Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Stanslaus Haroon Nyongo (39 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante sana. Kama ulivyonitaja mimi naitwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki. Kwanza kabisa naomba nitoe shukrani za dhati kabisa kwa wananchi wa Wilaya Maswa na hasa Jimbo la Maswa Mashariki, kwa kuikomboa Wilaya yetu kutoka Upinzani wa Majimbo mawili, Maswa Mashariki na Magharibi. Wametupa kura nyingi, mimi na mwenzangu wa upande wa Magharibi, tumemuondoa Shibuda na Kasulumbayi aliyekuwa anajiita Yesu kwa kura nyingi ambazo hata kwenda Mahakamani walikata tamaa. Tumeshinda vizuri kwa kishindo na napenda kusema kwamba hata kura za Magufuli, Mheshimiwa Rais wetu, tumempa kura nyingi sana Wilaya yetu ya Maswa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa napenda kuungana na wenzangu wengi walivyoongea kuunga mkono hotuba nzuri kabisa ya Mheshimiwa Rais, aliyoitoa tarehe 20 Novemba, hotuba hii ilikuwa imesheheni maudhui ambayo Watanzania walipenda wayasikie. Kero zilizokuwepo, ambazo zilikuwa ni wimbo kwa wenzetu wa upinzani, ndani ya hotuba ya tarehe 20 Novemba ya Mheshimiwa John Pombe Magufuli ilitoa majibu kwa kero zote zilizokuwa zinatukabili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hotuba hii ukiitazama kwa undani, ilikuwa imegawanyika katika sehemu kubwa mbili, lakini katikati kuna kiungo.
Sehemu ya kwanza ya hotuba hii ilikuwa ni matumizi makubwa, kwa maana ya ahadi zilizotolewa na Mheshimiwa Rais na ahadi zilizomo ndani ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambayo tumeitumia kuinadi kwa wananchi na wakatuamini wakatupa Kura nyingi. Ahadi ni nyingi ambazo zimegusa matatizo ya wananchi wa Tanzania. Ukitizama kwa upande huo, kweli kabisa kuna matumizi makubwa ambayo yanahitaji pesa nyingi kuhakikisha ahadi hizi zinakamilika na wananchi wanapata yale mabayo tuliwaahidi. Katika hotuba hii ya Meshimiwa Rais John Pombe Magufuli, upande wa pili wa hotuba unaonyesha ni jinsi gani tutapata pesa hizo, ni mikakati gani iliyopo, Serikali inaunda mikakati ipi kuhakikisha pesa zile zinapatikana na pesa zikipatikana basi ahadi hizi ziweze kukamilika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katikati ya mapato na matumizi kuna barriers ambazo zinafanya matumizi haya yasiweze kukamilika iwapo majipu aliyoyasema Mheshimiwa Rais yataendelea kuwepo. Majipu haya ndicho chanzo au kikwazo cha mapato makubwa ya nchi yetu. Jipu la kwanza alisema rushwa, jipu la pili alizungumzia mfumo mbovu, jipu la tatu akazungumza sheria mbovu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ukubali, katika mwili wa binadamu kweli anaweza akapata majipu, kwa tukisema majipu tunazungumzia mwili wa binadamu, kuna majipu mazuri, yamekaa sehemu nzuri, mtu anaweza kavaa shati mwingine asione, lakini kuna majipu mengine yamekaa sehemu mbaya. Na kuna majipu mengine yamekaa usoni, lakini majipu mabaya ndiyo yanayoharibu hata mwenendo wa binadamu kutembea, badala ya kutembea kawaida unatembea kama bata. Mojawapo ni hili jipu la Sheria ya Ununuzi. Ukienda katika Halmashauri nyingi kuna magari hayatembei, bado mazima eti kwa sababu ya Sheria ya Ununuzi. Kipuri hakinunuliwi kwa sababu ya Sheria ya Ununuzi. Tunashukuru Mheshimiwa Rais alisema hili litakuja Bungeni, Wabunge tumsaidie na mimi ninapenda kusema kwamba Wabunge tuwe tayari kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais kutengua sheria hii na kuirekebisha kwa manufaa ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hicho ni kiungo. Tukianza na matumizi, kuna matumizi makubwa, kuna ahadi kubwa, hizi lazima zitekelezwe na hakuna mjadala. Issue hapa ni kutafuta pesa, Serikali itumie mbinu kuweza kuhakikisha kwamba tunapata pesa, tunakusanya pesa za kutosha ili tuweze kukamilisha ahadi hizo. Sasa pesa itapatikana vipi? Ndipo tunarudi kule kule kusema kwamba kama tumeamua kuwekeza kwenye viwanda, tumeamua kuwekeza kwenye kilimo ni lazima tutengeneze miundombinu, miundombinu ambayo itakuwa ni friendly ku-invest kwenye kilimo, friendly ku-invest kwenye viwanda. Tuwe na miundombinu ambayo itafanya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali zinazotumika kila siku. Bidhaa kama toothpick, tissue paper, napkins, bidhaa ndogo ndogo ambazo kila siku zinatumika, tuna-import kutoka nchi za nje, basi iundwe miundombinu kuhakikisha kwamba na sisi tunaweza kufanya production kwa cheap cost ili tuweze kuingia kwenye competition ambayo itamfanya mwananchi wa kawaida aweze kununua bidhaa zetu, aache kununua bidhaa za nje.
Kwa mfano, ukitazama General Tyre. General Tyre kumbe ilizimwa tu, ilizimwa kwa sababu production cost ya General Tyre ilikuwa ni kubwa. Uki-produce tairi moja la General Tyre gharama yake ni sawa sawa na tairi nne za kutoka Malaysia. Wana-produce kwa cost ndogo, malighafi wanazo za kutosha, ile production in technology ni simple inafanya tairi inakuwa produced kwa low cost, matokeo yake inatoka nje kwenye market inakuwa competitive kwa sababu wananchi watanunua kwa bei nafuu. Lakini kwa sasa hivi technology ya General Tyre, ukifyatua tairi moja tairi lile linakuja kuuzwa laki nne halafu muuzaji ambaye ni mjasiriamali anayeuza matairi ana tairi lingine la kutoka Malaysia linauzwa shilingi 80,000/=. Lazima mwananchi atanunua tairi ya Malaysia ataacha tairi ya General Tyre.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Serikali ya John Pombe Magufuli, kwa kushirikiana na Mawaziri wake, Mheshimiwa Muhongo tupelekee umeme, tutengeneze barabara hata kama ni kwa kukopa, tupelekeeni maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisiendelee kuongea hayo, lakini naomba niongelee kuhusu Maswa. Maswa ni Wilaya kongwe, Wilaya ya siku nyingi. Tumeomba siku nyingi tupandishiwe hadhi ya kuwa Halmashauri ya Mji kutoka Halmashauri ya Mji Mdogo, haijapandishwa. Tunaomba tupandishiwe Halmashauri ya Maswa iwe Halmashauri ya Mji. Kuna faida ya Halmashauri kuwa ya Mji, tunaomba Halmashauri ya Mji wa Maswa. Tunaomba kilometa tatu za ahadi ya Mheshimiwa Rais alizoahidi Maswa, Waziri mhusika tunaomba Maswa mtupe kilometa tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ziwa Victoria lipo karibu na sisi, leo nimesikia majibu ya Mheshimiwa Waziri hapa, eti tunahitaji pesa katika mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria, tunahitaji zaidi ya bilioni 730 na zaidi, ambazo ni sawa sawa na Euro milioni 331. Pesa zinazotafutwa ni za wafadhili. Sijaona sehemu Serikali inasema ina mkakati wowote wa kutafuta pesa hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Mheshimiwa Waziri mchakato wa kuleta maji Maswa ufanyike haraka iwezekanavyo. Mtuletee maji katika Wilaya zetu zote za Mkoa wa Simiyu, na wewe ni shahidi unatoka Mkoa wa Simiyu, hatuna maji Mkoa ule, tunaomba mtuletee mitambo ya maji haraka iwezekanavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kuchukua nafasi hii, kwa sababu tunakwenda kwenye viwanda, Mkoa wa Simiyu unazalisha mazao yanayotokana na mifugo. Tunaomba wawekezaji waje, kuna ngozi tunauza, ngozi ya ng‟ombe inatupwa kwenye mnada ng‟ombe wakishachinjwa ngozi inatupwa, inauzwa shilingi 1,000 au shilingi 800 wakati ngozi moja ya ng‟ombe inatoa mikanda ya kiuno 50. Mkanda mmoja wa kiuno tunanunua shilingi 50,000 madukani, ng‟ombe mmoja anatoa mikanda 50, ni sawa sawa na shilingi milioni moja, lakini ngozi ile inatupwa kwenye minada yetu na ikiuzwa inauzwa shilingi 800/=, it is a shame. Ngozi ya mbuzi inauzwa shilingi 200/=. Sisi tukichinja mbuzi Mkoa wa Simiyu ngozi ya mbuzi tunatupa kule haina thamani yoyote. Tunaomba mtuletee viwanda vidogo, wawekezaji karibuni Maswa. Zaidi ya hapo naunga mkono hoja, ahsante sana kwa kunisikiliza. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi nichangie katika Wizara hii ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya yote, kwanza naomba nitoe shukrani zangu za dhati kabisa kwa Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi kwa kunipigia kura nyingi sana katika kugombea nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Nawashukuru sana kwa kunipa kura nyingi na naahidi nitawafanyia kazi, sitawaangusha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nichukue nafasi hii kwa ufupi nimpongeze mama yangu, Mheshimiwa Margaret Sitta kwa kazi nzuri aliyoifanya. Kwa kweli inadhihirisha wazi kwamba tunapokuwa na watu wazima basi mambo hayaharibiki. Tunamshukuru sana mama na akinamama wote kwa juhudi mlizozifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea labda nirekebishe wasemaji wenzangu waliomaliza kuongea sasa hivi, Mheshimiwa Anatropia aliyekaa sasa hivi alikuwa anajaribu kuongea kuhusu deni la EPZA. Ni kweli EPZA wanadaiwa kutoka shilingi bilioni 60 kwenda shilingi bilioni 190, ongezeko la deni hili si kama anavyosema ni kwa sababu ya inflation, hapana! Deni limepanda kwa sababu interest rate imepanda siyo inflation rate. Kutokulipa deni hili kunafanya interest inapanda matokeo yake ni kwamba leo EPZA wanashindwa kulipa deni hilo kwa sababu ya ucheleweshaji wa kupeleka pesa! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Serikali na mimi niungane naye, ipeleke pesa ilipe madeni ya EPZA waendelee ku-facilitate yale maeneo na wawekezaji waje wawekeze pale. Wananchi wanadai fidia zao mpaka leo hawajapewa pesa, deni linabaki kwa wale wenye maeneo wanadai, Serikali na yenyewe ongezeko la deni linaongezeka kutokana na interest rate. Kwa hiyo, tunaomba Serikali ifanye juhudi maalum kwa ajili ya kwenda kulipa deni hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimewahi kuchangia siku za nyuma kuhusu maendeleo ya viwanda lakini naendelea kusisitiza. Upande wa viwanda na hasa viwanda vidogo-vidogo, tunaomba Serikali iweke mkakati wa kutosha, tuna vijana wengi nchini wanamaliza vyuo, wanamaliza shule lakini hawana mitaji, wana ujuzi mbalimbali, hawana pa kuanzia! Wakienda benki interest inayotolewa ni kubwa ni more than 25%, ni 17% mpaka 25%! Ukienda kwenye commercial bank kwa mtu wa kawaida hawezi akakopesheka na hasa vijana wetu kwa sababu kwanza wanakosa collateral, inakuwa ni vigumu wao kupata mitaji.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba Serikali ije na mkakati maalum kwa vijana, iweze kutoa mikopo kupitia dirisha la TIB, mikopo maalum kwa ajili ya vijana, ikiwezekana wapunguziwe interest rate, yaani ile pesa ya riba, kutoka 25% inayotolewa na mabenki wapewe upendeleo maalum. Ikiwezekana wapewe 1% - 3% ili wakopesheke waweze kufanya kazi ya kuanzisha viwanda vidogovidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwenye masuala ya agro processing, tumezungumza vitu vingi sana kwamba tutaanzia na mazao yanayozalishwa na wakulima. Ni kweli, tuanze huko lakini kuna tatizo la kodi kero. Nami na-declare interest, tumezunguka kama Kamati ya Viwanda na Biashara tumekuta mfano, ukinunua alizeti kutoka Bariadi, Mkoa wa Simiyu kupeleka Singida kwa ajili ya kukamua pale Mkoa wa Simiyu anakutana na geti anatoa ushuru. Akifika Maswa anakutana na geti anatoa ushuru. Akifika Shinyanga anakutana na geti anatoa ushuru. Akifika Singida anakutana na geti anatoa ushuru, ndipo anapofikisha kwenye kiwanda. Huu ushuru mdogo mdogo unafanya production inakuwa ina-high cost, matokeo yake bidhaa unapoipeleka sokoni huwezi ku-compete na mtu anayeingiza mafuta ya kupikia kutoka nchi za nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kumbuka mafuta yanayoletwa hapa kutoka nchi za nje (crude oil) ina kodi ndogo sana. Sasa huyu mtu anayemnunua alizeti kwa ajili ya kukamua anakuwa ameingia gharama kubwa ya kulipa kodi ndogo ndogo. Hizo kodi wakati mwingine zinapokusanywa hazifiki mahali husika. Kwa hiyo, ni bora kodi hizi zingefutwa ikawezekana huyu mzalishaji ukampa kodi moja kubwa ya mapato kuliko kuingia gharama ya kulipa kodi ndogo ndogo na kero. Tunaomba hili suala lifanyiwe kazi kwa haraka kwa kweli ni kero kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine niliwahi kuongea nalisisitiza tena, tutafute mbegu bora, mbegu za kisasa ambazo zina mazao mengi. Kwa mfano, alizeti tunapata 70% tu ya ku-extract mafuta kama ukikamua, tunaomba mbegu bora. Ufanyike utafiti maalum kwa kuleta mbegu bora za uzalishaji kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo na Ufugaji. Mbegu zenyewe siyo za mazao tu, hata za mifugo, tunataka mbegu bora ili tuweze kuvuna mavuno bora. Tunasisitiza tena na hili liingie kwenye kumbukumbu na Serikali ifanye juhudi maalum kwa kazi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni suala la viwanda vinavyoajiri watu wengi na hasa viwanda vya nguo (textile). Ningekuwa naongea na Mheshimiwa John Pombe Magufuli leo ningemwambia katika mambo ambayo unatakiwa uyaanzishie Wizara ni Wizara ya Textile. Tungeanzisha Wizara au Idara Maalum kwa ajili ya Textile maana kwenye textile kuna mambo mengi, huwezi ku-produce shati bila kuweka vifungo. Huwezi ku-produce shati bila kuwa na material ya plastic, kuna vitu vidogovidogo vingi ambavyo vinaweza kwenda kutoa shati na suruali na vitu vingine. Tukiwa na Idara Maalum au Wizara Maalum basi itahakikisha sisi Tanzania tuna-specialise kwenye masuala ya textile tu. Pamba tunayo, watu tunao, maeneo tunayo, tuna uwezo wa kufanya production ya nguo kuliko nchi nyingine yoyote kwa East Africa na Bara zima la Afrika. Tunaomba hilo nalo lifanyiwe uangalizo maalum. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni Kiwanda cha Urafiki. Tulitembelea kiwanda hiki, 51% inakuwa owned na China na 49% ni Tanzania tunamiliki. Wachina hawafanyi production, capacity ya Urafiki ni kuzalisha mita za nguo milioni 30 kwa mwaka lakini production ya leo ni milioni tano kwa mwaka. Ukienda kwenye store ya Urafiki nje kuna magari yanasubiri production iishe ili wapakie kanga wapeleke Kariakoo. Ina maana demand is high, production is low. Wachina mkakati walionao siyo ku-modernize tena kile kiwanda, wanachotaka wao kufanya ni kuondoa kiwanda na kufanya iwe ni shopping mall, waweze ku-import product kutoka China, wapeleke ajira China, Tanzania tumelala. Mheshimiwa Waziri naomba kwa suala la Urafiki mtoe mkakati tusaidiane, nunueni hizo 2% za Urafiki ownership irudi Tanzania tuendeleze kile kiwanda tufanye production inayoeleweka.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la TANALEC, mwenzangu Mheshimiwa Anatropia kaliongea. Ukienda Kenya tulisoma tenda document za Kenya TANALEC wanafanya production ya transfoma lakini hakuna upendeleo wa nchi yetu kufanya TANALEC iweze ku-supply transfoma Tanzania. Wenzetu wa Kenya niliona tender form wanazotoa, wanatoa tenda za transfoma kwa vifaa vya umeme na wanatoa elekezo kwamba hii itajazwa na local manufacture tu. Sisi Sheria yetu ya PPRA inaangalia bei, turekebishe, TANALEC imekosa kazi kwa sababu ya sheria hii. Tulimwita Director General wa TANESCO akatuambia tunashindwa kununua TANALEC kwa sababu ya Sheria ya PPRA. Tunaomba sheria hii iletwe mapema tuirekebishe, tu-favor viwanda vyetu. Tunazungumzia viwanda halafu tenda tunapeleka India maana yake nini? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la uwekezaji, tunaomba zitoke special incentives kwa wawekezaji wanaokwenda kuwekeza mikoani. Sasa hivi eneo zuri la kuwekeza ni Dar es Salaam lakini limejaa, hakuna nafasi. Tunaomba watu wapewe incentive wakawekeze nje ya Dar es Salaam, wapewe special incentive.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa napenda kumpongeza Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa kuandaa hotuba nzuri sana yenye kuleta matumaini. Nawashukuruni sana na nawapa pongezi sana kwa kazi nzuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa niaba ya Mkoa wangu wa Simiyu na Wilaya yangu ya Maswa napenda niwapongeze Naibu Waziri pamoja na Waziri kwa kutembelea katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa. Kulikuwa kuna majengo mapya ya OPD na theater, nawashukuru jengo la OPD limeanza kufanya kazi baada ya kukamilika kwa muda mrefu, lakini lilikuwa halijaanza kufanya kazi. Kwa sasa wananchi wa Maswa wanapata huduma kupitia OPD mpya, nawashukuruni sana kwa hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda tu kuendelea kusema kwamba changamoto imebaki kwenye theater. Theater zimejengwa kubwa na nzuri, lakini hazina vifaa, madaktari ni wachache, tunaomba muendelee kuweka juhudi zenu basi theater ya pale Maswa ambayo ni theater kubwa na ya kisasa ianze kufanya kazi hasa tukizingatia kwamba Hospitali ya Wilaya ya Maswa ni tegemeo katika Mkoa wa Simiyu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu lingine katika Wilaya yangu hiyo ya Maswa ni kwamba hospitali hiyo basi ikiwezekana muipandishe hadhi kwa sababu ni hospitali ambayo ina vifaa vingi vya kutosha lakini haijapandishwa hadhi. Ki-capacity ni kubwa, tunaomba basi muangalie uwezekano wa kutuletea madaktari na vifaa vya kutosha ili iweze kutoa huduma zaidi katika Mkoa wetu wa Simiyu. Wagonjwa wengi wanaondoka katika Wilaya yetu ya Maswa na Mkoa wa Simiyu wanapokuwa referred katika Hospitali ya Rufaa wanakwenda Bugando. Ni mwendo mrefu, ni kilometa zaidi ya 120 wanakwenda kupata huduma kule. Basi naomba muweze kutusaidia hospitali hiyo muipandishe hadhi ili wananchi wangu wa Maswa waweze kupata huduma nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba vilevile nijadili bajeti. Bajeti ya Wizara ya Afya kwa kweli mimi bado inanisikitisha kwani ni ndogo. Kuna upungufu kweli wa shilingi bilioni 18 ukilinganisha na bajeti ya mwaka jana lakini kinachonipa moyo ni kwamba utekelezaji wa bajeti ya mwaka jana ulikuwa ni asilimia isiyofika 40 lakini nina hakika chini ya utawala wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli zimewekwa ceiling mpya, hizo ceiling mpya za kila Wizara nina hakika utekelezaji unaweza kwenda asilimia zaidi ya 80, hapo ndipo ninapopata matumaini makubwa. Tunaomba tushirikiane na Serikali hii tuweze kuhakikisha kwamba pesa zinakusanywa na utekelezaji wa kupeleka pesa katika Wizara ya Afya uwe wa kutosha na mambo yaweze kwenda vizuri kama ilivyopangwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wizara hii ya Afya kuna matatizo ya wazabuni. Kwa mfano, Chuo cha Uganga Wilaya ya Maswa, toka mwaka 2010 wazabuni wame-supply pale vyakula na bidhaa mbalimbali lakini hawajalipwa pesa zao. Kuna deni la shilingi milioni 270 na wazabuni wako 15, wengine wametaifishiwa mali zao na benki kwa sababu hawajalipwa pesa zao na benki zinawadai, kwa kweli wamebaki hohehahe kisa wamefanya biashara na Wizara ya Afya. Mimi nafikiri kufanya biashara na Wizara ya Afya siyo dhambi, ni vizuri mkawajali hawa watu mkawalipa madeni hayo. Pia sehemu zingine zote nchini wazabuni walipwe ili waweze kurudi kwenye kufanya biashara zao. Tunashirikiana na watu binafsi basi tusiwa-discourage kwa kutowalipa madeni hayo. Naomba mfanye juhudi ya kutosha muweze kuwalipa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine katika Wizara hii ni MSD. Nakubaliana kabisa na pande zote mbili ya Upinzani pamoja na Kamati ya Maendeleo ya Jamii, MSD wapelekewe pesa zao on time ili waweze kununua dawa na ku-supply. Kwa sababu tutaendelea kuwalaumu wakati kumbe Serikali na yenyewe inahusika kutokupeleka pesa zao kwa muda unaostahili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naomba niongelee kuhusu malipo ya madaktari. Madaktari wetu wanafanya kazi nzuri sana, wanapata shida kwa sababu wanafanya kazi, wanakwenda kwenye call zao lakini pesa haziji on time. Madaktari wengine wanadai pesa nyingi hawajalipwa mpaka leo.
Naomba Wizara iangalie uwezekano kwa mwaka huu wa fedha 2016/2017 muwalipe madaktari hawa. Madaktari hawa kwa kweli wanafanya kazi kubwa lakini malipo ni madogo, tushirikiane, tushikamane Mheshimiwa Waziri muwalipe madaktari pesa zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitaka kuwa frustrated nchi hii soma udaktari. Unasoma sana, unafanya kazi sana lakini malipo ni kidogo. Watu waliosoma mambo mengine unawakuta wanafanya vizuri tu na mambo yao ni mazuri, ukisoma udaktari inakuwa kama vile ni dhambi. Na-declare interest na mimi nilipitia huko huko, kwa kweli naomba muilee hii fani kwa sababu ni muhimu, ni fani ambayo huduma yake tunahitaji watu wote, kila mmoja hapa ni mgonjwa mtarajiwa na anakabiliwa na maradhi. Tunaomba mboreshe huduma za afya na muanzie kwa madaktari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kuzungumzia suala kuhusu mafunzo ya wafanyakazi, muongeze idadi za vyuo na kozi mbalimbali ambazo zinaweza ku-produce wafanyakazi wengi wa Wizara ya Afya. Mmepunguza tatizo kutoka asilimia 58 la upungufu wa wafanyakazi wa afya mpaka asilimia 51, bado haitoshi. Tunataka twende kwenye asilimia ndogo ya upungufu wa madaktari na wafanyakazi wa Wizara ya Afya. Tunaomba huduma iweze kuboreshwa na huwezi kuboresha huduma bila kuwa na wafanyakazi wengi wa kutosha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na ushauri wa Kamati kwamba Wizara hii ikiwezekana itenganishwe na TAMISEMI kwa sababu kunakuwa sasa na mlolongo ambao hauendi sawa. Unakuta madaktari walioajiriwa na Serikali Kuu na madaktari walioajiriwa na TAMISEMI wanagongana katika maslahi yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mfano mmoja japo siyo mzuri madaktari waligoma walikuwa wanataka mafao yao yalipwe na walikuwa wanataka walipwe stahili zao za kutosha, waligoma kutoa huduma ili kuisukuma Serikali ilete huduma. Hata hivyo, unapogoma wakati wafanyakazi au madaktari walioajiriwa na TAMISEMI wanaendelea na kazi ile impact ya kugoma inakuwa haipo, Serikali haiwasikilizi, mwisho wa siku Serikali inawagonganisha, inaonekana kama madaktari wanayumba au wanapishana. Wanayumba na kupishana kwa sababu wameajiriwa na waajiri wawili tofauti, huyu kaajiriwa na Serikali Kuu mwingine kaajiriwa na TAMISEMI. Wanapoungana pamoja kudai maslahi yao ya kutosha inashindikana kwa sababu wanakuwa na waajiri wawili tofauti.
Kwa hiyo, naomba hii Wizara ya Afya ishughulikie masuala yote ya afya pamoja na wafanyakazi wote wa afya kuanzia juu hadi ngazi ya chini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda vilevile kuongelea suala la huduma za afya. Mheshimiwa Waziri kwa kweli huduma za afya ni duni nchini kwetu. Ukitaka kujua nchi imeendelea ni pale unapopiga simu ya emergency uone muda wa waganga au gari la paramedical linavyokuja kutoa huduma. Ukienda nchi zilizoendelea ukipiga simu kuna dharura ni dakika tano tu hata haziishi unakuta huduma tayari imeshafika mlangoni. Nchini kwetu ni saa hata 24 unaweza ukapiga huduma haijafika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano mmoja wa ajali zinazotokea barabarani. Ikitokea ajali sasa hivi wanaokufa pale pale on the spot ni wachache sana wengi wa wanaokufa ni wale wanaokosa huduma ya afya. Mtu anapata bleeding kwa muda mrefu, anakata roho kwa sababu hakupata huduma ya afya ya haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri umefika wakati sasa Wizara iangalie uwezekano wa kuwa na unit inayoshughulikia emergency case. Tunapoteza wananchi wengi kwa sababu ya kukosa huduma ya haraka ya afya yaani huduma ya kwanza. Unapopata ajali labda upasuke kichwa au kifua hapo ndiyo unakufa on the spot lakini wengi wa wanaokufa ni kwa sababu wanakosa huduma ya mwanzo. Tunaomba hili suala Mheshimiwa ulitizame kwa kina ili uweze kulitafutia ufumbuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuunga mkono hoja, ahsante sana.
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa napenda nitoe shukrani kwa Wabunge wote waliotoa michango mizuri kabisa na ushauri mzuri. Vile vile nampongeza Mheshimiwa Waziri kwa uwasilishaji wake mzuri, napenda kusema kwamba naunga mkono hoja ya Mpango kwa asilimia mia moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mpango huu wa Pili kwa kweli ni Mpango mzuri iwapo utekelezaji angalau utafikia asilimia 50 au asilimia 80, tunajua inawezekana kwa namna moja au nyingine inaweza isiwe asilimia 100, lakini basi angalau ikiwa asilimia 80 tutakuwa tumekwenda mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango huu nizungumzie kidogo upande wa viwanda na maeneo mengine, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi tulipokuwa tunainadi wakati tunaomba kura kwa wananchi, tulisema kwamba tutajikita zaidi kwenye viwanda, tutaanzia kwenye viwanda vinavyotumia malighafi tunazozalisha nchini, kwa maana ya mazao yanayotokana na kilimo (Agro Processing Industry). (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika agro processing inabidi tujitahidi tujikite tufanye tafiti mbalimbali tuweze kutafuta mbegu zenye tija, kwa mfano, mbegu za alizeti tunazotumia kwa sasa ni mbegu za miaka ya nyuma, hakuna mkakati madhubuti wa kutafuta mbegu mpya ambazo zinaweza zikatoa mafuta mengi ya kutosha. Mbegu tunazozitumia sasa hivi ni mbegu ambazo tunapata mafuta kwa asilimia 60 mpaka asilimia 70, tunatakiwa tupate mbegu mpya, tafiti zifanyike, ili tuweze kupata mafuta mengi yanayotokana na mbegu tunazosindika nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mafuta ya alizeti tunapata asilimia 70 kumbe tungeweza kupata mbegu ambazo tunaweza tukapata mafuta asilimia 80 mpaka asilimia 90 tukipata mbegu bora, Mtanzania anayelima alizeti, anayelima pamba, atapata kipato kikubwa na mzalishaji au msindikaji wa mafuta atapata faida kubwa na tutapata mafuta mengi ambayo ni kwa gharama nafuu na tutakwenda kuyauza kwenye soko letu kwa gharama nafuu na vilevile tunapokwenda kwenye ushindani wa soko la Kimataifa basi tutauza kwa bei nzuri na bidhaa zetu za Tanzania zitaweza kuuzika katika masoko yote ya Afrika Mashariki na ya Kimataifa kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tulitangaza kwamba, tutajikita kwenye viwanda ambavyo vinazalisha au vinavyozalisha ajira kwa wingi. Viwanda vikubwa, kwa mfano viwanda vya textile (viwanda vya nguo), vinazalisha ajira kwa watu wengi. Unakuta kuna watu wengi wanafanya kazi ya kutengeneza nguo kwa mfano suruali au shati, kila mmoja ana kazi yake mmoja anapinda, mwingine anatengeneza tundu la kifungo, mwingine anafanya shughuli nyingine, kwa ujumla kunakuwa na ajira nyingi sana kwa Watanzania. Kwa hiyo, tutapata ajira kubwa, watu wataweza kufanya kazi, wataongeza kipato pia itaongeza uchumi wa nchi yetu. Kwa hiyo, tujikite kule tusisahau tuliyoahidi kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tujikite kwenye viwanda mama. Suala la Liganga na Mchuchuma, viwanda vinavyozalisha vyuma, viwanda vinavyozalisha nishati ya umeme, tujikite huko ili tuweze kupata umeme wa bei nafuu, tupate malighafi za bei nafuu na tuweze kuuza kwenye viwanda vidogovidogo hapa nchini, hapo tutaweza kujikwamua. Bila kufanya vile itakuwa ni tatizo kwa sababu hata wenye viwanda waliopo sasa hivi, wanaozalisha bidhaa mbalimbali, bidhaa nyingi tunadhani zinazalishwa nchini lakini ukichunguza kwa nyuma yake unakuta zinaingizwa kutoka nje ya nchi kama malighafi na malighafi zenyewe zinatozwa kodi kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, matokeo yake uzalishaji unakuwa ni wa gharama kubwa na uuzaji wa bidhaa unakuwa ni wa bei juu, tunashindwa kuingia kwenye ushindani kwa sababu bidhaa zetu ni za bei ya juu, tunakuta kwamba, bidhaa zetu haziuziki, zinazouzika ni za nje ya nchi na ndiyo maana uingizaji wa bidhaa za nje ni mkubwa kwa sababu bidhaa za nje zinauzwa kwa bei nafuu bidhaa zetu zinakuwa na bei ya juu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nizungumzie katika masuala ya Mkoa wangu wa Simiyu. Mkoa wa Simiyu ni mkoa wenye malighafi nyingi zinazotokana na kilimo, lakini Mkoa wa Simiyu ni Mkoa mpya, hatuna barabara. Ni miradi michache ya barabara ambayo tayari imeshaanzishwa, lakini utekelezaji ni mdogo.
Tunaomba Mkandarasi aliyeko site apewe pesa ili project iendelee, tutengenezewe barabara ya lami na tukishaunganisha Mkoa wetu wa Simiyu tukaweka kiwango cha lami kuunganisha na barabara ambazo zinakuja Dar-es-Salaam kuna uzalishaji mkubwa wa pamba ambapo marobota ya pamba yanayozalishwa katika Mkoa wa Simiyu yataweza kuja Dar-es-Salaam na kulisha viwanda vyetu vya textile na mambo yanaweza kuendelea na uchumi unaweza kuimarika zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ningependa kuongelea katika Mkoa huo wa Simiyu ni suala la mradi wa maji. Kuna mradi wa maji kutoka Ziwa Viktoria unaotakiwa kuleta maji katika Mkoa wa Simiyu, tunaomba utekelezaji wa mradi huu uharakishwe. Tunategemea maji mengi ya kutoka Ziwa Viktoria kwa matumizi ya aina mbili, kwa maana ya domestic use na vilevile tutumie maji kwa ajili ya irrigation. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mwanza ina mpunga wa kutosha. Tunaweza tukalima zaidi kwa maana ya kulima mpunga kwa chakula, tulime mpunga kwa maana ya zao la biashara. Sasa hivi duniani watumiaji wa zao la mpunga ni wengi wanazidi kuongezeka, waliokuwa wanaongoza ni wale watumiaji wa zao la ngano, sasa hivi zao la mpunga limeongezeka, watu wanatumia zaidi mchele, kidogo wanatumia na mahindi, lakini zao la mchele linatumika zaidi. Kwa hiyo, tujitoe katika zao la mchele kudhania ni zao la chakula, sasa tutambue mchele ni zao la biashara.
Mkituletea maji ya kutosha katika Mkoa wetu wa Simiyu, basi tuna hakika wakulima Mkoa wa Simiyu wataweza kulima mpunga kwa wingi na mpunga huo tutaweza kulisha kwa asilimia kubwa Tanzania nzima, tunaomba mradi huo utekelezwe mapema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo unahitaji pesa nyingi ambazo tuliambiwa kwamba, zimeshatolewa kiasi kidogo na feasibility study imeshafanyika. Tunaomba basi utekelezaji ufanyike mtuletee maji ya kutosha katika Mkoa wa Simiyu tuweze kulima, tuweze kulisha mifugo, tutumie maji yale kwa tija, ili tuweze kuleta maendeleo. Kuna Mikoa mingine ina ardhi kubwa kama Simiyu, lakini ardhi haitumiki kwa sababu hatujaweza ku-facilitate ardhi yetu itumike. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili tuweze kusonga mbele kuna suala la rasilimali watu. Nchi yetu ina watu zaidi ya milioni 46, kuna vijana wengi hawana ajira, vijana wengi wako mtaani ambao kwa kweli tukiweza kuweka mazingira mazuri ile tunasema ni human resources ambayo inaweza ika-generate uchumi wetu ukakua kwa hali ya juu. Tumeshindwa kutafuta namna ya kutumia nguvu za vijana tulionao mjini. Ukienda mjini, ukienda vijijini unakuta vijana wanacheza mpira, wanacheza pool! Mheshimiwa Rais juzi kazuia pool! Wanacheza pool kwa sababu, hawana kazi ya kufanya, tuna nguvu kazi kubwa katika nchi yetu ya Tanzania lakini tunashindwa kutafuta namna ya kuitumia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mpango huu wa miaka mitano kwenda 2025 tutafute namna nzuri ya kuweza kutumia nguvu ya vijana wetu. Ukienda mjini vijana wanacheza mpira, mpira wenyewe wanacheza wengine wanavuta bangi, wako kwenye vijiwe hawana kazi ya kufanya! Tunaomba tuangalie na upande huu, tusiangalie tu vitu vingine, lakini tuangalie tutatumia vipi nguvukazi za hawa vijana kwa maana ya kunufaisha uchumi wa nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna jambo lingine ambalo ningeweza kuliongelea katika sekta binafsi, ili tuweze kuimarisha uchumi ni lazima tukumbuke sekta binafsi ndiyo sekta pekee inayoweza ikasaidia kuongeza au kufanya industrialization, twende kwenye nchi ya viwanda, bila sekta binafsi hatuwezi kufika. Tuweke mazingira mazuri kwa sekta binafsi, mazingira mazuri ambayo yatawawezesha watu wa sekta binafsi wafanye kazi zao vizuri, wafanye kazi zao kwa tija. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama kwa harakaharaka katika masuala ya kodi, ni lazima tuitazame vizuri. Kwa mfano, mtu anaingiza bidhaa kwa maana ya uzalishaji, anaingiza mashine kubwa za uzalishaji, ukifika pale anatozwa kodi ya VAT, mtu analeta mashine ya kuja kutengeneza ajira, analeta mashine kubwa ya uzalishaji, lakini katika importation unakuta anachajiwa VAT! VAT ina-discourage kabisa watu kuingiza bidhaa kwa ajili ya uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia VAT nchi zingine mtu anapo-import capital goods kwa maana ya kwenda kuzalisha hatozwi kodi! Nenda Msumbiji, nenda nchi zingine, hawatozwi hiyo kodi! Sasa asipotozwa hiyo kodi na Tanzania tunatoza, basi mwekezaji huyu hawezi kuwekeza Tanzania atakachokifanya ni kwenda nchi nyingine na kuwekeza na akiwekeza kule ata-create ajira kule, ata-create production kule ya tija, tunajikuta tunabaki palepale na Mpango wetu unabaki kwenye makaratasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tubadilike, twende mbele, tuangalie nini tuanze nacho na nini tumalize nacho, lakini tukienda kwa kubeba mambo yote tunaweza tukajikuta tunamaliza miaka mitano bado hatujafika kule tunakotakiwa kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme suala lingine kuhusu uwekezaji kwa maana ya uwekezaji wa nje na ndani. Tunayo TIC, tutazame TIC ijikite kwa kuwawezesha wawekezaji wa ndani waweze kuwekeza vizuri. Wawekezaji wa nje wanapokuja nchini kwetu na wao wanakutana na mazingira mabaya vilevile. Ukiangalia nchi yetu katika huu Mpango wa Serikali wa miaka mitano tumeweka katika namba mia moja thelathini na kitu! Ina maana kwamba, hatuna mazingira mazuri ya uwekezaji! Ni lazima tuangalie leo tunapoamua kuwekeza au kukaribisha wawekezaji tuangalie Central Government inasemaje na Local Government inasemaje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna conflict kati ya Central Government pamoja na Local Government, Central Government tunakaribisha mwekezaji, lakini mwekezaji akienda kule kijijini, akienda kuwekeza, akikutana na watu wa Serikali za Mitaa kule wanamuona mwekezaji kama ni adui. Mwekezaji anakutana na mazingira magumu, anafukuzwa na wakija watumbua majipu wananchi wakisema huyu mwekezaji hafai watu wa chini wanashangilia. Tunamwona kama mwekezaji ni mwizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunaomba itolewe elimu, mwekezaji atambulike kwamba huyu ni mwekezaji anakuja kwa faida ya nchi yetu, mwekezaji anakuja kutengeneza ajira, mwekezaji siyo mwizi. Elimu maalum itolewe watu watambue kama mwekezaji ni mwenzetu. Kinachoendelea sasa hivi wawekezaji wamekutana na mazingira magumu, unakuta watu wa NEMC wanasimamisha kiwanda huyu anachafua mazingira, kiwanda kinasimamishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisimamisha kiwanda palepale umesimamisha ajira ya watu walioajiriwa pale, ukisimamisha kiwanda production inasimama, huyu mtu ana-fixed cost unamwingiza kwenye gharama kubwa, unadhani kesho atakuja kuwekeza Tanzania? Tunaomba uwekwe utaratibu, elimu itolewe, kama ni watu wa NEMC wanakwenda kusimamisha viwanda visifanye kazi eti kwa sababu ya mazingira, basi hao watu wa NEMC wawe wameshatangulia kwenda kutoa elimu ya kutosha kumwelekeza mwekezaji ni namna gani ya kutunza mazingira ili tusiwe tunasimamisha production unnecessary kusema kwamba huyu mtu anaharibu mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie mazingira mazuri ya kumfanya huyu mtu aone kwamba kuwekeza Tanzania ni vyema, kuwekeza Tanzania utapata faida, hakuna anayewekeza bila kupata faida, lazima tuwawekee mazingira mazuri ya wao kupata faida na tuweke mazingira mazuri ya sisi kama Watanzania kupata faida, tuweke mazingira mazuri kwa vijana wetu kupata ajira kama Watanzania kupitia uwekezaji wa nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumalizia kwa kusema kwamba kuna tafiti mbalimbali za kibiashara zinafanyika, tunazibeza hatuzifanyii kazi. Ukienda kwenye Vyuo Vikuu kuna tafiti mbalimbali zinafanyika, yaani Marketing survey na marketing research, tafiti hizo ziweze kutumika. Wengine wanafanya tafiti kwa maana ya kupata degree zao, kuna wengine wanafanya tafiti kupata masters zao na wanafanya tafiti ambazo ni za kweli, wanakwenda field wanakusanya data za kutosha, wana-interpret zile data walizozipata kule na vilevile wanakuja na mapendekezo nini kifanyike. Tunaomba tutumie tafiti hizo tuweze kusonga mbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi nichangie katika hoja hii ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nitoe pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri unazofanya. Mheshimiwa Waziri vilevile nikupe pongezi kubwa kwa kupokea ushauri mzuri wa Mheshimiwa Juma Nkamia na sote kwa kusema kwamba Bunge lianzishe studio yake, hongera sana.
Napenda kutoa pongezi pia kwa Wizara hii kwamba katika vyombo vya habari Tanzania imeonekana kuwa ni nchi ambayo imeruhusu kuwa na vyombo vingi vya habari, hongereni sana kwa hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijaongea yote kwa mustakabali mzima wa Taifa kuhusu Wizara hii, nianze Mheshimiwa Waziri katika mkoa wangu wa Simiyu tuna Chuo cha Michezo cha Malya, tunaomba Chuo cha Michezo cha Malya kitengewe pesa kwa maana ya kukiendeleza. Tunatambua eneo la Kanda ya Ziwa pamoja na mkoa wangu wa Simiyu kuna vipaji vingi sana vya utamaduni pamoja na michezo ya mpira. Hivyo tunaomba chuo hicho kiongezewe zana pamoja na walimu kuweza kutoa elimu ya michezo katika mkoa wetu na kwa manufaa ya Taifa zima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mkoa wetu wa Simiyu ni mkoa mpya ambao tulikuwa tumeji-attach na mkoa wa Shinyanga kabla, tulikuwa tuna kiwanja chetu kama mkoa maana ya kiwanja cha Kambarage kilikuwa kinawakilisha mkoa japo ni kiwanja cha Chama chetu cha Mapinduzi, lakini sasa mkoa wetu hauna kiwanja! Katika pesa ya maendeleo niliyoona hapa sijaona eneo ambalo imetengwa pesa maalum kwa kuendeleza viwanja au kujenga viwanja! Kwa hiyo, tunaomba katika mkoa wa Simiyu Wizara itutizame kama mkoa mpya, mtuwekee kiwanja cha mpira na hasa mpira wa miguu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kutoa maoni au ushauri pia kwa Wizara hii. Upande wa mpira wa miguu au timu ya Taifa kwa maana ya Taifa Stars, Tanzania tunategemea sana tutengeneze timu ya Taifa kupitia timu za ligu kuu. Kutengeneza timu ya Taifa kupitia timu ya ligi kuu ni kitu kimoja kigumu sana, tujikite katika kuanzisha football academy, hii ndiyo njia pekee ambayo inaweza ikatusaidia kutengeneza timu ya Taifa na kuipeleka katika Kombe la Dunia, lakini tukisema tutegemee premier league, wachezaji kutoka Simba na Yanga itakuwa ni tatizo kubwa sana kutengeneza timu ya Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wenzetu Nigeria na Ivory Coast wameweza kutengeneza timu zao za Taifa vizuri, kwa kuwa na football academies za kutosha zinazofaa, zinawajenga vijana, zinajenga wachezaji wazuri ambao wanawakilisha timu hizo kwenda kwenye makombe mbalimbali Afrika pamoja na Kombe la Dunia. Tunaomba Wizara hii katika mkakati tuliouona hapa, haijatengwa pesa nzuri ya kuanzisha football academies. Ukienda pale TFF wana mkakati na mpango mkubwa sana wa kuanzisha au wa kuboresha hizi timu, lakini kwa kutumia premier league peke yake hatuwezi kutengeneza timu ya Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika premier league, unapokuwa na timu za premier league tubadilike sasa! Tunapokuwa na ligi yetu ambayo mara nyingi inafadhiliwa na Vodacom tunataka iwe ni ligi ambayo ni commercial, ligi ya kibiashara. Tunapoweka wachezaji katika hizi timu zinazocheza premier league, tunataka tucheze kibiashara kama wanavyofanya Uingereza na nchi nyingine. Tunataka ule mkakati wa kusema timu isajili wachezaji wasizidi watano kutoka nje, hii naomba niseme Mheshimiwa Waziri haifanani na bidhaa. Tuna-discourage bidhaa kuingizwa au ku-import bidhaa kutoka nje, lakini kwenye football ni kitu kingine. Kwenye football tunahitaji ku-import wachezaji ili waweze ku-inspire wachezaji wetu local wacheze kiushindani na wachezaji wetu ambao ni wachezaji wa ndani waweze kuwa inspired kucheza kwa kiwango cha Kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano ukitizama timu kama Azam, leo tunamwekea Azam limit asisajili zaidi ya wachezaji watano kutoka nje, wakati akitoka hapo anakwenda kucheza champions league ya Afrika, champions league ya Afrika ni biashara. Akishinda kwenye champions league ya Afrika tunaingiza pesa na sifa katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia TP Mazembe ya Congo imesajili wachezaji kutoka nje karibu kumi na kitu! Na wanaposhinda champions league ya Afrika sifa inakwenda Congo. Lakini sisi tunazuia na wachezaji wetu hawawezi kufikia kile kiwango tunapowapeleka kule kushindana na wale wachezaji wengine timu zetu zinakuwa ni kichwa cha mwendawazimu, zinafungwa zinarudi. Yanga sasa hivi wameenda juzi wamefungwa huko wamerudi, wameenda kuungana na yale mashindano ya timu ambazo hazijui na yenyewe tuwaombee Mungu, lakini hatuna mikakati ya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningependa kuchangia kwenye suala hili hili la michezo, kuhusu rushwa kwenye michezo. Rushwa imetawala kwa marefa, tunaomba Wizara kwa kushirikiana na TFF muangalie hili suala, kwa kweli rushwa ni hatari, PCCB ikiwezekana ihusishwe katika kupambana na rushwa kwenye michezo. Waamuzi wanasababisha timu zifungwe ambazo hazistahili kufungwa! Waamuzi wanaharibu mpira na kusababisha fujo wakati mwingine kwa sababu tayari wameshachukua mlungula mfukoni! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, unakuta referee anaamua ndivyo sivyo, matokeo yake timu nyingine zimezoea kununua mechi kwa sababu wamezoea kuhonga ma-referee, wanahonga hadi wachezaji, mechi zinapangwa matokeo, mnashinda humu Tanzania mnakuwa mabingwa mkitoka nje mnafungwa. Mnajisifu mnajua mpira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili litizamwe kwa upana wa kutosha. Mheshimiwa Waziri tunaomba mshirikiane na TFF mkomeshe rushwa kwenye michezo. Leo hapa Mheshimiwa Zitto katoa ushauri mzuri kwamba betting na hizi bahati nasibu ndizo zinazoendesha hizi ligi kubwa duniani, huwezi kuendesha ligi kubwa duniani wakati tayari michezo ina rushwa. Huwezi kufanya betting ya kwamba leo Simba atafungwa na Yanga wakati kuna watu wameshaamua Yanga ifungwe mezani au wengine wameamua Simba ifungwe mezani. Uamuzi umeshatoka mezani. Hiyo betting itaingiza pesa kiasi gani? Siwezi ku-bet mimi kwenye kitu ambacho kiko corrupt. Ndiyo maana betting za Uingereza zinakuwa na maana kwa sababu wamepunguza kiwango cha rushwa, watu kweli wanakaa wanaanza ku-bet. Wana-bet, wana-predict kutokana na kwa sababu michezo inayochezwa kule Uingereza na sehemu zingine ile hali ya rushwa haipo. Kwa hiyo, ndugu zangu mlitizame kwa kina suala la rushwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kuzungumzia pia ufadhili wa timu. Sasa hivi kwa mfano, kuna timu zimeshinda ubingwa wa mikoa, zimegawanywa Kanda mbalimbali, kwa mfano sisi kwetu kuna timu inatakiwa iende Kagera kufanya kambi kwa maana ya kuingia kwenye mashindano ya Kitaifa, hakuna ufadhili. Wabunge ndiyo tunaoombwa tuchangie pesa ya kupeleka zile timu kwenye Kanda. Hakuna mkakati wa Serikali na TFF wa kuzifadhili hizi timu ziende zikacheze. Matokeo yake Wabunge ndiyo mnaokamuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano, kuna ndugu yangu mmoja tulishirikiana naye alikuwa anafadhili timu, timu ikawa inafanya vizuri, vijana wanacheza, tunatoa pesa. Yule mfadhili mkubwa anatoa pesa timu inakwenda kucheza, ikafika kiwango pesa hamna, timu ina uwezo. Yule bwana ikabidi ahonge timu ifungwe ili irudi nyumbani kwa sababu watu hawachangii pesa kwenye michezo na hawaoni umuhimu wa kuchangia pesa kwenye michezo. Kwa hiyo, tunaomba elimu itolewe, tunaomba Serikali iwe na mkakati kabisa thabiti wa kuweza kuhakikisha tunaendeleza michezo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna suala la viwanja nimeliongea hapo mwanzo, hata hatujui tuwaombe TAMISEMI Tuombe kwenye Wizara! Nani anahusuka na viwanja? Tunaomba Wizara ishikilie hili suala, ishikilie michezo kuanzia kwenye shule ya msingi tusiachie TAMISEMI, tusiachie Wizara ya Elimu, mshikilie michezo kuanzia chini mpaka juu, kwa maana ya kuanzisha football academies na kusimamia michezo kwa ujumla, ili tuweze kutengeneza timu bora za michezo ya aina mbalimbali. Sasa hivi uwezo huo uko Jeshini tu.
Mheshimiwa Mwenyekiit, kumbuka zamani tulipata watu waliotuwakilisha Tanzania kwenye michezo ya Kimataifa wakaleta sifa akina Filbert Bayi, akina Juma Ikangaa, Samson Ramadhan, Iswege Christopher, Ndassa Mafuru, Samwel Mwang‟a, Hatii Shamba, Restituta Joseph, Hawa wote walitokana na Jeshi, lakini sisi kama Wizara tumeshindwa kutengeneza hawa watu. Ina maana Jeshi peke yake ndiyo lina uwezo wa kutengeneza hawa watu. Kwa hiyo, tunaomba tushirikiane, ili tuweze kutengeneza timu zetu pamoja na timu ya olyimpic.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. Nakushukuru mno kwa kunipa nafasi. Naunga mkono hoja, lakini marekebisho hayo naomba yasikilizwe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Azimio la Bunge Kuridhia Mkataba wa Kimataifa wa Udhibiti wa Matumizi ya Dawa na Mbinu za Kuongeza Nguvu Michezoni
