Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. David Mwakiposa Kihenzile (69 total)

MHE. SALIM MUSSA OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza kabisa nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali yenye kutia matumaini, lakini nimuulize swali la nyongeza.

Je, haoni kama ipo sababu ya kuweza kuweka kipaumbele au Wizara yake iko tayari kutoa kipaumbele kwa hili jambo ili kuweza kutatuliwa kwa haraka sana, kwa sababu Wapemba wanalaghaiwa na issue hii imekuwa kubwa sana. Sasa hivi ili Wapemba waweze kukupa dua ili uweze kutoboa katika mikeka ijayo?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Salim Mussa Omar kwamba Serikali inafahamu na inatambua uzito mkubwa na umuhimu wa kupeleka ndege hiyo Pemba na ndiyo maana imeshaanza mchakato. Alichokifanya ni kutukumbusha, nasi tutajitahidi kuongeza kasi zaidi ili angalau ndugu zetu Wapemba waweze kusafiri kama inavyotakiwa. (Makofi)
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Waziri, swali la kwanza; kwa kuwa Mheshimiwa Waziri amesema kwamba uko mdaki mmoja utafungwa katika eneo la Azam Sea Link, tunataka kujua, ni lini mdaki huu utakwenda kufungwa ili kuondoa adha kwa wananchi wanaotumia eneo hili?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa vilevile Mheshimiwa Waziri amesema kwenye bajeti ya mwaka huu, wametenga fedha kwa ajili ya kununua midaki mingine. Je, ni midaki mingapi itakwenda kunuliwa kwa ajili ya eneo la Azam Sea Link ili kuendelea kuboresha eneo hili? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza kuhusu lini, ni ndani ya Mwaka huu wa Fedha 2023/2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili kuhusu ni midaki mingapi itajengwa kwenye eneo hili ni kwamba hakuna mpango wa kuongeza kwenye eneo la Azam Link kwa sababu tayari umeshapatikana mmoja na kama kutakuwa na uhitaji tutakwenda kwenye maeneo mengine yenye uhitaji mkubwa.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA : Mheshimiwa Spika, ahsante sana na nashukuru kwa majibu mazuri ila nina maswali mawili.

Je, ni kwa nini Serikali haifanyi utafiti wa suala la bei wa safari za ndege za ndani ya nchi kutokana na bei hizo kuwa kubwa sana, kwa mfano Dodoma - Dar es Salaam 200,000 na zaidi mpaka 500,000 kwa safari ya mara moja?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Serikali haioni hatari ya kupoteza soko la ndani endapo yakajitokeza mashirika mengine yakafanya biashara hii kwa mfano Flight-Link inafanya safari hiyo kwa dola 180 sawa na shilingi 450,000 kwa safari ya kwenda na kurudi Dodoma - Dar es Salaam na ni fixed. Kwa nini hamuoni mfanye bidii ili kuliokoa Shirika la Ndege Tanzania lisije likazama? Kwa nini hamjiongezi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Asha Abdullah Juma kama alivyoeleza.

Mheshimiwa Spika, moja kuhusu tafiti, Shirika letu kwanza, mashirika ya ndege sio moja yako mengi kama alivyosema Mheshimiwa Spika, lakini kwa kuwa amegusia kwenye ATCL specific, ni kwamba tafiti zinafanyika lakini kwa kuwa jukumu la Bunge ni kushauri Serikali tutaongeza pengine utafiti zaidi ili kwenda sambamba na hoja yake.

Mheshimiwa Spika, kuhusu hoja namba mbili ya kwamba je, hatuoni hatari ya kupoteza soko, nadhani ni jambo ambalo pia linazungumzika kupitia utafiti huo ambao tunaenda nao ambao ameusema kama alivyoshauri tutaendelea kujipima, lakini kwa sasa hivi ATCL haijapoteza soko kwa sababu ipo kwenye ushindani na viwango vilivyowekwa ni kwa mujibu wa ushindani kama nilivyosema kwenye jibu la msingi. (Makofi)
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana, nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba tunapata ndege za moja kwa moja kutoka Dodoma kwenda Kilimanjaro na Arusha au muda mfupi wa kuunganisha kwa kupitia Dar es Salaam?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri wa Mheshimiwa Priscus Tarimo kuhusiana na kuanzisha route inayokwenda Kilimanjaro, nafikiri Serikali itakapokuwa tayari basi ataweza kuarifiwa. (Makofi)
MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa niaba ya Serikali nashukuru kwa majibu mazuri, lakini nina swali moja la nyongeza.

Je, Serikali ina mkakati gani wa chuo hichi cha usafirishaji kuongeza wanafunzi wa kigeni? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asya kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Chuo cha Usafirishaji ambacho kiko pale Dar es Salaam kina wanafunzi 14,464 na katika wanafunzi hao asilimia 99.2 ni wanafunzi wa Kitanzania na asilimia 0.8 ni wanafunzi wa nje.

Mheshimiwa Spika, chuo kimeendelea na programu mbalimbali za kuhakikisha kinaongeza wanafunzi wengi kama ambavyo imeulizwa na Mheshimiwa Mbunge ikiwa ni kwa ajili ya kuhakikisha tunaongeza forex, lakini pia kwa ajili ya kuongeza experience kwa wanafunzi wetu.

Mheshimiwa Spika, programu mbalimbali zimefanyika katika chuo hicho ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Balozi zetu za nje kukitangaza chuo chetu kimataifa. Vile vile tumeshiriki katika mikutano mbalimbali mingine imefanyika Nchini Rwanda kwa ajili ya kuongeza na kutangaza chuo chetu.

Mheshimiwa Spika, kama hilo halitoshi, chuo chetu kwa sasa kinaandaa mkutano mkubwa tarehe 18 mpaka tarehe 20 mwezi ujao ambao ni First International Conference on Transport and Logistics and Management ili kuleta wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi kuhakikisha kwamba pengine tunaweza kujitangaza zaidi na kupata wanafunzi wengi zaidi, ahsante.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri yenye kutia moyo. Pia, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nyasa na jirani zao tunapenda kushukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay. Baada ya hapo naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Bandari ya Mbamba Bay itakuwa ni kubwa na ya kisasa na itahitaji mzigo mkubwa kwa ajili ya kuhudumia Tanzania pamoja na nchi za jirani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha sasa reli ya kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay inajengwa ili kuhakikisha kwamba bandari hii inatumika kiukamilifu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Bandari ya Mbamba Bay inategemeana sana mizigo yake na bandari ndogondogo zilizopo Kando ya Ziwa Nyasa. Bandari kama Liuli, Njambe, Lipingu na kule Manda katika Wilaya ya Ludewa. Nini mpango wa Serikali kuboresha bandari hizi ili ziweze kusaidia na kuhakikisha kwamba mizigo yote inachukuliwa vizuri?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali nipokee pongezi za dhati za Mheshimiwa Manyanya kwa sababu ni kwa muda mrefu Wananchi wa Ruvuma na mikoa ya jirani wamekuwa wakitamani kuona bandari hii inafanyiwa uboreshaji na tayari Serikali ya Awamu ya Sita imeshaanza utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake pili anauliza kuhusu bandari ndogondogo kama za Liuli, Njambe na maeneo mengine. Hizi bandari zote zimejumuishwa katika mpango kabambe ambao ni The Updated National Proposed Master Plan 2022/2023 mpaka 2026/2027 ambazo zipo kwenye mpango wa kuboreshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye swali la kwanza ambalo ndio swali kubwa linaulizwa na Wabunge karibu wote wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na Kusini. Kwamba ni lini sasa reli ya SGR ya kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay itaanza kujengwa na pengine reli hii wengine wanakwenda mbele zaidi wanataka kufahamu kuunganisha mpaka Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pengine nieleze kwa ufupi tu kwamba, Serikali inao mpango kwamba inatambua umuhimu na ukubwa wa mradi huu wa SGR ya Southern Corridor ambao ndani yake una miradi zaidi ya sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja reli hii ikijengwa ya kilometa 1,000 kutoka Mtwara kwenda mpaka Mbamba Bay kwenda mpaka Liganga na Mchuchuma utawezesha kusafirisha makaa ya mawe ambapo Mungu ametujalia zaidi ya metric tons milioni 400 na yaligundulika zaidi ya miaka pengine mia moja iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili itatusaidia makaa ya mawe yale yakishatengenezwa yataanza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 600; nusu yake yakayeyushe chuma pale Liganga, nusu yake yaingie kwenye Gridi ya Taifa lakini kama haitoshi meli hii pia inakwenda kutoa ajira na inakwenda kutoa pia chuma ambacho kinakwenda kutengenezea magari na vitu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnafahamu Watanzania kwamba kwa sehemu kubwa zaidi ya asilimia 100 tunaagiza chuma kutoka nje jambo ambalo linachukua fedha zetu nyingi zaidi. Hivyo basi, Serikali kwa kutumbua umuhimu huo mkubwa; moja, imeshaanza kutengeneza uboreshaji mkubwa wa Bandari ya Mtwara ili mzigo upatikane kwa wingi zaidi; lakini pili, inaongeza bandari nyingine ya pili ya kisiwa mgao ili bidhaa chafu zote kwa maana ya makaa ya mawe, simenti na kadhalika ipitie pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ipo kwenye mpango wa kuhuisha stadi iliyofanyika miaka ya nyuma kwa maana ya kutafuta mshauri mwelekezi kuhuisha ile reli ili tuweze kujua mahitaji yake ni yapi. Mara tu baada ya kukamiliisha tunategemea kuanza kuijenga kwa mfumo wa PPP na hatimaye tunaamini likikamilika hili ni moja kati ya mambo ambayo Mheshimiwa Rais wetu anayapigania na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu atakayakamilisha na hivyo kwenda kufufua uchumi wetu kwa kiasi kikubwa zaidi.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ukanda wa Ziwa Tanganyika yaani Mkoa wa Kigoma, Rukwa na Katavi tumesubiri kwa muda mrefu ukarabati wa meli ya MV Liemba. Je, ni lini Serikali itakamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kunusuru usafiri huo?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, Serikali ya awamu ya sita imejipambanua katika kutenda. MV Liemba ni kiungio kubwa la Ziwa Tanganyika na wananchi wote wanaotumia ziwa hilo. Tumekwishasaini mkataba mwaka jana mwezi Novemba na ndani ya mwaka mmoja tutakuwa tumeshakamilisha ukarabati na ili Wananchi wa Kigoma na maeneo jirani wasubiri kwa hamu tunakwenda kukamilisha meli yao.
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kuna agenda ya Mtwara Corridor na tunapozungumza Mtwara Corridor tunazungumza bandari, tunazungumza Airport pia tunazungumza reli ya Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umekuwa ni wimbo toka mwaka 2020 mpaka leo hii Serikali kila ikija hapa wanasema ipo kwenye mpango. Tunataka sasa tufahamu ni lini sasa ujenzi wa reli hii ya Liganga na Mchuchuma.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, nafikiri Mheshimiwa Mtenga anataka kupata pengine ufafanuzi wa ziada. Nimekwishasema na naomba nirejee. Tulishaanza SGR ya kutoka Dar es Salaam kwenda mpaka Isaka, tumekwishaenda na SGR kutoka Dar es Salaam tumekwenda mpaka Kigoma sasa tunakwenda mpaka Msongati Burundi. Awamu inayofuatia Serikali ya Awamu ya Sita imejipambanua na imejiwekea malengo ya kwenda SGR Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe mashaka uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita unakwenda kujenga reli ya SGR ya kusini ambayo ni Mtwara Corridor kama nilivyosema. Hii inakwenda kuungana pamoja na uboreshaji mkubwa wa Airport kama nilivyosema sambamba na uboreshaji mkubwa wa maeneo ambayo nimeyaeleza pale awali, kwa hiyo, nimtoe mashaka Mheshimiwa Mbunge.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kujenga meli kwa ajili ya abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika ili kutatua changamoto ya usafiri katika Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Je, ujenzi huo utatekelezwa lini?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, siyo tu meli ya mizigo na abiria kama alivyouliza Mheshimiwa Mbunge. Serikali imesaini tayari mkataba, tumeanza kujenga kiwanda cha kutengeneza meli nyingi nyingi katika Ziwa Tanganyika. Ambapo kiwanda hicho kitahusika na kutengeneza meli za mizigo na abiria na kukarabati zilizopo, hili linakwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa meli ambazo zipo za akina Mwongozo, Sangala pamoja na kina Liemba kama ilivyoulizwa na Mheshimiwa Sylvia pale awali.
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza niwapongeze Serikali kwa kujenga reli ya kisasa ambayo ya SGR kutoka Makutupora Tabora. Reli ile mpaka sasa hivi wamefukua makaburi ya watu wa Igalula, watu wa Goweko, Tula hamjawalipa mpaka leo. Je, ni lini mtawalipa fedha ambazo mliwarudishia msiba mpaka leo hamjawalipa kwa sababu reli inataka ipite?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, hii hoja ya Mheshimiwa Venant naomba niichukue tuifatilie halafu tuifanyie kazi baada ya kupata taarifa zake za kina.
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bandari ya Tanga ilifanya vizuri sana miaka ya 1980 na sababu kubwa ilikuliwa ni uwepo wa viwanda vingi ambavyo asilimia 90 sasa vimeshakufa. Kwa kuwa, meli kubwa na nyingi haziwezi kwenda mahali ambako zitapeleka tu mzigo bila kuchukua, yaani ile exchange of containers hakuna meli kubwa ambayo itakwenda bila kukutana na hali hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, tunamini kabisa bandari ndiyo uti wa mgongo wa Taifa hili; Je, Wizara hii ya Uchukuzi haioni haja ya kushirikiana kwa karibu na Wizara zingine kuhakikisha kwamba meli kubwa zinakuja kwa kufufua viwanda ambavyo Tanga vimekufa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, Bandari ya Mwambani ilipangwa kuendeshwa kwa ubia lakini kikwazo ilikuwa ni Sheria ya Ubia ambayo sasa imekwishafanyiwa marekebisho. Sasa Serikali itueleze wazi, mpaka sasa imeshachukua hatua gani kuhakikisha mpango ule wa kuendesha Bandari ya Mwambani kwa ubia unatekelezeka?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza sana Mheshimiwa Eng. Mwanaisha kwa kazi yake kubwa anayofanya ya kufuatilia mchakato wa miundombinu katika Mkoa wa Tanga. Serikali imeshaanza kufanya mambo mengi katika eneo hilo, mojawapo ni ukarabati wa hiyo Bandari ya Tanga lakini pia uwepo wa fursa kama bomba la mafuta ni hatua muhimu kwenye kuelekea Tanga kuwa eneo muhimu sana la kiuwekezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza kama je, tuko tayari kushirikiana na Wizara nyingine, ni kweli, tuko tayari kushirikiana na sekta nyingine ikiwemo Wizara ya Viwanda na Biashara kuhakikisha kwamba viwanda vilivyokuwa vimefungwa na vimefanya vizuri miaka ya 1990 na huko nyuma vinafufuliwa ili angalau bandari hiyo iweze kupata mizigo. Mojawapo ya mambo ambayo tunayafanya ni pamoja na kufufua pia uwanja wa ndege wa Tanga ili ndege kubwa na za kati ziweze pengine kuanza kutumia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili ameuliza kuhusu Bandari ya Mwambani, kwenye mpango wetu mkakati wa mwaka 2045 hiyo ni moja kati ya maeneo ambayo tunatazama kwa jicho la karibu zaidi. Kwa sasa hivi, moja tumeshakamilisha mabadiliko ya sheria ya PPP na hivyo tunakaribisha mtu yeyote anayetaka kuja kushirikiana nasi katika kuendeleza bandari hiyo ili kwa pamoja tuweze kuhakikisha kwamba Bandari ya Mwambani inafanya vizuri zaidi. Ahsante. (Makofi)
MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri ambayo yanatia moyo wa kuanza kufufuliwa kwa reli hii muhimu kwa uchumi wa Tanzania. Nina maswali mawili madogo ya nyongeza.

