Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. William Vangimembe Lukuvi (19 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kufungua Bunge la Kumi na Moja
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, na mimi napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa hotuba yake nzuri; na uzuri huu unajionesha pia kutokana na michango ya Waheshimiwa Wabunge na wananchi ambao sio Wabunge. Tunasoma kwenye magazeti, tunaona kila mtu amefurahia hotuba yake, lakini hata utendaji wa wa awali kabisa ya Serikali yake ya Awamu ya Tano. Kwa hiyo, nampongeza sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nawashukuru sana wananchi wa Jimbo la Ismani kwa kunirudisha tena hapa Bungeni. Nataka kuwaahidi tu kwamba kama nilivyozoea nitawatumikia na nadhani bado wana imani na mimi nitaendelea na nafasi yangu ile ile. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi niliyopewa na Mheshimiwa Rais ni kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Nataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge kwamba nimewasikiliza sana, yote yaliyosemwa mkifungua ukurasa wa 41 mpaka 46 mmezungumza katika maeneo hayo. Maeneo yote mliozungumza yako kwenye ilani, nataka kuwaahidi kwa sababu muda hautoshi, kwamba tunawawekea utaratibu wa kuyatekeleza katika miaka mitano hii. Kwa sababu tuko pamoja tumeshaunda na Kamati tutashirikiana katika kuhakikisha kwamba yote yaliyopangwa katika Ilani ya Uchaguzi wa Chama chetu yanatekelezwa katika kipindi hiki cha miaka mitano kwa ujumla.
Mheshimiwa Naibu Spika, yako mambo ya muda mfupi ambayo tumeamua kuyafanya na juzi mliniuliza. Moja kubwa mmezungumza ni habari ya migogoro, hili ni jambo la muda mfupi, liko kwenye ilani lakini halitaji miaka mitano. Tumekubaliana na rafiki yangu hapa kwamba mtuandikie migogoro; najua kuna migogoro ya mipaka ya vijiji kama nilivyosema, mipaka kati ya vijiji na hifadhi mbalimbali za misitu, wanyama na nini, mipaka kati ya Wilaya na Mikoa. Tukishapata hiyo orodha tutapanga utaratibu. Yale yanayohusu Wizara yangu na Wizara ya Maliasili tutaunda timu ya pamoja na bila kumsahau mwenzetu mwenye ardhi, Serikali za Mitaa ili kuhakikisa kwamba tunapitia migogoro yote na kuipatia majibu. Kwa hiyo, ni jambo ambalo tutaanza nalo sasa, haliitaji bajeti kubwa, ni lazima tuondoe hii migogoro kwa sababu imedumu na imewatesa sana wananchi, hilo tutalifanya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Wizara yangu sasa hivi tunafanya audit ya ardhi. Wako watu tuliyowapa mashamba makubwa lakini hawayatumii vizuri, vilevile wapo watu tumewapa mashamba makubwa, wameweka rehani na bahati nzuri mtu yeyote akiweka rehani mortgage, mimi najua kwa sababu lazima mortgage zile zinasajiliwa kwangu. Wameweka matirilioni za fedha lakini tunataka kujua kwenye mashamba yao hizo trilioni za fedha wameweka?
Mheshimiwa Naibu Spika, baadhi ya mashamba ambayo nimeshayapitia nimegundua pamoja na mamilioni ya fedha waliyochukua, mashamba yao yako vilevile kama walivyoyachukua. Kwa hiyo, tunataka tujue hizi fedha wamepeleka wapi? Kwa hiyo, tunafanya audit kwa watu waliochukua mashamba makubwa kwa maana ya kwamba kama wameshindwa, sheria iko wazi, tutawanyang‟anya, tutawapa wananchi wenye shida au tuawapa wawekezaji wengine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunataka tujue, wale walio mortgage fedha hizo wamepeleka wapi? Kwa sababu sasa iko tabia ya watu kuchua mashamba makubwa sana, tena watu wa aina fulani tu, wanachukua mashamba kila mahali, lakini hawawekezi, wala hawayatumii. Sasa wanachukua kama rehani ili wapate pesa, waende kujenga magorofa kigamboni kwa Mheshimiwa Ndugulile. Hiyo hatutakubali. Tunataka ukichukua fedha, lazima uwekeze katika mashamba yale yale.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hizi ni hatua za muda mfupi, kuondoa kero ya migogoro ya ardhi inayosababishwa na mipaka ambayo sisi watu wa Serikali tunaweza kufanya; lakini ya muda mrefu iko kwenye ilani. Lengo la Serikali katika Ilani ya Miaka Mitano ni kupima kila kipande cha ardhi. Tunaanza mpango huu mwezi ujao kwa Wilaya mbili ya Kilombero na Ulanga. Tunapima kila pande cha ardhi, lazima kiwe na mwenyewe na kumilikishwa kwa hati. Tunafanya Wilaya mbili za majaribio, Ulanga na Kilombero tunaanza mwezi ujao.
Mheshimiwa Naibu Spika, lengo letu tungependa hatua kwa hatua ardhi yote ya Tanzania ipimwe na ikipendeza zaidi, kila mwananchi awe na fursa ya kumiliki ardhi yake kwa hati ili aweze kuitunza, lakini na Serikali iweze kupata mapato.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, yako malengo ya muda mrefu. Nilitaka tu niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge mliosema mengi, tutatembea sana, tutawakuta huko huko, lakini nataka muwahakikishie wananchi kwamba ile migogoro mikubwa ambayo imewakera kwa muda mrefu, tutaisimamia.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nikushukuru sana wewe, lakini nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge waliochangia hoja hii kuanzia Jumamosi hadi leo. Najua kungekuwa na muda kwa hoja hii kila mtu angependa kusema. Kama wengi mlivyosema mtu unaweza ukachagua ukalala barabarani, unaweza kachagua nguo, chakula lakini hakuna mbadala wa ardhi. Kwa mujibu wa Katiba yetu na maisha yetu kila mmoja anahitaji ardhi kwa matumizi yake ya kawaida. Ndiyo lengo la Wizara yangu na Serikali kuhakikisha kwamba katika mpango kazi wetu wa miaka kumi ijayo tunataka nchi hii iwe imepangwa, imepimwa na imemilikishwa. Kila mtu anayestahili kuwa na ardhi awe amemilikishwa ili ardhi yake iwe salama, hilo ndio lengo letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nakushukuru sana na nawashukuru Waheshimiwa Wabunge wote. Nataka niwaambieni msingi wa kazi yetu sisi kama Wizara tunaanzia pale kwenye kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais. Kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi alikuwa anasema na hata sasa anasisitiza kwamba kazi yetu sisi watumishi na viongozi wa Serikali ni kuwahudumia Watanzania wote bila ya ubaguzi. Hiyo ndiyo kazi yetu ya msingi na huo ndiyo msingi uliyojikita katika Wizara hii.
Kwa hiyo, mimi najua na ninyi wenzangu leo mmechangia vizuri mkijua ardhi haina ubaguzi. Ndugu zangu wapinzani mmechangia vizuri sana kuanzia Waziri Kivuli, wenzangu wa Chama Tawala wamechangia vizuri sana, kwa msingi huo kwamba tunatambua na wote tunamuunga mkono Mheshimiwa Rais kwamba tunatakiwa tutekeleze majukumu yetu bila ubaguzi na sisi kama Wizara ya Ardhi ndio motto wetu. Kwa hiyo, matatizo yenu yote mliyoyasema bila kujali yanatoka upande gani, sisi kama Wizara tutayafuatilia huko huko yaliko bila kujali ni Jimbo au Wilaya ya nini ili kuyatolea ufafanuzi, kote tutafika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza zimetolewa hoja hapa kutoka kwenye Kamati yangu ya Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Injinia Nditiye ameunga mkono hoja na ametoa hoja nyingi sana hapa.
Moja, imetolewa hoja juu ya mfumo mpya ambao wengi mmeuzungumzia hapa wa Integrated Land Management Information System. Ndugu zangu katika menejimenti ya ardhi kisayansi ndiyo maana tumeamua kuingia kwenye mfumo huu ili kuondoa kasoro zote ambazo tumeziona na tumekuwa nazo katika miaka yote juu ya usimamizi wa ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kutoa taarifa kama ile niliyoitoa hapa kwamba mfumo huu siyo kwamba umekwama maana wengi nafikiri sikuwapa taarifa mapema kwamba hata yule mtekelezaji wa programu hii ameshapewa barua yaani ameshakuwa awarded na baada ya wiki mbili watakuja hapa Dodoma kusaini. Nimeagiza waje wasaini hapa mbele ya Mwenyekiti na Kamati yangu ili tuanze kazi ya kufunga mfumo huu ambayo itachukua si chini ya mwaka mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndani ya kabrasha nililowapa kuna kakitabu kadogo, kameandikwa Mradi wa Kuboresha Sekta ya Ardhi. Wale waliopata nafasi bila shaka wamefunuafunua kidogo. Ukija kwenye ukurasa wa mwisho huku ndio unaonesha mfumo wenyewe utakavyokuwa. Kwa hiyo, tutaachana kabisa na mfumo tuliouzoea na makaratasi mengi na mafaili ya hovyo hovyo kwenye Wilaya, Wizarani na Mikoani, tutaingia kwenye masuala ya kisasa.
Kwa hiyo, nataka kuwahakikishia wote wengi ambao wamezungumza kuanzia Kamati yangu na hasa Mheshimiwa Dkt. Mary Mwanjelwa amezungumza sana kwa sababu alikuwepo kwenye Kamati iliyopita na wale waliosema tulikwenda nao Uganda na Ethiopia ni kweli lakini sasa zamu yetu imefika kwa hiyo nataka kuwatoa wasiwasi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wote wanaozungumza kwamba fedha haziko kwenye bajeti hii, someni hii, humu ndani mna dola zaidi ya milioni 25 kwenye miradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mmezungumza habari ya upimaji na tatizo tulilonalo la vifaa vya upimaji kwenye Halmashauri, ukisoma hapa tuna fedha nyingi, tumeshaagiza vifaa vya upimaji lakini hatutavipeleka Wilayani, tutavipeleka kwenye Kanda nane, tunataka Halmashauri zenye kazi ya kupima zikachukue pale kwenye Kanda wakapime bila malipo yoyote. Kwa hiyo, vifaa tunanunua na fedha ziko hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mmezungumza habari ya master plan hasa ya Jiji la Dar es Salaam, ilikuwa mwezi uliopita ile ndege ya kupiga picha ya anga itusaidie katika kutengeneza master plan ingekuwa tayari, sasa hivi kwa sababu ya hali ya hewa wanategea tu. Hata hivyo, fedha ziko hapa kama dola milioni tatu hivi, tumeshamlipa contractor na hiyo ndege itapita angani kupiga picha za anga ambazo ndizo zitatusaidia kwa sababu hizi ndio base map za kutusaidia kutengeneza master plan, fedha ziko hapa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ununuzi wa vifaa hata magari yako hapa. Huo mtandao wenyewe wa ILMIS mnaousema ni dola milioni 12, hamtaziona kwenye bajeti yangu kwa sababu hizi fedha zilionekana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwa hiyo, ukiacha hizi zinazosomwa, nataka kuwaondoa wasiwasi na dola zaidi ya milioni 25, ziko kwenye mfuko mwingine na siyo za leo ni kweli ziko kwa miaka miwili iliyopita lakini zitatumika kwa mafao ya Wizara ya Ardhi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunaendesha zoezi la kukusanya maoni ya Sera ya Ardhi. Waheshimiwa Wabunge, katika kabrasha langu hilo nimewapeni bahasha fulani ina flash, ndani ya flash mle kuna barua nimeweka inayoonesha kwamba ndani ya barua ile kulikuwa na sera tatu.
Moja ya sera muhimu ambayo inazaa mikingamo yote ya haya mliyozungumza tangu asubuhi ni Sera ya Ardhi kwa sababu ndiyo imezaa Mabaraza ya Ardhi, sheria na kila kitu. Kwa hiyo, ili kuondoa mzizi wa fitina yote haya, ni muda mrefu sana kwa sababu tulianza kutengeneza sera ndiyo iliyotuelekeza kuwa na Sheria Na.4 na 5 ambayo wengine hapa wametoa mawazo kwa nini tuwe na Sheria mbili za Ardhi tuwe na sheria moja. Ndiyo iliyoanzisha hati za kimila na hati za kawaida na ndiyo iliyoanzisha Mabaraza ya Vijiji, Kata na Wilaya hayo yanayosiganasigana. Kwa sababu tunajua sasa ni muda mrefu umepita ndiyo maana tumeamua kuanzisha kazi ya kutafuta maoni ya wananchi juu ya Sera ya Adhi kuona ni namna gani leo baada ya miaka 50 hii tuweze kumiliki na kusimamia rasilimali ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndani ya bahasha ile kwenye kile wanachoita flash disk (kinyonyi), nawaombeni mnipe muda wenu kidogo Waheshimiwa Wabunge na ninyi nimewaleteeni questionnaire kubwa kidogo, dodoso kwenye kinyonyi nawaombeni sana, ninyi ni wadau muhimu sana katika marekebisho, shida zenu zote hizi zitakwisha tu kama tukishiriki kurekebisha sera halafu baadaye tupitie marekebisho ya sheria zetu. Kwa hiyo, naomba ndani ya kinyonyi nimewapa dodoso m-print ili msumbuke kidogo mtoe maoni yenu humu mkipata nafasi. Nitafurahi Bunge likiisha mwezi wa sita mwishoni kila mmoja wenu anipe maoni yake juu ya anavyofikiri turekebishe. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo maana nimewapeni sera zote, ndani ya flash kuna sera tatu zote tulizonazo na tunatengeneza kwa mara ya kwanza Sera ya Nyumba. Hatukuwa nayo, tunarekebisha Sera ya Makazi na tunatengeneza na Sera ya Nyumba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, humu ndani nimewapeni na Sera ya Nyumba na Sera ya Ardhi ili mpate nafasi Waheshimiwa Wabunge, najua mna majukumu mengi, lakini mtafunuafunua kidogo ili angalau m-print mtoe maoni, maana nyie ndio wadau muhimu. Ndani ya flash humo pia nimewapeni sheria 15 ambazo ndiyo zinasimamia utawala mzima wa ardhi, naomba mzisome.
Humu ndani kuna wasomi wengi, wengine wanasheria, wengine wazoefu tu, mambo ya ardhi, vita hizi na migogoro hii imetufundisha kusoma vitu vingi. Kwa hiyo na zenyewe kama mnafikiri kuna sheria fulani fulani zinakinzana au haziendi vizuri, someni tupate msingi wa kuzibadilisha. Nawashukuruni sana Waheshimiwa Wabunge na nitawashukuru sana kama mtanisaidia kurekebisha haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua muda hautoshi lakini nije kwenye suala la ujenzi holela limezungumzwa sana. Najua Serikali peke yake zamani ndiyo ilikuwa na jukumu la upimaji na upangaji hatukupanga na kupima vya kutosha. Kwa hiyo, wananchi wametutangulia na wamejenga wanavyotaka kwa sababu hawawezi kutusubiri. Sasa tumeanzisha programu ya kupanga na kupima kwenye miji na vijiji, lakini kazi hii lazima tushirikiane kwa sababu ni kazi ya msingi ya Halmashauri zetu, ndiyo wenye ardhi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi mmezungumza habari ya kupanga hata kwenye vimji vidogo, anayeamua mji mdogo upangwe ni ninyi Halmashuri ya Wilaya, mnaamua kwamba mji huu tunataka tuupange, mnaniletea mimi natangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba sasa Waziri ameridhia kaeneo fulani ka Tarime kapangwe kama mji mdogo; kama Mheshimiwa Esther anavyoomba, kwa hiyo leteni maombi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hamna uwezo wa kupanga sisi tutawasimamia na kuwasaidia watu wenye uwezo wa kupanga tunao wasomi wengi mitaani. Hivi sasa tumeanzisha kampuni 58 za wataalamu. Tuna wataalamu waliobobea kwenye masuala ya mipango miji wapo mitaani, tumeamua waanzishe kampuni za wataalamu wa kupanga na kupima tumezi-register ili ziwe mbadala ya shida ya wapangaji, wapimaji wa Halmashauri, ambao kwanza ni wachache lakini uzoefu wangu nao mara nyingi sana wapimaji wa Halmashauri hawafanyi vizuri kwa uadilifu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna mahali popote kwenye mchoro ambao tumeupitisha sisi ambao una viwanja 1,000 ambapo Wapimaji wa Ardhi wa Halmashauri yoyote wamepima wakavikabidhi Halmashauri viwanja 1000, lazima 100 watavikata. Kuondoa shida hiyo, kwa sababu vifaa tunavyo vitakuwa kwenye Kanda, tumeamua kushirikisha makampuni binafsi yatakuja kupanga, yatapima, umilikishaji utakuwa jukumu lenu Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua muda hautoshi kueleza, lakini concept hii nitaieneza nitakapopita mikoa yote mikoa yote kuelezea juu ya migogoro na namna ya kutatua na tutapanga hizi kampuni kwa mikoa ili zisaidie katika kupanga miji midogo midogo ili nayo isianze kujitanua kama squatter hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tunao mpango mwingine wapangaji hawa watakuja kuwafundisha zaidi; tumeshawafundisha, lakini Halmashauri tunataka sasa zijikite katika urasimishaji wa maeneo ambayo tayari yameshakuwa squatter. Hatuwezi kuyavunja yale watu wameshajenga. Kwa hiyo tunakuja kuwafundisha tunawaelimisha na tutatumia kampuni za watu binafsi kurasimisha makazi ili watu wanaoishi kwa makazi yanayoitwa si salama waweze kumilikishwa hati zao, miundombinu ipite wapate hati zao waweze kukopesheka. Kwa hiyo hayo ni mambo tunayokuja kuyafanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utoaji wa hati. Hati za kimila zinakopesheka kwenye kitabu changu nimesema na ninawashukuru sana benki ya TIB, Exim, CRDB na NMB wanakopesha na NMB ndiyo benki iliyopo kila mahali. Niambieni kama kuna mahali wamekataa kukopeshea kwa hati ya kimila, wanakopesha. Sasa nasema ushauri wenu nitaongeza nguvu ili mabenki mengine mengi yaweze kukopesha kwa hili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tutaongeza kasi vilevile ya upimaji na upangaji kwa kushirikiana na Halmashauri lakini kushirikisha kampuni nyingine ambazo hazitatoza hale kubwa, kwa sababu utozaji wa makampuni hawa mengine yanayoingia mikataba kama ya Bukoba na mahali pengine wameingia mikataba hata Lindi na wapimaji binafsi matokeo yake viwanja havinunuliki. Kwa hiyo Wizara yangu vile vile itajikitakatika kutoa bei elekezi ya upangaji wa bei za viwanja ili watu wasijiuzie wanavyotaka. Leo tumesimamisha uuzaji wa viwanja vya Temeke kwa sababu tumekuwa nao, Mheshimiwa Mbunge yupo hapa; yaani mtu anapima tu ardhi gharama ni shilingi 2000 kwa upimaji wa kiwanja halafu wanauza shilingi milioni 27. Haiwezi kuwa, ardhi hii haiwezi kuwa mbadala wa shida zenu zote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tutasimamia upangaji lakini tutasimamia na kuelekeza viwango vya kuuza bei vinginevyo mnalilia tu miji ipangwe nani atanunua kiwanja shilingi milioni 27. Ikiwa Wizara ya Ardhi inakopesha milioni 20 kwa mfanyakazi wa kawaida kukopa, kiwanja milioni 27 utapata wapi?
Kwa hiyo, nawaomba tusimamie. Wenzenu kule Halmashauri wana ingiza vitu ingawa hapa nimeona wengi mnasema gharama ya viwanja ni kubwa upimaji na hela zinakwenda wapi, hizi hewa zinajazwa kule. Kwa kuwa huwa hamshiriki mshiriki vizuri kuhoji gharama hasa hasa mliyoingia Halmashauri ya kupanga ni shilingi ngapi, kupima ni shilingi ngapi. Basi hata faida weka ten percent, twenty percent.
Mtu mmoja Halmashauri ya Jiji mmoja ambaye tumemfukuza, ananiambia mzee hapa bwana tumepata katika hii orodha ya viwanja hivi tumepata faida shilingi bilioni saba. Unawezaje kupata bilioni 7 kwa viwanja vya mkupuo 1500 ulivyopima kwa wakati mmoja? Lazima hizi shilingi billioni saba umewanyonya sana wananchi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nataka kuwaagiza halmashauri zote msifikiri ardhi ni suala la kujitajirisha tu. Na hata sasa nimezuia, ni marufuku kwa kampuni binafsi kwenda kununua mashamba na kujipimia viwanja, marufuku, haiwezi kuwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani leo Bagamoyo unaenda unanunua shamba heka kumi, kesho umebadilisha matumizi viwanja haiwezi kuwa. Kwanza ukibadilisha shamba kwenda matumizi ya viwanja umepandisha hadhi halafu unapima viwanja. Leo kuna mtu pale wamempa hati 600 za kwake binafsi kwa jina lake kwa sababu ni shamba lake amepima ameweka majina yake. Sasa ni marufuku mtu yeyote aliyenunua shamba litabaki shamba, ukitaka viwe viwanja kabidhi Halmashauri ndio wata deal na mimi kubadilisha matumizi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama mtu binafsi umenunua shamba ukilenga kwamba unataka kupima viwanja imekula kwako. Kabidhi hilo shamba Halmashauri itapanga, itapima, itamilikisha yenyewe, kwa sababu nimeona sasa watu wanakuja na briefcase zao wanatajirika kwa mashamba yetu kwa kupima viwanja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nirudie kidogo aliyoyasema Mheshimiwa Naibu Waziri juu ya fidia. Jamani fidia ipo kwa mujibu wa sheria, someni sheria sitaki kufafanua zaidi na tumeshasema kwamba ukiukwaji huo basi. Kama kuna mtu anataka kuchukua ardhi hata kwa maendeleo tenga fedha kwenye bajeti. Huo ndio msimamo wa sheria ambao hauna pande mbili ni upande moja tu, iwe ni kwa maendeleo au kwa huduma. Tenga fedha kwenye bajeti, nunua hilo shamba, fanya unachokitaka, huo ndio msimamo wa sheria. Mkitaka basi njooni mbadilishe sheria hapa ili iseme kwamba ardhi ichukuliwe bure kwanza au ikopwe halafu ndipo ifanye shughuli, hapana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo msimamo wa sheria ni huo na wote mnaochukua hayo ni lazima mfuate sheria. Mimi najua Halmashauri nyingi zimechukua maeneo ya watu wamepima viwanja, wanauza viwanja. Lakini angalau huyo mtu uliyechukua shamba ajue atalipwa kiasi gani aishi kwa matumaini. Lakini msiwe na hofu hata hao wanaocheleweshwa kulipwa fidia inabadilika kwa mujibu wa sheria kwa sababu ukichukua eneo la mtu bila kulipa fidia kwa miezi kadhaa inatozwa interest. Kwa hiyo, wale wote ambao wanafikiri hawajalipwa fidia kwa sababu maeneo yao yamechukuliwa na taasisi fulani fulani wajue wameweka fedha benki watalipwa na interest. Kwa hiyo, wasikate tamaa siku ambapo watalipwa, watalipwa pamoja interest kwa mujibu wa sheria. (Makofi)
Ndugu zangu mmezunguza sana habari ya migogoro ya ardhi. Kwa ufupi sana nataka niseme wale ambao wameniandikia nawashukuru na wengine wameboresha, tutajipanga. Wizara yangu peke yake haiwezi tutajipanga ndani ya Serikali Wizara zote zinazohusika na Maliasili, maana mimi sisababishi migogoro wanaosababisha ni watumiaji wa ardhi yangu. Kwa hiyo, tutajipanga na wenzangu TAMISEMI, Maliasili, Kilimo ili angalau tushirikiane tujipange tuifikie mpaka migogoro ya mipaka ya kijiji na kijiji. Tutajipanga na tutakuja kwenu, nataka kuwahakikishieni tutafika kote tutajipanga na wataalamu wetu ili tufike tuisome. Kama ni marekebisho ya mipaka tutafanya, kama ni ramani tutasoma, kama ni marekebisho ya jambo lolote tutafanya, kwa sababu Serikali ni moja na Mheshimiwa Rais ameagiza katika miaka mitano hii lazima tuwaondolee machungu wananchi, tuondoe migogoro ya ardhi. Kwa hiyo, kwa motto huo tutafika huko kote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Lwakatare amezungumza mengi sana lakini asishike shilingi yangu. Najua matatizo yake ya Bukoba ni makubwa, lakini kama tulivyoongea Chief Valuer wa Wizara yangu Evelyine baada ya Bunge hili pamoja na Kamishna wa Ardhi wa Kanda wanakuja Bukoba. Kuna mgogoro wa viwanja 5,000, sasa wanakuja kwa sababu tulishaelekezwa na Waziri Mkuu, wewe umeandika lakini sisi tulishaelekezwa na Waziri Mkuu kwamba lazima TAMISEMI na mimi nipeleke. Kwa hiyo, mimi napeleka watu wawili, lakini atakwenda na mtu wa TAMISEMI kuhakikisha kwamba mgogoro wa Bukoba sasa tunautafutia dawa once and for all, kwa hiyo, tunakuja huko. (Makofi)
Mheshimiwa Nassari kwanza yale uliyoyasema naomba radhi sana, yale yalioandikwa kwenye kitabu wamekosea, yale mashamba yote yalishafutwa.
Sasa wewe na mimi tunajua, nimehangaika sana ili mradi sasa unataka nije nikae nyumbani kwako wiki mbili nitakuja. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tulishahangaika sana nimetumia fedha zangu mpaka nimetoa shilingi milioni 271 za kuja kupanga vipande vidogo vidogo kwa kumilikisha wananchi wako wenye shida kutoka kwenye mashamba hayo. Lakini watendaji wangu wa upande ule wameniangusha, hawajafanya. Nimefanya sana na Arusha DC anajua nimempa watu wake 4,000 nimewapa vipande kwenye mashamba ambayo tumefuta, lakini hawajapanga kwa sababu sielewi wamenipa taarifa na fedha zangu za kupanga walikuwa hawana Halmashauri ya Arumeru na DC nimewapa 271 ya kufanya kazi hiyo. (Makofi)
Ndugu zangu, Chuachua wa Masasi kwanza ngoja nijipongeze mwenyewe pale unaposema tumejenga nyumba za National Housing nilikupa na bonus ya zahanati ila haukusema.
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Eee! Chuachua pale, nilikupa bonus ya zahanati lakini hukuisema, wewe umezungumzia fidia tu. Lakini nataka kuwahakikishia watu wote, wa Dar es Salaam mmezungumza kwa uchungu sana juu ya migogoro yenu yote, Kazimzumbwi tunaenda kuimaliza Alhamisi, tumeshaelekezwa na Waziri Mkuu mimi na Mheshimiwa Maghembe tunakwenda Dar es Salaam tunaenda kumaliza shughuli ya Kazimzumbwi haitakuwepo tena, tunamaliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wengi sana wamezungumza, rafiki yangu wa Siha naye amezungumza sana, lakini wewe mambo yako lazima tufike kule tumalize. Mzee wa Karagwe nakumbuka umezungumza sana, Mzee wa Efatha kule Malocha, wazee wa Sumbawanga kule wamezunguza sana habari ya Efatha. Efatha jamani sio jina la mtu maana mnazunguza hapa ni taasisi ya dini naona mmezungumza Efatha sana. Lakini nataka kuwahakikishia ndugu zangu wa Mkoa wa Rukwa, issue ile ya Efatha ipo mahakamani, siwezi kuizungumza sana, mimi nitakacho kifanya nitaimarisha nguvu ya mwanasheria wenu wa Sumbawanga ili kumsaidia ili kuharakisha ile kesi iishe haraka. Lakini dhamira ya Serikali ya kutwaa lile shamba iko pale pale, na madhumuni yake ni yale yale. Kwa hiyo, Mzee Malocha nafikiri umenisikia hapo. (Makofi)
Ndugu zangu mmechangia watu wengi waliochangia kwa maandishi mpo 57 naomba sana niwashukuru katika hoja hizi mbalimbali nilizozungumza hizi za mwanzo, Waheshimiwa waliochangia hasa hasa kwa kusema ni wengi lakini namkumbuka zaidi ndugu yangu Julius Laizer ambaye alifoka sana.
Nataka kukuhakikishia kwamba yale uliyoyasema nakubali kwamba lile shamba la Makuyuni lazima lirudi kwa wananchi. Lile shamba lilipangwa liende kwa wananchi na litarudi kwa wananchi. Ila ujue inakula kwako kwa sababu aliyejimilikisha hili shamba ni Edward Lowassa, nilitaka kukupa hiyo taarifa tu hapo umeingia pagumu kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, shamba hili lilidhamiriwa na Rais Mkapa wapewe wananchi, lilikuwa shamba la Stein Seed Vallay wanaokumbuka historia ile aliyefukuzwa na ndege na kila kitu..
Naam, Mheshimiwa Waziri wakati ule akiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu alisisitiza kwa Mheshimiwa Mkapa kwamba shamba hili naomba sana wapewe wananchi na vijiji vile wameshaniandikia mimi. Lakini bahati mbaya sana hati niliyonayo hapa imesainiwa na Mheshimiwa Lowassa. Kwa hiyo, mimi nakusaidia wewe kwamba hati hii tutairekebisha yeyeto aliyesaini hapa tutarekebisha na ardhi hii itarudi kwa wananchi. Nakushukuru sana tumeshirikiana kwa mengi na hili tutalimaliza na lazima tushirikiane mimi na Halmashauri ya Monduli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mary Mwanjelwa amezungumza kwa uchungu sana, Mheshimiwa Augustino Masele huyu leo amefunga bao la pili maana hata Jumamosi alichangia. Mheshimiwa Chatanda nasema hawa wote ambao wamezungumza hoja zinazofanana Mheshimiwa Abdallah Mtolea, Mheshimiwa Shangazi, Mheshimiwa Salma Mohamed Mwassa, Mheshimiwa Anatropia Theonest, Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mheshimiwa Joel Mwaka Makanyaga, Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mheshimiwa Angelina Adam Malembeka, Mheshimiwa Oran Manase Njeza, Mheshimiwa Richard Philip Mbogo, Mheshimiwa Rashidi Mohamed Chuachua, Mheshimiwa Joram Hongoli na Mheshimiwa Zuberi Kuchauka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine ni Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mheshimiwa Balozi Adadi Mohamed, Mheshimiwa Balozi Dkt. Diodorus Buberwa Kamala, Mheshimiwa Amina Saleh Mollel, Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay, Mheshimiwa Yussuf Salim Hussein, Mheshimiwa Omary Tebweta Mgumba, Mheshimiwa Sixtus Mapunda, Mheshimiwa Maria Ndila Kangoye, Mheshimiwa Riziki Mngwali, Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang‟ata, Mheshimiwa Joshua Samwel Nassari, Mheshimiwa Maulidi Mtulia, Mheshimiwa Stephen Ngonyani, Mheshimiwa Massay, Mheshimiwa Moshi Kakoso, Mheshimiwa Allan Joseph Kiula, Mheshimiwa Kiteto Koshuma, Mheshimiwa Kunti, Mheshimiwa Halima Mdee, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, Mheshimiwa Dkt. Godwini Mollel, Mheshimwia Zainab Katimba, Mheshimiwa Felister Bura, Mheshimiwa Emmanuel Papian, Mheshimiwa Agustino Masele again, Mheshimwia Rose Tweve na Mheshimiwa Juliana Shoza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia waliochangia hoja hizi, Mheshimiwa Edward Mwalongo, Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu, Mheshimiwa Sixtus Mapunda, Mheshimiwa Shally Raymond, Mheshimiwa Mwijage, Mheshimiwa Jenista Mhagama na Mheshimiwa Naibu Waziri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hoja hizi nimezijumlisha zote na majibu yake ndiyo hayo kwamba ndugu zangu hawa ndio wamechangia kwa kusema, lakini wapo waliochangia kwa maandishi na hoja zinafanana. Ninachoomba tu Waheshimiwa Wabunge mnivumilie. Najua hata mdogo wangu pale Mbunge wa Mikumi ananiangalia hajasema sana lakini huko nje anasema sana. Najua ndugu zangu mnaniangalia sana, lakini mengi mnasema hata nje huko tumeongea mengi sana. Nimewataja majina hapa ili wajue wananchi huko kwamba hawa wamechangia kwa kusema. Lakini pia zipo hoja hapa ambazo nitazizungumza zimezungumzwa na hawa wafuatao lakini kwa kuandika, wasije wakasema hawa wabunge wetu ni mabubu hawakusema, hapana upo utaratibu. (Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo waliochangia hapa kwa kuandika vilevile. Hoja hizi ni hizi ambazo nitazisoma baadae lakini waliochangia ni Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, Mheshimiwa Mwita Waitara, Mheshimiwa George Lubeleje, Mheshimiwa Charles Mwijage, Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mheshimiwa Mussa Sima, Mheshimiwa Juma Hija, Mheshimiwa Silafu Maufi, Mheshimiwa Halima Mohamedi, Mheshimiwa Risala Kabongo, Mheshimiwa Engineer Ngonyani, Mheshimiwa Aida Joseph, Mheshimiwa Shabani Omary na Mheshimiwa Mary Pius Chatanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengine ni, Mheshimiwa Allan Kiula, Mheshimiwa Paschal Yohana Haonga, Mheshimiwa Saumu Sakala, Mheshimiwa Cecilia Paresso, Mheshimiwa Lucy Owenya, Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mheshimiwa William Olenasha, Mheshimiwa Ritta Kabati, Mheshimiwa Omari Abdallah Kigoda, Mheshimiwa Desderius Mipata, Mheshimiwa Haji Kai, Mheshimiwa Zuberi Kuchauka, Mheshimiwa Ignas Malocha, Mheshimiwa Bhagwanji, Mheshimiwa Frank George, Mheshimiwa Mbarouk Salim, Mheshimiwa Maftaha, Mheshimiwa Gibson, Mheshimiwa Mendrad Kigola, Mheshimiwa Mary Deo Muro, Mheshimiwa Lucia Mlowe, Mheshimiwa Omari Abdallah Kigoda, Mheshimiwa Daniel Nicodemus, Mwenyekiti pia umechangia na lile shamba lako nitalifuatilia.
Waliochangia wengine ni Mheshimiwa Daniel Nicodemus, Mheshimiwa Constantine Kinyasi, Mheshimiwa Mbarouk Salim Ali, Mheshimiwa Esther Matiko, Mheshimiwa Omari Kigua, Mheshimiwa Dunstan Kitandula, Mheshimiwa Magdalena Sakaya, Mheshimiwa Ally Ungando, Mheshimiwa Joseph Haule, Mheshimiwa Japhet Hasunga, Mheshimiwa Willy Qambalo, Mheshimiwa Pascal Yohana, Mheshimiwa Sikudhani Chikambo, Mheshimiwa Cecil Mwambe, Mheshimiwa Esther Matiko, masuala yako ya upimaji wa Mji wa Tarime nimeyazungumza hapa.
Wengine ni Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Mheshimiwa Mpakate Daimu Iddi, Mheshimiwa Davidi Silinde, Mheshimiwa Jitu Soni, Mheshimiwa Harrison Mwakyembe na Mheshimiwa Daniel Mtuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimalizie kwa kuwashukuru sana benki ya dunia kwa msaada mkubwa sana wa fedha nyingi ambazo hazikuoneshwa hapa lakini zilipitia Ofisi ya Waziri Mkuu ambazo matumaini yangu ni kwamba mwakani mnaweza mkaona vitu fulani fulani kwa macho ambavyo vimefanywa kutokana na fedha ambazo hazikuombwa kwenye bajeti yangu. Bajeti yangu inaonekana nyepesi sana, lakini kuna fedha ambazo zipo kule kwenye Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kama nilivyosema zaidi ya dola milioni 25, hazijafanya kazi ya kutosha lakini katika kipindi cha mwaka huu wa fedha mtaona matokeo yake. Nawashukuru sana Benki ya Dunia.
Katika mradi huu wa awali wa kupanga, kupima na kumilikisha Wilaya tatu wenzetu wa Denmark, Sweden na Uingereza wanatusaidia sana nawashukuru sana nao. Lakini nawashukuru sana watu wa Benki Kuu ya Tanzania ambao wanasimamia sana masuala ya mortgage finance, tunashirikiana nao nazishukuru na benki zote 29 ambazo zinashiriki katika utoaji wa mikopo ya nyumba.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kwa uchache niwashukuru hao na kwamba tutaendelea kushirikiana nao. Kuna hoja nyingine ambayo imetolewa hapa kuanzia Bunge lililopita la uanzishwaji wa Real Estate Development Authority. Tunajua ujenzi wa majumba sasa na biashara ya majumba imekuwa kubwa, kwa hiyo tumeamua sasa tutaleta sheria hapa Bungeni. Imeulizwa sana kuanzia Bunge lililopita Bunge hili la mwaka huu tutaleta sheria ili angalau nchi iweze kutambua na kusimamia sekta hii muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho naommba nirudie tena kuwashukuru kwanza Kamati yangu nataka kusema Kamati yangu kama wenzangu mmepata Kamati mimi nimepata yakwangu nzuri sana, ina watu waliotulia, ingawa wengi wageni lakini ni watu wenye uzoefu na waliotulia wanatoa ushauri mzuri, nawashukuruni sana. Sikusema mengi kwa sababu ninyi mkisema kwangu ni maagizo, kwa hiyo maagizo yenu na maelekezo yenu nitayafanyia kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la KDA ndugu zanguni mnajua tulikotoka, tulikofikia, sasa naomba ushauri wenu huo, nimeupokea lakini narudi ng‟ambo kule Kigamboni nikakae na wadau wa KDA, wananchi wa Kigamboni ili tuzungumze tuelewane alafu tunashauriana ndani ya Serikali the way forward.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kuwahahakishieni, hakuna pesa humu lakini mimi ninazo shilingi bilioni saba tulikuwa hatujazitumia kwenye bajeti hii kwa ajili ya kuanza kulipa fidia ya watu wachache ambao wapo barabarani. Haziko hapa kwa sababu ziko kwenye bajeti hii ninazo ziko kwenye Mfuko wa Amana na Waziri wa Fedha anajua tunazo sio kwamba, pale hatufanyi, hatufanyi tu kwa sababu hatujamaliza kazi ya kuainisha lakini hatujaenda kujadiliana na wananchi wa Kigamboni juu ya utaratibu wa ulipaji wa fidia na kiwango cha fidia maana huwezi kuwashtukiza. Kwa hiyo kuna kazi inaendela kule. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimekubaliana na kwa watu wa kigamboni; madiwani wote wa Kigamboni wameshaniandikia barua niende kwao kwa sababu mambo haya huwa tunaenda hatua kwa hatua, tunazungumza na tunaelewana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwahiyo nataka kuwahakikishia wenzangu wote wenye hofu ya Kigamboni muondoe hofu. Lakini ushauri wenu tumeuchukua. Ikiwa kunahitajika marekebisho fulani kwa sababu mlitunga sheria ya kuanzisha mamlaka hii tutairudisha hapa ili mfanye marekebisho. Hata kama ikiwa ni kufuta tutairudisha ili tuifute.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwahakikishieni kwamba, tunazo fedha tutafanya mambo machache. Kuanzini sasa kama nilivyoagiza, masuala ya utoaji wa hati katika eneo lile nimeyafungulia, wataanza kupata hati. Kwa sababu kwa miaka yote hii watu walikuwa hawaruhusiwi kupata hati na kupata vibali vya ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, midhali sasa michoro imekamilika na yale wanayotakiwa kujenga kwenye site yao yanajulikana kwahiyo nimeshawaagiza wangu tuanze kutoa vibali vya ujenzi kwa watu wanaojenga kulingana na michoro inavyoelekeza katika maeneo yao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini watu wenye ardhi yao wapewe hati ili wapate nguvu ya ku-bargain na hao wawekezaji ambao watawekeza fedha katika maeneo hayo. Kwa hiyo, haya mawili nitayafanya lakini naomba nisiwapotezee muda mrefu nitazungumza na wadau wa Kigamboni kwa niaba yenu nafikiri tutaelewana maana tumeshaelewana mambo mengi hapa nafikiri tunaenda vizuri.
Kwa hiyo, ndugu zanguni nataka nikiri kwa mbali, mambo mlioniandikia ni mengi, mambo mlionishauri kwa mdomo ni mengi lakini mengi ni migogoro. Msingi wa migogoro kwanza nataka mnisaidie marekebisho ya sera, ambayo itarekebisha hata sheria zijazo, lakini pili maana yake naomba mnikaribishe tunapiga hodi tutakuja Mkoa kwa Mkoa kusimamia utatuzi wa migogoro hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sana mniunge mkono mnipe pesa hizi ili angalau nianze safari hata kesho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Ahsante sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana wewe na Waheshimiwa Wabunge, kwa heshima mliyotupa Serikali kupitia Wizara yangu kwa michango mizuri sana. Kila mmoja alikuwa anatamani kusikiliza michango kuanzia mtu wa kwanza mpaka wa mwisho, yaani tumefanya kazi ya kibunge vizuri. Hakuna jambo ambalo mimi sikuandika; kila jambo nimeandika. Ingawa sikuandika maneno yote, lakini angalau kila hoja ya mtu naijua. Naweza kusema tulikuwa very serious katika kujadili mjadala huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawapongeza sana nasi kama Wizara tutaendelea kutekeleza mwongozo wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Magufuli; yeye kila siku anasema kwamba yeye ni Rais wa CCM, ametokana na CCM ndiyo, lakini amechaguliwa na Watanzania wote na kila mara amekuwa anasisitiza tutoe huduma bila ubaguzi wowote. Kwa hiyo, ndiyo maana spirit ya Wizara yangu ni kutoa huduma kwa wananchi wote na wananchi wote tutaendelea kuwahudumia bila ubaguzi wa aina yoyote. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangu nawashukuru sana kwa niaba ya Wizara yangu na wenzangu wote, tuendelee kushirikiana, maana yake hii kama ninyi msingekuwa mnashirikiana nasi pengine tusingejua matatizo yenu. Kwa hiyo, tuendelee kushirikiana na moto ni huo huo. Tuna Ofisi hapa Dodoma, tuna Ofisi sasa kwenye Kanda na hapa nyuma yangu nimeleta viongozi wote wa Kanda nane. Kwa hiyo, kila jambo mlilolisema kama linahusu Mabaraza ya Ardhi, Msajili wa Mabaraza yupo hapa, Amina. Kama linahusu ardhi Kanda ya Magharibi, Kamishna na Msajili wapo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bunge lijalo Mungu akipenda, mtazungumza mkiwa na Mthamini wa Kanda, Mpima wa Kanda, Kamishna wa Kanda, Msajili wa Kanda na wote hawa watakuwa wamekamilika na watumishi wao na vitendea kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili alilosema Mheshimiwa Naibu Waziri, tumesema moja ya jambo ambalo mmelizungumza watu wengi humu ndani, kwamba tunakwama kupanga na kupima mashamba na wananchi kupata viwanja vyao kwa sababu hamna vifaa; tumeshaagiza vifaa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumetangaza kwenye gazeti, tutavisambaza hivi vifaa tena kwa teknolojia mpya, kwa sababu sasa tunatumia satellite na vifaa vya mapokezi ya satellite tumewaonesha jana, tumevinunua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tutakuwa na vifaa ambavyo vinapima kwa upana mkubwa kwa teknolojia mpya na tutawafundisha Maafisa wenu wote. Tutawaita hivi karibuni, Maafisa wenu wote Wapima, hawavijui hivi vitu, tutawafundisha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkipata nafasi, kule nyuma tumeweka Maonesho ya Wapima Binafsi, baadhi ya vifaa vya kisasa vya upimaji viko nyuma kule tunakofanyia sherehe. Atakayepata nafasi aende. Tunaposema RTK mtaziona kule, kwa nini kifaa hiki kinaweza kikapima mpaka kilometa 30 kwa wakati mmoja na kikatumia watu wawili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, Wilaya yako yote inaweza ikapimwa kwa siku tano au sita tukapima mashamba yote. Kwa hiyo, teknolojia hii tumeagiza na tutasambaza kwenye Kanda na awamu ya pili tunakwenda kuandika tunataka tupeleke vifaa hivi kila Wilaya ili hata kama unamwita mpima binafsi, basi uwe una kifaa chako inapunguza gharama. Kwa hiyo, tutatatua kero za ana kwa ana, lakini tunafikiri vilevile twende kwenye mifumo na baadaye tutakuja kwenu kuomba sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachowashukuru ni kwamba mmetusaidia sana kuainisha mambo mbalimbali na haya sasa siyo kujibu tu kwa maandishi lakini tutayapangia na ratiba, tutakuja Mikoani kote huko. Tutakuja Kilimanjaro kufanya audit, tutakwenda Chumbi kwa rafiki yangu Mchegerwa, tutakwenda Mikoa ya Kagera kule Karagwe, tutaenda kila mahali. Tutakuja mikoani. Sasa hatuji mikoani tukisubiri ratiba za mikoa, tutakuja kuthibitisha haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshajua mambo ya kuanza nayo. Tutakuja kila mkoa. Mkoa wa Manyara, Iringa, Ruvuma mpaka Mbinga tutakuja na kila mahali tutakuja, angalau tuna mambo ya kuanzia. Nataka kuwahakikishieni kwamba haya yote tutayaandika, lakini tutawapa majibu ili mjue lakini yatatusaidia sana tukija mkoani kufuatilia haya na kuhakikisha tunayatatua on the spot. Kwa hiyo, tutakuja ndugu zangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepanga Kanda vizuri, sasa tunateua Watendaji wetu wapya kwenye Kanda wafanye hii kazi, mambo yote tutayafanya. Dar es Salaam tutakuja wenyewe nami bado nipo pale, yale yote ya Dar es Salaam tutayamaliza; ya Dodoma hapa tutayamaliza na mikoa yote tutafika na kuyafanyia kazi. Kwa hiyo, nafikiri Waheshimiwa Wabunge hebu msubiri tuje. Tuna ratiba ya miezi 12 kabla hatujakutana hapa, tushirikiane huko huko mikoani kutatua haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mengi yatatatuliwa, tutaulizana tena huko mikoani na wenzangu wanaotoka hapa wanaanza kuyafanyia kazi. Inawezekana baadhi ya mambo mkirudi huko mtakuta yamekwisha kwa sababu viongozi wangu wa kanda wote wapo hapa wamesikiliza. Sasa tumewawezesha na magari mapya, wanakimbia kila mahali, kwa hiyo, hawana shida sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ndugu zangu nawashukuru sana kwa haya yote mliyoyasema nataka kuwaahidi kwamba tutawajibu kwa maandishi, lakini tutakuja huko mikoani, tutajadiliana sana, tutafanya makongamano, tutaitisha na viongozi wengine wa mikoa tuzungumze.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi inayoendelea kubatilisha mashamba ya watu ambao hawayatumii, tutaendelea kuifanya kila mahali; kazi ya kukagua mashamba yasiyotumika, tutafanya; kazi ya kupima kwa kasi ili kila mtu amilikishwe kiwanja, tutafanya. Leo ingawa bado mnazungumza gharama, lakini hizo gharama mnazozijua tumepunguza tozo kwa asilimia 67. Kwa hiyo, Mheshimiwa wa Mbinga hebu angalia taarifa yako. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama kubwa ambazo hata ninyi Waheshimiwa Wabunge mna offer nilizowapa, angalieni ile kitu inaitwa premium mlicholipa; 67 ya ile mliyolipa imepungua. Kwa hiyo, umilikishaji sasa utakuwa nafuu sana na tungependa kutoka sasa Halmashauri zote zisiruhusu hata kidogo watu kujenga katika maeneo au viwanja ambavyo havijapimwa na kupangwa. Kwa sababu kilio chao cha kupunguza tozo tumefanya, gharama za upimaji zitapungua sana na hivyo hakuna sababu mtu kuendelea kuvamia na kujenga katika maeneo ambayo hayajapimwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimwambie ndugu yangu Mheshimiwa Malocha, alizungumza juzi hapa kwa uchungu sana juu ya shamba lake la Malonjo. Watu wako mmelitoa nje ya Mahakama mzungumze. Malizeni mazungumzo, mimi nasubiri. Wakati ule niliwashauri mpeleke notice na mtu wangu alisaidia kuandika notice tuka-serve notice kwa Efatha, lakini akawapeleka Mahakamani. Ninyi mmetoa kesi Mahakamani mzungumze. Zungumzeni, mimi nawasubiri. Kwa hiyo, kabla mambo hayajaja kwangu, msinilaumu. Nilisema miezi sita mkileta kwangu nitakuwa nimeamua, lakini haijaja kwangu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri tutashirikiana na nimemwomba Mkuu wa Mkoa wa Rukwa asimamie hayo mazungumzo yenu, Mheshimiwa Malocha na Wabunge mshiriki haya mazungumzo ili yaishe vizuri. Kwa sababu hata yule mwekezaji ajue, lolote atakalofanya,

