu Spika, uwanja wa ndege wa Morogoro. Nashukuru Serikali kwa kutupatia Meneja wa Kiwanja cha Ndege Morogoro Ms Esta Mwigune. Morogoro ni Mkoa ulio katikati mwa Jiji la Dar es Salaam pamoja na Jiji la Dodoma. Kwa sababu hiyo na sababu nyinginezo, Manispaa ya Morogoro inakua kwa haraka sana. Tunashukuru kwa Serikali kwa kuliona hilo na kuutambua Uwanja wa Ndege Morogoro.

Pili, Mkoa wa Morogoro tuna sehemu za utalii ikiwepo Mikumi, Selou pamoja na Udzungwa. Kwa kuutambua na kuujenga uwanja wa ndege wa Morogoro, kutaongeza kuja kwa watalii wengi, hivyo kuinua uchumi wa nchi yetu

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo linalojitokeza sikuona fedha yeyote iliyotengwa ya kutengeneza/kujenga/ kukarabati uwanja wa ndege Morogoro, ingawaje tumeanza kupata wafanyakazi kama Meneja na wengineo. Ombi langu, naomba na kushauri uwanja huu wa ndege ukatengenezwe kwani ni wa manufaa kwa nchi yetu na hasa kufuatana na kukuza utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha ndege cha Selou tulishaambiwa kuwa kitajengwa. Je, ni lini kiwanja hiki kitajengwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana, nategemea nitajibiwa, baada ya hayo, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kupata nafasi hii kuchangia kwa maandishi ndani ya Bunge lako Tukufu. Napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu na Wataalam wote katika Wizara hii ya Fedha na Mipango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha za maendeleo zilizotolewa Hazina ni shilingi bilioni 5.8 kati ya bilioni 740.15 ya fedha zote zilizoidhinishwa na Bunge (sawa na asilimia 0.8), namna hii ya utoaji fedha za maendeleo kidogo (asilimia 0.8) ni dhahiri kwamba Hazina haijafanya vizuri kadri ilivyopangwa awali katika mambo ya maendeleo. Naishauri Serikali kuwa mara fedha zinapopatikana ziwe zinatolewa kadri zilivyopangwa na kupitishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumshauri Mheshimiwa Waziri kuwa ingawaje bado deni la Taifa linalipika, tuwe tunalipa kadri ipasavyo. Serikali ijitahidi kwanza kwa vyovyote vile kulipa deni hili la Taifa, jambo hili litasaidia kuendelea vizuri na miradi ya maendeleo kwa hiyo, pale inapowezekana Serikali iendelee kulipa na kupunguza deni hili la Taifa badala ya kuongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaweza kutoa au kulipa suala hili kipaumbele. Hata hivyo, naipongeza Serikali kwa kipindi hiki, kulipa Shilingi Trilioni 4.64 kwa deni la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri Serikali ihakikishe na kujitahidi ili madeni ya watumishi wote yaendelee kulipwa,ili kuwapatia moyo wa kufanya kazi kwa bidii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukusanyaji wa mapato; Serikali kusimamia mkakati kabambe wa ukusanyaji wa mapato kutoka kwa wafanyabiashara kwa kutumia mashine za kielektroniki (EFD). Ni vema kuwafuatilia wafanyabiashara ili wanaopaswa kulipa kodi wakalipe ni dhahiri wengine wanakwepa eti, hawana mashine au mashine mbovu, kiasi cha kupoteza mapato mengi. Wafanyabiashara hasa wafuatiliwe ili tuweze kupata mapato ya ndani yanayostahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi wa milioni 50 kwa kila Mtaa na kila Kijiji; ni kweli mwaka 2016/2017 hazikutolewa, tafadhali vikundi vya wajasiriamali wanazisubiri kwa hamu. Nashauri hizo shilingi bilioni 60 zilizotengwa kwa 2017/2018 jitihada iwepo, zipatikane na kutolewa kama ilivyopangwa. Naomba niwaambie Mheshimiwa Waziri, kuwa wananchi wanazisubiri sana, nashauri Serikali isichelewe kuanza kutoa fedha hizi angalau kwa awamu, isikike kuwa fedha hizi zimeanza kutolewa, hivyo itekelezwe kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu huduma kwa wastaafu; nawapongeza kwa kazi nzuri ya Serikali kwa kuwatambua wastaafu. Nashauri Serikali iendelee kuangalia pensheni zao, bado wale waliostaafu zamani pensheni zao ni ndogo sana. Wastaafu wanaomba na pia nashauri kwa sababu waliifanyia kazi nzuri Serikali yao, mara mishahara inapopandishwa na wenyewe angalau wapandishiwe pensheni yao ili kumudu maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala la mikopo, ni dhahiri kuwa wananchi kupokea mikopo kwa kutumia hati ya ardhi, bado benki nyingi hawatambui. Ni vema zijulikane benki zinazokubali hati hizi ili wananchi wa kawaida hasa waweze kupata mikopo. Nashauri Serikali, Benki ya Kilimo pamoja na mambo yote iweze kuongezewa fedha ili wakulima wakope kwa urahisi ingawaje matawi ya benki hii bado hayajasambaa mikoani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wote tunatambua kuwa asilimia 65 ya Watanzania wanategemea kilimo, pia viwanda (Tanzania ya Viwanda) vinategemea malighafi ya kilimo, ni kwa nini Serikali isichukue jukumu la kuongeza fedha kwenye Benki ya Kilimo ili wakulima wakope. Pia Serikali iangalie jinsi ya kuwaongezea fedha, Tanzania tunataka maendeleo ya viwanda ni vema wakulima tuwawezesha kwa njia ya mikopo nafuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira Kuanzia Januari, 2021 hadi Februari, 2022 pamoja na Taarifa ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kwa Kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI:
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa kwa mara nyingine ya pili nichukue nafasi hii kukupongeza kwa kupata nafasi hiyo, nakutakia majukumu mema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nawapongeza sana Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja yetu ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji ambao yapata kama Wabunge tisa ambao wamechangia. Pia nawapongeza Mawaziri ambao wametoa ufafanuzi, Mheshimiwa Bashe, Mheshimiwa Ndaki bila kumsahau Mheshimiwa Aweso ambaye na yeye yuko kwenye Kamati yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sio lazima wote niwataje majina ila Mheshimiwa Profesa Muhongo, Mheshimiwa Profesa Manya, Mheshimiwa Profesa Patrick Ndakidemi, Mheshimiwa Kunti, Mheshimiwa Mwijage; na Mheshimiwa Polepole amepongeza na yeye kuwa mapendekezo yote yaliyopendekezwa na Kamati yaweze kuchukuliwa. Mheshimiwa Neema Lugangira na yeye kwa sababu usalama wa chakula ni mtambuka uko pia kwenye upande wa kilimo, kwa hiyo na yeye amechangia pamoja na Mheshimiwa Nusrat amesema ubunifu kwenye sayansi na hasa tunaposema kuwa ubunifu wa chakula, Mheshimiwa Gambo kwenye upande wa ajira ambao ni Ilani ya Chama cha Mapinduzi, pamoja na mambo ya maua tunashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo yaliyoongelewa sana ni mengi ya kuhusu Tume ya Umwagiliaji, mambo ya pembejeo na mambo mengine yote yaliyoongelewa. Nawashukuru Waheshimiwa Mawaziri kama mmekubali kuwa mtachukua ushauri wetu na mapendekezo yetu na tumekuwa pamoja, naamini tutaendelea vizuri kama tulivyokuwa tunaendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba taarifa yetu yote iweze kuungwa mkono na mapendekezo yote pamoja na Wabunge wote waliomo humu ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja ya Kamati. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Ahsante, toa hoja.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI:
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri na Wafanyakazi wote wa Wizara hii. Pili, naomba kutoa pongezi kwa kazi wanayoifanya nzuri hasa Mkoa wa Morogoro kuhusu migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nyote mnafahamu kuwa Mkoa wa Morogoro ulikuwa na matatizo sana hasa kwa upande wa wakulima na wafugaji mpaka mapigano na mauaji yakatokea kwa upande wa watu na mifugo. Nashukuru Serikali kwa sababu Mawaziri walifika kwa kusaidiana na uongozi wa Mkoa pamoja na Wilaya waliweza kufanya kazi kadri walivyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa sababu dawa muhimu ya kumaliza hii migogoro ni upimaji wa ardhi. Upimaji wa ardhi ambao sasa hivi umefanyika kwenye Wilaya ya Malinyi, Ulanga pamoja na Kilombero kwa baadhi, nashukuru kwa sababu wametoa hata hati miliki na hiyo ndiyo ingekuwa mkombozi. Tufahamu kuwa hawa wanaopewa hati miliki ni wachache, naomba kwa sababu tumepata ufadhili kutoka Serikali ya Uingereza pamoja na Sweden na Denmark kupitia kwenye mashirika yao ya maendeleo ya DANIDA, DFID pamoja na SIDA nashauri Wizara kama inawezekana waweze hata watu wengine kupimiwa kwa sababu hata registry ambayo ni masjala wameweza kujenga lakini watu wangeweza kumilikishwa wote ingekuwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wa Morogoro ifahamike kuwa ni Wilaya zote zilikuwa na matatizo ya mifugo. Wilaya zote Mvomero nashukuru mmeweza kupima kiasi, Kilosa mmeweza kupima kiasi, lakini mfahamu kuwa watu walikufa Mabwerebwere, watu walipigwa na hasa wanawake ambao walikuwa wanalima mpunga wao, wengi walikimbizwa hawawezi kulima.

Naomba sana tena sana kwa kusaidiana jinsi mlivyoweza kupata ufadhili kutoka kwa mashirika hayo, Mheshimiwa Waziri una wataalam wazuri ambao wanaweza kuandika maandiko ya kuweza kuomba project pamoja na kusaidiana na Halmashauri zetu za Wilaya ya Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro Vijijini hata Manispaa pamoja na kule ambako tayari mmeshaanza kupima tuweze kupata kupimiwa ardhi kwa sababu ni majaribio yaweze kuwa majaribio ya Mkoa mzima watu wote mlikuwa mnajua kuwa Mkoa wa Morogoro ndiyo umeweka historia kwenye migogoro ya wakulima na wafugaji, kuweza kupimiwa ardhi kusudi tupate hatimiliki watu waweze kumiliki pamoja na tuweke historia ya kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nashauri kuwa kwa Wilaya zingine Mikoa yote ya Tanzania ambayo inajulikana kwa migogoro hii ya wakulima na wafugaji pamoja na migogoro ya ardhi, dawa ni kupima ardhi, kupata hati miliki, hati miliki ambayo inaweza kukusaidia hata kupata mikopo lakini kujua kuwa ni ardhi gani mifugo itaweza kuwa, ni ardhi gani wakulima wataweza kuwa na ni ardhi gani wafugaji wataweza kuwa na hii tutakuwa tumepanga mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujua kuwa kwa sababu wataalam ni wachache na kuna vyuo, Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Ardhi Morogoro pamoja na Chuo cha Ardhi Tabora, udahili uweze kuongezwa ili kusudi tuweze kupata watumishi wengi wataalam wa ardhi huko kwenye Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa niongelea kuhusu mipango ya miji. Bila ya kupanga miji itakuwa kuna ujenzi holela kama tunaoushuhudia watu wanajenga mpaka milimani na ninyi Wizara mpo, naomba na hilo mliangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kushukuru sana nyumba za National Housing zimejengwa pamoja na nyumba za watumishi ardhi hata Mkoa wa Morogoro tumepata lakini tatizo kama wenzangu wanavyosema gharama bado ni kubwa. Naomba muiangalie hiyo gharama ili kusudi hata wale vijana wanaoanza kazi sasa hivi, waweze kupata nyumba zao wakalipia kidogo kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo, wa Mwaka 2016
MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia Miswada hii miwili. Nitachangia kwa pamoja Muswada unaohusu Taasisi ya Utafiti wa Kilimo pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi (TAFIRI).
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukisema tafiti kwa kuanzisha hizi Taasisi na sheria naamini ni kitu kizuri sana ambacho kinamfanya Mtafiti aweze kumiliki tafiti zake badala ya kudhibitiwa pamoja na Taasisi nyingine. Naungana na Kamati jinsi ilivyoongea pale asubuhi na tuliweza kusema kuwa uwepo Mfuko wa Tafiti, kwa sababu ukianzishwa Mfuko huo, utamuwezesha hata Mtafiti yeyote yule anayetoka kwenye shughuli za kilimo pamoja na Mtafiti kwenye upande wa uvuvi kuweza kupata hela hasa za kufanyia tafiti zake.
Kitu kingine tulichoongelea ambacho inabidi kukazia ni kile ambacho kilikuwa kinasema kwenye Muswada ambao ulikuwa kwa upande wa uvuvi kuhusu yeyote yule ambaye atakuwa anafanya utafiti na kama utafiti wake haukwenda vizuri aweze kurudisha hela, hiyo, kwa kweli nasema hapana na bado nasema hapana. Haiwezekani ndiyo sababu ikaeleweka kuwa afadhali wawepo watu au group, Maprofesa au Bodi ambao wanaweza wakafuatilia huo utafiti wa huyo mtu tangu anapoanza mpaka anapoendelea. Mahali inapoonekana utafiti hauendi vizuri aweze kuachia hapo hapo badala ya kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuchukulie kwa mfano wanafunzi ambao wanasoma Vyuo Vikuu, unasema kuwa wafanye utafiti mpaka mwisho na kama pale ambapo hawata-succeed kuwa tafiti zao zimekubalika waweze kuleta hizo hela, hela hizo watazitoa wapi? Kwa hiyo, hapo naungana na Kamati kuwa kwa kweli tuangalie mlolongo wa utafiti unavyokwenda na pale inapoonekana kuwa utafiti haueleweki, hauendi vizuri aweze kuachia hapo hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ni la kuongelea ni wale watafiti kwenye deep sea. Kwa kweli hapa tunavyotunga Kanuni naomba kanuni zinavyotungwa Serikali iangalie jinsi ya kuangalia uvuvi wa kwenye deep sea kwa sababu tunaibiwa sana kwenye deep sea bila ya kuangalia na mapato mengi sana tunayapoteza pale ambapo hatuendi vizuri. Kuna vifungu ambavyo vinaongelea kuhusu umiliki wa tafiti.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mtafiti anayetafiti utafiti wake naomba aweze kumiliki huo utafiti. Bila ya tafiti hatuwezi kufika popote. Kwa hiyo, naunga mkono hizi sheria ziweze kupitishwa kusudi kwenye tafiti hizi tukitafiti, tafiti nyingi zimeshatafiti, Vyuo Vikuu vingi vimeshafanya tafiti, lakini kweli kufikia kwa mlengwa wakati mwingine inakuwa ni ngumu. Kwa hiyo, kwenye Kanuni iweze kuonekana jinsi inavyoweza kumfikia yule mlengwa na walengwa hasa ni wale wananchi ambao ni Wavuvi na ambao ni Wakulima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mengi nilikuwa nimechangia asubuhi nilipokuwa nachangia kwenye Kamati na sasa hivi naomba niongezee hayo machache ambayo nimechangia. Naomba Waheshimiwa Wabunge tuunge mkono Miswada hii yote miwili kusudi iweze kupita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. CHRISTINA G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha leo kupata nafasi na kuweza kuchangia angalau kwa maandishi. Pili, nichukue nafasi hii kukupongeza kwa kazi nzuri, pamoja na Mheshimiwa Spika, na Naibu Spika na Wenyeviti wenzako. Nizidi kuwapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wataalam na watendaji wote kwa kazi nzuri wanayoifanya, nawaombea Mungu wasonge mbele kwa kazi yao nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sote tunajua kuwa Morogoro ni mkoa ulioweka historia, kwa migogoro ya wafugaji na wakulima. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri inayoendelea nayo, ya kupima, kurasimisha na kutoa hati miliki kwa wananchi. Upimaji wa ardhi na kuwamilikisha wananchi kwa kupewa hati ya kumilikisha ardhi hii ni mkombozi wa kutatua migogoro. Naomba nimwambie Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri, upimaji wa vijiji na mashamba pia ni utatuzi tosha wa migogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ilifikia wakulima kushindwa kwenda mashambani na hasa Mbigili, Kilangali na sehemu za wakulima wa Mpunga Wilayani Kilosa kama Mabwerebwere. Kundi kubwa la wanawake, ambao ndio wakulima wakubwa, kweli, hali ilikuwa mbaya mpaka mapigano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mifugo pia ilifikia wakati ikakatwakatwa mpaka wengine kufa. Mifugo ilihamia katika Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro, Kilosa, Gairo, Mvomero, Morogoro Vijijini, Morogoro Manispaa, Kilombero, Malinyi na Ulanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na kuipongeza Serikali kwani baadhi ya Mawaziri walifika na hasa Mvomero na Kilosa ili kuona na kutatua migogoro hii kwa kusaidiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya, nawapongeza. Tatizo kubwa lilikuwa ni kutafuta malisho na maji katika ardhi iliyo wazi ambayo haijapimwa kisheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru na kupongeza Serikali ya Uingereza Sweeden na Dernmark kwa kupitia kwenye Mashirika yao ya Maendeleo DANIDA,SIDA,na DFID, kwa ufadhili wao wa upimaji ardhi mpaka kutoa Hatimiliki na kujenga Masjala ya Ardhi katika Wilaya ya Kilombero, Ulanga na Malinyi. Naamini, upimaji kiasi chini ya Serikali umefanyika Mvomero na kidogo Kilosa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upimaji ardhi ni gharama, Nashauri na kuiomba Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, fedha ziendelee kutafutwa, kama tulivyosaidiwa na nchi rafiki zetu kwenye mradi huu wa Kilombero, Ulanga na Malinyi, kusudi wananchi wote katika Wilaya hizi, kila mmoja apimiwe ardhi yake na kupewa hati miliki. Wakati mwingine tunashauri, taasisi Mheshimiwa Waziri, hata maeneo ya taasisi zetu zikapimwa na kupewa Hati miliki za maeneo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali yetu ione kuwa upimaji ardhi na matumizi bora ya ardhi ni muhimu kwa utatuzi wa migogoro ya ardhi. Nishauri maeneo yote ya wilaya zote za Morogoro yapimwe na wananchi wapewe hati miliki zao. Matumizi bora ya ardhi kwa kuchanganua ni wapi kilimo, mifugo, ifanyike na kadhalika. Hii itasaidia wananchi na kwa kuambatanisha na miundombinu kama mabwawa na majosho. Sasa hivi tumetulia kwa sababu malisho yapo baada ya mvua kunyesha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ikiwezekana Mikoa/ Wilaya zote zenye migogoro, ardhi yao ipimwe. Pia Hati miliki inaweza kutumika katika kuomba mikopo. Naomba benki (CRDB, NMB, NBC) wazipokee.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba (NHC) pamoja na Watumishi Housing, natoa pongezi kwa Serikali kwa kazi hii, liko tatizo nyumba hizi ni ghali. Nashauri, Serikali itathmini tena ili gharama zipungue, wananchi na hasa vijana wapate pa kuishi na kumudu maisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wataalam wa ardhi ni wachache, kwa hiyo, nashauri kwa kupitia Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo cha Tabora na Morogoro udahili uongezeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii. Kufuatana na takwimu ni asilimia 75 ya wananchi wanategemea kilimo na kilimo chetu kinachangia asilimia mia moja ya chakula. Mwaka 2016/2017, sekta ya kilimo imekua kwa asilimia 1.7 na katika kipindi cha nusu mwaka yaani Desemba kilimo kimekua kwa asilimia 3.1. Ukuaji huu wa kilimo hauridhishi, inabidi Wizara na Serikali ifanye jitihada za kuwezesha kilimo kukua na kuweza kuwasaidia wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwa na kilimo chenye tija ni bora kutumia kanuni bora za kilimo na kanuni bora za kilimo ni pamoja na kutumia pembejeo za mbolea, mbegu na kadhalika. Imekuwepo tabia ya wakulima kutotumia mbolea ya kutosha na mojawapo ya sababu ni bei kuwa ghali. Kwa mfano, hapa Tanzania wakulima wengi wanatumia mbolea kilogramu 10 kwa hekta ambapo kilogramu zinavyoshauriwa ni 90 kwa hekta. Kwa hiyo, nashauri hili jambo liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa kuja na huu mfumo wa ununuzi wa mbolea kwa pamoja. Hata hivyo, naishauri Serikali iufuatilie mfumo huu kwa karibu kwa sababu umeanza kuwa na changamoto yake kwani viashiria vimeanza kuonekana. Kwa mfano, kuna maeneo katika Mikoa inayozalisha chakula kwa wingi mbolea hii haikufika kwa wakati. DIP ni mbolea ya kupandia na urea ni mbolea ya kukuzia sasa unapeleka DIP wakati mazao yameshakuwa haiwezekani kwa sababu DIP ni mbolea ya kupandia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishauri Serikali na Wizara kupeleka mbolea hii kwa wakati muafaka. Tulipopitisha kwenye Bunge lako hili Tukufu kuwa tuweze kununua mbolea kwa pamoja tulisema ni ili tuweze kupata mbolea kwa wingi na kila mdau aweze kupata mbolea ambayo anaitaka baada ya kufuta ile mfumo wa kutumia ruzuku ambapo ilikuwa inatoa mianya ya rushwa. Naomba Wizara ijitahidi ili kila mdau wa kilimo aweze kuipata kwa wakati na bei elekezi iweze kutumika kwa sababu mahali pengine mpaka sasa hivi hiyo bei elekezi haifuatwi bado bei iko juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niongelee upande wa maji vijijini na mijini. Bado tuna tatizo kubwa kwenye maji mijini pamoja na vijijini, ni asilimia 56 vijijini na asilimia 69 mjini. Kwa hiyo, nashauri kwa upande wa maji Serikali yetu iweze kutilia mkazo kuona ni namna gani tunaweza kupata maji ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo cha umwagiliaji ni muhimu sana, lakini mpaka sasa hivi ni asilimia 1.6 tu ndiyo tunalima kwa umwagiliaji. Kwa namna hii hatuwezi kufika mbali kwa kilimo cha umwagiliaji na hatuwezi kusema kuwa tutakuwa na usalama wa chakula kama hatutatilia maanani kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasisitiza Serikali iweze kutoa hela za kutosha kwenye kilimo cha umwagiliaji. Kuna mabwawa, kwa mfano, Bwawa la Kidunda, usanifu wake ulifanyika tangu 2004 lakini pia kuna mabwawa mengi ya umwagiliaji ambayo mpaka sasa hivi hayajakamilika. Nashauri Serikali pamoja na Wizara tuweze kuona jinsi ya kukamilisha mabwawa haya kusudi tuweze kujikita kwenye kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni fedheha ambayo imetokea kweli kwenye upande wa korosho. Naomba Wizara iweze kuangalia hiki kitu kichotokea cha korosho zetu kukutwa na mawe na kokoto huko Vietnam. Kwa hiyo, naomba nalo liangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye wadudu waharibifu wa mazao kwenye Mikoa yetu hata Morogoro tuna tatizo la viwavijeshi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia bajeti ya Serikali. Nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipatia afya na kuweza kuchangia kwenye bajeti hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa sana anayoifanya. Kwa kweli, ni mtu anayestahili kufanya mambo anayoyafanya. Mheshimiwa Rais akisema anatenda, Mheshimiwa Rais amefanya mambo mengi kwa muda wa miezi 18 tu. Mheshimiwa Rais kwa kweli, kila mmoja anastahili kumpongeza kwa mambo yote anayowafanyia Watanzania. Amejitoa yeye mwenyewe na siyo yeye mwenyewe ni mkono wa Mwenyezi Mungu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana na namwombea Mwenyezi Mungu azidi kumlinda na azidi kumwongoza aweze kuishi maisha marefu. Hasa tendo hili la makinikia na kweli amelifanyia mambo mazuri, wengine wameanzisha lakini yeye mwenyewe nadhani atamalizia. Sasa hivi akikaa hivi karibuni mezani na hawa watu, fedha zitakuja, kila mmoja atatamani kuzitumia kwenye miradi yake. Kwa hiyo, naomba wote tuwe kitu kimoja, nchi yetu ni nzuri, nchi yetu ya Tanzania ina amani, naomba tuwe kitu kimoja hasa kushughulikia mambo haya yaliyo mbele yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri wa Fedha pamoja na Makatibu wa Fedha na Manaibu wake. Kwa kweli, bajeti hii ni nzuri sana, inawajali Watanzania, inawajali wakulima, inawajali watu wote kwa wastani. Kwa hiyo, tunashukuru kwa bajeti hii nzuri ambayo mmetueletea ya shilingi trilioni 31.7 na kati ya hizo wamesema asilimia 38 ni fedha za maendeleo. Naomba hizi fedha za maendeleo ziweze kuja zote kama walivyozipanga kusudi miradi ya maendeleo ile ambayo ni viporo na ile ambayo bado iweze kutekelezeka. Kwa hiyo, naomba kitu kama hicho. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya kati kwa ujenzi wa standard gauge, tunashukuru sana imeanza na wakandarasi wako tayari pale na itajengwa kwani tayari mkataba umeshawekwa saini ya kutoka Dar-es-Salaam mpaka Morogoro. Wamesema bado mnatafuta wafadhili kwa reli kuanzia Morogoro – Makutupora – Kigoma - Mwanza, naomba wafanye bidii sana kwa sababu reli hii inawasaidia watu wote. Reli hii haitachagua chama gani itawabeba watu wote wa kanda hizo hizo, kwa hiyo, naomba Serikali waifanyie kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopenda kuliongelea ni tatizo la maji, kila mmoja humu anazungumzia tatizo la maji.

TAARIFA . . .

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba unilindie muda wangu hata Mheshimwa Lowassa na yeye amemkubali Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia tatizo la maji, uwe Mbunge wa chama chochote kila mmoja anakiri kuwa ana tatizo la maji. Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi inasema kuja kufikia mwaka 2020 asilimia 85 vijijini wawe wamepata maji safi na salama na asilimia 95 mijini nao wawe wamepata maji safi na salama ili kusudi tuweze kuwatua ndoo kichwani wanawake. Kwa hiyo, naomba sana tena sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha hii ahadi iweze kutimilika maji yaweze kwenda vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawapongeza sana kwa kufuta leseni ya magari. Hii bajeti imepokelewa na watu wengi…

TAARIFA . . .