Moja, ningependa kujua ni lini hasa mchakato wote huu utakamilika (timeframe) ili wananchi wa Kilosa lakini Wananchi wa Mikumi na wananchi wa Kilombero wajue ni lini reli hii itaanza kukarabatiwa?

Swali langu la Pili la nyongeza; kwa kuzingatia kwamba Mji wa Kilosa sasa utaunganisha reli tatu, yaani reli ya sasa ya MGR, reli ya SGR na kwa sababu kutoka Kilosa mpaka Kidatu inaanza reli ya TAZARA Kidatu mpaka Mlimba. Maana yake sasa Mji wa Kilosa utaunganisha reli tatu.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuifanya sasa Kilosa kuwa ndiyo logistic hub kubwa katika nchi yetu inayounganisha reli hizi tatu, ukichukua reli ya TAZARA ina uwezo mpaka wa kufika Zimbabwe, Zambia, Afrika ya Kusini na Namibia ili mizigo katika reli hizi iweze kuhamishwa na makontena kwa urahisi katika Mji wa Kilosa ambao sasa una stesheni kubwa mbili ya MGR na SGR na uwezo wa kuungana na reli ya TAZARA. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Profesa kwa sababu swali lake linagusa sehemu kubwa sana ya maeneo ya Mashariki na Kati mwa Tanzania. Kwa kuwa reli hii ilikuwa ni muhimu sana miaka ya nyuma kwa nchi za SADC kuanzia nchi za South Africa mpaka Uganda, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Jemedari Dkt. Samia Suluhu Hassan inao mkakati madhubuti wa kufanyia kazi jambo hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ameuliza ni lini, jibu ni Mwaka huu wa Fedha 2023/2024, tumekwishaanza mchakato wa kimanunuzi na pengine ifikapo mwezi Februari tayari tutakuwa kwenye hatua kubwa zaidi.

Swali la pili anauliza ni upi mkakati wa Serikali wa kuifanya Kilosa kuwa logistic hub, kwa sababu tayari reli ya MGR, SGR na TAZARA zinaungana, kwanza nataka kumhakikishie kupitia SGR na MGR, tutajenga kituo kikubwa cha mizigo katika eneo hilo la Kilosa na tayari tumeshaanza upembuzi yakinifu katika kuhakikisha tunatimiza jambo hilo na hivyo kuifanya Kilosa kuwa ni Logistic hub kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameuliza hapo awali kwenye swali lake la nyongeza.
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa kuna malalamiko kwamba hata kazi ndogo ndogo kama za usafi, kufyeka na ulinzi, mkandarasi anatoa wafanyakazi maeneo ya mbali badala ya maeneo ya Seke, Malampaka na Malya. Je, Serikali inamshauri nini mkandarasi huyu?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kwa kuwa pia kuna malalamiko kwamba mkandarasi ambaye ndiyo mwajiri hapeleki au anapeleka michango kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kusuasua, je Serikali inasemaje juu ya malalmiko haya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mashimba Mashauri Ndaki.

Mheshimiwa Spika, la kwanza, amezungumzia kuhusiana na watu wengi kutoka nje ya eneo la mradi. Moja, nimetoa takwimu ya watu ambao wameajiriwa kutoka kwenye eneo hilo katika Mkoa wake wa Shinyanga.

Pili, nimkumbushe tu Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi huu ni wa Kitaifa. Hata hivyo, Serikali itaendelea kumsimamiwa na kumsisitiza kwamba, anatafuta kwanza wafanyakazi kwenye eneo husika kabla hajepeleka kipaumbele kwenye maeneo mengine ya nje ya eneo husika.

Mheshimiwa Spika, hoja yake pili ni kuhusiana na michango ya NSSF, kwamba pengine mkandarasi anasuasua. Tunafahamu Sheria ya NSSF (The National Social Security Act) Revised ya 2018 Cap. 50, inamtaka mkandarasi au mwajiri kuhakikisha kwamba anapeleka makato hayo NSSF mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba kuna changamoto kubwa sana kwenye upande wa mkandarasi huyu kwa sasa. Tayari tumeshaanza vikao kupitia wenzetu Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa ajili ya kukaa naye na kuweka commitment, mara tu anapolipwa fedha aweze kupeleka michango hiyo kwenye Mifuko ya Hifadhi za Jamii. Pia, aweze kuwalipa na wazabuni mbalimbali wa ndani. (Makofi)

SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, naona umesimama.

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, napenda tu kuongezea kwenye kile kipengele cha mkandarasi kutopeleka michango kwenye Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Mheshimiwa Spika, nakiri kweli kuna madai ambayo mkandarasi anadaiwa na Mfuko umekuwa ukifatilia madai hayo na kuna makubaliano ambayo NSSF imeweka na mkandarasi ambapo tunataka madeni haya yakamilike ndani ya mwaka mmoja.

