Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Dennis Lazaro Londo (1 total)

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali na Tanzania imeweza kufikia viwango vya uchumi mpana:-

(a) Je, ni nchi gani nyingize Afrika Mashariki zimeweza kufikia?

(b) Je, kama zipo hizo nchi, kwa nini sasa hizo zisianze halafu nyingine zitajiunga baadaye?
NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI (MHE. DENNIS L. LONDO): Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi, hakuna nchi mwanachama iliyokidhi vigezo vyote vya kuoanisha uchumi mpana. Tanzania ndiyo pekee ambayo imekidhi vigezo vinne kati ya vitano vya kuoanisha uchumi mpana kama inavyoelekezwa na Ibara ya Sita ya Itifaki ya Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Ibara ya Sita ambayo inahusu uanzishaji wa uchumi mpana, nchi nne ambazo ni Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda ndiyo nchi pekee ambazo zimetimiza vigezo vya kuwa na wastani wa mfumuko wa bei usiyozidi asilimia nane tangu mwaka 2021. Aidha, nchi tatu ambazo ni Tanzania, Rwanda na Kenya ndizo ambazo zimekidhi kigezo cha kuwa na akiba ya fedha za kigeni ambazo zinatosheleza mahitaji ya ununuzi wa bidhaa ambazo zinamudu ndani ya kipindi cha miezi minne na nusu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia nchi tatu wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Sudani ya Kusini na Uganda ndizo ambazo zimefikia kigezo cha Deni la Taifa kutozidi 50% ya pato ghafi la Taifa. Hivyo, hakuna nchi mwanachama ambayo imekidhi kigezo cha kuwa na kiwango cha juu cha nakisi ya bajeti ikijumuisha misaada isiyozidi asilimia tatu ya pato ghafi la Taifa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)