Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Rev. Peter Simon Msigwa (11 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2012, Mheshimiwa Mnyika alisimama hapa Bungeni akasema tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Bunge. Akasema tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa CCM na tumefika hapa tulipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais
Kikwete, mlimzomea, mkachukua Polisi mkamtoa. Leo wale wateule wa JK toka Magufuli ameingia amewaporomosha zaidi ya 30. Leo mnapiga makofi mnasema majibu yanatumbuliwa lakini miaka mitano iliyopita tulizungumza mambo ya safari za JK, mlitetea humu ndani na mkapiga makofi. Miaka mitano iliyopita tulizungumza sherehe, kofia, miavuli isiyo na tija mlipiga makofi, leo wengine mnajitoa ufahamu mnasema majipu yanatumbuliwa.
(Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunapozungumza hotuba ya Mheshimiwa Rais hii nchi ni ya wote. Mheshimiwa Rais tumempa kazi na Bunge hili lina wajibu wa kumsimamia, Tanzania ni yetu sote. Kwa hiyo, hatujaja hapa kumpambapamba, ana kazi anayotakiwa kuifanya kwa
Watanzania. Nikisema simuungi mkono katika mambo mengine anayofanya nitakuwa mwongo na nitakuwa mnafiki. Sisi kama Wabunge tunawajibu wa kutimiza wajibu wetu wa kuisimamia Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge lililopita lilikubali kutokuwa na meno na Mnyika alisema mkamzomea akatoka nje, tunataka turudie makosa yale yale ya kuwa na Bunge butu.
Wananchi wametutuma tuisimamie Serikali pamoja na kumwambia ukweli Mheshimiwa Magufuli. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Magufuli anasema anataka kubana matumizi, jambo ambalo ni zuri na Mbunge yeyote mwenye akili ataunga mkono. Hata hivyo, matumizi anayoyabana tumezungumza sana hapa, kuna idadi kubwa ya Wakuu wa Wilaya wanaendesha mashangingi hawana tija katika nchi hii akitaka kupunguza matumizi awatoe hao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, unamkuta Mkuu wa Wilaya naye ana chumba cha mikutano, kikao kikubwa anachoweza kufanya ni cha kuwa na wale walinzi na kazi yao ni kudhibiti mikutano ya CHADEMA. Hiyo kazi anaweza akafanya OCD, hatuhitaji Mkuu wa Wilaya. Wala Mkuu wa Mkoa hatumhitaji, kama ni kupunguza matumizi tumtoe huko. Kazi za Wakuu wa Wilaya wameishia kuomba hela kwa Wakurugenzi, abishe mtu kama haombi hela kwa Wakurugenzi hapa. Haya ndiyo mambo tunatakiwa tujadili kama tunataka tuisaidie Serikali ipunguze matumizi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunazungumzia masuala ya utawala bora, Mheshimiwa Mbarawa, wewe ni Mzanzibar na wenzako ambao hamjaapishwa, mnaondoka Zanzibar mnakuja kutaka kupiga kura Dar es Salaam, kuna utawala bora hapo? Hayo ndiyo majibu
mnatakiwa mumwambie Magufuli ayatumbue na muanze kutumbuliwa wenyewe. (Makofi)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina kaka yangu Maige kutoka Iringa, mwanadiplomasia, ameshiriki kwenye vikao vingi vya kutatua migogoro duniani hapa na yeye anaondoka mwanadiplomasia, Waziri wa Nchi za Nje, hajaapishwa anaenda kutaka
kupiga kura Kinondoni, huo ndiyo utawala bora? (Makofi/Kicheko)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, hii ni hypocrisy of the highest order. Kama Rais anataka utawala bora haya ndiyo mambo tunatakiwa tujadili ili Taifa tuliweke katika misingi bora.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivi kesho Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje kama ingemwagika damu Dar es Salaam angekwenda Rwanda kusuluhisha migogoro? Hebu tuwe wa kweli, tusijitoe ufahamu hapa. Hii nchi wote tunaipenda tuzungumze mambo ya msingi, hayo ndiyo mambo ya utawala bora?
Mheshimiwa Naibu Spika, jana Kilombero Mbunge mwenzetu anapigwa na kubebwa mzobemzobe na Polisi kwenye Jimbo lake mnakuja mnapiga vigelele hapa mnasema, utawala bora! Mbunge anazuiliwa kupiga kura kwenye Jimbo lake, haya ndiyo mambo tunayotakiwa
tuzungumze hapa lakini tunarudi kwenye mambo yale yale kwa akili ileile. (Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, mnasema utawala bora, rafiki yangu Kigwangalla anaondoka hata hafuati taratibu za Utumishi wa Umma unaenda kufungia watu kwenye ofisi. Najua nia nzuri ya Rais ya kutaka tulete mabadiliko lakini kama hatuja-change mindset za wafanyakazi wetu ni tatizo? Kama gari lako unaweza kuliendesha lina speed ya 120 hata unune, ukemee, haliwezi kwenda speed 200. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mmewajengea uwezo kiasi gani hawa watu? Human resources tuliyonayo ndiyo hii, hamjawajengea uwezo wa kufikiri vizuri, hamjawa-motivate, hamjawa-inspire, hamjajenga uwezo wa kwenda na kasi hii. Sasa hivi tunakwenda kwenye transformation hamjafanya hayo mambo kazi yenu ni kufukuzafukuza. Inawezekana nia ya Rais ni nzuri ya kutaka kuleta mabadiliko sasa wengine kwa sababu mmepewa vyeo siyo kwa merit mnataka muonekane eti mnafanya kazi, mnafungia watu milango, mnawafokea watu, anatoka hata Mkuu wa Mkoa anaenda kufokea watendaji wa mitaa ambao hawako chini yake wako chini ya Mkurugenzi, huo ni utawala gani bora wa sheria? Hebu tujihoji ndugu zangu.
(Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumekuja hapa tunapoanza hebu tuache kujitoa ufahamu. Tena nashukuru sasa hivi wengi mmekuja mnaufahamu, tuisimamie Serikali kama kweli tunataka maendeleo katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, akina Wassira wameondoka walikuwa hivyo hivyo, akina Malima walikuwa hivyo hivyo walikuwa kimbelembele, hebu tuwe wakweli tusijitoe ufahamu hapa. Kiukweli watu mnajitoa ufahamu matokeo ya Zanzibar yanaeleweka kabisa tunaanza
kuongea ngonjera na mashairi, tunaacha kusimamia ukweli. Kama tunataka tumsimamie Rais majipu ndiyo hayo, tuanze na majipu hayo, tusimame kiukweli tuitetee Serikali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, unasema tunapunguza matumizi lakini matumizi yako pale pale. Wakuu wa Mkoa wana kazi gani? Mnasema msimamizi wa usalama kwani RPC hawezi kufanya? Ni kazi ipi ambayo hawezi kufanya RPC mpaka awepo Mkuu wa Mkoa, ndiyo kazi
kubwa wanayofanya. Hawa hawana kaz, kama kweli tunataka tupunguze matumizi ndiyo hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama hatutabadilika na hatutasimama kama Bunge ambalo wajibu wetu ni kuisimamia Serikali siyo kumpambapamba tu Magufuli na Serikali ya CCM, hizi ni kodi za wananchi na wananchi wametuleta hapa tuisimamie Serikali. Kwa hiyo, niombe tusijitoe ufahamu ndugu zangu. Tulizungumza haya mambo mkatuzomea, mkaimba ni walewale na Kinana aliwaambia muisimamie Serikali lakini leo Mbunge wa CCM unasimama hapa unaipamba, unajikombakomba kwa Rais baada ya dakika mbili barabara ni mbaya, maji
hayapo. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninayezungumza pamoja na figisufigisu ambazo Chama cha Mapinduzi kilijaribu kuleta, nina barabara nzuri Iringa Mjini, nina maji asilimia 98, taa barabarani zinawaka, halafu wewe unakuja unajikombakomba hapa badala ya kuisimamia Serikali iwasaidie wananchi wako. Unajikomba kwa lipi, hiyo siyo kazi ya Kibunge! Wengine wamegeuka hapa wamekuwa Procurement Management Unit, siyo kazi yenu. Hata Halmashauri nimechukua pamoja na figisufigisu, nadhani Nape salamu anazipata hizi. Kwa
sababu nimefanya kazi ya kuwatumikia wananchi tuache unafiki, tuache kujikombakomba, tuisimamie Serikali.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, naona naishiwa muda, Mungu akubariki sana. (Makofi/Kicheko)
Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa kwa kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2016/2017 – 2020/2021
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Nami naona nijaribu kushauri na kutoa mchango wangu kuhusiana na agenda iliyo mbele yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nina maswali kadhaa ambayo napenda kumuuliza Waziri wa Fedha kwamba katika Mpango huu, ni kwa namna gani mambo haya ameyazingatia?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu toka tumepata uhuru, ni Taifa ambalo limekuwa tegemezi. Tumekuwa tukiendesha bajeti yetu na masuala mbalimbali ya kimaendeleo kwa kutegemea Wahisani au Wafadhili. Takwimu nilizonazo mpaka sasa ni kwamba kwa kipindi cha miaka 40, Jumuiya ya Ulaya imetoa zaidi ya Euro bilioni tatu kusaidia shughuli za kimaendeleo ambazo zimekuja kwa mfumo wa Kiserikali. Ukiacha mashirika kama Maria Stops na mashirika mengine kwa mfano kutoka Uingereza, hivi vyote vimekuja kuchangia na vimesaidia sana kukuza maeneo ya elimu, miundombinu na afya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye eneo la afya, Marekani na mashirika yake mengi sana yamesaidia sana Sekta ya Afya kusaidia wauguzi wetu namna ya kutatua kero mbalimbali za afya. Vile vile Kiserikali, mashirika kama DFID kutoka UK, USAID, UNFPA inayoshughulika na idadi ya watu duniani, haya yote yametoa michango kwa ajili ya kuisaidia nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunataka Taifa ambalo linajitegemea na tumekuwa tukijinasibu sana kwenye vyombo vya habari kwamba tunataka Taifa liwe la kujitegemea, kitu ambacho ni kizuri. Napenda Waziri wa Fedha aniambie, ni namna gani mpango wake una-reflect kuachana na huu utegemezi wa muda mrefu ambapo toka tumepata uhuru tumekuwa tukiwategemea hawa watu? Katika kipindi cha miaka kumi tumepoteza watoto zaidi ya 600,000 ambao wamekufa kwa utapiamlo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Taifa letu sasa hivi kila saa moja mama mmoja mjamzito anakufa. Maana yake ni kwamba kwa mwaka tunapoteza akinamama wajawazito 9,000. Ni namna gani Mpango huu una-reflect kwamba tutahama kutoka kwenye hii hali ambapo tunapoteza watoto na akinamama wajawazito? Huduma ya afya kwa kiwango chote tunaitegemea kutoka nje!
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Taifa hili asilimia karibia 50 ya watoto wanaozaliwa ni stunts. Kuna mental retardation ya kutosha katika nchi; na wanasema pale anapokuwa mtu mmoja amedumaa, kuna watu wengine ambao wana mental retardation watano. Ni namna gani Mpango huu una-reflect kujaribu kuliokoa Taifa hili kwenye maeneo haya?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa ambalo Kambi ya Upinzani imezungumza, ni jinsi ambavyo Mpango uliopita ulitekelezwa kwa asilimia 26 tu. Mheshimiwa Waziri, kabla hatujaenda mbele, you know speed is useless if you don’t know where you are going or if you lost. Kabla hatujaenda mbele unapotuletea huu Mpango, ni kwa nini Mpango uliopita tumeshindwa, ulitekelezwa kwa asilimia 26? Vitu gani vilisababisha tushindwe? Ni hatua gani zimechukuliwa? Kwa nini tulishindwa? Kwa nini hatutashindwa katika Mpango huu? Ni namna gani yale ambayo yalitushinda miaka iliyopita tutayarekebisha?
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya kabla hatujaenda mbele ni lazima tuwe na majibu ya kutosha. Kabla hatujaparamia huu Mpango tuanze kuupitisha, tuambiwe ni kwa nini tulishindwa na kwa nini hatutashindwa kwenye Mpango unaokuja?
