Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Dunstan Luka Kitandula (69 total)

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikitoa kifuta jasho kwa wahanga walioathirika na wanyamapori ikiwepo laki moja tu kwa heka nzima ya mazao yaliyoharibiwa au shilingi laki mbili kwa mtu aliyejeruhiwa, laki tano kwa aliyepata jeraha la kudumu na labda milioni moja kwa familia ya aliyeuawa na wanyama pori na pengine kuchelewesha kutoa malipo hayo kwa wahanga.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu matukio hayo yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku pengine kuwa mzigo mkubwa kwa Serikali na kushindwa kuwalipa kama ilivyo nchi ya jirani ni kwa nini sasa Serikali isione umuhimu wa kuanzisha huu mfuko wa fidia kwa wahanga?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa Serikali yetu ya Tanzania bado inatoa kifuta jasho kwa wahanga, haioni sasa ni muda mwafaka kurejea na kubadilisha baadhi ya mafungu katika Sheria hiyo ya Wanyamapori ya mwaka 2011 hasa kuongeza nyongeza hii ya fidia angalau iendane na hali ya maisha ya sasa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli imekuwepo changamoto ya viwango vya fidia au kifuta jasho kuwa vidogo. Vilevile ni kweli kwamba wakati mwingine imechukua muda mrefu kwa wananchi hao kufidiwa. Serikali imeliona hili na imelifanyia kazi na tuko kwenye hatua za mwisho za kuona kwamba kanuni zinafanyiwa marekebisho ili wananchi waweze kulipwa stahiki zao kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na hili la kusema tuanzishe mfuko maalum. Serikali imefanyia kazi jambo hili na imefanya utafiti kwa nchi jirani ambazo zimekuwa na mfumo huu na imejiridhisha kwamba wenzetu wamepata matatizo kuendana na mfumo huu unaopendekezwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Serikali inajielekeza kuweka mikakati ya dharula ambayo itatuhakikishia kwamba tunaondokana na tatizo hili, nakushukuru.
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kupata nafasi. Wako wananchi wangu wa Kata ya Maore, Karemawe, Bendera nakadhalika ambao wameuawa na Tembo takribani miaka miwili sasa lakini Serikali haijatoa kifutajasho wala chochote.

Je, hauoni kwamba Serikali inaonekana kama inawathamini Tembo zaidi kuliko ambavyo inawaona wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imechukulia kwa umuhimu na uzito mkubwa maisha ya Watanzania. Kutokana na changamoto hizi ambazo zimekuwa zikijitokeza kwa tembo kuvamia na kupoteza maisha ya wananchi wetu, Serikali imeandaa mkakati wa dharura ambao utatuondoa kwenye changamoto hii. Naomba tuipe Serikali muda, ndani ya kipindi mfupi tutaona matokeo ya utekelezaji wa jambo hili.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nampongeza sana; lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imeonesha wazi kwamba wameweka hiyo dawa. Hata hivyo, tatizo la popo katika maeneo ya Upanga, Sea View, Leaders Club, Kinondoni, Oysterbay, Masaki, Msasani Peninsula na maeneo mengine ya ukanda wa pwani linaongezeka siku hadi siku na kusababisha popo hao mpaka wanavunja vioo vya madirisha kwenye nyumbani.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza hiyo dawa ili popo hawa waweze kuondoka na kuwaondolea adha wananchi wa maeneo hayo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa changamoto inayowapata wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam katika maeneo ya Upanga na mengineyo, pia inawakuta wananchi wa Dodoma kuvamiwa na nyuki katika maeneo mbalimbali hasa maeneo ya Area D katika majengo ya TBA, Makole yote pamoja na maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma nyuki wanavamia na kuhama hama hovyo hovyo;

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwaondolea wananchi wa Jiji la Dodoma adha ya kuvamiwa na nyuki?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye swali la msingi, hatua ya kwanza ya kukabiliana na popo hawa ilikuwa ni kufanya utafiti wa kujua kiwango cha ukubwa wa tatizo na aina ya dawa ambayo inaweza kutumika ili kukabiliana na changamoto hii.

Mheshimiwa Spika, utafiti huu umekamilika, sasa jukumu lililopo mbele yetu ni kuhakikisha kwamba wadau wote wanaohusika na kukabiliana na jambo hili, zikiwepo Halmashauri zetu zinachukuwa hatua ya kuhakikisha tunasambaza dawa hizi kwa wananchi ili tuweze kukabilianana tatizo hili. Niombe wadau wote wanaohusika tushirikiane ili tuweze kuondokana na tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili la tatizo la uvamizi wa nyuki kwenye Mkoa wa Dodoma. Nitumie fursa hii kuwaagiza wataalamu wetu wa idara ya nyuki kushirikiana na wenzetu wa jiji la Dodoma ili kufanya tathmini ya haraka na kuona ukubwa wa tatizo hili na kuchukua hatua za haraka za kuangamiza nyuki hawa, ahsante sana.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri na kumpongeza, tunafanya kazi vizuri kwa pamoja na nimpongeza kwa majibu mazuri sana.

Mheshimiwa Spika, kwa kuongezea majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa upande wa popo, tayari tumeagiza dawa nyingine za majaribio ikiwemo Pepzol na Super Dichlorvos ambazo zinapatikana Marekani na Kenya. Imeonekana kwamba dawa hizo zikitumika ndani ya miezi miwili mpaka mitatu popo hao wanaweza wakatoweka.

Mheshimiwa Spika, pia nitoe rai kwa Halmashauri zetu za Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri nyinginezo katika maeneo ya miti ya barabarani waweze kununua dawa hizo ili waweze kupiga kwa ajili ya kuweza kufukuza na kudhibiti popo hao.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa Jiji la Dodoma kuhusu suala la nyuki, kama ambavyo Naibu Waziri ameeleza, nako pia tutoe rai kwa Halmashauri ya jiji Dodoma nao watenge fedha ili waweze kununua dawa hizo ili pale tutakapokuwa tumepata tathmini ya kuweza kujua ni dawa gani zinaweza kufanya kazi vizuri katika kudhibiti basi waweze kununua dawa hizo na kuweza kutumia.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia taasisi ya TAWIRI tutaendelea kushirikiana na wananchi pamoja na taasisi katika kuhakikisha kwamba tunadhibiti tatizo hili. Tuombe ushirikiano kwa wale wenye makazi pia waweze kununua dawa hizi katika maduka mbalimbali yanayozalisha dawa hizi. (Makofi)
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, pamoja na popo katika Mkoa wa Dar es Salaam, kuna tatizo kubwa la kunguru ambao wamekuwa wakitapakaa kila mahali, wanajerui watoto; na hasa katika fukwe, ambako wamekithiri, na hivyo kuharibu utalii wetu. Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha wanadhibiti kunguru hao?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, naomba kujibu swali la nyongezala la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli tumekuwa na tatizo la kunguru katika maeneo mbalimbali nchini. Serikali kupitia Wizara imekuwa ikifanya jitihada ya kuja na mipango mbalimbali ya kuweza kuondokana na tatizo hili. Changamoto tunayoiona ni kwamba wenzetu kwenye maeneo ya halmashauri zetu wameliacha jambo hili kuwa ni jambo la Wizara peke yake. Tunawaomba sana wadau wenzetu katika maeneo ya halmashauri, kwa kutumia teknolojia iliyoandaliwa na Wizara tushirikiane ili kupambana na tatizo hilo. (Makofi)
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Natumia nafasi hii kuipongeza Wizara na Serikali kwa ujumla kwa jitihada zinazofanywa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Napongeza Wizara kwa kutumia TTB na kuratibu ziara ya waandishi wa habari kwa ajili ya kubaini vivutio hivi. Hata hivyo, huwezi kutenganisha utalii na rika mbalimbali kwenye eneo husika kwa maana ya watu wazima, wazee, rika la kati na watoto katika kubaini na kuendeleza utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, ziara hii imefanikiwa, lakini bahati mbaya sana kuna rika la watu wazima, kuna kikundi cha KUMIDEU na vinginevyo ambavyo vinafahamu zaidi utamaduni, mila na desturi za watu wa Ukerewe, walitakiwa kuhusishwa. Nini sasa mkakati wa Serikali ili wakati mwingine vikundi kama hivi vishirikishwe ili kupata uhalisia wa vivutio vya utalii vilivyopo pale Ukerewe?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali, lakini tunakosa kiungo kinachoweza kuratibu mambo haya ya utalii. Halmashauri zetu zingeweza kutoa msaada mkubwa sana, lakini bahati mbaya sana hazina watu specific wanaoshughulika na utalii zaidi ya utamaduni. Je, ni nini mkakati wa Serikali sasa kuhakikisha Halmashauri zetu zote zinakuwa ama na idara au na vitengo vinavyohusika na utalii ili kuweza kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais katika kukuza Sekta ya Utalii? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ulimwenguni kote, custodian wa mila na desturi ni Machifu wakienda sambamba na wazee wa mila na desturi. Kwa bahati mbaya kwenye halmashauri zetu kumekuwa na upungufu wa kubaini makundi haya ya wazee wa mila na desturi. Natoa rai kwa halmashauri zetu, ziwe na mikakati ya kuwatambua wazee wa mila na desturi ambao ndio custodian wa tamaduni zetu ili tunapofanya jukumu la kutambua na kutangaza vivutio vilivyopo kwenye maeneo yetu, basi wazee hawa waweze kutumika.

Mheshimiwa Naibu Spika, natoa rai kwa halmashauri zetu, zijielekeze kwenye kutambua maeneo yote yenye sifa za kiutalii, wawasiliane na Wizara ili maeneo haya yaweze kusajiliwa tuweze kuweka mpango mkakati wa pamoja wa kutangaza maeneo haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la pili la uhaba au kukosekana kwa kiungo, kwa kukosekana wataalam kwenye halmashauri zetu. Mamlaka ya ajira ya watumishi kwenye ngazi ya halmashauri, ni Wizara ya TAMISEMI. Naomba sana halmashauri zetu zijielekeze kwenda kuomba vibali vya ajira kwa TAMISEMI ili jambo hili liweze kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hilo, kwa kutambua gap lililopo, Wizara ya Maliasili inao wataalam kwenye kanda zetu. Kwa mfano, kwenye Kanda ya Ziwa Victoria, tunao wataalam wetu wawili walioko Mwanza, Kanda ya Kusini, tunao wataalam watatu wapo Iringa, Kanda ya Kaskazini, tunao wataalam sita wapo Arusha, Kanda ya Pwani, tunao sita wapo Dar es Salam lakini vilevile hapa Makao Makuu tunao wataalam. Tunaomba halmashauri zetu ziwatumie wataalam hawa wakati wakijiandaa kupata vibali vya ajira kutoka TAMISEMI.
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Hifadhi za Taifa, Hifadhi za Misitu pamoja na Mapori ya Akiba, tumeanzisha kwa ajili ya kuhifadhi uoto wa asili na kulinda viumbe hai pamoja na wale ambao wako hatarini kutoweka. Hali kadhalika kwa kuwa hivi karibuni maeneo mengi ya hifadhi na mapori ya akiba, aidha tumeyamega ya kuyateremsha hadhi baadhi yake. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba utaratibu huu wa kumega maeneo na kuteremsha hadhi maeneno ya hifadhi haujirudii tena?

