Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Jesca Jonathani Msambatavangu (47 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nachukua nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi na nawashukuru wote kila mmoja kwa nafasi yake aliyechangia uwepo wangu mahali hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote napenda kupokea Hotuba ya Rais kwa mikono miwili na nampongeza sana kwa sababu sisi kama Wabunge, tumepokea dira na tumepata kitendea kazi cha kufanyia kazi katika uwakilishi wa wananchi wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa, naanza na sekta ya utalii, katika ukurasa wa 46, Mheshimiwa Rais ameongea kwamba ni sekta ambayo itawekewa mkazo mkubwa kutokana na umuhimu wake katika Taifa letu; kwanza, katika mchango wake mkubwa katika kuongeza pato la Taifa, pia ni sekta ambayo itatoa ajira kwa vijana wetu kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawapongeza upande wa Serikali; wenzetu hili wameshalianza, nasi watu wa Kanda ya Kusini au Southern Socket Tourism tunawashukuru sana kwa sababu tumeletewa mradi mkubwa wa REGROW ambao umetengewa dola milioni 150 kwa ajili ya kuendeleza utalii kusini; Iringa pia haikuachwa, itakuwa hub ya utalii huo, nasi tumepewa dola milioni sita kwa ajili ya kuanzisha Tourist Resource Center pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunawashukuru sana kuhusu msitu wa Kihesa Kilolo. Namshukuru Waziri wa Maliasili, tumeongea hili na amelifanyia kazi kwa haraka sana. Naamini ujenzi unaanza pale mara moja ili nasi southern socket au ukanda wa kusini tuwe sehemu ya kuchangia pato la Taifa kupitia utalii. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia naomba, ili utalii uweze kuwa mzuri, tunahitaji kuboresha huduma zetu kwa watalii. Kwanza, naomba tuboreshe huduma ya upatikanaji wa ubadilishanaji wa fedha za kigeni. Watalii wetu wengi wanapokuja kwenye zones za utalii wanakosa huduma hii kutokana na mchakato ambao ulipitishwa kwenye maduka yetu ya kubadilisha fedha za kigeni. Kwa hiyo, tunaomba Serikali iangalie hasa kwenye hizi nyanda za utalii, ni namna gani inalegeza masharti ili tuweze kuwahudumia watalii na lile neno lao, watakaporudi tutapata watalii zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile kuhusu kuboresha huduma za miundombinu, tunaomba barabara. Tumeshaanza kuboreshewa kiwanja cha ndege, sasa tunaomba barabara ile ya National Park, watakaposhuka pale ile barabara ya kutoka Iringa mpaka Ruaha National Park ya kilometa 104 basi nayo iboreshwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja kwenye suala la elimu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa ukarabati mkubwa uliofanyika kwenye Shule za Sekondari kongwe, tunaomba juhudi zile zile zielekezwe kwenye shule zetu za msingi kwani nazo zimechakaa.

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la mtaala haliepukiki, tunaomba Wizara ya Elimu tujipange kubadilisha mtaala kwa watoto wetu ili watoto wetu waweze kuajirika na kujiajiri nje na ndani ya nchi yetu. Tunaomba sana elimu ya kujitegemea irudishwe kwenye shule zetu ili watoto hawa wanapotoka waweze kujifunza kujitegemea. Vile vile tunaomba kuwe na masomo compulsory kama ya ujasiriamali kuanzia kwenye level ya shule ya msingi ili watoto waweze ku-develop visions zao wenyewe tangu wakiwa wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunashukuru sana kwamba kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais pia amesema kutakuwa na program mbalimbali za mafunzo ya ujuzi na maarifa ili kukuza uchumi. Tunaomba sasa vyuo vikuu vilivyoko kwenye zones zetu na mikoa yetu, kama kile Chuo Kikuu cha Mkwawa, kiwe independent, kiweze kusimama chenyewe ili kisaidie kutengeneza program zao kwenye kanda zetu zile ili kuwasaidia watoto wetu waweze kupata maarifa ya kufaidika na mazingira yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tusiendelee kuwa ni Vyuo Vikuu Shirikishi halafu vinaendelea kupokea program zinazopangwa Dar es Salaam wakati kule kule zinge-scan mazingira ya kule, zingepanga program za kule kule, zitawasaidia wananchi wetu. Tunaomba sana hili lichikuliwe. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye suala la uchumi, tunashukuru kwa ajili ya uzalishaji, lakini tunaomba sana mafunzo ya ujasiriamali yatiliwe mkazo kwa sekta binafsi lakini kwa informal sector na formal sector. Tunaomba makundi yale ya Madereva, Wamachinga, makundi ya bodaboda, yapewe mafunzo ya ujasiriamali ya kimkakati kutokana na kazi zao. Mafunzo ya ujasiriamali yasiandaliwe tu kwa ujumla, lakini yaende specific. Kwamba hawa ni Mama Ntilie, katika sekta yao tunawaboresha vipi? Hawa ni madereva wa bajaji, katika sekta yao tunawaboresha vipi? Tusitafute kupeleka mafunzo ambayo ni mafunzo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa kengele imeshagonga.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, dakika moja. Kulinda tunu za Taifa, naomba hili niliseme. Hapa yameongelewa masuala…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca kuna majina mengi hapa mbele. Ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Mimi nitaongelea jambo moja tu kuhusiana na urasimu katika utekelezaji wa Mpango huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitaomba nitoe mfano mmoja ambao uliwahi kutokea hapa kwetu, inaweza kuwa siyo hadithi nzuri sana, lakini itatusaidia kukumbuka. Kuna wakati fulani ilitokea hadithi ya mafuta ya upako; yalimwagwa kwenye carpet na watu wakapita wakiwa na malengo ya kupona pale, huzuni zitabaki pale, wakiwa na malengo kwamba kama waliingia na mawazo, yataisha pale na kwamba wataondoka hawana stress. Sasa basi, Mpango huu naufananisha kama mafuta ya upako, kumbe ndani ya yale mafuta ya upako kulikuwa kuna utelezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya watu kutoka wamepona pale, wakawa wanakatana mitama mle, wanalaliana, wanakanyagana, wengine wakatoka wamekufa, tukapata majeruhi na wengine ambao walikuwa mahututi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango ni mzuri na mambo yamekaa vizuri. Wasiwasi mkubwa ni urasimu ambao hauna maana katika utekelezaji wa Mpango. Lazima tukubaliane sasa kama tunakwenda kama nchi, tushirikiane mihimili yetu yote mitatu, Wizara zetu zote, pamoja na Idara zetu zote, tushirikiane na vyombo. Kwa sababu kuna wakati fulani tunaweka mipango mizuri lakini unaweza kukuta kuna mahali tunaweka vitu ambavyo vinasababisha tusiende mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tumeongea kwenye Mpango kwamba tuna miradi ya kimkakati. Miradi hii mingine imeanza siku nyingi, bado inahitaji gharama ndogo sana. Sasa kwa sababu ya urasimu usiokuwa na maana, utakuta kuna vikwazo vinatokea tu ama kutoka katika Idara moja ama kutoka katika Idara nyingine au kutoka katika Wizara fulani au kutoka katika chombo fulani tunakuwa hatuendi mbele.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tuna miradi kwa mfano ya utalii, tayari tuna capital kule kwa sababu tayari tuna Wanyama, tuna Mbuga za Wanyama, tuna kila kitu. Kuna miundombinu tu kuielekeza kufika kule kwenye utalii ili sisi tuanze kukamua dola, kunaanza kutokea urasimu usiokuwa na maana. Halafu wakati mwingine ku-connect sasa; tumeboresha viwanja vya ndege, tumenunua ndege, zinafika kwenye viwanja vya ndege. Kutoka pale kwenye kiwanja cha ndege kufika kwenye Mbuga ya Wanyama hapaingiliki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa huu ndiyo tunasema utelezi kwenye upako. Utelezi ndani ya Mpango, kwa nini sasa? Hii miradi ya kimkakati kama ya utalii ambayo inaweza ikatengenezewa tu miundombinu na tukaanza kupata fedha, isitolewe hiyo fedha tukafanya mambo haya na tukatekeleza ili tuanze kukamua hela huku wakati huo huo tukiboresha huduma zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tuna Wizara ya Viwanda na Biashara, tuna Wizara ya Vijana na Ajira, wanafanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba wanatengeneza ajira kwa vijana wetu. Tuna Wizara zinafanya juhudi kubwa au Idara zinafanya juhudi kubwa kuua vyanzo hivyo vya ajira. Ndiyo maana hapa unakuta Waheshimiwa Wabunge tunakuja kulalamika, ni kwa nini bodaboda zijae kwenye Vituo vya Polisi na vijana wetu wakati wamejiajiri na tumeruhusu kama sehemu ya ajira? Huo ndiyo unakuwa utelezi sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, tumekubaliana kwamba tunavutia wawekezaji kwenye Taifa hili. Tuna Wizara ya Uwekezaji kwenye nchi yetu, tulikuwa na TIC wakati ule inavutia wawekezaji kwa kuweka mazingira mazuri. Kuna Idara nyingine wanapofika ndani ya hii nchi, wanazuiliwa vibali, wanaanza kuwekewa urasimu wa vibali kibao, sijui kodi, vitu kama hivyo. Huo ndiyo utelezi sasa kwenye Mpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka uchumi shindanishi kikanda na Kimataifa. Leo hii tunataka Watanzania wakauze bidhaa kwenye Soko la Afrika Mashariki, Soko la SADC na Soko la AGOA. Rudi sasa kwenye utelezi; namna ya kupata Passport, namna ya kupata Hati tu ya Uraia, namna ya kupata cheti cha TBS, utelezi! Kina Mama wanatengeneza products zao, kuwekewa tu alama ya TBS kuna milolongo mirefu, akina mama wanashindwa kwenda mbele, tunashindwa kufanya biashara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati mwingine tunadanganyana humu. Unapofuatilia kibali kwa ajili ya wawekezaji au kuleta wawekezaji, utasikia kuna vyombo, kuna vyombo, kuna vyombo; sasa sijui ni bakuli, sijui ni thermos, sijui ni chupa! Vinazuia! Hapa vyombo vinafanya utafiti, uongo mtupu! Tunadanganyana, tunaweka utelezi kwenye Mpango. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii tuna miradi mikubwa ya umeme hapa imeanzishwa, kama Julius Nyerere Stiegler’s Gorge. Ule ni mradi ambao utatusaidia. Wapo Watanzania wanaubeza, zipo Idara nyingine ni utelezi. Wapo Watanzania wengine hawaoni umuhimu. Mradi ule utatuongezea nguvu ya umeme, utatupunguzia production costs, utasababisha bidhaa zetu kushuka bei. Hivyo utasababisha nasi tuweze ku- compete kwenye soko la East Africa na Kikanda. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi ule ukiwekwa maji pale, umeshatengewa tena hekta zaidi ya 150,000 kwa ajili ya irrigation scheme unakwenda kwenye ile irrigation, utakutana na watu wa bonde. Utelezi hutuzuia sasa tushindwe kufanya irrigation schemes. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kuna vitu ambavyo nasema kama hatutashughulika na utelezi kwenye mafuta ya upako, tutaondoka tumekufa, tutaondoka majeruhi. Lazima Serikali yenyewe ijipange. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nilikuwa nasoma taarifa ya CAG, anaongelea kuhusu kukusanya mapato na TRA jinsi ilivyokusanya, lakini moja ya mapendekezo ya CAG, aliwapa mapendekezo kama 338; ni asilimia 19 tu wameyafanyia kazi, mapendekezo 266 wameshindwa kuyafanyia kazi. Asilimia 38 ya mapendekezo 266 ni kwa sababu yako Idara nyingine, kwa hiyo, yameshindwa kutatuliwa, Idara nyingine imeleta utelezi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndugu zangu kama hatutaangalia haya na kuangalia urasimu tuliouweka ambao unatukata mtama wenyewe kwenye upako, hatuwezi kufika mbali. Lazima sasa Serikali iamue kwa nia ya dhati kuondoa urasimu usiokuwa na maana. Kama tumeamua tunajenga ajira kwa vijana wetu, walindwe; machinga walindwe; bodaboda walindwe; na mama ntilie walindwe. Wale hawajaenda shule lakini tuna wasomi, Maafisa Biashara wetu, siyo kazi yao kuingia kuwasumbua wale, ni kwenda kuwaelimisha wafuate taratibu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, siyo kazi ya Jeshi la Polisi tu kukamata bodaboda peke yake, ni kutoa na elimu. TRA leo ni chombo kinachokusanya mapato, siyo kazi yao kuwa innovator wa kesi kwenye nchi hii. Zipo kesi za biashara kwenye Mahakama ya Rufani 1,097 ambazo ziko created na TRA, wamehama kwenye lengo lao la msingi, wamehamia kwenye ku-create kesi. TRA wana kitengo cha kutoa elimu kwa wafanyabiashara, watoe elimu kwa wafanyabiashara na sio kuwavizia wafanyabiashara wamekosea ili wao wapate mazingira ya kuwashtaki. Kwa hiyo lazima tuondoe utelezi na urasimu usiokuwa na maana, twende tukatekeleze hii miradi ya kimkakati. Tujenge barabara kwenda kwenye National Parks zetu. Kwa mfano sisi tuna barabara ya kutoka Iringa - Ruaha National Park, ni park ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani. Ina tembo wakubwa kuliko National Park yoyote lakini miaka yote barabara iko kwenye Ilani lakini haitekelezeki mahali ambako tungekwenda kuchukua dollar bure. Unaona watu wanaingia Serengeti wanakwama kule ndani, wakati vitu tayari viko pale. Tuache, twende tukaamue sasa kufanya kazi kwa ajili ya ku-implement Mpango huu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tukifanya hivyo tutakwenda vizuri. Tukiangalia hawa watu wa chini, ameongea Mheshimiwa Mbunge mmoja kama tukiangalia hii micro enterprise ya wafanyabiashara wadogo tukaielimisha, leo tunaongelea ujuzi, kutoa elimu ya ujasiriamali. Tuna mkakati gani wa kuwapa hiyo elimu? Tunawapa mafunzo ya ujasiriamali kwa mtindo gani? Au tumeweka tu tunatengeneza mifuko ya wajasiriamali, sijui ya wafanyabiashara wadogo wadogo, hiyo mifuko inaishia juu. Kuna mmoja amesema hapa kuna Benki ya Kilimo ina majengo mazuri Dar es Salaam, Dar es Salaam kuna kilimo gani? Haya ndiyo mambo ya utelezi, yaani vitu ambavyo watu wanatengeneza dili ambazo hazieleweki! Twende kwenye grassroot tukatatue matatizo ya wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunaongelea akinamama wajengewe vituo vya afya, zahanati na hospitali, huduma za uzazi ziwe bure, wewe unakaa unazuia fedha ya matibabu kwa akinamama wasitibiwe, una hila gani? Utelezi huu. Sisi tunataka kuongeza wapigakura kwenye nchi hii, tunataka kuongeza raia bora kwenye nchi hii, wazaliwe watoto bora kwenye nchi hii, unazuia fedha bila sababu, huo ni utelezi. Tunataka sasa urasimu na Wizara zijione kama kila Wizara ina heshima, maana ipo ile kuona kwamba labda Wizara hii kwa sababu sisi ni Fedha, basi ni wa muhimu sana, samahani kaka yangu Mheshimiwa Mwigulu, wewe ni rafiki yangu sana. Labda wewe ndiyo wa maana zaidi kuliko yule Waziri wa Wizara ya Kilimo au Waziri yeyote, hapana! Kwa sababu ili Waziri wa Fedha awe na fedha, ni lazima kilimo kichangie mapato, ili awe na fedha, lazima bodaboda wachangie, ili awe na fedha, lazima mama ntilie wachangie. Leo hii tuna vitu vya ajabu, tunatakiwa kuangalia mambo ya utelezi, urasimu wa kijinga. Kwa nini tusifikirie Watanzania wetu…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Kengele ya pili imegonga Mheshimiwa…

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: … wanaofanya vizuri tukawatumia sisi wanaanza kuonekana kutumika kwanza Afrika Kusini.

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Naunga mkono hoja lakini utelezi uondolewe. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nami nitumie nafasi hii kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niongelee tu kwa ujumla sekta hii ya usafirishaji, kwanza sifa zake mahususi kiulimwengu ili sekta hii ionekane iwe bora. Sifa ya kwanza, ni lazima kuwe na mifumo mizuri iliyotengenezwa ya usafirishaji kwenye miji au tunasema well designed inter-city systems. Sifa nyingine ni ku-avoid unnecessary traffic flows au tunasema ni kuepuka ile misongamano isiyokuwa ya muhimu.


Mheshimiwa Naibu Spika, sifa nyingine ni kuhakikisha kwamba mifumo ya usafirishaji inapunguza gharama. Sifa nyingine ni kuhakikisha mifumo ya usafirishaji wetu inakuwa salama na ya uhakika. Nyingine ni kuhakikisha kwamba tunaweka mifumo mizuri ya usimamizi ya miundombinu yetu ya usafirishaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nichangie pale kwenye kuweka mifumo mizuri ya usafirishaji kwenye miji yetu. Ndugu zetu hawa wa Wizara ya Ujenzi wao ni wataalam na bahati nzuri sana Waziri tuliyenaye alikuwa Katibu wa Wizara hii. Napenda kushauri jambo moja kwenye Wizara hii. Kwanza, kuangalia mifumo ya usafirishaji kwenye miji yetu. Ipo miji imekuwa sasa kama ni vigogo vya usafirishaji kwenye mazao yanayotoka kwenye mikoa mbalimbali na yanayotoka kwenye vijiji vyetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, umeongea kuhusu Mji wa Mbeya asubuhi, lakini mimi nitaongea kuhusu Mji wa Iringa pia. Miji ile inapita au ipo katikati ambapo barabara kubwa zinapita katikati ya ile miji. Tunafahamu katikati ya miji mikubwa kama ile, kuna shughuli nyingi za kibinadamu zinafanyika. Sasa wenzetu hawa ni wataalam, walipokuwa wanajenga miundombinu ya barabara hizi, wakifungua mikoa mingine walijua kabisa geti kubwa litakuja kuwa ni Iringa; walijua barabara kubwa itakayosafirisha magari makubwa yote kutoka kwenye mikoa sita inayotegemewa kulisha nchi hii kwenda kaskazini na Kanda ya Ziwa mikoa sita itapita katikati ya Mji wa Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, walijua kabisa kwamba nchi zile ambazo ni landlocked countries, kwa mfano Zimbwabwe, zinapita katikati ya Jiji la Mbeya. Kwa hiyo, ilitakiwa wenzetu hawa watusaidie kutengeneza miundombinu ya kufungua yale majiji yasiwe barrier. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii viazi vinatoka Songwe vinaozea Mbeya, au vinaanza kuungua Mbeya; vikifika Iringa vinataka kupita vije Dodoma viende Mwanza, vinafia Iringa. Kwa sababu miji haipitiki. Ni sawa na umetengeneza barabara ya njia sita halafu unakwenda kuipitisha kwenye daraja la mita moja, lazima uvunje lile daraja; na ndicho kinachofanyika kwenye miji yetu. Mle kwenye miji ndiyo maana sasa kumekuwa na matatizo. Sisi Wabunge tumeongezewa kazi nyingine nje ya ilani kwenda kuanza kuzuia migomo inayotokea katikati ya vyombo vinavyopita kwenye miji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, umeongelea mgomo uliotokea Mbeya; wiki iliyopita sisi Iringa tulikuwa tuna mgomo wa watu wa barabara, bajaji na bodaboda. Sasa hivi ninavyoongea, kuna vijana wengine pia wamegoma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sisi tunafahamu, nami nawaomba Waheshimiwa Wabunge, mchawi bwana mkabidhi mtoto akulelee. Mimi nafikiri sasa TARURA tuwakabidhi hawa hawa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, iwe chini yao na wawe na full mandate ya kui-control TARURA ili sasa kule kulaumiana kwamba hapa alitakiwa atengeneze TARURA, kusiwepo. Wasimamie wenyewe kuanzia juu mpaka chini ili wanapofika kwenye mji ule waweze kuwasiliana na wenzao wa TARURA waangalie ni namna gani sasa mji huu tunaufungua? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, Iringa tuna bypass. Tunapoongelea miji hii mikubwa, kwa mfano pia Songea kuna bypass, Mbeya kuna bypass. Sasa hizi bypass waliziweka kabisa kitaalam, wamelipa fidia, wamefanya kila kitu, yaani kinachotakiwa ni kuzijenga. Kwa mfano, Iringa tuna kilometa 7.3, ili tuchepushe yale magari makubwa yapite pembezoni activities nyingine katikati ya mji ziendelee. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo tunakuja kwenye ile sifa nyingine ya kupunguza unnecessary traffic flows kwenye miji. Hizo ni unnecessary, tungekuwa tumejenga zile bypass tusingekuwa na sababu ya magari kuja pale. Njegere za akina mama zinaozea kwenye barabara, viazi vya vijana wetu…

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Twaha Mpembenwe.

T A A R I F A

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tu nimpe taarifa mzungumzaji kwamba tatizo hilo la kutoweza kuzijenga barabara kwa wakati kama mifano tunayopewa ya barabara ya kutoka Mbeya kwenda Tunduma na barabara nyingine za Iringa, barabara ya Kibiti mpaka Mloka, hii yote ni kutokana na sababu ya mambo ya utelezi. (Kicheko/Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Msambatavangu, unaipokea taarifa hiyo?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea taarifa hiyo kwa mikono miwili. Niseme kwamba huu utelezi ndiyo tunataka utolewe. (Kicheko/ Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bypass zijengwe kwenye miji yetu. Kwa nini tunasema bypass zijengwe? Kwa sababu mijini ndipo huduma za jamii zinakopatikana, watu wetu wanakwenda kupata huduma kule. Watu wanafia barabarani. Pia mijini ndiko kwenye masoko. Wewe umefikisha bidhaa mpaka stendi inashindwa kufika sokoni kwa sababu tu ya traffic jam. Sasa uangalie, huo ndiyo utelezi tunasema. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, angalia Mji kama Iringa, kwanza barabara yenyewe ya Tanzam inapita iko kwenye mlima, malori makubwa yote yanakwama pale. Lori likianguka katikati pale, Iringa haipitiki kwenda chini, kwenda juu; na malori ya dagaa zilizotoka Mwanza zinaozea pale. Tunawaomba wenzetu waangalie haya, tunaomba sana watusaidie. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ninachotaka kuongea hapa, sisi tumepitisha hapa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Sasa inaonekana kama Mpango tunaoupitisha hauendani na mipango ya Wizara nyingine. Nilimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi wakati anaapa, alisema kazi yake ni ku-coordinate hizi Wizara. Tunaomba kupitia Bunge hili aka-coordinate mambo ili Mpango wetu wa Miaka Mitano uende sambamba na mipango ya hizi Wizara.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo tunataka sekta ya utalii ichangie watalii wafike milioni tano ifikapo 2025, na share kubwa tunategemea kupata kwenye utalii wa Southern Zone. Leo tumeiwekea barabara inayokwenda National Park kujenga kwa usawa wa kilometa 1.5, barabara ya kilometa 104, hivi tunapomaliza huu Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2020 - 2025 ni kweli tutakuwa tumefikisha sisi kuchangia pato hilo la Taifa, kufika dola bilioni 6.0? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine tunajiuliza hii mipango tumeweka Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano halafu bado tunaongelea kuunganisha madaraja tu hatuongelei barabara zile zinazokwenda kwenye strategic areas. Tunaongelea kilometa mbili, kilometa tano kwenda kwenye miradi ile ya kimikakati ya kutuongezea pato la Taifa. Je, tupo serious? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana ndugu zangu tuwaangalie Watanzania kwa jicho la huruma, tuwaangalie hawa vijana wetu wa bajaji, wa bodaboda waliopo mijini kwa jicho la huruma. Askari wanafanya kazi kubwa yaani mpaka wanashindwa sasa. Leo TARURA inapewa fedha ya maintenance tu, asilimia 80 mpaka 90, lakini kwa maana ya miradi ya maendeleo wanapewa asilimia 10 mpaka 20. Miji yetu inakua, Waheshimiwa Wabunge tunaposema maintenance maana yake unapewa fedha za kutunza barabara tu zilizokuwepo, hawapewi pesa ya kuongeza mtandao wa barabara. Miji yetu sisi inakua, Iringa TARURA haijapewa fedha ya miradi ya maendeleo na mji unakua wale watu kule wanafuatwa vipi. (Makofi)


Mheshimiwa Naibu Spika, hizi bajaji sijui bodaboda zinafikaje kule kwenye makazi ya watu? Kama watu wanapewa fedha ya kutunza barabara ambazo hazipo, mtoto huyu akabidhiwe wenyewe, wakabidhiwe hawa Ujenzi na Uchukuzi wamchukue TARURA wakae nae ili yanapotokea matatizo tusilaumu kwamba huyu yupo TAMISEMI, tujue ni wenyewe Uchukuzi asilimia mia wamefeli hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba TARURA wapewe, nashukuru wamenipatia milioni 120 kwenye barabara yangu inayopita Kleruu, nayo inatakiwa itengenezwe kwa kiwango cha kokoto.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kiwango cha kokoto si kiwango. Sasa nashukuru kwa ajili ya hilo lakini niwaombe sana tujaribu ku-coordinate mpango wetu na mambo yetu tuliyoyapanga lakini tujaribu kuangalia hizi by pass kwenye majiji zifunguliwe ili huduma zingine za kiuchumi ziendelee. (Makofi)



Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Niipongeze Serikali kwa mpango mzuri ambao imetuletea. Pamoja na kuipongeza kwa sababu imekuwa ni bajeti ambayo imekwenda kugusa maeneo muhimu sana ya wananchi wetu na kutatua changamoto za wananchi wetu, lakini bado nina mchango katika sehemu tatu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwenye suala linalohusu elimu, kwa kuwa ili tuendelee tunahitaji tupate watu ambao watakuwa na elimu bora. Niombe sana katika mabadiliko ya mtaala wenzetu watu wa elimu waangalie na kuzingatia mazingira yetu ya Tanzania na kuona namna gani vijana wetu watafundishwa ili waweze kupambana na mazingira ya nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia na elimu yetu imekuwa nadharia sana, sio ya vitendo. Watoto wanakaa darasani muda mwingi sana, hawana practical, kwa hiyo wanapotoka inakuwa ni shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, kipo kipengele cha ujasiriamali, ni cha muhimu sana, mtoto lazima ajifunze kuwa ana maono au ana vision tangu kwenye elimu ya msingi. Kwa hiyo lazima tuangalie namna gani tutaingiza kipengele hicho kwenye elimu yetu ili tuwe na watoto wenye mipango kuanzia wadogo watengeze road map ya maisha yao kuanzia shule ya msingi mpaka watakapomaliza.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema maneno niende kwenye suala lingine linalohusiana na masuala ya miundombinu, leo tunajadili bajeti ya Serikali, lakini zamani wakati Taifa letu linaanza kwenye nchi hii tuliwahi kuwa na program ya vijiji vya ujamaa. Nia ilikuwa ni kusogeza huduma karibu na wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, leo hii katika mipango yetu ya ardhi hata tunapokuwa kwenye shughuli zetu za kisiasa kutafuta kura, unaweza ukaona kwamba tumeacha sasa ile program atuangalii ni namna gani tunawapanga watu wetu kwa makazi na namna gani tunaigawa ardhi yetu kwa ajili ya masuala ya kilimo na kazi zingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, watu wanaondoka, anakwenda anahamia kwenye mlima alikuwa mwindaji, anahamia huko analeta na mke wake na watoto wanazaliana wako mbali juu ya mlima na hakuna mamlaka yeyote iliyowaambiwa jamani hapa sio sehemu ya makazi, mrudi mkakae na wenzenu. Hii inazidi kutuongezea gharama na ndio maana sasa kumfuata yule mtu ili umpelekee huduma ya barabara, maji, afya ni mbali, yuko mbali na wenzie lakini tayari anataka kupata huduma kutoka kwenye Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, unaweka bajeti ya kujenga barabara kumfuata mtu au kuwafuata watu 600 ambao wako mbali, unatumia zaidi ya bilioni sita au nane na wale watu wamekaa kule wanalima mbogamboga, ukiangalia return kiuchumi pale ni hasara. Kulikuwa kuna sababu gani hawa watu wajitenge na wenzao waende mbali wakaishi peke yao, wakati wangeweza kuishi na wenzao, tukaweza kuwahudumia vizuri pale, wakiwa wamekaa pamoja. Kwa hiyo tunaomba wenzetu hawa wa ardhi waliangalie hilo na mipango yetu iwe hivyo makazi lazima yaimarishwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, duniani hawafanyi mambo mapya ila wanafanya mambo yaleyale katika ubora zaidi. Leo hapa tumevaa nguo lakini ni sawa tu na Adam na Eva walivyokuwa wanavaa nyasi, wao walivaa nyasi direct, magome ya miti na walivaa ngozi moja kwa moja, lakini sisi tunavaa ngozi zilizokuwa processed, vinakuwa viatu. Leo tunavaa magauni kutoka kwenye mimea ya pamba. Hicho ndicho tunachosema hatukutakiwa kuacha zile program za Vijiji vya Ujamaa, lakini kuitengeneza ile program iwe ya kisasa na kutusaidia zaidi kwa sasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, point yangu nyingine naomba leo kidogo tukumbushana na maneno ya Mungu humu ndani. Kwa sisi wa kristu wenye biblia ya Isaya 32 mstari wa 17 unasema: “Haki kazi yake duniani imetumwa kuleta amani, haki kazi duniani imetumwa kuleta utulivu na matumaini.”

Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ndio kazi kubwa ya haki tunaomba sana wenzetu hawa walioko Serikalini, tunapoongea watusikie na wafanyie kazi. Yapo mambo waliyofanyiwa Watanzania wenzetu kwenye nchi yetu hayana tija na yamewajeruhi na hayana tija kwa maendeleo na mustakabali wa nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, tumeongelea sana hapa maduka ya kubadilisha fedha za kigeni. Wenzetu wale wengine ukiangalia ni wajane, wenzetu wale wengine ukiwaangalia walianzisha zile biashara baada ya kupata viinua mgongo vyao, wengine walianzisha zile biashara mitaji waliipata kwa shida. Ni kweli kama Kamati ya Kudumu ya Bunge inavyosema katika Sura ya 56 ya bajeti yake na mapendekezo yake, kile kipengele cha 8.4, kwamba kulikuwa na lengo la Serikali la kuhakikisha kwamba haya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni yanafuata sheria za Serikali na kanuni za Benki Kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, operation iliyofanyika kwenye yale maduka, watu hawa bado hawakutendewa haki, tunaomba haki itendeke kwa sababu mwenye kuhukumu kwenye suala la haki ni Mwenyezi Mungu. Nchi yetu tumejipambanua sana kwamba tunamtegemea Mungu na hatuna ubishi kwenye hili. Ni kweli Mwenyezi Mungu ametusaidia na tumeona alivyotupigania hata wakati wa janga la corona, sasa basi sisi kama viongozi tufanye hiyo practice kwa matendo, kama tunamheshimu Mungu tuheshimu na watu aliowaumba sisi tuwaongoze. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuwatendee haki wale watu wanaolia kwa ajili ya vitu vyao walivyochukuliwa, fedha zao zilizochukuliwa, mali walizochukuliwa warudishiwe. Wenzetu TRA tunawaomba sana, wakati fulani unakuta Mheshimiwa Rais namshukuru sana, kwa sababu alitoa kauli mwenyewe, kwamba kweli tunahitaji kodi, lakini hatuhitaji kodi ambayo ni ya dhuluma. Tunahitaji kukusanya mapato, lakini hatuhitaji ya dhuluma ndani yake. Tukusanye mapato ambayo hata tunapokwenda kumwomba Mwenyezi Mungu atusaidie, atatusikia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tunaomba wenzetu wa TRA kwanza wawe wanaelewa, leo hii Mheshimiwa Rais anatoa kauli kwamba sasa kodi zote za miaka ya nyuma, miaka sita au saba iliyopita jamani basi, ukienda TRA ndio kwanza wanatoa demands note za kuwadai watu kodi miaka nane au tisa iliyopita. Unawauliza hili likoje, wanakuambia sisi tupo tunafuata maelekezo na sheria, ni kweli kauli ilitolewa kisiasa, lakini sisi tunafuata mwongozo, tunataka maelekezo.

Mheshimiwa Naibu Spika, naamini Rais anapokuwa anatoa, ameshafanya uchunguzi wa kina, kwa sababu yeye ana milango mitano ya fahamu ana vyombo vimeshamsaidia mpaka anafikia hatua ya kutoa tamko. Kwa hiyo wenzetu wafuate mambo ambayo tunawaambia tutende haki kwenye Taifa letu, tuwatendee haki, hii iendane na kesi zingine za biashara. Wapo wafanyabiashara wengi waliofanyiwa vitu vingi ambavyo havikuwa sahihi. Tunaomba sana kero zao zitatuliwe kesi zao na mashtaka yao yaangaliwe kwa kina ili kama kuna uonezi wowote uliofanyika, watu hawa waweze kusaidiwa na warudishwe kwenye hali ya kawaida ili tuendelee kujenga imani kwa wawekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la elimu, tumejipambanua kwamba elimu yetu haina ubaguzi na mimi hapa naomba niseme tumesema tunataka Watanzania washiriki kwenye uchumi, lakini wapo wawekezaji waliowekeza kwenye nchi hii kwenye sekta ya elimu, wamejenga shule, wamejenga vyuo, lakini namna ambavyo wakati mwingine tunawachukulia, hatuwachukulii kama ni watu ambao wanatusaidia kama Serikali kutoa huduma kwa jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba tuwachukulie kama ni watu ambao wamechukuwa nafasi ya Serikali kuwahudumia wananchi na wao wana-feel gap ya kutoa elimu kwa wananchi. Kwa hiyo suala la kutoa elimu bure, tuwasaidie basi hata hawa private pamoja na kwamba wao au shule binafsi wanachaji ada, leo Serikali inashindwa nini hata kuwachangia gharama za mitihani tu.

Mheshimiwa Naibu Spika, wale ni Watanzania wanaolipa kodi na walikuwa na haki ya kusoma kwenye public schools au kwenye shule zetu za Serikali, lakini wameamua kusomesha watoto wao kwa gharama na ndio walipa kodi wazuri wa nchi hii. Kwa nini leo shule ina wanafunzi 10 kwa sababu haijafikisha wanafunzi 35 inatakiwa ilipie wale wanafunzi 25 ada za mitihani hata kama hawapo. Kwa hiyo, katika nchi hii bado tuna malipo hewa kwenye elimu, imefanyika michakato ya wafanyakazi hewa, lakini sisi kwenye sekta ya elimu na Wizara ya Elimu bado watu wanalipa ada za mitihani hewa.

Mheshimiwa Naibu Spika, nikisema hivi namaanisha kwamba, ikiwa huna watoto 35, una watoto 10 unachajiwa fedha ya watoto 35. Hawa watu wanawekeza return on investment kwenye elimu inachukua miaka 10, ndio mtu aanze kupata faida kwa hiyo tunawaomba wenzetu wa Wizara wajue hawa ni partners wetu, hawa ni Watanzania, wamewekeza kwenye elimu, tunaomba wasaidiwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, nyaraka za elimu pia ziangaliwe. Tuna tatizo kubwa sana tunaweza kuona la kawaida, leo tunatangaza shule zote zitafunga tarehe 30 mwezi wa Sita, tunaomba tuulizane maswali, je, miundombinu ya kuwasafirisha wale watoto wetu kutoka kwenye mashule kwenda kwa wazazi wao tuna uhakika ipo?

Mheshimiwa Naibu Spika, tuna changamoto kubwa unakutana na watoto wamelala stendi, Mbunge unapigiwa simu sijui watoto wa shule gani wamekosa basi wamelala stand au mabasi ndio yametolewa mabovu wakati ule, wamepakiwa watoto wetu wanalala njiani unapigiwa, usalama wao unakuwaje? Kwa sababu mabasi yanayotumika ni yale yale ambayo siku zote ndio yanasafirisha abiria. Yakitoka mengine ni mabovu kwa sababu hakuna mtu atakayenunua basi asubiri tu msimu wa shule kufunga asafirishe tu wanafunzi. Kwa hiyo watu wa wizara tunaomba watusaidie katika waraka mbalimbali wanazozitoa na maelekezo wanayoyatoa, basi wawe wanaangalia na mazingira na hali halisi ya Watanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema maneno haya, nashukuru na naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie mpango huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango duniani ni mpango kama ilivyo mipango yote na ina sifa zake. Tumeletewa mpango na tumeusoma na taarifa yake na jinsi ulivyo. Mpango huu una chanzo chake ambacho ni Ilani ya Chama cha Mapinduzi; na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ni mkataba kati ya Watanzania na Serikali wanayoenda kuiunda na mambo ambayo wanategemea kwamba Serikali itakwenda kuwafanyia. Serikali ni Mkandarasi ambaye amepewa tenda na CCM kutekeleza yale ambayo iliahidi kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili mipango iweze kutekelezwa lazima kuwe na malengo. Malengo tumejiwekea na tunayaona yapo kwenye mpango, lakini Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inatambua kabisa kwamba, Mpango huu ndio unakwenda kutekelezwa katika ule Mpango wa Miaka Mitano ambayo tumeupitisha, ambao ndio unakwenda kutimiza dira ya maendeleo ya Taifa ambao tumeanza kutekeleza tangu mwaka 2000 mpaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa basi, ninachoona shida kwenye Mpango wetu ile kutokuwa unasomana na ule Mpango Mkuu wa Miaka Mitano kwa sababu malengo yake kama tunasema kwamba, mpango wote unatakiwa kuwa na malengo yanayopimika, yanayokuwa na muda maalum, yanayoweza kufikika, maana yake kuna sifa za malengo. Mpango huu kuna mambo ambayo ukiangalia katika miradi yetu ya maendeleo tumeweka malengo kwamba tutakuwa na miradi ya maendeleo ambayo itakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi ambayo ni ujenzi labda wa barabara. Barabara hizi zinakwenda kufungua fursa za kukua kwa uchumi, halafu barabara zile hazijawekewa muda lini zinakwenda kukamilika. Maana yake ni kwamba, yale malengo hayasaidii mpango huu wa muda mfupi kufikia mpango wa muda mrefu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tuna barabara inajengwa kuanzia Itono – Ludewa kwenda Manda, kilometa 211. Serikali inasema barabara hii imeanza ujenzi na ujue tupo kwenye utekelezaji wa Mpango huu wa Miaka Mitano, maana yake tuko mwaka wa tatu. Tumeanza ujenzi wa kilometa 50 kuanzia Lusitu mpaka Mawengi na umekamilika kwa asilimia 95. Sasa swali langu ni hili hapa, huyu mkandarasi kapewa kazi ya kujenga barabara hii kwenye Ilani ya CCM yenye urefu wa kilometa 211. Anatupa kukamilika kwa kipisi cha kilometa 50 kwa asilimia 95 ina maana gani?

