Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to supplementary Questions by Hon. Judith Salvio Kapinga (129 total)

MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Pia nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri yenye matumaini kwa wananchi wangu wa Rorya, lakini ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; kwa kuwa Sheria ya Uthamini inatamka wazi kwamba thamani ya ardhi inapaswa kulipwa ndani ya miezi sita, lakini wananchi hawa wamedai malipo yao toka mwaka 2011 na hawajalipwa. Nataka nipate commitment ya Serikali itakapofika Novemba kama wananchi hawa hawajalipwa uthamini wa ardhi yao, je, Serikali itakuwa tayari sasa kurudia uthamini kwa mujibu wa Sheria inavyotamka kwamba wananchi wale walipwe ardhi kwa mujibu wa Sheria inavyotamka?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa jambo hili limekuwa ni la muda mrefu toka mwaka 2011 na sasa liko ndani ya Ofisi ya Mkurugenzi nataka nipate commitment ya Serikali hasa Ofisi ya Wizara ya TAMISEMI, je, ni lini watalipa fedha ili wathamini warudi site wakamilishe uthamini na upande wa TANESCO waweze kulipa fidia kwa wananchi hawa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jafari Chege, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusu kurudia zoezi ikifika Novemba, zoezi hili limeshachukua muda mrefu nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge Serikali imeshatenga fedha kiasi cha milioni 350 ili wananchi 231 wanaodai fidia walipwe ikifikia Novemba, 2023. Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba zoezi hili tunaenda kulikamilisha na kwa sababu limechukua muda tutafuatilia kwa ukaribu kuhakikisha kwamba linakamilika.

Mheshimiwa Spika, kwenye swali lake la pili kuhusiana na kutoa fedha, tayari Serikali kupitia TANESCO imeshatoa fedha kiasi cha shilingi milioni 15 kwa ajili ya kukamilisha zoezi la uthamini. Tutafuatilia kuhakikisha kwamba Halmashauri ya Rorya inakamilisha taratibu hizi kwa wakati ili zoezi hili liweze kukamilika kwa wakati kwa kadri ambavyo imepangwa, ahsante. (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI): Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hii tena kumwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya kuhakikisha kwamba fedha hizi ambazo wenzetu wa TANESCO wameshazipeleka kwenye halmashauri ile ziweze kutumika mara moja na kulipa fida hiyo. (Makofi)
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mradi wa Geita - Nyakanazi na Nyakanazi - Rusumo kuna baadhi ya wananchi wa Biharamulo ambao wanapitiwa na mradi ule katika Kata nne za Rusahunga, Kaninha na Nyakahula nao pia bado hawajalipwa pesa zao za fidia. Je, ni lini Serikali itaweza kukamilisha malipo hayo kwa baadhi ya watu ambao walikuwa hajalipwa pesa zao? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba nijibu maswali ya Mheshimiwa Engineer Ezra Chiwelesa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na fidia ya Geita - Nyakanazi tayari Serikali ilishatenga fedha bilioni sita na tayari fedha bilioni 5.9 zilishalipwa kwa ajili ya wananchi na wananchi waliobakia ni wananchi 49 tu, tunaamini taratibu zikikamilika na wao wataweza kulipwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Nyakanazi -Rusumo pia Serikali ilishatenga fedha bilioni 3.8 na tayari bilioni tatu ilishalipwa, wananchi waliobakia ni 39 tu. Nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia na kwa sababu fidia hii imekamilika kwa zaidi ya asilimia 95, tutafuatilia kuhakikisha kwamba kidogo kilichobakia kinaweza kukamilika, ahsante sana. (Makofi)
MHE. GEOFFREY I. MWAMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri. Hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, tuna Kijiji cha Mlundelunde, Kitongoji cha Mchaka ambacho kina shule ya sekondari ambapo bahati mbaya umeme umepita juu yake na shule ile ya sekondari kama taasisi ya Serikali, haijapata ule umeme: Je, nini maelekezo ya Serikali kwa REA Mtwara ili waweze kufanya haraka kuunganisha umeme katika hiyo shule ya sekondari?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Tumepata changamoto kubwa kwa Jimbo letu la Masasi Mjini ambapo tuna Kata saba za Sururu, Mwengemtapika, Matawale, Chanikanguo, Temeke, Marika pamoja na Mmbaka ambazo ziko vijijini, lakini wanatakiwa kulipa shilingi 320,000/= kama sehemu ya ada ya uunganishaji wa umeme: Je, Serikali haioni ni wakati muafaka sasa, wananchi hawa wapate haki kwa maana wapo vijijini, waunganishiwe umeme kwa shilingi 27,000/= kama vijiji vingine?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Geoffrey Mwambe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na shule ambayo ameitaja, shule hii ipo katika moja ya kitongoji ambapo utaenda kutekelezwa mradi wa vitongoji 15 ambavyo tayari Serikali imeshatenga fedha kwa mwaka huu wa fedha. Tunaanza kufanya ufuatiliaji ili tuweze kuona ni namna gani tunaanza kutekeleza mradi huu wa vitongoji 15.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la pili juu ya maeneo ya vijijini ambayo yanakataliwa kutozwa shilingi 27,000/=, tayari Serikali tumeshaya-identify haya maeneo na tuko katika mchakato wa mwisho ili kuweza kutolea maelekezo kwa maeneo kama haya ambayo yanaleta mkanganyiko wa bei.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Mkandarasi aliyekabidhiwa vijiji 15 vya Wilaya ya Hanang’ kasi yake inasuasua sana: Je, nini kauli ya Serikali juu ya Mkandarasi huyu ili kuwapa matumaini wananchi wa Wilaya ya Hanang’?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Asia Halamga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkandarasi aliyekuwepo Hanang’ Nakurwa Investment Company ni kweli alikuwa anasuasua lakini tumemsimamia na katika vijiji 15 ambavyo vimebakia, vijiji tisa ameshasambaza nguzo, na tuna imani mpaka ifikapo Desemba, 2023 atakuwa amekamilisha kuweka umeme vijiji vyote, ahsante.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwanza naishukuru Serikali kwa majibu mazuri. Hali ya makali ya mgao wa umeme katika Wilaya ya Kahama pamoja na Halmashauri yake ni makali mno, hali ni ngumu, wafanyabiashara wanashinda wamekaa, umeme umekatika siku nzima. Sasa Mheshimiwa Waziri yupo tayari kufanya ziara katika Wilaya hii ya Kahama pamoja na Halmashauri zake ajionee hali ilivyo kwa wananchi hawa?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili. Je, Serikali ina mkakati gani sasa wa kuipa Mkoa wa ki-TANESCO Wilaya hii ya Kahama ambayo inakua kwa kasi kwa nchi hizi za maziwa makuu?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Nishati napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Emmanuel Cherehani.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mgao wa umeme, kwa sababu sasa hivi tumetengamaa na tumepunguza kidogo ule upungufu ambao ulikuwepo, niwaelekeze TANESCO na kituo chetu cha pamoja cha gridi (Grid Control Center) wahakikishe maeneo yote yanaendelea kupata umeme kulingana na jinsi ambavyo tunaboresha upatikanaji huo wa umeme.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na ziara, nitafika Ushetu Mheshimiwa Mbunge. Suala la pili kuhusiana na kuweka kituo cha kimkoa Ushetu, Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kuangalia tathmini kama Wilaya ya Kahama inafaa kuwekwa kama Mkoa wa ki-TANESCO kwa ngazi ya mkoa, na kama itafaa, basi tutafanya hivyo, lakini kama haifai, tutaendelea kuboresha huduma ili wananchi wa Ushetu waendelee kupata huduma bora na stahili za masuala ya umeme. (Makofi)
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa. Hospitali mpya ya Wilaya ya Mabogini imeshaanza kutoa huduma, je, Serikali ina mpango gani kupeleka umeme katika Hospitali yetu hii mpya?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Hospitali ya Mabogini tayari tumeshaifanyia tathmini na tupo katika mchakato wa kupata fedha ili ifikapo Januari, 2024 tuweze kuhakikisha Hospitali hii ambayo tayari inafanya kazi iweze kupatiwa umeme wa uhakika, ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Licha ya majibu mazuri ya Serikali, nina maswali madogo mawili.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Kata ya Mgambazi ipo kwenye Manispaa ya Morogoro, lakini mpaka sasa hivi Mtaa mzima wa Mgambazi pamoja na Chambilazi na Vilengwe hawajapatiwa umeme, licha ya kuwa kwenye Manispaa ya Morogoro: Je, ni lini watapata umeme? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kijiji cha Zongo ambacho kiko kwenye Kata ya Kisemo pamoja na Kijiji cha Bwakila Juu katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini, hawajapata umeme. Ni lini vijiji hivi vitapatiwa umeme? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Dkt. Christine Ishengoma kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na umeme katika Mitaa ya Mungazi, Chambilazi na Vilengwe tayari tumeshaiweka kwenye Mpango wa fedha wa 2025 na mitaa hii itapatiwa umeme.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Vijiji vya Zongo na Bwakila Juu, tayari wakandarasi wamepatiwa site na muda wowote kazi itaanza, ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Serikali iliahidi kufunga umeme katika shule zote za sekondari na taasisi za dini, lakini zipo shule ambazo hazijaweza kufungiwa umeme; je, ni lini Serikali itafunga umeme katika Shule ya Sekondari Kimenyi, katika Halmashauri ya Kasulu DC? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Genzabuke, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari kuna miradi inaendelea kwenye vijiji vyote ya kupeleka umeme. Mwanzoni ilikuwa kilomita moja, tumeongeza kilometa mbili ili taasisi nyingi zifikiwe. Kwa shule hii ya Kimenyi kama haipo katika scope ambayo ipo sasa hivi, tutahakikisha kwamba tunaweka fedha kwenye mwaka ujao ili na wenyewe waweze kupatiwa umeme, ahsante.
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Wananchi wa Kilwa wamekuwa ni wanufaika wakubwa wa umeme wa gesi unaozalishwa katika Kituo cha Somanga.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kukiboresha kituo hiki ili kumaliza changamoto kubwa inayokabili wananchi wa Kilwa katika huduma ya umeme? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ndulane, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari tumeanza mkakati wa kurekebisha kufanya matengenezo kwenye visima vyetu ambavyo vinazalisha gesi na tumeshaanza Mnazi Bay, Songosongo pamoja na Madimba. Kwa Somanga pia tutahakikisha tunaweka kwenye mkakati ili tuweze kukiboresha na wananchi wa Kilwa waweze kupata umeme wa uhakika, ahsante.
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa tatizo la kukatika umeme katika Manispaa ya Morogoro linafanana na tatizo lililopo katika Wilaya na Mkoa wa Kilimanjaro, hususan Kata ya Uru Kusini; ni lini sasa TANESCO itarekebisha tatizo hilo kabisa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shally Raymond, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tatizo la kukatika kwa umeme halipo tu Morogoro na Kilimanjaro, limekuwepo kwa Tanzania nzima. Serikali tumechukua hatua. Mwanzoni tulianza na upungufu wa Megawati 421 wastani hapo. Mpaka kufikia leo tumefanikiwa kupunguza upungufu kwa wastani wa Megawati 218. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunachukua hatua.

Mheshimiwa Spika, nilieleza hapa kwamba Bwawa la Mwalimu Nyerere tumefikia 94.01% na tumeshaanza majaribio. Pia, nimesema hapa tumeongeza uzalishaji kwenye visima vetu vya Songo Songo pamoja na Madiba ili kuweza kuongeza gesi ili tuweze kupunguza changamoto hii ya upatikanaji wa umeme. Tayari tunafanya matengenezo kwenye mitambo yetu yote ili kuboresha hali. Nina uhakika Waheshimiwa mmeona hali ya upatikanaji wa umeme imeanza kutengemaa.

Mheshimiwa Spika, niwahakikishie tutaendelea kufanya kazi hii nzuri ili kuhakikisha tunaiondoa nchi katika changamoto ya umeme, ahsante. (Makofi)
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Uyui Makao Makuu yake ni Isikizya, kilometa 35 kutoka Tabora Mjini, na lipo tatizo kubwa kweli la umeme. Watumishi pale; DC na Wakurugenzi hawafanyi kazi kutwa nzima, umeme unakatika zaidi ya mara tano kwa siku; je, Serikali ina mpango gani wa kuweka umeme wa kudumu pale Isikizya? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Almas Maige, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, tayari Serikali tumechukua hatua katika Halmashauri ya Uyui na katika Mkoa mzima wa Tabora. Tumechukua hatua na tuna mradi unaendelea wa kujenga vituo vya kupooza umeme na line za kusafirisha umeme. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, baada ya mradi huo kukamilika ndani ya miezi 18, tatizo la kukatikakatika kwa umeme unaotakana na line ndefu kutoka Tabora Mjini mpaka Uyui mpaka kwenye Jimbo la Mheshimiwa Sitta tutakuwa tumelipunguza.

Mheshimiwa Spika, pia nimwelekeze Meneja wa TANESCO Mkoa wa Tabora ahakikishe ratiba wanazozipanga zinazingatia maeneo ambayo yanatoa huduma kwa wananchi hususan maeneo ambayo yanatoa hospitali, vituo vya afya pamoja na shule na maeneo mengine ambayo yanatoa huduma kwa wananchi, ahsante.
MHE. ANASTAZIA J. WAMBURA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, wakati wa Bunge la Bajeti, Serikali iliahidi kupeleka turbine ya megawati 20 kule Mtwara kama hatua za dharura za kupunguza tatizo la upungufu wa umeme ambalo linasababisha kukatikakatika kwa umeme; je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hiyo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Anastazia Wambura kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli tuliaahidi kupeleka hii taibai kutoka Ubungo kwenda Mtwara. Baada ya tathmini ya kina tulijirididha mtambo huu hautafanya kazi vizuri pale Mtwara. Tumeshaongea na Kampuni ya CSI juu ya kuzalisha umeme hapo na tumeshakamilisha, na tuna kituo cha kupoza umeme tunakijenga hiyari ambacho tunategemea kitakamilika ndani ya mwezi huu. Kikikamilika basi, umeme ambao utatolewa na Kampuni ya CSI utaweza kwenda kwenye Mkoa mzima wa Mtwara na Lindi na hivyo tutakuwa tumeondoa kabisa changamoto ya umeme kwa Mikoa miwili.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunawaomba Waheshimiwa Wabunge na wananchi wa Mtwara na Lindi watuvumilie kidogo mpaka mwishoni mwa mwezi huu tutakuwa tumekamilisha na kuwapatia umeme wa uhakika, ahsante.
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ipo dhamira ya Serikali ya kupeleka umeme vijijini kote na umeme kufika maeneo ya mbali kabisa kutoka Mkoa wa Singida ambako ndio sub-station kubwa ilipo eneo la Rungwa, lakini umeme unafika ukiwa faint na Serikali ilikuwa na dhamira ya kujenga kito cha kupoza umeme kwa maana ya sub-station katika eneo la Mitundu. Je, Serikali inaanza lini kujenga kituo cha kupoza umeme Mitundu, ili kusaidia wananchi, ili waweze kujiwezesha na viwanda vidogo vidogo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Massare, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli mpango huo upo, na nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunatafuta fedha na pili, mchakato huo wa upatikanaji wa fedha ukikamilika basi tutaanza kujenga kituo hiki cha kupoza umeme, ahsante.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Spika, kwa kuniona. Naomba kuuliza swali. Je, ratiba ya mgawo wa umeme katika Jimbo letu la Temeke umekuwa ni wa muda mrefu sana na ratiba yake haifuatilii kadiri ya ratiba zinavyokuja kwamba, umeme utakatika kuanzia muda fulani mpaka muda fulani, sasa umekuwa ni wa muda mrefu sana. Kuanzia jana mpaka leo saa hizi Temeke hatuna umeme, je, una tamko gani Waziri, ili kule Temeke waweze kutuletea umeme kulingana na mgawo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dorothy Kilave, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema, kidogo tumetengemaa kwenye suala la upatikanaji wa umeme, na kwa Mkoa wa Dar es Salaam tunafahamu maeneo mengi kwa sasahivi yanaweza yakapitisha hata siku mbili mpaka tatu bila kukatika kwa umeme. Kwa hili ambalo ambalo ameniambia Mheshimiwa Mbunge inaonekana ni suala ambalo ni specific, yaani ni mahususi. Naomba nilifuatilie, Mheshimiwa Mbunge, nikitoka hapa na nitakupatia majibu, ahsante. (Makofi)
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, tarehe 10 Agosti, 2021 TANESCO na STAMICO waliasaini makubaliano ya kuzalisha megawati 200 kutoka kwenye Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira; je, mpango huo umefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Jumbe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mpango huu bado upo na tunautekeleza kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.
MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, nini mpango wa Serikali katika kupeleka umeme katika Shule ya Sekondari ya Tawa katika Halmashauri ya Morogoro Vijijini.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Kalogeris, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tayari tuna miradi ambayo inaendelea kwenye kila Mkoa kuhusiana na kupeleka umeme. Nitafuatilia kuona kama Shule ya Sekondari Tawa ipo katika mipango ambayo tunayo, na kama hamna, basi tutafanya jitihada za ziada, ili kuhakikisha Shule ya Sekondari Tawa inapatiwa umeme, ahsante.
MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Spika, ahsante, je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha maeneo ya uzalishaji pamoja na hoteli za kitalii kama za Mkoa wa Arusha hazipati adha ya ukatikaji wa umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Swai, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeshatangulia kusema hapo awali, Serikali tunafanya jitihada mbalimbali kuhakikisha tunapunguza adha ya upatikanaji wa umeme. Na kwa kadiri ya mipango hii, nimhakikishie, maeneo haya ya uzalishaji yataendelea kuendelea kupata umeme wa uhakika kwa kadiri ambavyo tunaboresha upatikanaji wa umeme. Ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naishukuru sana Serikali kwa majibu mazuri, nami nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza: Je, ni mikoa mingapi hapa nchini hadi sasa haijaunganishwa na Gridi ya Taifa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili: Nafahamu kwamba Kigoma nayo ipo katika mpango wa kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia vituo vya Urambo na Ipole Sikonge. Sasa swali ni kwamba wananchi watalipwa lini fidia kwenye ile njia ya kutoka Tabora kwenda Ipole?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Kakunda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na mikoa ambayo haijaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, mikoa miwili ya Katavi na Rukwa ndiyo ambayo haijaunganishwa kabisa kwenye Gridi ya Taifa. Mikoa ya Mtwara, Lindi, Kigoma na Kagera imeunganishwa kidogo kwa Msongo wa kilovolt 33, lakini miradi inaendelea ili tuiunganishe kwa Msongo Mkubwa wa Kilovolt 220 na Kilovolt 400. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na fidia ambayo ameuliza Mheshimiwa Mbunge, tayari tumeshafanyia kazi na tunategemea ifikapo tarehe 30 mwezi huu wa Novemba, 2023 wananchi wataanza kulipwa, ahsante.
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Spika, naomba niulize maswali mawili madogo ya nyongeza.