Mheshimiwa Spika, nimesimama pia kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, kuna utaratibu ambao umewekwa kati ya NSSF na mkandarasi kwa wale ambao wanatakiwa kulipwa mafao yao sasa, kuna utaratibu maalum wa fedha zao kupatikana ili wasiathirike na malipo hayo.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nikuhakikishie kwamba, kama Wizara ambayo tunasimamia mifuko ya hifadhi ya jamii, tutahakikisha kwamba madeni haya tunayafatilia ili haki za wafanyakazi zisipotee. Ahsante sana.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake mazuri yenye kutia moyo. Pia, kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Nyasa na jirani zao tunapenda kushukuru sana na kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay. Baada ya hapo naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Bandari ya Mbamba Bay itakuwa ni kubwa na ya kisasa na itahitaji mzigo mkubwa kwa ajili ya kuhudumia Tanzania pamoja na nchi za jirani. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha sasa reli ya kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay inajengwa ili kuhakikisha kwamba bandari hii inatumika kiukamilifu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa kuwa Bandari ya Mbamba Bay inategemeana sana mizigo yake na bandari ndogondogo zilizopo Kando ya Ziwa Nyasa. Bandari kama Liuli, Njambe, Lipingu na kule Manda katika Wilaya ya Ludewa. Nini mpango wa Serikali kuboresha bandari hizi ili ziweze kusaidia na kuhakikisha kwamba mizigo yote inachukuliwa vizuri?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali nipokee pongezi za dhati za Mheshimiwa Manyanya kwa sababu ni kwa muda mrefu Wananchi wa Ruvuma na mikoa ya jirani wamekuwa wakitamani kuona bandari hii inafanyiwa uboreshaji na tayari Serikali ya Awamu ya Sita imeshaanza utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake pili anauliza kuhusu bandari ndogondogo kama za Liuli, Njambe na maeneo mengine. Hizi bandari zote zimejumuishwa katika mpango kabambe ambao ni The Updated National Proposed Master Plan 2022/2023 mpaka 2026/2027 ambazo zipo kwenye mpango wa kuboreshwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nikija kwenye swali la kwanza ambalo ndio swali kubwa linaulizwa na Wabunge karibu wote wa Nyanda za Juu Kusini pamoja na Kusini. Kwamba ni lini sasa reli ya SGR ya kutoka Mtwara mpaka Mbamba Bay itaanza kujengwa na pengine reli hii wengine wanakwenda mbele zaidi wanataka kufahamu kuunganisha mpaka Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pengine nieleze kwa ufupi tu kwamba, Serikali inao mpango kwamba inatambua umuhimu na ukubwa wa mradi huu wa SGR ya Southern Corridor ambao ndani yake una miradi zaidi ya sita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja reli hii ikijengwa ya kilometa 1,000 kutoka Mtwara kwenda mpaka Mbamba Bay kwenda mpaka Liganga na Mchuchuma utawezesha kusafirisha makaa ya mawe ambapo Mungu ametujalia zaidi ya metric tons milioni 400 na yaligundulika zaidi ya miaka pengine mia moja iliyopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili itatusaidia makaa ya mawe yale yakishatengenezwa yataanza kuzalisha umeme zaidi ya megawati 600; nusu yake yakayeyushe chuma pale Liganga, nusu yake yaingie kwenye Gridi ya Taifa lakini kama haitoshi meli hii pia inakwenda kutoa ajira na inakwenda kutoa pia chuma ambacho kinakwenda kutengenezea magari na vitu mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninyi mnafahamu Watanzania kwamba kwa sehemu kubwa zaidi ya asilimia 100 tunaagiza chuma kutoka nje jambo ambalo linachukua fedha zetu nyingi zaidi. Hivyo basi, Serikali kwa kutumbua umuhimu huo mkubwa; moja, imeshaanza kutengeneza uboreshaji mkubwa wa Bandari ya Mtwara ili mzigo upatikane kwa wingi zaidi; lakini pili, inaongeza bandari nyingine ya pili ya kisiwa mgao ili bidhaa chafu zote kwa maana ya makaa ya mawe, simenti na kadhalika ipitie pale.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu ipo kwenye mpango wa kuhuisha stadi iliyofanyika miaka ya nyuma kwa maana ya kutafuta mshauri mwelekezi kuhuisha ile reli ili tuweze kujua mahitaji yake ni yapi. Mara tu baada ya kukamiliisha tunategemea kuanza kuijenga kwa mfumo wa PPP na hatimaye tunaamini likikamilika hili ni moja kati ya mambo ambayo Mheshimiwa Rais wetu anayapigania na kwa msaada wa Mwenyezi Mungu atakayakamilisha na hivyo kwenda kufufua uchumi wetu kwa kiasi kikubwa zaidi.
MHE. SYLVIA F. SIGULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, ukanda wa Ziwa Tanganyika yaani Mkoa wa Kigoma, Rukwa na Katavi tumesubiri kwa muda mrefu ukarabati wa meli ya MV Liemba. Je, ni lini Serikali itakamilisha ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kunusuru usafiri huo?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, Serikali ya awamu ya sita imejipambanua katika kutenda. MV Liemba ni kiungio kubwa la Ziwa Tanganyika na wananchi wote wanaotumia ziwa hilo. Tumekwishasaini mkataba mwaka jana mwezi Novemba na ndani ya mwaka mmoja tutakuwa tumeshakamilisha ukarabati na ili Wananchi wa Kigoma na maeneo jirani wasubiri kwa hamu tunakwenda kukamilisha meli yao.
MHE. HASSAN S. MTENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa kuna agenda ya Mtwara Corridor na tunapozungumza Mtwara Corridor tunazungumza bandari, tunazungumza Airport pia tunazungumza reli ya Liganga na Mchuchuma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, umekuwa ni wimbo toka mwaka 2020 mpaka leo hii Serikali kila ikija hapa wanasema ipo kwenye mpango. Tunataka sasa tufahamu ni lini sasa ujenzi wa reli hii ya Liganga na Mchuchuma.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, nafikiri Mheshimiwa Mtenga anataka kupata pengine ufafanuzi wa ziada. Nimekwishasema na naomba nirejee. Tulishaanza SGR ya kutoka Dar es Salaam kwenda mpaka Isaka, tumekwishaenda na SGR kutoka Dar es Salaam tumekwenda mpaka Kigoma sasa tunakwenda mpaka Msongati Burundi. Awamu inayofuatia Serikali ya Awamu ya Sita imejipambanua na imejiwekea malengo ya kwenda SGR Kusini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtoe mashaka uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita unakwenda kujenga reli ya SGR ya kusini ambayo ni Mtwara Corridor kama nilivyosema. Hii inakwenda kuungana pamoja na uboreshaji mkubwa wa Airport kama nilivyosema sambamba na uboreshaji mkubwa wa maeneo ambayo nimeyaeleza pale awali, kwa hiyo, nimtoe mashaka Mheshimiwa Mbunge.
MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Serikali imekuwa ikitoa ahadi ya kujenga meli kwa ajili ya abiria na mizigo katika Ziwa Tanganyika ili kutatua changamoto ya usafiri katika Mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Je, ujenzi huo utatekelezwa lini?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, siyo tu meli ya mizigo na abiria kama alivyouliza Mheshimiwa Mbunge. Serikali imesaini tayari mkataba, tumeanza kujenga kiwanda cha kutengeneza meli nyingi nyingi katika Ziwa Tanganyika. Ambapo kiwanda hicho kitahusika na kutengeneza meli za mizigo na abiria na kukarabati zilizopo, hili linakwenda sambamba na uboreshaji mkubwa wa meli ambazo zipo za akina Mwongozo, Sangala pamoja na kina Liemba kama ilivyoulizwa na Mheshimiwa Sylvia pale awali.
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwanza niwapongeze Serikali kwa kujenga reli ya kisasa ambayo ya SGR kutoka Makutupora Tabora. Reli ile mpaka sasa hivi wamefukua makaburi ya watu wa Igalula, watu wa Goweko, Tula hamjawalipa mpaka leo. Je, ni lini mtawalipa fedha ambazo mliwarudishia msiba mpaka leo hamjawalipa kwa sababu reli inataka ipite?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimwa Mwenyekiti, hii hoja ya Mheshimiwa Venant naomba niichukue tuifatilie halafu tuifanyie kazi baada ya kupata taarifa zake za kina.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali na nina maswali mawili ya nyongeza. Mchakato wa uboreshaji na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege Kilwa Masoko ni wa muda mrefu sasa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; nataka Mheshimiwa Naibu Waziri, awahakikishie Watanzania, Wanakilwa na Bunge hili, je, mpango wa Serikali wa uboreshaji na upanuzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kilwa Masoko bado uko pale pale?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri amefika Kilwa Masoko mara kadhaa. Alifika mwezi Juni akiwa Mwenyekiti wa Kamati na akafika mwezi Agosti akiwa Naibu Waziri katika Sekta hii ya Uchukuzi na alikuja mahususi kwa ajili ya masuala haya ya kiwanja cha ndege.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale kuna changamoto kadhaa, kwa wananchi wangu hawa 438 mpaka sasa bado hawajalipwa fidia. Je, yuko tayari sasa baada ya Bunge hili kwenda Kilwa Masoko akiambatana nami ili kwenda kusikiliza kero za hawa wananchi wangu 438?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. DAVID M. KIHENZILE): Mheshimiwa Naibu Spika, nataka nimpe uhakika Mheshimiwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita inayo dhamira ya dhati ya kuboresha Uwanja wa Ndege wa Kilwa Masoko. Pia, hiyo inakwenda sambamba na uwekezaji mkubwa unaofanyika pale wa kujenga bandari kubwa kwa ajili ya uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namhakikishia kwamba mpango wa Serikali uko pale pale, mara baada ya wenzetu wa Wizara ya Fedha kukamilisha taratibu za ndani, fidia hiyo kwa wananchi hao itaanza kulipwa. Hilo moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili anauliza je, niko tayari kuambatana naye baada ya kumaliza Bunge hili. Amekiri mwenyewe nilikwenda pale pamoja na wenzangu nikiwa Mwenyekiti wa Kamati Kilimo na Mifugo. Vile vile, nimekwenda hapo juzi kukagua bandari hiyo na uwanja huo. Niko tayari kwenda pamoja naye ili tukawape uhakika wananchi hao ambao wanamwamini Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ili waendelee kujenga imani naye.
MHE. RAMADHAN SULEIMAN RAMADHAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri amekiri mwenyewe kwamba, upembuzi yakinifu utakamilika Desemba, je, ni lini ujenzi utaanza rasmi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; je, ujenzi huo utazingatia kwa kiasi gani kuweka vifaa vya kisasa ili abiria wasikaguliwe na mbwa kama inavyofanyika sasa?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. DAVID M. KIHENZILE): Mheshimiwa Naibu Spika, nipende kumhakikishia Mheshimiwa Ramadhan Suleiman Ramadhan kama nilivyosema hapo awali. Hatua ya kwanza ambayo Serikali inafanya ni kufanya uthamini au upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambao utaweza kutusaidia kujua nini kinapaswa kufanyika. Pia, mara baada ya kukamilisha hatua hiyo, hatua itakayofuatia itakuwa ni kuanza kufikiria au kuanza mchakato kwa ajili ya ujenzi. Kwa sababu, Serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa sana kwenye bandari zetu nchini ikiongozwa na Bandari yetu kubwa ya pale Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, namba mbili; kama nilivyojibu swali la kwanza, katika usanifu huu unaoendelea kwa ajili ya ghati letu jipya la Dar es Salaam, utaambatana pamoja na ufungaji wa mashine ya ukaguzi wa kisasa ambao utatumia teknolojia ya kisasa ya ukaguzi kwa ajili ya abiria na mizigo.
MHE. AMINA ALI MZEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali. Naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha Sheria za Utumishi zinaendana na mradi wa reli?

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali inatuhakikishiaje vijana wengi wanaendelea kupata ajira nchini? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara ya Uchukuzi na Serikali kwa ujumla itaendelea kusisitiza na kusimamia sheria zote zilizowekwa kama nilivyotaja pale awali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kama nilivyoeleza, tunatambua na kuthamini ujuzi mkubwa walioupata vijana katika ujenzi wa reli inayoendelea. Pengine nitumie nafasi hii pia kulitaarifu Bunge lako Tukufu kwamba Taifa letu linaweza kuwa miongoni mwa mataifa ya awali ambayo yatakuwa na vijana wengi wenye uwezo mkubwa wa kujenga reli. Kwa sababu kama unavyofahamu, katika takribani kilometa 72,000 za reli iliyojengwa barani Afrika, zaidi ya nusu inajengwa Tanzania. Hivyo tunakwenda kuwa na manpower kubwa ya vijana wenye uwezo, uzoefu na ustadi mkubwa. Hivyo uzoefu na uwezo huo tutauthamini na kuhakikisha tunautumia ndani ya nchi yetu na hata wakati mwingine kuwa-recommend kwenye maeneo ya nje ya nchi yetu.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka jana, 2023, inaonesha dhahiri kwamba ni zaidi ya vijana 1,800,000 kila mwaka wanaingia kwenye soko la ajira. Je, Serikali ina mkakati gani mahususi inayoweza kuonekana ya kuweza kuhakikisha kwamba hao vijana wanaendelea kupata ajira?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa ajira kwa vijana na imefanya mambo mengi. Ajira mbalimbali zimeendelea kutangazwa Serikalini, kwenye taasisi zake na kadhalika, hiyo ni moja. Pili, tumeendelea kuvutia uwekezaji mkubwa kwenye Taifa letu. Katika kipindi kifupi kilichopita, wawekezaji wameongezeka zaidi na miradi imefunguliwa. Tatu, miradi yetu, kwa mfano ya sekta hii kama nilivyoeleza, kwa upande wa reli kuanzia Dar es Salaam mpaka Isaka, kutoka Tabora mpaka Kigoma na Kigoma mpaka Msongati, pia tunakwenda kujenga reli inayotoka Mtwara mpaka Mbamba Bay, Liganga na Mchuchuma, kote huko tunaenda kuajiri vijana wa Kitanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba tunapunguza gap la ajira nchini.
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa inaonekana katika hizo sheria alizosema za LATRA, watu wa bajaji na bodaboda hawamo kwenye hizo sheria, je, ni lini Serikali itatunga sheria za kuwalinda watu wa bodaboda na bajaji?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Katika nchi yetu tuna uhaba mkubwa sana wa ajira na hasa kwa vijana wetu wote wa darasa la saba, certificate, diploma mpaka degree, wote wamejiajiri kwenye bajaji na bodaboda, lakini kuna kodi nyingi sana katika sekta hii, na hasa kodi ya TRA na kodi ya parking; ni lini Serikali itafikiria namna ya kuwaondolea kodi ya TRA ambayo ni shilingi 120,000/= na kodi ya parking?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tupokee kama ushauri maswali mawili ya Mheshimiwa Mwita Getere, anamezungumzia kuhusu pengine kuboresha na kutazama sheria zetu ikiwa ni sambamba na suala la kodi ambayo kwa maelezo yake inawakwamisha vijana wetu. Tumepokea kama ushauri, tutapitia mchakato wa kawaida halafu tutaweza kufanyia kazi kulingana na uhitaji wa wakati huu.
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Moja ya nchi ambazo zimefanikiwa sana katika usimamizi wa biashara ya bodaboda ni nchi ya Rwanda. Je, Serikali ipo tayari kuwatuma maafisa wake kwenda kujifunza ni namna gani biashara hii inaweza ikadhibitiwa vizuri ili wananchi wangu pale Kinondoni waweze wakafaidika na utaratibu huo mpya? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ametoa ushauri mzuri, lakini pia huwa napenda kuwakumbusha Waheshimiwa Wabunge na viongozi, tunapofanya comparison ni vizuri tukatazama pia na mazingira halisi. Ukiangalia ukubwa wa nchi ya Rwanda ni takribani square meter 27,000, wakati Tanzania ina 904,500. Jiji la Dar es Salaam ni kubwa zaidi, lakini hata hivyo tunapokea ushauri wake, tunajifunza tuone wenzetu wamefanyaje? Ahsante sana. (Makofi)
MHE. JANETH E. MAHAWANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Nini kauli ya Serikali kuhusu usalama wa usafiri wa bodaboda kupakia abiria zaidi ya mmoja tena bila kuvaa helment?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatoa kauli wasafiri wote wa vyombo vya moto nchini, iwe bodaboda, iwe bajaji, na kadhalika, kuzingatia sheria pamoja na usalama kwa ajili yao wenyewe ikiwa ni sambamba na abiria wanaowabeba. (Makofi)
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nipate faraja kidogo kwa majibu ya Serikali kwamba hatua iliyofikiwa sasa hivi ni kwamba tayari daftari lipo kwa Mthamini Mkuu Hazina kwa maana ya Wizara ya Fedha. Wananchi hawa wamekuwa wakiathirika kwa muda mrefu tangu 2013 walikuwa ni 144, ukafanyika tena uthamini 2023 wakafikia wananchi 438. Hivi tunavyozungumza wananchi wangu hawa 438, hawana makazi kutokana na kushindwa kuziendeleza nyumba zao kwa kusubiri taratibu za Serikali. Hali ni tete kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; kutokana na ukweli kwamba tumeshakaa na Mheshimiwa Waziri pamoja na Wizara ya Fedha na kukubaliana kwamba, wananchi hao walipwe haraka iwezekanavyo. Je, ni nini kauli ya Serikali kulipa wananchi hawa fidia ndani ya kipindi kifupi kijacho kabla hawajaendelea kuathirika? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; Uwanja wa Ndege wa Kilwa Masoko ni moingoni mwa viwanja 12 ambavyo tuliviingiza katika mpango wa miaka mitano wa kuboresha na kupanua. Faraja tuliyonayo pale Kilwa Masoko tunajenga Bandari ya Uvuvi. Kufuatia ujenzi wa Bandari ya Uvuvi, umuhimu mkubwa wa kuimarisha kiwanja hiki upo na uhitaji mkubwa utahitajika huko mbele ya safari. Je, ni lini sasa Serikali baada ya kulipa wananchi wangu ndani ya muda mfupi, itaanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege Kilwa Masoko? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Ally Kassinge kwa ufuatiliaji makini wa Kiwanja hiki cha Ndege. Serikali inatambua umuhimu mkubwa wa Kiwanja cha Ndege cha Kilwa Masoko. Moja, ameeleza vizuri sana, Serikali imewekeza bilioni 268 kwa ajili ya ujenzi wa bandari kubwa katika Ukanda wetu wa East Africa, Bandari ya Uvuvi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia tunao Mradi mkubwa sana wa Gesi wa Mkoa wa Lindi. Hivyo, kiwanja hiki ni muhimu sana siyo tu kwa wananchi wa Lindi na ukanda huo, lakini kwa Taifa letu. Hivyo nimhakikishie Mbunge kwamba, Serikali kauli yake imeshafanya uthamini hatua ya kwanza na ya pili na mpaka wamefika wananchi karibu 454 ambao tunategemea kuwalipa karibu 6,200,000,000. Naomba Mbunge apokee kauli ya Serikali ninayoenda kuitamka sasa. Serikali italipa fidia wananchi hao, mara tu itakapokamilisha hatua za ndani na itaanza hatua za ujenzi mara moja.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri mwenye pesa kasimama.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Naomba nimpongeze sana Mheshimiwa Naibu Waziri mwenzangu kwa majibu yake mazuri, pia nimpongeze sana muuliza swali. Muuliza swali amehusisha Wizara ya Fedha. Ni kweli suala hili tunalitambua na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi wake kule Kilwa, wawe na amani kabisa fedha hiyo italipwa kwa wakati. (Makofi)
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, na pia napongeza kwa majibu haya ya Serikali. Naomba kupata ufafanuzi kwa maswali mawili. Moja, nilitaka kujua kwa sababu uchumi wa watu wa kwenye ukanda huu wa bahari hususan Pemba, Unguja, Tanga, Mtwara na Lindi wanategemea sana upatikanaji wa usafiri wa baharini. Ni lini fedha hizi zitapatikana ili kwenda kufanikisha upatikanaji wa Meli hiyo?

