Contributions by Hon. Elibariki Emmanuel Kingu (38 total)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa heshima na taadhima napenda kumshukuru Mungu wa mbinguni, aliyeziumba mbingu na ardhi kwa kunipa fursa hii mchana wa leo kuweza kuchangia hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa miezi michache iliyopita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitakwenda moja kwa moja kujikita katika hotuba ya Mheshimiwa Rais katika sekta ya kilimo. Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa Wilaya zilizopo katika Mkoa wa Singida. Nikiri kwamba Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa michache inayochangia katika Pato la Taifa hasa katika sekta mafuta ya kupikia. Kilimo cha alizeti ni zao kubwa la kiuchumi na kibiashara kwa wakazi wa Mkoa wa Singida, Wilaya yangu ikiwa ni miongoni mwao. Nikiri kwamba so far Serikali yetu bado haijafanya juhudi za makusudi na za kutosha kuhakikisha kwamba inawatafutia wakulima wetu masoko ya kuuza mafuta na kuhakikisha mazao mbalimbali yanayotoka katika Mkoa wa Singida yanapata masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitoe mfano katika Wilaya ninayotoka na Jimbo la Singida Magharibi. Wilaya na Jimbo ninalotoka tunakabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa masoko ya mafuta yanayozalishwa katika viwanda vidogo vidogo ambavyo kimsingi vinawasaidia wananchi wetu kupata kipato.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, nilizungumza hili pia na Waziri wa Kilimo tulipopata muda wa kuteta kidogo, tuna changamoto kubwa ya uharibifu wa ndege kwa lugha ya nyumbani wanawaita selengo. Mazao ya wananchi yamekuwa yakiliwa kwa kiwango kikubwa sana lakini kwa kipindi chote cha karibia miaka kumi Serikali haijaja na majibu ya kuweza kuwasaidia wananchi mazao yao yaache kuliwa na hawa ndege. Nilizungumza na kaka yangu Mwigulu Nchemba, ni rai yangu tena kwa Serikali yangu hii ya Awamu ya Tano, watu hawa wanatumia nguvu zao kuzalisha lakini kilio chao kimekuwa hakisikiki sawasawa Serikalini na hawapati majibu juu ya kutatua tatizo lao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mungu wamemchagua Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ni Waziri msikivu, Waziri mwenye moyo wa kuwasikiliza Wabunge, muda wote ukimpigia simu anakusikiliza.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwigulu Nchemba nakuomba kaka yangu spirit uliyonayo endelea nayo, Wabunge wengi wanakupenda kwa sababu huna kiburi, unajishusha chini ya miguu ya watu.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Nakuomba na natoa rai, panga ziara twende Jimboni kwangu ukaone uharibifu mkubwa unaofanywa na ndege wanaitwa selengo kwa mazao ya wanyonge hawa. Nakuahidi ukienda kutatua kero hii Mungu wa mbinguni atakukumbuka na thawabu zake zitakuwa juu yako. (Makofi)
Mhesheshimiwa Mwenyekiti, nizungumze pia katika sekta ya elimu, nitumie fursa hii kwa dhati ya moyo wangu kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Simbachawene kwa agizo alilolitoa kwa Halmashauri zetu zote kuhakikisha kwamba watoto wa Kitanzania, is a shame kwa nchi, watoto wa Kitanzania kukaa chini ya mbao fifty years of independence. Tunaweza tusielewane hapa tukaona kwamba tunaishambulia Serikali lakini ni aibu kwa nchi watoto wa Kitanzania kukaa chini ya mbao miaka 50 ya uhuru. Haya mambo tusipoyasema sisi Wabunge wa CCM tutawapa nguvu watu wa Upinzani watayasema watabomoa Serikali yetu. (Makofi)
Kwa hiyo, mimi nasema, wito uliotolewa na Waziri Simbachawene na kaka yangu Simbachawene nikutie moyo, toa circular ipeleke kwa Wakurugenzi wako wote nchini, wape deadline na mikakati. Mimi kwa mfano kwenye Jimbo langu nimepeleka proposal Halmashauri, nimewaambia tuko tayari sisi kutoa nguvu kwa kutumia fedha zetu na kutafuta fedha za wafadhili, tuna mapori mengi tunayalinda wakati watoto wa Kitanzania wanakaa chini. Watu waruhusiwe wapate vibali, tukakate mbao, tuchonge madawati, nakuhakikishia suala la watoto wa Kitanzania kukaa chini itakuwa na history katika Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya afya, niiombe Serikali na nimuombe Mheshimiwa Waziri wa Afya, Mheshimiwa Rais alipokuwa akifanya kampeni miongoni mwa ahadi alizozitoa alisema kwamba tutahakikisha tunakwenda kujenga zahanati katika kila kijiji cha Taifa hili. Nimuombe dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu, nina imani naye, ana uwezo wa kufanya kazi, Jimboni kwangu tumeshamuanzishia, tumeanza ujenzi wa zahanati katika vijiji 19. Namuomba Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Serikali pale ambapo Wabunge tunakuwa na initiatives zetu wenyewe na ku-solicit kutafuta fund kwa maarifa yetu, Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi isichelewe kutuunga mkono Wabunge kuhakikisha kwamba tuna-fulfil ndoto na njozi za Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niongeze jambo lingine, ndugu yangu amezungumza hapa kuhusiana na Madiwani lakini pia niwatetee Wenyeviti wa Serikali za Vijiji. Kama inawezekana, najua vijiji ni vingi lakini kama Serikali inaweza ikajipanga at least katika kipindi chao cha uongozi cha miaka mitano wakaangaliwa. Watu hawa wanaisaidia Serikali na kufanya mambo makubwa, naomba Serikali pia iweze kuwakumbuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala mwisho ni reli ya kati na reli ya Singida. Ikumbukwe kwamba kipindi cha utawala wa Mheshimiwa Benjamini William Mkapa, Serikali ilitumia mamilioni ya shilingi kufanya uwekezaji wa kujenga reli iliyotoka Dodoma kuja mpaka Singida. Leo ninapozungumza reli hii ya Singida imeachwa haifanyi kazi. Ushauri wangu kwa Serikali ya chama changu, najua tupo watu baadhi tuna interest katika sekta ya transport, tujenge reserve ya kutosha ya mafuta pale Singida, reli ifanye kazi ya kusafirisha mafuta kutoka Dar es Salaam mpaka Singida. Magari yanayotoka Mwanza, Bukoba, Kagera, Shinyanga, Tabora wachukulie mafuta pale Singida, hii reli tuliijenga kwa faida gani?
Ndugu zangu kwa nini tunawekeza vitu halafu hatuzingatii suala zima la value for money? Hii reli haina kazi! Najua watu wanaweza wakani-attack maana najua kuna watu wana interest kwenye mambo ya malori na transport, I don’t care, lakini suala la msingi reli ya Singida iliyojengwa inawezaje kutumika hata kusaidia sekta ya barabara ambazo zinaharibika kwa sababu ya malori. Pelekeni mafuta Singida pale tutawapa maeneo ya kuwekeza kama mko tayari. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima nirudie tena kwa mara ya mwisho kwa dhati ya moyo wangu na bila chembe ya unafiki na kwa unyenyekevu mkubwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Aidha, naongeza kumuunga mkono kaka yangu Kitwanga, suala la NIDA mlilolifanya jana, nakupongeza Kitwanga simama, we are behind you, tunakuunga mkono.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mimi nataka nikuhakikishie, nimefanya kazi Serikalini, nilikuwa nikifanya kazi Fair Competition Commission mwaka 2010 kabla sijateuliwa na Rais, nimepigwa picha ya kutengenezewa kitambulisho cha Taifa mpaka leo sijapata. Kitwanga kanyaga, tunakuunga mkono na watu wa Mungu tutafunga na kuomba kwa ajili yako. We will pray for you brother.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, kwa heshima na taadhima, naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia, ahsanteni sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kuweza kuchangia katika mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitajikita moja kwa moja katika ushauri kwa Serikali. Jambo la kwanza ambalo ninafikiri nitumie nafasi yangu ya uwakilishi kuishauri Serikali ni katika ongezeko la mahitaji ya matumizi katika fedha tunazozipata kutokana na deni la ndani na nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, itakumbukwa kwamba katika kipindi cha mwaka ulioisha 2015/2016 matumizi makubwa ya deni la nje na ndani la Taifa yalielekezwa katika sekta za nishati, barabara, madaraja na viwanja vya ndege. Nataka nimshauri kwa dhati kabisa Waziri wa Fedha, tunakopa fedha kutoka nje na ndani kwa lengo la kwenda kuwekeza kwenye sekta ambazo kimsingi hazina uhusiano wa moja kwa moja katika ku-stimulate ukuaji wa uchumi, kuna tatizo. Ninatoa mfano, tunakopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha za ndani na za nje ya nchi, tunajua sote kwa pamoja asilimia 80 ya Watanzania ni wakulima. Hivi ndugu zangu katika fikra tu za kawaida, nimeshawahi kuwa Mkuu wa Wilaya pale Igunga, katika vitu ambavyo lazima Waziri wa Kilimo na Waziri wa Fedha mfanye kazi kwa coordination. Ndugu zangu ukiangalia miradi tuliyonayo kama nchi, miradi mikubwa ya schemes of irrigation ni miradi ambayo ilijengwa na muasisi wa hili Taifa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema kwamba nchi tunataka tuwasaidie wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, hivi tunaachaje kwenda kukopa fedha na kwenda kuwekeza kwenye miradi ya kuwasaidia wakulima kufunga irrigation schemes? Nina mfano mmoja na Mheshimiwa Dalaly Kafumu utaniunga mkono.
Nilipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, tuna mto unaitwa Mto wa Mbutu kipindi cha mvua mto huu kuna maji ambayo ukienda kuyaangalia yanayotiririka na kupotea na chini ya Igunga kuna eneo la karibu mpakani mwa Singida na Igunga eneo ambalo ni fertile kwa ajili ya shughuli za kilimo. Tumepiga kelele tukiwa pale kwamba utengenezwe mkakati ifunguliwe irrigation scheme kubwa ajili ya kuongeza tija katika uzalishaji wa kilimo cha mpunga Igunga mpaka leo imekuwa hadithi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri nataka nitoe ushauri, tunapokopa fedha kutoka katika Taasisi za ndani na nje, pelekeni fedha hizi kwenye miradi ambayo itakwenda ku-stimulate ukuaji wa uchumi na kumgusa mwananchi moja kwa moja kilimo kikiwa cha kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya pili, tunazungumzia habari ya ku-industrialise nchi, how do we industrialise nchi wakati vocational education hakuna mipango yoyote ya kusaidia kwenye vocational education hapa? Nilitarajia Waziri wa Elimu kwa kushirikiana na Waziri wa Fedha kuwepo na coordination ya kuhakikisha ya kwamba tunapojiandaa nchi kui-industrialise lazima tuwaandae watoto wa Kitanzania kuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi kwenye viwanda tunavyotaka kuvijenga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano, ninawapongeza watu wa NSSF nimeona wameifungua National Milling, ninaona wanaelekea kujenga Kiwanda cha Sukari ambacho wanasema kinakwenda kuajiri watu zaidi ya laki moja, nani tumeshaanza kuwaandaa watoto wa Kitanzania ndani ya miaka tatu kitakwenda kusimama, tumefanya mikakati gani kuwandaa watoto wa Kitanzania kuwa na vocational skills ya kwenda kifanya kazi kwenye viwanda hivi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu niwashauri Mawaziri kwa nia njema Mawaziri wa Serikali yangu, Mawaziri wa Serikali inayotokana na chama changu, niwashauri. Ninawaomba ndugu zangu, mambo mengine hebu tuwe na creative sisi wenyewe tuwe na creativity, kwa mfano, hata suala hili la kumaliza tatizo la madawati tulisubiri mpaka Rais atoe tamko, lakini hivi leo tunaposema nchi tunataka iwe nchi ya viwanda hivi tunajua kwamba tuna walimu wetu mpaka leo hawana nyumba za kuishi? Hivi kwa nini asitokee Waziri mmoja aseme ninaweka mikakati ndani ya kipindi cha miaka mitatu hakuna mwalimu atalala nje, hakuna mwalimu atakwenda kukaa kwenye nyumba ya kupanga linashindikana hilo? Mambo haya tukiweza kuyafanya ndugu zangu tutajenga base ya kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa itakuwa ni elimu itakayoendana na zama hizi tunazozungumza, zama za viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wa pili, kudorora kwa uchumi. Ninaishauri Serikali yangu kwa nia njema, hakuna shaka kwamba kuna viashiria na dalili kwamba uchumi wa nchi yetu to some extent kuna mdororo. Ninatoa ushauri kwa kaka yangu Mheshimiwa Mpango, Mheshimiwa Mpango ninakujua nimefanyakazi na wewe nikiwa Serikalini, ninakujua uzalendo wako haya mambo ya kuteleza hapa na pale tutasaidiana kwa lengo la kulijenga Taifa letu.
Ninakupa ushauri, Mheshimiwa Waziri wa fedha fanyeni kila mnaloweza punguzeni base ya kodi kwa wananchi, kodi zimekuwa nyingi sana. Tume-tax kila maeneo na unapoongeza tax kila eneo definitely lazima utapunguza circulation ya fedha kwenye uchumi. Na ukishapunguza circulation ya fedha kwenye uchumi utakwenda kuathiri masuala mazima ya huduma na uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri ninaotoa kwa Serikali yangu, kuna fedha mlizichukua za mashirika na taasisi mkazipeleka kuziweka kwenye deposit ya Benki Kuu. Watu wa mashirika ya umma, NSSF na mashirika mengine walikuwa wakipata riba kutoka kwenye mabenki kwa hizo deposit. Ninawashauri Waziri wangu rudisheni fedha hizi kwenye mabenki, yaiteni mabenki myape maelekezo yapunguze riba ya mikopo kutoka asilimia 18 mpaka 13 mtakuwa mmeongeza wigo wa Watanzania kukopa na mtakuwa mmesaidia middle class katika business hapo tutakuwa tunajenga uchumi wa nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna theory inasema kwamba kiuchumi, mahali popote unapotaka ku-stimulate uchumi wa nchi kwa lengo la kukuza wafanyabiashara wa kati, ukifanya kitu kinaitwa kupunguza pesa kutoa pesa kwenye mzunguko katika uchumi maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba watu wanapokuwa hawana fedha kwenye uchumi inakwenda kuathiri hata shughuli za uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninatoa ushauri tusi-ignore suala la kusema kwamba pesa hakuna mtaani tukaishia kusema kwamba watu wanapiga dili, hapana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tuende extra miles na tutumie wachumi wa Taifa hili tulionao wafanye tafiti, watuambie Tanzania kwa uchumi tulionao ni fedha kiasi gani zinahitajika ziwepo kwenye circulation na watupe majibu ni fedha kiasi gani sasa hivi kwenye circulation hazipo, ziko wapi ili kusudi tuweze kuwa na remedy katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nizungumzie suala zima la sera za kifedha (monetary and fiscal policy). Ukiamua kujenga uchumi ambao utaleta ushirikishwaji wa wananchi lazima tuhakikishe ya kwamba uwepo wa fedha nyingi kwenye mzunguko. Inawezekana labda Waziri wa Fedha waliamua kubana fedha kwenye mzunguko kwa lengo la ku-control inflation kwenye nchi kwa maana ya kwamba bei zinakuwa juu na fedha inakisa thamani. Lakini nataka nikwambie kitu kimoja, bado tunaweza kulifanya hili kwa kuziagiza commercial banks zikaweka riba kubwa kwa watu wanaweka deposit. Watu watapeleka fedha kwenye mabenki lakini pia tukaziambia benki zikashusha riba ya mikopo kwa wafanyabisahara wa kati na wakubwa tuta-encourage private sector kuchukua mikopo na ku-invest. Tunaposema tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda tukiacha hali iendelee namna hii kuna hatari kubwa ya Serikali kukwama na kuna hatari kubwa ya nchi kukwama kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia jambo lingine ninalotaka kushauri kwa nia njema kabisa kuna mambo tumekuwa tukiyazungumza hapa kwa muda mrefu. Ninawashauri Mawaziri wangu wanaotokana na chama changu kilichoko madarakani kwa nia njema tunaomba sana Mawaziri wasiwe wanasubiri mpaka matukio ndiyo waweze kuchukua hatua kwa mfano, mwaka jana kipindi tunafungua Bunge la mwezi wa 11, nilikuja na kilio juu ya usumbufu wa ndege wanaokula mazao ya wakulima maskini watu wasio na kipato. Tunazungumza hapa Mheshimiwa Waziri, leo ninapozungumza Singida ndiyo Mkoa tuna-lead katika production ya sunflower lakini leo ninavyozungumza asilimia 70 ya sunflower iliyolimwa kwenye jimbo langu ililiwa na ndege wanaitwa silingwa na mpaka sasa hivi tunavyozungumza nina imani hata Waziri usikute wanasubiri msimu ufike tuanze kupiga kelele tena Bungeni hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba mtimize majukumu yenu kwa lengo la kumsaidia Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Sina mashaka na uzalendo wa Dkt. Magufuli, sina mashaka na uzalendo wa huyu Rais katika kutetea na kupigania maslahi ya Taifa hili lakini inawezekana kabisa kuna baadhi ya wasaidizi kwa makusudi yao wameamua kumkwamisha Rais wetu whether kwa kuogopa kumshauri vizuri. (Makofi/vigelele)
Kwa hiyo, ninatoa ushauri tusisubiri mpaka mambo yaharibike ndiyo tuje kwa ajili ya kuanza kupiga kelele. Wakulima wetu wanahitaji kuiona Serikali yetu iko proactive na kushughulikia matatizo na changamoto zao kabla athari hazijaonekana. (Makofi/vigelele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika sekta ya elimu, ni wazi kwamba Mheshimiwa Rais Dkt. John pombe Magufuli alipokuja na sera ya elimu bure, niitumie fursa hii kuipongeza sana Wizara ya elimu na kumpongeza Rais japokuwa changamoto ni nyingi lakini ninauona moyo wa kizalendo wa Rais wetu katika kulitetea suala zima la sekta ya elimu. Changamoto tuliyonayo na alizungumza kaka yangu Mheshimiwa Heche, alizungumza leo asubuhi, tumeongeza idadi ya enrolment. Mimi kwenye jimbo langu peke yake asilimia ya wanafunzi walioongezeka kwenye udahili ni asilimia 17.8 kwenye jimbo langu lakini ndugu zangu tunauhaba wa vyumba vya madarasa, hivi ndugu zangu hili nalo tunasubiri mpaka Rais atoke atoe declaration kwamba muanze vyumba vya madarasa? Kwa nini tusiweke mipango mikakati tuseme ndani ya kipindi cha miaka miwili tatizo la changamoto la uhaba wa vyumba vya madarasa litakuwa limetatuliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa changamoto kwa Mawaziri, ninatoa changamoto kwa Baraza langu la Mawaziri, nendeni mkakae mjifungie pelekeni proposal Dkt. Magufuli ni Rais msikivu suala la madawati nililizungumza mimi hapa Bunge la kwanza ndiyo nilikuwa Mbunge wa kwanza kulizungumza na alipokuja Singida sisi tulionyesha mfano na chama…(Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa heshima na taadhima nakushuru kwa kunipa nafasi. Waheshimiwa Wabunge na ndugu zangu Watanzania ambao tutapata fursa ya kulisikiliza Bunge letu, nina mambo ya msingi mawili ya kuyazungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ieleweke kwamba tunaposema kitu kinachoitwa Serikali lazima tujue ya kwamba wajibu na kazi ya Serikali ni kuhakikisha inasimamia masuala mazima ya ulinzi na usalama ukiachilia mbali masuala ya kiuchumi. Nimeshawahi kubahatika kuwa Kiongozi wa Dola katika mbili ya Wilaya katika Taifa hili. Nataka niwaambie tunaweza tukazungumza mambo hapa kwa sababu ya kishabiki na mihemko ya kisiasa, bila kuangalia masuala mazima ya hatma ya nchi. Ninachotaka kukisema, duniani kote ili watu waweze kukaa kwa amani na utulivu, ni lazima Serikali ijulikane kwamba ipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na suala zima la Serikali katika kuwekeza kwa Jeshi la Polisi. Yamezungumzwa maneno mengi, lakini nataka nikwambie sisi wenyewe Wabunge wa CCM haturidhishwi na hali ya Askari wetu wanavyoishi. Tunaiomba Serikali yetu ifanye hatua za makusudi, kwanza kuwapatia posho katika mazingira magumu ya kazi wanayofanya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, utakumbuka, kuna wakati mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Iringa, nimeletewa taarifa mabasi yametekwa pale Igunga.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza na Askari, OCD hana mafuta ya kupeleka Askari. Haya lazima tuyaseme kwa sababu tusipoyasema tutakuwa hatulitendei haki Taifa letu. Natoa wito kwa Serikali yangu, natoa wito kwa Jeshi la Polisi, tengenezeni unit maalum itakayokuwa ina-deal na suala la kuhakikisha supply ya mafuta kwa Ma-OCD nchi nzima. Mafuta haya yasipite kwa Ma-RPC yaende kwa Ma-OCD kule kwa sababu wakati mwingine OCD anaweza akashindwa kumwambia bosi wake, tunao uzoefu huo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, Sekta ya Madawa ya Kulevya. Wiki tatu zilizopita kabla Bunge halijaanza, Kamati yetu tumefanikiwa kwenda kuangalia depot inayohifadhi madawa ya kulevya. Tumekwenda pale, mazingira wanayofanya kazi Askari wetu, Mheshimiwa IGP uko hapa, najua utanisikiliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Jeshi la Polisi angalieni namna ya kuwasaidia Askari wanaopambana na watu wanao-deal na drugs muwa-treat kwa special treatment. Tumekwenda kumkuta binti mmoja anafanya kazi kwenye lile ghala ndani hana gloves, hana chochote, amevaa malapa ndani ya ghala la kuhifadhi madawa; ukiangalia ukuta umechakaa mpaka umeweka rangi ya njano. Sasa je, kwa binti wa Kitanzania anayefanya kazi; naliomba Jeshi la Polisi liweze kuwasaidia katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu, tumekuwa tukizungumza suala zima la kupambana na madawa ya kulevya, lakini leo tunazungumza kwamba Jeshi letu la Polisi hawana hata boti za doria baharini. Linapotokea suala la kufanya surveillance kwenye bahari, hawana boti. Wanawezaje wakafanya kazi watu hawa? Natoa wito kwa Jeshi letu la Polisi na Serikali, naiomba Serikali ifanye kila inaloweza, wapatieni Polisi boti za kisasa, angalau tatu wakafanye doria baharini kupambana na masula mazima ya dawa za kulevya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho. Kuna mengi yamezungumzwa hapa, mambo ambayo kimsingi nimeshangaa sana! Namheshimu sana dada yangu Mheshimiwa Esther Matiko, ni rafiki yangu, nampenda, lakini kusema kwamba hotuba ya upinzani imezuiliwa, nimeshangaa kidogo. Kama mmezuia hotuba ya upinzani, hili naomba mlitolee ufafanuzi, kama kuna hotuba imezuiwa kusomwa hapa. Kwa sababu sijaona kama kuna hotuba imezuiwa kusomwa hapa Bungeni, unless otherwise kama kutakuwa kuna jambo lingine.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nimtie moyo kaka yangu Mheshimiwa Kitwanga, tumekwenda kwenye unit inayo-deal na kuangalia sample za madawa, ndani ya kipindi cha miezi mitatu, Mheshimiwa Kitwanga amesimamia, tumeona sample 256 za madawa ya kulevya ndani ya miezi mitatu. Leo tunavyozungumza mipaka yote hakuna madawa yanaingia kwenye nchi yetu. Mheshimiwa Kitwanga fanya kazi, tunakuunga mkono na sisi tunajua mnachokifanya kwa maslahi ya Taifa hili. Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kukushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi hii adhimu ya kuchangia katika hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kukupongeza kwa uongozi wako na pia kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kazi kubwa anayofanya kwa kuhakikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa juhudi kubwa anazofanya yeye binafsi katika kuhakikisha Tanzania ya viwanda inafika na hatimaye kuleta matumaini mapya ya kiuchumi kwa Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa kuchangia bajeti ya Waziri Mkuu. Ukurasa wa 34 wa Hotuba ya Waziri Mkuu imeelezea hali ya kutatua migogoro ya mipaka kati ya vijiji na hifadhi. Lazima kama Taifa tujue idadi ya watu inaongezeka kila siku ilhali eneo la kiuchumi, yaani ardhi haiongezeki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamekuwepo na hali ya wanachi hasa Jimbo langu la Singida Magharibi ambapo wamekuwa wakipoteza mali zao ikiwemo mifugo, fedha, mazao na mambo mengine yanayoathiri maisha yao kwa ujumla. Katika Jimbo langu pekee wafugaji wamepoteza zaidi ya shilingi milioni 140 kwa kulipishwa faini kwa wanyama wao kukutwa katika maeneo yanayosemekana ni ya hifadhi. Hifadhi hii ambayo inafika maeneo ya Muhintiri, Ihanja, Ighombwe, Mwaru, Mtunduru, Minyashe na Makilawa haijawahi kutangazwa kisheria mahali popote kama hifadhi ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wetu wanaongezeka, wakulima na wafugaji wanakosa mahali pa kulima na kuchungia mifugo yao kwa sababu ya mipaka ya hifadhi. Ni wakati muafaka sasa kutokana na ongezeko hili la watu, tunaiomba Wizara ya Maliasili na Utalii sasa kushirikiana na TAMISEMI kuongeza maeneo ya wananchi na kupunguza ukubwa wa hifadhi ili kuondoa migogoro ya muda mrefu isiyokwisha ambayo inagharimu wakati mwingine maisha ya wakulima na wafugaji pamoja na mali zao. Naomba sana wananchi wetu wa kata nilizozitaja watengewe maeneo maalum ya kuchungia mifugo yao badala ya kila eneo lenye malisho kuonekana ni eneo la hifadhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mapendekezo haya, naunga mkono hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali Pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya mimi kuweza kuwa na mchango wangu kama Mbunge katika kuishauri Serikali yangu, Serikali ya Chama cha Mapindinzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nianze kwa unyenyekevu mkubwa kabisa kutambua kazi kubwa na commitment kubwa inayofanya na uongozi wetu katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ikiongozwa na jemedari wetu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, its an disputed kabisa kwamba amesema dada yangu Mheshimiwa Munde, legacy ambayo inakwenda kuandikwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya Awamu ya Tano is an questionable na inakwenda kuonesha vitu ambavyo Taifa litakumbuka vizazi na vizazi.
Mimi nitumie fursa hii kwa dhati ya moyo wangu kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye kwa muda mwingi tumekuwa naye humu Bungeni, tumekuwa tukisema na kupongeza watu wengine lakini tumemsahau kiongozi huyu mkubwa kabisa wa shughuli za Kiserikali Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhangaika mikoani na kwenye majimbo kupambana na mambo ya kahawa, kupambana na mambo ya korosho, kupambana na mambo ya maji, Mheshimiwa Waziri Mkuu leo mimi kijana wako nataka nitambue kazi yako kubwa unayoifanya katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nitumie fursa hii kumpongeza sana kaka yangu Dkt. Mpango, the good thing kwa Dkt. Mpango ninachokiona mimi miongoni mwa viongozi wenye msimamo hasa katika sekta na Wizara nyeti kama hii, Dkt. Mpango ninakupongeza. Mimi nimebahatika kufanya kazi na Dkt. Mpango nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, kuna kipindi nilifanya coordination ya kuwa-organize vijana wa vyuo vikuu katika sekta ya kilimo, Dkt. Mpango akiwa anafanya kazi Tume ya Mipango alifunga safari kuja kutembelea miradi ya vijana kwa muda wa siku tatu Igunga na kutoa ushauri. Kwa hiyo Dkt. Mpango mimi ninakupongeza wewe ni mzalendo na kubwa zaidi ni kiongozi usiyeyumba katika masuala ya kodi, hiyo ni sifa kubwa sana kwa kiongozi. (Makofi)
Naomba nijikite katika mchango wangu kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, kwanza, Rais wetu amekuja na vision akitekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya ku-industrialize nchi, hili nimelisema toka nilipoingia hapa katika Bunge hili kikao cha kwanza kabisa, tunapozungumzia habari ya kutaka ku-industrialize nchi hatuwezi kuacha kuweka connectivity kati ya mambo ya industrialization na masuala mazima ya kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niishauri Serikali ya Chama cha Mapinduzi, katika sekta ya kilimo mwanzo tulivyoanza nilianza kuona kwamba tunakwenda vizuri, lakini katikati naona kuna mahali tuna-stuck, tulianza kuzungumzia mazao ya kimkakati, Bunge la kwanza nilizungumzia na kaka yangu Dkt. Mpango uko hapa nilizungumzia habari ya wakulima wa pamba wa lake zone, nilizungumzia habari ya wakulima wa mazao ya alizeti katika mikoa ya kanda ya kati na baadhi ya mikoa ya mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilisema Tanzania (Taifa letu) tunapoteza fedha nyingi sana katika kuingiza mafuta kutoka nje ya nchi mafuta ya kula nikasema potential tuliyonayo katika kilimo cha alizeti tukiamua kufanya intensive investment Taifa letu litaondokana na habari ya importation ya mafuta tuta-save foreign currency na tutaweza kuinua uchumi wa nchi. Ninachokisema ni kwamba sijaona connection iliyopo kati ya Viwanda na sekta ya kilimo hasa katika kilimo cha alizeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishauri Serikali, ni wakati muafaka sasa kuhakikisha ya kwamba Serikali inatoa incentive package kwa wakulima wa mazao ya alizeti, kaka yangu Dkt. Mpango lichukue hili na mwakani kwenye bajeti
lilete toeni incentive katika mbegu za alizeti, toeni incentive katika masuala mazima ya pembejeo tuweze ku-boost productivity na kuongeza tija ili Viwanda viweze kupata raw material. Mimi hapa ninapozungumza Jimbo langu linapakana na Jimbo la Iramba, kuna kijana mmoja mjasiriamali amefungua Kiwanda cha Alizeti hapa ninapozungumza amepata market Rwanda, anauza Congo, anauza Zambia…
MHE. MARTHA M. MLATA: Anaitwa Yaza.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Anaitwa Yaza, ahsante Mheshimiwa Mama Martha Mlata. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya tukiweza kufanya Mheshimiwa Waziri tutaweza kulisaidia Taifa hili na tutaweza kutengeneza wajasiriamali wa kati watakaoweza kufanya investment kwa sababu hawa ndio wazawa wenye uchungu na hili Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili ushauri wangu ninaoutoa kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi, tunazungumzia suala la viwanda, Rais John Joseph Pombe Magufuli amekuja na ideology ya kutoa elimu bila malipo shule ya msingi, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango uko hapa na mama yangu Mheshimiwa Profesa Ndalichako najua uko hapa ninajua wewe ni mama bingwa ni Waziri uliyeimudu Wizara yako ya Elimu, mimi ninakupongeza sana mama yangu ushauri wangu ninaoutoa, mwakani njooni na mpango wa kuhakikisha vocational education inakwenda kuwa bure kuanzia mwakani, tukifanikiwa kuweka vocational education kuwa bure tutaweza kutengeneza class ya technocrats ambao watakwenda kutumika katika viwanda ambavyo tunampango wa kuhakikisha kwamba Taifa letu linakwenda kuwa Taifa la viwanda. Kama tumeweza kutoa elimu bila malipo kwa shule za msingi Mama Ndalichako ukiwasiliana na Mheshimiwa Dkt. Mpango mkafanya coordination ya kuangalia tuna vyuo vingapi vya ufundi Tanzania, skills zinazohitajika kwa ajili ya kwenda ku-feed watu kwenye viwanda, tukawekeza kwa vijana wetu wa vocational education mimi nataka niwaambie in next ten years viwanda vinavyojengwa hatutategemea technocrats kutoka nje ya nchi tutawatumia wazawa kutoka katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mpango huu ndio ushauri wa Kibunge mimi nataka muuchukue achaneni na watu wanaopiga blaa blaa! Watu wanaotaka kutukatisha tamaa, kazi ya Wabunge ni kuja kuishauri Serikali na kutoa mawazo mbadala kwa maslahi ya kuhakikisha Taifa letu linasonga mbele, habari ya kuja hapa kuja kuanza kumtukana Dkt. Mpango sijui mpango umefanyaje. Mimi nataka niwaambie jimbo ninalotoka la Singida Magharibi nimezaliwa kijijini mimi baba yangu alikuwa ni mwalimu for almost 30 years chini ya kipindi hichi nimeshuhudia kwa macho yangu najengewa vituo karibu vinne vya afya on the spot mambo haya hayakuwepo kwani hizi fedha zamani hazikuwepo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapozungumza habari ya kuja uchumi wa nchi ni pamoja na ku-improve social service ku-improve social welfare za watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Dkt. Mpango ushauri wangu mwingine ninaoutoa tuiangalie sasa sekta binafsi kwa kuwaangalia entrepreneurs wa Kitanzania tuwaangalia entrepreneurs wa Kitanzania na kuwalinda. Ndugu zangu nataka niwape mfano mdogo kwa nini tunasema kwamba Kenya is one of the largest ten investers kwenye nchi yetu, Kenya ni miongoni mwa mataifa kumi yaliyowekeza Tanzania sana kwa sababu gani wamekuwa wajanja sana wanachukua private sector yenye teknolojia kutoka nje, wanakuja wanazisajili kwao kazi zote zinatoka East Africa wanatokea Kenya wanakuja Tanzania wanachukua kwa sababu wameangalia fursa kwa jicho la pili. Niwashauri Mheshimiwa Dkt. Mpango na timu yako tusi-dicourage private sector kwa maana ya kuwalinda Wazawa wanapokuwa wamebuni na kuanzisha vitu ninaiomba Serikali yangu ya CCM iangalie hili kwa jicho la ukaribu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti tutakapoweza kutengeneza middle class na entrepreneurs ya kwetu hawa ndio watakaokwenda kuwekeza kwenye Viwanda vya korosho tunavyovitaka hawa wahindi wanaokuja Wafanyabiashara tunawapenda hawawezi kuwa na uchungu kwenda kuwekeza kwenye viwanda vya kubangua korosho tukiwezesha middle class ya kwetu, entrepreneurs wa Kitanzania hawa Mheshimiwa Dkt. Mpango wanatakuwa na uchungu viwanda ambavyo Rais Magufuli anavipigia kelele vitafunguliwa ninawashauri kwa dhati ya moyo wangu kila mahali alipo entrepreneur wa Kitanzania tusimvunje moyo, ninawashukuru sana ninajua hili linaeleweka na ninajua mna- take note na ninajua kaka yangu Dkt. Mpango unaelewa mdogo wako ninachokisema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja kidumu Chama cha Mapinduzi.