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, siikubali hiyo taarifa, kama hajui kusoma aende akasome aangalie ni kitu gani kinatendeka huko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nazungumzia kufutwa kwa leseni ya magari. Nendeni kwenye mitandao ongea na watu wote, ongea na wasomi, ongea na kila mmoja, hii kweli anaiunga mkono.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nizungumzie kuhusu kutoa ushuru wa Sh.40/= kwa kila lita ya mafuta, nashauri Mheshimiwa Waziri wa Fedha hizi hela ziweze kwenda kwenye Mfuko wa Maji. Nikiwa mwanamke nasisitiza hilo kwa sababu najua shida ya wanawake ambao wanatafuta maji pamoja na watoto wao, hizi hela ziweze kwenda kwenye Mfuko wa Maji. Nasisitiza kuwa asilimia 30 ya hizi fedha ziweze kwenda mjini pamoja na asilimia 70 ziende vijiji. Nasema hivi kwa sababu mjini inaweza kutokea taasisi zingine zikasaidia kugharamia maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo, asilimia 65 ya wananchi wanategemea kilimo na malighafi nyingi zinatoka kwenye kilimo. Kwa hiyo, namwomba sana sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha, fedha zilizotengwa kwenye kilimo ahakikishe zote zinakwenda kwenye kilimo kwa sababu bila ya kilimo hakuna viwanda, chakula na lishe ni duni. Kwa hiyo, naomba sana hizi hela ziweze kutoka zote tuweze kuinua pato la familia pamoja na pato la Taifa na hasa tukazanie kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa sababu wameweza kutoa tozo mbalimbali kwenye pembejeo na ushuru wa mazao asilimia tatu kwa bidhaa za biashara na asilimia tatu kwa bidhaa za chakula. Hata hivyo, katika mikoa mingine, kwa mfano, Morogoro tunalima mahindi, mpunga na viazi yote yanafanana ni biashara pamoja na chakula. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri tozo iwe moja kwa zao moja, iweze kufanana kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo tani moja ambayo wamesema kuwa kama unasafirisha kutoka Halmashauri moja kwenda Halmashauri nyingine ushuru umefutwa. Mheshimiwa Waziri akija kuwa-wind up hapo aweze kulifafanua kwa sababu kuna wakulima wengine kwa mfano nakaa Manispaa ya Morogoro lakini nalima Halmashauri ya Morogoro Vijijini na ukisema tani ni magunia kumi, magunia kumi kwa wakulima wa kisasa wanavuna mpaka magunia ishirini, je, tozo itakuwaje na mimi ni mkulima siyo mfanyabiashara, nimevuna magunia yangu ishirini utanitoza ushuru? Naomba sana Mheshimiwa Waziri aliangalie kusudi aweze kutushauri vizuri kama ushuru utakuwepo au hapana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakwenda kwenye ufugaji, wafugaji kusamehewa malighafi ambayo inatengeneza chakula cha kuku, naishukuru sana Serikali na naipa pongezi. Wananchi wote ambao wanafuga kuku na hasa wanawake itawasaidia sana katika kufuga kuku na itasaidia kuongeza kipato, lishe pamoja na ajira hasa kwa vijana ambao wanamaliza shule na hawana kazi. Ushauri wangu, naomba waangalie mazingira mazuri ya kukopa na hasa Benki ya Kilimo pamoja na Dirisha la TIB, hela zote hizo walizozitenga ziweze kutolewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye mayai yanayototoleshwa na yenyewe inasaidia sana wafugaji. Wale wafugaji vifaranga vilikuwa bei ya juu sasa kwa kufanya hivyo bei ya vifaranga itapungua na gharama pia itapungua, pato litapanda na lishe pia litapanda. Ushauri wangu ni kama huo huo waangalie mazingira mazuri ya ukopaji na hasa Benki ya Kilimo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea kuhusu shamba la kilimo Mkulazi na Mbigiri ambayo tayari yako kwenye mchakato wa kujenga viwanda vya sukari na kilimo cha sukari. Nashauri waangalie out growers, hawa wakulima wetu wa Morogoro ambao wanazunguka mashamba hayo watafaidikaje? Naomba waangalie kusudi na wenyewe waweze kuwa kwenye mpango wa kupata na ajira itaongeze kwa vijana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mapato, kwa kweli nashukuru kuwa Sh.10,000/= ambayo wameiweka kwenye nyumba ambayo haijathaminishwa pamoja na Sh.50,000/= kwa nyumba ya ghorofa itasaidia kuongeza mapato yetu na hasa mapato ya ndani ambapo itasaidia kufanya mipango yetu ya maendeleo. Ila Mheshimiwa Waziri kama maswali yalivyokuwa yanaulizwa akija ku-wind-up aelezee kuwa tumeanza na hizi za Manispaa na Halmashauri ni lini na ni nyumba ya aina gani ambayo itatozwa Sh.10,000/= kama Wabunge wenzangu walivyouliza.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia katika Bunge lako Tukufu. Nianze kwa kumpa pongezi Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya; kwa muda wa miaka miwili na nusu hii amefanya mambo mazuri sana. Mwenyezi Mungu ambariki katika kazi zake zote anazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia kumpa pongezi Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi nzuri naye anayoifanya pamoja na watendaji wake wote wa Serikali, kwa kweli mnafanya kazi nzuri sana; Mheshimiwa Jenista, Naibu Mawaziri pamoja na Makatibu wote na wafanyakazi wote nawapa pongezi sana kwa hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambayo ameitoka hapa Bungeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na mazuri sana ambayo yamefanyika katika Mkoa wangu wa Morogoro, nianze na viwanda. Katika Mkoa wangu wa Morogoro, Mheshimiwa Waziri Mkuu ni shahidi naye juzi juzi alikuja kwenye kiwanda cha sigara, Mheshimiwa Rais ameweza kufungua kiwanda cha sigara. Kwa kweli Morogoro tunakwenda vizuri kwa upande wa viwanda, si mbaya sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa viwanda tuna 21st Century, tuna Mazava na viwanda vingine vyote vinaendelea vizuri. Ila hapa naomba vile viwanda ambavyo havifanyi kazi ambavyo vimekufa, naomba itafutwe namna ya kuvifufua na wale ambao hawawezi kuviendesha naomba sana waweze kunyang’anywa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kiwanda cha magunia, wananchi wengi sasa hivi wanalima wanahitaji magunia ya kuhifadhi mazao yao, lakini hiki kiwanda hakifanyi kazi. Naomba sana Serikali ione jinsi ya kufufua hiki kiwanda cha magunia badala ya kuagiza magunia kutoka nchi za nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Morogoro tayari standard gauge inajengwa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro na naamini kuwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro wataitumia vizuri sana; nampongeza sana Mheshimiwa Rais na Serikali yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Daraja la Kilombero; kwa kweli wananchi wa Morogoro tunashukuru sana kuona kuwa Daraja la Kilombero sasa hivi linafanya kazi na unaweza ukapita wakati wowote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna shamba la miwa la Mkulazi ambalo linafaidisha sana hata wakulima wa nje (out growers), ambao tunaweza tukapata sukari, pamoja na shamba la Mkulazi II ambalo litaongeza sukari. Kwa hiyo kwenye matatizo ya sukari kuna kipindi ambacho huwa tunapata tatizo la sukari, naamini kuwa Watanzania tutaweza kupata sukari pamoja na ajira na mambo mengine; pia na umeme, tutaweza kuzalisha hata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimaliza hayo nakuja kwa upande wa TARURA; pale mjini Morogoro barabara kwa kweli zimeharibika, naomba watu wa TARURA waweze kutengeneza barabara za Morogoro Mjini kwa sababu Morogoro Mjini kuna barabara ambazo unapita zimekuwa mashimo, kwa hiyo naomba sana Serikali iweze kuwapatia hela ili waweze kututengenezea Mji wetu mzuri wa Morogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa afya; naomba niongelee hospitali yetu ya mkoa. Wabunge wengi wa Morogoro hapa Bungeni huwa tunaongelea hospitali ya mkoa, tunaomba kila siku X Ray. Hata Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokuja Morogoro wakati pale anaangalia kiwanda pamoja na Mkulazi II niliomba X Ray na humu ndani Wabunge wenzangu wamekuwa wakiomba kuhusu X Ray. X Ray ya Hospitali ya Rufaa ya Morogoro haifanyi kazi vizuri. Pia tumeomba vifaa vingine kama CT Scan. Naomba muiangalie vizuri Hospitali yetu ya Morogoro, inahitaji kuboreshwa zaidi na zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wetu wa Morogoro kuna Wilaya ambazo hazina hospitali kwa mfano Wilaya ya Mvomero na Morogoro Vijijini. Unakuta Wilaya hizi wagonjwa wengi wanakuja kutibiwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Rufaa na wanarundika sana. Kwa hiyo, naomba kwenye bajeti nijue hii Hospitali ya Morogoro Vijijini ni lini itajengwa? Naamini hela kiasi ilipelekwa lakini hakuna kinachoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haijengwi pale Mvuha iliposemekana basi naomba kiboreshwe Kituo cha Afya cha Dutumi au cha Tawa na kupata hadhi ya Hospitali ya Wilaya pamoja na Mvomero hatuna Hospitali ya Wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye upande wa maji, Mkoa wetu wa Morogoro Wilaya nyingi hazina maji safi na salama hasa Morogoro Mjini kwa kweli mitaa ipo, lakini unakuta kata nyingi hatuna maji safi na salama. Tuliambiwa kuwa Bwawa la Mindu litaweza kukarabatiwa na tukaambiwa kuwa usanifu tayari umefanyika, lakini mpaka sasa hivi haieleweke ni lini hili Bwawa la Mindu litaweza kukarabatiwa na tutaweza kupata maji, kwa sababu ukiongea na Mheshimiwa Waziri wa Maji inaonekana muda wake bado kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye maji pia niongelee kuhusu Wakala wa Maji Vijijini. Naomba Wakala wa Maji Vijijini iweze kuanzishwa kusudi tuweze kupata maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niongelee kuhusu Sh.50 kwa kila lita ya dizeli pamoja na petroli iweze kuwa Sh.100 ili tuweze kupata maji ya kutosha. Wananchi wote wanahitaji maji, hakuna hata Mbunge mmoja hapa ambaye hahitaji maji. Maji ni muhimu sana naomba Wabunge wote waunge mkono kuhusu jambo hili la maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuongelea kuhusu asilimia nne ya akinamama, asilimia nne ya vijana na asilimia mbili kwa walemavu. Ni kweli Halmashauri zingine zinatoa lakini Halmashauri zingine hazitoi. Kwa hiyo, naomba kuwa tamko litoke hapa Bungeni tena Wakurugenzi waweze kutoa hizi hela bila kujali wanapata mapato ya ndani kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa nishati ni kweli Waheshimiwa Mawaziri wanafanya vizuri mdogo wangu Mheshimiwa Subira pamoja na Mheshimiwa Kalemani mnafanya vizuri kwa upande wa REA. Hata hivyo, kuna vijiji mbalimbali kwenye Mkoa wa Morogoro hasa Kimamba, Kitongoji cha Diwani Frola ambacho mmekipitia, lakini wananchi wote wanaokaa hapo hawana umeme. Kwa hiyo, naomba mkiangalie pamoja na vijiji vingine ambavyo bado havijapata umeme wa REA kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa elimu, namshukuru Mheshimiwa Rais na viongozi wote wa Serikali kwa kweli elimu bure (bila malipo) ni nzuri sana. Hata hivyo, naomba mhamasishe kuchangia chakula cha mchana kusudi watoto wetu waweze kupata chakula cha mchana, naona wazazi wengi hawajaelewa. Kwa hiyo, naomba litoke tamko hapa Bungeni kuhamasisha kuchangia angalau chakula cha mchana kwa watoto wetu hawa wanaosoma kwenye shule hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Morogoro upande wa Walimu wa sayansi sekondari tuna upungufu wa Walimu 614 na kwa upande wa maabara tuna upungufu wa maabara 281. Kwa upande wa shule za msingi ambapo mara kwa mara huwa tuna Walimu wengi, lakini sisi tuna upungufu wa Walimu 4,643. Kwa hiyo, naomba wazifanyie kazi hizi takwimu ambazo nimezitoa ili tuweze kupata Walimu wa sayansi kusudi tuweze kwenda na sayansi na teknolojia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kilimo hasa cha umwagiliaji, naomba tukiangalie. Tusiseme tu green house, green house, no, lazima tuangalie tutahamasishaje kilimo kwa sababu bila ya kilimo…

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja ingawa muda ulikuwa kidogo, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii.

Kwanza kabisa nianze kwa kumshukuru Mungu na kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na watendaji wote wa Wizara ya Afya, napenda kutoa shukrani kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tano kwa mambo mazuri inayotufanyia Mkoa wa Morogoro. Imetupatia fedha kwa vituo vitano ambavyo ni Gairo, Mtimbira, Kidodi, Mkuyuni, Kibati na Rupiro. Kwa upande wa Mtimbira tumepata shilingi bilioni 500 kwa ujenzi pamoja na ukarabati na vituo vingine vilivyosalia tumepata shilingi bilioni 400 kwa kila kituo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwa Mheshimiwa Waziri Ifakara Mji, Ifakara hawana Hospitali ya Wilaya na mara kwa mara wanatumia kibaoni Kituo cha Afya Kibaoni kama hospitali yao ya Wilaya. Maombi yalishaletwa ya kukipandisha kituo hiki kiwe Hospitali ya Wilaya. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri aweze kuona kuna haja ya kuipandisha hadhi na kuwa Hospitali ya Wilaya kwa sababu wanakihitaji hasa akina mama na watoto ambao mpaka sasa hivi majengo yapo, lakini kinachokosekana hakuna wodi ya watoto njiti ambao wanazaliwa kabla ya muda wao na wanachanganywa pamoja na watoto ambao wanaumwa, namna hii wanaweza wakapata maradhi kutokana na mchanganyiko huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande mwingine naomba pia kwa upande wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa ambayo mara nyingi tumekuwa tunaomba x-ray pamoja na chumba pekee cha upasuaji wa mifupa, nyote mnajua kuwa Mkoa wa Morogoro unapokea watu wengi ambao wanapa ajali, pia tunaomba gari la wagonjwa tuweze kuongezewa gari lingine kwa sababu Manispaa yetu ina kata 29 pamoja na Wilaya zingine ambazo hazina hospitali na zinatumia Hospitali hii ya Mkoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuongezea hapo kuna Wilaya ambazo hazina hospitali kwa mfano Gairo, Kilombero nilivyosema pamoja na Morogoro Manispaa. Kwa hiyo, naomba sana kuwa tuweze kujengewa hospitali hizi kusudi kupunguza mrundikano wa wagonjwa kwenye Hospitali yetu ya Mkoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Bima ya Afya ni mpango wa Serikali kuwa kila mmoja aweze kutumia bima ya afya. Kwa hiyo, mkakati uliowekwa na Serikali wa kuona kuwa kila mmoja aweze kutumia Bima ya Afya kuangaliwa kwa makini.

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee kuhusu suala la lishe, kwa ukweli kwenye upande wa nchi yetu ya Tanzania bado lishe inahitajika kwa wingi, bado tuna udumavu, bado tuna ukondevu na ninasema kuwa tuna malnutrition ambayo imepitiliza. Naomba hii mikakati ya ambayo wameiweka waweze kuitimiza na naomba kwa sababu suala la lishe ni mtambuka waweze kushirikiana pamoja na Wizara ya Kilimo kwa sababu unaweza ukatumia vyakula na ukapata vitamini pamoja na minerals.

Mheshimiwa Naibu Spika, upungufu wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii. Ni ukweli usiopingika kuwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii ndiyo wanaosukuma maendeleo kwenye Mikoa yetu, kwenye kata zetu na kwenye vijiji vyetu, uliangalie suala hili ili kusudi tuweze kuwa na wataalam wa Maendeleo ya Jamii kwenye kila kijiji na kwenye kila kata kusudi tuweze kusukuma maendeleo ambayo ndiyo yanatakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuongelea uwezeshaji wa wanawake, kuna asilima tano ambayo pamoja na TAMISEMI naomba muweze kushirikiana na TAMISEMI ili kusudi hawa Maendeleo ya Jamii ndiyo wanasukuma maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kusema kuwa naunga mkono hoja na Mwenyezi Mungu akubariki kwa kunipatia nafasi hii na nawapenda sana. Ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naanza kwa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na Awamu zilizopita kwani tayari tumepata daraja la Kilombero. Wananchi wa Morogoro tunashukuru sana na hivi karibuni daraja letu la Kilombero litafunguliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni barabara ya Kidatu – Ifakara – Kitanda - Namtumbo. Hii barabara imetengewa fedha kidogo, lakini tunashukuru Serikali hata kwa kutengewa fedha hiyo. Fedha iliyotengwa ni ya kutoka Kidatu – Ifakara, tunaishukuru sana Serikali kwa sababu hivi karibuni itawekewa jiwe la msingi. Hata hivyo, kwa upande wa kutokea hapo Ifakara - Namtumbo bado haieleweki. Ni muda mrefu tumeisemea tunaomba sana iweze kutengewa hela kwa bajeti zinazokuja au hata sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni usafiri wa anga hasa nikimaanisha viwanja vya ndege vya mkoa. Mkoa wa Morogoro ni mkoa unaokua, una mbuga za wanyama ambazo ni Mikumi pamoja na Selous ambapo unapata watalii wengi na pia kuna ajali zinatokea. Juzi ajali ya ndege ilitokea kwenye kiwanja cha tumbaku ilibidi isukumwe kwa sababu ya kutokuwa na kiwanja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nashauri tufikirie kiwanja cha abiria ambacho kitajengwa Mvomero au Kisaki. Morogoro huwezi kujenga hovyo ovyo kwa sababu ya mambo mengine yanayoeleweka, lakini kwa upande wa Mvomero na Kisaki kinaweza kikajengwa kikatumiwa na watalii wanaokuja kwenye mbuga zetu na kwa abiria pia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Bigwa – Mvuha - Kisaki. Barabara hii tunaiongelea mara kwa mara ambayo ikijengwa kwa lami itasaidia watalii pia na kusafirisha mazao mengi ambayo yanaweza kulisha viwanda vyetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TARURA pamoja na TANROADS, naungana na wenzangu kusema kwamba TARURA iangaliwe kwa sababu bila kupata malighafi kutoka vijijini ambako barabara zake ni mbovu hatutaweza kwa kweli kufanikiwa vizuri sana. Naomba sana itengewe fedha zaidi ili kusudi tuweze kujengewa hizi barabara zetu kadri inavyowezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Ifakara – Mahenge - Mwaya - Ketaketa sijaisikia. Hii ndiyo barabara ya kwenda Selous ambako kuna watalii na malighafi. Kwa hiyo, naomba wakati wanatenga bajeti na yenyewe waifikirie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile barabara ya kutoka Ifakara - Mbingu - Chita na yenyewe sijaisikia. Naomba na yenyewe waiangalie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye mitandao ya simu, kuna sehemu mbalimbali ambazo Wabunge tumempatia Mheshimiwa Waziri ambazo hazina mitandao. Naomba sana waziangalie kusudi na zenyewe ziweze kupata minara ya simu tuweze kupata usikivu kwa upande wa Mkoa wetu wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee barabara ya Magole – Dumila - Kilosa – Mikumi – Mziha – Turiani, naishukuru Serikali imeanza kujengwa kwa lami, lakini kuna sehemu ambayo bado haijajengwa kwa lami. Naamini imetengewa fedha lakini fedha hiyo kidogo iliyotengewa ni kwa sababu ya fidia na hela za kuwalipa wakandarasi. Kwa hiyo, hiyo sehemu ya Ludewa - Kilosa - Mikumi - Mziha - Turiani naomba itengewe fedha kusudi iweze kupitika. Wakati wa mvua barabara ya Kilosa - Mikumi mawasiliano yanakatika kabisa ambapo huko ndiyo mahali ambapo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye Bunge lako tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuwapongeza Mawaziri, Waziri Kamwelwe ambaye ni Waziri pamoja na Naibu kwa sababu walifanya ziara kwenye Mkoa wangu wa Morogoro na walifanya ziara mpaka Malinyi, walifanya ziara Mlimba na Morogoro Mjini lakini ziara imefanyika ila bado kuna matatizo mbalimbali. Nashukuru Serikali kwa miradi ambayo tayari inatoa maji na kwa upande wa umwagiliaji ambayo tayari inafanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na mradi wa maji Morogoro Mjini. Mradi wa Maji Morogoro Mjini umechukua muda mrefu na hiki kilio tumekifikisha mpaka kwa Mheshimiwa Rais alipokuwa kwenye ziara Morogoro, naomba sana huu mradi uweze kumalizika kwa sababu unafadhiliwa na Wafaransa pamoja na Serikali ya Tanzania ambapo Serikali ya Tanzania kwenye bajeti hii imetenga shilingi bilioni nane pamoja na Euro. Naomba sana Waziri aione kuwa ni kazi kweli mradi huu wa maji Manispaa kukosa maji siyo vizuri sana. Kuna baadhi ya Kata ambazo hazipati maji kabisa zingine zinapata maji kwa mgao, kwa hiyo, naomba sana aifanyie kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wakala wa Maji Vijijini kama wenzangu walivyosema naomba na yenyewe ifanyiwe kazi na yenyewe iweze kuanzishwa. Miradi ya Benki ya Dunia ambayo haijamalizika iweze kumalizika. Miradi mingine ya umwagiliaji pamoja na maji viporo iweze kumalizika. Mradi wa Chalinze awamu ya tatu nao umechukua muda mrefu tatizo ni kuwa mkandarasi alisitisha mkataba, naomba ifanyiwe kazi ili kusudi uweze kuanza kwa sababu unatoa maji kwenye Mkoa wa Pwani, Kibaha pamoja na Morogoro kwenye vijiji vingine vya Morogoro kama Kidugalo.

Kwa hiyo, naomba na wenyewe ufanyiwe kazi uweze kufanya kazi, Mheshimiwa Waziri unajua kuwa umechukua muda mrefu naomba uweze kufanyiwa kazi. Bwawa la Kidunda naomba na lenyewe lifanyiwe kazi ni kweli limekuwa la muda mrefu lakini nashukuru naipongeza Serikali kwa sababu imetenga hela, kwa hiyo, hizo hela ziweze kusimamiwa na kuangaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo cha umwagiliaji ndiyo muhimu kwa nchi yetu ya Tanzania kutokana na tabianchi. Ni asilimia 1.6 mpaka sasa hivi ambayo inamwagiliwa, lakini kuna mpango kabambe ambao umepangwa naomba ufuatwe na uweze kukamilika kusudi tuweze kupata kilimo cha umwagiliaji.

Pia naipongeza Serikali kwa miradi ya kilimo cha umwagiliaji ambayo inafanyika Mkoani Morogoro. Kwa mfano, kilimo cha mpunga ambacho kinafanyiwa Msolwa Stesheni, Ujamaa, scheme za Ludewa pamoja na Rumuma na zingine ambazo kwa bajeti hii zimetengewa shilingi bilioni 7.2, naomba hizi hela ziweze kutolewa na ziweze kusimamiwa vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye mteremko wa fedha, mteremko wa fedha wengi wameshachangia lakini naomba hasa kwenye fedha za maendeleo ambapo lazima miradi ya maji iweze kuisha, scheme za umwagiliaji ziweze kukamilika. Naomba hizo hela tunazotenga kwenye Bunge kama inawezekana naiomba Serikali yangu ziweze kupatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu uvunaji wa maji kutokana na tatizo la tabianchi naomba tuweze kufuata uvunaji wa maji na hii sera iweze kufuatwa na kuwekewa mikakati kabisa pamoja na vyanzo vya maji viweze kutunzwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuomba sana tena sana miradi ya maji iweze kukamilika. Umenipatia dakika tano na point zangu nimeziongea kwenye dakika tano.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Nianze kwa kuunga mkono hoja hii. Pia nawapongeza Mheshimiwa Waziri, pamoja na Naibu Waziri na Watendaji wote kwa kazi nzuri waliyoifanya kwenye Sekta hii ya Mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ili uwe na mifugo na ufugaji wa kisasa ni lazima elimu itumike na hii elimu inatolewa na Afisa Ugani. Afisa Ugani ni watu muhimu sana. Kwa upande wa uvuvi kuna uhaba wa Afisa Ugani. Wanaohitajika ni 16,000 lakini waliopo ni 750 tu. Kwa hiyo, kuna Afisa Ugani 15,250. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwa upande wa mifugo na wenyewe kuna uhaba na hata hao waliopo, hawafanyi kazi vizuri. Kwa hiyo, nashauri Wizara kwa kushirikiana pamoja na TAMISEMI iangalie jinsi ya kuwapa mwongozo na utaratibu hawa Afisa Ugani wa Uvuvi na hasa wa Mifugo waliopo waweze kufanya kazi kwa kujituma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mpaka sasa hivi ninapoongea, hawawatembelei wakulima na hasa Maafisa Ugani wa Mifugo. Inabidi uwaite ndiyo waje wakutembelee. Siyo kama zamani walivyokuwa wanajituma. Kwa hiyo nashauri Serikali iangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna sekta nyingine ambayo huwa haiongelewi sana, nayo ni ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nikisema ufugaji wa kuku wa kienyeji, napenda sana nimpe pongezi rafiki yangu Profesa Salome Mtayoba kwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi. Hongera sana kwa upande wa ufugaji. Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni kitu kizuri sana kwa sababu unanufaisha sana familia kwa kuinua kipato na kuwapa ajira ya mara moja vijana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba licha ya Wizara kuona inaweka msisitizo, lakini naona kuwa msisitizo uwe zaidi na zaidi kuhusu hawa akinamama pamoja na vijana, pamoja na familia tuweze kuinua kipato, tuweze kuinua lishe. Sasa hivi tumefikia 32% ya Watanzania wengi hasa watoto ambao ni wadumavu (malnutrition). Kwa hiyo, kwa upande wa lishe, lazima tukazanie kwenye upande wa kilimo hasa ufugaji wa kuku wa kienyeji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nataka kuongelea ni ufugaji wa samaki kwenye upande wa mabwawa (fish ponds au aquaculture). Elimu hii haijaenea sana kwa wakulima au wafugaji. Hiki kilimo cha mabwawa ni rahisi sana kufanyika hata nyumbani kwako. Mahali popote unaweza ukafanya ili mradi una maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwa kuinua ufugaji wa samaki ambao hauna shida kukamatwa nyavu na kupigwa mabomu, naona Wizara ihimize kilimo cha uvuvi wa samaki kwenye mabwawa, kwa kifupi ni fish ponds, ambayo unaweza ukaenda wewe mwenyewe, hata mwanamke mwenyewe ukachukua samaki wako ukaja ukapika mara moja, watoto wako wakapata lishe na familia nzima ikapata lishe na kupandisha kipato. Kwa hiyo, nauliza upande wa Serikali, mkakati mkubwa sana waliouweka kwenye upande wa ufugaji wa samaki kwenye mabwawa ukoje? Naomba utiliwe mkazo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niongelee migogoro ya wafugaji pamoja na wakulima. Kwa upande wa Mkoa wa Morogoro, hii bado ipo, hatuwezi kusema imekwisha. Imetulia kidogo kwa sababu sasa hivi kuna mvua, majani yanapatikana, malisho yanapatikana, ndiyo sababu imetulia. Ukienda kilosa kwenye Kijiji cha Mabwegere bado kuna matatizo ya wafugaji pamoja na wakulima. Akinamama hawapati raha kwenda kulima, kama mnavyojua wakulima wengi, zaidi ya asilimia 70 wanaotoa chakula ni wanawake.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sana waliangalie hilo. Dawa yenyewe iliyopo ni matumizi bora ya ardhi. Kwa hiyo, tuendelee kupima ardhi kusudi watu waweze kupata ardhi yao na waweze kuona ni wapi pa kulishia.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni elimu ya malisho. Jambo lingine ambalo linaweza likaondoa migogoro ya wafugaji pamoja na wakulima ni Elimu ya Malisho. Elimu ya Malisho bado haijaenea sana. Naomba sana wawahimize hao wafugaji na hii inawezekana wakiipata hii elimu hata kuhama hama kwa hawa wafugaji kutaacha, kwa sababu wataweza kustawisha malisho yao na wataweza kuyatumia wakati wowote na inaweza ikasaidia hata wakati wa kiangazi kwa sababu watatengeneza hay ambayo wanaweza kulisha mifugo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, fedha za maendeleo, kama tulivyoona, kwa msimu wa mwaka 2017/2018 kwa upande wa mifugo iliinidhishwa shilingi bilioni nne na kwa upande wa uvuvi shilingi bilioni sita. Mpaka Machi mwaka huu 2018, hakuna hela yoyote ya maendeleo ambayo ilikuwa imeshatolewa. Sasa kama hela za maendeleo hazitolewi, miradi itaendeleaje au itafanyikaje? Kwa hiyo, naomba kama tunaidhinisha hela humu Bungeni, tujitahidi Hazina pamoja na Serikali kwa ujumla hela ziweze kutolewa kwa wakati.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuchangia katika Bunge lako Tukufu angalau kwa maandishi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri wote kwa kazi nzuri wanayoifanya. Napenda kumpongeza Waziri Jafo na Manaibu wote wawili, Katibu Mkuu na Watendaji wote chini ya Waziri wa TAMISEMI kwa kazi nzuri wanayofanya. Naishukuru Serikali kwa miradi yote ya maendeleo iliyotolewa kwa Mkoa wetu wa Morogoro, kutokana na Morogoro Vijijini kutokuwa na hospitali ya wilaya naiomba na kuishauri Serikali yangu kupandisha Kituo cha Afya Dutumi na kuwa hospitali ya wilaya, majengo yapo, iko kwenye baadhi ya majengo ambayo yaliachwa na wafadhili bila ya kukamilika, naomba Serikali ione jinsi ya kukamilisha majengo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hiki Kituo cha Afya Dutumi kiangaliwe kwa namna ya pekee kwani Wauguzi na Madaktari hawatoshi. Kituo hiki kinachukua takribani kata saba, lakini kata hizi ziko mbalimbali. Kwa sababu ya kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto, nawaombea wanawake wa Morogoro Vijijini gari la wagonjwa. Wanawake hawa wanapata shida sana kwa kuletwa kwenye kituo cha afya hiki. Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI tafadhali awasaidie wanawake wajawazito na watoto na watu wengine (wagonjwa) kwa kuwapatia gari la wagonjwa katika kituo hiki cha Dutumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa kutupatia hela za baadhi ya vituo vya afya katika Mkoa wetu wa Morogoro. Ombi langu licha ya kutokuwa na hospitali ya wilaya katika Wilaya ya Morogoro Vijijini, pia hatuna hospitali za wilaya katika Wilaya ya Mvomero na Gairo, pia Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ambayo inajengwa kuwa hospitali ya wilaya bado haijakamilika. Tunaomba hospitali za Wilaya katika Wilaya hizo nilizozitaja hapo huu na pia kukamilisha ambazo bado kukamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Afya Mafiga kinatoa huduma kubwa. Akinamama wajawazito na hasa wanawake wanapenda kujifungulia katika Kituo cha Afya Mafiga. Tatizo wagonjwa wajawazito hasa akinamama wanaishi katika mitaa na kata za mbali, kiasi wakati mwingine hupatwa na matatizo ya uzazi, kwani hakuna gari la wagonjwa la kuwakimbiza kwenye kituo hicho cha afya. Mheshimiwa Waziri nawaombea gari la wagonjwa wanawake hawa wenye matarajio ya kujifungua salama na kupunguza vifo vya akinamama wajawazito na watoto. Gari lililopo ni la zamani na mara kwa mara ni bovu, pia linatumika kwenye vituo vingine vya afya katika Manispaa ya Morogoro.