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa napenda kutoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Waziri wa Michezo kwa kuleta Azimio hili hapa Bungeni. Napenda kusema kwamba tumechelewa sheria hii ilitakiwa tuipitishe mapema kwa sababu wachezaji wetu ndiyo waathirika wakubwa wa matumizi ya madawa haya.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ningependa kusisitiza pamoja na kwamba tunapitisha hili Azimio naungana na Serikali kwa maamuzi haya kwa asilimia mia moja kwamba tupitishe. Matumizi ya madawa haya ya kuongeza nguvu hayatofautiani kabisa na upangaji wa matokeo. Upangaji wa matokeo unasababishwa na mambo mengi. Kwanza watu wanapanga matokeo kwa maana ya kuangalia zile award zinazotolewa kwenye michezo. Nchi ambazo zimeendelea zimekuwa ni za kwanza kuathirika na matumizi haya kwa sababu ya kutaka kupanga matokeo, walikuwa wanapanga matokeo ili watu waweze kuneemeka kifedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama sasa hivi ni kwamba idara ya michezo yaani ndiyo inayolipa zaidi, ukitaka kuwa na kijana ambaye anaweza akaleta kipato kikubwa ni yule kijana anayecheza mpira kwa mfano au wanaokimbia riadha. Wale wanapewa kipato kikubwa sana na kipato hiki ndicho inakuwa ni motivation yaani inasabisha watu kutumia madawa ili kuweza kupanga matokeo. Kwa hiyo, matokeo yanapangwa mtu anapata ushindi usio wa halali, anapata ushindi ili aweze kujilimbikizia pesa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hii tunasema kwa Tanzania tulichelewa ilitakiwa tuwe tumeanza na watu wakajifunza na wakaelewa kwa ufasaha. Ni toka zamani ukiangalia mwaka 1968 Olympic ndiyo walianzisha lakini lilikuwa ni tatizo la muda mrefu, watu walikuwa wanatumia hata vyakula vingine vya kawaida ili aweze kuongeza nguvu waweze kupata performance kubwa katika michezo. Kulikuwa kuna uyoga ulikuwa unaitwa ni hallucinogenic mushroom, ilikuwa ni mushroom maalum kwa kuongeza nguvu. Watu walikuwa wanatumia hata hizi mbegu za ufuta ili waweze kuongeza performance waweze kupata kipato.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, kwa pamoja hapa napenda kusema kwamba, nashukuru sana hii sheria imeletwa tuipitishe, tuipitishe kwa maana ya kwamba tuungane na Umoja wa Kimataifa UNESCO, kwa maana ya kwamba Tanzania nayo itambulike ni nchi inayopingana na haya madawa ya kuongeza nguvu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tungekwenda mbali zaidi, tukiangalia kuna matumizi ya pombe, matumizi ya bangi. Tunashukuru Serikali inapambana na matumizi ya bangi, kwa kweli kuna vita vikubwa vinavyoendelea na masuala haya ya cocaine na vitu vingine. Tunashukuru Serikali inafanya kazi vizuri kupambana, lakini kuna tatizo la viroba! Viroba na lenyewe ni tatizo kubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tungeangalia namna ya kupiga marufuku viroba; viroba vipigwe marufuku kwa sababu na vyenyewe ni tatizo kubwa, kuna vijana wengi wanaathirika na viroba wanashindwa kucheza, wanastua kidogo kwa maana ya kuongeza nguvu lakini baada ya muda wana develop kwenye addiction, tunaharibu nguvu kazi ya Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli vijana ni wengi, nimezunguka baadhi ya maeneo tulikuta watu wanatumia viroba kwa kweli inasikitisha, viroba vinatumika sijui kwa sababu ni cheap, sijui ile packing iko flexible mtu ananunua anatia mfukoni, ni rahisi kununua kwenye vibanda, kwenye vioski vinauzwa viroba. Ukitazama watu wanatumia viroba kabla hawajaingia kucheza mpira au kukimbia riadha mtu anastua kidogo, anasema anaongeza nguvu, lakini baada ya muda anakwenda kwenye drug dependence au alcohol dependence, ana-develop addiction. Kwa hiyo, tunaomba Serikali nayo itazame kwenye viroba tupunguze matumizi ya viroba. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ningependa kuongelea, kwa sababu tunaongelea upangaji wa matokeo, kutumia hizi nguvu za ziada ni kwamba unapanga matokeo kwamba unakwenda kushinda. Kuna tatizo Mheshimiwa Waziri la rushwa kwenye michezo na lenyewe linapanga matokeo. Unakuta ma-referee kwenye mpira wa miguu wanapewa pesa ili kuweza kupanga matokeo, ina-demoralize kabisa. Ukienda kuangalia mpira unakuta refa akishapewa mlungula pasipokuwa na penalty yeye anatoa penalty, pasipokuwa na offside yeye anazuia kuna offside. Kwa kweli ina-discourage watu kucheza mpira, hata watazamaji ina-discourage kwa maana unaangalia wakati matokeo yameshapangwa, timu zetu kubwa Simba na Yanga zinashiriki kwenye kupanga matokeo, wachezaji wanapewa rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tuangalie ni namna gani ya kutengeneza sheria kuweza kuhakikisha kwamba tunaondoa kwa sababu upangaji wa matokeo kwa kweli ni tatizo na tulishasema mpira au michezo ni afya, michezo ni uchumi, michezo ni burudani. Kwa hiyo, tuangalie uhalisia wa michezo, tuilete michezo katika hali yake halisi. Mtu ashiriki ashinde kwa halali kama ni mkimbiaji wa riadha aweze kushiriki kwa halali. Tunaomba muangalie hayo mambo matatu ambayo ni viroba, rushwa na hili Azimio tulipitishe kwa faida ya Taifa letu na kwa dunia nzima.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili nami niweze kuchangia katika huu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2017/2018 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitoe pongezi kwa Mheshimiwa Waziri kwa maelezo yake mazuri na mipango mizuri niliyoiona katika maelezo yake na hotuba yake. Vilevile naipongeza Kamati husika nao wametoa mapendekezo mazuri tunawapa pongezi sana kwa hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana kwamba Serikali inakwenda kuongeza kiwango cha Bajeti kutoka trilioni 29.5 kwenda kwenye trilioni 32.9. Nawapongeza sana kwa mawazo mazuri na mipango hii mizuri, kwa sababu hii ni ishara kwamba Serikali ya CCM imejipanga sawasawa kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wake ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure bila malipo, umeme vijijini, barabara za vijijini, maji safi na salama na huduma za afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi na changamoto nyingi ambazo zimeonekana katika Bajeti ambayo imepita, hivyo tunavyo-focus kwenda kwenye Bajeti hiyo kubwa ni lazima basi Serikali iwe na mikakati mizuri na mipango ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na vyanzo vizuri vya kuweza kupata pesa ili tuweze kukamilisha yale malengo tunayoyahitaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama katika Bajeti ya Mwaka 2016/2017, ambayo ndiyo tunaendelea nayo sasa hivi tuko katika quarter ya pili, kwa maana ya kwamba quarter ya kwanza tumeimaliza tunakwenda kwenye quarter ya pili leo ni tarehe moja ina maana tuna mwezi mmoja wa quarter ya pili. Tukitazama ni kwamba pesa za maendeleo zimekwenda kidogo sana, hii ni kwa sababu pengine kuna mikakati fulani haikukaa sawa, basi hili tunaomba lisijitokeze tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapokwena kwenye mwaka mpya wa fedha na tumeweka makadirio makubwa ya kiasi hicho cha shilingi 32.9 trilioni inabidi tujifunge kibwebwe kwelikweli kuhakikisha kwamba tunaongeza mapato ambayo yataweza kuwezesha bajeti hii kukamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningependa kuchangia kwenye masuala ya fedha. Pamoja na kwamba tunakwenda katika mkakati na mpango huu, kuna tatizo kubwa limejionesha katika taasisi mbalimbali za kifedha. Kulikuwa kuna tatizo la kupeleka pesa ambalo Mheshimiwa Mpango naye ni shahidi, ni kwamba waliamua kupeleka pesa kwenda BOT yaani Central Bank kutoka kwenye taasisi kubwa za kifedha, kwa mfano NSSF na taasisi nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa mabwana walikuwa wanapeleka pesa kwenye hizi commercial banks mara ya kwanza, kwa mfano, NSSF walikuwa wanapeleka mabilioni mengi kwenye hizi commercial banks na kule commercial banks walikuwa wanalipa interest kwa maana ya kwamba walikuwa wanawalipa kila mwezi kiasi fulani cha fedha ambazo hawa NSSF walikuwa wanaweza na wao sasa kutumia pesa zile za interest kuweza kuwalipa wateja wao, kwa maana ya zile benefits wanapojiondoa kwenye mafao. Sasa unapoziondoa zile pesa kupeleka Central Bank ina maana kwamba ile biashara umeiondoa kwa hawa wahusika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kunakuwa na impact nyingine kwenye commercial bank kwa sababu wanakuwa wamekosa pesa, sasa hivi na wao nao wanakosa pesa ya kuwakopesha wateja wao. Unapowakosesha pesa ya kuwakopesha wateja wao yaani wafanyabiashara, hizo benki na zenyewe zinakufa kwa sababu zinashindwa kupata interest kutoka kwa wafanyabiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mtindo huu naomba Serikali itazame kwa macho mawili huu mpango, iweze kubadilisha, kurudisha zile pesa kwenye commercial banks. Unavyoziondoa ina maana kwamba hizi benki za kibiashara unaziua na kwamba zisiwe na uwezo tena wa kukopesha wateja wao. Hivyo basi tunaomba Serikali itazame upya, kwa sababu kwa kupeleka pesa kule ina maana kwamba benki isingekufa na Serikali ingeendelea kupata pesa pale inapohitaji pesa, lakini mnapopeleka Central Bank ina maana kwamba mnakwenda kuziweka kwenye shelf hizi pesa, zinakosa mzunguko, hakuna anayelipa interest na mwisho wa siku tunashindwa kupeleka pesa kwenye maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni suala la bandari. Suala la bandari tunalipigia kelele kwenye mambo makubwa mawili tu. Jambo la kwanza ni VAT kwenye auxiliary services on transit goods. Sisi Tanzania tumesaini mkataba wa Vienna, tulisaini mkataba wa World Trade Organisation (WTC), mteja anayepita Tanzania au raia wa nchi nyingine anayepita Tanzania anapopewa huduma au anaponunua kitu, unapokwenda nchi nyingine yoyote wewe kama ni mgeni ukinunua hata shati, unapotoka kama ulilipa VAT unarudishiwa! Kwa nini tunaweka VAT kwenye mizigo ya watu wanaokwenda nje? Kwa nini tunakwenda kinyume na mikataba? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kukosa hivi ni kwamba tunaweka mazingira magumu, hawa wafanyabiashara wa Congo na sehemu zingine tunawa-charge hizi VAT, matokeo yake ile VAT inakwenda kwa wateja wao. Mwisho wa siku wanakwenda kwenye bandari zingine, wanaamua kwenda Mombasa, wanakwenda Beira kwa sababu kuna charge kubwa inayochajiwa katika Bandari yetu. Tunaomba hiyo VAT iondolewe. Tuliyazungumza kwenye mpango wa mwaka 2016/2017 na nalirudia leo katika huu Mpango wa 2017/2018, ondoeni! Tunazidiwa na bandari za majirani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo lingine katika bandari tumezunguka tumeliona, kuna kitu kinaitwa single customer territory, huo mkataba ni tatizo. Tulioingia mkataba ni nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Congo haipo kwenye huu mkataba. Sisi tumesaini, tumewahi, tumeingia kwenye huu mkataba leo Wakongo wanachajiwa kodi kwenye bandari ya Dar es Salaam, risk ya mteja anapochajiwa mzigo wake Dar es Salaam, mfano mafuta amechajiwa Dar es Salaam, akatembea katikati gari likapata ajali, mafuta yakamwagika yule mteja anapata hasara mara mbili kwa sababu anakuwa amenunua, hasara na amelipa kodi, hasara mara ya pili, tuna kiherehere gani cha kwenda kusaini hiyo mikataba? Matokeo yake hawa wateja wanahama wanakwenda Beira, wanakwenda Mombasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bandari iji-assess upya, Serikali iangalie bandari ina matatizo yapi na isitoshe bandari iwe na kitengo cha marketing, waweze kufanya research na kugundua ni nini tatizo limewafanya wateja wa Congo na sehemu zingine waondoke? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo mawili yamefanya wale watu wanaofanya biashara ya copper badala ya ku-export mzigo katika bandari ya Dar es Salaam wana-export kupitia bandari ya Beira. Meli kubwa hawawezi wakaja Dar es Salaam kama hawana uhakika wa kushusha mzigo na kupakia mzigo. Hizi shipping zinataka uhakika wa kushusha mzigo na kupakia mzigo, wasipokuwa na uhakika wa kupakia mzigo wa ku-export maana yake ni kwamba wataleta mizigo mingine kwa gharama kubwa kufidia ile mizigo wanayoikosa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ondoeni hizi sheria tuziangalie upya. Kwa kufanya hivi tumeondoa wafanyabiashara wakubwa. TATOA wana magari 26,000; magari asilimia 60 yamepaki ambayo ni magari 15,000 ina maana kuna madereva 15,000 wamesimama hawana kazi, utingo 15,000 wamesimama hawana kazi, vipuri hawauzi, wenye matairi hawauzi, ina maana wale wafanyabiashara wa mafuta hawauzi mafuta, mama ntilie anakosa biashara, mwenye guest anakosa biashara, mwenye M-PESA anakosa biashara. Maana yake tumedhibiti mapato ya milioni 600 halafu tukazuia circulation ya bilioni sita, what are we doing? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye kilimo na hasa kilimo cha pamba, kuna mpango wa C2C naomba uzingatiwe, tuna soko kubwa sana la nguo Afrika Mashariki, tuna nchi tano, Tanzania yenyewe tu ina watu karibu milioni 50 sasa, ukienda na nchi zingine tuna watu zaidi ya milioni 100, hawa watu wote wanavaa nguo kutoka China, wanavaa nguo kutoka India na sehemu zingine, Tanzania tuna uwezo wa kulima pamba ya kutosha, tuna uwezo wa kufungua viwanda vya nguo na hivi viwanda vya nguo vikaweza kuzalisha nguo za kutosha kuuza soko la East Africa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tusitegemee mtu binafsi atajenga kiwanda cha nguo. Kiwanda cha nguo ni jambo ambalo Serikali inatakiwa i-intervene iingie kwenye ku-invest kwenye viwanda vikubwa kwa kufanya spinning, kutengeneza vifungo, kutengeneza ribbons, kutengeneza vitu mbalimbali ambavyo vinaunda nguo, pawe na industry ya textile maalum kwa soko la Afrika Mashariki, tuende huko. Tukishafanya vile ina maana kwamba tutakuwa na soko la uhakika na kuweza ku-export nguo zetu katika soko la East Africa na mkulima wa pamba, pamba yake itauzika na mkulima wa pamba atapata soko la uhakika kuliko sasa hivi mnavyotuendesha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, upande wa viwanda napenda kumalizia, kuna watu wanaitwa TEMDO. TEMDO wana teknolojia ya kutengeneza mitambo midogomidogo ambayo inaweza ikamsaidia mwananchi wa kawaida, tukawa na viwanda vidogovidogo hata vya ndani, mtu akawa na kiwanda kidogo cha kukamua alizeti, kiwanda kidogo cha kutengeneza soksi, kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa ndogondogo ambazo ni highly consumed katika market yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ina maana kwamba, tukiwawezesha hawa ndiyo tutaweza kupata uchumi wa viwanda, lakini leo TEMDO hawapewi hela, leo tumekwenda kwenye quarter ya pili, TEMDO hata senti tano hawajapewa, wakati wanatakiwa wanunue vipuri, wanunue spare mbalimbali waweze kuvumbua zile teknolojia na kuwauzia watu wengine waweze kufyatua mashine mbalimbali ndogondogo kwa ajili ya viwanda vidogovidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka tuwabebe akinamama, tubebe vijana, tunataka kwenda kuwapa milioni 50 ya mitaji, lakini kama tutawapa mitaji kwa maana ya kuchuuza, kuchukua bidhaa moja iliyotengenezwa yaani finished product kwenda kwenye soko lingine kila mtu anafanya, tunataka twende kwenye uchumi wa uzalishaji, uchumi wa kila mtu aweze kuzalisha kuondoa state moja ya bidhaa ya kilimo, kwenda kwenye new state, haya ndiyo yanayoweza yakatuondoa, bila hivyo hatuwezi kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mwisho, tuangalie kodi hizi ndogondogo ambazo ni kero zimezungumzwa katika bajeti iliyopita, lakini bado kodi ndogondogo ni kero. Tumehesabu kodi zinazochajiwa ndogondogo ziko kodi zaidi ya 41 tumeziona ziko wazi, tuziondoe hizi kodi zinawafanya watu waweze kurudi nyuma, zinawafanya watu wasiweze kwenda mbele. Tunaomba hizi kodi ziangaliwe upya, tunapokwenda katika mkakati huu na mpango wa mwakani ina maana tuhakikishe kwamba tunaziondoa kodi ambazo ni kero, tunakwenda kwenye kodi chache zinazoweza kumwinua mwananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho wananchi wa kawaida wapewe mikopo midogomidogo ili waweze kujinasua pale walipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii na mimi kuchangia katika taarifa hii ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa shughuli zake katika kipindi cha kuanzia mwezi wa Januari, 2016 hadi Januari, 2017.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nachukua nafasi hii kwanza kupongeza Kamati kwa kazi nzuri waliyoifanya, tunawapongeza kwa ufuatiliaji mzuri na ukweli waliouzungumza katika ripoti yao. Na mimi nashukuru kwamba Serikali imefanya kazi nzuri ya kukusanya mapato. Naishukuru vilevile Serikali na kuipongeza kwa kuweza kulipa madeni kwa kiwango kikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza haya kwa sababu tumeona ripoti inaeleza wazi kabisa kwamba ulipaji wa madeni umelipwa kwa kiwango cha juu kabisa na hii ni dalili nzuri kwamba ulipaji huu wa madeni unaweza kutusaidia hata kwa wafadhili kuendelea kutuamini na kuweza kutupa pesa nyingi ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa imeeleza vizuri japokuwa tu mimi nina wasiwasi kidogo kwa baadhi ya mambo ambayo nafikiri tungehitaji uangalizi wa ndani zaidi au wa macho makali zaidi mawili. Kwa maana ya kwamba tunapoandaa bajeti ni lazima tuzingatie mambo ambayo yanatokana na bajeti ile. Tunaona kabisa kwamba bajeti hii haikuweza kutekelezwa kwenye baadhi ya miradi ya maendeleo kwa sababu nchi ilikwenda kulipa madeni. Tunakubali kulipa madeni ni wajibu, lakini tuna wajibu wa kuangalia bajeti zetu tunavyozipanga ni lazima wataalam watusaidie ku-forecast yale madeni ambayo Serikali inatakiwa iyalipe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitoka kwenye bajeti ya trilioni 22 tukaenda kwenye bajeti ya trilioni 29 kwa mwaka 2016/2017. Tulikwenda kwenye bajeti kubwa, kinachonishangaza ni kwamba, kumbe kulikuwa kuna madeni ambayo yako matured. Kama kungekuwa kuna madeni yako matured ambayo yamekuwa ni kikwazo cha Serikali kupeleka pesa kwenye miradi na kulipa madeni ya ndani na ya nje, basi inabidi wataalam wachunguze na waangalie wawe tayari kuisaidia Serikali, kutusaidia Wabunge tunapokwenda kupitisha bajeti basi tuweze ku-consider yale madeni ambayo Serikali inakwenda kuyalipa. Bila kufanya hivyo tutapanga bajeti, tutakutana na madeni katikati, tutalipa madeni, tutashindwa kupeleka pesa kwenye miradi ya maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitizama katika miradi ya maendeleo Serikali imepeleka fedha kwenye miradi ya maendeleo kidogo sana. Mfano mzuri ukiangalia kwenye kipaumbele cha Serikali ambayo tunasema Serikali ya viwanda, bajeti iliyopelekwa katika Wizara ya Biashara na Viwanda ni asilimia 10 tu ya bajeti iliyokusudiwa. Ukitizama kwenye Wizara inayohusiana na masuala ya mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, pesa ya maendeleo ni asilimia sifuri, haijaenda pesa yoyote. Sasa hivi ni vikwazo vinatukwamisha, inabidi kweli Serikali tujizatiti tuhakikishe tunapeleka pesa za maendeleo kwa wakati kama ilivyopangwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuongelea vilevile masuala ya vyanzo vya mapato. Suala la kodi, kuna kodi hapa ambazo zililalamikiwa sana, mfano kodi ya VAT kwenye utalii. Mimi nafikiri Serikali ijipime, Wabunge tunapozungumza na yenyewe Serikali itusikilize, siyo kukaa mnasikiliza tunaandika halafu tunakwenda kutoza kodi kwenye utalii. Utaendaje kuwatoza watu kwenda kuangalia nyumbu na swala unawawekea VAT! Mtu anayekwenda kuangalia nyumbu na swala hakuna haja ya kumuwekea VAT. Tuondoe VAT tuweze ku-invites watalii wengi waweze kutembelea katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona pato linavyozidi kuongezeka kwenye utalii tukiwaondolea kodi ya VAT tutakaribisha watalii wengi, wata-flow kwa wingi. Tuangalie na nchi ambazo tunashindana nazo kama Kenya wao wanafanya nini? Tujifunze kutoka kule ili na sisi tuweze kufanya inavyostahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kodi hiyo kuna suala la VAT kwenye capital investiment. Tunasisitiza watu tuondoe kodi kwenye kilimo, tunasisitiza tuondoe kodi kwenye vifaa vya kilimo kwa maana ya kwamba watu tulime zaidi tupate mazao mengi. Kwa mfano, mtu amelima akaenda kuuza mazao yale kwa wale watu ambao wanachakata mazao yetu, unakuta kwa mfano mtambo wa kutengeneza juice au mtambo wa kusaga unga, ile investiment anayoileta Mwekezaji, kwa mfano, Ndugu Bakhresa pale alitaka kuleta mtambo wa dola milioni 100, lakini akaukutana na VAT! Hebu piga asilimia 18 ya VAT ya milioni 100 ni shilingi ngapi! Ndipo alipoamua kuondoa mtambo huu na kuupeleka nchi jirani ambako hawana hiyo kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ni lazima tu-harmonize hizi strategy zetu. Kama tumeamua kuondoa VAT kwenye vifaa vya kilimo basi tuondoe kodi kwenye msururu mzima ambao hadi kwenye uchakataji wa bidhaa zile. Sasa kama wewe umeondoa kodi umemu-encourage mtu alime akalima mahindi, unamuwekea kodi mtu anaye-invest anayeweza kwenda kusaga unga na ku-pack, maana yake ni nini? Tunapoamua kuondoa basi tuangalie flow nzima ili tuweze ku-encourage wawekezaji waweze ku-produce zaidi na kuweza kupata kipato cha kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kodi hiyo kuna kitu kinaitwa single customer territory, mikataba ya single custom, tumepigia kelele. Ni kweli Tanzania sisi ni wanachama wa East African na tumekubaliana nchi zote za East Africa kuwa na single customer territory kwa maana ya kutoza kodi, kwa niaba ya nchi nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mkataba uko kwa nchi za East Africa, kwa nchi ya Kongo haupo, iIna maana Mkenya anaweza akafanya biashara na Mkongo bila kumtoza kodi. Ina maana sisi tunamtoza kodi mfanyabiashara wa Kongo Dar es Salaam, tukimtoza kodi ina maana kwamba huyu mfanyabiashara tunamu-encourage aende kwenye bandari za pembeni. Wamekwenda Beira, wamekwenda Durban, wanakwenda Mombasa, wametukwepa katika bandari yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya tuyatizame kwa kina, tunapoamua kutafuta vyanzo vya mapato tusione aibu. Tusiingie mikataba ambayo haina tija! Huu Mkataba wa single customer territory kati ya Tanzania na Kongo naomba muutizame upya, ikibidi muuondoe. Kwa nini tuwakusanyie Kongo zile pesa? Kuna malalamiko wameshaanza kusema kwamba, kumbe hata pesa zenyewe zinapokwenda kwenye mikono ya Serikali ya Kongo haifiki kwa wananchi! Sasa sisi tunawasaidia nini? Ina maana badala ya kuwasaidia Wakongo wote tunawasaidia Wakongo wachache!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini tuingie kwenye mkataba kama huo na unakimbiza wateja wetu wasije katika bandari yetu! Tuuondoe huo mkataba, ikiwezekana hata kesho tuuondoe ili kusudi tu-encourage biashara ya kongo na Tanzania ili bandari yetu irudishe uwezo wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile naongelea kuhusu vyanzo vipya. Katika kuongelea vyanzo vipya vya kodi ni lazima tujali viwanda vyetu na viwanda vipo vikubwa na viwanda vidogo. Viwanda hivi haviwezi kufanya kazi kama hatuna umeme wa uhakika, hatuna umeme wenye bei nafuu. Umeme wetu bado ni tatizo kubwa katika uchumi wa nchi yetu. Tunauza umeme kwa bei kubwa mno na bado umeme wenyewe hauna quality nzuri, unakatika mara kwa mara. Umeme unapokatika ni hasara kubwa sana kwa wawekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulitembelea EPZA pale kuna jamaa wanatengeneza hizi smart card, kadi za benki na nini, wanatengeneza kwa ajili ya kuwauzia makampuni ya simu, wanauzia mabenki, hizi unaziona visa card zinatengenezwa pale EPZ Dar es Salaam. Wanatumia system kubwa ya computer and very sophisticated. Ukiukata umeme mara moja wana-recover ile system kwa siku saba. Kesho akiona kuna nchi nyingine ina umeme wenye quality nzuri huyu mtu atatuhama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ni matatizo makubwa. Ilipeni TANESCO deni lake, walipeni waweze kuweka infrastructure nzuri. Tunaipongeza Serikali mmepeleka umeme hadi vijijini sawa kabisa mmepeleka umeme hadi vijijini, lakini quality ya umeme bado ni tatizo katika nchi yetu. Umeme kwa kweli ni tatizo, tusipo-improve umeme hii Serikali tunasema tunaenda kwenye viwanda, tutashindwa kwa sababu bila energy ya kutosha ni tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niende kwenye kilimo. Asilimia 70 ya Watanzania tumejiajiri kwenye kilimo, lakini kilimo chetu hakina tija, kilimo na ufugaji ndiko kwenye ajira kubwa katika nchi yetu. Hebu tuangalie namna gani ya kuwasaidia wakulima, sasa hivi bei ya mbegu ya mahindi inauzwa shilingi 13,000 mfuko wa kilo mbili! Shilingi 13,000 mwananchi wa kawaida mbegu kununua shilingi 5,000 kwa kilo, karibu shilingi 6,000 ni shida kununua, hawezi kununua. Ni bora Serikali mka-subsidize hizi mbegu mkatoa na mkawalipia wakulima wakanunua mbegu kwa bei nafuu ili waweze kupanda na kupata mazao mengi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachokifanya sisi kwetu kule Usukumani mtu akilima mwaka huu anahifadhi na madebe mawili/matatu ya mbegu, zile mbegu hazina ubora! Tunataka special mbegu ambazo mtu ukipanda unapata mavuno ya kutosha, sasa zile mbegu ni bei juu mno. Kama mnataka kweli wananchi waweze kulima wapate mazao ya kutosha punguzeni bei ya mbegu, Serikali iingilie kati i-intervene m-subsidize mzilipie kodi hizi mbegu. Wako watu wachache wanaozalisha hizi mbegu muwape mikataba wazalishe mbegu, muwasambazie wananchi kwa bei nafuu waweze kupata mazao mazuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kwa wanyama ng‟ombe tulionao hatuna ng‟ombe wa maziwa wala hatuna ng‟ombe wa nyama. Tuna indigenous ng‟ombe wetu ambao ukimwangalia amekondeana, tuna ng‟ombe wengi na ukame huu wengi wanakufa sasa hivi. Hatuna ng‟ombe ambao wana good quality kwa maana ya kula nyama, hatuna ng‟ombe kwa maana ya kupata maziwa bora. Tunaomba mbegu mpya, tunazungumza kila siku Serikali iingilie kati mlete mbegu za ng‟ombe wapya wenye kuweza kutoa nyama nyingi, ng‟ombe wapya wenye kuweza kutoa maziwa mengi ya kutosha ndipo tutaweza kuwainua wananchi wetu na kuweza kuwaingiza katika uchumi wa kati. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kusema kwamba bado Serikali ina kazi kubwa ya kufanya. Nawashukuru kwa kazi kubwa mnayoifanya kwa kweli, tumeangalia kwenye elimu, elimu bure, pesa zinakwenda, hivyo vitu tunasema tunatoa pongezi za dhati kabisa, muendelee kufanya kazi nzuri. Tunaona miradi mingine inakwenda ya barabara, tunajengewa barabara, lakini miradi ya maendeleo tunaomba Serikali iwalipe watu wanaoidai ili kusudi mzunguko wa pesa urudi na tuweze kupata mzunguko wa kutosha na watu waweze kulipa kodi na Serikali iweze kupata mapato ya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii niweze kutoa mchango wangu. Kwanza kabisa naomba ku-declare interest kwamba ni Mjumbe wa Kamati hii ya Viwanda na Biashara pamoja na Mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia napenda kutoa pongezi zangu za dhati kabisa kwa Mwenyekiti wangu kwa uwasilisho wake mzuri, amewasilisha vizuri na kwa kweli aliyoyaeleza ndiyo ambayo Kamati imeyasema niko hapa tu kwa ajili ya kusisitiza kwa baadhi ya mambo fulani ambayo nadhani ni muhimu tukayasisitiza na Serikali ikajua na Bunge likatambua nini cha kufanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la viwanda na biashara kwanza ni suala mtambuka ambalo si kazi pekee inayomwelemea Waziri mhusika wa Viwanda na Biashara lakini ni suala mtambuka ambalo kama Serikali au nchi nzima kupitia sekta nyingine basi inabidi tushikamane bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunaipeleka nchi yetu kwenda kwenye nchi ya viwanda kama Sera ya Chama cha Mapinduzi inavyosema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mengi yamezungumzwa katika Kamati na katika kusisitiza, ni suala la upelekaji wa fedha za maendeleo katika Wizara zilivyopangiwa bajeti zake yaani katika Wizara husika. Kwa mfano, Wizara ya Viwanda na Biashara, pesa walizopata ni asilimia saba nukta tano tu na leo tuko quarter ya tatu tunakwenda kwenye quarter ya mwisho. Asilimia saba nukta tano Wizara ya Mazingira chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais wenyewe hata sifuri, yaani hata percent kadhaa hawajapata wao ni sifuri kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa kweli hii inawanyong‟onyesha watendaji wetu na Serikali iangalie namna ya kupeleka pesa za maendeleo kwenye sekta husika kwa muda unaostahili ili kusudi yale yaliyopangwa yaweze kutekelezwa. Ucheleweshaji huu sijui Waziri atafanya muujiza wa namna gani, sijui watendaji watafanya miujiza ya namna gani, kazi wamepewa, pesa za mishahara wanapelekewa, pesa za mishahara wanakula lakini pesa za kufanyia kazi hawapati, ina maana kama pesa ya maendeleo haijaenda ina maana hawa wafanyakazi wanapewa mishahara ya bure. Tunataka pesa ziende kwa wakati ili waweze kutekeleza yale ambayo yamepangwa na yale ambayo yanatakiwa yatekelezwe kwa muda uliostahili au muda uliopangwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ripoti hii imeelezea kuhusu kodi, tunapiga kelele sana kuhusu kodi na tozo mbalimbali, tunaomba vyombo husika muangalie upya kuhusu hizi kodi na hasa kwenye kodi ya capital investment, kwenye capital investment kuna VAT, kuna VAT hadi kwenye vyombo vya Serikali. TBS anapokwenda kuagiza vifaa vya maabara ili aweze kukagua bidhaa mbalimbali kwa usalama wa Mtanzania, maabara zao wanapoagiza vifaa zinatozwa kodi ya VAT, haya masuala tunakwenda kwenye bajeti inayokuja wayaondoe, Serikali iondoe VAT kwenye kodi za maabara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwekezaji mkubwa anayetaka kuwekeza kwenye kiwanda cha kukamua bidhaa za mkulima anapoagiza bidhaa kubwa kwa maana ya mashine za kuchakata bidhaa mbalimbali za kilimo na zenyewe ana kodi kubwa amewekewa, tunaomba hizi kodi ziondolewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna masuala ya Sheria ya Manunuzi, ukienda pale TANELEC unakuta kabisa kwamba mmiliki wa TANELEC mmoja wa shareholders ni NDC na TANESCO ikiwemo, wana asilimia 10 mle ndani. Kutokana na Sheria hii ya Manunuzi inawafanya hawa TANELEC wakose biashara kwa TANESCO, yaani Mjumbe wa Bodi ya TANESCO ambaye ni Mkurugenzi wa TANESCO anaingia kwenye Board of Directors lakini biashara badala ya kuipa TANELEC ambayo yeye mwenyewe ndio mhusika mle ndani, TANESCO pamoja na REA wananunua transfoma na waya kutoka nje, wanaikosesha biashara pale. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii tumetazama katika nchi za jirani, tuliangalia tender board iliyotolewa kule Kenya kwenye shirika la umeme vilevile, wana-favour kampuni zao kwa kutoa tenda maalum kwamba tenda hii ijazwe na watu wanaofanya uzalishaji ndani ya nchi ile lakini sisi tunapeleka biashara nje. Sheria ya Manunuzi bado tunaendelea kuipigia kelele tuirekebishe na irekebishwe, kwa kweli inasikitisha sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la umeme nilishaliongelea, umeme sio wa uhakika. Quantity na quality ya umeme wetu bado ni tatizo kubwa, hatuwezi kwenda kwenye viwanda kama umeme wetu unaendelea kukatika namna hii na uzalishaji ukawa ni wa shida na bado umeme wetu ni bei ya juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijikite kwenye bandari, bandari yetu ni kivutio kikubwa sana cha watu kufanya biashara na naomba niseme kwamba bandari ipo chini ya Wizara ya Miundombinu, lakini bandari utekelezaji wake kikubwa ni kufanya biashara. Biashara ndicho chanzo kikubwa cha kuwepo kwa bandari pale, lakini ufanisi wa biashara wa bandari yetu hauvutii na ndiyo maana watu wanakwenda kuwekeza au kutumia bandari nyingine za jirani. Matatizo tumeyazungumza mengi – kuna single customer territory, tumeyaongea masuala ya kodi on auxiliary goods, yote tumekwishaongea, lakini ninachotaka kuzungumza leo, hata bandari yenyewe ndani ina matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama toka mwaka 2012 mpaka 2017 wakurugenzi wa bandari wamebadilishwa watano, alikuwepo mzee Mgawe, alikuwepo Kipande, Massawe, Matei na mpaka leo yupo Injinia Kakoko, kila siku wanabadilishwa, kwa watumiaji inatia wasiwasi. Ukimtazama hata huyu aliyepo sasa hivi Mheshimiwa Engineer Kakoko amefanya mabadiliko ndani ya bandari, katika ile top management kabadilisha watu saba, kamwondoa bwana Gawire Mkurugenzi wa Utumishi, kapiga chini, Kilian Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA kafukuza, Magesa Kaimu Mkurugenzi wa Utekelezaji kafukuza, bwana Masoud Kaimu Meneja wa Fedha kafukuza, bwana Muhanga Kaimu Meneja wa Bandari kafukuza, bwana Mosha Meneja Msaidizi wa Bandari kafukuza, bwana Macha Meneja wa Utumishi kafukuza. Cha ajabu kabisa badala ya kufukuza kuweka watu competent, kaondoa hapa Msaidizi Operations Manager katoa kaweka mlinzi kuwa Operations Manager. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, maana yake ni nini, kuna siku atapakua mzigo kwenye bandari upande mmoja upande mwingine meli inazama, tuwe makini, haya mabadiliko yanatia wasiwasi, wafanyabiashara hawawezi kuja bandarini watakwenda sehemu nyingine, mtu wa security anakuwa Operations Manager, tunaomba tuwe serious. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine, meneja halipi watu on time. Wapakuaji wa mizigo, wanasema ile ni casual labour, wale wapakua mizigo hawana mkataba wa kupakua mizigo, sio wafanyakazi wa kudumu, wanapakua kama vibarua, wanapakua leo wapewe pesa zao leo, anayesafisha leo apewe pesa yake ya kibarua leo, Mheshimiwa huyu hawalipi wale watu alio-outsource, wale watu wenye kampuni ambazo zinaendesha zile shughuli hawalipwi, wanalipwa kidogo kidogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanamwandikia barua awalipe anachelewa kuwalipa, hapa nina barua amepokea tarehe 23, mwezi wa kwanza, wanamwomba tulipe hela. Kuna kampuni inawadai hawalipi, ina maana wale wapakuaji, huyu mwenye kampuni itafika atashindwa kupata cash ya kuwalipa watu on a daily basis, atakosa ile pesa na akikosa pesa wale wafanyakazi watagoma na wakigoma hiyo habari itatoka nje, itakwenda Congo, itakwenda na nchi nyingine kwamba wafanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam wamegoma hawajalipwa, at the end of the day watumiaji wa bandari wanakwenda Beira, watakwenda Durban, watakwenda Mombasa, haya ndiyo yanayotuletea matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Meneja wa Bandari mwingine katolewa Mhasibu kutoka TANROADS amekwenda kuwa meneja pale, that’s a professional job, ni watu wataalam wanatakiwa wafanye zile kazi. Jana sikupata muda wa kuongea kwa watu wa miundombinu – chunguzeni hili, kuna kampuni nyingine pale zinaonewa, kuna wengine wamepewa kazi tatu, moja anapakua mizigo ya kontena wanamu-underpay kwa sababu ana kazi nyingine mbili, wana…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja, ahsante sana.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii kwa siku ya leo. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya bora kabisa. Awali ya yote kwanza kabisa Mheshimiwa Mwenyekiti naomba nitoe pongezi nyingi sana kwa wananchi wa Uyui kwa ushindi mkubwa walioupata. Kama tulivyosikia katika Uchaguzi Mdogo wa Vijiji CCM imepata viti 14 sawa na asilimia 93.3 hongera sana. Katika Vitongoji viti 58 CCM imechukua 51 sawa na asilimia 88 hongereni sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile napenda kutoa pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kutoka katika Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kazi nzuri wanayofanya na kwa hotuba nzuri kabisa ambayo imejaa ukweli na uwazi. Katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri aliyozungumzia zaidi masuala ya mazingira ameeleza kwa uwazi kabisa kwamba hali ya mazingira nchini kwetu siyo nzuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la mazingira ni suala mtambuka, tunatambua wazi kwamba nchi yetu sasa inakwenda kuwa ni nchi ya viwanda kwa hiyo tunapokuwa na mazingira ambayo siyo ya kuvutia inatupa hali ngumu sana kuona kama kweli nchi yetu inakwenda kwenye viwanda. Tunahitaji juhudi za ziada kuhakikisha kwamba tunatunza mazingira yetu ipasavyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tukitizama juhudi za Serikali kwa namna moja au nyingine tumejitahidi, lakini tunahitaji juhudi zingine nyingi za ziada kuhakikisha kwamba mazingira yetu yanakuwa siyo tishio tena kwa viumbe wanaoishi juu ya ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa mabadiliko ya tabianchi yameleta mabadiliko makubwa sana, ukitizama hata kimo cha bahari kinaongezeka. Kimeongezeka kwa sentimeta 12, maana yake ni kwamba zile kingo ambazo ziko kwenye upande wa baharini na zenyewe ziko katika mazingira hatari ya kuweza kufunikwa na maji na baadhi ya maeneo mengine kuna visiwa vimeanza kufunikwa. Hii ni hali mbaya kwa sababu bila kuchukua tahadhari ya kutosha tutajikuta tuko katika mazingira magumu sana miaka ijayo. Kwa hiyo, ndugu zangu tunahitaji tuungane na mikakati ya Kimataifa pamoja na ile mikataba ambayo Tanzania imesaini ya Kimataifa kuhakikisha kwamba tunashiriki katika kudhibiti uharibifu wa mazingira unaotokana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningependa kuongelea suala la Mfuko wa Mazingira. Tunatoa pongezi kubwa sana kwenye Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Februari, 2017 umeanzishwa huu Mfuko wa Mazingira ambao Mheshimiwa Ndugu Ali Mufuruki amechaguliwa kuwa Mwenyekiti. Huu Mfuko wa Mazingira ni muhimu sana tuufanyie kazi. Mfuko huu wa Mazingira tuuwezeshe, tuhakikishe kwamba tunaupa nguvu ya kuweza kufanya kazi ya kutekeleza au kusimamia ile Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004. Tunaomba Serikali izingatie kuusaidia na kuhakikisha kwamba huu Mfuko unafanya kazi ipasavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitizama suala la mazingira kama tunavyosema ni suala mtambuka, lakini ukitizama Wizara hii haipewi fedha za kutosha, haipewi facilities za kutosha kuhakikisha inafanya kazi inavyostahili. Ukitazama katika tozo kuna tozo mbalimbali zinazohusiana na mazingira, ukiangalia tozo kwenye magari chakavu, ukiangalia tozo kwenye mkaa, ukiangalia tozo kwenye mafuta, tozo kwenye majengo, kwenye migodi, kuna magogo yanatozwa kodi ya mazingira, lakini Mfuko huu haupewi chochote maana yake nini?(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hata katika Kamati ya Mazingira imeeleza angalau asilimia tano ya hizi tozo iende kwenye Mfuko wa Mazingira ili kusudi Mfuko huu uweze kupatiwa nguvu ya kuweza kufanya kazi yake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitazama hapa katika Mfuko huu wa Mazingira na juhudi kamili ambazo zinaendelea katika Wizara hii, utaona kuna mwingiliano wa hali ya juu katika Wizara zingine. Wizara ya Mazingira ina- insist watu waweze kutunza mazingira, waweze kupanda miti na kuacha ile misitu ya asili iendelee kukua, lakini kuna Wizara zingine kwa mfano, Wizara ya Maliasili kupanda miti siyo priority kwao, wao kuvuna miti ndiyo kipato kwao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, iangaliwe namna ya kuweza ku-harmonize hizi sheria ili kusudi hawa wote wawe na majukumu sawa ya kuweza kutunza mazingira. Ukitazama Wizara ya Maliasili wao misitu wanaitumia kwa ajili ya kutunzia wanyama lakini masuala ya kupanda na kuhakikisha kwamba misitu inalindwa hiyo inakuwa ni kazi ya Wizara ya Mazingira chini ya Mheshimiwa Makamu wa Rais. Sasa hapa hizi Wizara zote mbili au tatu zihakikishe kwamba wana- harmonize hizi sheria kuhakikisha kwamba Wizara ya Mazingira inakuwa na nguvu kuhakikisha kwamba inasimamia Sheria ya Mazingira na Sheria hizi zinahakikisha kwamba zinatunza mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ningependa kuongelea kuhusu bajeti ya mazingira, bajeti ya mazingira leo imeombwa hapa, lakini inasikitisha sana ukiangalia bajeti ya mwaka 2016/2017, walikuwa wametengewa shilingi billioni 20 lakini ile bajeti ceiling kwa mwaka huu imepungua. Tunaomba Serikali iangalie uwezekano wae kuitengea bajeti ya kutosha Wizara hii. Hii Wizara ni nyeti lakini inaonekana kama vile haipewi priority kama Wizara zingine, wanapewa pesa kidogo na kweli uharibifu wa mazingira ni mkubwa kiasi kwamba hapo baadae watashindwa kufanya kazi na mazingira yetu yatazidi kuwa mabovu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba kutoka billioni 20 ya mwaka 2016/2017, angalau wangerudia kupewa kiasi kile kile, sasa bajeti imepigwa panga imekatwa kutoka billioni 20 inakwenda kwenye billioni 15. Matokeo yake ni nini? Hawa wanafanya kazi kwa kutegemea Mfuko wa NEMC na NEMC ndiyo inayowalisha Wizara ya Mazingira na NEMC inalalamikiwa kwa kutoza watu tozo na penalty nyingi ambazo kwa kweli zinafanya watu wasijisikie vizuri na NEMC inavyofanya kazi. Kwa hiyo, naomba mambo haya yote yazingatiwe vya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri pamoja na Wizara yake kwa kutuwezesha Mkoa wa Simiyu kupata pesa za mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kiasi cha dola za Kimarekani millioni 100 sawa na billioni 230. Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Simiyu, kwa niaba ya wana-Maswa na Wilaya zingine zote za Mkoa wa Simiyu, tuna uhakika sasa tutapata maji kutoka Ziwa Victoria na tutahakikisha kwamba tutapata maji ambayo yatatusaidia kutunza mazingira ya Mkoa wetu wa Simiyu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tunavyotambua Mkoa wetu wa Simiyu ni Mkoa kati ya mikoa nane ambayo iko katika tishio ya kuwa jangwa hatuna vyanzo vya maji , hatuna vyanzo ambavyo ni vya uhakika kuweza kupata maji, kuweza kumwagilia na kufanya shughuli za kiuchumi kwa maana ya kilimo na shughuli zingine za kufuga na mambo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kupata mradi huu tunashukuru sana kwamba sasa Mkoa wa Simiyu utaamka na utakuwa ni mkoa ambao utalima mazao mengi kwa kupitia mradi huu kwa maana ya kumwagilia, tutalima mpunga mwingi wa kutosha na tutatunza mazingira ya kutosha na mkoa wetu utakuwa ni green, tunasema ni mkoa ambao ni wa kijani. Tunawashukuru sana na tunaomba wana Simiyu wajiandae kwa miradi hii mikubwa inayokuja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho ni matumizi ya plastiki, tumeona jinsi juhudi za Serikali ilivyofanya tunawapongeza Serikali kwa kuweza ku-burn viroba, viroba ilikuwa ni moja ya vitu vinavyochafua mazingira. Ninachotaka kusema ni kwamba katika vile viroba vya pombe, uchafuzi wa mazingira wa viroba vya pombe ulikuwa ni kama niasilimia 0.001 something kule. Sasa kuna mifuko ya plastiki na yenyewe tulishatoa tamko katika Kamati yetu kwamba watengenezaji wa vifungashio vya plastiki watoke katika teknolojia ya sasa hivi ya mifuko ambayo haiozi waende kwenye teknolojia ambayo ni bio-degradable ambayo mifuko ukiisha i-produce baada ya miezi mitatu ukiitupa kwenye udongo mifuko ile inaoza. Tunaomba waende kwenye hiyo teknolojia, dunia yetu itakuwa salama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, at the same time Serikali itoe elimu ya kutosha jinsi ya utupaji wa plastiki, watu wafahamu namna ya kutunza mazingira na mwisho Kamati iliishauri Serikali kwamba Serikali i-insist sasa kuwawezesha Wajasiliamali waweze kuanzisha viwanda vya bidhaa…...(Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema. Nianze kwanza na ushauri kabla sijaongea mambo mengine. Ushauri wangu kuhusu Mwenge, leo ni mjadala ulikuwa umeendelea kuhusu Mwenge, watu wameongea sana na wanaongea hasa kuhusu gharama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naomba niungane na wenzangu kutetea umuhimu wa Mwenge. Tuendelee kukimbiza Mwenge, uendelee kuangaza hadi nje ya mipaka ulete upendo na amani katika nchi yetu. Ushauri wangu ni kwamba, kama tunaona kuna gharama kubwa, tusiwe na haja ya kuukimbiza Mwenge kila siku nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuchague siku moja kama ni siku ya Uhuru tarehe 9 mwezi wa 12, tarehe 8 unawashwa katika Mkoa ambao wanaazimisha siku hiyo ya Kitaifa kama ni Mkoa wa Kilimanjaro mfano, unawashwa, tarehe 9 unazimwa na unafanya kazi zile zote ambazo Mwenge unafanya katika Mkoa husika. Mwaka unaofuata tunakwenda kwenye Mkoa mwingine tunafanya vile. Hayo ni mawazo yangu, lakini tunaweza tuka-discuss zaidi katika modarity ya kuukimbiza Mwenge kama tunaona gharama ni kubwa. Huo ni ushauri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili kuhusu TBC. TBC inavyoonekana kwa kweli, imewekwa pembeni. Tuangalie namna ya kuwasaidia TBC. Matangazo ya TBC yanakatika, quality ya picha ni mbovu, wakati mwingine unatazama sauti inakata na wakati mwingine unaona kabisa kwamba hapa kuna upungufu, teknolojia imeshawapita, wako nyuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri iangaliwe namna ya kuwasaidia hawa kupitia vile wanaita ving’amuzi. Wale wateja wa ving’amuzi waweze kulipa pesa na pesa zile zikilipwa TBC wapewe hela yao moja kwa moja kuliko kuanza kupeleka pesa Hazina, mara process zinafanyika za hapa na pale na matokeo yake wanachelewa kupata pesa. Wanahitaji mitambo mipya, wanahitaji teknolojia mpya. Wako nyuma, hawako kibiashara kabisa! Tunaomba muwaangalie kwa jicho la namna ya pekee ili kusudi muweze kuwasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lingine natoa pongezi kwa Serengeti Boys; kazi wanayofanya ni nzuri kabisa, wametuletea heshima katika nchi hii. Tunaomba hiyo timu muilee vizuri, hiyo timu itatufikisha mbali. Nakumbuka kuna timu ya vijana ilienda hadi ikachukua ubingwa wa dunia, lakini baada ya pale kuja kurudi ile timu sijui imepotelea wapi. Tunaomba muiangalie hii Serengeti Boys, itatupeleka mbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumze kwa kina kidogo, naomba ku-declare mimi ni Mwenyekiti wa Chama cha Mpira katika Mkoa wa Simiyu. Kwa hiyo, mimi ni mdau mkubwa wa mpira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kwamba katika timu ya Taifa ni lazima tuwe na utaratibu wa kutengeneza timu yetu ya Taifa. Watu tunadhani kwamba premier league ndiyo inayotengeneza timu ya Taifa. Hivi vilabu, huwezi kutengeneza timu ya Taifa kutoka kwenye hivi vilabu. Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu inatengenezwa kutokana na Football Academy.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiwa na Football Academy nzuri za kutosha tutakuwa na vijana wengi ambao tutaweza kutengeneza kutengeneza timu ya Taifa. Premier league ni typical commercial league. Hiyo ni commercial football, pale ni biashara, siyo timu ya Taifa. Mshindi wa Premier League anapokwenda kwenye Champions League anakwenda kucheza kibiashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo sisi tunadhani kwamba kutengeneza Timu ya Taifa ni lazima wachezaji watoke kwenye Premier League, ni makosa. Premier League ni biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapotegemea Premier League kutengeneza Timu ya Taifa, utajikuta huyu mwenye timu, kwa mfano Azam tumchukulie, Azam ana uwezo wa kununua wachezaji kutoka nje hata 20; leo bingwa wa Tanzania akipatikana, anapokwenda kwenye Champions League ya Afrika anaenda kukutana na TP Mazembe, ambapo TP Mazembe yeye amenunua wachezaji karibu ya 20 kutoka nje, kwa sababu anafanya biashara. Sisi leo Azam unamzuia kwa mfano asinunue wachezaji zaidi ya watano kutoka nje, hii sheria haina maana yoyote. Hii muiondoe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachezaji wapatikane first division kushuka chini kutokana na zile Football Academy zetu. Nawapeni mfano, Zambia walipoteza wachezaji walikuwa wanaenda Gabon, walianguka na ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Zambia wamepoteza wachezaji, makocha wakajiunga wakarudi kwenye Football Academy zao wakaangalia wachezaji wakatengeneza timu nyingine mpya ya watoto wadogo, wakaunda Timu ya Taifa ikaenda Gabon na ikacheza ikafika finali ikatolewa na Nigeria. Kila mtu anakumbuka hapa! (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda Brazil, kuna wachezaji kama Romario alikataliwa asiingie Timu ya Taifa, kocha akasema tuna mchezaji anaitwa Gaucho kutoka kwenye Football Academy. Alivyoingia Gaucho wakachukua kombe la dunia. Sisi leo tunang’ang’ania wachezaji wa Premier League ndio wacheze Timu ya Taifa. Hatuwezi kufika popote! Undeni Football Academies za kutosha, fufueni vile Vyuo vya Michezo vya kutosha ili kusudi mpate watoto wa kutosha kwenda kucheza Timu ya Taifa. Kwa mtindo huu hatutafika. Kwanza league zenyewe hazina quality, you cannot predict. Ukienda kuangalia mpira, mara refa amekula mlungula, anaamua penati, anaamua kitu cha ajabu ajabu. Leo kuna points zinanyang’anywa mezani, hakuna! Tunafanya nini?