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa nikiri kwamba mwaka 1999 na kuelekea mwaka wa 2000, Taifa letu la Tanzania lilipata msiba wa kuondokewa na Hayati Baba wa Taifa letu Mwalimu Nyerere. Taifa lilishuka sana na Watanzania waliingiwa na majonzi na wengi wakajiuliza nini itakuwa hatma ya Taifa letu. Hata hivyo, kutokana na uongozi madhubuti na uimara wa chama kilichopo madarakani Chama Cha Mapinduzi, Taifa la Tanzania liliendelea kuwa stable na nchi iliendelea kuwa moja na maendeleo ya kiuchumi na kijamii yaliendelea kuonekana katika nchi Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, pia mwaka huu pia Taifa la Tanzania lilimpoteza Rais wake ambaye alikuwa kipenzi cha Watanzania, Rais ambaye alikuwa mzalendo, shujaa, jasiri, mwenye kuongoza njia, Rais aliyeaminiwa na umma ambaye na kuleta imani kubwa duniani, kifo chake na maombolezo yake yamedhihirisha namna gani Watanzania na dunia kwa ujumla ilikuwa na imani kubwa na rais huyu, lakini Watanzania wengi waliingiwa na hofu wakaona sasa Tanzania itakwenda wapi. Kuonesha umahiri wa chama kilichopo madarakani kwamba ni chama kinachoweza kuwaandaa viongozi, leo tunapozungumza kila nchi, Raisi aliyepo madarakani Mama Samia Suluhu Hassan, kila mmoja anatoa makofi na pongezi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninachoweza kusema ni kwamba Chama Cha Mapinduzi ni ngalawa imara inayoweza kuwaandaa viongozi wa kuliongoza Taifa wakati wowote wa shida na raha. CCM ni tanuru la kuandaa viongozi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika,, naomba niende kwenye hotuba yangu. Sasa nakwenda kuzungumzia maeneo makubwa mawili hasa katika sekta ya kilimo. Nashukuru namwona kaka yangu Bashe huwa ni Naibu Waziri msikivu sana, mara nyingi Wabunge wanapozungumza huwa ana-take note kwa manufaa ya Taifa. Naomba nitoe takwimu zifuatazo:-
Mheshimiwa Spika, Nchi ya Misri, ambayo kwa asilimia karibu sabini kama sio themanini ni jangwa; nchi ya Israel ni jangwa. Naomba Bunge lako Tukufu lisikilize takwimu zifuatazo: Taifa la Misri katika sekta ya kilimo cha umwagiliaji licha ya nchi kuwa imezungukwa na mto mkubwa ambao kimsingi chanzo kikubwa cha mto huo kinatoka Tanzania, ukiangalia takwimu zinaonesha Taifa la Egypt moja ya vyanzo vikubwa vinavyofanya nguvu za kiuchumi za Nchi ya Egypt ni kilimo cha umwagiliaji. Kama haitoshi takwimu zinaonesha Taifa la Misri limewekeza zaidi ya hekta milioni 3.4 kwenye Sekta ya irrigation peke yake.
Mheshimiwa Spika, ukiangalia takwimu suitability ya land ya Misri na Tanzania ni tofauti kama mbingu na ardhi. Availability za resources kama maji, manpower na mengine, ni sawa na mbingu na ardhi, kwa maana ya kwamba Tanzania hiko katika competitive advantage ya ku-invest kwenye kilimo cha umwagiliaji, lakini angalia takwimu kwa nchi yetu. Namwomba kaka yangu Mheshimiwa Bashe na Mheshimwa Waziri wameaminiwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi. Mchango wangu wa kwanza nilipoingia kwenye Bunge hili nilizungumzia habari ya sekta ya Irrigation, that was my first mchango kwenye Bunge la Tanzania. Nilitoa mifano na nikatoa ushauri, namna gani Serikali ya Chama Cha Mapinduzi tunaweza tukalipindua Taifa hili likawa Taifa la ku- export mazao duniani kote na watu wote tukainua uchumi wa Taifa, kwa Tanzania sasa tunapozungumza eneo ambalo tumelitumia peke yake kwa umwagiliaji ni hekta elfu 19 wakati Egypt they have 3.4 million na hawana suitable land kwa ajili ya kilimo.
Mheshimiwa Spika, natoa takwimu hizi huku nikiwa natambua kabisa, Serikali yetu ya Chama Cha Mapinduzi, kama kweli wataamua kudhamiria kusaidia kilimo cha nchi hii katika sekta ya umwagiliaji, nakwenda kutoa mfano, nimekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga kwa miaka takribani minne. Irrigation scheme kubwa katikja Mkoa wa Tabora iko Wilaya ya Igunga inaitwa Mwanzugi. Production inayofanyika kwa lile shamba dogo, nataka nikuhakikishie, ndio irrigation inayolisha mchele wote wa Rwanda, Uganda pamoja na nchi za Burundi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa takwimu hizo, nilitoa mchango wangu nikashauri, suitable land tunayo ambayo inafaa kwa irrigation, kwa Tanzania tuna potential ya 2.1 million hekta za irrigation katika nchi zetu. Nilitoa mfano tukiamua kuwekeza, Mheshimiwa Bashe kaka yangu na Wizara na wataalam wakaenda pale Igunga peke yake wakaamua kuyatenga yale maji ya Mto Manonga, wakatengeneza mabwawa, irrigation peke yake Mkoa wa Tabora tuna uwezo wa kulisha nchi zaidi ya nne kwa chakula na mazao mengine ya kibiashara tunaweza kuyafanya. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niiombe Serikali yangu ya Chama Cha Mapinduzi, hili Bunge ndio mahali peke yake ambapo tunaweza kutoa mawazo ya kuisaidia Serikali, inapotengeneza mipango, Taifa hili likapiga hatua. Kama Rais Hayati Magufuli alivyokuwa anasema, Taifa hili sio maskini, nchi hii tunakosa kuwa na mipango mikakati na mambo ya vipaumbele ambavyo vinaweza vika-turn upside down maendeleo ya nchi hii. Niiombe sana Wizara ya Kilimo, kama kuna eneo Bashe na watu wako na Wizara wanatakiwa kufanya waende wakawekeze katika kilimo cha umwagiliaji, hicho peke yake kitaleta suluhu ya kuongeza export nje ya nchi na kufanya Taifa letu liweze kuendelea.
Mheshimiwa Spika, nimetoa mifano Egypt peke yake ukingalia statistic za dunia, fedha wanazoingiza Egypt kutokana na kuuza matunda, ulitupa fursa mwaka juzi, tulikwenda Egypt na timu ya Taifa, tulikwenda kutembelea miradi. Ile ilikuwa ni fursa ya kimichezo, lakini tulijifunza kitu, tulienda kutembelea Irrigation za zabibu, tukatembelea irrigation mbalimbali, Egypt is complete desert. Hata hivyo, kinachozaliwa nilipoona yale mashamba nikaangalia baraka za nchi yangu Mungu aliyonipa hii Tanzania, I was so much embarrassed. Tuna uwezo Tanzania tunakwama wapi? Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwenye mipango yetu waandike, walete fedha, wasaidie kilimo cha umwagiliaji kwenye Taifa hili.
Mheshimiwa Spika, ulikuja kunizindulia kampeni kwenye jimbo langu, mahali pekee yake ulipokuja kuzindua kampeni pale Mgungila, pale tuna maji ambayo yanapotea na nakwambia leo tunavyozungumza Mkoa wa Singida, mchele wote karibia asilimia 75 unatoka Mgungila, lakini wale wakulima they are just doing agriculture on their own skills, hakuna mipango ya Serikali, bonde kubwa lina…
Mheshimiwa Spika, haya mambo jamani, napata shida sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Kingu, watu wa kilimo kila wakileta bajeti ni ya kununua laptop, kunuua pikipiki, zinatakiwa zielekee huko.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimwa Spika, kabisa kabisa, yaani hili Taifa nawaambia, tukidhamiria kufanya mambo na hakika kwa hii style ambayo Serikali yetu ilikuwa inakwenda, nakwambia nchi hii in next ten years to come hili Taifa halitasogelewa na nchi yote kwa Afrika kwa sababu kila kitu tunacho. (Makofi)
Mheshimwa Spika, jambo la pili, kwa mfano tumechukulia hata ukiangalia katika kilimo amechangia kaka yangu pale, amezungumza habari ya pesa tunazotumia, sasa hivi potential iliyopo ya ku-import mafuta ya kupika, inakwenda karibia dola billion 275, that is the potential. Sasa tukiamua kufanya PPP aliyokuwa anaisema kaka yangu, tukashirikiana na Serikali, wakafungua block farming ambazo huwa tunazungumza na Mheshimiwa Bashe ya alizeti, nasema, fedha tunazozitumia kuagiza mafuta peke yake kwenye kilimo, block farming zikiwepo za mfano, sisi Singida tumemwambia Mheshimiwa Bashe, tuko tayari kumpa maeneo ya kutosha ya alizeti kufungua block farming ambazo zitakuwa mfano ili Taifa liweze kuzalisha mafuta.
Mheshimiwa Spika, hii nchi tunaweza kufanya mambo makubwa na mazito endapo Serikali itapokea ushauri wa Wabunge na kuacha kuona Wabunge tunaoshauri kama maadui. Maana kuna Mawaziri wengine ukiwashauri, we have to be honest, anakuona adui, yaani unaona kabisa Waziri anakuona huyu mtu adui. Kuna Waziri mmoja nilishauri kwa nia njema, Waziri mwenyewe ni Mheshimiwa Mwambe, nikasema angalieni kuna shida ya masoko ya Watanzania. Mheshimiwa aknijibu in very arrogant way, mimi ni Mbunge mwakilishi wa watu, Mawawiri tunapotoa michango tuheshimiane, we are doing this for interest ya nchi. Jibu alilonipa; wewe bwana kama nyama yako imekosa soko…, mimi siuzi nyama. Nikizungumza hapa kwa niaba ya wafanyabaishara, nisichukuliwe nimetumwa, wale ni Watanzania na sisi ni sauti yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, I am very sorry kama nitakuwa nimem-offend, lakini I was so embarrassed, hilo siyo jibu la Waziri anayetokana na Chama Cha Mapinduzi kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho, naomba nizungumzie upande wa marketing. Upande wa marketing natoa mfano mdogo, Taifa la Ethiopia lilifungiwa kupata market ya kuuza nyama kwa nchi za kiarabu, in within three days, Mawaziri zaidi ya sita walifunga safari kwenda kufungua masoko ya watu wao. Sisi hapa kwetu…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante sana.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima na taadhima, naomba nikishukuru kiti chako kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu mfupi katika bajeti hii ya Wizara ya Viwanda.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, namshukuru sana kaka yangu Mheshimiwa Mwijage na pia naishukuru Serikali ya Chama changu; Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika na ndugu zangu, Waheshimiwa Wabunge, nimesoma kitabu hiki cha hotuba ya Kambi ya Upinzani from page one mpaka page ya mwisho. Ukurasa wa tatu, hotuba ya Kambi ya Upinzani wamesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi imechoka kiakili na uwezo wa kufikisha ndoto za Tanzania ya Viwanda, it is impossible.
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Kilichojaa kwenye hotuba ya Kambi ya Upinzani ni malalamiko, hakuna alternative ya nini kifanyike kwa mustakabali wa nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma kitabu cha Mheshimiwa Mwijage, kuanzia mwanzo mpaka mwisho amejikita kwenye program, planning, strategy na namna ya ku-industrialize nchi. Kwa hiyo, kama ni watu waliochoka akili, it is the Opposition Camp ambao kimsingi this is nothing! Absolutely nothing! Malalamiko mwanzo mpaka mwisho.
T A A R I F A . . .
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei, kwa sababu nilichokisema from page one to the last page, hotuba imejaa malalamiko, hakuna alternative za ki-strategy, mikakati na source za kupata resources za ku- industrialize nchi. Naomba niendelee.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema, wengi wanapuuza mikakati ya Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi katika ku-industrialize; lakini nataka nikuhakikishie, ndani ya miaka michache ijayo Rais John Joseph Pombe Magufuli anakwenda kuli-surprise Taifa kwa kuhakikisha kwamba Tanzania ya viwanda inakwenda kujengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kulithibitisha hilo, Serikali ya Chama cha Mapinduzi ya Awamu ya Tano, tayari imeshaanza mikakati ya ku-modernize infrastructure za nchi. Wenzetu Kenya wamejenga standard gauge rail ambayo inatoka Mombasa kwenda Nairobi. Gharama walizozitumia ni Dola bilioni 3.8. Kwa Tanzania, Rais John Joseph Pombe Magufuli anajenga standard gauge kwa ukubwa huo huo kwa gharama ya takriban bilioni mbili US Dollars.
Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni kuonesha kwamba Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika ku-industrialize nchi amezingatia three E’s za economy; Efficiency, Effectiveness and Economy. Huyo ndiye Magufuli wa CCM na watu wanaotega masikio wakifikiri tutafeli, imekula kwao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nikuhakikishie, mimi binafsi nimesafiri, nimekwenda kutembelea programu mpya; dada yangu Mheshimiwa Jenista nakupa big up sana, wewe na Ofisi ya Waziri Mkuu. Nimekwenda Ngerengere; jana hapa tulikuwa tunawatetea wanajeshi, nimejionea barabara zinazochongwa kwa kiwanda kipya cha five thousand TCD tons; tani 200,000 kwa mwaka. Nimekwenda Kibigiri, nimejionea programu mpya ya 15 TCD kiwanda kinachojengwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa Dodoma tunapozungumza, ndani ya miezi mitatu National Milling inakwenda kufufuka. Kiwanda cha National Milling kinakwenda kuwaka. Tani 60 za unga zinakwenda kuzalishwa na tani 20 za mafuta. Yote ni kazi ya Chama cha Mapinduzi. Taarifa nilizonazo, viwanda vya Mwanza vinakwenda kuwaka na viwanda vyote; the former National Milling vinakwenda kuwaka. Wanaosubiri mkono wa mtu uanguke kama fisi, hii imekula kwao. Sisi Chama cha Mapinduzi tunakwenda kujenga viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu wa pili; naishauri Serikali yangu ya chama changu, Chama cha Mapinduzi…
(Hapa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge walisimama kutaka kumpa mzungumzaji Taarifa)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo ninaloishauri Serikali yangu ni kwamba wajomba zangu wa Kanda ya Ziwa wameteseka kwa miaka mingi katika kilimo cha pamba. Natoa ushauri Wizara ya Kilimo na Wizara ya Viwanda wafanye coordination. Tunahitaji tuanzishe large irrigation scheme za kikanda ambazo zitawa- accommodate wakulima wetu wa pamba waweze kuwa na sustainable agriculture ambayo itaweza ku-provide raw material kwenye viwanda tunavyotaka kuvijenga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi wa kwanza nilifanya private tour kwa nchi za Ujerumani, Turkey na Russia; textile industry tukiamua kuwa serious kaka yangu Mheshimiwa Mwijage, we have trust and confidence in you; tukiamua kufanya fully utilization ya resources tulizonazo, mito na ardhi, nataka niwahakikishie, ajira ya vijana wanaomaliza Chuo Kikuu tunakwenda kui-curb over just within three years. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, natoa ushauri kwa Serikali ya chama changu, tuanzishe large irrigation scheme; mito Simiyu tukaitege, mito ya Manonga na Igunga tukaitege, tuvune maji tuwe na large scale agriculture. Hii peke yake ndiyo itakwenda kulikomboa Taifa kutokana na adha tuliyonayo ya ukosefu wa ajira kwa vijana katika masuala mazima yanayohusiana na viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tu-engage protectionism approach kulinda viwanda vya ndani. Tunalindaje viwanda vya ndani? Hili nalizungumza, nina uhakika huenda hata vyombo vya usalama humu ndani; kuna watu wanataka ku-temper na uchumi wa nchi yetu, lazima tuwe very serious na lazima tuwe wakali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, hivi karibuni kuna watafiti fulani kutoka Marekani na nataka niwaambie haya maneno kwa sababu tabia ya Mataifa ya ki-capitalist wanapoona nchi changa zinataka kukomaa kiuchumi, wanaanza kupandikiza mambo ya hovyo ili kutuvuruga. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushuru sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kutoa mchango wangu, nimebahatika kuwa Mbunge hii ni term yangu ya pili kwa maana ni mara yangu kuwa Mbunge katika Bunge hili la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilishiriki kupitisha bajeti zote za Serikali kwa Bunge lililopita ninaomba niwe honest kwa mara yangu ya kwanza toka nimekuwa Mbunge nimeshuhudia bajeti iliyobeba dhima halisi ya wale waliotutuma kwa maana walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara ya kwanza, kama Mbunge nimeshuhudia kiwango kikubwa sana cha kasi ya upelekaji wa fedha za miradi ya maendeleo katika halmashauri zetu. Ninaomba niseme kwa dhati ya moyo wangu na Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali kipenzi chetu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yumo humu ndani. Mheshimiwa Waziri wa Fedha wewe na Naibu wako Mheshimiwa Eng. Masauni mmewatendea haki sana walipa kodi na wananchi waliotutuma katika Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndugu yetu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa alikuwa Singida ndani ya siku moja mbili zilizopita, na nitaka nilisema hili Mheshimiwa Waziri Mkuu nanijuwa na huko hapa na ninajua Mheshimiwa Gulamali atatulia niseme wema wa Waziri Mkuu aliyeuonyesha kwa watu wa Singida akiwa ameambatana na Waziri wa Kilimo na Naibu wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu wananchi wa Singida wanakupongeza kwa jambo kubwa moja, ulipokwenda Singida kwa agenda ya zao la Alizeti ambalo ni zao la Serikali la kimkakati, ulitumia zaidi ya masaa nane ukiwa umekaa kwenye meza ukisikiliza hoja za wananchi wetu na walipa kodi wetu mmoja baada ya mwingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri Mkuu usikivu wako wananchi wametutumia meseji na ushahidi tunao wanasema hawajapata kuona kiongozi wa kiserikali, wa nafasi kubwa kama Waziri Mkuu anaweza kukaa na akatulia kwa masaa zaidi ya nane akisikiliza michango ya wananchi tena wananchi wengine ambao hawana hata uelewa mpana wa mambo ya kimkakati ya kiuchumi, lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu uliwasikiliza wananchi wa Singida wakatoa mawazo yao wakatoa wanataka direction gani katika production ya sunflower katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niungane na wananchi wa Mkoa wa Singida kusema kabisa kwa dhati ya moyo wangu kama kuna karama za kiuongozi Mungu anazitoa, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, Waziri wetu Mkuu umepewa karama kubwa sana ya kiuongozi karama ya kuwa na unyenyekevu wa hali ya juu ya kujishusha to the ground na kuwasikiliza walipa kodi. Umetupa somo kubwa sana sisi vijana tunaokuwa katika uongozi ahsante sana kiongozi wetu Mungu akubariki sana kaka yangu. (Makofi/ Vigelegele)
Mheshimiwa Mwenyekiti, zao la Alizeti ni zao ambalo Serikali ya Awamu ya Sita na niwapongeze sana Mawaziri wa Wizara hizi mbili ni zao ambalo wameamua kwa dhati kulifanya kuwa zao la kimkakati na ninataka nitoe takwimu zifuatazo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tanzania tuna make seventy eight percent ya market share ya uzalishaji wa mafuta ya Alizeti katika ukanda wa East Africa na baadhi ya nchi za maziwa makuu ikiwemo Zambia, pamoja na Kongo. Asilimia 78 ya market monopoly Tanzania tumeikamata, nchi inayotufuata kwa mbali sana ni Uganda kidogo, wakifuatiwa na Rwanda ambazo production yao ni karibia tani kama 4,000 kwa mwaka mzima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kukisema na ninaomba kabisa Waziri Wizara ya Fedha na Naibu mnisikilize, hili mkiweza kulichukuwa wazo langu nina imani kabisa mtakwenda kuifanya Tanzania inakwenda kuwa another giant katika kuliteka soko la Afrika kwa sababu anayeongoza ni South Africa ambaye amekamata 48, 46 percent ya production ya mafuta haya katika ukanda mzima wa Afrika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri naomba unisikilize ushauri wangu tumeweka incentive kwa wale tunawaita strategic investors katika sekta ya sunflower production. Kwa Mkoa wa Singida strategic investor tunaye huyu mmoja katika kile kiwanda kikubwa cha uzalishaji, viwanda vingine huyu yeye amepewa zero VAT kwa maana ni muwekezaji mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nilipe Bunge lako taarifa katika zao hili la Alizeti takwimu zimeshasomwa na hapa Bungeni namna gani Serikali na Taifa tunatumia a lot of forexes kuagiza mafuta kuja ndani ya nchi. Na wakati mwingine mafuta haya uenda yanakuwa hata hayana ubora ule tunaoukusudia. Tanzania tukiamua kwa mipango thabiti na tumepata Waziri wa Fedha naomba nikiri msikivu sana anayefikika kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu na kiongozi wetu Mkuu wa Serikali yupo hapa Bungeni, ushauri wangu ninaomba Wizara ya Kilimo Wizara ya Biashara na Masoko sijui na vitu gani ninaomba kwa dhati ya moyo wangu chukueni ushauri huu. Nendeni mkaangalie wale wazalishaji wadogo wa mafuta katika Mkoa wa Singida na mikoa jirani, wazalishaji wale mkienda kuwaangalia wawezesheni wapate mashine za kisasa katika kuhakikisha ya kwamba ukamuaji wa mafuta unakidhi tija kwa sababu mashine nyingi wanazotumia hazina ubora wa kimataifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkiweza kulifanya hili Mheshimiwa Waziri pamoja na Wizara ya Viwanda na hii chachu mliyokuja nayo ya kuleta mbegu za kisasa katika zao la Alizeti nataka niwaambie kwa idadi ya wakulima tulionao wa Alizeti kwa Mkoa wa Singida peke yake Mkuu wa Mkoa amekuja na takwimu kwenye kikao cha Mkuu wa Mkoa Singida peke yake kwa wakulima wetu tunauwezo wa ku- cover production ya nchi nzima ya Alizeti na tukabusti uchumi wa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mheshimiwa Bashe ushauri wangu ninawaomba kwa kuwatumia wakulima hawa ambao umeamua kuwekeza kwao, nataka niwaambie Singida tunayo ardhi ya kutosha yenye rutuba, tuna watu akina baba wenye uwezo wa kufanya kazi tuko tayari tukiwezeshwa na Serikali kuhakikisha tunazalisha tuweze kupiga hatua katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninalotaka kuliongelea juzi nimetembelea Kisarawe nimetembelea Wilaya ya Mkuranga anapotoka kaka yangu na Waziri mahiri kabisa kijana Mheshimiwa Ulega usipokuwa makini unaweza ukafikiri hili Taifa watu wanafanya ngonjera hili Taifa linapiga hatua this country is moving nchi hii inapiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kiuchumi, tumekwenda pale kwenye kiwanda tukiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye Kamati ya Sheria na Katiba tumejionea uzalishaji wa gypsum kwenye kiwanda kile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumza kiwanda kile ambacho kipo kwenye nchi yetu ya Tanzania kime- capture market ya nchi saba Afrika Kenya, Zambia Malawa Msumbiji mpaka Zimbambwe wanauza gypsum. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu Mheshimiwa Waziri kiwanda kile cha kimkakati kina changamoto moja kubwa na nilizungumza hapa Bunge lililopita kuhusiana na mifugo watu wengine wakaniona na attack personality za watu leo Serikali mmefanya research ushauri niliutoa yale matozo yote ya kwenye nyama mmeyafuta wananchi kule wanapiga makofi production ya nchi itaongezeka ninawapongeza sana Mheshimiwa Waziri na Wizara ya Mifugo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsanteni sana Mheshimiwa Waziri Mkuu wamefanya kazi matozo niliyoyasema hapa Bungeni wamefanya utafiti wamejiridhisha leo nimesoma ripoti ya Waziri wamefuta zile tozo ninawapongeza sana Wizara ya Fedha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachokiomba nendeni mkakitembelee kile kiwanda Wizara ya Fedha mimi kila jambo nikilizungumza hapa ninazungumza kwa maslahi ya Taifa langu siweki maslahi yangu ninazungumza maslahi ya nchi mtu achukie apende asipende nimeiweka Tanzania yangu mbele kwa maslahi ya vizazi vinavyokuja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu nendeni mkakitembelee kiwanda kile cha Mkuranga wale watu wana changamoto moja Mheshimiwa Waziri karatasi wanazozitumia katika ku-cover ile gypsum haipatikana Tanzania karatasi ile inakuwa imported kutoka nje ya nchi na inapekelekea cost of production inakuwa kubwa inasababisha bidhaa inakuwa na bei kubwa na ninataka nikuambie.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanda kile wakati wana ki-acquire kilikuwa na uwezo wa kuzalisha milioni 4 waka- expand uzalishaji mpaka milioni 15 na actual production ni milioni nane wameweza kuliteka soko lote la Afrika na Mheshimiwa Waziri Mkuu nilifanya upelelezi kutaka kujua resources tulizonazo zinazoweza kukifanya kiwanda hichi ku- sustain tumeambiwa ma-gypsum powder tuliyonayo yanaweza yakazalisha gypsum kwa zaidi ya miaka 40 na yapo yakutosha kwenye Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba Waziri wa Fedha wewe na naibu wako fanyeni utafiti wa kitaalam tumieni vyombo vyetu vya kiserikali nendeni mkawasaidie mwekezaji huyu ajira aliyoitoa nilipoona sikuamini kama niko Tanzania, sikuamini kama niko kwenye nchi hii ya Tanzania, msaidieni mwekezaji huyu aweze kupata nafuu ya kodi kwenye hii kodi moja ya makaratasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mnaona hilo haliwezekani pelekeni fedha kwenye kiwanda chetu cha kuzalisha karatasi nunueni mitambo izalishe karatasi wapate market ya kuuza kwa mwekezaji huyu mtakuwa mmesaidia na mtakuwa mmeliongezea nguvu Taifa katika kuzalisha kodi wanayolipa wale watu na production wanayofanya nimekwenda kulala usingizi hata…
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti taarifa.
MWENYEKITI: Taarifa!
T A A R I F A
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa Mheshimiwa Mbunge anavyozungumzia suala la kiwanda kinachozalisha karatasi nchini ni Mgololo kiwanda kile kile nimefika pale na nimeona uzalishaji wa kiwanda na kina changamoto ya masoko ya ndani ahsante.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu malizia washa mic umalizie muda wako.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaipokea kwanza taarifa lakini aina ya karatasi ninazozizungumzia za gypsum sio karatasi kama hizi ni karatasi ni industrial paper zinazotumika kwenye gypsum. Ambazo mwekezaji huyo anatumia fedha nyingi kuzi-import Mheshimiwa Waziri Mkuu kaka yangu kama tunaweza tuone fedha kwenye kiwanda kile kilete mitambo ya kisasa kizalishe karatasi kwa sababu soko tayari lipo unless otherwise mpeni msamaha wa kodi mwekezaji huyu anayeleta ajira kwenye Taifa letu na kusababisha TRA kukusanya kodi ya kutosha katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho…
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nikushukuru sana kwa kunipa nafasi na mimi kuweza kushiriki kutoa mchango wangu katika mapendekezo ya mpango, lakini pia kwa mpango ambao tunaendelea nao kuutekeleza wa mwaka 2020/2021. Mimi ninakwenda kuzungumza maeneo mawili tu kwa kifupi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu la Tanzania idadi ya ajira ambayo ni active employment katika sekta ya kilimo ni zaidi ya Watanzania inakadiriwa kwa mujibu wa ripoti ya SAGCOT, inakadiriwa kwamba Taifa la Tanzania watu waliojiajiri katika kilimo ambao ni adult wanacheza kati ya watu Milioni Saba mpaka Milioni Nane na wakati mwingine ripoti zingine zinaonyesha kwamba watu walioajiriwa katika sekta ya kilimo wanafika milioni 9.6 mpaka milioni 10. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mara nyingi sana huwa nakufuatilia unapokuwa umekaa kwenye kiti chako unapokuwa unatoa dondoo za kuchomekea kwa upande wa Serikali. Huwa najifunza mambo mengi sana na huwa nayachukulia hayo madondoo unayoyasema huwa nayachukulia in a very serious way. Wiki iliyopita ulitoa dondoo ambayo ilikuwa inatoa msisitizo wa kuikumbusha Serikali katika suala zima la kuangalia nini Serikali inaweza ikakifanya, katika suala zima la kuwasaidia wakulima wetu kutokana na hali ilipo sasa ya masuala mazima ya mbolea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nataka niseme neno moja. Pamoja na kwamba Serikali yetu ya Awamu ya Sita chini ya Mama Samia Suluhu Hassan, imefanya vizuri sana katika mambo ya revenue collection kwa kweli hilo tunawapongeza sana, hatukutegemea kama revenue collection zingeweza kwa utulivu lakini mapato yakaongezeka katika kukusanya. Tunampongeza sana mama na Serikali yake sana sana! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme neno moja, nilipokuwa Mbunge kwa mara ya kwanza mwaka 2015 wakati ninakaa kiti cha pale nyuma mchango wangu wa kwanza kwenye Bunge lako hili Tukufu, niliishauri Serikali ya Chama changu kama kweli tumedhamiria kumkomboa mkulima wa Taifa hili, mkulima wa nchi hii atakombolewa peke yake kwa Taifa kujenga miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga mabwawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilienda mbali nikatoa mfano nilipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, tuna Mito inaitwa Mito ya Manonga inayounganisha Mikoa ya Tabora, Simiyu na Shinyanga, nikatoa mfano kwenye Bunge hilo Hansard zako zikipekuliwa zitasema. Mimi ninachojiuliza hivi kwa nini wenzetu upande wa Serikalini michango ambayo inaweza mkaichukua ikawapa hata ninyi Mawaziri legacy kwamba, mmeweza kulisaidia Taifa katika eneo fulani kwa nini kila mara tunakuja kama vile tu show? Tunazungumza mambo ya msingi yanayozungumzwa na Waheshimiwa Wabunge hayachukuliwi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, inaonekana kama tu basi fulani kesho Mheshimiwa Nape naye pia atachangia aonekane ametimiza jukumu lake la kuzungumza Bungeni, kwa nini constructive ideas zinazotolewa na Wabunge Serikali hawazichukui na kutekeleza? Mimi hapo napata wakati mgumu sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kujenga mabwawa nimetoa mfano kwa Wilaya ya Igunga bwawa pekeyake la Mwanzugi, lenye ujazo wa maji mililita milioni 20 lina uwezo wa kuzalisha mpunga unaozalishwa na lile bwawa moja lililojengwa toka enzi za Hayati Mwalimu Nyerere lina uwezo wa kulisha nchi karibia za Afrika Mashariki katika mchele ninaweza nikasema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini wewe ulikuja kuzindua kampeni kwangu hili huwa siachi kulisema. Ulikwenda kwenye Kata za Iyumbu na Mgungira sisi kule tuna mabonde, tukijenga bwawa moja tunaweza kutoa ajira ya watu wasiopungua zaidi ya 25,000 ajira za moja kwa moja, lakini mchele unaweza ukasafirishwa kwa Mataifa zaidi ya matano. Serikalini jamani kwa nini hamtaki kuweka hizi legacy? Mheshimiwa Nape amezungumza hapa kwa uchungu sana, mimi nasema na Bunge hili niseme wazi mbele ya Wabunge hawa, tukimaliza vikao vya Bunge kama hatujazungumza ultimatum ya kuwasaidia wakulima juu ya disaster iliyoko mtaani ya mbolea tutahukumiwa na Mungu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Bunge hili tutamaliza kukaa vikao vyetu vyote hatujaiagiza Serikali yetu iliyoko madarakani kwenda kuwasaidia wakulima, kuhakikisha ya kwamba kuna subsidies zinawekwa kupunguza ukali wa bei za mbolea pamoja na mbegu tutakuwa hatujalitendea haki hili Taifa. Nataka niseme kama tunaweza kuwaangalia wamachinga tukasema wamachinga tukapeleka Shilingi Bilioni Tano sijui ngapi, hapa leo tunazungumza voters of this country. Lakini mimi mwenyewe huku cha ajabu nimeshangaa nimesoma huu mpango kwa kweli lazima tukosoane ili tuweze kwenda mbele lazima tukosoane. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeangalia katika sekta ya kilimo na toka juzi nilikuwa namsumbua Naibu Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Bashe nimemsumbua sana kwenye simu, nilipoona yuko busy Kaka yangu alinijibu tu kwa haraka haraka nimemtafuta Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nikamwambia hebu naomba unipe takwimu masuala mazima ya mbolea na mambo kama hayo.
Ninachoweza kusema ni kwamba kama Serikali yetu itakuwa tunakuja Bungeni hapa Wabunge tunazungumza kutoa michango ya kulisaidia hili Taifa, lakini tunaonekana kwamba tu ni mazoea tu fulani atachangia, fulani atachangia, hatutalisaidia Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja ya kujenga mabwawa kwa ajili ya kuwa na zone za kilimo cha umwagiliaji wakati umefika msaidieni Rais, Mheshimiwa Bashe jengeni mabwawa angalau kila Mkoa pawe na mabwawa matatu makubwa. Kwa Dodoma jengeni bwawa litakalowasaidia wakulima wa zabibu, Singida kajengeni bwawa litakalowasaidia wakulima wanaolima mpunga pamoja na alizeti, pamba kwa upande wa Kanda ya kule kwa Wajomba zangu Wasukuma, Taifa hili litakwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, shida kubwa tuliyonayo Watanzania sisi tuna tabia moja ambayo ni nzito sana naomba niiseme kwa ruhusa yako. Sisi ni wazuri sana katika kuzungumza lakini katika kutekeleza mambo yanayoweza kuleta mapinduzi ya maisha ya Watanzania tuna kigugumizi kikubwa sana. (Makofi)
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Olelekaita.