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kambi ya Upinzani imezungumza kwamba tunapopanga mipango lazima iwe inaendana na mazingira, kuna mipango mingine ni kweli huwa inakuwa imposed, haiendani na uhalisia wetu. Huu Mpango wako unasema nini kuhusu kuendeleza Sekta ya Utalii ambayo inachangia asilimia 25 ya fedha za kigeni? Vile vile asilimia 17 zisizo na kodi, yaani GDP Mpango wako unasemaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema hivyo kwa sababu gani? Kumekuwa na uvamizi na nashukuru sasa hivi Waziri wa Ardhi amekuja; kumekuwa na uvamizi wa mifugo, wafugaji wamevamia maeneo mengi ambayo ndiyo yanakuza Sekta ya Utalii ambayo kimsingi ndiyo yanatuletea pesa nyingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tena na Waziri wa Mifugo yupo hapa! Nchi yetu ina asilimia 10 kwa ajili ya ufugaji. Kwa bahati mbaya haya mashamba makubwa mengi ambayo tulitenga asilimia kumi kwa ajili ya ufugaji yamehodhiwa na watu wachache ambao kimsingi hayatumiki. Sasa maeneo haya yamesababisha hawa wafugaji waanze kuondoka sehemu ambazo tumezipima. Sasa zinaathiri kwenye hunting industry, zinaathiri kwenye National Parks wakati hii ardhi ipo, haijapangwa vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeshangaa juzi Waziri wa Maliasili anahangaika na tumbili wale waliokamatwa KIA. Ni kweli sikubaliani wanyama wasafirishwe ovyo ovyo, lakini ukiangalia tumbili na athari zinazopatikana kwa wavamizi wafugaji wanaopeleka kwenye maeneo ya uhifadhi, ni athari kubwa sana kuliko tumbili ambao tunahangaika nao pale KIA. Ni sawa na nyumba inaungua moto, watu badala ya kuokoa vyombo, vinateketea, wewe unamshangaa binti aliyevaa sketi fupi. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ndiyo Serikali yenu! Hatuna priorities! Hii Sekta ya Utalii ndiyo inaiingizia Taifa asilimia 25 ya fedha za kigeni. Wafugaji najua wanapiga kelele sana, sio kwamba siwapendi, najua wengine watainuka hapa! Ufugaji katika nchi hii unachangia one point seven ya GDP, halafu mnaleta mchezo na inayochangia asilimia 17, hapa balance iko wapi? Naomba Mheshimiwa Waziri wa Fedha anipe majibu, mmejipangaje?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Iringa Mjini kwenye Sekta ya Utalii, hii Southern Circuit mlituambia katika Bunge hili kwamba tunataka na Southern Circuit kuwe na utalii, lakini Iringa Mjini pale ni mahali ambapo pamekaa kimkakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumelalamika sana miaka mitano hapa kwamba ule uwanja wa ndege uharakishwe, ujengwe vizuri na barabara ya lami ijengwe mapema iwezekanavyo kwenda kwenye Mbuga ya Ruaha ya National Park ambayo kimkakati ni hii Sekta ya Utalii. Sasa kumekuwa na maneno mengi, mara mnawapiga mkwala hawa wafadhili ambao wanatusaidia; Mheshimiwa Mpango umesema tunaweza kujitegemea, mmekejeli hata zile fedha za MCC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekwambia hii ni nchi ambayo watoto wanakufa kwa utapiamlo. Tuambieni hii mikakati yote kwa miaka 40 tumetegemea fedha za kutoka Ulaya, mmejipangaje kujiondoa kwenye eneo hili? Naunga mkono tujitegemee, lakini tuwe realistic, tunaachanaje na kujitegemea? Tunatoa elimu ambayo ni spoon feeding! Ni elimu ya watu ambao wanamaliza shule lakini hawana mchango! Tunasomesha wachumi ambao hawana uchumi, wanataka wafundishe uchumi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwenda kujifunza uchumi, bora niende kwa Mangi kwenye kaduka kake atanifundisha uchumi kuliko nimpate mchumi mwenye degree kwa sababu hana uchumi yeye mwenyewe, hawezi kuleta chakula mezani. What kind of economics is that? Huo Mpango wako ni lazima tuwe na majibu haya, ni namna gani tutapunguza vifo vya akinamama wajawazito? Huu Mpango tunataka utupe majibu ni kwa kiwango gani tumeshidwa miaka mitano iliyopita?
Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia 26 ni ndogo sana. Utupe majibu ya kutosha! Nami najua, tulikwambia mapema kabisa, wewe sio mwanasiasa, lakini sasa hivi naona siasa imeanza kuingia, unatoa majibu ya kisiasa. Tunataka utupe majibu ya uhalisia! Kama kweli tunajifunga mkanda, tujue tunajifunga mkanda kwa kiwango kinachotosha. Tuambiane ukweli! Zama za kudanyanyana hazipo, tuambiane ukweli kwamba hela hii walikuwa wanatusaidia Wamarekani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimesema ukifuatilia hizi hela, afya ya nchi hii tumeikabidhi kwa Wamarekani, hatuna uwezo huo! Nimetaja haya mashirika yote ya Kiserikali, achilia mbali hizi NGOs ambazo zote zinaleta pesa kusaidia akinamama. Haya ndiyo mambo ambayo Bunge tunatakiwa tujadiliane na tuambiane ukweli hapa! Kinachonishangaza kikubwa, ni kwa kiwango gani tunacheza na Sekta ya Utalii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tutengeneze Mpango in our context. Utalii ndiyo unaotuletea pesa nyingi katika nchi yetu, lakini matokeo yake, tunacheza na mifugo. Bahati mbaya wenzetu wa Kanda ya Ziwa, they speak a lot, wana influence. Akina Musukuma hawa wanaongea sana, wangependa hata hifadhi zile zote waingie wanyama tu. Nakubaliana kwamba mifugo ni ya muhimu katika Taifa letu, lakini hatuwezi! Hii inachangia one point seven GDP, tukaua inayochangia seventeen. Yaani tunaua uhifadhi kwa kiwango kidogo kwa sababu ya kufurahisha watu kisiasa. Naomba Mpango huu u-reflect ni namna gani tuta-boost uchumi wetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vile vile tunataka tuwe na uchumi wa kati, lakini ukiangalia idadi zote mlizotupa, wasomi tunaowaandaa katika sekta mbalimbali, kwa mfano, utalii una-boom katika nchi yetu. Sioni wale wanaohusika na industry hii tumewaandaa kwa kiwango gani; wale wanaohusiana na gesi tumechukua sababu za makusudi kiasi gani kuwaandaa kwa ajili ya uchumi wa baadaye badala ya kuleta siasa?
Mheshimiwa Waziri naomba haya maswali yangu niliyokuuliza kwenye Mpango wako, ina-reflect kiasi gani ili tuwe wahalisia, tusifanye vitu vya kubahatisha na siasa? Sasa hivi tumemaliza uchaguzi, hebu tuingie kwenye uhalisia, tusiende kwenye siasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi ninavyozungumza, bandari kwa taarifa zenu wenyewe, imeshuka kufanya kazi kwa kiwango cha asilimia 50. Wateja wengine kutoka Kongo wameondoka, wanakimbilia Beira. Haya mambo tutawezaje kuyafikisha kwenye uhalisia kama hatuambizani ukweli? Nasi kwenye Ilani yetu ya Uchaguzi tulisema angalau one third ya bandari ndiyo yangekuwa mapato ya Taifa. Sasa hivi tumeshashusha asilimia 50.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba uchumi pamoja na siasa mnazozifanya, hebu tu-balance kuwe na uwiano kati ya business na politics. Naona mizania ya siasa inapanda zaidi kuliko uchumi. Hebu tu-balance, kwa sababu mwisho wa siku, huu ni mtumbwi, tumepanda wote. Kama mwenzetu umeanza kutoboa, tutazama wote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba haya majibu yasawazishwe ili kwa pamoja turidhiane, tuishauri Serikali. Waziri wa Ardhi unanisikia, Waziri wa Mifugo unanisikia, bahati mbaya Waziri wa Maliasili hayupo, naomba m-balance haya mambo; kwa sababu siku moja nimemsikia Waziri wa Maliasili na Waziri wa Mifugo, kulikuwa na sintofahamu kidogo katika eneo hili. Mimi wale tumbili hata mngeacha waende, hakuna shida. Ingekuwa tembo au faru, hiyo sawasawa. Wale Tumbili si sawa na Kweleakwelea! Wapo wengi tu, tungeuza tupate hela; lakini mnaacha uhifadhi, ng‟ombe wanakwenda kule, wanaharibu uhifadhi! Hii ni kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadaye.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni hayo tu machache, nimejaribu kusaidiana kidogo katika hilo. Ahsante sana.
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017- Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi. Na mimi nataka nitoe mchango wangu kuhusiana na Wizara hii ya Viwanda. Mheshimiwa Waziri nashukuru umekuwa unaongea sana na unapojibu maswali kama vile bado tuko kwenye kampeni. Tunatagemea sasa hivi hapa utupe data za uhalisia namna utakavyokwenda ku-earth majukumu yale ambayo Mheshimiwa Rais amekupa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, natambua Mheshimiwa Rais amesema anataka nchi hii, jambo ambalo ni jema, iwe ni nchi ya viwanda kwa maana ya uchumi wa viwanda. Nchi hii wahitimu kwa mwaka ni 800,000. Katika majukumu ambayo Mheshimiwa Rais amekupa wewe kama Waziri amesema 40% ya wahitimu 800,000 anataka waende kwenye viwanda. Katika 40% ya hao watu 800,000 ni watu 320,000 maana yake hawa tunawaingiza kwenye viwanda. Kwa nchi hii kiwanda kikubwa ambacho kimewahi kuajiri watu wengi sana hawazidi 5,000. Sasa twende kwenye hesabu za haraka haraka maana ukija hapa unakuwa kama unafanya kampeni, twende kwenye hesabu za haraka haraka za kawaida tu. Ili lengo lako hilo la kuajiri watu 320,000 kwa mwaka lifikiwe maana yake unatakiwa uwe na viwanda 530 katika kipindi cha miaka mitano ya Ilani yenu ya Uchaguzi ambayo mnajisifu nayo. Hoja inakuja hapa mwaka huu sasa tunakwenda nusu una viwanda vingapi? Naomba utujibu hapo, una viwanda vingapi mpaka sasa? Utatutajia cha Dangote, alikiacha Mheshimiwa Kikwete ambaye sasa hivi mnamzomea, ninyi hamjatengeneza hata kimoja, una viwanda vingapi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii wafanyabiashara wanataka kuongea na Serikali yako, mnawakatalia, mnawa-frustrate, hamkai nao. Bado mnasema mna wawekezaji kutoka nje wakati hawa hawa waliomo ndani hamuwezi kuwa-handle vizuri. Ningekuomba Mheshimiwa Waziri hebu tuache mbwembwe tuwe realistic, hizi hesabu zinakataa, huna uwezo huo. Saa hizi hata viwanda viwili vipya huna! Ukinionesha viwanda vitatu umetengeneza nitakupa Land Cruiser yangu hapo nje kama unavyo, toka mmeingia Serikali hii, huna hivyo viwanda. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mnakuja hapa mnatupa takwimu za uongo, za kutuaminisha matumaini ambayo hayapo, hauna viwanda hivyo. Ukipiga hesabu hawa watu huwezi kuwapeleka, kiwanda kikubwa kinachoajiri watu sasa hivi ni Breweries inapeleka watu 3,000. Hawa watu 320,000 kwa mwaka where are you going to employ them, wapi utaenda kuwaajiri? Tunaomba unapokuja utuambie hesabu za uhalisia, hatuko kwenye kampeni, tunataka utuambie ukweli! Naomba hilo usije na majibu mepesi mepesi, hivyo viwanda hauna. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ndugu yangu hapa amezungumza, infrastructure ya umeme iko wapi, umeme wa uhakika uko wapi mpaka sasa unaowaita hao. Umetuambia Jumatatu tuje tugawane hapo, hatuwezi kugawana watu kama njugu wakati hakuna infrastructure yaani mimi nitaondoka na mwekezaji nasema naenda naye Iringa naenda naye wapi! Tukafanye nini? Mazingira yaliyoandaliwa yako wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri mimi ningeomba hebu tuambizane ukweli na ninyi ndio mtakaokwenda kumuangusha Mheshimiwa Magufuli kama mkija na mbwemwbwe ambazo hazina uhalisia. Mtupe mambo ambayo yanawezekana. Nimekupa hii takwimu uikatae! Unahitaji kuwa na viwanda 530 ndiyo uwapeleke hawa 40% kwenye hivyo viwanda unavyosema unakwenda kutupa na kuwaaminisha Watanzania kwamba nchi itakuwa ya viwanda, mambo yatakuwa mazuri, utupe figure ambazo ni za uhalisia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini lingine amezungumza Mheshimiwa mwenzangu hapa kuhusiana na hawa wafanyabiashara wadogo wadogo ambao tumezungumza sana hata miaka mitano iliyopita tunawaona kama ni kero katika nchi yetu badala ya kuwaona ni fursa. Kwa hiyo, hebu tu-change, is a mindset thing. Change what you see by changing how you see. Tunapowaona wale watu ni kero ndiyo tunagombana nao na mabomu badala ya kuweka mikakati ya kuwafanya hawa watu wawe na tija kwenye maeneo yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu ni wengi sana wangetafutiwa maeneo. Tumezungumza sana na mwaka jana tulitoa mpaka na maazimio kwenye eneo hilo kuhakikisha miji yote yatengwe maeneo walao kila weekend maeneo yale yafunguliwe, haya mambo yamekuwa yakisuasua katika maeneo mbalimbali. Naona hapa kwa mfano Dodoma imeshaanza na maeneo mengine lakini tumekuwa tukiwapiga hawa Wamachinga, tumekuwa tukiwaonea, hatuwatengenezei mkakati mzuri. Kwa sababu wao kama alivyosema ndugu yangu hapa, ndiyo wako kwenye field wengine wote hapa tunaongea nadharia tu lakini wao wako kwenye field ndio wanaliona soko lilivyo.