Mheshiiwa Mwenyekiti, nawashukuru TFF, wanafanya kazi nzuri. Hata ukitazama kalenda ya Kimataifa TFF wamefanya kazi nzuri. Ukitizama zile kalenda za michezo ya Kimataifa katika nchi 12 za CECAFA, TFF wamejitahidi badala ya mechi moja wanacheza mechi mbili, hilo nawapa pongezi, lakini waunde miundombinu ya kutafuta wachezaji wa Timu ya Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, twende kwenye Bongo Movies; hii ku-burn sinema za kutoka nje sijui imetoka wapi? Hivi una-burn sinema za kutoka nje mnatuuzia zile sinema zenu za jambazi ameingia na soksi! Eti jambazi ameingia na soksi kuvamia mtu, ulishawahi kuona wapi? Tuleteeni sinema; sisi tunamjua Rambo. Mimi nikiwa mdogo namjua James Bond. Kwenye miziki ya zamani tulikuwa tunamjua Bob Marley. Mbona wenye muziki wamejitahidi!

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilienda Kenya, kwenye club za Kenya unakuta watu wanapiga miziki ya Kenya. Sasa hivi ukienda unakuta wanapiga Bongo Flava, ina maana Bongo Flava wamejitahidi. Nyie Bongo Movie, mna-burn kuingiza sinema kutoka nje. Hii imetoka wapi? Naomba tusitafute kiki kwa shortcut …

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: …warudi nyuma, wajitahidi kutengeneza sinema vizuri, wataingia kwenye soko ndani na nje ya nchi. Sasa una-burn ku-import sinema kutoka nje: Je hao wa Kenya, Wanaigeria; sisi tunataka leo tuuze sinema Kenya na Uganda. Sasa tutaziuzaje kule? Tutaziuza iwapo tume-improve quality ya sinema zetu za Bongo. Warudi nyuma wajipange. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la Kiswahili. Ndugu zangu Waheshimiwa Wabunge, nilikwenda South Africa nikakuta kuna Wakalimani kwenye Mkutano. Mkalimani anaongea ki-Portugal na Kiingereza. Nikauliza, Mkalimani wa Kiswahili yuko wapi, kwa sababu nataka niongee Kiswahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnapokwenda kwenye mikutano, mwombe Wakalimani wa Kishwahili kule mnakokwenda. Kwa sababu mkiweka wakalimani wa Kiswahili, mtawapa soko wakalimani na watu watajifunza Kiswahili, wataona kwamba kina soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiswahili ni lugha kubwa, imekuwa ya pili kwa Afrika ikiongozwa na lugha ya Kiarabu. Lugha ya pili ni Kiswahili, ina maana lugha yetu ni kubwa, tusiibeze lugha yetu. Tuitukuze lugha yetu. Naomba tumjali, tumtetee na tumlinde na tumheshimu Mheshimiwa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kukitukuza Kiswahili. Turudi tuendelee kuongea Kiswahili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampa hongera Mheshimiwa Magufuli kwa kwenda kuongea Kiswahili nje ya nchi. Ombeni siku zote mnapokwenda kwenye Mikutano mwombe Mkalimani wa Kiswahili. Semeni, hatujui Kiingereza. Tatizo la Sisi Wabongo, tunajifanya tunajua Kiingereza, hatujui. Unafika kule hata ukipewa muda wa kuongea, unaongea point mbili, tatu, baada ya hapo umetoka nje ya line. Tuongee Kiswahili. Tuweke Wakalimani wa Kiswahili, Kiswahili ziwe na soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hongera Mheshimiwa Magufuli kwa kwenda kuongea kiswahili nje ya nchi. Siku zote mnapokwenda kwenye mikutano ombeni mkalimani wa kiswahili, semeni hatujui kiingereza. Tatizo la sisi wabongo (watanzania) tunajifanya tunajua kiingereza, hatujui. Unafika kule hata ukipewa muda kuongea unaongea point mbili, tatu baada ya hapo umetoka nje ya line. Tuongee kiswahili, tuweke wakalimani wa kiswahili, ili kiswahili kiwe na soko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoma za kienyeji, tv zetu, hawa TCRA mtu anayeomba leseni ya tv katika vipindi anavyoomba kwamba mimi nitaonyesha vipindi moja, mbili, tatu, kiwepo na kipindi cha ngoma za kienyeji kwenye tv. Iwe ni utaratibu kwa sababu sisi kwa mfano kule Usukumani tuna ngoma nyingi na nadhani hakuna kabila lenye ngoma nyingi kama Wasukuma. Tuna ngoma za gugobogobo, wigashe, bugoyangi na kadhalika kuna ngoma nyingi zionekane, mbona makirikiri tunaiona kutoka Zimbwabwe?
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hotuba au kuchangia makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Rais na nianze na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Kwanza, nakubaliana na makadirio ya matumizi ya Wizara hii, naunga mkono kwa asilimia mia moja.
Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwanza kabisa niwape pongezi kwa kazi kubwa wanayofanya, wanafanya kazi kubwa ambayo ni ngumu, Mheshimiwa Waziri Simbachawene naona kwa kweli anapambana, anastahili sifa ya pekee, nimpe hongera kwa kazi kubwa anayoifanya. Mheshimiwa Waziri naomba aendelee kupambana asiwe discouraged na maneno ya watu, aendelee kufanya kazi kwa ufanisi, Watanzania wanasubiri huduma yake kwa hali na mali.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kutoa baadhi ya ushauri kutokana na changamoto zinazokabili Wizara hii kwamba shule zetu za msingi kwa kweli tunahitaji bajeti kubwa ya kutosha kwa maana ya kujenga majengo na hasa vyoo. Nimesoma ripoti ya Waziri, ratio ya vyoo kwa kweli inakatisha tamaa. Unakuta tundu moja la choo watoto wanaotumia ni wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama kwa muktadha wa afya kwa kweli sisi katika mkoa wetu na hasa Wilaya yetu ya Maswa tulipata tishio la kipindupindu kwani kuna baadhi ya shule kwa kweli zilistahili kufungwa. Nafikiri ungewekwa mkakati mzuri hata kama madarasa bado hatujajipanga vizuri na bado tunahangaika na madawati lakini tuhakikishe kwamba pawe na mazingira mazuri ya kupata huduma ya vyoo. Kwa kweli hali ya vyoo ni mbaya na inatishia afya za watoto wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile hukohuko katika shule za msingi tunaomba basi Walimu waendelee kuboreshewa mafao yao, Walimu wana hali ngumu. Wilaya ya Maswa Walimu hawana nyumba za kutosha na wanaishi kwenye mazingira magumu. Ndiyo sisi kama Halmshauri tunafanya kazi kupambana kujenga na tunajaribu kuwaelimisha wananchi, lakini Wizara iweze kuongeza nguvu kuhakikisha kwamba Walimu wanaishi at least kwenye nyumba ambazo zinatia moyo. Ukienda katika vijiji vya Wilaya yangu ya Maswa ukienda Masanwa, Budekwa na maeneo mengine kwa kweli kuna hali ngumu sana ya nyumba za Walimu. Hivyo, tunaomba Mheshimiwa Waziri atazame kwa kina ni namna gani anaweza akatusaidia.Mheshimiwa Naibu Spika, napenda tu kutoa ushauri kwenye Halmashauri pengine Halmashauri yangu ya Maswa na Halmashauri zingine. Katika ujenzi wa maabara ukienda Wilaya zingine kwa kweli watu wamefanikiwa wamejenga maabara na wameweka vifaa. Mimi katika Wilaya yangu ya Maswa tuna mahitaji ya maabara 128, lakini tuna maabara nane tu ambazo zimekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri ukatafutwa uwezekano au utaratibu Halmashauri zikaweza kukopa benki fedha nyingi kuhakikisha miradi ya maabara inakamilika. Nina maana Serikali iziwezeshe Halmashauri ziweze kukopesheka. Ukipiga hesabu ya harakaharaka kwa mfano mimi nishapauwa maabara karibu 90 zinahitaji kukamilishwa na kuwekewa vifaa, inahitajika shilingi bilioni 3.5 ili kuweza kukamilisha. Halmashauri inakusanya fedha ndogo sana, ukienda kuwachangisha wananchi kwa kweli wananchi wangu hawana kipato kikubwa, kuchangisha kiasi hicho itachukua miaka, watoto wa Maswa hawataingia maabara kujifunza kisa wazazi wao hawana fedha, kisa wazazi wao ni walalahoi.
Halmshauri zetu zinakopesheka kwa riba ndogo na ikiwezekana tupewe muda mrefu. Mimi nilijaribu kwenda CRDB kuwaomba kwamba Halmashauri yetu ikope, tukapiga mahesabu ya shilingi bilioni 3.5 inahitaji tulipe zaidi ya milioni 80 kwa mwezi na hawataki kwa muda mrefu wanataka ndani ya miaka mitatu tuwe tumelipa lile deni.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunaomba Halmashauri zikopeshwe na zipewe muda mrefu wa kulipa ili kusudi tuweze kupata fedha nyingi kwa wakati mmoja, tutafute wakandarasi wanaoweza kujenga zile maabara, watoto wetu wakaingia kujifunza ili sisi wazazi na Halmashauri tukaendelea kulipa deni. Naomba sana utaratibu huu ufanyike ili kusudi Halmashauri nyingi ziweze kupata maabara.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha upande wa shule vilevile kwamba maabara zinajengwa, ndiyo, maeneo mengine wameshajenga lakini suala la madawati nalo linashughulikiwa. Napenda kutoa pongezi kwa suala hili na naomba nguvu ya kutengeneza madawati inayotumika iendelee. Nashukuru kwa Wilaya ya Maswa sasa hivi madawati tunapata na nashukuru kuna fedha imerudi, Naibu Spika umerudisha fedha kwamba Wabunge tutapatiwa madawati.
Mheshimiwa Naibu Spika, nami naungana na wenzangu kusema kwamba madawati yale tunayaomba yaje kwa wakati tuyapeleke na sisi Wabunge tushiriki kuhakikisha madawati yale tunayapeleka maeneo husika, kwa sababu ni fedha zinazotokana na Bunge basi tunaomba wakati madawati yanapelekwa, basi sisi twende tukayakabidhi tuoneshe kwamba yale madawati yaliochangiwa ni sehemu ya fedha zinazotokana na Bunge.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la wazabuni. Kuna maeneo mengine nafikiri Wizara ilitoa ahadi kwamba itahakikisha wazabuni wanalipwa madeni yao. Imefika wakati sasa waje Wilaya yangu ya Maswa wahakiki madeni hayo na kuhakikisha wazabuni wale wanalipwa madeni yao. Wilaya ya Maswa tumepata fedha kidogo, shilingi milioni 18 tu tunasema haitoshi, kuna shule ya Maswa Girls, Binza Day, kuna wazabuni wanadai madeni makubwa Serikali haijalipa. Nafikiri Mheshimiwa Waziri ataiangalia Wilaya ya Maswa ili waweze kulipa madeni hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kuungana na wadau wengine kwenye masuala ya utawala bora, naomba nichangie kidogo. Kwenye utawala bora tumeona jinsi watumishi hewa walivyokuwepo, natoa pongezi kwa Mheshimiwa John Pombe Magufuli kwa kuhakikisha watumishi hewa wanaondoka katika nchi hii. Tunaomba juhudi ziendelee kufanyika, tuendelee kuhakikisha kwamba wale ambao walishiriki kuhakikisha kwamba kuna wafanyakazi hewa wanachukuliwa hatua ili liwe fundisho haya mambo yasiendelee kujirudia tena. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini vilevile napenda kutoa ushauri kwa Serikali kwamba ili kuondokana na watumishi hewa kuna maoni yametolewa hapa kwamba tuwe na system ambayo ni nyepesi ya kuweza ku-identify nani amefariki, nani kaacha kazi na nani kaajiriwa ili pawe na system ambayo inaweza ika-respond haraka. Pia ikiwezekana pawe na intergrated systems ambazo zina-connect data zote kwa watu wote nchini kwa mfano, Kitambulisho cha Taifa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna dada mmoja alizungumza kwa upande wa pili alisema tuwe na intergrated system kwa maana ya kujua mtu aliyefariki, mtu ambaye ameajiriwa, pawe na system nyepesi kuweza kujua ni nani hewa, nani ambaye si hewa ili kusaidia Taifa lisiweze kuingia kwenye hasara kubwa ya kulipa mishahara mikubwa kwa watumishi hewa na kuondokana na hasara kubwa ambayo tulikuwa tunaipata.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumalizia kwa kusema kwamba nampongeza Mheshimiwa John Pombe Magufuli na Baraza lake la Mawaziri tumekwenda kwenye bajeti ambayo inaonekana ni ndogo lakini ni attainable. Ni bajeti ambayo tunaweza kukusanya fedha na tunaweza kuzitumia kwa jinsi bajeti ilivyopangwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatoa pongezi kwa sababu siku za nyuma, bajeti zilikuwa zinaonekana ni kubwa lakini utekelezaji wake ulikuwa hauzidi asilimia 50, utekelezaji wake ulikuwa ni asilimia 30 mpaka 40, unakuwa na bajeti kubwa ambayo haitekelezeki. Tunapenda kutoa pongezi kwa wakati huu hata kama inaonekana bajeti ni ndogo lakini ni ya ukweli, tuendelee kupambana na tufanye kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuunga mkono hoja na nakushukuru sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2015, Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 na Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa nianze kwa kukupa pongezi wewe mwenyewe kwa kazi nzuri unayoifanya. Tunamuomba Mwenyezi Mungu akujalie afya njema uendelee hivyo hivyo, kazi yako iko safi, tunaona juhudi zako, Mungu akubariki sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nitoe pongezi kwa Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwa hotuba yake nzuri aliyeitoa. Nimpongeze kwa bajeti nzuri ambayo kwa kweli ni ya kihistoria na utekelezaji wa bajeti hii kama kweli itatekelezeka kwa asilimia zaidi ya 80 Tanzania itakuwa imeweza kwenda mbele zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaipongeza bajeti hii kwa kuangalia umuhimu wa maendeleo. Kwa kweli katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi uliopita mwaka jana 2015 tuliahidi mambo mengi sana. Jambo kubwa tuliloahidi ilikuwa ni kuondoa umaskini na kuondoa umaskini ni lazima tujikite kwenye kilimo na kwenye shughuli mbalimbali ambazo zitaweza kuondoa umaskini wa wananchi wetu. Tukiangalia hata katika bajeti hii inaonesha asilimia 40 inakwenda kwenye matumizi ya maendeleo.
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile tunatoa pongezi kwa sababu maendeleo bila elimu na yenyewe ni tatizo. Tumeona katika bajeti hii asilimia 22.1 imekwenda kwenye maendeleo ya elimu, tunawapongeza kwa hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukumbuke kwamba katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi tuliwaahidi akina mama kwamba watakapochagua Serikali ya Chama cha Mapinduzi basi mama hatapata mzigo wa kutafuta maji kwenye vyanzo mbalimbali vya mito na visima na kwamba tunakwenda kukomesha tatizo la akina mama kujihimu asubuhi kwenda kutafuta maji. Katika bajeti hii tunaona imetengwa asilimia 4.8 kwa ajili ya maendeleo ya maji. Tunaomba juhudi zifanyike, utekelezaji uwe wa asilimia 100. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tuliwaahidi akina mama na watoto kwamba kwa kuchagua CCM mwaka 2015 huduma za afya zitaboreshwa. Tukiangalia katika bajeti iliyopo asilimia 9.5 imetengwa kwa ajili ya maendeleo ya afya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunawaombea na kwa kushirikiana na Watanzania wote tufanye kazi kwa juhudi ili yale malengo yaliyopangwa yaweze kutimia. Vilevile tuweze kuwaondolea kero wananchi na kutimiza ahadi ya Chama cha Mapinduzi ilizowaahidi wananchi katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi mwaka 2015. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika haya nina changamoto ninazoziona na naweza nikachangia zaidi. Tukienda kwenye suala la kodi ya majengo, Umoja wa Madiwani na Mameya wa Miji wamekaa na kutoa tamko kwamba hawakubaliani na maamuzi au mapendekezo aliyoyatoa Mheshimiwa Waziri katika bajeti hii. Wanayapinga kwa sababu wanasema kwamba Mkoa wa Dar es Salaam ulianza kama piloting katika ukusanyaji wa kodi ya majengo kwa maana ya Kinondoni,Temeke pamoja na Ilala, kwa Wilaya zote tatu za Mkoa wa Dar es Salaam lakini matokeo hayakuwa mazuri, ukusanyaji wa kodi za majengo haukuwa mzuri, wanakuja na maoni ya kusema kwamba mapendekezo haya yabadilishwe. Mimi nina maoni kwamba, kama tunaamua kwenda huko, nia ni njema tunataka tukusanye kodi za majengo lakini kama piloting results zake hazikuwa nzuri mmeona nini ambacho kitakwenda kurekebishwa ili TRA iweze kukusanya kodi za majengo? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama kuna changamoto zilionekana Dar es Salaam, je, tutazi-tackle vipi kuanzia tarehe 1Julai, 2016? Nasema hivi kwa sababu tunaweza tukaamua TRA kukusanya kodi ya majengo na ukitazama Halmashauri nyingi zinategemea kodi ya majengo kuanzia asilimia 30 mpaka asilimia 60 leo tunawaondolea, je, sisi tumejidhatiti kwa namna gani? Je, tutapeleka pesa zinapohitajika?
Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile wanalalamika kwamba wana changamoto za mikopo katika Halmashauri zao na wamekwishaingia mikataba na mabenki. Je, TRA ikikusanya hizi Halmashauri zitalipiwa madeni katika mabenki kupitia huu mfumo wa kupitia Hazina? Nafikiri Waziri aje atueleze na awape amani Mameya ambao wamekusanyika na wengine wamekuja hapa jana toka Dar es Salaam, wamegawa tamko lao kwa Wabunge wanalalamika kwamba uamuzi huu unakwenda kuwaondolea uwezo na hivyo Halmashauri zitakufa na njaa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni kuhusu kodi za mazao. Tunashukuru wameondoa kodi hasa kwenye mazao ya mbegu ambazo zinazalisha mafuta na kuweka kodi kwenye crude oil kwa maana ya mafuta yanayotoka nje kwa ajili ya mafuta ya kula. Tanzania tunatumia zaidi ya tani laki nne kwa mwaka na mafuta tunayo-import yanatokana na palm. Leo tumeyawekea kodi, nakubali nia ni nzuri lakini tumejipanga vipi kuzuia bei ya mafuta kupanda? Kwa sababu kama tumeweka kodi lazima bei ya mafuta itapanda na kama ikipanda hata chipsi mtaani itapanda bei kwa sababu mafuta ya alizeti kidogo gharama yake ni kubwa. Nafikiri kidogo tungeweza kwenda taratibu, tusiende pupa kwa sababu tutatengeneza bei kubwa ya mafuta ya kula na tutajikuta tunashindwa. Nia ni njema tunakubaliana na ninyi lakini tuangalie ni namna gani ya kuweka unafuu kusudi tupate mafuta kwa bei ya chini. Chakula kinacholika mtaani mama lishe wanapika kwa kutumia mafuta ya palm oil, japokuwa kweli yana matatizo kwa sababu yana cholesterol lakini tuangalie ni jinsi gani ya kuingia katika kuboresha uzalishaji wa mafuta ya ndani ambayo yatakidhi mahitaji ya mafuta tunayotoa nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine nilishatoa ushauri kwamba kuna zao la pamba, watu wa Mkoa wa Simiyu wanalima pamba, bei ya pamba inakwenda kuporomoka. Inaporomoka kwa sababu hakuna mikakati ambayo inaonesha kwamba Serikali iko serious kumuokoa mkulima wa pamba. Bei ya pamba inaelekea kudorora na percent kubwa ya pamba tunayolima tunapeleka nje, je, tunajiandaa vipi kuwa na viwanda vyetu vya ndani ambavyo vitafanya mkulima wetu alime kwa uhakika wa soko, alime bila kuogopa bei? Sasa hivi kuna directive price inatolewa ambayo inamkandamiza mkulima. Sasa hivi mkulima anayelima pamba anabadili kilimo cha pamba anakwenda kwenye alizeti kwa sababu kilimo cha pamba hakilipi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba ianzishwe Wizara ya textile kama inawezekana tuamue ku-specialize ku-produce nguo tuuze katika soko la East Africa ambalo lina population ya watu zaidi ya milioni 100 sasa hivi kwa sababu nguo zina demand kubwa. Mtoto akizaliwa leo anatumia nguo, unapoishi unakuwa unatumia nguo, unapofariki unafunikwa na nguo, matumizi ya ngua yako juu, lakini tunalima pamba tuna export, kwa nini tusiwe na viwanda vilivyojitosheleza kwa maana ya kuzalisha nguo na tukauza katika soko letu la East Africa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tumeweka kodi kwenye mitumba kwa sababu tunadhani tunaweza tuka-produce nguo. Nachosema tuna-promote soko la China, watatuletea nguo hapa mpya, nguo za mitumba tutaziwekea kodi lakini sisi wenyewe hatuzalishi nguo. Tunaomba Mheshimiwa Waziri mlitazame suala hili kwa upana wake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi hii, napenda kuunga mkono hoja. Ahsante sana.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi kwa upande wa Serikali basi tuanze kutoa maelezo kwa upande huu.

