Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Hamad Hassan Chande (151 total)

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushuru Mheshimwa Spika, kwa kunipa nafasi ya kuuliza. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa chande kwa kuteuliwa kupata nafasi hiyo, tunakuombea kwa Mungu akusaidie ili uweze kuona mbele zaidi, kwake nina swali moja tu. Kwa kuwa humu ndani ameandika sheria nyingi za mazingira, sasa swali ni lini atafika kwenye Jimbo la Bunda kwenye Vijiji vya Nyabuzume, Jabulundu na maeneo yaliyoharibiwa na barabara inayojengwa ya lami kutoka Butiama -Nyamswa na Sanzati ili kuangalia athari za mazingira katika maeneo hayo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, siku za karibuni mara tu baada ya Bunge kumalizika tutafuatana mguu kwa mguu mimi na yeye twende kuangalia hali hiyo na insha Allah tutekeleza. (Makofi)
MHE. SIMAI HASSAN SADIKI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanaendelea kuathiri vyanzo na miundombinu ya maji kule kijijini Nungwi jambo ambalo limepelekea kuwa na kero kubwa kwa Watanzania wanaoishi maeneo yale. Napenda kusikia kauli ya Serikali ni lini mradi huo unaozungumziwa hapa unatarajiwa kuanza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, Mheshimiwa Waziri ni lini atakuwa tayari kuongozana na mimi kwenda kuangalia moja kwa moja uhalisia wa athari ya mabadiliko ya tabia nchi?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Simai Hassan Sadiki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naomba kwa idhini yako nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Simai kwa juhudi yake ya kufuatilia miradi mbalimbali katika Jimbo lake ikiwepo miradi ya maji kwa kweli ni mwanaharakati mkubwa kufatilia maendeleo ya maslahi ya jimbo lake na wananchi kwa ujumla.

Mheshimiwa Naibu Spika, mara tu baada ya utaratibu wa kifedha utakapokamilika mradi huu utaenda kutekelezwa. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tupo katika harakati za kufatilia taratibu hizi za kifedha zikamilike ili kusudi kwenda kutekeleza mradi huo katika eneo lake.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili mara tu baada ya kumaliza kikao hiki mwishoni mwa mwezi huu tutafuatana mimi na yeye twende tukaone athari hiyo ambayo inajitokeza ndani ya jimbo lake, ahsante.
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri bado nina maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tumeona jitihada mbalimbali za wananchi wakizichukua kwa makusudi katika kupanda mikoko kwa lengo na madhumuni ya kuhifadhi mazingira, kuongeza mazalia ya samaki lakini kuzuia maji ya bahari kupanda nchi kavu. Mfano mzuri ni wananchi wa Kijiji cha Mjini Wingwi na Sizini Wilaya ya Micheweni. Swali la kwanza, je, Serikali inawapa matumaini gani wananchi hawa wa Mjini Wingwi na Sizini kwa kuwapatia misaada ya kifedha na vifaa kama boti kwa ajili ya patrol kama sehemu ya kuhamasisha na kuwapa moyo kuendelea na jitihada hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kufuatana nami baada ya Bunge hili mpaka kwenye Kijiji cha Mjini Wingwi na Sizini kwa lengo la kwenda kuona jitihada za wananchi hawa?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Omar Issa Kombo, Mbunge wa Wingwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu maswali haya, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Mbunge Omar Issa kwa juhudi yake ya kutunza mazingira katika maeneo yake.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza anauliza Serikali itawapa matumaini gani wananchi? Serikali kwa sababu inasikiliza na inathamini juhudi za wananchi, naomba hili tulichukue na baadaye tutakaa pamoja naye na wataalamu wetu tuone namna gani tunawapatia motisha wananchi ambao wanajitahidi kutunza mazingira.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la pili mimi niko tayari kabisa kufuatana naye baada ya Bunge hili kwenda kuona na kutafuta njia sahihi ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira.
MHE. RASHID ABDALLA RASHID: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nimshukuru Naibu Waziri kwa majibu mazuri ya Serikali na pia niishukuru Serikali kwa kupeleka fedha katika maeneo hayo ya ujenzi wat uta hilo. Na nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa, miradi hii inagharimu fedha nyingi katika utekelezaji wake, lakini katika utekelezaji huo Serikali haikutumia mafundi wazuri na hatukupata matokeo mazuri katika ujenzi wa tuta hilo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia mafundi bobezi ili wananchi waweze kunufaika na ujenzi huo wa tuta?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, Naibu Waziri atakuwa yuko tayari kufuatana nami ili kwa macho yake aende kushuhudia ujenzi wat uta uliofanyika katika phase II ya TASAF Awamu ya Pili?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali haifanyi shughuli zake kwa kubahatisha upo utaratibu maalum ambao umeandaliwa wa kutumia wataalamu bobezi. Wataalam ambao wana uwezo mkubwa wa kujenga miradi hiyo, ili ufanisi uweze kupatikana.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili, niko tayari kwa sababu ya juhudi zake ambazo nimeziona katika jimbo lake kufuatananaye bega kwa bega, hatua kwa hatua mpaka katika jimbo hilo kuona sehemu husika.
MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniruhusu kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo linalowaathiri wananchi wa Nanguji na Kiwani linafanana kabisa na tatizo linalowaathiri wakazi wa Kijiji cha Kojani. Na kwa kuwa, wananchi wa Kijiji cha Kojani wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusiana na suala la maji ya bahari kuwaathiri katika makazi yao ya kudumu. Je, Serikali ina mpango gani au inaweza kuweka mkakati gani ili kuweka ukuta, pamoja na alama, lakini ili kunusuru makazi ya wananchi wa Kijiji cha Kojani? Ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Kojani ni ndani ya jimbo lang na Kojani ni sehemu yangu nitashawishi Serikali na kuandika miradi tofauti kwa ajili ya kuhami kisiwa hicho cha Kojani. (Makofi)
MHE. MWANAKHAMIS KASSIM SAID: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuwa wazee hawa walifanya kazi kwenye Serikali hii, walitumia vigezo gani kuwa walipwe kiinua mgongo na wasilipwe pensheni yao ya kila mwezi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili: Je, Waziri yuko tayari kwa ruhusa yako kuungana nami kwenda kuwaona wazee hawa kuwapa maneno mazima? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA (MHE. HAMAD HASSAN CHANDE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mwanakhamis Kassim Said wa Jimbo la Magomeni kwa juhudi yake ya kufuatilia wazee kupata stahiki zao.

Mheshimiwa Naibu Spika, vigezo ambavyo tumetumia ni Kanuni, Taratibu na Sheria ambazo zimewekwa na kama hatukutumia vigezo hivyo, basi ingekuwa ni kinyume na taratibu. Hivyo basi, Serikali bado iko na usikivu. Serikali yetu ni sikivu, Mheshimiwa Mbunge anao uwezo wa kupeleka malalamiko tena na tutayazingia kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Naibu Spika, Swali la pili, niko tayari kabisa mimi na Waziri wangu kufuatana naye kwenda kushuhudia jambo hilo, Inshaallah. (Makofi)
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niipongeze Serikali kwa juhudi wanazozifanya katika kutafuta majawabu ya eneo hili. Lakini vilevile nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu ya matumaini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mto Msimbazi sasa hivi umepoteza kina kutokana na kujaa michanga mingi sana kiasi kwamba tupo katika kipindi cha mvua, kipindi ambacho maji hutapakaa na wananchi wa maeneo ya Kigogo Jaba, Kigogo Kati, Kata ya Mzimuni, Daraja la Magomeni na hata Kata ya Magomeni yenyewe, pale wanapata athari kubwa sana ya mafuriko.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba commitment ya Serikali kwamba wasaidie juhudi za wananchi katika maeneo hayo, juhudi ambazo zinaongozwa na Madiwani wangu Mheshimiwa Richard Mgana, Mheshimiwa Loto na Mheshimiwa Nurdin katika kuondoa mchanga katika maeneo yale ili mvua hizi zisilete athari tena.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, changamoto hii pia…

NAIBU SPIKA: Hilo swali la pili nenda moja kwa moja kwenye swali.

MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ningemuomba Mheshimiwa Waziri aambatane nami kutembelea Kata za Tandale, Magomeni, Ndugumbi, Makumbusho, Kijitonyama, Mwananyamala na Hananasif ili kwenda kuona athari za mto Ng’ombe kutokana na mafuriko vilevile ili aweze kusaidia juhudi za Serikali ambazo zimeshaanza kuujenga mto huo. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuchukua nafasi hii kwanza kumpongeza Mheshimiwa Abbas Tarimba Gulam kwa juhudi yake ambayo anaifanya katika jimbo lake la Kinondoni. Lakini pili kuwa ni Mwenyekiti wa Bunge Sports Club kwa awamu ya pili nadhani. (Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tarimba. Swali la kwanza, kwa kuwa juhudi imeshafanyika kwa wananchi wa Jimbo la Kinondoni katika kuhami, kuokoa mafuriko ambayo yanatokea katika Mto Msimbazi, basi Serikali ipo tayari kushirikiana nao kwa ajili ya kuondoa mchanga huo kuongeza kina cha maji, kuongeza kina cha mto ili maji yaweze kupita kwa usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, suala lake la pili, niko tayari Mheshimiwa Abbas kufuatana na wewe kwenda katika sehemu inayohusika. Ahsante sana.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, Mkoa wa Arusha una mito mingi ambayo ni vyanzo vizuri vya maji na vilevile ni vivutio vya utalii. Kama vile Mto Temi, Mto Nduruma na n.k. Lakini mito hii mingi imetekelezwa na kupelekea kukauka maji kutokana na shughuli nyingi za kibanadamu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu kwa Serikali, Je, Serikali inampango gani wa kuirudisha mito hii katika hali yake ya asili? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo katika harakati ya upandaji wa miti kuimarisha mazingira ili kuhami mito hiyo iweze kuwa salama na kurudi katika hali ya kawaida.
MHE. MICHAEL M. KEMBAKI: Mheshimiwa Naibu Spika, ningependa kuuliza swali ambalo linafanana na ambalo muuliza swali wa kwanza alivyouliza.

Swali langu ni kwamba katika Mji wetu wa Tarime Mjini lipo korongo maarufu kama korongo la starehe, na korongo hili limekuwa hasa wakati wa mvua linaleta madhara makubwa maana linapitisha maji mengi na hatimaye linahatarisha nyumba za wakazi ambao wanaishi kandokando ya korongo hili.

Je, Serikali ni lini litajenga Korongo hili ili at least wakazi ambao wapo katika mtaa huu waweze kuwa na uhakika wa makazi yao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tutatuma wataalam wetu kwenda kuangalia na kufanya tathmini katika Korongo hilo ili kusudi wataalam hao walete tathmini ambayo ni sahihi kwa ajili ya kufanyia kazi ndani ya mwaka wa fedha ujao. (Makofi)
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kuniona. Kwa kuwa changamoto zilizopo ndani ya Jimbo la Kinondoni kuhusiana na Mto Msimbazi ni sawa kabisa na changamoto zilizopo katika Mto Mbezi na Mto Mpiji ndani ya Jimbo la Kibamba.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ni lini sasa itaanza kutengeneza kingo za mto Mbezi ili kuokoa taasisi za Serikali mashule lakini vile vile na nyumba za wananchi, kuondolewa na maji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana kwa juhudi yake ya kupitia na kufanya mambo yaliyomengi ndani ya Jimbo la Kibamba. Kwa hakika Serikali ipo tayari kufanya tathimini ama inafanya tathmini juu ya jambo hilo mara tu mwaka wa fedha tutakapopata idhini ya fedha za kutosha basi tutapita ndani ya Jimbo hilo na kutatua changamoto ambazo zinazikabili Jimbo la Kibamba.
MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, kwa kuwa Korongo hili kwa msimu wa mvua wa mwaka 2020 na mwaka 2021, nyumba 29 za wananchi zimechukuliwa na maji.

Je, Serikali ina mpango gani kupitia Mfuko wa Maafa kuwasaidia wananchi hawa ambao wameathirika kwa kuchukuliwa na nyumba zao?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ili kuona ukubwa wa tatizo hili, ni muhimu sana Waziri na timu yake ya wataalam wa mazingira kutembelea eneo hili ili kuona wenyewe uharibifu ambao umetokea pale: Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kufuatana nami katika eneo lile ambalo imetokea shida hii ajionee mwenyewe?
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Awali ya yote naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Malima kwa juhudi yake ya ufuatiliaji katika mto huo na Jimbo lake kwa ujumla.

Mheshimiwa Spika, pili, nampa pole Mheshimiwa Mbunge kwa maafa ambayo yametokea katika mvua zilizopita. Ni kawaida ya Serikali, inapotokea maafa katika sehemu yoyote kufuatilia, kufanya tathmini na kuwafariji watu hao ambao wamepata maafa katika sehemu mbalimbali. Kwa hiyo, nimtoe shaka kwamba, Serikali itafuatilia na itakwenda kuwafariji watu waliopata maafa katika sehemu hiyo.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili. Mimi pamoja na timu yangu ya wataalam, niko tayari kabisa kufuatana na yeye baada ya Eid El-Fitr twende wote kuona hali ilivyo Inshallah. (Makofi)
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwanza nimshukuru Naibu Waziri kwa kunijibu vizuri na Watanzania wamesikia jinsi gani vyuma chakavu vilivyokuwa vinafanya kazi ya kusaidia jamii, lakini hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa suala la vyuma chakavu limekuwa sugu ingawa mazingira wameiwekea kanuni na kwa kuwa suala hili la mazingira limeshamiri la watu kuiba vyuma chakavu kwamba imekuwa kama ni mtaji wao na inaipa taabu Serikali katika kudhibiti ambavyo vyuma kama alivyozungumza Mheshimiwa Waziri.

Je, wako tayari kutuletea sheria itakayokuwa kali inayohusu vyuma chakavu ili tuipitishe hapa Bungeni iweze kusaidia jamii?

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa baadhi ya wezi wanaohujumu vyuma chakavu wengi wao wanatumia vilevi ambavyo havikubaliki na jamii ambao kama mfano wanaokula unga, hao ndio jamii kubwa inayofanya kazi hizo za kubeba vyuma chakavu ambavyo vimo katika mitaro ya maji.

Je, suala hili Serikali inalijua na kama inalijua imeliangaliaje…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Fakharia umeshauliza maswali mawili tayari.

MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS: Mheshimiwa Naibu Spika, Insha Allah nataka nijue hayo mawili ahsante.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli sheria zilizopo zinatosha kabisa, lakini ushauri unazingatiwa, kimsingi Mheshimiwa Mbunge tuondoe na tuache tu muhali wale watu ambao wamefanya makosa tuchukue hatua na kuwapeleka sehemu ambayo inayohusika. Ahsante. (Makofi)

WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo ameyaweka mbele ya Bunge lako Tukufu, lakini nimshukuru sana Mheshimiwa Fakharia, ni kweli kabisa wengi kati ya vijana ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli hiyo wamekuwa na dalili zote ambazo zinaviashiria vya matumizi ya dawa za kulevya za aina mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mamlaka ya Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kulevya na Biashara Haramu ya Dawa za Kulevya inachokifanya kwa sasa ni kuanzisha klabu mbalimbali katika mitaa na shule na maeneo mbalimbali kwenye nchi yetu ili kuweza pia kuwabaini hata hao vijana wanaojihusisha na shughuli hizo na shughuli nyingine tu, lakini wanaendelea kutumia dawa za kulevya na lengo letu ni kuwasaidia kuwaondoa huko na kuwaleta katika biashara ambazo hatawajihusisha tena na matumizi ya dawa za kulevya. Kwa hiyo tutaendelea kufanya kazi hiyo nzuri, lengo la Serikali ni kuhakikisha Tanzania bila matumizi na biashara ya dawa za kulevya iwezekane na tuweze kusonga mbele. (Makofi)
MHE. NAJMA MURTAZA GIGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na naishukuru Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Muungano kwa niaba ya Waziri wa Fedha kwa majibu mazuri ambayo nafikiri sasa yataielekeza nchi yetu kuwa shirika hili ni la Serikali kwa mujibu wa sheria.

Swali langu ni moja tu kwamba kwa vile Serikali imeelekeza taasisi za Muungano na taasisi zote za Serikali kutumia Shirika la Bima la Taifa sasa kwa nini Serikali hairudi na kuelekeza wananchi wake ili waelewe kwamba Shirika la Bima la Zanzibar ni Shirika la Kiserikali na wana wajibu pia wa kutumia kulingana na huduma zao wanakavyoona ni nzuri na mimi nikiwathibitishia wabunge kwamba huduma hizo ni nzuri? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Najma kwa juhudi yake ya ufuatiliaji wa kero za wananchi na kwa namna anavyopambana kwa wananchi wote, kwa kweli naomba hili tulichukue kama ni wazo, ni ushauri na tutalifanyia kazi. Tutashauriana na Serikali kulifanyia kazi jambo hili, ahsante.

MHE. AMOUR K. MBAROUK: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza sijajua kwa nini mikoa ya Zanzibar haijaorodheshwa hapa, lakini pia sijajua Serikali inawezeshaje makundi haya 157 ili kumudu kazi hii ngumu sana?

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Kwa kuwa zipo dini ambazo zinajinasibu na kujitahidi kusema kwamba kila kitu kitakachotokea duniani kwenye vitabu vyao wameeleza: Je, Serikali imeshaona umuhimu wa kuwashauri viongozi wa dini katika kuondoa tatizo hilo ambalo ni gumu sana hata pale Zanzibar ambapo visiwa ndiyo vinaondoka?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Khamis Amour Mbarouk kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Amour kwa juhudi yake ya kufuatilia masuala ya mazingira kule visiwani Zanzibar. Suala lake la kwanza ni kweli kwamba ipo haja ya kuhamasisha vikundi mbalimbali katika sehemu zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na tayari tumewasiliana na wenzetu, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais kule Zanzibar kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wa Kanda za Pwani ili kusudi kuanzisha vikundi kama hivi kwa lengo la kutunza mazingira. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kwa kweli tunachukua hoja yake hii kwamba upo umuhimu wa kushirikisha taasisi za dini. Tumeanza kuwaita viongozi wa dini na kuzungumza nao kuhusu suala la utunzaji wa mazingira. Kwa mwelekeo ambao tunakwenda nao sasa, ni lazima tuzishirikishe taasisi za dini kuhusu suala la utunzaji wa mazingira, kwa sababu wao kwa asilimia kubwa wanakaa na wananchi. Kwa hiyo, tutawaomba viongozi wa Makanisa ama Misikiti iwe ni sehemu ya mahubiri yao ya utunzaji wa mazingira ili mazingira yetu yawe salama kwa maslahi ya Taifa letu. Ahsante. (Makofi)
MHE. ASYA MWADINI MOHAMMED: Mheshimiwa Spika nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Huko nje hasa katika ukanda wa bahari, sisi tunatokea kwenye visiwa, hali ni mbaya sana kuhusu masuala mazima ya mazingira. Wakisema kwamba waanzishe vikundi, kwamba vikundi ndiyo viwe vinasimamia mazingira katika kukusanya taka, bado elimu haijafikiwa. Yaani wananchi walio wengi wanazalisha taka, lakini hawana taaluma ya utunzaji wa hizo taka hasa kwenye upande wa mazingira. Je, nini kauli ya Serikali juu ya usimamizi wa masuala mazima ya utoaji wa elimu ya usimamizi wa mazingira? (Makofi)
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asya, ni kweli kabisa anachokisema Mheshimiwa Mbunge kwamba elimu bado ni ndogo, lakini tumieandaa programu maalumu za kutoa taaluma kwa wanavikundi na wananchi wa kawaida.

Mheshimiwa Spika, jibu langu la pili la nyongeza nilisema kwamba tutaenda mpaka kwa taasisi za dini ili suala la taaluma liwe na wigo mpana. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba taaluma hiyo ya utunzaji wa mazingira itafika nchini kote.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, Waziri anaweza kutueleza ni mafanikio yapi yamepatikana katika mpango huo toka umeanza kutekelezwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Bagamoyo imekumbwa na changamoto kubwa sasa hivi ya kumegwa ardhi na maji ya bahari na hasa katika Chuo cha Sanaa Bagamoyo na maeneo mengineyo.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha inadhibiti hali hiyo isiweze kuendelea.
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu swali, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana Mheshimiwa Muharami kwa juhudi yake ya ufuatiliaji wa mazingira lakini na mabadiliko ya tabianchi katika Jimbo lake la Bagamoyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mafanikio ambayo yamepatikana katika miradi hii, moja; ofisi tano za BMUs tumejenga katika Wilaya za Bagamoyo na Pangani. Sehemu ambazo zimejengewa ofisi hizo na kuzipatia samani ni pamoja na Saadani, Chalinze; Zingibari, Mkinga; Kipumbwi, Pangani; Dunda, Bagamoyo; na Sudimtama na tumewanunulia viatu na makato kwa ajili ya kusimamia usafi huu wa mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kweli kwamba Bagamoyo ni moja ya kati ya sehemu ambazo zina changamoto kubwa za mabadiliko ya tabianchi, lakini tayari ofisi yetu imeshapeleka watalaam kufanya upembuzi yakinifu na kufanya survey ambayo ni sahihi na watalaam hawa wameshaleta majibu, siku za karibuni hivi basi mradi utaanza kutekelezwa katika eneo hilo. Ahsante.
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Wafanyabiashara wengi wenye mitaji midogo hawana elimu ya kutosha kuhusiana na suala zima la kufanya makadirio yao wenyewe ya kulipa kodi. Jambo hili limepelekea wafanyabiashara hawa mara nyingi kuajiri wataalam wa kuja kuwasaidia jambo ambalo hupelekea wao kutozwa fedha nyingi kuanzia shilingi laki tano, milioni moja na kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo hili limekuwa ni changamoto sana kwa wafanyabiashara na mwisho wa siku wafanyabiashara wengi wameshindwa kuendelea na biashara kwa maana wamekata tamaa kwa kuwa mwisho wa siku wanajikuta hawapati chochote, kila wanachokifanya kinaishia katika kulipa wataalam.