T A A R I F A
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nataka nimpe ndugu yangu taarifa tu hapa, kwa mujibu wa Ilani yetu mfano tu, kwa sekta ya mifugo tulisema tutajenga mabwawa 400 na change nyingi kidogo hivi, lakini kwa mwaka huu uliopita Wizara ya Mifugo peke yake wametengewa fedha ya kujenga mabwawa matano tu na ilitakiwa mabwawa 91. Sasa tukiendelea na trend hiyo kwa miaka mitano ijayo maana yake ni kwamba tutajenga mabwawa kama 20 hivi kati ya 450 na hiyo ni mfano tu. Kwamba tusipobadilisha mwelekeo na mipango ikaweza kujibu Ilani inavyosema maana yake tutakwenda hatutafanya vizuri zaidi. Ahsante sana. (Makofi)
SPIKA: Taarifa hiyo unaipokea Mheshimiwa Kingu?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa hii naipokea kwa unyenyekevu mkubwa kwa sababu ninajua Kaka yangu pia anatoka kwenye jamii ya wafugaji. Wafugaji na wakulima ni watu wamoja, ahsante sana kwa taarifa ninaipokea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nataka kumalizia kusema ni kwamba, chukulia tu mfano tunaposema kilimo kina ajiri adult kwa mujibu wa takwimu za SAGCOT, watu Milioni Nane mpaka Milioni Tisa ndugu zangu tunapozungumzia ajira ya watu Milioni Nane mpaka Milioni Tisa tunazungumzia ajira ya Taifa, yaani kama kuna jambo tunatakiwa tulifanye Bunge hili ni kuilazimisha Serikali yetu kwenda sambamba na matakwa ya wakulima ambao ndiyo voters wetu wengi waliotuleta katika Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawaambia Waheshimiwa Wabunge ikiwa tutakuja kwenye Bunge hili tukasahau kuwasemea wakulima, tukasahau kuwasemea wafugaji, tukasahau kuwasemea wafanyakazi na watu wengine, hakika mimi ninakuambieni vizazi vitaandika kumbukumbu na tutakuja kuhukumiwa, kwa sababu tutakuwa tumesahau kundi la watu ambalo ndiyo wanabeba roho ya uchumi wa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, tunajenga madarasa 3,000. Nampongeza sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kama alivyosema Mheshimiwa Nape. Mama ameonesha uwazi wa hali ya juu katika mikopo aliyoipata na namna mikopo ilivyotumika. Kwenye hilo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais, lakini madarasa haya 3,000 kuna jambo hapa kwenye Mpango sijaliona…
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
MWENYEKITI: Ndiyo, taarifa.
T A A R I F A
MHE. TABASAM H. MWAGAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, madarasa ni 15,000 siyo 3,000.
MWENYEKITI: Unapokea taarifa hiyo Mheshimiwa?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba kaka yangu Mheshimiwa Tabasam aende taratibu. Haya ninayosema ni ya shule za awali, shule shikizi na kuna madarasa mengine 12,000 kwa ajili ya sekondari. Kwa hiyo, nilikuwa natoa takwimu katika...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Mheshimiwa muda wako umeisha, wind-up.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapo-windup ni kwamba madarasa 3,000 katika shule shikizi ina maana tunakwenda ku- recruit wanafunzi 120,000; wapi? Tuna madarasa 12,000 ya sekondari, ina maana tunakwenda ku-recruit wanafunzi 480,000; wapi? Kwenye Mpango nilitegemea Serikali ituonyeshe namna gani imejipanga kuziba gap la upatikanaji wa walimu na vifaa vya kufundishia kwa madarasa haya tuliyoyajenga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipofanya hivi, tutajikuta tumejenga madarasa, wanafunzi wamekwenda, na jambo la uhaba wa walimu linazaliwa. Haya ni mambo ya planning na namna ya kuweza kutekeleza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana, naunga mkono hoja. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nakwenda kuzungumza mambo mawili tu na mambo haya mawili nayokwenda kuzungumza yapo katika level ya kitaifa kwa lengo la kuisaidia Serikali na kuwasaidia walipakodi ambao ni Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 7 Desemba, 2020, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kiongozi wetu Kassim Majaliwa Majaliwa kwa uzalendo kwa kutanguliza maslahi mapana ya Taifa alitoa maelekezo kwa kuangalia namna gani Watanzania walipita katika msuko msuko mkubwa ambao ulipelekea kupanda kwa bei kubwa ya bidhaa katika Taifa letu ikiwemo bidhaa ya cement na bidhaa zingine. Tarehe 7 Desemba Waziri Mkuu alitoa maagizo ya kufanyika kwa study ambayo ingeweza kuleta majibu katika Taifa letu kwa nini Watanzania wamepata burden kubwa katika sekta ya ujenzi kwa sababu ya kupanda kwa bei ya cement katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe taarifa; Fair Competition Act Na. 8 ya mwaka 2003 section 5(1) imeeleza namna gani kampuni inaweza kuwa na market share katika Taifa letu katika uwekezaji wa aina yoyote katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe taarifa hata ninapozungumza hapa, aliyekuwa Waziri wa wakati huo Professor Kitila Mkumbo; ninakupongeza kwa sababu wewe pia ulitanguliza mbele maslahi ya nchi na nina imani hata mwalimu wangu aliyenifundisha Mzumbe University Mwalimu Dkt. Ashatu akipewa na yeye maelezo mazuri atakwenda kuyatanguliza maslahi mbele ya nchi, wataweza kuzishauri mamlaka za nchi kuhakikisha ya kwamba maslahi ya Watanzania, maslahi ya walipakodi yanalindwa dhidi ya ma- cartel ya kijambazi yanayochukua nafasi katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikwambie, study iliyofanywa na vijana wazalendo wa Kitanzania waliosomeshwa na kodi za walalahoi wa Kitanzania. Study imeonyesha miunganiko ambayo Twiga Cement waliokuwa wanataka kumnunua Tanga Cement jambo la kwanza. Study zinaonyesha ilikuwa inakwenda ku-violate Fair Competition Act Na. 8 ya mwaka 2003 section 5(1) iliyopitishwa na Bunge hili tukufu kwa ajili ya kumlinda mwananchi mlalahoi kule mtaani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunapozungumza study imeonyesha gharama ya kutengeneza na kuzalisha mfuko mmoja wa cement kwenye taifa hili la Tanzania it is only 5,700 Tshs. Gharama ya kuzalisha mfuko mmoja wa cement ni shilingi 5,700. Kampuni ikiachwa ikauza kwa faida, bei ya cement kwenye Taifa letu hakuna namna bei ya cement inaweza ikazidi shilingi 8,700 na shilingi 9,000 lakini nini kinafanyika? Makampuni haya ya uzalishaji wa cement study zinaonyesha yanafanya kitu kinaitwa cartels zilizozungumzwa katika Fair Competition Act ambayo imepitishwa na Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nikupe taarifa, cartel hizi tunazozizungumza nataka niwaambieni na ndiyo maana Wabunge nataka niwashawishi. Mna kazi kubwa sana kumwombea Mheshimiwa Rais na Waziri Mkuu huyu na Mawaziri ili wawe na moyo wa kizalendo wa kufanya maamuzi ya kizalendo. Mambo haya wanapambana na watu matajiri wakubwa, watu wenye fedha, vita hii bila kumtanguliza Mungu taifa hili Watanzania watakuwa wanageuka kushoto wanapigwa, wanageuka kulia wanapigwa mamiradi ya Serikali Mheshimiwa Rais juzi amelalamika anasema Engineer estimates zinakuwa kubwa. Miongoni mwa vyanzo vinavyosababisha nchi yetu inapata hasara ni kwenye study kama hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninapozungumza, Umoja wa Wazalisha Cement wa Afrika Mashariki kwa study wamegundulika wanakaa vikao, wanafanya market allocation, wanapanga bei za cement na ninataka nikwambie hata Bunge hili kuna wakati tunakuja tunapitisha vitu hapa maskini ya Mungu bila kuelewa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninapozungumza, research inaonyesha ukuaji wa Sekta ya Ujenzi umekua kwa 13% lakini nenda kwenye viwanda, uzalishaji wa cement umeongezeka only kwa 3% na hiyo percent ninayoizungumza ya 3% kwa 13% ambayo sekta inakua; viwanda vimezalisha 3% lakini capacity yake vinatakiwa vizalishe 50% na tulichokifanya kibaya zaidi tumekwenda tukapandisha bei ya importation ya cement kutoka 25% mpaka 35%. Tunamlinda nani wakati wazalishaji wa ndani only wanazalisha 3% ya maximum capacity ya uzalishaji wa viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya yanaumiza sana kwa mtu yeyote mzalendo anaelipenda Taifa lake hawezi kunyamaza akaacha kuzungumza mambo haya yanayofanyika kwenye Taifa hili. Hapa tunapozungumza, cement inauzwa shilingi 18,000. Study zimefanywa na watoto wetu wa Kitanzania waliosoma kwa kodi zetu. Study inaonyesha zote hizi zimefanyika na ni ma-cartel. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hapa ukimuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu hii ripoti toka taarifa imesemekana ripoti ifanyike, hii ripoti haijawahi kuwekwa hadharani. It has never been published in the public, umma uweze kuona namna gani viwanda vya cement vimetengeneza ma-cartel kwa kushirikiana na wasambazaji, kwa kushirikiana na wafanyabiashara kuwaibia Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme neno moja, kama Bwana Mungu wetu aishivyo, Wabunge wazalendo hatutanyamazishwa kusema mambo yanayowaumiza Watanzania, mambo yanayoumiza watu wetu katika sekta nzima ya uzalishaji na hii inasababisha Serikali yetu inatekeleza grand project. Miradi ya SGR, miradi ya barabara, miradi ya ujenzi, gharama za ujenzi zinakuwa kubwa, nani wa kulihurumia hili taifa na kuwa na ujasiri wa kuyasema haya na ku-risk maisha yake? Nani wa kuwa na huo ujasiri? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumza hapa ninajua hayo ma-cartel kule yananisikiliza. Yataanza kutengeneza hata njama, wanafanya hata njama wakati mwingine ku-silence kila sauti itakayosimama kuwatetea Watanzania.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunazungumza hapa study imefanywa na hawa vijana na ninakuomba Waziri wangu Mkuu Kassim Majaliwa kwa uzalendo ule ule ulioufanya kaka yangu ya kuagiza study ifanyike, tumia uzalendo ule ule tena itisha ripoti hii mtakuja kuniambia Serikali tukiamua kuwa serious haifiki mwezi wa sita hapa, bei ya saruji inapaswa kuwa chini ya shilingi 9,000 kuwasaidia Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninaomba nizungumze. Tumezungumza hapa kuhusiana na mambo ya kulinda maadili ya Taifa. Nchi hii haiwezi kuwa na prosperity kama tutaacha kulinda tunu za maadili ya kitaifa hili. Hii nchi yetu ni nchi iliyopata uhuru na sababu kubwa ya Mwalimu Nyerere kupigania uhuru wa Taifa hili ilikuwa taifa liwe huru liweze kulinda misingi yake iliyopelekea Taifa hili kuheshimiwa nyakati zote toka Taifa hili limepata uhuru.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa wito, Bunge letu kama chombo cha kutunga sheria na kusimamia Serikali ninatoa wito kwa mahakama zetu za Taifa hili, ninatoa wito kwa viongozi wa dini zote. Katika Biblia katika imani yangu, neno la Mungu linasema; “Mungu wetu huwa hadhihakiwi.” Pia neno la Mungu katika kitabu kitabu kitakatifu Biblia inasema, “Mungu wetu huwa siyo Mungu wa Kujaribiwa kwa sababu yeye ni Mungu mwenye uwezo na mamlaka.”
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa wito kwa Serikali, kwa sababu hata haya ma-NGO tunayoyaona ambayo yanasababisha kuharibu maadili ya watoto ukiangalia yamesajiliwa na Serikali yetu hii hii ambayo tunazungumza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawezaje tukasema tunalinda hizi haki za watoto kama tutashindwa Serikali kuhakikisha kwamba tunajenga platform na mazingira ambayo yatampa Mungu heshima na tukampa Mungu wetu utukufu ili Taifa letu liendelee kubarikiwa? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa wito kwa Serikali, ninawaomba sana lindeni vizazi vyetu, walindeni watoto wetu wa Kitanzania kwa kuhakikisha kwamba jambo lolote ambalo litakuja ku-contravene na misingi ya Taifa hili inakwenda kudhibitiwa kwa maslahi ya nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho kama utaniruhusu.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, ahsante sana kwa mchango wako.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu kabisa naomba nichukue nafasi hii kukushukuru sana kwa heshima kubwa uliyonipa ya kuweza kutoa mchango wangu katika Wizara hii nyeti kabisa ambayo inahusiana kabisa na kuchochea maendeleo ya Taifa letu. Nakwenda kuzungumza maeneo mawili matatu kwa kifupi sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nitumie nafasi hii kama wengine walivyofanya kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Profesa Mbarawa na wasaidizi wake wawili Manaibu Waziri pamoja na Makatibu Wakuu wanaoongoza Wizara hii kwa ufanisi mkubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Singida, nimuombe Mheshimiwa Profesa Mbarawa, tunatambua kazi kubwa sana wanayoifanya Mheshimiwa Profesa na Wizara yake katika ujenzi wa kufungua barabara za kiuchumi. Barabara ya Tanga inayotokea Kiteto kuja kutokea Kondoa kwenda mpaka Singida, tunampongeza sana Mheshimiwa Profesa Mbarawa na Wizara yake. Sasa nimwombe, ili tuwasaidie wananchi wa Mkoa wa Tabora na Singida, wananchi wanapotoka Tabora wanazunguka Nzega, Igunga, Arusha, wanakwenda Same, wanakwenda Tanga, hiyo barabara ni ndefu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nampa Mheshimiwa Profesa alternative ya barabara. Hii ambayo ameifungua kutoka Tanga kuja mpaka Singida, aje jimboni kwangu kuna barabara inatoka kwangu inakwenda Mtunduru, inakwenda Igombwe, inakwenda Iyumbu, inakwenda mpaka Tabora, hapa atakuwa amekata zaidi ya kilometa 200 za watu kuzunguka kufika Tanga. Sasa namwomba kaka yangu Waziri na Wizara yake, afanye feasibility study, afungue barabara hii na kuna shughuli nyingi za kiuchumi zinakwenda kufanyika pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo naomba niwasemee watu wa Kusini. Inawezekana kabisa watu wa Kusini wametumia muda mwingi sana kujisemea wakaonekana huenda wanazungumza sababu wao wanatoka Kusini. Sasa huenda leo mimi Mbunge wa Singida Magharibi nikizungumza kwa maslahi ya Taifa na nchi, huenda naweza ninaweza nikaeleweka na kuleta tija kwa maslahi ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesoma statistics hapa, feasibility study inaonesha sasa hivi ndani ya miezi 14 zimesafirishwa tani za makaa ya mawe milioni 2.3. Ukienda kwenye statistics unahitaji kama lori moja litakuwa linafanya kazi ya kusafirisha haya makaa ya mawe, unahitaji malori 2,000 kuweza kuya-tap makaa ya mawe kule yanakozalishwa kuyafikisha kwenye bandari tayari kwa kusafirishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nchi, kupanga ni kuchagua. Hivi kweli barabara zetu zinaweza zika-afford malori 2,000 kupita barabarani na kuangalia gharama kubwa ambayo Serikali inaingia katika kujenga barabara? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa niaba ya watu wa Kusini. Leo nazungumza kama Mbunge wa Singida Magharibi, mimi sitoki Kusini, lakini nazungumza jambo hili kwa sababu limebeba maslahi mapana ya Taifa hili, limebeba maslahi ya kiuchumi ya Taifa hili. Mheshimiwa Profesa Mbarawa feasibility study iliyofanywa mwaka 2016 chini ya RAHCO inaonesha namna gani potential ya kiuchumi ya ile corridor ya Mtwara tunayoizungumza jamani. Kuna potential za kiuchumi kule, kuna potential za utalii, kuna potential za kilimo, kuna potential za investment nyingi zimewekwa kule. Naomba nitoe ushauri, wamwache Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aandike kitabu chake mwenyewe, wamwache mama Samia atengeneze legacy yake mwenyewe kwenye uongozi, wamwache mama yetu aruhusu mifumo ya uwekezaji. Tukajenge reli ya corridor ya Mtwara tuweze ku-tap coal inayozalishwa kule na kuileta katika Bandari ya Mtwara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikwambie, tukiwa kama Wabunge, tukiacha kuangalia ukanda tukaweka maslahi ya nchi mbele, Taifa hili litapiga hatua. Nataka nikwambie wapo wawekezaji wako tayari kufanya investment za build, operate na ku-transfer, wamejaa Mheshimiwa Profesa Mbarawa, lakini PPP pia zinafanya kazi. Kama Serikali hawana finance, watafute private sector wakawekeze, hawa watu wa Mtwara wakiwekeza haitakuwa kwa faida yao, itakuwa ni kwa faida pana ya maslahi ya hili Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namwomba Mheshimiwa Profesa Mbarawa chondechonde, kama kuna vitu atakuwa amemsaidia Rais wetu kuacha legacy ni kumruhusu Rais wetu wa Awamu ya Sita ajenge reli ya corridor ya watu wa Mtwara kwa lengo la ku- tap resources zilizoko kule kwa maslahi mapana ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, hili la bandari sikuwa na nia hata ya kulichangia sana kwa sababu, jamani kwa dunia ya sasa hivi Waheshimiwa Wabunge, hivi kweli kwa dunia ya sasa hivi tunaweza tukawa na hofu ya kubinafsisha mwendeshaji wa Bandari hii ya Dar-es-Salaam, kweli? (Makofi)
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Maimuna Pathan.
TAARIFA
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. naomba kumpa Taarifa Mbunge anayeongea sasa hivi, Rais wetu wa kwanza, Mwalimu Nyerere, alikuwa hataki mambo ya ukabila, ukanda, wala udini. Kwa hiyo, nampa pongezi kubwa sana bado anamuenzi Rais wetu wa kwanza kwa kuondoa ukabila, udini na ukanda. Big up na huo ndio Ubunge tunaoutaka wa kitaifa. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu, Taarifa unaipokea?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa hii kwa sababu imeni-recognize kwamba, ni Mbunge wa Kitaifa, nimeipokea kwa mikono miwili. Namshukuru sana Mheshimiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la bandari, jamani kwa wale tunaotembea duniani hebu tuwe na trust nak il ambacho mamlaka inafikiria kwa lengo la kuongeza revenue kwenye hii nchi. Hili la bandari, hivi kweli kuna mashaka kwamba, tukibinafsisha bandari yetu ile katika operation, si walikuwa wanafanya TICTS jamani, si walikuwa wanafanya TICTS juzi tu hapa, sasa kuna ubaya gani kampuni nyingine ikaja kuleta ufanisi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeambiwa, mimi natoa mfano, juzi kati niliingiza vitanda vya kusaidia akinamama jimboni kwangu, miaka miwili iliyopita. Ukiangalia gharama ya kukodi container moja mpaka hapa dola 4,000, lakini wenzetu wanalipa dola 1,600 au 1,800 jamani kuna shida gani kubinafsisha bandari, tija ipatikane, maendeleo ya nchi yapatikane? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo mengine jamani tuangalie maslahi ya nchi. Huyu Rais aliyeko madarakani hawezi kufanya jambo kwa maslahi ya familia yake na watoto wake. Chochote atakachokifanya mama yetu atafanya kwa ajili ya maslahi ya nchi na sisi Wabunge huwa tuko wazi hapa, mambo yakija ndivyo sivyo, hatuogopi kusema, tunasema wazi, lakini hili lina maslahi ya nchi. Rais wetu aungwe mkono, Bandari ya Dar-es-Salaam, tena nawaambia, nashangaa sana kwa sababu, Serikali sisi Wabunge kazi yetu ni kuwashauri, lakini nashangaa sana, hili jambo wanataka kulifanya kama vile mpaka sijui fulani aamue, hapana. Jambo linalohusiana na maslahi ya nchi na ndio maana tuna Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wafanye kazi wasiogope.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi matarajio yetu ni kuona bandari ile inapata ufanisi na mambo yanakuwa mazuri kwa maslahi ya Taifa hili. Wala wasisubiri eti kumuuliza na kuhoji mtu fulani aone nini kinafanyika. Ndio maana tuna Amiri Jeshi, yuko Kikatiba, yuko kisheria, hakuna mtu wa kuweza kuuliza kinachofanyika, zaidi tutahoji tunapoona kuna violation ya maslahi makubwa ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ambalo naomba nichangie, wengi wamezungumza kuhusiana na mambo mazima ya ujenzi wa SGR na mambo mengine. Nataka niseme kitu kimoja, lazima kwenye hili tuelewane, wakati mwingine tunaweza tukawa na hisia za kuhisiana tu ambazo zinaweza zisilisaidie hili Taifa. Niwaombe sana, Mheshimiwa Jerry Silaa leo amezungumza mchana na nimempa Taarifa, takwimu zinaonesha na kuna muda nilikosea nikatamka kwamba, engineering estimates nikazitaja kama BOQ.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa zinaonesha Tanzania ndio nchi ambayo kwa kutumia rasilimali zetu na mikopo tunayokopa tumeweza kujenga reli kwa bei nafuu sana ndugu zangu. Hii habari tunazungumza sijui ya mabehewa, sijui ya nini, hivi kweli leo kama nchi, tumepata mkandarasi anaambiwa na Serikali tunaomba utupe guarantee ya ubora wa mabehewa yako, anasema hapana najitoa, Serikali gani itakuwa tayari kumpa mtu huyo kazi? Haipo duniani. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Kingu, muda wako umekwisha.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, basi nikushukuru sana kaka yangu Mungu akubariki sana. Japokuwa Mheshimiwa Shigongo alikuwa anaomba niongezewe muda, lakini naomba kwa heshima yako nikae. (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante sana.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Nishati
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, niungane na Wabunge wenzangu kukushukuru sana wewe binafsi kwa uongozi wako mahiri katika Bunge letu hili, pia nichukue nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu kabisa kusema Taifa hili lina historia kubwa.
Mheshimiwa Spika, nchi hii imetoka mbali sana kwa ambao tunasoma historia tunajua Taifa hili limetoka wapi katika zana zote za maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kisiasa. Transformation katika Taifa letu ni kubwa sana. Ninaomba niseme maneno yafuatayo na hili ninaomba niseme kwa dhati ya moyo wangu.
Mheshimiwa Spika, kuendesha na kuongoza Serikali ni jambo ambalo kwanza wanaoaminiwa huwa ni watu wachache sana lakini pia kuendesha na kuongoza Serikali ni jambo ambalo linaweza kuwa captured na kumudiwa na watu walio makini sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita nilikuwa nafuatilia mienendo ya siasa katika Taifa hasa katika mikutano ya hadhara. Nimesikia baadhi ya vyama vya siasa nje wakimkejeli Rais wa Awamu ya Sita Dkt. Samia Suluhu Hassan na wamemkejeli katika maeneo wakisema kwamba Rais ameweka mabango mengi hata ndoto za kufikisha umeme kila kijiji hizi ni historia hakuna kitu kitakachowezekana.
Mheshimiwa Spika, naomba nikupe rekodi mimi kwenye Jimbo langu mimi Serikali ya Awamu ya Sita kwenye mambo ya umeme wametufanyia ndani ya miezi mitatu iliyopita. Ndani ya miezi mitatu iliyopita, Jimbo la Singida Magharibi na nina uhakika mifano hii iliyofanyika Singida Magharibi imefanyika nchi nzima. Hivyo nataka tutoe watu waelewe, Serikali ya Chama cha Mapinduzi iliyoko madarakani chini ya Rais Samia Suluhu Hassan siyo Serikali ya porojo, siyo Serikali ya maneno. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mawaziri wetu akiwemo Kaka yangu January pamoja na Naibu wako, trust mliyopewa na Rais nataka nikuambie January mchana kweupe Bungeni hapa leo, kazi hii wewe na Wizara yako mnaifanya kwa uadilifu na uaminifu mkubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ndani ya miezi mitatu, Jimbo la Singida Magharibi ndani ya miezi mitatu nimewashiwa umeme Kijiji cha Germany, Igombwe, Chungu, Irisya, Munyu, Mwasutianga, Kintandaa, Maswea, Kipunda, Mtunduru, Mpugizi, Mpetu, Kinyampembee na Mhintiri, nimewashiwa umeme ndani ya miezi mitatu iliyopita. Hapa ninapozungumza, ninakwenda kuwashiwa umeme mwezi huu Vijiji vya Igilansoni, Msosa, Minyughe, Misake, Makilawa, Mteva, Mtavira, Mayaa, Mlandala, Kaugeri, Mduguyu, Uyumbu, Makyungu, Mgungira mpaka wamefika mpakani mwa Tabora kilometa 225 kutoka Makao Makuu ya Wilaya. Nani kama Mama Samia? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jamani tunapozungumza utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, ndiyo maana nataka niseme watu wasije wakatuona sisi Wabunge tunakuja hapa, Wabunge wa kusifia. Sisi ni Wabunge wasomi. Hiki Chama chetu ambacho kiko madarakani humu ndani kimeleta cream ya Wabunge wenye akili kichwani. Hapa siyo watu wa kuja kupigapiga makofi. Mkiona tunapiga makofi mjue yale tuliyoiagiza Serikali kwenye Ilani yetu ya chama yanafanyika kwa uzalendo na uaminifu mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ndiyo maana nataka niseme kwa kazi inayofanyika wale wanaomkejeli Mama Samia nataka nikuhakikishie kwa sababu nimeona yamefanyika kwenye Jimbo langu, Rais Samia anakwenda kuandika rekodi ambayo mtangulizi wake Hayati Magufuli aliianzisha na Mama anakwenda kumaliza kazi, vijiji vyote vinakwenda kuwaka umeme. Nataka niwaombe Wabunge wote tuendelee kumuunga mkono January na Mama Samia na Wizara hii tuendelee kuwashika mkono, kazi wanayoifanya ni kubwa. Sisi kwenye Ilani tuliwatuma mtuwashie umeme, umeme unawaka unataka nisikusifie? Umeme unawaka tusiseme? Tutasema. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kule wanakopita watu wa CHADEMA wanapiga propaganda kwamba Rais anaweka mabango, nataka nikwambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako January.
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, nataka nimpongeze sana Mama Samia na kwa kweli haya mambo tunayafanya kwa sababu hata tusiposema Mungu atatushangaa. Mradi huu unazungumzwa wa LNG toka discovery imefanyika mwaka 2012, tumejaribu mazungumzo 2016, 2017 kwenye kitalu Namba Moja, Mbili na Nne mazungumzo yakakwama. Tukafufua mazungumzo miaka ya 2017, 2019 mazungumzo yakakwama, kwa dhati ya moyo wangu Mheshimiwa January Kaka yangu, kama kuna vitu ambavyo Taifa hili litakukumbuka ni kuyafufua mazungumzo ya mradi wa LNG na kuyafanikisha kwa kiwango kikubwa. Leo tunapozungumza hapa, tunapozungumza mradi ambao unakwenda kufanya generation ya fedha zaidi ya trilioni 80 huu ni uchumi mkubwa kwa Taifa, hakuna Mbunge ambaye ana akili ataacha kuunga mkono Serikali kwa jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninakupongeza sana Mheshimiwa Waziri, ninampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kukuamini, umekwenda kuyafufua mazungumzo haya na tunaona mafanikio yake. Ninataka nikuambie na wewe sasa kwa kazi uliyoifanya nzuri ya heshima, tunataka tuone matokeo mzee, transition ya dunia sasa hivi inakwenda kasi. Transition ya gesi sasa hivi dunia inakwenda kwenye umeme wa upepo, umeme wa jua na joto ardhi, mkichelewa kutekeleza mradi huu Mheshimiwa January mimi nakuambia hii gesi itabaki kuwa laana kwa Taifa. Harakisha haraka utekelezaji wa mradi huu, uweze kufanyika, Taifa liweze kupata revenue tuendelee kuwajengea watoto wetu mashule, tuendelee kuwekeza, tuendelee kutatua tatizo la ajira kwa Taifa, nchi yetu iweze kupiga hatua kwa maslahi ya watu wake, hongera sana Kaka yangu Mheshimiwa January. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo lingine ninalotaka kulizungumza, nikuombe Mheshimiwa January pamekuwa na maneno huko mtaani, watu wa SONGAS wanapiga kelele kuna uwezokano mkubwa SONGAS wanahisi kwamba Serikali haina mpango wa ku – renew mkataba. Wafanya kazi kule wana – tension kubwa January, kama January umeweza kufufua mazungumzo ya LNG yaliyokuwa yamekwama toka 2016, ukaleta matumaini kwa nchi, ukaleta matumaini kwa investor. January kakipengele cha SONGAS katakushinda kufanya nao majadiliano Kaka yangu? Nenda kakae na watu wa SONGAS fanyeni nao majadiliano kama kuna vitu mnaviona kwenye mkataba wa kwanza vilikuwa havina maslahi ya Taifa piga chini tutakuunga mkono. Wakikubaliana na masharti ya Serikali na ile ndiyo PPP ya kwanza January ambayo imeleta mafanikio kwenye Taifa hili.
Mheshimiwa Spika, tunapozungumza PPP best ambazo zimeleta mafanikio ni pamoja na watu wa SONGAS, wanatuuzia umeme kwa only senti sita na ninasikia wako tayari kushuka zaidi. January fanya nao mazungumzo tuweke tension hii tuiondoe, kazi mnayoifanya mimi nilikuja Ikulu niliona projection mlizokuwa nazo za kuwekeza umeme mpaka tuuze umeme nje ya nchi. Niliona mipango ya kaka yangu Ndugu Maharage wa TANESCO na ninasema kabisa kwa dhati, Maharage asivunjwe moyo, kijana huyu ana – vision kubwa sana, maana tumekuwa kwenye Taifa letu tunapo – hire brain zenye uwezo wa kuleta mabadiliko tunaanza kuwapiga vita mara huyu anafanya hivi, Maharage Chande ni moja ya vijana wazalendo wa Taifa hili, aungwe mkono ni kijana mwenye vision kubwa ameonesha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilikwenda Ikulu nikaona projection za namna nchi inataka kutengeneza umeme na kuuza nje ya nchi, nikaona plan zake ninawaomba Wabunge wenzangu tuwe wazalendo wa kuwaunga mkono vijana wote ambao ni zao la Taifa hili, ambao wanaweza wakalisaidia Taifa hili kupiga hatua. (Makofi)
Mheshimiwa Sika, jambo la mwisho naomba nimuombe Mheshimiwa January. Kwenye Jimbo langu la Singida Magharibi kuna vijiji vinne mliviruka, mliruka Kijiji cha Nkhoire Kata ya Isseke. Ninarudia Nkhoire ya Isseke January ninakuomba uikumbuke. Kijiji cha Mwaru ambayo ni Makao Makuu ya Kata mliiruka ninaomba muikumbuke, mimi kwa kazi hizi mlizozifanya 2025 niletee mtu yeyote mnayemtaka atapigwa saa mbili asubuhi, kwa kazi hizi za umeme. Ninachokuomba ni kwamba endeleeni kufanya kazi kwa uzalendo, Mungu awabariki sana, mnafanya kazi kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa niseme nataka niwaambie Wabunge Spika huyu na mimi narudia, hata jana Spika wa Afrika Kusini na watu wao wamesema wao wanamu–endorsed huyu Brigedia Jenerali akagombee Bunge la Dunia. Sasa kama Mabunge makubwa yanamu – endorsed, Congo wako nae, Zambia wako nae, Botswana wako nae, Thailand wako nae, jamani ama namna gani? Tutashindwa jamani? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kazi iendelee. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 - Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu mdogo kwa ajili ya bajeti hii ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa kwa dhati ya moyo wangu nianze kwa kuipongeza Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa kazi kubwa inayofanywa na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama hasa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na waswahili wanasema ukiona vinaelea ujue vimeundwa, nidhamu kubwa inayooneshwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni kielelezo cha utekelezaji bora wa sera za Chama cha Mapinduzi katika kipindi chote toka Taifa limepata uhuru. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, si siri, Jeshi la Wananchi wa Tanzania ni miongoni mwa majeshi duniani yenye nidhamu ya hali ya juu. Taifa letu la Tanzania tumepata sifa kitaifa na kimataifa, tumeshiriki operesheni mbalimbali duniani na Jeshi letu; ninataka nijivunie hata makamanda mliopo humu kwenye ukumbi; tunasema ya kwamba Chama cha Mapinduzi kinatakiwa kipongezwe kwa kuwa katika kipindi cha takribani miaka 50 ya Uhuru Jeshi letu limekuwa na nidhamu na dunia yote imetutambua kwa kazi kubwa inayofanywa na wapiganaji wetu.
T A A R I F A . . .
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli wa Chama cha Mapinduzi chini ya nidhamu ya Jeshi la Wananchi Tanzania huwezi ku-exclude kwa sababu utendaji na utekelezaji wa sera zote toka tumepata uhuru nchi hii imekuwa ikitawaliwa na Chama cha Mapinduzi, unawezaje ukakitenga Chama cha Mapinduzi, unawezaje ukaitenga CCM na mafanikio makubwa yanayopatikana kutokana na nidhamu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja niwaambie Waheshimiwa Wabunge, nidhamu ya Jeshi letu na ndiyo maana hata leo mchana wakati kuna hoja zimetolewa juu ya vijana wa Jeshi la Polisi wamepigapiga risasi pale juu kidogo jana kwa sababu ya tukio lilikuwa limetokea kwa Mheshimiwa Malima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, let me tell you one thing, tunapozungumzia nidhamu ya vyombo vya dola, unajua kuna mataifa mimi nimejaribu kutembeatembea kidogo duniani, kuna mahali haya mambo tunayoyaona Tanzania sisi tunayapuuza lakini nataka niwaambieni hawa wapiganaji wa Tanzania kama ni Bunge tukiamua leo tukasema kwamba kwa nidhamu wanayoionesha mimi natoa rai kabisa Waheshimiwa Wabunge kwa bajeti zinazokuja naomba Jeshi la Wananchi wa Tanzania tulipe kipaumbele cha kwanza kwa sababu wapiganaji hawa wameonesha nidhamu ya hali ya juu na Taifa letu limepata sifa kitaifa na kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niende katika sekta nzima ya suala la JKT.
MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM: Mheshimiwa
Mwenyekiti, taarifa.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba hizo interruption uzipuuze ili niweze kuendelea na mchango wangu kwa sababu nina muda mfupi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, JKT kama moja ya sehemu ya kuzalisha ajira, ninaomba nitoe ushauri kwa Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi. JKT, ninatoa ushauri, kwa sababu JKT ina-recruit vijana wengi wanakwenda kupata mafunzo, naiomba Serikali tutenge fedha za kutosha, vijana wanapokwenda JKT wakafanya training ya kijeshi, wakamaliza kwa kipindi cha miezi sita wapelekwe na watafutiwe mashamba makubwa wafanye uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii italisaidia Taifa kupata chakula lakini pia vijana hawa kwa kipindi hicho watakuwa wanapata ajira in phase, wamemaliza walichozalisha kinakuwa mali yao wanaondoka wanaingia wengine, hivi ndivyo wanavyofanya mataifa makubwa kama China na mataifa mengine duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ninatoa ushauri, wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania sasa hivi kuna chama chao kinaitwa MUWAWATA, huu ni umoja wa wastaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kwa maslahi ya usalama wa nchi si sahihi sana umoja huu kuwa nje ya mfumo wa usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hatari hii inaweza ikajitokeza wakaingiliwa na kuanza kulishwa sumu na kusababisha uasi kwenye nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri wangu kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi, MUWAWATA waendelee kuwa na uratibu chini ya Serikali kupitia Jeshi la Wananchi kwa sababu hawa ni wapiganaji wa akiba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina takwimu, miaka michache ya nyuma MUWAWATA ulikopeshwa bajaji na wakalipishwa hela nyingi na vikundi vya wafanyabiashara, this is very dangerous kwa security ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa ushauri, kaka yangu Kamanda Mabeyo najua uko hapa, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwinyi, najua uko hapa kipenzi cha Watanzania, ninaomba upeleke hii proposal mkahakikishe kwamba MUWAWATA inakuwa chini ya usimamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho… (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kiongozi wangu kwa kunipa nafasi na kwa kweli kimsingi kabisa mimi niungane na Wabunge wenzangu kuendelea kuipongeza na kuiunga mkono Serikali yetu. Mimi kwa leo nina mada kama tatu chache kwa kifupi kwa ajili ya kuishauri Serikali yangu Serikali ya Chama changu iliyoko madarakani, kuwashauri Mawaziri wake pamoja na Watendaji wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la kwanza utafiti wa kidunia unaonesha kwamba Global Oil and Gas Companies ni state owned enterprise ambazo zinaendeshwa na Serikali husika duniani kote. Ili Taifa lolote liweze kufanikiwa katika exploration, exploitation kwenye mambo ya refinery, uuzaji na usambazaji wa oil and gas Taifa lolote duniani Waheshimiwa Wabunge na Mheshimiwa Mwenyekiti lazima lifanye uwekezaji wa kutosha katika taasisi zake za nchi kwanza, kwa sababu za kiusalama za nchi, lakini pili; kwa sababu za kibiashara za kupunguza makali ya maisha katika nchi yoyote ambayo imebarikiwa kuwa na resources ya mafuta na gesi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia baadhi ya michango ya Wabunge humu na kidogo nimekuwa frustrated a little bit, katika dunia ya sasa hivi Waheshimiwa Wabunge itakuwa ni hatari kubwa sana, tukija hapa Bungeni tukatoa ushauri wa kui-discourage TPDC katika uwekezaji wa mafuta na gesi tutakuwa tunafanya kosa kubwa sana katika Taifa hili. Mataifa makubwa duniani yanayozalisha gesi na mafuta nenda nchi kama za Saudi Arabia angalia akina Saudi Aramco yale makampuni, nenda Venezuela, nenda Kuwait wameyawezesha mashirika yao ya ndani ya nchi kistratejia yameweza kuwa na mchango mkubwa wa kufanya biashara kubwa duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ombi langu kwa Serikali, Kaka yangu Mheshimiwa January ninakuomba mimi sihitaji kusema sifa zako, uwezo wako wa kiutendaji brother hakuna mtu ana mashaka nao, uzalendo wako kwa nchi yetu Brother January na Naibu wako hakuna mtu ana mashaka nao, good enough umepewa timu ya Katibu Mkuu mchapakazi sana, Kaka yangu Mramba na mimi sifa moja January ambayo kwa kweli inakupa uziada, wewe ni humble sana Brother utasemwa utatukanwa mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Brother umepewa spirit ya ku-hold na kuvumilia mambo, keep that spirit lengo letu ni kumsaidia Rais na Serikali ya Chama chake kilichoko madarakani kufanya transformation. Hoja yangu ya msingi ninaomba Mheshimiwa January tengeneza mikakati, tunahitaji kuiona TPDC ya ushindani ndani ya miaka 10 tuweze kuwa na Shirika lenye uwezo wa ku-compete na akina Saudi Aramco tuweze kujenga heshima ya Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninaloishauri Serikali yangu ndugu zangu tusitake kuishauri Serikali kuja kuangamia, wote tunajua gharama ya kupanda kwa mafuta duniani kumeathiri vitu vingi, leo tunazungumza hapa mimi January nakuambia hili usingekuja nalo kwenye mkakati, I swear mbele za Mungu wangu nilikuwa nakwenda kukamata Shilingi lakini brother mimi nasema kwamba mimi nimenyanyua salute kwako umefanya jambo la diversification ya umeme na umetuambia unakwenda kuongeza kilomita mbili kila kijiji hivi jamani kwa strategy hizo atajitokeza Mbunge hapa aseme mama Samia hafanyi kazi? Au akisimama mtu kusifia mnasema eti wengine wanatumika? Unatumikaje kwa mambo mazito kama haya Rais anayoyafanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambie wala msidanganywe Rais asidanganywe Wabunge wote humu ndani wanampenda Rais na wanamuunga mkono, watu wasiende kutaka kuwachongea Wabunge na Rais waonekane kwamba kuna baadhi ya watu wazuri baadhi ya watu wabaya, Mama Samia kwa kazi anazozifanya wewe Mbunge kama huungi mkono wewe ni kichaa. Leo tunazungumza hapa hii bajeti Mheshimiwa January umeleta hapa kwa diversification unakwenda kuifanya ya umeme ina maana Mama ameweka bajeti amekwenda kui-triple mara mbili, vijiji tunaongezwa kila kijiji kilomita mbili nani kama mama Samia jamani! Kweli na hili nikisema mje mseme kwamba Kingu anazungumza ili ajipendekeze hivi, mimi ni kijana msomi jambo la kwanza, halafu siyo msomi mimi hapa kichwani niko vizuri. Nikija kujenga hoja hapa ninajenga hoja kwa sababu walipa kodi waliotutuma wamepata matumaini makubwa ya kazi zinazofanywa na Serikali Awamu ya Sita.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu January kaka yangu ninawashauri ni kweli bei imepanda msije mkajidanganya hapa tukataka sifa hapa ooh! Wakandarasi wanaiba bei zimepanda msiwaumize Wakandarasi bei zimepanda za vitu fanyeni utafiti tumieni wataalam wakaangalie quoted BOQ zilikuwa ngapi? Waende kwenye market ya sasa hivi, waangalie bei inasoma ngapi, nendeni mkawaongeze wakandarasi pesa miradi ya mama iishe miradi ya Mama iishe, lengo letu ni kuhakikisha ya kwamba kwa hali Mama anavyoupiga mwingi coming 2025 Rais ajichukulie kura kutoka kwa Wabunge hawa ambao ndiyo wasemaji na wawakilishi wake huko kwenye Majimbo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho tulizungumza hapa Bunge lililopita and I was one of the MPs ambao tulishauri ile kampuni mliipa kazi ya kuweka vinasaba kwenye mafuta we spoke of this, ilikuwa ina-charge Shilingi 14 kwa lita watu wakapiga kelele hapa mbona tunaibiwa, Rais ameingia madarakani Mama Samia ametoa maelekezo tangazeni tender.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tender imetengazwa huyo ambaye yupo sasa SISPA ameomba na makampuni mengine, mchakato umeenda, kampuni imeshinda inatuambia itatuwekea vinasaba kwa shilingi 5.8 kwa lita hao SIPSA nasikia sijui wametenda shilingi nane, wameshinda kampuni lowest mmefuta tender hivi mnafanya kwa maslahi ya nchi au kwa maslahi ya nani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunapozungumza hapa projection zinaonesha Serikali inapokea loss ya shilingi bilioni 4.5 kila mwezi, hivi jamani hatuionei huruma hii nchi, hizi bilioni 4.5 kila mwezi tunazopata loss, sitaki kusema mengi. Ushauri wangu kwa Serikali…
MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Salome Makamba taarifa.
T A A R I F A
MHE. SALOME W. MAKAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifa mzungumzaji Mheshimiwa Elibariki Kingu hasa kwenye ile jambo analolizungumzia la ufutwaji wa tender. Sheria ya Manunuzi ambayo tulitunga wenyewe ndani ya Bunge hili kifungu cha 19(1), (2) na (3) kinataka utaratibu wa kufuta tender Bodi ya Zabuni waende kuomba PPPRA na baada ya kuomba uchunguzi ufanyike na waitwe wale walioathirika baada ya kufuta tender ile lazima waitwe ili waweze kutoa concern zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kama utaratibu wa ufutwaji wa hiyo tender ambayo wote humu ndani tulikubaliana kwamba wakapewe ile kampuni nyingine badala ya hii inayotia Taifa hasara, kama utaratibu haukufuatwa Mheshimiwa Waziri huu ni uendelezwaji wa uvunjwaji wa Sheria ya Manunuzi ambao unafanywa na Serikali katika idara mbalimbali za nchi hii naomba nikupe hiyo taarifa. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu unapokea taarifa.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu mkubwa taarifa ninaipokea kwa unyenyekevu mkubwa sana. (Makofi)
MWENYEKITI: Haya endelea.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, na ndiyo maana haya mambo tunasema, unajua hili taifa tunalipenda wote, ikiwa Rais aliona kuna mahali kuna shida, mama yetu akaagiza haya yafanyike, hayo yaliyofanyika ya kufuta tender na ninakwambia hapa leo nina kwa mambo haya I have statistics zinaonesha wale watu wa TBS wanapoteza shilingi 11,000,000 kila siku; shilingi milioni mita tatu karibia na sabini kwa mwezi ukiangalia hata trend nzima kwenye nchi ndio nimekuja kufanya compilation nimepata fedha zinazopotea 4.5 billion kila mwaka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wabunge mpo tayari bilioni 4.5 zipotee fedha ambazo zinaweza kwenda kutumika kusaidia watu wengine? Serikali chonde chode msimtie Rais wetu doa, msimtie narudia tena nazungumza nikiwa na macho nimeyakaza bila kumwogopa mtu msimtie Rais aliyepo madarakani doa, fuateni taratibu na sheria za nchi mama huyu kazi anazozifanya kwa Taifa hatutaki 2024 kwenda 2025 Rais wetu tunapomnadi tunataka ni kutoboa na kuteleza kwa maslahi ya Taifa…
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Mwambe taarifa.
T A A R I F A
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimuongezee taarifa Mheshimiwa Kingu kwamba Kampuni hii anayoitaja ya SISPA ndio pia inayoendesha sasa uchapaji wa zile stempu za kieletroniki za ETS. Kwa hiyo malalamiko haya ni mapata kwenye uwanda wa biashara zinazofanywa na SISPA wakati nchi nyingine zilimkataa na ushahidi upo hata mimi ukiniambia nitenge ushahidi kwako nitakuletea. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu, unapokea taarifa?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu mkubwa ninapokea taarifa…
MWENYEKITI: ...na muda wako sasa umekwisha.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutoka kwa Mbunge makini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo ninaunga mkono hoja Mheshimiwa January na Naibu wako fanyeni kazi mumsaidie Mama, Bunge na Watanzania tupo na ninyi mpaka kieleweke. (Makofi)
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuwa mmoja wa wachangiaji jioni, lakini kabla sijaanza mchango wangu ambao nitauelekeza katika maeneo makubwa matatu, kama ushauri kwa Serikali na kama maoni yangu nikiwa kama Mbunge muwakilishi kabisa wa wananchi wa Singida Magharibi, ukweli lazima tuuseme. Umuhimu wa kusema ukweli ni kuweza kulisaidia Taifa liweze kuwa na mtazamo ambao ni sahihi kutoka mtazamo ambao sio sahihi ambao unaweza ukajengwa katika mazingira tu ya kijamii, kiuchumi ama mazingira mengine ya kisiasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimezunguka Nchi ya Kenya kwa mwaka huu, nimekwenda Uganda na nimekwenda Rwanda. Nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu kwamba, standard za kuulinda uchumi wa Tanzania zinazofanywa kwa makusudi na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Waziri wake wa Fedha, kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba, kama hautembei unaweza usielewe haya ninayoyasema. Standard za kuulinda uchumi kwa Afrika Mashariki kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu, wewe na Serikali yako na Rais wetu mnalitendea haki sana Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia jambo zima la inflation toka dunia imetoka katika misukosuko ya Covid-19, angalia inflation katika Nchi ya Rwanda, angalia inflation katika Nchi ya Uganda na Kenya kwa statistics. Tanzania tunafanya the best katika ukanda wa Afrika Mashariki na ukanda wa Nchi za SADC. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa dhati ya moyo wangu na mimi niko proud na Waziri wa Fedha. Kwanza huenda kwa sababu tu nitasema, mtasema huyu anamsemea kwa sababu ni ndugu yake wa Singida. Mimi nazunguka duniani, mmenipa nafasi ya kuwa mwakilishi kwenye Bunge la Dunia, ninazunguka dunia yote. Viwango vya namna uchumi wa Tanzania unavyokwenda Mheshimiwa Waziri shikamoo, unajitahidi sana kaka yangu kuliweka Taifa katika misingi ambayo imewapunguzia economic shock Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikia baadhi ya wachangiaji wamezungumza wamesema…
MBUNGE FULANI: Eti, rudia.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri ananiambia nirudie. Nimesema kwamba, juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Wizara hii ya Fedha imesababisha kupunguza economic shock kubwa ambayo ingeweza kuleta frustration kwenye nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesikiliza wachangiaji, kaka yangu ametoka kuchangia hivi karibuni, hii Finance Bill mnayoileta mwaka huu, nawaambia mimi nitakuwa Mbunge wa kwanza kuiunga mkono kwa sababu kubwa zifuatazo, haiwezekani kama Taifa tukawa tumewapa monopoly watu wachache kuagiza sukari. Wamepewa monopoly na Serikali kuagiza sukari na wamepewa incentive, mimi ni muumini mzuri sana wa viwanda na sina maana kwamba, viwanda vyetu vya sukari vinafanya vibaya, lakini wanafanya vitu ambavyo vina-abuse soko na kumuumiza mlaji wa mwisho, ambaye ni mwananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya, nikupe mfano mdogo. Mwaka jana Wizara ya Kilimo ime-analyze gape la sukari kwenye nchi wakapata tani 60,000. Wakawaita wenye viwanda wakakaanao chini wakawaambia agizeni hii sukari. Nakwambia Mheshimiwa Waziri kama sio makusudi viwanda vyote vya sukari viligoma kuleta sukari nchini, why should be like this? Hivi kweli tuingie gharama ya kuwapa mzigo watanzania walaji wa mwisho?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sukari ilifika mpaka shilingi 7,000. Mheshimiwa Waziri, mimi leo nataka kusema harakisha, ikiwezekana mngekuwa mnaweza kurekebisha Kanuni, Finance Bill ije haraka, tutaipitisha kwa msimamo mmoja, Wabunge wote tutaipitisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Taifa hatuwezi kuruhusu monopoly ya kuagiza sukari inafanywa na watu saba. Wakipewa vibali wanachukua wanakwenda kuviuza kwa watu kwa expense ya kuja kuwapa mzigo walipa kodi ambao ni raia wa Taifa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo jambo nikiwa kama Mbunge ninayetokana na Chama Cha Mapinduzi, Mbunge ambaye kazi yangu ni kuja Bungeni, kusimama na kuyasemea masilahi ya walipa kodi ambao wamekiamini Chama changu kilichopo madarakani kwa ajili ya kuwapigania katika welfare zao, hatuwezi kuruhusu jambo hili. Kwa hiyo nataka nimwambie Waziri wa Fedha pamoja na Watu wa Mipango, hiyo Finance Bill tutaipigia debe kwa sababu inagusa masilahi mazima ya walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nalotaka kuishauri Serikali yangu; Hayo mengine sina lengo la kumwingilia Mheshimiwa Spika na Kamati yake, yako kwenye Kamati ya Maadili, Mheshimiwa Mpina amepelekwa kwenye Kamati ya Maadili, sitaki kuingilia. Hata hivyo, nachotaka kukuambia ni kwamba Serikali yoyote duniani itakapokosa kuwa na nguvu ya kuingilia soko inapoona raia wake wanafanyiwa makusudi na kuibiwa, Serikali hiyo inakosa legacy ya kuiongoza nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia na Serikali yake hawawezi kuona kuna wafanyabiashara wachache wanajipanga kuona bei sukari inafika shilingi 7,000 Rais akae ametulia aseme kwamba; “Eeh, tunalinda viwanda vya ndani.” Hata ingekuwa ni mimi nisingeruhusu hiyo hali. Jukumu la kwanza la Serikali yoyote iliyochaguliwa na wananchi ikaaminiwa jambo la kwanza ni kulinda welfare ya watu wake, hiyo ndiyo kazi ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna hoja huku zimezungumzwa, mimi sina lengo la ku-interfere mambo ya Kamati. Unaposema kwamba Serikali imepata hasara ya shilingi bilioni 500, where do you get these economic calculations? Unazitoa wapi? Siku zote tunapoagiza shortage ya sukari na tunapoangalia sugar gap tunatoa exemption ya uagizaji wa sukari. Sasa hizo shilingi bilioni 500 zinatoka wapi? Hili kama siyo lengo la kutaka kuichonganisha Serikali na wananchi walioko nje waone kwamba Mama Samia ameshindwa kuisimamia Serikali anataka kuumiza wananchi. Haya mambo kwa Wabunge makini, tuliosoma kwa kodi za walipa kodi, tunaojua thamani ya Taifa letu we will never allow them to happen over our dead body kwenye Taifa letu, hatuwezi kukubali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukachekeana, tukaoneana haya kwenye mambo, when it comes kwenye mambo yanayohusiana na masilahi ya Taifa letu tutailinda Serikali yetu kwa wivu na gharama kubwa kwa masilahi ya Watanzania. Hili nalisema wazi mchana kweupe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nilishauri kwenye bajeti ya Mheshimiwa Nape. Mheshimiwa Mwigulu nataka nikuongeze wigo wa kukusanya kodi. Tulizungumza na kaka yangu Mheshimiwa Sanga; tulisafiri na wewe kaka yangu kwenda Marekani, tulichojionea kwenye mataifa makubwa ambayo Watanzania siku zote mnatoa mifano; “Eti kwa nini Marekani wana barabara nzuri, kila kitu angalia Ulaya.” Those guys wanalipa kodi. Lazima tujenge utamaduni wa watu kulipa kodi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo kwenye Taifa letu mkiangalia kwenye statistics, zinaonesha wanaotubeba kwenye kulipa kodi ni watu wasiozidi 5,00,0000, Taifa lenye watu milioni 60 lakini nguvu kazi tuseme ni watu milioni 30, wangapi wanalipa kodi? Watu hawalipi kodi. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu nakupa mfano mdogo na nataka nikuulize swali, ni madereva wangapi wanaoendesha tax mtaani mmewasajili kidigiti na mnjua hela wanzokusanya kwenye tax? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo kuna taxi zinapaki Airport, kila siku natoka airport nashuka inanileta nyumbani na ninalipa shilingi 20,000. Nani analipa kodi kwenye ma-tax haya yanayoendeshwa barabarani? Nani analipa kodi kwenye majumba? Mimi mwenyewe nina nyumba zangu nimepangisha watu wanakaa, hata mimi nazungumza hapa sijawekewa mfumo na Serikali kuhusiana na hela ninazozipata kwa kulingana na kodi za nyumba zangu, kodi za Serikali zinakwenda wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanadanganya, mtu ananunua kiwanja anauza, value imepanda anadanganya Serikali ameuza kiwanja shilingi milioni 200, ameiba zaidi ya shilingi milioni 160. Serikali haya mnashindwa kuya-monitor. Kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu nataka nikusaidie mawazo, digitalize uchumi wa Tanzania, ondoeni cash economy. Ninawambia tax base ya nchi itaongezeka, Serikali mtakusanya mapato. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu, mtajenga uchumi wa kisasa utakaoweza kuwasaidia Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ninaloshauri Serikali yangu. Kaka yangu Mheshimiwa Bashungwa unafanya kazi nzuri na kubwa katika Wizara yako. Wewe pamoja na timu ya watu wako tunakuona mpaka umekwenda kula chakula sijui kinaitwa mlonge, tukasema labda utamsahau Mama Alaska na utahamia kule lakini tunamshukuru Mungu ulirudi. Ninaomba nitoe ushauri kwa Wizara yako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa na changamoto ya ma-engineer kule kwenye mikoa. Sometimes unakuta mtu ambaye hana fani ya engineer anakwenda kusimamia barabara. Nakushauri kupitia bodi zako sijui ERB na akina nani, tengeneza pool ya vijana waliomaliza chuo kikuu ambao ni ma-engineer wawekeni kwenye list hakikisheni kila mkandarasi anayepata kazi kwenye Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anawachukua vijana wasiopungua watano waliomaliza vyuo vikuu wapate skills. Wakimaliza mradi kwanza watapata kipato, pili mtakuwa mnatengeneza technology transfer kwa zile kampuni ngeni kwa vijana wa Kitanzania. Baada ya miaka mitano kampuni za wazawa wa Kitanzania zitakuwa na uwezo wa kuchukua tender kubwa. Mheshimiwa Bashunga ninalisema hili nikiwa na imani na wewe kama Waziri kijana unaweza ukalifanya kwa lengo la kusaidia nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la mwisho lakini siyo kwa umuhimu. Kaka yangu, Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo, umepewa Wizara kwa muda mfupi umefanya kazi kubwa na ya kizalendo. Kwa mara ya kwanza nimepata muda wa kusoma mpango wote, hongera sana. Hivi ndivyo watu wa Singida wanavyofanya, hivi ndivyo Singida inavyotoa watu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi naweza kusema kwamba, kwa mpango huu na kwa miaka ijayo, alisema Mheshimiwa Askofu Gwajima watu wakafikiri anatania, jitahidini mipango tunayoipanga tui-reinforce kwa sheria ili kiongozi yeyote anayekuja kwenye Taifa letu apite kwenye njia ya mipango na maono ya Taifa kwa miaka 100 inayokuja. Tukiweza kufanya namna hii tutakuwa tumelijengea heshima Taifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo na kwa haya niliyoyasema kwa uimara wa uchumi wa Taifa letu, Rais wetu anavyohangaika kutafuta fedha huku na huko, ninakiri na kusema hadharani mchana kweupe kwamba Rais Mheshimiwa Dkt. Samia ameonesha uzalendo mkubwa, ujasiri mkubwa na nguvu kubwa kama mwanamke. Mimi Mbunge wake nasema Mitano tena kwa Mama, mwenye wivu ajinyonge. Mimi Mbunge wa wananchi ndiyo nimekwishasema sasa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza kabisa na mimi niungane na baadhi ya Wabunge wenzangu kuwapa pongezi Waziri wa Maji, Mzee wangu Mheshimiwa Engineer Kamwelwe pamoja na kaka yangu Mheshimiwa Aweso. Kwa kweli, wanasema mnyonge mnyongeni, watu hawa wanajitahidi kujituma regardless ya changamoto za kifedha ambazo zipo katika Wizara yao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia nimpongeze Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Mkumbo. Profesa Kitila, kaka yangu huyu kwa kweli, hongera sana brother, tunaona kuna mabadiliko yanaonekana na unatuwakilisha vizuri watu wa Singida pia kwenye Wizara hii, ahsante sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naungana na Wabunge wenzangu kuishauri Serikali na hapa naomba tuelewane. Najua Mheshimiwa Waziri wa Fedha yuko hapa, sisi tunapozungumza kama Wabunge tunazungumza kwa niaba ya wananchi walipa kodi wa hii Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wabunge tumesema tunahitaji shilingi 50 ziingizwe kwenye petroli na dizeli kwa ajili ya kuwasaidia wapiga kura wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuishii kuagiza fedha hizi ziingizwe, tunatoa rai fedha hizi zikiingizwa, Wizara ya Fedha tunawataka sisi kama Wabunge, fedha hizi ziende Wizarani zikatatue kero na changamoto ya maji kwa wananchi wetu. Itakuwa ni jambo la aibu kama tutawapa wananchi wa Tanzania burden hii, fedha hizi ziingie zikatumike katika mipango ambayo Bunge hili halikuwa limependekeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi najua Mheshimiwa Waziri wa Maji, najua unyenyekevu wako mzee wangu na Waziri wa Fedha, mama yangu Mheshimiwa Kijaji, wewe ulikuwa mwalimu wangu, huyu mzee mkimpa fedha mimi nina imani kwa jinsi ninavyomjua huyu mzee tatizo na changamoto za maji, mnyonge mnyongeni…
MWENYEKITI: Mu-address kama Mheshimiwa Waziri au Mbunge.
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa hiyo, Wizara ya Fedha tunachowaomba hizi shilingi 50 tunaomba ziende Wizara ya Maji wakafanye kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, kuna watu wengine wanakuja wanachangia kuhusiana na mradi wa Stigler’s. Mimi nataka niwaambie, Ilani ya TANU kipindi cha nyuma, kwa watu mnaosoma historia, acha sisi watu wa Chama cha Mapinduzi, Mradi wa Stiggler’s umekuwepo kwenye Ilani ya TANU enzi za Mwalimu Nyerere, la kwanza. La pili, ndugu zangu tuache kushikiwa akili na Wazungu. Miradi yote ambayo Taifa linajua italeta tija Wazungu wanakuja wanasema environmental problem, achacheni na haya mambo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunachotaka Bwawa la Kidunda lijengwe, mradi huu wa Stiggler’s Gorge ukatekelezwe. Kinachotakiwa Serikali chukueni maamuzi magumu kafanyeni serious land conservation. Kuna mambo yataumiza watu, lakini fanyeni kwa maslahi ya vizazi vinavyokuja na kwa maslahi ya hili Taifa. Haiwezekani leo tuogope kutekeleza mradi kwa sababu tu kuna watu wanapiga kelele kwa maslahi ya Wazungu, tuwaache Wazungu wawili/watatu wakavae bukta wapige picha tuache kutengeneza mradi wa nchi kwa maslahi ya nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, megawati 2,400 zitaweza ku-curb problem ya umeme ambayo nchi tumekuwa nayo toka uhuru. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri na Serikali, kama Rais wetu alivyosimamia sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi tunawakilisha watu wengi humu ndani, nendeni mkatekeleze mradi wa Stiggler’s Gorge kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia ukiangalia hata ma-researchers wanavyosema, angalia gharama za uzalishaji umeme kwa kutumia mambo ya thermo technology, angalia mambo ya gesi, angalia mambo ya wave za bahari, angalia mambo ya nuclear, gharama ya uzalishaji umeme kwa njia ya maji ni ndogo, Wazungu wanajua. Hapa tunazungumzia tunajenga treni ya umeme itakwenda kuendeshwa na umeme upi? Kwa hiyo, tuwe wajanja hasa ninyi watu wa Serikali, simamemi imara kuhakikisha kwamba kile mnachoki- dream sisi tunawaunga mkono, tekelezeni kwa maslahi ya wapiga kura wa Jamhuri hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu ambalo nataka nilizungumze, Mheshimiwa Waziri nakuomba mzee wangu, kuna Wabunge wamechangia na mimi naunga mkono. Profesa Kitila Mkumbo kaka yangu, unda Tume ukachunguze kuna miradi hapa ya maji imefanyika, mfano mmoja ni kwangu, kuna miradi ya maji imetumia billions of shillings za walipa kodi haifanyi kazi. Nenda pale kwangu kuna Kijiji kinaitwa Nkwairee zaidi ya shilingi milioni 200 zimekwenda, jana nimetoka kufanya mkutano jimboni kwa wapiga kura mradi haufanyi kazi, watu wamepiga pesa, haya mambo hayawezekani. Hatuwezi kuruhusu Taifa letu fedha za walipa kodi zinatumika watu wanakwenda wanafanya miradi ambayo haina tija at the end of the day mradi unakwisha maji hayatoki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga pale kuna mradi ulitekelezwa kutoka Igunga kwenda mpaka kule Isakamaliwa. Nimeondoka nikiwa kama DC pale, DP zote hakuna centre hata moja inatoa maji. Watu wame-relax Wizarani as if nothing has happened, pesa za walipa kodi zimekwenda. Haya mambo kama kweli tunataka kumsaidia Rais na kuwasaidia wapiga kura na kwa maslahi ya chama chetu tuendelee kutawala na kushika dola lazima tutende haki na kuhakikisha kwamba tunawapelekea watu wetu maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, Mheshimiwa Waziri ulikuja jimboni kwangu, nakushukuru sana mzee wangu ukazindua mradi wa maji pale Sepuka na ulituahidi na najua kwa sababu Profesa Kitila Mkumbo uko hapa, Mheshimiwa Waziri alituahidi kutuchimbia visima vingine tisa katika maeneo yafuatayo; Mayaha, Misake, Iseke, Mpetu, Kaugeri, Ufana, Puma na Mpugizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba kwa heshima na taadhima na unajua sasa Profesa Kitila Mkumbo hapa na wewe ni home boy, hebu basi bwana fanya mambo yako huko kwa maslahi ya wananchi na wapiga kura wa Jimbo la Singida Magharibi. (Makofi)
Mheshimiwa Waziri nakuomba utakapokuwa unamaliza majumuisho ya Wizara yako uje na kauli ya kuwahakikishia watu wa Jimbo la Singida Magharibi kwamba kero za maji, kwa mfano, kuna maeneo mzee wangu niliyasema kuna watu wanabeba ndoo za maji kutoka Kata ya Kijiji cha Mlandala…
T A A R I F A . . .
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, aah, basi bwana kwa heshima kwa sababu huyu Mbunge pia ninamheshimu basi, lakini kwani hujui kwamba Profesa Kitila Mkumbo ni mwenyeji wa Singida? Nimeipokea taarifa yake kaka yangu huyu, naomba niendelee kumalizia mchango wangu. Natambua kama huyu bwana ni Katibu Mkuu wa nchi nzima lakini wewe kubali tu bwana huyu ni wa kwetu pia Singida kule bwana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kumalizia kwa kusema Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Dokta John Joseph Pombe Magufuli, mimi nataka nikupongeze sana Mheshimiwa Waziri, toka nimekua kwenye kijiji nilichozaliwa mpaka nimefikisha umri wa kuwa Mbunge sijawahi kuona miradi mikubwa ya maji ikitekelezeka kama kipindi hiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa napozungumza Waziri umeleta fedha shilingi milioni 300 tumechimba maji Mtunduru, shilingi milioni 300 tumechimba maji Irisya, shilingi milioni 81 tumechimba maji Mwaru, shilingi milioni 210 tumesambaza maji Sepuka, shilingi milioni 81 tumesambaza maji Nkwairee japokuwa mradi huu nimesema una matatizo, lakini kwa juhudi kabisa Mheshimiwa Waziri nataka nikupongeze wewe na Naibu wako, ahsanteni sana. Njooni tena tuendelee kutatua changamoto za maji kwenye jimbo langu, Mungu awabariki, endeleeni kuisimamia na kuitekeleza Ilani ya chama changu ili CCM tuendelee kushika dola na tuendelee kuwatumikia wananchi wa hii Jamhuri na walipa kodi wa nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Kumi na Moja wa Bunge
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia. Kwanza kabisa ni wazi inajulikana kabisa ya kwamba jukumu la kutunga sheria ni jukumu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba. Kinachofanyika kitendo cha ku-delegate mamlaka ya utunzi wa sheria kwenda kwenye mhimili wa executive ni kutokana na ukweli kwamba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haliwezi kukaa kila siku na kutunga hizi regulations ambazo zinatumika kwenye mamlaka za Serikali na Serikali Kuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kimsingi tukiri ya kwamba mimi nikiwa kama moja ya wajumbe wa Kamati ya Sheria Ndogo tumeshuhudia kwa kiwango kikubwa ukosefu wa umakini mkubwa sana sana sana kwa upande wa executive katika utunzi wa sheria na hasa regulation ambazo kimsingi ndizo zinagusa maisha ya wananchi ya kila siku.
