Answers to Primary Questions by Hon. Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya (332 total)
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa lami barabara yenye urefu wa Kilometa 50 toka Mbulu kwenda Haydom ambayo ipo kwenye mpango wa Bajeti tangu 2019/2020, 2020/2021?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kujibu swali na ni mara yangu ya kwanza, naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru kwanza Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwa Mbunge. Pia nimshukuru sana Mheshimiwa Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
Mheshimiwa Spika, pia nikishukuru sana chama changu Chama Cha Mapinduzi kwa kuniteua na hatimaye kunipitisha kuwa mgombea wa Jimbo la Ileje, lakini niwashukuru sana….
SPIKA: Sasa majibu Mheshimiwa Naibu Waziri.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba nijibu swali laMheshimiwa Zacharia Paul Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika,Barabara ya Mbulu - Haydom yenye urefu wa kilometa 70.5 ni sehemu ya barabara yaKaratu – Mbulu – Haydom– Sibiti – Lalago – Maswayenye urefu wa kilomita 398 inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Awali (Preliminary Design) wa barabara hii (kupitia mradi wa Serengeti Southern Bypass) ili kuijenga kwa kiwango cha lami umekamilika. Kazi hii ilifanywa na Kampuni iitwayo H.P. Gauff Ingenieure GmbH & Co. KG – JBG mwaka 2016 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa wananchi wa Mbulu pamoja na Hospitali ya Haydom, Serikali ilianza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi kwa sehemu ya Mbulu
– Haydom yenye urefu wa kilomita 50 kwa kiwango cha lami, ambapo katika mwaka wa fedha 2019/2020, ilitenga Shilingi milioni 1,450.00 na mwaka wa fedha 2020/2021, imetenga Shilingi milioni 5,000.00. Ujenzi wa barabara hii utatekelezwa kwa njia ya Kusanifu na Kujenga (Design and Build) na zabuni ya kazi hii itatangazwa wakati wowote katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Katika mwaka wa fedha 2020/2021, zimetengwa shilingi milioni 401 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -
Je, ni lini ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi wa Barabara ya kutoka Kahama - Nyang’holongo – Kharumwa – Nyijundu – Busolwa - Ngoma hadi Busisi Sengerema kwa kiwango cha lami itatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika,kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika,Barabara ya Kahama - Nyang’holongo - Kharumwa - Nyijundu - Busolwa - Ngoma hadi Busisi Wilayani Sengerema (yenye urefu wa kilometa 162.99), inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Barabara hii inaunganisha mikoa mitatu ya Shinyanga, Geita na Mwanza kupitia Wilaya za Msalala (Shinyanga), Nyang’hwale (Geita) na Sengerema (Mwanza).
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii, hivyo inatafuta fedha za kufanya usanifu, ikiwa ni maandalizi ya kuijenga barabara hiyo, kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, jumla ya shilingi milioni 581.827 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati kwa kiwango cha changarawe. Aidha, Wizara kupitia TANROADS inaendelea kufanya matengenezo mbalimbali ya barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. GODWIN E. KUNAMBI (K.n.y MHE. ABUBAKAR D. ASENGA) Aliuliza: -
Je, ni lini Ujenzi wa Barabara ya Kidatu hadi Ifakara utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshmiwa Abubakar Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kidatu – Ifakara ni sehemu ya Barabara Kuu ya Mikumi - Kidatu - Ifakara - Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha yenye urefu wa jumla ya kilometa 547. Barabara hii ni miongoni mwa barabara muhimu katika Taifa kwa kuwa inaunganisha Mkoa wa Morogoro na mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara ya Njombe, Ruvuma na Lindi kupitia Wilaya za Kilombero, Ulanga na Malinyi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara kati ya Kidatu hadi Ifakara yenye urefu wa kilometa. 66.9 pamoja na Daraja la Ruaha Mkuu vinajengwa na Mkandarasi M/S Reynolds Construction Company Limited (Nigeria).
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali, kupitia Wizara ya Fedha na Mipango na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii kwa gharama ya Euro 40,441,890.81 takribani sawa na shilingi bilioni 113.13 bila VAT. Mradi ulitegemea kukamilika tangu tarehe 29 Septemba, 2020. Mradi huu umechelewa kukamilika kwa sababu za kimenejimenti kwa upande wa Mkandarasi. Hata hivyo, Serikali inaendelea kumsimamia Mkandarasi kwa karibu ili akamilishe mradi kama ilivyopangwa. Mradi huu umepangwa kukamilika mwezi Oktoba, 2021.
MHE. JACQEULINE N. MSONGOZI (K.n.y MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA) Aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Sumbawanga Mjini utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ni miongoni mwa viwanja vya ndege vinne (4) ambavyo ni Kigoma, Tabora, Sumbawanga na Shinyanga vinavyotarajiwa kujengwa na kukarabatiwa kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB).
Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za makubaliano ya mkataba wa miradi hiyo baina ya Serikali (kupitia Wizara ya Fedha na Mipango) na Mfadhili (Benki ya Uwekezaji ya Ulaya – EIB) tayari zimekamilika na idhini (No Objection) ya kuanza utekelezaji wa miradi yote minne (4) imetolewa na Mfadhili wa miradi husika.
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa Mkandarasi (M/ s Sino Shine Overseas Construction & Investment East Africa Limited) na Mshauri Elekezi (SMEC International PTY Limited) ikishirikiana na Kampuni ya SMEC International Tanzania Limited) kwa ajili ya kutekeleza kazi hii, wamepatikana. Hivyo hivi sasa, Serikali iko katika hatua za awali za kuanza utekelezaji wa mradi huu.
MHE. FLATEI G. MASSAY Aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Karatu – Dongobesh – Hydom hadi Singida iliyotengewa fedha katika bajeti iliyopita utaanza?
NAIBU WAZIRI WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, suala kama hili lilijitokeza, swali namba 7 ambalo liliulizwa na Mheshimiwa Mbulu Mjini, kwa hiyo, inaonyesha ni kwa kiasi gani barabara hii ni muhimu na majibu yangu ni kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Mbulu – Haydom yenye urefu wa kilometa 70.5, ni sehemu ya barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti – Lalago – Maswa (km 398) inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Awali (Preliminary Design) wa barabara hii (kupitia mradi wa Serengeti Southern Bypass) ili kuijenga kwa kiwango cha lami, umekamilika. Kazi hii ilifanywa na kampuni iitwayo H.P. Gauff Ingenieure GmbH & Co. KG – JBG mwaka 2016 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW).
Mheshimiwa Naubu Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hii ambayo itawezesha wananchi wa Mbulu kupata huduma katika Hospitali ya Haydom, Serikali ilianza kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Mbulu – Haydom (km 50) kwa kiwango cha lami; ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021, shilingi bilioni tano zilitengwa. Utekelezaji wa mradi huu upo katika hatua za manunuzi na ujenzi wake utafanywa kwa njia ya Kusanifu na Kujenga (Design and Build). Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imetenga fedha shilingi milioni 401 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka.
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Flatei Massay, swali la nyongeza.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi kwa kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri mwenyewe kwamba barabara hii ina umuhimu na sasa kwa miaka miwili imekuwa ikiwekwa kwenye bajeti na haikujengwa na amesema imetegwa shilingi bilioni 5, je, atuambie ni lini atatangaza tenda ili barabara hii ianze kujengwa?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa anajua wazi kwamba bilioni 5 haiwezi kujenga barabara na barabara hii iko kwenye Ilani ya uchaguzi mwaka 2015-2020 na 2020-2025 na Mheshimiwa Rais ameahidi kwenye kampeni juzi hapa, je, yupo tayari kuweka fedha kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 ili kumaliza kilomita zingine 20 kufika 70 kufikia eneo la Haydom?
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Kitahi – Lituhi kupitia Ruanda itaanza kujengwa ili kurahisisha usafirishaji wa makaa ya mawe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali lililoulizwa na Mheshimiwa Benaya Liuka Kapinga, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, magari yote makubwa yanatakiwa yachukue makaa ya mawe katika eneo la Amani Makoro kwa ajili ya kupeleka maeneo mbalimbali nchini. Makaa ya mawe huchukuliwa na magari yenye uzito usiozidi tani 15 kutoka Mgodini (eneo la Ngaka) hadi Amani Makoro.
Ili kurahisisha uchukuaji wa makaa ya mawe kutoka Amani Makoro kwenda maeneo mengine nchini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Ujenzi) kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kitahi – Lituhi (km 84.5) kwa awamu ambapo mpaka sasa km 5 kuanzia Kitahi hadi Amani Makoro (Coal Stockpile) zimekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 9,000 katika mwaka wa fedha 2020/2021 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kiwango cha lami kwa kilometa tano nyingine. Kazi za ujenzi kwa sehemu hii zinatarajia kuanza mwishoni mwa Aprili, 2021. Aidha, ili kuhakikisha barabara yote inapitika kipindi chote cha mwaka, Serikali imetenga kiasi cha shillingi milioni 1,800 za matengenezo mbalimbali katika mwaka wa fedha 2020/ 2021.
MHE. HASSAN S. MTENGA Aliuliza: -
Je, Serikali haioni sababu kwa sasa kutumia Bandari ya Mtwara kusafirisha korosho zinazolimwa Kusini badala ya kutumia njia ya magari ambayo yanasababisha uharibifu mkubwa wa barabara kwenda Bandari ya Dar es Salaam?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Selemani Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, wafanyabiashara wamekuwa wakitumia bandari ya Mtwara kusafirisha korosho zinazolimwa kusini mwa nchi kwa kuzingatia ushawishi wa Serikali wa kutumia zaidi bandari hiyo badala ya kutumia njia ya magari ambayo ni kweli inachangia uharibifu wa barabara na wakati mwingine ajali za mara kwa mara. Katika kufanikisha nia hii, Serikali imeendelea kufanya vikao na wadau mbalimbali ili waweze kutumia Bandari ya Mtwara na hasa baada ya kufanya maboresho makubwa katika bandari hiyo kwa kujenga gati jipya na kuongeza kina cha maji ili meli kubwa zaidi ziweze kutia nanga katika bandari hiyo ya Mtwara.
Mheshimiwa Spika, changamoto za Bandari ya Mtwara ni utegemezi wa shehena ya aina moja tu ya korosho inayotoka Mtwara na hakuna shehena nyingine inayoingia katika Bandari hiyo. Hali hiyo inasababisha gharama za usafirishaji kuwa juu kutokana na meli kuja zikiwa tupu bila mzigo ili kufuata shehena ya korosho Mtwara tofauti na Dar es Salaam.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto hiyo Serikali inaendelea kuwashawishi wenye meli kupunguza gharama za usafirishaji ili kufidia gharama za kusafirisha korosho kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa njia ya barabara. Aidha, Serikali kupitia TPA (Mamlaka ya Bandari) inaendelea kuitangaza bandari ya Mtwara ili zipatikane shehena zinazoingia katika bandari hiyo, ahsante.
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE Aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani kuhusu kujenga daraja katika Mto Maragalasi Ilagala?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nashon William Bidyanguze, Mbunge wa Kigoma Kusini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, daraja katika Mto Maragalasi katika eneo la Ilagala liko katika barabara ya Mkoa wa Kigoma (Simbo – Ilagala – Kalya) yenye urefu wa kilometa 235. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 345 kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kwa kutambua umuhimu wa daraja husika kwa wananchi, hususan wa Mkoa wa Kigoma na maeneo ya jirani, baada ya kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika, Serikali imejipanga kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza na kukamilisha ujenzi wa daraja hilo.
MHE. HAMISI S. TALETALE Aliuliza:-
Je, ni lini barabara ya Bigwa – Kisaki itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mwaka 2020 – 2025 inavyoelekeza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamisi Shabani Taletale, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Bigwa – Mvuha – Kisaki ni barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilometa 133.28 ambapo kilomieta 18.4 ni za lami na kilomita 115.14 ni za changarawe. Barabara hii ni kiungo muhimu kwa Mkoa wa Pwani na Morogoro na pia ni barabara inayoelekea katika Mradi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere katika Mto Rufiji ambalo ujenzi wake unaendelea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ilikamilika mwezi Novemba, 2017 chini ya Kampuni ya Uhandisi ya UNITEC Civil Consultants Ltd ya Tanzania kwa ushirikiano na Kampuni ya Multi-Tech Consult (Pty) Ltd ya Gaborone, Botswana.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha. Wakati Serikali inatafuta fedha za ujenzi, imeendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali ili barabara hii iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Aidha, katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 1,492 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara husika. Ahsante.
MHE. FRANCIS L. MTEGA Aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Rujewa – Madibira – Mafinga (kilometa 151) utaanza kwa kuwa upembuzi yakinifu umekamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Leonard Mtega, Mbunge wa Mbarali, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Rujewa – Madibira – Mafinga yenye urefu wa kilometa 152.1 ni Barabara ya Mkoa ambayo ipo chini ya Wakala wa Barabara (TANROADS). Sehemu ya barabara hii, yani Rujewa hadi Madibira yenye urefu wa kilometa 97.1, inahudumiwa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Mbeya na sehemu iliyobaki kipande cha Madibira hadi Kinyanambo chenye urefu wa kilometa 55, kinahudumiwa na Wakala wa Barabara Mkoa wa Iringa. Barabara hii ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 na ahadi za Viongozi Wakuu wa Nchi kuijenga kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii ambayo inapita katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya mpunga na mahindi, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara ilifanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami. Baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kujenga barabara hii. Wakati Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi, Wizara kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea kufanya matengenezo ya barabara hii ili ipitike majira yote ya mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, barabara hii imetengewa kiasi cha shilingi milioni 757 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali na shilingi bilioni 3,380,000,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
MHE. AMANDUS J. CHINGUILE Aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Masasi – Nachingwea kwa kiwango cha lami utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amandus Julius Chinguile, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa barabara ya Masasi – Nachingwea inayounganisha makao makuu ya wilaya ya Masasi na Nachingwea, imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina tangu mwaka 2015. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami, barabara yenye urefu wa kilometa 45. Katika mwaka wa fedha huu 2020/2021, jumla ya shilingi bilioni 1.43 zimetengwa kwa ajili ya maandalizi ya kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha za ujenzi pia imeendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali kwa barabara hii ambapo katika mwaka wa fedha wa 2020/2021, jumla ya shilingi milioni 232.66 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ili barabara hii iendelee kupitika katika majira yote ya mwaka.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. GEORGE N. MALIMA Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kuanzia Njia Panda ya Kongwa hadi Mpwapwa Mjini yenye urefu wa takribani kilometa 30 ambayo ipo katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Njia Panda ya Kongwa hadi Mpwapwa ulianza kutekelezwa kwa kujengwa kwa kiwango cha lami kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014. Ujenzi huu ulianza baada ya kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina mwaka 2013 uliohusisha barabara ya Mbande – Kongwa Junction. Kongwa Junction – Ugogoni kilometa 17.5, Kongwa Junction – Mpwapwa – Ving’awe kilometa 38.85 na Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe kilometa 46.93.
Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ujenzi kwa kiwango cha lami ulianza, ambapo hadi sasa ujenzi wa sehemu ya Barabara ya Mbande – Kongwa Junction kilometa 16.7 umekamilika. Serikali kwa sasa inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Njia Panda ya Kongwa hadi Mpwapwa. Katika mwaka wa fedha huu tunaondelea nao Serikali imetenga shilingi bilioni 4.95 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami katika mji wa Mpwapwa. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa utaendelea kutekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imeendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali ya barabara hizi ili ziendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi bilioni 1.1 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Pandambili – Saguta – Mpwapwa – Ng’ambi na shilingi milioni 751.596 kwa ajili ya matengenezo ya barabara ya Manchali – Ng’ambi – Kongwa Junction – Hogolo Junction ambapo barabara ya Njiapanda ya Kongwa hadi Mpwapwa imezingatiwa. Ahsante.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya Likuyufusi - Mkenda yenye urefu wa kilometa 124 kwa kiwango cha lami ili kufungua zaidi fursa za kiuchumi kati ya nchi yetu na Msumbiji?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Likuyufusi – Mkenda yenye km 124 ni barabara muhimu kwa kuwa inaunganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji kupitia Mto Ruvuma.
Aidha, barabara hii inahudumia wasafiri wanaotumia uwanja wa ndege wa Songea wanaotokea Nchi jirani ya Msumbiji na maeneo mengine ya Mkoa wa Ruvuma. Vile vile, barabara hii ni muhimu kwenye suala la ulinzi wa mipaka ya nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali ilikamilisha usanifu wa kina wa barabara hii chini ya Kampuni ya Crown Tech - Consult Limited ya Tanzania. Hata hivyo, kufuatia uchimbaji wa makaa ya mawe kwenye eneo la Mhukulu lililopo kilomita 80 kutoka Songea na kilomita 60 kutoka Likuyufusi, Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS, ilikamilisha mapitio ya usanifu wa kina wa barabara hii (mwaka 2020) ili iendane na mahitaji na mazingira ya sasa. Vile vile, katika Mwaka huu wa Fedha 2020/2021, Daraja la Mkenda limetengewa shilingi milioni 110 kwa ajili ya kuendelea na usanifu wa kina.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa awamu ambapo katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 shilingi bilioni 1.59 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kilomita 10. Kazi inatarajiwa kuanza mwezi Aprili, 2021 baada ya kukamilisha taratibu za manunuzi. Aidha, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni
1.346 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ili barabara hii iweze kupitika majira yote ya mwaka.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Lupiro – Malinyi – Londo – Namtumbo, yenye urefu wa kilometa 296 ambayo ipo katika Ilani ya CCM 2020?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Antipas Zeno Mgungusi, Mbunge wa Malinyi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Lupiro – Malinyi – Londo – Namtumbo yenye urefu wa kilometa 296 ni sehemu ya barabara kuu ya Mikumi – Kidatu – Ifakara – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo – Lumecha yenye kilometa 547 ambayo inaunganisha Mikoa ya Morogoro na Ruvuma.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hii, Wizara kupitia TANRAODS, imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina mwaka 2018. Ujenzi wa sehemu ya Kidatu – Ifakara kilometa
66.9 kwa kiwango cha lami pamoja na Daraja la Ruaha Mkuu unaendelea. Fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu iliyobaki ikiwemo ya Lupiro – Malinyi – Londo – Namtumbo zinaendelea kutafutwa na Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati ikiendelea kutafuta fedha za ujenzi, Serikali pia imeendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali ya barabara hii, ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 720 na shilingi milioni 377.2 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hii katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma mtawalia ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itamaliza kipande cha barabara kutoka Mbagala Zakhem hadi Mbagala Kuu na kipande cha barabara toka Mbande – Kisewe hadi Msongola?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Jimbo la Mbagala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Mbagala Zakhem – Mbagala Kuu yenye urefu wa kilometa 5.1 ni miongoni mwa barabara ambazo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne alitoa ahadi mwaka 2017/2018. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ilijenga kilometa moja ya lami katika barabara hii ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipande cha barabara ya Mbande – Kisewe – Msongola ni sehemu ya barabara ya Chanika – Mbande – Mbagala Rangi Tatu yenye urefu wa kilometa 29.4 inayounganisha barabara ya Kilwa na barabara ya Nyerere. Kati ya kilometa 29.4 kilometa 22.8 zimekwishajengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 6.06 zilizobaki zipo kwenye kiwango cha changarawe. Barabara hii inasimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS).
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Msongola mpaka Mbande kilometa 6.06 kwa kiwango cha lami. Ujenzi unaendelea kwa awamu kupitia fedha za maendeleo ambapo kuanzia mwaka 2018/2019 hadi mwaka 2020/2021 jumla ya shilingi bilioni 1.05 zimetumika kujenga kilometa moja kwa kiwango cha lami nyepesi. Kazi hiyo imeanza Msongola kuelekea Mbande. Ahsante.
MHE. RASHID A. SHANGAZI Aliuliza:-
Je, ni lini ahadi ya Serikali ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Lushoto – Muyanta hadi Mlalo itaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Lushoto – Mlalo yenye urefu wa kilometa 41.93 ni sehemu ya Barabara ya Lushoto – Mlalo – Umba junction yenye urefu wa kilometa 66.23 ambapo kati ya hizo, kilometa tisa ni za lami na kilometa 32.93 ni za changarawe. Katika mwaka wa fedha wa 2020/ 2021 kiasi cha milioni 420 zimetengwa kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa mita 400 za barabara hii kwa kiwango cha lami. Ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu zilizobaki utaendelea kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa Barabara ya Lushoto – Mlalo – Umba Junction kiuchumi, kiulinzi na kiutalii na hivyo wakati ujenzi kwa kiwango cha lami kwa awamu ukiendelea, Serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo mbalimbali kila mwaka. Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 jumla ya Shilingi milioni 475.5 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo ili kuhakikisha kuwa barabara hiyo inapitika majira yote ya mwaka.
MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE Aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa Daraja la Mto Mbaka linalounganisha Jimbo la Busokelo na Rungwe litakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fredy Atupele Mwakibete, Mbunge wa Busokelo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Daraja la Mto Mbaka ambalo lipo katika barabara ya Katumba - Lwangwa - Tukuyu yenye jumla ya kilometa 81, linaunganisha Halmashauri ya Busokelo na Mji wa Tukuyu. Barabara hiyo ni ya mkoa na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, hapo awali daraja hili lilikuwa la chuma (Bailey) lakini kwa kuzingatia umuhimu wa daraja hilo lililopo kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya kilimo na mazao ya misitu, Serikali iliamua kulijenga kwa kiwango cha zege kuanzia mwaka 2018. Hata hivyo, wakati ujenzi ukiendelea kulijitokeza changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na usanifu ambao ilibidi urudiwe kuendana na hali halisi ya eneo husika. Usanifu huo ulikamilika mwezi Oktoba, 2019.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Mkandarasi anaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo ambapo kazi za ujenzi zimefikia asilimia 68 na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2021. Ahsante.
MHE. NAPE M. NNAUYE K.n.y. MHE. GODWIN E. KUNAMBI Aliuliza: Serikali ina mpango wa kuunganisha mikoa yote kwa mtandao wa barabara za lami, ikiwemo barabara yenye urefu wa kilometa 223 inayounganisha Mikoa ya Njombe na Morogoro kupitia Mlimba ambayo pia iko katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM):-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara anayozungumzia Mheshimiwa Mbunge ni Barabara ya Ifakara – Mlimba – Taweta – Madeke yenye urefu wa kilometa 220.22 ambayo ni barabara ya mkoa inayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu ya kutoka Ifakara hadi Kihansi (kilometa 126) ili kuunganisha na kipande cha barabara ya lami (kilometa 24) kilichojengwa hapo awali kati ya Kihansi na Mlimba.
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sehemu iliyosalia kati ya Kihansi na Madeke (kilometa 94.2) umepangwa kufanyika katika mwaka huu wa fedha wa 2020/2021 kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB). Kazi hii ipo katika hatua ya manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ina kamilisha usanifu wa kina, imeendelea kutenga fedha na kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika kipindi chote cha mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021, jumla ya shilingi bilioni 2.29 zimetengwa. Ahsante.
MHE. FLORENT L. KYOMBO Aliuliza:-
Pamoja na kazi nzuri ya miradi ya kutengeneza barabara Nkenge, viongozi wetu kwa nyakati tofauti wameahidi kufanya maboresho ya miundombinu ya barabara za Kabyaile/Shozi – Njiapanda ya Gera, Minziro – Mutukula, Kaja Hospitali ya Mugana (Bwanja).
Je, ni lini barabara hizo zitatengenezwa ili kuondokana na kero hizo zinazowapata wananchi wanaotumia barabara hizo kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Nkenge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Mutukula – Minziro (kilometa 15.8) ni barabara ya ulinzi na pia ni moja ya ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Barabara hiyo inatakiwa kufunguliwa na tayari kilometa mbili zipo na zinatumika. Kilometa 13.8 zilizosalia zinapita katika mashamba na Hifadhi ya Msitu wa Minziro na zitaendelea kufunguliwa kwa awamu. Makisio ya ujenzi wa barabara hiyo yamefanyika na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS)ambapo jumla ya shilingi bilioni 3.63 zinahitajika kwa ujenzi wa kiwango cha changarawe na shilingi bilioni 9.994 zinahitajika kwa ujenzi wa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara zingine ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja, Serikali itaendelea kuziboresha ili kuhakikisha kuwa zinapitika vizuri katika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. DAIMU I. MPAKATE Aliuliza:-
Je, ni lini barabara ya Mtwara Pachani – Nallasi – Tunduru itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mtwara Pachani – Lingusenguse – Nallasi Tunduru yenye urefu wa kilometa 300 kwa kiwango cha lami. Kazi hii ilitekelezwa na Mhandisi Mshauri GEG wa Ureno kwa gharama ya shilingi bilioni 2.559 na ilikamilika mwaka jana (2020). Kwa sasa, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati ujenzi wa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Barabara nchini, inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2.293 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hiyo.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI Aliuliza:-
Je, ni lini Daraja la Kisorya – Lugezi litakalounganisha Wilaya za Bunda na Ukerewe litajengwa ili kurahisisha ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Wilaya hiyo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa ujenzi wa daraja litakalounganisha Wilaya ya Bunge na Ukerewe ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba – Kisorya – Nansio yenye urefu wa kilomieta 121.6 ambao utekelezaji wake umeanza na uko katika hatua mbalimbali. Kazi ya upembuzi yakinifu na usaniifu wa kina wa barabara ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba hadi Kisorya yenye urefu wa kilometa 107.1 ilikamilika Machi, 2013. Aidha, usanifu wa kina wa sehemu ya barabara ya Kisorya – Rugezi – Nansio (Ukerewe) yenye urefu wa kilometa 14.5 pamoja na Daraja la Rugenzi – Kisorya ulikamilika Aprili, 2017.
Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa mradi huu umegawanyika katika sehemu tatu, yaani Lots tatu, ambazo ni Nyamuswa – Bunda – Bulamba (Lot I) yenye urefu wa kilometa 56.1; Lot II bulamba – Kisorya yenye km. 51 na Lot III Kisorya – Lugezi – Nansio yenye urefu km. 14.5 inayojumuisha na daraja la Kisorya – Rugezi yaani daraja lina urefu wa mita 1000. Hadi sasa ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Bulamba – Kisorya ambao ni Lot II umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba Lot I kwa kiwango cha lami unaendelea na umefikia asilimia tano. Aidha, ujenzi wa sehemu ya Rugezi – Nansio Pamoja na daraja la Kiisorya – Rugezi utaannza baada ya fedha kupatikana.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa sehemu ya Kisorya – Rugezi – Nansio ikiwemo ujenzi wa daraja Serikali kupitia wakala wa ufundi na umeme TEMESA inaendelea kutoa huduma ya kuvusha wananchi wa maeneo haya kupitia kivuko cha MV Ujenzi.
MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE Aliuliza:-
Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga reli ya TAZARA kutokea Tunduma kwenda Kasanga ili kuwa na manufaa mapana ya kiuchumi na matumizi mazuri ya Bandari ya Kasanga na kuufungua Mkoa wa Rukwa kiuchumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege, Mbunge wa Kalambo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na mkakati wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya reli nchini ambayo utekelezaji wake unazingatia kipaumbele kutokana na utekelezaji wa miradi ya reli kuhitaji fedha nyingi. Hivi sasa, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu wa Reli ya Mpanda – Karema na ni matumaini yetu kwamba, mradi wa reli hii utakapokamilika, utaifungua Mikoa ya Rukwa na Katavi kiuchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kujenga reli ya kutoka Tunduma hadi Kasanga, naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, ushauri wake umepokelewa na Wizara itaufanyia kazi. Aidha, kama nilivyosema awali, kwa kuwa miradi ya reli inahitaji fedha nyingi, utekelezaji wa ushauri huu utazingatia matokeo ya upembuzi yakinifu utakaofanywa kuhusu kipande hicho cha reli ikiwa ni pamoja na vipaumbele vya nchi. Ahsante.
MHE. OMARI M. KIGUA Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza ahadi ya muda mrefu ya ujenzi wa barabara kutoka Kilindi kwenda Gairo kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nitoe shukrani kwa Mwenyezi Mungu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuniamini ili niweze kumsaidia katika nafasi ya Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hivyo, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kilindi – Yogwe – Gairo yenye jumla ya kilometa 115.7 ni barabara ya Mkoa inayounganisha mikoa ya Tanga na Morogoro kupitia Wilaya ya Kilindi na Gairo na inahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) katika mikoa ya Tanga na Morogoro.
Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na ufinyu wa bajeti, kwa sasa Serikali haijapata fedha ya kuanza ujenzi wa barabara ya Kilindi – Iyogwe – Ngirori hadi Gairo kwa kiwango cha lami. Aidha, Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hii ili kuhakikisha kuwa inaendelea kupitika vizuri katika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO Aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Kolandoto hadi Kishapu kwa kiwango cha lami utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la na Mheshimiwa Boniphace Nyangindu Butondo, Mbunge wa Kishapu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kolandoto hadi Kishapu inayojulikana kwa jina la Kolandoto – Mwangongo yenye urefu wa kilometa 53 ni sehemu ya barabara ya Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Sibiti – Oldeani B, yenye urefu wa kilometa 328 inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ili kuijenga kwa kiwango cha lami imekamilika. Kazi hii ilifanywa na Mhandisi Mshauri M/S. Intercontinental Consultants and Technocrats pvt Ltd ya India.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeanza maandalizi ya kuanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami ambapo katika mwaka huu wa fedha tunaoendelea nao, jumla ya hilingi milioni 2,500 (bilioni 2.5) zilitengwa. Aidha, wakati maandalizi ya kuanza ujenzi yakiendelea, Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 443.31 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali.
MHE. ALFRED J. KIMEA Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Old Korogwe kwenda Kwamndolwa - Magoma - Mashewa - Bombomtoni - Maramba hadi Mabokweni yenye urefu wa kilomita 127.54 kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa Rais pamoja na Waziri Mkuu kwa wananchi wa Korogwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Alfred James Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Old Korogwe – Kwamndolwa – Magoma – Mashewa – Bongomtoni – Maramba hadi Mabokweni yenye urefu wa kilometa 127.69 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa barabara hii kiuchumi kwa wananchi wanaoishi maeneo inayopita barabara kama ilivyotajwa hapo juu. Ili kuweza kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 1,450.78 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali.
MHE. HAMIDA M. ABDALLAH Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itapeleka injini mpya ya Kivuko cha MV Kitunda - Lindi Mjini?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamida Mohamed Abdallah, Mbunge wa Lindi Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), umetenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 850 kupitia vyanzo vyake vya ndani kwa ajili ya ukarabati wa Vivuko nchini kikiwemo MV Kitunda ambacho ukarabati wake utahusisha ubadilishaji wa injini pamoja na matengenezo mengine. Ukarabati huu utaanza robo ya pili ya mwaka huu wa fedha. Ahsante.