hataweza kulima lile shamba kwa ustaarabu kwa sababu wale wananchi wamechukia. Kwa hiyo, kwa mwekezaji lazima ajue kwamba lile shamba ni moto na wananchi mtekeleze haya mazungumzo yenu vizuri, win-win situation, mwendelee na hilo shamba. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na shukrani zangu zote nimalizie kwa kusema changamoto zilizoainishwa kwenye mapendekezo yenu na hoja zenu ni nyingi sana, yaani nashindwa hata nianzie wapi; lakini ya Watumishi imezungumzwa sana hapa, Watumishi hatunao. Tutakachokifanya cha dharura kwanza, tutashirikiana na TAMISEMI kuangalia watumishi waliopo tuwapange vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika zunguka yangu nimegundua kuna Wilaya zimependelewa, kuna Watumishi wengi sana. Ilemela na Nyamagana wana Watumishi wasiopungua 100 Wilaya mbili wa Sekta ya Ardhi, tutawaondoa huko. Hii ni kwa sababu kuna Wilaya nyingine haina Mtumishi hata mmoja wa Sekta ya Ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutapita, kabla ya kuajiri wapya, tutaangalia uwiano wa jinsi walivyopangwa ili tuwa-switch angalau kazi za dharura ziweze kufanywa kwa watumishi waliopo tugawanye vizuri ili watumishi hawa wasambae maeneo mengine. Watu watapangwa upya halafu baada ya hapo ndiyo tutasimamia vibali kwa Mheshimiwa Angellah Kairuki ili wapya wakipatikana, tuwapange vizuri. Upangaji haukuwa mzuri tutaurekebisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi mmezungumza habari ya asilimia 30; masuala haya ya upangaji na kodi ya asilimia 30, kinachosisitizwa hapa ni kwamba tungependa miji yetu ipangwe, watu wajenge kwenye viwanja vilivyopangwa, lakini watu wamilikishwe mashamba angalau wapimiwe ili wapate hati. Sasa imekuja tu asilimia 30 lakini faida kubwa zaidi ya watu kujenga kwenye viwanja vilivyopangwa ni kuendeleza miji yetu vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, msiangalie tu asilimia 30, mwangalie vilevile kwamba hawa watu kodi tunazokusanya tunazikusanya kwenye viwanja ambavyo vimepangwa na kupimwa, kwa hiyo, Miji yetu imepangika. Kwa hiyo, tuendeleze kasi ya kushirikiana ya kupanga Miji yetu ili iweze kupangika vizuri na kuwawezesha wananchi kupata hati. Kila mwananchi akipata hati, tutaelewana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la mwisho, Mheshimiwa Kiongozi wa Upinzani, lile suala la kutoza kodi kwa viwanja vya mijini na mashamba madogo madogo ya mijini ambayo hayajapimwa, nina maelezo ya ziada. Nitakutafuta wewe na Mheshimiwa Mwassa wenye hoja hii, tuzungumze, tujadiliane. Kinachokufanya wewe useme ni shamba lako mjini ni nini? Hicho hicho tuta-register.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu haiwezekani wewe unapata faida kubwa pale mjini, una ekari 40 Dar es Salaam, una ekari 4,000 Dar es Salaam hutaki kupima, lakini unauza vipande vipande unapata hela; hulipi capital gain. Hivyo hivyo, unavyojifanya wewe vinavyokutambulisha kwamba ni shamba lako, tutavisajili hivyo hivyo na utatulipa pesa, lakini nitawatafuta ninyi wawili, msishike shilingi ili niwafahamishe vizuri. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana, Mwenyezi Mungu awajalie wale wanaoendelea kufunga na sisi wala futari, makobe, tupo, tutawasaidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017.
WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa hii na mimi nitoe mchango wangu kwenye hoja ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitumie fursa hii kuunga mkono hoja yetu ya Ardhi, Maliasili na Utalii kabla sijaenda mbali. Lakini pili, kumpongeze Makamu Mwenyekiti ambaye kwa sasa anakaimu Mwenyekiti dada yangu Mheshimiwa Kemilembe Julius Lwota na Wajumbe wote wa Kamati hii kwa kuendelea kutushauri na kutuunga mkono katika kutekeleza majukumu yetu tuliyopewa katika Wizara ya Maliasili na Utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, nitapenda kuanza kuchangia kwanza kwa kulitambulisha Bunge lako tukufu kwamba sekta ya maliasili na utalii ni katika sekta nyeti sana katika Taifa letu. Na unyeti wake unaanza pale ambapo Tanzania inatambulika kimataifa katika tafiti iliyofanyika mwaka 2012 kama nchi ya nne kati ya nchi 140 duniani zenye vivutio vya asili. Kwa hiyo, nchi yetu ina utajiri vikubwa sana wa vivutio vya utalii. Lakini pili, sekta ya maliasili na utalii inachangia pato la Taifa kwa kiwango cha asilimia 17.6 ya GDP yaani pato la Taifa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia sekta hii inachangia kwa kiasi kikubwa na niseme tu ni sekta namba moja kwa kuingiza fedha za kigeni nchini mwetu. Katika mwaka wa fedha uliopita sekta hii ilichangia jumla ya shilingi bilioni 2.1 za Kimarekani, lakini pia sekta hii ina changamoto nyingi mbalimbali na changamoto zake zinatokana na uasili wenyewe wa sekta hii. Sisi kwenye Wizara ya Maliasili na Utalii tunasimamia rasilimali ambayo inatumika lakini pia inajirudia, kwa maana kwamba wanyamapori wanazaliana; misitu inaweza ikaota ikakua. Kwa hiyo, ni sekta ambayo ina rejuvenate kadri ambavyo tunaendelea kui-manage kwa uendelevu.

Lakini pia sekta yetu inachangia kwa kiasi kikubwa sana kutoa ajira hapa nchini, inachangia takribani asilimia 12 ya ajira zote zinazotolewa katika Taifa letu na kwa msingi huo sekta hii ni nyeti sana na mimi katika hatua hii nikubaliane na Kamati yetu ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na Waheshimiwa Wabunge wenzangu wote waliosema kwamba sekta hii kwa hakika inahitaji umakini wa namna ya kipekee katika kuiongoza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tulipoteuliwa kwenye nafasi hizi nina hakika mamlaka ya uteuzi ilizingatia umuhimu huo kuweka watu wanaoweza kuiongoza sekta hii kwa weledi lakini pia kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu na ndiyo maana tunatekeleza majukumu yetu bila kumwangusha Mheshimiwa Rais lakini pia bila kuliangusha Taifa letu.

Pamoja na fursa zote zilizopo lakini sekta hii ina changamoto kubwa sana ya maeneo yake kuvamiwa na watu mbalimbali, ina changamoto ya mipaka kutokuwa wazi, kutokueleweka vizuri baina ya wahifadhi na wananchi, ina changamoto kwamba sekta ya utalii imekuwa ikichangia kidogo sana kwenye kuondoa umaskini wa watu wetu japokuwa inaonekana ni sekta nyeti. Lakini pia ina changamoto kwamba sekta hii imejikita katika ukanda mmoja tu wa nchi yetu na kwa kiasi kikubwa kwa zaidi ya asilimia 90. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hivyo sasa changamoto hizi tumeziwekea mikakati mbalimbali ya kuzitatua. Mojawapo ya mikakati tuliyoweka kwenye ya awamu ya tano ni utekelezaji wa mradi mkubwa wa kufanya diversification ya kijiografia kwa maana ya kutambua na kuwekeza nguvu zetu kwenye maeneo mengine zaidi ya kitalii. Lakini pia kufanya diversification ya mazao ya utalii yaani toursim product katika maeneo mengine mbalimbali na katika hili napenda kutambua diversification ya kijiografia ambayo tumeanza kuifanya na tutaifanya kwa mafanikio makubwa ya kuelekea kuifungua circuit ya utalii ya kusini ambapo tunaanza kuelekea kutekeleza mradi mkubwa unajulikana kama RIGRO ambao una dola za Kimarekani milioni 150 zaidi kidogo ya shilingi bilioni 300. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye mradi huo tutafanya mambo mengi ikiwemo kujenga uwanja wa ndege wa Nduli na kuufanya uwe wenye kiwango cha kutua ndege kubwa. Lakini pia kujenga barabara ya kutoka Iringa mpaka geti la kuingia Ruaha National Park pale Msembe, lakini pia kujenga viwanja vidogo vidogo vya ndege 15 katika mbuga nne ambazo zinapatikana kwenye circuit ya kusini. Na hapa nazungumzia Udzungwa, Ruaha National Park, nazungumzia Selous Game Reserve lakini pia nazungumzia Mikumi National Park. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na mambo hayo ambayo tunakusudia kuyafanya kwenye mradi wa RIGRO tunakusudia kuwekeza kwenye uhifadhi wa bonde la Usangu ambalo kwa kiasi kikubwa limeingiliwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu na hivyo kusababisha maji kwenye Mto wa Ruaha Mkuu kupungua kwa siku zaidi ya 60 katika kipindi cha miezi 12 ya mwaka hali ambayo inaweza kuhatarisha bionuai inayopatika kwenye hifadhi ya Ruaha na maeneo mengine yanayolindwa kwa mujibu wa sheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii ni diversification ya kijiografia kwamba kanda ya circuit ya kaskazini imeelemewa sana, lakini pia inafanya vizuri sana sasa tunaifungua circuit ya kusini ili na kwenyewe kuweze kuwa na hadhi ya kiutalii kama ambavyo circuit ya Kaskazini ipo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu pia unakuja na kufanya maboresho kwenye kituo cha treni cha Matambwe kilichoko pembezoni mwa Pori la Akiba la Selous lakini pia kujenga air strips zenye hard surface nne kwenye maeneo yote hayo niliyoyataja na mambo mengine mengi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na kufanya diversification ya kijiografia, tumejikita pia kufanya diversification kwenye mazao ya utalii yaani tourist product ambapo hatuangalii utalii wa wanyama pori peke yake tunaanza kufikiria kutanua wigo wa vivutio kwa kuwekeza kwenye kufanya maboresho ya utalii wa fukwe, utalii wa mikutano lakini pia…

KUHUSU UTARATIBU . . .

