Contributions by Hon. Dr. Charles Stephen Kimei (48 total)
Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii. Nami nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa nafasi siku hii ya leo nina afya tele. Pia nishukuru chama changu cha CCM kwa kunipa fursa ya kugombea kwenye Jimbo lile la Vunjo ambapo wananchi wake walitupa kura kwa wingi na CCM ikashinda kwa kishindo, kwa hiyo, CCM oyee.
WABUNGE FULANI: Oyee.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, niseme hivi, mimi niliyesoma hivi vitabu vitatu nasema ni kitabu kimoja ambacho bado kinaandikwa bado hakijaisha na naamini kwamba itakapofika mwezi Juni, 2025 tutaona chapter ya nne na pengine ikimpendeza Mheshimiwa Rais tutaona na chapter ya tano itakayokuwa inatuonesha kwamba dira ya 2025 kwenda 2050 itakuwaje lakini ni kitabu kitamu na utamu wake ni kwa sababu una happy ending, unaishia pazuri.
Mheshimiwa Spika, niliposoma nimeona kwamba katika hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyotoa Novemba 2015 anaanza na mambo magumu sana ya kuunda utawala bora na kutafuta uongozi ambao ungeweza ukapigana na mmomonyoko wa maadili ndani ya Serikali, kurudisha nidhamu na kuhakikisha kwamba mapato ya Serikali yanakusanywa vizuri na yanatumiwa vizuri. Naamini kwamba kwa kile alichokifanya kuunda uongozi ambao aliweza kufanya nao kazi lakini pia akawa anatumbuatumbua mpaka tukaona mambo yamesimama vizuri ndiyo sababu tunasema kwamba kusema kweli ni fundisho kubwa linalosema kwamba maendeleo ya Afrika, maendeleo ya Tanzania yanatokana na uongozi bora. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini uongozi bora siyo viongozi bora ni kiongozi mmoja ambaye anajitokeza, the leader, ana make a big difference katika mambo yote yanayofanyika kwenye nchi au kwenye kampuni inakuwa hivyo hivyo, kama ukiwa na kiongozi bora utaona matokeo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nashukuru na nasema kwamba kusema kweli ukisoma kitabu hiki ambacho kinaandikwa hakijaisha natumaini utaona wazi kwamba tumempata kiongozi ambaye anastahili sifa kwa kila Mtanzania. Hata mtiririko wa namna anavyoelezea dira na mkakati wake na malengo yake na milestone za kufikia na namna ya kutathmini utaona wazi kwamba ni kitu ambacho kinaeleweka kwa kila mtu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, utaona kitu kama hicho hata ukimuuliza bibi yangu pale mgombani kule Moshi wewe ni nani? Anakwambia mimi ni Mtanzania naenda kwenye uchumi wa kati, kipato cha kati na baadaye tutafika kwenye kipato cha juu. Kwa hiyo, kila mtu anaelewa ni kitu gani. Lengo kuu la nchi ni kuinua kipato cha Mtanzania.
Mheshimiwa Spika, katika hotuba yake aliyotupa kwenye ufunguzi anasema wazi kwamba sasa amejua kutakuwa na miundombinu lakini hailiwi, lazima sasa tuweze kuwezesha wananchi wetu na wale tunaowaongoza kuongeza kipato chao, wajasiriamali kwa kuwawezesha kupata mikopo na kadhalika ili waweze kuinua kipato chao. Kwa hiyo, nasema kwamba kwa logic ya hiki kitabu kiko vizuri sana.
Mheshimiwa Spika, nimsifu kwa kitu kimoja, katika nchi ambayo inaenda kwa kasi tunayoona, kasi ya ukuaji wa pato la Taifa kwa asilimia saba kwa wastani, lakini miradi mikubwa inatekelezwa. Utakuta kwamba mataifa mengi yanashangaa kwamba bado tumeweza kuendelea na utulivu wa uchumi mkubwa. Utulivu huo umetokana na umakini wa Mheshimiwa Rais, lakini pia tumpongeze Mheshimiwa Dkt. Mpango, Waziri wetu wa Fedha na Mipango pamoja na Gavana wa Benki Kuu kwa ushauri mzuri waliotoa. Kwa sababu wangeweza wakachukua njia rahisi ya kufanya inflation finance maana ku-print pesa na kukuza mfumuko wa bei. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wao hawakufanya hivyo, wametumia njia ngumu ya kukusanya mapato kutoka kwa Watanzania, hiyo njia ngumu kuliko ku-print pesa au kukopa tu na ni kweli kwamba hii miradi mikubwa ungekuta kwamba inashawishi watu sana kuchukua mikopo ya ziada, lakini nashukuru kwamba hawakufanya vile wamefanya kitu ambacho ni kigumu, lakini tunaona matunda yake ni mazuri na ndio hapa unasema hapa tunaona kuna happy early.
Mheshimiwa Spika, sasa niseme hivi tumeona kuna utulivu wa uchumi wa ujumla ndio, exchange rate imekuwa stable, mfumuko wa bei uko chini, riba zimetulia lakini hazijatulia mahali pake kwa sababu ziko juu bado watu wanalalamika riba asilimia 15 inflation asilimia tatu, really interest rate ni kubwa sana. Kwa hiyo, kinachohitajika sasa ni pengine tuhakikishe kwamba tunaendeleza sera hizo za kuhakikisha kwamba riba nazo zinashuka kwenye mabenki yetu. Utaona mabenki yanarekodi faida kubwa sana, mwaka huu kwa mfano, faida za mabenki ni kubwa sana kwa sababu wanatoza sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nitoke hapo niseme hivi, kwa kuona kwamba miundombinu inaboreshwa vizuri, sasa njia ya peke ni kuongeza uwekezaji na tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kusema kwamba ameunda Wizara ndani ya ofisi yake ambayo inashughulika na uwekezaji. Niseme hivi kwamba private sekta haitaweza kunufaika sana kama blue print aliyoizungumza Mheshimiwa Mwijage haitatekelezwa kwa umakini na kwa haraka zaidi. Inatekelezwa kwa speed tofauti tofauti kwenye kila Wizara, lakini ingetekelezwa kwa speed ile wanayotekeleza kwa mfano Wizara ya Viwanda naamini ungekuta vitu vinabadilika na pengine private sector ingeweza ikaanza kushika hatamu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kwamba tatizo kubwa katika sekta binafsi ni kusema kwamba uwekezaji lazima uwe mkubwa sana, kumbe sasa hivi uwekezaji hata kwenye nyumba yako unaweza kwa sababu kuna umeme. Ukishakuwa na umeme unaweza ukawa na kiwanda kidogo cha kuchakata hata ndizi na hiyo ndio njia peke kusema kweli ya kuinua kipato kule kwetu mashambani kwa kuunda viwanda vidogo kwa vikundi au kwa mtu mmoja mmoja ambaye ataweza kuchakata mazao akayaongezea thamani na yale mazao yakauzwa sehemu nyingine ambapo hayapatikani au ambapo yanahitajika kwa wakati ule.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kusema kwamba pengine tuangalie namna gani ya kuwawezesha vijana wetu au wajasiriamali wanawake na wengine na hata akinababa kwa kuwapa exposure. Nikasema exposure haiwezi kutolewa kwa kumpeleka mtu China kuangalia maonesho China hapana, exposure ni kwamba pengine Shirika letu la SIDO lingekuwa karibu zaidi kule kwenye vijiji sasa linashughulika kwa kuona kwamba kweli linaonesha watu kwamba kuna kiwanda kidogo cha shilingi milioni moja au laki tano na hiki kiwanda unaweza ukakitumia mkiwa vijana watano, mkakitumia mkaongeza thamani mkapeleka mkauza. Naamini kwamba hicho lazima kifanyike na naamini kwamba Wizara inayohusika itafanya hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunazungumza mambo ya mikopo, kupeleka watu vyuo vikuu, hii nataka kusema katika uchumi tunaojenga sasa hivi uchumi wa kati, tatizo kubwa ni skills study zile za watu kufanya vitu kwa mkono sio kuwa na degree sio kuwa na ma-Ph.D hayatasaidia sana. Utakuta kwamba unemployment kati ya watu waliomaliza chuo kikuu ni kubwa sana lakini mtu anayetengeneza simu, simu hizi tunazotembea nazo hizi mfukoni ukimtafuta mtaani humpati na wana kazi, mechanic wote wana kazi lakini tatizo moja tunasema tu kwamba elimu yetu inalenga chuo kikuu, hapana! Huko ni kwa zamani, elimu ilenge daraja…
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: …baada ya kumaliza form six watu wengi waende kujifunza kazi za mikono, study za mikono. Kwa hiyo, vyuo vya ufundi viongezeke…
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Lakini na vyenyewe vibadilishe mwelekeo sio kuangalia zile study zilizokuwa zinahitajika zamani tuangalie study za kisasa, electronic base na ambazo…
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kimei pokea taarifa, jitambulishe Mheshimiwa nani.
T A A R I F A
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, naitwa Mheshimiwa Musukuma, ningependa kumpa taarifa tu Mheshimiwa Dkt. Kimei kwamba anavyochangia anasema tuache kuamini ma-degree na ma-PhD. Nampa taarifa tu kwamba duniani kote matajiri wengi hawana degree. (Makofi/Kicheko)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, napokea taarifa!
SPIKA: Kabla Mheshimiwa Dkt. Kimei hujapokea taarifa hiyo, nisisitize tu Waheshimiwa Wabunge mumsikilize Mheshimiwa Dkt. Kimei hoja yake, ni hoja ya msingi sana. Hii habari kila mwanafunzi anaenda chuo kikuu anasoma vitu vya ajabu ambavyo tumezoea traditionally, sitaki kuyataja masomo, yako masomo yaani ni kama kumpotezea mtoto tu direction. Yalikuwa na maana enzi hizo, lakini leo hii dunia ya sasa, dunia ya uchumi wa kati, ndio hii anayopendekeza Mheshimiwa Dkt. Kimei. Skills na kwa hiyo hata mfuko wa mikopo uelekeze zaidi mikopo yake huko. Mheshimiwa Dkt. Kimei hebu rudia hiyo hoja yako bwana, nakupa dakika tatu. Katibu hebu iweke vizuri. (Makofi)
Waziri wa Elimu amekaa vizuri anakusikiliza sasa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ndio nasema hivyo kwamba, kusema kweli mahitaji ya uchumi wetu wa sasa hivi ni watu wanaoweza kutenda na mahitaji ni kwamba watu wana magari lakini hawawezi kutengeneza, ukitafuta fundi hakuna kwa sababu hakuna mtu anayefundisha vitu hivyo na siyo tena kutengeneza magari ambayo ni ya ajabu, sasa hivi tengenezeni magari ambayo lazima zile shule zetu za ufundi na zenyewe zi-adopt mahitaji ya sasa hivi. Ukienda uka-register wanafunzi utapata wanafunzi utapata wengi sana ukitafuta kwenye electronic base industry na nini utapata, lakini ukienda kwa ile ya zamani kwamba sijui unataka mtu wa kuranda. Tuna chuo cha ufundi pale kwetu Mamba pale lakini hakuna mtu anaenda kwa sababu wana mashine za kuranda wanafundisha kuranda au cherehani za kushona lakini ni zile za zamani sasa hivi kuna cherehani za kisasa.