Kwanza kabisa nipende kushukuru kwamba Waheshimiwa Wabunge wengi wametoa mawazo mengi tofauti katika kuchangia huu mpango wa mwaka. Mawazo ni mengi na nashukuru mawazo mengi ni mazuri lakini na mimi kwa kujikita kwa upande wa madini kulikuwa kuna mawazo machache kwa Wabunge ambayo waliyatoa hasa walijikita katika upande huu wa madini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kabla sijajibu hoja hizo awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayoifanya. Tumeona anafanya mambo mengi ambayo kwa kweli yalikuwa hayana majibu, lakini kwa uwezo wake Mheshimiwa Rais na uzalendo wake ameonesha dhahiri kwamba ana nia thabiti na ya dhati kuhakikisha kwamba analinda rasilimali ya nchi yetu, anahakikisha kwamba rasilimali ya nchi yetu inakuwa na tija kwa uchumi wa nchi yetu. Kwa hilo Mheshimiwa Rais tunampongeza sana kwa kazi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile nichukue fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha hii Wizara mpya ya Madini. Wizara hii ilikuwa imeungana na Wizara ya Nishati na Madini na ukitazama ni kwamba tunatambua kwamba madini ni sekta nyeti, ni sekta ambayo ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi yetu. Hivyo Mheshimiwa Rais aliniteua mimi na Mheshimiwa Angellah Kairuki tuweze kuongoza Wizara hii lakini ukitazama kwa kina ni kwamba Mheshimiwa Rais alitaka tija katika Wizara hii ya Madini. Wizara hii imeundwa kwa maana ya kwamba tuongeze efficiency ya kusimamia rasilimali ya nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua mchango wa uchumi katika nchi yetu rasilimali ya madini ilikuwa inachangia kiwango kidogo sana, asilimia 3.7 lakini sasa hivi kwa juhudi zake Mheshimiwa Rais ni kwamba sekta ya madini inachangia zaidi ya asilimia 4.3 katika uchumi wa nchi yetu. Hivyo basi mimi na mwenzangu tuna kazi kubwa kwa kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Madini kuhakikisha kwamba tunaongeza tija kupitia hii sekta ya madini kuhakikisha kwamba uchumi wetu unaimarika na tunakwenda kuimarisha uchumi kwa maana ya kwamba tunakwenda kupandisha kiwango hicho kilichopo cha asilimia 4.3 na kwenda mbele zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa na Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na tumefanya mabadiliko yake ambayo ni ya mwaka 2017. Mabaadiliko haya ni makubwa lakini yalitazama sana katika sehemu nne ambazo ni muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya kwanza ilikuwa ni kuua ile Tanzania Mineral Auditing Agency (TMAA) na jambo la pili lilikuwa ni kuunda Tume ya Madini ambayo mpaka sasa kama Wizara tupo katika kufanya restructuring kwa maana ya kuitengeneza hii Tume na kuianzisha ili sasa Tume hii iweze kusimamia sekta ya madini inavyostahili, kwa maana ya kutoa leseni, kusimamia ku-regulate sheria na kanuni za masuala ya madini ili kusudi madini yetu yaweze kuongeza tija katika uchumi wa nchi yetu. Kwa hiyo, kwa muda mfupi ujao, nadhani hadi kufikia mwisho wa mwaka huu Tume hiyo itakuwa tayari na itakuwa imeanza kazi kuhakikisha kwamba inasimamia vizuri sekta hii ya madini na tuweze kupata tija kutokana na madini ambayo tunachimba nchini kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu nyingine ya sheria hii ilikuwa ni sehemu ya kuongeza kodi ya royalty (mrabaha), kutoka asilimia nne kwenda asilimia sita na kutoka asilimia tano kwenda asilimia sita kwenye madini ya vito na madini ya metallic. Vilevile kuongeza gharama au kuongeza kodi ya clearance ambayo ni asilimia moja. Mchakato huu hata kabla ya kuanzisha Tume hiyo, umeshaanza, sasa hivi wachimbaji wanalipa royalty asilimia sita. Hii ni hatua kubwa, ni hatua nzuri ambayo itatuongezea kipato katika mrabaha na Serikali itaweza kuneemeka zaidi na madini haya tofauti na ilivyokuwa kipindi cha mwanzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya ndiyo mambo ya mwanzo, naweza kusema ni utangulizi kwa ujumla wake. Ninapenda kusema na niwaeleze Watanzania kwamba, tunakwenda kudhibiti utoroshaji wa madini kwa kuunda Tume hii na marekebisho ya sheria. Tunakwenda kuhakikisha kwamba, madini yetu tena hayatoroshwi, hayapiti njia za panya, hayapiti njia zisizo sahihi, tunataka kwamba wachimbaji wote wapitie utaratibu unaostahili ili waweze kulipa kodi zote kwa TRA na vilevile waweze kulipa mrabaha ili Serikali iweze kupata kipato chake ambacho kinastahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushahidi umeonesha Mheshimiwa Rais, tarehe 20 Septemba, 2017 alipokuwa Mererani, alitoa amri ya kujenga ukuta unaozuia yale maeneo yote ya machimbo ya Tanzanite. Ujenzi huo umeanza toka tarehe Sita mwezi huu na ujenzi huo unakwenda kwa kasi ya hali ya juu. Jeshi letu la JKT liko site linafanya kazi ya construction na kwa hali iliyopo sasahivi ni kwamba, kuna wanajeshi pale wa kutoka JKT zaidi ya 2,000 na wanafanya kazi hiyo na wataifanya kazi hiyo kwa mkataba unavyosema, watafanya kazi ndani ya miezi sita na fedha za ujenzi wa ukuta huo wamekwishapewa asilimia 80. Kwa hiyo, tuna hakika kwamba ukuta ule utajengwa na tutadhibiti utoroshaji wa madini kutoka eneo la Mererani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Mheshimiwa Rais alitoa amri ya kwamba, tujenge mnada ambao utakuwa ni Mererani ambao mnada huu utatumika kwa watu wanaokuja kununua madini ya Tanzanite katika Mnada wa Mererani. Hapa tunavyozungumza pale Mererani tumeshapata eneo la EPZA ambalo shilingi bilioni 2.2 imetolewa kwa ajili ya ujenzi wa haraka wa mnada ule, ukishakamilika ujenzi ule kwa muda mfupi ujao, basi mnada ule utafunguliwa, madini ya Tanzanite, maonesho ya madini, wanunuzi watakuja pale watanunua na watalipa mrabaha, watalipa ili tuweze kupata kipato chetu kama kinavyostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika michango mbalimbali kuhusiana na utoroshaji wa madini hata sheria inasema, sasa hivi tuna wataalam wazuri, wathaminishaji wa madini yetu. Ukiangalia kwenye upande wa Almasi tuna wataalam wazuri, mfano mzuri ni juzi tu hawa Wiliamson Diamond Limited (WDL) waliweza kuzalisha Almasi. Almasi ile katika kutolewa kuisafirisha Serikali kwa juhudi zake ilikamata na kuangalia, kulinganisha uthaminishaji wa mwanzo na wa pili, tukakuta thamani ya Almasi zile ni kubwa, Serikali ikazuia uuzaji wa zile Almasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, WDL waliendelea kuzalisha. Walizalisha tena carat 39,000 na zikathaminishwa kwa kiasi cha shilingi bilioni nane na wataalam wetu, lakini kupeleka Almasi ile kwenye soko la Almasi, soko la mnada la Antwerp, kwa mara ya kwanza tumeweza kuuza Almasi yetu kwa njia ya mnada kwa dola za Marekani bilioni 10. Hii ni hatua kubwa ambayo Serikali imechukua na ni ya kumpa moyo Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa anayoifanya. Kwa kweli hiyo ni hatua kubwa na Mheshimiwa Mwenyekiti na wewe ni shahidi unalielewa hili. Kwa kweli, utoroshaji wa Almasi ulikuwa ni wa hali ya juu, lakini kwa namna tunavyokwenda tunakwenda kudhibiti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa yako katika ule mzigo wa pili uliokwenda kuuzwa kwa dola milioni 10, ndani ya almasi zile ilikuwepo almasi adimu ambayo inapatikana Tanzania ambayo tunasema inaitwa pink diamond, iliuzwa kwa dola milioni mbili, kipande kimoja tu chenye carat tano. Kwa hiyo, tunaweza tukaona kwamba, kumbe tulikuwa na pink diamonds nyingi ambazo zinakwenda bila kuwa recorded katika zile takwimu ambazo zilikuwa zinaandikwa, kwa hiyo, hiyo ni hatua kubwa tumeweza kufikia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado tunaendelea na hatua za ku-control utoroshaji wa madini. Juzi tumekamata kilo nne za dhahabu katika Bandari ya Zanzibar, tumezikamata dhahabu ambazo zina thamani ya milioni 500. Tunaendelea kuimarisha ulinzi mipakani kuhakikisha kwamba utoroshaji wa dhahabu unasimamishwa, lakini wakati huo huo Serikali ina juhudi ya kuanzisha minada mitano mikubwa ambayo itakuwa inauza dhahabu. Tutauza dhahabu kwa njia ya wazi ili watu waje wanunue dhahabu na waweze kulipa ushuru, waweze kulipa na mrabaha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile minada yetu hii tunatakiwa tuitengenezee miundombinu mizuri kwa maana ya usalama, miundombinu ya umeme, miundombinu ya maji, miundombinu ya usafirishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mjadala uliokuwa unaendelea watu wamepiga sana kelele kuhusu kutengeneza Uwanja wa Ndege Chato. Kule Chato tunahitaji usafirishaji wa madini yetu, tunahitaji kusafirisha watu, tunahitaji kusafirisha vifaa, uwanja wa ndege wa Chato ni muhimu sana kujenga pale Chato. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda pale Bulyanhulu wana uwanja wa ndege. Wale mabwana wamejenga uwanja wao wa ndege wa kuweza kusafirisha bidhaa zao, Kwa nini Serikali tusiwe na uwanja wetu? Kwa nini Serikali tusiweke uwanja wa kisasa wa kuweza kusafirisha bidhaa zetu za madini kupitia uwanja wa Chato? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wameongelea kuhusu umbali wa kutoka Mwanza. Kutoka Mwanza hadi Geita ni kilometa 185, kutoka Geita kwenda Chato ni zaidi ya kilometa
120. Kwa hiyo ni kilometa 120 na hizo 180 ni zaidi ya kilometa 300 kutoka uwanja wa ndege wa Mwanza, hapa katikati usafirishaji wa dhahabu ni hatari sana kusafirisha dhahabu umbali wa zaidi ya kilometa 300.

Kwa hiyo, uwanja wa Chato ni muhimu kuuweka pale na hii ni kwa manufaa ya Watanzania wote na wala sio kwa manufaa ya watu wachache kama wenzetu walivyokuwa wakieleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017 na Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2017.
NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. STANSLAUS H. NYONGO): Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii jioni ya leo. Kwanza kabisa natoa shukrani za dhati kabisa kwa Kamati ya Nishati na Madini kwa kazi nzuri walioifanya. Kamati ya Nishati na Madini kipekee kabisa tumekuwa tukipokea mchango mkubwa, ushauri maelekezo mbalimbali kutoka katika Kamati hii. Kwa kweli ushauri wao tunaupokea na ni ushauri mzuri na tutaendelea kushirikiana na Kamati hii kwa maana kuisukuma Sekta hii ya Madini iweze kusonga mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile nawashukuru sana Waheshimiwa Wajumbe 14 waliochangia, wametoa michango mizuri michango yenye mashiko. Namshukuru na mama yangu Mheshimiwa Anne Kilango kwa complement aliyotupa. Kweli kabisa kwamba Wizara yetu imekuwa ikikusanya maduhuli kwa hali ya juu. Tunapambana usiku na mchana kuhakikisha tunakusanya maduhuli ambayo tunayapeleka katika Mfuko wa Serikali na Watanzania wote waweze kupata fedha au kupata huduma mbalimbali kutokana na makusanyo tunayokusanya kutoka katika Wizara yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli tunakusanya kwa kiasi kikubwa na ni mfano tuseme wa kuigwa kwa sababu mpaka hapa tulipo tuko katika nusu ya mwaka wa fedha wa kibajeti. Tumekusanya zaidi ya asilimia 80.4 ya maduhuli. Tunashukuru sana mama kwa kuliona hilo na tunashukuru kwa pongezi ulizotupa; na tutaendelea kukaza msuli kuhakikisha kwamba tunaendelea kukusanya maduhuli ili Watanzania wote waweze kupata huduma kutokana na mapato yanayopatikana katika Sekta ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, michango mingi imeongelewa, nami napenda kuungana na waliochangia hasa katika ukurasa wa tano wa taarifa ya Kamati kuhusiana na mradi wa Buckreef. Ni kwamba STAMICO iliingia mkataba na Buckreef na kampuni ya TAZAM 2000 wakatengeneza Kampuni ya Bacliff ambapo STAMICO wanashikilia asilimia 45.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama ilivyosema Kamati tumelitazama hili, huyu mbia kwa kweli havutii na tumeamua kuangalia kwa namna nyingine ambapo STAMICO inawabidi wakae chini na wanasheria waweze ku- review mkataba huu ili tuweze kuangalia na ikiwezekana tutafute mbia mwingine ili STAMICO wahakikishe kwamba yule mbia atayepatikana basi aweze kufanya kazi vizuri na uchimbaji uendelee na Serikali iweze kujipatia kipato. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna hoja nyingine ambayo imeongelewa kuhusu pesa za ruzuku pamoja na pesa za mikopo zilizokuwa zinatolewa na Wizara. Kweli kabisa kwamba kuna watu walikuwa wanapokea ruzuku kutoka Serikalini, yaani kutoka Wizara ya Madini kupitia Benki ya TIB, walikuwa wanapata fedha kwa ajili ya kuendeleza migodi. Ilikuwa ni fedha maalum kwa kuendeleza wachimbaji. Kuna wachimbaji wengine walifanikiwa, wamefanya vizuri sana. Kuna wachimbaji wengine wamekwama, lakini inaonekana kabisa walikuwa na juhudi za kufanya vizuri lakini wamekwama. Wachimbaji wengine walichukua zile fedha na kwenda kuzitumia kwa matumizi mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wachimbaki tisa kwa taarifa tulizonazo. Napenda kuchukua nafasi hii kuwaeleza kwa mara mwisho, nilitoa tamko nikiwa Singida, warudishe hizo fedha. Nachukua nafasi kusema kwamba nimetoa tena tamko la mwisho, wala sina haja ya kutoa siku nyingi, ni kwamba ndani ya hizi siku 14 zinazofuata, wajisalimishe wenyewe, wazirudishe hizo fedha kwa sababu wamewanyima Watanzania wengine kuweza kupata fedha hizo na kufanya shughuli za uchimbaji wakaweza kuendeleza Sekta hiyo ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la wachimbaji wadogo, Wizara imejipanga vizuri, sasa hivi tumeshatenga zaidi ya heka za mraba laki 238 kwa ajili ya kuwapa wachimbaji wadogo waweze kuchimba, lakini tunahakikisha kwamba wachimbaji hao wadogo wakae ndani ya vikundi, tuwatambue tuwarasimishe wachimbe ili na Serikali nayo iweze kukusanya kodi, maduhuli na Halmashauri husika ziweze kupata ushuru wa huduma (Service Levy).

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala la GST limezungumziwa. GST ndiyo Taasisi pekee ambayo inaweza ikafanya kazi vizuri kwa maana ya kufanya tafiti mbalimbali na kuweza kuwasaidia wachimbaji wadogo kuwapatia maeneo ambayo tayari yameshafanyiwa utafiti, yana taarifa za kutosha kwa maana maeneo ambayo yana dhahabu ya kutosha au madini mengine ambayo tayari yamefanyiwa utafiti wa kutosha ili kuepusha wachimbaji kuchimba kwa kubahatisha. Tumejipanga na GST na kuja kuleta taarifa hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumalizia. Kwa migogoro iliyopo, tunaifanyia kazi na hasa ule mgogoro wa North Mara na watu wa Nyamongo, maongezi yanaendelea. Taratibu zinafanyika na makundi yote tunayashirikisha. Tunachotaka ni Serikali itatue mgogoro wa Nyamongo ili wachimbaji waendelee na wananchi waendelee na shughuli zao za ujenzi wa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwa kusema kwamba Kamati imeshauri kwamba kuna wachimbaji wa Kitanzania tuwape maeneo, akiwepo mchimbaji wa Busolwa. Tunahakikisha mchimbaji huyo tunampa eneo ili aongeze muda wa mgodi, Watanzania waneemeke na ajira katika mgodi huo na Serikali tuendelee kupata kodi kutoka katika mgodi huo kwa sababu mgodi huo unafanya kazi. Hakuna haja ya kumnyima eneo ambalo tunadhani Serikali tunaweza tukampa na kukamsaidia mchimbaji mdogo na wa kati.

Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania wengine wote wanaotaka kuwekeza katika Sekta ya Madini, tuko tayari kuwasaidia kuwapa maeneo mazuri wachimbe na tutaweza kuwasaidia kwa namna ambayo watatoa ajira kwa Watanzania wengine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 – Wizara ya Madini
NAIBU WAZIRI WA MADINI (MHE. STANSLAUS H. NYONGO): Mheshimiwa Niabu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nimshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema na fadhila kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kusimama hapa mbele ya Bunge lako Tukufu ikiwa ni mara yangu ya kwanza kabisa kusimama ili kujibu hoja za Wabunge wa Kamati yetu ya Nishati na Madini katika hotuba yetu ya kwanza kabisa ya kuomba Bunge lako Tukufu kuidhinisha kupitisha bajeti ya Wizara hii mpya ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, kwa kuniamini na kuniteua kuwa msaidizi wake kwa kunipa majukumu ya kuwa Naibu wa Waziri wa Madini ambapo Wizara hii ni mpya na yenye majukumu mazito ya kulinda rasilimali hii muhimu kwa nchi yetu. Napenda kumhakikishia Rais wangu na Watanzania wote kuwa nitakuwa mwaminifu na mchapa kazi mkubwa, nitatumia uwezo wangu, nguvu zangu, uaminifu wangu, uadilifu wangu kusimamia na kuongoza sekta hii muhimu na bila kumuangusha Rais wangu na Watanzania wote kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kumshukuru Waziri wangu, Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki kwa ushirikiano na maelekezo anayonipatia katika kutekeleza majukumu ya Wizara hii mpya. Kipekee, namshukuru sana Mheshimiwa Kairuki maana yeye amekuwa ni mtu muhimu sana kwangu kwa jinsi anavyonipatia mbinu na maarifa ya kuongoza na kujiamini katika kutekeleza majukumu ya Wizara hii muhimu na yenye changamoto nyingi. Mheshimiwa Kairuki siyo mtu wa kujivuna kama mnavyomuona hapa ni mchapakazi na asiye mchoyo wa kukupa ujuzi na uelewa wa mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kunisaidia maarifa ya kutatua changamoto zinazotukabili katika Wizara yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze sana Mheshimiwa Doto Mashaka Biteko pacha wangu, kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Naibu mwenzangu wa Wizara ya Madini. Kipekee nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutuongezea nguvu katika Wizara yetu kwa kutambua uwezo usiokuwa na mashaka wa Mheshimiwa Doto Biteko. Basi ni uhakika kuwa changamoto na majukumu ya Wizara hii yenye changamoto nyingi sasa kwa umoja wetu, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Wizara hii wakiongozwa na Katibu Mkuu Prof. Simon Samwel Msanjila ni hakika kuwa tutaendelea kusimamia vizuri sekta hii na bila shaka yoyote tutaendelea kuhakikisha tunatekeleza Ilani ya chama chetu Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee kabisa niwashukuru sana familia yangu kwa ushirikiano mkubwa wanaonipatia katika kutimiza majukumu yangu. Kwa kweli wananivumilia sana kipindi napokuwa sipo nao katika kutimiza majukumu yangu ya kulitumikia jimbo langu na Taifa langu kwa ujumla. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa umuhimu wa kipekee kabisa napenda kuwashukuru sana wananchi wa Jimbo Maswa Mashariki, kwanza kwa kunichagua kuwa Mbunge wao. Nina imani kuwa hawakukosea kunichagua na ninawaahidi kuwa nitaendelea kuwatumikia kwa nguvu zangu zote na kwa kila hali na mali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niendelee kuwashukuru sana kwa kunivumilia kuwa mbali nao pindi napokuwa katika kutekeleza majukumu yangu ya Unaibu Waziri wa Madini. Napenda kuwaahidi kuwa nitaendelea kuwa nao katika kuhakikisha Maswa yetu inaendelea kupata maendeleo kadri tunavyotarajia na mambo mazuri zaidi wategemee yanakuja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla sijaendelea na hotuba hii, napenda kuunga mkono hoja ya Mheshimiwa Waziri wangu aliyoileta katika Bunge lako Tukufu. Baada ya kusema hayo, naomba sasa niendelee kwa kujibu baadhi ya hoja zilizojitokeza pindi Waheshimiwa Wabunge walipokuwa wakichangia bajeti hii ya Wizara hii ya Madini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wengi wamechangia na wamechangia vizuri sana. Kamati ya Nishati na Madini nayo imetoa mapendekezo yake, Wabunge waliochangia, wamechangia wengi kwa mdomo na wengine wamechangia kwa maandishi, napenda kuwaambia kwamba tumesoma maandishi yote na tumeona mawazo yao mazuri. Tunapenda kusema kwamba tutaendelea kuchukua ushauri wao na kuweza kuutendea kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile namshukuru AG kwa maneno mazuri aliyoyatoa leo, kwa lecture nzuri aliyotupatia, katueleza historia nzuri ya sheria za madini. Kwa kweli kila mmoja aliyesikia ameweza kuona tunatoka wapi na sasa tunakwenda wapi katika kusimamia hii sekta yetu muhimu kabisa ya madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Katiba na Sheria ambaye naye ameelezea vizuri kuhusu mikataba na leseni ambazo kwa kweli toka siku za nyuma jinsi zilivyokuwa zikitukandamiza na mikataba mbalimbali ambayo ilikuwa inakandamiza maslahi ya nchi yetu. Ameeleza vizuri, ametusaidia kutupa somo zuri ambalo kwa kweli kila mmoja aliyesikia ameweza kuelewa na kuona ni jinsi gani tunavyoenda sasa kusimamia rasilimali yetu hii ya madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wengi wamechangia, tumepata pongezi nyingi sana, mimi Naibu mwenzangu pamoja na Waziri wetu. Napenda kusema kwamba kwa pongezi mlizotupa mmezidi kutupa chaji/betri ya kuweza kufanya kazi kwa moyo kwa sababu tunaona ni jinsi gani mmeridhika na kazi tunazozifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi nyingine iliyokuja ni jinsi gani Wizara yetu imeongeza kukusanya maduhuli. Tumeweza kukusanya maduhuli kupita kiasi ambacho kilikuwa kimepangwa, mpaka sasa hivi tuna zaidi ya 130% ya makusanyo ya maduhuli tuliyoyakusanya. Tumeweza kufanikisha kwa sababu kwanza kabisa tumeweza kurekebisha Sheria yetu ya Madini ya mwaka 2017 ambapo tumeongeza kiasi cha mrabaha kwenye madini ya metali pamoja na madini ya vito ambapo sasa tunakusanya 6%. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, makusanyo yameongeza na kwa kweli hii inatia moyo tutaendelea kufanya kazi hii ya kukusanya maduhuli kwa sababu Wizara yetu typically kazi yake ni kukusanya maduhuli. Tukishakusanya maduhuli haya tunapeleka katika Mfuko Mkuu na wenyewe utapeleka fedha kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo na kuweza kuleta maendeleo kwa Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wameongea mambo mengi naweza nikachambua moja baada ya lingine na siwezi kumtaja kila mmoja. Wengi wameongelea kuhusu tafiti mbalimbali ambazo kwa kweli ziko chini ya Taasisi yetu ambayo tunaiongoza katika Wizara yetu ya Madini yaani GST - Geological Survey of Tanzania, wameongea kwa kirefu. Kwa ujumla inaonekana kabisa GST wanahitajika kufanya kazi kubwa ya kufanya tafiti mbalimbali ili tuweze kuwasaidia wachimbaji wetu kuwapa taarifa mbalimbali za kijiolojia waweze kuchimba maeneo ambayo yana tija, yenye deposit nyingi ya madini, waweze kutumia fedha au mitaji yao kwa kuchimba maeneo ambayo wanaweza wakachimba kwa kupata faida ili waweze kupata fedha ambazo kwa kweli zitawasaidia katika kuinua uchumi wao.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile katika GST mambo mengi yameongelewa kwamba tafiti wanazofanya ni zile za awali. Wabunge wengi wamependekeza kwamba tuende mbele, GST iwezeshwe fedha waweze kufanya tafiti ambazo zinaweza kuona kiasi gani cha madini tuliyonayo ili iwe rahisi sasa tunapokwenda kumpatia mtu leseni, aidha, tuuze leseni kwa njia ya mnada hapo baadaye kwa kuona kabisa kwamba tuna deposit ya uhakika, mwekezaji anapokuja ikiwezekana tumuuzie leseni ambazo tuna uhakika kuna madini kiasi gani. Hiyo itatuwezesha kupata wawekezaji ambao kwanza watanunua pengine kwa mnada na watakapoweza kununua itakuwa na tija na sisi tutakuwa tuna uhakika kwamba anaponunua kwenda kuchimba tuna uhakika atachimba kwa kiasi gani na sisi Serikali tutapata kiasi gani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengi yameongelewa kuhusu STAMICO. Mheshimiwa Waziri wangu atakuja na ataeleza msimamo uliopo kuhusiana na STAMICO.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile ni kwamba kuna madeni mengi katika Migodi ya Buhemba na Kiwira. Madeni hayo mengine yalikuwa makubwa, Mheshimniwa Naibu Waziri mwenzangu ameeleza kuhusu madeni ya STAMIGOLD. Kuna madeni ambayo yalikuwa ni makubwa mno ambayo kwa kweli tulikuwa tunaona yana forgery lakini sasa tutatuma timu kwenda kuhakiki madeni hayo na tukishakupata uhakika wa madeni hayo basi Serikali itakapopata fedha itahakikisha kwamba inawalipa wale ambao wanadai wakiwemo wafanyakazi na wale watu ambao walikuwa wamechukuliwa maeneo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Waheshimiwa Wabunge wameongea kuhusu vifaa duni kwa wachimbaji. Napenda kusema kwamba bado Wizara yetu ina kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba tunawasaidia wachimbaji wetu kwa kuwapa elimu lakini kuangalia namna ya kuwawezesha kupata mitaji na kuweza kupata vifaa vya kisasa ili wachimbe kwa gharama ndogo waweze kupata return kubwa na wao itakuwa imewasaidia katika kujiendeleza katika miradi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wameongelea kuhusu mikopo, ni kweli kabisa wachimbaji wengi hawana sifa ya kukopeshwa na mabenki yetu. Wanapokwenda kukopa benki, benki haziko tayari kuwapa fedha kwa ajili ya ku-rise mitaji yao ni kwa sababu hakuna taarifa za uhakika, hakuna taarifa zinazoonyesha kuna deposit kiasi gani. Hivyo basi, sisi kama Wizara kwa kushirikiana na GST tunaangalia namna bora ya kufanya tafiti vizuri kuweza kuona deposit zenye uhakika. Deposit hizi pamoja na ripoti za GST ziweze basi kutumika kupeleka benki na kuweza kuwa-identify kwamba huyu mtu anaweza akakopeshwa kiasi fulani na atakachokopeshwa basi benki inakuwa na uhakika kwamba huyu mtu atarudisha na huyu mtu atabaki na fedha kwa maana ya kupata faida zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, masoko ya madini pia yameongelewa. Kwa kweli tunakwenda kujiandaa kutafuta masoko ya madini mbalimbali yakiwemo madini ya vito, dhahabu na madini mengineyo. Tunaangalia namna bora ya kuweka masoko, ikiwezekana katika madini ya dhahabu basi tuanze walau na masoko ya kila mkoa watu waweze kuchenjua madini yao, wapeleke sehemu, wanunuzi wafike pale, waweze kununua madini na Serikali tutakuwa pale na tutawapa support ya kutosha. Pia Serikali tutakuwa imara kusimamia kuweza kupata kodi yetu na sisi kuwapa export permit, kuwapa urahisi na kupunguza ile bureaucracy ya kupata export permit. Kwa hiyo, tuko tayari, tumejipanga na tutahakikisha kwamba kila mkoa tutaweza kuwawekea mazingira ya kuanzisha soko la madini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengi yameongelewa na Waheshimiwa Wabunge ikiwemo kodi. Ni kweli kabisa kuna kodi zingine ni nyingi, kwa mfano, kwenye dhahabu kuna kodi nyingi ambazo pengine baadhi ya wachimbaji wanashindwa ku-comply na kodi hizo. Tutaendelea kutoa elimu ya kodi, tutaendelea kutoa elimu ya kulipa mrabaha (royalty) ili wachimbaji waweze kuzifahamu kodi hizo, waweze kutunza nyaraka mbalimbali zinazohusiana na kodi ili kuweza kuwapa unafuu na kuweza kujikinga na kutozwa kodi mara mbili mbili yaani double taxation. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano withholding tax mtu anapolipa anashindwa kuweka risiti, anapokwenda kutoa madini yake ku-export TRA wanamchaji tena, wanapomchaji tena analalamika kwamba anachajiwa mara mbili. Hii ni kwa sababu watu hawa wengine wanakosa ile elimu ya kutunza nyaraka. Tunaangalia namna bora ya kuondoa kodi kero lakini wakati huohuo tutaendelea kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wachimbaji ili kodi hizo zisiwe mzigo kwao, waweze kufanya biashara vizuri na waweze kupata faida katika biashara hiyo ya uchimbaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo mengine yameongelea kuhusu mikataba, Mheshimiwa Waziri wa Katiba hapa ameelezea kuhusu mikataba mibovu. Suala hili limeelezewa kwa namna mbalimbali na Waheshimiwa Wabunge wameongea vizuri sana. Kwa somo la leo, nina hakika kabisa kwamba wameweza kupata somo la uhakika kwa maana ya kwamba uwelewa utakuwa umeongezeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kusema sisi pamoja na Wizara yetu tutaendelea kujipanga kama walivyopendekeza Waheshimiwa Wabunge tuwe na semina za mara kwa mara ili kuweza kuwaelimisha Waheshimiwa Wabunge kuhusu kodi mbalimbali, mikataba mbalimbali pamoja na shughuli za uchenjuaji wa madini kama vile tulivyofanya katika maonyesho ya madini tuliyoyaleta. Kwa maonyesho haya, watu wamejifunza, wengine walikuwa hawajawahi kuona tanzanite, kwa mara ya kwanza Waheshimiwa Wabunge wameona tanzanite na dhahabu na jinsi ya ku-process madini hayo. Mungu akitujalia tutaendelea kutoa elimu zaidi kwa Wabunge waweze kupata ufahamu na tunapoingia katika Bunge lako watu wawe wanachangia kitu wanachokifahamu na iwe rahisi kuweka michango mizuri na kupata ushauri mzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya mwaka 2017 imezuia ku-export raw minerals yaani madini ghafi. Watu wa Mundarara, Mheshimiwa hapa Kalanga amezungumzia, tulikwenda kule Mundarara tukaenda kutoa ahadi kemkem. Ahadi mojawapo ilikuwa ni kwenda kuwaeleza kwamba sheria hii na mabadiliko yake siyo mzigo kwa wachimbaji wadogo wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli raw minerals zimezuiliwa kutoka lakini tunaangalia namna ya kuja na mwongozo bora na wa kitaalam ambao utaweza kuonyesha tutaweza ku-process madini yetu katika kiwango gani na kile kiwango ambacho kinakubalika ku-export. Tutakapoleta mwongozo huo basi kila mchimbaji ataweza ku-comply na sheria hiyo na itakuwa siyo mzigo tena. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hivi watu wa Mundarara niwaeleze kwamba wasiwe na wasiwasi, ahadi tulizowapatia ziko pale pale, tutawaletea mwongozo wataendelea kuchimba kwa faida kubwa. Kama alivyosema Naibu mwenzangu pale Mundarara wamejenga nyumba nzuri na majengo mazuri, kwa kweli hali ya pale ukifika unaona kabisa fedha inayotokana na machimbo inakuwa na tija katika jamii inayowazunguka. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, limezungumziwa suala la CATA Mining. CATA Mining ni mgodi wa mchimbaji wa kati ulio katika Mkoa wa Mara. Huyu mchimbaji alikuwa na leseni sita yaani Primary Mining Licences ndani ya eneo la jeshi. Watu wamesema kwamba kuna mgogoro, Waheshimiwa Wabunge niwahakikishie hakuna mgogoro katika mgodi ule. Sasa hivi tumewashauri kwamba wakae na Jeshi la Wananchi Tanzania waelewane, Jeshi la Wananchi Tanzania lina ile surface right yaani anamiliki ardhi ya juu, yule mchimbaji amepewa leseni ya kuchimba pale kwa maana kwamba yeye ana mining right, kwa maana ana haki ya kuchimba pale, sasa wao wakae kwa pamoja na wamekwisha
kuelewana, sasa hivi ule upande wa pili ni kwamba zile Primary Mining Lisences zao sita zitakwenda kuunganishwa na kupata kitu kimoja ambacho tunaita Mining Lisences. Hiyo Mining Lisences itakuwa chini ya kampuni inaitwa CATA Mining yaani kampuni ya Mtanzania mmoja anayemiliki 50% na Mkanada anayemiliki 50%. Kwa umoja wao wataingia mkataba na Jeshi la Wananchi ili waweze kuchimba haraka na iwezekanavyo. Kwa kweli tunaona mgodi huu una potential kubwa kwa wananchi wa maeneo hayo, wananchi zaidi ya 400 ajira zao ziko pembeni, wameshindwa kufanya kazi kwa sababu mgodi huo umesimama wakisubiri mikataba hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawahakikishia kwamba mgodi huo baada ya kupata Mining Lisence wataanza operesheni, wananchi wa maeneo hayo wataweza kupata ajira. Vilevile sisi kama Serikali tutaendelea kupata kodi kutoka katika mgodi huo ili nayo iweze kupeleka kwa wananchi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mengine Waheshimiwa Wabunge wameyaongea, wameongea maneno mazuri, Mheshimiwa Kanyasu ameongea, kuna Wabunge wengi hapa wameongea na mzee wangu hapa Mheshimiwa Mwambalaswa katupa hongera nyingi. Kwa kifupi, kuna malalamiko ya kuchanganya leseni, unakuta kuna leseni ya utafiti na watu wengine wameomba leseni za kuchimba madini ujenzi. Wizara yetu tutaendelea kuhahakisha kwamba tunawapa leseni hizo watu waweze kuchimba madini ujenzi na tuna hakika kwamba yatawasaidia wananchi kupata material ya kuweza kufanya ujenzi katika maeneo yao, vilevile sisi Serikali tutapata marahaba kutoka kwenye madini ujenzi na kuongeza maduhuli katika Wizara yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, niendelee kukushukuru wewe na Bunge lako Tukufu, niwashukuru Wabunge kwa mawazo na maneno ambayo wametupa toka jana yametupa afya njema kwa sababu tumeona kwamba kweli Bunge letu lina upendo. Bila kujali upande wowote, wametoa mawazo mazuri na wametupa hongera nzuri. Mawazo yao waliyoyatoa tunayachukua, tutaendelea kufanya kazi kwa uhakika na tutaendelea kuhakikisha kwamba tunafuata ushauri wanaotupatia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, napenda tena kusema kwamba naunga mkono hoja hotuba ya Waziri wangu wa Madini, Mheshimiwa Angellah Jasmine Kairuki. Ahsante sana kwa kunisikiliza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Madini
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, naomba nikushukuru kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuhitimisha hoja hii ya Wizara yetu hii ya Madini.

Mheshimiwa Spika, nianze ka kutoa pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya katika kusimamia Sekta hii ya Madini lakini vilevile nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa uteuzi alioufanya kwa kuweza kumteua Waziri wangu Mheshimiwa Dotto Biteko mimi na yeye kusimamia sekta hii muhimu ya madini kwa kweli namshukuru sana na tunapenda kumwahidi kwamba hatutamwangusha, tutaendelea kufanyakazi vizuri zaidi.

Mheshimiwa Spika, niendelee kumshukuru vilevile tena Mheshimiwa Rais wka kumteua dada yetu Angella Kairuki kushika nafasi ya kuwa Waziri wa Mambo ya Uwekezaji ambayo itakuwa chini ya Waziri Mkuu. Ni hatua kubwa sana mbapo hata sisi kwa upande wa madini ina tija kubwa na itatusaidia sana katika masuala yote ya uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, niendelee kuishukuru Wizara ya Madini ikiongozwa na Katibu Mkuu, Profesa Msanjila kwa kazi kubwa anayoifanya tunasaidiana nae lakini vilevile niendelee kuwashukuru sana Wabunge kwa michango yao ambayo kwa kweli leo wamechangia hapa tumeona Kamati ambayo nayo imeweza kutoa maoni yake. Nipende kusema kwamba tunashirikiana vizuri sana na Kamati ya Nishati na Madini na tunafanya kazi bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunapeleka sekta hii ya madini kule ambapo kunastahili.

Mheshimiwa Spika, vilevile niendelee kuwashukuru wapiga kura wangu wa Jimbo la Maswa Mashariki kwa kuendelea kunivumilia kwa kazi kubwa ninayoifanya maana muda mwingi nakuwa niko nao mbali lakini kwa kweli wamezidi kunipa ushirikiano mzuri, tunaendelea kushirikiana nao kuhakikisha kwamba naendelea kusimamia Jimbo langu la Maswa Mashariki kupeleka maendeleo ambayo tulikuwa tumewaahidi wananchi, lakini vilevile wanaendelea kuwa na uvumilivu wa kunivumilia mimi muda mwingi ninapokuwa sipo Jimboni. Vilevile bila kusahau niishukuru sana familia yangu ambayo inanipa nguvu katika kufanya kazi zangu za Wizara.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, niendelee sasa vilevile na kuchangia hoja ambazo Waheshimiwa Wabunge wamezizungumza hapa.

Mheshimiwa Spika, awali ya yote nipende kusema kwamba tunaendelea kupongeza, kumpongeza Mheshimiwa Rais na kupongeza Bunge lako Tukufu kwa kukubali kupitisha au kubadilisha Sheria yetu ya Madini ya Mwaka 2010 na hayo mabadiliko ambayo tumeyafanya mwaka 2017. Kwa kweli kwa muda ambao tumeanza kutumia sheria hii tumeweza kuona mabadiliko makubwa ambayo yameweza kusaidiwa na sheria hii baada ya kufanya haya mabadiliko.

Mheshimiwa Spika, cha kwanza kabisa ni ile Serikali kumiliki asilimia 16 kwenye miradi yote ya migodi ya madini. Kwa kweli imeonekana kuwa na tija kubwa na watu wote, wawekezaji wote wa upande wa madini wako tayari kutoa asilimia 16 ambayo Serikali itakuwa inazimiliki japokuwa Kambi ya Upinzani walikuwa na wasiwasi kuona kwamba labda inamilikiwa na nani, lakini niwatoe tu wasiwasi Kambi ya Upinzani kwamba hii asilimia 16 sasa hivi iko chini ya Treasury kwa maana ya Hazina. Vilevile mapendekezo yao walikuwa wanayatoa kwamba iwe STAMICO, ok fine, inaweza ikawa STAMICO lakini inaweza ikawa kwa upande wa Treasury, lakini bado iko upande ule ule wa Serikali. Ile ownership ya 16 percent bado inamilikiwa na Serikali na Serikali inapopata gawiwo basi itapeleka maendeleo kwa wananchi.

Mheshimiwa Spika, vilevile kwa mabadiliko haya haya tunashukuru na kuona tija kubwa ambayo imekwenda hasa katika kubadilisha kiwango cha mrabaha kutoka asilimia nne na asilimia tano sasa hivi tunatoza asilimia sita kwenye madini ya metali na asilimia sita hiyo kwenye madini ya vito. Tumeona jinsi ilivyoweza kupandisha mapato na kuweza kupata maduhuli makubwa kutokana na ku-charge asilimia hiyo sita ikiwa ni pamoja na tozo jipya la asilimia moja kwa maana ya clearance fee. Kwa kweli niwashukuru wachimbaji wamejitolea na wame-comply vizuri na sheria hii na wanatoa hiyo tozo na kwa kweli hawana malalamiko yoyote.

Mheshimiwa Spika, isipokuwa tu niendelee kumshukuru tena Mheshimiwa Rais pale tarehe 21 Januari, 2019 baada ya kukaa na wachimbaji akaongea nao kwa kweli walitoa malalamiko mengi na hasa katika kodi ambazo zilikuwa zinatozwa katika sekta hii ya madini. Nishukuru kwamba baada ya kuondoa hiyo VAT pamoja na withholding tax kwa kweli unafuu umeonekana mkubwa na sasa hivi wengi wa wachimbaji wanaonekana kutoa ushirikiano katika kufanya biashara kwa sababu tumepunguza kodo hiyo.

Mheshimiwa Spika, pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwamba kupitia Shera hii ya madini amekuwa na msisitizo mkubwa katika kuanzisha masoko ya madini. Kwa kweli uanzishwaji wa masoko ya madini imeonekana kuwa na tija kubwa. Mfano mzuri, soko moja tu la kule Chunya, siku ya kwanza ambapo tumefungua soko la madini tuliweza kupata zaidi ya kilo 13 za dhahabu na kupata zile kilo 13 za dhahabu tulipata zaidi ya shilingi milioni 68 kwa siku moja tu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ina tija kubwa na sasa tumefungua masoko 22 na kwa kweli ni kwamba ukusanyaji wa fedha umekuwa ni wa hali ya juu, tumeona jinsi fedha ilivyokusanywa kwa sababu dhahabu iliyopita kwenye masoko mpaka hivi sasa ninavyozungumza ni zaidi ya kilo 578 ambapo zina thamani zaidi ya bilioni 48 na sisi kama Serikali kupitia huo mrabaha tumeweza kupata zaidi ya bilioni 3.6.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli tukiendelea na kusimamia vizuri masoko haya basi tunaweza tuakajikuta tunakusanya vizuri zaidi na nipende tu kuishukuru Kamati ya Nishati na Madini imetoa mapendekezo yake na niseme tu kwamba tumeyachukua mapendekezo hayo, tunakwenda kuyatumia mapendekezo hayo katika kuboresha masoko haya na kuhakikisha kwamba masoko haya yanaendesha vizuri shughuli zake.

