Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions from Hon. Stephen Lujwahuka Byabato (5 total)

MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, naishukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kutoa fedha ya ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia roundabout ya Rwamishenye mpaka njia panda ya Kashabo Bukoba Mjini, sasa naomba kujua ni lini ujenzi huo utakamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara hii ya njia nne inaendelea kujengwa katika Mji wa Bukoba na ilikuwa imepangwa imalizike mwaka huu. Changamoto ambayo imejitokeza ni kwamba kuna kitu kama land slide ambayo imeonekana, maji yanatoka chini. Kwa hiyo, sasa hivi eneo hilo tunalipitia upya ili liweze kuangaliwa kama bado barabara itaendelea kupita hapo ama tunatakiwa tuibadilishe. Baada ya kupata majibu ya wataalam, barabara hiyo itaendelea kujengwa na kukamilishwa. Ahsante.
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru na nimshukuru Dkt. Samia kwa utekelezaji wa mradi mkubwa wa upanuzi mtandao wa Maji Bukoba Mjini unaogharimu shilingi 3,300,000,000 na Mheshimiwa Naibu Waziri alikuja kukagua na akatoa maelekezo. Kama alivyosema itaisha Desemba, lakini niliomba kujua ni lini 207,000,000 iliyobakia ya kuleta mabomba kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji zitaletwa Bukoba Mjini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Byabato, Mbunge wa Bukoba Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa tulifika Bukoba tukafanya ziara pia tukajionea hali ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi na hakika Bukoba kwa upande wa maji hali ni nzuri sana, lakini tunatambua kwamba uhitaji wa fedha hizo katika eneo hilo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutazisukuma haraka iwezekanavyo kuhakikisha kwamba, zinafika na mradi unakamilika kwa wakati.
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, naishukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kutoa fedha ya ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia roundabout ya Rwamishenye mpaka njia panda ya Kashabo Bukoba Mjini, sasa naomba kujua ni lini ujenzi huo utakamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara hii ya njia nne inaendelea kujengwa katika Mji wa Bukoba na ilikuwa imepangwa imalizike mwaka huu. Changamoto ambayo imejitokeza ni kwamba kuna kitu kama land slide ambayo imeonekana, maji yanatoka chini. Kwa hiyo, sasa hivi eneo hilo tunalipitia upya ili liweze kuangaliwa kama bado barabara itaendelea kupita hapo ama tunatakiwa tuibadilishe. Baada ya kupata majibu ya wataalam, barabara hiyo itaendelea kujengwa na kukamilishwa. Ahsante.
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi. Wanabukoba tunamshukuru Mheshimiwa Dkt. Samia kwa kufanya miradi ya kimageuzi katika mkoa wetu na Bukoba Mjini tukiwemo. Sasa ujenzi wa barabara ya njia nne katika Mji wa Bukoba Mjini unaogharimu shilingi bilioni 12.4 tayari umeshaanza, naomba kufahamu ni lini mradi huu utakamilika? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli tuna mradi wa kujenga kutoka barabara mbili kwenda barabara nne na tumegawanya katika vipande viwili. Kipande cha kwanza kiko karibu 44%. Kwa mujibu wa mkataba tunategemea kufikia mwishoni mwa mwezi Mei iwe imekamilika. Kipande cha pili kikihusisha na Mto wa Kanoni ambao tumetumia hela za emergency kwa sababu kunakuwa na mafuriko; kwa mujibu wa mkataba tunategemea ikamilike mwezi Desemba mwaka huu. Ahsante. (Makofi)
MHE. STEPHEN L. BYABATO: Mheshimiwa Spika, ahsante, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali madogo mawili.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ni ya kimkakati kwa Manispaa yetu ya Bukoba inaenda kwa mwekezaji mkubwa wa shule ambazo zinafanya vizuri kitaifa za Kaizirege na Kemebos na yeye amekuwa akishirikiana na Serikali kutengeneza barabara hii. Sasa ninaomba commitment ya Serikali kwamba ni lini itawekewa lami ili iendelee kuhudumia vizuri mwekezaji huyu, lakini na wakazi wengine wa maeneo hayo?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, nilimwomba juzi Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI kwamba Mradi wa TACTIC utakapokamilika basi usainiwe pale Bukoba Mjini ili Wana-Bukoba Mjini waweze kuona kwamba jambo hili linaanza kufanyika. Sasa ninaomba kujua ni lini mradi huo utasainiwa ili barabara zaidi ya kilometa 10 ziweze kutekelezwa katika Jimbo la Bukoba Mjini? (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nianze kwanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake ambayo nia ya kimsingi anataka kuona miundombinu ya barabara inaboreshwa katika jimbo lake. Kuhusiana na swali lake la mwanzo kama nilivyotangulia kujibu katika majibu ya msingi kwamba barabara hii ya Lake Oil - Ijuganyodo ipo katika mpango wa kufanyiwa ukarabati lakini lengo na nia ni kuijenga barabara hii katika hadhi ya lami.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba katika kipindi cha miaka minne tayari katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba jumla ya shilingi bilioni 9.6 zimewekezwa kwa ajili ya kukarabati na kujenga barabara za lami na mtandao wa lami umeongezeka kutoka kilometa 34.29 mpaka sasa mtandao wa lami ni kilometa 43.54. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itaendelea kuongeza mtandao huu wa lami na itaifikia barabara hii muhimu kabisa ya Lake Oil – Ijuganyodo.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali lake la pili Mheshimiwa Mbunge ameulizia kuhusiana na utekelezaji wa Mradi wa TACTIC, ni kweli Manispaa ya Bukoba Mjini na yenyewe ni miongoni mwa miji 45 ambayo inanufaika na Mradi huu wa TACTIC. Kwa awamu hii au kwa wakati huu tuliokuwa nao tayari mradi wa ujenzi wa barabara kilometa 10 katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge unaendelea na evaluation na tunatarajia mwezi Mei tutasaini mikataba ili mkandarasi sasa aweze kukabidhiwa site na aanze ujenzi.

Kwa hiyo, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge yeye na wananchi wake wa Manispaa ya Bukoba Mjini wakae mkao wa mapokeo, barabara hizi zinakuja kujengwa kupitia Mradi wa TATIC pamoja na miundombinu mingine ya soko na stendi. (Makofi)