Mheshimiwa Spika, niendelee kwa kusema hivi kwa kule kwetu kama anavyosema Mheshimiwa Saashisha, kusema kweli zao la kahawa limedorola sana na nashukuru kwamba Mheshimiwa Rais aliweka hilo pia katika zao la kimkakati. Hata hivyo, niseme hivi kule Kilimanjaro ile ardhi imeshadidimia haifai tena hata kulima kahawa, utatumia madawa mengi na watu hawajui kutengeneza composite, kwa hiyo unakuta kwamba ile kahawa ukiipeleka kuuza nje tena hupati hata wanunuzi. Halafu bahati mbaya pia vile vihamba vyetu, yale mashamba yetu yamekuwa tragmented mtu mmoja ana robo heka, atalima wapi.
Mheshimiwa Spika, sasa namwomba Mheshimiwa Lukuvi, Waziri wa Ardhi, sisi Wachaga wengine tunataka tuhamie mahali ambapo kuna ardhi, tukalime huko, mambo ya kusongamana kule haifai na wameniomba wananchi wangu wa Vunjo kwamba jamani ukienda tafuta mahali utakakoweza kutupeleka tukalime tupate eneo tulime na sisi tuwe na tija, tuwe na mabilionea na sisi, lakini kusema kweli kule Uchagani huwezi kuwa bilionea kwa sababu hakuna ardhi. Watu wa kule Vunjo tuna shida hiyo na nitakuja kumwomba Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, atusaidie.
Mheshimiwa Spika, mwisho, niseme hivi katika rasilimali tuliyonayo sisi kule Kilimanjaro, ni mlima Kilimanjaro na ni kweli wana Vunjo na wengine wote wanaozunguka ule mlima wanapata shida sana. Shida kubwa ni kwamba ajira haipatikani, vijana wengine wanaokuja kupata ajira kule ni kutoka maeneo mengine, lakini hata wale wanavijiji wanaozunguka ule mlima, ile nusu maili hawaruhusiwi kutumia, siku hizi wanapigwa, walikuwa wanasema ni wanawake tu waende huko, sasa wanawake wakaenda wenyewe, baadaye na wenyewe wakanyimwa kwenda huko kutafuta kuni, kutafuta majani ya ng’ombe na mbuzi na kadhalika. Sasa tunamwomba Waziri wa hifadhi naye atuangalizie hilo na ni jambo kubwa.
Mheshimiwa Spika, mambo ya barabara yameshazungumza sana. Naunga mkono hoja ya kuongeza Mfuko wa TARURA, kusema kweli barabara zetu zina matatizo japokuwa hata zile ambazo zinatakiwa ziwekwe lami zimeahidiwa lami tunazo hizo kama tatu hivi ambazo Mheshimiwa Rais naye alituruhusu…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Naona kengele imelia.
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Kimei, tunakushuru sana…
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa moyo moja na sisi tutatekeleza kila jambo ambalo liko kwenye hotuba hii. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026) na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Mwaka 2021/2022 pamoja na Mapendekezo ya Muongozo wa Maandalizi ya Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2021/2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa muda huu uliniopa nizungumze. Ninayo mengi kidogo,kwahiyo nitaenda moja kwa moja kwenye mjadala huu. Pia nikupongeze wewe kwa namna ambavyo unatuongoza, kusema kweli inatupa hamasa kubwa sana kuwa Bungeni hapa.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nasema kwamba naunga mkono kwa asilimia mia moja Mpango ambao umewasilishwa hasa kwasababu nafikiria kwamba mpango huu una uhalisia kwa kiasi kikubwa. Uhalisia kwamba assumptions zilizotumika kwa mfano ya kusema kwamba tunaweza tukaongeza pato la Taifa mwaka ujao kwa 6.3%,wangeweza wakasema 7%, lakini wamesema 6.3%, naamini ni achievable kwasababu ya misingi ambayo tumeijenga. Naamini kwamba kuna mambo mengi ambayo yanaweza yakatuteteresha kwasababu hatujajua dunia ina kwenda wapi kwasababu ya wingu ambalo bado lipo kuhusiana na corona kwenye nchi za nje, lakini naamini endapo hali itabadilika kidogo tunaweza tukafikia hiyo 6.3% kwa mwaka ujao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana pia wastani wa 8% utafikiwa mwishoni mwaawamu, lakini inawezekana pia hata 7%, ni nzuri sana kwasababu wale wanaojua kanuni ya ukuaji cumulative(limbikizo la ukuaji)wanaita ni the low ofcumulative growth. Kama unaongeza pato lako kwa asilimia 6.0 kwa mwaka unaweza uka-triple hiyo kwa miaka siyo zaidi ya miaka 10. Kwahiyo naamini kwamba tunaweza tukafikia hiyo nanihi yetu ambayo ni pato la uchumi wa kati, kiwango cha juu.Kwahiyo naamini tupo sawasawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho nakosa tu kwenye huuMpango, nilikuwa natamani sana nione mipango ambayo imekaa fungamanishi kama kwa mfano ulivyokuwa mpango wa SAGCOT ambao unaeleza vitu vingi ambavyo vinasaidianaili kuhakikisha kwamba ile corridor inatoa kitu. Sasa kuna mipango kama huo wa SAGGOTambao naamini kwamba bado uko unatekelezwa. Nilikuwa nataka tuone kamalogisticsmapaulogistics plan za kufanya Tanzania hususan Dar es Salaam kuwa ni logistichub ya nchi hizi ambazo zinapakana na sisi, lakini sijauona vizuri. Ndiyo tunajenga vizuri infrastructure ile ya kutufungulia mipaka na kupeleka vitu kwenye mipaka na tuweze kupata a lot of value additions, lakini bado naona haijafungamanishwa sawasawa,ili kuona zile corridor tulizonazo zote zitatusaidia namna gani kuongeza kipato chetu bila kutegemea sana vitu vingine ambavyo ni more primary.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba wengi wanasema kilimo, kusema ukweli ni kizuri, lakini nataka kuwatahadharisha kwamba Mheshimiwa yuko sahihi anaposema kilimo hakilipi kama hatuna viwanda. Bado watakaoweka bei kama tutawauzia primary product watakuwa bado ni walaji wa kule nje, ni walaji wa Ulaya na wanapoona kwamba tunataka kufanikiwa watazidi kutubana, watasema bei ziko hivi bei zitaanza kutuvuruga, kwahiyo njia tu pekee ya kuweza kuhakikisha kwamba beiya mazao yetu inaimarika ni kuhakikisha kwamba tuna-process, tunauza kitu ambacho kinaweza kikahifadhiwa, kikafika kwenye masoko tofauti tofauti kwa bei ambayo siyo ile inakuwa dictated by the consumers. Kama consumers ata- dictate bado utapata matatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti,kama ninavyosema kilimo lazima tunapokizungumzia tuseme tutafanyaje tukiunganishe na viwanda ili kiweze ku-process. Niseme kwamba tumezungumza mambo mengi kuhusiana naukuaji nakadhalika, lakini ni lazima tuzungumzie strength. Watu wanapotengeneza plan yoyote unaangalia strength zako ni nini na ni sawa tukasema ni uongozi bora, amani, utulivu, mshikamano na vitu vyote hivyo na siasa safi, lakini kitu ambacho hatujakiona ni ile strength tuliyojenga kwa kutuliza uchumi wetu ukawa tulivu ambao mfumuko wa bei upo chini, wenye exchange rate ambayo ni nzuri nakadhalika ambayo inatufungulia milango ya kuweza kuisaidia Serikali yetu kuweza kukopa kwa bei nafuu kabisa.(Makofi)
Mheshimiwa MWENYEKITI,tunapoangalia mipango hii mara nyingi tunajua tunatumia cash budget, sasa tukianza kuzungumza mpango kwa kuanzia kwenye matumizi kwa kuorodhesha vitu gani tunataka vifanywe, kwanza niseme naomba Mungu ajaalie kwamba pamoja na mafanikio tuliopata kwenye miundombinu, kule Vunjo wamesahau. Naomba wasisahau zile barabara zetu kule Vunjo,lakini kama tutaorodhesha kila mtu aorodheshe vitu, the shopping distance is huge,TARURA inataka pesa,TANROADs inataka pesa, halafu bado wengine wanasema Serikali ijenge viwanda, hili hapana, Serikali haiwezi kujenga viwanda, zaidi Serikali iwezeshe kwenye viwanda vya kimkakati ambavyo tunatakiwa Serikali kama tunavijua kwenye maelekezo ya hotuba za Rais. Hiyo ya kuwezesha viwanda vya kimkakati hata kama ikiingia ubia lakini kuhamasisha, sera ziwe safi,blue print iwepo, mambo yawe sawasawa.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti,kusema kweli hatuwezi kusema Serikali ikajenge viwanda vya alizeti nakadhalika hatutaweza hiyo, tuwezeshe watu na ndiyo kazi yetu kwenye zile kamati ambazo zinahusika. Kwahiyo nataka kusema hiyo tuwe makini,kwasababu hatuwezi kuorodhesha. Nimejifunza kitu cha msingi sana na nimefurahia sana Wabunge fulani wameanza kusema kwanini tusipate fedha namna hii. Kwasababu cha kwanza ni mapato, je, yanatoka wapi? Kuna Mheshimiwa Shabiby alisema pengine mapato tuongeze tozo kwenye matumizi ya mafuta na tena akatoa pia mawazo ya namna hii, yale ndiyo mambo tunataka tujue kwasababu ukishapata zile fedha ukimpa Rais wetu anazitumia vizuri, anajua kuzisimamia kwa ufanisi,zitazaa vyovyote tunavyotaka, lakini tuangalie na nashukuru wale wanaozungumzia kwamba tuzibe mianya ya pesa kupotea.