Swali la Pili, kwa kuwa upoteaji wa uoto wa asili unaenda sambamba na upoteaji wa viumbehai, mimea na wanyama ambao wako hatarini kutoweka. Je, Serikali ina mpango gani wa kuainisha na kuwea kutenga utaratibu maalum wa kuweza kuhifadhi viumbe adimu na wale ambao wako hatarini kutoweka? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iliridhia kuachia maeneo yenye migogoro vilevile kushusha hadhi baadhi ya mapori na hifadhi zetu baada ya kubaini kwamba ipo migogoro isiyokuwa na tija iliyokuwa inahatarisha usalama wa wananchi wetu. Serikali ilifanya hivyo baada ya kufanya utafiti wa kina kuona kiasi cha matumizi endelevu ya maeneo hayo, jinsi ambavyo yanaweza kutumika na kama yalikuwa yanatumika kwa jinsi ambavyo ilivyokuwa imekusudiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale inapoonekana kwamba pori au hifadhi imepoteza sifa yake ya awali ya msingi, basi maeneno hayo hushushwa hadhi na kuwa misitu ili tuweze kuendelea kutunza maeneno haya. Katika kujipanga kuhakikisha kwamba hali hii haijitokezi tena, Serikali inajipanga kutoa elimu kwenye maeneo yote yanayozunguka maeneo ya hifadhi zetu na mapori tengefu ili kujenga uelewa wa wananchi kuhusiana na umuhimu wa rasilimali hizi, vilevile Serikali imejipanga kuongeza doria katika maeneo haya ili uvamizi usijitokeze tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, Serikali inajitahidi sana kuhakikisha kwamba pale ambapo mimea imetoweka au wanyama wametoweka Serikali imekuja na mkakati wa kupanda miti kwenye maeneo yale yaliyoathirika, kwa mfano kupitia TFS tumeaza kupanda miti kule Mkoani Geita, vilevile tumeanza kupanda miti Mkoani Kigoma zaidi ya hekta 139,000 zimepandwa ili kuhakikisha uoto ule haupotei.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini pale ambapo tunaona kwamba kuna aina fulani ya wanyama inatoweka, tunakuwa na mkakati wa kuweka maeneo maalum ya kuhakikisha tunadhibiti kuzaliana kwa wanyama wale ili wasije wakatoweka. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Hifadhi ya Msitu wa Kihesa - Kilolo pia imekutana na athari hizo. Je, Serikali iko tayari kutusaidia na sisi kuja kupanda miti ili kuendela kuhifadhi eneo lile?

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, tumelichukua, wataalam wetu wataenda kufanya tathmini na kuona jinsi ambavyo tunaweza kusaidia.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Spika, Sera ya Ugatuaji ni Sera ya Kitaifa. Suala la mapato ya taasisi zetu na maduhuli ya Serikali kwenda moja kwa moja hazina inaenda kinyume na hii Sera ya ugatuaji. Ndio inayosababisha miundombinu muhimu kwenye hifadhi zetu kutotengenezwa mara kwa mara. Je, Serikali haioni wakati umefika sasa wa kurudisha walau asilimia 20 ya mapato kwenye hifadhi zetu, ili washughulikie miundombinu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Serikali inakiri kufunguliwa kwa geti hili katika Kata ya Kilangali na Tindiga kunaenda kufungua fursa za kiuchumi. Je, wamewaandaa vipi wananchi wa Kata za Tindiga, Dhombo, Masanze na Kilangali, ili wasije kuwa wageni wakati fursa hizi ambazo zitatokana na kufunguliwa kwa lango hili zitakapowadia? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na changamoto ya kukamilika kwa miundombinu kwenye maeneo yetu kutokana na kukosekana kwa fedha na mabadiliko tuliyokuwa tumefanya ya mfumo wa kukusanya mapato na kuyapeleka moja kwa moja kwenye Mfuko Mkuu wa Hazina. Hata hivyo, baada ya jambo hili kujadiliwa kwa kina ndani ya Bunge lako Tukufu na jambo hili kufikishwa Serikalini tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuridhia kurejesha tozo ya maendeleo ya utalii ambapo tayari Mheshimiwa Rais ameridhia asilimia tatu ya fedha hizi iweze kutumika kwa ajili ya shughuli hizi.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili; jukumu la kutoa elimu kwa wananchi wetu sio jukumu la Serikali Kuu peke yake ni pamoja na halmashauri zetu. Nitoe rai kwa halmashauri husika ziweze kutoa elimu kwa wananchi, tukiwepo sisi Waheshimiwa Wabunge, ili wananchi waweze kuchangamkia fursa za kimaendeleo zinazokuja katika maeneo yetu.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana; je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha lango la kuingia Mlima Kilimanjaro la Kidia kwani lango hili litakuwa linatumiwa na watu maarufu kupanda Mlima Kilimanjaro?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika kuongeza mapato katika nchi yetu. Kwa hiyo, ni makusudio ya Serikali kuboresha malango katika hifadhi zetu zote za Taifa katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, katika hili la Kidia, tayari Serikali inaendelea na kuboresha eneo lile. Tayari tunavyozungumza barabara ya kilometa karibu 28 ya watembea kwa miguu kwenye eneo lile imeboreshwa. Barabara karibu kilometa tisa inajengwa kwa kiwango cha changarawe na katika bajeti ya mwaka huu kupitia TANAPA zimetengwa karibu milioni mia tisa kwa ajili ya kujenga mageti kwenye eneo hilo.
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kumekuwa na wimbi kubwa la tembo kuvamia makazi ya watu na mashamba, lakini kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri amesema kuna askari wanatokea Ngara. Tumekuwa tukitoa taarifa ya uvamizi wa tembo huwa inachukuwa zaidi ya siku mbili mpaka nne kwenda kutatua tatizo hilo.

Mheshimiwa Spika, je, Serikali mtanipa lini askari watakao kaa katika Jimbo la Igalula siyo hao wa Ngara na siwajui na sijawahi kuwaona?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, tumekuwa na uvamizi na uharibifu wa mali za wananchi na mwaka jana tulikwenda kufanya tathmini wananchi zaidi ya hao 17 walivamiwa na uharibifu mkubwa. Lini mtawalipa fidia wananchi waliopata athari hizo? Nakushukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Venant Daud Protas, Mbunge wa Jimbo la Igalula kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli nchi yetu imekuwa na wimbi kubwa la matukio ya wanyama wakali na waharibifu kushambulia maeneo ya wananchi wetu. Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha kwamba pale tunapopata taarifa tunawatuma askari wetu kwa haraka kwenda kusaidia kukabiliana na changamoto hizi.

Mheshimiwa Spika, sasa tathmini iliyokuwa imefanyika ilionekana kabisa askari hawa tuliokuwa nao kwenye eneo lile wana uwezo wa kushughulikia jambo hili, lakini kwa sababu ya concern ya Mheshimiwa Mbunge baada ya kikao hiki cha leo nitakaa nae tuweze kuona ni jinsi gani tunaweza kushirikiana na halmashauri kutoa mafunzo kwa maafisa wanyama pori wa vijiji ili waweze kushirikiana na wale wa Serikali kuondokana na changamoto iliyopo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kuwalipa hawa wananchi ambao wamepata madhara haya kama nilivyosema kwenye jibu la msingi tuko kwenye hatua za mwisho za kufanya tathmini ili tuweze kuwalipa. Tathmini hii ikikamilika nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wale watakaostahili kulipwa watapata malipo yao kwa wakati.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana ninalo swali moja la nyongeza. Kwanza, niishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri ya kutia moyo. Kwa kuwa umekiri kuwepo kwa maporomoko hayo ambayo ni kivutio lakini yamepotea baada ya uchepushaji kwenye mradi wa umeme Rusumo. Je, huoni sasa ipo haja kupitia Wizara yako na Wizara ya Nishati mshirikiane kurejesha maporomoko hayo yawe kama awali ili yaendelee kuwa kivutio katika Wilaya yetu ya Ngara?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge Semguruka kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Ngara kwa kushirikiana na kampuni ya umeme ambayo itapewa jukumu la kuendesha mradi ule wa umeme pale Rusumo tayari wanamkakati wa kupanda miti katika eneo lote lile la ukanda wa mradi ule, ni imani yetu kwamba baada ya kufanyika upandaji wa miti ule hali ya upatikanaji wa maji katika eneo lile itaimarika na hivyo uwezekano mkubwa wa kivutio hiki kuendelea kutumika.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kutoa ajira kwa mkataba wa muda mfupi kwa askari wa VGS ilikuweza kupunguza tatizo kubwa ama uhaba wa askari wa wanyama pori nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inao mkakati wa kuhakikisha kwamba pale ambapo mafunzo ya askari wa vijiji yamefanyika na kumekuwa na uhitaji wa askari hawa kupatiwa ajira, tunashirikiana na halmashauri kuona jinsi ambavyo kupitia miradi mbalimbali tulioyonayo akari hawa badala ya kupewa ajira wanaanzishiwa miradi itakayowaingizia kipato ili wakati wakifanya shughuli hii ya uhifadhi lakini vilevile waweze kujiongezea kipato.