Je, Serikali ina mpango gani madhubuti wa kutoa elimu sahihi kwa wafanyabiashara hawa hususan wafanyabiashara wa vijijini ambao kimsingi elimu kwao haipo kabisa? Naomba majibu ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, wafanyabiashara hawa wenye mitaji midogo walikuwa wamewekewa utaratibu maalum wa makadirio ya shilingi 20,000/= kwa mwaka, lakini mpaka sasa ninapoongea utaratibu huu upo kimya kabisa, ni kama haupo: Je, Serikali ina kauli gani kuhusiana na utaratibu huu ambao upo kimya kwa wafanyabiashara hawa ikiwa ni sambamba na kwa wafanyabiashara wenye maduka siyo tu kwa machinga. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza naomba nimpongeze sana ndugu yangu Mheshimiwa Agnesta kwa namna anavyotetea Wafanyabiashara wadogo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la taaluma, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na hata wakubwa kupitia runinga, redio, na matamasha. Inawezekana baadhi ya vijiji elimu hiyo haijawafikia. Tutachukua ushauri huu kushuka chini vijijini kabisa kwa ajili ya kupeleka elimu ya kulipa kodi hasa kwa hiari. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili; kuhusu utaratibu wa wafanyabiashara wadogo kulipa ada ya shilingi 20,000/= kwa mwaka bado upo na unaendelea kwa wale wafanyabiashara wadogo wadogo kupitia vitambulisho vya Machinga. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Awali ya yote nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jitihada za kunijibu ingawa swali langu la msingi niliuliza ni lini sasa Serikali itakwenda mitaani, itashuka chini kwa maana ya TRA kuweza kuwabaini wafanyabiashara hawa waweze kuandikishwa na hatimaye waweze kupata tax clearance?

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika majibu tunaona kwamba, Serikali inasema kuna kampeni ya mlango kwa mlango, nataka nikiri, sijaiona kampeni hiyo na kwa hali hiyo kama utaratibu huo upo maana yake ni kwamba, utachelewesha sana kuweza kulifanya zoezi hili: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu; kwa kuwa, Serikali imeweza kufanikisha kuwepo kwa Maafisa kwenye kila kata, kwa mfano Maafisa wa Elimu, Maafisa Afya, Maafisa Kilimo, na kadhalika; ni kwa nini sasa Serikali isifikirie kuwa na Maafisa Kodi kwenye kila kata ili waweze kufanya kazi ambayo ni ya kuwafikia kwa urahisi wafanyabiashara ambao kila siku wanalalamikia masuala ya tax clearance na license? Kule Kinondoni shida ni kubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; ili kuweza kuwabaini wafanyabiashara hasa hawa wadogowadogo katika maeneo yetu, je, Serikali haioni busara kama inaweza ikaanzisha madaftari katika kila mtaa kuweza kuwabaini wafanyabiashara ndogondogo ili matatizo yao ya elimu ya ulipaji wa kodi na masuala mengine yakatatuliwa kwa urahisi, badala ya kuzungumzia elimu ambayo inatolewa na mamlaka kupitia kwenye ofisi za kodi kiasi kwamba, si rahisi jambo hilo kuweza kutekelezeka zaidi ya nadharia? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Abbas, Mbunge wa Kinondoni, kwa namna anavyowapigania na kuleta maendeleo katika Jimbo lake la Kinondoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nijibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Abbas, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza suala la kushuka chini ni kama ambavyo tumezungumza katika swali la mwanzo la Mheshimiwa Agnesta. Serikali yetu iko tayari kushuka chini kwenda hadi Serikali za Mitaa kwa ajili ya ukusanyaji wa kodi, lakini la kuanzisha maafisa ndani ya Serikali za Mitaa, hili tutachukua kama ni wazo na ushauri na tutautekeleza baadaye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe wasiwasi Mheshimiwa Abbas kwamba, kampeni ya mlango kwa mlango ipo na pengine tu kutokana na majuku yake mengi hajashuhudia. Hii ni kwa sababu, tayari mpaka kufikia tarehe 31 mwezi jana, basi walipakodi 432,323 ndani ya Kinondoni peke yake tumewasajili tayari na wafanyabiashara kati ya hao ni 171,973 kwa hiyo, suala hili la mlango kwa mlango liko Mheshimiwa Abbas. Ahsante sana.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Naibu Waziri ninayo maswali mawili ya nyongeza. Ufungaji wa Benki ya Wakulima ya Kagera iliyopo pale Manispaa ya Bukoba, iliwaumiza watu wengi ambao hawakuwa na hatia wakiwepo vikundi vya akinamama, SACCOS za akinamama, wakulima, wajasiriamali na hata wale wastaafu waliokuwa wameweka akiba zao. Serikali iliwalipa Sh.1,500,000/= pekee hata kama mtu alikuwa na akiba ya shilingi milioni 40. Sasa hivi anatuambia kwamba Serikali imekuwa ikikusanya madeni, pamoja na kuuza mali za Benki hiyo tangu mwaka 2018. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha hilo zoezi la kuwalipa hiyo Sh.1,500,000/= pamoja na akiba zote walizokuwa wameweka kwenye hiyo benki? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa nini Serikali isione umuhimu sasa badala ya kuzifunga, ikaziunganisha hizi Benki ndogo ndogo, kama ilivyofanya ikaunganisha Benki ya Wanawake, Benki ya Posta, Benki ya Twiga, TIB wakatengeneza Tanzania Commercial Bank kwa hiyo, mtaji ukawa umeongezeka kuliko kungoja sasa hizi Benki wakazifilisi na wakawaumiza wananchi ambao wanakuwa wameweka akiba zao kwenye hizo Benki? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasabago Mushashu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu awali ya yote napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Mushashu, kwa juhudi yake ya kuwatetea wananchi hao ambao walipata hasara hiyo katika benki iliyohusika, pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini ndugu yangu Byabato, kwa kuwa wanafuatilia kwa karibu suala hili lililojitokeza katika Benki hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la ulipaji wa fidia ya amana linaendelea mpaka hivi sasa tunavyozungumza. Wale wote ambao hawajajitokeza kwenda kuchukua amana hiyo, basi tunamwomba Mheshimiwa Mbunge, awashajihishe watu hao waende kupata fidia hiyo isiyozidi Sh.1,500,000/=. Wale ambao amana yao ni zaidi ya Sh.1,500,000/= waendelee kuwa na subira, mpaka zoezi la ufilisi wa benki hiyo utakapokamilika na watalipwa kwa mujibu wa taratibu za ufilisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili. Serikali tayari imeshaanza zoezi kwa upande wake kuziunganisha Benki, ambazo zilipata changamoto mbalimbali zikiwemo mitaji. Tayari Serikali yetu imeshaziunganisha Benki ya Posta, Benki ya Wanawake, Benki ya TWIGA na Benki ya TIB na kuunda Benki inayojulikana kwa jina la Benki ya Biashara Tanzania (TCB). Ahsante sana.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, majibu ya Serikali ni mazuri kama tulivyosikia, lakini swali: Mpaka sasa kiasi kinacholipwa kutoka kwenye dhamana ni shilingi 1,500,000 tu hata kwa mteja aliyeweka pesa nyingi sana na wanasubiri kuuza mali za benki ndipo waweze kuwalipa; na benki nyingine hazina mali za kutosha.

Je, Serikali haioni kuna haja sasa ya kuleta sheria kwenye Bunge hili ili kuweza kuwasaidia wateja wa benki hizi? Benki ya Greenland, pamoja na benki ya FBME na zenyewe zimefilisika kwa muda mrefu na sasa tunaona Covenant Bank lakini hakuna muda mahususi wa kufanya minada na kuwalipa wateja: -

Je, Serikali na yenyewe haioni kuna haja ya kupanga specific time ili kuweza kuuza mali hizo na ikishindikana Serikali ichukue dhamana hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Cecil Mwambe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Cecil Mwambe kwa maswali yake haya mazuri, maana yake maswali yake yanaonekana ni mawazo ushauri. Mfano swali la mwanzo, Serikali inalichukua wazo hili na ushauri huu wa kuongeza idadi ya kulipa hiyo fidia ya shilingi milioni moja na nusu kwa wale ambao amana yao iko zaidi ya shilingi milioni moja na nusu.

Mheshimiwa Spika, la pili pia inaonekana ni ushauri kwetu. Kwa hiyo, Serikali itatenga muda mahususi au wakati mahususi wa kukusanya mali na madeni kwa zile Benki ambazo zimefilisiwa na Serikali kwa mujibu wa sheria. Ahsante.
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Ninalo swali moja dogo la nyongeza; kwa kuwa vijana wengi kutokidhi vigezo na masharti yatolewayo na mabenki.

Je, Serikali haioni haja ya kuweka kigezo cha miradi ama business plan ili vijana wengi waweze kukopesheka? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Lucy John Sabu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali hilo, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa juhudi zake za kuwatetea vijana. Ni kweli kwamba vijana walio wengi wanamaliza masomo na wengine ni hodari sana, wana uwezo mzuri wa kielimu, lakini hawakopesheki kwa sababu hawana dhamana. Serikali italichukua hili kulipeleka kwa wataalam wetu kulifanyia uhakiki, ikionekana jambo hili linapendeza, basi business plan itatumika kama ni kigezo cha dhamana katika benki za Serikali.
MHE ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi, lakini kwa idhini yako nichukue nafasi hii kuwashukuru sana Watanzania ambao wamenifanya ni-trend wiki hii na kauli mbiu yangu ya kuchumba chima. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya pili sasa ninaulizia hii pesa ya shilingi milioni 204 ikizingatiwa kwamba kuna baadhi ya suppliers ambao tayari walikwisha- supply vifaa na leo hii ni miezi 18 wanaidai Serikali. Ninaomba kupata kauli thabiti ya Serikali, ni lini pesa hii itapelekwa ili tumalizane na hili tatizo kwa sababu wanadai zaidi ya miezi 18 baadhi ya watu pale?

Pili, kwa kuwa sasa wananchi wangu wa Biharamulo ambao ni wafanyabiashara wamelazimika kuingia kwenye hali y kuikopesha Serikali bila makubaliano ya mikopo.

Je, Serikali ipo tayari kuwalipa na riba hawa watu ambao wame-supply vifaa na leo wanatakiwa walipwe pesa yao? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante; kwa ruhusa yako naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Engineer Ezra Chiwelesa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu naomba nimpongeze sana kwa jinsi ambavyo anajitahidi kufuatilia wananchi wa Jimbo hilo kwa maendeleo na maslahi ya Wilaya yake.

Mheshimiwa Spika, suala la ulipaji madeni Serikali siku zote ipo katika harakati za kuhakikisha kwamba imelipa madeni ya wadai wote. Zipo taratibu ambazo zinafuatwa za kujiridhisha na kuhakiki madeni hayo ili baadae tuweze kulipa kwa utaratibu.

Mheshimiwa Spika, kwa wale ndugu zetu ambao walishatumikia miezi 18 lakini fedha hiyo haijapatikana, tumeshatoa mpaka kufikia Januari mwaka huu tumeshatoa shilingi milioni mia tatu kuja katika Jimbo lako la Halmashauri ya Biharamulo. Katika fedha hiyo mnaweza mkatenga fedha maalum kupunguza taratibu deni la wananchi ambao walitumikia Jimbo hilo. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naipongeza Serikali kwa kuanza kufanya malipo hayo. Je, ni lini Serikali itakamilisha malipo ya madai yaliyosalia?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Charles Kajege, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuhakiki na kupitia madeni yote ambayo maombi yao yameletwa. Mara tu utakapokamilika uhakiki huo, Serikali itaendelea kulipo kwa madeni yote yaliyosalia.
MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ingawa, Mheshimiwa Naibu Waziri amejibu vizuri kwenye swali la msingi, lakini naomba niulize swali la nyongeza. Serikali imeshafanya jitihada za makusudi kwenye kupunguza ukali kwenye bidhaa ya mafuta. Je, Serikali haioni haja ya kufanya jitihada hizo hizo ili kupunguza ukali kwenye bidhaa za vyakula?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhan, Mbunge wa Chake Chake, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi kwamba tayari Serikali imeshatoa ruzuku kwa upande wa mbolea na tayari Serikali imeshusha kodi ya uingizaji wa mafuta ya kula. Kwa hiyo, Serikali imeshachukua hatua ya kupunguza ukali wa mfumuko wa bei za mafuta.
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nimpongeze Waziri kwa majibu yake mazuri, lakini naomba niulize swali la nyongeza. Serikali imekuwa na majibu mazuri sana kuhusu mfumuko wa bei, lakini uhalisia ulivyo nje katika mitaa na vijiji, hali ilivyo haiko hivyo ambavyo Serikali imekuwa ikijibu. Je, Serikali inaliambia nini Taifa letu la Tanzania juu ya mfumko huu wa bei?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ussi Pondeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali na mipango yake ya Serikali ni kusimamia bei za bidhaa na kuona kwamba wananchi wanapata huduma zao kwa bei nafuu. Ahsante.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; kwa kuwa kwa mujibu wa Sheria hii ya PPP kwa maana ya Sheria Sura namba 210, kiwango cha mtaji kwa wazawa ni dola milioni 20. Je, Serikali haioni kwamba kiwango hiki ni sehemu ya kikwazo cha utekelezaji wa sheria hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali ina mpango gani wa kupunguza masharti ya kimkataba katika miradi hii inayoibuliwa na sekta binafsi ili iweze kutekelezwa kwa ufanisi kupitia PPP? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sheria ya PPP ipo katika mchakato wa kufanyiwa marekebisho na sasa ipo ngazi ya kukusanya maoni kutoka kwa wadau. Kwa hiyo nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira mpaka mchakato huo utakapokamilika bila shaka hiki hakitokuwa kikwazo kwa utekelezaji wa sheria hiyo.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, masharti hayo ambayo yapo pia ni kwa mujibu wa sheria na taratibu, kwa hiyo pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge masharti hayo huenda yakapungua baada ya kupata mapendekezo kutoka kwa wataalam wetu ambao wanakusanya maoni hayo. Ahsante.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa madeni haya shilingi trilioni 7.9 kama ulivyosema ni ya wafanyakazi, watoa huduma na wauzaji bidhaa na ni ya muda mrefu, hauoni kwamba Serikali mnakuwa sehemu ya kufifisha shughuli za kiuchumi za Watanzania? Swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili; Wizara yako ya Fedha ndio inayomsimamia Msajili wa Hazina, sasa ni lini mkakati huu utakamilika, nataka time frame ili mkakati huu upelekwe kwenye Kamati ya Bunge inayosimamia mashirika ya umma kwa ajili ya ufuatiliaji na utekelezaji? Ni lini? Time frame? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima James Mdee, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mipango ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tumelipa madeni yote hasa Serikali ya Awamu ya Sita, tumelipa madeni yote yaliyopo katika Serikali, lakini ni lini mkakati huu utaanza kutumika ni wakati wowote baada ya kupitia na kuhakiki wataalam wetu basi itatolewa taarifa rasmi. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZAHOR MOHAMED HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri naomba kuuliza maswali mawili ya ziada.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza; je, Serikali sasa iko tayari kutoa taaluma hii baada ya mkanganyiko wa mambo haya kwa upande wa Zanzibar?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; je, lini hili linaweza kuanza kufanyika kwa ajili ya kuondoa huo mkanganyiko? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyo ada ya Serikali kutoa taaluma kwa wananchi wake na taasisi mbalimbali, Serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi wote juu ya jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili anauliza, ni lini? Niseme, Serikali kutoa taaluma kwa wananchi wake ni suala endelevu. Kwa hiyo, tunaendelea kutoa taaluma kwa wananchi.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwanza napenda nianze na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuanza utekelezaji wa kutoa ruzuku kwenye pembejeo za mbolea na zoezi hilo linaenda vizuri sana na wananchi wamepunguziwa mzigo mkubwa kwenye pembejeo za mbolea kupitia hiyo ruzuku pamoja na soko la dunia mbolea kupanda bei kwa kiasi kikubwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu; kwa sababu kimuundo Benki Kuu huwa inakopesha mabenki kwa muda mfupi na katika hali hiyo haiwezi kukidhi mahitaji ya mikopo ya kilimo ambayo ni ya muda mrefu. Sasa je, ni kwanini Serikali haioni kuhamisha huo mfuko kutoka Benki Kuu na kwenda Benki ya Maendeleo ya Kilimo, hizo shilingi trilioni moja ziweze kusaidia wakulima? Nashukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njeza, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya Mheshimiwa Njeza kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalichukua na kulifanyia tathmini, tukiona kwamba upo ubora wa kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua stahiki. Ahsante.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nikijaribu kupitia huku kwenye benki hii, ni takribani miaka 10 sasa tangu benki hii ianzishwe. Ilianzishwa mwezi Septemba, 2012, lakini tunaona ina matawi matano tu. Matawi haya matano yako katika majiji haya makubwa, lakini tunajua wakulima wako kwenye vijiji vyetu na kata zetu ambako tunatoka. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa je, kwa sababu Serikali imesema itapanuka lakini based on kupata pesa ya mtaji mkubwa zaidi: Ni nini mpango wa Serikali kuiongezea pesa benki hii hata kupitia hazina ili wakulima wetu ambao wametutuma sisi hapa waweze kunufaika na benki hii ambayo ina miaka zaidi ya 10 lakini haijawafikia? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili: tarehe 9/6/2022 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kagera kwenye uwanja wa Kaitaba alitoa maelekezo maalum kwa Serikali ya Mkoa wa Kagera na akai-cite kwamba tumekuwa na shida ya mafuta ya kula katika nchi hii na mpango uliopo ni kuutumia Mkoa wa Kagera ambao una maeneo makubwa ambayo hayatumiki kwa ajili ya kufanya kilimo cha michikichi na kilimo cha alizeti; na ameelekeza tutenge hekta takribani 70,000 mpaka 100,000 kwa ajili ya kutatua tatizo hili: -

Sasa je, Serikali haioni kwamba iko haja ya kuielekeza benki hii pamoja na kwamba mtaji wao bado ni mdogo, ielekee Kagera ikaungane na Serikali ya Mkoa ili waone wanasaidiaje kutatua tatizo hili la mafuta ya kula? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Eng. Ezra kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza tunalipokea kama ushauri na tunaenda kulifanyia kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili pia tunaenda kulifanyia tathmini tuone kama upo umuhimu wa kuelekea kwa wakati huu; na kwa kuwa ni maelekezo ya Mheshimiwa Rais kunyanyua uchumi katika Mkoa wa Kagera, basi nalo hili tumelipokea na tunalifanyia kazi. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZAINAB A. KATIMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Kama Serikali ilivyosema kwamba imetoa utaratibu mzuri wa kwamba mtu anayeanzisha biashara awe ana miezi Sita kabla ya kuanza kulipa kodi, lakini sasa katika uhalisia (in practice) mazingira hayapo hivi. Mpaka sasa bado watu wanatakiwa. Kwa sababu mtu anapoanzisha biashara inabidi kwanza apate leseni ya biashara ili apate leseni ya biashara inabidi aende akapate TIN na ili apate TIN inabidi apate TAX Clearance, sasa ili apate hiyo TAX Clearance anapewa makadirio ya kodi na analazimika alipe robo ya kwanza ya yale makadirio ya kodi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa analipa kabla hata ya hiyo miezi Sita ambayo amepewa kama muda ambao hatakiwi kulipa kodi. Sasa naomba kujua kwa sababu ni mwongozo na ni utaratibu ambao umetolewa na Serikali lakini kiuhalisia haupo hivyo.

Je, Serikali inatoa majibu gani kuhusiana na changamoto hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Zainab Athman Katimba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba hili tulichukue tulifanyie uchunguzi, lakini nitoe maelekezo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kufuata Sheria, Utaratibu na Kanuni zilizowekwa na Serikali. Ahsante. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa nyakati tofauti Serikali imekuwa ikisisitiza kutokufungia akaunti wafanyabiashara, lakini tumeendelea kupokea malalamiko wafanyabiashara wanafungiwa akaunti. Hata kama kuna changamoto za kikodi lakini kumekuwa na tatizo hilo.

Je, ni ipi kauli ya Serikali kwa TRA kuacha utaratibu wa kufungia akaunti wafanyabiashara hata kunapotokea changamoto za kikodi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba kauli ya Serikali katika jambo hili ni ile kutaka mamlaka ya mapato kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na Serikali katika majukumu yao ya kila siku. Suala la kufunga akaunti bila vielelezo hili hakuna. Ahsante.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina maswali mawili. Kwanza nashukuru kwa majibu.

