Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Mwita Mwikwabe Waitara (254 total)

MHE. OMARI A. KIGODA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kutokana na suala la elimu bure, imeleta changamoto ya kuwa wanafunzi wengi sana ambao wamejiandikisha, lakini kuna uhaba mkubwa sana wa Walimu ambao unasababisha hawa wanafunzi wasipate elimu bora: Je, Serikali ina mpango gani mkakati wa kuajiri Walimu wengi zaidi ili hawa wanafunzi waweze kupata elimu bora?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli kwamba elimu ya msingi bila malipo imeleta chachu ya maendeleo na mwamko mpya na wanafunzi wengi wamejiandikisha na kuingia katika mfumo wa elimu Tanzania. Hili ni jambo jema na kupongezwa kwa maamuzi thabiti ya Mheshimiwa Rais kwa Awamu ya Tano.

Mheshimiwa Spika, mpango uliopo ni kwamba tunao Walimu zaidi ya 11,000 katika Shule za Sekondari, ambao hawa tunaona kwamba mzigo wao siyo mkubwa sana, tumeomba kibali washushwe waje kufundisha Shule za Msingi ili waweze kuziba gap la uchache wa Walimu.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, kumekuwa na wale Walimu ambao wanastaafu na wengine wanapata makosa ya kinidhamu kazini na wengine wanafariki dunia, lakini hapa katikati kumekuwa na mkwamo kidogo, Mheshimiwa Rais amesharuhusu kuajiri angalau kila mwaka kupunguza gap hili.

Mheshimiwa Spika, mpango wa tatu, tumepata kibali cha kuajiri Walimu zaidi za 6,000 ambao wakiajiriwa watapunguza upungufu wa Walimu katika Shule zetu za Msingi. Ahsante sana.
MHE. ALMAS A. MAIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa amjibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini umeona kwamba kuna utata wa maneno fundi sadifu na fundi mchundo na hilo limekuwa tatizo la elimu yetu. Fundi mchundo niartisan na Serikali imefanya vizuri sana lakini fundi sadifu ambaye ni Full Technician Certificate (FTC) holders ndio tuna upungufu mkubwa. Technical field inafanya kazi, ma-engineer wanawatelemshia hawa watu wa fundi sadifu na fundi sadifu wanawateremshia watu wa artisans.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo limekuwa tatizo, kuna gap kubwa kati ya wahandisi (engineers) wanaofanya kazi na kwenda kuunganisha huku chini nafasi katikati imepotea. Baada ya hapo nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imefanya sana kazi ya kuanzisha Shule za Kata, zimeenea maeneo yote ya vijijini na kata. Je, Serikali sasa haioni umuhimu wa kuzifanya baadhi ya Shule za Kata ziwe shule za ufundi ili kumwaga mafundi katika ngazi za vijiji na kata ili kuijenga sera hii ya viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imeamua kujenga VETA na kwa kuwa Jimbo langu la Tabora Kaskazini hakuna chuo hata kimoja cha VETA. Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Chuo cha VETA katika Jimbo la Tabora Kaskazini.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwanza kuna vyuo vya ufundi ambavyo vinasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lakini pia kuna shule hizi za ufundi ambazo zimekarabatiwa kama nilivyotaja na tunaomba tupokee wazo lake tulifanyie kazi, tukiona linafaa itafanyiwa kazi na kutekelezwa ili kuongeza na kupunguza gap ambalo amelizungumza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ameuliza kama kuna kuna uwezekano wa kuanzisha Chuo cha VETA katika Jimbo lake la Tabora Kaskazini, tunaomba tulipokee ni wazo jema likifanyiwa kazi atapata majibu kwa wakati muafaka. Ahsante.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwana naomba niweke kumbukumbu sawa. Mimi ni Mbunge wa Geita, siyo Geita Vijijini. Hakuna Jimbo la Geita Vijijini.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Geita DC ina population ya takribani watu 1,200,000 kwa sensa ya mwaka 2012/2013. Sasa kwa majibu ya Serikali, inavyoonekana, bado tutakwenda hata uchaguzi ujao tukiwa bado tunakaa Halmashauri moja. Je, Serikali inatoa kauli gani ya uharaka kwa ajili ya kuharakisha hizo taasisi zilizobaki ili tuweze kupata mgawanyo wa Halmashauri mbili?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba Mheshimiwa Waziri atamke kitu kwamba kulingana na ukubwa na wingi wa watu wa Halmashauri ya Geita DC, Serikali inaona umuhimu gani wa kutuongezea ceiling ya bajeti kwa wingi wa watu tulionao?

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi ni kwamba suala la kugawa Mamlaka za Serikali za Mitaa linatakiwa lianzishwe na mamlaka yenyewe kwenye eneo hilo. Nimesema tayari jambo hili limejadiliwa kwenye Halmashauri yao ya Wilaya ya Geita. Sasa ni wajibu wao kupeleka mjadala huo kwenye ngazi ya Wilaya na ngazi ya Mkoa, nasi tupo tayari kupokea mapendekezo yao na tuangalie uharaka na ulazima wa kufanya maamuzi ya kugawa Halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Spika, jibu la swali la pili ni kwamba bajeti ya Serikali inategemea na uwezo uliopo. Nia ya Serikali ni njema kabisa kwamba bajeti iongezeke na kila mtu angeweza kupata mgao ambao angehitaji. Hili nalo linategemea pia uwezo wa Serikali, kadri itakavyoruhusu basi bajeti itaongezeka ili huduma iweze kupelekwa kwa wananchi wa Geita na maeneo mengine ya nchi. Ahsante.
MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili nami niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro ambao una population kubwa sana: Je, Serikali inaonaje sasa hii mamlaka ya mji mdogo iwe mamlaka kamili ya mji?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kama nilivyosema, mchakato huu wauanzishe wenyewe watu wa Geita na hususan Busanda; nasi Ofisi ya Rais TAMISEMI tutapokea mapendekezo yao na tutawahisha jambo hili kadri itakavyohitajika kulingana na ukubwa wa bajeti na upatikanaji wa fedha.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, anasema kwamba halmashauri waongeze makusanyo ya mapato ya ndani (own source) na kwa kuwa Serikali ilichukua vyanzo vingi vya mapato ambavyo vilikuwa vinaipatia halmashauri mapato, sasa Serikali inasema halmashauri ziongeze makusanyo ya mapato ya ndani, hayo makusanyo ya ndani yatatoka wapi na kwa nini Serikali isiongeze ruzuku ili Madiwani waongozwe posho? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Madiwani ni viongozi kama sisi Wabunge; na kwa kuwa viongozi wa kisiasa wengi wamewekwa kwenye Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa, kwa nini hawa Madiwani nao wasiwekwe kwenye sheria hii ili waweze kutambulika kisheria kwa sababu ni viongozi muhimu? Katika Uchaguzi Mkuu ni mafiga matatu, baada ya uchaguzi figa la tatu linameguka wanakuwa viongozi wa kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba majibu.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa George Malima Lubeleje kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, Mheshimiwa Mbunge anauliza kwamba kwa sababu kuna vyanzo vimechukuliwa na Serikali Kuu na kwa hiyo mapato ya halmashauri yamepungua ni kwa nini tusitoe ruzuku. Kwanza naomba ieleweke kwamba vyanzo vilivyochukuliwa ikiwemo kodi ya majengo inakusanywa na TRA kwa niaba ya Serikali nzima lakini fedha hizi zinarudishwa kwenye halmashauri kwa ujumla wake kwenda kufanyia kazi shughuli za maendeleo katika halmashauri zetu hizo hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kwa sasa hili jambo la ruzuku halijafanyiwa kazi, naomba tulipokee tulifanyie kazi, kadri uwezo utakavyoruhusu basi tutaona kama kuna uwezekano wa kupeleka ruzuku. Kwa sasa kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi ni kwamba posho za Madiwani na malipo mbalimbali zinatokana na vyanzo vya ndani na sasa tupo kwenye mchakato wa kuandaa bajeti ya 2019/2020, naomba halmashauri zetu ziangalie uwezekano wa kuongeza posho na mapato ili waweze kujilipa wenyewe kwa sababu ndipo msingi wa malipo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili anazungumza habari ya sheria kuweza kuwatambua; hili ni jambo jema, lakini kwa sheria iliyopo huu ndiyo utaratibu wa kawaida, sasa kama kuna maoni mengine kama alivyopendekeza tupo tayari kuyapokea, tuyafanyie kazi na hatimaye kuyaingiza kwenye sheria ili waweze kulipwa kama watumishi.
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza nampongeza na niwapongeze TAMISEMI kwa kutupatia kiasi kilichotajwa kwa ajili ya shule zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri zetu nyingi hazina uwezo wa mapato, lakini natambua dhamira ya Serikali ya kutoa elimu bure. Nina maswali mawili ya nyongeza:-

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kukarabati shule kongwe ambazo ni za muda mrefu? Kwa mfano, Shule ya Msingi Masagali ya mwaka 1940 na Shule ya Msingi Songwe 1952? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kutembelea hizi ili ajionee hali halisi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA C. WAITARA):
Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Kigua kwa kazi nzuri ambayo anaifanya kutetea wananchi wake na hasa kuboresha miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba tunavyozungumza hapa kwenye mgawo ambao umeishia awamu ya saba ya EP4R amepata mgawo wa shule mbili; Shule ya Kikunde mabweni mawili, matundu sita ya vyoo, vile vile na Shule ya Mafisa ambayo imepata madarasa manne na bweni moja na matundu sita ya vyoo.

Mheshimiwa Spika, vilevile swali lake la kwanza ni kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejitahidi sana, tumekarabati shule 45 kwa zile shilingi bilioni 60, lakini sasa tunaenda awamu ya pili, tunakarabati shule 17 kwa zaidi ya shilingi bilioni 17. Sasa shule aliyoitaja, tutaangalia kwenye orodha yetu, lakini tutaendelea kadiri itakavyowezekana. Ni nia ya Serikali kukarabati shule zote 89 hizi kongwe, zikamilike, lakini tumeanza zile ambazo tulizirithi kutoka kwa Wakoloni, ili tumalize twende na nyingine zote pamoja na hizi za kisasa ambazo wananchi wanachangia pia.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba nimwarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba Mkutano huu ukimalizika tarehe 11 nitakuwa Tanga na Kilindi ni mojawapo. Tanga, Arusha na kuendelea. Kwa hiyo, niko tayari kutembelea shule hizi na kupata maelezo ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Serikali. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa kuwa fedha za mafunzo zimekuwa zikibaki kila mwaka kutokana na wawezeshaji kutoka Vyuo vikuu Vya Tanzania; fedha hizo zimekuwa zikibaki kwa sababu wakati wa kutekeleza, wawezeshaji kutoka Vyuo Vikuu wamekuwa na programu nyingine katika vyuo vyao. Je, Serikali haioni ipo haja ya kutengeneza TOT wa Mkoa ili hata kama mradi utakapokwisha wanafunzi waendelee kupewa mafunzo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya mimba katika Mkoa wa Simiyu bado ni kubwa. Kwa mwaka 2017 wanafunzi 37 wa Shule za Msingi walipata ujauzito; 2018 wanafunzi 38; halikadhalika katika Sekondari kwa mwaka 2017 wanafunzi 159 walipata ujauzito; na mwaka 2018 wanafunzi 153.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa uchungu huo mkubwa wananchi waliamua kuanzisha ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Mwanjoro: Je, Serikali ipo tayari kuunga nguvu za wananchi waliofikisha jengo usawa wa boma? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Leah Komanya kwa kuendelea kutaka watoto wa kike wapate elimu nzuri na juhudi hizi za kuunga mkono Serikali ambazo imeziweka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza anasema kuna fedha zinabaki kwenye programu hii. Ni kweli katika mazingira mbalimbali fedha inaweza kubaki, lakini maelekezo ya Serikali ni kwamba fedha ikibaki, wahusika wanapewa taarifa kwenye Wizara na inapangiwa majukumu mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mawazo Mheshimiwa Mbunge aliyotoa ni mazuri, tuyapokee; kuandaa TOT ili programu itakapoisha wawezeshwe watu wa eneo husika kwani itapunguza gharama, wenyewe kwa wenyewe watafundishana kwa lugha zao za nyumbani, hii kazi itaenda vizuri. Kwa hiyo, tunapokea wazo hili, tunalifanyia kazi. Ni wazo jema sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, anazungumza habari ya mimba na kuunga mkono juhudi za kujenga mabweni. Utakumbuka tangu juzi mpaka jana kumekuwa na mjadala katika Bunge hili Tukufu la kumalizia maboma ya madarasa lakini pia na mabweni na Vituo vya Afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme tu kwamba kazi hii inatekelezwa na Serikali inaunga mkono juhudi za wananchi, tunafanya mpango, tukipata fedha tutaweka nguvu katika maeneo hayo. Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa ambayo imepewa miradi mingi ya kuwezesha watoto wa kike wasome, kujenga madarasa, matundu ya vyoo na mabweni. Jambo hili tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba katika programu ijayo, fedha ikipatikana tutatoka hapa kuunga mkono nguvu za wananchi katika kumalizia mabweni ambayo wananchi wamechangia wenyewe.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mimba za watoto mashuleni ni jambo la aibu kweli kweli; nasi kama wazazi lazima tulichukulie very serious.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama tulivyoanza programu ya kujenga madarasa ya Shule za Kata, tukajenga mabweni, ni kwa nini Serikali isiagize Halmashauri kwa makusudi kabisa kwamba ni lazima katika Halmashauri bajeti itengwe ili mabweni yajengwe, lisiwe ni suala la hiari? Kwa sababu hawa watoto wanapata mimba kutokana na bodaboda, kutokana na njaa, watoto wamechoka kwa sababu ya umbali wa shule; kwa nini Serikali isiamue kabisa kwamba mwaka huu wa fedha kila Halmashauri ihakikishe angalau wamejenga mabweni mawili au matatu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli kwamba jambo la kujenga mabweni na hasa ya watoto wa kike ni jambo ambalo haliepukiki, ni jambo la lazima na naomba pia tulizingatie. Ndiyo maana kwenye miradi mbalimbali ya Serikali, kwa mfano mradi wa EP4R tumeshajenga mabweni 533 katika shule zote za Sekondari katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa sababu hoja ni kwamba tutenge fedha kwenye bajeti hii, Mheshimiwa Mbunge ni Mbunge; na Waheshimiwa Wabunge wote nawaomba sana, wakati huu ndiyo tunaandaa bajeti zetu za Halmashauri. Kila Halmashauri ina maelekezo mahususi ya Serikali, asilimia 40 au 60 kulingana na mapato ya Halmashauri inaenda kwenye shughuli za maendeleo na hasa miundombinu ikiwepo mabweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge kwenye bajeti ambazo zinaandaliwa sasa, hiki kipengele tumetoa maelekezo, Serikali ngazi ya juu ya Taifa tunapanga fedha, Halmashauri zitenge fedha. Wakuu wa Mikoa wameelekezwa, tunapozungumza maboma ni pamoja na madarasa na mabweni haya. Nasi tunapanga, Waheshimiwa Wabunge mtusaidie, tunalisimamia hilo. Kwenye ziara zangu zote, katika maeneo mbalimbali tunazingatia kukagua hosteli ambazo zinajengwa na wananchi, wadau mbalimbali na Serikali Kuu.
MHE. ALFREDINA A. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi mara ya pili kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawana ofisi za kufanyia kazi. Je, ni lini Serikali itawajengea ofisi za kufanyia kazi?

Mheshimiwa Spika, Wenyeviti wa Vitongoji, Vijiji na Mitaa wana wajumbe wanaosaidiana nao katika kazi za utendaji wa kazi za kila siku. Je, ni lini Serikali itawapa posho wale wajumbe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS – TAMISEMI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba ku-declare kwamba mimi pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa mstaafu. Naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge maswali yake mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza anaulizia kuhusu Ofisi za Serikali za Mitaa. Sasa hivi tunaenda kwenye Bunge la Bajeti na mpango wa kujenga ofisi za mitaa, vijiji na vitongoji ni mpango wa halmashauri husika. Kwa hiyo kama kuna upungufu mkubwa, tunatarajia kwamba halmashauri hizo na vijiji watakuwa wameweka kwenye bajeti yao ili waweze kuleta kwenye Bunge lako Tukufu iweze kupitishwa na waweze kujenga ofisi hizo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili anaulizia juu ya posho, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi ni kwamba posho za wenyeviti na wajumbe wao zinapatikana kwenye halmashauri husika kulingana na vipato vyao. Kwa hiyo kama kuna sababu ya kulipa posho tofauti na ilivyo kwa Wenyeviti wa Mitaa hili nalo pia lilifanyiwa kazi kwenye ngazi ya chini ya halmashauri husika kulingana na mapato yao, kama wana uwezo wataendelea kuwalipa.

Hata hivyo, sifa ya msingi ya kugombea kama ilivyo kwenye uchaguzi mwezi wa Kumi wajumbe hawa na Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji wanajua wanapaswa kufanya kazi ya kujitolea. Kwa hiyo tunatarajia kwamba watafanya kazi kama ambavyo waliamua kugombea na kupata nafasi hizo kama kuna uwezo wa posho watalipana, kama haupo wafanye kazi kama ambavyo waliamua kugombea nafasi hizo.
MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Pia naishukuru Serikali kwa kutuletea fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya viwili. Pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Ilani ya Chama cha Mapinduzi inaelekeza kwamba tujenge zahanati kila kijiji na Wilaya ya Igunga na Jimbo la Igunga mahsusi kuna vijiji ambavyo zahanati zimejengwa zikakamilika zaidi ya vijiji 10 kikiwepo Kijiji cha Kagongwa, Mgongolo, Makomelo, Chagana, Imalanguzu, Mwamakona na vijiji vingine. Ni lini Serikali itakwenda kukamilisha yale yaliyobaki pia kuleta watumishi ili zahanati hizo ziweze kuanza kufanya kazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Wilaya ya Igunga pamoja na Jimbo la Igunga na nchi nzima kwa ujumla wananchi walijenga maboma mengi sana ya zahanati ili kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini mpaka sasa hivi maboma hayo yapo tu na tumeomba sana tangu mwaka juzi Serikali itusaidie maboma haya yakamilike ili zahanati zianze kutumika kwa wananchi wetu katika vijiji vyetu. Je, ni lini Serikali itakamilisha maboma hayo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Dkt. Dalaly Peter Kafumu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mheshimiwa Dkt. Kafumu ameshatoa taarifa hii katika Ofisi ya Rais - TAMISEMI na ukilinganisha Igunga na maeneo mengine pia kuna maboma na zahanati nyingi ambazo zimekwishafanyiwa kazi. Tumeshaomba kibali kwa Mheshimiwa Waziri wa Nchi (Utumishi) ili tupate kibali cha kupata watumishi na wataalamu wa tiba katika maeneo haya ili waweze kutoa huduma. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvumilia, tukipata kibali hicho na kadri fedha zitakavyopatikana basi tutaajiri na kuhakikisha kwamba vituo vyote vinafanya kazi kama ambavyo nguvu za wananchi zimetumika katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kweli kwa taarifa tuliyonayo maboma ambayo yamekamilishwa nchini ni mengi kama ambavyo Jimbo la Igunga na Tabora kwa ujumla wamefanya. Hili nalo tunaomba tuahidi kwamba huu ni mwaka wa fedha, tumetenga fedha kwa bajeti ya mwaka 2019/2020 ili tumalizie maboma haya. Tunaomba wananchi waendelee kuisaidia Serikali kujenga maboma, tujitahidi kukamilisha ili huduma iweze kupatikana. Ahsante.
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni sera ya Serikali kuwa na hospitali katika kila wilaya. Wilaya ya Karatu haina Hospitali ya Wilaya na hivi karibuni Halmashauri imetenga eneo la kutosha kwa ajili ya kujenga hospitali hiyo na wananchi kwa kutumia mapato yao ya ndani pamoja na wadau mfano Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wameanza kujenga…

NAIBU SPIKA: Uliza swali lako Mheshimiwa Qulwi.

MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali sasa iko tayari kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli kwamba sasa hivi Serikali ipo kwenye hatua ya kujenga Hospitali za Wilaya mbalimbali nchini na hatua ya kwanza tulianza na hospitali 67 na awamu ya pili inaendelea. Tunawapongeza wananchi wa Karatu kwa kuendelea kuchangia huduma hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashauri tukamilishe kwanza hizi zilizopo baada ya hapo tutachangia na kumalizia Hospitali ya Mheshimiwa wa Karatu pia na maeneo mengine nchini. Hatua ya kwanza majengo yamekamilika tunapeleka vifaa tiba na kuna hatua ya pili ya wataalam mbalimbali. Tukianza kutoa huduma katika vituo hivyo nafikiri tutaenda na eneo letu la Karatu. Ahsante.
MHE. MENDRARD L. KIGOLA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kuna Vituo vya Afya vya Mtwango, Nunga na Iramba tushaezeka na kila kitu tayari. Je, Serikali itamalizia lini yale majengo ili wananchi waanze kuvitumia?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Mufindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mufindi kuna kituo cha afya kimekamilishwa na wananchi lakini vituo vingi vya afya vimejengwa nchini kama nilivyosema katika jibu langu la msingi. Tunawapongeza wananchi kwa kushirikiana na Serikali kuiunga mkono katika hatua hii muhimu ya kuboresha huduma za afya. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutawasiliana tuone wamefikia hatua gani kwa kushirikiana na Halmashauri na kama kuna mpango wao basi tuone namna ya kumaliza kituo hiki ili kuunga mkono nguvu za wananchi ili zisipotee bure.
MHE. ALHAJ ABDALLAH M. BULEMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swali la kwanza, Tarafa za Luoimbo, Suba na Nyancha ni tarafa zinazounganika, watu wanapita sehemu hiyo na Mheshimiwa Rais alitoa ahadi na muda wa ahadi za Rais kweli zitatekelezwa zote, je, imo ndani ya bajeti inayokuja kwamba inaanza kutengenezwa hata kama haitaisha kwa mwaka huu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni lini wananchi wa Rorya wataweza kuwa na matumaini kwamba Serikali yao inawakumbuka katika kilio chao hiki cha mafuriko ya kila mwaka?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdallah Bulembo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kwamba ipo kwenye bajeti ya mwaka huu, naomba anipe muda tupitie bajeti ya mwaka huu tutaangalia kama ipo. Cha muhimu ni kwamba mimi nilienda Rorya, nimefanya ziara ya kikazi, ni miongoni mwa wilaya za mwanzo kabisa nimezitembelea. Nimeenda Luoimbo, Suba na hii ni wilaya moja ilikuwa Tarime na Rorya imegawanywa hivi karibuni na imekuja na changamoto. Naomba wananchi wa Rorya, Mara na Watanzania wote waendelee kuiamini Serikali ya Chama cha Mapinduzi, ahadi hizi zote zitatekelezwa kabla ya uchaguzi wa mwaka wa fedha ujao. Tathmini imeshafanyika, tunahitaji shilingi bilioni 1.15 ya kukamilisha kazi hii. Ahsante.
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kazi kubwa inayofanywa na TARURA inapunguzwa faida au kufifishwa faida yake kutokana na ukosefu wa fedha za kujenga madaraja muhimu. Wananchi wa Korogwe wamekuwa wakipata shida ya muda mrefu ya Madaraja yao ya Mbagai, Makondeko na Mswaha. Serikali haioni kwamba iko haja ya kuweka jicho maalum kwenye bajeti inayokuja kwa ajili ya madaraja kwenye barabara ambazo zinatengenezwa na TARURA?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Korogwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge, ni Mbunge mpya lakini anafanya kazi kubwa sana ya kutetea wananchi wake wa Korogwe. Jambo la pili ni kwamba huu mpango mkakati ni wa kudumu na ndiyo maana imeanzishwa TARURA ili wataalam wetu hawa wakilala, wakiamka wafikirie barabara zetu za vijijini na mijini. Kwa hiyo, naomba tu aamini kwamba kazi hii inaendelea kufanyika vizuri na huu ni mwaka wa bajeti na bajeti ya barabara hizi inabidi ianzie katika vikao vyao vya ndani kuanzia kwenye mtaa, kijiji, halmashauri yao na hatimaye hapa Bungeni. Sisi kama Serikali tupo tayari kushirikiana na wananchi wa Korogwe na Mheshimiwa Mbunge wao ili kuhakikisha kazi hii inafanyika vizuri na kuondoa kero zilizopo pale.
MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Naibu Spika, asante sana. Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Mkuranga na wanaotumia barabara hiyo, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, barabara hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya wananchi wanozunguka eneo hilo; na kwa kuwa kuna haja ya kuiboresha; na kwa kuwa Serikali imesema wanasubiri TARURA wafanye tathmini ndiyo barabara hiyo ijengwe, je, hawaoni kwamba wakati wakifanya tathmini barabara hiyo iweze kutengenezwa angalau kwa kiwango cha kokoto?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa barabara hii inaungana na barabara ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam ambayo iko TANROADS. Je, Serikali haioni sasa kuna haja ya barabara hii kuipandisha hadhi na kuiweka TANROADS ili iweze kupata huduma ambazo zinalingana na kule inapoishia ambapo inahudumiwa na TANROADS?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, jirani yangu Mheshimiwa Zaynabu Vulu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni kwamba barabara hii inaweza ikapata matengenezo wakati tunasubiri mpango wa fedha ujao. Naomba niwaelekeze TARURA wa Wilaya hii ya Mkuranga wafanye utaratibu wa kukarabati maeneo korofi. Bahati nzuri katika mwaka huu wa fedha wametenga fedha shilingi milioni 270 ili zipelekwe katika eneo hili lakini tunaomba wafanye kazi hiyo mapema ili iendelee kupitika wakati wote na wananchi wasiendelee kupata shida katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kupandishwa hadhi kwa barabara hii. Suala la kupandishwa hadhi lina taratibu zake na mwongozo. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na Halmashauri yake wawasiliane na TANROADS, watafanya tathmini kama ikikidhi vigezo basi itakuwa ni vizuri ikapandishwa hadhi ili kupata huduma kubwa kidogo kulingana na mgao wa fedha ambao unatolewa. Ahsante.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi ili nami niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo kubwa la barabara hiyo ambayo inatoka Vianzi kwenda Marogoro mpaka Tundisongani ni daraja lililopo pale Tundisongani. Daraja hilo imekuwa ni shida mvua zinaponyesha wananchi wa Tundisongani na Wilaya ya Mkuranga wanakosa mawasiliano kabisa, hali ambayo imefanya Wabunge wa sehemu zote mbili Mkuranga na Kigamboni wamekaa pamoja lakini mpaka leo hakuna matunda yoyote juu ya barabara hii.

Je, Serikali sasa ina mpango gani wa kuboresha angalau lile daraja ili mvua zitakaponyesha wananchi wa Kigamboni na Mkuranga waweze kuwa na mawasiliano?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, naomba nimjibu Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mbunge wangu wa Mkoa wa Dar es Salaam kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa namna ambavyo ameuliza swali hili kwa uchungu na maeneo haya yote muhimu, kule Mkuranga kuna Naibu Waziri mwenzangu na kule Kigamboni Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya, naomba niwaelekeze TARURA, Mkoa wa Dar es Salaam walifanyie tathmini eneo hili na leo kabla ya saa saba nipate majibu nini kinaweza kufanyika ili kuondoa kero hii ya wananchi katika eneo hili. Ahsante.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba na mimi awaelekeze TARURA ili washughulikie barabara ya kutoka Shigara kwenda Ruangwe. Kijiji cha Ruangwe ni Kisiwa katika Wilaya ya Busega. Naomba maelekezo ya Waziri yaende kwa TARURA vilevile.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba niwaelekeze TARURA katika Wilaya ya Busega, watembelee maeneo yaliyotajwa na Mheshimiwa Mbunge Chegeni na wapate majibu ya kero hiyo ambayo ameitaja hapa Bungeni. Ahsante.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kuniona na kunipa nafasi. Pamoja na kazi nzuri wanayofanya TARURA Mkoa wa Iringa na katika Mji wa Mafinga, hali ya barabara za Mji wa Mafinga ambao ni kitovu cha shughuli za kiuchumi katika Wilaya ya Mufindi siyo ya kuridhisha, ni asilimia 24 tu ya baraba ambazo zinapitika kwa mwaka, ile tunaita good and fair. Je, Serikali ina mpango gani wa kuangalia Mji wa Mafinga kwa macho mawili ili kuhakikisha kwamba barabara za Mji wa Mafinga zinapitika kwa uzuri kwa mwaka mzima ili kusudi ku-speed up ukuaji wa uchumi ambao ndiyo kitovu cha Wilaya nzima ya Mufindi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nimjibu Mheshimiwa Cosato Chimi, Mbunge wa Mafinga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanzo wa kuanzishwa TARURA ilikuwa ni kuondoa kero ambazo Waheshimiwa Wabunge wengi hapa wanazungumzia. Kwa hiyo, naomba niwaelekeze TARURA nchi nzima, wafanye tathmini ya kero kubwa na za muda mrefu katika maeneo yao. Tunatarajia kwenye bajeti ambayo tunakwenda kuijadili, maeneo haya ambayo yanazungumzwa na Waheshimiwa Wabunge, ndiyo maeneo ambayo yatakuwa yamezingatiwa kuondoa kero katika maeneo hayo kwa pamoja na eneo la Mafinga, TARURA kufanya kazi pale na Mkoa wa Iringa, naomba wataalam wetu, Mainjinia nchi nzima wa TARURA, wafanye tathmini na walete kero mahsusi ambazo Wabunge wamezungumza na Viongozi mbalimbali wamewasilisha ili ziondolewe katika maeneo hayo. Ahsante.
MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa maswali ya kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. Awali ya yote kwanza napenda niishukuru sana Serikali kwa fedha ambazo imetupatia sisi kwa ujenzi kama alivyoeleza Mheshimiwa Naibu Waziri. Hata hivyo, hospitali teule ya Wilaya ya Mtinko ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameisema tangu ilipopandishwa hadhi mwaka jana haijapangiwa Madaktari wala Wauguzi wa kufanya kazi na kuongeza huduma katika hospitali hiyo. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kuwasiliana pia na Wizara ya Afya ili kuhakikisha kwamba hospitali hiyo inapata Wauguzi na Madaktari wa kutosha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri anajua tofauti ya kituo cha afya na hospitali ya Wilaya na wananchi wale ambao ni zaidi ya wananchi 80,000 hawana kituo chochote cha afya na wamejenga jengo hilo kwa zaidi ya miaka nane na halmashauri yetu imeshindwa kutenga fedha za kukamilisha jengo hilo. Je, Wizara iko tayari kutenga fedha ya kukamilisha jengo hilo la kituo cha afya cha Makuro na kutenga fedha kwa ajili ya majengo mengine ili kituo cha afya cha Makuro kiweze kuanza kufanya kazi kwa Tarafa ya Mtinko. Ahsante?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge Monko kwa kuendelea kuwasimamia wananchi wa Jimbo lake la Singida Kaskazini. Sasa naomba nimjibu swali lake la kwanza na la pili kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza anazungumzia habari ya kupata Wauguzi na Madaktari. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tumelipokea jambo hili, katika wale Wauguzi na Madaktari ambao tumewaomba kibali maalum Ofisi ya Utumishi wakipatikana, basi tutaangalia pia eneo hili ili wananchi waweze kupata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anazungumza habari ya kutenga fedha ya kukamilisha boma hili ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi. Namkaribisha Mheshimiwa Mbunge ofisini kwetu tuzungumze, tuone kitakachowezekana, lengo na makusudi ni kwamba jambo hili likamilike na nguvu za wananchi ziweze kuungwa mkono, zisipotee bure ahsante.
MHE. HAWA A. GHASIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kata ya Dihimba yenye vijiji zaidi ya 30 haina kituo cha afya hata kimoja na Kata ya Mangopachanne tayari wameshaanza ujenzi wa kituo cha afya. Je, Serikali iko tayari kuwaunga mkono katika kukamilisha kituo cha afya katika Kata ya Mangopachanne?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali hii ya Awamu ya Tano ya Chama cha Mapinduzi ipo tayari sana kuunga mkono wananchi hawa. Tuendelee kuwasiliana, tutatafuta fedha, zikipatikana tupeleke kukamilisha maboma yote na sio kule kwa Mheshimiwa Hawa Ghasia peke yake ila ni nchi nzima kwa Majimbo mbalimbali kukamilisha maboma yaliyojengwa na nguvu za wananchi.
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri lakini nina maswali mawili, kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, changamoto ya hosteli ambayo imejitokeza katika Jimbo la Mufundi Kusini haitofautiani sana na hali iliyopo katika Jimbo la Wilaya ya Kilindi. Ni ukweli usiopingika kwamba suala la hosteli ni kitu muhimu sana kwa sababu linachangia katika ufaulu wa watoto wetu. Je, Serikali iko tayari sasa kuhakikisha kwamba shule zote za vijijini ambazo watoto wanatembea kwa umbali mrefu zinakuwa na hosteli?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kwamba katika Jimbo la Kilindi ipo Shule ya Kwamkalakala ambayo ni miongoni mwa shule kumi za mwisho ambazo zimefanya vibaya kutokana na kutokuwa na hosteli. Je, Serikali ipo tayari kutoa msaada maalum kuhakikisha kwamba shule ile inajengewa hoteli? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza anataka kujua kama Serikali iko tayari kujenga hosteli kwenye shule zote za sekondari. Ni ukweli usiopingika kwamba hakuna mtu ambaye anapinga kutokuwa na hosteli katika shule zetu, zimeonesha tija na hasa kusaidia watoto wa kike waweze kupata muda mwingi wa kujisomea na kuweza kufanya vizuri katika masomo yao ambao pia wamekuwa wakifanya vizuri wale ambao wamebahatika kusoma vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunao mpango kupitia EPforR, tumepeleka fedha katika hosteli zetu na Kilindi wamepata hosteli moja ambayo nilienda kuitembelea. Tutaendelea kufanya hivyo kwa mwaka wa fedha huu ambao tumeleta bajeti leo mezani kwenu, Waheshimiwa Wabunge watuunge mkono ikishapita tutaangalia namna ya kuboresha.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tunawaomba wadau wote na Watanzania popote walipo hili jambo la kujenga hosteli za watoto wa kike katika shule zetu ni jambo shirikishi. Sisi Wabunge tushirikiane na wananchi wengine na Serikali tutasaidia kadri tutakavyokuwa na uwezo wa fedha wa kufanya jambo hilo.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu maswali mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, kabla ya kuuliza swali langu, naomba nichukue nafasi hii kupongeza Halmashauri ya Kusulu TC kwa kuweza kufanya vizuri kwa kutoa pesa hizo kila baada ya miezi mitatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, kwa kuwa wanawake wengi, vijana pamoja na walemavu wameweza kuhamasika kufungua vikundi lakini zipo Halmashauri ambazo zinasuasua na nyingine kutokupeleka pesa hizo kama sheria inavyotaka. Je, Wizara iko tayari sasa kutoa agizo ili Halmashauri hizo ziweze kutoa pesa kwa wakati?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, zipo Halmashauri ambazo bado ni changa mfano Halmashauri ya Kakonko pamoja na Buhigwe, makusanyo yao sio mazuri sana, ni kidogo. Je, Serikali inatoa kauli gani kwa kuzisaidia Halmashauri hizo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Josephine, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kwa kujali wanawake na kuwasemea ili waweze kupata mikopo na kujikwamua kiuchumi. Hii kazi inafanywa na Wabunge wote wa Viti Maalum kama nilivyosema jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli wakati wa bajeti bahati nzuri nimehudhuria kikao cha Kamati ya Utawala wa TAMISEMI, naomba niwapongeze wajumbe wakiongozwa na Mwenyekiti, Mheshimiwa Rweikiza kwa kazi nzuri waliyofanya katika mjadala ule. Kila Mkoa, Halmashauri, Mkurugenzi, Katibu Tawala alihojiwa na kutoa maelezo namna ambavyo amesimamia ukusanyaji wa fedha na kupeleka kwenye vikundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii hoja ya kusuasua kutokupeleka fedha ni jambo la kisheria na maagizo yametoka naomba nirudie, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala kwa maelekezo ya Kamati ya Utawala na TAMISEMI kwa mwaka wa fedha ujao kama kuna mtu atakuwa hajapeleka fedha hizi kikamilifu na kusimamia marejesho hali yake itakuwa mbaya sana. Haya ni maagizo ya Kamati na sisi kama Wizara tumeyachukua.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, maelekezo ni kwamba hakuna Halmashauri changa katika jambo hili, kama umekusanya Sh.100 umetoa makato yale ambayo ni ya msingi na makato mbalimbali ambapo yametolewa kwenye Halmashauri inayobaki 10% yake peleka kwenye vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu. Kwa hiyo, hata kama utakuwa umekusanya Sh.5, ondoa makato yote ya msingi ambayo yameelekezwa na Serikali inayobaki 10% peleka, usipopeleka sheria itachukua mkondo wake.
MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nilitegemea swali hili lingejibiwa na Wizara ya Mifugo na Kilimo lakini limejibiwa na TAMISEMI, kwa vile Serikali ni moja naamini tatizo la Mkoa wa Mara linaenda kutatuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu idadi ya ng’ombe nina mashaka nayo, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi wafugaji wengi wageni toka sehemu mbalimbali wanaingia mkoani kwa ajili ya malisho kwa kufuata mbuga. Malisho ni shida sana katika Mkoa wa Mara, Mkoa umeelemewa na ndiyo sababu kubwa sana Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na wakulima na wafugaji kuna mgogoro mkubwa sana. Kwa nini Serikali isione umuhimu wa kuweka sheria ya kuwasaidia wafugaji hawa?

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama, Bunda na Musoma Vijijini zimesahaulika ndio zenye wafugaji wengi sana na hakuna sehemu za malisho. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa elimu kwa wafugaji hawa ili wafuge ufugaji wa kisasa ili kuweza kujikwamua katika mahitaji yao ya kila siku?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joyce Sokombi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza namuomba Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi kama alivyosema Serikali ni moja, ulipozungumza habari ya Halmashauri na vijiji unazungumza TAMISEMI lakini pia tunafanya kazi pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhakikisha kwamba mambo yanaenda sawasawa. Kwa hiyo, swali lipo sehemu sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la msingi anasema idadi ya ng’ombe ina tatizo, sisi tumejiridhisha kwamba idadi hii ni kamili kwa sababu sensa imefanywa na Serikali na ni data kamili labda kama ana taarifa nyingine tofauti na hizi tutamkaribisha tu-compare notes.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumpongeze sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli baada ya kuona kwamba kuna shida kubwa ya malisho na migogoro mingi ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima ameunda timu ya Mawaziri wanane wanaendelea na vikao vyao maeneo mahsusi yamependekezwa na wadau wameshirikishwa, Tarime, Serengeti, Bunda na maeneo mengine nchi nzima yatatengewa maeneo.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya mpango huo kukamilika na taarifa kupewa Mheshimiwa Rais ataona itakavyofaa ili kuruhusu baadhi ya maeneo yawe kwa ajili ya wafugaji na wakulima na tunaamini baada ya zoezi hilo migorogoro ya wakulima na wafugaji itakuwa imefikia ukomo wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili anazungumzia kuhusu kutoa elimu, nimemsikiliza mara kadhaa hapa Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Mpina na Mheshimiwa Ulega wametoa taarifa mara nyingi na mipango mbalimbali na ni kweli kwamba wafugaji wetu wanashauriwa kufuga kwa tija, afuge mifugo michache kulingana na eneo lake lakini yenye manufaa ya kusomesha na kupata kipato. Hiyo kazi inafanywa na Serikali na inaendelea kuleta tija kubwa sana. Ahsante.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi. Pamoja na majibu ya Serikali, tunajua ongezeko la mapato. Tuna Halmashauri 185 lakini zinatofautiana kati ya Halmashauri na Halmashauri. Kwa hiyo, pamoja na ongezeko la kibajeti, bado Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imeathirika na mabadiliko ya Sheria hii. Sasa je, Serikali iko tayari kuongeza ruzuku toka hii ambayo tumeipata ya shilingi milioni 250 ambapo tumeweza kumalizia maboma ya shule mbalimbali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; tuna changamoto pia upande wa huduma za kiafya. Kata ya Itenka pamoja na Kata ya Ugara ziko mbali sana na upatikanaji wa huduma: Je, Serikali iko tayari kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya katika Kata hizi mbili?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Serikali iko tayari kuendelea kukamilisha maboma ya afya na elimu na ndiyo maana Mwezi wa Pili tumepeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 29.9 katika Majimbo mbalimbali likiwepo na hili la Nsimbo kukamilisha maboma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi nimesema, Serikali itaendelea kupeleka fedha ya ruzuku ya miradi ya maendeleo mbalimbali kadri ambavyo fedha itapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anaulizia kuwa na vituo vya afya. Ni nia njema ya Serikali kuendelea kuimarisha huduma za afya na tumefanya hivyo, vimejengwa vituo 352. Kwenye bajeti hii ambayo tunaendelea na mjadala kwenye Bunge lako Tukufu tunavyo vituo 52 vingine, hospitali 27, ukiongeza zile 67 zilizopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimtie moyo Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kufanya kazi hii ya kutoa huduma ya afya kwa wananchi wake kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na Halmashauri zetu kufanya vizuri, kuna baadhi ya vyanzo hawafanyi vizuri. Mfano, chanzo cha Kodi ya Ardhi, mwanzoni walikuwa wakikusanya wanapata retention ya 30 percent lakini sasa hawapati retention hiyo ambayo ilikuwa inawasaidia kujaza gari mafuta waweze kufuatilia wale ambao hawalipi Kodi ya Ardhi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nifahamu: Je, Serikali iko tayari kuangalia upya chanzo hili ili kisaidie kukusanya kodi hii ya ardhi kwa asilimia 100?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Gekul kwa kazi nzuri anayoifanya kule Babati kuwasemea watu wa Babati, lakini pili, naomba nilipokee suala hili kama sehemu ya changamoto, tuwasiliane na Halmashauri ya Babati Mjini, Wizara ya Ardhi na TAMISEMI tuone changamoto zilizopo tuweze kuziimarisha.
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niipongeze Serikali, nimpongeze Rais wangu Mungu azidi kumjaza hekima na maisha marefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, pamoja kwamba tumepata fedha zote hizo kama nilivyosema nashukuru lakini bado sekondari nyingi katika Jimbo la Lushoto hazina hosteli na hii imepelekea watoto wengi kufeli na watoto wengi wa kike kupata ujauzito. Je, Serikali ina mkakati gani sasa tena wa haraka kuhakikisha kwamba wanajenga hosteli katika sekondari ambazo hazina hosteli?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wananchi wa Jimbo la Lushoto kwa nguvu zao wamejenga majengo ya maabara tena yote matatu lakini mpaka sasa majengo yale hayajamalizika. Je, Serikali haioni kuwa kuna umuhimu sasa wa kumalizia maboma yale ili watoto wetu waweze kusoma elimu kwa vitendo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Shekilindi maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nampongeza Mheshimiwa Mbunge nimefika kwenye Jimbo lake la Lushoto, wananchi wa eneo lile na yeye mwenyewe wamefanya kazi kubwa kuongeza miundombinu ya elimu lakini pia afya na maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anaomba kujua mpango wa Serikali kuongeza hosteli. Katika bajeti ambayo inaendelea kujadiliwa sasa kila mtu akipitia kwenye kitabu cha bajeti cha Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, utaona kuna maeneo mbalimbali fedha zimetengwa kwa kazi hiyo lakini iko miradi mingine ya elimu itakayoimarisha hosteli mbalimbali. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge avumilie mwaka huu wa fedha tumetenga fedha na kadri zitakavyopatikana tutaweza kumaliza hiyo shida kwa watoto wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ni kuhusu maboma ya maabara, tumeanza kupeleka vifaa na kukamilisha maboma katika shule nyingi kadri itakavyowezekana. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane huenda shule au maeneo yake anayotaja tutapeleka vifaa vya maabara lakini pia tutamalizia maboma ya maabara hizo. Lengo ni ili tupate wataalamu wa sayansi ili tutakapoanza issue ya viwanda tuwe na wataalam wa kutosha.
MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa misingi ya elimu bora, sawa, shirikishi kwa wote, elimu ya msingi inaanzia darasa la ngapi mpaka la ngapi na elimu ya sekondari inaanzia darasa la ngapi mpaka la ngapi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa James Mbatia, Mbunge wa Jimbo la Vunjo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa utaratibu tunaotumia tuna darasa la awali, darasa la kwanza mpaka la saba, form one mpaka form four na kidato cha tano na cha sita baadaye elimu ya juu. Ahsante.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba hivi karibuni Serikali imefanya ukarabati mkubwa wa shule za sekondari kongwe ikiwemo Shule ya sekondari ya Mpwapwa lakini mimi nataka nimuulize Mheshimiwa Naibu Waziri mnafanya ukarabati wa shule tu lakini nyumba za walimu zimechakaa kweli kweli. Je, mna mpango gani wa kukarabati shule na nyumba ya walimu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa George Malima Lubeleje (Senator), kama lifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba tunakarabati shule tu ukweli ni kwamba tumekarabati shule nyingi zaidi kuliko nyumba za walimu. Hata kwenye kitabu cha bajeti tunachojadili sasa ambapo Mungu akipenda tutahitimisha Jumatatu tarehe 15 akipitia kwenye majimbo mbalimbali ataona fedha zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za walimu. Uwezo wa Serikali siyo mkubwa sana, tunaomba Mheshimiwa Mbunge na wadau mbalimbali tushirikiane katika jambo hili kupunguza shida ya walimu katika nchi hii. Ahsante.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kuwa tumeona shule nyingi kongwe zilizotoa viongozi mbalimbali zimekuwa zikikarabatiwa. Kwa Mkoa wangu wa Arusha, kuna Shule ya Arusha Sekondari ambapo miundombinu yake ni mibovu na chakavu. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutenga pesa kwa ajili ya kukarabati shule hii kongwe ya Arusha Sekondari?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Catherine Magige, msemaji mzuri sana wa Mkoa wa Arusha na Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni nia ya Serikali kukarabati shule zote kwa wakati mmoja kama ingewezekana lakini kwa sababu ya ufinyu wa bajeti jambo hilo halijawezekana, tutakarabati kulingana na uwezo lakini pia kuna vigezo mbalimbali. Kwa hiyo, naomba nichukue hoja ya Mheshimiwa Mbunge, tufanye tathmini, tumeshamaliza awamu ya kwanza tupo kwenye mpango wa awamu ya pili, huenda kwenye awamu ya tatu Shule ya Arusha Sekondari ikaingizwa kwenye mpango huu wa Serikali wa kukarabati shule hizi.
MHE. DKT. RAPHAEL M. CHEGENI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri sambamba na matatizo ya Lushoto, Wilaya ya Busega haikupata mgao wa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma. Je Mheshimiwa Naibu Waziri, unaweza ukatoa maelekezo katika mgao huu na Wilaya ya Busega tupate mgao huo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge wa Busega swali lake la nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza natambua kazi nzuri ambayo anaifanya katika Jimbo lake la Busega kuwasemea wananchi wake lakini sina hakika kwa sababu fedha zile zilisambazwa kwenye wilaya zote kwa maana ya Halmashauri inawezekana kwenye Jimbo hilo kuna bahati mbaya. Naomba tuwasiliane baada ya kipindi cha maswali na majibu tuone njia bora ya kumaliza shida hiyo. Ni nia ya Serikali kila Jimbo lipate mgao wa kupunguza shida ya maboma na kuchangia nguvu za wananchi ili wasilalamike.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, mpango unaotekelezwa sasa wa kilomita 0.4 ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na kwa kuwa ahadi hii ya Mheshimiwa Rais ni kilomita 5 katika Mji wa Mbulu, nini majibu ya Serikali kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 kwa kuwa Rais atakuwa anataka ahadi hiyo iwe imetekelezwa na mimi nimeshatimiza wajibu wangu wa kuikumbusha Serikali mara kadhaa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, ni kweli Mji wa Mbulu ni mji mpya ulioanzishwa lakini ni Halmashauri au Wilaya kongwe katika ya Wilaya kongwe Tanzania. Kwa hivi sasa Mji wa Mbulu una kilomita 1.8 katika mitaa yake kwa kiwango cha lami. Kwa kuwa hali ya barabara na madaraja katika kata kumi ukiacha kata zingine nane za vijijini ni mbaya; na kwa kuwa TARURA wanapewa fedha kidogo sana hivyo kushindwa kutekeleza mahitaji yaliyoibuka, nini kauli ya Serikali kuwezesha miundombinu ya barabara katika Miji wa Mbulu pamoja na ahadi hiyo ya Rais?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge Zakharia, Mbunge wa Mbulu Mji maswali mawili ya nyongeza kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anauliza kuhusiana na ahadi ya Mheshimiwa Rais, naomba nimhakikishie kwamba hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, kipenzi cha Watanzania, namhakikishia kabla ya 2020 ahadi hii itakuwa imekamilishwa ili Mheshimiwa Rais atakapoenda kuomba kura kwa awamu nyingine kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi, asipate vikwazo kwa wananchi wa Mji wa Mbulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, anapenda kujua tuna mpango gani, nitoe maelekezo kwa TARURA Mkoa na Wilaya yake ya Mbulu kama hali ya mji huu ni mbaya kiasi hicho wafanye mchakato walete maandishi hapa tujue namna ya kufanya ili tuweze kuboresha wakati tukisubiri kutafuta fedha nyingi zaidi za kuboresha Mji wa Mbulu. Ahsante.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Katika majibu yake Mheshimiwa Naibu Waziri ameeleza kwamba mipango ya kuendeleza barabara za miji ni pamoja na Mpango wa DMDP. Katika Manispaa ya Ubungo mpango wa DMDP, unatekelezwa kwa upande wa Jimbo la Ubungo peke yake lakini upande wa Jimbo la Kibamba kwenye Kata sita za Kwembe, Msigani, Mbezi, Saranga, Goba mpango huu hautekelezwi kabisa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupanua utekelezaji wa mpango wa DMDP ili kuzigusa kata sita za Jimbo la Kibamba kwenye masuala ya miundombinu ya barabara?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mnyika, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Mkoa wa Dar es Salaam ikiwepo maeneo ambayo ametaja ya Ukonga na maeneo mengine, tunatekeleza awamu ya kwanza ya mpango ya DMDP. Naomba niwahakikishie kwamba itakapokuja awamu ya pili Wabunge watashirikishwa waweze kuainisha maeneo yao ili tupanue wigo zaidi wa kuendeleza Mji wetu wa Dar es Salaam.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Mji wa Mafinga ulikuwa Mamlaka ya Mji Mdogo kwa miaka tisa na Julai 2015 ikawa Halmashauri kamili ya mji. Je, Serikali inaweza kuwahakikishia wana-Mafinga kwamba kwa kuwa Halmashauri ya Mji kamili na wao wameingia katika Mpango Kabambe wa Maboresho ya Miji? Kwa sababu sasa hivi Mafinga ni Halmashauri ya Mji kamili. Tunataka tu kuhakikishiwa na sisi tunaingia katika awamu ya pili? Kwa sababu ndiyo ukombozi wa barabara zetu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Cosato Chumi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge alikuwa na Mheshimiwa Rais amekubaliwa mambo yake yote manne leo amelala usingizi mnono kabisa. Katika suala hili, kama nilivyojibu swali la Mheshimiwa Zakharia, Mbunge wa Mbulu Mji, tutakapoanza kufanya mchakato miji mipya yote na huo mji wako utaingizwa katika awamu hiyo.
MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kwa kuwa matatizo ya wananchi wa Rungwe kuhusu barabara yanafanana kabisa na matatizo ya wananchi wa Chunya hasa hasa kwa barabara inayotoka Chunya – Kiwanja - Ifumbo - Mjele, ambayo sasa hivi inaunganisha Mikoa miwili ya Songwe na Mbeya; na kwa kuwa Mamlaka ya Wakala wa Barabara (TARURA) toka imeanzishwa Chunya hakuna barabara hata moja ambayo wameikarabati. Je, Mheshimiwa Waziri anatoa maagizo kwa TARURA ili waikarabati barabara hiyo iweze kupitika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Mheshimiwa Naibu Waziri kijana mchakapa kazi yupo tayari kuongozana name kwenda Chunya ili akaangalie kazi ambazo wanafanya TARURA katika Halmshauri ya Chunya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza kwa barabara ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja na mipango iliyopo na kwa sababu michakato hii inaanzia kwenye ngazi ya Halmashauri, inakuja kwenye Mkoa mpaka ngazi ya TAMISEMI, namwomba Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane baadaye tupate taarifa sahihi ya eneo hili na tuweke mipango mahususi ambayo inaweza kutatua shida hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anauliza kama nipo tayari. Mimi nipo tayari sana wakati wowote. Tupande ratiba twende tuone eneo hili, turudi kufanya mipango ya kukamilisha na kuondoa kero za wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. MUSSA A. ZUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naipongeza Serikali kwa mradi wake wa kuleta mpango wa DNDP kwenye Mkoa wa Dar es Salaam. Jimbo la Ilala tumepata Kilometa mbili tofauti na maeneo mengine wamepata zaidi ya Kilometa 40.

Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuboresha barabara za kata zote 10 za Jimbo la Ilala ili ziweze kuonekana za kupitika kwa sababu ni katikati ya mji na zinasaidia kupunguza msongamano katikati ya mji kuelekea pembezoni mwa mji?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M.WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kuna miradi inaendeshwa katika Mji wa Dar es Salaam, UNDP na sasa kilichobaki, baada ya kutengeneza barabara nzuri zaidi, ni vingumu zaidi barabara za pembezoni zikawa nzuri. Sasa kwa sababu Mheshimiwa Mbunge tupo wote Ilala na tunampongeza Meneja wa TARURA kwamba ni msikivu sana, tutawasiliana naye tuone mipango iliyopo na sisi tuishi kama Wabunge wa Dar es Salaam ili kuwezesha mipango ya kukamilisha barabara zetu na hasa wakati wa mafuriko watu wa Dar es Salaam wasiweze kupata shida zaidi.
MHE. ZAINABU AMIR MNDOLWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Barabara itaokayo Korogwe kupitia Kwa Mndolwa - Mkaalie - Tamota hadi kuunganishwa na Kiwanda cha Chai Mponde ni takribani kilometa 40 lakini haijajengwa kwa kiwango cha lami. Hii ni barabara muhimu sana katika nchi kwa sababu mazao mengi kutoka Jimbo la Bumbuli ambayo yanasafirishwa kwenda Dar es Salaam hupita pale, lakini wakati wa mvua barabara hii haipitiki kabisa na kuna maporomoko ya mawe:-

Je, ni lini sasa Serikari itajenga hii kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza kuendelea kuwasema wananchi wa Korogwe, lakini namwomba sana kwa sababu tupo kwenye wakati wa bajeti hii aunge mkono bajeti ya TAMISEMI Jumatatu tutakapofika kwa majaliwa ya Mwenyenzi Mungu tupate fedha hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nilijibu swali hapa nikasema, tuliunda timu ya wataalam, inapitia sasa namna ya ku-identify hizi barabara ili tuangalie ule Mfuko wa TANROADS na TARURA. Nimesikia michango ya Waheshimiwa Wabunge kwamba TARURA inafanya kazi nzuri sana. Shida hapa ni fedha. Tukipata chanzo realible cha fedha na formula ambayo ipo sawaswa na wadau mbalimbali na bajeti ikaungwa mkono. Nia ya Serikali ni kukamilisha barabara zote ikiwezekana kwa kiwango cha lami ikiwepo hiyo ya Korogwe. Ahsante.
MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza, nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini ningeomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Chuo hiki cha Mwalimu Nyerere kilijengwa na Wazalendo wa nchi hii, tena kabla ya Uhuru na Mwalimu Nyerere alikipa jina ya Kivukoni lenye maana ya eneo lililopo Chuo kilipo. Je, sasa Serikali haioni umuhimu wa kukipandisha hadhi Chuo hiki kuwa Chuo Kikuu, ili tumuenzi Baba wa Taifa, ukizingatia kwamba Barani Afrika kuna nchi nyingi ambazo wamezipa majina ya Waasisi kama Mandela South Africa, Kenyata Kenya lakini Nkurumah Ghana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Chuo hiki, Mheshimiwa Waziri kuna bweni ambalo limejengwa toka mwaka 2013 kwa ajili ya wanafunzi hawa wa Shahada ya Uzamivu, lakini mpaka sasa halijakamilika. Je, ni kwa nini halijakamilika na ni lini litakamilika na nini kauli ya Serikali katika kukamilisha bweni hilo. Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y. WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kiza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza linaenda kwenye majibu ya swali langu la msingi, tumesema mpango wa Serikali kwa sasa si kupandisha hadhi Vyuo. Vilevile tukubaliane kwamba ili kupandisha Chuo kuwa na level ya Chuo Kikuu, kuna vitu vingi inabidi kuzingatia, kwanza inabidi uunde Kikosi kazi cha Wataalam waende wapitie Mitaala, aina ya Walimu kama wanatosha, eneo lenyewe Hatimiliki ya eneo lao. Kwa hiyo kuna vitu vingi vya kuangalia, lakini kwa sababu tunazungumza kuna vitu vingi vya kufanya, tumesema tuboreshe hivi vilivyopo, itakapofika wakati, Serikali ikaona haja ya kufanya hivyo, tutafanya hivyo kwa kuzingatia taratibu na sheria za nchi ambazo zimewekwa kwa ajili ya kazi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, anasema kuna bweni ambalo halijakamilika, naomba hili tulichukue tulifanyie kazi, lakini kwa kweli kama kuna bweni lipo pale na kuna upungufu wa mabweni, tutafanyia kazi ili liweze kukamilika.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya msingi, kwenye swali la Kivukoni, mimi ni moja ya product ya Kivukoni. Kwa kuwa historia ya Chuo hiki kilikuwa ni Chuo cha ku-train Viongozi na kutokana na changamoto tunazoziona katika utekelezaji wa majukumu yao hasa Viongozi kwenye Local Government, wilayani, Wakurugenzi, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kukirudishia chuo hiki kazi yake ya msingi ya kufundisha viongozi skills za namna ya kutekeleza majukumu yao kwenye maeneo yao na nakubaliana na uamuzi wa Serikali wa kutokukipandisha hadhi badala yake tukibadilishie sasa majukumu kitoke kwenye ku-train social sciences kiende
kwenye ku-train viongozi wetu kwa sababu kwa kweli changamoto ya utekelezaji wa majukumu yao kwenye maeneo yao imekuwa ni kubwa sana?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NASERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA - K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba nimjibu Mheshimiwa Nape Nnauye swali lake la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaamini kwamba Chuo hiki kimeanzishwa kwa majukumu aliyoyataja Mheshimiwa Mbunge na yataendelea kufanyika hivyo, sasa kama kuna upungufu umeonekana, hilo ni jambo la kulichukua na kwenda kulifanyia kazi, lakini tunaamini kwamba kazi ya msingi iliyoanzishwa kwayo inaendelea kufanyika. Ahsante.
MHE. SUSAN P. MASSELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Serikali, ya Waziri, ambayo yanavunja moyo kabisa, kwa sababu hawajatoa commitment ni ni lini watamaliza huo ukarabati na ukizingatia Vyuo hivyo alivyovitaja viko kwenye hali mbaya sana na ukizingatia pia Jiji la Mwanza, ni Jiji ambalo linakua kila siku. Vyuo vingine viko uchochoroni kabisa ambapo ni mazingira mabaya kwa wanafunzi na Wakufunzi katika kufanya kazi. Sasa katika majibu haya nina maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, mwaka jana tuliona Serikali kupitia Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) ikivichukulia hatua Vyuo Vikuu binafsi ambavyo havikuwa na vigezo vya Vyuo Vikuu na kuviacha Vyuo Vikuu vya Umma ambavyo vilevile vilikuwa havina vigezo vya kuwa Vyuo Vikuu kama alivyojibu kwenye swali la msingi. Je, Waziri haoni kwamba zoezi hili lilikuwa linagandamiza Vyuo Vikuu vya binafsi ambavyo vinatoa nafasi kubwa kwa wanafunzi ambao wamekosa nafasi kwenye Vyuo vya Umma na kupata nafasi?

MWENYEKITI: Sema tu straight.

MHE. SUSAN P. MASSELE: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa Serikali ina ndoto ya Tanzania ya Viwanda ni lini sasa itajenga, Polytechnic College katika Mkoa wa Mwanza, ambapo itatoa ujuzi kwa ajili ya mahitaji ya viwanda ukiachilia mbali Chuo cha...

MWENYEKITI: Ahsante, inatosha. Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwa niaba.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Susanne Maselle, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kweli kwamba zoezi hili lililofanyika lilikuwa la ugandamizi na ndiyo maana vyuo ambavyo vilionekana vina matatizo havijalalamika, vimetii masharti, vimeboresha vyuo vyao na wale ambao wamekamilisha wamekabidhiwa kuendelea kufanya kazi. Kwa hiyo, hii siyo kweli lakini na vyuo vya umma pia vinazingatia utaratibu na ubora wa elimu kwa kadri ya miongozo iliyotolewa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, tumesema nia ya Serikali si kuanzisha vyuo kila mkoa bali ni kuhakikisha vyuo vilivyopo vinaendelea kuboreshwa kwa kuongeza miundombinu na wataalam waliobebea katika nyanja hizo. Vikiimarishwa vinatosha kutoa wataalam kwenye viwanda na kubaki na kutumia utaalam wao nje ya nchi yetu.
MHE. KIZA H. MAYEYE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali ya nyongeza. Nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri lakini naomba kuuliza maswali mawili, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, wapo walimu ambao mpaka wanastaafu walikuwa wako katika daraja jipya lakini mlipokuja ku-calculate mafao yao mka- calculate kwa kikokotoo cha mshahara wa zamani. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa wastaafu hawa mapunjo yao ya mafao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, pesa ya likizo na matibabu kwa walimu hawa ni takwa la kisheria kwa mujibu wa sheria za kazi lakini walimu hawa wamekuwa wakienda likizo au kwenye matibabu pasipo kupewa pesa zao kwa wakati. Je, ni lini sasa Serikali mtaona umuhimu wa kuwalipa walimu hawa pesa kwa wakati mara wanapokwenda likizo au kutibiwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Kiza maswali yake ya nyongeza mawili, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Mbunge ametaka kujua wale waliolipwa mafao yao kwa kikokotoo cha zamani, naomba nitoe maelekezo kwa waajiri wao na Maafisa Utumishi kwenye Halmashauri zetu, twende case by case walifanyie kazi halafu sisi tutashauriana namna bora ya kulishughulikia ili kuondoa changamoto na malalamiko kwa watumishi hawa.