Mheshimiwa Spika, tumeanza zoezi hilo kwa mradi wa REGROW ambao unajielekeza kwenye kufungua fursa za utalii katika mikoa ya Kusini tunaamini mafunzo tutakayoyapata kutokana na mradi huu yatatuonesha ni jinsi gani tunaweza kuendeleza katika maeneo mengine.
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, kwa kuwa kivutio chetu pekee cha maporomoko ya Rusumo sasa kimepunguza mvuto baada ya uwekezaji wa mradi wa umeme pale Rusumo, Serikali haioni kuna haja sasa ya kuisaidia Ngara kuendeleza vivutio vingine ili Ngara isiondoke kwenye ramani ya kupata watalii, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndaisaba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kivutio cha Rusumo siyo kivutio pekee kilichopo katika ukanda huu tunazo mbuga za wanyama zilizoko katika ukanda huu. Vilevile, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi tunaangalia kutumia uwepo wa mradi wa umeme kuufanya kama sehemu ya kivutio. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kuendeleza utalii katika ukanda huu tutaunganisha vivutio vingine vyote vilivyopo ili Sekta ya Utalii iweze kunufaisha ukanda huu na nchi yetu kwa ujumla.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, licha ya kupeleka umeme katika Kata za Chenzema, Langala na hizo nyingine zote, naishukuru Serikali kwa sababu inachukua huduma sana kwenye umeme: Je, ni lini vijiji vya Kidunda pamoja na Ngolehanga vitaweza kupatiwa umeme? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini vijiji na vitongoji vya Morogoro vijijini vitaweza kupata umeme? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, naomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro kwa ujumla wake una vijiji vilivyohitaji kupatiwa umeme takribani 668. Vijiji ambavyo vilikuwa vipo katika mpango wa kupelekewa umeme ni vijiji 239. Mpaka sasa tumeshapeleka umeme kwenye vijiji takribani asilimia 90. Makusudio yetu ni kwamba vijiji vyote vya Mkoa wa Morogoro ikifika mwezi Juni mwaka huu viwe vimepatiwa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile mkakati wetu ni kuhakikisha kwamba tupo katika hatua ya mwisho ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 vya kila jimbo la nchi yetu na matarajio yetu ni kwamba kazi hii itakamilika, uratibu wa kazi hii utakamilika hivi karibuni na tutaweza kuanza kufanya kazi hiyo.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Ndani ya Halmashauri ya Mji wa Njombe Kata ya Kambarage kuna mitaa miwili ya Pemba na Unguja mpaka leo haina umeme: Ni lini mitaa hiyo itapata umeme? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Mwanyika, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itahakikisha kwamba vijiji vyote ambavyo havina umeme, kufika mwezi Juni vinapata umeme na vile vile kufika Juni kazi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji vyote nchini, vile 15 kama nilivyosema awali, itakuwa imefanyika.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni lini Serikali itapeleka umeme katika Kata za Mwamashele, Lagana pamoja na Mwasubi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Mnzava, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, makusudio yetu ni kuhakikisha kwamba mikataba yote ya ukandarasi wa kupeleka umeme kwenye vijiji vyetu, ile mikataba iliyowahi kufika mwezi Juni mwaka huu 2024, umeme utakuwa umepatikana. Mikataba ambayo imechelewa tutasogea mbele kidogo ikiwezekana kufika mwishoni mwa mwaka huu wa fedha (2023/2024). (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Ni lini Serikali itatekeleza mpango wake wa peri urban kupeleka umeme katika mitaa yenye sura za vijiji katika miji yetu ikiwepo katika Manispaa ya Iringa Mtaa wa Ugere, Mosi, Msisina na Mtalagala.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mpango wa kupeleka umeme kwenye maeneo ya miji yenye sura za vijiji (peri urban) na kazi hiyo inaendelea kwa sasa. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, kazi hii itakamilika, maeneo haya yatapatiwa umeme.
MHE. EMANNUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Nashukuru kwamba, ameshindwa kuthibitisha kwamba mifugo inatakiwa kutozwa shilingi 100,000 kwa kichwa cha ng’ombe wanapoingia hifadhini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wafugaji wengi Tanzania wamekuwa wakitozwa shilingi laki moja kwa kichwa cha ng’ombe wanapoingia hifadhini na kuna wananchi wametozwa mpaka shilingi milioni sabini kwa wakati mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza nini kauli ya Serikali kwa Watumishi wa TANAPA, TAWA pamoja na NCAA ambao wamekuwa wakitoza shilingi laki moja kwa kichwa cha ng’ombe?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili je, Serikali ipo tayari kurejesha fedha za wananchi ambazo wametozwa zaidi ya shilingi milioni kumi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shangai kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jibu langu la msingi nimeonyesha sheria inataka nini? Lakini sambamba na eneo hilo niseme tu kwamba, kosa la kuingiza mifugo kwa mujibu wa Sheria ya Hifadhi ya Taifa lipo pia katika Kanuni Na. 7(1) ya Kanuni za Hifadhi ya Taifa GN Na. 255 ya mwaka 1970 kama ilivyorekebishwa ambavyo Kifungu kinazuia kuingiza mifugo Hifadhini na adhabu ya kosa kuingiza mifugo ni kwa kila mfugo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nchi yetu, Serikali yetu ina heshimu Utawala wa Sheria na chombo ambacho kimekasimiwa kutafsiri sheria pale ambapo kuna changamoto ni Mahakama zetu. Nitoe rai kwamba wale wote wanaoona kwamba imepita hukumu ambayo wanaona haikuwatendea haki basi twende kwenye mfumo wa kisheria ili sheria iweze kutoa haki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hili la kurejesha bado narudi pale pale yeyote anayehisi kwamba hakutendewa haki tuzitumie Mahakama zetu ili haki iweze kutendeka. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, naomba niulize swali moja la nyongeza, ila niruhusu nijieleze kidogo.

Mheshimiwa Spika, wakati kunatokea moto kwenye mlima watu wanaokimbizana kuuzima ni wale wanaoishi kandokando ya ule mlima; pale Marangu wanabebwa, wanasombwa, wanalazimishwa kwenda kuzima moto. Sasa tulikuwa tunaomba Serikali itoe kauli kuhusiana na uwezekano wa kutoa mwongozo ili wale tour operators wawe na uwiano fulani tuseme asilimia 70 ya wahudumu wanaopandisha watalii wawe wanatoka kwenye eneo lile la pale Marangu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na tunaenda kuufanyia kazi tuone ushauri wa kitaalam utatuelekeza vipi. (Makofi)
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuondoshwa kwa maeneo ya kinga (buffer zone) kunasogeza zaidi wananchi karibu na hifadhi na kuwahatarisha na wanyama wakali na waharibifu: Je, Serikali haioni haja ya kuja na mikakati zaidi ya kutoa elimu ili kuwasaidia wananchi hawa kuwaepusha na hiyo hatari? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa buffer zone kitaalam inalenga kuwatenga wananchi na maeneo ya hifadhi na hivyo, kupunguza vitendo vya uharibifu na vitendo vya uvamizi.

Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kwamba, utaratibu huu wa kuondoa buffer zone katika maeneo ya hifadhi haujirudii? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mohammed Soud Jumah, Mbunge wa Donge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, Wizara inajielekeza sana kwenye kutoa elimu. Sambamba na hiyo, kwenye maeneo ya namna hii vilevile tuna mikakati ya kuwahamasisha wananchi kufuga nyuki kwenye maeneo hayo. Vilevile, kuendesha utalii wa kiutamaduni, kupanda au kutunza misitu ili waweze kuja na mfumo wa biashara ya uvunaji wa Hewa ya Ukaa. Tunaamini wananchi wakijielekeza kwenye maeneo haya, basi huo muingiliano utapungua athari zake.

Mheshimiwa Spika, katika swali la pili, ni kweli kwamba maeneo haya ya buffer zone yanalenga kuwatenga wananchi na maeneo ya hifadhi ili kuwaondolea athari ya madhara ya uvamizi na hivi. Pamoja na kutoa elimu, Wizara inajielekeza kwenye kusimamia sheria, kanuni na taratibu za uhifadhi na kutoa elimu kwa viongozi na wananchi. Imani yetu ni kwamba, elimu hii ikiwaingia wananchi na wakazingatia maelekezo haya, basi migogoro hii itaondoka. (Makofi)
MHE. CHRISTOPHER O. OLE-SENDEKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa wanyama hao walioko katika maeneo yetu ya uhifadhi, mara baada tu ya kuvuka kwenye buffer zine wanaingia kwenye ardhi za vijiji.

Je, Wizara au Serikali haioni kwamba kuna haja sasa ya Wizara kukaa na vijiji vinavyozunguka maeno ya hifadhi ili kwa pamoja waweze kuweka utaratibu rafiki wa namna ya kusimamia wanyama pori nje ya hifadhi za Taifa na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza katika maeneo hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ole-Sendeka kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara imekuwa ikifanya jambo hili ambalo Mheshimiwa Ole-Sendeka amelishauri. Sambamba na hilo, tumekuwa tukishirikiana vilevile na Wizara ya Ardhi katika kufanya mipango ya matumizi bora ya ardhi. Tunaamini kwa kufanya hivyo tutaepuka changamoto tunazokabiliana nazo.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, naomba sasa niwe na swali moja tu la nyongeza. Kwa kuwa maelezo ambayo Mheshimiwa Naibu Waziri umeyaeleza, vikundi vingi vilivyopewa mizinga hiyo ni vya Wilaya ya Iringa lakini kutoka Iringa Vijijini na Iringa Manispaa ni lango la utalii Kusini.