Mheshimiwa, Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro tuna upungufu wa Walimu wa shule za msingi zaidi ya ……pia tuna upungufu wa Walimu wa sayansi 641 katika shule za sekondari. Naishauri Serikali izidi kuajiri Walimu wa sayansi mpaka shule za vijijini kadri Walimu wanavyohitimu vyuo. Pia ukosefu wa Walimu, nashauri kuwepo usambazaji wa Walimu hawa wa msingi sawasawa mjini na vijijini kadri nchi yetu inavyosonga mbele kwa miradi ya kisayansi ndivyo wanasayansi wanavyohitajika. Kwa hiyo, ombi na ushauri wangu, Serikali yangu ya Awamu ya Tano iliangalie suala hili la upungufu wa Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu lingine ni kuhusu TARURA. TARURA wawezeshwe ili barabara za Manispaa Morogoro zitengenezwe. Barabara nyingine kwa sasa zina mashimo. Je, hao TARURA mbona hawaendi speed inayotakiwa mpaka barabara za vijijini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu na hasa katika badhi ya mikoa na hasa mikoa inayozalisha sana mazao kuna utapiamlo uliokithiri pamoja za udumavu zaidi ya asilimia 42. Pia kumezuka tatizo la utapiamlo uliopitiliza, viriba tumbo. Nashukuru kwa Serikali kwa mikakati inayoiweka kuhusu masuala ya lishe na uhakika wa chakula Tanzania, tatizo hili bado ni tete kitaifa na hasa kwenye mikoa niliyoitaja inazalisha chakula kwa wingi. Naomba Serikali ilione hili ni tatizo la wananchi wake na izidi kulifanyia kazi na kuweka mikakati ya kutokana na tatizo hili kwa makundi yote ya Watanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya lishe ni mtambuka, watu wengine wanawake kwa wanaume, pia mna Wabunge wengi hawajui masuala ya lishe. Ombi langu kwa kuanzia hapa Bungeni na kushirikiana na Serikali masuala ya lishe, uhakika wa chakula yaangaliwe kwa umakini. Namna hii tutakuwa na Taifa la watu wenye afya nzuri na wachapa kazi, pia lishe nzuri, inasaidia kupunguza magonjwa yanayotokana na utapiamlo wa aina yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nashauri kuwe na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Lishe na Uhakika wa Chakula.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Kwanza naomba kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri na Naibu Mawaziri wote kwa jinsi wanavyofanya vizuri. Naomba pia kumpa pongezi Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kuiona hii sekta ya madini ni muhimu sana na jinsi anavyoiendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba niongelee Mkoa wangu wa Morogoro. Mkoa wa Morogoro una madini mbalimbali. Kwa mfano, Wilaya ya Morogoro Vijijini kule Mkuyuni pamoja na Matombo kuna madini ya dhahabu. Madini haya ya dhahabu yanachimbwa na wachimbaji wadogo wadogo. Hawa wachimbaji wadogo wadogo hawana elimu na mara kwa mara wanachimba na kusafishia kwenye mto mkubwa uliopo hapo hapo Mkuyuni na wanatumia zebaki ambayo wakati mwingine si nzuri kwa binadamu. Kwenye kitabu cha Wizara sikuona vizuri kama Mkuyuni na Matombo imeonekana kuwa tuna dhahabu na wanachimba sana na ipo miaka mingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Ulanga kuna rubi nayo ni ya muda mrefu, miaka nenda rudi. Kwa hiyo, naomba itambuliwe kuwa Ulanga kuna rubi na inachimbwa na wachimbaji wadogo na inaonekana hawana elimu na soko. Naomba sana hawa wachimbaji wadogo waweze kupatiwa teknolojia nzuri ya uchimbaji wa madini na kupatiwa soko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Afisa Madini wa Mkoa, naamini mikoa mingi au kila mkoa kuna Afisa Madini, lakini nilivyosikia na navyojua hakuna Maafisa Madini wa kutosha kwenye wilaya zetu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba hilo aliangalie kwa sababu hawa Maafisa Madini ndiyo wanapaswa watoe elimu kwa wale wachimbaji wadogo ili waweze kuelewa wachimbeje madini hayo na wauze wapi. Kwa sababu hawana elimu wanajichimbia wenyewe, hawana vifaa, wakiona jiwe hawaelewi kuwa ni kitu gani wanaendelea wenyewe bila ya kuelewa. Kwa hiyo, naomba hawa Maafisa Madini waweze kupelekwa mpaka huko wilayani ambako madini yanachimbwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Kilosa, kuna madini mengi hata mengine siyajui, ni majina ya watu kama Felista nilikuwa sijui kuna madini yanaitwa Felista. Felista ni jina la mama yangu, sasa nakuta kuwa kuna madini yanaitwa Felista. Pia kuna madini ya rubi, red garnet, moonstone lakini sikusikia kama yametajwa, naomba Mheshimiwa Waziri ayafanyie kazi. Mkoa wa Morogoro ni tajiri kwa madini naomba wauangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana, nimeona kwenye kitabu Mheshimiwa Waziri amesema kwamba utafiti wa awali umefanyika kwenye Mkoa wa Morogoro ila sikuona kama haya madini yametajwa kuwa yanatoka kwenye Mkoa wa Morogoro. Kwa hiyo, naomba iangaliwe kuwa tunatoa madini na tuweze kupata wawekezaji kusudi tuweze kuwa na maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wachimbaji wadogo wadogo hawana elimu, wapewe elimu na ruzuku ili kusudi waendelee vizuri na uchimbaji wao na waweze kuongeza mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naelewa unafahamu kuna Chama cha Wanawake Wachimbaji naomba nao waweze kupatiwa elimu kusudi waweze kuchimba. Unajua ukimuendeleza mwanamke hasa kwenye machimbo na sasa hivi tumesema kazi yoyote hakuna mwanaume hakuna mwanamke yeyote yule anaweza akafanya kazi hii, naomba Mheshimiwa Waziri awaangalie hawa wachimbaji wanawake waweze kuendeleza nchi yetu na kujiletea mapato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Morogoro kuna wawekezaji wamekuja, kuna mazungumzo yanaendelea hasa Ulanga. Naomba sana waangaliwe kwa sababu hawa wawekezaji tunaomba wawekeze lakini wasiwasumbue wachimbaji wadogo wadogo. Wachimbaji wadogo wapate nafasi yao na hawa wawekezaji waweze kupata nafasi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna graphite, sijui kama Mheshimiwa Waziri anajua kuwa Ulanga kuna graphite. Kwa hiyo, naomba Waziri aangalie na Ulanga ili iweze kuendelea na kunufaika na madini yanayopatikana huko. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais kwa ujenzi wa ukuta wa Mererani. Kwa kweli amefanya jambo zuri katika kudhibiti utoroshaji wa tanzanite ambayo ilikuwa inatoroshwa inaunzwa nje na haifahamiki kuwa imetoka Tanzania inafahamika imetoka mahali popote pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ninalokazia sana ni kuhusu soko la madini hapa nchini. Nashauri Waziri ahakikishe soko la madini linakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna tin kule Cherwa ambayo tangu nazaliwa naisikia kule lakini mpaka sasa hivi hakuna kitu chochote kimefanyika kuhusu madini haya.

Mheshimiwa Waziri anafahamu madini ya tin, naomba sana nayo yaangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi, ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Mpango wa 2019/2020. Nianze kwa kuwapongeza kuwa huu mpango ni mpango mzuri sana ambao kila mmoja kwa kweli ana uangalia na inabidi ajivunie kwa sababu ni mpango mzuri. Jambo ambalo naomba kuongelea naomba nishauri kuwa miradi ambayo imeshaanzishwa hasa kwa muda mrefu naomba sana iangaliwe kwenye vizuri kwenye Mpango huu, kwa mfano huu mpango wa Mchuchuma na Liganga uweze kumalizika na kuangaliwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba kushauri kwenye maendeleo ambayo yapo maboma wananchi wengi wamejenga maboma ya shule, maboma ya zahanati, maboma ya vituo vya afya na vyenyewe naomba viangaliwe kwenye mpango huu viweze kuhusishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni umeme, umeme ndio nashukuru na ninapongeza Serikali, nampongeza Mheshimiwa Rais anafanya vizuri sana, lakini kuna vijiji pamoja na vitongoji ambavyo bado havijapata umeme kwa hiyo ningeliomba viweze kuangaliwa kwenye mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba kuangaliwa kwenye Mpango huu, ni maji, maji ni muhimu sana, unakuta kweli Wizara ya Maji inafanya vizuri sana lakini kila mmoja ananikubalia kuwa licha ya kufanya vizuri bado kuna matatizo ya maji kwenye sehemu mbalimbali, kwa hiyo naomba sana hili jambo liangaliwe hata kwenye Kata yangu ya Magadu bado tuna tatizo la maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba liangaliwe ni kwenye mikopo ya elimu ya juu. Naomba sana vigezo viangaliwe kusudi wanafunzi wengi waweze kupata mikopo, kwa sababu unakuta amefaulu lakini hakujaliwa kupata mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine ninaloongelea ni kilimo, kilimo kinaajiri zaidi ya watu zaidi ya 65.5% na asilimia 100 ya chakula kinatoka kwenye kilimo, lakini tunafanya vizuri ndio kwenye kilimo, lakini bado hatujapata kipaumbele kabisa kwenye upande wa bajeti naomba sana, Mheshimiwa Waziri Dkt. Mpango uangalie kuwa kuna tulikubaliana kwenye Malabo kuwa ni 10% kwa hiyo tuangalie kuwa itakuwaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwenye upande wa utafiti hatuwezi kuendelea bila ya utafiti, kwa hiyo tutenge hela za kutosha kwenye mpango huu tuone kuwa utafiti utakwendaje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye upande wa pembejeo uzalishwaji wa mbegu nashauri na naomba mpango uwepo wa kuzalisha mbegu hapa nchini, yaani tuzalishe sana hapa nchini kuliko kuchukua mbegu za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba kuongelea kwenye kilimo, ni viwanda vya kuzalisha mbolea, ndio vimeanza lakini bado havijachukua kasi, kwa hiyo, kwenye mpango huu, licha ya kuwa na mbolea inayoingia kutoka nje, lakini naamini kuwa tukizalisha kwenye viwanda vyetu hapa Tanzania mbolea itakuwa chini na wakulima wengi wataweza kuinunua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni viwanda vya dawa za wadudu, yaani viwatilifu, nashauri kuwa tuwe na viwanda, mpaka sasa hivi tuna kiwanda kwa wastani kimoja ambacho kiko Njombe (Mafinga) cha Pareto naomba sana,.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana tuwe na viwanda vingi, naomba niongelee uvuvi, uvuvi bado hatujaendelea vizuri kwenye uvuvi wa bahari kuu, naomba sana tujikite kwenye mpango wetu huu kuangalia jinsi tukavyoendeleza uvuvi wa bahari kuu na yenyewe tukazie sana kwenye mpango huu ununuzi wa meli ili tuweze kuwa na meli zetu za uvuvi kwenye bahari kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, ni ujenzi wa bandari ya uvuvi, niko kwenye uvuvi, tuweze kuwa na bandari ya uvuvi, kusudi tuweze kuvua samaki ambao wanatoka kwenye bahari kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, cherezo, tukiwa na meli tuweze kuwa cherezo yetu, ambayo imejengwa hapa nchini kusudi meli zetu ambazo tutanunua kwenye mpango huu, ziweze kutengenezwa na kukarabatiwa kwenye nchi yetu badala ya kwenda Mombasa na nchi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine tuwe na viwanda, mpaka sasa hatuna viwanda vya kuchakata samaki, hasa wa bahari kuu, kwa hiyo naomba tuweze kuwa na mpango uweze kuhusisha viwanda vya kuchakata samaki bahari Kuu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa mifugo, mifugo tuweze kuwa na mpango ambao utahusisha kuwa na ufugaji wa kisasa, sio ufugaji wa kuhamahama na hasa tuki-focus sana kwenye malisho, uwepo mpango wa kwenye malisho pamoja na mpango wa kwenye viwanda, pamoja na mpango wa kwenye mambo ya miundombinu, nikisema miundombinu namaanisha ujenzi wa mabwawa pamoja na majosho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naongelea kwenye upande wa mazingira, mazingira yetu mpaka sasa hivi, hayafurahishi kwa hiyo naomba sana, mpango wetu huu, uweze kuhusisha mambo ya mazingira. Kwenye mpango huu wa 2019/2020 mipango iliyopita imeonesha changamoto, naomba kwenye mpango huu ambao tunakwenda nao wa 2019/2020 tuweze kuona jinsi ya kutatua hii changamoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ili niweze kuchangia machache kwenye Wizara hizi. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Waheshimiwa Mawaziri hasa wa Wizara hizi pamoja na Manaibu, nawapa hongeza sana kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na mambo ya afya; kwa Mkoa wetu wa Morogoro kwa kweli na Tanzania nzima afya imefanya vizuri sana, Nashukuru kuona kwenye bajeti hii ya mwaka 2019/2020 tumeweza kutengewa fedha kwenye vituo vya afya Mkoani Morogoro ikiwepo Mvumi, ambayo imetengewa milioni 200 ambayo na mimi nimeshaichangia matofali 2000. Pia napongeza kwa upande wa kituo cha afya cha Dumila ambao na wenyewe wametengewe milioni 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu ni kwa vituo vya afya vingine ambavyo bado havijaweza kutengewa, kikiwepo kituo cha afya cha Mzinga, ambacho tayari wamejenga kwa nguvu za wananchi, lakini hakijakwisha, kikiwepo na Magadu pamoja na Mafisa na vituo vingine ambavyo sikuvitaja kwenye Mkoa wetu wa Morogoro kwenye Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia natoa pongezi zangu kwa Serikali kwa upande wa kutenga fedha za hospitali za Halmashauri ya Wilaya. Tunashukuru sana kwa upande wa Gairo, tumeweza kutengewa milioni 500, Kilombero milioni 500, Mvomero milioni 500, pamoja na Morogoro Wilaya milioni 500. Hii kwa kweli nashukuru kwa sababu Hospitali ya Mkoa ilikuwa inapata matatizo sana ya msongamano wa wagonjwa hasa kwa upande wa wazazi ilikuwa ni kazi kweli, kwa sasa hivi naona tatizo hili litakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sijaona hela kwenye upande wa hospitali ya Wilaya ya Manispaa ya Morogoro ambayo inajengwa na inatumika, lakini haijatumika sawasawa kwa sababu bado haijakamilika. Kwa hiyo, naomba Serikali waweze kuangalia na waweze kunijibu kama kweli wamenitengea kwa sababu sijaona hela yoyote ya hospitali ya Manispaa pale mjini. Naomba hospitali hii iweze kuangaliwa vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa watumishi hasa kada ya afya pamoja na elimu kwa Mkoa wa Morogoro bado tuna matatizo. Kwa upande wa wataalam wa afya na hasa ukikuta kwenye vituo vile ambavyo viko pembezoni kwenye Wilaya za pembezoni kama Malinyi, Ulanga unakuta kuwa kituo cha afya au zahanati inaweza ikawa na Mganga mmoja ambaye hawezi. Halafu mimi mwenyewe nimeshuhudia, unakuta hivi vituo vya afya vingine vinafungwa saa tisa. Jioni havifanyi kazi, usiku havifanyi kazi, hapo kwa kweli sielewi. Naomba Wizara waliangalie kwa sababu ugonjwa hauchagui ni saa ngapi unaumwa, saa yoyote unaumwa, kwa hiyo naomba waliangalie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa elimu, Walimu ni pungufu na hasa kwa upande wa Walimu wa sayansi naomba watupatie hao Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo furaha sana kuipongeza Serikali kwenye miradi ya kimkakati kwa kweli Manispaa ya Morogoro tunaringa na wananchi wanajivuna na Mkoa wa Morogoro wote kwa sababu Manispaa ni kioo. Mpaka sasa hivi tuna soko ambalo tunajenga, soko zuri sana ambalo tumetengewa shilingi bilioni tati na milioni mia tano kwa bajeti hii. Kwa hiyo tunashukuru, pia tuna wale wanaopita pale Stendi, wote mnaiona kuwa Stendi ya Morogoro ni nzuri kwa hiyo tunaishukuru Serikali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu ya msingi bila malipo, Mkoa wa Morogoro kwa kweli Serikali inafanya vizuri chini ya Mheshimiwa Rais, lazima niipongeze kwa sababu upande wa elimu bila malipo, kwa upande wa shule za msingi tumeweza kutengewa zaidi ya billioni sita na pia kwenye sekondari zaidi ya bilioni sita. Tunaishukuru sana Serikali iendelee kufanya vizuri kama inavyofanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ninaloomba ni kwa upande wa hosteli, hospitali ambazo zitajengwa naomba ziweze zijengwe kwenye shule za wasichana kwa sababu watoto wa kike wanapata matatizo sana na wao wanayajua kwa mimba za utotoni na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeona kuwa kuna magari kama 40 ambayo yatanunuliwa na kutawanywa kwenye halmashauri ambazo zina mazingira magumu. Kwa kweli kwenye Halmashauri ambazo zina mazingira magumu naomba kuomba kupatiwa gari moja kwa Halmashauri ya Malinyi, ambayo iko mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uwezeshaji wananchi kiuchumi, asilimia nne kwa wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa walemavu ni jambo zuri sana ambalo limeweza kufanywa na Serikali, lakini kuna wale ambao hawatimizi masharti. Naomba hayo masharti yaangaliwe vizuri kusudi hao vijana waweze kurudisha kwa wakati na hizi hela ziweze kuwasaidia. Kwa upande wa wanawake wanarudisha vizuri, lakini vikundi viko vingi, kwa hiyo naomba Wizara wanisikilize, waweze kuangalia jinsi ya kuwasaidia hawa wanawake ili waweze kupata hela nyingi na za kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TARURA, ni kweli wanafanya vizuri lakini wanapata hela kidogo. Kwa upande wa Morogoro kwa barabara za vijijini naona hawajaweza kuendelea vizuri kwa sababu hela hazitoshi. Kwa hiyo, naomba waongezewa hela ili kusudi waweze kufanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Manispaa kuna barabara za pembezoni ambazo wanazisahau. Kwa mfano kama barabara za Magadu na SUA kwa wasomi. Naomba na zenyewe waweze kuzitengeneza vizuri kadiri inavyowezekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwa upande wa lishe. Tanzania yetu ina udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano ambapo 34% wamedumaa, kuna utapiamlo lakini Serikali imeweza kuona kuwa ni jambo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Dkt.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja za Wizara zote mbili, ahsante sana na Mwenyezi Mungu awabariki. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa natoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pia napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Wizara nzima kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza napongeza kwa kuongeza fedha za mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Ombi langu ni kwa ajili ya angalizo kwa wanafunzi waliotokea kwenye shule za private. Kigezo cha kutowapatia mikopo wanafunzi waliopitia shule za private, kuwanyima mikopo, nashauri lifanyiwe kazi. Wananchi siku hizi wamepata mwanga na wanapenda watoto wao wasome kwa hali yoyote ile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli wazazi wengine wanasomesha kwenye hali ngumu, hasa wenye mlezi mmoja kama mtoto wa mama ntilie au akina mama wengine wanadunduliza hela ili mtoto wake asome. Mimi ni shahidi Morogoro na mikoa mingine kuna akina mama wanasomesha watoto wao kwa kupitia kulima na kuuza mchicha au kwa kupika maandazi au chapati. Mheshimiwa Waziri, tafadhali sana kigezo cha wanafunzi kusoma private kifanyiwe uchunguzi wa ndani, watoto wengine waliopitia mkondo huu wanapaswa kukopeshwa asilimia kubwa kwani hali yao ni duni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napongeza kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa ukaguzi na kubaini vyuo vikuu venye upungufu kwa ubora wake kama Chuo Kikuu. Namshauri sana Mheshimiwa Waziri kuhusu ufuatiliaji wa mienendo ya vyuo hivi, ni muhimu kuliko kwenda kama zimamoto na kuvifunga vyuo (baadhi) kwa kutokuwa na ubora. Ni bora vyuo vikafuatiliwa na kupewa ushauri. Vyuo hivyo vikijirekebisha kufuatana na upungufu, viendelee na kutoa elimu kama kawaida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyuo hivi hasa ni vya binafsi vikiwepo vingi vya dini. Vinapofungwa ghafla wanafunzi wanapata shida kwa kubadilishwa na kupelekwa vyuo vingine. Walimu waliokuwa wanafundisha vyuo hivyo wanapoteza ajira zao na mpaka sasa hawajui kinachoendelea. Naomba Mheshimiwa Waziri anapokuja kuahirisha, nipate ufafanuzi kuhusu hatima ya wanafunzi na walimu waliokuwa kwenye vyuo hivi, hasa walimu na wafanyakazi, hatima yao ya ajira ni nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri kitengo hiki cha ukaguzi kipewe fedha zote zilizotengwa pamoja na miundombinu kama magari. Ili kuboresha elimu yetu, ni muhimu kuboresha kitengo hiki cha ukaguzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri kuna kanda ambazo hakuna technical college hata moja. Vyuo hivi vinasaidia sana wahitimu kujiajiri hasa wale waliomaliza Form IV na Form VI. Mheshimiwa Waziri, Kanda wa Ziwa wanaomba angalau chuo cha ufundi kimoja. Ni mengi mazuri yanayofanywa na Serikali yangu ya Awamu ya Tano, naomba nishauri hili liangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu bila utafiti na pia walimu wa sayansi ni tatizo. Nashauri fedha inayotengwa kwenye utafiti na hasa vyuo vikuu zitolewe zote ili utafiti uendelee. Ni muhimu sana kuendelea kupunguza hili tatizo la walimu wa sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sera ya Kila Wilaya Kuwa na Chuo cha VETA na hasa wilaya za pembezoni lipewe kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia katika bajeti hii ya Maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kukupongeza wewe na pia kwa kuwapongeza Mawaziri; Mheshimiwa Profesa Mbarawa pamoja na Mheshimiwa Aweso kwa kazi nzuri wanayoifanya. Kusema ukweli wanahangaika sana, wanafanya kazi sana, miradi ya maji imeongezeka, maji yameongezeka, lakini tatizo moja bado watu wanahitaji maji. Ninavyoongea sasa hivi, ni asilimia 64.8 ya wananchi wamefikiwa vijijini na asilimia 80 mijini wamefikiwa na maji. Kwa hiyo, watu bado wanahitaji maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikileta mfano mmojawapo kwa Mkoa wangu wa Morogoro, ambao ni mkoa uliojaliwa ambao una mito mingi sana, lakini mpaka sasa hivi sehemu nyingi za Mkoa wa Morogoro wana matatizo ya maji. Kwa mfano, nikija kwenye Mji mdogo wa Gairo, Malinyi, Vijiji vya Morogoro Vijijini, Mvomero pamoja na Kilosa bado wana matatizo ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa maji ambao ni wa Manispaa Morogoro ni tatizo mpaka sasa hivi kwani umechukua muda mrefu. Ni kweli naamini Serikali inajitahidi na imesema kuwa kuna Euro milioni 70 ambayo itafadhiliwa itasaidia pamoja Serikali pamoja na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), lakini tatizo ni kuwa mpaka sasa hivi umechukua muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri na Mheshimiwa Naibu Waziri wanajua tatizo la Morogoro na tatizo la manispaa, nilishaongea na Mheshimiwa Waziri na Waheshimiwa Wabunge wameongea naye na amekiri kuwa kweli ni tatizo. Naomba atuambie tufanyeje Mkoa wa Morogoro hususan manispaa ili upungufu wa maji uweze kwisha na wananchi waweze kupata maji. Ninavyoongea hivi, Kola A, Kola B na Mkundi hawapati maji kabisa na wale Kata zinazopata maji hazipati maji ya kutosha, wanapata maji pungufu. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri atujibu tufanyaje kama kuna uwezekano wa kuona tufanyeje ili waweze kupata maji waweze kuchukua hatua hiyo tukiwa tunasubiri huo mradi mkubwa unaoshirikisha Bwawa la Mindu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni miaka mitatu sasa hivi imepita tunajadili kuhusu kuongeza tozo ya maji kutoka Sh.50 kwa lita mpaka Sh.100 lakini mpaka sasa hivi bado utekelezaji ndio tatizo. Humu Bungeni tulishapitisha, lakini tatizo ni utekelezaji, sijui kwa nini; Mheshimiwa Waziri naomba atujibu. Naamini kuwa kama tungekuwa tumeongeza hiyo tozo au tumechukua njia nyingine ya kuongeza huo Mfuko wa Maji wa Taifa tungekuwa tumeweza kupata maji mengi ya kutosha na hasa maji huko vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inathibitishwa kuwa mwaka huu Aprili, fedha zilizotolewa kwa miradi ya maendeleo asilimia 67 zilitoka kwenye Mfuko wa Maji na asilimia 17 tu zimetoka kwenye vyanzo vingine vya maji. Naomba waweze kutueleza tutafanyaje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Bwawa la Kidunda. Ujenzi wa Bwawa la Kidunda tangu nimeingia humu Bungeni nasikia ujenzi wa Bwawa la Kidunda, ujenzi wa Bwawa la Kidunda. Naomba kujua ingawaje na leo wameweka ujenzi wa Bwawa la Kidunda, lakini inaonekana kuwa bado hakuna hela na bado hakuna mfadhili. Kupanga ni kuchagua, naomba tuone tufanyaje kwani kwenye Bwawa la Kidunda linasaidia sana kuongeza maji kwenye Mto Ruvu; Ruvu Chini na Ruvu Juu pamoja na megawatt 20 za umeme pamoja na maji ya umwagiliaji. Kwa hiyo, nafikiri na barabara ya kutoka Ngerengere kwenda mpaka Kidunda. Naomba na yenyewe iweze kupewa kipaumbele hili jambo la Kidunda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, uanzishwaji wa Wakala wa Maji Vijijini yaani huyu ni mfadhili mkubwa sana. Naishukuru na kuipongeza Serikali kwa kuanzisha Wakala wa Maji Vijijini, ila ninachoshauri ikisimamiwa vizuri na ikapewa hela ya kutosha, naamini kuwa itafanya kazi nzuri na maji yataweza kuongezeka Vijijini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji, nikiongelea Morogoro, vyanzo vya maji vingi vimeharibika. Tulikuwa na Misitu ya Uluguru, maji zamani na ninyi mnajua ilikuwa inaimbwa kuwa maji yatiririka milimani Morogoro lakini sasa hivi nenda hakuna maji yanayotiririka; vyanzo vimeharibika, mito inakauka, mito inakuwepo wakati wa mvua. Kwa hiyo, hii ni kama kokote kule, kwa hiyo naomba katika vyanzo vya maji waendelee kutoa elimu tuone wakisaidiana pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu kutunza vyanzo vya maji. Vyanzo vya maji sera zipo, naomba sera zitiliwe mkazo kusudi tuweze kupata maji ya kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umuhimu wa uvunaji maji. Miongozo na sera zilishatolewa kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi lakini sera hazitekelezwi. Naomba kwa kusaidiana na Wizara zingine, hii nasema nina uhakika nayo kuwa zilishatolewa, kwa hiyo naomba sana waweze kutekeleza na kusimamia hizi sera na miongozo kusudi uvunaji wa maji hasa kupitia kwenye mapaa ya majumba kwenye taasisi na nyumba ya mtu mmoja mmoja iweze kutekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa kulipia maji kabla ya kutumia (prepaid). Prepaid ni mfumo mzuri, huu mfumo hausumbui, kwenye ziara zetu tumekutana nao Arusha na Kishapu, watu hawasumbuliwi. Kwa hiyo, nashauri kuwa kwa kusaidiana na TAMISEMI na Wizara zingine, huu mfumo wa prepaid uweze kutumika kusudi watu waweze kutopata matatizo wakati wa kulipa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi mingi ya maji huchukua muda mrefu kukamilika kwa sababu fedha zinazotolewa hazitoshi, tumeona mpaka Aprili ni asilimia 51 tu imetolewa. Kwa hiyo, nashauri kuwa hela zote ambazo zitapitishwa za maendeleo ziweze kutolewa. Mheshimiwa Waziri wa Fedha naamini ananisikia kusudi tuweze kupata maji, maji ni muhimu, maji ni uhai; naomba sana fedha itolewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Maji Chalinze ni wa muda mrefu ambao huu Mradi wa Maji Chalinze Awamu ya Tatu umesimama, mkandarasi alishindwa na mpaka sasa hivi bado hajatafuta mkandarasi mwingine. Mheshimiwa Waziri wa Maji afanye juhudi sana ili tuweze kupata mkandarasi mwingine kwani huu mradi wa Chalinze unasaidia hata Vijiji vya Morogoro ikiwemo Kidugalo, Ngerengere pamoja na vijiji vingine vya Chalinze. Mtiririko wa fedha za miradi ya maendeleo naomba utiliwe mkazo kusudi ziweze kutolewa kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa ukusanyaji wa maduhuli, imejitahidi kukusanya maduhuli kwa sababu kufikia hadi Machi imekusanya asilimia 81. Kwa hiyo, naamini kuwa ikijitahidi kukusanya maduhuli hata miradi mingine itaweza kuendelea kuwa mizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa, naipongeza Serikali kwa miradi mikubwa yote inayotekelezwa ikiwemo mradi wa Lake Victoria ambao unaleta maji mpaka Tabora, Uyui, Shinyanga na mahali popote. Wanafanya vizuri ila naomba wajitahidi wananchi bado tunahitaji maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya hayo, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kusimama katika Bunge hili Tukufu na kuchangia machache kwa maandishi, hotuba ya bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. Pia, nachukua nafasi hii kumpa pongezi Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na wataalam wa Wizara nzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inafanya mambo mengi mazuri, hasa kuhusu mambo ya afya ikiwepo ujenzi wa vituo vya afya na upatikanaji wa dawa. Natoa shukrani kwa Hospitali yetu ya Mkoa/Rufaa Morogoro kwa kutupatia X-ray ya kidigitali, tunashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na umuhimu wa Hospitali ya Rufaa Morogoro, tunaleta ombi letu kuhusu kupewa mashine ya CT-Scan ambayo ni muhimu sana. Hii ni kukumbushia ahadi ambayo ilitolewa hapo awali na viongozi wetu wa taifa wakati wa ziara Morogoro. Nashukuru kwa yote mazuri yaliyotendeka kwa kutupatia gari la wagonjwa na X- ray, kwa imani hii naamini hata CT-Scan tutapewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri na naomba Hospitali za Wilaya za Mkoa wetu za Gairo, Ifakara, Morogoro Vijijini na Mjini ziendelee kupewa fedha na kujengwa na kukamilika. Mheshimiwa Waziri nasema haya kwa sababu Hospitali ya Mkoa inazidiwa na wagonjwa (mrundikano wa wagonjwa) kwani Wilaya za Mkoa hazina hospitali.