Swali la pili, ni nia ya Serikali kuendelea kulipa watumishi wake na kuwapandisha madaraja kwa wakati. Sasa hivi tumeshafanya calculation na tumejiridhisha kwamba tuna walimu zaidi 86,000 ambao wanaidai Serikali zaidi ya shilingi bilioni 43, tuna walimu wa sekondari zaidi ya 18,000 ambao wanadai karibu zaidi ya shilingi bilioni 18. Jumla ya madai ya walimu wote ya madaraja, likizo na malimbikizo mbalimbali kwa maana ya areas zao ni jumla ya zaidi ya shilingi bilioni moja. Kwa hiyo, Serikali imefanya utafiti na uhakiki sasa tunafanya mchakato wa kutafuta fedha ili walimu wetu waweze kulipwa madai yao na kupunguza malalamiko ambayo kwa kweli ni mengi sana. Ahsante.
MHE. BONNAH M. KALUWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ambayo ameyajibu Mheshimiwa Naibu Waziri; kwa kuwa Serikali imeanzisha miradi ya kimkakati katika mikoa mingine na ukizingatia katika Jimbo la Segerea kuna wananchi wengi sana ambao wanakaribia 1,300,000; je, Serikali ina mpango gani kujenga masoko ambayo yatakuwa yanawasaidia wananchi ili wasiweze kwenda mbali kama hivyo alivyosema Kisutu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, nimemsikia Mheshimiwa Waziri anaongelea kuhusiana na Soko la Kinyerezi. Kutokana na kwamba nilifanya ziara mwezi uliopita, hilo soko mpaka sasa hivi kwanza linavuja, halafu pia halijamaliziwa vizuri. Kwa hiyo, haliwezi kuzinduliwa mwaka 2019 kama anavyosema.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hayo, kuna Kata nyingi ambazo hazina masoko kama Kata ya Kisukulu, Kata ya Kipawa na Kata nyingine: Je, Serikali ina mpango gani kuhusiana na hizo Kata nyingine kuhakikisha kwamba zinapata masoko?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuelewa, nakushukuru. Swali la kwanza ningeomba niseme tu kwamba utaratibu unaotumika kuibua miradi ya kimkakati ni Halmashauri husika, inakaa na wataalam wake, wanaandika andiko, wanaliwasilisha Ofisi ya TAMISEMI pamoja na Wizara ya Fedha; wataalam wa Wizara ya Fedha wanaenda kufanya tathimini ya andiko lenyewe, gharama zake na mrejesho kwa maana ya faida itakayopatikana na baada ya hapo wataruhusiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ya kuwa na masoko ya Kinyerezi na maeneo mengine, itategemea Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nilitaka tu niseme kwamba inawezekana ni kweli Mheshimiwa Mbunge anasema, sasa nimwelekeze Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala aende akafanye utaratibu wa kukarabati na kurekebisha soko hilo ili liendane na ambavyo nimejibu katika swali langu la msingi, kwamba Kinyerezi ilizinduliwa mwaka 2017 na Mbio za Mwenge wa Uhuru lakini Mei mwaka huu linatakiwa lianze kufanya kazi. Mkurugenzi aweke pesa pale ili liweze kufanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja anayoizungumza Mheshimiwa Mbunge hapa, soko la Kisutu ni kweli lipo kwenye mkakati, limesharuhusiwa na Serikali na fedha imeshatolewa. Naomba nimhakikishie, kwa kadri anavyojua kwamba lazima lisimamiwe; na Mheshimiwa Mbunge nimridhishe kwamba yeye katika Manispaa ya Ilala ana ujenzi wa machinjio ya kisasa kabisa ya Vingunguti ambayo ipo pia kwenye mpango mkakati katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mji wa Karatu ni Mji wa Kitalii na hauna soko la uhakika. Hivi sasa wananchi wa Karatu kwa kutumia mapato yao ya ndani wameanza kujenga soko lenye hadhi ya Mji huo: Je, Serikali iko tayari sasa kuunga mkono jitihada za wananchi hao ili soko hilo likamilike?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Katika Mkoa wa Manyara tayari tuna mradi wa kimkakati katika Wilaya ya Hanang’. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge kama nilivyosema katika jibu langu la msingi, fedha zipo, Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano. Cha muhimu, Halmashauri husika ikae na kutoa andiko, likija hapa kwenye tathmini hili jambo litafanyika. Sisi tunakusudia kuweka masoko, stendi na majengo mbalimbali ya kimkakati ili baada ya kuwekeza katika maeneo hayo, Halmashauri zetu zipate mapato ya kutosha ili kuweze kuendeleza na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wetu.
MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kata yangu ya Mahenge Mjini ambapo ndiyo Mji wenyewe ulipo, kuna shida kubwa ya soko. Wananchi walijitolea wakajenga soko, Serikali ikatia hela zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018 Mwenge ulikuja ukafungua hilo soko, lakini mpaka leo hii soko hilo halijaanza kutumika. Kwa hiyo, Mwenge umedanganywa, Mbunge kadangaywa, wananchi wamedanganywa. Je, lini Serikali itasimamia ufunguaji wa soko hilo ili wananchi wapate kulitumia?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuhsukuru. Hili jambo tumelipokea, tutalifanyia kazi tuone tatizo liko sehemu gani ili liweze kufanya kazi.
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwa kuwa imekuwa ni ahadi ya muda mrefu ya Serikali kujenga Soko la Mto wa Mbu Wilayani Monduli Mkoani Arusha, lakini mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea na wananchi wa Mto wa Mbu wamekuwa wakipata taabu: Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Soko la Mto wa Mbu Mkoani Arusha?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni kweli hili suala hata Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mheshimiwa Julius Kalanga ameniuliza jana. Kama nilivyosema, namwomba Mheshimiwa Mbunge wakae na Halmashauri yao, fedha zipo kama ulivyosema. Ni kuandika andiko na sisi Ofisi ya Rais, TAMISEMI tupo tayari kusaidia utaalaam na namna ya kuboresha pamoja na Hazina ili andiko likamilike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua kuna wapiga kura wengi sana pale Mto wa Mbu, tungependa wapate soko zuri, wapate kipato, pia wachangie kodi katika maendeleo ya Watanzania wenzetu. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane hili jambo liweze kufanyiwa kazi.
MHE. ALBERT N. OBAMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nishukuru majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ni ukweli kwamba tuna upungufu mkubwa nchi nzima wa Walimu wa sayansi na hesabu na kwenye jibu lake la msingi ameonesha kwamba Buhigwe ina upungufu wa asilimia 46. Sasa na hiki kimekuwa ni kikwazo ambacho kinatufanya kwamba ufaulu wetu uwe mdogo na kule ni pembezoni, kwamba watoto hawawezi kupata namna ya kuweza ku--access namna ya kujisomea kwa kufundishana. Je, ni lini itaweka umuhimu wa kuongeza Walimu wa sayansi katika Wilaya ya Buhigwe?

Mheshimiwa Spika, la pili nipongeze wananchi wa Wilaya ya Buhigwe kwa juhudi na kujitolea kujenga maabara na kujenga madarasa. Je, ni lini Serikali italeta sasa vifaa vya maabara kwa sababu tunaendelea kukamilisha sasa maabara katika shule nyingine, ni lini italeta vifaa hivyo kwa wanafunzi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Obama kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna upungufu wa Walimu wa masomo ya sayansi na hisabati na kama nilivyoongea kwenye jibu langu la msingi ni kwamba sasa hivi tunafanya mchakato wa kumalizia kuajiri Walimu zaidi ya 4,500 na tumeyaweka mahsusi kabisa kwamba maeneo haya, Wilaya yako ya Kongwa, kule Buhigwe na maeneo mengine, tutazingatia maeneo ambayo yana upungufu mkubwa zaidi.

Tunaomba tupate taarifa kwa sababu kuna mahali unakuta kweli shule nzima haina hata Mwalimu wa hesabu, au baiolojia, kemia au fizikia, tutaweka vipaumbele maeneo hayo ambayo yana changamoto kubwa. Hii ni awamu ya kwanza ya ajira, awamu ya pili ikipatikana pia tutakuwa tunapeleka Walimu kadri uwezo utakavyokuwa unapatikana.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anauliza habari ya kumalizia maboma ya maabara. Nimesema kwenye majibu yangu ya msingi ni kwamba tayari hapa tulipo tunasambaza vifaa, tenda imeshatangazwa, kazi inafanyika. Inawezekana wakati tunaomba taarifa kwenye halmashauri mbalimbali labda watu wetu kule hawakuleta taarifa hiyo. Kwa hiyo Mheshimiwa Obama kama ana wasiwasi kwa hili la kupeleka vifaa vya maabara kwenye eneo lake, basi naomba tuwasiliane ili tuweze kuzingatia maombi yake. Ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Halmashauri hazina uwezo wa kuwalipa Madiwani na mpaka sasa Madiwani wengi wamekopa posho zao; na kwa kuwa mapato madogo na hali hii inapelekea Madiwani kutolipwa stahiki zao: Je, Serikali ina mpango gani kubadilisha namna hii ili Serikali ilipe toka Hazina kama walivyo Watumishi wengine sasa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Wenyeviti wa Vitongoji na Wenyeviti wa Vijiji nao wanafanya kazi sawasawa na Madiwani na Watendaji, hao Ma-VEOs na WEOs wanalipwa mishahara: Je ni lini sasa Serikali itawaona Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji ili kuwalipa posho au mshahara?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti nakushukuru. Swali lake la kwanza anapendekeza kwamba Waheshimiwa Madiwani walipwe posho kutokea Hazina na kwa maelezo yake anasema kwamba kuna Halmashauri ambazo hazina uwezo. Ukweli ni kwamba Halmashauri ambayo haina uwezo wa kujiendesha inapaswa kufutwa kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, lazima vyanzo viwe vimeainishwa na vinasimamiwa na hii hatujapata malalamiko rasmi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoelezea ni kwamba Halmashauri kwa mapato yake ya ndani wanajipangia namna ya kuweza kulipa Waheshimiwa Madiwani. Kama Serikali itapata uwezo mkubwa zaidi ya huu uliopo sasa, hili jambo litafanyiwa kazi. Kwa sasa Halmashauri zote zinapaswa kulipa na tunajua kuna Halmashauri ambazo Waheshimiwa Madiwani wanazidai fedha mpaka sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaelekeza kila Mkurugenzi ahakikishe kwamba Madiwani wanalipwa stahiki zao kwa sababu wanafanya kazi kubwa. Swali lake la pili, anapendekeza pia kwamba kuwe na mpango wa kulipa Wenyeviti wa Mitaa. Ni kweli, nami ni Mwenyekiti wa Mtaa Mstaafu kule Kivule Dar es Salaam Ukonga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna maelekezo ya Serikali kwamba kila makusanyo yote ya Halmashauri asilimia 20 inabidi irudi katika Mitaa yetu na Vijiji, inawezekana jambo hili halitekelezwi vizuri. Naomba niwaelekeze Wakurugenzi, Wenyeviti wa Vijiji kwa sasa, ile asilimia ambayo inapaswa kurejeshwa baada ya kodi kukusanywa katika eneo lao, ipelekwe na waweze kulipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuendelea kuwalipa asilimia nyingine zaidi hii au Serikali Kuu ichukue jukumu hili, kwa kweli itategemea uwezo wa Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na jibu la Mheshimiwa Naibu Waziri, asilimia 20 ambayo inatengwa ili irudi kwa ajili ya Wenyeviti wa Mitaa, kuna Halmashauri nyingine hiyo asilimia 20 ni ndogo sana. Ni kwa nini Serikali isitoe commitment ili hawa Wenyeviti wa Mitaa na Wenyeviti wa Vitongoji wapate mshahara kwa sababu wao ndio wanafanya kazi kubwa sana katika shughuli zote za maendeleo huko tunakotoka?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nia njema ya Serikali tungeweza kuwalipa Wenyeviti wa Mitaa mishahara. Hapa tunazungumzia hali ya uwezo wa Serikali kufanya kazi. Wenyeviti wa Mitaa ni wengi sana, pamoja na kazi kubwa wanayofanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachoelekeza, pamoja na kwamba hayo mapato ni madogo, kwa kinachopatikana, kuna Wenyeviti wa Mitaa hawalipwi kabisa fedha hizi na tuna malalamiko mengi wameleta. Tumeelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya wahakikishe hawa watu wanalipwa stahiki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la kuweza kuwalipa kwa sasa, tumelichukua, tutalifanyia kazi. Uwezo wa Serikali ukiruhusu, hawa viongozi wenzetu watalipwa stahiki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ukweli ni kwamba pamoja na maelekezo yanayoelekezwa kule chini, viongozi hawa wa Mitaa na Vijiji, Vitongoji hawalipwi posho zao; na kwa kuwa Serikali kwa namba ya viongozi hawa kuwa kubwa inashindwa kuongeza posho zao:-

Serikali haioni umefika wakati sasa kufikiria uwezekano wa kuwalipa kiwango fulani cha pesa viongozi hawa pale wanapomaliza muda wao wa Uongozi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, utaona Waheshimiwa Wabunge wanazungumzia posho za Madiwani na posho za Wenyeviti wa Mitaa; naomba nitumie nafasi hii kusema tu kwamba wakati tunamalizia hoja yetu ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, suala la posho za Madiwani zile ambazo zilikuwa zimezungumzwa, Mheshimiwa Waziri ameshatoa maelekezo kwa Madiwani wote wa Halmashauri watapata Waraka wa maelekezo kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuondoa sintofahamu ya posho za Madiwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali alilouliza Mheshimiwa Mkundi, tulipokee; ni kweli kwamba Wenyeviti wa Mitaa baada ya kustaafu kuna kiwango cha fedha wanapaswa kulipwa. Sasa maoni ya Mbunge ni kwamba tuangalie namna ya kuongeza kiwango hiki (lump sum amount) kama watasema ni shilingi 500,000/= au shilingi 1,000,000/= kwa mkupuo itaweza kuwasaidia. Jambo hili tunalipokea, tunalifanyika kazi, kadri uwezo wa Serikali utakavyoruhusu, tutalitekeleza kwa sababu ni jambo jema kwa ajili ya viongozi wenzetu hawa.
MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza kwa jambo muhimu kama hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanaofanya bidii na kushirikiana na Wabunge ni Madiwani na Wenyeviti katika kuhamasisha maendeleo katika maeneo yao; sasa kama Halmashauri inaweza kuwa na uwezo wa kulipa posho zaidi: Je, Serikali inaweza ikaruhusu Halmashauri ile yenye uwezo kuongeza posho kwa hawa ambao ndio wanaoweza kuongeza mapato hayo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge sawa na Wabunge wengine wote ambao wameendelea kuwasemea Waheshimiwa Wenyeviti wa Mitaa na Waheshimiwa Madiwani, nao ni viongozi wenzetu na hakuna namna ya kuweza kuwapuuza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeeleza hapa kwamba wakati wa Bajeti kulikuwa na mjadala; na kweli kuna Waraka ambao umepelekwa katika Halmashauri zetu ambao unaelekeza fixed amount kulipwa kwenye posho za Madiwani ukiacha ile posho ya mwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema Mheshimiwa Waziri aliahidi mbele ya Bunge lako Tukufu na naomba niseme, bado ametoa ametoa maelekezo, ndani ya muda siyo mrefu sana, Waraka kutoka Ofisi ya Rais, TAMISEMI kupitia Katibu Mkuu utaenda kwenye Halmashauri zote na suala hili la kulipana Madiwani kulingana na uwezo wa Halmashauri litatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi, kama uhitaji wa Walimu wa Sayansi kwa Mkoa wa Dodoma ni 916. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba uhitaji wa Walimu wa Sayansi ambao ndio Madaktari na Wahandisi na Wauguzi unakamilika kwa kuwaajiri Walimu wanaotesheleza mahitaji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na uhitaji mkubwa wa Walimu wa Sayansi kwa shule za sekondari, kuna uhitaji mkubwa wa Walimu wa shule za msingi. Kwa mfano, Wilaya ya Kongwa kuna uhitaji wa Walimu 1,088; Chemba, Walimu 786; Kondoa, Walimu 618; Dodoma Jiji, Walimu 656, hapo ni Wilaya nne tu nimezitolea mfano. Je, ni lini sasa Serikali itaamua sasa kuwaajiri Walimu wa shule ya msingi kwa sababu elimu ya msingi ni kujenga msingi wa mwanafunzi, Je, Serikali iko tayari kuwaaajiri Walimu wa kutosha pamoja na halmashauri zetu kujenga miundombinu, Jiji wamepanga bilioni 8.3 kwa ajili ya kujenga miundombinu kwa ajili ya shule za msingi na sekondari. Je, serikali iko tayari sasa kuwaajiri na Walimu wa shule za msingi ili kukidhi mahitaji?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Felister Bura, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli swali lake la kwanza anauliza upungufu mkubwa Walimu na naomba nikiri kwamba ni kweli kwamba tuna uhitaji mkubwa sana wa Walimu wa Hesabu na Sayansi, takribani nchi nzima na Wilaya zote na Wahesimiwa Wabunge wote hawa ukiona wanapiga makofi wanazungumza hilo. Hii ni ajira ya awamu ya kwanza, bado tathimini ile ya Walimu hewa na wengine, hii tumeomba kibali kupata Walimu 8,500 kama nilivyosema, lakini tunatarajia kupa kibali kingine mwezi wa Tano au wa Sita ambao watakuwa wengi zaidi ya hawa. Kwa kweli makusudi yetu ni kulenga kuajiri Walimu wengi wa Hesabu na Sayansi, lakini kama nilivyosema pale ambapo wana mahitaji makubwa sana, kwa mfano, unakuta kuna shule haina Mwalimu wa Hesabu, haina Mwalimu wa fizikia na kemia tutazingatia maeneo yenye upungufu mkubwa zaidi wakati tunapeleka Walimu hawa katika shule zetu za sekondari.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ameuliza ajira ya Walimu wa shule za msingi. Katika hao niliowataja Walimu 4,500 nimesema 1,300 ni masomo ya sayansi na hisabati, maana yake Walimu 3,200 wanaobaki wote hawa ni Walimu wa shule ya msingi pamoja na Walimu wa watoto wenye mahitaji maalum. Kwa hiyo, tutazingatia kupeleka pia na Walimu wa shule za msingi katika maeneo mbalimbali ambayo yana upungufu mkubwa. Tumefanya mawasiliano na Waheshimiwa Wabunge, wanafahamu, tutalizingatia, lakini tukipata kibali mwezi wa Tano kama nilivyosema au wa Sita tutazingatia maeneo gani ya kwenda.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kuna upungufu mkubwa, lakini tuna maelekezo mengine ambayo kama kutakuwa kwa mfano kwenye vibali vya muda, tukianza kutangaza nafasi unakuta pia inakuwa ni pungufu. Tumetoa vibali vya muda, Walimu ambao wamesoma masomo ya sayansi na hesabu lakini sio Walimu wanapata mafunzo ya muda mfupi ili waweze kuziba gape hili la Walimu wa Sayansi na Hisabati. Ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nasema tu kwamba Wilaya ya Kilombero na hasa kutokana na miundombinu yake ina upungufu wa Walimu 1,018 na sio wa sayansi tu, wa kada zote. Kwa mfano, Jimbo la Mrimba unakuta shule ina Walimu watatu lakini ina wanafunzi 800 au 1,000. Je ni lini sasa Serikali katika hawa Walimu wanaosema wanawaajiri sasa hivi watatupelekea Walimu kwenye Wilaya ya Kilombero, ikiwemo na wanawake kwa sababu kuna shule haina Mwalimu mwanamke hata mmoja. Sasa wale watoto wanaokuwa wakamuone nani? Kwa hiyo, ni lini sasa mtapeleka walimu hususan Jimbo la Mrimba ili watoto wale waendelee kukua wakiwa na chakula cha akili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Suzan Kiwanga, Mbunge wa Mrimba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tumeshatoa maelekezo zile shule ambazo zina Walimu wa kike peke yake au wa kiume peke yake ni lazima wachanganywe. Hii kwa kweli ni kazi ambayo inafanywa ndani ya Wilaya na Mkurugenzi mwenyewe kwani ana uwezo kupata taarifa na Mheshimiwa Mbunge anawasiliana naye halafu wanawabadilisha ndani, kama ni Mwalimu kutoka nje ya mkoa mwingine hilo ndio unakuja ngazi ya TAMISEMI. Kwa hiyo, nadhani hilo lifanyike na ningepeda kueleza kwa kweli itakuwa sio sawasawa kama kuna shule ina Walimu wa kiume tu na shule ile ni mchanganyiko. Kwa hiyo, naomba nitoe maelekezo kwa Wakurugenzi wote na Maafisa Elimu wa Mikoa na Makatibu Tawala, hili jambo walifanyie kazi sio zaidi wiki mbili kwa sababu inawezekana na ndani ya mazingira yao.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza, ajira hizi ambazo tumetangaza tutazingatia maeneo ambayo yana upungufu mkubwa na tuliomba Mheshimiwa Mbunge anajua kuna shule ambayo, shule za msingi inawezekana kwamba unaweza ukawa na Walimu wachache kwa sababu wanafundisha masomo mengi kwa wakati mmoja, lakini sekondari lazima kila mtu ana somo lake au masomo mawili ambayo anafundisha, haya maeneo ambayo yana changamoto kubwa na tutahakikisha kwamba tunapeleka Walimu katika maeneo haya. Ndiyo maana tumezuia pia na uhamisho, labda niliseme hili, kwa maana kwamba kuna maeneo ya halmashauri kwa sababu yana mazingira magumu, watu wamekuwa na sababu nyingi sana za kuwahamisha na kuomba uhamisho.

Mheshimiwa Spika, maelekezo yametoka kwa Serikali kwamba tusimamishe uhamisho kwanza wa Walimu nchi nzima ili tutengeneze mifumo ambayo, anapoomba uhamisho kwa sababu yoyote ile hata kama ni mgonjwa, kumfuata mume wake au mke wake au vyovyote itakavyokuwa tujue je, anapotoka kule Kaliua, Mrimba, Kilosa anapooenda kule balance ikoje kule ya Walimu, kwa maana ya kuangalia ikama hiyo. Kwa hiyo, tumelichukua hatua hiyo baada ya kugundua kwamba kuna maeneo wanakimbia mazingira magumu ya kazi, wanaenda sehemu ambayo kuna unafuu, anapaswa kufundisha mahali popote kulingana na mkataba wake wa kazi. Ahsante.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa taarifa tu ni kwamba na mimi ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, kwa hiyo, hiki nilichokuwa nakiuliza nahitaji Wenyeviti wengine wapate ufafanuzi wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, Serikali inatenga fedha nyingi kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Majibu ya Naibu Waziri amenukuu Katiba, Ibara ya 146, wanasema madhumuni ya kuanzisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa ni kuharakisha maendeleo ambapo kuchaguliwa huku na sisi Wabunge, Madiwani pamoja na Rais tunachaguliwa hivyohivyo lakini sisi tunalipwa posho na mshahara. Kama Serikali inaweza kutenga fedha kwa ajili ya uchaguzi, kwa nini haitengi fedha kwa ajili ya kuwalipa Wenyeviti hawa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa na Vijiji kuna Watendaji wa Vijiji na wa Serikali za Mitaa ambao wanalipwa na Serikali, wanaofanya kazi saa tisa lakini Wenyeviti wanaochaguliwa na wananchi wanafanya kazi saa 24 hawalipwi. Serikali haioni sasa kwa kuwa mpaka sasa haijawalipa Wenyeviti wala hakuna sheria yoyote iliyoletwa kwa ajili ya kuwalipa, kwa nini isiufute Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wabaki hawa wanaolipwa na Serikali?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nimjibu Mheshimiwa Aida Khenani, Mbunge wa Viti Maalum, maswali yake ya nyongeza mawili, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua kuhusu posho za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa. Mimi pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kabla ya kuwa Mbunge tangu 2014 mpaka 2017. Kwa hiyo, naomba niseme tu kwamba haya ni maswali ya uchonganishi na naomba niwaambie Wenyeviti wa Mitaa kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi inawapenda sana na ndiyo maana inataka kuwaeleza ukweli na naomba wanisikilize.

Mheshimiwa Spika, kabla ya kwenda kugombea kunakuwa na maelezo na kanuni zimetaja sifa za nani anapaswa kuwa Mwenyekiti wa Mtaa. Sifa mojawapo muhimu sana ni kuwa na kipato cha kumfanya aweze ku- sustain maisha yake binafsi. Kwa hiyo, mtu yeyote anapoenda kuchukua fomu na bahati nzuri mwaka huu mwezi Novemba tunafanya uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kila anayetaka kuwa Mwenyekiti wa Mtaa au Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au Kijiji, Kitongoji, anapaswa asome sifa, ajiridhishe ndiyo achukue fomu, hilo la kwanza.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, Wenyeviti wa Mitaa kwa mujibu wa maelezo ya Serikali watalipwa kwa viwango mbalimbali kulingana na uwezo wa Halmshauri yao. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge anapouliza swali ningetaka aseme kwenye Halmashauri yao wamejipangaje kuwalipa posho Wenyeviti wa Halmashauri kwa sababu pesa ziko kule na miradi iko kule wanaisimamia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kwa sasa uwezekano wa Serikali kulipa posho za Wenyeviti wa Mitaa kwa maelekezo tuliyotoa makusanyo yakipatikana kinachotakiwa kirudishwe kwenye Halmashauri asilimia 20 walipwe. Ni muhimu kuzingatia Mheshimiwa Diwani anapochukua fomu anafahamu mimi sina mshahara nitalipwa posho, anajiridhisha Sh.350,000 kwa mwezi inatosha.

Mheshimiwa Spika, tunaomba watenganishe kati ya kazi na posho. Wafanye kazi kwa weledi lakini wasiache kuwahudumia wananchi kwa sababu hawajalipwa posho, kwa sababu hayo ni makubaliano na wameridhika kabla ya kugombea. Serikali ikipata uwezo wa kutosha itapeleka posho kwa Wenyeviti wa Mitaa, kwa sasa uwezo haujapatikana, tunawaomba waendelee kufanya kazi kwa weledi, wanafanya kazi kubwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ipo pamoja na Wenyeviti wa Mitaa kinyume na hapo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua kwamba kwa sababu Wenyeviti wa Mitaa hawalipwi posho na Watendaji wa Mitaa na Vijiji wanalipwa kwa hiyo tufute wabakie wanaolipwa. Hawa Watendaji wa Mitaa, Kata na Vijiji ni watumishi wa Serikali, wanatajwa kwenye orodha ya watumishi wa umma.

Kwa hiyo, huyu ni mtumishi na ndiyo maana anapotaka kupata nafasi hii tunatangaza nafasi kwa uwezo wa Halmashauri na Serikali Kuu, analeta vyeti, anakuwa- vetted, anakaguliwa, anapewa mkataba wa kazi yake na huyu anapaswa kufanya kazi kwa niaba ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwenye ngazi ya Kijiji na Mtaa huyu Mtendaji ndiyo Mkurugenzi wa Halmashauri na kama kuna jambo lolote hawa wanawajibika. Kwa hiyo, naomba tutofautishe huyu ni mtumishi wa Serikali na huyu ni mtumishi wa wananchi kwa kazi ya kujitolea na wote ni watu muhimu sana katika eneo hili. Huyu Mtendaji na watu wengine watapata kile ambacho kinastahiki kwa kadiri ambavyo tumekubaliana. Ahsante.
MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nina swali moja la nyongeza. Pamoja na kwamba Serikali imejibu vizuri, nawapongeza sana; na uamuzi unaokuja wa kufuta madeni ni mzuri sana, nawapongeza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati hizi fedha zinakopesha huko nyuma, kuna baadhi ya Halmashauri zilipeleka fedha kidogo; pamoja na kwamba hazikupeleka zote, lakini fedha hizi wale waliokopeshwa au vikundi vilikopeshwa vimekuwa vikisuasua sana katika kulipa hizi fedha. Mfano Halmashuri ya Wilaya ya Njombe kabla, tulikuwa Halmshauri moja upande wa Wanging’ombe na Makambako. Baada ya kugawanya hizi Halmashuri, zile fedha zilizokopeshwa kwenye vikundi vya Halmashauri nyingine, kwa mfano, Wanging’ombe na Makambako, imekuwa ni vigumu sana kurejesha na wamekuwa wakisuasua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kauli ya Serikali kwa vile vikundi ambavyo vilikopeshwa na sasa wanasuasua kurejesha au hawarejeshi kabisa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nashukuru kwa pongezi ambazo ametoa na kwa hatua ambazo Serikali inachukua kufuta madeni na malimbikizo haya. Naomba nitoe maelekezo kwamba hizi fedha hazikuwa sadaka, wala zawadi. Hii ilikuwa ni mikopo; na dawa ya kukopa ni kulipa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwaelekeze Wakurugenzi wote nchini walipo na wale Maafisa Ustawi wa Jamii na Mikoa, Wilaya na Kata, vile vikundi ambavyo vilipewa fedha hii ya Serikali kwa ajili ya kujiendeleza na kuboresha maisha yao, ni muhimu warejeshe fedha hizi na waweke time frame baada ya muda fulani fedha irejeshwe. Kwa sababu makusudi ya Serikali ilikuwa, kikundi kimoja kikikopeshwa kikaboresha maisha yake, wakirejesha na wengine zaidi wanaendelea kukopeshwa ili waweze kuyaboresha maisha yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. AMINA N. MAKILAGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2018 katika bajeti tulipisha sheria kwamba kila Halmashauri ni lazima kutenga 10% ya wanawake na vijana watu wenye ulemavu. Hivi sana ninavyozungumza zipo Halmashauri hapa nchini, ikiwemo Wilaya Butiama hawatoi mikopo kama ambavyo sheria tulivyoipitisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujua, nini kauli ya Serikali katika kuhakikisha Wakurugenzi wanatekeleza maagizio ya Bunge kutenga 10% ya wanawake, vijana na walemavu ili kusaidia katika vikundi na kuleta tija kwa wanawake, vijana na walemavu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni kweli kwamba sheria imeshatungwa na kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi ni kwamba huko nyuma hatukuwa na sheria, sasa sheria ipo in place inafanya kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwapongeze Wajumbe wa Kamati ya Wizara ya TAMISEMI, walikumbusha Wajumbe, walitoa maelekezo kwenye mikoa na Halmashuri zote nchini na wakatoa masharti kwamba kipindi kijacho, kama kuna Halmashauri ambayo haijapeleka fedha hizo kwa mujibu wa sheria, hao watapata taabu sana katika Kamati ile wakati wanaleta bajeti yao mwaka ujao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo ni kwamba kama umekusanya shilingi 100/=, baada ya kuondoa yale makato ya kisheria kabla ya kupeleka zile fedha kwenye makundi muhimu yaliyotajwa, ni lazima 10% ya fedha hiyo ipekwe kwenye vikundi na igawanywe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kama Halmashauri ya Butiama haijapeleka fedha, najua walipokuja kwenye Kamati ya Bunge walikuwa wameweka asilimia ndogo karibu 15% au 25% ambayo wakikuwa wamepeleka, lakini tumepata manung’uniko ya hapa na pale; Mheshimiwa Mbunge najua ni mwenyeji mkaazi wa Mkoa wa Mara, naomba nitoe maelekezo tupate taarifa mahsusi kwa Halmashauri ya Butiama kama kweli hawajapata fedha hizi. Mkurugenzi, ikifika kesho saa 7.00 tupate taarifa kama amepeleka fedha kiasi gani; vikundi gani vimepelekewa? Ili tuweze kumaliza jambo hili. Ahsante.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Fedha nyingi hizi zimepotea kwa sababu ya maamuzi ya kisiasa ya kutoa hii mikopo, lakini mwarobaini tumeupata, ni hii sheria tuliyotunga hapa. Ila sasa ni lini Serikali italeta kanuni (najua zimeshaanza kuandaliwa) ambazo zitasimamia ugawaji wa hizi pesa ili kukomesha kabisa ugawaji holela wa hizi fedha na kuwabana hawa Wakurugenzi waweze kuzitoa vizuri?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Bahati nzuri Mheshimiwa Selasini ni Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya TAMISEMI na Utawala na mojawapo maelekezo ambayo yalitoka kwa Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Selemani Jafo ilikuwa kanuni hizi zitolewe mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe taarifa kwamba kanuni hizi zimeshatolewa, ilitangazwa kwenye gazeti la Serikali, zinasubiri utekelezaji. Kwa hiyo, kimsingi jambo hili limeisha; na mambo yote ambayo Kamati ilielekeza na maoni ya Waheshimiwa Wabunge yamezingatiwa; namna ya kugawanywa, namna ya kusimamiwa na hatua za kinidhamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hata kama kuna vikundi vitakopeshwa fedha, wasipozingatia sheria na kanuni watawajibishwa. Hili ni jambo la kikundi husika ili fedha hii iweze kwenda vizuri kama ambavyo Bunge na Serikali ilikusudia kuboresha maisha ya Watanzania hawa.
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Shule hii ni kongwe halafu iko kwenye eneo ambalo ni hatarishi, kuna bwawa ambalo lina wanyama wakali ambao wanaingia katika eneo la shule kwa sababu shule hii haina uzio kabisa; na shule hii ina upungufu mkubwa sana wa madarasa na vilevile ina upungufu wa mabweni; na kwa kuwa Serikali imepanga fedha na imesema hapa kuwa imeji-commit na pesa tayari zipo; sasa naomba commitment, ni lini Serikali itakarabati shule hii kwa sababu wanafunzi wa shule hii wanapata taabu sana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, shule hii ina wasichana takribani watoto 888, ni watoto wa kike ambao wanapata shida sana; usiku wakiugua hakuna gari katika shule hii: kwa kuwa hii shule ni kongwe, ni lini Serikali itatuletea gari katika shule hii ya Sekondari ya Mpanda Girls?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba zimetengwa fedha shilingi bilioni 16 kwa ajili ya kukarabati shule nyingine mwaka huu wa fedha na commitment ya Serikali ni kwamba ukarabati huu unaanza mara tu tutakapoanza kutekeleza bajeti ya mwaka 2019/ 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ametoa hoja ya gari na ni kweli kwamba kwa shule hizi kongwe na kutokana na mazingira ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge, naomba tupokee ombi hili tutalifanyia kazi kwa kadri uwezo wa Serikali utapopatikana.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, nikirejea hapo katika Shule ya Wasichana ya Mpanda kimechimbwa kisima kirefu, tatizo lililobaki ni ufungaji wa pump na ukizingatia ni shule ambayo ina watoto wa kike peke yake.

Ni lini Serikali itakamilisha suala la ufungaji wa pump kwenye shule hii?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Tunapokarabati hizi shule kwanza tunaangalia mfumo wa majengo, mabweni, bwalo, madarsa, Ofisi, majengo ya utawala, mfumo pia wa maji na mfumo wa umeme. Kwa hiyo, kama alivyozungumza kwamba kuna kisima ambacho kimechimbwa katika eneo hilo, wakati wa ukarabati litaangaliwa. Tutatenga fedha kwa ajili ya kupata maji katika eneo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huwezi kuwa na wanafunzi wengi katika shule hii kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba ni zaidi ya wanafunzi 800, watoto wa kike, halafu kusiwe na huduma ya maji. Ahsante.
MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi nami niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa matatizo ya ukarabati katika shule za sekondari yanafanana na shule za msingi, Mkoa wa Tabora katika Manispaa ya Tabora, Shule ya Kanyenye iliezuliwa karibuni madarasa manne tangu mwaka 2018 Machi, mpaka leo haijafanyiwa ukarabati, wanafunzi wanapata taabu. Nini kauli ya Serikali kwa leo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba nipokee maombi na maelekezo ya Mheshimiwa Mbunge tutayafanyia kazi. Mpaka Bunge lijalo tutakuwa tumepata majibu ya tatizo hili katika eneo la Tabora. Ahsante.
MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Shule ya wasichana ya Tabora (Tabora Girls) ni shule kongwe sana hapa nchini ambayo pia ina vipaji maalumu. Shule hii kwa muda mrefu imetelekezwa kuhusu uzio. Ile shule haina uzio kabisa kwa miaka mingi na tayari juhudi za viongozi mbalimbali nikiwemo mimi mwenyewe tumeshaanza mkakati wa kujenga uzio huo.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutusaidia katika kukamilisha uzio huo wa Shule ya Wasichana Tabora?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, nakushukuru. Namwomba Mheshimiwa Mbunge tuonane tuone. Kama wananchi wameanza kujitolea na wadau mbalimbali akiwepo Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri ya wananchi wake anaowawakilisha hapa Bungeni, basi tuonane tuone ni changamoto gani zilizopo na sehemu gani ya kuweza kusaidia kumalizia uzio huo.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami naulize swali dogo la nyongeza. Katika jitihada za kuboresha miundombinu ya elimu Mkoani Lindi, kwa misimu miwili, mitatu iliyopita tulikubaliana kukata fedha kutokana na malipo ya korosho ya shilingi 30/= kwa kila kilo ili kukarabati miundombinu na kujenga miundombinu mipya. Sasa iko miundombninu ambayo ilianza kujengwa kwa sababu ya hali ambayo sote tunaijua, miundombinu hiyo sasa imesimama kwa sababu hiyo fedha haikupatikana.

Je, Serikali iko tayari kusaidia kumalizia miundombinu hii katika Mkoa wa Lindi hasa upande wa elimu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa
Mwenyekiti, ni nia ya Serikali kuendelea kukamilisha miundombinu ya elimu na hasa ile ambayo imeanzishwa na wananchi na ndiyo maana tumepeleka fedha za kiutawala mwezi Januari, tumepeleka fedha za maboma karibu shilingi bilioni 29.9. Kwenye bajeti hii ambayo imepitishwa, zaidi ya shilingi bilioni 90 inaenda kusimamia miundombinu ya elimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nipokee maombi ya Mheshimiwa Mbunge, tutazingatia maoni yake. Ahsante.
MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza ningependa kuwapa pole sana wananchi wa Machame na hasa familia ya Marehemu Dkt. Reginald Mengi kwa msiba uliowapata. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho haye mahali pema peponi.

Mheshimiwa Spika, sasa niulize maswali mawili ya nyongeza, kwanza, uhaba wa walimu 384 tumepewa walimu 21! Katika shule zetu, shule 50 zina walimu wawili wawili na shule zingine 40 zina walimu watatu watatu, sasa ujue hizo zingine ndiyo… na shule za msingi zina madarasa nane, darasa la awali na madarasa saba, kwa hiyo, hali iliyoko pale ni ngumu sana.

Mheshimiwa Spika, na kwa sababu uhaba huu umetokana na walimu kustaafu, kuhama na kufariki. Suala la fedha halipo hapa, kwa sababu nafasi zipo, na mishahara ipo, ni kwa nini sasa Serikali haichukui hatua ikaajiri bila kutumia visingizio ambavyo havina msingi.

Mheshimiwa Spika, pili, ni lini Serikali itabadilisha urasimu huu, kama mwalimu yupo na yuko kwenye ikama, na amestaafu. Kwa nini Serikali hairuhusu halmashauri ikaajiri kutoka kwenye soko mara moja ili kutoathiri upatikanaji wa elimu katika shule. Inaacha mpaka shule zinakuwa na mwalimu mmoja?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Mwikwabe Mwita Waitara, maswali hayo muhimu sana, Mwanga upungufu wa walimu 300, Kongwa upungufu walimu 1000. Majibu tafadhali.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli, tuna upungufu wa walimu wa shule za msingi 66,000 nchi nzima, na upungufu wa walimu wa sekondari 14,000, kwa hiyo, ni kweli kwamba kuna upungufu, ni jambo ambalo liko wazi.

Mheshimiwa Spika, lakini kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, hizi ajira mpya ni ajira za kuziba nafasi. Sasa hivi inayofuata ni ajira zile za kawaida za kila mwaka za kuongeza na kupunguza upungufu uliopo. Kwa hiyo, naomba niwahakikishie kwamba Serikali imeshaliona hili, tulifanya uhakiki, pamoja na watumishi hewa, waliofariki, waliofukuzwa kazi na wengine wamestafu na wengine wameacha kwa sababu mbalimbali. Kwa hiyo, hili ilikuwa ni kuziba nafasi hizi, sasa inakuja ya ajira za kila mwaka za kuweza kuziba kwa utaratibu wa kawaida na hili linafanyiwa kazi na Serikali inajua kwa kweli kuwa kuna upungufu mkubwa nchini wa walimu.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ni kwamba, ni kuziba nafasi kwa maana ya kutoa kibali kwa halmashauri. Hizi ni ajira, cha muhimu hapa siyo kuruhusu utaratibu usioelekeweka utumike kuajiri walimu, kumekuwa na mambo mengi sana katika halmashauri zetu ambayo yanafanyika katika ajira hizi, kwa hiyo, tunajiridhisha kwanza. Lakini cha muhimu ni kwamba tumekubaliana kama Serikali kuchukua hatua mahususi kupunguza upungufu wa walimu shule za msingi na sekondari.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kama ilivyo kwa Mheshimiwa Maghembe Mwanga, Wilaya ya Kilombero yenye majimbo mawili ilikuwa na upungufu wa walimu 1,118 na hivi juzi tu tumeletewa walimu 34, wanne wa sayansi sekondari na 30 wa msingi na kufanya nakisi upungufu huo ubaki 1,084.

Je, Serikali ni lini sasa itapeleka walimu ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, ili watoto wale wapate chakula cha akili, ukizingatia na miundombinu yetu si rafiki?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli, kama nilivyosema, tumeajiri walimu 4,549, tuna shule za msingi 16,000 za Serikali na tuna shule zaidi ya 4000 za sekondari. Katika hali ya kawaida upungufu huo naupokea kama Serikali ni kweli, kuna upungufu mkubwa na tusingeweza kupeleka kila mahali. Lakini tuliangalia kwa mfano kuna shule ambazo pale kulikuwa na wakumu ambao wanapelekwa shule za msingi, wameenda mahitaji maalumu, wameenda na masomo ya sayansi na hisabati.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, angalau tukaangalia shule ambazo zina upungufu mkubwa zaidi tukapeleka pale, kwingine tumepeleka walimu mpaka watano, wengine wanne.

Mheshimiwa Spika, lakini, Mheshimiwa Susan Kiwanga wiki iliyopita aliuliza swali hap ana walimu hao. Tumeshatoa maelekezo, kwanza kuna walimu wapo kwenye halmashauri, makao makuu ya wilaya au ya mji, lakini unakuita pembezoni kule unakuta walimu ni wachache, lakini walimu wapo. Tumeshapeleka fedha katika halmashauri zote nchini za kuweza ku-balance ikama.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunatarajia kwamba kazi hii itafanyika kwa kusimamiwa na Makatibu Tawala Mikoa na Wakurugenzi, ndani ya wiki mbili mpaka tatu, tupate taarifa rasmi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ilikuwa kuhamisha walimu kupeleka pembezoni ilikuwa ni ngumu kwa sababu fedha hazipo, sasa fedha wameshapelekewa Halmashauri zote, zinatakiwa kazi ifanyike, halafu ajira inayofuata tutazingatia maeneo yote ambayo yana upungufu mkubwa. Shule za msingi, hisabati na masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Spika, ahsante, likiwemo na eneo la Kongwa.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali na tumeona kweli Serikali sasa imeonesha nia ya kupunguza kadhia hii ya watumishi wa kada ya afya. Nina maswali madogo mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, dhamira ya Serikali, lakini na wananchi katika Jimbo la Manyoni Magharibi, Halmashauri ya Itigi ni kujikwamua, wameanza kutumia nguvu zao katika kujenga zahanati na vituo vya afya katika vijiji vyao, lakini nguvu zao zinaonekana kuisha. Je, Serikali iko tayari sasa kuwasaidia wananchi wa vijiji ambao wameanza kujenga zahanati kwa nguvu zao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika swali ambalo niliuliza mwaka jana kipindi kama hiki majibu ya Serikali ilikuwa yameonesha kwamba na Hansard iko hapa ninayo kwamba, Serikali ilikuwa imetenga milioni 600 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Itigi, lakini hadi tunapozungumza leo hii bajeti nyingine ya Wizara ya TAMISEMI ilishasomwa, hospitali hii bado hatujaletewa pesa. Je, Serikali iko tayari sasa basi kupeleka hizi pesa ambazo iliahidi na wananchi walisikia kwamba zitapelekwa katika Halmashauri ya Itigi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na nimpe pole sana kwamba, alipata ajali mbaya hivi karibuni, lakini pamoja na kwamba, alikuwa na machungu ya maumivu aliweza kuwakumbuka wananchi wake wa Manyoni na akaanza kuandika swali hili ambalo nalijibu hapa leo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa naomba nijibu maswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, sisi Serikali tunahimiza wananchi na wenyewe Waheshimiwa Wabunge wamekuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi kushiriki kujenga vituo vya afya na zahanati na kuna maboma mengi.

Naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, jitihada na nia ya Serikali iko palepale, kadri ambavyo uwezo utapatikana tutapeleka fedha za maboma, lakini pia kupeleka wataalam na vifaa tiba ili kuweza kuboresha huduma za wananchi wetu katika maeneo yao na hii itakuwa ni kwa nchi nzima.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, anauliza habari za hospitali yake ya Itigi; naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutaendelea kuliangalia hili kulingana na uwezo wa Serikali. Kama mwaka huu bajeti hii haikupelekwa katika eneo lake la Hospitali ya Itigi kama alivyotaja Mheshimiwa Mbunge, basi tunalichukua kulifanyia kazi ili wakati ujao aweze kupata fedha na kuweza kupata huduma na kuboresha hospitali yake ya wilaya.
MHE. DKT. SHUKURU J. KAWAMBWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Nitangulize kutoa shukrani za wananchi wa Bagamoyo kwa juhudi kubwa ya Serikali katika kuboresha huduma ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Bagamoyo kwa muda mrefu sana wamehangaika na ujenzi wa zahanati katika Vijiji viwili, kimoja cha Buma Kata ya Kilomo, kingine Kitame katika Kata ya Makurunge. Hivi sasa zahanati ya Makurunge imekamilika na Buma wakati wowote tutamaliza, tunamalizia ujenzi wa choo. Swali langu kwa Mheshimiwa Waziri, je, ni lini tutaweza kupatiwa watumishi na vifaa tiba katika zahanati hizi kwa kuzingatia kwamba, kwa muda mrefu wananchi hawa hawajapata huduma?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Shukuru Kawambwa, Mbunge wa Bagamoyo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshaomba kibali maalum kwenye Ofisi, Wizara ya Utumishi cha kuajiri Madaktari, Waganga na Wauguzi. Naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba, maeneo yote ambayo zahanati zimekamilika na vituo vya afya ambavyo vinajengwa nchi nzima na hospitali za wilaya na pale palipo na upungufu mkubwa tutazingatia maeneo hayo ikiwepo na eneo lake la Bagamoyo na zahanati mbili ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, Wilaya ya Kilolo inapitiwa na barabara kuu (High Way) kutoka Tanzania kwenda Zambia, lakini pia ni barabara ambayo ukitoka Mikumi ni mpakani na Ruaha Mbuyuni mpaka ukifika Ilula ni kilometa zaidi ya 200, lakini hapo hakuna kituo cha afya. Mara nyingi accidents zimekuwa zikitokea, wananchi wa Mbeya, Malawi, Zambia, wamekuwa wakipata matatizo na wamepoteza maisha kwa sababu, inabidi waende wakatibiwe Iringa Mjini ambako ni mbali; na kwa kuwa, wananchi sasa wa Ruaha Mbuyuni wameonesha nia ya kujenga Kituo cha Afya, je, Serikali itakuwa tayari kuwasaidia kwa haraka ili kuokoa maisha ya watu ambao wamekuwa wakiyapoteza pale?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mbunge Venance Mwamoto, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwa swali mojawapo la nyongeza hapa, hivi leo asubuhi kwamba, ni nia ya Serikali kuendelea kuboresha huduma za afya na maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja yatazingatiwa katika kuboresha. Kama wananchi wamechukua juhudi za kuanza ujenzi tunawapongeza sana, sisi kama Serikali tuko pamoja nao na mimi hivi karibuni nitaenda kutembelea Jimbo la Mheshimiwa Mwamoto. Hivyo nitaomba tutembelee eneo hili tuone juhudi za wananchi ili tuweze kutia nguvu katika eneo hilo. Ahsante sana.
MHE. PASCHAL Y. HAONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. Mji Mdogo wa Mlowo ulioko Wilaya ya Mbozi una wakazi wapatao elfu 70 na zaidi, lakini bahati mbaya sana mji huu una zahanati tu ambayo inahudumia watu hao zaidi ya 70,000.

Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kujenga kituo cha afya ili kuweza kuwahudumia wale wananchi ambao ni wengi na wanapata tabu sana na wanasumbuka wakati wa kupata matibabu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mwalimu Paschal Haonga, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeanza kujenga vituo vya afya awamu ya kwanza bajeti hii ya 2019/2020 awamu ya pili, naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge awamu ya tatu tutazingatia maeneo yote ambayo hayajapata huduma hii, likiwepo Jimbo lake la Mbozi na hasa eneo mahususi ambalo amelitaja hapa asubuhi.
MHE. SAUL H. AMON: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii.

Kwanza nishukuru Serikali kwa kuboresha Vituo vya Afya vya Masukulu na Ikuti, hapo nashukuru sana, kwani sasa hivi vinaonekana kama hospitali, lakini wananchi wa Kata ya Mpuguso na Kata ya Isongole kwa nguvu zao wamejenga vituo vya afya kufikia hatua ya maboma, wengine mpaka kumalizia kwenye ceiling board.

Je, Serikali ina mpango gani wa kumalizia hivi vituo vya afya kwa hao watu wanaotoka mbali sana ili viweze kwisha kwa haraka na waweze kuvitumia?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la Mheshimiwa Amon la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tumeshaanza kutekeleza kuunga mkono juhudi za wananchi ambapo wameongeza nguvu zao. Tumeshapeleka fedha katika kumalizia maboma ya shule za sekondari, tupo kwenye mchakato wa kupeleka maboma kumalizia maboma ya shule za msingi; awamu ya tatu ni maboma ya zahanati na vituo vya afya na maweneo ambayo tutazingatia ni maeneo ambayo wananchi wameshaonesha juhudi zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba mchakato huu ukikamilika aneo lake pia, ambalo amelitaja tutalizingatia sana. Ahsante.
MHE. JOEL M. MAKANYAGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nashukuru kwa majibu mazuri sana ya Serikali ambayo ameyatoa hapa Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini kwa umuhimu wa eneo lile niombe tu Mheshimiwa Naibu Waziri tupate nafasi twende sote kwa pamoja tutembee katika kijiji kile tuone jiografia ya pale na umuhimu wake ili Serikali iweze kuona inaisaidia vipi Halmashauri ya Chamwino katika kukamilisha zahanati ile.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Namshukuru Mheshimiwa Mbunge wa Chamwino Makao Makuu ya Ikulu ya Nchi kwa kukubali na kutupongeza, lakini mimi nipo tayari sana wakati wowote mwezi huu wa Tano twende katika Jimbo lake tukatembee. Ahsante.
MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kijiji cha Kitifu kipo Kata ya Mgombezi kimejenga zahanati na kimekamilisha, isipokuwa tu tunaomba mtusaidie majengo ya daktari pamoja na majengo mengine ambayo hayajakamilika. Kwa hiyo, nilikuwa naomba sana, je, mtakuwa tayari kutusaidia angalau tuweze kupata fedha kwa ajili ya jengo la mganga?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge mwanamke wa Jimbo ambaye anafanya kazi kubwa sana pale Korogwe. Naomba nimhakikishie kwamba mimi, Wizara na Serikali tupo tayari kuwasaidia Wabunge wanawake ili waendelee ku-maintain Majimbo yao. Tutafanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Wiki tatu zilizopita niliuliza swali kuhusu Zahanati ya Kigarama ambayo wananchi wamejenga kwa nguvu zao, miaka miwili wamekamilisha OPD, lakini kuna upungufu wa choo na nyumba ya Mganga na haiwezi kufunguliwa kabla ya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itaweza kukamilisha majengo hayo yanayopungua ili Kituo hiki kiweze kutoa huduma kwa wananchi ambao wanahangaika muda mrefu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Jambo hili tunalifahamu na kama nilivyojibu tangu wiki iliyopita ni kwamba tupo kwenye mchakato wa kupeleka fedha za kumalizia maboma ya Zahanati na Vituo vya Afya na naomba jambo hili tulichukue kwa uzito, tutalifanyia kazi, Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi. Ahsante.
MHE. HASNA S. MWILIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri na ninaishukuru pia Serikali kwa hiyo fedha ambayo imetuletea.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ni kweli kwamba tunazo hizo High School mbili kwa maana ya Lugufu Boys na Lugufu Girls. Shule hizi kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, zimeanzishwa kwenye majengo chakavu yaliyokuwa yakitumika na wakimbizi. Hali ya hizo shule ni mbaya sana na hata hiyo shilingi milioni 150 waliyoleta, yaani inakuwa haionekani imefanya nini kutokana na mazingira halisi tuliyonayo pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata umeme na maji kwenye hizi shule, hakuna. Sasa swali langu kwa Naibu Waziri: Je, ni lini sasa Serikali itaweza kutatua changamoto ya miundombinu iliyoko Lugufu Boys na Lugufu Girls sambamba na kuwapelekea umeme na maji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili ni kweli kabisa kwamba Halmashauri inaangalia uwezekano wa kuanzisha Kidato cha Tano na cha Sita kwenye Sekondari zetu za Buhingu na Sekondari ya Sunuka. Kwenye majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ameonyesha kwamba Halmashauri inatumia pesa zake za ndani. Sisi wote ni mashahidi, hali ya kipato cha Halmashauri sasa hivi ni mbaya sana. Kwa hiyo, naiomba Wizara; swali langu ni: Je, Wizara haioni sasa ni vyema ituletee fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu kwenye Shule ya Sekondari ya Sunuka na Shule ya Sekondari ya Buhingu ili tuweze kuwa na Kidato cha Tano na cha Sita?

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge, hawa ni miongoni mwa Wabunge jembe wanawake wa Majimbo ambao wanafanya kazi kubwa sana kuwatetea Watanzania wenzao na hasa katika suala zima la elimu na unaona anazungumza habari ya wanawake ili na wao wafikie hatua kama yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anataka kujua ni namna gari Serikali imejipanga kuboresha majengo ya shule hasa ambazo amezitaja ambazo ni chakavu. Ni utaratibu wa Serikali kuboresha majengo haya na bahati nzuri kwenye Bunge hili Tukufu ambalo linaendelea tumeishapitisha bajeti ya TAMISEMI na tuna fedha mle karibu shilingi bilioni 90 ambayo itakwenda kufanyakazi EP4R. Kwa hiyo, tutagawa fedha katika maeneo yale na ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutazingatia hili katika kupeleka fedha kwenye eneo hilo kwa shughuli ambayo ameitaja.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, amezungumza habari ya Kidato cha Tano na Kidato cha Sita. Siyo kwamba Serikali imejitoa kushiriki. Tunachosema ni kwamba Halmashauri lazima ianze. Kuna mambo ya msingi kwa mfano ardhi, iwe na umiliki hatuna fedha ya kulipa fidia, lakini wachangie kupitia mapato yao ya ndani, nasi kama Wizara tunaongezea pale na kuboresha pamoja na kupeleka wataalam na maabara nyingine. Kwa hiyo, tutachangia jambo hili ila walianzishe. Kipaumbele ni kwamba kila Tarafa angalau iwe na High School moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kusema kwamba ni muhimu tungeomba kuhimiza, pamoja na kuanzisha Shule za Kidato cha Tano na cha Sita, ukweli ni kwamba hizi shule ni za Kitaifa, zikianzishwa maana yake utapeleka watoto kutoka nchi nzima. Kwa hiyo, unaweza kubadilisha miundombinu mingine ili watoto wa eneo lile kama ni Uvinza, utaenda kuwasaidia Nguruka. Ni muhimu kuhimiza elimu ya msingi, sekondari, halafu wengine tunaenda huko mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. SELEMANI M. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika wamejitahidi sana kwa kushirikiana na wananchi, wamejenga shule za sekondari zipatavyo sita, lakini kwa bahati mbaya sana bado baadhi ya majengo hayajapata kuezekwa. Kwa hiyo, tulikuwa tunauliza, Serikali ina mchango gani wa kuwasaidia hao wananchi ambao wametumia nguvu kubwa ili waweze kukamilisha hayo majengo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mwezi wa Pili mwanzoni tumepeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 29.9 kumalizia majengo kwa maana ya maboma katika Shule za Sekondari. Ninaamini Halmashauri karibu zote, kuna baadhi ya maeneo tu hatukupeleka, lakini maeneo mengi tumepeleka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, ni kwamba vile vile mwaka huu wa fedha tuna miradi mingi na fedha ambazo zipo kwenda kumalizia maboma. Sasa kama kuna changamoto katika eneo hili kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, tutazingatia maombi yake ili tuweze kumalizia majengo haya na watoto wetu waweze kukaa sehemu salama na waweze kupata elimu kama ambavyo ndiyo makusudio na matarajio ya Serikali ya Awamu ya Tano. Ahsante.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Hali ya Jimbo la Same Mashariki na Shule za High School haiko tofauti sana na ile ya Kigoma Kusini. Serikali ilishatupa hela ya kujenga bweni la wasichana ili Kidato cha Tano kianze na bweni hilo la kuchukua wanafunzi 80 limeisha. Sasa hivi wananchi wameshatengeneza matofali na wanaanza ujenzi wa kupandisha madarasa mawili ili Form Five ianze. Je, Serikali inaweza kutusaidia katika vile vifaa kama mabati na kumalizia umeme? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kama ambavyo umesema, tunaposema Serikali inamalizia maboma, tumepiga mahesabu maana yake ni pamoja na kumalizia majengo yenyewe, kuezeka kuweka madirisha na kuweka madawati ndani ya vyumba vile. Tumekadiria karibu shilingi milioni 12,500,000/= kila boma moja kukamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu tumeshapeleka fedha mwezi wa Pili kama nilivyosema, ambapo sasa tunarajia watakuwa wanaendelea kumaliza, kwenye bajeti hii pia kuna mpango wa kupeleka fedha za kumalizia maboma ya Shule za Msingi na Sekondari. Kwa hiyo, nimtie moyo Mbunge kwamba tutapeleka fedha hizo. Hayo aliyozungumza ya umeme na miundombinu mingine itazingatiwa katika kurekebisha. Hiyo ni nchi nzima kwenye Majimbo yote. Ahsante.
MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Mara chache nimeuliza kwenye sehemu ya Walimu. Nnataka kuuliza, kwa nini kwenye Shule za Halmashauri na nje ya Halmashauri Walimu wanatengwa na wake zao wanapelekwa shule nyingine hata zaidi ya kilomita 100? Hamwoni hiyo itaathiri familia ile ya Walimu na kwamba ni hatari kwa watoto kupata mimba?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nia ya Serikali tungependa kila mtu akae na mwenza wake karibu, kwa maana kwamba mume akae na mke na mke akae na mume. Hayo ndiyo yalikuwa mapenzi na matarajio ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Waheshimiwa Wabunge wenyewe mmekuwa mkilalamika kwamba kuna maeneo mengine walimu hawapo kwa sababu wanahama sana; na sababu kubwa ni hiyo kwamba anamfuata mume wake au mke wake au sababu nyinginezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tulisema, jambo hili baada ya kupata malalamiko hata kutoka kwa wananchi na Wenyeviti wa Halmashauri, Madiwani, Wabunge na wananchi wengine, kwamba kuna upungufu na kwa hiyo, ikama hai-balance katika maeneo yetu. Serikali ikalichukua na kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatengeneza mfumo ambao kama Mwalimu anataka kuhama kutoka shule A kwenda shule B, pale anapotoka asilete shida, na hapo anapoenda asiende kujaza watu kuliko mahitaji yake. Mfumo huo unaikaribia mwisho. Ukikamilika, hii shida ya walimu kuhama na ku-balance haitakuwa shida, tutaimaliza hilo tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfumo; hata Mbunge ukiomba, ukiwaambia mkoa mzima usambazaji ukoje, Halmashauri ikoje, hakutakuwa na shida. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira. Pia Walimu wanalalamika sana, kuna mambo mengi ya uhamisho. Tutayafanyia kazi yote na hii kero itaisha. Ahsante sana.
MHE. ZAINAB MUSSA BAKARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Sijaridhika na majibu ya Serikali. Swali la kwanza, ni takribani miaka sita au saba huko nyuma, kwamba hizo nyongeza hazitolewi na Serikali. Je, hatuoni kwamba Serikali inafanya makusudi kufinya bajeti ili kuwakosesha Walimu hao nyongeza hizo za mishahara?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kama hii ipo kisheria, ni kwa nini Serikali inashindwa kutoa hiyo nyongeza ya mishahara na mara ya mwisho imetoa lini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge maswali yake ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma hapa kwenye jibu la msingi kwamba kulingana na kanuni za kiutumishi ambazo watumishi wote Tanzania sio Walimu tu watumishi wote wanajua, kwamba Serikali inapanga kuamka, kwa mfano kwaka huu wa fedha 2019/2020 kwenye bajeti yetu, kama hatukuuingiza kipengele cha nyongeza ya mishahara ambapo najua kuna tamko pale litatolewa kwenye Sherehe za Mei Mosi, maana yake ni kwamba mwaka huu kama hawataongeza mishahara halipaswi kuwa deni. Hili kwa mujibu wa kanunu za kiutumishi watumishi wote wanajua.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya Serikali kutathimini, tumesema mara ya mwisho nyongeza ya mishahara imetolewa mwaka 2017/2018, kwa hiyo hili kimsingi sio deni. Serikali inapanga kuinua mapato yake kama kuna uwezo wa kuongeza inaongeza na haya hayapaswi kuwa malalamiko.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, moja ya tatizo linalopoteza morality ya utendaji kazi katika watumishi wetu wa umma ni pamoja na kutokuweka wazi namna ambavyo Serikali italipa madeni ya huko nyuma ya watumishi wetu; na kwa kuwa kwa jambo hili watumishi wanakosa moyo wa kufanya kazi, je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka wa kukaa na vyama vya wafanyakazi ili waweze kuona namna gani ya kutatua tatizo hili la madeni ya huko nyuma ili watumishi wetu wote waweze kufahamu namna ambavyo Serikali kama mlezi wao na mwajiri wao itawatendea katika jukumu hili la kulipa madeni?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshafanyia kazi madai ya Walimu na watumishi wengine na ilishakutana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi na utaratibu upo wa kuweza kulipa fedha hizi. Kwa sasa hakuna mgogoro kati Serikali na wafanyakazi, madeni yanajulikana. Tunatafuta fedha na uwezo wa Serikali kuanza kulipa madeni haya. Hata hivyo tunalipa kila muda, sio kwamba bajeti ni kubwa kiasi hicho, kwa hiyo madeni yanalipwa, lakini pia tumeshakubaliana namna ya kwenda, deni halisi linajulikana kwamba kila mtu anadai kiasi gani na hilo linafanyiwa kazi.
MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kukosekana kwa nyongeza ya mwaka kwa Walimu na wafanyakazi wengine (annual increment) kunapelekea wakati wakistaafu wanakosa haki yao ya msingi ya mafao ya kijumla, sambamba na pension yao wakati watakapostaafu.

Je, Serikali inawaambia nini Walimu ambao tayari wamestaafu mwaka jana na mwaka juzi ndani ya awamu hii ambao sasa wamekosa hiyo increment ambapo inaenda kuathiri mafao yao ya kustaafu na pension yao ya kila mwezi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Masoud kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe maelezo kwa ufupi sana. Jambo la kwanza kuna tofauti kati ya madai na nyongeza ya mishahara. Tumesema kwenye nyongeza ya mshahara Serikali inapanga bajeti kulinga na mwaka husika wa bajeti. Kama hujaongezewa hilo sio deni la hupaswi kudai na nimejibu kwenye jibu la msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, madeni, haya ndio haki ya watumishi kudai na utaratibu wake ni kama nilivyoeleza namna ya kuweza kuyafidia. Walimu hata juzi Waziri wa Nchi ametoa tamko hapa, hata kupandisha madaraja imeelekezwa vizuri kwenye Waraka wa Waziri kwamba ni muhimu izingatiwe kama kuna watu wanakaribia kustaafu na hawajapandishwa daraja na wamekidhi vigezo, tuanze na hao.