Mheshimiwa Spika, niendele kuwaasa wachimbaji, walete madini kwenye masoko haya kwa sababu ukileta madini kwenye masoko haya unapata uhalali wa Serikali, utaingia kwenye ule utaratibu sahihi wa Kisheria ambapo madini yako sasa yatatambulika Kiserikali na wee utalipa kodi yako lakini vilevile Serikali itapata kipato chake na Serikali itakulinda, itakupa usalama wa madini hayo na itakupa usalama wa soko.

Mheshimiwa Spika, vilevile niwaase wanunuzi; bado wanakwenda kununua madini katika masoko ya pembeni au ya uchochoroni. Tuwaase na kuwashauri kwamba waje katika masoko ya madini kwa sababu masoko haya tumeyatengeneza kukutanisha wauzaji na wanunuzi wa madini. Wakifika katika soko utaratibu wote unachukuliwa na wataalam wetu wako pale, wanapima madini hayo na kuhakikisha madini siyo feki, madini ni sawasawa, kipimo utatolewa sawa sawa lakini vilevile ni kwamba utakuwa na uhakika na kile ambacho wewe umekinunua.

Mheshimiwa Spika, niendele kushukuru katika marekebisho haya haya ya Sheria ambayo tuliweza kuyafanya, kuna suala la local content; wafanyabiashara wengi au wachimbaji wengi wame-comply na Sheria ya Local Content, mpaka sasa hivi tuna uhakika kampuni nyingi sasa hivi wanaajiri Watanzania, lakini Kampuni nyingi vilevile sasa hivi zinakwenda kutumia bidhaa za Tanzania.

Mheshimiwa Spika, pia tushukuru kwamba kwa kweli hata wafanyabiashara wa Kitanzania wameonekana kuwa na kufanya biashara ambayo iko katika viango ambavyo wenye migodi wanahitaji. Zamani ilikuwa ni shida kupeleka bidhaa au wafanyakazi ambao wana ile quality au ule ubora ambao wachimbaji wanautaka, lakini kwa kutumia Sheria hii, Watanzania wamekuwa tayari kufanya biashara na migodi mikubwa na kuhakikisha kwamba wanakidhi yale mahitaji na ubora ambao wachimbaji wetu wanataka.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika sheria hii tuliona suala la CSR na Wabunge wengi wameliongelea. Katika suala hili la CSR kuna Halmashauri nyingi ambazo sasa hivi wameanza kuona matunda yake ikiwepo Halmashauri ya Manispaa ya Geita. Geita sasa hivi wanakwenda kupata zaidi ya bilioni tisa na bilioni tisa hiyo itakwenda kufanya maendeleo katika Mji wa Geita. Hapo awali ni kwamba hii CSR ilikuwa ikitoka unakuta wanatueleza tu kwamba leo wamejenga shule, ukiuliza bei ya shule wanakwambia tumejenga kwa bilioni moja. Ukiangalia thamani ya shule hiyo haiendani na bilioni moja hata milioni 200 haifiki.

Mheshimiwa Spika, lakini sasa hivi Madiwani watasimamia fungu hili na wanaposimamia fungu hili watahakikisha kwamba value of money ipo kuhakikisha kwamba miradi hiyo sasa inakuwa na tija na ubora lakini inalingana na kiwango cha fedha ambayo imetengwa.

Mheshimiwa Spika, kuna suala la service levy; niendelee tu kutoa ushauri kwa halmashauri zote, watu wote wanaotoa huduma kwenye migodi watupe ushirikiano kwa kushirikiana na halmashauri. Mtu yoyote ambaye hayuko tayari kutoa service levy katika Sekta hii ya Madini sisi tutambana. Tuhakikishe kabisa kwamba watu wote wana comply na sheria ya ya kulipa service levy ambayo ni asilimia
0.3 na waweze kutoa kwa halmashauri husika. Mfano mzuri juzi nilikuwa Shinyanga, yule mchimbaji mmoja ambaye alipata almasi kubwa kabisa ambayo haijawahi kutokea hapa Tanzania yenye carat zaidi ya 512, palepale tumemchaji katika soko la madini amelipa mrabaha wetu zaidi ya milioni mia moja na themanini na kitu; lakini vilevile katoa fedha kwa ajili ya clearance fee na palepale tukatoa fedha ambayo ni 0.3 percent kwa ajili ya Halmashauri ya Kishapu; na halmashauri imepata fedha. Huo ndio mfano mzuri kwa wachimbaji wote waweze kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile nishukuru kwamba katika Wizara yetu tumeendelea kusimamia masuala ya uongezaji wa thamani ya madini (value addition), sasa hivi katika kituo chetu cha TGC cha pale Arusha tunaendelea kutoa mafunzo kuhakikisha kwamba vijana wetu wanajifunza namna ya kukata madini na kuweza kuongeza thamani katika madini hayo.

Mheshimiwa Spika, tuna Taasisi ya GST ambayo ni muhimu sana kwa wachimbaji Waheshimiwa Wabunge wameiongelea. Nipende kukuhakikishia katika Bunge lako kwamba tunaendelea kufanya tafiti mbalimbali na kuchora ramani ambazo zinaonesha uwepo wa madini kwa kila mkoa na kwa kila Wilaya. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wangu imeeleza, kwamba tumeshatengeneza ramani hiyo na wachimbaji wote wanaweza wakaja GST kuweza kupata taarifa mbalimbali za uwepo wa madini mbalimbali katika yale maeneo tuliyonayo.

Mheshimiwa Spika, STAMICO; kwa mara ya kwanza sasa hivi STAMICO imefufuka na hapa tunavyozungumza mgodi wa STAMIGOLD ambao ulikuwa unatengeneza hasara tulikuta hasara ya zaidi ya bilioni 64. Sasa hivi mgodi wa STAMIGOLD unatengeneza faida tumeshapata faida zaidi ya bilioni moja; ni kwa sababu ya usimamizi mzuri na tulibadilisha pale menejimenti sasa hivi wanachimba kwa faida. Nipende tu kuwahakikishia ile STAMICO iliyokuwa inazungumzwa zamani vibaya na Bunge lako hili Tukufu, kwa sababu Waheshimiwa Wabunge kweli ilikuwa inawachefua sasa hivi tunakwenda kuongelea faida katika uchimbaji au katika miradi ya STAMICO. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuzungumzia issue ya Mheshimiwa Kishimba. Amezungumzia katika ufungaji wa Mgodi wa Buzwagi; ni kweli kuna shimo kubwa pale ambalo liko pale na ndani ya shimo hilo au tuseme chini bado kuonaonekana kuna chembechembe au kuna uwepo wa dhahabu zaidi ya ounce milioni moja. Ni kweli, lakini katika masuala ya uchimbaji dhahabu inaweza ikawa chini haina tatizo lakini namna ya kuichukua dhahabu hiyo chini kuna gharama, gharama inapokuwa kubwa; kwa mfano sasa hivi ounce moja iko kwenye dola 1200, ukaweza kuchimba kwa gharama ya dola 1100, 1200, bado kuna wasiwasi inawezekana ukatengeneza hasara kubwa. Lakini kama unaweza ukachimba, sasa hivi pale Buzwagi mpaka wanafikia mwisho walikuwa wanachimba ounce moja kwa gharama ya dola 900, kwa hiyo ukienda kuuza kwa dola 1200 unapata faida.

Mheshimiwa Spika, lakini sasa hivi ni kwamba wana mitambo mikubwa, ukisema uchimbe dhahabu iliyoko pale kwao hawataweza kutengeneza faida; labda aje mchimbaji ambaye anaweza kuchimba kwa gharama ndogo, akichimba kwa gharama ndogo kwa hali iliyoko pale anaweza akatengeneza faida. Lakiini kinachotokea shimo lile ni kubwa kuna matetemeko yanapita yanahatarisha usalama wa wananchi wanaoishi maeneo yale. Tuna mfano mzuri pale katika mgodi wa Lisolute pale Nzega mashimo yameachwa, ni hatari kweli kweli. Sasa katika uchimbaji sheria inasema unapotaka kuanza kuchimba lazima utupe mining plan yako lakini lazima utupe mining closure yako plan ikoje na Kamati ya mining closure lazima ione na iridhie. Sasa hivi wameshawasilisha mining closure plan yao na ni lazima wafukie shimo hilo.

Mheshimiwa Spika, lakini kama Mheshimiwa Mbunge anaendelea kutushawishi kwamba inawezekana mtu anaweza akachimba kwa gharama nafuu atuhakikishie ufunikaji wa shimo hilo; kitu ambacho tunaona ni kitu kigumu. Kwa hiyo bado majadiliano yanaendelea ya kuona namna ya kufanya.

Mheshimiwa Spika, lakini vilevile niendelee kumueleza Mheshimiwa Kishimba, amezungumzia hoja ambayo hata sisi tunakubaliana nayo; kuhusu service levy kwa yale makampuni yalikuwa yanatoa huduma ya bima katika migodi hiyo. Huduma ya bima ilikuwa inatolewa katika migodi hiyo, wale waliokuwa wanatoa huduma hiyo ni makampuni ya nje. Niliwahi kuzungumza tukiwa na Mheshimiwa Mbunge, tukiwa Kahama tukiwa katika msafara wa Mheshimiwa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu; nikasemaje; hatuna shida sisi kuwabana makampuni haya yatoe ushirikiano wa kutambua yale makampuni ambayo yalitoa huduma na kutueleza walioweza kuwalipa shilingi ngapi ili tuweze ku-charge asilimia 0.3 ambayo ni service levy kwa halmashauri ya Kahama.

Mheshimiwa Spika, niliwaeleza kwamba halmashauri hiyo ifanye ufuatiliaji huo lakini mpaka sasa tunavyozungumza hawajatuletea kutueleza ni nani wamewasiliana naye, je amekubali au amekataa? Nimshauri tu Mheshimiwa Mbunge kwamba atuletee taarifa hiyo ili tuweze kufanya mawasiliano na hawa watu waliohusika. Lakini vilevile tutambue kwamba wale wote waliokuwa wanatoa service kwenye migodi kila mmoja ana wajibu wa kulipa service levy ambayo ni asilimia 0.3

Mheshimiwa Spika, kuna hoja nyingine ambayo imezungumziwa hapa na Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusiana na mradi wa Tancoal. Kuna mengine yataelezwa na Mheshimiwa Waziri atazungumzia na wahusika, Mheshimiwa Waziri wa Viwanda na Biashara amezungumza. Lakini nipende tu kuongelea mambo mawili kuna suala la barabara kilomita 40 kutoka pale Ngaka kwenda Kitai; kwa kweli hili suala linaongeza gharama ya uendeshaji au uzalishaji wa makaa ya mawe kwa sababu gani, kutoka Ngaka kwenda Kitai…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante malizia Mheshimiwa Waziri dakika moja.

NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kutoka Ngaka kwenda Kitai ni kilomita 40 na madaraja yaliyopo pale katikati ni madaraja 12 na kila daraja lina uwezo wa kupitisha tani 15 tu za makaa ya mawe na wakati magari yale ambayo yanabeba makaa ya mawe kwenda Rwanda na Burundi yanatakiwa yabebe tani 30, kwa hiyo inabidi magari madogo yaliyo chini ya tani 15 yapitishe kwenye yale madaraja mpaka Kitai halafu Kitai pale ndipo yapakiwe sasa kuingia kwenye magari makubwa ambayo ni Semi trailer. Kwa kweli hii inasababisha ongezeko kubwa la uzalishaji, nikubaliane na tumeshakuongea na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na watu wa utengenezaji wa barabara (TARURA) ambao wamesema watakwenda kujenga madaraja hayo na kuhakikisha kwamba sasa baada ya muda wakishajenga madaraja hayo usafirishaji pale utakuwa wa bei nafuu kwa sababu magari ya tani 30 yataweza kufika kule Ngaka.

Mheshiimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana kwa kunipa nafasi, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nichukue fursa hii kuwapongeza sana Simba Sports Club, kwa kuweza kufika katika nafasi ya robo fainali ya kombe la Afrika kwa maana ya African Champions League na hili nichukue fursa hii vilevile kuwapongeza Young African kwa sababu kwa kitendo cha Simba kufika katika robo fainali itawafanya Yanga kama watafanikiwa, basi na wao kuwa na nafasi ya pili kwa maana ya kwenda katika mashindano ya Champions League. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ni nafasi ambayo imetengenezwa na Simba, kwa hiyo, niwapongeze sana na wao kama watafanikiwa basi wajue kwamba Simba imefanya kazi nzuri na wao kupata nafasi ya kwenda Champions League. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini niendelee tu kuwaambia watu wa CAF ikiwezekana wabadilishe kanuni kwamba, anayefanikiwa kusababisha timu nyingine kwenda kwenye mashindano hayo, waangalie hizi kanuni upya isiwe nafasi ya pili ikiwezekana huyu aliyeshinda ndio achague nani wa kwenda naye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hili kwa sababu haiwezekani mtu anayekuzomea, anapokea wageni ambao ni maadui zako yeye ndio anawapokea airport na kuwa- support halafu mwisho wa siku tukishinda yeye apate nafasi ya kuendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutawaomba CAF waangalie namna nyingine ya kupanga kwasababu, haiwezekani anayetuzomea twende naye. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo niendelee na mchango wangu, niwaombe tu Watanzania wote, niwaombe Wabunge na watu wote kwa ujumla. Tunawanamuziki wazuri sana Afrika, lakini Diamond ameonesha kuwa ni mwanamuziki ambaye ameonekana duniani kote na leo ametajwa kuwa ni mmoja wa wanamuziki bora duniani wanaokwenda kupigiwa kura. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Diamond katika ile BET Award yaani Black Entertainment Award ametajwa kwamba ni mmoja wa nominee yaani wanaopendekezwa wapigiwe kura. Na niseme tu waliotajwa duniani yuko mwanamziki anaitwa Aya Nakamura wa Ufaransa, Burna Boy wa Nigeria, Diamond wa Tanzania, Emicida wa Brazil, Headie One wa UK, Wizkid wa Nigeria, yaani sijui na nani mwingine huyo wa UK. Kuna Youssoupha wa Ufaransa. Kwa Afrika wapo watatu na kwa Afrika Mashariki ni mwanamuziki mmoja tu kutoka Tanzania ambaye ni Diamond Platinum. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini cha kusikitisha ameanza kupata vikwazo tena kutoka kwa watanzania wenyewe na kibaya zaidi wanaingiza hadi masuala ya kisiasa, na kibaya zaidi wanamsema kwa sababu ali-support CCM, wana-CCM mliomo humu na wana-CCM Tanzania wote tumpigie kura Diamond. Sasa hivi sio suala la chama, hili ni suala la Tanzania, tumpigie kura nyingi, tumpigie kampeni aweze kushinda na hii atakuwa amekwenda kutanga nchi yetu katika nyanja za muziki duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee na mchango wangu vilevile kuhusiana na masuala haya ya TBC. TBC wamefanya kazi nzuri, niishukuru Serikali imeweza kutoa shilingi bilioni tano kwa ajili ya kuongeza usikivu wa TBC. Tunawaomba TBC hizo shilingi bilioni tano mlizopewa mzifanyie kazi usikivu uongezeke, wananchi wanataka kusikia habari za uhakika kutoka TBC. Kuna mikoa ambayo ipo pembezoni mwa nchi yetu usikivu sio mzuri wa TBC, watu wanasikia redio za nchi za jirani. Tunaomba muongeze usikivu ili kusudi watanzania waweze kupata habari za uhakika kutoka TBC.

Mheshimiwa Spika, kuna suala ambalo Mheshimiwa Tarimba alikuwa analiongea hapa kuhusiana na masuala ya mpira wa miguu. Ni lazima tufike sehemu tuamue kuna timu ya Taifa na mashindano ambayo yanashirikisha timu za Taifa, lakini kuna ligi za ndani pamoja na champions league katika mabara yetu. Sisi Tanzania tuna Simba na Yanga zimejitangaza vizuri kuna Azam na timu nyingine. Vilevile kuna timu za Taifa ambazo kwa mfano timu za Nigeria na nchi nyingine wamekuwa na timu nzuri sana za Taifa. Niombe tu kueleza kwamba timu za ligi zinazocheza ligi, hii siyo mpira wa kawaida inaitwa commercial football ni mpira wa kibiashara. Uingereza leo hana timu nzuri kweli World Cup, lakini amejitangaza kwa maana ya ligi yake imekuwa ni ligi maarufu duniani na amejikita hapo tu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo tunaona timu za Waingereza zimeingia fainali champions league, Chelsea na Manchester City na wanaingiza fedha nyingi sana. Hata sisi Afrika, Simba tumekomea robo fainali sawa, lakini Simba ingechukua ubingwa wa champions league ingeingiza fedha nyingi, ingetangaza Tanzania. No matter what katika timu ya Taifa hatuna timu nzuri, lakini tunapojikita kwenye commercial football tunaangalia kwenye champions league tunakwenda kufanya nini. Sasa niwaomba TFF, niwaombe na Wizara msi- limit sana wachezaji kuajiri wachezaji kutoka nje ya nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama Azam, kama Simba, kama Yanga amekwenda kwenye commercial football ambayo ni ligi kuu hapo ni biashara hata kama angeweza kuleta wachezaji kutoka sehemu nyingine alete lengo lake ni kwenda kushinda champions league ili aingize fedha atangaze na nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia timu kwa mfano ile timu ya Congo ile TP Mazembe ambayo ilikuwa inakwenda kushinda inakwenda kwenye champions league ilikuwa inaingiza wachezaji, ilikuwa inasajili wachezaji wakati mwingine hata timu nzima, angalia Real Madrid alikuwa anasajili wachezaji sio kutoka Spain, alikuwa anasajili wachezaji kutoka Portugal na maeneo mengine analenga kwenda kwenye champions league kwa sababu akishinda tayari anaingiza fedha na ameitangaza Spain.

Mheshimiwa Spika, sisi Simba tukishinda ni Tanzania no matter Morison anatoka wapi? Sasa tukitaka kutengeneza timu ya Taifa twende kwenye football academy.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, tutengeneza football academy hizo zitakwenda kutengeneza timu ya Taifa.

T A A R I F A

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Unapewa taarifa Mheshimiwa Haroon Nyongo.

MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na mchangiaji kueleza vizuri sana lakini lengo la Serikali nakupa taarifa tu, ni kuimarisha ligi yetu na kuhakikisha vijana wetu ndio wanakuwa na uwezo mzuri kabisa kwa ajili ya soka letu hili badala ya kuleta vijana wengine kutoka nchi zingine. Nadhani lengo ndio hilo.

SPIKA: Je, uko tayari na vijana wa Tanzania wasiende nje pia kwenye nchi za wenzetu? Kwa taarifa hiyo unapewa Mheshimiwa Haroon Nyongo. (Makofi)

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana umeuliza swali la msingi zuri sana, kwamba je, wachezaji wetu wasiende nje?

Mheshimiwa Spika, leo Mbwana Samatta amekwenda kucheza huko nje, amekwenda kucheza hadi Aston Villa naomba niwaeeleze mbona Samatta angepeleka Aston Villa ingekwenda kucheza champions league ya Ulaya ina maana ile timu ingeshinda wale wangejitangaza kama Waingereza wala siyo Mbwana Samatta kutoka Tanzania. The same na sisi timu yetu ikifika huko tutaitangaza kwamba ni Tanzania, Simba imeshinda au Yanga imeshinda iliyoshinda champions league ni timu kutoka Tanzania no matter hawa wachezaji waliomo humu wanatoka nje ya nchi nyingine.

Mheshimiwa Spika, kingine timu ya Taifa ninachotaka kusema, tutengeneze football academy nzuri mfano mzuri ni Zambia ilipopata ajali kule Gabon watu walivyofariki karibu timu nzima wale makocha walirudi kwenye football academy zao wakawa kumbe tayari wana-infrastructure nzuri ya kutengeneza wachezaji wao, wakatengeneza timu nyingine ikaenda kwenye mashindano hayo hayo na timu ile ikafika hadi fainali, ikaenda kufungwa na Nigeria. Wasingekuwa na football academy nzuri wasingekuwa na timu bora hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba niwaeleze hakuna timu ya Taifa inayotengenezwa na timu za ligi, timu ya Taifa inatengenezwa na Serikali kwa kutengeneza miundombinu mizuri na walimu wazuri wanaoweza kutengeneza na ukishapata wachezaji wazuri utawauza sasa kwenye ligi yako ya ndani kwa maana hiyo inayochezwa champions league na wachezaji wengine utawauza nje ya nchi ikacheze kwenye vilabu vingine. Ukizungumzia timu ya Taifa ndio maana leo utaizungumzia Brazil na Ujerumani, lakini ukizungumzia ligi bora inayoweza kuifikisha timu kwenye champions league ni Uingereza. Watu tubadilishe mindset zetu, tuangalie kama tunaamua kwenda kwenye commercial football twende na kama tunaamua kutengeneza timu Taifa ni jukumu la Waziri na Serikali yake.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana mchezo wa Simba na Yanga; amezungumza kidogo Mheshimiwa Gulamali hapa. Derby ni mechi za watani wa jadi na hizi mara nyingi zinakuwa na sifa ya kukusanya watu wengi na kuteka hisia za watu. Ukichukua ten derbies za Afrika; ya kwanza alikuwa anajinanii hapa ya kwanza Al-Ahly pamoja na Zamalek; ya pili ni Kaizer Chiefs na Orlando Pirates; ya tatu ni Club Africana na Esperance ya Tunisia; ya nne ni Wydad Casablanca na Raja Casablanca za Sudan; ya tano kwa Afrika ni Simba na Yanga ambayo ni Kariakoo derby inafuatiwa na ya sita ya kule Kenya wanajiita Mashemeji derby. Hizi zinabeba hisia za watu na mara nyingi huwa zinasababisha fujo na sintofahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ina jukumu la kulinda hizi mechi, mechi ya Simba na Yanga sio suala la vilabu ni suala la Serikali, lazima muangalie usalama, muzipe usalama na ulinzi wa kutosha. Kwa sababu hizi mechi zinavuta hisia za watu wapenzi wa mpira ndani na nje ya nchi. Kuna wapenzi kutoka Zambia, Kenya, Rwanda, Burundi walikuwa tayari kuangalia ile mechi ikasogezwa mbele, mimi nakubali kuwa Yanga walichukua uamuzi sahihi, lakini na wao wawe wazalendo ilisogezwa kwa masaa mawili wangevumulia tu wapate kichapo chao. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Nyongo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Masuala ya UKIMWI kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
MHE. STANSLAUS H. NYONGO – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA YA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Niendelee tu kushukuru na kupongeza sana Wabunge wote. Tumepata wachangiaji 15; na kwa kweli Wabunge wote wameunga mkono hoja, hakuna hata mmoja aliyepinga. Vilevile, tumepata wachangiaji ambapo tumesikia Naibu Mawaziri wawili ambao wamechangia pamoja na Mawaziri wawili ambao wametoa ufafanuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Kamati niendelee kupongeza sana Mawaziri hawa, wamefanya kazi vizuri na Kamati yangu kama unavyoifahamu ina sasa Wizara nne. Kwa kweli mambo ni mengi na tulipata muda mdogo kidogo wa kuweza kutoa ufafanuzi. Pia tumetoa kwenye maandishi na kila Mbunge anaweza akapitia na imeonesha ni jinsi gani ambapo Kamati imeweza kutoa ushauri kwa kina kwa wizara zote hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu nisisitize mambo mawili matatu kwa kila sekta. Mambo makubwa yaliyojitokeza, kubwa ni hili suala la; kwanza kabisa tunaipongeza Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwenye fedha hii ya mkopo ambayo ni shilingi trilioni 1.3 ambapo kwa kweli Mheshimiwa Rais ameitendea haki nchi yetu kwa kuweza kuelekeza hizi fedha ziende zikajenge miundombinu ya elimu na afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika fedha hizi zimekwenda karibu shilingi bilioni 800 na ushei, ambazo zimekwenda kwenye miundombinu ya elimu na afya. Nii sawa sawa na kama 75% hivi zimekwenda kujikita kwenye kupeleka huduma kwa wananchi. Jambo hili kwa kweli Mheshimiwa Rais tunampongeza sana kwa sababu hii changamoto ilikuwa ni kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ulivyosikia Wabunge, pamoja na kutoa pongezi hii, ni kwamba tuna upungufu mkubwa sana wa watumishi wa afya na elimu. Kwa wastani, kwa sekta zote hizi mbili tunaona kabisa tuna upungufu wa watumishi karibia 50% kwa kila sekta. Walimu pamoja na madaktari na watumishi wa afya, kwa kweli naipongeza Serikali, Waheshimiwa Mawaziri wamezungumza, lakini kwa kweli Serikali ichukue juhudi za kipekee kuhakikisha kwamba tunaajiri watumishi wa sekta ya elimu na afya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa walimu, tuhakikishe tunazalisha walimu wenye ubora. Tunaweza tukawa na madarasa ya kutosha lakini kama hakuna walimu, bado watoto wetu wanaweza wasipate elimu inayostahili.

Kwa hiyo, tunapenda kuishauri Serikali na kuisisitiza kwamba tuzalishe walimu wa kutosha ili waende wakawafundishe watoto hawa. Kwa kweli juhudi zilizofanyika ni kubwa, kwa hiyo, lazima tukamilishe kwa kuweza kupeleka walimu wa kutosha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo huo, tunawapongeza sana Wizara ya Afya, walitoa mwongozo wa masuala ya kuulinda au kuhakikisha kwamba wale wafanyakazi au watumishi wasiokuwa na ajira, wanaojitolea (volunteers) waweze kwenda kufanya kazi kwenye vituo vya afya na zahanati. Kwa kweli hili nalo lifanyike kwa Wizara ya Elimu. Volunteerism ifanyike ili kusudi watu wapelekwe kule hata ambao hawana ajira, basi itafutwe namna bora au program bora ya kuajiri kama parttime ili waweze kutoa huduma kwa wananchi, kwa sababu wananchi wanahitaji huduma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fikiria kijiji kilikuwa hakina zahanati, leo kina zanahati, majengo yamejengwa pale, lakini hakuna mganga; what do you expect? Wale ambao hawajaajiriwa, basi waende pale wakatoe huduma kwa wananchi halafu iangaliwe namna ya Serikali kuwalipa hawa hata kama ni kidogo, basi waweze kutoa huduma. Ajira ikija, siku mkiamua kuajiri hawa waliojitolea muwape kipaumbele cha kuwapa ajira. Kama ni walimu wapewe ajira kwa kipaumbele kwa sababu walijitolea; na kama ni waganga na manesi, nao wapewe kipaumbele cha kupewa ajira kwa sababu wamejitolea na kwa kweli wametoa huduma na wameshirikiana na Serikali katika wakati mgumu, nao muweze kuwajali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la MSD limezungumzwa na kila Mbunge hapa. Suala la upatikanaji wa dawa, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri ametoa ufafanuzi, lakini MSD iwezeshwe. MSD kama haijawezeshwa, bado litakuwa ni tatizo. Tunashukuru kwamba fedha zimetolewa shilingi bilioni 373 lakini kuwezeshwa huko, na mfumo urekebishwe wa kuweza ku-monitor usambazaji wa dawa. Kama hakuna mfumo thabiti, upotevu wa dawa utakuwepo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tunawapongeza sana MSD kwa kuamua kuzalisha dawa, tumeona essential drugs zinazalishwa na Keko Pharmaceuticals; tumekuta uzalishaji a hundred percent. Sasa kama uzalishaji wa essential drugs upo kwa 100%, kwa nini kunakuwa na upotevu na huu upungufu wa dawa kwenye vituo vya dawa? Kwa sababu wanaangalia mahitaji na uzalishaji, sasa huu upungufu umetokea wapi? Inaonekana hapa katikati kuna upotevu wa dawa. Basi ingaliwe namna ya kuwekeza katika kuweka mifumo mizuri ya kuweza kuhakikisha dawa inasimamiwa wakati wa kuzalisha, wakati wa kununua,wakati wa ku-stock, kusambaza na kupeleka kwa wagonjwa na watumiaji. Hili ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasisitiza hivi kwa sababu gani? Kama tumeweza kujenga Kituo cha Afya kwa shilingi milioni 400, umejenga zahanati kwa shilingi milioni 100, umejenga Hospitali ya Mkoa kwa mabilioni ya fedha, tunashindwa nini ku-invest kwenye Kituo cha Afya shilingi milioni tano ya kuweka mfumo ambao uta-monitor mapato, dawa, matumizi na kuwezesha kujua kwamba stock hii ipo eneo hili na hili na stock hii kuna upungufu eneo lingine, mfumo unakueleza?

Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mzuri, kwenye blood bag imeonekana. Kuna maeneo MSD wametueleza blood bag ipo Mkoa X, halafu Mkoa Y hakuna blood bag. Maana yake nini? Pangekuwa na mfumo unao-monitor Mkoa X una blood bag in excess, basi huo mfumo umwelekeze blood bag zitoke Mkoa X kwenda ku-supply Mkoa Y ili hawa watu wa Mkoa Y nao wapate blood bags. Hili ni suala la mfumo tu. Kwa hiyo, tunasisitiza sana mfumo ufungwe katika ku-monitor hizi shughuli za ku-control stock.

Mheshimiwa Mwenyekiti, issue ya mitaala, tunaishukuru sana Serikali, wameeleza vizuri na mwaka 2026 tunategemea kwamba tutapata mitaala mipya na ianze kufundishwa. Tunasisitiza waendelee kufanya kwa haraka, lakini lazima uangalie, mtoto anayemaliza Kidato cha Nne ambayo sasa hivi tumesema ndiyo basic education, mnapomfundisha, basi afundishwe na utaalam, atoke na utaalam fulani ili hata asipoendelea Kidato cha Tano, akienda mtaani awe utaalamu fulani wa kuweza kufanya kazi. Atakapomaliza chuo cha kati, awe na ujuzi, yaani tupate namna ya kupata wataalam wadogo wadogo ambao wanaweza kwenda kuzalisha katika viwanda vidogo vidogo. Hili ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la michezo limezungumzwa vizuri, tuwekeze. Hizi kampuni zinapotoa misaada kwenye michezo, basi ile gharama inayotolewa kwenye michezo iwe inatambulika kwenye mahesabu ya kikodi, kwamba mtu anaye-finance; mfano, kampuni imetoa fedha ya kununua mipira, iweze kutambulika kikodi ili waweze kupunguziwa katika corporate tax. Hili ni jambo la muhimu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimalizie suala la Mheshimiwa Mulugo; suala hili linatisha kwa kweli kama kweli hiyo hali ipo. Tunaomba wadau pamoja na Serikali tukae, tujadili tuone. Ku-control ufundishaji kwamba mwezi wa Tatu topic moja na mbili ziwe zimeshafundishwa, hiyo sawa; lakini kumzuia mtu kufundisha zaidi eti kwa sababu anawahi sana, hilo tunaomba tukae na kuweza kuli-review. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, kuhusu mimba za utotoni Mheshimiwa Bidyanguze amezungumza vizuri, tunahitaji elimu, watoto tuwafundishe. Biologically mtoto akishakuwa matured anapokwenda kwenye secondary growth ana-develop kitu kinaitwa ovulation period, ndiyo kipindi cha hatari yeye kupata ujauzito. Aambiwe kipindi hiki kina dalili zipi, ili asijihusishe. Bila ya kufanya hivyo, tutaendelea na dropouts kwa watoto na utoro utaongezeka na hii inakuwa ni hasara kwa Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Basi baada ya kusema hivyo, naomba kutoa hoja. (Makofi)

MHE. KASSIM HASSAN HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti naafiki.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. STANSLAUS H. NYONGO - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, mimi tu niendelee kuchukua au kuomba fursa hii kwa maana ya kwamba nitoe pongezi za dhati kabisa kwa Waheshimiwa Wabunge ambao wamechangia siku ya leo na hasa katika kuchangia hoja ya Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii.

Mheshimiwa Spika, tumepata wachangiaji wengi, Wabunge takribani 15 wamechangia na Mawaziri ambao wamechangia moja kwa moja kuhusiana na Kamati yetu ni Mawaziri wanne.

Mheshimiwa Spika, nishukuru tu kwamba wachangiaji wote wameungana na Kamati, wameungana na hoja zote za Kamati na mapendekezo ya Kamati. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niendelee tu kumpongeza, nimpongeze Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya na hasa ya kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee kuwapongeza Mawaziri ambao wanasimamiwa na Kamati yetu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, kwa kweli wamekuwa wanafanya kazi na kazi hiyo wanayoifanya ni ya ushirikiano wa hali ya juu na Kamati yetu. Hapa leo wamekuja kujibu hoja mbali mbali kwa kweli Mawaziri hawa wameonesha commitement ya hali ya juu kwa maana kwamba wanakwenda kutekeleza yale majukumu au yale maoni ambayo Kamati yetu imeyatoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niendelee tu kusema kwamba maazimio ya Kamati ambayo tunakwenda kuyapitisha leo hapa katika Bunge lako tukufu basi waende wakayasimamie, wayafanyie kazi kadri jinsi walivyotoa maelezoyao na jinsi tulivyoweza kutoa maelekezo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kamati baada ya kutoa maoni, wachangiaji wengi wameweza kuchangia na kabla sijaenda kwenye Wizara moja moja kuna hoja za jumla ambazo zimetolewa na Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Spika, katika michango yote ya Wabunge, jambo lililojitokeza kubwa zaidi ni suala zima la upungufu wa watumishi hasa katika sekta ya afya na sekta ya elimu kwa maana ya walimu.

Mheshimiwa Spika, katika taarifa yetu ya Kamati iliyopita ya mwaka jana, tulisema na tulisisitiza kwamba Serikali ichukue jukumu maalum au jukumu mahsusi kuhakikisha kwamba inaajiri walimu, madaktari na manesi ili kusudi waende wakatoe huduma kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninaendelea kusema kwamba ninaishukuru Serikali imechukua hatua za dhati, lakini bado jukumu ni kubwa, wanatakiwa waajiriwe walimu wa kutosha pamoja na watumishi wa sekta ya afya.

Mheshimiwa Spika, leo umesikia hapa masomo ya sayansi ni kilio kikubwa, upungufu wa walimu wa sayansi umeonesha unaendana kabisana failure ya wanafunzi katika masomo ya sayansi. Kwa maana hiyo, kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya ufaulu mdogo wa wanafunzi katika masomo ya sayansi na upungufu wa walimu wa masomo hayo. Hivyo basi jukumu hili Serikali tunaomba ilichukuwe, ilibebe kwa hali ya upekee ili kusudi tuondokane na changamoto hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo limezungumzwa zaidi ni ukatili wa kijinsia kwa kina mama na watoto. Nimshukuru sana na Mheshimiwa Waziri Mkuu leo ndiyo ilikuwa mada yake kuu. Ukatili wa kijinsia umezidi kukithiri na hata leo hapa Waheshimiwa Wabunge wamesema hata kwa watoto wa kiume napo tutupie jicho. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hili halipingiki ni lazima tuchuke hatua za kipekee. Sasa hivi ukiwa na mtoto wa kike unatakiwa umlinde, lakini ukiwa na mtoto wa kiume naye unatakiwa umlinde tena zaidi, haya yote nadhani ni vizuri tuamue kwa pamoja, tupambane na ukatilii huu wa kijinsia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine katika masuala ya kijumla ni afya ya akili; suala la afya ya akili limekuwa ni changamoto kubwa, tuchukue sasa juhudi za kipekee kuhakikisha kwamba tunapambana na matatizo ya akili ambayo wanachi wetu yanawakabili.

Mheshimiwa Spika, kwa Wizara ya Afya ni kwamba namshukuru sana Mheshimiwa Waziri ametoa commitement kubwa na kwa suala la MSD, tunaomba sana wawekezaji wa ndani wapewe nafasi na fursa kwa ajili ya kuzalisha dawa kwa ajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa dawa, lakini vilevile kwa ajili ya kufanya biashara katika nchi ambazo tuna mahusiano nazo kwa maana ya nchi za SADC na nchi za Afrika ya Mashariki.

Mheshimiwa Spika, vilevile suala la TMDA pamoja na TBS; yale majukumu ya TBS aliyozungumza Mheshimiwa Waziri na yeye ametoa support hiyo ni kwamba kweli majukumu ya chakula basi yarudishwe kwa TMDA aweze kuyashughulikia kwa sababu ana utaalamu wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, kwa Bodi ya Mikopo kwenye suala la Wizara ya Elimu, wewe katika Bunge lako hili hapa majuzi, Bunge lililopita uliweza kutoa, ulituongoza na Bunge likatoa ushauri kwa Serikali kwa wanafunzi ambao walikuwa hawajapata mkopo wapatiwe mikopo mara moja na waweze kuingia madarasani waendelee na masomo.

Mheshimiwa Spika, uamuzi huu ulikuwa ni uamuzi wa busara na wa kipekee na umakini wa hali ya juu uliotoka katika Bunge lako la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Jana nashukuru Kaka yangu, Ndugu yangu Mheshimiwa Mwigulu Nchemba hapa alisema kwamba Bunge hili, Wabunge wangekuwa kidogo makini wangetoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais. Naomba niseme umakini wa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wa kusahauri Serikali iongeze fedha kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi ulikuwa ni umakini wa hali ya juu kupita kiasi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nikupongeze sana wewe, ninakupongeza sana na Bunge lako kwa maamuzi haya, tunaomba na tumesema katika taarifa ya Kamati, Bodi ya Mikopo iongezewe fedha. Udahili wa wanafunzi siyo suala la dharura. Udahili wa wanafunzi ni suala linaloweza kufanyiwa forecasting ya kutosha, fedha iliyotoka, Shilingi Bilioni 570 ilijulikana, na udahili wa wanafunzi kwa mwaka huu uliongezeka na Bodi ya Mikopo ilitoa taarifa kwa Wizara ya Fedha ili iongeze fedha kwa ajili ya mikopo, tunaomba siku nyingine Wizara itambue kwa wepesi na kwa haraka kwamba kuna ongezeko la udahili ili iweze kuongeza fedha kwa ajili ya kuwapa wanafunzi mikopo hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile suala la maendeleo katika Sekta ya Maendeleo ya Jamii, tunampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kuanzisha sekta hii au Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii. Ukatili unaoendelea, msimamizi mkuu wa masuala haya ni Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum. Waziri huyu ana instrument yake. Yanapotokea matukio kama haya wakati mwingine yeye ndiyo anatakiwa akemee. Hivyo basi, tuangalie Serikali iangalie kwa umakini, Wizara hii ikiwezekana iwe chini ya ofisi kubwa za Serikali, aidha iwe chini ya Waziri Mkuu au iwe chini ya Makamu wa Rais, au iwe chini ya Ofisi ya Rais ili Waziri huyu anapoona kuna suala lolote la kukemea au suala lolote ambalo linaonekana kuna uvunjifu wa amani au ukatili wa kijinsia awe na power ya kumwambia Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Sheria, Waziri wa Elimu au Waziri yeyote ambaye anashughulika na watoto na akina mama awe na power hiyo, nadhani hili tutakwenda vizuri zaidi tukilirekebisha. (Makofi)

SPIKA: Dakika moja malizia Mheshimiwa.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mwisho kwa Wizara ya Utamaduni na Michezo, tunawashukuru sana na tunampongeza Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa anayoifanya. Wizara hii ilikuwa haionekani sasa hivi imekuwa ni Wizara ya mfano, wanafanya kazi vizuri sana, hivyo waendelee kujenga viwanja, waendelee kuhakikisha kwamba vijana wa Kitanzania wenye talent za kufanya michezo au kucheza michezo mbalimbali waweze kuonesha talent zao, na iwe chanzo cha vijana hawa kupata fedha.

Mheshimiwa Spika, matajiri vijana na watoto wanatokana na talents. Matajiri wanaotengenezwa katika umri mdogo ni wale wenye vipaji maalum. Wizara hii tukiiwezesha, tutapata matajiri vijana kutokana na vipaji walivyonavyo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, niseme sasa naomba kutoa hoja. Ahsante.

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
NAIBU WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii. Kwanza kabisa, napongeza Kamati zote mbili kwa uwasilishaji mzuri na ushauri mzuri uliotolewa. Sisi kwa upande wa Sekta hii ya Madini kuna hoja kama mbili au tatu ambazo zimejitokeza, nazo ningependa kuchangia kidogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, Kamati zimeelezea namna ya kuimarisha utendaji wa Shirika la STAMICO. Napenda tu kukueleza kwamba Serikali imeendelea kuimarisha utendaji wa STAMICO kwa kuteua Bodi mpya na Menejimenti mpya ili ifanye kazi kwa ufanisi zaidi ya ilivyokuwa inafanya awali. Tumechagua watu wenye weledi na Mheshimiwa Rais alituteulia Mwenyekiti wa Kamati ya STAMICO, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, anafanya kazi vizuri na kwa kweli Bodi inatoa ushauri mzuri na kwa kweli kazi inaenda vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile limeongelewa suala la ukosefu wa mtaji. napenda kueleza kwamba Serikali pia imeendelea kuliwezesha Shirika la Madini la Taifa kadri fedha zinavyopatikana. Aidha, STAMICO imekuwa inatumia assets zake na hasa leseni ilizonazo kuzibadilisha kuwa sehemu ya mtaji. Kwa hiyo, ukiangalia maeneo mengi ni kwamba leseni ambazo zinamilikiwa na STAMICO, tunapokuwa tunaingia katika joint venture na makampuni mengine katika miradi hiyo, basi zile leseni za STAMICO zimekuwa ndiyo sehemu ya mtaji. Kwa hiyo, badala ya kutegemea mtaji sana kutoka Serikalini, tumeamua kutumia leseni zetu kuwa kama ni mchango wa mtaji katika miradi hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile limezungumzwa sana suala la kupunguza gharama za uendeshaji. Tumepunguza muundo wa Shirika kutoka Kurugenzi zilizokuwa tano, sasa hivi tuna kurugenzi tatu. Hivyo, tumepunguza gharama ambapo zilikuwa zinatumika fedha nyingi kulipa au kuendesha zile kurugenzi kutoka Kurugenzi tano kuwa Kurugenzi tatu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumepunguza gharama za uzalishaji wa madini hasa katika mradi wa STAMIGOLD. Tulikuwa tunazalisha wakia moja kwa dola za Kimarekani 1,800 ambapo hata katika mauzo katika Soko la Dunia unakuta wakia moja kwa mfano sasa hivi ni dola 1,400 kwa wakia moja. Kwa hiyo, tulikuwa tuna-produce kwa gharama kubwa, tunapokwenda kuuza tunauza kwa gharama ndogo. Tumeona kwamba Shirika lilikuwa linapata hasara na linatengeneza madeni makubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tumepunguza gharama za uzalishaji ya wakia moja kutoka dola 1,800 kuwa dola 940. Hata tunapopeleka katika soko tunakuta wakia moja inauzwa labda dola za Kimarekani, sasavi tumepambana hadi kufikia dola 1,500. Kwa hiyo, tunatengeneza faida. Ile difference ya 1,500 na 940, ile difference tunayoipata, ndiyo faida kwa Shirika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile Shirika limeanza kuuza madini yake. Badala ya kupeleka nje, kwa sababu kupeleka nje kuna gharama na ilikuwa inatugharimu kwa trip moja kupeleka dhahabu nje ya nchi, ilikuwa inatugharimu mpaka shilingi milioni 38, sasa hivi tumeshaanzisha masoko ya madini nchini na tumeamua sasa hivi katika mgodi ule wa STAMIGOLD, badala ya kupeleka nje na kwa sababu bei inajulikana, tunauza katika masoko yetu ya ndani. Hii inatuondolea ile ghrama ya kusafirisha madini yao kupeleka nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni moja ya hatua ambazo tumechukua na tumeweza kupunguza gharama za uendeshaji. Hatua hizo zimesababisha shirika letu, kama mlivyosikia hapo majuzi, tumeweza kutengeneza faida na tumeweza hadi kutoa gawio kwa mchango wa Serikali, tumetoa kiasi cha shilingi bilioni moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Hoja ya Dharura kuhusu Mikopo ya Elimu ya Juu Nchini
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Nami niungane na Mheshimiwa Ezra Chiwelesa kwa hii hoja aliyoitoa.