Swali la kwanza; kwa kuwa Mvomero ni miongoni mwa Wilaya ambazo ziko vijijini; na kwa kuwa, Kijiji cha Madizini, Lusanga, Manyinga, Turiani, Kilimanjaro na Kichangani, havikuwahi kupata hadhi ya kisheria kuwa miji midogo; Mheshimiwa Naibu Waziri, huoni sasa kuna haja ya kutoa maelekezo wananchi wa vijiji hivi walipie umeme kwa shilingi 27,000 badala ya kulipia umeme kwa shilingi 321,000? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Wananchi wa Tarafa ya Turiani wamekuwa wanapata adha kubwa sana ya kukatika kwa umeme: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, huoni sasa ni wakati muafaka kutenga bajeti ya kwenda kuboresha miundombinu hii inayotoka Morogoro kuelekea Turiani ya kupeleka umeme kwa sababu miundombinu hii ni ya muda mrefu na imechakaa kwa kiwango kikubwa sana? Nashukuru sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jonas Zeeland, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Vijiji vya Madizini, Lusanga, Manyinga, Kilimanjaro, Kichangani na Turiani, vilitolewa tangazo, lakini havijaidhinishwa kama miji midogo. Kwa hiyo, niwaelekeze TANESCO Mkoa wa Morogoro kuendelea kuwa-charge wananchi 27,000 kwa maeneo haya yote ambayo hayajaidhinishwa kama miji kidogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la pili la line ya umeme inayotoka Turiani kwenda Kilosa na Gairo, mwaka huu wa fedha tumetenga bajeti ya matengenezo. Nikuahidi, kama matengenezo hayatakamilika, mwaka ujao wa fedha tutaendelea kutenga bajeti ili kuhakikisha tunaboresha miundombinu hii ili wananchi waendelee kupata umeme wa uhakika, ahsante. (Makofi)
MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona; ni lini Serikali itapeleka umeme kwenye vitongoji zaidi ya asilimia 70 katika Wilaya ya Kyerwa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver Semuguruka, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tayari Serikali tumeanza mpango wa kupeleka umeme kwenye vitongoji vyote vilivyobakia 36,000. Kwa kuanza, tumeanza kwa miradiya ujazilizi ambayo tumeshaweka wakandarasi na vilevile tunategemea kuendelea kutafuta wakandarasi kwa Mradi wa Vitongoji 15 kwenye kila jimbo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, vitongoji katika Jimbo la Kyerwa na vyenyewe vitafikiwa, ahsante. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujua, lini wananchi wa Jimbo la Bunda watapata umeme wa REA II C kwa vijiji 147?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mradi wetu wa II C tumetenga vitongoji 17 na kwa mradi ujao pia, vitongoji 15 Jimbo la Bunda litapata. Kwa hiyo, kwa kuanzia wataanza na vitongoji 32, ahsante.
MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa, tulisema mpaka mwezi wa 12 mwaka huu, vijiji vyote vitakuwa vimepata umeme na bado kuna vijiji kama Kiteto hatujapata umeme. Nini kauli ya Serikali kwa mpango huu wa mwezi wa 12 vijiji vyote vipate umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Edward Olelekaita, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli, Wakandarasi wote ambao tumewapatia mikataba ya kwisha Desemba 30, kupeleka umeme kwenye vijiji vyote, lazima wakamilishe kupeleka umeme kulingana na mikataba yao. Wale ambao walipewa ziada mpaka Juni, 2024 wata-cross kwenda 2024. Niwaelekeze Wakandarasi wote, yeyote ambaye hatahakikisha anamaliza mkataba wake kwa muda, bila sababu za msingi, hatutasita kuchukua hatua na kuweza kutokuendelea na mkataba wake ikifika Desemba, 30 mwaka huu, ahsante.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, kwa kuwa vitongoji vinavyopewa umeme ni vile ambavyo line za umeme kubwa tayari zilishapita, lakini kwenye jimbo langu kuna Kitongoji kama Nindi na Songeapori ambavyo viko mpakani na kuna changamoto kubwa za kiusalama.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuvisaidia vitongoji hivi viwili kwa jicho la kipekee? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Stella Manyanya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, vitongoji hivi viwili kwa kweli, vimekaa kimkakati. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa awamu hii ya ujazilizi utaweka addition scope ili vitongoji hivi viweze kufikiwa na umeme kwa umahususi wake, ahsante.
MHE. ALLY M. KASSINGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa nafasi ya swali la nyongeza:-

Mheshimiwa Spika, usambazaji wa umeme wa REA katika Kata ya Nanjirinji na Kata ya Likawage, umekwama kwa sababu ya mgogoro kati ya TFS pamoja na mkandarasi. Nini Kauli ya Serikali katika kutatua mgogoro huu ili wananchi wapate umeme huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ally Kassinge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mbunge nikuahidi, nitafuatilia suala hili ili kuhakikisha linatatuliwa kwa wakati na wananchi waweze kupata umeme katika maeneo yao, ahsante.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwenye vijiji sita vilivyobakia kwenye Tarafa ya Mikumi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Christine Ishengoma, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkandarasi katika vijiji hivi yuko site anaendelea na kazi. Nimhakikishie tu, ifikapo Juni, 2024 vijiji hivi vyote vitakuwa vimepatiwa umeme, ahsante.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kufanya rejea kwenye zana nzima ya local content ambayo imeweka takwa la kisheria kwamba, katika miradi wakandarasi kwa maana fursa za zabuni pamoja na ajira ziweze pia kupatikana kwa wale wanaotoka kwenye maeneo ya mradi (host community). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa msingi huo nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, katika hao 42 waliowasilishwa hapa na Serikali ambao amesema kwamba ni wakandarasi pamoja na watoa huduma. Ukweli ni kwamba hao 42 ni watoa huduma (local suppliers) na siyo wakandarasi (local contractors). (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, swali langu la kwanza. Je, Serikali ipo tayari kufanya tathmini ya kina, kuweza kuainisha maeneo na fursa ambazo wakandarasi wa Mkoa wa Kagera wanaweza wakapewa kinyume na ilivyo hivi sasa? Fursa zingine wamepewa wakandarasi kutoka mikoa mingine, kama Mwanza ili hali Mkoa wa Kagera wanao wakandarasi wanaoweza kufanya kazi hizo. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, Serikali kupitia Wizara ya Nishati wapo tayari kuja Mkoa wa Kagera ili kukaa na Uongozi wetu wa Mkoa wa Kagera chini ya Mkuu wa Mkoa wetu Mheshimiwa Fatma Mwasa, kujadili na kuona namna bora ya kuhakikisha kwamba Wakandarasi wa Mkoa wa Kagera wanapata fursa (local contractors), jambo ambalo litaweza kuhakikisha ulinzi wa mradi (host community) kinyume na ilivyo hivi sasa jambo ambalo linasikitisha, ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Neema Kachiki Lugangira, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kufanya tathmini, kwa kuwa Mradi huu wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima Uganda mpaka Chongoleani Tanga umefikia 32.6%. Nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunavyoendelea kwenye utekelezaji wa mradi, tutahakikisha wakandarasi wadogo ambao wanatokea maeneo ambapo mradi unatekelezeka wanaendelea kupewa fursa, kadri ambavyo tunaendelea na utekelezaji wa mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kutemebelea Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Mbunge nikuhakikishie, tutakuja ili kuweza kuona ni namna gani tunaweza tukashirikiana kwenye masuala haya ya msingi ambayo tunaamini yanagusa jamii ya watu wa Kagera. Lakini vilevile kwa kwa jamii zote ambazo mradi unatekelezeka tutahakikisha tunafanya hivyo kwa maslahi ya wananchi vile vile kwa maslahi ya utekelezaji wa mradi, ahsante.
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Spika, ukizingatia kwamba Bandari ya Dar es Salaam ni bandari ya nchi nzima siyo Dar es Salaam peke yake, lakini tumeona kwamba mafuta kwa maana ya petroli na dizeli zimekuwa rahisi zaidi Dar es Salaam kuliko maeneo mengine ya pembezoni. Kwa mfano, kwa Taarifa ya EWURA ya jana petroli Dar es Salaam ni 3,257 na dizeli 3,210 lakini ukienda Songwe ni 3,374 na dizeli ni 3,227 na maeneo mengine hali kadhalika.

Mheshimiwa Spika, maswali yangu mawili ya nyongeza; la kwanza; je, Serikali inategemea kumaliza lini tathmini hiyo ili utekelezaji huu uanze mara moja na wananchi walioko nje ya Dar es Salaam waepuke hiyo changamoto? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali imejipangaje kuhakikisha kwamba inatatua changamoto za nyuma kama ambavyo imezisema kwenye majibu yake ya leo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kumaliza tathmini yalikuwa ni maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, kufanya tathmini hii kwa haraka sana ili kuweza kujua kama tunaenda kwa mfumo huo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge suala hili ni la kipaumbele na tathmini itakamilika hivi karibuni na kisha tutaweza kufanya tathmini, ili kuweza kujua kama kweli tunaweza kwenda kwenye mfumo huo. Kwa hiyo, ni suala la kipaumbele kwa upande wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tathmini itatueleza namna ambavyo tulipata changamoto huko nyuma na kwa sasa tujipange vipi ili kuelekea kuwa na mfumo huu kama tathmini itatuelekeza hivyo. Ahsante.
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, naomba niulize swali moja dogo lenye sehemu (a), (b), (c), (d) kama ifuatavyo: -

SPIKA: Mheshimiwa ni (a) na (b) pekee. Kwa hiyo, katika hayo manne chagua mawili.

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante.

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuongea na wadau ili waweze kuondoa gharama kubwa iliyopo ya ununuzi wa mtungi wa gesi na gesi yenyewe, wakati mchakato wa kupunguza au kuweka ruzuku kwenye nishati ya gesi unaendelea kwa Serikali?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Shule ya Ufundi Mtwara Tech. imefunga mfumo wa gesi asilia suala ambalo limepunguza gharama kubwa ambayo ilikuwa inatumika wakati wakitumia nishati mbadala ya kuni na mkaa. Wakati wakitumia nishati hiyo walikuwa wanatumia shilingi milioni saba. Sasa baada ya kuweka mfumo wanatumia shilingi milioni 1.8.

(b) Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka mfumo huo kwenye Taasisi zote za Serikali ikiwemo Chuo cha Ualimu Matogolo na Shule za Sekondari zote katika Mkoa wa Ruvuma na nchi yote ya Tanzania? Ahsante sana. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa namna anavyofuatilia matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la ruzuku, ajenda ya nishati safi ya kupikia ni ajenda ya Mheshimiwa Rais mwenyewe. Wote mnakumbuka wakati wa mkutano wa COP28 Dubai, alizindua Mkakati wa Nishati ya Kupikia kwa Wanawake Afrika. Kwa hiyo, jambo hili tumelibeba kwa uzito sana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu ruzuku tayari tuna programu na miradi kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya tunayo programu ambapo mawakala wanawezeshwa kifedha ili kupunguza bei ya mitungi kwa wale wanunuaji wanaonunua gesi kwa mara ya kwanza. Tutaendelea kubuni miradi na kutafuta fedha ili kuhakikisha wananchi wanapata mitungi ya gesi kwa gharama rahisi zaidi.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusiana na kuwekeza mifumo ya gesi katika taasisi; kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) tumeshaanza mradi kwa ajili ya kuweka nishati hii safi ya kupikia ya gesi kwenye magereza, kambi za Jeshi pamoja na shule za msingi na sekondari. Tutaendelea kutafuta fedha ili kuhakikisha tumefikia taasisi nyingi zaidi.

Mheshimiwa Spika, kwa taasisi alizosema za Mkoa wa Ruvuma tutazingatia pia, ili kuhakikisha wanawekewa mifumo hii, ahsante.
MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Julai mwaka huu mkataba huu unatakiwa kusainiwa, nataka kujua majadiliano haya yatakamilika lini?

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Mkataba wa Songas kwa takriban miaka 20 umekuwa una changamoto kubwa sana eneo la shareholding structure. Sasa, kwa lengo la kuongeza uwazi na uwajibikaji pamoja na kwamba tuna TEIT, Je, serikali haioni kuna umuhimu wa ku-list shares zake kwenye stock market kwa sababu kule kuna scrutiny ya hali ya juu na hesabu zinawekwa wazi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na lini majadiliano yatamalizika, majadiliano haya tunategemea yatamalizika ifikapo mwezi wa tatu mwishoni. Kuhusiana na suala la pili la Serikali kuweka shares zake kwenye stock market, tumezingatia ushauri wa Mheshimiwa Mbunge na tutafanyia kazi wakati tunaendela na majadiliano, ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa vijiji 29 vilivyopo Jimbo la Ludewa vinahudumiwa na mzalishaji binafsi wa umeme na vinakabiliwa na changamoto ya bajeti kwa wazalishaji binafsi; na kwa kuwa Serikali imeshafanya kazi kubwa ya kutambua gharama za kufikisha umeme kwenye vitongoji na kuwasha umeme Mawengi na Milo: Je, nini ahadi ya Serikali kwa wananchi wale ikizingatiwa sasa tunaenda kwenye bajeti?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali moja la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na uzalishaji wa umeme kwenye vijiji hivyo 29, nafahamu kuna changamoto ya umeme kwa sababu ya wazalishaji ni wawezeshaji binafsi, lakini Serikali kupitia REA tunao mpango wa kuwawezesha wazalishaji binafsi wa umeme na utaratibu upo. Vilevile, tutaendelea kushirikiana nao kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata umeme wa uhakika. Pia, tunao mkakati wa kuhakikisha wananchi hawa wanapata umeme kupitia miradi ya Serikali ambayo tunayo na tutahakikisha hilo linafanyika haraka iwezekanavyo ili wananchi waondokane na kadhia hiyo, ahsante.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID: Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza hapa. Kwanza, ningependa kujua katika maeneo haya ambayo yanafanya utafiti wa gesi na mafuta ni leseni ngapi zimetolewa kwa ajili ya uchimbaji wa gesi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, napenda kujua Serikali ina mkakati gani wa kuendelea kunadi vitalu hivi ili kupanua wigo wa uwekezaji na kuweza kuthibitisha zaidi kiasi cha rasilimali hizi ambazo tunazo nchini?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hadi sasa kwa maeneo haya 84 ambayo tunafanya tafiti, tunazo jumla ya leseni 11 ambapo leseni nane ni za utafutaji na leseni tatu ni za uzalisahaji wa gesi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, kwa sasa hivi Wakala wa Udhibiti wa Mkondo wa Juu Wa Petroli (PURA) akishirikiana na Wizara tunao mkakati wa kuendelea kufanya maandalizi ya kunadi zabuni za vitalu kwa ajili ya kuleta wawekezaji zaidi ili kufanya tafiti na kuthibitisha rasilimali hii, ahsante.
MHE. MRISHO M. GAMBO: Mheshimiwa Spika, ukizingatia kwamba Bandari ya Dar es Salaam ni bandari ya nchi nzima siyo Dar es Salaam peke yake, lakini tumeona kwamba mafuta kwa maana ya petroli na dizeli zimekuwa rahisi zaidi Dar es Salaam kuliko maeneo mengine ya pembezoni. Kwa mfano, kwa Taarifa ya EWURA ya jana petroli Dar es Salaam ni 3,257 na dizeli 3,210 lakini ukienda Songwe ni 3,374 na dizeli ni 3,227 na maeneo mengine hali kadhalika.

Mheshimiwa Spika, maswali yangu mawili ya nyongeza; la kwanza; je, Serikali inategemea kumaliza lini tathmini hiyo ili utekelezaji huu uanze mara moja na wananchi walioko nje ya Dar es Salaam waepuke hiyo changamoto? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; Serikali imejipangaje kuhakikisha kwamba inatatua changamoto za nyuma kama ambavyo imezisema kwenye majibu yake ya leo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kumaliza tathmini yalikuwa ni maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, kufanya tathmini hii kwa haraka sana ili kuweza kujua kama tunaenda kwa mfumo huo. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge suala hili ni la kipaumbele na tathmini itakamilika hivi karibuni na kisha tutaweza kufanya tathmini, ili kuweza kujua kama kweli tunaweza kwenda kwenye mfumo huo. Kwa hiyo, ni suala la kipaumbele kwa upande wa Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vilevile tathmini itatueleza namna ambavyo tulipata changamoto huko nyuma na kwa sasa tujipange vipi ili kuelekea kuwa na mfumo huu kama tathmini itatuelekeza hivyo. Ahsante.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza napenda kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa mkakati wake wa kuhakikisha kwamba sasa tunakwenda kupata nishati safi na salama ya kupikia. Ni jambo kubwa, tunampongeza sana na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamelipokea.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu ni kwamba, kwa kuwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamehamasika na wako tayari katika matumizi ya nishati safi ya gesi ya kupikia, lakini kwa kuwa changamoto kubwa ni gharama ya hiyo gesi na Serikali imeonesha mipango ya kusambaza gesi hiyo ambayo ina gharama nafuu kwa wananchi, je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuelekeza nishati hiyo au mabomba hayo kwenye maeneo yenye wananchi wengi kama Kawe, Mwenge, Mbagala, Manzese na maeneo mengine, badala ya ku-base kwenye eneo hilo hilo la Mbezi Beach na Mikocheni peke yake?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Tunao mpango wa kuhamasisha matumizi ya gesi asilia nchini, na kwa sasa hivi tunao mkakati wa kupeleka gesi kwenye nyumba takribani 10,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba maeneo hayo ambayo ameyataja yenye watu wengi yatafikiwa na huduma hii ili waweze kutumia gesi kwa gharama nafuu zaidi kwa sababu gesi hii inayounganishwa majumbani ina unafuu zaidi kuliko gesi ile ya LPG ya mitungi. Ahsante.
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, Serikali imehamasisha matumizi ya nishati safi na Watanzania wengi hasa wa vijijini wamehamasika, lakini bei, kwa maana ya gharama ya ujazaji wa gesi ni kubwa sana. Nataka kujua, nini mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inatoa ruzuku ili kupunguza gharama za gesi kusudi wale wananchi maskini wa kijijini waache kutumia kuni na mkaa, watumie gesi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunao mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia ambao tunaenda kuukamilisha hivi karibuni ili kuweka mkakati wa kukabiliana na changamoto zote ambazo zinawazuia wananchi wasiweze kutumia gesi katika kupikia. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, baada ya mkakati huu kukamilika, tutakuwa na mikakati madhubuti wa kuwawezesha wananchi wote kutumia gesi safi ya kupikia ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni.
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kule Tunduru Kusini na Jimbo langu la Nanyumbu tunao madereva pamoja na mafundi sanifu ambao sasa hivi wapo katika ajira za muda kati ya miaka mitano na miaka saba. Je, wizara ipo tayari sasa katika ajira zinazokuja kuwafikiria madereva hawa ambao wamekuwa muda mrefu katika shirika? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, jukumu la kupeleka umeme vijijini lipo chini ya REA. REA jukumu lake ni kupeleka umeme vijijini na baadaye kuwaachia TANESCO kuwaunganishia wateja. Je, Serikali haioni wakati umefika REA baada ya kupeleka umeme vijijini iwaunganishie wateja ndipo iwakabidhi kwa TANESCO wateja wote badala ya kuwaachia TANESCO kufanya kazi ya kuwaunganishia wateja hao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na ajira kwa ajili ya madereva, kwanza niwapongeze Waheshimiwa Wabunge, Mheshimiwa Mhata na Mheshimiwa Mpakate, kwa kazi nzuri wanazofanya katika majimbo yao. Kuhusiana na ajira za vibarua hawa, kama wizara tunathamini sana mchango wa wafanyakazi wetu vibarua hususani mafundi na madereva. Nataka niwahakikishie kwa kuwa ni wafanyakazi wetu ambao wanafanya kazi kwa jitihada kubwa sana kulitegemeza shirika letu, tutahakikisha ajira zinapotoka wanazingatiwa ipasavyo kulingana na sheria na taratibu za utumishi wa umma. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la REA kuendelea na kuunganisha wateja pale ambapo miradi inakamilika. Ushauri wa Mheshimiwa Mbunge tumeupokea na tutauchakata kuona kama unatekelezeka na kama unatekelezeka hatutasita kuufanyia kazi, ahsante. (Makofi)
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wanaotumia umeme wa REA vijijini wamekuwa wakipata changamoto kubwa sana za huduma za haraka pale inapotokea hitilafu ya umeme na hii ni kwa sababu ya mafundi wengi wanakaa Makao Makuu. Swali langu, je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuajiri mafundi hawa maalum kwa ajili ta kitengo cha dharura na kuwasambaza huko vijijini ili wananchi hawa waweze kupata huduma za haraka? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa mawazo mazuri. Nataka nimhakikishie kuhusiana na suala la huduma kwa wateja tayari tumeshaanza kufanyia kazi kuhakikisha tunakitegemeza kitengo hiki ili kiweze kuwa na huduma nzuri kwa wateja. Kuhusiana na suala la mafundi tayari tumekuwa tukiongeza viunga kwenye maeneo ya mbali ili wananchi waweze kupata huduma za uhakika. Kwenye suala la mafundi, kuongeza mafundi Mheshimiwa Mbunge tumelipokea na tutaendelea kulifanyia kazi kuhakikisha wananchi wanapata huduma nzuri. (Makofi)
MH. ALLY J. MAKOA: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali yenye kutupa matumaini naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; baada ya Serikali kutupatia katika kipindi hiki hiyo mitaa 15, vipi sasa kuhusiana na ile mitaa ambayo haikutajwa hapo ambayo imebaki mfano Chora, Damai, Ngereli pamoja na Hurumbi na yenyewe mpango wao ukoje?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; je, ni lini Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kufuatana na mimi twende Kondoa kwa ajili ya kuona yale mazingira na namna watu wanavyohitaji huo umeme. Nashukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kazi nzuri anayoifanya kwenye jimbo lake. Katika mitaa ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge tutazingatia katika bajeti inayofuata kuona kama mitaa mingine imebakia tunaweza kuiingiza baadhi ili kuweza kuwafikishia wananchi huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na kuambatana na yeye jimboni, tutapanga na Mheshimiwa Mbunge siku za hivi karibuni ili tuweze kwenda kuona utekelezaji wa miradi katika jimbo lake, ahsante. (Makofi)
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru swali langu la msingi linauliza ni lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nina maswali mawili ya nyongeza; swali la kwanza narudia, ni lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, nini mpango wa Serikali katika kunusuru Mji wa Mpanda dhidi ya katikakatika ya umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia mradi huu wa kufikisha umeme wa Gridi ya Taifa Katavi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na lini mradi huu utakamilika? Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Wana-Mpanda na watu wa Katavi wote kwa ujumla. Suala la kupeleka Gridi ya Taifa Mpanda na Katavi ni suala la kipaumbele chini ya Awamu ya Sita kuhakikisha mikoa yote ambayo haijaunganishwa na Gridi ya Taifa inaunganishwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunamwomba kwa niaba ya watu wa Katavi watuvumilie kidogo, mradi unaenda vizuri na kwa maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati tunasimamia kwa weledi mkubwa sana na nina imani miezi michache ijayo tutakuwa tumekamilisha hii njia ya kusafirishia umeme, uzuri kituo cha kupooza umeme kimeshafikia 98%. Kwa hiyo, ni njia tu hii ya kusafirishia umeme itakamilika hivi karibuni na watu wa Katavi watapata umeme wa Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, tunaelewa umuhimu wa umeme wa uhakika Mpanda na Katavi kwa sababu wananchi wa Katavi ni wafanyakazi wazuri sana. Sasa kwa hatua za haraka, kwa maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati leo mafundi wetu watafungua mtambo wa megawati moja Biharamulo ili kuweza kuupeleka Mpanda pale ili kuweza kuongeza uzalishaji kwa sababu mahitaji ni megawati saba, lakini tunazalisha karibia megawati 6.15 tutaongeza megawati moja ili tuweze kupunguza mgao Katavi pamoja na Mpanda, ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, Serikali inatambua kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kukamilika bila kuwalipa wananchi wa Sikonge fidia ya shilingi bilioni 2.2 ambayo bado Wizara ya Fedha haijaipa Wizara ya Nishati hizo hela.