Mheshimiwa Mwenyekiti,tax effort yetu we mention kwenye hizi documentis 13%,12.9% ndiyo revenue effort tuliyofanya mpaka mwaka jana na tunaendelea kusema mwaka unaokuja 13.3% ndiyo tax effort, nchi nyingine hata hapo Kenya 23% ya GDP, uwiano kati ya mapato ya Serikali na GDP, pato la Taifa ni 20%, sisi tunasema 13% ni ndogo sana, ina maana kwamba njia tunazotumia kutoza kodi na njia tunazokusanya mapato yetu ni finyu. Aidha, vile vyombo vyetu vinavyoshughulika na ukusanyaji wa mapato vijiunde upya vi-think out of the box, what is happening?Effort yoyote Mheshimiwa Rais aliyofanya kupata hela kwenye madini na nini lakini bado eti revenue effort 13% ofGDP isnothing, tunataka tupate 20% whichmeans tunapata 28 trilioni, tunge- finance vitu gani? TARURA ingepatapesa mpaka tushindwe kuzungumza, lakini ninavyoona ni kwamba kuna kitu kiko hafifu hapo katikati kwenye ukusanyaji, sijui zinaenda wapi hizo hela. Kwanini iwe 13% au sisi tuna overstateGDP yetu pengine I do not know, lakini kama kweli takwimu ziko sahihi 13% ni ndogo toka tukiwa kule sisi miaka ya 1996, kwahiyo tunazungumza kwamba effort yetu lazima ifikie 20%, sasa mpaka leo hii 13%, tuna matatizo lazima tuanzie hapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tunaposema tuna-demand barabara na vitu vingine, je, mapato yanatoka wapi? Kwasababu hutapata kule kwenye Wizara ya Viwanda wanapata 6%, kilimo wanapata 6% of approved budget, it willnever work. Kwasababu hiyo tuna over state hizi revenue ndiyo sababu tunapanga vitu ambavyo ni hewa,havitatekelezeka,where is the money?The money is the cash budget, sasa niseme hivi kwanini nimeanza kusema kwamba tuna strength moja ya kukopesha. Revenue ya Serikali ya matumizi inatokana na vitu viwili taxrevenueyaani mambo ya kodi na tozo; pili, mikopo. Sasa mikopo inaweza ikatokana kwenye mabenki ya ndani napensionfunds nakadhalika yaani vianzio vya ndani, lakini pia zinaweza zikatoka nje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa kwa nje na tunaambiwa kwamba nanii yetu iko chini sana, yaani uhimilivu wetu wa ukopaji bado tunaweza tuka-affordhata mara tano, sasa kwanini tusikope zaidi, tunaogopa nini kukopa kwasababu tunajenga rasilimali, tunajenga mtaji, nchi hii ina balance sheet yake,liabilities and assets. Watu wanaposema sijui deni hili siyo himilivu, deni walikuwa wanapiga ile gross hawaondoi ile rasilimali tuliyotengeneza,assetskwahiyo lazima uchukue asset - liabilities unapata net liability au netasset.
Sasa sisi ukiangalia kwa mfano vitu ambavyo vimejengwa Awamu hii ya Tano thamani yake na deni letu, ni kama hatuna deni yaani ukiangalia kwa uhimilivu watu wa Taifa letu,uhimilivu wa balance sheet ya kwetu,network yetu ni nzuri kwasababu tumekopa tumeweka kule, hata kama tungekuwa tumekopa mara ngap,i tutaingiza kwenye asset inazaa vizuri.
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Kimei.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nizungumzie…
MWENYEKITI: Tayari ni kengele ya pili.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Sasa nina mengi sana, lakini...
MBUNGE FULANI: Unga mkono hoja.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI:Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.(Makofi)
Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa Kipindi cha Miaka Mitano kuanzia mwaka 2021/2022 – 2025/2026
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kuniona na napenda kwanza nimshukuru sana na nimpongeze Waziri wa Fedha na timu yake pamoja na Kamati ya Bajeti kwa namna ambavyo wamewasilisha Mpango huu. Natumaini wote imetufurahisha. Nataka nianze kwa kusema kwamba naunga hoja yake mkono, japokuwa nitakuwa na maoni mawili au matatu ili kuweza kuboresha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme hivi kwamba kusema ukweli kwanza tunawapongeza pia Wizara na Serikali kwa ujumla kwa kuweza kutuwekea uchumi wetu kwenye hali ya utulivu. Tunajua kwamba ukuaji umekuwa mzuri sana, hata wakati huu wa covid, lakini pia mfumuko wa bei uko chini, uko vizuri, japokuwa namuunga mwenzangu mkono aliyezungumza kwamba pengine asilimia tatu ni ndogo sana, inatunyima fursa fulani ya kuweza kukuza zaidi kwa kuipa Sekta Binafsi na wale wanaouza, nafasi ya kuona faida watakayopata wakiendelea kuzalisha Zaidi.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia tumeona kwamba hali ya deni la Taifa ni himilivu. Pili, tunaona pia kwamba thamani ya shilingi yetu iko vizuri na pia tuna International Reserves ambazo ni nzuri. Hiyo ina maana kwamba ni strength kubwa sana ambayo tunaweza tukaitumia tukafanya assessment ya nchi yetu kwa athari ya wawekezaji na hivyo tukaanza kukopa kwa riba ya chini sana. Riba ya asilimia tano au sita unaweza ukapata kwa mfumo huo wa infrastructure bond au pia kwa kukopa moja kwa moja kwa direct placement ya bond yetu kwa wale wanaotaka kuwekeza Tanzania kwa sababu Tanzania imekaa vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwamba hakuna sababu ya kuchelewesha utekelezaji wa miradi elekezi. Hii miradi tunasema ya vielelezo kama SGR na mradi wa umeme wa Mwalimu Nyerere wakati tunaweza tukakopa, tukahamasisha na tukafanya haraka haraka tukaanza kuona matunda kutokana na miradi hii mikubwa ambayo itatoa chachu katika ukuaji wa Taifa letu. Nataka niseme kwamba tutumie hiyo kama fursa, kama ni strength na hiyo strength tuweze kuitumia kuweza kufanya mchakato huo wa kuweza kwenda kwenye soko la Kimataifa na kukopa na tusizingatie sana kukopa ndani kwa sababu tukikopa ndani maana yake tunai-crowd out private sector. Watu binafsi hawawezi kwenda nje kwa sababu hawajulikani, lakini Serikali inajulikana kwa sababu ni Serikali na Serikali is as good as gold.
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini tukihamasika sisi Serikali tukakopa nje, tukaacha resources za ndani zinakopwa zaidi na watu binafsi, kwanza riba zitakuwa chini. Sasa hivi tuliambiwa kwamba riba nashangaa kwamba licha ya vigezo hivi vizuri vya uchumi, riba bado ziko kwenye asilimia 15. Nimekutana na watu wa BOT walituambia kwamba kwa sababu tunakopesha Serikali kwa asilimia 15, sio kweli! Serikali inalipa asilimia 15 kwa bond ya muda kati ya miaka 15 na 20, lakini Benki zinakopesha mikopo ya mwaka mmoja mpaka miwili sanasana pengine ni michache sana kwa miaka zaidi ya hapo. Sasa wakikopesha kwa asilimia 15 ni kubwa sana ambapo Serikali ikikopa kwa kipindi hicho kifupi riba inakuwa ni kwenye asilimia chini ya 10. Kwa hiyo unaona kwamba kuna uwezekano wa kushusha hizi riba kwa kuwezesha Sekta Binafsi kukopa zaidi na hivyo kuwezesha Sekta Binafsi kuwekeza na tukaona matokeo ya Mpango wetu huu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kitu kimoja ambacho nimekisikiliza hapa. Tunafanya mambo kimazoea mazoea sana, yaani tatizo la sisi Waafrika pengine ni kwamba tunaanza kuzalisha halafu ndiyo tunatafuta soko. Kumbe uzalishaji unatakiwa uanze sokoni, unatafuta soko liko wapi. Ukishaona soko liko wapi na bei zake zikoje, ndiyo unasema sasa niki-incur au nikitumia gharama hizi kuzalisha nitapata faida, lakini mtu anazalisha ndizi heka 20 halafu zimeshaiva, anasema anatafuta soko liko wapi, hamna soko lolote namna hilo, huwezi kupata na mtu akijua unazo ndizi zinaoza anakupa bei ya chee! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima tujifunze kufanya biashara kitofauti kwanza tufanye utafiti tujue kwamba ni kitu gani kinauzika wapi. Tunapoendelea kulima, tunazungumzia mazao haya ya asili siku zote, pamba, kahawa, tumbaku. Hivi tumeshajiuliza ni wapi masoko haya yakoje duniani kwa sasa hivi? Bei za huko mbele za kahawa zinaenda wapi, bei za tumbaku zinadidimia na tunaendelea kusema tumbaku na kadhalika. Ukweli tukifanya tathmini sahihi tukajua kwamba ni kitu gani cha kuzalisha hapa kwetu, sio lazima iwe ni mazao haya tunayoona, tumeona kwamba tulivyowaambia Wachaga kule kwamba hawa jamaa wenzetu wa Kyela wanalima avocado halafu wanapata kilo moja shilingi 1,500; kila mtu anatafuta mbegu ya avocado, huna haja ya kumtafutia mbolea, anatafuta mwenyewe kwa sababu anajua kwamba ina faida kulima avocado.