Mheshimiwa Mwenyekiti, umakini huu umesababisha sisi kutilia mashaka ni kwa kiwango cha namna gani wananchi wetu wanaweza wakawa vulnerable kuathirika kutokana na matumizi ya regulation ambazo tunaweza tukazipitisha na wakati mwingine kwa kiwango kikubwa zinaletwa hapa zikiwa tayari zimeshakuwa gazetted na ziko kwenye operation.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshuhudia kanuni nyingi zinatungwa, kanuni inasema hivi lakini ukienda kwenye sheria unakuta ni kitu tofauti hakiendani na kitu hata kimoja kuhusiana na sheria husika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfano mdogo, ukienda kuangalia GN. 80 ambayo inaongelea habari za Urban Planning Building Regulation ya mwaka 2018; ukienda kusoma kanuni ya tatu inatoa tafsiri ya neno vehicle ambayo kimsingi ukiangalia tafsiri hiyo iko kabisa kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani kifungu cha 168.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukizingatia hilo, ukiachilia mbali kanuni hiyo kutoa tafsiri ya neno vehicle tofauti, lakini bado regulation yenyewe inaongelea habari za Urban Planning Building Regulation, sasa mambo ya vehicle kwenye mambo ya urban yanaingiliana wapi? Hii inaonesha kwa kweli kuna ukosefu wa umakini mkubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niiombe Serikali, regulations hizi ndizo zinazotumika ku-govern maisha ya kila siku ya wapiga kura na wananchi wetu. Kama mhimili wa Serikali hautachukulia suala la utungaji wa regulation ni kuwa ni suala serious kama alivyosema dada yangu Mheshimiwa Katimba, kuhakikisha kwamba mnapata manpower na skilled labour ambayo itaweza kusaidia Ofisi ya Mwanasheria na watu wa TAMISEMI katika kuhakikisha kwamba regulation zinazokuja ziweze ku-reflect misingi ya uandishi wa sheria katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hilo halitoshi, bado ukienda katika masuala ya uandishi wa majedwali, katika taratibu za uandishi wa sheria majedwali ni sehemu ya sheria, lakini unaweza ukakuta jambo limezungumzwa ukienda kwenye jedwali halipo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya mambo kwa namna moja ama nyingine yasipoangaliwa kwa umakini na kwa trend tuliyonayo ya ku-gazette regulation na kuzifanya zitumike na zinakuja baadae kwa sababu ya wingi italeta madhara makubwa sana kwa wananchi wetu. Nina imani ninayasema haya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ananisikiliza ili kusudi yaweze kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia pamekuwa na makosa makubwa ambayo yamekuwa yakifanyika. Misingi ya uandishi wa sheria imekuwa ikikiukwa sana, nikiwa na maana ya drafting principles katika uandishi wa regulations. Mfano mdogo unaweza ukaenda kwenye GN. 90, ukienda katika GN. No. 90 utakuta kwenye ile sheria nyuma ya sheria kuna maelezo ambayo ndani ukiangalia hayana explanation yoyote. Ili maelezo yoyote katika sheria yaweze kupata nguvu ya kisheria, lazima yawe na kifungu kinachotoa support ambacho kinayapa maelezo hayo nguvu ya kisheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ukienda katika hiyo sheria niliyoisema katika GN. 90 ambayo kimsingi inaongelea The Urban Planning (Urban Farming) Regulations, 2018 ambayo inayotoka na sheria mama The Urban Planning Act Sura ya 355, ameizungumzia Mheshimiwa Katimba, lakini nyuma ya sheria nenda kasome utakuta kuna maelezo, hakuna kifungu chochote kinachoyapa maelezo hayo nguvu ya kisheria, huu ni udhaifu mkubwa sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, nitoe ushauri kwa Serikali. Kwa sababu sisi katika Kamati tume-observe makosa ya kimsingi ambayo kimsingi unaona kabisa ya kwamba kuna ukosefu wa umakini wa hali ya juu katika suala zima la utunzi wa regulation. Niiombe Serikali, kupitia Ofisi ya TAMISEMI, kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, toeni semina kwa maafisa ili watu wanapofanya kazi zinazoletwa kwenye Bunge tuweze kuona kwamba Mhimili wa Serikali uko serious katika kuandaa regulation ambazo zinatumika kwa wananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, niiombe Serikali kwa umakini mkubwa kabisa, ni muda muafaka sasa regulation zetu kabla hazijakuwa gazette, kwa sababu nyingi sisi kama Wabunge ambao tunasimama kwa niaba ya wananchi zinaweza kuleta madhara makubwa kwa wananchi, tuiombe Serikali kabla hawaja- gazetted regulation na kanuni zozote wazilete kwenye Bunge tuweze kuziridhia ndipo ziende zikawe gazetted kwa ajili ya maslahi ya wapiga kura wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, ninaunga mkono hoja nina imani Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wamesikia na nina imani Ofisi ya TAMISEMI pia wamesikia.
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2018/2019 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa kwa heshima kabisa nianze kwa kuzishukuru Wizara zetu hizi mbili, TAMISEMI na Wizara hii inayoshughulikia mambo ya Utumishi wa Umma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naanza kwa kumshukuru sana kaka yangu na mzee wangu Mheshimiwa Mkuchika. Mzee Mkuchika nampongeza kwa sababu miongoni mwa Mawaziri wasikivu yeye ni miongoni mwa Mawaziri wasikivu sana. Nakumbuka lilipotokea tatizo la watumishi kuondolewa kazini mimi binafsi nilikwenda ofisini kwake na alipopata taarifa kupitia kwa aliyekuwa anakaimu kama Katibu Mkuu pale Wizarani ambaye pia alinihudumia niliona public service pale, Mheshimiwa Mkuchika nataka nimpongeze sana na watumishi wake wa Wizarani hakika ni watu ambao wana commitment ya kazi. Naomba hilo nilitambue. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nataka nimpongeze Mheshimiwa Jafo. Mheshimiwa Jafo nampongeza sana kwa sababu kwa muda mfupi katika Wizara ambayo Mheshimiwa Rais amemweka kuweza kulitumikia Taifa letu amekuja Jimboni kwangu na Wilaya yangu ya Ikungi zaidi ya mara mbili, Mungu ambariki sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu ni kwa Mheshimiwa Jafo naelekeza ushauri wangu kwa taasisi ambayo Rais amemweka kuiongoza. Taifa letu linakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa nyumba za Walimu wa shule za msingi na sekondari. Nataka nimshauri kaka yangu Mheshimiwa Jafo, kama tulivyofanya mikakati ya kulisaidia Taifa kuondokana na uhaba wa madawati nchi nzima, natoa rai ni wakati muafaka kwa Serikali yetu kuamua kwa makusudi kukomesha tatizo la ukosefu wa nyumba za Walimu nchi nzima. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi natoka Jimbo la Singida Magharibi. Kuna maeneo unakwenda Walimu wanatembea zaidi ya kilometa saba mpaka nane hawana mahali pa kukaa. Changamoto hii inapelekea utulivu wa Walimu ku-concentrate katika kuwafundisha watoto wetu kuwa mdogo sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tuliweza kutatua changamoto za madawati kwa kipindi kifupi namwomba Mheshimiwa Jafo, kaka yangu, nina imani na yeye bado ni kijana mwenzetu namwomba akae na Wizara yake, akae na watendaji, wafanye tathmini ya upungufu wa nyumba za Walimu nchi nzima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi Wabunge wa Chama cha Mapinduzi kwa sababu ya uzalendo wetu na kulipenda Taifa letu tutakuja kumuunga mkono atakapoleta mapendekezo ya kujenga nyumba za Walimu nchi nzima hapa Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niongelee suala zima la afya. Ilani ya Chama cha Mapinduzi ilielekeza kujengwa kwa zahanati katika vijiji vyote na vituo vya afya katika kata zote katika Taifa letu. Mimi katika Jimbo langu nimeshaanza kujenga zahanati vijiji vyote kwa nguvu za wananchi na kwa kushiriki mimi Mbunge binafsi na kwa kutumia fedha za Jimbo. Mpaka sasa hivi tunavyoongea, kuna changamoto ya kumalizia pale ambapo wananchi wamefanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa Mheshimiwa Jafo, Jimbo la Singida Magharibi sasa hebu alitumie jimbo hili kama mfano wa majimbo katika Taifa hili kwa sababu sisi hapa tunapozungumza vijiji vyote vya jimbo tumeanza kujenga zahanati. Mimi juzi nimegawa zaidi ya vitanda 85 na nimevipeleka hata pale ambapo zahanati bado hazijakwisha lengo ni kuipa Serikali changamoto ili waone ya kwamba tuna kila sababu ya kuhakikisha wananchi hawa wanafikiwa na huduma za afya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuna maeneo ambapo wananchi wamemaliza kujenga maboma kwa zaidi ya miaka mitatu. Tuna kijiji cha Mnang’ana pale Sepuka wamejenga boma mpaka leo Serikali bado haijapeleka nguvu kwenda kumalizia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kazi nzuri na changamoto ambazo Mheshimiwa Jafo anakabiliana nazo katika sekta hii lakini bado kuna kila sababu ya kuhakikisha kwamba zahanati ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi, mimi mpaka sasa hivi tuna maboma zaidi ya 17 ambayo tumeanza kuyajenga kipindi mimi nimeingia hapa kama Mbunge lakini bado msukumo wa halmashauri kwenda kumaliza ni mdogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata Mheshimiwa Waziri kaka yangu Mheshimiwa Jafo akitoka hapa leo, akifanya mawasiliano na Mkurugenzi wangu atamwambia ni maboma mangapi tumeyasimamisha. Mheshimiwa Naibu Spika anapiga makofi kwa sababu alikuja jimboni kwangu akajionea. Kwa hiyo namwomba kaka yangu Mheshimiwa Jafo maboma ambayo tumeshayasimamisha watuletee fedha tuweze kuyamaliza ili tuweze kuwaunga mkono na kuwatia moyo wananchi hawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu, nakwenda kuzungumza habari ya vyumba vya madarasa. Nimpongeze sana kaka yangu Mheshimiwa Jafo. Amefanya kazi kubwa ya kutuunga mkono pale ambapo wanafunzi wetu walikuwa wanatembea umbali mrefu, sisi tumeanzisha programu ya kuanzisha shule za msingi ikiwezekana hata shule tatu katika kijiji. Kwa mfano, Kata yangu ya Minyuge tumeanzisha shule mpya za msingi katika maeneo ya Mayaha, Minyughe na Misake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, changamoto kubwa ni kwamba kuna baadhi ya maeneo watoto wanatembea kilometa 14 kwenda kutafuta shule katika makao makuu ya kijiji. Sasa maeneo ambayo tayari sisi kama Wabunge kwa kushirikiana na wananchi wetu tumeanzisha ujenzi wa shule mpya, tunaomba Serikali isichelewe kwenda kuweka nguvu kuhakikisha kwamba madarasa haya yanapauliwa na kumalizwa. Hilo ni la msingi sana katika kuwasaidia watoto. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kuna Kata moja inaitwa Mwaru, kuna eneo linaitwa Mtakuja, watoto wanatembea umbali wa kilometa 16 kipindi cha mvua mito inakuwepo, watoto hawawezi kwenda shule, lakini sisi tumejenga shule pale Mtakuja tumeshamaliza. Kwa kushirikiana na wananchi tumeshamaliza kuipaua. Namwomba Mheshimiwa Jafo anapofanya location ya Walimu Jimbo la Singida Magharibi aliangalie kwa jicho la karibu sana kwa sababu tumeweka commitment na tumeweza kuwasaidia watu wetu katika eneo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la nne, nizungumze kuhusiana na barabara. Ombi langu kwa Mheshimiwa Jafo na Serikali yangu kwa ujumla, Serikali yangu sikivu, Serikali ya Chama cha Mapinduzi, naomba Mfuko wa TARURA ikiwezekana asilimia waliyoiweka waiongeze kwa sababu idadi kubwa ya barabara ambazo zinahudumiwa na halmashauri changamoto ya barabara bado ni kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nina barabara yangu ambayo haijafanyiwa ukarabati wa kutosha kwa takriban miaka miwili inayotoka Puma - Ihanja - Muintiri - Igeransoni. Halmashauri yangu ya Ikungi sehemu kubwa ya mapato inategemea kutoka katika hizi kata ambazo ziko mpakani wa Tabora ikiwemo Igaransoni. Kwa hiyo, naomba kaka yangu Mheshimiwa Jafo chonde chonde…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 - Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba kutumia wasaa huu kukushukuru wewe kwa kunipa nafasi ya kuchangia Hotuba ya Waziri Mkuu kwa Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa naomba nitumie nafasi hii kumpongeza sana Waziri wetu Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa kwa juhudi zake chanya katika mchakato mzima wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitano. Waziri wetu Mkuu huyu amekuwa akitekeleza majukumu yake kwa ufanisi na unyenyekevu mkubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mchango wangu katika bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu utajikita katika sehemu mbili; bandari kwa masaa ya mchakato wa uagizaji mafuta na usambazaji wake na suala zima la biashara ya magari, hasa bonded warehouse.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2012 kilianzishwa chombo kilichokuwa kinaitwa Petroleum Importer Coordinator (PIC) ambapo chombo hiki baadaye kilivunjwa na kuanzishwa PBPA Wizarani ikiwa na majukumu ya kusimamia uagizaji wa mafuta na ku-discharge mafuta kwa wasambazaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo shida katika Taifa letu, shida hii lazima kama Taifa Bunge letu litimize wajibu wake kuishauri Serikali kwa maslahi ya nchi. Serikali yetu ina umiliki wa asilimia 50 katika Kampuni ya Tipper lakini vita inayoikumba kampuni hii utashangaa. Inawezekanaje tunaagiza mafuta nje ya nchi, yakifika Dar es Salaam kila importer anapelekewa mafuta moja kwa moja kwenye deposit yake wakati tunayo Tipper, chombo ambacho kina capacity kuhifadhi mafuta yote ya nchi hii na yaliyopo kwenye transit? Tipper wanapigwa vita eti wanaiba mafuta, sisi tumerogwa na nani? Serikali tuna hisa fifty percent Tipper ina maana Serikali tunaiba mafuta?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaiba mafuta against nani? Tunawaamini zaidi importers wakiwemo Engen, Oryx, Oilcom, Lake Oil kuliko chombo hiki cha umma ambacho tukiweza kuwa na one au single terminal receiving matanki ya Tipper yana uwezo wa kuhifadhi mafuta lita milioni 220, sawa na capacity ya kupakua meli tatu kwa wakati mmoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tipper ambayo ni sehemu ya Serikali ikipewa jukumu la kusambaza mafuta yote ya Oil Marketing Companies (OMC) wanaweza kusambaza mafuta ndani ya siku tatu baada ya ku-deliver na jambo hili linaweza kufanyika ndani ya siku sita tu kwenye depots. Ni muda muafaka sasa Tanzania kuepuka ujanja na wizi unaofanywa na wafanyabiashara wa mafuta kwa kupiga vita single terminal receiving.
Mheshimiwa Mwenyekiti, single terminal receiving ya mafuta ndiyo mfumo pekee unaotumika duniani kote. Hata mafuta ya transit wanunuzi wa nje ya nchi watachukulia mafuta kutoka Tipper na hivyo kuliingizia Taifa mapato na pia kuisaidia TRA kukusanya mapato yake kutoka eneo moja tofauti na practice ya sasa ya kufuatilia mapato kutoka kwa OMC moja moja kutoka depots zao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, damage charges tunazoingia kwa meli kuwa katika foleni, OMC wanalipia wastani wa dola 25,000. Dola 25,000 USD kwa siku, sasa unajiuliza kama hakuna ujanja kwa nini tunafifisha efficiency kwa chombo ambacho Serikali tunaweza ku-monitor uingiaji wa mafuta na usambazaji na kuliingizia Taifa ajira.
Mheshimiwa Waziri Mkuu najua yeye ni mzalendo na mtu wa haki, weka historia katika nchi hii kwa kuhakikisha kuanzia leo mafuta yote yanayoagizwa nchini yanamezwa na Tipper na waagizaji wote wapeleke kwenye deposits zao toka Tipper.
Mheshimiwa Mwenyekiti, faida za kuwa na single receiving terminal ni hizi; moja, hapatakuwa na damage sababu meli zitaweza kumwaga mafuta kwa wakati. Mbili, ili kuepuka wizi au diversion ya mafuta mabomba ya mafuta kati ya SBM na Tipper itenganishwe; na tatu, tutaongeza wigo wa Transit Cargo Consignment.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wetu Mkuu na Serikali wajue kwamba wafanyabiashara wanapoteza wastani wa shilingi milioni 330 kwa gharama za demurrage kwa wastani wa siku @25,000 USD kila meli inapokuja kupakua mafuta, wastani wa call za vessel za mafuta ni 24 kwa mwaka, hivyo wastani huu unapelekea kupoteza pesa karibu 19,776,970,608 kila mwaka zinapotea sawa na wastani wa milioni 824,040,422 kwa kila shipment.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge hili ni kazi yake kuishauri Serikali, ni wakati muafaka katika majumuisho ya hotuba ya Waziri Mkuu Serikali sasa wakubali kufanya mabadiliko ya haraka kwa maslahi mapana ya nchi yetu kwa kuifanya Tipper iwe mpokeaji na msambazaji wa mafuta yote ya nchi kutoka kwa petroleum traders.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa sasa kwa upakuaji wa mafuta bandarini una kasoro kubwa na unatia walakini wa ukweli wa idadi halisi ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa mfano kwa idadi ya terminal 18 – saa kati ya 36- 54 zinapotea kutokana na kuhamisha umwagaji kutoka terminal moja kwenda nyingine. Taifa letu tuna shida moja tunalalamika sana, tunatengeneza vitu vizuri lakini hatutaki kutekeleza wakati mwingine kwa viongozi wetu kupotoshwa kwa makusudi au kwa kutokujua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Tipper ni chombo ambacho Serikali yetu ina umiliki, ukifanya analysis ya kimapato nje ya gawio, Serikali imepata revenue karibu asilimia 68 kutoka Tipper moja kwa moja, Serikali tunapata revenue ya almost 70% kutoka Tipper na oryxy mbili anachukua asilimia 30% tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya ushauri huu, naiomba Serikali yangu sikivu ya CCM kuanza mara moja matumizi ya single terminal receiving. Naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020
MHE. ELIBARIKI E. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima na taadhima nitumie fursa hii kukushukuru wewe binafsi na Bunge lako tukufu kwa kunipa nafasi ya mimi kutoa mchango katika ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishi na Utawala Bora.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa mimi binafsi naomba ku-declare kwamba Mheshimiwa Freeman Mbowe namuheshimu sana kama kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwa sababu ni mtu makini nina imani. Hata hivyo, kuna vitu ambavyo kaka yangu Mheshimiwa Mbowe amevizungumza naomba nivitolee ufafanuzi kidogo sana hasa katika suala zima la ulinzi wa Mheshimiwa Rais.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ulinzi wa Rais, naomba nieleweke, kwa namna ambavyo Rais wetu amechukua maamuzi katika masuala mazima ya uchumi wa nchi, usalama wa Rais wetu lazima utakuwa kwenye mashaka makubwa kwa sababu ya maamuzi Rais wetu aliyoyachukua. Wewe ni shahidi, Bunge lililopita Mheshimiwa Zitto Kabwe na timu yake walileta hoja hapa kuna watu walipiga fedha katika masuala ya ESCROW, Mheshimiwa Rais Magufuli ameingia madarakani, watuhumiwa wote waliokuwa wamefanya ubadhirifu kwenye mambo ya ESCROW, amewakamata, sasa wako magerezani. Kwa kiwango cha fedha zilizokuwa zimeliwa, Rais amekamata watu hawa mnataka kuniambia hawa ma-Taikun hawana watu wanaoweza wakaleta insecurity kwa usalama wa Rais? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema Serikali inatekeleza miradi ambayo Wazungu wanaipiga vita, Stiegler’s George, tunakwenda kuzalisha MW2400 za umeme, Wazungu wanapiga vita, Rais kwa ujasiri anatekeleza hilo. Hizi ni ahadi zilifanywa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jasiri na jemedari Rais wa Awamu ya Tano anayetokana na Chama cha Mapinduzi ameingia madarakani, hajaangalia Wazungu ameangalia maslahi ya nchi, Stiegler’s George inajengwa, mnafikiri Wazungu wanafurahi? Mnafikiri usalama wa Rais utakuwa sawasawa? Leo tunavyozungumza Rais anajenga Standard Gauge, mnafikiri mataifa ya Ulaya wanapenda? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nitoe taarifa, ulinzi wa Rais tena uongezwe mara dufu kwa sababu usalama wa Rais wetu kwa mambo anayoyafanya kwa maslahi ya Taifa hili hatuwezi kuacha usalama wa Rais ukawa katika stake kwa sababu tunaogopa kupiga makofi, Wazungu walikuwa wanataka wavae vichupi wakapige picha kwenye Stiegler’s George kule Ruvu, haiwezekani. Tunaomba Wabunge wa Chama cha Mapinduzi na sisi ndiyo majority, ndiyo sauti ya nchi humu Bungeni, ulinzi wa Rais wetu ikiwezekana uongezwe hata mara kumi zaidi kwa sababu usalama wake hauko sawasawa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine nalotaka kulizungumza ni suala la utawala bora. Mwaka mmoja baada ya kuingia hapa Bungeni tuliona Taifa letu lilivyojaribiwa na hapa mimi nazungumza kwa sababu toka nimemaliza kusoma chuo kikuu sijawahi kufanya kazi mahali popote zaidi ya kuitumikia Serikali hii. Tumeingia Bungeni hapa kuna mambo mengine Serikali haiwezi kuya-disclose kwa sababu ya siri za nchi, Mataifa ya Ulaya kwa kushirikiana na watu ndani ya nchi mmeona kilichokuwa kinatokea kule Rufiji, watu wameuawa Kibiti, ili Taifa kudhihirisha kwamba lina utawala bora, dola ya Tanzania imekwenda kudhibiti upumbavu uliokuwa unafanyika pale Kibiti na nchi imetulia. Nataka niseme katika suala la utawala bora hakuna mahali ambapo tunaweza tukapigia kelele utawala bora, tunafanya vurugu, tuache Taifa letu liwe torn apart, never shall we allow this. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudi kwenye michango, moja ya vitu pia ambavyo tunaweza tukavizungumza katika utawala bora ni equal distribution of national cake. Nampongeza sana Mkurugenzi wa TARURA na timu yake na Mheshimiwa Jafo na timu yake na Mzee wetu Mheshimiwa Mkuchika, toka nimeingia madarakani fedha zilizoletwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuwasaidia wapigakura wanyonge, walipa kodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tumeletewa fedha shilingi bilioni 1.3 na tumejenga madaraja; tumeletewa fedha za vituo vya afya Sepuka, Ihanja na sasa hivi tuna kituo cha afya kule Iyumbu, yote haya ni mambo ya utawala bora. Zaidi ya hapo, hata kwa Jimbo jirani la kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye amepata matatizo, hapa napozungumza Serikali ya CCM bila kujali hayupo na anaumwa, zimepelekwa fedha vijiji 19 watu wake wanachimbiwa maji. Leo mnataka kusema nini hapa?
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Mheshimiwa Esther Matiko anazungumza hapa, Serikali ya CCM hapa napozungumza imemjengea Kituo cha Afya cha Mkende kwa shilingi milioni 400. Hapa tunapozungumza Serikali imemtengea shilingi bilioni 8 kumjengea soko la kisasa pale kwake Tarime. Hapa tunapozungumza boma lake la Halmashauri amepelekewa shilingi bilioni 2 na shilingi milioni 500 zimeshakwenda. Msije hapa kuwadanganya Watanzania, msije hapa kuudanganya umma, sisi tunachokisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi, chini ya Dkt. John Joseph Magufuli inafanya kazi. Nataka niwaambie, mimi kwenye Jimbo langu Rais alipata asilimia 73 ya kura ya uchaguzi uliopita lakini kwa kazi hizi 2020, Rais anakwenda kuchukua zaidi ya asilimia 95 ya kura. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba nitoe rai kwa Wabunge wa Chama cha Mapinduzi…
KUHUSU UTARATIBU
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuomba unilindie muda wangu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilichokuwa nasema sina maana kazi yangu hapa ni kuja kusifu tu lakini upotoshwaji unaofanywa juu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi, nikiwa kama Mbunge nayetokana na chama hiki lazima tuje hapa Bungeni tuweze kufafanua ili dunia na Watanzania waweze kujua ni kweli chama chetu na Serikali yetu inatekeleza au haitekelezi. Ndiyo maana nimetoa mfano, Jimboni kwa kaka yangu Mheshimiwa Tundu Lissu aliyepata matatizo, hayupo hapa Bungeni lakini Serikali ya Chama cha Mapinduzi imepeleka miradi ya maji katika vijiji 21 na hapa tunapozungumza miradi ya maji inaendelea kutekelezwa. Nimesema miongoni mwa mambo ambayo yanaweza yakaingia katika components za good governance ni pamoja equal distribution of resources na national cake na ndivyo Serikali ya Chama cha Mapindizi inavyofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka nimalize kwa kusema…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana, muda wako umekwisha.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, kidumu Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa heshima kubwa naomba kuleta mchango wangu kwa maandishi katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Kwanza pongezi zangu kwa Waziri na Naibu kwa kazi kubwa mnazofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niishauri Serikali yetu ya CCM, lazima tujikite katika kuandaa mitaala ambayo itawapa fursa wanafunzi wanaohitimu waweze kuwa na skills ambazo zitawafanya waweze kujiajiri au kumudu kuendesha maisha yao binafsi katika mazingira ya sasa ya ushindani. Wanafunzi wengi wanaomaliza vyuo na elimu za kawaida za sekondari, wamekuwa wakitegemea sana kupata ajira rasmi kutoka katika taasisi za Serikali na binafsi. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa wimbi kubwa la nguvu kazi mtaani ambayo haitumiki kwa maana ya kwamba hawana ajira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ufike wakati muafaka sasa Serikali yetu iandae mitaala ya namna ya kuwapa elimu ya kujitegemea wahitimu wetu ili wapate technical skill ambazo zitawasaidia kujiajiri au kujitegemea. Hapa tunaweza kupata wahitimu wakaandaliwa katika vikundi mbalimbali tukawapa mikopo ya mitaji hawa ambao tumewaandaa vema ili waweze kuanzisha miradi ya kujiajiri na kujitegemea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tulimaliza shule za msingi na kulikuwa na mafunzo ya elimu ya kujitegemea kama vile uselemara, umeme, ufundi wa magari na kadhalika. Naishauri Serikali yangu kuhakikisha watoto wetu wanaohitimu wanapata skills ambazo zitawasaidia kujiajiri na nchi pia kupata wataalamu ambao tutaweza kuwatumia katika viwanda ambavyo tunavihamasisha vijengwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, naishauri Serikali kupitia mfumo wa kuhakiki vyeti vya wanafunzi wanaoomba mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ambapo kwa sasa utaratibu umetolewa kwa waombaji wanaoomba kupitia online kulazimika kuhakiki vyeti jambo ambalo naona ni kuwapotezea muda na gharama watoto wa Kitanzania. Nashauri Serikali irudishe jukumu la kuhakiki vyeti lifanywe na Bodi ya Mikopo yenyewe na liwe well-coordinated. Wanafunzi wanapoomba mikopo wanaambatanisha na vyeti vyao vya kuzaliwa moja kwa moja, Bodi ichambue na kupeleka majina na nakala za vyeti viweze kuhakikiwa na hivyo kuwasaidia watoto wetu kupunguza gharama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya ya Ikungi, sisi ni wazalishaji wakubwa sana wa alizeti hivyo uhitaji wa ujenzi wa vyuo vya ufundi hauepukiki ili kupata vijana wenye technical skills watakaojiajiri katika usindikaji wa mazao ya kilimo yanayopatikana katika Wilaya yetu. Naomba sasa ujenzi wa VETA utekelezwe katika Kata ya Minyughe, Wilaya ya Ikungi, mahali ambapo tayari tumeandaa eneo la ujenzi wa chuo hiki ambacho kitakuwa chachu ya maendeleo katika kuwasaidia vijana wa Kitanzania watakaokuwa na uwezo wa kujiajiri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, natoa rai kwa Serikali kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuja na mkakati madhubuti wa namna ya kuandaa mkakati wa ujenzi wa nyumba za walimu nchini. Walimu wetu wanateseka sana katika kupata makazi ya kuishi hivyo kuathiri taaluma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Nishati
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii muhimu ya kuchangia kwa maandishi Hotuba ya Wizara ya Nishati. Nianze kwa kuipongeza Wizara na hasa Waziri Kalemani na Naibu wake kwa namna ambayo wamekuwa wasikivu na wachukuaji wa hatua wa haraka katika suala zima la kusambaza umeme vijijini.
Mheshimiwa Spika, wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi walikuwa nje ya REA Phase II; sasa Mheshimiwa Waziri na timu yako nikuombe REA Phase III isitupite tena. Watu wetu wamekuwa wavumilivu na kusubiri ahadi ya utekelezaji wa REA III ambavyo nina imani Vijiji kama, Kitumtu, Minyushe, Igelansoni, Mtunduru, Mwami, Kintandaa, Masweya, Germany, Msosa, Ishombwe, Iyumbu, Magunguruka, Kipunda, Mlandala na Vijiji vyote.
Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikimsumbua sana Mheshimiwa Waziri kuhusu REA II, baada ya mkandarasi kushindwa kumaliza vijiji vya REA II; ambapo aliondolewa na kupewa mkandarasi mpya ambapo makubaliano yalikuwa nikumnunulia vifaa lakini mpaka leo REA wameshindwa kununua vifaa na kumkwamisha mkandarasi katika kutekeleza majukumu yake.
Mheshimiwa Spika, naomba sana katika suala la Tipper Serikali ianzishe one stop center ya kuhifadhi mafuta badala ya utaratibu wa sasa wa kila muagizaji kupakua mafuta kutoka nchini na kuyapeleka kwenye matanki yao. Hili linapelekea kuwepo kwa wizi mkubwa ambao Serikali haiwezi ku-control kiwango cha mafuta yanayopakuliwa kutoka kwenye meli kwenda kwenye matanki ya kuhifadhi.
Mheshimiwa Spika, faida ya mafuta yote kuhifadhiwa Tipper ni kwanza tutaweza ku-control na kuwa na uhakika wa kiwango cha mafuta yanayoingia nchini na kuuza nje ya nchi.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo ninaunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa dakika hizo tano, lakini mimi pia ninaona tu kwamba ninamshukuru Mungu kwa sababu ili la Bagamoyo miongoni mwa nondo ambazo pia ambazo nilikuwa nimeziandaa nilikuwa nimejiandaa sana kuja kuchangia katika hii project ya Bagamoyo kwanza nikushukuru wewe binafsi kwa uzalendo mkubwa ambao umeuonyesha kulizungumzia hilo, ahsante sana.
Mheshimiwa Spika, mimi nakumbuka mwaka 2012 alipokuja Rais wa China kabla ya hapo Serikali hii ya Chama cha chetu cha Mapinduzi mwaka 2008 ili hire consultant ambaye alifanya kazi ya kufanya feasibility study wakaja na recommendation za ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, lakini kama alivyosema mama yangu Nagu kipindi hicho mimi nilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda nilikuwa nikifanya fair competition, Mama Nagu alikuwa bosi wangu, nataka nikuambie kitu kimoja not only kwamba hii Bandari ya Bagamoyo tunaizungumza hapa kwamba ilikuwa ina muhimu, lakini ilikuwa inakwenda kuwa the biggest port in Africa.
Mheshimiwa Spika, namba mbili Bandari hii ya Bagamoyo ilikuwa inakwenda kufanya circulation ya kuingiza makontena zaidi ya milioni 22 kwa mwaka ukilinganisha na Bandari ya Dar es Salaam, kwa wachumi waliokuwa wamefanya feasibility study pamoja na consultant, bandari hii ilikuwa inakwenda kuwa hub ya kuzifungua nchi ambazo ni land locked na mradi huu, nataka nikwambie ulikuwa unakwenda kuongezwa, wawekezaji hawa walikuwa wanakwenda kujenga Standard Railway Gauge ambayo ilikuwa inakwenda ku-connect kutoka Bagamoyo mpaka kwenye Reli ya TAZARA.
Mheshimiwa Spika, mimi nataka nikwambie ndugu zangu wa Serikali mimi ninawaomba hapa sisi kama Wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwa maslahi ya hili Taifa, hatuwezi tukaja hapa Bungeni tukazungumza kwa lengo la kuikwamisha Serikali, nimesoma kitabu hichi, kinachozungumzwa ni kwamba inaonekana kwamba mkandarasi sijui kuna mambo hayako kwa maslahi ya nchi, hatuwezi tukaishia hapo tu, tuangalie vipengele ambavyo vinakwamisha tuviondoe, mradi huu ukatekelezwe kwa maslahi ya hili Taifa.
Mheshimiwa Spika, leo Rais tayari Serikali yetu imeanza kujenga Standard Gauge Railway kutoka Morogoro - Dar es Salam kuja Dodoma, kama tutafanikisha mradi huu tayari hii Reli ya Standard Gauge itaweza kupata access ya kuwa fade na mizigo ambayo tutaichukuwa kutoka Bandari ya Bagamoyo.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo mimi kwa unyenyekevu mkubwa ninaungana na Wabunge wengine kuisisitiza Serikali this is the grand project kama Spika ulivyosema, tunaishauri Serikali ikakae iangalie wapi tumekwama mradi huu uweze kutekelezwa.
Mheshimiwa Spika, la pili naomba niende jimboni. Katika jimbo langu la Singida Magharibi na Mheshimiwa Waziri nimeshakuona zaidi ya mara tatu mwaka jana watu wangu wa Kata ya Iyumbu walivamiwa na majambazi saa tisa mchana, maduka yakaporwa kila kitu, watu wakakosa access ya kufanya mawasiliano hata polisi kuja kuwasaidia, hakuna minara ya mawasiliano. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwaka jana tumeletewa kitabu hapa na hili lazima tuliseme, Serikali Watanzania pia wanaona, msiwe manakuja hapa jamani wakati mwingine mnatupiga longolongo tunapata shida huko, tuliletewa vitabu hapa vinavyoonesha takwimu za minara itakayokwenda kujengwa na makampuni ikiwemo TTCL, mpaka leo tunapozungumza, wale wananchi wangu mimi kutoka makao makuu ya Wilaya mpaka ufike Kiyumbu ni zaidi ya kilometa 190 hawana minara ya mawasiliano, makampuni ya private mmeyazuia, sasa tunataka TTCL ikuwe lakini it must be competitive ili tuweze kuwasaidia watu wetu.