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati huo hajatuambia hizi asilimia 161 zinazobaki atakamilisha katika hii miaka miwili iliyobaki. Hapa ndipo kunakuwa na tatizo la mpango na tusipowekana sawa maana yake ni kwamba, tutakuwa tunaweka hii mipango halafu haitimii. Sasa tumeshamaliza dira ya maendeleo ya miaka 25 na Serikali ya CCM inaitambua hiyo na imeeleza kwenye ilani kwamba, itaisimamia Serikali yake kuhakikisha inaandaa mpango mwingine wa dira ya miaka mingine 25, maana yake itakwenda mpaka 2050.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa najaribu kuuliza kama hatutawekeana malengo kwamba, ninyi mwaka huu mkiingia katika hii barabara jengeni kilometa 40, mwaka unaofuata tutajenga kilometa 42, mwaka unaofuata tutajenga kilometa 42, mpaka miaka mitano tufikishe zile kilometa 211 hii mipango yetu tutakuwa tunafikiaje? Kama watu watakuja tu ofisini, sisi tumejenga kwa asilimia 95 kilometa 50, ndizo ulizotumwa? Wewe umetumwa kutengeneza kilometa 211, tuambie hiyo asilimia uliyojenga katika hiyo kilometa 211, usituambie katika hizo ulizoamua wewe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni sawa na unakwenda kumkagua mkandarasi mradi, halafu anakwambia nimekamilisha kwa asilimia 90 kipande hiki, wakati wewe unajua kipande kile ni kidogo sicho ulichompa. Kwa hiyo, tunataka mpango unaokuja sasa uwe una time ya kutuhakikishia kwamba, hizi barabara tunazosema zinafungua uchumi wa Taifa letu katika miaka mitano zinaishaje? Kwa mwaka wa kwanza zinajengwa kilometa ngapi, ngapi, kwa miaka inayofuata mpaka tutakapofikia kwenye zile ambazo tunajua kabisa kwamba, ndani ya miaka mitano tutakuwa tumekamilisha ile barabara yote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama tutaendelea kujenga hizi barabara kwa kilometa moja, kilometa mbili, tunafungua uchumi. Kwa mfano, barabara ya Iringa MR mpaka Itunundu kilometa 70, kila siku wanajenga kilometa moja moja miaka 70 watakua lini kwenda kwenye uchumi wa kukua kwa asilimia nane na watu watakuwa answerable vipi? Yaani unamuulizaje mtu kwamba, wewe Wizara yako ya Uchukuzi imefanya kazi nzuri kama hukumwekea lengo kwamba, lazima barabara hizi zinazofungua uchumi ujenge kwa asilimia 40 au 50?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa ndio kwenye shida ya mpango. Kwa hiyo, mipango tunayokuja nayo huku mbele ifanyiwe mapinduzi tuambiwe barabara hii uliyosema unaijenga kwa miaka mitano umejenga kilometa ngapi? Nimejenga kilometa 150; hizi zilizobaki unamaliza ndani ya hii miaka miwili iliyobaki na kama hujamaliza kwa nini? Hapo ndipo tutakuwa tunakwenda sawa na mipango mingine yote duniani, lakini tukienda hivi itakuwa kama ile michezo ya kuchezea vile viberiti chekundu cheusi, chekundu cheusi, kila mtu atakuja atatuambia hapa sisi tumejenga kilometa mbili kwa asilimia 90. Kilometa mbili kwa asilimia 90 out of kilometa ngapi? Haya ndio maswali ya kujiuliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kikubwa ambacho kipo kwenye huu Mpango; pamoja na kwamba tunakusanya fedha, udhibiti wa fedha zetu umeendelea kuwa weak. Tumeelekeza sana kelele nyingi kwamba, Serikali za Mitaa ndiko fedha nyingi zinakopotea, lakini iko miradi hapa ambayo imewekwa na Wabunge wengine wameisema na yenyewe inapoteza tu fedha za Serikali, haina tija. Katika karne hii kuipatia taasisi fedha, unaipatia taasisi fedha bilioni moja, inakwenda kufanya ubunifu na ndio wanasema inakwenda kuwa ni kitivo cha kubuni zana za kilimo vijijini kama CARMATEC, unaipatia bilioni moja, inakuja imekutengenezea mikokoteni ya kuvutwa na ng’ombe nane. Imetengeneza sijui mashine za kubangua korosho mbili, huu ni utani wa uwekezaji kwa watu wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu ambao tunatumia gharama kubwa tumewekeza, tunawafundisha, tunawapa mafunzo, especially vijana. Tunawapeleka katika majeshi, kwa mfano JKT, wanafanya kazi kubwa sana ya kuwafundisha wale vijana uzalishaji mali, uhodari, ushujaa na wale wanaweza kufanya kazi popote. Wao JKT lengo lao la kuanzisha si kwamba kutoa ajira kwa vijana, lakini sisi Serikali ya CCM imetutuma kuandaa ajira milioni nane. Hawa vijana wanaangaliwa vipi? Wanaachwa vipi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, unamwachaje mtu ambaye umesham-train anaweza kufanya kazi, anaweza kulima, anaweza kutengeneza, anaweza kupambana na mazingira ya Kitanzania, kulala popote akaweza kulima, akafanya nini, ukamuacha kama kijana wako, kama nguvukazi, kumwendeleza na wakati umeshatumia gharama kubwa ya uwekezaji kwake. The same applies tunafanya kwa watu tunaowasomesha, tunafanya kwa vijana ambao wanamaliza vyuo vikuu, hatuna mpango kabambe kwamba, vijana wamemaliza, hawa wana elimu hii, vijana hawa wamemaliza SUA wana elimu hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunahangaika mpaka vijijini; China waliamua kwa pamoja wakasema sasa tunachukua vijana milioni tano, tunawapeleka vijijini na wengine tutawapeleka nje ya dunia wakajifunze namna ya kufanya kazi. Hawa nao waende vijijini kule, wakakae na wanakijiji, waangalie wanafanya nini, halafu watupatie njia mbadala za kufanya mambo wanayofanya kisasa zaidi. Sisi tuna mpango gani kwa vijana wetu na hizi milioni nane? Hizi ajira milioni nane tulizopewa na chama? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, rasilimali watu na rasilimali vitu hatuweki vizuri. Leo tuna LNG, mradi wa gesi, taarifa imekuja hapa kwamba, mradi ule wa gesi tumejenga barabara kuzungushia eneo lile, ndio kazi zilizofikiwa kwa bilioni nne karibu na. Tumezungushia barabara kwenye ule mradi, halafu mambo mengine yaliyofanyika kwenye mradi ule tunaendelea na utafiti wa kisayansi, tunaendelea na utafiti wa kuweka mipango, sasa kipi kinaanza kati ya kuku na yai? Unaanzaje kujenga barabara na kuzungushia eneo ambalo bado unaendelea kufanyia utafiti wa kisayansi, hujajua kwamba, utatakiwa uweke mitambo ya kiasi gani? Kwenye hizo barabara hiyo mitambo itapita au haitapita?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante. Kengele ya pili.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Naomba Mheshimiwa Waziri akija hii miradi mingine ambayo haina tija aitoe na taasisi ambazo zinachukua hela hazina tija zitolewe. Ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi pia niungane na Wabunge wengine kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungnao wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya katika Taifa letu na hasa kwa kuangalia wananchi wetu wa chini kuhakikisha kwamba anashughulika zaidi na masuala ya elimu na afya na tumeona kwa vitendo siyo kwa maneno. Nimtie moyo kwamba tupo nyuma yake na tutaendelea kupigana na kuhakikisha kwamba kazi inaendelea na zaidi sana kwa kuwa amesimama kama taa ya mabinti zetu na sisi wanawake tutahakikisha haizimi, ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo nitakuwa naongea mambo mawili na hayo yote yanahusu ukatili. Jambo la kwanza nitaongelea ukatili wa kijinsia lakini dhidi ya watoto, lakini nitaongelea pia ukatili wa kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa leo tumekaa hali ya watoto wetu kwenye Taifa hili si salama hata kidogo. Mheshimiwa Waziri amesema hapa kati ya mashtaka yaliyopelekwa mahakamani ya ukatili wa kijinsia asilimia 33 ni kwa ajili ya watoto na 67% ni kwa wanawake. Lakini nimuongezee hajasema wanaume, lakini upo ukatili pia dhidi ya wanaume na tafiti zinaonesha kabisa kiwango cha wanaume kupigwa kimeongezeka mpaka 71.7% wakati wanawake wamepigwa kwa 73.5%. Ukichukua takwimu hizo zinaonesha wanaume wanashuka kwa sababu wao walikuwa juu zaidi kwenye kiwango cha kupiga na wanawake wanapanda kwa kasi kubwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasema hivi kwa sababu hizi zote zinaonyesha namna gani sasa athari inakwenda kuangukia kwa Watoto, kwa sababu vipigo vinavyoendelea usitahimivu wa ndoa unakuwa haupo, watu wanaachana wanaacha watoto katika hali hatarishi. Katika hiyo 33% watoto wa kiume waliofanyiwa ukatili ni 11.5% na watoto wa kike ni 22%. Tunaposema watoto wa kiume wamefanyiwa ukatili wa kingono maana yake wameingiliwa kinyume cha maumbile. Ipo miaka kumi inayokuja usishangae kuona mtoto wako wa kiume anakuja nyumbani na mkwe wako wa kiume na tusije tukaanza kuleta maneno astaghfilillah, tusije tukaanza kuleta maneno God for bid, tusije tukaanza kuleta maneno Mungu niepushie mbali, atakuwa hajakuepushia mtoto wako wa kiume, atakuwa amekuja na mwanaume mwenzie na anataka kumuoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu katika watoto waliofanyiwa ukatili 3% ndiyo waliopata ushauri nasihi na kutibiwa, 7% wako mitaani na wale wanageuka kuwa makonki master na watoto wa kike 13% tu ndiyo waliopata ushauri. Nasema hivi kwa sababu sisi Iringa tumepata tatizo hili, mtoto mmoja ambaye ameweza kuwalawiti wenzie 19 ndani ya mwezi mmoja, sasa wale saba wanaobaki ambao hawajafanyiwa matibabu wala ushauri nasihi wanarudi mitaani na wanaendeleza ile tabia. Nilivyoongea na yule mtoto aliniambia kwa uchungu sana akaniambia nilifanyiwa matendo haya nikiwa nursery school miaka mitano, leo hii tumepata takwimu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri watoto walioandikishwa nursery school ni karibu 1,198,564 lakini watoto walio nje ya shule kwa maana ya pre-primary kwa data zilizoko na utafiti ulioko wa UNICEF ni 61.8%. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hatujaona mpango hapa tumesema tumewaandikisha hawa ni awali na tunapongea awali hawa ni watoto wa shule ya msingi miaka sita chini ya hapo wako nyuma na yule mtoto anasema alifanyiwa akiwa chini ya miaka sita.

Leo aliachwa amekwenda mtaani na akaniambia Mheshimiwa Mbunge nikasema nikusaidiaje kama Mbunge wako maana mtoto ana miaka 13; akaniambia naomba uhamishe watoto wote wanaokaa lile eneo uwapeleke shule ya bweni au uwapeleke kwenye vituo maana yake pale watoto wote ndiyo tunachofanya.

Sasa nikawa nasoma pia maendeleo ya wenzangu Wizara mpya ambayo mama ametuanzishia ya Maendeleo ya Jamii, wanasema wameanzisha kamati za kulinda watoto na wanawake. Kamati 18,186 kati ya kamati 20,750 walizotaka kuanzisha kwenye nchi hii kwa ajili ya kulinda wanawake kwenye mitaa na vijiji, kamati hizo hazipo na hazifanyikazi, hatujaziona. (Makofi)

T A A R I F A

NAIBU SPIKA: Taarifa.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii. Jambo hili la ulawiti kwa watoto wadogo, ukatili wa kijinsia kwa Watoto, limeshika kasi sana katika nchi yetu na kumekuwa na kesi nyingi sana ambazo mwisho wake haueleweki kumekukuwa na rushwa mbalimbali na hakuna hatua madhubuti ambazo zinachukuliwa mimi niombe sasa kupitia hili kwamba Mheshimiwa Mbunge anachokisema ni sahihi kabisa na wale wote watakaobainika basi wahasiwe iwe ndiyo adhabu kubwa ikiwa ni pamoja na kifungo, ahsante.

NAIBU SPIKA: Taarifa hiyo?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea kasoro ile ya kuhasiwa. Sipokei ya kuhasiwa kwa sababu tuna namna tutawashughulikia na kuwashughulikia hawa kwa sababu zipo sababu zinazosababisha wafanye mambo haya ikiwepo ukata, nitaongezea yaani yale mambo ya uchumi yale.

Sasa hivi mapenzi au huduma ya mapenzi ni product kama product zingine watu wamepunguza purchasing power hawana nguvu ya kununua kwa hiyo wanakwenda kwenye kundi la watoto wadogo na kuwaonea. Kwa nini wamepunguza purchasing power? Ni kwa sababu ya ukatili mbalimbali unaofanyika kwenye jamii kiuchumi ikiwepo pamoja naweza nikasema sasa hivi na sisi tunachangia kama kuna Wizara hapa inafikiria kutowapa kipaumbele Watanzania katika miradi inayotolewa na Serikali hao ndiyo wanaosababisha matatizo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, leo ukiniambia nguzo za umeme zitanunuliwa nje ya nchi una maana vijana wangu wote walioko Iringa, Songwe, Tanga wote wamepanda miti wakose fedha, watakapokuwa wanahitaji la mapenzi watafanya nini? Kwa sababu kiuhakika sasa hivi hamna mwanamke atakupenda sura kwa sababu wanaume kwanza hawana sura nzuri unampendaje mwanaume sura. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, mwanamme anapendwa kitu alichonacho anapendwa fedha leo tunapoharibu mazingira ya utendaji kazi wa machinga hatuangalii kama mimi Mheshimiwa Bashungwa Iringa hujanipa hela yoyote ya kuandaa mazingira ya machinga. Wanakaa katika mazingira hatarishi wanapoteza mitaji wale ni watoto wa kiume rijali unategemea unaenda wapi? Inapofika hatua anataka hamu ya mapenzi anafanyaje?

Mheshimiwa Naibu Spika, hayo ndiyo tunayoyasema, lakini pia kuendelea kuwanyanyasa vijana wetu waliojiajiri kwa mfano kwenye bodaboda, kwenye bajaji wanafanya kazi zao unawabana unawanyanyasa kwa leseni wasifanyekazi vizuri una mnyanyasa yule kijana akikosa hela atafanya nini? Huo ndiyo unyanyasaji wa kiuchumi.

Sasa tuhakikishe kwamba Watanzania wanajengewa mazingira mazuri ya kufanyakazi, wanajengewa mazingira mazuri ya tiba, mimi naomba vijana wangu pale watibiwe vizuri zile hela za vijana naomba jamani kutoka mfuko wa Waziri Mkuu shilingi milioni 200 tu tukawawezeshe vijana wa pale wafanyekazi wawe na uwezo wa purchasing power za mapenzi, wasibake watoto wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba sana tuangaliwe masuala ya huduma za afya tuboreshe, watoto hawa wengine wanabakwa wamekosa nimekuambia ni asilimia tatu katika 11 wanaopata matibabu lakini hata wakienda hospitali sisi tumetoa watoto wengi kuwapeleka Muhimbili pia wakatibiwe baada ya kuwa wamefanyiwa ubakaji hatuna Hospitali ya Wilaya na leo sioni kama imetengwa hapa nimetengewa milioni 500 tu ya kukarabati lakini tuliwaomba tujengewe kwa sababu ile iliyokuwa ya Wilaya mmechukua Mkoa na inahudumia mkoa mzima tunaomba hospitali yetu ya Wilaya ili sisi watoto wetu waweze kutibiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme hivi katika masuala ya ukatili haya mimi nasimama leo kama Mheshimiwa Mbunge hapa kwa sababu kuna masuala ya ushirikina yapo ndani yake, sasa ushirikina ni mambo ya rohoni na tunayashughulikia kiroho. Walioko humu ndani watumishi wa Mungu watanielewa, mimi nasema hapa sasa kama Mbunge na ninyi wenzangu kama mnaniunga mkono mtajibu amina mwishoni nasema hivi Mungu tusaidie hatutawafanyia hatutawahasi kama alivyosema Mheshimiwa lakini ninaomba hivi tuachilie nguvu za Mungu kuanzia hapa zikawashughulikie wote kwenye kile kiungo wanachotumia kulawiti watoto wetu, kipigwe nguvu kisifanye kazi na zile mashine mbili zinazozalisha nguvu, zipotee kabisa na madaktari watakapoona mtu mwenye dalili hizo mnitafute ili tumuombee arudi katika hali ya kawaida na tumfanyie counselling ili watoto wetu waendelee kuwa salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kwenye masuala ya kiuchumi tuwatengenezee vijana wetu mazingira rafiki ya kufanyakazi tusiwanyanyase mama ntilie sijui akina nani wanapoonekana wanafanyakazi usimwage bidhaa zao, uangalie namna utakavyotumia hekima kuwasaidia ili wajijengee uchumi. Tumesema hapa tuwape vipaumbele Watanzania kwenye miradi tuwape vipaumbele tuwape elimu ili Watanzania waweze kuwa na purchasing power ya mahitaji yao ya muhimu ikiwepo suala la mapenzi, ahsante. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022, Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi nami nichangie. Kwanza nichukue nafasi hii kupongeza sana Ofisi ya CAG kwa kazi kubwa wanayoifanya kuhakikisha kwamba Bunge hili linakwenda siyo kama kipofu, bali tunakwenda huku tukiwa tunaona. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo mambo ambayo nataka niongee kutoka kwenye ripoti ya CAG, nami ni Mjumbe wa Kamati. Kwanza kabisa, yapo mengi ambayo Waheshimiwa Wabunge wameshaongea. Cha kwanza nilichotaka kuongea ambacho CAG amekiongea na kinaonesha wasiwasi, nami binafsi pia nikapata wasiwasi, kwanza ni kuhusiana na fedha za ruzuku ya maendeleo ambazo zinapelekwa kwenye Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, CAG anasema pesa za maendeleo zinazopelekwa kwenye Halmashauri zetu baadhi yake zinaonekana zimepelekwa bila kupitishwa au kupatiwa idhini kutoka kwenye Bunge hili. Wasiwasi wangu unaanzia hapo. Zipo zaidi ya Halmashauri 19 ambazo zimepelekewa fedha zaidi ya shilingi bilioni 47 bila idhini ya Bunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi yetu kubwa hapa kama Wabunge ni pamoja na kuisimamia Serikali na kupitisha hizi bajeti za Serikali. Sasa nashindwa kuelewa, ni kwa nini fedha hizi shilingi bilioni 47 zipelekwe katika Halmashauri, hata kama nia ni njema, ndiyo zipelekwe katika hizi Halmashauri bila Bunge kujua au kuidhinisha matumizi yake kwenye hizi Halmashauri?

Mheshimiwa Naibu Spika, wasiwasi wangu unakuja, pale ninapojiuliza, wenzetu Serikali wana mpango gani na Bunge? Je, wanataka kutunyang’anya ajira zetu? Kwa sababu sisi kazi yetu ndiyo hiyo, tuje hapa tupitishe bajeti, tuwahoji na kadhalika. Sasa unapokwenda moja kwa moja unapeleka fedha hizi bila kunipa mimi, una nia gani? Kwamba unanifuta kazi yangu, au una mpango gani? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine, fedha zimepelekwa kwenye miradi ya maendeleo zikiwa pungufu. Hapa naipongeza Serikali. Zaidi ya Halmashauri 163 zimepelekewa shilingi bilioni 500 kama ruzuku ya miradi ya maendeleo, lakini wamejitahidi kwa sababu upelekaji wa miaka mitano mfululizo ni wastani wa asilimia 46; lakini kwa mwaka 2020/2021 wamepeleka asilimia 62 kwenye ruzuku ya miradi ya maendeleo. Hapo tunawapongeza na tunaona nia njema ya Serikali, lakini bado kuna upungufu wa asilimia 38 zaidi ya shilingi bilioni 300 ambazo hazijapelekwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaiomba Serikali iangalie namna, kwa sababu tunapopeleka fedha hizi kwenye miradi ya maendeleo ndivyo tunavyokwenda kuchakachua uchumi kule chini kwa watu wetu. Halmashauri tatu zenyewe zimepelekewa fedha kama ambavyo jinsi tulikuwa tume-plan bila kuwa na mambo yoyote meusi ndani yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, hoja yangu ya pili; ili tuendelee tunahitaji watu; lakini tunahitaji watu tu, tunahitaji watu walioongezewa thamani. Hatuwezi kuendelea kama tuna watu ambao hawana thamani kubwa. Taarifa ya CAG inaonesha bado yako madai kwa watumishi wa umma wa nchi hii. Wanatudai mishahara shilingi bilioni 63. Yapo madeni ya malimbikizo ya posho, likizo kwa watumishi milioni karibu 96,650,000,000. Hawa ndio rasilimali watu tunaotegemea kwamba wafanye kazi kubwa kwenye Halmashauri zetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama hatutaweka uwekezaji kwa watu hawa, ina maana utendaji wao ndio maana unakuwa ni duni. Watu hawa ndio tunaopelekea mabilioni ya fedha kwenye miradi ya maendeleo, halafu hujampa fedha yake ya nauli anapokwenda likizo, ndio maana unakuta sasa wana-temper na mifumo, wanafanya mambo meusi meusi ili angalau waweze kufidia ule upungufu na makali wanayopata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo tumeelezwa hapa, Manispaa moja tu ya Ilemela kwenye mitando tayari wame-temper na shilingi bilioni karibu nane, zimefutwa vocha za karibu 822 kwenye mfumo bila utaratibu unaoeleweka. Tumeelezwa hapa, Ubungo wameingiza figure kwenye mfumo ambao Mwenyekiti wangu wa Kamati amesema tu kwamba ni shilingi milioni 500 ambayo haieleweki yaani. Ukiwauliza, wanakwambia ilikuwa ni namba ya simu. Unashindwa kuelewa, namba ya simu gani inaanza na kodi ya 500? Ni ujanjaujanja na ubadhirifu ili kuhakikisha kwamba wanakuja ku-temper na fedha za Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, tusipoangalia, na kuwaangalia watumishi wa umma, hatuwezi kufanya mambo makubwa yakaenda sawa sawa na maendeleo kwenye Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, bado kuna malalamiko ya kikokotoo kwenye nchi hii…

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, Taarifa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, …

NAIBU SPIKA: Taarifa.

T A A R I F A

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa mchango wake, lakini nadhani Bunge hili pia linapaswa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa sababu baada ya CAG kuwa ametoa taarifa hiyo na hasa kwenye malimbikizo ya mishahara kwa watumishi wa umma; na kwa kuwa Mheshimiwa Rais alishajipambanua kwamba anahitaji rasilimali watu iweze kupatiwa haki na stahiki iweze kutekeleza wajibu sawa sawa; mpaka tarehe 31 Januari, Serikali ya Awamu ya Sita imeshalipa malimbikizo ya mishahara kwa watumishi wa umma 116,792. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, haikuishia hapo. Katika hayo malimbikizo ya mishahara imekwishakutumia fedha za Kitanzania shilingi bilioni 199.365. Kwa hiyo, tunampongeza CAG kwa kazi nzuri, lakini hapo hapo pia tumpongeze Mheshimiwa Rais kwa kuona jambo hilo na kulipa stahiki za watumishi wa umma. (Makofi)
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba unilindie muda wangu, lakini nashukuru kwa taarifa hiyo ya Serikali na naipokea. Hata hivyo tunayojadili hapa ni ile iliyoishia Juni, 2021. Kama wamekwenda hatua hiyo, tunawapongeza zaidi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuwaombe, suala lingine linaloleta malalamiko, pamoja na mambo mengi tuliyoambiwa kuhusiana na kikokotoo, lakini kikokotoo kile ndani ya watumishi wa umma kinasumbua. Tunaomba Serikali ione namna ambavyo itakaa na watumishi wa umma na kuona wanafanya kazi kwa moyo bila kuwa na malalamiko.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimejaribu kukaa hata na Jeshi la Polisi tu, wakielezea hali yao ya utendaji wa kazi wanakwambia sisi hatuna hata muda wa kupumzika kusema tutatafuta hela ya ziada kwa ajili ya kuweka kibanda. Tunategemea tukilipwa mafao yetu ndiyo tuweke kibanda. Leo ukiniambia unanipa kidogo halafu unanilipa kidogo kidogo unakuwa hunisaidii. Tunaomba Serikali ikakae ili kuendelea kupunguza malalamiko haya kwa watumishi wa umma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu kingine ambacho nataka kuongea, upo ubadhirifu wa mikataba ambayo Halmashauri zetu zinaingia, na uwekezaji ambao Halmashauri zetu zinaingia. CAG ameelezea. Yapo mambo ambayo Halmashauri zinafanya bila upembuzi yakinifu, kwenda kuwekeza miradi ya ujenzi wa mastendi na masoko. Unakuta kwa sababu tu Halmashauri hii imejenga soko, na wengine wanataka wakajenge soko na wangine wanataka wakajenge stendi na wengine wakaige kitega uchumi hiki, lakini bila kuangalia mazingira yao yanaendana na hicho kitega uchumi wanachotaka? Ndiyo maana yapo majengo mengi sana yamejengwa kwa gharama kubwa lakini hayatumiki ipasavyo kwa sababu Halmashauri zetu hazifanyi upembuzi yakinifu wa kujua mradi ule kama unaweza ukawa sahihi kwa mazingira yao na kama watu wao wanauhitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba sana Serikali iwasimamie. Hizi Halmashauri, Wizara husika, isimamie. Ile ya kwamba tunakwenda kujifunza mahali fulani, Waheshimiwa wanasafiri wanakwenda kujifunza mahali, anachukua tu ile utaratibu wa kujenga Machinga Complex ya Dar es Salaam anataka labda ajenge Iringa, wakati ni tofauti kabisa. Yaani Machinga wa Iringa ni tofauti kabisa na Machinga wa Dar es Salaam, na hawawezi kuendana katika biashara zao wanazozifanya. Kwa hiyo, hii imeipotezea Serikali mapato hela nyingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia zipo taasisi nyingine…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Haya, nakuongezea sekunde 10.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo taasisi nyingine ambazo nazo zinasababisha Halmashauri zetu kupata hasara. Taasisi kama TEMESA ni za Serikali, lakini nazo zimekuwa funza kwenye Halmashauri zetu. Kwanza, ukitaka kupeleka gari TEMESA watakuandikia vifaa vya bei kubwa kuliko hata kwa Mangi, unakwenda unatengeneza kwa gharama kubwa, wanakufungia kifaa kimekufa, yaani hawaeleweki. Kwa nini tutumie TEMESA kama tunajua kabisa hii inatuletea tatizo?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia kuna NHIF, kila wakati kwenye hela za vituo vyetu vya afya wanatafuta visingizio vidogo vidogo, kwamba hawa wameshindwa kujaza fomu…

NAIBU SPIKA: Ahsante. (Kicheko/Makofi)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika Mpango wa Tano wa Maendeleo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yapo mambo ya msingi tunapotaka kufanya mabadiliko ya kiuchumi na kwenye biashara. Ukichukua mfano wa nchi ya China ilipotaka kufanya mabadiliko yake kwenye masuala ya uchumi na biashara zaidi ya miaka 40 walikuwa wakiendelea kusuguana na sheria na sera zao. Mipango na mikakati yao ilikuwa imekaa vizuri; ilikuwa ikijali muda, lakini ukienda kwenye mambo ya sheria na sera zao zilikuwa zinawarudisha nyuma na zikafanya uchumi wao kuendelea kuwa duni, ulishindwa kuendelea kukua, tegemezi na usiozingatia ushindani wa kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baadaye walipoamua sasa kuanza kubadili sera na sheria zao ndipo walipoanza kuleta maendeleo makubwa na ndani ya miaka nane kwa ripoti za Benki ya Dunia, walikuwa wanakua mara mbili zaidi ya GDP ambayo ilikuwa ni kwa asilimia 9.5. Ndipo walipoweza sasa kutoa umaskini kwa watu wao zaidi ya milioni 800 maana tunapoongelea China ni watu zaidi ya milioni 1,400.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo sasa Mpango huu wa kwetu wa Maendeleo wa Miaka Mitano ni mzuri na umezingatia standard na spidi au umejikita katika muda lakini kikwazo kikubwa kitakachokuja kutukuta, katika ukurasa wa tano wa maeneo ya muhimu ya kuzingatia ambao Mpango unaeleza, umeeleza mambo mazuri lakini haukuweka msisitizo katika kuhakikisha kwamba tunabadili na sisi sheria na sera zetu ambazo huwa zinatusababisha tusiende kwa spidi au tusiende kwa wakati ule ambao tumeupanga, hicho kipengele hakijawekwa. Kwa hiyo, tunaomba tushauri kwamba katika Mpango huu tujaribu kuangalia namna gani tutabadilisha sheria na sera zetu ili ziweze kuendana na muda ili tuweze kuutekeleza huu mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara nyingi sana tumekuwa tukipanga vitu vingi lakini unakuta kuna sheria zinakinzana. Tunakwenda kwa spidi tunataka kuinua utalii, Mpango unatuambia kwamba tutoke katika watalii 1,500,000 mpaka itakapofika 2025 tuwe tumefika watalii 5,000,000, lakini kuna sera nyingine ambazo zipo sasa zinahusiana na masuala ya kutoa vibali au permit za kuishi, unakuta zinakinzana na ile sera ya sisi kuboresha spidi ya kuendeleza utalii wetu au kuboresha spidi ya uwekezaji. Mwekezaji anakuja katika taifa letu, amekuja na mtaji, anakuja kupambana na Sheria ya Labour ambapo yeye anataka kuja na mke wake lakini sheria inamkatalia asije na mke wake au anapata usumbufu kupata permit ya kuishi na mke wake. Sasa unakuta vitu kama hivi vinakuwa vinakinzana, tusipoziangalia sheria na sera zetu, bado hatutaweza kuutelekeleza huu Mpango kwa wakati kama ambavyo tunatarajia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaweza tukajifunza kutoka kwenye Sekta ya Madini, namna ambavyo madini yamechangia kwenye maendeleo yetu katika Mpango wa Pili, ni kwa sababu pia yalifanyika mabadiliko makubwa ya kisheria kwenye sheria za madini na ile ikatusababisha tukaenda vizuri. Kwa hiyo, ushauri ni kwamba tunaomba sheria na sera nazo ziangaliwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitaka kujua kwamba tuna mkinzano wa kisheria na mipango yetu utaona mara nyingi sana mambo yetu mengi yanakwenda kwa waraka, matamko, yanakuwa kama ya zimamoto hivi. Kwa sababu kama sheria ingekuwa inakwenda sawasawa na mipango, hivi vitu vya zimamoto, kwenda kwa matamko na nyaraka visingekuwa vinakwenda namna hii. Hii inaonesha namna gani sheria yetu inawezekana haiko sawasawa na mipango ile ambayo tunaiweka. Kwa hiyo, tujitahidi kubadilsiha sheria zetu na tujitahidi kuangalia mabadiliko makubwa kwenye sera zetu ili tuweze kwenda sawasawa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi wetu unatakiwa ujengwe sasa kwa misingi ya soko. Tusitengeneze tu mpango kwamba tulime mazao haya zaidi, tulime kitu hiki au kile zaidi, hebu tuangalie soko lina uhitaji gani. Kama tunasema tuna uhitaji mkubwa wa mafuta ya alizeti, huko ndiko sasa tutengeneze mpango namna gani tunawashawishi wakulima ili waweze kulima alizeti na namna gani tunatengeneza sheria ambayo itazuia uingizaji wa mafuta ya alizeti kwenye nchi yetu ili soko letu la ndani lenyewe lianze kuwa ni soko kabla hatujategemea soko la nje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndugu zangu, lazima …

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Kengele imeshagonga Mheshimiwa, ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nianze na suala la utafutaji wa masoko ya bidhaa za kilimo.

Mheshiiwa Spika, ushauri Serikali iangalie mahitaji ya ndani ya bidhaa au mazao ya kilimo, kisha ifanye zoning ya kuhakikisha hitaji hilo litashughulikiwa na wakulima wa kanda fulani. Mfano tunahitaji mafuta ya kupikia nchini, hivyo ianishwe mikoa ambayo itatakiwa kuchangia market share hiyo. Hii itasaidia Serikali, kuelekeza nguvu kubwa za uwekezaji hasa katika utafiti, mbegu bora, upatikanaji wa masoko, kuweka miundombinu bora, pia itavutia wawekezaji.

Pili, miji yetu pia ni masoko ya bidhaa za kilimo kama mbogamboga, iangaliwe miji ambayo mito inapita katikati yake, halafu ifanyiwe mkakati wa kilimo bora cha mbogamboga na ufugaji wa samaki wa kizimba, bila kuathiri mazingira. Mfano Mji wa Iringa unapitiwa na Mto Ruaha, Njombe, Mto Ruhuji na kadhalika.

Tatu, fedha za wafadhili katika kilimo ziwafikie walengwa ikiwa ni pamoja na za Serikali zilizowekezwa kwenye mabenki ya Kilimo.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Afya
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante nakushukuru kwa kunipa nafasi na mimi pia nishukuru kwa ajili ya juhudi kubwa za Wizara ya Afya na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna ambavyo anaendelea kuimarisha afya katika Taifa letu. Nawashukuru kwa ajili ya Kituo cha Afya Mkimbizi ambapo mmetupatia Shilingi milioni 250 na baadaye mmeongeza tena Shilingi milioni 250 nawashukuru sana, kwa ajili ya Wodi zinazojengwa katika Hospitali ya Frelimo ya Wilaya pale mawili na ICU pamoja na Mochuari. Nawashukuru pia kwa utanuzi unaoendelea wa Hospitali yetu ya Mkoa wa Iringa ingawa tuna changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi, maana tunahitaji kuwa na watumishi karibu 466 na tuna watumishi 266 tu na nyinyi mmeipangia ile kwa ajili ya huduma ichangie zaidi ya Shilingi Bilioni 5.8 kwa hiyo tunaomba tuongezewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naomba leo niongelee hoja ya afya ya akili. Mheshimiwa Waziri nimesoma katika mambo yako sijaona sana unaongelea suala la afya ya akili, lakini afya ya akili ni kitu cha muhimu sana na ni lazima kama nchi tuhakikishe kwamba tunakichukulia uzito mkubwa na kukiwekea mipango. Kwa sababu, suala la afya ya akili tunaposema mtu awe na afya ya akili maana yake kwanza awe na uwezo wa kujitambua. Mtu anaonesha ana uwezo wa kutatua changamoto zake, mtu anaweza kufanya kazi na kuzalisha lakini mtu huyo anaweza akatoa mchango kwenye jamii yake. Sasa ukitaka kujua mpo kiwango gani cha afya ya akili kama wananchi lazima mjielekeze kuangalia hoja hizo. Kwanza kabisa tukienda namna gani labda kama Watanzania tunachangia ukiona mara nyingi raia wanajiuliza, Serikali inatufanyia nini na sio wao wanataka kusema sisi tunaifanyia nini Serikali ujue kuna tatizo kubwa kwenye afya yao ya akili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wote wenye afya za akili wanajiuliza mimi nitaifanyia nini Tanzania na sio Tanzania itanifanyia nini. Sasa sisi mara nyingi tunatumia Technic ya walevi au ya watu wanaopenda kunywa mara nyingi wako baadhi yao, wakiwa na tatizo anaahirisha tatizo kwa kulewa halafu kesho anajua akiamka mambo yatakuwa safi. Lakini kiuhalisia haiwi hivyo kwa sababu akiamka kesho fedha ile, ambayo anatakiwa aanze kutatulia changamoto ameitumia yote imekwisha. Suala hili lipo kwetu inapotokea changamoto mara nyingi tunakimbilia kutaka Serikali ifanye jambo bila kuangalia sisi wenyewe tunakwendaje kutatua lile jambo. Uwezo wetu wa kutatua changamoto kama wananchi/viongozi inaonekana umeshinda na hiyo ndio ina- comprise afya ya akili mna afya ya aina gani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, juzi juzi ikishuka bei ya mazao tunataka Serikali iweke ruzuku ikishuka bei ya mbolea tunataka Serikali iweke ruzuku imepanda bei ya mafuta tunataka Serikali iweke ruzuku. Sasa mimi najiuliza ni kwa nini hatufikirii kutatua changamoto na siku nyingine kutumia akili walizotumia wazee wetu, yamkini akili zao zilikuwa zina afya wakasema tunapita kwenye kipindi cha vita ni wakati wa kujifunga mikanda tuhakikishe tunapambana ili tujenge uchumi. Mimi leo najiuliza ile Shilingi Bilioni 100 tunayoiweka huku haijatoka kwenye TARURA kweli hatutaanza kutembea kwenye barabara zina makorongo, hatutaanza kukosa dawa? Sasa Mheshimiwa Waziri wa Afya tuangalie sana kwenye suala la afya ya akili, unatusaidia vipi tuweze kutatua changamoto zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kujitambua ni ukweli usiopingika Taifa lolote linalotegemea kuendelea kuwa na nguvu, linafanya uwekezaji mkubwa kwa vijana wake na tunaposema vijana hapa ni miaka 15 mpaka 35. Sasa tuangalie kama Taifa tunawekezaje kwa vijana wetu unapofika mahali unaona vijana wa miaka 35 hawapewi priority wakati nchi nyingine sasa hivi zinahama zinaelekea hata kumpa kijana mwenye miaka 27 kuwa Rais wa nchi. Lakini sisi kwenye nafasi tu za Umeneja kwenye nafasi tu za Uenyekiti wa Bodi, tunajaa wazee na tunakaa sisi tu wakina bibi hili Taifa ni Taifa ambalo litafika mwisho. Kwa sababu, kama unaendelea kuwekeza kwa wazee unaendelea kila siku kuhuisha mikataba watu wamestaafu unakazi ya kuhuisha mikataba wazee waendelee wazee waendelee, maana yake ni kwamba vijana wako utawatumia lini? Utawapa practice lini maana huo ndio udumavu wa akili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu udumavu wa akili ni kama unashindwa kuwa na adequate simulation ile Sy social simulation ukishindwa kuwa nayo ile ina maana unashindwa kuwandaa vijana wako wajipange. Kwa nini kwenye hizi nafasi kama Profesa ni bibi basi msaidizi wa Profesa awe kijana mdogo ili kumuandaa. Kwenye nafasi kubwa tunashika sawa wewe umeshika nafasi kubwa ni mtu aged kwa nini hufanyi succession plan ya kumuandaa kijana. Sasa Taifa letu litakuwa halina nguvu kama siku zote tutaendelea kufikiri kwamba wanaoweza kushika nafasi kubwa, ni watu wenye umri mkubwa na kusahau vijana na hilo ni tatizo la afya ya akili. Kutotambua kwamba wewe ni mzee utaondoka nchi unatakiwa umuachie kijana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Waziri afya ya akili tunaiangalia sehemu nyingine sisi tunaweza tukaleta hoja kutoka huku chini lakini wenzetu mkikaa huko Wizarani mnatuona sisi kama... sisi tuko juu ndio wenyewe. Unaona sisi tuliwaambia ile Hospitali ya Mkoa wa Iringa mmeng’ang’ania kuitanua pale kwenye car seater pamejaa hata hapatanuliki mmebanwa na Magereza mmebanwa na Mahakama, pelekeni kwenye heka 35 kule mkaitanue vizuri nyinyi wenzetu mmekataa mmetuona sisi hatuna afya ya akili lakini kimsingi nyinyi ndio hamna afya ya akili. Kwa sababu, wewe unaweza kubadilisha Magereza iwe ICU kwa kuwaondoa Magereza pale? Nyinyi ndio hamna afya kwa hiyo sisi tunaomba muangalie. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, lakini Mheshimiwa Ummy hilo lisikupe taabu unafanya kazi vizuri mimi ninachoomba niletee Hospitali ya Wilaya ya Iringa, hujaiingiza hapa na uliniahidi kwamba basi tutakujengea Hospitali ya Wilaya lakini kwenye bajeti haipo mama yangu. Naomba kwa sababu sisi ile hospitali hatutibu watu wa Iringa tu na Majimbo yote yanayotuzunguka wanakuja pale, Isimani wanakuja, Kilolo wanakuja, kule kwa Kiswaga wanakuja, Kalenga na Mafinga wanakuja pale katikati tunaomba mtujengee hiyo hospitali yetu ya wilaya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunapoongelea afya ya akili angalia hali halisi ya performance ya Watanzania wetu. Leo hii unaweza kumuona mama amebeba begi zuri ukafikiri labda ndani ya begi mule sijui kuna nini lakini ukiangalia kuna maji ambayo amepewa sijui kwa Nabii gani yamletee magari, yamletee nyumba, yamletee utajiri, ana tango ameombewa sijui la kuimarisha ndoa, ana chumvi sijui ya kumwaga avute wateja, ana vitu kibao yaani vitu vinavyoonesha watu hawana afya ya akili. Wanadanganywa kwa hiyo Mheshimiwa Waziri wa Afya hiki ni kitu cha msingi, tunaomba ukiweke kwenye bajeti yako utatusaidiaje Watanzania hawa wawe na afya wasidanganyike? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hakuna namna hata Mungu mwenyewe anasema nitabariki kazi ya mikono yako sio kwa kutembea na maji yaliyochotwa Jordan au maji yamechotwa Mto Meru sasa hili ni tatizo la afya ya akili. Hebu tuangalie afya za akili zetu wanasema afya ya akili ni kujitambua. Leo hii tuna vijana wengi wanaogopa kuoa wanaogopa kuolewa ukimuuliza wewe kwa nini huolewi anasema nipo nipo kwanza umri unakwenda, wewe kwa nini huoi nipo nipo kwanza. (Makofi)

Kosa la afya ya akili. Akili yake hai-reason sawasawa. Umri umefika, bado hajitambui. Sasa hiki kitu ni cha muhimu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hii afya ya akili tusipoishughulikia, ina tabia ya kuleta umasikini kwenye nchi, kwa sababu uwezo wa watu kuzalisha unapungua kwa sababu hawafikirii. Umenielewa? Leo nimekuja nikasema hapa jamani, wanaume hawa wanapendwa wakiwa na kitu (fedha), lakini kuna mwanaume mmoja anaitwa Heche, amelalamika kwa nini nimesema wanaume, sio warembo? Hilo ni tatizo la afya ya akili. Mimi siamini kama kuna mwanaume hapa atataka kuitwa mrembo. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, afya za akili za watu haziko sawasawa, mtusaidie. Watu wanalalamika ndoa zinavunjika kwa sababu ya suala la afya ya akili. Tumepeleka mikopo akina mama wakope, leo anakopa FINCA, anaenda PRIDE, anaenda huku anaenda huku. Ndoa nyingi zinavunjika kwa kuwa watu wanakimbia kwa sababu ya mikopo. Hajui namna ya kuzalisha. Unaona! Kwa hiyo, anakosa afya ya akili nini? Ya akili! Kwa hiyo, inatuletea matatizo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa Jesca dakika zako zimeisha, lakini nakuongezea dakika moja, malizia mchango wako. (Makofi/Kicheko)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, naendelea. Kama tunafikiri kwamba umasikini wa nchi hii utaisha kwa sababu ya kutoza kodi, mama aliongea categorically, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatutaki kodi zenye dhuluma. Tunataka kodi kwa haki. Kama kuna kiongozi, bosi amekaa kwenye Ofisi ya TRA, anajua kabisa huyu mfanyabiashara uwezo wa kulipa hii kodi hana, halafu yeye anambambika kodi na kumtoza kodi kubwa, ni afya ya akili hana. Yeye mwenyewe analipwa kwa hiyo biashara, halafu anachagiza kuiua hiyo biashara. Ina maana mtu huyo hana afya ya akili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unapokwenda na nguvu kufunga biashara, badala ya kumwelimisha mtu kwamba hii biashara fanya hivi na hivi, au nipe mpango wako wa kulipa kodi; wewe kazi yako ni kufunga biashara na wakati umetumwa ukalate na kuongeza mapato ya Taifa hili, afya yako ya akili ina mgogoro. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba sana na viongozi wetu, tupo kwenye idara na kwenye Serikali, bado tunaona kuna vitengo. Mimi niko Kamati ya Nishati, nashukuru sana. Sisi tuna Kitengo cha Geothermal. Geothermal ni umeme wa jotoardhi, wamejipanga vizuri kupitia Waziri wetu anawasimamia, yule mzee tumefika anatusomea taarifa kwamba mimi nastaafu, lakini nimemwandaa kijana huyu hapa, anakuja kuchukua hii nafasi. Zipo Wizara na wapo mabosi wengine wa Wizara hapa, bado wanafikiri kuendelea ku-renew mikataba kwa wazee na wamesha-renew mikataba mara sita, mara saba. Wakati una-renew mkataba mara tatu mara nne, tayari tuna workforce ambayo ni vijana wamesoma hatuwaandai, ni kutokuwa na afya ya akili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Nami naomba Mheshimiwa Ummy unapokuja hapa, useme hiyo afya ya akili unaiwekaje tupone?

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa hii leo tena.

Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru kwa hotuba nzuri ambayo Waziri Mkuu ameisoma jana ambayo imesheheni matumaini makubwa, lakini hoja yangu leo itakuwa ni umuhimu wa binadamu kutoa fursa kwa binadamu mwingine kuishi.

Mheshimiwa Spika, upo ukatili unaendelea juu ya binadamu na sisi tusipokuwa makini specie yetu kama viumbe hai kama binadamu tunakwenda kupotea.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu amesema jana namna ambavyo Serikali imetekeleza mambo yake kwa mwaka ulioisha na fedha nyingi tulizowekeza huko, zaidi ya trilioni nane kwa ajili ya kutengeneza miundombinu mbalimbali ya kuhakikisha kwamba, ustawi wa binadamu katika nchi yetu unaendelea kuwepo. Naamini kabisa fedha nyingi tunazowekeza kwenye miradi ya kimkakati nia na madhumuni yake sio kutusaidia sisi tunaoishi leo peke yetu, tuna nia ya kuwasaidia watoto wetu, tuna nia ya kuwasaidia wajukuu zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumewekeza zaidi ya bilioni 762 kwenye reli ambayo tunategemea itaishi zaidi ya miaka 100 ijayo na yamkini sisi katika miaka 100 ijayo sisi hatutakuwepo. Tumewekeza katika bwawa la umeme zaidi ya bilioni 800, Bwawa la Mwalimu Nyerere, hatutakuwepo. Tunawekeza katika miundombinu ya viwanja vya ndege zaidi ya bilioni 77 na Iringa tumepata bilioni 41 kwa ajili ya kujenga Kiwanja cha Nduli, kimefika asilimia 42 lakini tunajua tuliambiwa mpaka Septemba kitakuwa kimekamilika, tunajua zitaletwa fedha, lakini nia na madhumuni ni kwamba, tusaidie watoto wetu na wajukuu zetu na vizazi vijavyo, kama Watanzania na Waafrika.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameeleza mipango ya maliasili za Taifa letu, jinsi tunavyotaka kuendelea kulinda maliasili zetu sio kwa ajili yetu sisi tu, kwa ajili ya watoto wetu na uzao ujao. Mama alivyojitolea kwa ajili ya kufanya ile movie ya Royal Tour, nia na madhumuni sio ataiona yeye peke yake na Awamu yake ya Sita, nia na madhumuni wajukuu wetu pia waje waione.

Mheshimiwa Spika, yapo mambo yanayoendelea katika jamii yetu. Tusipokuwa makini na tukienda kwa ku-copy na ku-paste kwa sababu, watu fulani wamesema au mataifa fulani yamesema, sisi tusipoamua kutumia akili zetu na kwamba, tumepewa fursa na Mungu na sisi kama Watanzania kuamua mambo yetu, upo wakati na sisi kama Watanzania tutoe fursa mataifa mengine yaje yajifunze kutoka kwetu namna ambavyo tunalea watoto wetu, namna ambavyo tunakuza watoto wetu.

Mheshimiwa Spika, sisi kama Waafrika hatukufundishwa kujifunza tu kwa watu wengine. Afterall Mungu aliumba mtu mke na mume hakuangalia color ilikuwa ni color gani, kwa hiyo, na sisi watu wengine, mataifa mengine wanatakiwa waje wajifunze namna ambavyo Afrika inatunza watoto wake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hapa katikati ukatili kwa watoto wetu umezidi mno. Tunashangaa, hatuelewi imetokea wapi? Imekuwaje? Waziri Mkuu ameeleza hali ya usalama wa nchi yetu na utulivu iko vizuri, mipaka yetu iko vizuri na ni kweli, wote tunashuhudia tuko vizuri, lakini kumbe ndani ya nchi kwenye uzao wetu tayari hatuko salama. Watoto wetu wamefanyiwa vitu vya hovyo mno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo kumbe humu ndani tuna taasisi, tena Mheshimiwa Waziri Mkuu katika ku-wind up hotuba yake ameeleza mambo muhimu ambayo anataka yafuatwe. Moja katika yale sita, ameeleza jambo la tatu anasema, viongozi wetu wa Serikali, dini, mil ana vyama vya siasa wakemee kwa nguvu zote ushiriki wa sehemu yoyote ya jamii katika matendo yasiyoendana na mila, tamaduni na desturi za Watanzania. Hii ni pamoja na wazazi na walezi wote kushiriki kikamilifu katika makuzi na malezi bora ya watoto yatakayosaidia kuwaepusha na vitendo viovu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, it is a high time suala hili linalohusiana na ukatili kwa watoto wetu, ulawiti kwa watoto wetu, ubakaji kwa watoto wetu, masuala ya ndoa za jinsia moja yasifumbiwe macho. Tuyaongelee Makanisani, tuyaongelee Misikitini, tunaanza hapa Bungeni, tuyaongelee Serikalini, tuyaongelee kwenye familia zetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutapotea. Hizi reli zitakuja kupandwa na popo kama ilivyokuwa Sodoma na Gomora. Huu umeme hautakuwa na maana. Haya majengo makubwa tunayojenga hayatakuwa na maana. Barabara ile wanayotujengea Iringa kwenda Ruaha National Park nani atapanda nani ataangalia wale tembo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nimesema lazima binadamu mmoja atoe fursa kwa binadamu mwingine. Kama babu yangu mimi asingetoa fursa kwa baba yangu mimi leo ningekuwa wapi? Angemua babu yangu mimi aolewe na babu mwingine wa Kijiji kile ingekuwaje? Mimi leo ningekuwa wapi? Kama mama yangu angeona ndoa zina shida akaamua kuolewa na mwanamke mwingine, mimi leo ningekuwa wapi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lazima vijana wetu waambiwe ukweli. Sisi tunawapenda, tunawaheshimu ndio maana tunawekeza, ndio maana mama hakawii anazunguka huko na huko kwa sababu ya kuhakikisha kwamba, tunalinda Watanzania na uzao wao. Sasa leo tukikaa kimya kwa sababu, ni human right, ni human right ipi wakati sisi hatutoi fursa? Sisi tulipewa right ya kuishi na moja among the human rights ni haki ya mtu kuishi na wewe unatakiwa kutoa fursa kwa mtu mwingine aishi, you don’t give the right halafu unataka upewe right, haiwezekani! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, twende kwenye shule zetu na si suala tu la Serikali kusema kwamba, sasa Serikali ije hapa maendeleo ya jamii watwambie hiyo jamii wanayoitunza ni ipi? Hii mipango tunayoitenga ya nini? Haya mabilioni ya fedha tunayaweka ya nini kama hayataangalia uzao wa tumbo letu? Kama hatutaangalia watoto wetu wanaishi vipi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo watoto wako kwenye vulgar environment, hawaelewi waende wapi. Wakija majumbani tafiti za UN zinaonesha kwamba, 66% ya watoto wanafanyiwa ukatili majumbani kwa wazazi wao, 44% inayobaki ni shuleni na sehemu nyingine. Wanakwenda shuleni tena wale guardians ambao tumewakabidhi watoto nao tena wanawalawiti watoto, wanawafanyia ubakaji watoto. Tanzania where is this country heading to? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sisi we need to be a role modal in this world. Other people should come also and learn from Tanzania kwamba na sisi tumeweza kuwa-groom watoto wetu, sio lazima tuige kila kitu from them. Hata wao wenyewe wame-confuse. Nimemsikia Biden mwenyewe anasema, anashangaa anasema my mum alisema tu it is sinful, halafu akasema it is cruelty kwa binadamu, ni ukatili kwa binadamu. Wenyewe hawaelewi, yaani they don’t know what to say. They find somewhere to read, wanataka mahali wakajifunze. Tanzania we are ready, tulikuwa tuna-raise vipi watoto wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo Japani wanahangaika kwamba, uzao wao unakwisha kwa sababu, mwanamke ana uwezo wa kuzaa mtoto 1.3 kwa sisi tuliosoma hesabu maana yake kati ya wanawake wanne anayezaa watoto wawili ni mmoja tu. Wengine wanazaa mmoja wengine labda hawazai. Watu wanaona population yao inashuka, they are fighting, Waziri Mkuu yule ana-fight namna gani ainue population yake. Sasa kama it is a human right wao kuoana wanawake kwa wanawake na wanaume kwa wanaume kwa nini wanawa- force watoto wetu waingie kwenye hizo kwa kuwalazimisha kufanya vitu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wao nao wa-grow wafike waamue wenyewe. Nashindwa kuelewa NGO ndani ya nchi hii. Nimerudi Iringa nimekutana na hiyo, vijana wananiambia kuna mahali mmetupeleka tukafundishwe tukopeshwe, lakini madam mbona kama vile wanatufundisha mambo fulani? In this country! (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumewaruhusu, halafu hiyohiyo Wizara ya Maendeleo ya jamii, hiyo hiyo ndio inasajili NGO, hiyo hiyo ndio inatakiwa kulinda jamii, hiyo hiyo ndio inatuletea watu wanagawa vilainishi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, look here, we are privileged to be leaders in this country. Ni neema, it is a grace. Tusije tukajiona kwamba, sisi ni wa maana sana kuliko watu wengine, we are graced na tusipotumia neema hii vizuri, leo tukikaa kimya Mungu atainua mawe yatasema, ila sisi na uzao wetu utapotea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, narudia tena, binadamu atoe fursa ya binadamu mwingine kuishi. We love them, they are our kids. Ni watoto wetu, tunawapenda, hata hawa walioingia kwenye mifumo hiyo ya ndoa za jinsia moja au ushoga hatuwachukii ni watoto wetu, mtoto wako hata akiwa kibaka utamkataa?

Mheshimiwa Spika, tutafute mbinu za kuwasaidia wale watoto wetu. Tuone namna gani tutakaa, kama we think kwamba, dunia ime-advance scientifically let that science prove kwamba, inaweza ku-solve problems kama hizi. Science ituhakikishie kama inaweza kumsaidia kijana wetu wa kiume aliye-engage huko, amepoteza kabisa viungo vyake, nguvu zake hazi-function, itusaidie. Hatujamaliza bado kupambana na matatizo ya uzazi wa wanawake, leo tuanze kupambana na kubadilisha matumbo ya wanaume yawe ya akinamama, inawezekanaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya tu ambayo ni original tumepewa bure tumeshindwa kuyashughulikia…

SPIKA: Mheshimiwa Jesca Msambatavangu muda wako umeisha. Dakika moja, malizia.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame kwa pamoja. Kwa agizo hili twende kwa pamoja, ukisimama hapa wekaweka kidogo mbwembwe, haiwezekani, Ubunge wetu hauna maana kama watoto wetu hawatakuwepo baada ya miaka 10. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatuko tayari kuacha Tanzania iwe ni nchi kama ilivyo Sodoma na Gomora wanazaliana popo. We are not ready, we are here ku-make sure Watanzania wanaendelea kuwepo katika ulimwengu huu mpaka ukamilifu wa dahari, ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Afya
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia kwenye Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote na mimi nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya afya, akisaidiwa na Waziri wetu Ummy, Waziri makini kabisa na Naibu Waziri Kaka yangu Mollel. Tunawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nami niungane na Kamati, nawashukuru sana kwa kuja Iringa na kuona changamoto zilizopo katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Tunawashukuru sana kwa ajili ya Digital X-Ray Scan na ukarabati wa lile jengo la Radiology ambalo mmetumia zaidi shilingi bilioni moja na milioni mia saba na tisini na moja, tunawashukuru sana pia kwa ukarabati wa ICU shilingi milioni 150, tunawashukuru sana. Tunawashukuru pia kwa ajili ya fedha nyingi mlizozileta kwenye hospitali yetu ya Wilaya ya Manispaa ya Iringa ambayo ni zaidi ya shilingi bilioni moja na milioni milioni mia mbili. Tunawashukuru kwa ajili ya fedha ya Kituo cha Afya Mkimbizi shilingi milioni 500. Tunawashukuru kwa ajili ya fedha katika Kituo cha Afya Ipogoro shilingi milioni 357. Tunawashukuru kwa ajili ya fedha mlizoleta kwenye zahanati zetu, Zahanati ya Mkwawa shilingi milioni 50, Zahanati ya Isakalilo pale shilingi milioni 150, Zahanati ya Nduli shilingi milioni 50, Zahanati ya Ugele shilingi milioni 50. Nawashukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema haya changamoto zilizotokea tunaomba muendelee kutuongezea watumishi katika Hospitali yetu ya Referral ya Mkoa wa Iringa na pamoja na kwamba mmeshatupatia watumishi wengine karibu 26 lakini bado tuna upungufu. Mmetupatia watumishi 46 kwenye Hospitali yetu ya Wilaya bado tuna upungufu na katika vituo vyetu vya afya kwa mfano Mkimbizi mmetupatia watumishi Saba. Tunawashukuru sana na kwenye zahanati watatu, watatu tunawashukuru tunaomba muongeze.

Mheshimiwa Naibu Spika, Manispaa ya Iringa kwa geographical location yake inahudumia siyo Manispaa ya Iringa tu. Tunahudumia Jimbo la Kalenga, tunahudumia Isimani, tunahudumia Kilolo. Kwa sababu watu hawawezi kupita pale Mjini wakaenda kutibiwa Kilolo wakati pale kwenyewe kuna Hospitali. Hawawezi kutoka Kalenga wakapita mjini wakaenda kutibiwa Igodivaa wakati pale kuna hospitali. Hawawezi kutoka Ifunda wakaja kutibiwa huko Igodivaa. Kwa hiyo location yetu tunaomba sana mtusaidie. Mtuongezee kituo cha afya Kitilu, mtuongezee kituo cha afya Igumbilo kwa sababu huko ndiko kunakopokea watu kutoka kwenye Majimbo mengine na sisi tupo tayari kwa sababu kwa mfano Igumbilo pekeyake zahanati inahudumia zaidi ya watu 600. Sasa unaweza kuona mzigo unavyokuwa mkubwa. Kwa hiyo tunaomba.

Mheshimiwa Naibu Spika, ufinyu wa eneo katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa ni changamoto ambayo kamati imesema. Mimi niwaombe rejeeni mapendekezo yetu na RCC ya Iringa, kwamba Hospitali ya Wilaya ile ina eneo kubwa sana na wala pale siyo mbali hazifiki hata kilometa Sita. Mnaweza mkaamua structure zenu nyingine mkaziweka pale na mkatenga kama mkoa ili tuendelee kupata huduma za referral kwenye hospitali yetu ya Mkoa kuliko kufikiria kuihamisha pale Wizara ya Mambo ya Ndani ianweza ikawa shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini tunaomba wataalamu wa mifupa. Mnaona geographical location ya Iringa, ipo kati kati pale, barabara kubwa zote zinapita pale, ajali ni nyingi. Kwa hiyo, wote wanategemea kuja pale kwa ukaribu wake. Tunaomba sana wataalam wa mifupa, masikio tupate ili watu wakipata ajali kuliko kuanza kuwakimbiza Benjamin kuwapeleka Muhimbili, na distance ni ndefu, basi pale tupate wataalam wa mifupa ili waweze kutusaidia lakini tunawashukuru kwa ajili ya wataalam mliotuletewa wanne kwa ajili ya viungo bandia kwa ajili ya wagonjwa wa ajali.

Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niwashukuru sana pia kwa kuniteua kuwa Balozi wa Afya ya Akili Tanzania. Nakushukuru sana Waziri wa Afya na ninaona jambo hili linaongelewa kwa mapana yake. Sasa katika huo ubalozi naomba basi wale Isanga wanatibu tibasheria, kwa ajili ya wale wenzetu wanaoonekana kule kwenye sheria walipelekwa kimakosa kumbe ni matatizo ya afya ya akili wanapelekwa pale kusaidiwa kutoka Magereza. Wapeni basi hiyo shilingi bilioni moja na milioni 600 walizoomba changamoto ya kibajeti ili waweze kuwahudumia wenzetu wenye matatizo ya afya ya akili kutoka kwenye vyombo vya sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, nawashukuru pia kwa ajili ya Mirembe kuifanya kuwa Taasisi ya Afya ya Akili Nchini. Ilingane lingane basi sasa na taasisi ya afya. Tumesherehekea mwaka jana miaka 100 pale lakini bado hapaeleweki. Ilingane na taasisi ya afya ya akili.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri kama Balozi nisipoongelea masuala ya afya ya akili nitakuwa sijaitendea haki nafsi yangu mimi mwenyewe. Masuala ya matatizo ya afya ya akili ni makubwa. Ninakushukuru umeweka katika vipaumbele vyako Namba Sita kuimarisha huduma za afya ya akili, huduma za utangamano na tiba shufaa. Tunakushukuru sana kwamba umeiingiza lakini ipe uzito unaowezekana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Ummy, matatizo ya afya ya akili yanakuletea cost kubwa sana kwenye vifaatiba na matibabu. Kama WHO wanasema afya ya akili ni kutojitambua, ni kushindwa kupambana na changamoto, ni kushindwa kutoa msaada kwenye jamii, ni kushindwa kufanya kazi kuzalisha kwa faida, hiyo ilitakiwa ipewe kipaumbele cha kwanza. Tukiwapa watu wetu wakawa na uelewa mzuri kwenye akili zao. Kwanza mimi nataka ile pre copying kwanza. Kabla hujafikia kutupa dawa za afya ya akili, tujifunze kwanza masuala ya mambo yanayosababisha tukafikia kule kwenye kutumia dawa.

Mheshimiwa Naibu Spika, na hiii tuifanyaje? Tufanye kampeni maalum. Marekani tangu miaka ya 50 wana mwezi wa kampeni maalum kwa ajili ya masuala ya afya ya akili na wao wanaifanya Mei. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nasi tuchague mwezi maalum ambao tutaongelea masuala ya afya ya akili, tutawaambia watu wafanye meditation, tutawaambia watu mwezi huu nendeni mkafanyiwe massage, tutawaambia watu mwezi huu walie wasiolia, tutawaambia watu mwezi huu ni wa kusema matatizo yenu ili watu waseme, watu walie, watu wapate nafasi ya kwenda kufanya massage, watu wapate nafasi ya kwenda kutembelea misitu, waende national parks, waka-relax akili zao. Wakirudi wawe salama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Waziri haya matatizo ya afya ya akili ndiyo yanakufanya wewe unakuwa na wogonjwa wengi wasio na magonjwa ya kuambukiza hospitali. Unatumia fedha nyingi, kumbe watu wanatakiwa kufanyiwa tu mazoezi, watu wakishachangamana humu kwenye ndoa wakashindana wakidundana ngumi wanakuja kushonwa kwako wewe. Wanapiga x-ray mzigo unaongezeka kwako. Watu wakishindwa kufanya maamuzi sahihi wanawasababishia wengine presha. Ndiyo unapata taabu kubwa wengine veins zina-fail ndiyo tunapata taabu kubwa ya kununua ma-CT Scan kumbe mambo mengine yangetibika. Hapa umetuambia umetibu watu milioni 35.

Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa naongea na daktari mmoja akasema katika watu 10 wanaoenda hospitali, wagonjwa ni Watatu, Saba wote hawa wameenda kwa sababu tu ya afya ya akili. Mtu tu mke wake kaamua kumletea tatizo kwenye nyumba, mume amefyatuka presha iko juu, anahitaji CT scan anahitaji vitu kama hivyo. (Makofi/ Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tunatakiwa sisi tuone kwamba kampeni ya afya ya akili ndiyo kitu cha mwanzo kuliko vitu vingine. Ukija mimi ukaniahidi hapa leo kama Jesca Mbunge, ukaniahidi kwamba chinga wa Iringa tunakwenda kuwaletea shilingi milioni 700 watengenezewe structure zao, halafu usipoleta zile fedha mimi umenifanya niwe chizi, na wale machinga wangu wote wamekuwa machizi, hivi hatueleweki afya zetu zimeyumba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hii kampeni ianze kwenye Wizara za wenzio wasiwe motor behind kusababisha afya za akili waambie mnanivurugia watu afya zao. Ahadi ziwe zinatekelezeka, mipango itekelezeke ili watu wawe na afya nzuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, afya ya akili inakwenda kwenye masuala ya imani. Mtu akili ikishashindwa kufika mahali ikaamua jinsi ya kutatua tatizo lake anajipeleka sasa kwenye imani potofu, ndiyo kule wanafikia sasa mtu anaambiwa ukienda ukambaka mzee, ukambaka mtoto, ukambaka dada yako, ukambaka mama yako unapata utajiri. Sasa mwisho wa siku wakibakwa wanakuja kwako Waziri wangu Ummy wanahitaji dawa, wanahitaji huduma za afya, tunaongeza mzigo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo suala hili liweke mwanzo. Kampeni ifanyike kubwa ili watu wetu waelewe kwanza. Katika vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Kitu cha kwanza kinachomuangamiza binadamu ni kiuchumi, kisiasa, kinachomuangamiza kwenye jamii ni kukosa maarifa. Kama mtu hana understanding ya kwamba kulia ni deal, kulia kutaniponya, kwenda National Parks kutembea Selous kutaniponya, anafikiri ni anasa peke yake inatupa shida, mtu aelewe kwamba kwenda National Park siyo anasa unakwenda kufanya healing. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenda na watoto wako kuogelea wakati mwingine kutembea na watoto wako porini wakasikia harufu tofuti tofauti, sauti za ndege badala ya sauti za magari peke yake, ile nayo ni healing ya kutosha. Wewe kuendelea kusema mimi leo namtoa outing mke wako na ukasema leo simtoi mchepuko outing, namtoa mke wangu outing umemfanyia healing akirudi hatakusababishia matatizo ya afya ya akili, lakini watu wanadhani ni anasa.!

Sasa hivi Mabalozi tuko well empowered, tunaweza kufundisha watu Mheshimiwa Ummy hapa sasa bajeti ya Balozi iwepo maana yake sasa hata bajeti ya Balozi haipo. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa mambo haya Mheshimiwa Ummy nimekuwa nayafanya mwenyewe kivyangu, hayawezi kwenda kwenye upana huo. Tengeneza timu sisi twende tukawaambie watu. Tukaongee na vijana wetu, tuwaeleze. Hii tabia ya mtu kujiona eti mimi mwanamke lakini I am feeling, I am a man yaani yeye ni mwanamke anajiona ni mwanaume, no! hatuangalii jinsia kwa kujihisi, tunaangalia kwa structure uliyonayo kwa physical appearance yako. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa leo tunaongea hapa ushoga, tunaongea sijui usagaji kumbe watu wangekuwa vizuri tu, hana sababu ya kujiona mwanamke mwanaume, mwanaume mwanamke kwa sababu tayari akili yake inge- sense tu kwa kiungo nilichonacho mimi ni mwanamme sina sababu ya kujiona mwanamke. Kwa kiungo nilichonacho mimi ni mwanamke, sina sababu ya kujifanya mwanaume.

SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Balozi.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika ya Mwaka 2012
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia suala lililopo mbele yetu, Azimio la Kuridhia Itifaki ya Biashara ya Huduma ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Bara la Afrika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba leo niongee mambo mawili makubwa ambayo huwa tunayapata baada ya kupitisha maazimio katika Bunge lako Tukufu. Awali ya yote, nipongeze mtazamo wa Wizara kwa ujumla kwa sababu dunia inapokwenda sasa hivi, sisi hatuwezi kukaa kama kisiwa. Dunia imeshakuwa globalized, mambo yanafanyika kwa pamoja. Kwa hiyo, nawapongeza sana kwamba inawezekana hata kuridhia Azimio hili tumechelewa. Kwa kuwa sasa tumeamua kuridhia, nitakuwa na ushauri wangu katika mambo mawili kwa Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la kwanza ni timing au kwenda na muda. Jambo la pili ni mindset, jinsi ya kuandaa akili za Watanzania ili kwenda sawa na mipango ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikianza na timing, kila kitu lazima kiwe na muda maalum na ili ufikie malengo unayopanga, lazima ujipangie muda. Kamati imeeleza vizuri sana na imetoa ushauri mzuri sana kwamba tunakwenda kuridhia itifaki hii, cha msingi, ni lazima Serikali iangalie sera zetu, kanuni zetu na sheria zetu ziendane na wakati. Maana tunaweza tukaridhia hili, bado sheria zetu zikachelewa kurekebishwa, na kanuni zetu zikachelewa, bado na sera zetu zikawa ni zile zile, haitakuwa na maana ya sisi kuridhia haya. Kwa hiyo, tunaomba haya mambo tunapoyapitisha, yaendane na kasi na muda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule kwetu Iringa kuna usemi tunasema hivi: “Ng’ombe anayewahi kufika mtoni, ndiye anayekunywa maji masafi.” Kwenye biashara kuna watu wanaoitwa innovators. Wale watu ambao ni innovators mara nyingi hawafilisiki na ndio ambao huwa wanaendelea, wanarithisha utajiri kizazi na kizazi. Wale ambao wanajifunza kwa kuangalia matokeo, mara nyingi ndio wale ambao wanafilisika kila wakati. Mtu ambaye anabuni kitu akakianzisha mwenyewe, mwingine anasubiri mwenzie abuni, aangalie kama atanufaika, yule ndiye ambaye sasa anakuja kufilisikafilisika na biashara zake haziendi vizuri; lakini mtu yeyote anayeangalia mapema akawahi ile fursa mapema, ndiye anayeweza kufaidi na kunufaika na hiyo fursa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaridhia Azimio hili kwa nia ya kwamba sasa tunaenda kuboresha utalii wetu, tunaenda kutanua mipaka yetu ya kunufaika kibiashara kwenye nchi ambazo zinaridhia Azimio hili, lakini wenzetu watanufaika, watafaidi kwenye nchi yetu, na sisi watu wetu wakawa bado wana-lag behind au bado hatujawaandaa katika ile attitude, ndiyo unakuja sasa kwenye aspect namba mbili ya mindset. Ni namna gani tunawaandaa watanzania kwenye haya maazimio mazuri ambayo Bunge linayapitisha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, akili za Watanzania huwa zinashibishwa vipi maarifa, wakaelewa nia dhabiti ya Serikali inayokuwemo ndani ya haya maazimio? Kama tunapitisha hapa maazimio na Watanzania akili zao hazijaelewa vizuri, bado wanaona tunapoteza muda, lakini huwa yanageuka yanakuwa fimbo. Tunapitisha kwa nia njema kwa kuangalia ustawi wa Watanzania, kwa kuangalia kukua kwa uchumi kwa Watanzania, kwa kuangalia tunavyoongeza fursa za ajira, kwa kuangalia tunavyobadilisha maendeleo ya Watanzania, lakini kwa kuwa mindset zao ambazo zinakuja kuleta attitudes zao hazikusetiwa vizuri, yanatugeuka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumepitisha maazimio, lakini watu hawajui. Mheshimiwa Waziri lazima tukubali kwamba katika bajeti zetu tunatumia gharama kuwaelimisha watu. Mwalimu alishasema, kama wewe unaona kwamba elimu ni gharama, basi jaribu upumbavu au jaribu ujinga. Kama tunafikiri kwamba tutapitisha maazimio halafu Watanzania hawayaelewi yakaenda yalivyo, hebu tujaribu sasa kuyapitisha maazimio, watu hawayaelewi, halafu uone yakifika kwenye jamii jinsi yanavyoturudi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatakiwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye kuhakikisha kwamba watanzania wanaelewa nini hasa nia nzuri na dhabiti ya Serikali kwa kuwapa elimu waelewe. Usipom-set mtu vizuri kwenye akili aka-download uongo akauweka kwenye moyo wake, kuja kuutoa huo uongo aliouweka moyoni ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naiomba Serikali, kwenye maazimio kama haya yasiishie tu hapa, lazima kuwe na program maalum ya kuhakikisha Watanzania wanaelimishwa, wanawekwa sawasawa, waelewe nia thabiti ya Serikali yao, kwamba nia ya Azimio hili ni kutanua mipaka yetu hata ya ajira. Hatuwezi tukakaa humu ndani ya Tanzania…

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: … na Watanzania milioni 61 tukafikiri kwamba tunaweza kuajiri wote humu tukapata fursa, wakati kuna fursa ya ajira sehemu ya watu milioni 360…

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jesca, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ulenge.

TAARIFA

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda kumpa taarifa mzungumzaji Mheshimiwa Msambatavangu kuwa katika hilo analolisema, ni jambo jema sana na Umoja wa Mataifa tayari imeshaweka Azimio la kwamba sharing misinformation can seriously harm those around you. Nafikiri ni wakati sahihi sasa ili watu waweze kuelewa maazimio yanayotolewa na Serikali kwa usahihi, tuunge mkono jitihada za Umoja wa Mataifa katika kampeni hii ya watu kuto-share taarifa zisizokuwa sahihi bila kuwa na uhakika wa taarifa hizo, ahsante.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jesca, taarifa unaipokea?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea kwa mikono miwili, taarifa ya Engineer iliyoenda shule.

Mheshimwia Mwenyekiti, tunaambiwa kwamba taarifa ni nguvu. Azimio hili limeongelea, na sifa kubwa ya nchi yetu ni kuwa na amani na utulivu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikwambie amani na utulivu huwa inaanza kwanza kwenye choko choko za kupotosha taarifa. Tutachokonoa Mhimili wetu wa amani na kukorofishana humu ndani na tukapigana na tukaonekana hatuko sawa sawa baadaye tunakuja kuambizana kumbe kuna muongo mmoja alianzisha tu taarifa akaipeleka yeye isivyo wakati wenye taarifa sahihi hawakuzifikisha wakati sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niombe maazimio haya yamilikiwe na Serikali kama mnavyotumilikisha Wabunge na Watanzania wayamiliki haya ni mambo ya nchi yetu, wawe wanaelewa tuna desturi moja. Isiwe rahisi mtu anakuja tu kutuambia tumeuzwa, watu wengine pressure zinapanda mmeuzwa, mmeuzwa, mmeuzwa watu wanafikili. Mtu mwingine anaweza akatoka hapa na hili hili azimio akaenda kusema mmekodishwa, mmekodishwa SADC watu wakaona tumekodishwa au tumepangishwa. Kumbe nia siyo hiyo nia ni thabiti watu wapewe elimu tutumie fedha kutoa elimu kwa Watanzania wawe wanaelewa mambo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, utali ni package, Watanzania waelewe utalini package, mtalii anataka kutoka Afrika Kusini mpaka Cairo atumie ile nini wanasema Cape to Cairo apite nchi zote ndani ya Afrika akafike Cairo atoke Kusini mpaka kule. Sasa sisi tukikaa tumejifungua hapa hatujaridhia azimio hili tumetanua utalii wetu kupitia royal tour watu watatoka Marekani watakuja Tanzania watataka kwenda Congo tayari kuna vifigisu figisu sisi hatujafungua mipaka na kushirikiana na wenzetu wa Congo utalii hautokua? mindset za Watanzania hapo wengine tayari ukishaambiwa tu nchi nyingine kama Congo unajua ni vita tu, ukumbuki kumbe na akina Awilo Longomba nao watatoka huko huko kama kuna vita tu hakuna mambo mengine ya starehe kwanini wanaweza kupata muda wakajifunza na muziki?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii ni ku-unset mind zao wajue kwamba kuna fursa kwenye nchi zingine; lazima Watanzania wapate maarifa haya. Ndugu zangu tusipo wekeza kwenye mind set na altitude tunapitwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ukienda nchi kama Nigeria wanakwambia moja ya sehemu ambapo wameajiri watu wengi ni kwenye utume ni missionary namna ambavyo wameshirikiana na Taasisi za kidini halafu wamezifundisha zile Taasisi za kidini wamezi-empower kwa kutengeneza kanuni na sera nzuri wamewaruhusu dini waende nje ya mipaka ya nchi yao. Kwa hiyo, wameweza kufungua huko mamisikiti, wameweza kufungua huko makanisa kwa watu wengine wamekwenda kuajiriwa hata nje ya Nigeria.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunajipanga vipi kuhakikisha kwamba tunashirikiana na wenzetu, siyo tu sisi Watanzania, Taasisi za dini kuona kwamba tunawaita Viongozi wa dini tukawaambia kuna fursa hizi tunaomba mnaposimama mkitoa maelekezo yenu, mkitoa na nyaraka nyingine toeni na fursa hizi hapa ili Watanzania wajue kuna fursa sehemu mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama hayo hatutayafanya tutabaki kulaumiana na tutaonekana sisi tunaandika vizuri sana, tunamipango mingi sana, tunamaazimio mengi tunapitisha lakini hayana tija kwa Watanzania…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jesca ahsante sana, malizia sentesi ya mwisho.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimuombe Mheshimiwa Waziri, narudia tena lazima tuhakikishe tunawekeza kwenye fahamu. Watu wetu wajue na wewe ndiyo Waziri wa Viwanda na Biashara, watu wetu wajue ni kitu gani hasa kiko ndani ya hili azimio?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Azimio la Bunge Kuhusu Pendekezo la Kuridhiwa Mkataba Baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Dubai kwa Lengo la Kuanzisha Ushirikiano wa Kiuchumi na Kijamii katika Uendelezaji wa Maeneo ya Bandari Nchini
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi niungane na wenzangu, lakini kabla nataka na mimi niweke msingi kama ambavyo makubaliano haya yanaweka msingi na msingi wangu nitauweka kutoka kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu, nita-refer Biblia.

Mheshimiwa Spika, Hosea 4:6 inasema; “Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, kwa kuwa wameyakataa maarifa.” Mathayo 22:29 inasema; “Yesu akajibu akawaambia mwapotea kwa kuwa hamyajui maandiko.” Yohana 8:32 inasema; “Tena mtaifahamu kweli na hiyo kweli itawaweka huru.” Methali 11:9 inasema; “Asiyemcha Mungu, humpoteza jirani yake kwa kinywa chake, bali wenye haki watapona kwa maarifa.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naanzia hapo, hofu zetu zote ni kutokuwa na maarifa na Serikali inachokifanya sasa hapa leo imetupa maarifa ya kutosha, tuondoe sasa ile dhana yetu tuliyokuwa nayo kwenye vichwa, tukubali kuingiza vitu vipya, ili tusiendelee kudanganywa na kuangamia. Mimi kwa kuwa somo la sheria na mimi pia nilipata kidogo ukakasi, lakini sikutaka kuangamia kwa kukosa maarifa. Nilijipa muda wa kusema nitafute maarifa. Kwenye huu mkataba kwanza kitu cha kwanza unachotakiwa kujua unakwenda kwanza malengo yake ni nini.

Mheshimiwa Spika, kwa sisi tusio wanasheria, watu wa biashara tunapoandika research huwa kuna general objectives na kuna specific objectives. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lengo la jumla la mkataba huu ni kati ya nchi na nchi na hawa nchi na nchi wanaingia makubaliano ya kushirikiana kwenye masuala ya biashara kwenye maeneo ya bandari, automatic bandari zinakuwa kwenye maziwa, kwenye bahari, kwenye mito, hiyo ni ya ujumla na hii utaipata kwenye ibara ya pili; malengo ya mkataba.

Mheshimiwa Spika, ukija Ibara ya nne ya mkataba ambayo inaeleza mawanda au upana ndiyo hiyo tulikuwa tunasema scope, hii imejaribu kuelezea mawanda ya huu mkataba lakini imekwenda specific kwamba hawa nchi wameshaingia makubaliano na wenzetu wale wanafikiri kwamba kampuni ambayo labda inaweza tukaanza nayo ni ya kwao ya uwekezaji kwenye bandari ambayo ni DP World.

Mheshimiwa Spika, wakai-bind kabisa kwa specific objective kwamba ninyi mkienda Tanzania mtaingia mkataba baada ya kuwa hatua zote zimefikiwa pamoja na Bunge kuridhia, mkataba wenu mtakwenda kuingia kwenye maeneo haya. Ndio hiyo appendix moja tuliyoisema imeeleza kwa undani, lakini kilichonifurahisha katika kujua malengo, siyo kwamba bandari zote au maziwa yote au Tanga sijui huko Mtwara wapi zimeingia, hapana. Kwenye hiyo hiyo article four namba mbili inasema; Tanzania will inform Dubai of any other opportunities relating to ports, freezones and logistics sectors in Tanzania to allow Dubai or Dubai entities to express interest and submit proposals for consideration in respect of such other opportunities.

Mheshimiwa Spika, kwamba sisi Tanzanaia ndiyo tutakuwa na mamlaka ya kuwaambia wale Dubai tuna fursa nyingine huku labda kuna Bandari ya Mtwara tunaomba kwa sababu hapa mmefanya vizuri, tunaomba basi na Mtwara mkafanye kitu kama hiki. Wao watakuwa na responsibility ya kutafuta mtaji na kwenda kuendeleza, kusiamia na kuhakikisha wanaboresha. Hivyo ndivyo mkataba. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa wanasheria wakisoma wanatudanganya kwamba maziwa yote yamechukuliwa, bahari zote zimechukuliwa, mbona namba mbili hamuiangalii kwamba consideration ni sisi ndio tutakao-inform hawa kwamba tuna opportunities nyingine katika hizi water bodies za uwekezaji wa bandari, hapo mimi nikajiridhisha, nikaondoka na kuangamizwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama mwanasiasa kuna hoja nyingine utaifikiria kwamba je, ardhi ya Watanzania inachukiliwa? Maana ardhi ikishachukuliwa Tanzania maana mimi watu wangu watakaa wapi? Wapiga kura wangu Iringa watakaa wapi au wataenda wapi? Nikaenda Ibara ya nane inaeleza ukurasa wa 18 haki ya ardhi, lakini hapa Ibara hii inaitaka Serikali ya Tanzania kuhakikisha hatua muhimu zinachukuliwa ili kuwezesha DP World kupata haki ya matumizi ya ardhi. Yes, lazima sisi kama Watanzania tuwa-guarantee wale matumizi ya ardhi yetu. Wanaleta mitambo, sawa, watawekeza pale. Sasa kama hatutawalinda kwa sheria zetu tukaendelea kuwa na urasimu, tukaendelea kuwa-disturb, unategemea wawekezaji wataendelea kuwepo?

Mheshimiwa Spika, sisi tumepewa jukumu la kuwalinda hawa wawekezaji na ni jukumu la msingi, sio kumiliki ardhi. Katika hii ukurasa wa tisa inaeleza tafsiri, hakuna mtu anakuja kumiliki na kuchukua ardhi ya Watanzania. Ukurasa wa tisa, Land Rights inavyoeleza interpretation inasema; “Land Rights shall mean all those rights (excluding rights of ownership of the land in Tanzania.” (Makofi)

Mheshimiwa Spika, imeondoa hilo suala la umiliki wa ardhi, kwa hiyo wao watakuwepo kwenye matumizi ya ardhi. Sisi tunasoma hivi, ili tusiangamie hata kama sio wanasiasa. (Makofi)

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, manufaa kwa Watanzania...

SPIKA: Mheshimiwa Jesca Msambatavangu kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei.

TAARIFA

MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba huu mkataba na anavyozungumza vizuri sana Mheshimiwa wetu, jina lake gumu sana, Mheshimiwa Jesca, ni kwamba wanaangalia logistic ya from Dar es Salaam na kufikisha mzigo Burundi, Rwanda kote na Uganda. Kwa hiyo, lazima wafikirie kwamba ili iwe ni efficient lazima waweze kuboresha bandari za Ziwa Victoria, kama itakuwa hivyo na pia waweze kuweka maeneo ya bandari kavu sawasawa na kadhalika na pia kuwezesha hizi export… (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Jesca Msambatavangu, unapokea Taarifa hiyo?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, nashukuru sana kwa Taarifa; fahari ya wazee ni mvi kichwani, hiyo ndio hekima ya mzee. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwamba wewe huwezi kumpa mtu atoe makontena pale usimpe sehemu ya kuweka makontena. Huyu DP World ana bandari kavu Rwanda, usimpe access ya treni kwenda Rwanda kupeleka makontena yake; ana-supply na South Africa, sijui na wapi huko na Djibouti huko ana mikataba inaendelea, usimpe access kwamba atakwenda hadi huko kupeleka makontena, haiwezekani. Kwa hiyo, ndio maana kuna appendix II kwamba, badae tutakuja kuendelea kuongea sisi tutakapokubali tutamshirikisha yeye.

Mheshimiwa Spika, kama mwanasiasa manufaa hayo mengine ya ushirikishaji, tatizo kubwa tulilonalo saa hizi ni ajira. Mimi nikaangalia changamoto, hivi mimi watu wangu wa Iringa wanaosoma pale Chuo cha Bandari, Dar es Salaam watapata kazi au ndio zinakwisha au wanafukuzwa?

Mheshimiwa Spika, nikaangalia Ibara ya 13 - ushirikishwaji wa wazawa, ajira na majukumu kwa jamii. Tunahangaika hapa kutoa ajira, tunaleta wawekezaji ili tupate ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, anasema ibara hii, inaelekeza kuwa mikataba itakayosainiwa ya utekelezaji wa mradi lazima iainishe mpango wa ushirikishwaji wa wazawa katika utekelezaji wa mradi husika, unaona? Na maeneo yafuatayo yatapewa kipaumbele kwenye hii article. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hiyo inasema kutoa kipaumbele kwa kampuni za ndani katika zabuni na ushauri pale ambapo makampuni hayo yatakidhi vigezo. Baadhi ya miradi inayokwenda kutekelezwa iwe imetolewa kwa kampuni za ndani na raia wa Tanzania; kutekeleza mpango wa mafunzo ya uendelezaji wa raia wa Tanzania; kusaidia kujenga uwezo wa vyuo/mafunzo katika tasnia ya usafiri majini na usafirishaji; na kuwezesha tafiti na uhamasishaji wa teknolojia kwa wazawa.

Mheshimiwa Spika, hii tayari msingi umewekwa wazawa wetu sisi…

SPIKA: Sekunde 30 malizia.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, wazawa watapata ajira, lakini na wale waliokuwepo wataboreshwa kwa kupewa mafunzo. Maana asije akasema nimeweka kitu cha kisasa hapa Mtanzania hawezi, tunataka ampe mafunzo aweze kuki-operate kile kitu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunataka nini?