Mheshimiwa Naibu Spika, mbili; kwa kuwa Ilani ya CCM inahimiza zaidi kwenye ushirikiano baina ya taasisi ambazo siyo za Muungano, ni maeneo yapi ya ushirikiano ambayo Kampuni hii ya Meli ya Tanzania inashirikiana na Shirika la Meli la Zanzibar? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Bakar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kuhusu ni lini mchakato utakamilika wa upembuzi yakinifu, tumeshaingiza kwenye bajeti katika mwaka huu wa fedha 2023/2024. Tunategemea kabla hatujakamilisha mwaka huu, tutakuwa tumeshakamilisha upembuzi yakinifu kwa kujua lini, kiasi gani, na kwa namna gani pengine inapaswa ifanyike?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ameuliza swali kuhusu ushirikiano kati ya Kampuni ya Meli ya Tanzania (ATCL) pamoja na ile ya SHIPCO (Shirika la Meli la Zanzibar). Tumeshaanza katika hatua za awali ushirikiano kati ya pande hizi mbili na yapo maeneo makuu matatu ambayo tunaweza kuyatazama katika hatua za kuanzia. Moja, tunaangalia ushirikiano katika taarifa na wataalam; pili, tunaangalia uwezo na kuwajengea uwezo wataalam wetu katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na mabaharia, TEHAMA, mipango, utafiti, rasilimali watu pamoja na masoko; tatu, tutaongeza zaidi kwenye eneo la kubadilishana uzoefu katika pande zote mbili.
MHE. JOSEPHAT. S. KANDEGE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya kutia matumaini kutoka Serikalini, naomba niulize maswali mawili kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, juu ya efficiency ya TAZARA ni suala ambalo hatuna ubishani kama Taifa na hasa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, juu ya ufanyaji kazi bora wa TAZARA. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba ukarabati unafanyika na mtaji unawekwa ili TAZARA iweze kufanya kazi kwa jinsi ambavyo tunatarajia? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kwa kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa na hivi tunavyoongea tayari imeshafanya upanuzi katika Bandari ya Kasanga, na lami imeshajengwa mpaka kufika Kasanga, je, Serikali haioni kwamba ni wakati muafaka wa kuishirikisha sekta binafsi ili kuhakikisha kwamba kutoka Kasanga kwenda DRC na kui- decongest Bandari ya Dar es Salaam; na bahati nzuri Mheshimiwa Naibu Waziri anajua tuna makubaliano mazuri na DRC, ni wakati muafaka wa kufanya extension ili tuweze ku-decongest bandari yetu?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, TAZARA ni reli muhimu kwa uchumi wa Taifa letu. Sisi sote tunafahamu tangu ilipoanza kujengwa na kuanza kutumika mwaka 1976 kwa Sheria ya Bunge Na. 23 ya mwaka 1975 yenye urefu wa kilometa 1,860. Pia, sisi Watanzania tuna faida kubwa zaidi kwa sababu asilimia 52 ya reli hiyo ambayo ni 975 iko Tanzania na wenzetu ni 885.

Mheshimiwa Spika, ilipokuwa inatengenezwa wakati huo, ilikuwa imelenga kubeba mzigo wa tani milioni tano, lakini karibu miaka yote hiyo, hatukuwahi kufikia ufanisi huu, ni miaka michache tulifikia asilimia 24. Mamlaka za nchi kwa maana ya Tanzania, Zambia pamoja na wenzetu Wachina, baada ya kuitazama reli hii ndefu kabisa barani Afrika ambayo ina madaraja karibu 318, ina mahandaki karibia 22 na makaravati karibu 2,229, wakasema ipo haja ya kuanza kuitafakari upya.

Mheshimiwa Spika, hii inakwenda sambamba na uboreshaji mkubwa tunaoufanya pale bandarini. Tayari Rais wetu na Marais hawa wawili wako kwenye mazungumzo. Tunategemea ukarabati mkubwa sana kwenye miundombinu pamoja na vitendea kazi unaweza ukaanza kufanywa mwaka huu 2024 ili kuiboresha bandari hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwenye hoja ya pili aliyoisema ya PPP, tunatambua ni hoja yake ya muda mrefu Mheshimiwa Mbunge, anajenga hoja kwamba kutoka Kaprimposhi mpaka kule Lubumbashi ni Kilometa 1,000 wakati kutoka kutoka pale Kasanga - Mlilo ukivuka ng’ambo ni kilometa 400.

Mheshimiwa Spika, tumepokea ushauri wake, tutaufikisha Serikalini ili tuuchakate kama tunavyochakata mambo mengine ili tuone namna gani tunakwenda kuutekeleza, ahsante.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Ni lini Serikali itajenga reli kutoka Bandari ya Mtwara kuja Tunduru – Namtumbo - Songea, pale Matomondo - Mbinga mpaka Mbamba Bay? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, tayari tuko kwenye hatua ya kuhuisha design hiyo ya southern corridor kwa maana ya kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay mpaka Liganga na Mchuchuma. Itakapokuwa tayari, nafikiri Serikali itaanza kutekeleza mara moja.
MHE. ORAN M. NJEZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kupewa nafasi. Kwa kuwa kuna ushindani mkubwa wa Lobito Corridor, je, Serikali ina mkakati gani wa haraka kuhakikisha miundombinu ya TAZARA inakuwa katika kiwango cha SGR?

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, katika majibu ya nyongeza nimezungumza mpango wa Serikali wa kuiboresha vizuri sana TAZARA, ambapo tayari viongozi wetu wameshaanza mazungumzo na yatakapokuwa tayari tutaanza kuyatekeleza mwaka huu wa 2024.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Ni kwa muda mrefu sasa Serikali imekuwa ikiahidi ujenzi wa Reli kutoka Tanga – Arusha – Loliondo – Mugumu hadi Musoma, lakini ni miaka sasa imepita. Napenda kujua nini kauli ya Serikali kuhusiana na ujenzi wa hiyo reli?

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Mbunge hoja hii aliyoizungumza ya Tanga – Arusha na Musoma baada ya hapa tupate muda wa kuijadili halafu tuweze kupata majibu kamili.
MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, inasemekana kwamba Kampuni inayomilikiwa na Serikali ya Uchina imeshatoa pendekezo la ukarabati wa reli husika kwa thamani ya shilingi trilioni 2.5 na majadiliano yalianza na Serikali ya Zambia kupitia Waziri mwenye dhamana kama wewe. Hiyo imekuwa reported na gazeti la Citizen la tarehe 10 Februari, 2024. Serikali mnatuambiaje kuhusiana na hili? Hayo unayoyasema ndiyo kampuni inayomilikiwa na Serikali ya China?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, mazungumzo yanaendelea na kwa kuwa hatujafika hatua ya mwisho, itakuwa ni mapema sana kuanza kuzungumzia gharama na hatua tuliyofikia. Namuomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira, yakishakamilika taarifa hizi ni za wazi, basi ataweza kufahamu pengine ni mkandarasi gani anayefanya kazi hiyo.

SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri kwa sababu swali hili limekuwa likijirejea mara kwa mara na hili swali alilouliza Mheshimiwa Msongozi na umejibu hapa kwamba 2024 nafikiri ulikusudia kusema 2024/2025. Sasa ni muhimu ili 2024/2025 linahusu hii ya TAZARA au inahusu ile ya Mheshimiwa Jacqueline aliyouliza ile ya kuanzia Mtwara mpaka Mbamba Bay. Hii 2024/2025 inahusu ipi kati ya hizi mbili?

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, mwaka huu 2024 nilichokizungumzia ni uboreshaji wa Bandari ya TAZARA kutoka Dar es salaam mpaka Kapirimposhi kilomita 1860 hii Reli ya TAZARA kutoka Dar es salaam mpaka Kapirimposhi huu ndio uboreshaji tunaozungumza kwamba mazungumzo yanaendelea kati ya nchi hizi tatu na tunategemea mwaka huu pengine tuanze utekelezaji wake.

SPIKA: Sawa umerejea tena 2024, ukisema 2024 maana yake ni mwaka huu wa fedha ule unaokuja unaitwa 2024/2025 wewe unakusudia kusema upi 2023/2024 au 2024/2025?

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nilikusudia kusema kwa maana kuanzia Januari hii mpaka Desemba hapa katikati tutakuwa tumefikia hatua nzuri ya utekelezaji.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri juu ya mradi huu wa ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi huko Mbamba Bay. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu kwa Serikali, kwa kuwa mmeamua ku-engage private partnership kushiriki katika mradi huu, mimi nawapongeza sana na naiomba Serikali iongeze jitihada ili reli hii iweze kufunguliwa na iwe mkombozi kwa wananchi wa Kusini hasa usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka Liganga, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mhata kwa kutoa pongezi, wachache sana wakitendewa mambo mema wanasimama na kushukuru. Kwa hiyo nakushukuru sana Mheshimiwa Mhata kwa kuwa na moyo wa shukrani ambao utazidishiwa yaliyo mema zaidi. (Makofi)
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza baadhi ya mabehewa kuweka mfumo wa ubaridi (cold room) katika reli ya TAZARA ili tuweze kusafirisha parachichi zetu na mazao ya mboga mboga yamfikie mlaji wa mwisho yakiwa na ubora? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Mgaya kwa sababu ni mdau mkubwa sana wa reli ya TAZARA na tukubali ukweli kwamba kwa sasa katika reli yetu na mabehewa yaliyopo hatuna cold rooms, lakini kila mtu anafahamu umuhimu wa ukuwaji wa sekta ya parachichi katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu mkubwa Wizara tunapokea ushauri huu na tunapokwenda kwenye hatua ya pili ya maboresho makubwa ya reli yetu kutoka Dar es Salaam mpaka Kapiri Mposhi tutaona namna ya kuweza kuweka hicho alichokizungumza cha cold room.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali imeboresha miundombinu ya Bandari ya Tanga kiasi kwamba shehena zimeongezeka, lakini reli ya kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na kutoka Tanga kwenda Arusha bado ni chakavu sana, je, kuna mpango wowote wa kuboresha reli hii ili sasa shehena hii iweze kutoka kwa urahisi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Shangazi, Mbunge wa Mlalo na Katibu wa Bunge la CCM kwa swali lake kubwa na zuri la maslahi ya watu wa Tanzania na watu wa Kaskazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inao mpango mzuri na kabambe kwa sababu inatambua umuhimu wa upande wa Kaskazini kwanza kwenye utalii, kilimo pamoja na sekta nyingine, hivyo katika mwaka wa fedha 2023/2024 tumeshafanya kazi kubwa, tulishasaini mkataba wa kununua materials za kukarabati reli inayotoka Tanga kuelekea mpaka Arusha kilometa 533.