Je, ni lini zoezi hili litakamilika ukizingatia umuhimu wa kukusanya kodi na kwa vile ni muda tangu Mheshimiwa Rais alipotoa agizo hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, Serikali na TRA ina mkakati gani rafiki wa kufanya makadirio ya kodi kwa wafanyabiashara yanayoendana na mapato halisi ili kuzuia wafanyabiashara wasishindwe kulipa kodi hizi? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali kwanza, inategemea ushirikiano ya mteja wakati wa kufanya majadiliano. Kama mteja atakuwa na ushirikiano mzuri basi suala hili linamalizika kwa kipindi kifupi sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili; mikakati ambayo tumechukua sisi Serikali ni kutoa fursa kwa wateja, yaani wafanyabiashara, kufanya self assessment, yaani kujifanyia tathmini wenyewe halafu na sisi tunajiridhisha. Mkakati wa pili ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara wote ili wafate taratibu za kulipa kodi.
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, halmashauri hii makusanyo yake ya mwaka 2021 ilikuwa bilioni 5.3 kwa mwaka na Jimbo hili la Muhambwe liko mpakani ambapo tuna biashara za ujirani mwema kwenye Masoko ya Mkarazi na Kumshwabure. Je, Serikali haioni ni muda muafaka sasa kujenga TRA ya kudumu lakini pia na kujenda ushuru wa pamoja mpakani ili kudhibiti biashara holela za mpakani? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, wananchi wa Muhambwe wanafuata huduma za leseni Mkoani Kigoma ambapo ni kilomita 240 kutoka Jimbo la Muhambwe. Je, ni lini Serikali itaanzisha huduma za leseni katika Jimbo la Muhambwe ili kuwaondolea adha wananchi hawa wa Muhambwe?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake la kwanza, Serikali imelichukua na tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba ikimpendeza Mheshimiwa Mbunge niambatane naye kwenda kuona hali halisi ya Wilaya ya Kibondo, tuone namna gani tunaweza tukatatua usumbufu huu ambao wanapata wananchi wetu wa Kibondo. Ahsante.
MHE. ESTHER E. MALLEKO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwanini Serikali isipunguze riba inapokopesha benki za biashara ili gharama hizo ziweze kushuka na Watanzania wengi waweze kukopa.

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwanini Serikali isipunguze riba inapouza hati fungani ili Watanzania wengi waweze kupeleka fedha zao katika benki hizo kama fix deposit.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Esther Malleko kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, viwango vya riba vimepungua kwa asilimia 16.60 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 16.41, mwaka 2022 ili kuwezesha benki kukopesha wananchi kwa riba nafuu na kupunguza mikopo chechefu.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, riba za hatifungani haziwekwi au kupangwa na Benki Kuu ya Tanzania bali ni matokeo ya mchakato wa mauzo na ununuzi wa hatifungani kutoka soko la fedha linaloendeshwa kwa mfumo wa soko huria. Hata hivyo, takwimu za karibuni zinaonesha kuwa riba za hatifungani zimepungua.
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini nina uhakika kwamba tathmini ya mwisho kufanyika katika eneo hilo ni mwaka 2008.

Mheshimiwa Spika, basi naomba kumuomba Mheshimiwa Waziri kama inawezekana ili kuthibitisha yale anayoyasema tuongozane akaongee na wafanyabiashara wa Wilaya ya Ngorongoro ambao ndio wahitaji wa kituo cha forodha.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa
Spika, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Emmanuel Shangai, Mbunge wa Ngorongoro, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote kabla ya kujibu swali hilo naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyofuatilia na kufanyia kazi katika Jimbo lake. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama yetu Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania ni Serikali sikivu sana. Kwa hiyo, niko tayari kufuatana na yeye Mheshimiwa Mbunge kwenda katika eneo hilo na kuona uwezekano na kuongea na wananchi na wafanyabiashara kwa jumla. (Makofi)
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika,
nianze kwa ushauri mdogo kwamba Serikali iende ikaziangalie hizi gharama, bado ni kubwa sana na zinadumaza ubunifu. Maswali mawili yangu ya nyongeza; vijana wengi wamejiajiri kupitia ubunifu na wengi wanafanyakazi na taasisi za nje, changamoto imekuwa ni malipo.

Je, ni lini sasa Serikali itaruhusu mfumo wa pay poll ili vijana hawa ambao wamejiajiri na kufanya kazi za consultancy huko nje ya nchi waweze kupata malipo yao. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; tuna vijana wengi wabunifu ambao wanaandaa mifumo ya software. Software ambazo tunazinunua online hazitozwi VAT, lakini zile ambazo zinatengenezwa nchini, zinatozwa VAT. Ni lini sasa Serikali itafanya mapitio ili kuhakikisha kwamba wabunifu wa ndani ya nchi wanapata nafuu katika mifumo ambayo wanaitengeneza hapa nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ndugulile kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba kumpongeza sana Mheshimiwa Ndugulile kwa kiasi ambacho anapigania wananchi wa Jimbo la Kigamboni na Watanzania kwa jumla. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mfumo wa Paypal bado haujazuiliwa na unaendelea kutumika nchini. Mwaka 2016 wawakilishi wa Paypal walifika Benki Kuu ya Tanzania ili kupata taratibu zinazotakiwa katika kutekeleza huduma hiyo. Hata hivyo, Serikali ipo tayari kupokea maombi ya leseni kwa sababu hawawezi kuendesha huduma hiyo bila kuwa na leseni. Serikali iko tayari kupokea leseni hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, ni kweli kabisa. Naomba nikiri kwamba ni kweli huduma hii ya software au huduma za mtandao hulipiwa VAT ni suala la kweli kabisa kwamba lazima ilipiwe VAT na ni tofauti, yaani VAT ambayo inalipiwa kwa software ambazo zinatengenezwa nchini, zinakuwa na ongezeko hilo la thamani tofauti na ambazo wananunua ndani ya mtandao online.

Mheshimiwa Spika, suala hili tayari utafiti umeshafanyika kwa kina na mapendekezo yake tayari. Nalihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba mapendekezo hayo yatawasilishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/ 2023 mwaka huu. Ahsante. (Makofi)
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Makampuni mbalimbali ya simu yanatoa huduma za mikopo kupitia mitandao na riba zake ziko juu sana: -

Je, Benki Kuu inafanya nini kuhakikisha inasimamia huduma hizi?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Benki Kuu ya Tanzania inapitia maombi yote ambayo yanaletwa na makampuni mbalimbali. Itakapojiridhisha, basi itatoa leseni kwa kampuni yoyote ikizingatia masharti kwamba lazima waambatane au washirikiane na kampuni au taasisi ambayo ipo ndani ya nchi yetu. (Makofi)
MHE. KHADIJA S. TAYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali na kuonyesha namna gani Serikali imejipanga kwa kutumia hizi takwimu.

Mheshimiwa Spika, kwa kutumia takwimu zilizopita, za 2010 na sasa hivi tuko 2022/2023 kwenye maandalizi ya bajeti ya Mpango wa mwaka 2022/2023.

Je, Serikali imejipangaje kupitia Wizara yake hii ya Fedha na Mipango kuondoa matatizo ya watu wenye ulemavu; kwa sababu hii Wizara ndiyo ambayo ina bajeti Kuu ya Serikali? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Khadija Shaaban Taya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha Sensa yetu tukapata takwimu sahihi na kuweza kujua idadi ya watu wenye ulamavu na aina ya ulemavu ambayo ipo nchini, tutaandaa mipango rasmi na kutoa vipaumbele ambavyo vinaweza kuingizwa hadi katika bajeti yetu kwa maslahi ya wananchi wote.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan haiko tayari kuacha kundi lolote nyuma, makundi yote yataainishwa katika vipaumbele vya nchi hii na kwa maslahi ya umma. Ahsante. (Makofi)
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwanza naishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri na naipongeza TRA na wadau mbalimbali kwa ubunifu huo wa mashine ambayo inarahisisha, sasa maswali yangu mawili ya nyongeza ni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa bado yapo matukio ambayo baadhi ya wafanya biashara ya kutotoa risiti hasa katika maeneo yenye biashara mfano Kariakoo. Je, Serikali kupitia TRA kwa kuwa imepewa kibali kwa mara ya kwanza kaujiri watumishi wengi kwa wakati mmoja, inawatumiaje watumishi wale katika mapambano dhidi ya vitendo hivi vya kutotoa risiti? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili, kwa kuwa katika jibu lake la msingi ameeleza kwamba, wafanyabiashara wanaruhusiwa kusheria kurejesha gharama za mashine za EFD wanazozinunua wakati wanakokotoa mapato ya kutoza kodi. Je, Serikali inajipangaje kutoa elimu hii kwa wafanyabiashara wengi ili kuondoa dhana ya kwamba mashine za EFD ni gharama zaidi? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote kabla ya kujibu maswali haya, kwa idhini yako, naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyofuatilia na pia ni Balozi wa TRA.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, Serikali iliwapatia mafunzo yale ambayo ni muhimu kabisa, awali kabla ya kuanza kufanya kazi, lakini kama hilo halitoshi, Serikali imeandaa Mkakati wa kutoa mafunzo ya watumishi hawa, mafunzo maalum kwa watumishi hawa wapya kila baada ya miezi minne.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Serikali kupitia TRA ina program ya kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, tv pamoja na redio. Nichukue fursa hii kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, kuwaelekeza TRA kuendelea kutoa mafunzo hayo kimkakati. Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. FATMA H. TOUFIQ: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuweza kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kuna kipindi kumekuwa kukitokea tatizo la upatikanaji mfumo hasa kwa watu wanaohitaji zile mashine za EFD, hivyo kuchelesha kupata zile mashine za EFD nini mkakati wa Serikali wa kuimarisha mfumo ili wafanyabiashara waweze kupata hizi mashine za EFD kwa wakati? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Toufiq, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, changamoto hizo zilikuwepo za mfumo huo wa mashine ya EFD na ndiyo maana tukaamua sasa kuleta mfumo mpya na kifaa kipya ambacho kinajulikana kwa VFD. Ahsante. (Makofi)
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa jibu zuri ambalo nimelipata: -

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mkakati upi ambao imeuweka wakati mwingine isijirudie kukaa muda mrefu bodi za wataalam kutokuwepo?

Mheshimiwa Spika, Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Maimuna Ahmad Pathan, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imejiandaa na imeweka mipango, mikakati na taratibu maalum ambazo zitakuwa ni suluhisho sahihi la kutokuwa na muda mrefu wa kuunda ama kuteuwa bodi hizo. Ahsante.
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Naibu Spika, nishukuru Serikali kwa majibu yake lakini nikiangalia majibu haya naona kana kwamba yanakinzana na azma ya blue print ambayo inataka wafanyabiashara kwa maana ya walipa kodi waweze kufanya biashara zao wa urahisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Siku zote ukaguzi husababisha interest na penalties kitu ambacho kinafanya ulipaji wa kodi ule unakuwa mgumu. Kuna ukakasi gani kwa Serikali kuweza kuleta mabadiliko kwamba tax audit sasa zifanyike kila mwaka?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kwa kuchelewesha hizi tax audit wafanyabiashara wanabambikiziwa makodi makubwa sana kiasi kwamba wanakimbilia kwenda mahakamani, fedha za Serikali hazikusanywi inavyopaswa na kwa wakati. CAG anazungumza trillions of moneys zimekwama kule katika mahakama. Hivi Serikali haioni kwamba ni wakati sasa kurahisisha shughuli za ukokotoaji wa kodi ili fedha za Serikali ziweze zikapatikana kwa urahisi?
NAIBU WAZIRI FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Abbas Tarimba, Mbunge wa Kinondoni kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza tunalichukua kama ushauri, Serikali itaenda kufanya utafiti tukiona kwamba umuhimu wa kuwekwa sheria hiyo basi Bunge lako tukufu tutapeleka mapendekezo yetu na kutunga sheria nyingine ambayo tufanye ukaguzi wa kila mwaka kwa wafanyabiashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini swali lake la pili pia nalo tunaenda kulifanyia ukaguzi na utafiti kama kweli fedha zinapotea basi atatusaidia na Wabunge wenzangu atatusaidia namna gani ya kuweza kudhibiti na kukusanya fedha hizo kwa wakati stahiki. (Makofi)
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, nchi yoyote ambayo inahitaji kukusanya mapato kwa wingi na kuwatengenezea mazingira mazuri wananchi wake wamekuwa wakiweka mazingira mazuri ya kodi yaani kodi zinakuwa rafiki si kubwa kulingana na biashara ya mtu anayoifanya. Lakini hapa katikati kodi zimekuwa kubwa kulingana na biashara ya Watanzania wanazozifanya na kumekuwa na malalamiko mengi.

Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali inamkakati gani wa kuweka kodi rafiki ili mtanzania ajivunuie kulipa kodi ili kuchangia maendeleo katika Taifa lake?
NAIBU WAZIRI FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Bulaya kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeandaa mazingira rafiki ya ulipaji kodi isipokuwa baadhi ya wafanyabiashara wanakuwa ni wababaishaji katika biashara zao baadhi yao, lakini nalo niseme kwamba tunalichukua kwenda kulifanyia kazi.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la Mheshimiwa Tarimba lilisema Serikali inachukua muda mrefu wa kufanya Tax Audit matokeo yake watu wanabambikiziwa kodi kubwa. Waziri umesema unataka ukafanye utafiti, CAG ameainisha kwamba kuna kesi za kikodi zenye thamani ya zaidi ya trilioni 350…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Halima uliza swali lako.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, trilioni 350 zimekwama kwa sababu ya kesi za kikodi. Unahitaji kufanya utafiti gani zaidi juu ya suala la Mheshimiwa Tarimba ni muhimu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima Mdee kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, tuliposema kufanya utafiti lazima tujiridhishe na kama kesi zipo mahakamani tunaiachia mahakama ifanye shughuli zake.
MHE. NG'WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini bado jukumu la msingi la kulinda maslahi na vipato vya Watanzania linabaki kuwa la Serikali, basi swali langu la kwanza; je, Serikali inatambua uwepo wa makampuni haya ambayo Watanzania wamewekeza kwa kununua hisa yanafanya biashara, yanatengeneza faida na bado hayalipi magawio kwa Watanaznia hawa waliowekeza?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali inasemaje au ina mkakati gani wa kuja na mpango madhubuti na wa wazi wa kuhakikisha kwamba inalinda maslahi ya Watanzania hawa waliowekeza dhidi ya wizi huu wa kuaminiwa?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kamani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza tumepokea shauri hilo na tunafuatilia mara moja. Nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge tuwe na mashirikiano ya pamoja katika kuzitambua kampuni hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, nielekeze DSE na CMA kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hii ya wizi na mara tu zitakapobainika hatua za kisheria zitachukuliwa.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Nafahamu pamoja na kwamba sheria hiyo ipo na sisi ndio tunaosimamia utawala wa sheria, lakini nafikiri pia makampuni haya yanasimamiwa kwa regulation za taratibu zetu za nchi.

Sasa tunaomba kujua Serikali ina mpango gani sasa wa kuitisha taarifa za mashirika hayo ili kujua wametoa gawio kiasi gani na tangu walipoanza kuuza hisa wametoa gawio kiasi gani na kuwapa wananchi taarifa nini hatma yao?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jesca, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hili ni shauri na shauri lake tumelichukua, tunaenda kulifanyia kazi.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Pia niipongeze sana Serikali kwa kupunguza riba katika hati fungani kwenye level tofauti. Ningependa kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika swali la kwanza; kwa sababu sasa hivi Serikali inafungua uchumi, inafungua nchi na kila mtu anatakiwa ashiriki katika suala zima la uchumi. Je, Serikali inaonaje kwamba ipunguze idadi ya minada ya hati fungani kusudi mabenki ya biashara yaweze kufanya biashara yaweze kupata wawekezaji, ili tuweze kuongeza mzunguko wa fedha nchini?

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili; ningependa kuiomba Serikali miaka saba iliyopita Serikali ilikuwa inapitisha fedha zake kwenye mabenki ya biashara na zile fedha zilikuwa zinakaa pale muda mrefu, kwa hiyo kulikuwa na mzunguko mkubwa wa fedha na wananchi walikuwa wanaweza kukopa na hata riba zilikuwa zimepungua kwa sababu kulikuwa na fedha nyingi kwenye mabenki ya biashara. Je, Serikali haioni muda umefika sasa wa kufungua tena kwamba fedha zake ziwe zinakaa kwenye mabenki ya biashara kusudi wananchi waweze kukopa, mzunguko wa fedha uongezeke lakini pia na riba ziweze kushuka?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. David Mathayo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kupunguza idadi ya riba katika hati fungani ni swali la kisheria, lakini Serikali imelichukua na tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Dkt. Mathayo alileta ombi kwamba minada iwe inapungua mwenendo wake wa riba, basi nalo Serikali imelichukua na tutalifanyia kazi.
MHE. OMAR ALI OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; je, ni viwanda vingapi vya wazawa ambavyo vimepata msamaha huo?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, vimewasaidiaje viwanda hivyo? ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli swali la kwanza ni suala la takwimu naomba hili tulichukue tutampelekea kwa maandishi. Swali la pili, ni hakika kabisa viwanda vyote vya wazawa nchini vinapata misamaha kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na Serikali.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru Serikali kwa kuonesha commitment ya kutaka kujenga stendi hii ya kisasa, lakini nimewasiliana na watu wa Halmashauri, wanasema kwamba kwa upande wa Halmashauri mchakato umeshakamilika kutoka kwenye ngazi ya Wilaya mpaka kwenye ngazi ya Mkoa. Sasa hivi Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari kuwasiliana na watu wa TAMISEMI kwa kuona kwamba mradi huu umekwama kwenye ngazi hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili kwa sababu kumebakizwa miezi miwili bajeti aliyoitaja hapo inakwenda kukamilika. Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari kututengea tena fedha kwenye bajeti hii iwapo kama fedha zile za mwanzo zitakuwa bado hazijatumika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu maswali hayo naomba nimpongeze sana Kaka yangu Kuchauka kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo la Liwale.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Fedha na Mipango ipo tayari kuwasiliana na Wizara ya TAMISEMI nachukua nafasi hii nitoe maelekezo kwa wataalam wetu kufanya mawasiliano ya haraka sana kuona hadhi ya project hii imefikia wapi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, suala la pili kwa kuwa Serikali ina nia njema ya kujenga stendi ya kisasa, basi kama haikukamilika mwaka wa 2021/2022 basi bajeti inayokuja tutatenga tena fedha hiyo ili kusudi tuone mradi huo umekamilika. Ahsante. (Makofi)
MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa
Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Baada ya majibu mazuri ya Wizara kuhusiana na swali nililouliza, nina swali moja la nyongeza. Ni kwamba kumekuwa na uvumi wa muda mrefu kwamba VAT inayotoka kwenye miamala ya mtandao ya simu inakusanywa na mamlaka moja tu ambayo ni ya TRA. Halafu TRA ndio wanakisia kiwango ambacho wanawapa Zanzibar. Wizara wanasemaje kwenye uvumi huo?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ramadhan Suleiman, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni suala la taaluma tu katika nchi yetu kwa jamii yetu kwamba TRA ndio wanakusanya mapato ya pande zote mbili katika suala la miamala. ZRB wanakusanya kwa upande wa Zanzibar na Tanzania Bara ni TRA. Kwa hiyo nichukue fursa hii kuwaagiza TRA na ZRB kuendelea kutoa taaluma kwa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wajue makato haya yanakatwa vipi kwa mujibu wa sheria. Ahsante.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ahsante pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; kama inavyoonesha, kwamba kila mwaka na kila muda tunalipa Deni la Taifa ni kwa nini sasa Deni la Taifa halioneshi dalili ya kupungua ilhali kila mwaka tunalipa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, ni lini sasa Serikali italeta mchanganuo wa madeni yote tunayodaiwa kama nchi ili Wabunge tupate fursa ya kushauri katika ulipaji wa madeni hayo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati iliyo mikubwa nchini kwetu. Tunarejesha fedha lakini tuna uhitaji mkubwa tunaendelea kukopa.

Mheshimiwa Spika, kwa swali lake la pili, Serikali inawasilisha taarifa ya madeni yake kwenye Kamati ya Bajeti kila mwaka na kila inapohitajika. Tunaishukuru sana Kamati ya Bajeti kwa miongozo yake inayotusaidia kuendelea kufanya deni letu kuwa himilivu, ahsante.
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niulize maswali madogo ya nyongeza. Kwa kuwa katika Hospitali ya Ocean Road kuna changamoto ya baadhi ya mashine za mionzi kukaa muda mrefu bandarani kutokana na kutokamilika kwa taratibu za kikodi; je, Serikali ina mpango gani wa kuweka utaratibu mzuri wa vifaa tiba hivyo kuondolewa mlolongo wa taratibu hizo? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali sasa haioni haja ya kuondoa kodi zote kabisa ya vifaa tiba vyote vya wagonjwa wa kansa, figo na kadhalika ili hospitali nyingi ziweze kutibu hayo magonjwa na kutibu Watanzania walio wengi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, utaratibu uliopo sasa ni mzuri, kwani Mheshimiwa Waziri wa Afya akisharidhia tu, basi vifaa hivyo vinapatiwa msamaha wa kodi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, ni kwamba vifaa tiba vyote vikiwa vya kansa, figo na kadhalika vinapatiwa msamaha wa kodi baada ya kupata ridhaa tu ya Mheshimiwa Waziri wa Afya, ahsante.

SPIKA: Kwa hiyo, tutakuwa sahihi kwamba anayechelewesha vifaa ni Wizara ya Afya na siyo Wizara ya Fedha.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, sisi tukipata tu barua ya Mheshimiwa Waziri wa Afya kuhusu vifaa tiba, basi tunatoa msamaha bila pingamizi yoyote.