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na kuwa na taarifa hizo lakini ukweli ni kwamba taarifa hizi hazimfikii mkulima, tunakaa na hizo taarifa, hujui kwamba unaweza sasa badala ya kulima kahawa ukalima avocado, kwa nini? Ukiendelea kulima kahawa kwenye ule udongo wa kule kwetu umeshakwisha kabisa kwa sababu umelima kahawa miaka 40 au 50, kwa hiyo hauna tena rutuba na hauna tija. Kwa sababu hauna tija badilisha uzalishe linguine, baada ya muda mwingine unaweza ukarudia tena kahawa na ndiyo mambo ya crop rotation, wale wanaojua mambo ya kilimo. Kwa hiyo naweza kusema kwamba pengine kuna haja ya kusema kwamba ni eneo lipi nibadilishe zao lile, kama kule Uchagani kahawa haiendi tena, pengine twende upande wa avocado na mambo kama hayo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo mengine pia unaona kwamba unatumia gharama nyingi kwa sababu ule udongo unatakiwa ufanye rotation, uzalishe kitu kingine. Naamini kwamba tunaposema tutafutiane masoko, cha kwanza ni hizo taarifa na hizo taarifa sasa hivi ni kielektroniki, tufungamanishe masoko yetu. Mtu hajui kwamba kama nina ndizi, Mbeya wananunua namna gani ndizi, Moshi wananunua namna gani, Nairobi wananunua namna gani kwa kutumia hizi gadgets zetu za mawasiliano hizi ambazo zinatupa bei kila mahali duniani virtually unaweza ukajua kila kitu kinauzwa namna gani. Kwa hiyo watu watajua bei zake na sio lazima ukutanishe mtu physically, unaweza ukakutanisha watu kwa mawasiliano haya tuliyonayo na hiyo ni bei nafuu ya kukutanisha watu, ni bei nafuu ya kumpa mtu tija ya kuzalisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme hivi, mimi nafikiri kwamba katika huu Mpango wetu, suala zima la ushirikishi, kujenga uchumi shirikishi na uchumi shindani. Issue iliyopo ni kwamba tutafanyaje vijana hawa wapate ajira na hawawezi kupata ajira bila kujiajiri wenyewe sasa hivi kwa sababu watu ni wengi ambao hawana ajira na hawataki kuingia kwenye kilimo kwa sababu kilimo hakina tija na kwa sababu hawajafundishwa namna ya kulima kwa tija au kwa faida. Kwa hiyo naomba hivi, kwamba pengine umefika muda sasa tujaribu kutengeneza mfumo wa kuwa-organize vijana kwenye vikundi na kuwaonesha namna gani ya kutengeneza mashamba yenye tija, kutengeneza viwanda vidogo vidogo vyenye tija na mtu asifikirie kwamba kiwanda ni kiwanda cha Mchuchuma, hapana. Tena sasa hivi hata kuzungumza mambo ya chuma ni kitu tofauti kidogo kwa sababu dunia haiendi kwenye mambo haya, inaenda kwenye software zaidi sasa hivi, kwa hiyo Sekta ya Huduma ndiyo itakuja kuwa ni sekta muhimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Sekta ya Huduma maana yake ni sekta ya kuhudumia viwanda, kwa sababu ukiwa na kiwanda lazima kihudumiwe, maintenance na kadhalika. Sasa kama wewe unakimbizana tu hiki unasahau kule, haitawezekana, lazima tuingize fedha, lakini ili vijana waweze kufanya hivyo wanahitaji mtaji, mtaji unatokana na nini? Tunasema tutawapa vimikopo vidogo dogo kwenye halmashauri, haina kitu hiyo! Tuunde ile Mifuko ya Serikali ambayo imetawanyika kila mahali, tuunde National Credit Guarantee Scheme or Fund au kuwe na misingi ya kibiashara lakini nafuu ambayo itakuwa imewekwa na Serikali ili watu wanaotaka mikopo wanajua tunaenda pale ambapo kutakuwa na kitengo cha wakulima, vijana, vinakaa mahali Pamoja. Pia unaweza uka-leverage ile guarantee scheme ikazalisha maradufu kwa sababu kama default rate kwa mkopo, hiyo iliyotoka kwa vijana pengine ni only ten percent ina maana kwamba ukiwa na mkopo wa ku-guarantee watu 100 unazidisha mara 10, uta-guarantee watu mara 10 yaani kiasi cha fedha mara 10. Sasa hivi unatumia kile unam- guarantee mtu mmoja ambapo tunaweza tukapeleka kwenye guarantee fund tukawapa watu wakaendesha kibiashara, tukaweza kuwezesha watu kupata mikopo kwa wingi na mitaji kwa wingi kwa muda mrefu na muda mfupi.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimalizie kwa kusema kwamba, mimi ni muumini wa masuala ya kwamba, kilimo cha sasa hivi ni lazima kibadilike na kubadilika kwa kilimo hicho ni lazima tusifanye mambo ya mazoea, tujaribu kuona ni kitu gani kitaoteshwa wapi na wakulima wapewe taarifa za masoko ambayo ni sahihi. Kwa kumalizia niseme hivi, ili tuweze kuongeza lile fungu la kukopesha au kuwezesha watu kupata mitaji, lazima tuunde National Credit Guarantee Fund or Corporation ambayo itashughulika na Mifuko yote na ile fedha inakaa mahali pamoja na inatumika kwa faida ya wengi. Hapa nataka kukuhakikishia kwamba inaweza ikawa ni kubwa kuliko Benki zote hapa Tanzania. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kuniona na kunipa fursa hii nichangie kwenye mjadala huu.
Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kabisa kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo ameanza kazi yake vizuri, amerejesha amani na matumaini mapya kwa watu wengi. Lakini pia kwa kuzingatia kwamba ametuambia tunaendeleza yale yaliyoanzishwa chini ya uongozi wa Mheshimiwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, na tunaamini pia kwamba kwa jinsi ambavyo tunmfahamu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ataongeza hata ile kasi ambayo tunaipokea.
Mheshimiwa Spika, nataka niseme kwamba kielelezo kikubwa cha kuonesha kwamba kweli Mheshimiwa Rais wetu anatekeleza kama anavyoahidi ni timu ya Mawaziri aliyoweka kumsaidia yeye, akiwemo Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye amekuwa ni kichocheo kikubwa na naamini kwamba ataendelea na kasi ileile, ataendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais kwa namna hiyo lakini pia na Mheshimiwa Makamu wa Rais aliyechaguliwa, naamini wote ni watu poa kabisa, siyo poa, ni bomba kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naamini tukiangalia timu iliyopo mtu anapokwenda kwenye kiwanja cha mpira unaangalia kwamba amebeba timu gani na yeye ameingia kwenye uwanja huu akiwa amebeba timu ya Yanga au ya Simba? Ya Yanga tuseme, lakini itabadilika. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nataka niseme hivi; nampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa uwasilishaji wake mzuri, wa kina na unaoeleweka, ripoti ambayo imeandaliwa kweli kitaalam na ina-cover kila kitu ambacho mtu unataka kuona. Lakini nimpongeze zaidi kwa jinsi ambavyo amesimamia shughuli za Serikali kwa miaka hii yote ya Awamu ya Tano na mwaka huu ambao tumeanza na jinsi ambavyo amejitoa kutembea kwenye maeneo mbalimbali, na nina matumaini kwamba kule kuona kwake kumesaidia sana kusukuma utekelezaji wa miradi na mikakati ambayo ilikuwa imewekwa mbele yake.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka nimpongeze na niseme kwamba tunaamini na mimi naamini kwamba hatasahau kutembelea Vunjo. Na ninaamini pia kwamba Mheshimiwa Rais kule Vunjo hatujaona viongozi wa kitaifa wa kubwa kwa miaka mingi, takribani miaka saba – naamini tutaanza kuwaona pia kule wajue kwamba kule pia sisi CCM tumejipanga vizuri na tumejipanga kwa safu ambayo italeta maendeleo kwa jimbo letu sana sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakupongeza wewe na Naibu Spika kwa jinsi ambavyo mnatuweka pamoja na kutupa fursa na kujua ni yupi aseme saa ngapi na kadhalika. Nawapongeza sana, naamini naona ufahari sana.
Mheshimiwa Spika, nianze kwa kusema kwamba huu utani wa darasa la saba na maprofesa siyo mzuri sana. Kule nilikotoka mtu anajulikana kwa kazi na umuhimu wake na wote tuna kazi moja ya Ubunge, hatujuani kwa elimu tulizonazo na elimu tulizonazo hazina maana yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tunapofika hapa tupeane heshima kwamba wewe uko darasa la saba au gumbaru umetoka huko we don’t care unajua kusoma na unaweza kuchangia vitu vizuri. Naamini kwamba sisi kila mtu ana nafasi yake lakini tusianze kuingiza utani, utani huo ni mzuri lakini, hasa Mheshimiwa Musukuma akiwepo…
SPIKA: Haya, sasa endelea na hoja Mheshimiwa Dkt. Kimei.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Endelea na hoja iliyopo Mezani.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Spika, niache Mheshimiwa.
SPIKA: Ukiwachokoza nawajua hawa, endelea tu Mheshimiwa Dkt. Kimei. Ukiwachokoza darasa la saba utatafuta mlango wa kupitia.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nawafahamu, nawafahamu sana. Nawafahamu na ninawapenda sana lakini…
SPIKA: Maana yuko Rafiki yangu mmoja, Mheshimiwa Dkt. Mwakyembe, alikosa kuona mlango wa kupitia baada ya kuwagusa darasa la saba. Ndiyo maana nasita, usije ukawagusa huko Vnjo watakuvunja mguu, endelea tu na hoja ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, darasa la saba waache.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Niseme hivi; kuna jambo moja ambalo linatakiwa liangaliwe kwa ujumla, hasa kwenye hii nyanja ambayo inahusiana na mambo ya uajiri wa wafanyakazi serikalini na kadhalika. Ni suala zima la kutathmini skimu ya mishahara ili kuiweka bayana ili mtu kama ni profesa atake kukaa kwenye uprofesa wake. Lakini ukweli ni kwamba mtu anafuata pale penye maslahi, lakini kuna wengine tunakuja hapa kwa sababu tunataka kutekeleza mambo fulani fulani kwenye maeneo yetu.
Mheshimiwa Spika, na ninataka kusema kwamba ninashauri kwamba skimu ya mishahara iangaliwe ili stadi zile ambazo ni rare professions na kadhalika na ambao tunataka wabaki kule kwenye specialties zao waweze kufanya utafiti, walete innovation, wasaidie nchi hii kwenda forward professionally, tuweze kuwabakiza kule zaidi kuliko kuwatoa na kuwaleta kwenye siasa na kuwavutia kwa sababu huku kuna maslahi mazuri mengine, lakini naamini kwamba tutaangalia hili ili mambo yawe vizuri zaidi na watu wakae kwenye professions. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninataka kuchangia kwenye maeneo matatu; eneo la kwanza kabisa ni eneo la utawla bora, utawala bora unaendana na span of control. Sasa imekuwa kwamba kuna halmashauri nyingine ambazo ni kubwa sana, zinaweza zisiwe kubwa sana kwa maeneo lakini kwa wingi wa watu.