Mheshimiwa Spika, sisi katika Kamati yetu tumeshauri katika bajeti ya mwaka huu na katika bajeti iliyopita. Tumeyaona na tumeyasikia malalamiko ya vijana wanaoomba mikopo kwa ajili ya kujiunga na elimu ya chuo kikuu. Ni kweli kabisa, sisi tumewaita watu wa Bodi ya Mikopo, tumekaa nao, tumeongea nao, tumeangalia vigezo wanavyovitumia katika kutoa mikopo. Inachanganya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanasema wanatoa mikopo kwa watoto waliofaulu vizuri, sawa, tunakubaliana nayo. Lakini wanatoa mikopo kwa watoto ambao wazazi wamefariki, yaani Watoto yatima. Kuna watu wengine wamepata mikopo wazazi wapo, kuna watoto wengine ni yatima hawapati mikopo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na kibaya asilimia 62 ya mikopo iliyotoka wamekwenda kuwakopesha vijana wanaosoma masomo ya arts. Ukiwapa watoto wanaosoma masomo ya arts wanapofaulu wengi wamekwenda mtaani kutafuta kazi hawana ajira. Kwa hiyo unakuta watoto asilimia 62 hawana ajira, maana yake ni nini, hawarudishi mikopo. Asilimia iliyobaki ni kama 20, wamewapa watoto wanaosoma masomo ya sayansi, asilimia tano ni wale ambao hawakuomba mkopo.

Mheshimiwa Spika, tumeshauri hivi, na mimi nilizungumza humu kwa niaba ya Kamati, kwamba watueleze ni shilingi ngapi inahitajika kwa mwaka kuwapa mikopo wanafunzi wote Tanzania wanaostahili kuingia chuo kikuu. Wakatuambia fedha wanayopata ni bilioni 570, lakini wakipata bilioni 800 watatoa mikopo kwa wanafunzi wote Tanzania.

Mheshimiwa Spika, tukaomba Serikali itafute hiyo bilioni 800, mtu yeyote anayehitaji kuingia chuo kikuu ana shida ya kifedha, no matter ni mtoto yatima au ana wazazi, kwa sababu kuna wazazi wengine hawana uwezo, wapewe mikopo watu wote waingie chuo kikuu wasome. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, elimu iende kutolewa, kwamba mzazi mwenye uwezo kumkopesha mtoto wako kuingia kuchukua mikopo, kumbuka kwamba akiingia kazini atakuwa na jukumu la kulipa mkopo ule. Kama hiyo elimu ikitolewa mzazi kwenda kuchukua mkopo iwe ni last resort, kwamba umekwama ndipo mtoto wako umuingize akachukue mkopo kwa sababu ule mkopo siyo wa mzazi, mkopo ni wa mtoto ambaye akishaingia kazini atastahili aulipe.

Mheshimiwa Spika, na la mwisho tukasema kwamba Bodi ya Mikopo kwa sababu ilianzishwa kwa ajili ya kusaidia wanafunzi kwenda kusoma ibadilishwe iwe commercial, wawe na utaratibu na mfumo mzuri wa kufuatilia ulipaji wa mikopo. Kwa sababu unafika sehemu wanakwama kukusanya madeni kwa hiyo wawe na utaratibu mzuri, ianzishwe kama ni benki ambayo itasaidiwa na Serikali kupewa ruzuku ili iweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naungana na Mheshimiwa Ezra. Hali ni mbaya, inabidi Serikali iliangalie hili na mrudi kwenye maoni ya Kamati muweze kuhakikisha tunatafuta hiyo fedha. Kama ni Bunge kupitisha tutafute hiyo fedha ili wanafunzi wote Tanzania wapewe mikopo waende wakasome. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa uhai. Nishukuru sana wana Maswa kwa kunichagua kwa kura nyingi sana, nimepata ushindi mkubwa kuanzia kwa Rais, Ubunge hadi kwa Madiwani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niendelee kutoa pongezi sana kwa Mheshimiwa wetu Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa aliyoifanya hasa kukusanya maduhuli na kuhakikisha kwamba matumizi ya fedha inayokusanywa na Serikali inafanya kazi iliyotakiwa. Kwa kweli usimamizi umekuwa ni mzuri sana kwa Serikali na matokeo tunayaona kwamba fedha inayokusanywa na Serikali inatumika ipasavyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nitajikita kwenye jambo moja muhimu. Mheshimiwa Rais wakati anatoa hotuba alisema kwamba jambo ambalo atalipa kipaumbele au Serikali italipa kipaumbele ni kulinda na kudumisha tunu ya taifa letu yaani amani, umoja na mshikamano wa uhuru wa nchi yetu. Nazungumza hili kwa makusudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna janga kubwa la corona ambalo limeitikisa dunia. Naomba nikuambie kitu kinachompeleka mtu hospitali siku zote, nazungumza hili ili watu waweze kunielewa, cha kwanza huwa ni maumivu (pain). Jambo la pili linalompeleka mtu hospitali huwa ni hofu. Hofu ziko mbili; ya kwanza hofu ya disability yaani kupata ulemavu na hofu ya pili huwa ni ya kifo. Haya ni mambo makubwa yanayompeleka mwanadamu hospitali kwenda kupata huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, imetengenezwa hofu na hofu hii ni ya kifo, dunia imetengenezewa hofu ya gonjwa la corona, taarifa zimekuwa exaggerated as if kwamba corona ni gonjwa jipya litakwenda kuangamiza dunia hii. Ni mwamba mmoja tu Dkt. John Pombe Magufuli amesimama imara na kupingana na hofu hii. Naomba Watanzania na Waheshimiwa Wabunge tuungane na juhudi za Mheshimiwa Rais wetu kuondoa hofu hii ambapo ni janga kubwa linakwenda kuleta vifo kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, magonjwa yalikuwepo mengi, kuna ugonjwa ulikuwa unaitwa smallpox (ndui), ulikuwa eradicated mwaka 1977 kwa chanjo na ulikuwa unasababishwa na virus. Kuna ugonjwa mwingine wa surua uliuwa watoto wengi, ulipatiwa chanjo na sasa hivi umekuwa controlled. Kuna tatizo kubwa la malaria, tunapata infection ya malaria milioni 200 kila mwaka, hawa watu wangekuwa wanatupenda ugonjwa wa malaria wangeukomesha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya nyuma, kuna Profesa mmoja Mjerumani alileta genes ambapo angeweza kuwasambaza kwa mbu wote na wangebadilisha behavior ya kutafuta damu kwa kwa ajili ya ku-nourish mayai yao kutoka kwa binadamu kwenda kwa wanyama na mbu hao wasingesababisha malaria ingekuwa historia kama walivyofanya kwenye chickenpox au smallpox.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ugonjwa wa HIV umeanza toka mwaka 1981 na wanamjua huyu retrovirus yupo type one na type two, wanajua behavior yao, biashara ipo kwenye antiretroviral, hapo ndipo wanapokunywa maziwa. Wameanza na vidoge vingi kwa wagonjwa wameenda kwenye kidonge kimoja na sasa hivi wanakwenda kwenye innovation ya sindano moja kwa miezi sita. Biashara hii inaenda kwisha kwa sababu muamko umeeleweka, vifo vimepungua kwa asilimia 60 na maambukizi yamepungua kwa zaidi ya asilimia 40 na Tanzania tumepambana nayo vizuri sasa deal imeisha kwenye HIV, the deal now is corona. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna ugonjwa huu wa corona umetambulika China type ya kwanza na type ya pili ambayo wanasema imetokea South Africa wanakuja na chanjo wanasema hii ndiyo chanjo ambayo inakwenda ku- solve corona, chanjo ya HIV ya toka mwaka 1981 iko wapi? Kwenye malaria nimedokeza biashara ipo kwenye vimelea vya malaria, neti, antimalaria na ugonjwa huu ni biashara kwao na ndiyo maana wanaendelea kuufuga. Kuna Waitaliano wameleta genes wanasambaza, mbu wamembadilisha anakuwa na jinsia mbili; anakuwa hana mdomo wa kunyonya damu, badala ya kumng’ata binadamu anakwenda kufa kwa sababu hawezi kumng’ata binadamu na spread ya malaria inaisha. Aliyegundua hizi genes alikufa mazingira ya kutatanisha kisa biashara ya antimalaria na neti na wanaotutengenezea net bure tunawajua. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana, kengele imeshagonga.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. (Makofi)
The Finance Bill, 2016
kunipa nafasi. Kwanza kabisa napenda kupendekeza marekebisho kidogo, Mheshimiwa Waziri ameeleza katika Hotuba yake na kwenye sheria ipo kwamba wasiotumia mashine ya EFD, wasiotoa risiti, watanyang‟anywa leseni kwa muda wa miaka miwili.
Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa hiyo iondolewe mtu atakayepatikana na tatizo hili, basi bora apigwe penalty kubwa kuliko kunyangw‟anywa leseni kwa miaka miwili. Kwa sababu ukimnyang‟anya leseni kwa miaka miwili ni kwamba, hatalipa tena ushuru kwa miaka miwili, ina maana unamwondoa kwenye biashara. haina maana yoyote kumnyang‟anya leseni kwa miaka miwili. Bora mtu achajiwe penalty kubwa kama ilikuwa ni 25 percent iende kwenye 50 percent kwa maana ya kwamba ajifunze na bado kwa upande wa Serikali inakuwa ni kipato. Hiyo moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, kuna hii migodi kwa mfano kampuni ya ACACIA, tulikuwa tunafahamu kwamba kampuni ya ACACIA itaanza kulipa kodi mwakani, tunachoshangaa Kamati imekuja na ripoti kusema kwamba itaanza kulipa kodi mwaka 2019, kwa nini wamesogeza mbele? Hawa watu ni wawekezaji wanamigodi mikubwa mitatu na migodi hii ni mikubwa kiasi kwamba tukiitumia katika kukusanya kodi, tutapata mapato makubwa Serikalini.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba hii tax holiday ifuatwe kama ilivyokuwa mwanzo. Tunashangaa kwa nini tax holiday imekuwa extended? Ni rushwa au ni nini? Kwa nini Waziri wanapendekeza ku-extend muda wa kuwatoza ushuru hawa watu? Hawa ni wawekezaji na wanawekeza kwa faida, ndiyo maana wako hapa, ni lazima walipe tax, kuna mamilioni na mabilioni ya pesa ambayo wanatakiwa wayalipe.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ni suala la hawa hawa wawekezaji kwenye migodi mikubwa. Hawa ACACIA na migodi mingine wanapata tax exemption kubwa. Kuna zaidi ya bilioni 60 wanapewa tax exemption, tunaomba wachajiwe, waondolewe hiyo exemption kwa sababu bado makampuni haya yanafanya kazi kwa faida kubwa na ndiyo maana wanawekeza hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Niabu Spika, suala lingine la mwisho sitaki kuongea muda mrefu, ni suala la kufanya reallocation ya pesa. Mandate aliyopewa Waziri wa Fedha pamoja na Rais, tukae tuangalie upya, kufanya reallocation ya pesa ni kuondoa umaana wa Bunge lako. Tunakaa hapa tunapitisha bajeti, tunakaa muda mrefu, tunafanya allocation ya pesa, lakini unapompa mandate Waziri bila ku-consult Bunge ku-reallocate pesa, ni tatizo kubwa na ndiyo maana maendeleo hayaendi yanavyostahili. Kwa sababu tunaweka hapa allocation ya pesa kwa maana ya kuleta maendeleo, lakini kama kuna mtu mmoja anaweza akafanya reallocation, which means Bunge hili linakaa for nothing.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Bunge liheshimike, pesa zinazokuwa allocated kwenye Bunge ziheshimike, pesa za maendeleo ziende, pesa zifanye kazi iliyokuwa imekusudiwa na Bunge. Tunapotaka kufanya reallocation ya mamilioni ya walipa kodi, tunaomba Bunge likae lipitishe, liangalie umuhimu wa hiyo reallocation na Bunge liweze kupeleka hizo pesa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni hayo tu nashukuru kwa kunipa nafasi na ahsante sana kwa kunisikiliza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Kwanza kabisa na mimi nipende kutoa shukrani nyingi sana kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Maswa Mashariki na niendelee kuwapa pole kwa msiba uliotukuta sote. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile naomba nitoe pongezi kwa Serikali kwa kukubali kuondoa TMX kwenye manunuzi ya mazao yetu. Tatizo lilikuwa kubwa sana na kule kwenye Jimbo langu kwa kweli ilikuwa ni tatizo, hata kwa wale wanaokwenda kuuza choroko kilo tatu, nne, tano ilikuwa inawapa shida sana kuuza mazao yao kwa kupitia mtandao huu. Kwa hiyo, tunaishukuru Serikali kwa usikivu na kwa kutoa maamuzi haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ushauri kwa mambo kama mawili au matatu. La kwanza, naomba nitoe ushauri kuhusiana na bandari yetu. Serikali yetu imeamua kujenga reli ya standard gauge, reli hii ina manufaa makubwa sana katika uchumi wa nchi yetu. Reli hii inakwenda kujengwa kwenda kwenye mipaka ya nchi yetu lakini bado reli hii itategemea mzigo mkubwa sana kutoka nchi za jirani kwa mfano nchi ya Kongo, kila mwaka tumekuwa tukisafirisha shaba kutoka Kongo zaidi ya tani 500,000 hadi 700,000 kupitia bandari yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunajenga reli hii ni lazima tuone namna ya kuungana na wenzetu wa nchi za jirani ikiwezekana na kadri tunavyokuwa tukijinasibu na Rais wetu Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alikuwa anasema nchi yetu ni tajiri, nchi tajiri lazima isaidie na nchi jirani kuwa matajiri ili na yenyewe iwe tajiri zaidi. Ikiwezekana kwa namna yeyote ile tuingie mikataba kuhakikisha kwamba Kongo, Zambia na nchi nyingine kwa mfano Rwanda na wenyewe wanakwenda kwenye standard gauge. Nia yake ni kuhakikisha mizigo hii inakuja kwenye bandari yetu na bandari yetu iweze kusafirisha mizigo mingi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivyo kwa sababu gani? Bandari yetu ina uwezo wa kubeba au kuhudumia tani zaidi ya milioni nne kwa mwaka ya mizigo migumu yaani hard cargo lakini kuna mizigo ya liquid zaidi ya tani milioni 4.5, mizigo hii inapitia kwenye bandari yetu kwenda upande wa nchi kavu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nalotaka kuzungumza leo, nimesoma Mpango wa Maendeleo, nimeangalia strategy za watu wetu ambazo wanaziandaa kwenye masuala ya bandari zetu nimeona ujenzi wa meli za kufanya huduma katika nchi yetu. Ni lazima sasa tufikirie kutengeneza reli kubwa za kusafirisha mizigo kutoka bandari yetu kwenda nchi nyingine za mbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tukibeba shaba tukaileta kwenye bandari yetu ikakomea hapo zikaja meli nyingine kubwa zikabeba mzigo kupeleka nchi nyingine tunakuwa tumewapa biashara watu wengine. Faida ya pili meli kubwa zikibeba mzigo kutoka kwenye bandari yetu kwenda nchi za mbali mfano China, India na maeneo mengine zitakwenda kubeba bidhaa nyingine zitaleta kwetu; huduma au bidhaa kutoka nchi nyingine zilizoendelea cargo hizo zitaletwa kwa bei nafuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, meli haiwezi kuja nchini kwetu bila kuwa na uhakika wa kubeba mzigo mwingine. Kwa hiyo, inapokuja kwenye bandari yetu ikakuta mizigo mingi imeletwa kwa standard gauge railway kwenda kuipakia kwenye ile meli nyingine itakwenda kutusaidia kuleta commodities nyingine kutoka nchi nyingine. Lazima hiyo biashara tuichungulie tuifanye. Tusiachie Rainier, Messina na Maersk wanakwenda kuchukua mizigo yetu kutoka kwenye bandari yetu kwenda kwenye bandari nyingine wanafanya biashara halafu sisi tumepaki tupo idle, tunaomba tufanya biashara kupitia bandari yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine nataka kuliongelea ni kuhusiana na Ofisi ya Waziri Mkuu kushughulikia masuala ya UKIMWI. UKIMWI tumeudhibiti, sasa hivi magonjwa ya UKIMWI yanauwa kwa kiwango cha asilimia 4.2 tu. Magonjwa yanayouwa Watanzania wengi ni non- communicable diseases na ugonjwa unaoongoza ni wa moyo unauwa asilimia 30.6, unafuatiwa na cancer inauwa asilimia 15 inafuatiwa na magonjwa ya figo na magonjwa mengine pamoja na kisukari.

Mheshimiwa Naibu Spika, kumtibu mgonjwa mmoja wa magonjwa ya moyo na kisukari kwa mwaka siyo chini ya shilingi milioni nne. Ofisi ya Waziri Mkuu ibebe suala la non- communicable diseases. Kitu kikubwa ambacho kinashauriwa na wataalam ni watu kufanya mazoezi na kula chakula bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mpango wa Miaka Mitano pamoja na Wizara ya Afya nimepitia katika Kamati mipango yao, hatuoni juhudi za kufanya mazoezi, hatuoni juhudi za kuzuia magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba waingize hili katika mipango yao kila Wizara ije na mikakati ya magonjwa ya kuambukiza.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya, naunga mkono hoja, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kwanza kuanza kuchangia katika Wizara hii ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kipekee kabisa kwanza nitoe pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais wetu, Mama Samia Suluhu Hassan, hasa pale alipoweza kupata mkopo wa Trilioni 1.3. Ni kwamba, fedha zaidi ya Bilioni Mia Nane na Hamsini na kitu ambayo ni sawa na asilimia kama 75 ya fedha hizo zimekwenda kwenye huduma za jamii, kwa maana kwamba, zimekwenda kujenga madarasa, kwa maana ya sekta ya elimu, lakini vilevile fedha zimekwenda kujenga miundombinu ya sekta ya afya. Kwa hiyo, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa uamuzi wake huo mzuri wa kupeleka huduma za jamii kwa wananchi wake. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nitoe pongezi kubwa sana kwa Waziri wa Wizara hii, Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda na Naibu wake Mheshimiwa Omari Kipanga, vilevile nimpongeze sana Katibu Mkuu wa Wizara hii, Profesa Eliamani Sedoyeka, pamoja na Makamu wake wawili ambao ni Profesa James Mdoe pamoja na Profesa Caroline Nombo, watu hawa wamekuwa waungwana sana Pamoja na Watumishi wote wa Wizara hii kwa sababu wamekuwa ni watu wasikivu na wanapokuja kwenye Kamati yetu kwa kweli tunaongea kwa kuelewanana nia yetu ni moja na njema ya kutumia wanachi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, watu hawa wamekuwa waungwana sana pamja na watumishi wote wa Wizara hii kwa sababu wamekuwa ni watu wasikivu na wanapokuja kwenye Kamati yetu kwa kweli tunaongea kwa kuelewana na nia yetu ni moja na nia ni njema ya kutumikia wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusema kwamba, Wizara hii ni muhimu sana na ni Wizara nyeti kwa kizazi chetu cha Tanzania. Kwa hiyo niendelee kusisitiza yale malengo endelevu ya milenia ambayo yanatuelekeza angalau 20% ya fedha za bajeti ziende kwenye sekta ya elimu, hilo tulizingatie. Tukifanya hivyo at least kwa 17% tutakuwa tumeweza kutatua changamoto nyingi ambazo zipo katika sekta hii au zinazoikabili sekta hii ya elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, niungane na Kamati na wajumbe wenzangu wa Kamati ambao kwa kweli tumefanya kazi kubwa ya kuishauri Serikali. Katika yale maoni ya Kamati ninaendelea kusisitiza kwa mambo mawili matatu; la kwanza, ni kwenye mikopo ya elimu ya juu. Mikopo ya elimu ya juu tumekuwa na tatizo kubwa malalamiko yamekuwa ni mengi sana vijana, wazazi wanalalamikia hii Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kwa sababu tumekuwa tukipata fedha, lakini fedha hizo hazitoshi kwa Watanzania wanaohitaji mikopo kwa ajili ya kwenda kujiendeleza katika elimu za juu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Kamati tumeliona hili na wakati mwingine tumekuwa tunachanganyikiwa kwa sababu hatuelewi lengo kubwa lilikuwa ni nini? Lengo zuri la Serikali tunalitambua kwamba ni kuwawezesha watoto wa elimu ya juu waweze kusoma kwa kupata mikopo, lakini uchaguzi wa watoto hawa au wale ambao wanapewa kipaumbele kupewa mikopo inakuwa inachanganya, wakati mwingine inaonekana kwamba watoto yatima ndiyo wapewe mikopo, ni kweli mtoto yatima anatakiwa apewe mkopo, lakini wakati mwingine watoto yatima hao hawapati hiyo mikopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati mwingine tunasema kwamba wale waliofaulu vizuri masomo ya sayansi ndiyo wapewe mikopo 100%, wakati mwingine hawapati 100%, wanakomea 40% na 50%. Wakati mwingine tunasema haya basi, wapewe wale watoto ambao wanaonekana wana ufaulu mzuri kwenye masomo labda ya art na masomo mengine, bado tunaona kwamba mkanganyiko na watu wengi wameshindwa kuelewa kwamba kipaumbele cha mfuko huu ni kitu gani.

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tuliwauliza Bodi ya Mikopo, hivi kwa nini tusiwape mikopo watoto wote wa Kitanzania wanaohitaji mikopo ya elimu ya juu bila kujali ufaulu, bila kujali ni mtoto yatima, so long anahitaji mkopo huyu mtu anahitaji fedha kwa ajili ya kujiendeleza apewe mikopo. Wakasema kwamba mfuko huu ni mdogo, una bilioni 400 umeongezeka mpaka sasa bilioni 500. Je, ni shilingi ngapi inahitajika ili watoto wote wapewe mikopo hiyo? Wakasema tunahitaji bilioni 800. Hivi kweli kama mikopo hii inatolewa na baada ya muda fulani inarudishwa na hii kumbe ni biashara na wanalipa na interest kwa nini tusitafute bilioni 800, mtoto yoyote anayehitaji kukopa fedha apewe mkopo aende akasome.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kwa sababu mikopo hii inalipwa mtoto atakwenda kulipa tatizo ni nini? Tatizo hapa ni kwamba ni elimu, tuwaelimishe wazazi kwamba mzazi mwenye uwezo wa kumsomesha mtoto wake elimu ya juu amsomeshe, amuondolee ile burden ya kuja kulipa mikopo baadaye, lakini yule ambaye anahitaji kwa nini anyimwe mkopo? Hivi ni nani apate mkopo na nani akose mkopo, nani aende shule nani asiende shule.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tukasema kwamba ni vizuri Bodi hii ya Mikopo kwa sababu ilianzishwa kuwawezesha Watanzania, ifanye kazi kwa mfumo wa kibenki, wapewe fedha, watoe mikopo kwa riba nafuu baada ya pale wawafuatilie waliochukua mikopo walipe taratibu na watoto wengine waende wakasome. Kwa hiyo hili ni jambo ambalo tumesisitiza katika Kamati yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile mabenki binafsi yapewe na yenyewe fursa ya kuwakopesha wanafunzi kwa riba ndogo, itafutwe incentive kwenye mabenki haya waweze kuwapa mikopo wanafunzi wakasome.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue fursa hii nimesoma taarifa ya Mheshimiwa Waziri nawapongeza sana NMB Mungu awabariki, wametoa bilioni 200 kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kusoma elimu ya kati. Waendelee na moyo huo waendelee kutoa mikopo kwa sababu tumekuwa tunasisitiza hata wale wanafunzi wa elimu ya kati wanaosoma Diploma ufundi mchundo, wanaosoma haya masomo ya VETA, wanaotaka kupewa ada shilingi 800,000, shilingi 700,000 au shilingi 600,000 kwa nini wasipewe mikopo? Tunatoa kwenye elimu ya juu tu na kwa elimu ya juu tu yenyewe tunatoa mikopo, tumefuatilia tumekuta 62% ya mikopo inayotolewa inapelekwa kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya art, wakishamaliza kusoma masomo ya art wanapokwenda kwenye soko la ajira hawapati ajira.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kama watoto hawapati ajira 62% wametoa kwa watoto wanaosoma art, watarudisha vipi hizi fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ni vizuri kuwapatia mikopo wanafunzi wanaosoma elimu ya kati na kwa kweli Benki ya NMB imefanya jambo jema na nawaomba na mabenki mengine wajitolee, wawape mikopo wanafunzi wanaosoma elimu ya kati kwa sababu ndiyo wanaoajirika kwa haraka na ndiyo wanaopata ajira haraka na ndiyo wanaoweza kurudisha mikopo hiyo kwa haraka. Tunaomba sana hilo lifanyike.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie, suala la watumishi, sekta ya elimu inahitaji Walimu, Walimu hatuna. Sasa hivi tunajenga VETA kila wilaya na nawaomba nichukue fursa hii kuomba wilaya yangu ya Maswa wanijengee VETA. Wakishajenga VETA Walimu wa kuwafundisha watoto ufundi wako wapi? Tuwe na special program ya kufundisha Walimu watakaokwenda kufundisha ufundi kwenye VETA. Walimu wanaofundisha sasa hivi wana ile teknolojia ya zamani chuma wanaunganisha kwa zile sticker wakati siku hizi kuna teknolojia mpya wafundishwe teknolojia mpya, wapewe vifaa vya kisasa, watoto hawa wafundishwe elimu ya ufundi katika shule hizi, lakini wafundishwe na Walimu walio-qualify. Tumejenga madarasa vizuri tunashukuru, tunajenga VETA tunashukuru, lakini program ya Walimu ianzishwe ili kusudi ikawafundishe vijana hawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, Vyuo Vikuu vyetu ukienda kuangalia Vyuo Vikuu tumekwenda Chuo Kikuu cha Mkwawa, kuna Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanafunzi wamejaa wanaosoma undergraduate simply kwa sababu wanapata mikopo ya elimu ya juu. Tumeenda Mkwawa tumekuta wanafunzi zaidi ya 8,600 wanasoma undergraduate, tukauliza wanafunzi wanaosoma Masters wako wangapi? Tukaambiwa wako 57 tu kwa nini? Hakuna wanaojiunga, kwa nini hawajiungi? They are comfortable kwa sababu wanafunzi wanakuja wana mikopo ya elimu ya juu. Wanaosoma Masters na PhD hawana mikopo sasa hawawezi kuja hawa watu kama hakuna sensitization.

Tunaomba Vyuo Vikuu viwape fursa watu wanaofanya marketing waka-market kwa watu wanaotaka kusoma Masters wajiunge katika kozi hizi ili vyuo vikuu hivi viweze kuwadahili wanafunzi wa masters na PhD.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, ahsante kwa kunipa fursa. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nami awali ya yote nitoe pongezi sana kwa Mheshimiwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu Samia Suluhu Hassan, kwa fedha nyingi anazozitoa kwa ajili ya ujenzi wa sekta ya elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni. Mama ametoa fedha nyingi sana kwa maana ya kupeleka fedha kwenye sekta ya elimu pamoja na sekta ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kutoa pongezi zangu kwa Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Ndugu yangu Mheshimiwa Profesa Adolf Mkenda, kwa kazi kubwa anayofanya, pamoja na Naibu Waziri wake ambaye ni Mheshimiwa QS Kipanga. Vilevile nimpongeze sana Katibu Mkuu wa Wizara hii, Dada yangu Profesa Carolyne Nombo, anafanya kazi vizuri sana na Naibu Makatibu wakuu wake wwili ambao ni Profesa James Mdoe na Dkt. Rwezimula.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitoe pongezi kwa Kamishna wa Elimu ambaye ndiyo Mwalimu Mkuu wa Tanzania pamoja na Wakuu wa Taasisi zote ambazo ziko chini ya Wizara hii ya Elimu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nikueleze, katika Wizara ambazo wanasikiliza ushuri, Wizara ya Elimu wanasikiliza sana ushauri na hasa wa Kamati. Mnafahamu mimi nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, nimefanya nao kazi, kwa kweli Wizara ina viongozi wanaosikiliza sana ushauri wa Wabunge. Mwenyezi Mungu awabariki kwenye jambo hili, endeleeni kusikiliza ushauri na kuishinikiza Serikali kutimiza yale ambayo Wabunge wanayashauri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kupongeza Wizara na hasa katika Jimbo langu la Maswa Mashariki. Wamenipa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Mwabalatulu katika Kata ya Mpindo, lakini vilevile wamenipa fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana katika Shule ya Mwangala Sekondari, wamenipa fedha kwa ajili ya ujenzi au ukarabati wa shule kongwe ambayo fedha tulipeleka katika Shule ya Msingi Shanwa. Kwa kweli ukarabati umefanyika na kwa kweli wamefanya kazi kubwa na nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bado niendelee kushukuru kwa fedha walizozitoa katika programu ya ujenzi wa shule 63 za VETA, Maswa nayo imekuwa mnufaika, tumepata fedha ambayo inakwenda kujenga shule ya VETA na kwa kweli ujenzi huu unaendelea. Niwaombe Wanamaswa wenzangu kwamba tuusimamie vizuri ujenzi huu ili tuweze kupata shule kwa haraka na watoto wetu waweze kujifunza.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kupongeza Wizara hii, kama nilivyosema wanasikiliza ushauri. Niwapongeze sana kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kuandaa mitaala na sera ya elimu. Tumeona hapa juzi Tarehe 12 – 14 kongamano kubwa hapa Dodoma. Haijawahi kutokea, watu 1,500, wataalam mbalimbali wadau wa elimu wamekuja katika Mji wa Dodoma kutoa mawazo yao kuhusu namna ya kuboresha sera na mitaala ya elimu yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bado taarifa kupitia kwa Mheshimiwa Waziri inasema kuna Watanzania 250 nao ni wataalam, wametoa maoni yao na ushauri wao kupitia njia ya mtandao katika kuhakikisha kwamba wanatoa michango yao ili kuboresha suala la elimu katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kutoa ushauri katika sekta ya elimu ya ufundi. Tumeona ujenzi wa VETA, kila Wilaya VETA zinakwenda kujengwa. Tumeona mikakati ya Wizara ya Elimu katika kutoa elimu ya ufundi, sawa kabisa. Ushauri wangu tuendelee kuwafundisha walimu ambao watakwenda kufundisha elimu ya ufundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru mkakati wa Wizara ya Elimu mmetenga vyuo kumi vya mwanzo kwa ajili ya kutoa elimu ya walimu wanaokwenda kufundisha ufundi. Mahitaji ya walimu wa ufundi yanakwenda kuongezeka, tunaomba sana vyuo hivi ambavyo mnakwenda kuviandaa basi mviandae vizuri na kuhakikisha kwamba mnafanya udahili wa kutosha kuhakikisha kwamba vijana wengi wanakwenda kupata elimu ya ufundi na ufundi wenyewe ni ule wa kisasa kwa teknolojia za kisasa ili hawa waende kuwafundisha wanafunzi katika hivi vyuo ambavyo tunakwenda kuvianzisha katika kila Wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema haya kwa sababu tunakwenda kujenga vyuo vya VETA lakini tusipokuwa makini tutaanza tena mgogoro uleule wa kutafuta walimu wa ufundi. Kwa hiyo, ni lazima tujiandae kwa hili. Tunajenga vyuo, basi tuandae na human resources kwa maana ya walimu wanaokwenda kufundisha elimu hii ya ufundi katika vyuo hivyo, hili ni jambo la msingi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika vyuo hivi vinavyokwenda kujengwa, baada ya muda kidogo, miaka miwili, mitatu kutakuwa na uzalishaji wa wanafunzi ambao wamepewa elimu katika vyuo hivi. Baada ya kuzalishwa katika vyuo hivi, hao wanafunzi wanakwenda wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitoe ushauri. Kwanza Wizara hii pamoja na Serikali kupitia Hazina, Waziri wa Fedha kama yupo ananisikia, tuanze kutenga fedha kwa ajili ya training factories katika Wilaya zote hapa nchini. Hizi training factories zitaendelea kupokea wanafunzi, watajifunza wanafunzi mbalimbali, lakini hizi factory zitumike kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali ambazo zinatokana na mazingira husika katika eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano mzuri ambao ninaweza nikautoa katika hili, kuna maeneo ya uchimbaji wa madini, kwa mfano uchimbaji wa dhahabu, kuna mitambo mingi inatumika maeneo yale na kuna vipuli vinaagizwa kutoka maeneo mbalimbali, lakini tukiwa na factory industries, yaani kwa maana ya kwamba viwanda vidogo ambavyo vinaweza vikazalisha vipuli katika maeneo hayo, na wanafunzi wa maeneo yale wakaingia kwa ajili ya uzalishaji wa vipuli katika maeneo hayo hayo, hili litakuwa na tija kwa maana ya kwamba wataendelea kupata mafunzo na pia wataendelea kupata kipato kwa sababu watakuwa wanazalisha. Kwa hiyo, hizi factories ni very very important. Serikali sasa ianze kuangalia kwa sababu tayari tunakwenda kupata output kubwa ya wanafunzi waliojifunza katika vyuo hivi vya VETA.

Mheshimiwa Naibu Spika, niendelee kushauri tena, tumeambiwa, hata msemaji aliyepita amezungumza kwamba tukitaka kujenga Taifa, tujikite katika kuwekeza kwenye elimu, lakini vile vile tuelewe kabisa kuwekeza kwenye elimu ni njia ya kumkomboa kijana wa Kitanzania. Pia kuna jambo lingine la michezo ambalo Mheshimiwa Waziri amezungumza, kwenda kuanzisha vyuo vya michezo kwa maeneo mbalimbali. Kwa kweli lazima tufundishe vijana wengine ambao wanakwenda kufundisha elimu ya michezo katika vyuo mbalimbali. Tuna vijana wa kitanzania wana uwezo mkubwa, wana vipaji vya mpira, michezo mbalimblia ikiwa ni pamoja na vipaji vya usanii kwa maana ya kuimba na kucheza ngoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tupate walimu wa kufundisha na kuweza kufanya talent identification. Siyo hivyo tu, ni lazima tuweke na mkakati wa kufanya talent development, kwa maana ya kwamba lazima vipaji hivi viendelezwe ikiwa ni pamoja na yale masuala ya uvumbuzi mbalimbali ambao tayari Wizara ya Elimu imeanza kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwenye suala la UNESCO. Niungane na Kamati, imetoa ushauri mzuri, na tumekuwa tukitoa ushauri mara kwa mara. Tume ya UNESCO iko chini ya Wizara ya Elimu. Tume ya UNESCO haifai kukaa chini ya Wizara ya Elimu. Serikali naomba msikie, Tume ya UNESCO inasimamia mambo mbalimbali na mambo mtambuka ikiwemo masuala ya urithi wa dunia. Kwa mfano, yule mjusi mkubwa aliyeko Ujerumani, mtu wa kwanza kwenda kumdai yule mjusi ni Tume ya UNESCO. Sasa lini Wizara ya Maliasili itaongea na Wizara ya Elimu kuhusu UNESCO aibuke aende kule kumdai yule mjusi?