SPIKA: Haya, ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, mimi naunga mkono hoja, ahsante. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuchangia katika Mpango huu wa mwaka 2022/2023. Pia nami niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine kuendelea kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama yetu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anajali sana hali za wananchi wetu, hasa kwa kuangalia kuwekeza kwenye elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara. Tunamshukuru sana na tunamwombea Mungu aendelee kumpa afya na hekima katika kuliongoza Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapomshukuru Mheshimiwa Rais naomba pia Mheshimiwa Waziri wa Fedha anapoandaa hii Mipango, kwa kuwa Mama sasa ameshafanya lile jukumu lingine ambalo lilikuwa ni madarasa na sehemu nyingine, kwenye afya na vituo vya afya, basi awe anatuletea pia na taarifa ya yale mengine tuliyoyapanga sisi wenyewe humu ndani, yanakwenda vipi? Zile chenji za fedha ambazo zingebaki au zilitakiwa zitumike, hazijatumika, zimeendaje? Tunaomba hilo tuwe tunaambiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Mheshimiwa Waziri wa Fedha awe anatuambia pia, katika Mpango huu aliousoma na Kamati ya Bajeti imeelezea kwamba, kuna wakati fedha hazikupelekwa MSD kwa sababu ya wizi uliokuwa unatokea pale MSD. Basi tuwe tunapewa pia mrejesho, chenji, wakati ule walipozuia zisiende; zile ambazo zilizuiwa ziko wapi? Au zimefanya nini? Itakuwa ni vizuri sana tukijua. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuchangia Mpango huu, moja kwa moja kwanza, nichukue fursa hii kuuelezea Mpango wenyewe na kuangalia kwamba Mpango huu ndiyo mwanzo, ukiwa ni mwendelezo wa Mpango wa Miaka Mitano ulioanza mwaka 2016/2017, ambao unaisha mwaka 2021 na sasa tunaingia Mpango mwingine wa Miaka Mitano. Katika vipaumbele vya ule Mpango wa nyuma, mojawapo ilikuwa ni kukuza uchumi na kuendelea kujenga msingi wa uchumi wa viwanda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tunapoongelea msingi wa uchumi wa viwanda, huwezi kuacha miundombinu ya barabara, miundombinu ya umeme, vile vitu ambavyo vitachochea kukua kwa uchumi. Sasa nimepita katika Mpango na tuna miradi yetu ya kimkakati na tuliposema ni miradi ya kimkakati, maana yake ni miradi ile ambayo inajenga msingi ambao utakuza uchumi wa viwanda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, tunasema miundombinu ya barabara, miundombinu ya reli na mambo ya umeme. Sasa tuna barabara na tuna miradi ya kimkakati ambayo sehemu nyingine ilikuwa inatupelekea kuingiza mapato zaidi au kuongeza pato zaidi la Taifa ambalo lingeweza kufufua sekta nyingine za viwanda. Kwa hiyo, tuna barabara kwa mfano, tuna miradi ya utalii kama ambavyo katika Mpango wake anasema; kukuza utalii ili kuongeza pato la Taifa na tunajua Ilani ya CCM inatutaka tuongeze pato la Taifa kufikia dola bilioni sita ifikapo mwaka 2025. Pia tuongeze watalii wafike milioni tano ifikapo mwaka 2025 na tunategemea sana kutanua uwanda wetu wa utalii ikiwepo utalii Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna mbuga kubwa ambayo ni ya pili Afrika ambayo ni Ruaha National Park. Tunaposema utalii wa kusini, unachukua Mikoa yote ya Kusini. Tunaiona Katavi, tunaangalia Kimondo cha Songwe, tunaangalia Njombe Kitulo, tunaangalia Selous, tunaangalia ule utalii wote wa kusini pamoja na Ruaha yenyewe. Sijaona kama Serikali imeweka kwenye Mpango suala la kutengeneza barabara zinazoingia kwenye ile Mbuga. Zaidi sana naona shilingi bilioni 90.2 ambayo itashughulika na miundombinu kufidia hasara zilizotokana na Uviko kwenye Mashirika yale yale ya Utalii kama TANAPA na wengine, lakini hatuoni Mpango ukituambia kuna kutengeneza zile barabara zinazoingia kwenye ile Mbuga ili watalii wanapofika waweze kuingia kwa urahisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna barabara ile kuanzia Iringa, kilomita 104 kuelekea Ruaha. Tuna barabara nyingine ambayo inaanzia Iringa pia inaingilia Idodi Jimbo la Isimani huko. Hatuoni kama Serikali ina Mpango, zaidi sana waliweka Mpango wa kutengeneza madaraja. Sasa tunatengeneza madaraja wakati sehemu nyingine za barabara ni mbovu. Hii ni miradi ya maendeleo ambayo ingechochea uchumi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine, tunaishukuru sana Serikali kwa namna ambavyo inaonyesha uchumi wetu wa Tanzania, pamoja na athari za Uviko bado uchumi wetu umekua chanya. Tusipojiangalia, sisi ni nchi mojawapo katika nchi 11 zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa chanya. Nchi nyingine zote 33 zinakua hasi, ukiondoa Gabon na ile Afrika ya Kati ambayo uchumi wake ni zero. Sasa tusipojiangalia tulikuwa tunakua uchumi chanya, lakini tutakuja kupitwa na wale waliokuwa na uchumi hasi, kwa sababu ya (nitumie neno lile lile) utelezi ambao tunauweka wenyewe kwenye mipango yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kurudia hapa ni hiki hapa; moja ya sababu kubwa ya kufanya uchumi ukue hasi au kushuka kwa uchumi imeonekana ni Uviko na sababu zilizosababisha ni kufungwa kwa uzalishaji kwenye nchi nyingi kwa jina la kuaminika ambalo lilikuwa ni lockdown. Sisi Tanzania Mwenyezi Mungu alitusaidia tukiwa na Serikali yetu mahiri na shupavu, hatukuwa na lockdown, lakini viongozi wetu walifuatilia ile misingi ya afya tukaweza kuwa salama, tukaendelea na uzalishaji na uchumi wetu ukaendelea kukua katika hali ya kuwa chanya, siyo hasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine kilichoathiri; kwa nini sisi tulikuwa tunaendelea na shughuli za uzalishaji? Kwa sababu, kwa kawaida pia linapotokea tatizo ni fursa, ni mwanya pia wa kuendelea kiuchumi. Kama ninyi ambao mtakuwa mmejipanga vizuri mnaendelea kuzalisha, mngeweza kuwa-serve wenzenu wengine ambao walikuwa wamejifungia.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa. Ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nashukuru sana. Basi naomba kuunga mkono hoja. Mengine nitachangia kwa maandishi. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nashukuru kwa kunipa nafasi nichangie lakini nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya hasa ya kupeleka fedha nyingi kule chini kwenye grassroot kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie jukwaa hili na nafasi hii kipekee kabisa kuwashukuru sana Watanzania wanaolipa kodi kwenye Taifa letu. Tumeambiwa takwimu zao kwamba ni wachache sana lakini wanabeba mzigo mzima wa watu milioni 61 na sisi tuna walipakodi tumeambiwa walioandikishwa hapa milioni nne na wanaofanya vizuri wapo. Nichukue nafasi hii niwashukuru sana Watanzania mnaolipa kodi kwa ajili ya Taifa letu. Kama unaona kuna mtoto anakwenda shule, kuna hospitali zinajengwa, kuna barabara zinajengwa ni kwa sababu yako wewe Mtanzania unayelipa kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna hiyo nitoe wito kwa Watanzania wengine na sisi tujisikie wivu kuchangia maendeleo ya Taifa letu. WHO wameainisha maeneo ambayo yanaweza yakasababisha tuka-improve biashara au tukafanya biashara zetu zifanikiwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa wanasema lazima tuweke mazingira mazuri kwenye biashara. Hawa Watanzania milioni nne wanaolipa kodi hebu tuwawekee mazingira mazuri tuwaheshimu, tuone kwamba jambo wanalolifanya kwenye Taifa hili ni kubwa sana. Kwanza tunapoweka mazingira mazuri tutaweza kukuza biashara, tutakuza uwekezaji, tutakuza ajira lakini tutajiletea maendeleo ya Taifa letu na wanaendelea kusema kwamba yapo mazingira tunayotakiwa kuongelea ambayo tutatakiwa kuyaweka.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza tuwe na mazingira huru ya biashara, tuwe na kanuni nzuri rafiki kwa ajili ya wafanyabiashara, tuwe na soko huria lakini tuwe na mipango ya kutafuta masoko mapya na kukuza masoko tuliyonayo. Kubwa zaidi tuwe na mipango ya kuwahakikishia wafanyabiashara mazingira mazuri ya kufanya biashara. Hapo ndipo tutakapoongeza hiyo tunasema tax base yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunapoongelea suala la kuongeza au kutanua masoko tumeshaambiwa hapa. Tumeona kazi moja tu ambayo Mheshimiwa Rais ameifanya ya Royal Tour, namna ambavyo imeongeza fursa mpya katika soko letu la utalii ilivyotanua soko letu la utalii na kuvutia utalii. Sasa tunatamani katika hiyo hali na sekta nyingine ziige ili kuweza kupalilia kile ambacho Mheshimiwa Rais amekifanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunasema kwamba tunataka kuweka mazingira mazuri, tuongee tu kwenye utalii. Leo watalii wameongezeka lakini watalii wakija kutalii wanapenda wapate huduma stahiki, wanapenda wale bata. Leo watalii wetu wakiingia Tanzania hata uwezo wa kupata kubadilisha fedha za kigeni ni shida kutokana tu na kutokuwa na maduka ya fedha za kubadilisha yaani maduka ya kubadilisha fedha za kigeni hakuna. Taarifa inasema hapa mpaka Mei, 2023 tayari tuna maduka ya fedha tuliyoyasajili 11. Kule wakati kwenye semina tuliambiwa ni maduka nane yenye matawi 36. Kutoka kwenye Bureau de Change tulizokuwa nazo 2019, 400. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii wazungu wakija Iringa hawana kwa kubadilisha dola ili waende wakale bata Ruaha. Sasa wale Mama aliokwenda kuwaita wanakuja, wanakuja huku wanakutana na broke hakuna pa kubadilisha fedha za kigeni wanarudi mwaka mwingine? Hayo ndiyo mazingira lakini kilichosababisha ni kutokuwa na kanuni rahisi za kufanya biashara hiyo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo naona kwanza kwenye biashara hii kuna ubaguzi. Huwezi kuniambia umewapa watu leseni nane wana matawi 36 nchi nzima. Wenye capital requirement ya shilingi bilioni moja moja mmeanza kutubagua Watanzania kwa kuwapa fursa za kufanya biashara kwenye nchi hii watu wenye uwezo wa fedha. Tusio na uwezo wa fedha maana yake tusiwekeze wenye mitaji yetu midogo midogo. Hao mabilionea ndiyo wawekeze. This is not right! Lazima Watanzania wapewe fursa sawa ya kufanya biashara, huo ni ubaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kujenga imani kwa wafanyabiashara ni pamoja na kauli za viongozi kuzingatiwa. Watanzania wana imani kubwa sana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Leo hii kama Rais atatoa kauli au atatoa maelekezo kwa idara yoyote au Wizara yoyote ya Serikali isipozingatiwa ni kumdharau Rais wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa leo Watanzania watamwamini nani? Hata Mbunge nikaenda kusema kuna mpango mzuri huu hapa, kama Rais alitoa kauli haikuzingatiwa haikufanyiwa kazi, tunapoteza imani kwa wafanyabiashara kuendelea kuwekeza. Leo tuliambiwa kodi za miaka mitano Rais kasema miaka mitano ya nyuma, miaka sita zisichajiwe lakini hakuna lolote lililofanyika kwenye Mamlaka zetu kuhakikisha hilo halifanyiki na sana sana ukienda wanasema sisi tunasimamia sheria. Nchi hii Watanzania watamsikiliza nani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu Rais anapokuja anapotoa maagizo anakuwa ameshafanya tit for tat amejua hili linatakiwa mabadiliko ya haraka lakini haya mambo hayafanyiki ndiyo kuweka ugumu kwenye mazingira ya biashara. Watu wanashindwa kutanuka, watu wanashindwa kuwekeza kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii ahadi za viongozi zitekelezwe. Mheshimiwa Waziri wa Fedha pale Iringa mwaka jana mwezi wa nane saa hizi tunakaribia mwaka mzima Mheshimiwa Rais alisema na kupitia wewe kinywa chako Mheshimiwa Waziri naongea na Mwenyekiti lakini kwa maelekezo ya Spika kwamba shilingi milioni 700 tutapewa kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya machinga. Wale machinga wakiwezeshwa kwenye mazingira yao hayo madogo wata-graduate watakuwa wafanyabiashara wakubwa kuja kuungana huku kwenye shilingi milioni nne. Tukiwawekea mazingira saa hizi ya kumaliza mitaji yao na kuua mitaji yao hatutapata wafanyabiashara wengine wanao-graduate kuingia shilingi milioni nne. Waongeze idadi ya shilingi milioni nne ifike sita wote wanatakiwa watoke huko kwenye biashara ndogo. Kwa nini tunashindwa kuona umuhimu wa kuwatengenezea mazingira mazuri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo hii Mheshimiwa Waziri amesoma taarifa yake hapa kwamba anaziwezesha benki, Tanzania Postal Bank na ile benki nyingine wanazipa mitaji lakini kuna benki nchi hii Mheshimiwa Waziri ni community banks, benki ambazo mama ntilie wamechanga hela zao wamepata mtaji wamefungua community bank kama Mkoba Bank ya Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo TRA mmewachukulia shilingi milioni 600 kutoka kwenye account yao kwamba wanadaiwa kodi za miaka hiyo ya nyuma sita, saba huko. Shilingi milioni 600 za mama ntilie wa nchi hii. Hivi Tanzania sisi huwa hatusamehewi kweli madeni huko na mataifa makubwa? Sisi tunakosa kuwasamehe mama ntilie unakwenda ku-freeze account yao, shilingi milioni 600 mama ntilie waliochanga wakaanzisha community bank yao kwa mtaji wao Benki ya Mkoba Tawi la NMB Mkoa wa Iringa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tusipotengeneza mazingira dunia hii kila nchi inatengeneza destiny yake yenyewe. Tunaongea haya maneno ili wenzetu wayafanyie kazi. Kama benki nyingine unazipa mtaji unaziwezesha, kwa nini community bank usizisamehe madeni yao hii ili wale wakinamama waendelee kukopeshana wenyewe? Tusipoangalia tunapigana wenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu kingine ni cha mwisho. TRA nawaomba sana TRA wao ni Watanzania wanapata mental health bila sababu za msingi. Wanakuwa hawana afya nzuri za akili bila sababu za msingi wanakuja kustaafu wanakufa mapema bila sababu za msingi. Wanakosa marafiki mitaani bila sababu za msingi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiajiriwa TRA siyo kwamba umepewa kazi ya kutoa roho za watu. Salimia watu tengeneza mazingira mazuri, hawa Watanzania unayekuwa umemnunia unampa hiyo waliyosema Mheshimiwa Nyamoga lazima alipe shilingi 200,000 lazima akulipe wewe shilingi 50,000 ndiye aliyekuajiri, ndiyo anayekulipa hapo mshahara na kodi yako.

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: …Kwa nini usimhudumie vizuri umbambikize kodi kwa sababu hajasoma halafu unakuja unasema usipojua sheria siyo sababu ya kutosamehewa sheria? Wewe ulisomeshwa na kodi yake ili umsaidie kumuelimisha. (Makofi)

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante na mimi nashukuru kwa kunipa nafasi hii kuweza kuchangia katika ripoti hizi tatu ambazo zimewasilishwa.

Mheshimiwa Spika, mimi na-declare interest kwamba ni Mjumbe wa Kamati ya LAAC. Nachukua nafasi hii kwa kweli kuwashukuru Wajumbe wa Kamati ya LAAC, haya ambayo Waheshimiwa Wabunge ninyi mnakutana nayo sasa hivi sisi kwetu imekuwa ni kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, unaweza ukaona uzito wa kazi yetu kwa kweli kama Wajumbe wa LAAC na namna ambavyo tunaathirika sana kwenye akili tunapokuwa tukichambua ripoti hizi za CAG hasa kwenye suala la Serikali zetu za Mitaa.

Ndugu zangu mimi nawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa namna ambavyo mmeongelea kwa uchungu na sisi mmetuunga mkono kwenye uchungu wetu na hayo ndiyo ambayo yapo ndani ya nchi yetu na kwa kusema hivyo hatuna maana kwamba pamoja na haya ambayo yapo haina maana kwamba hakuna mazuri yaliyofanyika. Mazuri yapo mengi sana lakini katika hayo mazuri madoa yake makubwa ndiyo haya.

Mheshimiwa Spika, CAG ni chombo ambacho sisi wenyewe tumeridhia, tumeweka utaratibu ili kuiendesha nchi yetu, lakini inaonesha kwamba baadhi ya wenzetu wanaona anakuwa kama adui. Hili tunalipata kutokana na namna ambavyo CAG akitoa maoni yake yanashughulikiwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, zipo Halmashauri nyingi sana hazijibu hoja za CAG, hoja ambazo zinaelezea ubadhirifu na upotevu wa hivi vitu na rasilimali za nchi katika Taifa letu. Sasa mimi nashindwa kuelewa kama sisi wenyewe tumepitisha na tumekubali kiwe ni chombo ambacho kinaweza kutusimamia, ni kwa nini hatuwezi kusimamiana na kuhakikisha kwamba hoja za CAG zinajibiwa? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kitu cha kwanza ambacho mimi nakiomba, kwanza zile Halmashauri ambazo hazijibu hoja za CAG ndiyo indicators za kwanza kwamba haziko tayari kuhakikisha kwamba zinasimamia rasilimali za nchi hii zinatumika kama zilivyopangwa na hiyo iwe ni indicator ya kuanza kuwafuatilia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine nilichokiona, mfumo wetu wa uendeshaji, hapa kila mtu analalamika. Mheshimiwa Rais amekabidhiwa hii ripoti analalamika, Wabunge tumekuja tunalalamika na Serikali nayo ikija italalamika, watendaji nao wanalalamika, sasa ni nani atakayekwenda kutatua hili tatizo?

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Spika, Taarifa.

SPIKA: Mheshimiwa Jesca Msambatavangu kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Jenista Mhagama.

TAARIFA

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, nampongeza Mheshimiwa Jesca kwa mchango wake, lakini naomba niweke sawa mchango wake pale anaposema kwamba Mheshimiwa Rais analalamika, hapana, Rais hajalalamika, kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 34 ama 36 Mheshimiwa Rais amepewa majukumu ya kukasimu madaraka yake kwa watendaji mbalimbali kwenye taasisi.

Mheshimiwa Spika, alichokuwa anakifanya Mheshimiwa Rais ni kujaribu kuwakumbusha watendaji wote wajibu wao wa kusimamia na kuhakikisha kila jambo linakwenda sawasawa. (Makofi)

Kwa hiyo, ukimtafsiri Rais kwa kuendelea kuwasimamia watendaji wake na kuwaelekeza kazi zinavyotakiwa kufanywa kule siyo kulalamika. Kwa hiyo, nilikuwa naomba kumpa taarifa Rais hajawahi kulalamika, anaendelea kutoa maelekezo. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika,…

SPIKA: Ngoja Mheshimiwa. (Kicheko)

Mheshimiwa Msambatavangu unaipokea taarifa hiyo?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, sijui niipokee au nisiipokee? Nitabaki neutral lakini nataka kusema hivi, wakati Mheshimiwa Rais anakabidhiwa taarifa hii sisi wote ni Watanzania na tulikuwa tuna masikio, tulimsikia akilalamika kutokana na ubadhirifu uliofanywa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuendelea kujipamba hapa na kujitekenya wenyewe kwamba hakulalamika haisaidii. Kulalamika siyo dhambi, ni kutoridhika na hali inavyokwenda. Sasa sisi Wabunge hapa tunalalamika, Rais analalamika, ninyi Mawaziri ndiyo mnatetea, kwa hiyo ninyi mnakubaliana na huu uovu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Watanzania wamelalamika, sisi tunalalamika kwa sababu hatukubaliani na hii hali kwamba hiki kinachoendelea siyo sawa. Kwa hiyo, hakuna aliyepongeza, Rais hakupongeza kwamba hii taarifa iko sawasawa. Sisi tunachowaomba wao waende wakasimamie na mimi naomba tusichekeane, unajua kila mtu Mungu kamuumba kwa ajili ya uwezo wake. Kuna mahali…,kwa mfano naweza nikatoa mfano mdogo hapa kuna mahali tunahitaji daktari mpole wa kumfariji mgonjwa, kuna mahali tunahitaji nesi mkali wa kumpiga mama ili ajifungue. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi kuwalaumu manesi wote kwamba wote wanafanya kitu…hapana, kwa sababu watoto hawatazaliwa kama manesi wote wakianza ku-act kama wapole fulani hivi kama wachungaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lazima tufike mahali tusimamiane, Mheshimiwa CAG anaongea hapa mass dropout ya watoto, amesema watoto wa shule za msingi karibu 19,000 wameacha shule. Watoto hawa ni kati ya umri wa miaka sita mpaka 13 - 17 wamekwenda wapi? Tuna Wizara inashughulika na watoto, watoto leo ukipita wanavuta shisha, watoto leo ukipita kuna snacks zinawekwa bangi watoto wanakula. Serikali ipo mnaona, Waziri Mkuu alisimama hapa akazuia package za viroba ili watoto wetu wapone. Leo mmerudisha tena vinywaji vilevile vyenye package ndogo watoto wetu wanalewa mitaani, wanakufa tu haya yote CAG ameyasema. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tunakaa hapa tunachekeana mimi nataka niwaambie hivi Taifa hili lina Mungu na nafasi uliyopewa Mungu ameamua uwepo. Ikishindikana sisi humu tunasema halafu hatua hazichukuliwi sisi tunaingia kwenye maombi Mungu atusaidie namna ya kuwa-overhaul, hatuwezi kuacha watoto wetu wanangamia. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, CAG anasema hapa, leo kuna sababu CAG ametoa za mass dropout; ngoma, watu wanakwenda kwenye ngoma. Mkurugenzi wa Bagamoyo tunamuuliza kwa nini watoto wengi hawaendi shule namna hii anasema ngoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hivi kweli watu tumekaa ni viongozi…, wewe nikuulize kina mama tupo humu ndani, Wabunge wanawake tupo humu ndani, wewe unaweza kuolewa na miaka 13 ukashika mimba kwa ile labor pain ukaenda kujifungua?

Mheshimiwa Spika, leo CAG anasema watoto wanapata mimba wakiwa na umei kati ya miaka 13 – 11. Watoto darasa la saba hawamalizi, tuna Wizara ya Elimu, tuna Maendeleo ya Jamii sijui tuna nini, watoto wanapotea hatuoni. Watoto wa sekondari, mass dropout sekondari, sisi zaidi ya asilimia 50 watoto wanatoka na division zero na division four kwenye public schools.

Mheshimiwa Spika, tuwashukuru Manispaa ya Moshi; Moshi tulipowauliza kwa nini watoto wanatoroka shule? Mkurugenzi akasema Moshi watoto wengi wametoka kwenye public schools wamehamia kwenye private schools. Sasa ndiyo tuulizane humu ndani wengine wanatoka kwenye shule za Serikali kwenda kwenye shule za watu binafsi, ni dropout hiyo. Lakini wengine wamekwenda ngoma, ni dropout hiyo, lakini wengine wanakwenda masoko ya usiku. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, Buhigwe, Kasulu eti kuna watoto wanakwenda masoko ya usiku; mnauza nyama kule, mnauza vitu, mnauza na watoto huko huko. Watoto wanashindwa kusoma, tumekaa hapa kama viongozi tunafanya nini? (Kicheko)

SPIKA: Sekunde 30 Mheshimiwa malizia mchango wako.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kitu kingine wafanyakazi; watumishi bado wanadai shilingi bilioni mia moja naa, kweli leo kuna Halmashauri moja ya Pwani watumishi saba wameamua wachange hela wapeleke kwenye Mfuko wa NSSF kwa sababu Serikali haikuwachangia ili walipwe mafao yao, wazee wa nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mbunge wa Kigoma alisema hapa kule mnafanya ni sehemu ya adhabu ni kweli. Kigoma na Nkasi watumishi wanadai mishahara, hawajalipwa mafao yao, tumesema kwa nini? Mkurugenzi anasema mimi nilikuwa bado sijafanya uhakiki. Kuna mtu anaitwa Urassa kutoka Kigoma ni Afisa Uchaguzi anadai shilingi milioni 63, mwingine anadai shilingi milioni 71. Kuna Godigodi anadai shilingi milioni 53 hawa ndiyo mnategemea wakasimamie miradi ya shilingi bilioni mbili, bilioni sita wakati wanawadai fedha zao, arrears za mshahara zaidi ya shilingi milioni 19 wataweza wapi? (Makofi
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2021
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nashukuru kwa kunipa nafasi. Nitaanza na Wizara ya Miundombinu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza niishukuru Serikali kwa kazi kubwa inayofanya katika kutujengea miundombinu. Lakini ninaomba tu, tulikuwa tumepitisha hapa mpango wa miaka mitano na tukaomba wenzetu waweke kipaumbele katika kuimarisha miundombinu inayoelekea kwenye miradi ya kimkakati ikiwepo Ruaha National Park.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani sisi Iringa tupo tayari kuwajaza dollar, kuwajaza pound sterling, kuwajaza ma-euro, lakini utelezi unatokea Wizara ya Miundombinu. Tunaomba barabara zile zinazoinga Ruaha National Park zifikike, tujengewe kwa kiwango cha lami. Ili tazalishe madola tutatue matatizo mengine ya sehemu zingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naingia Wizara ya Nishati na Madini, nitaanza na Shirika la STAMICO. Tunaomba sana STAMICO tuwapongeze kwa kazi nzuri mnayofanya, na limekuwa ni shirika sasa ambalo linakwenda kujitegemea baada ya kuwa ICU muda mrefu. Lakini sasa tumejitahidi kuweka maafisa madini kwenye kila mkoa, na tumejitahidi kutanua wigo wa ulipaji madini mpaka kwenye madini ya ujenzi, tunasema mchanga, mawe na kokoto.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba sana kwenye mchanga, mawe na kokoto wamejiajiri vijana wetu wa hali ya chini sana. tuwaombe sana Serikali muangalie namna ya kuwabeba wale vijana wasije tena wakafukuzwa na ma- tycoon halafu vijana wetu wakabaki tena wanahangaika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Posta lifanyiwe rescheduling. Shirika la Posta lipambane kutokana na mazingira ya biashara yaliyopo, tuondoe urasimu. Hawawezi kupambana na Vodacom Tanzania wakati wao bado wana urasimu na mautelezi kibao, mlolongo mrefu wa maamuzi, timing inakuwa iko nyuma, wafanyakazi wanalipwa bila kuangalia marupurupu kutoka na kwenye industry. Wajitahidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TANESCO; TANESCO tunaweza tukailaumu sana lakini wafanyakazi wa TANESCO na TANESCO yenyewe siyo kwamba wanawajibika wako kutengeneza umeme kwenye nchi hii. Lazima Serikali iwawezeshe. Tuliwaambia TANESCO wasambaze umeme kwa 27,000 wakati hatujawapa hela yoyote ya kusambazia umeme huo, wakati tunajua vijijini wao wanasambaziwa kwa fedha inayokatwa kwenye mafuta kutoka kwenye REA.

Mheshimiwa Mwenyekiti, TANESCO walijiongeza. Inawekezana fedha za kukarabati mitambo wakatumia kupeleka umeme kwa wananchi. Sasa mitambo imeshindwa kukarabatiwa ndiyo inatokea kwamba umeme unakatika kila wakati. Serikali iliangalie hilo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna ishu ya Kitengo kinaitwa TEITI. TEITI ni Kamati ya Usimamizi, Uhamasishaji, Uwazi na Uwajibikaji kwenye Sekta ya Madini, Mafuta na Gesi Asilia. Kazi yake kubwa ni kutuweka wazi kupitia mikataba, kuangalia mapato ya madini yanayopatikana kwenye nchi yametumikaje kwa maslahi mapana ya wananchi. Yapo maswali mengi sana kwenye jamii, kila ukitaka kuwaambia jamani tuchangie hiki wanakwambia ninyi mna madini, mna gesi, kwa nini hamuwezi kutumia hizo fedha?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa TEITI ni kitengo ambacho kinaweza kutusaidia na kipo rasmi kwa ajili ya kazi hiyo. Lakini TEITI ina changamoto, watumishi wa TEITI wako saba wakati TEITI inakitaji kuwa na watumishi 60. Tunategemea hawa wakaangalie uwajibikaji, wakaangalie uwazi kwenye madini, wakapitie mikataba, watuelimishe wananchi mapato tuliyopata kwenye madini, kwenye mafuta, kwenye gesi asilia – watumishi saba. We are not serious. Kwa hiyo tuwasaidie TEITI ili waweze kufanya vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini na bajeti yao iongezwe. TEITI leo tumewatengea milioni 443, wakati hata watu wa nje wanaotusaidia, wale wahisani, wameona TEITI kazi yake ni nzuri, wamewatengea bilioni moja na milioni 725 na wameshalipa, wameshawapa nusu ya hiyo fedha. Na sisi tumewapa milioni 200.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kupunguza maswali mengine yasiyokuwa na msingi; madini mnatumiaje, mapato ya gesi yanatumikaje, mapato ya mafuta yanatumikaje. Taasisi kama hizi ambazo tumeziunda zifanye kazi. TEITI inatakiwa iwe na wajumbe nane wa kutoka kwenye Wizara wanne, lakini wanaotoka kwenye NGOs wale wanaharakati wa kupigania mapato ya wananchi wawili na wengine wanatoka kwenye makampuni hayo ya mafuta na gesi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni shirika la Uwazi ambalo limekubali na sisi tumeridhia kwa Sheria Na. 23 ya mwaka 2015 ambapo tumeungana na mataifa mengine yenye rasilimali hizi za madini, mafuta na gesi ili kuweka uwazi. Sasa basi tuwasaidie TEITI waweze kufanya kazi yao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namalizia kwa kusema ndugu zangu, Wizara ya Miundombinu msitupe utelezi. Tunaomba lami tuwajaze madola na mayuro, Iringa tuko tayari jamani. Ahsante.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia katika mpango huu, pia nichukue nafasi hii kupongeza kwa ajili ya mpango huu na nitakuwa na mambo machache ambayo naamini nitachangia na kupata ufafanuzi ili tuweze kwenda vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachangia mpango na hii ndiyo dira ya utendaji wa kazi katika nchi yetu, katika Wizara zote na Idara zote. Kama ambavyo mpango unasema tunaangalia dira ya maendeleo ya Taifa lakini pia tunaangalia mipango mingine iliyopangwa ya muda mrefu lakini tunaangalia mpango uliopita mwaka jana, tunaangalia na Ilani ya CCM.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maana hiyo nilitegemea kama ambavyo Kamati wameeleza kwamba kuna mapungufu ya jumla yaliyotokea kwenye Mpango, ni kitu cha muhimu sana ambacho Mheshimiwa Waziri akisimama atuambie. Tunakwenda kupitisha mpango huu lakini mapungufu yake ya jumla ni kwamba tumemaliza mpango ambao umeisha, hatujaambiwa katika Mpango ule ulioisha kuna ajira ngapi zilitengenezwa kutokana na ile miradi ya maendeleo. Sisi 2025 tunakwenda kwa wananchi waliotupa ridhaa ili tuwaambie yale maelekezo ya CCM tutengeneze ajira 8,000,000 mwaka huu tulitengeneza hizi, mwaka huu tulitengeneza hizi lakini mpango haujaeleza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunakwenda mpango huu una miradi ya maendeleo baadhi yake haijaelezwa bayana na sisi tunakwenda kupitisha kwamba uwe ni mpango wetu ambao unabeba miradi yetu ya maendeleo ambayo haijaelezwa bayana. Tunaomba miradi hiyo Mheshimiwa Waziri ukisimama tupate kwa ubayana wake. Pia hatujaelezwa kinagaubaga mafanikio tunayokwenda kuyapata kwenye huu mpango, akisimama atueleze mafanikio tunayokwenda kuyapata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namba nne mpango huu kama ambavyo upo sasa, kwa kuwa tumesema mipango yetu sasa hivi tunayopanga iendane na Sensa tuliyoifanya na kuimaliza mwaka jana. Haijatoka ile ripoti yote ya Sensa lakini anagalau tumepata baadhi ya ripoti. Sasa kama walivyosema mzungumzaji Mheshimiwa Mbunge aliyepita Mheshimiwa Ng’wasi tumetumia zaidi ya bilioni 400 kufanya Sensa, yale matokeo ya Sensa yanatakiwa kutusaidia kupanga mipango yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatamani kuona tumeambiwa kwenye Sensa work force ya nchi yetu ambayo tunaitegemea watu wenye umri kati ya miaka 15 – 64 ni asilimia 53.1. lakini ukiangalia katika hao watu asilimia 34.5 ni watu wenye umri kati ya miaka 15 – 35 ambao ni vijana tunabakiza work force ya 18% tu ndiyo wale ambao ni miaka 36 – 64.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, mpango huu ni namna gani umezingatia umri huo wa nguvukazi ya Taifa letu, kuwaweka mipango. Tunakwenda kukopa mkopo wa ndani, sijaelewa mkopo wa ndani ni vipi, tutakopa kwenye mabenki yetu au tunakwenda kukopa kwa wazabuni au tunakwenda kukopaje Waziri atatuambia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya dola 6,000 hizo sijui milioni elfu sita sijui, hlafu nje tunategemea kukopa hizo 2,200 na ngapi. Sasa katika huu mkopo ni namna gani hii workforce ya vijana miaka 15 – 34 tunakwenda kuitumia. Mheshimiwa Waziri umeongea vizuri sana kwenye ripoti yako, kwamba tunatakiwa tuwe na watu wa kutosha na tuwe na watu bora, watu wa kutosha kwa mujibu wa Sensa na ambao ni bora kwa ajili ya workforce hii ni hawa asilimia 34.5 wenye umri kati ya 15 mpaka 34.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukitoa walioko shule, milioni tano na kidogo, unabaki na watu karibu 16,000 ambao ni vijana. Hao wengi wao ni wale ambao wameajiriwa kwenye Machinga, boda boda, bajaji, kilimo na ufugaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ripoti inaeleza vizuri sana kwamba Serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 62 kupitia NFRA na CPB kununua mazao ya wakulima. Nilitamani Waziri wa Kilimo angekuwa hapa, naye kama akipata fursa atuambie ni kwa nini fedha wamepewa za kutosha lakini bado kuna malalamiko kwamba wakulima hawajalipwa mazao yao?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Iringa wameuza mahindi NFRA na wameuza CPB lakini hawajalipwa fedha zao. Tatizo liko wapi? Kwa sababu hii ndiyo workforce ambayo tunaitegemea kwa mujibu wa sensa. Sasa ile mipango ambayo tumesema, kwa mfano, vijana, tuwe na programme kabisa ya kuchakachua kuona kwamba tuna programme gani? Tuache ile 4:4:2 peke yake, kwa sababu workforce kubwa ukiangalia kwenye Taarifa ya CAG, wanaopewa ile mikopo wengi ni akina mama, ndio waliopewa zaidi ya asilimia 50 lakini vijana wamepunjwa na watu wenye ulemavu wamepewa kidogo. Kwa hiyo, hii workforce bado tunai-neglect na kuiacha nje wakati hii ndio nguvu ya Taifa ambayo tunategemea ibadilishe uchumi wetu, tuwe na huo uchumi shindanishi ambao tumeuandika kwenye mpango.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hii nguvu ya kuchochea tunaiwekea mpango gani? Tuache ile kwamba Ofisi ya Waziri Mkuu ilipewa shilingi bilioni moja ikakosa vijana wa kukopa, wakakopesha tu shilingi milioni 200 tu, shilingi milioni 800 sijui ikaenda wapi; tuwe na mpango madhubuti kabisa. Leo hii tunapoongelea hiyo workforce, vijana wengine, nimewatoa wale milioni tano ambao ni wale walioko sekondari, form one mpaka six, lakini tuna vijana wako vyuo vikuu. Hawa ni workforce ambao tunategemea baada ya miaka miwili, mitatu wana-mature wanaingia sokoni. Mpaka sasa hivi tunavyoongea, wako foleni wameandikiwa kupewa mikopo lakini hawajapewa na masomo hayajaanza tunaingia Novemba, Desemba, muhula unaisha. Bodi ya Mikopo hawajatoa. Hawa ndio watu tunaowaongelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa namna gani mpango huu uta-accommodate hii workforce ya nchi yetu ili kutusaidia ku-push uchumi wetu? Hii mikopo tunayosema tunaomba ya ndani zaidi, nataka kujua, kwa sababu kama tutaendelea kuwa-drain watu wetu, wazabuni wetu na kuwakopa, ku-drain benki zetu, Serikali ikawekeza nguvu kubwa kukopa huko kwenye benki, halafu wakija sekta binafsi ambayo wewe kwenye mpango wako unasema tuna nia ya kuinua sekta binafsi, kuwaboreshea waweze kuwekeza na kuacha zile shughuli nyingine ambazo Serikali inafanya zinazoweza kufanywa na sekta binafsi, sasa Serikali tuki-drain kwa kwenda kukopa kule na kutowaachia wawekezaji binafsi hiyo fursa, bado tutakuwa tumechukua fedha mfuko huu, tumehamishia mfuko huu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tungetamani fedha kubwa na ajira nyingi zijengwe na sekta binafsi. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri, ukisimama naomba utuambie, hiyo ndio workforce tuliyonayo? Ndiyo mashine yetu, ndiyo kiwanda chetu cha kuzalisha na kuinua uchumi wetu. Hawa vijana tunawawekea mpango gani kabambe? Tukiachana na miundombinu, tunawawekea mpango gani kabambe?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuna mpango wa kusema, sasa katika hii fedha, sijui ni shilingi trilioni tatu au ngapi tutakayochukua, hatuna mpango wa kusema hizi shilingi bilioni 500, hebu sasa tukakopeshe kwenye sound organisation za vijana wetu wanaofanya biashara ndogo ndogo ili watulipe kodi, lakini uchumi utakuwa umefunguka, kama ambavyo tulikuwa tunasema mabilioni ya mama. Tulivyo-inject shilingi milioni 1.3, tayari nchi yote ilikuwa inatetemeka kwamba kuna mabilioni ya Mama Samia yameenea nchi nzima.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hebu tutafute fedha ambayo tutakwenda ku-inject kwa vijana, Machinga. Tutafute namna ya ku-inject kwa bodaboda au bajaji tukaziweke biashara zao kuwa rasmi, wasimame kutoa ajira. Sasa hivi tuna vijana wengi wame-graduate wanafanya vizuri kwenye kilimo cha irrigation. Hata ukija kwangu Mkalama wamenitengenezea, kila mwezi nauza nyanya hapo kwa zaidi ya shilingi milioni mbili au tatu. Wametengeneza vijana wadogo tu wa kutoka SUA. Tukiwawezesha hawa katika kila wanachokifanya, tukakiboresha kuwe cha kisasa, tukawatafutia masoko na kuwa-connect kwenye masoko nje ya nchi, tunaondokana na umaskini kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Waziri, naomba ili tuendane na sensa sawasawa, utakaposimama uje utujibu haya, miradi hiyo ni miradi gani? Iwe bayana; ajira ngapi utakwenda kutengeneza? Mwaka jana ngapi tumezitengeneza? Manufaa gani tunakwenda kuyapata kupitia Mpango huu?

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba upelekaji wa umeme kwenye maeneo ya mijini yenye sura za vijiji, lifanyiwe kazi maeneo hayo yapate umeme. Mfano maeneo ya Mitaa ya Ugele, Msisina, Mtalagala, Mosi, Ulonge, Machinjio ya Nguruwe ndani ya Manispaa ya Iringa. Umeme upelekwe kwa gharama za upelekaji wa umeme vijijini, kwa kuwa mazingira yao ni sawa na vijiji tu, ingawa vinatambulika viko mjini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nina ombi maalumu; tunaomba kujengewa makazi ya polisi katika Kituo cha Polisi Iringa Mjini.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nashukuru kwa kunipa nafasi. Naipongeza Wizara hii kwa kazi kubwa wanayoifanya pia kwa lile jambo la Mchuchuma, tunawapongeza sana na tunawatakia kila la heri kuhakikisha kwamba linafika mwisho na tunaanza kuona matunda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa ku-quote hotuba ya Mheshimiwa Waziri ambayo anasema “Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda na biashara kwa kiasi kikubwa inategemea shughuli za sekta binafsi ambayo ndiyo inayowekeza mitaji yao viwandani na kwenye miamala ya kibiashara ili kuhakikisha upatikanaji wa bidhaa na huduma nchini unakuwepo wakati wote.” Hivyo, Mheshimiwa Waziri anasema jukumu kubwa la Wizara yake yeye ni kusimamia masuala ya utafiti, ushauri, uratibu, kutoa mwelekeo kwenye tasnia hii ya viwanda na biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haipingiki kwamba sekta binafsi ndiyo imebeba viwanda na biashara. Wakristo tunaambiwa katika Mhubiri 10:19 fedha ni majawabu ya mambo yote. Kwa maana hiyo ni kwamba, walioshika majawabu ya mambo mengi ya Taifa letu ni hawa wafanyabiashara ambao Mheshimiwa unawasimamia wewe na ambao umesema ni sekta binafsi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuainisha majukumu yako Mheshimiwa Waziri umesema mnaratibu masuala ya utafiti yanayohusiana na biashara, mnatoa ushauri na mnaonesha mwelekeo. Kwa maana hiyo, sekta hii binafsi inakutegemea sana wewe Waziri wa Viwanda uwasaidie katika kuratibu mambo yao na sekta nyingine au Wizara nyingine ili wafanye vizuri zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri wa Fedha alitusomea hapa mapato ambayo tumekusanya mwaka 2023 nayo yana-reflect hii taarifa yako, kwamba tulikuwa tumekusanya shilingi trilioni 38, ambapo shilingi trilioni 23.6 ilitoka kwenye mapato ya ndani ambayo Mamlaka yetu ya Mapato ilikusanya shilingi trilioni 23.6, hizo shilingi trilioni 13.4 ni fedha za mikopo, hiyo shilingi trilioni moja ni kutoka vyanzo vingine. Kwa hiyo, utaona kwamba fedha nyingi inayokusanywa hata kwenye mapato ya nchi hii inatoka kwenye sekta binafsi, kwa maana hiyo sekta hii inatakiwa iangaliwe kwa umakini mkubwa sana, wafanyabiashara na wawekezaji kwenye viwanda wanatakiwa kutunzwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunafahamu manufaa ya biashara kwamba inafanya kuanzisha ajira kubwa sana katika nchi. Biashara inaleta makusanyo ya mapato, biashara inasaidia ujenzi wa miundombinu. Nikafikiria nikaona kumbe katika Mawaziri hawa wewe hapo ndiye Waziri mkubwa wao na wengine wote hawa wangekuwa ni Mawaziri wadogo wadogo kwako. Kwa sababu hakuna barabara bila biashara na fedha wala hakuna afya bila biashara na fedha. Hatuna miundombinu yoyote itakayofanyika kwenye nchi hii kama hatuna fedha. Pia, tumekusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara ambao ni sekta binafsi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Mheshimiwa Waziri lazima ajifunge kibwebwe bila kuwa mpole ahakikishe mtu anayeivuruga Sekta ya Biashara anapambana naye. Kama anashindwa kupambana naye yeye kwa jinsi alivyo kwa sababu wote wana rank moja, basi aangalie hata namna ya kumchongea sehemu ili ashughulikiwe. Kwa sababu hapa kuna dhambi ambayo inawasumbua sana watoza ushuru tangu enzi za Yohana. Yohana alishughulika nayo akashindwa, amekuja Yesu akawaacha nayo mpaka sasa hivi kizazi hiki Manabii na Mitume wanashindwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ipo dhambi ya watoza ushuru na hii imeandikwa katika Kitabu cha Luka 3:12-13 maneno ya Mungu yanasema hivi, “Watozaushuru nao au wakusanyakodi wakamwendea yule Nabii Yohana wakamwuliza hivi, “nasi tunataka kwenda mbinguni, tufanye nini? Nabii Yohana akawaambia, “msibambikize kodi watu.”