Kwa hiyo, mara baada ya kusaini mkataba huo katika mwaka wa fedha huu unaofuatia tunakwenda kuanza kutoa reli iliyokuwepo, tunataka tuweke reli nzito ambayo itakuwa na capacity ya ratilika 80 kwa yard, iliyokuwepo ilikuwa 45 kwa yard.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii reli iliyopo sasa hivi speed inayokwenda treni ni karibu speed ya 15 - 20 kwa saa moja, hivyo inawachukuwa muda mrefu sana kufika kwenye destination inayotakiwa. Tukifanya maboresho haya speed itaongezeka mpaka 75, kwa hiyo muda kama ilikuwa ni saa 12 tutakuwa tunatumia saa karibu nne. Kwa hiyo, habari njema hii kwa watu wa Kaskazini, Tanga na Watanzania kwa ujumla juu ya maboresho makubwa ya reli ya Kaskazini. (Makofi)
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Uchukuzi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Mlimba usafiri wa reli ya TAZARA ndiyo usafiri unaotegemewa, sasa lini mpango wa Serikali katika kuboresha reli hii ikiendana sambamba na kuongeza mabehewa na route za safari ya reli hii kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya TAZARA kama inavyofahamika ilijengwa miaka 1975 baina ya Serikali tatu, China, Tanzania na Zambia na kipindi chote hicho designed capacity ilikuwa ni metric tons milioni tano, lakini kutokana na ubovu wa miundombinu hatukufikia lengo. Habari njema kutoka kwa daktari wa maendeleo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania amefanya kikao na Waziri wa Zambia pamoja na Rais wa China, hivi ninavyozungumza tupo kwenye hatua za mwisho za majadiliano, reli nzima inakwenda kufumuliwa upya. Moja, kuongeza uwezo wa reli wa kubeba mzigo, lakini pili tutaongeza mabehewa pamoja na vichwa vya kutosha ya mizigo na abiria. Kwa hiyo, Wana-Mlimba na watumiaji wote wa reli hii inayotoka Dar es Salaam mpaka Kapiri Mposhi kilometa 1,860 waendelee kusubiri habari hii njema ambayo inakuja kwa Watanzania wote. (Makofi)
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali. Napenda kuiuliza Serikali, ni sababu zipi ambazo zimefanya wabadili uamuzi wa awali ambapo ilikuwa wanatoa eneo la meta 700 kutoka kwenye njia ya kurukia ndege na sasa wanachukua eneo lote mpaka nje ya milima upande wa pili ambapo hapahitajiki kwa upanuzi wa Uwanja wa Ndege? Hilo ni swali la kwanza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, naishukuru pia Serikali kwamba zoezi la uthamini limeanza na lilipangwa kufanyika kwa siku 55, mpaka sasa hivi siku 38 zimekamilika, ni mitaa miwili tu ambayo imefikiwa ambayo ni Mtaa wa Bulyanhulu na Shibula bado mitaa mitatu; mtaa wa Kihili, Monze na Nyamwilolelwa. Je, ni lini kazi hiyo itakamilika kwa mitaa yote mitano ili wananchi waweze kupata haki yao?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na eneo ambalo awali lilikuwa limepangwa, lakini baada ya tathmini ya kina na tukiangalia kwamba Serikali ina mpango mkubwa wa kufanya Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuwa wa Kimataifa, vipo vigezo mbalimbali, kimojawapo ni usalama. Tathmini ya kiusalama ilipofanyika, ilidhihirika kwamba ni muhimu na ni lazima wananchi wa eneo lote lile wapishe ili tuweze kuwa na uwanja ambao siyo tu ni mkubwa, lakini pia unakidhi takwa la kisheria pamoja na la ukubwa kwa maana ya kiusalama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, kuhusiana na muda. Pendekezo la Mkoa kupitia Mkuu wa Mkoa la kuwatoa wananchi katika eneo lile kwa sababu za kiusalama lilipokamilika lilibidi liwasilishwe Serikalini na baada ya kupata idhini, tayari uongozi wa Mkoa pamoja na Kamishna wa Ardhi wa Mkoa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wameshaanza mchakato kwa ajili ya uthamini. Mara tu tutakapokamilisha, tutaanza zoezi la kulipa.
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeshaanza mchakato wa kuwalipa fidia wananchi wanaopisha upanuzi wa uwanja wa Moshi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, wale wanaostahili tumeshaanza kuwalipa na wengine tumeshawalipa, lakini kuna wananchi waliovamia ambao hawatastahili kulipwa katika eneo hilo.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Fidia imekuwa ikicheleweshwa sana kwa muda mrefu kwa hawa wanaopisha upanuzi wa viwanja na mmekuwa mkiahidi mtalipa riba, mfano pale Uwanja wa Manyara - Karatu. Je, ni lini mtalipa hizo riba? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, malipo ya fidia katika viwanja vyote nchini ikiwemo Kiwanja cha Manyara yatalipwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za ulipaji fidia Serikalini.
MHE. MARTHA N. GWAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza: Je, ni lini Serikali italipa fidia kwa wananchi waliopisha maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa SGR, ambao ni wananchi wa Halmashauri ya Itigi na wananchi wa Halmashauri ya Manyoni?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili: Ni lini Serikali italipa Service Levy kutokana na ujenzi wa reli ya SGR kwa hizi Halmashauri ambazo zimepitiwa na reli hii; Halmashauri ya Itigi na Halmashauri ya Manyoni? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia malipo hayo, nataka nimjulishe kwamba mfumo wa utoaji wa ardhi katika eneo hilo umekuwa ukienda sambamba na kulipa fidia. Maeneo ambayo hayajalipwa fidia kwa sasa ni yale maeneo ambayo tuna uchimbaji wa malighafi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na Tambukareli, Centre pamoja na Milembela. Maeneo hayo yataendelea kulipwa kulingana na hatua za uthamini zitakapokamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili kuhusiana na Service Levy kwa Halmashauri zote mbili kwa maana ya Itigi pamoja na hiyo nyingine ya Manyoni, tulifanya vikao mwaka jana, 2021 kati ya TRC pamoja na Halmashauri zote mbili, namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake baada ya kukubaliana ikaonekana kwamba pengine inatakiwa waanze kulipwa shilingi 1,500,000,000 kwa kila Halmashauri moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyozungumza, tayari wameshalipwa shilingi 214,000,000 kila mmoja na malipo mengine yataendelea kufanyika kulingana na jinsi tutakavyokuwa tumechimba zile material. (Makofi)
MH. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali langu la kwanza; kwa kuwa nchi iko katika ushindani wa kibiashara baina ya mataifa mengine, je, Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha mchakato?

Mheshimiwa Spika, swali langu namba mbili, kutokana na changamoto kubwa ya msongamano wa malori ndani ya mpaka wa Mji wa Tunduma ambayo yanavuka mpaka nataka kujua hatua zilizofikiwa mpaka sasa katika kujenga kituo cha maegesho cha muda ili kuepusha changamoto ya mlundikano wa magari makubwa. Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Stella Fiyao, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza kuhusu kuharakisha mchakato, Serikali inaendelea kufanya kazi hiyo ya kuharakisha kama nilivyosema, bila kuathiri taratibu ambazo zimewekwa ikiwa ni pamoja na kufanya huo uthamini na baadaye kulipa fidia katika mwaka wa fedha ambao unafuatia.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kuondoa msongamano, hii imekuwa ni changamoto kubwa na ndiyo maana Serikali imefanya mambo mawili makubwa kwa sasa kama unavyofahamu. La kwanza, tayari tumeshakaa kama nchi mbili, Zambia na Tanzania. Hii ilikuwa ni maamuzi yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa nchi kupitia ziara ya Rais wetu alipokwenda Zambia ili tuondoe vikwazo vyote vilivyopo mpakani.

Mheshimiwa Spika, tunaamini suluhu hii ni ya kudumu zaidi pengine kuliko kuweka kipande pembeni pale Tunduma. Pia, Serikali inaendelea na mchakato mkubwa wa kuboresha reli yetu hii yote ili mzigo mkubwa zaidi uweze kubebwa kupitia Reli ya TAZARA kutoka Tanzania mpaka Kapiri Mposhi, Zambia.
MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Tabora, Wilaya ya Manispaa, Kata ya Ifucha waliahidiwa kujengewa bandari kavu kwenye mkutano wa hadhara alipokuja Mheshimiwa Waziri Mbarawa; na mpaka sasa hivi Halmashauri ya Manispaa ya Tabora imeshalipa fidia ya heka 600 katika Kata ya Ifucha, je, Serikali inatupa status gani wananchi wa Mkoa wa Tabora ili kusubiri kwa hamu ujengaji wa bandari kavu katika mkoa wetu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Mbunge, dada yangu Munde kwa kuweza kukumbushia jambo hili. Nimhakikishie kwamba Mheshimiwa Waziri ameshanituma katika Bunge hili niende Tabora kwa ajili ya kuona sehemu hiyo ili kuendelea kupanga namna bora ya kufanya kuendana na jambo hilo.
MHE. STANSLAUS S. MABULA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali ilishakuwa na makubaliano ya awali kuchukua eneo ambalo siyo zaidi ya ndani ya meta 700 kulipa fidia na sasa inaonekana itakwenda zaidi ya kata tano zikiwemo Kata za Shibula pamoja na Bulyanhulu na wakazi zaidi ya 1,400, je, Serikali haioni kuchukua eneo lote hili kwa wakati mmoja kutaathiri maisha ya baadhi ya wananchi ambao wako nje kabisa ya eneo la uwanja wa ndege?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Serikali kwa kuanza ujenzi wa jengo la abiria, ni lini mkakati wa Serikali kuhakikisha Uwanja wa Ndege wa Mwanza na wenyewe unakuwa moja ya viwanja vya Kimataifa hapa nchini? Nashukuru.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la pili kisha nirudi swali la kwanza.

Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kuufanya wa Kimataifa na tayari mambo kadhaa yameanza kufanyika. La kwanza, tuko kwenye hatua za ndani za documentation. Ili uwanja uweze kuwa wa Kimataifa, kuna taratibu za kisheria ambazo lazima zizingatiwe.

Mheshimiwa Spika, la pili, ni pamoja na kuondoa wavamizi wapatao 1,000 katika uwanja huu ili waweze kupisha kiwanja hicho kiweze kuwa salama. Pale kuna milima na maeneo mbalimbali ambayo wananchi wamevamia. Kwa hiyo, huwezi kukifanya cha kimataifa wakati huo huo usalama wa kiwanja uko mashakani.

Mheshimiwa Spika, la tatu, tunafanya kazi ya uboreshaji wa miundombinu. Kama unavyofahamu, tarehe 28 mwezi huu Waziri wetu Mheshimiwa Mbarawa alikwenda kushuhudia ujenzi wa jengo la abiria. Iko mikakati mingi, lakini nimetaja mitatu ya kuufanya uwanja huu kuwa wa kimataifa.