MHE. KASALALI E. MAGENI K.n.y. MHE. SHANIF M. JAMAL Aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Hungumalwa - Ngudu hadi Magu kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) Alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shanif Mansoor Jamal, Mbunge wa Kwimba kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya kutoka Hungumalwa – Ngudu hadi Magu ni barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilometa 71. Barabara hii ni kiunganishi muhimu kati ya Wilaya za Kwimba na Magu kupitia Hungumalwa - Ngudu - Bukwimba hadi Isandula Wilayani Magu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) ilikamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Hungumalwa – Ngudu – Bukwimba – Magu yenye urefu wa kilometa 71 mwaka 2019. Katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 1,500 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami, Serikali kupitia (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka ambapo katika mwaka huu wa fedha jumla ya shilingi milioni 926.711 zimetengwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. MAIMUNA A. PATHAN Aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa barabara ya Masasi hadi Liwale kupitia Nachingwea kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GEOFREY K. MSONGWE) Alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Ahmad Pathan Mbunge Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Masasi hadi Liwale kupitia Nachingwea kwa kiwango cha lami ambapo kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa sehemu ya Masasi – Nachingwea – Nanganga yenye urefu wa kilometa 90 ilikamilika mwaka 2014 na sehemu ya Liwale – Nachingwea yenye urefu wa kilometa 130 imekamilika mwezi Juni, 2021. Katika mwaka huu wa fedha 2021/2022, jumla ya shilingi milioni 1,500 yaani sawa na shilingi bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Masasi – Nachingwea.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili kuhakikisha inaendelea kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022, jumla ya shilingi milioni 634 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali.
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Kinyata kwa njia nne kutoka Mwanza Jiji kuelekea Usagara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Shing’oma Mabula, Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyamagana – Usagara ni sehemu ya barabara Kuu ya Mwanza – Shinyanga Mpakani yenye urefu wa kilometa 104. Barabara hii ni muhimu katika kukuza uchumi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na ni kiunganishi kati ya Mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Mara, Geita na nchi jirani.
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imeanza mipango ya kuanza ujenzi wa barabara ya Mwanza hadi Usagara kwa njia nne. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii unaendelea ambapo umezingatia kupanua barabara hii kuwa na njia nne kuanzia Mwanza Mjini hadi Usagara yenye urefu wa km 22. Kazi hii inafanywa na Mhandisi Mshauri M/s NIMETA Consult (T) Ltd ya Tanzania kwa gharama ya Shilingi Milioni 980.84. Aidha, usanifu wa kina unatarajiwa kukamilika Septemba, 2021 na baada ya kukamilika barabara hiyo itaingizwa kwenye mpango wa ujenzi ikiwa ni pamoja na upanuzi wa njia hizo nne kutoka Mwanza Jiji hadi Usagara kutegemea na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-
Je, lini ni Serikali itatekeleza ahadi iliyotolewa na Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni ya kumaliza mgogoro wa ardhi uliopo kati ya wananchi na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege KIA?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kusimama hapa mbele baada ya kupewa kura za kutosha na wananchi wa Tarime Vijijini, naomba niwashukuru sana kwa ushirikiano. Pia, namshukuru Mungu kwa yote yaliyotokea na namshukuru sana Mheshimiwa Rais, Samia Suluhu Hassan kuniamini na kunipa nafasi ya kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Ujenzi na Uchukuzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Hai, kama ifuatavyo: - (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwaka 1969 Serikali ilitenga eneo lenye ukubwa wa ekari 11,085 kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA). Eneo hilo lilipimwa mwaka 1989 kwa ramani ya upimaji Na. E255/18 iliyosajiliwa na namba 231264 inayofahamika kama FARM No.1 lenye Hati namba. 22270 iliyotolewa 20 Machi, 2005.
Mheshimiwa Spika, mnamo mwaka 2001 Serikali ilibaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kutoka vijiji vinavyopakana na KIA vya Sanya Station, Chemka, Tindigani na Mtakuja vilivyopo Wilaya ya Hai na Vijiji vya Majengo, Samaria na Malula vilivyopo Wilaya ya Arumeru kuingia kwenye eneo la KIA na kuweka makazi ya kudumu.
Mheshimiwa Spika, Serikali ilichukua hatua za kufanya tathmini shirikishi wa mali za wananchi ili kuwaondoa kwa lengo la kutimiza azma ya Serikali kuendeleza KIA na pia kulinda usalama wa Kiwanja. Katika utathmini huo, ilibainika kwamba ndani ya eneo hilo kuna kaya 289 zenye thamani ya fidia iliyotakiwa shilingi 426,020,500/=. Fedha za kulipa fidia hizo hazikuwepo wakati huo, kwa hiyo, fidia haikulipwa.
Mheshimiwa Spika, mwaka 2013, 2018 na 2019 kwa nyakati tofauti, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kushirikisha TAMISEMI, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Mipango, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha, Ofisi ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Wilaya za Hai na Arumeru imekuwa ikishughulikia suala hili kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji husika ili kupata suluhu kwa kubaini idadi ya kaya zenye makazi ya kudumu katika eneo la KIA na kufanya tathmini upya.
Mheshimiwa Spika, mwezi Juni, 2018 zoezi la uwekaji wa alama lilianza ambapo Vijiji vya Majengo na sehemu ya Kijiji cha Mtakuja viliwekwa alama za kudumu. Vijiji vya Samaria na Malula vilivyopo Wilaya ya Arumeru, Vijiji vya Tindigani na Sanya Station katika Wilaya ya Hai vilikataa kutoa ushirikiano kwa Timu ya Wataalam kwa kukataza wataalam katakata kuingia katika eneo hili.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imejipanga kukamilisha zoezi hili kwa kurudishia mipaka ya kudumu ya KIA na kubaini idadi ya kaya zilizopo ndani na kufanya tathmini upya na kupata kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa ili zoezi hili liweze kumalizika. Ahsante.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaweka taa katika barabara kuu ya Mji wa Maswa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki, kama ifuatavyo:- Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ilishaanza kazi ya uwekaji taa katika barabara kuu ya Mwigumbi hadi Maswa eneo la Maswa Mjini katika mwaka wa fedha 2020/2021. Jumla ya taa za barabarani 18 zimeshawekwa ambazo zimegharimu jumla ya Shilingi milioni 81.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROADS, imepanga kuendelea na uwekaji wa taa katika barabara kuu katika Mji wa Maswa katika mwaka wa fedha 2021/2022. Ahsante.
MHE. IDD K. IDDI aliuliza:-
Je, nili ni Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Geita – Bukoli hadi Kahama kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasimu Iddi Iddi, Mbunge wa Msalala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na maandalizi ya makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Geita – Bukoli hadi Kahama yenye urefu wa kilomita 139 inayounganisha mikoa ya Geita na Shinyanga.
Mheshimiwa Spika, kazi hii ilifanywa na Mhandisi Mshauri ENV Consult (T) Ltd kwa gharama ya Shilingi milioni
440. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Aidha, Kampuni ya Uchimbaji Madini BARRICK imeonyesha nia ya kufadhili ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Kahama – Bulyanhkulu – Geita yenye urefu wa kilometa 120.2. Kwa sasa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Wizara ya Madini zinaendelea na mazungumzo na Kampuni ya BARRICK Kuhusu utaratibu wa ujenzi wa barabara hii.
Mheshimiwa Spika, wakati ujenzi wa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha Wizara yangu inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka ambapo katika mwaka wa fedha huu wa 2020/2021, jumla ya shilingi milioni 872.966 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hiyo.
Aidha, ninapenda kulifahamisha Bunge lako tukufuku kuwa ili ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ufanyike, hatua mbalimbali hufuatwa ambazo ni pamoja na upembuzi yakinifu, usanifu wa kina. Utayarishaji wa Nyaraka za zabuni na taratibu za ununuzi za kumpata mkandarasi wa ujenzi. Hivyo, kukamilika kwa hatua tajwa, maana yake nikuanza kwa mradi husika. Ahsante.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Makofia kupitia Mlandizi hadi Vikumbulu Kisarawe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimwa Michael Costantino Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Makofia – Mlandizi – Vikumbulu yenye urefu wa kilometa 135.97 ni barabara ya mkoa inayounganisha Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Kisarawe. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina pamoja na uhakiki wa mali zitakazoathiriwa na mradi sehemu ya Makofia – Mlandizi – Maneromango yenye urefu wa kilometa 100 umekamilika. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii utaanza baada ya kupata fedha ambazo Serikali inaendelea kutafuta.
Mheshimiwa Spika, wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Wizara yangu inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka ambapo katika Mwaka huu wa Fedha wa 2020/21 jumla ya shilingi 1,524.000.07 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hii. Ahsante.
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatengeneza kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mbalizi – Mkwajuni ili kuepusha adha wanayokutana nayo Wananchi hususani kipindi cha mvua?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mbalizi – Chang’ombe – Mkwajuni – Patamela – Makongolosi yenye urefu wa kilometa 117 ni barabara ya Mkoa inayounganisha Mkoa wa Mbeya na Songwe na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Mbalizi hadi Galula yenye urefu wa kilometa 56.
Aidha, taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zizonaendelea kwa sehemu ya Galula – Mkwajuni - Makongolosi kilometa 61 zinaendelea. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Mbalizi hadi Galula chenye urefu wa kilometa 56 ambayo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika.
Mheshimiwa Spika, wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), inaendelea kuifanyia matengenezo ya aina mbalimbali kila mwaka barabara hii. Ahsante.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza:-
Kasi ya ujenzi wa barabara ya Muheza – Amani sio ya kuridhisha na hadi sasa maeneo korofi bado hayajafikiwa:-
Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwa na awamu ya pili katika ujenzi wa barabara hiyo kuanzia Amani kuelekea Muheza ili kutatua changamoto zilizopo wakati ujenzi wa barabara ukiendelea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamis Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara ya Muheza – Amani yenye urefu wa kilometa 40, Serikali iliamua kuijenga kwa kiwango cha lami kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina mwaka 2015. Awamu ya kwanza ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sasa yenye urefu wa kilometa saba kuanzia Muheza kuelekea Bombani inaendelea na imefikia asilimia 70.
Mheshimiwa Spika, mara baada ya kukamilika kwa sehemu ya kwanza ya mradi huu unaoendelea, ujenzi wa sehemu ya pili ya kuanzia Bombani hadi Amani utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha. Lengo ni kukamilisha ujenzi wa barabara yote kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha za kukamilisha ujenzi wa sehemu ya barabara iliyobaki, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ikiwemo sehemu korofi ili kuhakikisha inapitika majira yote. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, barabara hii ilitengewa shilingi milioni 600 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali, ahsante.
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kilometa 200 kutoka Kilyamatundu kupitia Ilemba, Muze, Mfinga mpaka Majimoto?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kilyamatundu – Muze – Mfinga – Kasansa hadi Majimoto yenye urefu wa kilometa 206 ni barabara ya Mkoa inayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini yaani TANROADS. Barabara hii inaunganisha Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Songwe eneo la Kilyamatundu na Kamsamba katika Daraja la Momba.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hii, Serikali ilianza kuchukua hatua za kuimarisha barabara hii kwa kuanza na kukamilisha ujenzi wa Daraja la Momba lenye urefu wa mita 84 na barabara za maingilio zenye urefu wa kilometa 1.2 ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa sana cha mawasiliano baina ya Mikoa ya Rukwa, Katavi na Songwe.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Ntendo – Muze – Kilyamatundu ambao unahusisha sehemu ya Kilyamatundu – Muze yenye urefu wa kilometa 142. Kazi ya usanifu imefikia asilimia 50. Mara usanifu wa kina utakapokamilika, maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami yataanza kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza:-
Barabara ya kutoka Kibena (Stop Lupembe) mpaka Madeke C Mfiji, kilometa 125, imeshafanyiwa usanifu na upembuzi yakinifu tangu mwaka 2015.
Je, ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kibena - Lupembe – Taweta yenye urefu wa kilometa 125 ni Barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Njombe. Kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina pamoja na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya taratibu za ununuzi wa Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha huu wa 2020/2021, Serikali imetenga jumla ya Shilingi bilioni 5.96 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya barabara ya Kibena – Lupembe yenye urefu wa kilometa 50. Aidha, wakati Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa vipande vingine, Wizara yangu inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Makamu wa Rais kwa Wananchi wa Mbinga ya kujenga barabara ya Mbinga – Litembo – Kigonsera hadi Matiri kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Liuka Kapinga Beyana, Mbunge wa Mbinga Vijiji kama ifuatavyo;
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imeanza kutekeleza kwa awamu mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara tajwa kwa kuanzia na sehemu ya Mbinga – Mbuji – Litembo yenye urefu wa kilometa 24. Hadi sasa jumla ya kilometa 4.89 zimekwishajengwa kwa kiwango cha lami. Kazi hiyo itaendelea kwa awamu kila mwaka kulingana na upatikanaji wa fedha. Aidha, wakati Serikali ikiendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami, barabara hii itaendelea kufanyiwa matengenezo mbalimbali ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 674.896 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu barabara ya Kigonsera – Matiri hadi Kilindi yenye urefu wa kilometa 35.32, Serikali inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iweze kupitika majira yote ya mwaka.
MHE. SILLO D. BARAN aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Dareda – Bashnet – Dongobesh kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Sillo Daniel Baran, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Dareda – Bashnet hadi Dongobesh yenye urefu wa kilometa 54 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania- TANROADS ambapo kilometa 10 zimejengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 44 ni za changarawe. Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Dareda – Bashnet hadi Dongobeshi kwa kiwango cha lami. Kazi hii ilifanywa na Mhandisi Mshauri Luptan Consults Ltd kwa kushirikiana na Mhandisi Consultancy Ltd kwa gharama ya shilingi milioni 398. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Wizara yangu kupitia TANROADS inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 513.594 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hiyo. Ahsante.
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza:-
(a) Je, kwa nini barabara ya Mpanda – Ulyanhulu – Kahama haikujengwa katika kipindi cha 2015 – 2020 kama ilivyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi 2015 - 2025?
(b) Je, ni lini sasa ujenzi wa barabara hiyo utaanza kama ilivyoelekezwa na Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimwa Rehema Juma Migilla, Mbunge wa Ulyanhulu, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyanhulu yenye urefu wa kilometa 457 inayounganisha Mikoa ya Katavi, Tabora na Shinyanga ni moja ya barabara zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020. Barabara hii ipo kwenye kundi la miradi inayotakiwa kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.
Mheshimiwa Spika, mkataba kwa ajili ya Upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa barabara ya Mpanda – Ugala – Kaliua – Ulyankulu – Kahama ulisainiwa tarehe 18 Agosti, 2020 kati ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Kampuni ya Crown Tech Consult Ltd kwa gharama ya shilingi milioni 940.30. Kazi hii itafanyika ndani ya miezi 12 na inatarajiwa kukamilika Septemba, 2021. Mara baada ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa Kina kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiendelea, Wizara yangu kupitia TANROADS, inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Aidha, ninapenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa ili ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ufanyike, hatua mbalimbali hufuatwa ambazo ni pamoja na upembuzi yakinifu, usanifu wa kina, utayarishaji wa nyaraka za zabuni na taratibu za ununuzi wa kumpata mkandarasi wa ujenzi. Hivyo, kuanza kwa hatua tajwa, maana yake ni kuanza kwa mradi husika. Ahsante.
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya Tingi – Kipatimu yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami hasa ikizingatiwa kuwa barabara hiyo inapita katika maeneo yenye kumbukumbu za Vita vya Majimaji na vivutio muhimu vya Utalii?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa barabara ya Tingi – Kipatimu yenye urefu wa kilometa 50 kwa kiwango cha lami. Hata hivyo, mkakati wa Serikali kwa sasa ni kuunganisha makao makuu ya mikoa kwa barabara za lami zilizoainishwa kwenye shoroba za maendeleo (development corridor). Serikali itakapokamilisha mpango huu barabara nyingine za mikoa zitafuata ikiwemo barabara ya Tingi – Kipatimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na matengenezo ya kawaida na matengenezo ya muda maalum ili kuifanya barabara hii kupitika majira yote ya mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 496.569 zimetengwa kwa ajili ya kuifanyia matengenezo barabara hii. Aidha, Serikali imepanga kuimarisha baadhi ya sehemu korofi kwa kuziwekea lami. Ahsante.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja kwenye Mto Malagarasi ili kuunganisha Kata ya Ilagara na Kata ya Sunuka katika Wilaya ya Uvinza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Josephine, Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Daraja la Malagarasi (Lower Malagarasi Bridge) linaunganisha Kata ya Ilagala na Kata ya Sunuka katika Wilaya ya Uvinza kupitia Barabara ya Simbo – Ilagala hadi Kalya.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa daraja hili katika bajeti ya mwaka huu wa 2020/2021, Wizara yangu imetenga shilingi milioni 345 kwa ajili ya kufanya kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Daraja hili la Malagarasi. Aidha, katika mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2021/2022 daraja hili limetengewa shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuendelea na kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina. Kwa sasa taratibu za ununuzi wa Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi hiyo zinaendelea. Baada ya kazi hiyo kukamilika, ujenzi wa daraja hili utaanza kadiri ya upatikanaji wa fedha utakavyokuwa. Asante.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya mpakani kutoka Mtawanya kwenda Nanyumbu kupitia Mpilipili – Mapili –Chikoropola – Lichele – Lupaso hadi Lipumburu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Lulindi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mpilipili – Mapili –Chikoropora – Lichele – Lupaso hadi Lipumburu ni sehemu ya barabara ya ulinzi ya Mtwara – Madimba – Tangazo –Mahurunga – Kitaya – Namikupa hadi Mitemaupinde yenye urefu wa kilometa 365.5. Sehemu ya barabara hii yenye urefu wa kilometa 258.0 imeshafunguliwa na inaendelea kufanyiwa matengenezo ya kila mwaka na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Aidha, Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuendelea kuifungua barabara hii kwa sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilometa 107.3.
Mheshimiwa Spika, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) unaendelea kuiboresha barabara hii kwa kuhakikisha inapitika majira yote ya mwaka ambapo jumla ya kilometa 10.8 zimejengwa kwa kiwango cha lami katika maeneo korofi ya milima ya Mtawanya, Kilimahewa, Mdenganamadi, Mnongodi na Dinyeke. Ahsante.
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya kutoka Magu – Bukwimba hadi Ngudu itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuu nganisha Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Makao Makuu ya Mkoa wa Mwanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Emmanuel Mageni Kasalali, Mbunge wa Sumve ,kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya kutoka Magu – Bukwimba hadi Ngudu ni sehemu ya barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilomita 71 inayoanzia Magu – Bukwimba – Ngudu hadi Hungumalwa. Barabara hii nikiunganisha muhimu kati ya Wilaya ya Magu na Kwimba kupitia Isandula (Magu) – Bukwimba – Ngudu – Nyamilama hadi Hungumalwa.
Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha kazi ya Upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Magu – Bukwimba –Ngudu hadi Hungumalwa kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 71. Kazi hii ilifanywa na Mhandisi Mshauri M/s Advanced Engineering Solution kwa gharama ya shilingi milioni 638.486 na kukamilika mwaka 2019. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za kugharamia ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Wizara yangu kupitia TANROADS inaendelea kuihudumia barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2020/ 2021 jumla ya Shilingi milioni 475.551 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hii.
MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Nyololo – Mtwango – Mafinga hadi Mgololo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GEOFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyololo – Mtwango yenye urefu wa kilomita 40.4 na barabara ya Mafinga – Mgololo yenye urefu wa kilometa 81.14 zinasimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS). Barabara ya Nyololo – Mtwango ni barabara ya mkoa ya kiwango cha changarawe na barabara ya Mafinga – Mgololo ni barabara kuu ya kiwango cha changarawe na kiwango cha lami katika maeneo korofi. Barabara hizi zinapita katika maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya biashara na chakula na pia zinahudumia viwanda kadhaa ikiwa ni pamoja na Kiwanda cha Karatasi cha Mgololo.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hizi, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nyololo – Mtwango kwa kiwango cha lami. Aidha, inaendelea kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Mafinga – Mgololo kwa kiwango cha lami, ambapo kwa sasa kazi hii ipo katika hatua za mwisho.
Mheshimiwa Spika, barabara hizi zitaingizwa katika mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Wakati Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hizi kwa kiwango cha lami, kwa sasa barabara hizi zinaendelea kufanyiwa matengenezo mbalimbali kila mwaka ili kuhakikisha kuwa zinapitika katika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. SAMWEL X. HHAYUMA aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya Kondoa – Gisambalang – Nangwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Samwel Xaday Hhyuma, Mbunge wa Hanang’, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kondoa - Nunguri - Mtiriyangwe - Gisambalang - Nangwa yenye urefu wa kilometa 81.4 ni barabara inayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROADS baada ya kupanda hadhi mwaka 2010 kutoka barabara ya wilaya na kuwa barabara ya mkoa.
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya ukarabati ili ipitike kwa mwaka mzima. Katika mwaka wa fedha huu 2020/2021, barabara hii ilitengewa jumla ya milioni 888.8 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali na ukarabati na Shilingi milioni 60 kwa ajili ya usanifu wa Daraja la Mungurwi. Serikali itaiweka barabara hii katika mpango wa kuijenga kwa kiwango cha lami kulingana na upatikanaji wa fedha. Hata hivyo, Serikali itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii kuhakikisha kuwa inapitika vizuri majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:-
Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Lumecha – Londo – Kilosa kwa Mpepo, inayounganisha mkoa wa Ruvuma na Morogoro kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Lumecha, Londo, Kilosa kwa Mpepo ni sehemu ya barabara Kuu ya Mikumi, Kidatu, Ifakara, Lupiro, Malinyi Kilosa kwa Mpepo, Londo hadi Lumecha yenye jumla ya kilometa 512 ambayo inaunganisha Mikoa ya Ruvuma na Morogoro. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ulikamilika mwaka 2018 ikiwa ni lengo la Serikali kujenga barabara yote kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, hadi sasa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mikumi hadi Kidatu kilometa 35.2 na ujenzi wa Daraja la Magufuli lenye urefu wa mita 384 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilometa 9.142 umekamilika. Aidha, ujenzi wa sehemu ya Kidatu – Ifakara ambayo ina urefu wa kilometa 66.9 unaendelea na umefikia asilimia 22.6.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa barabara hii kuanzia Lupilo, Malinyi Kilosa kwa Mpepo, Londo hadi Lumecha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami ikiwemo sehemu ya Lumecha, Londo hadi Kilosa kwa Mpepo. Aidha, wakati juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zikiendelea, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania yaani TANROADS Mkoa wa Ruvuma na Morogoro itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii kutoka Ifakara, Lupiro, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo, Londo hadi Lumecha kila mwaka ili iweze kupitika majira yote ya mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha huu wa 2020/2021, barabara hii imetengewa jumla ya shilingi milioni 3,610.54 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali. Kati ya fedha hizo shilingi milioni 985.585 ni kwa ajili ya sehemu ya barabara ya Lumecha, Londo ambayo iko Mkoa wa Ruvuma, ahsante. (Makofi)
MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-
Je, ni lini barabara ya Ibungu – Kafwafwa hadi Kyimo itafanyiwa upembuzi yakinifu na kuanza ujenzi kwa kuwa imetajwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anton Albert Mwantona, Mbunge wa Rungwe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Ibungu –Kafwafwa – Kyimo ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 68.2 ambapo kilometa 21.8 zipo Mkoa wa Mbeya na kilometa 46.4 zipo katika Mkoa wa Songwe. Barabara hii ni ya changarawe na udongo na inapita sehemu zenye miinuko mikali hivyo kupitika kwa shida wakati wa mvua kutokana na utelezi. Barabara hii ni muhimu kwa kuwa imekuwa ikitumika katika usafirishaji wa mazao mbalimbali ya chakula na biashara kwa kuwa imepita katika maeneo ya wakulima.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Ibara ya 55(c)(iv): Chama cha Mapinduzi kiliahidi kuielekeza Serikali kukamilisha/kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara mbalimbali hapa nchini zenye jumla ya urefu wa kilometa 7,542.75 ambapo miongoni mwa hizo ni hiyo Barabara ya Ibungu – Kafwafwa – Kyimo yenye urefu wa kilometa 68.2.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ibungu – Kafwafwa – Kyimo ili hatimaye iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekuwa ikifanyia matengenezo mbalimbali ili kuhakikisha inapitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE K.n.y. MHE. VUMA A. HOLLE aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Kasulu - Uvinza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino Vuma Holle, Mbunge wa Kasulu Vijijini kama ifuatavyo;
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Kasulu – Uvinza yenye urefu wa kilometa 65.9 kwa kiwango cha lami ambapo kilometa 8.9 kutoka Kasulu njiapanda ya Kanyani ni sehemu ya mradi wa barabara ya Kidakhawe – Kasulu yenye urefu wa kilometa 63 ambayo ujenzi wake kwa kiwango la lami umekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, wakati Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa sehemu ya njia panda ya Kanyani hadi Uvinza, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali kila mwaka ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 barabara hii imetengewa jumla ya shilingi milioni 1,887.9 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali. Ahsante.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Maswa hadi Lalago?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroun Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Maswa – Lalago yenye urefu wa kilometa 34 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Barabara hii ni sehemu ya Mradi wa Serengeti Southern by-pass ikianzia Maswa – Lalago – Mwanhuzi – Sibiti hadi Karatu yenye urefu wa kilometa 338. Mradi huu ulihusisha kazi ya Upembuzi Yakinifu chini ya ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na umeshakamilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza usanifu wa kina na ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali sehemu hii ya Maswa – Lalago na inapitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. EZRA J. CHIWELESA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Nyamirembe – Chato mpaka Katoke Biharamulo ya kilomita 50 kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ezra John Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Nyamirembe Port – Katoke yenye urefu wa kilometa 50 ni barabara ya Mkoa inayounganisha Bandari ya Nyamirembe ambayo ipo Mkoa wa Geita na Mji Mdogo wa Katoke ambao upo Mkoa wa Kagera kupitia vijiji mbalimbali na Hifadhi ya Burigi Chato. Barabara hii inahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeshaanza taratibu za kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwa kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa gharama ya Shilingi milioni 861.046 kwa kutumia fedha za ndani. Katika mwaka wa fedha ujao 2021/2022, fedha zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa Nyamirembe Port – Katoke, urefu wa kilomita 50.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii inaendelea kuiimarisha kwa kuifanyia matengenezo ya aina mbalimbali kila mwaka kabla ya ujenzi kwa kiwango cha lami kuanza ili barabara hiyo ipitike katika vipindi vyote vya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha 2020/2021, jumla ya Shilingi milioni 447.771 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali na kwa sasa barabara hiyo ipo katika hali nzuri. Ahsante.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara inayotoka Mtwara Mjini kwenda Msimbati ambako kuna mitambo ya visima vya gesi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shamsia Azizi Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mtwara Mjini kuanzia Mangamba – Madimba – Msimbati inayokwenda kwenye visima vya gesi vya Mnazi Bay yenye urefu wa kilometa 35.63 na barabara ya Madimba – Kilambo inayokwenda kwenye Kivuko cha Kilambo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji yenye urefu wa kilometa 16.87 ni barabara za mkoa zinazosimamiwa na Wizara yangu. Barabara hizi zinafanyiwa matengenezo kila mwaka na Wakala wa Barabara nchini Tanzania (TANROADS) na zinapitika wakati wote. Katika mwaka wa fedha ujao wa 2021/2022 zimetengwa jumla ya shilingi milioni 231 kwa ajili ya matengenezo.
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hizi pamoja na kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya kuzijenga kwa kiwango cha lami. Ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara hizi utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza:-
(a) Je, nini sababu ya barabara ya Kibiti – Lindi kuharibika mara kwa mara licha ya kufanyiwa ukarabati?
(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatiza hilo ili kuzuia ajali za mara kwa mara katika barabara hiyo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anastazia James Wambura, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kibiti – Lindi kwa sasa inabeba magari mengi na yenye uzito mkubwa zaidi ya ilivyokusudiwa wakati wa usanifu uliotumika kujenga barabara hiyo. Hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda na migodi katika Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini uliojitokeza miaka ya hivi karibuni baada ya ujenzi wa barabara hii kukamilika. Aidha, ujenzi wa viwanda vikubwa kama cha Dangote, Mkoani Mtwara na uwepo wa migodi mikubwa ya Makaa ya Mawe, Mkoani Ruvuma kumechangia ongezeko la magari yanayobeba uzito mkubwa kuliko ilivyotarajiwa wakati barabara hii inafanyiwa usanifu.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa sasa, Serikali inaendelea na mpango wa ukarabati mkubwa utakaowezesha barabara hiyo kustahimili wingi na uzito wa magari kwenye barabara hii. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 7,500 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Aidha, pamoja na juhudi za Serikali zinazoendelea, ninaomba nitoe wito kwa wasafirishaji kutumia Bandari ya Mtwara ambayo upanuzi wake umekamilika na hivyo kuwa na uwezo wa kupokea meli nyingi na kubwa kwa wakati mmoja.
Mheshimiwa Spika, kutumia bandari hii ya Mtwara itasaidia sana kupunguza usafirishaji wa mizigo mikubwa kwa njia ya barabara na hivyo kunusuru barabara hiyo kuharibika mara kwa mara.
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-
Je, ni lini barabara kutoka Kolandoto hadi Meatu itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge Viti Maalum, Simiyu kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kolandoto hadi Meatu ni sehemu ya barabara ya Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Sibiti hadi Oldeani Junction yenye urefu wa kilometa 328. Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ulishakamilika na ujenzi kwa kiwango cha lami utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha.
Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 5,000 zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Kolandoto – Mwanhuzi yenye urefu wa kilometa 62.5 na kipande cha Lalago – Ng’oboko – Mwanhuzi yenye urefu wa kilometa 74.
Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa Daraja la Mto Sibiti pamoja na barabara unganishi kwa kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 25 mpakani mwa Wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu na Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ni hatua za awali za ujenzi wa barabara hiyo ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA aliuliza:-
(a) Je, nini sababu ya barabara ya Kibiti – Lindi kuharibika mara kwa mara licha ya kufanyiwa ukarabati?
(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatiza hilo ili kuzuia ajali za mara kwa mara katika barabara hiyo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anastazia James Wambura, Mbunge Viti Maalum, lenye sehemu (a) na
(b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kibiti – Lindi kwa sasa inabeba magari mengi na yenye uzito mkubwa zaidi ya ilivyokusudiwa wakati wa usanifu uliotumika kujenga barabara hiyo. Hali hiyo inatokana na uwekezaji mkubwa wa viwanda na migodi katika Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini uliojitokeza miaka ya hivi karibuni baada ya ujenzi wa barabara hii kukamilika.
