Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Questions from Hon. Dr. Medard Matogolo Kalemani (1 total)

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:-

Je, lini Serikali itakarabati shule kongwe za msingi katika Jimbo la Chato?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi 476,200,000, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 10 na matundu ya vyoo 77 katika Shule Kongwe za Bwanga, Bwina, Busalala, Ilemela, Itanga, Katale, Katende, Mwangaza, Nyantimba, Nyarutembo na Nyisanzi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Katika Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali imepanga kutumia shilingi 890,300,000, kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 25 na matundu ya vyoo 75 katika Shule Kongwe za Bukiriguru, Busaka, Buzirayombo, Ihanga, Katete, Kibumba, Kinsabe, Katende, Kitela, Mwabasabi, Minkoto, Mwangaza, Nyakato, Nyamirembe na Nyangh’omango.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuboresha shule kongwe za msingi zikiwemo za Halmashauri ya Chato kadri ya upatikanaji wa fedha.