Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Esther Lukago Midimu (16 total)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora kwa mwaka wa fedha 2016/2017
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya. Vile vile nampongeza Waziri Mkuu kwa kazi nzuri anazozifanya, wananchi wote wanaziaminia. Pili, nawapongeza akinamama wa Mkoa wa Simiyu kwa kunipa kura ili niweze kuwawakilisha katika Bunge lako Tukufu na nawaahidi utumishi uliotukuka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nawapongeza sana Mawaziri wote wawili kwa hotuba yao nzuri. Naanza na uboreshaji wa maslahi ya Madiwani. Madiwani wanafanya kazi katika mazingira magumu sana hawana hata usafiri. Naiomba Serikali yangu sikivu iweze kuwapatia hata pikipiki ili waweze kufanya kazi vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la afya Wilaya ya Maswa; hospitali ya Wilaya ya Maswa ina tatizo la umeme, umeme siyo wa uhakika unasuasua, miundombinu imekuwa ya kizamani. Naiomba Serikali yangu iweze kuboresha miundombinu ya hospitali ya Wilaya ya Maswa. Vile vile hospitali ya Wilaya ya Maswa ina majengo ambayo yameshakamilika, jengo la OPD, theater na wodi ya wazazi, lakini hayajaanza kutumika. Naomba Serikali yangu sikivu ya Chama cha Mapinduzi hayo majengo yaanze kutumika yaweze kuhudumia wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile katika Wilaya hospitali ya Maswa ina tatizo la maji. Jambo la kusikitisha Maswa Mjini kuna maji na hospitali ya Maswa na Maswa Mjini ni pua na mdomo, lakini hospitalini hakuna maji. Naiomba Serikali yangu ifanye haraka ivute maji kutoka pale Maswa Mjini ipeleke hospitali ya Maswa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu afya katika Wilaya ya Itilima, Wilaya ya Itilima tunayo zahanati kubwa sana Kata ya Luguru. Hiyo zahanati ina majengo mengi sana. Tunaomba kibali kwa zahanati hiyo ili iweze kupandishwa hadhi iwe kituo cha afya. Tuna jengo kubwa la upasuaji limejengwa na Mfuko wa Mkapa Foundation na vifaa tiba tayari vipo, tatizo hatuna wataalam wa upasuaji. Naiomba Serikali yangu itupelekee Madaktari Bingwa wa upasuaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna kituo cha afya Zagayu. Kituo cha afya cha Zagayu kina wafanyakazi watano ambapo mahitaji ni wafanyakazi 32. Tunaomba mtupelekee watumishi 32 ili waweze kuhudumia vizuri. Tunacho kituo cha afya Kata ya Nkoma, tunaiomba Serikali itupatie kibali kama kuna uwezekano tukipandishe hadhi kwa Wilaya ya Itilima tuwe na Hospitali ya Wilaya, kwa sababu wananchi wa Itilima wanahangaika sana, wakipata matatizo wanaenda kutibiwa Bariadi, Somanda. Tukikipandisha hadhi kile kituo cha afya cha Itilima, nina imani hata msongamano wa wagonjwa Somanda utapungua. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya maji; naipongeza sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kuahidi kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria kuleta Mkoani Simiyu kupitia Wilaya zake za Busega, Bariadi, Maswa, Itilima na Meatu. Naiomba Serikali yangu ihakikishe hayo maji itakapovuta, maji yapitie kwenye shule zote za Mkoa wa Simiyu za Sekondari, vituo vya afya vyote na zahanati ili yaweze kusaidia kwa sababu maji ni muhimu kwenye vituo vya afya na hospitali, ukizingatia na sera yetu ya sasa hivi ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kila Kijiji kutakuwa na zahanati na kila Kata kutakuwa na kituo cha afya. Naomba na maji yafike huko. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile kuna vijiji katika Wilaya ya Maswa havina maji kabisa ambavyo ni Gudekwa, Masanwa, Mwabalatulu na Isegenge, akinamama wa vijiji vile wanahangaika sana. Naiomba Serikali yangu iweze kuchimba visima virefu kwa hivyo vijiji nilivyovitaja ili mradi akinamama waweze kupata maji. Wameshindwa kufanya kazi zao za ujasiriamali na mambo mengine ya maendeleo wamebaki kutafuta maji, wanasafiri kilometa nane mpaka kilometa 10. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu sekta ya elimu; naishukuru sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kujenga shule nyingi za Kata, naipongeza sana. Naiomba Serikali yangu kama kuna uwezekano kwa Mkoa wetu wa Simiyu iweze kutenga kila Wilaya shule ya bweni kwa watoto wa kike, kwa sababu watoto wa kike wanahangaika sana, watoto wa kike tukijenga shule za bweni tutawaepusha na vishawishi vya chipsi na bodaboda wakiwa wanarudi makwao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Bariadi tuna Chuo cha Ufundi, Bunamhala, chuo kile naomba kiboreshwe, vijana wengi wapate ujuzi ili waweze kujiajiri wenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mkoa wetu una changamoto, una upungufu wa nyumba za Walimu 1,471, madarasa 563 na matundu ya vyoo 2,107. Tunaiomba Serikali iweze kutuletea pesa kupitia TAMISEMI ili tuweze kukamilisha ujenzi huu. Vile vile naomba Serikali iweze kuweka Chuo cha VETA Mkoani Simiyu na iweze kutuletea pesa haraka sana tuweze kujenga hospitali ya Mkoa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi, naunga mkono hotuba ya Waziri Mkuu kwa asilimia mia moja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa namshukuru Waziri kwa hotuba yake nzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nianze kuchangia mchango wangu. Mkoa wetu wa Simiyu ni wakulima wazuri wa pamba lakini cha kusikitisha zao hilo linaenda kufa kabisa, wananchi wamekata tamaa kabisa kwa sababu ya bei kushuka. Suluhisho pekee la bei ya pamba ni kutuletea kiwanda cha nguo na nyuzi. Mkituletea kiwanda cha nyuzi, nina imani vijana wengi watapata ajira na bei ya pamba itapanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wetu wa Simiyu tuna viwanda vitano vya kuchakata pamba. Naona na wenye ginneries wamekata tamaa, nashindwa kuelewa kwamba zao la pamba likifa viwanda vile vitafanya kazi gani. Naomba mtuletee kiwanda cha nyuzi na kiwanda cha nguo, nina imani hata wao watauza marobota yao karibu zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pia mkoa wetu ni wa wafugaji, tunaomba mtuletee kiwanda cha nyama. Nasema hivyo kwa sababu wafugaji wetu wanaibiwa sana, wakipeleka mnadani ng‟ombe mmoja anauzwa shilingi laki mbili mpaka shilingi laki tatu lakini ng‟ombe huyo huyo ukimlisha na kumnenepesha ukimpeleka kiwandani unamuuza shilingi laki nane mpaka shilingi milioni moja, naomba mtuletee kiwanda cha nyama. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Simiyu kuna akinamama wajasiriamali wakubwa na wazuri sana, wana vikundi vikubwa. Naomba Serikali iwaletee viwanda vidogo vidogo vya SIDO vya kusindika mazao ili waweze kujikwamua na umaskini.