Aidha, ujenzi wa viwanda vikubwa kama cha Dangote, Mkoani Mtwara na uwepo wa migodi mikubwa ya Makaa ya Mawe, Mkoani Ruvuma kumechangia ongezeko la magari yanayobeba uzito mkubwa kuliko ilivyotarajiwa wakati barabara hii inafanyiwa usanifu.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto hiyo kwa sasa, Serikali inaendelea na mpango wa ukarabati mkubwa utakaowezesha barabara hiyo kustahimili wingi na uzito wa magari kwenye barabara hii. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 7,500 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Aidha, pamoja na juhudi za Serikali zinazoendelea, ninaomba nitoe wito kwa wasafirishaji kutumia Bandari ya Mtwara ambayo upanuzi wake umekamilika na hivyo kuwa na uwezo wa kupokea meli nyingi na kubwa kwa wakati mmoja.
Mheshimiwa Spika, kutumia bandari hii ya Mtwara itasaidia sana kupunguza usafirishaji wa mizigo mikubwa kwa njia ya barabara na hivyo kunusuru barabara hiyo kuharibika mara kwa mara.
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:-
Je, ni lini barabara ya Kisamba – Sayaka hadi Salama inayounganisha Mkoa wa Mwanza na Simiyu itaanza kuhudumiwa na TANROADS?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kisamba – Sayaka hadi Salama ni barabara ya Wilaya inayohudumiwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).
Mheshimiwa Spika, ili barabara yoyote iweze kuhudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) zipo taratibu ambazo lazima zifuatwe ikiwa ni pamoja na maombi ya kupandishwa hadhi ya kuwa barabara kuu ama ya mkoa kuwasilishwa kwenye mamlaka zinazohusika kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa kwenye Sheria ya Barabara ya mwaka 2007 na Kanuni zake za mwaka 2009 ambayo imeainisha pia vigezo vinavyohitajika katika kupandisha hadhi barabara. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Kilosa hadi Mikumi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine G. Ishengoma, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Kilosa – Mikumi ni sehemu ya barabara ya Dumila – Rudewa – Kilosa – Mikumi yenye urefu wa kilometa 142.3 ambayo ni ya Mkoa inayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROADS.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kwa awamu kama ifuatavyo:-
(i) Ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya barabara kutoka Dumila hadi Rudewa yenye urefu wa kilometa 45 ulishakamilika na barabara inatumika.
(ii) Ujenzi wa kiwango cha lami wa sehemu ya barabara kutoka Rudewa hadi Kilosa yenye urefu wa kilometa 24 ulianza Februari, 2019 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2021.
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu ya barabara iliyosalia kutoka Kilosa hadi Mikumi yenye urefu wa kilometa 73.3 kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami imeshakamilika. Serikali inaendelea na utafutaji wa fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu hiyo ya barabara. Ahsante.
MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Ifakara – Mahenge utaanza kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alaudin Hasham Salim, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Ifakara –Mahenge ni sehemu ya Barabara Kuu ya Mikumi, Kidatu, Ifakara, Lupiro, Mahenge/Malinyi, Kilosa kwa Mpepo, Londo hadi Lumecha yenye urefu wa kilometa 547 ambayo inaunganisha Mikoa ya Ruvuma na Morogoro. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii ilikamilika mwaka 2018 kwa lengo la kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi sasa ujenzi wa Daraja la Magufuli lenye urefu wa mita 384 pamoja na barabara unganishi yenye urefu wa kilometa 9.142 umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya Ifakara – Lupiro – Mahenge utaanza kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zikiendelea, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara husika ili ipitike majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi wa barabara ya Mianzini, Sambasha, Ngaramtoni hadi Hospitali ya Selari kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Noah Lemburis Ole Saputu, Mbunge wa Arumeru Magharibi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, aliagiza barabara ya Mianzini – Sambasha – Ngaramtoni hadi Hospitali ya Selari yenye urefu wa kilometa 18 kupandishwa hadhi ili isimamiwe na Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) na aliagiza ijengwe kwa kiwango cha lami. Awali barabara hii ilikuwa inasimamiwa na Halmashauri za Arusha DC.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ilifanya usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami pamoja na utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kazi ambayo ilikamilika mwaka 2019. Zabuni za ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kwa kilometa zote 18 zimetangazwa tarehe 17 Mei, 2021.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi za ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami zitaanza mara baada ya tathmini ya zabuni kukamilika na mkandarasi kupatikana. Katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 jumla ya shilingi bilioni 2.5 zimetengwa kwa ajili ya mradi huu. Ahsante.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara kutoka Mnivata hadi Masasi kupitia Newala kwa kiwango cha lami utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara Mnivata, Newala, Masasi yenye urefu wa kilometa 160 ni sehemu ya barabara ya Mtwara, Nanyamba, Tandahimba, Newala hadi Masasi yenye urefu wa kilometa 210.
Mheshimiwa Naibu Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Mtwara, Nanyamba, Tandahimba, Newala hadi Masasi yenye urefu wa kilometa 210 umekamilika. Ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo awamu ya kwanza ya sehemu ya Mtwara hadi Mnivata yenye urefu wa kilometa 50 imekamilika.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga shilingi milioni 3,000 kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mnivata, Newala, Masasi yenye urefu wa kilometa 160.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea kuifanyika matengenezo mbalimbali barabara hii ili kuhakikisha kuwa inapitika majira yote ya mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya Shilingi Milioni 1,017.33 zimetengwa. Ahsante
MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-
Je, ni lini Bandari ya Sota eneo la Shirati itaanza kurekebishwa ili kuinua uchumi, lakini pia kuboresha shughuli za kibiashara eneo la mpakani mwa Tanzania na Kenya?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege Mbunge wa Rorya kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Bandari ya Sota ni miongoni mwa Bandari za kati na ndogo 693 zilizoainishwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Bandari (TPA) ili kutangazwa katika Gazeti la Serikali kwa lengo la kuzirasimisha. Aidha, mpango huo wa urasimishaji unakwenda sambamba na zoezi la kuhuisha Mpango Mkuu wa TPA wa kuendeleza Bandari zote nchini unaojumuisha Bandari ya Sota.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa mpango huo unafanyiwa mapitio na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, mwaka huu 2021. Baada ya mpango huo kukamilika, orodha ya bandari kwa ajili ya uendelezaji ikiwemo Bandari ya Sota eneo la Shirati itatolewa kwenye tangazo la Serikali ili zihuishwe, ahsante.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Katesh – Hydom kwa kiwango cha lami ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za afya katika Hospitali ya Hydom pamoja na usafirishaji wa mazao hasa ngano?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Samweli Xaday Hhayuma, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Katesh – Hydom yenye urefu wa kilometa 67 ni sehemu ya barabara ya mchepuo wa Mbuga ya Serengeti (Serengeti Southern Bypass) ambayo inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya upembuzi yakinifu wa Barabara ya Mchepuo ya Mbuga ya Serengeti (Serengeti Southern Bypass) yenye urefu wa kilometa 575.6 inayojumuisha barabara ya Karatu – Hydom – Lalago hadi Maswa yenye kilometa 446.6, Katesh – Hydom yenye kilometa 67 na Kolandoto – Lalago yenye kilometa 62 inatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Ujerumani. Upembuzi yakinifu unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, mwaka huu 2021. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Katesh – Hydom utaanza pindi usanifu wa kina utakapokamilika na kadri ya upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya kutoka Katumbasongwe hadi Ileje kilometa 90.7 itaanza kujengwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyigulile Mlaghila, Mbunge wa Kyela, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Katumbasongwe – Ileje ni barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilometa 114.51 inayounganisha Mkoa wa Mbeya na Songwe kupitia Wilaya ya Kyela na Wilaya ya Ileje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Katumbasongwe - Kasumulu – Ngana – Ileje ipo katika taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina taratibu za ujenzi zitaanza. Aidha, Serikali inaendelea kuihudumia barabara hii kwa kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka wakati taratibu za ujenzi wa kiwango cha lami zikiendelea. Katika mwaka wa fedha huu wa 2021/ 22 barabara hii imetengewa Shilingi milioni 141.45 za matengenezo. Ahsante.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -
Je, ni lini Barabara ya kutoka Kibaoni – Kasansa – Muze – Ilemba – Kilyamatundu hadi Mlowo itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakangáta, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kibaoni hadi Mlowo ni barabara ya mkoa yenye jumla ya urefu wa kilomita 363 na inaunganisha mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe. Barabara hii inapita katika bonde la Ziwa Rukwa ambalo ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na uvuvi na hivyo kuwa kichocheo kikubwa cha kiuchumi katika mikoa ya Rukwa, Katavi na Songwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali ilianza mipango ya kuijenga kwa kuanza na ujenzi wa Daraja la Momba ambalo lilikuwa kikwazo kikubwa cha mawasiliano kati ya mikoa hii mitatu ya Rukwa, Katavi na Songwe ambao umekamilika. Ili kukamilisha ujenzi wa barabara yote kwa kiwango cha lami kuanzia Kibaoni hadi Mlowo ambayo ni kilomita 363, Serikali ipo katika hatua ya awali ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambapo kazi inaendelea kwa sehemu ya Kibaoni – Majimoto yenye urefu wa kilomita 27 iliyopo mkoani Katavi na sehemu ya Muze – Kilyamatundu yenye urefu wa kilomita 141 iliyopo Mkoa wa Rukwa. Kwa upande wa Mkoa wa Songwe, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sehemu ya Mlowo – Kamsamba yenye urefu wa kilomita 130.1 imekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Tanga – Mabokweni – Maramba – Daluni – Mtoni – Bombo – Magoma hadi Korogwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula, Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Tanga – Mabokweni – Maramba – Daluni – Bombo Mtoni – Korogwe yenye urefu wa kilometa 127.69 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Aidha, Sehemu ya barabara ya Tanga – Mabokweni yenye urefu wa kilometa 11.2 tayari imejengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kiuchumi wa barabara ya Tanga – Mabokweni – Maramba – Daluni – Bombo – Korogwe kwa wananchi wa maeneo ya Mashewa, Mabokweni, Maramba, Bombomtoni, Magoma na Daluni. Kwa kutambua umuhimu huo, Wizara imetenga fedha katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao 2021/ 2022 kiasi cha shilingi milioni 1,275.4 ambayo ni sawa na bilioni 1.2754 ili kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii. Mara baada ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii. Aidha, barabara hii itaendelea kufanyiwa matengenezo mbalimbali ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mbulu – Haydom – Singida kwa lami, ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais tangu mwaka 2015?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Mbulu - Hydom hadi Singida yenye urefu wa kilometa 160.5 inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Barabara hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili za Mbulu – Haydom urefu wa kilometa 70.5 na Haydom – Singida urefu wa kilometa 90.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sehemu ya pili ya Mbulu –Haydom imetangazwa kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa kuanza na kilometa 25 na sehemu zingine zilizobaki zitaendelea kuongezwa wakati sehemu ya kwanza ya kilometa 25 ikiendelea. Sehemu iliyobaki ya Haydom – Singida ipo katika hatua ya manunuzi ili kumpata mhandisi mshauri atakayefanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kabla ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza ujenzi wa barabara ya kutoka Manyoni - Sanza - Chipanga - Bahi hadi Dodoma kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Manyoni East – Heka - Iseke - Sanza - Chipanga katika Wilaya ya Bahi; Chidilo Juction – Bihawana Juction Dodoma yenye urefu wa kilometa 194 ni barabara ya mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS ambapo ni Mkoa wa Singida na Dodoma. Kati ya hizo kilometa 126 zinasimamiwa na TANROADS Mkoa wa Singida na kilometa 68 ni Mkoa wa Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii kiuchumi, Serikali imeanza na hatua ya kwanza ya ujenzi wa daraja la Sanza ambapo kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja lenye urefu wa mita 75 na barabara unganishi zenye jumla ya urefu wa kilometa 14.5 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami umekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya Shilingi milioni 1,500, sawa na bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Daraja la Sanza ambalo ni kiungo muhimu kwa barabara hii inayounganisha Mkoa wa Singida na Dodoma. Aidha, mipango ya ujenzi wa sehemu ya barabara inayobaki kwa kiwango cha lami itaendelea kufanyika kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. MASACHE N. KASAKA K.n.y. MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itamaliza ujenzi wa barabara ya Njombe – Mdandu – Iyayi kuelekea Mbeya?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Njombe (Ramadhani) – Mdandu – Iyayi yenye urefu wa kilometa 74 ilikamilika tangu mwaka 2015. Kwa sasa ujenzi unaendelea kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo jumla ya kilometa 14.11 kati ya kilometa 74 tayari zimejengwa kwa kiwango cha lami ikiwemo sehemu ya Mji wa kihistoria ya Mdandu.
Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021 kipande cha kilometa 1.5 kinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi milioni 929.288 na katika mwaka wa fedha 2021/2022 kipande kingine cha barabara chenye urefu wa kilometa 1.5 kinatarajiwa kuanza kujengwa na inakisiwa kugharimu shilingi milioni 929.288. Ahsante.
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -
Je, ujenzi wa barabara ya Tabora – Mbambali – Bukene – Itobo hadi Kahama umefikia hatua gani baada ya kutengewa fedha kwenye bajeti mwaka 2020/2021?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na utayarishaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Tabora – Mbambali – Bukene – Itobo yenye urefu wa kilometa 114. Kazi hii ilitekelezwa na Mhandisi Mshauri NIMETA Consult ya Tanzania na ilikamilika Aprili, 2020 kwa gharama ya shilingi milioni 790.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 jumla ya shilingi milioni 1,000 sawa na bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, aidha, wakati Serikali inaendelea na maandalizi ya kuanzia ujenzi wa barabara hii, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Ahsante. (Makofi)
MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mkwiti – Amkeni inayounganisha Mkoa wa Lindi na Mtwara kupitia Mtama?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Newala Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mkwiti – Amkeni yenye urefu wa kilometa 74.23 inayounganisha Wilaya ya Tandahimba na Newala katika Mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lindi Vijijini mkoa wa Lindi unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2020/2021, jumla ya shilingi milioni 1,807.00 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa kilometa tatu ambapo jumla ya kilometa 2.8 zimekamilika kujengwa na kazi za ujenzi zinaendelea kwenye kipande chenye urefu wa mita 200. Wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukiendelea kutekelezwa kwa awamu, Wizara yangu itaendelea kuifanyia matengenezo barabara hiyo ili iweze kupitika majira yote ahsante.
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Magu –Ng’hungumalwa kwa kiwango cha lami utaanza baada ya upembuzi yakinifu kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami, barabara ya Magu – Bukwimba - Ngudu – Ng’hungumalwa yenye urefu wa kilometa 71 ilikamilika mwaka 2019.
Katika mwaka wa fedha wa 2021/2022, Serikali imetenga shilingi milioni 1,500 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kilometa 10 kwa kiwango cha lami barabara hii. Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kadri ya upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. CECILIA PARESSO K.n.y. MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -
Je, ni lini ahadi ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege Tanga aliyoitoa Mheshimiwa Rais wakati wa uzinduzi wa Bomba la Mafuta pale Chongoleni Mkoani Tanga itaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ng’azi Ulenge, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Kiwanja cha Ndege cha Tanga ni miongoni mwa viwanja 11 vya ndege vinavyofanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Transport Sector Support Project.
Mheshimwa Spika, Benki ya Dunia imeonesha nia ya kufadhili upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga kupitia programu iitwayo Development Corridor Transport Programme.
Mheshimwa Spika, kwa sasa majadiliano kati ya Serikali na Benki ya Dunia kuhusu malipo ya fidia kwa wananchi watakaopisha utekelezaji wa mradi wa upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga, mapitio ya awali ya ripoti ya mradi huu pamoja na maandalizi ya taarifa mbalimbali zinazohitajika kabla ya mkataba wa mkopo kusainiwa yanaendelea.
Mheshimwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumhakikishia Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ng’azi Ulenge kuwa Serikali ina nia ya dhati ya kufanya upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege cha Tanga. Aidha, majadiliano kati ya Serikali na Benki ya Dunia yatakapokamilika utekelezaji wa mradi huu utaanza mara moja. Ahsante.
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza: -
Kwa muda mrefu Jimbo la Arusha Mjini limekuwa likisumbuliwa na changamoto ya mafuriko kwenye Kata ya Sembetini, Levolosi, Osunyai, Sekei, Unga Ltd, Sakina, Baraa na Olerian yanayosababishwa na miundombinu mibovu ya barabara ya Sakina – Tengeru na Airport – Soko la Kilombero?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Sakina – Tengeru umehusisha upanuzi wa barabara iliyokuwepo kutoka njia mbili kwenda njia nne na katika mito yote yamejengwa madaraja makubwa yanayopokea maji kutoka mlima Meru na kupeleka katika makorongo makubwa ya asili. Hivyo, mafuriko yanayotokea katika maeneo husika hayasababishwi na miundombinu mibovu ya barabara ya Sakina – Tengeru.
Mheshimiwa Spika, tatizo la mafuriko katika maeneo yaliyotajwa na Mheshimiwa Mbunge yanasababishwa na sababu zifuatazo: -
(i) Mabadiliko ya kimazingira yanayohusiana na ujenzi uliofanyika katika maeneo ya juu na hivyo kuongeza maji katika maeneo ya juu kuelekea kwenye maeneo ya chini;
(ii) Ujenzi holela katika mikondo asili ya maji na kupunguza upana wa njia ya maji; na
(iii) Utupaji taka ngumu kwenye mitaro ya maji na kusababisha kuziba kwa makalvati na kupelekea maji kupita juu ya barabara na kusambaa katika maeneo ya wananchi.
Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na tatizo la mafuriko, Serikali kupitia Tanzania Strategic Cities Project unaotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Arusha, inafanya utafiti wa kina ili kuona ni jinsi gani mafuriko haya yanaweza kuzuiwa kwa kujenga miundombinu ya kukusanya maji yote yanayotoka Mlima Meru na kuleta madhara ya mafuriko. Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Cheil Engineering ya Korea Kusini anaendelea na utafiti huo, ahsante.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Iringa Mjini hadi Kilolo ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Iringa Mjini hadi Kilolo yenye urefu wa kilometa 33.6 ni sehemu ya barabara ya Iringa iliyoanzia Ipogolo – Idete yenye urefu wa kilometa 67.7 ambayo ni barabara ya Mkoa inayosimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS). Kilometa 9.9 za barabara hiyo ni za lami na kilometa 23.7 nyingine ni za changarawe.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara ya Iringa Mjini hadi Kilolo, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) ilikamilisha Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo mwaka 2009. Kwa sasa ujenzi wa kilometa 10 kwa kiwango cha lami kati ya kilometa 23.7 za changarawe unaendelea huku marejeo ya usanifu wa mwaka 2009 yakiendelea.
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itaendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami wa kilometa 13.7 zilizosalia kadri ya upatikanaji wa fedha. Aidha, Serikali itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara yote kutoka Iringa Mjini hadi Idete kuhakikisha kuwa inapitika vipindi vyote vya mwaka, ahsante.
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kolandoto – Oldean Junction utaanza kwa kuwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ulishafanyika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Meatu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Kolandoto –Lalago – Mwanhuzi – Sibiti – Qangded – Oldean Junction yenye urefu wa kilometa 328 ni barabara kuu inayounganisha Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Singida na Arusha.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 2,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa awamu kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya barabara ya Kolandoto – Mwanhuzi yenye urefu wa kilometa 62.5 na shilingi milioni 3,000 kwa ajili ya barabara ya Lalago – Ngóboko – Mwanhuzi yenye urefu wa kilometa 74 ambayo ni sehemu ya barabara aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge. Ujenzi wa barabara hizi utaendelea kutekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, wakati juhudi za kuanza ujenzi wa barabara hizo zikiendelea, Serikali itaendelea kutenga fedha za matengenezo ya barabara hii ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 shilingi milioni 849.97 zimetengwa kwa sehemu ya Kolandoto hadi Mwangongo mkoani Shinyanga, shilingi milioni 540.995 zimetengwa kwa sehemu ya Mwangongo hadi Sibiti mkoani Simiyu, shilingi milioni 579.118 zimetengwa kwa sehemu ya Sibiti hadi Matala mkoani Singida na shilingi milioni 1,507.352 zimetengwa kwa sehemu ya Matala hadi Oldean mkoani Arusha. Ahsante.
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye kilometa 258 itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 25 inavyoelekeza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa, Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mchakato wa zabuni wa kumpata Mhandisi Mshauri atakayefanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kwa ajili ya kuijenga Barabara ya Nangurukuru – Liwale yenye urefu wa kilometa 258 kwa kiwango cha lami umeshakamilika na mkataba wa kazi hii unatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwezi Juni, 2021. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni
548.603 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Kazi ya usanifu itakapokamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ya ujenzi wa Barabara ya Bugene kupitia Pori la Kimisi hadi Benaco kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Oliver Daniel Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza kutekeleza ahadi ya Rais ya ujenzi wa barabara ya Bugene kupitia Pori la Kimisi hadi Benaco kwa kiwango cha lami ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Bugene – Kasulo – Kumunazi yenye urefu wa kilometa 128.5 ulikamilika mwaka 2019. Taratibu za manunuzi ya Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park yenye urefu wa kilometa 60 zipo katika hatua ya mwisho kwa kutumia fedha za ndani. Katika mwaka wa fedha huu wa 2021/2022 shilingi bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Aidha, Serikali imewasilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika maombi ya fedha za ujenzi kwa sehemu iliyobaki ya Burigi Chato National Park hadi Kumunazi yenye urefu wa kilometa 68.5. Ahsante.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kutenga fedha za kuvunja Mlima Londo ili kuunganisha Wilaya ya Malinyi na Namtumbo hata kwa kiwango cha changarawe ili njia hii iweze kupitika huku Serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami wa Barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa –Kwa Mpepo – Namtumbo Lumecha ya kilomita 296?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Antipas Zeno Mgungusi, Mbunge wa Malinyi, kama ifuatayo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ilikamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Ifakara – Lupiro –Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha mwaka 2018. Katika usanifu huo, barabara itakayojengwa imeukwepa Mlima Londo kutokana na gharama kubwa ya kuuvunja mlima itakapopita barabara hiyo. Hivyo, Serikali itajenga barabara kwa kiwango cha lami kupita katika maeneo yaliyoainishwa katika upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo, namsihi Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Aidha, Serikali itaendelea kuifanyia matengenezo barabara hii na kuendelea kuifungua kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara za Mbezi Shule – Mpiji Magohe – Bunju kupitia Mabwe Pande na Kibamba Njia Panda – Mpiji Magohe kama zilivyoainishwa kwenye Ilani ya CCM ya mwaka 2020 - 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Issa J. Mtemvu, Mbunge wa Kibamba kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mbezi Shule – Mpiji Magohe – Bunju kupitia Mabwe Pande ni barabara inayotambulika kwa jina la Mbezi Victoria – Mpiji Magohe hadi Bunju yenye urefu wa kilometa 25; na barabara ya Kibamba Njia Panda – Mpiji Magohe inatambulika kwa jina la Kibamba Shule hadi Mpiji Magohe ambayo ina urefu wa kilometa 8.7.
Mheshimiwa Spika, barabara hizi ni sehemu ya barabara ya Mzunguko wa Nje wa jiji la Dar es Salaam (Outer Ring Roads) inayoanzia Bunju – Mpiji Magohe – Kibamba – Pugu Kajiungeni – Mzinga – Tuangoma mpaka Kigamboni ambayo ina urefu wa kilometa 61.
Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika mpango wa kujenga barabara hizi kwa kiwango cha lami. Katika Mwaka wa Fedha wa 2021/2022 jumla ya Shilingi milioni 600 zimetengwa kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya mzunguko wa nje inayoanzia Bunju – Mpiji Magohe – Kibamba – Pugu Kajiungeni – Mzinga – Tuangoma mpaka Kigamboni na mzunguko wa ndani inayoanzia – Mbezi Mwisho – Kifuru – Banana – Kipara hadi Kigamboni. Taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri wakufanya kazi hiyo zipo katika hatua za mwisho za uchambuzi wa zabuni. Mara baada ya kazi hiyo kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. SUBIRA K. MGALU K.n.y. MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza Ujenzi wa barabara ya Nyamisati hadi Bungu katika Jimbo la Kibiti?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Twaha Ally Mpembenwe, Mbunge wa Kibiti kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Bungu – Nyamisati yenye urefu wa kilometa 40.2 ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) iliyopo katika Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Pwani.
Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha wa 2021/ 2022, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania, imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii. Taratibu za kumpata mshauri elekezi wa kufanya kazi hiyo, ziko katika hatua za mwisho za kusaini mkataba. Baada ya usanifu kukamilika na gharama kujulikana Serikali itatafuta fedha za ujenzi.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea na maandalizi ya kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania, inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii. Ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka na katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022 jumla ya Shilingi milioni 732.67 zimetengwa. Ahsante.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza: -
Barabara ya Mlimani kutoka Mwembe – Mbaga hadi Mamba - Myamba ni kero kubwa kwa wakazi zaidi ya 150,000 katika Majimbo ya manne; Same Magharibi na Same Mashariki ambapo zaidi ya 70% ya wakazi wake wanaishi milimani.
Je, ni lini barabara hiyo yenye urefu wa Km 120 itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami nyepesi (Surface dressing) ili kufanikisha shughuli za maendeleo katika Wilaya ya Same?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mwembe – Myamba hadi Ndungu ni barabara ya changarawe yenye urefu wa kilometa 90.19. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Aidha, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Serikali imetenga shilingi milioni 1,848.97 kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hiyo. Vilevile, ujenzi wa Daraja la Yongoma lililokatika wakati wa msimu wa mvua umekamilika kwa gharama ya shilingi milioni 453. Ahsante. (Makofi)
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -
Je, Serikali imeweka vivutio gani maalum ili kuwavutia wasafirishaji kutumia Bandari ya Mtwara kusafirisha mizigo ya nchi za Msumbiji, Malawi na Zambia?
NAIBU WIZIRA YA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika hatua za awali za kuvutia wasafirishaji kutumia Bandari ya Mtwara, Serikali imepunguza asilimia 30 ya gharama za tozo za bandari kwa shehena ya Korosho. Gharama hizo zinahusisha kupanga na kupokea shehena kwenda au kutoka melini, usafiri wa kati wa kusafirisha bidhaa kutoka melini hadi kwenye eneo la kuhifadhia mizigo na kinyume chake; kupokea na kupeleka mizigo kutoka kwenye mabehewa au malori kwenda melini; na upakuaji na uhifadhi wa mizigo kutoka kwenye meli.
Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imetoa punguzo la ada inayotozwa kwa matumizi ya gati kushusha mizigo ndani ya meli (wharfage) kutoka dola ya Kimarekani hadi nusu Dola na kurefusha muda wa makasha ya kupakia Korosho kuwa bure katika msimu wote wa korosho.
Mheshimiwa Spika, vile vile, Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeendelea kutoa punguzo la tozo maalum kwa wasafirishaji wa makaa ya mawe na saruji ili kuifanya Bandari ya Mtwara kufanya kazi katika kipindi chote cha mwaka. Serikali itaendelea kufanya tathmini na kuchukua hatua stahiki kwa lengo la kuvutia matumizi ya Bandari ya Mtwara.
Mheshimiwa Spika, napenda kutoa wito kwa wasafirishaji kutumia punguzo hili la tozo lililofanywa na Serikali kusafirisha mizigo ya nchi za Msumbiji, Malawi na Zambia kupitia Bandari ya Mtwara. Ahsante.
MHE. ABEID I. RAMADHANI aliuliza: -
Barabara ya kutoka Singida kupitia Mji Mdogo wa Ilongero – Mtinko hadi Hydom ni muhimu kwa uchumi wa Mkoa wa Singida, Manyara na Simiyu.
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Ilongero – Mtinko hadi Hydom kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Abeid Ighondo Ramadhani, Mbunge wa Singida kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Ilongero – Mtinko hadi Hydom yenye urefu wa kilometa 93.3. Mkataba wa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ulisainiwa mwezi Oktoba, 2021 na kazi inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2022. Mara baada ya kazi ya Usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante. (Makofi)
MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Kolandoto hadi Meatu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kolandoto – Mwanhuzi (Meatu) yenye urefu wa kilometa 117.57 ni sehemu ya Mradi wa Barabara ya Kolandoto – Lalago – Mwanhuzi – Sibiti – Oldeani B Junction yenye urefu wa kilometa 328 usanifu wake ulikamilika mwaka 2017. Serikali inaendelea na jitihada na juhudi za kutafuta fedha ili kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 1,240.246 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo, ahsante. (Makofi)
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya kutoka Magu – Bukwimba hadi Ngudu itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ili kuunganisha Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba na Makao Makuu ya Mkoa wa Mwanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Mageni Kasalali, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Magu – Bukwimba hadi Ngudu ni sehemu ya Barabara ya Magu – Bukwimba – Ngudu hadi Hungumalwa yenye urefu wa kilometa 71. Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii tangu mwaka 2019. Baada ya kukamilika kwa usanifu Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya Shilingi milioni 596.576 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali. Ahsante.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaipandisha hadhi barabara ya Igurubi – Mbutu – Igunga hadi Itumba yenye zaidi ya km 140 kuwa chini ya TANROADS ili ijengwe kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, taratibu za kupandisha hadhi barabara ni kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni za Menejimenti ya Barabara za Mwaka 2009. Kwa vile suala hili ni la kisheria, ninamshauri Mheshimiwa Mbunge awasilishe maombi yake ya kupandisha hadhi Barabara ya Igurubi – Mbutu – Igunga – Itumba, yenye kilometa 102.8 kwenye Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Tabora. Bodi ya Barabara ya Mkoa itajadili maombi hayo na ikiridhia itawasilisha maombi kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ambaye ndiye mwenye dhamana ya kupandisha hadhi ya barabara nchini. Ahsante.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa kilometa 20 kutoka Nkome hadi Nzera?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Musukuma Joseph Kasheku, Mbunge wa Geita Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Nzera – Nkome ni sehemu ya Barabara ya Geita – Nzera hadi Nkome yenye urefu wa kilometa 54 inayounganisha Mji wa Geita ambayo ni Makao Makuu ya Mkoa na Miji Midogo ya Nzera, Nkome na Ziwa Victoria.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kuandaa makabrasha kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina Barabara yote kutoka Geita – Nzera hadi Nkome (kilometa 54) kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 2,000 kwa ajili ya maandalizi ya kuanza ujenzi. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea na maandalizi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iweze kuendelea kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 jumla ya shilingi milioni 1,162 zimetengwa kwa kazi hiyo. Ahsante.
MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -
(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Barabara ya Bihawana – Chali hadi Sanza Manyoni kwa kiwango cha lami kwa kuwa barabara hii muhimu huwa haipitiki wakati wa masika?
(b) Je Serikali ina mpango gani wa kuinua tuta la barabara katika eneo la Chali ili liweze kupitika wakati wote?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Bihawana – Chali hadi Sanza Manyoni ni barabara ya Mkoa inayojulikana kwa jina la Bihawana - Chidilo – Chipanga – Chali Igongo ambayo ina urefu wa kilomita 69, ambayo inaunganisha Wilaya za Bahi na Manyoni kupitia Sanza. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha za kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 shillingi milioni 759.252 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo.