SPIKA: Waziri wa Nchi, naona Waziri wa Afya hayupo wala Naibu wake. Huu ndiyo uhalisia? Kwa sababu haya maneno ya Mheshimiwa Mariam Kisangi, maana yake atakuwa kayatowa Ocean Road, wanasubiria vifaa viko bandarini.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE NA URATIBU: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba suala hili tulichukue, tutalifanyia kazi vizuri Serikalini ili tuwe na majibu ambayo yana uhakika na tuweze kumkabidhi Mheshimiwa Mbunge na kuona tatizo hilo linaweza likahitimishwa namna gani. (Makofi)
MHE. NG’WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, la kwanza: Pamoja na Bunge lako hili Tukufu kupitisha Sheria hii ya Fedha mwaka 2019 inayotoa nafuu ya mjasiriamali kwa mtu anayeanza biashara kulipa kodi baada ya miezi sita, lakini bado wananchi wakienda kutafuta leseni kwenye Halmashauri zetu wanatakiwa kupeleka Tax Clearance kutoka TRA. Ili aipate hii Tax Clearance anatakiwa afanyiwe makadirio ya kodi na alipe kodi ya mwanzo. Sasa nini Kauli ya Serikali juu ya mkanganyiko huu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, Sheria ya Uwekezaji Tanzania ikisomwa pamoja na Sheria mbalimbali za Kodi nchini, inatoa ruhusa kwa mamlaka mbalimbali za mapato kutoa msamaha wa kodi kwa wawekezaji wa nje mpaka mitano; na hii ni nzuri kwa ajili kukuza uwekezaji nchini. Sasa ni lini Serikali itaona haja ya kufanya mapitio ya Sheria hii ya Fedha ya mwaka 2019 ili kuongeza muda wa msamaha wa kodi kwa wazawa angalau kwa miezi 12 mpaka 18 ili: moja, kuendelea kutoa motisha kwa wawekezaji hawa wa ndani: na pili, kuwapa mazingira bora ya ushindani wawekezaji hawa wa ndani sambamba na wawekezaji hawa wa nje katika biashara? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kamani, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa idhini yako, naomba nielekeze Kamishna wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania kufanya kazi kwa mujibu wa Sheria. Sheria hii imepitishwa, hakuna Mjasiriamali yeyote mpya anayetakiwa kulipia chochote kabla ya biashara yake. Kwa hiyo, naomba nimwelekeze kufanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, naomba nipokee maoni ya Mheshimiwa Mbunge tuyachukue kwenda kuyafanyia kazi.
MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ningeomba kuuliza maswali mawili madogo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, la kwanza, kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitoa misamaha ya kodi ya VAT kwa taulo za kike na vishikwambi lakini tija haikuwepo kabisa. Je, Serikali inachukua hatua gani kukabiliana na changamoto hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa misamaha hii ya VAT kwa bidhaa zinazotoka nje ya nchi imekuwa ikichelewa sana na inasababisha hata miradi ya maendeleo mingi kutokamilika kwa wakati. Je, Serikali inachukua hatua zipi kutatua kadhia hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Issa Mtemvu kwa ufuatiliaji wa misamaha hii ama harakati za ulipaji kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba misamaha ilitolewa kwa vishikwambi na taulo za kike lakini wako ambao walienda kinyume na taratibu lakini Serikali ilichukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta misamaha hiyo na kuhakikisha kwamba wafanyabiashara hao wamelipa kodi inayostahiki. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili mikakati ambayo imechukuliwa na Serikali. Moja ni kubadilisha sheria, sheria iliyokuwepo zamani lazima Baraza la Mawaziri ndiyo litoe msamaha lakini kwa sasa iko juu ya Waziri wa Fedha na Mipango. Jingine Serikali imetengeneza mfumo ambao kwa sasa inaratibu misamaha yote hiyo na inatolewa kwa wakati.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Nashukuru kwa majibu ya Mheshimiwa Waziri, lakini kwanza kabla ya swali langu nitoe utangulizi, katika majibu ya Mheshimiwa Waziri anasema msamaha wa kodi uliotolewa ni baiskeli pamoja na magari mahususi kwa matumizi ya watu wenye ulemavu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mlemavu wa macho au asiyoona hivi gari lake linafananaje? Naomba kuuliza swali la kwanza; Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba inatoa msamaha wa kodi kwa watu wenye ulemavu wa macho na vifaa vingine vyote wanavyoleta iwe sawa kama wale wenye ulemavu wengine waweze kupata msamaha wa kodi hiyo na kuleta unafuu wa maisha yao? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; kumekuwa na baadhi ya Watendaji wa Wizara hiyo ambao wanahusika na utoaji wa msamaha wa kodi wakiwatoza kodi wenye ulemavu na katika majibu ya Mheshimiwa Waziri ameonyesha msamaha wa kodi unatolewa. Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari nimletee watu wenye ulemavu ambao wametozwa kodi wakati wanahitaji msamaha huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa
Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Tendega, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu maswali hayo, naomba nimpongeze sana kwa kiasi ambacho anawapigania ndugu zetu wenye ulemavu. Swali lake la kwanza kama nilivyojibu katika swali la msingi ni vifaa tu mahususi ambavyo wanatumia ndugu zetu wenye ulemavu ndivyo ambavyo vinapata msamaha, lakini maoni yake tunayachukua, tunaenda kuyaangalia kama yanaleta tija kwa pande zote mbili kwa walengwa na Taifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, siwezi kukataa kukutana na ndugu zetu, wananchi wenzetu wenye ulemavu na watu wengine wote mimi niko tayari kukaa nao, lakini naomba baada ya kipindi hiki cha maswali na majibu nikae na Mheshimiwa Mbunge tuone kwa kiasi gani tunaweza tukapata ufumbuzi wa suala hilo na kuwasaidia ndugu zetu hawa wenye ulemavu, ahsante. (Makofi)
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza hili suala sio jipya, limeanza toka mwaka 1997 kupitia TGNP, mwaka 2000 Serikali ikafanya mradi wa majaribio, mwaka 2010 kikaundwa hicho kikosi kazi anachokisema. Sasa kwa maelezo ya Waziri leo mwaka 2023 anasema kikosi kazi, maana yake anatuambia kwamba Serikali haiko serious, haijawa tayari bado kutimiza commitment zake za Mikataba ya Kimataifa iliyosaini? Kwa sababu sio jipya. Hilo la kwanza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa hili jambo ni la muda mrefu hamwoni sasa kwa mwaka ujao wa fedha 2024/2025 ni wakati muafaka kwa Serikali kupitia Wizara hii kuelekeza kila Wizara kuja na tamko la kijinsia katika upangaji na utekelezaji wa bajeti yake? Dhamira ni Serikali ama wananchi wajue kila shilingi iliyopangwa mwanababa amefaidika vipi, mwana mama amefaidika vipi, kijana amefaidika vipi, mlemavu amefaidika vipi? Ndio spirit ya hii concept. Sasa hamdhani kama Wizara ya Fedha...

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mdee, uliza swali.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Naibu Spika, Hawaoni sasa kwa mwaka ujao wa fedha 2024/2025, mwelekeze kila Wizara ije na tamko la bajeti la kijinsia?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima James Mdee, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza Serikali haiko serious? Naomba nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali iko serious na tuko tayari kufanyia kazi masuala yote na maoni ambayo yanatolewa na Waheshimiwa Wabunge.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, maoni yake tumeyachukua na tutakwenda kuyafanyia kazi. (Makofi)
MHE. HAJI MAKAME MLENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mbali na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa benki hii haikufilisika bali ilifilisiwa na inasemekana walikuwa na fedha za kulipa waathirika wa benki hii. Je, Serikali inajua maumivu wanayoyapata waathirika wa benki hii?

Swali la pili, kwa kuwa Serikali ndiyo dhamana wa mabenki yote Tanzania na Watanzania wengi wameathirika na benki hii. Je, haioni haja hivi sasa Serikali ikachukua jukumu la kuwalipa Watanzania wlioathirika katika benki hii na wao wakasubiri jibu la Mahakama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Haji Mlenge kwa namna anavyofuatilia kwa karibu sana suala hili la benki ya FBME. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inajua kadhia hii na ndiyo maana Serikali inafuatilia kwa karibu sana siku hadi siku, mpaka kutoa wataalam wetu hapa kwenda kusimamia kesi hiyo kule Cyprus.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, naomba Mheshimiwa Mlenge uwe na subira mara tu maamuzi ya Mahakama yatakapotolewa na taratibu kukamilika nakuhakikishia kwamba Serikali itawalipa wateja hao bila pingamizi yoyote.
MHE. JUDITH S. KAPINGA: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa majibu mazuri, ila nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tayari Serikali ina kitengo maalum na tayari inafanya utambuzi na ukusanyaji wa kodi hizi: Je, tangu jitihada hizi zifanyike, mapato yanayotokana na biashara hizi yameongezeka kwa kiasi gani?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Pamoja na mikakati mizuri ambayo Serikali inafanya, bado biashara nyingi za kimtandao hazijafanyiwa utambuzi na hazifanyiwi ukusanyaji ikiwemo biashara ya D & D; Serikali ina mkakati gani wa kuimarisha mikakati hii ili biashara hizi ziweze kufanyiwa utambuzi wa ukusanyaji mapema ili kuongeza mapato? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Judith, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza ni kiasi gani, naomba hili nijibu kwa njia ya maandishi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, Serikali imeendelea kulipa VAT na kwa taratibu zote na imechukua suala hilo na inaendelea kulifanyia kazi.
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri napenda kupata commitment ya Serikali kwamba wakati tukisuburi kukamilika kwa mchakato wa Itifaki ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kati ya nchi yetu na nchi ya DRC ambayo ni mdau mkubwa wa kibiashara wa nchi yetu; je, Wizara yako ipo tayari kukaa na wafanyabiashara wa Kigoma ili kuwapa elimu ya Itifaki hiyo kurahisisha shughuli za kibiashara baina yetu na DRC?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kilumbe kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kutoa mafunzo na kwa ujumla tayari Serikali imeandaa programu maalum kwa ajili ya kutoa mafunzo ya wafanyabiashara hao, lakini siyo tu waliopo Kigoma bali nchi nzima.
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kuna idadi ndogo sana ya usajili kwa maana ni asilimia 16 tu ya nguvu kazi ya walipa kodi: Je, Serikali haioni wakati umefika sasa kwa Wizara ya Fedha, TAMISEMI na Wizara ya Viwanda na Biashara kukaa pamoja na kuona namna bora ya kusajili wafanyabiashara na walipa kodi katika ngazi ya vijiji badala ya kugombania leseni kwa maana ya leseni B?

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo ya kimkakati, mfano Jimbo la Mikumi ambalo siyo wilaya wala siyo halmashauri, lakini ni maeneo ya kimkakati ya biashara na kodi: Serikali ina mpango gani wa kuchechemua maeneo haya ili wafanyabiashara washiriki kikamilifu katika ujenzi wa Taifa letu?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ni kweli kama nilivyosema, bado idadi ya walipa kodi ni ndogo na tayari Serikali ina mikakati mbalimbali ili kuhakikisha tunaongeza idadi ya walipa kodi kulingana na nguvu kazi iliyopo.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, ni kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Ufanyaji Biashara nchini (MKUMBI), na hili tumeendelea kutoa elimu na hatua mbalimbali ambazo zinapelekea kuvutia wafanyabiashara na wazalishaji mbalimbali kurasimisha biashara zao ikiwa ni pamoja na kuondoa kodi, tozo na ada ambazo ni kero kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumeendelea kuweka mazingira ambayo yanarahisisha usajili wa biashara kwa wananchi wote. Kwa hiyo, tayari Serikali inafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, TAMISEMI lakini pia Wizara ya Viwanda. Sasa hivi tunataka tuone namna ya kuhakikisha tunapeleka maelekezo kwenye ngazi ya vijiji ili kuwa na dirisha la pamoja la kuratibu masuala ya biashara kutoka ngazi ya Kijiji, lakini tayari tumeshafika kwenye halmashauri ambako tunaweka Idara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji ambao watafanya kazi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, maeneo mkakati, ni kweli tunaona umuhimu wa kuhakikisha maeneo ya kimkakati ambayo yana fursa nyingi za kibiashara kuyawekea miundombinu wezeshi ikiwemo masoko na kuweka vituo maalum vya kuhamasisha wananchi kusajili biashara zao. Tayari Wizara kupitia BRELA tumeshaanza kupeleka elimu na kuhamasisha wananchi kusajili biashara zao katika maeneo husika kwa maana ya halmashauri na hata katika maeneo yale ya kimkakati ambayo tunaona yana biashara ambazo zinaweza kuleta tija kwa uchumi wa nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
MHE. SALIM MUSSA OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Nachukua fursa hii kuwaombea tu kwa Mwenyezi Mungu waweze kutimiza yale ambayo wananchi wana-wish. Nina swali lingine la nyongeza: Je, utaratibu huu ambao unafanyika kwa makampuni katika kujikadiria kodi yao kwa kufanya ukokotoaji wa kile ambacho wanaingiza, ni lini utaenda kwa maduka ya kawaida ya retails? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nina ushauri kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa nini sasa kutokana na sintofahamu kubwa iliyojitokeza ndani ya nchi yetu baina ya mlipa kodi na mtoza kodi, kwa nini sasa usiwepo mfumo wa kutengeneza activities za kimichezo baina yao hata kutengeneza ligi baina ya wafanyabiashara pamoja na TRA na viwanja tunavyo pale Kariakoo? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge. Kabla ya kujibu naomba nimpongeze sana kwa namna anavyojitahidi kutetea kampuni changa vile vile na wafanyabiashara wadogo wadogo. Swali lake anasema ni lini? Namwomba tu Mheshimiwa Salim awe na subira, mchakato huu unaendelea kufanywa na Serikali kwa nia safi. Mara tu baada ya kumalizika tutaleta katika Bunge lako tukufu, ahsante. (Makofi)
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Kalemie na Uvira ni miji ambayo iko karibu sana na Mikoa ya Kigoma, Katavi na Sumbawanga: Je, Serikali haioni haja ya kufanya haraka kuhakikisha kwamba maeneo haya ya Uvira na Kalemie yamefunguliwa hizo branches za CRDB? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Nashon William Bidyanguze, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli Serikali imeona haja hiyo na ndiyo maana kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, kwamba Benki Kuu ya Tanzania ilishatoa kibali kwa CRDB sasa, lakini tumetoa wito kwa benki nyingine zote nchini ambazo ziko tayari kuwekeza katika miji hiyo ya Congo, basi Serikali imetoa idhini ya kufanya zoezi hilo. (Makofi)
MHE. LUCY J. SABU: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa fursa hii, naomba sasa niulize swali dogo la nyongeza.

Kwanza naipongeza Serikali kwa majibu mazuri, kwa kuwa katika mkutano wa vijana Mkoa wa Mwanza na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi kwamba tutaanzisha Benki ya Vijana Wajasiriamali.

Je, ningependa kufahamu ni hatua zipi zimefikiwa katika mchakato wa uanzishwaji wa benki hiyo. Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, awali ya yote naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Lucy pamoja na Wabunge wengine wote kwa kufuata nyanyo za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutaka kujua au kuona hali ya vijana wetu kiuchumi inaimarika.

Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sabu kwamba suala hili lipo katika hatua ya majadiliano katika kikao kazi cha Makatibu Wakuu, litakapokamilika tu hatua iliyopo sasa, basi tutajulishwa ili wananchi wote wajue na hatua nyingine ziweze kuendelea.
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mwezi Septemba ni mwezi ambao tunategemea kuanza kilimo katika maeneo yetu;

Je, Serikali haioni haja ya kuwataka Benki ya CRDB waanze kutoa mikopo kwa wakulima ili waweze kutayarisha mashamba yao? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Kata za Msikisi, Kijiji cha Namalembo na Matutwe, Chiwalwe, Namajani pamoja na Mpanyani zipo mbali sana na makao makuu ya wilaya ambako ndiko zinatolewa huduma za kibenki kwenye Jimbo la Ndanda;

Je, Serikali haioni haja ya kuwasogezea wananchi huduma kwenye maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu Maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwambe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba benki itatoa huduma zote mara tu baada ya kukamilika kule Liwale ikiwemo mikopo CSR na mengineyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la pili, tutashauriana na benki ili wapeleke huduma hizo za kibenki katika zile kata ambazo hazijafikiwa na benki ili kuepusha utapeli ambao unafanyika katika shughuli za wanadamu kiuchumi za kila siku.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Niishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa mabenki mengi hapa nchini bado yana uhaba wa fedha tofauti na Mheshimiwa Waziri ulivyosema. Hali ambayo imepelekea sasa hivi wafanyabiashara wengi wa Soko la Kariakoo, hawa wadogo wadogo na wengine wakubwa wanapata shida ya kupata pesa za kigeni, kiasi kwamba CRDB in a day sasa hivi huwezi kupata zaidi ya dola 1,000 na mabenki mengine kama NMB na NBC huwezi kutoa zaidi ya dola 500 kwa siku. Kitu ambacho kama mtu anahitaji kutuma pesa nyingi nje ina mchukua muda mrefu sana kuzunguka kwenye benki mbalimbali kukusanya hela na haruhusiwi ku-change hizo hela;

Je, sasa ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha tunawapeleka wafanyabiashara katika dreams zao za kupata fedha za kigeni ili waweze kufanya shughuli zao za biashara vizuri bila kukwama? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kihalisia Nchi zetu zimekuwa zinafanya trading kubwa sana na Nchi za Asia ikiwemo China, India na Uturuki pia, lakini wafanyabiashara wa Tanzania wanalazimika kubadilisha pesa zao kuwa kwenye shilingi kupeleka katika dola na wanapofika kwenye yale Mataifa wana-change tena kutoka kwenye dola kupeleka kwenye pesa za wale mataifa;

Je, sasa wanakuwa wanapata hasara ya exchange rate hapo, hamuoni kwamba iko hajia ya Serikali ya Tanzania kuongea na mataifa haya makubwa ambayo tunafanya nayo biashara na tunatembelea kwa kiasi kikubwa na uanguko wa dola hasa zinaposhindwa kupatikana, wakaturuhusu tukaanza kufanya exchange rate ya pesa za nchi zao; kwa mfano anaenda China akaondoka na Yuan akiwa hapa hapa akifika kule asipate usumbufu wa kubadilisha kwenye dola halafu watoke kwenye dola warudi kwenye pesa ya Mataifa yao?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Engineer Chiwelesa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi, tayari Serikali imechukua hatua kadhaa ili kupunguza au kuondoa changamoto hiyo. Kwa hiyo naomba nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na Subira, hivi karibuni changamoto hiyo imeondoka katika nchi yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, shauri lako Mheshimiwa Engineer tumelichukua na tunalifanyia kazi. Ninachotaka kukuambia, hivi karibuni tumeanza mazungumzo na India katika shauri ambalo umelitoa na Nchi nyingine tutaenda.
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Mheshimiwa Waziri aliahidi kuja Mtwara kuzungumza na wadeni hao. Je, Mheshimiwa Waziri upo tayari kuja Mtwara kuja kuzungumza na hawa ambao wana wadai? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wananchi wa Jimbo la Mtwara wameahidiwa mara kwa mara juu ya majibu ya Mheshimiwa Waziri. Sasa ni lini sasa mtakuja kuwapa fedha zao hao wananchi wa Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Hassan Mtenga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mimi niko tayari kabisa kwenda kuwasikiliza na kukaa na wananchi wa Mtwara Mjini kuhusu madai yao mara tu baada ya Bunge kumalizika tutakaa na Mheshimiwa Mtenga tuende kukutana na wananchi hao.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba taratibu za ufilisi zinaendelea na kuanzia Julai mwaka wa fedha unaokuja tunaenda kuwalipa wananchi kwa mujibu wa sheria. (Makofi)
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa, kumekuwa na taarifa kwa wachuuzi wadogo wadogo maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Wilaya ya Nyang’hwale, kwa kupungukiwa na silver ama sarafu ndogo ndogo kuanzia shilingi 50, 100, 200 na 500 na kusababisha mfumuko wa bei kwenye masoko yetu madogo madogo.

Je, Wizara inalitambua hilo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Amar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ninamuomba tu Mheshimiwa Mbunge kwamba hili tulichukue tukalifanyie kazi, tukafuatilie tuone kwamba hivyo ndivyo hali halisi ilivyo na tuone ni njia gani ya kulipatia utatuzi suala hilo. (Makofi)
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali ina mpango gani wa kusimamia taasisi ndogondogo zinazoumiza wananchi katika mikopo yake kama hizi zinazojulikana kama kausha damu, komandoo, rusha roho na kadhalika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango na mikakati na ndiyo maana tumeanzisha sheria na taratibu kwa hiyo taasisi yoyote ambayo inaanzisha mikopo lazima ifuate sheria na taratibu na iwe imesajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania. (Makofi)
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante. Yaliyotokea Mtwara Mjini kwa PRIDE pia yametokea ndani ya Iringa Manispaa. Je, zoezi hilo Julai mtalifanya kwa wote nchi nzima pamoja na Iringa Manispaa walioathirika?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Jesca kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tuliposema kwamba Kampuni hii ya PRIDE tayari imefanyiwa taratibu na Sheria ya Ufilisi, tunaenda kulipa fedha hiyo kwa wadai walioko Mtwara nina maana kwamba ni nchi nzima wale ambao wana madai Julai tutaanza kulipa fedha hiyo. (Makofi)
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya ziada. Namshukuru Waziri kwa jawabu lake zuri lakini ningeomba sasa Serikali ituambie, kwa sababu vijana wanapata tabu sana kupata malipo yao, Je, ni lini Serikali itaruhusu mifumo kama ya PayPal ili watu waanze kulipwa fedha zao? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Kampuni ya PayPal haijaomba leseni. Mara tu itakapoomba leseni na kukidhi vigezo vya kisheria basi Serikali itaruhusu kampuni hiyo kutoa huduma nchini.

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Ilikuwa niseme kwa niaba yake kwa sababu aliwasiliana na mimi pia. Nakushukuru.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba hili tulichukue tukalifanyie kazi. (Makofi)
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa nafasi. Kwanza niipongeze sana TRA kwa hatua walizozichukua kuongeza uwezo wa kukagua hii miamala ya transfer pricing, ikiwemo ununuzi wa Kanzidata ya Orbis na kuiwezesha Serikali kupata mapato stahiki. Sasa ninayo maswali mawili ya nyongeza:-

Swali la kwanza; hizo hatua ambazo amezizungumza Mheshimiwa Naibu Waziri zimesaidia kwa kiwango gani kuongeza mapato ya Serikali?