Mheshimiwa Spika, sasa nikirudi kwenye swali lake la kwanza, nafikiri litakuwa limeshajibiwa na hoja hii ya pili, kwa sababu hatuwezi kuacha eneo ambalo nimeshalisema pale juu, kwa sababu tu tunataka tuufanye uwanja wa kiamataifa. Kwa hiyo, lazima watu wapishe ili tuweze kuupa hadhi inayostahili, ahsante.
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali kwa kuchelewa kulipa pesa ya wananchi zaidi ya miaka mitano sasa, haioni kwamba imerudisha nyuma maendeleo ya wananchi hao kwa kukosa sehemu za kulima? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, naomba kauli thabiti ya Serikali, je, ni lini wananchi hawa wa Nachingwea wataipata pesa yao?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba tuna viwanja takribani 15 nchi nzima ambavyo tunafanya uhakiki na hatua mbalimbali za utwaaji wa ardhi ili kuweza kufanya maendelezo makubwa ya viwanja vya ndege. Hilo moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, la pili, ningependa kujibu maswali yake kwa umoja wake. Tunafahamu umuhimu mkubwa wa Uwanja wa Ndege wa Nachingwea, siyo tu kwa ajili ya korosho, madini ambayo yamegundulika na LNG, lakini pia kwa ajili ya mazao kama ufuta na kadhalika. Hivyo basi, Serikali kwa maana ya kutoa kauli thabiti, inaliarifu Bunge lako Tukufu kwamba tunao mpango wa kujenga uwanja huu na ndiyo maana sasa tulifanya uhakiki kwa wale wananchi 116. Awali ilikuwa tuwalipe shilingi bilioni 3.5, lakini baada ya kufanya uhakiki na ongezeko la gharama ya mazao, tukapata ni shilingi bilioni 3.4 – 3.5. Hii yote ni dhamira ya Serikali katika kuona kwamba wananchi hao wanakamilishiwa mradi wao. Hivyo basi, tunaendelea na taratibu mbalimbali za Serikalini, tukikamilisha tutaweza kuanza ujenzi huo. Ahsante.
MHE. VEDASTUS M. MATHAYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Uwanja wa Ndege wa Musoma, watu wanadai fidia sasa ni zaidi ya miaka mitatu ambayo ni fedha isiyopungua bilioni 3.9. Hakuna biashara inayoendelea kwa kuwa wanategemea wapate fidia ili waendelee na maisha yao. Je, ni lini sasa hawa watu watalipwa fidia ili waweze kuendelea kuondoka pale? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunafahamu madai mbalimbali ya Uwanja wa Ndege wa Musoma na hivi juzi Mheshimiwa Waziri Mkuu alikuwa hapo na alitoa maelekezo kwa sisi wasaidizi wake Serikalini tukamilishe haraka iwezekanavyo. Tupo kwenye hatua mbalimbali hususan za mwisho kwa wenzetu Wizara ya Fedha. Mara watakapokamilisha tutakwenda kulipa mara moja, kwa sababu tunafahamu umuhimu wa Uwanja wa Ndege wa Musoma kwa maana ya madini pamoja na vitu mbalimbali ambavyo viko pale. Ahsante.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naishukuru Serikali kwa kutupa shilingi bilioni 11 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi wale waliokuwa Uwanja wa Ndege wa KIA ili waweze kuondoka. Hata hivyo, kumejitokeza changamoto ndogondogo, baadhi ya wananchi kufanyiwa tathmini ndogo tofauti na hali halisi na baadhi yao kusahaulika. Changamoto hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais aliiagiza Wizara ya Uchukuzi iifanyie kazi. Je, ni lini sasa Serikali itamaliza changamoto hii ikiwa ni pamoja na kurudia tathmini kwa wale ambao walifanyiwa tathmini ambayo siyo sahihi? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tulifanya uhakiki kwa baadhi ya waliolalamika kwamba walipunjwa malipo yao katika Uwanja wa KIA, lakini kwa kuwa Mheshimiwa Mbunge ameleta hoja hiyo, tuko tayari kama kuna malalamiko mengine, kuyapitia upya ili waweze kupata stahiki zao. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Wananchi wa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambao kwa muda mrefu waliambiwa wasiendeleze maeneo ambayo yako karibu na barabara ambazo ni Barabara kutokea Omugakorongo kwenda mpaka Murongo zikiathiri Kata za Kibale, Bugara na maeneo mengine. Je, ni lini sasa fidia hizo zitatoka ili wapishe hayo maeneo ya uendelezaji wa barabara kwa sababu wameshindwa kuendelea na maendeleo au kufanya chochote kwa sababu ni issue ya muda mrefu? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema kwenye maelezo wakati namjibu mwenye swali la msingi, tupo kwenye hatua mbalimbali za utwaaji wa ardhi, tuna viwanja 15 nchini kote. Pamoja na hoja aliyoisema Mheshimiwa Mbunge, tunaichukua tuifanyie tathmini na tutaona namna bora ya kuonana naye ili kuweza kuzifanyia kazi hoja za wananchi hao.
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini wananchi wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Manyara watalipwa fidia?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hatua tuliyopo ni uandaaji wa taarifa ya uthamini, mara tutakapokamilisha, tutawalipa fidia.
MHE. KILUMBE S. NG’ENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Moja ni kwamba, tangu mkataba wa ukarabati umefanywa mwaka 2023 mpaka leo kipande cha Tabora - Kigoma chenye urefu wa kilometa 411 hakuna kazi yoyote mpaka sasa inayoendelea. Haijafanyika kazi yoyote na bajeti ya mwaka 2023 na mwaka 2022 mmekuwa mkitenga fedha kwa ajili ya ukarabati na hakuna kazi inayoendelea.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili ni kwamba, mliongeza mabehewa katika reli hiyo ili kuongeza safari za train kutoka tatu kwa wiki mpaka nne kwa wiki, na mpaka leo bado safari ni tatu na mabehewa yaliyoongezeka yapo na ya ukarabati yapo lakini hakuna kinachoendelea. Nini mpango wa Serikali kwenye jambo hili?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Kilumbe Ng’enda kwa kukubali majibu ya Serikali ambayo tumeyatoa na kimsingi katika swali lake la kwanza la nyongeza anaweka mkazo kwamba dhamira hii ya Serikali ambayo imeonekana inafaa mpaka tumefika hatua ya kupitisha na hatimaye kusaini mkataba pengine angependa kuona ianze mara moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea ushauri huu na tunaendelea kujipanga kuhakikisha katika muda ambao tumeusema, basi ukarabati huu tunauanza mara moja kwa ajili ya kusaidia wanakigoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, hii inakwenda sambamba na kwenda kutazama hii habari ya route ambayo amezungumza pamoja na kuongeza mabehewa, lakini bado hatujaanza route, tumelipokea, nashukuru sana.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naishukuru Serikali kwamba imeona umuhimu wa uwanja ule kwa sababu ni uwanja ambao ulitumika kukomboa nchi za Kusini mwa Afrika na ule ni miongoni mwa viwanja hivyo. Kwa hiyo, nataka kujua kama Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kwenda Newala ili kuona hali ya uwanja ule?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili ni kwamba, ni zaidi ya miezi mitatu sasa imepita tangu mkataba wa jengo la abiria kwenye uwanja wa Mtwara usainiwe, lakini mkandarasi hajalipwa advance payment ili ujenzi huo uanze. Je, ni lini Serikali italipa advance payment ili ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa Mtwara uanze kujengwa? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Serikali napokea shukurani, na ninaomba shukrani hizi ziende kwa Rais wetu mpendwa ambaye anajenga viwanja takribani nchi nzima. Pia, niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge kwa ajili ya kutembelea eneo hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili amezungumza kuhusiana na jengo la abiria Mtwara. Serikali katika awamu ya kwanza imefanya kazi kubwa ya kujenga runway katika uwanja wa Mtwara, kuweka taa za barabarani, maegesho, na kadhalika. katika hatua ya pili Serikali imeshasaini mkataba wa takribani shilingi bilioni 67 ambapo tunajenga jengo la abiria, control tower, jengo la zimamoto, hali ya hewa, na kadhalika. Vilevile, hivi ninavyozungumza tayari mkandarasi amekabidhiwa site na ujenzi unaanza mara moja.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, suala hili nimelizungumza hapa Bungeni hii ni mara ya saba, ikiwa maswali ya msingi matatu, ya nyongeza mawili na nimechangia mara moja. Mheshimiwa Waziri wa Fedha wakati anahitimisha Mpango na Bajeti wa mwaka 2024/2025 alizungumza masuala ya fidia kuwa yatakuwa kipaumbele. Mwaka wa fedha umeanza na hii ni robo ya kwanza: -

(a) Je, ni lini wananchi wangu hawa watalipwa fedha hizi kiasi cha shilingi bilioni 6.2?

(b) Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari baada ya Bunge hili aambatane na mimi kwenda Kilwa Masoko ili tukakutane na wananchi wangu hawa tukawape majibu ya Serikali yenye matumaini?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwa swali la pili, mara tu baada ya Bunge niko tayari niongozane na Mheshimiwa Mbunge twende huko.

Mheshimiwa Spika, swali lake la kwanza, kwamba ni lini; ni mwaka huu wa fedha 2024/2025.
MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; je, ni lini Serikali itaongeza viti mwendo vya umeme katika viwanja vyetu vya ndege na stesheni zetu, hasa SGR kwa kuwahudumia watu wenye mahitaji maalum?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa tumeshuhudia watu wenye mahitaji maalum wanapata shida sana wakisafiri hasa kwenye stesheni zetu za SGR. Je, ni lini Serikali itatoa mafunzo maalum kwa wahudumiaji wa watu hawa wanaposafiri katika stesheni zetu za SGR na viwanja vya ndege na vituo vya mabasi?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi anavyopigania haki ya watu wenye mahitaji maalumu katika viwanja vyetu katika SGR, treni na usafiri mwingine wa mabasi. Serikali inayo nia na imekuwa ikifanya hivyo. Kama ambavyo nimesema kwenye swali la msingi, ujenzi wowote unaojengwa katika viwanja vyote unazingatia watu wenye mahitaji maalum.