Mheshimiwa Naibu Spika, napongeza kwa ujenzi wa Kituo cha Afya Mikumi, majengo ni mazuri na hivi karibuni kitaanza kutumika. Mpaka sasa ameletwa daktari mmoja, naomba na kushauri waletwe wataalam wengine zaidi kusudi wananchi wapate matibabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo nililoliona katika kituo hiki ni ukosefu wa jengo la mortuary. Ujenzi mzima unaendelea kukamilika ila hakuna mpango wa mortuary. Naiomba Serikali yangu ifikirie jambo hili kwani Mikumi, hususan Wilaya ya Kilosa, kuna watu wengi na hivyo hata jengo hili ni muhimu ingawaje watu hatutaki kusikia kifo.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kwa vituo vya afya vinavyoendelea kujengwa. Nashauri mpango huu uendelee kuvifikia vituo vya afya ambavyo wananchi wamejenga na kuachia ngazi ya maboma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati wa Vituo vya Afya Dutumi na kumalizia majengo yaliyokaa muda mrefu, hilo ni ombi letu wananchi wa Morogoro Vijijini. Katika ziara zangu Zahanati ya Hembeti ambayo inatumika pia kama Kituo cha Afya kwenye Kata ya Hembeti, Wilaya ya Mvomero, majengo yake yamechakaa sana tena sana. Naiomba Serikali zahanati/kituo cha afya hiki kikarabatiwe. Pia, hakuna wataalam wa kutosha kuanzia madaktari hadi manesi. Kituo hiki nashauri kiangaliwe vizuri ili kizidi kutoa huduma nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu ina tatizo la utapiamlo na hasa udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano. Tatizo kubwa ninaloliona ni elimu kwa wananchi. Nashauri elimu ya lishe ya mkakati na ya vitendo itolewe zaidi. Wananchi wakipata elimu ya kutosha kuhusu mambo ya lishe hasa kwa akina mama wajawazito na akina mama wanaonyonyesha utapiamlo utapungua au utakwisha kabisa hapa nchini Tanzania kwani kwa ujumla vyakula vya kutosha tunavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vituo vya maendeleo ya jamii. Naomba na kushauri ukarabati wa vituo hivi. Ni kweli wataalam wa maendeleo ya jamii wanatakiwa sana na muhimu kwa kusukuma maendeleo ya jamii yetu hapa nchini. Watumishi hawa ni muhimu sana kwa kusukuma maendeleo. Nashauri kila kijiji kiweze kupata Afisa Maendeleo ya Jamii ili kuharakisha maendeleo ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Ndoa. Na mimi naungana na Wabunge wenzangu kusema kuwa kutokana na hali na maendeleo tuliyonayo sheria hii ni ya muda mrefu na imepitwa na wakati. Nashauri iletwe humu Bungeni ili ibadilishwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ugonjwa wa malaria udhibiti wake uangaliwe kwa undani.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuchangia hayo, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuchangia kwa maandishi hotuba ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa ununuzi wa ndege sita, ujenzi wa reli ya mwendo kasi na mambo mengi sana ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kuhusu barabara ya Bigwa – Mvuha – Kisaki (Morogoro Vijijini) kwa kiwango cha lami. Wabunge wa Morogoro tumekuwa tunachangia mara kwa mara na kuambiwa kuwa itatengenezwa lakini kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri sikuweza kuiona kama kweli imetengewa fedha. Naomba Mheshimiwa Waziri atueleze wananchi wa Morogoro Vijijini ni lini barabara hii ya Bigwa – Mvuha - Kisaki itajengwa kwa kiwango cha lami na ikakamilika?

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa kutengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 2,020.00 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi sehemu ya Rudewa – Kilosa (km 24). Barabara hii nimekuwa nikiizungumzia mara kwa mara na hasa kipande cha Kilosa – Mikumi. Kipande hiki wakati wa mvua kinakuwa kibaya sana na kupitika kwa shida. Maelezo ya mara kwa mara ni kuwa wafadhili hawajapatikana. Je, ni lini kipande hiki kitatengewa fedha na Serikali au kitapata wafadhili kwa ujenzi wa kiwango cha lami?

Mheshimiwa Spika, napongeza kwa fedha zilizotengwa shilingi 12,135.00 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya Kidatu-Ifakara (Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo – Lumecha – Songea). Nashauri fedha zilizotengwa 2019/2020 zitolewe zote na kwa wakati kwani mpaka sasa ujenzi huu unafanyika polepole au unasuasua.

Mheshimiwa Spika, Serikali chini ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano, imefanya mambo mengi mazuri. Hata hivyo, nakumbushia barabara muhimu sana ya Lupiro – Mahenge – Mwaya kwa ujenzi wa kiwango cha lami. Kwenye hotuba hii sijaona kuwa barabara hii imetengewa fedha. Barabara hii nimekuwa nikiisemea pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ulanga kwani kuna faida zinazopatikana Ulanga kama madini, utalii pamoja na mazao mbalimbali kama mpunga. Naomba maelezo ni lini barabara hii itaanza kuongelewa, kutengewa na kupatiwa fedha na ujenzi wa lami kuanza?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Magole – Turiani – Mziha – Handeni. Nianze kwa kutoa pongezi kwa barabara hii, ujenzi wake unaenda vizuri na wananchi wa Wilaya ya Mvomero wanaipenda na kuishukuru Serikali yetu inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, nashukuru Serikali kwani mradi huu umetengewa shiling milioni 1,170.00 katika mwaka wa fedha 2019/2020 kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya barabara ya Turiani – Mziha – Handeni (km104). Naamini kuna wakati barabara hii itakamilika na wananchi wa Mvomero na Handeni watafurahi zaidi kwani miundombinu itakuwa vizuri.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa ujenzi wa reli ya mwendokasi. Wananchi wanaisubiri kwa hamu ikamilike, hasa wa Mkoa wa Morogoro Vijijini, Morogoro Mjini, Kilosa na Mkoa mzima wa Morogoro kwa ujumla. Wananchi waliopisha umeme wa reli hii ya mwendokasi wanaulizia ni lini watalipwa fidia yao? Ni vyema wakaelezwa kwani ni muda sasa umepita tangu evaluation imefanyika.

Mheshimiwa Spika, natoa hongera kwa Mheshimiwa Rais kwa ununuzi wa ndege sita na ukarabati wa viwanja vya ndege unaoendelea. Tuliahidiwa ujenzi wa viwanja vya ndege sehemu za utalii, Mkoa wa Morogoro ujenzi wa kiwanja cha watalii Selou Kisaki (Morogoro Vijijini). Kwa kushirikiana na Wizara husika ya Utalii, nashauri uwanja huu ujengwe.

Mheshimiwa Spika, mawasiliano. Kuna orodha ya vijiji na kata vya wilaya ya Mkoa wa Morogoro ambavyo amepewa Mheshimiwa Naibu Waziri. Naomba wakajengewe minara ili waweze kupata mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, usalama wa usafiri kwenye barabara ya Dar es Salaam – Morogoro – Dodoma. Kuna magari makubwa/malori mengi na baadhi ya ajali husababishwa na magari haya. Nashauri mwenendo wao barabarani udhibitiwe.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa uliokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niweze kuchangia kwenye mpango huu wa maendeleo, napenda kumpa pongezi kwanza Mheshimiwa Rais kwa mambo mazuri aliyeyafanya na anaendelea kuyafanya hasa kwenye miradi yote ambayo inatekeleza na ambayo imeshatekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili nimpongeze Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake na watendaji wote kwa mambo mazuri kutuletea huu mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuongelea kwenye mambo ya vipaumbele hasa vinavyowagusa wananchi nikianza na kilimo, kilimo kama tulivyosema kina ajiri asilimia 65 ya wananchi na kimekuwa kwa asilimia 5.3 na kinachangia pato la Taifa kwa asilimia 28. Licha ya hivyo nilikuwa naomba huu mpango tukiweza kuondoa umasikini hasa kwa watanzania naona kilimo kiweze kiweza kipaumbele kwa sababu wananchi wengi tunaona kuwa wanaajiriwa pamoja na kilimo. Kwa upande wa kilimo hasa kuna utata wa afisa ugani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nashauri kuwa tuelekeze kwenye mpango wetu huu kutumia TEHAMA kutokana na tatizo hili tutumie TEHAMA hasa kwenye simu zetu kwa kuwafikia wakulima kuwapa ushauri kutokana na TEHAMA tunaweza tukafikia wakulima wengi, hii teknoloji tayari imeanza kutumika kama kwa kuanzia kufuatana na NGO’s mbalimba na taasisi mbalimbali na watafiti na imeonekana kuwa inafaa. Kwa hiyo, kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo Mheshimiwa Dkt. Mpango naomba tuangalie jinsi ya kuwekeza kwenye kilimo na kwa kutumia IT hasa kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na nikisema kilimo kuwa kinapunguza umasikini siyo kilimo cha kawaida ninyi mnajua ni mashahidi mmeona kuwa mabadiliko ya tabia nchi. Kwa hiyo, naomba huu mpango uwekeze sana kwenye kilimo cha umwangiliaji tukiwekea kwenye kilimo cha umwangiliaji tutakuwa na uhakika kuwa tutawasaidia wakulima wengi kutokana na kilimo kwa sababu wakulima wengi wanalima mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo jingine ambalo nilikuwa nataka kuongelea kuhusu kilimo ni kuwa hatujawekeza sana kwenye uvuvi wa bahari kuu kwenye upande wa uvuvi naomba huu mpango safari hii ujiwekeze na kujielekeza sana kwenye uvuvi wa bahari kuu na hii iendane pamoja na viwanda vya kuchakata mazao ya uvuvi kwa sababu ukiangalia hatuna viwanda vingi vya kuchakata mazao ya uvuvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye ufugaji, kwenye upande wa ufugaji tunafuga ndiyo lakini huu mpango uangalie licha ya kuwa na mifugo mingi lakini hatuna viwanda hasa vya kuchakata mazao ya ndani hasa kama maziwa mnaona mpaka sasa hivi viwanda vya maziwa ni vichache sana na bado tuna import maziwa ya unga kuja kufanya maziwa fresh kwahiyo nilikuwa naona huu mpango uweze kuwekeza kwenye viwanda vya ndani ambavyo vitaweza kuchakata mazao yetu ya kilimo uvuvi pamoja na ufugaji na hasa hasa ni kimaanisha kwenye upande wa viwanda vya maziwa na matunda na mafuta kwa mfano unaona hatuna viwanda vingi vya mafuta ninyi nyote ni mashahidi mnaona mafuta yanakaakaa barabara yana grow rancidity yanafanya nini kwa hiyo nilikuwa nashauri kuwa tuweze kupata uwekeze kwenye viwanda kusudi tuweze kufufua na kuendeleza viwanda ambavyo vinastahili kwa mazao yetu ya ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kinachogusa kwa upande wa mpango ni maji upande wa maji naona kweli Wizara inafanya vizuri sana lakini mpaka sasa hivi wananchi wote hawajapata maji tukitaka kwenda vizuri kwenye mpango huu wa 2020/2021 naomba sana tuwekeze sana kwenye maji kwa sababu wananchi wote waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ni asilimia 64 tu vijijini na asilimia 80 mijini kwa hiyo mwaka ni kesho 2020 tuweze kupata maji ya kutosha angalau vijiji vyote viweze kupata maji ya kutosha. Hivyo hivyo nakwenda pamoja na umeme, umeme nashukuru mawaziri mnafanya vizuri sana kwa upande wa nishati, lakini naomba vile mpango na wenyewe huu mpango uweze kujikita usiache umeme ingawaje wanafanya vizuri hasa tuweze kuona kufikia vijiji vyate kwenye umeme kusudi twende vizuri kwenye umeme na wananchi wote waweze kupata umeme ingawaje wanafanya vizuri naomba tusivisahau.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ninalopenda kuongelea haraka haraka TARURA inafanya vizuri lakini kama wenzangu walivyosema ni kweli wanapewa asilimia kidogo asilimia 30 haiwezi kutoza barabara zote za mjini za TARURA na barabara za vijijini zinazoendeshwa na TARURA na hasa barabara za mashambani kwahiyo naomba huu mpango uweze kuelekeza kwenye mambo haya na wenyewe waweze kupata fungu zuri kwenye mpango wetu huu tunaokwenda nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kuongea hayo naomba kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais tena na tena kwa Standard Gauge kwa sababu sasa hivi inakwenda kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro asilimia 63 na kuendelea mpaka kutoka Makutopola kuendelea ningependa iweze kufikia mwanza pamoja na Kigoma iende haraka kusudi barabara zetu ziache kuharibika barabara zetu zinaaribika kwa sababu lori. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kwa mfano tukipata hii ikaisha itaweza kusafirisha mizigo na barabara zetu zitaendelea kuwa nzuri kwa hiyo huu mpango unawenyewe ujielekeze huko tuone jinsi tutakavyomaliza na pongezi nyingine natoa kwa bwawa la Nyerere nasema ahsante sana naamini wananchi wote likiisha wataweza kupata umeme wa kutosha kwa hiyo, na hapo hapo nasema Mpango wa ardhi waweze kuangali mpango wa ardhi kwa sababu kuna mambo ya utalii hapo na kuna mambo ya kilimo cha umwangiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naomba kupongeza kwa kutupatia Halmashauri pale Morogoro kutupatia Halmashauri ya Kilombelo pamoja na Halmashauri ya Mlimba naamini mambo yatakwenda vizuri na sisi nikiwa Mbunge wa viti maalum naamini tutafanya kazi nzuri kwenye halmashauri hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru ahsante sana na Mwenyezi Mungu akubariki naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia. Kwanza kabisa nawapa pongezi Wenyeviti wote wawili wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji pamoja na Kamati ya Ardhi. (Makofi)

Mheshimimwa Mwenyekiti, nianze mchango wangu kwa kuwapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri hasa kwa upande wa Kilimo, Maji pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Nawapa pongezi sana hasa kwa upande wa mifugo, kwa kweli mambo waliyoyafanya yote yanaonekana ni mazuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa kilimo, naomba nichangie kuwa wote tunajua kuwa asilimia 80 ya Watanzania wanategemea kilimo. Pia kilimo kinachangia kwa asilimia 30 ya pato la Taifa na asilimia 95 ya chakula kinatokana na kilimo, asilimia 30 ya mauzo ni ya nje na asilimia 70 malighafi inachangia malighafi ya viwanda.

Mheshimiwa Spika, nikisema hivyo, naomba na ninashauri kuwa kilimo kipewe kipaumbele na hasa kwenye bajeti tunayokuja kutunga hapo baadaye kuwa asilimia 10 ya bajeti nzima iweze kwenda upande wa kilimo ili kuweza kutekeleza Azimio la Abuja pamoja na Malabo.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana na ninaipongeza Serikali kuona Tume ya Umwagiliaji imerudishwa Wizara ya kilimo kutoka Wizara ya Maji kwa sababu tangu wameingia huko kwenye Wizara ya Kilimo, ndiyo wenyewe tunategemea sana kilimo cha umwagiliaji. Huwezi kuongea kilimo cha umwagiliaji bila ya kuongea kilimo. Kilimo cha umwagiliaji ndicho tunachotegemea sana kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Mheshimiwa Spika, Tume ya Umwagiliaji tangu wamehamia Wizara ya Kilimo, nawapongeza Serikali pamoja na Benki ya Dunia kwa kuweza kukamilisha vizuri mradi wa kuongeza mpunga unaotekelezwa huko Mkoani Morogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia Tume ya Umwagiliaji imeweza pia kukamilisha miradi mingine, pamoja na skimu 10 kama Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo alivyoisema kwenye Kamati yetu ambayo tumeiorodhesha. Ila tatizo lililopo ni kuwa walikuwa watekeleze tena miradi mingine mitano lakini hawakuweza kuitekeleza kwa sababu ya tatizo la fedha. Ninaloshauri na tunaloshauri ni kuwa fedha za maendeleo na hasa zinazotoka kwenye nchi yetu naomba ziwe zinatengwa za kutosha na ziwe zinatolewa kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, wote tunaelewa kuwa mboga mboga na matunda ni muhimu sana kwa afya ya binadamu na hasa kwa upande wa lishe ya binadamu kutoka kwa mtu mzima mpaka kwa mtoto, tunahitaji kupata matunda pamoja na mboga mboga pamoja na vyakula vingine. Kwa hiyo, kilimo cha mboga mboga na matunda kinaajiri watu zaidi ya 8%.

Mheshimiwa Spika, ninachoshauri hapa ni kuwa soko lipo ila uzalishaji bado haujawekwa sawa sawa. Kwa hiyo, nilichokuwa nashauri, uzalishaji kwa wingi uweze kuangaliwa, pia na soko la uhakika liweze kuonekana vizuri sana kwa sababu kilimo cha mboga mboga na matunda unakuta ni vijana wengi na akina mama ndiyo wanaolima kilimo hiki.

Mheshimiwa Spika, tatizo kubwa lililopo ni tozo na kodi ambapo Kamati imeona kuwa ni zaidi ya 45 hivi. Hii tuliongea na TAHA ambao ndiyo sana sana wanaoshughulika na mambo ya kilimo cha mboga mboga na matunda.

Mheshimiwa Spika, kilimo mseto wote tunakijua. Kilimo mseto ni kuchanganya changanya mazao mbalimbali, hasa ndiyo kilimo mseto ambapo wakulima wadogo wadogo Tanzania tumekizoea sana. Kilimo hifadhi ni ile unalima mazao yanafunika udongo, unyevunyevu unabaki, halafu unaweza ukafanya kilimo cha kubadilisha badilisha kiasi rutuba inabaki kwenye udongo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nilikuwa nashauri kuwa kilimo mseto pamoja na kilimo hifadhi viweze kuhimizwa kwa wananchi kwa sababu kama unatumia kilimo mseto na unatumia unachanganya kwa mfano mahindi pamoja na karanga au pamoja na maharage, zile nodules mizizi yake inatengeneza nitrogen. Kwa hiyo, kama inatengeneza nitrogen unaweza ukapunguza matumizi ya mbolea ya kemikali na ukatumia hiyo mbolea ya asili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi nawapongeza sana kwa upande wa mifugo. Mmefanya vizuri, mmepunguza mambo mengi, samaki wameongezeka kwenye mifugo, lakini soko bado samaki bei iko juu. Kwa hiyo, tunaomba sana kuhusu hilo. Pia nawapongeza kwa sababu ya kutoa 0.4 mrabaha ambao inaweza ikachangia kuleta mapato mengi kwa muda hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, kuhusu bandari, nilikuwa nashauri tena, najua Serikali iko kwenye mkakati wa ujenzi wa bandari, lakini mpaka sasa hivi bado hawajaamua ni wapi itajengwa hii bandari. Hapo naongelea uvuvi wa bahari kuu. Kwa hiyo, naomba ili tuweze kuongeza kipato cha nchi yetu lazima tuangalie uvuvi wa bahari kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine ni ufugaji wa viumbe kwenye maji.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na Mwenyezi Mungu akubariki zaidi na zaidi. Ahsante.
Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya pamoja ya ziada ya Nagoya – Kuala Lumpur kuhusu Uwajibikaji Kisheria na Fidia kwa Madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi ya Bioteknolojia ya Kisasa katika Kutekeleza Itifaki ya Cartagena (Nagoya – Kuala Lumpur Supplementary Protocol on Liability and Redress on Cartagena Protocol on Biosafety) pamoja na Azimio la Kuridhia Itifaki ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika kuhusu Kulinda Haki Miliki za Wagunduzi wa aina mpya za Mbegu za Mimea. (Protocal for Protection of New Varieties of Plants (Plant Breeder’s Rights) in The Southern African Development Community – SADC) pamoja na Azimio la Kuridhia Mkataba wa Marrakesh wa mwaka 2013 unaowezesha upatikanaji wa kazi zilizochapishwa kwa watu wasioona, wenye uoni hafifu au ulemavu unaomfanya mtu kushindwa kusoma (The Marrakesh Treaty to Facilitate Access to Published Work For Persons Who Are Blind, Visually Impaired or Otherwise Print Disabled)
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii. Nami najikita kwenye Azimio la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Afrika (SADC) kuhusu kulinda hatimiliki ya Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu Pamoja na Mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu hawa, wagunduzi, ambao wamefanya utafiti wao wa muda mrefu, kama hii ikiridhiwa itakuwa nzuri sana kwa sababu ya kupata motisha. Watakuwa wanamotisha sana na wataona kuwa wametambuliwa na watazidi kufanya utafiti wao kusudi waweze kupata huo ugunduzi na waweze kugundua aina mpya za mbegu pamoja na mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Azimio hili likiridhiwa, nchi yetu nayo itaweza kufaidika kwa njia mbalimbali kupitia mapato kwa sababu aina mpya hii ya mbegu za mimea tunaweza kubadilishana pamoja na nchi nyingine za SADC kwa njia ya uhalali. Hapo mwanzoni ilikuwa haibadilishwi kwa njia ya halali kwa sababu tulikuwa tumejifunga kwenye nchi yetu ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, vijana wetu na wenyewe watapata motisha kuweza kuchukua haya masomo ya Plant Breeding ambayo yatawawezesha kufanya utafiti na kugundua aina hizi mpya za mbegu za mimea kusudi waweze kutambulika na waweze kuendelea vizuri pamoja na nchi yetu kuweza kunufaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema kwenye Kamati, nchi yetu itaweza kufaidika pamoja na wagunduzi kwenye mrabaha ambao pia unaweza kutumika mrabaha mwingine kuendeleza ugunduzi mpya kwenye mambo haya ya aina mbegu za mimea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe mwenyewe na watu wengine walikuwa wanafahamu kuwa tatizo la mbegu hasa hapa nchini ni kubwa sana, lakini kwa kuridhia huu mkataba, hawa watafiti baadaye wakigundua na kuwa wagunduzi, wataweza kujikita sana kwenye tafiti zao na kugundua aina mpya za mbegu za mimea ambazo zitaweza kuzalisha mbegu nyingi hapa Tanzania na tutaweza kupata mbegu hizi kwa urahisi bila matatizo yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikisema wagunduzi, simaanishi wale ambao wamesoma tu, kuna wagunduzi wakulima ambao na wenyewe wanagundua na hawa wakulima na wenyewe itawalinda kusudi waweze kugundua aina mpya za mimea pamoja na mbegu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ajira itazidi kuwepo kwa sababu vijana wengi na wakulima watajikita kwenye ugunduzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo naweza kuongelea hapa ambalo nchi yetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Dakika tano zako zimekwisha. Mheshimiwa Eng. Chiza.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa hilo. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye bajeti hii ya mifugo pamoja na uvuvi. Kwanza nianze kwa kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais, Waziri Mkuu, kwa kazi nzuri wanayoifanya, pia na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo, Mheshimiwa Mpina, Mheshimiwa Ulega, Naibu, Katibu Mkuu Prof. Elisante, pamoja na Katibu Mkuu wa Uvuvi, Tamatama.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema kuwa, Wizara ya Mifugo, pamoja na Uvuvi, inajitahidi ninapenda kuwapa pongezi kwa kazi nzuri sana wanayoifanya. Licha ya bajeti kupungua pungua au kufanya nini, lakini wanajitahidi sana kwa kazi nzuri wanayoendelea nayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kuwapongeza, naomba niongelee kwenye bajeti ya maendeleo, ni kweli, bajeti ya maendeleo imeshuka, imeshuka kwa asilimia 40. Kwa hiyo, nashauri kuwa, hiyo fedha ndogo mnayoipata na kuwa wasiwasi na hiyo miradi ya maendeleo itatekelezwaje kwa hiyo fedha kidogo bilioni tano, naomba sana, tena sana hiyo fedha itakayotolewa, iweze kutekelezwa vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, operations za uvuvi, operations za uvuvi zimekuwa zikiendeshwa hapa nchini, Pwani, Kanda ya Ziwa, Tanga, pia hiyo ni Pwani pia. Lakini tunaweza kukutana na wavuvi, kwa kweli operation ni nzuri, naipenda, ni nzuri na Serikali inaipeda, kwa sababu inainua kipato, hao samaki wanaweza kuzalia kwa sababu operation hiyo inasaidia samaki waweze kutaga vizuri, kuliko waweze kuvuna samaki wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mpina nilikuwa nashauri elimu endelee; kabla ya kuchoma nyavu za hao wafugaji waweze kupata elimu ya kutosha ya ni saizi gani ya matundu inayotumika kwa samaki, dagaa, kwa samaki sangara, kwa samaki terapia? Ni aina gani na ni wapi wanapatikana? Swali linakuja, je, tukishazichoma hizo nyavu wale wanaoleta nyavu hapa nchini wanafanywaje? Nilikuwa naomba pia waweze kulifuatilia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna migogoro ya ardhi na watumiaji ardhi. Hii migogoro ya ardhi inatokana na; kwa mfano kwa upande wa wafugaji na wakulima, nina mfano kidogo; juzi juzi pale Ulanga mifugo imeingia kwenye shamba la mpunga pale Nakafulu, wamekula mpunga wote wamemaliza. Kwa hiyo nilikuwa nashauri kuwa mikakati iwepo ya kuwaeleza kuwa wafugaji na wakulima waheshimiane ili migogoro iweze kupungua.

Mheshimiwa Spika kuna mikakati inayoendelea ambayo imepangwa na Serikali, naomba hiyo mikakati iweze kutimilika isiwe mikakati tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Malisho.Tatizo hili la migogoro linaletwa na malisho. Nikisema malisho ya mifugo naamanisha mikunde pamoja na nyasi. Mtoe elimu ya jinsi ya kustawisha hayo malisho (shamba darasa).

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nashauri kuwa haya mashamba darasa yawe kwenye kila kata, hasa kwenye mikoa ile ambayo ni ya wafugaji, ili waweze kujua ni malisho gani na jinsi ya kustawisha hayo malisho.

Mheshimiwa Spika, vilevile tatizo lililopo ni mbegu; mbegu za malisho hazipatikani kwa urahisi. Kuna wakulima wafugaji ambao wanatafuta mbegu lakini hazipatikani madukani. Ningeliomba Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri hizi mbegu ziweze kupatika mashambani kusudi Maafisa Ugani waweze kufanya kazi yao ya kuwaelimisha hawa wafugaji jinsi ya kustawisha haya malisho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kuhusu Ufugaji wa Kisasa. Ni kweli mifugo iko mingi, iko hata hapa Dodoma, iko Manyara, iko Mwanza, na iko kila mahala. Hata hivyo ninaishauri Wizara kuwa ule mpango mkakati mliouweka naomba ufuatwe ili tuweze kufuga kwa kisasa na tuweze kupata mazao mema mazuri kutoka kwenye mifugo yetu. Mifugo tukiiendeleza vizuri tunaweza kupata kuinua kipato chetu pamoja na lishe kutokana na mifugo. Kwa hiyo nilikuwa nashauri jambo hilo.

Mheshimiwa Spika, Vyakula vya Mifugo Hasa Kuku. Ni kweli kuwa tulitoa tozo na ada tulipunguza kwenye vyakula vya kuku hapa Bungeni. Hata hivyo, licha ya kupunguza hizo tozo na ada tatizo bado liko palepale kwenye vyakula vya kuku. Akina mama na vijana wangeweza kweli kufuga kuku, lakini wanapata tatizo kwa sababu vyakula vya kuku bado viko juu. Najua Mheshimiwa Waziri utaweza kuniambia kuwa watumie malighafi inayozalishwa hapa nchini. Ni kweli, nimefanya utafiti, viwanda hivi ni vya hapa nchini, vinazalisha chakula cha kuku na vinatumia malighafi inayozalishwa hapa nchini lakini bado chakula kiko juu. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri naomba ulifanyie kazi kusudi wanawake, vijana, na wakulima wengine waweze kuendelea kwenye tasnia hii ya ufugaji wa kuku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tozo kwenye Sekta hii ya Mifugo imekuwa kubwa na nyingi lakini nashukuru na naipongeza Serikali. Kwenye hotuba ya Waziri amesema…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante Dkt. Ishengoma.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kabla sijamaliza naunga mkono hoja, lakini uvuvi wa aquaculture, naomba utiliwe mkazo.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye mapendekezo ya bajeti ya 2019/ 2020. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri Mpango pamoja na Naibu wake, Katibu Mkuu na wataalam wote kwa kazi nzuri waliyoifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kusema ukweli, bajeti hii iliyosomwa safari hii, mimi nimefanya utafiti huko nje, nimeongea na watu na wasomi na kila mmoja, bajeti hii wameipenda vizuri sana. Wanasema hawajawahi kuona bajeti nzuri kama ya safari hii, Mheshimiwa Waziri songa mbele. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu na Mawaziri wote kwa kazi nzuri mnayoifanya, bajeti hii wameipenda, imegusa kila mmoja, wanasema ni bajeti nzuri mbayo hawajawahi kuiona. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza kuipongeza Serikali kwa kufanya uhakiki na kulipa madeni ya wazabuni pamoja na watoa huduma, mmefanya kazi nzuri, bado mnahakiki. Licha ya hivyo naomba kukwambia kuwa kuna baadhi ya vyuo ambavyo ni vya kilimo, baadhi ya shule za sekondari kwenye Mkoa wangu wa Morogoro ambao bado hawajalipwa kama MATI Ilonga kuna na sekondari ya Morogoro kuna wanaodai. Naomba waifanyie kazi na ninavyosema hivi, bila shaka kuna na mikoa mingine kuna wazabuni na wakandarasi ambao hawajalipwa naomba waendelee kuhakiki Serikali iweze kuwalipa kama ilivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kuongelea mambo ya vipaumbele kwenye bajeti hii na nianze kwa viwanda pamoja na kilimo. Ili viwanda viweze kuendelea lazima tuangalie kilimo, kilimo ndiyo kinacholeta malighafi kwenye viwanda na ninaposema kilimo hapa namaanisha kilimo mazao, uvuvi na mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa kilimo asilimia 65.5 ya wananchi wanategemea kilimo na hasa huko vijijini na asilimia ya chakula asilimia 70 ni wanawake wanaozalisha chakula hiki. Kwa hiyo, naomba tunavyoongelea kilimo tuwape kipaumbele wanawake na hasa kuangalia kwenye upande wa mikopo na kuangalia jinsi watakavyoendeleza kilimo hiki. Hakuna kilimo/chakula bila ya kumuangalia mwanamke. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ila kuna changamoto kidogo kwenye upande wa kilimo, bado tunatumia kilimo cha jembe sana sana ingawa naipongeza Serikali kwa upande wa matrekta yameongezeka, lakini unakuta bado tuna matatizo tunatumia kilimo cha mvua, bado ni kilimo cha mvua kinashamiri. Kwa hiyo nilikuwa naiangalia na kuiomba Serikali yangu iangalie kilimo cha umwagiliaji. Tukifanya kilimo cha umwagiliaji, tutaweza kusonga mbele na tutaweza kupata malighafi ya kutosha kwenye mazao yote ambayo tunalima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa jambo lingine kubwa sana kwenye matatizo ya kilimo ni mbegu. Mbegu hapa nchini tunazalisha asilimia 21 tu, mbegu nyingine zinatoka nje, tatizo ni nini? Tatizo ni ASA ambao ndiyo wanadhibiti na wazalisha mbegu, ASA hawana bajeti ya kutosha. Mheshimiwa Waziri naomba ASA wapate bajeti hiyo waliyoomba fedha ziweze kupitishwa zote kwa pamoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kuzalisha hizo mbegu, wanaodhibiti hizo mbegu ni TOSCI, TOSCI na wenyewe hawana fedha, naomba na wenyewe waweze kupewa fedha za kutosha kusudi tuweze kupata mbegu za kutosha. Huko ni kwa upande wa mazao hasa nafaka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwenye mbogamboga (horticulture) pamoja na matunda ni asilimia moja tu ya mbegu tunazalisha hapa nchini na sanasana ni vitunguu. Kwa hiyo, naomba sana kwa sababu mbegu nyingi zinatoka nje, je, tatizo ni nini? Naomba sana na yenyewe ni ASA hawana fedha za kutosha, naomba muwapatie fedha za kutosha, huo ndiyo ushauri wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ni mbolea; tunategemea mbolea kutoka nje. Tuna kiwanda kimoja cha Minjingu, Minjingu nayo haipendwi sana hapa nchini, kwa nini, ni baadhi ya wachache wanaipenda. Kwa hiyo, nilikuwa naomba Serikali yangu na hapa wanaohusika watuambie Kiwanda cha Mbolea cha Lindi ni lini kitaanza kuzalisha mbolea? Kwa sababu tukipata mbolea yetu, naamini tutaweza kulima na kuzalisha vizuri sana kwa sababu mbolea pamoja na mbegu bora tutaweza kupata mazao bora ambayo yanaweza kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana hii programu ya SAGGOT pamoja na ASDP, Serikali wamepanga mkakati mzuri kwenye upande wa kilimo, naomba hela zote zilizopangwa kwenye mkakati huo ziweze kutoka na zikitoka tutaweza kupata mazao ya kutosha.