Kwa hiyo, nikuombe Mheshimiwa Waziri, tungeomba hili tatizo nalo lipate ufumbuzi wa kudumu na wa moja kwa moja badala ya kuwaona hawa watu ni kero tuone kama ni fursa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikirudi kwenye suala la viwanda, kwa mfano Mwanza kuna kiwanda kilikuwa cha nyama ambacho kilikuwa cha Tanganyika Packers, wakaja wakawekeza wawekezaji hakikwenda vizuri. Wakaja watu wa nje, baadaye wakaja Wamarekani, Wamarekani baada ya matatizo yao ya uchumi, hakipo. Leo Mheshimiwa unasema kwamba watu waje, kile kiwanda kule tatizo ni nini? Vilivyopo vimeshindwa nini na sasa hivi unatuaminisha kitu gani kitasababisha hivyo viwanda vilivyopo kwenda mbele? Vile vilivyoshindwa vilishindwa kwa nini na sasa hivi kwa nini unatuaminisha kwamba hivyo vilivyopo tutasonga mbele? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hebu tuache mambo ya kampeni. Uchaguzi mlishashinda whether mlituibia kwa magoli ya mkono, it is fine, mlishinda, Serikali ni ya kwenu.
Sasa hapa hatuhitaji kampeni, tupeni vitu ambavyo mnakwenda ku-earth. Hatutaki mbwembwe! Mheshimiwa Mwijage acha mbwembwe, tupe vitu ambavyo ni practical. Mwalimu wangu alikuwa anasema how can you earth it?
Tuambie unawezaje kutuambia kwenye ground? Tuna viwanda vingi sana, Iringa tulikuwa na viwanda vingi vya akina-TANCUT vile vyote vimekufa. Ukienda Mbeya hivyohivyo, ukienda Morogoro hivyohivyo. Sasa hivi mnakuja na lugha nzuri sana, very testy lakini ukienda kwenye uhalisia, hii hesabu ni ndogo sana nimekupa, it doesn’t work brother. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba atakaporudi hapa atatupa majibu. Hii ni hesabu ndogo sana huhitaji kuwa na elimu ya Chuo Kikuu, ndogo tu. Utupe majibu namna gani hii kazi aliyokupa Mheshimiwa Magufuli ya kuhakikisha 40% ya wahitimu 800,000 wanaingia kwenye viwanda, ni viwanda vipi? Mpaka saa hizi huna hata kimoja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka niliweke wazi hilo, tuache mbwembwe, tuambizane ukweli hapa ili tuisimamie Serikali. Nikushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Baada ya kumaliza uchaguzi wetu wa nchi mwaka 2015, mlishangilia kwa mbwembwe nyingi sana kwamba Serikali na Chama cha Mapinduzi mmeshinda kwa kishindo, mkawaaminisha Watanzania kwamba mnaweza kuongoza nchi hii. Watanzania wakawasikiliza, mkaunda Serikali yenu. Tukaja Bungeni hapa tukaapishwa. Siasa za nje tukazileta Bungeni na ndiyo maana hivi vipaza sauti vimewekwa hapa kwa ajili kuzungumza. It is about talking! Ni juu ya dialogue hapa Bungeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali mnakuja na hoja zenu mnaendelea kuwashawishi wananchi kwamba sisi tuna uwezo wa kuongoza nchi hii, mnaleta hoja. Nasi tuliowapinga tunakuja na hoja zetu kuwakatalia kwamba hizi hoja haziwezekani. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo hii Serikali inayosema ni ya Hapa Kazi Tu, Wabunge 250 wa Chama cha Mapinduzi na Serikali yao inashindwa kujibu hotuba ya kurasa 34! Inataka kuwaambia nini Watanzania? Kama kurasa ya 34 Wabunge 250 wa Chama cha Mapinduzi wanaogopa isisomwe, ninyi ni mature wa kuongoza nchi hii? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yetu tunakuja hapa tuna-dialogue, sisi ndivyo tunavyoiona Serikali, tunaoliona Jeshi la Polisi linafanyaje? Mikataba ya hovyo ikoje? Mtazamo wetu wa pili kwenye view yetu, this is how we see. Njooni na hoja mwoneshe udhaifu wetu uko wapi? Muwaaminishe Watanzania kwamba we are not matured. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kabla hatujaendelea, hatujazungumza, mnaweka mpira kwapani, mnataka msaidiwe na marefa. Suala la kujiuliza, you guys are you fit to lead this country? Kama hotuba ya ukurasa 30 hamwezi kuijibu, nani asiyejua mizengwe ya nyumba zilizouzwa katika nchi hii? Nani asiyejua nchi hii ina mikataba mibovu?
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Ambaye anatakiwa ashangiliwe kama King Kanuti, hatakiwi kuguswa katika Bunge hili. Nirudie maneno aliyozungumza Mheshimiwa Sugu; huyu Rais Mwema mnamfanya wananchi wasimwelewe. Yeye siyo Mungu, ana hali ya ubinadamu anaweza akakosea. Lengo letu hapa tupo kuisaidia Serikali na ndiyo dhana nzima ya kuwa na mfumo wa vyama vingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wamezungumza wenzangu hapa jinsi ambavyo mnawatumia Polisi, wakati wa uchaguzi mnawapa majina mazuri yote, lakini maisha wanayoishi ni ya shida sana. You are just using them! Mnawatumia wakati wa uchaguzi. Nawaomba ndugu zangu na niseme nyie mnaosema usalama wa nchi hii ni sababu ya ulinzi na usalama wa Jeshi la Polisi.
Mimi kama Mkristo na Mchungaji, Biblia inasema, Mungu asipoulinda mji, wakeshao wafanyakazi bure.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba utunze muda wangu tafadhali. Narudia tena, Bwana asipoulinda mji, wakeshao wafanya kazi bure! Biblia inasema mji haulindwi kwa wingi wa silaha anazokuwanazo mfalme. Ni Mungu ameamua ku-sustain amani ya nchi hii. Kama tutaendelea kucheza kwa kuamini kwamba bunduki na vifaru vitalinda amani ya nchi hii, tunapoteza muda. Ulinzi wa Muammari Gaddafi ulikuwa ni mkubwa kwa mbali kabisa kulinganisha na ulinzi wa nchi hii; lakini yuko wapi leo? Bwana asipoulinda mji, wakeshao wafanya kazi bure? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Jeshi la Polisi, msitumike vibaya kisiasa, nchi hii ni ya mfumo wa vyama vyingi, sisi hapa hatujaja kwa fedha, tumekuja hapa kwa merit. Tuna haki hizo! Mnabambika watu kesi! Kama Mbunge, mimi nimebambikwa kesi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, siku ya uchaguzi, kulikuwa kuna yule Mungi sasa mmempandisha cheo ameenda bandarini. Ameagiza Polisi wanakuja kunivamia, wamepiga watu, wamevunja miguu, mikono, mwisho wa siku, wiki mbili zimepita sipelekwi Mahakamani mpaka nikaanza kudai na Wakili wangu kwamba mmetupiga, wakatulaza kwenye bwalo wanawake na wanaume! Mimi ninayezungumza! Tunadai kwa nini hamtupeleki Mahakamani? Napelekewa charge eti wewe umemjeruhi Kamanda wa Field Force. (Makofi)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mimi Msigwa namjeruhi Kamanda wa Fied Force; na la pili nimejeruhi gari la Polisi. Kesi imekwenda Mahakamani wiki mbili, imefutwa; haina mkia wala miguu. (Kelele/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba Jeshi la Polisi, hebu acheni kutumika kisiasa. Tupo kwenye nchi ya vyama vingi. Kazi yetu kubwa hapa ni kuiweka Serikali sawasawa mwone wenyewe, nanyi Makamanda wa Polisi mnaona jinsi gani Serikali inashindwa kujitetea hapa! Kurasa 34 wanashindwa kujibu, they cannot! Nchi imejaa hofu, watu mmejaa hofu, huyu Rais mwema sana amewatia hofu mnaogopa kujitetea na kusema. Why? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Plato anasema: “if you cannot die for something, you are not worth living.” Sisi tupo tayari kwa lolote kwa sababu tunataka tuinyooshe nchi kwa faida ya vizazi vijavyo; na wajibu wetu ni kuikosoa Serikali, kuiweka vizuri. Haya tunayoyashauri, mangapi tuliwashauri? Tuliwashauri jambo la Katiba, mkalichukua, ila kwa sababu hamna ubongo wa kuku, mkashindwa. Si mlishindwa! Tuliwashauri, mkachukua. (Kicheko/Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliwashauri suala la elimu bure, mmejikanyagakanyaga, mnashindwa na yenyewe. Mngetupa hapa, hiki ni kisima cha kupata hekima na busara tunataka tuwashauri. You are incapable of leading this nation. Hapa ni mahali pa ku-dialogue. Ambao hamjasoma historia, nendeni Ugiriki mkaangalie Wagiriki walikuwa wanafanyaje kule Heathen. Unakuja na hoja unazijenga! Tumehamisha siasa kule, hapa ndiyo tunajadiliana, njooni na hoja. Sasa mmetunua macho, hamwezi kujitetea, mnajaza hofu watu, wafanyakazi na watu wote wana hofu, tutaendeshaje nchi hii? Bunge mmelifunga, halisikikii, humu ndani mnataka kutu-paralyse, sasa hiyo siasa tutafanyaje?
MHE. PETER S. MSINGWA: Ila saa hizi ni watu ambao hawaaminiki hata huko msiwaamini, hawaaminiki, saa hizi wanajikosha kusema sema maneno mazuri hapa wanawadanganya, tulikuwa nao usiku, waongo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, muda ukifika muafaka tutawataja, walikuwa wanatuletea na hela za kampeni sasa leo hapa wanajifanya wanadanganya danganya wanatuzunguka waongo, ni wanafiki hawa, hawawafai hata ninyi na hawa hawaifai hata Serikali kuwepo kwa sababu wata… (Makofi)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Msigwa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 20 16/2017 - Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi ningeanza kwa kuchangia utawala bora. Mtu mmoja aliwahi kusema, it takes a political consciousness and political will for the good governance to prevail. Utawala bora na utawala wa sheria hauanzi na bajeti, bajeti sio takwa la msingi la utawala bora. Kwa hiyo, inaanza political will kwamba tunataka tuwe na utawala bora ndiyo bajeti inakuja.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nini nazungumza haya? Toka Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani neno na dhana nzima ya utawala bora halionekani. Mtu mmoja pia naomba nimnukuu amesema, utawala bora ni kuongoza nchi kwa ufanisi na tija, kwa uwazi, uadilifu, uwajibikaji na ushirikishwaji wa watu kwa kufuata utawala wa sheria. Tangu Serikali hii imeingia madarakani, kuna mambo kadhaa ambayo imekanyaga huo utawala bora, halafu leo Waziri bila hata kuwa na uso wa soni anakuja kuomba hela zaidi ya shilingi bilioni mia nane hapa za utawala bora ambao haupo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze na la kwanza. Serikali hii imeanza kufanya kazi kienyeji. Mawaziri wote hawa wameanza kazi bila kupata instrument, huko ni kukanyaga sheria maana yake hawa Mawaziri ni sawa na sisi Mawaziri Vivuli walikuwa wanatoa maagizo wakati hawako kwa mujibu wa sheria, huo siyo utawala bora. Aidha, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumekaa kimya, hatusemi wakati wajibu wetu ni kuinyoosha Serikali, watu wote tumekaa kinafiki.
Hata Mawaziri wengine tukiwa kwenye chai mnalaumu utaratibu huu, mkija hapa mnageuka kama vinyonga, hamsemi na wakati hii ni kazi ya Bunge. Mkibisha tutataja mmoja mmoja ambao mnapinga utawala huu kwa taratibu hizo na wengine tumewarekodi kama Rais anavyosema amerekodi, kama mnabisha tuweke hapa. Hata ninyi hamkubali halafu tukikaa humu ndani ya Bunge hamsemi na kazi ya Bunge ndiyo hiyo tumekuja hapa kusema. Tunazungumzia utawala bora, mnafanya kazi bila instrument, that is wrong and thas is not good governance, shame with you.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, toka Bunge la Tisa…
KUHUSU UTARATIBU.....
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, lakini wakati wa kuchangia tunakuwaga na taarifa hatuna mwongozo, nashangaa huyu ameomba mwongozo umempa, Kiti bado kinayumba tu. Naendelea kuchangia, unayumba bado, hakuna mwongozo wakati wa kuchangia, sheria ndivyo inavyosema.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba muda wangu uzingatiwe. La kwanza nililokuwa nachangia ni Serikali kuongoza bila instrument.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, toka Bunge la Tisa la Mheshimiwa Sitta na utawala uliopita pamoja na kwamba kulikuwa na upungufu lakini utawala uliopita ulijitahidi kukuza demokrasia kwa kiwango fulani, Bunge lilikuwa linaoneshwa live, tumeona wakati wa madam Spika, Wabunge tulikuwa na uhuru. Kwa Wabunge wengine ambao ni washabiki Bunge halijaanza Tanzania, tusome kidogo kutoka Ugiriki, Wagiriki walifanyaje Bunge mpaka tukafikia hatua hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, Bunge ni mkutano wa wazi wa wananchi wote. Serikali hii inaanza kuminya inaweka siri, huu siyo mkutano wa unyago, tunaongelea matumizi ya hela za Watanzania, tunahitaji Watanzania waone kila kinachojadiliwa kwa manufaa yao. Serikali inayokandamiza uwazi ni Serikali ambayo ni oga, ni Serikali inayoficha madudu. Kama mnasimama hapa mnasema mnakusanya pesa za kutosha, mmevunja rekodi, haijawahi kutokea, mmeikuta Hazina tupu, mnaficha nini tusiwaoneshe Watanzania hayo mnayoyafanya? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo la pili, mnakanyaga wenyewe sheria halafu mnakuja kuomba bajeti ya utawala bora ambao hamnao. Pamoja na udhaifu wa Serikali iliyopita lakini Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete alikuwa jasiri, aliruhusu humu ndani tuongee, tuikosoe Serikali kwa uwazi na hilo nampongeza bila aibu. Tulimsema, tulimkosoa na mambo mengine aliyafanyia kazi pamoja na kwamba mengine hakuyashughulikia. Leo mnakuja hapa kwa ujasiri mnasema Hapa Kazi Tu, kukosolewa hamtaki, kazi gani ambayo hamtaki kukosolewa?
Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wote bila aibu wakati ule tunamkosoa Kikwete hapa mlikaa kimya, mlituzomea lakini leo mnaufyata. Inaonekana Mheshimiwa Magufuli hata akidondosha kijiko ninyi mtapiga makofi kwa sababu ya uoga wenu. Wabunge hatuwezi kuwa waoga kwa kiwango hicho, wajibu wetu ni kuisimamia na kuikosoa Serikali. Waliosoma physics sasa imegeuka kama ile pendulum swing, Serikali iliyopita alikuwa upande huu, sasa hivi tumeendelea upande huu badala ya kukaa katikati, lengo letu ni kuinyoosha Serikali, huo ndio wajibu wa Bunge. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, Waziri unapata wapi uhalali wa kutuletea bajeti hii wakati Serikali yako inakanyaga utawala bora wa sheria? Serikali inayoogopa uwazi ni Serikali isiyojiamini, ni Serikali ambayo inaficha uovu.
Tulitegemea demokrasia sasa inapanda ngazi kutoka pale tulipofika, kwa sababu mambo haya ni ya wazi, ni ya nchi, ni ya wananchi, tulitegemea sasa uwazi uwepo ili tukosoe, tudadisi, tuhoji kwa manufaa ya wananchi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Sugu alizungumza hapa alisema numbers don‟t lie, imagine Serikali inayosema uwazi Dar es Salaam mmezidiwa, Mameya 11 lakini bado mnang‟ang‟ania, hata hiyo shule sasa imetusaidiaje kama hesabu tu inakataa, mmezidiwa, mnapiga danadana, mnakataa, huo ni uwazi gani mnaozungumza hapa?
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, naikataa taarifa kwa sababu anasema uongo.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo na wewe umemwita bwege, kuna mtu kule Arusha alimwita Mheshimiwa Magufuli bwege akapelekwa Mahakamani na wewe utakwenda Mahakamani. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Naibu Spika, mna dhana ya kusema tutumbuane majipu, ili Serikali ya Chama cha Mapinduzi ipone lazima tuwe na Bunge imara. Kama ni jipu linaanzia kwenye Bunge, Bunge hili ni jipu, limekuwa dhaifu, haliwezi kuikemea Serikali. Kuna maamuzi ya msingi na makubwa ambayo Bunge hili linayatoa na mimi kama Kamishna na Makamishna wengine hatushirikishwi, hili ni jipu, lazima tutumbuane humu ndani.
NAIBU SPIKA: Muda wako umekwisha,
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa mwaka wa Fedha 2016/2017.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana kwa kunipa nafasi. Mimi nianze na Wizara kama ambavyo mchangiaji Mheshimiwa Lucy Owenya amesema, ili tupandishe uchumi wa Southern circuit lazima tufungue milango.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ningeomba sana Bunge lililopita tumezungumzia sana kuhusiana na uwanja wa Nduli Iringa pamoja na barabara inayotoka Iringa Mjini kwenda National Park. Ningeomba Wizara kama inawezekana hebu tushirikiane basi hata na TANAPA tutengeneze ile barabara kusudi tuweze kuzalisha pesa nyingi zinazotokana na hifadhi ambayo ni kubwa ya pili hapa Afrika, ningeomba hilo mlifanyie kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, ninataka nizungumzie kuhusu wanyama waliotoroshwa, hiki ni kiporo. Kwa bahati mbaya Wabunge huwa tunasahau tulikotoka, hiki ni kiporo. Bunge lililopita tumezungumza sana juu ya ujangili, lakini kuna wanyama waliokuwa wametoroshwa uwanja wa KIA. Bunge lililopita tulitoa azimio, AG wewe ni shahidi hapa tulikubaliana wote kwamba lazima ufanyike uchunguzi ni akina nani walitorosha wale wanyama, sasa hivi hakuna kesi, mwanzoni mlikuwa mnasingizia kuna kesi mahakamani, sasa hivi hakuna kesi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, iliingiaje ndege ya kijeshi? Jeshi lilionaje hapa? Usalama wa Taifa ulionaje? Hayo mambo bado hayajatolewa majibu. Serikali ya Qatar, nilibahatika kwenda Qatar walisema wamezoea kuchukua wanyama kwa style hiyo. Tulitoa Azimio kwenye Hansard inaonyesha Bunge lililopita. Ninaomba Waziri haya mambo hayawezi kulala kiporo kama tunataka tukomeshe ujangili, maana yake Serikali hii imesema inafukuwa makaburi, tuendelee kufukuwa makaburi hayo ni nani alihusika kutorosha hawa wanyama kuwapeleka Qatar, lazima turudishe na Bunge liliazimia. Naomba AG utasaidia Wizara hii namna gani tulifanye.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la tatu ni hili suala ambalo Kambi ya Upinzani imezungumzia kuhusu Kampuni ya Green Miles. Kampuni ya Green Miles, amezungumza Mheshimiwa Mbunge Mzee wangu hapa, mimi nilkuwa miongoni mwa Kamati ya Wabunge wanne, tuliokuwa tunachunguza utoroshaji wa wanyama. Tulipochunguza kampuni ya Green Miles, kama alivyosema haikupewa vitalu vya uwindaji kwa sababu ilikuwa haina sifa. Kamati ya ushauri ilimshauri Waziri kwamba hii kampuni haina sifa, imesema uongo, lakini haihifadhi kwa sababu kwenye kuwinda kunahitaji uhifadhi, kwa bahati mbaya au vinginevyo mambo yalivyokwenda hii kampuni ikapewa. Ilivyopewa tukayashuhudia yale ambayo walivunja kanuni za uwindaji na kulikuwa na infringement zaidi ya 11.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tarehe 4 Julai niliweka CD hapa kuonesha jinsi ambvyo wanawinda vibaya! Hawa watu hawana sifa za uhifadhi na Waziri aliyepita aliamua kuifutia leseni ya uwindaji kwa sababu wanawinda vibaya, suala hili lilivuta hisia za Kimataifa katika masuala ya uwindaji, suala hili lilivuta hisia za Watanzania vituo karibu vyote vya televisheni vilionesha jinsi ambavyo hawa watu wanawinda vibaya wanyama, hawana sifa ya kuwinda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kushangaza Mheshimiwa Waziri umetoa barua tena. Hapa Mheshimiwa Maghembe, kwenya masuala ya uhifadhi niko na wewe, sikubaliani kwamba ng‟ombe waende kila mahali, lakini kwenye suala hili sikubaliani na wewe. Kwa sababu tunakubali kuwa uwindaji ni pamoja na uhifadhi, hunting is about conservation. Mwindaji yoyote ambae hawezi ku-conserve nature hatustahili katika nchi yetu! Sasa inawezekanaje hawa watu ambao hawana sifa, kuna infringement zaidi ya kumi na ngapi? Lakini Waziri aliyekutangulia alifuta, kulikuwa na makosa sita aliyaona. Walikuwa wanawinda ngedere hawaruhusiwi kuwinda ngedere.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtoto wa chini ya miaka 16 anawinda, sheria inakataa, walikuwa wanatumia bunduki ambazo zinaziba sauti, sheria inakataa, wewe mwenyewe unaijua kwenye sheria ya mwaka 2009 na regulations za mwaka 2010. Hawa watu wamevunja sheria, leo wanarudi wanarudi kwa mlango gani? Ninaomba Waziri utuambie hawa watu ambao hawana sifa za kuwinda wamerudije tena kwenye maeneo hayo? Tutakuwa tunaleta mchezo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo niwaombe Waheshimiwa Wabunge hebu tuwe consistance kama tunataka tufanye uhifadhi. Wale waliokuja kuchukuwa wanyama wetu, watu walipiga kelele sana Bunge lililopita wakasema tunataka hata mifupa irudi. Nani alichukuwa hao wanyama? Hiyo ndege ya Qatar iliingiaje? Tulizungumza hapa kwamba mpaka na Ikulu ilikuwa inahusika, hatujapata majibu ya kutosha. Lakini hawa ambao walizuiwa wanarudi tena kwa mlango wa nyuma wamerudije? Naomba Mheshimiwa Waziri haya mambo utupe majibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala lingine kuna Mbunge, asubuhi amezungumza kwamba mpaka kwenye magazeti wanaandika kwamba kuna Wabunge wengine ni majangili. Hii ni kashfa kwa Bunge, hatuwezi kukaa kimya. Hili Bunge tumeambiwa kuna wala rushwa, Bunge hili wengine wanapiga mtindi, Bunge hili tena tunaambiwa kuna majangili. Tutakuwa na chombo cha umma kipi ambacho haya mambo kama hatuwezi kuyasemea? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu mtu kama kweli imeandikwa Jambo Mills gari yake hii hapa, kama ni kweli lazima tupate majibu na kwa bahati mbaya labda yeye hayupo na inasemekana, taarifa zinasemekana mpaka na gari lingine la Jambo Mills lilikamatwa na pembe za ndovu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama vile halitoshi, huyu mtu kuna leseni moja ya madini na yeye anahusika. Haya madini yako kwenye kitalu kule Meatu ambacho kuchimba madini hairusiwi kwenye hifadhi Waziri unajua Huyu mtu sijui amepataje kulikuwa hakuna EIA? Amepata, wanatumia wafugaji kuwaingiza eneo la uwindaji kwa kisingizio kwamba hawana malisho ili waweke pressure kusudi wakachimbe madini mpaka wamepata hiki kibali.