Swali la pili; ni kauli gani Serikali inatoa juu ya ongezeko kubwa la taarifa shuku juu ya fedha haramu ambapo miamala ya usafirishaji wa fedha kwa njia ya kielektroniki na fedha taslimu imeongezeka kutoka trilioni 123 hadi trillioni 280 mwaka wa 2023. Sasa ishara hii inaonesha kwamba, kuna ongezeko kubwa la rushwa, ufisadi, transfer pricing, elicit financial flow, capital flight, sasa haya matukio haya kwa ongezeko hilo la hizi takwimu Serikali inatoa kauli gani kama FIU ilivyotoa taarifa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Awali ya yote kabla ya kujibu maswali naomba kumpongeza Mheshimiwa Mpina pamoja na Wabunge wengine kwa namna wanavyopigania kuona kwamba, ukusanyaji wa mapato unapatikana kwa ufanisi.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, kwa kweli, hatua hizi zimesaidia kwa kiasi kikubwa sana. Ndiyo maana inadhihirika hata hivi karibuni tumeona TRA wamevunja rekodi katika ukusanyaji wa mapato hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili kupitia TRA Serikali imeimarisha mifumo ambayo itadhibiti mianya yote ya rushwa na hata njia nyingine za ukwepaji wa kodi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, Serikali kupitia TRA imeongeza rasilimali watu kwa kiasi kikubwa sana na hata hivi karibuni nafasi 524 zimetangazwa na mchakato unaendelea.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, pamoja na hayo Serikali imekwenda mbali sana, iko sasa hivi kwenye FATAF (Financial Action Task Force), anti-money laundering, anti-terrorism financing, Serikali iko vizuri sana. Mimi niko kwenye kikao cha European Union na tumeona namna European Union wanavyoisifia Serikali ilivyodhibiti utakatishaji pesa na ku-finance terrorism katika Taifa letu.

Mheshimiwa AG.

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, nilitaka tu kuongeza ya kwamba, kwa mujibu wa Sheria ya Anti-Money Laundering, taarifa shuku zinapowasilishwa kwa FIU, baada ya kufanyiwa analysis hupelekwa na kufanyiwa kazi na vyombo vyenye dhamana ya kuchunguza na baadae kuchukua hatua za kisheria. Kwa hiyo, taarifa ambazo zimekwishatolewa kwa sasa zinaendelea kufanyiwa kazi na vyombo vyenye dhamana hiyo vilevile. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Mkoa wa Kagera anaosema unachangia 2.6% ni mkoa ambao una rutuba ya kutosha, unazalisha kahawa ya kutosha na pia una ardhi ya kutosha: Je, huo mkoa kuchangia kwenye pato la Taifa 2.6% haioni kwamba ni kushindwa kwa Serikali? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Mkoa wa Kagera umezungukwa na nchi mbalimbali ikiwepo Rwanda, Burundi na maeneo mengine: Nini mkakati wa kuusaidia au kusaidia kuvutia wawekezaji katika huu mkoa ili uweze kuzalisha vya kutosha na hasa katika viwanda ili uongeze pato la Taifa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Anatropia, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali haijashindwa na ushahidi wa hilo, Serikali imeweka mazingira wezeshi ili wananchi wenyewe wafanye shughuli zao za kiuchumi na kijamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, Serikali imefanya mikakati mbalimbali na hatua mbalimbali. Hivi leo tunaona sekta za uzalishaji ndiyo ambapo Serikali imeweka nguvu zaidi ya kuwekeza mfano kama kilimo cha umwagiliaji, mifugo na uvuvi, ahsante. (Makofi)
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Je, lini Serikali italipa fidia kwa wananchi wanaopisha ujenzi wa kituo hicho cha forodha? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango yupo tayari kuambatana nami twende Manyovu baada ya Bunge hili ili akaongee na wananchi hao wanaopisha ujenzi wa kituo hicho cha forodha? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Felix kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze hilo la pili. Niko tayari kuambatana naye kwenda sehemu husika na kuongea na wananchi kule. Swali lake la kwanza, Serikali iko katika hatua za uchambuzi wa fidia hiyo ya wananchi. Namwomba tu Mheshimiwa Mbunge awe na subira. Mara tu taratibu zitakapokamilika, basi wananchi watapata haki yao.
MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, natambua msamaha ambao umetajwa na Serikali, lakini pamoja na msamaha unaotolewa wa kodi unakuwa sawa kwenye hizi taasisi lakini wanapotoa hizi huduma, wanatoa kwa gharama tofauti tofauti. Serikali ipo tayari kutoa mwongozo sasa katika hizi gharama zinazotelewa kwenye hizi taasisi binafsi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani bado kuna changamoto ya Kodi ya Forodha kwa vifaa tiba pamoja na dawa.

Je, Serikali iko tayari kutoa hizi kodi zote kama ilivyotangaza kwenye magari yanayotumia umeme ili kutoa kipaumbele kwa afya za Watanzania? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Aida kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa taasisi ambazo zinafanya biashara zinastahiki kutoa kodi inayostahiki kwa mujibu wa sheria, ambazo zinatoa huduma tu zinapata hadhi ya charitable organization na zitapata unafuu wa kodi.

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili, Serikali inatambua umuhimu uliopo katika elimu na afya, tunaendelea kuboresha miongozo mbalimbali ya kodi ili kila wakati tuweze kufikia malengo ya utoaji huduma bora kwa wananchi wetu, ahsante.
MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa naomba kuuliza Serikali, je, iko tayari kuwa na mpango mahsusi wa kuisadia SUMA JKT katika kuhakikisha kwamba tunajitosheleza katika suala zima la chakula na mafuta ya kula? Mipango mahsusi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Chumi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo tayari kuangalia vipengele mahsusi vya kusaidia mashirika yake na mashirika mengine, lakini ushauri wake pia tumeuchukua na tunaenda kuufanyia kazi.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Pamoja na majibu ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba alienda Bikonge na Nyamuhonda; wananchi wa Jimbo zima walienda kwake wakitaka kujua ni lini wataweka pale kituo kwa sababu kitasaidia kuokoa fedha za Serikali na kufanya biashara mpaka watu wa Serengeti watanufaika hapa. Kwa hiyo niliomba nijue ni lini kituo hicho kitajengwa kama ambavyo Mheshimiwa Waziri wa Fedha aliahidi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, ninapozungumza hapa Kanda ya Ziwa yote Shinyanga, Simiyu, Mwanza, Geita, Mara biashara ya mazao imesimama kwa sababu Sirari kuna vurugu kubwa kwa zuio ambalo limetolewa na Mheshimiwa Waziri kwa Niaba ya Serikali. Watu wa Sirari na kanda ya ziwa wangependa kujua ni lini zuio hili litaondolewa kwa sababu wakati wanatoa tamko la kuzuia tayari wafanyabiashara wa mazao walikuwa na mazao kwenye maghala yao, hawafanyi biashara; na ulikuwa ukipeleka mazao Kenya unaleta bidhaa nyingine kutoka Kenya. Kanda imesimama biashara haifanyiki;

Je, ni nini kauli ya Serikali katika jambo hili?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mwita kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba nimpongeze sana kwa namna anavyofatilia kituo hiki kidogo cha forodha pale mpakani. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kituo hiki mara tu upatikanaji wa fedha utakapopatikana basi kituo hiki kitajengwa, asiwe na hofu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili naomba tulipokee kwa sababu limechanganya Wizara tofauti, Wizara ya Kilimo, Biashara na Fedha. Naomba tulipokee tukakae kama kamati tutakutana na wewe Mheshimiwa Mbunge tuone namna gani tutatatua changomoto.

WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kutoa majibu ya ziada katika swali alilouliza Mheshimiwa Waitara. Mimi na yeye tumeshaongea zaidi ya mara moja mara mbili, naomba nirejee na Watanzania wanielewe. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haijazuia watu kufanya biashara ya mazao na kuuza mazao nje ya nchi. Serikali ilichokizuia ni watu kufanya biashara bila kufuata utaratibu wa Kisheria. Haiwezekani mtu unanunua mahindi Songea unapakia kwenye malori huna business license ya aina yoyote, hata business name kusajili ambayo ni huduma inayotolewa. Huna tin number, huna tax clearance, huna export permit, huna phytosanitary halafu unataka nchi ikuruhusu kwenda kuuza nje mazao hayo. Malipo hayaonekani katika mfumo rasmi wa fedha, hatuzipati data katika export statement zetu za nchi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, maelekezo ya Mheshimiwa Rais yako wazi, Mtanzania yeyote anayetaka kufanya biashara ya mazao kwa ajili ya kuuza nje ama kuuza ndani ya nchi akate leseni ya biashara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nipitie kwenye Bunge lako Tukufu kuwaambia wafanyabiashara wa mazao, nendeni kwenye halmashauri kateni leseni za biashara, nendeni TRA chukueni Tin Certificate ili muingie kwenye mfumo rasmi na formalization ya biashara ya mazao ya kilimo. Hatuwezi kuendelea katika mfumo huu unao endelea. Na nia ya Serikali ni kurasimisha shughuli za kilimo na shughuli za biashara za mazao. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, jana mtu yupo tayari apigwe penalty ya shilingi laki nane au milioni moja kwa sababu hana leseni avuke upande wa pili. Wiki iliyopita tumeruhusu malori Sirari, wiki hii tumeruhusu zaidi ya malori 506 na wote wamelipa faini ya shilingi milioni moja. Hatuwezi kuruhusu mfumo huu. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwaombe Wafanyabiashara, mazao ya kilimo yatauzwa popote, nendeni mkajirasimishe muwe na business license, muwe mna TIN, mna tax clearance. This is how we formalize economy. (Makofi)
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Je, ni lini Serikali itajenga kituo cha forodha Oloika katika kata ya Ololosokwan Wilayani Ngorongoro ili kupunguza usumbufu kwa wananchi lakini kuongeza mapato ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema Serikali kupitia TRA walifanya utafiti nchi nzima. Kwa hiyo upatikanaji wa fedha katika nchi yetu basi kituo alichokitaja Mheshimiwa Mbunge kitajengwa.

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kulikuwa na ujenzi wa vituo vikubwa vitatu vya forodha, kipindi inajengwa Vigaza kulikuwa na cha Manyoni halikadharika kulikuwa na Kituo cha Nyakanazi Biharamulo ambacho kilikuwa kimeshaanza kujengwa na tayari majengo yako pale, lakini kimetelekezwa kile kituo na kiko chini ya Wizara ya Fedha.

Sasa nilitaka kujua ni lini ujenzi wa Kituo cha forodha Nyakanazi Biharamulo ambacho kilishaanza ujenzi utafufuliwa ili uweze kukamilika kwa manufaa ya Biharamulo?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ezra kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo hiki kilikuwa na mgogoro kati ya Mkandarasi na upande mwingine lakini tumechukua hatua na ninacho mhakikishia Mheshimiwa Mbunge, hivi karibuni tutapata mwafaka wa jambo hilo na kituo hicho kitaendelea na ujenzi kama kilivyopangwa.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mwaka 2021 Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango alifanya ziara kwenye Jimbo la Momba kumwonesha mahali ambapo tunapendekeza kujenga kituo cha forodha. Mwaka huu mwezi wa pili Mheshimiwa Waziri Mkuu pia tulimshirikisha wazo hilo na akaona ni jema;

Je, Serikali imefikia hatua gani kujenga kituo kipya cha forodha ndani ya Jimbo la Momba ili kunusuru kituo cha forodha kilichopo Tunduma kwa sababu kimezidiwa ili kiweze kutoa huduma kwa ufasaha?
NAIBU WAZIRII WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo hicho ni kweli Mheshimiwa Waziri wa Fedha alienda lakini Mheshimiwa Waziri Mkuu alienda. Tuna mpango wa kujenga kituo hicho. Namwomba tu Mheshimiwa Mbunge awe na subra mara tu fedha zitakapopatikana tutajenga kituo hicho.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza nishukuru Wizara kwa majibu mazuri yanayotia matumaini. Jambo hili linaenda kutatua tatizo kubwa la ununuzi, na hasa katika taasisi zetu za umma ambazo zinaingia kwenye ushindani ambazo zinashindwa kufanya manunuzi kwa sababu ya ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa miradi mingi kwenye halmsahuri zetu sasa hivi inatekelezwa kwa force account na watu wanaoingia kwenye manunuzi ni watu ambao hawana taalum; Je, Serikali iko tayari kutoa mwongozo mahsusi ili kuongoza kuona namna gani hayo manunuzi yanayokwenda kufanya kusiwe na mgongano ambao sasa hivi nani ambaye anatakiwa kujibu maswali hayo ya ununuzi?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ili kupunguza safari nyingi za maafisa ununuzi kwenda na kurudi kwa ajili ya kwenda kufanya manunuzi, Je, Serikali haioni umuhimu wa kuongeza yale masurufi (imprest) kutoka milioni tatu ili kufika milioni kumi, kwa sababu sasa hivi hakuna bidhaa inayoweza kununuliwa kwa shilingi milioni tatu? Kwa hiyo matokeo yake wale maafisa manunuzi wanakwenda na kurudi zaidi ya mara tatu kwa bidhaa moja.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mohamed Kuchauka kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kwa ridhaa yako nijibu maswali yote mawili kwa pamoja. Taratibu, mwongozo na kanuni zinatolewa mara baada ya kutunga Sheria hiyo katika Bunge lako Tukufu. Hii ndiyo nafasi adhimu baada ya Muswada kuja Bungeni ya Wabunge kutushauri na kutuelekeza. Serikali yao ni sikivu sana tutaendelea kupokea ushauri huo na kuufanyia kazi, ahsante.

MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante nami kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sheria ya Manunuzi ya Umma inaelekeza asilimia 30 kwenda kwenye makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu lakini Sheria hii inaonekana kuto tekelezeka.

Je, ni lini Serikali itatilia mkazo Sheria hii ili iweze kuleta tija kwa jamii?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Njau kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, sheria hii ipo na inatekelezwa. Tuna toa maelekezo kwa maafisa masuhuli wote ambao hawajatekeleza hili watuletee ripoti na tuwaambie kabisa watekeleze sheria hii kama ilivyowekwa.

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika manunuzi ya Serikali kumekuwepo na utamaduni wa kuongeza bei bidhaa zinazonunuliwa na Serikali ukilinganisha na bei halisi iliyoko sokoni.

Je, Sheria hii mpya inayofanyiwa marekebisho itagusa eneo hili kuhakikisha Serikali inanunua kulingana na bei ya soko?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge katika hili. Itakapopita Sheria hiyo basi zitafuatwa taratibu zote za manunuzi katika bei halisi ambayo ipo nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.

MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa miradi mingi ya Halmashauri inasimamiwa na walimu wakuu, waganga pamoja na walimu wakuu shule za msingi.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapa semina hao walimu wakuu baada ya sheria hiyo mpya kupitishwa upya?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mpakate kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema awali taratibu, kanuni na miongozo itatoka mara tu baada ya Bunge lako Tukufu kupitisha Sheria hii. Naomba Mheshimiwa Mbunge awe na subra itakapopita Sheria hii basi hayo yote anayoyatarajia yatapatikana.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Waziri uko tayari kuja Kigoma baada ya Bunge hili ili uweze kuongea na wafanyabiashara wa Wilaya zote zinazopakana na nchi ya Congo na Burundi?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Felix kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida mtoto hufuata kichogo cha mlezi wake. Kwa kuwa Mheshimiwa Rais mara nyingi anawasikiliza wafanyabiashara na hata Kariakoo alimtuma na kumwelekeza Mheshimiwa Waziri Mkuu akaenda kusimama kwa zaidi ya masaa sita kusikiliza wafanyabiashara, kwa hiyo na mimi niko tayari kwenda Buhigwe na mipakani kuwasikiliza wafanyabiashara. (Makofi)

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Mpaka wa Mutukula ambao ni mpaka wa Tanzania na Uganda ndani ya Wilaya ya Misenye ni mpaka ambao kiuchumi unakusanya mapato makubwa, lakini wafanyabiashara wa pale wanakabiliwa na utitiri wa tozo ambazo kama mazingira mazuri ya kiwekwa biashara hiyo itakua…

SPIKA: Swali lako.

MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Spika, ni lini sasa Serikali itaboresha mazingira ya biashara katika mpaka wa Mutukula?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika jitihada za kuweka mazingira mazuri ya kibiashara, kwa hiyo, siyo tu sehemu ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge, sehemu zote ambazo ziko mipakani na ambazo sio za mipakani tutajitahidi kuondoa changamoto hiyo ya biashara. (Makofi)
MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru; tatizo sio tozo peke yake kuna utitiri wa vituo bubu vya ukaguzi wa bidhaa barabarani; je, na hivyo vitaondoka lini?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kajege kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ndio inawezekana lakini naomba hili tulichukue tulifanyie utafiti tuone kama zipo changamoto hizo ambazo zinakwamisha harakati za biashara tuweze kuzipunguza ama kuziondoa kabisa.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, ni lini mtahakikisha mnaondoa askari polisi kujihusisha na ukusanyaji wa kodi kwenye mipaka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni lini tutaondoa askari polisi? Askari polisi ni chombo cha usalama, usalama wa mali na usalama wa wananchi. Hatuwezi kuwaondoa sehemu za mipakani, kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutafuatilia nini kinatokea huko katika biashara hiyo ya mipakani. (Makofi)
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tayari sasa Serikali imeshazindua Tume ya Mipango ya Taifa, je, Serikali haioni ni wakati sahihi sasa kuwa na mipango ya miaka 100 na kuendelea ya Taifa letu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, je, Serikali haioni ni wakati sahihi sasa kuanza kuwa na mpango wa maendeleo wa miaka 100 na kuanza kuitekeleza kwa kipindi cha miaka mitano mitano?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Saashisha Mafuwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa ridhaa yako naomba nijibu kwa pamoja. Ni jambo zuri kuwa na mpango wa muda mrefu sana wa hiyo miaka 100 au zaidi ya hapo lakini kwa kuwa Tume ya Mipango imeshaanzishwa au inaendelea kuanzishwa kwa sasa, huko siku za mbeleni tutaangalia suala hilo. Serikali imechukua shauri hilo na litafanyiwa kazi kadiri uwezekano utakapopatikana ikionekana kama iko tija. Kwa kuwa tayari sasa hivi tupo tunaandaa Dira ya Taifa 2050 itakayoanzwa kutekelezwa mwaka 2026 mara tu Dira ya 2025 itakapohitimishwa, ahsante.
MHE. NUSRAT S. HANJE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kusuasua kwa utekelezaji wa bajeti kadri tunavyotenga kwenye Bunge hili kipindi cha bajeti, wakati mwingine kuchelewa kufika au kufika kwa asilimia ndogo. Sasa naomba kufahamu mkakati wa Serikali kutatua changamoto hii, kwa sababu tukitenga bajeti tunatarajia ifike kama tunavyotenga.

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Natamani kufahamu mpaka sasa hivi Serikali imechukua hatua gani kwa Watendaji ambao wamekuwa siyo waaminifu na wabadhilifu wa mali za umma hususan bajeti kadri tunavyotenga badala ya kusubiri taarifa ya CAG pamoja na Mwenge? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nusrat Hanje, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutoa fedha kama zilivyotengwa katika bajeti kadri ya fedha zinavyopatikana. Kwa kuwa, mfumo wetu wa bajeti ni cash budget, pesa zitakusanywa ili ziweze kutumika katika bajeti, hivyo Serikali itaendele kukusanya na kuongeza uwezo wa ukusanyaji wa mapato ili tuweze kutekeleza bajeti kama ilivyopangwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili. Serikali imechukua hatua mbalimbali kwa wale watumishi ambao siyo waadilifu. Hatua hizo ni pamoja na kuwafikisha Mahakamani, wako wale ambao wamefungwa sasa, wako ambao wamesimamishwa kazi na wako ambao wamefukuzwa kazi. Ahsante. (Makofi)
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, Serikali sasa haioni kuwa ni wakati muafaka wa kukitumia kitengo cha Ukaguzi wa Ndani kuweza kufatilia bajeti?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inakitumia ipasavyo kitengo hiki cha Ukaguzi wa Ndani na tumekiongezea uwezo mwaka huu uliopita na mwaka ujao tumetenga kuongeza uwezo wa kufanya ukaguzi unaostahiki.

MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Moja ya eneo ambalo Serikali inatekeleza chini ya asilimia 50 kwenye bajeti na mpango ni ahadi za Viongozi wa Kitaifa.

Je, ni upi mkakati wa Serikali kumaliza ahadi zote za Viongozi wa Kitaifa za miaka ya nyuma? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mtemvu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuimarisha mawasiliano lakini inaendelea kuimarisha makusanyo ya fedha, na hivi nimuombe Mheshimiwa Mbunge naye awe ni Balozi wa kushawishi na kuwashauri wafanyabiashara pamoja na yeye na mimi kuendelea kukusanya kodi ili tuweze kutekeleza ahadi za viongozi wetu kwa wakati.
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Katika taasisi ambazo zinalalamikiwa sana kwa uonevu na kukithiri kwa rushwa ni pamoja na TRA, hili linasababishwa na kujadili kodi ana kwa ana kupitia utaratibu wa sasa. Sasa kwa kuwa taratibu hizi zimekuwepo kwa miaka 22 iliyopita, TRA haioni kwamba inahitaji mabadiliko ya haraka ya kuondoa mawasiliano ya ana kwa ana ili kudhibiti jambo hilo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; dunia sasa inafanya biashara zaidi kupitia mitandao na imethibitika kwamba TRA bado wanaendesha makadirio yao kianalogia. Ni hatua zipi za haraka ambazo inachukua ili kuweza kukusanya kodi ambayo inapotea kwenye mitandao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kanyasu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa ipo changamoto ya mifumo na ipo changamoto hiyo ya kukutana ana kwa ana kati ya Mlipa Kodi na Afisa Kodi. Serikali hatua ambayo imechukua ni kuimarisha mifumo kuhakikisha kwamba Mlipa Kodi na Afisa Kodi hawatokutana ana kwa ana ili kuepusha hiyo mianya ya rushwa.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili. Serikali kupitia Bunge lako Tukufu lilifanya marekebisho ya sheria pamoja na kuanzisha Kitengo Maalum kwa ajili ya kusimamia kodi za biashara, mtandao na kuhakikisha kwamba utambuzi wa mfanyabishara ya kimtandao amesajiliwa na kulipa kodi inayostahiki.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa nafasi, katika majibu ya msingi ya wizara inaonesha wanazungumzia zaidi biashara kati ya nchi ya Zambia na Tanzania, lakini geti la Tunduma ninaongelea ni biashara kati ya nchi ya Zambia na nchi ambazo ziko SADC ambazo ni zaidi ya saba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maswali yangu ya nyongeza kama yafuatavyo; kabla ya maboresho ya bandari zetu lile ilikuwa asilimia 70 ya mizigo inapitia geti lile, kwa hiyo tafsiri yake kama tumeboresha bandari zetu na Kongo wameingia kwenye East Africa ina maana kwamba nchi zingine zitapitisha mizigo pale.