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, asante, ni Mjumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii na hii ni hoja ya Kamati kama Mbunge ninachangia hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi huo tunafanya jitihada nyingi mbalimbali ikiwepo jitihada kuongeza mazao ya utalii kama nilivyosema na hapa tunazungumzia mbali na hizo talii za fukwe, utalii wa kuvutia mikutano na matukio mbalimbali ya michezo ya kimataifa tunawekeza nguvu zetu kwenye kuandaa mwezi maalum wa urithi wa Mtanzania, ambapo tumekusudia mwezi wa tisa kuandaa…(Makofi)

(Hapa kengele ililia na kuashiri kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

T A A R I F A . . .

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, huyo ndio Mnyamwezi Kingwangalla huyo. (Makofi)

Naomba niipongeze sana Kamati yangu chini ya Makamu Mwenyekiti na Waheshimiwa Wajumbe wote wa Kamati hii kwa michango, lakini pia kwa maelekezo yao ya kila mara ambayo yamesaidia sana katika utendaji wa Wizara yangu. Lakini nawashukuru pia Wabunge wengine wote wa Bunge hili kwa ushirikiano wao mkubwa ambao unatusaidia kama Wizara ya Ardhi katika kutatua na kufanya kazi mbalimbali za kusimamia sekta ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nawapongeza vilevile Waheshimiwa Mawaziri wenzangu wa sekta zilizotangulia ambazo ni watumiaji wa ardhi wote waliotanguliwa wa Mifugo, wa Kilimo, wa Maliasili wote ni watumiaji wa ardhi nawapongeza sana kwa mikakati yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikua tu niwakumbushe kwamba tunajua kwamba tuna migogoro mingi sana na kwa upande wa ardhi tuna migogoro ndani ya vijiji na ndani ya miji na tunajua kila Mbunge hapa alishawahi kuorodhesha migogoro yake kutoka kwenye Jimbo lake na hata tungeorodhesha yote tusingeweza tukaimaliza hata tungepata kipindi cha Bunge la mwaka mzima. Nataka muamini tu kwamba migogoro yote mliyoorodhesha kuanzia kwenye Kamati Teule ya Sendeka na ndiyo maana hata mdogo wangu Mheshimiwa Nape hapa mimi naona hakuna sababu ya kuunda Kamati Teule nyingine kwa sababu ile Kamati ya mwisho ya mwaka 2015 ndiyo tunafanyia kazi kama Serikali hivi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, orodha yenu ya migogoro ndio tunafanyia kazi ndiyo iliyosababisha tuunde Kamati ya Mawaziri watano, nataka kuwaambia tunaendelea vizuri isipokuwa kama mnavyojua baadhi ya Mawaziri wameingia karibuni tumepeana muda ili kila mtu akaangalie sekta yake, halafu tutakutana tena nafikiri wakati wa Bunge la Bajeti kila Wizara itakuwa na maeneo mapya ya kusemea kuliko ilivyo sasa. Kwa hiyo, Kamati yetu inaendelea vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwakumbushe tu kwa sheria ya mipango miji na za vijiji za ardhi zote za mwaka 1999 masuala yote yanayohusu ardhi yanasimamiwa na Halmashauri zetu za Wilaya. Halmashauri za Wilaya ndio zinazohusika na mipango mijini lakini ndizo zinazohusika na mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji.

Kwa hiyo, kila tunachosema tujue mamlaka ya mwisho ya kuandaa mipango ya matumizi bora mjini au mipango ya matumizi bora vijijini ili kuepusha mapigano ya wakulima na wafugaji na wavamizi wengine ni sisi Halmashauri ndio tumepewa dhamana hiyo kwa mujibu wa sheria zote hakuna mtu mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ningependa kila mara tuwe tunashiriki vizuri katika kusimamia ardhi yetu kwa kushiriki katika upangaji mijini lakini vijijini. Nawapongeza sana Halmashauri ambazo hivi sasa mijini wameshaandaa master plan ziko Halmashauri 23 za miji, lakini ziko Halmashauri nyingine 24 na miji midogo ambayo wameandaa mipango ya kati na ziko Wilaya karibu asilimia 20 ambao wameshaandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi.

Kwa hiyo, nawahimiza tu Waheshimiwa Wabunge angalau kila Wilaya kwenye bajeti ingeweka angalau kila mwaka kufanya matumizi bora ya ardhi vijiji vitano vile vyenye migogoro mikubwa ambavyo vinashirikisha jamii nyingi pengine tungepiga hatua. Kwa hiyo, nawaomba sana Waheshimiwa Wabunge tujue kwamba jukumu la mipango ya matumizi bora ya ardhi ni la kwetu sisi. (Makofi)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Lukuvi dakika moja samahani kidogo. Kwa mamlaka niliyokuwa nayo naongeza nusu saa mpaka saa mbili na robo, endelea Mheshimiwa Lukuvi.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Wizara kwa kutambua hilo na ninyi wote Waheshimiwa Wabunge mnajua sehemu kubwa ya nchi hii haijapangwa, mijini na vijijini hakujapangwa yaani utambuzi na upangaji wa matumizi mbalimbali mijini na vijijini haujafanyika kwa zaidi ya asilimia 75.

Kwa hiyo, Wizara yangu na Serikali kwa sasa tunaandaa mpango wa kitaifa wa kupanga na kupima kila kipande cha ardhi cha nchi hii. Kwa sababu hiyo tutakuja na mapendekezo kwenye budget speech yetu pengine kuanzisha fund maalum ambayo itasababisha zoezi hili la upangaji wa vijiji na upimaji na mijini liweze kutekelezeka. Kwa hiyo, tunakusudia angalau kila eneo na kila kipande cha ardhi kiweze kupangwa ili ulinzi wa ardhi uwe madhubuti. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, na zoezi hilo tumeliona linawezekana kwa sababu hivi sasa tuanza katika Wilaya ya Kilombero, Malinyi na Mahenge. Tumeanza kupanga kila kipande cha ardhi na katika mwaka ujao tutakuwa tunakamilisha mpango wa Wilaya hizo tatu tutakuwa tuna uwezo wa kutoa hati za Kimila zaidi ya laki nne katika Wilaya hizo tatu. Kwa hiyo, tunafikiri kwamba kila mwananchi akiwa na hati katika eneo analomiliki ikiwa kijijini hati ya kimila na mjini title deed itamwezesha kutumia rasilimali ardhi vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na zoezi hilo kwa sababu hii nchi hii haijapangwa kwa muda mrefu mijini hata vijiji kwa mijini tumekuja na programu ya urasimishaji wananchi wote ambao walijikuta wamejenga katika maeneo ambayo hayakupangwa na kupimwa kwa matatizo mbalimbali pengine kwa Serikali kuchelewa kupanga maeneo hayo. Tumeanzisha programu ya urasimishaji katika maeneo hayo ili wananchi hao waweze kupata huduma za msingi katika maeneo hayo kama vile barabara maeneo ya upitishaji miundombinu ya umeme na maji, lakini pia tuwawezeshe kuwa title deed waweze kumiliki ardhi kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wajumbe mjue jambo hili linahimizwa na Serikali kama una squatter, kama una wananchi katika Jimbo lako wanaishi katika makazi holela, jitahidi sana kuhakikisha mnashirikisha wananchi katika mitaa ile wanafanya urasimishaji ili watoke kwenye makazi holela wakae kwenye makazi yaliyo rasmi. Tunafanya zoezi hilo ni rasmi, najua wote mnaokaa mjini mna maeneo ambayo yanamakazi holela. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni fursa imetolewa na Serikali ya Awamu ya Tano kurasimishwa maeneo hayo na mpaka sasa mikoa ambayo inaongoza kwa urasimishaji ni Mkoa wa Mwanza ambao kwa sasa Wilaya mbili tu za Ilemela na Nyamagana wanakaribia kutoa hati 30,000 kuwawezesha wao…

T A A R I F A . . .

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kila Wizara inasimamiwa na sheria zake. Sheria yangu inaniruhusu kurasimisha makazi holela, lakini halitakuwa jambo la kudumu, ndiyo maana tunahimiza master plan na tunakuja na mpango wa kupanga na kupima kipande cha ardhi. Tukiweza kupanga na kupima kila kipande cha ardhi, kwa vyovyote vile urasimishaji utakoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niwapongeze sana viongozi na wananchi wa Wilaya za Ilemela na Nyamagana peke yao wamewezesha wananchi wao ambao walikuwa wamejenga majengo ya fahari na hayana hati, leo wanamiliki wakiwa na hati katika makazi holela. (Makofi)

Pia Mkoa wa pili ni Dar es Salaam, Dar es Salaam kuna maeneo mazuri wanafanya vizuri Kimara, Makongo kule kwa maprofesa wanafanya kazi nzuri wamechanga wenyewe. Lakini na mikoa mingi wanaendelea kufanya zoezi hilo, kwa hiyo, nawapongeze sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakubaliana na mapendekezo ya Kamati kwamba kuanzia sasa hatutatumia makampuni ya nje kufanya master plan. Tumefanya master plan kwa kutumia Kampuni ya Singapore kama walivyosema watu wa Kamati, Wajumbe wangu wa Kamati kwa gharama kubwa. Tumefanya Mwanza na Arusha ni kweli, lakini nimesema nimekubaliana na mapendekezo ya Kamati yangu ya Ardhi kuanzia sasa haitawezekana kabisa kuajiri makampuni ya nje kwa ajili ya kufanya master plan, kwa sababu vyuo vyetu vya ndani vimetoa wataalam wengi, na hizi master plan…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 - Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa fursa hii uliyonipa mara ya pili baada ya ile kusoma. Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote kwa kutupa moyo mimi na Naibu wangu na Watendaji wetu. Nataka kuwahakikishieni kwamba hatutawaangusha. Leo mmetuchaji zaidi, tutaongeza speed. Nataka mhakikishe kwamba mwakani mkija kuzungumza wote ambao mmeandika na kusema, mje mtoe ushuhuda kwamba tumefika kwenu na tumezungumza haya mliyotutuma tukiwa kwenye Majimbo yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na hoja yako, ulipokuwa unachangia hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenye maswali yako wiki mbili zilizopita, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi kwamba ile issue ya Chama cha Wapangaji na National Housing wakutane, Mheshimiwa Waziri Mkuu ni Kiongozi wetu, nawe ni Mwenyekiti wetu. Nataka kukuhakikishia kwamba National Housing watakutana na viongozi wa Chama cha Wapangaji. Jana nimekutana na Mwenyekiti yuko hapo nje. Naagiza wakutane kabla ya tarehe 15 Mwezi wa Sita, halafu waniambie wamekubaliana nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, yale maagizo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu yatatekelezwa, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi yuko juu hapa ananisikia na Kaimu Mkurugenzi wa National Housing yuko hapa. Naagiza wakutane kabla ya tarehe 15 Mwezi Juni baada ya hapo, wanione mimi kama Waziri nijue nini naweza kuamua. Kama liko ndani ya uwezo wangu au la kupeleka kwenye Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa pendekezo hilo na namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa maagizo na namhakikishia kwamba nitatekeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waheshimiwa Wabunge wamezungumza wengi, nianze na rafiki yangu hapa Mheshimiwa Bobali. Amri yangu niliyoitoa ni kwa mujibu wa Sheria ya Mchinga. Lile eneo nataka wasikie wote, ni eneo la Serikali. Zile ekari zote zilizochukuliwa na kampuni ile iliyochukua kuzunguka Bahari ya Hindi, lote ni eneo la Serikali. Walichukua kinyume cha sheria na nilikwenda na viongozi wote, walitoa hati kinyume cha sheria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama kuna mazungumzo na migongano inafanyika huko, haiwezekani. Nimeshatoa amri na amri siyo yangu ni ya kisheria. Kwa hiyo wajue tu hili eneo ni la Serikali. Halmashauri ya Wilaya ya Lindi wajue hili ni eneo la Serikali na lazima walipange kwa mujibu wa sheria. Nilitangaza siku ile walipandishe hadhi kwa sababu walianza kutoa hati kabla, eneo lenyewe likiwa kwenye hadhi ya vijiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hili hatubabaishani ndani ya Serikali. Mimi ndio nimepewa jukumu hili na Mheshimiwa Rais, namsaidia kufanya jambo hili. Zile Zahanati zitafunguliwa, vinginevyo anayetaka azibomoe akazijenge huko alikotaka. Zile Zahanati zimejengwa kwenye ardhi yenu.

Kwanza nashangaa, mnasubiri nyie kufunguliwa na nani? Nani awafungulie? Ziko kwenu, nani anawafungulia? Kufuli gani hizo zimewekwa? Mwambieni azichimbe azitoe. Nani alimpa kibali cha kujenga? Hakuna makubaliano? Kwa hiyo, nasema, hilo la Zahanati siyo langu, lakini ardhi ile haitoki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimewasikiliza vizuri Mheshimiwa Bobali na issue zenu za mipaka, Mheshimiwa Kuchauka na Mheshimiwa Maftaha, ninyi mnatoka Mkoa wa Lindi na Mtwara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nimepanga, sasa mmenipa nguvu. Nitatembelea Mkoa wa Mtwara na Lindi. Nitarudi tena pale Mjini Mtwara ili nione yule tapeli kama anaendelea kunyanyasa, maana sehemu nyingi nimemkaba. Huyo huyo ndiye amehusika na huko Lindi, huyo huyo ndio Mtwara. Anatafuta watu wa Dar es Salaam wanakwenda kuchukua ardhi Mtwara kana kwamba Mtwara hawapo. Nitakuja Mtwara, Lindi na Newala kwa rafiki yangu Rashid. Kule nako ule mpaka kati ya Masasi na Newala tutakuja kuzungumza huko kwenye site, tutaelewana. Ni kweli baadhi ya Watendaji wa Ardhi kwa siku za nyuma walikuwa sio waaminifu. Tunapowatuma kwenda kurekebisha mipaka, wanarekebisha mipaka kutokana na eneo; wale wajanja wanaowapa fungu, basi mpaka unahamia huko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumejifunza juzi kwenye mpaka wa Kilindi na Kiteto; zaidi ya kilomita 15,000 zilikuwa zimehama. GN inaeleza watu waende Kaskazini Mashariki wenyewe wanakwenda Magharibi bila sababu. Sasa kutokana na nidhamu iliyowekwa n a Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, hakuna mtumishi anaweza kula hela tena. Kwa hiyo, sasa hivi mjue kila palipoandikwa GN, tutarekebisha kwa mujibu wa maandishi ya GN unless wananchi wakubaliane upya. Maana inawezekana GN na yenyewe imepitwa na wakati, lakini mkikubaliana, sisi tunakuja kuiandika tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie kwamba sasa hivi utumishi wa Umma umebadilika, watu wana nidhamu, tutakuja kurekebisha hiyo mipaka ya Masasi na Newala na maeneo yote ambayo yana migogoro mipaka tutapitia na mingine tumeshaiandika, kama ile ya Makambako, Njombe na Mufindi, rafiki yangu Mheshimiwa Kigola amesema na mingine tuliyoandika tutakuja kuishughulikia ili angalau watu wakae vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI naye ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa wahakikishe kwamba mipaka ya vijiji na vijiji migogoro yao wanaimaliza kwa sababu iko ndani ya uwezo wao. Alishaandika siku nyingi na nadhani hili wanalitekeleza. Maana haiwezi kuwa wanasubiri Mawaziri waende huko kushughulikia mipaka ya vijiji na vijiji wakati GN wanazo na mipaka hii ilibuniwa na Wilaya zao. Kwa hiyo, nawaomba Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wasimamie ukamilishaji wa utatuzi wa migogoro ya vijiji na vijiji kwa sababu iko ndani ya uwezo wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimeyasikia ya Mheshimiwa Bobali, Mheshimiwa Kuchauka na Mheshimiwa Maftaha. Lile la Mheshimiwa Maftaha la mjini kuhusu mgogoro wa fidia, kwa sababu wananchi waliingia mkataba na UTT; na UTT ni chombo cha biashara, kiko chini ya Wizara ya Fedha, hata mimi niliwashangaa. Kwa sababu waliosema watalipa mwaka 2017 ni wao, nami nilikuja Mtwara na nyie tulikutana na wewe ulikuwepo. Baadaye wamesema hailipi, wameenda kwa mwenye Wizara yake, Wizara ya Fedha wakamwambia, Mzee huu mradi haulipi, Bodi ya UTT wamekataa kuchukua ile ardhi kwa sababu ule mradi wakipima viwanja watauza ghali na wananchi wa Mtwara hawataweza, hailipiki. Kwa hiyo, wameacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi Wizara ya Ardhi hapa nilikuwa upande wa wananchi, lakini yamenishinda kwa sababu wenye mradi ambao mlikubaliana nao wamesema hailipi. Ardhi haijachukuliwa, imerudi mikononi, kwa hiyo, tushirikiane tuipange wenyewe, tupime viwanja ili kila mtu apate faida ya ardhi yake. Hatuwezi kuwang’ang’ania wale kwa sababu ilikuwa ni biashara. Nilitaka niseme hivyo, lakini nitakusaidia kuwaeleza zaidi nitakapokuja Mtwara. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mtuka amezungumzia habari ya master plan kule Manyoni, yeye ni mtalaam, anajua kabisa kwamba masuala ya master plan yanaanza kwao. Waazimie wao kutengeneza master plan halafu tutashirikiana. Waazimie kwenye Council kwamba wanataka kutengeneza master plan na kupanga mji wao, tunajua wana matatizo ya vifaa, vitakavyokuja tutawaelezeni, wataviazima hivi vifaa kila Halmashauri ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuanzia mwezi wa Saba tutakuwa na vifaa nchi nzima, mtaviazima kila Halmashauri bure. Kabla ya mwezi wa Saba wataalam wa Serikali wa Halmashauri tulionao tutawafundisha sisi Wizara namna ya kutumia hivyo vifaa vya kisasa kupanga. Kwa hiyo, yeye kwa sababu anajua kupanga, yeye ni surveyor, hivi vifaa atavitafuta, tutampa avitumie ili angalau vimsaidie katika kuharakisha. Tunajua jitihada zake, anafanya kazi vizuri pale, lakini tutashirikiana naye kuhakikisha anakwenda kwa kasi nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alivyosema Mheshimiwa Mwakasaka ni kweli Tabora kuna migogoro mingi, wajanja walishaiharibu pale siku nyingi. Nimekuja mara mbili, amekuja Naibu wangu lakini tutakuja tena. Tunajua siyo tatizo la Tabora, viongozi wengi wameshiriki katika kuharibu mipango miji na kudhulumu watu. Siyo Tabora, sehemu nyingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadhi ya viongozi, hata sisi wa kisiasa na Madiwani wakati mwingine huwa tunagombea kwa ajili ya viwanja. Kwa hiyo, kila mji umekwisha, umeshapangwa lakini umeingia kwenye madaraka, lazima upate viwanja. Sasa Watendaji wale walikuwa wanawaajiri ninyi, kwa hiyo, wakiwatisha kidogo wanabadilisha, wanawauzia. Sasa hawatawatisha tena. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais ameondoa hicho kichaka, wamekuja kwangu, maana walikuwa wanawatisha kwamba watawafukuza wasipotekeleza matakwa yao. Mheshimiwa Rais amewahamisha huko, amewaleta kwangu. Kwa hiyo, nataka niwaonye watumishi wote wa Serikali, sasa hakuna kwa kujificha, kitendawili kimeteguliwa, lazima watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa sheria na hakuna vitisho. Mtu yeyote sasa atakayekosea huko hatajificha kwamba nililazimishwa na Kamati ya Mipango Miji, ni lwake, atakakufa na lwake na hahamishwi mtu, atafia hapo hapo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mwakasaka kwamba kwa issue ya Tabora lazima tuje twende tena. Kuna mambo ambayo yamekaa vibaya pale. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, alichozungumzia Mheshimiwa Mabula ni kweli, katika zoezi la urasimishaji Tanzania watu wanaoongoza wamefanya vizuri, kwa nidhamu na kwa heshima na kujitolea ni Wilaya ya Nyamagana na Ilemela. Amesema kweli kabisa. Kwa hiyo, nami nawapongeza sana. Mheshimiwa Mabula anajua watu wake aliowaleta wiki iliyopita, tumekubaliana tukutane mwezi wa Sita katikati kule Jimboni. Kwa hiyo, namshukuru sana na yeye ametoa ushirikiano sana kule Nyamagana katika zoezi hili. Nyamagana na Ilemela peke yake wameshatoa Hati zaidi ya 25,000. Namshukuru sana na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ametoa ushirikiano mkubwa katika zoezi hili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nawaomba wananchi na viongozi wote wa Wilaya, wajue zoezi la urasimishaji halina mwenyewe. Watu wamejenga kwenye maeneo yasiyopangwa nchi nzima mijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kila wilaya ijipange ihakikishe inawaokoa wananchi wao katika maeneo yale yasiyopangwa yanayoitwa makazi holela wayapange ili waweze kupata Hati, iwaongezee mzunguko wa fedha, kipato kwa sababu watu wakipangiwa, wakipewa hati, wataingia benki, watazitoa zile hela za mabenki zitakuja mtaani, zitaongeza mzunguko wa fedha katika Halmashauri. Kwa hiyo, zoezi la urasimishaji ni la wote na viongozi wa Wilaya tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba jambo hili linafanyika vizuri kama walivyofanya wenzetu wa Nyamagana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mheshimiwa Shekilindi, tukipata Wenyeviti wengine wa Mabaraza, tumeahidiwa tutarekebisha upungufu tunaopata kule Lushoto. Suala la upimaji, nafikiri halmashauri yake lazima ijipange. Kama watu hawana Hati, basi ni uzembe wa Halmashauri yake. Kwa sababu Wizara haiwezi kwenda kupanga na kupima kila mahali, lazima tujipange tufanye wenyewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimemsikia Mheshimiwa Mgumba, ni kweli leo amenipa siri kwamba Morogoro walinipiga changa la macho. Nitakwenda tena na kabla sijaenda nitashirikiana naye ili aniambie siri hiyo. Ni kweli yapo matatizo Morogoro, nakiri kabisa, lakini kwa sababu ya muda, nafikiri kwa sababu amenipa kidogo ufunguo, tutakwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Kigola, nimeshamwambia. Mheshimiwa Malecela Kilango amenialika kule, mimi nakwenda katika hizo Kata zote mbili. Mheshimiwa Lupembe amenialika Katavi, nitakwenda. Nikitoka Tabora nataka kwenda Katavi na nitakwenda na Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi ili twende kuangalia hilo eneo mgogoro kati ya maeneo ya ulinzi na ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusema nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge, hatuna nafasi ya kuwataja kwa majina lakini wamechangia kwa maandishi na wengine kwa kusema. Mengine yaliyotoka kwenye Kamati ni maelekezo yetu. Haya yote waliyoyasema yametusaidia sasa kupanga ratiba ya kazi na Mheshimiwa Naibu Waziri. Kutokana na hayo waliyoandika na waliyoyasema sasa tumejua twende wapi. Tutawafikia kwenye Wilaya zao ili mtufafanulie zaidi. Kabla hatukwenda tutahakikisha tutawatafuta kwa simu ili tushiriki wenyewe kwenye Mikutano katika Wilaya zao. Tungependa wafunguke zaidi tukiwa pale ili angalau tushirikiane katika kukomesha hii migogoro katika maeneo yenu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nisisitize mambo matatu ya mwisho. Nataka kusisitiza kwa wananchi wote na viongozi na wananchi kwamba ulipaji wa kodi ni suala la kisheria, tumeongeza muda, hatuongezi tena, naomba wananchi wote walipe kodi. Baada ya mwezi nilioutangaza, sasa wale ambao wana malimbikizo wataanza kupelekwa Mahakamani kuanzia mwezi wa Sita. Naomba tulipe kodi kwa maendeleo ya Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia ziko taasisi za Serikali ambazo tunafikiri hazifanyi biashara kuzifutia madeni haya, lakini pia kuziangalia namna ya ulipaji wao wa kodi. Hatuwezi kutoza kodi kwenye Zahanati, Shule za Msingi na Shule za Sekondari ambazo hazitengenezi faida. Vile vile vipo Vyuo na Taasisi za Serikali ambazo zimeomba zifutiwe, lakini zinafanya biashara. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnataka kufutiwa. Tutaangalia ardhi ambayo mnaitumia kwa mabweni na kwa madarasa, lakini yale maeneo mnayofanya Mlimani City tutawatoza kodi. Kwa hiyo, siyo kwamba kila Taasisi ya Serikali tutaisamehe. Yale maeneo ambayo mnatoza hela na sisi tutatoza kodi. Yale ambayo mnafanyia bure nasi tutawasamehe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, nizungumzie habari ya urasimishaji. Nimesema nawaombeni viongozi wote tushirikiane tufanye suala hili la urasimishaji, lakini partners wa urasimishaji makampuni binafsi lazima tuwe na nidhamu katika kufanya jambo hili. Imeonekana kama jambo hili sasa halina mwenyewe, mnaingia ingia hovyo, wasio na sifa na wenye sifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeagiza bodi zangu zote zinazoshughulika na upimaji na upangaji zisimamie na kuhakikisha zinayafuatilia makampuni binafsi yanayokwenda kufanya kazi hii kwa kukiuka utaratibu. Jana nilisema, wananchi wanachanga wenyewe gharama za urasimishaji, Serikali haichangii, lakini fedha zile zisiende mikononi kwa kampuni, zikae kwenye kikundi cha urasimishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie kwa kusema nawaomba sana Halmashauri zote zisimamie suala la matumizi bora ya ardhi. Kupanga matumizi bora ya ardhi katika vijiji na miji ni kazi yetu wote. Naahidi kama nilivyosema, vifaa vya upimaji tutavisambaza kwenye kanda ili Halmashauri ivitumie. Lengo ni kupunguza gharama kwa wananchi ili kasi ya upangaji na upimaji iende kwa kasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, narudia kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kama nilivyomshukuru mwanzo kwa kasi na ushauri mbalimbali ambao amekuwa anatupa. Sisi tunafanya kazi na pongezi hizi, lakini mjue kuna mtu anatusukuma tunafuata vision yake na mnajua aliwahi kuwa Wizara hii na kasi yake, vision yake tunaifuata. Tunamshukuru sana kwa msukumo na ushauri wa mara kwa mara ambao anatupatia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaahidi kwamba baada ya bajeti hii, tutapanga ratiba ili tupate fursa ya kuwatembelea Waheshimiwa Wabunge kwa sababu ratiba yenu sasa tumeshaipanga kulingana na kero mbalimbali mlizotupatia hata ambao wameandika kwa maandishi tumeona kero zao. Tumejipanga, mpaka mwezi wa Saba ninyi wenyewe mtakuwa mashahidi kwamba kweli mlikuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2018
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa muda ulionipa. Nami nakupongeza sana kwa utendaji wako na usimamizi mkubwa wenye tija wa Bunge letu Tukufu, nawapongeza sana Kamati yangu ya Ardhi, Maliasili na Utalii kwa ushauri wao ambao wamekuwa wanatupa kila wakati, mimi na Naibu wangu tumefurahi, na tumenufaika sana na ushauri wa Kamati hii, tukiwa kwenye mikutano, tukiwa kwenye ziara, tumefaidika sana na Wajumbe wote kwa pamoja wakiongozwa na aliyekuwa Mwenyekiti. Kwa hiyo nawapongeza sana na tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika utendaji wa kazi ambazo tumekabidhiwa mara zote sisi tunatekeleza kwa malengo ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Pili, tunatekeleza kwa maelekezo mahsusi, ya Mheshimiwa Rais na Viongozi Wakuu, Makamu na Waziri Mkuu maagizo ya Cabinet lakini pia maelekezo ya Bunge lako Tukufu. Maelekezo ya Bunge lenyewe lakini kupitia Kamati yetu ambayo tunayo kwa muda mrefu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya shukrani hizi nafikiri niseme machache ambayo yamesemwa kwenye Kamati, naunga mkono sana, Kamati hii na maoni yake, lakini niseme mambo matatu yaliyogusiwa ndani ya ripoti hii, la kwanza nataka niseme, kwamba pamoja na kutekeleza kwa misingi niliyoisema lakini tunatekeleza kwa mujibu wa Sheria. Kwetu sisi Wizara ya Ardhi, Sheria kuu zaidi tunazozisimamia ni mbili kwa upande wa ardhi; Sheria Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999. Sheria Na. 4 inahusu zaidi ardhi hizi ambazo mara nyingi sana zinasimamiwa na kila anayemilika ardhi kwa kutumia sheria hii huwa tunampa karatasi hii, hati ya namna hii. Hii ni hati inayotolewa kwa kusimamiwa na Sheria Na. 4 ya mwaka 1999, inaitwa ardhi ya jumla.