Mheshimiwa Spika, sasa kama halmashauri ni kubwa sana, zaidi ya watu laki tatu, inakuwa ni ngumu sana kusema kweli halmashauri ile kutenda kwa kuwafikia watu ambao tunataka tuwafikie kwa karibu, tuwapelekee elimu ya uwezeshaji na tuwasaidie kwa kuwaonesha kwa vitendo. Lazima halmashauri hizi zinagaliwe ili kama zinaweza zikapangwa kivingine zipangwe. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais Hayati wetu, mpendwa wetu, JPM, alipokuja kwetu alisema kwa mfano tuwe na Halmashauri ya Himo, alikubaliana na hilo. Na ninaamini kwasababu naunga mkono mambo mengi nasema Mungu atujalie na Mheshimiwa Rais wetu mpya, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aweze kukubali pia twende na Halmashauri yetu ya Vunjo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pili, nataka nizungumzie suala la Kamati ya UKIMWI kudhibiti UKIMWI. Naomba hii ijiongeze kidogo na kuhusu la gonjwa la COVID, ninaomba hii Kamati iingize masuala hayo kwenye mchakato wake ili tuweze kujua tunapoendelea huko mbele na tuweze kudhibiti, siyo tu UKIMWI, kwasababu UKIMWI naamini tumeshaanza kuu-contain na mtu ambaye kweli amejipeleka hovyohovyo natumaini ni... lakini ukweli UKIMWI kwenye rate ya three to five percent siyo mbaya, at least tunaweza tukadhibiti. Lakini naamini kwenye magojwa haya mapya yanayojitokeza, hasa COVID, pia tuangalie.
Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, niseme kwamba kwenye suala zima la COVID Private Sector Foundation ilitoa mchango wake, ilifanya utafiti wkae kuhusiana na athari na ninaamini kwambs Serikali itaendelea kusoma na kuona mapendekezo gani yalifanyika hususan kwenye sekta ya utalii, kwamba sekta ya utalii iliathirika sana na ukiwaambia kwamba walipe tozo zile walizokuwa walipe NGOs fees ambazo ni fixed, waendelee kulipa wakati hawajawa na watalii, zitakufa. Hawataweza kuendelea. Kwa hiyo, tukasema kwamba wale waangaliwe kwa namba yao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na siyo sekta ya utalii tu, na sekta nyingine pia zimeathirika lakini ile ripoti najua ilikuja Serikalini na tunaomba kwamba Serikali iisome tena ione kama inaweza ikaitumia ili kuweza kupunguza makali ya gonjwa hili. Kama kwetu halipo limekuwa nje kwa hiyo, limeathiri wale wateja wet, na kadhalika. Lakini nataka kusema kwamba ni lazima tuangalie namna ya kusaidia watu.
Mheshimiwa Spika, suala la uwezeshaji. Uwezeshaji naamini kila Mbunge hapa amejipanga kwa namna moja kwasababu hii miundombinu tunayoijenga haitakuwa na maana kama haitatumiwa kuzalisha, na ndiyo sababu moja nasema lazima tuangalie kwamba tumejenga barabara, ni kitu gani kimetokea hapo kwenye barabara.
Mheshimiwa Spika, kulikuwa na Central Corridor Programme ambayo ilikuwa isaidie ku-develop vitu fulani fulani along the central corridor ya railway na ile railway baadaye iweze kuwa na tija zaidi na watu wengi wanavutiwa na jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, uwezeshaji ni jambo la msingi lakini kuna masuala ambayo lazima tuyaangalie. Kwanza ishu ya finance kama alivyosema mwenznagu, kwamba mtaji ni kitu kikubwa. Sasa mitaji tunayotegemea, kwa mfano ukiwa kwenye halmashauri, haijawa revolving fund, mtu anachukua mkopo lakini ukiuliza ni mingapi imerejeshwa kwenye halmashauri wale waliokopa utakuta kwamba urejeshaji ni very low.
Mheshimiwa Spika, ndiyo sababu inakuwa kila mwaka lazima uingize hela mpya na ukiuliza leo hela ya kukopesha ni ngapi watakwambia ni ile waliyopokea mwaka huu, hawakwambii ukichanganya na ile ambayo tumekopesha mwaka jana ikarudi na hii ambayo leo imetolewa tunaweza tukakopesha mara tano, haijatokea namna hiyo.
Mheshimiwa Spika, ni kwasababu kuna weakness kwenye level ya halmashauri kutoa ile mikopo, ile mikopo inatolewa na watu ambao kwanza ni wale maafisa maendeleo wako wachache, hawana staff wa ku-follow up, hawashirikishi sana watu wa kwenye vijiji. Kwa hiyo, ikiwa kama mtu amechukua mkopo ijulikane anatumia kwa njia ya uzalishaji na kadhalika, kwa hiyo inatokea kwamba yule mtu anayechukua hela hawezi hata kuitumia vizuri na anakuwa hajaandaliwa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naamini kwamba ni vizuri hizi hela halmashauri…
SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Dkt. Kimei, tunakushukuru sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza Waziri na Naibu wa Wizara hii kwa kazi nzuri na ubunifu mkubwa kwenye kutatua matatizo ya migogoro ya ardhi. Ninapongeza pia Katibu Mkuu pamoja na uongozi mzima wa Wizara.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Wilaya ya Moshi Vijijini, hususan Mji Mdogo wa Himo, kumekuwepo na migogoro mingi inayosababishwa na Maafisa Ardhi kufanya double allocation kwa nia ya kujipatia rushwa. Aidha, wafanyabiashara wachache wamejirundikia maeneo makubwa na mji ni kama vile umekuwa mali ya matajiri wachache. Tunaomba Wizara iingilie kati na kugawa maeneo yaliyohodhiwa bila kuendelezwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo kubwa kwenye Wizara ni ucheleweshaji wa vibali vya kujenga, pamoja na utoaji wa electronic titles jambo ambalo tuliahidiwa lingefanyika kwa haraka, inachukua muda mrefu na ingekuwa vizuri kuchapisha kwenye vyombo vya habari titles ambazo ziko tayari.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna umuhimu wa kutenga maeneo ya kilimo kwenye kila Halmashauri kwa wawekezaji wakubwa.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Viwanda Na Bishara
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapongeza hotuba nzuri ya Waziri wa Viwanda na Biashara, nampongeza yeye mwenyewe Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na uongozi mzima wa Wizara kwa kazi nzuri na ubunifu katika kutekeleza Sera na Ilani ya chama tawala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachosikitisha sana ni Wizara hii inayobeba dira ya Taifa letu kwa sehemu kubwa kutokupewa kipaumbele cha kufikishiwa fedha zilizoidhinishwa kwenye bajeti ya maendeleo. Kwa mwaka 2020/2021 ilipata chini ya asilimia 50 ya bajeti na hivyo kushindwa kutekeleza miradi ambayo ingewezesha kujenga misingi bora ya kuwezesha wananchi wajasiriamali kuanzisha shughuli za uzalishaji na kutengeneza ajira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa majengo/ mabanda ya kuwapangishia wajasiriamali wadogo wadogo na wa kati ni falsafa nzuri kwani inawezesha pia kuwafikishia wajasiriamali hawa huduma na mafunzo mbalimbali, na pia kuwasimamia wale wanaopewa mikopo na SIDO kutumia mikopo hiyo vizuri. This be Serikali ikubali kutenga fedha nyingi zaidi kwa utekelezaji wa mkakati huu na kwa Mfuko SIDO wa kuwezesha wajasiriamali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mashirika ya TIRDO, CAMARTEC, TEMDO yanafanya ubunifu mzuri na unaozingatia uwezekano wa kupeleka kwenye soko letu teknolojia sahihi kwa mazingira yetu na kwa bei nafuu. Hata hivyo taasisi hizi hazipati bajeti za kutosha kujitangaza na kupeleka taarifa sokoni kwa walengwa ili wazijue na wazinunue. Kwa namna hii zinapoteza tija. Wapewe rasilimali fedha na watu wa kueneza kile walichobuni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mashirika mengi yaliyo chini ya Wizara hii hayana bodi. Hii inapunguza kiwango cha utawala bora. Tuiombe mamlaka husika ifanye uteuzi kwa wakati.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa blueprints unastahili kuongozwa na Wizara hii licha ya kwamba Wizara nyingine zina maeneo yao. Blueprint inatekelezwa kwa kasi ndogo, lakini kuna haja ya kufanya tathmini mpya kuhusu kero mpya zilizoibuka kwa wafanyabiashara na wawekezaji. Kero zilizoorodheshwa miaka mitatu iliyopita zimepitwa na uhalisia wa sasa.
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2020 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nashukuru kwa nafasi hii. Mimi pia nimpongeze Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuja na bajeti yake ya kwanza nzuri sana. Nampongeze Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu wake na uongozi wa Wizara kwa ujumla kwa bajeti hii ambayo kusema kweli imezingatia maoni ya Wabunge pamoja na maoni ya wadau wengi na ninaamini kwamba imewafurahisha wananchi kwa ujumla katika nchi yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme tu makubwa ambayo siyo sana ya kutaka kuingia ndani in detail, lakini niseme mambo matatu makubwa ya kisera. Kwanza, nikiangalia bejeti hii, kusema ukweli ni contractionary budget. Yaani ni bajeti ambayo haitaweza kukuza uchumi kwa kiwango kile ambacho tungetarajia. Kwenye wasilisho la hali ya uchumi wa sasa hivi tumeambiwa kwamba tumekua kwa asilimia 4.8.