Mheshimiwa Spika, la pili kwenye kitabu nimeangalia barabara inayojengwa kutoka Sepuka - Mlandala kwenda Mgugila, ninaomba nimalizie hili kwa uchache sana, barabara hii nimeanza kuiona toka nikiwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga mwaka 2012/2013; imejengwa madaraja yasiyopungua 40, ni mwaka wa kumi hii barabara Serikali wameshindwa kuipandisha/kuijengea tuta la moramu, leo naangalia kwenye kitabu imeombewa milioni 90.
Mheshimiwa Spika, mimi naiomba Serikali wananchi hawa wa Iyumbu, Mheshimiwa Waziri nimeshakufuata zaidi ya mara mbili.
Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ikungi asilimia 90 ya revenue inapata revenue kutokana na wakulima wanaotoka kwenye Jimbo langu Singida Magharibi kwa sababu tunazalisha mpunga na mchele kwa kiwango kikubwa, lakini wananchi hawa tumeshindwa kuwakamilishia ujenzi wa hii barabara for ten years madaraja yamejengwa. Mimi nasema safari hii sitaingua mkono bajeti ya Wizara hii kama sita pata majibu ya ujenzi wa barabara ya watu wangu kwa sababu watu hawa wamekuwa wakipata shida, nimekwenda personal kulizungumza nimefanya njuhudi na sijapata majibu yoyote nashukuru sana.
Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa, 2022
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana sana kwa kunipa heshima hii kubwa ya ku-second huu Muswada ambao umeletwa na Serikali. Kwa kweli kwa kifupi sana nitumie fursa hii kumpongeza sana Waziri na Naibu.
Mheshimiwa Spika, mimi ulinipa nafasi na heshima ya kuhudumia Kamati hii ya Katiba na Sheria. Nimeshiriki katika kuujadili Muswada huu. Kwa kweli nitumie nafasi hii kumpongeza sana kaka yangu Simbachawene na Ummy kwa usikivu wao mkubwa kwa maoni ambayo sisi Wanakamati tuliwapa kwa lengo la kuboresha Muswada huu na kufanya harmony katika implementation ya Muswada huu mzima. Hongera sana kwa Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi niseme kitu kimoja. Ibara alizozitaja kaka yangu Olelekaita, Ibara hizi zimekwenda mbali zaidi. Ibara ya 13 ya Muswada huu imewataja Wabunge wa Viti Maalum wote nchini, kwamba wamepewa fursa ya kushiriki katika zile Oversite Committee tunazozitaja katika mikoa yao. Jambo hili limeonesha namna gani Muswada huu umeamua kuwa inclusive katika kuwafanya Wabunge katika kushiriki katika level za mikoa. Kwa maana Wabunge wa Viti Maalum ukija kwenye majimbo wanaweza wasionekane, lakini Muswada umeweza ku-reflect. Kwa hiyo, hili Mheshimiwa Simbachawene nafikiri darasa langu la kuwashirikisha kinamama katika uongozi na maamuzi ulilielewa vizuri. Ninakupongeza sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, eneo la pili ambalo nataka niipongeze sana Serikali; tulipata fedheha sana tulipopata maafa mwaka 2017 pale Bukoba. Tuliona namna gani Serikali ilivyokuwa ikihangaika kuwaita wadau ku-mobilize fund kwa ajili ya kwenda kutatua na kurudisha hali iliyokuwa imetokana na madhara ya earthquake ambayo ilikuwa imewapata watu wetu wa kule Bukoba. Kitendo cha Serikali kuja na Muswada unaoipa Ibara ya 34 Mamlaka ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha fund maalum ambayo itakuwa inatibu matatizo na majanga yakitokea katika nchi hii imeipa Serikali heshima na kuepuka Serikali kukimbia majukumu yake ya Kisheria na Kikatiba katika kupambana na majanga katika Taifa. Kwa hiyo, Mheshimiwa Simbachawene tunakupongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na fund hii itakayoanzishwa itawekewa utaratibu wa namna itakavyotumika.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa namsikiliza sana kaka yangu Kuchauka. Kama angekuwa amepata nafasi, huenda ameusoma Muswada labda kwa sababu pia alishapata matatizo, lakini akipata nafasi kuusoma Muswada hivyo vitu vyote alivyokuwa anauliza kwamba nani ata-determine janga hili ni la level gani na lichukuliwe na nani; Muswada huu umejitosheleza kueleza kila kitu, Mheshimiwa Waziri tunakupongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema maneno hayo machache ninaomba, na ninawashawishi Waheshimiwa Wabunge, kwamba tuunge mkono Muswada huu kwa sababu umekuja wakati muafaka ili sasa tuweze kuipa Serikali forum ya kukabiliana na majanga katika Taifa letu kwa namna ya ufanisi zaidi.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana ninaomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru wewe binafsi kwa kunipa nafasi katika kuchangia mchango wangu na ushauri kwa Serikali katika Wizara hii ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mheshimiwa Spika, katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM Serikali iliahidi kutekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami katika barabara ya Singida – Sepuka – Ndago – Kizaga yenye urefu wa takriban kilometa 92. Barabara hii imekuwa barabara muhimu sana kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara kama vile alizeti, mahindi na kadhalika. Wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 Mheshimiwa Rais alipita barabara hii na kuwaahidi wananchi kuwa barabara hii itajengwa kama ambavyo Ilani ya Uchaguzi wa CCM ilielekeza, lakini mpaka hapa tunapoongea utekelezaji wa Ilani katika ujenzi wa barabara hii bado unasuasua na hivyo kuwafanya wananchi kuendelea kupata adha katika kusafirisha mazao na hata mafuta yanayozalishwa katika viwanda ambavyo vimejengwa maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, Serikali yetu imekuwa ikitumia sana fedha nyingi katika matengenezo ya muda mfupi na mrefu ya barabara hii, jambo ambalo kama Serikali itaweka dhamira ya dhati katika kujenga barabara hii kwa Mwaka wa fedha 2018/19 Serikali ilitenga fedha za upembuzi yakinifu wa barabara hii lakini mpaka leo hatua za utekelzahi haueleweki.
Mheshimiwa Spika, katika Sekta hii hii ya barabara, Serikali tangu mwaka 2010 imejenga madaraja katika barabara ya Sepuka – Mkandala – Mgungira tangu madaraja yakamilike leo miaka 9 ujenzi wa tuta la barabara umeshindikana, hivi tumetumiaje pesa za umma kwa mamilioni na kushindwa kukamilisha ujenzi wa tuta tu? Barabara hii ni muhimu sana katika kusafirisha mazao ya chakula na biashara kama vile mchele, alizeti na barabara hii ambayo inaungana na barabara ya Magereza –Mtuduru – Iyumbu imekuwa ya muda mrefu sana mvua zimenyesha watu hawa wanakosa mawasiliano. Ni muda muafaka sasa kwa Serikali kutekeleza ujenzi wa barabara hii muhimu kwa wapiga kura wa Jimbo la Singida Magharibi.
Mheshimiwa Spika, jambo la tatu, mawasiliano ya minara ya simu; jiografia ya Jimbo la Singida Magharibi iko very complicated. Toka nimekuja Bungeni tumekuwa tukipewa vitabu vinavyoonesha distribution ya minara ya simu, lakini hakuna utekelezaji wa mnara hata mmoja ambao uliahidiwa na Serikali ambao umejengwa.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2018 wananchi wa Kata ya Iyumbu walivamiwa na majambazi mchana na maduka yote kuporwa pesa, watu wetu hawakuweza kupata msaada sababu ya ubovu wa barabara na ukosefu wa minara ya simu, hakuna mawasiliano ya barabara wala ya simu na kata hizo ndizo zinaendesha halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ambapo asilimia 90 ya mapato yanatoka kule kutokana na kiwango kikubwa cha uzalishaji wa mchele ambao unauzwa Uganda, Rwanda na Burundi na kuliletea Taifa mapato ya ndani.
Mheshimiwa Spika, mwaka jana vilitolewa vitabu hapa ambavyo TTCL wamepewa market share ili kufungwa minara katika maeneo hayo, lakini hakuna lolote lililofanyika katika kuwasaidia Watanzania hawa.
Mheshimiwa Spika, haya mambo yanatuweka mahali pagumu sana. Naomba minara ya mawasiliano ikafungwe Ikungi, Igholwe na maeneo yote ambayo wananchi wanapata matatizo katika Jimbo la Singida Magharibi.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi na kimsingi naomba ninukuu maneno yafuatayo yaliyosemwa na Mheshimiwa Rais wakati analihutubia Bunge lako Tukufu. Alisema: “Nakwenda kuchangia kwenye maeneo mawili kwa kifupi sana. Nitumie fursa hii kuikaribisha sekta binafsi kuwekeza kwenye viwanda vya kutengeneza bidhaa za mifugo, nyama, ngozi, maziwa, kwato na kadhalika. Katika hilo tunaahidi kutoa vivutio maalum kwa watakaowekeza katika viwanda hivyo ambavyo vitasaidia kuinua vipato vya wafugaji wetu na pia kuongeza fursa za ajira kwa Watanzania. Hapa nataka niweke bayana kuwa watendaji watakaokwamisha ujenzi wa viwanda tutawashughulikia”. Haya ni maneno ya Mheshimiwa Rais aliyatoa hapa Bungeni.
Mheshimiwa Spika, nataka nilipe taarifa Bunge lako Tukufu, global practice na najua hii ni theory kwa international trade mahali popote duniani, Tanzania, Uganda, Kenya, Ethiopia, Somalia na ukisoma katika statistics za dunia Tanzania tumetajwa kuwa nchi namba mbili kwa wingi wa mifugo barani Afrika. Katika hili namuomba sana Waziri wa Viwanda atulie anisikilize lakini pia namuomba Waziri wa Uwekezaji atulie na kunisikiliza.
Mheshimiwa Spika, nataka nilipe Bunge lako Tukufu hotuba ya Rais iliyokuwa imejikita katika kulisaidia Taifa kupiga hatua katika masuala mazima ya viwanda, nimeamua kuchagua eneo dogo na kulifanyia utafiti eneo la mifugo. Angalia hiki kinachofanyika katika nchi yetu ya Tanzania ili kama sisi Bunge tuweze kutoa mchango wa kulisaidia Taifa na kuwasaidia wakulima na wafugaji wetu.
Mheshimiwa Spika, nakupa taarifa wewe na Bunge lako Tukufu gharama za uwekezaji na export ya nyama ambayo imeshasindikwa katika Taifa la Tanzania kwa kiwanda ambacho mtu amewekeza na ameajiri watu, kwa mfano, kiwanda cha Kenya, kilichowekeza na kuwa na uwezo wa kuzalisha kwa mfano nimechukulia mifugo, ng’ombe 1,000 kwa siku, Ethiopia nako ng’ombe 1,000 kwa siku Kenya na Uganda, angalia gharama hizi uone namna gani we are the witch of our own development. Nataka nikuambie wewe na Bunge lako Tukufu mipango ya Serikali na nia ya Rais najua asilimia mia moja ni nia thabiti ya kuhakikisha Taifa linapiga hatua lakini bado hatujafanya harmonization ya sheria, regulation zinakwamisha kupiga hatua kwa sekta nzima ya viwanda katika Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, nakupa mfano, kiwanda kinachochinja ng’ombe 1,000 kwa siku Tanzania kikafanya uzalishaji wa ng’ombe 1,000 kwa kipindi cha mwaka mzima Kenya ili uweze kuzalisha ng’ombe 1,000 kwa mwaka mzima, gharama unazozilipa zile za kawaida tu achana na mambo ya tax, kuna kuja kulipa cooperate tax, PAYE na mambo mengine kwa Kenya inagharimu 1,900,000 kiwanda kinapata kama tozo tozo kutoka Serikalini. Ethiopia kiwanda kinachozalisha nyama ya ng’ombe 1,000 kwa siku, kwa mwezi, kwa mwaka wanalipa 1,008,000.24. Uganda wanalipa 1,900,000. Njoo kwa Tanzania na hii nataka nikuambie na Waziri wetu Mkuu yupo hapa state intervention katika kulinda viwanda vinavyowekezwa na Watanzania au investors wanaotoka nje imekuwa changamoto kubwa kwa Taifa letu. Ndiyo maana tunajenga viwanda vinakaa mwaka mmoja vimekufa, state intervention.
Mheshimiwa Spika, kwa Tanzania kuna bodi na matitiri mengi naomba niyasome uone picha na ninyi Mawaziri mliopo hapa mkasaidie kufikisha vision ya Mheshimiwa Rais katika sekta ya viwanda. Kwa Tanzania kuna kitu kinaitwa livestock and fisheries, ukizalisha nyama kila kilo wanaku- charge shilingi 150 wanasema gharama zao.
Mheshimiwa Spika, cha pili, kuna kitu kinaitwa Bodi ya Nyama, Mawaziri nyie mpo hapa kama nasema uwongo prove me wrong, nimefanya utafiti. Kuna kitu kinaitwa Bodi ya Nyama they take one percent ya FoB kwenye production ambayo imezalishwa na kiwanda. Kuna kitu kinaitwa Chamber of Commerce wanachukua shilingi 55,000 kila certificate per consignment ambayo inakuwa exported. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukifanya calculation mwekezaji atakayekwenda kuwekeza kwenye kiwanda cha kuzalisha nyama kwa mwaka mmoja kwa Tanzania nje ya cooperate tax na mambo mengine analipa fedha zisizopungua 860,000,000 wakati Kenya mtu analipa 1,000,000 peke yake. We cannot survival, hatuwezi ku-survival Mawaziri wangu na ndiyo maana viwanda vingi vinafunguliwa tunapiga makofi tunafungua viwanda haviwezi kukabiliana na ushindani. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wenzetu wanafanya state intervention na maana ya state intervention ni kwamba wawekezaji wanapoingia na Rais hapa nimeisema vision ya Rais wa Nchi, vision ya Rais wa nchi anasema tutatoa some sort of incentive katika viwanda, lakini wito wangu ninaotoa kwa Serikali yangu sikivu, ndiyo maana mnalalamika hapa, amesema kaka yangu pale, mbuzi wanakwenda kuuzwa Kenya, kiwanda wanawezaje ku-compete na Wakenya, Mkenya mimi juzi nilikuwa Dubai niliamua tu kufanya survey,nimekwenda nyama zote Dubai zinaandikwa imported from Kenya wakati Kenya hawana mbuzi. Afrika nchi zenye mbuzi hata Ethiopia tunawasifu, lakini hawana mbuzi, Ethiopia wanakondoo, mbuzi wanatoka Tanzania na kiasi kidogo Somalia.
Mheshimiwa Spika, ninachokwambia nenda kwenye masoko ya nje,kama utakuta kuna nyama imeandikwa imetengenezwa kutoka Tanzania, hakuna nahii nawaambia Mawaziri wa Mifugo, wasisubiri Rais Magufuli aje atoe matamko wachukue hatua. Yaani if I was the Minister, today ingetoa declaration ya kuhakikisha tozo zote ya ovyo zinazokwamisha viwanda vya nchi hii na kufanya Watanzania wanakosa ajira, ni bora utumbuliwe umefanya maamuzi kwa maslahi ya Taifa. Wafanye kazi Mawaziri wangu, wasiogope Rais yupo nyumayao. Mheshimiwa Mwambe you are Minister kaka yangu tunakuamini, bado kijana mdogo tunajua uwezo wako, shirikiana na Wizara ya Mifugo saidieni Taifa hili kwa mustakabali wa Taifa hili.
Mheshimiwa Spika, la pili, Rais jana alizungumza, nilisikiliza hotuba yake na hiyo pia iko katika packageya hotuba aliyotoa hapa Bungeni, suala la uwekezaji tuna changamoto kubwa sana, naomba nikwambie, kazi inayofanywa na Ofisi ya Waziri Mkuu hakika tunaweza tusiitambue kwa sababu kuna mambo mengine tunaweza tusiyaone Waziri Mkuu na Ofisi yake wanafanya kazi nzito sana katika kusaidia uwekezaji kwenye Taifa hili.(Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba nilipe Bunge lako Tukufu taarifa, Rais jana alipokuwa anatoa takwimu watu wanakwenda kwenye benki wanakopa hela kubwa sana za kuwekeza, wanakimbilia mahakamani. Natoa mfano mdogo sanasana, nenda kachukue takwimu za iliyokuwa Bank M take statisticsangalia list ya watu waliokwenda kuchota bilioni za shilingi za Watanzania mle halafu uwekezaji fedha zimetoroshwa sijui Canada, sijui Kenya na mpaka leo ninavyokwambia its true Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya kazi kubwa sana angalau kuna bilioni 200 zimeokolewa kupitia Bank ya Azania.
Mheshimiwa Spika, hili nalisema kwa uchungu kwa sababu hapa Bungeni tunayo Kamati inayoshughulikia Uwekezaji na Mitaji, sina maana waanze kufukua makaburi kujua nani kakopa, lakini ukiangalia kwenye list ya waliokopa, mbaya zaidi hukuti mtu wa ngozi ya namna yangu,I am very sorry to say this, tunaweza tukapigiana kelele na Wabunge hapa vimikopo tunachukua vidogo vidogo kwenye taasisi za fedha, nataka niseme with confidence na with evidence,Taifa hili bado linapigwa sana. Wizi wa rasilimali za nchi bado haujakoma kwenye nchi hii, lazima kama Bunge tudhamirie kwa dhati kusaidia vision ya nchi, Rais atiwe moyo na Bunge sisi.
Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kukushukuru sana wewe binafsi kwa kunipatia nafasi kuwa msemaji wa mwisho, kwenye hoja iliyoko mbele yetu. Jambo la kwanza ambalo nataka nilizungumze kuna dhambi moja kubwa sana watu wanaifanya kwa sababu tu wanajua kwamba Rais Magufuli amekufa na hawezi kujitetea. Gwajima katika mahubiri yake niliyoyasikia aliyoyatoa kule Kanisani, amesikika akisema toka Rais Magufuli afe mambo yamekuwa yakienda ndivyo sivyo akiwa ananukuu jambo la chanjo ya Corona.
Mheshimiwa Spika, baba wa watu Rais Magufuli amefanyakazi yake ametimiza muda wake Mungu amemruhusu apumzike. Ametenda haki na mema mengi kwenye Taifa hili, Hayati Magufuli aachwe apumzike asihusishwe na mambo ya hovyo. Rais Magufuli alipokuwa madarakani alichokishauri alilishauri Taifa tusiwe na haraka ya kukimbilia chanjo lakini hakuzuia Taifa likijiridhisha lisichukue chanjo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hii imekuwa ikitumika kama kichaka, Magufuli, Magufuli, Magufuli, Magufuli muacheni Rais Magufuli apumzike na ninasema huko aliko, kaka yangu Askofu Gwajima anisikilize kwa sababu kama mdogo wangu Ditopile alivyosema, sio mnafiki. Nilimfuata Gwajima kwenye simu yake ya kiganjani nikamuambia haya unayoyafanya ninakushauri unyamaze hayana maslahi na Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nayasema haya kwa sababu, Askofu Gwajima anasema ana Kanisa na anatumikia watu wa Mungu. Neno la Mungu katika Warumi 13:1 linasema: Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Na ndio maana kwa watumishi wa Mungu wanaomjua Mungu vizuri, Yesu wakati anazaliwa utawala wa Herode palikuwa pana sensa inaendelea Jerusalemu. Yusufu na Mariamu wakiwa ni wasomi wazuri wa Biblia wale watu wakiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu wali-comply na agizo la Herode la Serikali tena wakati huo, Jerusalemu iko chini ya utawala wa Rumi wakaondoka kwenda kuhesabiwa kwa kutii mamlaka ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, na wakati huo nayasema hayo kitabu cha Mathayo 2:1 kinaonyesha namna Yesu alivyofanya msafara kwenda kutii agizo la mamlaka tena chini ya utawala ambao tunaweza tukasema kwamba walikuwa chini ya ukoloni. Lakini kama hiyo haitoshi Luka 12:7- 9 neno la Mungu linasema, Mungu huyu anajua idadi mpaka ya nywele zilizoko katika kichwa chako. Sasa kama Mungu anajua idadi ya nywele kwa nini Mariamu hajasema kwamba Herode anatuita kwenda kuhesabiwa, Mungu anajua idadi ya nywele wagomee mamlaka ya wakati huo. Hiki anachokifanya Gwajima ni kiburi kilichojaa, kuvimba na kulewa sifa za dunia na sio sifa za kumuwakilisha Mungu katika madhabahu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninayasema haya kwa sababu, Askofu Gwajima ametoa tuhuma nzito sana kwa nchi na nafikiri haya mambo nimejiuliza maswali. Hivi ni kweli Jeshi la Polisi hawaoni criminality iliyopo kwa statement za Gwajima? Hivi kweli Jeshi letu la Polisi halioni hatari ya kauli za Gwajima kwamba zinaweza zikasababisha hata Serikali ikapinduliwa kwamba Rais ameamua kuuza watu wake? Nimejiuliza maswali nimekosa majibu!
Mheshimiwa Spika, jambo ninalotaka kulisema Askofu Gwajima yuko hapa jirani na ninajua watu watampelekea clip na zimfikie kwa sababu tabia ya unafiki msabato mimi sijawahi kufundishwa, nimefundishwa kuita nyeusi nyeusi kuita nyekundu nyekundu. Kitendo alichokifanya Askofu Gwajima jambo la kwanza, kwa mujibu wa uchambuzi wangu Askofu Gwajima alidhamiria kuichonganisha Serikali ya Mama Samia Suluhu na wananchi ili watu waache kuwa na imani na Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kitendo cha Askofu Gwajima kujitokeza hadharani na kuwaambia watanzania kwamba chanjo hii mnayokwenda kuchanjwa haijafanyiwa utafiti, chanjo hii mkiitumia italeta madhara hilo jambo ni it is a very big if not huge is subordination kwa mamlaka za nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema naungana na Mariamu Ditopile, adhabu zitakazotolewa kwa Askofu Gwajima kwa hili, zisiishie hapo hata huyu Halima Mdee aliyekuwa Mbunge wa Kawe hajawahi kutufanyia vitimbi vya namna hii anavyovifanya Askofu Gwajima. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hili jambo nataka niseme kwa dhati kabisa limetufedhehesha na mimi nilikuwa nashangaa sana kwa nini chama changu mpaka leo wamekaa kimya hawajachukua hatua? Mwanachama anafikia stage ya kufanya haya mambo mazito mpaka Spika unaamua kumuita, Chama cha Mapinduzi kile tunachokijua. What is wrong with my party? Kuna shida gani? Jambo hili ni kutaka kukwamisha mipango. Hivi nilikuwa najiuliza amesema Kilumbe Ng’enda Rais Dkt. Magufuli kama Mungu angekuwa hai mpaka leo, Gwajima angeweza kufungua mdomo wake na kuleta hizi chokochoko? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakuambia Wabunge tuko hapa kama kuna Mbunge anafikiri ya kwamba atatumia forum kwa sababu tu hakupendezwa na Rais Samia kuwa madarakani walahi nakuambia tuta-deal naye. Sisi tuta-deal naye. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka nikuambie kama kuna mtu alikuwa anategemea kupata mamlaka Serikalini imetokea bahati mbaya wote hatuwezi kuwa Mawaziri walioko Mawaziri ukaanza kuwachokonoa walahi nakuambia tuta- deal na wewe. Ninasema ikitokea mmoja wetu anataka kujenga umaarufu binafsi badala ya umaarufu wa Taasisi na kulinda mifumo ya Taifa letu, kabla hawajaja kwako tutatwangana makonde huko, tuweke heshima. (Kicheko/ Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kusema pamoja na kwamba naunga mkono maazimio yote ya Bunge, nimemshauri rafiki yangu Mheshimiwa Jerry Silaa kwa dhati ya moyo wangu ninalisema moja ya marafiki zangu wa karibu sana Mheshimiwa Jerry Silaa. Na hata tukio lilipotokea nilimuandikia ujumbe anajua, zaidi ya mara tatu na ninalisema from the bottom of my heart tusiposimama kushauriana kwa lengo la kuelekezana sisi bado vijana nina imani Mheshimiwa Jerry atakutafuta, nina imani atakutafuta kwa wakati wake.
Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba amechelewa chelewa nina imani atakuja, akija baada ya haya wewe mpokee kama baba akiomba radhi mpokee. Kwa sababu, ninajua wakati mwingine kuna mambo yanatokea hapa mtu unashindwa kuelewa huyu ni huyu ninayemjua? Unajiuliza maswali. Lakini baada ya kusema hayo binafsi nikushukuru sana na nikupongeze sana kwa namna ambavyo umesimama kulinda heshima ya Mhimili huu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukiacha Mhimili huu udharauliwe hata huko nje heshima yetu sisi Wabunge haitaonekana. Baada ya kusema maneno haya ninataka nimtie moyo Rais wetu aliyeko madarakani asije akadanganywa na mtu. Hatuwezi wote kuwa Mawaziri, Mawaziri walioko tuwaheshimu tuwaunge mkono. Hatuwezi wote kuwa Mawaziri ikitokea hatujapata nafasi tusiwe chanzo cha kuanza kulidhalilisha Baraza la Mawaziri la kumdhalilisha Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakuambia Rais Samia Suluhu Hassan, Mheshimiwa Spika, nguvu yake kwa umma ni kubwa wananchi wanampenda haijawahi kutokea katika historia ya Taifa, fedha zinapelekwa kwa wananchi kwa kiwango hiki anachofanya Rais Samia Suluhu Hassan. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninaomba jambo moja Mungu aendelee kulibariki Taifa letu, Mungu aendelee kuulinda umoja na mshikamano wa Taifa letu. Mungu amlinde Rais wetu na Mihimili yake yote mitatu ukiwemo wewe Spika. Wasalaam aleykum. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja na kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Nishati
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu kwenye Wizara hii ya Nishati.
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, tunasema kwamba tunapaswa kutambua na kuthamini kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa miaka mitano nyuma katika suala la nishati na umeme.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi na kwa kweli katika hili mimi nitajikita zaidi katika kutoa complement na kuongelea maeneo mawili, matatu ya kitaifa, lakini pale ambapo tunaona Wizara zinafanya vizuri na kuleta mapinduzi chanya yanayobadilisha uchumi wa Taifa sisi kama Wabunge tuna nafasi ya kutoa complement ili Taifa lijue nini kimefanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kwa dhati ya moyo wangu uzalendo ulionyeshwa na Waziri Kalemani, mimi kwa hili naomba niwe wazi. Nasema kwa dhati kabisa unyenyekevu wa Waziri Kalemani kwa kiasi kikubwa sana umefanikisha mapinduzi makubwa katika sekta ya kusambamba umeme nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nasema hili kuweka rekodi katika Bunge lako Tukufu. Waziri huyu ukimpigia simu saa sita ya usiku lazima akupokelee na Waziri huyu ukimtumia ujumbe lazima akujibu. Kwetu sisi Wabunge kama kuna jambo linatupa faraja ni kuona namna tunahitaji kufanya mawasiliano na Mawaziri na wanakuwa wepesi katika kuitika. Kwa dhati ya moyo wangu, naomba nitumie Bunge lako kumpongeza sana Waziri Mheshimiwa Kalemani hili ameweza kulishinda. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini nampongeza tena Waziri huyu Mheshimiwa Kalemani, juzi tuliona sintofahamu ikitokea katika Shirika letu la Umeme la TANESCO, LUKU zikaleta matatizo. Mimi kwa upande wangu nilihisi ni some sort ya sabotage kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi lakini nampongeza sana Waziri alichukua hatua za haraka za kuwasimamisha kazi watumishi wa TANESCO na Waziri Mkuu akaliunga hilo mkono kwa kuruhusu uchunguzi zaidi ufanyike, hilo tunawapongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani, Rais wa Awamu ya Sita kwa muda mfupi na kwa haraka ameshasaini mkataba wa zaidi ya shilingi bilioni 300 kwa ajili ya kuzalisha umeme mwingine kule Kigoma. Naipongeza sana Wizara na Serikali ya Awamu ya Sita kwa sababu changamoto zinazozungumzwa kwa watu wa Katavi ni wazi umeme utakaozalishwa sasa katika Mkoa wa Kigoma utaingizwa kwenye Gridi ya Taifa na utahudumia mikoa ambayo ilikuwa haipati umeme wa Gridi ya Taifa, kwa hilo pia tunawapongeza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kubwa natoa pongezi kwa sababu wananchi wa Jimbo la Singida Magharibi wamepata faraja. Waziri alipotoa namba za wakandarasi waliowapa kazi mimi nimepigiwa simu na mkandarasi anaitwa Central, nimepewa uhakika tutaanza kusambaziwa umeme katika vijiji vyote 34 kuanzia mwezi huu. Mheshimiwa Waziri tunakushukuru na tunakupongeza sana wewe na Serikali na tufikishie salamu hizi kwa Mheshimiwa Rais maana huenda tulidhani kwamba vijiji 2,000 vilivyoahidiwa na Serikali ya Serikali ya CCM kwenye uchaguzi uliopita vinaweza vikasuasua. Peleka pongezi kwa mama yetu Mheshimiwa Samia Suluhu ametutendea haki Wabunge wa Chama cha Mapinduzi na wapiga kura wote kwa kuyaenzi na kuyashikilia yale mapambano yaliyoanzishwa na Hayati Dkt. John Joseph Pombe Magufuli katika suala zima la kusambaza umeme kwa wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nina taarifa Vijiji vyangu vya Mwaru, Mduguyu, Mlandala, Kaugeri, Mpungizi, Irisya, Munyu, Mwasutianga, Mtunduru, Kintandaa, Maswea, Jerumani na vingine vingi siwezi kuvitaja vinakwenda kuanza kuunganishiwa na umeme. Hapa mimi nasema, Mungu akinipa uzima mwaka 2025 nachukua, ninaweka waaa, kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Spika, nimalize kwa kuiomba Wizara, Singida tuna mradi mkubwa wa kutengeneza umeme kwa kutumia upepo. Mradi huu umezungumzwa kwa muda mrefu, kaka yangu Mheshimiwa Kalemani unajua watu wa Singida tunakupenda pamoja na Naibu wako mdogo wangu Mheshimiwa Byabato, mdogo katika umri lakini kiongozi wangu kwa maana ni Naibu Waziri, nawaomba kabisa kwa niaba ya watu wa Singida…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Elibariki Kingu.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, oooh, naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii na Kamati ya Kudumu Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu shughuli za Kamati hizo kwa Mwaka 2021
MHE. ELIBARKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nami niungane na Wabunge wenzangu kukupongeza wewe binafsi kwa nafasi ambayo Wabunge tumekuchagua kwa kishindo. Hongera sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Taifa hili la Tanzania bado nina imani kwa dhati ya moyo wangu kwamba mambo mema na ya msingi ambayo Taifa letu yameyarithi toka kuanzia zama za Waasisi wa Taifa letu, it is my trust kwamba kizazi hiki cha leo kikiamua kwa dhati na kwa dhamira ya kuangalia maslahi ya nchi mbele na maslahi ya vizazi vinavyokuja, tuna uwezo kabisa wa kulilinda Taifa hili tukafanya maamuzi Taifa hili likabaki moja, Taifa hili likabaki kuwa la mshikamano, Taifa hili likaendelea kuwa la upendo na likadumisha tunu za umoja na mshikamano ambazo ndizo zimekuwa asili ya Taifa hili ambalo limekuwa likipigiwa chepuo kwa mifano duniani bila kuleta migogoro. Tumekuwa na sifa hiyo ya Watanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Watanzania tumekuwa na sifa ya kutatua matatizo yetu wenyewe na kuliacha Taifa likiwa moja na likiwa na mshikamano. Naomba niseme maneno mafupi yafuatayo: -
Mheshimiwa Spika, demographic projection ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa miaka 35 inayokuja, naiona Ngorongoro ya miaka 35 inayokuja ikiwa na population ya zaidi ya watu 800,000 mpaka 900,000. Naiona Ngorongoro ya miaka 40 inayokuja ikiwa na viwanda ndani ya hifadhi, naiona Ngorongoro inayokuja ikiwa na mitambo ya mashine kwa ajili ya ku-cater for population ambayo itakuwa pale.