Mheshimiwa Spika, tunaposema habari ya ufutaji wa ardhi wa hati unaoanzia kutoka kwenye Halmashauri kama alivyoeleza Mbunge wa Korogwe Vijijini ni hati hizi ndizo zinahusika na utaratibu ule lakini pia tunayo Sheria Na. 5 ya Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, inahusu ardhi ya vijiji. Kabla ardhi haijageuzwa haijahaulishwa kuja kutolewa hati hii, ardhi zote za vijiji zinatolewa hati ya namna inaitwa hati za kimila. Wanaopata ardhi hii hawana ukomo wa umiliki hawalipi kodi, lakini imeweka kiwango kila kijiji hakipaswi kutoa zaidi ya ekari 50. Kwa hiyo tuna ardhi zinatawaliwa na Sheria mbili, lakini na hati za utambulisho ziko mbili.

Mheshimiwa Spika, nimesema nianze na hii ili angalau Waheshimiwa Wabunge tuelewane. Sasa katika usimamizi wa sheria kama nilivyosema Sheria ya Ardhi hii inayotawala Sheria ya Vijiji, mamlaka makubwa zimepewa Serikali za Vijiji zenyewe, ila inapozidi 50 uhaulishaji sasa inabidi ngazi ya Wilaya izungumze, ije kwetu Wizarani, tumpelekee Mheshimiwa Rais, ikimpendeza anakubali kuibadilisha ile ardhi ya kijiji kuja ardhi ya jumla na ndipo mtu anaweza akamiliki ardhi kwa hati kama hii, kama ni ekari 50 kwa matumizi yoyote, kama ardhi iko kijijini.

Mheshimiwa Spika, sasa hati hizi ziko nyingi sana, hatutozi kodi lakini tunaamini masikini wa Tanzania wanaopendwa sana Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli ndio wanatumia hati hizi na ndio maana hazitozwi Kodi. Wanaotumiwa hati hizi sasa hivi wanakaribia milioni moja katika vijiji vyetu, lakini hawa ni mashamba, wanakaribia milioni moja. Kwenye hati hizi wa mashamba wanakaribia 2,000, mashamba makubwa, wanaomiliki kwa hati hizi, yako mashamba yasiyopungua 2,000 yenye ekari zisizopungua milioni sita zinazotumika kwa shughuli mbalimbali za kilimo za ufugaji na wamilika hao 2,000 wanazo hati hizi.

Mheshimiwa Spika, sasa moja ya jambo ambalo tumeshauriwa hapa na ambalo limezungumzwa na ndugu yangu Mheshimiwa Msigwa hapa, alitaka kuzungumza kwamba utekelezaji wa Sheria hii una mashaka na amefika mahali mpaka amemhusisha Rais, lakini nashukuru Waheshimiwa Wabunge wengi mmechangia hapa, kwamba utoaji wa ardhi au ufutaji wa hati hizi unafuata Sheria na hata siku moja, haijawahi kutokea Rais akaniagiza mimi nifute hati ya mtu fulani au nimpelekee hati ya mtu fulani afute, hajawahi kuniambia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wanaoanza kupendekeza ardhi hii kwanza, mnakumbuka tulipoanza Awamu ya Tano, mimi mwenyewe nilileta dodoso hapa kwa kila Mbunge kuuliza kero zenu, ninyi ndio mlijaza dodoso na kueleza kero zenu, tukatengeneza kitabu, asilimia 60 ya kero zile ilikuwa mashamba pori na migogoro ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, baada ya hapo tukatengeneza ratiba ya utekelezaji na …

MHE. ZITTO R. Z. KABWE: Mheshimiwa Spika, kuna ushahidi wa maagizo ya Rais.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Wewe Zitto una kelele sana, sikiliza wenzako waseme.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Mheshimiwa Spika, achana naye huyo.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ninyi mlipoleta zile kero ndipo tukatengeneza ratiba ya utekelezaji, kwa hiyo kutokana na maelekezo yenu, tumefuatilia, tumerudisha yale maelekezo yenu kule Wilayani, wamefuatilia. Katika uhakiki wa mashamba haya 2,000 mpaka sasa katika miaka mitatu hii, tumeshafuta mashamba 46 kwa mujibu wa Sheria, lakini chanzo ni ninyi, lakini pia outcry ya wananchi na Viongozi mbalimbali wamepita kwenye Kampeni wamesikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sababu ni moja tu, watu katika hawa 2,000 tuliowapa hizi hati, wanayo mashamba makubwa kama walivyosema Wajumbe Fulani. Hati hizi ukipewa kuna masharti ya matumizi huku nyuma, umri wa matumizi umeandikwa kwenye hati hizi, hati hizi hakuna umri wa matumizi, lakini unatakiwa ukipata ardhi ya shamba, angalau uhangaike moja ya nane kwa mwaka uendeleze. Kwa hiyo matarajio ya hati hii angalau katika kipindi cha miaka minane utakuwa umejiendeleza kumaliza hili shamba, lakini wako watu wengi, wengi sana, ambao wamepokea mashamba haya, matokeo yake siku zote hizi za nyuma walikuwa wanatumia kwa ajili ya kuweka rehani kupata mtaji wa biashara na kufanya biashara nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa mbele yangu nimekuja na daftari hili, mimi nina privilege ya kujua siri zenu zote, humu ndani kuna watu ambao wamepewa ardhi na wamechukua mkopo, hapa kuna zaidi ya trilioni moja nimeshika, kuna zaidi ya dola mia tano hapa na kuna fedha tasilimu zaidi ya bilioni 800 watu wamekopa, kwa rehani na hii ni taarifa ya Benki kuu, kwa rehani ya ardhi, lakini ninyi wenyewe mnajua, hivi kama kweli kilimo cha Tanzania kingewekeza zaidi ya trilioni moja si nchi ingetikisika, fedha ziko wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi tunao ushahidi baada ya kufanya uhakiki kwamba watu walichukua hizi fedha kwa sababu usimamizi ulikuwa hafifu, wamechukua kama kinga, wamechukua Benki, pamoja na kuandika madhumuni ya kuendeleza yale mashamba, lakini Benki hazifuatilii, Benki zinataka tu return ya biashara zao, wameenda kuwekeza Dubai, wamenunua apartment, wanawekeza biashara na kulipa papo kwa papo mashamba yamebaki pori, hayakuendelezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi Wabunge mkisema kuna mashamba pori huku, watu wamekopa hela benki, lakini watu wanapambana kulima yale mashamba, halafu anatokea siku moja mtu anatishatisha hivi, miaka 10 au 20 yeye anaendelea kuongeza thamani ya Kampuni yake, kutokana na mtaji unaotokana na thamani ya ardhi, lakini kule kwenye shamba haendi.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kuwahakikishia kwamba kwa maelekezo ya Ilani, Chama cha Mapinduzi kimetuelekeza tufanye uhakiki na tuchukue mashamba haya na ndiyo maana tumefanya hivyo. Kwa sasa tumechukua mashamba 46 katika mikoa ifuatayo: Arusha (2); Kilimanjaro (1); Dar es Salaam (2); Morogoro (18) na Kilosa peke yake ni 12; Iringa (1); Pwani (4); Simiyu (2); Tanga (17); Kagera (1); Mara (1); Lindi (1) alilotaja Mheshimiwa Nnauye. Shamba limetoka kwenye Jimbo lake na bado namba 38, umetaja namba 37 na 38 tumepeleka. Kwa hiyo, huu ni utekelezaji wa maelekezo yenu kumbe tufanye nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo ndugu zangu wakati mwingine, Mheshimiwa Peter hayuko hapa, huna sababu ya kuunda Kamati Teule ya kwenda kuchunguza uhalali wa kazi aliyoifanya Rais kisheria. Ninyi mnaofikiria maneno haya hangaikeni na Majimbo yenu tu kwa sababu Mheshimiwa Rais ametimiza wajibu kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, aliyesababisha hii ni ninyi, wananchi wana shida na tumetekeleza. Fikiria tumefanya uhakiki wa mashamba 2,000 tumegundua 46, kumbe tungefanya nini? Mashamba haya mnaachiwa wenyewe ili muwapangie wale wananchi walioko pale wanaitwa wavamizi ili nao wawe wamiliki wa mashamba hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme tu kwa Waheshimiwa Wabunge tushirikiane, hili jambo ni jema, hakuna sababu ya kutafutiana maneno hapa, Mheshimiwa Rais anatekeleza wajibu wake na ni msikivu sana. Yeye hafuti, mapendekezo yanatoka huku.

Mheshimiwa Spika, mashamba yaliyotajwa ya Mohamed Enterprises Company hapa amesema Mheshimiwa Peter. Mohamed Enterprises anamiliki mashamba makubwa 21 nchi hii…

WABUNGE FULANI: Eeeee.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Yako Tukuyu, Rungwe, Mombo, Korogwe na Same.

MBUNGE FULANI: Efatha.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hivi asipoendeleza tunafanyaje? Kwa hiyo, tumefanya uhakiki, kwanza niwaambie mashamba yaliyofutwa ni sita lakini onyo alipata mashamba 12. Baada ya kupata onyo, Afisa Ardhi pale akawa anachezacheza Naibu Waziri akamdhibiti amemuondoa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya hapo nilipomwagiza Naibu Waziri, tumepiga na picha na vielelezo vyote tunavyo, tukagundua ukweli mashamba sita hana la kufanya. Nataka nimwambie hayo sita na yenyewe tumempa angalizo tunamtazamia, asipotekeleza tuliyomwambia nayo yako kwenye mstari mwekundu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kuwaambia sheria itasimama na itachukua mkondo wake bila kumuonea mtu lakini bila kumuogopa mtu. Sisi tumeelekezwa kulinda rasilimali za Taifa. Kwa hiyo, naomba kama Wabunge tushirikiane, haya maneno madogo madogo ya watu wamechukua rushwa sijui wamefanya nini hayana maana, tushirikiane katika kusimamia mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana wote mliochangia na najua wengi mmesoma kwenye mitandao kwamba katika kutekeleza mambo haya mimi na Naibu wangu tumechukua rushwa. Kama tunaweza kuchukua rushwa na tukafuta basi hiyo nzuri. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Bado Rukwa.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kule Rukwa kulikuwa na shamba kubwa ambalo lina mgogoro mkubwa na Nabii wa Efatha, Mheshimiwa Mwingira, kwa hiari yake mwenyewe amekubali kutoa ekari 3,000 na kuwarudishia wananchi wa vijiji vitatu. Kule Same Mheshimiwa Mama Kilango tumekwenda wenye mashamba makubwa wamekubali kutoa mashamba yao. Ulanga juzi wawekezaji wamekubali kuweka ekari 9,000 kwa wananchi ili angalau na wenyewe wasitazame tu macho kwenye ardhi ambayo inamilikiwa na wenye mashamba makubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kusema kwa kweli Wabunge wote tushirikiane kumpongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi hii kubwa anayoifanya. Anafanya kwa ajili yenu, Wabunge wa CCM wote tumeahidi kwenye Ilani kwamba tutafanya jambo hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, Mheshimiwa Rais mmempongeza sana ametangaza Wizara saba tushirikiane, tunataka kuwahakikishia kwamba Wizara saba tutafanya lile jambo ambalo ametuagiza Mheshimiwa Rais la kutokomeza migogoro. Nimemwomba Mheshimiwa Spika tuwashirikishe na ninyi Waheshimiwa Wabunge, mimi ndiyo Mwenyekiti. Tuwashirikishe na ninyi Wabunge kama mna ziada zaidi ya yale ambayo mlisema tuko hapa wiki hii. Mtu yeyote ambaye anafikiri ana kero ya ardhi ya ziada atuandikie ili tuongeze katika agenda tulizonazo na tumepewa muda mfupi sana tupeleke kwa Mheshimiwa Rais. Kwa hiyo, kwa niaba yake na kwa niaba yenu, tunashukuru sana kwamba angalau wazo hili la Mheshimiwa Rais mmelichukua na tumeona watu wote wananchi wenye nia njema wamefurahia jambo hili.

Mheshimiwa Spika, National Housing haina matatizo ya kulipa deni, ina uwezo wa kulipa deni na kila mwezi inalipa shilingi bilioni tano na milioni mia sita kutokana na fedha yake yenyewe. Kwa hiyo, ina uwezo wa ku-service madeni na ina mali ambayo zina thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 5.

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, nawashukuru sana Wabunge wote kwa kunisikiliza na kwa kuchangia hoja hii. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020 Pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu Shughuli Zilizotekelezwa na Kamati Hiyo Katika Kipindi cha Mwezi Februari, 2019 Hadi Januari, 2020
WAZIRI WA ARDHI NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, natoa pongezi kwako kwa kunipa nafasi ya kuchangia hoja hizi za leo na katika kuchangia kwangu nilitaka nitoe baadhi ya fafanuzi ya mambo yaliyozungumzwa hasa kuhusiana na Shirika la Nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza nataka niseme kwamba huko kunakoitwa kudorora kwa miradi ya National Housing hakuna uhusiano wowote na maamuzi ya Serikali kuhamia Dodoma. Kwa sababu uamuzi wa kufanyia Dodoma umefanywa katika Awamu ya Kwanza, sisi Awamu ya Tano tungepozwa tu kwamba tumetekeleza mambo ambayo yameshindwa kutekelezwa kwa zaidi ya miaka 40. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hakukuwa na uhusiano na siamini kwamba Naibu Wangu Waziri alizungumza haya kwamba tunashindwa kutekeleza miradi ya National Housing kwa sababu tume-divert fund kuja Dodoma kwa sababu miradi ya Dodoma ya National Housing ilikuwepo na ilikuwa na fedha zake. Kwa hiyo, nilitaka niseme kwamba uamuzi huu hauna uhusiano na ile miradi lakini najua ni kweli kulikuwa na matatizo katika utekelezaji wa baadhi ya miradi ya Shirika la Nyumba hasa miradi mikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Nyumba lilikuwa limejiingiza katika miradi mingi sana ya gharama nafuu ambayo ndio yalikuwa maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi lakini pia ilijiingiza kwenye miradi mikubwa sana ya kibiashara. Sasa ndani ya miradi hiyo kulikuwa na matatizo ya usimamizi, uongozi wa bodi lakini na utekelezaji. Kwa hiyo, kabla hatujafikiria kuingiza Shirika la Nyumba kwenda kukopa hizo fedha wanazotaka zikopwe, nimetoa maagizo kwa bodi mpya ambayo tumeiunda hivi karibuni ambayo naipongeza sana imegundua na imeanza kazi kwa kasi sana. Mambo ambayo tumeyafanya ambayo tumeagiza yafanyike ni kama ifuatavyo:-

(i) Tumeagiza kufanya restructuring ya mikopo, ile mikopo yote iliyokuwa imechukuliwa na kujenga hii miradi mbalimbali mnayoona tumeamua tufanye restructuring ya ile mikopo kwanza tuchunguze na tufanye restructuring na huo utaratibu umeshaanza kuzaa matunda tangu tumeagiza mpaka sasa tumeanza na mkopo mkubwa kwa mfano wa Shelta Afrika peke yake tulikuwa tunakopa kwa dola 17% baada ya kukaa tumezungumza sasa tumefikia asilimia 14 kwa shilingi. Kwa hiyo, tunapitia mikopo yote tunafanya restructuring itatupa nafuu zaidi kuliko hata hiyo kupoteza hizo mnazosema shilingi bilioni 20 kwa mwaka;

(ii) Tunapitia mikataba ndani ya mikataba ya ujenzi ile kuna baadhi ya vifungu ambavyo vilikuwa vinaongeza gharama ambavyo havina msingi na contractors tumewa-engage bahati nzuri ule mradi wa Morocco na huo 711 wa Kawe ni contractor mmoja. Tunapitia ile mikataba ili kuondoa mambo ambayo yalikuwa yanaweza kutekelezwa bila kuwepo na gharama hizi na kupunguza gharama na tukipunguza gharama hizi zitatusaidia wote, zitasaidia Serikali kupunguza gharama ya ujenzi lakini itawasaidia hata walaji, ununuzi wa zile unit tunafikiri hata ununuzi wa zile units zile apartment ulikuwa mkubwa kwa sababu ya baadhi ya mikataba iliyoingiwa, kwa hiyo, tunafanya hili la pili.

Pia mjue ndani ya Shirika la Nyumba kuna joint ventures 194 mikataba yake ina mashaka sana kwa hiyo na yenyewe hii tumeikabidhi tunaipitia upya ili kuona hizi joint ventures hazikuingiwa sasa zipo joint ventures muda mrefu lakini baada ya kuchunguza baadhi ya joint ventures tunafikiri tulipigwa nazo zitatusaidia kupunguza gharama za uendeshaji la shirika.

(iii) Tumeamua hivi sasa kuanzisha na kuendeleza kampuni tanzu ya National Housing ya ujenzi. Tunayo daraja la kwanza ya ujenzi kampuni yetu ambayo kwa sasa peke yake kwa kipindi cha mwaka huu mmoja tumeingia na tunajenga miradi mikubwa 35 ikiwepo ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mara, na Hospitali ya Mkoa wa Mtwara tunakwenda vizuri sana. Miradi hii 35 peke yake itatuongezea faida ambayo itawezesha kukamilisha baadhi ya miradi hii;

(iv) Tumeamua kwamba katika maamuzi ya bodi zilizopita na management waliweza kununuanunua mali nyingi ambazo kwa kweli tunafikiri haikuwa msingi tulikopa pesa lakini wakanunua baadhi ya ardhi kwa mfano Arusha kule na sehemu nyingine. Mali kama zile tunafikiri hazikuwa na sababu kununuliwa kwa fedha za mikopo kwa hiyo bodi inaangalia uwezekano. Bodi ya sasa ina wataalam waliobobea inaangalia uwezekano wa kuuza baadhi ya asset ambazo zilinunuliwa bila kufanya utafiti wa kutosha ili fedha hizi zirudi ndani ya shirika ziweze kutekeleza miradi hii, na kazi inaendelea vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini zile kazi za msingi za ujenzi wa nyumba za gharama nafuu hapa makao makuu hazitaathirika na ndio maana nimesema haina uhusiano wa kuhamia hapa kwa sababu ipo program ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu tulishajenga pale 150 na hivi sasa tunamalizia Iyumbu 68 na mwezi ujao tunaanza apartment 100 hapa Dodoma. Kwa hiyo, hii ni miradi tofauti na hii yote inatekelezwa kwa fedha za ndani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niwaambie Waheshimiwa Wabunge, kwamba shirika lisipimwe kwa sababu ya ile miradi miwili, kazi za shirika zinakwenda vizuri kuliko wakati mwingine wowote. Hivi sasa miradi mingi sana iliyoko mikoani imekamilishwa na mingi ambayo nyumba nyingi ambazo tulikuwa tunatarajia tuuze tumebadilisha utaratibu, sasa tunataka tuuze kwa gharama nafuu zaidi kwa tenant purchase yaani mwananchi akiingia akipanga kodi yake ile tutaihesabu kama sehemu ya mauzo baada ya muda itakuwa mali yake badala ya kumlazimisha mwananchi aende benki kukopa mapesa mengi alipe interest huku alipe kodi, kwa hiyo kodi yake peke yake itamwezesha kununua nyumba. Nyumba nyingi tunafanya tumefanya Kahama, tunafanya sehemu zote ambapo tunajenga hivi sasa, huo ni ubunifu mpya wa bodi mpya na Serikali ya Awamu ya Tano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilitaka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba tukishamaliza kazi hii ya restructuring ya mikopo tukikamilisha kupitia hii mikataba mipya ya ujenzi najua tutapata nafuu kubwa sana. Kwanza hata Waziri wa Fedha sijamwambia tunasubiri tupate return ya restructuring hii na upitiaji wa mikopo hii ndio tujue exactly kiasi gani tunataka kukopa kumalizia na wapi tutakopa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukachukua hela ya Serikali kwa sababu Serikali ina pesa sio lazima twende benki, lakini tunazo Taasisi hivi sasa tuna Taasisi ya TMRC ambayo inawezesha mabenki kukopesha kama push money kwa ajili ya wajenzi wa nyumba za gharama nafuu tunaweza tukakopa hata huko. Kwa hiyo vyanzo vya kukopa vingi lakini lazima tujikite katika ukopaji wenye tija na ukopaji wa gharama nafuu ambao utatuwezesha kushusha gharama ya ujenzi lakini kushusha gharama za wanunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo mmezungumzia habari ya gharama ya ujenzi lakini hamkwenda zaidi kwenye gharama za wanunuzi wa hizi nyumba, hizi nyumba ni ghali sana. Sasa kwa nini ilikuwa ghali tunafikiri ni kwa sababu yah ii mikataba ambayo wajenzi wenyewe wamekubali kukaa na sisi ili kupunguza hizi gharama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo Mwenyekiti wa Kamati na Waheshimiwa Wabunge bahati mbaya kwenye hizi Kamati za Bunge sisi mawaziri huwa hatuingii lakini haya ndio maelekezo niliyotoa. Nimetoa maelekezo kwa bodi mpya na inafanya kazi nimeridhika kwamba wameanza vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini la mwisho pia nimeagiza bodi ifanye re-structuring ya muundo wa Shirika la Nyumba. Muundo wa Shirika la Nyumba vilevile ulikuwa hauna haki sawa ndani ya watumishi, kwa hiyo, hata utendaji wa kazi ulidorora kidogo. Wako watu wachache walikuwa wanapata zaidi kuliko walio wengi. Kwa hiyo, sasa hivi wamepitia nashukuru kwamba juzi wamekaa Baraza la Wafanyakazi Nashukuru kwamba juzi wamekaa Baraza la Wafanyakazi, tunataka tujenge morale mpya ya watumishi wote wa Shirika la Nyumba ili kasi ya uendelezaji wa Shirika la Nyumba tuanze vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka kuwahakikishia kwamba Serikali ya Awamu ya Tano inasimamia vizuri kazi ya Shirika la Nyumba. Mapato ya Shirika la Nyumba hayajatetereka na sasa Bodi hii ambayo tumeiunda inasimamia vizuri. Leo tumeanza kuona uwezo wa shirika lenyewe kuendeleza hii miradi kwa fedha za ndani. Wamebana matumizi na wanaendelea kubana matumizi lakini kuangalia upya hii miradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Mbunge wa Kawe asiwe na wasiwasi. Tutamaliza ule mradi wa Morocco Square mwaka huu 2020, lakini pia tutamaliza na ule wa seven eleven. Ila tupe nafasi kidogo tuondoe ile hewa. Ni ngumu sana watu kujua, lakini mwenzenu niko ndani kidogo, nakiri kwamba nafikiri kuna hewa kidogo. Kwa sababu kama re-structuring ya mkopo mmoja umeweza kupunguza, kwanza kuondoa uwezekano wa kulipa kwa dola lakini kupunguza interest kwa 4% kutoka seventeen mpaka fourteen, huo mkopo mmoja tu, tunafikiri tunaweza. Kwa hiyo, tupeni nafasi, tuna uwezo na tutatekeleza hii miradi kwa gharama nafuu inayolipika na tutawapunguzia wanunuzi wa hizi nyumba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa heshima uliyoipa Wizara yetu ya kuwa kwenye kiti kuanzia asubuhi mpaka jioni na kusimamia Mkutano huu wa leo, nakushukuru sana. Nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa heshima kubwa waliyotupatia, nataka kuwahakikishia kwamba tutaendeleza kasi yetu ya utendaji na ushirikiano kama tulivyoanza, Mungu atusaidie.

Mheshimiwa Spika, pia namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa nguvu anayotupa maana hii nguvu yote tunapumua, tunaishi na tunafanya kazi kutokana na msimamo na nguvu anayotupa. Kama yeye angekuwa hatupi nguvu, tusingekuwa na nguvu, kwa hiyo sisi tunapata nguvu kutokana na kiongozi wetu kwa nguvu anayotupatia na msimamo alionao, sisi tunafuata humo humo, barabara anayopita na sisi kwa sababu ya nguvu yake na imani aliyonayo kwetu ndiyo maana na sisi mnatuona tunachacharika. Kwa hiyo, nawashukuruni sana Wabunge wote kwa shukrani, wengine hawakusema lakini wamepiga makofi, tunashukuru sana, Mungu awabariki. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawashukuru sana wale waliopata nafasi ya kusema leo asubuhi na mpaka jioni. Labda nianze na wachache niliowaandika hapa; Mheshimiwa Yussuf namshukuru sana kwa shukrani zake, lakini amesema machache hapa, nataka kumwambia kwamba tutayazingatia na ushauri mwingi aliosema ila nataka nimhakikishie kwamba ni kweli kama alivyosema migogoro kati ya wilaya na wilaya na vijiji na vijiji, hata maelekezo ya Mheshimiwa Rais ameagiza kwamba Viongozi wa Mikoa na Wilaya lazima washughulikie kutatua migogoro hii ya mipaka ya wilaya na wilaya na vijiji na vijiji. Sisi kama Wizara tutaendelea kusimamia jukumu hili.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Saed Kubenea nashukuru kwa ushauri wake wa National Housing, lakini juu ya kiwanja hicho cha 20,000 ambacho amesema binafsi nilimwalika, aje anikumbushe kidogo ili tuweze kuona kama tunaweza tukakishughulikia, tupo hapa hapa wiki nzima ijayo tuonane hapa. Si vizuri jambo lake binafsi nikalizungumza hapa ndani, tutaonana.

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Mabula kwa pongezi zake na suala la urasimishaji nakubali kwamba Nyamagana wanafanya vizuri sana na yeye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba watu wake wote wanamilikisha zile squatter. Sasa asilimia kubwa ya wananchi wa Wilaya ya Nyamagana hawaishi kwenye squatter, wanaishi kwenye mazingira halali na wamepata na hati za kumiliki. Sasa hilo tatizo la milimani namwahidi nitakwenda huko milimani, tutali-solve huko huko milimani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia namshukuru sana Mheshimiwa Hawa Ghasia kwa shukrani alizonipa na ushirikiano wake aliotuwezesha kupanga master plan ya kwanza. Kwa Awamu hii ya Tano tumepanga master plan kule Mtwara, lakini Mheshimiwa Hawa Ghasia alitupa ushirikiano mkubwa, tumepanga master plan nzuri ambayo imeshirikisha Mtwara Mjini na maeneo mengine ya Mtwara Vijijini.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Dkt. Kiruswa na Mheshimiwa Julius wasiwe na wasiwasi, habari ya mipaka ya Longido, Arumeru na Monduli itashughulikiwa. Bahati nzuri aliyekuwa msimamizi wa masuala ya upimaji wa mkoa nimempandisha cheo, ndiyo Mpimaji Mkuu wa Tanzania sasa na kazi anaijua, atarudi kule kwenda kuhakikisha mgogoro wa mpaka kati ya Arumeru, Monduli na Longido anahuisha pamoja na mgogoro wa kijiji cha Mheshimiwa Julius lazima ataukamilisha. Kwa hiyo, nashukuru sana asiwe na wasiwasi Daktari tutakwenda kukamilisha huu mgogoro, lakini ushauri mwingine alioutoa, tutaushughulikia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Julius namshukuru sana, naomba tu watu wa Monduli wakamilishe, tumefuta mashamba 15, watupe mapendekezo wanataka kuyatumia namna gani, lakini nashukuru sana kwa ushirikiano. Kila nilipokwenda Monduli nimemkuta Mheshimiwa Julius tumeshirikiana naye na nashukuru kwa ushirikiano wake na tutafuatilia kuhakikisha kwamba hii ardhi ya Jeshi la Wananchi inakuwa mali ya Jeshi na hatutoi fidia kutokana na ushauri wake kwa sababu ni maoni ya Halmashauri ya Wilaya ya Monduli siyo maoni ya Mheshimiwa Julius. Halmashauri yenyewe ilishaandika kwamba wangependa hili eneo liwe mali ya Jeshi kwa sababu wananchi hawakatazwi kuchunga ndani ya eneo la Jeshi. Kwa hiyo, nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Devotha Minja namshukuru kwa ushauri wake. Wakati mwingine mimi shemeji yako awe ananidokeza huko nje halafu anakuja, kwa hiyo asinichukie nikienda kule, huwa nakwenda wakati mwingine ananiambia.

Mheshimiwa Spika, Morogoro nimechukua hatua wiki iliyopita nimeamua kuwaondoa watendaji wote wa ardhi wa Mkoa wa Morogoro kwa sababu mimi ni mtu mzima, siwezi kuagiza leo, nikirudi yanafanyika yale yale. Pamoja na uhamisho ninaofanya kwa watendaji wa sekta nzima ya ardhi, lakini wa Morogoro wote lazima watoke. Hata kama sina ushahidi kwamba hawafai, nitawatafutia kazi, siwafukuzi kazi, lakini watoke kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka nianzishe Kanda Maalum ya Morogoro, ardhi ya Morogoro ina rutuba, iko katikati ya uzalishaji, nitaweka kanda maalum lakini pia na watendaji watakuja wapya ili tuipange na tuisimamie vizuri Morogoro. Kwa hiyo, nashukuru kwa ushauri wake Mheshimiwa Devotha Minja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunafanya haya tunajituma kwa sababu Mheshimiwa Rais wetu ametutuma twende kwa watu. Kwa hiyo, siwezi kukaa ofisini, lazima niende kwa watu na nitakwenda tena Morogoro nitafunua hayo mafaili machafu, ataniona tena, kwa sababu sisi lazima tutoke twende kwa watu. Kwa hiyo, isimkere sana akiniona nakwenda kwa watu, lazima niende.