Nimshukuru Mkuu wa Mkoa alizuia hiki kibali na nimuombe Waziri wa Madini alifuatilie hili suala, ni nani alitoa kibali hiki, watu waingie kwenya hifadhi, sheria yetu inakataa kwamba wasiingie kwenye hifadhi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa huyu kama kweli haya mambo yanafanyika na yeye anahusika, Bunge lijisafishe, tujue kuna tatizo gani kama ni ya uongo asafishike, lakini vyombo vya habari vimeandika, vyombo vya habari vimetoa, anahusika, wanasema kuna Mbunge anahusika wamemtaja kwenye magazeti, ukienda kwenye mitandao na yeye hajakanusha. Lakini kuna wakati walivyokamatwa hawa watu waliachiwa, wakatoa fedha kidogo tu wakati wengine wanasota.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wanasafirisha tumbili, umewaweka ndani sasa hivi wanasota, lakini hawa watu wanatembea, inaoneka waliokamtwa wana nasaba na huyu mtu alyetajwa hapa, lakini wametoa faini wakaachwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanyama wanaonekana hapa hawakuchukuliwa hatua zozote, lakini wengine wamesafirisha tumbili tu wale tena wana haki, wale walikuwa wanasafirisha tumbili vizuri hawana makosa, akina Mzee Mlokozi wale wanalala tu kule ndani. Hawa wanatembea barabarani na wanatumia kisingizio, nikuombe hata hili suala la Toya Mheshimiwa Waziri hebu liangalie kwa upana wake. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kwa bahati nzuri miaka yote mitano nimekuwa kwenye hilo eneo kidogo naelewa, watu wa Toya muwaangalie kwa jicho la karibu sana. Manyanyaso wanayoyapata na taabu wanayoipata kwa kweli haiwahusu. Tunajaribu kuwarudisha nyuma hawa ambao ni Watanzania wazawa, wanafanya biashara zao, tunawa-drag chini bila sababu. Niombe Watanzania wenzangu the fact sisi ni Wabunge hapa, tupo kwa ajili ya maslahi ya Watanzania na Taifa kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna msemo mmoja unasema: „it is not economical to go to bed early and save all the candles if the result is twins (siyo jambo la kiuchumi kwenda kulala mapema ukatunza mishumaa yote kama matokeo yake yatakuwa ni mapacha). Kama tutadhani ni uchumi kupeleka ng‟ombe kila mahali kusiwe na mipaka, tusidhani litakuwa jambo la kiuchumi, baadaye tutapata hasara ya Taifa hili, ni lazima tu-save nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi hii ni ya wafugaji, nchi hii ni ya wakulima, nchi hii ni ya wafanyakazi, nchi hii ni ya viwanda, kwa hiyo, lazima tutenge maeneo. Ndiyo maana China walivyoona nchi ni ndogo wakaweka sheria ya kuzaa mtoto mmoja. Kwa hiyo, hatuwezi tukasema ng‟ombe wawe kila mahali, hatuwezi kusema ufugaji uwe kila mahali, tukabaliane wote kama viongozi, tutenge maeneo maalum. Mheshimiwa Waziri, kuna asilimia 10 nchi hii ya ufugaji wa ng‟ombe, ambao ng‟ombe tulionao milioni 25, wakiwekwa vizuri tunaweza tukawatunza. Lakini hatuwezi kukubali kutumia mifugo tukaharibu uhifadhi, tukaharibu utalii ambao unatuletea fedha za kigeni asilimia 25 na GDP ya asilimia 17. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, badala ya kugombana hapa na wananchi wametuita hapa kama viongozi, kama watu wenye busara, badala ya kugombana hapa kuwa na mawazo madogo ya kuwaza Jimbo lako hebu tuwe na national interest, tukae wote kwa pamoja tukubaliane. Hii nchi ni yetu sote, tukubaliane mifugo ikae wapi, samaki wakae wapi, ng‟ombe wake wapi? Mheshimiwa Waziri tukiruhusu jazba zitutawale hapa tutaishia kugombana. Kama wananchi huko wakituona, mfugaji anagombana na mkulima, mkulima anagombana na mfugaji, huko nje tutaanzisha vita.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa Fedha 2017/2018
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianzie hapo alipoishia Mheshimiwa Lema, Bunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linao uwezo wa kumu- impeach Rais. Sasa kama tuna uwezo wa kumu-impeach Rais halafu watu tukimtaja Rais hapa mnatetemeka maana yake tunataka tukiuke Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Bunge pekee, ni chombo hiki pekee, waliotunga Katiba walijua kuna wakati Rais anaweza akakosea na hiyo mamlaka iko mikononi mwetu. Mimi nashangaa Wabunge tukimtaja Rais kama anakosea tutamui-impeach vipi kama anakosea anapoingoza nchi yetu? Kwa hiyo, hebu turudi kwenye senses zetu kwamba mamlaka hiyo tunayo na wala hatumuonei kama anafanya makosa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe sana Mheshimiwa Mpango, wengi wamezungumza mimi narudia na juzi nilisema na tunasema ukweli kwa sababu tunalipenda hili Taifa. Nikuombe sana unapoleta mambo yako hapa usilete kama vile upo kwenye lecture room kwamba unataka kutupa lecture. Sisi ni wawakilishi wa wananchi, wametutuma wananchi na ndiyo maana mnapoleta huu mpango hapa ni ili sisi Wabunge wote tuujadili vinginevyo msingekuwa mnaleta mngekaa nao huko Serikalini muendelee. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka jana ulipoleta, tena mimi tulikutana pale nje, mimi huwa nasema openly, tulikutana pale nje nikakuambia hizo kodi unazoleta kwenye VAT utaleta chaos, nikakuambia hizo kodi unazoleta bandarini utaleta taabu. Bandarini sikuwa na utaalam sana walau kwenye maliasili nilikuwa najuajua kidogo, lakini zimesababisha shida kubwa kwenye nchi yetu halafu hapa tunalindanalindana, tunafichamafichama kuelezana ukweli na mnamdanganya mfalme kwamba mambo yapo vizuri. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye kitabu chake hiki najua kanuni zinaeleza kwamba hatuwezi ku-review bajeti iliyopita kwa sababu haijapita miezi sita, lakini haya mambo yote uliyoandika yame-based kwenye bajeti ile iliyopita ambayo hata wewe mwenyewe Waziri hukuwepo hapa Bungeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, huu mpango unaouleta hapa haupo realistic kwa sababu Ilani ya Chama cha Mapinduzi aliyomaliza Mheshimiwa Jakaya Kikwete kipaumbele hakikuwa viwanda, hii sasa ya Mheshimiwa Magufuli inazungumzia viwanda. Huu Mpango wako umetuletea mambo ya DARTS na kadhalika ambayo ni mafanikio yaliyopita ya Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Kwa hiyo, mpango huu haupo realistic, upo baseless, tunajadili kitu ambacho hakina miguu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini Serikali hii kwa sasa tunapozungumza mipango Mheshimiwa Waziri Mpango lazima tuwe na watumishi ambao wana confidence. Amezungumza Mheshimiwa Lema hapa ukienda kwa watumishi wote wa umma hawana ujasiri katika nchi hii, mmewa-terrorize wote, hawana confidence, hawajiamini kila mtu akiamka asubuhi hajui kitu gani kitatokea. Haya mambo tunayopanga tutawezaje kuyatekeleza kwa watu ambao hawajiamini! Umma umeaminishwa kwamba watumishi wote wa umma ni wezi, wafanyakazi wote hawana ujasiri wa kukaa kazini, ile morale haipo kwa sababu kila mtu ni mwizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, amezungumza vizuri sana Mheshimiwa Lema tukisema dhamira ya Mheshimiwa Rais ya kutaka kuleta mabadiliko na nidhamu katika nchi hii au ku-restore glory haipo tutakuwa tunasema uongo. Kuna mambo ambayo ameonyesha dhamira nzuri, wote tunakataa rushwa, wote tunakataa mambo mabaya ndani ya nchi lakini njia anazozitumia za kutisha watu na kuvunja sheria hizo ndiyo tunazozikataa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma Ripoti ya Utafiti wa Amani Duniani iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Institute of Economics and Peace ya mwaka 2015, Tanzania ni moja ya nchi 64 duniani zinazokaribia hatari ya kuvunjika kwa amani kwa sababu ya ukandamizaji wa kidemokrasia. Sasa tusipokuwa na amani na kuheshimu na mipaka na mipango tuliyojiwekea wenyewe tutawezaje kusonga mbele na mipango hii mizuri? Hii nchi ni yetu sote, pale Rais anapofanya vizuri tutakubaliana naye, lakini mazuri yake yote anayoyafanya yanaharibika pale alipozungukwa na watu ambao hawamwambii ukweli. Sisi hapa tutamwambia ukweli, mtukate vichwa tutamwambia tu, kama yupo uchi tutamwambia upo uchi, we are not scared of him. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Zitto amezungumza hapa Serikali hii haipo coordinated. Ukienda kwa mfano kwenye mipango yako hii hakuna mahali popote ambapo umezungumzia espionage (uchumi wa kijasusi). Wizara ya Mambo ya Nje ndiyo jicho la nchi ambapo mimi nashangaa katika mipango yako ya mwaka jana haikukuambia jinsi ambavyo Congo ni ya muhimu sana katika bandari yetu ya Dar es Salaam, Wizara ya Mambo ya Nje ilikuwa wapi? (Kicheko)
Leo Wizara ya Mambo ya Nje kama ni jicho, kama ipo coordinated ingeweza kusema unapopeleka mpango huu kwamba bandarini tutaongeza kodi kiasi hiki Mheshimiwa Mpango unakosea tutapoteza potential customers. Kama Serikali hii ipo coordinated ulipopandisha VAT kwenye mambo ya tourism Waziri wa Maliasili angekuambia you are wrong tunaenda kupoteza watalii. Hata hivyo, kwa sababu mkiamka kila mtu afanya la kwake, anawaza la kwake na mnashindana kwenda kujipendekeza kwa Magufuli matokeo yake ndiyo mnatuletea mipango ya ovyo ovyo. Tupo hapa kama Bunge, hampo coordinated ndiyo maana Mheshimiwa Kigwangalla anaweza akasema dawa zipo kidogo, Mheshimiwa Ummy anasema zipo za kutosha na Makamu wa Rais anasema hazipo, tumsikilize nani sasa, the same government! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri najua ni msomi, Mpango huu kuna tafiti nyingi ambazo hata rafiki yangu asubuhi amezizungumza hapa. Ukiangalia tafiti zilizofanywa na Taasisi ya Kimataifa ya GCI kuhusiana na mazingira bora ya uwekezaji Tanzania inashika nafasi ya 120 kati ya nchi 140 zilizotajwa kwenye uwekezaji huo. Ukiangalia moja ya matatizo tuliyonayo Tanzania nchi yetu imekuwa ni ya nne, mazingira ya uwekezaji hayajawa mazuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Tanzania inahesabiwa kwamba hatujawa wazuri katika matumizi ya teknolojia. Huu mpango hautafsiri ni namna gani tunapambana na hayo maeneo ili tutengeneze mazingira mazuri ya uwekezaji. Kwa hiyo, hizi tafiti zinaletwa halafu Mheshimiwa Mpango na wewe unaenda njia yako. Serikali nzuri na jasiri inaweza ikasimama na mimi ningekuwa wewe ningekuja hapa kwa sababu kimsingi hili joto tunaloliona mwezi wa sita mwakani litakuwa kubwa sana na inawezekana Bunge likaondoka na kichwa chako hapa. Inawezekana Mheshimiwa Waziri huu mpango labda ali-copy New Zealand au Australia, ni busara tu kuja hapa na kusema jamani this things it is not going to work here nili-copy mahali nika-paste hapa hai-work, tutaambizana ukweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo ambayo ni kweli tumeshindwa kuyafanya kwa visingizio mnavyovileta, lakini kuna mambo we told you, ulishupaza shingo ukakataa. Kuna data nyingi zinaonyesha jinsi ambavyo Serikali yetu haina mazingira mazuri ya uwekezaji. Zimekuwa ni ngonjera nyingi hapa na kukandamiza demokrasia na kupiga wapinzani na yote yanayoletwa hapa yanakuwa hayatekelezeki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi niwaombe Wabunge, hii nchi ni yetu sote na wala hatuitaji kugombana, tunahitaji kama Wabunge tuongee lugha moja lakini kwenye ukweli tumwambie mtu amefanya vizuri na kama amefanya vibaya tumwambie amefanya vibaya. Msingi wa kwanza lazima turudishe demokrasia katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii hali mnayotaka kuiweka kwenye Chama cha Mapinduzi ya kuogopa watu mnaitoa wapi? Hata Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema tusiogope watu, tuwaheshimu watu. Leo ndani ya chama chenu mmeanza kuogopa watu hicho chama chenu hakina wazee cha kuwaonya watu wasiogopwe? Hivi vyeo ni dhamana, alikuwepo Baba yetu wa Taifa na nataka niwaambie Serikalli ya Awamu ya Tano msidhani wale wa Awamu za Kwanza, ya Pili, ya Tatu na ya Nne hawajafanya mazuri na hata wapinzani hatusemi hivyo, kuna mambo mazuri ambayo Baba wa Taifa aliyafanya lazima tuyaenzi na kuyaheshimu, lakini kuna mambo mabaya aliyoyafanya tutayakataa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi kuna mambo mazuri aliyafanya na mabaya aliyafanya mazuri tutayaheshimu na alikosolewa, alisikiliza, tukampenda. Akaja Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alifanya mambo mazuri tukampigia makofi, tulipenda hata hotuba zake za kila mwisho wa mwezi zilikuwa ni hotuba zilizoshiba siyo za vijembe za kutukana watu, lakini kuna mambo mabaya tulimsema. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, akaja mzee wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na kwamba tulim-challenge ni kweli, pamoja na kwamba kuna mambo hatukukubaliana naye lakini alisaidia nchi hii kwenda mbele. Kipindi chake aliweka mazingira walau watu duniani walianza kupenda kuja kuwekeza Tanzania na walau aliruhusu demokrasia. Tulimsema humu ndani lakini alihakikisha kila mtu kama Mtanzania anatoa mawazo yake, leo kwa nini Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli asisemwe? Tulikuwa tunakaa naye pale kwenye kiti tunamfuata pale leo tunamuogopa ana mapembe? (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe Wabunge wa CCM hebu tuweke itikadi zetu pembeni, tusimame kama Bunge, Rais akikosea tuwe na uwezo wa kusema no, wewe ni Rais wetu lakini hapa no. Hatuwezi tukawa waoga, anatisha kila mtu na kila mtu anajipendekeza kusema uongo. Hii nchi ina hali mbaya lazima tushirikiane. Ninyi mnaopeleka hiyo mipango kwa sababu mnamzingira akisimama kwenye vyombo vya habari anasema wale waliokuwa wanaiba pesa ndiyo wanapata taabu, hivi maskini wanaouza vitumbua kule…
T A A R I F A...
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa ya Mheshimiwa Simbachawene siipokei na haya ndiyo niliyoyasema ndiyo uoga tunaouzungumza huo. (Makofi)
La pili hayo maneno aliyoyazungumza Mheshimiwa Simbachawene wakaongee kwenye party caucus. Hapa tunaongea...
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja yangu ndugu zangu nimesema hapa hakuna mpinzani yeyote anayesema Serikali zilizopita hakuna mazuri yaliyofanyika, hakuna anayesema hivyo. Tunachosema mabaya tutakosoa na tutaendelea kukosoa. Kama ninyi mnamuogopa Mtukufu Rais sisi tutamsema, tutamkosoa ndani ya Bunge na nje ya Bunge na akifanya vizuri tutamwambia.
Niombe Wabunge wote tushikamane, tunapojadili mambo mazuri ya nchi wote tuwe pamoja uchumi uko vibaya, hakuna pesa mifukoni hakuna pesa kwa watu. Mheshimiiwa Rais mnam-mislead eti anasema waliokuwa wanapiga rushwa ndiyo wana shida huko mitaani mama ntilie kwenye majimbo yenu walikuwa wanapiga rushwa wapi?
Watu wana hali mbaya. Wanashindwa kulipiwa ada halafu mnakuja hapa mnasema wapiga rushwa walikuwa wanapiga rushwa wapi kwenye majimbo yenu. Hivi ninavyozungumza nyuso zenu zinawashuka kwa sababu mnajua ukweli huo kwamba hali ni mbaya. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nawaomba wote tuchangamke tumdhibiti Waziri wa Fedha alete mipango na bajeti inayoeleweka. Mawaziri wengine mnabeba mzigo sio wenu, wakati wa bajeti mwaka jana tulikuwa tukiwaambia pesa hazitoshi mnasema aah zinatosha hivyo hivyo. Sasa hivi kwenye Kamati mmerudi tena mnasema kwa kweli hazitoshi mtusaidie ninyi ninyi, sasa hivi mnasema hazitoshi. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, suala tumbane Waziri wa Fedha alete mipango inayoeleweka siyo mipango ya ku-copy na ku-paste sijui kutoka wapi iwe katika mazingira ya kwetu. Tuletee mipango in our context siyo mme-copy New Zealand au sijui Australia huko it doesn’t work here.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mkataba wa Ubia wa Uchumi baina ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. In principle, nakubaliana na mawazo ya Serikali kwamba mkataba huu tusiusaini, lakini kuna mambo ambayo kama Wabunge na kama wawakilishi wa wananchi lazima tuyajadili kwa pamoja tuone faida na hasara. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napingana sana na wenzangu wanaofika hapa wanasema kwa sababu Mheshimiwa Mkapa amesema, Mheshimiwa Magufuli amesema, kwa hiyo, hatuusaini.