Mheshimiwa Naibu Spika, tunasema kwamba tutakua kwa asilimia 5.6 mwaka ujao, 2022. Kwa nini tufikie asilimia 5.6 badala ya kurudi asilimia saba ambapo ndiyo long term trajectory yetu kwa miaka mingi? Wakati tumeshashuka mwaka huu tukapunguza ile kasi, tutawaona kwamba kwenye nchi nyingine ambazo wametekeleza aina fulani ya sera, utaona kama Ulaya zinaanza kurudi na kuwa mara mbili ya ile waliyokuwa wamebajeti mwaka uliopita.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri tatizo ni kwamba ukiangalia bajeti, sera zilizomo humu ndani za fiscal na monetary utakuta zote ni contraction. Kwa nini? Kwa mfano, ukisoma bajeti ya mwaka jana, 2020 na ukisoma Monetary Policy Statement ya mwaka 2020 na ya miaka mitabo iliyopita kwa ujumla hutaona tofauti. Wanabaki pale pale kwamba tutakua kwa asilimia saba. Naamini kwamba ndiyo sababu tumebakia tunakua kwa asilimia saba kwa sababu hatubadilishi zile sera za ujumla, zinabakia ni zile. Kwa hiyo, kama hubadilishi ile sera uka-promote growth, ni kwamba hutaweza ku-break through out of your long term hiyo ambayo tumekuwa tunaiendeleza asilimia sita au saba kwa miaka zaidi ya 10 toka wakati wa awamu ya nne na ya tano. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ninaamini ukweli ni kwamba ukiangalia sekta ya fedha, utakuta kwamba tatizo ni kwamba kama unashikilia inflation kwenye tarakimu kati ya tatu na tano kwa miaka 10 au 20, umejenga fiscal space kubwa sana ya kuweza kukopa na kuongeza fedha za kuendesha miradi katika nchi yetu; ya Serikali in this case, lakini pia inafungua fedha zile zilizo benki ziweze kwenda kwa sekta binafsi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ni kwamba sera hii ya kushikilia inflation kwenye asilimia tatu, maana yake ni kwamba mikopo isikue. Kwa sababu the only way unavyoingiza fedha kwenye uchumi ni kwa mikopo au kwa kuuza fedha za kigeni. Sasa sisi mikopo yetu tumeishikilia, Serikali inakopa kidogo na sekta binafsi inakopa kidogo, kwa hiyo, kwenye uchumi kunakuwa na ukwasi mdogo sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, unajua Marekani ni nchi ambayo the rate of employment kule Marekani ni 5% au 6% na wao inflation yao inakuwa ni tatu kwa sababu wakichochea kidogo uchumi tayari inflation mambo yatakuwa magumu, hawatapatikana watu wa kufanya kazi. Hapa kwetu tuna unemployment kubwa, kwa hiyo, tunaweza tukaweka mkopo kwa sekta binafsi, sekta binafsi ikaajiri na uchumi ukaanza kukua kwa 7%, 8%, 9% au 10%. Ni very easy. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ni kwamba utakuta kwamba riba ni zile zile miaka hii yote. Toka mimi nianze kusoma hii serious, riba zinazotokana na Sera ya Fedha ni zile zile za zaidi ya asilimia 10. Ukiangalia nakisi ya bajeti ambayo sasa ni budgetary policy ni nakisi ile. Ukiangalie, yaani kitu unapotaka kuangalia zaidi kwenye bajeti ni nakisi.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukiangalia nakisi ya bajeti ambayo sasa ni Budgetary Policy, yenyewe Budgetary Policy ni nakisi ile. Uiangalie yaani kitu unavyotaka kuangalia zaidi kwenye bajeti nakisi. Ukiweka nakisi ndogo maana yake Serikali inajinyima kwenda kukopa fedha kwa sababu, maana yake ni kitu ambacho lazima ukipate nje ya mapato uweze kukiingiza kwenye uchumi wako. Na sasa hivi kwa sababu kuna fiscal space ya muda mrefu ya low inflation unaweza ukakopa hata kwenye Benki Kuu, tumeona sasa wameanza kukopa Benki Kuu kwa kasi kubwa kidogo na hiyo ni kitu kizuri kwa sababu, tunaingiza fedha kwenye uchumi, na watu wakishaleta bidhaa zao wanaweza wakaongezea mikopo yao wakazalisha. (Makofi).
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hiyo nasema kwamba, bila kufanya marekebisho hapo na niwakumbushe wale waliosoma kidogo, kuna trade off kati ya inflation na growth. Trade off kati ya inflation na, unaongeza inflation unaongeza na rate of wealth growth mpaka a certain level hapo inflation inapokuwa kwamba, ina cause employment imeshafikia mwisho ndio unasema hapa sasa nikienda zaidi nitajikuta napata hasara kwa sababu hata labor cost inakuwa sasa ni structural inflation imejitokeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka kusema kwamba, hii issue ya contraction monetary policy na fiscal policy tuiangalie, nakisi sasa imeshuka wameishusha kutoka asilimia 3 kwenda asilimia 1.5 maana yake Serikali isikope, isitafute fedha mahali pengine ikaingiza kwenye uchumi uchumi ukakua; uchumi hauwezi kukua bila kuwekeza, sasa hiyo ni moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme pili,nasema kwamba, ukiangalia kwa upande wa mapato ijapokuwa wana-protect ifike kwenye 23 plus, lakini ukweli ukiangalia mapato ya mwaka huu hayatafikia trilioni 18. Mpaka sasa hivi ukichukua takwimu za mwezi Mei ziko itafikia, nimepiga hesabu haiwezi kuzidi trilioni 18, sasa trilioni tano utazipata wapi? Uongeze ufike 23 trillion?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo una over estimate, tumesha-over estimate kwenye hii bajeti, lazima tuangalie ni wapi tupate au tuongeze vipato wanavyoshauri wengine kwenye simu, whatever. Japokuwa wanawema ukiweka kwenye simu au ukiweka kwenye miamala hii watu watarudi kule kwenye matawi ya benki, benki zitafurika watu. Watu watasema kwa nini nikachukue kwenye M-Pesa? Nitaenda kwenye benki kwenye matawi nichukue pesa yangu cash kwa kulekule hudai kwa hiyo, sasa tatizo utaongeza mpaka wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna vitu hivi ambavyo vina alternative ways tukivishika tutapata matatizo. Kwa hiyo, nasema kwamba, ukweli ni kwamba, hilo ni tatizo na niseme hivi kuna hii issue kwa mfano kwenye upande wa mapato unpredictability, again mambo ya policy unpredictability yamejiingiza hapo. Kwamba, unaweka ushuru kwa mwaka mmoja, nasema tumeweka huu kwa mwaka mmoja, hii kwa mwaka mmoja, sasa wewe mtu utafanyaje maamuzi ya kuwekeza wakati wewe unajua kwamba, huu ushuru umepata unafuu wa mwaka mmoja tu? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tunataka ushuru ukae kwa miaka mitatu, minne, kabla hujajigusa. Tatizo hapa tunasema tax current kuwe na tax current ya kwamba, nikipandisha mwaka huu nitakaa miaka mingine mitatu kabla sijapandisha. Kwa hiyo, mtu akitaka kutumia ile opportunity anawekeza kweli kama unpredictability tunazidi kuiongeza hapa haitasaidia sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, halafu nasema hivi kodi hii ambayo wanakamati wa bajeti wameisema ya LUKU; LUKU, eehee, LUKU ni watumiaji wengi ni wapangaji. Sasa wewe ukaenda kutumia unamtoza mwenye property au unamtoza aliyepanga property?
Mheshimiwa Naibu Spika, tuangalie vizuri namna ya kukusanya. Ni kodi nzuri ni ubunifu, lakini tuiangalie namna ya kukusanya na kitu kama hicho. Lakini niseme hivi kwenye upande wa ku-allocate resources zetu tunaziweka sana kwenye miundombinu, sawa, lakini tujiulize ni kitu gani tunafanya ili watu waanze kuona opportunities kwenye central corridor kwa mfano kwa sababu sasa SGR is coming, lakini hebu niambie toka tuanze kujenga SGR mpaka Morogoro ni watu wangapi wameenda kuanza kuwekeza au hata kuulizia nijenge kiwanda gani? Niweke kitu gani? Niweke shamba gani? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hamna watu wamekaa kimya tu kwa sababu, kuna vitu vingine ambavyo havijafanyika kuweza ku-motivate production na investment katika hii nchi. Mwisho, but not the last kwa sababu muda tu. Niseme execution, execution unakuja kuona mwisho wa mwaka, unaona hela nyingi zinaanza kutolewa quarter ya tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, issue ninayoomba ni kwamba, fedha hasa hizi za maendeleo tujaribu kuzipangilia kwa mpango kwamba, zile ambazo tunakopa tuzikope mapema, ili zianze kutekeleza miradi ya maendeleo tusingojee mpaka quarter ya nne ndio tuanze kupata pesa kwa sababu hizi zinakusanywa kwenye kodi mostly for the current purpose, lakini hizi za maendeleo ni fedha ambazo zinatakiwa zipatikane immediately. Tutafute wale watu wanaotukopesha watukopeshe, tutafute donors wazilete mapema tuanze kuzitumia kwenye miradi ya maendeleo, tuanze kuzi-disburse mara moja hasa kule kwenye wananchi zifike mara moja. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini cha mwisho ni issue hii ya ahadi za viongozi. Tuliahidiwa na Wabunge hapa tulipokuja tuliahidiwa kwamba, zile ahadi za viongozi kwa wananchi wetu kule kwenye majimbo zitaorodheshwa ziwekwe kwenye vipaumbele tuambiwe kwamba, hii ya kule Vunjo itatekelezwa mwaka wa tatu. Nikitajiwa hivyo nitasema haleluya, lakini kama hatujajua kwamba, zile ahadi zimewekewa mchakato gani wa kutekeleza itakuwa kwamba, tunabakia tunaenda kule wataanza kutupa mawe wewe ulizungumza hivi, tupeni tuende na hicho kitu. Nimesema hapa kwa sababu najua ni kwenye mambo ya execution. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba unisamehe kwa kuzidisha kidogo, lakini nataka kusema naunga mkono hoja hii vizuri sana. Na haya niliyosema ni mambo tu ya kuboresha tunaenda mbele, ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa Unaokusudiwa Kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa fursa hii. Nikupongeze kwa namna ambayo unaendesha Bunge hili kwa weledi. Pia nijiunge na wenzangu kutoa pongezi na shukurani nyingi, kwa Mheshimiwa Rais wetu mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa jinsi ambavyo anaendeleza kazi hii kwa kasi na kusema kweli anatekeleza kwa mafanikio. Sio mafanikio tu, lakini huku akizingatia kile ambacho watu wengi wanakisahau; Katiba, Sheria, Sera na Kanuni. Jambo hili limeanza kuvutia sana wawekezaji kutoka nje na hapa ndani na watu kujisikia wako nyumbani. Naamini hiki kitachangia sana katika ukuaji wa pato letu katika miaka inayokuja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha na timu yake yote kwa yote ambayo walifanya. Wameleta mapendekezo ya Mpango ambayo yanakubalika. Nimpongeze pia Mheshimiwa Daniel Silo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti, kwa namna ambavyo aliwasilisha ushauri na maelekezo fulani fulani ambayo, yametoka kwenye Kamati yake kuhusiana na mapendekezo haya ya Bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kabla sijajikita kwenye lile ambalo nataka nizungumzie zaidi ambalo ni la mambo ya sera ya fedha, niseme kwamba licha ya mipango mingi na mikakati mingi ambayo inatekelezwa kwa sasa hivi, ikiwepo ile ambayo inaendana na mpango wa kupambana na athari za COVID-19. Utaona kwamba bado Mpango huu umekuja na maoteo ya ongezeko la pato la Taifa ambalo nafikiri ni chini sana asilimia 5.2. Ni ongezeko kidogo sana ukizingatia kwamba mambo mengi yanatokea na yanatokea kwa haraka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, licha ya hivyo, naamini kwamba, sisi hatutoki kwenye uchumi ambao ulikuwa kwa hasi, uchumi wetu umekuwa chanya, kwa hiyo tuna kila sababu ya kutegemea kwamba, kile kinachotokea kwenye ground na ukweli ni kwamba maoteo ya ukuaji wa chumi zilizoendelea ni asilimia sita kwa mwaka 2020/2021 na mwaka unaokuja unaotea wakue kwa asilimia 4.9, yote hii itachochea ukuaji wa uchumi wetu. Kwa hiyo, ni lazima pengine tuangalie vizuri kwamba tusiwe-conservative sana bali, tujaribu kuangalia ni namna gani tutachukua hatua na nafikiri kwamba, hatua zitakazochukuliwa zilete matokeo ni hizi ambazo nazungumza sasa hivi ndio hizo zitaweza na ndio kitu kimekuwa kikwazo kikubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaona kwamba ukuaji wa pato la Taifa unatokana zaidi na sekta zile ambazo zinanufaika na uwekezaji wa Serikali. Miundombinu, ujenzi ndio utaona hizo sekta ndio zinanufaika na zinakua kwa kasi mpaka asilimia 13 mpaka 14, lakini sekta nyingine hizi za watu binafsi binafsi za kilimo na kadhalika, zinakua kwa kiwango ambacho naamini bado kiko chini. Ukuaji huu mdogo kwenye sekta hizi naamini unatokana zaidi na kile ambacho hakijafikiwa licha ya kwamba tuna uchumi ambao tunasema ni uchumi tulivu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, uchumi tulivu maana yake ni uchumi ambao una-low inflation (mfumuko mdogo wa bei). Hata hivyo, utakuta kwamba, mahitaji kwa uchumi kukua kwa kasi sio tu kwamba uwe na mfumuko mdogo wa bei, wanasema necessary but not sufficient conditions ziko tatu. Moja ni hiyo mfumuko wa bei mdogo; lakini huu mfumuko wa bei mdogo lazima uweze kutupelekea kupata riba zilizo chini. Cha kwanza, riba ziwe chini na tulivu na maana ya riba kuwa chini na tulivu ni riba ziwe chini kwa maana ya kwenye tarakimu moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, ni kwamba, thamani ya sarafu yetu iwe nayo tulivu; exchange rate stability. Kwa hiyo, the three ni necessary but not sufficient conditions za rating growth. Sasa niseme hivi, tutaona kwamba uchumi wetu kwa miaka mingi umekuwa na inflation ambayo ni chini ya asilimia 10. Imekua kwenye zaidi ya miaka 10 iliyopita, tuna inflation ambayo iko kati ya tatu sasa na sita au saba, lakini utakuta kwamba bahati mbaya licha ya kuwa na hiyo, bado kuna matatizo ya sera ya fedha haijaweza kutuletea riba ambazo ziko chini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, issue ni kwamba tujiulize ni kwa nini sera hizo haziji chini? Benki Kuu imefanya mambo mazuri, imeweza kupunguza ile riba ambayo wanatoza mabenki wanakwenda kukopa kwao. Imepunguza fedha ambayo mabenki wanalazimika kuweka kwenye Benki Kuu ambayo haipati riba. Zote hizi zimejaza mabenki ukwasi wa kutosha. Hata hivyo, bahati mbaya hatua hizi zilizochukuliwa siku za karibuni zimesaidia yale mabenki kutengeneza faida kubwa kwa manufaa ya wana hisa wao tu, hazijaenda kwa walengwa, yaani hizi hatua zimguse yule mzalishaji wa sekta binafsi ambaye ili yeye aweze kuongeza uzalishaji au awekeze kwenye uzalishaji mpya, ni lazima apate mkopo ambao ni acceptable kwa riba. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hiyo haijatokea. Nafikiria kwamba, siku itakapotokea kwamba riba zishuke ziwe kwenye tarakimu moja, ndio utaanza kuona kwamba mahitaji ya mikopo yataanza kuongezeka. Kwa sababu, unajua kwamba unaenda kuzalisha, lakini huhatarishi ile dhamana yako, hawaji kuiuza kwa sababu utaweza kulipa ule mkopo na u-service. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kwa hizi riba za asilimia 16 mkopo unaji-multiply mara mbili baada ya miaka mitano. Hebu niambie ni kitu gani duniani hapa utawekeza halafu kiji-multiply mara mbili kwa miaka mitano. Hata nyumba yako wewe mwenyewe miaka 20, 30 ndio unarudisha fedha yako. Kwa hiyo, nasema hiyo haitawezekana mpaka wafanye hivyo. Sasa napenda kutoa hoja kwamba, kitu kinachopelekea mabenki wasishushe riba sio kana kwamba hawana ukwasi, ni kwamba kuna riba ambayo ni bench mark, kigezo ambacho wao ndio wanaangalia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachofanyika wao wanaangalia kwamba kwenye soko la dhamana za Serikali, je, riba inayopatikana pale ni kiasi gani? Wakishapata pale wanasema ok, hii ni risk free rate kwa hiyo ile ndio kigezo chetu. Hatuwezi kushuka chini na ukweli ni kwamba fedha hizi zilizopatikana zote kwenye huu mlegezo uliotolewa na Benki Kuu, nyingi zimekwenda kwenye dhamana za Serikali, hazikwenda kwenye sekta binafsi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme hivi, ukweli ni kwamba hata deni la Taifa linachochewa zaidi na riba hizi za dhamana za Serikali za muda mrefu ambazo ni asilimia 15, 16. Kwa hiyo, tunaposema deni la Taifa tatizo sio tu kwamba eti wanakopa sana, hapana. Rate service burden inakuwa kubwa kwa sababu riba hizo ziko hivyo. Ukiangalia miaka ya nyuma riba kwa dhamana za Serikali hazikuwa hivi. Kwa hiyo, nasema ule mfumo wa ku-auction dhamana za Taifa, una-auction kwa kutaja bei, kwamba, nauza dhamana za bilioni 400 kwa asilimia 16 nani atashusha bei? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hilo ni soko au una-dictate? Nakuapia hazitakaa zishuke hizo riba ilimradi namna ya kuendesha hiyo minada ni hiyo hiyo. Kuna mwanaume anaitwa Dutch Auction natumai wajaribu kuangalia namna gani ya kufanya au waanze kushusha waseme tuta-auction kwa asilimia 10, tuone kama hawatanunua. Mabenki yatakimbilia hata mimi nitanunua kwa sababu asilimia 10 it is a big real interest rate. Real kwa sababu ukitoa hii asilimia tatu, nne ya inflation bado nina real benefit ya six, seven percent. Kwa hiyo, kuna kila haja tumwombe Waziri atekeleze kwa sababu, hiyo itasaidia kwenye kupunguza burden kwa kila mtu na kuanza kuona tena hali inarudi kikawaida, watu kuchukua mikopo, biashara kukua na sisi wote tukafaidi na utakuta hata kwenye kilimo watu watapata mikopo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme kwamba, nafikiria hilo ni la msingi na tuseme kwamba pamoja na kwamba mfumuko wa bei umetufaidisha kuhakikisha kwamba exchange rate bado imekuwa stable, lakini bado haujatufikisha pale ambapo, that is the most critical issue ni riba na niseme hivi nazungumza riba kwa sababu gani?
Mheshimiwa Mwenyekiti, sera ya fedha sio kitu kingine isipokuwa riba, basi ukienda nje huko duniani kwenye masoko yaliyoendelea, nenda US, nenda wapi kitu cha maana wanaangalia bank rate, that is all, mambo mengine yanaji- set yenyewe kwenye soko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naambiwa muda umeisha. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa fursa hii. Ninayo mengi kidogo, lakini nitajaribu kuzungumza machache. Niseme na najiunga na wenzangu kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais wetu kwa mafanikio mengi tunayoyaona na ambayo yameorodheshwa vizuri kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu. Pia nimpongeze Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi na Makamu wa Rais wetu Philip Mpango na wewe pia Mheshimiwa Spika nikupongeze jinsi unavyofanya kazi yako.
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hivyo, naomba niseme, tumesikia mengi yametekelezwa kwenye uchumi wetu, miradi mikubwa sana, lakini naomba Serikali ielewe kwamba, wakati unapofanya makubwa usahau kwamba kuna vikero vidogo vidogo ambavyo ukiviondoa vitakupa amani na kutekeleza yale makubwa.
Mheshimiwa Spika, ukiingia kwenye mtihani usianze na maswali magumu, anza na yale madogo na yale rahisi ambayo utayamaliza mara moja, halafu uende kwenye makubwa. Hasa ukienda kwenye halmashauri zetu kwa mfano, kuna vijikero kama kwa mfano kule Vunjo, barabara ya kilometa saba toka Mji Mdogo wa Himo kwenda Lotima, kitu ambacho unaweza ukakimaliza kwa fedha utakayoita ni chenji tu.
Mheshimiwa Spika, ukienda kwenye barabara tunayoita ni ya Mandaka - Mkirema kilometa saba ni pesa kidogo, ukienda Uchila – Kisomanji - Kikolarii ni kilometa saba au nane, kwa hiyo unaweza ukaviondoa na mimi nisije tena hapa nikiwa naomba kuuliza maswali hapa na pale, nitawaachia na wengine wakiuliza maswali kwa sababu vile vidogo vimetoka, mimi nina amani na Serikali ina-implement vitu vizito itaweza kui-implement bila kusema kule Vunjo kuna matatizo gani mbona huyu jamaa anasimama kila siku. Naomba Serikali ichukulie hilo na iweze kuvikamilisha vile vidogo.
Mheshimiwa Spika, tunaipongeza sana Serikali kwa miradi mikubwa iliyotekelezwa na tunasema kwamba hii miradi ina maana kubwa sana hasa hii tunayoizungumza ya huduma za jamii, mashule na hospitali na kadhalika. Nafikiri tuangalie vizuri kwamba je, the current costs implications zake zikoje. Unapojenga shule ufikirie OC na mishahara itakayotosheleza ile shule, iende ifanye kwa ufanisi.