Sasa ni lini Wizara ya Fedha itatoa fedha hizo ili Wizara ya Nishati walipe fidia hiyo ili kukamilisha huo mradi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la fidia la wananchi hawa wa Sikonge tayari tunalifanyia kazi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tupo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kufanya malipo haya na uzuri Wizara ya Fedha wameshaji-commit kwamba wanatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hawa. Tunaomba wananchi wa Sikonge, Tabora na yale maeneo ambayo wanadai fidia katika mradi huu wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Mpanda waendelee kutuvumilia, tutalipa fidia hiyo kwa sababu tayari tulishaji-commit kwamba tutalipa, ahsante.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Naibu Spika, naishukuru Serikali kwa majibu yake.

Kwa kuwa maeneo yote ya mitaa iliyotajwa na Mheshimiwa Naibu Waziri maeneo mengi makazi ya watu yamerukwa na uingizaji wa umeme; je, Serikali haioni kuwa sasa ni wakati mwafaka wa kuingiza yale maeneo ya huduma ya afya, elimu na maeneo ya makanisa kuingizwa kwenye mradi huu wa kuingiza umeme kwa shilingi 27,000?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa tayari katika eneo la Mbulu Mjini, maeneo mengi yaliyopelekewa huduma ya umeme yamekuwa na changamoto nyingi ya wananchi kushindwa kuingiza umeme kwa yale yaliyofikiwa.

Je, Serikali haioni kuwa ni wakati mwafaka kutazama upya nchi nzima maeneo yote ambayo wananchi wameshindwa kuingiza umeme kwa gharama kubwa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge, kwanza, kwenye upande wa maeneo ambayo yamepitiwa na umeme, lakini taasisi hazina umeme, tayari nimeshajibu kwenye jibu la msingi kwamba, mitaa ile 12 iliyobakia tunao mkakati wa kupelekea umeme kupitia mradi wa vitongoji kwa mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile niwasihi REA waweze kufanya tathmini kwenye maeneo haya na kuweza kuona kama maeneo haya yanaweza yakaingizwa kwenye Mradi wa Peri Urban na kisha taasisi zilizopo katika maeneo haya na yenyewe yaweze kupata umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, kwenye maeneo yenye sura ya vijiji lakini yapo mijini tayari Wizara ya Nishati kupitia Shirika la Umeme (TANESCO) tumeshafanya mapitio kwenye maeneo 1,570 ya maeneo ambayo yana sura ya vijiji, lakini yapo mijini ili kuweza kuona uwezekano wa kutoka shilingi 320,000 hadi shilingi 27,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, maeneo yake ambayo yana picha hiyo na yenyewe tutayapitia kuweza kuona kama yanakidhi vigezo vya kuingia kwenye utaratibu huu wa shilingi 27,000. Ahsante. (Makofi)
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Katika Jimbo la Tarime Vijijini maeneo ya Vijiji vya Nyangoto, Kerende, Mjini Kati, Nyabichune na Nyamwaga wananchi wangu wanalipia umeme shilingi 320,000 kinyume na sera ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, nini kauli ya Serikali wananchi wapate umeme kwa bei nafuu ambayo imeelekezwa vijijini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye maeneo haya ambayo ameyataja Mheshimiwa Mbunge, tutayapitia kuona kama yapo kwenye yale maeneo 1,570 ambayo tumeshayaainisha na kama hayapo tutayafanyia tathmini kuweza kuona kama na yenyewe yanaweza kuingia katika mpango huo ili wananchi waweze kupata huduma ya kuunganisha umeme kwa shilingi 27,000. Ahsante. (Makofi)
MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itawapatia umeme wananchi waliopo katika Mtaa wa Msisina, Msalagala na Kisowele, Iringa Mjini kwa sababu maeneo hayo yalikuwa katika Jimbo la Ismani? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, mitaa hii ambayo ameitaja Mheshimiwa Mbunge ya Msisina, Msalagala na Kisowele itaenda kupatiwa umeme kupitia mwaka wa fedha 2024/2025. Ofisi yetu ya TANESCO - Mkoa wa Iringa, imeshaweka kwenye mpango huo, lakini vilevile katika mitaa hiyo kuna Mtaa mmoja pia wa Kipululu na wenyewe hauna umeme. Tulishawaelekeza TANESCO kupitia Ofisi ya Mkoa waweze kutenga special fund ili mitaa yote hii minne ambayo haina umeme waweze kupatiwa umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mitaa hii tayari ipo kwenye mpango na yote itapata umeme kwa mwaka ujao wa fedha, ahsante. (Makofi)
MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa nishukuru Serikali kwa kutupatia umeme kwenye vijiji vyote 70, lakini changamoto kubwa iliyopo ni size ya transformer zilizofungwa. Wamefunga size ya transformer kVA 50 na mahitaji ni makubwa, wananchi wana viwanda vya alizeti na viwanda vya kuchomelea. Swali la kwanza; je, Serikali haioni kuna haja ya kufunga transformer za kVA 200 mpaka 345 ili kupata umeme wa uhakika?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; nimesikia Serikali kwamba wako kwenye hatua za kutafuta wakandarasi kwa ajili ya kutengeneza kwenye vitongoji. Kumekuwa kuna kasumba miaka yote ya kupata wakandarasi wasiokuwa na sifa. Nataka kujua Serikali wamejipanga vipi kuhakikisha katika eneo la due diligence hawafanyi makosa? Nakushukuru. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, tumepokea maoni ya Mheshimiwa Mbunge na maoni ya Waheshimiwa Wabunge wengi na kwa hivyo tumefanyia kazi, kuanzia mwaka huu unaokuja wa fedha 2024/2025, tutaongeza ukubwa wa transformer. Zitakuwepo transformer za ukubwa wa KVI 50, KVI 100 na KVI 200 na zitafungwa kulingana na mahitaji ya eneo husika. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, jambo hilo tumelipokea na lipo tayari kwenye utekelezaji.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na wakandarasi wanaosuasua kwenye miradi; maelekezo ya Serikali, kupitia Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, yalishatoka. Hatutawavumilia wakandarasi wote wanaotekeleza miradi kwa kusuasua na kutoendelea mbele, kupitia Taasisi zetu za TANESCO na REA hatutawapatia kazi wakandarasi wanaosuasua katika miradi yetu, ahsante.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Spika, ahsante, Wilayani Rungwe vijiji saba mpaka sasa hivi havijafikiwa na umeme wa REA. Vijiji hivyo ni Mpindo, Kata ya Bulyaga; Isumba Kata ya Kinyala; Kyobo Juu, Kata ya Ikuti; Ngumbulu, Kata ya Isongole; Mpombo, Kata ya Lupepo; Isabula, Kata ya Kisiba; na Kasanga, Kata ya Mpombo. Je, ni lini vijiji hivyo vitapata umeme wa REA? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge, katika vijiji vyote hivi saba vilivyopo katika Jimbo la Rungwe mkandarasi yuko site. Namhakikishia kwamba, tutaongeza usimamizi kuhakikisha vijiji hivi vinapatiwa umeme kulingana na mikataba yetu ambayo ni Juni, mwaka huu. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge, tutasimamia vizuri na tutahakikisha wananchi wa Jimbo la Rungwe wanapata umeme katika vijiji hivi saba, ahsante.
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kumaliza kuweka umeme katika vijiji vyote 70 vya Mkalama. Naomba commitment ya Serikali kuhusu vitongoji 15 ambavyo nimeviombea umeme, ni lini umeme utawashwa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, vitongoji hivi 15 katika Jimbo la Mkalama na katika majimbo yote, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge na ninalitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, tupo katika hatua za manunuzi. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa, hivi karibuni tutakamilisha na tutaenda kwenye utekelezaji wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 katika kila jimbo, ahsante.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itasambaza umeme kwa bei ya vijiji katika Kata ya Katindiuka, kama ilivyokuwa imeahidi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, katika maeneo yote ambayo tunatekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini bei ya kuunganisha umeme ni 27,000. Katika maeneo ya vijiji-miji ambako bei ni zaidi ya hiyo, tunaendelea kufanya mkakati wa kuona namna ambavyo tunaweza tukaenda kwa ajili ya ku-incorporate hata wananchi ambao hawana uwezo wa kulipa 321,000, lakini katika maeneo yote tunayotekeleza miradi yetu ya vijiji bei ya kuunganisha umeme ni 27,000 na tutaendelea kufanya hivyo, ahsante.
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, je, ni lini Serikali itamaliza kusambaza umeme katika vijiji vilivyobaki katika Mkoa wa Singida?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, katika vijiji ambavyo vimebakia katika Mkoa wa Singida wakandarasi wanaendelea na kazi ya kufikisha umeme kwenye vijiji hivyo. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kusimamia kwa weledi mkubwa sana ili vijiji vilivyobakia viweze kupata umeme kwa wakati. Ahsante.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, zipo shule za sekondari ambazo bado hazijapata umeme. Pamoja na shule hizo, mwaka jana, 2023 niliomba Shule ya Sekondari Kimenyi ipatiwe umeme, lakini mpaka sasa shule hiyo iliyopo Kata ya Kagera Nkanda haijaweza kupatiwa umeme. Ni lini sasa sekondari hiyo ya Kimenye itapelekewa umeme? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili. Mkoa wa Kigoma una wilaya saba. Kati ya wilaya hizo, ni wilaya nne tu ambazo zimepatiwa umeme wa gridi ya Taifa. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika wilaya zilizosalia kwa maana ya Kigoma Vijijini, Kigoma Mjini na Uvinza? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kupeleka umeme katika Shule ya Kimenyi iliyopo katika Kijiji cha Kagera Nkanda, tayari mkandarasi ambaye anatekeleza mradi wa kupeleka umeme katika Kijiji cha Kagera Nkanda yupo site. Sasa nimwelekeze Meneja wa Mkoa wa Kigoma ahakikishe anatenga fungu la ziada kwa sababu shule hii ipo mita 900 kutoka kwenye njia ya umeme anayojenga mkandarasi. Kwa hiyo, pale ambapo njia hii itakamilika, basi watenge fungu la nyongeza kwa ajili ya kuunganisha umeme kwenda kwenye shule hii ya sekondari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kupeleka umeme wa gridi katika hizi wilaya tatu, Serikali inatekeleza mradi wa kupeleka umeme wa gridi katika Mkoa wa Kigoma ambapo mradi huu kwa sasa umefikia asilimia 94. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa mradi unaendelea vizuri sana na tunajenga njia ya umeme ya kilovoti 400 kutoka Nyakanazi hadi Kidahwe. Umeme ukifika Kidahwe utaenda Kigoma Mjini pamoja na Uvinza kwa kadiri ya utekelezaji wa mradi ambao upo kwa wakati.

Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie wananchi wa Kigoma kuwa mradi wa kupeleka gridi ya umeme Kigoma unaendelea vizuri sana na utamalizika kwa wakati. (Makofi)
MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itakamilisha zoezi la kupeleka umeme katika shule na taasisi zote zikiwepo za dini katika Mkoa wa Lindi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika miradi ambayo inaendelea, ni maelekezo ya Serikali kwamba shule na taasisi ambazo zipo mita chache katika maeneo ambayo tunapitisha njia za umeme, basi taasisi hizi ziweze kuunganishwa. Zile ambazo zipo umbali wa zaidi ya mita 900 kwenda nyuma, ni maelekezo kwamba Ofisi zetu za Mikoa na Ofisi za TANESCO za kimkoa zihakikishe zinatenga bajeti ya ziada na nyongeza kuhakikisha zinapeleka umeme katika taasisi hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni maelekezo ya Serikali kuhakikisha taasisi zote za msingi zinapata umeme kwa ajili ya ustawi wa watu wetu na shughuli za maendeleo za wanajamii.
MHE. DOROTHY G. KILAVE: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini umeme unaopita eneo la Uhasibu utakamilika ili Jimbo la Temeke tuweze kupata umeme usiokatikakatika tena?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Kurasini ni kweli limekuwa lina changamoto ya umeme, lakini tuna ujenzi wa laini ya chini ya umeme kwa ajili ya kuboresha umeme katika Wilaya ya Ilala. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba mradi unaendelea vizuri sana na upo katika hatua za mwisho za umaliziaji. Pindi utakapokamilika, wananchi wa jimbo lako watapata umeme wa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakuhakikishia tunasimamia mradi huu kwa weledi mkubwa sana kuhakikisha unakamilika kwa wakati.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itapeleka umeme kwenye vijiji vilivyobakia kwenye Wilaya ya Kilosa pamoja na Morogoro Vijijini? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI:Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Kilosa na Morogoro Vijijini wakandarasi wapo site. Tunaendelea kuwahimiza wakandarasi kutekeleza miradi hii kwa weledi kuhakikisha wananchi wanapata umeme kwa wakati na kuhakikisha wanakamilisha majukumu yao kulingana na mikataba yao, ahsante.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Jimbo la Muleba Kusini ina vijiji vitatu ambavyo havijapata umeme; Kijiji cha Kiholele, Burungura na Bihanga. Ni lini Serikali itapeleka umeme katika vijiji hivyo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika hivi vijiji vitatu kwenye Jimbo la Mheshimiwa Dkt. Kikoyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba mkandarasi yupo site. Tutaendelea kumsimamia ili aongeze kasi kuhakikisha vijiji hivi vinawaka umeme.
MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri yaliyotolewa na Serikali nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa hii gesi asilia (CNG) sasa inatumika kwenye gari nyingi, je, hamuoni kuwa sasa ni wakati mwafaka wa kufungua vituo njiani ili mtu anapokuwa anasafiri kutoka Dar es Salaam kuja hapa kuwe na vituo maalumu kabisa vya gesi asilia ambako mtu anaweza kujaza kwenye gari lake?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Askofu Josephat Gwajima. Ni kweli kwamba Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi tumeanza mkakati wa kutafuta namna ya kuwa na vituo kwa gari binafsi kuanzia Dar es Salaam mpaka Dodoma kwa awamu ya kwanza. Tayari tumekwishaanza kuwa na mkakati huo na tayari wadau wa sekta binafsi wameshaanza kujitokeza kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa vituo barabarani kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma. Hata kwa upande wa magari ya Serikali tayari TPDC imeanza kuongea na Bohari za GPSA ili kuongeza vituo vya CNG kwenye hivi vituo vya bohari kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ili pia hata magari ya Serikali nayo yakiwa yamekwishabadilishwa yaweze kujazwa gesi kutokea Dar es Salaam – Dodoma ambapo ndiyo njia kuu ya magari haya kwa kiasi kikubwa yanapopita.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa kwa pande zote mbili za magari binafsi pamoja na magari ya Serikali tumekwishaanza kulifanyia kazi suala hili ili kuongeza idadi ya magari ambayo yanatumia CNG, ahsante.
MHE. MUNIRA MUSTAPHA KHATIB: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa Serikali ina mpango kuwa ifikapo mwaka 2030/2034 wananchi wote wawe wanatumia nishati safi na salama.

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wanasambaza mabomba kwenye nyumba ili ifikapo mwaka 2030/2034 wananchi wote wawe wanatumia nishati safi na salama? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, na nimshukuru Mheshimiwa Munira kwa swali zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari Serikali tulikwishaanza awamu ya kwanza ya majaribio kwa ajili ya kuweka miundombinu kwenye maeneo ya Mikocheni pamoja na Mbezi. Aidha, kwa sasa tayari tumeanza mchakato wa kuendelea kuwekeza katika miundombinu hii kwa maeneo mengi zaidi hususan kwa Mkoa wa Dar es Salaam kwanza ili wananchi wengi waweze kutumia gesi nyumbani, kwa sababu ni ukweli kwamba gesi ya nyumbani kwa miundombinu ina bei nafuu kuliko ile ya mitungi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tayari mikakati ipo ya kuendelea kuongeza miundombinu nyumbani ili wananchi wengi waweze kutumia gesi nyumbani na tufikie azma ya Mheshimiwa Rais ya kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034. (Makofi)
MHE. TARIMBA G. ABBAS: Mheshimiwa Mwenyekiti, niipongeze Serikali kwa juhudi zake za kuleta teknolojia ya gesi katika gari, lakini sasa hivi teknolojia imepanda sana kiasi kwamba kuna magari ya kutumia umeme.

Je, Serikali ina juhudi gani katika kuangalia vilevile uwezekano wa kuhamasisha kuleta magari ya umeme nchini ili kuendelea kupunguza matumizi ya mafuta na gesi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nishukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali inaangalia njia mbalimbali kwa ajili ya kuhamasisha matumizi mbadala, kwa sababu tunaamini ajenda zote hizi zinalenga kwenye kuongeza jitihada za kupambania suala la mazingira. Kwa hiyo, kama ambavyo tunawekeza kwenye nishati ya gesi kwenye magari ndivyo ambavyo tumeshaanza mikakati ya kuweka pia mazingira wezeshi kwa ajili ya kuleta magari yanayotumia umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nikuhakikishie Mheshimiwa Mbunge jambo hili pia Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu kuanzia mwaka jana alishalianza na sisi tunaendelea nalo ili kuhakikisha kwamba tunaweka mazingira wezeshi kwa ajili ya matumizi ya magari ya umeme, ahsante.
MHE. MOHAMED SAID ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, hapa katika majibu yake ya msingi Mheshimiwa Naibu Waziri anasema Serikali inahamasisha kwa kupunguza kodi magari ambayo yanatumia gesi, lakini magari yaliyopo nchini ni mengi sana na yanahitaji kutumia gesi. Gharama za ku-install mitambo ya gesi kwenye magari ni kubwa sana, ni takribani shilingi milioni 2.5. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kwamba gharama hizi zinashuka?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nishukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, gharama hizi ziko juu kidogo ndiyo maana Serikali tumeendelea kuhamasisha watu wengi zaidi na kampuni nyingi zaidi ziweze kuwekeza katika kuwa na karakana. Tunakubali mwanzo huwa ni mgumu sana, lakini tunakoelekea ni kuzuri kuliko tulikotoka. Mwaka 2021 wakati tunaanza kuhamasisha matumizi ya gesi kwenye magari, kwa wastani tulikuwa tuna-convert takribani magari 1,159, leo tunavyoongea tuna magari 5,100 katika mwaka huu wa 2022/2023. Hii ni kwa sababu karakana zimeongezeka kutoka ile moja ya DIT hadi nane. Kwa hiyo, wawekezaji wengi wanavyokuja ndivyo ambavyo gharama inavyoendelea kushuka kutokana na ushindani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tunaendelea kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza zaidi na kuja na teknolojia bora zaidi. Tukiwa na karakana nyingi zenye teknolojia ambayo ni bora gharama zitapungua. Kwa hiyo, tunaendelea kulifanyia kazi ili kuhakikisha kuwa gharama hizi zinapungua, ahsante.
MHE. REHEMA J. MIGILLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipa nafasi na kwanza tuipongeze Serikali kwa kuanzisha hii teknolojia ya kutumia gesi kwenye magari yetu, lakini magari mengi yanayotumia hii gesi ni magari ya petroli tu.