Kwa hiyo hilo jambo la kuwa karibu na kustaafu limezingatiwa na hakuna mtu atakayenyimwa haki yake, deni ni deni hata kama mtu atakuwa amestaafu, atapewa na tutakapoanza kulipa madeni kimsingi tunaangalia wale wenye shida, wale waliostaafu ndiyo tunaanza kuwalipa na wengine wanaendelea. Ahsante.
MHE. EDWIN M. SANNDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana na nashukuru kwa majibu ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza, kwanza fursa za vyanzo vya mapato na uwezekano wa kuongeza mapato inatofautiana baina ya halmashauri na halmashauri. Hili suala la malalamiko lina kosa msingi linabaki kuwa dhana.

Sasa je, Serikali huwezi kulinganisha kati ya Kondoa au Geita au hata Dar es Salaam fursa za mapato zilizopo, na Madiwani ni sehemu ya wanaoweka nguvu ya kukusanya mapato na kuongeza mapato. Serikali haioni umuhimu wa kuwaruhusu walipe kadiri ya uwezo wa halmashauri zao ili pia iwe sehemu ya motisha?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, lini sasa maana tulipata Waraka wa kutuambia tulipe 40,000 na hapa tunazungumzia posho za vikao peke yake, lini sasa maslahi mengine tunaendelea kuruhusu kadiri ambavyo inafanya kazi. Lini sasa tutapata Waraka wa kufafanua ili ule Waraka uliotolewa mwezi Januari uweze kupitwa maana Serikali inafanya kazi kwa maandishi?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Waheshimiwa Madiwani wanafanya kazi kubwa sana ya kusimamia mapato, kwa kukusanya lakini pia na ndiyo maana fedha nyingi hapa tunapeleka halmashauri Waheshimiwa Madini kupitia vikao vyao na Kamati mbalimbali ndiyo wanapaswa kusimamia na kwa kweli tunawashukuru sana wamekuwa wakifanya hivyo. Majibu yangu ni kwamba ni kweli Mheshimiwa Waziri wa Nchi wakati anamalizia hoja yetu hii ya bajeti ya TAMISEMI, aliahidi mbele ya Bunge lako Tukufu kwamba jambo hili linafanyiwa kazi na naomba niwaahidi kwamba, Waheshimiwa Wabunge wote na Waheshimiwa Madiwani popote walipo wavute subira ndani ya wiki hii Mheshimiwa Waziri atatoa maelekezo na jambo hili litafikia mwisho ambapo tunaamini kwamba utakuwa ni mwisho mwema, ahsante.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, suala linaloulizwa na Mheshimwa Sannda na sisi pia watu wa halmashauri ya Masasi linatuletea shida. Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ilipanga kulipa posho Madiwani na stahiki zao nyingine kutokana na makusanya yaliyokuwa yanakusanywa kutoka kwenye ushuru wa korosho ambao Mheshimiwa Rais amesema hatapeleka tena. Sasa swali langu, ni je, Serikali haioni umuhimu wa kuwalipa Madiwani hawa posho moja kwa moja kutoka kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba suala la posho za Madiwani, kwanza kimsingi yanatokana na mapato ya ndani na suala lingine ni uwezo wa halmashauri yenyewe na Mheshimiwa Rais alishatoa maelekezo kwa Wilaya hizi ambazo zilikuwa zinakusanya mapato kupitia korosho wajipange kwa msimu mwingine wa korosho wafanye kazi vizuri ili waweze kupata mapato hayo. Sisi maelekezo yetu ni kwamba tutatoa maelekezo na halmashauri italipa Madiwani kulinga na uwezo wao wa ndani, ahsante.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa halmashauri ambazo zinalima korosho maamuzi yanayohusiana na ununuzi wa korosho ndiyo yaliyopelekea wao kupoteza mapato. Kuna halmashauri ambazo makusanyo yake sasa hivi ni 6% tu kwa sababu fedha zake zote walikuwa wanategemea korosho, Serikali haioni ni busara kufanya compensation ya fedha hizi ili halmashauri hizi ziweze kuendelea na shughuli zao kama kawaida ikiwemo kuwalipa Madiwani?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nadhani jambo hili kila halmashauri inapanga mipango yao na kilichofanyika na Serikali ni kwamba ilikuwa ni lazima tuchukue hatua kuwawezesha watu wetu waweze kuuza korosho zao, lakini halmashauri zenyewe maelekezo ya Serikali ni kwamba kwa kuwa hiki kilikuwa ni kipindi cha mpito tunaamini kwamba msimu ujao watajipanga vizuri waweze kukusanya kwa kuzingatia Sheria na miongozo yao. Kwa sasa suala la compensation halitakuwepo kwa sababu hiyo bajeti hatuna, ahsante.
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kuna baadhi ya halmashauri hufanya matumizi ya fedha hizi bila kumshirikisha Mheshimiwa Mbunge, na hayo yako hasa kwa upande wa Zanzibar. Je, Serikali inatoa kauli gani ili waache tabia hiyo mbaya na kujua kama Mbunge ndiyo mhusika mkuu na msimamizi wa Mfuko huo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, sijui huku Bara lakini kwa upande wa Zanzibar Mheshimiwa Mbunge baada ya kupitisha matumizi ya fedha hizi, halmashauri inakuwa haimshirikishi katika suala lolote tena. Je, mamlaka ya Mbunge katika kusimamia fedha zile kwa upande wa Zanzibar ni ya halmashauri au ni Mbunge anahusika mwanzo hadi mwisho? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, anataka kujua kama fedha hii inaweza ikatumika bila Mbunge kuhusika. Kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu langu la msingi ni kwamba Mwenyekiti wa fedha hii ya Mfuko wa Jimbo ni Mbunge mwenyewe na wametajwa vizuri wajumbe wa Mfuko wa Jimbo, Madiwani wawili kwa kuzingatia jinsia, Watendaji wawili wa Kata au Viti Maalum lakini na mtu mmoja ambaye anakuwa ni kutokana na NG’O katika Jimbo husika, halafu anaongeza na Katibu wa Mfuko huu anakuwa ni Mchumi katika halmashauri husika.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kama kuna fedha inataka kutumika, kwa vyovyote vile hata kama Mbunge hatakuwa Jimboni ni lazima Mkurugenzi wa halmashauri hiyo afanye consultation na Mbunge wa Jimbo kama Mwenyekiti na kama hatakuwepo maana yake Mbunge ataridhia labda Diwani miongoni mwa wale Madiwani kwa sababu shughuli haziwezi kusimama ili aweze kufanya kazi hiyo. Miradi inapopitishwa Mkurugenzi kazi yake ni kwenda kupitisha fedha ikatumike na siyo kupanga kwamba ongeza, punguza hiyo hairuhusiwi kabisa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili linafanana na la kwanza, kama nilivyosema na naomba nirudie tumepata malalamiko kwa kweli karibu Wabunge wengi hapa wanalalamika. Wakurugenzi wa halmashauri hawana maamuzi katika fedha hizi, hizi fedha zinaenda kwenye vikao na Wabunge ambao ni Wenyeviti wenyewe wanajadili, na inawezekana Mbunge akaenda kwenye eneo A au Kijiji B akasikiliza kero za wananchi au Mwenyekiti wa Mtaa au Mheshimiwa Diwani au wananchi wa kawaida wakalalamika, Mbunge anaweza akasema napeleka shilingi laki tano hapa. Kwa hiyo Mkurugenzi hawezi kubadilisha haya maelekezo ya Mbunge kwa sababu ndiyo uwezo wake. Ndiyo maana inaitwa Fedha ya Kuchochea Maendeleo ya Jimbo, kwa hiyo, wale Wakurugenzi ambao wana tabia ya kutumia fedha bila Mbunge tunaomba majina yao tutawashuhulikia kwa sababu Sheria imetaja vizuri namna ambavyo wanapaswa kufanya.

Mheshimiwa Spika, tumeelekeza, ukishapitisha fedha hizi kwenda kutumika ni lazima Kamati ya Mfuko wa Jimbo iende kufanya ziara ikakague hiyo miradi kama kweli ipo na kama imetekelezwa na anayetajwa pale ni Mbunge. Hii ni fedha ya Serikali, lazima isimamiwe vizuri na Sheria imeelekeza kwamba Mbunge inawezekana hana fedha mfukoni kutoa lakini kupitia Mfuko huu unaweza ukatamka neno kwa wananchi na roho za wananchi zikapona, ahsante.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, makofi kwa majibu ya Serikali kutoka kwa Wabunge yanaashiria kwamba yako matatizo katika uendeshaji na matumizi na usimamizi wa Mfuko wa Jimbo ambao lengo lake mahsusi ni kuhakikisha kwamba Wabunge wanachochea shughuli za maendeleo katika Majimbo yao.

Mheshimiwa Spika, ninaomba Serikali sisi mtuachie pia twende tukashauriane na Waziri mwenye dhamana ikiwezekana Serikali itoe waraka wa maelekezo tena kusudi kila halmashauri iweze kusimamia utekelezaji wa kisheria wa mfuko huo, lakini vilevile tuwaombe Waheshimiwa Wabunge kama Wenyeviti wa Mifuko hiyo, waone kwamba wana wajibu pia wa kuhakikisha kwamba matumizi ya fedha ya Mfuko wa Jimbo yanafanyika kwa kuzingatia Sheria.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nilikuwa na maswali madogo mawili ya nyongeza. Ni hatua zipi zilizochukuliwa kwa Wakurugenzi walioshindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato; kuchangia asilimia 40 katika miradi ya maendeleo; na kuchangia asilimia 10 kwa akina mama, watu wenye ulemavu na vijana?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, katika nafasi za Wakuu wa Idara zilizo wazi Serikali imechukua hatua gani kuhakikisha zinajazwa na watumishi wenye sifa za kuwa Wakuu wa Idara ili kuwepo na uwajibikaji katika matumizi ya fedha za maendeleo ukizingatia Serikali inapeleka fedha nyingi sana katika miradi ya maendeleo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Leah Jeremia katika swali lake, anataka kujua ni hatua gani zimechukuliwa kwa Wakurugenzi na Watumishi wengine ambao wameshindwa kupeleka asilimia 40 na asilimia 10 kama ambavyo ndivyo ilivyo maelekezo ya Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba hata hivi karibuni Mheshimiwa Waziri wa Nchi alitoa taarifa ya tathmini ya makusanyo ya Halmashauri mbalimbali na Halmashauri ya kwanza mpaka za mwisho zimetajwa na alitoa muda ambao Halmashauri watachukua hatua kurekebisha mapato hayo na kila Mkurugenzi amepaswa kujieleza na kuonesha mikakati hiyo. Kwa hiyo, hatua zinachukuliwa na wana maelekezo mahususi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ni kweli kwamba kuna fedha zimetengwa asilimia 40 ili ikaendeshe miradi ya Halmashauri. Tumetoa maelekezo, sisi viongozi wa Wizara hii, sisi Manaibu wenzake na Watendaji wengine, tukifanya ziara kwenye Halmashauri zetu, pamoja na kwenda kukagua fedha kutoka Serikali Kuu, ni lazima pia kila Halmashauri itupeleke kwenye mradi mmojawapo ambao ni own source; fedha ambazo wamekusanya kutoka kwa wananchi, zimefanya miradi? Hii ni ili tuwe na connection kati ya fedha ambayo inatolewa kama kodi, lakini pia na miradi ya maendeleo, kweli jambo linafanyika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kweli kwamba kuna maeneo mengi wako Wakuu wa Idara na Vitengo wanakaimu na tumetoa maelekezo kufanyike utaratibu, wale ambao wana sifa wathibitishwe kazini na wale ambao hawana sifa waondolewe ili tuwe na watu ambao kimsingi wana uwezo wa kufanya maamuzi. Kwa sababu ni kweli kwamba kama mtu anakaimu, wakati mwingine amekaimishwa na Mkurugenzi, akipingana naye katika mambo fulani, anamwondoa anamweka mtu mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunataka watu wawe na uwezo, wakaelezee Idara, wawe na mipango na pia waweze kubuni kwa sababu ofisi ni ya kwake..

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. AHMED A. SALUM: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante, pamoja na majibu yasiyoridhisha ya Mheshimiwa Naibu Waziri na ni mepesi mepesi sana, naomba sasa niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema hivi, katika Jimbo la Solwa tuna maboma 158, kati ya hayo maboma 40 ni zahanati kwa maana zahanati 32 na nyumba za watumishi ni 10 na maboma 50 ni shule za msingi, 58 tupo kwenye sekondari kwa maana ya maabara. Fedha zinazohitajika ni zaidi ya bilioni 4.7 lakini sijaona commitment ya Serikali ya kuniambia kwamba katika mwaka huu wa fedha au mwaka unaofuata tutatenga kiasi fulani kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma haya. Kwa majibu haya, ninaona kabisa kwamba hata miaka kumi hatuwezi kukamilisha maboma haya ambayo ni nguvu za wananchi tulikwenda kuyakamilisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini sasa Serikali inatoa commitment majibu sahihi kwa wananchi wa Jimbo la Solwa kwenda kukamilisha maboma haya hata kwa awamu tatu polepole ili tukamilishe maboma haya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza haya siyo majibu mepesi, kwa sababu Serikali imepeleka fedha shilingi bilioni 29.9 nchi nzima, siyo jambo dogo ni jambo kubwa na la kupongeza. Na Majimbo yote yamepata na Mheshimiwa Mbunge tumetaja kiasi cha fedha ambazo amepata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kumalizia maboma haya ya zahanati, msingi na sekondari ni jambo mtambuka, tunahusisha wadau mbalimbali wa elimu, Serikali yenyewe, Mheshimiwa Mbunge, halmashauri yake na wadau wengine, kwa hiyo hili jambo ni la pamoja. Niseme tu kwamba commitment kwa mfano Halmashauri ya Shinyanga wametenga fedha mapato ya ndani milioni 140 kumalizia maboma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapozungumza niseme tu kwamba wiki iliyopita Serikali hii ya Chama cha Mapinduzi ya Awamu ya Tano imepeleka fedha shilingi bilioni 68.48 kumalizia maboma ya shule za msingi na halmashauri yake imepata. Kwa hiyo, hii ni commitment kubwa, tunaomba hizi fedha zitumike vizuri, cha muhimu wakurugenzi wa halmashauri wanapoleta maboma kule TAMISEMI wawasiliane na Wabunge wao ili wawe kwenye lugha moja, fedha zikienda Wabunge wajulishwe ili waweze kusimamia utekelezaji, fedha iweze kutumika vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba nimuulize swali Mheshimiwa Waziri katika Mkoa wa Mwanza, katika mgao wa fedha za maboma kwa ajili ya sekondari, Wilaya ya Kwimba haikupangiwa hata senti tano kwa maana hata boma moja, ilisahaulika na tayari tulikuwa tumeshaleta Shule za Sekondari za Wala, Kikubiji, Malya, Wungumarwa, Ndami, Mwabomba, Shilembo, Iseni na Mwangalanga. Mheshimiwa Waziri, tunaomba tupate majibu kwa nini Wilaya ya Kwimba katika mgao huo wa bilioni
29.9 ilirukwa yenye Majimbo mawili na tayari tulikuwa tumeshaweka majina.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameshawasilisha hoja yake hiyo Wizarani na nilimuahidi kwa niaba ya Wizara kwamba watakapoanza kugawa fedha za EPFR sekondari maeneo yote siyo kwake tu, maeneo yote ambayo yalivukwa kwa bahati mbaya maana huo haukuwa mpango mahsusi wa makusudi, ilikuwa ni bahati mbaya tu, tutazingatia Kwimba pamoja na maeneo mengine yote ambayo yalirukwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, niombe, wakati tunaomba taarifa hizi, ndiyo maana nikasema hapa Wakurugenzi na maafisa elimu wetu wa sekondari na msingi, wanapoombwa walete taarifa ya maboma TAMISEMI tunawaelekeza washauriane na kupeana taarifa na Wabunge ili wazungumze kwenye lugha moja. Imegundulika kuna maboma mengine yameletwa na Waheshimiwa Wabunge lakini kule wanasema kwamba hiyo siyo shida kubwa sana. Kwa hiyo, tumesema tunaposema tunahitaji maboma, wakurugenzi na maafisa elimu wakitoa taarifa wapitishe au kushauriana na Waheshimiwa Wabunge ili tuzungumze pamoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo, fedha zikipelekwa kama zilivyopelekwa sasa, tumepeleka bilioni 29.9 kuna baadhi ya Wabunge hawakupewa taarifa, tumepeleka bilioni 68.48 wiki iliyopita, inawezekana Wabunge hawajui;
kwa hiyo, Wabunge wajulishwe ili wajue lakini kama kuna mahali pesa imeletwa kwenye halmashauri una hali mbaya sana kwenye shule ya msingi au sekondari, mkurugenzi anajua anaandika barua kwa Katibu Mkuu TAMISEMI anaomba kubadilisha matumizi ili kutibu shida kubwa, hii nyingine itaendelea kusubiri, asante.
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ni wazi kwamba kwa nchi nzima tuna matatizo makubwa sana ya upungufu wa madarasa. Sasa nilitaka kujua Serikali ina mpango mkakati gani wa kuhakikisha kwamba walau kwa kila mwaka wanajenga madarasa kadhaa wakati wanajua kabisa kwamba projection ya idadi ya watoto wanaijua. Sasa nilitaka kujua wana mkakati gani mahsusi wa kuhakikisha kwamba hili tatizo walau kila mwaka watakuwa wanajenga madarasa kadhaa kwa kila mkoa na wilaya.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tumeona hiyo changamoto wakati ambapo watoto wanaenda kuingia kidato cha kwanza, darasa la awali na darasa la kwanza ilionekana kuna upungufu mkubwa wa madarasa. Tumeshawaelekeza wakurugenzi wanafahamu, mwaka huu projection darasa la saba wanamaliza wangapi, kwa hiyo vacancy itakuwa ni kiasi gani, form four wanamaliza wangapi, vivo hivyo kidato cha sita, wafanye hiyo kazi na kila halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wameelekezwa lakini sisi kwenye bajeti tumetenga zaidi ya bilioni 90 kwa ajili ya kazi hiyo, ahsante.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kupata nafasi hii. Pamoja na jitihada kubwa za Serikali zilizofanywa za kupeleka fedha kwa ajili ya kumalizia maboma, bado Wilaya ya Tanganyika kuna uhitaji mkubwa wa kumalizia majengo ambayo yalianzishwa kwa nguvu za wananchi hasa ya shule za sekondari Ablulamatam, Kapalamsenga, Tongwe na Mnyagala kwenye kituo cha afya. Je, ni lini Serikali itawaunga mkono wananchi ambao wamejitolea kwa kiwango kikubwa.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunatambua kuna uhitaji mkubwa na kuna majengo ambayo yamejengwa kwa nguvu za wananchi na wadau mbalimbali na Serikali yenyewe. Na ndiyo maana tuliekeza kwenye fedha ile ya maboma, kazi mojawapo ni kuchangia na kumalizia nguvu za wananchi. Na hata hizi ambazo zimepekwa sawa bilioni 68.48 ambayo ni wiki iliyopita tu, hizi fedha zina maelekezo, humu kuna fedha ambazo zinaenda kwenye ujenzi lakini pia kuna fedha za ku- balance ikama, kuna hoja ilikuwepo hapa kwamba kuna walimu wa kike shule moja hakuna walimu wa kiume, au walimu wa kiume hakuna walimu wa kike; wakurugenzi watumie fedha hii walimu walipwe ili waweze ku-balance kama kule halmashauri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa ambalo tumeomba, shule ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja, fedha zimeenda kwenye halmashauri yake, ni wao sasa kuangalia je, hiyo fedha itumike namna gani. Lakini kadri tutakapopata uwezo tutakuwa tunazingatia maeneo ambayo yana changamoto kubwa ili kuweza kuondoa hiyo kero lakini hasa kuchangia na kushiriki katika nguvu za wananchi ili wasiendelee kulalamika.
MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza Mheshimiwa Naibu Waziri katika jibu lake amesema ujenzi umeshaanza. Je, yuko tayari kuongozana na mimi kesho ili akaone ujenzi kama umeanza au watu wake wamemdanganya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kutokana na kunyesha kwa mvua barabara nyingi siyo tu zimeharibika bali zimeoza na hii imepelekea wazazi kupata shida kufika hospitali hasa kwa barabara ya Huzi kuja Manda ambapo ukitoka Manda kuja Huzi kuja kwenye Kituo cha Afya cha Mpwayungu, lakini Mvumi Mission hakuingiliki pande zote, madaraja yamezingirwa na maji na yamevunjika.

Mheshimiwa Naibu Waziri anatuambiaje kuhusu kutengeneza kwa haraka ili kunusuru maisha ya akinamama na watoto na wagonjwa akinababa ili waweze kufika hospitali? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru na naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Lusinde, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, jibu langu la msingi nimesema kwamba maandalizi ya ujenzi wa barabara umeshaanza si kwamba barabara umeanza, maandalizi yamekwishaanza. Kama tumeshaanza niko tayari nipo tayari kuongozana naye kwenda kuangalia hatua ambayo imekwishafikiwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ambalo kimsingi ni swali ambalo linahusu Wabunge wote humu ndani kwamba baada ya mvua ambazo kimsingi zimeanza na zinaendelea sana barabara nyingi zimeharibika, Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameshaagiza Meneja wa TARURA wa Tanzania na Mameneja wa Mikoa na Wilaya wafanye tathmini na walete bajeti ili tufanye utengenezaji wa haraka katika maeneo mbalimbali ili huduma muhimu ziweze kufanyika.

Kwa hiyo, naomba nitumie nafasi hii kuwaelekeza pia, Meneja wa TARURA wa Mikoa na Wilaya kwamba kazi ambayo wamepewa na Mheshimiwa Waziri wa Nchi waifanye haraka sana na kuchukukua hatua ya dharura ili kuhakikisha kwamba huduma za afya zinaendelea, vijana wanaenda shule na watumishi wa Serikali na watumishi wengine wanafanya shughuli zao za maendeleo. Ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Spika, nakushuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Mtama, napenda kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake wa kuamua kutupa watu wa Mtama Halmashauri yetu. Sasa je, Serikali iko tayari kumuunga mkono Mheshimiwa Rais kwa kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya kujenga barabara za Mji wa Mtama na kuzikarabati zile ambazo zimeharibiwa na mvua ili Mji wa Mtama sasa uwe na hadhi ya kubeba Halmashauri hii ambayo Mheshimiwa Rais ametupa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru na naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nape, Mbunge wa Mtama, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Nape na Halmashauri zingine zote kwamba Serikali ipo tayari kutenga fedha za kutosha kujenga barabara katika Makao Makuu ya Halmashauri mpya na zile za zamani, pia na kujenga majengo muhimu katika maeneo hayo ili huduma ziweze kutolewa kwa uhakika zaidi. Ahsante.
MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Shule Shikizi ya Muungano ilijengwa na nguvu za wananchi kwa muda mrefu na mpaka leo tunaambiwa kwamba hiyo shule itakamilika Februari. Je, Serikali haina takwimu za wanafunzi wanaomaliza kusudi hii miundombinu ianze kutengenezwa mapema ili wanafunzi waweze kwenda kwenye shule zao?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; je, umeme ni lini utaunganishwa katika hiyo shule? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza angependa kujua kama Serikali ina takwimu; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ina takwimu za idadi ya wanafunzi ambao wapo katika maeneo yetu mablimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika eneo hili, Jimbo la Mkuranga kwa Mheshimiwa Abdallah Ulega pamoja na Mheshimiwa Mbunge na wengine wamefanyakazi kubwa sana ya kusaidia na kuchangia kupitia Mfuko wa Jimbo, wadau mbalimbali na Mbunge mwenzake wa Viti Maalum katika Mkoa ule wamefanyakazi kubwa sana ya ziada. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nimwmabie Mheshimiwa Mbunge kwamba tumeshafanya tathmini, tunajua ni kweli kwa mwaka huu wanafunzi baadhi walibaki kwa muda mrefu nyumbani baada ya kuwa na upungufu wa miundombinu, lakini tulivyofanya tathmini sasa hivi tumekubaliana, tumefanya projection kwamba hii changamoto ya miundommbinu itakwenda kupungua, lakini tushirikiane, Serikali, Wabunge, wadau mbalimbali ili tuweze kuboresha miundombinu yetu hii. Ni matarajio yetu ni kwamba hii hali ya kuwa na uoungufu itaendelea kupungua kadri muda utakavyokuwa unakwenda.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la pili, ametaka kujua kama ni lini umeme utaunganishwa katika shule hii; naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba suala la umeme ni suala ambalo sisi wote tushirikishane pale kwa sababu hii ni sehemu ya umma tunatoa huduma. Lakini kwamba tutaweza kuweka miundombinu katika shule zote haiwezekani kwa maana ya Serikali sisi wenyewe. Mheshimiwa Mbunge ni mdau muhimu na wadau wengine wote tushirikiane tuone, tujue ni kiasi gani kinaweza kikasaidia shule hii kupata umeme ili tuweke katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali ambayo kidogo yana ukakasi, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ya Mkiwa - Rungwa hadi Makongolosi imekuwa ikitengewa pesa kwa muda mrefu toka nimeingia katika Bunge hili na hata Mheshimiwa Rais aliwahi kusimama katika mkutano wa hadhara akiwaambia wananchi wa Itigi kwamba sasa inajengwa na mkandarasi alipatikana lakini hatujui kilichotokea.

Sasa je, Serikali hususani Wizara hii ambayo inayohusika na barabara hii ambayo inahusika na TANROADS, Wizara ya Ujenzi, wako tayari sasa kusema mbele ya Bunge lako tukufu ni lini wataanza kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami kilometa 56.9 ambazo zimetajwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, barabara hii inapita katikati ya Mji wa Itigi, mji wa kibiashara na wananchi wanajishughulisha katika kuhangaika kutafuta maisha yao vizuri, barabara hii sasa imegeuka mto inapitisha maji. Je, ni lini Serikali itafanya haraka kukarabati barabara hii kwa dharura?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, tumemsikia Mheshimiwa Mbunge na kama nilivyosema kwenye jibu la msingi ni kwamba tumeshafanya usanifu na tutawasiliana na wenzetu wa TANROADS tuangalie namna bora ya haraka zaidi kuweza kurekebisha hali hii katika Jimbo lake. Lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama sasa anavyozungumza Mji wa Itigi unapitisha maji; naomba nimuagize Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida na Wilaya hii afanye tathmini ili alete maombi tuone hatua ya haraka zaidi ya kuweza kurekebisha hali hii ili maji yasiweze kupita katika eneo hili na huduma ziweze kuendelea. Ahsante.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza na kabla ya swali la nyongeza ningependa kuwasilisha shukrani zangu kwa TARURA Mafinga na TARURA Iringa kwa jinsi ambavyo wanajituma kufanya kazi pamoja na mazingira ya uhaba wa fedha. Pia na Wakala wa Misitu Tanzania kwa maana ya shamba la Sao Hill ambao mara kwa mara tumeshirikiana nao kwa kutusaidia Greda na sisi halmashauri kujaza mafuta kusembua barabara zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa nina maswali mawili ya nyongeza swali la kwanza kwa mujibu wa mgao wa fedha za mfuko wa barabara kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri mpaka hapa tulipo TARURA inapata asilimia 30 na TANROADS inapata asilimia 70 na wote wanashughulika na barabara ambazo ni za muhimu katika Taifa letu, lakini bado TARURA barabara zao ndiyo zinazobeba mazao zinabeba biodhaa, zinabeba mbolea.
Je, mbali ya hiyo kanuni Serikali iko tayari kutafuta namna nyingine ya kuwa chanzo maalum cha kuiwezesha TARURA ifanye kazi zake kwa ufanisi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili Mji wa Mafinga Mjini unakuwa kwa kasi na ndiyo kitovu cha uchumi wa mazao ya misitu katika Wilaya Mufindi na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Je, Serikali iko tayari japo kuiangalia Mafinga kwa macho mawili ili kusudi miundombinu yake iweze kuboreshwa na hivyo mchango wake katika uchumi wa Taifa ukaongezeka?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tumekuwa na changamoto ya mgao wa fedha na tumepokea pongezi kwa niaba ya Serikali kwa kazi nzuri ambayo inafanyika na TARURA na nchi karibu kila halmashauri. Changamoto kubwa ni ufinyu wa bajeti na upungufu wa fedha ambao upo inapelekea changamoto hizo kuendelea kuwepo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na mambo mengine kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge jambo hili la mgao wa fedha linafanyiwa kazi kuna Kamati maalum iliundwa naifanyia kazi na Waheshimiwa Wabunge humu ndani walishatoa maoni mbalimbali kutafuta chanzo mbadala, pia kuangali formula ambayo itatumika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, pamoja na mambo mengine tutaendelea kufanya pia kazi hiyo huu mchakato tutakamilisha na ikishindikana kupata mgao wa fedha hizi au hata 50 kwa 50 basi tuangalie vyanzo vingine vya kusaidia barabara zetu ziweze kupitika. Ni kweli kwamba barabara hizi ni muhimu sana ndipo walipo wananchi wengi, huduma za kijamii nyingi tunajua zinapitika wakati wote na hasa wakati huu wa mvua.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili Mheshimiwa Mbunge anataka kujua kama Serikali inampango wa kuboresha Mji wa Mafinga. Niseme tu kwamba Serikali ina mpango wa kuboresha maeneo yote ya Miji ikiwepo Mafinga Mjini pindi tukipata uwezo wa fedha wa kutosha na kuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba kazi hiyo itafanyika kwenye eneo lake ili uchumi uweze kukua na huduma iweze kupatikana kwa haraka na kwa gharama nafuu, ahsante.
MHE. DEVOTHA M. MINJA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru sana yapo mambo ya ajabu sana, barabara hii ya Meimosi ni barabara ambayo imelalamikiwa kutumia fedha nyingi sana za walipa kodi na hili limekuwa question kwa LAAC walipokwenda kuitembelea barabara hii CAG mwenyewe ali-question barabara hii, Mainjinia wa TANROADS wali-question barabara hii na cha kushangaza mpaka sasa kama kweli Waziri anasema barabara haina shida

Ni kwa nini mpaka Serikali haijazindua barabara hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili Mheshimiwa Rais alikuja Morogoro mwaka 2018, na akamuagiza Waziri wa TAMISEMI kuunda tume ya kuchunguza barabara hii baada ya kubaini kuna ubadhirifu.

Je, ni kwa nini toka miaka hiyo miwili mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya barabara hii?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ameuliza swali na ukweli kwamba majibu haya kule kuna Mkuu wa Mkoa tena makini ameleka juzi karibuni kazi imefanyika kwa sasas hayo ndiyo majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili anazungumza maelekezo ambayo Mheshimiwa Rais alitoa, Mheshimiwa Rais akitoa maelekezo kwamba ufanyike uchunguzi sehemu fulani aliyetoa maelekezo uchunguzi ufanyike ndiyo unapewa taarifa. Kwa hiyo, sitarajii kwamba taarifa ya Mheshimiwa Rais tutaileta Bungeni hapa labda kama Bunge litaagiza vinginevyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara hii imejengwa kwa makubaliano na mikataba iliyokuwepo ndiyo imepitiwa. Kama kuna jambo ambalo analizungumza yeye na tofauti na maelezo yetu haya tutalifanyia kazi, lakini kimsingi kwa sasa majibu ya Serikali ni hayo tumetuma wqatu wetu wameenda site Mheshimiwa Waziri amefanya kazi yake na haya ndiyo majibu ya Serikali kwa sasa katika eneo hili, la barabara ya Meimosi Morogoro Mjini, ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana licha ya barabara ya Meimosi kuwa haina matatizo yoyote, lakini Manispaa ya Morogoro barabara za pembezoni ni mbovu kiasi hazipitiki kwa muda wa mvua. Kwa hiyo, kuna mkakati gani wa kutengeneza hizi barabara ? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili jana limeuliza naomba nirudie majibu ya Serikali kama ambavyo amesema Mheshimiwa Naibu Waziri yule wa Ujenzi, tumeshafanya tathimini kuangalia maeneo mbalimbali ambayo kwa kweli yameathirika na mvua na baadhi ya maeneo hayapitiki, tumeagiza watu wetu Meneja wa TARURA SO, tumeagiza Meneja wa Mikoa yote na Meneja Wilaya walete tathimini yao taarifa tumeshaipata tunaifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuwahakikishie hivyo Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa watanzania kwamba ndani ya muda mfupi sana maeneo yote ambayo hayapitiki kwa dharura, lakini tutaendelea kuwa tunaboresha ili kuimarisha barabara zetu katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, niwaelekeze TANROAD Meneja wa TANROAD Mkoa wa Morogoro apitie maeneo ambapo Mheshimiwa Mbunge amezungumza na yako mambo ambayo unaweza kufanya ndani ya uwezo wao kwa bajeti ndogo iliyopo katika halmashauri na mikoa yetu, lakini yale maeneo makubwa ambayo ni changamoto kwao tumewaambia tuwapokee TAMISEMI ngazi ya taifa tuweze kuyafanyia kazi lengo ni kwamba barabara hizi zipitike wakati wote na huduma kwa jamii yetu iendelee kutolewa kama kawaida. Ahsante.
MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa majibu yake mazuri. Napenda nithibitishe kabisa kwamba jibu lake ni sahihi na nimshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, alikuja Bariadi na kuzindua barabara hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya shukrani hizo nina swali moja tula nyongeza.

Mheshimiwa Spika, chini ya mradi huu halmashauri ya Mji wa Bariadi imenunua vifaa mbalimbali kwa kuendeleza maboresho hayo ikiwemo magari ya maji taka, grader na vifaa vingine. Vifaa hivi viko bandarini kwa muda mrefu sana; na hili siyo kwa Bariadi tu lakini kwa vifaa kama hivyo kwa miji mingine ambayo iko chini ya mradi huu ambao unafadhiliwa na World Bank.

Mheshimiwa Spika, napenda nifahamu suala la VAT kwa miradi inayotekelezwa na Serikali ambayo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alishalitolea maelekezo, ni lini sintofahamu hii kati ya TAMISEMI na Wizara ya Fedha itamalizika ili vifaa hivi vitoke bandarini viende vikafanye kazi iliyokusudiwa chini ya mradi huu? Naomba majibu.
NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa fursa hii, na nimshukuru Mheshimiwa Andrew Chenge Mtemi kwa swali hili muhimu. Pia nimshukuru yeye kwa sababu ni mmoja wa wajumbe wa Kamati yetu ya Bajeti, Kamati inayofanya kazi kubwa katika kuishauri Serikali na kutoa maelekezo mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, Mheshimiwa Rais alitoa maelekezo ni sahihi na tayari tulishaanza kuyafanyia kazi kupitia Sheria ya Fedha ya Mwaka 2018, Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 na sasa tunaanza mchakato wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2020 ambapo nina uhakika tulikofika sasa tutaweza kushughulikia tatizo hili la miradi inayofadhiliwa na Benki ya Dunia tutaweza kuikamilisha katika mwaka huu wa fedha. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana Naibu Waziri kwa majibu mazuri, kwa kuwa Wilaya ya Mbinga ni Walaya ambao iko pembezoni sana na wananchi wake wnachangamoto nyingi sana pamoja na majibu mazuri bado kuna tatizo kubwa la kuwa gari la wagonjwa katika hospitali hiyo.

Je, Serikali ina mkakati saa wa kuhakikisha wanawapelekea gari la wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa matatizo ya hospitali haya yanaendana kabisa na hali ya hospitali Zakiemu Mbagala.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongezea hospitali ya Zakiem Mbagala ambayo imezidiwa wagonjwa ni wengi lakini majengo ni machache na wahudumu ni wachache, nakushukuru.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kusimamia Mkoa wa Dar es Salama, pia ni Tanzania kwa ujumla wake hususan jambo la afya ya akinamama na watoto na wazee.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba unapokua unajenga kuboresha huduma za afya ni muhimu kuwa na gari la wagonjwa ili inapokea dharura iwe ni rahisi kumuwaisha katika huduma nyingine ya ziara ya pale alipokuwa, lakini naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba kadri kwa uwezo wa Serikali uwezo ukipatikana basi eneo hilo la Mheshimiwa Raphaeri Mapunda litapata gari la wagonjwa kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameulizia hapa.

Mheshimiwa Spika, naomba niseme tu kwamba mpango wa Serikali ni kuboresha huduma zaafya na kupeleka hufuma karibu na wananchi, tumepokea hoja Mheshimiwa Mbunge bahati nzuri tunaenda kwenye mwaka wa bajeti 2020/2021 basi tuangalie uwezekano wa kupatikana ili tuweze kupeleka fedha katika eneo hili kuboresha huduma ya pale Mbagala pia Mkoa wa Dar es Salam kwa ujumla wake. Na natambua kwamba wnanchi wangu wa Jimbo la Ukonga pia wanaweza wakapata huduma pale Mbagala Zakiemu, ahsante sana.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza, wnanchi wa Jimbo la Bunda Mjini na Wilaya ya Bunda kwa ujumla walikubaliana kwamba hospitali ya Manyamanyama iwe hospitali ya Wilaya. Lakini kuna baadhi ya mambo ambayo hospitali hiyo haina pamoja jokofu la kuhifazia maiti. Wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini wanapata tabu kupeleka maiti Nyamswa Jimbo la Bunda.

Sasa ningependa kujua ni lini Serikali itapeleka jokofu katika hospitali ya Manyamanyama?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli maneno yako yako ya utangulizi yanafaa sana ndiyo maana tufanye mabadiliko makubwa katika eneo hili ikiwa na Wabunge wanaopatikana wakatI wote Bungeni kusemea watu wao kama Mheshimiwa Ester Bulaya.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kwanza Bunge imepata Kituo cha Afya ni suala la kuishukuru Serikali ya Awamu ya Tano ya Dkt. John Pombe Magufuli tumepata hospitali pale inajenga katika eneo hili lengo ni kupunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali hii. Mheshimiwa sema Mheshimiwa hoja yako imepokelewa tuangalie uwezo wa Serikali tupeleke jokofu katika eneo hili ili maiti ikipatikana pale basi iweze kuhifadhimiwa eneo la karibu na kupunguza gharama zausafirishaji wa ndugu wa marehemu, ahsante sana.
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba niulize maswali mawili ya nyongeza, swali la kwanza Mheshimiwa Naibu Waziri, ukweli ni kwamba halmashauri nyingi hasa za Mijini wamesha exhaust karibia vyanzo vyote vya mapato. Sasa nilifikiri kwamba Serikali ingetusaidia kuweka mpango wa haraka kwa ajili ya nyumba za walimu.

Ni lini Serikali itaweka kwenye bajeti kuu fedha za ujenzi wa nyumba za walimu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili nishukuru kwanza Serikali ilitupatia fedha milioni 152 kwa ajili ya kukamilisha bweni la Sekondari ya Nakwa katika Halmashauri ya Mji wa Babati lakini ujenzi umefika katika upauzi bado finishing, niombe serikali itupatie fedha kwa sababu tatizo la vyanzo vya mapato kuwa vichache kati Halmashauri ya Kalenga ina fafana pia Halmashauri ya Mji wa Babati.

Ni lini Serikali itatupatia fedha kwa ajili ya finishing ya bweni la Sekondari ya Nakwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli tungependa kuona nyumba za walimu katika maeneo ya jirani ili walimu wetu wasiweze kupata shida wnapotoa huduma na kuhudia vijana wetu katika maeneo mbalimbali na hasa Vijijini. Vilevile tungependa pia kuwa na mabweni ya kutosha kwa watoto wa kike ili kuwapunguzia majanga ya kupata mimba na wakati mwingine mazingira magumu kuplekea kufanya vibaya katika mitihani yao.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tuko kwenye bajeti ya mwaka huu tumetenga fedha ya kukamilisha nyumba zaidi ya 364 katika maeneo mbalimbali, pia kumalizia mabweni na kumbi mbalimbali. Ningependa niseme tu kwa mfano fedha hizi ambazo zinazungumzwa hapa ambazo tungeweza mkopo ambayo wenzetu humu ndani wametuhujumu kwa kufanya hizi fedha zisiweze kuchelewa zingeweza kunufaisha vijana, watanzania wazalendo wenzetu zaidi ya milioni sita, tungeweza kujenga matundu ya vyoo kwenye mashule ya Sekondari, 1000, tungejenga matundu ya vyoo 2000 katika maeneo mbalimbali, kutengeneza kumbi za mikutano, mabwalo na hosteli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, naomba tu niseme katika jambo hili ni jambo la mkakati la pamoja Serikali, Waheshimiwa Wabunge na wadau mbalimbali tushirikiane tunapoona kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato wenzetu wanapokula kitumbua wasitie mchanga ili fesha ije katika eneo hili na watanzania wapate huduma kama ambavyo imetupasa kufanya, ahsante.
MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza, kwa kuwa Serikali imetueleza kwamba ina mikakati mbalimbali ya kuongeza nyumba za walimu na tatizo hili lililopo katika Jimbo la Kalenga linafafana sana na Jimbo la Singida Kaskazini.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa katika bajeti hii ya mwaka 2020/2021 kuanza kutenga fedha kwa ajili kutoa posho maalum kwa walimu ili waweze kukodisha nyumba na waishi katika maeneo ambayo yanastahili, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni mapenzi ya Serikali hii ya Awamu ya Tano kwamba tuwe na uwezo wa kuwawezesha walimu wetu wafanye kazi katika mazingira raisi sana na lipokee ushauri wake na kwa sababu yeye ni Mheshimiwa Mbunge na mchakato huo bahati nzuri unaanzia kwenye ngazi ya halmashauri.

Kwa hiyo, ningeomba Waheshimiwa katika halmashauri zetu pale mchakato unaondelea sasa tunatengeneza bajeti tuangalie uwezekano wa kupunguza adha hii kwa walimu wetu; na sisi kama Serikali ngazi ya TAMISEMI tutalipokea na kuanza kulifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, lakini nitoe wito kwa watanzania tunaoishi katika maeneo ambayo tunatoka hata Waheshimiwa Wabunge na wadau mbalimbali wa elimu hata tukijenga zile nyumba za kawaida na kuweza kuwapangisha walimu kwa bei nafuu walimu wataishi karibu maeno ya shule wataweza kutoa huduma mbalimbali. Tushirikiane pamoja kuweza kupunguza changamoto ya walimu, walimu wafundishe katika maeneo salama, rafiki pia na kodi ambayo ni affordable ili waweze kufanya kazi katika urahisi wake, ahsante sana.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona pamoja na ukosefu wa nyumba za walimu katika Jimbo la Kalenga ni mwaka wa nne sasa walimu hawa hawajapandishwa madaraja na wamekuwa wakipata adha kubwa sana katika masuala hayo ya nyumba.

Ni lini sasa Serikali itawapandisha madaraja walimu hawa ili waweze kuongeza morale katika utendaji kazi wao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tuna malalamiko mbalimbali mengi ya walimu katika maeneo mbalimbali ya nchi wakionesha kukerwa na kutopandishwa madaraja.

Niwaombe pia katika jambo hili pia kwa sababu ya mchakato wa kupandisha madaraja unaanzia kule ngazi ya halmashauri zetu ambako kila Mbunge pale yupo, mchakato unaanzia pale ngazi ile inaenda kwa Afisa Utumishi inakuja kwa Mkurugenzi mpaka maeneo mengine. Tupeane taarifa tumeshatoa maelekezo tumekutana walimu wote na mawakilishi wao kwa maana Maafisa Elimu wa Wilaya na Mikoa na Wakurugenzi na Makatibu Tawala, juzi walikuwa hapa Dodoma, tukaagiza kwamba tupate taarifa.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu unakuta, mwalimu yupo kwenye halmashauri yako Mheshimiwa Mbunge, lakini mwenzake yeye kapanda mara ya kwanza, mara ya mwisho 2013 mpaka leo hajapanda, lakini kuna wengine wamekuwa wakipandishwa. Kwa hiyo, tukipata taarifa mahusui katika maeneo haya tutazifanyiakazi haraka sana. Walimu wanalalamika na wanakwazwa, tungependa tuwaondolee adha, yale mambo ambayo yapo ndani ya uwezo tuyaondoe ili tuondoe kero kwa walimu wetu waendelee kufundisha kwa moyo. Ahsante sana.
MHE. SHAABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Hata hivyo, kabla ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza, naomba nitumie nafasi hii kuwapa pole wananchi wa Wilaya ya Lushoto kwa mvua zinazoendelea kunyesha takriban sasa ni miezi minne bila kujua zitaisha lini. Niwatoe hofu kwamba taarifa za mvua zimefika sehemu husika, ni imani yangu kubwa sasa kwamba baada ya mvua kupungua miundombinu ile itarejeshwa na wananchi watapata huduma kama ilivyokuwa awali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa naomba niulize maswali mwili ya nyongeza. Kwanza nimpongeze kwa majibu mazuri Mheshimiwa Naibu Waziri kwa kusema kuwa ametupatia fedha za maabara, ni kweli. Hata hivyo, kuna shule nyingi sana katika Wilaya ya Lushoto zaidi ya 50 lakini zenye maabara hazifiki sita. Kwa nini sasa Serikali isitumie mfumo kama ule wa mwaka jana wa kutoa fedha za kukarabati maboma ya madarasa ili kukarabati maabara kuepusha usumbufu kwa wanafunzi wetu hasa wasichana ambapo tutaepusha mimba za utotoni?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Jimbo la Lushoto lina sekondari nyingi sana zaidi ya 28 lakini zenye hosteli naamini hata tatu hazifiki. Je, kwa nini sasa Serikali isitupe hata fedha kwa mwaka huu ili kukarabati maboma ya hosteli ambayo yameshajengwa kwa nguvu za wananchi mfano Mlongwema…

SPIKA: Mheshimiwa Shekilindi nafikiri umeeleweka, majibu ya maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFlSI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shekilindi, Mbunge wa Lushoto, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza umeona Mheshimiwa Mbunge amehemewa, mimi nimeenda Lushoto pamoja na kwa Mheshimiwa Shangazi ni kweli wana shule nyingi na wanajenga kwa nguvu za wananchi. Nawapongeza sana Mheshimiwa Shekilindi na Mheshimiwa Shangazi kwa kazi nzuri ambayo wanafanya katika kupeleka elimu katika maeneo yale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia nimetembelea baadhi ya maboma ya maabara ambayo kwa kweli hayajakamilika. Maombi ya Mheshimiwa Mbunge tumeyapokea, Serikali ina mkakati wa kuhakikisha kwamba tunapata maabara katika kila shule ya sekondari kwa sababu ni lazima tuwe na masomo ya sayansi ambayo yanafundishwa kwa vitendo na siyo nadharia.

Mheshimiwa Spika, kwa bajeti ya mwaka huu na bajeti ambayo tunaendelea nayo, nimhakikishie kwamba katika maombi ambayo ameshayaleta pale ofisini tutayafanyia kazi, hawezi kukosa baadhi ya maabara ambazo zitakamilika. Hatujengi maabara tu, tunajenga maabara lakini pia kupeleka vifaa ili wanafunzi waweze kufanya mazoezi kwa vitendo.

Mheshimiwa Spika, napenda kumjulisha Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine wote mwaka huu ambao tunaendelea nao tumetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maabara na majengo mbalimbali lakini na mwaka huu ambao tunaanza mchakato wa bajeti tutatenga fedha. Nitoe wito kwa Waheshimiwa Wabunge Halmashauri huko wanaendelea kutengeneza bajeti ni muhimu kwenye bajeti hii ambayo tunaenda nayo 2020/2021 tutenge fedha kuanzia vyanzo vya Halmashauri na sisi Serikali Kuu tutatafuta fedha tuwekeze pale ili tuweze kuboresha maabara, majengo ya hosteli, kumbi za mikutano na nyumba za walimu. Ahsante sana.
MHE. EDWIN M. SANNDA: Mheshimwa Spika, nakushukuru. Labda tu kabla ya kuuliza maswali yangu ya nyongeza, nikuombe tu univumilie kidogo kwa sababu haya majibu ya Serikali sioni matumaini kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwanza tunazungumzia uchumi wa viwanda na tegemeo kubwa lazima tuweze kuzalisha wanasayansi wa kutosha kabisa. Sasa mimi natoa mfano tu wa Mkoa wetu wa Dodoma tulikuwa kwenye vikao vya ALAT hata kwako Mheshimiwa Spika tuko chini ya 20% ya ukamilishaji wa maboma ya maabara. Sasa huu uchumi wa viwanda unakwenda kulishwa na watu kutoka wapi kama tunawapeleka watu wa masomo mengine na siyo wanasayansi?

Mheshimiwa Spika, unapozungumzia shilingi milioni 8 ambazo Halmashauri ya Mji Kondoa tumeidhinisha hizi ni zile fedha ambazo nimezitoa mimi kupitia Mfuko wa Jimbo mwaka jana na tulikwishazitoa. Boma moja la darasa linajengwa kwa shilingi 25 sisi tunazungumzia shilingi milioni nane. Hebu Serikali ione ni namna gani tunakuja na mkakati wa dharura sasa kama ambavyo tumefanya kwenye maboma ya madarasa na kwenye nyumba za walimu ili tuweze kukamilisha hizi maabara nchi nzima. Swali la kwanza hilo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, walau mimi nina maabara moja tu kati ya sekondari nane (8) ambayo imekamilika na yenyewe haina vifaa. Ni lini tutapata angalau hivyo vifaa vya maabara kwenye hata hiyo moja ambayo mpaka sasa imeshakamilika? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba majibu ya Serikali tafadhali.
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFlSI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Sannda, Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ameuliza maswali mawili, moja anauliza mkakati wa Serikali wa kumalizia maabara ambazo wananchi wameweka nguvu zao lakini jambo la pili anataka kujua ni lini tutapeleka vifaa katika shule yake.

Mheshimiwa Spika, tulisambaza vifaa vya maabara kwenye shule na maabara mbalimbali. Nafikiri baada ya kutoka hapa mbele tuwasiliane tuone ni kwa nini maabara yako moja ambayo imekamilika haikupata vifaa ili tuweze kupeleka vifaa katika shule yako hiyo.

Mheshimiwa Spika, lakini nikupongeze sana kwa swali muhimu, ni kweli kwamba tunahitaji uchumi wa viwanda na tunahitaji zaidi wanafunzi wetu wasome masomo ya sayansi na huwezi kusoma sayansi kama hauna maabara zenye vifaa na wale wataalam wa maabara ili waweze kufanya mazoezi kwa vitendo. Tunampongeza Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine ambao kwa kupitia Mfuko wa Jimbo wamepeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha maabara. Najua wengine wamejenga madarasa, wengine wamenunua madawati na wengine wamejenga nyumba katika maeneo ya jirani ili walimu wetu waweze kupanga kwa bei nafuu sana.

Mheshimiwa Spika, nilichosema hapa ni kwamba Serikali ina mpango, kwenye bajeti hii Waheshimiwa Wabunge wote tumetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maabara. Tulishatoa taarifa kwenye Halmashauri walete taarifa ya maabara ambazo zimekamilika, vifaa vinanunuliwa na vinasambazwa katika maeneo yale. Tunaendelea kutoa wito tupate hizo taarifa ili tuendele kukamilisha zoezi hili.

Mheshimiwa Spika, umesema vizuri hapa kwamba hapa tunazungumzia maabara katika shule za sekondari na katika mpango wetu ule wa kupata fedha zile ambazo zina kizungumkuti huko na wenzetu wameshiriki, katika mpango ule nilisema juzi hapa tunajenga shule mpya za watoto wa kike maalumu 26, tunajenga madarasa na mabweni kwa maana ya mabwalo zaidi ya 300 na tunakamilisha maabara zaidi ya 400. Kwa hiyo, huenda hii fedha ingekuja kwa wakati na ndiyo ulikuwa mpango wa Serikali hii kazi ya kulalamikia maabara hata kama isingeisha ingepungua sana. Tutoe wito Waheshimiwa Wabunge kama nilivyosema juzi hii kazi Serikali ni yetu sote tulishirikiane fedha zikitafutwa tunapeleka fedha Halmashauri, tunapeleka fedha kutoka Mfuko Mkuu lakini pia tunatumia wadau mbalimbali ili tuweze kupata fedha tuweze kukamilisha miundombinu mbalimbali ya elimu.

Mheshimiwa Spika, tushirikiane katika jambo hili na kama ambavyo umeshazungumza katika Bunge hili. Pia sisi kama Wizara tunakwazwa sana na mambo haya kwa sababu tunaweka mipango na Wabunge wameleta maombi mbalimbali pale Wizarani, fedha zimeiva halafu kuna watu wanaweka kitumbua mchanga. Ahsante sana.
MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Ukiangalia malengo endelevu ya dunia yanaenda kwa vipaumbele. Kipaumbele cha Nne ni elimu bora, sawa Jumuishi/Shirikishi kwa wote. Kipaumbele cha Tisa ni viwanda, ubunifu na miundombinu. Serikali imekuwa ikiwekeza kwa kasi kubwa kwenye miundombinu lakini ili uweze kutekeleza na kusimamia vizuri miundombinu yafaa kuwekeza zaidi ya mara mbili kwenye elimu kabla ya miundombinu. Serikali haioni umuhimu wa kuja na mpango mkakati bila kupepesa macho ili wawekeze kwenye elimu na hasa sayansi ili maabara zetu zikiwa kwenye hali nzuri ikiweko ya Rasesa ambayo Mbunge naijenga kule Vunjo waweze kuwekeza na watoto wetu wawe wabunifu waweze kuendesha karne ya sanyansi na teknolojia na hasa viwanda?
NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFlSI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa James Mbatia, Mbunge Vunjo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maoni na mawazo yake mazuri na ya kisayansi. Nimhakikishie kwamba mpango wa Serikali upo mkubwa sana wa kuhakikisha kwamba tunaondoa changamoto hii. Tunaweka mpango mzuri wa kumalizia maabara zetu, kupata mabweni ya kutosha kwa watoto wa kike lakini kupata walimu wa sayansi hasa masomo ya hesabu, fizikia, kemia na biolojia ili masomo hayo yaweze kufundishwa.

Mheshimiwa Spika, lakini wakati tunatekeleza mkakati wa muda mrefu tunao mpango wa muda mfupi. Kama nilivyosema kwenye bajeti hii tunazo fedha na vyanzo vipo katika maeneo mbalimbali. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kabla ya mwezi wa pili au wa tatu tutakuwa tumepeleka fedha katika majimbo yetu ili kukamilisha miundombinu ya elimu. Mpango wa mwaka huu tumeelekeza Wakurugenzi na nyie Waheshimiwa Wabunge hakikisheni kwenye mpango mnaoanzisha pale kuwe na kipengele hicho cha kuwekeza katika walimu na madarasa lakini pia maabara katika halmshauri zile.

Kwa hiyo, tukishirikiana na Halmashauri zetu sisi Wabunge na wadau mbalimbali wa maendeleo na Serikali Kuu jambo hili linawezekana. Hatuwezi kuwa na viwanda halafu wageni ndiyo waje kufanya kazi hapa kwetu lazima tuwe na viwanda na vijana walioandaliwa vizuri wafanye kazi katika viwanda hivyo ili tuweze kuwekeza katika uchumi wa viwanda na uchumi wa kati.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi Serikali imekwepa kujibu msingi wa swali kwa sababu msingi wa swali langu ni kwamba Ibara ya 74(6)(e) ya Katiba imesema Bunge linaweza kutunga sheria ya kuipa tume jukumu la kusimamia suala lingine lolote na Ibara hiyo ya Katiba pamoja na kuwa kwenye majukumu ya Tume kulikuwa hakuna jukumu la kusimamia kura ya maoni ya mabadiliko ya Katiba, sheria ikatungwa na Bunge ya kura ya maoni…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mnyika uliza swali.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Sasa ndio najenga msingi wa swali kwa sababu amejibu tofauti kabisa. ni kwa nini Serikali imeogopa kuleta Bungeni Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambayo ingeondoa mamlaka kwa Waziri wa TAMISEMI ingeweka daftari la kudumu kutumika na ingepeleka majukumu yote kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili uchaguzi usimamiwe na Tume ya Uchaguzi badala ya kusimamiwa na Serikali yenyewe kwa maana ya Waziri wa TAMISEMI ambaye ni interested part ndio alazimike kutunga kanuni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwenye sehemu ya mwisho ya majibu amesema kwamba kanuni zimeandaliwa kushirikisha wadau, bahati nzuri nilikuwepo kwenye kikao kilichofanyika mwezi Aprili cha kujadili kanuni. Tumekaa kikao kama vyama, anasema vyama vimeshirikishwa; tumekaa kikao Aprili, Aprili hiyohiyo tarehe
25 mwezi wa nne, Waziri akatoa Kanuni kwa siri zilizochapishwa, zimekuja kutolewa hadharani mwezi Agosti na Kanuni zile hazijazingatia maoni ya vyama, wadau na tayari Kanuni hizo zimeanza kutumika vibaya, tunaona Wakuu wa Mikoa ambao ni viongozi wa kisiasa, Wakuu wa Wilaya, Maafisa Tarafa sasa ndio wanapewa jukumu la kusimamia uchaguzi wakati ni makada wa Chama cha Mapinduzi, kutakuwa na uchaguzi wa uhuru na haki katika mazingira kama hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, majibu ya Serikali ni sahihi kulingana na swali ambalo ameliuliza. Nikirejea swali la Mheshimiwa Mbunge anasema je, ni kwa nini Ibara ya 74(6)(e) isitumike ili kusimamia uchaguzi wa Vitongoji na Vijiji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hoja anayosema swali la kwanza kwamba kwa nini Serikali isilete mabadiliko ya Katiba, Serikali inaweza ikaleta Muswada wa kubadilisha Katiba lakini pia Mheshimiwa Mbunge ana nafasi hiyo na hajafanya hivyo. Kwa hiyo, angeleta mabadiliko hayo tungeyajadili lakini kwa sasa tunazungumza uchaguzi wa Serikali za Mitaa as by now kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zilizopo utasimamiwa na Waziri mwenye dhamana, hakuna mabadiliko ya Katiba ambayo yamekwishafanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili; Mheshimiwa Mbunge ananiuliza kwamba kanuni hizi hazikuzingatia miongozo, sio kweli na yeye mwenyewe bahati nzuri amethibitisha kwamba alihudhuria, sasa mkiitwa kwenye kikao kujadili na kutoa maoni siyo lazima Serikali ichukue kila kitu mnachokisema, maoni yakitolewa wataalam wanakaa, wanaangalia katiba, sheria, miongozo mbalimbali na practice ya kawaida halafu tunaamua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kanuni hizo sasa hivi wala hazikumpa dhamana yoyote Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya kwamba wakasimamie uchaguzi, muongozo huu hapa. Mheshimiwa Mnyika Naibu Katibu Mkuu wa chama chake cha CHADEMA alikuwepo siku hiyo Mheshimiwa Waziri anatangaza kanuni, amepewa kanuni za uchaguzi, mwongozo wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Mwongozo wa Mpiga kura. Na kanuni inasema pia asasi za kiraia na mtu yeyote yule anaweza akapewa hii akasoma na akaomba miongozo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe Mheshimiwa Mnyika asiwe ana hofu, Mheshimiwa Mnyika uchaguzi huu utakuwa ni huru na haki na kanuni imeeleza vizuri nani anapaswa kusimamia uchaguzi huu. Tujipange, tukutane kazini, ahsante. (Makofi)
MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kupigania afya yangu, sasa hivi naendelea vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana kwa watu wasioitakia mema nchi hii, wamekuwa wakiweka dosari ambazo hazipo kwenye suala hili la uchaguzi. Je, Serikali imejipangaje kuwaelimisha zaidi Watanzania ukweli ambao wamekuwa wakifanya hivyo na uchaguzi umekuwa ni huru na ndio maana wapinzani ni wengi ndani ya Bunge, Madiwani, Wenyeviti na kadhalika. Mmejipangaje kuwaelimisha Watanzania hawa wanaopenda amani katika nchi yao? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwanza nampongeza na kumpa pole sana kwa kupata shida ya afya na Mungu amemjalia na aendelee kuimarika Mbunge mwenzetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ni swali muhimu sana, nasema ni muhimu kwa sababu ni kweli kwamba hata swali la msingi la leo utaona ni swali ambalo limejaa tu hofu bila sababu yoyote ile kwa sababu uchaguzi wa Serikali za Mitaa si kwamba unaanza kufanyika kwa mara ya kwanza Tanzania leo mwaka huu, ni uchaguzi ambao tumefanya awamu kadhaa huko nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na bahati nzuri niliyesimama hapa pia nimekuwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa kupitia chama cha upinzani CHADEMA kama ingekuwa uchaguzi sio huru mwenyewe mwaka 2014 nisingekuwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa pale Kivule, nilishinda uchaguzi na nikawa Mwenyekiti wa Mtaa kupitia chao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili; uchaguzi wa nchi hii ni huru, nilikuwa Mbunge kupitia CHADEMA, nilishinda kwa kanuni hizihizi na Katiba hiihii iliyopo na leo nimesimama mbele yako kama Mbunge kupitia Chama cha Mapinduzi. Hii yenyewe inaonesha kwamba uchaguzi wa Tanzania ni huru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nirudi kwenye Serikali za Mitaa, mchakato wa uchaguzi huu kanuni zimeandaliwa na wadau waliitwa wakatoa maoni yao, tukachakata na wataalam wakashauri kanuni hii hapa imeshatolewa na Mheshimiwa Waziri wa Nchi ameshatoa nakala hizi kwa Wakuu wa Mikoa wote na vyama vya siasa wanazo hizi kanuni. Hakuna mtu ambaye amekuja mbele ya Watanzania akakosoa kifungu chochote kwenye kanuni kwamba kimekinzana na Katiba kina mapungufu, wamepokea na wameridhia, tunaendelea na mchakato.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeenda mbali zaidi, tumetoa mwongozo kwa wapiga kura, hapa inaeleza nani ana sifa za kugombea, mchakato ndani ya chama namna mbalimbali za michakato na usimamizi na imetaja nani anapaswa kusimamia uchaguzi na imewakataa mpaka Watendaji wa Kata ukisoma vizuri. Kwa hiyo, nitashangaa sana watu ambao wanakuja hapa wana hofu ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tarafa, Watendaji na watumishi wa Serikali lakini kanuni imeeleza ni nani ambaye anapasa kusimamia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitabu cha tatu ambacho kimetolewa ni Mwongozo kwa Mpiga Kura na kanuni imeeleza kama mtu yeyote ama asasi za kiraia anataka kutoa elimu ya uraia, kuchunguza ndani na nje kanuni imetoa mwongozo kuna utaratibu wa kufanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niseme kwamba Serikali imejipanga vizuri sana kuendesha uchaguzi wa Serikali za Mitaa na utasimamiwa na Waziri mwenye dhamana na Watanzania wapo tayari sana kufanya uchaguzi huru na haki, wapate viongozi wao, wazingatie maelekezo ya Serikali ili tupate viongozi ambao watatuwakilisha. Wananchi wasiwe na hofu, uchaguzi utasimamiwa na vyombo vipo na kama kuna mtu yeyote ambaye ana jambo lolote ambalo anadhani kwamba linataka maelezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ipo wazi, tunawakaribisha tupate maoni tujadiliane kwa maana ya kuboresha,

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuulizwa maswali madogo mawili ya nyongeza. Kwa kuwa ukamilishaji wa maabara katika sekondari ni sehemu muhimu sana ya utoaji wa mafunzo kwa vitendo; na kwa kuwa Halmashauri nyingi nchini zimeshindwa kukamilisha maabara kwenye sekondari zetu: Je, Serikali ina mpango gani wa kukamlisha maabara hizo ili vijana wetu waweze kufanya mafunzo kwa vitendo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa katika swali la msingi, Mheshimiwa Waziri amesema, Mkoa wa Singida utapata vifaa kwenye shule 59: Je, ni shule zipi katika Jimbo la Singida Kaskazini zitakazopatiwa vifaa vivyo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza namshukuru Mheshimiwa Mbunge sawa na Waheshimiwa Wabunge wengine kwa kuendelea kufuatilia na kusimamia elimu ili vijana wetu wapate maisha mazuri huko baadaye kwa kujiendeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anauliza, kama Serikali ina mpango wa kupeleka fedha kukamilisha maabara katika mashule yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Serikali ina mpango mkakati, fedha hizi ambazo tunapata za kutoka Halmashauri zetu, fedha za kutoka Serikali kuu, fedha za kutoka katika wafadhili mbalimbali, pamoja na kazi nyingine za kujenga madarasa, lakini pia tunatumia kukamilisha maabara hizi. Naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwa ujumla kwamba, mwaka huu wa fedha tumetenga fedha nyingi pia. Wakati ukifika tutaanza kutekeleza mradi huu na kila Halmashauri na kwenye mashule tutapeleka fedha ili kukamlisha maabara, likiwemo la Jimbo la Mheshimiwa Monko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anauliza, shule ambazo zina mpango wa kupelekewa vifaa vya maabara. Katika Jimbo la Mheshimiwa Monko, Singida Vijijini, shule kwa mfano ya Sekondari Madenga, Shule ya Sekondari Nyeri, Shule ya Sekondari Ugandi, Shule ya Sekondari Dokta Salmini, Shule ya Sekondari Mandewa, Shule ya Sekondari Mtururuni, Shule ya Sekondari Mganga na Shule ya Sekondari Utemini. Shule hizi pamoja na nyingine zitapata vifaa vya maabara mwaka huu ambao tunaendelea nao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kuniona niulize swali dogo na nyongeza. Kumekuwa na taarifa za kupotosha juu ya michango mashuleni hasa baada ya elimu bure:-

Je, ni nini maelezo ya Serikali kuhusu suala hili? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, kwa kufuatilia suala la elimu na hasa hususan watoto wa kike, kama ambavyo Waheshimiwa Wabunge wengi hasa wanawake wanafanya kusemea wanawake wenzao ili na wenyewe baadaye wawe wana mambo mazuri huko mbele.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, nimefanya ziara mbalimbali kwenye Halmashauri nyingi tangu nimepata nafasi hii ya kuaminiwa na Mheshimiwa Rais, lakini ni kweli kwamba kumekuwa na watu wanapotosha. Wengine wanapotosha kwa kutojua, lakini wengine wanapotosha kwa makusudi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, michango mashuleni haijazuiliwa. Kilichofanyika, umewekwa utaratibu. Huko nyuma ilikuwa kuna michango mingi mashuleni na inaratibiwa na Walimu. Ilikuwa wanaunda timu yao, kiasi kwamba badala ya kuwa na jukumu kubwa la kufundisha na kusimamia elimu, ikawa wengi wanagombana na wanafunzi na wazazi ili michango iende pale shuleni. Baada ya Serikali kuliona hilo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetoa waraka wa mwaka 2015 ambao umeanza kutumika mwaka 2016.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba waraka huu Waheshimiwa Wabunge waupate kwa kuwa unapatikana, wausome. Waraka huu unaelekeza namna michango inavyoweza kuratibiwa katika shule zetu na umetaja kila mtu na kazi yake. Kama ni ngazi ya kijiji, kama ni ngazi ya mtaa, kama ni Kamati ya Shule au Bodi ya Shule, kama ni Waheshimiwa Madiwani kwa maana ya WDC, kama ni Waheshimiwa Wabunge na Halmashauri ngazi ya mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango kama ni kwenye shule kwa mfano, kuna upungufu wa Walimu na tunajua kwamba tuna upungufu wa Walimu hasa masomo ya sayansi kwa sekondari na msingi. Wazazi wenyewe kwa utashi, wakaamua kuona kuna ulazima wa kupata mwalimu hata wa kujitolea kwa michango kidogo. Kikao cha wazazi kinaitishwa, kinasimamiwa ama na Mkurugenzi au na Mkuu wa Wilaya ili wazazi ambao hawana uzwezo wasilazimishwe. Pia baada ya kukubaliana, watoto ambao wazazi wao au walezi hawatakuwa na uwezo kuchanga, ni marufuku kuwazuia kutoenda shuleni kusoma ili wakatafute michango hiyo, wachange wale wenye uwezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, huo ndiyo utaratibu uliotolewa na walaka unaeleza, Waheshimiwa Wabunge wausome, wale ambao wanapotosha wananchi kwamba michango hairuhusiwi. Haiwezekani kuna watu wanakaa kwenye kijiji fulani, kwenye kata fulani, wana uwezo kwa mfano kuchimba kisima cha maji katika shule, hawawezi kuzuiliwa. Cha muhimu, ni lazima tujue nani anachanga na fedha inasimamiwa na nani? Walimu wabaki na jukumu la kufundisha na watu wengine tusaidie miundombinu hii. Kazi ya kuifanya elimu iwe bora Tanzania, ni kazi ya Serikali, kazi ya Wabunge na kazi ya wadau mbalimbali wote ambao wanapenda maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. JOYCE B. SOKOMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda tu kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Zahati ya Kenyamanyori ambayo inatoa huduma kwa Kata mbili ambayo ni Nyandoto na Ketare. Wananchi wa maeneo yale wamejitolea kwa nguvu zao, wamejenga jengo la wazazi ambalo ni kiliniki ya wanawake kufikia lenta, pia nguvu ya Mbunge, ameweka pake mifuko 20: Je, ni lini Serikali, itaongeza nguvu kuweza kufikia kumaliza jengo lile la kiliniki ya mama na mtoto? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili: Je, ni lini Serikali itapeleka dawa katika Zahanati ya Gamasara kulingana na kiasi cha fedha kilichobaki MSD?