Mheshimiwa Naibu Spika, ya kwangu yalikuwa ni machache tu ya kuomba viwanda, Serikali yangu ni sikivu, naomba ituletee viwanda hivyo katika Mkoa wetu wa Simiyu. Ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Maji na Umwagiliaji
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanazozifanya. Kwa namna ya pekee nampongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya. Kwa muda mfupi amefanya kazi na zimeonekana, Mwenyezi Mungu ambariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ahadi ya kuleta maji kutoka Ziwa Victoria mpaka Mkoa wa Simiyu na Wilaya zake tano za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa na Meatu, na hela tayari zimeshakuja, wananchi wana imani na Rais wao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yangu sikivu maji yakifika Mkoa wa Simiyu iweze kusambazwa kwenye shule za msingi na sekondari pamoja na vituo vya afya na zahanati. Nasema hivyo kwa sababu wanafunzi wanahangaika sana, muda mwingi wanachota maji usiku, asubuhi wakienda darasani wanashindwa kusoma wanasinzia tu, ni bora Serikali itoe kipaumbele katika mashule yetu yapate maji ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Mkoa wa Simiyu ni wachapakazi wazuri na ni wakulima wazuri, nina imani maji yakifika watalima kilimo cha umwagiliaji, njaa itakuwa ni ndoto katika Mkoa wa Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali yangu kwa ajili ya kutuletea shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya ukarabati wa mabwawa Wilaya ya Itilima na mabwawa yale ni Mwamapalala, Nobora, Sunzula, Sawida, Chinamiri na Lugulu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yangu sikivu sasa iweze kusambaza maji kwenye kata ili kutimiza azma ya Mheshimiwa Rais ya kumtua mwanamke ndoo kichwani. Iweze kusambaza kwenye kata zifuatazo, kata za Nkuyu, Migato, Mwaswale, Mwamtani, Nkoma, Kindilo na Sawida. Maeneo haya niliyoyataja wanawake wanahangaika sana, muda mwingi wanaupoteza kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na ukizingatia wanaochota maji ni wanawake si wanaume. Mwanamke anachota maji usiku, saa zingine anakutwa na matatizo huko njiani. Naiomba Serikali iweze kuzingatia hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER L. MUDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya Mwenyezi Mungu ambariki sana. Pili, nampongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu Waziri kwa hotuba yao nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kutenga fedha shilingi bilioni 15 kwa ajili ya kuvuta maji toka Ziwa Victoria kuleta Simiyu, pamoja na Wilaya zake za Busega, Bariadi, Itilima, Meatu na Maswa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sasa nianze kuchangia, kuna Mradi wa Chujio Wilaya ya Maswa ni wa muda mrefu sana umeshindwa kabisa kukamilika. Mkandarasi kila akiongezewa muda ameshindwa kabisa kukamilisha, wananchi wa Wilaya ya Maswa wakiendelea kunywa maji siyo safi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inakigugumizi gani cha kuvunja mkataba na kumpa au kufunga mkataba na mkandarasi mwingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa namshukuru Rais kwa kazi nzuri anazozifanya kwa kazi nzuri anazozifanya Mwenyezi Mungu ambariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, namshukuru Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mwenyezi Mungu awabariki sana kwa kazi nzuri wanazozifanya. Pia nampongeza sana Waziri wa TAMISEMI na Naibu Mawaziri wake pamoja na Katibu Mkuu kwa kazi nzuri wanazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya afya. Katika Mkoa wetu wa Simiyu tuna tatizo la upungufu wa wafanyakazi. Katika vituo vya afya na hospitali hatuna watumishi kabisa. Tunaiomba Serikali yangu sikivu itusaidie ili tuweze kupata watumishi katika hospitali zetu za Mkoa wa Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa kutenga pesa ili tuweze kujenga Wilaya mpya ya Itilima na Busega, wametenga bilioni tatu. Naiomba Serikali yangu sikivu hizo pesa zije kwa wakati, tujenge hospitali kwa wakati ili iweze kusaidia Wanabusega na Wanaitilima kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Wilaya ya Busega wanahangaika sana na wa Itilima, wanafuata matibabu Wilaya ya Bariadi na Wilaya ya Bariadi inategemewa na Wilaya tatu, hivyo, kuna msongamano wa wagonjwa sana. Sasa naiomba Serikali yangu sikivu iweze kukamilisha hizo hospitali haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali ya Wilaya ya Meatu haina Daktari bingwa kabisa wa magonjwa ya akinamama. Akinamama wa Wilaya Meatu wanahangaika sana, wanafuata matibabu Wilaya ya Bariadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni mtu wa Simiyu, mtu atoke Kata ya Mwabuzo kufuata matibabu Bariadi na hiyo hiyo Wilaya ya Bariadi ina Daktari bingwa mmoja anategemewa na Wilaya nne; Wilaya ya Bariadi, Wilaya ya Meatu, Wilaya ya Busega na Wilaya ya Itilima. Tunaomba katika hospitali ya Meatu mtuletee Daktari Bingwa wa magonjwa ya akinamama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu, naishukuru Serikali kwa mpango wake wa elimu bure. Katika Wilaya Maswa tuna sekondari 36, maabara zilizokamilika ni saba, maabara 29 bado, zimejengwa na zimeezekwa kwa kupitia Halmashauri na nguvu za wananchi. Naiomba Serikali sasa itusaidie ili maabara ziweze kukamilika na shule bila maabara bado haijakamilika kwa sababu wanafunzi wanatakiwa kusoma masomo ya sayansi yaani chemistry na physics. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine ni upungufu wa Walimu katika shule za msingi na shule za sekondari. Naiomba Serikali yangu itusaidie Walimu katika shule zetu za Simiyu za sekondari na za shule ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi wa maji wa Ziwa Victoria, kwanza niishukuru sana Serikali mwaka jana kwa kutenga pesa za mradi wa maji wa Ziwa Victoria unaokuja Simiyu. Mradi huu mpaka sasa haujaanza na hakuna dalili zozote zinazoonekana kwamba mradi unaweza ukaanza. Mheshimiwa Waziri wa Maji nilimuuliza swali kuhusu mradi huu, Waziri akanijibu vizuri sana kwamba mradi huo unaweza ukaanza mara moja. Huo mradi utaanza na Wilaya ya Busega, Bariadi pamoja na Itilima kwa awamu ya kwanza ambao ujenzi wake utachukua miaka miwili. Akasema awamu ya pili atamalizia na Maswa na Meatu, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni mtu wa Simiyu unajua akinamama wanavyohangaika kutafuta maji, hivyo, mradi huu utawasaidia sana akinamama ambao wanahangaika kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. Pia utasaidia kwenye taasisi za Serikali kama shule, zahanati na vituo vya afya. Vilevile tutalima na kilimo cha umwagiliaji, sisi ni wachapakazi njaa kwetu itakuwa ni ndoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi mwingine wa Maswa wa chujio, yaani huu mradi umekuwa ni kizungumkuti. Mradi huu una miaka mingi wananchi wa Maswa wanakunywa maji siyo safi na salama. Nilishawahi kuuliza swali humu, Mheshimiwa Waziri akanipa moyo akasema baada ya miezi mitatu huo mradi utakamilika, huu mradi unasua sua. Mkandarasi huyu kila akiongezewa muda hamalizi, miaka nenda rudi anaongezewa muda huu mradi hauishi, wananchi wetu wanaendelea kuhangaika. Serikali ina kigugumizi gani kuvunja huo mkataba na mwekezaji huyu, ikafunga mkataba na mwekezaji mwingine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuishukuru Serikali yangu sana ya Chama cha Mapinduzi ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mchapakazi, Mwenyezi Mungu ambariki, naendelea kuishukuru sana kwa Wilaya ya Itilima inaendelea kutuletea fedha za kujenga miundombinu. Sasa hivi tumejenga jengo la utawala, zahanati zinaendelea na vituo vya afya vinaendelea, Mwenyezi Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsate sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa namshukuru Rais kwa kazi nzuri anazozifanya kwa kazi nzuri anazozifanya Mwenyezi Mungu ambariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, namshukuru Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mwenyezi Mungu awabariki sana kwa kazi nzuri wanazozifanya. Pia nampongeza sana Waziri wa TAMISEMI na Naibu Mawaziri wake pamoja na Katibu Mkuu kwa kazi nzuri wanazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza sana Wizara ya Afya kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya afya. Katika Mkoa wetu wa Simiyu tuna tatizo la upungufu wa wafanyakazi. Katika vituo vya afya na hospitali hatuna watumishi kabisa. Tunaiomba Serikali yangu sikivu itusaidie ili tuweze kupata watumishi katika hospitali zetu za Mkoa wa Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa kutenga pesa ili tuweze kujenga Wilaya mpya ya Itilima na Busega, wametenga bilioni tatu. Naiomba Serikali yangu sikivu hizo pesa zije kwa wakati, tujenge hospitali