Je, Serikali ina mpango upi wa kuhakikisha kwamba magari yanayotumia dizeli nayo yaanze kutumia gesi kwani tunaona Kampuni ya Dangote magari yake yanatumia dizeli, lakini wamefanya installation ya mitungi ya gesi, mpango ni upi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tumeanza programu hizi na kwa sasa hivi tulikuwa tuna vituo vitano tu, lakini ili kuelekea kuwa na vituo vingi zaidi tumeanza mazungumzo na hao wawekezaji wa kwenye sekta binafsi ili kuhakikisha wanaona namna ya kuwa na mifumo yote miwili, yaani petroli pamoja na dizeli. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tunaendelea kulifanyia kazi ili kupata namna ya kuyafanya magari yanayotumia dizeli nayo kuweza kubadilishwa mfumo.
MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali na naipongeza Serikali kwa namna ambavyo inafuatilia vizuri na kukamilisha matatizo na kero za umeme.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilayani Kyela kuna shida za vijiji ambavyo havijafanikiwa kupata umeme wa REA. Sasa je, ni lini Serikali itakamilisha vijiji hivyo ambavyo vipo kwenye Wilaya ya Kyela pamoja na kule Wilaya ya Mbarali na Wilaya ya Mbeya Vijijini? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji ambavyo hivi vimebaki katika hizi wilaya ambazo amesema Mheshimiwa Mbunge, ni vijiji vichache na wakandarasi wapo site. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa tunasimamia kwa weledi mkubwa sana kwa sababu muda wa kumalizika huu mradi ulishafika, kwa hiyo, wakandarasi tumewahimiza kuhakikisha wanamalizia miradi hii na vijiji viweze kuwashwa ili tuweze kumaliza kabisa mradi huu. Kwa hiyo, tunafuatilia kwa karibu na tutaendelea kufuatilia kuhakikisha kwamba vijiji hivi sasa vinakamilika na vinawashwa umeme, ahsante. (Makofi)
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyouliza swali la msingi, Kijiji, Kata ya Kinyala ni kata ambayo ni kubwa sana na kiukweli transformer mpaka sasa haijafika. Mheshimiwa Naibu Waziri, ninajua weledi wako wa kazi, ni lini mtatuletea transformer hiyo ili watu hawa wa Kinyala waweze kupata umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge baada ya hapa nitafuatilia kwa Meneja wa Wilaya na Meneja wa Mkoa, kuhakikisha kama kweli transformer haijafika basi mkandarasi aweze kuharakisha, aweze kupeleka na wananchi hawa waweze kupata umeme kwenye hivi vijiji ambavyo miradi inaendelea, ahsante. (Makofi)
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza: Je, Serikali kwa kuonyesha mfano ina mpango gani sasa wa kubadilisha magari ya Serikali kutoka matumizi ya mafuta kwenda gesi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili: Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kusambaza karakana ya kubadilisha mfumo wa matumizi ya mafuta kwenda kwenye matumizi ya gesi katika mikoa yote Tanzania? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante na nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Spika, kwanza kuhusiana na mkakati wa Serikali kubadilisha magari ya Serikali kwenda kwenye mifumo ya gesi, kama Serikali kwa kweli jambo hili tunalihitaji sana kwa sababu lina manufaa makubwa sana ikiwemo kupunguza gharama na matumizi. Tumeshatafuta mtaalamu mshauri ambaye kwa sasa hivi atatusaidia kufanya study za kimazingira pamoja na kuweka michoro ya kihandisi ili kufanya tathmini kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma pamoja na vituo vya GPSA ili kujua tunaongezaje suala hili ili magari haya yakishabadilishwa mfumo yaweze kujaziwa gesi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari Serikali tumeanza kulifanyia kazi suala hili.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusiana na karakana, kwa kweli kwa kushirikiana na sekta binafsi tunao mkakati mahsusi wa kuhakikisha mpaka itakapofika Disemba, 2025 tutakuwa na zaidi ya vituo 30.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli jambo hili kama Serikali tumelibeba kwa dhati kwa ajili ya kuendeleza jitihada za Mheshimiwa Rais za kutumia nishati safi, si tu ya kupikia bali pia katika maeneo mengine kwa ajili ya manufaa kwenye mazingira yetu na manufaa mengine ya kiuchumi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari tumeanza kwa Dar es Salaam kwa ajili ya vituo na karakana na tutafanya vivyo hivyo kwa kadiri muda unavyokwenda kwa ajili ya mikoa mingine, ahsante.
MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kasi ya usambazaji wa vituo hivi ni ndogo sana ukilinganisha na hamasa iliyopo. Je, Serikali inatuambia nini...

SPIKA: Mheshimiwa Agnes, subiri.

Mheshimiwa Waziri keti, anayeuliza yuko nyuma yako, Mheshimiwa Agnes Marwa.

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, kasi ya usambazaji wa vituo hivi ni ndogo sana ukilinganisha na hamasa iliyopo, je, Serikali inatuambia nini katika hili hasa katika Mkoa wa Mara?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kasi ya usambazaji, ni kweli hili tuliliona na tulianza kwa kurahisisha vigezo vya kupata vibali kwa ajili ya wawekezaji binafsi ili waweze kuwekeza kwa urahisi. Kwa hiyo, kwa sasa hivi tumebadilisha mifumo na kuongeza kasi kwenye kutoa leseni kwa ajili ya kuanzisha vituo ili kuzialika sekta binafsi ziweze kushiriki katika uwekezaji huu kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi kwa ajili ya kutatua changamoto ambayo tunayo, tumeagiza vituo vya kuhamishika vya gesi (Mobile CNG Stations) kwa ajili ya kutatua changamoto hii kwa uharaka. Vilevile tunajenga vituo zaidi ya vitano pale Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wanaendelea kupata huduma hii kwa uharaka.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa kweli tumeongeza kasi kwenye kutoa leseni kwa haraka na kwenye kujenga, sisi Serikali pia kwa kushirikiana na sekta binafsi, ili tuweze kutoa huduma kwa haraka, ahsante.
MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali langu la kwanza: Je, Serikali kwa kuonyesha mfano ina mpango gani sasa wa kubadilisha magari ya Serikali kutoka matumizi ya mafuta kwenda gesi? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili: Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kusambaza karakana ya kubadilisha mfumo wa matumizi ya mafuta kwenda kwenye matumizi ya gesi katika mikoa yote Tanzania? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante na nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Spika, kwanza kuhusiana na mkakati wa Serikali kubadilisha magari ya Serikali kwenda kwenye mifumo ya gesi, kama Serikali kwa kweli jambo hili tunalihitaji sana kwa sababu lina manufaa makubwa sana ikiwemo kupunguza gharama na matumizi. Tumeshatafuta mtaalamu mshauri ambaye kwa sasa hivi atatusaidia kufanya study za kimazingira pamoja na kuweka michoro ya kihandisi ili kufanya tathmini kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma pamoja na vituo vya GPSA ili kujua tunaongezaje suala hili ili magari haya yakishabadilishwa mfumo yaweze kujaziwa gesi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari Serikali tumeanza kulifanyia kazi suala hili.

Mheshimiwa Spika, la pili, kuhusiana na karakana, kwa kweli kwa kushirikiana na sekta binafsi tunao mkakati mahsusi wa kuhakikisha mpaka itakapofika Disemba, 2025 tutakuwa na zaidi ya vituo 30.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli jambo hili kama Serikali tumelibeba kwa dhati kwa ajili ya kuendeleza jitihada za Mheshimiwa Rais za kutumia nishati safi, si tu ya kupikia bali pia katika maeneo mengine kwa ajili ya manufaa kwenye mazingira yetu na manufaa mengine ya kiuchumi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tayari tumeanza kwa Dar es Salaam kwa ajili ya vituo na karakana na tutafanya vivyo hivyo kwa kadiri muda unavyokwenda kwa ajili ya mikoa mingine, ahsante.
MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, ahsante, kasi ya usambazaji wa vituo hivi ni ndogo sana ukilinganisha na hamasa iliyopo. Je, Serikali inatuambia nini...

SPIKA: Mheshimiwa Agnes, subiri.

Mheshimiwa Waziri keti, anayeuliza yuko nyuma yako, Mheshimiwa Agnes Marwa.

MHE. AGNES M. MARWA: Mheshimiwa Spika, kasi ya usambazaji wa vituo hivi ni ndogo sana ukilinganisha na hamasa iliyopo, je, Serikali inatuambia nini katika hili hasa katika Mkoa wa Mara?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kasi ya usambazaji, ni kweli hili tuliliona na tulianza kwa kurahisisha vigezo vya kupata vibali kwa ajili ya wawekezaji binafsi ili waweze kuwekeza kwa urahisi. Kwa hiyo, kwa sasa hivi tumebadilisha mifumo na kuongeza kasi kwenye kutoa leseni kwa ajili ya kuanzisha vituo ili kuzialika sekta binafsi ziweze kushiriki katika uwekezaji huu kwa urahisi.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi kwa ajili ya kutatua changamoto ambayo tunayo, tumeagiza vituo vya kuhamishika vya gesi (Mobile CNG Stations) kwa ajili ya kutatua changamoto hii kwa uharaka. Vilevile tunajenga vituo zaidi ya vitano pale Dar es Salaam kwa ajili ya kuhakikisha kuwa watu wanaendelea kupata huduma hii kwa uharaka.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa kweli tumeongeza kasi kwenye kutoa leseni kwa haraka na kwenye kujenga, sisi Serikali pia kwa kushirikiana na sekta binafsi, ili tuweze kutoa huduma kwa haraka, ahsante.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, nashukuru na nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa Visiwa vya Ilugwa na Ukara wananchi wananunua umeme kwa shilingi 1,800 kwa unit, mbaya zaidi wanapata umeme huo kwa saa 10 pekee, kuanzia saa tano asubuhi hadi saa tano usiku, je, Serikali ina kauli gani kuhusu kuwarahisishia maisha wananchi wa visiwa hivi?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, mradi wa kutoa umeme Bunda na kuongeza nguvu kuelekea Nansio, mkandarasi anachelewa kwa sababu wananchi wanaopaswa kupisha mradi huu hawajalipwa fidia, je, ni lini Serikali italipa fidia ili mkandarasi huyu aweze kuendelea na kazi yake?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ni kweli Visiwa vya Ukara na Ilugwa vina umeme jua ambao unapelekwa na Kampuni ya JUMEME na ni kweli wanalipa wastani wa shilingi 750 mpaka 800 kwa unit. Hii ni kutokana na kwamba mwekezaji yule mchana anatumia solar na usiku anatumia jenereta na diesel kuzalisha umeme. Kwa hiyo, gharama zinakuwa kubwa.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa hivi ndiyo maana changamoto ya muda mrefu ni hii ya kujenga kituo cha kupooza umeme ambapo Serikali tunatumia takribani shilingi bilioni 132.5 kujenga njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupooza umeme Ukerewe ili kuweza kutatua changamoto ya umeme Ukerewe.

Mheshimiwa Spika, lakini kwa kipindi hiki cha muda mfupi, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) anafanya jitihada za kuweza kutoa ruzuku ya mifumo midogo (solar pannels) za nyumbani ili wananchi waweze kununua kwa nusu bei na waweze kupata umeme usiku wakati tunasubiria kujenga kituo cha kupooza umeme na hii njia ya kusafirisha umeme ili viweze kukamilika.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la pili la fidia, tunaendelea kuwasihi wananchi waweze kuachia maeneo yao ili kuweza kutekeleza miradi wakati tunasubiri kulipwa fidia. Niwahakikishie wananchi wote ambao wako katika miradi hii, kwamba watalipwa fidia zao na tuko katika mchakato huo ili kuweza kukamilisha fidia zao.

Mheshimiwa Spika, tunaendelea kuwasihi wananchi, miradi hii ni kwa manufaa ya wote, waiamini Serikali, watupishe tupitishe miradi na fidia tunaendelea kuzifanyia kazi na watalipwa kwa wakati, ahsante.
MHE. ERIC J. SHIGONGO: Mheshimiwa Spika, wananchi wa Visiwa vya Maisome, Kaserazi pamoja na Yodzu wana changamoto kutoka kwa mzalishaji wa umeme (JUMEME) ambapo hivi sasa nimeongea nao wananunua umeme kwa unit moja shilingi 2,200. Ahadi ya Serikali ilikuwa ni kupitisha umeme wa cable mpaka Kisiwani. Je, ahadi hiyo itatimizwa lini?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kwa maeneo haya ya visiwa ambavyo amevisema Mheshimiwa Mbunge, kwa yale maeneo ambayo yako kilometa mbili kutoka pale ambapo umeme upo tutajitahidi kuanzia sasa hivi tuweze kuyafikishia umeme wa cable. Yale yaliyokuwa mbali kwa hatua hii ya muda mfupi tutaendelea kutoa hizi solar pannels za ruzuku ili wananchi waweze kupata umeme wa uhakika huku tukiendelea na mikakati ya muda mrefu ya kuwafikishia umeme, ahsante.
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Spika, Kampuni ya Rex Energy inafanya kazi ya kusambaza umeme katika visiwa vidogo vidogo saba katika Jimbo la Ukerewe, lakini mpaka sasa mradi huu unasuasua kwa sababu mkandarasi hajalipwa ruzuku. Nini kauli ya Serikali?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Mkandarasi Rex Energy ni mkandarasi binafsi na amepewa leseni na halmashauri kwa ajili ya kufikisha umeme kwenye maeneo hayo. Utoaji wa ruzuku una vigezo na moja ya kigezo ni uwezo mzuri wa mwekezaji katika kutoa huduma. Tutajiridhisha juu ya vigezo hivi na kama mwekezaji huyu ana vigezo basi tutampatia ruzuku kwa vigezo ambavyo tunavyo, lakini kama hatakidhi vigezo tunataka tuwahakikishie kwamba tutatafuta mkandarasi mwingine ambaye ana uwezo wa kufikisha umeme katika maeneo haya, ahsante.
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, je, ni lini kituo cha kupozea umeme kinachojengwa eneo la Uhuru, Wilayani Urambo kitakamilika? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Kupoza Umeme cha Uhuru kimeshafikia zaidi ya 97% na kwa sasa hivi tupo katika hatua za kufanya test kwa kutumia jenereta huku tukisubiri line ya kusafirisha umeme inayojengwa na ITDCO ambayo imeshafikia ziadi ya 67% iweze kukamilika. Kwa hiyo, kituo kile kwa kweli kimekamilika kwa zaidi ya 97%. Tunachosubiria ni line ya umeme ambapo pia tunategemea hivi karibuni itakamilika na kituo hiki kuanza kufanya kazi, ahsante.
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kukamilisha usambazaji wa umeme vijiji vyote 62 Wilaya ya Nyang’hwale, lakini kuna changamoto, tranformer hizo zimeanza kuzidiwa kwa sababu wananchi wengi wamefungua viwanda vidogovidogo, je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kumwelekeza Meneja wa TANESCO Wilaya ya Nyang’hwale afanye tathmini kwenye transformer ambazo zimezidiwa na kubadilishwa tuwekewe nyingine kubwa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, niwape pole wananchi wa Nyang’hwale kwa changamoto hiyo. Ninamwelekeza meneja sasa hivi wafanye tathmini kuweza kuona maeneo ambayo yanahitaji kubadilishiwa transformer ili wananchi wa Nyang’hwale ambao ni wazalishaji wazuri sana waweze kupata huduma na kuwasaidia katika shughuli zao za kiuchumi.
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na pia nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa nishati ya LNG ni nyenzo muhimu ya kiuchumi ili kuweza kuchochea uchumi wetu hali kadhalika ni tiba sahihi ya mazingira yetu na hasa upoteaji wa misitu. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza akatuambia kuna jitihada gani ambazo amezianzisha za kuweza kushirikiana na Sekta za Maliasili na Mazingira ili nazo ziwe katika utaratibu mzima huo wa mchakato wa uanzishaji wa matumizi ya gesi ya LNG?