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Zahanati ya Kenyamanyoli kuna nguvu ya ujenzi inaendelea pale na kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema, lakini kwa mwaka huu wa fedha Halmashauri ya Mji wa Tarime imetenga fedha lakini kutoka kwenye Bajeti ya Serikali Kuu tutaangalia kitachowezekana ili kusaidia nguvu za wananchi hawa ambao wamejitolea ili nguvu yao isiweze kupotea bure. Kwa hiyo, tuendelee kuwasiliana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI tuone tunafanya kitu ili kuongeza nguvu watu wote katika eneo hili waweze kupata huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anauliza kama tunapeleka dawa kwa fedha ambayo imebaki. Nimesema katika jibu la msingi kwamba waliomba milioni 17, bado zimebaki milioni 13. Wizara hatuna shida kupeleka madawa katika Zahanati hii wala mahali pengine popote pale, maelekezo ya Serikali ni kwamba kadri ambavyo bajeti imepangwa mahitaji ya wananchi ni Watumishi wetu katika eneo hili wajitahidi kuagiza dawa, dawa zipo kwa hiyo kama wanauhitaji fedha zimebaki zipo ni wao wapeleke madai yao tutoe maelekezo, wananchi wa Kamasala, Kenyamanyoli na maeneo mengine waweze kupata huduma ambayo ilitarajiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Pamoja na maelekezo yaliyotolewa kwa Halmashauri kutenga fedha kwa ajili kuyawezesha Mabaraza haya, lakini ni ukweli usiopingika kwamba Halmashauri nyingi bado hazijaona umuhimu wa kutenga fedha ili Mabaraza haya yafanye kazi zao kwa weledi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza; kwa kuwa suala kutoa maamuzi kwenye masuala ya ardhi ni suala muhimu sana: Kwa nini Serikali isichukue sasa jukumu hili kama ambavyo imechukua jukumu la kuyawezesha yale Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya ili haki iweze kutendeka vizuri? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Wajumbe wa Mabaraza haya wanapoteuliwa, wanapewa semina ya masaa kadhaa, baadaye wanaapishwa, lakini semina ya masaa kadhaa kwa mtazamo wangu haitoshi kwa watu wanaofanya kazi muhimu ya kutoa maamuzi kama haya: Kwa nini Serikali isije na mpango mahsusi wa mafunzo kwa Wajumbe hawa ili waweze kufanya kazi yao kwa weledi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni kweli kwamba mabaraza haya yanasimamiwa na Halmashauri na Mheshimiwa Mbunge anasema Serikali ichukue jukumu hili la kusimamia Mabaraza ya Kata. Katika mgawanyo wa kazi kwa maana ya Ugatuzi wa Madaraka (D by D) tumegawana kwamba Halmashauri itasimamia Mabaraza ya Kata ya Ardhi halafu na Serikali Kuu itaanzia ngazi ya Wilaya kwenda kule juu na Mheshimiwa Mbunge ni Diwani katika Halmashauri yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kwamba, Mabaraza haya hata baada ya kuwa yameteuliwa, usimamizi wake na uangalizi unasimamiwa na Halmashauri chini ya ulezi wa Mwanasheria wa Halmashauri zetu. Kwa hiyo kama kuna upungufu katika eneo hili ni muhimu kama Mheshimiwa Mbunge anavyosema tuchukue hatua na kuelekeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe maelekezo hapa kwa Wakurugenzi wote na Waheshimiwa Wabunge mtusaidie. Kwenye Bajeti ambayo inatengwa pale, mpaka wameelekezwa vikao vingapi wakae katika maeneo hayo ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka. Kwenye Bajeti ambayo inaendelea sasa tupitie: Je, kipengele hiki kimewekwa katika Bajeti yetu? Kama kuna tatizo, Bajeti ikifika hapa tuwasiliane ili tuweze kufanya marekebisho hayo. Wakurugenzi wana wajibu huo wa kusimamia, kutenga fedha na kuwezesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili Mheshimiwa Mbunge anataka kujua kwamba mafunzo yanatolewa kwa muda mfupi sana, lakini suala la mafunzo ni jambo endelevu. Kama kuna upungufu katika eneo lile Mwanasheria na Viongozi wa Halmashauri; na kama wanashindwa wataomba usaidizi katika ngazi ya Taifa, wanaweza kufanya mafunzo kadri inavyohitajika kutoka muda hadi muda mwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ndiyo maelekezo ya Serikali, naomba wazingatie. Kama kuna upungufu tuwasiliane tuweze kuchukua hatua kwa maana ya case by case. Ahsante.
MHE. TUNZA I. MALAPO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa bahati nzuri nimewahi kwenda mara kadhaa kwenye Mabaraza ya Kata. Pamoja na kwamba Mheshimiwa Naibu Waziri amesema Mwanasheria wa Halmashauri anasimamia Mabaraza hayo, lakini kiukweli kabisa hakuna usimamizi wa kisheria unaopatikana pale. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali langu: Je, Serikali iko tayari kuweka utaratibu mahsusi ili kusudi Mwanasheria apatikane wa kueleza na kuhakikisha wananchi wanatendewa haki kwa sababu unakuta Baraza la Kata linahukumu kesi ya shilingi milioni 10 wakati wao mwisho wao ni shilingi milioni tatu. Ni kwa sababu ya kukosa Mwanasheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kujua, Serikali imejipangaje kuhusu hilo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Siyo kweli kwamba Wanasheria hawasimamii haya Mabaraza ya Kata. Kama nilivyosema, kwenye majibu yangu yaliyotangulia hapa, kama kuna malalamiko kwenye eneo specific, Mheshimiwa Mbunge ni vizuri akataja ili tuweze kuchukua hatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nina mfano. Kule Kivule tulikuwa na shida kwenye Baraza la Kata, tulimwita Mwanasheria wa Halmashauri ile ya Manispaa ya Ilala akaja akasikiliza malalamiko yaliyokuwepo, gharama kubwa ya uendeshaji wa kesi, uonevu na kuvuka kiwango ambacho kimewekwa kwa mujibu wa sheria, tulivunja Baraza tukaweka viongozi wengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama kuna malalamiko katika eneo mahsusi tupewe taarifa. Vilevile tujue kwamba Wanasheria wako kwa mujibu wa Sheria hii ili haya Mabaraza ya Kata na yanaendeshwa kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1985 na imeendelea kufanyiwa marekebisho kadri muda unavyoenda.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kama kuna malalamiko, lazima tuchukue hatua. Hata hivyo, Mwanasheria wa Halmashauri ana uwezo, kwa sababu hazungumzi mtu mmoja, Idara ya Sheria kwenye Halmashauri ina wajibu huo. Ila kama kuna Mwanasheria kwenye Halmashauri yoyote hapa Tanzania, ameshindwa kufanya wajibu wake na haendi kila siku, Mbunge umepeleka malalamiko, wananchi wamelalamika, wamehukumu kesi kinyume na utaratibu, tupe taarifa tuweze kuchukua hatua kwa Mwanasheria huyo wakati wowote kuanzia sasa. Ahsante.

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa. Kwanza namshukuru Naibu Waziri, TAMISEMI kwa kujibu vizuri. Pia pamoja na hiyo aliyosema Naibu Waziri, changamoto hii kama Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pia tumeiona kwa sababu watu wale mashauri yao mengi yanahusiana na ardhi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, Wizara yetu kwa kusaidiana na Msajili wa Mabaraza, akishirikiana na Wanasheria katika Halmashauri, tumeweka utaratibu wa kutoa mafunzo kwa zile Kamati zote za Mabaraza ya Ardhi ya Kata pamoja na Vijiji ili kuweza kuwapa elimu na ukomo wa namna wao wanavyotakiwa kusimamia. Kwa sababu wanapokwama, mashauri mengi yanaenda kwenye Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumeona kwamba tujenge msingi kule chini ili watu waweze kufanya kazi zao vizuri kwa weledi ili kupunguza malalamiko ambayo Waheshimiwa Wabunge wanayasema.
MHE. ENG. EDWIN A. NGONYANI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nitoe shukurani za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa makubwa aliyoyafanya katika Wilaya ya Namtumbo. Alipofika tarehe 5 Aprili, 2019 katika Kijiji cha Nchomoro katika mambo ambayo wananchi walimlalamikia ni pamoja na kutaka maeneo ya kulima mpunga katika maeneo ambayo wamezoea kuyalima. Maeneo hayo ni Luvele, Bomalili, Nahimba, Makangaga na Mpigamiti katika Kijiji cha Nchomoro na Nangunguve, Namayani na Mkuti katika Vijiji vya Mteramwai na Songambele pamoja na eneo la Nandonga la Kijiji cha Likuyu Sekamaganga. Jibu ambalo Mheshimiwa Rais alilitoa linafanana kabisa na kauli iliyotolewa na Mheshimiwa Naibu Waziri, nashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, tatizo langu tu katika utekelezaji, Halmashauri pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya bado hawajapata fedha za kupitia upya hayo maeneo ili kupata maeneo ya kilimo, ufugaji pamoja na hifadhi na hivyo kuondoa mgogoro huo moja kwa moja lakini fedha za kufanya doria kila wakati zinapatikana. Sijui suala hili la fedha kama Wizara inaweza kutusaidia zipatikane ili tatizo hili liondoke moja kwa moja? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, mimi kama Mbunge wao katika maeneo hayo kila napopita changamoto hii ya kukosa ardhi ya kilimo hasa kilimo cha mpunga katika maeneo yote yanayozunguka hifadhi za Mbalang’andu, Kimbanda na Kisungule ndiyo kubwa. Dawa pekee ni kupitia upya mipaka ya maeneo hayo na kupata maeneo rasmi ya kilimo, uhifadhi na mifugo. Je, ni lini Serikali itatusaidia kuondoa hili tatizo moja kwa moja kwa kufanya hayo mapitio haraka inavyowezekana kama makubaliano yalivyokuwepo toka awali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ngonyani, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuwasemea na kuwatetea watu wake ili kupunguza migogoro kati ya wafugaji na wakulima katika Jimbo lake na maeneo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la msingi anataka kujua kwa nini ahadi ya Mheshimiwa Rais haijatekelezwa lakini pia kazi ya kupitia na kutenga maeneo haijafanyika kwa maana ya Halmashauri na Mkuu wa Wilaya labda kama kuna upungufu wa fedha. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika mambo ambayo hatuwezi kufanya mchezo nayo ni pamoja na kuchezea ahadi za Mheshimiwa Rais kama amepita mahali na kuahidi. Kwa hiyo, naomba nimuelekeze Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo na Mkurugenzi wakae pamoja wajadiliane, watuambie changamoto iliyopo ili tuweze kusaidiana kwa pamoja na Wizara kuondoa changamoto hii lakini pamoja na kuondoa kero kwa wananchi wale na magomvi yasiyokuwa na lazima lakini kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais katika eneo hilo la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili Mheshimiwa Mbunge anauliza namna ambavyo tuliweza kusaidia kupima maeneo haya kuondoa changamoto mbalimbali katika mazingira ambayo ameyazungumza. Mheshimiwa Mbunge tumeshazungumza juzi na jana na Mheshimiwa Waziri ameshalipokea hili, tumetoa maelekezo maeneo yote ambayo kuna migogoro hii ya ardhi kama kuna changamoto ya fedha, mambo ya mipaka na vitu mbalimbali viangaliwe. Ndiyo maana Mheshimiwa Rais amechukua hatua hata maeneo ya hifadhi zile za Taifa (National Parks) ametoa maelekezo Mawaziri wamepita kuchukua changamoto mbalimbali. Mheshimiwa Rais angependa wananchi wakulima na wafugaji wapate maeneo yao, mipaka itambuliwe na waishi kwa amani bila magomvi ili waweze kujiletea maendeleo. Mheshimiwa Mbunge naomba utupe fursa tuifanyie kazi, viongozi wa eneo hili watoe taarifa, tushirikiane pamoja na tuondoe changamoto katika maeneo haya ya mipaka. (Makofi)
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ningependa kuuliza swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya Mtaa, lakini ukiangalia kazi kubwa anayoifanya katika kusimamia majukumu mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuwanganisha wananchi kwenye Mtaa wake pamoja na kusimamia ulinzi na usalama kwenye Mtaa wake, kiwango cha posho wanazopewa na Halmashauri ni kidogo…

SPIKA: Sasa swali.

MHE. HAMIDA M. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, napenda kujua, ni lini sasa Serikali itaongeza kiwango hiki cha posho wanayopata ya shilingi 10,000/= kulingana na kazi ambayo wanaifanya?

Mheshimiwa Spika, swali la pili la nyongeza, napenda kujua kwamba Waheshimiwa Madiwani sasa wanadhaminiwa kukopeshwa mikopo kutoka kwenye vyombo vya fedha: Ni lini sasa Serikali itasimamia kuhakikisha kwamba Wenyeviti nao wanakopeshwa katika vyombo vya fedha? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, swali la kwanza anazungumzia kiwango cha posho kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa. Kama ambavyo nimejibu kwenye swali langu la msingi ni kwamba ni kweli kwamba Wenyeviti hawa wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wanafanya kazi kubwa na Serikali inawadhamini.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, mapato ambayo wanapewa ya asilimia 20 ni makusanyo katika Halmashauri husika. Hivi viwango vya shilingi 10,000/=, shilingi 20,000/=, shilingi 50,000/= mpaka shilingi 100,000/= vinategemeana pia na uwezo wa Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wengine wote, kadri tunavyokuwa tunabuni vyanzo mbalimbali kwenye Halmashauri zetu, zikipata uwezo mkubwa Wenyeviti hawa watapata posho kulingana na mapato ya ndani kulingana na Sura ya 290 ya fedha za Serikali za Mitaa kama nilivyotaja.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, anauliza ni lini Wenyeviti wataanza kupata mikopo? Yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbunge amesema hiki kiwango ni kidogo na wakati mwingine ni kweli kwamba Wenyeviti wa Mitaa wanaendelea kudai. Kwa hiyo, namna ya kurejesha ukikopeshwa fedha benki inakuwa na ugumu wake, inaonekana mapato pia hayana uhakika. Halmashauri wanaweza wakapata kiasi kidogo, wakapata kidogo. Wakati mwingine kulingana na msimu wakapata fedha nyingi, wakapata nyingi kidogo. Sasa mabenki yatakuwa ni ngumu sana kuweza kuwawezesha.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuja na mpango wa kuwezesha Halmashauri kuwa na miradi ya kimkakati, Halmashauri ikiwa na uwezo mkubwa wa kutosha kuanzisha kama masoko, stendi na vitu vingine vile vikubwa itawawezesha Halmashauri kuwa na uwezo, kuwa na kipato cha uhakika na Wenyeviti wetu watakopeshwa na watasimamiwa na Halmashauri na Waheshimiwa Wabunge katika maeneo yao ya kazi. Ahsante.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili nami niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mwaka 2000 mpaka 2010 Serikali iliunda Tume ya Kushughilikia maslahi ya Madiwani na tume hii iliongozwa nami na iliitwa Tume ya Lubeleje kwa ajili ya maslahi ya Madiwani, kwamba Madiwani waongezwe posho kulingana na majukumu yao:-

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri unasema nini kuhusu kuongeza posho ya Madiwani pamoja na kuwalipa Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni nia na lengo kubwa la Serikali ikiwa na uwezo mkubwa unaotosha tungependa kuongeza posho hii ya Waheshimiwa Madiwani ili waweze kujikimu kulingana na kazi wanazofanya katika Halmashauri zetu ambazo ni kubwa.

Mheshimiwa Spika, swali la msingi hapo mwenyewe umeshuhudia, Mheshimiwa Mbunge anauliza, ni lini Wenyeviti wa Mitaa na Vitongoji wataongezwa posho?

Mheshimiwa Spika, nchi hii tuna mitaa zaidi ya 4,200 na kitu hivi; tuna vijiji zaidi ya 12,000; tuna vitongoji zaidi ya 64,000; na kila mtaa una Wajumbe sita, Kijiji kina Wajumbe 25. Ukipiga hesabu kwa ujumla wake, ni watu wengi kwelikweli; ongeza Madiwani wa Kata na Madiwani wa Viti Maalum.

Mheshimiwa Spika, naomba Waheshimiwa Madiwani waendelee kuchapa kazi, Serikali ya CCM inawaheshimu sana. Uwezo ukipatikana watapata posho, lakini tumeelekeza Halmashauri, wale Madiwani ambao wanadai posho zao na kukopwa, wasikopwe, walipwe kile ambacho kinawezekana kupatikana ili wachape kazi yao. Nakushukuru sana.
MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana katika maeneo yetu lakini wengi wao hawana ofisi na wengineo wanatumia nyumba zao kama ofisi:-

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba Wenyeviti wetu wanapata ofisi ili waweze kufanya kazi zao vizuri sana katika Halmashauri zetu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nashukuru. Ni kweli kuna baadhi ya maeneo ambayo Wenyeviti wetu wa Vijiji na Mitaa hawana ofisi, lakini wengine wamepanga katika nyumba za watu binafsi na wakati mwingine wanalazimika kufanya kazi hizo za kuhudumia wananchi katika majengo yao binafsi. Maelekezo ya Serikali ni kwamba Wenyeviti wa Mitaa ofisi zao zinasimamiwa na Halmashauri na Wakurugenzi katika maeneo yao, kwa sababu Watendaji wa Mitaa na Vijiji ni Wawakilishi na wanafanya kazi kwa niaba ya Mkurugenzi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nielekeze Halmashauri zote, kwenye bajeti zao za kila mwaka lazima watenge bajeti ya kujenga ofisi hata kama siyo zote, ndiyo maelekezo. Nasi tunaendelea kufuatilia na tuna taarifa za Halmashauri kuna baadhi wameanza kujenga ofisi hizo kwa kupitia michango mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza Waheshimiwa Wabunge pia, nimeona kwenye taarifa kwamba kwenye Mfuko wa Jimbo baadhi ya Wabunge tena wengine wa Viti Maalum wamechangia ujenzi wa Ofisi za Mitaa na Vijiji, lakini kuweka zana kama photocopy machine na kusaidia utendaji uweze kuboreshwa.

Mheshimiwa Spika, tuwahimize Wakurugenzi kile kinachopatikana kila mwaka kwenye bajeti yao na Waheshimiwa Wabunge wafuatilie, tutenge kiasi kidogo ili kuweza kupunguza shida za Ofisi za Wenyeviti wetu wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji. Ahsante.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Serikali ilichukua vyanzo vingi vya mapato katika Halmashauri zetu, kwa hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa haina mapato ya kutosha ya kuweza kujenga soko; je, kwa nini Serikali isitoe fedha kwa ajili ya kujenga soko la Mpwapwa kama vile inavyotoa fedha kujenga majengo mengine kama vile Vituo vya Afya na majengo mengine?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa mimi niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa na kwa kuwa jukumu la Mikopo ya Serikali za Mitaa ni kukopesha Halmashauri ili ziweze kujenga masoko, kujenga Vituo vya Mabasi; je, huo mpango umeishia wapi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa George Malima Lubeleje, kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kwamba kuna vyanzo vingine vilichukuliwa na Serikali Kuu kutoka Serikali za Mitaa kwa maana ya Halmashauri, lakini hizi fedha ambazo zilichukuliwa kuletwa Serikali Kuu, kwa maana Mfuko Mkuu wa Serikali ni fedha ambazo zinatumika kujenga miradi mikubwa ya Kitaifa ambayo inanufaisha maeneo yote ya nchi. Zingeachwa kama ilivyokuwa maana yake kuna Halmashauri zingine zingepata miradi zingine zingekosa miradi, kitendo cha kupelekwa Hazina maana yake fedha hizi zinasimamiwa na Serikali na inapeleka miradi mikubwa ambayo kila Mtanzania mahali popote alipo wananufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niliweke sawa jambo hilo, lakini jibu langu la swali la pili ni kwamba, ni kweli kwa sasa kuna miradi ambayo Halmashauri Kuu inapewa fedha kutoka pengine kwa Wafadhili wa nje, kadri muda ulivyokuwa unaenda miradi hii ilikuwa unapanga mipango ambayo huna uhakika nayo. Sasa Serikali imeleta Mpango Mkakati ambayo ina uhakika hata mikopo kutoka Mfuko wa Serikali za Mitaa ilikuwa ni fedha ambayo ina riba na wakati mwingine haina uhakika sana na kuna Halmashauri zingine zimekopa fedha zinadaiwa mpaka leo hawajawahi kurejesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa hiyo Serikalia imetengeneza Mkakati pamoja na Wizara ya Fedha, fedha zipo Halmashauri inaandika andiko na Mheshimiwa Mbunge ni Mjumbe katika Halmashauri yake vikao vya Kamati ya Fedha wanaainisha mradi ambao wanadhani wao utakuwa ni mkakati wao kupata fedha nyingi, wanaleta Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa unaenda Hazina unapitiwa na Wataalam, wakipata fedha hizo wataanzisha mradi mkubwa kama hilo soko Mbunge alivyosema hiyo, hiyo fedha ikipatikana watafanya miradi ambayo wana uhakika nayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, yako maeneo juzi nilikuwa Manispaa ya Moshi, wana Mradi wa zaidi ya shilingi bilioni ishirini na nane, Jiji la Dar es Salaam wana bilioni hamsini na nane, maeneo mengine bilioni kumi na sita, kumi na saba, kumi na nane, kwa hiyo fedha zipo Mheshimiwa Mbunge na Halmashauri husika waandae Andiko la Kimkakati, tufanye tathmini wapate fedha wajenge mradi ambao utapata fedha za uhakika ili waweze kufanya miradi ya maendeleo katika eneo lao. Ahsante.
MHE. QAMBALO W. QULWI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mji wa Karatu ni Mji wa Kitalii na ni mji ambao unakua kwa kasi sana, lakini bahati mbaya mji huo hadi wa sasa hauna soko la uhakika, Halmashauri kwa kutumia mapato yake ya ndani imeanza ujenzi wa soko la kisasa, je, Serikali lini itaunga mkono jitihada hizo za Halmashauri ya Karatu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Qambalo Mbunge wa Karatu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba Halmashauri zote hizi Wakurugenzi wameelekezwa, wameitwa Dodoma Wakurugenzi wote nchi nzima, Waweka Hazina, Maafisa Mipango wakapewa utaratibu, Serikali inachofanya kama soko lenu mnadhani kwamba linakidhi viwango walete kama nilivyosema andiko ili fedha zitolewe waweze kufanya kazi, wanakopeshwa fedha, wanawekeza, wanasimamia wenyewe, wanaanza kurejesha kidogo kidogo. Hiyo ni fedha ambayo ina uhakika tofauti na kuahidiwa bilioni kumi halafu haiji au unapata bilioni moja. Fedha za Miradi ya Kimkakati zipo, walete andiko tupitie, wapate fedha wasimamie na Mheshimiwa Mbunge awepo ili wapate fedha ya uhakika na soko lisimame wapeleke huduma na kupata mapato mema ya kujenga Halmashauri yao.
MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Kama ulivyo Mji wa Mpwapwa kuna Mji wa biashara unaitwa Endasak Wilaya ya Hanang ni mahali ambapo wanahitaji soko kama hilo wanalolihitaji Mpwapwa, naomba kujua kwa Mheshimiwa Waziri ni nini kitakachofanyika kushirikiana na Halmashauri yetu pale tujenge soko kwa sababu imezungukwa na vitunguu saumu, vitunguu maji, makabichi na nini na hakuna soko, Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA) Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, Mbunge wa Hanang kama ifuatavyo:-

Naomba majibu haya pia yaende kwa Waheshimiwa Wabunge wote ambao wana maswali yanafanana na hayo; maelekezo ni kwamba Wakurugenzi na Wataalam wetu katika Halmashauri wameelekezwa, hii ni fursa tunaomba waitumie. kila Halmashauri inaangalia fursa ya kibiashara iliyopo, kuna wengine wameandika Miradi ya Kimkakati kujenga masoko, wengine wamependekeza kujenga stendi na miradi mbalimbali kama hiyo na wale ambao wamefanikiwa tunavyozungumza fedha wamepewa wanaendelea na ujenzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa wengine wote Halmashauri zote walete maandiko katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa pamoja na Hazina tutapitia, fursa iliyopo waitumie, fedha hizi zipo pale, isipokuwa wale ambao walileta mkakati wakapewa fedha na fedha zile hawakuzitumia, maelekezo yametoka vinginevyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, waandike haraka andiko lao, washirikishe Wataalam wao, Waheshimiwa Wabunge washiriki, fedha zipo waanzishe miradi ya kimkakati tupate fedha za uhakika ili kukamilisha miradi ya maendeleo ya wananchi na kuondoa kero katika maeneo yetu. Ahsante.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Serikali haioni kwamba imewavuruga Walimu wa sekondari ambao wamesomea kufundisha watu wa rika ya sekondari na kuwapeleka katika elimu ya msingi, haioni kwamba imewachanganya na imeshusha morari ya utendaji kazi zao? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali haioni umuhimu wa kuajiri Walimu ambao wako mtaani hawajaajiriwa kwa kukosa ajira kwa muda mrefu, kwa nini wasiwaajiri Walimu hawa wakaenda kufundisha shule za msingi katika ngazi ambayo wao wameisomea? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwakagenda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza anazungumza kwamba tunashusha morari, siyo ya kweli, hayo yalikuwa ni mapokeo tu, sisi wengine Walimu tunafahamu kwanza mzigo wa kufundisha sekondari na shule ya msingi unatofautiana, ni heavy duty sekondari kuliko shule ya msingi, ile inawaelekeza kwamba watu walipopelekwa pale hatukuwa na maandalizi mazuri, watu wakapokea tofauti, lakini waliopokea vizuri wameendelea kufundisha na hakukuwa na shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo kupanga Mwalimu afundishe shule ya msingi au shule ya sekondari siyo kushusha morari yake, hili tu nimesema kulikuwa na upungufu mkubwa, kama Serikali, kama una watu zaidi ya 11,000 wako wanafundisha vipindi vichache sana kwa siku na kuna Walimu katika shule ya msingi wanafundisha vipindi vingi, ilikuwa ni busara kutumika kuwapeleka kule kufundisha, lakini tumeshachukua hatua, tuliwaelekeza Maafisa Elimu wa Mikoa na Halmashauri zetu, wakakaa wakazungumza nao wanaendelea kufanya kazi vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la ajira, ni kweli kwamba tuna upungufu mkubwa wa Walimu katika shule za msingi na sekondari, lakini juzi hapa tumeajiri Walimu 4,500, tumeomba kibali cha Walimu 22,000 hasa masomo ya shule za msingi, masomo ya fizikia na hisabati katika maeneo hayo. Kwa hiyo, kadri Serikali itakapopata uwezo ndivyo inaweza kuajiri, huwezi kuajiri tu kwamba kuna Walimu mtaani, hapana, lazima uajiri Walimu lakini wapate stahiki zao na uwezo wa kuwalipa kila mwisho wa mwezi pamoja na mahitaji mengine. Ahsante.
MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lako Tukufu kila mwaka linatenga jumla ya shilingi elfu 10 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi. Katika fedha hizo shilingi elfu sita zinapaswa kwenda moja kwa moja kwenye mashule na shilingi elfu nne zinakwenda TAMISEMI kwa ajili ya ununuzi wa vitabu, lakini Serikali inafahamu kwamba katika mpango wa GEP, Serikali ilipata zaidi ya shilingi bilioni 45 kwa ajili ya kununua vitabu, na kwa jumla ya idadi ya wanafunzi waliopo nchini wa shule za msingi, kuna zaidi ya shilingi bilioni 144 zilipaswa zinunue vitabu na shule hazina vitabu na kuna vitabu ambavyo viliondolewa, Serikali….

NAIBU SPIKA: Uliza swali.

MHE. KABWE Z. R. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali haioni kwamba, ni muafaka sasa kufanya ukaguzi maalum ili kuweza kutambua jumla ya fedha hizi shilingi bilioni 190 zimetumika namna gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, katika uchunguzi uliofanywa kwenye jumla ya halmashauri za wilaya 12 hapa nchini, katika shilingi elfu sita inayopaswa kwenda kwenye mashule kwa kila mtoto, fedha inayofika, kwenye hii sample ya wilaya 12 ni shilingi elfu 4200 tu. Serikali haioni haja ya kufanya ukaguzi maalum ili kuweza kufahamu hii shilingi 1200 ambayo haifiki kwenye shule inakwenda wapi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza si kweli kwamba TAMISEMI tunanunua vitabu, tumegawana kazi, suala la vitabu na kiwango chake na ubora wake linafanywa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kwa kuwa ameuliza swali la kitakwimu na Mheshimiwa Naibu Waziri mwenzangu yupo hapa, basi unaweza ona namna ya kutenda hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini suala la kujibu hapa ni kwamba, Mheshimiwa Zitto, anasema halmashauri zimekaguliwa, sisi kama Serikali hatuna taarifa ambayo anaizungumzia hapa Mheshimiwa Zitto, kwamba fedha
hazifiki katika shule zetu, na Mheshimiwa Zitto Kabwe, bahati nzuri kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya LAAC, Halmashauri ya Kigoma Ujiji ambayo ni Halmashauri ya chama chake cha ACT, ndiyo halmashauri ambayo imekuwa na hati chafu miaka minne mfululizo, lakini vilevile miradi ya elimu iliyopo pale, ina hali mbaya kweli kweli. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama kuna halmashauri imekaguliwa tuna takwimu za kutosha ni halmashauri ya Mheshimiwa Mbunge. Jibu ni kwamba, hakuna taarifa ambazo anazitoa, siyo za kweli, hakuna ukaguzi uliofanyika mahususi na hakuna malalamiko ambayo yameletwa kwamba Serikali tufanye ukaguzi maalum, tukipata taarifa hizo na maombi hayo, Serikali itachukua hatua kufanya ukaguzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukaguzi wa fedha ya elimu na miradi ya Serikali inafanyika kila wakati, kuna Kamati za Bunge, imeenda TAMISEMI, imeenda watu wa Ustawi wa Jamii wamekagua na taarifa zipo. Kila wakati tunachukua hatua kabla ya bajeti na baada ya bajeti hii ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Zitto kasema kwamba fedha za Global Partners for Education dola milioni 46 zinatumika kwa ajili ya vitabu. Naomba nimfahamishe kwamba, fedha hizo zinatumika kwa ajili ya kuendeleza sekta ya elimu kwa ujumla na siyo specific kwa ajili ya vitabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia naomba nimhakikishie kwamba, fedha zote ambazo zinakwenda kwenye vitabu, zimeenda kwenye Taasisi yetu ya Elimu na kwa sasa tumefikia sehemu ambayo karibia vitabu vyote vinapatikana. Kuna vitabu ambavyo tunaendelea kuvichapisha lakini kwa sehemu kubwa vitabu vinapatikana sasa isipokuwa kama kuna changamoto kwenye halmashauri moja moja, inakuwa ni kesi ambayo ni specific lakini kwa ujumla kwa sasa tumeshaondokana na shida ya vitabu, tulichapisha vitabu vipya na tena vitabu ambavyo havina makosa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini zaidi, ninaweza nikakutana na Mheshimiwa Zitto nimueleweshe zaidi kwa sababu takwimu yeye ndiyo kaja nazo ambazo ziyo takwimu za Serikali, kwa hiyo, akitaka ufahamu zaidi anaweza akakutana na mimi nikamfahamisha.
MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, katika kuibadilisha dunia, ku-transform dunia, kigezo cha elimu kimepewa kipaumbele namba nne na kigezo cha elimu bora. Je, fedha hizi zaidi ya bilioni 900 ambazo zimekwenda kwenye shule zetu, kigezo cha kupima zimefanikisha kwa kiasi gani ubora wa elimu na viashiria vyake vyote ukoje!
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS (TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tumepeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 900 kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi la swali la Mheshimiwa Zitto, na Mheshimiwa Mbunge anataka kujua vigezo vya kuonyesha kwamba elimu imeboreka ni kwa kiwango gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza, fedha hii inafanya mambo mengi sana ikiwepo ni pamoja na uendeshaji wa shule, usimamizi wa elimu Tanzania umeimarika sana. Tumenunua pikipiki katika Waratibu Elimu wa kata zote nchini, sasa wanaweza ku-move kutoka shule moja kwenda nyingine, maana yake ni kwamba hata utoro rejareja umepungua shuleni, kiwango cha watoto kupata mimba na kuchukua hatua, tuna kesi mbalimbali mahakamani na baadhi ya watu ambao wametuhumiwa kuwapa wasichana wetu mimba wameshafikishwa mahakamani na wengine wamefungwa, kesi ziko katika hatua mbalimbali. Hiyo ni kwa sababu fedha hiyo imekwenda, imepeleka vifaa vya utendaji, pikipiki na imewezesha.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili, tumejenga hosteli maeneo mbalimbali, kitendo ambacho kimepunguza watoto wa kike wengi sasa wanakaa katika shule zetu na utaangalia matokeo mbalimbali, darasa la saba, form four na form six, kiwango cha ufaulu cha watoto wa kike kimeongezeka sana. Tumejenga mabweni na hosteli maeneo mbalimbali, watoto wa kike wengi wanakaa katika maeneo ya shule na usimamizi wao umekuwa ni mzuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini elimu msingi bila malipo, sasa hivi tunapozungumza, vijana wetu wa kidato cha nne wanafanya mitihani. Mwaka 2018 wanafunzi ambao walisajiliwa, watahiniwa wa kufanya mitihani, walikuwa 427,000, mwaka huu ni 485,866, maana yake ni ongezeko la wanafunzi ambao wameingia kidato cha nne zaidi ya asilimia 1.37, huu ni ufaulu mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vijana wengi wa Tanzania maskini ambao walikuwa hawana uwezo wa kusoma wa kike na wakiume, wengine walifanya kazi za house girl, wengine walikuwa makuli kwenye masoko, walikuwa wapiga debe, ninapozungumza hapa, vijana wengi kitendo cha Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuondoa ada katika masomo yao, watoto wengi wapo mashuleni, hata wananchi ambao wanataka ma-house girls wanapata shida sana kuwapata, vijana, wasichana wengi wanasoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ni kwa uchache, lakini Mheshimiwa Mbatia ni kweli kwamba, yeye anafahamu, hata matokeo ya form six yameongezeka, elimu ya high school imekuwa ni kubwa sana, kwa sababu ya fedha hizi ambazo zimekwenda kuimarisha huduma. Ndiyo maana, hata wananchi ambao walitoa nguvu zao kuchangia kujenga maboma, tumepeleka fedha zaidi ya bilioni 29, angalia halmshauri zote nchini ili tumalize maboma, watoto wetu waendelee kukaa katika madarasa ambayo yapo sawa na wapate matundu ya vyoo. Ahsante.
MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kumekuwa na matumizi ya hovyo kabisa katika halmashauri zetu na kupelekea halmashauri hizo kupata hati chafu. Kwa mfano, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga imepata hati chafu kwa mwaka mmoja, mimi najiona kama natembea bila nguo, lakini halmashauri kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri, Halmashauri ya Ujiji ambayo inaongozwa na ACT anapotoka Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe, miaka minne mfululizo imepata hati chafu wakati yeye akishinda twitter na instagram. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzifuta halmashauri hizi? (Kicheko)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge wa Ulanga, alikuwa anasema maneno mengi sana hapa Bungeni wakati mwingine akaonekana kwamba ni kituko, lakini naomba niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge, kauli ya Mheshimiwa Mbunge wa Ulanga imetusaidia sana TAMISEMI na watu wengi wamewajibishwa katika halamshauri ile na uchunguzi mahususi umefanyika tukagundua kuwa ni kweli kwamba watumishi wetu wamwekuwa wabadhilifu, fedha nyingi zililiwa, kama alivyokuwa analalamika.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, ni kweli, Kamati ya Bunge ya LAAC wapo, Mwenyekiti yupo hapa na Wajumbe wenzake wanafamu. CAG alipopitia baadhi ya halmashauri, hata mimi nilishangaa, halmashauri mbili, wamepoteza fedha zaidi ya shilingi bilioni kumi na kitu, lakini Halmashauri ya Kigoma Ujiji, halmashauri hii imekuwa na hati chafu mfululizo miaka minne, lakini tulipowahoji viongozi wa pale, wakatuambia viongozi wetu wa kisiasa, wanaingilia mpaka manunuzi ya kisheria, mpaka tenda ambazo zinagawanywa pale Kigoma Ujiji, wanapewa kwa itikadi za kivyama, hizi ni taarifa rasmi za Bunge, ninazozitoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumetoa maelekezo, ni kweli kwamba, ile halmashauri ikiendelea kupata hati chafu ya tano na itapewa ukaguzi mahususi, kuna uwezekano mkubwa Mheshimiwa Zitto halmashauri yako kufutwa kwa sababu husimamii vizuri, na wewe ni mtaalam wa mahesabu. Ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, hoja ya msingi hapa ni kwamba tunayo changamoto siyo tu katika Jimbo hili, lakini katika Majimbo mengine pia ya namna ya kusaidia hasa watoto wa kike kuwapunguzia suluba wanayoipata ya kwenda shuleni na kurudi, ndiyo maana hawa wananchi wa Msalala wakawekeza fedha kwa ajili ya kujenga mabweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jibu la Serikali ni kwamba mnasaidia kwenye shule ambazo zinachukua wanafunzi wa kitaifa. Hawa ambao wako wengi kwa nini Serikali haioni iko haja sasa ya kuwekeza hata kwenye hizi shule ambazo zinachukua katika eneo dogo lakini kwa lengo la kuwasaidia mabinti zetu wapate mahali pa kukaa na kupata masomo yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; uwekaji wa miundombinu katika hizi shule na hasa suala la umeme kwa maeneo mengi kwa miradi ya REA imekuwa kama ni hisani ya Wakandarasi, kwa sababu wanaambiwa wakipata nafasi waweke. Maeneo mengi ushahidi unaonesha kwamba hawafanyi mpaka ambapo panakuwa na msukumo maalum. Serikali haioni umefika wakati sasa suala la kuweka umeme kwenye shule liwe ni suala la lazima kwa Wakandarasi waliopewa miradi ya REA na iwe ni kazi ambayo inafanyika bure badala ya kuwa sasa hivi inafanyika kama hisani?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni kweli kwamba nia njema ya Serikali kama tungekuwa na uwezo mkubwa tungepeleka mabweni ama mabwalo katika shule zetu hizi za kutwa. Tumesema hizi shule za kutwa zipo karibu na makazi ya wananchi na tumeelekeza pia Waheshimiwa Wabunge, wananchi wengine na wazazi waendelee kuchukua tahadhari juu ya kulinda watoto wa kike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeanza na hizi shule za mabweni za Kitaifa kwa sababu wanafunzi wanatoka maeneo ya mbali sana katika makazi yao huku majumbani kwao kwenda katika hizi shule. Naomba tupokee ari ya Mheshimiwa Mbunge na maoni yake; tukipata uwezo wa kutosha tutafanya kazi na tungependa pia watoto wetu waendelee kusoma vizuri. Ni kweli kwamba kumbukumbu zinaonesha watoto wengi wa kike hawamalizi shule kwa sababu wanapewa mimba wakati wa kutoka nyumbani kwenda shuleni na wakati wa kurudi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anazungumzia habari ya umeme kupelekwa katika shule zetu za sekondari za Umma. Ni kweli kwamba tumepata malalamiko mengi katika maeneo mbalimbali, nami nimefanya ziara maeneo hayo. Walimu wetu, Wenyeviti, wazazi, viongozi, Madiwani na Wabunge wanalalamika kwamba kunakuwa na bill kubwa pia ya kuunganisha umeme katika shule zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tumesikia mara kadhaa Mheshimiwa Waziri wa Nishati akitoa maelekezo. Tupokee wazo hili pia, tuongee na viongozi wenzetu wa Wizara ya Nishati ili ikiwezekana umeme upelekwe kwenye maeneo ya Umma tena iwe ni bure kwa sababu hii ni huduma ya Serikali. Shule za Serikali, vijana wa Kitanzania, Serikali ni ya kwetu, ipo namna ya kulifanya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli tungependa unapopeleka umeme katika maeneo ya shule za jirani, hata vijana ambao wanakaa maeneo ya jirani, hata wakati wa usiku wanaweza wakajisomea kujiandaa na mitihani yao na kufanya discussion mbalimbali hata kutoka shule mbalimbali za jirani katika maeneo hayo. Ahsante.
MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Lupembe, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ina shule tatu zenye Kidato cha Kwanza mpaka cha Sita; Shule ya Lupembe Sekondari, Magilu Sekondari na Itipingi Sekondari. Katika shule hizi zote kuna uhaba mkubwa sana wa vyumba vya madarasa na mabweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye shule moja hii ya Itipingi wananchi wameshaanza kujenga bweni moja ambalo sasa hivi limefikia kwenye hatua ya lenta: Je, Serikali ipo tayari kutoa fedha kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hawa ili waweze kukamilisha mabweni na hawa vijana waweze kuishi katika mazingira mazuri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni kweli kwamba Waheshimiwa Wabunge wengi na wadau mbalimbali wamejenga maboma mengi katika maeneo yao ya Shule za Sekondari na Msingi, kwa maana ya maboma ya shule lakini pia na maboma ya kujenga mabwalo na mabweni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka huu wa fedha uliopita tumetoa shilingi bilioni 29.9 kukamilisha maboma ya nchi nzima zaidi ya maboma 2,900. Naomba niwaahidi mwaka huu pia, kwenye bajeti ambayo nimesema kwenye jibu langu la msingi tumetenga shilingi bilioni 58.2, pamoja na mambo mengine fedha hiyo imejumuishwa na fedha ya kwenda kukamilisha maboma, mabweni, mabwalo, nyumba za walimu lakini pia na matundu ya vyoo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge nikutie moyo kwamba wakati ukifika wa kusambaza hizo fedha tutaendelea kuwa tunawasiliana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Waheshimiwa Wabunge, fedha zinapoenda katika maeneo yenu, ni muhimu mkapendekeza maeneo ya vipaumbele. Tumepeleka fedha ya kukamilisha maboma, lakini fedha nyingine zimerudishwa kwa sababu kuna shule zimepelekewa kumbe hazikuwa na maboma. Fedha ambayo inapelekwa na Serikali ni kukamilisha maboma na siyo kuanza ngazi ya msingi mpaka kwenye lenta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu ya Mheshimiwa Waziri anasema kutakuwepo na uchaguzi wa huru na haki. Nataka nimwambie tu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 3(1) inasema, “Tanzania ni nchi ya kidemokrasia yenye kufuata mfumo wa vyama vingi.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwepo na malalamiko kila kona juu ya tabia mbaya iliyoonekana, kuhusu kuondolewa kwa Wagombea wa Upinzani hasa katika uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa unaofanyika tarehe 24 kwa vyama vya ACT Wazalendo, CUF, CHADEMA, NCCR-Mageuzi. Imeonekana huu ni mkakati maalum wa Serikali katika kudhoofisha upinzani hapa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwomba Mheshimiwa Waziri utuambie, mna makakati gani wa ziada kuhakikisha kwamba tabia hii mbaya, chafu iliyofanywa makusudi na Serikali kwamba wagombea hawa wa upinzani wanarejeshwa na wanashiriki uchaguzi tarehe 24 mwaka huu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili,…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Masoud, hilo siyo swali.

MBUNGE FULANI: Ni swali.

MWENYEKITI: Endelea swali lingine.

MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Waziri mhusika, Mheshimiwa Jafo alisema, wasimamizi wa uchaguzi na wote waliohusika kuwaondoa Wagombea wa Upinzani, wasilikilize malalamiko hayo na baadaye kutoa haki ambayo italeta tija katika uchaguzi huu ndani ya mfumo wa vyama vingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uniambie, pamoja na kauli ya Waziri ambapo hadi sasa baadhi ya watendaji hawa, wasimamizi wanakimbia katika ofisi: Je, mna mkakati gani wa kuhakikisha kwamba maandalizi haya yataweza kufanikisha uchaguzi huu na ukawa wa haki na huru?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Hili swali ni muhimu kwa ajili ya uelewa. Nalitumia jukwaa lako ili uniruhusu nitoe elimu pia kwa wale wote ambao hawajaelewa utaratibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni kwamba Waheshimiwa Wabunge wamelalamika sana kwenye Bunge hili, naomba niwaarifu kwamba Wabunge hawana haki ya kuweka pingamizi wala kulalamikia uchaguzi kama wametendewa haki ama lah! Wenye haki ya kulalamika ni wale watu wote ambao walijaza fomu na kusema wameondolewa. Utaratibu umeainishwa vizuri kwenye Kanuni yetu na Waheshimiwa Wabunge na Vyama vya Siasa wamepewa Kanuni hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, muda wa vipingamizi haujaisha. Kanuni imeeleza, baada ya uteuzi, kuanzia tarehe 5 mpaka tarehe 6 ambayo ilikuwa ni jana, wale wote ambao wamekuwa hawajaridhika na uteuzi au kuondolewa ama kuteuliwa kugombea walipaswa wapeleke pingamizi kwenye Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi. Kama hawajaridhika na maamuzi hayo, pia wanayo fursa mpaka tarehe 9 kwenda kupeleka pingamizi kwenye Kamati ya Rufaa.

Pia kama hawataridhika na maamuzi ya Kamati ya Rufaa ambayo inapatikana kwenye ngazi ya Wilaya, wanayofursa ndani ya siku 30 kwenda kwenye Mahakama yoyote kuanzia na wilaya kwenda kuweka pingamizi kuweza kupata haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hayupo hapa Bungeni leo, lakini jana alikuwa Singida. Yanayozungumzwa Bungeni na kule site hali ni tofauti sana. Ameenda Manyara na sasa hivi ninavyozungumza yuko Iringa, ataenda Njombe. Tumetuma watu kule Liwale na Moshi. Mazungumzo mengi ya Waheshimiwa Wabunge humu ndani yanatofautiana sana na hali halisi kule site.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, yaliyozungumzwa hapa kuna Wabunge wamechukua clip wameweka kwenye mtandao. Nimeuliza kwa mfano Tarime Mjini, Mheshimiwa Mbunge alitoa taarifa hapa kwenye clip akisema wagombea wote wameondolewa, siyo kweli. Taarifa za leo asubuhi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge, maelekezo ya Mheshimiwa Waziri wa nchi ni kwamba, Kanuni inaelekeza, yule ambaye hajaridhika na uteuzi wake apeleke pingamizi kwenye vyombo vile na asiporidhika ndiyo aseme. (Makofi/ Vigelegele)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwatie moyo Waheshimiwa Wabunge, Waheshimiwa Watanzania, utaratibu unaeleweka, lazima ufuatwe…

MBUNGE FULANI: Wamefunga Ofisi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SRIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): …na uchaguzi huu utakuwa ni huru na haki kwa wale ambao watazingatia taratibu na sheria za uchaguzi.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu yake, anasema kwamba watumishi wanaweza kulipwa na Halmashauri lakini Halmashauri hizi hazina fedha. Kwa hiyo, nataka kujua kwa sababu Halmashauri hazina fedha Kifungu cha kuwalipa kitatoka wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na matatizo ya Bima ya Afya kwa sababu kuna wakati mwingine Halmashauri zinashindwa kurejesha fedha katika Mfuko wa Bima, kwa hiyo, kunakuwa na matatizo ya upatikanaji wa dawa. Je, tatizo hili mtalimaliza namna gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Mheshimiwa Mbunge anaulizia uwezekano uliopo wa Halmashauri kulipa. Kwanza utaratibu uliopo kama nilivyosema, ni kwamba manunuzi mengi ya dawa yanafanyika na wale Phamasists katika maeneo yetu ya wilaya. Ila kama Halmashauri ina uhitaji, huwa inaangalia pia na uwezo wake wa fedha; na kwa kawaida wanaomba kibali hapa TAMISEMI, tunawaruhusu wanaendelea kuwaajiri watu kwa mkataba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimejibu kwenye swali langu la msingi kwamba kama Serikali itapata uwezo itawajiri wawe wa kudumu panapokuwa na mahitaji, kwa kuwa tayari shughuli kubwa ya manunuzi inafanywa na wataalam wenyewe kuangalia vizuri viwango na tunawasiliana na wenzetu wa MSD moja kwa moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge alitaka kujua namna ambavyo kunakuwa na changamoto ya dawa katika maeneo haya. Hatujapata sehemu ambayo wameshindwa kununua madawa haya. Naomba tupokee hoja ya Mheshimiwa Mbunge tuifanyie kazi. Kama kuna Halmashauri imepata changamoto hii, basi tuwasiliane ili tupate namna ya kuitatua ili mradi wananchi wetu waendelee kupata huduma kama ambavyo Serikali imekusudia kuwapa huduma bora katika maeneo yao ya karibu. Ahsante.
MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa vyanzo vingi vya mapato vya Halmashauri vinaenda Mfuko Mkuu: Je, Serikali ina mikakati gani kuhakikisha vyanzo vile vya Halmashauri vinarudi kwa wakati muafaka ili changamoto ambazo zinakabili Halmashauri zipate kutatuliwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SRIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Juzi nilikuwa najibu swali hapa katika Bunge lako Tukufu ambalo liliuliza namna ambavyo Serikali imejipanga kuwezesha Halmashauri. Tukasema kwamba fedha hizi ambazo zimekusanywa kutoka maeneo ya Halmashauri yale, kuna Halmashauri kulingana na mapato yao walikuwa wanapata fedha nyingi zaidi kuliko Halmashauri nyingine na matokeo yake kuna baadhi ya maeneo mengi ya nchi yalikuwa hayawezi kupata miradi ya maendeleo hasa miradi ile mikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imejiandaa na imetoa maelekezo kwa Halmashauri zote nchini kwamba ziko fedha ambazo zitasimamiwa na Hazina, tumewaambia wataalam wetu katika Halmashauri zetu waandae miradi ya kimkakati kama ni stendi au soko kadri watakavyoona wenyewe katika maeneo yao fursa ni ipi, wakiandika andiko linakuja TAMISEMI, linapitiwa na wataalam wa TAMISEMI, linapitiwa pia na wataalam pia wa Wizara ya Fedha kupitia Hazina na baadaye wanaridhia kuanzisha mradi huo mkubwa. Mradi huo ukianzishwa ukakamilika watakuwa watakura wanarejesha lakini pia watapata fedha ambayo ina uhakika, changamoto zingine zote katika maeneo yao zitamalizika kwa sababu wana fedha ya uhakika. Tunataka wakipata fedha hizo wapange miradi ya maendeleo ili waweze kuitekeleza kwa fedha ambazo wenyewe wanazisimamia na zinapatikana kwa wakati. Ahsante.
MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Serikali inakiri kwamba, sheria na taratibu zinaruhusu uchaguzi huo; na kwa kuwa, wanatambua kwamba, maeneo mengi yalikuwa pia yana makaimu na chaguzi hizo hazikufanyika. Je, Serikali sasa inatoa maelekezo gani kwa watendaji wanaohusika ili wawe wanachukua hatua zinazostahili kwa wakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa sasa hivi tuko kwenye mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utaondoa kabisa makaimu hawa ambao wamekuwa ni kero kwa maeneo mengine na tumesikia chama kikuu cha upinzani, CHADEMA, wametangaza kujitoa katika uchaguzi huu na kuwakosesha wananchi haki yao ya kimsingi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa mujibu wa Katiba yetu na Serikali ya Vyama Vingi. Je, Serikali ina kauli gani kuhusiana na kadhia hii ambayo inaendelea nchini? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Monko, Mbunge wa Singida Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujua kwa nini nafasi hizo zilikuwa hazijazwi kama ambavyo inatakiwa na kanuni. Ni kweli kwamba, kumekuwa na nafasi wazi mpaka tunaingia kwenye uchaguzi wa mwaka huu na hii ilitokana na aidha, watendaji wetu katika ngazi zile kutokuwa na uelewa mkubwa wa kanuni zetu, lakini vilevile tumeshaelekeza sasa kwamba, tunacho chuo hapa cha Serikali za Mitaa cha Hombolo. Baada ya uchaguzi huu Wakurugenzi na sisi Wabunge tunaomba tushiriki kuhakikisha kwamba, viongozi wetu watakaopatikana wa vijiji, vitongoji na mitaa wapate mafunzo pamoja na watendaji wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ziko sababu mbalimbali zimeainishwa ambazo Mwenyekiti wa Mtaa au Kijiji au Kitongoji anaweza kupoteza nafasi yake, mojawapo ni kwamba, kama Mwenyekiti kwenye Kijiji hajasoma mapato na matumizi kwa muda wa miaka mitatu mfululizo inaweza ikamfanya akapoteza nafasi yake. Vilevile Mwenyekiti huyo kama atakuwa hajaitisha mikutano mara tatu mfululizo bila sababu za msingi, au inaweza ikaitishwa mikutano ya kisheria yeye Mwenyekiti asihudhurie katika hii mikutano, sababu nyingi ambazo zimetolewa ikiwepo kufukuzwa na chama au kufariki au kujiuzulu mwenyewe. Kwa hiyo, tunaomba tutoe wito kwamba, baada ya uchaguzi huu basi viongozi wetu ngazi husika hasa Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zetu na Miji watoe elimu, watoe maelekezo na Waheshimiwa Wabunge wakati wowote ikitokea nafasi wazi au ukahisi, tuwasiliane tutachukua hatua kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anazungumzia habari ya CHADEMA kujiondoa katika nafasi za kugombea. Ni kweli na sisi kama ofisi tumepata taarifa kwenye mitandao labda huenda wakatoa tamko rasmi, lakini Kauli ya Serikali ni kwamba, uchaguzi huu unaendelea kama kawaida kama ulivyopangwa kwenye ratiba. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utafanyika tarehe 24 Novemba, mwaka huu 2019, wananchi wote ambao wamejiandikisha na vyama vile ambavyo vipo kwenye mchakato waendelee na mchakato wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri wametoa tamko jana kwenye mitandao, lakini itakumbukwa kwamba, kwenye taratibu zetu ni kwamba, wale ambao walikuwa na malalamiko wameandika mapingamizi yao na kesho ndio siku ya mwisho, wao jana ndio wametoa tamko. Kwa hiyo, kama wamejiondoa hawana sababu yoyote ya kulalamika kwamba, hawakutendewa haki, tulieleza tukarudia mara kadhaa kwamba, watu wenye sifa ya kutoa mapingamizi ni wale ambao ni wagombea. Wenzetu walitaka watoe kauli Bungeni, kwenye mitandao, mtaani na Serikali iamue, Serikali inafanya kazi kwa karatasi kwa mawasiliano, hatuna document mezani hatuwezi kujadili jambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe wito, yale maagizo ya kuhamasisha wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo bahati nzuri Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya kazi kubwa Watanzania wanamuunga mkono. Mwenye mamlaka ya kutoa maelekezo nchini Tanzania ni Rais wa Jamhuri ya Muungano pekee na sio kiongozi wa chama cha siasa. Kiongozi wa chama cha siasa atatoa maelekezo kwenye chama chake kwa wanachama wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya ambao ni Wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama, tumepata taarifa kwenye mitandao wanahamasisha watu, wanaharibu mazao ya watu na wanatishia watumishi wa umma. Wakuu wa Wilaya popote mlipo kama kuna mtu anahisi hakutendewa haki kwenye uchaguzi huu na anafanya fujo mtaani, sheria stahiki zichukue mkondo wake. Hatujawahi kutunga sheria katika Bunge hili Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosema ukigombea ukinyimwa haki au ukahisi kunyimwa haki ukafanye fujo. Ukigombea ukinyimwa haki au ukahisi kunyimwa haki ziko taratibu za kisheria wazifuate, wasipofuata vyombo vya usalama vitashughulika nao na Watanzania wawe na amani, uchaguzi uko palepale, amani na tulivu, tunachapa kazi na hakuna ambaye atawaambia wananchi wasishiriki shughuli za maendeleo, sisi TAMISEMI tupo pale kila mahali, ukishiriki kuhamasisha fujo na viongozi wetu wachukue taarifa mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii, atakayebainika tusilaumiane mbele ya safari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu Katiba inatambua uwepo wa Serikali za Mitaa na uwepo wa Serikali Kuu. Serikali za Mitaa kwa juu zinaanzia kwenye ngazi ya Halmashauri. Je, Serikali haioni kwamba, umefika wakati sasa wa kuunganisha uchaguzi wa Madiwani na uchaguzi wa vijiji, vitongoji na mitaa ili Serikali za Mitaa wafanye uchaguzi pamoja na Serikali Kuu kwa maana ya Bunge na Rais, uchaguzi wao uwe pamoja?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nape Moses Nnauye, Mbunge wa Mtama, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba, hili jambo ni jambo la kisheria. Tunayo Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura Namba 287 na Sura Namba 288, lakini pia tuna uchaguzi wa Serikali Kuu, Wabunge na Madiwani na Mheshimiwa Rais; tupokee wazo hili tulifanyie kazi, ni jambo la mchakato, kama itawezekana kufanya hivyo ni jambo jema tutalifanyia kazi, lakini hili ni jambo la kisheria tunalipokea na kulifanyia kazi kwa mujibu wa taratibu zetu. Ahsante.
MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, ni kwa nini sasa hawa viongozi ambao mara kwa mara maana huwa tunashuhudia, kiongozi akifika mahali wanawapiga wakinyanyua mabango yao, wanapigwa, wanafukuzwa na kwa tamko hilo sasa ni kwa nini hawa viongozi wanaofanya mambo haya ya kunyanyasa wananchi wasichukuliwe hatua za kinidhamu?

Mhshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; mara nyingi huu utaratibu wa kutatua kero za wananchi, unakuta hata leo mfano Waziri wa TAMISEMI akifika pale ziko kero nyingi za wananchi yeye ndio anazitatua, au Waziri wa Ardhi akifika pale zinaonekana ziko wazi ambazo labda Mkurugenzi angeweza kuzitatua, lakini ameshindwa kuzitatua mpaka kiongozi afike pale. Hali hii sasa inaonesha dhahiri kwamba, leo baadhi ya kero nyingi zinaweza kutatuliwa tu pale ambapo viongozi wa Kiserikali au viongozi wakuu wanaenda pale. Serikali inao mpango gani wa kuhakikisha kwamba, hayo matatizo yanaisha na matatizo ya wananchi yanatatuliwa kule kwenye ngazi za wilaya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge wa Musoma Mjini, ndugu yangu, kaka yangu Vedastus Mathayo Manyinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujua ni kwa nini kuna baadhi ya watu wanazuia wananchi kutoa kero zao au kuonesha mabango ambayo yamejaa hisia za changamoto zao katika maeneo yao na amesema kwamba, wanapigwa. Tunachojua ni kwamba, Mheshimiwa Rais na viongozi wengine wakifanya ziara wamekuwa wakiruhusu maswali kujibiwa na wananchi kutoa kero zao. Tukumbushane kwamba, pia kwenye mikutano ile ambayo kiongozi hasa Mheshimiwa Rais anapokuwepo ni mkusanyiko mkubwa sana. Sasa wakati mwingine ni watu wa usalama wanaangalia mazingira yalivyo, bahati mbaya sana yale mabango hayaratibiwi, kwa hiyo, wao wanachukua tahadhari kwanza ya kiusalama halafu wakigundua kwamba, ni ya hoja genuine, wana lengo la kupeleka kero, inaruhusiwa na wamekuwa wakifanya mara kadhaa tumeshuhudia sisi wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo nitoe wito kwamba, viongozi wetu hawa kwenye maeneo yetu ya mikoa na wilaya, tunao ugatuzi wa madaraka katika nchi hii kutoka ngazi ya kitongoji mpaka ngazi ya kitaifa na hii itaenda sambamba na kujibu swali lake la msingi, kimsingi Mheshimiwa Rais ameshatoa maelekezo, tumeeleza kwamba, viongozi wetu watoke ofisini, kama ni Mkuu wa Mkoa awe na utaratibnu wa kusikiliza wananchi wake katika eneo lake husika. Kwanza akutane na Wakuu wa Wilaya kwenye mkoa wake husika na watendaji wake, anapokea changamoto katika mkoa wake, wanaweka mikakati namna ya kutatua zile changamoto, halafu badae anafanya ziara kwenda kusaidia yale ambayo yameshindikana ngazi ya wilaya wasaidiane kama mkoa kuyamaliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi maana yake ni kwamba, jambo ambalo lipo kwenye ngazi ya kitongoji limalizwe na viongozi wa kitongoji kwa tatizo husika. Jambo likitoka kwenye kitongoji kuja kwenye kijiji au mtaa liwe na uwezo huo walimalize, kwenye kata vivyo hivyo na kwenye ngazi ya wilaya na mkoa. Tukifanya kazi kwa pamoja kila mtu akaenda site, watu wasikilizwe, kero zitatuliwe, hakuna sababu ambayo itakuwepo tena Mheshimiwa Rais au Viongozi wa Kitaifa Mawaziri kwenda mahali mbalimbali kutatua kero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba nitoe wito kwa viongozi wetu kimsingi ni kuonesha kwamba, mtu huyo kwenye mkoa au kwenye kata ameshindwa kufanya kazi. Kama kuna changamoto inatolewa mbele kiongozi wa Kitaifa akiwa kwenye ziara wakati pale kuna mtu ambaye ni wa kisiasa mwakilishi, lakini pia kuna mtu ambaye ni mteuliwa wa Rais au mamlaka nyingine halafu kuna watendaji wa Serikali. Tukifanya kazi kila mtu kwa ngazi yake hii habari ya kupeana mabango wakati viongozi wamekuja haitakuwepo, tutakutana na viongozi watafanya mambo ya jumla makubwa ya Kitaifa na tutaenda na maendeleo yetu kama kawaida. Ahsante.
MHE. MARYAM SALUM MSABAHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kumuuliza Naibu Waziri swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa ma-DAS na Wakuu wa Mikoa na wateuliwa wa Rais wengi wao wengine hawataki kufuata taratibu kusikiliza kero za wananchi na hata pale wananchi wengine wanapodhulumiwa haki zao hawatatui kwa wakati, mpaka wanasubiri msafara wa Rais na kwenda kulalamika mbele ya Rais wale wananchi ambao wamedhulumiwa haki zao. Je, Serikali ina mkakati gani hawa ma-DAS na Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa wasiowajibika katika nafasi mbalimbali walizoteuliwa ili kuwahakiki na kuchukuliwa hatua za kisheria?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MIAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Maryam Msabaha, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba, kuna baadhi ya maeneo kumekuwa na malalamiko, lakini Mheshimiwa Rais alipokuwa anahutubia katika eneo la Mbarali, Mkoani Mbeya alitoa maelekezo mahususi kwamba, kila Mkuu wa Mkoa, kila Mkuu wa Wilaya, kila mteule wa Serikali na mamlaka yake mpaka ngazi ya chini waweke ratiba ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua. Zile ambazo zitakuwa zimeshindikana kwenye ngazi yao wapeleke ngazi ya juu, lakini tumeenda hatua mbele zaidi tunafuatilia, Mheshimiwa Maryam na Wabunge wengine kama kuna maeneo ambayo Mheshimiwa Rais ataenda au viongozi wengine watu wananyanyua mabango kulalamikia kero ambazo zipo ndani ya uwezo wa viongozi wale, hao watu ndio wanapaswa kimsingi kuondolewa katika nafasi hiyo kwa sababu, wameshindwa kutimiza wajibu wao. Ahsante.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara hii inapita kata nane huko kuna wananchi ambao wanafanya shughuli nyingi sana za kiuchumi lakini pia kuna taasisi hata shule iliyokuwa ya kwanza kitaifa iko eneo hilo.

Je, ni kwanini Serikali isione kwamba kuna umuhimu sasa wa kuipandisha hadhi ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami? Kwa sababu pia iko kilomita mbili kutoka mpaka wa Kilimanjaro na Arusha.
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba hii barabara ina changamoto lakini Mheshimiwa Mbunge hapa anaomba kama barabara inaweza ikapandishwa hadhi, kupandishwa hadhi ni mchakato maana yake unaitoa barabara kutoka TARURA kwenda TANROAD ambayo ni Wizara nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nimuombe Mheshimiwa Mbunge jambo hili inabidi lianzie kwenye halmashauri yake liende kwenye ngazi ya mkoa kwenye kikao cha halmashauri cha barabara halafu walete kwenye ngazi nyingine ya kitaifa tutaona namna ya kufanya kama inakidhi vigezo basi itapewa hadhi hiyo ili iweze kupata fedha za kutosha na iweze kutengenezwa na wananchi wa eneo hilo waweze kupata huduma kama ambavyo ndiyo matarajio Serikali.
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza kabla ya kuuliza swali la nyongeza ninaomba kutoa ufafanuzi kwamba hawaitwi wasiosikia au wasioongea kwa ujumla wao wanaitwa viziwi kwa hiyo, ni vizuri zaidi kuwa makini na haya majina ili kuepuka wakati mwingine kuonekana kwamba kwasababu neno asiyesikia ina maana ni mtu mtukutu. Asante naomba sasa niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwasababu tatizo hili ni kubwa maeneo mengi na kwa namna moja au nyingine wanaochagua hawazingatii kwa kujua kwamba huyu mtoto ana mahitaji pengine maalum au asiye na mahitaji maalum. Sasa je, ni lini Serikali itaweka mchakato maalum kwa kuzingatia kwamba katika kila mkoa angalau kuwepo na shule zitakazosaidia watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo viziwi?

Swali la pili uhaba wa waalimu ambao hawana ujuzi wa kufundisha wanafunzi kwa maana kwamba wanafunzi wote wanachanganywa pamoja hata wale viziwi.

Je, sasa upi mkakati maalum wa Serikali katika kuhakikisha kwamba walimu wenye mahitaji maalum wanasambazwa katika shule zetu za msingi ili basi waweze kusaidia wanafunzi wetu hasa wenye mahitaji maalum? Ahsante.
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tunao upungufu wa shule hizi katika maeneo mbalimbali ya nchi na kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi tumeanza na hizo na kuna baadhi ya maeneo kuna shule zingine uwezo wa Serikali ukiruhusu basi tutajenga karibu kila mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungependa hao watoto wapate huduma ya taaluma katika yao ya karibu bila kupata usumbufu ili kwasababu pia kuna kuwa na shida hata kuwatoa nyumbani na kuwapeleka hata kwenda kuwaangalia wanapata matatizo ya magonjwa na mambo mengine hiyo ndiyo shida. Lakini tunatoa wito pia kwenye jibu letu kwamba hata wale wadau ambao wanaweza wakajenga shule kama hizi tumeshuhudia shule nyingi zipo Tanzania hapa za private na za watu binafsi na wadau mbalimbali lakini nyingi zinalenga watoto hawa ambao wanauelewa wa kawaida na hawana aina yoyote ya ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tukipata mdau mwingine pia ambaye anaweza akajenga shule za aina hii za mahitaji maalum tutampa support kama Serikali ili shule iweze kufunguliwa haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia swali lake la msingi anaulizia kama kuna namna ya kuweza kupeleka walimu katika kila mahali. Ni kweli kwamba kuna upungufu lakini kila tunapokuwa na ajira ya walimu tunazingatia pia walimu wa mahitaji maalum. Na swali lake anapozungumza hapa kwamba tusaidiane pia namna ya kutambua watoto katika kila eneo ilitokea pia kwamba tunatoa taarifa kuwatambua watoto hao katika maeneo yao lakini pia maeneo mengine wanafichwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nitumie fursa kuwaomba pia Waheshimiwa Wabunge na watanzania wote inapotokea kuna mwanafunzi wenye ulemavu katika eneo hilo lakini pia tukasema hawa watoto ukiwatenga wenyewe wenyewe pia imekuja hoja inaitwa elimu jumuishi ili watoto hawa waanze kuzoeana wanasaidiana ili hata mtoto akizaliwa katika jamii yetu kwenye familia ni mlemavu asitengwe hiyo ni nia ya Serikali tuwe na elimu jumuishi lakini wanapokuwa na ulemavu mkubwa zaidi wanapata mahitaji mahsusi na usimamizi mahsusi ili waweze kupata huduma vizuri sana. Ahsante!
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kuniona sambamba na majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali wilayani Moshi Vijijini kuna shule ya viziwi ya Vona wamejitahidi kwa muda mrefu sana kupata ushirikiano na Serikali lakini imeshindikana. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kufuatana na mimi mpaka Vona ili aone ni jinsi gani Serikali itaisaidia shule hiyo?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nipo tayari sana kuambatana na mwalimu tukatembelee watoto wetu hao wazuri tukaone mazingira hayo na ni kuhakikishie Mheshimiwa Mbunge huo ushirikiano uliokosekana sasa utapatikana. Ahsante sana.
MHE. RICHARD P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru Serikali kwa kuangalia na kutoa ruzuku kwenye Halmashauri zetu, hususan ambazo zina vipato vya chini. Swali la kwanza; kwa kiwango hiki ambacho Serikali imetoa, bado kulingana na uhitaji kwenye Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo ni kidogo. Je, wako tayari kutuongezea ili tuweze kukidhi ukamilishaji wa maboma na uhitajikwenye upande wa elimu pamoja na afya?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; katika upande wa mahitaji haya je, Naibu Waziri yupo tayari kurejea ziara yake atembelee Halmashauri ya Nsimbo kujionea na aweze kuona namna bora ya kuiwezesha Halmashauri ya Nsimbo?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba nipokee pongezi hizi za Mheshimiwa Mbunge, na hii pia imezingatia sana kwamba amekuwa akilisemea sana eneo lake hili ili kuweza kuondoa kero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anauliza kama Serikali ipo tayari kuongeza fedha. Naomba nimhakikishie yeye na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba Serikali nia yake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaondoa changamoto ya miundombinu ya elimu na afya na kazi hiyo itakuwa inaendelea kufanyika kadri ya upatikanaji wa fedha kwa Serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili ananiuliza kama nitarejea ziara katika eneo hili. Ni kweli nimeshapanga ziara karibu mara mbili ikikaribia kwenda kule eneo la Katavi na Rukwa, ziara hii imekuwa ikiahirishwa. Naomba nimhakikishie ratiba nimeshaipanga, tukiahirisha Bunge hili Mheshimiwa Mbunge nitakuja Katavi na Rukwa na ntatembelea majimbo yote ya ukanda ule. Ahsante sana.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua hivi karibuni TAMISEMI wamekuwa wakitoa rating kwenye Halmashauri zetu kwa maana ya kuwapa namba kutokana na makusanyo na utekelezaji wa makusanyo wanayoyafanya. Kwa bahati mbaya sanaHalmashauri nyingi ambazo walipanga mipango yao ikitegemea makusanyo ya mazao ya kilimo hawakuweza kufanikiwa kupata hizo pesa kwa wakati kwa sababu Serikali iliamua kuingilia mchakato fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kuuliza kwa Mheshimiwa Waziri, kwamba miradi mingi imesimama kwenye Halmashauri zetu, pesa za posho kwa ajili ya Madiwani hazilipwi kwa wakati na hasa miradi ya afya kwa sababu hivi karibuni – na niipongeze Serikali kwamba wametupatia pesa za 4PRkwa mfano Jimbo la Ndanda tumepata zaidi ya madarasa 13. Sasa ninataka kufahamu; ni lini Serikali mtapeleka pesa kwa ajili ya kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwenye Kata za Ndanda, Lukuledi, Mihima na Mpanyani kwa ajili ya vituo vya afya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Mheshimiwa Mwenyekiti, ameeleza maelezo mengi lakini kwa ufupi ni kwamba kama kuna mahitaji mahsusi unaandika TAMISEMI ili waweze kuyafanyia kazi. Lakini mpango wa Serikali ni kwamba hata Mwaka wa Fedha tunapoanza 2019/2020, fedha zimetengwa kwenda kumalizia maboma ambayo yapo ya msingi na sekondari katika Halmashauri zenu. Kwa hiyo tuvute subira lakini kama una jambo mahsusi tuandikie ili tuweze kuchukua hatua za haraka zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini niseme hii haisemwi amesema 4PR, hii EP4R ndiyo lugha sahihi, maana yake ni kwamba Education Payment For Results. Ahsante.
MHE.DKT. RASHID M. CHUACHUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa kuwa sasa kuna upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi katika Halmashauri ya Masasi na walimu 46 wanahitajika ili kukidhi Ikama ya walimu wa masomo ya sayansi;

Je, ni lini Serikali italeta Walimu hao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ni kwamba kwa kuwa suala la kukosekana kwa walimu wa sayansi ni suala la Kitaifa, na kwa kuwa wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha nne na kidato cha sita hawachagui kwenda kujiunga na masomo ya ualimu wa masomo ya sayansi, hivi Serikali haioni kunatakiwa kuwe na jitihada za maksudi za kuchochea watoto hawa ili waweze kujiunga na masomo ya ualimu wa sayansi hususan kwa kuondoa ama kupunguza ada kwa masomo ya Diplomaya Ualimu wa Sayansi na Degree ya Ualimu wa Sayansi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia suala la elimu hasa katika masomo ya sayansi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza anataka kujua ni lini walimu wa sayansi watapelekwa katika maeneo haya. Ni kweli kwamba kuna upungufu wa walimu wa sayansi na hisabati katika shule zetu za sekondari lakini tumepata kibali mwaka wa fedha uliopita tukaajiri walimu 4,500 na sasa tunasubiria kibali kingine takribani walimu 15,000. Tukipatakibali hicho tutaajiri, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge maeneo yote ambayo yana upungufu tutaanza nayo, pale palipo na upungufu mkubwa tunaanza na kuendelea katika maeneo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nia ya Serikali ni kuwa na walimu wa kutosha katika masomo ya sayansi ili kuweza kuboresha elimu hii ya sayansi hasa kwenye dhana nzimainayohusiana na Serikali ya Awamu ya Tano ya sera ya maendeleo ya viwanda na uchumi endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anazungumzia kama kuna uwezekano wa kupunguza ada katika masomo na hasa katika Diplomaili wanafunzi wengi na vijana wengi wajiunge katika masomo ya sayansi na hasa Ualimu ili waweze kupunguza changamoto hii. Kwanza gharama inayotumika sasa siyo kubwa ni gharama ya kawaida kabisa na Serikali imejitahidi sana kupunguza michango mingi ambayo ilikuwa inafanyika. Sasa hivi tumeshapeleka vijana wengi katika Vyuo hivi, wataendelea kusoma na ada ni ya kawaida. Ahsante.(Makofi)
MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Naibu Waziri kwa majibu mazuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mahitaji ya walimu wa sayansi ni makubwa sana na ukizingatia wananchi ambao tunaishi pembezoni unakuta shule moja kama Rungwa Sekondari pale Mpanda ina watoto 1,150, walimu wa sayansi kuanzia Form One mpaka Form Six walimu wako wanne tu. Na ukiangalia sehemu nyingine kama Usevia shule Form One mpaka Form Six walimu wawili.

Je, Serikali itatuletea lini Mkoa wa Katavi walimu kwa sababu tunahitaji sana walimu kutokana na uhitaji wa wanafunzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili,kwa kuwa Serikali ilifanya kazi kubwa ya kuhamasisha kujenga maabara katika shule zote za Kata nchini, na wananchi walihamasika sana wakajenga maabara na maabara zile zimekamilika lakini walimu wa sayansi hakuna kabisa.

Je, lini Serikali itaweka mikakati maalum kama ilivyofanya kuhamasisha kujenga maabara ili tuweze kupata sasa walimu wa sayansi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza ninampongezasana Mheshimiwa Mbunge Anna Lupembe kwa kuendelea kuwasemea watu wake wa Mkoa wa Katavi ili waweze kupata elimu bora.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba tuna changamoto ya upungufu wa walimu wa sayansi na hasa katika masomo ya sayansi na hisabati. Vilevile Serikali imefanya kazi kubwa sana ya kuongeza juhudi ya kutafuta fedha ili tuweze kuajiri walimu hawa wakasaidie kuondoa changamoto ya walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwataarifa tu mwezi Mei mwaka huu Serikali ilipeleka fedha za EP4R motisha ili moja, zikamalizie maboma ya shule za msingi na sekondari, pili ilikuwa ni ku-balance ikama katika shule zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niwaelekeze Waheshimiwa Wakurugenzi katika Halmashauri zetu na Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, zile fedha za Serikali ilikuwa ni kuangalia kama kuna shule moja ina upungufu, shule nyingine ina walimu wa ziada, ilikuwa ni kuwahamisha kutoka eneo moja kwenda lingine ili kuweza ku-balance Ikama na kupunguza changamoto ya Walimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kama nilivyosema katika maswali yaliyopita leo asubuhi, tumeshaomba kibali cha kuajiri walimu hawa, zaidi ya 15,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na maeneo mengine ya pembezoni, tutakapopata kibali cha kuajiri walimu wa sayansi na hisabati, maeneo ya pembezoni yatakuwa kipaumbele, tutaanza na maeneo ambayo yana upungufu mkubwa wa walimu kwenda pale ambapo pana upungufu ambao siyo mkubwa sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili anaulizia maboma ya maabara zetu. Ni kweli, tumekubaliana tunagawana kazi, Waheshimiwa Wabunge, Serikali na wadau mbalimbali wa elimu na maendeleo.Kazi ya kumalizia maboma haya ya maabara ni ya kwetu sote kama nilivyotaja. Serikali tumejipanga, hapa tulipo tupo kwenye manunuzi, wakati wowote kuanzia sasa taratibu za manunuzi zitakamilika tutapeleka vifaa katika maabara zetu. Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge na wadau wengine tuendelee kuchangia kwa namna mbalimbali tumalizie maboma yetu, vifaa tutapeleka, wataalam tutapeleka na hii changamoto hatimaye itaisha ili watoto wetu waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki. Ahsante. (Makofi)
MHE. MARTHA J. UMBULLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nami nampongeza sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri na ya kina. Nachukua nafasi hii pia kuipongeza sana Serikali, hasa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais wetu, John Pombe Magufuli kwa jinsi ambavyo inashughulikia kwa ukamilifu migogoro mingi ya ardhi hapa nchini na hususan katika Mkoa wetu wa Manyara. Hapa pia nimpongeze sana Mheshimiwa RC wetu, Alexander Mnyeti na ma-DC wote wa mkoa huu kwa sababu migogoro hii sasa hivi inaenda ikipungua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina swali moja tu la nyongeza. Hivi karibuni Mheshimiwa Rais wetu ametoa tamko kwamba kuhusiana na migogoro hii ya ardhi ya wananchi kuvamia maeneo mbalimbali kwa ajili ya makazi, kwa ajili ya kilimo na ufugaji yapatiwe ufumbuzi haraka ili kuleta utulivu na amani kwa wananchi katika maeneo mbalimbali:-

Je, Serikali imeweza kushughulikia kwa kiwango gani matatizo haya ya migogoro ya wananchi tukijua kwamba kule Manyara kuna mgogoro unaofukuta kule vilima vitatu kuhusiana na wananchi kukosa amani na kuvamia maeneo kwa ajili ya makazi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza naomba nipokee pongezi zangu kwa niaba ya Wizara na pongezi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. Nampongeza Mheshimiwa Mbunge Umbulla kwa kutambua kazi kubwa inayofanyika na Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Alexander Mnyeti na Wakuu wenzake wa Wilaya, Wakurugenzi wote pamoja na Watumishi wa Serikali katika eneo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Rais kwa mapenzi na ukarimu alionao kwa Watanzania aliamua kuunda kikosi kazi cha Waheshimiwa Mawaziri wanane, wamezunguka maeneo yote yenye migogoro, Wakuu wa Mikoa wameshirikishwa, Wakuu wa Wilaya wameshirikishwa, taarifa zikakusanywa. Kazi hii imeshafanyika, sasa wameandaa ripoti wamempelekea mwenye mamlaka ili aweze kuangalia na kutoa maelekezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wabunge wote wa Tanzania kwamba, Mheshimiwa Rais dhamira yake ni kuondoa migogoro kati ya wananchi na wakulima, wakulima na wafugaji, ili kazi iendelee kuwa nzuri sana. Tumpe muda alifanyie kazi, kama ambavyo alikuwa na nia njema ya ku- control migogoro hii, tuwe na amani kwamba, migogoro itaisha na wananchi wetu watafurahi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
MHE. HASNA S. K. MWILIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Katika timu hiyo ya Mawaziri saba ambayo Mheshimiwa Rais aliunda, walipata pia fursa ya kutembelea Jimbo la Kigoma Kusini kwenye Kata ya Buhingu, Kijiji cha Kalilani. Tangu wamekuja kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kuhusiana na migogoro ya ardhi, mpaka leo wananchi hawajapata majibu kuhusu hatima ya maamuzi ni kitu gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Waziri leo hii aweze kuwaambia wananchi wa Kijiji cha Kalilani na wananchi wa Kijiji cha Sibwesa, kwa sababu wanaishi kwa mashaka hawajui watatolewa kwenye ardhi yao au wataendelea kubaki: Je, ni lini? Maamuzi ya Serikali yanasema nini kuhusiana na timu ile iliyoundwa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA):
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nimetoka kujibu swali la nyongeza hapa la Mheshimiwa Umbulla kwamba hii kazi ya kuondoa migogoro na kupanua baadhi ya maeneo ili wakulima wetu na wafugaji wapate maeneo na kupunguza migogoro, ni kazi ambayo Mheshimiwa Rais kwa ukarimu wake yeye mwenyewe aliamua kuunda timu ya Waheshimiwa Mawaziri na akawatuma, wamezunguka nchi nzima. Namaomba Mheshimiwa Mbunge na Watanzania wote, Mheshimiwa Rais ameona tatizo, amechukua hatua, mambo haya yanahitaji mambo mbalimbali ya kiutaratibu yafanyike na kila sekta ijiridhishe na kuangalia sheria mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumpe nafasi Mheshimiwa Rais nia yake njema itimie. Mgogoro huu utaisha Mheshimiwa Mbunge na wananchi wako wa Kigoma Kusini wataendelea kuwa na amani, kwa sababu Rais mwenyewe ameshika mpini na ameamua migogoro ipunguzwe. Jambo jema ni kwamba hata maeneo ambayo yalikuwa na malalamiko, ameelekeza watu wengine wasivunjiwe kuna uwezekano wa kuongeza maeneo au kupunguza maeneo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamwamini Mheshimiwa Rais, ana nia njema. Jambo hili litafika mahali pazuri sana. Ahsante.
MHE. ZAYNABU M. VULU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri na juhudi za Serikali kuhakikisha kunakuwa na kituo maalum cha kuzalisha mitamba, nina maswali yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo hilo ni kubwa, na kwa kuwa eneo hilo tayari limeshakuwa na wakazi zaidi ya 300 kwenye sehemu inayoitwa Vingunguti na wakazi hao wako kwa muda mrefu sana, na wanajiendeleza na wamejiendeleza kwa muda mrefu. Je, haioni sasa ni wakati wa Serikali kulitoa eneo hilo na kuwapa wananchi hao ili waweze kuishi kwa usalama na amani?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa suala hili linahusu mambo ya mifugo na ardhi, hii Tanzania ni nchi ya amani, upendo na ushikamano, na Tanzania yetu ina wakulima, wafugaji, wafanyabiashara na wafanyakazi sehemu mbalimbali. Kumekuwa na tatizo la migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji. Je, Serikali haioni sasa ikatafuta mbinu mbalimbali mbadala za kuepukana na migogoro hiyo kwa kuwapatia maeneo wafugaji wakakaa wakaweka mifugo yao na wakulima na wananchi wengine wakaishi kwa amani na utulivu?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba eneo hili lilikuwa na hekta zaidi ya 1,000 na baada ya Serikali kugundua kwamba wananchi wameshaingia eneo hili, wamejenga, wamejiendeleza, tumefanya tathmini, tumewaachia wananchi zaidi ya hecta 2,900 ili waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo.

Sasa naomba tupokee pia hoja ya Mheshimiwa Mbunge ya kwenda kufanya tathmini tuangalie kazi ya kuzalisha mitambo ambayo inafanyika eneo hili, faida yake, lakini pia na huduma za jamii za wananchi halafu tutaona busara tunafanye ili tuweze kuamua, ama tuwaachie au tuendelee kuweka mifugo pale ya kuzalisha mitambo.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili anazungumzia migogoro ya ardhi; muda mfupi uliopita Mheshimiwa Waziri Mkuu ametoka kuzungumza hapa namna ambavyo Mheshimiwa Rais na Serikali kwa ujumla wamepokea jambo hili la migogoro na kwamba haipaswi kuendelea. Mheshimiwa Waziri umefanya kazi hiyo, lakini pia wakuu wa mikoa na wilaya wamepewa maelekezo, lakini Wizara ya Ardhi inafanya pia mpango mahususi wa matumizi bora ya ardhi, sasa hili nalo kama kuna mgogoro pale unaendelea naomba tulipokee tuwasiliane na wenzetu mamlaka katika eneo lile tulifanyie kazi. Nia ya Serikali ni kwamba migogoro isiwepo, tunahitaji wakulima, tunahitaji wafugaji na wananchi na shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo biashara ili waendelee kufanya kwa amani na waweze kuchangia pato ikiwa ni pamoja na kulipa kodi. Ahsante.
MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nchi yetu kwa sasa ina miundombinu mizuri kuliko enzi za ukoloni au enzi zilizopita. Je, Serikali inaonaje kwa muda huu kupunguza idadi ya wilaya, idadi ya majimbo ya mikoa ili Serikali ipate pesa, i-save pesa kwa ajili ya kupunguza idadi ya mikoa, idadi ya majimbo na idadi ya wilaya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, tumemsikia Mheshimiwa Ally Keissy kwa maoni yake na mtazamo wake lakini maeneo haya kiutawala yakiwepo majimbo ya uchaguzi ya Waheshimiwa Wabunge hawa wapendwa, wilaya, mikoa na maeneo mengine ya kata na vijiji yanaanzishwa kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa utakapofika wakati wa kuona kwamba kwa hilo wazo la Mheshimiwa Keissy ni muhimu kufanyiwa kazi tutalifanyia kazi. Kwa sasa msimamo ni kwamba tutaendelea kuimarisha maeneo yaliyopo kujenga miundombinu, kupeleka huduma mbalimbali za kijamii ili watu wote waweze kupata maisha ambayo ni bora zaidi.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana ningependa kuuliza swali la nyongeza mji mdogo wa Mbalizi ulipewa mamlaka miaka 15 iliyopita na sasa hivi ina wakazi zaidi ya 100,000 na pia uwanja wa kimataifa wa Songwe uko katika eneo hilo. Sasa ni lini Mji mdogo wa Mbalizi utapewa hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mji wa Mbalizi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba kwa sasa tunaendelea kuimarisha maeneo ya kiutawala yaliyoanzishwa. Wanapozungumzia kuanzisha halmashauri maana yake unaongezea miundombinu unahitaji huduma ya ukubwa zaidi na watendaji watakuwepo na majengo yataongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvumilia tuimarishe kwanza hii miji midog iliyopo halmashauri zetu na katika nchi hii kuna mikoa mingi pia bado haina majengo ya kutosha ya kuwa mikoa na watendaji wengine. Tuna upungufu wa miundombinu katika halmashauri zetu pia Waheshimiwa Wabunge wenyewe bado wanadai ofisi za Wabunge hazijajengwa. Kwa hiyo, nadhani ukiangalia mahitaji yaliyopo na kuongeza eneo la utawala nadhani tupeane muda kidogo tutekeleze haya yaliyopo tukamilishe tutazingatia baadaye maoni yake, ahsante.
MHE. BALOZI DKT. DIODORUS B. KAMALA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nina maswali mawili ya nyongeza. Utafiti uliofanywa na watafiti katika vyuo vikuu vya Tanzania umebainisha kwamba upungufu wa wahadhili katika vyuo vikuu kwa Tanzania ni asilimia 44, na umebainisha pia kwamba, chuo kama Muhimbili, kuna upungufu wa wahadhili asilimia 65, chuo kama cha Mbeya, kina upungufu wa wahadhili asilimia 54 na utafiti huo umebainisha pia, kati ya hao waliopo pamoja na upungufu huo, asilimia 53 tayari wameshastafu kwa sheria za sasa.

Je, Wizara iko tayari kutafakari upya uamuzi wa kwamba, wahadhili wakifikisha miaka 65 wastaafu na wasiongezewe mkataba?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa taasisi nyingi duniani zilishapandisha umri wa kustaafu, kwa mfano, Nairobi University umri wa kustaafu kwa maprofesa ni miaka 70 na baada ya hapo anaweza akaendelea kwa mkataba. Ujerumani hakuna neno kustaafu kwa maprofesa, ukistaafu unapewa cheo cha Emeritus Professor, unaendelea kufundisha na kutafiti mpaka pale utakaposema sasa umechoka, na Uingereza wamebadilisha sheria kabisa sheria ya Bunge, neno kusitaafu katika kufundisha vyuo vikuu limefutwa kabisa, kwa sababu wamegundua akistaafu mmoja leo, inawachukua miaka 40 kuweza kutengeneza mtu kama huyo.

Je, Wizara iko tayari kufikiria na kujifunza kutoka kwa wenzetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, Mheshimiwa Mbunge ametoa utafiti alioufanya na ninaomba niamini kwamba huyu ni Dokta na ni Balozi atakuwa amefanya utafiti wa kutosha, lakini tutaongezea kufanya ili kupata taarifa sahihi sana juu ya jambo hili. Lakini ni kweli kwamba wako wahadhili wengine wengi ambao wanastaafu wakiwa na umri wa kuweza kufanya kazi, hilo jambo ni ko wazi, hili jambo ni ushauri mzuri naomba tuupokee, tufanyie kazi tuone uwezo utakavyoruhusu, tutashauriana na tutaomba Mheshimiwa Mbunge kukutane zaidi katika jambo hili ili liweze kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile, pamoja na kwamba tunataka maprofesa hawa na wataalamu wengine waongezewe muda wa kufanya kazi, lakini tunao mpango pia wa Serikali wa kuendelea kusomesha wataalamu wetu ndani na nje ya nchi. Kwa mfano sasa hivi tunavyozungumza tuna wataamu 65 kati yao ni wadhamivu wanasoma nje ya nchi na watatu wanasoma katika udhamili. Kwa hiyo, tutataangalia namna ya kuweza kuongezea muda wa kufundisha wale hasa wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo, na kwenye fani mahususi na jambo hili Serikali itakwenda kulifanyia kazi, ahsante sana.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza, majibu haya Serikali ni mazuri na yana dhamira njema ya kuijenga nchi hii ifikie katika malengo mazuri. Lakini kuna majibu ya swali kama hili ambao niliuliza mwaka 2016 kama 2016/2017 na bahati nzuri kwenye hansard ninalo lilipata majibu ambao yalionyesha matumaini kwamba kuna siku Halmashauri ya Itigi inaweza kuwa Wilaya. Lakini kwa kuwa Halmashauri ya Itigi ni engeo ambao lina ukubwa wa Squire kilometa 17,000 ni sawa sawa baadhi ya mikoa ambao ipo katika nchi hii na ni tarafa moja.

Je, sasa Serikali ipo tayari kuwa tuachane na suala la kuongeza Wilaya tuondoe walau tuongeze tarafa ambazo hazitakuwa na ghamara kubwa za uendeshaji ikiwemo ofisi ya Wakuu na nini au madiwani?

La pili, katika eneo langu kuna kijiji kinaitwa Mitungu ambacho nacho kina eneo kubwa ukubwa wa eneo ni mkubwa sana lakini wananchi ni wengi. Kutoka katikati ya kijiji mpaka pembeni ni kilometa 40 upande mmoja na upande wa pili hivyo hivyo.

Je, Serikali iko tayari kufanya kazi nzuri kama nazofanya Mheshimiwa Dkt. Medard Kalemani ambaye anatamka jambo na linafanyiwa kazi na haraka unapata matokeo. Je, kwenye kijiji hiki kimoja tu ambacho tunataka kugawanywa angalu kupata vijiji viwili kina watu zaidi elfu 30 Serikali ipo tayari angalu kusaidia na kunipa uwezekano wa mwaka 2020 kuona wepesi katika eneo hili?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge tunakusudia na kutengependa apate wepesi mwaka 2020 na kwa kazi nzuri anayoifanya kuwasemea wananchi wake wa Manyoni tunaamini kwamba wataendelea kumwani na kumunga mkono.

Mheshimiwa Naibu Spika, ameuliza maswali mawili ya nyongeza kwa uchungu na akionyesha ukubwa wa nchi ulivyo na ameonyesha namna ambavyo alishapata majibu ya matumaini hapa Serikali inafanya tathimini kutoka mwaka hadi mwaka. Baada ya kufanya tathimini ya kuangalia maeneo ambayo bado yanazidi kuimarishwa kwa maana ya Ofisi na vitendea kazi vingine miradi ya maendeleo iliyopo na uwezo wa Serikali ndio maana tukaja na jibu la namna hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo amezungumza hapa kwanza maeneo haya yanafanya uchanguzi kwa mfano vijiji vya mwaka huu tayari timu yetu imeshatembelea maeneo mbalimbali kuangalia maeneo ya migoro mahali ambapo ilikubadilisha GN wameshafanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tulipokee hili tuendelee kushauliana tuone kama haitaingiza gharama kubwa Serikalini. Kama ambavyo tunajua tukiongeza maeneo itakauwa gharama zaidi tutaona namna ambavyo kama kuna wepesi wa kuifanya ile kazi ili hawa wananchi waweze kupata huduma karibu. Lakini nawaomba waendelee kuwahimiza nia ya Serikali ni njema sana na Wabunge watakubaliana na sisi kwamba kwa kweli kama unaanzisha maeneo mapya na kati ya hapa kuna watu ambao wadai ofisi za mikoa kuna ofisi za wilaya, Ofisi za Wabunge, Ofisi za kata vijiji na mitaa kwa kweli ukiangalia huo ukubwa na wingi wa shughuli hiyo unahitaji tutulie kuimalisha maeneo ambayo kweli tunayo sasa ili tuweze kuongeza baadaye ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza. Pamoja na kutambua nia njema ya Serikali katika kusitisha kuongeza maeneno mengine mapya ya utawala hasa kwa maeneo ya mikoa na wilaya na halmshauri ambazo pengine gharama ya kuanzisha ni kubwa lakini kule chini kwenye kata na vijiji na mitaa hali ni mbaya sana na gharama yake sio kubwa kiasi hicho, badala kuyabeba yote pamoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali kwa nini isifikirie hasa tunapokwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kwenye mitaa, kwenye kata na vijiji kwenda kuongeza maeneo ya kiutawala kwa sababu hali halisi inakataana na huo msimamo wa Serikali?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema ni kweli kuwa tunaangalia gharama ni kubwa lakini naomba nikubaliane na maoni ya Wabunge walio wengi humu kwamba tuangalie kama nilivyomjibu Mheshimiwa Massare tuangalie kama kuna maeneo ambayo hatutakuwa na gharama kubwa tuyazingatie.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu lengo la Serikali nikusogeza huduma karibu na wananchi na kuna maeneo kwa kweli wanatembea km 40, 30 kwenda kuomba barua ya mtendaji wa kata kitendo ambacho sio sawa sawa. Kwa hiyo, tulipokee hili kwa niaba ya Bunge hili Tukufu na kwa niaba ya Serikali tumelifanyia kazi kwa pamoja na tutashirikisha Wabunge wa maeneo husika namna kuweza kulifanya hili kutekelezeka. Ahsante.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo Naibu Waziri amesema kwamba swali hili liliulizwa kuhusu Tanga wiki iliyopita ningependa kujua Mkoa ambao una halmashauri 11 na tunaposema pamoja na kupeleka maendeleo karibu na wananchi lakini lengo haswa ni kuboresha huduma. Huoni kama ni mzigo kubwa sana kwa mkoa mmoja kuwa na halmashauri nyinigi wakati baadhi ya mikoa halmashuri zake hazizidi nne hadi tano?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri nimewahi kuwa katibu wa vijana wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Tanga, nina zifahamu halmashauri 11 na ukiangalia jiografia kwenda mpaka kule kilindi mpaka Tanga kule Nkinga ni jiografia kubwa. Lakini tunajua kuna mikoa mingine pia ni mikubwa sana ukiangalia kwa mfano Lindi, Ruvuma kule kwa kweli kuna maeneo makubwa sana kiuongozi labda kwa jibu la jumla tu ni kwamba msimamo wa Serikali ni kwamba kwa gharama iliyopo kama ilivyotajwa kwenye REA ujenzi wa miundombinu ya mkoa na wilaya ni kubwa sana ni mabilioni ya fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tulipokee tushauriane ndani ya Serikali tuone kama tunaweza kulifanya kesi by kesi kulingana na ukubwa wa eneo hili tuone kama tunaweza kulifanyika kazi kwa sasa siwezi kuahidi kama tutafanya kesho. Tunaona ile ku-concern ya huduma karibu na wananchi jiografia yetu kubwa mikoa ni mikubwa lakini tulipokee kama maoni ya Wabunge tuendelee kuyafanyia kazi wakati ambapo ikiwa wakati muafaka hili litatekelezwa. Lakini hayo ndio majibu ya Serikali kwa sasa.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nisikitike kwa majibu ya Serikali ambayo yametolewa na Naibu na Waziri sasa hivi Serikali ya Awamu ya Tano tunasema tunaelekea kwenye Tanzania ya Viwanda na kwa kasi kubwa sana ununuzi wa ndege ambao tuahitaji pilot na Ma-engeneer, mnajenga SGR, stiegler’s gorge zote zitahitaji wataalam.

Mheshimiwa Naibu Spika, haya majibu hayatoi uhalisia ni mwezi Mei mwaka huu tumepewa mwalimu mmoja wa sayansi sasa kama Mheshimiwa Naibu Waziri anazungumzia walimu toka Tanzania tupate uhuru kweli tunao walimu 59, na upungufu ni mkubwa. Maswali yangu sasa.

Ningependa kujua katika sekondari tisa ambazo zipo ndani mji wa Tarime ni sekondari mbili ambayo ni High School ya Tarime na sekondari ya Mogabili ndio maabara zimekamilika sekondari saba zote maabara hazikamilia majengo ni yale ambao wananchi wamejenga na kwa kufanya hivi inazorotesha ufaulu wa wanafunzi. Ningependa kujua Serikali ni lini mtaleta fedha ili tuweze kukamilisha maabara ya hizi sekondari saba ambazo hazijakamilika zikisubiri Serikali ikamilishe pamoja na vifaa?

Katika Halmashauri ya Mji wa Tarime tuna sekondari moja tu A-Level na kama unavyojua kwamba tuna sekondari tisa. Wanapomaliza form four wanafunzi wetu wengi na hasa wasichana wanashindwa kupata nafasi kuendelea na high school. Ni lini sasa Serikali itapandisha hadhi walau Mogabili Sekondari au Nyandoto kuwa A-level nayo ili kuchukua wanafunzi mchanganyiko kwa maana wavulana na wasichana ili watoto wetu wa kike waweze kwenda High School?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upole kabisa haya ndio majibu ya Serikali, yeye Mheshimiwa Esther kama ana majibu yake nadhani abaki nayo. Majibu ya Serikali majibu haya yanaandaliwa kutoka Halmashauri ya Tarime. Hakuna taarifa za uwongo ambazo zinatolewa hapa mbele ya Bunge letu Tukufu na ndio taarifa ya hali halisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili suala la kupeleka walimu na kupeleka vifaa vya maabara haliwezi kabisa kulinganishwa na miradi mingine ya maendeleo kwa sababu kila kitu kinajitegemea na vyote ni muhimu sana na vinafanyika sambamba. Tumeajiri walimu awamu hii ya juzi 4500 ndio imepata walimu wachache, awamu iliyopita walimu walipelekwa Tarime lakini bahati nzuri na mimi nimefika wanazungumza ukifika Tarime pale tunazungumza.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala shule kupandishwa hadhi Waheshimiwa Wabunge mnafahamu ni suala la mchakato ni lazima ninyi wenyewe kama Mbunge wa eneo husika kupitia halmashauri yako kupitia vikao vya halmashauri kamati ya fedha, bajeti ya ndani na wadau mbalimbali ikiwepo na mfuko wako wa jimbo mleta maoni TAMISEMI Wabunge walioleta maoni yakupandishwa shule zao kuwa high school yanafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, na ninaomba nitoe taarifa kuanzia mwezi mwaka huu tuna shule nyingi zinaanzishwa ambao tumepata maoni kutoka kwa Wabunge wenyewe kwa vyanzo vya ndani tumpelekee Serikali na walimu tunawapeleka katika maeneo hayo. Ahsante.
MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, matatizo ya Tarime ni matatizo ya nchi nzima. Na utakubaliana nami kutokana na matatizo maabara ndio maana wanafunzi wengi wanapofika kidato cha pili majority wana-opt kwenda masomo ya Arts kutokana na upungufu mkubwa wa maabara lakini vile vile upungufu mkubwa wa walimu wa sayansi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri anapojibu hapo anasema kwamba wametenga takribani bilioni 59 mara nyingi fedha hizo tunatambua zinaenda walau nusu. Sasa nilitaka kujua Serikali ina mkakati gani mahususi katika miaka hii inayobakia mpaka tunapoenda kwenye Bunge la mwisho kuhakikisha kwamba wanatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha maabara ili wanafunzi wetu wa opit kwenda masomo ya sayansi ili waendane na Tanzania ya viwanda.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, labda nitoe taarfa kwamba hapa tulipo sasa hivi tumepata shilingi bilioni 16.6 na tumeshaomba taarifa labda hili nisema inawezekana kuna tatizo la mawasiliano tukiomba maabara ambazo zimekamilika tunaomba kwa maafisa wetu wa elimu kuhamia mikoa na wilaya. Tumeshapata taarifa mbalimbali za halmashauri zote nchini. Mchakato unaendelea kupeleka vifaa tulitaja juzi hapa kwenye bajeti zaidi ya maabara 2500 nchi hii watapata vifaa vya maabara mpya.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini fedha inayozungumzwa hapa kwenye bajeti hii inazungumzia 2019/ 2020 ndio inayozungumzwa hapa. Lakini tunazingatia maeneo lakini tumeeomba taarifa kama kuna maabara zimekamilika tupate taarifa zao. Lakini kuna halmashauri zinatofautiana kutoka moja kwenda nyingine na tunaanza kama tunapeleka vifaa au wataalamu wa maabara au walimu wa sayansi tunapeleka mahali ambapo kuna changamoto kubwa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tukipata taarifa zile labda niwaelekeze Waheshimiwa Wakurugenzi tunapoomba Taarifa kupitia Maafisa Elimu wa Mikoa, Msingi na Sekondari na Walimu, ni lazima wale watoe taarifa lakini pia na Waheshimiwa Wabunge mshirikishwe, maana yake tumepata kweli taarifa hapa hata ya maboma, ikaonekana tunapata taarifa ambazo ni old fashion Mbunge ana taarifa zake, na Mkurugenzi ameleta taarifa hapa zinatofautiana, ndiyo picha. Lakini, tukiomba taarifa ya Elimu au ya Afya au huduma nyingine kwenye halmashauri zetu, basi Wakurugenzi na Makatibu Tawala kabla ya kuleta taarifa kwenye Ofisi Kuu za Serikali wawasiliane na Waheshimiwa Wabunge ili wote tuwe kwenye line moja na tuweze kuzungumza lugha moja. Ahsante. (Makofi)
MHE. SHAABAN O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona, kutofaulu kwa wanafunzi hasa wa masomo ya sayansi kuna changiwa sana na kutomalizika kwa maabara, Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za kutosha katika maabara hizi ili ziweze kumalizika hasa katika Jimbo la Lushoto? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge, na anajua nimetembelea kwenye Jimbo lake, na anafanya kazi kubwa sana kuwasemea wananchi wake, na wananchi wa Lushoto wamejenga Shule nyingi ikiwepo shule ya high school, na nilienda akaniambia kuna upungufu wa Walimu, na namuahidi kwamba tulipomaliza kugawa mgao wa Walimu hawa wa Sekondari naye amepata mgao, na hili tumelipokea, vifaa ambavyo tumeelekeza, kama ile Shule ambayo nilitembelea ilikuwa na changamoto kubwa ya watoto wa kike wengi hawajapata vifaa ambavyo vya kuwasaidia ili waweze kusoma masomo ya sayansi. Ahsante.
MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: Mheshimiwa Spika, nimejibiwa, kwa kuwa nchi yetu itahitaji wanasayansi huko mbele tuendako, na hivi sasa tunavyojenga uchumi wa viwanda. Je, Serikali haioni kwamba hali tuliyonayo katika shule zetu za sekondari ambapo shule za Serikali zina walimu wazuri sana lakini hazina maabara na shule zile za binafsi zina maabara, walimu siyo wazuri kama wale wa Serikali, lakini watoto wale ndiyo wanafaulu mitihani. Serikali ina mpango gani hasa kuhusu kuwaandaa wanasayansi watakaoiendeleza nchi yetu huko mbele? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, nimeona fedha hapa vimetengwa, kwa ajili ya maabara, si maabara peke yake kama ulivyoona swali lenyewe. Nilikuwa nataka nimuulize Waziri, kati ya fedha hizi ni shilingi ngapi zitapelekwa Mwanga kwa ajili ya kusaidia wananchi kujenga maabara ya Msalagambo yale yaliyojengwa sasa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Profesa ameuliza kwa uchungu na yeye pia ni mwanasayansi ni Profesa katika eneo hilo na tunatambua changamoto iliyopo ya masomo ya sayansi na hasa maabara, lakini niseme, fedha ambazo nimetaja hapa shilingi bilioni 58.2 ni mwaka wa fedha huu 2019/2020, lakini mwaka wa fedha uliopita tumepeleka fedha kwenye shule za sekondari 1964, lakini hapa tulipo tunafanya mchakato wa kupeleka tena fedha za vifaa vya maabara katika shule zetu zaidi ya 2000.

Mheshimiwa Spika, lakini ujue kwamba sisi sekondari za Serikali ni 3632, kwa hiyo tunaamini baada ya mpango huu kukamilika ndani ya mwaka huu mpaka 2020 karibu kila maabara itakuwa na vifaa vya kutosha katika eneo hilo. Kwa hiyo, Mheshimiwa Profesa nimtoe wasiwasi kwa jambo hili na kwamba tumejipanga namna ya kufanya vuzuri, lakini tumeshatoa maelekezo, maeneo ambayo kuna upungufu wa maabara kuna namna njia mbadala zimefanyika ndiyo maana leo ukiangalia hata pale viwanja vya Jamuhuri kuna maonesho yanafanyika na walimu wetu wamefundishwa kufanya njia mbadala ili tuweze kufundisha watoto wetu kwa vitendo na ufaulu utakuwa unaongezeka kutoka mwaka hadi mwaka.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili la kuuliza, kama ulivyosema, kwamba sina data hapa lakini nadhani baada ya kipindi cha maswali na majibu ninaweza nikampa kumbukumbu, data kamili kwamba yeye katika eneo lake la Mwanga atapata shilingi ngapi katika shule aliyoitaja, ahsante.
MHE. KITETO Z. KOSHUMA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali, lakini kwa umuhimu mkubwa sana wa suala hili, Serikali nimeuliza ni hatua zipi zinazochukuliwa, lakini Serikali imeniletea majibu kusema kwamba sheria imetungwa. Sheria tumeitunga sisi wenyewe Wabunge na tumeipitisha sisi wenyewe na imesainiwa na Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, lakini je, ni hatua gani zimechukuliwa? Ndiyo lilikuwa swali langu la msingi, lakini nasikitika kwamba halijajibiwa kwa sababu hakuna hatua amabazo zimeonyeshwa kuchukuliwa katika halmashauri ambazo hazitengi fedha hizi na ukizingatia kwamba fedha hizi zinasaidia maendeleo ya kiuchumi kule kwa yale makundi maalumu ambayo yametajwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba Serikali iweze kusema ni hatua zipi ambazo zimechukuliwa hasa baada ya Serikali ya kutungwa kwa sheria.

Mheshimiwa Spika, lakini pia, kwa kuwa zipo halmmashauri ambazo zina changamoto ya mapato, je, Serikali ina mkakati gani wa kuzisaidia halmashauri hizo ili ziweze kutenga asilimia 10 ya haya makundi ili waweze kuchochoe maendeleo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ni kweli alitaka kujua hatua, lakini nimesema kwenye jibu la msingi kwamba, sheria hizi na kanuni zimetungwa mwaka jana 2018 na mwaka huu wa bajeti tumepitisha fedha ambazo zinakwenda kwenye mwaka 2019/2020. Sasa hizi halamshauri ambazo zitashindwa kutekeleza sheria hii, baada ya sheria hii kuwa in place, tumetangaza kanuni wanazo, then hatua zitachukuliwa dhidi ya hawa watu ambao wamekuwa wakichukua hizi fedha. Kwa sababu mwanzoni sheria haikuwepo na kanuni hazikuwepo ilikuwa halmashauri inatenga kwa kujisikia. Hayo ndiyo majibu ya Serikali na Mheshimiwa Mbunge avute subira.

Mheshimiwa Spika, na maelezo ya nyongeza ni kwamba, kwa bahati nzuri halmashauri zote, mikoa yote na wakurugenzi, kwenye mwaka huu wa fedha wakati wa mjadala wa bajeti ya TAMISEMI, kila Mkurugenzi alikuwa anaji- commit kwamba anarudi kwa hii awamu ya robo ya nne ya mwisho, ni lazima wakamilishe kutenga fedha kwa kiwango tulichokubaliana na mwaka wa fedha wa bajeti ujao, kama kuna mkoa utakuja bila kukamilisha zoezi hili na niwaombe Waheshimiwa Wabunge kwenye ziara zetu katika majimbo na wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, nendeni kwenye halmashauri, Wakurugenzi wawaonyeshe fedha zilizotengwa, vikundi vilivyokopeshwa, miradi ambayo imeanzishwa ili mtupe taarifa tuweze kuchukua hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, anauliza habari ya changamoto za mapato. Nimezungumza vilevile kwenye jibu la msingi, hata kama halmashauri inakusanya shilingi 100, imeelekezwa, ndani ya hicho ilichokusanya kidogo hicho, itenge asilimia 10 ya fedha hizo baada ya kuondoa mapato lindwa. Kwa hiyo, katika hoja hii na katika sheria hii na kanuni zetu, hakuna halmashauri ambayo itapata utetezi wa kwamba mapato ni ya chini. Hatukumlazimisha apeleke bilioni mbili, bilioni 10, bilioni 100, tumesema, 10% ya makusanyo ya mapato lindwa.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, ukifuatilia trend ya utoaji wa hizi fedha za vikundi asilimia 10, mara nyingi Wakurugenzi wamekuwa wakijificha kwenye revolving fund, wakitoa ile revolving fund ambayo imerudishwa na vikundi, utadhani ya kwamba imetolewa aislimia 10. Wizara mko tayari kuweka mchakato ambao utaweka wazi revolving fund na 10% ya mapato ya kila mwaka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba nikubali kwamba kwa maelekezo yako tutafanya hivyo ulivyosema kwa maana ya kupeleka nakala kwa kila Mbunge kueleza ufafanuzi tunamaanisha nini katika hii 10% ambayo inapaswa kuwa imetengwa.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nijibu sasa swali la nyongeza la Mheshimiwa Ryoba, ni kweli, wakati wa mjadala wa bajeti Waheshimiwa wa Kamati ya Utawala na TAMISEMI waliliona hili, na kweli imeonekana kuna halmashauri zingine wakichukua fedha wamekopesha, wakizirudisha, wengine walituambia ilionekana wanatoa taarifa ya kwamba walishapata mpaka asilimia 180, 120, wakaulizwa, hii nyingine ya ziada mmeitoa wapi. Ikaonekana kwamba, kikundi kikitoa fedha, wakikirudisha wanajumuisha wanasema imekusanywa, kwa hiyo, tukaelekeza kwamba na sasa hivi tumefungua akauti, kwenye kanuni mpya iliyotengenezwa, kutakuwa na akaunti mahususi ambayo fedha hii inaingia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, umapokusanya fedha zitaonekana, zinaporejeshwa zitaonekana kwa hiyo, hakutakuwa na kuchanganya kati ya fedha ambayo imekopesha na fedha ambayo imekusanywa, lakini Waheshimiwa Wabunge kama nilivyosema, na hili nalo tutaona na nakala na kanuni watazipata ili kuweza kusimamia vizuri utengaji wa hizi fedha lakini usimamizi wake na utekelezaji wake.
MHE. GOODLUCK A. MLINGA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza kwa niaba ya wananchi wa Ulanga, naomba niishukuru Serikali ya CCM kwa kutupa kipaumbele kwenye Sekta ya Afya. Maana yake tumepata shilingi milioni 400, Kituo cha Afya cha Lupilo kimeisha na shilingi milioni 400 imeingia juzi.

(a) Hospitali hii ya Wilaya wakati inajengwa, mwaka 1905 wilaya ilikuwa na watu 23,000, leo hii wilaya ina watu zaidi ya 200,000: Serikali haioni kiasi hiki cha fedha, shilingi milioni 400 kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa hospitali hii ni kidogo sana?

(b) Hospitali yetu ya Wilaya ya Ulanga imekuwa na changamoto kubwa sana ya watumishi wachache na wasio na sifa: Je, lini Serikali italeta watumishi wa kutosha na wenye sifa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza tunapokea pongezi za Serikali kutoka kwa Mheshimiwa Mbunge na kwa niaba ya wananchi wa Ulanga. Mheshimiwa Mbunge ana maswali mawili ya nyongeza. La kwanza, tumepeleka shilingi milioni 400, anadhani kwamba ni pesa kidogo.

Naomba tu nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba hii ni awamu ya kwanza, tunapeleka fedha katika maeneo mbalimbali ya nchi hii kama alivyosema kwa kuzingatia kipaumbele cha afya. Baada ya awamu hii kwisha tutaangalia pia kutokana na uwezo wa Serikali tutaongeza fedha nyingine. Lengo ni kuimarisha hospitali hii iweze kutoa huduma inayostahiki na hata kadri ambavyo wananchi wapya wataendelea kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, swali la pili Mheshimiwa Mlinga anauliza habari ya watumishi. Muda uliopita Naibu Waziri mwenzangu, Mheshimiwa Kandege, alitoa taarifa kwenye Bunge hili Tukufu kwamba tumeshapeleka barua kuomba kupata kibali cha kuajiri watumishi kwa upande wa Sekta za Elimu na Afya. Kwa hiyo, wakati wowote tukipata kibali hicho, tutakapoajiri tutazingatia maombi ya Mheshimiwa Mbunge lakini pia na maeneo mengine ya nchi hii. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Hospitali yetu ya Ulanga ina tatizo na tatizo ni kuwa haina gari la wagonjwa: Je, Serikali ni lini itatupatia gari la wagonjwa kwenye Hospitali yetu ya Ulanga?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli kwamba kuna maeneo mengi ambayo bado tuna upungufu wa vitendea kazi. Tunaomba tulipokee swali hili. Kadri tutakavyopata uwezo tutapeleka gari katika eneo hili pamoja na maeneo mengine ya nchi ambayo kwa kweli kuna changamoto ya mawasiliano.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa tumeelekeza kwamba katika maeneo ya jirani au kwenye Hospitali ya Wilaya ya jirani inapotokea shida au hata magari ya Halmashauri yatumike kutoa huduma hiyo. Tutajitahidi kadri itakavyowezekana magari yapatikane katika Hospitali ya Wilaya, ikitokea shida ya mgonjwa basi apate huduma haraka kupelekwa kwa hatua nyingine ya mbele.
MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Majimbo ya Kibamba na Ubungo kabla hayajaondolewa kwenye Manispaa ya Kinondoni yalikuwa yanahudumiwa na Hospitali ya Mwananyamala. Sasa baada ya kuanzishwa kwa Wilaya mpya ya Ubungo, huduma tunazipata kwenye Hospitali ya Sinza Palestina ambayo hailingani na wingi wa watu wa Majimbo haya mawili ya Kibamba na Ubungo na haina eneo kubwa kwa ajili ya kuipanua kuwa hospitali kubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, sasa je, Serikali iko tayari sasa kwa kuwa Makao Makuu ya Wilaya ya Ubungo yako ndani ya Jimbo la Kibamba eneo la Kwembe na kuna ardhi kubwa imepimwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa satellite town Luguruni: Je, Serikali iko tayari sasa kwenda kujenga hospitali ya wilaya kule ili wananchi wa maeneo ya kule wapate huduma ya eneo la karibu zaidi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ni kweli kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge anazungumza, lakini katika Mkoa wa Dar es Salaam tumepeleka fedha kuimarisha kituo pale Kinondoni, tumepeleka fedha shilingi milioni 200 pale Sinza, tumepeleka fedha Kigamboni shilingi milioni 1.5 kwa awamu ya kwanza na pale Ilala na tumeongeza shilingi milioni 500.

Mheshimiwa Spika, naomba tupokee ombi hili. Ukweli ni kwamba kila palipo na Makao Makuu ya Wilaya patakuwa na huduma ya wananchi. Awamu hii ikimalizika tutapeleka fedha katika eneo hilo ili wananchi wetu waweze kupata huduma. (Makofi)
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Asilimia 10 ya EP4R inayotolewa kwa ajili ya msawazisho wa ikama, imekuwa siyo suluhu katika Mkoa wa Simiyu kwa kuwa walimu wengi sana wamekuwa wakihama. Walimu 60 wanahama kwa robo moja katika Wilaya ya Meatu na watano ndio wanahamia. Je, Serikali haioni haja ya kuwa na mkakati ili walimu wanaoajiriwa wakabaki kuitumikia Halmashauri angalau kwa miaka mitano kabla ya kuruhusiwa kuhama?