Je, mpo tayari sasa kutupatia na Iringa Manispaa ili angalau uoto wa asili urudi kwa kufuga nyuki? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mara tutakapopata orodha ya vikundi vilivyoanzishwa kwa jambo hili, Wizara itaona jinsi ambavyo inaweza kushirikiana na hamashauri ili kuweza kuwapatia mizinga. (Makofi)
MHE. NDAISABA G. RUHORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Kwa kuwa tayari Ngara kuna mkandarasi anayeendelea kujenge miundombinu ya kupeleka umeme maeneo ya Ngoma, Kata ya Bugarama, Kibogora, Mganza na Keza, na kwa kuwa mkandarasi huyu mpaka sasa hajapeleka umeme kwenye kata hizo na vijiji ambavyo viko viko kwenye kata hizo, ni upi mpango wa Serikali wa kumsukuma mkandarasi huyu ahakikishe anakamilisha kazi yake ya kupeleka umeme kwenye maeneo haya, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo ya Serikali, yako wazi kwa wakandarasi wanaoendelea na miradi ya kupeleka umeme vijijini kwamba wanapaswa kuheshimu mikataba yao. Wale ambao hawataweza kupeleka umeme kwa mujibu wa mikataba yao, basi wanakuwa wamejiweka kwenye mazingira ambayo hawatapata mikataba mingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kuwakumbusha wakandarasi wote, wafanye kazi walizopewa kwa mujibu wa mikataba yao, maana kushindwa kufanya hivyo wanajihakikishia kwamba hawatapata mikataba mipya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, natoa maelekezo kwa watendaji wetu katika mkoa ule, wamsimamie kwa karibu mkandarasi huyu ili aweze kutimiza wajibu wake. (Makofi)
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nimemwelewa vizuri sana Mheshimiwa Naibu Waziri, ni kwamba Serikali imekubali kutoa hekta 2943.8 kwa wananchi wa Kisiwa cha Maisome. Kwa niaba ya wananchi hao naomba niwasilishe furaha yao kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa Bunge lako Tukufu kwani kwa muda mrefu wameishi kwa mateso sana wakiwa hawana eneo la malisho.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu ni moja tu ni lini? Ni lini? Ni lini, kwa mara tatu mchakato huu wa kuweka mpaka utatekelezwa ili wananchi waifurahie Serikali yao? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa sheria, zoezi hili linapaswa kuchukua miezi sita. Siku 90 za kuweka mipaka, kutengeneza ramani na vilevile siku 90 ambayo ndiyo itahusisha lile tangazo nililolisema. Tumefika hatua nzuri, naomba Mheshimiwa Mbunge atupe muda, tunalikamilisha muda siyo mrefu.
MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ni Septemba niliuliza swali Na. 76 juu ya wananchi ambao wamevamia Msitu wa Bono uliopo Kijiji cha Mswaki kwenye Kata ya Msanja na Serikali ilisema itawaondoa itakapofika Desemba 30, kwa maana ya mwaka 2022. Nataka kujua: Ni nani ambaye anazuia kuondoa wananchi wale ambao wanafanya uharibifu mkubwa na msitu huo tunaoutegemea kwa ajili ya mvua? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, bado Serikali inasimamia maazimio yake yale kwamba wananchi wale wataondolewa kwenye msitu ule. Naomba Mheshimiwa Mbunge, atupe fursa tulifanyie kazi ili tutekeleze kusudio letu.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza naipongeza Serikali kwa juhudi kubwa inazofanya kuhakikisha umeme unapatikana. Wananchi wa Kyela wamekuwa ni wavumilivu sana kwa muda mrefu, umeme pamoja na ratiba ya mgao wa umeme, lakini bado kuna hitilafu za umeme ambazo zinatokea mbeya na Rungwe zinawaathiri wananchi wale. Je, Serikali haioni sasa kwamba ni wakati muafaka kuachana na mlolongo mrefu huu wa upembuzi yakinifu na kuleta mambo mengine yanayoathiri uharakishaji wa ujenzi wa kituo hiki cha umeme? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, miaka ya nyuma ya 1990, umeme Kyela ulikuwa unatoka pale Kiwira Coal Mine na wananchi wa Kyela walikuwa wanapata umeme bora kabisa, lakini sasa hivi umeme huo haufanyi kazi na haupo. Kwa kuwa tarehe 10 Agosti, 2021 TANESCO iliingia makubaliano na STAMICO ili wazalishe megawat 200 ambazo zingetokea Kyela moja kwa moja, je, Serikali haioni sasa kwamba ni wakati muafaka wa kuharakisha kuanza kwa mradi huu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaelewa kadhia wanayopata wananchi wa Jimbo lake la kukatika kwa umeme mara kwa mara. Serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha changamoto hizi zinaondoka, lakini hitimisho la muda mrefu ni ujenzi wa kile kituo cha kupoza umeme katika Wilaya ya Kyela. Kama nilivyosema, mradi huu ni sehemu ya mradi wa gridi imara ambapo katika kipindi hiki Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 470 kuhakikisha mradi ule unaweza kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kuhusu kuharakisha na kuachana na mlolongo, hatua hizi zinazofanyika sasa za upembuzi yakinifu, kufanya tathmini ya maeneo ya wananchi ambayo yakichukuliwa watahitajika kufidiwa na mambo kama hayo, ni hatua muhimu sana ili mwisho wa siku tuweze kupata mradi ambao hautakuwa na matatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira Serikali imejidhatiti kuhakikisha kwamba ndani ya kipindi kifupi kama tulivyosema mradi huu unatekelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu jibu lake la swali la pili ni kweli kwamba pale kuna mradi wa makaa ya mawe unaokusudiwa kujengwa kati ya TANESCO na wenzetu wa STAMICO. Nafurahi kusema kwamba, mwezi uliopita wataalam wa TANESCO na STAMICO wamekaa na kukubaliana kuharakisha mchakato wa ujenzi wa mradi huu katika kupitia upembuzi yakinifu uliofanyika ili kuakisi mahitaji ya sasa. Takribani shilingi milioni 400 zimetengwa kwa ajili ya kuharakisha kazi hiyo. Nimuombe awe na subira tunauhitaji sana mradi huu.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kupata jibu zuri linaloashiria uendelevu wa kumbukizi hizi. Pia napenda kuipongeza Serikali mwezi uliopita tarehe 15 ilitoa GN ya Maadhimisho haya ya Kumbukizi za Majimaji. Kwa hiyo, kwa niaba ya mashujaa 30 walioongoza vita hii pamoja na wananchi wa Jimbo la Kilwa Kaskazini, naipongeza sana Serikali kwa hatua hii, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa GN imepatikana ya kumbukizi hizi, je, ni lini Serikali itaanza kutenga fedha kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukizi hizi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Serikali ina mkakati gani kwa kushirikisha Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi ya TARURA na TANROADS kuwezesha barabara zinazokwenda kwenye kumbukizi hizi ziweze kupitika katika kipindi chote cha mwaka mzima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea pongezi za Mheshimiwa Mbunge. Kama tunavyofahamu tupo kwenye kipindi cha bajeti, niwaombe Waheshimiwa Wabunge kipindi bajeti ya Wizara hii itakapofika, basi tuweze kuipitisha ili tuweze kufanya haya ambayo yanayoombwa na Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na hili suala la barabara, barabara zote ambazo zipo kwenye maeneo ya hifadhi tunaishukuru Serikali imetupatia vifaa na fedha za kuweza kufanya ukarabati kwenye maeneo haya. Vilevile kama tulivyomsikia Waziri wa Miundombinu muda mfupi uliopita kwamba Serikali imetoa fedha za kuhakikisha inafanya ukarabati kwenye maeneo ambayo yamepata changamoto ili ziweze kupitika. Nimwombe Mheshimiwa Mbunge kwa barabara mahsusi ambazo zina tatizo hili, awasiliane na Wizara husika ili ziweze kufanyiwa kazi. (Makofi)
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, sasa kwa kuwa Serikali imeamua kuchukua hatua hizo ni namna gani imejipanga ili tatizo hili lisitokee tena na kuathiri upatikanaji wa umeme kwenye maeneo ya Sengerema kama ilivyokuwa mwanzo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini swali la pili, kwa kuwa bado kuna tatizo kubwa la kukatika kwa umeme kwenye maeneo ya visiwa vya Ukerewe na hasa kwenye maeneo ya visiwa vidogo ambako wanategemea umeme wa jua. Ni lini Serikali sasa itaondoa moja kwa moja matatizo ya umeme kwenye maeneo ya visiwa vidogo ya Visiwa vya Ukerewe?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu masala mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mkundi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye jibu langu la awali, kwamba mara baada ya tatizo hili kutokea Serikali ilikuwa inaipatia Sengerema umeme kutoka Kituo cha Mpovu kilichopo Geita. Mpango wetu wa pili sasa ni kuweka waya kupitia kwenye daraja badala ya kupitia chini ya maji ili vilevile Sengerema ipate umeme kutokea Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimhakikishie kwamba, pamoja na kwamba, lilitokea tatizo hili, lakini sasa imekuwa ni bahati kwao kwa watu wa Sengerema. Kwamba, sasa watakuwa na njia mbili za uhakika za kupata umeme. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba, umeme kwa Sengerema itakuwa tatizo hilo limeondoka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na hili la kukatikakatika kwa umeme katika maeneo ya visiwa, Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba maeneo yetu ya visiwa yanapata umeme wa uhakika. Pale ambapo teknolojia ya solar inaweza kutupatia umeme huo, tutatumia teknolojia ya kisasa kuhakikisha kwamba umeme unapatikana. Pale ambapo mazingira yataruhusu kupata umeme kutoka kwenye gridi, Serikali itafanya hivyo.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, mkandarasi anayejenga Mradi wa Umeme Kijiji cha Kigurunde na Kijiji cha Makanka amechelewesha mradi ule sasahivi ni zaidi ya miezi sita.

Je, nini kauli ya Serikali juu ya mkandarasi huyu kuchelewesha mradi ule?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Shekilindi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapenda kurudia kauli yake na maelekezo kwa wakandarasi, kwamba wanapaswa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ya kupeleka umeme kama ambavyo tumekubaliana nao kwenye mikataba. Mkandarasi yeyote ambaye atashindwa kutimiza wajibu wake aelewe kwamba, amejihakikishia, kwamba hatutampatia tena kazi katika nchi yetu. (Makofi)

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwa kuwa Serikali iliweka mkakati wa kukarabati mitambo na njia za umeme, ili kumaliza tatizo la katakata ya umeme na migawo ya umeme.

Je, tangu programu hiyo ilivyoanza mwaka 2022 Serikali imeweza kupunguza kwa kiasi gani katakata na migawo ya umeme inayoendelea wakiwemo wananchi wangu wa Jimbo la Kisesa?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, mambo haya ya teknolojia huwezi kuwa na uhakika wa asilimia mia moja. Mambo haya ya umeme tatizo linaweza kutokea wakati wowote, unaweza kufanya matengenezo leo, kesho likatokea tatizo umeme ukakatika. Niombe tu aendelee kuiamini Serikali kwamba, tutajitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuhakikisha tunaondokana na matatizo haya. (Makofi)
MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama za ujenzi katika Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ni takribani trilioni 6.5 na CSR ambayo inatakiwa kulipwa kwa Halmashauri ya Morogoro Vijijini na Halmashauri ya Rufiji ni takribani bilioni 276. Siku za nyuma Serikali kupitia Wizara ilitaka fedha hizo za CSR za ujenzi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere ziende zikajenge Uwanja wa Mpira Dodoma. Mkandarasi alikataa kwa sababu, utaratibu wa mkataba unakataza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini katika Bunge hilihili katika Taarifa iliyoletwa na Kamati ya Bajeti ilisema kwamba, fedha za CSR zinataka kwenda kujenga Chuo cha TEHAMA Kigoma bilioni 80, kujenga Chuo cha Gesi Asili ya Lindi bilioni 80, lakini kujenga vyuo vya utabibu Dodoma na Tanga bilioni 80. Juzi Mheshimiwa Rais wakati anasimamia uitiaji saini wa vitalu vya gesi alisema, fedha za CSR ziendelee kunufaisha wananchi katika maeneo husika na sababu za kunufaisha wananchi katika maeneo husika ni kwamba kwanza wananchi wale ni walinzi wa mradi, lakini wananchi wale ni waathirika kwa sababu, kuna mahali kushoto au kulia wanakosa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali; hizi fedha bilioni kumi-kumi ambazo tunapewa Halmashauri ya Morogoro Vijijini kwa ajili ya ujenzi wa hospitali yenye hadhi ya Wilaya katika Kata ya Kisaki na Wananchi wa Rufiji katika Kata ya Nyamwage ni nini? Ni sehemu kwamba, bado tutaendelea kupata fedha katika mradi huu au ndio zimekwisha? Na kama zimekwisha, Serikali inasema nini kwa Wananchi wa Halmashauri ya Morogoro Vijijini na wananchi wa Halmashauri ya Rufiji kuhusu fedha yao hii ambayo ni haki Kikatiba, je, kuna double standard katika nchi hii katika CSR, kwamba kuna wengine wanapewa wengine hawapewi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa naba ya Waziri wa Nishati, naomba kujibu swali moja la Mheshimiwa Kalogeris, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nitumie fursa hii kusema kwamba Serikali inaelewa concerns za Wabunge wa Morogoro na Pwani. Jambo hili limekwishafika Serikalini, Mkuu wa Mkoa wa Pwani alitufikishia, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro alitufikishia na hata kwenye Kamati ya Nishati jambo hili lilifikishwa, itoshe kusema jambo hili ni la kimkataba, hizo changamoto zilizojitokeza tumeziona, Serikali inafanyia kazi changamoto hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ipo tayari kwa kushirikisha wadau wote wanaohusika na jambo hili, kupitishana kwenye yale ambayo tunayafanyia kazi ili mwisho wa siku tuweze kupata ufumbuzi wa pamoja. Namuomba Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, Serikali imeelewa na tupo tayari kulifanyia kazi. (Makofi)
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kulipa fidia kutokana na madhara wanayopata raia kwa vitendo vya baadhi ya watumishi wabaya wa TFS? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Almasi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, masuala yote ya haki za binadamu yanatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo. Nimhakikishie Mheshimiwa Almasi, pale watumishi wetu watakapokuwa wamefanya makosa chini ya sheria hizo, fidia stahiki zitatolewa kwa mujibu wa sheria iliyopo. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itawalipa fidia kwa kifuta machozi kwenye Vijiji vya Hunyari, Kihumbu, Mariwanda, Sarakwa, Mugeta Kyandege na Tingirima?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za kufanya uhakiki na uthamini wa madai ambayo tumeyapokea na pindi uthamini huo utakapokamilika, tutawalipa wahusika haraka iwezekanavyo.
MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali moja la nyongeza kwa Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi hawa wa Kijiji cha Ngombo wamekaa muda mrefu wakisubiri hiyo fidia ili waweze kuondoka kiasi ambacho wameshindwa kulima lakini pia wameshindwa shughuli nyingine zozote za kijamii ili kuweza kukidhi mahitaji yao na familia zao; je, nini kauli ya Serikali?