Mheshimiwa Naibu Spika, masoko yanaenda pamoja na mazao na viwanda. Nashukuru kuona viwanda vimeanza kujengwa, kuna viwanda vya korosho vipo, naipongeza Serikali wanajitahidi kwenye kuangalia na kuangalia wakulima wa korosho wawasaidiaje, siyo kusema wamewaachia wanawasaidia kadri wanavyoweza na najua kila kitu kitakwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mazao ya mikunde tumeweza kupata kiwanda hata Morogoro tuna kiwanda kimejengwa ambapo tutaweza kununua mbaazi, karanga na maharage. Kwa hiyo, hata matatizo yaliyokuwepo kwa upande wa mbaazi yatakwisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikisema kilimo inakwenda na miundombinu/barabara; kuna barabara za mashambani, barabara za mashambani zingine zimesahaulika, naomba sana ziangaliwe. Kuna barabara za uchumi; nikisema barabara za uchumi kwa upande wa Morogoro kuna barabara ya kutoka Kidatu – Lupilo – Malinyi – Songea, Namtumbo. Tumetengewa hela kidogo, naomba Mheshimiwa Waziri hela hizo zilizotoka ziweze kutolewa na zenyewe ni za ukarabati. Hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, iweze kujengwa kwa lami kwa hiyo ndiyo hivyo uchumi utaendelea na kwa sababu inaunganisha mikoa miwili; Mkoa wa Ruvuma pamoja na Mkoa wa Morogoro iweze kuangaliwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikija kwa upande wa mifugo, mifugo tuweze kufuga mifugo ya tija. Kwa upande wa mifugo waangalie sana kuhusu malisho. Naomba bajeti yote iliyopangwa kwenye malisho iweze kutoka pamoja na matumizi bora ya ardhi. Tulisema kuwa ardhi iweze kupimwa, ikipimwa hakutakuwepo matatizo yoyote na wafugaji wataweza kufuga vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uvuvi; uvuvi wa bahari kuu bado hatujautendea haki. Naomba sana Serikali yetu iangalie uvuvi wa bahari kuu, maziwa, mito na uvuvi ambao tunasema ni wa mabwawa. Ili tupate samaki wengi, lazima wananchi wahamasishwe kufuga kwenye mabwawa na hii itasadia hasa na kwenye utapiamlo kwenye mambo ya lishe. Fedha zote zilizotengwa kwenye mambo ya lishe ziweze kutolewa na ziweze kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ukuaji wa uchumi kwa maendeleo; naomba kuongelea kuhusu Stiegler’s Gorge. Stiegler’s Gorge tunaifurahia sana na tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuiona hii na kuiendeleza na tunaamini haturudi nyuma, tunasonga mbele pamoja na umeme huu wa Stiegler’s Gorge na ninaamini tutapata umeme mwingi na tutaweza kuzalisha kwenye viwanda vyetu na tunaweza kufanya mambo mengine kuhusu huu umeme. Pamoja na hii Stiegler’s Gorge kuna mambo ya umwagiliaji pamoja na barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa maji…

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Miradi yote iliyolala iweze kukamilika, nakushukuru sana naunga mkono hoja. Ahsanteni sana, nashukuru. (Makofi)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi, Mwenyezi Mungu akubariki.

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyeniwezesha kusimama hapa. Kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kwa Bunge hili la Kumi na Mbili, nichukue nafasi hii kuwashukuru wanawake wa Morogoro walionipa kura za kishindo na za heshima yake. Nasema nawashukuru sana akina mama wa Morogoro, nakishukuru sana Chama changu cha Mapinduzi kwa kunileta humu Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru pia Mheshimiwa Rais kwa mambo yote aliyoyafanya. Hotuba zake mbili ni nzuri sana, unaangalia ya kuongelea na kuacha unakosa, unatamani uwe na muda mrefu kusudi uongee kila kitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza na maji. Serikali imefanya vizuri kwenye maji ingawa siyo vizuri sana lakini imejitahidi. Nawashukuru na kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri kwa upande wa maji. Mheshimiwa Rais jinsi alivyosema kwenye upande wa maji, naomba kila kitu kilichoongelewa kiweze kutekelezeka, kuna miradi ambayo imekamilika na mengine bado haijakamilika. Wananchi wanaomba na wanataka maji, kwa hiyo, miradi ambayo haijakamilika nashauri iweze kukamilika kusudi wananchi waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa pongezi kubwa kwa hotuba ya Mheshimiwa Rais na jinsi anavyofanya hasa kwa kuchukua kutoka Ziwa Viktoria kuyaleta mpaka Tabora na tunategemea yatakuja mpaka Dodoma, hiyo tunashukuru. Mkoa wangu wa Morogoro una mito mingi lakini mpaka sasa hivi tuna shida ya maji. Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri wananisikia muuangalie vizuri sana Mkoa wa Morogoro tuweze kupata maji ya kutosha na miradi ile kichefuchefu iweze kuisha kabisa twende vizuri na nikiwa Mwenyekiti wa Kamati naamini nitakuwa pamoja nanyi bega kwa bega. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa miundombinu, Mheshimiwa Rais ameongelea vizuri sana kwenye ukarabati wa reli ya kati, sasa hivi imekarabatiwa vizuri na ukarabati na ujenzi wa reli ya mwendo kasi. Sisi wananchi wa Morogoro kwa kweli tunafaidika vizuri sana na reli hii ya mwendo kasi. Kinamama, kinababa na vijana wote nawashauri muwe tayari kwa sababu ajira imepanda reli hii ikianza. Ila tunauliza ni lini reli hii itafunguliwa kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro ili wananchi waweze kujiweka vizuri kwa mwendo kasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naweza kuliongelea ni kwenye uchumi. Mheshimiwa Rais amesema kwenye uchumi hasa ataangalia upande wa kilimo, mifugo na maji na hasa mifugo na uvuvi kwani ndiyo sekta zinazoleta ajira kwa wananchi wengi. Kwa upande wa kilimo unakuta asilimia 65.5 wanategemea kilimo na asilimia 100 inazalishwa na wakulima wa vijijini na kila mmoja anategemea chakula kutoka kijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, amesema ataangalia upande wa pembejeo, mbegu na mbolea. Nachoomba kwa Mawaziri wanaohusika ambao tupo pamoja waangalie sana upande wa mbegu. Mpaka sasa hivi hatujitoshelezi kwa upande wa mbegu, kwa hiyo, tuangalie jinsi ya kuzalisha mbegu hasa kwa upande wa taasisi hivi zinazozalisha mbegu pamoja na wananchi waweze kufundishwa na kuelekezwa jinsi ya kuzalisha mbegu tuweze kupata mbegu za kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia jambo lingine ambalo naomba kuliongelea ni kuhusu mbegu zetu za asili. Naomba sana tusidharau mbegu zetu za asili tuone jinsi ya kuziboresha kusudi ziweze kutumika.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusu Maafisa Ugani. Nashukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Kilimo ameanza kuwaita Maafisa Ugani na kuongea nao. Nashauri Maafisa Ugani wawe karibu na wakulima kusudi waweze kuwapa elimu ya kutosha tuweze kuzalisha kwa wingi. Tukizalisha kwa wingi ndiyo tutaweza kupunguza umaskini na ajira kwa kila mmoja.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili tayari Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, nimeongelea kitu kimoja kinatosha na kuwashukuru wanawake wa Morogoro, ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia Mpango wa Maendeleo awamu ya tatu na Mpango wa Mwaka mmoja. Nitaanza kwa kuchangia kuhusu kukuza uchumi wa nchi pamoja na pato la nchi na hasa kukuza uchumi wa viwanda. Nikianza kuchangia kwenye uchumi wa viwanda siwezi nikasema viwanda vitakua bila ya kilimo, uvuvi, ufugaji, maji pamoja na umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia zaidi ya 66 ya wananchi wamejikita kwenye kilimo. Kwa hiyo, lazima tuangalie kwa undani kuhusu kilimo ndiyo tutaweza kukuza pato la Taifa na pato la mwananchi yeye mwenyewe mfukoni mwake. Kwa hiyo jambo la muhimu sana hapa la kuangalia ni kuhusu kilimo kiwe rafiki, kiwe cha kisasa, kilimo kiweze kuvutia kwa wananchi na hasa kwa vijana na kiwe kilimo cha maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubali kuwa Mawaziri wa Kilimo, Uvuvi pamoja na Mifugo, wanafanya vizuri sana. Pamoja na mikakati iliyowekwa, inabidi tuweze kutimilika vizuri sana. Kwa upande wa vijana wanapata shida, lazima tuone jinsi ya kuwavutia vijana na watu wazima, wote waone kuwa kilimo ni rafiki ili kila mmoja avutiwe kuingia kwenye kilimo. Tufanyaje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu cha kwanza tuangalie zana za kilimo. Nakumbuka zamani yalikuwepo matrekta ya vijiji ambayo yalikuwa yanasaidia wananchi kulima kwenye mashamba yao. Kwa hiyo, kama hiyo inawezekana naamini hata vijana wanaotoka vyuo vikuu wanaweza wakaingia kwenye kilimo, hata vijana wanaomaliza VETA, hata vijana ambao hawajasoma, wote wanaweza kuingia kwenye kilimo kwa sababu hawatatumia nguvu, watatumia zana za kilimo ambazo zinapendekezwa kama matrekta na kadhalika ili kusudi tuepukane na jembe la mkono ambalo linatoa jasho kweli.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo linavutia kwa vijana hasa kuwekeza kwenye kilimo waweze kukopesheka na watakopeshekaje? Tuweze kupata wawekezaji binafsi na hasa kilimo cha mkataba. Kilimo cha mkataba ni kizuri sana kwa sababu hicho kilimo wataweza kulima na baada ya kuvuna na kuuza wataweza kukata zile hela ambazo watakuwa wameingia pamoja na mkataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la muhimu sana kwa hawa vijana pamoja na kilimo kuwa rafiki na kukibadilisha kilimo lazima tuwe na mbegu bora. Tuwe na mbegu za mafuta, ni kweli kila mmoja sasa hivi anasema bei ya mafuta ni ghali. Unajiuliza kwa nini, Tanzania tuna ardhi nzuri, tuna wasomi wazuri, tuna kila kitu kwa nini iwe hivyo? Kwa hiyo tuangalie hata michikichi hiyo sio lazima izalishwe Kigoma peke yake, hata Morogoro tunazalisha mchikichi, hata Kagera wanaweza wakalima mchikichi, hata Mbeya hata Kilimanjaro. Kwa hiyo ni kiasi cha kuweka uzito kuona tutafanyaje tuweze kuondokana na umaskini kwa kupitia kilimo hasa kwa kuangalia pamoja na masoko. Kabla hujaanza zao uweze ku-focus kwenye soko, ukiwa na soko bila shaka utaweza kuzalisha kwa wingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la viwanda, lazima tuweze kuwa na ufugaji. Kwenye ufugaji tufuge mifugo ambayo ni ya kisasa, sio bora kufuga. Ni kufuga kwa kisasa na kuzalisha kwa kisasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye uvuvi, tuwe na blue economy, tuone kuwa tunafanyaje kwenye uvuvi kusudi tuweze kuwa na viwanda ili wananchi wote waweze na wenyewe kunufaika kwenye mambo ya kilimo, uvuvi, mifugo na kwenye ufugaji wa nyuki pia, asali ipo lakini hatuna soko…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, kengele imeshagonga.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi, lakini naamini imeeleweka. Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Azimio la Bunge la Kutambua na Kuenzi Mchango wa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa Utumishi wake Uliotukuka Pamoja na Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia katika maazimio yote haya mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze kwa kumpa pole Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuondokewa na Rais wetu, na Watanzania wote pia nawapa pole kwa msiba tulioupata, msiba mkubwa sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili naomba kusema kuwa Mheshimiwa hayati Dkt. Magufuli hakuna mtu ambaye haoni mambo aliyoyafanya. Alifanya mambo mengi mazuri na kweli inabidi tuyaenzi na tumuenzi kwa mambo yote aliyoyafanya. Amegusa kila kitu, kila Nyanja, kila sekta, kila mkoa, amefanya mambo mengi. Siwezi kuyarudia kwa sababu yote yameshasemwa, lakini afadhali niseme machache hasa kama reli ya mwendokasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa reli ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro ambayo sasahivi ujenzi umeshafika Morogoro nadhani alitamani kuiona, kuingia na yeye kuona anatembea kwenye reli hiyohiyo, lakini Mwenyezi Mungu hakupanga; lakini Watanzania ametuachia naamini Mheshimiwa Mama Samia, Rais wetu, ataendelea pamoja na wengine. Viongozi bado tunao watamalizia wataiendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia alifanya mambo ya Mwalimu Julius Nyerere ambayo na yenyewe ilikuwa imekaa kwa muda mrefu. Amefufua viwanda, ameanzisha viwanda, Mheshimiwa Rais kwa kweli Hayati Magufuli kila mmoja inabidi amuenzi, kila mmoja ameona aliyoyafanya. Hakuna kipofu kila mmoja ameona aliyoyatenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naomba tumuombee kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Na ninamalizia kusema amina. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba kusema kuwa Mheshimiwa Rais, Hayati Magufuli ameondoka lakini ametuachia viongozi, ametuachia Mheshimiwa Mama Samia, ametuachia Rais wetu Mheshimiwa Mama Samia, mama shupavu, mama mahiri, mama mtulivu, mama mnyenyekevu ambaye atatuvusha kwa yale yote ambayo yalikuwa yanafanywa Mheshimiwa Hayati Magufuli. Mheshimiwa Mama Samia alikuwa Naibu wake, Makamu wake na alikuwa anafanya mambo bega kwa bega pamoja na Hayati Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miradi yote iliyokuwa inaendelea Mheshimiwa Rais Samia anaifahamu vizuri sana. Mheshimiwa Rais wetu Samia ametembea nchi nzima anajua kila kitu kinachotendeka Tanzania. Kupitia kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi anaifahamu miradi pamoja na watendaji wake wa Serikali. Hatuna shaka Mheshimiwa Rais wetu atatuvusha, tuna imaninaye, tutafika mahali kule Kaanani, tutafika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Rais Mama Samia naamini na Watanzania wanamuamini; na yeye alisema kwenye mambo ya maji ataweza kuwatua. Yeye pamoja na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Mama Samia alikazania sana maji hasa kwa upande wa akinamama. Mheshimiwa Mama Samia tulifanya kampeni naye, wote mlikuwanaye mikoa mingi, mliona mambo mengi aliyokuwa anasisitiza sio tofauti na Mheshimiwa Hayati Magufuli aliyokuwa anayatenda kwa sababu walikuwa wanafanya kazi pamoja. Kitu cha msingi tuzidi kumuombea Watanzania wote, wananchi wote, Serikali tushikamane nao, Wabunge, kusudi tuweze kufika kule ambapo tumeanza na ambapo tunakwenda. Nani haoni ndege ambazo zinaendelea?

Mheshimiwa Naibu Spika, najua Mheshimiwa Mama Samia ataendeleza yale yote, tuna imani naye hatuna tatizo. Mnaona hata mijadala kwenye TV, wananchi wote wanamsifia Mheshimiwa Mama Samia hakuna ambaye anasema ooh. Wale ambao wanabeza hawapo, nadhani kama wapo hawajui wanalolisema, Mheshimiwa Mama Samia atafanya kila kitu.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Samia ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais hapa Tanzania na Afrika Mashariki. Naamini atafanya; kama wanawake wanaweza na wanaume wanaweza hakuna tofauti. Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na Eva aliwaumba wote sawa. Naamini tutafanya kazi naye na tutampa ushirikiano na tutafika kila kitu kitakwenda. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho wa yote ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Watanzania, naomba tuzidi kumuombea Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Hassan Suluhu, azidi kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, na ninashukuru kwa kumpata Mheshimiwa Dokta Mpango. Tunampa pongezi Dokta Mpango, tunampa pongezi Mheshimiwa Rais wetu kwa kumpendekeza na Kamati Kuu kumpendekeza na Bunge tukampitisha kwa asilimia 100. Mheshimiwa Mpango ni mpole, mchapakazi, anaweza, Makamu anafanya kazi, tunashukuru.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimefurahi sana mpaka moyoni mwangu. Nilivyofurahi ndivyo Wabunge walivyofurahi. Nilivyofurahi ndivyo Watanzania walivyofurahi. Napata message nyingi kutoka kwa Watanzania. Napata message nyingi kutoka kwa wananchi wa Morogoro. Napata message nyingi kutoka wanawake wote na wanaume wote Tanzania. Mwenyezi Mungu aijenge Tanzania. Mwenyezi Mungu ambariki Rais wetu. Mwenyezi Mungu ambariki Makamu wa Rais. Na Mwenyezi Mungu awabariki Watanzania wote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana. Mwenyezi Mungu tubariki Bunge zima, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ya kuchangia hotuba ya Wizara ya Afya. Kwanza nianze kwa kuwapongeza Wizara hasa Waziri na Naibu kwa kazi kubwa wanayoifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niongelee hospitali yangu ya Mkoa wa Morogoro ambayo nilishaiongelea hapa ndani. Kwanza napongeza kwa upanuzi ambao wanaufanya kwenye hospitali hii ila ni upanuzi wa kwenda juu. Kwa hiyo sehemu ya hospitali ile kama wanavyojua Hospitali ya Mkoa wa Morogoro inapokea wagonjwa wengi hapo na majeruhi wengi sana, kwa hiyo sehemu hiyo haitoshi. Hapa nilishaomba kuwa kijengwe kituo au hospitali kubwa ya kisasa ya Morogoro ambayo inaweza ikapokea wagonjwa wengi na majeruhi wengi ambao huwa wanapokelewa hapo kutoka kwenye mikoa mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia hospitali hii ni kubwa lakini haina CT-SCAN. Kutokana na matatizo yaliyo hapo nilishaongea na Mheshimiwa Naibu Waziri na Waziri wakaniambia kuwa CT-SCAN ipo kwenye meli inakuja, sasa je, imefikia wapi na itafika lini hapa hospitalini Morogoro au itakaa bandarini mpaka lini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo kwenye Hospitali yetu ya Morogoro tunaloomba kutokana na umuhimu wa hospitali hii ni mtambo wa oxygen ambao nilishaongea na wenyewe, nikaambiwa kuwa nitaambatana na Naibu Waziri aende kunionesha mahali pa kujenga hicho kituo cha mtambo wa oxygen. Mheshimiwa Waziri akija kuhitimisha hapa aniambie kwamba ni lini tutaambatana na Mheshimiwa Waziri au Naibu Waziri kwenda kuona hicho kituo cha oxygen kitakapojengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo naomba kuliongelea kwenye Hospitali hii ya Morogoro ni wataalam Mabingwa, nalo naomba liweze kuangaliwa kwenye Hospitali yetu hii ya Morogoro ambayo inatibu wagonjwa wengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo nimekumbana nalo, naomba nisisitize sana kuhusu upungufu wa dawa kwenye hospitali zetu na upungufu wa dawa kwenye vituo vyetu vya afya. Upungufu wa dawa kila mahali ni tatizo. Hata hivyo, nashukuru Mheshimiwa Waziri kwenye hotuba yake amesema viwanda vinajengwa vya kutengeneza dawa, basi naomba viangaliwe ili basi tatizo hili liweze kupungua kwa sababu limekuwa kubwa sana kwenye nchi yetu na kila mmoja anazungumzia upungufu wa madawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukija kwenye taarifa ya Serikali wanasema dawa zipo, lakini namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Doroth naye tuliongea mara nyingi kuhusu upungufu wa dawa, naye akakiri kweli kuwa atafuatilia upungufu wa dawa na wale wote wanaoiba dawa atawafuatilia. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri naomba aliangalie hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo kwa uharaka naomba kulizungumzia ni Bima ya Afya. Unakuta mtu amelazwa ICU anaandikiwa dawa ya kutibiwa wakati yeye amelazwa, yaani anaumwa sana kwa sababu kupelekwa ICU ni kuwa unaumwa sana, lakini unaandikiwa dawa ambazo hazipatikani, inabidi eti uende kununua, inawezekana hiyo? Kwa hiyo naomba hiyo Bima ya Afya nayo iangaliwe, iendane na madawa yanayotolewa pia na Bima ya Afya kwa wote ijulikane ni lini itaweza kutolewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niongelee utafiti, uangaliwe...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele imeshagogwa Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana lakini utafiti ufanyike kwa magonjwa ambayo…

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

NAIBU SPIKA: Kwa magonjwa ambayo…

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa magonjwa ambayo hayaambukizi yakiwepo kisukari, kansa, pressure, ugonjwa wa Ini na figo naomba utafiti ufanyike sio kutuambia kuwa hayatibiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nianze kwa kuunga mkono hoja.


Mheshimiwa Naibu Spika, nitachangia kuhusu barabara, mipango mizuri ya Serikali ipo lakini nachoomba ni utekelezaji. Naongelea barabara ya Ngiloli – Iyogwe - Kilindi (Tanga). Tatizo hapa tunaomba ijengwe kwa kiwango cha lami. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, halafu jambo kubwa lingine ni kuhusu madaraja. Kuna madaraja ya Chakwale na Nguyami. Madaraja haya yanajengwa kila mwaka lakini mwaka mvua ikinyesha yanakatika. Je, ni lini haya madaraja ya Chakwale na Nguyami yaliyopo Gairo yatajengwa kwa ukamilifu ili kuondoa tatizo la kukatika kila mwaka kwani tunaharibu fedha za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine nayoongelea ni ambayo imeshaongelewa ni ya Kidatu – Ifakara – Malinyi – Londo - Kitanda -Namtumbo. Barabara hii tumeiongelea mara nyingi humu Bungeni inasuasua na ni ya muhimu sana. Kwa hiyo, mipango yote iliyopangwa tunaomba itekelezwe kwa sababu tumeiongelea muda mrefu na lakini hakuna utekelezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ni ya Bigwa – Mvuha - Kisaki ambayo inakwenda mpaka Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere. Tunashukuru imewekwa kwenye mpango na imetengewa kiasi kidogo cha fedha, lakini kwa umuhimu wake tunaomba mipango yote iliyopangwa iweze kutelezwa kwa sababu nayo hii barabara tumeiongelea miaka nenda miaka rudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ni Ubena - Zamozi - Ngerengere - Mvuha – Kisaki. Barabara hii nayo imetengewa fedha kiasi lakini kutenga sio kutenda, tunaomba itekelezwe kama ilivyopangiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara nyingine ni Dumila - Magole - Turiani - Mziha – Handeni. Hii barabara nayo tumeiongelea lakini nashukuru kipande cha Magole - Turiani kimetengenezwa kwa lami, kipande cha Turiani - Mziha - Handeni bado hakijatengenezwa. Naomba kufahamu hiki kipande kitatengenezwa lini? Kipande hiki pia kimetengewa fedha lakini naomba utekelezaji uende kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Dumila – Ludewa – Kilosa - Mikumi tumeiongelea mara nyingi. Barabara ya Dumila - Ludewa tayari imejengwa kwa kiwango cha lami na barabara ya kutoka Ludewa - Kilosa ujenzi unaendelea. Tatizo ni kipande cha barabara ya kutoka Kilosa - Mikumi, usanifu ulishafanyika muda mrefu, sasa mnasema mipango ya kutafuta hela inaendelea, sasa itaendelea mpaka lini? Naomba kujua kipande cha barabara ya kutoka Mikumi - Kilosa kitatengenezwa lini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Ifakara – Lupilo
– Mahenge - Mwaya, sijaiona kwenye mpango wowote. Watu wa Mahenge tunaomba hii barabara kwa sababu Mahenge ni Wilaya inayozalisha sana mpunga na kuna madini. Naomba na barabara hii iweze kuonekana kwenye mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Ifakara – Mlimba – Lupembe; wakati wa mvua huwezi kupita. Tunaomba na yenyewe itengenezwe vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna barabara ya kutoka Kihansi - Madeke – Njombe. Hii ni barabara inayounganisha mikoa miwili ambapo tunaweza kufanya biashara kama itatengenezwa mpaka Njombe.

Mheshimiwa Naibu Spika, reli ya mwendo kasi. Tuinashukuru sana Serikali kwa kujenga hii reli ya mwendo kasi ambapo kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri amesema kuanzia Dar es Salaam - Morogoro imefikia asilimia 91, tunashukuru. Tunaomba ujenze uende vizuri kusudi tuweze kuifaidi kama ilivyokusudiwa ambapo wananchi wa Morogoro wataweza kunufaika kwa kufanya biashara na kadhalika.

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ndiyo nilipenda kuchangia, nakushukuru sana. (Makofi)


Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipatia nafasi na kwa sababu muda ni mfupi nitachangia kidogo na ninaanza kwa kuunga mawazo yote ya Kamati.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kweli inafikia haiwezi kufanya maajabu bila ya kupata fedha za kutosha na hasa fedha za kutosha za maendeleo kama nilivyosema kwenye taarifa ya Kamati mpaka mwezi Aprili kwa upande wa uvuvi ilipata asilimia 31 tu na miaka yote mitatu iliyopita ilikuwa inapata fedha pungufu kwenye fedha za maendeleo. Kwa hiyo, ninaomba na ninaishauri Serikali iongezee fedha hizi Wizara kusudi iweze kufanya mambo mazuri kwenye uvuvi pamoja na mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninalotaka kuongelea ni ufugaji wa kisasa; wananchi wote waelewe kuwa kufuga siyo kuchunga, tuweze kufuga ufugaji wa kisasa Wizara waweze kujikita kutoa elimu ili kusudi tuweze kufuga ufugaji wa kisasa, tuweze kupata maziwa ya kutosha, ng’ombe mmoja anaweza akatoa maziwa lita 32 kwa siku. Nenda mkajifunze kwa mwekezaji wa Iringa yule ASAS ambaye anafuga ufugaji wa kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikifika hapo naomba Wizara pia iangalie hawa wawekezaji iweze kuwapa mazingira mazuri ya uwekezaji, kwa mfano uwekezaji kwenye viwanda vya samaki, unakuta wawekezaji wengine wanapata shida, uwekezaji kwenye mifugo waweze kuwawekea mazingira mazuri tuweze kupata uwekezaji wa kisasa. Kwa mfano, kwa upande wa maziwa bado tunaagiza maziwa mengi kutoka nje, mimi nashangaa tuna mifugo mingi ni nchi ya tatu Tanzania, lakini bado tunaagiza maziwa kutoka nje. Wizara tuangalie jinsi ya kuboresha maziwa tuweze kuzalisha na kusindika maziwa yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niende tena kwenye Bwawa la Mindu wote mnalijua Bwawa la Mindu pale Morogoro, naomba wale wananchi wawekewe utaratibu mzuri unaoeleweka waache kuvua kwa kujiiba, waweze kuvua kwa utaratibu uliopo kusudi waweze kunufaika na Bwawa hilo la Mindu.