Mheshimiwa Spika, wajibu wetu sisi kama Wabunge hapa na hii ndiyo tabia ya Watanzania wengi, hatupendi kuhoji, hatupendi kudadisi, hatupendi kubishiwa. Hiki kitu kimekuja hapa, tuna haki ya kuhoji, kudadisi na kuuliza ili tukubaliane. Sisi siyo nyumbu kwamba tuingie tu mtoni, kwa nini mnataka tusidadisi? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, huu mkataba wataalam walipokuja juzi hapa, Profesa Kabudi alifafanua vizuri sana, lakini katika article 140 na kitu, alizungumza article karibu 20 au 15. Alizijadili hapa vizuri sana kwa weledi. Sisi kama Taifa amezungumza vizuri sana dada yangu hapa, tuna tabia ya ku-complain, tuna tabia ya kulialia! Complainers attract complainers. Kila wakati tunalalamika. Nakubaliana kabisa kwamba hii ni vita. Kila mtu anataka kupata hii keki ya uchumi duniani; kwa nini mnadhani Kenya wakubaliane na sisi kama wao hawapati maslahi? Kwa nini mnafikiri Europeans waje hapa kufanya mikataba kama wao hawana maslahi?
Mheshimiwa Spika, ni wajibu wetu sisi kama Taifa kutengeneza mazingira ambayo na sisi tuta-capitalise kupata faida. Siyo kila saa tunakuja hapa tunalialia, Kenya wametuzidi, Kenya wametuzidi. Kama wewe ni mpumbavu, upumbavu wako hauwezi kutoka kwa sababu unamchukia mwenye akili. We are responsible kujifunza kwa nini Kenya kila siku wanakuwa pro-active na sisi tunachelewa ku-capitalise huko mbele? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wenzetu tunalia nao hapa kwamba wana mazingira mazuri. Sisi hapa tunalalamika; Mzee wa sound hapa kila siku ana viwanda vya kwenye mabegi. Sasa kama tuna viwanda vya kwenye mabegi, tutaenda kuuza nini Ulaya? Kutokuwa na kitu cha kuuza Ulaya is that their problem or is our problem? Badala ya kwamba sisi tukae hapa tujadiliane ni kitu gani tutapeleka Ulaya, tunalaumu kwa sababu hatuna kitu cha kuuza Ulaya. Is that their fault? That is our fault. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumezungumza kwenye bajeti iliyopita, tumelalamika sana jinsi ambavyo Wizara ya Mambo ya Nje, imekuwa dhaifu katika masuala ya diplomasia ya kiuchumi. Ni kwa sababu hatuna wataalamu ambao wanaangalia mbele kuangalia Tanzania tunahitaji nini.
Mheshimiwa Spika, amezungumza dada yangu hapa, ukianza kujiuliza kaka yangu Mwijage hivi tunahitaji nini? Kwenye East Africa tunataka kupata nini? Tunataka kufanya biashara ipi? Iko kwenye makaratasi hapa halafu mnataka kutuambia Waheshimiwa Wabunge tukienda kwa wananchi...
Taarifa...
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Nakushukuru kwa taarifa, lakini wazungu sio watawala wa Kenya. Kenya inatawaliwa na Uhuru Kenyatta ambaye ni Mswahili.
Mheshimiwa Spika, ninachotaka kusema hili suala la blame shift, kila siku tuna-blame wengine tunashindwa kuwa responsible kwa uchumi wetu, hebu tuliache. Kwa sababu Wizara ya Mambo ya Nje ina udhaifu mkubwa sana katika nchi hii katika masuala ya diplomasia ya kiuchumi.
Mhemiwa Spika, nimemuuliza ni kitu gani tunataka kama Taifa upande wa Afrika Mashariki, ni kitu gani tunataka SADEC? Tunakuja hapa tunalialia tu, lakini hatujui tunataka nini. Hebu tuambie kwa mfano Wabunge tunataka tufanye biashara vipi na Afrika Mashariki, Ulaya, Marekani, Afrika ya Kusini au na Brazil? Tunataka tufanye biashara gani? Tunayo mikataba.
Mheshimiwa Spika, la pili, tumezungumza juzi kwenye ripoti ya …
Mheshimiwa Spika, naomba unilinde kwenye muda wangu, naona wanani-disturb sana.
Mheshimiwa Spika, kwenye ripoti ya GCI imezungumza sana jinsi ambavyo mazingira hata ya kufanya biashara katika nchi yetu ni magumu sana; mojawapo ya mazingira magumu ni kwamba Tanzania hatuna utaalam hata wa TEHAMA.
Mheshimiwa Spika, nchi za nje zinashindwa kufanya biashara na sisi kwa sababu hatuna utaalam huo. Mazingira ya rushwa, ufisadi na urasimu katika kufanya biashara, haya mambo hatu-deal nayo, matokeo yake tunaanza kuwalaumu Kenya, tunailalamikia Kenya, Kenya wanatuzidi, wametutangulia. Is that their problem or our problem?
Mheshimiwa Spika, pamoja na haya mambo yote ambayo Serikali ilileta wataalam hapa ambayo nakubaliana nayo kwamba lazima tuwe waangalifu, lakini lazima tuji-position mahali ambapo tuwe na uwezo wa ku-compete Kimataifa, siyo kulialia. We are like babies, every time tunalia, Kenya wametutangulia. Kwani wewe kutanguliwa unaona tatizo gani? Tulipata uhuru kwa pamoja; kila siku tunalialia Kenya wajanja, Kenya wajanja. Hapa Tanzania tunalalamika, Kenya wajanja; ukienda kwenye aviation, Kenya wanatuzidi; hata hapa Tanzania, wao wako zaidi.
Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye tourism, Kenya wametuzidi. Tunalialia. Hatuandai watu wetu, hamweki mipango madhubuti ya kuandaa watu wetu kwenye mazingira ya kibiashara, tunabaki kulialia, mwisho wa siku tunakuwa kwenye mkia.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, namshauri Mheshimiwa Kaijage.
Si Kaijage jamani!
MBUNGE FULANI: Mwijage!
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwijage, nakushauri, hivi viwanda vyako vya kwenye mabegi na kwenye mifuko ni kweli hatutapeleka bidhaa Ulaya, haiwezekani. Ni lazima tutengeneze mazingira. Mnalalamikia Kenya eti viwanda vya Wazungu viko Kenya, kwa nini nyie msilete viwanda vya wazungu hapa? Kwani si Watanzania wataajiriwa? Hiyo Dangote ni ya Mtanzania? Si ni Mnaigeria amekuja hapa Watanzania wanaajiriwa? Tusitafute visingizio tunashindwa kujipanga wenyewe, tunashindwa kutengeneza mazingira mazuri, halafu inapokuja mikataba hii tunaanza kulaumiana.
Mheshimiwa Spika, kubwa zaidi, nimemwona Mheshimiwa Hawa Ghasia hapa, mazungumzo mengine anayozungumza siyo ya kidiplomasia; ya kusema watu wengine tuna- support kwa sababu ya ushoga, hii siyo lugha za kidiplomasia. Tanzania siyo kisiwa, tunahitajiana vizuri sana.
Mheshimiwa Spika, la pili ambalo tunatakiwa tujue, kwa nini Kenya wamesaini? Lazima tujue kwa nini Kenya wamesaini? Haya masuala ya kidiplomasia ni vizuri tukatoa michango ya kidiplomasia kwa sababu tunahitajiana na watu wengine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, leo wakenya wamesaini, Watanzania tunakaa pembeni; lakini kumbuka kuna siku kutakuwa na jambo ambalo Watanzania tutakuwa na faida nayo kubwa, lakini kuna uwezekano tukamhitaji Kenya au Rwanda. Wao watakapochomoa, itakuwaje? Kwa hiyo, haya ni mambo ambayo ni lazima tujadiliane kama Taifa, siyo tukiwa blind; lazima tujadiliane tu-dialogue.
Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na Taarifa ya Mwaka ya Shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kwa Kipindi cha Januari, 2016 hadi Januari, 2017
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi, nianze kwa kusema kwamba na mimi ni Mjumbe wa Kamati hii, kwa hiyo ninaunga mkono hoja na nipongeze Wajumbe wenzangu wa Kamati pamoja na Mwenyekiti wa Kamati, ninaamini tumefanyakazi nzuri na tunaiomba Serikali ipokee ushauri ambao tumeishauri kwa ajili ya manufaa ya Taifa letu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi kama Mjumbe nilitaka nizungumze kwa ujumla mambo yanayohusiana na amani na utulivu wa nchi yetu. Ripoti ya utafiti iliyotolewa na Instituteof Economics and Peace inazungumzia na inaonesha kwamba Tanzania ni nchi ya 64 kati ya nchi 64 ambayo ipo hatarini kutoweka kwa amani. Kwa hiyo, Kamati yetu inahusika na mambo ya nje, ulinzi na usalama na ili ustawi wa amani katika nchi yetu ni lazima eneo hili liendeshwe kwa weledi, kwa utaalam, huku demokrasia ikishamiri katika nchi yetu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ripoti hii imetaja ma-group manne ya nchi namna ambavyo yana-exercise utawala wake. Inasema pale ambapo kuna full democracy kunakuwa kuna amani ya kutosha na kunakuwa na maendeleo ya kutosha kwa sababu watu wanakuwa na uhuru wa kutoa mawazo yao, watu wanaweza waka-challenge na kukosoana kwa amani kwa sababu kuna full democracy. Kwa hiyo, katika ripoti hii inaonesha kwamba kukiwa na full democracy nchi huwa ina flourish. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ripoti hii imeeleza vilevile kuna frauddemocracy, democracy ya kiasi; kunapokuwa kuna democracy ya kiasi kunaanza kuwa na viashiria vya uvunjivu wa amani. Kipengele cha tatu kuna hybrid regime ambayo ndiyo Tanzania tunaangukia hapo kwamba tuna utawala wa kichotara ambapo kuna aina fulani ya demokrasia, lakini kuna aina fulani ya udikteta. (Makofi) Katika ripoti hii inasema nchi yoyote ambayo inaangukia katika eneo hili inakuwa kwenye hatari ya kupoteza amani na Tanzania tupo kwenye hatari ya kupoteza amani kwa sababu tupo kwenye hybrid regime. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni authoritarian regime ambayo hiyo ni ya kidikteta kabisa ambako bado hatujafika na tumeona madhara ya kuwa na regime za namna hii. Kwa hiyo, tunapozungumzia suala la ulinzi na usalama ni jambo la msingi na ni jambo la muhimu sana tukifuata taratibu, sheria na kanuni tulizojiwekea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeyazungumza yote haya kuweka kama msingi. Taifa letu ili tusiingie kuwa eneo la mwisho kabisa ambalo ni hatari, ni lazima tuzingatie sheria na taratibu ambazo tumejiwekea wenyewe. Kwa hiyo, ningeomba vyombo vya ulinzi na usalama na ningeomba watawala wanaohusika sheria ambazo tunazitunga hapa tukizifuata wote tutajikuta tunaiweka nchi yetu katika usalama na hatimaye uchumi wa nchi yetu utakua. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, nikiangalia Wizara ya Mambo ya Ndani nataka nimnukuu Mheshimiwa Kafulila jana ali-tweet, amezungumzia tuna chombo kwa mfano hiki cha National Drug Control Council ambapo ndani ya chombo hiki yupo Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani, ambao hawa wote wanashughulika na chombo hiki kwa ajili ya kudhibiti pamoja na Waziri wa Afya naye yumo na wengineo. Hawa wote ni chombo ambacho kimeundwa kwa ajili ya kudhibiti dawa za kulevya na kipo kisheria. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nimezungumzia masuala ya ulinzi, kila Kiongozi ana mipaka yake na kila Kiongozi amepewa majukumu yake. Kuna chombo kama hiki nilitaka niulize Wizara ya Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mwigulu upo hapa, kumetokea kitu gani badala ya hiki chombo kushughulika na masuala ya msingi kama haya ambayo sisi sote tunaunga mkono vita ya kupambana na dawa za kulevya, leo siwaoni Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani na Waziri wa Afya mkishughulika na mkitoa matamko kwa sababu ninyi ndiyo wenye chombo hiki, tunamuona Makonda ndiyo amebeba bango la nchi nzima ambaye ni kiongozi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam sawa tu na Mheshimiwa Amina Masenza, Mkuu wangu wa Mkoa pale Iringa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini Mheshimiwa Makonda yeye ndiyo abebe bango na chombo kikubwa ambacho kinatakiwa kifanye kazi hiki kikae kimya. Ningeomba haya mambo Serikali ijaribu kufafanua, kwa sababu haya ndiyo mambo ambayo yanasababisha utengamavu na utulivu wa nchi yetu upotee bila sababu. Mtoto aliyehongwa na mama yake huwa tunamuita mummy’s boy au mummy’s girl lakini inaonekana Makonda labda ningemuita daddy’s boy. Kwa sababu anaweza akasema chochote anachotaka wakati wowote hajui na mipaka yake, hii inaweza ikatuletea matatizo katika nchi yetu. Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda siyo mtaalam wa mambo ya uchunguzi. Mwenyekiti wangu wa Kamati umekaa kwenye kitengo hicho utaweza kutusaidia. Polisi wamesomea, wanaweza kufanya investigation ya mambo haya, sasa watu wote tumekaa kimya nchi hii where are the lawyers? tuna Tanganyika Law Society,where are thelawyers, tunapoona mambo yanaenda vibaya tumekaa kimya. Where are thejudges hatuoni Majaji wakitoa matamko kuonesha kwamba kila mtu akae kwenye msimamo wake ili nchi yetu iweze kuwa na utulivu na amani, watu wote wamekaa kimya, tunalipeleka wapi Taifa ambalo kila mtu akiamka asubuhi anaamua kufanya jambo analolitaka na wachungaji wamekaa kimya, lakini wengine tunaona wakipewa zawadi wanasema at least mimi nasema hapa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana kuna checks and balance, wahenga/wataalam wa mambo ya utawala walivyoamua kuweka mihimili mitatu hawakuwa wajinga, waliona anaweza akatokea kichaa mmoja akaamua kufanya anavyotaka, Bunge letu hili lipo kwa ajili ya kazi hiyo mambo yanapokwenda hovyo lazima tusimame kama muhimili kumrudisha nyuma yule anaekwenda vibaya na maamuzi tuliyoyafanya. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, my question is where are the judges in thiscountry and where are the lawyers, tunawasomesha kwa gharama kubwa wanasoma sheria ili iweje? Lengo tunataka tukae katika nchi yetu kwa usalama na haki. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ripoti hii imezungumza vizuri sana juu ya jinsi ambavyo amani inaweza kutoweka. Lakini kwa sababu ya muda ninataka kusema Bunge hili kwa sababu ya kutokujua au kwa makusudi tulitoa maamuzi ambayo mengine ni ya hovyo katika nchi yetu, ni wakati sisi kama watunga sheria na muhimili ambao ni wa muhimu katika Taifa letu tufike mahali tujitafakari. Kwa mfano, tulipitisha sheria ambayo inaminya upatikanaji wa habari ambayo inawasaidia watu wachache, hii sheria tulipitisha hapa lakini mwisho wa siku itatugeuka ni kiashiria ambacho kinaweza kikasababisha tuvunje amani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile Bunge letu hili ambao ni muhimili muhimu katika taifa letu limekosa uhuru, limekuwa ni Bunge ambalo linaminywa, hatuwezi kuikemea Serikali tena, why are we here? Mheshimiwa Mwenyekiti, tupo hapa kufanya nini kama hatuwezi kuidhibiti Serikali na tunapoidhibiti Serikali siyo maana yake tunataka kuiangusha, tunataka itembee katika mkondo wake ili amani yetu itulie na ndiyo kazi ya Bunge. Kazi ya Bunge ni kuidhibiti na kuisimamia Serikali ienende kama inavyopaswa. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mwenzangu hapa ametoa mwongozo tunaye Katibu wa Bunge hapa anayetakiwa atuongoze tunapokaa hapa; sasa leo anaenda kwenye vyombo vya habari anasema Bunge limekosea. Na yeye anafanya kazi yetu ya Bunge hatujaajiriwa na yeye hapa with duerespect, anafanya kazi ya Bunge hajatuajiri yeye sisi hapa; anatakiwa afuate maagizo yetu. Na ana wataalam wanaotushauri anatakiwa atuelekeze where are we heading? Haya ni masuala tunahitaji tujadiliane siyo kwa kugombana ni kwa kujadiliana wote kwa pamoja. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine la pili ni Serikali kupiga marufuku vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara, huko ndiyo tunaweza kuona mambo mengi ambayo yanaenda hovyo, tukaongea kwa uhuru, tukaisaidia Serikali ienende vizuri. Haya mambo tunakaa kimya tunashangilia mtu mmoja anaamua halafu tunakaa kimya watu wote, where are we heading? (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine Asasi za Kiraia zikijaribu kuzungumza nazo zinazuiwa na zinakatazwa, haya ni masuala ambayo tunapaswa tujiulize tunakwenda wapi. Ni maoni yangu kwamba ni vizuri tukasonga mbele na ni vizuri tukatafakari kama Bunge, je, tunafanya wajibu wetu, tunatimiza wajibu wetu kama muhimili? MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa, dakika moja tu.
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho niseme hii nchi yenye Bunge kibogoyo, TAKUKURU kibogoyo, vyombo vya habari bubu, NGO bubu na siasa bubu, polisi kibogoyo na National Drug Control kibogoyo, hatuwezi kuepusha michafuko katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niwaombe wote kwa pamoja na kwa kumalizia dakika ya mwisho kabisa mchungaji mmoja kule Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia aliwahi kusema; “Silence in the face of evil it is evil itself, God will not hold us guiltless not to speak is to speak, not to act is to act.” Kwa hiyo, hatupaswi tukae kimya katika haya mambo haya mabaya, ningewaomba Wabunge tushirikiane wote kwa pamoja tuulinde muhimili wetu, nashukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, takwimu zinaonyesha kwamba toka mwaka 1980 mpaka 2010 Afrika pamoja na resources tulizonazo tumepoteza kiasi cha dola trilioni 1.4. Takwimu hizi zinaonyesha hii yote imesababishwa na uongozi mbovu katika Bara la Afrika. Mojawapo ya sababu ni
kutokuwepo mwendelezo wa viongozi wanapobadilishana madaraka. Nchi yetu katika Serikali hii ya Awamu ya Tano kumekuwa na changamoto kubwa sana ambazo takwimu hizi zina-cement kwamba na sisi kama Taifa tunaweza tukaendelea tena kupoteza mali tulizonazo kwa sababu ya tatizo la uongozi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Mtawa mmoja wa Kikatoliki aliishi miaka 1953 kule Marekani anaitwa Bishop Sheen, aliwahi kusema; “Civilization is always in danger when those who have given the right to command have never learned how to obey.” (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nchi yetu iko kwenye kiza kinene kwa sababu kuna watu wengi sana ambao wamepewa mamlaka ya kuamrisha lakini wao wenyewe hawajawahi kujifunza namna ya utii. Nazungumza haya kwa masikitiko makubwa sana kwamba tatizo kubwa tulilonalo
katika Serikali ya Awamu ya Tano ni poor leadership skills ambayo hii inaweza ikatupelekea tukaingia kwenye matatizo makubwa sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri amezungumzia sana masuala ya Chuo cha Uongozi, lakini nina wasiwasi sana kama hiki chuo kina mtaala wa namna ya kuwa-train hawa watu. Kwa bahati mbaya katika nchi yetu uongozi unakuwa defined kwa title au status badala ya
function. Uongozi wa sasa hivi tulionao wa Awamu ya Tano ni uongozi ambao ni bully, ni uongozi ambao ni una-scream, ni uongozi ambao una-shout, ni uongozi unao-intimidate badala ya kuonyesha njia. Kwa sababu ya uongozi huu umeparalyze civil service na tuki-paralyze civil service maana yake itashindwa ku-produce. Watu wako intimidated na uongozi huu hauko based kwenye merit kwa sababu watu hawajawa
trained.
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini utanitunzia muda wangu lakini na wewe mwenyewe umechanganya actually, sasa sijui hapo umesemaje, sijui ni Kiswahili hicho?
Mheshimiwa Naibu Spika, katika society ambayo nimeritocracy the blind cannot lead the sighted, uninformed cannot lead the wise and the unskilled cannot direct the skilled. Katika uteuzi wa Mheshimiwa Rais, amechukua makada wengi wa Chama cha Mapinduzi amewaingiza
kwenye civil servant ambayo hiyo ina-cripple utendaji wa kazi. Haya mambo hatuwezi kuyanyamazia kwa sababu hili Taifa ni la wote na ni kinyume kabisa na utaratibu. Ndugu zangu wote tukumbuke hapa tunapokwenda kwenye uchaguzi watu wote sisi tunakuwaga hatuna madaraka sisi wanasiasa, huwa wanabaki civil service, ukii-cripple civil service maana yake unaua utendaji kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimshauri tu Mheshimiwa Rais ambapo wenzangu wengi wanaogopa sana hata kumshauri, maana yake Mheshimiwa Rais akisema mkikamata watu wanavunja sheria ng’oa matairi kuna watu wanapiga makofi kinyume cha taratibu. Mheshimiwa Rais akisema mimi sikuleta matetemeko wanapiga makofi.
Mheshimiwa Rais akisema mkikutana na jambazi huko hata kabla hajapelekwa mahakamani kinyume cha sheria watu wanapiga makofi, wanadhani kumsifu Mheshimiwa Rais kwa kile anachokifanya ni uzalendo. Tunatengeneza Taifa la waoga ambapo tuna cripple national kama hatuwezi kucriticise viongozi wetu. Tuko hapa kuwafanya viongozi wetu wawe accountable na ndiyo wajibu wetu, (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Thomas Jefferson, Rais wa Marekani aliwahi kusema ukiona wananchi wanaiogopa Serikali jua Serikali hiyo ni ya kidikteta. Ukiona Serikali inawaogopa wananchi jua Serikali hiyo ni ya kidemokrasia kwa sababu Serikali lazima iwe accountable kwa wananchi.
Sisi hapa kama Wabunge tuko hapa kuwawakilisha wananchi, the government must fear us. Serikali lazima ituheshimu sisi kwa sababu lazima iwe accountable kwetu.
Leo tunafika Bungeni tunanyamazishwa eti tusiikemee Serikali, why are we here? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi kama kiongozi, wewe kama kiongozi you are accountable to us, Serikali mko accountable kwa Bunge hili. Sasa kila kitu mna-protect, chochote mnachofanya mna-protect, Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa ni ku-scream, shouting. Huwezi kujua leo ni msiba au leo ni harusi, huwezi kujua leo wako kwenye matatizo, leadership is about inspiring people, putting people to work is not about screaming and shouting. Tuna uongozi wa Awamu ya Tano ambao una-shout, una-scream unaintimidate everybody kwa hiyo ume-paralyze watu kufanya kazi. Halafu wengine wasomi hapa na ninyi mnakaa kimya mnapiga makofi mambo ambayo ni kinyume na utaratibu wa sheria ya nchi yetu, where we heading? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, the unskilled cannot direct the skilled. Tumekubali kuweka akili zetu mfukoni tunaongozwa na wale ambao ni unskilled. Leo tuna watu kama akina Bashite amesema Sheen hapa, those who have never learned how to obey they have given the right to
command, mtu kama Bashite anachokijua ni kuvaa shati la kijani na kumtukana Lowassa, ndicho alichoweza. Leo anakuwa Mkuu wa Mkoa anatoa amri kubwa halafu tunampigia makofi. Wale ambao ni incompetent wanawaongoza competent, kwa hiyo, utendaji kazi
unashuka wanaona sasa hata maana ya kusoma haipo. Kwa hiyo, mtoto yeyote anachoona ili niwe kiongozi ni kujua kumtukana mtu mmoja wa chama kingine, wapi tunakwenda jamani?
Mheshimiwa Naibu Spika, tuna wanasheria kwa mfano Mwanasheria Mkuu hapa, wajibu wake mkubwa yeye ni kuhakikisha Serikali inafanya kazi lakini na yeye amegeuka amekuwa Mbunge anatetea Serikali. Badala ya yeye kunyoosha akiona Serikali inakosea anasema Chief Whip
hebu ili jambo tu-withdraw tukajipange vizuri kwa sababu yeye ni kuweka mambo vizuri mwisho wa siku huu ni mtumbwi wa sisi wote lakini kilichotokea ni kati ya upinzani na sisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna mtaalamu mmoja anasema Taifa ambalo linazalisha soft minded people linanunua kifo kwa installment cha Taifa lenyewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mnadiscourage criticism katika Bunge, mna-discourage dialogue mnataka tuwe tunapiga makofi, why are we here? Kama mngetaka tusije hapa mngetuzuia kule kule Iringa wakati wa uchaguzi, the fact kwamba watu wa Iringa wamenileta
hapa I will speak, I will talk.
Mheshimiwa Naibu Spika, leo tuna TISS (Usalama wa Taifa) ambapo kazi yake kubwa ni ku-protect Chama cha Mapinduzi badala ya ku-protect nchi. Ukija kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi robo tatu utawakuta watu wa TISS wamevaa nguo za kijani, they are busy na Chama cha Mapinduzi. Tunazungumza hapa kuna mauaji, utekaji lakini ni kwa sababu wameacha mambo ya msingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, in this country kila mtu anaweza akafanya jambo lolote. Jeshi linaweza likakusanya kodi na bunduki, leo tunakusanya kodi na bunduki (with guns). Hujui nani anafanya nini na kwa ajili ya nini ni kwa sababu nchi haina priority, poor leadership.