kwa wakati ili iweze kusaidia Wanabusega na Wanaitilima kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Wilaya ya Busega wanahangaika sana na wa Itilima, wanafuata matibabu Wilaya ya Bariadi na Wilaya ya Bariadi inategemewa na Wilaya tatu, hivyo, kuna msongamano wa wagonjwa sana. Sasa naiomba Serikali yangu sikivu iweze kukamilisha hizo hospitali haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali ya Wilaya ya Meatu haina Daktari bingwa kabisa wa magonjwa ya akinamama. Akinamama wa Wilaya Meatu wanahangaika sana, wanafuata matibabu Wilaya ya Bariadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni mtu wa Simiyu, mtu atoke Kata ya Mwabuzo kufuata matibabu Bariadi na hiyo hiyo Wilaya ya Bariadi ina Daktari bingwa mmoja anategemewa na Wilaya nne; Wilaya ya Bariadi, Wilaya ya Meatu, Wilaya ya Busega na Wilaya ya Itilima. Tunaomba katika hospitali ya Meatu mtuletee Daktari Bingwa wa magonjwa ya akinamama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu, naishukuru Serikali kwa mpango wake wa elimu bure. Katika Wilaya Maswa tuna sekondari 36, maabara zilizokamilika ni saba, maabara 29 bado, zimejengwa na zimeezekwa kwa kupitia Halmashauri na nguvu za wananchi. Naiomba Serikali sasa itusaidie ili maabara ziweze kukamilika na shule bila maabara bado haijakamilika kwa sababu wanafunzi wanatakiwa kusoma masomo ya sayansi yaani chemistry na physics. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine ni upungufu wa Walimu katika shule za msingi na shule za sekondari. Naiomba Serikali yangu itusaidie Walimu katika shule zetu za Simiyu za sekondari na za shule ya msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi wa maji wa Ziwa Victoria, kwanza niishukuru sana Serikali mwaka jana kwa kutenga pesa za mradi wa maji wa Ziwa Victoria unaokuja Simiyu. Mradi huu mpaka sasa haujaanza na hakuna dalili zozote zinazoonekana kwamba mradi unaweza ukaanza. Mheshimiwa Waziri wa Maji nilimuuliza swali kuhusu mradi huu, Waziri akanijibu vizuri sana kwamba mradi huo unaweza ukaanza mara moja. Huo mradi utaanza na Wilaya ya Busega, Bariadi pamoja na Itilima kwa awamu ya kwanza ambao ujenzi wake utachukua miaka miwili. Akasema awamu ya pili atamalizia na Maswa na Meatu, lakini mpaka sasa hakuna kinachoendelea kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe ni mtu wa Simiyu unajua akinamama wanavyohangaika kutafuta maji, hivyo, mradi huu utawasaidia sana akinamama ambao wanahangaika kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. Pia utasaidia kwenye taasisi za Serikali kama shule, zahanati na vituo vya afya. Vilevile tutalima na kilimo cha umwagiliaji, sisi ni wachapakazi njaa kwetu itakuwa ni ndoto. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mradi mwingine wa Maswa wa chujio, yaani huu mradi umekuwa ni kizungumkuti. Mradi huu una miaka mingi wananchi wa Maswa wanakunywa maji siyo safi na salama. Nilishawahi kuuliza swali humu, Mheshimiwa Waziri akanipa moyo akasema baada ya miezi mitatu huo mradi utakamilika, huu mradi unasua sua. Mkandarasi huyu kila akiongezewa muda hamalizi, miaka nenda rudi anaongezewa muda huu mradi hauishi, wananchi wetu wanaendelea kuhangaika. Serikali ina kigugumizi gani kuvunja huo mkataba na mwekezaji huyu, ikafunga mkataba na mwekezaji mwingine? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuishukuru Serikali yangu sana ya Chama cha Mapinduzi ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, mchapakazi, Mwenyezi Mungu ambariki, naendelea kuishukuru sana kwa Wilaya ya Itilima inaendelea kutuletea fedha za kujenga miundombinu. Sasa hivi tumejenga jengo la utawala, zahanati zinaendelea na vituo vya afya vinaendelea, Mwenyezi Mungu ambariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsate sana na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa naipongeza Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi nzuri inazozifanya. Sisi Mkoa wa Simiyu katika majimbo yote tumeletewa gari za kubeba wagonjwa, hongera sana Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili nampongeza Mheshimiwa Ummy kwa kazi nzuri anazozifanya pamoja na Naibu Waziri, kwa kweli wanafanya kazi nzuri. Waheshimiwa Wabunge juzi juzi tu tumeshuhudia Serikali inakabidhi magodoro, vitanda pamoja na mashuka, hongera sana kwa Serikali kwa kazi nzuri inazozifanya.Pia Serikali yetu inajitahidi sana dawa kwenye hospitali zetu, asilimia 85 mpaka asilimia 90 ya dawa zinapatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naishukuru Serikali yangu kwa kutuletea pesa za ujenzi wa hospitali ya mkoa, naishukuru sana. Serikali imetuletea pesa tumemudu kulipa eneo la hospitali ya mkoa, ni ekari 121, fidia tumelipa zaidi ya milioni mia mbili, ujenzi wa ground floor tumelipa zaidi ya milioni mia tano, ujenzi wa kumalizia ghorofa moja tumelipa zaidi ya bilioni moja, jumla kuu ya pesa tulizolipa zaidi ya bilioni mbili tulizotumia kwenye ujenzi. Naishukuru sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, sasa hivi jengo la OPD limekamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana Serikali yangu; naiomba sasa iweze kutujengea wodi za wagonjwa. Wodi ya wazazi, wodi ya watoto na wodi ya akinamama. Hospitali ya mkoa bila wodi itakuwa bado haijakamilika, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali teule ya mkoa haina gari la kubebea wagonjwa kuwapeleka Hospitali ya Rufaa ya Bugando. Tunaiomba Serikali itununulie gari la kubebea wagonjwa ituletee ili tuweze kupeleka wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando na hospitali nyinginezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naiomba Serikali ituletee gari la mpango wa damu salama. Akinamama wengi wanapoteza damu kwa ajili ya kujifungua; inaweza ikanusuru akinamama pamoja na watoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hospitali yetu ya mkoa ina upungufu sana wa watumishi, tunaiomba Serikali ituletee watumishi. Watumishi waliopo katika hospitali ya mkoa ni watumishi asilimia 25, asilimia 75 hawapo. Tunaomba watuletee Madaktari Bingwa ili waweze kuhudumia na kukidhi mahitaji ya hospitali yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo moja baya linajitokeza katika nchi yetu, halifai kuigwa katika jamii na linaleta taswira mbaya katika nchi yetu. Jambo hilo ni ubakaji wa watoto wadogo wa miaka miwili. Watoto wadogo wanabakwa na baba zao, wajomba zao, pamoja na majirani kutokana na imani zao za kishirikina; inaumiza sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna kipindi nilikuwa ziara nilienda wilaya fulani ambayo sitaitaja; kuna mtoto mdogo wa miaka mitatu alikuwa amebakwa akaharibiwa sana na ikabidi wampeleke rufaa Bugando. Naiomba Serikali ikemee hilo kwa nguvu zote ikiwezekana wanaofanya hivyo wanyongwe, hiyo itasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni mimba za utotoni; sana sana zinatokea kwa maeneo ya wafugaji; naiomba Serikali iweze kudhibiti tatizo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru Serikali kwa kuanzisha Benki ya Wanawake, lengo ni kuwakomboa wanawake wote kiuchumi. Naiomba Serikali wakati Waziri anakuja kujibu hapa naomba aniambie benki hiyo ni lini itafika katika Mkoa wa Simiyu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Mwenyekiti wa Bodi kupitia vyombo vya habari alisema kuna madeni hayalipiki, ni bilioni nane. Naomba Mheshimiwa Waziri akisimama aje atueleze hiyo bilioni nane imekwenda wapi na ni akina nani waliokopa ambao hawarudishi? Naiomba Serikali yangu ijitahidi sasa kukusanya yale madeni ya bilioni nane ili hizo pesa ziwafikie wananchi wa Mkoa wa Simiyu. Akinamama wa Mkoa wa Simiyu nao wana hamu ya kupata zile pesa za Benki ya Maendeleo ya Wanawake halafu na wanawake wa mikoa mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi, niendelee kuipongeza Serikali yangu kwa kazi nzuri inazozifanya. Mwenyezi Mungu awabariki sana Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pia niwapongeze Mawaziri wote kwa ujumla wanajitahidi, wametembelea mikoa yetu pamoja na wilaya zetu wanafanya kazi nzuri, hongera sana, nawatia moyo, wachape kazi, wasonge mbele. Ahsanteni sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wetu wa Simiyu una mito miwili muhimu sana. Mito hiyo ni Mto Simiyu na Mto Duma. Kwa miaka ya hivi karibuni mito hiyo imekuwa inakauka muda mfupi tu baada ya mvua za masika kwisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo kubwa, miti mingi imekatwa ili kutengeneza mkaa na kuni kwa ajili ya kupikia na hii ni kwa sababu hakuna chanzo kingine cha nishati. Imefika hatua akina mama wanatumia kinyesi kupikia, kitu ambacho kinasababisha macho yao kuwa mekundu. Hii ni sababu ya lawama na kusingiziwa ni wachawi na hatimaye kuuawa kwa kukatwa na mapanga.