Mheshimiwa Spika, ni dhahili kwamba, siyo wasichana wote hupata hisia (pre-menstrual syndrome) kabla ya kuanza hedhi na wakati huo hakuna mwalimu yeyote wa kike ambaye anaweza kutoa msaada. Je, Serikali haioni haja ya kuwapatia Waheshimiwa Madiwani wanawake elimu ya hedhi pamoja na afya ya uzazi angalau mara moja kwa mwaka ili kwa kushirikiana na Wabunge wanawake, angalau tuwe tunatoa elimu ya uzazi kwa watoto wetu wa kike? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wa Viti Maalum wote kwa kuzingatia mambo ya wanawake na hasa waschana katika shule zetu ili kuimarisha afya zao.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza anapendekeza kwamba walimu ikiwezekana wakae miaka mitano ili waweze kuhudumia katika maeneo haya. Ndiyo maana Mheshimiwa Waziri Mkuu alishatoa maelekezo katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kwamba walimu wote kwa ujumla pamoja na wahudumu wengine wa afya, tunaandaa mfumo wa kisayansi ambao utakuwa unaweza kuonyesha kama mwalimu anataka kuhama kutoka point ‘A’ kwenda point ‘B’ ikiwa tunaweza kuangalie ile ikama.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni kwamba, tunavyozungumza hapa, mwezi huu mwanzoni, tumepeleka fedha za EP4R, motisha kila Halmashauri. Nawaomba Waheshimiwa Wabunge wakafuatilie fedha zimeenda katika Halmashauri zao na kwenye majimbo yao, Halmashauri zote nchini zimepelekewa fedha hizi za ku-balance ikama, vilevile na fedha za kumalizia maboma ya shule za msingi. Naomba mkasimamie ili zifanye kazi iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, nitasikitika sana kama kuna shule ambayo ina walimu katika Halmashauri yake, tumepeleka fedha za ku-balance ikama halafu bado iendelee kubaki shule moja ambayo haina mwalimu wa kike, itakuwa ni bahati mbaya; na kwa kweli Mkurugenzi huyo, au Afisa Elimu wa Mkoa na viongozi wa mkoa huo watakuwa hawakuitendea haki Serikali. Maelekezo ni kwamba, fedha iliyopatikana wazingatie kuhamisha walimu wa kike, wahakikishe kila Halmashauri ina mwalimu wa kike. Kwa sababu unakuta Halmashauri mbalimbali zina walimu wengi katika maeneo mbalimbali. Tulipeleka fedha ili mwalimu akihamishwa asianze kulalamika. Hili nadhani lizingatiwe na lifanyiwe kazi. Waheshimiwa Wabunge, tusaidiane kufuatilia hili ili liweze kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, hoja ya miaka mitano kuelekeza, ziko taratibu mbalimbali za Utumishi wa Umma, hizo ndizo zinazingatiwa. Hata hili la kuzuia kwa muda, kimsingi tumezuia kwa sababu baada ya malalamiko mengi, kama Mheshimiwa Mbunge alivyosema kwamba kuna maeneo walimu wanafika. Hata juzi tumeajiri walimu, walipaswa kuripoti tarehe 21 mwezi huu ndiyo ilikuwa waripoti kama ajira ndiyo tupange, lakini wameshaanza kuomba uhamisho. Hata kuripoti hajaripoti, hajapewa hata namna ya ajira, hajaanza kulipwa mshahara.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tukizuia ajira kunakuwa na malalamiko mengi sana kwamba watu wanaonewa, lakini kimsingi matatizo hayo ndiyo tunayazingatia. Kwa hiyo, tunaomba walimu waendelee kubaki maeneo yale na uhamisho umeendelea kusitishwa mpaka tutakapokamilisha mfumo ili tuweze kumhamisha mwalimu tukijua kwamba eneo analotoka au kwenda haliathiri sana utoaji wa elimu katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, anashauri kwamba Waheshimiwa Madiwani wa Viti Maalum wapewe semina hii ili waweze kusaidia na Waheshimiwa Wabunge. Hili jambo tunalipokea, lakini ukweli ni kwamba elimu hii ya uzazi inatolewa; ni elimu endelevu, inatolewa kwa wazazi wenyewe, kwa wanafunzi wenyewe, kwa walimu wa kike na wa kiume. Pia Mheshimiwa Waziri wa Afya alishauri juzi hapa; na hata akina mama katika nyumba zetu, unaweza ukamlea mtoto vizuri zaidi, kwa sababu unakaa naye muda mwingi zaidi ili kusaidia kuboresha mambo haya. Tunaupokea ushauri huu, tutaona utakapofika wakati muafaka tuufanyie kazi. Ahsante.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, watoto hawa wanapopelekwa kwenye shule wazazi wao wanawatelekeza, hawafuati watoto wao kuhakikisha kwamba wanapata mahitaji maalum hasa mavazi. Siyo hiyo tu, shule hizo zinakosa pesa za kulipia walinzi, kulipa, maji, kulipa mapato na Matron na wengine wanahitaji misaada maalum na hasa wale wenye uoni hafifu au wasiyoona.

Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu sasa kuwepo na mpango maalum wa kuhakikisha kwamba watoto hawa fedha hizo zinapelekwa kwa kuzingatia kwamba Halmashauri hazina mapato, zimezinyang’anywa mapato yote, haziwezi kuhimili kumudu kusaidia shule hizo; Kuwepo na mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba huduma kama hizo zinapatikana kwa watoto hawa.

Mheshimiwa Spika, shule ambazo mimi nimeuliza swali ni za Serikali, sikutegemea kwamba Serikali inaweza ikakosa takwimu maalum kwa ajili ya kuweza kutoa huduma.(Makofi)

Je, Serikali inataka kutuambia kwamba inafanya kazi bila kuwa na takwimu sahihi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Swali lake la kwanza Mheshimiwa Conchesta amezungumza hoja ambayo kimsingi inatakiwa Watanzania wote tuichukue na kuifanyia kazi. Ni kweli kwamba wako wazazi ambao wametelekeza watoto wao, hata akimpeleka shuleni, anamwacha pale moja kwa moja, hawezi kumfuatilia.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli ni jambo hili ni jukumu la kijamii, haliwezi kuwa la Serikali peke yake, tulichukue na tuwashauri kwamba hawa ni watoto wenye haki sawa na watoto wengine, tuwapokee, tuwakubali, na tuwasaidie. Tukishikamana sisi Watanzania na jamii kwa ujumla na Serikali, jambo hili litakuwa jepesi sana.

Mheshimiwa Spika, vile vile Mheshimiwa Conchesta anapendekeza kwamba kama kuna uwezekano wa kupeleka fedha zaidi, tufanye hivyo. Ninachokizungumza hapa, tunapeleka huduma kwenye shule kulingana na idadi ya wanafunzi kulingana na taarifa tuliyopokea hapa. Hili swali nalijibu kwa pamoja na swali lake la pili. Tunapozungumza kwamba taarifa hazipatikani, kama alivyosema mwenyewe ni kwamba kuna watoto wengine wanafichwa katika jamii, kuna wengine kweli hawako kwenye mfumo rasmi, kuna wengine wapo mashuleni, lakini taarifa ya Serikali Kuu hapa TAMISEMI pamoja na Hazina ambao wanatuma fedha moja kwa moja kwenye mashule, tunapata taarifa kutoka kwenye Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, katika jambo hili natoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge, Madiwani, Viongozi wa Vijiji na Mitaa, tupatieni taarifa sahihi. Tukipata taarifa sahihi, tutapeleka fedha kwa kiwango kinachotosha katika eneo lile; na hiyo ndiyo ambayo inakosekana hapa. Kwa hiyo, jambo hili ni la kwetu wote, tunaendelea kufanya kazi. Inawezekana kuna upungufu katika maeneo mbalimbali, tumetembea katika shule mbalimbali, lakini kuna upungufu, lakini kadri Serikali inavyopata uwezo imekuwa ikiimarisha huduma hizi.

Mheshimiwa Spika, tumesema hakuna mtoto ambaye atakufa katika shule hii au kupata shida kubwa bila kupata huduma. Cha muhimu tusaidiane, Mheshimiwa Mbunge kule wa Kagera ameona taarifa ipo, tuwasiliane, tutaipokea, tutalifanyia kazi. Lengo ni kuhakikisha kwamba watoto hawa wanapata elimu na ushahidi upo kwamba huko watoto waliachwa, walitelekezwa, wamechukuliwa na Serikali na wasamaria wema, wameingia kwenye mfumo rasmi, sasa hiivi ni viongozi wakubwa katika nchi hii, wamejiajiri na wanasaidia wenzao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa katika Mkoa wa Dar es Salaam kumekuwa na ongezeko la watoto wenye mahitaji maalum; na kwa kuwa shule ambazo zinapokea watoto wenye mahitaji maalum kama Majimatitu Maalum, Mtoni Maalum, Salvation Army, Wailesi Maalum, Uhuru Mchanganyiko, Mgulani Inclusive na Sinza Maalum zinakuwa hazitoshelezi mahitaji, watoto wale bado wanabaki majumbani:-

Je, Serikali haioni haja sasa ya kuongeza katika shule zote za msingi vitengo vya watoto wenye mahitaji maalum ili nao waweze kupata elimu katika maeneo yao wanayotoka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mariam Kisangi kwa mawazo haya mazuri ya kuunga mkono Serikali ya Chama cha Mapinduzi. Naomba nitoe taarifa kwamba sasa hivi baada ya kuona kwamba unapotenga shule maalum ni kama wale watoto unawatenga, wanakuwa isolated sana katika mazingira yao. Kwa hiyo, sasa hivi tumekuja na kitu kinaitwa Elimu Jumuishi. Ndiyo maana tumetoa maelekezo nchi nzima, tunapojenga miundombinu mipya, hata kama ni Kituo cha Afya izingatie mahitaji maalum, kama ni shule zetu za msingi na sekondari ziwe na mahitaji maalum.

Mheshimiwa Spika, ukienda kule Buhangizo utawakuta, Chaibushi utakuwata, Kilosa Sekondari utawakuta. Kwa hiyo, hiyo imeshaanza. Cha muhimu, ametoa warning, tuendelee kuzingatia. Tumeendelea kuwaeleza wanafunzi wa kawaida kwamba hawa watoto wenye mahitaji maalum ni wenzao, wawapokee, wawakubali, wawasaidie na wasome kwa pamoja pale inapowezekana. Hilo kwa kweli linafanyika. Cha muhimu hapa tutaongeza nguvu zaidi na kwa maoni ya Mheshimiwa Mbunge tutayafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. JOSEPH K. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kupata nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa vile uhaba huu wa walimu kwa sehemu nyingine unachangiwa na kutokuwa na msawazisho sawa wa shule zetu mbalimbali hasa baina ya shule za mijini na vijiji na hivi kusababisha shule za vijiji ziwe na walimu wachache zaidi ukilinganisha na sehemu za miji. Ni lini sasa Serikali itakamilisha mchakato wake wa kuhakikisha kwamba kuna kuwa na msawazisho wa walimu ili uhaba au toshelevu wa walimu ulingane mijini na vijijini?

Mheshimiwa Spika, pili, kwa vile tumeona vijana wengi waliohitimu taaluma ya ualimu bado wapo mtaani kwa muda mrefu sasa na wengine zaidi ya miaka minne/mitano na bado Serikali inawekeza fedha nyingi kwenye kusomesha vijana hawa katika vyuo vyetu vikuu kwa nini sasa Serikali isiangalie utaratibu mpya wa kusomesha vijana wetu kwa kulingana kwa mahitaji ya soko la ajira na mahitaji ya Taifa katika ujumla wake na kuwawezesha vijana wetu waweze kuwekeza zaidi katika ujasiliamali? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maoni na mtazamo wake, lakini wiki iliyopita nilitoa taarifa kwenye Bunge lako tukufu kwamba tumepeleka fedha katika Halmashauri zote ambazo kazi, moja, nikumalizia maboma ya shule za Msingi lakini pia lingine ni kusawazisha au ku- balance ikama katika shule zetu. Tumeelekeza Wakurugenzi, Walimu na Makatibu Tawala wa Mikoa kwamba wahahakishe kwamba fedha hii inatumika kuwahamisha walimu ili moja, kuangalia kusambaza walimu katika upungufu uliopo katika maeneo ya mjini ili waende maeneo ya pembezoni; lakini la pili kuangalia zile hoja kwamba kuna shule ina mwalimu kike haina mwalimu wa kiume au wakiume haina wakike pia izingatiwe hilo. Kwa hiyo kazi inafanyika tunatarajia kwamba Wakurugenzi na viongozi wa mikoa watasimamia hili na Waheshimiwa Wabunge ni kwa sababu ni sehemu ya mikoa yenu hili ni taarifa rasmi naomba mtusaidie kusimamia.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anasema tufundishe wanafunzi wetu kulingana na mahitaji, juzi Mheshimiwa Waziri wa Nchi alitangaza matokeo ya form four na mojawapo ya kazi iliyofanyika ni kugawanya wanafunzi katika maeneo mbalimbali, sasa hili la kusema tuweke kulingana na idadi, ni kweli kwamba walimu wapo mitaani lakini ukweli kwamba tunahitaji walimu wengi katika sekta zote shule ya msingi na sekondari.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu kila mwanafunzi amelekwa mahali ambapo anahitaji, na tunatarajia kuna shule za Serikali na watu binafsi lakini pia na shughuli binafsi na tunaendelea kuangalia mchakato wa kuhakikisha wanafunzi hawa badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali ambalo ni jambo la kitaifa kwa kweli ni lazima tuanzishe utaratibu wa watu kufanya kazi hata kwa shughuli binafsi yaani isiwe ile knowledge based, iwe ni competent. Kwa hiyo tunalichukua tunafanyia kwa siku za usoni tutaweza kulizingatia, ahsante.
MHE. SUSAN L. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, matatizo ya walimu wa sayansi yameikumba sana Wilaya Kilombelo hususani jimbo la Mlimba karibuni ina shule 26 za sekondari. Lakini hivi karibu tumepata walimu wa sayansi wanne tu na kupelekea shule nyingi za sekondari kukosa walimu wa sayansi.

Je, Serikali ina mpango gani kutupelekea walimu wa sayansi Wilaya ya Kilombero husani jimbo la Mlimba ukizingatia tunakula samaki, kwa hiyo, watoto wana akili sana ya mahesabu na sayansi kwa mfano bora angalia tumemtoa Mheshimiwa Likwelile alikuwa kule Wizarani tumemtoa Benno Ndulu kwa hiyo sasa hivi tunakosa wasomi kwa sababu hatuna walimu wa sayansi. Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge ameuliza mara kadhaa swali hili tunamshukuru, lakini tumepeleka walimu wachache kulingana na mahitaji yaliyopo, lakini tumeomba kibali cha kuajiri walimu wa kutosha mwezi huu wa sita au mwaka wa fedha mpya ukianza. Kwa hiyo, pindi tutakapopata hicho kibali Mheshimiwa Mbunge ndio maana nakuhakikisha kwamba suala Mlimba na maeneo mengine yenye upungufu mkubwa kama kwako kule tunazingatia maombi yako muhimu. Ahsante.
MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, elimu ya msingi ni kumjengea mtoto uwezo wa kujua, wa kuelewa na wa kuendelea na maisha ya elimu na ujuzi katika siku za mbele; na unapoacha kumpa mwanafunzi wa shule ya msingi mwalimu wa kumsaidia hata huko sekondari hawezi kufanya vizuri.

Mheshimiwa Spika, tuliomba walimu 4,410 lakini tumepewa walimu 699 hata nusu ya kiwango tulichoomba hatujapata; na hapo kuna walimu waliostaafu, waliotolewa kwa vyeti fake, kuna wanaougua ambao wamesafishwa kwa ajili ya kuugua. Walimu 699 hawakidhi mahitaji ya walimu wa shule za msingi na kutokana na ujio wa makao makuu kuna uhitaji mkubwa sana wa walimu wa shule za msingi.

Serikali ina mkakati gani sasa wakuongeza walimu wa kutosha katika mkoa wetu wa Dodoma?

Mheshimwa Spika, swali la pili, tuna walimu 203 ambao wamestaafu ambao mahitaji yao ya fedha wanazotakiwa kulipwa ni shilingi milioni 260. Walimu hawa tangu mwaka 2014 hajalipwa stahili zao na wamekwishastaafu wapo nyumbani.

Ni lini sasa Serikali itawalipa walimu hawa 203 ambao wamestaafu wameshindwa kurudi kwao kutokana na kutolipwa stahiki zao?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimwa Spika, ni kweli kwamba tulipata kibali cha kuajiri walimu 4500 lakini uhitaji wa walimu wa shule za msingi ni zaidi 66,000; uhitaji wa walimu wa sekondari ni zaidi ya 14,000; walimu 3,088 tuliwapeleka shule za msingi na walimu waliobaki ndio tulipeleka sekondari. Kwa hiyo katika hesabu hiyo katika hali ya kawaida lazima kutaendelea kuwa na upungufu na kuna Halmashauri na shule nyingine hazikupata walimu kabisa, huo ndio ukweli.

Mheshimwa Spika, lakini kama nilivyosema kwenye swali lililotangulia tuliomba kibali cha kuajiri walimu tukipata kibali hicho tunaongeza walimu lakini tutapeleka maeneo ambayo wana uhitaji makubwa ikiwepo na Mkoa wa Dodoma.

Mheshimwa Spika, swali la pili anauliza walimu wastaafu; malipo ya stahiki za walimu ziko za aina mbili, kuna malipo yanayolipwa na Halmashauri zetu lakini pia kuna malipo ambayo yanatoka katika Serikali Kuu. Katika Mkoa wa Dodoma amezunguzumza walimu 203 lakini sisi tunajua kwamba tuna walimu hapa 599 katika Mkoa huu ambao wamestaafu na wadai fedha zaidi ya shilingi milioni 652. Lakini madi yalipokuja TAMISEMI yamerudishwa kule kwa mambo manne.

Moja, ni kwamba madai hayo pia yanabidi yahakikiwe kamati za ukaguzi za mikoa na halmashauri hazikufanya hivyo; lakini jambo la pili kwa mfano nauli za walimu inabidi Wakurugenzi walipe. Wakurugenzi hawakuwa wameonesha wana mkakati gani wa kulipa walimu wastaafu fedha kutoka kwenye mipango ambayo ni maelekezo ya Serikali; lakini jambo la tatu ni lazima fedha hizo baadhi ya watumishi waliomba wameletwa kwamba wadai wengine wanastaafu mwaka 2019 yaani mwaka Juni kimsingi walikuwa hawajastaafu. Sasa tulipoangalia namna ya ukokotoaji wa zile nauli kwamba nani analipwa nini kutoka wapi kwenda ilikuwa imekosewa.

Mheshimwa Spika, kwa hiyo tukarudisha madai hayo katika viongozi wetu wa Mikoa na Halmashauri wayafanyie kazi tutawasiliana na Wizara ya Fedha, ukweli ni kwamba wataafu wa Serikali wakiwemo na walimu baada ya kufanya kazi kubwa kutumikia taifa hili kwa unyenyekevu mkubwa na uaddilifu mkubwa ni lazima walipwe stahiki zao.

Kwa hiyo, naomba kwa Wakurugezi wahakikishe kabla ya kuleta madai ni lazima wahayahakiki ili kondoa usumbufu ambao walimu wetu na wastaafu wengine wanaupata, ahsante.
MHE. JANETH M. MASABURI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuweza kuniruhusu niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza nichukue fursa hii kuipongeza TAMISEMI kupitia Mawaziri wake wote kwa kazi nzuri wanayoifanya hapa nchini. Tumekuwa tukiwaona wanatekeleza wajibu wao ipasavyo, lakini katika eneo hili la vijana na wanawake ninaomba niulize maswali kama yafuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa vijana wengi na wanawake hapa nchini wameshindwa kufanya biashara zao kwa tija kutokana na ukosefu wa ujuzi na maarifa wa kufanya biashara hizo. Je, Serikali iko tayari kuiwezesha kutoa mafunzo makundi haya ya ufugaji wa samaki ya uhakika na kwa idadi kubwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa, sekta ya uvuvi imeonesha kuwa na fursa kubwa ya kukuza ajira, kukuza kipato, kuboresha lishe na hata kuiingizia Serikali fedha za kigeni. Je, Serikali iko tayari kuanzisha mpango wa kujenga vizimba pembezoni mwa maziwa na mabwawa na hata kandokando ya mwambao wa bahari?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKO NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru kwa pongezi ambazo ametutumia kwenye Ofisi ya TAMISEMI kwa kazi ambayo inafanyika tunamshukuru sana.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Masaburi ametoa maswali mawili, swali la kwanza anatuhimiza tuwe na mafunzo kwa vijana na akinamama na kweli hili jambo linafanyika, kwa sababu jambo la msingi ni kwamba tumeshatoa maelekezo kila Halmashauri ina maelekezo na baada ya kugundua kwamba kuna … pia na mafunzo … mtaji ndio maana Bunge hili tukufu likapitisha sheria kwamba kila Halmashauri itatenga mapato yake ya ndani asilimia nne kwa akinamama, nne kwa vijana na mbili kwa watu wenye mahitaji maalum au wenye ulemavu kwa hiyo hii pia ni sehemu ya mtaji.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili kila Halmashauri ina Maafisa wa Ustawi wa Jamii na kuna Maafisa wa Vijana katika Halmashauri zote nchini. Naomba nitumie nafasi hii kuwaelekeza washirikiane na Maafisa wa Ugani kwenye Wizara ya Kilimo waende wakatoe mafunzo kwa vijana hawa na kimsingi hata ziara ambazo Mheshimiwa Waziri anafanya, Manaibu, Makatibu Wakuu na Wakurugenzi ndio tunaangalia miradi ambayo imeanzishwa na Halmashauri na kukagua ikiwepo ni pamoja na ufugaji wa samaki katika maeneo yetu.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba tupokee ushauri wake tuwasiliane na viongozi wenzetu wa Wizara ya Uvuvi. Tutalifanyia kazi, ahsante sana.
MHE. ALEX R. GASHAZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, katika Jimbo langu la Ngara tumehamasisha vijana wanaosoma vyuo vikuu nchi nzima wanaotoka Wilaya ya Ngara kwa ajili ya kuweka umoja na ushirika na miaka miwili mfululizo wamekuwa wakija kujitolea wakati wa likizo ndefu kufundisha kwenye shule zetu za sekondari na tayari wamesajili shirika lao linaitwa Mzalendo Education Organisation (MEO). Serikali iko tayari kuwashika mkono ili kusudi waweze kuendelea kutengeneza mazingira ya ajira kwa vijana wenzao kwa sababu tayari Halmashauri imeshawapatia ekari 10 kwa ajili ya kuanza miradi ya mfano.

Je, Serikali wako tayari kuweza kuwashika mkono ili vijana hawa wawe mfano kwa vijana wenzao nchi nzima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKO NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuunganisha vijana katika eneo lake na kuwapa mawazo haya ambayo ni mawazo mema kweli kweli. Ni kweli, tupo tayari na utayari wetu umeshaanza kutekelezwa. Naomba nitoe maelekezo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ngara na Afisa Elimu pale waende katika eneo hili wakutane na vikundi hivi vya vijana, wazungumze nao halafu walete maoni ni kitu gani hasa wanataka kusaidiwa ili waweze kufanya kazi hii nzuri ambayo imeanza. Ahsante sana.
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na utaratibu ambao ni kinyume cha Sheria Wakuu wa Mikoa, Wilaya, Makatibu Tarafa na hata Watendaji wa Kata kuwafukuza Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji papo kwa papo kwenye mikutano ya hadhara.

Je, Serikali ina tamko gani kuhusu jambo hili ambalo ni kinyume cha sheria? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni kwamba Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wamekuwa wakifanya kazi kubwa sana wakiwasaidia Madiwani na Wabunge na kwa kweli ndiko Serikali za wananchi ziliko, lakini wamekuwa hawapati posho, posho zao zinasuasua, hawapati mishahara, wamekuwa wakifanya kazi kwa taabu sana.

Je, Serikali inasema nini hasa katika hiki kipindi cha Bajeti kuhakikisha kwamba watu hawa wamepata posho kidogo kwa ajili ya kuwasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba ni-declare interest kwamba na mimi pia kuanzia mwaka 2014 hadi 2017 nilikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule, Ukonga - Dar es Salaam, swali lake la kwanza anaulizia juu ya namna ambavyo Wenyeviti wa Vijiji Vitongoji na Mitaa wanavyoondolewa madarakani.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa sheria, kwanza kama unataka kumuondoa Mwenyekiti wa Kijiji, hayo maeneo niliyoyataja, la kwanza ni lazima wapatikane watu ambao wana watuhumu hao viongozi katika eneo lao la kiongozi ambalo wamechaguliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili lazima hao watu waandike malalamiko kwa maandishi wampelekee Mkuu wa Wilaya wakitaja tuhuma moja baada ya nyingine ambayo muhusika na mlalamikiwa ametenda na jambo la tatu ni lazima Mkuu wa Wilaya au anayehusika ataandika maana yake sheria inamtambua Mkuu wa Wilaya kwenye ngazi ya Wenyeviti wa Vijiji kuja chini, atamwandikia Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji au Mtaa tuhuma zake kwa maandishi, ndani ya muda usiozidi siku saba mtuhumiwa atalazimika kujibu tuhuma alizopewa na baada ya hapo, baada ya kupokea majibu ya tuhuma zile Mkuu wa Wilaya ataitisha mkutano wa wananchi wa eneo husika na sheria inasema watakao hudhuria siyo chini ya nusu ya wakazi wa eneo husika na wawe wamekuwa registered kwenye registration ya mtaa husika wanaotambulika, watu wazima wenye akili timamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya hapo watapewa nafasi ya kujitetea mbele ya mkutano huo, atasomewa tuhuma zake, atapewa nafasi ya kujitetea na baada ya hapo wananchi baada ya kumsikiliza watapiga kura sasa kuonesha kwamba hawamtaki, mbili ya tatu (2/3) ya mkutano uliohudhuriwa wakikubali kwamba hafai ataondolewa madarakani na huo ndiyo utaratibu na naomba viongozi wazingatie muongozo huo wa kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni habari ya posho au mishahara kwa Wenyeviti wa Mitaa, Vitongoji na Vijiji. Swali hili nimejibu mara nyingi, naomba nirudie; kwa mujibu wa sheria hizi kazi, zetu hizi, Wenyeviti wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji hawapewi mishahara, lakini hata hivyo kwa sababu ya kuangalia umuhimu wa shughuli ambazo wanafanya na unyeti na ni kweli wanafanya kazi zaidi ya masaa 24 sheria imeelekeza na TAMISEMI tumeelekeza, naomba nielekeze pia kulingana na mapato ya Halmashauri kwenye eneo husika Wakurugenzi wetu wamekuwa wakipanga namna ya kuwapa posho za kujikimu, kuweza kulipia ofisi zao, kuwapa vitendea kazi ikiwepo na photocopy. Maeneo mengine kulingana na mapato yao wamepanga wanalipwa shilingi 50,000 kwa mwezi, kule Dar es Salaam najua wanalipwa shilingi 100,000 kwa mwezi, kwa hiyo, inategemea na mapato.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa sheria haijabadilishwa na Waheshimiwa Wabunge Bajeti ya TAMISEMI imeshapitishwa na kwa kweli hatukupokea maoni yoyote ya Halmashauri wakitaka kupandisha posho za Wenyeviti wa Mitaa au wa Vijiji, hili jambo tulipokee, tutafakari kwa pamoja tukipata uwezo tuboreshe utaratibu huu ili Wenyeviti wa Mitaa waweze kulipwa kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya, wanatusaidia sana katika kazi hii na wanafanya kazi ya kipolisi, mahakama, kifamilia na mambo mengi kadha wa kadha ambayo yanafanyika. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo Mheshimiwa Waziri amejibu mimi kwanza nimpongeze kwa majibu yake mazuri, lakini bado kuna tatizo la hawa watendaji wetu yaani kwa maana kwamba Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani ni kwamba hawajapata semina, pamoja na kwamba sheria/sera bado haijaletwa ya ugatuzi wa madaraka lakini bado uko umuhimu wa kuwapa semina mara kwa mara ili waweze kujua mipaka yao ili waweze kuboresha utendaji wao wa kazi.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwapa semina hawa watu, Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji ili waweze kufanya kazi vizuri? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, inawezekana kuna maeneo hawa viongozi hawajapata semina lakini ninachojua na maelekezo ya TAMISEMI ambayo na mimi nimesema nilikuwa Mwenyekiti wa Mtaa tulifanyiwa baada ya uchaguzi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wale viongozi wakishapatikana kabla ya kuanza kazi wanapewa semina ikiwa ni pamoja na kuapishwa, hawa wajumbe wanakula viapo vya uaminifu kwenye ngazi ya Halmashauri na wanapaswa kuapishwa na Mwanasheria Mkuu wa Halmashauri husika, hilo linapaswa kufanyika, kama kuna mahali halikufanyika nitaomba kwa sababu tunaenda kwenye uchaguzi wa mwaka huu tutalisimamia ili viongozi wakishapatikana wapate semina, waapishwe lakini kubwa zaidi ni lazima wajue mipaka yao ya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yako majukumu na kuna tofauti kubwa kwa mfano ya Wenyeviti wa Mitaa na Wenyeviti wa Vijiji, Wenyeviti wa Mitaa ni waratibu wa shughuli za Serikali za Mitaa, wakati Wenyeviti wa Vijiji ni Serikali kamili wana maamuzi wanaweza hata wakachukua rasilimali za eneo fulani wakauza wakafanya miradi ya maendeleo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo hayo mambo tutayasimamia ili yaweze kufanyiwa kazi na naomba viongozi wetu wa Halmashauri na Mikoa wajipange, baada tu ya uchaguzi haitakiwi Mjumbe wa Serikali ya Mtaa au wa Kijiji au Mwenyekiti aanze majukumu yake bila semina, kiapo na mafunzo tutayazingatia na chuo chetu kikuu cha mafunzo ya Serikali za Mitaa za Hombolo kina nafasi hiyo na hata nyie Waheshimiwa Wabunge mnakaribishwa hata sasa mkitaka na wajumbe wenu mnawapeleka pale, tuna nafasi ya kutosha walimu waliobobea, karibu Hombolo Chuo cha Serikali za Mitaa wapate mafunzo ili wafanye kazi kwa kuboresha huduma za kijamii. (Makofi)
MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kuna baadhi ya Wenyeviti katika vijiji vyetu baada kuteuliwa tu baada ya miezi mitatu/minne wanajiuzulu wengine wanafariki, lakini hakuna chaguzi zinafanyika na mfano hasa kwenye Wilaya yangu kunakaa wazi, wanateuliwa tu mtu anakaimu anakuwa pale, sasa demokrasia inasemaje kuhusu watu wanaojiuzulu na wanaofariki kwa nini uchaguzi haufanyiki?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, inawezekana kweli, nimesikia sikia naomba nitoe maelekezo, kwanza, hakuna mtu anaitwa Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji au Mtaa kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, haipo hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachofanyika ni kwamba Wajumbe na kuna watu wengine mtu akijiuzulu anakaimu kwa muda mrefu na anatembea na muhuri kwamba ni Mwenyekiti, hilo zoezi kama lipo kuanzia sasa na leo muda huu, likome halipo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachofanyika mtu akijiuzulu Wajumbe wa Serikali ya Mtaa wanapokutana kwenye kikao, miongoni mwao anakuwa Mwenyekiti wa kikao hicho na uenyekiti wake unakoma mara tu baada ya kikao kuisha wakati ule, anayepaswa kufanya kazi ya kiutendaji ni Mtendaji wa Kijiji au Mtendaji wa Mtaa mpaka uchaguzi ufanyike, lakini uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wakati wowote ikitokea gap tunategemea kupata taarifa kutoka ngazi ya Kijiji au Mtaa inakuja TAMISEMI, tunaruhusu wafanye uchaguzi kwa sababu kwanza unasimamiwa na eneo husika pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mtu akijiuzulu, kwa mfano mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu kama sasa, hatukuruhusu kwa sababu sheria inazuia huu muda hauruhusiwi, lakini muda wowote wa nyuma Mheshimiwa Ally Keissy kama ilitokea ni bahati mbaya sana na tunaisimamia tupate taarifa baada ya uchaguzi huu, kama inatokea mtu amejiuzulu baada ya muda siyo mrefu sana inabidi achaguliwe ili wananchi wahudumiwe na mtu ambaye wamempigia kura, waweze kumwajibisha kwa ile imani waliyompa. Ukikaimisha mtu ambaye hawakumchagua wao watashindwa kumwajibisha na ukienda kumuhoji anasema mimi siyo Mwenyekiti nilikuwa nakaimu na anakimbia majukumu yake. Ahsante. (Makofi)
MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwa na tatizo la kuingiliwa katika maamuzi ya kesi na wanasiasa hasa kwenye maeneo ya vijijini na hivyo kuathiri yale maamuzi.

Je, Serikali inatoa maelekezo gani kwa maeneo hayo ya vijijini ambako kumekuwa na mwingiliano wa viongozi wa kisiasa hasa Madiwani?

Lakini pili kumekuwa na tatizo kubwa la Mabaraza haya kutokuwa na vifaa vya kufanyia kazi, lakini kutokuwa na ofisi, posho za kuweza kujilipa na mwisho wa siku imekuwa wakiona yule anayedaiwa au anayehukumiwa ndiyo mwenye uwezo, wanaangalia nani mwenye uwezo basi wanamu-award ili waweze kupata hizo fedha na mwisho wa siku waweze kujilipa au kuweza kununua hivyo vifaa?

Je, ni nani mwenye wajibu wa kutoa hivi vifaa na kutoa hizi posho lakini pia na ofisi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya wanasiasa ambao wanaingilia mambo hayo ya uendeshaji wa Mabaraza ya Usuluhishi ya Kata.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimeeleza kwenye jibu langu la msingi, haya mambo ni mambo ya kisheria ya tangu mwaka 1985 na yamefanyiwa marejeo mwaka 2002 wale Wajumbe wa Mabaraza ya Kata ni Wajumbe ambao wanatoka kwenye Kata husika kwa hiyo lazima uwe mkazi wa Kata husika kama siyo mkazi hupaswi kuingia katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili la kuangalia wakati unapata Wajumbe wa Uendeshaji wa Mabaraza ya Kata, ni lazima hao watu wasiwe na tuhuma zozote za jinai na makosa mbalimbali kwa lugha nyingine lazima wawe ni waadilifu katika eneo lile, lakini majina haya ambayo yanaombwa yanapaswa kubandikwa kwenye notice za matangazo ili kama kuna mwananchi ana pingamizi dhidi ya mtu yeyote mjumbe aliyeomba aondolewe, lakini hakuna nafasi kabisa ya kiongozi wa kisiasa kuingilia kwa sababu kuna Kamati ya Ward DC inapendekeza majina kwa maana ya maoni, lakini uteuzi wa mwisho wa wajumbe hawa unafanywa na Halmashauri akiwepo Mwanasheria wa Halmashauri na Mkurugenzi na viongozi wengine, na ikiwezekana Mkuu wa Wilaya anaingia katika eneo hilo kwa maana ya kufanya consultation.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mujibu wa sheria hakuna namna ya kuingilia, lakini kama kuna eneo ambalo viongozi wa kisiasa wanaingilia hayo ndiyo maeneo tunayohitaji kupata taarifa ili tuweze kuchukua hatua na kutoa maelekezo na kuendesha vizuri katika maeneo hayo bila kuingiza siasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, ni vitendea kazi ambayo inapelekea pia maamuzi ambayo yameyumbishwa kulingana labda na vipato na kuangalia nani amepeleka kesi katika eneo hili. Ni kweli kwamba tumepata pia maneno maeneo mbalimbali wanakosa vitendea kazi, lakini haya Mabaraza yanasimamiwa na Wakurugenzi wa Utendaji wa Halmashauri na Wanasheria wa Halmashauri na ndiyo maana baada ya kuchaguliwa wanapaswa waende watoe semina na mafunzo, lakini Bajeti za Halmashauri lazima ziwe na kipengele ambacho kinasaidia uendeshaji wa Mabaraza haya ya Kata na hata fedha ambazo wanapanga kwa mfano kesi imeamuliwa kutoka eneo moja ofisini kwenda kuangalia mahali ambapo kuna malalamiko inabidi gharama ile iwe ni gharama iwe ni gharama ya kawaida kabisa ndogo ambayo mtu wa kawaida ataifanya, na lengo la Mabaraza haya ni kupunguza umbali wa kuwafanya wananchi kutoka kwenye Kata yake kwenda kwenye Mahakama za mwanzo na Wilaya, lakini vilevile kuwasaidia watu wa kawaida kabisa ngazi ya chini.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba nielekeze Wakurugenzi Watendaji na Wanasheria katika Halmashauri zetu kama kuna maeneo kuna malalamiko makubwa na watu wanakuwa charged gharama kubwa, naomba wachukue hatua ili tuweze kusimamia, tuweke viwango vya kawaida kabisa ambavyo mtu wa kawaida anaweza kufanya, lakini mwisho isije ikatokea hata siku moja kwa sababu kuna mtu ana malalamiko yake na kwa sababu hana uwezo wa kifedha asisikilizwe hili litakuwa ni kosa kwa viongozi wetu ambao wanasimamia katika eneo lile na itakuwa inaenda kinyume kabisa na maelekezo ya Baraza na Uanzishwaji wa Baraza la Usuluhishi wa Kata, nakushukuru sana.
MHE. VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba unisikilize vizuri.

Kwa kuwa ni-declare interest kwamba niliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya kwa hiyo najua matatizo ya Mabaraza ya Kata. Mara nyingi wanaolalamika ni wale ambao hawana uwezo, ndiyo wanadhulumiwa ardhi na mashamba yao, wanaowadhulumu ni watu wenye uwezo na kwa sababu Halmashauri hazina uwezo wa kifedha wanaotoa gharama ya kuendeshea kesi hizo mahakama hiyo ni wale waliolalamikiwa wenye fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri haki itapatikana? Mimi nafikiri naomba unijibu. (Kicheko)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, haki inapaswa kupatikana hata kama hauna pesa, maelekezo ni kwamba zile bei ni kweli wanakubaliana, kwanza bahati nzuri viwango vya kutoza ni viwango ambavyo kwenye ngazi ya Kata ya Diwani na Ward DC yake wanaweza ku-moderate, Halmashauri zinaweza kusimamia, Mkuu wa Wilaya anaweza kuingilia, Mkuu wa Mkoa anaweza kuingilia, kwa hiyo, kuna flexibility kubwa sana ambayo unaweza ukaangalia hapo, lakini mahali pengine ilipotokea tumetoa maelekezo isitokee mtu ambaye hana uwezo asitendewe haki.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanapanga viwango vya kawaida na maeneo mengine tumetoa maelekezo unakuta kwamba kwa mfano hata hukumu imetoka, lakini ile gharama ya kwenda kuchapisha ni kubwa anatozwa mwenye kesi, ikikosa anapeleka mtu mwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba nitoe maelekezo ni kwamba hili jambo ni jambo muhimu, jambo la kisheria na lililenga kimsingi kusaidia watu wa ngazi ya chini au maskini ndiyo Mabaraza ya Kata lililenga naomba viongozi wetu wakiwemo na Waheshimiwa Wabunge tuwasiliane, kama kuna mahali Mheshimiwa Mwamoto kuna mwananchi amedhulumiwa au hakusikilizwa kwa sababu hana fedha nipo tayari twende sasa hivi tukamsikilize na apate haki yake, ahsante.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, report ya UNESCO ya mwaka 2018 inaeleza kwamba huwezi kuwa na viwanda kama huna nishati ya kutosha na maji ya kutosha. Je, Serikali inajua suala hilo? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; suala la viwanda 100 kila Mkoa ni suala lililotamkwa kisiasa. Serikali inaweza ikatuambia ni viwanda vingapi vilivyotengenezwa tayari katika Taifa hili la Tanzania ikiwepo Mkoa wa Mbeya kuna viwanda vingapi vimeshajengwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza anataka kujua kama Serikali inatambua umuhimu wa nishati ya umeme wa kutosha ili kuendesha viwanda hivi. Jibu ni kwamba Serikali ya Chama cha Mapinduzi, Awamu ya Tano inatambua sana na ndiyo maana imeanzisha mikakati mbalimbali ya kuboresha na kuongeza umeme, kuna umeme wa gesi unazalishwa, lakini pia mpango mkakakti mkubwa sana ambao namuomba Mheshimiwa Sophia auunge mkono, ule wa kupata umeme kutoka Bonde la Mto Rufiji ili tupate umeme wa kutosha kwenye viwanda lakini pia matumizi ya majumbani. Lakini hata na wananchi wa kawaida hawajasahaulika ndiyo maana kuna umeme wa REA unalipwa kwa gharama ndogo sana ya shilingi 27,000 kwa kila Mtanzania na kila Kijiji, na nyumbani kwao watapata umeme wa kutosha sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anataka kujua idadi ya viwanda ambavyo vimepatikana katika kila Mkoa na anasema ni tamko la kisiasa. Kwanza naomba nimwambie Mhehsimiwa Mbunge kwamba hili ni tamko mahususi la mpango mkakati wa Chama cha Mapinduzi, siyo tamko la kisiasa linatekelezeka, tumeshazindua, tumetuma mwongozo nchi nzima, Wakuu wa Mikoa wameitwa hapa Dodoma, Wakuu wa Wilaya wameelekezwa, Mamlaka ya Serikali za Mitaa imetenga maeneo mbalimbali ya kuanzisha viwanda, imeshiriki Mbeya, tumeenda Lindi na maeneo mengine. Tumeshapata viwanda vipya zaidi ya 3000 katika nchi nzima na nitawasiliana na viongozi wa Mkoa kupata idadi haliis ya Mkoa wa Mbeya ambao anatoka yeye kupata hivyo. (Makofi)

Kwa hiyo, naomba nimuombe Mheshimiwa Sophia ashiriukiane na Serikali ya Chama cha Mapinduzi na ikiwezekana na mwenyewe awezeshe, awe na kiwanda ili akina mama kama yeye waweze kupata uchumi jumuishi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. JOSEPH R. SELASINI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu wa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya vijana, akinamama na walemavu umeonesha kwamba katika baadhi ya mikoa fedha hizi zinatumika vibaya, lakini baadhi ya Mikoa kama Simiyu na Dar es Salaam wamebuni utaratibu wa kuwakopesha vijana na kuanzisha viwanda vidogo vidogo ambavyo vinajumuisha vijana, akinamama na walemavu kwa pamoja na hivyo kuanza taratibu utekelezaji wa hii sera ya viwanda katika jamii.

Sasa je, Serikali haioni kwamba upo ulazima wa mawazo haya na utekelezaji huu wa Simiyu na Dar es Salaam kuenezwa katika mikoa mingine ili fedha hizi ziweze kusaidia kuanzisha viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kutekeleza huo mkakati wa viwanda?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, Mheshimiwa Selasini ni Mjumbe wa Kamati ya Utawala ya Bunge hili tukufu pamoja na Mheshimiwa Rweikiza, Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora, lakini Wajumbe hawa wa Kamati hii tunawashukuru sana Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwenye bajeti iliyopita tumeshirikiana vizuri, haya ni mawazo ya Kamati ya Utawala ambapo Mheshimiwa Selasini alikuwepo pale. Simiyu tumeenda na mimi nimetembelea Kiwanda kile cha Chaki lakini pia Dar es Salaam tunafahamu na juzi Jumatatu iliyopita nimefanya ziara katika Mkoa wa Dodoma na wenyewe wamesaidia kununua mashine ya kutengeneza matofali na vijana wanaendelea kujiajiri.

Mheshimiwa Naibu Spiika, naomba nitoe maelekezo ambayo yatakuwa ni marudio; tumetoa maelekezo asilimia 10, asilimia nne ile ya akinamama, nne kwa vijana na mbili kwa watu wenye ulemavu au mahitaji maalum. Tumeelekeza badala ya kutoa fedha kwa vikundi au mtu mmoja mmoja ambazo kimsingi hazileti tija, lengo la kukopesha fedha hizi ni kuwasaidia akinamama na makundi haya muhimu ili yaweze kuboresha maisha yao. Wakurugenzi wameelekezwa, Makatibu Tawala wameelekezwa ili iete tija. Wanaweza wakaatenga maeneo ya viwanda, wakawakusanya vijana, akinamama na watu wenye ulemavu na tumeshatoa kanuni ipo mtaani ili waelekezwe na wanapata mafunzo wakianzisha viwanda vidogo vidogo watajiajiri, fedha itapatikana, wataboresha maisha yao, lakini pia warudishe fedha ili makundi mengine zaidi yaweze kupata huu msaada na mchango wa Serikali. Ahsante. (Makofi)
MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, nina maswali mawili ya nyongeza kama yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, la kwanza; kumekuwepo na hofu na malalamiko makubwa juu ya mbinu chafu ambazo zimeweza kujitokeza hivi karibuni wakati wa urejeshaji wa fomu kwa vyama vya upinzani kuambiwa kwamba viongozi hao/wagombea hao wa upinzani hawana sifa jambo ambalo limekuwa likileta hisia mbaya kwamba Chama cha Mapinduzi kinataka ibaki peke yake katika uchaguzi.

Je, huoni Mheshimiwa Waziri mbinu hii chafu ya kusema wagombea wa upinzani hawana sifa kwa hila na ujanja kutaweza kupelekea uchaguzi huu usiwe wa haki na huru na kweli atakayeshinda mtatangaza? La kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili; kumekuwa na taratibu ambazo zimekuwa zikiendelea hivi sasa katika baadhi ya maeneo kuanza kufanya kampeni kwa njia ya ujanja ujanja. Mfano, pale Morogoro kumekuwa na uzinduzi wa Morogoro ya Kijani huku wakieleza kwamba tunaelekea chaguzi za Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji wakati uchaguzi uko Oktoba.

Je, ni kwa nini basi matangazo haya, mabango haya na utaratibu huu unaofanywa kwa upande mmoja tu wa Chama Tawala usidhibitiwe mapema ili kutuondoa na matatizo ambayo yanaweza kujitokeza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, kwanza hakuna mbinu chafu. Utaratibu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utatangazwa tarehe na mwenye mamlaka, uwekwe utaratibu wa kujiandikisha kwa muda utakaotajwa, yatabandikwa majina kwenye mbao za matangazo kila watu watahakiki wakazi katika mtaa husika na kijiji au kitongoji, wataenda kwenye kampeni sawa kwenye vyama vyote na uchaguzi utafika watachaguliwa ila kwa sababu Mheshimiwa Masoud anajua kwamba watakaochaguliwa wengi wagombea wa Chama cha Mapinduzi hiyo ndiyo hofu uliyonayo kwa sababu kazi nzuri ya Chama cha Mapinduzi ambayo imefanywa chini ya Dkt. John Pombe Magufuli, miradi mikubwa ya kimkakati, Rais ambae ni wa mfano katika Afrika na dunia anayekutana na makundi mbalimbali, uchaguzi ukitangazwa uwezekano mkubwa wa kupata asilimia 98 wagombea wa Chama cha Mapinduzi ndiyo huo ambao unakutisha, lakini tutakwenda kwenye uchaguzi, watu wako wajiandae vizuri, kanuni zipo, kuna Kamati za Rufaa, kama hujaridhia unaweza ukaenda Mahakamani ukapata haki yako Mheshimiwa Mbunge usiwe na hofu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili Mheshimiwa Mbunge anauliza kuanza kufanya kampeni na CCM ya Kijani. Hapa ni mipango ya Chama cha Mapinduzi. Chama hiki ni Chama Tawala, kinakagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na kujipanga na uchaguzi ujao. Chama makini, chama kikongwe lazima kiwe na mbinu nyingi kila wakati na ndizo zonachanganya watu akiwepo Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kinachofanyika na CCM wanaita wanachama wao, wanakagua kadi za uanachama, wanapata taarifa ya uchaguzi, usiwe na hofu na hata hivyo ukiangalia CHADEMA wale CHADEMA ni msingi walikuwa Katavi, wameenda Rukwa, wapo kila mahali tuna taarifa hizo na wanafanyakazi.

Sasa ndugu yangu Mheshimiwa kama wewe hujajipanga usiwaonee nongwa wenzako. CCM ipo kazini, CCM ya Kijani itaendelea kila mahali hata mimi Bunge likiaihirishwa nifanya Ukonga na nakushauri uende kwenye chama chako andaa mkakati. Watanzania wake mkao tayari, Serikali ya Chama cha Mapinduzi iko makini imejiandaa, sheria zitafuatwa, kanuni zitafuatwa na sheria zipo. Kama hujaridhika mahali popote uko aggrieved unakeenda Mahakamani lakini uchaguzi huu utakuwa uchaguzi mzuri sana, hofu yako nikutoe, wananchi ndiyo watakaochangua, wana macho wanaona, wana masikio wanasikia, CCM ndiyo habari ya mjini. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Watendaji wa Vijiji na Mitaa ni muhimu sana katika uchaguzi huu, lakini kuna vijiji vingi havina watendaji. Je, Serikali ina mpango gani wa haraka wa kujaza nafasi hizi kabla ya uchaguzi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu unasimamiwa na watendaji wa ngazi za chini wale Watendaji wa Vijiji na Mitaa, Watendaji wa Kata na mpaka ngazi ya Halmashauri na ni kweli kwamba kuna baadhi ya maeneo ambayo hayana watendaji hawa, lakini nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, uko utaratibu wa Kiserikali bahati nzuri hawa ni watumishi wa Serikali. Tunaendelea kuchukua hatua kuajiri na kuziba mapengo. Ikitokea uchaguzi unafika eneo fulani au kijiji hakuna Mtendaji, wale watumishi wa Serikali wakiwepo watumishi wa afya, walimu wanapewa jukumu watasimamia kwa sababu wote wanaitwa, wanapewa semina na mafunzo na wanaapishwa kiapo cha utii, halafu wanafanyakazi za Kiserikali na wakimaliza kazi hii wanarudi kwenye majukumu yao ya kawaida. Ahsante.
MHE. KHATIB SAID HAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, baadhi ya matukio yaliyojitokeza katika baadhi ya chaguzi za marudio ni lile tukio la Wakurugenzi kujificha pale inapotokea wagombea wa vyama vya upinzani wanarejesha fomu na hivyo kuwakosesha sifa ya kuwa wagombea.

Je, Mheshimiwa Waziri amesema Chama cha Mapinduzi kina mbinu nyingi, hii ni moja kati ya mbinu mnayoitumia ili kuhalalisha ushindi wa haramu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, mbinu za CCM ni za ushindi safi siyo ushindi mchafu, kwa hiyo siyo mbinu chafu hizo anazozungumza, ni ushindi safi, mipango, mikakati.

Sasa naomba nirudie kumjibu Mheshimiwa Khatib kwamba Wakurugenzi wala hawajakimbia, hakuna Mkurugenzi aliyekimbia na ndiyo maana maeneo yote ambayo maana yake wagombea wa Chama cha Mapinduzi walikuwa na sifa kuliko wagombea wengine wote na walijua mapema kwamba wasingeweza kuchaguliwa, lakini mpaka leo hatuna taarifa ya nani anayesema Mkurugenzi wa Halmashauri fulani amekimbia na amefungua kesi Mahakamani kudai hiyo haki yake, hakuna hiyo kesi mpaka leo. Kama wamekimbia wangeweza kulalamika, hatuna malalamiko officially. Ofisi ya Rais, TAMISEMI ndiyo inasimamia Halmashauri zote nchini na mamlaka za mitaa, hatuna taarifa ya hiyo kesi.

(Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila kufuata utaratibu)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nirudie; Waheshimiwa wananchi wasitiwe hofu na watu ambao wanaogopa siasa za ushindani. Kinachofanyika hapa ni kushindanisha Chama cha Mapinduzi na kazi yake nzuri na vyama vingine ambavyo havijafanyakazi nyingine yoyote na huenda wakifanya ni mambo madogo madogo sana, mambo makubwa makubwa ya Tanzania haya yamesimamiwa na Serikali kwahiyo mnapopeleka wagombea kwanza lazima utegemee mambo mawili, aidha, unashinda au unashindwa. Ukishindwa kubali na ukishinda mshukuru Mungu. Ahsante. (Makofi)
MHE. MAFTAHA A. NACHUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza kwa kuwa hawa Wenyeviti wa Serikali za Vijiji na Mitaa wanafanya kazi inayofanana kabisa na hawa Watendaji wa Vijiji na Mitaa, lakini Serikali inawalipa Watendaji tu. Je, Serikali haioni kwamba inawabagua Wenyeviti hawa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa kuwa Halmashauri nyingi hivi sasa mapato yake yamechukuliwa na Serikali ikiwemo kodi ya majengo pale Mtwara Mjini na nchi nzima kiujumla ambayo ilikuwa inasaidia sana kupata makusanya ili kuweza kuwalipa posho kwa mujibu wa sheria hawa Wenyeviti wa Vijiji Serikali ama Vijiji vingi ama Halmashauri nyingi zinashindwa kutoa hata posho ya shilingi 20,000 kwasababu haina vyanzo vya mapato ikiwemo kodi ya majengo.

Je, Serikali ni lini itarudisha kodi hii ili halmashauri nyingi ziweze kukusanya na kuwapa posho Wenyeviti wa Mitaa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge swali lake la kwanza anasema Serikali inawabagua Wenyeviti kwa sababu Watendaji wanalipwa. Suala hili siyo kweli kwa sababu wanapokuwa wanaomba hizi kazi utaratibu unatofautiana, Wenyeviti wa Mitaa wanachaguliwa na wananchi wao na wale Watendaji wanaomba kazi na wanaajiriwa na Serikali na nimeeleza kwenye jibu la msingi ni kwamba malipo ya Wenyeviti wa Mitaa na Wenyeviti wa Vijiji na Wajumbe wao inategemea makusanyo ya mapato ya ndani na tumeshapitisha bajeti, hatujazuia Halmashauri kuwa na uwezo wa kuwalipa Wenyeviti tukazuia, ndiyo maana tukasema tunatambua kazi nzuri inayofanywa kwa sasa utaratibu uliopo Halmashauri yenye uwezo italipa posho kulingana na uwezo ule na Wenyeviti wa Mitaa waendelee kutuvumilia uwezo ukiruhusu hatujakataa kuwalipa ila uwezo ukiruhusu watalipwa.

Kwa hiyo, Halmashauri zetu kama watabuni vyanzo vingine vya mapato wakipata uwezo wa kuwalipa watalipa Serikali haijazuia kabisa. Lakini hakuna ubaguzi na Wenyeviti wanajua kwamba hawa ni waajiriwa, wanaombwa na vyeti, wana-qualify na hawa ni watumishi wa wananchi ambao wamechaguliwa na wananchi wale na wanafanyakazi nzuri sana kama tulivyosema.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili anazungumza kurudisha kodi ya majengo, kwa hiyo, kuwezesha Serikali zetu kwenye Halmashauri kuwalipa Wenyeviti wa Mitaa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kodi hii kuchukuliwa kodi ya majengo pamoja na mabango pamoja na kodi zingine hii fedha inachukuliwa yote kwa ujumla wake nchi nzima inapelekwa kwenye kapu kuu la Serikali, kwa hiyo, hata miradi ya kimkakati barabara zinazojengwa, miradi ya maji, mishahara ya watumishi hii ni fedha ambayo inatumika kule, kwa hiyo siyo kwamba haina kazi. Lakini tumeelekeza Halmashauri na tumewaambia wabuni miradi mbalimbali ya kimkakati na Wizara ya TAMISEMI, Wizara ya Fedha tunawezesha kuanzisha miradi mikubwa mikubwa na Mtwara nimekuja pale kuna miradi mikubwa inaanzishwa.

Kwa hiyo ukipata uwezo kama huu ukapata fedha katika eneo lile na vyanzo vingine ukibuni bila kunyanyasa wananchi wataongezewa posho zao. Kwa sasa Halmashauri itaendelea kulipa kwa kadri itakavyoweza na pamoja kazi nzuri inayofanyika hatujazuia Halmashauri kulipa kulingana na uwezo wake.
MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kuwa Halmashauri nyingi nchini zinalipa hiyo posho ya Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kati ya shilingi 5,000 mpaka shilingi 10,000. Je, Serikali haioni sasa kwamba imefika wakati ambapo wanapaswa kutoa maelekezo viwango vya posho hizo kupanda na vikawa vinafanana kwa Halmashauri zote nchini?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Moshi Mjini ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Mstaafu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hoja ya nyongeza ya posho ya Wenyeviti wa Mitaa inategemea na uwezo wa Halmashauri, mimi nafahamu natoka katika Halmashauri ya Ilala. Ilala wanalipa posho kwa mwezi shilingi 100,000 Wenyeviti wa Mitaa na wanalipa kila baada ya miezi mitatu, mitatu, lakini hiyo inategemea na mapato makubwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Temeke.

Kwa hiyo, kama Moshi na maeneo mengine yana uwezo kama nilivyosema hatujazuia kabisa, fedha inayokusanywa kwenye Halmashauri kuna maelekezo yametoka, kwa mfano asilimia 10 itaenda kwenye vijana, akinamama na watu wenye ulemavu. Fedha zingine kuna maelekezo mengine yametoka, lakini inayobaki fedha ya maendeleo itatengwa, lakini inapohusika na uendeshaji kama ni Halmashauri ngazi ya Kata, Vijiji na Vitongoji inahusika. Kwa hiyo Halmashauri yenye uwezo itaendelea kulipa posho kubwa kulingana na uwezo wake. H lo linaruhusiwa hatujazuia. Ahsante.
MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, bahati nzuri mimi nimekuwa niliwahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya wakati ule Halmashauri zote vyanzo vyote vilikuwa pale, lakini kwa kuwa Serikali imechukua vyanzo vyote na tulikubaliana mpeleke ruzuku ya kutosha kwenye Halmashauri ili viongozi hawa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji na Madiwani walipwe. Kwa nini hamuongezi ruzuku kwenye Halmashauri za Wilaya?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Senator Mzee Lubeleje kama ifuatavyo:-

Ni kweli ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mstaafu na alivyozungumza ni kweli wakati huo, lakini sasa hivi ni kweli kwamba baadhi ya vyanzo vimechukuliwa ili viweze kuratibu kwa sababu kuna Halmashauri ambazo zilikuwa na majengo mengi na mabango mengi na walikuwa wanaweza kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja tofauti na maeneo mengine, Serikali imetumia busara kwamba fedha hizi zikusanywe centrally, lakini zipelekwe kwenye miradi ya wananchi ambayo ni nchi nzima hata Halmashauri ambayo ilikuwa na mapato machache ya mabango au na majengo inapata miradi mikubwa ya kimkakati ili maendeleo yaende katika msambao unaofanana katika nchi yetu.

Lakini hoja yake ya kuongeza posho na kupeleke ruzuku, miradi mingi ya ruzuku ilikuwa inategemea pia na wafadhili kutoka nje, sasa hivi ndiyo tukasema fedha zipo za kuanzisha miradi ya kimkakati na maelekezo yameenda kwenye Mikoa yote na Halmashauri zote. Ni wataalamu wa Halmashauri yako Mheshimiwa Lubeleje wanakaa, wanaandaa andiko, wanakaa na watu wa Wizara za Fedha na TAMISEMI, miradi inapelekwa ndiyo maana nikasema ukipata miradi ya kimkakati, masoko, stand kubwa kubwa zile mapato yataongezeka na kwa hiyo Halmashauri itaweza kulipa posho za Wenyeviti wa Mitaa.

Mheshimiwa Spika, niseme maneno ya nyongeza wenyeviti wa mitaa tunatambua kazi kubwa sana ambayo wanafanya na ndiyo maana miradi yote mikubwa ya kimkakati ipo kule wanaisimamia kwa kushirikiana na viongozi wa Kata na Madiwani na wengine, uwezo wetu wa Serikali ukiwa mkubwa tungeweza kulipa mishahara na posho kubwa kubwa, kwa sasa hatujafikia huko.

Mheshimiwa Spika, tunaomba Wenyeviti wa Mitaa waendelee kufanya kazi kwa sababu wameaminiwa na watu wao, uwezo wa Serikali …, lakini Halmashauri zetu wajipange kila kinachopatikana wasiwasahau Wenyeviti wa Mitaa, wawawezeshe ili waweze kufanya kazi zao vizuri. Ahsante.
MHE. MARY D. MURO: Mheshimiwa Spika, ahsante nafikiri hata wewe umeshangaa ukiwa kwenye kiti hicho hicho mwaka jana nilisimama mbele yako nikiuliza kwa nini chuo hiki hakifanyiwi ukarabati na ilijibiwa na Wizara ya Elimu mpaka mwaka jana ilikuwa haijulikani kama chuo hiki kiko chini ya Wizara ya Elimu au TAMISEMI, walipeleka Wizara ya Elimu pesa ya chakula wakaenda kuwanyang’anya wakasema kwamba chuo hiki hakiko chini ya Wizara ya Elimu na mpaka tunavyoongea saa hizi watoto wa shule pale hawana chakula sasa hivi tunajibiwa na TAMISEMI ina maana mpaka sasa hivi ndiyo imejulikana kwamba chuo hiki kiko chini ya TAMISEMI.

Sasa swali je, ni lini chuo hiki kitapata ruzuku ya chakula kwa sababu makusanyo yao ni madogo sana?