Mheshimiwa Mwenyekiti, dhambi hii ya kubambikiza kodi watu ndiyo inayoharibu sekta binafsi. Mheshimiwa Waziri wewe ni kuratibu, ni ku-coordinate, ni kufanya mambo yawe fair kwenye sekta zote na kuongea na wenzio professional wengine ili kuona umuhimu wa biashara. Wao wanaona tu fedha zinatiririka Hazina hawajui wewe unazidi kuwa mfupi kwa kuhakikisha kwamba biashara huku zinakomaa zinazalisha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri sasa asiwachekeechekee, awasemee kama anashindwa kupambana nao kwa sababu leo hii kuna watu bado wanafunga biashara. Iringa kwangu mimi wafanyabiashara wangu wananipigia simu wiki nzima, wanafungiwa biashara karne hii. Tunajifunza kwenye biashara kuwa meneja yeyote mwenye akili anatumia watu kufikia malengo yake na siyo nguvu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa wenzetu hawa wakusanyaushuru na watoza ushuru waangalie kama wana mameneja ambao bado wanatumia nguvu, hawatumii akili wawatoe wawaweke wale wanaotumia akili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikwambie, Wahasibu sio Mameneja wazuri sana kwa sababu moja ya theory za uhasibu ni conservatism, kuwa rigid tu bila sababu. Yaani mtu anajimwambafai tu, yuko rigid, hataki kumsikiliza mtu, akipita amenuna tu, ndio style. Yaani rigidity au conservatism ni one of the theories ya wahasibu. Tafuteni mameneja. (Makofi)

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa. (Kicheko)

MWENYEKITI: Taarifa.

TAARIFA

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, mchangiaji anachangia vizuri sana nataka tu nimpe taarifa mchangiaji kwamba wahasibu hawa huwa wanachojua ni debit and credit wala siyo conservative by nature.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Jesca, unapokea hiyo taarifa?

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Twaha, mwakilishi wa wananchi kutoka Kibiti ni Mhasibu lakini mimi pia nilisema siku ile ni Daktari wa DBA. Najua theory za wahasibu ni conservatism abishe kama siyo. Conservatism ni one of their theories, yaani ndiyo utaratibu wao na wewe sio mhasibu kama hauko conservative. Sasa ni kanuni na hawa sio mameneja, lakini mameneja ni watu ambao wanaweza wakaongea na mtu wakamtia moyo akamwelewa kwa maneno na akalipa kodi willingly. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nimekwambia Iringa leo watu wanafungiwa biashara, wanaandikiwa kodi za miaka iliyopita. Mtu amepewa notice ya kodi ya mwaka 2013. Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema jamani hizi kodi za miaka sita hizi hebu tuachane nazo. Ukishaona mtu siku zote anafuatilia viporo, huyo ameshafika mwisho hana uwezo wa ku-deliver kitu kipya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwenye uwezo wa ku-deliver kitu kipya atatafuta mbinu mpya na vyanzo vipya vya mapato siyo kurudi kutafuta viporo walivyoviacha wenzie huko nyuma. Leo hii unaenda kufunga biashara, umeshindwa kuongea na haya mambo ilishasemwa yasifanyike.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapo tena tuna jambo lingine hapo kwa wenzetu hawa wakusanya kodi. Nimesema kudai kodi za zamani, kubambikiza kodi na kutengeneza uadui na wafanyabiashara. Mheshimiwa Waziri lazima wakusanya kodi wajue kwamba hata mishahara yao na suti zao na viti wanavyokalia kule maofisini vinatoka kwa yule mfanyabiashara mdogo anayekuja kumkadiria kodi pale. Yaani wao sio mabosi wao ni watumwa, wale wanaokwenda pale ndiyo wameshika majawabu ya maisha yao na mishahara yao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hicho ndicho kinachotuangusha. Hawa TRA wangekuwa na uwezo wa kukusanya zaidi ya hizi shilingi trilioni 23.6. Halafu lazima wajue kwamba wafanyabiashara ni ma-genius na ma-intelligent ndiyo maana wako wachache. Ni watu wanaotumia akili kubwa sana huwezi kumshinda. Uchumi ukishaharibu mazalia yake ni kama uyoga kuurudishia ni shida.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tunahangaika na dola kwamba hazipo. Hapa ni practice iliyofanywa wakati ule wa ku-harass Bureau De Change leo tumepoteza style mpaka turudi kwenye line itatupa shida. Kwa hiyo, Mheshimiwa Waziri vitu kama hivi hutakiwi kuviruhusu semelea maana wengine watakusumbua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine naomba sasa, kuna mtu anauliza asemee wapi? Yeye anajua, mbona hajauliza! (Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine tunamwomba sana Mheshimiwa Waziri, muwe karibu na hawa wafanyabiashara wadogo kwa sababu kila unayemwona ni tycoon; leo alianza kama mbuyu ulioanza kama mchicha. Kwa hiyo, harassment ya wafanyabiashara wadogo kama machinga ndio hatuna future ya kuja kuwa na wafanyabiashara wakubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri hii ni Sekta yake na anawasimamia Mama yangu. Naomba pamoja na kwamba wamepelekwa kule Maendeleo ya Jamii lakini wale ni wafanyabiashara. Ninyi Wizara zenu zinaingiliana; washikiliwe hawa wakuzwe watakua. Wakikua watatuletea kodi kubwa, wakishatuletea kodi kubwa hapa tuta-solve majawabu ya mambo mengi sana. Tunalalamikia umeme humu, tunadai barabara, tunadai madaraja, tunadai dawa na tunadai bima za afya. Wale ndiyo wameshika majawabu.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wa umma nchi hii siyo wengi, nao wanajitahidi sana, wanalipa kodi sana na ni kati ya walipakodi wazuri; nao ni wa kuangaliwa. Wazabuni wa nchi ndio wafanyabiashara, ndio walioshika majawabu. Leo unam-starve mtu ana-save chakula kwenye shule, mama tu anasaga unga humlipi ile hela. Usipomlipa ile hela kwa miezi sita umemuua anaenda kununuaje mahindi aje aendelee kulisha na yeye aendelee na biashara? Kwa hiyo, wafanyabiashara wa ndani, wazabuni, walipwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna ombi lingine.

MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa, nimekuvumilia kidogo ili umalizie.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, muda umeisha?

MWENYEKITI: Ndiyo.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nashukuru kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii ya Maliasili na Utalii katika nchi yetu na hoja yangu ya kwanza kabisa itakuwa kwa heshima na taadhima kubwa kutoa pongezi na shukrani kwa uongozi wa Wizara hii nikianzia na Mheshimiwa Waziri mwenyewe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namuomba sana Mheshimiwa Waziri anipelekee salamu zangu kwa Mheshimiwa Rais za kumshukuru sana. Sisi kama wana-Nyanda za Juu Kusini tuna kila sababu ya kumshukuru sana Rais. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuona umuhimu wa kupanua wigo wa utalii kwenye nchi yetu kuja Kusini, kama Southern Circuit na hilo amelifanya kwa matendo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nikianzia katika Jimbo langu la Iringa, kwanza Mheshimiwa Rais kwa Awamu ya Sita, kupitia Wizara zake, ameweza kutujengea uwanja wa ndege mkubwa ambao umekamilika kwa asilimia 86 ambao unaleta watalii wengi, lakini pia, matendo mengine aliyotuonesha ni kuimarisha miundombinu ya barabara zinazoingia kwenye mbuga yetu kubwa ya Ruaha National Park. Barabara ya Iringa – Samora kama kilomita 103 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami, Barabara ya Ruaha – MR – Itunundu – Pawaga na yenyewe tumetengewa kilomita 20, tuna uhakika 25 zitajengwa mwaka huu, lakini pia, Iringa By Pass, kwa ajili ya kuweka mji wetu kuwa wa kitalii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu. Mheshimiwa Waziri wewe ni shahidi ulikuja wakati wa Maonesho ya Kusini pale, kile kituo ambacho tumekuwa tukilalamika. Tumeuliza humu maswali zaidi ya nane na hapa nachukua nafasi hii kumpongeza sana Naibu Waziri aliyekuwepo, dada yangu, Mheshimiwa Mary Masanja ambaye mimi huwa namuita kivutio cha utalii, yaani yeye mwenyewe ni kivutio cha utalii, kwa kazi kubwa aliyofanya tukiwa tukipambana, kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho. Leo Naibu Waziri, dada yangu, Mheshimiwa Mary kile kituo kimeanza kwa hiyo, tunakushukuru sana Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizi imesababisha sasa mimi kutoa hoja, kwa ajili ya kuwatetea tembo waliopo ndani ya nchi yetu. Kwa nini nawatetea tembo? Ninawatetea tembo na wanyamapori wengine, lakini ninawatetea tembo nikiwa nina sababu za msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, species ya tembo duniani, wanasema miaka ya milioni sitini iliyopita 37 mpaka 34 tembo, walikuwa wa aina karibu 175 mpaka tunapoongea leo tembo wamebakia species tatu tu. Specie mojawapo ipo Asia, specie nyingine iko Savannah na specie nyingine tuko nayo sisi Forest Africa ambao ni tembo tulionao huku Tanzania na East Africa in General, wakiwemo tembo kwenye mbuga zetu za Tanzania na tembo waliopo Mbuga ya Ruaha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tembo wamekuwa wakipambana muda mwingi. Inasemekana, unajua Waheshimiwa Wabunge tukilia sana Mungu anaweza akasema sawa, nyie wote ni viumbe wangu, kama hawa wanawasumbua sana ngoja niwachukue wote kama alivyowachukua kwenye nchi nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tutakuwa hatueleweki kwa sababu, tembo, kama Wanyama, ni moja kati ya big five na ni moja kati ya wanyama wanaovutia watalii wengi kuja Africa baada ya kuwa zile species zimepotea huko kwao. Tembo ni mnyama kati ya wanyamapori wengine wanaotusaidia katika kupambana na umaskini wa nchi hii, kupambana na maradhi, kupambana na wale maadui watatu ambao tuna changamoto nao. Hawa wanapokuja kuwaona tembo wanalipa fedha za kigeni, tunaweza kununua dawa, tunaweza kujenga vituo vya afya, tunajenga shule na tunajenga miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo inanisababisha kuona kwamba, hawa wanyamapori sisi tunaweza tukaishi nao. Ndio maana hata Mungu alivyomuumba Adamu alimuweka kwenye bustani na wanyama. Tunachotakiwa sisi kutumia ni akili zetu, sisi ni binadamu, tumepewa utashi, wao hawajapewa utashi. Wakati mwingine unajiuliza, sisi kila wakati tunaenda Ruaha National Park tunakwenda kutalii, tunakutana na wanyamapori, tunakutana na simba na tembo, tunarudi tukiwa salama tume-enjoy, afya zetu za akili zimekaa sawa, lakini wao wakija kwetu tayari shughuli inakuwa ni nzito, sisi tunashindwa kutumia akili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachowaomba, kama Wizara, hebu fanyeni utafiti wa kina. Tembo wame-undergo evolution mbalimbali, inaonekana tembo wa zamani kwanza walikuwa wadogo tu, wana kilo kama tano tu, sasahivi tuna tembo wana kilo 4,000 wame-undergo evolution ya kukua size, kuongezeka zile trunk zao, wameongezeka skull ya kichwa, wameongezeka rims zao mpaka yamekuwa majitu yale ya kilo 6,000/7,000 kwa tembo tulionao sisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, isijekuwa tembo hawa nao wanabadili tabia baada ya sisi kwenda kuwatembelea sana manukato yetu yanawavuta na wao kuja huku kwetu. Mnachotakiwa ninyi ni mkasome, tembo wasijekuwa wana-undergo evolution wanatamani, kwani India jamani, tembo wao si wanapakia maharusi? Hamuoni kule India wanapakia maharusi? Inawezekana na wa kwetu wameshatokea species nyingine inayotaka kuishi karibu yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukitoa ushauri kama huu wataalam wanatujibu tu, tukianza kuwaruhusu waje huku kwa watu watabadili tabia, watakuwa na tabia za watu, wanabadilika ndio. Kwa sababu, hata wale wa India walikuwa kwanza wa pori, lakini baadae wamekuja kuwa huku, kama wapo huku tujifunze, muwafundishe wananchi wanaokaa karibu na hao tembo, maeneo yanayosumbua zaidi, ili wawe marafiki na wale Wanyamapori kwa sababu, wanatusaidia kutuletea fedha za kigeni na ni katika species ambazo Mungu amezilinda amezilinda Africa na anatuamini kwamba, tutaendelea kuwalinda. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine, sisi tulikuwa tunaongea siku moja nikawaambia hivi kama tembo wanakuja huku wanafuata matikiti, wanafuata mpunga, sisi ni binadamu na wale ni herbivores. Herbivores wanakula vegetation, wameamua kula mpunga, wanakula matikiti, ni vegetation. Kwa nini msiwapandie kwenye buffer zone hayo matikiti nao wakiwa wanatoka, kabla hawajaingia kwenye matikiti ya wananchi wakutane na matikiti yao kwenye buffer zone kule? Mnasema ooh, watabadili tabia, kule ndani kuna mibuyu gani saa hizi wanayopata maji ya kutosha? Wanakutana na climate change, wanakutana na kupungukiwa kwa makazi kutokana na wanadamu kuwasogelea. Tembo wanakutana na changamoto ya kuibiwa viungo vyao zikiwemo pembe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vitu kama hivi wale nao Mungu ametupa tu, kama tunaona tabu sana sawa, watu watafunga na kuomba tembo watapotea and then tutapata wapi hela za kigeni? Hata kama tuliambiwa tuwatawale, Mungu alimwambia Adamu awatunze maana yake ni kwamba, mwishoni tutaulizwa, uliwatunza vipi? Sasa inaonekana kama akili zetu sisi zinazidiwa na akili za tembo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani tembo wanatuzidi akili sisi binadamu? Tumeshindwa ku-control kuishi na Wanyama? Mbona leo tuko na simba hapa? Kule kwenye maonesho hatuko na simba? Iringa, simba wamekuja wametutembelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba ninyi fanyeni utafiti. Tumekutana na kundi la simba walivyokuja pale, sijui wale wazee wamefanyaje kwa sababu, mhifadhi wa kwanza kuwa Ruaha National Park alikuwa ni Chief Mkwawa, ulikuwa hauruhusiwi kwenda kuwinda kwenye ile mbuga bila kibali cha Chief na alikuwa anakuelekeza wanyama wa kuwinda, hauwindi tu kila mnyama. Leo wamekuja simba, wazee wanaenda, muulize Mkuu wa Mkoa wa Iringa dada yangu Halima Dendegu yuko pale, wakamwambia usiwe na wasiwasi hawa tunajua jinsi ya kuishi nao hapa. Walichofanya wale ni kuwazuia wale simba wasile watu na wasile mbwa, lakini waliwaruhusu kula vitu vinginevingine, ng’ombe, mbuzi na vitu vingine. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, simba wamekula ng’ombe, wamekula mbuzi, hawajala mtu hata huyu. Wana akili timamu, lakini ninyi kama binadamu mmekaa tu, utafiti wa kwenda kusoma utakuta watu wanasema tunaenda Dubai kwenda kusoma jinsi ya kuishi na tembo, sasa Dubai wana tembo? Unaenda Ulaya kujifunza jinsi ya kuishi na nyani, wanapata wapi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hao ndio ujanja-ujanja, wasomi wetu watusaidie, wafanye uchunguzi watuambie Watanzania kuishi na tembo unaishi naye hivi, sisi tuta-enjoy. Wakija wakakaa sehemu nyingine, mmeshajua wanapita, mnasema wanafuata kule walikofanya nini?

Mheshimiwa Mwenyekiti, tembo wana akili sana. Sisi wengine tangu tuondoke kwa bibi zetu hatujawahi rudi, lakini wao kwa babu zao na bibi zao wanarudi. Wanaenda kutembea ndio wanakutana na majengo, sasa tujifunze kama wanapita zone hii tunawalindaje?

MWENYEKITI: Ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru, naunga mkono hoja. Tembo walindwe kwa gharama yoyote.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu Zilizokaguliwa za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2023; Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishia Tarehe 30 Juni, 2023; na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia na nitaanzia pale ambapo mjumbe mwenzangu alipoishia ili niendelee. Katika hizi hotuba ambazo zimesomwa hapa, suala la madeni na kikubwa mimi nitaenda kwenye madeni madogo madogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inabidi tujiulize kwa sababu, upo utaratibu mzuri ambao Serikali imeshauweka kwamba, Halmashauri yoyote ikikusanya mapato yake ina percent ya kutumia na ya kupeleka kwenye miradi ya maendeleo, 40% kwa 60%. Zipo Halmashauri nyingine zinapewa %30 kutokana na ukubwa wa mapato yake, nyingine zinapewa mpaka 80%, lakini bado Serikali kuu inaongeza ruzuku kwenye matumizi ya kawaida, shilingi milioni 79 kwa mwaka huu uliofanyiwa ukaguzi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, bado ukiangalia sisi Kamati yetu ya LAAC tukapita, Halmashauri 55 bado zinadaiwa na wale wazabuni wadogo wadogo, hawa wanao-supply stationaries, chakula na wanaowapa mafuta. Halmashauri zile zinadaiwa shilingi bilioni 29, sasa total ya madai yote inakuwa shilingi bilioni 87, lakini kwa zile 55 tulizoangalia ni shilingi bilioni 29. Sasa unajiuliza, hawa wana ile 60% ya kwao ya kuendeshea shughuli zao, ikiwa ni pamoja na kulipia chakula, kulipa mafuta na stationary.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukienda kwenye miradi ya maendeleo inaeleza kabisa fedha ya ufuatiliaji isizidi asilimia tano ya ile fedha nzima ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa. Kwa hiyo, kule kwenye miradi ya maendeleo kumeshaji-set kwenyewe, kwamba, atakwenda kuangalia kituo cha afya, shule inavyojengwa kwa kutumia zile fedha, asitumie zile fedha zaidi ya asilimia tano. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa unakuta Halmashauri ile imetumia zile asilimia tano, imetumia ruzuku iliyoletewa na Serikali kati ya hii 79, imetumia ile 60% waliyokusanya wenyewe na bado imewakopa mama ntilie chakula, haijawalipa. Hizi hela za OC zinakwenda wapi? Yaani hiki ndiyo tunachoiomba Serikali irudi kule chini, itupe mchanganuo, hizi hela za OC huwa zinakwenda wapi kwenye halmashauri zetu? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna Halmashauri moja katika Mkoa wa Iringa, siyo Manispaa ya Iringa, mama ntilie anadai zaidi ya shilingi milioni 150 amelisha chakula kwa mwaka huu wa fedha, nafikiri anaitwa Turumba Food and Catering. Shilingi milioni 150 wamekula chakula kwenye vikao vyao, mama yule anadai shilingi milioni 150, sasa wamemwacha wamehamia tena kumfilisi mwingine na hii ndiyo trend kwenye Halmashauri nyingi. Tunawauliza hao wanaowadai bado wanawahudumia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanasema hapana. Sasa ina maana sisi tunapeleka hizi fedha au Serikali inapeleka hizi fedha ikachechemue ule uchumi wa watu wetu wa chini, kumbe zinaishia hapa juu kwenye Halmashauri, watu wetu hawapati na ndiyo maana malalamiko ya hali ngumu. Watu mifukoni hatuna kitu, yanakuwa makubwa. Kwa hiyo sasa tunaomba hii ikaangaliwe, OC zinatumika vipi, ile inayopeleka Serikali?

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kuna issue ya ceiling. Kuna Halmashauri nyingine ukiangalia CAG anasema zinatakiwa zikusanye shilingi bilioni 911, zimekusanya shilingi bilioni 912, lakini Kigamboni wamekuja tumewahoji kwenye Kamati yetu, Kigamboni wamewekewa ceiling ya shilingi bilioni 11, lakini wao wamekusanya shilingi bilioni 13, wana-exceed shilingi bilioni mbili. Kwa hiyo, Halmashauri nyingine zina uwezo wa kujitanua, zikatanua yale mapato yake, lakini zinabanwa na ceiling ambayo Serikali sijui, Wizara ya Fedha sijui, ni Sheria za Umoja wa Mataifa au whatever, IMF wanatubana kwa hiyo, wale wanashidwa kuongeza effort kwenye kukusanya mapato. If that is the case, basi tuangalie namna, tutatumia akili gani, ili kuona zile halmashauri zikusanye mapato zinavyoweza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hoja ya NHIF. Kwanza NHIF yenyewe inajiendesha kwa hasara sasa hivi. Nilipata mtu mmoja aka-calculate akasema, tukitaka NHIF ijiendeshe labda kila anayechangia sasa aongeze asilimia 2.2 ya mchango wake ndiyo itafika kwenye balance ya kwamba, inazalisha faida kwa hiyo, maana yake ni ipo chini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini NHIF inadai kila Halmashauri wanawakata hela; mmeshindwa kujaza fomu, mmekosea kujaza fomu, nimesikia hapa nimeambiwa na Benjamin kumbe wanakosea kujaza fomu mpaka wanadaiwa penalty ya shilingi bilioni tatu. Sasa mimi najiuliza na ukiangalia makosa yenyewe, kosa lenyewe tumeliona juzi pale; NHIF wanasema dawa au huduma iliyotolewa kwenye kituo cha afya haikutakiwa kutolewa kwenye kituo cha afya, kwa hiyo, hiyo huduma tunawakata hela. Vifaa tiba kwenye nchi hii vinapelekwa na Serikali. Mnapelekaje dawa mnayojua haitakiwi kutumika kwenye vituo vya afya ili NHIF wazikate halmashauri? Kwa hiyo, wanadumaza huduma za afya kule chini. Sasa hivi tunajua vituo vya afya vimejengwa, vya kisasa, lakini wenzetu wa NHIF waende kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilitaka kutibiwa siku moja, daktari kani-diagnose akaniambia nataka nikutibu, nikufanyie operation hii. Wao wakasema haiwezekani, sisi kwenye mikataba yetu hatuna operation ya hivyo, labda ufanye operation ya analogy. Sasa, yaani kule kuna madaktari, sisi tukiwa diagnosed na madaktari wetu, madaktari bingwa wenye huduma za kisasa wao hawataki wanataka kuturudisha kwenye huduma according to wao wanavyotaka na ndivyo wanavyokwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi NHIF hawajui kwamba, leo hii katika vituo vya afya tunafanya operation za akinamama wajawazito? Halafu unamshtaki nesi kwa kutoa matibabu ambayo hayakutakiwa kutibiwa kwenye kituo cha afya, ilitakiwa kuwa hospitali ya wilaya, hawajui leo tuna Madaktari Bingwa kwenye hospitali za wilaya? Kwa hiyo, halmashauri nyingi zimepigwa penalty ya kukataliwa zile fedha, sio kweli. Tunataka Wizara ya Afya wakakae na NHIF warudishe fedha za watu, waache uporaji. Halafu hii Serikali ni yetu, watu tunataka tuwahudumie wananchi wetu, sio suala la penalty. Wenyewe zikirudi huko juu wanafanya nini? Ziende zikatibu wananchi kule. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuja kwenye suala lingine. Pamoja na mambo haya niliyoyaongea, CAG safari hii amefanya kazi kubwa sana. Amefanya ukaguzi wa ufanisi kwenye masuala ya afya ya akili kwenye nchi hii. Sasa wote mtakuwa mmesoma fedha, mmesoma kampuni, mmesoma nini, hamjasoma afya ya akili. Tatizo kubwa ni afya ya akili. CAG amesema kabisa, mtu yeyote mwenye afya nzuri ya akili anaweza ku-contribute vizuri kwenye nchi yake, kutoa mchango sahihi kwenye jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tuna watendaji ambao hawatoi michango sahihi kwa sababu, huduma za afya ya akili hazijawekewa msingi kwenye nchi hii. Leo hii tumekwenda kukagua shule moja Chaduru huko, watu wamejenga msingi, kozi ya msingi wa jengo inakwenda kozi 18. Fedha yote imeishia kwenye msingi, huyo mtu ana afya nzuri ya akili? Anatoa mchango gani kwenye hii nchi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unajua kabisa thamani yangu. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, mwanamke, unalazimisha nikatibiwe kwenye analogy, ili nife? Halafu utanipata wapi mtu kama mimi kwenye nchi hii? Sasa hawa wenzetu nao wana afya nzuri? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jamani afya ya akili hata humu ndani tukisema watu wanafikiria ni mambo ya uchizi. Sio mtu amekuwa kichaa, lile ni tatizo tayari. Afya ya akili ni ustawi tu wa akili zetu na CAG kasema kumbe kuna Sheria ya Afya ya Akili ya Mwaka 2008, Kipengele cha 31(1)(b), kinataka Wizara iunde Baraza la Afya ya Akili Nchini, ili kutoa huduma za kisaikolojia na huduma saidizi. CAG kasema kama hatutoliangalia hili watu watazidi kupata matatizo mengi, watashidwa ku-perform katika ile standard tunayotaka wa-perform, vijana wetu watazidi kulewa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, unashangaa humu ndani leo hii watu wamekwenda kutoa huduma za afya ya akili wamewaangalia wazee, wamewaangalia watoto wale waliopata mimba za utotoni, watoto wa mazingira magumu na wamewaangalia watu wenye ulemavu. Tuulizane humu ndani, kati ya wazee wetu wa zamani waliokuwa wanachukuwa majembe wanakwenda kuchimba barabara, wanajitolea na sisi leo tunajengewa barabara za lami, tunamwaga takataka, tunataka Serikali ituzindulie, nani ana afya mbaya ya akili? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa nini ukawaangalie wazee badala ya uanze kutuangalia sisi kwanza afya zetu zikoje?

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala ni sheria. Tunataka Baraza la Afya ya Akili Nchini hii liundwe. Sheria inaelekeza tangu Mwaka 2008, ili vijana wetu wapate support ya ushauri. Tunasema si kwamba, mambo hayaendi kule chini, mambo yanakwenda, mikopo inakwenda.

Mheshimiwa Mwenyekiti, haya, wenzangu wameongelea hiyo 4:4:2 inakwenda kwenye vikundi, lakini vikundi vile vikipewa mikopo tumeshaambiwa mikopo ile hairudi. CAG anasema, ili mtu aweze kurudisha mkopo lazima akili yake iweze ku-perform, yaani a-produce productively siyo tu suala la kwenda kazini, anakwenda kazini anazalisha kwa tija?

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunakwenda Milembe, dawa ya afya ya akili iliyopo Milembe ni moja tu, ya aina moja, wakati ubongo una sehemu tatu na sehemu zote zikiathirika zinahitaji matibabu tofauti. Tunaomba suala hili lichukuliwe kwa uzito, tutapunguza matatizo mengi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunawacheka wenzetu si ndiyo? Tunaona wenzetu sijui vijana wao wamefanyaje, wameingia humu wanaleta vituko, wanaleta maandamano na sisi tusipohangaika na kuwaweka vizuri vijana kwenye akili tuna changamoto kubwa; CAG amesema suala hili limesababisha tukakosa ushauri wa kisaikolojia na vijana wengi wameingia kwenye ulevi uliokithiri, ni nani hapa sio shahidi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, unachukua kabisa kijana, umepanda bodaboda unaona kabisa huyu tukifika ni kudra za Mwenyezi Mungu. Watoto wadogo, leo tuna viongozi ambao sasa hivi ukienda kwenye mitaa ya mijini kote kuna casino zimewekwa kila mahali. Wanaotoa vibali ni wasomi wa nchi hii ambao wanajifanya wana afya ya nzuri ya akili, kutuletea casino kwenye makazi ya watu, watoto wanashinda wanakimbia humo, wanakunywa, wanavuta bangi, hawana akili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema suala la afya ya akili tuanze kufundishwa sisi tulioko juu. Huku ghorofani kukishakuwa kumechanganyikiwa hata tufanyaje, ndiyo maana leo watu wanatafuta, kila zikipelekwa fedha za madarasa hazitoshi, tumeongeza wanasema hazitoshi. Kituo cha afya mara ya kwanza tumepeleka shilingi milioni 470 hazitoshi, tumepeleka shilingi milioni 580 hazitoshi, tunataka shilingi milioni 640. Tunapeleka shilingi milioni 640 hazitoshi. Mtu anajenga nyumba, anajenga shule mahali penye mwinuko, anatafuta level ya mlima kuanzia kule chini mpaka apate level ya pale juu, halafu ndiyo ajenge darasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwani kama huyu mtu ana akili timamu kwa nini asijenge kwa leveling? Waheshimiwa, si tulikuwa Rwanda hapa? Si tuliona zile nyumba zao zilivyo juu ya milima, hivyo? Sasa wangekuwa wanatafuta level wale, mpaka wakakutane kule juu, hela yote shilingi milioni 600 si inaishia huko? Huku juu Wizara, wenzetu TAMISEMI, kule kwenye wasomi tunawashukuru, hivi hawajui nchi hii kama kuna Southern Highlands of Tanzania? Tuna ukanda wa ziwa, tuna ukanda wa kati, hawajui? Wametoa ramani zote za flat rate, afya zao zikoje? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Wizara ya Afya jambo hili siyo la kulifanyia mzaha. Kampeni zenyewe, Marekani wameanza kampeni za afya ya akili tangu Mwaka 1958 na unakuta wale ma-first ladies kama akina nani, ndiyo wanakuwa ma-organizer wa zile kampeni. Sisi hatufanyi kampeni, tunasubiri siku ya kujinyonga duniani ndiyo tunafanya kampeni ya afya ya akili. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunataka hizi kampeni ziwe intensive, watu wajue. Humu ndani mimi nakutana na watu, siwezi kuwataja ninyi jamaa zangu, Waheshimiwa wenzangu, muda wenyewe tuliopo sio mzuri tutalipuana vichwa, lakini wengi wao humu na ninyi pia, hamuelewi. Mkiniona mimi mnaniambia balozi wa afya ya akili, mnafikiri balozi wa machizi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sio maana yake. Nawaambia kila siku suala la afya ya akili ni ustawi wa akili ya mtu kichwani.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, unapokuja ukichaa, tayari ni tatizo. Niombe sana, CAG ametusaidia, ametoa mapendekezo ya namna ambavyo tunaweza tukashughulika na suala la afya ya akili, kutojibu hoja za CAG ni kukosa afya ya akili. Wajibu hoja za CAG, anawasaidia wao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, location ya Jimbo la Manispaa ya Iringa, lipo katikati ya majimbo mengine ya Mkoa wa Iringa, hivyo kusababisha watu kutoka katika Mkoa wote wa Iringa kuona urahisi wa kufuata huduma za muhimu ndani ya Manispaa ya Iringa. Hii imesababisha uhitaji wa huduma za jamii kama afya, elimu, miundombinu ya barabara kuwa changamoto, kwani tunalazimika kuhudumia watu wengi zaidi ya wakazi waliopo ndani ya mji. Mfano Hospitali za Wilaya za Jimbo la Kilolo imejengwa Wilayani Kilolo ili watu wafuate huduma hiyo Kilolo wanatakiwa kupita Manispaa ya Iringa.

Mheshimiwa Spika, sasa kwa hali ya kawaida hawezi kupita mjini kwenda kuifata hospitali iliyoko Kilolo. Wanatakiwa kutibiwa Manispaa, jiografia hiyo iko pia kwa Jimbo la Isimani na Kalenga.

Hivyo tuna umuhimu wa kuongeza vituo vya afya pembezoni mwa Jimbo la Iringa, ambayo ni Kata ya Kitwiru, Kata ya Igumbiro na Kata ya Isakalilo. Pia utanuzi wa Hospitali ya Frelimo uende kwa kasi na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ili kuhimili uhitaji uliopo.

Pia shule kongwe kama Iringa Girls, Lugalo Sekondari na Mawele Wele Sekondari, ziongezewe mabweni kwa kuwa ni shule za kitaifa halafu zinachukua watoto wenye ulemavu wa kila aina. Sasa zinazidiwa sana wakati zina maeneo ya kutosha kufanya expansion. Iringa Girls imaliziwe yale mabweni mawili ambayo hayakumaliziwa wakati wa ukarabati wa shule kongwe ambayo ni bweni la Mshikamano A na B.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa madarasa kwenye maeneo yetu uzingatie uhitaji, kuna sehemu nyingine shida kubwa inakuwa sio tu madarasa bali majengo mengine. Pia fedha za ujenzi wa mabwalo ziangaliwe upya na zitolewe sawa kati ya TAMISEMI na Wizara ya Elimu, wengine wanatoa chache wengine nyingi, baadhi mabwalo yanaisha kwingine inashindikana. Ndani ya Manispaa tunaomba mabwalo yamaliziwe katika sekondari zetu ambayo hayajakamilika. Kama Kwakilosa Sekondri, Mlandege Sekondari, Tagamende Sekondari na kadhalika.

Pili, Iringa Manispaa imekuwa na shida kubwa ya mara kwa mara vifungu ku-burst hivyo kusababisha uendeshaji wa halmashauri kuwa mgumu na kuwakosesha Madiwani kulipwa posho za vikao kwa wakati na kuwalipa wazabuni wa Manispaa na kuendesha shughuli nyingine, hili lifanyiwe kazi.

Mheshimiwa Spika, pia ulipaji wa madeni makubwa kama deni la Kampuni ya SIETCO, wanaoidai Manispaa pesa za ujenzi wa stendi ya Igumbiro na soko la Mlandege vilipwe ili kuondoa hasara ya kulipa penalt na kuja kuzuia wahisani kutoa misaada pia.

Mheshimiwa Spika, TARURA tunaomba sana kwa namna Mji wa Iringa ulivyokaa, unapitiwa na barabara kubwa za kimataifa mbili (TANZAM). Iringa Manispaa inapitiwa na barabara kubwa ya kutoka mikoa kumi ya Kusini kwenda Mashariki ya nchi yaani Mbeya – Dar es salam; pia inapitiwa katikati na barabara inayotoka Cape Town to Cairo yaani mikoa 10 ya Kusini mwa Tanzania ikiwemo Nyanda za Juu Kusini kwenda mikoa sita ya Kanda ya Ziwa na Kaskazini mwa nchi mikoa sita. Sasa jaribu kufikiria huo mzigo unaopita Iringa wakiwemo na wakazi kutumia barabara hizo hizo. Ni shida kubwa sana na kumekuwa kuna mkwamo na ajali nyingi sana.

Mheshimiwa Spika, tunaomba barabara za ndani za Mji na Manispaa ya Iringa zijengwe kwa kiwango cha lami ili kuufungua mji ule ili angalau wanancchi watumia barabara za pembezoni ili kupisha watumiaji wa Kimataifa watumie hizo nyingine. Mfano barabara ya Ipogolo – Kagrieolo - Kitwiru; Wilolesi - Mtwivila; Magereza - Ipogolo; Don Bosco - Kihesa Kilolo kupitia Magic Site, pia kukamilishwa kwa Iringa bypass.

Mheshimiwa Spika, otherwise tunawashukuru sana kwa juhudi kubwa na kazi inayotukuka inayofanywa na TAMISEMI kwa ujumla.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Iringa ni mkoa wa kilimo hususani hata Manispaa ya Iringa. Sasa sisi hatuna eneo la kufanya block farming na Iringa Manispaa ndiyo lango la utalii Kusini na tunajengewa uwanja wa ndege ambao utaruhusu hata ndege ya mizigo kutua na kuchukua kama mboga mboga.

Mheshimiwa Waziri wewe unajua utalii ni pamoja na huduma nzuri ya chakula. Hivyo basi, rejea mazungumzo yetu, tunaomba sana sana tupewe eneo la Serikali lililokuwa la Kilimo au Utafiti Gingilanyi, katika Kata ya Nduli ili tutumie kama block farming kwa vijana wa manispaa ya Iringa, pia tunaweza tukatumia eneo lililokuwa Kituo cha Utafiti cha Kilimo kilichopo Ipogolo Kata ya Ruaha.

Mheshimiwa Spika, pia tunaeneo la umwagiliaji la Mkoga Kata ya Isakalilo. Tunaomba litengewe bajeti kwa ajili ya kuboresha ili kuwa na kilimo cha umwagiliaji na chenye tija.

Mheshimiwa Spika, tunaomba changamoto ya upatikanaji wa mbolea karibu na wakulima itatuliwe, kwanza, kwa kuweka mfumo madhubuti ambao utafanya kazi kwa wakati wote bila kukatikakatika, kuwa na wasambazaji wa kutosha mpaka vijijini hivyo kuimarisha utendaji kazi wa mawakala wadogo kwa kuondoa urasimu usio kuwa wa msingi kwa mawakala wadogo. Pia kuufanya mfumo usiruhusu QR code kuwa scanned zaidi ya mara mbili, iwe kama ilivyo kwenye voucher za simu au namba za LUKU ukiingiza mara moja haiwezi kuruhusu tena kuingiza au ku- scan. Pia zisitolewe zinazofanana kwa makampuni mawili.

Mheshimiwa Spika, mbolea hii ya ruzuku ikiwezekana iwe na limit ya mifuko itakayotolewa. Labda Serikali iseme itatoa ruzuku kwa mifuko kadhaa tu. Wale wenye mahitaji makubwa maana yake wana uwezo mkubwa hivyo waweze kununua kwa bei ya kawaida isiyokuwa na ruzuku. Wakulima wakubwa wengine huchukua mbolea ya kutosha wakulima wa Wilaya nzima hawa wanaweza. Mbolea ya ruzuku itolewe kwa mwaka mzima. Pia usajili wa wakulima kama wapo ambao bado hawajamaliza basi waendelee kutumia mpaka wamalize na usajili wa wakulima uwe ni endelevu.

Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kuwasilisha na naunga mkono hoja.
Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu, katika Nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuasisiwa kwa Taifa letu Mwenyezi Mungu ametusaidia kupata Miamba Sita kwa Awamu Sita za Uongozi, na katika Miamba Sita hii Mwenyezi Mungu ametusaidia kuonesha jinsia zote mbili miongoni mwa Miamba Sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja ya mambo ambayo yalikuwa yakitusumbua katika Taifa letu ni katika kugusa sheria hizi tatu ambazo zimeletwa leo mbele yetu. Maneno yalitokea mpaka 2014 tulikuwa tuna nia ya dhati ya kuona kwamba sasa tuandike Katiba mpya, hata hivyo ilishindikana. Leo tumempata Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jinsia ya kike amethubutu kwamba sasa tunataka tufanye marekebisho kwenye zile sehemu nyeti kabisa ambazo ukizigusa unakuwa umegusa utamu wa Madaraka ya Rais na ya sisi tulioko hapa leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya ameonesha kwa nia ya dhati kutoka kwenye moyo wake na kuyajengea falsafa na kuamua kuchukua hatua thabiti za kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kufanya mabadiliko. Katika Biblia kitabu cha Mwanzo 11:6 inasema hivi; “Mungu akasema tazama watu hawa ni Taifa moja na lugha yao ni moja na haya ndiyo wanayoamua kuyafanya, hawatashindwa na hakuna kitakachoweza kuwazuilia”.