Mheshimiwa Spika, sehemu (b) kuhusu kuinua tuta eneo la Chali, Serikali imefanya kazi zifuatazo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2019/ 2020, Serikali imejenga kalavati kubwa na kuinua tuta lenye urefu wa mita 500. Katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 Serikali imejenga makalavati makubwa mawili na kuinua tuta lenye urefu wa mita 100. Vilevile, katika mwaka wa fedha huu wa 2021/2022, Serikali imepanga kunyanyua tuta lenye urefu wa mita 500 ambapo mkataba wa kazi hii upo katika hatua za kusainiwa. Ahsante.
MHE. KAVEJURU E. FELIX Aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kupanua Uwanja wa Ndege wa Kigoma ili Ndege kubwa ziweze kutua?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa idhini yako naomba nitumie nafasi hii kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuniamini ili niweze kumsaidia katika nafasi hii naomba nimuahidi yeye Mheshimiwa Rais, Waheshimiwa Wabunge pamoja na watanzania kwa ujumla kwamba nitaendelea kuwatumikia kwa uaminifu na uadilifu kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kavejuru Eliadory Felix Mbunge wa Buhigwe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanja cha Ndege cha Kigoma ni miongoni mwa Viwanja vya Ndege vinne (4) ambavyo ni Kigoma, Tabora, Sumbawanga na Shinyanga vinavyotarajiwa kujengwa na kukarabatiwa kwa Ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank -EIB). Ambapo miradi mingine yote imekwishapata Makandarasi isipokuwa mradi wa upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma. Kwa sasa, taratibu za makubaliano ya Kimkataba tayari zimeshakamilika kati ya Serikali na Mfadhili huyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na Mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma kuwa na Mfadhili, kazi zingine ambazo ziko nje ya makubaliano zitatekelezwa na Serikali moja kwa moja. Aidha, Serikali itahusika na kazi ya urefushaji wa barabara ya kuruka na kutua Ndege kutoka mita 1,800 zilizopo kwa sasa hadi mita 3,100. Ambapo tayari Usanifu wa kina umefanyika kwa lengo la kuwezesha ndege kubwa kutua na kuruka bila matatizo yoyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa kazi zinazofadhiliwa na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank - EIB) katika mradi wa Kiwanja hiki cha Ndege, Serikali inasubiri idhini (no objection) kutoka kwa Mfadhili ili kukamilisha mchakato wa manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi atakayetekeleza mradi huu. Aidha, kazi ambazo zinatarajiwa kufanywa kwa ufadhili wa Benki hiyo ni Ujenzi wa Jengo jipya la Abiria, Jengo la Kuongozea Ndege, Upanuzi wa Maegesho ya Ndege, Usimikaji wa taa za kuongozea ndege pamoja na uzio wa usalama.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali imejipanga kuanza upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma mara baada ya kumpata Mkandarasi atakayetekeleza mradi huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza upembuzi yakinifu wa ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Manyoni East – Heka – Isseke - Sanza hadi Dodoma?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GEOFREY G. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Manyoni East – Heka – Isseke – Sanza – Chali – Igongo hadi Bihawana Junction Dodoma ni barabara ya Mkoa inayohudumiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS). Barabara hii ina urefu wa kilometa 193 na kati ya hizo kilometa 124 ziko Mkoa wa Singida na kilometa 69 ziko Mkoa wa Dodoma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali imekamilisha usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni kwa daraja la Sanza lenye urefu wa mita 75 lililopo kwenye barabara hii. Kazi hii ilikamilika mwaka 2018. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha za kulijenga. Kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara hii zitafuata kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili kuhakikisha kuwa inaimarika na kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka huu wa fedha wa 2021/2022, jumla ya Shilingi milioni 1,513.284 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali ya barabara hii. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara za kuunganisha Mkoa wa Katavi na Mikoa ya jirani utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi ya barabara za kuunganisha Mkoa wa Katavi na mikoa jirani ya Kigoma, Rukwa na Tabora ni kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na jitihada za kuunganisha Mkoa wa Katavi na Mkoa wa Kigoma ambapo ujenzi wa barabara ya Mpanda – Ifukutwa - Vikonge yenye urefu wa kilometa 37.65 umekamilika kwa kiwango cha lami. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 sehemu ya barabara ya Vikonge – Mishamo Junction yenye urefu wa kilometa 62 imetengewa shilingi milioni 3,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Aidha, Serikali kupitia TANROADS iko katika hatua za mwisho za mchakato wa zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Mikoa ya Katavi na Rukwa, ujenzi wa sehemu za Sumbawanga – Kanazi urefu wa kilometa 75, Kanazi – Kizi – Kibaoni kilometa 76 na Mpanda – Sitalike kilometa 36.5 kwa kiwango cha lami umekamilika. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi milioni 4,000 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Kibaoni – Sitalike yenye urefu wa kilometa 71. Serikali kupitia TANROADS iko katika hatua za mwisho za mchakato wa zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kwa Mikoa ya Katavi na Tabora, utekelezaji wa barabara ya Tabora – Ipole – Koga – Mpanda yenye urefu wa kilometa 359 ni kama ifuatavyo; Tabora – Sikonge yenye urefu wa kilometa 30 ujenzi umekamilika; sehemu ya Usesula – Komanga yenye urefu wa kilometa 108 na barabara ya kuingia Mji wa Sikonge yenye urefu wa kilometa 7.5; sehemu ya Komanga – Kasinde yenye urefu wa kilometa 108 na barabara ya kuingia Mji wa Inyonga kilometa 4.8; sehemu ya Kasinde – Mpanda kilometa 108 na barabara ya kuingia Mji wa Urwira yenye urefu wa kilometa 3.7 ujenzi wake umekamilika. Ahsante. (Makofi)
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali – Ishihimulwa – Shitage – Muhulidede kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Athuman Almas Maige, Mbunge wa Tabora Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Tabora – Mambali – Bukumbi – Ishihimulwa – Shitage – Muhulidede yenye urefu wa kilomita 109.4 ni sehemu ya barabara inayounganisha mikoa ya Tabora na Shinyanga. Sehemu ya barabara kutoka Tabora hadi Bukumbi yenye urefu wa kilometa 84 ni barabara ya mkoa. Kutoka Bukumbi hadi Muhulidede yenye urefu wa kilometa 25.4 ni barabara ya wilaya iliyokasimiwa kwa Wakala wa Barabara (TANROADS) kuanzia mwaka wa fedha 2018/2019.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sehemu ya barabara hii kutoka Tabora hadi Mambali yenye urefu wa kilomita 56, imefanyiwa usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Kazi ya usanifu ilikamilika mwezi Aprili, 2020. Baada ya kukamilika kwa usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sehemu ya barabara iliyobaki ya kutoka Mambali – Bukumbi hadi Muhulidede yenye urefu wa kilomita 53.4, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuhakikisha kuwa barabara hii ya Tabora - Mambali – Bukumbi hadi Muhulidede inapitika vizuri majira yote, katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya Shilingi milioni 443.989/= zimetengwa kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali. Ahsante.
MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza:-
Je, ni nini kinachosababisha mabadiliko makubwa ya bei za tiketi za ndege za Air Tanzania kwa safari za Dar es Salaam na Dodoma ambapo mara nyingi hufika hadi shilingi laki sita?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salim Mussa Omar, Mbunge wa Gando, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfumo wa uuzaji wa tiketi katika biashara ya usafiri wa anga ni mojawapo ya mikakati ya ushindani ili kuvutia wateja. Mashirika ya Ndege hushindana kwa kutumia mkakati huu ambapo tiketi hupangwa katika ngazi mbalimbali kufuatana na vigezo mbalimbali kama vile bei ya tiketi, ujazo wa ndege, muda wa kukata tiketi, masharti ya tiketi na daraja la usafiri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutumia kigezo cha ujazo wa ndege na muda ambao abiria anakata tiketi, mteja anayekata tiketi mapema na kukuta ndege haijajaa hupata bei ya chini ukilinganisha na mteja anayekata tiketi muda mfupi kabla ya safari yake na kukuta ndege imejaa, ambapo mara nyingi huwa siku chache au muda mfupi kabla ya safari, hupata bei za juu. Mfumo huu unatumika Kimataifa na mashirika yote ya ndege.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa ATCL bei hizi zimepangwa katika ngazi mbalimbali. Kwa mfano, katika safari ya Dodoma kwenda na kurudi, ATCL ina jumla ya ngazi 13 katika daraja la kawaida (economy class) ambapo bei zake zinaanzia shilingi 331,400/= hadi shilingi 678,400/=. Bei ya juu ya wastani wa shilingi 600,000/= ni viti 10 kati ya jumla ya viti 76 vya ndege nzima sawa na takribani asilimia 13 ya ujazo wa ndege. Hivyo, abiria wakiwahi kukata tiketi wana nafasi kubwa ya kupata bei za chini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, kuna daraja la biashara (business class) ambalo kuna viti sita tu na ni kwa abiria yeyote ambaye yupo tayari kulipa katika daraja hilo. Daraja hilo linatoa huduma maalum, kwa mfano, mteja anapewa kilo saba zaidi za mzigo ukilinganisha na daraja la kawaida, mteja hupatiwa mhudumu wa kumsikiliza kwa haraka muda wowote akiwa ndani ya ndege, mteja kutokuwa na gharama za kubadilisha safari akifanya mabadiliko hayo kwa mara ya kwanza na pia mteja hupewa kipaumbele wakati wote wa safari kuanzia wakati wa ukaguzi (check in). Kutokana na sababu hizi, gharama za daraja hili ni kubwa kuliko daraja la kawaida. Daraja hili la biashara lina ngazi nne zenye bei kati ya shilingi 721,600/= hadi shilingi 953,000/=.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na maelezo hayo, namwelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL kufanya utafiti wa nauli zinazotozwa na mashirika ya ndege washindani kwa safari za ndani ili kuziwianisha na kisha kupanga nauli zinazoweza kuvutia Watanzania wengi kutumia ndege za ATCL. Ahsante. (Makofi)
MHE. ALEXANDER P. MNYETI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Mwanangwa – Misasi – Kahama?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwanangwa – Misasi – Kawekamo – Solwa – Kahama yenye urefu wa kilometa 150, ilifanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kukamilika mwaka 2017 kwa gharama ya shilingi milioni 798.8. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea na juhudi za kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ya barabara hii ili iendelee kupitika kipindi chote cha mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya shilingi milioni 2,809.304 zimetengwa kwa matengenezo mbalimbali pamoja na ujenzi wa madaraja saba katika maeneo yanayoathiriwa na mafuriko. Madaraja hayo ni madaraja mawili katika eneo la Mwanzugi, madaraja matatu katika eneo la Mwakitolyo na madaraja mawili katika eneo la Solwa.
Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi wa kilometa 5.15 kwa kiwango cha lami katika eneo la Kahama kuelekea Solwa. Ahsante.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Geita kupitia Nyarugusu kwenda Bukoli hadi Kahama ambapo upembuzi yakinifu ulishafanyika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bryceson Magesa Tumaini, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuandaa nyaraka za zabuni kwa barabara ya Geita – Nyarugusu – Kahama yenye urefu wa kilometa 133.9 imekamilika mwaka 2017. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Aidha, mwaka 2021, Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick ilionesha nia ya kufadhili ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Kwa sasa, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Madini na Wizara ya Fedha na Mipango zinaendelea na mazungumzo na Kampuni ya Barrick kuhusu utaratibu wa ujenzi wa barabara hii.
Mheshimiwa Spika, wakati ujenzi kwa kiwango cha lami ukisubiri upatikanaji wa fedha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS), inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya shilingi milioni 838.97 zilitengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali katika barabara hii. Aidha, Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Shinyanga kwa kutumia fedha za maendeleo inakamilisha ujenzi wa mita 600 kwa kiwango cha lami katika barabara hii kuanzia eneo la Busoka katika Manispaa ya Kahama. Ahsante. (Makofi)
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza: -
Je, ni lini Ujenzi wa Barabara ya Ifakara – Kihansi – Madeke utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Ifakara – Kihansi hadi Madeke yenye kilometa 220.22 ni sehemu ya barabara ya Ifakara – Mlimba – Taweta – Madeke – Lupembe hadi Kibena Mkoa wa Njombe ambayo ni barabara ya mkoa inayounganisha mikoa ya Morogoro na Njombe katika Kijiji cha Madeke.
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuandaa nyaraka za zabuni kwa sehemu ya Ifakara hadi Kihansi yenye urefu wa kilometa 126. Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza maandalizi ya kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata Mkandarasi wa ujenzi wa kilometa 50 kati ya Ifakara hadi Mlimba kwa kiwango cha lami ndani ya mwaka wa fedha wa 2021/2022. Aidha, kipande cha barabara kati ya Kihansi na Mlimba chenye urefu wa kilometa 24.26 kimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, sehemu iliyobaki itaendelea kujengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha hadi barabara yote ikamilike kwa kiwango cha lami. Pamoja na juhudi hizi, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali ili kuhakikisha inapitika majira yote ya mwaka ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya shilingi bilioni 2.729 zimetengwa. Ahsante. (Makofi)
MHE. JOHN M. SALLU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Kwamsisi mpaka Mkata kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa John Marko Sallu, Mbunge wa Handeni Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kwamsisi hadi Mkata yenye urefu wa kilometa 35 ni sehemu ya barabara ya Mkalamo Junction hadi Mkata yenye urefu wa kilometa 73.1. Barabara hii ni ya mkoa na inahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, sehemu ya barabara hii kutoka Mkalamo Junction hadi Kwamsisi yenye urefu wa kilometa 38.51 iliingizwa katika mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Pangani – Tungamaa – Mkwaja hadi Mkange yenye urefu wa kilometa 95.2. Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami amepatikana ambaye ni China Railway 15 Group na Mkataba umesainiwa tarehe 6 Septemba, 2021. Gharama za ujenzi ni shilingi bilioni 94.539 na muda wa utekelezaji wa mradi huo ni miezi 48.
Mheshimiwa Spika, sehemu iliyobaki ya Kwamsisi hadi Mkata iliingizwa katika mpango wa RISE (Roads to Inclusion and Socioeconomic Opportunities) ambao inafadhiliwa na Benki ya Dunia. Mradi huu upo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mhandisi Mshauri atakayefanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mtwara Pachani, Lusewa, Nalasi hadi Tunduru yenye urefu wa kilomita 320 kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mtwarapachani – Lusewa – Nalasi – Tunduru yenye urefu wa kilomita 300 ni barabara ya mkoa na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Ruvuma.
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina pamoja na utayarishaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami imekamilika mwaka 2020. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati tukisubiri upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, Serikali itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hiyo ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, jumla ya shilingi milioni 1,960.583 zimetengwa kwa ajili ya matengenezo mbalimbali na ukarabati wa madaraja kwenye barabara hii. Ahsante.
MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mzumbe hadi Mgeta?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas Van Zeeland, Mbunge wa Mvomero, kama ifuatavyo: -
Barabara ya Mzumbe – Mgeta yenye urefu wa kilometa 26 ni sehemu ya barabara ya Mkoa ya Sangasanga – Langali – Luale hadi Kikeo yenye urefu wa kilometa 59.16 na inahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, Ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mzumbe - Mgeta yenye urefu wa kilometa 26 imeanza kutekelezwa kwa awamu ambapo mwaka 2020 Serikali ilikamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa kipande cha mita 400 kuanzia Mzumbe na katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inaendelea na ujenzi wa kipande kingine cha mita 700 kwa shilingi 216,800,000 na kazi ilianza Novemba, 2021 na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2022. Sehemu iliyobaki itaendelea kujengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha shilingi 664,557,000 kimetengwa kwa kazi hiyo. Ahsante.
MHE. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa Daraja la Kalebe utaanza na kukamilika kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Daraja la Kalebe lenye urefu wa mita 32.56 lipo katika barabara ya Kyaka II – Kanazi – Kyetema yenye urefu wa kilometa 60.65. Barabara hii ni ya Mkoa na inahudumiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja la Kalebe umejumuishwa katika mradi wa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kyaka II – Kanazi – Kyetema ambao unatekelezwa chini ya Mhandisi Mshauri Luptan Consult Ltd. kwa kushirikiana na Mhandisi Consultancy kwa gharama ya shilingi milioni 340.035. Kazi hii imeanza tarehe 31 Disemba, 2021 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Oktoba, 2022.
Mheshimiwa Spika, baada ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo pamoja na barabara hiyo. Ahsante.
MHE ISSA J. MTEMVU aliuliza: -
Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutatua mgogoro wa bomoabomoa wa nyumba za wananchi zilizokuwa pembezoni mwa Barabara ya Morogoro kutoka Kimara hadi Kibamba ulioanza mwaka 2017?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Jimbo la Kibamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwaka 2017/2018, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, sekta ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Dar es Salaam iliondosha nyumba na mali za watu zilizokuwa zimejengwa kinyume cha sheria ndani ya eneo la hifadhi ya Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kibamba ikiwa ni maandalizi ya kupanua barabara hiyo toka njia mbili hadi njia nane ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kulingana na Sheria ya Barabara ya mwaka 1932 pamoja na Kanuni zake za mwaka 1955 na marekebisho yake Na. 13 ya mwaka 2009, imeainishwa kwamba upana wa hifadhi ya barabara hiyo kuanzia Kimara Stop Over hadi Kibaha (TAMCO) ni mita 121 kutoka katikati ya barabara kila upande. Hivyo, nyumba na mali zote zilizokuwa ndani ya eneo hili walikuwa wako ndani ya eneo la hifadhi ya barabara kinyume na sheria.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la kuwaondoa wananchi waliokuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara ili kupisha utekelezaji wa mradi huu lilifanyika kwa kufuata Sheria ya Barabara na hadi sasa Serikali haina mgogoro wowote na wananchi walioondolewa ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, endapo kutatokea mgogoro kati ya wananchi wa eneo la Kimara hadi Kibamba kuhusiana na bomoa bomoa ya nyumba zilizojengwa ndani ya hifadhi ya barabara ya Morogoro kinyume na sheria, mgogoro huo utatatuliwa kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Ahsante.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Lushoto – Magamba – Lukozi – Mlalo hadi Umba Junction kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Lushoto – Magamba – Lukozi – Mlalo hadi Umba Junction ni barabara ya Mkoa yenye urefu wa kilometa 66.23 na inasimamiwa na Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Tanga.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitekeleza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kwa awamu kutegemeana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 9.1 kati ya Lushoto na Mazinde Juu zimejengwa kwa kiwango cha lami. Mwaka huu wa fedha 2021/2022, jumla ya Shilingi milioni 420 zimetengwa ili kuendeleza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kwa kipande chenye urefu wa mita 400. Kazi za ujenzi zilianza mwezi Januari, 2022 na kazi zinategemewa kukamilika mwezi Juni, 2022. Hadi tarehe 10 Februari, 2022 kazi zilikuwa zimefikia asilimia 15.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa awamu kulingana na upatikana wa Fedha. Ahsante.
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Chemba hadi Singida utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi wa ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo - Chemba – Kwa Mtoro hadi Singida ni barabara ya mkoa yenye urefu wa kilometa 461 inayounganisha Mikoa ya Tanga, Dodoma, Manyara na Singida. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi ya ujenzi wa barabara hii umeanza ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami ulikamilika mwaka 2018. Zabuni ya kazi ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Handeni – Mufulate (Kilometa 20) zilishatangazwa na Mkandarasi kupatikana. Rasimu ya Mkataba imepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kupata idhini (vetting) ya kusaini Mkataba.
Mheshimiwa Naibu Spika, maandalizi ya kutangaza zabuni ya ujenzi kwa sehemu ya kutoka Mafuleta – Kwediboma yenye urefu wa kilometa 30 yanaendelea na zabuni itakuwa imetangazwa kabla ya Juni, 2022. Aidha, Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante. (Makofi)
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -
Je, nini kauli ya Serikali kutokana na mkanganyiko uliotokea kuhusu fidia katika barabara ya Tanga – Pangani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Mwanaisha Ng’anzi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya Tanga – Pangani yenye urefu wa kilomita 50 ni sehemu ya barabara ya Bagamoyo kuanzia Makurunge – Saadani – Pangani hadi Tanga ambayo ina urefu wa kilomita 256. Awali Benki ya Maendeleo ya Afrika ilionesha nia ya kufadhili barabara yote ya Bagamoyo kuanzia Makurunge – Saadani – Pangani hadi Tanga urefu wa kilomita 256.
Mheshimiwa Spika, aidha, mfadhili alitoa sharti la kulipia fidia kwa mali zote zitakazoathiriwa na mradi ndani na nje ya eneo la hifadhi ya barabara. Hivyo, uthamini wa mali zitakazoathiriwa na mradi ulifanyika kwa kuzingatia sharti hilo. Wananchi walifahamishwa kwenye mikutano ya uelimishaji umma na kujulishwa kuwa endapo mfadhili hataendelea na nia hiyo na Serikali ikajenga kwa fedha za ndani, wale wenye mali zilizopo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hawatalipwa fidia.
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hiyo, na kwa kutochelewesha mradi, Serikali ilianza ujenzi kwa sehemu ya Tanga, hadi Pangani urefu wa kilomita 50 kwa kutumia fedha za ndani.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka, 2017 ujenzi wa aina yoyote hauruhusiwi ndani ya eneo la hifadhi ya barabara. Hivyo, wananchi waliofanya maendelezo ndani ya eneo hilo hawastahili kulipwa fidia.
Mheshimiwa Spika, kwa kufuata matakwa ya sheria za nchi wale wote ambao walikuwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara, hawakustahili kulipwa fidia na waliondolewa kwenye orodha ya malipo kabla ya taarifa ya fidia kuwasilishwa kwa Mthamini Mkuu wa Serikali. Ahsante.
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Mpanda kwenda Karema kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante; kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mpanda – Kagwira - Karema yenye urefu wa kilometa 122 ambapo kipande cha Mpanda – Kagwira chenye urefu wa kilomita 10, ni sehemu ya barabara Kuu na sehemu ya Kagirwa – Karema yenye jumla ya urefu wa kilometa 112 ni barabara ya Mkoa.
Mheshimiwa Spika, mnamo mwezi Machi, 2021 Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ilisaini Mkataba na Kampuni ya M/s Crown Tech. Consultant Ltd. kwa ajili ya kufanya Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kagwira – Karema yenye urefu wa kilometa 112 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami na kazi hii inategemea kukamilika mwezi Aprili, 2022.
Mheshimiwa Spika, mara baada ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Ahsante. (Makofi)
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA K.n.y. MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga bandari kavu eneo la Old Korogwe katika Halmashauri ya Mji Korogwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Alfred James Kimea, Mbunge wa Korogwe Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa bandari kavu hufanyika ili kuongeza ufanisi wa bandari zilizopo mwambao wa bahari na maziwa. Ujenzi wa bandari kavu huzingatia vigezo maalum ikiwa ni pamoja na kuondoa msongamano katika bandari iliyo karibu na bandari kavu na kusogeza huduma karibu na watumiaji wa mwisho. Aidha, kigezo kingine ni uwepo wa upembuzi yakinifu unaobainisha mahitaji ya bandari kavu husika ili kuwa na msingi wa kufanya maamuzi sahihi.
Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo hayo, eneo la Old Korogwe halijabainishwa kwa sasa kwamba linafaa kujengwa bandari kavu. Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari itafanya tathmini kuona umuhimu wa uwepo wa bandari kavu katika eneo la Old Korogwe. Ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA K.n.y. MHE. JERRY W. SILAA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Pugu – Kifuru hadi Mbezi Mwisho kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jerry William Silaa, Mbunge wa Jimbo la Ukonga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Pugu – Kifuru – Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 12.7, sehemu ya kutoka Mbezi Mwisho hadi Kifuru (kilometa 6.7) imejengwa lami kwa njia mbili na sehemu ya kutoka Kifuru – Pugu Station (kilometa 6) ni barabara ya vumbi.
Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga fedha kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sehemu ya Pugu Station hadi Kifuru (kilometa sita) kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami kwa njia nne na kwa sehemu ya Kifuru - Mbezi Mwisho (kilometa 6.7) kuipanua kutoka njia mbili kuwa njia nne. Zabuni kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi hiyo zimetangazwa na zitafunguliwa tarehe 10 Oktoba, 2022. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -
Je, kuna mpango wowote kubadili mwelekeo wa ujenzi Barabara ya Tanga kupitia Handeni, Kiberashi, Mrijo, Mondo Bicha hadi Kwamtoro?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Kondoa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kulingana na taarifa ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, ujenzi wa barabara inayounganisha Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida utaanzia Handeni - Kibirashi - Kijungu - Kibaya - Goima - Chemba - Donsee – Kwamtoro hadi Kititimo (Singida) ambayo itakuwa na urefu wa kilometa 463.5.
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara hii umeanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa kujenga Kilometa 20 kwa sehemu ya Handeni – Mafuleta, ahsante.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Kolandoto - Mhunze hadi Mwangongo itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Nyangindu Butondo, Mbunge wa Kishapu kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilishakamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kolandoto – Mhunze hadi Mwangongo (kilometa 53) kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Zabuni kwa ajili ya kazi hiyo zitatangazwa mwezi Novemba, 2022. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO K.n.y. MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga uwanja wa ndege wa Omukajunguti?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Nkenge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa kujenga Kiwanja kipya cha Ndege katika eneo la Omukajunguti, mkoani Kagera ili kuwezesha ndege kubwa ziweze kuruka na kutua.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, utekelezaji wa mradi huu utaanza kwa kadri ya upatikanaji wa fedha baada ya Serikali kukamilisha taratibu za utwaaji wa ardhi na ulipaji wa fidia. Ahsante.
MHE. TABASAM H. MWAGAO K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Kahama – Nyangh’wale – Busisi hadi Sengerema itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu Swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyangh’wale kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Katika mwaka wa fedha 2022/23 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 300 kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kahama – Nyangh’wale – Busisi hadi Sengerema yenye urefu wa kilometa 163. Baada ya kazi hiyo kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya zege ya kilometa tatu kwenye Mlima Magara katika Jimbo la Mbulu Mjini?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu la Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, eneo korofi na hatarishi katika Mlima Magara lina urefu wa kilometa saba. Kati ya hizo kilometa saba, Serikali imekamisha ujenzi kwa kiwango cha zege kilometa nne. Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali itaendelea na ujenzi kwa kiwango cha zege kwa kiasi cha kilometa moja. Kilometa mbili zilizobaki zitaendelea kujengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. SYLVESTRY F. KOKA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa la Mheshimiwa Sylvestry Francis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni kwa ajili ya Expression of Interest kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze hadi Morogoro yenye urefu wa kilometa 205 kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F). Gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (Build Operate and Transfer) ambapo sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari. Ahsante.
MHE. STANSLAUS H. NYONGO K.n.y. MHE. NJALU D. SILANGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya kutoka Sibiti – Kisesa – Itilima – Bariadi
– Salama - Sayaka hadi Kisamba kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Njalu Daudi Silanga Mbunge wa Itilima kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Sibiti hadi Mwandoya Junction ama Loboko ni sehemu ya barabara ya Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti – Lalago – Maswa yenye urefu wa kilometa 389 ambayo imepangwa kujengwa kupitia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction & Financing (EPC + F).
Mheshimiwa Spika, sehemu ya Mwandoya Junction hadi Kisesa – Itilima – Bariadi yenye urefu wa kilometa 100, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inaendelea na sehemu ya kutoka Bariadi – Salama hadi Magu kupitia Ng’haya (kilometa 76) ipo katika hatua ya manunuzi ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Ahsante.
MHE. MWANTATU MBARAK KHAMIS aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kuweka miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu katika vyombo vya usafiri ikiwemo mabasi ya mwendokasi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwantatu Mbarak Khamis Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikisimamia upatikanaji wa huduma bora na salama kwa watumiaji wa usafiri kwa makundi yote ya jamii wakiwemo wenye ulemavu. Serikali imekuwa ikizingatia mahitaji ya makundi maalum hasa wenye ulemavu katika ujenzi wa miundombinu ya usafiri ikiwemo miundombinu ya mabasi ya mwendokasi.
Mheshimiwa Spika, miundombinu ya mabasi ya mwendokasi inayotumika sasa na inayoendelea kujengwa imezingatia watu wenye mahitaji maalumu. Aidha, mabasi yote ya mwendo kasi yamezingatia watu wenye mahitaji maalumu hususan wenye ulemavu, wazee na wajawazito. Ahsante.
MHE. ABDULLAH ALI MWINYI aliuliza: -
Je, Serikali imechukua hatua gani kutatua changamoto zinazoelezwa za ukiritimba zilizopelekea Kampuni ya Uber kusitisha huduma zake nchini Tanzania?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abdullah Ali Mwinyi, Mbunge wa Mahonda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) ilianza kudhibiti huduma za taxi mtandao mwezi Mei, 2020 kwa kutumia Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Na. 3 ya mwaka 2019 pamoja na kanuni zake.
Mheshimiwa Spika, baada ya LATRA kuanza kudhibiti eneo hili kisheria, iliweka viwango vya tozo kwa huduma za taxi ili kupunguza migogoro kati ya madereva na wamiliki wa mifumo ya taxi ambao ni pamoja na Kampuni ya Uber. Kutokana na hatua ya LATRA kuweka tozo katika huduma za taxi mtandao, Kampuni ya Uber iliamua kusitisha kutoa baadhi ya huduma hapa nchini mwezi Aprili, 2022.
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia LATRA inaendelea na mazungumzo na Kampuni ya Uber kwa lengo la kuhakikisha inarejesha huduma za taxi mtandao. Ahsante.
MHE. EDWARD K. OLELEKAITA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Arusha – Simanjiro – Kiteto hadi Kongwa kilometa 430 itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami kama ilivyoahidiwa katika Ilani ya Uchaguzi (CCM) 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Edward Kisau Olelekaita, Mbunge wa Kiteto, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mnamo tarehe 27 Juni, 2022 ilitangaza zabuni kwa ajili ya kuonesha nia (Expression of Interest) kwa Makampuni ya Ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Arusha – Simanjiro – Kiteto – Njiapanda ya Kongwa yenye urefu wa kilometa 453.42 kwa utaratibu wa EPC + Jumla ya Makampuni kumi na moja (11) yalikidhi vigezo na tarehe 22 Novemba, Zabuni hizi zitafunguliwa.
MHE. ZAINAB A. KATIMBA K.n.y. MHE. ASSA N. MAKANIKA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mwandiga – Chankele – Mwamgongo hadi Kagunga?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Assa Nelson Makanika, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mwandinga – Chankele- Mwamgongo hadi Kagunga yenye urefu wa kilometa 65 ni barabara ya wilaya. TANROADS wanaendelea kuifungua kutoka njia panda ya Chankele hadi Kagunga kilometa 47 na tayari kilometa nane zimeshafunguliwa.