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la UNESCO ni suala mtambuka. Kamati imesema kwamba iende kwenye Wizara mtambuka. Ingesema tu moja kwa moja straight kwamba UNESCO iende chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ikafanye kazi yake vizuri. Hilo naomba nitoe ushauri, na kwa kweli bila kufanya hivyo UNESCO itaonekana kama vile ni mtoto ambaye hajaliwi na Wizara ya Elimu, na kwa kweli hana kazi na Wizara ya Elimu. Ana component moja tu. Tunaomba sana, ushauri wa kamati unaposema kwamba UNESCO iondolewe chini ya Wizara ya Elimu, ushauri huo uzingatiwe, iende chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ikafanye kazi yake inavyostahili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii nami kwa siku ya leo niweze kuchangia kuhusiana na Muswada huu wa Sheria ya Upatikanaji wa Taarifa (The Access to Information Bill of 2016).
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitoe pongezi kwa Serikali yetu ya Awamu ya Tano kwa kuja na Muswada huu. Nchi yetu itakuwa ni moja ya nchi tano tu kwa Afrika ambazo zitaruhusu wananchi wake waweze kupata taarifa zinazowahusu katika jamii wanayoishi kwa mujibu wa sheria. Ni nchi chache zinazotoa loophole hii kwa wananchi wake kuweza kupata taarifa tena kwa mujibu wa sheria. Kwa sababu nchi nyingi zinaficha mambo yao yanavyokwenda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi nyingi hazina transparency Government, hazina ile transparent ya kutosha ndiyo maana unakuta information zingine zinafichwa kwa makusudi kwa sababu ya watu wachache wanaoongoza hizo nchi. Tanzania kwa kuruhusu watu wapate taarifa kisheria ni progress kubwa ambayo tunahitaji pongezi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli napenda kusifia na namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kufikia hapa mlipofikia kweli tunakwenda kwenye demokrasia ya kweli yenye uwazi na kila mmoja aweze kuwa na uhuru wa kuhoji mambo yanayomhusu katika jamii inayomzunguka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri kwa kazi kubwa aliyoifanya kuandika Muswada huu, niipongeze Kamati ya Sheria kwa kazi kubwa waliyoifanya, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na wadau wote. Tumeona katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri, wamesema kwamba wadau wengi walishirikishwa katika kujadili, kuweza kujadiliana na kufikia muafaka wa kuweza kutengeneza Muswada huu ambapo utakwenda kutumika kwa hali ambayo ni ya kimaendeleo, kuleta maendeleo katika jamii inayotuzunguka. Kwa hiyo tunawapongeza sana kwa kazi nzuri waliyoifanya, Mungu awabariki sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi nyingine naileta kwa Mheshimiwa Rais wetu kwa kukubali kwamba wananchi waweze kupata taarifa katika mambo ambayo yanawahusu wao wenyewe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba basi katika Muswada huu au sheria hii izingatie zile quality za taarifa ili taarifa iwe na quality nzuri kuna mambo matano ya kuzingatia. Jambo la kwanza iwe ni taarifa ambazo ziwe ni short and clear, taarifa ziwe measurable, ziwe na accuracy yaani uhakika, ziwe reliable na ziwe in time yaani taarifa ambazo ziko katika muda unaostahili. Tukisema leo tunapitisha taarifa, lakini basi sheria ilinde, kwa mfano mtu yupo kijijini anapoomba taarifa ya jambo fulani asiletewe mlolongo wa mambo mengi ambayo hayamhusu. Taarifa ziwe ni short and clear, mtu aletewe taarifa kutokana na mahitaji ya taarifa anayoitaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ni kwamba, taarifa ziwe measurable, ina maana kwamba tunapoombwa taarifa za mambo ambayo kwa mfano mambo ya kifedha, mambo ya BOQ, ziwe ni taarifa ambazo ni zinaonekana, zenye vipimo, zenye quality ya kutosha kwa maana ya kuonesha vipimo halisi ili mtumiaji aweze kuzitumia zile taarifa kwa uhakika zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile pawe na source zinazoeleweka za kutoa taarifa hizi, elimu itolewe kwenye ngazi ya vijiji, ngazi za Kata, Tarafa, Wilaya kwamba mtu anapotaka taarifa ya jambo fulani wapi aende apewe taarifa ile, ili kusudi taarifa anayopewa iwe ni taarifa ambayo ina uhakika na aweze kuitumia katika yale masuala ambayo anataka ayafanyie kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba pia katika Muswada huu kwa sababu katika quality za kupata taarifa suala la time ni muhimu, suala la kuweka siku 30 litazamwe upya, kwa sababu kama nataka taarifa ya aina fulani kwa wakati ule, taarifa ile ikachelewa kuna uwezekano mkubwa wa mwombaji taarifa, kutoweza kuitumia taarifa ile ipasavyo kwa sababu inaweza ikamrudia muda ambao yeye hahitaji tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa inapokuwa inakuja kwa muda muafaka ndipo inakuwa na standard au quality ya kuitumia lakini taarifa nimeomba leo let say nimeomba taarifa ya BOQ ya utengenezaji wa barabara inayopita kijijini kwangu, nataka nijue hawa wanajenga kwa kiasi gani, BOQ inasemaje, wafanyakazi wanawatoa wapi, je wamekuja na wafanyakazi wao au watapata vibarua katika kile kijiji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo taarifa ikichelewa maana yake ni kwamba siku ikija inaniambia kwamba hawa watu wanatakiwa wapate vibarua kutoka kijiji husika, unakuta zile shughuli zimekwisha, ina maana hiyo taarifa haina maana yoyote. Kwa hiyo, tunaomba litazamwe kwa namna nyingine katika hizo siku 30, basi taarifa zipatikane kwa haraka na ziwe za uhakika.
Nashukuru sana kwa kutambua kwamba katika Muswada huu taarifa hizi zinakuwa wazi na kweli zitumike kwa ngazi zote kwa maana ya vijiji na maeneo yote ambayo yanatuhusu ili tuweze kupata taarifa za kiuchumi tuweze kujua bei za mazao yetu tunayolima. Mfano zao letu la pamba mkulima wa pamba anakaa analima toka mwanzo anakwenda palizi tatu mpaka anakwenda kuvuna pamba, hana taarifa ya bei inakuwaje, anakuja kupata taarifa ya bei mwishoni ameshavuna pamba, ina maana huyu mkulima amelima bila kujua atakuwa na return ya kiasi gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unakwenda ku-invest halafu hujui revenue yake itakuwaje, lazima tuwape taarifa wakulima mapema ili tujue kwamba bei ya mwakani ya pamba itakuwa kiasi fulani ili na wao kuwapa nafasi ya kuweza kutumia resources walizonazo kununua mbolea, kununua mahitaji ya kilimo ili wanapokwenda kulima wajue kwamba nitakapomaliza kulima na kuvuna return yangu itakuwa ya namna hii. Mkulima awe na uhuru wa kuamua nilime ama nisilime, kwa sababu atajua atapata faida au atapata hasara. Hivyo, tunaomba taarifa ziwe za uhakika za mapema tupate forecast information ili tuweze ku-forecast mambo mbalimbali ya kilimo na kujua bei. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika taarifa hizi za kiuchumi tupate taarifa zinazohusiana na masoko mengine, isiwe taarifa ya kupata masoko tu ya Tanzania hapana, tujue na masoko ya nchi zingine kwa maana ya kujua masoko ya kiushindani na masoko ambayo kama wakulima tunapotaka twende nje ya nchi tukauze mazao yetu, basi tujue kwamba tukilima mahindi au tuna mazao ya aina fulani, nikienda kuuza Congo au nikiuza Malawi nitapata faida kiasi gani na zile taarifa zitanisaidia kama mkulima ambaye nitaamua kufanya biashara niweze kujua mazao yangu niuze wapi kwa maana ya ushirika au kwa mtu mmoja mmoja. Hizi taarifa zije zenye uhakika tuweze kufanya kazi vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tupate taarifa za kisiasa za uhakika. Kuna taarifa za kisiasa za upotoshaji kuna taarifa za kisiasa ambazo ziko bias unakuta kuna watu wana vyombo vya habari wanazitumia zile taarifa kwa maana ya kutengeneza habari, lakini habari wanazozitengeneza ziko bias kwa kuvutia upande mmoja. Tunataka taarifa ambazo ziko neutral, taarifa ambazo mtu akisoma anakuwa anapata uelewa wa kutosha. Vyombo vingi vya private yaani vyombo vingi vya habari viko bias.
Mheshimiwa Mwenyekiti, unakuta kwa mfano, ukisoma gazeti fulani linazungumzia habari ya chama fulani, ukisoma gazeti hili linazungumzia chama kingine, ukisoma gazeti hili linazungumzia dini hii, kuna magazeti mengine na TV zinaongelea habari za mtu mmoja, kuna magazeti sijui nilikuta gazeti la Simba litaongelea Simba, hilo sikatai, gazeti la Yanga litaongelea Yanga, hilo sikatai hatutaki biasness kwenye habari, tunataka habari ziwe za uhakika ili tuweze kuzipata na kuweza kuzitumia. Kwa hiyo, watumiwaji au watumiaji wa hizi taarifa hasa watu wa media wajitahidi wawe neutral waweze kutoa taarifa za kufaa ili tuweze kuziona na tuweze kuzitumia vya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile habari za kijamii hakuna taarifa za kutosha unakuta tunakwenda kuomba taarifa pengine labda taarifa za UKIMWI, hatupati taarifa za uhakika. Kuna watu wangapi wameathirika, mnapima hawa watu je, faida ya kupima hawa watu ni ipi kwa mhusika, mtu mwenyewe ambaye ana matatizo, faida iko wapi kwa mtu ambaye ni mtumiaji wa hizi data kwa maana ya Serikali au kuna advantage ipi ya kuwapima watu kwa maana na ya clinical level, kwa maana ya wale watu ambao wanatibu wagonjwa yaani Madaktari. Tunataka tupate taarifa za uhakika ili tuwe tunajua kwamba janga hili limetufikia kwa kiasi gani na nini kifanyike.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tujue efforts zinazotumika kwa maana ya kutoa elimu ya kujilinda na magonjwa hayo mbalimbali. Sasa hivi hatujui elimu inatolewa kwa kiasi gani kuna NGO‟s zinazunguka kutoa taarifa na kutoa elimu ya kinga ya UKIMWI, lakini hatujui zinafanya kazi vipi zina-spend hela kiasi gani, unakuta NGO inapewa mamilioni ya pesa lakini hatuna access ya kuwauliza hizi hela mmepewa na mmezitumia kwa kiasi gani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba na hata hizi NGO‟s iongezeke transparency ya kupata taarifa kwenye NGO’s zinazotoa elimu; je, hizo hela wanazozipata kwa wafadhili wanatumia shilingi ngapi, kuna pesa zingine zinaweza zikarudishwa kwenye Halmashauri zetu au Serikali yetu, pesa zile zikafanya kazi vizuri na elimu ya kujikinga na magonjwa mbalimbali kama UKIMWI ikawa ni more effective na ikawafikia wananchi ipasavyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala mengine ni miradi ya maendeleo; tupate taarifa za kutosha kwenye ngazi za chini; Katibu Kata au Katibu Tawi wa eneo lolote au Mtendaji wa Kijiji aende wapi akapate accurate information ili aje awaletee wananchi wake waweze kujua nini kinachoendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna Wabunge humu hawapati taarifa za kutosha, kuna mambo yanaendelea kule Majimboni mwao hawajui, unakuta kuna kijiji tu kimesimikwa pale nguzo za umeme, umeme unakwenda kijiji kingine, kile kijiji hakina taarifa, unakuta umeme unaenda kijiji kinachofuata. Anayejua kwamba kile kijiji kinachopitishiwa umeme lini kitapata umeme, hakuna anayejua, ukimuuliza Mbunge hajui, ukimuuliza Diwani hajui, anaona tu kuna nguzo zimepita zimeenda Kata nyingine, ukimuuliza kwamba je, Kata hii itapata umeme lini hana habari mpaka uende TANESCO ukaulize na unaweza ukapewa information kwa sababu wewe ni Mbunge. Hata hivyo, tunashukuru kwa Muswada huu, tutapata taarifa hizo kwa sheria, tutakuwa na haki ya kuhoji na kupata information. Tunaishukuru Serikali kwa kazi kubwa walioifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nisiongee mengi zaidi, nashukuru sana, napenda kuunga mkono hoja hii na naipongeza Serikali kuja na hoja hii nzuri na muhimu sana.
Mhshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunisikiliza.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nashukuru sana kwa kunipatia nafasi, mimi kwanza niendelee kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa kazi nzuri anayoifanya yeye na watumishi wote katika Wizara hii ya Viwanda na Biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mchangiaji aliyekuwa akichangia/aliyemaliza sasa hivi naye amekumbushia suala la Kiwanda cha Vifaa Tiba katika Mkoa wa Simiyu hasa vifaa vinavyotokana na zao la pamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sioni tatizo ni nini, nani kakwamisha kibali hivi kama sisi tunataka nchi iwe ya viwanda sisi wenyewe tena tunakuwa vikwazo maana yake nini. Naiomba Serikali mjitahidi kuhakikisha kwamba kiwanda hiki cha vifaa tiba kinaanza kufanyakazi kwa sababu ndiyo mkombozi wa Watanzania kwa maana vifaa tiba, lakini bado ni mkombozi kwa wakulima wa pamba katika mikoa inayozalisha pamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la pamba linalimwa katika mikoa takribani minne, mitano zaidi na bado kuna mikoa mingine zaidi. Mkoa wetu wa Simiyu, Mkoa wa Mwanza, Mkoa wa Shinyanga, Mkoa wa Mara na Mkoa wa Kagera ni wazalishaji wazuri wa pamba, na sisi katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 tumesema kabisa kwamba tutajikita katika kuhakikisha tunasimamia uzalishaji wa mazao na hasa mazao ya biashara pamba ikiwemo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamba ndiyo mkombozi wa wakulima wa maeneo haya, lakini naomba nikuambie uzalishaji wa pamba huu kila siku umekuwa na maneno, umekuwa na kelele kwa sababu zao la pamba limekosa soko la kudumu. Mkulima wa pamba ananyanyasika miaka yote, sisi kwetu pamba imebadilika imekuwa siyo zao tena la biashara limekuwa zao la kisiasa, is a political crop kwa sababu wewe Mbunge, wewe Diwani unapoomba kura inabidi uongelee maslahi ya zao la pamba ndipo upewe kura. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo sisi Wabunge tuliomo humu wa mikoa tunayozalisha pamba tukirudi hivi hivi mimi naomba niwaeleze hatutarudi tena humu Bungeni kwa sababu wakulima wengi wa pamba wanaona kama vile hatuwatetei. Zao la pamba linakwenda kuzalisha nguo, market ya nguo iko Tanzania, iko Kenya, iko Uganda nchi zote za Afrika Mashariki wanahitaji nguo na binadamu anapozaliwa leo mpaka kufa kwake anahitaji nguo; ukizaliwa unafunikwa nguo, ukikua unavaa nguo, ukilala unajifunika nguo, ukienda msibani, ukifa tunakuzika umevalishwa nguo. Hakuna product iliyokuwa muhimu kutoka baada ya chakula kinachofata ni nguo na market hii ya East Africa ni kubwa mno. Lakini nguo zinazozalishwa zinaingizwa kutoka nchi za nje na tunalipa kodi kubwa tunatumia fedha za kigeni kupeleka fedha nje na tunalipa kodi hizo na tunaponunua fedha za kigeni tunakwenda kuingiza nguo kwa ajili ya matumizi ambayo ni basic kwa mwanadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamba tunayozalisha asilimia 75 tuna export hebu ona hiyo miujiza yaani raw material inayohitajika kwa bidhaa ambayo ni muhimu raw material yake badala yaku-consume sisi hata Tanzania kuitumia katika viwanda vyetu vya kuzalisha nguo, bidhaa hiyo tuna gin tuna-process kwa asilimia 25; asilimia 75 ya process yaani kwa maana ya mnyororo wa thamani tunaupeleka nje, halafu tukishaupeleka nje tunakwenda kuzalisha ndiyo tuna import tena, haya ni maajabu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Serikali msimame na miradi ya kimkakati mlijali suala la zao la pamba kuna mkakati wa CC (Cotton to Cloth) nimeona imekuwa ni maneno tu hatujui mkakati huu ni wa Wizara ya Kilimo, hatujui mkakati huu ni wa Wizara ya Viwanda, hatujui mkakati huu ni wa nani? Tunaomba Serikali mkae muamue leo kwamba tunakwenda kulipa soko zao letu la pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusitegemee wafanyabiashara watutengenezee kiwanda cha nguo, ni lazima Serikali i-invest kwa sababu gani, mnyororo wa thamani wa kutoka pamba kwenda nguo hapa katikati kuna viwanda vingi sana kuna uzalishaji wa pamba, kuna kufanya mambo ya ku-gin, kuna kutengeneza majora na kutengeneza majora kuna kuhitaji hapo katikati kuna process nyingi, hapo kuna utengenezaji wa rangi za nguo, kuna utengenezaji wa label za nguo, pakken material kwa maana ya plastic kuna vitu vingi hapa katikati mjasiriamali mmoja hawezi kutengeneza value chain ya pamba mpaka kwenye nguo ni lazima Serikali intervene, ni lazima Serikali itengeneze miundombinu wa wajasiriamali kila mmoja katika value chain hii ya pamba alenge sehemu moja afanye biashara. Kama ni mtengeneza rangi atengeneze rangi, kama ni mtengeneza vifungo atengeneze vifungo, kama ni mtengeneza uzi atengeneze uzi, kama mtengeneza label atengeneze label, the end of the day hii value chain ikikamilika ndipo unaweza ukatengenezewa shati ukavaa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo nguo uliyovaa hapo Mheshimiwa Waziri nguo uliyovaa hapo kifungo ni kiwanda kingine, label ni kiwanda kingine hiyo rangi ni kiwanda kingine viatu ni kiwanda kingine. Kila kitu ni kiwanda kingine bila Serikali ku-intervene ikatengeneza value chain nzima hatuwezi kuwa na cotton to cloth, hiyo strategy yenu haitafanikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi vitu havihitaji elimu sijui ya namna gani, kwani hamuoni kuna kiwanda kinachotengeneza baiskeli? Baiskeli inatengenezwa na fundi chini ya mti tu, lakini anayetengeneza tairi mwingine, anayetengeneza rim mwingine, anayetengeneza wire, ni mwingine ni Serikali ndiyo inayotengeneza utaratibu huu kama mnasema sijui mnaanzisha sijui industrial park tengenezeni industrial park ya tairi, tengeneza ya spoke, tengeneza ya kengele, tengeneza ya mpira, tengeneza ya wire; the end of the day mtu anakwenda ku-assemble baiskeli chini ya mti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wewe leo mnasema leo mfanyabiashara atengeneze kiwanda cha nguo! Mimi nawaeleza haitawezekana mtu akatengeneza eti nguo kamili ukienda hata pale EPZ Dar es Salaam kuna watu wanatengeneza nguo wana-export wanapeleka Marekani, lakini leo unakuta kifungo kimetoka Malaysia, unakuta sijui majora yametoka India, sijui zipu imetoka sijui wapi, rangi imetoka sijui wapi, ndiyo wanakwenda ku-assemble pale wakisha-assemble ndiyo wanapeleka wanakwenda kuuza sehemu zingine. Serikali na kama mimi leo ningeongea na Mama Samia Suluhu Hassan - Rais wetu ningemwambia aanzishe Wizara inaitwa Textile Ministry, iangalie kutoka pamba mpaka nguo kwa sababu Wizara ya Viwanda na Biashara hamtaweza peke yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba hili mlizingatie bila hivyo sisi wakulima wa pamba tutaendelea kulia na wakati tunazalisha pamba nzuri yenye thamani nzuri ambayo sisi kama Serikali tunaomba muiongezee thamani pamba yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani leo pamba tunauza shilingi 1000 tu na bado tukiuza shilingi 1000 mkulima bado analaliwa, mkulima anacheleweshewa fedha, mara tunaanzisha Ushirika, mara sijui tunafanya nini tuna chemka. Tengeneza demand ya pamba katika nchi yetu sisi tuweze kuuza pamba yetu na tuongeze thamani ya pamba yetu, tukauze Kenya, tukauze Uganda, tukauze sehemu zingine. Market ipo binadamu wote wanahitaji nguo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Mimi kwanza napenda kuchukua fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, yeye na timu yake kwa kazi nzuri wanayofanya, Mwenyezi Mungu awabariki sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi kwa Jimbo langu la Maswa Mashariki na Maswa nzima kwa ujumla kwa kweli tatizo la kukatika umeme limekuwa sugu. Kila siku tunasikia mipango mizuri na nini lakini hatuoni juhudi ya kuondokana na kero hii ya kukatikakatika kwa umeme. Kwa hiyo, nakuomba sana Mheshimiwa Waziri mfanye basi jitihada za ziada ili kuweza kuondokana na kero hiyo.

Mheshimiwa Spika, vilevile kuna vijiji vyangu vingi ambavyo havina umeme. Tumeona mradi wa REA umefanya kazi vizuri sana lakini wamefanikiwa kufikisha umeme kwenye Makao Makuu ya Kata, tunakubaliana na hilo, hata hivyo, vijiji vya pembeni mwa kata hizo havina umeme. Kwa hiyo, katika records zetu zinaonesha kama vile kata zote Wilaya ya Maswa zimepata umeme lakini ukiangalia vijiji vya pembeni mwa kata hizo hakuna umeme.

Kwa hiyo, tunaomba sana msifikishe tu umeme kwenye kata basi mpeleke na vijijini, maeneo ya pembezoni mwa kata hizo. Kwa mfano pale Maswa kuna Kijiji cha Jilago, Mwabadini, Mbugamita, Mbalagane, Chugambuli, Mwabalogi, Mlimani, Mwabalatulu, Mwamashindike, Ikungulyankoma, kote huko tunaomba umeme ufike jamani. (Makofi)

SPIKA: Yaani majina hayo, sijui urudie tena ili Waziri aandike? Endelea Mheshimiwa. (Kicheko)

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, naomba nirudie; Jilago, Mwabadini, Mbugamita, Buhangija, Chugambuli, Mwabalogi, Mlimani, Mwafumbuka, Mwabalatulu, Ifungilo, Mwamashindike na Ikungulyankoma. Mheshimiwa Kalemani atakuwa amenielewa vizuri sana, tunaomba umeme ufike tumetoa ahadi siku nyingi. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nichukue tena fursa hii kukushukuru na kukupongeza wewe na Mheshimiwa Waziri kwa uamuzi wenu mliouamua wa kupeleka ile huduma ya vinasaba kwenda TBS. Pamoja na kwamba Mheshimiwa Spika umeshaamua na Wabunge tumeshaamua kwamba tubadilishe sheria, lakini kuna data fulani napenda Watanzania waielewe; tunapopeleka huduma ya vinasaba TBS kuna advantage kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, nimezunguka kuna watu wengine mpaka wakawa wananiuliza tena wengine mpaka Wabunge wanakuuliza, hivi vinasaba ni nini? Vinasaba kwa lugha nyepesi ni rangi ya kutia kwenye mafuta na uamuzi huu tuliuamua mwaka 2010. Mafuta yanapotoka bandarini kuyatofautisha na mafuta yanayokwenda nchi za jirani ilibidi mafuta yetu tuyatie rangi, ni uamuzi mzuri sana ili kuepukana na yale mafuta yanayokwenda nje ya nchi kushushwa njiani. Hata hivyo, kitendo kinachofanyika kwa kweli kilikuwa kinafedhehesha sana kwa sababu bado mafuta yalikuwa yanashushwa njiani na kwa sababu vinasaba vilikuwa vinamilikiwa na mtu binafsi ilikuwa rahisi kuwauzia watu wengine kisha wanaenda kutia ile rangi kwenye mafuta ambayo yako on transit. Tunawashukuruni sana kwa uamuzi huu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini kwa harakaharaka hii Kampuni ya Global Fluid International (GFI) tunakubaliana walikuwa wanalipa kodi lakini naomba nikutaarifu kodi waliyolipa mwaka 2020, corporate tax, ilikuwa ni shilingi bilioni 1.86 tu na VAT walikuwa wanalipa wastani wa milioni 650 kila mwezi. Mafuta yanayopita kwa siku tuna wastani wa lita milioni tisa, wana-charge shilingi 14 kwa lita, ukichukua milioni 9 mara shilingi 14 mara siku 365 za mwaka walikuwa wanachuma Sh.45,990,000,000 halafu wanalipa corporate tax bilioni 1.86 na VAT wastani wa milioni 650 kwa mwezi.

Mheshimiwa Spika, tukiwapa TBS kwa bei hiyohiyo ya shilingi 14 mara lita milioni 9 kwa siku mara siku 365 wanapata hiyo bilioni 45.9 gharama zao ni bilioni 33. Vilevile watatoa fedha kwa ajili ya development bilioni 2.5 na bilioni 9 itakwenda kwenye Government Consolidated Fund, tutapata bilioni 9. Hii ni fedha nyingi. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Nyongo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi. Kwanza kabisa na mimi nitumie fursa hii kuipongeza sana Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kazi nzuri wanazofanya. Kwa kweli mnyonge mnyongeni haki yake mpeni; wanafanya kazi vizuri sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa harakaharaka; kwanza katika Mkoa wangu wa Simiyu. Mkoa wangu unaitwa jina la Simiyu, maana yake ni mto. Kuna Mto unaitwa Simiyu, hauna maana yoyote. Ni mto ambao mvua zikinyesha unapata maji, mvua zikikatika kwa muda mchache mto unakauka. Hauingizi shughuli yoyote ya kiuchumi, hauna chochote kiutalii, hauna tija yoyote. Isipokuwa tu tuliita Simiyu, ilikuwa ni vita vya makao makuu ya mkoa, yatakuwa Maswa na wapi, kuna wenzetu wakaamua kubadilisha jina badala ya kuuita Mkoa wa Maswa ukawa Mkoa wa Simiyu ili kuchengesha tu Makao Makuu ya Mkoa. Sasa vita hivyo vimeisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Game Reserve inaitwa Maswa Game Reserve; kwa nini Mkoa huu usiitwe Mkoa wa Maswa tuka-promote hiyo game reserve, tukai-market, tukau-market mkoa wetu. Najua sikuwepo wakati wa michakato hii, sikuwa Mbunge na nadhani ningekuwa Mbunge pangechimbika. Hata kama makao makuu yangekwenda sehemu nyingine, lakini mkoa ule ungeitwa Mkoa wa Maswa tuka-promote Game Reserve ya Maswa kuliko mto ambao unakausha maji na usiyokuwa na maana yoyote.

Mheshimiwa Naibu Spika, Ruvuma wame-promote mto wao, una maana na historia. Kilimanjaro kuna Mlima Kilimanjaro; Manyara wana Mbuga ya Manyara; Katavi kuna Mbuga ya Katavi; hata huko Chato mnataka leo tuweke Mkoa wa Chato, uitwe Burigi. Ni hilo tu nimesema nianze nalo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna suala lingine la ng’ombe kwenda kwenye hifadhi. Control ya ng’ombe kwenda kwenye hifadhi, wewe ni shahidi, inahitaji brain ya mtu mmoja tu. Just the brain of one person; anaswaga ng’ombe hata 5,000 wanakwenda sehemu fulani. Kwa hiyo decision ya ng’ombe kwenda kwenye hifadhi ni ya binadamu, tena mmoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa Serikali tunapo-charge kila ng’ombe, yaani adhabu inakwenda kwa ng’ombe mmojammoja, hiyo hapana. Hebu turudi tujipange upya tufikirie adhabu. Hivi kwani adhabu ya mtu ambaye anaendesha gari ndogo aka-overspeed na anayeendesha gari kubwa adhabu yake ni tofauti? Au kusema unaendesha basi, basi wewe kwa sababu umebeba watu wengi ukivunja sheria ina maana adhabu yake inakuwa ni tofauti na gari ndogo? Adhabu ni adhabu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu anapoingiza ng’ombe wengi kwa sababu discretion ni ya mtu mmoja, basi adhabu iangaliwe, kama alivyozungumza Mbunge wa Kiteto hapo, aadhibiwe aliyewapeleka ng’ombe, lakini siyo ku-charge gharama ya ng’ombe mmoja mmoja. Huo kwa kweli ni uonevu.

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, nimesikia na wewe umekuwa balozi wa kutetea mjusi. Huyu mjusi ambaye yuko Ujerumani ambaye ni dinosaur, juhudi hizo…

NAIBU SPIKA: Nani huyo kanitunukia ubalozi? Maana sina taarifa.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa mama Riziki Lulida amekunukia.

NAIBU SPIKA: Ahaa, amenitunikia? Nilikuwa sina habari.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, amekutunikia, u-champion wa kutetea yule mjusi arudi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba niseme hivi; Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sisi ni wajumbe au tuseme ni member wa Umoja wa Mataifa. Sisi ni member state, tuko katika mikataba ya Umoja wa Mataifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, UNESCO inasimamia masuala yote ya elimu pamoja na haya masuala ya maliasili. Mwaka 1970 tuliingia mkataba ambao unajulikana kwa jina la Convention on the Means of Prohibiting and Preventing the Illicit Import, Export and Transfer of Ownership of Cultural Property. Huu mkataba tuliuingia Paris tarehe 14, Novemba mwaka 1970 na nia ni kulinda maliasili za nchi hizi wanachama.

Mheshimiwa Naibu Spika, UNESCO ndio anayesimamia masuala yote ya ulinzi wa hizi mali za urithi katika nchi husika. Sisi tumeanza juhudi za kufuatilia mjusi huyu toka mwaka 2005. Cha kushangaza Wizara ya Maliasili badala ya kwenda UNESCO kupeleka malalamiko kule kwa sababu UNESCO ina tume yake hapa nchini na tume hiyo ndiyo yenye kazi ya kwenda kupeleka hizi hoja kule UNESCO kuishtaki Serikali ya Ujerumani ili iweze kuturudishia mjusi wetu, lakini badala yake Wizara ya Maliasili inaongea na watu wa museum (makumbusho) ambayo inahifadhi mjusi yule.

Mheshimiwa Naibu Spika, yule anayehifadhi mjusi ni mtu ambaye tunaweza tukasema labda ni mwizi. Haiwezekani wewe unadai kitu chako cha wizi, badala ya kwenda mahakamani kuomba kitu chako unakwenda kwa mwizi kwenda kujadili naye akurudishie hicho kitu. Naomba nikwambie, Kamati za Bunge zitakwenda huko, watakwenda watu wa maliasili watapokelewa vizuri na balozi, watapokelewa vizuri na watu wa museums, watakwenda watamwona mjusi lakini hakuna chochote kitakachofanyika.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Serikali, tunaomba Wizara waongee na Tume ya UNESCO waandike barua kwenda kwenye tume ambayo itakwenda kwenye vikao vinavyokubalika kisheria kutokana na mkataba wa mwaka 1970, tudai officially mjusi huyu arudishwe. Atarudishwa kwa gharama ya Serikali ya Ujerumani na atakuja kupangwa na kuwa assembled kwa gharama ya Ujerumani. Naomba hilo nikuombe sana Mheshimiwa Waziri.

NAIBU SPIKA: Muda wako umeshakwisha Mheshimiwa Nyongo.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwanza kabisa nami nitoe shukrani nyingi sana kwa Serikali kwa kuweza kutoa fedha kwa kila jimbo kwa maana ya kupeleka fedha TARURA shilingi milioni 500 kwa kila jimbo hongereni sana na ninawashukuruni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa muda ni mdogo nitataja mambo kwa juu juu tu, ninachokiomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwenye upande wa Kilimo kuna mpango wa kilimo Agricultural Sector Development Programme, mpango huu ni mzuri sana umeelezea namna ya kuongeza uzalishaji, imeongelea namna ya kuweza kufanya processing kwa mazao yetu ya kilimo, ni namna gani ya kuweza kufanya packaging, namna gani ya kuuza na kufanya masuala yote ya environmental protection haya mambo ni muhimu sana katika kukuza uchumi wa nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri wa Fedha habari tulizonazo sisi Wabunge na taarifa tulizonazo mpango huu hamuupi fedha, kama hamuupi fedha tutaendelea kupiga kelele siku zote hapa tunaongeza kilimo tuongeze kilimo, tuongeze uzalishaji kama ASDP Phase II hamuipi fedha tutakuwa tunaendelea kupiga mark time, naomba muwapelekee Wizara ya Kilimo fedha mpango huu uweze kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa utalii ongezeni matangazo, utalii wetu hautangazwi na kibaya zaidi, Waziri humu wa Utalii ulishawahi kusema vivutio tulivyonavyo sisi ni vingi hatuna haja ya kutangaza, tangazeni tunataka biashara ya utalii iongezeke katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, China ina 1.7 bilioni population ya watu wa China, mkitangazia watu wa China mkapeleka matangazo kwenye CCTV ya China 1.7 bilioni population wakisikia watu nusu ni milioni zaidi ya 800 watakuwa wamesikia habari hiyo, wakasikia na kuelewa nusu yao ni milioni 400 nusu yao wakaamua kuja kutembelea Tanzania ni milioni 200, nusu yao wakafanikiwa kufika Tanzania ni milioni 100, mkitangaza China tu tumeongeza idadi ya watalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo mnasema hakuna haja ya kuongeza kufanya matangazo ya utalii, nawashukuru Simba mmekwenda mbele, mmekwenda kwenye mashindano makubwa mmeandika visit Tanzania hiyo ni hatua nzuri endeleeni kutoa matangazo ya utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sekta ya elimu Mulugo ameongelea kuhusu mambo ya PPP nendeni kwenye PPP. Watoto wanaokwenda kumaliza darasa la saba ni wengi hatutaweza kuwa accommodate watoto kwenye madarasa tuliyonayo ya Sekondari muwa-involve private sector watusaidie na kazi ni nyepesi tu, kama mtoto anagharama tunamgharamia fedha inatoka BOT inakwenda kwenye shule za msingi na sekondari kuna gharama ya kila mtoto, gharama hiyo pelekeni kwenye shule ya Serikali na gharama hiyo hiyo wapeni watu binafsi wata-accommodate hawa watoto wawafundishe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa afya ndugu yangu hapa Mheshimiwa Shigongo kaongea vizuri kwenye preventive measures, preventive medicine, mama yangu hapa Mheshimiwa Dkt. Gwajima anakuja kuomba siku zote anaomba bajeti ya tiba, mishahara na kununua vifaa tiba pprevention haipo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba Ofisi ya Waziri Mkuu isimamie suala la prevention kuna tatizo kubwa na non-communicable diseases limeongezeka sana bila utaratibu na uratibu wa Waziri Mkuu hatuwezi kufanikiwa wananchi wetu wanakwenda kupotea kwa sababu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, vyanzo vya vifo ni zaidi ya asilimia 36 tunapata vifo kutokana na non-communicable diseases. Ukiangalia ni magonjwa ya kisukari, magonjwa ya moyo na magonjwa ya kansa pamoja na ajali, tunaomba sana uratibu wa Waziri Mkuu katika kuhakikisha tunawanusuru Watanzania kutokana na majanga ya magonjwa yasiyokuwa kuambukiza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho bandari yetu ninasoma mipango ya uchumi siku zote. Upande wa bandari yetu ni kubwa ina uwezo wa kupakia tani nyingi sana kushusha na kupakia, lakini hatuna ujenzi wa meli kubwa ya kupeleka bidhaa abroad, kupeleka nje ya Tanzania. Tumekalia kuzungumzia bandari ujenzi wa meli, meli ndogo ndogo Ziwa Victoria, Ziwa Nyasa, Ziwa sijui Tanganyika, tuamue sasa kujenga na meli kubwa ya kupeleka bidhaa nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada kusema hayo naunga mkono hoja ahsante sana kwa kunipa nafasi (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi.

Kwanza kabisa niendelee kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI na timu yake, pamoja na Katibu Mkuu pamoja na Naibu Makatibu Wakuu kwa kazi nzuri wanazozifanya. Kabla sijaendelea kwanza na mimi niunge mkono hoja, lakini vilevile niendelee kutoa shukurani zangu kwa Wabunge wenzangu wameongea vizuri sana kuhusiana na suala la Madiwani. Suala la Madiwani kukosa mishahara kupewa posho mimi naona ni kama kutokuthaminiwa, anayepewa posho ni yule mtu anayefanya kazi kwa siku ni kibarua hivi kweli Diwani amekuwa kibarua? Diwani anayefanya kazi ya kusimamia maendeleo anakuwa hatambuliki kiajira, matokeo yake analipwa posho kama vile kibarua. Mimi ninawashukuru sana Wabunge na kwa kweli Serikali imefika wakati sasa muwaone kabisa kwamba, Madiwani ni Wabunge kama walivyo Wabunge wa Majimbo na wao ni Wabunge wa Kata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Madiwani na sisi ni sawa sawa kabisa tofauti yetu na wao sisi tunakuja huku Bungeni Dodoma na wao wanabaki kwenye Halmashauri na wakati mwingine wao ndiyo wako karibu zaidi na wananchi na ndiyo wanaosikiliza shida za wananchi kila siku. Tunaomba sana Serikali iwajali Madiwani walipwe mishahara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hilo niendelee kumshukuru sana na kumpongeza Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi. Ninakushukuru sana Mheshimiwa Waziri unavyofuatilia kwa kweli kazi yako ni nzuri na kwa kweli kila mmoja anapongeza na tunaona juhudi zako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi kubwa iliyobaki ni kusimamia fedha hizi tuone thamani ya fedha katika miradi ambayo imetengewa fedha. Mimi noamba nitoe tu ushauri mdogo. Kuna Mwenge wa Uhuru unapita na unakagua miradi mbalimbali, miradi hii inapokaguliwa wanafanya ukaguzi wa ghafla. Wanafika pale jana na juzi tumeona mmoja ameshika sululu anachimba kwenye lami anakagua, mwingine tumeona juzi anabonyeza nondo kwa mikono. Ukaguzi huu ni wa ghafla wakati mwingine wanaweza kweli wakaibua hoja zenye mashiko, lakini wakati mwingine wakawa labda wanawaonea wale wahusika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kabla Mwenge haujafika eneo husika pawe na timu maalum iwe inatangulia inafanya ukaguzi wa kina, Mwenge unapofika wanapata ripoti wanatoa mapendekezo na maoni yao kisha wanafungua mradi au kutokufungua mradi. Wafanye hivyo badala ya kushtukiza, huo ni ushauri wangu wa haraka haraka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ni TARURA. TARURA mnafanya kazi nzuri nishukuru sana Maswa mmetupa kilomita za lami, kuna kilomita moja kuna kilomita moja na nusu na fedha zinakwenda, lakini hawa Wakandarasi wanapoleta zile certificate mnachelewa kuzilipa, mkichelewa kulipa miradi inasimama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maswa pale kuna mradi mmoja wa kilomita moja soko la jioni umechelewa kumalizika ule mradi wa toka mwaka 2015. Kuna Mkandarasi anadai fedha ali-raise certificate wakachelewa kulipa Shilingi Milioni 188 leo ndiyo wamemlipa sasa hivi anaendelea na shughuli lakini nchi nzima mnachelewesha kuwalipa naomba mfanye kazi nzuri, mnafanya kazi nzuri lakini tunaomba muwahi kuwalipa Wakandarasi hawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine katika Halmashauri yangu ya Maswa kuna jengo la Halmashauri, nawaombeni sana mtoe fedha mtujengee jengo la Halmashauri, Wilaya ya Maswa ni kongwe lakini jengo la Halmashauri ni la kizamani kabisa, tunaomba fedha tujenge Halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tuna ujenzi wa stendi pale Maswa tunaomba mtujengee stendi ya mabasi, kwa kweli hali siyo nzuri tunaomba fedha mtujengee stendi ya mabasi. Huo ndiyo ujumbe wangu kwenu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, kuna mazao ya mkakati, pamba ni zao la mkakati tunalima pamba sisi, kuna korosho, kuna tumbaku, kuna kahawa, kuna chai. Mazao haya kwenye maeneo wanayolima mazao haya tumeona miradi ya kutengeneza barabara kwenye maeneo wanakolima mazao haya kwa ajili ya kusafirisha mazao haya kutoka maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Maswa na maeneo mengine tunayolima pamba hatuoni mkakati wowote wa kuboresha zao la pamba, kulitengenezea miundombinu ya kusafirisha zao la pamba katika maeneo hayo. Kama miradi ya mkakati mnaitambua au mazao ya mkakati mnayatambua kwa nini pamba hamlitambui zao hili? Kwa nini mnatambua korosho, kwa nini mtambue chai, kwa nini mtambue kahawa? Mnapeleka barabara, mnatengeneza barabara nzuri katika maeneo hayo, kwa nini msitengeneze barabara za kusafirisha zao la pamba katika maeneo hayo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi tunakwenda kuivisha zao la pamba hakuna barabara, pamba imelimwa kwa wingi, watu wamevutika kulima pamba, lakini barabara ni mbovu ni mbovu haijawahi kuonekana. Tunawaomba sana TARURA muongee na Wizara ya Kilimo katika mazao ya mkakati, tunaombeni mtutengenezee miundombinu ya kusafirisha mazao haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine naomba nikupe tip moja nafahamu. Kwenye hospitali zetu za Wilaya Madaktari wana-enjoy kuandika dawa fulani na dawa fulani hazipo. Hawatoi maoteo mapema kupeleka MSD wana- enjoy kukosekana kwa dawa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wana-enjoy kwa sababu gani? Dawa inapokosekana MSD akaambiwa hii dawa iko out of stock yeye anapata nafasi ya kwenda kwa washitiri na kutangaza tender kununua kwa kutumia Local Purchasing Order. Akitangaza tender hiyo akiongea na mshitiri kule deal inapigwa huko wanapata fedha. Wakurugenzi jirekebisheni muwe wazalendo katika Taifa lenu. Ukifanya hivyo unamsababisha Mtanzania kukosa dawa, akikosa dawa Mtanzania kwa kweli hili ndilo linaleta tatizo kubwa. Mheshimiwa Waziri wekeni mfumo wa kusimamia dawa kwenye Hospitali za Wilaya, Zahanati na Vituo vya Afya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Naibu Waziri hapo anafahamu ni Daktari anajua hili. Washitiri wanafanya deal na Waganga wa Wilaya tunaombeni sana muweke mfumo mzuri kwa kushirikiana na Wizara ya Afya muwe na mfumo wa ku-monitor dawa kuanzia mwanzo mpaka inavyokwenda kutumika kwa mtumiaji. Tunaomba sana suala hilo mlizingatie. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo nashukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuwa mchangiaji wa mwisho kwa siku hii ya leo kabla Serikali kuanza kujibu.

Mheshimiwa Spika, Wabunge wengi wameongea kuhusiana na uadilifu wa Jeshi la Polisi na kweli wewe ni shahidi, malalamiko ya raia kwa askari yamekuwa ni mengi sana, lakini bado hata askari wenyewe wana malalamiko yao. Wakati mwingine unakuta raia wanalalamikia askari kwa sababu ya kubambikwa kesi na mambo mengine. Ukienda kule katika Majimbo yetu ukimkuta askari kwenye kijiji fulani labda askari Mkuu wa Kituo ni kama Mungu mtu hivi, yaani ukikorofishana na yeye ni kwamba wewe wakati wowote unaweza ukabambikiwa kesi na ukaozea ndani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini wakati mwingine kuna malalamiko kwa raia kuhusiana na ajira za askari, sasa hivi kila Mbunge hapa anaandikiwa ki-memo na wapiga kura wake, naomba unisaidie unifanyie mpango nipate ajira ya uaskari. Tatizo limekuwa kubwa, utaratibu wa ajira haueleweki, kuna hali fulani ya sintofahamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile kuna malalamiko ya wafungwa magerezani, wafungwa na wenyewe ni binadamu wana haki zao, lakini vile vile kuna malalamiko ya maaskari wenyewe kupanda vyeo, wakati mwingine wanasema kabisa kuna kupanda vyeo kwa sababu ya upendeleo fulani. Kwa hiyo kuna sintofahamu, nimejaribu kufuatilia na kuona tatizo ni nini, kuna chombo tunatakiwa tukiunde na chombo hiki ni lazima kiwepo kwa ajili ya kusimamia kitu wanaita code of conducts kwa ajili ya askari wetu au jeshi letu la Polisi na Magereza.

Mheshimiwa Spika, ni vizuri kama tungeanzisha kamisheni ambayo inaitwa Police Force and Prisons Service Commission ambayo itasimamia code of conducts ya askari, suala la kupanda cheo, kuhamishwa lisiwe suala la kufahamiana, uwe ni utaratibu ulio sahihi unaoeleweka na ulio wazi kwa Jeshi la Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kenya, Nigeria na nchi nyingine kama Jamaica na maeneo mengine wameunda kamisheni kama hii ambapo hata sisi tuna Tume ya Utumishi, mtumishi akiwa na malalamiko yake anapeleka kwenye Tume akiwa na kesi au tatizo anapeleka kwenye Tume, anatafutiwa haki yake, lakini Jeshi la Polisi ni kwamba, leo Rais wa nchi akitaka kutafuta IGP anatafuta wale watu ambao yupo karibu nao, wakati kumbe kungekuwa na chombo hiki, kingemsaidia Rais kupendekeza majina matatu au manne halafu Rais anasema katika haya mawili, matatu, manne mlioniletea yeye anakuwa na uhuru wa kuteua mmoja kuwa IGP.

Mheshimiwa Spika, leo IGP akiwa na tatizo na askari wa chini, hawawezi kumlalamikia IGP, lakini pangekuwa na chombo hiki, angepeleka malalamiko yake, chombo kikampa haki. Kwa hiyo naona kabisa kwamba tuna haja ya kuwa na kamisheni ya utumishi wa Jeshi la Polisi na Magereza, mfano mwingine kuna watu wanahamishwa kwa sababu tu ya ugomvi kati ya yeye na bosi wake, pangekuwa na chombo hiki kingeweza kusaidia kuondoa hayo matatizo.