Mheshimiwa Spika, bomoabomoa ya Ubungo – Kibamba Naibu Waziri ameshaelezea na Waziri wa Ujenzi alishawahi kueleza hapa na aliwahi kuja na hukumu kwamba wakati mwingine Serikali sikivu hii ya Awamu ya Tano lazima isikilize na itii amri ya mahakama, kama watu wameshindwa kesi mahakamani unafanyaje?

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rhoda namshukuru kwa ushauri wake, lakini bado narudia kwamba, pamoja na kwamba kuna matatizo kati ya maeneo ya Jeshi na wananchi huko Mpanda, lakini mara nyingi utafiti wetu umegundua, sehemu nyingi wananchi wanafuata maeneo ya Jeshi kwa sababu hiyo hiyo kwamba maeneo ya Jeshi hayana mipaka na hayana alama zinazoonekana. Mimi nimeelekeza taasisi zote za Serikali ziweke mipaka inayoonekana, wapime maeneo yao na waweke alama zinazoonekana ili kila mwananchi ajue ni ardhi ya Serikali/ taasisi inaanzia wapi kwenda wapi, lakini kutokuona alama isiwe kisingizio kwa watu kuvamia ardhi za maliasili, jeshi au mali za taasisi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Rhoda kama anajua kwamba watu wamekaa kwenye ardhi ya Jeshi, awashauri tu waondoke kwa sababu sisi tusingependa wafanye hivyo, ardhi ya jeshi kwanza inakuwa ni ardhi ya akiba kwa wote, Jeshi linatunza tu ardhi, lakini kuna installation kwa ajili ya manufaa ya Watanzania. Kwa hiyo, najua migogoro ya mwingiliano wa Jeshi na wananchi.

Mheshimiwa Spika, katika Kamati yetu na Mheshimiwa Mwinyi, Waziri wa Ulinzi amejitahidi sana kupitapita katika maeneo mbalimbali. Kule ambako Jeshi limevamia ardhi ya watu, kuna mpango wa kuwalipa fidia lakini maeneo ambayo wananchi wamevamia ardhi ya jeshi hawatalipwa fidia.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rashid nashukuru sana kwa ushauri wake, hivi viwango nilivyosema vya Sh.150,000 ni vya urasimishaji ambao wanakubaliana kwenye mitaa kila mtu anachangia ili apate hati, siyo kodi ya ardhi. Kodi ya ardhi inatozwa kulingana na thamani ya ardhi kwa kila eneo la Tanzania; kodi ya ardhi ya Dodoma haiwezi kuwa sawa na Tunduru. Kwa hiyo, Sh.150,000 ni viwango vya sasa, tulianza na Sh.300,000 kwa makampuni binafsi, sasa ni Sh.150,000 na fedha hizi zinatunzwa na Kamati za Urasimishaji za maeneo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunafanya uchunguzi kwa sababu tumegundua sehemu nyingine wanarasimisha kwa Sh.100,000 na wengine chini ya Sh.100,000. Mungu akipenda Bunge lijalo watagundua viwango hivi vimepungua zaidi, tunataka kufanya utafiti ili tupunguze gharama ya urasimishaji kwa wananchi. Hivi karibuni tutatangaza gharama za upimaji wa mashamba maana hawa warasimishwaji ni nyumba za mijini, tutatangaza gharama za upimaji wa mashamba ili watu wajue kwa sababu gharama za mashamba za upimaji zinapaswa kuwa ndogo zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, huu ni urasimishaji, lakini kodi ya ardhi kwa ushauri wake kama alivyotuahidi, tutafanya utaratibu ili Maafisa Ardhi waweke viwango hata huko kwenye notes board za Wilaya kwamba ukiwa na square meter kadhaa, kodi ya ardhi ni kiasi fulani, wataweka. Hii ni kwa sababu kuna kodi zinatofautiana, maeneo ya biashara ni tofauti, maeneo ya makazi tofauti na maeneo ya mashamba ni tofauti na ni kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbarouk nashukuru sana kwa ushauri wake. Maeneo ya Jeshi haya nimeyasikia, nilikwenda pale nilimjibu siku ile, bahati mbaya sikuwa nimemwona, lakini Mheshimiwa Ummy alinialika kwenda pale, alinialika nilishakwenda pale na haya maneno yote ya Tanga nilishayasikia, lakini nikipata fursa siku nyingine nitarudi. Maneno mengi tulizungumza siku ile nilipokwenda, nilipoalikwa na Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Tanga, tulizungumza pale na nikafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Tanga kuna matatizo mawili, hayo anayozungumza na airport. Jambo la airport linashughulikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kwa sababu ipo tabia na iko fununu kwamba yupo Mwenyekiti wa Mtaa pale aliuza yale maeneo kwa watu, kwa hiyo, hatuwezi kuingia kichwa kichwa kulipa fidia kwa watu wakati tunajua kuna mtu nyarubanja pale alijifanya ni ardhi yake akauzauza. Kwa hiyo, uchunguzi unafanywa na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwanza ya Mkoa ili wahakikishe kwamba wale waliojenga ni wananchi ndiyo, lakini walipataje. Hatuwezi kuwalipa fidia wao wakati wao kuna mtu mwingine alinufaika kwa njia haramu. Kwa hiyo Kamati ya Ulinzi na Usalama inashughulikia na mengine haya tutakuja kushughulikia pamoja na hilo eneo la Ramsim.

Mheshimiwa Spika, shamba la Ramsim lote ni la Umoja wa Vijana. Nilikwenda kwenye mkutano shida yao ilikuwa wanataka kujua gharama tu za urasimishaji na nini, lakini wananchi walikiri kwamba lile ni shamba la Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Susan Kiwanga nashukuru sana kwa kutufariji kwa kufiwa kwa hawa vijana, lakini nataka nimuhakikishie kwamba nilichokisema mimi ni kwamba, kuna tofauti kati ya mipango miji, nimetumia sheria inayonipa madaraka ya kupandisha hadhi maeneo ya vijiji kuwa ya mipango yaani yapangwe kimji, lakini sina mamlaka ya kutangaza Mamlaka za Miji. Kwa hiyo, asishangae kuona kwamba Mlimba kuna vijiji vimetangazwa vipangwe kimji na watu wapewe hatimiliki lakini mamlaka ni ya kijiji.

Mheshimiwa Spika, hata maeneo yote niliyotangaza humo 455 kwenye mikoa yetu, mamlaka bado ni za vijiji ila vijiji vyenyewe vimepata hadhi vinapangwa kimji, yaani upangaji wake ni kama upangaji wa mjini siyo vijijini na wamiliki wa maeneo hayo tunawapa hatimiliki za miaka 99 siyo hati za kimila. Kwa hiyo, mwenye mamlaka ya kutoa utawala au mamlaka ya kujitawala katika miji ni TAMISEMI lakini sisi tunatoa hadhi ya upangaji wa ardhi. Kwa hiyo, sisi tumetoa upangaji wa ardhi vijiji 455 tumevipandisha hadhi, mamlaka ni vijiji lakini ardhi inapangwa kimji.

Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ya Stiegler’s tutaoa taarifa baadaye maana haya maeneo anayosema Mheshimiwa Susan ndiyo zile Ramsar site ulizosema juzi. Hii miradi tumeshirikiana na Wizara ya TAMISEMI pamoja na Halmashauri zote, ni kweli waliwaondoa watu ambao walikuwa wamevamia kwenye maeneo oevu, maeneo ya TAMISEMI lakini mradi wangu huu unashughulika sana vilevile na kuondoa migogoro. Si kweli kwamba wakifika migogoro wanaiacha, hapana, Mheshimiwa Susan atakuwa hawatendei haki, wamejitahidi sana kusuluhisha migogoro labda huo mmoja anaoujua, lakini sehemu kubwa tumetatua migogoro ya mipaka ya vijiji, hata migogoro ya mashamba kwa sababu tusingeweza kuwapimia watu hati zao bila kutatua migogoro. Kwa hiyo, sehemu nyingi tumeweza kutoa sasa hati 200,000, tusingeweza kutoa hati za kimila za mashamba 200,000 kweli bila kuwa na migogoro ya mipaka, kwa hiyo tumejitahidi sana. Akikaa nao aendelee kuwapongeza, asiwavunje moyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Agnes namshukuru sana na kwa kweli mipaka ya hifadhi na ndiyo maana nimezungumza kwenye mambo ambayo yalikuwa yana hitilafu katika Wilaya zile za Tarime, Serengeti na Bunda, ni ule mpango wa buffer zone ambao kwenye Kamati yetu tumeuangalia na nafikiri wakati ukifika majibu yakitoka tutatoa taarifa, lakini nashukuru kwamba kweli migogoro imekwisha na leo tunapanga matumizi bora ya ardhi Bunda, Serengeti na maeneo mengine.

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Serukamba kwa pongezi zake na ushauri wake mkubwa kuhusu National Housing tutauzingatia juu ya namna ya kujenga nyumba za kupangisha na za kuuza na masuala yote ya micro financing.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rose Kamil tutafuatilia hayo mashamba, lakini ufutaji wa mashamba yasiyoendelezwa ni kazi ya Halmashauri, ndiyo inaanzaisha hiyo process. Fursa ya kwanza imetolewa na Halmashauri yenyewe kufanya ukaguzi juu ya mashamba yaliyomilikishwa katika Halmashauri kubaini kama yamekiuka utaratibu, watu hawalipi kodi na hayaendelezwi.

Mheshimiwa Spika, pale kwenye Halmashauri ya Hanang tumewapelekea mtu anaitwa Afisa Ardhi Mteule, yule ni Kamishna pale ndiye mwenye jukumu pekee la kutoa notice kwa yule mwenye shamba ili aweze kujieleza hatimaye lifutwe, asipotekeleza yeye, wasipotupa jicho lao kwanza kule, mimi siwezi kuchukua hatua. Kwa hiyo, ningependa arudi na maelekezo yangu kwa Afisa Ardhi Mteule kwamba yeye amesema Bungeni, lakini nimewatupia mpira halmashauri, amwambie Mkurugenzi wayakague, wamtume Afisa Ardhi Mteule achukue hatua, hizo hatua wakichukua ndiyo zitakuja kwangu, nampelekea Mheshimiwa Rais anayafanya hayo mambo kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo, ningependa mambo hayo kidogo tuanzie kule Wilayani, yakifika kwangu inakuwa rahisi, mashamba haya yote aliyoorodhesha waende wakafanye ukaguzi watuandikie kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Mnzava, nitapita kwenda Tanga hivi karibuni kuangalia hayo mashamba aliyoniambia. Namshukuru sana Mheshimiwa Mnzava, lazima tushirikiane. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Selasini kwa pongezi zake, tutaendelea kushirikiana. Hana matatizo sana kule kwake lakini tutakwenda kuangalia hayo matatizo. Napokea ushauri juu ya Wakala wa Nyumba ila kwa bahati mbaya mimi na Wizara yangu tumeamua kwamba tutaendelea kufanya kazi kidogo za uwakala kupitia Shirika la Nyumba kwa sababu Shirika la Nyumba nalo limeshafanya utafiti na kujua aina ya nyumba zinazoweza kujengwa vijijini na nini, lakini ile taasisi tunataka tuipeleke Chuo Kikuu itafanya vizuri zaidi kuliko ikibaki kwetu. Nakubali kwamba standard za ujenzi ndivyo zinavyokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunaposema tunatoa kibali cha ujenzi nyumba yoyote ya mjini tunakupa kibali cha ujenzi lakini tunakutajia na aina ya nyumba, tunajua kabisa. Tunapopanga miji na master plan inajulikana kabisa eneo hili unatakiwa ujenge nyumba ya ghorofa moja, eneo hili nyumba ya ghorofa mbili; eneo lililopangwa kujengwa nyumba ya ghorofa moja huwezi kujenga nyumba ya ghorofa mbili hata kama una hela, hutapata kibali.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni mahali ambapo wale watoa vibali wamelegea, ndiyo maana hawazingatii standards, lakini kwa mujibu wa ujenzi wa nyumba mijini unaenda kwa standards na ndiyo maana hapa Dodoma Mjini ukijenga sasa hivi unaambiwa na bati weka rangi fulani, hizo ni standards za wapangaji miji lazima na CDA zamani walikuwa unataka kujenga mahali, ramani hii hapa nenda kajenge. Kwa hiyo, tutaendelea kuelimishana juu ya ushauri wake kwa sababu ni muhimu sana huu ushauri katika upangaji wa miji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Pallangyo karibu sana, namkaribisha sana na nampongeza sana kwa ushindi, tutafanya kazi pamoja. Tulikwenda Arumeru pale bila shaka nimemwambia juzi, yapo mashamba ambayo tumeyafuta pale kwa niaba ya wananchi, tena moja lilikuwa la Chama cha Ushirika, walikuwa hawafanyi nalo kazi, wakataka wananchi wakalime kwenye mawe halafu huku wakodishe, tumelifuta. Hata hivyo, bado wana deni hawajaniambia utaratibu wa namna ya kulitumia. Kwa hiyo, Mheshimiwa Pallangyo tunamkaribisha sana, nampa fursa kama ana mengine pengine kwa sababu ya dakika tano nipo hapa tuzungumze ili tushirikiane mambo yaende haraka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nirudie hili la watendaji wa Serikali, ni kweli nimesema asubuhi kwamba watendaji wa Serikali ni wachache lakini pia tumegundua hawakupangwa vizuri, kwa hiyo tunarudia kuwapanga upya. Kwa uchache huo huo nataka kuahidi maeneo ambapo kulikuwa hakuna watendaji wa Serikali wa sekta ya ardhi watapatikana. Tunataka hawa watendaji watumike kama wasimamizi kwa sababu sasa kazi nyingi za sekta ya ardhi za upangaji na upimaji makampuni binafsi wanatusaidia lakini hawawezi kufanya kazi hizi ndani ya Wilaya kama hatuna mtu wa sekta ya ardhi pale wilayani. Kwa hiyo, tutawapanga vizuri na kuhakikisha kwamba wanaenea kila mahali.

Mheshimiwa Spika, masuala mengine ya RERA ambayo Msemaji wa Upinzani amezungumza Real Estate Regulatory Authority, najua kila mwaka huwa wanazungumza. Sheria hii sisi draft tumeshamaliza, tunakamilisha utaratibu wa Serikali, naamini ipo siku itaingia hapa. Sheria hii tunataka itusaidie kusimamia haki za wapangaji, haki za Serikali kwa kodi, lakini pia kusimamia sekta yenyewe ya ardhi kwa sababu tumegundua katika sekta ya ardhi inatumika sana na baadhi ya watu kwa ajili ya kutakasa fedha na kuingiza fedha haramu kwenye ardhi. Kwa hiyo, tunaifanyia kazi hii sheria na Mungu akipenda itafika hapa.

Mheshimiwa Spika, suala la ulipaji wa kodi nataka kusisitiza tena, kila mtu ambaye anadaiwa kodi, wakiangalia kwenye kile kitabu mbele ya jalada safari hii sikuweka sura yangu, nimeweka maneno fulani. Ukiangalia yale yamewakumbusha Waheshimiwa Wabunge ukitaka kujua deni lako, angalia pale, ukitaka kulipa kodi ya ardhi angalia juu ya kitabu nimefanya makusudi. Kwa hiyo, waangalie huo mfano kila mtu ajue, kama anadaiwa tafadhali asisubiri nimtangaze tarehe 30 Juni kwenye gazeti maana majina yote ya wanaodaiwa nitawaaibisha mwisho wa mwezi wa sita. Kwa hiyo, naomba waangalie hilo jedwali nimewatumia ili uangalie kama unadaiwa, mimi nisingefurahi sana Waheshimiwa Wabunge niwatangaze kwamba wanadaiwa kodi ya ardhi maana sheria zenyewe wametunga wenyewe.

Mheshimiwa Spika, nyuma ya jalada la kitabu nimeonesha aina mpya ya hati tunayotoa ya kielektroniki ya karatasi moja. Halafu ndani ya jalada la nyuma nimewaonesha leseni ya makazi ya elektroniki moja ambayo tunatoa na tunataka leseni za makazi zisambae baada ya bajeti hii, mpango huu uingie mikoa yote kwa sababu ni jambo rahisi. Watanzania vijana wataalam wa Wizara yangu wametengeneza teknolojia moja, wametengeneza app moja ambayo tutaambukiza katika Halmashauri zote halafu watu wachangie shilingi 5,000 wapate leseni. Ni kama hati lakini ya miaka mitano, itawasaidia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika kitabu hicho kuna alama ambazo nimezitumia safari hii zitawasaidia Waheshimiwa Wabunge, hasa hiyo iliyopo ukurasa wa kwanza, ninaomba kila mtu ajaribu, utumbukize plot numbers zake zile halafu itamjulisha anadaiwa kiasi gani ili mlipe na Watanzania wote nawaomba walipe kodi ya ardhi.

Mheshimiwa Spika, mwisho wa mwezi wa sita nimeagiza mabaraza yote ya ardhi, hakuna kesi nyingine isipokuwa kuwaswaga mbele ya mabaraza yale watu ambao hawajalipa kodi ya ardhi; na Serikali, mimi Waziri asiniandikie mtu hata mmoja akiomba nimpunguzie penalty, hapana, sina madaraka hayo. Ukitaka sasa upunguziwe penalty, lipa kabda ya mwezi wa sita, ukiruka mwezi wa sita penalty yako iliyopo sasa inaruka kwa asilimia 300.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naomba Watanzania wote kupitia tangazo hili angalieni mnadaiwa kiasi gani, kila mtu anayemiliki ardhi kwa hati ahakikishe kwamba analipa kodi ya ardhi ya kila mwaka. Wenye leseni ya makazi wanalipa, wenye hatimiliki wanalipa, isipokuwa wale wananchi maskini, Serikali ya Awamu ya Tano imewaonea huruma, wale wanaomiliki kwa hati za kimila, wale hawalipi kodi ya ardhi, wale wenye vishamba vya vijijini kule wenye hati za kimila Serikali imewasamehe, hawalipi kodi za ardhi. Lakini wale wanaomiliki hatimiliki, iwe ya shamba, iwe ni kiwanja mjini au shamba la mjini, lazima walipe kodi.

Mheshimiwa Spika, lakini wale wote wanaomiliki kishamba au nyumba ambayo ina kiwanja kilichopimwa mijini lazima aingie kwenye process ya urasimishaji apate hati ya muda mrefu, alipe kodi au aingie kwenye leseni za makazi alipe kodi. Hata kama una kishamba mjini, lazima upime uchukue leseni ya makazi tukutoze hela.

Mheshimiwa Spika, kuna watu wana maeneo makubwa mjini hawataki kuyapima kwa sababu wanajua mwisho wake watalipa kodi kila mwaka lakini wakivamiwa kidogo wako kwa Waziri. Tunataka mtu mwenye shamba mjini, mwenye kiwanja mjini, mwenye nyumba mjini, hana hati achukue hati kupitia urasimishaji au leseni ya makazi ambayo gharama yake ni shilingi 5,000, shilingi 4,000 zinakwenda Halmashauri kwa kazi ya kutayarisha leseni yenyewe, shilingi 300 anachukua Mwenyekiti atakayemsindikiza yule kijana anayekwenda na simu kupima zile nyumba na shilingi 700 ni yule kijana mwenye simu anayekwenda kupima. Kila nyumba yule kijana atapata shilingi 700.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo hii inatengeneza hata ajira kwa vijana wetu wa Wilayani kwenu; ni simu tu. Sisi tutamuwekea kifaa mule kwenye simu, akipita kwenye nyumba, uzoefu wetu unaonesha kijana anaweza kupima nyuma 20 kwa siku moja, Dar es Salaam wameweza, kwa hiyo nyumba 20 kwa siku moja na leseni zitatoka. Kwa hiyo nyumba 20 tunapata shilingi 5,000, shilingi 4,000 zinaingia kwenye Halmashauri, shilingi 300 anapewa Mwenyekiti wa Mtaa anayemtembeza huyu kijana anayepima, na 700 anapata yule kijana mwenyewe, kwa hiyo hii ni ajira. Mtakuta vijana wengi hata waliosomea masomo mbalimbali huko wenye simu za aina hii wanaweza kufanya hiyo kazi na kila siku akawa anaingiza mfukoni hata shilingi 10,000. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo tuchangamkie fursa hii, nataka baada ya zoezi hili kufanikiwa Mkoa wa Dar es Salaam tutahakikisha sasa tunakwenda mikoa yote ili kila mtu awe na hatimiliki au leseni ya miaka mitano. Lakini tungependa kila Mtanzania awe na hatimiliki ya ardhi yake ili aweze kulipia kodi. Kwa hiyo ni suala la msingi na la lazima.

Mheshimiwa Spika, Naibu Waziri amesema hapa, watu wote ambao tayari tumeshawapimia halafu wamepewa invoice wanakaa nayo miaka mitatu, tunawatoza kodi kuanzia mwaka huu lazima walipe. Haiwezekani tumeshakupimia tumekupa na invoice hutaki kuchukua hati eti kwa sababu utalipa kodi, kwa hiyo lazima wote tulipe kodi.