La pili, ni lini majengo na miundombinu ya chuo hicho yatafanyiwa uboreshaji?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ni kweli Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia suala hili na fedha zilipelekwa pale, hiki chuo kiko chini ya TAMISEMI, kwa hiyo ilipogundulika kwamba fedha zimepelekwa pale na Wizara ya Elimu, ikabidi zirudishwe zipelekwe kwa malengo yaliyokuwa yamekusudiwa. Lakini nimesema kwamba chuo hiki kimeshafanyiwa tathmini, tumepeleka fedha pale milioni 70 kwa mapato ya ndani kwa maana ya kupunguza shida iliyopo, lakini tunaendelea kutafuta fedha zikipatikana wakati wowote hata leo kitaanza kufanyiwa ukarabati huo mkubwa wala hamna shida.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili anauliza habari ya chakula, hili naomba nilipokee tulifanyie kazi kwa sababu utaratibu ni kwamba wanafunzi wote ambao wapo maeneo yote nchi nzima wanaosoma lazima wapewe chakula na tunapeleka fedha ya chakula kulingana na idadi ya wanafunzi katika eneo hili na hawezi kukaa shuleni bila kuwa na chakula.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba niahidi kwamba hili tutalifanyia kazi mapema iwezekanavyo liweze kufanyiwa kazi kama kweli ni tatizo katika eneo hilo.
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri juu ya tatizo hili, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo;

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la migogoro ya ardhi imekuwa ni changamoto kila eneo katika nchi hii na kama swali la msingi linavyosema kwamba katika Jimbo la Wilaya ya Handeni kuna changamoto ya migogoro ya ardhi. Je, nini mpango mkakati wa Serikali hususan kwa kupima maeneo haya ya ardhi kwa kuainisha maeneo ya wakulima na wafugaji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, changamoto hii ya migogoro ya ardhi iliyopo Handeni inafanana sana na changamoto iliyopo kuna mgogoro baina ya Wilaya ya Kilindi na Wilaya ya Kiteto ambayo imedumu muda mrefu sana. Je, nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba inatatua mgogoro huu? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Mbunge wa Kilindi kwa niaba ya Mbunge wa Handeni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba kuna maeneo mengi ambayo hayajapimwa katika Halmashauri zetu na katika Tawala za Mikoa, lakini bahati nzuri Serikali imepunguza sana gharama za upimaji na najua wapo wadau mbalimbali ambao wanaendelea katika maeneo mbalimbali ya kupima maeneo yetu. Mimi naomba nitoe maelekezo kwa viongozi na ushauri kwa wananchi kwamba ukipima eneo lako thamani yako inapanda, unaweza ukakopesheka na ukapata fedha ili kujiendeleza katika eneo lako. Kwa hiyo, wale watu muhimu ambao wanafanya huo upimaji katika maeneo yetu ambao unatambuliwa na viongozi wetu wa vijiji, mitaa, kata, halmashauri na mikoa wawape ushirikiano na wapime maeneo yao ili kuweza kupata hati lakini pia kuweza kupata fedha katika benki mbalimbali katika kuendeleza maeneo yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili anauliza suala la mgogoro ambao upo kati ya Kilindi na Kiteto. Yako maeneo mbalimbali ambayo tumepokea malalamiko yao, iko migogoro ambayo ipo katika Wizara ya TAMISEMI ya mipaka, tunaishughulikia na tunafanya hivyo kwa sababu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili angalau maeneo haya yaweze kutambulika vizuri na uchaguzi usiwe na maneno maneno mengi ya kuhusu mipaka. Yapo mambo ambayo yanahusiana pia na matumizi ya ardhi ambayo yapo kwenye Wizara ya Ardhi, haya pia tunashirikiana na wenzetu wa WIzara ya Ardhi ili kuweza kuyatatua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama kuna mgogoro ambao ameutaja hapa sasa tuwasiliane baadae ili tuweze kupata details/taarifa sahihi za eneo hili na ninamhakikishia tutafanya kazi nzuri kuweza kuhakikisha kwamba eneo hili mgogoro unamalizika na watu wetu waendelee kuishi kwa amani na kushirikiana kama ni wafugaji au wakulima, Mheshimiwa Rais tayari ameshatoa maelekezo ili maeneo yatengwe na kuheshimiwa ili watu wetu wafanye kazi bila kugombana kwa kuleta maendeleo katika nchi yetu. Ahsante.
MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Upo mgogoro wa ardhi wa kimpaka kati ya vijiji vya Msandamuungano, Sikaungu na Gereza la Molo, je, ni lini Serikali itatatua mgogoro huo? Bahati nzuri na Waziri wa Mambo ya Ndani nilishamuona juu ya mgogoro huu.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kutoa hoja hii, lakini iko migogoro mingi kama nilivyosema kwenye swali langu la msingi kwamba yako maeneo ambayo yana matatizo ya mipaka. Tumeshayapokea, tunayafanyia kazi na naomba nimuombe Mheshimiwa Mbunge, baada ya kumaliza kipindi cha maswali na majibu, tukutane ofisini kwa sababu akizungumza mpaka wa kijiji na kijiji hii inakuwa ni kazi ya TAMISEMI inahusiana na mambo ya GN. Ukizungumza habari ya magereza maana yake ni gereza kati ya wananchi lakini pia na Wizara yetu ya Mambo ya Ndani. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge tuonane, tuone kama maeneo haya ni miongoni mwa maeneo ambayo tumeyaainisha yenye malalamiko ili tuyafanyie kazi, mgogoro huu utaisha. Kama ni mipaka na mipaka na wenzetu wa Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, maelekezo ya Mheshimiwa Rais ni kwamba maeneo yote ambayo yana migogoro yaishe mapema iwezekanavyo, kama kuna magereza iko pale inafanya kazi nzuri ya watu wetu, kama kuna vijiji ni kazi nzuri ya watu wetu ili malalamiko yasiwepo tuyamalize sisi kama viongozi kwa niaba ya Mheshimiwa Rais. Ahsante.
MHE. JUSTIN J. MONKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, upo mgogoro kati ya Manispaa ya Singida pamoja na Halmashauri ya Singida DC katika eneo la Kata ya Muhamo kijiji cha Muhamo, eneo la njiapanda ambapo tuna uongozi wa kitongoji na wakati huo huo eneo hilo hilo lina Mwenyekiti wa Mtaa na Mheshimiwa Naibu Waziri alipofika kwenye ziara Singida aliambiwa na anazo taarifa za mgogoro huu. Je, ni lini mgogoro huu utatatuliwa ili wananchi hao waweze kukaa kwa amani? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, ni kweli kwamba mimi nilifanya ziara Singida Mjini na Vijijini na katika kikao changu na watumishi Waheshimiwa Madiwani wa eneo lile walitoa taarifa za mgogoro huu na kuna GN pale mbili. Wakati Singida inaanzishwa kuwa mji mdogo, waligawana mali na mipaka ikatengenezwa na GN ikawekwa. Baada ya kuwa Manispaa kulikuwa na GN nyingine. Sasa yapo mambo ambayo nimeshaelekeza wataalam wetu wanafanyia kazi na Mheshimiwa Mbunge anafahamu, tulizungumza mara kadhaa, ninaomba nitoe maelekezo kwamba mgogoro ili tuutatue sisi TAMISEMI ni lazima watu wa Halmashauri ile na Manispaa wafanye kazi yao na watu wa Mkoa wafanye kazi yao halafu watuletee taarifa hapa. Lakini inavyoonekana ni kwamba bado kama kuna mambo ambayo hayajaenda sawa kwa maana ya ngazi ya Wilaya ya Manispaa lakini pia na Mkoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge jambo hili tumeshalichukua kama TAMISEMI, nimeshatoa maelekezo kwa wataalam wetu wapitie zile GN mbili zinaleta mgogoro ili kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019 mwaka huu ambao utafanyika Novemba, hili jambo tuwe tumelimaliza ili watu wetu kwa kweli waendelee kufanya kazi kwa kushirikiana vizuri sana kwa sababu Singida ni moja haiwezi kuwa na malalamiko ya hapa na pale ambayo hatuwezi kuyafanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hili tunalifanyia kazi kabla ya uchaguzi ujao tutakuwa tumelipatia majibu na Mheshimiwa Mbunge Monko waendelee kuwa na amani na watu wako wajue kwamba tutalifanyia kazi kama Serikali na litaisha mapema sana. Ahsante.
MHE. YOSEPHER F. KOMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kama ambavyo aliyejibu swali amekiri kwamba Shule hii ina changamoto nyingi. Shule hii imeanza mwaka 1995 lakini iko ndani la eneo la shamba ambalo lilikuwa la Mkonge la Mjesani Estate, na mpaka sasa tunavyoongea shule hii haina hatimiliki ya lile eneo, kwa hiyo walimu na watendaji pale wamekuwa wanaishi kwenye shule ile kama vile wamepanga. Kwa hiyo nilitaka nifahamu, Wizara ina mkakati gani wa kuhakikisha shule hii inapata hatimiki ya eneo ili iweze kufahamu mipaka ya eneo lake kama Shule?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kama ambavyo amesema Mheshimiwa Waziri. kuhusu suala la maj. Pale kuna Mto Zigi ambao ndio wanaoutumia wanafunzi kuchota maji kwa ajili ya matumizi pale shuleni, na kumeshatokea ajali zaidi ya mbili ya wanafunzi pale kutaka kuuawa na mamba, ule mto una mamba. Je, Serikali kama mdau mkuu kwenye hili suala la elimu wako tayari kushirikiana na halmashauri na wadau wengine kuhakikisha milioni 7.6 inapatikana kwa wakati ili kupeleka maji kwenye shule ile?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Yosepher Komba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tunahitaji maeneo yote ya Umma yapimwe na yapate hatimiliki ili kuwa na uhalali wa eneo hilo lakini pia kupunguza migogoro ambayo inatokana na wananchi kuvamia maeneo hayo ya umma ikiwemo Mashule kama alivyotaja. Naomba nimuelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri hii ya Mkinga atume wataalam wapimaji wakapime eneo hilo ili waweze kupata hati na kuondoa migogoro ambayo inaweza kuwepo katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili anazungumzia habari ya maji. Tumesema kwamba tathmini imeshafanyika, zinatakiwa shilingi milioni 7.6, na Serikali ipo tayari kushirikiana na halmashauri, na pia Mheshimiwa Mbunge ashirikiane na sisi. Sote kwa pamoja tuhakikishe kwamba tumepata maji katika eneo hili na watoto wetu waweze kupata huduma nzuri na masomo yaendelee.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na changamoto za maji na umeme katika shule zetu kumekuwa na tatizo kubwa sana katika shule nyingi nchini hasa Mkoa wa Mara pamoja na Jimbo la Bunda Mjini; tatizo la matundu ya vyoo. Athari kubwa ni kuleta magonjwa ya mlipuko kwa wanafunzi wetu pamoja na shule kufungwa. Sasa ningependa kuiuliza Serikali, ina mpango gani wa kushirikiana na taasisi mbalimbali katika kuhakikisha kwamba matundu ya vyoo yanajengwa shuleni ili kuwafanya wanafunzi wetu wasome wakiwa katika hali ya usalama zaidi wasipate magonjwa ya mlipuko?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tuna upungufu mkubwa sana wa matundu vyoo nchi nzima kwa shule za msingi na sekondari.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili linapaswa kuwa jambo shirikishi, haiwezi kuwa kazi ya Serikali peke yake. Serikali imetoa Waraka ambao umeanza kutumika, wa mwaka 2016 ambao unaonesha namna ambavyo wadau mbalimbali wakiwepo na wananchi wa kawaida wanaweza kushirikiana kuweza kupunguza changamoto za miundombinu ya elimu. Serikali imekuwa ikifanya kazi hii awamu kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha; na mwaka wa fedha ambao unaanza Julai mwaka 2019/ 2020 tumetenga fedha zaidi ya shilingi bilioni 184 kwa ajili ya kuondoa kero katika miundombinu ikiwepo matundu ya vyoo. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge na wadau wengine tushirikiane; unapokuwa unaweza kuchangia tuchangie ili kuweza kupunguza adha hizi ambazo zipo katika shule zetu, ahsante.
MHE. AMINA S. MOLLEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Changamoto hii ya vyoo inawaathiri zaidi watoto wenye mahitaji maalum; watoto wenye ulemavu wanalazimika kutambaa katika uchafu, vinyesi vya watoto wenzao; na hiki ni kilio changu tangu nimeingia Bungeni.

Naomba mkakati madhubuti wa Serikali, wana mkakati gani wa kuhakikisha kwamba watoto wenye mahitaji maalum wanasoma katika mazingira mazuri na tunawaondoa katika hiyo hali hatarishi ya kuweza kupata magonjwa mbalimbali? Ahsante?. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, (Makofi)
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amina Mollel kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba watoto na watu wote wenye mahitaji maalum wanahitaji special treatment ili aweze kuishi pamoja vizuri katika jamii yetu. Serikali imekwishaelekeza majengo yote mapya ambayo yanajengwa, si ya elimu tu, majengo yote ya Umma; wanapojenga jengo la Mkuu wa Wilaya, Mkoa, vituo vya afya zahanati na hospitali za mikoa pamoja na shule zote tunazingatia mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum. Lazima kuna chumba maalum cha choo kwa ajili ya watu hao, lakini pia na watoto wa kike wakujisitiri wakati wao wa hedhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kwa hiyo, mambo hayo tunaomba yazingatiwe na uongozi wote katika ngazi ya mikoa ya wilaya wafuate maelekezo ya Serikali. Tunapofanya ziara mbalimbali katika mikoa yetu miongoni mwa kazi ambazo tunafanya tunakagua kama kweli katika choo kilichojengwa kuna choo maalum. Maeneo yote tumefanya hivyo na jambo hilo linaendelea kufanya kazi vizuri. Hata hivyo majengo ya zamani yanapofanyiwa maboresho pia na jambo hili lizingatiwe; mahitaji maalum ni muhimu na limekubalika lazima lifanyiwe kazi, ahsante.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona, Shule ya Sekondari ya Mumiterama iliyopo Wilaya ya Ngara imeanzishwa mwaka huu na haijawahi kupatiwa fedha yoyote kwa ajili kuendesha.

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka pesa katika shule hiyo, kwa sababu ina changamoto nyingi, maji usafiri na makazi ya watumishi?
NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushuruku, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver Semuguruka kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nipokee ombi lake, kwa sababu shule inapokuwa inaanzishwa kwanza kuna mambo ya kuzingatia, tunaangalia vigezo mbalimbali, Ofisi ya Rais TAMISEMI, pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Sasa kama shule imesajiliwa imeanza kweli haijawahi kupelekewa fedha naomba Mheshimiwa Mbunge baada ya kipindi cha maswali na majibu tuwasiliane tuone ni kwa nini haijapata na kama kuna ukweli wowote tuweze kuchukua hatua, ahsante. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, Mheshimiwa Waziri, hivi karibuni alikuja Lushoto ambako kulikuwa na tatizo la upangaji wa ardhi katika Mji Mdogo wa Mnazi ambapo pesa ambazo zimetumika vibaya nje ya utaratibu na ulitoa maagizo. Sasa nataka kujua ni kwa kiasi gani jambo lile Ofisi ya Rais, TAMISEMI imelishughulikia?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mji Mdogo wa Lushoto umeshatangazwa takribani miaka tisa, lakini mpaka sasa mamlaka ile bado haijaanza kazi, bado inapatikana ndani ya Halmashauri ya Lushoto. Sasa je, ni lini sasa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Lushoto itaanza kufanya kazi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, asante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shangazi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli nilifanya ziara katika Wilaya ya Lushoto, Mkoa wa Tanga na nikakuta kuna matumizi mabaya ya fedha shilingi zaidi ya milioni 300. Nikatoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya, namshukuru uchunguzi umeshafanyika, tumeshapokea taarifa ile watu wote waliohusika namhakikishia Mheshimiwa Mbunge watashughulikiwa kwa mujibu wa tararibu za kisheria, tunalifanyia kazi jambo hilo, naomba tupeane muda, tuvute subira kidogo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anaulizia habari ya Mji Mdogo ambao ulitangazwa na haujawa mamlaka kamili. Nimejibu maswali haya mara kadhaa, nirudie tu kusema kwamba kama jambo hili haliongezi gharama za kuendesha Serikali, tumeelekeza na ni msimamo wa Serikali kwamba kwa sasa tujielekeze kuboresha maeneo na kukamilisha maeneo ambayo yalishaanzishwa kabla ya kuanzisha maeneo mengine ya mji.

Mheshimiwa Spika, sasa kama hili linaongeza gharama, kuongeza watumishi, majengo ya Serikali na bajeti kuongezeka, kwa kweli Serikali haitakuwa tayari kufanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hayo ndiyo majibu ya Serikali na Mheshimiwa Mbunge aendelee kutoa ushirikiano. Kadri tutakavyopata fedha ya kutosha, yale maeneo ambayo yameshaanzishwa yakaimarishwa vizuri kwa kupeleka huduma muhimu, vifaa, watendaji wa kutosha, basi maeneo mengine mapya yataanzishwa ili kupeleka huduma karibu na wananchi wetu. Ahsante.
MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru sana kwa majibu ya Serikali, hata hivyo nina maswali mawili madogo ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, Ofisi ya Rais, TAMISEMI haiwezi ikatoa waraka kwa halmashauri zetu zote nchini ikiainisha kodi zote za kero ambazo zilifutwa na Bunge hili? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa vitambulisho vya wajasiriamali pamoja na nia njema iliyo nyuma yake, utekelezaji wake bado ni kero kubwa nchini. Je, Serikali pia haiwezi ikatoa maelekezo ya jinsi ya kutekeleza zoezi hilo ili tuwe na usare nchi nzima kuliko hali ilivyo sasa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, anauliza kama Serikali inaweza ikatoa waraka ambao unaainisha kodi za kero ambazo zilifutwa na Bunge hili Tukufu.

Naomba tupokee ushauri huo na naomba niahidi kwamba waraka huu utatengenezwa na utasambazwa nchi nzima na Waheshimiwa Wabunge watapata nakala wa kuonesha kodi ambazo ni kero zilizofutwa na Bunge hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ameuliza habari ya vitambulisho vya wajasiliamali. Ni kweli kama ambavyo wewe mwenyewe umeongezea, nilitoa tamko la Serikali katika Bunge hili Tukufu ulinipa fursa hiyo, lakini vilevile pamoja na waraka wetu ambao umetolewa nchi nzima na maelezo uliyotoa mara kadhaa katika Bunge hili, bado inaonesha kuna changamoto katika utekelezaji wa jambo hili.

Mheshimiwa Spika, tulisema tunapoanza 1st July, mwaka wa fedha mpya wa 2019/2020, tutatoa waraka mahsusi na Waheshimiwa Wabunge watapata nakala ukianisha nani anapaswa kutozwa kodi ya wajasiriamali na nani anapaswa kupewa kitambulisho. Kwa kweli baada ya kutoa waraka huo, wale wote ambao watakiuka wakaienda kinyume na maelekezo haya ambayo kimsingi siyo matamanio ya Serikali na siyo matakwa ya Mheshimiwa Rais. Mheshimiwa Rais alimaanisha kuwasaidia wajasiriamali wadogowadogo wasipate usumbufu mtaani kwao wanapofanya biashara ndogondogo ya kujikimu kutozwa kodi kubwa na watu wa TRA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania waendelee kuvuta subira, jambo hili tunalifanyia kazi na kwa kweli baada ya hapo itakuwa ni utekelezaji, hakutakuwa na msalia Mtume. Watu wote wafanye shughuli zao bila kuvunja sheria lakini wasipate bughudha ambazo kwa kweli ni kero. Ahsante. (Makofi)
MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali moja la nyongeza. Ninavyofahamu mimi, service levy haichajiwi kwa mfanyabiashara mmoja ambaye amefungua duka lake na amelipa leseni na kodi ya mapato, lakini wafanyabiashara wadogowadogo kwenye baadhi ya Halmashauri wanachajiwa service levy, nini kauli ya Serikali juu ya hili?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Pauline Gekul, Mbunge wa Babati Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli, ulipaji wa kodi ni kwa mujibu wa sheria na taratibu na sheria zipo na wasimamizi wanatakiwa kufuata taratibu hizo. Sasa Mheshimiwa Mbunge kama kuna maeneo ambayo watu wanachanganya analipa service levy ambayo imeelekezwa na bado anatozwa kodi nyingine, nafikiri tupate maelekezo yake na taarifa muhimu tuweze kulifanyia kazi.

Hata hivyo, kodi italipwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na sheria ipo, tunaomba hao wote wanaosimamia jambo hili watende haki na wasikilize watu na kutoa elimu ya umma. Ahsante.
MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kuipongeza Serikali yetu kwanza katika suala la afya ambapo tayari ilitupatia milioni 500 kwa upanuzi wa Kituo chetu cha Afya Mkoani na imetekelezwa, lakini vilevile bilioni moja na laki tano kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya mradi ambao unaendelea, sambamba na hilo nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, ikama ya Watumishi wa Afya ni 360 na tulio nao ni 255 tunao upungufu wa Watumishi 105 katika Idara yetu ya Afya jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi wanapokwenda kupata huduma na tukizingatia kwamba sasa Hospitali ya Wilaya inakwenda kukamilika mapema; je, ni lini sasa Serikali itakamilisha ajira kwa upungufu huu ili kusudio la kutoa huduma hii liweze kukamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa vilevile ikama ya Watendaji wa Mitaa ni 73 na tunao 50 na tuna upungufu wa Watendaji 23 na tunapata malalamiko sana hasa tunapofanya ziara katika mitaa yetu kwa wananchi wetu na ikizingatia kwamba tunakwenda sasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa; je, ni lini sasa Serikali itajazia upungufu wa watumishi hawa ili huduma hii iweze kuwafikia wananchi na tusiwe na malalamiko?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Silvestry Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tunamshukuru sana kwa pongezi zake kwa kazi nzuri ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi Awamu ya Tano. Swali lake la kwanza ametaka kujua ni lini tutapata Watumishi kwenye Sekta ya Afya.

Tulizungumza mara kadhaa, turudie tu kwamba tumeshaangalia changamoto hii katika maeneo mbalimbali pamoja na Kibaha, lakini tumeshaomba Kibali Utumishi kupata Watumishi wa Sekta ya Afya 12,000. Kwa wakati huo tukipata kibali hiki na kuajiri tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba watumishi hawa watapelekwa katika eneo hilo wakatoe huduma kwa watu wetu ili waendelee kufurahia maisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili anasema kuna upungufu katika Watendaji wa Mitaa na Vijiji na kwa sababu kuna Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ni kweli kwamba kuna baadhi ya maeneo katika mitaa yetu na vijiji hatuna watendaji, lakini jambo hili la uchaguzi naomba Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi na Watanzania wengine wote, hao hao wanaosimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni Watumishi wa Umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunahitaji kupata Watendaji wa kila siku kutoa huduma kwa watu wetu, lakini wakati wa uchaguzi kama itatokea kuna kijiji au mtaa ambao hauna Mtendaji wa Kijiji, basi wale Watumishi wa Umma waliopo pale watafanya kazi hiyo kwa niaba ya Serikali na tunahakikisha kwamba jambo hilo litaenda vizuri bila tatizo. Ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, pamoja na miundombinu mizuri iliyopo katika Kituo cha Bwisya, kuna upungufu mkubwa wa watumishi pale kituoni na kuathiri utoaji wa huduma.

Mosi, je, ni lini Serikali itapeleka madaktari na wahudumu wengine wa afya Bwisya?

Pili, Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe (Nansio), Vituo vya Afya na Zahanati Jimboni Ukerewe vina upungufu mkubwa wa watumishi (chini ya 50%): Ni lini Serikali itapeleka watumishi wa kutosha na hasa ikizingatiwa ugumu wa jiografia ya visiwa vya Ukerewe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, imepata kibali cha kuajiri madaktari 610 na kuwapanga kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kutoa kipaumbele kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa. Hivyo baadhi ya Madaktari hao watapangwa kwenye Vituo vya kutolea huduma za Afya Wilaya ya Ukerewe.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuajiri wataalam wa huduma za Afya kwa awamu kwa kadri ya upatikanaji wa fedha.
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Ahsante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kama tunavyofahamu kwamba mifuko hii ya Adaptation Fund pamoja ile ya LDCF yaani Least Developed Country Fund hutengewa fedha maalum na Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi kupitia hii mifuko na fedha hizi hutakiwa zitumike katika muda maalum na ni fungu maalum, na kutokana na utaratibu ambao unaendelea katika Serikali au katika Wizara zetu imekuwa ikichukua muda mrefu sana kutayarisha maandiko na kuweza kuyawasilisha na mpaka kupata hizi fedha.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba, fedha hizi ambazo zinakuwa zinatengwa kwa ajili ya Tanzania zinaombwa kwa haraka na kuweza kupatikana katika muda muafaka ili kupunguza hatari ya kuweza kuja kuzikosa hizi fedha au kuzipoteza?

Mheshimiwa Spika, swali namba mbili, je, kuna utaratibu gani wa uwiano wa fedha hizi kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS,
MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Soud, Mbunge wa Donge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, kumekuwa na, kwa namna moja au nyingine ucheleweshaji wa fedha hizi, lakini tunaendelea kuimarisha utaratibu wa mawasiliano. Fedha hizi kwanza lazima mradi uandikwe, lakini vilevile tunashiriki na wenzetu wa Wizara ya Fedha ambao wana taratibu zao, tunahitaji tax exemption katika jambo hili. Kwa hiyo, lazima wataalam wetu wapitie kwanza halafu kisha wamshauri Mheshimiwa Waziri wa Fedha namna bora ya kuweza kuruhusu mradi uweze kuendelea. Wakati mwingine unalazimika kwenda site, hiyo ndio inasababisha muda unakuwa mrefu kidogo, lakini tunaahidi mbele ya Bunge lako tukufu kwamba tutachukua hatua za haraka na miradi hii itakuwa haichukui muda mwingi sana kutekelezwa, ili tuweze kupata fedha hizo ambazo ni manufaa makubwa kwa nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili ambacho Mheshimiwa Mbunge anataka kujua ni kwamba kuna uwiano. Hii miradi kama nilivyotaja katika miradi mitano mradi ukiibuliwa kule upande wa Zanzibar kiasi hicho cha fedha mradi utatekelezwa fedha zinapelekwa bila kuwa na mgawo, kwa hiyo, hapa kazi kubwa ni kujiimarisha, kuandaa watu wetu, wataalam wetu, waandae maandiko ya kutosha fedha zinapatikana. Sisi kama Ofisi ya Makamu wa Rais ni ku- facilitate na kuratibu mambo haya yaweze kufanyika kwa haraka zaidi. Ahsante sana.
MHE. KAVEJURU A. FELIX: Mheshimiwa Spika, nina swali moja la nyongeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, reli ya kutoka Tabora kwenda Kigoma na ujenzi mzima wa SGR kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma ni wa muhimu kweli, kwa kuzingatia kwamba nchi ya Congo DRC inaitegemea reli hiyo kwa ajili ya kusafirisha mizigo yake, ambacho ni chanzo kikubwa sana cha uchumi wa nchi yetu. Naomba kujua ni upi mkakati wa Serikali wa kuharakisha ujenzi wa reli hiyo baada ya upembuzi huu ambao unakamilika mwezi huu wa Septemba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kavejuru Aliadory Felix, Mbunge wa Buhigwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kwamba kazi ya upembuzi yakinifu inafanyika na inakamilika mwaka huu, Septemba, 2021. Pia nimesema kwenye majibu ya swali la msingi kwamba tunatafuta mkopo wa gharama nafuu usio na masharti magumu ili ujenzi uweze kuanza.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge naomba atupe nafasi tulifanyie kazi jambo hili. Limepewa uzito mkubwa na Mheshimiwa Rais ameshaelekeza kwamba miradi yote ya kimkakati ikiwepo hii SGR, kama nilivyotaja kwenye majibu yangu ya msingi, ni lazima ijengwe kwa wakati.

Mheshimiwa Mbunge naomba awe na amani, eneo hili reli itajengwa na watu wa eneo hili watapata huduma ya usafiri. Ahsante sana.
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Spika, kwanza, nashukuru sana kwa majibu yaliyotolewa na Serikali na katika majibu hayo inaonekana kwamba imekadiriwa tani 500,000 ndiyo zitakazokuwa zinapita kwenye bandari hiyo kavu lakini mpaka sasa ni tani 200,000 tu, kwa hiyo, wanasema bandari haijazidiwa.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo la msingi ambalo nilitaka Serikali ilifahamu ni kwamba kutokuongezeka kwa mizigo kumetokana na kukosekana kwa mabehewa ya mizigo na ubovu wa reli vitu ambavyo vinakwenda kutengenezwa katika bajeti ya mwaka huu. Je, Serikali haioni kama ni busara kwenda sambamba na kukamilisha bandari hiyo badala ya kusubiri bandari izidiwe wakati ile bandari kavu ya kuhifadhi makasha itakuwa haijakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA W. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kilumbe Shabani Ng’enda, Mbunge wa Kigoma Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba shehena ilikuwa imepungua na mwaka huu wa fedha tunaongeza mabehewa na katika jibu la msingi utaona tayari fidia ya eneo hilo lote hekta 69 imeshafidiwa na mwaka wa fedha ujao tunaanza ujenzi. Kwa hiyo, kwa kadri tutakuwa tunapata fedha tutakuwa tunajenga kwa kadri ya mahitaji yanavyokua. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba bandari hii haitazidiwa na itajengwa kadri tutakapokuwa tunapata fedha. Kwa hiyo, asiwe na wasiwasi wowote ule, tunalifanyia kazi, ahsante.
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Naishukuru sana Serikali ya Chama Cha Mapinduzi kwa kuunganisha wilaya na wilaya, mikoa na mikoa. Hata hivyo, ipo barabara inayoanzia Njuki – Ilongero – Kidarafa hadi Hydom. Barabara hii nimekuwa nikiiulizia mara kwa mara ambayo inaunganisha Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Singida. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha barabara hii kwa kiwango cha lami ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi kwa Mikoa ya Manyara na Singida? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Aysha Mattembe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa sasa tupo kwenye Mpango wa Bajeti ya Mwaka mpya wa Fedha. Naomba nimwahidi Mheshimiwa Mbunge baada ya Bunge hili Tukufu kipindi cha maswali tukae pamoja tuone utaratibu uliotumika. Kwa sababu, barabara zinaibuliwa kutoka ngazi ya Mkoa kuja ngazi ya Wizara, basi kama barabara hizo ambazo zina mahitaji muhimu sana katika maeneo uliyoyasema hazikuingizwa kwenye Mpango wa Bajeti mwaka huu tujipange kwa Mwaka wa Fedha ujao. Wananchi wa pale wavute subira, tupo tayari kufanya kazi ya kuhakikisha kwamba maisha yao na bidhaa zao zinapata nafasi na gharama nafuu kusafirisha ili kuweza kubadilisha maisha yao.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kuulizwa maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa barabara hiyo sasa inaitwa kwa jina la dhihaka kwamba ni barabara ya kuombea kura na kwamba katika jibu la msingi Mheshimiwa Naibu Waziri amesema jumla ya Shilingi Bilioni 10 zimetengwa kwa bajeti ya mwaka 2020/2021 na sasa imebaki miezi miwili, naomba kuuliza swali, ni lini hasa ujenzi huo unaanza na kukamilika kwa kuwa hata Mkandarasi na ukusanyaji wa vifaa haujaanza? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kutokana na ubovu wa barabara hiyo vyombo vya usafiri vimekuwa vikitoza nauli kubwa. Umbali wa kutoza Sh.750 unatozwa Sh.3,000 na kuendelea. Je, Serikali inawaambia nini wananchi wa Mtwara namna inavyoweza kukomesha ama kuwasaidia kumudu gharama za usafiri ili waweze kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawahitaji kusafiri? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA
M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Agnes Hokororo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nimpongeze Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwasemea wananchi wake katika jambo muhimu sana la mawasiliano ya barabara. Kwenye swali lake la kwanza amesema ni kweli kwamba zimetengwa Shilingi Bilioni 10 na muda wa bajeti ya mwaka huu imeyoyoma sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa tu baada ya maswali na majibu tutakaa naye kwa sababu hapa kuna mchakato fedha zipo zimetengwa kama kuna changamoto kama nilivyosema hakuna taarifa kule eneo la Mtwara hasa TANROADS tuwasiliane, tumpe majibu sahihi ili aweze kueleza wananchi wake ni lini barabara hii inaanza kutengenezwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali lake la pili anasema nauli imepanda kwa sababu ya ubovu wa barabara kutoka 750 hadi 3,000 na nini kauli ya Serikali. Kauli ya Serikali ni kwamba, Serikali itajenga barabara hii kwa kiwango cha lami kama ambavyo ilivyoahidi kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Naomba niwaambie wananchi wa Mtwara na maeneo ya jirani kwamba sasa barabara hii haitakuwa barabara ya kura itakuwa jambo halisi na litatekelezwa. Ahsante sana.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa barabara hii ya Mtwara inafanana kabisa na ahadi ya Serikali kupitia Ilani ya Uchaguzi katika barabara ya kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Babati kupitia Sukuru – Olkasmenti - Simanjiro – Kibaya, Wilaya ya Kiteto. Je, Serikali ni lini itaanza ujenzi wa barabara hii ili kurahisisha huduma kwa wananchi wa Manyara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA
M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, Mbunge wa Vijana, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niseme tu kwamba kazi inaendelea ilikwishaanza baadhi ya barabara tathmini imekamilika na ujenzi unaendelea. Zile barabara ambazo hazikufanyika mwaka wa fedha 2020/2021, zimewekewa mpango mkakati wa bajeti ijayo 2021/2022. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge wa Vijana, Mkoa wa Manyara, watu wa Manyara wasiwe na wasiwasi mpaka Simanjiro, tutatekeleza Ilani ya Uchaguzi kama ilivyoelekezwa na kama ambavyo ndio maagizo ya Viongozi wetu Wakuu hasa Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Naibu Spika, ninadhani kwamba majibu haya kidogo sijaridhika sana, lakini niseme ni mwanzo.

Mheshimiwa Naibu Spika, faru weusi pamoja na wanyama wengine wanapatikana katika Hifadhi za Taifa tatu tu katika nchi hii zikiwemo Serengeti, Ngorongoro pamoja na Hifadhi ya Mkomazi. Upande wa Kenya wana kiwanja cha ndege pale Tsavo, upande wa Kenya Hifadhi ya Tsavo ndiyo inayopakana na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi, na hivyo wanapata watalii wengi kwa sababu wao wana kiwanja cha ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile umbali wa kutoka Arusha na KIA ni mkubwa sana ukizingatia na uhitaji wa watalii kuja kuona faru weusi walioko kwenye sanctuary pale Mkomazi National Park. (Makofi)

Ninaomba Serikali iangalie uwezekano wa kukarabati Uwanja wa Ndege wa Same ili watalii hao waweze kufika kwa urahisi na kuongeza Pato la Taifa kama Mheshimiwa Rais alivyosema jana.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la pili, ninaomba inapowezekana Mheshimiwa Waziri aje pale Same ili aweze kuona mazingira hayo ninayozungumzia, kwamba uwanja upo unahitaji marekebisho ili tuweze kukuza uchumi kupitia utalii. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kuleta wazo zuri sana ambalo kimsingi siyo la Same Magharibi peke yake, hili ni jambo la Kitaifa.

Ninaomba nitumie nafasi hii kumuelekeza Katibu Mkuu Ujenzi na Uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi, awatume wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege waende Same Magharibi wafanye tathmini, tuangalie cost implication ili kiwanja hiki kikarabatiwe mapema iwezekanavyo, fedha itakapopatikana kupitia watalii katika eneo hili itasaidia kuboresha hotuba nzuri ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya jana ya kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili; naomba nimuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba niko tayari kabla Bunge hili halijaisha naomba kibali cha Mheshimiwa Spika na Mheshimiwa Waziri Mkuu, twende Sa me kwa sababu kuona ni kuamini, tushuhudie hali halisi na tuongeze maelekezo ya ziada. Ahsante. (Makofi)
MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia fursa ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, unakuwa umekamilisha kumlipa mtu fidia unapoweka pesa kwenye akaunti yake. Kwa nini sasa Serikali isiwalipe wananchi wa Kyamkwikwi kwa kuhakikisha pesa zinaingia kwenye akaunti zao kabla ya mwisho wa mwezi huu ili jibu la Mheshimiwa Waziri liweze kuwa sahihi? Hawa watu hawajalipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; tunapozungumza Bandari ya Kyamkwikwi tunamaanisha huduma kwa Visiwa vya Bumbile, Makibwa, Nyaburo, Kerebe na Gooziba. Sasa kwa nini Serikali isichukue maoni ya wananchi waliyoyatoa kwa Kepteni Mwita wa MV Clarias juu ya chombo muafaka cha kuweza kwenda katika hivyo visiwa nilivyovirejea? Kwa sababu unapozungumzia MV Chato, MV Chato haiwezi kupita kwenye mkondo wa Makibwa kuelekea Kerebe.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI(MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Charles Mwijage, Mbunge wa Muleba Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimuelekeze Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi atumie wataalam wake atueleze status ya fidia ya wananchi hawa, itakapofika Bunge la jioni Mheshimiwa Mbunge atapewa majibu sahihi ni lini wananchi wake watalipwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili Mheshimiwa Mbunge anasema ni kwa nini tusichukue maoni ya wananchi waliyotoa kwa Kepteni Mwita kama alivyotaja, ili yaweze kufanyiwa kazi kwa lengo kubwa la kuboresha huduma ya usafiri katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuyapokee maoni haya tuyafanyie kazi, yapitiwe na wataalam wetu tupate ushauri sanifu ili tuweze kutekeleza kama ambavyo tunapaswa kukidhi mahitaji ya wananchi. Kwa sababu lengo la Serikali hii ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhudumia wananchi, tena wananchi wale ambao wana uhitaji mkubwa hasa wa pale Muleba Kusini na Kaskazini.
MHE. SIYLVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu haya ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, toka barabara ile ya njia nane kutoka Kimara hadi Kibaha kukaribia kukamilika kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magari katika Mji wa Kibaha kiasi kwamba kutoka Kibaha Mjini mpaka pale Mlandizi kiasi cha kilometa 15 unaweza ukatumia hata masaa mawili na nusu wakati kuna barabara ya zamani kutoka pale Picha ya Ndege kupita Kongowe hadi Visiga ambayo ingelirekebishwa tu ingeweza kuondoa huu msongamano wakati mpango wa ujenzi unaendelea. (Makofi)

Swali la kwanza, je, ni lini sasa Serikali inakamilisha ujenzi/inajenga barabara ya njia nane kutoka Kibaha Mjini mpaka Mlandizi angalau kuondoa usumbufu huo?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, barabara ya kuanzia pale TAMCO hadi Mapinga na kuanzia kwa Mathias hadi Msangani zinazojengwa kawa kiwango cha lami zinasuasua sana ujenzi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kutoa fedha na kukamilisha ujenzi huo ili matunda mazuri ya kazi ya Serikali yaweze kupatikana kwa wananchi wa Kibaha Mjini?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Koka Mbunge wa Kibaha Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba nielekeze Meneja na TANROADS Mkoa wa Pwani ahakikishe kwamba anaondoa changamoto zote ambazo amepelekea barabara hii ujenzi wake unasuasua na kama kuna changamoto ambazo ameshindwa kuchukua hatua basi Wizara ipo tayari kutoa ushirikiano ili jambo hili na barabara ijengwe kwa wakati na kiwango kinachotarajiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake la pili naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba changamoto ambazo ametoa hapa na msongamano wa magari tutauchukulia hatua, Serikali inafanya kazi hii na Mkandarasi yupo site Sasa kwa sababu tunaenda kwenye weekend hii naomba nimuhakikishe kwamba kabla ya Jumatatu atakuwa amepata majibu sahihi nini kinafanya barabara isuwesuwe iweze kurekebishwa mapema sana na hata jana nilipigiwa simu na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi ambao leo tuna kazi maalum wakikwama barabarani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimwelekeze Katibu Mkuu tunapojiandaa sasa muda mfupi ujao Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwenda kupiga kura za ndio za Mama Samia kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, changamoto hizo kwa wajumbe wanaporudi kwenda makwao hasa Dar es salaam hasa na maeneo jirani ziwe zimekomesha mara moja ahsante sana. (Makofi)
MHE. REGINA N. QWARAY: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi uliyonipa ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, Mkoa wetu wa Manyara ni miongoni mwa mikoa yenye vivutio vingi kama vile Hifadhi ya Wanyama Tarangile, tuna Mlima Hanang, tuna Ziwa Babati. Kutokana na ukosefu wa Kiwanja cha Ndege katika mkoa wetu watalii wengi wanapokuja katika mkoa wetu hutumia Uwanja wa Ndege uliopo Manyara kule Mto wa Mbu umbali wa kilometa 160, hutumia Uwanja wa Ndege uliopo KIA kilometa takribani 200, hutumia Uwanja wa Ndege wa Arusha kilometa zaidi 164. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, je, Serikali haiwezi sasa kuweka msukumo wa pekee kusogeza huduma ya Uwanja wa Ndege katika Mkoa huu wa Manyara ili kuchochea shughuli za maendeleo katika mkoa wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa tayari eneo hili limekwishatengwa kule Mwada, ni lini sasa Serikali itaona kuboresha ili kuweka airstrip katika eneo hilo litumike wakati tunaendelea kusubiri ujenzi wa Uwanja wa Ndege katika mkoa wetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Regina Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Manyara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kufanya kazi za kibunge wa Mkoa, kwa sababu nina uhakika uwanja huo ukijengwa na kukamilika huduma itakuwa ya mkoa na mikoa ya jirani. La pili naomba nimuhakikishie kwamba jambo hili Mheshimiwa Pauline Gekul Mbunge wa Babati Mjini na wengine wenye majimbo wamekuwa wakifuatilia kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, majibu ya Serikali ni kwamba tuna- engage Mkandarasi Mshauri tuelekeze fedha katika eneo hili, tunajua umuhimu wake na vitu vyote katika Mkoa wa Manyara ukamilike.

Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali lake la pili linalohusu wazo lake la kutengeneza airstrip katika eneo hili, tunalipokea na tutalifanyia kazi ili huduma iweze kupatikana katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Takwimu mbalimbali za wataalam zimeonesha kama Uwanja wa Ndege wa Serengeti ukiboreshwa utakuwa uwanja pekee katika Kanda ya Ziwa utakaoleta tija kubwa kiuchumi, kiuhifadhi na kijamii kwa wananchi wa Serengeti na Tanzania kwa ujumla. Kwa kuwa mpaka sasa tayari wadau mbalimbali na wananchi wamekwishachangia ujenzi wa uwanja huu. Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa uwanja huu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Serengeti, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza ni kweli Uwanja wa Serengeti ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi lakini pia katika eneo la Serengeti na Mkoa wa Mara kwa ujumla. Pia naomba nitambue kwamba ni kweli wananchi na Mheshimiwa Mbunge amejiunga, wametengeneza group la WhatsApp, wanachangisha fedha na Mheshimiwa Mbunge leo ameomba appointment watu wakija awapokee tuzungumze.

Mheshimiwa Spika, naomba nimwelekeze Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege atume watalaam wetu katika eneo hili ili juhudi nzuri za wananchi zisipotee, atuongezee utalaam wa Wizara yetu kazi hii ifanyike na uwanja ujengwe ili watalii wasizunguke Zaidi, washuke pale karibu na tutape huduma na fedha iongezeke.
MHE. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa muda wa kuuliza swali la nyongeza, nina swali moja tu. Sasa kwa sababu zoezi la ukamilishaji wa ujenzi litachukua muda mrefu kwa kuzingatia majibu ya Mheshimiwa Waziri. Sasa je, Serikali haioni haja sasa ya kujenga japo daraja la dharura kwa kupitia vyombo vyetu vya jeshi ili kunusuru kesi za vifo pamoja na upotevu wa mali za wananchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia changamoto za wananchi wake wa Jimbo lake waliompigia kura kumleta hapa Bungeni. La pili, naomba nimwambie kwamba jambo hili tumelipokea, kabla ya kwenda kuomba vyombo vyetu vya Jeshi kuna taratibu zake, naomba nimwelekeze Katibu Mkuu Ujenzi atume mtaalam wetu katika eneo hili ili tuone kama kuna haja ya kujenga daraja la dharura kwa wakati huu na tuweze kulifanyia kazi wananchi wetu waendelee kupata huduma kama ilivyo matarajio ya Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan. Ahsante.
MHE. JERRY W. SILAA: Mheshimiwa Spika, pamoja na salamu za shukrani na pongezi kwa Mheshimiwa Waitara kwa kuchaguliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na shukurani zetu kwa Mheshimiwa Rais kwa kumpa nafasi hii, tunaamini swali hili angeweza kulijibu bila hata kusoma, kwa nasaba yake na Jimbo la Ukonga. Naomba kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Jimbo la Ukonga na Jimbo la Mbagala ndiyo majimbo pekee kwenye Mkoa wa Dar es Salaam ambayo hayaunganishwi na barabara ya lami; na barabara hii ni barabara muhimu sana kwa wananchi wa Kata ya Chanika, Msongola kujiunga na Jimbo la Mbagala.

Naomba commitment ya Serikali kipande hiki kidogo kilichobaki cha kilometa 4.95 ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa mazingira ya Jimbo la Ukonga yanafafana na Jimbo la Mbeya Mjini, ni lini Serikali itapanua barabara ya TANZAM inayotoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma, kipande cha Uyole – Tunduma kilometa 104, na kipande cha Uyole – Igawa kilometa 116. Barabara hii inasomeka ukurasa wa 66 wa Ilani yetu ya Uchaguzi yenye kurasa 303. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jerry William Silaa, Mbunge wa Ukonga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ili ni swali la kihistoria, Waswahili wanasema mtoto mpe mchawi akulelee. Ni kweli kwamba barabara ya Mbagala – Mbande naifahamu na Mheshimiwa Jerry pamoja na Mheshimiwa Chaurembo Mbunge wa Mbagala, nilipoteuliwa kuwa Naibu Waziri katika eneo hili suala la kwanza, hata hawakunisalimia, walitaja barabara hii na kwa sababu ya umuhimu wake. Barabara hii ikijengwa vizuri kiwango cha lami wananchi wanaweza wakatoka Ukonga wakaenda Mbagala wakaenda Kusini au Kusini anakuja Dodoma haina sababu ya kupitia mjini kuepuka foleni anaweza akapita eneo hili.

Mheshimiwa Spika, nimekwishaongea na Chief wa TANROAD Engineer Mfugale, kwamba walikuwa wametenga fedha vipande vipande vya matengenezo mbalimbali katika eneo hili. Kuanzia mwezi Julai mwaka mpya wa fedha 2021/2022 Mheshimiwa Jerry na Mheshimiwa Chaurembo barabara hii kilometa 4.9 zitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ili watu waweze kupata huduma katika eneo hili.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, wiki iliyopita Mheshimiwa Naibu Spika alikalia kiti hapo ulipokaa, akatoa malalamiko kwamba eneo lake daraja lilivunjika tangu 2019 na mpaka leo anapozungumza na asubuhi amenikumbusha mkandarasi hayupo site na nilitoa maelekezo hapa kwamba mkandarasi aende site wafanye kazi ya dharura ili kuwa na uunganisho katika eneo hilo ili watu wapite.

Mheshimiwa Spika, leo nazungumza habari ya barabara. La kwanza, kabla leo jua halijazama nipate maelezo kwa nini mkandarasi hajawa site katika eneo lile, daraja lile halijatengenezwa tangu 2019 mpaka leo. La pili, kwa kibali chako na kibali cha Mheshimiwa Waziri Mkuu weekend ijayo nitaenda Mbeya kutembelea barabara hii pamoja na daraja nione kama kweli mkandarasi hayupo site, baada ya hapo tutaongea vizuri. Ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza. Barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa wananchi wa Ukerewe, inasaidia wananchi wanaoenda Kivuko cha Bugorora kwenda Ukara ambako kuna hospitali mpya sasa ya Wilaya ya Bwisya; barabara hii inasaidia wananchi wanaoenda Kakukuru ambapo ndiyo msingi wa uchumi wa Ukerewe, pia inasaidia wananchi wanaoenda Mliti mpaka Lubya kwenye msitu wa Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pesa hizi za matengenezo ya kawaida zinazotengwa zimekuwa hazisaidii sana kwa sababu inakuwa nzuri kwa muda mfupi, lakini inakuwa haipitiki kwa muda mrefu. Ni kwa nini sasa Serikali isianze kuifanyia Barabara hii upembuzi na hatimaye upembuzi yakinifu ili hatimaye sasa ianze kujengwa kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ambalo kimsingi siyo swali, ni ushauri; kwenye Kivuko cha Bugolola kwenda Ukara kumekuwa na shida ya kivuko kile na inaweza kusababisha ajali hata gari kutumbukia majini. Kinachohitajika ni kuweka Moorum au trip kadhaa za mawe ili kutengeneza gati lile ili wanananchi waweze kuvuka kwa usalama. Kwa hiyo, nitoe ushauri kwa Wizara, kwa haraka na kwa dharura, ifanyie kazi jambo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Swali lake la kwanza Mheshimiwa Mkundi ameomba barabara yake hii ifanyiwe upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge wa Ukerewe Mkundi kwamba tumepokea ombi, tutalifanyia kazi ili tufanye tathimini ya kina halafu tuweze kujua gharama ambayo inahitajika kuwekwa kiwango cha lami ili barabara iweze kutengenezwa na kupitika kwa wakati wote.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili tumepokea ushauri ambao naomba nimwelekeze Mkurugenzi wa vivuko Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kwa kuwa amesema kuna hali hatarishi ya maisha katika eneo hili, afanye tathmini, aangalie hali halisi, halafu tuweze kuchukua hatua ya dharura ili kuweza kuokoa maisha ya watu wetu katika eneo hili. Ahsante.
MHE. HAMISI S. TALETALE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya swali dogo la nyongeza. Naomba kuuliza, Serikali iliahidi kutangaza tender ya ujenzi wa barabara ya Bigwa – Kisaki.

Je, ni lini Serikali itatangaza barabara hii?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ni kweli kwamba kwa sasa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ipo kwenye hatua mbalimbali za kutangaza baadhi ya barabara ili ziweze kujengwa kwa hatua mbalimbali, nyingine kwa kiwango cha lami na mengine ni madaraja ya kujengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira na maelezo mengine ya ziada yatatolewa kwenye bajeti yetu ambayo inatarajiwa kusomwa Jumatatu ijayo tarehe 17 na tarehe 18. Ahsante.
MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Barabara ya Stalike – Kibaoni yenye urefu wa kilometa 71 ni ahadi ya Mheshimiwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli na tayari barabara hiyo imeshafanyiwa upembuzi yakinifu.

Swali langu kwa Serikali: Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami katika barabara hii, ukizingatia Mkoa wa Katavi ni moja kati ya mikoa michache sana ambayo bado haijafanikiwa kuunganishwa Mkoa na Mkoa kwa kiwango cha lami? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba barabara hii ni muhimu na Mkoa wa Katavi upo kwenye mchakato wa kupata barabara za lami. Kama nilivyosema, naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira, bajeti yetu inaanza kujadiliwa tarehe 17 na tarehe 18 hapa Bungeni. Nitapata fursa ya kuwatajia barabara ambazo tumetangaza kwa mwaka huu na mwaka wa fedha ujao.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie katika barabara muhimu ambazo zinajengwa kwa kiwango cha lami ni pamoja na kuunganisha Mkoa wa Katavi na maeneo mengine. Ahsante sana.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Marais wetu waliopita akiwemo Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli waliahidi ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mbalizi – Shigamba:-

Je, ni lini sasa hiyo barabara itajengwa kwa kiwango cha lami? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Njeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, ahadi zote za Viongozi Wakuu wa Nchi akiwemo Dkt. Hayati Magufuli, Mama Samia, Mheshimiwa Waziri Mkuu na viongozi wengine, ahadi hizi lazima zitekelezwe kwa sababu ni ahadi ya Serikali na Serikali ipo kazini inafanya kazi na kazi inaendelea.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwaa Mbunge kwamba, barabara yake hii kama ilivyoahidiwa itafanyiwa kazi, itajengwa kwa kiwango cha lami, tupeani ushirikiano na muda si mrefu ahadi hiyo ya viongozi itatimia kabla ya 2025. Ahsante. (Makofi)
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Umuhimu wa barabara ya Mkundi ni sawasawa na barabara ya Mugala kwenda Busambala. Je, ni lini Serikali itafikiria kuijenga barabara hii katika kiwango cha lami? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge wa Mwibara, mdogo wangu Mheshimiwa Kajege, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza eneo hili nalifahamu, mimi natoka katika Mkoa wa Mara na tumeshapata taarifa, Mheshimiwa Mbunge hapa ameulizia ili wananchi wasikie kama analisemea katika Bunge hili Tukufu. Mheshimiwa Mbunge tuliwahi kuzungumza nje ya box, inafanyiwa kazi na asubiri tarehe 17 na 18 atapata majibu sahihi. Kwa hiyo, watu wa Mwibara na Mkoa wa Mara kwa ujumla na mikoa mingine yote tutazifanyia kazi. Ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru pamoja na majibu ya Serikali naomba niulize maswali madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; hii hadithi ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege Sumbawanga ni hadithi ya muda mrefu na wananchi wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu. Sasa naomba kupata majibu ya Serikali ni nini ambacho kinakwamisha upatikanaji wa fedha kwa sababu tumekuwa tukisubiri muda mrefu ili ujenzi huu uanze mara moja? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa sababu ujenzi wa uwanja ulioko Sumbawanga uko katikati ya Mji na kwa kuliona hilo Serikali iliamua kwa makusudi mazima kutenga eneo lingine na si kama airstrip kama ambavyo Naibu Waziri amejibu. Aliyekuwa Makamu wa Rais Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Dkt. Ghalib Bilal alifika eneo la Kalambo na kuweka jiwe la msingi ili eneo lile liendelee kulindwa. Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba eneo lile halivamiwi ili itakapofika wakati wa kujenga uwanja mkubwa kusiwe na haja ya fidia? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Kandege, Mbunge wa Kalambo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyotoa maelezo yangu kwenye jibu la msingi ni kwamba jambo hili linafanyiwa kazi na Mheshimiwa Kandege anafahamu taratibu za Serikali, kama jambo ni makubaliano ya kimkataba lazima yakamilike. Hata hivyo, nipokee hoja yake kama kweli kuna ucheleweshaji tutalifanyia kazi ili uwanja huu ukamilike kama ambavyo tumeahidi kwenye jibu letu hapa kwa niaba ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nipokee ushauri wake wa pili kwamba eneo hili ni kweli kwamba juzi nilikuwa Mtwara, hoja mojawapo iliyopo kule ni kwamba wananchi wamesogea karibu na eneo na wahitaji kulipwa fidia ambayo ni gharama nyingine kubwa tena kwa Serikali. Eneo hili litasimamiwa, lipimwe liwekwe mipaka na vizuizi ili libaki kwa matumizi ambayo limekusudiwa na wananchi wasianze kugombana na Serikali kwa kudai fidia ambayo itaongeza gharama pia katika maeneo hayo. Ahsante.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa wananchi wale wamesubiri kulipwa fidia kwa muda mrefu; na kwa kuwa, hawawezi kuendeleza kufanya shughuli yoyote katika maeneo yaliyozuiliwa, wanapata shida katika nyumba zao, hawawezi kuongeza kitu: Je, sasa Serikali imejipangaje; ni lini itawalipa fedha zilizobakia ili waweze kupisha ujenzi wa mradi huu wa One Stop Centre? (Makofi)

Swali la pili; kwa sababu fedha za kujenga mradi huu zilishatengwa na zipo; nilipofuatilia fedha hizi zipo: sasa ni lini mradi huu ambao una manufaa makubwa kwa wananchi wa Makambako utaanza kujengwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA) Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia fidia kwa wananchi wake wa Jimbo lake la Makambako.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba mradi huu una maslahi makubwa na mapana kwa nchi yetu na kwa uchumi wa nchi yetu hasa kwa wasafirishaji upande wa SADC na East Africa Community, hata hivyo, fedha hizi ni za World Bank. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imelipa uzito, litafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo tulipe fidia kwa wananchi hawa ili wapishe kazi ya ujenzi ifanyike na huduma ya uchukuzi iweze kuboreshwa katika Wizara yetu ya Ujenzi na Uchukuzi. Ahsante.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, Mto Ruvuvu una tabia ya kujaa, hali inayoweza kusababisha kivuko hiki kutofanya kazi, hasa nyakati za masika; na kwa kuwa vivuko hivi vina tabia pia ya kupata hitilafu, hali ambayo inasababisha huduma ya kuvusha wananchi isiwepo. Swali la kwanza; je, Serikali iko tayari kutuletea mtumbwi wa kisasa ili uweze kutoa huduma pindi ambapo kivuko kitakuwa hakiwezi kufanya kazi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuambatana na mimi twende kwenye Jimbo la Ngara akashuhudie changamoto zetu za vivuko pamoja na miundombinu mingine, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninampongeza kwa swali lake zuri kwa sababu anatu-alert kwamba tunapojenga vivuko tuweke pia na mitumbwi kama backup ikitokea tatizo tuweze kupata huduma katika maeneo hayo. Naomba nimuelekeze Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi atume wataalam wetu waende katika eneo hili la Mto Ruvuvu akafanye tathmini tujue aina ya mtumbwi na gharama zake ili tuweze kupeleka huduma hii muhimu katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Ndaisaba kwamba kwakuwa ni mjukuu wangu nitaenda pale Kagera kutembelea Ngara katika eneo hili baada ya Bunge hili kumaliza Bunge la Bajeti, ahsante.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali ya nyongeza. Pia nashukuru sana kwa Mheshimiwa Naibu Waziri na hata pacha wake kwenye Wizara hiyo, wanaifahamu sana jiografia ya Wilaya ya Mbeya na hasa Mbalizi. Swali la kwanza, ahadi nyingi zimetolewa, hata wewe utakumbuka kuwa, eneo la miteremko ya Iwambi – Mbalizi lina ajali nyingi na zinaendelea. Mheshimiwa Rais wa sasa tarehe 15 alipotembelea na kuwapa pole wananchi wa Mbalizi kwa ajali mbaya iliyoua watu zaidi ya 20, aliahidi ujenzi wa Barabara ya By-pass ya Uyole – Songwe na By-pass ya Mbalizi – Iwambi. Sasa ni lini ahadi hiyo itatekelezwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; bandari kwa muda mrefu walitwaa eneo la Inyala kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Kavu, lakini kwa miaka mingi sasa hawajaweza kuwalipa wananchi na wananchi hawafanyi shughuli zozote za uzalishaji. Sasa ni lini Wizara itaipa nafasi na kuiamuru Mamlaka ya Bandari walipe fidia kwa wananchi wa Inyala, Mbeya? Nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza ni kweli kwamba, Mheshimiwa Rais, Mama Samia, alipita katika eneo ambalo ametaja na akatoa maelekezo. Bahati nzuri tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kupitisha bajeti yetu jana na miongoni mwa fedha ambazo zimetengwa ni pamoja na malipo ya Barabara hii ya By-pass pale Uyole – Songwe. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge awe na amani tutakapoanza utekelezaji wa bajeti hii hili eneo tutazingatia maelekezo ya kiongozi mkuu wa nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, anazungumza habari ya fidia ya Bandari Kavu, Inyala. Miongoni mwa maeneo muhimu ambayo tumepanga kujenga Bandari Kavu ni pamoja na Inyala, ambayo itahudumia ukanda wa Nyanda za Juu Kusini. Kwa hiyo, kwa sababu anasema kwamba, kuna shida pia ya mawasiliano naomba nimhakikishie kwamba, shida hiyo itamalizika fidia iweze kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukubaliane baada ya maswali na majibu tuongee na Mheshimiwa Mbunge tupate exactly hasa malalamiko yako wapi, ili utekelezaji wa jambo hili ufanyike, wananchi walipwe fidia zao, wafanye shughuli za maendeleo, lakini pia bandari hii ijengwe na Serikali iweze kumiliki eneo hili ili na kupunguza migogoro kati ya wananchi na Serikali yao pendwa ya Chama Cha Mapinduzi.
MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwenye majibu ya Waziri, Barabara hii ya Karatu – Mbulu – Haidom – Sibiti, lakini kwenye Ilani kuna barabara hii ya Lalago – Mwanhuzi – Kolandoto – Matala – Karatu. Sasa kwenye majibu ya Waziri amesema kilometa 25 kupitia Barabara ya Karatu – Mbulu, sasa ni lini Barabara ya Lalago
– Kolandoto – Mwanhuzi – Matala – Karatu itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba barabara zote mbili ambazo amezitaja ziko kwenye bajeti lakini pia zinajengwa kwa awamu kwa Kulandoto na maeneo mengine ambayo yametajwa tutaenda hatua kwa hatua kadri ambavyo tutapata fedha. Lakini bahati nzuri kwamba ipo kwenye bajeti, pia vipande baadhi vimeanza kujengwa kwa mwaka wa fedha huu ambao unaendelea, ahsante.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali, barabara ya kutoka Makutano, Butiama Nyamswa na Sanzati ni barabara imejengwa kwa muda mrefu sana mkataba wake ulikuwa miaka miwili sasa ni miaka minane toka imeanza kujengwa kama ni bajeti ilikuwa na bajeti ya shilingi bilioni 46 sasa inaenda mpaka Bilioni 50 ni lini sasa hiyo barabara itakamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI – (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba barabara hii imechukua muda mrefu ni miongoni mwa miradi ya barabara ambayo ilikuwa na mkwamo na Mheshimiwa Mbunge anajua kwamba changamoto zimetatuliwa barabara inaendelea kujengwa na kazi itakwisha matarajio mwaka huu kabla haujakwisha hadi mwaka ujao itakuwa imeshakamilika barabara hii, na tumepanga baada ya Bunge kukamilika tutaenda kutembelea barabara ile ili kuona hali halisi katika eneo la ujenzi. Ahsante.
MHE. IRENE A. NDYAMKAMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa meli hii imedumu takribani miaka 100 na ilikuwa mkombozi wa Wana-Ziwa Tanganyika, nikimaanisha Rukwa, Katavi na Kigoma. Je, ni lini sasa Serikali itakarabati meli hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa Ziwa Tanganyika lina uchumi mkubwa na Serikali imetujengea bandari mbili, Bandari ya Kasanga na Bandari ya Kabwe. Ni lini Serikali itatujengea meli mpya Mkoa wa Rukwa kama mikoa mingine ili wananchi wa Mkoa wa Rukwa wafaidike na Serikali yao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, asante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Irene Ndyamkama, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi ni kwamba, tayari Mv. Liemba ipo kwenye hatua nzuri kwa sababu mkandarasi amekwishapatikana na mwezi ujao tuna-sign mkataba ili kazi iendelee. Kwa hiyo, katika hili la Mv. Liemba kama ambavyo Wabunge wengi wa Mkoa wa Katavi na maeneo ya jirani walizungumza wakati wa bajeti, tumezingatia linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali la pili tumepokea hoja yake ya kupata meli ya Mkoa wa Katavi kama mikoa mingine. Tutalifanyia kazi kadiri ambavyo Serikali itapata fedha za kutekeleza hilo, ahsante.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, bandari hiyo sasa imesharasimisha na ninaipongeza sana Serikali: Je, Serikali sasa ina mpango gani wa muda mfupi kuboresha eneo hilo ili liweze kufikika?

Swali la pili; kwa kuwa wanawake wa Kata ya Mbweni ni wadau wakuu katika eneo hilo la bandari: Je, Serikali ina mpango gani ya kuwatengea eneo mahususi kabisa ya kufanya shughuli za ujasiliamali ili nao waweze kufahidika na fursa hiyo ya bandari? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya muda siyo mrefu sana tutatembelea eneo hilo. Anasema kuna shida ya barabara kwamba eneo halifikiki; tutarekebisha miundombinu ili waweze kupata huduma nzuri pale.

Mheshimiwa Spika, swali la pili amewasemea akina mama wa nchi hii na hasa Mkoa wa Dar es Salaam maeneo ya Mbweni; naomba niseme tumepokea wazo hili nzuri na jema, tutalifanyia kazi akina mama wapate sehemu maalum ya kufanya shughuli zao katika Bandari ya Mbweni. Ahsante.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa na mimi nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyojibu kwenye jibu la msingi kwamba barabara hii inaharibika sana kutokana na malori hasa ya Dangote na malori ya gypsum. Lakini usafirishaji kama anavyosema ni kweli Bandari ya Mtwara imeboreshwa kwa kiwango kikubwa, lakini gharama ya usafirishaji wa mzigo kutoka kwenye Bandari ya Mtwara na Bandari ya Dar es Salaam ni sawa sawa na ndiyo maana wafanyabiasha wana option kusafirisha mzigo kwa barabara kuja kusafirisha kwa Bandari ya Mtwara na ndiyo maana hata mafuta watu wa mafuta wameambiwa wachukulie Mtwara, lakini bado malori ya mafuta yanatoka Tunduru, yanatoka Liwale, yanatoka Nachingwea yana option kuja Dar es Salaam badala ya kuchukulia Mtwara.

Kwa hiyo, mimi naiomba Serikali sasa Serikali wataangalia namna yaku-adjust hizi bei ili iwe kivutio kwa Bandari ya Mtwara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kuchauka Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo:-

Kwanza majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri mwenzangu ni sahihi lakini niongezee tu kusema kwamba tumeshafanya mazungumzo ni kweli barabara imeharibika kwa sababu ya mzigo mzito wa Dangote lakini pia na tungependa pia hata korosho zisafirishwe kupitia Bandari ya Mtwara. Tumefanya ziara pale, tulikuwa na changamoto ya gharama ambayo Dangote alilalamika tumefanya negotiation tumekubaliana kupunguza gharama hizo.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili wenzetu wa korosho wanasema kwamba kulikuwa hamna makontena tumewapa nafasi katika Bandari ya Mtwara ili waweze kuhifadhi korosho zao na kwa sababu hiyo tunaamini kwamba hata mazungumzo yakikamilika mzigo utapita sehemu kubwa pale. Tumeboresha Bandari ya Mtwara lakini pia na uwanja wa ndege unaboreshwa, kwa kweli barabara ile kwa namna ilivyo ikiendelea kutumika vile ilivyo watu wa Kusini wataendelea kupata gharama kubwa ya mizigo yao.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna shida kwamba hata uiharibifu wa barabara gharama yake ambayo inachangiwa
hatuwezi ku-replace kwa hiyo alternative njia nzuri ni kuhakikisha kwamba bandari ile inatumika vizuri na imeshaboreshwa tumetumia gharama kubwa zaidi, hayo mengine mazungumzo ya kiutawala itakamilika ili mizigo iweze kupita kwenye eneo hilo, ahsante.
MHE. MARIAM D. MZUZURI: Mheshimiwa Spika, niseme wazi tu sijaridhika na majibu ya Serikali kwenye swali hili ambalo ni la mkakati na lina umuhimu sana na niseme tu mimi kama Mbunge mwenyeji nimeshafuatwa sana na Naibu Mawaziri huku kuwatafutia nyumba za kuishi na kwa kweli wanatusababishia mtaani watu wengi kukosa.