Mheshimiwa Naibu Spika, niwaombe ndugu zangu hebu tujipange Serikali ni ya kwenu, tuji-reorg, tujipange vizuri kwa sababu ni kama ubongo ambao uko scattered, you are every where, there is no priority. Mara tunaenda Dodoma, mara leo Bashite anakamata sijui watu gani, mara huyu ametumwa nini na kwa sababu hatuna priorities hatujui tunataka kufanya nini. Ni kama vile wataalamu hawapo katika nchi hii.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunatoa mawazo yetu lengo ni kuifanya Serikali yetu iwe nzuri. Tume-discourage fikra ambazo zina criticize kwa sababu hakuna mtu ambaye hawezi kuwa challenged katika ulimwengu huu. Kuwa challenged ni sehemu ya uongozi ili ujipime, sisi ni mirror yaani sisi ni kioo chenu huwezi kwenda kwenye kioo nywele hujachana unakipiga ngumi kioo sasa utajionaje, mnatupiga sisi sasa mtajionaje?
Mheshimiwa Naibu Spika, sisi ni kioo chenu tunawaona hivyo mnavyofanya, wote mmekuwa waoga (terrified). Mawaziri wote mko-terrified hapo, Wabunge mkoterrified tukitoka huko nje ndiyo mnatuambia ee bwana lakini hapa mnasema kweli na wengine nikitoka nje mtaniambia
lakini humu ndani hamsemi.
Mheshimiwa Naibu Spika, niombe Usalama wa Taifa wafanye kazi yao vizuri. Tumezungumza mauaji hapa sina muda wa kusema, baada ya Wabunge kusema kuna watu wako-tortured sana kule Mpingo wanafungiwa kwenye kachumba kadogo, wanakojoa humo humo, wanajisaidia
kwenye rambo wanateswa halafu wakionekana hawana hatia wanawadampo kwenye kituo cha mabasi pale wengine wako kwenye Jimbo langu toka Iringa wanaachwa na nauli tu. Hatuna muda wa kusema tu lakini haya mambo yapo watu wanakuwa totured tukisema hamtaki kusikia.
Muswada wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari wa Mwaka 2016
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie kwa kifupi. Niseme tu tuliku-miss wewe Mheshimiwa Chenge, karibu tena tunafurahi kukuona. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti…
MWENYEKITI: Hebu acha matani yako, ulini-miss mimi? (Kicheko)
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nchi yetu ni ya kidemokrasia na naomba ninukuu maneno machache, Novemba 1883, aliyekuwa Rais wa Marekani wakati huo, Abraham Lincoln aliwahi kutoa hotuba moja maarufu sana inayoitwa The Gettysburg Address ambayo alisema Serikali ya watu, inayotokana na watu, kwa ajili ya watu. Sisi kama Tanzania tumeamua kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi, mfumo wa kidemokrasia. Nikirudi kidogo kwenye historia, dunia imepitia hatua mbalimbali, mifumo ya kidikteta, mifumo ya kichifu mpaka tumefika kwenye mfumo wa kidemokrasia ambapo Serikali ya watu, kwa ajili ya watu, haiwi mali ya mtu mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nayasema haya kwamba kama Taifa tunajitungia utaratibu ambao kila mtu ataufuata kwa mujibu wa Katiba yetu ambayo tumeiweka wenyewe. Napata ukakasi sana kwa kaka yangu, Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe anapouleta huu Muswada, niwe mkweli kabisa naona una agenda ya siri. Ni Muswada ambao tunatengeneza sheria ambapo tunaangalia kipindi chetu cha utawala na wengi wetu hata lifespan ya maisha inakwenda ukingoni, ndiyo tunateremka hatuliangalii kama Taifa kwa siku zinazokuja baadaye. Napata ukakasi kwamba hivi hizi sheria tunazozitunga na tunazileta, mmeshaleta bills nyingi, zipo kwa ajili ya kufurahisha kwamba tuna Bunge la kutunga sheria na tunaweka bills nyingi, kwa sababu sheria tulizozitunga zilizopita hazifuatwi, hazizingatiwi, hazifuatiliwi, kwa nini tunaleta sheria tena? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mihimili yetu mitatu hii, sasa hivi Bunge ndiyo mhimili ambao hauna heshima katika nchi hii. Ni kwa sababu Wabunge tumekosa heshima, tunaamua mambo ya hovyohovyo, mambo ya kipuuzi ambayo hatutafakari. Nimekuta Wabunge wengine wanalalamika jinsi ambavyo hata polisi wanatudharau kwa sababu Wabunge tumeshindwa kusimama kwenye nafasi zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini nasema haya? Mimi binafsi nasikitika kwamba huu Muswada unakuja, tunaye Mwanasheria wa Serikali na Waziri, tunaamini hawa ni wasaidizi hata wa Mheshimiwa Rais, hawa ndiyo wanatakiwa wamwoneshe Mheshimiwa Rais awe anang‟ara Tanzania na nje ya Tanzania. Hata hivyo, kuna mambo ambayo nasema nasikitika Miswada kama hii inakuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe kwamba napata ukakasi na Muswada huu, wakati ule tulikuwa hatuko humu Bungeni, Mheshimiwa Nkamia alisimama hapa ana-challenge hukumu ambayo mhimili mwingine umetoa kule Arusha na Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, huyu ni mtaalam, msomi, anadiriki kusema ule mwenendo wa kesi atam-task DCI aulete wakati taratibu hazisemi kama mtu hajaridhika kwenye mahakama anakata rufaa kwenye mhimili mwingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa napata ukakasi ni nini agenda ya Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe kwenye Muswada huu ambapo haya aliyoyaeleza humu ndani kwa mfano hizo haki za kupata habari za hao Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa, hizo excess zipo, wote si tupo kwenye council kule, nani anamzuia mtu kupata habari hizo kwenye Councils zetu kule, wote wanakuja wanapata hizo habari. Napata tatizo, naanza kujiuliza, hivi nchi yetu inafika mahali, kwa wale walioiona ile movie ya Gods must be Crazy, yule bushman, ametoka porini haelewi kwamba watu huwa wanafuga mbuzi anachukua kamshale kake anapiga mpaka wanampeleka mahakamani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kweli nchi hii sheria hazifuatwi kiasi hicho, Mwanasheria wa Serikali amekaa kimya, Waziri amekaa kimya, anadiriki kutokutafsiri, sasa mimi nauliza hizi habari mnazoleta zitakuwa practiced wapi? Ndiyo hoja ambayo naiuliza, hii miswada uliyoileta itakuwa practiced wakati Katiba inakanyagwa kabisa. Tulitegemea Waziri asimame aseme this is not right, kama hii haikubaliki mimi na-step down, AG anafanya nini ofisini kwa sababu vitu vya hadharani vinakiukwa! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nasema Bunge hili linadharauliwa. Leo katika nchi hii mtu anaona kwamba hata kumpa mtu mafao ya kisheria ni kama favour, AG hasemi, Waziri husemi, halafu leo unatuletea Muswada mwingine tutunge ukatekelezwe wapi sasa? Kwa watu civilized na dunia iliyopevuka kama mambo hayafuatwi kwa mujibu wa sheria wana-step down, sasa hivi mngekuwa mmeficha nyuso zenu. Ndiyo maana nasema napata ukakasi, mnatuletea huu Muswada utakwenda kutekelezwa wapi wakati Katiba inakanyagwa lakini hamsemi na ninyi ndiyo mnatakiwa mseme Mheshimiwa Kwamba this is not right, tumekaa kimya, sasa Bungeni tunafanya nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa hatusemi, tutapataje hiyo heshima huko nje kwamba sisi ni watunga sheria na hizo sheria tunataka zisimamiwe? Hao polisi wana haki kabisa ya kutuburuza na kututania kwa sababu hatuna hiyo hadhi, tulitakiwa tuulinde mhimili huu. Leo mnaleta huu Muswada na kuwazuia whistleblowers. Kwa mfano, Bunge lililopita tulizungumza kuhusu wale wanyama waliotoroshwa. Hivi kwa Muswada huu mnaouleta hapa yule mwandishi aliyeandika atakuwa na uwezo wa kuandika hizi habari.
KUHUSU UTARATIBU.....
MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, dakika zangu nane naomba utanitunzia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na wewe kumuunga mkono Mheshimiwa Mhagama lakini when you talk about Sweden ni watu wako civilized, demokrasia iko wazi siyo kama hapa. Ukimwona Waziri wa Sheria wa Sweden anaji-behave anafuata taratibu, ukimwona AG wa Sweden anaheshimu nchi anafuata Katiba, kwa hiyo, tukilinganisha Sweden na hapa tunakuwa tunajidanganya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunajilinganisha na Rwanda, ndiyo tunachojilinganisha hapa. Hizo reference zote wanazozichukua hizo ni kujificha, it’s just political gimmicks, reference wanazozitoa siyo kwa nchi hii hakuna civilization. Nimesema kwa nchi nyingine yanayotokea na sintofahamu katika nchi hii, Waziri wa Sheria na AG walitakiwa wawe wame-step down kwa sababu ni aibu kwa dunia!
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaikanyaga Katiba halafu watu tunachekacheka hapa, ndiyo maana nasema napata ukakasi kwamba tunaleta sheria wakati Katiba inakanyagwa na hii sheria inatokana na Katiba. Leo anasimama mtu mmoja anasema watu wote wanyamaze halafu tunapiga makofi halafu unasema I am a Member of Parliament, kwa nini polisi wasikudharau? Haya ndiyo ninayoyazungumza, watu hawataki kuzungumza hapa, wote tuko kwenye mess na ndiyo tunatakiwa tujadili hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napata ukakasi kwamba Waziri na AG wanaleta huu Muswada wanao uwezo wa kusimamia hii sheria, ambao nasema kuna kitu kimefichwa nyuma yake. Kwa hiyo, ukiniambia tufuate kifungu cha ngapi, hiyohiyo sheria inanipa uhuru, mimi sijasoma sheria lakini being a theologian najua mme-copy mambo mengi kutoka kwenye mosaic law, namna ya kutafsiri, walau naijua context, principle ambayo interpret scripture na ninyi mnafuata, Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe huwezi kuikata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sheria za nchi hii kama tunafuata tafsiri, Waziri anasimama kutetea kitu ambacho kiko wazi atawezaje kutetea hii? Anatetea kitu cha uwazi kabisa hata mtu asiyesoma sheria anaona kuna makosa. Ndiyo hoja yangu kwamba what is it behind, Wenyeviti wa Mitaa ndiyo wanaitaka hii? Hii ndiyo kazi ya sisi Wabunge tutoe vitu vya maana. Vilevile mimi kutoa mchango wangu sidhani kama natakiwa nipangiwe na wewe na wewe toa mchango wako. Kwa nini usubiri mimi niseme uanze kunisema mimi? Toa mchango wako hapa tukusikilize. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo…
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo. Kwa hiyo, suala langu ninalolizungumza, inakuwa haina maana kuendelea kutuletea bills hapa ambazo hazitekelezwi. Ina maana mawili na mimi nawa-challenge hawa wakubwa wawili, AG pamoja na Waziri, aidha kwenye ofisi hiyo viatu ni vikubwa mno wanatupotezea muda hapa, maana yake hawawezi kufuatilia hizi sheria au hawatoi ushauri au wanaogopa, lakini vyote hivyo viwili wangesema watoke hadharani kwa sababu lazima tulinde Katiba ya nchi, ndiyo hivi vitu vingine vifuatwe. Sasa Katiba ya nchi haifuatwi halafu watu wote mnakaa kimya mnachekelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue hekima zake Shibuda, aliwahi kusema siku moja maabara ikisema Mheshimiwa Mfalme anaharisha usibomoe maabara unatafuta dawa. Hii yote ni kuviziba vyombo vya habari, vyombo vya habari vinasaidia kusema mfalme anaharisha, mfalme anatakiwa atafutiwe dawa ili apone. Sasa mnaziba, hamtaki watu waseme, mnataka tuje hapa tupongezane tu. Humo sisi hatumo na tunaongea kwa nia nzuri Tanzania ipone, wote tufuate Katiba hii si ndiyo imetuleta humu ndani. Wote tufuate Katiba hii hakuna mtu ambaye yuko juu ya Katiba sasa tunaogopana, watu wanajificha, wanakuwa kwenye uvungu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nakumbuka kwenye Biblia wakati wa Gideoni walikuwa wanakwenda kwenye mapango kule wanajificha, everybody is hiding, wengine wanajibembeleza kutaka vyeo, tufanye kazi zetu. Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe nashindwa sana kujadili kipengele baada ya kipengele kwa sababu naona dhana iliyoko nyuma siyo nzuri kwa ajili ya Taifa letu. Niwaombe Wabunge tuache ushabiki, tuchukue nafasi yetu kama Wabunge tulisaidie Taifa. Mwisho wa siku tunamaliza vipindi wengine hawakuwepo wapo barabarani, wengine hizi sheria zinawatafuna saa hizi wamekwenda huko mbali, tuweke sheria ambazo kila mtu ata-comply na kila mtu ataishi kwa raha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kwamba wengine hawayapendi haya, lakini lazima tuyaseme. Anafika mtu mmoja, hivi kwa sheria za nchi kweli Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, Sheria Na.5 ya 1992 ya Vyama vya Siasa ndivyo inavyotafsiriwa vile, seriously?
Mheshimiwa Mwenyekiti, haya. Nilikuwa nasema, namshangaa AG anasimama anatetea, hivi sheria za Tanzania ndiyo zinavyotafsiriwa vile? Hizo ndiyo principles za kutafsiri sheria? Kweli kabisa wanasheria wakubwa tumesomesha anasimama anasema, eeh, hiyo ndiyo hivyohivyo.