Mheshimiwa Spika, narudia tena kukushukuru wewe, nawashukuru Wajumbe wote, Wabunge wa Bunge hili, kwa heshima mliyotupa, Mungu awabariki sana mliochangia, mlioweza kuchangia kwa kusema nawashukuru sana, mliochangia kwa maandishi nawashukuru sana, Mungu awabariki sana. Sisi majibu yetu yatakuja kwa maandishi lakini wengine nitawafuata, ambao kuna hoja ambazo zinahitaji ufafanuzi zaidi, nimeshachukua majina yenu, nitawafuata tutakaa hapa tutaelewana zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini msisite kama nilivyosema, kama kuna wengine hawakupata nafasi ya kuandika na kusema, tupo na Mheshimiwa Spika ametupa chumba namba 11 hapa. Ukileta watu wako wawili kutoka Kasulu walete hapa, tutakuhudumia hapa hapa; ukileta watu wako watatu kutoka wapi, tutakuhudumia hapa hapa, mpaka Bunge liishe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ndugu zangu, kwa hiyo sisi tunafikiri kwamba tuna wajibu mkubwa wa kuwatumikia ninyi, lakini kuwatumikia na wananchi wote wa Tanzania. Hii ndiyo kazi tuliyopewa na Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Spika, naafiki.
Mapendekezo ya Mpango wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango na Bajeti ya Serikali katika Mwaka wa Fedha 2016/2017
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi ya dakika tano. Kama tulivyokuwa tunajadili hotuba ya Mheshimiwa Rais, Wabunge wengi wamerudia maneno mengi ambayo yalisemwa wakati ule. Nataka kurudia kuwaahidi kwamba katika kutayarisha Mpango huu, sekta ya ardhi ni msingi na muhimu sana katika maandalizi ya kujenga uchumi kama ilivyoandaliwa. Hivyo, nataka kuwaahidi kwamba yale yote waliyozungumza tutashirikiana na Mheshimiwa Waziri wa Fedha kuhakikisha mikakati mbalimbali ya kuboresha ardhi ili iweze kutumika vizuri katika uchumi tutaifanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na michango hii, nataka niseme moja, jana Mheshimiwa Mbunge mmoja Anatropia Theonest, kwanza nataka nimwombe radhi Mheshimiwa uncle wangu Tundu Lissu amejitahidi lakini naona niliseme kwa sababu tunamaliza. Jana alinihusisha kwa jina kwamba mwaka 2011 nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa hiyo nilihusika sana katika kupora viwanja vya Mabwepande.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mbaya zaidi hata waandishi wa habari wamerekodi kama ilivyo hata kutafakari kidogo, mimi 2011 nilikuwa kwenye kiti hiki hapa, nilikuwa Chief Whip. Sasa mdogo wangu wa Segerea, ungechanganya kidogo tu ungejua kwamba unayoyasema hata kama umeambiwa ungetumia na akili yako, ungejua, lakini sikutaka kuingia kwenye huo mjadala kwa sababu nilimwomba Chief Whip wa Upinzani ashughulikie nafikri imeshindikana, lakini nimekuandikia Mheshimiwa Mwenyekiti barua nafikiri kama ana ushahidi atakuletea ili tuendelee na safari hii kwenye Kamati ya Maadili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, nataka kusema, Mpango wa Serikali, mpango unaosimamiwa na Wizara yangu ni kuhakikisha kila kipande cha ardhi kinapimwa ili kila mwananchi aweze kumiliki. Ni kwa kumiliki ardhi kila mtu ndipo tutaongeza na mapato ya Taifa na ndiyo maana speed ya umilikishaji sasa tunaitilia umuhimu na hata sasa nimeagiza, speed ya utoaji hata tittle ambayo ilikuwa ni miezi sita sasa tumeanza kutoa hati kwa mwezi mmoja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili la migogoro, hatuwezi kuujenga uchumi kama hatuna utulivu. Wananchi wanagombana kati ya hifadhi, vijiji na watu binafsi. Kwa hiyo, nataka kuwahakikishieni taarifa zenu tumeshazipata. Hili halihitaji Mpango kuandikwa, sisi tukitoka Bunge hili tunaanza. Taarifa zenu zilizokuja na Mheshimiwa Maghembe na TAMISEMI tutaanza kushughulikia ili kuhakikisha kwamba watu tunawapa raha, waweze kusimamia shughuli zao za maendeleo ya kiuchumi kwa kupunguza migogoro iliyopo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuanzia upimaji kama nilivyosema, mwezi huu tutaanza Wilaya ya Kilombero na Ulanga kama Wilaya za mfano za upimaji wa kila eneo. Upimaji huu hautanyang’anya ardhi ya mtu, lakini tutahalalisha ardhi yake na tumpe karatasi zitakazomwezesha kutambulika Kiserikali kwamba ni mmiliki halali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kumaliza hizo wilaya, tutaona mfano huo na gharama zake ili twende kufanya nchi nzima. Kwa hiyo, nataka kuwahakikishia tu Waheshimiwa Wabunge, sekta ya ardhi tutasimamia mawazo yenu, haya yaliyopo kwenye mpango na yale ambayo ni ya utekelezaji wa muda mfupi maana yake haya ya mpango yanaweza kuwa yameandikwa machache, lakini tuliyoyasikia ni mengi, tutasimamia ili kuhakikisha kwamba Sekta ya Ardhi inakuwa kwa manufaa Watanzania wenyewe wa nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, naomba tu kwamba, wakati mwingine kumekuwa na dhoruba za kutupiana maneno, upande wa rafiki zangu hawa, wakati mwingine wanatumia maneno makali sana kwa Mawaziri, wanasahau kwamba Mawaziri hawa ni Wabunge kama ninyi. Hata hivyo, haipiti dakika moja, wana-cross kwa Mawaziri hao hao wanataka kuteta. Sasa mfikirie jamani, binadamu hawa wote tunafanana, haiwezekani huyo Waziri umwite tapeli, mjinga halafu una-cross hapa akusikilize kama vile hukusema kitu. (Makofi)
Ningependa tujenge hoja kama Mbatia, kama Zitto Kabwe, hoja nzito lakini hazina kashfa wala matusi kwa mtu mmoja mmoja, kwa sababu Mawaziri hawa siyo vyuma, ni binadamu. Kwa hiyo, naomba tu, wote hapa ni marafiki na Serikali haitawabagua, itawatumikia wote, lakini tukiwa…
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. WILLIAM V. LUKUVI: Kwa kuwa Jimbo la Isimani lina shule zaidi ya 50 za msingi na 13 za Sekondari na lipo vijijini, vijana wengi wanaomaliza sekondari hawana chuo chochote cha mafunzo ya ufundi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Isimani ndilo lenye eneo lote la Ruaha National Park na wazalishaji wakubwa wa mazao ya kilimo hususan mpunga. Pia wana nia ya ujenzi wa nyumba bora, hivyo kuwapo kwa Chuo cha Ufundi chini ya VETA itasaidia vijana wa Iringa vijijini hususan Jimbo la Isimani kujifunza masomo ya ufundi mbalimbali na masomo ya utalii na hoteli. Kwa hiyo, naomba sana Wizara ikubali kujenga Chuo cha Ufundi – VETA Jimboni Isimani wilaya ya Iringa Vijijini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kushukuru kupata nafasi ya pili ya leo angalau nihitimishe hii hoja. Kwanza nianze kwa kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia kwa kusema ambao katika orodha yangu hii wapo 25 akiwepo Naibu Waziri wa Ardhi. Majina yenu nayajua kuanzia msemaji wa kwanza Mheshimiwa Silaa mpaka msemaji wa Mwisho Mheshimiwa Malembeka.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia nawashukuru wachangiaji wengine ambao wamechangia kwa maandishi ambao wapo tisa. Maandishi yenu tunayo, tunatafakari na tumezijua hoja zenu na tutazijibu vile vile kwa maandishi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii baada ya maelezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri, namshukuru sana. Nitumie muda mfupi kwanza kutoa maelezo juu ya sheria. Wengi mmezungumzia juu ya masuala ya upangaji wa miji. Kwanza kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya Mwaka 2007 inatamka wazi kwamba Mamlaka za Upangaji wa Ardhi ni Halmashauri za Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge tujue kwamba sisi kama Wabunge na wenzetu Madiwani kwenye Halmashauri ndiyo Mamlaka halali ya kisheria ya kupanga ardhi ndani ya Wilaya yetu. Waziri wa Ardhi hatakuja kukupangia ardhi ya Tarime hata mahali pamoja. Sisi tunafanya tu udhibiti wa ile michoro, kuhakikisha kwamba mkishapanga, tukishakubaliana hambadilishibadilishi kila mara, lakini Mamlaka ya Upangaji ni Halmashauri. Kwa hiyo, wewe ndio mwenye kitambaa unapeleka kwa fundi ushonewe suti kwa mshono unaoutaka, haiwezi kuwa Wizara. Kwa hiyo, nataka hilo tuelewane kuhusu Mamlaka ya Upangaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ujenzi holela, mdhibiti ni Halmashauri. Baada ya kutunga sheria hii, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Kamati ya TAMISEMI bila shaka mnajua ipo kanuni za Udhibiti na Uendeshaji Miji Sura 244, ni kanuni za TAMISEMI. TAMISEMI ndiyo anayepaswa kudhibiti. Mamlaka za Upangaji ndizo zinazopaswa kudhibiti masuala yote ya ujenzi na uendelezaji wa miji. Kwa sababu ukishapanga, kama hili ni eneo la makaburi, mtu akijenga si wewe uliyepanga ndiyo lazima umwondoe.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, suala la udhibiti na suala la upangaji ni mamlaka. Yaani Jiji, Manispaa, Miji na Halmashauri, hii ni ardhi yenu. Yaani ukipewa kipande kile cha utawala, ni ardhi yenu; na vijijini kupanga matumizi bora ya ardhi ya vijiji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa namwona kule Mheshimiwa Aleksia, amezungumzia habari ya ardhi za vijiji, pengine akapendekeza lichimbwe shimo, yaani mpaka; wakulima wawe huku na wafugaji wawe huku. Bahati mbaya kuna rafiki yangu mmoja ameondoka hapa, aliwahi kujaribu pale Mvomero, tukachimba tuta wakulima wawe huku na wafugaji kule, ilishindikana. Hivi binadamu unamwekeaje mpaka, kwamba umwekee shimo hapa asiende upande huu, asiende huko, ilishindikana kabisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawaambia ndugu zangu, dawa ni kupanga matumizi bora ya ardhi ya vijiji. Kwa mujibu wa Sheria Na. 5 ya Mwaka 1999 ya Vijiji, ardhi na yenyewe kijiji ndiyo mali yao chini ya usimamizi wa Halmashauri. Wao katika mkutano wao wakiamua kwamba eneo hili ni la kufuga, eneo hili ni la makazi, eneo hili ni la kilimo, ile ni sheria tayari. Wakishaileta kwangu maana yake hawaruhusiwi kubadilisha mpaka waombe kibali kwangu. Kwa hiyo, wanaopanga matumizi bora ya ardhi ni vijiji husika, lakini chini ya usimamizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningefurahi bajeti ijayo mwulize vijiji vimepanga bajeti kiasi gani ya kupanga matumizi bora ya ardhi? Kwa sababu ardhi ni mali yao. Halmashauri nazo lazima zijue ardhi ile waliyokasimiwa na wale viongozi waliochaguliwa kwa ardhi ile na viongozi wa kuteuliwa walioteuliwa kusimamia ardhi, wajue kwamba Mamlaka ya Sheria ya Mipango Miji imewapa kupanga ardhi yao.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengi wamejua hilo, wamepanga ardhi yao na imewanufaisha. Wananchi wamejenga kwenye viwanja vilivyopangwa na kupimwa na Halmashauri zimepata mapato kwa sababu wametekeleza vizuri sheria hiyo. Nilitaka nianzie hapo ili tujue.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, sisi kama wasimamizi wa sera tumeona haiwezekani kuacha Mamlaka za Upangaji peke yake ndiyo maana tunashirikiana kupanga mipango mikubwa. Bajeti ile iliyopita tulikuwa tumetengewa fedha za World Bank nyingi, zaidi ya shilingi bilioni 60, sasa bahati mbaya mazungumzo hayajamalizika, mnajua tena mambo ya Corona watu wanafanyia majumbani, lakini lengo letu ilikuwa ni kushirikiana na Halmashauri ili kukamilisha zoezi la Upangaji na Upimaji nchi nzima; kwa vijijini kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi na kwa mijini kwa kutumia Sheria Na. 4 kupanga miji yetu kwa kushirikisha watalaam wetu. Hayo makampuni binafsi, tulitaka yashiriki kikamilifu kwa sababu tunajua kweli hayana hela, lakini tungeyashirikisha na kupeana maeneo ya kusimamia upangaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka huu tunashukuru, mmeona kwenye vitabu vya fedha, tuna fedha nyingine ambazo Serikali imetupatia kutoka Korea, bado tunaendelea. Hizi fedha zinapita kwetu tu, lakini washiriki wakubwa wa upangaji ni Mamlaka za Upangaji ambazo ni Halmashauri. Kwa hiyo, bado zikitokea hizi fedha tutashirikiana. Moja ya gharama kubwa ambayo inawapata Halmashauri katika upangaji ni ununuzi wa vifaa. Tunataka fedha hizi zitusaidie kidogo kununua vifaa, vipatikane vifaa vya kisasa vya kupima ili wasiwe wanakodisha.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja ya gharama kubwa ya upimaji, huwezi kupanga mezani, kuchora kwamba hapa nitaweka makaburi, nitajenga nyumba, lazima upige picha juu ya ardhi, picha ya anga ili ikupe sura hapo chini unapotaka kupanga pakoje? Hiyo ni gharama kubwa sana. Wengine wanatumia hizi za kwenye mtandao, copy, copy hizi, lakini hazitoi taswira nzuri. Kwa hiyo, tunanunua vifaa mtaona; tunanunua drone na ndege kwa ajili ya kurahisisha kazi ya wapangaji Halmashauri ili tuwasaidie kuwapa picha za anga zirahisishe ununuzi na upigaji wa picha zile ambao ni gharama sana ili kupata picha zenye sura halisi ili wapangaji waweze kupanga jambo hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunashirikiana na Mamlaka za Upangaji ili kurahisisha kazi hizi. Ndiyo maana katika fedha za Maendeleo tulizozipata sisi Wizara tuliona siyo vizuri kufanya ziara tu, tukafikiri tuwarudishie Halmashauri wajitahidi kupanga maeneo yao. Watatafuta maeneo mazuri ya kupanga, lakini tuwape fedha shilingi 10/=, warudishe shilingi 10/=. Ndiyo maana wengine kama Jiji la Mbeya na wengine wamechukua zaidi ya bilioni, wamepima viwanja wamerudisha bilioni, wamepata zaidi ya bilioni nao wanaendelea vilevile. Wengine wamefanya bila pesa ya Serikali, lakini wameendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tumeona hili jambo ni jema. Badala ya kuzipeleka fedha kwa miradi ambayo itasimamiwa na Wizara, sisi wataalam wa Wizara tupeleke Wilayani kule kwenye ardhi ili Mamlaka za Upangaji zifanye. Nataka kuahidi, fedha zozote nitakazopewa na Mheshimiwa Mwigulu mwaka huu, zote zitakuja Wilayani, hazitabaki Wizarani. Hazitabaki kwa sababu sisi ni Wizara ndiyo, lakini hatuwezi kwenda kufanya kazi Halmashauri wakati Halmashauri ina wataalam wenye weledi na waliosoma kama sisi na wale wanasimamiwa na mamlaka ya upangaji. Mamlaka ya Upangaji, Halmashauri ndiyo wanaojua, wanaotaka kujua na wanaotakiwa kuwaambiwa hawa wanataka kupimiwa viwanja vya namna gani; na mji wao uwe namna gani? kwa hiyo tutaendelea kushirikiana ndugu zangu Wabunge. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nachotaka tu niwaambie kwamba safari hii Kamati hizi mbili za TAMISEMI na Ardhi tumekubaliana tuunde timu ya pamoja ambayo itaweka masharti na mwongozo ili ijulikane nani mwenye sifa ya kupata na asipopata afanywe nini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kila Halmashauri ina uwezo wa kuomba. Kwa hiyo, kama Mbunge hapa unatamani Halmashauri yako ingependa kuingia katika program hii, mwambie Mkurugenzi aombe tu. Zikifika hizi fedha, ninyi mnajua kona hii nikipanga leo viwanja vitanunulika kesho. Msianze kupanga maeneo ya makaburi, hutapata hela. Anza kwanza kupanga maeneo mazuri ili upate hela ya kurudisha, halafu baadaye ndiyo utakuja kupanga maeneo ya makaburi. Sasa wengine wameanza kupanga maeneo ya makaburi; nani atanunua makaburi? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni jukumu la Halmashauri kujua fedha za mwanzo upeleke wapi ili upate mtaji, baadaye ujitegemee? Kwa hiyo, mipango hiyo mtafanya wenyewe. Kwa hiyo, waambieni Wakurugenzi waombe kwa Katibu Mkuu, vigezo vitawekwa wazi na Wizara yangu wataalam wangu, wa Katibu Mkuu wa TAMISEMI na Katibu Mkuu wangu, wataunda timu, wataweka vigezo na ikiwezekana baadaye hata Kamati ya TAMISEMI mkienda kukagua miradi, mtakagua pamoja na miradi hii inayotekelezwa katika hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nawaombeni ndugu zangu tukumbushane tu huko kwenye Halmashauri, tujitahidi angalau Halmashauri kwa mwaka iweke bajeti hata ya kupanga matumizi bora ya ardhi ya vijiji viwili, vitatu, kumi; Inshallah Mwenyezi Mungu akitupa hizi fedha tulizobajeti mtakuta kama tulivyofanya katika wilaya tatu za Mkoa wa Morogoro, tulipata fedha kidogo tukaenda kufanyafanya vijiji vingi zaidi. Vinginevyo kwa kweli, kazi ya msingi hii ya kupanga matumizi bora na kusimamia kwenye Halmashauri ni kazi ya Mamlaka ya Upangaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi karibuni tulikuwa tumependekeza kwamba zamani tulikuwa na ikama ya mtu anaitwa Land Ranger kwenye mitaa huko; kama kiherehere hivi, akiona mtu amechimba msingi, basi ameshatoa ripoti, watu wamebomoa. Sasa hivi hawa watu hawapo. Dodoma walikuwa wengi sana. Tunafikiria namna ya kutumia Watendaji wa Mitaa, kwa sababu Watendaji wa Mitaa wapo pale, yule anaweza akamwona kila mtu anayevunja kanuni za Mipango Miji na akatoa taarifa. Kwa hiyo, tunafikiria namna ya kuwatumia hawa ili angalau wasimamie mambo haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, urasimishaji limezungumzwa sana. Jambo hili ni jema, nimelipigia debe kwa nguvu tangu nimeingia. Haya makampuni nimeruhusu mimi yakasajiliwa na tumeyasimia. Ni kweli mwanzo walikuwa wanapanga bei vibaya, tukarudi na hivi, tumeenda mbele nyuma, lakini kidogo wengine wanafanya kazi nzuri, lakini kweli ni masikini, hawana fedha. Pia namna ya uendeshaji wake ulikuwa wa ovyo, ovyo siku za mwanzo. Ilikuwa wanakwenda kuomba kazi kwa Mwenyekiti wa Mtaa, wanapatana, kumi, ishirini, wanachukua fedha kwa masikini halafu hawafanyi kazi. Tumedhibiti.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaambie, mpaka sasa makampuni yaliyochukua fedha za wananchi na hawajafanya kazi inafikia shilingi bilioni 45. Mmoja amesema hapa, makampuni yanadai wananchi shilingi bilioni 70, lakini kwa sababu michoro wanayo, wananchi watalipia tu; lakini makampuni yamechukua amana hizi laki moja na nusu, laki moja na nusu, karibu shilingi bilioni 45 na hawajapima hivyo viwanja. Ndiyo hao wa Kimamba tunaopambana nao. Nataka kuwahakikishia watazirudisha hizi fedha na kazi watafanya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sina nia kuwafukuza, najua wamegawa gawa barua humu; wameandika barua, wametia kwenye box za watu wanaofikiri watawasaidia, bahati nzuri wengi wao wamenirushia zile barua ninazo. Ila wengine wamezitumia kusema humu, lakini wengine wamenirudishia, haiwasaidii sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, watendaji wangu walitoa taarifa fulani, nataka wajue zile kampuni za kupima wangekuja kwangu kuniambia badala ya kuandika barua. Sasa Mtendaji wangu kasema atawafuta badala ya kuja kwa Waziri ku-appeal, ninyi mnaandika barua mitaani, itawasaidia nini? Mimi ndio niliyetoa fursa hii ya makampuni kufanya urasimishaji. Mimi ndio niliyepanga hata bei na ndio niliyewasha moto mpaka wakasambaa kufanya kazi zote pamoja na Dodoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndugu zangu wenye makampuni binafsi, njooni tuzungumze, nitawaita tena, nitakuja kila mkoa nizungumze na makampuni yanayoshiriki na kazi ya urasimishaji kila mkoa tuzungumze kulikoni? Ni kweli hatuwezi kufanya kazi hii ya urasimishaji Serikali peke yetu, hatutaweza, lazima tushirikiane na hawa jamaa, hatuwezi. Hiyo lazima niwaambie ukweli, hatuwezi. Hata tungepata ikama ya kuweka mpima mmoja mmoja kila wilaya hatutaweza. Kazi ni tushirikiane sasa na ninyi mmeshapata ufahamu, tushirikiane katika udhibiti; win, win situation.

Mheshimiwa Naibu Spika, watendaji wangu wasiombe rushwa kwa hawa jamaa, wapitishe michoro bila bahasha, lakini na hawa wafanye kazi kwa uadilifu. Hata mabenki wajue hapa kuna fedha, wangeweza kuwakopesha hawa, wakabaki na michoro halafu watu wakawa wanalipa benki kuchukua hati zao. Hili tunaendelea nalo, najua litakwisha, tutaenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niwaambie urasimishaji utaendelea, tutashirikiana. Nitakuja Mkoa wa Dar es Salaam, nitapiga kambi pale mwezi mmoja tufanye kazi yote iishe. Tupite maeneo yote yenye kero tumalize hili jambo, tuzungumze tuone namna ya kuwasaidia hawa. Ni lazima wananchi wapate haki yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika na ndugu zangu wote, najua wengi katika hotuba zenu mmenipa mialiko. Mheshimiwa Jerry Silaa nakuja kumalizia kazi yangu kule;

Mheshimiwa Massay ingawa umeomba mambo mengi, lakini nilikuwa na mpango wa kuja Mbulu, nitakuja; Mheshimiwa Halima Mdee lile jambo la Chasimba, Chatembo na Chachui, wewe unalijua sana, ila leo umepiga chenga, hukusema mpaka mwisho. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie Waheshimiwa Wabunge, hili analolizungumza siwezi kulisema sana, ni la kimahakama. Wale watu wa Chasimba, Chatembo na Chachui ipo hukumu ya Mahakama ya Rufaa kabisa iliyowataka zile kaya 4,000 lazima waondoke. Sasa mimi kuwa Waziri wa Makazi nikaona watu 4,000 waondoke kweli nyumba zibomelewe! Ndiyo nikawa-engage wale wazungu wa kiwanda, ee bwana, kwani wewe unataka nini? Akasema bwana mimi nina madini hapa, lakini nina-surface right. Kama watu wako wataweza kunirudishia kidogo, mimi nitawaacha wakae hapo hapo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tukaenda kutangaza na aliyekuwa Mbunge pale, watu hawatoki. Tuelewane sasa kiasi gani nikurudishie ili anunue ile raw material mahali pengine kiwanda kiendelee. Sasa ile naona Mheshimiwa Halima hakuisema. Hawawezi. Nataka kuwaambia hivi, hawataweza kubaki pale kwa sababu kuna hukumu ya Mahakama ya Rufaa na hakuna mtu ambaye yupo juu ya Mahakama. Ni lazima tuelewane; na ndiyo maana thamani ya ardhi pale ni square meter moja ni shilingi 20,000 wakati ule; hawa kiwanda wamesema wawape shilingi 6,400/= wawapimie wawabakize pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ingawa sehemu nyingine ya pili kuna wengine wenye mashamba, wanachaji mpaka shilingi 100,000/= per square meter. Hawa Wazungu wana hati. Siwezi kuwapa hati hawa wananchi wa Chasimba ya mtu mmoja, mmoja juu ya hati ya kiwanda. Maana yule Mzungu lazima nimlipe hii fidia ndipo arudishe ile hati. Fursa ya kubaki, watabaki, hawaondoki, wale Wazungu wameshakubali, lakini wawalipe kidogo fidia ya ardhi. Hivi nani huyo Dar es Salaam anaweza kupata kiwanja bure kulipa chochote? Nani? Sasa mvamizi ndio apate privilege ya kubaki na kiwanja bure! Ilitokea wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Halima ulisahau element ya fidia. Sasa hapa tusifungue mjadala, mara nyingi wewe tunakutana Dar es Salaam. Mimi nitakukumbusha yale makaratasi ya Kamati ile ya mwanzo ambayo tulikuwa tunazungumza tulikwama wapi na ndiyo maana mgogoro huu umenichukua miaka sita. Nitakukumbusha Dar es Salaam. Tusiwape faida, maana Mahakama wasije wakafiri Bunge huwa linatafsiri hukumu zao, maana hii ni hukumu; nawe ni mwanasheria, wakili. Kwa hiyo, tuzungumze Dar es Salaam, nitakupa ushirikiano, nitakupa makaratasi ili usome vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niwaahidi kwamba Mheshimiwa Mtemvu, Mheshimiwa Gambo nitafika Arusha na Arumeru zote mbili, nitakuja. Pia Mheshimiwa Mbunge wa Mtama, timu ile uliyoomba ya kuja kuangalia ule mpaka itakuja ili tuone namna gani, halafu baadaye tutashirikiana na Waziri wa TAMISEMI namna ya kumshauri Mheshimiwa Rais ikibidi, tukiona kama kuna sababu juu ya mipaka hiyo. Lakini kule…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, kengele ya pili imegonga.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuwaahidi tu Wabunge wote mliozungumza hapa, mliohitaji migogoro yenu kutatuliwa kwenye site, mimi mmenipa mwaliko, nitafika; na ratiba hii naanza wiki ijayo. Kote huko nitakuja. Nitaenda Mtama, nitaenda Mbogwe, nitaenda Hanang, Arumeru zote, Nyamagana narudi tena na Kaliua nitakwenda. Kaliua kulikuwa na ratiba ambayo tulishaombwa na Mheshimiwa Mama Sitta na Waziri wa Utalii, tutakuja huko. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, omba fedha, kwa sababu hata mimi nitataja hapo kwamba uje na Mbeya. Orodha ni ndefu, wewe omba hela tukupe halafu uje tuonane huko.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuruni sana kwa kunisikiliza. Naomba mnipe pesa na yote haya mliyoyasema watu wote yatatimizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naafiki.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nami nashukuru kwa muda huu niliopewa kuchangia hoja hii kuu ya Wizara ya Fedha. Kabla sijasema yangu machache nami niseme nampongeza sana Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita, Mheshimiwa Mama Samia Suluhu kwa kazi nyingi, kwa muda mfupi usiozidi siku 100 ambao tumeshuhudia. Tumeshuhudia maelekezo, tumeshuhudia kazi, tumeshuhudia na mfumo mpya wa utendaji wa kazi na tumeshuhudia na kasi mpya ya utendaji wa kazi. Kwa hiyo, nami nampongeza sana, angalau katika siku hizi ambazo hazizidi 100 ambazo amekaa madarakani wananchi tumepata matumaini makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepata matumaini na mengi Waheshimiwa Wabunge mnayaona hata humu kupitia Bungeni. Yapo mambo mapya ambayo tulikuwa hatujashuhudia, mnayaona. Haya makofi mengi ya Mheshimiwa Waziri Ummy ni matumaini mapya ambayo yamekuja na utaratibu mpya. Bajeti ni ile ile, pesa ni zile zile, lakini huu ni ubunifu mpya wa namna ya kusimamia na matumizi mazuri. Kwa hiyo, haya ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Sita katika siku zisizozidi 100. Sasa fikiria tukifika mpaka 2025, Mheshimiwa Ummy atasema maneno mangapi huyu? Tunajua yako mengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunampongeza. Kwetu sisi tulioko wote, maana ni Wabunge wote tuna matumaini makubwa kutokana na mageuzi makubwa anayoyafanya. Nami nimepewa shilingi milioni 500 zile barabara, nimeelekeza zitumike kwenye barabara zangu. Haya ni mapinduzi makubwa kwamba sasa na Wabunge tunashiriki katika kupanga miradi ya maendeleo. Yaani tunashiriki kupeleka pesa na kusimamia pesa tuliyopeleka wenyewe kwa maelekezo ya barabara na miradi tunayoitaka. Tumeulizwa hapa habari ya shule tunazotaka zipelekewe pesa, Wabunge wote tumechagua shule. Ni mapinduzi makubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, napenda sana kupongeza haya, yatatupa ule usimamizi wa karibu ambao tulikuwa tumepewa kwenye Katiba, sasa tunapewa kiuhalisia kwamba kuna upangaji wa bajeti unaokwenda kwenye milango ya Serikali na mwingine upande wa jimbo tunakwenda kusimamia. Kwa hiyo, napongeza sana juhudi hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi Wizara ya Ardhi ni Sekta wezeshi. Katika miradi yote inayopangwa humu ndani, yote inatekelezwa kwenye ardhi. Kazi kubwa na maelekezo makubwa tuliyopewa na Mheshimiwa Rais ni kupunguza urasimu katika upatikanaji wa ardhi katika kutekeleza yote yanayopangwa hapa hasa ya uwekezaji. Tumeshuhudia katika kipindi hiki cha siku zisizopungua 100 Mheshimiwa Rais kwa kutumia madaraka ya kisheria aliyopewa ameweza kufuta mashamba yasiyopungua 11 yenye ekari ya zaidi ya 24,119. Mashamba haya yamefutwa kwa sababu yalikuwa hayaendelezwi vizuri. Haya mashamba yako kila mahali, hata Waheshimiwa Wabunge mlipokuwa mnachangia sehemu nyingine, mnayaita mashamba pori. Kwa hiyo, ni fursa Waheshimiwa Wabunge, kama kuna mashamba kama haya watu wanamiliki sehemu mbalimbali lakini mnayaona kwa macho hayaendelezwi, tuambizane kutoka huko huko ili tuchukue hatua za kisheria tuyafute ili waweze kupewa watu wengine wenye uwezo wa kuyaendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mashamba haya ameelekeza sehemu wagawiwe wananchi ambao hawana ardhi ya kutosha na sehemu tumehifadhi kwa ajili ya uwekezaji. Pia tulikuwa na mashamba yenye ekari 45,788 ambayo yalifutwa siku nyingi lakini maelekezo ya namna ya kutumia yalikuwa yatoke kwa Mheshimiwa Rais na yalikuwa hayajatolewa. Mama ametoa maamuzi kwamba mashamba haya angalau ekari 33,672 kati ya ekari 45,000 wagawiwe wananchi wayatumie na sehemu iliyobaki ya ekari 15,000 ziwekwe kwa ajili ya uwekezaji kupitia taasisi ambazo zinasimamia uwekezaji za EPZA na TIC, kulima mashamba ya katani, kujenga viwanda na vitu vingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tumeshuhudia katika kipindi hiki cha siku zisizozidi 100 uwekezaji maombi ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji yamekuwa makubwa sana. mpaka tarehe 01 mwezi wa sita ofisi yangu imeshapokea maombi 305 ya watu wawekezaji mbalimbali wanaokuja kutaka ardhi kwa ajili ya uwekezaji mbalimbali. Na kati ya hayo, kama nilivyosema juzi, sasa tumeanza kukaa Kamati ya Kitaifa ya Ugawaji wa Ardhi inakutana kila wiki kwa hiyo, katika maombi 305, mia tatu na tatu yameshapewa majibu na wawekezaji wameshapewa ardhi ya uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, uwekezaji huu tunakwenda kushuhudia Morogoro kuna uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha sukari. Kigoma kuna watu wameomba kwa ajili ya viwanda vya sukari, lakini Kilwa kule kuna kampuni kubwa zinakuja kulima mihogo, lakini yanaweka viwanda vya kuchakata mihogo kwa soko la China kwa ajili ya kununua vilevile mihogo inayolimwa katika Mikoa ya Kusini, lakini hapa Kibaha tumeshuhudia kampuni zimeanza kuomba sasa maeneo ya industrial park. Iko kampuni moja ambayo imepewa ekari 1,000 na imeahidi itawekeza viwanda 73 katika hiyo industrial park. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, hayani mambo yanayotokea ndani ya siku zisizozidi 100 kwa hiyo, uwekezaji nao unaenda kwa kasi. Na sisi kama sekta wezeshi tunaahidi mbele yenu Bungeni hapa, tunamuahidi Mheshimiwa Rais kwamba, tutatimiza wajibu wetu, tutaondoa urasimu na kuhakikisha uwekezaji unakuwa wa tija katika nchi hii, hasa katika matumizi ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, na ardhi hii imetengwa mikoa yote. Nawashukuru sana Waheshimiwa Wakuu wa Miko ana Wakuu wa Wilaya wametenga ardhi za kutosha na halmashauri, kama mamlaka za upangaji ziko huko. Kwa hiyo, nataka kuwahakikishia wawekezaji wote Tanzania ni salama kwa uwekezaji na ardhi ya kuwekeza ipo. Mtu yeyote ambaye anafikiri nataka kuwekeza, kujenga majengo, kujenga viwanda, ardhi ipo; kokote kule kama wakikusumbua tuonane huko wizarani sisi tunajua ardhi ilipo mahali popote katika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini la mwisho, ndani ya Bunge hili tumeshuhudia Waheshimiwa Wabunge mkisema gharama za umilikishaji ni kubwa na wengi mlikuwa mnaitaja tozo ya premium. Kama walivyosema Wabunge wengine, inaelekea Mheshimiwa Rais huwa anasikiliza kule, leo tumemsikia Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametangaza hapa kwamba toso ya asilimia mbili na nusu kwa kila anayemiliki ardhi kwa mara ya kwanza ya thamani ya ardhi sasa imepunguzwa na inakuwa 0.5. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, maana yake nini? Hawa wote wawekezaji ambao tumewapa ardhi zaidi ya 303 wangepaswa kulipa asilimia 2.5 ya thamani ya ardhi na hii si kodi ni tozo. Na wote hawa kila anayemiliki kiwanja, hata urasimishaji wakipata invoice wanamfuata Waziri awapunguzie, nilikuwa nawapunguzia, lakini je, mtu wa Kigoma atamuona Waziri? Je, mtu wa Kilosa kule atakuja kwa waziri?