Mheshimiwa Spika, swali namba mbili, kwa kuwa kuna ushirikiano mzuri katika matumizi ya grid ya Taifa ya umeme baina ya Tanzania Bara na Visiwani; Je, Mheshimiwa Waziri ameshaanza mchakato wa ushirikiano katika utaratibu mzima wa uanzishwaji au mchakato mzima wa LNG ili na Zanzibar nayo iweze kutumia fursa hii mara tu utaratibu utakapokamilika? Ahsante sana (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Moja, ni kuhusiana na kushirikisha idara ya maliasili pamoja na mazingira. Suala la mazingira ni suala mtambuka, halihusishi sekta moja, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama anavyosema, wakati wote ambapo tunafanya majadiliano kuelekea utekelezaji wa mradi huu, sekta zote muhimu zinashirikishwa, kwa sababu ni kweli mradi huu unalenga kutuimarisha kiuchumi, lakini vilevile unalenga kuimarisha utunzaji wa mazingira. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sekta muhimu zote ambazo zinatakiwa kushirikishwa zinashirikishwa katika hatua zote.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusiana na manufaa ya mradi huu kwa upande wa Tanzania Zanzibar. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sasa bado tupo katika hatua za majadiliano, lakini masuala yote yanayohusisha unufaika wa mradi huu yatazingatiwa pale ambapo mradi unakamilika na unaenda kutekelezwa, ahsante. (Makofi)
MHE. FURAHA N. MATONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa line kubwa ya umeme kutoka Bunda kupita Nansio, Wilaya ya Ukerewe ambao unachelewa kwa sababu ya wananchi kutokulipwa fidia. Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi wale ili mradi ule uweze kuendelea? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tunafahamu juu ya umuhimu wa mradi huu wa kujenga njia kubwa ya kusafirisha umeme kutoka Bunda, Nansio kwenda Ukerewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tunashirikiana na wenzetu wa Wizara ya Fedha ili tuweze kulipa fidia kwa wananchi katika maeneo haya na ili mradi huu uweze kuendelea. Kadri ambavyo mradi unaendelea, tunaendelea kuwasiliana na ku-engage na wananchi ili tuweze kukubaliana ili mradi uweze kuendelea taratibu taratibu huku tunasubiri fidia. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge suala hili linafanyiwa kazi na wananchi hawa watalipwa fidia yao kuanzia mwaka huu wa fedha. Ahsante
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Nyarukoba ya Kijiji cha Msege umeme ulifika Makao Makuu ya Kijiji lakini katika eneo hilo kuna wachimbaji wadogo ambao wako tayari kutoa fedha zao wapelekewe umeme ili kupunguza gharama ya uzalishaji wa dhahabu. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yupo tayari kwenda kuwasikiliza wachimbaji wale kwa gharama zao ili wapate umeme wafanye kazi ya uchimbaji? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake. Katika Kata hii ya Nyarukoba tayari nilishamwelekeza Meneja wa TANESCO, Mkoa wa Mara afanyie kazi na tayari wameshaanza kupeleka umeme kwenye hilo eneo. Niwahakikishie wachimbaji hawa wadogo tutawafikishia umeme kwa ajili ya kuboresha shughuli zao za kiuchumi. Ahsante.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lini Serikali itawalipa fidia Wananchi wa Wilaya ya Tunduru waliopisha Mradi wa Gridi ya Taifa? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, tayari wenzetu wa Wizara ya Fedha wanafanyia kazi jambo hili. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuanzia mwaka huu wa fedha wananchi hawa wa Wilaya ya Tunduru watalipwa fidia kwa ajili ya mradi huu wa kupeleka gridi kutoka Songea kwenda Mtwara mpaka Masasi na Lindi, ahsante.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza nipongeze Serikali kwa juhudi hizo zinazoendelea kuunganisha Mkoa wa Kagera na Gridi ya Taifa. Swali langu la kwanza; Mkoa wa Kagera umekuwa ukipata adha kubwa sana ya kukatika kwa umeme ambao kwa siku unakatika zaidi ya mara nane na wananchi wameendelea kupata adha kubwa. Je, nini mkakati wa Serikali wakati tunasubiria mpango wa kuunganisha na Gridi ya Taifa kuweza kuondoa adha hii wanayoipata? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Wilayani Kyerwa tuna vitongoji 668 na ambavyo vina umeme ni 245. Je, nini mkakati wa Serikali wa kupeleka umeme kwenye vitongoji hivi ambavyo bado havijafikiwa na umeme? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge katika Wilaya za Kyerwa, Karagwe na Missenyi umeme unakatika katika na hii ni kwa sababu kituo cha kupoza umeme kimezidiwa. Serikali tumeshaliona jambo hili na tulishalifanyia kazi. Tumepeleka transformer Kyaka lenye ukubwa wa MVA 20. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kazi ya kufunga transformer hii inaendelea na wataalam wameniambia ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba, transformer hii itaanza kufanya kazi. Hivyo maeneo yote ya Kyerwa, Karagwe na Missenyi suala la kukatika katika kwa umeme litapungua.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali la pili, la vitongoji 245 kuwa na umeme kati ya vitongoji 668, kwa sasa tumeshasaini mkataba wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 3,060 na mwaka huu wa fedha tunaenda kusaini mkataba pia wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 10,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge watu wa Kyerwa pia watanufaika na miradi hii mikubwa miwili ya kupeleka umeme kwenye vitongoji. Ahsante.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa kuwa huu Mkoa haujaunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kumekuwa na changamoto ya kukatikakatika umeme kama ilivyokuwa katika Mkoa wa Kagera. Changamoto ya kukatika kwa umeme imekuwa ikipelekea kuharibika kwa vifaa na kuungua kwa nyumba za watu. Natoa mfano kuna mwananchi wa Wilaya ya Kyerwa anaitwa Ramson Greshen ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Mkombozi. Adha ya kukatika kwa umeme imesababisha kuungua kwa nyumba yake. Nataka kauli ya Serikali watu wanaopata adha ya kukatika kwa umeme kama huyu wanapewa fidia namna gani?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la pili; kwa sasa imepata taarifa kwamba waratibu wa REA maeneo mbalimbali ikiwepo Mkoa wa Kagera wamepewa barua za kusitisha mikataba yao na kumaliza kazi. Nataka kujua hatma ya miradi ya REA wakati ambapo waliokuwa wanaratibu wamepewa barua ya kusitishiwa mikataba yao? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na suala la fidia, wahanga wote ambao wanapata madhara yanayosababishwa na hitilafu za umeme utaratibu upo. Utaratibu ni kwamba EWURA wanashughulikia kupitia taasisi zao, kujiridhisha kama madhara hayo yanatokana na mifumo ya taasisi zetu na baada ya hapo kama inafanyika hivyo basi kuna taratibu za mwananchi kupatiwa fidia.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namshauri mwathirika huyu ambaye tunampa pole sana afuate taratibu za kisheria zilizopo na kama ana manufaa yake kwa majanga aliyopata basi tunamhakikishia ataweza kulipwa fidia kutokana na hasara aliyoipata, ahsante.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa mkandarasi anayejenga hiyo line kutoka Songea hadi Masasi anafanya kazi kwa kusuasua kwa sababu ana madai ambayo hajalipwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kumwezesha haraka ili aendelee na ujenzi wa mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, Mkandarasi anayepeleka umeme kutoka Songea hadi Mahumbika ni Kalpataru. Mkandarasi huyu tayari alikuwa site. Serikali tunafahamu umuhimu wa Mkoa wa Mtwara na Lindi kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa. Kwa hiyo, kwa umuhimu huo tunawasiliana kwa karibu na wenzetu wa Wizara ya Fedha ambao hivi karibuni wametuhakikishia kwamba mkandarasi huyu atawezeshwa ili kazi iweze kufanyika kwa haraka zaidi. Ahsante.
MHE. DEUS C. SANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Naomba niulize maswali madogo mawili ya nyongeza:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mabadiliko ya bei, hasa katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Namanyele na Laela, ziliathiriwa ambapo kutoka shilingi 27,000 mpaka shilingi 320,000 kutokana na Sheria ya Mipango Miji, lakini kiuhalisia Sura ya Mamlaka ya Miji hii midogo ni ya vijiji. Je, Serikali mna mpango gani wa kushusha bei kurudi kuwa, shilingi 27,000 ili kuwapa nafuu Wananchi wa Mamlaka ya Miji hii kuunganisha umeme?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Mkandarasi anayetekeleza mradi wa umeme Mkoa wa Rukwa, hasa Jimbo la Kwela, speed yake ni ya kusuasua, hasa katika Kata ya Mnokola, Kilangawala na Milepa. Nataka kupata kauli ya Serikali, ni lini mtamsimamia mkandarasi huyu kikamilifu, ili aweze kutekeleza majukumu kwa sababu, tumelalamika mara nyingi hapa Bungeni? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Mbunge kuhusiana na maeneo ambayo wana-charge shilingi 320,000 badala ya shilingi 27,000 katika maeneo ya Namanyele na eneo lingine ambalo Mheshimiwa Mbunge amesema.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kweli, tumefanya mapitio ya maeneo ambayo tuliona hayastahili kuwekewa kiasi cha shilingi 320,000 na tumeshauri, ili iweze kushuka mpaka shilingi 27,000. Katika maeneo haya tumeshapitia maeneo 1,500 na tumejiridhisha kwamba, inabidi yaende kwenye shilingi 27,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na maeneo haya mawili ambayo Mheshimiwa Mbunge amesema tutaenda kupitia kuona kama yapo katika yale maeneo ambayo tumesema, inabidi yatoke shilingi 320,000 mpaka shilingi 27,000. Kama yapo hapo tutaendelea na utekelezaji kwa kadiri muda unavyoenda na upatikanaji wa fedha, lakini kama hayapo, basi tutajiridhisha kuona kama maeneo haya yanatakiwa kushushwa mpaka shilingi 27,000 na baada ya hapo tutayaingiza katika mpango huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na haya maeneo ya Kwela, Mnokola, Kiwangawala na hilo lingine ambalo amesema Mheshimiwa Mbunge; kwa kweli, ni kweli huu Mradi wa Tanzania – Zambia Interconnector ulikuwa unasuasua kidogo kwenye baadhi ya maeneo. Mapema mwaka huu Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati walifanya ziara kwenye mradi huu na kukwamua yale matatizo ambayo yalikuwa yanasababisha mradi kutoenda kwa kasi ambayo sisi tumetarajia. Nakuhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wameshafanyia kazi na tutaendelea kumsimamia mkandarasi, ili aweze kutekeleza vizuri mradi huu uweze kukamilika kwa wakati. Ahsante.
MHE. MOSHI S. KAKOSO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza, naishukuru Serikali kwa kupeleka Miradi ya Umeme wa REA kwenye Wilaya ya Tanganyika. Kwenye Wilaya ya Tanganyika mmepeleka Umeme wa REA kwenye Kata ya Mwese ambao umewafikia wananchi. Kwa bahati mbaya sana zile taasisi muhimu kama soko, Parokia na eneo la Msikiti na shule ya sekondari na msingi hakujapelekwa umeme. Ni lini mtapeleka huduma hiyo iwafikie wananchi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Kakoso, Mbunge wa Tanganyika. Ni kweli katika maeneo mengi, ikiwemo hii Mwese, kuna baadhi ya taasisi hazijafikiwa, lakini tumeshatoa maelekezo kwa yale maeneo ambayo hayadizi mita 500, basi wafanyie kazi kuona taasisi ambazo zipo kwenye ukubwa wa sehemu ambapo umeme ulipo mpaka mita 500 yaweze kuunganishwa na umeme kwa sababu, wote tunafahamu umuhimu wa taasisi hizi katika mendeleo ya jamii.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, katika Kata hii ya Mwese ambapo Mheshimiwa amesema maeneo ya parokia, msikiti, shule za msingi na sekondari tutafanyia kazi. Tutakwenda, ili kuweza kuona kama maeneo haya yapo kwenye ukubwa huo na kuweza kupatiwa umeme, lakini kama maeneo haya yapo mbali tutaangalia kuona kwenye mradi wa vitongoji kuona namna gani maeneo haya yanafikiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile, ni azma na nia yetu ya dhati kuhakikisha maeneo yenye taasisi zote za muhimu yanafikiwa na umeme kwa sababu, Serikali inawekeza fedha nyingi sana, hususan kwenye shule za msingi na sekondari. Na dhamira yetu ni kuhakikisha maeneo haya yenye taasisi zinazoleta huduma kwa jamii na zenyewe zinaweza kupata umeme, ili tuweze kuboresha zaidi mazingira ya kujifunza na kujifunzia kwenye shule za msingi na sekondari. Ahsante.
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Utekelezaji wa Miradi ya REA katika Wilaya ya Muleba unasuasua. Serikali ina kauli gani kumuhimiza mkandarasi amalize ile kandarasi aliyopewa? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na pia, nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Kikoyo. Nataka nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwa kweli, ni mkakati wetu kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati. Namhakikishia nitafanya ziara katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge, ili kujionea na kuendelea kumsisitiza mkandarasi aweze kuongeza kasi hii ya kupeleka umeme kwenye vijiji ambavyo vimebakia, ili iweze kufanyika kwa haraka wananchi waweze kupata umeme. Ahsante. (Makofi)
MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba vijiji vyote 785 vya Mkoa wa Mtwara tulipokea taarifa ya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa kwamba vimeshapatiwa umeme. Isipokuwa, kazi hii sasa inaendelea kwenye vitongoji. Kijiji cha Mnyambe, Mitema pamoja na Kijiji cha Mapinduzi tayari wakandarasi wako huko. Tunaiomba Serikali itoe maelekezo ya kuhakikisha kazi hii inafanywa kwa spidi ili iweze kukamilika mapema.

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na mwingiliano wa kazi, kama utakumbuka, kulikuwa na vitongoji 15 ambavyo sisi Waheshimiwa Wabunge tulipendekeza, lakini kuna kazi ya ujazilizi katika maeneo mbalimbali ikiwemo Chiwata, Mkalinga, Ngalole, Chikoweti, Maswela pamoja na Kitongoji cha Magomeni na Mjimwema…

SPIKA: Mheshimiwa Cecil Mwambe, swali la nyongeza.

MHE. CECIL D. MWAMBE: Mheshimiwa Spika, tunaomba sasa Serikali iweze kufanya review ya ramani kwenye maeneo hayo, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu maswali mawili ya Mheshimiwa Cecil, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa yale maeneo ambayo miradi inaingiliana, huu wa vitongoji 15 na miradi ya ujazilizi ambayo pia imeanza, kwa niaba ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, naomba nimwelekeze Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini, waweze kufanya mapitio pamoja na wakandarasi ili kuhakikisha miradi hii haiingiliani, ila yote inatekelezwe kwa kasi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa haraka, ahsante.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, je ni lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha upendo, Tupendane, Ikwambi na Mission katika Halmashauri ya Mji wa Ifakara?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Vitongoji hivi alivyovisema Mheshimiwa Mbunge vya Upendo, Tupendane, Ikwambi pamoja na Mission, vipo katika miradi ya vitongoji ambayo inaendelea. Tuna Mradi huu wa Vitongoji 15, lakini tuna mradi mwingine wa vitongoji ambao unatarajia kuwepo. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendelea kupeleka umeme kwenye vitongoji, na kwa vitongoji hivi ambavyo amevisema, tutahakikisha na vyenyewe vinakuwepo katika mradi na wananchi wapate umeme, ahsante. (Makofi)
MHE. BAHATI K. NDINGO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Vitongoji vya Iduya “A” na Iduya “B”, Kata ya Utengule Usangu pamoja na Kitongoji cha Ngolongolo Kata ya Ihai, ni Vitongoji vyenye watu wengi sana na mpaka leo havina. Nini mkakati wa Serikali wa kutusaidia kupeleka umeme kwenye vitongoji hivyo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Vitongoji vya Iduya “A” na Iduya “B”, pamoja na Mngolongolo, vipo katika miradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji 15. Tumefanya mapitio ya vitongoji hivi kutoka kwenye ile list ya kwanza kwenda list ya pili. Kwa hiyo, kwa sababu kuna miradi iliyokuwa inaendelea kwenye baadhi ya vitongoji, basi vitongoji hivi vitaingia kwenye vile vitongoji ambavyo tayari vimeshapelekewa miradi, ahsante.
MHE. ALLY I. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Spika, jimboni kwangu kuna vitongoji vingi sana vyenye hadhi ya kuwa Kijiji, lakini havina umeme kabisa. Je, Wizara ina mpango gani wa kuviangalia vitongoji hivi kwa jicho la huruma?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kama ambavyo nimeshasema, tayari Serikali tumeanza utekelezaji wa miradi kwenye vitongoji baada ya kufika karibia na mwisho kwa mradi mkubwa wa kupeleka umeme kwenye vijiji. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote kwamba dhamira yetu ni kuhakikisha tunaendelea kupeleka umeme kwenye vitongoji ikiwemo vitongoji katika Jimbo la Mheshimiwa Mchungahela.

Mheshimiwa Spika, tumeanza na vile vitongoji 15 na tuna miradi mingine ya vitongoji inakuja. Vilevile, katika Mkoa wake tuna mradi wa ujazilizi ambao pia umeanza. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa, miradi ipo na wakandarasi wako site na tutaendelea kupeleka kwenye vitongoji kwa kadri miradi na upatikanaji wa fedha unavyoendelea, ahsante.
MHE. MIRAJI J. MTATURU: Mheshimiwa Spika, Vitongoji vya Mipetu, Kairo na Majengo katika Jimbo la Singida Mashariki, ni vitongoji vyenye shughuli nyingi za uchumi. Je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji hivyo? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, Vitongoji vya Kairo, Mipetu na Majengo, ipo miradi ambayo inaendelea, lakini kama vitongoji hivi havipo katika miradi ambayo wakandarasi wako site, basi tutavichukua ili kuweza kuviweka katika miradi ya vitongoji ambayo inakuja, ahsante.
MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Pamoja na majibu ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, yako maeneo ya vijiji ambayo mpaka sasa hayaunganishiwi umeme kwa gharama ya shilingi 27,000 badala yake wanaunganishiwa kwa shilingi 320,000. Mfano ni eneo la Manyata Kata ya USA River kule Arumeru Mashariki. Je, nini kauli ya Serikali juu ya jambo hili?

Mheshimiwa Spika, swali la pili: Wilaya ya Korogwe mpaka sasa kazi ya kuunganishiwa umeme wa kilometa mbili, pamoja na ujenzi wa vile vitongoji 15 haijaanza. Ni lini kazi hii itaanza kwenye Wilaya ya Korogwe, Jimbo la Korogwe Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kuhusiana na swali la kwanza la hili eneo la Manyata - USA River, maeneo yote ya vijiji, umeme unaunganishwa kwa shilingi 27,000 labda isipokuwa maeneo haya ni maeneo ya mamlaka ya Mji mdogo ambayo yanatambulika kama mitaa.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, niendelee kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge wote kuwa, maeneo yote ya vijijini, ada ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000. Kwa hiyo, tutaangalia eneo hili la Manyata ambalo lipo USA River, kama wanachajiwa zaidi ya hapo na ni eneo la vijiji, basi tutachukua hatua ili kuhakikisha wanarudi kwenye shilingi 27,000; lakini kama ni eneo ambalo liko kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo, basi ndiyo maana ada yake inakuwa ni shilingi 321,000.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na mkandarasi ambaye yupo Korogwe, tayari Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu alitoa maelekezo kwa mkandarasi kutoa commitment ya kumaliza mradi kwa wakati kwa sababu alikuwa anasuasua. Tayari imeshafanyika hivyo na ndani ya wiki hii tutasaini na mkandarasi ili aanze kupeleka umeme katika kilometa mbili kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge, ahsante.
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, Haydom ni Kijiji na Dongobesh ni Kijiji, lakini umeme wake unaingizwa kwa shilingi 320,000. Je, ni lini utatoa mwongozo katika vijiji hivyo ili walipe shilingi 27,000 kama vijiji vingine vyote?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimesema kwenye swali la msingi, maeneo yote ya vijiji gharama ya kuingiza umeme ni shilingi 27,000. Kama maeneo haya kulingana na miongozo ya TAMISEMI ni maeneo ya vijiji, tutafuatilia kuhakikisha gharama ya kuunganisha umeme ni shilingi 27,000, ahsante. (Makofi)
MHE. SOUD MOHAMMED JUMAH: Mheshimiwa Spika, ahsante sana na pia nampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri, pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa nishati ya LNG ni nyenzo muhimu ya kiuchumi ili kuweza kuchochea uchumi wetu hali kadhalika ni tiba sahihi ya mazingira yetu na hasa upoteaji wa misitu. Je, Mheshimiwa Waziri anaweza akatuambia kuna jitihada gani ambazo amezianzisha za kuweza kushirikiana na Sekta za Maliasili na Mazingira ili nazo ziwe katika utaratibu mzima huo wa mchakato wa uanzishaji wa matumizi ya gesi ya LNG?

Mheshimiwa Spika, swali namba mbili, kwa kuwa kuna ushirikiano mzuri katika matumizi ya grid ya Taifa ya umeme baina ya Tanzania Bara na Visiwani; Je, Mheshimiwa Waziri ameshaanza mchakato wa ushirikiano katika utaratibu mzima wa uanzishwaji au mchakato mzima wa LNG ili na Zanzibar nayo iweze kutumia fursa hii mara tu utaratibu utakapokamilika? Ahsante sana (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge. Moja, ni kuhusiana na kushirikisha idara ya maliasili pamoja na mazingira. Suala la mazingira ni suala mtambuka, halihusishi sekta moja, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kama anavyosema, wakati wote ambapo tunafanya majadiliano kuelekea utekelezaji wa mradi huu, sekta zote muhimu zinashirikishwa, kwa sababu ni kweli mradi huu unalenga kutuimarisha kiuchumi, lakini vilevile unalenga kuimarisha utunzaji wa mazingira. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sekta muhimu zote ambazo zinatakiwa kushirikishwa zinashirikishwa katika hatua zote.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusiana na manufaa ya mradi huu kwa upande wa Tanzania Zanzibar. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kwa sasa bado tupo katika hatua za majadiliano, lakini masuala yote yanayohusisha unufaika wa mradi huu yatazingatiwa pale ambapo mradi unakamilika na unaenda kutekelezwa, ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri na hatua hiyo waliyofikia ni muhimu sana. Hata hivyo, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Swali la kwanza. Sasa hivi Ludewa inakwenda kuwa na viwanda vikubwa sana, lakini bado inategemea power station kutoka Wilaya ya jirani ya Madaba. Je, Serikali haioni haja ya kujenga kituo cha kupooza umeme pale Ludewa, ili kupunguza adha kwa wananchi ya kukatika kwa umeme mara kwa mara?