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati kipindi hiki tunasubiri kupata fidia, je wananchi waendelee kuandaa mashamba yao ili kusudi waweze kujipatia chakula na kipato kwa ajili ya familia zao?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninawashukuru wananchi hawa kwa jinsi ambavyo wamekuwa na subira kuruhusu mchakato huu wa fidia ambao ni muhimu sana kufanyika uweze kukamilika. Nawaomba waendelee kuwa na subira, tunaamini ndani ya kipindi kifupi fidia hii itapatikana, kwa hiyo, wataendelea na maisha yao kama kawaida.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, hivi sasa utaratibu wa fidia nchini kwa wanaoathiriwa na wanyama haueleweki vizuri. Serikali ina mpango gani wa kuweka wazi utaratibu huu wa fidia kwa wananchi wanaoathiriwa na wanyama katika mali zao na maisha yao?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, fidia kwa wananchi wanaopata madhara ya wanyama inafanyika kwa mujibu wa sheria na kanuni ambayo iko wazi na tumekuwa tukiisema mara kadhaa katika Bunge hili na kwa bahati nzuri kanuni hizi zimesambazwa kwa Maafisa Hifadhi wote wa halmashauri zetu ambao tunaamini na wao wanafanya kazi ya kutoa semina kwenye vijiji vyetu, lakini kama haieleweki natoa rai kwa Maafisa Wanyamapori katika halmashauri zetu waendelee kufanya kazi nzuri hii ya kutoa elimu kwa wananchi ili jambo hili lieleweke.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, wananchi wa Vijiji vya Mvugwe, Makere, Kitagata, Nyachenda, Nyamidaho, Mugombe na Nyakitonto na kata nyingine ambazo sikuzitaja zimezunguka Hifadhi ya Makere Kusini na kwa sasa wananchi hao wanazuiliwa kuvuna mazao yao; je, Serikali iko tayari kuiagiza TFS na watu wa Kitalu cha Kagerankanda kilichopo Kabulanzwili ili wananchi waweze kuvuna mazao yao?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kati ya ekari 10,000 zilizotolewa na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Magufuli ni vijiji viwili tu vilivyoweza kupata ambapo ekari 2,496 ziligaiwa Kijiji cha Kagerankanda na Kijiji cha Mvinza kilipata hekta 2,174, lakini ekari hizo 5,000 zilizobaki zimechukuliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu. Vijiji vyote hivyo nilivyovitaja kwa maana ya Mvugwe, Makere, Kitagata, Nyachenda, Mugombe, Nyakitonto, Nyamyusi na Kulugongo vyote vinategemea hifadhi hiyo ya Makere.

Je, Serikali iko tayari kukaa na Wizara ya TAMISEMI ili hizo hekta 5,000 zilizochukuliwa na Halmashauri ya Kasulu DC zirudishwe kwa wananchi wa vijiji hivyo niulivyovitaja?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Genzabuke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo hili la wananchi kulima kwenye hifadhi limekuwa likiendelea kwa muda mrefu, lakini vilevile tulipata maombi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kigoma na Kagera tulipokaa nao kwamba yale maeneo ambayo wananchi wamelima kwenye hifadhi waruhusiwe kuvuna mazao yao, lakini wasiruhusiwe kulima tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara imekwishatoa maelekezo kwa wahifadhi wetu wa maeneo haya kwamba wananchi waliolima kwenye hifadhi waruhusiwe kuvuna mazao yao, lakini wasiruhusiwe kuendelea kupanda kwenye hifadhi hizi. Ninawakumbusha wahifadhi wetu agizo hili bado linasimama na sasa Serikali au Wizara tutafuatilia wahifadhi wetu wote ambao hawajatekeleza agizo hili na hatutasita kuchukua hatua. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, wakati tulipopata maelekezo ya kumega ardhi kwa vijiji hivi, vilevile tulipewa maelekezo ya kutenga eneo kwa ajili ya halmashauri kwa shughuli za uwekezaji, lakini vilevile kuwa akiba endapo yatatokea mahitaji ya ziada, wananchi waweze kupewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa sababu eneo hili sasa hizi hekta 5,000, zinamilikiwa kisheria na halmashauri, tutaendelea kuwasiliana na wenzetu wa halmashauri kuona namna bora ya ardhi hii kutumika kwa mujibu wa sheria kwa sababu halmashauri hii wananchi hawa ni wananchi wake. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kwanza majibu hayo ni kweli kabisa, nawapongeza sana Serikali na mratibu wa REGROW Ndugu Saanya pamoja na Wizara kwa kazi kubwa mliyofanya kuanza ujenzi wa kituo hiki, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa moja ya mkakati mkubwa uliotumika kuinua utalii nchini kwa miaka mitatu iliyopita ni kupitia Royal Tour, je, ni lini mkakati kama huu utatumika pia ku-promote utalii Kusini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, utalii wa vyakula ni moja ya vitu ambavyo watalii wanapenda, ni namna gani Wizara iko tayari kutusaidia kama Manispaa ya Iringa ili tuweze kujikita kwenye utalii wa vyakula hasa ukizingatia kwamba sisi huwa tuna vyakula vingi ambavyo watu wengine kama nyama? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyoneza ya Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama tulivyoeleza wakati wa bajeti yetu, baada ya uzinduzi wa filamu ya Royal Tour tumezindua filamu nyingine inaitwa Amazing Tanzania. Sasa hivi tuko kwenye kazi ya ku-promote filamu hiyo ili tuweze kuona jinsi ambavyo inaweza kufungua soko la utalii kwenye Bara la Asia. Tutafanyia monitoring ya mafanikio ya filamu hiyo ili tuweze kujipanga kuweza kutangaza maeneo mengine zaidi kupitia filamu za namna hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili, katika kukuza utalii wa Nyanda za Juu Kusini tumekuwa na shughuli mbalimbali tunazozifanya, mojawapo ni utalii wa kiutamaduni. Ninawaomba wananchi wa ukanda huu kupitia dirisha hili la utalii wa utamaduni waweze kuendelea kujiunga na kuonesha mahitaji ya kufanya shughuli hii ya utalii wa utamaduni kupitia mambo haya ya chakula ili mradi uweze kuwafadhili.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa kuwa Mradi huu wa REGROW ni package mojawapo kuhakikisha kwamba wananchi wa Iringa na Nyanda za Juu Kusini wanapatiwa elimu ili waweze kujiajiri kupitia utalii.

Je, ni kwa kiasi gani sasa mmejipanga kuhakikisha wananchi wa Iringa na Nyanda za Juu Kusini wanaopatiwa hiyo elimu ili waweze kuupokea utalii?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, swali lake moja la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kupitia Mradi wa REGROW tayari tunavyo vikundi takribani 600, ni vikundi vya kijamii ambavyo vinatokana na maeneo haya ambayo yana ufadhili wa eneo hili na kumekuwa na ufadhili mbalimbali wa miradi yao kijamii ikiendelea, lakini vilevile tukifanya shughuli ya kutoa mafunzo kwa vikundi hivi ili vifikie mahali ambapo tunaweza kuvifadhili.