Mheshimwia Spika, nikienda Kilombero kwenye Mto Kilombero sasa hivi Samaki wamepungua zamani samaki walikuwepo wawekee mazingira mazuri kusudi samaki waweze kuzaliana na wananchi wa Kilombero na wa Morogoro waweze kupata kitoga ile waliokuwa wanavua kwenye Mto wa Kilombero. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, uzalishaji wa vifaranga wananchi wengi sasa hivi wamehamasika kufuga vifaranga kwa hiyo iwepo uzalishaji wa vifaranga na elimu kutoka kwa Maafisa Ugani wa Uvuvi ambao sasa hivi ni wachache. Naomba liangaliwe ufugaji huo huo wa vifaranga ili kusudi waweze kupewa wananchi waweze kufuga kwenye mabwawa pamoja na vizimba, uvuvi ni uvuvi mzuri sana kwa hiyo inaweza ika…

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa NARCO naomba matatizo yote yaliyopo kwenye NARCO yaweze kutatuliwa, pia muda wa kupewa vitalu usiwe mwaka mmoja wapewe vitalu kwa muda mrefu kusudi aweze ku-own kwani kitalu chake na aweze akawekeza vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wale wananchi wanaozunguka ranchi hizo hizo waweze kunufaika na ranchi hizo. Nikija kwenye Ranchi ya Kongwa mpaka sasa hivi naomba iangaliwe vizuri kwa sababu sasa hivi imezungukwa na magugu ya Kongwa, hayo magugu ya Kongwa yaweze kutolewa kusudi iweze kuonekana kuwa ni ranchi na wananchi waliozunguka ranchi hiyo waweze kunufaika na vitalu hivyo.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa kuwa masoko kuna masoko vijana wanaweza wakanufaika na masoko kusafirisha wanyama na nyama nje, kwa hiyo waweze kupewa elimu jinsi ya kuweza kuwanufaisha vijana na watu wengine nje bado wanahitaji nyama, bado wanahitaji maziwa kusudi tuweze kunufaika na masoko ya nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuimarisha afya ya wanyama…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, namalizia kwa kusema naunga mkono hoja, lakini naomba tasinia hii ya uvuvi na mifugo iangaliwe vizuri inanufaisha wananchi wengi, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kunipatia nafasi na nianze kwa kuunga mkono hoja na pili naunga yote yaliyoongelewa kwenye taarifa ya kamati.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema kuwa ili tufanikiwe katika kilimo chetu kwa kuzalisha kwa tija lazima tuangalie kweli masoko kwa sababu tukiangalia masoko mambo yote yatajituma na wakulima watajituma wenyewe kwa wenyewe. Kwa mfano, tukiangalia kuna kitengo cha masoko katika wizara, nilikuwa nakuomba kuwa Mheshimiwa Waziri akiangalie hicho kitengo cha masoko kifanye kazi kisikae tu kitafute masoko kusudi wakulima waweze kupata masoko ya mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa mfano kuna mazao ya miwa, Mheshimiwa Waziri alitembelea viwanda vyote vya miwa anajua matatizo yote ya viwanda vya miwa, anajua matatizo yote ya skimu zote za miwa, nilikuwa nashauri kuwa Mheshimiwa Waziri tulikuwa wote kwenye baadhi ya viwanda naomba kuwa matatizo yote yaweze kutatulika. Leo asubuhi nimeongea na wakulima wa miwa Kilombero, Iyovu bado matatizo yapo palepale, kwa upande wa masoko naamini kuwa wale wakulima miwa matatizo yote yakitatuliwa wakulima wa miwa hawatakuwa na tatizo la masoko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na hapa Tanzania tutaweza kuzalisha sukari ya kutosha kuweza kuwa hatutakuwa na deficit yoyote kwenye sukari. Kwa mfano kule Iyovu wanatupa miwa ambayo haiwezi kuzalisha kwa sababu kiwanda ni kidogo, lakini kulikuwa na tatizo la kupanua kiwanda, hilo tatizo likiisha wataweza kufanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tulikuwa tatizo wanachoma miwa ya wakulima na hiyo miwa hainunuliwi inakaa tu, ukienda Dakawa kiwanda bado hakijaisha, ukienda kule Mtibwa bado wanamatatizo yao kwa hiyo matatizo yakiisha hiyo ni mfano mmoja wa masoko. Kwa mfano kama masoko yapo chukulia kuwa uzalishaji wa wakuku wa singida unaona kuwa wanauzwa tu kwa sababu masoko yapo ili masoko yaendane pamoja na miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikisema miundombinu naelezea barabara za mashambani, nikisema miundombinu naelezea viwanja vya ndege, kwa mfano wakulima wa parachichi, wakulima wa mazao ya bustani najua Mheshimiwa Jacqueline yupo pale wakati mwingine wanapata matatizo kwa sababu ya usafirishaji kwenda nje lakini soko lipo. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri tuangalie mazao ya bustani kwa sababu yanazalisha kwa mara moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naongea haraka haraka nakwenda kwenye pembejeo, najua wewe ulisemea pembejeo hasa kwenye mbegu, mbegu za alizeti kama kamati pamoja na wizara tuliwaambia kuwa lazima tusimamie uzalishaji wa mbegu za alizeti na kweli tutasimamia kusudi hizo mbegu za alizeti ziweze kuzalishwa kwa wingi na hasa kilimo cha umwagiliaji kama mlivyoona kuwa hela nyingi zitakwenda kwenye kilimo cha mbegu na hasa kwenye umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia upande wa mbolea pamoja na viwatilifu lazima na vyenyewe viangaliwe kusudi tuzalishe kweli kilimo chenye tija lazima tuangalie masoko, tuangalie pembejeo pamoja na kilimo cha umwagiliaji. Ukiangalia sasa hivi tuna tatizo la mvua kama hatutajikita kwenye kilimo cha umwagiliaji tutakaa tunasema tunalima, lakini tunalima vitu vyetu vinakauka. Uvunaji pamoja na mabwawa pamoja na skimu zetu lazima zitengenezwe tuweze kupata kilimo cha umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni tafiti, tafiti hapa nasema tafiti wa udongo lazima udogo ufanyiwe utafiti huwezi kuweka mbolea tu kama utafiti kwenye udogo haujafika ili tuzalishe vizuri lazima tutoe hela za tafiti, lazima tufanye tafiti kwenye sehemu mbalimbali. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, Mwisho Afisa Ugani pamoja na bajeti lazima itolewe na mfumo wa ushirika lazima uangaliwe. Ahsante nakushuru sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushkuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia bajeti hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kumpongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhi Hassan, Kwa kazi nzuri sana anayoifanya. Pili nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu wake pamoja na wataalamu wote wa fedha kwa kazi nzuri wanayoifanya, hongereni sana. Kwa kweli nimeipita hii bajeti yote nzima nimeiona kweli bajeti nzuri sana, ambayo kila mmoja anaisifia na kila mmoja hata kule nje wanaisifia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hapa niweze kuongelea kuhusu mambo ya kilimo. Kila mmoja anaelewa kuwa kilimo inaajiri asilimia 65 ya wananchi, pia kilimo 100% ya chakula kinachotolewa na kinachozalishwa kinaliwa na sisi wananchi kwa 100% wanazalisha hichi chakula. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo licha ya hayo yote imetengewa bajeti kidogo, kwa mwaka huu wa bajeti ya 2021/2022 imetengewa kiasi cha fedha ya bilioni 294.2 ambayo hii ni kidogo sana. Kilimo inamambo mengi, kilimo ina umwagiliaji, kilimo ina mambo ya mbegu, kilimo ina utafiti, kilimo ina kupima udongo, kilimo ina mambo kweli mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba mambo yote ambayo yametengwa kwenye bajeti hii iweze kutolewa, kusema kuwa ni ndogo kwa upande wa nchi zinazoendelea, kufuatana na Azimio la Malabo ilitupendekeza kuwa, bajeti ya kilimo iwe angalau asilima kumi ya bajeti nzima ya Taifa. Sisi bajeti yetu iko chini ya asilimia moja, unaweza ukaiona kuwa kweli tunakazana na kilimo hatuwezi kuwalaumu Mawaziri ni sisi wenyewe, nilikuwa nashauri kuwa Mheshimiwa Waziri unanisikia kuwa safari ijayo mwaka wa bajeti unakuja 2022/2023, hii bajeti ya kilimo kama kweli tunataka kupunguza umasikini iweze kuongezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuongelea ni kuhusu mikopo ya elimu ya juu, mikopo ya elimu ya juu wote tunafahamu, wote wabunge tunajua, kuwa Watoto wa vyuo vikuu huwa wanatusumbua huko vijijini na mjini, wengi wamedahiliwa na wamepata vyuo na hawakuweza kupata mikopo, kwa hiyo bado wapo vijijini wako huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru naipongeza Serikali kwa kuweza kutenga bilioni 500, ambayo itaweza kwenda kwenye mikopo ya elimu ya juu. Saa nashauri hawa wanafunzi ambao walidahiliwa na wakapata vyuo na wakakosa mikopo, wawe wa kwanza kuwapa kipaombele kuona je, kama watawe kuomba wanaweza wakamit requirement ya kupata hii mikopo.(Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lengine ambalo naongelea ni ukusanyaji wa mapato, nashukuru kwa kupunguza ushuru wa mashine za kukusanyia mapato. Jambo muhimu ambayo inabidi tuangalie na wote tunajua watu hawadai risiti na watu hawatoi risiti, na ukienda anaweza akakwambia nikupe risiti feki, na wewe kama unataka vitu vya rahsi unakubali pia nilikuwa naomba tutoe elimu kuhusu ukusanyaji wa mapato ndio tunaweza kuendeleza nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea kuhusu lishe, miaka mingi lishe huko nyuma ilikuwa ni kwa Wizara ya Kilimo, na kwenye Wizara ya Kilimo ilikuwa inaenda vizuri sana, kiasi kinamama walikuwa wanafundishwa vizuri hata kupika uji, wanafundishwa lishe vizuri sana, hakuna mtu aliyeongelea kuhusu lishe humu ndani. Jambo ninalo omba bajeti ya lishe iweze kuangaliwa, na ikiwezekana lishe itolewe huko kwenye Wizara ya Afya iweze kwenda kwenye Wizara ya Kilimo kama zamani, au iweze kwenda TAMISEMI ambavyo inaweza ikaratibu vizuri mambo ya lishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa elimu imetolewa asilimia tatu ya bajeti tu ambayo haitoshi, kwa hiyo, nilikuwa nashauri kuwa iweze kutengewa zaidi ya asilimia tatu…

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Neema Lugangira taafira.

T A A R I F A

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nashukuru, ningependa kummpa taarifa mzuingumzaji kwamba, Chama cha Mapinduzi tayari kimeona umuhimu wa suala la lishe kuwa kwenye sekta ya kilimo, na kwenye ilani yake ile lengo la kushusha hali ya udumavu kutoka asilimia 32 mpaka asilimia 24 imewekwa chini ya sekta ya kilimo. Kwa hiyo, kilichobaki ni Serikali na yenyewe kufanya kama hivyo, ahsante. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ishengoma unaipokea hiyo taarifa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naipokea kwa mikono miwili, halafu kuongezea hapo hata wale maafisa lishe wanafundiswa na vyuo vya kilimo, kuanzia kwenye cheti mpaka kwenye Chuo Kikuu cha Sokoine wanafundisha hadi lishe. Inakuwaje inaratibiwa na afya?

Naomba sana afya iungane kama idara nyengine lakini mratibu mkubwa aweze kuwa ni kilimo. Pia tuweze kutunga sera na sheria ambayo inaweza kuwabana watu wa halmashauri, kutenga hiyo elfu moja kwa kila mtoto chini ya miaka mitano kusudi iweze kuratibu mambo ya lishe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu TARURA, watu wengi wameongelea lakini na mimi nashukuru kwa shilingi milioni mia tano ambazo zinatolewa kila Jimbo kusudi kutengeneza barabara zetu za TARURA. Ukweli barabara ni mbaya zinaweza zikaenda vizuri, halafu napongeza kuwa kwa ushuru ambao utakuwa ni shilingi 100 kwa kila lita ya diesel na kila lita ya petroli ambazo hizi fedha zitakwenda kutengeneza barabara za TARURA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye mafuta. Naishukuru na kuipongeza Serikali kwa kupunguza ushuru na kwa kuongeza ushuru wa mafuta yanayotoka nje ili kusudi kulinda viwanda na kulima mbegu zinazozalisha mafuta ndani ya nchi yetu. Hii hapa nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye juzi kule Singida alizindua kampeni ya kilimo cha alizeti na kilimo cha alizeti ndugu zangu Wabunge mnapotoka hapa nendeni kwenye Majimbo yenu, hamasisheni kilimo cha alizeti ili kusudi tuweze kuondokana na kuagiza mafuta kutoka nje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu pia kwa kuhamasisha kilimo cha michikichi ambayo na yenyewe inazalisha mafuta ya mawese.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni kuhusu kilimo cha umwagiliaji. Vifaa vya umwagiliaji ukweli ni ghali hasa ukileta kwenye mipira ile ya matone ya maji. Mheshimiwa Waziri, angalia kama kuna VAT kwenye vifaa hivi vya umwagiliaji VAT iweze kutolewa kusudi tuweze kumwagilia kwa urahisi mambo yetu ya mboga mboga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hapa napongeza kwa kutoa ushuru hasa cold chain au chumba cha baridi. Hii itasaidia kwa ukulima wa bustani, wakulima wa bustani kwa sababu wataweza kulima mbogamboga na matunda na wanaweza wakaweka kwenye chumba cha ubaridi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni nzuri sana kwa sababu inaendeleza kilimo cha bustani ambacho ni rahisi sana kwa kumtoa mkulima kwenye umaskini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ninaunga hoja na hayo yote niliyoyaongea naomba yachukuliwe. Ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye mapendekezo ya Mpango wa mwaka 2022/2023. Kwanza nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipatia nafasi hii.

Pili, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana anayoendelea kuifanya kwa Nchi yetu ya Tanzania. Mwenyezi Mungu amwongezee maisha marefu. Amina. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuchangia kwenye vipaumbele vya Mwongozo wa Mpango huu ambao tunauongelea na sana sana nitajikita kwenye vipaumbele viwili kati ya vipaumbele vitano. Navyo ni vile vipaumbele vinavyogusa kilimo. Nitaongelea kilimo tu. Nikisema kilimo ni zile sekta ambazo ni kama hazipewi kipaumbele, kwenye kilimo naongelea kilimo, uvuvi pamoja na mifugo. Hizi sekta ni za uzalishaji, lakini ukiangalia kwa kweli hazipewi kipaumbele na ningependekeza kuwa kwenye Mpango unaokuja zipewe kipaumbele namba moja kwa umuhimu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiongelea kilimo, wananchi wote asilimia 100 wanategemea kilimo kwa upande wa chakula, nyote humu ndani mmekula, kama hujala utakula, hiyo yote ni kilimo. Wafanyakazi wanakula, wananunua chakula kinachotoka shambani, hiyo yote ni kilimo. Asilimia 66.3 ya Watanzania wanategemea kilimo kama ndiyo ajira yao na ndiyo uchumi wao, lakini bado hatujakipa kipaumbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwa upande wa asilimia kwa kukua kwa kilimo ni asilimia tatu mpaka nne tu, hii kwa kweli inasikitisha kwa sababu kwa nini! kwa sababu hakuna uwekezaji, lakini tungekuwa tunawekeza kwenye kilimo kingekuwa na chenyewe kinakua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo chetu kinachangia asilimia 26.9 ya pato la Taifa, lakini bado hakipewi kipaumbele. Naomba mwaka huu katika Mpango huu na kwenye bajeti inayokuja ya 2022/2023, kipaumbele namba moja kiwe kilimo. Tukiweza kuwakwamua wananchi wetu wanaoishi huko vijijini na mijini wanaotegemea kilimo, ndiyo tutaweza kutoa umaskini na kuleta ajira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge wengi humu Bungeni wanawakilisha asilimia kubwa ya wakulima huko wanakotoka kwenye majimbo yao. Wabunge wengi humu ndani zaidi ya asilimia 60 na wenyewe ni wakulima. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tuungane na Serikali, tuiambie Serikali kilimo iwe kipaumbele namba moja, ndiyo tutaweza kuondoa umaskini na kuweka ajira kwa Watanzania wetu na vijana wengine na akinamama ambao tunategemea kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivi kwa nini? Maazimio ya Malabo, tuliazimia kuwa asilimia 10 ya bajeti nzima iende kwenye kilimo, lakini sasa sisi bado hatujafika popote kwenye maazimio haya ya kilimo, bado bajeti ipo chini.

Naungana na Kamati ya Bajeti kwa mambo yote waliyoyasema kuhusu kilimo. Hongera sana kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Wajumbe wa Kamati ya Bajeti kwa mambo yote waliyoyaongelea. Wameongea na Kamati yangu ya Kilimo nikiwa Mwenyekiti I declare the interest, tumeongea kuhusu mambo ya Bajeti, kuwa bajeti ya kilimo iweze kupandishwa. Bajeti ya kilimo kwenye upande wa Kamati ya Bajeti ambayo nimeisifia na kuipongeza, wamesema Bajeti itoke kwenye bilioni 250 ya mwaka uliopita iweze kufikia angalau bilioni 450. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati yangu na mimi mwenyewe, nasema bado na hiyo ni kidogo, iweze kupanda zaidi ya hapo, ikiwezekana iende kwenye bilioni 500 kwa kuangalia Mpango wetu ambao unategemea kuwa mazao ya kilimo ndiyo yanalisha na viwanda, malighafi za kilimo ndiyo zinazolisha viwanda vyetu. Sasa tunasema twende na dhima hiyo ambayo inasema kuwa tuweze kuwa ina viwanda, lakini je, viwanda vitatoka wapi kama hatuna mazao ya kilimo? Lazima tuweke kipaumbele kwenye kilimo kwenye uzalishaji, uzalishaji ndiyo namba moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mambo haya ya uzalishaji kuna mambo mengi…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Sijui hiyo ni kengele ya pili au ya kwanza.

MWENYEKITI: Ya pili.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, lakini kubwa ninalosema, bajeti ya kilimo ipandishwe juu, ndiyo tutaweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia bajeti ya Wizara hii, Sekta hii ya TAMISEMI.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuwashukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana anayoifanya kwa nchi yetu katika maendeleo. Pili, nakushukuru na kukupongeza wewe kwa jinsi ambavyo unatuongoza humu Bungeni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimpongeze ndugu yangu Waziri Bashungwa, kwa kweli tunamtegemea anafanya kazi nzuri pamoja na Manaibu wake na Makatibu wake wazuri. Nikianzia hapo hapo nakuja kwa Manaibu Katibu Wakuu. Kuna Naibu Katibu Mkuu kwenye Afya anafanya vizuri sana, Naibu Katibu Mkuu kwenye mambo ya Elimu anafanya vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwenye mambo ya uzalishaji ambayo wananchi wengi wanategemea sana, haionekani wazi wazi Katibu Mkuu yuko wapi? Ambaye anaweza akasimamia wazi wazi kwa kusaidiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwenye mambo ya kilimo ambayo wananchi wengi wanakitegemea na mifugo ambayo watu wengi wanaitegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naamini kuwa tungekuwa na Naibu Katibu Mkuu ambaye yuko assigned kwenye mambo ya kilimo, mifugo na uvuvi, sekta hii ya uzalishaji ingefanya mambo mazuri sana. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri akija kuainisha hapa ni vizuri atueleze vizuri Serikali imejipangaje kama tunaweza tukapata Naibu Katibu Mkuu ambaye anashughulikia mambo ya Sekta ya Uzalishaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee kwa kusema kuwa Wabunge tuko humu ndani kuwawakilisha wananchi waliotutuma. Nimetumwa na Waheshimiwa Madiwani, Madiwani hasa wakiwakilishwa na Madiwani wa Mkoa wa Morogoro. Madiwani hasa wakiliwakilishwa na Madiwani wa Manispaa ya Morogoro. Madiwani wanafanya kazi kubwa sana na wewe mwenyewe na Wabunge wote tunaamini kuwa wanafanya kazi kubwa. Wanachoomba posho yao ni ndogo na maslahi yao, waongezewe kiasi na wenyewe waweze kufanya kazi vizuri. Tuko humu Bungeni lakini wenyewe ndiyo wanalinda majimbo yote. Tuko humu Bungeni ndiyo wanaofanya kazi zote za kijamii, za Serikali na za kichama. Kwa hiyo naomba sana tuwaangalie Waheshimiwa Madiwani kwa upande wa elimu na kwenye maslahi yao. Hapo hapo na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Wenyeviti wa Vijiji na wenyewe waangaliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siko mbali sana, naongelea asilimia 10. Asilimia 10 hiyo mahali inatumika vizuri, mahali pengine siyo vizuri. Ni kweli haitoshi vikundi ni vingi sana, lakini ingeweza kutosha kama ingesimamiwa vizuri sana. Kwa mfano miradi ya maendeleo kwa upande wa akinamama asilimia nne hiyo, miradi ya kimaendeleo kwa upande wa vijana asilimia nne hiyo na miradi ya kimaendeleo kwa watu wenye ulemavu ingeweza kuwanufaisha wanufaika hao.

Mheshimiwa Spika, kwa mfano hela zinazorejeshwa hazina mpangilio mzuri wa marejesho. Halmashauri zingine hawajui jinsi ya kuzipangilia. Kwa hiyo naishauri Serikali iangalie jinsi ya kuwanufaisha walengwa kusudi waweze kunufaika na hizi asilimia 10. Pia uwepo ufuatiaji, ufuatiliaji mahususi wa kuona hizi fedha zinatumikaje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu TARURA. Kwa upande wa TARURA wanafanya vizuri sana. Wameongezewa hela naamini kuwa watafanya vizuri hasa kwenye barabara za vijijini na hata kwenye barabara za mijini pembezoni. Nikichukua barabara ya Mjini Morogoro ambayo inaanzia Mziga mpaka Mgambazi ni mbaya sana. Nikichukua ya Fokoland ni mbaya sana na barabara zingine za pembezoni. Vijijini Bwakila Juu ni mbaya sana, Kweuma ni mbaya sana. Kwa hiyo, hiyo ni mifano midogo ambayo TARURA naamini wanafanya vizuri lakini kwa kuongezewa hela naamini watafanya vizuri zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa makandarasi wanaofanya miradi ya barabara na wanaofanya miradi ya maji, naomba waangaliwe vigezo vyao kama wametimiza? Wakimaliza kazi zao walipwe kwa wakati wasiwacheleweshe kuwalipa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo ninaloongelea sasa ni upande wa elimu. Hapa elimu namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi aliyoifanya kwa hiyo hela ya trilioni 1.3. Kwa kweli kila mmoja anayaona mambo mazuri anayoyafanya Mheshimiwa Rais kwa upande wa kujenga shule, madarasa na upande wa matundu ya vyoo, lakini kuna shule zingine za sekondari, kuna shule zingine za msingi kama SUA Sekondari bado hawana maabara, bado hawana matundu ya vyoo. Kwa hiyo ningeomba kuwa na wenyewe waangaliwe.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine la elimu ambalo natoa ushauri ni kwa upande wa chakula cha mchana. Chakula cha mchana hasa kwenye shule za kutwa bado ni changamoto kwenye baadhi ya shule. Kwa hiyo naomba waweke mkakati, waandike barua au mwongozo kwa shule zote za sekondari za kutwa na kwa shule zote za msingi waweze kupata chakula cha mchana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Walimu, ni kweli mgawanyo wa Walimu bado hauendi vizuri hasa kwa shule za pembezoni. Naomba waweze kupata Walimu wa kutosha hasa wa sayansi pamoja na sanaa tunaajiri. Pongezi sana Serikali kwa kuajiri, kuomba vibali, lakini mgawanyo uangaliwe.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa afya, tumejenga vituo vingi vya afya, tunamshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Rais na hata Mkoa wetu wa Morogoro tumejenga vituo vya afya zaidi ya vitatu. Tumejenga hospitali zaidi ya sita. Kwa hiyo tunampongeza Mheshimiwa Rais lakini tatizo bado ni wafanyakazi, wataalam wa afya. Tatizo unakuta kuwa hospitali au zahanati moja kwa mfano, Zahanati ya Mvuha. Zahanati ya Mvuha kuna Daktari mmoja na Nurse mmoja, siku Daktari akiumwa au Nurse akiumwa hakuna kazi siku hiyo. Kwa hiyo tunaomba waongezwe wataalam wa afya pamoja na dawa na vifaa tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikija kwa upande wa afya hiyo hiyo, naomba waangaliwe hasa kinamama kwenye maternity zao. Kuna maternity ward nzuri sana ambazo zimejengwa, lakini wataalam na madawa hakuna. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, nampongeza sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri sana anayoifanya Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Amefanya mambo mengi. Kila mkoa, kila Mbunge aliyepo humu ndani, kila mwananchi anaona mambo yote aliyoyafanya kwenye mkoa wake, kwenye kata yake kwa maendeleo yetu Watanzania. Kweli tunampongeza sana.

Mheshimiwa Spika, pili, naomba kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa hotuba yako nzuri ambayo umeitoa, ni nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, nawe pia nakupongeza kwa jinsi unavyoendesha Bunge letu hili. Hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mkoa wangu wa Morogoro umefaidi mambo mengi sana kwenye maendeleo anayoyaleta Mheshimiwa Dkt. Samia, Rais wetu. Nianze na ujenzi wa Reli ya Mwendokasi. Kama ulivyosema kwenye Speech yako, kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro ambayo ina kilomita 300 na inagharimu jumla ya Shilingi za Kitanzania bilioni 792.99 ambazo zinajenga reli hii na kuendelea mpaka Dodoma, yaani inakwenda vizuri, imebakia asilimia kidogo kumalizika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunaomba sana na Watanzania wengi wanaisubiri sana hii reli ambayo Mheshimiwa Rais anaisimamia iweze kukamilika na kuleta manufaa ya kiuchumi, mawasiliano, na mengine mengi ya kuinua pato kwa wananchi na nchi yetu ya Tanzania kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu kwa upande wa wananchi, hii reli tuisimamie na kuitunza na siyo kuiharibu kama tunavyoharibu miradi mingine wakati mwingine.

Mheshimiwa Spika, mradi mwingine ambao tunajivunia sana ni wa kufua umeme wa Mwalimu Julius Nyerere. Bahati iliyoje tuliyonayo kwa Mkoa wa Morogoro? Hili bwawa liko kwenye Mkoa wa Mororogoro Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini pamoja na Mkoa wa Pwani. Hii itafua umeme kwa megawati 2015 na inagharimu hela za Kitanzania shilingi bilioni 869.93. Kweli tulijivunia, tulikwena, nami nilikuwepo wakati inawekwa maji na Mheshimiwa Rais alishuhudia maji yanawekwa. Kwa kweli Mheshimiwa Rais tunajivunia sana kwa Bwawa letu la Mwalimu Nyerere.

Mheshimiwa Spika, hili Bwawa la Mwalimu Nyerere licha ya kuwa na lengo la kufua umeme ambao utatosheleza nchi yetu, ambapo tutaweza kuuza nchi za nje, pia ni kivutio tosha cha utalii kwa watu wa Tanzania, hasa na watu wengine.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naweza kusema kwa Bwawa la Mwalimu Nyerere, limeleta ajira kwa vijana wetu na hasa vijana wa Mkoa wa Morogoro na Mkoa wa Pwani ambao wanajivunia kuwa na bwawa na Watanzania wote kwa ujumla. Bwawa hili la Mwalimu Nyerere limeweza kukuza Kata na Miji ambayo imeizunguka. Mfano, mzuri ni Kata ya Mvuha pamoja na Kisaki ambayo ukienda unaona kweli maendeleo yanakuja.

Mheshimiwa Spika, sasa tufanye nini? Ushauri wangu; ili kuendeleza na kulifikia hili Bwawa la Mwalimu Nyerere, ili paweze kufikika kwa urahisi, miundombinu mpaka sasa hivi siyo mizuri. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri, barabara ya kuanzia Ubena - Mvuha mpaka Kisaki na barabara ya kuanzia Bigwa - Mvuha - Kisaki mpaka kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere ziweze kujengwa kwa kiwango cha Lami ili kusudi liweze kufikika kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naomba kuongelea ni kuhusu Mradi wa Sukari pale Mkulazi. Bahati nzuri hii Mkulazi na yenyewe iko kwenye Mkoa wa Morogoro. Kuna Mkulazi Na.1 na Mkulazi Na. 2 ambako kuna kiwanda kinachojengwa pale Dakawa Mkulazi kwa shilingi bilioni 39.84.

Mheshimiwa Spika, ninachoomba ni kuwa, miwa inalimwa ambapo mpaka sasa hivi imeshalimwa na kiwanda kimejengwa na kimefikia asilimia 75. Mara kitakapokamilika, kitazalisha tani 50,000 za sukari; ambapo zitakapozalishwa hizo tani 50,000 zitasaidia kupunguza uhaba wa sukari katika nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni hekta 2,974 mpaka sasa hivi zimelimwa. Ushauri wangu, wakulima wamejitokeza wengi kutoka Kijiji cha Mbigili, Kata ya Mbigili Wilaya ya Kilosa ambao na wenyewe wamewekeza kwa wingi, kwa hiyo wamepata ajira. Tatizo lililopo, hawapati maji ya kutosha. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri Serikali waweze kuwapa maji, kwa maana ya kilimo cha umwagiliaji kusudi tuweze kuzalisha sukari kwa wingi na wakulima waweze kufaidi katika kazi hii ya kilimo kwenye Mkulazi Na. 1 na Mkulazi Na. 2. Zikifanya vizuri itaweza kwenda vizuri.

Mheshimiwa Spika, mradi mwingine ni ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege. Naipongeza Serikali na Mheshimiwa Rais kwa kukarabarti viwanja vya ndege vilivyopo kama Geita na Dodoma kama nilivyovitaja na viwanja vingine.

Mheshimiwa Spika, swali langu moja kwa Serikali, ilikuwa ni kiwanja cha Ndege cha Morogoro; kwa niaba ya wananchi wa Morogoro, habari ya hiki kiwanja tulishaiongelea humu Bungeni. Kwa hiyo, naomba kujua hatima yake na bajeti ya fedha ya kiwanja hiki kitajengwa lini, ili kusudi wananchi wa Morogoro pia waendelee kufaidi matunda ya Serikali. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni Benki ya Kilimo. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais anaitolea fedha ambazo mpaka sasa hivi imeshapata takribani Shilingi bilioni
78.54 ambayo imenufaisha wakulima takribani 119,797.

Mheshimiwa Spika, tunavyofahamu ni kuwa, takribani wananchi wa Tannzania asilimia 65.5 wanategemea kilimo. Kwa hiyo, wakulima hawa wamehamasika sana kwenye kilimo, uvuvi pamoja na mifugo. Kwa hiyo, ushauri wangu, kwenye Benki hii ya Kilimo ambayo ni mkombozi kwa mkulima iweze kuongezewa fedha kusudi wanufaika waweze kuwa wengi kwenye benki hii ya kilimo ambayo inapata fedha hizo lakini hazitoshelezi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningeomba kuongelea ni kuhusu masuala ya Lishe. Bila kuwa na lishe nzuri hatuwezi kuwa na Taifa lenye afya na lenye kuendeleza mambo kiutaalamu. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri kuwa masuala haya ya lishe tuyachukulie kiundani na twende nayo vizuri. Kwa sababu sasa hivi tunaona kuwa kuna ukondefu ambao umepungua ndiyo kwa jitihada zilizotolewa, lakini tufuate ushauri wa lishe, tuweze kutumia chakula cha lishe.