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo Mheshimiwa Rais ameleta tiba kwamba, wote wanaomiliki ardhi kwa mara ya kwanza wamilikishwe kwa tozo ya 0.5 yaani nusu ya asilimia moja. Kwa hiyo, hii itaongeza ari ya uwekezaji, lakini na wananchi masikini ambao wanataka kumiliki ardhi zao kwa kupata hati, hasa katika zoezi la urasimishaji. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais, lakini nampongeza sana rafiki yangu Mheshimiwa Dkt. Mwigulu kwa hotuba yake nzuri sana ambayo ameisoma hapa ambayo imewezesha tozo hii kupunguzwa kutoka asilimia 2.5. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa jinsi nilivyosikia mazungumzo ya Waheshimiwa Wabunge wengi naona tozo hii mmeikubali kwamba, ipungue. Na pengine tunavyoendelea inaweza ikafutwa kabisa kwa sababu, hii sio kodi ni tozo. Kodi za msingi za umilikaji zipo na mtu akimiliki ardhi kwa mara ya kwanza maana yake anakuwa mlipa kodi wa kila mwaka kwa miaka 99. Kwa hiyo, ni vizuri mtu amiliki kwa gharama ndogo kwa sababu bado anatupa japo kidogo kidogo, lakini kwa miaka 99. Hawa ni walipa kodi wa kudumu wa uhakika, yaani akinunua shati maana yake atalilipia kodi kwa miaka 99, akipewa hati miliki maana yake huyo anaingia kwenye daftari la ulipa kodi la Serikali kwa miaka 99. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, huu ni mwanzo mzuri. Nafikiri tukiona inaenda vizuri mwaka huu tunaamini hata mapato yatokanayo na kodi ya ardhi yataongezeka kwa sababu, leo tuna viwanja laki tisa ambavyo tumevipima, lakini watu hawajachukua hati kutokana na tozo hiyo. Kwa michoro ya survey ambayo inaonesha viwanja mbalimbali vilivyopimwa nchi hii kwa urasimishaji na viwanja na mashamba tunayo michoro ya viwanja elfu tisa ambavyo vimepimwa, lakini hatujatoa hati. Watu wanasita kuchukua hati kwa sababu tozo hii ilikuwa kubwa kuliko kodi ya asili ambayo imetungwa na Sheria ya Bunge. Kwa hiyo, tunahisi baada ya kuondoshwa hii premium then tunaamini kwamba, wananchi watamiliki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wananchi Waheshimiwa Wabunge wamewasemea na Mheshimiwa Rais amesikia ameondoa hii kodi. Kwa hiyo, hakuna kizuizi chochote sasa kisingizio cha kuweza kumilikishwa kwa sababu, gharama kubwa ya umilikishaji imeondoka.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaelekea na sisi kama Wizara, kama ambavyo wameanza kodi ya majengo kwenda ki-electronic, na sisi tumejipanga kuja ki-electronic vilevile. Tunaangalia uwezekano pengine mwakani tutakuja na bajeti tofauti, tunaangalia namna nzuri zaidi ya ukusanyaji wa kodi ya ardhi pengine kwa kuunganisha na majengo, lakini tutajipanga vizuri. Na sisi tunaunga mkono hili la ukusanyaji tujaribu ukusanyaji huu wa kutumia bili za umeme, lakini na sisi kwenye kodi ya ardhi kwa sababu, majengo yako kwenye ardhi na taariza zote tunazo kwa hiyo, na sisi tunajipanga ki-electronic.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa tumefunga mfumo mpya ambao umetengenezwa na vijana wa kitanzania. Mwezi ujao tutaanza kutoa Hati za Electronic hapa Dodoma. Mfumo huo utatuwezesha sisi kutokutumia mabavu sana kufuatilia kodi ya kila mwaka kwa sababu, ndani ya mfumo ule tuna namba za simu, tuna taarifa za kila mmiliki wa ardhi. Ikifika siku ya kulipa kodi message itakujia kwenye sim una kukuomba ulipe kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, huu ni mfumo ambao umetengenezwa na wataalamu wa Wizara na utaanza kutumika. Wale wote ambao watachukua hapa Dodoma hati kuanzia tarehe 01 mwezi wa saba wataanza kupata hati za electronic. Na pengine tutaachana na hii tabia ya kufukuzana kwa sababu, kila mwananchi atakumbushwa siku ya kulipa kodi. Tunataka tufanye jambo hili nchi nzima, ili tupunguze kasi ya kukamatana na kufukuzana kwa ajili ya ukusanyaji wa kodi, turahisishe, lakini tupate mapato ya kutosha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nakushukuru sana kwa muda ulionipa, lakini nataka nirudie kuunga mkono kwa nguvu zangu zote hotuba hii ya Wizara ya Fedha kama walivyofanya wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Rais, lakini kuwapongeza sana wenzetu Mawaziri wa Wizara ya Fedha na watendaji wote wa Wizara ya Fedha. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini wa Mwaka 2016
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo na majibu yote ya Mheshimiwa Naibu Waziri, kwanza nampongeza sana kwa kusimamia kwa muda mrefu sana Muswada huu na kutoa majibu ya uhakika. Nadhani hata wenzangu waliotoa hoja wataridhika kwamba amesema kitu anachokifahamu na nampongeza sana kwa hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, muhimu ni kwamba kama tulivyosema Wabunge wengi jambo hili halikuwepo, kila jambo lina mwanzo. Kwa hiyo, naomba niwapongeze sana Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia lakini nawapongeza sana mlioleta amendments, leo nafikiri tutafika saa nane maana ziko amendments 20 hapa lakini bahati nzuri wengi wameandika mambo yanayofananafanana muhimu ni kwamba sheria ipo na mtakubali tuanzie mahali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Mheshimiwa Naibu Waziri anazungumza kuna mwingine alichangia mwisho hakumsikia, Mheshimiwa Mtuka. Mheshimiwa Mtuka alikuwa amependekeza juu ya masuala ya makosa yaliyopo kwenye Ibara ya 67. Maoni aliyopendekeza yapo kwenye sheria nyingine za nchi, lakini mengine aliyosema yamejibiwa na Mheshimiwa Naibu Waziri. Ni kweli kwamba taasisi za Serikali zitakapokuwa zinafanya tathmini yake mara nyingi huwa tunatumia Wathamini wa Serikali kwa sababu tunao Wathamini kwenye Halmashauri na kwenye Wizara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sheria hii hatuwezi kutoa exemption kwa sababu exemption ni suala la Wizara ya Fedha. Kwa hiyo, exemption itatolewa wakati wa tathmini ya kazi ya Serikali kwa kutumia Sheria nyingine ya Fedha siyo kwa sheria hii maana mimi siyo Waziri anayehusika na exemptions. Exemption kwa shughuli kama hizi kwa non-profit making organisations, kwa Serikali, itatolewa kama inavyotolewa siku zote na sheria nyingine. Kwa hiyo, tathmini za binafsi zitalipiwa na Bodi itatengeneza fee lakini za Serikali zitapewa exemption kwa mujibu wa sheria ya exemption.
Mheshimiwa Mwenyekiti, karibu yote ambayo mmechangia yamejibiwa lakini nataka niseme moja. Nimewasikiliza sana, nataka nifanye marekebisho kidogo kwenye jambo la sifa za Wathamini Wasaidizi. Waheshimiwa Wabunge, tukipitisha Muswada huu mambo yatakuwa kama yafuatayo:-
Kule Wilayani watu wa Serikali kutakuwa na Wathamini lakini Wilaya moja inaweza kuwa na Wathamini watatu, kila Wilaya kuna mtu atapewa uteule na Chief Valuer anaitwa Mthamini Msaidizi Mteule ambaye ndiye atakuwa na uwezo wa kuidhinisha na ku-sign nyaraka zote za tathmini ndani ya Wilaya ile, atapewa ile kofia ya uthamini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye ardhi mnao hawa watu wanaitwa Afisa Ardhi Mteule, hata kama mna Maafisa Ardhi watano lakini ndani ya Wilaya kuna mtu anaitwa Afisa Ardhi Mteule ambaye ndiye anayeidhinisha hati na zinakwenda kwa Kamishna. Kwa hiyo, Mthamini Msaidi Mteule ndiye atakuwa muidhinishaji wa tathmini kabla hazijakwenda kwa Chief Valuer hata kama Wathamini wako wengi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi sasa uzoefu tulionao ni kwamba tathmini za nchi nzima, ziwe za watu binafsi kutoka Kibondo au Rombo au za Serikali kutoka Rombo au Kibondo lazima zifike Dar es Salaam alipo Chief Valuer, ni mtu mmoja tu peke yake ndiyo anaruhusiwa kuthibitisha au kuidhinisha tathmini yoyote ya nchi nzima.
Waheshimiwa Wabunge, Muswada huu mnaotunga leo hawa Wathamini Wasaidizi watafanya kazi hiyo ili kupunguza mzigo kwa wananchi na taabu wanayoipata na muda unaopotea kwa Serikali au wananchi kusubiri tathmini eti kwa sababu makabrasha yako kwa Chief Valuer. Wakati mwingine zinaweza kuja tathmini za mashamba ekari 100,000, 10,000, vitabu 100, 200, vyote vinajaa kwenye chumba cha mtu mmoja, inachukua muda mrefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa nini katika Muswada huu tunasisitiza uzoefu ufanane na Chief Valuer ni kwa sababu hawa ma-Valuer Wasaidizi tunawaweka kwenye kanda zile, tunayo Kanda ya Kaskazini (Moshi), Nyanda za Juu (Mbeya), tunayo Tabora na Mwanza, kule hatukuwa na hawa watu ndiyo maana valuations zilikuwa zinakuja Dar es Salaam, mkitupa hawa watu kwenye sheria hii tunawaweka kule kwa hiyo valuation ya kila kanda haitakwenda kwa Chief Valuer, itaishia kwa huyu wa kanda kama ilivyo kwa hati zenu. Tumefanikiwa sasa hati zote zinatolewa kwenye kanda na zinasajiliwa kwenye kanda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tungependa sasa hata valuation ripotizisije Dodoma anapohamia Chief Valuer ziishie kwenye kanda. Kanda ya Kasakazini Chief Valuer Msaidizi wa Moshi awe na uwezo sawa na yule kwa sababu ndiye atakayegonga mhuri wa mwisho na hatahojiwa na Chief Valuer. Ndiyo maana tunasema angalau hawa watu wawe na sifa na uzoefu unaofanana kidogo kwa sababu itafika mahali huyu atakuwa anachunga nidhamu ya hawa, wakati mwingine itafika huyu hana kazi ya kugonga muhuri kwa sababu kazi nyingi zitakuwa zinafanywa kwenye kanda. Kwa hiyo, tusiwapuuze sana hawa ni watu muhimu, ndiyo watakaofanya kazi na ninyi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ninachotaka ku-compromise hapa, tumejadiliana sana na AG na tume-research, miaka mingi nchi yetu haikuwa hata na degree za valuation. Chuo cha Ardhi kimetoa advanced diploma kwa miaka mingi, tukilazimisha kwamba Assistant Valuers wawe na masters hatutawapata, hawapo!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka nikubaliane kwa jumla na wote mnaosema angalau uzoefu uwepo lakini watu wenye shahada ya kwanza au elimu inayofanana na shahada ya kwanza wawe na sifa hiyo ya kuwa ma-Valuer Wasaidizi. Kwa sababu wote tunajua vyeti havifanyi kazi, hii kazi anayofanya valuer ni ileile katika maisha yake yote, kwa hiyo uzoefu ni muhimu kuliko cheti. Maana kila siku kukicha uzoefu na utaratibu uliowekwa kwenye kanuni na Bodi ya namna ya kufanya valuation ni uleule, ni kazi ya mazoea, kazi ya mazoea inahitaji uzoefu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nakubaliana na ninyi kwamba kwa kazi hizi bachelor inatosha au elimu inayofanana na hiyo. Zamani tulikuwa na advanced diploma ambazo zinafanana na hizo, zimefundishwa sana na Chuo cha Ardhi na Valuers wengi ndiyo wanazo hizo, tukisema masters hapa watasajiliwa wachache sana. Kwa hiyo, hilo nakubaliana na ninyi, tutakapofika kwenye marekebisho nimeona mtu fulani ameleta, tutafanya masahihisho juu ya suala hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kwamba uzoefu ni muhimu katika kazi hii. Leo huyu mtu Halmashauri nzima kule ndani kuna private sector kuna Serikali, Serikali inataka kufanya valuation ya property tax kwenye majengo, kuna mambo ya mortgage, hata wewe tu unaweza kuwa na dhahabu yako unataka kujua thamani yake ili ujue tu una mali kiasi gani siyo kwa maana ya mortgage au nini, ni huyuhuyu atafanya. Ili aweze kujua namna ya kufanya tathmini ya mambo yote haya, maana ndiyo mnayemtegemea, lazima awe na uzoefu, degree peke yake haitoshi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nasema naweza ku-compromise habari ya cheti kwamba vijana hawa waliosoma degree ya kwanza akipata uzoefu huo anaweza kuwa na ngazi hiyo, lakini uzoefu ni muhimu kwa sababu kama mlivyoona valuation hii inahusu mambo mengi sana. Kwa hiyo, ndugu zangu nafikiri hapo tunaelewana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sasa kutakuwa na mnyumbuko. Mnajua Wathamini wa Wilaya wako chini ya TAMISEMI, wale wa Kanda wako chini ya Wizara lakini leo hakukuwa na mahusiano kati ya Mthamini Mkuu na Mthamini wa kwenye Wilaya. Kwa kumweka Mthamini kiungo pale au mteule maana yake umemuunganisha Chief Valuer na huyu Valuer wa Wilaya. Kwa hiyo, sheria hii imekamilika kutokana na structure iliyowekwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mwassa hapa amesema tuorodheshe maeneo, si rahisi kuorodhesha yote hapa ndani, nafikiri ni rahisi zaidi tukitulia tukaorodhesha kwenye kanuni kwa sababu maeneo haya yanaongezeka, technology inaongezeka sasa, mahitaji ya maeneo mapya ya valuation yanaweza yakaongezeka, kurudi Bungeni hapa kuyaongeza kila mara kwenye sheria itakuwa ngumu. Kwa hiyo, tukubaliane tu Mheshimiwa Mwassa kwamba twende kwenye kanuni ili kuorodhesha haya mambo yote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wengi mmezungumza hapa kuhusu Valuers wawili katika mradi mmoja, haiwezekani! Kama Valuer mmoja tathmini yake inapingwa, inafutwa, anateuliwa mwinginehuwezikuajiri kampuni mbili zinafanya valuation ya kitu kimoja, lazima itakuwa valuation moja at a time. Kwa sababu kama kweli huyu amesajiliwa na inapita kwenye Bodi ileile, haziwezi kuwa valuation mbili, unataka nini? Au huyu unaikata, una-appeal, unatafuta mwingine hii inafutwa, kwa hiyo, valuation itakuwa moja tu haziwezi kuwa mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kidogo juu ya ndugu yangu Mheshimiwa Mtulia, ameunganisha hili na mambo ya Magomeni Kota. Haya mambo hayahusiani lakini basi wacha niseme tu. Kwanza kama alivyompongeza Mheshimiwa Rais nami nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uamuzi huu wa kibinadamu na upendo wa Kitanzania kwa kuwahurumia wale maskini na kufanya uamuzi mgumu sana. Nilifikiri Mheshimiwa Mbunge wa eneo lile asingeongeza yale mengine yanayoonesha kuna kasoro, angempongeza moja kwa moja, angeishia pale pengine wananchi wake wangemwelewa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hakuna kasoro katika hili, hili jambo lililofanywa na Mheshimiwa Rais ni jema na asilinganishe jambo hili na yaliyopita na asifiche. Sisi tunaojua historia pale kulikuwa na harufu ya ufisadi, halikuwa jema, wala asisingizie ya juzi, habari ya TAMISEMI kazuia, kwa nini TAMISEMI kazuia, huo uendelezaji ulitaka kufanywa na nani? Mnataka niseme hapa hao waendelezaji mliotaka kuwapa pale?
Tuishie tu kusema Mheshimiwa Rais amefanya uamuzi mgumu lakini wa busara, kwa upendo na kwa kuzingatia maadili aliyonayo. Jambo hili ni baya, lilikosewa na ndiyo maana amesema halifai kurudiwa tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watu walipewa ahadi…
Muulizeni Mheshimiwa Mtulia anayetetea kwamba TAMISEMI ndiyo imechelewesha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka kumwambia Mheshimiwa Mtulia jambo hili ni jema na halikuwa na makosa. Nataka wale wananchi wa Magomeni Kota waendelee kumwombea Mheshimiwa Rais ili Mwenyezi Mungu amjalie nia njema hii ikamilike. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili ni jema kabisa na wala asilinganishe na la mabondeni. Hilo la mabondeni nalijibu kabisa, nyumba hizi 644 zitakapojengwa watapewa tu wale waliovunjiwa nyumba waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota. Watu wa mabondeni waliovunjiwa wana sababu nyingine zaidi ya hii, nyumba hizi haziwahusu. Wale wameondoshwa kwa sababu walikuwa wanakaa kwenye maeneo hatarishi, kwa hiyo, hawatapewa nyumba hizi. Siwezi kuendelea zaidi kwa sababu Mheshimiwa ana kesi mahakamani, nafikiri aendelee na ile kesi kwanza. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa amelaumu kidogo kwamba hakutambulishwa na angefikiri kwamba mimi ningemtambulisha. Sasa wewe na mimi, wewe si ulikuwepo pale juzi, mimi si uliona nimewekwa kwenye ratiba kama mgeni uliniona mimi ni MC? Mimi nimetangazwa pale nimepewa nafasi yangu, Mheshimiwa Waziri njoo mbele, waliopewa kazi ya kutambulisha wamemaliza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Meya pale ametambulishwa na Mheshimiwa Rais mwenyewe na wengine wametambulishwa na mimi na nimepewa nafasi yangu moja tu ya kusema. Sasa lawama hizo rafiki yangu kutoka kule Dar es Salaam mpaka kuja Bungeni kwa kutokutambulishwa tu na Waziri na mimi nilikuwa mgeni na MC ulimwona!
Nafikiri ungeangalia maudhui ya sherehe yenyewe. Nafikiri maudhui ya sherehe yenyewe na mafanikio ya sherehe yalikuwa makubwa zaidi kuliko kutambulishwa mtu mmoja. Kwa hiyo, mzee mimi nilikuwa mgeni kama wewe nisingeweza kuchukua jukumu la kutambulisha watu kwa sababu sikupewa kazi hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nimjibu kwa sababu amesema, hata kama wengine hampendi lakini mtu anayesema lazima ajibiwe maana mimi siyo bubu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, narudia kwa kuwashukuru sana wachangiaji wote waliochangia hoja hii kuanzia Kamati yetu ya Ardhi, Msemaji wa Kambi ya Upinzani na wachangiaji wote waliochangia humu ndani wa vyama vyote pamoja na wale walioandika amendments. Nataka kuwahakikishia kwamba baada ya Muswada huu kupita Serikali itajitahidi kukamilisha kanuni zilizoahidiwa ili kuhakikisha kwamba sheria hii inatekelezwa kwa malengo yaliyokusudiwa na Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono sana hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nampongeza sana yeye, Naibu wake, Katibu Mkuu, timu ya wataalam na wote walioshiriki katika kupanga jambo hili.

Mheshimiwa Spika, nataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwamba Serikali imejipanga vizuri sana katika kuondoa kero hasa za uwekezaji kwa sababu tunajua uwekezaji wote unaanza kwenye msingi wa ardhi. Baadhi ya uwekezaji mkubwa ambao tunautarajia kama wa LNG Wabunge wamezungumza, nataka kuwahakikishia kwamba wizara yangu imeshatoa hati ya eneo lote kwa TPDC, hakuna tatizo la ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika eneo la uwekezaji wa bomba la mafuta kutoka Uganda, nataka kuwahakikishia kwamba Wizara yangu kwa kushirikiana na wabia tumeshapiga picha ya anga ya upana wa mita 200 katika eneo lote la mpaka. Kwa hiyo, najua kuna speculators ambao wameshaanza kupanda miti na vibanda humo, picha tunazo; hamtapata fidia watu ambao mnaweka weka katika maeneo hayo kwa sababu tumeshapiga picha za anga na kazi inaendelea katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumejianda kabisa kuondoa kero katika eneo la ardhi ili kuhakikisha wawekezaji wa ndani na nje wanawekeza wa ndani na nje wanawekeza na Watanzania wanapata unafuu katika kumiliki ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka huu wa fedha tutapanga master plan katika miji 30, tumeshaanza. Master plan ambazo zitaelekeza maeneo mbalimbali ya uwekezaji pamoja na hao wamachinga ambao wanasajiliwa, master plan hizi lazima zielekeze maeneo ya kufanya biashara. Wizara yangu haitasaini master plan yoyote ambayo haitaelekeza maeneo ya kufanya biashara hasa za watu wadogo wadogo katika miji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, katika umilikaji wa ardhi, EPZ tumewapa maeneo makubwa, lakini sheria tumetunga mwaka huu EPZ na TIC tumewapa jukumu lingine la kutoa hati. Zamani ilikuwa wawekezaji wanapewa hati na Wizara ya Ardhi. Kwa hiyo, EPZ na TIC sasa wanatoa wenyewe derivative right ili kupunguza urasimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika umilikaji wa Watanzania na wageni, uwekezaji na ujenzi wa Mipango Miji, jambo moja lililokuwa linawakwaza Watanzania ni gharama ya umilikaji wa ardhi. Mwaka huu pekee tumeamua kama Serikali kuondoa asilimia 67 ya tozo kubwa ambayo ilikuwa inawakwaza sana watanzania na wawekezaji katika katika umilikaji wa ardhi inaitwa premium. Kwa hiyo, fikiria kama wewe ulikuwa unatakiwa kulipa shilingi milioni 100 sasa kuanzia tarehe moja mwezi wa saba utalipa milioni 33. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Serikali imeamua hivi ili kuwapa nafuu watu wengi zaidi waweze kumiliki ardhi na Serikali kila mwaka iendelee kupata kodi. Kwa hiyo, tumefanya makubwa sana katika kuhakikisha kwamba tunarahisisha suala zima la uwekezaji ili kuhakikisha kwamba kila mwananchi anamiliki ardhi bila kikwazo kikubwa.

Mheshimiwa Spika, hapa Dodoma ilikuwa ni eneo pekee ambalo wawekezaji wa nje hawawezi kufika kwa sababu ya mkanganyiko wa umilikaji wa ardhi. Mheshimiwa Rais aliagiza na utekelezaji umenza, imefutwa CDA na sasa watu wote wanaomiliki ardhi Dodoma wataanza kupata title deed kama wananchi wengine katika maeneo mengine ya Tanzania, na watapata title deed zenye miaka 99.

Mheshimiwa Spika, wale wote waliokuwa wanapata lease tumeanza utaratibu wa kubadilisha ili waweze kupata title deed za miaka 99. Walikuwa wanapata lease za miaka 33 lakini sasa tutawaongeza kila mwenye hati ataongezewa miaka 66 na kwa agizo la Mheshimiwa Rais kwamba hawa watu wote wabadilishiwe hati bila kuongezwa gharama yoyote, bure. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kila mmoja sasa mwenye lease aliyekuwa na hati Dodoma ni fursa aende Manispaa ili aweze kupata title deed ya miaka 99. Maana yake ni nini? Ukipata title deed sasa TIC wanaweza kumpa derivative right yule mwekezaji ambaye utampata kutoka nje ambaye anaweza akaingia ubia na wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tunaendelea na jitihada za kufanya audit, tunajua katika kupanga mipango hii ya uwekezaji, wako matapeli wanaingia wana-take advantage kuchukua ardhi ya Tanzania kwa ajili ya kujipatia mitaji au kuhamisha mitaji, wanatumia ardhi yetu kufanya mortgage na kuhamisha pesa. Kwa hiyo, tunafanya audit kuwatambua wale wote ambao wamemiliki ardhi. Kwanza hawana sifa, wengine si raia, lakini wale ambao wamemiliki ardhi kubwa na bila kuziendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita Mheshimiwa Rais amefuta mashamba yenye ekari zaidi ya elfu ishirini Mkoa wa Morogoro, na katika kipindi cha mwaka huu mmoja na nusu Mheshimiwa Rais ameshafuta mashamba yenye ekari zaidi ya 100,000 katika nchi hii, na mashamba haya yanapangwa ili kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania wa wawekezaji walio mahiri wanamilikishwa kwa kufuata sheria. Tunajua wapo watu wamemiliki hata maeneo ya madini kwa sura za Tanzania na hati za Kitanzania.

Vilevile wapo wenzetu wengine wana hati mbili mbili za kusafiria, kwa maana wana uraia wa nchi mbili. Tunafanya uhakiki na wale wote ambao watagundulika wana hati mbili mbili lakini wamemiliki ardhi ya Tanzania tutanyang’anya kama ambavyo tumeshawanyang’anya watu wengine. Ule wakati wa longo longo umekwisha sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kila mmoja anayetaka kumiliki ardhi atapewa na nataka kukuhakikishia Mheshimiwa Spika kwamba Serikali tumejipanga, tumerahisisha sana utaratibu na tumeondoa kero nyingi sana katika ardhi, umilikaji umekuwa smooth. Zamani ilikuwa ili uweze kupata hati unasubiri mwaka mmoja, leo maximum ni mwezi mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumejipanga twende katika lengo la wiki moja, na kutokana na mfumo tuliouanza kuufunga Dar es Salaam, tumeshaanza kufanya scanning ya document mbalimbali katika Wilaya ya Kinondoni na Ubungo; kwa Dar es Salaam
tutaanza kufikia lengo hilo la wiki moja mwakani. Tukifunga mitambo hii Nchi nzima, tunaweza kufika mpaka siku mbili. Vile vile Ulipaji wa kodi mwakani tutaanza kutumia mtandao; tutalipa kodi kwa kutumia mtandao wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie kwamba jitihada zinazofanywa na Mheshimiwa Rais lazima na sisi Wizara mbalimbali kama Wizara yangu ya Ardhi, tumuuunge mkono kwa kufanya yale yanayotuhusu ndani ya wizara yetu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono sana hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha, nampongeza sana yeye, Naibu wake, Katibu Mkuu, timu ya wataalam na wote walioshiriki katika kupanga jambo hili.

Mheshimiwa Spika, nataka kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kwamba Serikali imejipanga vizuri sana katika kuondoa kero hasa za uwekezaji kwa sababu tunajua uwekezaji wote unaanza kwenye msingi wa ardhi. Baadhi ya uwekezaji mkubwa ambao tunautarajia kama wa LNG Wabunge wamezungumza, nataka kuwahakikishia kwamba wizara yangu imeshatoa hati ya eneo lote kwa TPDC, hakuna tatizo la ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika eneo la uwekezaji wa bomba la mafuta kutoka Uganda, nataka kuwahakikishia kwamba Wizara yangu kwa kushirikiana na wabia tumeshapiga picha ya anga ya upana wa mita 200 katika eneo lote la mpaka. Kwa hiyo, najua kuna speculators ambao wameshaanza kupanda miti na vibanda humo, picha tunazo; hamtapata fidia watu ambao mnaweka weka katika maeneo hayo kwa sababu tumeshapiga picha za anga na kazi inaendelea katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumejianda kabisa kuondoa kero katika eneo la ardhi ili kuhakikisha wawekezaji wa ndani na nje wanawekeza wa ndani na nje wanawekeza na Watanzania wanapata unafuu katika kumiliki ardhi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mwaka huu wa fedha tutapanga master plan katika miji 30, tumeshaanza. Master plan ambazo zitaelekeza maeneo mbalimbali ya uwekezaji pamoja na hao wamachinga ambao wanasajiliwa, master plan hizi lazima zielekeze maeneo ya kufanya biashara. Wizara yangu haitasaini master plan yoyote ambayo haitaelekeza maeneo ya kufanya biashara hasa za watu wadogo wadogo katika miji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la pili, katika umilikaji wa ardhi, EPZ tumewapa maeneo makubwa, lakini sheria tumetunga mwaka huu EPZ na TIC tumewapa jukumu lingine la kutoa hati. Zamani ilikuwa wawekezaji wanapewa hati na Wizara ya Ardhi. Kwa hiyo, EPZ na TIC sasa wanatoa wenyewe derivative right ili kupunguza urasimu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia katika umilikaji wa Watanzania na wageni, uwekezaji na ujenzi wa Mipango Miji, jambo moja lililokuwa linawakwaza Watanzania ni gharama ya umilikaji wa ardhi. Mwaka huu pekee tumeamua kama Serikali kuondoa asilimia 67 ya tozo kubwa ambayo ilikuwa inawakwaza sana watanzania na wawekezaji katika katika umilikaji wa ardhi inaitwa premium. Kwa hiyo, fikiria kama wewe ulikuwa unatakiwa kulipa shilingi milioni 100 sasa kuanzia tarehe moja mwezi wa saba utalipa milioni 33. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo Serikali imeamua hivi ili kuwapa nafuu watu wengi zaidi waweze kumiliki ardhi na Serikali kila mwaka iendelee kupata kodi. Kwa hiyo, tumefanya makubwa sana katika kuhakikisha kwamba tunarahisisha suala zima la uwekezaji ili kuhakikisha kwamba kila mwananchi anamiliki ardhi bila kikwazo kikubwa.

Mheshimiwa Spika, hapa Dodoma ilikuwa ni eneo pekee ambalo wawekezaji wa nje hawawezi kufika kwa sababu ya mkanganyiko wa umilikaji wa ardhi. Mheshimiwa Rais aliagiza na utekelezaji umenza, imefutwa CDA na sasa watu wote wanaomiliki ardhi Dodoma wataanza kupata title deed kama wananchi wengine katika maeneo mengine ya Tanzania, na watapata title deed zenye miaka 99.

Mheshimiwa Spika, wale wote waliokuwa wanapata lease tumeanza utaratibu wa kubadilisha ili waweze kupata title deed za miaka 99. Walikuwa wanapata lease za miaka 33 lakini sasa tutawaongeza kila mwenye hati ataongezewa miaka 66 na kwa agizo la Mheshimiwa Rais kwamba hawa watu wote wabadilishiwe hati bila kuongezwa gharama yoyote, bure. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo kila mmoja sasa mwenye lease aliyekuwa na hati Dodoma ni fursa aende Manispaa ili aweze kupata title deed ya miaka 99. Maana yake ni nini? Ukipata title deed sasa TIC wanaweza kumpa derivative right yule mwekezaji ambaye utampata kutoka nje ambaye anaweza akaingia ubia na wewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia tunaendelea na jitihada za kufanya audit, tunajua katika kupanga mipango hii ya uwekezaji, wako matapeli wanaingia wana-take advantage kuchukua ardhi ya Tanzania kwa ajili ya kujipatia mitaji au kuhamisha mitaji, wanatumia ardhi yetu kufanya mortgage na kuhamisha pesa. Kwa hiyo, tunafanya audit kuwatambua wale wote ambao wamemiliki ardhi. Kwanza hawana sifa, wengine si raia, lakini wale ambao wamemiliki ardhi kubwa na bila kuziendeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wiki iliyopita Mheshimiwa Rais amefuta mashamba yenye ekari zaidi ya elfu ishirini Mkoa wa Morogoro, na katika kipindi cha mwaka huu mmoja na nusu Mheshimiwa Rais ameshafuta mashamba yenye ekari zaidi ya 100,000 katika nchi hii, na mashamba haya yanapangwa ili kuhakikisha kwamba wananchi wa Tanzania wa wawekezaji walio mahiri wanamilikishwa kwa kufuata sheria. Tunajua wapo watu wamemiliki hata maeneo ya madini kwa sura za Tanzania na hati za Kitanzania.