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, tayari tuna vitimwendo vya umeme ambavyo vinasimamiwa na watoa huduma katika maeneo mbalimbali ikiwemo Swissport na wengine. Pia, hata kwenye upande wa SGR au hata kwenye ndege unapokwenda kupanda usafiri huu wako watu wenye mafunzo, si tu pale unapokuwa unapanda lakini pia wapo na madaktari pamoja na fani mbalimbali katika afya ambao kama kutakuwa na changamoto yoyote wako tayari kwa ajili ya kuja kuhudumia.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, tunapokea ushauri wake. Tutaendelea kuongeza ubora katika viwanja vyetu kulingana na mahitaji ya watu wenye mahitaji maalum hatua kwa hatua.
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza tunaishukuru Serikali kwa ujenzi wa bandari. Swali la kwanza; kwa kuwa bandari imeshakamilika na kwa kuwa ujenzi wa reli hii unakwenda kuunganisha Nchi yetu ya Tanzania na Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, pia inakwenda kutoa fursa kwa wananchi wa Tanzania hususan wananchi wa Mkoa wa Katavi kufanya biashara na Nchi ya Congo. Je, Serikali ina mkakati gani wa kupata fedha kuharakisha ujenzi wa reli hii?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa upembuzi yakinifu umeshakamilika wa kilometa 321 kutoka Kaliua Mpanda hadi Kalema kwa ajili ya ujenzi wa reli hii, lakini katika ujenzi huo kuna wananchi ambao watapisha ujenzi wa reli hii. Je, ni lini wananchi wanaopisha ujenzi wa reli hii watalipwa fidia yao?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama utaridhia kabla sijajibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Taska Mbogo, ninaomba nitumie nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa tukio kubwa linaloendelea sasa hivi Nchini China, ambapo yeye pamoja na Marais wenzake, Rais wa China pamoja na Mheshimiwa Rais wa Zambia, wamesaini hati ya makubaliano ya kuboresha reli yetu ya TAZARA. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hapa Bungeni mara kadhaa hoja hii imeulizwa kila wakati, ni lini TAZARA itaboreshwa, leo hati maalum ya makubaliano imesainiwa ili kuifumua TAZARA iweze kubeba mzigo na kufungua biashara kati ya nchi yetu na Nchi za Congo na nchi ya Zambia na sote tunafahamu tuna potential ya mzigo wa ten million metric tons Congo pamoja na seven million metric tons upande wa Zambia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nikirudi kwenye swali la Mheshimiwa Taska Mbogo, namba moja anauliza mkakati wa kupata fedha. Serikali ya Tanzania imejitambulisha kwamba ndiyo Serikali inayoongoza Barani Afrika kwa kuwa na agenda maalum kwenye reli, ndiyo maana tunajenga reli ndefu kuliko reli nyingine yoyote katika Bara letu na duniani tukiwa ni nchi ya tano. Ninamwomba Mheshimiwa Mbogo pamoja na Waheshimiwa Wabunge wengine wa mikoa hiyo wavumilie kidogo, tupo kwenye kipande cha saba sasa kwa maana kutoka Dar es Salaam mpaka Mwanza wakandarasi wapo site tayari na kutoka Tabora mpaka Kigoma wapo site tayari na kutoka Kigoma Uvinza kuelekea mpaka Burundi tupo kwenye hatua za kumpata mkandarasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe Mheshimiwa Mbogo avumilie, tukimaliza hapa tutarudi kwenye vipande vingine vinavyoendelea ikiwa ni pamoja na kwake Kaliua - Mpanda, pamoja cha Mtwara Corridor ambacho najua Wabunge wa Mtwara lazima wangeuliza, leo pamoja na kutoka Rusumo kwenda mpaka Kigali na kutoka Tanga, Arusha na Musoma. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu hoja ya pili, Serikali hii inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, inajali wananchi wake. Nimhakikishie pale itakapobainika kunahitaji fidia wananchi hawa kwa mujibu wa taratibu na sheria za nchi yetu watapewa fidia zao. (Makofi)
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Wilaya ya Kahama imekuwa ndiyo kitovu cha kibiashara kwa Mkoa wa Shinyanga, lakini pia na Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Nchi hizi za Maziwa Makuu. Kwa nini Serikali isitenge japo fedha kidogo ili kuukarabati uwanja huu ambao ni wa kiwango cha moramu?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Manispaa ya Kahama imekuwa ikikusanya fedha nyingi zaidi ya shilingi bilioni 13 mpaka shilingi bilioni 15 kwa mwaka. Kwa nini Serikali isitoe kibali sasa kwa Manispaa hii ya Kahama angalau uwanja huu uwekwe kwa kiwango cha lami pamoja na miundombinu yetu ili kuondoa adha wanayoipata wasafirishaji?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Cherehani kwa ufuatiliaji wake wa karibu wa Uwanja wa Ndege wa Kahama lakini hata ule wa Shinyanga. Pili, napenda kumwarifu Mheshimiwa Cherehani pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwa ujumla kwamba katika kipindi ambacho Serikali imewahi kutenga fedha nyingi kuliko wakati mwingine wowote, ni sasa. Hivi ninavyozungumza, takribani Shilingi trilioni moja zinajenga viwanja vya ndege karibu vyote kwenye nchi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, moja, tumepokea ushauri wake mzuri kwa ajili ya kuweka moramu ili uwanja huu uendelee kutumika zaidi na ikizingatiwa ni jengo la ubia ambalo limejengwa na wenzetu wa Madini. Pili, namwomba pia awe na subira kidogo, tutakapokamilisha Uwanja wa Ndege wa Shinyanga, tutapima mahitaji makubwa yaliyopo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kahama halafu tuone ni hatua ipi ambayo inahitajika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, izingatiwe kwamba, tunapozungumza hapa hata maeneo mengine kwenye viwanja vya mikoa, kuna mahitaji makubwa ya fidia pamoja na viwanja hivyo vifanyiwe maboresho. Kwa hiyo, watupe muda kidogo, baada ya hapo tutaona cha kufanya kama Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, nampongeza kwa sababu amekuja na mawazo ya kimapinduzi. Anazungumza juu ya Halmashauri ya Kahama kwamba ni halmashauri kubwa ambayo inakusanya mabilioni ya pesa na anaomba kibali kwamba pengine waruhusiwe kufanya ukarabati. Kimsingi Serikali hii ya Awamu ya Sita inaunga mkono jitihada za halmashauri na Waheshimiwa Madiwani wa aina yake katika kuiunga mkono Serikali kusaidia maboresho mbalimbali ya viwanja vya ndege.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yetu chini ya Mheshimiwa Waziri Mbarawa pamoja na Mamlaka yetu ya Viwanja vya Ndege haitakuwa kikwazo, bali itakuwa msaada katika kurahisisha azma yenu hiyo kutokana na umuhimu mkubwa ambao mmeuona endapo mtatenga fedha kwa ajili ya kufanya maboresho.
MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Mara ni mkoa wenye historia katika nchi hii, kwani anatoka Muasisi wa Taifa letu Baba Julius Kambarage Nyerere. Tumeona mkiwa mnamuenzi kwa matembezi na kwa vitu mbalimbali. Sisi watu wa Mkoa wa Mara, moja ya kumuenzi Baba wa Taifa ni kuhakikisha mnakamilisha Uwanja wa Ndege wa Musoma kwa kiwango cha lami. Ni lini mtatenga fedha za kutosha kuhakikisha Uwanja wa Ndege wa Musoma unakamilika? Wabunge tumechoka kushukia Mwanza.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Ester Bulaya kwa swali lake ambalo ameuliza kwa umakini mkubwa. Serikali hii ya Awamu ya Sita inatambua, inazingatia na inafahamu umuhimu wa Baba wa Taifa. Pia inatumbua umuhimu wa viwanja vya ndege nchi hii, ndiyo maana pamoja na viwanja vyote nilivyosema vinaendelea kujengwa na kukarabatiwa, Uwanja wa Ndege wa Musoma upo, umeshatengewa fedha na unajengwa. Hivi ninavyozungumza, upo 60%. Labda ninachoweza kumhakikishia, ni kuiagiza mamlaka inayosimamia iharakishe ujenzi huo ukamilike ili uweze kuanza kutumika.
MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali ya kutia matumaini, naomba kuuliza. Swali la kwanza; je, Serikali au Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kutaja kiwango kilichotengwa kwa ajili ya kuanza kazi hii ya kufunga taa katika Kiwanja cha Ndege cha Mafia? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; kwa kuwa Uwanja wa Ndege wa Mafia licha ya kwamba hauna taa lakini una uwezo wa kuruhusu ndege kubwa kutua na kwa kuwa Serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwenye Shirika letu la Ndege ATCL. Je, ni lini Shirika la ATCL litaanza safari ya kwenda Mafia ili kuwawezesha watalii hasa kipindi cha Mwezi wa Kumi mpaka wa Tatu ambapo utalii wa samaki mkubwa anayepatikana kwenye nchi sita tu hapa duniani aina ya samaki potwe?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa jinsi anavyojenga hoja kuhusiana na Uwanja wa Ndege wa Mafia na nimhakikishie swali lake la pili kwamba tumeshaanza tathmini ya kina kufahamu mahitaji na habari za kutosha kuhusiana na Uwanja wa Mafia na tukikamilisha tutapeleka Ndege ya ATCL.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la kwanza kuhusiana na habari aliyozungumza, kwanza nimkumbushe Serikali inafahamu umuhimu mkubwa sana wa Kiwanja cha Ndege cha Mafia kilichojengwa miaka mingi iliyopita kuanzia wakati wa mkoloni na tumefanya kazi kubwa pale. Tulirekebisha runway tukajenga ambayo ina urefu wa mita 1,500 na upana wa mita 30, tukaongeza eneo la kuegesha ndege kiasi kwamba ndege sita ndogo Caravan C208 zinaweza kutua pale. Kama hiyo haitoshi, tunapozungumza hapa tunafanya usanifu kwa ajili ya kuongeza jengo la abiria ili liwe na uwezo wa kubeba abiria zaidi kwa sababu jengo lililopo linabeba abiria 50.

Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, katika mwaka huu wa fedha nimeshamtamkia, Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia inao mpango na inakwenda kuweka taa za kuongozea ndege katika kiwanja hicho. Atupe muda tu tutakwenda kukamilisha.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, Uwanja wa Ndege wa Kahama unapokea watu zaidi ya 200 kwa siku. Je, Serikali ina mpango gani wa kuupanua na kuujenga kwa kiwango cha lami?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, Uwanja wa Kahama ni moja ya viwanja muhimu kwa Taifa letu na kwa kushirikiana na wadau tumeshajenga jengo la abiria zuri sana. Tuko kwenye hatua za tathmini ili kuhakikisha kwamba tunajenga njia kwa ajili ya kuruka na kutua ndege.
MHE. IDDI K. IDDI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Waziri ametueleza kwamba Uwanja wa Ndege wa Kahama uko kwenye process, sasa ni lini wakati wanasubiri mchakato huo wataanza kuleta safari za Ndege za ATCL ambazo zitatua Kahama? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa ameleta kama ushauri, tumepokea.
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza; Meli ya MV Victoria husafirisha abiria kwa madaraja matatu, daraja la tatu, daraja la pili na daraja la kwanza. Mimi nilisafiri na meli hiyo kupitia daraja la kwanza, nikalala usingizi nilipoamka saa saba badala ya watu wawili nilikuta tupo watu sita. Sasa napenda kujua ni taratibu gani zinatumika ili hao watu wa TASAC au kama ni Marine Service wanahakikisha usalama wa abiria kwa kufuata taratibu zilizowekwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; huko nyuma Afisa Kazi wa Mkoa alikuwa katika daraja la kwanza kwenye meli, alifuatwa ndani ya meli, akachukuliwa na akatupwa ndani ya maji akafariki. Je, Marine Service au kama ni TASAC sasa wako tayari kuweka ulinzi thabiti ndani ya meli kuhakikisha kwamba kunakuwa na usalama wa kutosha hasa ule usiku mkuu maana hii meli inasafiri usiku ndani ya maji? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpe pole Mheshimiwa Mbunge kama alivyoeleza kwa aliyoyasema Bungeni, lakini nimhakikishie na nitumie nafasi hii kutoa maelekezo maalum kwa Wakala wa Meli pamoja na TASAC kuhakikisha kwamba wanadumisha ulinzi na usalama kwa abiria kwa vyombo vyote majini siyo tu Ziwa Victoria na maeneo mengine yote ikiwemo Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa na kwingineko kote.
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa ujenzi wa bandari kavu ilikuwa ni ahadi ya Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Mheshimiwa Mkapa na kwa kuwa Serikali imesema haijakidhi vigezo, je, Serikali iko tayari kwenda kuwaelezea wananchi ili sasa wazo hilo lifutwe kwenye mawazo yao kwa sababu walikuwa wanasubiria?
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, lengo hasa ilikuwa kuongeza uchumi kupitia shughuli za usafirishaji wa mizigo hasa kutoka Bandari ya Mtwara na kupitia Daraja la Mtambaswala lile la Umoja, je, Serikali inafikiria shughuli gani sasa ili kuweka shughuli mbadala katika lengo la awali?
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mhata na Mheshimiwa Hokororo kwa maana ya swali lao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, unapojenga bandari kavu vipo vitu unavyovitazama na kikubwa tunaangalia shehena na ndio maana kwa sasa hivi ninapozungumza, Serikali ya Awamu ya Sita inajenga reli kutoka Dar es Salaam mpaka Kigoma, inaunganisha mpaka Burundi, lakini pia inajenga reli kuelekea Mwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika ushoroba huu kilometa 2,300 tunajenga Bandari Kavu ya Kurasini, Bandari Kavu ya hapa Ihumwa - Dodoma, Bandari Kavu ya Fela kule Mwanza na Katosho, Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hatua ya pili tukishatoka kwenye upande huu wa central corridor kwa maana ya CSGR Serikali inaendelea na mchakato kwa ajili ya kujenga reli ya kusini inayotoka kwenye bandari yetu ya Mtwara pamoja na Kisiwa Mgao, inaunganisha kwenda Liganga na Mchuchuma ambako kuna madini pamoja na makaa ya mawe, lakini inakwenda mpaka Mbamba Bay ambayo tayari ninavyozungumza mjenzi wa Bandari ya Bamba Bay yupo site. Sasa hii Bandari Kavu ya Nang’omba itakuwa ni bandari muhimu tukishafika hatua hiyo ili tutoe mzigo bandari tuupeleke Msumbiji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutauingiza katika mchakato huu wa southern corridor kuhakikisha kwamba na yenyewe inakuwa sehemu ya mradi wetu wa reli hiyo.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa fursa ya kuuliza swali moja dogo la nyongeza lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