Mheshimiwa Spika, swali la pili. Ninapenda kufahamu iwapo Serikali ipo tayari kunipa wataalam kutoka TANESCO na REA niweze kwenda nao Kata za Lumbila na Kilondo ambako bado vijiji vingi havijapata umeme hadi sasa. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninapongeza Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mawili ya nyongeza. Kuhusu kujenga kituo cha kupooza umeme Ludewa; tutaenda kulifanyia kazi kuona kama uwezekano upo na kama upo basi tutaweka. Kama haupo, kwenye ule mradi wa grid imara basi tutaona ni namna gani tutaweza kujenga kituo cha kupooza umeme pale Ludewa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninafahamu Wananchi wa Ludewa ni wachapakazi sana kwa hiyo, wanahitaji umeme wa uhakika, kwa ajili ya viwanda vidogo na vikubwa. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge tumelipokea na tutalifanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kupewa TANESCO na REA, ili kuhakikisha kwamba, vijiji vya Nsele, Kilondo, Mkanda, Lumbila na Changali wanapata umeme kwa sababu, nafahamu vijiji hivi havina umeme; tulipata changamoto ya mkandarasi, kwa sababu vijiji hivi vipo Mwambao wa Ziwa Nyasa akaona ni vigumu katika utekelezaji, hivyo akaamua kuvirudisha REA. Hata hivyo, kwa sababu tulisaini naye mkataba na alifanya survey na akakubali mwenyewe kuvifanya, tumekataa yeye kuvirudisha vijiji hivi REA na tayari tumeshampa schedule, ili atuambie ni lini atapeleka umeme kule, otherwise tutamchukulia hatua kali za kisheria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, namuambia mkandarasi huyu ahakikishe anatekeleza mradi kwa wakati. Otherwise tutachukua taratibu za Kisheria kuhakikisha ya kwamba na sisi tunapata haki yetu kwa sababu, alisaini mkataba baada ya kufanya survey na akahakikisha kwamba, anaweza kupeleka umeme kwenye vijiji hivi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kama mwishoni kabisa tutajiridhisha hawezi kupeleka umeme katika vijiji hivi kwa wakati, sisi kupitia TANESCO na REA, tuna uwezo wa kupeleka umeme kwenye vijiji hivi. Kwa hiyo, tutachukua hatua zote za kisheria kuhakikisha umeme unaenda, lakini kama hataweza kupeleka kwa wakati tutafanya wenyewe. Vilevile, tutamchukulia hatua kali za kisheria. Hatuwezi kukubaliana na wakandarasi wababaishaji. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tutalifanyia kazi kwa hakika, ahsante. (Makofi)
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri kutoka kwa Naibu Waziri. Nawapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya Mbulu Vijijini. Swali la kwanza; je, ni lini sasa mtatupatia umeme kwenye vitongoji vilivyobaki kwa sababu, kule ni sawasawa na vijiji?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; tulikubaliana kwenda kufanya uzinduzi wa kuwasha vijiji hivyo sita, je, Mheshimiwa Naibu Waziri ni lini sasa tunakwenda kuwasha hivi vijiji, ili Jimbo la Mbulu Vijijini lipate umeme wa kutosha?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mawili ya nyongeza. Jimbo la Mbulu lina jumla ya vitongoji 361 ambapo kati ya hivyo, vitongoji 80 ndivyo ambavyo vina umeme. Tutaongeza upatikanaji wa umeme kwenye vitongoji kupitia mradi wa vitongoji 15 vilevile tuna mradi wa ujazilizi pale kwa vitongoji 16. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tutapunguza idadi ya vitongoji zaidi kupitia mradi wa REA ambao unatarajiwa kupeleka umeme kwenye vitongoji 20,000 kwa awamu.

Mheshimiwa Spika, ahsante. Samahani, kuna hili swali la pili la Mheshimiwa Mbunge, kuhusu kwenda kuwasha.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, nilimuahidi Mheshimiwa Mbunge, tutaenda kuwasha vijiji hivi sita. Kwa kuwa, natambua vijiji vitatu vitakuwa vimekamilika Tarehe 27, vijiji viwili vitakuwa vimekamilika Tarehe 28 na kimoja kitakuwa kimekamilika Tarehe 30 mwezi huu, basi tutapanga, ili kuona namna gani baada ya kukamilika Bunge hili tutaenda kuwasha vijijini kwako, Mheshimiwa Mbunge, ahsante sana. (Makofi)
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, mkandarasi anayeitwa Silo anasuasua kupeleka umeme Kijiji cha Kigulu. Yapi ni maelekezo ya Serikali kwa mkandarasi huyu?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake. Kuhusu kijiji hiki, tutamsimamia mkandarasi kwa weledi sana kuhakikisha anamaliza kufikia mwezi huu kwa sababu, ndiyo makubaliano ya kumaliza mradi huu ikifika Tarehe 30 ya mwezi huu. Kwa hiyo, namuelekeza Mkurugenzi wa Mradi huu wa REA ahakikishe anamfuatilia mkandarasi na kuhakikisha anatimiza kazi yake kwa kadiri ya muda wa mkataba. Ahsante sana. (Makofi)
MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi hii. Kwanza naipongeza Serikali kwa kazi nzuri ambayo imeifanya kule Arumeru Mashariki, kwa ajili ya kusambaza umeme wa REA. Hata hivyo, pamoja na juhudi hizo, ukanda wa mashariki, hususan Tarafa ya King’ori, bado vitongoji vingi viko gizani. Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwenye ukanda huo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kuhusu hii ya kupeleka umeme huku King’ori; namhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutapeleka umeme katika vitongoji hivi, kwanza kupitia mradi wa vitongoji 15 na pia, tutaendelea kupeleka kupitia miradi ya REA ambayo tunayo kwa Mwaka huu 2025 na kuendelea. Ahsante. (Makofi)
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Majibu yanasema Serikali inaendelea na majadiliano, hivyo niiombe Serikali kutoa commitment kwa kuwa imeshatangaza kusitisha matumizi ya kuni na hasa kwenye taasisi na matumizi ya Gesi ya LPG ni gharama. Tungetaka kauli ya Serikali itakamilika lini kwa sababu ilivyo kwa sasa inaweza kuchukua muda mwingi na sijui hatima yake.

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; kwa kuwa matumizi ya gesi nchi nzima kwa sasa wananchi wengi wanatumia LPG, LPG ni gesi ambayo ni ghali na Serikali haitumii Mfumo wa Bulk Procurement. Nataka kauli ya Serikali juu ya kutumia mfumo huu ambao utaweza kusaidia ku-regulate price tofauti na ilivyo leo ambapo wauzaji ndiyo wanaoweza ku-determine price tofauti na ilivyo kwenye bidhaa nyingine ya petroli. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Spika, moja kuhusiana na lini majadiliano haya ya Mradi wa LNG yatakamilika, mradi huu ni mradi wenye manufaa makubwa sana kwa Taifa letu. Majadiliano haya ni muhimu kwa sababu ndiyo ambayo yanaweka msingi wa kodi, mirabaha pamoja na ulinzi wa vigezo vya sisi kunufaika kiuchumi. Kwa hiyo nataka niwahakikishie suala la Mradi wa LNG ni kipaumbele katika Serikali na majadiliano haya yanaendelea vizuri sana.

Mheshimiwa Spika, ni lini? Nitashindwa kusema tarehe mahususi, lakini nataka niwahakikishie ni kipaumbele na tunafanya kazi hii kwa weledi mkubwa sana kuhakikisha majadiliano yanaendelea vizuri, yanakamilika na mradi unaenda kutekelezwa. Nataka niwahakikishie suala hili Mheshimiwa Mbunge kwa kweli tumejizatiti kuhakikisha tunafanya majadiliano ya maslahi kwa Taifa na mwisho wa siku yanakamilika na mradi kutekelezeka.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la pili la kuagiza gesi ya LPG kwa Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja (Bulk Procurement System - BPS). Kwa kweli ni wazo zuri na sisi tunalichakata, lakini unafuu wa bei ama uuzaji wa bei kwa kweli EWURA wanachokifanya soko halipo huru, hivyo ni tunahakikisha soko linakuwa himilivu ili kuhakikisha bidhaa inaweza kusambaa na inapatikana kwa urahisi. Suala la BPS lina vigezo mbalimbali ikiwemo kwa sasa hivi tunaenda kujenga gati ambalo litatuwezesha kuleta meli kubwa za LPG. Kwa hiyo tutaendelea tathmini kadri ambavyo tunaendelea kuwekeza kwenye kuleta gesi hii ili kuhakikisha tunaenda kutumia Mfumo huu wa BPS lakini ni wazo ambalo tunalichakata na tutaenda kulifanyia kazi kulingana na mahitaji ya soko, lakini kwa kadri vile tunavyoenda kuboresha miundombinu ya kuleta gesi nchini, ahsante. (Makofi)
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa Gridi ya Taifa ni muhimu sana katika Jimbo langu la Nanyumbu na kwa Serikali kwa ujumla. Sisi tunaamini kabisa kwamba mradi huu ukimalizika ile katika katika ya umeme kwenye Jimbo la Nanyumbu itakwisha, lakini nina maswali mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wamekwishaachia mashamba yao huu ni mwaka wa pili sasa na mashamba yale ya mikorosho ndicho kilichokuwa chanzo kikuu cha uchumi kwa wananchi wale. Sasa nataka nipate commitment ya Serikali: -

(a) Je, ni lini itawalipa wananchi wale fedha zao ili kufidia yale machungu ya kuyaacha maeneo yale?

(b) Je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari hiyo commitment atakayoitoa akaja ndani ya jimbo langu akaongea na waathirika wa hili eneo ili wananchi wale waridhike kupata majibu moja kwa moja kutoka Serikalini?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na nimpongeze, amekuwa akifuatilia juu ya fidia hii ya wananchi wa Nanyumbu kwa muda sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu ni mradi wa kimkakati ambao unalenga kupeleka umeme wa gridi kwenye Mikoa ya Mtwara na Lindi, kwa hiyo, ni mradi ambao kwa kweli ni kipaumbele kwa Serikali. Vivyo hivyo suala la fidia pia ni suala ambalo tunaliangalia kwa jicho la kipekee. Niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa wananchi wake wa Nanyumbu watalipwa fidia hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Rais wakati anafanya ziara katika Mkoa wa Mtwara aliwahakikishia wananchi wale kwamba watalipwa fidia. Mimi niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali itawalipa fidia wananchi wake wa Nanyumbu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu mimi kwenda kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge nitafika na tutaenda kwa wananchi pamoja na Mheshimiwa Mbunge, ahsante sana.
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa changamoto ya ukosefu wa umeme wa Gridi ya Taifa, lakini pia mitambo mizuri ya umeme inawakumba wananchi wa Kigamboni katika Kata za Kigamboni, Vijibweni, Mji Mwema, Gezaulole, Somangira, Kibada, Kisarawe II na Mwasonga kukosa umeme wa uhakika kwamba ikifika saa 12.00 jioni kunakuwa na low voltage kiasi kwamba maeneo hayo huwezi kupika, huwezi kuwasha microwave, huwezi kuwasha chombo chochote na umeme unakuwa kama wa kibatari.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ni kweli kwa yale maeneo ya Kigamboni ikifika jioni umeme unakuwa na low voltage. Serikali tayari imekwishaanza kulifanyia kazi jambo hilo. Kupitia Kituo cha Kupooza Umeme cha Mbagala tumeongeza transfoma nyingine ili kuhakikisha kwamba tunaongeza nguvu ya umeme kwa ukanda wote ule kuanzia Kigamboni, Mbagala mpaka kwenda Pwani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, transfoma ile imekwishafika na mkandarasi yuko site. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ya Awamu ya Sita inafanya kila jitihada ili kuhakikisha kwamba wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam hususan maeneo ya Mbagala, Kigamboni na Pwani wanaendelea kupata umeme wa uhakika na hivi karibuni mradi utakamilika na umeme utakuwa wa uhakika, ahsante.
MHE. ANTON A. MWANTONA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujua ni lini Mradi wa REA kwa vitongoji 15 katika Jimbo la Rungwe utaanza?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante mradi wa vitongoji 15 katika Jimbo la Rungwe, mkandarasi yuko site na sasa hivi anafanya manunuzi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mradi umeanza na tumeshasaini mkataba na huu mradi wa vitongoji 15 utaenda kutekelezeka, ahsante.
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kazi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji imeanza hata Jimboni kwangu Bukene Kampuni ya Sinotech imefika na imeanza kazi hiyo. Hata hivyo wanapeleka umeme kwenye vitongoji ambavyo tu vimepitiwa na line kubwa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha hata vile vitongoji ambavyo havipitiwi na line kubwa (high tension) navyo vinapata umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba huu mradi wa vitongoji 15 ni mradi jazilizi, kwa hiyo unatekelezwa kwenye maeneo ambayo tayari yana miundombinu. Kwa maeneo ambayo hayana miundombinu tunakuja na mradi kuanzia mwezi wa 12 ambao utahusisha kujenga MV na LV lines, lakini vilevile utahusisha kuweka transfoma kulingana na ukubwa wa maeneo tofauti tofauti. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba yale maeneo ambayo hayana miundombinu na kwa hiyo, yameshindwa kunufaika na huu mradi wa ujazilizi wa vitongoji 15 yataendelea kupata umeme na yataendelea kujengewa miundombinu kwa mradi unaokuja wa kupeleka umeme kwenye vitongoji, ahsante.
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itapeleka umeme katika vitongoji vya Mkoa wa Simiyu ambavyo bado havijapata umeme ili kuondoa kero kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa kupeleka umeme kwenye vitongoji katika Mkoa wa Simiyu na sasa hivi tuna huu mradi wa ujazilizi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 15 katika majimbo yote ya Mkoa wa Simiyu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mkoa wa Simiyu ya kwamba Serikali itaendelea kupeleka miradi kwa kadiri tunavyoendelea mbeleni, ahsante.
MHE. FRANCIS I. MTINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa vitongoji ambavyo vinapitiwa na umeme mkubwa bado viko vingi sana kwenye majimbo yetu.

Je, Serikali haioni kuwa kuna sababu ya kuwaongeza hawa wakandarasi ambao wako site vitongoji zaidi ili kuokoa muda na kwamba tayari miundombinu ipo kwenye baadhi ya vitongoji?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maendeleo ni hatua na Tanzania nzima tuna vitongoji zaidi 36 ambavyo havina umeme. Ni azma ya Serikali kuhakikisha kwamba vitongoji vyote vinapelekewa umeme. Hata hivyo ni mradi ambao ni lazima uende kwa awamu kwa sababu vitongoji hivi ni vingi. Tumekwishaanza, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge waendelee kutuvumilia, tunatafuta fedha mwezi wa 12 tunakuja na mradi mwingine na vitongoji vingi zaidi vitanufaika na miradi hii ambayo kiukweli ina tija kubwa sana kwa maeneo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wetu wa Tanzania, ahsante.
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa jitihada za makusudi za kunusuru kukatika kwa umeme Wilayani Meatu zinazochukuliwa na Serikali ikiwemo kutoa umeme Mkalama Mkoani Singida hadi Bukundi na hatimaye Makao Makuu ya Mji wa Mwanhuzi. Nina swali moja tu Mheshimiwa Waziri. Naomba kuuliza, je, Serikali haioni haja ya kumwezesha mkandarasi anayejenga line ya kutoka Ibadakuli kwenda Imalilo Bariadi kwa kumlipa deni lake la shilingi bilioni saba ili kumjengea uwezo? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Azma ya Serikali ni kuhakikisha tunaendelea kuboresha upatikanaji wa umeme kwa wananchi, hususan wananchi wa Meatu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutayafanyia kazi madai ya mkandarasi ili kuhakikisha anafanya kazi hii kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa kwa manufaa ya watu wa Meatu, ahsante.
MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, je, ni lini Serikali itakamilisha suala la usambazaji wa umeme katika mitaa ya Halmashauri ya Mji wa Bunda?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na namshukuru Mheshimiwa Mbunge amekuwa akifuatilia hii mitaa kwa muda mrefu. Tayari tuna mradi pale kupitia Wakala wa Nishati Vijijini wa Vitongoji 15 lakini kwa mitaa ambayo inabakia tutaendelea kufuatilia na kutafuta fedha kuhakikisha umeme unawekwa katika mitaa ambayo bado haijafikiwa na umeme, ahsante.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa nafasi. Kukatika katika kwa umeme Wilayani Liwale imekuwa ni adha kubwa sana. Ukiwauliza wataalamu wanasema sababu kubwa ni umbali uliopo kutoka Mahumbika mpaka Liwale ambako kuna kituo cha kupozea umeme. Je, Serikali haioni umefika wakati sasa wa kujenga kituo cha kupozea umeme Wilayani Liwale?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge. Umuhimu wa kuweka kituo cha kupoza umeme Liwale upo, kwa sababu utaboresha upatikanaji wa umeme kwa wananchi wa Liwale. Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwa sasa tunatekeleza mradi mkubwa wa kupeleka umeme wa gridi kwenye Mikoa ya Mtwara na Lindi kutokea Ruvuma, Songea Tunduru, Masasi mpaka Mahumbika. Tukikamilisha mradi huu mkubwa, tutaona uwezekano wa kuweka vituo vya kupoza umeme, ili pamoja na umeme wa gridi ambao ni wa uhakika zaidi, basi kwenye eneo la Liwale pia kuwe kuna kituo cha kupoza umeme. Kuhakikisha kwamba tunapunguza adha ya kukatika katika kwa umeme, ahsante.
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Tulipata wakandarasi kwenye majimbo yetu na hasa pale Tarime Vijijini na vitongoji zaidi ya 300 havina umeme. Walienda wakapima kupitia Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji wakaweka beacon. Sasa ni lini mradi huu wa umeme utaanza kutekelezwa katika jimbo la Tarime Vijijini ili watu wangu watoke kwenye giza nene? Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge. Tayari tumeanza utekelezaji wa kupeleka umeme kwenye vitongoji. Tumeanza na vitongoji 15 ambavyo yeye mwenyewe Mheshimiwa Mbunge alituonyesha kwa list yake na kuanzia mwezi Desemba mwaka huu tuna mradi mwingine wa vitongoji 4,000. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, katika mradi unaofuata tutaendelea kupunguza vitongoji katika jimbo lake ili kuhakikisha vitongoji hivyo ambavyo havina umeme vinapelekewa umeme na wananchi wananufaika, ahsante.
MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Tuna mradi mkubwa huu wa umeme ambao Mheshimiwa Naibu Waziri ameusema hapa hivi punde wa kutoka Songea – Namtumbo - Tunduru kwenda Masasi. Mradi huu mkandarasi hayupo site sasa hivi. Pia, wananchi hawajalipwa fidia yao. Je, ni lini wananchi watalipwa fidia yao na kwa nini mkandarasi hayupo site sasa hivi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, cha kwanza, mradi huu unaendelea. Mkandarasi hayuko site kwa sababu kulikuwa kuna changamoto za malipo, lakini siyo kwamba mradi umesimama. Mradi unaendelea na tayari kazi imeanza. Tutaendelea kufuatlia kuhakikisha mkandarasi analipwa kwa sababu fedha ya advance ya mwanzo alishapatiwa, lakini ana madai mengine. Tutaendelea kuhakikisha kwamba analipwa ili aendelee na kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya Songea - Tunduru, Tunduru – Masasi na Masasi – Mahumbika inaendelea. Nif changamoto za fedha ambazo kwa kushirikiana na wenzetu wa Wizara ya Fedha tutahakikisha mkandarasi analipwa ili kumwongezea uwezo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili kuhusu fidia, hivi karibuni Mheshimiwa Rais alienda ziara Mkoa wa Ruvuma na aliwaahidi wananchi wa Tunduru kwamba watalipwa fidia yao. Nataka niwahakikishie, Seirikali ya Awamu ya Sita itahakikisha wanalipwa fidia waendelee kutupa ushirikiano wanaotupa kwa kupisha maeneo yao ili miradi iweze kuendelea. Niwahakikishie ahadi ya Mheshimiwa Rais iko pale pale, watalipwa fidia yao na tunawashukuru sana kwa kupisha hayo maeneo ili miradi iendelee, ahsante.
MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa majibu mazuri ya Naibu Waziri, katika Kitongoji cha Changwahela kilichopo katika Kata ya Mapinga, mradi kama huo wa kupeleka umeme katika migodi ya wazalishaji chumvi umefanyika lakini wananchi wa kitongoji hicho hawajapata umeme. Je, ni lini sasa Serikali itawapatia umeme wale wananchi walio katika kitongoji hicho ili na wao waweze kufaidika na huduma hiyo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante nashukuru kwa swali la Mheshimiwa Mbunge, katika hiki kitongoji ambacho kipo katika Kata ya Mapinga, Mheshimiwa Mbunge, tumepokea changamoto hiyo na tutaenda kufanya survey kuona ni namna gani tutaweza kufikisha umeme katika kitongoji hiki na wananchi hao waweze kupata umeme wa uhakika. (Makofi)
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO: Mheshimiwa Spika, je, ni lini tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara katika Jimbo la Mbagala litaisha?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, ahsante, nashukuru kwa swali zuri la Mheshimiwa Abdallah Chaurembo. Nimhakikishie kwa kweli siyo kama ilivyokuwa mwaka jana, kwa kiasi tumepunguza kukatiwa kwa umeme katika Jimbo la Mbagala. Lakini, Mheshimiwa Mbunge, tunatekeleza mradi wa kuongeza transfoma pale kwenye kituo cha kupooza umeme cha Mbagala.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tukimaliza mradi huu wa kupanua kituo kile cha kupooza umeme pale Mbagala, basi tutakuwa tumemaliza kwa kiasi kikubwa changamoto ya kukatika kwa umeme. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge atupe subira kidogo ili tuweze kukamilisha mradi. (Makofi)
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa majibu mazuri ya Serikali na nipongeze kwa hatua hizo kubwa ambazo zimefanyika za uwekezaji huo mkubwa wa Kituo cha Nyakanazi na hatimaye kuweza kutuondolea tatizo la kukatika katika kwa umeme, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu wa Nyakanazi tulikuwa tunapata mradi wa umeme unaotoka Biharamulo kwenda Mkoa wa Kigoma au tunauita Kigoma – Nyakanazi ambao ulikuwa na vijiji 32, vijiji saba vikiwa Wilaya ya Biharamulo katika Kata za Kalenge na Nyanza na vijiji 25 Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujua sasa katika Wilaya ya Biharamulo, hivyo vijiji saba vya Kata za Kalenge na Nyanza mpaka sasa baada ya kumalizika mradi ule ni wateja wangapi wameunganishiwa umeme kutokana na vijiji hivi saba?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, mradi huu mkubwa wa kutoka Geita kuja Nyakanazi na kutoka Rusumo kuja Nyakanazi ulipitia maeneo ya watu na walistahili fidia. Nadhani mwaka jana Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati akiwa Biharamulo tuliomba wale watu ambao hawajalipwa pesa zao waweze kupatiwa pesa zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka kusikia kauli ya Serikali, mmefikia wapi na maandalizi ya kuwalipa pesa wale waliokuwa wamepitiwa na ule mradi ili sasa kwa sababu umeme unawaka na walipisha maeneo yao wao waweze kupata haki yao ya kulipwa fidia ambayo imechukua muda mrefu sana, wale waliokuwa wamebaki wachache kama 32? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge, Engineer Ezra Chiwelesa kwa kazi nzuri anayoifanya kuwatetea wananchi wa Biharamulo na ninaomba kujibu maswali yake kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika vijiji saba vilivyopo katika Kata za Kalenge pamoja na Nyanza mpaka sasa tumeshaunganisha wateja 615 na kwa sababu kazi hii ni endelevu, tunaendelea hivyo kadiri wananchi wanavyofanya wiring tunaendelea kuwaunganisha na umeme. kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kazi hii inafanyika vizuri sana na REA kwa kushirikiana na TANESCO.