Mheshimshiwa Spika, mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga Shilingi bilioni 1.85 kuendelea kuifungua barabara hii kwa kiwango cha changarawe. Baada ya kuifungua barabara yote, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. AHMED A. SALUM aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mwanangwa – Mwakitolyo hadi Bulige Wilayani Kahama kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ahmed Ally Salim, Mbunge wa Solwa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mwanangwa – Mwakitolyo hadi Bulige yenye urefu wa kilomita 118.8 ni sehemu ya barabara itokayo Mwanangwa – Misasi - Salawe – Solwa - Kahama yenye urefu wa kilomita 148.8. Serikali tayari imeanza ujenzi kwa awamu ambapo kilomita 5.65 kuanzia Kahama kuelekea Solwa na sehemu ya mita 450 katika mji wa Bulige zimekamilika kwa kiwango cha lami. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, kiasi cha Shilingi milioni 750.62 zimetengwa kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kilometa 1.2. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -
Je, ni lini kipande cha barabara ya Turiani hadi Handeni kitajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara yote kutoka Magole - Turiani – Mziha hadi Handeni yenye urefu wa kilometa 147.7. Aidha, ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Magole – Turiani (Km 45.27) umekamilika na sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kukamilisha ujenzi wa sehemu iliyobaki ya Turiani - Mziha – Handeni yenye urefu wa kilometa 102.
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaendelea na matengenezo ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Kigoma uliosimama kwa muda wa mwaka mzima?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kilumbe Shabani Ng’enda, Mbunge wa Kigoma Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya matengenezo ya Upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma yatafanyika kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, matengenezo yalisimama kwa sababu Mfadhili alichelewa kutoa idhini ya kumpata Mkandarasi atakakayetekeleza kazi hizo. Kwa sasa, idhini (No Objection) imeshatolewa.
Mheshimiwa Spika, mfadhili wa mradi huu ameshatoa fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huu. Kwa sasa rasimu ya Mkataba imepelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya mapitio.
Meshimiwa Spika, mara baada ya taratibu za vetting kukamilika na Mkataba kusainiwa, utekelezaji wa kazi za matengenezo ya upanuzi wa mradi wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma utaanza. Ahsante.
MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Barabara ya Sengerema – Nyamazugo – Nyehunge na Nkome kwa kiwango cha lami ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais wakati wa Kampeni?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Erick James Shigongo, Mbunge wa Buchosa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ipo katika hatua za Manunuzi ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Sengerema – Nyamazugo – Nyehunge yenye urefu wa kilometa 54.4. Zabuni zilifunguliwa mnamo tarehe 30 Agosti, 2022. Uchambuzi wa zabuni unaendelea na mkataba wa kazi za ujenzi unatarajiwa kuwa umesainiwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022.
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Simiyu utaanza baada ya kukamilika zoezi la uthamini wa eneo la Uwanja utakapojengwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Kiwanja cha Ndege cha Simiyu kilifanyiwa Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2017 kupitia Mradi wa
Transport Sector Support Project (TSSP).
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imekamilisha uthamini kwa maeneo na mali zitakazoathiriwa na utekelezaji wa mradi na kuandaa jedwali la uthamini ambalo tayari limeidhinishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuendelea na taratibu za malipo.
Mheshimiwa Spika, mara baada ya taratibu za kulipa fidia kukamilika, mipango ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Simiyu itaanza kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Singida hadi Sepuka kuelekea Kizaga itajengwa kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Ikungi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Elibariki Immanuel Kingu, Mbunge wa Singida Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni kwa barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago hadi Kizaga yenye urefu wa kilometa 77.6 na inategemea kutangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022. Ahsante.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -
Je, nini hatma ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Geita – Nyarugusu hadi Kahama hususani kipande cha Geita – Nyarugusu – Bulyanhulu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Tumaini Bryceson Magessa, Mbunge wa Busanda kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika makubaliano ya msingi ya awali kati ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Barrick, Kampuni ya Barrick ilikubali kutoa dola za Kimarekani milioni 40 kugharamia ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. Hivyo, Serikali na Kampuni ya Barrick zimekubaliana kuwa fedha hizo kiasi cha dola za Kimarekani milioni 40 zitumike kwa ujenzi wa barabara ya Kahama – Bulyanhulu junction – Geita yenye kilometa 120 na kipande cha Bulyanhulu junction hadi Kakola (kilometa 11.3). Kwa sasa Serikali iko katika hatua ya kukamilisha majadiliano hayo ili kuwezesha mradi huo kuanza kutekelezwa, ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kuu ya Mwanza - Shinyanga kwa kiwango cha njia nne kutoka Mwanza Mjini hadi Usagara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Shing’oma Mabula, Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu ya Mwanza, Shinyanga, yenye urefu wa kilometa 104 ambao utahusisha na upanuzi wa barabara kutoka njia mbili kuwa njia nne kwa sehemu ya kutoka Mwanza Mjini hadi Usagara, kilometa 25. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa barabara hii iko katika hatua za mwisho na inatarajiwa kukamilika tarehe 27 Aprili, 2022.
Mheshimiwa Spika, baada ya usanifu wa kina kukamilika na gharama za ukarabati kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati utakaohusisha upanuzi wa sehemu ya kutoka Mwanza Mjini hadi Usagara, kilometa 25 kutoka njia mbili kuwa njia nne. Ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Igawa hadi Tunduma kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Igawa hadi Tunduma yenye urefu wa kilometa 218 ikiwa ni maandalizi ya kufanyia ukarabati kwa kiwango cha lami. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ilikamilika mwezi Agosti, 2021. Aidha, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umejumuisha barabara ya mchepuo katika Jiji la Mbeya kipande cha Uyole – Songwe Bypass yenye urefu wa kilometa 48.9.
Mheshimiwa Spika, Serikali itafanya ukarabati na upanuzi wa Barabara ya Igawa hadi Tunduma kwa awamu, ambapo awamu ya kwanza itahusisha upanuzi wa barabara kutoka njia mbili kuwa njia nne kwa sehemu ya Uyole – Ifisi yenye urefu wa kilometa 29 ili kupunguza msongamano katika Jiji la Mbeya. Taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi zinaendelea na inatarajiwa kazi itaanza mapema katika mwaka wa fedha 2022/2023.
Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa sehemu iliyobaki pamoja na kujenga Barabara ya Mchepuo ya Uyole – Songwe bypass. Ahsante. (Makofi)
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mahenje - Ndolezi - Hasamba hadi Vwawa ambayo ni muhimu kwa utalii wa Kimondo cha Mbozi na usafirishaji wa mazao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe inajenga kwa kiwango cha lami barabara hii kwa awamu. Hadi mwishoni mwa Machi, 2022 Kilometa 4.5 zimekamilika kujengwa kuanzia Mji wa Vwawa hadi Kijiji cha Mtambwe katika hospitali ya Mkoa wa Songwe. Aidha, ujenzi unaendelea kwa sehemu ya mita 800 na inatarajiwa ifikapo mwishoni mwa Mwezi Juni, 2022 ujenzi utakuwa umekamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu ya barabara hii iliyobaki kilomita 26.56 kwa sasa inafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na kampuni ya Mhandisi Mshauri M/S Inter Consult Ltd ya Dar es Salaam. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022. Baada ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -
Je, ni nani mwenye jukumu la kusafisha mifereji na kuzibua makaravati ya barabara zinazojengwa chini ya TARURA au TANROADS?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Naghejwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, jukumu la usafi wa barabara na mifereji ikiwa ni pamoja na kuzibua makaravati ni la msimamizi wa barabara husika. Hivyo, kwa barabara za TANROADS mhusika ni TANROADS na za TARURA mhusika ni TARURA.
MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Kiwanja cha Ndege Singida Mjini?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha Ndege cha Singida kilifanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2017 kupitia mradi wa Transport Sector Support Project (TSSP) kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa Kiwanja hiki cha Ndege.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kutoka vyanzo vya Ndani na Washirika wa Maendeleo ili kuanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida.
MHE. HAJI MAKAME MLENGE aliuliza: -
Je, ni kwa nini wafanyabiashara wanaoweka bustani kando ya barabara hulipishwa fedha nyingi na TANROADS na TARURA?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Makame Mlenge Haji, Mbunge wa Chwaka, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Tozo kwa Wafanyabiashara wanaoweka bustani kando ya barabara hutozwa kulingana na Mwongozo wa Udhibiti wa Uwekaji Huduma ndani ya eneo la hifadhi ya barabara (Manual for Control of Utilities Installation within the Road Reserve) ambao unatokana na Kanuni ya 3 (1) ya Kanuni za Barabara (Fedha na Ushirikishwaji wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi) za mwaka 2011 zilizotolewa chini ya Sheria ya Barabara, Na.13 ya mwaka 2007. Kulingana na Mwongozo huo Wafanyabiashara wanaoweka Bustani kando ya barabara hutozwa Shilingi 4,639.5 kwa mita ya mraba kwa mwaka. Fedha hizo hupelekwa Bodi ya Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya barabara.
MHE. ALAUDIN H. SALIM aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itafungua barabara ya kimkakati inayotoka Mahenge mpaka Liwale kupitia Malinyi, Mlimba, Njombe na Songea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Alaudin Hasham Salim, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara inayotoka Mahenge kwenda Liwale ni Mahenge - Mwaya – Ilonga – Liwale ambapo sehemu ya Mahenge hadi Ilonga imefunguliwa na inapitika majira yote ya mwaka. Hata hivyo, kutoka Ilonga kwenda Liwale hakuna barabara kwa Mwalimu Nyerere na itahitaji kufanyiwa upembuzi yakinifu wa awali kuona iwapo inakidhi vigezo vya mazingira kabla ya kufunguliwa.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Choma – Ziba – Nkinga hadi Puge?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali Mbunge wa Manonga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa Barabara ya Choma – Ziba – Nkinga hadi Puge yenye jumla ya kilometa 109.56 ambayo inapita katika maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ndala na Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, Serikali kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROAD, imeamua kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mwaka huu wa fedha 2022/2023 kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Fulo kupitia Nyambiti hadi Malya itafanyiwa upembuzi yakinifu na kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuifanyia Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina barabara ya Fulo – Sumve – Nyambiti hadi Malya kwa lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikitafuta fedha za Usanifu, Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), itaendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili kuhakikisha kuwa inapitika vizuri majira yote. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shilingi milioni 668.345 zimetengwa kwa ajili ya kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hiyo. Ahsante.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: -
Je, nini kinakwamisha ujenzi wa barabara ya Mnivata – Masasi kupitia Tandahimba na Newala?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Lulindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imepata mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara kutoka Mnivata hadi Masasi yenye urefu wa kilometa 160. Zabuni kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii zilitangazwa mwezi Julai, 2022 na kufunguliwa tarehe 18 Oktoba, 2022 na kwa sasa uchambuzi wa zabuni unaendelea. Aidha, Serikali imetoa jumla ya Shilingi bilioni 3.086 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi watakao athirika na ujenzi huo, na zoezi la kulipa wananchi hao fidia linaendelea. Ahsante.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya mzunguko katika makutano ya Barabara ya Dar es Salaam, Morogoro na Bagamoyo kuelekea Mlandizi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Michael Constantino Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Makofia, Mlandisi hadi Mzenga kilomita 35, makutano ya barabara ya Dar es Salaam -Morogoro na Makofia- Mlandizi-Mzenga eneo la Mlandizi limesanifiwa kwa ajili ya kujenga barabara ya mzunguko yaani round about. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuanza ujenzi wa barabara ya Makofia – Mlandizi hadi Mzenga utakaohusisha na ujenzi wa round about katika eneo la Mlandizi. Ahsante.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya kutoka Buza-Kilungule hadi Nzasa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Buza-Kilungule hadi Nzasa ina urefu wenye jumla ya kilomita tisa. Barabara hii imekasimiwa kwenye mtandao wa barabara zinazohudumiwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa barabara TANROADS Mkoa wa Dar es Salaam.
Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika hatua za utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kuanzia Nzasa hadi Buza kupitia Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam yaani Dar es Salaam Metropolitan Development Project. Mradi huu wa DMDP unasimamiwa na Wizara ya Ofisi ya Rais, TAMISEMI na kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini (TARURA). Aidha, kwa sasa mkandarasi yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -
Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kuunganisha barabara za Mkoa wa Tanga na mikoa jirani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mhandisi Mwanaisha Ng’azi Ulenge, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mpango wa Serikali ni kuiunganisha mikoa yote kwa barabara za lami. Mkoa wa Tanga unapakana na Mikoa ya Pwani, Morogoro, Manyara, Kilimanjaro na nchi jirani ya Kenya. Tanga imeunganishwa na barabara zifuatazo: Tanga – Chalinze (Mkoa wa Pwani), Handeni – Tuliani hadi Magole (upande wa Mkoa wa Morogoro), Handeni - Kibilashi – Kibaya, (Mkoa wa Manyara), Tanga – Korogwe hadi Same (Mkoa wa Kilimanjaro) na kwa upande wa Kenya ni Tanga - Horohoro.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, zipo barabara nyingine ambazo zinaunganisha Mkoa wa Tanga na mikoa ya jirani. Ahsante.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kimataifa wa Omukajunguti ili kuruhusu ndege kubwa kutua Bukoba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa kujenga kiwanja kipya cha ndege katika eneo la Omukajunguti, Mkoani Kagera ili kuwezesha ndege kubwa ziweze kuruka na kutua.
Mheshimiwa Naibu Spika, Uthamini wa awali kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi watakaoathirika na utekelezaji wa mradi ulishafanyika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ujenzi wa kiwanja hicho cha ndege. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Shinyanga kama ilivyoanishwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mhe. Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga ni miongoni mwa miradi ya ujenzi na upanuzi wa viwanja vya ndege vinne ambavyo ni Kigoma, Tabora, Sumbawanga na Shinyanga inayotarajiwa kutekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank - EIB).
Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa matakwa ya kimkataba kati ya Serikali na EIB yamekamilishwa na mfadhili tayari ameshatoa fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi hii. Aidha, Mhandisi Mshauri pamoja na mkandarasi wameonesha utayari wa kuanza kazi na mikataba kati yao na Serikali ilishasainiwa tangu mwaka 2017.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa mradi huu umechelewa kuanza kwa wakati, Mhandisi Mshauri pamoja na mkandarasi wameomba ongezeko la fedha katika kipengele cha price adjustment ili kuweza kuendana na mabadiliko ya bei ya bidhaa kwa soko la sasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo naomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali imejipanga kuanza utekelezaji wa mradi huu kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 haujaisha, nah ii itatokana na endapo mkandarasi atawasilisha hati ya dhamana ya malipo ya awali kwa wakati. Ahsante.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango wa kukamilisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Sumbawanga Mjini?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga ni miongoni mwa miradi ya Ujenzi na Upanuzi wa Viwanja vya Ndege Vinne (4) ambavyo ni Kigoma, Tabora, Sumbawanga na Shinyanga inayotarajiwa kutekelezwa kwa Ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank - EIB).
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka sasa, matakwa ya kimkataba kati ya Serikali na EIB yamekamilishwa na mfadhili tayari ameshatoa fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa miradi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mradi huu ulichelewa kuanza kwa wakati, kwa sasa taratibu za kimkataba kati ya Serikali na Mkandarasi zinaendelea. Aidha, Mkandarasi amewasilisha maombi ya kufanyika kwa marekebisho ya Mkataba wa awali. Hivyo, marekebisho haya yameshafanyika na kuwasilishwa kwa Mfadhili (EIB) kwa ajili ya kupata idhini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali imejipanga kuanza utekelezaji wa mradi huu kabla ya mwaka wa fedha 2021/2022 haujaisha endapo idhini itatolewa na mfadhili kwa wakati.
MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Kiwanja cha Ndege katika Mkoa wa Manyara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utaratibu wa kutwaa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mkoa wa Manyara.
Mheshmiwa Mwenyekiti, hadi sasa Serikali imeshamaliza kuandaa hadidu za rejea kwa ajili ya kumpata mhandisi elekezi atakayefanya upembuzi yakinifu pamoja na usanifu wa kina ili kubaini gharama za ujenzi. Hivyo, ujenzi wa kiwanja hicho utaanza baada ya usanifu kukamilika, ahsante.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itazijenga barabara za Kibada – Mwasonga – Tundwi – Songani na Ngomvi – Kimbiji hadi Pembamnazi kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa naiaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, zabuni kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami kwa Barabara ya Kibada-Mwasonga, Tundwi-Songani hadi Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 zimetangazwa tarehe 6 Januari, 2023 na zitafunguliwa tarehe 17 Februari, 2023. Kwa upande wa Barabara ya Ngomvu – Kimbiji hadi Pemba Mnazi yenye urefu wa kilometa 27, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika na sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE K.n.y. MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kuweka taa za barabarani katika Miji ya Magu, Kisesa, Nyanguge, Lugeye na Ilungu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Wakala wa Barabara Tanzania Mkoa wa Mwanza umepanga kuweka taa katika Miji ya Magu, Kisesa, Nyanguge, Lugeye na Illungu. Uchambuzi wa zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi unaendelea na unatarajiwa kukamilika tarehe 15 mwezi Februari mwaka huu wa 2023 na kazi inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu wa 2023, ahsante.
MHE. HAJI MAKAME MLENGE aliuliza: -
Je, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inashirikiana vipi na Ofisi ya Makamu wa Rais kuweka mazingira mazuri kandokando ya barabara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Haji Makame Mlenge, Mbunge wa Chwaka, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika kuweka mazingira mazuri kandokando ya barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inashirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kuhamasisha utunzaji wa mazingira ya barabara ikiwa ni pamoja na upandaji miti kandokando ya barabara. Aidha, Wizara inaendelea kuzingatia Sera ya Taifa ya Mazingira ya mwaka 2021, Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na Miongozo ya Usimamizi wa Mazingira katika kutunza mazingira ya barabara.
Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia NEMC inaendelea kuzingatia sheria hiyo kwa kuhakikisha miradi ya barabara inafanyiwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment) kabla ya ujenzi na kufanyia kazi matokeo ya tathmini hiyo ili kutunza mazingira ikiwemo kuweka mazingira mazuri kandokando ya barabara, ahsante.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Mlowo – Utambalila – Chitete na Utambalila – Kamsamba kilometa 145 inayounganisha Mikoa ya Songwe na Katavi itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Mlowo – Utambalila – Kamsamba yenye urefu wa kilometa 145 umekamilika mwaka 2020. Ujenzi wa Daraja la Momba lenye urefu wa kilometa 80 lililopo kwenye barabara hii eneo la mpakani mwa Songwe na Rukwa na barabara unganishi zenye urefu wa mita 950 kwa kiwango cha lami umekamilika mwezi Julai, 2019. Baada ya ujenzi wa daraja kukamilika, Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuendelea na ujenzi wa barabara hiyo, ahsante.
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -
Je, ni nini kinachelewesha ujenzi wa barabara kutoka kutoka Tabora – Mambali – Bukene hadi Kangogwa ilihali ilishatengewa bajeti?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (ENG.GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo: -
Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Tabora – Mambali – Bukene hadi Kagongwa yenye urefu wa KM 114 umekamilika mwaka 2020. Baada ya kukamilika kwa usanifu na gharama za ujenzi kwa kiwango cha lami kujulikana, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Aidha, Serikali imejenga kilometa 9.6 kwa kiwango cha lami kutoka Tabora Mjini kuelekea Mambali.
Mheshimiwa Spika, wakati Serikali ikiendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami, Wizara yangu kupitia TANROADS imeendelea kuifanyia matengenezo mbalimbali barabara hii ili iendelee kupitika wakati wote. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya Shilingi Milioni 1,200 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Ahsante.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga walau kilometa chache barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo – Londo mpaka Lumecha kilometa 296?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Antipas Zeno Mgungusi Mbunge wa Malinyi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imepokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na itaanza kujenga kilometa chache chache za barabara ya Lupiro – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo hadi Londo mpaka Lumecha yenye urefu wa kilometa 296 hasa kwa kuanza na maeneo korofi ili barabara hii iweze kupitika kwa urahisi wakati wote wa mwaka. Aidha, Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: -
Je, ni lini Barabara inayounganisha Wilaya ya Kyela na Ludewa kupitia Matema, Ikombe mpaka Liuli itaanza kujengwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFRY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyingulile Jumbe Mlaghila, Mbunge wa Kyela kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara inayounganisha Wilaya ya Kyela na Ludewa yenye urefu wa km 156 inapita kwenye safu ya milima ya Livingistone yenye miteremko mikali na miamba kubwa ya mawe.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kufungua barabara hii kwa awamu kwa kufyeka misutu na kupasua miamba. Azma ya Serikali ni kuifungua barabara yote kuanzia Lupingu (Ludewa/ - Lumbila-Matema (Kyela).
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Korogwe – Dindira – Bumbuli hadi Soni ambayo ilitengewa fedha kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi katika mwaka wa fedha 2020/2021?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFRY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami Barabara ya Korogwe – Dindira – Bumbuli – Soni (km 77) unafanyika kwa awamu. Sehemu ya kutoka Soni hadi Bumbuli (km 21.7) upembuzi yakinifu na usanifu wa Kina umekamilika. Kwa Sehemu iliyobaki ya kutoka Bumbuli hadi Korogwe (km 55.3), kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina inaendelea na imefikia asilimia 81.
Mheshimiwa Spika, baada ya Kazi ya Upembuzi Upembuzi yakinifu na Usanifu wa Kina kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya ulinzi kutoka Mtwara – Newala – Masasi hadi Songea kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu Swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Nanyamba kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, barabara ya ulinzi ya kutoka Mtwara – Newala – Masasi hadi Songea yenye urefu wa KM 358, inaambaa na Mto Ruvuma. Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa sasa inaendelea kuifungua barabara hii kwa kiwango cha changarawe na ujenzi wa madaraja makubwa na madogo katika mito na mikondo ya maji inayokatisha barabara hii ili iweze kupitika. Kiasi cha kilometa 208 zimefunguliwa na daraja kubwa la Mbangala lenye urefu wa mita 120 mkataba wa ujenzi umesainiwa tarehe 11 Aprili, 2022. Baada ya kuifungua barabara yote Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya kilometa 73 kutoka Fulo – Nyambiti – Malya itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Sumve, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara ya Fulo – Nyambiti – Malya yenye urefu wa kilometa 73 wakati wowote pindi fedha itakapopatikana. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kazi hii. Ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa kilomita 50 za barabara ya Mugakorongo kuanzia mpaka wa Uganda na Tanzania utaanza ili kuvutia biashara na watalii?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa barabara ya Omugakorongo – Kigarama hadi Murongo yenye urefu wa kilometa 110.1 utatekelezwa kwa awamu. Awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa sehemu ya barabara kutoka Murongo hadi Businde eneo la Kigarama yenye urefu wa kilometa 50. Ujenzi wa sehemu hii utaanza Murongo na pia utahusisha ujenzi wa Daraja la Murongo lililopo mpakani mwa Tanzania na Uganda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Kalebe – Bukoba Vijijini ili kuwezesha magari yenye uzito zaidi ya tani kumi kupita kwenye daraja hilo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya kujenga Daraja la Kalebe ambapo kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja hili inaendelea chini ya Mkataba wa Usanifu wa Barabara ya Kyaka II – Kanazi – Kyetema. Kazi ya usanifu imepangwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka huu wa 2022.
Mheshimiwa Spika, ahsante.
MHE. RITHA E. KABATI K.n.y. MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga daraja la Ugalla lililopo katika Kata ya Ugalla?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina wa Daraja la Ugalla lenye urefu wa mita 150, ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa ujenzi. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha ili kuanza ujenzi wa daraja hilo. Ahsante.
MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara za Dareda – Dongobesh, Katesh – Haydom, Karatu – Mbulu – Haydom – Singida na Babati hadi Orkesumet kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara za Dareda – Dongobesh (km 60), Katesh – Hydom (km 70), Karatu
– Mbulu – Hydom – Singida (km 246) na Babati - Orkesumet (km 145). Kwa kipande cha Mbulu – Garbab chenye urefu wa kilometa 25, taratibu za zabuni ziko kwenye hatua za mwisho za kusaini mkataba. Kwa kipande cha kutoka Garbab – Muslur chenye urefu wa kilometa 25 maandalizi ya kutangaza zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi yako kwenye hatua za mwisho. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu zilizobaki. Ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Haydom kwenda Mogitu - Katesh itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Wizara kupitia TANROADS tayari imeingia mkataba na mhandisi mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kufanya tathmini ya athari za kimazingira na uandaaji wa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Haydom – Katesh yenye urefu wa kilometa 70. Kazi ya Usanifu imeanza mwezi Februari, 2023 na inategemewa kukamilika mwezi Februari, 2024. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Mto Lumpungu katika Jimbo la Muhambwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi, Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mto Lumpungu unatenganisha nchi ya Burundi na Tanzania katika Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma kwenye Kijiji cha Kibuye, Kata ya Kumsenga. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha nchi mbili Burundi na Tanzania, Serikali itaanzisha mazungumzo na nchi ya Burundi ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hili, ahsante.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE K.n.y. MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza: -
Je, ujenzi wa barabara ya njia nane kutoka Kibaha – Chalinze hadi Morogoro umefikia hatua gani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), imekamilisha upembuzi yakinifu wa awali kutathimini uwezekano wa kujenga barabara ya Kibaha – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilomita 205 kwa utaratibu wa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi. Matokeo ya utafiti huo yalionesha mradi kuwa na manufaa makubwa ya kiuchumi na kifedha iwapo itajengwa barabara ya njia nne ya kulipia katika ushoroba mwingine (new corridor). Barabara ya sasa inayotumika itaendelea kutumika na watumiaji ambao hawatakuwa tayari kupita katika barabara ya kulipia.
Mheshimiwa Spika, Mtaalam Elekezi ameanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali ili kumpata mwekezaji wa kufanya ujenzi wa barabara ya kiwango cha expressway yenye njia nne ambapo sehemu ya Kibaha – Mlandizi – Chalinze kilometa 78.9 imekamilika na kuidhinishwa na Wizara ya Fedha na Mipango tarehe 7/3/2023. Tangazo la kuwataka wazabuni kuonesha nia ya kuwekeza katika mradi huu limetolewa tarehe 14/3/2023 na mwisho ni tarehe 18/4/2023.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya Chalinze hadi Morogoro kilomita126.1, upembuzi na usanifu wa awali unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2024, ahsante.
MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha Ujenzi wa Barabara ya Njombe – Ludewa – Itoni hadi Manda kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi kwa kiwango cha zege wa Barabara ya Itoni - Ludewa hadi Manda yenye urefu wa kilomita 211.42. Ujenzi kwa kiwango cha zege wa sehemu ya Lusitu – Mawengi kilomita 50 umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Itoni – Lusitu kilomita 50 unaendelea.
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa sehemu zilizobaki utaendelea kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya Luhindo hadi Ndondo katika barabara Kuu ya Nyoni hadi Mitomoni Wilayani Nyasa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Eng. Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Nyasa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.046 kwa ajili ya matengenezo mbalimbali kwenye barabara ya Nyoni - Liparamba hadi Mitomoni. Tayari Mkandarasi yupo eneo la kazi akiendelea na kazi za matengenezo ambapo katika sehemu korofi zenye miinuko na miteremko mikali anazijenga kwa zege na kuweka makalvati maeneo kadhaa. Kazi hizi zinategemewa kukamilika tarehe 30 Juni, 2023, ahsante.
MHE. JOHN M. SALLU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itamalizia ujenzi kwa kiwango cha lami kipande cha barabara ya Turiani hadi Handeni kilometa 104?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa John Marko Sallu, Mbunge wa Handeni Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii inayoanzia Magole, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya kuanzia Magole hadi Turiani yenye urefu wa kilometa 45.27, katika mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya shilingi bilioni moja zimetengwa kwa ajili ya kuanza maandalizi ya ujenzi wa sehemu iliyobaki kati ya Turiani – Mziha hadi Handeni kilometa 104 kwa awamu, ahsante.
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Masasi – Nachingwea kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Waziri Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Masasi – Nachingwea yenye urefu wa kilometa 45 ni sehemu ya barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale yenye urefu wa kilometa 175 ambayo ipo katika hatua ya Manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa kutumia utaratibu wa EPC+F. Uchambuzi wa zabuni upande wa technical umekamilika na sasa unafuata uchambuzi wa financial ambao utafanywa na Wizara ya Fedha na Mipango.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. (Makofi)
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya kutoka njia panda ya Iyula – Idiwili - Nyimbili hadi Ileje itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza kujenga barabara ya Njiapanda ya Iyula – Idiwili – Nyimbili hadi Ileje (kilometa 79) kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Mkandarasi amepatikana kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 2.1 kwa sehemu ya barabara ya kuanzia Njiapanda ya Iyula kuelekea Idiwili. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu iliyobaki.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -
Je, ni lini Barabara ya Kilosa hadi Mikumi itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza kujenga barabara ya Kilosa – Ulaya hadi Mikumi kilometa 77 kwa awamu kulingana na kiasi cha fedha kilichotengwa. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha shilingi milioni 1,300.00 zimetengwa. Mkataba wa ujenzi umesainiwa kujenga kipande cha kilometa moja katika eneo la Ulaya, ahsante sana.
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaweka taa za barabarani katika Mji wa Mpwapwa ili kuongeza usalama nyakati za usiku?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga kiasi cha Shilingi milioni 350 kwa ajili ya kuweka taa za barabarani katika Mji wa Mpwapwa kwa urefu wa kilometa 2.5. Kazi za uwekaji wa taa umeanza na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023, ahsante.
MHE. GEOFFREY I. MWAMBE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa stendi mpya ya Mji wa Masasi ikiwa ni mradi funganishi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Masasi hadi Mnivata?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Geoffrey Idelphonce Mwambe, Mbunge wa Masasi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa ushirikiano wa Benki ya Maendeleo ya Afrika ipo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya Mnivata – Newala – Masasi yenye urefu wa kilomita 160. Taarifa ya uchambuzi wa zabuni za kumpata mkandarasi zimekamilika na kuwasilishwa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya kupata idhini ya kuendelea na hatua ya kusaini mkataba (no objection). Kwa vile mradi wa ujenzi wa Stendi mpya ya Mji wa Masasi ni moja ya miradi itakayotekelezwa kama mchango kwa jamii chini ya mradi wa ujenzi wa barabara hii, kazi za ujenzi wa stendi mpya ya Mji wa Masasi itaanza baada ya mkataba wa ujenzi wa barabara kusainiwa na kazi za ujenzi kuanza. Ahsante.
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza: -
Je, ni lini wananchi wa Kata ya Sitalike waliopisha ujenzi wa barabara ya Sitalike hadi Mpanda Hotel watalipwa fidia?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wananchi wa Kata ya Sitalike hadi Mpanda wanaodai fidia ni wale walio kwenye eneo la nyongeza la upana wa hifadhi ya barabara la kutoka mita
22.5 kwenda mita 30.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuwalipa fidia wananchi hawa, ahsante.