Mheshimiwa Spika na ndugu zangu Wabunge, naomba nizungumze haya kwa dhati ya moyo wangu, nikitanguliza maslahi ya Taifa langu mbele na kuweka ubinafsi wangu nyuma. Nataka niwaambie Watanzania, na naomba Bunge linisikilize kwa makini. Haya mambo tunayozungumza habari ya heritage ya dunia kwa Ngorongoro hatuzungumzii tu heritage ya dunia kwa sababu inaleta revenue zinazolisaidia Taifa letu, lakini tunazungumzia misingi ya historia ambayo Taifa hili Mungu amelipatia tuvirithishe vizazi vya wajukuu zetu na wajukuu wa wajukuu zetu kwa nature ya utajiri ambao Mungu amelipatia Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nayasema hayo kwa sababu na nitakuwa mtu wa hovyo sana kama nitatanguliza mambo ya ukabila kuzungumza sijui Umasai, kwangu mimi hoja siyo Mmasai aliyeko Ngorongoro, kwa sababu wale ni Watanzania, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hoja ninayoizungumza; je, Taifa hili la kizazi cha sasa hivi tuko tayari kuona heritage ambayo Mungu ametupatia kama nchi ikipotea bila kufanya maamuzi? Hiyo ndiyo hoja ya msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tukienda kwenye hoja hiyo ya msingi wote kwa pamoja tutarudi kama Taifa, tutatengeneza resolutions za kwenda ku-approach lile eneo. Nataka nikuhakikishie jambo hili litamalizika kwa amani na utulivu na maslahi ya Taifa hili yatakuwa yamelindwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ndugu zangu, nataka niwaambie kitu kimoja; ukiachilia mbali habari ya mifugo tunayoizungumza, lakini kuna taarifa ambazo kama siku moja ukiniruhusu nitazileta mezani kwako kama ushahidi. Kuna taarifa ambazo zinaonesha, sitaji kwa jina, mataifa ya jirani kuna hujuma kubwa inafanyika katika Hifadhi ya Ngorongoro. Kuna idadi ya wanyama wengi wanaletwa na mataifa jirani na lengo lake ni vita vya kitalii kupambana kati ya Mataifa ya East Africa. Sisi kizazi cha leo we are not ready kuona Ngorongoro inatufia katika mikono yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nayasema haya kwa uchungu mkubwa kwa sababu haya yanayofanyika kule ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ukiachilia mbali modernization ya housing ambayo inaendelea kule ndani, lakini ninachotaka kusema ni kwamba population ya watu kutoka mwaka 1959, watu 8,000 na kwa kweli huwezi kuzuia watu walikuwepo mle kwa mujibu wa sheria, lakini tujiulize swali; sheria ile iliundwa wakati ule ilikuwa imelenga nini kwa wakati ule? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama sheria tulikuwa tumeiunda sisi wakati ule Bunge hili ndicho chombo peke yake cha Kitaifa chenye mamlaka ya Kikatiba ya kubadili sheria na kutunga sheria zinazolinda maslahi ya nchi na kulinda maslahi ya vizazi vinavyokuja katika Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, ombi langu kwa Serikali na nataka niliseme hili kwa dhati kabisa kwa Serikali; mzigo huu tusiutupe kwa ile jamii ya watu walioko pale Ngorongoro peke yao. Serikali kwa upande mwingine kuna mahali ilikosea, kwa sababu haiwezekani nyumba za ghorofa zinajengwa Ngorongoro inaangalia, modern houses zinajengwa inaangalia, watu walitakiwa kuchukua hatua mapema. Hivi ninavyozungumza naona kabisa yaani kama vile maamuzi haya tulikuwa tuyafanye jana na siyo leo kwa maslahi ya kulinda ile Hifadhi ya Ngorongoro. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali ya chama changu chini ya Rais wetu shupavu, mama Samia Suluhu Hassan, juzi Rais amefanya royal tour tumeona impact ya ongezeko kubwa la watalii katika Taifa letu. Tumeona impact kubwa ya ongezeko la mapato katika Taifa kutokana na royal tour. Ombi langu, Serikali ifanye engagement ya Kimungu kwa hawa watu walioko katika hifadhi. Imani yangu ni kwamba engagement ya kuzungumza na wafugaji hawa ikifanyika kwa ustaarabu Watanzania ni Taifa la watu wasikivu, tutamaliza mgogoro ule bila kuleta vurugu ambazo dunia inaweza ikatucheka kesho. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa yale yanayoendelea katika Hifadhi ya Ngorongoro nitakuwa Mbunge ambaye nimeweka rekodi mbaya kwa Taifa langu nikisema Serikali msichukue hatua ya kulinda ile hifadhi. Hatua hii ya kulinda hifadhi inatakiwa ifanyike haraka na kwa maslahi mapana ya Taifa, lakini wakati huohuo tulinde mambo yote yanayohusiana na humanity kuhakikisha kwamba watu hawa wanatafutiwa mahali ambapo watakuwa comfortable na shughuli zao za ufugaji, watakuwa comfortable na shughuli zao nyingine za kiuchumi. Lengo ni kuhakikisha kwamba Taifa hili linabaki kuwa moja.
Mheshimiwa Spika, hizo statistics alizokuwa nazisema Mheshimiwa Salome Makamba, mimi nimekwenda mbali, hizo statistics nina orodha kama utaniruhusu naweza siku moja nikakuletea kwenye meza, ya baadhi ya watu ambao ni wafanyabiashara wa mifugo, wamewatumia watu ndani ya hifadhi na kuweka mifugo ndani ya hifadhi na ndiyo hao wamekuwa wakipaza sauti kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wewe jiulize kama statistics za Serikali zinaonesha ufukara ni asilimia 50, inakuwaje watu wawe na mifugo zaidi ya 800,000 au 900,000 wasemekane ni maskini? Hayo ni maswali ya kujiuliza kama nchi.
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu wetu yuko hapa.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa unyenyekevu mkubwa, naunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Kuhusu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutofuata Maelekezo ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwa mtazamo wangu tunapokutana na changamoto, kwanza nianze na kukushukuru. Kuna kauli umeitoa hapo kabla, binafsi nimeona ni kauli ya kiuongozi. Jambo hili tusipolisema hapa ndani ya Bunge tunaweza tukajenga taswira kwamba Serikali hii ya Awamu ya Sita imeingia madarakani, kuna matatizo makubwa, wanafunzi hawapati mikopo, Serikali haitoi fedha, ndiyo notion ambayo imejengeka huko nje. Sasa nataka tuweke mambo vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Samia toka ameingia madarakani, ameongeza fedha za mikopo ya Elimu ya Juu kutoka Shilingi bilioni 464 mpaka Shilingi bilioni 570, ambalo ni ongezeko la Shilingi bilioni 100 na kitu kwa wanafunzi wa elimu ya juu. Hilo nataka tuliweke sawasawa. Kwa sababu ilivyozungumzwa itaonekana kwamba, sasa yaani bodi pamekuwa panayumba, kuna myumbo. Namna hii tukifanya tutakuwa hatumtendei haki Mheshimiwa Rais aliyeko madarakani, tutakuwa hatutendei haki Serikali kwa juhudi wanazozifanya kuhakikisha watoto wetu wanapewa mikopo. Hilo lazima tuliweke vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kiti chako kimetoa maelekezo kwamba tunavyozungumza it is like kwamba hakuna kitu kinafanyika kwenye bodi, jambo ambalo nimeshukuru sana umetoa hayo maelekezo na huo ndiyo msimamo wangu. Kwa sababu takwimu zinaonesha, Mama Samia toka ameingia madarakani, Rais wetu amefanya deliberate decision ya kuongeza fedha kuwasaidia watoto wa Kitanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama kuna changamoto zimejitokeza za kiutendaji, hatuwezi kufumbiana macho hapa. Mimi sifungwi mdomo na mtu, kama kuna changamoto naiona for the interest ya nchi nitasimama hapa kusema ukweli bila kufungwa mdomo na mtu; na ndiyo kazi ya Mbunge na ndiyo jukumu la Kibunge. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumesikia ripoti hapa, naomba niseme kwa unyenyekevu mkubwa sana. Hii ripoti iliyosomwa hapa na Mwenyekiti wa Kamati, siyo ripoti ya Kamati, hii ni ripoti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa sababu Kamati imepewa majukumu kama wanafanya kwa niaba ya Bunge.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Yahaya Massare.
T A A R I F A
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mdogo wangu Mheshimiwa Elibariki Kingu. Tunachokizungumza hapa ni kwa maslahi mapana ya wananchi wetu, na mjadala huu unalenga amri yako ambayo uliitoa kwa Serikali. Uliiambia Serikali kuwa watoto wote waende vyuoni wakati tunaandaa taratibu namna gani watapatiwa mikopo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa tujadili namna ya kuwasaidia watoto wa masikini, wa wakulima na wafanyakazi wa nchi hii. Mheshimiwa Rais alishatoa fedha. Sasa kama changamoto ni utekelezaji, ndiyo tulizungumze hilo. Nani kakosea; nani kafanya nini; lakini dhamira yetu ituweke wapi? Tuna nia ya kuwasaidia, Mheshimiwa Rais upande wake kashamaliza, sisi kama Bunge tulishatoa na wewe kama Mkuu wa Mhimili huu ulishatoa maelekezo kwamba wanafunzi hawa waende vyuoni.
Mheshimiwa Spika, ili kumaliza changamoto hii, watoto walioko vyuoni hawajalipwa tuition fees, zinatoka wapi? Matarajio yao ni hii Bodi ya Mikopo na Wizara ya Elimu. Ndiyo tujadili hao watu ili namna gani waende kama timu moja. Watoke huku na kule; nani ni nani; na nani ni nani; na afanye nini; kwa kipindi hiki? Tuisaidie nchi hii, tusaidie watu wetu na tusaidie watoto wa wananchi masikini ambao wazazi wao nao wenyewe walipiga kura kwa ajili yetu na tumo ndani ya nyumba hii.
Mheshimiwa Spika, naomba nimpe taarifa mdogo wangu. (Makofi/Kicheko)
SPIKA: Mheshimiwa Elibariki Kingu, malizia mchango wako.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, wewe ni kiongozi mstahimilivu na mvumilivu sana. Ahsante. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilichokuwa nakisema, taarifa hii iliyoletwa katika Bunge lako ni Taarifa ya Bunge kwa sababu Kamati imekasimiwa madaraka na Bunge lako. Hoja yangu ya msingi, hivi kweli Bunge hili lije kuanza kufanya kazi ya kumfundisha Waziri namna ya kufanya communication na watu wake wa Wizarani? it is impossible. Unajua tusichukulie mambo haya kimzaha mzaha, at the end of day tunaharibu hali ya hewa ya siasa nje, tunaona kwamba ni mambo ya kawaida. Bunge hili lianze kumfundisha Waziri namna ya kuwasiliana na watu wa Bodi ya Mikopo? Bunge lianze kumfundisha Waziri umeipa kazi Tume uliyoiunda wewe…
T A A R I F A
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, terms of reference zinatengezwa na mtu mwingine, aliyempa kazi bodi nani ametengeneza terms of reference? Tunaambiwa hapa kwenye ripoti, kama tumeamua kufunika kombe mwanaharamu apite tulifunike, lakini ukweli utabaki Waziri na timu yake wapange mawasiliano vizuri na Wizara, hatutaki kuharibiwa hali ya hewa ya siasa nje. Ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na mimi leo nina maeneo matatu ya kuchangia kwa ajili ya kuishauri Serikali yangu katika masuala mazima ya biashara na uchumi wa nchi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nimesoma research iliyofanywa na Price Waters Cooper kwa projection ya uchumi na biashara ya dunia kwa miaka 27 inayokuja. Ripoti inaonesha the imaging seven economies ambazo zinajumuisha mataifa ya Indonesia, Uturuki, China, Brazil, Mexico na mataifa mengine. Utafiti huu unaonesha kwamba baada ya miaka 27 kufika mwaka 2050 mataifa kama Indonesia yanakwenda kuwa moja ya mataifa yanayokuza chumi zao sana kutokana na biashara na uwekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nalisema hili kwa sababu sisi Tanzania we cannot be jack of all trade, kama nchi alikuwa anazungumza mdogo wangu Mheshimiwa Ezra na Mbunge mwenzangu hapo nimemsikia kwa makini sana. Sisi kama nchi lazima tuwe na vipaumbele vichache ambavyo vitaweza kulifanya Taifa letu liweze kuwa na mambo ya msingi ya kujivunia katika biashara ya dunia. (Makofi)
Leo tunapozungumza habari ya nchi iko katika shortage ya mafuta, hivi ni kweli watanzania mnataka kuniambia sisi Tanzania tumeshindwa kabisa kuwa na uwezo wa kuwa na sufficient ya mafuta katika Taifa letu, mafuta ya kula? hili jambo mimi nimelizungumza Bunge lililopita nilizungumza alikuwa anazungumza Mheshimiwa Ezra. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, uzalishaji wa mafuta kweli tumeshindwa kuwa na mikakati ya kuwa na mashamba na hili mimi nalizungumza Wizara ya Biashara najua mnafanyakazi nzuri na kuna recommendation zenu nitawapa. Wizara ya Kilimo iko na Waziri makini najua it’s doing the best ila ninachotaka kusema ni kwamba hivi ni kweli Tanzania leo sisi ni wa kulia tuna shortage ya mafuta ya kula? With all arable land ambayo Mungu ametupatia kama nchi tunalia habari ya mafuta ya kula. Can we give excuse ya habari ya war in Ukraine for habari ya mafuta ya kula kwa wananchi wetu?
Mheshimiwa Naibu Spika, shida moja tuliyonayo ni kwamba we plan a lot, hatuchukui maamuzi serious ya kufanya maamuzi ya kuleta mageuzi katika Taifa letu. Huu mfano alikuwa anauzungumza Mheshimiwa Ezra Serikali tukiamua kwa kupata wawekezaji tukawa na mashamba peke yake ya mashamba ya alizeti ya mfano maelfu ya heka, mimi ninawaambieni hili Taifa hatuhitaji kuagiza mafuta hapa haturuhusu tu kuwapa deal wafanyabiashara lakini we are killing the economy of the country na biashara kwenye nchi haiwezi kwenda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi natoa ushauri Serikali Wizara ya Kilimo kaka yangu Bashe you are very smart Waziri wangu. Waziri wa Biashara mwalimu wangu umenifundisha Mzumbe University fanyeni coordination tuhakikishe na tuweke mipango ndani ya kipindi cha miaka kumi hili Taifa liondokane na habari ya utegemezi wa kuagiza mafuta. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo lingine ambalo linatu-cost pia sasa tunavyozungumza haya mambo mipango lakini hata ukiangalia Tume ya Mipango yenyewe tumeiua. Tume ya Mipango tumeiua hatuna Tume ya Mipango, all these great things tunazozizungumza hatuna Tume ya Mipango. (Makofi)
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa taarifa.
NAIBU SPIKA: Taarifa.
T A A R I F A
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa taarifa ndugu yangu Kingu kwamba Serikali imechukua hatua na kufuatia ushauri uliotolewa na Wabunge katika Bunge la bajeti lililopita, Serikali imegawa mbegu katika mikoa mikuu mitatu ya alizeti ikiwemo Mkoa wa Singida na mwaka huu peke yake mkoani Singida tumegawa jumla ya tani 1,039 na Mkoa wa Singida baada ya crop survey itatuzalishia jumla ya tani 365,000 za ziada za alizeti zitakazotupatia lita 115,000 za mafuta katika uzalishaji wetu na mwaka ujao wa fedha tutagawa tani 5,000 kwa nchi nzima. (Makofi)
Kwa hiyo, siyo kwamba Serikali haijachukua hatua Serikali inachukua hatua na hii ni budgetary na tumeshaanza kufanyia kazi. (Makofi)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Kingu taarifa unaipokea?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa taarifa ya Mheshimiwa Bashe, kwa kweli sina mashaka na utendaji wa Waziri Bashe, lakini tungependa kuona sasa kwenye market haya anayoyazungumza Mheshimiwa Bashe tuone uzalishaji unapatikana. Kwa sababu sasa hivi scarcity ya mafuta ninyi mnajua wote mnajua nchi iko kwenye scarcity kubwa ya mafuta, lakini kwa sababu ni hatua zinaendelea it’s well and good ndiyo tunahitaji vitu vya namna hiyo vitokee. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo la pili ambalo nilikuwa nataka kulizungumza tulikuwa tuna mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo, mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mimi nimesoma ripoti ya utendaji kazi wa Bandari ya Salala iliyoko huko Mashariki ya Kati. Ujenzi wa mradi wa Bagamoyo sisi si tumezubaa sasa hivi tumekuwa tunazungumza, lakini nakwambia tukiacha kutekeleza ujenzi wa mradi wa Bagamoyo in next ten years mtaona wenzetu Mombasa ama Msumbiji wame-peak na sisi Tanzania tutabaki kuwa observer. Tukiweza kutekeleza mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo sasa hivi tunazungumza habari za usafirishaji kwenye bahari zimekuwa kubwa, tukiweza kujenga mradi ule wa Bandari ya Bagamoyo, tutaweza kuleta meli kubwa za fifth generation ambazo zitaweza kuifanya Tanzania kuwa hub ya kuchukua mizigo na kuipeleka kwenye nchi za interior ambazo ziko land locked na hiyo itafungua biashara katika nchi.
Sasa shida kubwa ni kwamba tunapozungumza mambo kama haya tunayachukulia taratibu taratibu lakini lazima twende kwa speed ambayo dunia inatutaka kwenda kwa speed kwa lengo la kuwasaidia watanzania katika masuala mazima ya biashara. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini jambo lingine ambalo nilikuwa nataka kulizungumza niipongeze sana Wizara, Wizara niwapongezeni sana...
(Hapa kengele ililia kushiria kwisha muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante, kengele ya pili hiyo. Lakini sasa upate ulifanya nini? Hebu rudia ulifanya haya sekunde mbili. (Kicheko)
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, niitumie nafasi hii kuipongeza sana Wizara na kwenye hili kwa kweli niwapongeze kwa mara ya kwanza nimeona mikataba iliyokuwa yamesainiwa Dubai, nimeona utekelezaji wa ujenzi wa viwanda 200 Kwala ukiendelea kwa macho yangu nimeenda kutembelea, nitoe pongezi sana kwa Katibu Mkuu wa Wizara na Waziri Mwalimu wangu Profesa Kahyarara ni mtu wa matokeo alipokuwa NSSF alisimamia ujenzi wa viwanda vya Bodi ya Nafaka vimetokea na sasa naona ujenzi wa viwanda 200 unaendelea hayo ndiyo mambo tunayoyataka kwa hili Serikali nawapongeza. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa nawashukuru Wizara ya Elimu chini ya Profesa Mkenda, kaka yangu, nawapongeza sana kwa juhudi kubwa mnazofanya kuhangaika katika kuhakikisha kwamba mnainua elimu ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukifuatilia michango ya Wabunge wote waliozungumza kuanzia asubuhi mpaka sasa hivi tunaelekea mchangiaji karibu wa kumi na kitu, utaona namna gani Wabunge wengi wamezungumzia changamoto ambayo haioneshi consistence katika mfumo wetu mzima wa elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Watanzania tunajua uwezo wa Mheshimiwa Prof. Mkenda na Naibu wako. Nchi inatambua ya kwamba yeye ni msomi, mzalendo aliyesomeshwa kwa kodi za Watanzania, ana uwezo mkubwa, ni zao la watoto wa kizalendo wa nchi hii. Tumaini la Watanzania ni kuona nchi inapata transformation kwa lengo la kusaidia sustainable development katika masuala mazima ya elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria Na. 25 ya mwaka 1978 imempa mamlaka Waziri wa Elimu kuunda chombo cha kisheria; Baraza la Ushauri katika masuala ya elimu katika nchi yetu. Ndugu zangu Watanzania na Wabunge wenzangu, nataka niwaambie with a very big disappointment; toka sheria hii imeundwa, hapa tunazungumza alikuja Waziri fulani akafuta hiki; akaja fulani, akafuta hiki; huyu anazungumza habari za mitaala; hivi leo tukiuliza, toka Sheria ya mwaka 1978, ni mwaka gani Serikali yetu tumetekeleza kuunda chombo chenye watalaam wazalendo wanaoona direction na vision ya nchi wakamshauri Waziri juu ya mwelekezo na mustakabali wa nchi katika elimu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri, kaka yangu, Mheshimiwa Profesa Mkenda, tunakuomba ukawe shujaa wa kwanza Waziri katika Taifa letu utakayekwenda kutekeleza takwa hili la kisheria Na. 25 ya mwaka 1978. Nenda kaunde chombo cha kisheria, Baraza litakalokuwa linakushauri katika masuala mazima ya elimu. Hizi kelele unazozisikia kwa Wabunge, hautazisikia mpaka siku Yesu anarudi. Ni kweli watu wamekuwa wakijichukulia hatua na kufanya maamuzi bila ku-reflect demand na nini dunia inakihitaji hasa Taifa letu katika dunia tunayokwenda ya globalization. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ni matumaini yangu Mheshimiwa Prof. Mkenda ninamshauri kama mdogo wako na kama Mbunge mwenzio, sheria imekupa mamlaka, tukimaliza ikiwezekana hata kesho teua watu watangaze tupate chombo cha kuanza kukushauri katika masuala mazima ya elimu. Hizi kelele za Wabunge hautazikisikia na utaona changamoto nyingi zinazozungumzwa kuhusu elimu yetu na mitaala, tutakwenda ku-harmonize na kulisaidia hili Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu wa pili; asilimia 25 ya sekondari katika Taifa letu zinatokana na private investmate kwa maana shule za private. Leo tunapozungumza, kaka yangu Mheshimiwa Innocent, Waziri wa TAMISEMI, nampongeza kwa huruma yake kubwa sana, juzi akaamua kuongeza nafasi ya watu kufanya application zilizotangazwa katika Serikali. Naomba Bunge lako linisikilize kwa makini; kama private sector inafanya asilimia 25 ya shule, Mheshimiwa Innocent juzi ametutangazia nafasi takribani 10,000. Kwa taarifa nilizonazo mpaka sasa hivi, waliyoomba ni zaidi ya waombaji kama 120,000 kwa nafasi 10,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu kwa Serikali, Profesa Mkenda kaka yangu mnisikilize. Tukitaka kusaidia changamoto ya upatatikanaji wa walimu kupata ajira na walimu wa masomo ya sayansi kuongezeka lazima private sector ipewe nguvu, na kwamba shule za private lazima zipewe nguvu. Leo tunapozungumza shule za private tumeziwekea mpaka cooperate taxi, jamani elimu hii ni huduma! Tukiweza kupunguza kodi kwenye shule za private mimi nakwambia tutasaidia Watanzania wengi kufungua shule, walimu wetu wanaokosa ajira wataajiriwa kwenye private. Tutasaidia kutatua changamoto kwenye Sekta ya Elimu na kaka yangu Mwigulu Madelu na ninaju upo hapa, ninajua hiyo kodi utakwenda kusaidia kuzifuta kwa lengo la kusaidia Private Sector Investment katika Sekta nzima ya elimu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu wa tatu. Serikali inachukua mikopo mingi, na ninampongeza sana Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan. Uwekezaji unaofanywa katika miundombinu ya elimu ni uwekezaji unaotia moyo sana. Rais wetu asivunjwe moyo aungwe mkono na apongezwe. Uwekezaji unaofanyika ni wa hali ya juu. Hata hivyo, ninaomba nikosoe na kushauri. Tuna programu za EP4R ambazo wastani tunakopa kama Dola milioni 500. Tuna programu EQUIP ambazo pia tuna Dola kama milioni 500.
Mheshimiwa Naibu Spika, Hivi mtoto anayesoma private ni mtoto wa Kitanzania au siyo wa Kitanzania? Mtoto anayesoma shule ya Serikali anatafuta elimu ni wa Kitanzania au siyo wa Kitanzania? Tukitaka tusaidie Taifa letu kwenye suala la elimu, ninatoa ushauri, kwamba fedha za mikopo katika investment katika masuala ya walimu Serikali msione haya kuzisaidia shule za private katika investments, kwenye masuala ya vifaa, Maabara na walimu. Kwa sababu mikopo hii hata wale wa private wanalipa tusiwabague kwa lengo la kujenga hali ya kuwasaidia wananchi wetu kuweza kupata unafuu katika kupatikana kwa walimu katika maeneo hayo; huo ni ushauri wangu.
Mheshimiwa Naibu Spika, amezungumza kaka yangu Erick Shigongo, nimekusikiliza kwa makini sana brother. Lakini kuna muda pia alizungumza Profesa asubuhi. Leo tunapozungumza ukienda katika vyuo vya Uganda, fanya research, nenda katika vyuo vya Makerere na Bukene, nenda kwenye vyuo vya Kenya kama vile Nairobi University, halafu njoo fanya comparison na vyuo vya Tanzania. Nenda kaangalie idadi ya Watanzania wanaosoma Kenya na Uganda na idadi ya waganda wanaosoma Tanzania, utakuta kuna huge gape. Sababu kubwa ya msingi bado tuna mediocracy mind set ya kung’ang’ania vitu ambavyo havilifungui taifa katika kufanya Taifa letu la Tanzania liweze ku-integrate na ku-absolve mambo mengine ya technological transfer yatakayosaidia nchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano sisi tumeweka kigezo cha mtu kwenda Chuo Kikuu mpaka asome kidato cha sita. Hapo Kenya mtoto anamaliza kidato cha ana- qualify kwenda Chuo Kikuu akija Tanzania refraction. Haya mambo hayawezi kulisaidia taifa. Ushauri wangu ninaotoa Profesa Mkenda kaka yangu nenda kakae na timu yako. Na timu hiyo najua hata hili ninalolishauri, Baraza la kiufundi ambalo limeundwa kwa Sheria namba 25 ya mwaka 1978, ninajua kabisa ushauri ninaoutoka ukienda kuzungumza huko Serikalini mka-harmonize faida ya kuwa na integration ya watoto kutoka mataifa mengine kuja kusoma kwetu kwanza vyuo vikuu vitaongeza mapato ya kudaihili wanafunzi, pili tutaweza kurahisisha ku-harmonize technological transfer kutoka Mataifa ya wenzetu kuja kwetu lakini pia tutajiendelea kujenga mshikamano na undugu katika block zetu za kikanda na katika masuala mazima ya kisiasa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ushauri wangu wa mwisho. Vyuo Vikuu, ninatoa ushauri tumeweka retirement age ya walimu wa vyuo vikuu...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Kengele ya pili hiyo Mheshimiwa Kingu.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naama.
NAIBU SPIKA: Kengele ya pili.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa heshima yako.
NAIBU SPIKA: Sekunde mbili malizia.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kaka yangu. Ninatoa ushauri tumeweka retirement age kwa vyuo vikuu miaka 65, lakini nataka niwaambi kule vyuo vikuu mimi nilifundishwa na akina Profesa Kuzilwa walikuwa ni watu umri umeshakwenda. Wekeni taratibu watu wakishafikisha huo umri waanze kusaini mikataba, kule vyuo vikuu hawabebi zege, tunapoteza maarifa kwenye nchi, watu tunawaacha bado wana uwezo wanakwenda wanakaa nyumbani. Maprofesa… (Makofi)
NAIBU SPIKA: Ahsante, mengine andika kwa Waziri.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nitumie nafasi hii kukushukuru kwa kunipatia nafasi ili kutoa mchango wangu mfupi katika Wizara hii ya Afya ambayo kimsingi ni Wizara muhimu sana kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa letu na sustainable development kwa ujumla katika Taifa letu.
Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nataka niseme kwamba, imani kubwa ambayo Watanzania wameendelea kuwa nayo kwa Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kiwango kikubwa imani hiyo inachagizwa na mambo makubwa ya msingi yanayotokana na upelekaji wa huduma za msingi kwa wananchi. Jambo ambalo limeendelea kuwafanya Watanzania waendelee kuwa na trust na Serikali iliyoko madarakani.
Mheshimiwa Spika, nayasema haya kwa sababu kubwa mbili. Kwanza kabisa, Rais wetu Mama yetu aliyoko madarakani Mama Samia Suluhu Hassan amefanya juhudi kubwa sana na hatuwezi kuacha kulisema hili. Tumekuwa tukizungumza habari ya revolution kubwa iliyofanyika katika kuboresha masuala mazima ya Afya katika Mikoa, Wilaya mpaka Kata. Rais wetu tunampongeza sana na jambo hili mimi nasema kwamba tukiendelea kumpongeza Rais kwa mambo haya anayoyafanya tukaacha kuifanya Serikali na baadhi ya watendaji kuwajibika kwa makosa ambayo yanaweza yakamtia Rais doa tutakuwa hatulitendei haki Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nayasema hayo kwa sababu kubwa mbili. Miezi minne iliyopitia tumemsikia Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akipita na kulalamika nchi ikiwa inakumbwa na upungufu mkubwa wa madawa kuanzia kwenye Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Hospitali za Mikoa mpaka Hospitali za Rufaa. Kama hilo halitoshi, tumemsikia Waziri wa Afya akilalamika upungufu wa madawa kwenye hospitali zetu.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme na Mheshimiwa Ummy naomba anisikilize kwa makini sana Bunge hili sisi tuko hapa kwa sababu ya legacy ya kuhakikisha kwamba wale wananchi waliotuchagua ambao ndiyo walipa kodi tunakuja kuwasemea na kuhakikisha kwamba welfare zao zinatekelezwa na Serikali iliyoko madarakani. Kitendo cha wapiga kura wetu ambao ndiyo wananchi tunakwenda kwenye mikutano ya hadhara, tunahutubia mikutano tukimaliza tunaambiwa Mbunge mmetujengea Kituo cha Afya dawa ziko wapi. Jambo hili lazima lifike mahali likome kwenye Taifa letu, watu wanaotuchagua na sisi kama Wabunge ambao tunatokana, kwa mfano kama mimi natokana na Chama Tawala. Chama changu kimepewa ridhaa ya kuongoza Taifa kwa sababu kilikuwa na election manifesto, kimeahidi mambo ya kutekeleza.
Mheshimiwa Spika, jambo la ukosefu wa dawa nakwambia limekuwa kero kubwa kwa wananchi huko mtaani na wananchi wetu wapiga kura wamekuwa hawatuelewi. Jambo la kusikitisha Serikali inatoa fedha, MSD inapelekewa pesa, Mheshimiwa Waziri Ummy watuambie jambo gani linatokea dawa haziendi kwa wananchi? Jambo gani linatokea MSD huko dawa hazifikiwa kwa wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Waziri Mkuu analalamika, Waziri analalamika, what’s going on kule MSD. Hili jambo nalisema kwa dhati ya moyo wangu, sisi kama Wabunge na mimi kama Mbunge ninayetokana na chama kilichopo madarakani, tunawapa Wizara muda wa matarajio, tunaomba jambo la ukosefu wa dawa kwenye Taifa hili, tunawapa miezi minne au mitano, tutakuja hapa Bungeni… (Makofi)
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Kingu, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Lucy Thomas Mayenga.
T A A R I F A
MHE. LUCY T. MAYENGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kutokana na tatizo kubwa lililotokea MSD, naomba Bunge na nimwongezee Mheshimiwa Kingu kwenye taarifa yake, ni vizuri Wizara hii ifanye special audit MSD ili ambaye anatuhumiwa, kazi iendelee.(Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Kingu, unapokea taarifa hiyo.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, taarifa hiyo naipokea kwa sababu mimi nimetumwa na wananchi nije niwe sauti yao kwenye matatizo yao. Wananchi wa jimboni kwangu moja ya changamoto zinazowakumba hakuna madawa, Mama Rais anatoa fedha na Serikali sisi Wabunge tunaidhinisha hapa bajeti, Bunge lako linaidhinisha bajeti zinakwenda kwa nini dawa hazifiki? Hili jambo nataka niwaambie Wabunge sisi ndiyo tutakaoenda kuulizwa kule, sisi ndiyo tunaounda Serikali, lazima tusimame imara hapa Bungeni kuhakikisha Serikali yetu tunai-task, kuhakikisha kwamba dawa zinawafikia wapigakura wetu na walipakodi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, hilo hilo linaloendana na dawa. Nataka nimshauri Waziri waende wakalete Sheria tuje tuwapitishie. Tuunde kitu kinaitwa Health Commodity Revolving Fund, tuweze kuwaundia chombo cha Kisheria. TANROAD wana chombo chao cha kuleta fedha kwa ajili ya dawa, maji wana chombo chao. Afya ni jambo muhimu linalohusiana na masuala mazima ya usalama wa Taifa, waende wakalete Sheria tutawaundia Mfuko wa Fedha wa Dawa. Mfuko huo utafutiwe vyanzo vya uhakika vya fedha ili kuwasaidia watu wetu waweze kuhakikisha kwamba wanapata uhakika wa dawa.
Mheshimiwa Spika, Mfuko huu tutautafutia vyanzo vya uhakika vya fund ili kusudi uweze kuwasaidia watu wetu na tuweze kulisaidia Taifa letu. Nataka niwaambie nipo kwenye Kamati ya Katiba na Sheria, Makamu wangu Mwenyekiti yuko jirani hapa, hapa kuna wajumbe tuko tayari, Wizara ilete hiyo sheria, tutaichakata, tutaileta Bungeni, tulisaidie Taifa waweze kuwa na special fund ya kusaidia mambo ya dawa katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mchango wangu wa tatu, Madaktari wetu, naomba wanisikilize kwa makini sana Waheshimiwa Wabunge. Tunapozungumzia jambo la Madaktari kwenye Hospitali za Umma, public facilities, Daktari anakwenda pale anakaa dakika 20 anatibu, anakimbia anakwenda hospitali B, anatoka hospitali B anakaa dakika 10 anakimbia, anakwenda hospitali C. wanahangaika kujikimu maskini, Mheshimiwa Ummy dada yangu niwaombe Madaktari hawa kama walivyo watumishi wengine ni watu wamesoma hizi taaluma zao, wanatibu, haya mambo ni mambo ya usalama wa Taifa.