Mheshimiwa Spika, ni kwamba wameamua kuwa wamoja, kuongea lugha moja na wana mambo wamekusudia kuyafanya kama Taifa lao moja hakuna kitakachowazuilia. Ili sisi kuwa wamoja, kuweza kujiletea maendeleo, kujenga Taifa letu lazima tuongee lugha moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutaongeaje lugha mmoja tusipokuwa na maridhiano? Mheshimiwa Rais akaamua kwamba sasa tufanye maridhiano na ili ufanye maridhiano, kwa nafasi yake ilivyo kubwa, mambo ya maridhiano au mahusiano hata Mwenyezi Mungu aliyafanya. Wanadamu walipopotea Mungu aliamua kuja kufanya reconciliation lakini ili kufanya reconciliation ile ilimtaka ashuke aje kwenye level ya binadamu. Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike, akashuka kuja kwenye level ya watu wa kawaida, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu. Akatengeneza urafiki na wale wenye maneno maneno akaenda nao hadi kwenye sherehe zao akala nao. Akawaita watu bila kuangalia itikadi za imani zao, dini zao, uwezo wao, vyama vyao vya siasa, watu wa chini akakaa nao kwa pamoja, akatengeneza Kamati ya Maridhiano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakakaa kwa pamoja ni kipi ambacho kinasemwa semwa kwenye Taifa letu kinatufanya tusiende pamoja? Wakakaa wakiongozwa na kiongozi mkubwa wa dini wakajadili. Wakapata mambo 83 yanayofanya tusiwe wamoja kwenye nchi yetu, yamkini tushindwe kufikia maksudi yetu. Katika 83 Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mambo 64 wameyatekeleza ikiwepo na pamoja kwamba sasa kama mikutano ya hadhara ilikuwa haipo fanyeni mikutano ya hadhara, na wengine waliokimbia wakajiona wakimbizi kwenye nchi hii rudini, enjoy maisha kwenye nchi yenu. Sasa walioko nje sasa hivi siyo wakimbizi wako tu wana-enjoy wanatumia haki yao ya msingi universal right ya kuishi popote wanapotaka lakini si kwa wasiwasi wa kukaa kwenye nchi hii. Hiyo ni nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, walipotaka kuandamana wasaidizi wake wakasema siku hiyo tutakuwa tunafanya usafi wa mitaa, akasema tulieni waacheni waandamane, wapeni na ambulance, wapeni na ulinzi waseme wanachokitaka. Nia ni reconciliation tufikie maridhiano tuwe wamoja, sisi ni Taifa moja tuongee lugha moja, lolote tunalokusudia katika kujenga uchumi wa nchi yetu tutaweza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi kufanya haya bila kuwa mstahimilivu, kuamua kuacha yale matashi yako yote ya Uamiri Jeshi Mkuu ukashuka ukakaa na watu huwezi kuyafanya, akafanya yeye kwa matendo kuja kukaa na watu wa chini kabisa, lakini hatuwezi kufanya hii bila reform lazima tukubali kufanya mageuzi ya dhati. Watu wameogopa kuigusa Tume ya Uchaguzi, kuitengenezea sheria mimi naigusa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakwenda kushughulika na Tume. Kama tatizo ni Tume tuishughulikie Tume, kama tatizo ni mimi Rais kuwa na Madaraka mengi basi sawa naachia Madaraka kwenye Kamati ya Usaili nipendekezeeni hao watu mnaowataka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ingekuwa ni kifaru alinyofoa pembe yake akampa mtu mwingine, ingekuwa ni tembo amenyofoa meno yake akampa mtu mwengine. Nia yake ya dhati ni kuona kwamba tunakuwa wamoja tulijenge Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, akasema, kufanya mageuzi haikuwa rahisi, hata sisi tulio wa kwake, maana katika watoto wa mama kuna mtoto mmoja yaani huyo huwaga yuko kwenye pochi, lakini kuna mwingine anaweza kuwa yuko pembeni kidogo; hata watoto wake wengine hawakuelewa. Akasema, mtatakiwa kuelewa, lazima twende kwa style hii ili tufanye reformation ili tufanye rebuilding, tuwe wamoja.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameanza kufanya rebuilding kwa kusema sasa tunaenda kufanya mageuzi ya kuandika. Tunaleta sheria Bungeni, tunafanya mabadiliko ili watu wajisikie wako huru, halafu baada ya hapo twende mbele tufanye kazi ya kujenga Taifa letu. Sasa tupambane na umasikini, tupambane na maradhi, tupambane na upungufu wa ajira kwenye Taifa letu, tuijenge nchi yetu, tuache maneno maneno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba Watanzania tufike mahali na sisi tuungane na Mheshimiwa Rais kwenye nia zake za 4R, tufanye rebuilding ya Taifa letu. Hili ndilo Taifa Mungu alilotupa, hatuna Taifa lingine, na wengine wana-quote na kujifunza kutoka kwa watu wengine, lakini nataka nikwambie huko tunakojifunza ndiyo kubaya zaidi.

Mheshimiwa Spika, amesema hapa Mheshimiwa Tadayo wengine mataifa yao yalipata uhuru tangu miaka ya 1776 mpaka 1919 bado walizuia wanawake miaka 144 mbele, bado haki ya demokrasia kwa wanawake ilikuwa haiwezi kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mpaka miaka ya 1960 sisi tumepata uhuru bado kuna mataifa haya tunayodhani kwamba ni bora sana, watu weusi walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura. Ili upige kura lazima kwanza ufanye; kuna kile kipengele kimoja wanasema ukatengeneze mazingira mazuri na jirani yako mweupe ili kupiga kura ulipe kodi ya kura, ili kupiga kura kama wewe ni mlafi mlafi tu, huruhusiwi kupiga kura. Sijui huo ulafi walikuwa wanaupimaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hao ndiyo tunataka tujifunze kutoka kwao! Watanzania tutakurupuka kutoka kwao. Haya huwa wanasema, ilikuwa ni miaka 144 baada ya kupata uhuru, sisi Taifa letu lina miaka 62. Ina maana tungekuwa kwenye nchi hizo mpaka leo sisi wanawake humu tusingekuwepo, kwa sababu haturuhusiwi kuchagua wala kuchaguana, wala Mheshimiwa Rais asingekuwepo. Sasa wakati mwingine, nasi tumepewa akili. Usipende kulazimisha ubongo au unajizima data unabaki airplane mode. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wanatakiwa kuja kujifunza kutoka kwetu sisi. Rais wetu miaka 62 amewezaje kufanya demokrasia? Waliwezaje wale miamba sita akiwepo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwashirikisha wanawake kwenye harakati za mapambano ya uhuru na kuwafanya wachaguliwe day one from the day of independence? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wao wameshindwa! Tuache kujizima data, wanatamani kuja kujifunza. Ukiona mtu anakushawishi bwana, unajua kule sijui Marekani, sijui wapi, sijui wapi; mwambie sisi ni Watanzania, ni Taifa moja na Mungu alitupa ubongo, tuna uwezo wa kupanga mambo yetu wenyewe kabla hatujaiga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Watanzania tumuunge mkono Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili sasa tuache hizi kelele na mbambamba za haturuhusiwi kusema; haturuhusiwi sijui nini; tuelekeze akili zetu kufanya innovation na creativity ya kulijenga Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwasihi wanawake, tujifunze kutoka kwa mwamba huyu wa Awamu ya Sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike. Tusilielie. Mungu akawaambia watu fulani Taifa moja, nawapeleka ninyi vitani siyo kwamba siwapendi, nawapeleka vitani ili mkajifunze vita. Kwa hiyo, wakati mwingine wanawake ukitukanwa mwambie yes, hapa ndiyo kwenyewe; unafundishwa vita ya kupambana. Usipoenda vitani utakuwa huwezi kupigana; na majibu huwa yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naweza nikatolea mfano, nilitukanwa Iringa pale, nikaambiwa Jesca Msambatavangu huwa mnamchagua Mbunge hana mume. Nikajibu tu jukwaani, wewe unayelalamika kwamba sina mume, ndio mwanaume, katoe posa Kamati Kuu ya CCM, njoo unioe, vinginevyo utakuwa una matatizo ya kiume. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Weweee!

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, tusilie, mama ameshaonesha njia, mwamba wa Awamu ya Sita, unalilia nini? Simama tumepata fursa sawa. Wanawake tusimame twende tukagombee, tuitetee nchi yetu, na tunamwona mama ndiye Rais aliyesema, natoa mamlaka yangu ya Tume ya kuteua sijui Wajumbe wa Tume, nayatoa napeleka kwenye Kamati, si amepeleka! Si mambo mazuri! Watu wanaandamana, situmii nguvu, natumia akili. Ndiyo maana Biblia inasema, “Ishi na mwanamke kwa akili.” Kwa sababu mwanamke ni very intelligent, anatumia akili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wanaandamana, peleka ambulance, peleka Polisi awasindikize, watafanya nini? Hata sisi mama siku ile amebeba khanga ameingia kwenye ule ukumbi anacheza, nikasema jamani, yule ni mama ana khanga ya chama kile, hee! Yaani mimi alinifundisha kitu kipya sana. Nikapiga magoti nikamwambia Mungu, nakushukuru. Akaingia, akatoka salama. Wewe unaogopa nini? Huyo aliyekusema, utanyofoka ngozi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi nchi tunasema hizi, nchi hizi ambazo tunawasifia, mtu huruhusiwi kupiga kura, hiyo miaka hiyo sasa. Mpaka miaka ya sitini sitini, huruhusiwi kupiga kura kama hujui kusoma na kuandika wala huruhusiwi kupelekwa na mwenzio kukupigia kura. Kama huwezi kutoa kiapo kwa mdomo, huruhusiwi kupiga kura. Sasa kama mtu ni kiziwi, labda ana ulemavu inakuwaje? Sisi tunataka tuwaambie jamani eh, msitupeleke mputa. Sisi Taifa hili ni changa, lina miaka 62, ninyi mna miaka 200, mtusubirishe kidogo, tunajipanga. Afterall, we are well off kuliko ninyi mlivyokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niseme, haya mambo yalitukuta kule nyuma. Kule nyuma watu walileta vurugu kwenye Katiba Mpya, wakafikiri kuna mtu wanamkomesha, lakini ile Katiba Mpya mimi nilivyoiona, ilipendekeza hata Tume hiyo huru waliyosema. Afterall hii Tume ni huru kwa sababu hiyo ibara ya 74 (7) inasema Tume hiyo itakuwa huru, kwenye Katiba iko.

Mheshimiwa Spika, Mgombea binafsi aliruhusiwa, haya mambo yote ambayo tunayafanyia amendments yaliruhusiwa, lakini watu wakajizima data, wakabaki airplane mode, wakajifanya wanatoka, leo tena wanatusumbua turudi kwenye mambo yale yale. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi hamna kubaki kindege, mtu ajifungue data, tuunge mkono hii hoja, tupitishe nchi yetu. Tuna mambo ya maana ya kufanya kuliko haya maandamano ambayo tunafanya kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tutamsemea, tutamtetea popote na Mungu atusaidie. Wanawake sikilizeni niwaambie, watu wa Taifa fulani wakamwambia Mfalme Daudi; “Wewe ni mfalme wetu.” Alikwenda kwenye vita akanusurika kufa, aliporudi, walivyopata ile habari wakasema, “Wewe ni mfalme wetu, hatutaruhusu tena uongozane na sisi kwenye vita ili hiyo taa isije ikazima, halafu wote tukazima Taifa zima.” Wanawake tunatakiwa tutoke na kauli moja. Sisi lazima tumtetee Mama Samia ili ile taa ya wanawake isije ikazima kwenye Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba wanaume, mnapomuongelea Mama Samia muongelee kama binti yako wa kike, mwongelee kama mama yako mzazi, mwongelee kama your baby ambaye unataka kumuoa, sio yule ambaye mmetengana vyumba. Taa hiyo ikizima, mmezima ndoto za binti zenu, taa hiyo ikizima mmezima ndoto za mama zenu, taa hiyo ikizima, tumezima ndoto za wanawake wa Tanzania, na Afrika inataka kujifunza kutoka Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatumpi sifa za bure, kasema Mheshimiwa Mwakagenda, kura siyo namba, kura ni uwezo na umahiri. Wale miamba sita walifanya mambo mema, lakini hili waliogopa kuligusa, mwanamke ameligusa na tunakwenda kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maneno haya, nawaomba Watanzania, tuache ushabiki, sisi ni Watanzania, wala tusijidhalilishe, Mungu anatupenda, nchi hii imekuwa ya ahadi, siku zote imepokea watu wanaopata shida kwenye nchi zao, tumekuwa wa kwanza kupigania uhuru upande wa Southern SADC; sisi ndio tumeongoza mapambano, tuliwasaidia hata South Africa, no matter economically wako mbali, lakini tulishirikiana; na ndiyo chama kimebakia ambacho hatusemi kama ni vipi, lakini ndicho kilichozaa na vyama vingine vyote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi ni nchi makini, tuko strategically, spiritually, physically and mentally. Kwa hiyo tusijidhalilishe Watanzania tupambane twende na hoja zetu. Tunapitisha Muswada huu kwa nia njema Miswada mitatu ili muwe huru kugombea, kuchagua wagombea mnaowapenda. Mliambiwa kwamba ooh, mtu anapita bila kupingwa hampati fursa ya kuchagua; sasa mnakwenda kupata fursa, akipita peke yake mpeni kura za ndiyo au hapana halafu ataonekana kama mnamhitaji, lakini tumewapa fursa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nimalizie.

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie moja tu. Naomba tuaminiane, tupendane, tuheshimiane, hakuna mtu mwingine atakuja kuijenga nchi yetu. Leo humwamini Jaji wa Mahakama ya Rufani, leo humwamini Mkurugenzi, hivi ninyi wanaume, sasa hii nchi ataongoza nani? Tukakodi Wakurugenzi? Tukodi Majaji wa kuja kutuongoza na ninyi mpo na mmesoma?

Mheshimiwa Spika, haiwezekani, huwezi kusema Wakurugenzi wote wabaya, majaji hawafai, wako presidential officials kivipi? Ninyi ndio ninyi, nchi hii mmepewa kurithi, tutatumia majaji wetu, wasomi wetu kwa ajili ya mambo yetu kama ambavyo tukipata shida wanatusaidia. Tutatumia Wakurugenzi kama ambavyo wanasimama Maafisa Waandamizi; kama vituo vya afya wanasimamia, ujenzi wa shule wanasimamia, leo unashindwa kumwamini kulinda kura, kivipi? (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu, katika Nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuasisiwa kwa Taifa letu Mwenyezi Mungu ametusaidia kupata Miamba Sita kwa Awamu Sita za Uongozi, na katika Miamba Sita hii Mwenyezi Mungu ametusaidia kuonesha jinsia zote mbili miongoni mwa Miamba Sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja ya mambo ambayo yalikuwa yakitusumbua katika Taifa letu ni katika kugusa sheria hizi tatu ambazo zimeletwa leo mbele yetu. Maneno yalitokea mpaka 2014 tulikuwa tuna nia ya dhati ya kuona kwamba sasa tuandike Katiba mpya, hata hivyo ilishindikana. Leo tumempata Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jinsia ya kike amethubutu kwamba sasa tunataka tufanye marekebisho kwenye zile sehemu nyeti kabisa ambazo ukizigusa unakuwa umegusa utamu wa Madaraka ya Rais na ya sisi tulioko hapa leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya ameonesha kwa nia ya dhati kutoka kwenye moyo wake na kuyajengea falsafa na kuamua kuchukua hatua thabiti za kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kufanya mabadiliko. Katika Biblia kitabu cha Mwanzo 11:6 inasema hivi; “Mungu akasema tazama watu hawa ni Taifa moja na lugha yao ni moja na haya ndiyo wanayoamua kuyafanya, hawatashindwa na hakuna kitakachoweza kuwazuilia”.

Mheshimiwa Spika, ni kwamba wameamua kuwa wamoja, kuongea lugha moja na wana mambo wamekusudia kuyafanya kama Taifa lao moja hakuna kitakachowazuilia. Ili sisi kuwa wamoja, kuweza kujiletea maendeleo, kujenga Taifa letu lazima tuongee lugha moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutaongeaje lugha mmoja tusipokuwa na maridhiano? Mheshimiwa Rais akaamua kwamba sasa tufanye maridhiano na ili ufanye maridhiano, kwa nafasi yake ilivyo kubwa, mambo ya maridhiano au mahusiano hata Mwenyezi Mungu aliyafanya. Wanadamu walipopotea Mungu aliamua kuja kufanya reconciliation lakini ili kufanya reconciliation ile ilimtaka ashuke aje kwenye level ya binadamu. Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike, akashuka kuja kwenye level ya watu wa kawaida, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu. Akatengeneza urafiki na wale wenye maneno maneno akaenda nao hadi kwenye sherehe zao akala nao. Akawaita watu bila kuangalia itikadi za imani zao, dini zao, uwezo wao, vyama vyao vya siasa, watu wa chini akakaa nao kwa pamoja, akatengeneza Kamati ya Maridhiano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakakaa kwa pamoja ni kipi ambacho kinasemwa semwa kwenye Taifa letu kinatufanya tusiende pamoja? Wakakaa wakiongozwa na kiongozi mkubwa wa dini wakajadili. Wakapata mambo 83 yanayofanya tusiwe wamoja kwenye nchi yetu, yamkini tushindwe kufikia maksudi yetu. Katika 83 Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mambo 64 wameyatekeleza ikiwepo na pamoja kwamba sasa kama mikutano ya hadhara ilikuwa haipo fanyeni mikutano ya hadhara, na wengine waliokimbia wakajiona wakimbizi kwenye nchi hii rudini, enjoy maisha kwenye nchi yenu. Sasa walioko nje sasa hivi siyo wakimbizi wako tu wana-enjoy wanatumia haki yao ya msingi universal right ya kuishi popote wanapotaka lakini si kwa wasiwasi wa kukaa kwenye nchi hii. Hiyo ni nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, walipotaka kuandamana wasaidizi wake wakasema siku hiyo tutakuwa tunafanya usafi wa mitaa, akasema tulieni waacheni waandamane, wapeni na ambulance, wapeni na ulinzi waseme wanachokitaka. Nia ni reconciliation tufikie maridhiano tuwe wamoja, sisi ni Taifa moja tuongee lugha moja, lolote tunalokusudia katika kujenga uchumi wa nchi yetu tutaweza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi kufanya haya bila kuwa mstahimilivu, kuamua kuacha yale matashi yako yote ya Uamiri Jeshi Mkuu ukashuka ukakaa na watu huwezi kuyafanya, akafanya yeye kwa matendo kuja kukaa na watu wa chini kabisa, lakini hatuwezi kufanya hii bila reform lazima tukubali kufanya mageuzi ya dhati. Watu wameogopa kuigusa Tume ya Uchaguzi, kuitengenezea sheria mimi naigusa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakwenda kushughulika na Tume. Kama tatizo ni Tume tuishughulikie Tume, kama tatizo ni mimi Rais kuwa na Madaraka mengi basi sawa naachia Madaraka kwenye Kamati ya Usaili nipendekezeeni hao watu mnaowataka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ingekuwa ni kifaru alinyofoa pembe yake akampa mtu mwingine, ingekuwa ni tembo amenyofoa meno yake akampa mtu mwengine. Nia yake ya dhati ni kuona kwamba tunakuwa wamoja tulijenge Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, akasema, kufanya mageuzi haikuwa rahisi, hata sisi tulio wa kwake, maana katika watoto wa mama kuna mtoto mmoja yaani huyo huwaga yuko kwenye pochi, lakini kuna mwingine anaweza kuwa yuko pembeni kidogo; hata watoto wake wengine hawakuelewa. Akasema, mtatakiwa kuelewa, lazima twende kwa style hii ili tufanye reformation ili tufanye rebuilding, tuwe wamoja.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameanza kufanya rebuilding kwa kusema sasa tunaenda kufanya mageuzi ya kuandika. Tunaleta sheria Bungeni, tunafanya mabadiliko ili watu wajisikie wako huru, halafu baada ya hapo twende mbele tufanye kazi ya kujenga Taifa letu. Sasa tupambane na umasikini, tupambane na maradhi, tupambane na upungufu wa ajira kwenye Taifa letu, tuijenge nchi yetu, tuache maneno maneno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba Watanzania tufike mahali na sisi tuungane na Mheshimiwa Rais kwenye nia zake za 4R, tufanye rebuilding ya Taifa letu. Hili ndilo Taifa Mungu alilotupa, hatuna Taifa lingine, na wengine wana-quote na kujifunza kutoka kwa watu wengine, lakini nataka nikwambie huko tunakojifunza ndiyo kubaya zaidi.

Mheshimiwa Spika, amesema hapa Mheshimiwa Tadayo wengine mataifa yao yalipata uhuru tangu miaka ya 1776 mpaka 1919 bado walizuia wanawake miaka 144 mbele, bado haki ya demokrasia kwa wanawake ilikuwa haiwezi kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mpaka miaka ya 1960 sisi tumepata uhuru bado kuna mataifa haya tunayodhani kwamba ni bora sana, watu weusi walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura. Ili upige kura lazima kwanza ufanye; kuna kile kipengele kimoja wanasema ukatengeneze mazingira mazuri na jirani yako mweupe ili kupiga kura ulipe kodi ya kura, ili kupiga kura kama wewe ni mlafi mlafi tu, huruhusiwi kupiga kura. Sijui huo ulafi walikuwa wanaupimaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hao ndiyo tunataka tujifunze kutoka kwao! Watanzania tutakurupuka kutoka kwao. Haya huwa wanasema, ilikuwa ni miaka 144 baada ya kupata uhuru, sisi Taifa letu lina miaka 62. Ina maana tungekuwa kwenye nchi hizo mpaka leo sisi wanawake humu tusingekuwepo, kwa sababu haturuhusiwi kuchagua wala kuchaguana, wala Mheshimiwa Rais asingekuwepo. Sasa wakati mwingine, nasi tumepewa akili. Usipende kulazimisha ubongo au unajizima data unabaki airplane mode. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wanatakiwa kuja kujifunza kutoka kwetu sisi. Rais wetu miaka 62 amewezaje kufanya demokrasia? Waliwezaje wale miamba sita akiwepo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwashirikisha wanawake kwenye harakati za mapambano ya uhuru na kuwafanya wachaguliwe day one from the day of independence? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wao wameshindwa! Tuache kujizima data, wanatamani kuja kujifunza. Ukiona mtu anakushawishi bwana, unajua kule sijui Marekani, sijui wapi, sijui wapi; mwambie sisi ni Watanzania, ni Taifa moja na Mungu alitupa ubongo, tuna uwezo wa kupanga mambo yetu wenyewe kabla hatujaiga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Watanzania tumuunge mkono Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili sasa tuache hizi kelele na mbambamba za haturuhusiwi kusema; haturuhusiwi sijui nini; tuelekeze akili zetu kufanya innovation na creativity ya kulijenga Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwasihi wanawake, tujifunze kutoka kwa mwamba huyu wa Awamu ya Sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike. Tusilielie. Mungu akawaambia watu fulani Taifa moja, nawapeleka ninyi vitani siyo kwamba siwapendi, nawapeleka vitani ili mkajifunze vita. Kwa hiyo, wakati mwingine wanawake ukitukanwa mwambie yes, hapa ndiyo kwenyewe; unafundishwa vita ya kupambana. Usipoenda vitani utakuwa huwezi kupigana; na majibu huwa yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naweza nikatolea mfano, nilitukanwa Iringa pale, nikaambiwa Jesca Msambatavangu huwa mnamchagua Mbunge hana mume. Nikajibu tu jukwaani, wewe unayelalamika kwamba sina mume, ndio mwanaume, katoe posa Kamati Kuu ya CCM, njoo unioe, vinginevyo utakuwa una matatizo ya kiume. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Weweee!

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, tusilie, mama ameshaonesha njia, mwamba wa Awamu ya Sita, unalilia nini? Simama tumepata fursa sawa. Wanawake tusimame twende tukagombee, tuitetee nchi yetu, na tunamwona mama ndiye Rais aliyesema, natoa mamlaka yangu ya Tume ya kuteua sijui Wajumbe wa Tume, nayatoa napeleka kwenye Kamati, si amepeleka! Si mambo mazuri! Watu wanaandamana, situmii nguvu, natumia akili. Ndiyo maana Biblia inasema, “Ishi na mwanamke kwa akili.” Kwa sababu mwanamke ni very intelligent, anatumia akili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wanaandamana, peleka ambulance, peleka Polisi awasindikize, watafanya nini? Hata sisi mama siku ile amebeba khanga ameingia kwenye ule ukumbi anacheza, nikasema jamani, yule ni mama ana khanga ya chama kile, hee! Yaani mimi alinifundisha kitu kipya sana. Nikapiga magoti nikamwambia Mungu, nakushukuru. Akaingia, akatoka salama. Wewe unaogopa nini? Huyo aliyekusema, utanyofoka ngozi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi nchi tunasema hizi, nchi hizi ambazo tunawasifia, mtu huruhusiwi kupiga kura, hiyo miaka hiyo sasa. Mpaka miaka ya sitini sitini, huruhusiwi kupiga kura kama hujui kusoma na kuandika wala huruhusiwi kupelekwa na mwenzio kukupigia kura. Kama huwezi kutoa kiapo kwa mdomo, huruhusiwi kupiga kura. Sasa kama mtu ni kiziwi, labda ana ulemavu inakuwaje? Sisi tunataka tuwaambie jamani eh, msitupeleke mputa. Sisi Taifa hili ni changa, lina miaka 62, ninyi mna miaka 200, mtusubirishe kidogo, tunajipanga. Afterall, we are well off kuliko ninyi mlivyokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niseme, haya mambo yalitukuta kule nyuma. Kule nyuma watu walileta vurugu kwenye Katiba Mpya, wakafikiri kuna mtu wanamkomesha, lakini ile Katiba Mpya mimi nilivyoiona, ilipendekeza hata Tume hiyo huru waliyosema. Afterall hii Tume ni huru kwa sababu hiyo ibara ya 74 (7) inasema Tume hiyo itakuwa huru, kwenye Katiba iko.

Mheshimiwa Spika, Mgombea binafsi aliruhusiwa, haya mambo yote ambayo tunayafanyia amendments yaliruhusiwa, lakini watu wakajizima data, wakabaki airplane mode, wakajifanya wanatoka, leo tena wanatusumbua turudi kwenye mambo yale yale. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi hamna kubaki kindege, mtu ajifungue data, tuunge mkono hii hoja, tupitishe nchi yetu. Tuna mambo ya maana ya kufanya kuliko haya maandamano ambayo tunafanya kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tutamsemea, tutamtetea popote na Mungu atusaidie. Wanawake sikilizeni niwaambie, watu wa Taifa fulani wakamwambia Mfalme Daudi; “Wewe ni mfalme wetu.” Alikwenda kwenye vita akanusurika kufa, aliporudi, walivyopata ile habari wakasema, “Wewe ni mfalme wetu, hatutaruhusu tena uongozane na sisi kwenye vita ili hiyo taa isije ikazima, halafu wote tukazima Taifa zima.” Wanawake tunatakiwa tutoke na kauli moja. Sisi lazima tumtetee Mama Samia ili ile taa ya wanawake isije ikazima kwenye Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba wanaume, mnapomuongelea Mama Samia muongelee kama binti yako wa kike, mwongelee kama mama yako mzazi, mwongelee kama your baby ambaye unataka kumuoa, sio yule ambaye mmetengana vyumba. Taa hiyo ikizima, mmezima ndoto za binti zenu, taa hiyo ikizima mmezima ndoto za mama zenu, taa hiyo ikizima, tumezima ndoto za wanawake wa Tanzania, na Afrika inataka kujifunza kutoka Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatumpi sifa za bure, kasema Mheshimiwa Mwakagenda, kura siyo namba, kura ni uwezo na umahiri. Wale miamba sita walifanya mambo mema, lakini hili waliogopa kuligusa, mwanamke ameligusa na tunakwenda kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maneno haya, nawaomba Watanzania, tuache ushabiki, sisi ni Watanzania, wala tusijidhalilishe, Mungu anatupenda, nchi hii imekuwa ya ahadi, siku zote imepokea watu wanaopata shida kwenye nchi zao, tumekuwa wa kwanza kupigania uhuru upande wa Southern SADC; sisi ndio tumeongoza mapambano, tuliwasaidia hata South Africa, no matter economically wako mbali, lakini tulishirikiana; na ndiyo chama kimebakia ambacho hatusemi kama ni vipi, lakini ndicho kilichozaa na vyama vingine vyote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi ni nchi makini, tuko strategically, spiritually, physically and mentally. Kwa hiyo tusijidhalilishe Watanzania tupambane twende na hoja zetu. Tunapitisha Muswada huu kwa nia njema Miswada mitatu ili muwe huru kugombea, kuchagua wagombea mnaowapenda. Mliambiwa kwamba ooh, mtu anapita bila kupingwa hampati fursa ya kuchagua; sasa mnakwenda kupata fursa, akipita peke yake mpeni kura za ndiyo au hapana halafu ataonekana kama mnamhitaji, lakini tumewapa fursa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nimalizie.

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie moja tu. Naomba tuaminiane, tupendane, tuheshimiane, hakuna mtu mwingine atakuja kuijenga nchi yetu. Leo humwamini Jaji wa Mahakama ya Rufani, leo humwamini Mkurugenzi, hivi ninyi wanaume, sasa hii nchi ataongoza nani? Tukakodi Wakurugenzi? Tukodi Majaji wa kuja kutuongoza na ninyi mpo na mmesoma?

Mheshimiwa Spika, haiwezekani, huwezi kusema Wakurugenzi wote wabaya, majaji hawafai, wako presidential officials kivipi? Ninyi ndio ninyi, nchi hii mmepewa kurithi, tutatumia majaji wetu, wasomi wetu kwa ajili ya mambo yetu kama ambavyo tukipata shida wanatusaidia. Tutatumia Wakurugenzi kama ambavyo wanasimama Maafisa Waandamizi; kama vituo vya afya wanasimamia, ujenzi wa shule wanasimamia, leo unashindwa kumwamini kulinda kura, kivipi? (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu, katika Nchi yetu, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuasisiwa kwa Taifa letu Mwenyezi Mungu ametusaidia kupata Miamba Sita kwa Awamu Sita za Uongozi, na katika Miamba Sita hii Mwenyezi Mungu ametusaidia kuonesha jinsia zote mbili miongoni mwa Miamba Sita. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, moja ya mambo ambayo yalikuwa yakitusumbua katika Taifa letu ni katika kugusa sheria hizi tatu ambazo zimeletwa leo mbele yetu. Maneno yalitokea mpaka 2014 tulikuwa tuna nia ya dhati ya kuona kwamba sasa tuandike Katiba mpya, hata hivyo ilishindikana. Leo tumempata Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa jinsia ya kike amethubutu kwamba sasa tunataka tufanye marekebisho kwenye zile sehemu nyeti kabisa ambazo ukizigusa unakuwa umegusa utamu wa Madaraka ya Rais na ya sisi tulioko hapa leo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, haya ameonesha kwa nia ya dhati kutoka kwenye moyo wake na kuyajengea falsafa na kuamua kuchukua hatua thabiti za kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kufanya mabadiliko. Katika Biblia kitabu cha Mwanzo 11:6 inasema hivi; “Mungu akasema tazama watu hawa ni Taifa moja na lugha yao ni moja na haya ndiyo wanayoamua kuyafanya, hawatashindwa na hakuna kitakachoweza kuwazuilia”.

Mheshimiwa Spika, ni kwamba wameamua kuwa wamoja, kuongea lugha moja na wana mambo wamekusudia kuyafanya kama Taifa lao moja hakuna kitakachowazuilia. Ili sisi kuwa wamoja, kuweza kujiletea maendeleo, kujenga Taifa letu lazima tuongee lugha moja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tutaongeaje lugha mmoja tusipokuwa na maridhiano? Mheshimiwa Rais akaamua kwamba sasa tufanye maridhiano na ili ufanye maridhiano, kwa nafasi yake ilivyo kubwa, mambo ya maridhiano au mahusiano hata Mwenyezi Mungu aliyafanya. Wanadamu walipopotea Mungu aliamua kuja kufanya reconciliation lakini ili kufanya reconciliation ile ilimtaka ashuke aje kwenye level ya binadamu. Mama Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike, akashuka kuja kwenye level ya watu wa kawaida, akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu. Akatengeneza urafiki na wale wenye maneno maneno akaenda nao hadi kwenye sherehe zao akala nao. Akawaita watu bila kuangalia itikadi za imani zao, dini zao, uwezo wao, vyama vyao vya siasa, watu wa chini akakaa nao kwa pamoja, akatengeneza Kamati ya Maridhiano. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wakakaa kwa pamoja ni kipi ambacho kinasemwa semwa kwenye Taifa letu kinatufanya tusiende pamoja? Wakakaa wakiongozwa na kiongozi mkubwa wa dini wakajadili. Wakapata mambo 83 yanayofanya tusiwe wamoja kwenye nchi yetu, yamkini tushindwe kufikia maksudi yetu. Katika 83 Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, mambo 64 wameyatekeleza ikiwepo na pamoja kwamba sasa kama mikutano ya hadhara ilikuwa haipo fanyeni mikutano ya hadhara, na wengine waliokimbia wakajiona wakimbizi kwenye nchi hii rudini, enjoy maisha kwenye nchi yenu. Sasa walioko nje sasa hivi siyo wakimbizi wako tu wana-enjoy wanatumia haki yao ya msingi universal right ya kuishi popote wanapotaka lakini si kwa wasiwasi wa kukaa kwenye nchi hii. Hiyo ni nia ya dhati ya Mheshimiwa Rais. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, walipotaka kuandamana wasaidizi wake wakasema siku hiyo tutakuwa tunafanya usafi wa mitaa, akasema tulieni waacheni waandamane, wapeni na ambulance, wapeni na ulinzi waseme wanachokitaka. Nia ni reconciliation tufikie maridhiano tuwe wamoja, sisi ni Taifa moja tuongee lugha moja, lolote tunalokusudia katika kujenga uchumi wa nchi yetu tutaweza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huwezi kufanya haya bila kuwa mstahimilivu, kuamua kuacha yale matashi yako yote ya Uamiri Jeshi Mkuu ukashuka ukakaa na watu huwezi kuyafanya, akafanya yeye kwa matendo kuja kukaa na watu wa chini kabisa, lakini hatuwezi kufanya hii bila reform lazima tukubali kufanya mageuzi ya dhati. Watu wameogopa kuigusa Tume ya Uchaguzi, kuitengenezea sheria mimi naigusa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunakwenda kushughulika na Tume. Kama tatizo ni Tume tuishughulikie Tume, kama tatizo ni mimi Rais kuwa na Madaraka mengi basi sawa naachia Madaraka kwenye Kamati ya Usaili nipendekezeeni hao watu mnaowataka. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ingekuwa ni kifaru alinyofoa pembe yake akampa mtu mwingine, ingekuwa ni tembo amenyofoa meno yake akampa mtu mwengine. Nia yake ya dhati ni kuona kwamba tunakuwa wamoja tulijenge Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, akasema, kufanya mageuzi haikuwa rahisi, hata sisi tulio wa kwake, maana katika watoto wa mama kuna mtoto mmoja yaani huyo huwaga yuko kwenye pochi, lakini kuna mwingine anaweza kuwa yuko pembeni kidogo; hata watoto wake wengine hawakuelewa. Akasema, mtatakiwa kuelewa, lazima twende kwa style hii ili tufanye reformation ili tufanye rebuilding, tuwe wamoja.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais ameanza kufanya rebuilding kwa kusema sasa tunaenda kufanya mageuzi ya kuandika. Tunaleta sheria Bungeni, tunafanya mabadiliko ili watu wajisikie wako huru, halafu baada ya hapo twende mbele tufanye kazi ya kujenga Taifa letu. Sasa tupambane na umasikini, tupambane na maradhi, tupambane na upungufu wa ajira kwenye Taifa letu, tuijenge nchi yetu, tuache maneno maneno. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba Watanzania tufike mahali na sisi tuungane na Mheshimiwa Rais kwenye nia zake za 4R, tufanye rebuilding ya Taifa letu. Hili ndilo Taifa Mungu alilotupa, hatuna Taifa lingine, na wengine wana-quote na kujifunza kutoka kwa watu wengine, lakini nataka nikwambie huko tunakojifunza ndiyo kubaya zaidi.

Mheshimiwa Spika, amesema hapa Mheshimiwa Tadayo wengine mataifa yao yalipata uhuru tangu miaka ya 1776 mpaka 1919 bado walizuia wanawake miaka 144 mbele, bado haki ya demokrasia kwa wanawake ilikuwa haiwezi kufanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mpaka miaka ya 1960 sisi tumepata uhuru bado kuna mataifa haya tunayodhani kwamba ni bora sana, watu weusi walikuwa hawaruhusiwi kupiga kura. Ili upige kura lazima kwanza ufanye; kuna kile kipengele kimoja wanasema ukatengeneze mazingira mazuri na jirani yako mweupe ili kupiga kura ulipe kodi ya kura, ili kupiga kura kama wewe ni mlafi mlafi tu, huruhusiwi kupiga kura. Sijui huo ulafi walikuwa wanaupimaje? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hao ndiyo tunataka tujifunze kutoka kwao! Watanzania tutakurupuka kutoka kwao. Haya huwa wanasema, ilikuwa ni miaka 144 baada ya kupata uhuru, sisi Taifa letu lina miaka 62. Ina maana tungekuwa kwenye nchi hizo mpaka leo sisi wanawake humu tusingekuwepo, kwa sababu haturuhusiwi kuchagua wala kuchaguana, wala Mheshimiwa Rais asingekuwepo. Sasa wakati mwingine, nasi tumepewa akili. Usipende kulazimisha ubongo au unajizima data unabaki airplane mode. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu wanatakiwa kuja kujifunza kutoka kwetu sisi. Rais wetu miaka 62 amewezaje kufanya demokrasia? Waliwezaje wale miamba sita akiwepo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwashirikisha wanawake kwenye harakati za mapambano ya uhuru na kuwafanya wachaguliwe day one from the day of independence? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wao wameshindwa! Tuache kujizima data, wanatamani kuja kujifunza. Ukiona mtu anakushawishi bwana, unajua kule sijui Marekani, sijui wapi, sijui wapi; mwambie sisi ni Watanzania, ni Taifa moja na Mungu alitupa ubongo, tuna uwezo wa kupanga mambo yetu wenyewe kabla hatujaiga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naomba Watanzania tumuunge mkono Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili sasa tuache hizi kelele na mbambamba za haturuhusiwi kusema; haturuhusiwi sijui nini; tuelekeze akili zetu kufanya innovation na creativity ya kulijenga Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, niwasihi wanawake, tujifunze kutoka kwa mwamba huyu wa Awamu ya Sita, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwenye jinsia ya kike. Tusilielie. Mungu akawaambia watu fulani Taifa moja, nawapeleka ninyi vitani siyo kwamba siwapendi, nawapeleka vitani ili mkajifunze vita. Kwa hiyo, wakati mwingine wanawake ukitukanwa mwambie yes, hapa ndiyo kwenyewe; unafundishwa vita ya kupambana. Usipoenda vitani utakuwa huwezi kupigana; na majibu huwa yapo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, naweza nikatolea mfano, nilitukanwa Iringa pale, nikaambiwa Jesca Msambatavangu huwa mnamchagua Mbunge hana mume. Nikajibu tu jukwaani, wewe unayelalamika kwamba sina mume, ndio mwanaume, katoe posa Kamati Kuu ya CCM, njoo unioe, vinginevyo utakuwa una matatizo ya kiume. (Makofi/Kicheko)

MBUNGE FULANI: Weweee!

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, tusilie, mama ameshaonesha njia, mwamba wa Awamu ya Sita, unalilia nini? Simama tumepata fursa sawa. Wanawake tusimame twende tukagombee, tuitetee nchi yetu, na tunamwona mama ndiye Rais aliyesema, natoa mamlaka yangu ya Tume ya kuteua sijui Wajumbe wa Tume, nayatoa napeleka kwenye Kamati, si amepeleka! Si mambo mazuri! Watu wanaandamana, situmii nguvu, natumia akili. Ndiyo maana Biblia inasema, “Ishi na mwanamke kwa akili.” Kwa sababu mwanamke ni very intelligent, anatumia akili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wanaandamana, peleka ambulance, peleka Polisi awasindikize, watafanya nini? Hata sisi mama siku ile amebeba khanga ameingia kwenye ule ukumbi anacheza, nikasema jamani, yule ni mama ana khanga ya chama kile, hee! Yaani mimi alinifundisha kitu kipya sana. Nikapiga magoti nikamwambia Mungu, nakushukuru. Akaingia, akatoka salama. Wewe unaogopa nini? Huyo aliyekusema, utanyofoka ngozi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hizi nchi tunasema hizi, nchi hizi ambazo tunawasifia, mtu huruhusiwi kupiga kura, hiyo miaka hiyo sasa. Mpaka miaka ya sitini sitini, huruhusiwi kupiga kura kama hujui kusoma na kuandika wala huruhusiwi kupelekwa na mwenzio kukupigia kura. Kama huwezi kutoa kiapo kwa mdomo, huruhusiwi kupiga kura. Sasa kama mtu ni kiziwi, labda ana ulemavu inakuwaje? Sisi tunataka tuwaambie jamani eh, msitupeleke mputa. Sisi Taifa hili ni changa, lina miaka 62, ninyi mna miaka 200, mtusubirishe kidogo, tunajipanga. Afterall, we are well off kuliko ninyi mlivyokuwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi niseme, haya mambo yalitukuta kule nyuma. Kule nyuma watu walileta vurugu kwenye Katiba Mpya, wakafikiri kuna mtu wanamkomesha, lakini ile Katiba Mpya mimi nilivyoiona, ilipendekeza hata Tume hiyo huru waliyosema. Afterall hii Tume ni huru kwa sababu hiyo ibara ya 74 (7) inasema Tume hiyo itakuwa huru, kwenye Katiba iko.