Je, Serikali ina mpango gani mahususi na wa dharula ili kuleta nishati mbadala na wenye gharama nafuu ili kuwanusuru akina mama wenzetu wa Mkoa wa Simiyu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, watalii wengi wanatokea Arusha kuelekea Serengeti, lakini sisi Mkoa wa Simiyu hatuna barabara wala mlango wa kuingilia Hifadhi ya Serengeti. Je, ni lini sasa barabara hiyo itajengwa ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu nao wapate fursa ya kuitumia hifadhi ya Serengeti na kufurahia urithi wa Taifa letu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mkoa wa Simiyu miradi ya barabara hatuioni na wakati kuna Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Pori la Akiba la Maswa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mazao yatokananyo na nyuki yana mchango mkubwa sana katika uchumi wa nchi yetu, pia kuna nchi hapa Afrika, kwa mfano Ethiopia, mazao ya nyuki yana mchango mkubwa sana katika GDP. Tanzania ina mazingira mazuri sana kwa ufugaji wa nyuki kwa mfano Mikoa ya Katavi, Rukwa, Tabora na Kigoma pamoja na Singida, lakini hata hivyo sioni mpango mkakati wa kuliendeleza jambo hilo. Vilevile hakuna watalaam wa nyuki kwa sababu hata chuo kilichopo Tabora ni kidogo utadhani ni chuo cha mtu binafsi. Tunaomba chuo hicho kiongezewe miundombinu ili kiongeze udahili. Serikali iendelee kuchukua hutua madhubuti ya kuwezesha chuo hiki na kutengeneza ajira kwa vijana na kuliwezesha zao hili kuongoza Kimataifa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ESTER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya, Mwenyezi Mungu ambariki sana. Pili, nampongeze Makamu wa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya, Mwenyezi Mungu ambariki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampogeza Waziri Mkuu kwa kazi nzuri anazozifanya, Mwenyezi Mungu ambariki sana. Nampongeze Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI pamoja na Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu kwa hotuba nzuri waliyoisoma, inaridhisha, imesheheni mambo mazuri. Pia nampongeza Mheshimiwa Mkuchika, Waziri wa Utawala Bora. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nianze kuchangia. Naipongeza Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kutujengea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu, ambayo imezinduliwa na Mheshimiwa Rais juzi, inafanya kazi vizuri. Hata hivyo, kuna changamoto katika hospitali ya mkoa. Changamoto ya kwanza, hatuna genereta ya dharura umeme ukikatika; hospitali hiyo haina uzio na ina upungufu wa vifaa tiba. Naiomba Serikali iliangalie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi nzuri inazozifanya, imetuletea shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya; Wilaya ya Itilima, Busega na Bariadi DC mchanganuo wake, kila Wilaya inapata shilingi bilioni 1.5. Hospitali hizo zikikamilika, nina imani matatizo yatapungua hususan katika wilaya hizo nilizozitaja; huduma itakuwa karibu; na vifo vya akina mama na watoto havitatokea tena. Vikitokea ni bahati mbaya, siyo kwamba vinatokea kwa kukosa matibabu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naiomba Serikali yangu katika hospitali yetu teule ya Mkoa wa Simiyu haina Madaktari Bingwa wa magonjwa ya akina mama; na hospitali hiyo ina msongamano sana. Inahudumia wilaya tatu; Busega, Bariadi na Itilima. Msongamano unakuwa mkubwa sana, akina mama wakienda pale, inachukua siku mbili au tatu kupata matibabu. Tunaiomba Serikali itusaidie kutuletea daktari wa magonjwa ya akina mama kwa vile akina mama tuna maradhi mengi. Kuna maradhi mengine yanahitaji kumwona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Akina Mama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuipongeza Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kuboresha Hospitali ya Wilaya ya Maswa. Imetujengea genereta nzuri, imetujengea x-ray nzuri, inafanya vizuri. Vilevile imetujengea wodi ya akina mama na watoto, tunapongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naenda sasa Wizara ya Maji. Naipongeza sana Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi kwa kutuletea mradi wa maji wa Ziwa Victoria. Mradi huo ukifika utatusaidia wananchi wa Mkoa wa Simiyu hususan akina mama kwa sababu muda mwingi wanaupoteza kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. Nina imani mradi huo ukifika, tutafanya kazi za maendeleo, tutalima mboga mboga, tuta-supply Dodoma na Dar es Salaam mpaka nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na pongezi hizo kuna changamoto Wilaya ya Maswa kata ya Zanzuni. Kuna mradi wa chujio ambao umechukua muda mrefu sana. Kila kandarasi akiongezewa muda mradi huo umeshindwa kukamilika. Nashindwa kuelewa tatizo ni nini, huku wananchi wa Maswa wakiendelea kunywa maji ambayo siyo safi na salama. Fedha zipo ila mradi haukamiliki. Naiomba Serikali iangalie hilo kwa mapana yake. Kila siku nikisimama hapa hilo nalipigia kelele. Naomba sasa Serikali yangu kwa vile ni sikivu, iweze kunisikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pia niipongeze Serikli kwa mradi mkubwa wa maji wa Busega ambao upo kata ya Ramaji. Niliuliza swali juzi juzi hapa Bunge lililoisha. Mheshimiwa Naibu Waziri alinipa majibu mazuri sana, akasema, mradi huo utaanza kufanya kazi mwezi wa Nane. Nami nimeenda kufanya ziara, nimewaambia akina mama, mradi huo utaanza kufanya kazi mwezi wa Nane. Kwa hiyo, wananchi wa Busega wanasubiria hiyo neema ya maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa kazi nzuri anazozifanya, Mwenyezi Mungu ambariki sana, tunamwombea, atabaki kuwa juu, atabaki kuwa mawinguni. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Awali ya yote napenda kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuongeza bajeti katika miradi ya maendeleo na maeneo mbalimbali hii inadhihirisha kuwa kweli uchungu wa mwana aujuae mzazi na hasa mama.

Mheshimiwa Spika, nipende kutoa shukrani kwa Serikali kwa kuongeza bajeti ya maendeleo inayogusa moja kwa moja kwa wananchi hasa bajeti ya Mradi wa TASAF, ujenzi wa barabara za vijijini, upimaji wa ardhi na miradi ya maji. Pia niipongeze sana Serikali hasa kwa kuongeza bajeti ya kushughulikia masuala ya maafa, wote ni mashahidi kuwa nchi yetu hivi karibuni ilikumbwa na maafa, hivyo niipongeze sana Serikali kwa hatua hii.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa kutoa ushauri wangu; kwanza mchakato wa kuchagua wanufaika wa Mradi wa TASAF uongezwe umakini ili tuweze kupata wanufaika wanaostahili, tofauti na sasa maana kuna baadhi ya watumishi wasiokuwa waaminifu wamekuwa wanaingiza wasiostahili bila sababu za msingi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ardhi, kumekuwa na migogoro mingi japo utatuzi wa migogoro umekuwa wa kusuasua na baadhi ya Mabaraza ya Ardhi yamekuwa chanzo cha migogoro kuongezeka, hivyo nashauri Serikali kuangalia mabaraza haya kwa jicho la kipekee ili yatende haki.