Mheshimiwa Spika, nimtoe shaka kwamba tutaendelea na kazi hii ya kutoa elimu. Sasa hivi tunavijengea uwezo vikundi hivi 600, kazi itaendelea. Naomba tuwasiliane ili tuone ni vikundi vya namna gani viko kwenye maeneo hayo aliyoyasema na tuweze kuviingiza kwenye mpango wetu. (Makofi)
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Spika, ahsante, katika Mradi wa REGROW kuna sehemu ya mradi wa uwekezaji wa kijamii ikiwemo vijana katika sehemu inayotekeleza miradi hii. Je, Serikali inaweza kuniambia ni kwa namna gani makundi ya vijana yanafaidika na Mradi huu wa REGROW?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Munira swali lake kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema hapo awali, utaratibu wa mradi huu ni kufadhili vikundi na mpaka sasa tunavyo takribani vikundi 600. Tayari tumeshatoa uwezeshaji au mikopo kwa vikundi visivyopungua 150. Zaidi ya shilingi bilioni tano zimetolewa kwa ajili ya miradi ambayo inaibuliwa na vikundi hivi.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Mbunge kama kuna kikundi mahususi anadhani hakijaingizwa kwenye utaratibu huu tuweze kushirikiana ili tuweze kuvipatia uwezeshaji.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, REGROW Phase One Kitulo tuliwaacha, REGROW Phase Two ni ipi ahadi ya Serikali mtatupatia miradi barabara, miradi ya accommodation na uwanja wa ndege? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kwa sababu tuko kwenye maandalizi, tuko kwenye kukamilisha REGROW Phase One lakini vilevile maandalizi ya REGROW Phase Two, nimhakikishie tutachukua mawazo yake ili tuweze kuyajumuisha kwenye mchakato wa kuona jinsi ambavyo tutakuja na miradi ya ziada kwenye eneo hilo.
MHE. NEEMA G. MWANDABILA: Mheshimiwa Spika, kupitia huu Mradi wa REGROW natamani kufahamu wana mkakati gani wa kuwekeza kwenye hoteli kwenye maeneo ambayo wanakuwa wamejenga vituo vya utalii, mfano ile Ngorongoro Reservation ambayo iko pale Ndolezi, Mkoa wa Songe?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, msingi wa REGROW ni kujenga mfumo ambao utawezesha kutangaza utalii kwenye maeneo haya. Sasa yapo maeneo ambayo mradi kama mradi unafanya wenyewe, lakini yapo maeneo ambayo tunafanya kutoa chachu kwa sekta binafsi ione umuhimu wa kuja kuwekeza kwenye maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa sekta binafsi iliyoko kwenye maeneo haya iweze kujiingiza kwenye utekelezaji wa miradi hii na hata yale maeneo ya hoteli ambayo tunaanzisha bado tutahitaji sekta binafsi ije ishirikiane na sisi kuendeleza.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tuko tayari kupokea mawazo yake na baada ya hapa tukae pamoja tuone jinsi gani kuweza ku-accommodate mawazo aliyonayo.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Wilaya ya Kyerwa Kata ya Kamuli ina eneo linalovutia sana utalii kupitia hot spring na ni eneo ambalo hutumika kwa ajili ya kuponya magonjwa, watu wanaweza kutumia yale maji kuweza kupona magonjwa mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, nataka kujua ni kwa kiwango gani tunaweza kutumia Mradi wa REGROW kulitangaza hilo eneo likaingiza fedha kwenye wilaya lakini na Taifa kwa ujumla kwa sababu ni potential sana?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Mradi wa REGROW ni kwa ajili ya Nyanda za Juu Kusini, sasa kwa eneo hili ambalo Mheshimiwa Mbunge amelisema tutawaagiza wataalamu wetu waende wakalione eneo hilo ili tuione fursa iliyopo kwa sababu tunafahamu kwamba maeneo mengi ya namna hii wenzetu wa Wizara ya Nishati wameyaainisha kama maeneo ya kujenga mifumo ya umeme wa joto ardhi. Kwa hiyo, tutaenda kuangalia eneo hilo tuone potential iliyopo na tuone ni jinsi gani tunaweza kuliendeleza.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa ni miaka 86 toka kimondo hiki kichukuliwe kule Ivuna Jimbo la Momba, kimekuwa kikihifadhiwa kwenye hiyo museum iliyopo huko London. Je, sisi kama Wana-Momba tutanufaika vipi na kile ambacho wanakipata kwenye museum yao na Taifa kwa ujumla, baada ya miaka 86?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Mahali hapo ambapo kilichukuliwa kimondo kwenye Kijiji cha Itumbula Kata ya Ivuna zipo taarifa nyingi ambazo zinazunguka eneo hilo ambazo zinavutia kwa ajili ya mambo ya utalii. Je, ni lini Wizara ya Maliasili na Utalii mtafika eneo hilo la Itumbula, Ivuna ili mweze kukutana na wazee wa mahali hapo tuweze kuwasimulia historia nzuri ya kupendeza katika eneo hilo?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi kwamba Serikali imeunda timu ya Kitaifa ya kuishauri namna bora ya kunufaika na uwepo wa malikale katika nchi za wenzetu ambazo zimetokea katika nchi yetu. Namwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira, Kamati hii au timu hii inafanyia kazi mambo haya na itaishauri Serikali namna nzuri ya sisi kunufaika na malikale hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye swali lake la pili kwamba ni lini tutakwenda kwenye eneo lile, nataka kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara tayari imeshafika kwenye eneo lile na imeanzisha tamasha ambalo hufanyika kila mwezi Juni. Tamasha hilo linaibua fursa za kiutalii kwenye eneo hilo na wataalamu wetu wanakamilisha michakato ya kujumuisha eneo hili liwe sehemu ya tamasha linalofanyika katika mkoa ule.
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa kupitia Ilani ya Chama chetu tuliwaahidi wananchi kwamba kwenye mapori yetu tutatenga maeneo ya kuishi watu, lipo pori la Kigosi ambalo limepakana na Kata ya Iponya na Kata ya Bukandwe: Ni lini Serikali itatenga maeneo ya kuishi watu ili waweze kufanya shughuli zao na kuishi kwa uhuru na amani kwenye hiyo hifadhi?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali hili lililoulizwa ni tofauti sana na swali la msingi. Naomba kumshauri Mheshimiwa Mbunge alilete swali hili kama swali mahsusi ili niweze kulijibu kikamilifu.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na pia nashukuru kwa majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa maeneo yaliyotajwa yanatumiwa na wananchi wa kata hizo kwa kilimo kwa karne kadhaa na hawa wananchi wamekuwa vinara wa kutunza mazingira na kwa uthibitisho hao viongozi wawili wa kimila walitambulishwa hapa Bungeni wiki iliyopita kulipokuwa na maadhimisho ya kutunza mazingira.

Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari sasa akatembelee hayo maeneo akaongee na wananchi na vilevile pamoja na kutatua mgogoro ambao haujaisha akawapongeze kwa ajili ya kutunza mazingira? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa vile hawa wananchi wamekuwa vinara wa kutunza mazingira na wamefanya vizuri sana na kiasi kwamba wao ni walinzi wazuri kuliko hata hao askari.

Je, Wizara haioni umuhimu wa kuanza kushirikiana na wananchi kutoa misaada ya CSR kwa ajili ya kuwashirikisha ili kuwapa motisha ya kutunza mazingira? Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali lake la kwanza, niko tayari kwenda kutembelea eneo hili ili tuweze kufanya hayo ambayo ameeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na swali la pili, Wizara kupitia taasisi zetu tuna mipango ya ujirani mwema kwa wananchi wanaozunguka kwenye maeneo ya hifadhi zetu. Niwaagize wataalamu wetu walioko uwandani waende kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi hii ili wakafanye kazi ya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uibuaji wa miradi ya kijamii ili hatimaye miradi hiyo iweze kupata ufadhili.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itamaliza mgogoro wa mpaka kati ya Pori la Akiba la Selous na Kijiji cha Mtepela? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utatuzi wa migogoro ni mchakato na tunavyozungumza kuna mchakato wa utatuzi unaendelea. Namwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira tukamilishe kazi ile ili tuweze kuondokana na changamoto hii.
MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lini Serikali itamaliza mgogoro uliopo katika Kitongoji cha Isela, Kijiji cha Ndolezi na eneo la Kimondo kati ya wananchi na Ngorongoro?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema kwenye swali lililopita, utatuzi wa migogoro ni mchakato naomba tutoe fursa kwa Serikali iweze kushughulikia migogoro hii ili iweze kumalizika.
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, mgogoro kati ya TFS na Kijiji cha Kapyo, Kata ya Mahongole, Wilaya ya Mbarali tayari ulishamalizika baada ya wataalamu wa TFS wa Kanda kukaa kikao cha pamoja na wataalamu wa halmashauri pamoja na wanakijiji. Kinachosubiriwa kutoka Wizarani ni barua ambayo itawaruhusu sasa wale wanakijiji kuendelea na shughuli zao. Ni lini sasa tutapata hiyo barua ili kijiji hiki kiendelee na shughuli zake? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie fursa hii kuuagiza uongozi wetu wa TFS kwa haraka sana uweze kutoa barua hiyo ili kumaliza jambo hili. (Makofi)
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati gani thabiti wa kukomesha ukataji miti hovyo? Swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Serikali inawachukulia hatua gani wale waliobainika kukata miti hovyo na kusababisha nchi yetu kuwa jangwa?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kwa pamoja kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TFS imekuwa ikifanya doria mbalimbali za kuhakikisha ukataji miti hovyo unazuiliwa. Vilevile, imekuwa ikichukua hatua kwa wale wote ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivi kuwafikisha Mahakamani kwa mujibu wa sheria ili kuchukuliwa hatua.
MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa hatua nzuri ambazo imezichukua, je, Serikali haioni tija kuharakisha jambo hili kwa sababu limekuwa ni jambo la muda mrefu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kutokana na Jimbo la Ulanga kuwa limezungukwa na msitu pamoja na hifadhi na tembo wamekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba inadhibiti tembo hao kwa sababu imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaona nia, inaona haja ya kuharakisha jambo hili na ndiyo maana kazi kubwa imefanyika ya kuhakikisha mchakato wote umekwenda kama unavyotakiwa, sasa tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kisheria. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ndani ya mwaka huu wa fedha jambo hili litakamilika. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika kwamba biashara ya hewa ukaa ni biashara ambayo ni mpya kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo elimu inahitajika kutolewa ili maeneo mengi ikiwemo Halmashauri ya Kalambo iweze kufaidika. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunanufaika na biashara hii? Nakushuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba ipo haja ya elimu ya jambo hili kutolewa na ndiyo maana Ofisi ya Makamu wa Rais, eneo la Mazingira imekuwa ikiendelea kutoa elimu hii. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Maliasili kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira tutaendelea kufanya jambo hili ili uelewa uweze kusambaa kwa wananchi.
MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa hatua nzuri ambazo imezichukua, je, Serikali haioni tija kuharakisha jambo hili kwa sababu limekuwa ni jambo la muda mrefu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kutokana na Jimbo la Ulanga kuwa limezungukwa na msitu pamoja na hifadhi na tembo wamekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba inadhibiti tembo hao kwa sababu imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaona nia, inaona haja ya kuharakisha jambo hili na ndiyo maana kazi kubwa imefanyika ya kuhakikisha mchakato wote umekwenda kama unavyotakiwa, sasa tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kisheria. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ndani ya mwaka huu wa fedha jambo hili litakamilika. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika kwamba biashara ya hewa ukaa ni biashara ambayo ni mpya kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo elimu inahitajika kutolewa ili maeneo mengi ikiwemo Halmashauri ya Kalambo iweze kufaidika. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunanufaika na biashara hii? Nakushuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba ipo haja ya elimu ya jambo hili kutolewa na ndiyo maana Ofisi ya Makamu wa Rais, eneo la Mazingira imekuwa ikiendelea kutoa elimu hii. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Maliasili kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira tutaendelea kufanya jambo hili ili uelewa uweze kusambaa kwa wananchi.
MHE. SALIM A. HASHAM: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naipongeza Serikali kwa hatua nzuri ambazo imezichukua, je, Serikali haioni tija kuharakisha jambo hili kwa sababu limekuwa ni jambo la muda mrefu?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kutokana na Jimbo la Ulanga kuwa limezungukwa na msitu pamoja na hifadhi na tembo wamekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga. Je, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba inadhibiti tembo hao kwa sababu imekuwa ni kero kubwa sana kwa wananchi wa Jimbo la Ulanga? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaona nia, inaona haja ya kuharakisha jambo hili na ndiyo maana kazi kubwa imefanyika ya kuhakikisha mchakato wote umekwenda kama unavyotakiwa, sasa tuko katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za kisheria. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ndani ya mwaka huu wa fedha jambo hili litakamilika. (Makofi)
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni ukweli usiopingika kwamba biashara ya hewa ukaa ni biashara ambayo ni mpya kwa nchi yetu ya Tanzania, hivyo elimu inahitajika kutolewa ili maeneo mengi ikiwemo Halmashauri ya Kalambo iweze kufaidika. Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunanufaika na biashara hii? Nakushuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba ipo haja ya elimu ya jambo hili kutolewa na ndiyo maana Ofisi ya Makamu wa Rais, eneo la Mazingira imekuwa ikiendelea kutoa elimu hii. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Maliasili kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira tutaendelea kufanya jambo hili ili uelewa uweze kusambaa kwa wananchi.