Kuhusu swali la pili la fidia, ipo katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni Geita – Nyakanazi. Kwa Geita – Nyakanazi malipo ya Serikali yaani statutory compensation tayari imeshafanyika kwa wananchi wote, ambacho kimebaki ni top up compensation ambapo mkandarasi anatakiwa kuongeza ili waweze kulipwa kwa viwango vya kimataifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari tumeshaambiwa mshauri elekezi anatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuweza kufanya survey pamoja na masuala mengine ya kiutendaji ili wananchi hawa waweze kumaliziwa ile top up compensation ya mfadhili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipande cha Rusumo – Nyakanazi kulikuwa na wananchi 1,024 na wananchi takribani 986 wameshalipwa fedha shilingi bilioni 3.7 na wannchi waliobaki ni 38 tu ambapo wanadai shilingi milioni 81.02. Wananchi hawa hawajalipwa kwa sababu ya changamoto za mirathi na migogoro mingine, lakini fedha zao zipo na kadiri ambavyo wataweza kukamilisha taarifa zao na kuweza kumaliza migogoro na kukamilisha taratibu za mirathi watapatiwa fedha zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, fedha za wananchi hawa zipo, taratibu zikikamilika hawa 38 waliobaki katika kipande cha Rusumo – Nyakanazi na wenyewe watalipwa fedha zao, ahsante.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kahama ina mkandarasi mmoja tu wa kupeleka umeme wa REA vijijini pamoja na halmashauri zake tatu. Sasa ilhali amezidiwa na malalamiko ni makubwa sana kwa wananchi wetu, ni nini mkakati wa Serikali wa kupeleka kila halmashauri mkandarasi wake ili kuondoa malalamiko haya kwa wananchi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumpa pole Mheshimiwa Cherehani kwa changamoto hii ya mkandarasi. Nataka nimhakikishie kuwa tunafahamu changamoto ya mkandarasi huyu wa Kahama na tayari tumeshachukua hatua ikiwemo kukaa naye na kuweza kujua ni namna gani tunamwongezea nguvu ili aweze kuongeza kasi ya utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwombe Mheshimiwa Mbunge, ndani ya hizi wiki mbili, tatu mimi na yeye tuongozane twende Kahama ili tuweze kuangalia utekelezaji wa miradi hii katika eneo hili kwa sababu ni kweli kuna changamoto, lakini sisi dhamira yetu ni kutatua changamoto hizi ili wananchi wapate umeme kwa uhakika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunafahamu changamoto za mkandarasi na tutaendelea kumsimamia kwa weledi mkubwa sana kuhakikisha anamaliza kazi ambayo alitakiwa kuimaliza kwa wakati, ahsante.
MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, pamoja na pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Naibu Waziri na Wizara kwa ujumla kwa kazi ya kusambaza umeme vijijini. Mara ya mwisho nilikuwa nimekuomba kuhusiana na unyeti wa kupeleka umeme katika Vitongoji vya Songea Pori pamoja na Nindi ambavyo viko mpakani na Msumbiji. Nilikuwa napenda kukumbusha na kujua labda pengine kama kuna hatua ambazo tayari zimeshaanza kuchukuliwa, ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nianze kwa kumpongeza mama yangu Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya kwa kazi nzuri anayoifanya katika Jimbo lake la Nyasa. Serikali kwa mwaka huu wa fedha unaokuja 2024/2025 tayari tumetenga fedha ya kupeleka umeme kaika vitongoji 4,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Engineer Stella Manyanya kwamba hivi vitongoji viwili ambavyo amevitaja hapa kwa unyeti wa maeneo haya kwa sababu yako mpakani, tutazingatia ili na yenyewe yaingie katika mpango wa mwaka wa fedha unaokuja ili wananchi wa vitongoji hivyo waweze kupata umeme, ahsante.
MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali italipa fidia kwa wananchi waliopisha mradi wa umeme wa Gridi ya Taifa katika Jimbo la Tunduru Kaskazini? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze pia kaka yangu Mheshimiwa Zidadu Kungu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini kwa kazi kubwa anayoifanya katika jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipande hiki ni muhimu sana kwetu sisi kwa sababu ni sehemu ya mradi wa kupeleka umeme wa Gridi ya Taifa katika mikoa ya Mtwara na Lindi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, fidia katika eneo hili ni kipaumbele kwenye Serikali ya Awamu ya Sita na tunaendelea kufanyia kazi ili hivi karibuni wananchi hawa waanze kulipwa fidia zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie kaka yangu Mheshimiwa Zidadu na wananchi wa Tunduru kuwa fidia hii Serikali tunaenda kuilipa, watulie na watupe muda kidogo tumalizie taratibu ili tuanze kuwalipa, ahsante.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu mazuri aliyoyatoa, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwenye miradi hii ya vitongoji ambayo nimeitaja concern kubwa ni Kijiji cha Madeke ambacho mradi huu ulianza mwaka 2021 mpaka leo bado. Inaelekea kama kuna uzembe unaosababisha mradi huu usifanyike kwa spidi kubwa. Je, ni lini sasa Serikali itahakikisha Kijiji cha Madeke kinapatiwa umeme?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, katika Halmashauri ya Mji wa Njombe tuna maeneo ambayo yalikuwa identified ya uwekezaji na bajeti imeshaletwa kwenye Wizara, kwa ajili ya maeneo ya Ngaranga na Magoda. Ni lini sasa Serikali itakamilisha kupeleka umeme kwenye maeneo haya ya uwekezaji? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Mbunge Mwanyika kwa maswali mawili ya nyongeza. Moja ni kuhusiana na Kijiji cha Madeke; namhakikishia Mheshimiwa Mbunge wakandarasi ambao wanatekeleza mradi wa kupeleka umeme vijijini tunawasimamia kwa weledi mkubwa sana na ndiyo maana mpaka leo ni vijiji 400 tu kati ya vijiji 12,800 ndiyo vimebaki kupelekewa umeme. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge tutamfuatilia mkandarasi na tutamsimamia kwa nguvu sana, ili kuhakikisha anatumia muda ambao tumeutenga, kwa ajili ya kupeleka umeme kwenye vijiji ifikapo Mwezi Juni mwaka huu. Pia, tutafuatilia, ili kuona mkandarasi ana changamoto gani na kisha baada ya hapo tutamsimamia kwa nguvu sana, ili mradi huu ukamilike kwa wakati. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na sehemu ya Ngaranga pamoja na Mbagoda, ambapo kumetengwa fedha kwa ajili ya uwekezaji; kwa hili namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tutaendelea kufuatilia kwa karibu, ili kuhakikisha kwamba, mradi huu unaanza kutekelezeka. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge na ninamuahidi tutaendelea kufuatilia kuona utekelezaji wake unaanza hivi karibuni. Ahsante. (Makofi)
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Serikali imedhamiria kupeleka umeme vijijini kote nchini ikiwemo kwenye jimbo langu ambako vijiji vingi vinapatiwa umeme. Ni lini mtaanza kutekeleza kupeleka umeme katika vitongoji 15 katika Jimbo la Manyoni Magharibi, Halmashauri ya Itigi, ambavyo tulileta hapa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Namshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa swali kuhusu vitongoji 15. Kama nilivyosema mapema wiki hii, tupo katika hatua za mwisho za kumalizia, ili kuweza kuwapata wakandarasi katika maeneo haya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, suala la kupeleka umeme kwenye vitongoji, ambako tuko mwishoni kumalizia, ni suala ambalo ni la kipaumbele kwenye Serikali ya Awamu ya Sita. Ndiyo maana hata mwaka wa fedha unaokuja, 2025, tumetenga fedha nyingine, kwa ajilai ya kuanza mradi wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 20,000 ambapo kwa mwaka wa fedha 2025 tutapeleka umeme kwenye vitongoji 4,000. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunalifanya jambo hili kwa kasi kuhakikisha kwamba tunaanza kupeleka umeme vitongojini. Kwa jimbo la Mheshimiwa Mbunge, tutahakikisha pia kazi inaanza na vitongoji 15 vinapatiwa umeme huku tukisubiri mradi wa 2024/2025 ambao unaanza kupeleka umeme kwenye vitongoji 20,000, ahsante. (Makofi)
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, Serikali ya CCM imefanya kazi kubwa sana ya kupeleka umeme kwenye vitongoji mbalimbali na vijiji lakini sasa kwa sababu tuna-sort vitongoji, unakuta kitongoji A kimetoka kimekwenda kupata umeme, nguzo zimepita katika vitongoji C, B zimeacha, wenyewe wale A wamepata.

Serikali ina mkakati gani wa kutafuta transformer na nguzo ndogo, kuwapelekea mameneja wa TANESCO wa maeneo ya Bunda hasa Jimbo langu la Bunda ili vitongoji ambavyo vina nguzo kubwa, vipewe umeme kwenye maeneo ambayo yamepitiwa na nguzo?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, namshukuru Mheshimiwa Mbunge Getere kwa swali lake zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na kupeleka umeme kwenye vitongoji ambavyo viko mbele zaidi lakini havijapatiwa umeme na cha nyuma kimepatiwa umeme. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, maendeleo ni hatua, ilibidi tuanze kupeleka umeme kwenye vijiji ili tuweze kufikia yale maeneo ya vitongoji ambavyo havina umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kama vile ambavyo tulianza kazi ya kupeleka umeme kwenye vijiji, tunavyomaliza sasa, tunakuja hatua ya kupeleka umeme kwenye vitongoji. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, vitongoji vitapata umeme kulingana na jinsi ambavyo tunasogea. Vilevile, namuhakikishia kwa kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha vitongoji vinapata umeme na Mheshimiwa Mbunge atakumbuka kwamba tumetoka kwenye vitongoji elfu sitini naa, lakini leo hii tupo kwenye vitongoji 33,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tayari kazi kubwa imefanyika, naomba atuazime imani ili tuendelee kupeleka umeme kwenye vitongoji. Nataka kumtia moyo yeye pamoja na Wananchi wa Jimbo la Bunda kwamba watapata umeme, ni kwamba tu inabidi tuvumiliane kwa sababu maendeleo ni hatua, ahsante.
MHE. PROF. PALAMAGAMBA J. A. M. KABUDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu ya Serikali ya swali langu, ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza la nyongeza, je, ni lini Serikali itaimarisha ofisi ya TANESCO Dumila ili iweze kutoa huduma bora na kuweza kusambaza umeme katika Mji wa Dumila ambao unakua kwa kasi kubwa sana na sasa una wakazi zaidi ya 40,000?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, nguzo zimekuwa zinabadilishwa katika line ya sasa ya umeme na nguzo hizo bado ni bora na zinaweza kutumika. Je, Serikali inafikiriaje kuhusu kutumia nguzo hizo kueneza umeme katika vitongoji mbalimbali vya eneo la Jimbo la Kilosa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nampongeza Mheshimiwa Mbunge Profesa Palamagamba John Kabudi kwa maswali yake mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja, kuhusu kuimarisha ofisi ya Dumila ambapo kwenye hilo eneo la Mheshimiwa Mbunge kuna makazi zaidi ya 40,000. Kwa kweli, ni dhamira ya Serikali kuendelea kuboresha huduma kwa wananchi ili waendelee kupata umeme wa uhakika. Kama mtakumbuka, yalikuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, katika kuhakikisha kwanza, wafanyakazi wa shirika wanafanya kazi kwa weledi na kwa kweli amefanikiwa sana katika hilo. Pili, kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za umeme katika majimbo yote na katika maeneo yote ya Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kuimarisha Ofisi ya Dumila, tayari tulishaanza kufanyia kazi, siyo tu kwa Dumila, bali kwa majimbo mengine yote ambapo ofisi za TANESCO zipo. Kwa hiyo namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, pale kwenye mapungufu, tutaenda kuyaangalia na kuhakikisha kwamba Wananchi wa Dumila wanaendelea kupata huduma nzuri ya umeme ili kuboresha shughuli zao za maendeleo na za kijamii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na nguzo za umeme, tumepokea Mheshimiwa Mbunge na tunao mkakati wa kueneza nguzo kwa miaka mitano ijayo. Tutaenda kuangalia kwa eneo hili la Dumila mkakati wake umekuwaje ili kuhakikisha kwamba nguzo ambazo zinatakiwa zinaenda. Nafahamu Wananchi wa Dumila ni wananchi ambao kwa kweli wanajishughulisha sana hususan katika viwanda vidogo vidogo vya kukoboa mpunga. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tutaenda kuliangalia hili ili liweze kutekelezeka nawananchi waweze kuendelea vizuri na shughuli zao za maendeleo, ahsante.
MHE. BENAYA L. KAPINGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, mwaka jana niliuliza swali hapa kuhusiana na ujenzi wa sub-station Wilaya ya Mbinga na Serikali iliahidi kujenga sub-station mwaka huu. Je, ni lini sasa sub-station ya Wilaya ya Mbinga itajengwa?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na namshukuru Mheshimiwa Benaya kwa swali lake zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kweli, mradi wa kujenga kituo cha kupoza umeme pale Mbinga, upo katika hatua za kuweza kutekelezwa. Kama mnafahamu, mradi huu unatakiwa uanze kwa awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza ya sasa hivi kukamilika. Kwa kweli kwa awamu ya kwanza tumefanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ilivyokuwa kwa Mheshimiwa Profesa Kabudi kwamba unatekelezeka ndani ya awamu ya pili na ndivyo hivyo kwa kituo cha kupooza umeme Mbinga. Kwa kweli tutasimamia kwa weledi mkubwa sana na nguvu kubwa sana ili sub-station ya Mbinga iweze kujengwa. Kwa kweli kwa pale Mbinga, kwa sasa hivi tumefanya miradi mikubwa sana, kwanza tumeanza ku-stabilize line ambayo inapeleka umeme kutoka Songea hadi Mbinga. Vilevile, line za Mbinga Vijijini kwa sababu umeme ulikuwa unakatika katika sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo tumeanza kupeleka miradi ikiwemo miradi ya ujalizi ambayo kwa kweli Mbinga Vijijini ina miradi mingi sana, ina vitongoji vingi sana vya ujazilizi na inategemea kuanza hivi karibuni. Tutaendelea kuboresha ili kuhakikisha wananchi hawa wa Mbinga Vijijini wanendelea kupata umeme mzuri ili waweze kuboresha shughuli zao za maendeleo kwa sababu wananchi wa Mbinga Vijijini ni wachapakazi na wanajiendeleza sana katika maeneo ya viwanda vidogo katika maeneo ya kahawa na mahindi, ahsante sana. (Makofi)
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali iliahidi kuanza ujenzi wa kituo cha kupooza umeme pale Hanang mwaka 2022 na iliahidi itakamilisha mwaka 2023 mpaka sasa hakuna kilichoanza. Je, Serikali inaahidi nini Wana-Hanang ambao umeme kila siku unakatika?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa swali lake zuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu kupeleka kituo cha kupooza umeme Hanang, ni kweli kituo cha kupooza umeme Hanang, kipo pia katika awamu ya pili ya utekelezaji. Kwa hiyo nampongeza kwa kazi yake nzauri anayofanya na namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kama ambavyo tunaleta miradi mingi Hanang, tunamhakikishia kwamba baada ya kumaliza awamu ya kwanza, basi tutaenda awamu ya pili. Wananchi wa Hanang watapata umeme mzuri kwa ajili ya shughuli zao za maendeleo. Namwomba Mheshimiwa Mbunge awe subira tutatekeleza, ahsante.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Mheshimiwa Neema ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu la kwanza, sasa hivi bei au gharama ya kuunganisha umeme nyumba ambayo tayari ina umeme kwa maana ya extension na bei ya gharama ya nyumba mpya ambayo haijawahi kuwa na umeme inafanana.

Je, Serikali haioni kwamba ipo haja ya kutenganisha bei hii hasa kwa nyumba ile ambayo tayari ina umeme ili iwe nafuu? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, tunaishukuru sana Serikali imetuletea miradi zaidi ya minne ya umeme katika Jimbo la Hai, lakini bado vipo vitongoji ambavyo havijafikiwa na umeme. Kata ya Weruweru, Kata ya Mnadani, Kata ya Maili Sita, Kata ya Mnadani maeneo ya Maili Sita, pia Muungano, Boma Ng’ombe na maeneo mengine ambayo vitongoji vile havijafikiwa na umeme. Je, lini sasa Serikali itapeleka umeme kwenye vitongoji vilivyobaki katika Jimbo la Hai? (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kuhusiana na gharama za kuunganisha umeme kwenye nyumba mpya na gharama za kuunganisha umeme kwenye nyumba ambayo tayari ilikuwa ina umeme na labda mita imeharibika.