Je, Serikali haioni kuna ulazima na uharaka sana kuhakikisha wanaongeza geti lingine ili kuboresha huduma na ufanisi unaotakiwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kama ambavyo ziko nchi nyingine ambazo tunapakana nazo, mfano Kenya, kuna mageti ya forodha zaidi ya mawili au matatu, mfano Holili, Namanga, Tarakea na lile geti la Mombasa na Mheshimiwa Waziri alifanya ziara kwenye Jimbo la Momba mwaka jana.

Je, hamuoni sasa kuna haja kabisa ya kuhakikisha nchi ya Zambia ambayo inahudumia nchi zaidi ya saba ya SADC kupata geti lingine ndani ya Jimbo la Momba ili kuhakikisha tunaongeza mapato?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Momba kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama yanafanana maswali yake yote mawili kwa hiyo ni suala moja na nimesema katika majibu yangu ya msingi kwamba Serikali inafanya uchambuzi na tathmini kupitia katika sehemu hiyo pamoja na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi tukiona Serikali ipo haja ya kuongeza geti basi Serikali yetu ni sikivu, na iko tayari kufanya hivyo, ahsante.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, majibu ya Waziri yanaonesha kwamba deni la pre-1999 ni shilingi trilioni 4.4 lakini ripoti ya kikosi kazi cha Serikali yenyewe pamoja na ripoti ya CAG ambayo ilitolewa mwaka 2015 inaonesha deni la Serikali la pre-1999 ni shilingi trilioni 7.1.

Sasa nataka Waziri uniambie hiyo tofauti ilitokea lini na wapi na kwa sababu gani?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili Mfuko wa NSSF umesema Serikali inadaiwa shilingi bilioni 292 ripoti ya CAG iliyotoka juzi inasema Serikali inadaiwa shilingi trilioni 1.17 hiyo tofauti kati ya bilioni 200 na trilioni moja imetokana na nini?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza alikuwa anaulizia tofauti imetokeaje, naomba hili tulichukue kama ni ushauri na tutamjibu kwa njia ya maandishi.

Mheshimiwa Spika, swali la pili pia amehitaji tofauti tunaomba pia tulichukue na kwenda kufanya review bila shaka tutapata majibu yaliyo sahihi. (Makofi)
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwenye tathmini ya Serikali kati ya bidhaa ambazo zimeathiriwa na vita ya Urusi ya Ukraine ni mafuta ya nishati, mbolea na ngano.

Je, Serikali haioni umuhimu wa kufuta VAT kwa wazalishaji wa mafuta ya kula ndani ya nchi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Nancy Hassan Nyalusi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, suala hili limejadiliwa na suala hili ni ushauri, linahitaji wataalam, tutakaa pamoja tutatoa majibu. Nadhani pengine leo ama kesho tutatoa jibu la suala hilo.
MHE. ABDUL-HAFAR IDRISSA JUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali lakini ningependa kujua: -

Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na Maafisa Maalum walio chini ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watakaokuwa wanasimamia fedha hizi kwa upande wa Zanzibar badala ya kutegemea Maafisa wa Serikali ya Mapinduzi ambao hawawajibiki moja kwa moja katika Bunge letu?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Abdul-hafar Idrissa Juma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali hilo, kwa ruhusa yako naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Abdul-hafar kwa namna anavyopigania Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo lake na majimbo mengine ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, Sheikh Abdul-hafar swali lako kama ushauri tumelichukua tunakwenda kushauriana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tuone kama ufanisi utapatikana zaidi kwa kuweka Maafisa kule basi Serikali yako ni sikivu na inaweza ikafanya hivyo. (Makofi)
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Spika, ahsante kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Wananchi na wafanyabiashara wamekuwa na mwamko mdogo wa kudai risiti.

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu ili wananchi na wafanyabiashara wawe wanadai risiti?

Swali la pili; Wafanyabiashara wengi hawana mashine hizi za EFD pia zilizopo nyingi ni mbovu, unapokwenda madukani unakuta hawana mashine.

Je, Serikali sasa ina mpango gani wa kununua mashine kusambaza kwa wafanyabiashara wote ili kuongeza mapato? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Innocent Bilakwate kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wananchi wengi wana mwamko mdogo wa kudai risiti na baadhi ya wafanyabiashara wanakuwa wazito kutoa risiti. Mikakati ya Serikali ni kutoa elimu, kuendelea kuhamasisha na nitoe wito kwa TRA kuendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari vyote ndani ya nchi ikiwezekana hata nje ya nchi, vile vyombo ambavyo huwa vinasikilizwa sana. Pia ninawaomba Wabunge wenzangu kutoa taaluma hiyo kwa wananchi wetu kudai risiti baada ya kununua bidhaa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, tunaliangalia kwa kweli kutoa mashine za EFD tunaweza tukatoa hivyo hapo baadaye, kwa mwaka huu wa fedha hatutaweza kutoa lakini tutalingalia baadaye ikionekana ipo haja na fedha ipo ya kutosha basi tutatoa mashine hizo kwa wananchi wetu.
MHE. BENARDETA K. MUSHASHU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana naomba kuuliza swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, mashine za EFD ni za gharama sana lakini mtu akibadilisha biashara kwa maana ya TIN analazimika kununua mashine mpya. Kwa nini Serikali isiweke utaratibu wa badala ya kununua mashine mpya wakaondoa ile program akaendelea kutumia mashine ile ile kwa kubadilisha tu program? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mbunge huo ni shauri tunauchukua na tunaufanyia kazi. (Makofi)

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Kwanza, namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri ambayo yametuwekea kumbukumbu kwamba, mara ya mwisho tulibadilisha fedha mwaka 1997 lakini jibu langu bado sijalipata. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, ni mara ya kwanza kupata Rais Mwanamke Tanzania na Afrika Mashariki, ambaye ni mchapa kazi, jasiri na ameonyesha uwezo wa wanawake. Ambaye ameweza kutupa sifa Tanzania, Afrika na dunia nzima. Je, Serikali haioni kwamba, sasa ni wakati mwafaka wa kuweka sura ya Rais wa Kwanza Mwanamke katika Noti za Tanzania? (Makofi)

Swali langu la pili, kwa kuwa, Rais wa Kwanza wa Zanzibar amepewa nafasi katika sarafu ya Shilingi 500 na kutokana na kupanda kwa uchumi sasa hivi, Shilingi 500 haitumiki sana. Je, Serikali haioni kwamba sasa hivi ni fursa pekee ya kupandisha pia hadhi ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, kumuongezea noti juu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Angelina kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu suala hili zipo taratibu mbalimbali ambazo hutumika katika uwekaji wa alama kwenye noti zetu au sarafu yetu. Hizi lazima zizingatie kufuata Taratibu, Sheria na Kanuni. Muda wa suala hili ukifika basi, maoni yake tumeyachukua na tunaenda kuyafanyia kazi. Muda ukifika zitawekwa, Inshallah. (Makofi)
MHE. JUMA OTHMAN HIJA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa changamoto zinazoikabili mtaji wa sekta binafsi ni viwango vya riba katika benki zetu. Je, Serikali ina mpango gani kudhibiti viwango hivi vya riba? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Juma Othman Hija, Mbunge wa Tumbatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania ilishatoa trilioni moja kwa benki ili kutoa mikopo hasa ya kilimo kwa riba nafuu, isiyozidi asilimia 10 na zipo Benki zetu kama vile CRDB, NMB katika dirisha la kilimo wapo na single digit. Nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imezingatia na itaendelea kuangalia viwango vya riba kulingana na hali ya uchumi nchini, ahsante.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa Benki Kuu ya Tanzania ndio custodian wa waendesha biashara za benki nchini Tanzania.

Je, ni lini Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania itachukua hatua ya kuwafidia waliokuwa wateja wa SBNE pamoja na wafanyakazi kuwalipa haki zao kama vile inavyofanya SMZ - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imewalipa wateja wa Master Life waliopata kadhia kama hiyo? Sasa Serikali hii yetu ya Tanzanzania itafanya nini na kwa nini haiwapi taarifa wananchi kuhusu kadhia hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asha Mshua, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua hatua mbalimbali kutoa fidia kwa wale waathirika wa benki kama zilivyotokea wakati huo na bado Serikali ipo inafanya upembuzi, fedha itakapojitosheleza na kujiridhisha Serikali itatoa fidia kwa wananchi wake. (Makofi)
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Tunatambua kwamba kuna mwongozo ambao umetolewa na Wizara ya fedha ku-regulate riba kwenye microfinace hapa nchini, lakini mwongozo huo haufuatwi na hizo taasisi za kutoa fedha wakati mwingine zinachukua hadi kadi za ATM za watumishi wanaokwenda kukopa pale, Serikali inasema nini juu ya hili ili miongozo hiyo iweze kufuatwa?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali siku zote inafuata miongozo na taratibu ambazo zimewekwa, kama zipo changamoto ambazo ameziona acha tuzichukue twende tukajadili, tuangalie, tukijiridhisha basi tutazifanyia kazi. (Makofi)
MHE. JUMA USONGE HAMAD: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bidhaa ambazo tayari za mifugo hususan ng’ombe pamoja na mbuzi kwa Zanzibar ni adimu sana, lakini pia bei yake inakuwa ni ghali sana. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuhakikisha kwamba kufuta, lakini pia kupunguza kodi zote zile ambazo zinakuwa-charged pale bandarini kwa upande wa Tanga pamoja na Kitumbwi, bandari ya Tanga ili sasa kumpunguzia Mtanzania wa Zanzibar gharama nafuu bidhaa ile ya ng’ombe kama wa Bara?

Mheshimiwa Spika, lakini swali la pili; je, ni lini hasa Mheshimiwa Waziri utapanga safari ya kwenda bandarini kwenda kushuhudia namna Watanzania wanavyolazimishwa kulipa kodi maeneo ya bandarini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Juma Usonge Hamad kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, suala la usafirishaji wa nyama za mbuzi, ng’ombe na wanyama wengine ni kweli kwamba kupeleka Zanzibar ni nyama adimu hazipatikani sana, lazima tunavusha kutoka bara kwenda kule. Lakini suala la ufuataji wa kodi na tozo naomba hili tulichukue tulifanyie mchakato kwa sababu ni suala la kisheria.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili kuhusu kwenda kutembelea ili kuona hali halisi naomba niambatane mimi na yeye mara tu Bunge hili litakapomalizika tuende tukatembelee katika sehemu husika. (Makofi)
MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri kwa kweli ya Naibu Waziri lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, maboresho aliyoyasema Mheshimiwa Naibu Waziri ni makubwa. Je, hayo maboresho yametusaidia kuongeza kaguzi kiasi gani ikilinganishwa na kaguzi zilizokuwepo ambayo ilikuwa ni asilimia 1.2 kati ya makampuni 504 yanayojihusisha na miamala ya transfer pricing?

Swali la pili, Je, maboresho hayo yaliyofanywa na TRA yametuwezesha kuokoa fedha kiasi gani zilizokuwa zinapotea kutokana na kukosekana uwezo ndani ya nchi wa kukagua miamala ya transfer pricing?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Luhaga Joelson Mpina, kama ifuatavyo:-

Maboresho hayo ambayo tumefanya kupitia TRA yameongeza asilimia 4.5, mwaka uliopita kabla kufanya maboresho hayo ilikuwa tuko asilimia 1.2 lakini sasa tuko asilimia 4.5 kwa hiyo ni hatua kubwa sana ambayo tumepiga.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni suala la kitakwimu naomba tumpelekee kwa maandishi. (Makofi)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali katika huduma za miamala hapa kwetu nchini, mara nyingi mashine za huduma kwenye maeneo ya huduma za fedha, zinaonyesha kwa muda huu hatutakuwa na huduma ya upatikanaji wa risiti.

Je, kama ni tatizo la kimfumo Serikali haioni kuwa inapoteza mapato?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama kulikuwa na tatizo hilo la risiti ilikuwa ni tatizo la muda mfupi na tayari tatizo hilo tumeshaliweka sawa. Sasa manunuzi yoyote yatakuwa yanatolewa risiti kwa njia ya elektroniki bila shaka nikutoe shaka Mheshimiwa Mbunge, kwa sasa hakutokuwa na mwanya wowote wa kupoteza mapato yetu. (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi, kwa kuwa Julai, 2021 Waziri wa Fedha na Mipango alifanya ziara na kutembelea Kituo hicho cha Forodha na majibu ya Serikali yanasema kwamba, wanafanya tathmini kwa kina.

Je, tathmini hiyo ya kina itachukua muda gani kukamilika (time frame)?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kutokana na umuhimu wa Kituo chenyewe cha Forodha cha Tunduma, kwa sababu kimebeba nchi nyingi za Kusini mwa Afrika - SADC na kituo kile kuonekana kuzidiwa katika kutoa huduma za forodha. Je, Serikali haioni kuna haja na uharaka sana wa kuongeza Kituo kingine cha Forodha kwenye ule mpaka ambako ni Kakozi, kwa ajili ya kunusuru mapato yanayopotea na kuongeza mapato kwa Taifa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Condester. Hata hivyo, kabla ya kujibu naomba nimpongeze sana kwa namna anavyofuatilia kituo hiki.

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini itakamilika ndani ya mwaka huu wa fedha. Nimwombe tu Mheshimiwa Mbunge awe na subira, Serikali iko kazini na atapata mrejesho.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, naomba nimwelekeze Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, aangalie uharaka wa ujenzi wa kituo hicho huko Kakozi – Momba, endapo atajiridhisha kutokana na tathmini yake.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ambayo Mheshimiwa Waziri ameyatoa lakini kwa kuwa ni Wizara yake ya Fedha nilitaka nitoe maelezo haya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Benki Kuu inafanya juhudi kubwa ku-rescue Benki ya MUCOBA ya watu wananchi wadogo kabisa mamantilie na wafanyabiashara wadogo waliochanga fedha zao kuanzisha benki hiyo, chombo chao kimoja chini yake TRA kinafanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba benki hii inakufa kwa kuwachukulia fedha zaidi ya milioni 600 ambazo zilichukuliwa katika Benki ya NMB Tawi la Mkwawa kwa kisingizio cha kodi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hao mliowatafutia kupitia Benki Kuu, Benki ya Watu wa Zanzibar kuwekeza katika Benki ya MUCOBA Community, wameshindwa kuendelea na azma ya kuwekeza ku-rescue benki ile kwa sababu wameogopa TRA watakuja tena kuchukua fedha, kwa hiyo, wametoa fedha zao bilioni mbili katika benki ile na kuacha benki ile ikiwa mufilisi, haiwezi kujiendesha tena na fedha za watu wa chini kushindwa kuendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la nyongeza kwenye hapo, mimi naomba kujua nia yenu ya Wizara ya Fedha ya dhati katika kutekeleza 4R za Mheshimiwa Rais hasa kuhakikisha mnarudisha fedha hizo ambazo TRA wamechukua katika Benki ya MUCOBA, kuhakikisha mnarudisha fedha mlizochukua kwenye Bureau de change, kuhakikisha hamuendelei kuwabuguzi wafanyabiashara kwa madeni ya miaka iliyopita. Mpo tayari kama Wizara kuzitekeleza 4R za Mheshimiwa Rais?
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge makini kwa ufuatiliaji wa jambo hili linalohusu wananchi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niweke kumbukumbu sawa kwamba lile jambo la kwanza fedha hazikuchukuliwa kwa kisingizio cha kodi bali ilikuwa ni kodi halali, lakini naielewa hoja yake kwamba Benki hii inahudumia watu wakawaida na Serikali ya Mheshimiwa Rais imeshafanya jitihada za kuwasaidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niombe, kwa kuwa Mbunge amekuwa akilifuatilia sana jambo hili, tayari tulishaongea na mamlaka ya mapato Tanzania na wameridhia kukutana na uongozi wa benki hii ili kuweza kuona namna bora ya kuwasaidia na wananchi wale wasiweze kuondoa fedha hizo na kuweza kulimaliza ili benki iweze kujiendesha na kutoa zile huduma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo naomba Mheshimiwa Mbunge, wataarifu Viongozi wa Benki hii waonane na viongozi wa juu kabisa wa Mamlaka ya Mapato ili kuweza kuli-sort hili na kuweza kutoa fursa ili benki iweze kuendelea kufanya kazi. (Makofi)
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kabla ya swali Mheshimiwa Deo Sanga anashukuru sana kwamba malipo ya fidia ile yamefanyika na swali lake namba moja ni kwa sababu malipo yameshafanyika na lile eneo la makaburi siyo kubwa, Serikali haioni umuhimu wa kulipa haraka ili ipate uhuru wa kuendelea na ujenzi wa One Stop Centre pale Makambako?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; pale Kilolo ambapo Makao Makuu ya Wilaya yamejengwa, kuna madai ya fidia ya muda mrefu na yalikwishawasilishwa Hazina mara kadhaa. Je, Serikali haioni umuhimu wa kuyaharakisha malipo yale ili wale wananchi pia waweze kupata haki yao? Nakushukuru.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Nyamoga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kuhusu ulipaji wa fidia kule Idefu, Makambako, kwa kuwa tumeshalipa fedha nyingi sana shilingi bilioni 4.6 kilichobakia ni kidogo tu ni shilingi milioni 100. Naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ndani ya mwaka huu wa fedha tunaenda kulipa fidia iliyobakia. Upande wa Kilolo Serikali ipo tayari kufanya haraka, tunasubiri tu Mthamini Mkuu aweke idhini, akishatoa idhini yake tunaenda kulipa hiyo. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Je, ni lini Serikali italipa fidia kwa wananchi wa Gona, Sehemu ya Njia Panda pale Himo na Mabungo pale Uchira ambao nao wamepisha Serikali kujenga one stop center ya customs? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali ya nyongeza la Mheshimiwa Kimei, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Kimei suala hilo linatambulika Serikalini na tunalifanyia kazi. Awe na subira, fidia hiyo katika eneo alilolitaja italipwa kwa wakati mahususi. Ahsante. (Makofi)
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia fursa hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mamlaka ya utoaji msamaha wa kodi yamewekwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, sasa Serikali haioni haja ya kugatua madaraka na kuwapatia mamlaka mameneja wa mikoa ili waweze kutoa misamaha hiyo ya kodi ili kurahisisha kazi za ujenzi wa barabara ufanyike kwa haraka? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na malimbikizo ya madai ya VAT kwa wakandarasi, sasa Serikali haioni haja ya kuweka mchakato rahisi wa kuweza kuwalipa haraka wakandarasi hao ili waweze kutumia fedha zao ili kuijiendeleza kwenye miradi yao ya ujenzi wa barabara? Ahsante (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, ushauri wake Mbunge umepokelewa na unaenda kufanyiwa kazi hasa katika kipindi hiki cha ukusanyaji wa maoni, Serikali itaangalia na wataalamu wetu watatushauri, kama ipo tija ya kupeleka mikoani, basi Serikali itafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, madeni ya makimbikizo ya madai ya VAT Refund, yaliyo mengi tayari yameshahakikiwa na yamelipwa na yale ambayo yamewasilishwa siku za karibuni, yanahakikiwa na yakikamilika tu Serikali italipa refund hiyo. (Makofi)
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU: Mheshimiwa Spika, namshukuru Waziri kwa majibu mazuri. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Tanzania ilipoingia kwenye uchumi wa kati wa chini, baadaye lilikuja tatizo la Corona na sasa hivi tuna-experience mgogoro wa kivita wa Ukraine; dunia inatabiriwa kuwa na mgogoro mwingine wa kiuchumi; Tanzania itaathirika vipi iwapo mgogoro huo utatokea? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini swali langu la pili, katika jibu lake la swali langu la msingi Mheshimiwa Naibu Waziri amesema moja ya sifa ya nchi inapoingia kwenye uchumi wa kati ni kuwa na sifa ya kukopeshwa mikopo ya kibiashara. Hata hivyo zimekuwepo lawama baada ya Tanzania kukopa kibiashara: Ni nini mtazamo wa Wizara iwapo tutaendelea kukopa kibiashara wakati wengine wanaona pamoja na sifa hiyo tunayo, tusikope kibiashara? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Constantine John Kanyasu, Mbunge wa Geita Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimhakikishie Mbunge kwamba, nchi yetu bado haijashuka katika uchumi wa kati chini, bado tuko pale pale. Pamoja na changamoto zote hizo, kilichotokea ni kushuka kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja tukatoka 7% kuja 4.8%.

Mheshimiwa Spika, lakini swali lake la pili, kauli ya Serikali ni kwamba wananchi waache kuwa na lawama kwa sababu Serikali yao iko makini sana katika kufanya tathmini aina gani ya mkopo nchi yetu iingie, na una tija gani kwa maslahi ya Taifa letu?
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, naomba kuishukuru Serikali kwa majibu yake mazuri, lakini naomba niulize maswali mawili ya ziada.