Kuhusu sekta ya afya nazidi kuipongeza Serikali kwa kuendelea kujenga hospitali kwa kila Wilaya, vituo kwa kila kata na zahanati kwa kila Kijiji. Katika mkoa wetu wa Simiyu tunaomba sana kupewa watalaam zaidi wa afya ili waweze kuendana na mitambo mipya na ya kisasa ambayo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imekuwa ikileta mkoani kwetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu zao la pamba; hili ni moja ya zao la mkakati ambapo kwa asilimia 50 linazalishwa katika mkoa wa Simiyu, pia niipongeze Serikali hasa Wizara ya Kilimo kupitia Waziri Hussein Bashe na wenzie kwa kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani nchi nzima. Nashauri pia motisha iende pia kwa wakulima wa pamba kwa kupandisha bei ya kununulia zao hilo ili kuleta tija kwa wakulima kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeweza kuitekeleza ajenda 10 kwa 30, kilimo ni biashara.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya nashukuru sana na naunga mkono bajeti hii.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia Wizara ya Maji. Kwanza kabisa nampongeza Waziri kwa hotuba yake nzuri iliyosheheni matumaini ya Watanzania. Mheshimiwa Aweso unafanya kazi nzuri pamoja na Naibu wako.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Rais wangu, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama. Haijawahi kutokea mwanamke kuwa Mwenyekiti wa Taifa. Wanawake tunajivunia hilo, Mheshimiwa Rais ametuheshimisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ana dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani, ni mwanamke mwenzetu, shida zote zitaisha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sasa niongelee mradi wa Ziwa Victoria. Toka mwaka 2010 tunaongelea mradi huu, tunaomba maji kutoka Ziwa Victoria, hatimaye Serikali yetu sikivu ikatusikia, ikakubali kutuvutia maji kutoka Ziwa Victoria kuleta Mkoa Simiyu. Nilishawahi kusimama mwaka juzi kuuliza swali hapa kuhusu mradi huo utaanza lini.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa kipindi kile alinipa majibu mazuri akasema mradi huo utaanza na Wilaya tatu; utaanza na Busega, Bariadi na Itilima, lakini hadi sasa hakuna kitu kinachoendelea. Baadaye wakati wa kampeni, Mheshimiwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli wakati anafanya kampeni zake alisema Mkoa wa Simiyu tayari wameshatenga shilingi bilioni 800 kwa ajili ya kuvuta maji kuleta wapi Mkoa wa Simiyu kutoka ziwa Victoria, lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea. Naiomba Serikali yangu Sikivu, kwa vile inasema hizo fedha imetupa, itoe sasa mradi uendelee. Mradi huo utainua uchumi wa Simiyu na Mikoa ambayo ni ya pembezoni mwa Simiyu. Kwa sababu wanawake wa Mkoa wa Simiyu ni wakulima wazuri, wachapakazi, tutalima kilimo cha umwagiliaji, tutalima mboga mboga na matunda, tutauza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sera ya Serikali ni kuwa na uwanja wa ndege kila Mkoa. Simiyu tumetenga tayari eneo la uwanja wa ndege, nina imani utajengwa na ndege zitatua, tutasafirishva mboga mboga kwenda nje. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika maji waathirika wakubwa ni akina mama. wanaume muda mwingi nyie mmepumzika, mmelala tu, sisi tunakwenda kutafuta maji, tukirudi ndani tunapika. Ninaomba Serikali ibaini sasa maeneo ambayo yana shida na hali mbaya kabisa ya maji, ichimbe visima vidogo vidogo kwa sababu tunaoathirika ni sisi wanawake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee kuishukuru Serikali yangu na kuipongeza kwa mradi mkubwa wa maji wa Lamadi ambao umejengwa kwa shilingi bilioni 12.8 na unahudumia vijiji vitatu; Kijiji cha Lamadi, Kijiji cha Lukungu na Kijiji cha Mwabayanda. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, bado kuna vijiji vingine vina uhitaji zaidi, hawana maji kabisa; Kijiji cha Mirambi na Mwanhari. Wilaya ya Meatu ina shida kubwa sana, haina maji kabisa na wanawake wa kule wanahangaika sana. Muda mwingi wanaupoteza kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. Halafu jiografia ya Meatu ni mbaya sana, maeneo yale yana ukame sana, hata kama maji yakichimbwa kule chini unakutana na magadi, unakutana na maji ambayo hayafai katika matumizi ya binadamu. Naiomba Serikali ifanye utaratibu kila mwaka itenge fedha iwe inachimba hata mabwawa mawili mawili wapate maji watu wa Meatu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna bwawa la Mwanjoro huko huko Meatu. Kipindi kile Mheshimiwa Rais wa sasa wa Awamu ya Sita alikuwa Makamu wa Rais, alikwenda kulizindua. Sasa hivi limejaa tope. Naiomba Serikali yangu itoe fedha hilo bwawa likarabatiwe, kwa sababu linahudumia vijiji vitano ili wanawake waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa maji Mkoa wa Simiyu asilimia 60.3 Wilaya ya Meatu, asilimia 62 Wilaya ya Maswa, asilimia 69.2 Wilaya ya Itilima na asilimia 50.8 Wilaya ya Busega. Upatikanaji wa maji bado upo chini, tunaomba Serikali ituletee fedha ili tuchimbe visima virefu viweze kusambaza maji. Bahati nzuri kwa Simiyu tuna Meneja mwana mama mchapakazi, anachapa kazi, ni mtu mzuri, yeye anasubiri fedha tu aweze kusambaza maji kila kona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, ubarikiwe sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Esther Lukago Midimu.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Kicheko/Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi hili niwese kuchangia kwanza kabisa nampongeza Waziri na Naibu waziri kwa hotuba yake nzuri iliyosheheni matumaini ya watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naipongeza Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi kwa kutupatia pesa bilioni 5.4 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya, Wilaya ya Busega Bariadi DC na Itilima. Mchanganuo wake kila wilaya tumepata bilioni 1.8 lakini pia tunachangamato ya ukosefu wa vifaa tiba pamoja na madawa. Changamoto hii ni kubwa sana katika vituo vyetu vya afya pamoja na Hospitali za Wilaya wananchi wanatoka vijijini kwenda kutibiwa kwenye Vituo vya Afya wakifika wanakosa madawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo inasikitisha sana mwananchi akitibiwa anaambiwa kwenda kununua dukani kuna wananchi wengine wana hali duni hawana uwezo wa kununua dawa, naiomba Serikali iweze kutuletea dawa za kutosha katika hospitali zetu. Lakini pia katika vituo vyetu vya afya mkoa wa Simiyu hatuna x-ray mashine, hiki kifaa ni muhimu sana ikiwezekana naiomba Serikali ibaini vituo vyote vya afya nchi nzima ambavyo havina x-ray mashine ili waweze kufunga. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vijana wetu hawa wa bodaboda wanapata ajali, wakienda kwenye kituo cha afya wanapewa tiba ya dharula ambayo ni ya mwanzo kwamba atibiwe halafu baadaye aende katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Kwa vile vijana wetu wanaimani potofu wanaendea kwa waganga wa kienyeji hatimaye kidonda kinaoza wengine wasukuma wetu kule anaweza akapata ugonjwa wa TB hajapigwa x-ray anaenda kwa waganga wa kienyeji anatumia dawa za kienyeji akienda kwenye kituo cha afya hamna kipimo cha x-ray anaishia kutumia madawa ya kienyeji anaathirika naiomba Serikali ifanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine katika vituo vyetu vya afya hatuna umeme mbadala ambao ni jenereta, daktari akiwa anamfanyia mama mjamzito operation umeme ukikatika inakuwa ni shida naiomba Serikili ifanye utafiti katika vituo vya afya vyote ambavyo havina umeme mbadala ambayo ni jenereta ili waweze kufunga. (Makofi)