Mheshimiwa Spika, ushauri mwingine, nilikuwa naomba elimu iweze kutolewa kwenye kliniki...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Kengele imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, namalizia kwa kusema kuwa ukatili wa watoto naomba kwa kweli kama ilivyoongelewa humu ndani utiliwe maanani.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Nakushukuru sana, na ubaraikiwe na Mwenyezi Mungu. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii ya kuchangia kwenye sekta hii ya Wizara ya Kilimo. Kwanza kabisa naunga Taarifa yote ya Kamati ya Kilimo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais, Mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa mambo yote anayoyafanya. Na tatu, nataka kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Hussein Bashe, pamoja na Naibu Waziri, Makatibu wote pamoja na wafanyakazi wote wa sekta ya Wizara ya Kilimo. Pia, bila kuwasahau kamati yangu nzima, wajumbe wote wa Kamati ya Kilimo kwa kazi nzuri waliyoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuwapongeza wakulima wote wa Tanzania kwa kazi wanayoifanya ya kutupatia chakula tunachokula kila siku. Kwa kusema hayo ninasema kuwa maendeleo ya uchumi tukubali kuwa yanatokana na sekta za uzalishaji ikiwemo sekta ya kilimo. Kwa pamoja tukishikamana na kilimo tukakipa kipaumbele namba moja naamini umasikini utapungua kama hautakwisha kwa watu wote hapa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa bajeti. Napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kukiona kilimo na kukipa kipaumbele kwa kuwaongezea Wizara fedha kutoka bilioni 274 mpaka bilioni 751. Mheshimiwa Rais tunakupongeza sana kwa kuliona hili na Mwenyezi Mungu azidi kukubariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, madhumuni ya Kamati na madhumuni ya Serikali, hasa Wizara ni kukibadilisha kilimo kikawa kilimo cha mageuzi chenye tija na chenye biashara. Kilimo ni ajira, kinaleta chakula, ni lishe. Kilimo ni kila kitu. Huwezi kukaa bila ya kula ukadhani kuwa utaishi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naomba kusema mambo muhimu yanayopaswa kufanyika kwenye kilimo, nikianza na utafiti. Mheshimiwa Waziri naomba; hela zimetengwa za utafiti, Waziri mmepewa hela nyingi, hizo hela kuna vituo mbalimbali vya utafiti ambavyo tunaviita TARI pamoja na vyuo vingine vikuu kikiwepo Chuo Kikuu cha Sokoine na pia Chuo Kikuu cha Nelson Mandela.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa TARI ihakikishwe kuwa ni fedha kiasi gani inapelekwa kwenye kila kituo cha utafiti. Tafiti mbalimbali zimefanyika, na tafiti hizo ziwwafikie wakulima. Kuna tafiti rafiki ambazo ziko kwenye kituo cha Kibaha ambako wanafanya tafiti za biological control ambazo bado hazijawafikia wananchi. ninaomba hizo ziweze kuwafikia wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo ninaweza kuongea ni kwenye huduma za ugani. Huduma za ugani nakuhakikishia haiajawahi kutokea. Maafisa Ugani walikuwa hapa, naamini wengine bado wako hap ana wengine wananisikia. Ninachokiomba maafisa ugani fanyeni kazi. Mmepewa vitendeakazi, mmepewa pikipiki, kila mmoja atapata pikipiki yake, pikipiki 7,000 zimetolewa, visikwambi vimetolewa, extension kit imetolewa, pia mmepewa na vi-sample vya kufanyia sampling na ubora wa udongo kila Halmashauri. Kwa hiyo, nawaomba ninyi maafisa ugani fanyeni kazi tuweze kuona matokeo ya kilimo, kilimo kiweze kubadilika na kilimo kiweze kuwa cha tija. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa huduma za ugani ni mambo mengi yametolewa haijawahi kutokea, hawajawahi kupata vifaa kama hivyo. Kwa hiyo, waweze kuwafikia wakulima, siyo kukaa nyumbani bila kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni umwagiliaji. Wewe mwenyewe ni shahidi, watu wote ni mashahidi. Mnaona kuwa kwa upande wa tabia-nchi hasa kwa sasahivi, kama ninavyosema, unaona kuwa hakuna mvua, lakini kusema ukweli watu wengi wamelima na haya mazao ya mafuta ya alizeti mnayoyasema pamoja na mawese yamelimwa, lakini ni ukame. Dawa yenyewe ni umwagiliaji, lakini kusema ukweli mpaka sasahivi sehemu tunayoimwagilia ni sehemu ndogo. Sehemu inayofaa kumwagiliwa ni kubwa ambayo sasa hivi tunamwagilia asilimia 2.5 tu ndiyo inayomwagiliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hamjui hela zimeongezwa za umwagiliaji, lakini ni asilimia 2.5 tu ndiyo inayomwagiliwa. Naamini kuwa mmejikita kweli, pesa zimetolewa, kwahiyo simamieni umwagiliaji. Ili tufanikishe kilimo chetu lazima umwagiliaji upewe kipaumbele kwa hiyo, angalieni umwagiliaji kusudi tuweze kumwagilia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye mbegu. Kwenye mbegu, mbegu zinazalishwa na mbegu zinazalishwa na ASA…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Ishengoma, mda wako naona kama umeisha.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, bado kidogo. Niongezee dakika moja. (Makofi/Kicheko)

MWENYEKITI: Mheshimiwa, haya nakuongeza dakika moja basi ili uweze kumalizia. (Makofi)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa upande wa mbegu, uzalishaji wa mbegu ambao unafanya kusambazwa na ASA, na hasa sanasana tumeona wamesambaza mbegu za alizeti pamoja na mbegu za mahindi. Naomba wakulima tutumie hizi mvua chache ambazo zitakuwa zinanyesha, lakini sanasana kumkomboa mkulima ni kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba sana tena sana tuzingatie kilimo, kwa pamoja naamini tutatok. Hakuna kitu chochote kitatutoa kwenye umasikini bila ya kuangalia kilimo. Kwa hiyo, kilimo kipewe kipaumbele kusudi kiweze kututoa na sisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, siachi kuongelea Morogoro. Kwenye mabonde mengine ya Morogoro, mkoa ambao unazalisha chakula kwa wingi, yapewe kipaumbele. Ingawaje Serikali naiona kwenye umwagiliaji, lakini kwenye mabonde yote ambayo yako Mkoa wa Morogoro yaweze kuzalisha kwa wingi yaweze kuulisha Mkoa wetu wa Morogoro pamoja na mikoa mingine Tanzania kwa ujumla nan chi nyingine zinazofuata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru na ninaunga mkono hoja, ahsante sana nawashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mifugo na Uvuvi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi nami niweze kuchangia Sekta hizi za Mifugo pamoja na Uvuvi. Nianze kwanza kabisa kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa mambo mengi mazuri anayoyafanya kwenye sekta hii, kwa sababu tulivyoona Bajeti ya Mifugo imeongezeka, ingawa Bajeti ya Uvuvi imepungua kidogo; lakini yote ni mazuri, Wizara hii inakwenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ni mahususi sana kwa sababu inachangia asilimia saba kwa upande wa mifugo na asilimia moja kwa upande wa uvuv; na inachangia ajira kwa wananchi, pia na pato kwa wavuvi pamoja na wafugaji. Kwa hiyo, hii ni sekta mahususi kwa sababu inainua hata lishe ya wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri, hotuba yake aliyoisoma ni nzuri sana, imejaa vipaumbele vizuri sana, imejaa mikakati mizuri sana ya kuendeleza miradi kama ilivyopangwa. Ushauri wangu ni kuwa, mambo yote yaliyopangwa yaweze kutekelezwa kwa wakati na pia bajeti ambayo tunaomba, nawaomba Waheshimiwa Wabunge tuweze kuipitisha kwa sababu hii ni sekta mahususi, na ni sekta nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Mifugo ina mambo mengi. Ukitaka kupata mifugo bora lazima ufuate kanuni mbalimbali ambazo lazima mifugo iwe nazo. Kwa upande wa kwanza lazima iwe na malisho. Nimeona Mheshimiwa Waziri kwenye sekta yako una mipango mizuri sana ya kuboresha malisho. Malisho kwa upande wa sekta binafsi pamoja na malisho kwa upande wa Serikali, na malisho yanayoanzishwa tena.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nashauri Mheshimiwa Waziri pamoja na Serikali kuwa jambo muhimu sana hapa ni malisho. Malisho yaangaliwe kwa umakini sana. Malisho yasitengwe kwenye mikoa fulani au kwenye Halmashauri fulani. Yawepo mashamba darasa ya malisho, na ikiwezekana mashamba darasa kwenye kila Halmashauri, kwa sababu mtu akiona, anaweza akaenda aka-practice yeye mwenyewe akaweza kuwa na malisho. Kwa upande wa malisho, pia kuna suala la mbegu. Kama wanavyosema, bado kuna tatizo la mbegu, lakini naona kwenye hotuba kwamba kuna mashamba ambayo yametengwa kuzalisha mbegu pamoja na shamba la vikugwe na mashamba mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba hizo mbegu ziweze kupatikana madukani kusudi wafugaji waweze kupata mbegu na kuwa na mashamba na hii itapunguza migogoro mingine ambayo inaendelea au isiyo na lazima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine, ili wafugaji waweze kufuga kwa tija lazima waangalie yale mambo ya afya ya mifugo. Hii inaenda pamoja na chanjo na maji. Hapa nasemea upande wa mabwawa na malambo. Ni jambo la muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, malambo na mabwawa yanachimbwa. Tumetembelea mabwawa mbalimbali, lakini unakuta mwisho wake yanakuwa siyo bora, kwa nini?

Nilikuwa nashauri ianzishwe mamlaka kama Mheshimiwa Waziri alivyosema kwenye hotuba yako. Hiyo mamlaka shughuli zake hasa, ziwe ni ufuatiliaji wa miradi hii ambayoe ni majosho, malambo ili kusudi yaweze kuendelea vizuri. Miradi ipo, lakini ufuatiliaji wake siyo mzuri. Naamini ikianzishwa mamlaka, mambo yatakuwa mazuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa madume bora ni jambo muhimu sana. Nimeona kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri; najua kuwa madume bora 366 yameshanunuliwa na kusambazwa. Kwa hiyo, nilikuwa naomba kuwa hata hivyo, kuna wafugaji wazuri ambao wanaweza wakazalisha na madume bora kusudi hawa wananchi wafugaji hasa waweze kupata elimu ya kutumia madume bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye madume bora, kuna uhimilishaji. Wananchi wengi hawana elimu ya uhimilishaji. Nilikuwa namshauri Mheshimiwa Waziri kuwa Maafisa Ugani tulionao ambao ni wazuri, ni wasomi, wanafanya kazi nzuri, waweze kuwafikia wakulima na wafugaji, na kuwaelimisha kuhusu mambo ya uhimilishaji. Kwa mfano nina ng’ombe mmoja na una ng’ombe mmoja; natoa mfano wa ASAS mwenye ng’ombe wengi, lakini unakuta lita kwa ng’ombe mmoja anapata lita ya maziwa 36 kwa siku. Kwa nini uwe na ng’ombe wengi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja tena kwenye upande wa Maafisa Ugani. Nashukuru kwa Serikali kuwapitia pikipiki 1,012 hivi ambazo wamewanunulia. Ni jambo zuri sana. Mmewapatia na simu za kinganjani, mkiwemo na wenyewe kama Wizara ya Kilimo. Kwa hiyo, naomba, ingawa wako TAMISEMI, lakini Wizara pamoja na Serikali waweze kuwafuatilia kuona wanawafikia wafugaji. Wakati mwingine hawafiki kwa wafugaji, mpaka uwaite wewe mwenyewe, lakini kwa sababu wamepatiwa pikipiki, naamini watafika kwa wafugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili twende na sayansi na teknolojia, ni lazima tuboreshe huduma za mafunzo pamoja na utafiti. Kwa hiyo, fedha za bajeti zilizotengwa kwenye mambo ya utafiti, naomba zikishatolewa zote, waweze kupata bila kukata hata senti moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya wafugaji na wakulima pamoja na watumiaji wa ardhi, kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Mheshimiwa Waziri wa Ardhi naamini unanisikia, uweze kushirikiana pamoja na Wizara hii ya Mifugo kusudi hawa wafugaji waweze kutengewa ardhi yao waimiliki, wasibughudhiwe kusudi waweze kupata malisho yao, waweze kupanda malisho yao kwenye ardhi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru mmetatua migogoro mbalimbali kwa upande wa Morogoro na wenyewe umetatua lakini kwa upande wa Morogoro, kwenye Bonde la Kilombero kwa upande wa Kilosa, Mabwelebwele, Tindiga, Kilangali bado migogoro ipo. Mheshimiwa Waziri naomba ulifanyie kazi kusudi tuweze kulitatua hilo pamoja na sehemu nyingine ambazo sikuzitaja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa utambuzi wa mifugo,…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nasisitiza, kwa faida yake, utambuzi wa mifugo uweze kuangaliwa, na mwisho ni uchumi wa bluu, na ufugaji wa vizimbani pamoja na malambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, samaki wanapotea, lakini tukifuga kwenye vizimba, naamini tutapata samaki wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye bajeti hii ya kilimo. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa jambo hili zuri la kuona kilimo na kuipandishia bajeti yake kila mara. Pili naomba kumpa pongezi Mheshimiwa Bashe ambaye ndiye Waziri wetu wa kilimo pamoja na Mheshimiwa Mavunde ambaye ndiye makamu wake na Wizara nzima yote ya Kilimo, nasema hongereni sana mnafanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nikianza kwa upande wa bajeti, ndiyo bajeti inaongezeka na sasa hivi imeongezeka mpaka bilioni 970, lakini lazima na ni vizuri tuendane pamoja na Makubaliano ya Malabo na Maputo ya asilimia 10 ile yote ni ya kilimo kutokana na bajeti yote ya taifa; kwamba asilimia 10 iwe ya kilimo. Kwa hiyo ninashauri kuwa, licha ya kuongeza bajeti mara kwa mara naomba bajeti iendelee kuongezwa kadiri bajeti inavyokwenda mwaka kila mwaka tuweze kuwa na kilimo chanye tija.

Mheshimiwa Mwenyekiti, siwezi kwenda mbali bila ya kumpongeza Mheshimiwa Rais pamoja na Mheshimiwa Waziri Bashe kwa upande wa BBT ambayo wameianzisha, hasa kwa upande wa vijana pamoja na wanawake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii inasaidia sana kwa upande wa kulima mashamba makubwa (block farming) ambayo tunaweza kupata mazao kwa wingi tunaweza kupata maafisa ugani ambao wanatoa service mara moja kwa watu hao wote; kwa hiyo ni kitu kizuri sana; na inatoa ajira kwa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, angalizo ni moja tu; ninaomba kuwa wale vijana muwaangalie kwa undani kabisa kuwa ni kweli wanakwenda wana interest ya kilimo kweli? Au wanakwenda kwa sababu hawana ajira? Hiyo tuiangalie kusudi BBT iweze kuendelea, na iweze kuendelea hata kwa kanda, kama ulivyosema Mheshimiwa Waziri pia kwa mikoa. Naamini mkuu wangu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Waziri Bashe mmeshaongea tayari. Kwamba Mkoa wa Morogoro tumeshatenga eneo la kuendeleza BBT kusudi vijana wetu waweze kulima kilimo chenye tija kwenye sehemu hiyo. kwa hiyo naomba hiyo uikumbuke, kuwa mkoa wa Morogoro, inawa hukuutaja kwenye mikoa ambayo ina kipaumbele, lakini mkoa wa Morogoro ni mkoa wenye mikakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwa upande wa kilimo lazima tukumbuke kuwa kuna kanuni bora za kilimo na hasa ukitaka kuwa na kilimo chenye tija. Kanuni ya kwanza hasa ni kuwa na mbegu bora. Mbegu bora hizi ambazo sana sana zinazalishwa na ASA, ASA kazi yake ni kuzalisha mbegu hizo bora pamoja na wakulima wengine ambao wanaratibiwa pamoja na TOSCI ambayo inaangalia ubora wa mbegu, pamoja na TARI ambayo inafanya utafiti. Vitu hivi vitatu, ASA, TARI, TOSCI wakiungana kwa pamoja wanzalisha mbegu bora ambayo ikitumika kwa mkulima anaweza akapata mazao bora na mazao yenye uhakika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo muhimu ni kuwaongezea fedha, naamini wamewaongezea fedha inakwenda inapanda, kuna wakati walipata bilioni 11.6, wakaja bilioni 43 na kitu na sasa hivi imepanda. Kwa hiyo tujaribu kuwaongezea kwa sababu hizi ni taasisi ambazo ni muhimu kwenye upande wa mbegu bora. Nikija kwenye mbegu bora pia tusisahau mbegu za asili au mbegu za mkulima. Mbegu za mkulima hizi unaweza ukazitumia kila wakati, mwaka hadi mwaka. Cha msingi wapate elimu ya kuzichambua hizi mbegu kuona ni mbegu zipi atatumia kwa mwaka ujao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni mbolea; tunashukuru Mheshimiwa Rais tumepata mbolea ya ruzuku, lakini hii mbolea ya ruzuku imesambaa kwenye mikoa mingine vizuri, lakini kwenye mikoa mingine haijafanya vizuri kwa sababu ya usambazaji. Naomba safari ijayo waangalie kwa umakini kuhusu usambazaji. Ni kweli kwenye ushirika imesambazwa vizuri lakini kwa wakulima wengine haikwenda na kwa madukani, maduka ya kilimo wengine walikataa kabisa kuwa na hii mbolea kwa sababu ya milolongo mirefu ambayo ilikuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mbolea, nashauri kuwa kwa kuungana pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara tuweze kuanzisha viwanda vyetu vingine vya mbolea kusudi kupunguza makali ya bei. Hapa mpaka sasa hivi tuna Kiwanda cha Minjingu pamoja na kiwanda hiki kilicho hapa Dodoma ambavyo ndivyo vinazalisha mbolea ambayo haitoshi. Mpaka sasa hivi mbolea nyingine inatoka nje, kwa hiyo tungeliomba tuweze kuwekeza kwenye uzalishaji na kujenga viwanda vya mbolea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nataka kuongelea ni maji. Lazima mbegu ipate maji, ikipata maji na hapa naongelea kilimo cha umwagiliaji. Kilimo cha umwagiliaji ni muhimu sana na kilimo cha umwagiliaji ni muhimu sana kwa sababu kuna mabadiliko ya tabianchi, ukame hasa. Kwa hiyo tukimwagilia tunaweza kupata mazao yenye tija na mazao ambayo, kwa mfano upande wa mpunga, unaweza ukavuna magunia 40 mpaka 80 kwenye hekta moja. Kwa hiyo kama ndio hivyo kwa nini tusilime kilimo cha umwagiliaji? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namshukuru Mheshimiwa Waziri, namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuleta mitambo 33 ambayo itaweza kuchimba mabwawa na magari 53 ya ufuatiliaji. Jambo la msingi kwenye ufuatiliaji sio magari, kwenye ufuatiliaji ni wafanyakazi. Kwa hiyo lazima tuwe na wataalam wa kutosha na nashauri kuwa kadri fedha zinavyotolewa, kadri bajeti inavyokuja kila mwaka magari yaweze kuongezwa kusudi tuweze kuchimba na kufuatilia hawa watu kwa ujumla. Hiyo inaendana pamoja na kilimo cha umwagiliagi Mkoa wa Morogoro. Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, Mkoa wa Morogoro ni mkoa uliojaliwa mito mingi, ni mkoa wenye skimu mpaka sasa hivi tuna Dakawa, tuna Mkula tuna na skimu nyingine nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ila ningeliomba kuwa tupate skimu nyingine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Christine.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: …ili tuweze kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie na Maafisa Ugani…

MWENYEKITI: Muda wako umeisha Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari bado?

MWENYEKITI: Muda wako umeisha Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Maafisa Ugani waangaliwe vizuri. Ahsante na Mwenyezi Mungu ambariki Bashe, Mwenyezi Mungu ambariki Mheshimiwa Rais, tuweze kuendeleza kilimo chetu. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia kwenye Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu aliyenipatia nafasi ya kuchangia. Pili, nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri anayoifanya na kwa kutenga fedha kwenye Wizara hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana kumpongeza Mheshimiwa Waziri Dokta Angeline Mabula, Naibu Waziri wake Mheshimiwa Pinda, Katibu Mkuu Injinia Sanga, Naibu pamoja na Wizara nzima kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ardhi ni mali, ardhi ni vizuri tuitunze, ardhi tuithamini kwa sababu watu wanaongezeka lakini ardhi haiongezeki. Kila mmoja anaongelea migogoro, kila mmoja anatamani ardhi yake iweze kupimwa. Namuomba Mheshimiwa Waziri aangalie suala la upimaji wa ardhi ili kusudi tuweze kwenda vizuri kadri tunavyokwenda kwa sababu ardhi haiongezeki lakini binadamu wanaongezeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya ardhi katika Mkoa wa Morogoro. Nyote mnaamini kuwa Mkoa wa Morogoro unaongoza kwenye migogoro ya ardhi. Mheshimiwa Waziri wewe ni shahidi, naamini ulishafika Mkoa wa Morogoro, Mawaziri wengine wengine wamefika kwenye Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Mkoa ameweza kutatua migogoro ya Morogoro, Wakuu wa Wilaya wameweza kutatua migogoro na wataalam lakini migogoro bado iko hapo hapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hii migogoro hasa ninayoisema kwa Mkoa wa Morogoro hasa ni kwa upande wa wakulima na wafugaji. Ninaomba Mheshimiwa Waziri wa upande wa Ardhi uweze kushirikiana na upande wa Wizara ya Mifugo muweze kutatua tatizo hili ambalo limekuwa sugu kwenye Mkoa wetu wa Morogoro. Migogoro hii ya ardhi ambayo iko kwenye upande wa wakulima na wafugaji iko kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Morogoro ikiwepo Malinyi, ikiwepo Kilombero, hasa Kilombero ni hatari sana kwa sababu iko kwenye Bonde la Kilombero. Kwenye Bonde hili la Kilombero ndiyo linatoa maji ambayo yanakwenda kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere. Kwa hiyo, kama litaharibika hatutaweza kupata maji ya kutosha na umeme hatutaweza kupata umeme wa kuzalisha umeme kwenye bwawa hili. Kwa hiyo naomba muiangalie. Mvomero pamoja na Wilaya zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sitaacha kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa jitihada alizozifanya kwa Mkoa wetu wa Morogoro, licha ya matatizo hayo lakini angalau ameweza kupima maeneo machache kwenye Mkoa wetu wa Morogoro kwenye Wilaya mbalimbali ikiwepo Wilaya ya Malinyi, Kilombero, Ulanga na Kilosa pamoja na Mvomero lakini upimaji umesimama, ninaomba Mheshimiwa Waziri utakapokuja kujibu pale tuweze kujua kuwa upimaji huu unaendelea lini? Kwa sababu migogoro bado inaendelea na kutatua migogoro hii ni kupima ardhi kwa sababu ukipima ardhi watu watajua watapata hati miliki yao na wataweza kuwa na ardhi yao na wataweza kuzitumia bila ya mgogoro. Wakulima watakuwa na ardhi yao na wafugaji watakuwa na ardhi yao, itakuwa hakuna kuingiliana. Kwa hiyo, ningeliomba kujua ni lini upimaji tena utaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikifuatia hapo pia naongelea kuhusu vyuo vyetu vya ardhi ikiwepo Chuo cha Tabora pamoja na Chuo cha Morogoro na Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar es Salaam. Naomba sana kwa sababu wataalam inaonekana kuwa wanahitimu na wataalamu hawatoshi. Naomba udahili hasa kwenye vyuo vya kati uweze kueleweka, uweze kudahiliwa wanafunzi wengi kwa sababu hawa wa vyuo vya kati hasa ndiyo wanafanya sana upimaji wa ardhi, kusudi waweze kuajiriwa na tuweze kupata wataalam kwa sababu matatizo haya ya ardhi yatakwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kusema kuwa utafiti wa migogoro wala siyo utafiti, migogoro inayoeleweka, huu utafiti wa kubainisha hii ardhi uweze kufanyika kwa sababu ili tuende na sayansi na teknolojia lazima tufanye utafiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa naomba kuongelea bajeti. Bajeti inatolewa lakini naomba bajeti ya maendeleo iweze kuangaliwa kwa sababu hii bajeti licha ya kuongeza fedha na kutupatia fedha ndiyo ikitolewa kwa wakati na fedha zote tunazoziidhinisha humu Bungeni zikatolewa kwa wakati na zikatolewa zote miradi yote ya maendeleo ikiwepo upimaji wa ardhi itaweza kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia kwa kusema kuwa namsihi sana Mheshimiwa Waziri uliangalie hili suala la upimaji wa ardhi kwenye nchi yetu nzima, kusudi tuondokane na hii migogoro ya ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nakushukuru na Mwenyezi Mungu akubariki. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia bajeti ya Waziri wa Fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa namshukuru na nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mambo anayoyafanya sana miradi anaisimamia na ametoa hela nyingi kwenye bajeti hii. Ni kweli bajeti hii imemgusa kila mmoja kwenye kila nyanja kweli tunamshukuru Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninapoanza kuchangia nianze na ukusanyaji wa mapato. Naomba sana Serikali inakusanya mapato na ina njia ambayo imetumia ya kukusanya mapato lakini nilikuwa nashauri kuwa ifanye utafiti mzuri ambao utaweza kukusanya mapato. Mimi ni mmojawapo nikienda dukani kununua kitu naomba risiti, mmoja mmoja atakupa risiti lakini wengi watakuambia kuwa EFD machine zimeharibika hazifanyi kazi, kwa hiyo unakuta Serikali tunapoteza sana mapato kwa kutodai risiti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu, kuna viongozi wengi ambao wako Wilayani, ambao wako Mkoani, ambao wako kwenye Halmashauri naamini tukiwa-task waweze kufuatilia Maafisa Biahsara wataweza kufuatilia na kuwachukulia hatua hao wafanyabiashara ambao hawataki kutoa hela zetu kusudi tuweze kupata mishahara pamoja na wale watu wafanyakazi waweze kupata mishahara yao pamoja na miradi ya maendeleo iweze kutimilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kuwa mapato tunapata lakini kuna Wakandarasi, Wakandarasi kwa kweli wana shida wanafanya kazi zao lakini hawalipwi. Kwa hiyo, nilikuwa nashauri Mheshimiwa Waziri wa Fedha waangalie hawa Wakandarasi wanaishi maisha mabaya na huku wameshafanya kazi. Kwa hiyo, naomba muwaangalie walipwe hela zao ili kusudi waweze kuendelea na kazi zingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naongelea kuhusu asilimia kumi ya mapato ya Halmashauri. Hii asilimia 10 ambayo akina mama pamoja na vijana pamoja na wenye ulemavu ambayo wanatengewa ni nzuri sana, lakini kwa sababu ya changamoto Serikali imesema kuwa bado wanaifanyia kazi. Naomba na ninashauri kuwa kwa sababu ni jambo muhimu sana ambalo linawakomboa sana hasa wanawake wakiwepo na wanawake wa Morogoro na wanawake wote waliokuwa wanapata mikopo hii, naomba muifanyie haraka sana kusudi tuweze kupata ufumbuzi wake, waweze kuendelea na mikopo yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naongelea ni reli ya mwendokasi. Naipongeza Serikali nampongeza Mheshimiwa Rais kwani anafanya mambo mazuri sana. Tumeambiwa kuwa kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro ambacho kina kilomita 300 karibu kinakamilika kina asilimia 98.14 ambayo sasa hivi kinakamilika na mabehewa ninyi mmeyaona mabahewa ya ghorofa ambayo yameletwa, vichwa ambavyo vimeletwa naaamini kuwa hivi karibuni na kama sikosei labda mwezi ujao kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro kitaanza safari zake. Kwa hiyo, naomba na ninatoa ushauri kwa wananchi ambao watatumia hii reli waitunze, tuzidi kuitunza kusudi iweze kuendelea vizuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuja kwenye barabara, Mheshimiwa Rais ameunganisha barabara, Mkoa kwa Mkoa na ameunganisha mpaka nchi yetu na nchi jirani. Kwa hiyo, licha ya kumpongeza naomba barabara ya kuanzia Kibaha hadi Morogoro ambayo ina njia nne ingawaje imefanyiwa usanifu, hela zikitengwa iweze kukamilika kwa ni kuna foleni ya malori. Nanyi ni kweli mnasafiri kwenye barabara hii mnaiona hiyo foleni ya malori inavyosumbua, kwa hiyo naomba sana hiyo barabara kwenye bajeti hii iweze kufanyiwa kazi ili kusudi tuweze kupata usafiri ambao unaeleweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna barabara ambayo huwa tunaisemea mara kwa mara ya Bigwa mvua inakwenda kwenye Bwawa la Mwalimu Nyerere, tunayo barabara tunaisema Ubena - Zomozi mpaka kwenda mpaka Bwawa la Mwalimu Nyerere ndiyo kwenye mpango ilikuwepo, lakini naomba itengenezwe kwa sababu ni muda mrefu tumeiongelea hii barabara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu kilimo. Kilimo kinaajiri wananchi ambao ni asilimia 65.5 na zaidi. Kwa hiyo, kilimo ukitaka watu waweze kutoka kwenye umaskini ni sekta za uzalishaji ambazo sekta za uzalishaji ni kilimo. Kwa hiyo, kilimo namaanisha uvuvi, mifugo ambazo zinaweza kuwakomboa wananchi. Kwa hiyo, fedha zilizotengwa huko huko wakati mwingine tunatenga fedha hazitoki, kwa hiyo, tutakapopitisha hiyo bajeti naomba fedha tutakazozitenga zitoke na hasa kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kutokana mabadiliko ya tabianchi ambacho kitaweza kumkomboa mwananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na nampongeza Mheshimiwa Rais kwa bajeti ambayo imetengwa ambayo tunaiongelea sasa hivi bilioni 98.8 kitu kama hicho, hiyo bajeti ni kubwa sana. Bilioni 970.8 ambayo ndiyo bajeti ya kilimo, naamini ni kubwa sana ikisimamiwa vizuri sana itaweza kumkomboa mwananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa angalizo kuwa hiyo hela ambayo imetengwa naomba kadri bajeti zinapokuja hizi zinazokuja mbele mwaka kwa mwaka tuweze kupata bajeti zaidi ya hii ili tuweze kufikia Azimio la Malabo na Maputo ambayo ni asilimia kumi ya bajeti nzima iende kwenye kilimo. Kwa hiyo, naamini Mheshimiwa Rais anayependa kilimo na kukipa kipaumbele naamini atafanya hivyo, Mama ni mzuri Mama anafanya vitu vizuri anafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu mazingira. Nampongeza sana Mheshimiwa Makamu wa Rais kwa kuisimamia hiyo kampeni ya kupanda miti. Naomba sana wananchi, itaendelea kutenga fedha zinazotengwa kwa mambo ya Maliasili na Mazingira, tuweze kusimamia hiyo miti tuipande ambayo kila Halmashauri, kila Wilaya ni 1,500,000 inapandwa lakini ikipandwa tuweze kuifuatilia kuwa kweli inastawi na haikauki, hayo tunaweza kwa sababu ya mazingira. Pia licha ya kupanda miti tumehamasisha, wanahamasishwa, tuwahamasishe wananchi waweze kutumia nishati mbadala hasa kwa kupika, ili kusudi tuweze kupunguza kutumia mikaa pamoja na kuni tuweze kwenda vizuri kutunza mazingira yetu na yatatutunza naamini tukiweza kutunza haya mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu elimu. Tunamshukuru Mheshimiwa Rais, tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa mambo inayofanya ambayo ni wanafunzi wetu watasoma mpaka kidato cha sita bila ya malipo ya school fees, pia imetoa mambo ya vyuo vya kati itayafanyia vizuri sana. Pia na Vyuo Vikuu inatoa mikopo ya kutosha kwa hiyo naamini itaendelea kutoa mikopo kwa kila mwanafunzi kwa sababu hapo baadae wataweza kurudisha mikopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niongelee kuhusu umeme, tunashukuru Serikali yetu, ni kweli watu walikuwa hawajui umeme lakini miaka hii umeme umesambaa kila mahali na tunaamini tunakwenda kwenye vitongoji kila mmoja anayeweza kuweka umeme kwa shilingi 27,000 huko vijijini ataweza kuweka umeme. Kwa hiyo, tunampongeza mama anafanya kazi kubwa. Lakini naomba kuna Kata za Morogoro, Mgeta, Tarafa ya Mgeta ambayo bado Kata nzima vijiji vyote Kata kama nne hazijapata umeme. Kwa hiyo nashauri, namuomba Mheshimiwa Waziri anayehusika, aweze kuliona hilo jambo kuwa vijiji vyote vya Kata nzima havina umeme, Kata, Tarafa ya Mgeta vijiji vya Kata nne na zingine kwenye Wilaya ya Mvomero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisemee kuhusu barabara. Barabara za Mkoa wa Morogoro hasa za vijijini zikiwepo zinazosimamiwa na TARURA naomba ziangaliwe. Nakuomba sana ziweze kuangaliwa ziweze kutengenezwa ziweze kukamilika watu wa TARURA waweze kuona wana jukumu la kuweza kuona hizo barabara zinatengenezwa kwa sababu tuweze kwenda vizuri maendeleo ni maendeleo namshukuru Mama Samia namshukuru Rais wetu anatupenda na sisi tumpende.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nakushukuru na nasema ubarikiwe na Mwenyezi Mungu, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio na Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa SGR, nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali, Wizara na viongozi wote na watendaji wa Wizara kwa ujenzi wa SGR.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda sana kumpongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia ujenzi huu wa SGR.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipande cha kutoka Dar es Salaam kuja Morogoro kilometa 300 tumeambiwa tumefikia asilimia 99.54; tunaipongeza sana Serikali kwa ujenzi huu na hii ilikuwa mwezi Aprili. Pia tumeambiwa majaribisho ya umeme tayari yameshafanywa.