(a) Je, Serikali inajua faida zitakazopatikana kutokana na ujenzi wa njia ya reli ya mwendokasi kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay Wilayani Nyasa? (Makofi)
(b) Je, ni kwa nini Serikali inachelewesha kuanza ujenzi wa njia ya reli ya mwendokasi kutoka Mtwara kwenda Mbamba Bay? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kama nilivyosema kwenye swali la msingi, kwanza nianze kumshukuru Mheshimiwa Msongozi kwa sababu yeye pamoja na Wabunge wengi ambao nina uhakika watasimama tu kwa ajili ya kuhoji swali hili, wamekuwa wakihitaji kwa muda mrefu kuona SGR inajengwa kutoka upande wa Southern Corridor na Serikali inafahamu umuhimu wa jambo hili. Unapozungumza SGR ya Kusini lazima ufungamanishe Liganga na Mchuchuma pamoja na Bandari. Nini Serikali imefanya mpaka sasa? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya kwanza tumekwishalipa fidia mwaka jana wananchi 1,142 takribani shilingi bilioni 15.4. Hii ni commitment ya juu kabisa ya kuona jinsi ambavyo tunataka jambo hili likamilike mapema iwezekanavyo. Hatua ya pili tumekwishaanza ujenzi wa bandari ya Mbamba Bay na hivi ninavyozungumza tupo hatua za mwishoni kuanza kujenga Bandari ya Kisiwa Mgao – Mtwara. Kwa sababu unapozungumza reli hiyo lazima uzungumzie namna ya kusafirisha chuma pamoja na makaa ya mawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya tatu tunaboresha viwanja vya ndege kuanzia Njombe ambayo tupo kwenye usanifu wa kina lakini Mtwara pamoja na Lindi ambayo tunajenga pia kingine kipya. Kama nilivyosema hata katika bajeti hii tumetenga takribani milioni 702 yote hiyo ni kuelekea kuhakikisha kwamba tunafanya jambo hilo linakamilika mapema iwezekanavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hatua nyingine ambayo tunaifanya tunapojenga Reli ya SGR kutoka Dar es Salaam - Mwanza mpaka Kigoma takribani kilometa 2,102 hiyo ni kuonesha utayari wa Serikali katika kujenga Reli ya SGR Kusini. Kwa sababu unaanza hatua ya kwanza unamaliza hatua ya pili halafu unakwenda hatua zingine ambazo zinafuatia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi ninavyozungumza tayari tumejenga 2,102 reli kwa maana kama nchi na inakuwa ni nchi ya tano. Kwa hiyo, tukijenga na kilometa 1,000 na Mtwara Corridor 1,000 tutakuwa na 3,000 kama na mia tatu au na mia nne. Hivyo, tutakuwa ni nchi ya tatu duniani kwa kujenga reli ndefu zaidi na kwa nchi ya kwanza kwa nchi zinazoendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, faida zake kama alivyouliza Mheshimiwa Mbunge. Tuna faida nyingi ambazo tunazipata tukifanikiwa kujenga Reli ya Kusini kama nilivyosema Reli ya Kusini inafungamanishwa pamoja na Liganga na Mchuchuma ambayo Liganga na Mchumchuma tuna madini ya Vanadian, takribani pengine asilimia 0.4 kila mzigo unaopata pale ndani. Tuna vanadian na titanian ambayo inatengenezea engine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili inatusaidia kwenda kupata umeme megawatt 600 ambayo takribani 250 inakwenda kuyeyusha chuma na 350 inakwenda kuingia kwenye Gridi ya Taifa, nchi yetu ina changamoto ya umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama haitoshi reli hii itatusaidia sasa kuchukua malighafi zile zote kwa maana ya Mchuchuma yale makaa ya mawe kusafirisha, kuyatoa pale yale yalipo kuyapeleka duniani yanapohitajika kwa wingi zaidi sasa hivi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo taifa letu litapata fedha nyingi zaidi. Kama haitoshi pia itatuwezesha kufungamanisha nchi yetu kwenye viwanda, takribani milioni 2.9 ya chuma tutazalisha kwa mwaka wakati sisi mahitaji yetu tunakalibia milioni moja. Hivyo, basi niendelee kumuomba Mheshimiwa Mbunge, nafahamu yeye ni mkulima na angependa kujua faida kubwa ambazo zinapatikana kusafirisha mazao mbalimbali kwenye ukanda wa Kusini kupeleka nchi jirani na nchi za mbali kupitia reli hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, niendelee kumuomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati Serikali inakamilisha mchakato huu na hatimaye tutaenda kuanza ujenzi huo.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, awali ya yote naomba kuipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri juu ya mradi huu wa ujenzi wa reli kutoka Mtwara hadi huko Mbamba Bay. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, rai yangu kwa Serikali, kwa kuwa mmeamua ku-engage private partnership kushiriki katika mradi huu, mimi nawapongeza sana na naiomba Serikali iongeze jitihada ili reli hii iweze kufunguliwa na iwe mkombozi kwa wananchi wa Kusini hasa usafirishaji wa makaa ya mawe kutoka Liganga, ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mhata kwa kutoa pongezi, wachache sana wakitendewa mambo mema wanasimama na kushukuru. Kwa hiyo nakushukuru sana Mheshimiwa Mhata kwa kuwa na moyo wa shukrani ambao utazidishiwa yaliyo mema zaidi. (Makofi)
MHE. NEEMA W. MGAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali haioni umuhimu wa kutengeneza baadhi ya mabehewa kuweka mfumo wa ubaridi (cold room) katika reli ya TAZARA ili tuweze kusafirisha parachichi zetu na mazao ya mboga mboga yamfikie mlaji wa mwisho yakiwa na ubora? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana dada yangu Mheshimiwa Mgaya kwa sababu ni mdau mkubwa sana wa reli ya TAZARA na tukubali ukweli kwamba kwa sasa katika reli yetu na mabehewa yaliyopo hatuna cold rooms, lakini kila mtu anafahamu umuhimu wa ukuwaji wa sekta ya parachichi katika mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa na kadhalika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa unyenyekevu mkubwa Wizara tunapokea ushauri huu na tunapokwenda kwenye hatua ya pili ya maboresho makubwa ya reli yetu kutoka Dar es Salaam mpaka Kapiri Mposhi tutaona namna ya kuweza kuweka hicho alichokizungumza cha cold room.
MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali imeboresha miundombinu ya Bandari ya Tanga kiasi kwamba shehena zimeongezeka, lakini reli ya kutoka Tanga kwenda Dar es Salaam na kutoka Tanga kwenda Arusha bado ni chakavu sana, je, kuna mpango wowote wa kuboresha reli hii ili sasa shehena hii iweze kutoka kwa urahisi? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Shangazi, Mbunge wa Mlalo na Katibu wa Bunge la CCM kwa swali lake kubwa na zuri la maslahi ya watu wa Tanzania na watu wa Kaskazini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inao mpango mzuri na kabambe kwa sababu inatambua umuhimu wa upande wa Kaskazini kwanza kwenye utalii, kilimo pamoja na sekta nyingine, hivyo katika mwaka wa fedha 2023/2024 tumeshafanya kazi kubwa, tulishasaini mkataba wa kununua materials za kukarabati reli inayotoka Tanga kuelekea mpaka Arusha kilometa 533.

Kwa hiyo, mara baada ya kusaini mkataba huo katika mwaka wa fedha huu unaofuatia tunakwenda kuanza kutoa reli iliyokuwepo, tunataka tuweke reli nzito ambayo itakuwa na capacity ya ratilika 80 kwa yard, iliyokuwepo ilikuwa 45 kwa yard.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hii reli iliyopo sasa hivi speed inayokwenda treni ni karibu speed ya 15 - 20 kwa saa moja, hivyo inawachukuwa muda mrefu sana kufika kwenye destination inayotakiwa. Tukifanya maboresho haya speed itaongezeka mpaka 75, kwa hiyo muda kama ilikuwa ni saa 12 tutakuwa tunatumia saa karibu nne. Kwa hiyo, habari njema hii kwa watu wa Kaskazini, Tanga na Watanzania kwa ujumla juu ya maboresho makubwa ya reli ya Kaskazini. (Makofi)
MHE. GODWIN E. KUNAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Uchukuzi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwa kuwa wananchi wa Jimbo la Mlimba usafiri wa reli ya TAZARA ndiyo usafiri unaotegemewa, sasa lini mpango wa Serikali katika kuboresha reli hii ikiendana sambamba na kuongeza mabehewa na route za safari ya reli hii kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, reli ya TAZARA kama inavyofahamika ilijengwa miaka 1975 baina ya Serikali tatu, China, Tanzania na Zambia na kipindi chote hicho designed capacity ilikuwa ni metric tons milioni tano, lakini kutokana na ubovu wa miundombinu hatukufikia lengo. Habari njema kutoka kwa daktari wa maendeleo Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania amefanya kikao na Waziri wa Zambia pamoja na Rais wa China, hivi ninavyozungumza tupo kwenye hatua za mwisho za majadiliano, reli nzima inakwenda kufumuliwa upya. Moja, kuongeza uwezo wa reli wa kubeba mzigo, lakini pili tutaongeza mabehewa pamoja na vichwa vya kutosha ya mizigo na abiria. Kwa hiyo, Wana-Mlimba na watumiaji wote wa reli hii inayotoka Dar es Salaam mpaka Kapiri Mposhi kilometa 1,860 waendelee kusubiri habari hii njema ambayo inakuja kwa Watanzania wote. (Makofi)
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza maswali ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri mimi kwanza naipongeza Mamlaka ya Hali ya Hewa inafanya kazi nzuri sana ya kutoa tahadhari ya hali ya hewa ya nchi yetu na tahadhari ambazo ni za ukweli kwa asilimia kubwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa taarifa za hali ya hewa zinatolewa mapema sana, lakini Serikali haichukui hatua za mapema matokeo yake kunatokea madhara makubwa sana kama vile inaponyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali. Je, mamlaka zinazohusika zina mpango gani sasa wa kuhakikisha wanafanyia kazi taarifa za hali ya hewa?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa tumeshuhudia kunyesha kwa mvua kubwa katika maeneo na kusababisha mafuriko kama vile ya Rufiji, Kibiti, Kilwa, Lindi na Arusha - King’ori kulitokea mvua kubwa, madaraja yakavunjika mpaka gari la wanafunzi likaingia kwenye daraja.

Je, Serikali imejipanga vipi sasa kutoa taarifa pale inapotokea mvua inanyesha angalau kusimamisha masomo kwa wanafunzi wa shule za msingi na nursery school? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kutoa pongezi kwa Mamlaka yetu ya Hali ya Hewa kwa kazi kubwa ambayo wanafanya na hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa sana ambao Serikali imefanya katika kuiwezesha mamlaka hii itoe taarifa sahihi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili, amezungumza kuhusu kufanyia kazi, Mamlaka ya Hali ya Hewa ina jukumu kubwa la kuangaza, kukusanya, kuchakata pamoja na kuhifadhi na kusambaza taarifa za hali ya hewa na mara baada ya kukamilisha jukumu hilo la kwanza, jukumu la pili ambalo linafanyika sasa ni namna gani taarifa hizo zinakwenda kuwafikia wananchi mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, bahati nzuri tunayo sheria ya mwaka 2006 ambayo ni Sheria yetu ya TMA inaipa mamlaka kufanya kazi hiyo, lakini pia tuna Sheria ya Maafa Namba 6 ya mwaka 2022 ambayo kimsingi inatoa nafasi kwa Kamati zetu za Maafa mbalimbali nchi nzima. Mara baada ya kupokea taarifa za TMA, kuhakikisha kwamba zinasambazwa na kufikishwa katika maeneo mbalimbali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo Serikali kwa kushirikiana na mamlaka mbalimbali imeendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wananchi kupitia vyombo vya habari, kuimarisha mifumo yetu ya tahadhari pamoja na kujenga uwezo wa watendaji ili kuhakikisha kwamba taarifa zinakuwa sahihi, lakini pia zinafika kwa wananchi wetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru pia kwa swali lake la pili juu ya ushauri alioutoa kwamba pengine inapotolewa taarifa hizo za hali ya hewa pengine kutakuwa labda na kimbunga na kadhalika, ni vyema shule zikafungwa. Ushauri huu ni mzuri na sisi kama Serikali tumeupokea, tutaenda kuuchakata na kuufanyia kazi hatua kwa hatua. (Makofi)
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru, ni kweli kwamba Mamlaka yetu ya Hali ya Hewa inafanya kazi nzuri hivi sasa kutokana na uwekezaji mkubwa ambao Mheshimiwa Rais ameuwekeza, lakini kumekuwa na changamoto kwa wadau na taasisi mbalimbali zinazotumia taarifa hizi, kuchelewesha malipo kwa mamlaka yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa ni ipi kauli ya Serikali kuhusiana na taasisi hizi ambazo zinachelewesha malipo baada ya kutumia taarifa za hali ya hewa ili taarifa zetu za hali ya hewa ziendelee kuwa endelevu na bora zaidi? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninamshukuru Mheshimiwa Bakar kwa swali lake la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninatumia nafasi hii kuomba taasisi mbalimbali ambazo kimsingi ni wanufaika wa taasisi hii au taarifa za taasisi hii ili waweze kulipa ndani ya muda kwa ajili ya kusaidia mamlaka yetu ipate fedha na kuongeza uwezo zaidi, iweze kutengeneza au kuandaa taarifa zingine sahihi zaidi kuliko pengine livyokuwa hapo mwanzoni. (Makofi)
MHE. MWANTUMU DAU HAJI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza namshukuru Waziri wangu wa Miundombinu kwa majibu yake mazuri aliyoyatoa sasa hivi, yana kina ndani yake. Kama ingelikuwa sitaki kumwuliza swali lingine, basi ilikuwa mimi niseme basi, maana nimeridhika nalo, lakini nina swali moja dogo la nyongeza nimpe Waziri wangu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Serikali imejenga meli Maziwa Makuu, je, ni lini itajenga meli ya baharini kwa ajili ya abiria na mizigo ikiwemo kwenda Zanzibar? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwanza Serikali inamiliki meli pamoja na Serikali ya China kwa hisa ya 50% kwa 50%, ambayo ilijengwa mwaka 1967. Kwa sasa kutokana na umuhimu mkubwa wa usafiri kwenye Mwambao wa Pwani, kwa maana ya Malindi, Comoro, Tanga, Pwani, Zanzibar na maeneo mengine, Serikali ipo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 ili kufahamu gharama, wahitaji na fursa zilizopo katika bahari yetu, hatimaye kuweza kuanza kununua meli hizo.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Wananchi wa Mkoa wa Geita wanategemea Bandari ya Mwanza na Bukoba. Sasa Mkoa wa Geita unakua na unajitegemea; tunalo eneo zuri kabisa la bandari ambayo haijaboreshwa ya Nkome ambayo ingetumika kushusha mizigo kutoka Kenya na Uganda. Je, Serikali ina mpango gani wa kuiboresha Bandari ya Nkome ili wananchi wa Mkoa wa Geita tuweze kuitumia kushusha mizigo yetu kutoka nje? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, tayari Serikali inafanya maboresho makubwa kwenye Ziwa Victoria kwa namna mbili; moja, tunajenga Bandari ya North Mwanza, Bandari ya Kemondo na Bandari ya Bukoba pamoja na kununua meli mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilisha hatua hiyo, tutakwenda kwenye hatua ya pili ya kutazama maeneo mengine kulingana na uhitaji wake ambayo ni pamoja na eneo la Nkome ambalo Mheshimiwa Mbunge ameulizia.