Mheshimiwa Spika, naomba Wizara waende wakahakikishe zile package za percentage wanazozipata private, wawape wanapofanya kazi kwenye hospitali za umma. Waende wakawape Madaktari wetu, hili jambo la Madaktari kukimbia hawataliona, wata-concentrate kuwatibu watu katika public facility. Jambo hili litaongeza tija ya utendaji na tutakuwa tumewasaidia Watanzania na tutaleta tija na sisi wataturahisishia kazi ya kwenda kuomba kura 2025 kuhakikisha kwamba Mama ambaye huyu ameleta matumaini kwa Taifa na kwa kweli kwenye hili wanawake shikamooni, mmetisha sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye hili nasema kwa dhati ya moyo wangu, kwenye hili mimi mwenyewe sasa hivi kwa dhati ya moyo wangu nimeamua kuwa advocate wa akinamama. Akinamama mkiaminiwa uwezo wenu wa kufanya kazi na sema kwa dhati ya moyo wangu, wanawake shikamooni, uwezo wenu wa kufanya kazi ni mkubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ukiangalia hapa hata utulivu huu wa Bunge aliyekaa hapo ni mwanamama, ukiangalia hata namna Taifa linavyokwenda, mimi juzi nilikuwa nasoma statistic, Afrika nzima Rais wa Tanzania mwanamama amepandisha mishahara Afrika nzima 23 percent, nani kama mama? Kwa uwezo huu akina mama, nashawishika kabisa hata kuamini hata baadaye tukileta sheria hapa wanawake tuawaongeze kwenye Uongozi watalisaidia sana Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo langu…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa Kingu kengele imeshagonga. Ahsante sana.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Point zangu zingine nitaziwasilisha kwa maandishi. Ahsante sana. (Makofi)
(Hapa baadhi ya Wabunge walimtunza fedha Mhe. Elibariki Kingu kutokana na mchango wake)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu mkubwa kabisa nitumie fursa hii kukushukuru wewe na kiti chako kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu kwa ustawi wa Taifa langu na watu wake.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa ninaomba ni– declare Mwalimu Dkt. Ashatu ni mwalimu wangu alienifundisha Mzumbe University masomo nikiwa mwaka wa kwanza alinifundisha masomo ya uchumi. Kwa hiyo, ninachangia Bajeti ya Waziri ambaye ana sehemu ya kunifanya kuwa hivi nilivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwanza kabisa ninakwenda kuchangia maeneo matatu la kwanza Statistics za Nchi zinaonyesha Kanda ya Mikoa zaidi ya kumi na nne inayojihusisha katika shughuli za kilimo cha pamba ambacho takwimu zinaonyesha ndani ya Taifa letu la Tanzania wakulima waliyojiajiri katika Sekta ya Kilimo ya Pamba wanakadiriwa kuwa takribani wakulima laki sita mpaka laki saba na wengi wanatoka kwenye Mikoa ya Mara, Geita , Mwanza, Simiyu, Tabora, Shinyanga, Singida na baadhi ya Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, chama kilichopo madarakani kwa mara ya kwanza ninaona dhamira ya Rais Samia kwenda kuandika unique record katika Taifa letu kwa sababu ya initiative hizi zilizofanyika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza; nimesoma Hotuba ya Mheshimiwa Waziri na Mwalimu wangu Hotuba ya Waziri inaonyesha Serikali imedhamiria kuhakikisha kwamba wawekezaji wote wanaofanya uwekezaji katika viwanda vya pamba mwaka huu pamba yote ya kulima niliyowataja kutoka Mikoa hiyo ambayo wanafanya jumla ya watu waliyojiajiri hizi ni ajira zaidi ya laki saba Rais wetu ameonyesha uzalendo mkubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nalisema hili kwa sababu toka nimekuwa Mbunge term yangu ya kwanza mwaka 2015 nimekuwa nikiwasemea wakulima wa pamba juu ya uhaba wa bei ndogo wanayoipata katika mazao yao ya pamba. Lakini kwa juhudi hizi za Rais tunaambiwa ya kwamba wakulima wote watakwenda kuuza pamba yao kwa viwanda vya ndani na nini kinakwenda kufanyika? Tunaona mikakati ya Serikali kuhakikisha kwamba viwanda hivi vinakwenda kutengeneza vitambaa vitakavyo ongeza thamani ya pamba ya mkulima na kuongeza export nje hilo litakwenda kuleta nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, statistics Waziri alizozisoma zinaonyesha sales yetu ya nje ime–raise kwa asilimia 64.4 na vitu vilivyochangia ku–raise kwa hiyo sale ya nje ambayo ni dollar kama milioni 4,000 bidhaa zinazo ongoza ni gold, cotton, coal na mengine kwa mpango huu Mheshimiwa Waziri nataka nikwambie mwalimu wangu ninakupa big up sana, tunampa big up Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hichi anachokifanya anatafsiri kwa vitendo yale yote yaliyoainishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kumsadia mkulima wa zao la pamba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikuambie, nataka nilipe Bunge lako tukufu taarifa; wakulima wa pamba katika Taifa letu wanachukua idadi ya ajira ya watu wanaokadiriwa laki saba. Tukiweza kuwasaidia wakulima kuuza pamba ndani na bei yao ikapanda hiyo ni sawa na kusema ya kwamba dollar milioni 4,000 tulizozirekodi za sale kwa sababu tutakuwa tumeongeza thamani tutakwenda kuifanya Tanzania kupata fedha za kigeni na wakati huo tutakwenda kuinua pato moja moja la zaidi ya ajira laki saba nje ya ajira ambazo zitakuwa zimeguswa kutokana na spiral over impact ambayo itatokea katika uwekezaji huu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali mkija na mipango mizuri lazima tutawaunga mkono, lazima tutawasemea hongera sana Waziri, hongera sana Mwalimu wangu Dkt. Ashatu sisi tuna kuunga mkono katika hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kuweka rekodi nyingine Taifa letu lilikuwa linakumbwa na uhaba mkubwa sana wa uzalishaji wa sukari katika nchi. Nimesoma ripoti kutokana na Hotuba ya Mheshimiwa Waziri statistics zinaonyesha kwa juhudi za makusudi zilizofanywa na Serikali ya Rais Samia uwekezaji katika viwanda vya sukari umeongezeka na tume–observe ongezeko la tani 80,000 kwa mwaka peke yake wa 2022/2023 nani kama Mama Samia jamani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli kwenye hilo hatuna sababu ya kuacha kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, kwa kuwezesha mikakati hii na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais katika kuhakikisha ya kwamba tunapanua uwekezaji wa zao hili la miwa pamoja na kuongeza uwekezaji katika uzalishaji wa sukari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeambiwa nimesoma ripoti viwanda vinaonyesha TCDS zao walizokuwa wameziweka mwanzo expansion itafanyika zaidi kuhakikisha ya kwamba sukari inakuwa ya kutosha katika taifa letu tuweze kutosheleza soko la ndani na kufanya exportations na kiusababishia Serikali yetu kupata faida zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la tatu; nalotaka kulizungumzia nina mpongeza sana dada yangu Mheshimiwa Tauhida inawezekana ameondoka. Mheshimiwa Tauhida amesema Mheshimiwa Waziri wewe ni msimamizi karibia wa Wizara zote katika masuala ya uwekezaji jambo ninalokushauri Mheshimiwa Waziri wangu na Mwalimu wangu Ashatu tunakuomba uweke jicho lako la karibu sana katika Taifa letu lazima tuwe na kitu kinaitwa continuity katika investment hili ni tatizo kubwa sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, inajitokeza wakati mwingine makampuni yamekuja yamewekeza, wamefanya uwekezaji mkubwa, wanapotaka ku–renew mikataba wanakuja na plan kubwa za kuweka uwekezaji, sisi tunaona kwamba mtu akiwekeza eti miaka kumi, ishirini eti miaka mingi. Kuna mataifa mengine makampuni yanawekeza mpaka miaka mia mbili na rekodi zipo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo Tanzania makampuni yanakuja mtu anawekeza miaka ishirini, kwa mfano nilikuwa natolea mfano hawa watu wa Songas. Kampuni ya Songas imewekeza kwenye umeme na wamefanya juhudi kubwa kuzalisha umeme wa uhakika chini ya Wizara ya Kaka yangu Mheshimiwa January Makamba leo kwenye kusaini mkataba tunasikia eti wanabembeleza Serikali muwaongeze mkataba hivi jamani kwa umeme tuliokuwa tunauziwa senti sita na watu hawa na hawa ni mashirika ambayo wamekeza Serikali za Uingereza na Norway kweli watu hawa sasa hivi waanze kutuomba kuongeza mkataba na Taifa letu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa wito. Tujenge utamaduni wa kuwa na continuity ili tujenge trust kwa investors walioko nje wajue umuhimu wa kuwekeza Tanzania watapewa nafasi ya kutosha. (Makofi)
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.
MWENYEKITI: Taarifa kutoka wapi?
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, unilindie muda wangu hizi taarifa hizi…
MWENYEKITI: Mheshimiwa Stanslaus Mabula.
TAARIFA
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya kumlindia muda nataka nimpe tu taarifa kwa sababu amewataja Songas, TPDC ambao ni wabia wakubwa wa Songas kwa miaka yote waliyokuwepo hapa nchini wameokoa zaidi ya trilioni kumi na sita kwa hiyo nadhani Mheshimiwa Kingu anahoja ya msingi namuongezea tu nyama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Kingu, unapokea taarifa? Na muda wako umekwisha.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa taarifa hiyo ninapokea nimalizie, nimalizie na kama ametaja Shirika la Serikali mimi naunga mkono Mheshimiwa Waziri, tunakuomba Wizara yako inagusa Wizara zote katika mambo ya biashara, usiwekewe mipaka fuatilia uwekezaji katika Wizara zote tumsadie Rais na sisi tuna kuunga mkono mwalimu wangu, kiongozi wangu tuko pamoja na wewe kazi iendelee. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nitumie nafasi hii kukushukuru sana wewe Kiongozi wetu wa Muhimili huu kwa kazi kubwa ya kulitumikia Taifa kwa njia ya Muhimili wako unayoifanya. Pia, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuchangia Wizara hii muhimu kabisa ambayo inagusa maslahi mapana ya amani, ulinzi, usalama na maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongrza sana Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. Samia Suluhu Hassan, ni wazi toka Dkt. Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani chini ya uongozi wake, mipaka ya Taifa letu iko salama, ndani na nje Taifa letu liko salama, pale ambapo pamejitokeza mambo ambayo yangeweza kufanya instability ya amani ya Taifa letu Rais wetu kupitia Vyombo vyake vya Ulinzi na Usalama wameendelea kusimama imara, Taifa letu liko salama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kumpongeza sana Waziri wetu wa Ulinzi, Kaka yangu Mheshimiwa Innocent Bashungwa, kwa unyenyekevu wake na uzalendo wake mkubwa uliompelekea Rais kumwamini na kumpa kuongoza Wizara hii muhimu sana katika Taifa letu. Hongera sana Mheshimiwa Bashungwa, endelea kuwa mnyenyekevu namna hiyo, uendelee kuwatumikia Watanzania kwa maslahi ya Taifa letu na kwa maslahi ya welfare ya watu wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninaomba nitoe ushauri ufuatao kwa Taifa langu na kwa Wizara yangu hii muhimu ninayoipenda sana. Kwanza kabisa, takwimu zinaonesha mwaka 2016 vijana waliohitimu Kidato cha Sita walikuwa 65,000. Takwimu za mwaka jana zinaonesha vijana waliohitimu Kidato cha Sita walikuwa takribani 95,000. Ninaomba nitoe wito kwamba pawepo na mwingiliano wa Wizara zifuatazo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Kilimo, Wizara inayoshughulikia Mambo ya Vijana ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, pamoja na Wizara ya Mifugo.
Mheshimiwa Spika, ninachokisema hiki ni kwamba amezungumza Kaka yangu Mheshimiwa Cosato Chumi, vijana wanaohitimu JKT, tunazungumza habari ya kujenga ajira za vijana, hili jambo ni rahisi sana, fedha ambazo Serikali inazitenga katika Wizara ya Kilimo, pakiwepo na mikakati kati ya Wizara ya Ulinzi, Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo pamoja na Wizara hii iliyoko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia mambo ya vijana, tunaweza tukafanya mkakati rahisi sana.
Mheshimiwa Spika, fedha za kilimo za kimkakati kwa vijana ambazo sasa hivi, kwa mfano Wizara ya Kilimo walikuwa wanakimbizana kwenda kule kwenye maeneo yetu kutafuta vijana ni jambo jema, nataka nikwambie kwa nidhamu ambayo Jeshi letu la Wananchi wa Tanzania inalijenga kwa vijana wa Kitanzania, vijana wale huwa wanachukuliwa wanajenga component ya uzalendo wa nchi nzima. Wanachukuliwa kutoka Jimboni kwangu, wanachukuliwa Mtwara, Mwanza na maeneo yote ya nchi na wengi wao wanatoka vijijini, kuna ugumu gani vijana hawa JKT wakatafutiwa mashamba ya kuzalisha, wakaingizwa kwenye kilimo? Fedha zinazotokana na bajeti tunapeleka kwenye kilimo, tatizo la ajira tunalolizungumza litatafutiwa solution ya kudumu tutakuwa tumelitibu tatizo la ajira. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, natoa wito na ninawaomba Wizara, nina imani Rais ameteua vijana mahiri tunawaamini, Kaka yangu Mheshimiwa Katambi tunajua uwezo wako, Kaka yangu Mheshimiwa Mavunde Kijana mwenzangu tunajua uzalendo na uwezo wako, Mheshimiwa Bashungwa tunajua uzalendo na uwezo wako. Fanyeni coordination ya vijana wa JKT haya mabilioni Mama Samia aliyoyatoa mama yetu aandike record ya ku-recruit vijana wengi katika kuwapa ajira wanaotokana na Sekta ya Kilimo kupitia JKT. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hili nakuambia likifanyika jambo la kulia kwa sababu hamna ajira litakuwa historia na jambo hili nalizungumza ni mara ya tisa mchango huu nautoa katika Bunge hili lako Tukufu, ninawaomba Mawaziri wangu tekelezeni jambo hili litapata baraka na mtafanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la pili, pamoja na kumpongeza Kaka yangu Jacob Mkunda, Jenerali wetu na Kiongozi wetu wa Majeshi yetu, ninatoa wito kuwa dunia inabadilika, sayansi na teknolojia inabadilika, ninaamni kabisa Jeshi letu ni Jeshi lenye nidhamu limefanya ukombozi wa mataifa ya Kusini, limefanya ukombozi wa kulinda mataifa mengi dunia, natoa wito ni wakati sasa ya kuli - modernize Jeshi letu liwe na vifaa vya kisasa, adui akitaka kuweka mguu kwenye nchi yetu wakati wowote tunao uwezo wa kukabiliana naye. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, natoa wito, Rais wetu sasa hivi anatekeleza miradi ya kimkakati, tunajenga mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyeyere, tunajenga mradi wa SGR tunataka kwenda kwenye uchumi wa bahari, tunahitaji bahari yetu iwe salama, tunahitaji miundombinu tunayojenga iwe salama. Kwa maana hiyo, ninatoa wito tununue vifaa vya kisasa vya kijeshi tuwe na ma – artillery ya kisasa tuwe na anti-aircraft ya kisasa ili kusudi tuwe na uhakika. Taifa letu lina ulinzi na usalama wakati wote na Mungu aendelee kuwapigania wazalendo wetu wanaotoa maisha yao kwa ajili ya kulinda Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la tatu ninalotaka kulisemea ni wakati muafaka sasa Jeshi letu la Wananchi lipewe fursa ya kujenga chuo cha kisasa, Chuo Kikuu cha kisasa kitakachoweza kutoa mafunzo ya teknolojia ya kisasa Jeshini. Itakayoweza kutoa mafunzo kwa wanajeshi wetu kuji-equip na teknolojia za kisasa kwa sababu dunia imebadilika. Mambo ya kutumia mavifaru yale ya mwaka 1961 yameshapitwa na wakati, dunia sasa hivi imekwenda mbele. Ninatoa wito Jeshi letu litengewe bajeti kwa siku zinazokuja, wajengewe chuo cha kisasa kitakachoweza kutoa mafunzo ya kiutalaam ya Wanajeshi wetu ambao baadhi yao ndiyo watakwenda kui-feed Nyumbu, hao baadhi yao watakwenda ku- feed vyuo vyetu vya kisasa ambavyo Jeshi letu linavimiliki kwa maslahi ya Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho siyo kwa umuhimu lakini ni la mwisho, nilikua naomba nitoe ushauri. Naomba hili ya vijana nililolizungumza wa JKT katika miradi niliyoitaja tuwekeane malengo. Tuseme kwa mfano, mwaka huu umemaliza vijana 95,000 katika sekondari zetu za high school, tunaweza tukasema mwaka huu tunaweka project ya miaka kumi, mwaka huu wa kwanza tutaanza na asilimia 33, mwaka unaokuja asilimia 40 na kuendelea, nataka nikuambie Mawaziri hawa wazalendo vijana wenzangu watakuwa wamesaidia Taifa hili kuweka record kubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa niwapongeze sana Jeshi la Wananchi wa Tanzania, nimeona leo Mabregedia Jenerali wanawake, nimeona leo wanawake wakitajwa humu kwenye Jeshi lao lakini kubwa zaidi nimefarijika sana na mimi nataka niwaambie nasi humu Bungeni tunae Brigedia Tulia. Huko nje mnaupiga mwingi na sisi humu ndani yuko Brigedia Tulia anaendelea kufanya kazi ya kizalendo na hivi karibuni Taifa na watu wake tunamuombea Brigedia huyu akaongoze chombo kikubwa duniani akawe Rais wa Bunge la Dunia, ama namna gani jamani Wabunge? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pia niwaombe Jeshi la Wananchi wa Tanzania hawa Makamanda tumewaona wamekuja hapa, tumeona wamechukua mikanda ya medeni kwenye kupigana, wapo akina Simbu wamechukua medani kwenye riadha. Jeshi Kamanda Mkunda nakuomba unanisikiliza Kaka yangu pamoja Waziri hembu nendeni mkawa - promote hawa vijana. Tunataka tuwaone kwa kazi kubwa wanayoifanya vijana hawa waje Bungeni wamechafuka nyota, wanaleta sifa na heshima kwa Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu libariki Jeshi la Wanachi wa Tanzania, Mungu mbariki Amiri Jeshi, Rais Mama yetu Daktari Samia Suluhu Hassan, amani ya Taifa letu iendelee kutawala. Ahsanteni kwa kunisikiliza. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa heshima na kutoa mchango wangu mdogo katika Wizara yetu hii muhimu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nianze kwa kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mwanadiplomasia Namba Moja ambae ni Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan. Uimara wa Wizara hii ya Mambo ya Nje, chini ya Dada yangu na Kiongozi wetu Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax pamoja na Naibu wake, kwa kiwango kikubwa mafanikio na kukimbia kwa kasi kubwa sana katika diplomasia ya uchumi hatuwezi kutaja mafanikio haya na kumuacha Mheshimiwa Waziri wetu wa Mambo ya Nje, Dkt. Stergomena Tax na Naibu wake. Hongereni sana viongozi wetu wazalendo mnampa Rais wetu heshima Kubwa, mnalipa Taifa letu heshima kubwa sana katika masuala mazima ya diplomasia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme mambo yafuatayo; Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania ndiyo roho ya mambo yote yanayohusiana na maendeleo ya uchumi ya Taifa la Tanzania. Wizara ya Mambo ya Nje inajihusisha na mambo makubwa yafuatayo ambayo baadhi ya Wabunge wameyasema. Hauwezi kuzungumzia suala la uwekezaji kwenye nchi yetu ya Tanzania bila kuigusa Wizara ya Mambo ya Nje, hauwezi kuzungumzia masuala ya utafutaji wa masoko bila kugusia Wizara ya Mambo Nje, hauwezi kuzungumzia Mambo ya Grants and loans bila kuzungumzia Wizara ya Mambo ya Nje, hauwezi kuzungumzia habari ya kuwavuta watalii kutoka katika pande zote za dunia bila kuzungumzia Wizara ya Mambo ya Nje, hauwezi kuzungumzia mafanikio ya mikutano mikubwa ya Kitaifa na Kimataifa ambayo Viongozi wote wa Kidiplomasia wa nchi wanahudhuria bila kuigusia Wizara ya Mambo ya Nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kimkakati (Strategically) Wizara ya Mambo ya Nje tukiamua kuiweka kuwa Wizara ya Kimkakati ndiyo roho ya kufanya transformation ya uchumi na uwekezaji katika Taifa letu. Nimeyasema hayo kwa sababu tumekuwa tukiichukulia Wizara ya Mambo ya Nje kama Wizara tu ya watu kwenda kwenye mikutano. Nataka nikwambie, ninatoa rai kwa Serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ni Wizara inahitaji kupewa fedha za bajeti kubwa ya kwanza kwenye Taifa hili ni Wizara ya Mambo ya Nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikupe mfano mdogo, hapa tunaposema tumejenga, tumejenga barabara kubwa, tukisema tunapanua bandari, juzi tumezungumza jambo la bandari hapa, ni nani walifanya juhudi kuhakikisha kwamba wawekezaji hawa wanapatikana ni Wizara ya Mambo ya Nje. Kitu cha ajabu inapofika kwenye kuzindua miradi hii hawa watu hata hakuna mtu anayejali wala kujua kwamba kazi kubwa ya kizalendo imefanywa na Wizara ya Mambo ya Nje. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikuambie strategically as a nation kama tunataka kufanya transformation ya kiuchumi, transformation ya uwekezaji, transformation ya kukuza diplomasia ni sharti Serikali tubadilishe mindset watu hawa wapewe fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ninapozungumza ni nani anaetafuta masoko ya parachichi za Tanzania ni Mambo ya Nje. Nani anamsaidia Mheshimiwa Mwigulu kwenda kutafuta mikopo? Mambo ya nje. Halafu, nenda ukaangalie bajeti yao utaona kama nchi bado hatujadhamiria kulibadilisha Taifa hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa wito Serikali kama tutakuwa tumechelewa mwaka huu na tunae Mwanadiplomasia Mama Tax, Kiongozi mtulivu na mwenye uwezo mkubwa sana, yeye na Naibu wake, kama tutakuwa tumechelewa mwaka huu tujipange mwaka unaofuata tudhamirie kuleta transformation ya kiuchumi tuweze ku–empower Wizara yetu ya Mambo ya Nje ili FDI zije za kutosha Taifa letu liweze kupiga hatua ili changamoto za ajira alizozisema Daktari na watu wengine ziweze kumalizika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nataka nizungumzia Zanzibar leo.
MWENYEKITI: Malizia nusu dakika.
MHE ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante naomba nimalize tu Zanzibar. Zanzibar hawana Wizara ya Mambo ya Nje, hili naomba niliseme na univumilie kidogo sana. Zanzibar hawana Wizara ya Mambo ya Nje, wanategemea Wizara yetu hii ya Mambo ya Nje kuweza kuwasaidia watu wetu wa Zanzibar katika kuleta FDI katika kuleta utalii na masuala mazima ya uwekezaji katika nchi yetu ya Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe Wizara ya Mambo ya Nje, chochote mnachokifanya Mambunge mengine yatakuja tutawahoji ni uwekezaji kiasi gani umekwenda kwa wenzetu wa Zanzibar ambao ni partner iko kabisa katika Muungano huu tulionao wa Tanzania. Wazanzibari wanatakiwa wasaidiwe sana kwa sababu wao hawana Wizara inayojitegemea nje ya hii. Mheshimiwa Waziri tunaimani na wewe tunakuomba, Rais Mwinyi anafanya kazi kubwa na nitaoa rai Rais Mwinyi apatiwe utulivu Zanzibar, aendelee kuijenga Zanzibar. Choko choko ziachwe Zanzibar ili Rais Mwinyi kwa uwekezaji huu ninaouzungumza aweze kufanikiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwishop lakini siyo kwa umuhimu ninaunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya uchache wa muda tuliopewa, kwanza kabisa nitumie nafasi hii kukushukuru sana wewe binafsi kwa kunipa nafasi ya kutoa mchango wangu katika Bajeti Kuu ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza, tukiwa kama Wabunge sisi tuna nafasi ya kusema vitu ambavyo vinatoa direction ya nchi. Kwa dhati ya moyo wangu niseme mafanikio yote tunayoyazungumza ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Nyanja za kiuchumi, kijamii, kisiasa, nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu, sisemi kwa sababu Waziri huyu wa Fedha ni kaka yangu. Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba kaka yangu nataka niseme kwa dhati ya moyo wangu umeitendea haki sana Serikali ya Awamu ya Sita katika masuala mazima ya usimamizi wa fiscal policy and monetary policy na ndiyo maana tunapoangalia hali ya uchumi wa nchi za Afrika ya Mashariki ukiangalia masuala mazima ya inflation, bei za vyakula na bidhaa Taifa la Tanzania ndilo nchi peke yake stable katika mataifa yote ya Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa credit kama hizi hatuwezi tukaku-ignore kaka yangu Mwigulu. Niseme kwa dhati ya moyo wangu, unamfanya Rais wetu kuwa proud, na sisi kama Wabunge tunalisema mchana kweupe, wewe ni moja ya mawaziri bora kabisa kuwahi kutokea katika sekta ya fedha katika nchi yetu, keep it up kaka yangu kaza Kamba kazi iendelee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili nalotaka kulisema; kuna maneno mengi yamesemwa mtaani, kuna watu wamefikia hatua ya kutaka kuligawa Taifa, na hili nalisema kwa sababu ni Bajeti Kuu ya Serikali. Rais anahangaika kutengeneza base za kuleta kodi kwenye nchi, uwekezaji unaozungumzwa, Rais wetu anahakikisha ili tuache kukimbizana na mikopo Taifa liwe na revenue zake. Rais amefanya mipango kupitia Serikali, tunao watu wa DP World. Kuna watu wamekwenda kusema nchi imeuzwa. Mimi nataka nisome vipengele vya kisheria ambavyo vinaonesha upotoshwaji uliofanywa mtaani ulikuwa ni makusudi na lengo la kuchafua na kuleta instability ya umoja wa kitaifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Article One ya Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ukurasa wa 9 katika land right; kwa sababu unaposema nchi inauzwa unamaanisha tumeuza mamlaka ya nchi na tumeuza ardhi. Article 1 inasema “land right shall mean all those rights excluding the right of ownership of land”, huu mkataba. Sasa hoja ya kusema nchi imeuzwa inatoka wapi? mkataba unasema right of ownership, exclusion imewekwa kwenye right ya ownership ya ardhi. Acheni kudanganya watu, achene kuchafua nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu Rais hawezi kuliuza hili Taifa na ndiyo maana ni Amiri Jeshi Mkuu. Tumemwamini, tumempa madaraka na hafanyi maamuzi kwa sababu ni Mzanzibar. Nataka niwaambie, Mzanzibar ana haki ya kuwa Waziri kwenye Serikali ya Jamhuri ya Muungano na hatma iko kwenye muungano huu. Haiwezekani tukaanza kuleta mambo huyu Mzanzibar, tutavunja muungano wetu. Tunaomba wanaofanya hayo wakome mara moja Mama apewe maua yake kwa kuleta kampuni hii kuja kufanya uwekezaji utakaoleta tija katika Taifa letu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine na mambo mengine kwenye mkataba wamezungumzia article 22 wanasema mkataba huu tumejifunga, amendment zimezungumzwa kwenye article 22. Jambo lingine wamesema mkataba huu, sheria sijui tukishtakiana wapi article 21 imesema governing laws zitakazotumika ni za Serikali ya Tanzania. Mheshimiwa Waziri nataka niwaambie kafanyeni kazi, sisi kazi yetu tulihaidi, sisi ndiyo tuna Ilani, msitishwe na mtu, tunawaunga mkono. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ninalotaka kumshauri kaka yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu na Serikali. Wananchi wetu na viwanda vimekuwa vikilalamika, bei ambayo imekuwa ikitozwa katika electronic stamp imekuwa ikisemekana ni kubwa. namshauri Mheshimiwa Waziri kwa nini wasiwaite wawekezaji wa SICPA wakae nao, wawaombe washushe bei ili kusudi wafanyabiashara waweze kuwa na manufaa katika gharama hizi zinazozungumzwa. Najua wamefanya kazi kubwa pamoja nao ya kizalendo, mapato ya Serikali yameongezeka, uchumi wa Taifa unakua, miradi inaendelea kuwa financed kwa sababu ya mapato anayokusanya kaka yangu. Wakae na watu wa SICPA, wazungumze nao ili washushe gharama…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la mwisho, nakuomba radhi sana dada yangu. Jambo la mwisho nataka niseme kama alivyosema kaka yangu Kwagilwa Mama Samia apewe maua yake. Ripoti zinaonyesha mwaka 2001 net in flow ya foreign direct investment ilikuwa asilimia moja. Mwaka mmoja baada ya Mama kuingia madarakani ikapanda mpaka 1.4
Mheshimiwa Spika, UNCTAD wametoa ripoti wanaonyesha uwekezaji kwenye Taifa umeongezeka kwa asilimia 34, ripoti ambazo alikuwa anasema kaka yangu, inaonyesha kwamba Taifa limepanda katika ratio za kimataifa katika masuala mazima ya kiuchumi. Nani kama Mwigulu jamani? Hivi kweli tutasema hatuna Waziri imara wa Fedha. Naomba kaka achape kazi, Wabunge tunamuunga mkono, Rais tuko nyuma yake, waharakishe katika uwekezaji wa bandari, wasitishwe, tutatoka hapa, tutakwenda mtaani, tutawaeleza wananchi umuhimu na manufaa ya uwekezaji huu kwa maslahi ya Taifa letu, ahsante sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2023.
MHE. ELIBARIKI I. KINGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nakwenda kuzungumza eneo moja na kwa kweli kwa dhati ya moyo wangu niungane na mchangiaji wa mchana pamoja na kaka yangu Shigongo, kwanza kwa kuishukuru sana Serikali na kumpongeza Rais wetu kwa dhamira hii njema ya kuleta mabadiliko katika kuwasaidi Watanzania katika masuala ya uwekezaji na biashara. Kaka yangu Shigongo alikuwa anazungumza hapa nilikuwa namsikiliza kwa makini sana, amezungumza kwa uchungu sana.
Mheshimiwa Spika, ukisoma Ibara ya 61 inasema; “Baada ya kushaurina na vyombo husika vilivyoanzishwa kisheria, taasisi nunuzi itatenga mikataba itakayotumika kwa lengo la kujenga uwezo wa makampuni ya ndani.”
Mheshimiwa Spika, kifungu hiki ukikisoma na ukaendelea mbele kuna mahali zile sub-article inasema kwamba; “A Minister may,” kwamba Waziri anaweza kutunga kanuni.
Mheshimiwa Spika, naomba nitoe ushauri, kwa alichokuwa anakisema kaka yangu Eric Shigongo nataka nikupe ushahidi, tuna kampuni nyingi sana za Kitanzania zenye uwezo wa kutoa huduma na kazi ambazo ni za msingi na zina uwezo wa kufanywa na kampuni za Kitanzania. Lakini kwa bahati mbaya sana nikiri kwa moyo wangu kuwa baadhi ya wataalam wetu, technocrats walioko Serikalini na sizungumzii technocrats wote, baadhi ya technocrats wetu hawajali maslahi mapana ya kampuni za Kitanzania.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano unaweza ukasema umetangaza kazi, kwa mfano South Africa wenzetu kwa hiki hiki kifungu cha 61, wametunga sheria inaitwa Black Women Procurement Act. Black Women Procurement Act imetoa msisitizo kwa nchi ya South Africa mgeni anakuja amepata contract, sub-contract inafanywa na mzawa na sheria hii inamlazimisha mgeni huyu kwa miaka miwili anayofanya kazi na mzawa anafanya technological transfer mpaka miaka minne inakwisha makampuni yanapata uwezo wa kujitegemea.
Mheshimiwa Spika, nitoe rai, niiombe sana Serikali tusiishie kutunga sheria, tusimamie na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kule Serikalini kwa wale wanaokwenda kutekeleza kwa sababu inatia uchungu sana Watanzania wanakwenda kwenye tender hawashindi, wanafanya hiki lakini hawashindi. Kampuni zote za kigeni zinakuwa zinashinda ilhali kuna vijana wa Kitanzania wana uwezo wa kutengeneza vitu local na vikauzika kwa Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tutabaki kwenye Taifa hili kuwasindikiza wageni mpaka lini katika vitu ambavyo wazawa watoto wa Kitanzania wanaweza? Tanayo kampuni hapa zina uwezo wa kutengeneza mifumo ya kisasa, lakini ni nani anawapa nafasi? Tunazo kampuni zina utaalam wa hali ya juu katika fani zote za IT, lakini ni nani anawasikiliza? Any way.
Mheshimiwa Spika, mimi kwa leo nimesema hilo; naomba kwa kipekee sana nitumie nafasi hii, na utanisamehe sana haliendani na mada hii; nitumie nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu kulishukuru sana Bunge la Kenya. Wiki mbili zilizopita Bunge la Kenya lilipeleka taarifa ya utekelezaji wa Wana-IPU (Wajumbe wa Bunge la Dunia wa Kenya).
Mheshimiwa Spika, katika Bunge la Kenya, Wakenya majirani zetu wamejipambanua, wamekusemea vizuri sana Mheshimiwa Spika kwenye Bunge lao. Kuna Mbunge ametoa hoja, akalieleza Bunge la Kenya namna ya uwezo alionao Spika wa Tanzania, ndani ya Bunge la Kenya. Hivi ninavyozungumza Kenya Bunge limefanya adoption ndani ya Bunge ya kuku-endorse wewe kama mgombea wa Bunge la IPU. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, siishii kulipongeza Bunge la Kenya peke yake, ninayapongeza Mabunge yote ya Afrika Mashariki ambayo yalikutana yakaku-endorse wewe kama mgombea wa kiti cha Urais wa Bunge la Dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kama hiyo haitoshi sitapata nafasi nyingine baada ya Bunge hili, tunakwenda kwenye Uchaguzi wa Kiti cha Urais wa Bunge la Dunia.
Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Wabunge wenzangu ambao walituamini kutupeleka kwenye Bunge la IPU, kupongeza sana Mabunge yote ya SADC. Tulipokutana Arusha kikao kile nchi zote za SADC kwa sauti moja zilinyoosha mikono zikaku-endorse Dkt. Tulia Ackson kuwa Mgombea wa Kiti cha Bunge la Dunia hapo mwezi wa 10, Angola. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini kama hiyo haitoshi nitumie nafasi hii kuishukuru sana taasisi yetu muhimu na chombo muhimu cha maamuzi cha Afrika (African Union.) Katika kikao cha African Union kilichokaa Nairobi kimekupitisha na kuku-endorse wewe kama mgombea peke yake wa nafasi ya kiti cha dunia katika Bunge la Dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nisipoyasema maneno haya, tutamaliza Bunge hili hatutakuwa na nafasi ya kuonesha uzalendo uliyooneshwa na Mataifa ya Kiafrika. Nataka nitumie nafasi hii pia kumshukuru sana aliyekuwa Waziri wetu wa Mambo ya Nje, Mheshimiwa Stergomena Tax na Mheshimiwa Rais wetu Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Spika, diplomasia ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo tunafanya kampeni nje, tumeona heshima ya Taifa letu imekuwa kubwa, tumeona mapokeo ya Taifa letu yamekuwa makubwa na In Shaa Allah naamini Spika wangu mwezi Oktoba utakwenda kushinda kiti cha Urais wa Dunia na kuliletea Taifa letu heshima jambo ambalo litaendelea kuifanya Tanzania ing’are katika medani za Kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nakushukuru sana. Naomba Wabunge tuendelee kumwombea Spika wetu. Kwa muda mfupi nimekuwa naye karibu, dada yetu huyu ni mtu mnyenyekevu sana, Spika huyu ni mtu mtulivu sana, Spika huyu ni mtu mwenye maono makubwa sana na ndio maana dunia iko tayari kumuunga mkono katika uchaguzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunazo nchi kadhaa bado zimekataa kujitoa kwa sababu Africa Union wamesema kwamba wanakwenda na huyu, lakini In Shaa Allah kwa neema za Mwenyezi Mungu endeleeni kutuombea tupate ujasiri wa kuendelea kumsemea Mheshimiwa Dkt. Tulia tuweze kuleta trophy nyumbani kwa ajili ya heshima ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema haya, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)