Mheshimiwa Spika, chombo hiki rahisi tu kuunda, tungetunga sheria, tungepitisha hapa, tukawa na chombo hiki kinachoweza kusimamia code of conducts ya maaskari wetu. Kkuna maaskari waliostaafu Jeshi, kwa mfano ma IGP waliostaafu muda mrefu, wangekuwa wanateuliwa wanaendesha chombo hiki kama ilivyo kwenye Tume ya Utumishi, kuna majaji wastaafu, wanasimamia taratibu za utumishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutaendelea kulalamika askari wanaonea raia, raia wanalalamikia askari kila mmoja anamlalamikia mwenzie na msuluhishi wa hili tatizo hatumwoni, njia kubwa ni kutunga sheria ya kusimamia au ya kuhakikisha kwamba tunakuwa na kamisheni hii.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, ombi langu kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Maswa ni Wilaya Kongwe, hatujawahi kuwa na kituo cha Polisi, toka tumepata uhuru mwaka 1961. Nilishawahi kuuliza swali hapa, Maswa Kituo cha Polisi cha kwanza kilichovunjwa kilikuwa ni jengo la halmashauri, sasa hivi tumepeleka kwenye jengo la misitu, Ofisi ya Misitu ndio imekuwa kituo cha Polisi. Tunaomba watujengee kituo chetu cha Polisi ambacho kitasimamia shughuli zote za Polisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile nyumba za Polisi za Wilaya ya Maswa ni nyumba ambazo hazijakarabatiwa miaka na miaka, ni nyumba ambazo zimechoka, askari kupelekwa Maswa kwenda kufanya kazi, ukimpa nyumba ya Askari kuishi ni kama vile umempa adhabu. Tunaomba Wizara ya Mambo ya Ndani watujengee nyumba za wafanyakazi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Madini
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipatia nafasi. Awali ya yote, naomba nitoe pongezi nyingi sana kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya hasa katika usimamizi wa Sekta hii ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kutoa pongezi nyingi sana kwa Waziri wa Madini, ndugu yangu Mheshimiwa Dotto Biteko pamoja na Naibu wake Mheshimiwa Dkt. Stephen Kiruswa kwa kazi kubwa wanayoifanya. Vile vile, niendelee kutoa pongezi kwa Katibu Mkuu wa Wizara hii ndugu yangu Kheri, wanafanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Wakuu wa Taasisi zote ambazo zinasimamiwa na Wizara hii ya Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba hazidanganyi, tumeona jinsi gani Sekta ya Madini inavyozidi kupaa kwa kuongeza pato la Taifa kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017 mpaka sasa hivi tunaongelea asilimia 9.7. Hii ni hatua kubwa sana, inastahili pongezi na kwa kweli kazi kubwa sana imefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Madini tunaweza tukawa na madini yako chini ya ardhi na sisi Tanzania asilimia 90 ya madini tuliyonayo hatujayachimba. Pia madini yakiendelea kukaa chini maana yake ni kwamba uchumi wake hatutauona katika mchango wa pato la Taifa. Sasa nini kifanyike? Tunaona juhudi kubwa zinazofanyika, tuiombe leo Serikali, Wizara ya Fedha waangalie kwa jicho la kipekee hasa hizi Wizara ambazo zinazalisha fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Wizara ziko hapa nyingi tofauti, Mheshimiwa Rais anatengeneza Serikali yake kwa kuunda Wizara mbalimbali, lakini tunatambua kabisa kuna Wizara za matumizi na tunawapongeza Mawaziri humu kwa kufanya kazi kubwa ya kutumia. tunawagongea makofi, wamejenga zahanati, madarasa, barabara na wamejenga na vitu vingine. Wizara zao zinafanya kazi ya kutumia fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tuangalie kipekee Wizara zinazokusanya fedha kwa ajili ya matumizi hayo na Wizara zinazokusanya fedha mojawapo ni hii Wizara ya Madini. Wizara zinazokusanya fedha ikiwemo hii Wizara ya Madini, ni lazima tuzipe fedha za kutosha ili zilete fedha zaidi. Haiwezekani tukapata fedha nyingi bila ku-invest fedha kwenye Wizara hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Wizara ya Madini wanaipatia Bilioni 22 kwa ajili ya Maendeleo, leo tunawapa Bilioni 23, halafu tunawapa lengo la kukusanya trilioni 1.006, ni lazima tutambue kwamba ni lazima tuingize fedha kwenye miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha tunawawezesha wachimbaji wadogo wadogo ili kusudi wachimbe kwa tija, wapate fedha wao wenyewe, lakini wapeleke pato kubwa kwa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna wachimbaji wadogo ambao wanachangia asilimia 40, tuna wachimbaji wakubwa ambao wanachangia asilimia 60. Wachimbaji wakubwa ni wachacvhe lakini wanachangia kingi. Hawa leo na kesho mmoja au wawili waki-drop, itatokea shake kubwa kwenye mchango wa mapato, kwa sababu wanachangia kingi na wako wachache. Kwa hiyo, wawili au watatu kwa namna moja au nyingine ikitokea tatizo mmoja au wawili wakashindwa kuchimba, madhara yake ni makubwa kwenye pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachimbaji wadogo wanaochangia asilimia 40, ndio walioingiza ajira asilimia 80 ya uchimbaji na ndio Watanzania wengi wako kule wanachimba. Pia hii asilimia 40 wawili, watatu, wanne wakishindwa, impact haitaonekana kwa sababu ni wengi wako wachache wadogo wadogo wanachangia kingi asilimia 40. Tukiwawezesha hawa tuna hakika ni ajira ya Watanzania na wakati huo huo ndio watakuwa wazalishaji wakubwa na kuingiza fedha katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nini kifanyike? Tuendelee kuwapa fedha GST na STAMICO ili wajikite katika uwekezaji wa kufanya utafiti, kwa sababu utafiti ndio njia pekee ya kuwafanya watu wachimbe kwa uhakika na kuleta pato la Taifa. Wachimbaji wadogo wakichimba kwa uhakika, pato la Taifa litaongezeka. Hivyo basi, tunaomba GST wawezeshwe, waendelee kuongezewa fedha kwa ajili ya mikakati ya kufanya tafiti mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya kitu kinaitwa resource estimation.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wachimbaji sasa hivi wanatoka nje ya nchi na wengine wanatambua kuna dhahabu hapa, lakini hawatambui dhahabu hiyo ipo kwa kiasi gani na wa-invest kwa kiasi gani ili waweze kupata kipato. Tukifanya resource estimation vizuri kupitia GST, itakuwa ni rahisi kupata wawekezaji na watakuja kwa masharti nafuu na watachimba kwa uhakika kwa sababu tayari utafiti umefanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, GST leo wamekosa kibali cha kuajiri watafiti kwa maana ya watumishi wa GST. Naomba nishauri, kwenye Sekta ya Afya pamoja na Sekta ya Elimu tulitoa watu wa kujitolea volunteerism, watu wa kujitolea wameorodheshwa wakafanya kazi kwenye hizo Sekta za Afya na Elimu. Niwaombe hata GST ikiwezekana wako vijana wengi wana hizo taaluma za utafiti, Serikali itafute fedha, wajitolee, waingie kule wafanye kazi za kujitolea bila kuajiriwa. Hawa wafanye, ikitokea nafasi ya kuajiri wawaajiri hao. Waende wakafanye utafiti watawasaidia wachimbaji wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina mengi ya kuongea. Kingine ni suala la ufungaji wa migodi. Ufungaji huu huwa unaanza wakati migodi inaanza. Mpango wa kufunga migodi pamoja na kulinda mazingira huwa ni mpango unaoanza wakati mgodi unaanza. Leo Mheshimiwa Waziri ametueleza hapa kuna baadhi ya migodi imezuiliwa kufunga kwa sababu hawajafuata tu taratibu. Niwaombe Wizara wawe karibu na wale wanaoanzisha migodi. Ile migodi mipya, wanapoanzisha migodi hapo hapo na plan ya kufunga iwepo. Leo ukienda Buzwagi kuna pit kubwa imeshindwa kufunikwa, ni kwa sababu inawezekana kabisa kulikuwa kuna utaratibu umekiukwa toka mwanzo wakati mgodi unaanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Liganga na Mchuchuma. Nimwombe Mheshimiwa Waziri, leseni ya Liganga na Mchuchuma mwenzangu Mheshimiwa Profesa Manya alikuwa anazungumza hapa akaishia njiani. Liganga na Mchuchuma leseni zimetoka mwaka 2016, tuna chuma kingi zaidi ya tani milioni 150, tuna makaa ya mawe zaidi ya tani milioni 400 zipo zimekaa dormant, hazifanyi kazi yoyote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtu ameshindwa kuchimba kuna Sheria ya Madini, kwa nini Waziri asifute hizi leseni? Kwa sababu kutokuchimba kwa madini ya Liganga na Mchuchuma pale yale madini ya makaa ya mawe pamoja na madini ya chuma anayekosa fedha ni Waziri haingizi kwenye wizara yake.

Kwa hiyo, mchango wa Shilingi Trilioni moja, nina hakika ni mdogo kama tutajikita vizuri katika mipango yetu tutapata fedha zaidi. Kesi ya NDC na wale wawekezaji sijui Wachina Waziri aache waendelee na kesi, yeye afute leseni, ampe STAMICO achimbe, watu waendelee kufanya kazi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Nyongo.

MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushuru sana kwa kunipa nafasi na naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya
MHE. STANSALAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kwanza kabisa ya kuchangia katika hotuba hii ya Wizara hii ya Afya. Kabla sijachangia nichukue fursa hii kwanza kumpongeza Mwenyekiti wa Wabunge wa Afrika Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson, Spika wetu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jinsi alivyoaminiwa kuwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Kanda ya Afrika kule IPU. Basi tumtakie kila la kheri katika safari yake ya kugombea Urais wa Bunge au moja ya Mabunge ya Duniani (IPU). (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa makofi haya Waheshimiwa Wabunge wote wanamuombea uende ukashinde uwe Rais wa wa Wabunge wote duniani, na Inshaalah Mwenyezi Mungu atakubariki na utakuwa Rais wa IPU. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze sana Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kipaumbele chake cha kutoa fedha katika sekta ya afya, na kwa kweli tunaona uwekezaji mkubwa ambao anaufanya Rais wetu katika kuwekeza katika sekta hii ya afya na kupeleka huduma kwa wananchi, tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kazi hii kubwa unayoifanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi kama Kamati ya Afya tumefanya kazi kubwa, tumechambua kwa kina, tumeangalia kuona ni namna gani Serikali inafanya kazi kwa niaba ya Bunge lako. Tunatambua maadui wakubwa, hatujawasahau; wa kwanza ni maradhi umaskini na ujinga hawa ndio maadui zetu wakubwa katika nchi yetu. Lakini si hivyo tu maadui hawa ni maadui wa Afrika nzima; maradhi ujinga na umaskini ndio maadui wetu wakubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya nyuma viongozi wetu walikaa kule Abuja, walikaa chini wakatafakari wakasema kwamba kila nchi inapoandaa bajeti basi itengwe walau asilimia 15 ya bajeti ya nchi iende ikahudumie masuala ya afya. Mpaka sasa hivi tunavyozungumza tuna asilimia 2.8 tu ya bajeti yetu tunatenga kwa ajili ya huduma ya afya. Bado tuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha kwamba tunapeleka huduma za afya kwa Mtanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna mambo mengi ya kufanya, hakuana anayekataa, lakini mtaji wa kwanza ni afya yako. Kabla hujaenda kutafuta kitumbua au kwenda kutafuta chakula kwa ajili ya watoto wako ni lazima afya yako iwe imara. Ni lazima tuwe na mikakati ya pamoja kuhakikisha kwamba afya za Watanzania zinakuwa ni jambo la kipaumbele; kwa maana ya kwamba kila Mtanzania asiwe na wasiwasi pale anapopata shida ya maradhi yoyote basi aende akapate tiba, tiba ya uhakika na tiba ambayo ni ya hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Afya yeye na timu yake, Naibu Waziri viongozi alionao katika Wizara ya Afya, Katibu Mkuu wataalamu wetu wakuu wote wa taasisi, hiki kidogo ambacho wanapewa wanakitendea haki kwa kufanya kazi kubwa kwa kuona ni namna gani tupeleke hiki mwanzo na hiki kiwe kipaumbele cha pili. Keki hii ndogo tunayoipata ya taifa wao wanalala hawalali wanapanga ni namna gani Watanzania wapate huduma bora za afya, hongera sana Mheshimiwa Waziri Ummy kwa kazi unayoifanya.
Nakupongeza wewe kwa sababu wakati mwingine umekuwa huogopi kuchukua maamuzi kwa ajili ya Watanzania. Kuna wakati tunakuwa kama hatumuelewi, lakini tuna kuelewa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu maradhi ni adui mkubwa ni lazima tuwe na mkakati wa kutenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia wananchi. Majuzi tulikuja na mkakati wa kuwa na bima kwa watu wote. Serikali imefanya kazi kubwa kupitia mikataba ya kimataifa, kuna kitu kinaitwa Universal Health Coverage, kwamba kila nchi lazima ipeleke Huduma ya Afya kwa wananchi wake.

Mheshimiwa Naibu Spika, Tanzania imefanya kazi kubwa kupitia Serikali yetu. Tumejenga vituo vya afya tumejenga zahanati, hospitali za kanda na hospitali za rufaa. Tumefanya kazi kubwa na sasa hivi ninyi Waheshimiwa Wabunge ni mashahidi, kwamba kila Mbunge katika eneo lake kuna vituo vimejengwa, kuna zahanati imejengwa, vituo vya afya vimejengwa na hospitali za wilaya zimejengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni moja ya sehemu ya universal health coverage kwa sababu lazima tupeleke matibabu, lazima tupeleke huduma za kinga lazima tupeleke huduma za chanjo, pawe na parental care pawe na dedication; hizi zote zinaletwa. Changamoto kubwa iliyopo ni kwamba huduma imeshasogezwa kijijini huyu mwananchi anakwenda kulipia vipi huduma katika kituo ambacho ameletewa; na ndio maana tunapiga debe kwamba tuwe na universal health insurance kwamba kila mwananchi awe na bima ya afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hali iliyopo mfuko wa bima iliyopo ina-suffocate kwa upungufu wa fedha. Toto Afya Card Mheshimiwa Waziri juzi umeifuta, mimi nilishangaa, lakini tumekuja kukaa Waheshimiwa Wabunge kuona hali halisi hapakuwa na njia, njia iliyopo ni kutafua namna nyingine mbadala ya kuhakikisha watoto hawa wanapata huduma kwa kupitia huduma za bima; na bima iwe ni kuhakikisha kwamba watoto wanaingia katika package za wazazi na shule zetu zihakikishe kwamba watoto wote wawe na bima ya afya. Sasa, tunahakikisha kwa namna gani, lazima tuwe na ushirikiano kati ya wananchi wenyewe na Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi naishauri Serikali, kwa upande wa Serikali tuanzishe mfuko maalumu kwa ajili ya kuwahudumia wananchi kupitia bima zao. Tuna asilimia 28 ya Watanzania ni masikini, ni lazima Serikali iwahudumie kwa kuwapatia bima. Lakini Serikali inaingia gharama kubwa ya kuwasafirisha wananchi kwenda nje kwa ajili ya matibabu ya kibingwa. Kuna gharama nyingine kwa ajili ya ubingwa bobezi ndani ya nchi. Lakini bado tuneona hospitali zetu za mikoa na kanda zinatoa misamaha kwa wananchi zaidi ya bilioni 600 wanatoa msamaha kwa mwaka mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tuwe na mkakati wa kuhakikisha kwamba tunatoa fedha kwa ajili ya bima kwa wananchi. Suala jingine nataka kutoa ushauri, na kwenye Kamati yetu tumeeleza na Mheshimiwa aliyesoma amesoma vizuri; MSD amekuwa ni mtu anayepokea fedha kwenda kununua dawa. Tunaomba tuipatie MSD mtataji iliyoomba, inataka bilioni 592 kwa ajili ya kununua dawa. kuna kununua dawa kwenda kujenga maghala pamoja na kuanzisha viwanda vya dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, wanahitaji bilioni 92 kwa ajili ya kuwawezesha watu binafsi kujenga viwanda ili waweze kuzalisha dawa kwa matumizi ya Watanzania; na si hivyo tu watazalisha dawa hadi kwenda kuuza nje ya nchi. Tunaomba na naomba sana, Wizara ya Fedha mnatusikia, wasikilizeni MSD. Msipo wasikiliza tatizo la upungufu wa dawa ambao tunauona kwa wananchi wetu litaendelea kujitokeza. Leo tunaona kabisa kwamba MSD anafika sehemu akisema leo apelike dawa atumie fedha zote anakuwa na upungufu wa zaidi ya bilini 133.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima tufanye jambo tuihakikishie kwamba MSD anapata mtaji aweze kufanya kazi zake ambazo amepangiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimalizie kwa kusema, kwamba huduma za afya, Wizara ya Afya inafanya vizuri tunaona hospitali za kanda za mikoa zinafanya vizuri, kule chini kwenye hospitali za wilaya, zahanati na vituo vya afya bado tunaona kuna tatizo. Nadhani inafika wakati sasa, aliyeshikilia Sera ya Afya, Mheshimiwa Ummy unafanya kazi vizuri, ushikilie hivyohivyo kutoka hospitali za rufaa tukupe power ya kushikiria huduma hii ya afya mpaka kwenye zahanati na Vituo vya Afya uisimamie wewe ili…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Mwenyekiti, kengele ya pili hiyo.

MHE. STANSALAUS H. NYONGO: ...wananchi waweze kupata huduma bure bora na safi. Baada ya kusema hayo nami naunga mkono ahsante sana.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi na mimi leo niweze kuchangia katika hotuba hii ya bajeti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninampongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kwa Watanzania, kwa kweli tumeona miradi mingi sana katika Majimbo yetu. Haijawahi kutokea kuona fedha nyingi za miradi zinazokwenda katika Majimbo yetu na jinsi wananchi wanavyopokea miradi hiyo wanaipokea kwa furaha, wanaipokea kwa bashasha na naomba niseme tu kwamba mwaka 2025 Watanzania wengi watatoa pongezi hizo au watatoa ahsante kwa Mama kwa kumpa kura nyingi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile niipongeze sana Serikali kwa kujali Jimbo langu la Maswa Mashariki, tumepata fedha nyngi katika miradi, tumejenga vituo vya afya tumejenga barabara tumejenga barabara za Mjini Maswa tumeweka hadi mataa barabarani na sasa hivi kuna miradi mingi inaendelea ambayo kwa kweli wananchi wa Maswa wanashukuru na wanapongeza na watakwenda kumpa kura Mama mwaka 2025 bila kikwazo chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kupongeza Serikali juzi tumeshuhudia Serikali imeingia mikataba ya ujenzi wa barabara saba zenye jumla ya kilomita 2090 na zenye thamani ya zaidi ya trilioni 3.7. Mkataba huu tumesaini kwa mtindo ule wa EPC+F (Engineering Procurement Construction and Financing). Huu mtindo ni mpya tunaishukuru sana Serikali kwa kukubali kuingia katika mtindo huu mpya wa ujenzi wa barabara tunaona kabisa sasa barabara zinakwenda kujengwa maeneo ambayo tulikuwa hatutegemei barabara hizo kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona Ilani za Chama cha Mapinduzi mara nne au mara tano Ilani zimeandikwa zinasema kwamba barabara ya Karatu -Mbulu – Haydom – Meatu - Lalago, Maswa inakwenda kujengwa. Ilani zimepita tatu, Ilani hii inakwenda kutekelezwa kwa vitendo chini ya Mama Samia Suluhu Hassan, kazi kubwa kwa kweli Serikali imefanya, tunaomba mtindo huu kwa sababu ni mpya Serikali iusimamie kwa karibu, tuone ujenzi huu unafanyika kwa haraka na hata ndani ya mikataba hiyo kama kuna interest kutokana kuchelewesha kulipa au namna ile yoyote ambayo iliwahi kutokea katika ujenzi wa barabara tunavyojenga miaka ya nyuma, basi kuepusha hilo ni kwamba Serikali itekeleze wajibu wake kwa upande wake na wale wajenzi watekeleze kwa upande wao kwa muda uliopangwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile ninakupongeza wewe Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Serikali yako pamoja na Watendaji wako wa Wizara yako kwa jinsi mlivyokaa na kukubaliana kwamba sasa MSD ipewe mtaji. Tunawapongeza sana, tunaomba MSD wafanye kazi kwa weledi, wafanye kazi kwa uhakika Watanzania wanategemea makubwa kutoka kwao. MSD walikuwa wanaomba sana wapewe mtaji tunashukuru Serikali imekubali na mtaji umetolewa, tunaomba sasa mtekeleze kwa kupeleka fedha na MSD ianze kununua dawa ili iweze ku-supply dawa kwa wakati. Vilevile kuna ujenzi wa vifaatiba vinavyotokana na Pamba niwaombe sana MSD, kiwanda kijengwe kwa haraka, tunatambua mnakwenda kujenga kiwanda hicho katika Mkoa wa Simiyu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumzia hili kwa sababu gani? Zao la pamba tumekuwa na changamoto kubwa sana, wakulima wa Pamba tunapolima Pamba, tunapouza Pamba hii baada ya ku-gin inakwenda kuuzwa lint nje ya nchi tuna-export Pamba asilimia 70 mpaka 75, tunatumia asilimia 20 hadi 25 tu kwa ajili ya viwanda vya ndani, tukiendelea hivi Mkulima wa Pamba siku zote ataathirika na bei ya Soko la Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi lint inauzwa kwa dola 0.73, ukisema mnunuzi wa Pamba anunue kwa faida inabidi anunue Pamba kwa shilingi 800 au 900 maximum shilingi 1000. Indicative price ya Pamba ni shilingi 1,060 ukisema huyu mnunuzi anunue siku zote atakwenda kutengeneza hasara, wakati siku za nyuma bei ya Pamba ilikuwa inaongezeka, siku za nyuma tulikuwa tunaona bei ya Pamba inaongezeka kutokana na soko la dunia linavyosema, lakini tukiendelea kutegemea soko la dunia ambalo linakuwa na direct impact kwa mkulima wa Simiyu, mkulima wa Mwanza hatutamkomboa mkulima. Serikali lazima ifanye intervention kuangalia namna ya kumuokoa Mkulima wa Pamba, anapolima Pamba basi alime kwa uhakika na auze kwa bei ya uhakika inayompa faida, bila hivyo hatuwezi kuliinua zao letu la Pamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru Wabunge wengi wamepiga kelele baada ya kusikia kwamba bajeti inakwenda kupunguza kodi ya mafuta ambayo yanaingizwa kutoka nje yaani kwa maana ya crude oil kwenye palm oil.

Mheshimiwa Mwenyekiti, palm oil siku zote inajulikana duniani ni rahisi, ukiileta kwa bei ambayo umepunguzia kodi huyu muingizajiwa crude oil ya palm oil, muuzaji wa mafuta ya Pamba, mafuta ya Alizeti hawezi kuingia kwenye competition kwa sababu mafuta yake yatauzwa kwa bei ya juu. Crude oil bei yake ni chini na kibaya zaidi au kizuri zaidi kwa upande wa crude oil ukimpa huyo kodi ya asilimia 35 akiingiza atafanya refine aka-refine yale mafuta, by product yake anakwenda kutengenezea sabuni akitengeneza sabuni atapata faida huko. Mkulima wa Alizeti mafuta yake akikamua Alizeti by product yake ni mashudu, Pamba by product yake ni mashudu hayana thamani kubwa zaidi ya kuwa chakula cha Wanyama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukimshushia kodi mwenye crude oil ya palm oil, mimi niliona kwamba ina mantiki lakini baada ya Wabunge wengi kulalamika tumekuja kugundua kwamba ukiweka asilimia 35 ya crude oil ukamuwekea import duty, akiingiza mafuta akafanya refine atauza kwa bei ambayo inafaida kidogo sana lakini atatenengeza faida kwenye sabuni ambayo ni by product ya crude oil. Kwa hiyo, nadhani Mheshimiwa Waziri hebu tujaribu kukaa na ku-rethink, kuona ni namna gani ya kufanya ili kusudi Mtanzania asije akanunua mafuta kwa bei ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua crisis ya mafuta inakwenda mpaka kwa muuza chips, crisis ya mafuta inakwenda kwa Watanzania moja kwa moja. Kwa hiyo, tuiangalie mahitaji ya mafuta ni tani 680,000 kwa mwaka, Watanzania tunaweza kwa kutumia mbegu zote uwezo wetu ni ku-produce tani 300,000 tu. Sasa tani 380,000 inabidi tutoe nje sasa tuangalie ni namna gani ya kufanya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwenye Ngano. Kuna Mbunge mmoja jana hapa amepiga kelele sana jana kuhusiana na suala la Ngano, lakini Ngano tunaambiwa kwamba mahitaji ya Ngano kwa mwaka ni metriki tani 1,000,000, production yetu Tanzania ni only 20 percent, sasa hatuwezi kuishi bila ku-import Ngano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa lile sharti lililowekwa na Wizara ya Kilimo la kwamba mfanyabiashara anayetaka ku-import muwekeeni sharti, asilimia 20 mpaka asilimia 30 ya Ngano anayonunua anunue ndani, 70 percent anunue kutoka nje, liwe ni sharti ili kusudi aweze kununua Ngano ya ndani anunue na Ngano ya nje, kwa sababu yeye ni mfanyabiashara wa Ngano afanye hivyo ili kuipa soko Ngano yetu ya ndani vilevile na ngano ya nje iweze kuingia lakini mkipandisha sana kodi impact inakwenda kwa Mtanzania moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Watanzania wengi sasa hivi asubuhi Mama Lishe anapika chapati, chapati ikibaki inalika mchana na ikibaki anaenda kuwapa wanae jioni wanakula. Kwa hiyo, ngano imekuwa ni chakula kikubwa sana. Vilevile hata ukiangalia kwenye mafuta chips imekuwa ni chakula kinachoshindana na wali, zamani tulikuwa tunakula wali jioni siku hizi watu wanakula chips jioni. Kwa hiyo, ni lazima tuwe makini tukicheza vibaya tukakuta kodi imepanda impact inakwenda kwa Watanzania moja kwa moja kwa hili Mheshimiwa Waziri lazima tuwe makini na tuweze kuishauri vizuri Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo naunga mkono hoja ahsante sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa nakushukuru sana wewe na nikupongeze kwa kazi yako nzuri ya kutuongoza, wewe pamoja na Mheshimiwa Spika. Nichukue fursa hii kuendelea kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan Mheshimiwa Rais wetu kwa kazi nzuri anayoifanya. Vile vile nawapongeza sana Mawaziri hawa wawili ambao leo wameweza kuwasilisha mpango na masuala yote na mikakati ya utekelezaji wa mpango. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niendelee kusisitiza na niendelee kupongeza kwamba Mheshimiwa Rais wetu amekuwa na maono makubwa sana kwa maana ya kujenga miundombinu kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa nchi yetu. Miundombinu inayojengwa, kwa mfano SGR, tunatambua kabisa ndio msingi wa kwenda kuinua uchumi wa nchi yetu; na vile vile ujenzi wa barabara pamoja na miundombinu mingine kwa mfano uboreshaji wa ujenzi wa bandari na mambo mengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimwambie Mheshimiwa Waziri wa Mpango, Mheshimiwa Waziri kama utafikiria SGR na ambao utekelezaji unaendelea, tusipofikiria kujenga barabara na kuimarisha barabara kubwa, kwa mfano, barabara kutoka Dar es Salaam, Morogoro, Dodoma kwenda Kanda ya Ziwa Pamoja na kwamba kuna SGR tunajenga mfikirie kujenga hizi barabara na kuzitanua. Haiwezekani leo tupo karne ya 21 tunapishana barabara moja, malori makubwa, mabasi, magari madogo tunapishana kwenye barabara moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kwa sababu tukipata breakdown kidogo barabara hizi inakuwa ni chaos, watu wanasimama wanashindwa kutembea, barabara zetu zaina hali mbaya. Tusije tukaegemea kwenye SGR tukasahau barabara. Fikiria kujenga barabara nne Dar es Salaam - Morogoro, Morogoro – Dodoma, Dodoma – Singida kwenda Mwanza na upande wa Magharibi. Jengeni barabara hizi highway ziwe nne watu waweze kutembea, ndiyo uchumi wenyewe, siyo starehe. Barabara siyo starehe, barabara ni uchumi. Jengeni barabara watu waweze ku-move usiku na mchana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaona uchumi wetu unavyokua, trend ya ukuaji ni mdogo. Ukiangalia mwaka 2022 ukuaji wa uchumi wetu ulikuwa ni asilimia 4.7, mwaka 2021 asilimia 4.9, ina maana kuna difference ya asilimia 0.2. Mwaka 2023 asilimia 5.2 na tunategemea kuwa na asilimia 6.1 mwaka 2024. Ni lazima tuangalie uchumi wetu umekaa vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukitazama uchumi wetu, amezungumza Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo kwenye hotuba yake kwamba sekta ya kilimo ndiyo inayoongoza kwa ukuaji kwa asilimia 15.9, ikifuatiwa na sekta ya ujenzi pamoja na uzalishaji kwa maana ya viwanda. Ukiangalia ukuaji huu wa sekta ya kilimo ni nani anayeukuza huu uchumi? Nani yupo kwenye sekta ya kilimo? Ukitazama aliyeko kwenye sekta ya kilimo ni Watanzania wa kawaida. Asilimia 80 ndio wanaolima kilimo cha kawaida. Sasa kama wewe unategemea uchumi wako kukua na unayemtegemea ni mkulima, unamfanyia nini mkulima huyu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Bashe, amekuja na BBT na mambo mengine, lakini tuna hii document ambayo ameizungumza hata Mheshimiwa Mkumbo ya ASDP (Agriculture Sector Development Program). Hii program itekelezwe kwa asilimia 100. Kwa sababu gani? Katika SDP 2 tumeona mipango mizuri ya uzalishaji kwenye sekta ya kilimo, tumeona mipango mizuri ya uchakataji wa bidhaa za kilimo, tumeona mipango mizuri ya packaging kwa maana kutengeneza na kuweza kuongeza thamani ya bidhaa za kilimo ikiwa ni pamoja na kufanyiwa promotion na masuala ya ulinzi wa mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mpango wa SDP ushughulikiwe, utekelezwe ndiyo mkombozi mkubwa wa uchumi wa nchi yetu. Kwa mfano, zao la pamba. Nazungumzia pamba kwa sababu natoka kwenye kilimo cha pamba. Tunalima pamba miaka yote toka tumepata uhuru mwaka 1961, tuna-process asilimia 25 tu. Tunachukua pamba tunai-gin kwa ginners asilimia 75 tunaipeleka nje ya nchi. Kupeleka nje ya nchi asilimia 75 ni kupeleka ajira nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba value chain; uchakataji wa zao la pamba uongezeke. Ule Mkoa wa Simiyu mtusaidie. Serikali lazima mwekeze kwenye ku-add value zao la pamba. Badala ya ku-export pamba lint, kwa maana ya nyuzi, tu-export majora ya nguo, tu-export nguo. Bila kufanya hivyo na Serikali ku-intervene hatuwezi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukimtegemea mfanyabiashara mmoja awekeze kwenye ku-gin pamba, atengeneze kiwanda cha kufanya spinning, kiwanda cha kutengeneza nguo, mfanyabiashara mmoja hawezi. Hili tunalizungumza kila siku. Katika Mpango huu tunaomba mje na mkakati na mtenge fedha tutengeneze textile industry kwa maana ya kuhakikisha kwamba ule mpango wa cotton to cloth uweze kutekelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumesikia cotton to cloth toka enzi zile Mzee Mwijage, mzee wa vyerehani anaongelea cotton to cloth. Hivi mpaka leo cotton to cloth iko wapi? Miaka saba sasa tunaongelea cotton to cloth. Bila intervention ya Serikali kuwekeza kwenye textile kuhakikisha kwamba value chain ya zao la pamba ina-take place, bila kufanya hivyo, zao la pamba litaendelea kubaki vile vile.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkulima wa pamba mwaka jana 2022 tuliuza pamba kwa shilingi 2,000/=. Mwaka huu 2023 tumeuza pamba kwa shilingi 1,160/=, hii inakwenda wapi? Mwakani inawezekana tukauza kwa 1,000/= au chini ya shilingi 1,000/=. Huyu mkulima wa pamba mnampeleka wapi? Mkulima wa pamba analima kwa gharama kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwenye ule mpango wa ASDP imeeleza namna ya ku-increase productivity kwenye zao la pamba mwongeze productivity kwa maana ya ku-improve mbegu za pamba; kwenye heka moja ya mtu anayelima pamba, basi mfanye namna ya kuongeza uzalishaji kwa sababu sasa hivi mtu anazalisha kwenye heka moja kilo 200 mpaka 300., wakati nchi nyingine wanazalisha mpaka kilo 1,000. Ukishaongeza productivity maana yake ni kwamba tayari hawa watu umeshawaongezea ajira. Ukiweka vile viwanda vya ku-process zao la pamba tuta-add value zao la pamba na tutauza nguo badala ya kuuza lint kama tunavyofanya sasa hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana, Mheshimiwa Rais wetu ni mtu msikivu, ni mtu ambaye ana upendo, tunakuomba sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu na Mheshimiwa Prof. Kitila Mkumbo tunaomba mfanye jambo kwenye zao la pamba. Bila hivyo hatutakuwa na maendeleo yoyote katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kengele imegonga, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii.
Muswada wa Sheria ya Madaktari, Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa Mwaka 2016
MHE. STANSLAUS H. NYONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia Muswada huu ulioletwa mbele yako na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Kwanza kabisa nata pongezi kubwa kwa Mheshimiwa Waziri na Naibu wake kwa kazi kubwa waliyoifanya. Niwape pongezi kubwa wataalam waliokaa kwa pamoja kuweza kuhakikisha wanarekebisha muswada huu vizuri, niwape pongezi vilevile Kamati ya Huduma za Jamii kwa kazi nzuri waliyoifanya. Wamefanya kazi kubwa, nzuri kwa maana huu muswada ulivyoletwa kwa mara ya kwanza kila mmoja au kila mdau hakuweza kuridhika nao. Katika kufuata taratibu na kanuni ni kwamba muswada huu ulivyorudishwa basi Kamati imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kwamba inapata maoni ya kutosha na kuweza kuboresha muswada huu ipasavyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na yote kabisa naomba kwanza nitoe pongezi kwa muswada huu kuhakikisha kwamba linaundwa Baraza la Madaktari. Baraza hili la Madaktari ambalo Mwenyekiti wake badala ya kuteuliwa na Mganga Mkuu wa Serikali kama ilivyokuwa mwanzo sasa Mwenyekiti atateuliwa na Waziri hii ni hatua kubwa sana. Ni hatua kubwa kwa sababu kama Baraza litakuwa na Mwenyekiti anayeteuliwa na Waziri na huyu Waziri atazingatia masharti, atazingatia profession za huyu Mwenyekiti wa Baraza, maana yake ni kwamba Baraza hili litakuwa huru, litatenda kazi kwa kuzingatia misingi ya taratibu, misingi ya kitaalam na Mwenyekiti huyu atahakikisha kwamba analinda maslahi ya madaktari na wataalam wote wa afya, hii ni hatua kubwa ambayo inastahili pongezi ya hali ya juu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wito wangu kwa Waziri ni kwamba sasa umefika wakati wa kuangalia mtu mwenye weledi, watu wanaostahili kuongoza Baraza hili na Baraza hili litakuwa limebeba taaluma mmoja muhimu sana katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunavyofahamu ni kwamba, madaktari wanayo kazi kubwa sana ya kutibu Watanzania ambao kwa kweli wanakutana na matatizo makubwa ukizingatia hali halisi ilivyo ni kwamba madaktari pamoja na kutoa huduma kubwa na nzuri lakini wao wenyewe wana mazingira magumu sana ya kikazi. Hawana mazingira mazuri ya kufanyakazi, profession yao hailindiwi, hawana zile motivations ambazo zinawafanya wao wafanye kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama ni kwamba hata maslahi yao hayapo kama Kambi ya Upinzani walivyosema, izingatiwe wapewe bima, wapewe awards mbalimbali ambazo zitawafanya waweze kufanyakazi kwa moyo, lakini kwa sasa hivi ni kwamba hali sivyo inavyokwenda na unakuta madaktari wengi hawafanyi kazi kwa moyo, hawazingatii zile taratibu za kidaktari hivyo basi watakapokuwa na Baraza hili na Mwenyekiti wao ambae ni huru, watakuwa na nafasi sasa nzuri ya kujieleza, watakuwa na nafasi nzuri ya kuweza kutatua matatizo yao na kuweza kushughulikiwa ipasavyo, kwa hiyo tunawashukuru sana Wizara kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa maana ya kwamba sasa fani hii itatazamwa kwa macho mawili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada a kutoa pongezi hizi ningependa kutoa vilevile wito katika hii profession ya madaktari na hasa kwenye vyuo, Tunao madaktari wengi wanasoma kwa mfano pale Muhimbili wanasoma, wana- graduate, wanakwenda kufanya kazi, lakini ukitazama wale wanaoomba nafasi za kwenda kusoma masters, ukiomba nafasi ya kwenda kusoma masters wanaangalia performance yako ya undergraduate.

Mheshimiwa Naibu Spika, madaktari wengi tulionao ni wazuri, they are very bright lakini ukiangalia matokeo yao wamepewa marks ndogo ndogo sana pale Muhimbili, wanakosa nafasi ya kujiendeleza kwenda kufanya masters, hilo ni tatizo kubwa sana matokeo yake ukitazama vyuo vingine nje ya Muhimbili, kuna vyuo vingine kama IMTU na sehemu zingine unakuta madaktari ni wa kawaida wenzangu na mimi, ni bachelor holders lakini ukitazama kule performance yao wale walimu wao wamewapa marks nzuri kwa hiyo ukienda kwenye masters wale wakipeleka zile pass marks zao wanaonekana wao wame-perform vizuri zaidi, ukimtazama daktari anayetoka Muhimbili ana-performance ambazo ziko poor ha-qualify kwenda masters.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hizi Sheria na hii miswada imetengenezwa vizuri lakini nafikiri wangetazama na kwenye taaluma kule nako kuna tatizo kubwa sana, watu wanaonekana kama hawana uwezo wa kwenda kufanya masters lakini ukienda back to the roots unamkuta yule Daktari aliyetoka Muhimbili ni mzuri kabisa ana uwezo mkubwa kuliko yule ambae amesoma IMTU na vyuo vingine. Hii ni kisa tu kwamba Muhimbili ukisoma pale kufaulu kupata “A” au kupata GPA nzuri ni ngumu kwa sababu Muhimbili ni chuo kigumu. A is A uende dunia yoyote ile A ni A, B is B wherever you go B ni B. Sasa hakuna B wala hakuna C ya Muhimbili na hakuna C ya IMTU. Ukienda Uturuki, ukienda Russia, ukienda wapi C is C. Sasa wewe mwanafunzi wako unampa pass mark mbovu, anakwenda ana-graduate, anapata registration, anafanya kazi halafu kutaka kwenda kusoma masters ili sasa awe Daktari Bingwa wakitazama vyeti unakuta performance ni ndogo, anapita yule wa chuo kingine anakwenda anachukua masters. Sasa hilo warudi nyuma wajitazame kwa sababu hii ni profession sasa inakwenda kulindwa na hata kwenye masuala ya taaluma na wenyewe wayazingatie, waangalie.(Makofi)

Mheshimwia Naibu Spika, lingine nashukuru kwa kupitisha Muswada huu vilevile kwenye masuala ya leseni, nashukuru sana na napongeza kwamba hata AMO’s sasa wanapewa leseni kwasabbu AMO’s walikuwa wana- operate, mgonjwa akipata cesarean infection, kwa mfano hizi operation za kawaida ambazo zinahitaji ku-take measures ambazo ni za emergence walikuwa wanazifanya.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda kwenye vituo vikubwa vya afya wanafanya, hospitali zingine za Wilaya wale ndiyo Madaktari wakubwa wa Wilaya. Ule Muswada wa mwanzo ulikuwa unakataa kuwapa leseni hawa ilikuwa ni disaster kubwa. Kwa sasa hivi tunashukuru kwamba kwamba na wao wanaingia kupewa leseni ya kuweza kufanya au ku-practice hivyo vitu. Kama wameingia kupata hizo leseni tunashukuru kwamba sasa na wao watafanya kazi with confidence, watafanya kazi katika hali ambayo na wao watajisikia kwamba ni watu ambao wanathaminiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wito wangu mwingine wa mwisho, kuna kitu kinaitwa Medical Association of Tanzania yaani Chama cha Madaktari Tanzania. Tuache ubaguzi, Madaktari wengi wanaoingia kwenye hiki chama ni wale ambao tu tayari ni graduates, lakini kumbe kwa kupitisha hii sasa mpaka leo watu wanapata leseni ya AMO’s na CMO’s wanapata leseni sana AMO’s, CMO’S sina hakika, lakini kama na wao wanapata hizi leseni basi na wao waingie kwenye hicho chama. Ukienda Kenya mpaka wauguzi wamo. Kwa hiyo, wanaposimama kwa pamoja wanakuwa na nguvu ya pamoja kuongea, wanakuwa na nguvu ya pamoja ya kutetea maslahi yao. Wakisimama hata Serikali inatikisika kwamba sasa hawa watu wanazungumza kwa kauli moja, lakini Medical Association of Tanzania haina nguvu yoyote hata ofisi waliyonayo ni chumba kimoja tu lakini ukienda Kenya wamejiendeleza.

Mheshimiwa Naibu Spika, Medical associateion yao ni kubwa hata ukitazama jengo lao ni kubwa, wana facilities nyingi, watu wanaweza wakatolewa mafunzo mule, wakajifunza mambo mbalimbali. Kwa hiyo, na wao naomba warudi nyuma waweze kuangalia ni namna gani sasa ya kuweza kuimarisha hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukitazama Baraza limepewa kazi kubwa kama litakuwa huru na limepewa nafasi vilevile ya kuweza kumiliki mali tumeona katika Muswada huu basi wamiliki mali kwa maana ya kwamba wawe na uwezo wa kujiendesha wao wenyewe ili wawe na nguvu, hata wanapotetea maslahi yao basi Serikali inaweza kuwasikiliza na kuwatekelezea mambo yao.

Mheshimwa Naibu Spika, otherwise nashukuru sana na naunga mkono hoja. Ahsante sana.