Sasa kiu cha wananchi wa Morogoro wanauliza Mheshimiwa Waziri usafiri wa reli hii hasa kwa wasafiri wa wananchi ni lini utaanza kuanzia Dar es Salaam kuja mpaka Morogoro ili uweze kurahisisha usafiri. Naomba Waziri wakati anamalizia aweze kutueleza wananchi wa Morogoro tuweze kujua kwa sababu hii inasaidia katika mambo mengi ya uchumi, ya biashara pamoja na usafiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikiongelea hapo kuna kipande cha kutoka Kihonda mpaka kwenye kituo kikubwa hicho cha SGR. Katika hotuba ya Waziri amesema kitajengwa kwa upande wa lami, nashukuru sana. Ombi langu, naomba kuwa mara kwa mara huwa naongelea barabara ya mzunguko ili kurahisisha na kupunguza foleni hapo ya Msamvu pale Manispaa. Kwa hiyo, nilikuwa naomba badala ya kurudia hapo kwenye kituo iendelee mbele mpaka kwenye ofisi ya TAFORI kwa lami kusudi iweze kupunguza foleni ya hapo Msamvu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuongezea tena kuna baadhi ya wananchi wa Kihonda pale Manispaa na wananchi wa Kilosa ambao bado wanadai fidia zao ambao walihamishwa na walichukuliwa ardhi yao kutokana na ujenzi wa reli ya mwendokasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo furaha sana hasa mimi mwenyewe na wananchi wa Mkoa wa Morogoro kuona sasa hivi Mkoa wa Morogoro umefikiriwa kwenye uwanja wa ndege, hiyo ni furaha sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Morogoro wanausubiri kwa hamu ujenzi wa kiwanja cha ndege kusudi kurahisisha usafiri wa kusafiria kwani tulikuwa hatuna uwanja wa ndege kwenye Mkoa wetu wa Morogoro ambao utarahisha usafiri pamoja na ajira na uchumi. Kwa hiyo, tunashukuru sana kwa kuliangalia hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mweyekiti, jambo lingine ujenzi wa barabara wa kutoka Bigwa kuelekea mpaka Mvuha, tumetengewa fedha nashukuru sana kwa sababu hii barabara ni muhimu inaelekea kwenye Bwawa la Julius Nyerere ambalo ni muhimu sana kwa kufua umeme. Kwa hiyo, kuanzia pale Mvuha kuelekea mpaka Kisaki mpaka kwenye Junction naomba na yenyewe ifikiriwe, tuweze kuona itafanyaje. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi ni kubwa kwa Serikali kuona pia barabara ya Ubena mpaka Ngerengere Jeshini na yenyewe imetengewa fedha, itajengwa kwa kiwango cha lami. Hapo hapo naomba kuwa kuanzia hapo kipande cha Ngerengere kuelekea mpaka Mvuha nacho kiangaliwe ili kusudi kiweze kujengwa kwa lami kufuatana na umuhimu wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Magore kwenda mpaka Turiani ilitengewa fedha lakini tumeambiwa kuwa hizo fedha za kulipa makandarasi na ni madeni. Kwa hiyo, barabara ya kuanzia kipande cha Turiani mpaka Mziha pale kipo palepale wanasema wanafanya maandalizi. Namuuliza Mheshimiwa Waziri, hiki kipande cha Turiani mpaka Mziha ni lini kitajengwa na ni lini fedha zitapatikana, kwani kinaunganisha Handeni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Dumila – Ludewa – Kilosa nashukuru inaendelea vizuri, lakini na yenyewe ilitengewa fedha lakini na zenyewe ni za kulipa madeni ya wakandarasi. Kipande cha Kilosa mpaka Mikumi wanasema maandalizi yanafanyika; je, hayo maandalizi yatafanyika mpaka lini Mheshimiwa Waziri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa barabara ya Kidatu – Ifakara - Lupilo mpaka kuelekea Malinyi mpaka kuelekea Songea ambayo inaendelea na ujenzi. Ni kweli barabara kuanzia Kidatu mpaka Ifakara inaonekana hata ukipita inaonekana kuwa ujenzi unaendelea. Kwa hiyo, kwa kweli tunaipongeza Serikali na tunaishukuru Serikali kuona ujenzi unaanza kuendelea. Ni barabara muda mrefu, ni barabara ambayo tumeiongelea humu Bungeni mara kwa mara, kwa hiyo naomba hata Ifakara kuendelea mpaka Malinyi mpaka Songea iweze kuonekana kuwa inajengwa kwa sababu upande wa Ruvuma ni kama walishamaliza upande wa Morogoro ndiyo bado. Kwa hiyo, naomba na yenyewe iweze kuonekana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Chalinze – Magindu - Lukonge pamoja na Serengeti B mpaka Mziha kwa kweli nimeshukuru na nimefurahi sana kwa sababu barabara ya Mziha huwa ni mbaya sana kiasi kufika kwenda mpaka Mziha huwa ni kazi sana, lakini sasa hivi wamesema wanaiangalia. Nakuomba Mheshimiwa Waziri usiiangalie tu, naomba itengenezwe kwa kiwango cha lami kusudi wananchi waweze kupita kwa sababu inaanzia Mkoa wa Pwani mpaka inakuja kwenye Mkoa wa Morogoro. Kwa hiyo, nilikuwa naomba iendelee kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye madaraja; madaraja ya Chakwale pamoja na Nguyani sijayaona vizuri Mheshimiwa Waziri, haya madaraja ni muhimu sana kwa sababu wanafunzi wanapata shida, watu wanakufa humo kwenye maji wakati wa mafuriko inabidi usubiri kwa muda mrefu mpaka mafuriko yapite. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri unayajua hayo madaraja, naomba hayo madaraja yaweze kujengwa kwa uimara yaache kujengwa mwaka kwa mwaka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa nilikuwa naona barabara ya Ifakara – Kihansi - Madeke mpaka Njombe na yenyewe imetengewa fedha lakini imetengewa fedha kidogo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri naomba kwa sababu na hii inaunganisha Morogoro pamoja Njombe ni mikoa miwili totauti muiangalie vizuri kwa sababu ya uchumi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara nyingine ambayo haikutajwa kabisa ambayo sikuiona labda ni macho yangu ni barabara ya Newala kuja mpaka Ulanga, Mkoa wa Morogoro. Inaanzia Mkoa wa Mtwara inaunganisha Mkoa wa Morogoro. Mheshimiwa Waziri naomba hiyo barabara iangaliwe na baada ya hapo kwa kweli mimi napongeza na ninashukuru na mawazo niliyoyatoa naomba yachukuliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi na mimi kuchangia. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa kuianzisha hii Wizara ya Maendeleo ya Jamii kwani ilipokuwa pamoja na Afya niliona kama ilikuwa inamezwa.

Mheshimiwa Spika, tena niwapongeze sana wanawake wote wa Tanzania, kwa kweli wanawake sasa hivi hakuna mwanamke aliyelala. Hata ninyi wanaume mliyo humu ndani mnajua wake zenu wanafanya kazi, hakuna mwanamke aliyelala, kwa hiyo nawapongeza sana. Na wanawake wengi wamejitolea sana kufanya usindikaji, kufanya biashara mbalimbali, wanafanya kazi kweli, tatizo nilikuwa naomba Wizara waone jinsi ya kuwapatia mafunzo ya biashara wanawake kwa sababu wengi wanaanzisha biashara bila ya kupata mafunzo. Wapate mafunzo ya biashara pamoja na ujasiriamali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikiendelea hapo hapo nimekazia kuwa wapatiwe mafunzo ya biashara pamoja na ujasiriamali. Wanawake wamejitoa sana, hakuna mwanamke aliyelala sasa hivi.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ninasema ni asilimia nne kwa akinamama. Kwa kweli hawa akinamama wanarudisha mikopo yao vizuri sana na wanaitumia, lakini wanawake ukweli wamenituma wanasema kuwa hii asilimia nne haitoshi. Kwa hiyo, tuangalie pamoja na kushirikiana na Wizara zingine jinsi ya kuona tufanyeje ili ionekane hizi asilimia nne ambao wanapewa hawa akina mama, pamoja na vijana, pamoja na makundi ya watu wenye ulemavu ionekane kuwa kweli inafanya kitu ambacho kinaonekana kweli kweli kuwa ni kitu chenyewe.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kwenye usindikaji; akinamama ambao wamejikita sana ni masoko waweze kutafutiwa masoko na waweze kuonyeshwa kuwa wafanye vitu ya vyakula ambacho kina quality kweli. Wakati mwingine vyakula havina quality unakuta kuwa TBS inawababaisha, kwa hiyo tuangalie tuweze kuwasaidia hawa akinamama.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine na mimi nawaunga mkono akinamama wote waliongelea kuhusu ukatili wa akinamama pamoja na watoto. Unaona kwa kweli ni mambo haya wanafanya kwa kweli, tunaomba wajirudi akina baba kuacha kufanya ukatili kwa watoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninaloongelea ni watoto wa mitaani; tutaongelea watoto wa mitaani mpaka lini na yenyewe tuweke mtazamo jinsi ya kukatiza kuachana na kuongelea mambo ya watoto wa mitaani. Wizara pamoja na Afisa Maendeleo tukiwa pamoja na Ustawi wa Jamii tuone jinsi ya kuwaangalia hawa watoto waache kwenda kwenye mambo ya mitaani.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo halijaongelewa humu ni jukwaa la akinamama; majukwaa ya akinamama namshukuru Mheshimiwa Rais Samia ameanzisha majukwaa ya akinamama tangu alipokuwa Makamu wa Rais. Lakini mpaka sasa hivi haya majukwaa ya akinamama hawajui yanafanya nini, wapo tu, hawana uwezeshwaji, wanaendelea tu. Kwa hiyo, naomba sana wangepewa Mwongozo wangeliweza kufanya vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naomba kuliongelea ni vituo vya wazee; nilitembelea vituo vya wazee vya Morogoro, Kituo cha Fungafunga pamoja Chasi. Unakuta kuwa vituo vya wazee wanamuomba Mheshimiwa Waziri na Naibu awatembelee, hawajawatembelea kwa sababu kuna matatizo mengi, lakini viongozi wengine tumekwenda ndiyo sababu tunayachangia. Unakuta hao wazee wanaishukuru kwanza Serikali inawapatia chakula, ila kwa chakula wanapongeza. Lakini kuna tatizo unakuta hawa wazee majengo yao ni mabovu, kwa hiyo nilikuwa naomba haya majengo yaweze kukarabatiwa.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine wazee hao wengine siyo wazee sana kwa sababu kuna na vijana ambao wameumwa ukoma, hawana vidole, wamekatika vidole na nini nao wako humohumo. Wanaomba Kituo cha Fungafunga waweze kupatiwa uzio kwa sababu wazee wanatoroka wanakwenda mjini.

Jambo lingine wanashukuru kuna ma-nurse, lakini kuna tatizo moja wakipata magonjwa dawa hazitoshi, kwa hiyo wanaomba wapatiwe dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naongelea hapohapo ni maji; wana tatizo la maji naongelea Fungafunga ya Morogoro, kwa hiyo ushauri wangu waweze kupewa maji kusudi na na wenyewe waweze kutumika vizuri.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni watumishi; nikija kwenye watumishi, kuna watumishi wa Ustawi wa Jamii ambao inabidi wa wasaidie. Watumishi ni wachache kiasi wazee wengine hawajiwezi kabisa. Kwa hiyo, naomba muwaongezee watumishi. Hapo hapo kuna watumishi wengine wamekaa muda mrefu kwenye ngazi hiyo hiyo kuanzia mwaka 1999 hajapandishwa cheo chochote, yuko palepale, kwa hiyo, naomba muwaangalie na wenyewe waweze kuonwa kuwa wanafanyiwa mambo mazuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu uhaba wa watumishi kwa ujumla na wajibu wao, maendeleo ya jamii ni watu wazuri na inabidi waweze kufanya kazi zao vizuri, waweze na wenyewe kupewa vitenda kazi kama Wizara zingine walivyopewa vitendea kazi kama pikipiki na nini. Kwa sababu masuala yote kwa Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye anajijua masuala yote ya lishe yako kwako, masuala yote ya ujenzi wa vyoo yako kwake, masuala yote ya nini kusudi waweze kufanya kazi zao vizuri naomba Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii waweze kuangaliwa kwa vitendea kazi.

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo nakushukuru kwa kunipatia nafasi. Kwa hayo niliyoyaongea, naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi hii kuchangia kwenye bajeti.

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuleta bajeti nzuri sana, pia nampongeza Mheshimiwa Waziri, Dkt. Mwigulu, kwa kuileta hii bajeti hapa Bungeni. Kusema ukweli hii bajeti imekidhi ni nzuri sana kwa wananchi wote, wote wanaipenda sana.

Mheshimiwa Spika, nianze na suala la kuondolewa ada kwa kidato cha tano na sita. Hii imepokelewa vizuri na inaonekana kuwa wanafunzi watasoma bure bila ya kulipa ada kuanzia shule za msingi mpaka Kidato cha Sita, hii ni nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, inaonekana kuwa mikopo ya Vyuo Vikuu imeongezewa fedha katika bajeti hii. Kwa hiyo, jambo ninaloomba na kushauri ni kwamba vyuo vya kati viangaliwe ili na vyenyewe ulipaji wa ada uweze kuwa nafuu kwa wanafunzi hawa na kwa wazazi. Kwa hiyo, huo ni ushauri wangu, kuwa na vyenyewe viangaliwe, visiachwe katikati peke yao.

Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ambalo ninapenda kuongelea ni kuhusu hii asilimia 10. Kwa kweli hii asilimia 10 Mheshimiwa Waziri ukija kuhitimisha naomba uitolee ufafanuzi ili tuweze kuelewa. Hii asilimia 10 umesema kwenye hotuba yako kwamba asilimia tano imependekezwa kuwa iende kwa wamachinga ili kuboresha miundombinu. Miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa masoko.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia Wamachinga tayari kuna fedha ambazo zimeshatengwa, lakini hii asilimia 10 umesema asilimia mbili ndiyo itakwenda kwa vijana na asilimia moja ndiyo itakwenda kwa watu wenye ulemavu kwa kweli hapo haieleweki!

Mheshimiwa Spika, ninachoomba hii asilimia 10 ibaki kama ilivyokuwa, kuwa asilimia nne ibaki kwa akinamama, asilimia nne ibaki kwa vijana na asilimia mbili ibaki pia kwa wale watu wenye ulemavu. Kwanza kilichokuwa kinaombwa hapa ni kuongeza hii bajeti kwa upande huu wa asilimia 4:4:2, sasa badala ya kuongeza inaonekana kuwa inapunguzwa. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri aingalie vizuri sana kusudi isipangwe kama anavyokusudia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la kufurahisha kwa wananchi wote na hasa wakulima na wafugaji na wavuvi ni kujali sekta za uzalishaji na hizi sekta za uzalishaji hasa ni Sekta ya Kilimo, Sekta ya Uvuvi na Sekta ya Mifugo ambapo asilimia 65.5 ya wananchi inategemea kilimo. Asilimia 100 ya chakula tunachokula Watanzania inategemea kilimo. Kwa hiyo, kwa kuongeza bajeti ya kilimo kutoka bilioni 274 mpaka bilioni 954, ni jambo la neema sana. Pia fedha za mifugo kutoka bilioni 168.2 mpaka 268.2, nalo ni jambo safi kabisa na hapo hapo kuna mchanganuo kuwa bilioni 92 ni fedha za mifugo na bilioni 176.2 ni fedha za uvuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikienda kwenye kilimo jambo linalotakiwa hapa ni kilimo chenye tija, ufugaji wa tija pamoja na uvuvi wenye tija. Kwa upande wa kilimo nashauri na nampongeza Waziri wa Kilimo kama walivyosoma sekta zao pamoja na uvuvi na mifugo. Nashauri mipango iliyopangwa kwenye Wizara hii iende kama hivyo hivyo ilivyopangwa. Jambo la muhimu ni utekelezaji, ufuatiliaji na kuona kuwa mipango yote inaenda kama ilivyopangwa. Kwa mfano, nikija kwenye upande wa kilimo cha mbegu, sasa hivi tunamashamba ya mbegu 17 lakini unakuta mashamba mengine hayafanyi kazi vizuri. Kwa hiyo, nashauri mashamba yote ya mbegu yafanye kazi vizuri na yaweze kutumia kilimo cha umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, mpaka sasa hivi mashamba hayatumii kilimo cha umwagiliaji, naamini tukizalisha mbegu sisi wenyewe za hapa ndani tutatokana na tatizo la mbegu. Kwa mfano, mbegu za alizeti na michikichi, Tanzania tuna ardhi kubwa sana hatuna sababu ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nchi za nje, tunaweza kulima mbegu zetu za alizeti, tukaweza kuwatosheleza wakulima wote, tukaeneza elimu ya kulima michikichi kwenye mikoa ambayo imepangwa na tukaweza kuzalisha kwa wingi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kilimo cha ngano; tuna ardhi, tuna mikoa ambayo pia bado haijaangaliwa kuwa inaweza ikalima ngano. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kutoa ngano kwenye nchi za nje, tunaweza tukalima sisi wenyewe tukajitosheleza. Nashukuru Wizara ya Kilimo ambayo tayari imetoa vitendea kazi kwa Afisa Ugani. Kwa hiyo, Maafisa Ugani hawa wakisimamiwa vizuri naamini kuwa tutaweza kutoa na kuzalisha mbegu za kutosha na kuweza kujisimamia kupata mafuta ya kutosha ya kula badala ya kupeleka fedha zetu kununua mafuta nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, nikija kwa upande wa mifugo, tayari kuna elimu ya uimilishaji; wananchi wengi hawatumii elimu hii, elimu hii ni nzuri sana ikitumika vizuri bajeti itakwenda vizuri na watu wataweza kupata mazao bora ya mifugo. Kwa upande wa uvuvi nilikuwa nataka wananchi waweze kufundishwa vizuri elimu ya ufugaji wa samaki.

Mheshimiwa Spika, nikija kwenye ukusanyaji wa mapato; mapato mengi yanapotea tungeweza kupata fedha nyingi za kutosha kwenye ukusanyaji wa mapato. Tuje kwenye ukusanyaji wa mapato, hata sisi tulio humu ndani tunasema yule anayeuza aweze kutoa risiti na yule anayenunua aweze kudai risiti, lakini unakuta hiyo njia haitumiki. Kwa hiyo, naomba uwepo mfumo mzuri kama ulivyo kwenye sheli zetu za kuuzia mafuta, whether unaomba risiti, huombi risiti, lakini tayari mahesabu yanaonekana kuwa umechangia Serikali. Kwa hiyo, hata kwenye maduka yetu ya wafanyabiashara ionekane kuwa hizo EFD machines zinafanya kazi na zimewekewa mfumo wa kukusanya ada zetu ambazo tunaweza tukaongeza bajeti ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naongelea ni kuhusu TEHAMA. Hii TEHAMA ikienda mpaka vijijini vijana wetu kupitia kilimo, mifugo na uvuvi wanahitaji kutumia TEHAMA, wanahitaji kutumia umeme, wanahitaji maji safi na salama, wanahitaji mambo ya afya. Naamini hivi vyote vikiwa huko vijijini vijana watatamani kukaa vijijini na wataweza kuendesha maisha yao huko vijijini, watajiajiri huko vijijini, hakutakuwa na sababu ya kuvutiwa kuja mijini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naomba kuongelea baada ya kuwavutia vijana kukaa huko vijijini, nashukuru kwa upande wa kilimo, tayari na uvuvi na mifugo wameshaweka mazingira mazuri ambayo yatawavutia lakini yasimamie kwani kuwatengea ardhi, kuwapa matrekta ya kulimia ni jambo zuri ambalo litawavutia hawa watu hukohuko.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo naomba kuendelea ni kuhusu miundombinu ya SGR. Nashauri Mheshimiwa Waziri anasema SGR inakwenda vizuri, naipongeza Serikali ujenzi wa SGR unakwenda vizuri kipande cha Dar es Salaam kuja Morogoro kinakwenda vizuri, Waziri amesema kuwa tumefika asilimia 96.5. Kwa hiyo, naomba kipande hicho kiweze kukamilika na kiweze kufanya kazi kusudi na vipande vingine viendelee vizuri. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru, lakini mambo hasa niliyosema kuwavutia vijana ikiwemo TEHAMA na kila kitu, hivyo naomba kifanyiwe kazi.

SPIKA: Muda wako umeshaisha Mheshimiwa.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja, na bajeti hii ni nzuri naomba itekelezwe na isimamiwe. Ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira wa Mwaka 2018
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze
kuchangia katika Muswada huu ambao una manufaa kwa maisha ya binadamu. Kwanza nianze kutoa pongezi kwa Serikali kwa kuleta huu Muswada na pia naipongeza Serikali kwa sababu majadiliano mengi ambayo yalijadiliwa na Kamati yaliweza kuchukuliwa na Serikali, kwa hiyo, naipongeza kwa hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tulivyosema kwenye mjadala wetu ambao Mwenyekiti alitoa taarifa yetu kuwa utangulizi wa Ibara hiyo ya Kwanza iliyoanza na maana ya majina na Ibara ya Pili inaongelea matumizi kuwa, sheria hii itatumika tu Tanzania Bara. Ibara ya Tatu inaelezea maana ya maneno mbalimbali na nashukuru Serikali haya maneno, maana ya maneno, tulikubaliana kwa pamoja ila kuna mahali pengine ambapo ni kidogo tu tulitofautiana na mwisho wa yote tukakubaliana kwa definition kama hiyo ya RUWA kuwa RUWASA kwa sababu inachukua pamoja na mazingira na mazingira nayo ni jambo muhimu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya tano kuanzishwa kwa Wakala wa Maji Vijijini ni muhimu sana kwa sababu, huyu Wakala wa Maji Vijijini itatumika sana na pia kwenye uchimbaji wa visima na pia itatumika kwenye uanzishaji wa miradi mingine ya maji. Jambo hili ni muhimu sana, ila inabidi iangaliwe kuwa, hii miradi itaendeleaje hapo mbeleni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye Ibara ya 11 ikienda pamoja na Jedwali kuhusu asilimia 50 na theluthi moja kwa upande wa Serikali; hapa ni muhimu sana niongee kwa kirefu kidogo kwa sababu, kwa kuangalia bodi, mfumo wa Bodi ya Maji ambavyo utakuwa, inaonekana kuwa mfumo huu unaweza ukaleta asilimia kubwa ya akinamama kwenye Bodi hii ya Maji, kwa sababu, hawa akinamama ndio unakuta kuwa ndio wanashughulikia maji kwa hiyo, kama Kamati yangu ya Kilimo naungana nayo kuwa badala ya theluthi moja iwe asilimia 50.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kutokana na muundo wa bodi; kwenye muundo wa bodi unakuta kuna Mwenyekiti na hii bodi inateuliwa na Mheshimiwa Waziri. Kuna Mwenyekiti, ambaye huyu Mwenyekiti anatokana na mahali pale ambapo anaishi, anaweza akawa kwenye miji au anaweza akawa wapi. Pia, Mkurugenzi Mtendaji ambaye anaweza akawa mwanamke, pia Mwakilishi wa Wizara ya Maji ambaye anaweza akawa mwanamke au akawa mwanaume, pia Mwakilishi wa Ofisi ya Afisa Tawala wa Mkoa ambaye anaweza akawa mwanamke au akawa mwanaume, pia Mkurugenzi wa Manispaa ambaye anaweza akawa mwanamke au mwanaume.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuongezea hapo, kuna watu tena watano ambao wanachaguliwa na Waziri kwa kushauriana pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo unakuta kuna representative wa RAS, anayemwakilisha RAS, ambaye anaweza akawa mwanamke. Kuna Diwani anaweza akawa mwanamke, kuna mwakilishi wa watumiaji maji kwa wingi au biashara anaweza akawa mwanamke au mwanaume; kuna mwakilishi wa watumiaji maji kwa wingi anaweza akawa mwanamke au mwanaume; kuna mwakilishi wa watumiaji maji majumbani anaweza akawa mwanamke au mwanaume; kuna mwakilishi wa vikundi vya akinamama. Kwa hiyo, kwa kuangalia huo muundo wa bodi naungana na Kamati kuwa inaweza ikawa asilimia 100, lakini hasa asilimia 50. Kwa uwakilishi huu wanaweza wakateuliwa wanawake ndio wakawa wawakilishi kwenye bodi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mfuko wa Maji wa Taifa. Tulikubaliana kwa pamoja kwenye Kamati kuwa huo ni pamoja na Serikali kuwa ni kweli huu Mfuko wa Maji ni muhimu sana, lakini kama tulivyosema tulikubaliana na Serikali kuwa iwekwe kwenye kanuni na hizo kanuni kabla hazijaanza kutumika tuweze kukaa pamoja Kamati, pamoja na Serikali kuzipitia na kukubaliana kama ni kweli tunakubaliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ibara ya 61 kuhusu offensive and panalties; baada ya kupitia kwa kina, Kamati tuliona kuwa kwa kweli, adhabu nyingine ni kubwa sana. Kwa hiyo, makosa na adhabu zifanyiwe marekebisho makubwa na Serikali kusudi yaweze kuendana na makosa ambayo yametendeka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna neno muhimu kwenye definition ambalo tulisema kuhusu misuse of water au utumiaji vibaya wa maji. Hata ukiwa nyumbani unaweza ukawa unaosha vyombo, unaendesha maji, ikaonekana unatumia vibaya maji au wale wanaochepusha maji ikaonekana unatumia vibaya maji; kwa hiyo, kuna aina mbalimbali za matumizi ya maji, hivyo, tuliona itolewe maana yake, tafsiri, kusudi iweze kueleweka vizuri maana ya misuse of water ni nini kuliko kuiweka kwenye Muswada ambao utakuja kutumika kisheria na kupitishwa bila ya kujua misuse of water maana yake ni nini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudie kusema kuwa, mambo mengi naishukuru Serikali tulikubaliana pamoja na yale tuliyokubaliana yaende kama yalivyo na naomba Wabunge wajadili huu Muswada uweze kupita, lakini yale ambayo Kamati tumependekeza kama asilimia 50 wawe wanawake kwenye Bodi ya Maji, naomba ichukuliwe na Serikali kusudi iweze kutumika kuanzia pale itakapoweza kusainiwa na kuwa kama sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja kwa sababu mambo mengi yameshaongelewa. Ahsante kwa kunipa fursa. (Makofi)