Mheshismiwa Naibu Spika, lakini pia katika vituo vyetu tuna upungufu mkubwa wa madaktari hasa madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, sisi akina mama tuna maradhi mengi, ukienda hospitali huwezi ukatibiwa na daktari wa kawaida kuna malazi mengine ambayo unatakiwa umwone specialist wa magonjwa ya wanawake. Sisi Mkoa wa Simiyu tuna mmoja tu ambaye yupo Somanda, na katika Mkoa wa Simiyu tuna Wilaya tano huyo daktari anahudumia wilaya tano unakuwa msongamano mkubwa, daktari anachoka tunaiomba Serikali ituletee madaktari bingwa katika hospitali zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hospitali yetu ya mkoa, kwanza niipongeze Serikali kwa kutupatia pesa kujenga hospitali yetu ya Mkoa katika hospitali yetu ya mkoa bado haijakamilika hatuna wodi ya akinamama, hatuna wodi ya watoto, na hatuna wodi ya akina baba. Jengo la mama la mtoto bado halijakamilika na pesa ipo sijui tatizo ni nini, Mkandarasi anasuasua sana tunaiomba Serikali waziri akija aje na majibu kwa nini hilo jengo linasuasua na pesa ipo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hospitali yetu ya mkoa hatuna uzio kabisa, na hospitali ikikosa uzio ni hatari sana hospitali yetu ya Mkoa wa Simiyu iko karibia na barabara ya lami, wagonjwa katika hospitali wanaenda wa kila aina kuna mwingine anaweza kwenda amerukwa na akili anakimbilia kwenye lami anagongwa gari lakini pia uzio unadhibiti hata kuibiwa madawa na vifaa tiba. Naiomba Serikali itupatie pesa ili tuweze kujenga uzio. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru sana Serikali kwa kutuboreshea hospitali ya Maswa tuna theatre nzuri na tuna wodi nzuri za kulaza wagonjwa lakini tatizo mortuary ni ndogo inachukuwa watu watatu Tunaomba tupatiwe friji ili tuweze kuipanua hiyo mortuary. Lakini pia katika Vituo vya Afya vya Mkoa wa Simiyu hauna friji za kuhifadhi maiti. Tunaiomba Serikali iweze kutuletea friji katika vituo vyetu vya afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hospitali inayotibu saratani ni moja tu hiko Dar es salaam ambayo ni Ocean Road na wagonjwa wengi wanatoka kanda ya ziwa, tunaomba Serikali iboreshe hiyo hospitali ya Bugando ili kuweze kurahisha matibabu wananchi wanaotoka vijijini kanda ya ziwa watibiwe hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana baada ya kusema hayo naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maji
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais wangu mpendwa Mama Samia Suluhu kwa kazi nzuri alizozifanya, Mwenyezi Mungu ambariki sana.

Pili nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kazi nzuri anazozifanya Mwenyezi Mungu ambariki sana. Tatu nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Maji pamoja na Naibu Waziri na cabnet yake, wanafanya kazi nzuri. Mheshimiwa Aweso unafanya kazi nzuri mwanangu, Mungu akubariki.

Mheshimiwa mwenyekiti, tunamuona Mheshimiwa Waziri anazunguka nchi nzima kukagua miradi ya maendeleo; Mungu ambariki sana pamoja na Naibu Waziri. Nawapongeza Mawaziri wa Wizara pamoja na Naibu Mawaziri, wanafanya kazi nzuri, wanazunguka nchi nzima kukagua miradi ya maendeleo, Mungu awabariki sana. Nampongeza sana Meneja wetu wa Maji wa Mkoa, Mariam, kwa kazi nzuri anazozifanya, Mungu ambariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa nianze kuchangia. Namshukuru Mheshimiwa Rais kwa kutupatia milioni 400 kwa ajili ya Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Mkoa wa Simiyu katika Wilaya za Busega, Bariadi, Itilima, Maswa pamoja na Meatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, waziri tayari ameshasema, bilioni 400 zimeshapatikana. Mheshimiwa Rais ana dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani. Na Mheshimiwa Waziri amesema kwamba pesa, hizo bilioni 400 zimepatikana 400, ila bado wanatafuta mkandarasi. Niiombe Serikali yangu sikivu ya Chama Cha Mapinduzi mkandarasi apatikane haraka ili wananchi wa Mkoa wa Simiyu tuweze kupata maji ya Ziwa Victoria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanachi wa Mkoa wa Simiyu ni wakulima wazuri, maji yale yakifika tutalima kilimo cha umwagiliaji kwa mazao ya mbogamboga, mazao ya biashara na mazao ya chakula. Sasa, tukipata mazao ya chakula tuta-supply hata mikoa ya Jirani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Sera ya Serikali ni kuwa na uwanja wa ndege kila mkoa kwa maana hiyo na Mkoa wa Simiyu tutapata uwanja wa ndege na eneo tumeshatenga. Kwa hiyo tutalima mbogomboga, cabage biringanya pilipili hoho nyanya tutasafirisha na kuuza nchi za nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Simiyu ni miongoni mwa mikoa tisa iliyo hatarini kukumbwa na janga. Kama tutapata Maji ya Ziwa Victoria yatatusaidia sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Simiyu ni mkoa wa wafugaji, tuna ng’ombe milioni mbili tuna mbuzi zaidi ya milioni nne tuna Kondoo zaidi ya milioni tatu, tuna bata na kuku pia. Wanyama wote hao wanahitaji maji; na maji ni uhai. Wanyama hawa wakipata maji watazaliana lakini vilevile na wafugaji watapata utajiri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeza Serikali kwa Wilaya ya Meatu Kata ya Mwanuzi ambayo ilikuwa na shida sana ya maji, ilikuwa inakunywa maji ya tope, maji meusi ambayo yalikuwa yamechanganyika na tope lakini. Sasa hivi Serikali imejitahidi toka mradi ule ukamilike sasa hivi maji ya Meatu ni mazuri na ni meupe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo la maji Meatu kukatikatika linasababishwa na kukatikatika kwa umeme. Ombi kubwa kwa Mkoa wa Simiyu kitu tunachokiomba Serikali itusaidie ni kutujengea kituo kile cha kupoza umeme ambacho kitasaidia sana. Vilevile miradi yote iliyoko sasa hivi Wilaya ya Meatu inayoendelea ikikamilika Wilaya ya Meatu itapunguza shida za maji kwa sababu itafikia asilimia 84.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwa mradi wa maji unaotoka Lamadi kwenda Mkula mradi huu umesaidia sana umegharibu bilioni mbili. Niiombe Serikali yangu sikivu, kuna vijiji viwili vimebaki kupitiwa na huo mradi ambavyo ni; Kijiji cha Chabutwa na Kijiji cha Mwanale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu, kuna Kata ya Nyaluande vijiji vyote vitatu havijapata maji. Vijiji hivyo ni Nyaluande yenyewe Mwagindi na Mwamkale. Pia Kata ya Igalukiro ina changamoto kubwa ya maji Kijiji cha Runala na Mwamagigisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naendelea kuiomba Serikali yangu Sikivu, Wilaya ya Bariadi Kata za Sima, Gudui na Isanga kuna shida sana ya maji. Naomba Serikali ibaini mitaa yenye shida sana ya maji ili iweze kutupatia maji. Lakini vilevile naendelea kuipongeza Serikali kwa ajili ya Wilaya ya Itilima ambako tuna miradi mingi inayoendelea iliyokamilika. Hata hivyo, kuna Kata ya Kinamweri ina tatizo sana la maji. Naiomba Serikali itusaidie.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie hapa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante, muda wako umekwisha Mheshimiwa.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa nakupongeza wewe kwa kazi nzuri unazozifanya. Ni ukweli usiopingika wewe ni kichwa, unafanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais, Mama yetu kipenzi Dkt. Samia Suluhu kwa kazi nzuri anazozifanya. Waheshimiwa Wabunge ni ukweli usiopingika Mheshimiwa Rais anahangaika sana huku nahuku kutafuta pesa, ana uchungu na nchi yake, anataka nchi yake ipate maendeleo mapema. Mama ni mama tu, mama tuko nyuma yako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Angela Kairuki, pamoja na Manaibu kwa kazi nzuri wanazozifanya, lakini pia nawapongeza Mawaziri wote wakiongozwa na jembe Mheshimiwa Jenista Mhagama na Manaibu Waziri kwa kazi nzuri wanazozifanya. Nampongeza mkuu wetu wa Mkoa, Yahya Dhewanda, anafanya kazi vizuri, anasimamia pesa za maendeleo, anazunguka huku na huku, majimbo yote anafanya ziara anasikiliza kero za wananchi na kutatua kero za wananchi. Simiyu tunapaa hatutembei, Mheshimiwa mkuu wa Mkoa unafanya kazi vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kutupatia pesa Wilaya ya Itilima kujenga hospitali ya Wilaya, zaidi ya bilioni nne. Haitoshi, wakatupatia milioni 800 kununua vifaa tiba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika hospitali ya Wilaya ya Itilima hakuna uzio. Hospitali ya Wilaya ikikosa uzio ni hatari sana. Mtu anaweza akatokea popote pale kuivamia hospitali na hospitali ile ina wodi nzuri za kisasa na vifaa vyote vipo, wananchi wanalazwa pale. Ni mbaya sana, tunaiomba Serikali itupatie pesa tuweze kujenga uzio. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali itujengee ma-corridor ya kupitisha wagonjwa. Hospitali ya Itilima haina corridor za kupitisha wagongwa. Vilevile hatuna generator, pindi umeme ukikatika upasuaji hauwezi ukaendelea. Tunaomba Serikali ibaini hospitali zote za Wilaya nchi nzima ambazo hazina generator iweze kununua generator. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Hospitali yetu ya Wilaya ya Itilima kuna mortuary, hatuna fridge. Tunaiomba Serikali itununulie fridge ya mortuary. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini tunaomba tujengewe mashine ya kufulia, hatuna jengo la mashine ya kufulia. Wilaya ya Itilima hiyohiyo ina zahanati kumi, ina vifaa vyote, lakini haina watumishi. Tunaomba Serikali ituletee watumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na mama yetu kipenzi, Mama Samia Suluhu, imetupatia zaidi ya bilioni tatu kujenga hospitali ya Busega. Busega tuna vituo vya afya, Kituo cha Afya cha Mkula kina upungufu wa maabara, wodi na nyumba za watumishi. Kituo cha Afya cha Kasamo kina upungufu wa wodi na nyumba za watumishi. Kituo cha Afya cha Badugu kina upungudu wa maabara na nyumba za watumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile naendele na pongezi za hospitali ya wiyala. Naendelea na pongezi za hospitali za Wilaya kwa sababu gani, hospitali za Wilaya zimesaidia watu sana. Sisi Mkoa wa Simiyu tulikuwa na hospitali moja ambayo ni Somanda tu, hizi zote ni hospitali mpya, naipongeza Serikali kwa kutoa zaidi ya bilioni tatu kujenga hospitali ya Wilaya Bariadi iDC. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Bariadi tuna hospitali kongwe ambayo ni Somanda, ni ya kwanza kabisa katika Mkoa wa Simiyu, lakini haina jengo la dharura. Tunaomba Serikali itupatie pesa ili tuweze kujenga jengo la dharura na kuna vituo vya afya Ng’wang’wali na Ngulyati hawana vifaa tiba tunaomba Serikali ituletee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niendelee na pongezi kwa Maswa. Naipongeza Serikali kwa kuendelea kuboresha hospitali ya Maswa. Hospitali ya Maswa imeboreshwa, ina wodi zote, tumejengewa theatre na tumejengewa jengo la dharura. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ombi kwa Maswa kuna zahanati nne hazina watumishi, tunaomba Serikali itupatie watumishi. Kuna kituo cha afya cha Mwasai kimekamilika, lakini hakina wodi na jengo la mama na mtoto tunaomba liweze kukamilishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa hospitali ya Wilaya ya Meatu imeendelea kuiboresha. Kuna ombi Wilaya ya Meatu, kuna kituo cha afya cga Mwandoya, ni kikubwa sana, ukikiona hivi unaweza ukafikiria kwamba, ni hospitali ya Wilaya, kinahudumia watu zaidi ya laki moja. Naiomba Serikali kituo hicho kiweze kupandishwa hadhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, elimu, namshukuru Mheshimiwa Rais wangu kwa kutoa pesa kujenga madarasa, nchi nzima amejenga madarasa. Mheshimiwa Rais kwa kazi hii ya kujenga madarasa na kuboresha madarasa mazuri yana vigae na madawati mazuri, hao wanafunzi wanaosoma shule hiyo nakwambia wanafunzi hawa hawawezi wakamsahau Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Kengele ya pili imegonga. Sekunde 30, unaomba?

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ombi langu naomba shule za kata za sekondari waweze kujenga mabweni…

SPIKA: Waheshimiwa mnaotembea mbele ya mchangiaji mketi. Subiri kwanza, eenhee, haya endelea. Malizia hizo sekunde 30.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, lakini vilevile naomba tuweze kuongezewa watumishi, tuna upungufu mkubwa wa watumishi Mkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia. Kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais kwa dhamira yake ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani. Pili, nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu; Waheshimiwa Wabunge ni ukweli usiopingika Waziri Mkuu anazunguka nchi nzima kukagua miradi ya maendeleo. Nampongeza sana Mungu ambariki. Tatu, nampongeza Waziri Mheshimiwa Aweso pamoja na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanazozifanya. Wizara ya Maji wanafanya kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali yangu kwa kutuletea miradi mingi midogo midogo ya maji, nashukuru sana. Wilaya ya Maswa kuna Mradi wa Chujio, Kata ya Zanzui umegharimu bilioni tatu. Naishukuru sana Serikali, lakini pia naishukuru Serikali kwa kutuletea tenki la maji Maswa Mjini. Watu wa Maswa Mjini wanakunywa maji mazuri, safi na salama sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi langu kwa Maswa, kuna Vijiji vya Mwamashindike, Budekwa, Mwabalaturu na Busilili, kuna changamoto sana ya maji. Naiomba Serikali ituchimbie visima. Nasema hivyo kwa sababu gani, juzi tu Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mkoa wa Simiyu amezindua gari la kuchimba visima, hicho ni kishindo cha Mama Samia Suluhu. Naomba hilo gari liweze kutuchimbia visima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Busega naipongeza Serikali, Kata ya Mukura kuna mradi mkubwa wa bilioni 2.7, naipongeza sana. Kata ya Kabita kuna mradi unaendelea kujengwa na Serikali, tumeanzia bilioni sita naipongeza sana Serikali. Ombi langu kwa Busega, naomba Kata ya Shigala na Igalukilo kuna shida kubwa sana ya maji, naomba Serikali iweze kutuchimbia visima virefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naenda Kata ya Bariadi. Naipongeza sana Serikali kwa Mradi mkubwa wa Maji wa Ngulyati, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameuzindua juzi, umegharimu bilioni 1.3, naipongeza sana Serikali kwa hilo. Watu wa Kata ya Ngulyati wanaishukuru sana Serikali, wamenituma, sasa hivi hawana shida ya maji tena, wenyewe sasa hivi wanatafuta pesa tu hawana shida na maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi kwa Bariadi, naomba kuna changamoto kubwa Kata ya Sapiwi, Kata ya Sakwe, Kata ya Lukindwabiye, Kata ya Mwasuguya na Kata ya Likungulyabashashi. Tunaomba waweze kuchimbiwa visima kwa sababu, muda mwingi wanaupoteza kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Itilima, naipongeza sana Serikali kwa Mradi wa Gangabiriri, ni mradi mkubwa na ni mradi mzuri, lakini Wilaya ya Itilima, Gangabiriri ni Makao Makuu, Wilaya inaendelea kupanuka, naiomba Serikali ituongezee tenki, lakini vilevile naomba Serikali ichimbe kisima kirefu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Serikali iweze kufanya ukarabati katika mabwawa; la kwanza, Noghbora, Mwamapalala, Sawida, Habia na Nkoma. Nikija Wilaya ya Meatu, kuna Bwawa la Mwanjoro limepasuka na halijaanza kufanya kazi, naiomba Serikali iweze kukarabati. Bwawa hilo likikamilika litahudumia vijiji vitano. Mheshimiwa Aweso ananisikia, Meatu kuna ukame mkubwa sana, naomba ajitahidi ikiwezekana Meatu kila tarafa wachimbe bwawa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naendelea kuipongeza Serikali yangu kwa mradi mkubwa wa maji. Mheshimiwa Waziri ametupa matumaini na namshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kwa kutoa zaidi ya bilioni 444 kwa ajili ya Mradi wa Ziwa Victoria, ahsante sana mama kuwajali wanawake. Wanawake wa Mkoa wa Simiyu muda mwingi walikuwa wanaupoteza kutafuta maji kuliko kufanya kazi za maendeleo. Mama suluhisho la ukame Mkoa wa Simiyu ni Mradi wa Ziwa Viktoria, hongera sana mama yangu. Hicho ndio kishindo cha Mama Samia Suluhu, nani kama mama? (Makofi)

WABUNGE FULANI: Hakuna.