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa biashara ya kaboni, je, Serikali ina mkakati gani wa kuimarisha biashara hiyo ya kaboni Tanzania Bara na Zanzibar?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na kampeni endelevu ya upandaji miti nchini, je, kampeni hii inakidhi utunzaji wa mazingira? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kwamba elimu hii inatolewa, Ofisi ya Makamu wa Rais imekuwa na jukumu la kusimamia jambo hili na kwa mahsusi kabisa Kituo cha Taifa cha Uratibu wa Usimamizi wa biashara hii inafanya kazi kubwa ya kuwaelimisha wananchi na kama mnavyofahamu tayari Serikali ilitunga kanuni za usimamizi na udhibiti wa biashara ya kaboni ya mwaka 2022. Niwaombe wadau wetu wapate fursa ya kutembelea kwenye kituo chetu cha Taifa cha Uratibu na Usimamizi ili kupata taarifa za msingi za jinsi ya kuweza kushiriki kwenye biashara hii.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo wananchi takribani 400,000 kutoka kata sita za Jimbo la Busanda wanaofanya shughuli za kiuchumi kwenye maeneo haya kwa sababu hayana miti, lakini Serikali imesema wazi kwamba inakwenda kuanza kupanda hekta 100 kati ya hekta 50,000. Kwa hiyo, hekta karibu 50,000 zinabaki hazijafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili. Kwa nini Serikali isiruhusu eneo fulani litumiwe na wananchi kwa shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo kwa sababu hekta 50,000 zitakuwa zimebaki?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa nini wananchi wasigaiwe miche na TFS ili waanze kupanda miche hiyo wakati wakiendelea na shughuli za kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge yote kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, eneo la msitu lililoharibika ni hekta 2,000 na siyo hekta 50,000 kama Mheshimiwa alivyokuwa anasema, lakini kwa sababu jambo analolishauri lipo katika taratibu zetu, pale ambapo tuna mpango wa kupanda miti huwa tunatoa ridhaa kwa wananchi kushiriki kwenye kupanda miti kwenye maeneo hayo, lakini vilevile kufanya shughuli za kilimo kwenye maeneo yale ambayo yamepandwa miti. Pale inapotokea kwamba miti hiyo imeshakua mikubwa, wananchi wanaacha kufanya shughuli hiyo ya kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hili tunalichukua, namwomba Mheshimiwa Mbunge tuwasiliane ili tuweze kuweka mkakati utakaokuwa jumuishi kwa wananchi wote wanaohitaji kufanya shughuli hii na kuona mahitaji ya miche ya miti inayohitajika ili tuweze kujipanga na kuweza kutoa ridhaa na kuwasaidia.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, vitongoji 115 vilivyosalia ni vingi kwa idadi na wananchi wanahitaji umeme, je, ni lini kwa uhakika wananchi hao watapelekewa huduma hiyo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mkandarasi aliyepewa kazi ya ujazilishi bado anatusuasua kutekeleza mradi huo, nini kauli ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na vitongoji 115 kwa sasa REA inakamilisha hatua za mwisho za kumpata mkadarasi, ni imani yetu ni kwamba ndani ya wiki moja ijayo mkandarasi huyu atakuwa amesaini mkataba. Aidha, kazi hiyo inatarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao.

Mheshimiwa Spika, kwa lile swali lake lingine, ninaielekeza REA wamsimamie kwa ukaribu mkandarasi yule aweze kutimiza wajibu wake.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Nina maswali mawili ya kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali la kwanza; Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro ni wadau muhimu sana wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwashirikisha Wabunge hawa kwenye hii programu ya kupanda miti ili hili zoezi liweze kufanikiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tafiti nyingi zinazofanywa hapa nchini kuhusiana na Mlima Kilimanjaro, zinafanywa na watafiti kutoka nje ya Tanzania. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwashirikisha watafiti wazawa na kuwawezesha ili waweze kushiriki kwenye kuulinda huu mlima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, siku zote wamekuwa ni wadau muhimu katika kushajihisha shughuli za kimaendeleo katika nchi yetu. Kwa hiyo, Wizara tuko tayari kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro katika upandaji wa miti. Taasisi yetu ya Hifadhi ya Kilimanjaro ina mpango wa kutoa miche kwa watu ili waweze kuipanda nje ya maeneo ya Mlima Kilimanjaro. Kwa hiyo, tuko tayari kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge na kuwapatia miche hiyo, nitaomba leo mchana tukutane na Waheshimiwa Wabunge wote wa Mkoa wa Kilimanjaro ili tuweze kuainisha mahitaji yao na tuweze kuona jinsi ambavyo tunaweza kushirikiana nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la tafiti, ni kweli kwamba zipo tafiti zaidi ya tano ambazo zimefanywa na watafiti kutoka nje, lakini wakati wote walipofanya tafiti hizi walishirikisha watafiti wa Kitanzania, lakini kwa sababu tunafahamu kwamba suala la mabadiliko ya tabianchi ni suala mtambuka, taasisi zetu sasa za hapa nchini kama SUA, University of Dar es Salaam, UDOM, Nelson Mandela na nyinginezo zimeshiriki kikamilifu katika kufanya tafiti zinazoendana na kupata afua zitakazosaidia kwenye mabadiliko ya tabianchi. Ni imani yetu kwamba tafiti hizi zitatusaidia sana kama nchi kuwa na uelewa mpana wa tatizo tunalokabiliana nalo. (Makofi)
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri. Mwaka 1955 wakati hifadhi hii inaanzishwa Wananchi wa Vijiji vya Maisome walikuwa wakiishi mahali pale. Kwa sasa hivi eneo lililopo haliwatoshi kwa sababu, idadi ya watu imeongezeka. Mwaka jana wakati wa bajeti Wizara ilitoa siku 90 peke yake, ingekuwa imekamilisha mchakato huu. Swali la kwanza; sasa, wananchi wa Kata ya Maisome pamoja na Buhama wanataka kujua Serikali inatoa siku ngapi tena ili suala hili liweze kukamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa sababu, sasa hivi wananchi wakienda kusenya kuni msituni wanakamatwa na Maafisa wa TFS. Je, Serikali kabla mchakato huu haujakamilika, iko tayari kuwaruhusu wananchi waendelee kusenya kuni badala ya kukamatwa wanapokwenda kufanya kazi hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shigongo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, tulipojibu swali kama hili Bunge lililopita, tulisema Serikali inakamilisha taratibu hizi ambazo nimezisema sasa kwamba, zimekamilika. Tunasubiria sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ipitishe mabadiliko yale, ili tangazo rasmi litoke. Wakati ule nilisema tangazo lile likitoka, ndipo ambapo wananchi watapewa siku 90 za kuweza kueleza either kukubaliana na mabadiliko yale au kama wana hitaji lolote la nyongeza. Kwa hiyo, siku 90 ni baada ya tangazo kutolewa ndipo ambapo wananchi watapata muda huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, kuhusiana na wananchi kuruhusiwa kuokota kuni. Nataka nimhakikishie tayari mpango huo upo na sasahivi wananchi hawazuiliwi kukusanya kuni, kwa ajili ya matumizi yao ilimradi wanafuata utaratibu uliopangwa.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Je, ni lini Wizara ya Maliasili na Utalii itafika Jimbo la Momba kufanya ziara ili kushuhudia changamoto ya wananchi wa Mbao, Itumbula, Moravian, Tontela pamoja na Mbalwa. Changamoto ambazo wanazipitia baada ya kukosa sehemu ya kulima na hata sehemu ya kuokota kuni kwa sababu, wamezungukwa na hifadhi?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ipo tayari kwenda kufanya ziara hiyo mara baada ya kuahirishwa kwa Bunge hili. Tutakaa na Mheshimiwa Mbunge ili tuweze kupanga kipindi sahihi cha kwenda kufanya ziara hiyo.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Nyatwali yenye Vijiji vitatu, Tamau, Serengeti na Nyatwali, imekuwa katika mgogoro mrefu wa kusubiria malipo, lakini vilevile wamekuwa wakiilaumu Serikali kwamba, wanataka kulipa fidia ndogo, tathmini wamefanya zaidi ya mwaka na tunasikia kuanzia Tarehe 05 wana mpango wa kuwalipa. Wanataka kujua wanalipwa kwa fidia ipi? Ileile ya malalamiko, mbali ya kwamba, wamekiuka taratibu zaidi ya miezi sita na hawajawalipa? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Bulaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za fidia zinafahamika kwa mujibu wa Sheria. Uthaminishaji unapofanyika wananchi wanapaswa kulipwa kwa vigezo hivyo, lakini kama malipo yatakuwa yamechelewa zaidi ya miezi sita, upo utaratibu wa kuwalipa pamoja na riba, kwa ajili ya kufidia muda uliopotea. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na imani kwamba, wananchi watapatiwa haki yao kama vile wanavyostahili. (Makofi)
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapongeza Serikali kwa majibu mazuri ambayo wameyatoa lakini nataka kufahamu tu kwamba, yapo maeneo mengi katika nchi yetu ambayo yanafaa sana kwa ufugaji wa nyuki. Ninashukuru wamesema wanaanza mikakati ya kuelimisha Watanzania, lakini naomba niulize; swali la kwanza; ni upi sasa mkakati ambao Serikali imejiwekea ili wale wananchi ambao wanaishi kule vijijini wapate kwa uhakika elimu hii ili ilete manufaa kwa wafugaji wa nyuki wanaoishi vijijini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Mheshimiwa Waziri anaweza kuongozana nami kwenda katika Jimbo la Newala Vijijini ili aone namna ambavyo mazingira yetu ni mazuri kwa ufugaji wa nyuki na kuleta hamasa kwa wananchi wa Newala Vijijini? Nakushukuru (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Maimuna, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tumekuwa na mipango mbalimbali ya kutoa elimu kwa wananchi na kama mnavyofahamu kwenye kila Halmashauri tunao Maafisa Nyuki. Kwa hiyo, tumekuwa tukiwajengea uwezo ili waweze kutoa elimu hiyo. Vilevile, kupitia makongamano ambayo tumekuwa tukiyaandaa tumekuwa tukitoa elimu kwa wananchi na pale ambapo kuna vikundi ambavyo vinahitaji kupatiwa elimu, tumeweza kuwasaidia Maafisa Nyuki waliopo kwenye Halmashauri zetu kuweza kutoa elimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninatoa wito kwa wananchi kujiingiza kwa nguvu kubwa katika ufugaji wa nyuki, kwa sababu biashara ya asali na bidhaa zinazoambatana nazo ni kubwa na hivi karibuni Serikali imefanya jambo kubwa. Tumeweza kupata soko kubwa kule Nchini China ambalo kwa mwaka wanahitaji tani 38,000,000. Kwa hiyo, hii ni fursa kwetu sasa kuweza kuchangamkia soko hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali la pili, nipo tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwenda Newala kuona jinsi ambavyo tunaweza kushirikiana, kuhamasisha ufugaji wa nyuki na biashara hii katika eneo hilo.
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Nina maswali mawili ya kumuuliza Mheshimiwa Naibu Waziri. Swali la kwanza; Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro ni wadau muhimu sana wa Wizara ya Maliasili na Utalii. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwashirikisha Wabunge hawa kwenye hii programu ya kupanda miti ili hili zoezi liweze kufanikiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, tafiti nyingi zinazofanywa hapa nchini kuhusiana na Mlima Kilimanjaro, zinafanywa na watafiti kutoka nje ya Tanzania. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwashirikisha watafiti wazawa na kuwawezesha ili waweze kushiriki kwenye kuulinda huu mlima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Waheshimiwa Wabunge, siku zote wamekuwa ni wadau muhimu katika kushajihisha shughuli za kimaendeleo katika nchi yetu. Kwa hiyo, Wizara tuko tayari kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro katika upandaji wa miti. Taasisi yetu ya Hifadhi ya Kilimanjaro ina mpango wa kutoa miche kwa watu ili waweze kuipanda nje ya maeneo ya Mlima Kilimanjaro. Kwa hiyo, tuko tayari kushirikiana na Waheshimiwa Wabunge na kuwapatia miche hiyo, nitaomba leo mchana tukutane na Waheshimiwa Wabunge wote wa Mkoa wa Kilimanjaro ili tuweze kuainisha mahitaji yao na tuweze kuona jinsi ambavyo tunaweza kushirikiana nao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la tafiti, ni kweli kwamba zipo tafiti zaidi ya tano ambazo zimefanywa na watafiti kutoka nje, lakini wakati wote walipofanya tafiti hizi walishirikisha watafiti wa Kitanzania, lakini kwa sababu tunafahamu kwamba suala la mabadiliko ya tabianchi ni suala mtambuka, taasisi zetu sasa za hapa nchini kama SUA, University of Dar es Salaam, UDOM, Nelson Mandela na nyinginezo zimeshiriki kikamilifu katika kufanya tafiti zinazoendana na kupata afua zitakazosaidia kwenye mabadiliko ya tabianchi. Ni imani yetu kwamba tafiti hizi zitatusaidia sana kama nchi kuwa na uelewa mpana wa tatizo tunalokabiliana nalo. (Makofi)
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Spika, mgogoro wa Hifadhi ya Kituro na Vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Kituro ngazi ya Wilaya ya Makete, ngazi ya Mkoa wa Njombe ulishapeleka mapendekezo Wizarani. Kazi iliyobakia ni kwa Wizara tu kuthibitisha ili mapendekezo hayo yaweze kufanyiwa kazi.