Mheshimiwa Naibu Spika, gharama za kufanya connection kwenye nyumba ni zile zile. Gharama ya mita, gharama ya waya na labour charge kwa nyumba ambayo inabadilishwa na nyumba mpya gharama hazitofautiani. Kwa hiyo, gharama hizi zinakuwa calculated kulingana na mita, waya, pamoja na labour labda kama kwa maeneo ya mjini kunahitajika nguzo ndiyo pale kwa nguzo moja huwa tuna-charge shilingi 518,000 na ukiwekewa nguzo mbili tuna-charge shilingi 696,000. Hivyo, gharama za msingi za kuweka connection kwenye nyumba ni zilezile, ni constant hazibadiliki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali la pili la Mheshimiwa Mbunge tunayo miradi ya vitongoji ambayo inaendelea pamoja na kwenye Jimbo la Hai mkandarasi yupo site kwa ajili ya vile vitongoji 15. Pia tuna mradi mwingine wa vitongoji ambao unakuja wa vitongoji 4,000. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Jimbo la Hai na wenyewe watanufaika, ahsante. (Makofi)
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kituo hiki kinasubiriwa kwa hamu sana na wananchi wa Mkoa wa Songwe kutokana na matatizo ya umeme yaliyopo ndani ya Mkoa wa Songwe kwani itaondoa utegemezi wa Mkoa wa Songwe kutoka Kituo cha Mwakibete pale Mbeya. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, tangu kuwashwa kwa mtambo wa umeme Na.9 katika Bwawa la Mwalimu Nyerere, sisi Mkoa wa Songwe bado hatujafaidika na kuwashwa huko kwani bado tatizo la umeme limeendelea kuwa kubwa Mkoani Songwe especially line ya Mlowo-Kamsamba na line ya Tunduma. Nini hasa kinachosababisha matatizo ya umeme kuendelea katika Mkoa wa Songwe licha ya kuwashwa kwa mtambo Na.9 katika Bwawa la Mwalimu Nyerere?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia maendeleo ya watu wa Mbozi na Mkoa mzima wa Songwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na umeme kukatika katika line ya Mlowo-Kamsamba pamoja na Tunduma. Mkoa wa Songwe unapata umeme kutoka katika Kituo cha Kupoza Umeme cha Mwakibete kilichopo Mbeya. Line kutoka Mbeya mpaka Songwe ni ndefu sana na hivyo kupelekea tatizo la low voltage. Serikali tumeshaliona, kwa sasa kupitia Mradi wa Gridi Imara tunakwenda kujenga switching station pale Songwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile kupitia Mradi wa Tanzania-Zambia Interconnector tunakwenda kujenga Kituo cha Kupoza Umeme Songwe kwa ajili sasa watu wa Songwe waweze kupata umeme kutoka Kituo cha Kupoza Umeme Songwe na switching station ambayo itakuwa Songwe. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wote wa Mkoa wa Songwe, tumeliona tatizo hili na tutalifanyia kazi kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Songwe, ahsante. (Makofi)
MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri alifika Urambo kuangalia Kituo chetu cha Kupozea Umeme kinachojengwa sehemu ya Uhuru. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri naweza kutwambia lini kituo kile kitaisha ili na sisi tupate umeme kwa sababu tuna tatizo kubwa sana la umeme Urambo? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia Kituo hiki cha Uhuru. Kituo cha Uhuru kipo katika hatua za kwenda kumalizika. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunakisimamia kwa hali na mali kuhakikisha kinakamilika na kinaanza kuwanufaisha watu wa Urambo. Kwa hiyo, kwa sababu kimeenda vizuri sana na hata fidia watu wa eneo la Urambo wamelipwa, nimweleze Mheshimiwa Mbunge azma ya Serikali ni kuhakikisha wananchi wa Urambo wanaendelea kupata umeme wa uhakika na tutasimamia Kituo hiki kimalizike ili wananchi wako wa Urambo waweze kupata umeme wa uhakika zaidi.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri ametoa ufafanuzi mzuri sana na kutoa matumaini mazuri sana juu ya Kituo cha Nkangamo kilichopo ndani ya Jimbo la Momba. Sasa kwa kuwa maisha ya wananchi yanaendelea na wanahitaji umeme; je, upi mkakati wa dharura wa Serikali kwa ajili ya kutusaidia kuondoa changamoto hiyo wakati tunasubiri mpango wa muda mrefu huu ambao ametoa ufafanuzi, naomba majibu ya kuridhisha? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mipango ya dharura tayari inaendelea. Kwanza tunaendelea na kuboresha miundombinu iliyopo katika Mkoa wa Songwe na majimbo yote yaliyopo katika Mkoa wa Songwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya pili ya dharura nimeelezea ni kujenga switching station pale Songwe kwa ajili ya kuboresha low voltage ya umeme ambayo inatokea Mwakibete hadi Songwe. Kwa hiyo niendelee kuwahakikishia Waheshimiwa Wabunge, tumeshaanza kuchukua hatua za dharura ikiwemo kuboresha miundombinu kuhakikisha umeme haukatiki katiki.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili; tunaenda kuanza utekelezaji wa kujenga switching station kwa ajili ya kuhakikisha tunapata umeme wa uhakika zaidi. Ahsante.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru swali langu la msingi linauliza ni lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile nina maswali mawili ya nyongeza; swali la kwanza narudia, ni lini mradi huu utakamilika?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, nini mpango wa Serikali katika kunusuru Mji wa Mpanda dhidi ya katikakatika ya umeme?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa kuendelea kufuatilia mradi huu wa kufikisha umeme wa Gridi ya Taifa Katavi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na lini mradi huu utakamilika? Nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Wana-Mpanda na watu wa Katavi wote kwa ujumla. Suala la kupeleka Gridi ya Taifa Mpanda na Katavi ni suala la kipaumbele chini ya Awamu ya Sita kuhakikisha mikoa yote ambayo haijaunganishwa na Gridi ya Taifa inaunganishwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamwomba kwa niaba ya watu wa Katavi watuvumilie kidogo, mradi unaenda vizuri na kwa maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati tunasimamia kwa weledi mkubwa sana na nina imani miezi michache ijayo tutakuwa tumekamilisha hii njia ya kusafirishia umeme, uzuri kituo cha kupooza umeme kimeshafikia 98%. Kwa hiyo, ni njia tu hii ya kusafirishia umeme itakamilika hivi karibuni na watu wa Katavi watapata umeme wa Gridi ya Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, swali lake la pili, tunaelewa umuhimu wa umeme wa uhakika Mpanda na Katavi kwa sababu wananchi wa Katavi ni wafanyakazi wazuri sana. Sasa kwa hatua za haraka, kwa maelekezo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati leo mafundi wetu watafungua mtambo wa megawati moja Biharamulo ili kuweza kuupeleka Mpanda pale ili kuweza kuongeza uzalishaji kwa sababu mahitaji ni megawati saba, lakini tunazalisha karibia megawati 6.15 tutaongeza megawati moja ili tuweze kupunguza mgao Katavi pamoja na Mpanda, ahsante. (Makofi)
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana, Serikali inatambua kwamba njia hiyo ya umeme haiwezi kukamilika bila kuwalipa wananchi wa Sikonge fidia ya shilingi bilioni 2.2 ambayo bado Wizara ya Fedha haijaipa Wizara ya Nishati hizo hela.

Sasa ni lini Wizara ya Fedha itatoa fedha hizo ili Wizara ya Nishati walipe fidia hiyo ili kukamilisha huo mradi?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Naibu Spika, suala la fidia la wananchi hawa wa Sikonge tayari tunalifanyia kazi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tupo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kufanya malipo haya na uzuri Wizara ya Fedha wameshaji-commit kwamba wanatoa fedha kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hawa. Tunaomba wananchi wa Sikonge, Tabora na yale maeneo ambayo wanadai fidia katika mradi huu wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Mpanda waendelee kutuvumilia, tutalipa fidia hiyo kwa sababu tayari tulishaji-commit kwamba tutalipa, ahsante.
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipongeza Serikali kwa majibu mazuri. Mradi huu umechukua muda mrefu na wananchi wa Wilaya ya Misenyi wamekuwa wavumilivu, lakini kupitia Serikali sikivu wameendelea kufanya kazi ili kuhakikisha wananchi wanapata haki yao. Sasa nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, je, kwa kuwa fidia hii imechukua muda mrefu na tathmini ilishafanyika, ni nini mpango wa Serikali kuhakikisha kwamba tathmini hii inakidhi muda wa kisheria wa tathmini ili wananchi hao waweze kupata fidia ambayo inaendana na wakati?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, je, niwaambie nini wananchi wa Misenyi kwamba watalipwa hiyo fidia kwa kuwa wameisubiri kwa muda mrefu sana? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kufuatilia fidia ya wananchi wake kwa karibu sana. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba sisi kama Serikali tunahakikisha fidia ambayo inalipwa kwa wananchi ni ile ambayo inaakisi muda na wakati. Kwa sasa tupo tayari kwa ajili ya kuanza kulipa na wenzetu wa Wizara ya Fedha wametuhakikishia mpaka ifikapo mwishoni mwa Juni, labda tutakuwa tunaanza kulipa fedha hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa jimbo lake wakae kwa utulivu, Serikali ni sikivu sana na tupo tayari kwa ajili ya kuanza kulipa fedha hizi, ahsante.
MHE. JAFARI W. CHEGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa ni mara ya tatu sasa nasimama ndani ya Bunge kuulizia fidia ya wananchi zaidi ya 246 waliopisha mradi wa umeme toka mwaka 2011. Mheshimiwa Waziri nataka kupata kauli ya Serikali, kwa kuwa sasa ni miaka 13 imepita, ni lini wananchi hawa watalipwa fidia yao kwa mujibu wa sheria?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Chege amekuwa akifuatilia suala la fidia la wananchi hawa ambao wako 246 ambapo gharama ya fidia yao ni shilingi 220,000,000/=. Nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa jimbo lake kwamba, tayari fedha hizi tunazo na tunaanza kulipa wananchi 211 ambao taarifa zao zipo vizuri. Wale wananchi 35 ambao taarifa zao haziko vizuri, tumeielekeza halmashauri jimboni kwake waweze kuzifanyia kazi ili na wenyewe wakae katika mpango wa kulipwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, mpaka tunafika Juni 30, wananchi hawa watakuwa wameshaanza kulipwa kwa sababu fedha tayari tunazo.
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Mradi wa REA, kuna vijiji vitatu vya Wilaya ya Chemba vilisahaulika; Kijiji cha Kelema Kuu, Kijiji cha Birise na Kijiji cha Muungano na bahati nzuri hatuhitaji sisi fidia, tunahitaji umeme tu. Naomba kujua, ni lini sasa vijiji hivyo vitawekewa umeme? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Monni amekuwa akifuatilia kweli vijiji hivi vitatu ambavyo vilisahaulika katika mpango, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshafanyia kazi na vijiji hivi vya Kelema Kuu, Birise na Muungano, tayari tumeshaongea na mkandarasi kwa ajili ya kumwongezea wigo ili aweze kuanza kufanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa hakuna kijiji kitaachwa kupelekewa umeme katika mradi huu ambao unaendelea. Kwa hiyo, wakae kwa utulivu, Serikali tumesikia na tutapeleka umeme katika hivi vijiji vitatu, ahsante.
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, wananchi wa Wilaya ya Makete wamepisha ujenzi wa Bwawa la Lumakali na ni takribani mwaka mzima umeisha toka watu wa ardhi wafanye tathmini. Wanauliza, ni lini Serikali itawalipa fedha ili wananchi wetu waendelee na shughuli za kiuchumi kwenye eneo lile?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba katika bajeti ya mwaka unaokuja wa fedha 2024/2025, tumetenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia wananchi hawa ambao wamepisha Mradi wa Lumakali. Tunaendelea kufanya tathmini ili kuweza kuelekea kwenye zoezi la fidia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kuwa malipo ya fidia yapo katika bajeti kwa sababu mradi wa Lumakali ni mradi mmojawapo ambao sisi kama Serikali tunautegemea katika kuzalisha umeme, kwa hiyo, wananchi hawa watalipwa fidia. (Makofi)
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa maswali mawili ya nyongeza. Nataka kukiri mbele yako, kwamba lazima tuuseme ukweli kwamba umeme umepungua kukatika na tangu Waziri wa Nishati na Naibu Waziri Mkuu, Mheshimiwa Dkt. Biteko afike Kilombero atoe tamko lile kwamba tuna mgodi wa kuzalisha umeme, umeme usikatike, umeme haujakatika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka nikiri mbele yako, ukiona umekatika ujue basi yule anayeshika switch amezoea tu kukatakata lakini haukatiki umeme sasa hivi. Tunaishukuru Serikali ya Chama cha Mapinduzi, tunamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Zaidi ya mara mbili nimeuliza maswali mawili madogo ya nyongeza katika Bunge lako kuhusu bei. Kwangu kunaitwa Halmashauri ya Mji wa Ifakara, lakini nina vijiji 48. Katika vijiji hivyo 48, kuna maeneo ya vijiji Kata ya Katindiuka na Kata ya Kidatu wanatozwa bei ya mjini kwa sababu ya hilo jina la Halmashauri ya Mji wa Ifakara.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu, tuliomba Kata ya Katindiuka na Kata ya Kidatu katika hivyo vijiji ambavyo wanatozwa bei ya mjini, warudushiwe bei ya zamani. Je, ni lini Serikali itarudisha bei hiyo? Hilo swali la kwanza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, niliiomba Serikali vijiji vyangu 15, nikaleta na orodha kwamba viunganishiwe umeme. Je, ni lini vitaanza kuunganishiwa umeme? Ahsante.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Asenga amekuwa akifuatilia sana maendeleo na hususan masuala ya umeme katika jimbo lake. Nakiri kwamba ni kweli hizi kata mbili za Kidatu na Katindiuka amekuwa akizifuatilia kwa karibu sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, maeneo ambayo yanapaswa kufanyiwa marejesho kwa Tanzania nzima ni mengi sana. Mwaka 2023 wakati Mheshimiwa Rais anafanya ziara Mtwara, alituelekeza Aizara kwamba tupitie maeneo haya upya ili tuone yale ambayo yanatakiwa kulipa shilingi 27,000 na yale ambayo yanatakiwa kulipa shilingi 320,960. Zoezi hili tumeshalifanyia kazi, tumeshaainisha maeneo 1,500 na kwenye jimbo la Mheshimiwa Mbunge, tumeainisha maeneo 10, lakini nakiri, maeneo ya Kidatu na Katindiuka, bado tunaendelea kuyachakata ili kuona na yenyewe kama yanaweza kuingia katika list ya yale maeneo 10 na yenyewe tuweze kuyaweka katika mchakato wa kupunguza bei.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi na Waheshimiwa Wabunge wote, yale maelekezo ya Mheshimiwa Rais tumeanza kuyafanyia kazi. Tumeshaainisha maeneo 1,500 na tunaendelea kufanya hivyo ili baadaye tutafute mafungu kwa ajili ya kubadilisha kutoka shilingi 320,960 hadi shilingi 27,000.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na suala la pili la vitongoji 15, tunamaliza, tupo katika hatua za mwisho za zoezi la zabuni ili kuweza kumpata mkandarasi kwa ajili ya kuanza kufanya kazi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kabla ya mwezi huu kwisha, tutakuwa tumepata mkandarasi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa kupeleka umeme katika vitongoji hivi 15, ahsante.
MHE. GRACE V. TENDEGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi. Kumekuwa na changamoto kwenye miundombinu ya line za umeme hasa Mkoa wa Iringa na kusababisha kukatikakatika mara kwa mara na hii kuleta adha kwa wananchi wetu. Je, ni lini mtamaliza changamoto hizi ili wananchi waweze kupata umeme wa uhakika?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Grace Tendega. Suala la kukatikakatika kwa umeme ni kweli linaweza kuwa hivyo kutokana na changamoto ya miundombinu. Kwa kila mwaka wa fedha, tunatenga bajeti kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya umeme kwa ajili ya kupunguza na kumaliza kabisa changamoto ya kukatika katika kwa umeme.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa Mkoa wa Iringa kwa kiasi kikubwa, tumekuwa tukifanya matengenezo makubwa kwa ajili ya kupunguza kukatikakatika kwa umeme. Mheshimiwa Mbunge ni shahidi, suala la kukatikakatika kwa umeme kwa upande wa Iringa, limepungua kwa kiasi kukubwa sana. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Mkoa wa Iringa, tunaendelea kufanyia marekebisho kwenye miundombinu yetu ya umeme ili kuweza kuiondoa kabisa changamoto hii ya kukatika katika kwa umeme.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kukatikakatika kwa umeme katika Jimbo la Kilombero ni sawasawa na kukatikakatika kwa umeme katika Manispaa ya Morogoro. Je, ni lini umeme utaacha kukatikakatika katika Manispaa ya Morogoro?
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Manispaa ya Morogoro, tumekuwa tukiboresha miundombinu na hata pale katika Kituo cha Kupooza Umeme cha Morogoro, tumefanya extension ya kuongeza transformer nyingine kwa ajili ya kuimarisha nguvu ya umeme na kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Manispaa ya Morogoro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kwa kiasi kikubwa katika Manispaa ya Morogoro, kutokana na kuongeza miundombinu hii, tumeweza kupunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme. Kama nilivyosema hapo awali, kukatikakatika kwa umeme ni changamoto ya miundombinu, na kadiri ambavyo tunaendelea kutenga bajeti, tunaendelea kufanya kazi changamoto hii ili mwisho wa siku tuondoe kabisa changamoto hii katika Manispaa ya Morogoro.
MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Spika, taarifa za CAG pamoja na Kamati za Kudumu za Bunge toka mwaka 2009 zimekuwa zikieleza mapungufu makubwa yaliyopo kwenye mkataba wa SONGAS, nataka kujua Serikali ilishachukua hatua gani kwa GNT (Government Negotiation Team) ya wakati huo ili ya sasa Government Negotiation Team isifanye makosa yale.

Mheshimiwa Spika, swali la pili, chanzo cha Tanzania kupata alama ya chini kwenye tathmini ya EIT ya mwaka 2023 ni kutokana na mikataba kutowekwa wazi kinyume na sheria ya Tanzania Extractive Industry Transparency Act ya Mwaka 2015. Nataka kujua Serikali ni lini mtaleta mkataba huo Bungeni, sisi kama Wabunge tuujadili kabla ya kuusaini. Ahsante. (Makofi)
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maswali yake mawili ya nyongeza, kwanza kuhusiana na hii timu ya wataalamu. Mwaka jana mwezi Aprili timu ya wataalam iliundwa na walipewa jukumu la kuchambua mikataba yote ya Mradi wa SONGAS ikihusisha mikataba ya msingi (basic agreements) vilevile mikataba ya fedha (financial agreements).

Mheshimiwa Spika, ilivyofika mwezi Disemba tulianza majadiliano, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Bunge lako hili Tukufu kwamba, timu hii ya wataalamu ambayo imewekwa kwa ajili ya majadiliano ya nyongeza ya mkataba wa mauziano ya umeme kati ya TANESCO na SONGAS na mikataba mingine ambayo inahusiana. Ni timu ya wataalamu wenye weledi mkubwa sana na imehusisha maeneo yote ya msingi, lengo kuu ni kuhakikisha hatufanyi makosa yoyote tunapoenda kwenye mikataba ya namna hii.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na suala la pili la mikataba kuwa wazi, kwa sababu sasa hivi hatujafahamu kama tutaendelea na mkataba huu ama hatutaendelea na mkataba huo, inaniwia vigumu kusema ni lini tutaleta mkataba huo Bungeni lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, section 16 ya Sheria ya Extractive Industry ni kweli inataka uwazi kwenye mikataba na leseni za sekta ya uziduwaji na sisi kama Serikali tunahakikisha mara zote tunaenda kwa mujibu na matakwa ya sheria hizo. Kwa hiyo nimhakikishie kama tutafikia hatua hiyo basi tutawajibika kulingana na sheria. (Makofi)
MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nina maswali madogo mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; umeme ni maisha na sasa watu wanatumia umeme kufanya mambo yao yaende vizuri, sasa lakini kutoka shilingi 320,000 kwa vijiji ambavyo ni vidogo, ambavyo wamevionesha kama ni vijiji mji.

Je, Serikali ipo tayari sasa vile vijiji vidogo vilivyokusanyika pamoja kama vijiji vya Itigi ambavyo ni vijiji saba kwa pamoja, Kijiji cha Mitundu, viwalipe 27,000?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; wananchi wanapolipa hizo gharama za kuunganishiwa umeme Serikali inachukua muda mrefu sana. Je, Serikali inasemaje, ni muda gani mahsusi, mtu akishalipia umeme anakuwa anajua kwamba atafungiwa mita? Ahsante sana.
NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Spika, nimshukuru Mheshimiwa Mbunge kwa maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza kuhusiana na gharama kwenye maeneo ya vijiji mji, Serikali tumeshaanza kufanya mapitio kwenye maeneo ambayo tunadhani yanatakiwa kupunguziwa gharama kutoka 320,960 hadi shilingi 27,000.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa tumeshaainisha maeneo 1,500 na kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hiki Kijiji alichokisema na vijiji vingine vya Itigi pia vimepitiwa. Tutaenda kufanya mapitio zaidi ili kuona kama hicho Kijiji ambacho Mheshimiwa Mbunge amekitaja kinaweza kuingia katika mapitio haya.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kuunganisha umeme tunaendeleza kuboresha huduma kuhakikisha wananchi wanaunganishiwa umeme kwa wakati. Suala la kuunganisha umeme lina sehemu mbili yaani mwananchi kufanya wiring na sisi kisha kupeleka huduma ya kuunganisha umeme. Tuendelee kuwasisitiza wananchi pale ambapo huduma ya umeme inafika kwenye maeneo yao waweze kufanya wiring kwa wakati na sisi tutaendeleza kuboresha huduma ili kuhakikisha huduma ya kuunganisha umeme kwa wananchi inakuwa ya haraka na ya uhakika, ahsante.