Swali la kwanza, kwa kuwa suala la utafiti ni suala linalochukua muda, je, Serikali inaweza ikawaambia wananchi ni lini wanategemea kumaliza utafiti huu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa sababu mifumo ni jambo kubwa, je, Serikali iko tayari kuendelea kutoa taaluma zaidi kwa wadau ambao wanasumbuka sana na mifumo hii? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zahor, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tathimini hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Fedha wa mwaka 2024 ambao unatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lako Tukufu ndani ya mwaka huu na Bunge hili la Bajeti.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, Serikali kupitia taasisi zake imekuwa na utamaduni na imekuwa na desturi ya kutoa mafunzo siku hadi siku kwa wadau wanaostahiki, ahsante sana.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa sheria hii inataka kwenye kila manunuzi asilimia 30 ziweze kunufaisha makundi maalum ya vijana na wanawake;

Je, Serikali haioni umuhimu wa kutoa maelekezo mahususi kwa Maafisa Masuhuli wote nchi nzima ili waweze kufuata sheria hii? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zaytun Swai kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kila siku inayokwenda tunatoa maelekezo kwa maafisa wetu wa ununuzi; na hivi karibuni tarehe 30 Mei tulizindua kanuni maalum ambazo tumeziweka meno zitakazosaidia katika kuzingatia masuala yote ya kisheria na taratibu. Pia nachukua fursa hii kutoa maelekezo kwa maafisa masuhuli wote wa ununuzi nchini wazingatie sheria na taratibu zilizowekwa. (Makofi)
MHE. MUSSA R. SIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, lakini nina swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa, ziko ofisi za muda zinatumiwa katika Wilaya ya Mkalama pale na maafisa wa TRA na wakimaliza kazi wanarudi kwenye Wilaya ya Iramba.

Je, wakati wanasubiri kujenga ofisi zao kamili, Serikali haioni haja sasa ya kuweka wafanyakazi wakawepo kwa muda wote hapo Wilaya ya Mkalama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mussa Sima. Kabla ya kujibu swali hilo naomba nimpongeze sana kwa juhudi zake katika kuwatetea wananchi wa jimbo lake. Serikali itaangalia uwezekano wa kuweka watumishi wa kudumu wakati wa kusubiria ujenzi huo wa ofisi katika eneo husika, ahsante. (Makofi)
MHE. USSI SALUM PONDEZA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza napenda kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa vile majibu mazuri ya Serikali Naibu Waziri amesema kama kuna maduka yalikuwa yamefungwa na Serikali kutokana na utakatishaji wa fedha. Yako maduka ambayo yamefungwa na baadaye ikajulikana kama hayana makosa hayo ya utakatishaji wa fedha. Je, Serikali iko tayari kuwarudishia wale ambao walifungiwa lakini hawana shutuma hizo za utakatishaji wa fedha ambao fedha zao na mali zao zilizochukuliwa na Serikali?

Mheshimiwa Spika, la pili, je, ni lini sasa wale wote ambao wameonekana hawana hatia maduka yao yatafunguliwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan haiko tayari kuona kwamba kuna rasilimali fedha ya mtu au rasilimali yoyote imebaki Serikalini kumnyima mtu huyo haki yake. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba wale wote ambao wameonekana maduka yao hayana makosa yoyote watarejeshewa fedha zao na rasilimali nyingine zote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, maduka yaliyosalia, maduka yote ambayo yamefungwa yalikuwa ni 68 wakati ule. Maduka yaliyobaki sasa ni maduka saba tu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika hayo saba yatafunguliwa muda wowote. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Fedha.

WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kwanza kumpongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri. Naungana naye kuongeza taarifa kwamba hiki alichokisema Mheshimiwa Naibu Waziri kwamba Serikali ya Awamu ya Sita haiko radhi kuona fedha za raia mwema zinashikiliwa na Serikali. Kwa kipande kingine kulikuwa na component ya kodi ambayo ilikuwa imezidishwa, niongezee na hiyo kwamba kile kipengele cha kodi ambayo ilikuwa imezidishwa tayari kilisharejeshwa kwa wale waliokuwa wanahusika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, hiki alichosema Mheshimiwa Naibu Waziri na chenyewe kitaendelea kwa wale ambao walikuwa na baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa kwenye mikono ya Serikali. (Makofi)
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa fedha hizi Serikali imekaa nazo kwa muda mrefu na kwa kuwa fedha hizi zilikuwa ni za biashara. Je, wakati inarejesha fedha hizo zitaambatana pamoja na riba? (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Agnesta, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kweli nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali haitorejesha fedha hizo kwa riba kwa sababu wafanyabiashara walifanya makosa na wenyewe wamekiri makosa hayo.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nampa pole Mheshimiwa Mbunge Twaha na wananchi wa Kibiti kwa mafuriko makubwa yanayoendelea kule, lakini pamoja na hayo, nina maswali mawili ya nyongeza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kwa kuwa, jibu la msingi limeonyesha utayari wa Serikali kufungua Ofisi ya Forodha katika Bandari ya Nyamisati; na kwa kuwa, Bandari ya Nyamisati imeonesha ofisi katika Mamlaka ya Mapato (TRA). Naomba kujua, je, Serikali ipo tayari mpaka Desemba, 2024 ofisi hiyo iwe imefunguliwa kwa umuhimu wake wa kuongeza mapato? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa, wafanyabiashara wa vyombo vya mashua kutoka Zanzibar wapo tayari kusafirisha bidhaa kwa kutumia Bandari ya Nyamisati kwa sababu ina miundombinu iliyo kamili. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kushirikiana na Mbunge Twaha pamoja na mimi Mbunge wa Mkoa kukutana na wafanyabiashara hao ili kuzungumza na kuwatia moyo katika maandalizi ya kutumia Bandari ya Nyamisati? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Subira, Balozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iko tayari na ndiyo maana katika jibu la msingi tumesema Mwaka huu wa Fedha 2024/2025 forodha hiyo itafunguliwa. Kwa hiyo, Serikali iko tayari haitafika Disemba tutakuwa tumeanza zoezi hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili, Naibu Waziri yuko tayari kuambatana na Mheshimiwa Mbunge Twaha na Mheshimiwa Balozi wetu Bi. Subira kwenda kukaa na wafanyabiashara hao. Ahsante sana.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa majibu mazuri ya Serikali yanayoonesha kwamba kuna juhudi kubwa inafanyika, lakini kwa sababu ya magari haya ya mitambo hii kwenye halmashauri zetu huwa zinachukua muda mrefu sana kiasi kwamba inafanya kwamba Serikali ipate hasara na vingenevyo ni kuwa uchafu kwenye halmashauri zetu.

Je, ni mkakati upi unaofanywa na Serikali kuhakikisha magari haya yanaondolewa kwa wakati na Serikali isiendelee kupata hasara? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, mchakato mzima wa kuyaondoa hayo magari tangu gari linapooneka kwamba haliwezi kutengenezeka mpaka unaenda kuliingiza kwenye mnada mchakato huo unachukua muda gani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Kuchauka, naomba nimpongeze kwa ufuatiliaji wa suala hili.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza ni wajibu wa taasisi husika na halmashauri wanaotakiwa kuzipitia na kubaini gari chakavu au vyombo vya moto chakavu na kuripoti kwa kufuata taratibu Serikalini. Kwa hiyo, nielekeze ama niwaombe ndugu zangu wanaoongoza taasisi hizo kufuatilia na kuhakiki, wakibaini kwamba gari hizo ni chakavu basi walete taarifa kwa Wizara ya Fedha, Wizara ya Fedha itahakiki na kutoa vibali kwa ajili ya kuuza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, hakuna muda maalumu, sipokuwa vipo vigezo ambavyo vinaashiria kwamba sasa gari limekuwa chakavu vigezo hivyo kwa mfano kama mileage yaani kama imetembea kilometa zaidi ya 500,000, ama gari umri ambao imeishi umri mrefu zaidi ya miaka nane, lakini ajali kubwa, mazingira ya gari, lakini mabadiliko ya teknolojia, ahsante.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwa kuwa magari haya yapo mengi pia katika Wizara na Taasisi za Serikali na tuna Vyuo vya VETA tulivyojenga nchini vinahitaji magari ya kufundishia.

Je, Serikali haioni ipo haja sasa ya baadhi ya magari haya yakapelekwa kwenye Vyuo vya VETA kwa ajili ya kufundishia utengenezaji wa panel beating (uundaji wa magari) na mechanics na umeme wa magari? Wakati ndio huu. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Kawawa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Kawawa ametoa ushauri, ushauri wake umepokelewa tunaenda kuufanyia kazi. (Makofi)
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza, swali la kwanza; kwa kuwa Serikali imekiri kwamba, kuna athari hasi kwenye michezo hiyo na kwa kuwa vijana wa kiume ndiyo waathirika wakubwa wa michezo ya kubashiri ambayo inachangia ukatili wa kudhuru mwili, ukatili wa kingono, ukatili wa kiuchumi na kusababisha hata matatizo ya afya ya akili. Je, Serikali iko tayari kupitia utoaji leseni wa makampuni haya ya kubashiri hasa yale ya mabonanza ambayo yametapakaa kote nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa michezo hii ya kubashiri mtandaoni inafanya vizuri, makampuni kama SportPesa, M-Bet na kadhalika na yako chini ya Wizara ya Fedha ambayo kimsingi ina majukumu mengi na inashindwa kuisimamia kwa ufanisi. Je, Serikali ipo tayari sasa kuihamisha Bodi ya Michezo kutoka Wizara ya Fedha ambayo kwa msingi wa hoja hii imeshindwa kuratibu eneo hili vizuri na kuipeleka kwenye Wizara ya Michezo ambayo kimsingi ndiyo inayosimamia eneo la burudani na sehemu hii ya michezo ya kubashiri ya mtandaoni ni sehemu ya burudani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Shangazi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kumpongeza sana kwa kiasi alichofuatilia jambo hili na kimsingi najua dhamira yake ni kuimarisha maadili ya vijana wetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake la kwanza, nataka nimwambie kwamba, Serikali ipo tayari kupitia na kuangalia uhalali na wale wote ambao watakuwa wanaendesha michezo hii, kinyume na taratibu na sheria zetu basi zitaondolewa leseni zao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, Serikali imechukua ushauri wake wataalamu watakaa, wachambue, tukiona upo umuhimu au ipo haja ya kwenda huko, basi Serikali haitasita kuchukua hatua.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Kwa kuwa Serikali imeonesha nia ya kuhamisha sports betting kutoka Wizara ya Fedha kwenda Wizara ya Michezo, je, ni kwa namna gani Serikali inajipanga kushirikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya kulinda maadili ya watoto hasa kwenye michezo inayochezwa majumbani, maarufu ya Kichina? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba, Serikali ina mikakati tofauti tofauti ya kulinda ipasavyo maadili ya vijana wetu. Suala la kushirikisha Serikali za Mitaa bado ni eneo la Serikali, kwa hiyo, ushauri wake tumeuchukua na tutaufanyia kazi, ahsante.
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nimesema watoto wanaoathirika ni kuanzia miaka tisa mpaka 17, watoto hawa wote bado wako shuleni. Ili kuweza kuokoa kizazi hiki, Serikali mko tayari kusitisha michezo hii hususani michezo ya kubahatisha ya bonanza ambayo ndiyo ipo huko kwenye halmashauri zetu na ndiyo hao watoto wadogo wanayoicheza ili kutoa elimu na kwa ajili ya kuokoa kizazi chetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kulinda maadili ya vijana wetu na siyo tu vijana hata wananchi wake. Tunachomhakikishia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, Serikali itaenda kufuatilia na ikijiridhisha kama yanayofanyika yako kinyume na sheria na taratibu, basi Serikali inaweza kuchukua hatua yoyote ambayo inastahiki. Ahsante. (Makofi)
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na kwamba wamefanya kazi nzuri ya kuliona hili. Je, Serikali sasa haioni haja ya kwenda mbali zaidi, kwa sababu hata nyuzi ya kiatu ya Askari bado ni silaha. Serikali haioni sasa kuwaachia vyombo vyetu vya ulinzi fursa kamili ya kuwa na msamaha? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ushauri wake umepokelewa, kwa sababu amesema huoni haja ya kutanua wigo. Tumepokea ushauri huo na tutaufanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa nchi hii ili ufanye biashara unahitaji tax clearance na tax clearance inahusisha ulipaji wa kodi. Je, ni kwa nini Serikali isiainishe aina za biashara ambazo unaweza kupata leseni bila kuwa na tax clearance mpaka u-run biashara kwa muda fulani ili uweze ku-file na kulipa kodi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida tax clearance hutolewa, aah! Kiingereza. Cheti kile hutolewa baada ya biashara na Serikali inasema kwamba, mtu aanze kufanya biashara kwanza ndiyo anaenda kuomba hicho cheti cha ruhusa ya kufanyia biashara. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Sasa hoja yake si ni kwamba, hiyo biashara hawezi kuanza bila leseni? Yaani ni kwamba yale maombi ya leseni ili biashara yake afanye kwa utaratibu wa kisheria, unataka hiki cheti kwanza, ndiyo swali lake liko hapo.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, nakumbuka mwaka jana tulijibu swali kama hili na tukatoa maelekezo kwa Commissioner General wa TRA kwamba, yeyote ambaye ameanzisha biashara, lakini biashara ile bado haijafanya kazi na faida yake kuonekana, apewe cheti hicho ili aende akapate leseni ya kufanya biashara. Asiwe na kikwazo kwa sababu hajapata hiyo tax clearance.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali na nimefuatilia ndiyo inavyokuwa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Serikali ilifanya utaratibu mzuri wa kurekebisha kile kikokotoo, lakini kuna wastaafu ambao walituahidi kwamba wale ambao waliathirika na kikokotoo basi ile sehemu yao ambayo ilikuwa imeathirika kwa marekebisho mapya watawalipa, je, wataanza kuwalipa lini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili ni hili; kwanza na-declare interest kwamba nilikuwa ni mdau au ni mhanga kwenye jambo hili ninalokwenda kuliuliza. Tuna changamoto kubwa ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini ambapo fedha zao na vifaa vyao vilichukuliwa na Serikali iliahidi kurudisha, lakini mpaka sasa baadhi bado hawajarudishiwa zile fedha na vifaa vyao. Naomba kujua, Serikali itarudisha lini?

Mheshimiwa Spika, nisiporidhika na majibu yake, nitakuomba ule utaratibu uliotumia jana kwenye lile Shamba la Rukwa, utumike pia na hapa. (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Msambatavangu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, baada tu ya taratibu kukamilika na wale waathirika wa suala hili la kikokotoo watafanikiwa na wao kupata stahiki zao kama ilivyopangwa ambavyo watapata wale wengine.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusu maduka ambayo yalifungwa na Serikali kuahidi kurejesha fedha hizo, maduka haya yalikuwa jumla ni 67 na tayari 62 Serikali imesharejesha vifaa na fedha yao. Bado maduka matano akiwemo na dada yangu Msambatavangu, lakini nimhakikishie kwamba na haya matano yaliyobaki tutafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ameuliza specific na yeye mwenyewe, naomba uniruhusu baada ya kipindi hiki cha maswali na majibu nikae naye kama Kamati tujadili suala hili. (Makofi)
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; eneo hili la Kikatiti liko Tarafa ya King’ori ambayo ina Kata 10 zenye watu 124,000, pia eneo hilo ndilo kapu la chakula kwa Jiji la Arusha na viunga vyake. Kikatiti yenyewe ina watu .....

SPIKA: Swali Mheshimiwa Pallangyo.

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, swali langu ni je, kwa takwimu ambazo zipo katika Sensa ya Mwaka 2022, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka benki hizi zifungue matawi pale?

Mheshimiwa Spika, kama ni ngumu sana, ni kwa nini benki hizi zisifungue mashine za kutolea fedha (ATM’s) Eneo la Maji ya Chai, Kikatiti yenyewe na King’ori Madukani? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge Pallangyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, takwimu aliyotaja ni kweli inaleta ushawishi kufungua tawi la benki huko, lakini jukumu la Serikali kama nilivyojibu ni kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji. Kwa hiyo, naomba tu Benki za NMB, CRDB na nyingine waende kuangalia hiyo fursa ili ikiwezekana wafungue tawi katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni ushauri, naomba tuchukue na tunaenda kuufanyia kazi.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa kuendelea pale nilipoishia kwenye mchango wangu wa jana kwamba, kulingana na jiografia ya nchi yetu kupakana na Nchi ya Kenya kuna mageti (stop border post) Namanga, Tarakea na Holili. Je, kama sisi tunapakana na Nchi ya Zambia, upi ni mkakati wa Serikali kuona namna ya kuongeza mageti, ili utoroshaji huu usiendelee? Tuna Geti moja la Tunduma, liongezeke Geti la Chipumpu, Kapele pamoja na Geti la Kasesha, Kalambo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa, mchango huu kwa kuongeza geti, ili kuzuia utoroshaji wa mazao na bidhaa nyingine ambazo zinaingia nchini kinyume na utaratib nimekuwa nikichangia kuanzia Mwaka 2021. Natamani Serikali itueleze je, mmeshawasiliana na wenzetu wa Zambia kuwapa wazo hili na wao kuona kama ni fursa tunaweza tukaitumia kuongeza chanzo cha mapato? Kama ndio, Zambia wanasemaje? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza. Serikali kupitia TRA inafanya survey kwenye milango yote ya mipaka kwa Nchi yetu ya Tanzania na nchi nyingine za jirani. Kwa hiyo, Serikali itakapofika hatua imejiridhisha, basi tunaweza tukachukua hatua ya kujenga au kuongeza geti kutoka moja yakawa mawili na hadi kufikia matatu, ikionekana ipo tija ya kufanya hivyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Serikali ya Tanzania pamoja na Serikali ya Zambia kupitia TRA na ZRA tunafanya mawasiliano ya kila siku, ili kuona tunaboreshaje kuzuia bidhaa hizi zisipite kwa njia za panya au za magendo, ili kuongeza mapato kwa nchi yetu. Ahsante sana.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wakandarasi wengi wale ambao wana sifa za kuendana na mfumo kwenye miradi midogo hawapatikani vijijini, mara nyingi wanatoka mijini. Muda wao wa kuji-mobilize kufika site kutoa huduma unakuwa mwingi na kazi huwa zinachelewa. Je, Serikali haioni haja ya kuhakikisha kwamba inawapa upekee local fundi au wakandarasi wadogo kutotumia mfumo au kujengewa uwezo ili waweze kutosheleza vigezo vyao kusudi kazi ziweze kufanyika kwa wakati?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Antipas, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba baadhi ya wakandarasi wale wadogo wadogo bado iko changamoto ya uelewa juu matumizi ya mfumo huu, lakini Serikali itaendelea kutoa elimu kwa local fundi na wale wote wenye mahitaji ya matumizi ya mfumo huu, ahsante.
MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza na ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa miongoni mwa makusanyo ya kodi ni pamoja na utoaji na upokeaji risiti pale tunaponunua bidhaa dukani, na kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara bado hawajaelewa suala la umuhimu wa kutoa risiti pale wanapouza bidhaa kwa visingizio kwamba kumekuwa na utitiri wa kodi kwa wafanyabiashara bila kuangalia mtaji wa mfanyabiashara huyo tangu bidhaa inatoka bandarini hadi kufika dukani, je, Serikali inalichukuliaje suala hili?
Swali la pili, kwa kuwa…

SPIKA: Mheshimiwa uliza kwa kifupi.

MHE. MAIDA HAMAD ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa hivi karibuni tulipitisha sheria ya adhabu kwa wafanyabiashara wote wanaokwepa kodi, je, kutokana na malalamiko haya kwa wafanyabiashara, Serikali inasema nini au inalifanyia kazi kwa kiasi gani? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kwa ridhaa yako nijibu maswali yote mawili ya Mheshimiwa Maida, Mbunge wa Viti Maalum kwa pamoja. Kwanza, naomba nimpongeze sana kwa ufuatiliaji mkubwa wa jambo hili. Niseme tu kwamba ni kosa kisheria kwa mfanyabiashara kutotoa kodi na hata mnunuzi (mteja) kutodai risiti, tuwajibike. Tuna programu inaitwa Tuwajibike, inatakiwa mfanyabiashara lazima atoe risiti, ni wajibu wake na mteja wajibu wake ni kudai risiti.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tuseme kwamba yule ambaye anafanya biashara, lakini hatoi risiti kwa bidhaa ambayo ametoa au kutoa risiti ambayo haiendani na uhalisia wa biashara ni kosa kwa mujibu wa sheria, ahsante sana.
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na kwamba wamefanya kazi nzuri ya kuliona hili. Je, Serikali sasa haioni haja ya kwenda mbali zaidi, kwa sababu hata nyuzi ya kiatu ya Askari bado ni silaha. Serikali haioni sasa kuwaachia vyombo vyetu vya ulinzi fursa kamili ya kuwa na msamaha? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zahor kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ushauri wake umepokelewa, kwa sababu amesema huoni haja ya kutanua wigo. Tumepokea ushauri huo na tutaufanyia kazi. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa nchi hii ili ufanye biashara unahitaji tax clearance na tax clearance inahusisha ulipaji wa kodi. Je, ni kwa nini Serikali isiainishe aina za biashara ambazo unaweza kupata leseni bila kuwa na tax clearance mpaka u-run biashara kwa muda fulani ili uweze ku-file na kulipa kodi? (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, kwanza zungumza Kiswahili ama zungumza Kiingereza maana hiyo nayo unatuchanganya. Haya uliza swali lako upya.

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Sijui tax clearance inaitwaje kwa Kiswahili lakini kwa biashara nyingi...

SPIKA: Basi zungumza Kiingereza kwa sababu Kanuni zinaruhusu. Uliza swali lako kwa Kiingereza. (Makofi)

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, aah! Kwa Kiingereza? (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ni lazima...



NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa kawaida tax clearance hutolewa, aah! Kiingereza. Cheti kile hutolewa baada ya biashara na Serikali inasema kwamba, mtu aanze kufanya biashara kwanza ndiyo anaenda kuomba hicho cheti cha ruhusa ya kufanyia biashara. Ahsante sana. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Sasa hoja yake si ni kwamba, hiyo biashara hawezi kuanza bila leseni? Yaani ni kwamba yale maombi ya leseni ili biashara yake afanye kwa utaratibu wa kisheria, unataka hiki cheti kwanza, ndiyo swali lake liko hapo.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, nakumbuka mwaka jana tulijibu swali kama hili na tukatoa maelekezo kwa Commissioner General wa TRA kwamba, yeyote ambaye ameanzisha biashara, lakini biashara ile bado haijafanya kazi na faida yake kuonekana, apewe cheti hicho ili aende akapate leseni ya kufanya biashara. Asiwe na kikwazo kwa sababu hajapata hiyo tax clearance.
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali na nimefuatilia ndiyo inavyokuwa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; Serikali ilifanya utaratibu mzuri wa kurekebisha kile kikokotoo, lakini kuna wastaafu ambao walituahidi kwamba wale ambao waliathirika na kikokotoo basi ile sehemu yao ambayo ilikuwa imeathirika kwa marekebisho mapya watawalipa, je, wataanza kuwalipa lini?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili ni hili; kwanza na-declare interest kwamba nilikuwa ni mdau au ni mhanga kwenye jambo hili ninalokwenda kuliuliza. Tuna changamoto kubwa ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni nchini ambapo fedha zao na vifaa vyao vilichukuliwa na Serikali iliahidi kurudisha, lakini mpaka sasa baadhi bado hawajarudishiwa zile fedha na vifaa vyao. Naomba kujua, Serikali itarudisha lini?

Mheshimiwa Spika, nisiporidhika na majibu yake, nitakuomba ule utaratibu uliotumia jana kwenye lile Shamba la Rukwa, utumike pia na hapa. (Makofi/Kicheko)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Msambatavangu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, baada tu ya taratibu kukamilika na wale waathirika wa suala hili la kikokotoo watafanikiwa na wao kupata stahiki zao kama ilivyopangwa ambavyo watapata wale wengine.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusu maduka ambayo yalifungwa na Serikali kuahidi kurejesha fedha hizo, maduka haya yalikuwa jumla ni 67 na tayari 62 Serikali imesharejesha vifaa na fedha yao. Bado maduka matano akiwemo na dada yangu Msambatavangu, lakini nimhakikishie kwamba na haya matano yaliyobaki tutafanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ameuliza specific na yeye mwenyewe, naomba uniruhusu baada ya kipindi hiki cha maswali na majibu nikae naye kama Kamati tujadili suala hili. (Makofi)
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nitakuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; eneo hili la Kikatiti liko Tarafa ya King’ori ambayo ina Kata 10 zenye watu 124,000, pia eneo hilo ndilo kapu la chakula kwa Jiji la Arusha na viunga vyake. Kikatiti yenyewe ina watu .....

SPIKA: Swali Mheshimiwa Pallangyo.

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, swali langu ni je, kwa takwimu ambazo zipo katika Sensa ya Mwaka 2022, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka benki hizi zifungue matawi pale?

Mheshimiwa Spika, kama ni ngumu sana, ni kwa nini benki hizi zisifungue mashine za kutolea fedha (ATM’s) Eneo la Maji ya Chai, Kikatiti yenyewe na King’ori Madukani? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge Pallangyo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, takwimu aliyotaja ni kweli inaleta ushawishi kufungua tawi la benki huko, lakini jukumu la Serikali kama nilivyojibu ni kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji. Kwa hiyo, naomba tu Benki za NMB, CRDB na nyingine waende kuangalia hiyo fursa ili ikiwezekana wafungue tawi katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili ni ushauri, naomba tuchukue na tunaenda kuufanyia kazi.
MHE. ASIA A. HALANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza kwa niaba ya Mheshimiwa Priscus Tarimo, Mbunge wa Moshi Mjini. Nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali katika kipindi cha bajeti Mheshimiwa Waziri alitueleza kwamba zimetolewa zaidi ya shilingi bilioni 949 kwa ajili ya ulipaji wa madeni mbalimbali. Tunataka kufahamu katika ulipaji huo wa zile fedha shilingi milioni 949 watoa huduma shuleni na wao wako kwenye huo mpango?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, je, mnatumia muda gani ili wananchi hawa waweze kujua watakaa muda gani na madeni hayo kwa sababu watoa huduma shuleni wengi ni wajasiriamali wadogo wadogo?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa Asia kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza, bila shaka wazabuni ambao wanatoa huduma shuleni ni sehemu ya fedha ile ambayo ililipwa mwaka uliopita na wanaendelea kulipwa ndani ya mwaka huu na mwaka unaokuja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kwamba ni lini, inategemea upatinaji wa mapato na kukamilika kwa uhakiki. Basi nimwomba Mheshimiwa na Wazabuni wote nchini wawe na Subira, muda ukifika, fedha zao watalipwa.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Miongoni mwa wanaoidai Serikali kwa muda mrefu ni pamoja na wakandarasi wanaotengeneza barabara hapa nchini, na wako wengi wana madai ya muda mrefu. Ikumbukwe watu hawa wanapochukua hizi kazi wengine wanaenda kukopa benki. Wakati wanapotakiwa kufanya marejesho, Serikali haijawalipa. Nini kauli ya Serikali kuhusiana na hawa wakandarasi wanaodai, na wapo wengine wanafilisiwa na benki husika kwa sababu walienda kukopa? Nini kauli ya uhakika ya Serikali kuwapa matumaini watu hawa na ikiwezekana walipwe?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kauli ya Serikali ni kwamba madeni yote yanaendelea kuhakikiwa na Serikali. Uhakiki utakapokamilika na upatikanaji wa mapato, wazabuni wote pamoja na wakandarasi watalipwa.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri, alipojibu alisema wanafanyia uhakiki ndipo walipwe, lakini wapo watu au wakandarasi wengine wana miaka mitatu hawajalipwa. Je, huo uhakiki unachukua muda gani ili hawa watu wapate fedha zao?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mbunge amechukua eneo moja tu. Nilisema kulingana na upatikanaji wa mapato na uhakiki wa madeni. Kwa hiyo, mapato ya fedha yakipatikana watalipwa. Dawa ya deni ni kulipa. Nawahakikishia Waheshimiwa Wabunge fedha ikipatikana wakandarasi wote watalipwa.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Changamoto ya madeni ya wazabuni wa chakula shuleni inasababisha kuathiri moja kwa moja upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi na ubora wa chakula hicho hivyo kuathiri elimu kwa maana ya uwezo wa watoto kusoma. Sasa, ningependa kufahamu, Mei mwaka huu nilichangia hapa Bungeni kwenye Wizara ya Elimu kuhusu suala hili na Agosti; Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Zainab Katimba, alisema kwamba TAMISEMI imewasilisha Wizara ya Fedha madeni ya wazabuni wa chakula takribani shilingi bilioni 21.7. Sasa, je, uhakiki huo utakwisha lini? Kwa sababu nikitoa mfano kwenye Jimbo la Bukoba Mjini kuna shule sita za sekondari za Serikali ambazo zinaidai Serikali jumla ya shilingi milioni 935, na madeni hayo ni kati ya mwaka mpaka miaka sita.
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba baadhi ya wazabuni malipo yao hayajakamilika na hayajawafikia, lakini naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama nilivyoendelea kusema, kadri mapato yatakavyoendelea kupatikana ndivyo wazabuni wetu watakavyolipwa. (Makofi)
MHE. SALUM MOHAMMED SHAAFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kucheleweshwa huko kuundwa akaunti ya fedha ya pamoja ya Serikali, je, Serikali haioni kwamba haina nia njema ya ufunguaji wa akaunti hii?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, ufunguaji wa akaunti hii ya fedha ya pamoja ni takwa la kikatiba na siyo la kimashauriano. Nataka kufahamu, ni sababu zipi zilizosababisha mashauriano hayo kutokukamilika hadi leo? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Al-imam Shaafi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina nia njema kabisa na Mheshimiwa Mbunge mwenyewe ni shahidi kwamba ndani ya Jamhuri ya Muungano tulikuwa na changamoto 25, lakini 21 tayari zimeshapatiwa ufumbuzi, yaliyobaki ni machache na Serikali ipo katika mchakato wa kukamilisha na kupata ufumbuzi wa hizo nne. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali la pili, kila kitu kinahitaji utaratibu, kufuata kanuni na mashauriano. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba akaunti hiyo haitecheleweshwa, awe na subira na itafunguliwa baada ya pande mbili kukamilika. (Makofi)
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, naomba kuuliza maswali madogo mawili. Sasa hivi nchini kuna biashara ya foreign currency markets inazofanyika kwenye mitandao, Pamoja na biashara ya crypto currencies. Nini mkakati wa Serikali wa kusimamia na kuratibu biashara hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kuna Watanzania wengi wanafanya kazi nje ya nchi na wengine waliopo nchini wanafanya kazi za kisanii, kibiashara na kishauri kupitia mitandao, wanalipwa kwa fedha za kigeni, lakini fedha zile kuingia nchini imekuwa ni changamoto kubwa sana kwa sababu ya gharama kubwa za makato wanazopitia.

Mheshimiwa Spika, waweze kupitia nini makakati wa kupunguza gharama za makato ili Watanzania wale wanufaike na jasho lao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, mkakati wa Serikali, moja kati ya Mkakati wa Serikali ni kuboresha mifumo ya utumaji na upokeaji fedha ili kupunguza gharama ikiwa ni pamoja na kupunguza tozo na makato mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili Serikali inaendelea kufuatilia suala hili na tumechukua ushauri wake tukiona ipo haja ya kufanya hivyo basi tutafanya, wala hakuna shida yoyote. (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa nafasi. Ili nchi yoyote iweze kujiendesha vizuri kutoa miradi mijini na vijijini ni pamoja na kuongeza vyanzo vya mapato. Kwenye eneo hili la digital currencies kumeonekana kwamba kuna fursa nyingi sana na vijana wengi wa Kitanzania wanafanya biashara hii.

Mheshimiwa Spika, swali langu kwa Serikali, Serikali inaonaje kwa kushirikiana na Ofisi ya CAG mumpe kazi CAG aweze kufanya forensic audit kwa ajili yaku-audit transaction zote ambazo zinafanyika kwenye currencies mfano Bitcoin, Ethereum, LEPO, USDT na currency zingine ili tuweze kujua ni kiasi gani tunapoteza ili tuweze kukitumia kama chanzo cha mapato kwa ajili ya kusaidia Taifa letu? (Makofi)
WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri pamoja na swali zuri lililoulizwa na Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, Serikali inaendelea na utafiti kuhusu the whole scenario ya matumizi ya other currencies zikiwemo hizi za kieletroniki pamoja na matumizi ambayo yanaendelea na currencies hizi za kawaida ambazo ni hard cash, ambazo tumekuwa tukizitumia katika baadhi ya maeneo kuangalia kama kuna benefit tunazoweza kuzipata endapo tuka-shift kwenda kwenye matumizi ya alternative currencies hizi digital currencies.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo utafiti unaendelea na sasa wanaangalia experience kutoka katika mataifa yakiwemo ya Afrika ambayo yameishaenda kwenye digital currency kama Nigeria pamoja na nchi za Asia ambao wameshaanza kutumia utaratibu huo. Baada ya kuwa imekamilika tutaanza hatua kwa hatua kama tutaona ni jambo lenye faida na ambalo litatupigisha hatua zaidi. (Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali yanayotia matumaini, lakini kwa sababu ya mradi huu ni wa muda mrefu sana, una zaidi ya miaka sita sasa, umekumbwa na misukosuko mingi sana. Sasa naomba kupata kauli ya Serikali nini uwezo wao wa kusukuma mradi huu mwaka huu ukaanza kwa sababu tu umechelewa sana na wanaliwale wanauhitaji sana.

Swali la pili sambamba na mradi huu wa Stendi ya Kisasa, Liwale tulikuwa na shida kubwa sana ya kuwa na soko la kisasa, iliandikwa miradi hii yote miwili sambamba. Je, Serikali iko tayari sasa kutupatia fedha na mradi huu wa soko la kisasa ukaanza? (Makofi)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, naomba kabla ya kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kuchauka nimpongeze sana kwa namna anavyofuatilia miradi hii hasa huu wa stendi ya kisasa kule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la kwanza kama nilivyozungumza au kama nilivyojibu katika swali la msingi kwamba tayari fedha imetengwa milioni 412 ya mwaka ujao wa fedha 2024/2025, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi ule hautasimama utaendelea kujengwa kama ulivyopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili naomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira katika soko ila nimhakikishie tu kwamba ndani ya bajeti ya mwaka huu soko lile limetengewa fedha na Serikali ipo tayari kwa ujenzi wa soko hilo.
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Kumekuwa na hii mikopo kila mahali na ina athari kubwa kwa wanawake na vijana. Mikopo hii imesababisha wengi kupata tatizo la afya ya akili na ndoa nyingi kuvunjika. Mheshimiwa Waziri, haoni ni wakati mwafaka sasa hivi kukomesha mikopo hii ili kunusuru wananchi wetu? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Mwongozo wa Benki Kuu wa Mwaka 2018 na Kanuni ya Mwaka 2019, bado mikopo hii imeendelea kuwepo hasa Kausha Damu katika mikoa zaidi ya 17 na hasa Mkoa wa Kilimanjaro, Jimbo la Moshi Vijijini. Nini kauli ya Serikali kulingana na hawa wanaokiuka sheria hii? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Njau kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwanza nampongeza sana kwa kufuatilia jambo hili. Serikali inatoa maelekezo kwa taasisi hizo kuacha mara moja mwenendo huu na Serikali itafuatilia kwa karibu sana.

Mheshimiwa Spika, swali namba mbili, naagiza na kuelekeza BOT wafuatilie kwa karibu sana, kama kuna taasisi yoyote ambayo inaenda kinyume na sheria, Serikali haitakuwa na muhali kwa yeyote yule ambaye anaenda kinyume na sheria na taratibu ikiwemo kufuta leseni ya taasisi hiyo. (Makofi)
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa makampuni ya simu sasa ndiyo yanaongoza kwa kutoa hiyo mikopo ya haraka haraka bila kujaza fomu wala chochote; vijana wetu ni wengi ambao inakuwa kivutio na pia akina mama wajasiriamali wakiwepo akina mama wa Mkoa wa Kilimanjaro, lakini mikopo hiyo ni Kausha Damu. Ni lini makampuni haya yatalazimishwa kutoa elimu?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Shally, mama yangu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutoa elimu siku hadi siku kupitia vyombo vya habari tofauti, lakini hasa na taasisi zetu za kifedha ikiwemo Benki Kuu.
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni muda gani wa mwisho ulifanyika upembuzi yakinifu kwa benki hizi katika Wilaya yetu ya Micheweni? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, kuna maombi yoyote ya ufunguzi wa matawi mapya ya benki katika Wilaya yetu ya Micheweni yaliyopelekwa, ukizingatia kazi kubwa ya maeneo ya uwekezaji inayofanywa na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ally Mwinyi katika Wilaya yetu ya Micheweni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Omar Issa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu ninaomba kumpongeza sana yeye pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Micheweni kwa namna wanavyopambana ili huduma za kibenki kupatikana ndani ya Wilaya ya Micheweni hasa makao makuu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba uridhie nijibu maswali yote mawili kwa pamoja kuwa hadi sasa bado Serikali haijapokea maombi kwa Benki za NMB na CRDB kufungua tawi jipya pale makao makuu ya Wilaya ya Micheweni, lakini kutokana na uwekezaji ambao umewekwa na Serikali ya Awamu ya Nane, inayoongozwa na Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi katika Wilaya ya Micheweni, mfano, kama ujenzi wa bandari mpya ya kisasa na viwanda mbalimbali na ni eneo husika la uwekezaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba benki zetu za NMB na CRDB na benki nyingine, waende kuangalia fursa hii na wafanye upembuzi yakinifu kwa ajili ya kufungua tawi katika makao makuu ya Wilaya ya Micheweni. (Makofi)
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali yanayoonesha namna wanavyojali wastaafu, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, wapo wastaafu ambao wanaishi vijijini na mbali sana na makao makuu ya halmashauri na afya zao wakati mwingine siyo nzuri, wakati Serikali inatengeneza mfumo mpya wa kidigitali, je, haioni haja sasa ya kuwasogezea huduma wazee hawa wastaafu ambao hali zao siyo nzuri kwa kutumia watendaji wa kata na vijiji?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, je, ni mshahara gani hutumika katika kutengeneza pension hizi za wastaafu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kabla ya kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge ninaomba nimpongeze sana kwa kazi nzuri ambayo anaifanya, kwa kufuatilia jambo hili siku hadi siku. Ni mara kadhaa tunakutana ofisini kujadili suala hili. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nichukue swali lake la kwanza kama ni ushauri, hivyo ushauri wake umepokelewa, tunaenda kuufanyia kazi, kwa sababu Serikali imeona hilo na ndiyo maana tukasema tunaenda kuanzisha mfumo maalumu wa kidigitali ambao utawawezesha wastaafu kujihakiki wenyewe kupitia simu zao za mkononi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili, mshahara ambao unazingatiwa wakati wa kutengeneza pension ni ule mshahara wa mwisho wa mtumishi. (Makofi)
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Maboresho hayo ni lazima yaendane na nyongeza ya kima cha malipo ya pensheni. Ni lini mtawaongezea hawa wastaafu wanaolipwa na Wizara ya Fedha kiwango cha malipo kila mwezi?
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, suala la ongezeko la fedha ama la peshneni kwa wastaafu wetu ni suala ambalo linafuata taratibu na mchakato sasa hivi upo unaendelea nimwombe Mheshimiwa Mbunge awe na subira ataona matokeo chanya baada ya siku chache...
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipatia fursa hii ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mamlaka ya utoaji msamaha wa kodi yamewekwa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, sasa Serikali haioni haja ya kugatua madaraka na kuwapatia mamlaka mameneja wa mikoa ili waweze kutoa misamaha hiyo ya kodi ili kurahisisha kazi za ujenzi wa barabara ufanyike kwa haraka? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na malimbikizo ya madai ya VAT kwa wakandarasi, sasa Serikali haioni haja ya kuweka mchakato rahisi wa kuweza kuwalipa haraka wakandarasi hao ili waweze kutumia fedha zao ili kuijiendeleza kwenye miradi yao ya ujenzi wa barabara? Ahsante (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza, ushauri wake Mbunge umepokelewa na unaenda kufanyiwa kazi hasa katika kipindi hiki cha ukusanyaji wa maoni, Serikali itaangalia na wataalamu wetu watatushauri, kama ipo tija ya kupeleka mikoani, basi Serikali itafanya hivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, madeni ya makimbikizo ya madai ya VAT Refund, yaliyo mengi tayari yameshahakikiwa na yamelipwa na yale ambayo yamewasilishwa siku za karibuni, yanahakikiwa na yakikamilika tu Serikali italipa refund hiyo. (Makofi)
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba niulize maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa awali huduma hii ilikuwa inapatikana kwenye Jimbo la Micheweni ambalo lipo Wilaya ya Micheweni; sambamba na hilo, Serikali ya Awamu ya Nane ya Mheshimiwa Dkt. Mwinyi imeweka maeneo ya Maziwang’ombe kama maeneo ya uwekezaji; miundombinu tayari ipo lakini pia kuna ujenzi wa Bandari Rasmi Shumba Mjini ambapo tunatarajia mzunguko wa fedha utakuwa mkubwa. Je, Serikali haioni haja ya kupeleka huduma hii ya Benki kwenye Makao Makuu ya Wilaya ambayo yako kwenye Jimbo la Micheweni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Kwa kuwa wananchi wa Wilaya ya Micheweni wanatumia benki nyingine ikiwemo CRDB na NMB na Mheshimiwa Waziri amesema wametia mkazo kwenye PBZ, je, hawaoni haja ya kuwapelekea wananchi wa Wilaya ya Micheweni huduma ya Benki nyingine ikiwemo CRDB na NMB? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla ya kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Omar Issa, naomba nichukue fursa hii kumpongeza sana kwa namna anavyofanya kazi kwa ufanisi na kwa ufuatiliaji wa maendeleo ama wa huduma hizi za kibenki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la kwanza. Serikali inatambua ukuaji wa uchumi uliopo katika Mji wa Micheweni ambao umechochewa na uongozi thabiti wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Hivyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba benki hizi zitaendelea kufanya utafiti na upembuzi yakinifu katika eneo la Mji wa Micheweni. Ikionekana tija ipo, basi huduma hiyo itafunguliwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili. Benki zote hizo nyingine ambazo amezitaja CRDB na NMB zinaendelea kufanya tathmini katika Wilaya hiyo ya Micheweni, hivyo inawezekana baadaye kufungua Tawi la CRDB na NMB katika Wilaya hiyo. (Makofi)
MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa taarifa za wakopaji ni muhimu kwa financial institutions zote. Je, na hizi microfinance ndogo ndogo nazo zinapeleka taarifa za wakopaji BOT?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ili kuepuka default rate kwa financial institution zetu. Je, BOT wana-update hizo taarifa kwenye credit reference kwa muda gani; kwa wiki au kwa mwezi kwa sababu tunajua wakopaji wanakopa kila siku, nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Martha, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, taasisi zote za fedha kubwa na ndogo zinatakiwa zipeleke taarifa sahihi kwenye kanzidata inayosimamiwa na BOT.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kila baada ya mwezi taarifa hizo zinapokelewa na kusambazwa kwa taasisi zinazohusika. Ahsante.