Mheshimiwa Spika, Mgombea binafsi aliruhusiwa, haya mambo yote ambayo tunayafanyia amendments yaliruhusiwa, lakini watu wakajizima data, wakabaki airplane mode, wakajifanya wanatoka, leo tena wanatusumbua turudi kwenye mambo yale yale. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa hivi hamna kubaki kindege, mtu ajifungue data, tuunge mkono hii hoja, tupitishe nchi yetu. Tuna mambo ya maana ya kufanya kuliko haya maandamano ambayo tunafanya kila siku. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nataka niseme, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan tutamsemea, tutamtetea popote na Mungu atusaidie. Wanawake sikilizeni niwaambie, watu wa Taifa fulani wakamwambia Mfalme Daudi; “Wewe ni mfalme wetu.” Alikwenda kwenye vita akanusurika kufa, aliporudi, walivyopata ile habari wakasema, “Wewe ni mfalme wetu, hatutaruhusu tena uongozane na sisi kwenye vita ili hiyo taa isije ikazima, halafu wote tukazima Taifa zima.” Wanawake tunatakiwa tutoke na kauli moja. Sisi lazima tumtetee Mama Samia ili ile taa ya wanawake isije ikazima kwenye Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nawaomba wanaume, mnapomuongelea Mama Samia muongelee kama binti yako wa kike, mwongelee kama mama yako mzazi, mwongelee kama your baby ambaye unataka kumuoa, sio yule ambaye mmetengana vyumba. Taa hiyo ikizima, mmezima ndoto za binti zenu, taa hiyo ikizima mmezima ndoto za mama zenu, taa hiyo ikizima, tumezima ndoto za wanawake wa Tanzania, na Afrika inataka kujifunza kutoka Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hatumpi sifa za bure, kasema Mheshimiwa Mwakagenda, kura siyo namba, kura ni uwezo na umahiri. Wale miamba sita walifanya mambo mema, lakini hili waliogopa kuligusa, mwanamke ameligusa na tunakwenda kufanya vizuri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa maneno haya, nawaomba Watanzania, tuache ushabiki, sisi ni Watanzania, wala tusijidhalilishe, Mungu anatupenda, nchi hii imekuwa ya ahadi, siku zote imepokea watu wanaopata shida kwenye nchi zao, tumekuwa wa kwanza kupigania uhuru upande wa Southern SADC; sisi ndio tumeongoza mapambano, tuliwasaidia hata South Africa, no matter economically wako mbali, lakini tulishirikiana; na ndiyo chama kimebakia ambacho hatusemi kama ni vipi, lakini ndicho kilichozaa na vyama vingine vyote.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi ni nchi makini, tuko strategically, spiritually, physically and mentally. Kwa hiyo tusijidhalilishe Watanzania tupambane twende na hoja zetu. Tunapitisha Muswada huu kwa nia njema Miswada mitatu ili muwe huru kugombea, kuchagua wagombea mnaowapenda. Mliambiwa kwamba ooh, mtu anapita bila kupingwa hampati fursa ya kuchagua; sasa mnakwenda kupata fursa, akipita peke yake mpeni kura za ndiyo au hapana halafu ataonekana kama mnamhitaji, lakini tumewapa fursa... (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nimalizie.

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie moja tu. Naomba tuaminiane, tupendane, tuheshimiane, hakuna mtu mwingine atakuja kuijenga nchi yetu. Leo humwamini Jaji wa Mahakama ya Rufani, leo humwamini Mkurugenzi, hivi ninyi wanaume, sasa hii nchi ataongoza nani? Tukakodi Wakurugenzi? Tukodi Majaji wa kuja kutuongoza na ninyi mpo na mmesoma?

Mheshimiwa Spika, haiwezekani, huwezi kusema Wakurugenzi wote wabaya, majaji hawafai, wako presidential officials kivipi? Ninyi ndio ninyi, nchi hii mmepewa kurithi, tutatumia majaji wetu, wasomi wetu kwa ajili ya mambo yetu kama ambavyo tukipata shida wanatusaidia. Tutatumia Wakurugenzi kama ambavyo wanasimama Maafisa Waandamizi; kama vituo vya afya wanasimamia, ujenzi wa shule wanasimamia, leo unashindwa kumwamini kulinda kura, kivipi? (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)
The Prevention and Combating of Corruption (Amendment) Act, 2024
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili nami niweze kuchangia. Napi pia nitachangia kwenye huu Muswada wa Kupambana na Rushwa na niungane na wenzangu kuwapongeza Wizara kwa kazi kubwa waliyoifanya na Kamati pia kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa ajili ya kuchambua vipengele hivi ambavyo tunakwenda kufanyia marekebisho hasa kwenye issue ya kupambana na rushwa. Interest yangu kubwa pia itakuwa katika kipengele kile kile cha 25 na nitakuwa na mambo mawili ya muhimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ni kuomba kipengele kile kibaki kama kilivyokuwa kwa sababu zipo sababu za msingi, lakini pia nitaongelea na suala linahusu adhabu. Kwanza kabisa, niungane na Mbunge ambaye amemaliza kwamba ahadi hizi ambazo tunapenda ziwekwe katika sheria hii ya Kupambana na Rushwa hasa kwenye rushwa za ngono ziwe ni adhabu ambazo zinakwenda kuzuia lile jambo lisiendelee tena, zisiwe ni zile adhabu ambazo tuna-intend kwamba iende ikamrekebishe mtu. Iwe ni adhabu inayokwenda kuzuia mtu aone kabisa kwamba hatakiwi kufanya hiki kitendo kwa sababu ya madhara yanayotokana na tendo lenyewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, wengine wameongelea sana hapa masuala ya afya ambapo kama kutatolewa hiyo rushwa ya ngono mtu gani anaweza akaathirika kisaikolojia, lakini pia na afya yake. Mimi nitakwenda mbali zaidi kuona ambavyo madhara yanaweza yakatokea kwenye jamii. Ni kwamba unakwenda kumpa mtu kazi kwa sababu alitoa rushwa ya ngono, na unakwenda kumpa mtu kazi labda tuchukulie ya udaktari, haujaangalia professional yake, hujaangalia uwezo wake, uelewa wake na unyeti wa ile kazi anayokwenda kufanya ila wewe umeangalia professional yake katika performance katika suala la mapenzi au kwenye rushwa ya ngono, halafu huyu mtu anakwenda kuhudumia watu na hiyo kazi ameshaipata.

Mheshimiwa Naibu Spika, hebu fikiria! Ndiyo maana unakuta sasa hivi ukiangalia katika tafiti za dunia zinasema 43% ya watu wanaokufa duniani ni kwa sababu ya matibabu yasiyo sahihi yaliyotolewa na wauguzi. Watu zaidi ya 40% wanapoteza maisha kwa sababu muuguzi hakumpa tiba sahihi yule mgonjwa. Sasa ndiyo tunasema hapo, ndiyo hao watu sasa wanaweza kuwepo wengi wao wapo katika makundi kama haya especially kwa Afrika.

Mheshimiwa Naibu Spika, mtu anapewa nafasi ile lakini uwezo wake wa ku-perform kwenye ile nafasi haupo. Kwa hiyo, anatusababishia vifo, lakini anaweza kutusababishia madhara, anaweza kutusababishia ulemavu kwa watu kwa sababu hana hiyo skill ya kufanya ile kazi, kwa sababu hakupata kwa vigezo vya kwamba ana uwezo huo, bali alipata kwa vigezo vya kwamba alitoa rushwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo maana tunasema adhabu hii haitoshi. Inabidi iwe ni adhabu ambayo inakwenda kuzuia kwa sababu madhara yake yanakuwa ni makubwa yanakwenda mpaka kwenye jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ameongelea Mheshimiwa Mbunge pia, tunapoongelea hii sheria itakwenda kufanya kazi siyo tu kwenye masuala ya kazi, inaweza kwenda kufanya kazi pia hata kwenye masuala mengine, kwa mfano kwenye shule au kwenye vyuo. Kuna malalamiko mengi ya kwamba hata watoto wanapokwenda kwenye vyuo ili kufaulu anadaiwa rushwa ya ngono ili apate maksi za kuridhisha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ukienda kusema huyu mtoto au huyu mwanafunzi alienda akamshawishi mwalimu wake ili ampe rushwa, ampe maksi nzuri inakuwa haileti maana. Sisi tunategemea kwamba yule mwalimu aliyepo pale Chuo Kikuu yeye ni mlezi. Kwa hiyo, hatutegemei kwamba ushawishi wa mwanafunzi utamzidi Lecturer mpaka ashawishike, akubali kumpa mwanafunzi maksi kwa rushwa ya ngono eti kwa sababu mwanafunzi amemshauri, hapana!

Mheshimiwa Naibu Spika, hatutegemei kwamba mwanafunzi aliyemaliza chuo kikuu anakwenda kuomba kazi mahali, yeye ndiye mwenye shida ya kazi akawa ana nguvu kuliko yule bosi mwenye power ya kumpa kazi. Moja ya uwezo wa hawa viongozi wanaokuwepo kwenye hizo nafasi wawe na uwezo wa kukabiliana na masuala hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama yeye atakuwa ni mdhaifu kwa mtu tu anayekuja kufanya interview kwa muda mfupi, huyu ndiyo bosi tumemkabidhi labda kitengo, wakina dada wengi mle, tuna binti zetu wanaajiriwa mle, kuna wake za watu wanaajiriwa mle, kama ni mdhaifu namna hivyo kwenye interview tu anavutika kimapenzi, wale wake za watu walio chini yake! Wakija naye kumshawishi atavutika pia! Hao mabinti zetu wadogo wadogo wanaokuwa wameajiriwa ni wachumba za watu, yeye kama bosi ni mdhaifu wa kuathirika kiasi hicho, si nao watamvuta na yeye nao ataathirika nao, atataka afanye nao mapenzi!

Mheshimiwa Naibu Spika, tunategemea a-demonstrate nguvu ya kupambana na hiyo rushwa kwenye interview, lakini apambane na hiyo rushwa hata anapokuwa katika mazingira ya kazi ili watu wawe na uhakika wa usalama wa wake zao wanaofanya kazi kwenye ofisi mbalilmbali. Kama ndiyo hivyo, mabosi watakuwa wadhaifu tu kwenye rushwa za ngono wanapofanya interview, huko maofisini itakuwaje? Wafanyakazi wa kike watakuwaje salama? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunadhani kipengele kile cha 25 kibaki kama kilivyokuwa mwanzo ili kiendelee kumbana yule yule mwajiri, yule bosi ambaye ndiye mwenye nguvu; hasa tunasema aliyeshika mpini ili yeye, ajue namna ya kupambana asianguke kwenye ule mtego wa majaribu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kingine tukishasema tena hapa kwamba na yule anayeomba kazi naye aonekane na yeye alimshawishi, hapa itatuwia ngumu sana kumkamata yupi ndiyo mwenye makosa kwa sababu mosi, atamkandamiza bwana unataka kazi eeh! Leta rushwa ya ngono, huleti rushwa ya ngono ukienda kuniambia mimi nimekupa rushwa ya ngono nakwambia na wewe ulinishawishi. Sasa hapo itatokea contradiction, lazima atokee mmoja ambaye atakuwa anakamatwa na sheria …

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa

NAIBU SPIKA: Taarifa.

TAARIFA

MHE. TWAHA A. MPEMBENWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Naomba nimpe taarifa mzungumzaji. Mheshimiwa Mbunge anachangia vizuri sana, lakini nataka nimpe taarifa tu kwamba jambo lenyewe hili lipo very subjective kwa sababu ni jambo linalohusiana na mambo ya makubaliano. Sasa kwenda kuli-justify kwenda kwenye ngono bado kidogo lina utata utata lakini ni makubaliano inakuwa kati ya pande mbili.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea taarifa yake. Ni makubaliano ambayo mtu mwingine anasema amekubaliana kutokukubaliana. Nafikiri Mheshimiwa Twaha amewahi kusikia hicho kitu. Tunakubaliana kutokukubaliana. Huyu mazingira; turejee jana. Jamani tulikuwa tunapitisha hapa sheria kuhusiana na kuwalinda watoto, kwamba mtu yEyote asiwatumie watoto kwa sababu tu yule mtoto ana uhitaji, basi mtu amtumie vibaya kwenye shughuli za uhalifu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa sababu huyu; awe ni mama au ni kaka labda anahitaji kazi, amekwenda pale amekutana na bosi mwanamke, kwa sababu yule kijana wa kiume anahitaji tu kazi, basi yule mama anamfanyia vituko kumshawishi kwanza mpaka wafanye mapenzi ili aruhusu kumpa ile kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, au hivyo hivyo kwa mwanaume ambaye naye anataka kazi, na yule anakubaliana kwa sababu ya mazingira, hana option. Huyu ni inferior lakini yule mwingine ni superior. Huyu mwingine sisi tuna-assume yeye bosi ni mlezi na ndiyo tumemwajiri, amechukuwa dhamana ya kusimamia sheria na maadili ya kazi. Kwa hiyo, hatutegemei yeye awe part and parcel ya kuungana na yule ambaye ni inferior katika kuvunja maadili na sheria zilizowekwa. Kwa hiyo, yeye ili aonekane wa maana, lazima a-demonstrate uwezo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo maana tunasema kile kifungu kibaki kama vile kilivyokuwa ili wenzetu waliopo kwenye zile nafasi wasitumie zile nafasi kwa ajili ya kutuharibia vijana wetu, wawe wa kiume au mabinti zetu ambao ni wa kike, ambao wanakuwa inferior wanapokwenda kutafuta kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, narudia tena, adhabu hizi kwa mfano tunapokwenda kwenye ngono za watoto wetu na zitakwenda mpaka kwenye vyuo vikuu, kwa sababu unafikiria huyu mtoto aliyepata maksi kutoka chuo kikuu kwa kutoa rushwa ya ngono amefaulu, ana first class GPA anatakiwa kuajiriwa kuwa daktari wa binadamu. Amekuja huku anajua anayo silaha tena ni ile ile anakutana na rushwa naye anaajiriwa anaonekana ana maksi nyingi, amefaulu vizuri, nako anatoa ngono anapata kazi. Huyu mtu performance kwenye industry inakwenda kuwa ni very poor. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo maana zisiwekwe adhabu hizi za shilingi milioni mbili. Shilingi milioni mbili ni kitu gani? Bosi atashindwa nini? Ndiyo maana tunakubaliana na Kamati kwamba hizi adhabu ziongezwe. Mtu atashindwa kutoa shilingi milioni mbili? Kama tu hiyo rushwa yenyewe ya ngono mtu mwingine anaweza akanunua hiyo ngono zaidi ya shilingi milioni mbili kwa mara moja tu. Sasa atashindwa kusema kwamba nikalipe hiyo adhabu?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba, hii adhabu kwanza ipande kama Kamati ambavyo imeshauri na ikiwezekana wanasheria wetu mpo humu mweke adhabu ambayo inakwenda kukomesha vitendo hivi ili tuwasaidie watoto wetu, vijana wetu wawe salama ili tuwasaidie wanafunzi wetu huko kwenye vyuo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi hii tunaulizana wakati mwingine unamchukuwa mtu ambaye ni graduate unamwajiri kwenye kampuni, unamchukua mtu ambaye ni certificate graduate unakuta yule wa certificate ana-perform vizuri kuliko hata yule graduate. Unajiuliza, huyu na flying colors za ‘A’ zote hizi, GPA kubwa namna hii anashindwaje ku-perform kwenye kitu hiki? Kumbe hata siyo performance za kweli, ni viini macho. Kumbe wewe unamwona ana professional ya ‘A’ kwenye somo lile la sayansi kumbe ana professional ya ngono, ana ‘A’ kwenye mapenzi. Sasa anapokuja ku-perform kwenye field inashindikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ndiyo maana tunasema adhabu lazima ziongezwe ziwe zinakwenda kuzuia ili tupate watu ambao wana uwezo watakapokwenda kwenye industry waweze ku-perform. Tukiwa na ma-engineer waweze ku-perform.

Mheshimiwa Naibu Spika, huwa tunakwenda kukagua miradi ya Serikali, unakuta kweli tumepeleka engineer, lakini unajiuliza, hata mimi nisiye engineer, kweli ninge-propose nijenge msingi wa nyumba ndefu namna hii, hela yote iliyotakiwa kumaliza madarasa nane imeishia kwenye msingi wa darasa moja. Huyu ni engineer aliyesoma wapi?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, unakuta yale madhara yanatoka kule yanakuja moja kwa moja mpaka kwenye jamii, yanakuja yanaendelea kututia umaskini, yanakuja yanazuia innovation. Tuna watu wengine inawezekana kabisa kumbe na wao ni walimu wanafundisha watoto wetu, kumbe nao wamepewa zile nafasi za ualimu kwa sababu ya kuonekana ali-perform vizuri kwenye mapenzi na siyo kwenye skills. Sasa huyu anakwenda kuzalisha tunda gani? As a results ndiyo maana sasa hivi ukitaka kuongelea rushwa za mapenzi kwenye vyuo unaweza ukapata upinzani mkubwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, siku moja mpaka nilijiuliza, mama mmoja amesimama, ni lecturer wa Chuo Kikuu kimoja hapa nchini, anapinga rushwa ya mapenzi chuoni, yeye akiwa ni mwalimu wa pale, wenzie walim-punch vibaya mno. Nikaona aah, kumbe this is the system kwenye shule na kwenye vyuo vyetu! Sasa tunalalamika, kwa nini watoto wetu hawaajiriki? Kwa nini watoto wakienda kupambana kwenye East Africa na duniani wakifanya interview hawa-perform? Sasa ni namna gani wanapata hizo ‘A’ wanazozipata?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaomba adhabu iongezwe, lakini kipengele kile Na. 25 kibaki kama kilivyokuwa na yule mwingine ambaye ni victim kifutwe kabisa atolewe, yeye asiwe anaweza kuhukumiwa, ahukumiwe yule mkubwa ambaye sisi tunaamini kwamba tumempa ile nafasi kama mlezi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maji
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kwanza niwapongeze kwa kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Maji chini ya Waziri Aweso, kipekee sana kwa heshima na taadhima wananchi wa Iringa tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa unayofanya ya kuliongoza Taifa letu, na kusimamia maendeleo ya Taifa letu, na hususani katika Manispaa yetu ya Iringa. Tunashukuru kwa kuwa maji ndani ya Jimbo la Iringa imekidhi utekelezaji wa Ilani.

Mheshimiwa Spika, maombi; kwanza, tunaomba maji yafikishwe kwenye maeneo ya vijijini ndani ya Jimbo la Iringa ambayo ni eneo la Ugele, Kata ya Mkimbizi na Mosi Kata ya Kitwiru. Pia ninaomba kisima katika eneo letu la Uwanja wa Samora pale tulipofanyia mkutano ulipotuahidi kutuletea visima, siku ya ziara ya Rais, pamoja na zile shule tulizoomba kuchimbiwa visima.

Mheshimiwa Spika, Mkurugenzi wako IRUWASA amesema maji yapo kwenye shule hizo, na wamefungiwa prepaid, lakini hawatumii kwa kuwa bills hawawezi kulipia.

Pili, ninatoa ushauri kuwa katika bill ya maji muongeze hata shilingi 10 au tano kwa unit ili fedha hizi zichangie huduma za maji mashuleni, kwenye zahanati na vituo vya afya. Shule hizi zinawekewa miundombinu ya kisasa sana inayohitaji matumizi ya maji. Sasa kutegemea capitation pekee yake itakuwa vigumu sana.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe shukrani za dhati kwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kulinda raia na mali zao. Hata hivyo nina mambo kadhaa ya msingi sana ya kuchangia katika Wizara hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ni kuhusu kuwajumuisha polisi kutumia kikokotoo kama watumishi wengine wa Serikali tofauti na askari wengine wa majeshi mengine. Yapo malalamiko makubwa miongoni mwa askari kutoridhika na utaratibu huo. Askari hawa wa Wizara hii wanaona ni vyema utaratibu unaotumika kutoa mafao au kikokotoo kinachotumika kwa askari wengine mfano toka Wizara ya Ulinzi utumike na kwao pia kwani mazingira yao ya ufanyaji kazi yanalingana na askari wengine, lakini pia hawana muda wa kufanya mambo yao wanapokuwa katika ajira ukilinganisha na watumishi wengine wa umma, hivyo hawana muda wa kutafuta fedha nyingine kwa ajili ya kujiandaa na maisha ya kustaafu kama ilivyo kwa watumishi wengine wa umma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia viinua mgongo vyao au pensheni zao kwa walio wengi sio kubwa, hivyo, kutumia kikokotoo cha asilimia 33 hakiwasaidii kujiweka vizuri kwa maisha ya kustaafu, na pia umri wao wa kustaafu ni tofauti na wastaafu wengine wa kada nyingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo ni vyema kwa ufanisi bora wa majukumu yao wakiwa na afya nzuri ya akili wawapo kazini na baada ya kustaafu, tunaiomba Serikali ilipe uzito jambo hili la kutumia utaratibu wa kuwalipa mafao kama askari wengi wa Wizara ya Ulinzi na sio kikokotoo hiki cha asilimia 33 kama kinavyotumika kwa watumishi wengine wa umma ili kuweka heshima sawa kwa askari wetu wote na kuimarisha usalama wa raia na mali zao.

Pili, Serikali iweke mpango mahususi kwa kutumia nguvu kazi yake wakiwemo wafungwa na mahabusu kuhakikisha inaboresha makazi ya askari. Mfano makazi ya askari polisi ndani ya Jimbo la Iringa hayaridhishi. Hata makazi ya askari polisi wa Dodoma Kituo Kikuu cha Polisi Iringa Road hayaridhishi, ni aibu kwetu kama viongozi kuridhika kuwa na makazi duni namna hii ya askari wetu ambao ndiyo wanalinda mali na wananchi wetu wote yakiwemo mahoteli makubwa, maghorofa na roho zetu Watanzania wote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, wenza au wanawake wa askari polisi waangaliwe kwa namna ya kipekee katika kuwawezesha kiuchumi ili kusaidia ustawi wa familia za askari wetu. Kwa kuwa mara nyingi kupata ushirikiano wa kukopeshwa kwenye vikundi mitaani inakuwa ni changamoto kutokana na kazi za wenza wao. Uwepo mpango mahsusi wa kuzisaidia familia za askari kiuchumi kwa kuwawezesha wenza wao.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara hii ione namna ambavyo itakuza utamaduni kwenye maeneo ambayo yanapakana na mbuga zetu au maeneo ambayo watalii wengi hutemebelea kwa nia ya kusaidia kukuza utalii na kuongeza ajira nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba Iringa kama lango la utalii liangaliwe pia hasa ukizingatia historia ya watu wa Iringa na Chifu Mkwawa. Pia kuanzisha matukio mbalimbali kama mashindano ya ngoma, mbio na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Wizara ibuni njia muhimu za kushirikiana na wadau kuinua utamaduni wa sehemu husika na kuibua vivutio mbalimbali vilivyopo kwenye miji nchini ili kuimarisha ustawi wa afya ya jamii miongoni mwa jamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru kwa kunipa nafasi hii na mimi niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu katika kulipongeza Jeshi letu kwa kazi kubwa wanayofanya, hasa kuhakikisha usalama wa nchi yetu na ulinzi wa nchi yetu tunakuwa salama sana.

Mheshimiwa Spika, leo ningeomba niongelee kipengele cha JKT, yapo mambo mengi yanatuumiza akili, tunachanganyikiwa hatujui tunafanya nini, kumbe tuna vyombo humu ndani ambavyo hatujavitumia sawa sawa na kama tungevitumia matatizo yetu makubwa yanayotukosesha usingizi, mambo kama ajira kwa vijana, mambo kama maadili kwenye Taifa letu, mambo kama uzalendo, mambo kama ukakamavu, tayari tungekuwa tumeweza kwa kiasi kikubwa sana kuyatatua.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri amesoma utekelezaji wa Ilani kile kipengele (H) na wote hapa tupo kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, na Chama cha Mapinduzi kina viongozi makini wenye uelewa mkubwa wanaoona mbali sana. Wametuelekeza au wamekuelekeza Mheshimiwa Waziri katika utekelezaji wa Ilani (H), kuimarisha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) ili viwe vyombo vya kuwapatia vijana ujuzi wa kujiajiri na kuajiriwa na pia kuwa vyombo mahiri vya huduma na uzalishaji mali hasa katika ujenzi wa kilimo, ufugaji, uvuvi na maeneo mengine. (I) inasema hivi, ili uweze kutekeleza hilo (H) lazima sasa kupanua na kuongeza idadi ya Kambi za JKT na JKU. Ili kuwezesha vijana wengi zaidi, wakiwemo wahitimu wote kwa sababu JKT ina makundi mawili ya vijana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuna vijana tunawachukua kwa mujibu wa sheria na tunao vijana tunaowachukua kwa kujitolea. Wale wa kwa kujitolea ndiyo Ilani inasema kuwawezesha wengi, wale wa mujibu wa sheria Kidato cha Sita ni wote. Utalitekelezaje hili lazima uhakikishe kwamba unapanua na kuongeza Kambi za JKT na JKU.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ukisimama hapa utuambie safari hii unafanya nini katika kuongeza makambi, tunataka vijana wote wanaomaliza Kidato cha Sita waende JKT. Tunataka uongeze idadi ya vijana walioko mitaani waende JKT, kwa sababu JKT kwanza ina majukumu, objectives zake iliyopewa. Objective ya JKT namba moja ni malezi kwa vijana wetu, objective nyingine ni kuzalisha mali, kuwafundisha vijana wetu kuondokana na mentality ya kufikiria kwamba kazi za ofisini ni bora kuliko kujiajiri, kuzalisha mali lakini ni ulinzi wa Taifa letu. Kutoa mafunzo ya uhakika kwa vijana wetu kuhakikisha kwamba wanakuwa wazalendo, wakakamavu, kuendelea kulinda Taifa letu. Malezi ya vijana, kuwa na vijana wenye nidhamu, wakakamavu, wenye kujitegemea, wenye uwezo wa kufanya kazi ili kuleta maendeleo kwenye nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kumbe ni wakati muafaka sasa kama alivyosema kaka yangu Mheshimiwa Kingu, kumbe Wizara nyingine hizi zilitakiwa zifanye coordination na JWTZ na JKT kupeleka programu zao waseme sisi tunayo programu ya kuwafundisha vijana kupitia BBT hawa hapa. Kwa sababu Mheshimiwa Waziri kinachosumbua sasa hivi kwa vijana wetu, shule tumejenga nyingi, vyuo vingi ujuzi wanao, kinachosumbua ni ukakamavu, ni nidhamu na kujitegemea, hivi watavipata kule! Tunao Maafisa Kilimo yes, tumewadahili kwenye vyuo vya kilimo lakini Afisa Kilimo anaogopa nyoka, na nyoka wanaishi mashambani, akapate ukakamavu jeshini. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, tuna vijana tumewafundisha sasa hivi tumewapelea BBT watajifunza vizuri na mimi nashukuru nimetembelea kituo kimoja wanafanya vizuri lakini akishika jembe, akinyanyua tu jembe analiangusha lina mkata, ukakamavu haupo. Tunao vijana wengi tunawafundisha au tunawadahili wanakwenda vyuo vikuu wanamaliza form six, wanakuwa wasomi wazuri, madaktari wazuri lakini uzalendo hakuna. Mtu anaona bora mgonjwa afe yeye akimbie na dripu akauze. Kwa hiyo, kumbe mwarobaini wetu ni JKT na wazazi wetu waliliona hilo na ndio maana nikawa najiuliza ni kwa nini Waziri Mkuu Hayati Rashidi Kawawa aliamua kwenda JKT, ni kwa nini Mzee Aboud Jumbe aliamua kwenda JKT, ni kwa nini Mzee wangu mimi Adam Sapi, Spika wa kwanza wa Bunge hili aliamua kwenda JKT. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kule ndiko alikopata uzalendo na ukakamavu, wakajifunza nidhamu, leo tuna vijana tumewaendeleza sayansi na teknolojia Mheshimiwa Nape alikua anazindua minara 700 tunaweka huko lakini wengine wanatumia tu kutukanana au kutukana viongozi wetu au kui - defend Serikali yetu. Tusipowapeleka hawa JKT kujifunza uzalendo haina maana uwekezaji tuliofanya.

Mheshimiwa Spika, Serikali lazima mkae kama kitu kimoja mkubaline kwamba chombo kilichopitishwa kisheria na Bunge Tukufu kwa ajili ya malezi rasmi ya vijana wetu ni JKT, hatuhitaji tu akili za darasani Intelligent Quotient, ukishamjengea mental structure tunahitaji physical structure yake kwenye performance. Ana akili nzuri ni Afisa Kilimo mzuri lakini kuna mahali atatakiwa a - demonstrate ashike jembe achimbe, amuoneshe mkulima namna ya kufanya lazima huyu awe mtu makini, awe mtu mkakamavu, awe mtu mzalendo, awe ni mtu mwenye nidhamu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, JKT lazima iwezeshwe Waheshimiwa Wabunge, hiki ndiyo chombo kinachotuunganisha vijana wetu kama Taifa pekee yake. Huku kwingine tukiungana tunaungana kama Vyama vya Siasa, tunaungana kama CCM, tuna green brigade wetu, wanaungana kama CHADEMA wana red brigade. Huku ndiko tunakounganishwa kama Watanzania, tunaongea maslahi ya Watanzania, huku ndiko tunapelekwa bila ukabila, huku ndiko tunakopelekwa bila kujali itikadi za imani zetu. Tunakwenda kuambiwa sisi ni Watanzania we are blessed to be Tanzanians, tunaijenga Tanzania. Vijana wetu lazima wakue na mentality hiyo, wasifikirie tu kuona kwamba nchi zingine wanafanya vizuri, wanaishi vizuri natamani kutorekea huku, natamani kutorekea huku. Haina maana nchi hii, humu humu ndiyo nchi ya asali na maziwa hapa hapa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri nikuombe sana JKT, halafu kulala kule JKT namshukuru Mungu alinipa privilege nikaenda. Majengo ya JKT wala hayahitaji gharama kubwa wala is not a mansion kama hili Bunge letu. Wao wanapiga tu yale mahanga, bati na nini na nini, Waziri utuambie ukija hapa, CCM imekuelekeza hapa, wewe unajenga kambi ngapi? Vijana wengi tunataka kuona wanapungua mitaani unaniambia…

SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Ninataka kuona unanimbia Mheshimiwa Jesca leta vijana toka Iringa tuwapeleke JKT, wakajifunze uzalishaji mali, uzalendo na jinsi ya kulitumikia Taifa na kujitegemea wao wenyewe.(Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Jesca Msambatavangu kengele ya pili imeshagonga.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kuhusu utalii Kanda ya Kusini (REGROW), utekelezaji wa mradi huu umesaidia kuboresha miundombinu katika hifadhi na utatuzi wa migogoro.

Mheshimiwa Spika, naomba kuipongeza Wizara hii kwa kazi kubwa ya kukuza utalii na maliasili zetu. Pongeza pia za kipekee zimuendee Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake binafsi katika kuendeleza Wizara hii kupitia Royal Tour.

Mheshimiwa Spika, mchango wangu utajikita katika kujenga kituo cha Utalii Kusini chini ya REGROW kiitwacho Kihesa-Kilolo ambacho kinatakiwa kujengwa katika Manispaa ya Iringa ambalo ni lango la utalii Kusini. Umuhimu wa vituo hivi vya kitalii duniani ni kutoa taarifa na elimu kwa watalii kuhusiana na mwelekeo au ramani ya eneo husika ambalo mtalii anatakiwa kutembelea, kutoa taarifa ya huduma zilizoko katika eneo hilo la utalii, ni sehemu inayomuunganisha mtalii na eneo la utalii. Hivyo basi, ni lazima tukubaliane kuwa pamoja na uboresha mbalimbali unaofanyika kwenye mbuga na hifadhi zetu, bado tujue ni muhimu sana kuwa na kituo cha utalii au information centre ambacho ni Kihesa Kilolo.

Mheshimiwa Spika, Kituo hiki kitatakiwa kutoa taarifa za Utalii Kusini yote, sio Iringa pekee yake. Utafiti unaonesha ili tufikie lengo la Ilani yetu ya kufikia watalii milioni tano ifikapo mwaka 2025; basi ni muhimu kujenga kituo hiki. Sababu ni kwamba huwezi kupeleka watalii wote hawa Kaskazini, utaharibu kabisa ikolojia ya utalii wenyewe Kaskazini. Tabia za watalii hutaka kupata taarifa mapema kutoka kwenye vituo hivi kabla hawajaanza safari ya kutembelea eneo husika. Sasa kwa wale wanaotaka kuja Kusini wanapata taarifa wapi?

Mheshimiwa Waziri, msiseme tu muda unaturuhusu mpaka mwaka 2025, utakuwa unaenda kinyume na Mpango wa Miaka Mitano na Ilani ya CCM, inayotutaka tuongeze pato la Taifa. Mchango wangu namba mbili, moja ya sababu kubwa inayowafanya watalii kutorudi nchini ni kukosekana kwa huduma bora muhimu ikiwepo, kupatikana kwa fedha za kigeni. Mheshimiwa Waziri fanya jitihada zako binafsi bila kuwategemea Wizara ya Fedha kuhakikisha, maduka ya fedha za kigeni yanarudishwa nchini, hasa maeneo ya utalii. Pigania Wizara ya Fedha kupitia BOT waondoe masharti yasiyokuwa rafiki yanayosababisha maduka ya kubadilishwa fedha za kigeni yasiwepo.

Mheshimiwa Spika, tatu, Iringa Mjini kama lango au reception ya Utalii Kusini, lazima sasa tukuombe Mheshimiwa Waziri kuweka msukumo mahsusi wa kuwaandaa watu wa Iringa kuwa wakitalii. Mamlaka za Iringa kuwa kitalii, mazingira ya Iringa kuwa kitalii ikiwemo kuhakikisha misitu ya asili inalindwa kwa kushirikia na programu za TFS, kama kupanda miti, kutunza miti ya asili, kutoa mizinga ya nyuki ili kupunguza ukataji wa miti hovyo kuifanya Iringa kwa Southern Geneva); ikiwemo kuanzisha zoo, hili mimi mwenyewe naweza kusaidia.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri atakapo wind-up atoe kauli thabiti amejipanga vipi kuwafanya watu, viongozi, mji wa Iringa, mazingira ya Iringa kuwa ya kitalii (Southern Geneva of Africa). Naunga mkono hoja naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Mapitio ya Hali ya Uchumi wa Taifa 1.3.1. Pato la Taifa na Ukuaji wa Uchumi katika kipindi cha Januari hadi Septemba, 2022, Uchumi wa Taifa ulikua kwa wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2021. Ukuaji chanya wa uchumi ulichangiwa na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali ikiwemo mikakati ya kukabiliana na athari za vita kati ya Ukraine na Urusi; ruzuku kwenye mafuta shilingi milioni 100 kila mwezi, uwekezaji wa kimkakati katika miundombinu ya nishati (trilioni 6.55 limefika 86.89%), maji (trilioni 1), afya (trilioni 1), elimu, barabara, reli na viwanja vya ndege; kuongezeka kwa uzalishaji wa madini, hususan dhahabu na makaa ya mawe na kuongezeka kwa mikopo katika sekta binafsi ambayo imechochea shughuli za kiuchumi.

Aidha, ukuaji huu ulichangiwa na kuongezeka kwa shughuli za utalii kutokana na kampeni ya Royal Tour. Ukuaji huu wa uchumi unaashiria kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika sekta mbalimbali pamoja na kuongezeka kwa ajira na mapato ya ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, mambo matatu ambayo yatasababisha Watanzania kuhamisha uwanja wa vita; kwanza Bureau De Change - BoT/masharti ya kuanzisha Bureau De Change yawe rahisi ili kurahisisha upatikanaji wa dola nchini na kukuza utalii; pili, madeni ya kodi za muda mrefu - TRA lifanyiwe kazi; tatu, gawio kwa Watanzania kwenye makampuni ya hisa- kama Vodacom wafuatiliwe ili wawe wanatoa gawio.

Mheshimiwa Naibu Spika, madaraka ya Kamishna ni makubwa mno kiasi cha kukiuka haki za binadamu na baadhi ya sheria hasa Kamishna akiwa negative thinker.

Mheshimiwa Naibu Spika, machinga wa Iringa waliahidiwa na Rais fedha zao shilingi milioni 700; tunaomba Wizara ya Fedha itoe.

Kuhusu utoaji maamuzi chanya kwa viongozi wa juu wa taasisi unazoziongoza uko chini sana, wawe wanatoa maamuzi mapema na kwa wakati ili kuepusha migogoro kama migomo na kufifisha uzalishaji kwa wananchi; kupuuza maagizo ya viongozi ikiwemo Mheshimiwa Rais, mfano kutotoza kodi za miaka ya nyuma na ya muda mrefu, kutorudisha fedha za Bureau De Change na kusingizia Bunge na vyombo vingine vya sheria waache. Wawajibike! Nia ovu isiwepo kama ku-seize fedha za Community Banks kama Mucoba bank milioni 600, ni kutowatendea haki wananchi.
Azimio la Bunge la Kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa miongoni mwa viongozi wenye ushawishi mkubwa Duniani na kupewa Tuzo ya mafanikio ya ujenzi wa miundombinu
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nami nichukue fursa hii kwa kweli kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tuzo hii aliyoipata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa mimi ni Balozi wa Afya ya Akili, nitaomba nitumie mfano ili watu waelewe, kwa sababu kuna watu wengine huwa pia hawaelewi. Mimi niseme hivi, hii tuzo ni kama kombe ambalo huwa zinacheza ligi zetu humu ndani ya nchi. Hapa hii tuzo ilikuwa inagombaniwa na nchi 54. Nchi zote za Bara la Afrika na wachezaji walikuwa ni Wakuu wa Nchi kwenye timu hizo, lakini aliyekuwa kashikilia tuzo hii ilikuwa ni wenzetu Nigeria. Kwa hiyo, naweza nikaendelea kutoa mfano; nichukulie kama Nigeria ilikuwa ni Yanga na Mama Samia ni Simba; wameingia kwenye fainali. Zilikuwepo sheria, kama zilivyo sheria 18. Hapa kamati ile ikaangalia, maana kuna watu hawaelewi wanafikiri labda imetolewatolewa tu kwa sababu ya hivi hivi, hapana. (Makofi/Kicheko/Kigelegele)

Mheshimiwa Spika, jambo mojawapo Mbunge mwenzangu aliyemaliza kusema ameshamaliza. La kwanza, ilikuwa wameangalia shilingi milioni 290 ambazo Tanzania tume-qualify kwa vigezo kupewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya kuendeleza miundombinu chini ya usimamizi wa Rais Samia Suluhu Hassan, tukashinda kwa vigezo, tukaonekana tunafaa kupewa fedha hiyo kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya barabara, reli na usafiri wa anga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ya pili ikaangaliwa maono yetu baada ya kuwa tunajenga reli, tutai-manage vipi? Tutaiendeleza vipi? Tukaingia mkataba na kampuni nyingine ya China kutupatia modern flit cars kwa ajili ya kuendeleza sekta hii ya reli ambapo tutakuwa na magari 1,430 kwa ajili ya kusimamia uendelezaji wa sekta hii ya miundombinu ya reli. Hii iligharimu karibu dola milioni 172.2. Hayo ndiyo tuliyomtoa knockout Nigeria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ya tatu, ikaonesha nia ya Serikali ya Rais Samia; nimewahi sikia tetesi tetesi kwamba ule Mji Mkuu wa Nigeria, Abuja ule ramani yake inafanafana na masterplan ya Mji wa Dodoma. Sasa wao wamejenga ule Mji lakini walishindwa kwenye ring road hawajafanya. Sisi Tanzania tarehe 11 Februari, Rais wetu amezindua na kuanza rasmi ujenzi wa ring road katika Mji wetu wa Dodoma. Hiyo moja ilikuwa ni credit. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu zangu Watanzania tunaposema Mama anafanya kazi kubwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hata vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasema, wakati mwingine Nabii hapati heshima kwao. Ila mimi kama Balozi wa afya ya akili, naweza nikasema ni matatizo pia ya afya ya akili kutotambua kwamba una kitu cha thamani au una kiongozi bora ndani ya nyumba yako na kubeza juhudi za mama anapotoka kwenda kutafuta chakula; au baba anapotoka kwenda kupambana na maisha ili arudi na kitu kuendeleza familia. Ile nayo ni matatizo ya afya ya akili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ndugu zangu mama anapokuwa katika harakati za kuwepo ndani ya Tanzania, au anapokuwa katika harakati za kuwepo nje ya nchi ya Tanzania, ni kwa maslahi mapana ya Taifa letu. Leo hii katika hiyo fedha kila Mbunge hapa alipewa shilingi milioni 500 na wengine wamepewa shilingi bilioni moja. Leo hii nikifika Iringa, nikienda katika Kata yangu ya Mkimbizi pale, Namtivila kuna barabara tumejenga ambayo tumepeleka shilingi milioni 500 kutoka katika mgao huu. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

SPIKA: Mheshimiwa, kengele imeshagonga, ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa hiyo, nawaomba ndugu zangu tumuunge mkono mama, anaupiga mwingi!