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba sasa Mheshimiwa Waziri, akija hapa kutoa majibu, aniambie mradi huo unaanza lini? Kwa sababu, maeneo ambayo mradi unapita tayari fidia zimeshalipwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi wananchi wa Mkoa wa Simiyu sio wavivu, ni wakulima wazuri na ni wachapakazi. Maji yale yakifika tutalima kilimo cha umwagiliaji, tutalima mbogamboga, tutalima michicha, tutalima kabichi, tutalima bilinganya, tutalima nyanya, tutalima vitunguu. Tutalima mazao ya chakula na tutalima mazao ya biashara, lakini vilevile tutasaidia na mikoa ya jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sera ya Serikali sasa hivi ni kuwa na uwanja wa ndege kila Mkoa. Nina imani na Simiyu utajengwa na eneo tayari tumeshatenga, tutauza mbogamboga zetu na nje ya nchi. Tutauza mbogamboga zetu Dar-es-Salaam, Mbeya na kila sehemu watakula mboga za kutoka Simiyu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo nashukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya
MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuongea, kwanza kabisa nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anazozifanya anaboresha miundombinu ya afya.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais amejenga zahanati, vituo vya afya, hospitali za wilaya na hospitali za mkoa. Mheshimiwa Rais amefanya kazi nzuri, Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan hayuko tayari watu wake wafe kwa kukosa matibabu. Mama yupo vizuri tunampongeza sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, cha kwanza hapa duniani ni afya, bila afya hata ukiwa na mamilioni ya pesa haisaidii. Tunampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuboresha afya ndio maana vifo vya mama na watoto vimepungua.

Nampongeza Mheshimiwa Waziri Ummy na Naibu wake kwa nzuri wanazozifanya. Mheshimiwa Waziri anafanya kazi nzuri, hotuba yake ni nzuri, namjua yeye ni mchapakazi, nina imani atasimamia hotuba yake ambayo imesheheni matumaini ya Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea na pongezi kwa Mheshimiwa Rais kwa kuboresha Hospitali ya Muhimbili. Hospitali ya Muhimbili, sasa hivi inafanya operesheni ya kichwa, inapandikiza figo, inafanya operesheni ya moyo. Hata wagonjwa kutoka nchi za nje wanakuja kutibiwa. Hiyo ni kazi ya Mheshimiwa Samia Suluhu, Mama yetu ametuheshimisha, tuko vizuri Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuboresha huduma ya matibabu ya kansa Bungando. Mwaka juzi tulisimama hapa Wabunge wa Kanda ya Ziwa tukaomba matibabu ya kansa yasogezwe Bugando kwa sababu wagonjwa wengi wa kansa wanatoka Kanda ya Ziwa. Mheshimiwa Rais alisikia kilio chetu sasa hivi matibabu yanatolewa hapo karibu, hawawezi kuhangaika tena kwenda Dar es Salaam kutibiwa. naishukuru Serikali kwa kuanzisha utafiti wa kuweza kujua ugonjwa wa kansa unasababishwa na nini Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea na pongezi kwa Serikali imetujengea hospitali ya mkoa, lakini pia tuna jengo la mama na mtoto, Mheshimiwa Ummy analifahamu yeye ni mwanzilishi. Bajeti yake ni bilioni 5.7, jengo hilo limefikia asilimia 85. Tunamwomba Mheshimiwa Ummy akija kutoa majibu hapa, atupatie bilioni 1.7 ili tuweze kukamilisha hilo jengo la ghorofa na ni zuri la kisasa. Hiyo ni kazi ya Mama Samia Suluhu, hongera sana Mama yangu kwa kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naendelea na pongezi kwa majengo yafuatayo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imetujengea jengo la kutakasia vifaa, ufuaji wa nguo, nyumba mbili za watumishi, nyingine ni three in one, lakini pia katika hospitali yetu hiyo tumeletewa CT scan. Tulikuwa tunahangaika na kipimo hicho, watu wa Mkoa wa Simiyu walikuwa wanaenda kupata hicho kipimo Mwanza, lakini sasa hivi wanapata Mkoani Simiyu, hiyo ni kazi ya Mama Samia Suluhu, Mama yuko kazini. Ahsante sana Mama kwa kazi nzuri kwa kujalia afya za watu wako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ombi, hospitali yetu ya mkoa haina uzio kabisa na mwaka jana nilisimama nikasema hospitali haina uzio. Upande wa kushoto tumepakana na mlima, upande wa kulia tumepakana na barabara ya lami. Mlimani kuna vichaka vichaka, hospitali ikikosa uzio, utoroshwaji wa vifaa tiba na madawa ni rahisi sana. Mtu anaweza akasomba akaenda kuficha mlimani, halafu baadaye usiku anavisafirisha. Pia na hospitalini wanaenda wagonjwa wa aina mbalimbali. Kuna mwingine anaweza akaenda amechanganyikiwa wa afya ya akili akakimbilia barabara akagongwa gari. Naomba Serikali itujengee uzio, Mheshimiwa Ummy mtani wangu ameinisikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia hospitali hiyo hiyo haina wodi za kulaza wagonjwa. Hatuna wodi ya wanaume, hatuna wodi ya wanawake na hatuna wodi ya watoto. Naiomba Serikali iweze kutujengea halafu na jengo la bima. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, eneo la hospitali ya mkoa halijapimwa, halina hati. Naiomba Serikali iweze kupima eneo hilo halafu iweze kutupatia hati miliki. Katika hospitali yetu ya mkoa tuna upungufu wa watumishi. Watumishi walipo ni 231, upungufu wa watumishi 437, specialist wa nne, specialist wanaohitajika 21, Wauguzi waliopo 102 upungufu 97, upungufu wa Madaktari 27, upungufu wa Wafamasia 12. Tunaomba Serikali ituletee watumishi wa kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niendelee kumpongeza Rais wetu katika hospitali zetu za wilaya ametuletea X-Ray. Kama unakumbuka nilisimama hapa mwaka jana nikaomba X-Ray kila wilaya. Sasa hivi Serikali yetu ni sikivu imeshaleta X-Ray, hata kama mtu akipata ajali sasa hivi hawezi akakimbia kwa waganga wa kienyeji, atatibiwa hapo hapo, matatizo yatagundulika mapema. Ila naomba sasa wataalam wa mionzi hatuna. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, tuna Hospitali ya Somanda wakati hospitali ya mkoa hawajaanza kujenga ile hospitali ilipandishwa hadhi ikawa hospitali teule ya mkoa. Hiyo hospitali ni ya muda mrefu, majengo yamechakaa, tunaomba pesa ili yale majengo yaweze kukarabatiwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)