Vilevile wapo wenzetu wengine wana hati mbili mbili za kusafiria, kwa maana wana uraia wa nchi mbili. Tunafanya uhakiki na wale wote ambao watagundulika wana hati mbili mbili lakini wamemiliki ardhi ya Tanzania tutanyang’anya kama ambavyo tumeshawanyang’anya watu wengine. Ule wakati wa longo longo umekwisha sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, kila mmoja anayetaka kumiliki ardhi atapewa na nataka kukuhakikishia Mheshimiwa Spika kwamba Serikali tumejipanga, tumerahisisha sana utaratibu na tumeondoa kero nyingi sana katika ardhi, umilikaji umekuwa smooth. Zamani ilikuwa ili uweze kupata hati unasubiri mwaka mmoja, leo maximum ni mwezi mmoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumejipanga twende katika lengo la wiki moja, na kutokana na mfumo tuliouanza kuufunga Dar es Salaam, tumeshaanza kufanya scanning ya document mbalimbali katika Wilaya ya Kinondoni na Ubungo; kwa Dar es Salaam
tutaanza kufikia lengo hilo la wiki moja mwakani. Tukifunga mitambo hii Nchi nzima, tunaweza kufika mpaka siku mbili. Vile vile Ulipaji wa kodi mwakani tutaanza kutumia mtandao; tutalipa kodi kwa kutumia mtandao wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie kwamba jitihada zinazofanywa na Mheshimiwa Rais lazima na sisi Wizara mbalimbali kama Wizara yangu ya Ardhi, tumuuunge mkono kwa kufanya yale yanayotuhusu ndani ya wizara yetu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kuisha kwa muda wa mzungumzaji)

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.
Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019 pamoja na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2019
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nami nianze kuwapongeza Wenyeviti wa Kamati zote mbili na zaidi Kamati yangu ya Ardhi na Maliasili. Nakubali kwamba tumepokea ushauri wao waliotushauri.

Mheshimiwa Spika, lakini niseme mambo mawili; la kwanza nianze na National Housing. Kamati imeshauri juu ya mapendekezo yao ya ukamilishaji wa miradi ile mikubwa ya National Housing. Nataka kuwahakikishia kwamba miradi ili itakamilika.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema juzi mimi nilifanya uamuzi wa kusimamisha ukopaji wa zile fedha makusudi kwa sababu tulitaka kujiridhishe mambo fulani. La kwanza hatua ya kwanza nimeunda bodi mpya yenye ueledi yenye uwezo wa kusimamia, lakini kazi ya pili ya bodi ile nimewapa ni kuhakiki ile miradi na mikataba. Tumeanza kufanya mazungumzo na contractors, tunataka tuhakiki ili kuondoa mambo fulani fulani yatakayotuwezesha kupunguza gharama za ujenzi wa ile miradi mikubwa. Lakini tatu, tunazungumza na mabenki, tuna- renegotiate ili angalau tupunguziwepunguziwe hivi mariba yao yale. Na tumeanza kufanikiwa.

Mheshimiwa Spika, tukishamaliza haya yote tunajua sasa tutapata picha ni kiasi gani cha pesa kinahitajika ili kukamilisha ile miradi. Kwa hiyo, nataka niwahakikishie Kamati na Waheshimiwa Wabunge, Serikali iko makini sana, lakini kama tulivyo sisi kazi yetu ni kuhakikisha kwamba pesa yetu tunaitumia kwa madhumuni yaliyo sahihi, kwa hiyo hii miradi itakamilika. Tumeanza vizuri na ule mradi wa Morocco, utakamilika kabla ya Juni, na baada ya hapo tutaenda Seven Eleven ile ya Kawe.

Mheshimiwa Spika, lakini ipo miradi mingi ambayo inaendelea. Hapa Dodoma tumejenga nyumba 150 na tunaendelea kujenga nyingine 30 na mwezi ujao tutaanza kujenga apartments nyingine mpya 100; hii ni kwa fedha ya ndani.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uhakiki huu na kubana matumizi, Shirika la Nyumba sasa linaweza likajenga miradi mingine kwa pesa yake yenyewe. Na Shirika la Nyumba sasa limeanza kuaminika kwa kutumia kampuni tanzu ya National Housing ya ujenzi, sasa tuna miradi 35 mikubwa ambayo tumeaminika tunajenga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja ya miradi hiyo ni Hospitali ya Rufaa ya Musoma na Hospitali ya Rufaa ya Mtwara, wanaotoka huko wanajua. Hii ni kazi ambayo ilikuwa haifanywi na National Housing, sasa tumeamua katika Awamu ya Tano Shirika la Nyumba halitatumia contractor katika kujenga majengo yake na litashiriki katika ujenzi wa majengo mengine ya nchi. Kwa hiyo, Shirika la Nyumba sasa awamu hii inaenda vizuri zaidi kuliko awamu nyingine.

Mheshimiwa Spika, nataka msitafsiri uwezo au uendeshaji wa Shirika la Nyumba kutokana na ile miradi miwili mnayoiona pale Dar es Salaam. Ipo miradi mingi inaendelea, shirika limetulia, muundo umekamilika, bodi yenye weledi imekamilika inafanya kazi yake vizuri na yale yote ambayo yalikuwa yameshindikana sasa yatawezekana.

Mheshimiwa Spika, na zile nyumba ambazo zilikuwa zimejengwa kule mikoani tumebadilisha utaratibu sasa, watu watakuwa wanapanga zile ndogondogo zilikuwa zimejengwa muda mrefu lakini zilikuwa hazipati wanunuzi, tumeamua sasa kutengeneza utaratibu wa mpangaji mnunuzi. Kwa hiyo, mwananchi atakuwa na uwezo wa kupanga lakini hela yake mwisho wa yote atakabidhiwa nyumba. Tumeanza Kahama na sehemu nyingine, kwa hiyo zile nyumba ndogondogo kote kule tutaenda kwa utaratibu wa tenant purchase. Shirika la Nyumba nataka kusema linakwenda vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nije kwa baadhi ya mafanikio mengine ambayo yamezungumzwa kwenye Sekta ya Ardhi. La kwanza, Mheshimiwa Mch. Msigwa, katika miaka hii minne tumeweza kutatua migogoro zaidi ya 10,000 kwa njia ya utawala, maana yake nini? Kama wananchi hawa tusingewafikia na kutatua hii migogoro, wote wangekuwa mahakamani. Sasa wewe uniambie, wale wananchi wakiwemo wa Iringa niliowafikia juzi, miezi miwili iliyopita 500, leo wangekua kwenye mahakama wanatozwa hela na mawakili lakini leo wamepata nafuu kwa sababu Mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano wamekwenda kuwasuluhisha kiutawala, wame-save gharama wananchi lakini pia wamewatua mizigo na kuleta amani na utuivu. Na hivi sasa nina mwaliko wa Iringa tena, wanachama wako 200 wananchi wameomba niende kule, na wewe unajua. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo utatuzi wa migogoro kwa Wizara ya Ardhi iko kisheria. Pia tunatumia utatuzi mwingine kutumia mabaraza ya ardhi. Lakini pia Mheshimiwa Rais ametusaidia kutatua mgogoro ambao ulikuepo maisha, huu aliozungumza Mheshimiwa wa Maliasili. Vijiji 975 vilijikuta vimesajiliwa kwenye hifadhi za taifa, hifadhi za misitu, kwa miaka yote. Wamesajiliwa humu hati za TAMISEMI wamepewa, hati za ardhi wamepewa lakini bado kwenye GN za maliasili wanaonekana kama ni wavamizi. Na wakati huohuo baadhi ya watumishi wasio waaminifu walikuwa wanawatishatisha ili waondoke. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais kwa kutumia usuluhishi wa namna hii wa kutatua migogoro ameamua kuumaliza kabisa mgogoro huu kwa mara ya kwanza katika nchi hii. Vijiji 920 ambao walikuwa hawana matumaini ya kuishi katika vijiji vile sasa wamepewa matumaini mapya, watamilikishwa ile ardhi na hawataondoka katika ardhi yake. Haya ni matumaini mapya ambayo yamejengwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Magufuli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hili angelijuaje maana nao huu ni usuluhishi. Sasa kama nao huu kuwapa matumaini mapya vijiji 920 vikiwepo vya Iringa, ipo mitaa minne pale Iringa Mjini ambavyo vilikuwa kwenye msitu lakini navyo mitaa ile imeambiwa ibaki pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kuwaambia kwamba utatuzi wa mgogoro umetusaidia sana katika kuleta utengamano, amani na utulivu katika nchi hii. Siyo hayo, Mabaraza ya Ardhi nayo yamesaidia katika kutatua migogoro. Kuna kesi zaidi ya 112,243 zimetolewa maamuzi kati ya kesi zilizofikishwa kwenye mabaraza 139,943. Pia tumefanikiwa katika kipindi hiki kutayarisha Hati Miliki nyingi zaidi. Katika mwaka uliopita mwaka 2019 tumeweza kutayarisha Hati Miliki 325,000 ukilinganisha na hati zilizotolewa mwaka 2015 hati 54,000. Maana yake nini? Tumewapa matumaini watu zaidi ya 300,000 kumiliki ardhi yao na hivyo sasa wameweza kukopesheka katika mabenki.

Mheshimiwa Spika, zoezi la urasimishaji limefanywa kwa huruma ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Awamu ya Tano. Watu waliokuwa wamejenga katika maeneo mijini bila kuwa na vibali, bila kuwa na hati, bila kuwa na viwanja vilivyopangwa na kupimwa, mara zote walikuwa wametishiwa usalama wao na Manispaa na Halmashauri za Miji kwamba waondoke, lakini Mheshimiwa Dtk. John Pombe Magufuli amesema hawa ni Watanzania walijenga tukiwaona, warasilimishiwe wapewe hati zao katika makazi yao mijini. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante, malizia Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, zoezi hilo limefanikiwa sana tumetoa hati zaidi ya 500,000. Kwa hiyo, nakushukuru sana. Nataka niwahakikishie Wajumbe wa Kamati ile ya Maliasili na Ardhi kwamba tutaendelea kushirikiana na yale mapendekezo mengine yote tumeyachukua, tutayafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, kama kuna wanachi wenye kero waleteni tu, sisi kazi ya Serikali ni kusikiliza kero za wananchi, hatutachoka. Tutafanya, hii ni kazi yetu ya kuwahudumia wananchi kama tulivyohaidi.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.(Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili nichangie hotuba hii ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo ada nami nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ndumbaro na Naibu wake na watendaji wote wa sekta ya maliasili kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusimamia na kulinda rasilimali muhimu sana ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kusema mambo machache miongoni mwa mengi ambayo yamezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge. La kwanza nafikiri nifafanue tena kazi ambayo Serikali imeshafanya, nataka kuwapa tu taarifa Waheshimiwa Wabunge kwa kutambua mengi ambayo yanasemwa hapa kwamba idadi ya watu na shughuli zao zinaongezeka na wananchi sasa wamekuwa wengi sana, lakini hifadhi zimebaki vilevile.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka kuwakumbusha kwamba Serikali ilishafanya uamuzi na imefanya uamuzi baadhi ya maamuzi ni kama yafuatayo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, kwa kutambua hilo Serikali imefuta Mapori Tengefu 12 yenye ukubwa wa ekari laki 707,659.4. Haya mapori yalikuwa na GN zao yamehifadhiwa kwa mujibu wa sheria na Serikali imechukuwa jukumu la kuyafuta ili yapangwe yaweze kutumika kwa shughuli za binadamu za kilimo na mifugo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji umeshafanyika, Wizara ya Maliasili imeelekezwa na Waziri amesha-degazette, yaani ameshayaondowa kwenye orodha ya Mapori Tengefu ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, baada ya hapo Serikali imeshafuta, iliagiza misitu yenye ekari 46,715, hifadhi saba za misitu ambazo zimekosa sifa kwa sababu ndani yake kuna watu, kuna shughuli za binadamu na nini, hizi nazo zimefutwa, ekari 46,715 za misiti zimefutwa ili wananchi waendeleza shughuli zao za kilimo na mifugo katika maeneo hayo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haya maeneo ni yale yaliyokutwa angalau tunasema wavamizi, lakini wananchi wameingia katika maeneo hayo, wameanza kujishugulisha na shughuli mbalimbali za kibinadamu humu ndani. Kwa hiyo Serikali ilishafanya uamuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, la tatu, uamuzi mwingine uliofanywa pamoja na kwamba haya yameshakuwa degazetted, lakini bado Serikali ikasema hapana tuangalie tena maeneo mengine ya hifadhi za misitu 14 ili tukayapunguze na yenyewe yatumike kwa shughuli za kibinadamu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naweza nikasema haya ni kwamba, kwa sababu Waheshimiwa Wabunge labda shughuli za kutekeleza haya hamjaziona, lakini kama nilivyoahidi mara ya mwanzo kwamba sasa mwaka huu tumeweka bajeti wizara husika ili sasa tushirikiane na wananchi wa maeneo hayo na viongozi wa maeneo hayo, tuwaonyeshe kabisa, tunaposema hizi ekari laki saba ni zipi na watu gani watanufaika nazo.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaposema misitu hii ekari 46,000 zimepunguzwa au zimefutwa ni ipi na iko katika maeneo gani. Tunaposema misitu mingine au hifadhi za misitu
14 zitapunguzwa ni maeneo gani, lakini haya naweza nikasema baadhi ya maeneo ya hifadhi ambayo tunatarajia kwenda kuyapunguza mengine yanapatikana katika maeneo ya Uliyankulu, Geita, Rwamgasa, Lwande, Usindankwe, Ushirombo, Mbogwe, Bukombe, Runzewe, Biharamulo, Kahama, Miyeze, Tongwe East, Masanza, Uyui Kigwa Rubuga na Loasi River. Haya ni baadhi ya maeneo ambayo yana hifadhi za misitu ambazo Serikali imefanya uhamuzi lazima hifadhi hizi zipunguzwe ili wananchi waendelee na shughuli zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, uamuzi mwingine ni ule ambao tumekuwa tunausema mara zote kwamba Serikali ililetewa orodha ya kitaifa kwamba vijiji vipatavyo 975 inaelekea ndio vina mgogoro. Ni bahati mbaya sana hii orodha iliandikwa na Wabunge waliopita, lakini na Wakuu wa Mikoa na Wilaya, tutaileta kwenu muione hiyo orodha ya vijiji 975, kila mkoa na kila wilaya pengine ninayoyasema sio vijiji hivi. Kitaifa tulishafanya uhakiki na tukajua ni vijiji 975. Uamuzi wa Serikali ni kwamba vijiji 920 vinabaki na usajili wao lakini kuna kazi ndogo baadhi ya vijiji itafanywa ya kurekebisha mipaka, lakini haitafuta usajili wa vijiji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji 55 vilivyobaki ndivyo tuliambiwa tuendelee kufanya utafiti, tumeshamaliza kama nilivyowaambia, tunapeleka taarifa kwenye Baraza la Mawaziri na watatupa uamuzi. Kwa hiyo, ninachotaka kuwaambia Waheshimiwa Wabunge, ni kwamba concern yenu na sisi ndio concern yetu kama Serikali, nimeongea na mwezangu Waziri wa Maliasili, inaelekea pengine tumefanya uhakiki mara nyingi sana, wahifadhi zetu tunapofanya uhakiki maana yake ni kwamba kila hifadhi imesajiliwa kwa GN namba na mipaka inajulikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, pengine uhakiki tuliokuwa tunaufanya ulikuwa haushirikishi wananchi, kwa hiyo wapo wananchi ambao hawajui hiyo GN iliyoandikwa kwenye karatasi inatafsirika vipi kwenye ardhi. Kwa hiyo tumekubaliana, pamoja na kwamba tumeshafanya mara nyingi sana tutakuja kufanya uhakiki mpya. Tunayo maandishi hakuna mtu ambaye anania mbaya kwamba ataongezaongeza mipaka nje ya ile mipaka ambayo imetafsiriwa na imeandikwa na imeruhusiwa na GN.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunazo GN tutakuja na mimi ndio custodian ambaye ni kama msuluhishi wa mambo haya, nitaunda timu za wataalam wangu ambao wako chini ya Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, nitatumia GN za Maliasili, tutashirikiana na watu wa Maliasili, maana wenzangu ndio wana bajeti, tutafanya mara moja, tutakuja kuhakiki kwa mujibu wa GN na tutakapofanya, tutakapofika Uyui, Mbunge wa Uyui tutamwita. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii ndio GN na hii ndio mipaka uthibitishe, leo kuna vifaa ambavyo ukipima hivi kinaweza kikakupa mwelekeo hata kilometa 25 hatutachukuwa muda, tutaunda timu nyingi. Kwa hiyo nataka tu niwaambie tu Waheshimiwa Wabunge, mengi wamezungumza, inaelekea kwamba wananchi hawajui exactly na wala hawajawahi kushirikishwa kujua mpaka wa hifadhi hii umeanzia wapi na umeishia wapi. Hilo tunataka tulifanya safari hii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, si lazima tufanye kwa hifadhi zote, ningeomba kwa sababu tupo hapa, kila mmoja anayefikiri ana hifadhi ambayo ina mgogoro mkubwa wananchi wanataka kujua mipaka yao imeingia vipi, wakati wa kufanya uhakiki wale vijana wetu wana macho wataona na yaliyopo. Naomba kila mmoja wetu aandike hiyo hifadhi anayofikiri ihakikiwe ampe Waziri. Tukiwa hapa Bungeni maana hatuwezi kufanya zote hata ambazo hazina matatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge yeyote anayefikiri wananchi wanamghasighasi sana kujua mipaka imeishia wapi tupeni hiyo hifadhi iko wapi na inaitwa nini, msitu gani hifadhi ya wanyama ipi hata kama ni national park mpeni Waziri sisi tukishapa hiyo orodha tutaunda timu, zitaanza kazi mara moja ya kufanya huo uhakiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nilitaka nisimame hapa kutoa ufafanuzi wa haya ambayo yamezungumzwa sana. Ni kweli wamesema tunafanya kazi pamoja Wizara ya Ardhi, ni kweli Serikali ni moja na haya ninayoyasema tumeshazungumza na Waziri wa sekta na yupo tayari, mnamwona alivyokuwa mpole Waziri huyu, msikivu, hana shida na Naibu wake ndio yule, hana shida. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tutayafanya haya mambo waliyoyaomba Waheshimiwa Wabunge. Tukifika tutawashirikisha Viongozi wa Mikoa wa Wilaya na wale vijiji wanaohusika lakini kama Mbunge aliyeleta ile orodha tutamshikisha na ataweza kutusaidia pengine tusihakiki maeneo yote, tukaenda kwenye kona ambayo anafikiri ina mgogoro zaidi katika pori au katika hifadhi inayohusika.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka nichangie hayo ili niwaondolee wasiwasi Waheshimiwa Wabunge, tumewasikia, maneno yamesikika sana na kila leo yamekuwa yanarudiwarudiwa sana kana kwamba waliofanya uhakiki walifanya usiku au kuna watu wanaendelea kupanua hifadhi mpaka leo. Tutakuja kuhakiki kwa mujibu wa GN ambazo zimetangaza hifadhi hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na naunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 5) wa Mwaka 2017
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda ni mfupi; nataka niwapongeze Kamati na Waheshimiwa Wabunge kwa kuchangia hoja hii ya marekebisho ya sheria ya ardhi, lakini pia naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, labda niseme kwa ufupi waliochangia, Mheshimiwa Sakaya, Mheshimiwa Mbogo na Mheshimiwa Makamba; nataka niwakumbushe kwamba marekebsho ya sheria ya mwaka 1999 yalitambua kwamba ardhi inathamani hata isiyoendelezwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nataka kuwaambia wengi ambao mna mashaka kwamba ardhi peke yake mtu hawezi kukopea, inakopesheka kwa sababu ina thamani yenyewe. Valuers wanatathimini na wanaandika business plan zinakwenda benk wanapata mkopo. Inawezekana huwezi kupata kama thamani ya ardhi yako ni bilioni 1,000,000, bank hutoa 50 per cent 20, lakini unapewa. Hata kwenye viwanja vya majengo tunakopa kutokana na viwanja vile. Isipokuwa hati zile zinakuwa mali yao mpaka utakapomaliza mkopo wa benki, wanakuja kuzisajili. Kwa hiyo hiyo inakopesheka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hati za kimila tumesema wenye hati za kimila, wale wananchi masikini hawatahusika katika mpango huu kwa sababu kwanza hawakopesheki nje ya nchi kwa kutumia hati za kimila. Pili wale wanaokopa kwa kutumia hati za kimila tayari hati za kimila kwa sheria ina masharti yake. Benki wanakopesha kupitia hati ya kimila, lakini wanapokuja kuuza yale mashamba hawauzi sawasawa kwa sheria kama hati hizi za miaka 99.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanatakiwa kwanza wawauzie family members. Hati ya kimila ukichukua kama dhamana uki-default yule anayekuja kuuza ile adhi lazima auzie family members; kwa hiyo hati za kimila zipo protected. Kama ikishindikana wanatakiwa wanunue within the village. Kwa hiyo hati za kimila ziko protected ndiyo maana tukasema tusiwaingize kwenye mgogoro huu kwa sababu ya protection ile ile ardhi ile haipotei iko bado mikononi kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kukuhakikishia Mheshimiwa Makamba, hivi sasa tumefanya ukaguzi zaidi ya ekari laki moja ambazo hazijaendelezwa, zimewekwa rehani pamoja na business plan. Kwenye business plan wanasema watatoa ajira, vile vile watajenga viwanda na mali ghafi itatumika hiyo ya mashamba na mazao yatakayozalishwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini yote haya yanayeyuka, watu wanachukua pesa kwa mashamba yasiyoendelezwa, wanachukua zile pesa wanakwenda kufanya biashara za haraka haraka na fedha zile zinalipwa benki. Benki interest yao ni kwamba mikopo yao imelipwa, lakini ukiangalia miamala yao kupitia ile business plan Serikali inakosa. Kwa sababu kama mtu hakulima maana yake hajafanya biashara, maana angefanya biashara according to business plan tungepata kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama angetekeleza ile business plan lazima angeajiri watu, kama angetekeleza business plan angetengeneza kiwanda cha kutengeneza zile bidhaa au cha kuchakata zile bidhaa. Kwa hiyo Serikali inakosa vingi sana na hayo mambo yanafanyika. Wizara yangu imeshafanya ukaguzi sasa hivi tumeshapata zaidi ya ekari laki moja ambazo zimeshakopewa kwa utaratibu huu. Tumeshuhudia madalali kutoka nje ya nchi wakija kunadi ardhi za watu ambao wame-default lakini wamekopa nje ya nchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo marekebisho haya Waheshimiwa Wabunge hayakuletwa kimchezo mchezo. Naamini kwa sababu sisi Wabunge ni wazalendo namba moja ndiyo maana tumeunga mkono hoja hii. Nataka kuwaondoa mashaka kwamba hoja hii haina mgongano wowote wa kimaslahi na benki. Kamishna baada ya wewe kukopa, kabla hujakopa, Kamishna hana habari. Tuna kwambia ukishakopa baada ya miezi sita umeshakopa mpe tu taarifa kamishna kwamba nimekopa kiasi hiki na niko katika process, hii basi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, si kwamba miezi sita kwamba umeshamaliza, lakini ujue mpaka unapopeleka business plan benki. Unapokopa Kamishna hana habari, ukishakopa basi mjulishe Kamishna na sisi kama Serikali tuna vitengo vyetu vya kufuatilia. Kwa sababu kule benki na kwenyewe nao ni binadamu Loan Officers wamekuwa wanadanganya watu wengine. Wanaweza ku-collude na mkopaji lakini benki sipate faida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho nataka kusema kwamba mikopo ambayo watu wamekopa kwa kutumia dhamana ya ardhi ambayo haijaendelezwa hati zile zinafutika, sisi tunawashauri benki…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana na nawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge kwa kuunga mkono.
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na 2) wa Mwaka 2021 (Toleo la Kiingereza)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana na ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wengi ambao wamechangia vizuri katika hoja ya Muswada huu wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, niseme tu kidogo kwamba baadhi ya Waheshimiwa wamezungumzia mambo kadhaa kuhusiana na sheria hii inayohusisha Mabaraza ya Ardhi. Kilichofanyika hapa, la kwanza ni kuondoa utumishi wa muda kwa Wenyeviti wa Mabaraza, hawa Wenyeviti waliopo hivi sasa walikuwa wanateuliwa na Waziri kwa kipindi cha miaka mitatu mitatu na kwa sababu ni utumishi wa muda basi kulikuwa na mashaka kidogo kwamba pengine mtu akifanya miaka miwili, mitatu ule mwaka hata udhibiti wake ulikuwa ni mgumu sana, hata mamlaka ya udhibiti na nidhamu ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu hata wakikosea ilikuwa inanilazimu niteue Tume ya Majaji kwenda kupekua huko, inachukua muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, pia ajira zao hizi za muda zinakuwa ngumu, ndiyo maana Serikali sasa imefanya marekebisho kwamba hawa wawe watumishi kama kawaida, kama Mahakimu, watumishi wa Serikali wa kudumu. Zitangazwe nafasi, Mheshimiwa Salome alifikiri kwamba labda hatutatangaza, nafasi hizi zitatangazwa kama zinavyotangazwa, waombaji wataomba lakini wakishapewa watakuwa watumishi wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana hivi sasa Waziri wa Ardhi ameshatangaza Wilaya ambazo zinastahili kuwa na Wenyeviti wa Mabaraza zaidi ya 150, waliopo sasa hivi Wenyeviti hawa wa muda hawafiki hata 60. Kwa hiyo, unakuta Mwenyekiti mmoja anakwenda Wilaya tatu hadi Wilaya tano lakini tukiwa na watumishi wa kudumu wa Serikali wenye sifa tutakuwa nao kila Wilaya. Kwa hiyo, tuna hakika kwamba kwa utaratibu huu tuna uwezo wa kuwa na Mwenyekiti ambaye kwa lugha nyingine ni kama Hakimu wa Mabaraza ya Ardhi kila Wilaya kwa pamoja. Kwa hiyo, tumerahisisha hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia kuwa na mashaka tu kwamba huyu mtu hana uhakika na ajira yake kila baada ya mwaka wa tatu anajua ah! Labda Waziri atanitoa. Sasa huwezi kujua mwaka wa mwisho, si lazima nae ajiwekee maana yake hana kinga! Lazima ajiwekee kinga, kila baada ya mwaka wa tatu lazima ajiwekee kinga. Kwa hiyo, hii inatusaidia sana Waheshimiwa Wabunge wengi mmeniuliza hapa kwamba tutapata lini Wenyeviti Wenyeviti! Ni taabu sana kuwapata hawa kwa muda.

Mheshimiwa Spika, vilevile ukiangalia taaluma na kazi wanazofanya ni kama Mahakimu wa Mahakama za kawaida lakini hata ulipaji wao unakuwa ni tofauti kidogo. Kwa hiyo, hii Waheshimiwa Wabunge tumeifanya vizuri ili kurahisisha utendaji kazi na kuweka uwezekano wa kuwa na Wenyeviti wa Mabaraza katika Wilaya zote za Tanzania.

Mheshimiwa Spika, pia kwenye Kata. Sheria hii tumefanya marekebisho kwenye Kata kule mnakumbuka na ninyi mlikuwa mmependekeza siku nyingi, walikuwa wanafanya maamuzi na mnajua Wenyeviti, Kamati za Ardhi za Mabaraza ya Kata bahati mbaya sana unaweza kukuta wenye taaluma ya ardhi hakuna hata mmoja lakini walikuwa wanafanya uamuzi, maamuzi kabisa mpaka ya kukamata na mali za maskini, wanaita na madalali kabisa wanakamata mali za maskini. Kwa hiyo, sheria hapa inaweka utaratibu kwamba huku watafanya tu usuluhishi lakini maamuzi yatabaki kwenye Baraza la Ardhi la Wilaya. Huku watafanya usuluhishi ule wa kirafiki yaani mediation na baadaye ikishindikana wanaenda Wilayani badala ya kufanya maamuzi huku ambako kwa kweli wanaosimamia Mabaraza yale ni shida kidogo, kwa hiyo, haya ndiyo marekebisho makubwa ambayo yamefanyika.

Mheshimiwa Spika, ninataka nimuondoe wasiwasi Mheshimiwa hapa kwamba anasema wanapofanya mashauri lazima Mwenyekiti wa Baraza aende site kuangalia mgogoro, ni kweli wanaenda mpaka sasa na siyo lazima kutunga sheria maalum kwa sababu kwa sheria tu zilizopo civil procedure inaruhusu kufanya mambo haya siyo lazima kuwe na sheria nyingine hivi sasa wanalazimika kwenda huko.

Mheshimiwa Spika, hata Wakili mmoja akipendekeza ndani ya Mahakama kwamba anapenda jambo hili likaangaliwe kwenye site ya mgogoro Mwenyekiti wa Baraza anakwenda. Hata sasa inafanyika lakini siyo kila mahali lazima muende site, kuna jambo mnaweza kwenda site ikishindikana kama Wakili wako anaona jambo hilo haliwezi kuamuliwa mpaka muende site anaweza akaomba Mahakamani wakaenda site.

Mheshimiwa Spika, hivyo nilitaka niseme tu kwamba yote haya ambayo yamezungumzwa na Waheshimiwa Wabunge ndiyo yaliyoifanya Serikali ikalazimika na Muswada huo wa Marekebisho madogo ya Sheria hii na ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote mmeunga mkono marekebisho haya, nataka kuwahakikishia kwamba baada ya marekebisho haya, marekebisho haya yatasaidia sana utendaji wa haki wa Mabaraza haya kuanzia kwenye ngazi ya Kata mpaka ngazi ya Wilaya, hasa kwenye Kata ambako maamuzi mengi yalikuwa yanafanywa na watu ambao pengine hawana taaluma ile ya kufanya maamuzi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha na ninaunga mkono hoja. (Makofi)