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba kutoa mchango wangu kama ifuatavyo, nalipongeza sana Jeshi letu imara kwa namna linavyofanya kazi zake kwa weledi. Pamoja na mambo hayo mazuri binafsi naona wanayo fursa ya kuongeza kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, usalama wa wananchi ni matokeo ya usalama binafsi kwa wanajeshi wenyewe, asipo kuwa salama itapunguza motisha ya kuangalia usalama wa watu wengine. Tunaomba usalama wa wanajeshi wetu hasa huko Congo uimarishwe, inatuuma sisi tunajitolea kuwalinda majirani zetu, halafu wenzetu hawa sijui kama wanajali usalama wa vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kuhusu huduma za afya ya akili Jeshini ni muhimu zikaimarishwa, pamoja na kwamba hawa ni wanajeshi, bado ni binadamu, hali ya kwamba hawaruhusiwi kugoma wala kuandamana ni sawa kijeshi, lakini kibinadamu ndiyo wanahitaji zaidi huduma za afya ya akili kwa ujumla kuliko watu wengine waliopewa fursa ya kuongea au kuandamana au kubisha. Hivyo, Kituo cha Afya ya Akili kama ilivyobadilishwa Mirembe sasa ni muhimu sana. Wanajeshi wanahitaji kupata huduma hizo za kisasa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Jeshi letu katika maono yake ni kuwa Jeshi lenye weledi mkubwa. Hivyo basi, elimu ni muhimu sana kwa wanajeshi wetu. Kuhakikisha wanapata elimu bora, lakini na wale wenye elimu watumike vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne, tunaomba Jeshi letu litumike sana hata kutoa mafunzo kwa baadhi ya taasisi zetu au baadhi ya viongozi wetu ili kuongeza uzalendo kwa watu muhimu hasa viongozi wetu wasimamizi wa taasisi kama Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi, Waheshimiwa Wabunge na kadhalika. Hii itasaidia sana kuimarisha uhodari, uzalendo na kuondoa uvivu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tano, tunashukuru kwa Jeshi kuchukua hatua kwa vijana wote wanaomaliza form six, hiyo ifanyike na kwa wale ambao wanaenda vyuo vya kati bila kusahau Jeshi la Mgambo litoe mafunzo kwa vijana wote walioko mitaani ambao hawajapitia jeshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru pia kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia katika Wizara hii ya Ardhi na nitakuwa na mambo makubwa mawili. Niwapongeze kwanza kwa kazi nzuri pia ambayo wanafanya kwa sababu yapo mazuri mengi pia ambayo wanayafanya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nataka kuchangia kuhusiana na mpango wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa makazi. Kama Mbunge mmoja alivyokwishasema hapa; ardhi ni nguzo moja wapo katika nguzo nne ambazo Mwalimu Nyerere alisema, tunahitaji ili tuendelee, kwa sababu kila kitu kinafanyika kwenye ardhi. Sasa basi, kwenye upande wa makazi na matumizi bora nimeona kwamba wanasema mpaka 2025 inatakiwa vijiji vyote viwe vimepima na wamejiwekea namna hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miji tunayotoka pia kuna maeneo ambayo ni peri urban, haya sijaona mpango wake wamewekaje, yaani kwenye miji hakuna vijiji lakini tuna mitaa, lakini ile mitaa inaitwa mitaa kwa sababu tu ipo kwenye municipals au kwenye majiji; lakini ukiangalia hali halisi ni kama vijiji. Sasa sijui hii inaingizwa kwenye mpango gani. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine ni cha muhimu sana kukizingatia kwa sababu inatuletea shida hata kupeleka huduma kama hatuweki huu mpango wa matumizi bora ya ardhi mapema; hata kupeleka huduma kwa wananchi inakuwa ni kazi. Wakati ule Mwalimu Nyerere alianzisha zile program za vijiji vya ujamaa, of course yeye alianzisha kwa sababu ya mambo yake ya ujamaa na siasa za ujamaa na kujitegemea, lakini zilikuwa zina msaada kwa sababu hata wanapopeleka huduma wanawakuta wananchi wapo sehemu moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunataka kujenga barabara, unamkuta mtu alikuwa ni mwindaji, akaenda kuwinda mbali na wenzie, baadaye akajenga nyumba, akaanzisha familia iko mbali sana, sasa kule wanaendelea wanatengeneza familia wapo watu 200, wapo watu 150 kutoka kwa wenzao walipo ni kilometa zaidi ya 70 au 60; Serikali inalazimika kupeleka barabara mpaka kule, kuwapelekea shule lakini hawa watu wangekuwa sehemu moja kwenye kijiji ingelikuwa ni rahisi au kwenye mtaa, ingekuwa ni rahisi ku-concetrate kwamba tunawapelekea mahitaji ya muhimu pale ya huduma; lakini yale maeneo mengine wakatumia kwa ajili ya uwindaji au kwa ajili ya kilimo kama ambavyo wametumia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wamesema wanaimarisha TEHAMA, naomba katika zoezi la kuimarisha TEHAMA waangalie pia kuwapa mafunzo watu wao wa chini hasa kwenye kada hizi za chini kwenye halmashauri. Nasema hivi kwa sababu wengi, leo ukienda kwenye halmashauri wanatoa risiti za kuwadai kodi za ardhi wananchi ambazo siyo halisi. Ukiwauliza wanasingizia mfumo, wakati mfumo ule anau-feed mtu, hakuna mfumo ambao unajiweka peke yake halafu una generate data peke yake, ni watu ndiyo wana feed zile information kwenye mfumo. Sasa inaonekana watu wanakuwa hawapewi mafunzo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kingine tunaomba kwenye mambo ya MKURABITA, sasa hivi kwenye miji yetu MIKURABITA haipo tena, zile program za MKURABITA za kupima yale makazi ambayo hayakuwa rasmi haziendelei, sasa ujenzi holela unaendelea. Hata hivyo, kipo kipengele waliotoa kwenye Kamati zetu za Mipangomiji, cha kupitisha vibali vya ujenzi, wakaacha inawezekana walikuwa na nia njema kwamba vitolewe kwa wakati, viende na kasi na wananchi kwa sababu zile Kamati zina muda maalum. Hapa nafikiri wanatakiwa warudie waangalie ili kwamba Kamati zile zipewe mandate tena ya kuwa zinatoa vile vibali; kwa sababu tayari katika miji yetu ujenzi holela unaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili ninalotaka kuongea linahusiana na kodi ya ardhi (land rent) hasa kwenye taasisi; Taasisi za Dini, Taasisi za Shule na Taasisi za Vyuo. Ukiangalia hasa kwenye shule binafsi na kwenye vyuo binafsi. Suala hili limekuwa ni tatizo kubwa lakini katika hotuba ya Mheshimiwa Rais, alikuja hapa tarehe 22 Aprili, 2021, akatuambia kasome ile hotuba yake kitabu chake ukurasa wa 10, paragraph ya kwanza, ya pili mpaka ya tatu; alielezea ni namna gani ambavyo mazingira yetu ya uwekezaji wa biashara hayajaboreshwa; hasa kwenye Sera, Sheria na Kanuni zetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, akaahidi katika paragraph ya kwanza kuonesha anaboresha sera, sheria na kanuni. Paragraph ya pili na kuelezea hatua zinatakiwa kuchukuliwa ili kuvutia uwekezaji na sekta binafsi kuwekeza; lakini paragraph ya tatu akasema, nchi yetu imekuwa ikilalamikiwa kwa kutokuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji. Kwanza kutokuwa na kodi zisizokuwa na utulivu, lakini pia kuwa na sera ambazo zinabadilika badilika, hiki ni kitu ambacho hakivutii wawekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tuna watu wamewekeza kwenye elimu, uwekezaji kwenye elimu ni investment ya muda mrefu, return yake on investment ni zaidi ya miaka 10. Leo land rent unapokwenda kumchaji mtu mwenye shule binafsi, kwenye eneo la eka tatu katikati ya mji kwa mwaka anatakiwa kulipa milioni tisa, milioni sita inatoka wapi? Sasa uwekezaji umeanza kuwa kwa sababu hizi shule binafsi ndani ya manispaa lazima awe na eka tatu ndani yake kuna choo, viwanja vya michezo, madarasa, maabara, library vyote hadi choo kinachajiwa land rent, leo katika nchi yetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, inakuwaje wakati hawa watu binafsi ni wawekezaji, wametupunguzia msongamano kwenye shule zetu za public; lakini hawa watoto ni watoto wa Watanzania, Watanzania hawa wanaosomesha kwenye shule binafsi wana haki kabisa ya kuhudumiwa kielimu na Serikali hii, lakini wameamua kulipa kodi, wameendelea kusomesha watoto wao kwa gharama zingine, kwa nini tuwaongezee mzigo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tuangalie katika hizi shule binafsi, Serikali inatumia zaidi ya gharama za asilimia 97 kumsomesha mtoto kwenye shule ya public, lakini haichangii chochote kwenye shule ya private. Leo hii shule ya private inalipia fire, yaani shule ikitaka kuungua lazima ilipe ili ije izimiwe moto. Leo hatuna hata grant ya temptation tunayopata, unalipa land rent wakati fulani Katibu wa Wizara ya Fedha aliona kwamba suala la kuchaji kodi kwenye shule wakati ni taasisi zinazotoa huduma akazuia tukatolewa kodi ya SDL; lakini kodi hii imerudishwa kwa mtindo wa ardhi.

Mheshimiwa Spika, vile vitu alivyoongea mama Samia kuangalia sera na kanuni zetu; kanuni mojawapo inayowatesa wananchi wa Tanzania ni ile kumpa commissioner room na kumpa power zaidi ya Bunge, nasema zaidi ya Bunge kwa sababu gani haiwezekani kwenye hati mtu aandikiwe hati hii utalipa kwa mwaka Sh.1,000,000 labda ndiyo itakuwa land rent yako; Kamishna anakaa anabadilisha mtu alipe milioni sita au milioni tisa nani hapo mwenye mamlaka kuu? Hivi ndivyo vipengele ambavyo Rais alisema viondolewe kwenye kanuni, sera zetu na sheria kama zinawakandamiza Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, haiwezekani leo tukafikiri viwanja vya michezo navyo vilipiwe kwa utaratibu upi? Tuwaangalie hawa watu kwa sababu ni wawekezaji wa ndani na tuwasaidie; na kwenye maeneo ya Makanisa, maeneo ya Vyuo, hawa wamechukua jukumu la Serikali la kuelimisha Watanzania, kwa nini tusiwasaidie kama hatusaidii hata kulipa mishahara, watu hawa hata fedha ya kukaguliwa, kuletewa mitihani, wanalipa mitihani, kukaguliwa lakini hawajalalamika. Unaposema watu hawa wanachaji fedha, basi umchaji kodi, ujue ile kodi inapelekwa moja moja kwa Mtanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunawaomba ndugu zetu wa ardhi, kwa sababu wao ni msingi mmojawapo wa maendeleo kwa hiyo wasiposimamia vizuri sera hii na wakaweka kodi za aina hii maana yake ni kwamba huo mhimili hautasimama vizuri na hatutaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.

MWENYEKITI: Ameshamaliza muda wake; ahsante sana Mheshimiwa Jesca.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana nakushukuru sana. Naomba hilo lishughulikiwe.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante na mimi nikushukuru kwa ajili ya kunipa nafasi hii, lakini pia na mimi nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuona umuhimu wa kuanzisha Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, lakini pia nimpongeze Waziri pamoja na wenzie wote kwa kazi kubwa ambayo wameanza kuifanya kwenye Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, mimi leo naomba niongelee watoto wa kiume; tangu uumbaji Mungu alivyoumba utaratibu kila kitu kina namna ya kuongezeka na katika baraka ambazo Mwenyezi Mungu alizitoa kwa viumbe alivyoviumba tukiwepo wanadamu alisema tukaongezeka, tukatiishe, tukazalishe na tukatawale, hivi ni vitu ambavyo Mwenyezi Mungu, lakini sasa tunakwenda kuongelea pale kwenye kuongezeka.

Mheshimiwa Spika, kuongezeka kwa wanadamu au mbegu ya wanadamu Mwenyezi Mungu ameiweka ndani ya mtoto wa kiume, hakuna namna utabisha hilo. Na hata katika wanyama mbegu yao ya kuongezeka ipo ndani ya yule mnyama wa kiume, kwenye samaki hivyo hivyo yaani kwenye viumbe vyote ni hivyo. Sasa watu wote wenye afya nzuri ya akili wanaitunza mbegu kuliko kituo chochote, mkulima yeyote mwenye busara anaitunza mbegu yake vizuri kuliko kitu chochote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, na ndio maana mimi siwezi kuwa mshabiki wa kwamba mwanaume akifanya kosa ahasiwe kwa sababu mwisho Watanzania tutakosa mbegu na tukikosa mbegu tukaenda kuagiza kutoka nje sio Watanzania; na tukiitwa mbinguni kule tutaonekana Taifa letu liliisha siku nyingi sisi ni Taifa lingine. Sasa ninachotaka kusema, namna ambavyo tunaangalia watoto wetu wa kiume nchi hii sio sawa, naomba Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii alichukue ile ni mbegu, tukianza kwenye level ya familia tuangalie namna tunavyowalea watoto wetu wa kiume. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mbegu unajua inaweka kwenye kihenge inatunzwa vizuri isibunguliwe, lakini leo kwenye level ya familia ukiangalia mtoto wa kike ameweka karibu kabisa na chumba cha baba na mama ili hata akitoka usiku washtuke wamlinde, mtoto wa kiume amewekewa chumba banda la uani huko, arudi hakurudi hakuna anayejua. Leo hii kwenye familia tunasema kwamba hawa ndio vichwa vya familia, lakini ukiangalia namna tunavyowalea sio kuja kuwa vichwa, ndio maana kunatokea mgongano sasa hivi, huwezi kutegemea kumlea mfalme halafu ukamlea kilezilezi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, leo hii tuangalie wengi hapa tunaweza tukawa tunaangalia kwenye Azam pale sinema ya Ertugul angalia Ertugul jinsi alivyo m-raise Ottoman, alivyompeleka vitani, alivyomsimulia kwamba wewe ni mfalme, alivyomfundisha na kumpa mbinu, alivyomlisha, alivyompeleka shule na kumpa maarifa ya kwamba yeye ni mfalme, lakini sivyo tunavyowalea watoto wetu wa kiume. Leo hii tunaanza kuwapa sifa za ufalme kabla hajafika kwenye kuwa mfalme, mtoto wa kiume anapendelewa, anapewa vitu hata akiumia tu wakati mwingine anahitaji faraja alie, amwambie mama mimi nimefanyiwa kitu kibaya leo watoto wetu wanalawitiwa kwenye majumba kwa sababu ameshaambiwa mtoto wa kiume halii lii, mtoto wa kiume hasemi semi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo anasindwa hata kujieleza tatizo lake, leo hii ukienda mitaani waliojaa ni watoto wa kiume, sio wa kike, wameachwa, leo hii tukienda kwenye elimu tukianza kuweka kipaumbele hapa tunaweka kipaumbele cha kujenga hostels tunajenga za wanawake sio za watoto wa kiume. Sisi tunaangalia equality hatuangalii equity, sasa huyu unayetegemea aje kuwa kichwa leo hii twende kwenye style tunavyowaozesha watoto wetu, watoto wa kike wanaitwa wanapewa kitchen party wanapewa mafunzo…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha muda wa MzungumzajI

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ninachotaka kusema lazima sasa tubadilishe style ya kuangaia watoto wetu wa kiume na kuwapa haki sawa kwenye elimu, kwenye matibabu kwenye mafunzo kwenye kila kitu ili tuanze kuwa na kichwa kilichoenda shule, kama tunajua ile ndio mbegu yetu lazima tuitunze kwa ubora wote bila kuangalia kwamba …

SPIKA: Haya ahsante sana.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: … hawa ni watu wa aina gani, ahsante naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza tumekuwa tukileta ombi letu mara nyingi la kuomba kujengewa kizimba kwa ajili ya wafugaji wadogo wadogo wanaofuga samaki kando ya Mto Ruaha na katika mabwawa yao ili waweze kujifunza. Tunasikitika ombi letu halijafanyiwa kazi licha ya kuahidiwa kufanyiwa kazi na Mheshimiwa Waziri mwenyewe akiwa Naibu Waziri na sasa ni Waziri kamili. Sasa basi kwa heshima na taadhima tunaomba ombi letu lifanyiwe kazi, tujengewe kizimba ndani ya Manispaa ya Iringa.

Pili, wananchi wa Iringa mmoja mmoja na kwa vikundi wamekuwa wakijishughulisha sana na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na wanyama, hivyo tunaomba katika mpango wa kukopesha au kusaidia ng'ombe nasi pia tukumbukwe. Tunaomba pia kufanyiwa mafunzo ya kunenepesha ng'ombe.

Tatu, Mradi wa Machinjio ya Kisasa Ngelewala ulianza kwa awamu ya kwanza mwaka 2008/2009 hadi 2015/2016; mwaka 2019/2022 ulitekelezwa kama mradi wa kimkakati. Hadi sasa mradi haujakamilika kwa kiwango cha kutoa huduma za uchinjaji wa nyama kwa mfumo wa kisasa ikiwa ni pamoja na kuchakata nyama (processing) ikiwa ni kiwanda cha nyama. Tunaiomba Serikali ifanyie kazi ombi letu maalumu la kuomba fedha kiasi cha shilingi 1,902,077,650 yenye Kumb. Na.BC 134/164/01/13 ya tarehe 21 Juni, 2023 kwa ajili ya kukamilisha miundombinu na kununua vifaa kwa ajili ya machinjio hii ya Ngelewala katika Manispaa ya Iringa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Chombo hiki cha Polisi ndiyo kimepewa dhamana ya usalama na ulinzi wa mali na raia wa Tanzania. Wana dhamana hiyo ili wazalishe amani na utulivu na wakishazalisha amani na utulivu wananchi waweze kufanya kazi zao kwa amani, weledi na uhuru na tuweze kuliletea Taifa letu maendeleo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ili waweze kuzalisha hiyo amani na utulivu, ni lazima na wenyewe wawe na amani na utulivu. Kwa sababu kama ilivyo kawaida, hutegemei kwamba utapata nyanya chungu kwenye mwembe. Mwembe unatoa embe na nyanya chungu zinatoa nyanya chungu. Sasa ili sisi tupate amani na utulivu, raia na mali zetu tuwe salama, ni lazima polisi na wao wawe na amani na utulivu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa tumesomewa bajeti ya Wizara nzima kwa ujumla kwamba wamepelekewa 55% na hii 55% wamepelekewa robo ya tatu, maana yake ni Januari pale Februari. Ina maana hawa polisi kuanzia mwezi Julai mpaka Januari waliishi vipi? Wamefanya kazi zao vipi? Magari yao yametembea kwa vipi? Wamelipa bill kitu gani, maji na umeme? Wale tuliowapeleka kule cell wamekula kitu gani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni wazi kwamba kama tunataka kufanya kazi zetu kwa amani na utulivu na tunategemea tupate zao kutoka kwa polisi hatuna ujanja ni lazima tuwekeze kwao kama ambavyo ukitaka kupata maziwa mengi kwenye ng’ombe lazima umlishe. Tunataka amani na utulivu wa Taifa letu uwe kwa asilimia kubwa na 100%, lazima tuwekeze, bajeti yao iende kwa 100% na iende kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, leo tunalalamika hapa namna ambavyo polisi wanafanya kazi. Tunalalamika namna ambavyo watoto wetu wako kwenye risk, watoto wa shule sasa hivi wako kwenye risk. Watoto mitaani wanapita wamelewa, yaani polisi wangekuwa tu wana kazi nyingine ya kuchunguza hata vile viashiria vya uovu kwenye nchi, viashiria vya hatari kwa raia, maana wao ndiyo wanatuangalia usalama wetu na viashiria vya hatari kwa watoto wetu; hana hata mafuta. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Polisi Kata yupo lakini hawezi, kata zetu tunajua, kuna kata nyingine unakwenda kilomita 80 kata moja. Polisi Kata anakwendaje? Polisi wanapataje muda wa kuzunguka zunguka hata kwenye shule na taasisi kuona usalama uliopo kwenye shule hiyo kama nusu mwaka nzima hawajapelekewa hata shilingi kwa ajili ya kuendesha shughuli zao? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, polisi wanakuwa frustrated, hawana amani na utulivu. Leo hawa tuna think tank ambao ni polisi, hawa wengi karibu wanastaafu. Ni vile tu wanaishi kwenye chain ya command, kwamba mambo yao ni amri lakini wengi wao unaweza kuwaona serious ukajua ndiyo tabia ya polisi kuwa serious lakini kumbe hawana utulivu. Kikokotoo peke yake kimewachanganya kwanini haya mambo ya sera hizi mnakwenda ku-impact kwa polisi, yaani hawa mkishawachanganya na sisi wote tunachanganyikiwa, utulivu wetu unakuwa hatarini. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaomba kwanza polisi wawe regarded kama majeshi mengine kwa sababu salute wanapiga kama majeshi mengine. Polisi wasichukuliwe kama watumishi wa kawaida. Ile biashara ya kikokotoo wawe regarded kama majeshi mengine. Tunashukuru kwamba hicho kikokotoo wamesema kwamba watakishughulikia lakini hawa polisi tunataka jeshi la kisasa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumeshaambiwa sasa hivi majambazi hawaibi tena kwa mitutu wanatumia akili, ndiyo hicho alichokuwa anasema Mheshimiwa Swalle. Wanatumia akili zaidi ndiyo maana wanaiba kidijitali, wanaiba kwenye mitandao siyo tena wanakujia na mapanga na nondo. Hao wa mapanga na nondo ni vibaka wale ambao bado hawaja-graduate kwenye ule uhalifu wa hali ya juu. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa polisi wetu nao wanatakiwa wawe na IQ kubwa zaidi. Leo hii katika Jeshi la Polisi, mimi nina polisi wangu Iringa pale. Iringa sisi tuna bahati nzuri ya kuwa na vyuo vikuu vingi, wamesoma, wana vyeti, wana degree, wana masters, wakipeleka kwa mabosi wao hawavitambui vile vyeti, wanavikataa kwa sababu tu hawakupata kibali kwa bosi kwamba akasome. Tunataka polisi ya aina gani? Kijana kajitolea mwenyewe polisi kasoma wewe hutaki ku-accept, kutambua mchango wake kwamba huyu sasa ana masters, huyu ana degree, kwa sababu wewe huna, hapana. Tunataka jeshi lenye weledi na Kamati imeelekeza hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, lazima polisi waangaliwe wawe na amani. Kwa makazi yale wanayokaa, nyumba zile wanazolala. Mimi polisi wangu pale wana hati hati ya kugongwa na cobra kwa sababu kwanza wako porini lakini nyumba zenyewe zimejengwa tangu ukoloni. Polisi hata kwa kulala, wengine wana-enjoy futi sita kwa ngapi. Nyumba za polisi, leo tuondoke twende Kituo Kikuu cha Polisi cha Dodoma tuangalie nyumba za polisi, ndiyo mfano capital city, tukaangalie makazi ya askari, tuangalie jinsi yalivyo. Pale watapata usingizi wenye amani ipi ili watuzalishie sisi amani? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, wanapata utulivu upi? Nilikuwa naongea na akinamama wangu pale wa Line Police, tunaongea mambo yetu ya VICOBA na vitu vingine. Wakasema tunapata changamoto kubwa sana, sisi waume zetu hata kurudi kulala huku wanaona tabu. Wengine wanajiingiza tu kwenye shift za usiku siyo kwa sababu wamo, ila kwa sababu pa kulala panachekesha. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hatuwezi kuwa na chombo ambacho tunategemea kilinde amani ya nchi yetu, Waziri wetu, Mheshimiwa mwenye dhamana ya fedha umewanyima robo mbili hawana hela. Nawapongeza Watanzania, endeleeni kuwawezesha polisi kwa sababu kama mambo yenyewe ndiyo haya, tupeane tu hela mitaani humo. (Makofi)

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Msambatavangu, muda wako umeisha.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, kwanza, naomba kuchukua nafasi hii kwa heshima na taadhima kumshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia na kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri Bashungwa kwa kazi kubwa wanayofanya katika kujenga na kuimarisha miundombinu hasa ya barabara katika mkoa wetu wa Iringa na nchi nzima kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, ninawashukuru kwa kuendelea kuufungua Mji wa Iringa ambao ulikuwa haupitiki kutokana na kupitiwa na barabara kubwa mbili, yaani Mbeya-Dar es Salaam na Mbeya-Dodoma. Hii ilisababisha msongamano mkubwa Mjini Iringa, lakini ujenzi wa Iringa Bypass na ujenzi wa Daraja la Kitwiru - Isakalilo na Ipogolo - Kilolo. Hizi tunaomba zikamilike kwa kweli zitatoa changamoto kubwa sana ndani ya Mji wa Iringa. Ahsanteni sana!

Pili, ninaomba barabara ya Iringa - Pawaga ijengwe pia kama ambavyo tuliomba wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, lakini pia imo kwenye Ilani kwa zaidi ya miaka 30. Aidha, tunashukuru kwa kilometa ambazo tumepewa kwa barabara hiyo. Barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi na usafari kwa majimbo yote matatu au Manispaa na Halmashauri ya Iringa Vijijini. Tunaomba hata kilometa tano kuanzia mjini, kwa sababu wananchi wa Kata ya Kiwele na Mkwawa wanapata shida sana hasa wanapofuata huduma za matibabu, shule mjini.

Mheshimiwa Spika, tatu, tunaomba eneo la upande wa mto wa barabara ya Mbeya -Dar es Salaam, eneo la Iyofi zisifanyike shughuli za ujenzi au kilimo hatarishi, maeneo hayo yatunzwe ili kulinda hizo barabara, kwa mazingira yake hiyo barabara itamegeka.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba kutoa mchango wangu kama ifuatavyo, nalipongeza sana Jeshi letu imara kwa namna linavyofanya kazi zake kwa weledi. Pamoja na mambo hayo mazuri binafsi naona wanayo fursa ya kuongeza kufanya vizuri zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, usalama wa wananchi ni matokeo ya usalama binafsi kwa wanajeshi wenyewe, asipo kuwa salama itapunguza motisha ya kuangalia usalama wa watu wengine. Tunaomba usalama wa wanajeshi wetu hasa huko Congo uimarishwe, inatuuma sisi tunajitolea kuwalinda majirani zetu, halafu wenzetu hawa sijui kama wanajali usalama wa vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili ni kuhusu huduma za afya ya akili Jeshini ni muhimu zikaimarishwa, pamoja na kwamba hawa ni wanajeshi, bado ni binadamu, hali ya kwamba hawaruhusiwi kugoma wala kuandamana ni sawa kijeshi, lakini kibinadamu ndiyo wanahitaji zaidi huduma za afya ya akili kwa ujumla kuliko watu wengine waliopewa fursa ya kuongea au kuandamana au kubisha. Hivyo, Kituo cha Afya ya Akili kama ilivyobadilishwa Mirembe sasa ni muhimu sana. Wanajeshi wanahitaji kupata huduma hizo za kisasa zaidi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tatu, Jeshi letu katika maono yake ni kuwa Jeshi lenye weledi mkubwa. Hivyo basi, elimu ni muhimu sana kwa wanajeshi wetu. Kuhakikisha wanapata elimu bora, lakini na wale wenye elimu watumike vizuri sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nne, tunaomba Jeshi letu litumike sana hata kutoa mafunzo kwa baadhi ya taasisi zetu au baadhi ya viongozi wetu ili kuongeza uzalendo kwa watu muhimu hasa viongozi wetu wasimamizi wa taasisi kama Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi, Waheshimiwa Wabunge na kadhalika. Hii itasaidia sana kuimarisha uhodari, uzalendo na kuondoa uvivu.

Mheshimiwa Naibu Spika, tano, tunashukuru kwa Jeshi kuchukua hatua kwa vijana wote wanaomaliza form six, hiyo ifanyike na kwa wale ambao wanaenda vyuo vya kati bila kusahau Jeshi la Mgambo litoe mafunzo kwa vijana wote walioko mitaani ambao hawajapitia jeshi.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ninaomba mchango wangu huu kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi uchukuliwe kwa uzito. Kwanza tunawapongeza kwa kazi kubwa inayofanywa na Wizara ya Ardhi nchini, bila kumsahau Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Spika, naomba mchango wangu upokelewe kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza kuongeza kasi ya upimaji na kuongeza mapato kutoka katika ardhi ni muhimu sana. Sasa tuongeze wigo wa walipakodi na kupunguza viwango kwa square metre kwa walipakodi ya ardhi, yaani land rent ili kodi iweze kulipika kirahisi na watu wengi na kwa wingi kuliko kuwa na madai makubwa yasiyolipika.

Mheshimiwa Spika, pili, viwango vya kodi kwa taasisi kama shule, itumike flat rate kutokana na maeneo ya majiji, manispaa au vijiji; kwa kuwa vipo viwango vya ardhi inayohitajika kwa ajili ya ujenzi wa shule. Kumekuwa na shida ya ulipaji wa hizi kodi za ardhi kwa taasisi kama shule kutokana na ukubwa wake unaohitajika, na umuhimu wake kwa wananchi. Huwezi kutumia market price ilhali hii ni service, lakini pia ina maeneo ambayo viwanja vya michezo havitoshi na hivyo, inakuwa ni vigumu kwa wawekezaji hawa wa shule na taasisi nyingine za mtindo huo.

Mheshimiwa Spika, tatu, kuhusu viwango vya ulipaji wa kodi ya ardhi kwenye vijiji vinavyopandishwa hadhi kama miji wakati bado ni vijiji, tunaomba liangaliwe upya na sehemu hizo zichukuliwe kama vijiji kwa uhalisia wake. Kwa kuwa tuna vijiji ambavyo vipo mijini, hata sekta nyingine kama nishati, wameliweka na kutengeneza peri-urban plan.

Mheshimiwa Spika nne, viwango vya kodi za nyumba za NHC za Iringa Mjini vimekuwa ni mgogoro mkubwa. Tunaomba kodi iendane na kiwango cha bei ya soko kwa kuzingatia ubora wa nyumba hizo. Pia tunaomba ukarabati ufanyike kwenye majengo mengi yaliyochakaa ndani ya Manispaa ya Iringa. Tano, tunawaomba NHC waje wawekeze katika mji wetu katika maeneo ya utalii, kwenye makazi ya watu na hoteli.
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, contribution to Tanzania National Development Plan 2025/2026; The Importance of Mental Health in National Development.
Mheshimiwa Mwenyekiti, as Tanzania works towards its National Development Plan for 2025/2026, it is crucial to consider mental health as an integral component of national development. Mental health is not only a personal matter but a societal issue that affects social, economic, and physical well-being. According to the World Health Organization (WHO), mental health is defined as a state of well-being where an individual realizes their own abilities, can cope with the normal stresses of life, work productively, and contribute to their community. Therefore, mental health is essential to fostering a productive, healthy and stable society, all of which are central to Tanzania’s development goals.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mental health and its impact on development; mental health affects all aspects of society. Individuals with mental health challenges often experience poor economic outcomes, lower educational achievements, reduced productivity and increased rates of disability. Mental health issues can also lead to strained healthcare systems and significant social costs. This is particularly concerning in a developing country like Tanzania, where the population faces numerous socio-economic challenges, including poverty, unemployment, and limited access to quality healthcare services.

Furthermore, untreated mental health conditions can exacerbate social inequalities and hinder the realization of Tanzania’s sustainable development goals (SDGs), particularly in health (SDG 3), quality education (SDG 4), and decent work (SDG 8). To achieve a prosperous and equitable society, addressing mental health must become a priority.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Performance Audit of Mental Health Services in Tanzania (2024 Report); in March 2024, the Controller and Auditor General (CAG) of Tanzania conducted a Performance Audit Report on the availability of mental health care services in the country. The audit revealed significant gaps in mental health care services, including limited access to mental health professionals, inadequate infrastructure, and a lack of public awareness about mental health issues. Key findings include:-
(i) Inadequate Mental Health Professionals: There is a severe shortage of trained mental health workers, including psychiatrists, psychologists, and social workers, with many regions in Tanzania lacking such professionals entirely.

(ii) Limited Mental Health Infrastructure: Public health facilities often lack the necessary resources and infrastructure to provide adequate mental health care, such as specialized psychiatric wards or necessary medical equipment.

(iii) Stigma and Public Awareness: Mental health is often stigmatized in Tanzanian society, which leads to underreporting and untreated cases. There is a critical need for public awareness campaigns to reduce stigma and promote early intervention.

(iv) Funding and Budgetary Allocation: Mental health services are underfunded and the current national budget allocation for mental health is insufficient to address the growing demand for services.

Mheshimiwa Mwenyekiti, recommendations from the 2024 Performance Audit Report; the CAG's report outlined several key recommendations to improve mental health services in Tanzania:-

(i) Increased Investment in Mental Health Care: The government should allocate more funds to mental health services, including the expansion of psychiatric care infrastructure, hiring more mental health professionals and providing necessary training.

(ii) Public Awareness Campaigns: Launch national campaigns to raise awareness about mental health, reduce stigma and encourage early treatment.

(iii) Integration of Mental Health into Primary Health Care: Mental health services should be integrated into primary health care systems to make them more accessible in rural and underserved areas.

(iv) Strengthening Mental Health Policies: Review and update existing mental health policies to ensure they align with international best practices and address the evolving mental health needs of Tanzanians.

Mheshimiwa Mwenyekiti, recommendations for Inclusion in the National Development Plan and Budget 2025/2026; to ensure mental health is adequately addressed in Tanzania’s National Development Plan and Budget for 2025/2026, the following actions are recommended:-

(i) Allocate Adequate Budget for Mental Health: The government should allocate a specific percentage of the national health budget to mental health services. This would ensure that resources are dedicated to improving mental health infrastructure, hiring professionals and creating awareness campaigns.

(ii) Policy Implementation and Monitoring: Include mental health in national policies and establish a monitoring framework to track progress on the availability of mental health services. This should be linked to Tanzania’s overall development goals, ensuring that mental health is not sidelined.

(iii) Integration into Education and Workplace Programs: Mental health services should be integrated into schools, universities and workplaces to promote early detection and prevention. The national plan should also consider providing mental health education as part of the curriculum at various levels.

(iv) Public-Private Partnerships: Encourage collaboration between the public and private sectors to build and sustain mental health infrastructure. Private sector investment can help meet the growing demand for mental health services, especially in urban areas.
(v) Public Awareness Campaigns: Launch national campaigns to raise awareness about mental health, reduce stigma, and encourage early treatment. Let us make this a stepping Stone.

Mheshimiwa Mwenyekiti, conclusion; addressing mental health is vital for Tanzania's social and economic development. By incorporating the recommendations from the 2024 Performance Audit Report into the National Development Plan for 2025/2026, Tanzania can improve the mental health of its population, reduce the social stigma associated with mental illness and create a more productive, healthy and prosperous society. Mental health is not merely a healthcare issue but a development issue and its prioritization in national planning will be essential for the success of Tanzania's growth and prosperity in the coming decades.
Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa Mwaka 2022
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi lakini nichukue nafasi hii pia na mimi kuipongeza Serikali kwa juhudi kubwa ambayo inafanya kuimarisha huduma za afya katika Taifa letu. Pia, kuangalia mipango mbalimbali ambayo inaweza ikawakwamua watu wetu kutokana na matatizo ya afya ikiwepo mpango huu wa Bima ya Afya chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, lakini bila kuwaacha Waziri wetu wa Afya na Naibu Waziri pamoja na Viongozi wetu Wizara ya Afya.

Mheshimiwa Spika, nashukuru tumesoma tumeambiwa na Waziri tumepitia Muswada huu. Nitaongelea sehemu mbili tu, sehemu ya kwanza inahusu ufafanuzi nitaomba Mheshimiwa Waziri utakaposimama ujaribu kutushibisha, kwa sababu sisi pia tunataka tukawashibishe wananchi.

Mheshimiwa Spika, kwanza ni Ibara ya 21, Mheshimiwa Waziri pale panakupa nafasi wewe na Waziri mwenye dhamana ya Fedha kukaa na kuangalia viwango. Hilo ndilo suala kubwa ambalo tungetamani kuona namna gani mtafanya consideration, kwa sababu ibara inasema mtaangalia uhai wa mfuko na uendelevu wake. Natamani mngeangalia pia na vipato vya Watanzania kwa jinsi walivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Ibara ya 32, nitaomba ufafanuzi sitaielezea. Kutokana na namna ambavyo Ibara ya 22, inasema lakini niwapongeze kwa sababu mmeshatoa yale masharti ambayo yalikuwa yanakwenda kutubana kidogo. Hasa ukuiona kwamba kwenye kutoa leseni, kupata NIDA lazima ifungamane na hii kidogo ingetupa changamoto.

Mheshimiwa Spika, nakwenda kuongelea sasa ibara nyingine. Ibara ya 22, watu wasiyojiweza namna ya kubaini watu wasiojiweza. Hapa lazima tuwaeleze Watanzania, Watanzania watambue kwamba bima siyo msaada. Bima ni kitu ambacho mwenyewe unawekeza, bima ni kama kibubu ni kibubu cha kuchangia afya yako, bima ni kama mchango wa msiba, ukichanga kwa wenzako na wenzako wakichanga siku moja ukifiwa na wewe utanufaika. Mfuko huu ili uwe endelevu, lazima tuwaeleze, maana tunaposema hapa ni Bima kwa wote, watu wanafikiri sasa wote watakwenda kutibiwa bure bila ya kuwa na backup nyuma yake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, backup yake ni kwamba kadiri wengi tutakavyochanga kwenye hicho kibubu cha Bima ya Afya, ndivyo tutakavyoweza kutibiwa wengi. Faida utakayopata ni kwamba unachanga kwenye msimba wa mwezako lakini wewe hufiwi leo unaweza ukafiwa miaka mitatu ijayo. Kwa hiyo, ukatumia fedha za mwenzako na wewe ukija kuwa hai, mwenzako atakapoumwa wewe pia fedha zako zitatumika kumtibu.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwaombe Watanzania tuchukue kwamba hii ni njia itakayotusaidia siku usiyotarajia, utakayoumwa wewe kama ulichanga na wewe utanufaika kutibiwa kwa fedha uliyochanga. Inawezekana ulichanga fedha kidogo ukatumia gharama kubwa kwa ugonjwa wako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa nini nasema hivi, lazima tujue kwamba ni wajibu wa kuziangali afya zetu ni wajibu wetu sisi. Sisi tuna mtu mmoja Paulo kwenye kile Kitabu cha Biblia aliwaambia Wafilipi, Wafilipi sikilizeni, kufa kwa Mungu ni faida na kuishi ni Kristo. Kuishi wako unamtegemea Mungu na ukifa pia ni faida, kwa sababu Mungu amekupa wajibu wa kuiangalia afya yako wewe mwenyewe. Usipoiangalia anaweza akakuonea huruma kwamba mwanangu anapata tabu ngoja afe, aje akae na mimi huku Mbinguni. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ili afya hiyo uweze kuingalia lazima ulichangie. Hii ni sawa na Mkulima anavyolima mahindi yake, analima wakati akiwa na nguvu siyo wakati wa njaa anahifadhi mahindi wakati wa chakula kingi siyo wakati wa njaa. Tunatakiwa tukate Bima tukiwa wazima siyo wakati tunaumwa ili iweze kutusaidia ndio mwelekeo jinsi ulivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tukate Bima hii tukiwa wazima kwa ajili ya siku tutakayoumwa. Mheshimiwa Waziri amesema hapa na sisi wenyewe Waheshimiwa Wabunge tunafahamu. Watu wengi wanapokuwa na changamoto ya kuumwa, ndio anaulizia ukimuuliza huna Bima anakwambia sina labda nikakate. Sasa ndio maana mfuko wetu una-suffocate unakufa imeshindikana. Kwa hiyo, Watanzania tutambue kwamba tunatakiwa kuchangia kwenye mfuko huu ili utusaide siku tutakapokuwa na shida. Tusitegemee kwamba Serikali itachangia, jamani kwanza vyanzo vyenyewe tumesema kwenye betting, vyanzo vyenyewe tunasema kwenye pombe kali na sisi tulio Wahubiri tunaongeza mahubiri watu waache kulewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mfuko unaweza ukakosa michango, kwa sababu hatuna mpango wa kuruhusu watu waendelee kulewa kwenye nchi hii, ili wewe utibiwe kwa sababu huyo anayelewa naye ni mgonjwa mtarajiwa hatupo tayari. Kwa hiyo, tunachomba Watanzania usisubiri uumwe ili uwe na Bima ya Afya kata Bima yako mapema hiki ndio kibubu kwa ajili ya afya yako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna Mheshimiwa mmoja amesema tuache tabia ya watu wakifa ndio tunawachangia, hapana. Ukifa ni jukumu letu kwa sababu wewe huna uwezo huwezi kujisema tutakusemea. Wewe mzima kwa nini tukuchangie jichangie mwenyewe Bima yako ila siku ukifa lazima tukuzike, kwa sababu hata tukikuacha sisi ndio tutakao pata matatizo, lazima tukuzike. Tutakuzika kwa namna yoyote ila kwa wakati huu unapohitaji matibabu weka utaratibu wako, watoto wako na wale wanaokutegemea kuhakikisha kwamba umejikatia Bima yako na unakaa kukiwa free.

Mheshimiwa Spika, hata kwenye Bima nyingine ndivyo ilivyo hata ya magari, unakata Bima ya gari ili gari inapopata ajali usiapate stress, kupata kuchanganyikiwa, kupata matatizo ya afya ya akili, kwamba utapata wapi gari nyingine? Kwa sababu tayari ulisha ilipia Bima. Kwa hiyo, unapoumwa hauhitaji kupata stress yoyote, kwa kuwa huitaji kupata stress yoyote kuwa na Bima ya Afya. Ukiwa na Bima yako unajua kabisa nina uhakika ninaweza nikatibiwa popote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Waziri atakapokwenda kukaa na Waziri mwenye dhamana ya Fedha cha msingi ni kwenda kuangalia Watanzania wetu kwa uwezo wao. Vile vitita mtakavyo viweka tofauti tofauti, kila mtu apate fursa ya kuchangia. Tena mimi niliipenda vile mlivyoi-cam average kwamba huwezi kupata hiki bila kuwa na Bima hii, kwa sababu sasa hivi kuumwa tunaumwa. Kuna magonjwa tunaanzisha wenyewe na mengine tuna ya-import kutoka nje kama corona. Wakati usiyodhani unaumwa na unaumwa vibaya.

Mheshimiwa Spika, suala la Bima ya Afya kwa sasa hivi haliepukiki ni la msingi. Kila Mtanzania ajue kama anavyoweka akiba ya mchele nyumbani kwake, unaweka akiba ya sukari, unaweka akiba ya fedha za ada, ujue una wajibu wa kuweka akiba kwa ajili ya afya yako. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa Serikali imekurahisishia kwamba itakutunzia hiyo akiba na utakwenda kutibiwa kwenye hospitali zetu ambazo watu wote ni mashuhuda tunaona namna Serikali inavyofanya kazi kubwa kuimarisha huduma za afya kwenye nchi hii. Ndugu zangu ninaomba Vitabu vya Mwenyezi Mungu vinasema masikini hawata koma kwenye nchi. Ni kweli lakini watu wengine na wenyewe wameshakaa hapa tayari tumeshajipanga.

Mheshimiwa Spika, walivyosikia Bima ya Afya bure, tayari ameshaanza kujipanga kuwa kwenye kundi la wasiyo na uwezo. Usijipange kuwa kwenye kundi la wasio na uwezo, kwa sababu hata Biblia inavyosema masikini hawatakoma kwenye nchi, anamwambia. Kwa hiyo, wewe mwenye kutoa endelea kutoa kusaidia masikini, kwa sababu mimi Mungu wako nitakubariki. Wewe unayeendela kujipanga kuwa kwenye kundi la masikini hutabarikiwa. Hebu sema mimi nataka kutoka huko na mimi nibarikiwe na Mwenyezi Mungu, fikiria wewe kutoa. (Makofi)

SPIKA: Haya. Mheshimiwa Msambatavangu, muda wako umekwisha. Ahsante.

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nashukuru Sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)