Mheshimiwa Spika, iliwezekana Dar es Salaam kule Masaki, kule Mikocheni kujengwa nyumba kwa ajili ya viongozi. Kwa nini ishindikane mbona mji wa Serikali tumeujenga? Kwa hiyo naomba kwa kweli nitakuja kulirudia hili swali na lije na majibu yanayoeleweka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini tumeona jitihada za Serikali katika ujenzi wa makao makuu katika kuendeleza miundombinu yetu.

Maswali mawili ya nyongeza; la kwanza naomba kuuliza je wamefikia hatua gani katika ujenzi wa airport ya kule Msalato? Lakini la pili katika ujenzi wa barabara ya mzunguko kwenye Jiji letu la Dodoma? Nnashukuru.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali ya nyongeza mawili ya Mheshimiwa Mariam Ditopile kama ifuatavyo:-

Kwanza ni kweli kwamba Waheshimiwa Wabunge wameleta maombi mbalimbali ya nyumba pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali. Lakini tumeshatoa maagizo kwa Meneja Mtendaji Mkuu wa TBA na kuna viongozi wengine ambao walishastaafu yaani walikuwa Wabunge siyo Wabunge tena hapa Dodoma. Wengine walikuwa ni viongozi wa Serikali siyo viongozi wa Serikali walikuwa wanatumia hizo nyumba mpaka tunavyozungumza hapa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo wameshapewa notice nadhani ndani ya wiki mbili zijazo utapata taarifa halisi na baadhi ya Wabunge watapata nafasi ya nyumba hizi.

Mheshimiwa Spika, lakini maswali yake mawili kama ifuatavyo; la kwanza ni kweli kwamba Kamati ya kwako ya Kudumu ya Miundombinu, mwezi huu unaoishia walitembelea eneo la uwanja wa ndege wa Msalato, lakini pia na barabara za mzunguko hapa Dodoma naomba niseme tu kwamba fedha zipo za kulipa fidia. Pale Msalato kuna baadhi ya wananchi ambao hawakuwepo wakati wa fidia, fedha zipo zoezi linafanyika ndani ya muda mfupi sana zoezi litakamilika.

Mheshimiwa Spika, kujenga uwanja wa ndege wa Msalato pamoja na ring roads ni ahadi ya Serikali na Mheshimiwa Rais Mama Samia ameshatoa maagizo na maelekezo tutasimamia na itatekelezwa, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, lakini tumeona jitihada za Serikali katika ujenzi wa makao makuu katika kuendeleza miundombinu yetu.

Maswali mawili ya nyongeza; la kwanza naomba kuuliza je wamefikia hatua gani katika ujenzi wa airport ya kule Msalato? Lakini la pili katika ujenzi wa barabara ya mzunguko kwenye Jiji letu la Dodoma? Nashukuru.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana; kwa nini Serikali isijenge nyumba ambazo watakuwa wanaweka mkataba kwa Wabunge kila baada ya miaka mitano ambao wanaendelea wataendelea kukaa kwenye nyumba hizo, lakini ambao watakuwa hawaendelei basi nyumba hizo Wabunge wapya wanaokuja wakaweza kukaa. Kwa nini Serikali isiwe na mpango wa kujenga nyumba namna hiyo?(Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vita Kawawa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba kama nilivyosema kwenye maelezo yangu ya awali hizi nyumba zimekuwa na matumizi ambayo ni mabaya na tumekuja kugundua kuna baadhi ya watu wana nyumba zao hapa kwa sababu hizi za Serikali gharama ni chini kidogo wanapangisha za kwao hizi wanakaa nazo.

Mheshimiwa Spika, tumeshatoa maelekezo TBA kwamba wapitie na kimsingi ni nchi nzima ikiwepo ni madeni ambayo ni makubwa yapo watu wanadaiwa hawajalipa fedha ya Serikali na kupelekea wanashindwa hata kukarabati nyumba hizo.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili kwamba kama kuna mtu alikuwa ni Mbunge hapa Dodoma, ameshamaliza kipindi chake ile nyumba inapaswa irejeshwe au alikuwa ni mtumishi wa Serikali hizi nyumba zinapaswa kutumiwa na viongozi waliopo kwa wakati huu katika nafasi zao. Wazo lako ni jema Mheshimiwa Mbunge tulipokee tutalifanyia kazi ahsante sana. (Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa na mimi nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyojibu kwenye jibu la msingi kwamba barabara hii inaharibika sana kutokana na malori hasa ya Dangote na malori ya gypsum. Lakini usafirishaji kama anavyosema ni kweli Bandari ya Mtwara imeboreshwa kwa kiwango kikubwa, lakini gharama ya usafirishaji wa mzigo kutoka kwenye Bandari ya Mtwara na Bandari ya Dar es Salaam ni sawa sawa na ndiyo maana wafanyabiasha wana option kusafirisha mzigo kwa barabara kuja kusafirisha kwa Bandari ya Mtwara na ndiyo maana hata mafuta watu wa mafuta wameambiwa wachukulie Mtwara, lakini bado malori ya mafuta yanatoka Tunduru, yanatoka Liwale, yanatoka Nachingwea yana option kuja Dar es Salaam badala ya kuchukulia Mtwara.

Kwa hiyo, mimi naiomba Serikali sasa Serikali wataangalia namna yaku-adjust hizi bei ili iwe kivutio kwa Bandari ya Mtwara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kuchauka Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo:-

Kwanza majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri mwenzangu ni sahihi lakini niongezee tu kusema kwamba tumeshafanya mazungumzo ni kweli barabara imeharibika kwa sababu ya mzigo mzito wa Dangote lakini pia na tungependa pia hata korosho zisafirishwe kupitia Bandari ya Mtwara. Tumefanya ziara pale, tulikuwa na changamoto ya gharama ambayo Dangote alilalamika tumefanya negotiation tumekubaliana kupunguza gharama hizo.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili wenzetu wa korosho wanasema kwamba kulikuwa hamna makontena tumewapa nafasi katika Bandari ya Mtwara ili waweze kuhifadhi korosho zao na kwa sababu hiyo tunaamini kwamba hata mazungumzo yakikamilika mzigo utapita sehemu kubwa pale. Tumeboresha Bandari ya Mtwara lakini pia na uwanja wa ndege unaboreshwa, kwa kweli barabara ile kwa namna ilivyo ikiendelea kutumika vile ilivyo watu wa Kusini wataendelea kupata gharama kubwa ya mizigo yao.

Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna shida kwamba hata uiharibifu wa barabara gharama yake ambayo inachangiwa hatuwezi ku-replace kwa hiyo alternative njia nzuri ni kuhakikisha kwamba bandari ile inatumika vizuri na imeshaboreshwa tumetumia gharama kubwa zaidi, hayo mengine mazungumzo ya kiutawala itakamilika ili mizigo iweze kupita kwenye eneo hilo, ahsante.
MHE. REUBEN N. KWAGILWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Swali langu la msingi lilikuwa: Ni lini, Serikali kwa kiasi kikubwa inatoa maelezo ya kipande cha barabara cha Magole – Turiani badala ya Handeni – Mziha –Turiani. Naomba kurudia: Ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kipande hiki cha Handeni – Mziha – Turiani? La kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili; tunayo barabara inayofanana na hiyo ya kutoka Handeni – Kibilashi – Kiteto – Kondoa – Singida, mikoa minne inaunganisha barabara ile; Na bomba la mafuta linalotoka Hoima mpaka Tanga linapita kwenye barabara hiyo: Ni lini Serikali pia itaanza ujenzi wa barabara hiyo muhimu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati njema sana, kwenye bajeti ya Wizara hii tarehe 27, 28 mwezi uliopita Mheshimiwa Waziri alisimama hapa kwenye Bunge Tukufu akataja kwamba tumepata kibali cha barabara 16 kati ya barabara 29 na barabara hii ya Handeni – Kibilashi – Kiteto – Kondoa – Singida imetengewa kuanza ujenzi wa kilometa 25 na wakati wote kuanzia sasa itatangazwa, ipo kwenye mchakato mbalimbali wa kisheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri Wabunge wa maeneo ya Mkoa wa Tanga, Dodoma, Manyara na Singida ni kwa sababu tumepata activation kubwa, bomba la mafuta linapita hapa na mmeshuhudia Mheshimiwa Rais Museveni amekuja hapa na Mheshimiwa Mama Samia walikuwa pamoja wameweka sahihi ya ujenzi wa bomba hili la mafuta. Maana yake ni kwamba barabara hii ni lazima ijengwe ikamilike ili huduma hii iweze kufanya vizuri. Kwa hiyo, msiwe na wasiwasi ujenzi wa barabara hiyo utakamilika mapema sana. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Swali langu dogo ni hili kwamba: Je, Serikali itaanza lini ujenzi wa barabara inayotoka Chekereni – Kahe kwenda Mabogini? Hii ni barabara pekee ambayo ni bypass kwa magari ambayo yanatoka Dar es Salaam kwenda Moshi na hakuna bypass nyingine. Kwa hiyo, ni lini wataanza ujenzi huo ambao pia upo kwenye Ilani? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba eneo ambalo anataja tunalifahamu, lakini tumeweka mipango ya Serikali kutafuta fedha. Tutaanza mara moja baada ya kupata fedha kujenga barabara hiyo ambayo ni muhimu ili kuendeleza shughuli za kiuchumi katika eneo lake. Ahsante.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikushukuru sana na kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza pia kukuona umekaa kwenye hicho kiti kwa kweli kimeku-fit sawasawa. Kama Mbunge kijana nakupongeza sana, hongera sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la nyongeza ni kwamba imekuwa ni habari kwa kweli ya muda mrefu sana, wananchi wa Mkoa wa Singida tumeendelea kupata ahadi, ahadi, ahadi ambazo kwa kweli kimsingi ningependa sana kaka yangu na mtani wangu ninaye muheshimu sana watupe commitment kama Serikali; uwanja huu wa ndege wa Mkoa wa Singida. ambao kimsingi tuko jirani kabisa na Makao Makuu ya nchi lini Serikali inakwenda kuanza ujenzi wa uwanja huu kwa maslahi ya wananchi wa Mkoa wa Singida? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka nipate commitment. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Immanuel Kingu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza katika ujenzi wa uwanja wa ndege au kama ilivyo kwenye barabara tayari uwanja huo umefanikiwa kupata hatua ya kwanza. Tumesema usanifu na upembuzi yakinifu umeshafanyika; maana yake tayari hapa tulipo tunajua angalau inahitajika gharama kiasi gani. Tunatafuta mapato ya ndani, lakini pia na washirika wetu wa maendeleo. Tukipata fedha hata kesho Mheshimiwa Kingu, uwanja huu utaanza kujengwa.

Naomba nikuhakikishie kwa niaba ya Serikali kwamba tuna nia ya dhati kwamba kila Makao Makuu ya Mkoa kuwe na uwanja wa ndege ili uweze kutoa huduma katika maeneo yale. Kila Mheshimiwa Mbunge angeweza kupenda baada ya Bunge kuahirishwa apande ndege itue nyumbani kwake kwenye mkoa wake, achangie mapato, lakini pia na wageni wengine wapate huduma kirahisi sana. Ahsante.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Kwa kuwa uhitaji wa uwanja wa ndege Mkoa wa Singida ni sawa na uhitaji wa uwanja wa ndege Mkoa wa Simiyu na tumekuwa tukipata majibu kwamba Serikali iko kwenye mchakato.

Sasa na mimi nataka tu commitment kwamba je, ni lini sasa Serikali itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege Mkoa wa Simiyu pale Igegu ili wananchi waweze nao kupanda ndege nikiwemo na mimi?
NAIBU WAZIRI, UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye swali la Mheshimiwa King una kwa kuwa mkoa huu ni mkoa mpya, Mkoa wa Simiyu na usanifu wa kina na upembuzi yakinifu umeshafanyika, gharama zimeshajulikana, Serikali inatafuta vyanzo mbalimbali, tukipata fedha Mheshimiwa Mbunge wa Busega naomba nikuhakikishie kwamba utapata uwanja katika Mkoa wa Simiyu. Kama ambavyo ameanza mapema lakini wanafanya kubwa sana. Hongereni sana kwa kazi nzuri ambayo mnafanya katika mkoa huo. Ahsante sana.
MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kuniona; kwa kuwa Mkoa wa Njombe nao ni mkoa mpya na kwa kuwa uwanja wa ndege upo kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kwa kuwa Njombe tumekuwa tukilima sana maparachichi.

Swali, ni lini Serikali itaanza kutekeleza kuujenga uwanja wa ndege katika Mkoa wa Njombe na kwa sababu Mbunge amekuwa akiuliza mara nyingi sana Mbunge Mwanyika juu ya uwanja wa ndege? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Sanga, Mbunge mzoefu na maarufu katika Bunge hili tukufu; ni kweli kwamba Mkoa huu ni mkoa mpya na ni maarufu kwa kilimo cha maparachichi ambayo pia sasa hivi yamepata soko nje ya nchi. Wanahitaji uwanja wa ndege ili maparachichi yale yatoke moja kwa moja Njombe yaende popote ambapo yanahitajika huko duniani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema ana bahati kwamba eneo lake hili usanifu umeshafanyika, gharama zimeshajulikana na kwa maelekezo ya Mheshimiwa Rais Mama Samia kwamba Watanzania walipe kodi bila shuruti, pamoja na vyanzo vingine tukipata fedha za kutosha hata kesho tutajenga uwanja huu. Ahsante.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, kwa kuwa ipo barabara ambayo ilitolewa ahadi na hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, barabara ya Kibamba – Mpiji – Mabwepande na tayari bajeti ya Wizara hii imepita.

Sasa nataka kauli ya Serikali juu ya bajeti husika juu ya barabara hii; ni nini kimefanyika juu ya utengenzaji wa barabara hii katika mwaka huu ikitegemea Hayati alisema wapelekewe kwa udharura?
NAIBU WAZIRI, UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mtemvu, Mbunge wa Kibamba kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba bajeti yetu imepitishwa tarehe 27 na 28 Mei, 2021 hapa Bungeni tunawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kupitisha bajeti yetu. Tunaomba tuwahakikishie kwamba ahadi zote za viongozi wakuu, Mheshimiwa Rais Hayati Magufuli, Mama Samia aliyepo madarakani sasa, Mheshimiwa Waziri Mkuu na ambazo zimetajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi zitatekelezwa. Tupeane muda tu. Mheshimiwa Mbunge, tutapitia kwa haraka haraka tuweze kujua ni barabara gani zimetajwa, zipo nyingi nchi nzima. Siwezi kukudanganya hapa lakini tukipitia kama ipo na fedha yake imetengwa tutaisimamia na kazi itafanyika na bahati nzuri tumepanga kwamba eneo hilo tutoe malalamiko mkoa wa Dar es Salaam, tumewekeza fedha za kutosha kuboresha barabara ili uchumi wa Tanzania uendelee kuku ana fedha hizo zifanye kazi za kujenga uchumi wa Watanzania kutoa huduma za kijamii. Ahsante sana.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri ameyatoa, naomba niulize swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Njombe ni moja katika mikoa mitano bora ambayo imefikia kiwango cha uchumi wa kati kwa watu wake, mkoa huu ni moja kati ya Halmshauri 10 bora kwa makusanyo zinazizidi hata Manispaa zaidi ya 10 katika nchi hii. Mkoa wa Njombe ni mkoa ambao una miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo parachichi pamoja na Liganga.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa swali langu; hivi ni kigezo gani kinachotumika maana wasiwasi wetu hata katika viwanja 11 tunaweza tukawa wa mwisho kwa sababu sioni ni vigezo gani, ukienda kwa niliyoyasema Mkoa wa Njombe unatakiwa uwe mkoa wa mwanzo kupata uwanja wa ndege? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deodatus Phillip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tunatambua mchango mkubwa wa kiuchumi kutoka Mkoa wa Njombe kwa ujumla wake pamoja na Njombe Mjini. Lakini vilevile uwezo wa Serikali siyo mkubwa kiasi hicho kujenga viwanja hivi vyote 11 kwa wakati mmoja. Safari ni atua upembuzi yakinifu umefanyika sasa tunajua gharama ya kujenga uwanja wa ndege wa Njombe ni gharama kiasi gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini ukweli ni kwamba unaangalia, ameuliza vigezo kwa mfano, pale Iringa mjini kuelekea Mkoa wa Iringa karibu kabisa na Makambako na Mkoa wa Njombe, sasa hivi tunazungumza mkandarasi yuko site anaendelea kufanya kazi ya kumaliza runway ili ndege aina zote ziweze kutua eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa wakati ambao Serikali inaendelea kupata fedha kutoka mapato ya ndani na washirika wengine wa kimaendeleo, watu wanaotaka kwenda Njombe wanaweza kutumia alternative kutumia uwanja Iringa baada ya kuwa umekamilika.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali yake ni njema tungependa kila Mkoa uwe na uwanja wa ndege na Waheshimiwa Wabunge wakitoka hapa baada ya Bunge kuahirishwa wangependa kutoa katika mikoa yao, lakini kwa kuwa fedha nyingi kiasi hicho tuvumiliane tupeane muda kazi hii itakamilika, ahsante sana.
MHE. MKUNDI M. JOSEPH: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, pale Ukerewe tuna kiwanja kidogo cha ndege na kama kitaboreshwa kitasaidia sana kuchochea vivutio vya utalii na kuvitangaza vilivyopo Ukerewe, lakini na kuchochea uchumi wa Ukerewe na wananchi wa ukanda ule kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, nini mkakati wa Serikali kukiboresha kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kwenye visiwa vya Ukerewe? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Joseph Mkundi Mbunge wa Ukerewe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Ukerewe ni eneo la kisiwa na kwa sababu hiyo usafiri pekee ambao unatumika ni aidha, kutumia anga au kupita majini. Mheshimiwa Mbunge nampongeza kwa kuombea wananchi wake wameshapata kivuko inafanya kazi katika eneo lile na hili wazo tunaomba tulipokee.

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni ya kuboresha viwanja vyetu vya ndege na hasa eneo kama Ukerewe ambalo kuna mambo ya kiutalii, wageni wanaweza wakatua pale, kuna shida ya kiusafiri, hili tunalipokea tunalifanyia kazi, tukipata fedha za kutosha Mheshimiwa Mbunge nakuhakikishia eneo lako litaboreshwa zaidi ya hapo lilipo ahsante sana.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kunipa nafasi naomba kufahamu Serikali lini itaanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Manyara ili kurahisisha usafiri na usafirishaji kwa wakulima wafugaji na wafanyabiashara wa Mkoa wa Manyara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge la nyongeza juu ya uwanja wa Manyara kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika swali nililoulizwa na Mheshimiwa Phillip Mwanyika kutoka Njombe Mjini, nimesema kwenye jibu la msingi kwamba viwanja 11 vimefanyiwa tathmini na upembuzi yakinifu, tunajua gharama zilizopo, uwanja wake Mheshimiwa Mbunge na Mkoa wa Manyara kwa ujumla upo kwenye mpango huu, tunatafuta fedha na zikipatikana wakati wowote uwanja wake wa Manyara, pamoja na viwanja vingine 11 ambavyo nimevitaja hapa vitajengwa ili ndege iweze kutoa huduma katika mikoa hiyo. Ahsante.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipatia nafasi hii. Mkoa wa Kagera kwa muda mrefu kumekuwa na uwanja wetu wa ndege wa kimataifa Omukajunguti.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujua ni lini uwanja huu wa Omukajunguzi utajengwa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa kipaumbele cha Serikali ni kuboresha uwanja wa ndege wa Bukoba, uwanja wa kimataifa na kwenye bajeti ya mwaka ambayo imepitishwa mwezi uliopita tarehe 27 na tarehe 28. Uwanja ule tunatarajia kujenga jengo la abiria maarufu kama VIP, lakini pia na kuongeza runway ili ndege nyingi kubwa ziweze kutoa katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka huu wa fedha Mheshimiwa Mbunge watu wa Bukoba na maeneo ya jirani muwe na Amani tunajenga uwanja ule jengo la abiria maarufu lakini pia na run way utapata usafiri.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mchakato wa kuhakiki mali za wananchi pamoja na majedwali haya ya fidia ulianza toka mwaka 2018, je, wananchi wa Kokoto hadi Kongowe wanataka kujua wavumilie mpaka lini?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, ni nini hatma ya wananchi wa Mbagala Rangitatu eneo la Charambe hadi kule Mbande ambao wamewekewa mawe ya hifadhi ya barabara toka mwaka 2010 na bila kupewa maelezo yoyote? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Chaurembo, Mbunge wa Mbagala kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza Mheshimiwa Mbunge wa Mbagala ambaye ni Meya Mstaafu wa Manispaa ya Temeke kilio chako kimesikika Mheshimiwa Mbunge na ndio maana Mheshimiwa Rais alitembelea katika eneo lako na ametoa maelekezo. Kiongozi Mkuu wa nchi akitembelea nchi hayo ni maelekezo sisi ni watekelezaji.

Mheshimiwa Spika, kilichofanyika ni kwamba ni fidia imefanyika, mkandarasi yupo pale site ataleta taarifa, watu wa TANROADS Mkoa wa Dar es salaam watapitia taarifa hiyo, tutafanya joint verification kwa maana ya Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Fedha na Valuer wa Serikali baada ya hapo wananchi wale watalipwa fidia. Maelekezo ni kwamba ujenzi hautaanza mpaka tuondoe vikwazo vya kulalamikiwa na wananchi baada ya kulipwa haki zao. Kwa hiyo, naomba wavute subira katika jambo hilo tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili Mheshimiwa Mbunge anauliza habari ya mawe ambayo imewekwa pale katika road reserve ya Mbande kwenda Msongola mpaka Mvuti. Ni kweli kwamba wananchi baadhi walilipwa wakati huo, lakini tumekubaliana kwamba tukianza upanuzi wa barabara hiyo, yule mwananchi ambaye anafikiwa kwa wakati huo atakuwa analipwa fidia yake, hayo ndio majibu ya Serikali, ahsante sana.
MHE. GHATI Z. CHOMETE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali lakini nina maswali madogo tu ya nyongeza: -

(a) Serikali imetangaza tarehe 4 Juni zabuni je, ni lini sasa kilometa 76 zilizobaki zitafanyiwa kazi? (Makofi)

(b) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha barabara hii inaendelea kupitika wakati wote. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Zephania Ghati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwamba ametoa kibali barabara hii imetangazwa inajengwa kwa awamu, kwa kuanzia na kilometa 25 tuna bilioni Sita za kulipa advance payment baada ya kumpata mkandarasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia swali lake la pili kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Mkoa wa Mara kupitia TANROADS imetenga shilingi milioni 411 kwa ajili ya kuendelea kufanyia maboresho barabara hii hadi hapo itakapokuwa imekamilika. Ahsante.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa, sera ya Serikali ni kuunganisha kwa kiwango cha lami barabara za Mikoa na Wilaya na kwa kuwa barabara ya Idete – Iringa ni barabara ambayo inaunganisha Majimbo matatu, Iringa Mjini, Jimbo la Kalenga na Jimbo la Kilolo.

Je, ni lini sasa Serikali itaijenga kwa kiwango cha lami barabara hii kwa sababu kwanza ni ya kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA
M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum maarufu wa Mkoa wa Iringa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba barabara aliyoitaja ni muhimu sana, na mpango wa Serikali ni kuunganisha mkoa na mkoa na wilaya na wilaya.

Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa niaba ya Serikali, kwamba fedha zikipatikana wakati wowote barabara hizi zote muhimu zitajengwa kwa kiwango cha lami. Ahsante sana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itaikumbuka Barabara ya Bujera – Masukulu mpaka Matwebe katika Wilaya ya Rungwe kuweza kutujengea? Mheshimiwa Waziri naomba jibu la Serikali.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge wa Mkoa wa Mbeya, wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba Rungwe mimi nimefika, na maeneo ya Mbeya kwa ujumla wake; na tumekubaliana kwamba tunapotaka kujenga barabara za eneo hili usanifu wa kina lazima ufanyike kwa sababu ya miundombinu yake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mbheshimiwa Sophia kwamba, pesa ikipatikana wakati wowote, barabara hii itajengwa kiwango uliyoitaja muhimu sana kwa watu wa Rungwe cha lami. Ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Uwanja wa Ndege wa Musoma ni uwanja wa kimkakati, kwa maana Mkoa wetu wa Mara umejaaliwa madini, mbuga za wanyama, makumbusho ya Baba wa Taifa, samaki na biashara mbalimbali,hivyo ungeweza kunufaisha taifa iwapo ungejengwa kwenye kiwango cha kimataifa ili ndege ziweze kutua moja kwa moja tofauti na ilivyosasa hivi watalii wanatua Nairobi au Arusha ndipo wanakuja kwenye mbuga ya Serengeti.

Ningependa kujua sasa, huu ujenzi na ukarabati ambao unaokadiriwa kukamilika ndani ya miezi 18, unatarajia kuwa na run ways pamoja na jengo la abiria la kiwango cha kimataifa? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, pale Tarime tuna Uwanja mdogo wa Magena ambao hutumiwa na watalii na wale ambao wanakwenda migodi kwa kutua na ndege ndogondogo. Na sasa hivi upo chini ya halmashauri ambapo unaikosesha mapato Serikali, kwa maana imekodiswa kwa makampuni binafsi.

Je, Serikali haioni sasa ni wakati mwafaka wa kuchukua uwanja ule ili uje kwenye Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwenye Serikali Kuu ili pia uweze kukarabatiwa na kuweza kutumika na kuongeza kipato cha taifa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Matiko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza uwanja wa ndege wa Musoma ni uwanja ambao ni wa kihistoria, ni uwanja ambao uliasisiwa na Baba wa Taifa hili. Vilevile upo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi na viongozi wetu wa mkoa wanausimama pamoja na Wabunge wote wa Mkoa wa Mara. Na mimi pia ni sehemu ya eneo hilo la mkoa huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimuhakikishie kwamba uwanja tayari, kulikuwa na eneo limebaki, kama mita 105, ili kila aina ya ndege hata kama iwe kubwa iweze kutua pale. Tumeshalipa, fidia imekamilika. Kwa hiyo, ndege zote muhimu zitatua katika eneo hilo na watalii kutoka Kenya watatua Musoma watakwenda Serengeti kwenye shughuli zao, na uchumi wa Mkoa wa Mara na maeneo mengine utafunga.

Vilevile swali lake la pili linalohusu Uwanja wa Ndege mdogo pale Magena. Wiki iliyopita Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi alikuwa pale, amefungua mnada wetu pale wa Magena, maana yake itaongeza soko la kibiashara katika eneo hilo, kuna mifugo itauzwa katika eneo hilo. Uwanja huu upo chini ya Halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunalipokea wazo hili, tufanye tathmini, tuangalie uwezo wa Serikali, ikiwezekana upanuliwe na kusimamiwa ili ndege ndogo za watalii ziweze kutua pale, na hivyo itapunguza msongamano pia kuja Musoma na badala yake watakuja kule Tarime ambapo kimsingi watalala Tarime, watakula Tarime, watafanya kazi Tarime na uchumi wa Tarime utafunguka. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza niishukuru sana Serikali kwa kuingia mkataba na mkandarasi huyu ili ujenzi uanze tarehe Mosi, Julai, kwa hilo kwanza napongeza sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, ili niweze kuuliza maswali yangu mawili ya nyongeza, ni kwamba swali la kwanza; mikataba mingi ya ujenzi inasainiwa, lakini ujenzi unapopita maeneo yao, watu wanakuwa hawajalipwa compensation ili ujenzi ule uanze. Je, Serikali imekwishalipa compensation kwa wale watu wa sehemu ambako mradi huo unapita ili mradi huo uanze?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; mkandarasi huyu waliyepatiwa wa CHICO Construction ndio huyu huyu aliyejenga barabara ya kilometa 50 kutoka Mwigumbi kwenda Maswa. Barabara hii hata kabla haijakabidhiwa ilikuwa tayari imekwishaanza kupata mashimo na kuharibika. Mkandarasi huyo sasa hivi anafanya mobilization ku-bypass ili aanze kukarabati barabara ambayo hata bado hajaikabidhi. Je, Serikali ina uhakika gani kwamba baada ya kumpa mkandarasi huyu kazi hiyo ya bypass atajenga kwa kiwango kinachostahili? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nyongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, utaratibu wa Serikali ni kwamba barabara haiwezi kuanza kujengwa kama wananchi hawajalipwa fidia katika eneo hilo. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kabla barabara haijaanza kujengwa, wananchi watalipwa fidia na baada ya hapo ndiyo ujenzi utaendelea; hilo namuondolea wasiwasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, anauliza mkandarasi ambaye amepewa barabara hii, M/S CHICO, kwamba alijenga barabara kutoka Mwigumbi kwenda Maswa na imeharibika. Bahati nzuri mwenyewe Mheshimiwa Mbunge amesema kwamba barabara hii haijakabidhiwa, utaratibu ni kwamba ukipata kazi, unafanya kazi yako, kabla hujakabidhi kuna muda wa matazamio na lolote likitokea, kama kuna sehemu imeharibika, unapaswa kutengeneza kwa gharama zako. Ameshaelekezwa maeneo yote ambayo yameharibika ayarekebishe ili aendelee na kazi nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge, kwamba huyu tutamfuatilia na kumsimamia kwa ukaribu, kazi lazima ikamilike. Kama kuna mahali kuna shida tutawasiliana mara kwa mara na Mheshimiwa Mbunge ambaye yuko karibu na wananchi wake, ili fedha ya Serikali ifanye kazi ambayo imekusudiwa. Ahsante.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ili kuuliza swali. Napenda kuuliza swali; ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Igawa, Mbeya mpaka Tunduma, zikiwemo njia nne za Mbeya Bypass kwa ajili ya kupunguza msongamano uliopo pale Mbeya? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwenisongole, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba barabara ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja ni barabara muhimu sana na kwako Mbeya Mjini ni shida. Bahati nzuri mwezi uliopita tulikwenda kule Mbeya, kulikuwa na mgomo wa bajaji, pikipiki na daladala, shida ni kwamba kuna msongamano mkubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mpango mkubwa wa Serikali wa kujenga barabara ya njia nne. Tunafanya mpango na majadiliano na Benki ya Dunia, tukipata fedha hiyo wakati wowote kuanzia sasa, barabara hii itajengwa ili kuweza kupunguza msongamano katika Mji wa Mbeya na maeneo ya jirani. Ahsante.
MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Naibu Waziri, lakini majibu haya vilevile yaliwahi kutolewa huko nyuma kwa swali hilihili ambalo limewahi kuulizwa, lakini tukaambiwa hela imepatikana ya msanifu na msanifu huyo hakuonekana na barabara hiyo mpaka leo haijawahi kujengwa. Sasa naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, je, Wizara inafahamu umuhimu wa barabara au inajibu tu ilimradi kujibu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa vile Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka jana imeiweka barabara hii kwamba ijengwe kwa kiwango cha lami na kwa ville hata Ilani iliyopita ya mwaka 2015 ilikuwa na barabara hii, je, naweza leo kupata commitment ya Serikali kwamba ni lini ujenzi huu wa barabara hii kwa kiwango cha lami unaanza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru, na naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jasson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inatambua umuhimu wa barabara hii na ndio maana mwenyewe anafahamu kwamba ana vijiji karibu 29, vijiji 18 vipo katika barabara hii kwa hiyo ikijengwa ni wazi kwamba uhakika wa yeye kuendelea kuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini utakuwa umetimizwa.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2020/2021 kuna fedha milioni 557 zilitengwa kwa ajili ya kuendelea kufanya maboresho ili barabara hii iendelee kupitika wakati wote.

Vilevile mwaka wa fedha 2021/2022 zimetengwa fedha zaidi ya milioni 217 kwa ajili ya kuendelea kufanya maboresho. Kwa hiyo, hii inaonesha kwamba Wizara inajua umuhimu wa barabara hii na ndio maana imekuwa ikitenga fedha kutoka mwaka hadi mwaka ili kuendelea kuiboresha ili wananchi wa Bukoba Vijijini waendelee kupata huduma hiyo ya barabara.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili; ametaka kujua commitment ya Wizara. Kwenye jibu la msingi nimesema barabara hii tayari kuna mhandisi mshauri ambaye atafanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Na barabara hii kuna wahandisi wawili ambao wamepatikana; Mhandisi consultant ambaye atafaya kazi ya kutoka Kyetema – Kanazi – Katoro – Kyaka yenye urefu wa kilometa 60.7 atafanya kazi hiyo ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

Mheshimiwa Spika, mhandisi wa pili Age Consultant yeye atafanya kazi sehemu ya barabara ya Bukoba, Bosimbe na Maluku yenye urefu wa kilometa 19.

Kwa hiuyo, wahandisi hao wawili wakifanya kazi hii ikikamilika sasa tutaanza angalau kilometa chache kufanya kazi ya ujenzi wa lami katika eneo hili ili Mheshimiwa Mbunge Jasson Rweikiza aendelee kuwa na uhakika wa kuendelea kuwa Mbunge wa eneo hili, ahsante.
MHE. NUSRAT SH. HANJE: Mheshimiwa Spika ahsante, pamoja na majibu Mheshimiwa Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Mkoa wa Singida ni mkoa muhimu sana pamoja na Mkoa wa Dodoma na Simiyu katika uchumi wa nchi, kwa sababu inatambulika kwamba Singida sasa hivi ni pilot kwenye zao la alizeti mahususi kwa ajili ya nchi, kwa hiyo pamoja na jibu lake kwamba mwaka 2022/2023 kwamba ndio ataweka kwenye mpango.

Je, Wizara haioni umuhimu wa kutafakari upya jambo hili kulinganisha na umuhimu wa Mkoa wa Singida kwa sasa kwenye bajeti ya mwaka huu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Mkoa wa Singida kwenye miundombinu ya barabara bado kuna changamoto sana. Je, Wizara ina mpago gani wa kuhakikisha kwamba inaunganisha Mkoa wa Singida kwa barabara za lami ili kuhakikisha kwamba wakulima wa alizeti na vitunguu wanafikiwa mpaka kwenye vijiji vyao? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba nijibu mswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge Nusrat kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nifanye marekebisho huu mwaka unasomeka 2021/2022; maana yake kuanzia Julai tathmini inafanyika tuweze kupata gharama ili tulipishe eneo la kipande cha reli ambacho kimetajwa.

Sehemu ya pili; Mheshimiwa Mbunge amesema kuunganisha barabara hizi za lami kwenye eneo lake Mkoa wake wa Singida, ni kweli kwamba tunao utaratibu mzuri wa kila Mkoa, kwa maana Meneja wa TANROADS Mkoa anapaswa kuratibu zoezi la barabara katika Mkoa wake husika. Sasa tupokee hoja yako kama kuna eneo ambalo halipitiki kabisa kwa sasa, nielekeze Meneja wa TANROADS wa Mkoa wa Singida afanyie kazi kama kuna sehemu ya kuchukua dharura tufanye hivyo ili kufanya maboresho kwa wakulima wa alizeti, vitunguu na maeneo mengine wapate huduma nzuri ya usafiri, ahsante.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, nakushkuru sana kwa kunipa nafasi na mimi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ni miundombuni ya reli ni muhimu sana katika usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria, na kwa sababu reli hii ilianzishwa na Baba wa Taifa; Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kumuenzi Baba wa Taifa kwa kuifanyia haraka kuijenga reli hii na iweze kutumika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtaturu, Mbunge kutoka Mkoa wa Singida kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi kwamba Serikali inatambua umuhimu wa reli hii, kama alivyosema imeasisiwa na Baba wa Taifa, na tukifanya tathmini ya kujua gharama tutaiboresha reli hii. Hii reli iliopo ni ya zamani itabadilishwa tuweke iwe kubwa zaidi iweze kubeba mzigo mkubwa zaidi.

Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge tupe muda mwaka huu mpaka mwakani utapata majibu ya ujenzi wa reli Singida
– Manyoni na maeneo mengine.
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA Mheshimiwa Naibu Spika, nakuskuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswli madogo mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa barabara hii itakapokamilika itakuwa imekamilisha mzunguko wa Mlima Kilimanjaro kwa barabara ya lami, na hivyo itaongeza na kuchochea kasi ya ukuaji wa utalii wa Mlima Kilimanjaro na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro vilevile. Kuna barabara nyengine ambayo ilipendekezwa kwenye ilani tangu mwaka 2015, inayotoka Longido kuja kuungana na hii ya lami katika eneo la Sanya Juu, na barabara hii pia itapita ndani ya Hifadhi ya Jamii ya Indumet.

Je, Serikali imeweka mpango gani wa kuhakikisha kwamba barabara hii ya kuunganisha hiyo Wilaya ya Longido na Mkoa wa Kilimanjaro na maeneo ya hifadhi na uzalishaji wa zao ya West Kilimanjaro inakwenda kujengwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kuna barabara pia muhimu ya TANROADS inayotoka Longido mpaka Oldonyolengai mlima mwingine wa kitalii na maarufu duniani, pale ambapo itaungana na ile inayotoka Loliondo kuja mpaka Mto wa Mbu.

Je, Serikali itaanza lini kama ilivyo ahidiwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020/2025 kufanya usanifu wa barabara ya lami kwa ajili ya barabara hiyo muhimu kwa biashara ya utalii?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza ya Mheshimiwa Kiruswa, muhimu sana kama ifutavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge kwamba wote kwamba ahadi zote ambazo zipo kwenye Ilani ya Uchaguzi za Chama cha Mapinduzi na zile ambazo zinazotolewa na viongozi wakuu wa Serikali zitatekelezwa kama zilivyopangwa, hiyo ni kwa awamu kutokana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa naibu Spika, barabara mbili ambazo umezitaja zote ni muhimu sana, na unapojenga barabara hizi, hii Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi unajua ni Wizara wezeshi, ukijenga barabara pale Mlima Kilimanjaro, utaongeza idadi ya watalii na mapato yataongezeka na utekelezaji wa Ilani utatekelezwa vizuri zaidi.

Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge nikwambie kwamba barabara ya Longido-Sanya Juu itaanza kujengwa kadri tukipata fedha pia Longido Oldonyolengai ambayo umeitaja nayo ni muhimu sana na tutaifanyia kazi, lakini nikupongeze kwa kazi unayoifanya ya kuwasemea wananchi wako wa Jimbo lako, ahsante sana.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, suala liliopo Longido hata Mbogwe lipo; na ni mpango wa Serikali kila Halmashauri kuunganisha barabara za lami kwenda Makao Makuu ya Mkoa.

Je, Wizara inampango gani kulingana na Jimbo langu la Mbogwe sina barabara inayounganishwa Wilaya kwa Mkoa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza Mheshimiwa Mbunge ni kweli kwamba tumekuwa tukizungumza mara kwa mara kufatilia ujenzi katika jimbo lake na tumeshawaelekeza Meneja wa TANROADS Mkoa ili waangalie mipango iliyoko ndani ya mkoa wao, lakini pia tuangalie na hii ya Wizara. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mpango uliopo wa Serikali ni kuunganisha Mkoa kwa Mkoa, Wilaya na Mkoa na Wilaya kwa Wilaya. Kwa hiyo hoja yako tumeipokea Mheshimiwa Mbunge tutaifanyia kazi kadri ambavyo Serikali itapata fedha. Ahsante.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nikupongeze wewe kwa kutaja jina langu vizuri na nimkumbushe tu Naibu Waziri, naitwa Simon Songe Lusengekile.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa barabara hii inachochea sana uchumi wa wananchi wa Jimbo la Busega na Jimbo la Bariadi, kwa maana ya Ngasamo, Shigara, Dutwa pamoja na Mariri.

Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu sana wa kuipa kipaombele barabara hii ili iweze kutengeneza kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa tunaelekea sasa mwisho wa Bunge letu la Bajeti; je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa kutembelea Jimbo la Busega ili aone umuhimu wa hii barabara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Lusengekile, Mbunge wa Busega kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara hii ni muhimu sana na ndiyo maana kwanza Mheshimiwa Mbunge tayari kuna fedha zipo anajengewa madaraja mawili hapa kama nilivyoyataja katika jimbo lake. Lakini, la pili tumeahidi kwenye jibu langu la msingi kwamba barabara hii inafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina mwaka huu wa fedha ambao unaanza Julai ambayo ni keshokutwa. Kwa hiyo, hii ikikamilika tutajenga barabara hii kwa kiwango cha lami tunajua umuhimu wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili mimi niko tayari kufanya ziara kule Busega. Kwanza kuna shemeji yangu pale kwa hiyo nitaenda kumsalimia. Tuko tayari, tutaambatana. Ahsante sana.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa ninalo swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo la Buyagu sasa linaelekea kufikia hatma, lakini bado wananchi wa Kata ya Ilunda Wilayani Sengerema wana adha ya namna hiyo ya kuwa na kivuko kidogo: Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka kivuko kikubwa katika eneo hili la Ilunda? (Makofi)

Mheshmiwa Naibu Spika, swali la pili: Kwa kuwa Wilaya ya Sengerema inayo majimbo mawili; lipo Jimbo la Buchosa na Mheshimiwa anafahamu kwamba watu wa Kome, Nyakalilo, Nyakasasa, Mtama wana matatizo makubwa ya usafiri: Je, Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka kivuko kikubwa katika maeneo haya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shigongo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza katika eneo la Sengerema – Buchosa wana bahati kwamba tunajenga daraja kubwa pale Kigongo – Busisi na kuna vivuko kadhaa vinafanya kazi katika Ziwa Victoria. Baada ya barabara hiyo na daraja kukamilika, maana yake vivuko vile vitahamishwa kwenda maeneo mengine; na maeneo haya ambayo Mheshimiwa Mbunge anataja ndiyo sehemu mojawapo tunaenda kumaliza changamoto hii ili kuweza kutoa huduma katika eneo hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyozungumza sasa tunajenga kivuko kipya ambacho kitafanyakazi Kata Nyakarilo na Kome kitaenda katika eneo hilo. Vile vile tunafanya ukarabati wa kivuko cha MV. SabaSaba ili kiende kusaidia MV2 Kome kuweka huduma katika eneo hilo. Kwa hiyo, naomba nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ipo makini sana kupeleka vivuko kwa sababu mbili; moja, ni sehemu ya biashara na pili, ni sehemu ya kutoa huduma. Watupe subira kazi zitakamilika na shida ya usafiri katika eneo hili kwenye visiwa mbalimbali Ziwa Victoria itakuwa imekamilika. Ahsante. (Makofi)
MHE. CATHERINE V. MAGIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa barabara hii ya kutokea Wasso kwenda Mto wa Mbu ina kilometa 206, lakini kwa miaka minne barabara hii imejengwa kilometa 49 tu; na barabara hii imekuwa inaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa Ngorongoro. Hivi juzi tu kuna mama amefia njiani akiwahishwa hospitali kujifungua na tumeona Mheshimiwa Mama Samia akitangaza utalii na barabara hii inahusu utalii. Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara hii? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili: Kwa kuwa mkandarasi huyu anadai shilingi bilioni 21 na walimwongezea muda, alikuwa amalize kujenga barabara hiyo Oktoba, 2019: Je, hamwoni kwamba mnaingiza Serikali katika hasara ya kulipa penalty? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI: Mheshimiwa
Naibu Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Catherine kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kweli kwamba Mkandarasi anadai shilingi bilioni 21; na anapokuwa amewasilisha hati ya madai, lazima kuna kazi ya kuhakiki madai yao yanafanyika. Kazi hiyo imeshafanyika na Juni mwaka huu 2021, Mkandarasi huyo amelipwa zaidi ya shilingi bilioni 12. Kwa hiyo, mchakato unaendelea, wakikamilisha uhakiki huko Wizara ya Fedha atalipwa fedha ili kazi iweze kuendelea. Mimi mwenyewe nimefika katika barabara hii na nilipata shida kweli barabarani, anachokisema ni kweli, ni barabara ngumu sana, tulipata pancha za kutosha, lakini Serikali imeweka nguvu barabara hii ikamilike.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la pili, barabara hii ni kweli ina urefu wa kilometa 206, inavyo vipande vinne. Kwa hiyo, tunaanza na hiki cha kwanza; kutoka Wasso kwenda Sale na twende mpaka Mto wa Mbu. Tuna- engage vyanzo mbalimbali kupata fedha ili barabara hii iweze kukamilika. Mheshimiwa Mbunge ambaye pia ni Naibu Waziri wa Serikali hii ya Awamu ya Sita tulikuwa pamoja na anajua tulifanya juhudi kubwa. Tukifanya mpango kumaliza barabara hii, itabadilisha uchumi wa wale watu wa Ngorongoro, itapeleka huduma za kijamii na pia itafungua milango ya watalii na pato la Taifa kwa ujumla wake litaongezeka katika eneo hili. Ahsante.
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, katika ukanda huu kuna barabara tatu ambazo ni Gohole, Nyigu, Mtwango, Nyololo na Mafinga Mgololo.

Je, Serikali ina mkakati gani kuhakikisha kwamba barabara hizo zitapitika katika kipindi hiki cha mvua ambazo zinaanza? Kwa sababu hazipitiki. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nancy Nyalusi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba eneo hili Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ameshaji-commit. Tulikubaliana kwamba mwaka wa fedha unaofuata 2022/2023 tutaanza kujenga eneo hili kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, lakini la pili naomba nitumie nafasi hii kutoa maelekezo kwa Meneja wa TANROADS Mkoa wa Iringa, atembelee maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja. Afanye tathmini na kama kuna shida basi matengenezo yafanyike, wananchi wapate huduma ya usafiri wa miundombinu wakati wote wa mvua. Ahsante.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru na nashukuru majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa barabara ya Mwanuzi hadi Mwabuzo, kilometa 42 imekuwa ni barabara muhimu kutokana na wafanyabiashara wanaotoka Wilaya ya Meatu na Maswa kwenda Igunga kufanya biashara na hata magari ya kusafirisha pamba. Kikao cha DCC kilipeleka maombi Mkoani na RCC walishapeleka Wizarani. Je, Serikali haioni haja ya kuipandisha barabara hiyo kuwa ya TANROADS? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kipande cha Mwabuzo – Igunga, kilometa 36 kimekuwa ni cha muhimu kutokana na biashara inayofanyika hadi mabasi saba yanapita katika barabara hiyo na wakati wa masika yanalazimika kupitia Shinyanga mpaka Igunga, kilometa 300. Je, Serikali haioni haja ya kuifungua barabara hiyo kutoka Mwabuzo kilometa 36 hadi daraja la Manonga kilometa 36? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba nitoe maelezo ya maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jeremiah ambayo yameulizwa kwenye Ofisi ya Rais, TAMISEMI kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara hii ambayo Mheshimiwa Mbunge ameitaja walipeleka maoni yao katika ngazi ya wilaya kama utaratibu ulivyo, yamefika kwenye ngazi ya mkoa wakajadili kwenye RCC yao na sisi Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi tumeshatuma watalaam wetu katika eneo hilo, ma-engineer wameenda wametafuta tafuta taarifa mbalimbali. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Mbunge avute Subira, watalaamu wetu walete majibu yale, halafu kama itakidhi vigezo barabara hiyo itapandishwa hadhi na kuhudumiwa na TANROADS ili iweze kutengenezwa na ipitike wakati wote.

Mheshimiwa Spika, swali la pili; barabara yake ya pili ambayo ameizungumza, tumeipokea kwa uzito tutaifanyia kazi, tuombe ushirikiano ili barabara hiyo iweze kufanyiwa matengenezo ya kudumu na wananchi wa eneo hilo waendelee kupata huduma muhimu kwa njia ya barabara. Ahsante. (Makofi)
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Barabara ya Mtila - Lugenge mpaka Usalule ni barabara ya muhimu sana nani barabara inayounga wilaya tatu ikiunga pamoja na Hospitali kubwa ya Mkoa wa Njombe. Je, Serikali haioni kwamba ni muhimu sana hii barabara na yenyewe ikaingizwa katika mpango wa TANROADS kwa sababu mchakato umeshaanza na umekwama mahali Fulani? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwanyika, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba hoja hii Mheshimiwa Mbunge amefikisha ofisini katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Kama alivyosema mwenyewe kwamba mchakato unaendelea, naomba a-speed up process hiyo na sisi tutatoa ushirikiano, itakapokidhi vigezo tutaipokea kama TANROADS, tutaitengeneza na wananchi wake watapata huduma muhimu katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Kwa kuwa barabara ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Meatu Mheshimiwa Leah Komanya ni barabara ambayo pia inaungana na barabara ya kutoka pale Mwabuzo ikaenda Kabondo, Itinje, Mwandwitinje mpaka Mwaukoli na inaunganisha na zote hii inatoka Bariadi nyingine inatoka Meatu zinaenda zote Mkoa wa Tabora na Wilaya ya Igunga.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa sababu mapendekezo haya yote tuliyapeleka kwa pamoja kama ambavyo Naibu Waziri wa Ujenzi amejibu, sasa anaweza kunihakikishia kwamba haya maombi yote yanafanyiwa kazi kwa pamoja na muda mfupi ujenzi utaanza wa barabara hizi sasa kuwa za mkoa na baadaye ujenzi kuanza mara ili kuondoa changamoto zilizopo kwa sasa kutokana na TARURA kushindwa kumudu kukidhi mahitaji yake?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mpina, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, naomba nitumie Bunge lako Tukufu kumwagiza Meneja wa Mkoa wa Simiyu, Shinyanga na Mwanza na maeneo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge wameshaleta mapendekezo kwenye maeneo haya, wafanye kazi ya tathmini haraka iwezekanavyo, wawasilishe majibu Wizarani na sisi kama Serikali tuweze kuchukua hatua ili maeneo hayo yaweze kutengenezwa kwa haraka na wananchi wote waweze kupata huduma ya barabara. Ahsante. (Makofi)
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu hayo ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, suala la barabara hii limekuwa sasa kama ni hadithi. Hata watangulizi wangu wamekuwa wakipigia kelele sana barabara hii lakini pamoja na umuhimu wake bado Serikali inatuletea hadithi ya kwamba inatafuta bajeti. Wananchi wamechoka na hii hadithi, wanataka wajue je, ni lini barabara hii sasa itawekwa kwa kiwango cha lami?

Swali la pili; kwa kuwa Serikali bado inaendelea kutafuta bajeti kwa hii barabara lakini barabara hii ni muhimu sana, inapitisha mizigo kutoka sehemu mbalimbali na inapitisha abiria na mambo mengine. Lakini barabara hii mpaka leo inatumika kama uchochoro kwa baadhi ya magari ambayo yanakwepa kupima uzito sehemu nyingine. Sasa je, Serikali ipo tayari kutujengea mzani ili barabara hii iweze kuwa katika ubora wake ule ule?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Rehema Migilla kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza siyo kweli kwamba hizi ni hadithi nimesema tu kwamba kwa niaba ya Serikali tunaendelea kutafuta fedha tufanye upembuzi yakinifu na usanifu wa kina tuweze kujua tunahitaji upana wa lami kiasi gani na uzito wa mizigo unaoweza kupita katika eneo hilo, madaraja, ili tupate makisio ya bajeti ili tuweze kutafuta fedha. Kwa hiyo naomba Mheshimiwa Mbunge avute subira katika wakati huo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ameomba mizani. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa wazo hili limepokelewa na litafanyiwa kazi na watapata majibu kwa wakati muafaka. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli hali ya madaraja ya TAZARA, hasa kwa upande wa mataruma ya mbao, yana hali mbaya sana kiasi cha kuhatarisha maisha ya wasafiri pamoja na usalama wa mizigo. Je, Serikali ina mkakati gani na mpango wa haraka kupeleka fedha ili hayo madaraja yaweze kukarabatiwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; TAZARA ni muhimu sana katika ushindani wa Bandari yetu ya Dar es Salaam, huu ushindani wa kikanda unaifanya bandari yetu kuwa katika pressure kubwa sana. Je, Serikali haioni umuhimu wa kutenga pesa ya kutosha kupitia TPA Shirika letu la Bandari ili liweze kushiriki katika kujenga na kuboresha miundombinu ya TAZARA? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Oran Manase Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, anatoa taarifa ya hali mbaya ya Reli yetu ya TAZARA. Ninaomba nimuelekeze Mtendaji wetu wa TAZARA atembelee maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyataja, afanye tathmini ya haraka ili tuone kama hali ni mbaya kiasi hicho Mheshimiwa alivyozungumza basi ufanyike utaratibu wa kawaida kufanya marekebisho ili kuepuka madhara kwa mizigo na abiria ambao wanatumia eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Mheshimiwa Mbunge anauliza kama kuna uwezekano wa TPA kuwekeza katika eneo hili. Mheshimiwa Mbunge ni Mjumbe wa Kamati tumekutana kule TPA Dar es Salaam, wazo hili alilitoa ni wazo jema. Tumewapa maelekezo watu wa TPA waangalie uwezekano wa kuwekeza katika eneo hili kwa sababu wanaihitaji TAZARA katika kusafirisha mizigo, walifanyie kazi, wafanye tathmini, tukijiridhisha basi wazo la Mheshimiwa Mbunge tutalifanyia kazi. Lengo ni kuweza kutoa huduma kwa watu wetu, hasa upande wa Tanzania. Ahsante. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa njia pekee ya kuisadia TAZARA ni kubadilisha hiyo sheria iliyoanzisha TAZARA, Serikali inatoa tamko gani la haraka kuhakikisha sheria hiyo inabadilishwa ili Tanzania iwekeze zaidi kuliko wenzetu wa Zambia wanaosuasua? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spik, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba sheria hii imekuwa ni kikwazo kwa upande wa Tanzania kuwekeza katika reli hii kwa sababu kama nilivyosema, hisa ni asilimia 50 kwa 50. Kila ukiwekeza upande wa Tanzania haiongezi hisa katika upande wetu, lakini nia ya Serikali ni kwamba ingewezekana hata leo sheria hii ingeweza kubadilishwa tuwekeze katika upande wetu kuweza kutoa huduma kwa watu wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto, kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni kwamba sheria hii hatuwezi kuibadilisha upande wa Tanzania mpaka tukutane na watu wa Zambia. Wenzetu walikuwa na uchaguzi wameshamaliza, wamefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali, tumeshawaandikia barua tunasubiri wakijibu tukikutana jambo hili nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge litafanyiwa kazi haraka sana. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuuliza kuhusu hii reli kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi na Arusha ilifufuliwa, sasa imekufa, ni kitu gani kimeiua? Naomba Waziri hebu tueleze. (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Kimei kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hii reli haijafa ila zipo changamoto ambazo tunaendelea kuzifanyia kazi, kuongeza vitendeakazi pamoja na wafanyakazi katika eneo hili. Mheshimiwa Mbunge avute subira tunalifanyia kazi, reli hii itaendelea kufanya kazi ambavyo imekusudia Serikali, ndiyo maana ikaanzishwa baada ya muda mrefu sana. Ahsante.
MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, hivi karibuni sote tumeona jitihada kubwa sana za Rais Samia za kuvutia watalii katika nchi yetu, lakini pia sasa hivi tayari Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Hapi, pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii walianza jitihada za pamoja, wameanza vikao vya kuona namna ya kujenga uwanja ule. Hii ni kuzingatia pia kwamba kuna ushindani mkubwa kwa wenzetu, watu wa Masai Mara kule Kenya ambao wana-share ikolojia moja na Serengeti.

Mheshimiwa Spika, sasa namwomba sana Mheshimiwa Naibu Waziri nipate nafasi ya kukutana naye kwa mazungumzo maalumu kuona ni namna gani tutapata mwelekeo wa pamoja wa kuweza kujenga uwanja huu kwa viwango vikubwa kabisa.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, barabara hii ya Sanzate mpaka Natta, na ile ya Tarime – Mugumu – Natta, barabara hizi hazi-connect Makao Makuu ya Wilaya ya Serengeti pale Mugumu. Mwaka wa jana, 2020 aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano alitupa ahadi ya ujenzi wa kilometa 30. Kwa hiyo, namwomba sana…

SPIKA: Unasema Tarime – Mugumu – Natta, haifiki Mugumu tena!

MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Spika, Tarime – Mugumu – Natta halafu kuna ile ya Makutano na Sanzate – Natta. Sasa zote hizi kwa jinsi ya ule mpango wa ujenzi, zitachukua muda mrefu kuja kuunganisha Makao Makuu ya Wilaya. Kwa hiyo, tukawa tumemwomba aliyekuwa Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwamba kipande cha Natta – Mugumu kiweze kupewa fedha kijengwe haraka ili barabara ile ya Makutano – Sanzate – Natta sasa itoke pale Natta mpaka Mugumu. Halafu na ile inayotoka kule Tarime – Nyamwaga – Mugumu iweze kuungana nayo mapema zaidi.

Mheshimiwa Spika, sasa ni lini Wizara inaweza kutekeleza mpango huu na ile ahadi ya Rais? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Amsabi Jeremiah, Mbunge wa Serengeti kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza ameomba tufanye mazungumzo namna bora ya kupata fedha ya kujenga uwanja wa ndege wa Serengeti.

Mheshimiwa Spika, naomba tu nitumie nafasi hii kusema kwamba kwa sasa pia Mheshimiwa Rais ameshatoa fedha za kutosha za kuanzia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Musoma na mkandarasi ameshapatikana, yupo site anafanya kazi, lengo ni kuboresha huduma katika Hifadhi ya Serengeti.

Mheshimiwa Spika, tangu anazungumza Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, walifanya kazi nzuri sana pamoja na Wizara ya Maliasili ya kufanya mjadala. Sisi tunaona kwamba uwanja ambao walipendekeza kujenga ni uwanja ambao unamilikiwa na TANAPA na Halmashauri, ambao ni uwanja mdogo. Sisi tunataka tujenge uwanja mkubwa wa Kimataifa ili tushindane na wenzetu wa Kenya ambao wanajenga kule Masai Mara uwanja mkubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumewaelekeza watu wa Maliasili Uongozi wa Mkoa wa Mara watuletee andiko maalumu, tukae pamoja na Wizara ya Ujenzi, tujenge Uwanja wa Ndege wa Kimataifa ili tusigawane watalii wanaotaka kupata huduma katika mbuga yetu ya Serengeti. (Makofi)

SPIKA: Huo uwanja mnataka kujenga wapi?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, tunafikiria kujenga uwanja wa ndege Serengeti pale Mugumu, wanalo eneo pale la kutosha.

SPIKA: Haya endelea.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, sawa, ahsante.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni kweli kwamba barabara ya Sanzatte inajengwa na ameleta ombi la kilometa 30, tumepokea ombi hilo na linafanyiwa kazi. Wakati huo huo, kilometa 25 zinajengwa kutoka eneo la Tarime kwenda Serengeti ili wananchi wa eneo hilo waweze kupata huduma.

Mheshimiwa Spika, mawazo yote ni mazuri, lakini kupanga ni kuchagua. Kadri tunavyopata fedha za kutosha, barabara hizo zitakamilika kwa wakati ili huduma iweze kupatikana katika eneo la Serengeti. Ahsante. (Kicheko)
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nashukuru pia, majibu mazuri yenye kutia matumaini kutoka Serikalini. Hata hivyo, nina maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; nafahamu tulikuwa na behewa la daraja la pili, lakini kwa bahati mbaya behewa hili lilipata ajali ya moto. Ni lini Serikali itaturejeshea huduma hiyo ya behewa la daraja za pili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Kituo cha Mpanda kwa bahati mbaya sana wakati wananchi wakisubiri huduma ya usafiri, jengo lao la kusubiria huduma hiyo halipo. Ni lini Serikali pia, itatusaidia huduma hii muhimu ya jengo la kusubiria abiria? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA M. WAITARA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kapufi, kwa faida ya wananchi wa Mpanda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge anataka kujua kama tutarejesha daraja la pili katika eneo hili. Naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge maombi haya yamepokelewa. Tutazingatia maombi haya hasa katika mabehewa mapya ambayo yanaendelea kununuliwa angalau huduma hiyo iweze kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, tumepokea pia hoja ya pili ya jengo la kusubiri abiria. Hili ni eneo muhimu kwa sababu kama kunakuwa na jua abiria wanahitaji kivuli, lakini pia kama ni wakati wa mvua inapaswa kujikinga. Namwelekeza Mtendaji Mkuu wa TRC atembelee eneo hili ufanywe mpango wa haraka kujenga jengo la kusubiria abiria ili wananchi waweze kupata huduma muhimu. Ahsante.
MHE. KHLAIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza namshukuru Waziri kwa majibu yake ya kina, lakini hata hivyo nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali langu lilihusu hasa usalama wa raia wanaporushwa katika ndege. Usalama wao huu siyo kwa sababu ya uchache na udogo wa ndege. Ndege nyingi takribani ndogo ndogo hizi ambazo tunaruka nazo ni chini ya kilogramu 4,000, lakini bado ni abiria: Je, Serikali itabadilisha sheria hata kuwa ndege ni ya watu watatu, kilogram 3,000 kuleta marubani wawili?

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusu marubani kufanyiwa uhakiki wa afya zao miezi sita au 12; mgogoro wa afya unaweza kutokea wakati wowote akiwa ndani ya anga. Sasa unaonaje, unanusuru vipi abiria wale ambao rubani wao amepata changamoto ya afya akiwa angani peke yake? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. MWITA
M. WAITARA): Mheshimiwa Spika, nakushukuru. naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khalifa, Mbunge wa Mtambwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza Mheshimiwa Mbunge anataka kujua, ni kwa nini ndege ambazo zinabeba watu chini ya kilo 3,000 haziwezi kutumia marubani wawili?

Kwanza, ndege inapokuwa inatengenezwa, yule mtengenezaji anatoa maelekezo marubani wangapi wanapaswa kuitumia hiyo ndege.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili, ni kweli kwamba kutumia marubani wawili kwenye ndege moja ndogo pia ni gharama, maana yake huyo rubani inabidi alipwe. Ila sisi kisheria tumeruhusu kwamba unaweza ukatumia marubani wawili, lakini waendeshaji wadogo kwenye ndege zao hawazuiliwi kisheria kutumia marubani wawili.

Mheshimiwa Spika, la tatu, wanaangalia pia ile ndege aina ya mitambo na vipuri vinavyotumika. Ndege hizi ndogo zinabeba chini ya abiria 19 na haziendi umbali mrefu zaidi na hazitembei kwa saa nyingi na haziendi juu ya anga kwa maana ya kupata mikikimikiki ile ya mawimbi makubwa. Hata hivyo ikitokea kuna viashiria vya hali ambayo siyo nzuri kwa afya, kwa kuchukua tahadhani wanaweza kuongeza rubani wa pili katika ndege hiyo.

Mheshimiwa Spika, la pili ni uhakiki wa afya za marubani kwamba wale ambao wana miaka chini ya 40 ni mizei sita, lakini wale zaidi ya miaka 40 ni miezi 12. Hii ni ukweli kwamba kisayansi kwa mazoea ni kwamba hawa wenye chini ya miaka 40 ni vijana, tunaamini kwamba wana afya na nguvu ya kuweza kufanya kazi zaidi. Ila ikitokea kwamba kuna viashiria vya hali ya usalama kiafya wanaweza kufanyiwa utaratibu wa kupimwa afya zao hata chini ya miezi mitatu. Ni jambo ambalo linawezekana.

Mheshimiwa Spika, tunafanya mambo yote haya kwa kuzingatia Sheria ya Anga ya Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, ahsante.