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -
Je, lini barabara ya kilometa 0.8 kutoka Benki ya NMB hadi National Milling Kondoa Mjini itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) katika mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kuanza ujenzi wa barabara za Mji wa Kondoa kwa kiwango cha lami kwa urefu wa kilomita 3, ikiwemo kipande cha barabara ya kutoka Benki ya NMB hadi National Milling chenye urefu wa km 0.8. Ahsante.
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa Barabara ya Mbuyu wa Mjerumani hadi Mbulu, yenye urefu wa kilomita 50 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA K.n.y. MHE. AHMED A. SALUM aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa kiwango cha lami wa Barabara ya Mwanangwa – Mwakitolyo hadi Bulige utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ahmed Ally Salum, Mbunge wa Solwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Mwanangwa – Mwakitolyo hadi Bulige yenye urefu wa kilometa 148.8 kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Jumla ya kilometa 5.65 za sehemu ya Kahama kwenye barabara hii zimejengwa kwa kiwango cha lami na mita 540, sehemu ya Bulige imejengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Spika, aidha, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali imetenga shilingi milioni 750.62 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 1.2, sehemu ya Solwa na Bulige ambapo mkandarasi tayari amepatikana na ameshakabidhiwa mradi ili kuanza kazi. Ujenzi umepangwa kukamilika mwezi Septemba, 2023, ahsante.
MHE. EDWIN E. SWALLE aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa barabara ya Kibena Stop – Lupembe hadi Madeke kwa kiwango cha lami utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Edwin Enosy Swalle, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepanga kuanza ujenzi wa Barabara ya Kibena – Lupembe hadi Madeke yenye km 126 kwa awamu, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 itaanza ujenzi wa km 25 kwa sehemu ya kutoka Kibena hadi Nyombo. Kwa sasa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) wanaendelea kuandaa nyaraka kwa ajili ya kutangaza zabuni. Zabuni zinatarajiwa kutangazwa mwishoni mwa mwezi Juni, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kulingana na upatikanaji wa fedha hadi ikamilike yote, ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kahama – Solwa hadi Mwanza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Kahama – Solwa hadi Mwanza kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo kipande cha kilometa 5.65 kuanzia Kahama kuelekea Solwa pamoja na kipande cha mita 540 katika Mji Mdogo wa Bulige tayari imejengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga jumla ya shilingi milioni 750.62 kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 1.2 kati ya Solwa na Bulige ambapo mkandarasi tayari amepatikana na amekabidhiwa mradi ili kuanza kazi. Kazi imepangwa kukamilika mwezi Septemba, 2023.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa awamu hadi kukamilika yote kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. TUNZA I. MALAPO K.n.y. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Iyari hadi Mkunwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Shamsia Azizi Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania imepanga kujenga kilometa 2.2 katika barabara ya Iyari – Mkunwa (kilometa 79) kwa kiwango cha lami na mkandarasi yupo anaendelea na ujenzi ambapo kazi zinatarajiwa kukamilika Juni, 2023. Serikali itaendelea na ujenzi wa barabara hii kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha hadi kuikamilisha yote, ahsante.
MHE. FRANCIS I. MTINGA K.n.y. MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya mchepuko kutoka Kisaki – Unyamikumbi - Unyambwa hadi Mtipa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhan Sima, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa kina wa barabara ya mchepuko katika Mji wa Singida (Singida Bypass) kutoka Kisaki – Unyamikumbi – Unyambwa hadi Mtipa yenye urefu wa kilometa 46. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: -
Je, ni lini kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Mabokweni – Maramba – Daluni – Bombomtoni – Magoma – Korogwe utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dustan Luka Kitandula, Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania imeanza na inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Mabokweni – Bombomtoni – Mashewa – Magoma – Kwamndolwa hadi Old Korogwe urefu wa kilometa 127.69. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ilianza mwezi Agosti, 2022 na inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2023, ahsante.
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -
Je, ni hatua gani ya upembuzi yakinifu wa barabara ya Chimala – Matamba hadi Kitulo imefikiwa na lini ujenzi utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Makete kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Chimala – Matamba yenye urefu wa kilometa 20.1 ni barabara ya Wilaya ambayo imekasimiwa kwa TANROADS kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024. Baada ya kukasimiwa TANROADS, barabara yote kuanzia Chimala – Matamba hadi Kitulo ambayo itakuwa na urefu wa kilometa 41.1 itaingizwa kwenye mpango wa kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, ahsante.
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa kivuko cha waenda kwa miguu katika eneo la Kisimani barabara kuu itokayo Custom kwenda Sumbawanga itaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika eneo la Kisimani lililoko kwenye Barabara ya Tunduma kwenda Sumbawanga, kumewekwa alama za kuvuka (Pundamilia – Zebra Crossings) na Taa za kuongoza magari na watembea kwa miguu zimewekwa sehemu mbili; ya kwanza mita 300 kutoka eneo la Kisimani na ya pili mita 500 kutoka taa za kwanza za kuongozea magari na watembea kwa miguu (Traffic Signals). Aidha, Serikali ina mpango wa kujenga kivuko cha chini (underpass) katika eneo la Kisimani na utekelezaji wake unategemea upatikanaji wa fedha ahsante.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa kivuko kipya ya Kigamboni utaanza baada ya kutengewa fedha mwaka 2022/2023?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GEDFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, Mbunge wa Kigamboni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) katika mwaka wa fedha 2022/2023 umetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa kivuko kipya katika Kituo cha Magogoni – Kigamboni.
Mheshimiwa Spika, uzoefu uliopatikana kwa kutumia vivuko vidogo (sea taxi) vilivyokodishwa toka Kampuni ya Azam Marine umeonesha kuwa vivuko hivyo vina ufanisi zaidi katika kutatua kero ya ucheleweshwaji wa abiria. Hivyo, Serikali imeamua
kununua vivuko vidogo viwili. Taratibu za manunuzi ya vivuko vidogo viwili kwa ajili ya abiria (Sea Taxi) ambavyo vitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 250 kila kimoja zinaendelea, ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa kiwango cha lami barabra ya Kigonsera hadi Matiri na Mbinga hadi Litembo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Benaya Liuka Kapinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni kwa ajili ya kupata Mhandisi Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara ya Mbinga – Litembo – Mkiri sehemu ya Mbinga – Litembo/Mbuji kilometa 22 kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami ambapo zabuni zimefunguliwa tarehe 19 Aprili, 2023 na uchambuzi wa zabuni unaendelea. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana Serikali itatafuta fedha za kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Spika, aidha, kwa barabara ya Kigonsera – Matiri – Mbaha kilometa 55, Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga daraja litakalounganisha Tanzania Bara na Zanzibar?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mazungumzo kuhusu ujenzi wa daraja litakalounganisha Tanzania Bara na Zanzibar yalishaanza kwa kuzihusisha Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, sekta ya ujenzi kwa upande wa Tanzania Bara na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa upande wa Zanzibar, ambapo mnamo tarehe 11 Machi, 2023 kwa pamoja walikutana na Wawekezaji Kampuni ya China Overseas Engineering Group Company waliokuwa wameonesha nia ya kujenga daraja hilo. Yatokanayo na kikao hicho bado yanafanyiwa kazi kwa pande zote mbili Tanzania Bara na Zanzibar, ahsante.
MHE. JUDITH S. KAPINGA K.n.y. MHE. JERRY W. SILAA aliuliza: -
Je, Serikali haioni ni busara kuuza nyumba kwa Wapangaji wa kota za Ukonga kwa kuwa wameishi miaka mingi bila kufanyiwa ukarabati?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jerry William Silaa, Mbunge wa Ukonga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeweka mpango mahsusi wa kukarabati na kuendeleza maeneo yote ya kota nchini ambazo ni nyumba zilizorejeshwa TBA kutoka TAMISEMI.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, Serikali kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeanza kukarabati nyumba za kota za Ukonga ambapo kwa sasa TBA imekarabati maghorofa mawili yenye uwezo wa kubeba familia Nane. Ukarabati umehusisha maeneo ya paa, dari, mfumo wa umeme, mfumo wa majisafi na majitaka na upakaji wa rangi, ahsante.
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kurudia ujenzi wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa ambayo imejengwa chini ya kiwango na imeshaharibika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, mkandarasi alianza kazi za kurudia ujenzi wa maeneo yote ambayo yalionekana hayakidhi viwango vya ujenzi kwa gharama zake mwenyewe mnamo tarehe 10 Juni, 2021. Kazi za marudio ziko katika hatua za mwisho ambapo zimefikia asilimia 98 na zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO K.n.y. MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itapanua barabara ya Tegeta kuelekea kiwanda cha Saruji Wazo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Askofu Josephat Mathias Gwajima, Mbunge wa Kawe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kipande cha barabara ya Tegeta – Wazo Hill kilikarabatiwa Mwaka 2014 kwa kiwango cha lami kwa njia mbili (Single Carriage Way) ya upana wa mita 7 na njia za waenda kwa miguu zenye upana wa mita 1.5 kila upande. Upana huo unakidhi viwango vinavyohitajika kwa matumizi ya barabara ya njia mbili. Hata hivyo, kutokana na kuongezeka kwa wingi wa magari katika sehemu hii ya Tegeta – Wazo Hill, Serikali ina mpango wa kupanua barabara hii kuwa njia nne na utekelezaji wake utategemea upatikanaji wa fedha.Ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Vituo vya Abiria vya Bugorola, Ukara na Kisorya Ukerewe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) katika mwaka wa fedha 2022/2023, umetenga fedha kiasi cha shilingi 332,220,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Abiria vya Bugorola, Ukara na Kisorya katika Wilaya ya Ukerewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, TEMESA imeingia makubaliano na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA - Mwanza) kwa ajili ya kufanya usanifu wa miundombinu ya majengo na mchanganuo wa makadirio ya gharama husika. Taratibu za kumpata Mkandarasi atakayejenga miundombinu hiyo zitatekelezwa baada ya usanifu kukamilika ndani ya mwaka huu wa fedha 2022/2023, ahsante.
MHE. REHEMA J. MIGILLA aliuliza: -
Je, Serikali imetoa mwongozo gani kuhusiana na kiwango cha ubora wa taa zinazowekwa barabarani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rehema Juma Migilla, Mbunge wa Ulyankulu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haijatoa mwongozo rasmi kuhusiana na ubora wa taa zinazowekwa barabarani. Kwa sasa, Wizara imekasimisha shughuli za usimikaji wa mifumo ya umeme ikiwemo taa za kuongozea vyombo vya moto (traffic lights) na taa za usalama barabarani (street lights) kwa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ambapo hutoa msawazo (specifications) wa taa kwa Taasisi nunuzi unaoendana na mazingira na teknolojia ya wakati husika kwa viwango vya kimataifa.
MHE. AMOUR KHAMIS MBAROUK aliuliza: -
Je, kwa mujibu wa master plan ya miundombinu ya barabara Tanzania, tunahitaji fedha kiasi gani kukamilisha miundombinu hiyo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amour Khamis Mbarouk, Mbunge wa Tumbe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu kilometa 36,760.29, kati hizo kilometa 12,223.04 ni barabara kuu (Trunk Roads) na kilometa 24,537.25 ni barabara za mkoa (Regional Roads). Kati ya kilometa 36,760.29, kilometa 11,587.82 sawa na asilimia 31.50 zimejengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 25,172.48 zilizobaki ni za changarawe, sawa na asilimia
68.50. Ili kujenga kwa kiwango cha lami kilometa 25,172.48 zilizobaki, inakadiriwa kiasi cha shilingi trilioni 45.3 zinahitajika kwa wastani wa gharama za ujenzi bilioni 1.8 kwa kilometa kilometa moja, ahsante.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -
Je, lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya kutoka Geita – Bukoli hadi Kahama?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tumaini Bryceson Magessa, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepata fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 40 sawa na shilingi bilioni 92 kupitia Mkataba wa makubaliano na Kampuni ya Kuchimba Madini ya Barrick kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Kahama – Bulyanhulu hadi Kakola urefu wa kilometa 73. Kwa sasa kazi ya kupitia usanifu inafanyika kwa pamoja kati ya wataalam wa Serikali na Kampuni ya Barrick. Kazi zimepangwa kutangazwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023 na ujenzi unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2023/2024.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali itatenga fedha katika mwaka wa fedha 2023/2024 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa kipande kilichobaki cha barabara kutoka Geita – Bukoli – Bulyanhulu Junction kilometa 57.4, ahsante.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Simbo hadi Kalya?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Simbo – Kalya yenye urefu wa kilometa 234 kwa kuanza na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Daraja la Lower Malagarasi ambalo lipo katika barabara hii. Kazi za Usanifu zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika Novemba, 2023. Baada ya Usanifu kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja na kuanza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Simbo – Kalya urefu wa kilometa 234.
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Singida – Ilongero hadi Haydom?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Abeid Ramadhani Ighondo, Mbunge wa Singida Kaskazini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TANROADS tayari imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina pamoja na kuandaa nyaraka za zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Singida – Ilongero – Haydom yenye urefu wa kilometa 93. Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi, ahsante.
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Karema kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya kilometa 10 ya kutoka Mpanda hadi Kagwira na kwa sehemu iliyobaki ya kuanzia Kagwira hadi Karema (kilometa 112) zabuni za kuwapata Makandarasi zilitangazwa tarehe 20 Aprili, 2023 na zimepangwa kufunguliwa tarehe 31 Mei, 2023, ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mzumbe hadi Mgeta?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Mzumbe kuanzia Eneo la Sangasanga – Langali – Luale hadi Kikeo, yenye urefu wa kilometa 59.16 ambapo jumla ya kilometa 13.5 za lami zimejengwa na zimekamilika kwenye maeneo korofi yenye maporomoko na milima mikali. Aidha, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara hii kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA K.n.y. MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga kwa kwango cha lami barabara ya kutoka Ifakara hadi Mahenge?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salim Alaudin Hasham, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Ifakara Kibaoni hadi Mahenge Mjini yenye urefu wa kilometa 55.4 ni sehemu ya Barabara ya Ifakara – Mahenge– Malinyi – Kilosa kwa Mpepo
– Londo hadi Lumecha yenye urefu wa kilometa 435 ambayo Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa utaratibu wa EPC+F. Uchambuzi na tathmini ya zabuni za kumpata Mkandarasi na Mwekezaji atakayetekeleza mradi huu zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa Juni, 2023, ahsante. (Makofi)
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Kilambo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hasan Seleman Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Daraja la Kilambo linalopendekezwa kujenga litaunganisha Nchi ya Tanzania na Msumbiji katika Barabara ya Mangamba – Madimba – Tangazo – Kilambo yenye kilometa 36.8 Mkoani Mtwara. Kwa kuwa ujenzi wa daraja hili utahusisha Nchi mbili za Tanzania na Msumbiji, Serikali tayari imeanza mazungumzo ya awali na Nchi ya Msumbiji ili ziweze kukubaliana kuhusu ujenzi wa daraja hilo, ahsante.
MHE. NASHON W. BIDYANGUZE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Simbo - Kalya yenye urefu wa km 234?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nashon William Bidyanguze, Mbunge wa Kigoma Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Simbo – Kalya yenye urefu wa kilometa 234 kwa kuanza na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa daraja la Lower Malagarasi ambalo lipo katika barabara hii. Kazi za usanifu zinaendelea na zinatarajiwa kukamilika Novemba, 2023. Baada ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja na kuanza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Simbo hadi Kalya, yenye urefu wa kilometa 234, ahsante.
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -
Je, lini Daraja la Lyusa na Itembe na kalavati la Nkoma, Lyusa na Mwanjolo vitajengwa ili Daraja la Sibiti lipitike mwaka mzima?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, daraja la Lyusa na makalavati ya Nkoma, Lyusa na Mwanjolo yamejumuishwa katika mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa yenye urefu wa kilometa 389 ambapo Mkandarasi ameshapatikana na mkataba wa ujenzi unatarajiwa kuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa daraja la Itembe lenye urefu wa mita 150 lililopo katika Mkoa wa Simiyu, kazi za ujenzi zinaendelea na zimepangwa kukamilika mwezi Oktoba, 2023; ahsante.
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: -
Je, ni lini Serikalii itajenga barabara ya mchepuko ya Mlima Nyoka (Uyole) hadi Uwanja wa Ndege wa Songwe ili kuondoa msongamano na ajali?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oran Manase Njeza, Mbunge wa Mbeya Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ipo kwenye maandalizi ya kujenga barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma yenye urefu wa kilomita 218 pamoja na barabara ya mchepuo ya Mlima wa Nyoka pale Uyole hadi Uwanja wa Ndege wa Songwe (Uyole – Songwe Bypass) yenye urefu wa kilomita 48.9 kwa utaratibu wa EPC+F. Hadi sasa Mkandarasi amekwishapatikana na mkataba wa ujenzi utakuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023, ahsante.
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa barabara ya Mangaka hadi Morogoro kupitia Mbuga ya Selous utaanza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imepanga kuunganisha Mikoa ya Mtwara na Morogoro kwa barabara ya kutoka Masasi – Nachingwea – Liwale hadi Mahenge Mkoani Morogoro. Sehemu ya kutoka Masasi – Nachingwea – Liwale yenye urefu wa kilometa
175 itajengwa kwa utaratibu wa EPC + F. Kutoka Liwale – Mahenge kupitia Hifadhi ya Mbuga ya Selous Serikali imepanga kuanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mwaka wa fedha 2023/2024. Ahsante.
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Daraja la Kijiji cha Kalema Maziwani linalounganisha Wilaya za Kiteto, Chemba na Kondoa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), tayari imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kujenga upya Daraja la Kalema Maziwani katika barabara ya Kondoa – Bicha – Dalai ambalo lilititia kutokana na mvua kubwa za mwaka 2019. Ili kujenga daraja hilo mnamo tarehe 19 Mei, 2023 Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi na zabuni hizo zimepangwa kufunguliwa Tarehe 05 Juni, 2023, ahsante.
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Mlowo – Kamsamba kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Mlowo – Kamsamba yenye urefu wa kilometa 130.1 kwa awamu kwa kuanza na ujenzi wa Daraja la Momba lenye urefu wa mita 80 pamoja na barabara zake unganishi zenye urefu wa mita 950 na kazi ya ujenzi imekamilika. Aidha, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii. Katika mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imepanga kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mwembe – Mbaga hadi Mamba kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Mwembe – Mbaga hadi Mamba ambayo inaitwa Mwembe – Myamba – Ndungu yenye urefu wa kilometa 90.19. Baada ya usanifu kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga angalau kilometa tano kwa kiwango cha lami Barabara ya Tunduru - Mtwara Pachani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Mtwara Pachani – Lusewa – Lingusenguse – Nalasi hadi Tunduru yenye urefu wa kilometa 300 kwa awamu ambapo jumla ya kilometa 3.23 zimejengwa kwa lami nyepesi katika maeneo ya miji midogo ya Mkongo, Ligela, Lusewa na Sasawala. Aidha, mwezi Machi, 2023 Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imesaini mkataba kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa kipande cha mita 500 katika eneo la Tunduru Mjini. Vile vile, Serikali imekamilisha kazi ya Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii.
Mheshimiwa Spika, baada ya Usanifu kukamilika Serikali inaendelea kutafuta fedha za kuendelea na ujenzi, ahsante.
MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Gairo hadi Nongwe itajengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Gairo – Labeho hadi Nongwe yenye urefu wa kilomita 54.06 kwa kiwango cha lami baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Tayari maandalizi ya nyaraka za zabuni yamekamilika na zabuni kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya usanifu zitatangazwa mwezi Septemba, mwaka huu 2023 na zitafunguliwa mwezi Oktoba, 2023. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -
Je, lini TANROADS Mkoa wa Mara wataondoa vigingi katika maeneo ya Wananchi baada ya kushindwa kulipa fidia?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi wa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Bunda Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, upana wa eneo la hifadhi ya barabara zinazosimamiwa na Wakala ya Barabara Tanzania upo kwa mujibu wa Sheria ya Barabara ya mwaka 1932 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1962 na baadaye mwaka 1967 ambapo lilikuwa ni mita 22.5 kutoka katikati ya barabara kila upande. Aidha, Sheria mpya ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 na kanuni zake za mwaka 2009, ziliongeza upana wa eneo la hifadhi ya barabara kutoka mita 22.5 hadi mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa wananchi ambao wamo ndani ya nyongeza ya mita 7.5 kwa nchi nzima Serikali inaangalia upya nyongeza hii na itaandaa mapendekezo ya maeneo gani yabakie na nyongeza hii ya mita 7.5 ili fidia ilipwe na maeneo gani wananchi waruhusiwe kuendelea na shughuli zao. Ahsante.
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: -
Je, ni lini Serikali italipa fidia eneo la Nanganga ambako ujenzi wa barabara iendayo Ruangwa unaendelea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kanuni zake za Mwaka 2009 wananchi ambao mali zao zipo ndani ya mita 22.5 hawatastahili kulipwa fidia kwani wamo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara. Kwa upande wa wananchi ambao wamo ndani ya nyongeza za mita 7.5 kwa nchi nzima Serikali inafanya kazi na kuandaa mapendekezo ambayo yatabainisha maeneo gani wananchi wataruhusiwa kuyaendeleza na yapi Serikali itayachukua na kuyalipa fidia. Ahsante.
MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Choma - Ziba – Nkinga - Simbo - Puge utaanza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Said Gulamali, Mbunge wa Manonga kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami kwa barabara ya Choma – Ziba – Nkinga – Simbo – Puge yenye urefu wa kilometa 109 ambapo Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina amepatikana na ameanza kazi tarehe 24 Agosti, 2023 na anatarajia kukamilisha mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2024. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. GODWIN E. KUNAMBI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani kuhusu ujenzi wa barabara ya Mafinga hadi Mlimba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, nami kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako kama Naibu Waziri wa Ujenzi, naomba nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema, maana ametoa kibali hiki. Nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini ili niweze kumsaidia katika nafasi ya Unaibu Waziri wa Ujenzi, pia nikuahidi kwamba nitatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge lako Tukufu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba sasa nijibu swali. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Godwin Emmanuel Kunambi, Mbunge wa Mlimba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imepanga kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara inayoanzia Mafinga, eneo la Kinyanambo ‘C’ hadi Kihansi (Mlimba) yenye urefu wa kilometa 126.39, ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya milioni 250 zimetengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Baada ya kukamilika usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya Njia Panda - Mangola - Matala hadi Lalago kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Tlemai Awack, Mbunge wa Karatu kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Njia Panda kuanzia Karatu – Mang’ola – Matala – Sibiti River hadi Lalago, yenye urefu wa kilometa 328 inayojulikana kama Eyasi Route.
Mheshimiwa Spika, sehemu ya kuanzia Sibiti River hadi Lalago yenye urefu wa kilometa 121 imejumuishwa kwenye mradi wa EPC+F kupitia barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago hadi Maswa ambayo ina jumla ya kilomita 389 ambapo mkataba wake wa ujenzi umesainiwa. Kwa sehemu iliyobaki ya Njia Panda – Mang’ola hadi Matala kilometa 137, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante (Makofi)
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -
Je, lini barabara ya Ulinzi ya Hifadhi ya Mwalimu Nyerere inayojengwa toka Liwale hadi Mahenge itakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mohamedi Kuchauka, Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara hii kiulinzi na kijamii na inayounganisha Mikoa ya Lindi na Morogoro, katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya shilingi milioni 143.04 zimetengwa kwa ajili ya kazi za upembuzi yakinifu wa awali. Kazi ya upembuzi yakinifu wa awali itakapokamilika katika barabara hii inayopita katika Hifadhi ya Mbuga ya Wanyama ya Selous, itaonesha iwapo mradi unakidhi vigezo vya uhifadhi mazingira ili kuwezesha kujengwa, ahsante.
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:-
Je, Serikali ipo tayari kujenga kivuko cha juu barabara ya njia nane eneo la Magari Saba Mbezi ili kulinda uhai wa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Kibamba kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, eneo la Magari Saba, eneo la Mbezi, limekwishawekwa kivuko cha pundamilia (zebra crossing) kwa wapita kwa miguu ili kuwawezesha watumiaji wa barabara hiyo kuvuka kwa usalama katika eneo hilo, ahsante.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO K.n.y. MHE. JONAS V. ZEELAND aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Turiani hadi Mziha kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jonas Van Zeeland, Mbunge wa Mvomero, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Turiani hadi Mziha, yenye urefu wa kilometa 35.5 kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami imekamilika. Serikali imepanga kujenga ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami kwa awamu katika mwaka wa fedha 2023/2024. Ahsante.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaweka taa za kuongoza magari Igunga Mjini kwenye makutano ya barabara kuu ya Singida – Mwanza ili kuepusha ajali?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2022/23, imepanga kuweka taa za kuongozea magari katika Mji wa Igunga sehemu tatu tofauti kulingana na uhitaji wa sehemu hiyo. Mkandarasi wa kufanya kazi hiyo amepatikana na kukabidhiwa kazi tangu tarehe 01 Aprili, 2023, ahsante. (Makofi)
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga daraja linalounganisha Kata ya Bokwa na Songe Kilindi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya ujenzi wa Daraja la Songe katika barabara ya Kwaluguru – Kiberashi linalounganisha Kata ya Bokwa na Songe na barabara zake unganishi imekamilika tarehe 30 Novemba, 2022. Kwa sasa mkataba upo katika kipindi cha uangalizi hadi tarehe 29 Novemba, 2023, ahsante.
MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-
Je, lini Serikali itaboresha Madaraja ya Kampimbi na Mgandu Wilayani Same?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Madaraja ya Kampimbi yapo kwenye Barabara ya Same – Kisiwani hadi Mkomazi yenye urefu wa Kilometa 98. Mkataba kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Same – Kisiwani hadi Mkomazi yenye urefu wa Kilometa 98 umepangwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023. Ujenzi utajumuisha barabara na madaraja hayo na utaanza katika mwaka wa fedha 2023/2024, ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO K.n.y. MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -
Je, lini barabara ya Makongolosi – Mkiwa – Chunya itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Lupa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbeya – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (km 503.36) kwa awamu, ambapo sehemu ya Mbeya – Chunya – Makongolosi (kilometa 111) ujenzi umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya Noranga – Itigi – Mkiwa (kilometa 56.9) sehemu ya Noranga – Itigi (Mlongaji) (kilometa 25) umefikia asilimia 12 na kwa sehemu ya Noranga – Doroto (kilometa 6) na Itigi – Mkiwa (kilometa 25.6) mkataba wa ujenzi tayari umesainiwa. Kwa sehemu iliyobaki ya barabara za Makongolosi – Rungwa – Noranga (kilometa 356) na Mbalizi – Makongolosi (kilometa 50) Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi, ahsante.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Barabara za Itoni – Ludewa – Manda na Mkiu – Liganga – Madaba kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Zacharius Kamonga, Mbunge wa Ludewa kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Itoni – Ludewa – Manda yenye urefu wa kilometa 211.42 inajengwa kwa kiwango cha zege kwa awamu. Hadi sasa, Serikali imekamilisha Sehemu ya Lusitu – Mawengi kilomita 50. Kwa sehemu ya Itoni – Lusitu kilomita 50 kazi za ujenzi kwa kiwango cha zege zinaendelea. Kwa sehemu iliyobaki ya kutoka Mawengi – Manda kilomita 98.1, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu Barabara ya Mkiu – Liganga – Madaba yenye urefu wa kilomita 112 inayounganisha barabara ya Itoni – Ludewa hadi Manda na barabara kuu ya Makambako – Songea katika maeneo ya Mkiu na Madaba Mtawalia, tayari imefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikihusisha sehemu ya Liganga Nkomangómbe kilomita 70 na Nkomangómbe – Coal Power kilomita 4.14. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.
MHE. MWITA W. WAITARA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa barabara ya Tarime – Mugumu utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Tarime – Mugumu kilomita 87.14 kwa kiwango cha lami kwa awamu. Ujenzi kwa kiwango cha lami awamu ya kwanza sehemu ya Mogabiri – Nyamongo kilomita 25 unaendelea na utekelezaji wake umefikia asilimia 15. Aidha, Serikali ipo katika hatua za mwisho za manunuzi za kumpata Mkandaraasi atakayetekeleza ujenzi wa sehemu ya pili ya kutoka Tarime Mjini – Mogabiri na Nyamongo hadi Mugumu zenye jumla ya kilometa 62.14.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Arusha – Mirongoine – Simanjiro – Terati hadi Kongwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Noah Lemburis Saputu Mollel, Mbunge wa Arumeru Magharibi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Arusha – Mirongoine – Simanjiro – Kongwa inajulikana kwa jina la Arusha – Kibaya – Kongwa yenye urefu wa kilometa 453. Serikali itajenga barabara hii kwa kiwango cha lami kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction plus Finance (EPC + F). Hadi sasa Mkandarasi amekwishapatikana na mkataba wa ujenzi utasainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023. Ahsante.
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. TWAHA A. MPEMBENWE aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Bungu hadi Nyamisati Wilaya Kibiti?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Twaha Ally Mpembenwe, Mbunge wa Kibiti, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Bungu hadi Nyamisati yenye urefu wa kilometa 40.03. Kazi ya usanifu inatarajiwa kukamilika tarehe 30 Juni, 2023. Baada ya kukamilika kwa usanifu, Serikali itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa njia nne kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kilwa kipande cha Mbagala Rangi Tatu hadi Kongowe utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kuanza ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Mbagala Rangi Tatu hadi Kongowe, kilometa 3.8 katika mwaka wa fedha 2023/2024, ahsante.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ukarabati mkubwa wa barabara kuu ya Makambako - Njombe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa kuifanyia ukarabati barabara yote ya kutoka Makambako – Njombe – Songea yenye urefu wa kilometa 295. Sehemu ya Lutukila – Songea kilometa 95 ipo katika mpango wa ukarabati kupitia Mradi wa Tanzania Transport Integrated Project (TANTIP) ambapo Mkataba wa Mkopo nafuu kati ya Serikali na Benki ya Dunia umesainiwa na zabuni za kumpata Mkandarasi wa ujenzi zinatarajiwa kutangazwa mwezi Juni, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, sehemu iliyobaki ya Lutukila – Makambako ikiwemo na sehemu ya Makambako – Njombe urefu wa kilometa 59, Serikali inaendelea kutafuta fedha toka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje kwa ajili ya ukarabati. Ahsante.
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa meli tatu kwa ajili ya Ziwa Tanganyika kama ilivyoahidi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) imetenga bajeti katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya ujenzi wa meli mpya mbili; meli moja ya kubeba mizigo tani 3,500 na meli moja ya kubeba abiria 600 na mizigo tani 400 katika Ziwa Tanganyika. Kwa sasa MSCL ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na mkandarasi ili kuwezesha kuanza ujenzi wa meli hizo. Mikataba ya ujenzi wa meli hizo inatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa Juni, 2023.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, jitihada zinafanywa na Serikali za kukarabati Meli ya MV Liemba. Kwa sasa Serikali ipo katika hatua za mwisho za majadiliano na mkandarasi kabla ya mkataba wa ukarabati wa Meli ya MV Liemba kusainiwa, ahsante.
MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaboresha Kivuko cha Kinesi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ghati Zephania Chomete, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa miundombinu (jengo la abiria, ofisi, vyoo na uzio) katika Kituo cha Musoma maarufu kama Mwigobero. Mkandarasi amekabidhiwa eneo la ujenzi kwa ajili ya kuanza kazi. Aidha, ujenzi wa miundombinu upande wa Kinesi umepangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2023/2024, ahsante.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Tengeru utaendelea ikiwa ni mwendelezo wa barabara ya Sakina – Holili?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imepanga kuendeleza ujenzi wa barabara ya njia nne kuanzia Tengeru kwa kutumia fedha za mkopo nafuu kutoka Shirika la Maendeleao la Japan (JICA). Ujenzi utahusisha sehemu ya barabara ya Tengeru – Usa River yenye urefu wa kilometa 9.3, sehemu ya Moshi Mjini yenye urefu wa kilometa 8.4 na ujenzi wa daraja jipya la Kikafu lenye urefu wa mita 360. Kwa sasa mchakato wa manunuzi ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya kazi ya usanifu wa kina wa barabara na daraja upo katika hatua za mwisho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilika kwa usanifu, kazi ya ujenzi itaanza. Ahsante.
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya kutoka Kibada – Tundwi hadi Songani kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nipokee marekebisho ya Mheshimiwa Mbunge aliyoyasema.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nassoro Kisangi, Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Dar-es-Salaam, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imepanga kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kibada – Tundwi, Songani, Kimbiji yenye urefu wa kilometa 41 ambapo kwa sasa upo kwenye hatua za mwisho za manunuzi ya kumpata Makandarasi atakayetekeleza ujenzi wa mradi huu. Mkataba unatarajiwa kuwa umesainiwa kabla ya mwisho wa mwezi huu Juni, 2023. Ahsante.
MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:-
Je, Serikali inaonaje ikapunguza au kuondoa nauli kwenye vivuko vyote nchini kwa watu wenye ulemavu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inafahamu kuwepo na Watu Wenye Ulemavu wa aina mbalimbali ambao wanatumia huduma za vivuko kote Nchini. Aidha, suala la kupunguza au kutolipa nauli kwenye vivuko halijatamkwa kwenye Sheria ya Leseni za Usafirishaji.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, suala la kupunguza au kuondoa nauli limekuwa likifanyika kwa Watu Wenye Ulemavu waliopo kwenye mazingira hatarishi katika vyombo mbalimbali ikiwemo usafiri wa vivuko. Hii imefanyika kupitia ofisi za Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Maafisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri husika.
Mheshimiwa Spika, aidha, nichukue nafasi hii kuwaomba Waheshimiwa Wabunge kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu utaratibu huu wa kupunguza au kuondoa nauli kwa Watu Wenye Ulemavu au wenye mahitaji maalum. Ahsante.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami kwa Barabara ya Mlowo - Utambili hadi Kamsamba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Ranwell Mwenisongole, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami mwaka 2020. Aidha, Serikali imeanza kuijenga kwa awamu barabara hii ambapo imekamilisha ujenzi wa Daraja la Momba lenye urefu wa mita 80 na barabara za maingilio zenye urefu wa mita 950.
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha ujao wa 2023/2024 barabara hii imetengewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Babati Galapo hadi Orkesumeti kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS, imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami mwezi Februari, 2023. Kwa sasa Serikali inaendelea na zoezi la kufanya uthamini wa mali za wananchi watakaoathirika na mradi lililoanza tarehe 5 Juni, 2023 na inatarajiwa kukamilika tarehe 5 Julai, 2023. Baada ya zoezi la uthamini kukamilika na waathirika kulipwa fidia, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza:-
Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa barabara ya Karatu – Mbulu – Singida kilometa 190?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Karatu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Karatu – Mbulu – Singida ni sehemu ya barabara ya Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa yenye urefu wa kilometa 389. Serikali imeanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii ambapo sehemu ya Mbulu – Garbabi kilometa 25 kazi zinaendelea, sehemu ya Labay – Hydom kilometa 25) mkataba wa ujenzi umesainiwa tarehe 19 Mei, 2023 na sehemu iliyobaki itajengwa kupitia Mpango wa EPC + F wa barabara ya Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa ambapo mkandarasi amepatikana na mkataba wa kuanza ujenzi umesainiwa tarehe 16 Juni, 2023, ahsante. (Makofi)
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaendeleza barabara ya Mpanda - Kahama ili ifike Ulyankulu - Urambo - Ussoke - Tutuo - Sikonge hadi Mbeya?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Urambo kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANROADS inaendelea na kazi ya ujenzi wa barabara hizi kwa awamu kwa kiwango cha lami ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya kutoka Mpanda – Ugalla – Kaliua – Ulyankulu hadi Kahama urefu wa kilometa 457 umekamilika na sehemu ya barabara kutoka Urambo hadi Ussoke kilometa 45 tayari imejengwa kwa kiwango cha lami. Kwa sasa Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara za Ulyankulu hadi Urambo na Tutuo hadi Ussoke na baada ya kukamilika kwa usanifu huo Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hizi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya kutoka Ibanda hadi Itungi Port (kilometa 25) utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyigulile Jumbe Mlaghila, Mbunge wa Kyela, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Ibanda – Kajunjumele – Kiwira/Itungi Port yenye urefu wa kilometa 32 ulisainiwa rasmi mnamo tarehe 27 Desemba, 2022 na kupewa kibali cha kuanza ujenzi mnamo tarehe 31 Machi, 2023. Kwa sasa Mkandarasi yupo eneo la mradi anaendelea na ujenzi wa Kambi za Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ikiwa ni pamoja na maandalizi mengine kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: -
Je, ni lini Serikai itajenga kwa kiwango cha lami km 76 za barabara ya Karatu – Mbulu kwa kuwa usanifu wake ulifanyika 2021/2022?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ipo kwenye maandalizi ya kujenga kwa kiwango cha lami kwa utaratibu wa EPC+F (Engineering, Procurement, Construction plus Finance). Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti – Lalago – Maswa (km 389) ambapo barabara ya Karatu – Mbulu (km 76) ni sehemu ya barabara hii. Hadi sasa Mkandarasi amepatikana na mkataba wa kuanza ujenzi umesainiwa tarehe 16 Juni, 2023.
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa barabara ya Mtwara Pachani – Nalasi hadi Tunduru utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) tayari imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa barabara ya Mtwara Pachani – Nalasi hadi Tunduru yenye urefu wa kilometa 300. Katika mwaka wa fedha wa 2023/2024, Serikali imepanga kuendelea na ujenzi wa kilometa mbili katika Mji wa Tunduru. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi kwa sehemu iliyobaki, ahsante.
MHE. HALIMA J. MDEE aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Bunju B – Mabwepande – Kibamba utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima James Mdee, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Bunju B – Mabwepande – Kibamba yenye urefu wa kilometa 24.4 imeanza na inatarajiwa kukamilika mwezi Machi, 2024. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami kilometa 2.8 za barabara ambazo ni mchepuko kwenye barabara ya Pipeline?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa kilometa 2.8 za barabara za mchepuo eneo la Inyala. Kazi za ujenzi zilikamilika tarehe 24 Juni, 2023, ahsante.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya Lupingu hadi Kyela inayopita kandokando mwa Ziwa Nyasa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Zacharius Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Lupingu hadi Matema yenye urefu wa kilometa 126 ni barabara ya Mkoa na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Njombe na Mkoa wa Mbeya na inapita sehemu zenye mvua nyingi, milima na miteremko mikali. Kwa upande wa Mkoa wa Njombe barabara hii inafunguliwa kwa awamu ambapo jumla ya kilometa 3.6 zimefunguliwa na kwa upande wa Mkoa wa Mbeya jumla ya kilometa 4.0 zimefunguliwa ikiwa ni pamoja na kufanya ujenzi wa daraja moja (box culvert) na drift moja. Serikali kupitia TANROADS itaendelea kuifungua barabara hii kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Handeni – Kibirashi - Kondoa hadi Singida kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa, Mbunge wa Handeni Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kibaya – Chemba – Kwa Mtoro hadi Singida yenye urefu wa kilometa 424.24 kwa awamu. Ujenzi wa sehemu ya Handeni – Mafuleta kilometa 20 umefikia 11.61% na sehemu ya Mafuleta – Kileguru kilometa 30 mkataba umepelekwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa mapitio (vetting).
Mheshimiwa Spika, Kwa sehemu iliyobaki ya Kibirashi – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) utekelezaji wake upo kwenye miradi itakayojengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing EPC+F). Hadi sasa Mkandarasi wa kujenga barabara hii amepatikana na mkataba wa kuanza ujenzi umesainiwa tarehe 16 Juni, 2023. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza: -
Je, lini Serikali italipa fidia kwa maeneo ya Kahe/Chekereni na Njiapanda yaliyochukuliwa na TANROADS mwaka 2013?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, mwaka 2015 Serikali ilifanya na kukamilisha uthamini kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi 146 watakaoathirika na ujenzi wa mradi wa vituo vya ukaguzi wa pamoja wa magari ya mzigo (One Stop Inspection Station) ambapo kiasi cha shilingi bilioni 5.048 kilihitajika kuwalipa waathirika hao lakini hawakulipwa kutokana na Sheria Na. 7 ya Mwaka 2016 ya Uthamini na Usajili.
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANROADS Mkoa wa Kilimanjaro, inarudia zoezi la uthamini ulioanza tarehe 10 Mei, 2023 ambapo zoezi hilo lipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Baada ya zoezi hilo kukamilika waathirika watalipwa fidia zao, ahsante.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi wa Magari cha Muhalala – Manyoni?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja cha Muhalala Manyoni ulisimama kutokana na mkandarasi kusitisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho tarehe 11 Septemba, 2018 ukiwa umefikia 60.1%.
Mheshimiwa Spika, kusitishwa kwa ujenzi wa mradi huo kulisababisha mkandarasi kuingia katika mgogoro wa kimkataba na Serikali. Hivi sasa Serikali iko katika hatua ya kukamilisha makubaliano ya stahili za pande zote mbili kati ya Serikali na mkandarasi. Aidha, kwa kuwa Mkataba wa Ufadhili chini ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) bado unaendelea, Serikali itaendelea na mchakato wa kutafuta mkandarasi mwingine atakayemalizia kazi zilizobaki mara baada ya makubaliano ya stahili kukamilika, ahsante.
MHE. MIRAJI J. MTATURU K.n.y. MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga mitaro ya kuchepushia maji katika Kata za Bulyanhulu, Segese, Ngaya na Bulige?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Idd Kassim Idd, Mbunge wa Msalala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kata za Bulyanhulu na Segese zinapitiwa na Barabara ya Kahama hadi Kakola ambayo ipo kwenye mpango wa kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami katika mwaka wa fedha 2023/2024. Taratibu za manunuzi kwa ajili ya ujenzi zinaendelea na ujenzi wa mitaro utafanyika wakati wa utekelezaji wa mradi huo. Aidha, Mji Mdogo wa Bulige unapitiwa na Barabara ya Kahama – Solwa ambapo ujenzi kwa kiwango cha lami unaendelea na utahusisha ujenzi wa mitaro. Vilevile, mitaro iliyopo katika Kata ya Ngaya inakidhi mahitaji ya barabara hiyo na itaendelea kufanyiwa matengenezo, ahsante.
MHE. TASKA R. MBOGO aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Mpanda hadi Uvinza, yenye kilometa 159, utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mpanda hadi Uvinza yenye urefu wa kilometa 194 kwa awamu. Ujenzi wa Barabara ya Mpanda hadi Vikonge kilometa 37.6 umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Vikonge hadi Luhafwe kilometa 25 unaendelea. Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Luhafwe hadi Mishamo unatarajiwa kusainiwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2023. Kwa sehemu iliyobaki ya Mishamo – Uvinza kilometa 94, Serikali iko kwenye mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Afrika ili kuruhusu bakaa ya fedha za Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Tabora – Koga hadi Mpanda zitumike katika ujenzi wa sehemu hii, ahsante.
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza:-
Je, ni lini ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Mbuguni kuanzia Tengeru Sokoni, Arumeru hadi Mererani utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Tengeru Sokoni – Arumeru hadi Mererani yenye urefu wa kilometa 28 ambapo TANROADS wanaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina itakamilika Agosti, 2023. Baada ya usanifu kukamilika Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. FURAHA N. MATONDO K.n.y. MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: -
Je, lini kipande cha barabara cha Kisorya hadi Nansio kitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Ukerewe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inajenga barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya – Nansio yenye urefu wa kilometa 121.9 kwa awamu. Ujenzi kwa kiwango cha lami awamu ya kwanza sehemu ya Bulamba – Kisorya kilometa 51 umekamilika. Kwa sehemu ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba kilometa 56.4 ujenzi umekamilika na upo kwenye kipindi cha matazamio huku Mkandarasi akimalizia kazi ndogo ndogo zilizobaki. Kwa sehemu iliyobaki ya kutoka Kisorya hadi Nansio ambayo ina urefu wa kilometa 12.8 Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa barabara ya Mkiwa – Itigi hadi Rungwa inayounganisha Mkoa wa Mbeya na Singida utaanza kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Mkiwa kwa awamu. Taratibu za manunuzi ya mkandarasi wa kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Noranga – Itigi eneo la Mlongoji yenye urefu wa kilometa 25 zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba. Aidha, Serikali inaendelea na taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa kujenga sehemu ya kilometa 31.9 kati ya Itigi Kitongoji cha Mlongoji na Mgandu kwa kiwango cha lami. Kwa sehemu iliyobaki Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi. Ahsante.
MHE. SANTIEL E. KIRUMBA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Uwanja wa Ndege katika Mkoa wa Shinyanga?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Santiel Eric Kirumba, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga kitajengwa kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (European Investment Bank – EIB).
Mheshimiwa Mwenyekiti, mfadhili wa mradi huu tayari ameshaleta fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi. Aidha, Serikali imekwishafanya marekebisho ya mkataba na kuwasilisha kwa Mfadhili ili atoe idhini (no objection) kwani kutakuwa na mabadiliko ya gharama ikilinganishwa na wakati mkataba huo uliposainiwa mwaka 2017. Kazi za ujenzi wa mradi huu zitaanza mara moja tutakapopata no objection kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Handeni Kibirashi, Kondoa hadi Singida kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa, Mbunge wa Handeni Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro hadi Singida kwa awamu. Taratibu za manunuzi za kumpata Mkandarasi kwa sehemu ya Handeni – Mafuleta (km 20) zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba. Aidha, maandalizi ya kutangaza zabuni ya ujenzi kwa sehemu ya kutoka Mafuleta – Kwediboma yenye urefu wa kilometa 30 yanaendelea na zabuni itakuwa imetangazwa kabla ya mwezi Juni, 2022. Kwa sehemu iliyobaki Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante.
MHE. ASSA N. MAKANIKA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi watakaoathirika na ujenzi wa barabara ya Mwandiga – Manyovu Mkoani Kigoma?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Assa Nelson Makanika, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, barabara ya Mwandiga – Manyovu yenye urefu wa kilometa 53 ilianza kujengwa kwa kiwango cha lami mwezi Agosti, 2008 na kukamilika mwezi Oktoba, 2010. Wakati wa ujenzi wa barabara hii Wananchi wote waliostahili kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria kutokana na mali zao kuathirika na ujenzi huo walilipwa fidia. Ahsante.
MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi iliyotolewa na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa ya Ujenzi wa barabara ya Kharumwa yenye urefu wa kilometa mbili kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyang’hwale kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hii, Serikali kupitia Wizara yangu imeweka barabara yote ya Nyankumbu kuanzia Geita – Nyang’hwale hadi Nyang’holongo yenye urefu wa kilometa 123.11 inayojumuisha sehemu ya Kharumwa – Nyang’hwale katika mpango wa kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 hii ikiwa ni maandalizi ya ujenzi wa kiwango cha lami ambao utahusisha pia kilometa mbili katika eneo la Kharumwa anazozizungumzia Mheshimiwa Mbunge. Ahsante.
MHE. MWANTUMU M. ZODO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Bweni Wilayani Pangani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Mzamili Zodo, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, tararibu za manunuzi kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Pangani katika Mto Pangani litakalounganisha Vijiji vya Bweni na Pangani lenye urefu wa meta 525 ziko katika hatua za mwisho kwa ajili ya kusaini mkataba.
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:-
Je, ni lini barabara inayotoka Karagwe kupitia Nkwenda hadi Murongo itatengenezwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY KASEKENYA MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, zabuni kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Kyerwa hadi Chonyonyo (Kilometa 50) zimetangazwa na kufunguliwa tarehe 10 Mei, 2022. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali ipo kwenye hatua ya manunuzi ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo, ahsante.
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Seleman Mtenga, Mbunge wa Mtwara Mjini, kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Naibu Spika, jengo la abiria katika kiwanja cha ndege cha Mtwara litajengwa katika awamu ya pili ya ukarabati na upanuzi wa kiwanja hicho. Hivyo, fedha itatolewa baada ya kukamilika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mradi huu, ahsante.
MHE. NORAH W. MZERU aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Morogoro – Malinyi – Namtumbo kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Norah Waziri Mzeru, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafuata fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Ifakara – Malinyi – Kilosa kwa Mpepo - Londo hadi Lumecha (Namtumbo) kwa kiwango cha lami. Kwa sasa maeneo yote korofi yataainishwa na kujengwa ili barabara hii ipitike mwaka wote, ahsante.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Handeni Kibirashi, Kondoa hadi Singida kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa, Mbunge wa Handeni Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Handeni – Kiberashi – Kibaya – Chemba – Farkwa – Kwa Mtoro hadi Kititimo Singida kwa awamu ambapo mkataba wa mkandarasi wa kujenga sehemu ya Handeni – Mafuleta kilometa 20 ulisainiwa tarehe 11 Aprili, 2022. Ahsante.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -
Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara nyingi nchini zilizokwisha kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuzijenga kwa kiwango cha lami barabara zote zilizokwishafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Mpango huo unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga daraja katika eneo la Jangwani barabara ya Morogoro Jijini Dar es Salaam ili kuondoa usumbufu na adha wanazopata wananchi hasa wakati wa mvua?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Abdullah Juma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa daraja jipya la Jangwani chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ili kutatua tatizo la mafuriko imekamilika na Serikali inaendelea na mazungumzo na Benki ya Dunia ili kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo. Ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza: -
Je, ni lini ahadi ya Mheshimiwa Rais ya ujenzi wa barabara ya Mkuyuni hadi Mhandu itatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Shing’oma Mabula, Mbunge wa Nyamagana, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeanza kuifanyia upembuzi yakinifu na usanifu wa kina barabara ya Mkuyuni hadi Mhandu ili kuijenga kwa kiwango cha lami. Kazi hii ilianza tarehe 6 Juni, 2021 na inatarajiwa kukamilika Julai, 2022. Aidha, baada ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika, Serikali itatafuta fedha ili kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Unyoni hadi Maguu?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Benaya Liuka Kapinga, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali tayari imekamilisha kufungua barabara yote kuanzia Unyoni hadi Maguu yenye urefu wa jumla ya kilometa 25 kwa kiwango cha changarawe. Aidha, jumla ya kilometa 4.22 katika eneo la Mapera zimejengwa kwa kiwango cha lami nyepesi katika sehemu korofi. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza: -
Je, kuna juhudi gani za kufanya matengenezo ya kudumu katika eneo la Kyabalamba lililopo kati ya Kata za Rubale na Izimbya – Bukoba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imeendelea kuinua tuta la barabara eneo la Kyabalamba kwa kifusi cha mawe na kujenga madaraja madogo manne. Hadi sasa tuta la mita 400 na madaraja mawili yamekamilika na kazi itaendelea mwaka wa fedha wa 2022/2023. Ahsante.
MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUNGULILE aliuliza:-
Je, ni kiasi gani cha fedha kimekusanywa tangu Daraja la Nyerere lianze kutumika na ni lini huduma ya daraja hili itatolewa bila malipo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Faustine Engelbert Ndungulile, Mbunge wa Kigamboni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa Mfuko wa NSSF ulianza kupokea fedha zitokanazo na tozo kwa watumiaji wa Daraja la Nyerere mnamo tarehe 14 Mei, 2016 baada ya kuzinduliwa. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, 2022, Mfuko ulikuwa umekusanya jumla ya shilingi bilioni 66.86.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kupunguza tozo kwa watumiaji wa daraja hilo tangu kuzinduliwa kwake kwa kuzingatia tathmini ya uwezo wa wananchi kumudu tozo hizi. Kwa mara ya mwisho, Serikali imepunguza tozo husika tarehe 21 Mei, 2022. Ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Old Shinyanga kupitia Iselamagazi, Solwa hadi Salawe kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE): alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa sehemu ya Solwa - Salawe yenye urefu wa kilometa 15.35. Kwa sehemu iliyobaki kutoka Solwa kwenda Iselamagazi hadi Old Shinyanga yenye urefu wa kilometa 64.66 kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inaendelea. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika na gharama ya ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha ili kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:-
Je, lini barabara ya Makofia - Mlandizi itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Muharami Shabani Mkenge, Mbunge wa Bagamoyo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Makofia - Mlandizi, kilomita 35 ambapo kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imekamilika. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imepanga kujenga daraja dogo (box culvert) katika eneo la Mbwawa. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa barabara hii, ahsante.
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza:-
Je, nini mkakati wa Serikali kuboresha miundombinu ya barabara na kuinua maendeleo mikoa ya Lindi na Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tecla Mohamedi Ungele, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifautavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa Mkoa wa Mtwara, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi yenye urefu wa kilometa 210, ambapo sehemu ya Mtwara – Mnivata kilometa 50 ujenzi umekamilika na sehemu iliyobaki ya Mnivata – Newala – Masasi kilometa 160 pamoja na Daraja la Mwiti ujenzi umeanza na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026. Aidha, Serikali imepanga kuifanyia ukarabati barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi kilometa 200 ambapo maandalizi ya kutangaza zabuni za ukarabati wa barabara hii yako katika hatua za mwisho.
Mheshimwia Spika, kwa upande wa Mkoa wa Lindi, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ya Nanganga – Ruangwa kilometa 53.2 ambapo umefikia asilimia 74 na ujenzi wa barabara ya Nachingwea – Ruangwa kilometa 52.8 upo hatua za mwisho za manunuzi. Aidha, ujenzi wa barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale kilometa 175 utatekelezwa kwa utaratibu wa EPC + F na tayari mkataba wa ujenzi umesainiwa, ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-
Je, kwa nini Serikali isitumie teknolojia na vifaa vya kisasa kusafisha barabara za TANROADS?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imelichukua wazo la Mheshimiwa Mbunge na itaona ni namna gari nzuri ya kujumuisha teknolojia na vifaa vya kisasa katika kufanya usafi wa barabara pasipo kuathiri ajira za vikundi maalum ambavyo vimesajiliwa na Halmashauri za Miji, Wilaya, Mikoa, Manispaa na Majiji kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na Kanuni zake za mwaka 2016, ahsante.
MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza:-
Je, ni lini TANROADS watalipa fidia kwa kujenga shule mbadala baada ya shule ya Msingi Unkuku kupitiwa na Barabara ya Dodoma – Arusha?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Kondoa Mjini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mkoa wa Dodoma ilikwishalipa fidia kwa jengo la Shule ya Msingi Unkuku, miti pamoja na sehemu ya eneo la shule ambavyo viliathiriwa na ujenzi wa barabara ya Dodoma – Babati ambapo mnamo tarehe 10 Septemba, 2014 kiasi cha shilingi 8,370,221.00 kililipwa kwa Mkurugenzi wa Halmasauri ya Wilaya ya Kondoa, ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga barabara ya lami kutoka Kawajense – Ugalla hadi Kahama?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kawajense ambapo ni Mpanda – Ugalla – Kaliua – Ulyankulu – Kahama yenye urefu wa kilomita 456 ambapo kazi ya upembuzi yakinifu imekamilika na kazi itakayofuata ni kufanya usanifu wa kina. Aidha, usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Ugalla pamoja na madaraja saidizi sita yaani relief culverts umekamilika na kazi ya ujenzi wa madaraja hayo imeanza na inatarajia kukamilika mwaka 2024. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo, ahsante.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza:-
Je, lini Serikali itabadili Mitaala ya Elimu ili kwenda na wakati?
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekamilisha uandaaji na uidhinishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la mwaka 2023 na Mitaala katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Mafunzo ya Ualimu kwa lengo la kufanya elimu yetu iende na wakati. Mitaala iliyoboreshwa imezingatia mahitaji ya sasa ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo katika stadi za karne ya 21 ili kumjengea mhitimu stadi za Kuwasiliana, Kushirikiana, Ubunifu na fikra tunduizi. Aidha, ratiba ya utekelezaji wake inatarajiwa kuanza rasmi Mwezi Januari, 2024 na kukamilika mwaka 2027.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Elimu ya Kati na Elimu ya Juu, mapitio ya programu mbalimbali pia yanaendelea kwa lengo la kuifanya iende na wakati, vipaumbele vya nchi na mahitaji ya soko la ajira. Kwa mfano, kwa upande wa Elimu ya Juu kupitia Mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET) programu zaidi ya 300 zitahuishwa au kuanzishwa, nakushukuru.
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza: -
Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya malipo ya fidia kwenye miradi ya barabara za TANROADS zinazopita kwenye makazi ya watu Kibamba?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ulipaji wa fidia kwa wananchi ambao mali zao zinaathiriwa na miradi ya ujenzi wa barabara hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Namba 13 ya mwaka 2007. Wananchi wote ambao mali zao ziko nje ya eneo la hifadhi ya barabara wanalipwa fidia na wale ambao mali zao zimo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara hawastahili kulipwa fidia. Hii ni kwa wananchi wote nchi nzima ikiwemo na wananchi wa Jimbo la Kibamba, ahsante.
MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -
Je, ni lini upembuzi yakinifu utakamilika na kuanza ujenzi wa barabara ya Kahama – Nyang’hwale – Busisi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Nyang’hwale, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, zabuni ya manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Kahama, Nyang’hwale hadi Busisi yenye urefu wa kilometa 162.9, inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari 2024. Kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zinatarajiwa kuchukua muda wa mwaka mmoja. Hivyo kazi zitakamilika mwezi Februari, 2025. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa fedha zote za ujenzi wa barabara ya lami Karatu – Mbulu – Hydom hadi Sibiti ili ujenzi uendelee?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti – Lalago mpaka Maswa yenye urefu wa kilometa 389 inatekelezwa kwa kutumia fedha za ndani na kwa utaratibu wa EPC+F. Awamu ya kwanza: Mbulu – Garbabi (kilomita 25) Mkandarasi yupo eneo la mradi anaendelea na kazi. Eneo la Labay – Haydom (kilomita 25) Mkandarasi anakamilisha taratibu za kimkataba ili aweze kulipwa Malipo ya Awali (Advance Payment) ili aweze kuanza kazi. Sehemu iliyobaki ya Karatu – Mbulu na Haydom – Sibiti – Lalago – Maswa yenye urefu wa kilomita 339 itajengwa kwa utaratibu wa EPC+F ambapo Mkataba wa ujenzi ulisainiwa tarehe 16 Juni, 2023, ahsante.
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa Vibanda vya Wajasiriamali pembezoni mwa Barabara ya Njia Nane Kimara hadi Kiluvya utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS,) imekamilisha Usanifu wa Vibanda 950 vya Wajasiliamali vitakavyojengwa pembezoni mwa Barabara ya Morogoro kuanzia Kimara hadi Kiluvya. Zabuni ziko katika hatua ya uchambuzi (evaluation) na ujenzi unatarajiwa kuanza Mwezi Desemba, 2023 na utekelezaji wake unakadiriwa kuchukua muda wa miezi sita, ahsante.
MHE. MWANTUMU DAU HAJI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani kupunguza msongamano wa malori barabarani?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mwantumu Dau Haji, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango ya Serikali na jitihada za kupunguza msongamano wa magari ikiwemo malori barabarani ni pamoja na kujenga Madaraja na Barabara za juu kwenye majiji makubwa nchini, kufanya upanuzi wa barabara kutoka njia mbili kwenda njia nne hadi nane kwa maeneo yenye msongamano mkubwa, ujenzi wa maegesho ya malori, ufungaji wa mifumo ya kielektroniki ya kupima uzito wa malori yakiwa kwenye mwendo (Weigh in Motion System – WIMS) katika vituo vya mizani na barabara za michepuo katika miji na majiji mbalimbali, ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -
Je, nini kauli ya Serikali kwa Barabara ya Murushaka - Murongo ambayo Mkandarasi amepatikana zaidi ya mwaka mmoja bila Mkataba kusainiwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Seba Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Murushaka – Murongo yenye urefu wa kilometa 125, sehemu ya Kyerwa – Omurushaka kilometa 50, kati ya TANROADS na Mkandarasi Shandong Company Limited umesainiwa tarehe 19 Februari, 2024. Ahsante.
MHE. JOHN M. SALLU aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza kupanua barabara ya kutoka Segera – Manga hadi Chalinze?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa John Marko Sallu, Mbunge wa Handeni Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni kwa ajili ya kupata Mhandisi Mshauri wa kufanyakazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa Kina wa barabara ya Segera - Manga - Chalinze yenye urefu wa kilomita 175 na zitafunguliwa tarehe 14 Febuari, 2024. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inatarajiwa kukamilika Agosti, 2025. Baada ya kazi hiyo kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa barabara hiyo. Aidha, Serikali imekuwa ikipanua maeneo hatarishi kama kwenye milima na miinuko ili kupunguza ajali za barabarani. Ahsante.
MHE. PRISCUS J. TARIMO aliuliza:-
Je, kwa nini Serikali inachelewesha malipo kwa wakandarasi wazawa ambao wamekamilisha miradi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Priscus Jacob Tarimo, Mbunge wa Moshi Mjini kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Fedha zimekuwa zikishirikiana kuhusu upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi ikiwa ni pamoja na kulipa madai na madeni ya wakandarasi. Malipo kwa wakandarasi wote nchini hufanyika kulingana na upatikanaji wa fedha. Aidha, wakandarasi wazawa wamekuwa wakipewa kipaumbele katika malipo pindi fedha zinapotolewa. Ahsante.
MHE. MASACHE N. KASAKA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Makongolosi – Rungwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka, Mbunge wa Lupa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Mbeya – Chunya – Makongolosi – Rungwa – Mkiwa (kilometa 503.36) kwa awamu; ambapo sehemu ya Mbeya – Chunya – Makongolosi (kilometa 111) ujenzi umekamilika. Ujenzi wa sehemu ya Noranga – Itigi – Mkiwa (kilometa 56.9) sehemu ya Noranga – Itigi (kilometa 25.) umefikia asilimia 72 na kwa sehemu ya Noranga – Doroto (kilometa 6) na Itigi – Mkiwa (kilometa 25.6) kazi ya ujenzi imeanza na utekelezaji wa mradi unaendelea. Kwa sehemu iliyobaki ya barabara ya Makongolosi – Rungwa – Noranga (kilometa 356) Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi, ahsante.
MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza: -
Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa barabara kutoka Njiapanda/Ikungu kwenda Malampaka kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki, Mbunge wa Maswa Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Ikungu kwenda Malampaka yenye urefu wa kilometa 15 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 2.9 zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, Mkandarasi anaendelea na ujenzi wa kilometa 1.7 na kazi inategemewa kukamilika mwezi Juni, 2024. Kwa sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilometa 10.4, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-
Je, nini kauli ya Serikali kwa Barabara ya Murushaka - Murongo ambayo Mkandarasi amepatikana zaidi ya mwaka mmoja bila Mkataba kusainiwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Seba Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Ujenzi wa Barabara ya Murushaka – Murongo yenye urefu wa kilometa 125, sehemu ya Kyerwa – Omurushaka kilometa 50, kati ya TANROADS na Mkandarasi Shandong Company Limited umesainiwa tarehe 19 Februari, 2024. Ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA K.n.y. MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza: -
Je, ni lini barabara ya Nyashimo – Ndutwa – Shigala – Malili hadi Ngasamo itajegwa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), tayari imekamilisha taratibu za zabuni kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri atakayefanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Nyashimo – Ndutwa – Shigala – Malili hadi Ngasamo yenye urefu wa kilometa 48. Mkataba wa Mhandisi Mshauri unatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwezi Februari, 2024 na kazi ya usanifu inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2024. Baada ya kazi hiyo kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Ahsante.
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaacha kuwafukuza na kuwavunjia vibanda wajasiriamali wanaofanya biashara barabara kuu ya Segera – Korogwe – Moshi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Timotheo Paul Mnzava, Mbunge wa Korogwe Vijijini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, zoezi la kuondoa vibanda vilivyojengwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara kwa barabara kuu za Mkoa wa Tanga ikiwemo ile ya Segera – Korogwe – Moshi, lilifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 ambayo inapiga marufuku uwekaji wa miundombinu yoyote kwenye eneo hilo bila idhini ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS). Hivyo, TANROADS ilibomoa vibanda vya wafanyabiashara ambavyo havikupangwa kwa mpangilio mzuri na kuwepo na vibali na TANROADS. Wale ambao walikuwa na vibali na vibanda vyao kupangwa vizuri hawakuondolewa, ahsante.
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -
Je, nini kinakwamisha ujenzi wa barabara ya Same - Kisiwani - Ndungu hadi Mkomazi licha ya kutengewa fedha miaka minne mfululizo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Same – Kisiwani – Ndungu hadi Mkomazi yenye urefu wa kilometa 98 ulikamilika mwezi Novemba, 2020 na uthamini wa mali za wananchi watakaoathirika na mradi ulikamilika mwezi Septemba, 2022. Baada ya kukamilika kwa kazi ya usanifu, Serikali ilianza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa kipande cha kilometa 5.2 kutoka Maore hadi Ndungu mwezi Septemba, 2021 ambapo kazi za ujenzi zinaendelea na zimefikia asilimia 55 na zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024.
Mheshimiwa Spika, Serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kusaini mkataba na makandarasi wawili ili kuanza kujenga sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilometa 92.8 kwa kiwango cha lami ambayo imegawanywa katika sehemu mbili ambazo ni Same - Maore yenye urefu wa kilometa 56.8 na Ndungu - Mkomazi yenye urefu wa kilometa 36, ahsante.
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza:-
Je, lini Mkandarasi wa Barabara ya Lupilo, Malinyi, Kilosa kwa Mpepo hadi Londo ataanza kazi kwa mtindo wa EPC + F?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa barabara kwa utaratibu wa EPC+F unahusisha kufanya usanifu wa barabara kabla ya kuanza ujenzi. Kwa sasa Mkandarasi ameanza na anaendelea na usanifu wa kina. Aidha, Serikali na wakandarasi wanaendelea na taratibu za kupata fedha kwa ajili ya malipo ya awali kwa miradi yote ya EPC+F ukiwemo huu wa barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupilo – Malinyi – Londo hadi Lumecha Mkoani Ruvuma. Ahsante.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuepuka mzigo mkubwa wa ulipaji wa fidia wakati inapoongeza ukubwa wa barabara?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007, iliongeza upana wa hifadhi ya barabara kutoka meta 45 hadi meta 60 kwa barabara kuu na za Mikoa ili kukidhi mahitaji ya uendeshaji wa miundombinu ya barabara kwa wakati huu na wakati wa baadaye, ili uendane na ongezeko la watu na ukuaji wa shughuli za kiuchumi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kupunguza ulipaji wa fidia Wizara, kupitia TANROADS, imefanya tathmini ya awali ya gharama inayohitajika kwa ajili ya kulipa fidia kwa mali zilizomo ndani ya eneo la hifadhi ya barabara lililoongezeka la meta 7.5 kila upande na kuonesha kuwa, gharama kubwa za fidia ziko katika majiji na miji. Kutokana na hali hiyo, Serikali inaangalia uwezekano wa kuchepusha barabara kwenye maeneo hayo. Aidha, uchambuzi wa kina unafanyika, ili kubaini ni barabara zipi kweli zinahitaji upana wa eneo la hifadhi ya barabara wa meta 60 kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na ya hapo baadaye ya kuzipanua kulingana na ongezeko la wingi wa magari. Zoezi hili likikamilika taarifa kamili itatolewa, ahsante. (Makofi)
MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Ikungi – Mang'onyi – Londoni hadi Kilimatinde?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, zabuni ya manunuzi kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya kutoka Ikungi – Mang’onyi – Londoni hadi Kilimatinde yenye urefu wa kilometa 117.8 iko katika hatua za mwisho. Mkataba wa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina utakuwa umesainiwa kabla ya mwezi Juni, 2024. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inatarajiwa kuchukua kipindi cha mwaka mmoja na nusu, hivyo zitakamilika mwezi Disemba, 2025.
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante. (Makofi)
MHE. FLORENT L. KYOMBO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kyaka Katoro – Ibwera hadi Kyetema Nkenge kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Kyaka – Katoro – Ibwera hadi Kyetema yenye urefu wa kilometa 60.7 pamoja na daraja la Kalebe kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa taratibu za kutangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi wa kilometa 10 za barabara hiyo kwa kiwango cha lami pamoja na ujenzi wa daraja la Kalebe zinaendelea na inategemewa zabuni za kazi zitakuwa zimetangazwa kabla ya mwisho wa mwezi Juni, 2024. Kwa sehemu iliyobaki Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi, ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Kigonsera hadi Matiri?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kigonsera – Matiri yenye urefu wa kilometa 25 ni sehemu ya barabara ya mkoa ya Kigonsera – Kilindi – Mbaha yenye urefu wa kilometa 55 inayounganisha barabara kuu ya Songea – Mbinga na mwambao wa Ziwa Nyasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuifungua barabara hii inayoanzia Kigonsera hadi Mbaha ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Hadi sasa jumla ya kilometa 35 zimejengwa kwa kiwango cha changarawe, kilometa 12 zimefunguliwa na jitihada za kufungua sehemu iliyobaki ya kilometa nane zinaendelea. Mara baada ya kazi hii kukamilika, barabara hii itafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Madaraja ya Bujonde na Ilondo Mwaya - Kyela utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ujenzi wa Daraja la Bujonde linalounganisha Kata ya Kajunjumele na Bujonde. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imefikia 85% na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2024. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Daraja la Ilondo - Mwaya, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kulijenga daraja hili, ahsante.
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kiberashi hadi Songe Kilindi kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kiberashi – Songe (Kilindi) – Kwaluguru yenye urefu wa kilometa 127 imeingizwa kwenye Mpango wa Bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kazi hii ikikamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. TABASAM H. MWAGAO aliuliza:-
Je, lini mradi wa ujenzi wa Feri ya MV Buyagu utakamilika ikizingatiwa kuwa mkataba wa ujenzi umekwisha muda wake Aprili, 2024?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga kivuko kipya kitakachokuwa kiunganishi muhimu kati ya Wilaya ya Sengerema na Wilaya ya Misungwi kupitia eneo la Buyagu lililoko Sengerema na eneo la Mbalika lililopo Misungwi. Mkataba wa ujenzi wa kivuko hiki ulisainiwa mwezi Aprili, 2023 kati ya Serikali kupitia TEMESA na mkandarasi Songoro Marine Transport Mwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi za ujenzi wa kivuko hiki zimepangwa kukamilika mwezi Agosti, 2024 baada ya muda wa awali kuongezwa, ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Utegi hadi Kirongwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI NA UCHUKUZI (MHE. GODFREY K. MSONGWE) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Utegi – Kirongwe yenye urefu wa kilometa 48 inaendelea kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2022. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. JANETH M. MASSABURI aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kujenga barabara kwa kiwango cha lami pembezoni mwa reli ya SGR wakati ujenzi unaendelea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Sheria ya Reli Na. 10 ya mwaka 2017, hifadhi ya reli ni meta 30 kutoka katikati ya reli kila upande. Katika eneo hili hairuhusiwi kujenga barabara kwa matumizi ya kawaida. Hivyo, haitawezekana kujenga barabara ya lami pembezoni mwa reli ya SGR, ahsante. (Makofi)
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Tabora – Mambali – Bukene hadi Itobo kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Tabora – Mambali – Bukene hadi Itobo kilometa 114, unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa nane kuanzia Tabora Mjini hadi Nyuzi Round-about zimejengwa kwa kiwango cha lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, ujenzi wa kilometa moja kuanzia Kijiji cha Uduka kuelekea Kabanga unaendelea na umefikia 60%. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na kazi za ujenzi, ahsante. (Makofi)
MHE. EDWIN E. SWALLE K.n.y. MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa Barabara ya Katoro hadi Ushirombo hususani kipande cha Katoro hadi Luhembero utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Katoro hadi Ushirombo yenye urefu wa kilometa 58.2 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Nyikonga hadi Kashelo kilometa 10.5 yanaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia ambapo mkataba kwa ajili ya kuanza ujenzi unatagemewa kusainiwa mwezi Agosti, 2024. Kwa sehemu zilizobaki za Katoro – Nyikonga kilometa 26.2 na Kashelo – Ushirombo kilometa 21.5, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: -
Je, lini Barabara ya Pacha ya Mindu – Ngapa hadi Nachingwea itajengwa kwa Kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya kutoka Pacha ya Mindu – Ngapa hadi Nachingwea yenye urefu wa kilomita 153 yameanza, ambapo zabuni kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ipo katika hatua ya tathmini (evaluation). Kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zinatarajiwa kuchukua kipindi cha mwaka mmoja, hivyo zitakamilika mwezi Juni, 2025.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante. (Makofi)
MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Bandari ya Mtwara inatumika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GEORGE K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa viti maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha uboreshaji wa miundombinu ya Bandari ya Mtwara na ununuzi wa vifaa vipya ambavyo vitawasili mwezi Agosti, 2022 kwa ajili ya Bandari ya Mtwara. Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) inaendelea kuitangaza Bandari ya Mtwara pamoja na kupunguza tozo za Bandari ya Mtwara, ahsante. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. JEREMIAH M. AMSABI aliuliza:-
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa barabara ya lami kipande cha Sanzate hadi Natta.
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jeremiah Mrimi Amsabi, Mbunge wa Serengeti, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa Barabara ya Sanzate – Natta, urefu wa kilometa wa kilometa 40 ambapo hadi kufikia Machi, 2024 utekelezaji umefikia asilimia 45 na mradi unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Januari, 2025, ahsante.
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. NOAH L. SAPUTU aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itazuia kupaki magari ya Serikali sehemu za starehe baada ya saa za kazi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, napenda kujibu swali la Mbunge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Waraka wa Rais Na. 1 wa Mwaka 1998 kuhusu Hatua za Kubana Matumizi ya Serikali, ilielekezwa kuwa Magari yote ya Serikali yanatakiwa kuwa yameegeshwa sehemu zilizotengwa kwa ajili hiyo ifikapo saa 12.00 jioni bila kukosa. Vinginevyo, kiwepo kibali rasmi kinachoruhusu Gari la Serikali kuwepo barabarani baada ya saa 12.00 jioni.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, Serikali kupitia Kanuni Na. 21 ya Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za Mwaka 2009, imezuia Watumishi wa Umma kutumia Magari ya Serikali kwa matumizi binafsi. Hivyo, mtumishi anayekwenda kinyume na maelekezo hayo anatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa fursa hii naomba kuwakumbusha Maafisa Masuuli wote kusimamia maelekezo hayo. Ahsante.
MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -
Je, upi ukomo wa kuweka alama za upana wa Barabara Vijijini na kuwataka Wananchi kubomoa nyumba kutumia Sheria ya Mwaka 1932 na 2007?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na Sheria ya Barabara Na. 40 ya Mwaka 1932, hifadhi ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS ilikuwa mita 22.5 kutoka katikati ya barabara kila upande isipokuwa kwa barabara ya Morogoro ambao hifadhi yake ilikuwa kati ya mita 22.5 hadi 121.9 kuanzia Dar es Salaam City Hall hadi Daraja la Ruvu. TANROADS imeweka alama ya ‘X’ ya rangi nyekundu kwa mali za wananchi zilizopo ndani ya mita 22.5 na kuwataka wananchi waondoe mali hizo kwa gharama zao wenyewe kwa kuwa wamevamia eneo la hifadhi ya barabara.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Barabara Na. 13 ya Mwaka 2007 iliongeza hifadhi ya barabara zinazosimamiwa na TANROADS kutoka mita 22.5 kuwa mita 30 kutoka katikati ya barabara kila upande. Katika kutekeleza Sheria hii, TANROADS imeweka alama ya ‘X’ za rangi ya kijani kuonesha eneo la mita 7.5 liliongezeka kila upande ambapo wananchi waliopo katika eneo hili hawapaswi kuondoa mali zao mpaka watakapolipwa fidia.
MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza: -
Je, Serikali imefikia hatua gani katika ujenzi wa barabara za juu kwenye makutano ya barabara katika Jiji la Mwanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Mwanza, Serikali tayari imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya juu katika makutano ya Buzuruga yaliyoko katika barabara ya Mwanza Mjini hadi Nyanguge yenye urefu wa kilomita 35. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -
Je, hadi sasa ni kilometa ngapi zimejengwa kwa kiwango cha lami Barabara ya Mbalizi - Mkwajuni?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Mbalizi – Mkwajuni yenye urefu wa kilometa 92 ni sehemu ya barabara ya Mbalizi – Chang’ombe – Mkwajuni, Mkwajuni hadi Makongolosi yenye urefu wa kilometa115 inayounganisha Mkoa wa Mbeya na Songwe. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 10.4 zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, taratibu za manunuzi ya Mkandarasi kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa kilometa tano katika Mji wa Mkwajuni Mkoani Songwe na kilometa 3.5 kwa upande wa Mkoa wa Mbeya zinaendelea, ahsante.
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. ASSA N. MAKANIKA aliuliza: -
Je, nini mpango wa fidia kwa wananchi walioguswa na ujenzi wa Barabara ya Kigoma -Kasulu ambao nyumba zao zimewekewa X?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI aljibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 na kanuni zake za mwaka 2009 iliongeza upana wa eneo la hifadhi ya barabara kuu na za mkoa kutoka meta 45 hadi 60 ikiwa na nyongeza ya meta 7.5 kutoka katikati ya barabara kila upande. Kufuatia utekelezaji wa sheria hii, alama ya “X” yenye rangi ya kijani iliwekwa kwenye nyumba zote za wananchi zilizopo katika eneo hii ikiwa na maana kuwa wananchi hao waendelee kuwepo katika eneo hilo hadi watakapolipwa fidia, ahsante.
MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa barabara ya lami kutoka Choma - Ziba na Ziba - Puge utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Barabara ya Puge – Ziba – Choma yenye urefu wa kilometa 109 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imepanga kuanza ujenzi wa kilometa 11; kwa sehemu za Puge – Ndala kilometa tano; Ziba – Choma - kilometa mbili na Ziba – Nkinga kilometa nne. Kwa sasa kazi ya mapitio ya makabrasha ya zabuni inaendelea na mara baada ya kazi hiyo kukamilika zabuni zitatangazwa. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo, ahsante.
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuuza nyumba za TBA kama ilivyo kwa NHC ili ijiondoe kwenye biashara ambayo ina changamoto kwao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imefanya mabadiliko Hati Idhini iliyoanzisha Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kupitia Tangazo la Serikali (GN) Na. 595 la tarehe 25 Agosti, 2023 ili kuwezesha Wakala kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa TBA imeanza kujenga nyumba za kuuza kwa umma wote kama ilivyo kwa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Tayari Wakala umeandaa orodha ya miradi ya ujenzi wa nyumba zitakazouzwa kwa wananchi wote.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA aliuliza:-
Je, lini Serikali itakabidhi majengo yaliyotumiwa na Mshauri wa Ujenzi wa Barabara ya Mbinga hadi Mbamba Bay kwa Halmashauri ya Nyasa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, majengo ya kambi yaliyokuwa yanatumiwa na mhandisi mshauri wa ujenzi wa Barabara ya Mbinga – Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 67 yalirudishwa Wizara ya Ujenzi mnamo Tarehe 13 Aprili, 2023. Kwa sasa majengo hayo yanatumika kama nyumba za watumishi, wauguzi na madaktari, wa Hospitali ya Wilaya ya Nyasa. Ahsante.
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya kutoka Karatu – Mang’ola – Matala hadi Lalago kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Karatu – Mang’ola – Matala – Lalago yenye urefu wa kilomita 229 umekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Karatu – Mang’ola – Matala hadi Sibiti yenye urefu wa kilomita 156. Ahsante.
MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza:-
Je, lini Serikai itajenga Barabara ya Ifakara – Malinyi – Namatumbo – Mahenge Mjini hadi Lupiro kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imeshasaini mkataba wa ujenzi wa Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Londo – Lumecha kwa utaratibu wa EPC + F. Kwa kawaida, ujenzi wa barabara kwa utaratibu wa EPC + F unahusisha kufanya usanifu wa barabara kabla ya kuanza ujenzi. Kwa sasa mkandarasi ameanza na anaendelea na usanifu wa kina. Aidha, Serikali na wakandarasi wanaendelea na taratibu za kupata fedha kwa ajili ya malipo ya awali kwa miradi yote ya EPC + F ikiwemo barabara hii, ahsante.
MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Solwa hadi Kahama kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Kahama – Solwa yenye urefu wa kilometa 79.96 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 6.1 zimekamilika kujengwa. Aidha, kazi za ujenzi wa jumla ya kilometa 1.2 zinaendelea katika Miji ya Ngaya (meta 400), Bulige (meta 400) na Solwa (meta 400) na umefikia 68%. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na kazi ya ujenzi, ahsante.
MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kutoka Masasi kwenda Liwale kupitia Nachingwea?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale yenye urefu wa kilometa 175 ni miongoni mwa miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa utaratibu wa EPC+F. Kutokana na mabadiliko ya uchumi duniani, eneo linalohusu fedha limekuwa na changamoto ya upatikanaji. Ili kuepuka kuchelewa zaidi kwa utekelezaji wa miradi hii, Serikali imeanza kuangalia utaratibu mbadala ili mikataba iliyopo ifanyiwe mapitio yatakayowezesha miradi hii kujengwa kwa utaratibu wa kawaida wa “design and build” na ujenzi wake ufanyike kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati Barabara ya Kongowe hadi Mjimwema?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekuwa ikifanya ukarabati wa maeneo korofi katika Barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kivukoni yenye urefu wa kilometa 25.01, hasa yale yaliyoharibika sana katika kipindi cha mvua. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500, kwa ajili ya ukarabati wa maeneo yote yaliyoharibika, ahsante.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Nangwa – Gisambalang hadi Kondoa kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Nangwa – Gisambalang hadi Kondoa yenye urefu wa kilometa 79 yameanza kwa kutangaza zabuni ya kumpata mhandisi mshauri kwa ajili ya kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. manunuzi ya mhandisi mshauri yatakamilika mwezi Julai, 2024 na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inatarajiwa kuchukua muda wa miezi 12. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina itakapokamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-
Je, lini zabuni ya ujenzi wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda kwa kiwango cha lami itatangazwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda yenye urefu wa kilometa 18.13. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. NG'WASI D. KAMANI K.n.y MHE. MARY F. MASANJA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Nhungumalwa – Ngudu mpaka Magu kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Nhungumalwa – Ngudu yenye urefu wa kilometa 71 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, jumla ya mita 500 pamoja na roundabout zilijengwa katika eneo la Isandula. Aidha, mkataba wa ujenzi kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya kuanzia Magu hadi Ngudu yenye urefu wa kilomita 10 umesainiwa mwezi Mei, 2024 na kwa sasa mkandarasi yupo katika maandalizi ya kuanza ujenzi. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na kazi za ujenzi, ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaipandisha hadhi Barabara ya kutoka Mkolani Darajani – Nyakagwe hadi Busisi kwa kuiondoa TARURA na kuipeleka TANROADS?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kupandisha au kushusha hadhi barabara upo kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Sheria ya Barabara, Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kifungu cha 44(1) cha Kanuni za Menejimenti ya Barabara za Mwaka 2009. Kwa utaratibu huo, namshauri Mheshimiwa Mbunge awasilishe maombi ya kuipandisha hadhi barabara hiyo. Maombi hayo yatakapowasilishwa yatafanyiwa kazi na ikionekana barabara hiyo inakidhi vigezo, itapandishwa hadhi. Ahsante.
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Kilambo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatafuta fedha ili iweze kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Daraja la Kilambo. Baada ya kufanyiwa usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:-
Je, lini Serikali itawalipa fidia Wananchi wa Kahe/Chekereni na Njiapanda ambao maeneo yao yalichukuliwa na TANROADS Mwaka 2013? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, uthamini wa Mali za Wananchi wa Kahe/Chekereni – Njiapanda (Himo) watakaoathiriwa na mradi huo ulifanyika Mwaka 2013. Hata hivyo, kutokana na muda mrefu kupita bila kulipa fidia hiyo, Serikali imerudia zoezi la uthamini na taarifa ya uthamini imeidhinishwa na Mthamini Mkuu wa Serikali Tarehe 8 Machi, 2024. Kwa sasa, Serikali inaendelea kutafuta fedha, kwa ajili ya kulipa fidia kwa mali za wananchi watakaoathiriwa na mradi huo. Ahsante.
MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: -
Je, lini wananchi waliowekewa alama ya X kwenye barabara ya Masasi mpaka Liwale watalipwa fidia?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa wananchi wote ambao wamewekewa alama ya X kwenye barabara ya Masasi mpaka Liwale. Serikali itahakikisha inalipa fidia kwa mujibu wa sheria kabla ya ujenzi wa barabara hiyo kuanza, ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE K.n.y. MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE aliuliza:-
Je, lini zabuni ya ujenzi wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda kwa kiwango cha lami itatangazwa?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mbambo – Ntaba hadi Ipinda yenye urefu wa kilometa 18.13. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante.
MHE. NG'WASI D. KAMANI K.n.y MHE. MARY F. MASANJA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Nhungumalwa – Ngudu mpaka Magu kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Nhungumalwa – Ngudu yenye urefu wa kilometa 71 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, jumla ya mita 500 pamoja na roundabout zilijengwa katika eneo la Isandula. Aidha, mkataba wa ujenzi kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu ya kuanzia Magu hadi Ngudu yenye urefu wa kilomita 10 umesainiwa mwezi Mei, 2024 na kwa sasa mkandarasi yupo katika maandalizi ya kuanza ujenzi. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na kazi za ujenzi, ahsante.
MHE. STANSLAUS S. MABULA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaipandisha hadhi Barabara ya kutoka Mkolani Darajani – Nyakagwe hadi Busisi kwa kuiondoa TARURA na kuipeleka TANROADS?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kupandisha au kushusha hadhi barabara upo kwa mujibu wa Kifungu cha 11 cha Sheria ya Barabara, Na. 13 ya Mwaka 2007 na Kifungu cha 44(1) cha Kanuni za Menejimenti ya Barabara za Mwaka 2009. Kwa utaratibu huo, namshauri Mheshimiwa Mbunge awasilishe maombi ya kuipandisha hadhi barabara hiyo. Maombi hayo yatakapowasilishwa yatafanyiwa kazi na ikionekana barabara hiyo inakidhi vigezo, itapandishwa hadhi. Ahsante.
MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Daraja la Kilambo?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatafuta fedha ili iweze kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Daraja la Kilambo. Baada ya kufanyiwa usanifu na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Igawa hadi Tunduma utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Igawa – Tunduma kwa njia nne inajengwa kwa awamu, ambapo sehemu ya kuanzia Uyole eneo la Nsalaga – Ifisi, kilometa 29, ujenzi wake unaendelea na hadi sasa umefikia 15.5%. Kazi za ujenzi zimepangwa kukamilika tarehe 13 Aprili, 2025. Kwa sehemu iliyobaki ya Igawa – Uyole, eneo la Nsalaga na Ifisi – Tunduma zitajengwa kwa utaratibu wa EPC+ F. Ahsante. (Makofi)
MHE. PAULINE P. GEKUL aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwalipa fidia wananchi wa Babati waliopisha ujenzi wa barabara za mchepuko takribani miaka minne iliyopita?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, baada ya usanifu wa kina na uthamini wa mali zitakazoathiriwa na Mradi wa Barabara ya Mchepuo wa Mji wa Babati (Babati Bypass), tathmini ilionesha kwamba barabara pendekezwa ya Babati Bypass yenye urefu wa kilometa 27 inapita katika maeneo ya Mji wa Babati yenye nyumba nyingi na kusababisha gharama ya fidia kuwa kubwa kiasi cha shilingi bilioni 9.05. Kutokana na hali hiyo, Serikali imemwelekeza Mhandisi Mshauri kupendekeza njia nyingine mbadala ambayo itapita nje ya Mji. Hivyo, fidia kwa njia ya awali imesitishwa. Ahsante.
MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza Ujenzi wa Barabara ya Chela - Busengi hadi Kahama kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, zabuni kwa ajili ya kumpata mhandisi mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Nyang’oholongo ambayo ipo mpakani mwa Geita na Shinyanga kwenda Chela – Busangi hadi Nyambula yenye urefu wa kilometa 40.45 ipo katika hatua ya tathmini ambayo inatarajiwa kukamilika na kusainiwa kwa mkataba mwishoni mwa mwezi Julai, 2024. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2025. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza: -
Je, Serikali imefikia hatua gani ya ujenzi wa barabara ya Haydom hadi Mogitu kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Haydom – Mogitu yenye urefu wa kilometa 70 imekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza:-
Je, lini wananchi wanaopisha ujenzi wa barabara ya Ibanda – Itungi Port wa Iponjola - Kiwila Port watalipwa fidia zao?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la uthamini wa mali za wananchi zitakazoathirika wakati wa ujenzi wa barabara ya Ibanda – Itungi Port na Iponjola – Kiwira Port limekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kulipa fidia kwa wananchi hao.
MHE. KUNTI Y. MAJALA K.n.y. MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -
Je, ni lini matengenezo ya pantoni ya MV. Magogoni iliyopo nje ya Nchi yatakamilika na kurejeshwa nchini ili ianze kutoa huduma kwa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ukarabati wa kivuko MV. Magogoni unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa wezi Desemba 2024 na kurejeshwa nchini ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi, ahsante.
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Kisangara – Nyumba ya Mungu kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kisangara – Nyumba ya Mungu yenye urefu wa kilometa 17.5, inaendelea na inategemewa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu wa 2024. Baada ya Usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi, ahsante. (Makofi)
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami barabara ya Utegi hadi Kilongwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Utegi – Kilongwe yenye urefu wa kilometa 47.4 imekamilika. Kwa sasa taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya barabara hiyo kuanzia Utegi – Shirati itakayokuwa na urefu wa kilometa 27 zinaendelea, ahsante.
MHE. KAVEJURU E. FELIX aliuliza:-
Je, lini barabara inayounganisha Wilaya ya Kigoma Vijijini na Buhigwe itajengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Mahembe, Kinazi hadi Buhigwe?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya kuunganisha Wilaya ya Kigoma na Buhigwe unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hii kuanzia Kalela, Munzeze, Janda hadi Buhigwe imekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hiyo. Aidha, Serikali itaendelea kuifanyia matengenezo barabara hii ili iendelee kupitika majira yote ya mwaka, ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Kigonsera hadi Matiri?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kigonsera – Matiri yenye urefu wa kilometa 25 ni sehemu ya barabara ya mkoa ya Kigonsera – Kilindi – Mbaha yenye urefu wa kilometa 55 inayounganisha barabara kuu ya Songea – Mbinga na mwambao wa Ziwa Nyasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuifungua barabara hii inayoanzia Kigonsera hadi Mbaha ili iweze kupitika majira yote ya mwaka. Hadi sasa jumla ya kilometa 35 zimejengwa kwa kiwango cha changarawe, kilometa 12 zimefunguliwa na jitihada za kufungua sehemu iliyobaki ya kilometa nane zinaendelea. Mara baada ya kazi hii kukamilika, barabara hii itafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya ujenzi kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa Madaraja ya Bujonde na Ilondo Mwaya - Kyela utaanza?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ujenzi wa Daraja la Bujonde linalounganisha Kata ya Kajunjumele na Bujonde. Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imefikia 85% na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2024. Baada ya kazi ya usanifu kukamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu Daraja la Ilondo - Mwaya, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ikiwa ni maandalizi ya kulijenga daraja hili, ahsante.
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Kiberashi hadi Songe Kilindi kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara ya Kiberashi – Songe (Kilindi) – Kwaluguru yenye urefu wa kilometa 127 imeingizwa kwenye Mpango wa Bajeti ya mwaka 2024/2025 kwa ajili ya kufanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina. Kazi hii ikikamilika, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami, ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. TABASAM H. MWAGAO aliuliza:-
Je, lini mradi wa ujenzi wa Feri ya MV Buyagu utakamilika ikizingatiwa kuwa mkataba wa ujenzi umekwisha muda wake Aprili, 2024?
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inajenga kivuko kipya kitakachokuwa kiunganishi muhimu kati ya Wilaya ya Sengerema na Wilaya ya Misungwi kupitia eneo la Buyagu lililoko Sengerema na eneo la Mbalika lililopo Misungwi. Mkataba wa ujenzi wa kivuko hiki ulisainiwa mwezi Aprili, 2023 kati ya Serikali kupitia TEMESA na mkandarasi Songoro Marine Transport Mwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kazi za ujenzi wa kivuko hiki zimepangwa kukamilika mwezi Agosti, 2024 baada ya muda wa awali kuongezwa, ahsante.