Je, ni lini Wizara itafanyia kazi suala hilo ili tumalize ule mgogoro kule Makete? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge swali lake kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inashughulikia migogoro hii kupata utatuzi wa migogoro ili kuondokana na changamoto hii. Katika kushughulikia migogoro hii umakini mkubwa unahitajika ili kuhakikisha kila mtu anapata haki stahiki, namuomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati tunalishughulikia jambo hili ili mwisho wa siku tukilimaliza lisiwe na changamoto nyingine yoyote.
MHE. ALEKSIA A. KAMGUNA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Naomba kuuliza je, Serikali imejipangaje kumaliza mgogoro katika Mbuga ya Kikwachi iliyopo Wilayani Ulanga ili wale wananchi wasiendelee kupata usumbufu katika kilimo?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa sababu swali hili ni specific kwa eneo tofauti na swali la msingi namuomba Mheshimiwa Mbunge baada ya kipindi cha maswali na majibu tukutane ili tuweze kupata majibu ya uhakika kwa eneo hili.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, niombe watekeleze ambayo wamekuwa wakiahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuiuliza Serikali, kama ambavyo kwenye mashirika na taasisi nyingine wamekuwa wakilipa CSR, je, Serikali haioni sasa kuna haja ya kubadilisha sheria na kanuni ili wananchi wanaozunguka Mlima Kilimanjaro waweze kupata CSR kama yalivyo maeneo mengine ya migodi na kwingineko?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, tayari tumeshaunda vikundi mbalimbali katika Jimbo la Hai kwa ajili ya kusaidia vijana wetu wanaopandisha wageni kwenye Mlima Kilimanjaro, lakini kumekuwa na tatizo, zile kampuni za watalii nyingi zinakuja na vijana wao kutoka maeneo mengine.

Je, Serikali haioni ni wakati sahihi sasa kuzielekeza kampuni hizi zichukue vijana waliopo pale Machame Gate na mageti mengine yaliyopo Mkoa wa Kilimanjaro ili vijana wanufaike na mlima wao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hii ya kijamii imekuwa ikifanya vizuri isipokuwa tu baada ya tatizo la Covid ambalo mapato ya hifadhi zetu yalishuka ndipo miradi hii ilianza kupata changamoto. Baada ya mafanikio makubwa ya kudhibiti ugonjwa huu na kazi kubwa ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii, tumeona mapato yameendelea kukua siku hadi siku na tumeweka mfumo mahsusi kwa sasa unaotuelekeza kwenye kutekeleza miradi hii ya kijamii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtakumbuka Waheshimiwa Wabunge katika bajeti ya mwaka huu tumetenga takribani shilingi 3,000,000,000 kwa ajili ya miradi hii ya kijamii. Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge mtupe muda tuendelee na utaratibu huu wakati tunafanya tathmini ya mwenendo wa ukuaji wa sekta ya utalii ili tukiona imetengemaa basi tunaweza kuja na huo mpango ambao utapendekezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye eneo la ajira; suala la ajira kisheria ni fursa kwa Watanzania wote kuweza kufanya kazi mahali popote katika nchi yetu mradi hawavunji sheria. Sasa nimesikia changamoto hii ambayo Mheshimiwaa Mbunge ameisema, lakini tukumbuke vilevile kwamba ajira hizi zinatolewa na sekta binafsi na wao katika kutoa ajira hizi vipo vigezo, sifa ambazo wanaziangalia na kubwa zaidi kwao ni uaminifu kwa hawa vijana wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tutaendelea kushirikiana na wenzetu wa Hai kuona uwezo wa vijana wale, kama kuna mapungufu tupo tayari kushirikiana nao kuwajengea uwezo, lakini vilevile kuwahamasisha katika suala zima la uaminifu, ili tuhakikishe kwamba vijana hawa nao wanapata fursa ya kuajiriwa katika eneo lile na kuweza kunufaika na rasilimali iliyopo kwenye eneo lao. (Makofi)
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana na naipongeza Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa sasa, sekta ya utalii imekua sana hasa baada ya Mheshimiwa Rais Kutangaza utalii wetu na kutengeneza Filamu ya Royal Tour, je, Serikali haioni umuhimu wa kurejesha utaratibu wa zamani ili fedha hizo ziende kusaidia kwenye miundombinu pamoja na huduma nyingine zinazotolewa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kazi kubwa imefanyika ya kutangaza sekta ya utalii. Hapa nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amechukua jukumu hili yeye mwenyewe na kushiriki kwenye filamu ile ya Royal Tour ambayo imekuwa na matokeo mazuri sana kwa nchi yetu. Vilevile, ameshiriki kwenye filamu ya Amazing Tanzania ambayo kesho tunaenda kufanya uzinduzi wake kwa upande wa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeona ukuaji wa kasi wa sekta hii na imekuwa ikifanya tathmini ya kina kuhusu mwenendo wa ukuaji wa sekta hii na mahitaji yake. Ndiyo maana nilipojibu swali la msingi nimeonesha kwenye ule upande wa OC jinsi ambavyo Serikali imeongeza fedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mtakumbuka katika bajeti ya mwaka huu tuliidhinisha hapa, asilimia sita kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Sekta ya Utalii. Vilevile asilimia tatu kwenye eneo la sekta ya wanyamapori. Hizi ni fedha ambazo mwanzoni zilikuwa hazitolewi, lakini ni fedha ambazo sasa zinatoka ili kuimarisha sekta yetu kama nilivyosema kwenye upande wa OC na kwenye upande wa maendeleo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeona ongezeko kubwa la karibu dola bilioni tano kwa TANAPA dola karibu bilioni nne kwa ajili ya TAWA. Kwa hiyo, tathmini hii inayofanyika ya ukuaji wa sekta, ninaamini kabisa kwamba, tutaweza kukidhi mahitaji ya sekta hii na kuweza kuhakikisha kwamba, fedha zinatoka kwa kutosheleza ili tuweze kuiboresha sekta yetu ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia sana kwenye pato la Taifa na ajira katika nchi yetu.
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni ukweli usiopingika kwamba utalii unatuongezea fedha za kigeni kwa kiasi kikubwa sana. Pia, upatikanaji wa OC kila mtu anajua jinsi ambavyo inapatikana kwa kusuasua. Je, Serikali iko tayari kuhakikisha kwamba kunakuwepo na utaratibu wa kuwepo retention kwa ajili ya taasisi hizi ili yale matengenezo yanayotakiwa kufanywa kwa muda, yafanywe kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kama nilivyosema kwenye majibu ya awali, retention imeanza ndiyo maana nimesema tuna asilimia sita inayokwenda kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Utalii; pia, tunayo asilimia tatu ambayo inaenda kwenye World Life Protection Fund.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa jinsi ambavyo tathmini zinafanyika kuhusiana na ukuaji wa sekta hii, tathmini hiyo itatuelekeza juu ya umuhimu wa kuwa na 100% retention au twende hatua kwa hatua ili tusiweze ku-suffocate maeneo mengine ambayo fedha hizi za utalii zinaweza kuchangia.