Mheshimiwa Spika, nafikiri kwamba hilo jambo ambalo kila saa nikiangalia najisikia na-shrink sana. Hivi itakuja kufika mahali kwa mfano leo naamini kama tungesema mahitaji yote ya Walimu, watoa huduma za afya na wafanyakazi wengine wa Serikali ambao wanatakiwa kwenye Wizara ambao hawapo kama wote wangepewa, tungepewa ile ikama kama inavyoombwa, naamini kwamba bajeti nzima isingetosheleza kukidhi mahitaji yale.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naamini kwamba ni lazima tuangalie vizuri na tufanye uchambuzi vizuri, tusije tukaishia kukopa ili tule. Nakubaliana na mambo haya mnayosema inflation, kwani hii inflation niseme na ni lazima tujue, leo hii mfumuko wa bei Marekani na nchi za kanda za ulaya imefikia asilimia 7.5 kwa wastani.
Mheshimiwa Spika, ni mfumuko mkubwa kuliko wakati wote kuanzia mwaka 1982. Kwa hiyo hili ni suala la kidunia ni structural na kitu ambacho hatuwezi kuki-address kusema kwamba tunaenda kuomba pesa, ni kufanya nini, ni kukaza mikanda, this is the time to belt tighten, ni wakati kusema kwamba there is no way tutaepuka makali haya, kama ulikuwa unaenda jimboni kila siku nenda mara mbili, mara tatu kwa sababu hela utakayokuwa nayo haitatosheleza.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka kusema kwamba hilo ni jambo ambalo tuliangalie, sio kwamba ni letu na sio jambo la kufanya haraka haraka na sio kitu ambacho Benki Kuu inaweza ikashughulikia mara moja, haiwezi it is not monetary policy ya hapa ndani itafanya hicho kitu kwa sababu kinakuwa given na imported inflation.
Mheshimiwa Spika, sasa turudi hapa, ambacho nimepongeza kwenye hii miradi mikubwa, kuna kwa mfano hili suala la Vyuo vya VETE, naishukuru sana Serikali imeanza kutoa vipaumbele stahiki kwa VETA, vyuo hivi ambavyo vinatupa study na ufundi. Hata hivyo, naambiwa kwa takwimu ambazo sio rasmi, VETA ina upungufu wa Walimu 1400 na ni kabla havijaongezwa hivi vyuo vingine ambavyo vinakamilika kwenye mwezi huu wa Juni na mwaka unaokuja wanaweka vyuo vingine thelathini.
Mheshimiwa Spika, ukiweka pengine upungufu utakuja kuwa ni mkubwa sana wa watu, lakini sio tu upungufu wa Walimu, lakini ni upungufu pia wa vitendea kazi, vifaa vile vya kufundishia. Watu wanataka kujifunza cherehani, wanahitaji kushona kwa sababu sasa hivi tunavaa nguo zimeshonwa hapa, kwa hiyo lazima wawe na basic equipments kwenye hivi vyuo. Kwa hiyo, ni lazima tufikirie tunafanyaje pesa inatoka wapi ili tuweze kuhakikisha kwamba wanajenga ndiyo tusije tukajenga magofu, yaani kuwa na majengo tu it doesn’t help, haitasaidia.
Mheshimiwa Spika, mchango wangu mkubwa nilitaka kuingiza kwenye uwekezaji ambao Mheshimiwa Rais wetu ameufanyia kazi sana na naamini utaanza kuona miradi mingi inasajiliwa. Wamesajili miradi 294 kutokana na hotuba tuliyopewa na Mheshimiwa Waziri Mkuu na kweli kama miradi hii yenye kubeba thamani ya Dola Bilioni Nane itatekelezwa ajira zitaongezeka, kipato cha Taifa kitaongezeka, tutabakia kwenye kundi lile la watu walioendelea vizuri kipato cha kati na pengine tutaenda juu, lakini miradi hiyo inatakiwa kutekelezwa, tutafanyaje mimi nataka nishauri mambo matatu, manne.
Mheshimiwa Spika, kwanza nataka uwekezaji huu wenzetu majirani zetu wameanza kupunguza kodi ya makampuni, kwa sababu tunashindania wawekezaji hawa, wanapunguza kodi ya makampuni kutoka 30 kuja asilimia 25. Hiyo ni kivutio ambacho hatuwezi kukibisha hata tungesema tunafanya nini. Pili; kuna perception kwamba gharama za kuanzisha mradi hapa ni kubwa sana kumbe wala si kubwa sana ukilinganisha na kwingine, tatizo la watu kuona gharama hizi za uanzishaji miradi kubwa ni utitiri wa mamlaka zinazotoza tozo hizi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, utakuta kwamba kama tungeweka lamp sum tukasema kuanzisha kitu hiki ni Shilingi Milioni Moja unaenda kulipa kama ni TRA au mahali pengine lakini mamlaka nyingine zikagawiwa na huyo anayekusanya inakuwa ni rahisi mtu anajua kabisa ok, nataka kuanzisha kampuni ya simu ni Shilingi Milioni Tano basi its transparent and open and no need ushauri wa mtu. Kwa hiyo, mimi naomba hilo lifanyiwe kazi ili tuweze kupata wawekezaji hawa waje upesi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tatu; ni suala zima nitalizungumza tena kwa bahati mbaya suala la riba ambalo najua mamlaka imeshatoa amri imeshatoa directive kwamba lishughulikiwe, lakini hatuwezi kupata wawekezaji ambao hawawezi kukopa ndani kwa sababu utakuja na mtaji wako ndiyo mashine na nini, lakini ule mtaji wa working capital lazima utoke kwenye mabenki ya ndani. Hasa huwezi kukopa kwa asilimia 16 wakati kule nje mtu anayezalisha kama huyo anakopa kwa asilimia tano uende ukashindane naye kwenye mauzo ya nje it is impossible! What you need ni kwamba lazima kweli au tuweke special windows na tunajua kwamba kuna watu wanataka kuongeza uzalishaji wao hapa kwa mfano kule NIDA tulikwenda, lakini hawawezi kukopa hapa ndani kwa sababu hiyo tu kwamba riba ni kubwa na wakipeleka kuuza vile vitu nje hawataweza kushindana kwa hiyo inakuwa matatizo, naomba hicho kifanyiwe kazi na tusichukue tu mzaha mzaha kwamba basi tu tuna njia ya kupunguza hizo riba, tunajua zipo! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niongeze kingine ni kwamba mimi naamini pia kwamba miradi mingine kwa mfano Bagamoyo Port, sijui Mchuchuma – Liganga, tunasema kwamba tatizo lililopo ni kwamba wanajadili vitu ambavyo hatuna, wanajadiliana maslahi ya Taifa letu tuyalinde lakini tuangalie maslahi mapana yanatokana au faida nzima zinazotokana na mradi ule kwa muda mrefu, tuangalie tusiangalie kesho utakosa ushuru wa kiasi hiki na hiki, kwa sababu huo ushuru huna anyway haupo kama ile kampuni haitaanzishwa wewe hutapata huo ushuru. Kama Bagamoyo port haitaanzishwa ianze kufanya kazi hutapata hicho kitu, kwa hiyo afadhali tukubali tuangalie tuwe na long term view ya issues badala ya kuwa na short term issues.
SPIKA: Ahsante sana muda wako umeshaisha Mheshimiwa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja. Ahsante sana. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo kwa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 pamoja na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nashukuru sana kwa fursa hii. Natumaini nami utanipa dakika 15. Kwanza nianze kwa kusema kwamba nampongeza sana Mheshimiwa Rais na Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Tunaona jinsi ambavyo wanakimbizana kutafuta wawekezaji kutoka nje, na zaidi kutafuta resources, fedha kutoka kwenye Mataifa rafiki na kutoka kwenye mashirika ya Kimataifa ili waweze kuongezea kile tulichonacho na kuweza kusukuma na kutekeleza mipango ambayo tulikuwa nayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kwamba wote tunaelewa kwamba lengo kuu la mipango tunayotunga hapa na bajeti ni ukuaji wa pato la Taifa ili wananchi waweze kuinua maisha yao kwa kujipatia kipato cha juu na kuweza kuboresha huduma wanazopata. Kwa hiyo, ndiyo lengo kuu. Kama tukishindwa kufikia hilo, basi hatujakamilisha kazi yetu kama tunavyostahili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami naamini kwamba tumefeli kidogo. Kwa sababu gani? Katika lengo la mwaka huu kubwa kwenye bajeti ya mwaka uliopita na mpango wa mwaka huu ambao tunautekeleza pia, ni kwamba tuweze kufufua uchumi wetu. Sasa kufufua uchumi wetu siyo kupata 4.8% ambayo ilijitokeza baada ya madhara ya Uviko. Kufufua uchumi wetu maana yake ni kurudisha kasi ya ongezeko la pato letu kwenye 7% au zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Profesa Muhongo amesema sawa kwamba hatuwezi; na miaka hiyo ya nyuma kabla, tulipokuwa kwenye 7%, nia ilikuwa kwamba lazima tuongeze ile kasi ifike asilimia 8, 9 hata 10 ambayo ndiyo inaweza kupelekea kusema kwamba sasa tumejiondoa kwenye umasikini na kufika katika vurugu ya nchi ambazo zipo kwenye kipato cha kati na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama hatujaweza kufufua, tumebakia na asilimia 4.9; na ninashangaa kwenye huu mpango tulionao sasa hivi, tunasema kwamba hata mwaka unaokuja 2023 pato letu litakuwa kwa asilimia 5.3. Hata maoteo yanayofanyika kwenye mpango wetu huu hatujaweza kuwa courageous tukasema turudi kule tulipokuwa ndani ya kipindi cha miaka mingine miwili. Bado tuko chini ya 7% pengine mpaka mwaka 2025, ndiyo maoteo yaliyopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nafikiria kuna tatizo moja hapa, kama siyo kwenye takwimu, ni kwenye maandishi mengine. Ukweli ni kwamba haiwezekani nchi nyingine kama Botswana, Kenya na Rwanda; Rwanda imeongeza uchumi wake na kasi ya ukuaji wa pato lake ni asilimia 9.5 na Kenya ni asilimia 7.2. Sasa tunapoanza kusema kwamba aah, ni mvurugano wa logistic industry kwenye dunia, ni vita vya Ukraine, tusing’ang’anie huko. Tujaribu kuangalia ni kitu gani tunaweza tukafanya, tukarudisha uchumi wetu kwenye ukuaji wa 7% au zaidi ya 7%. La sivyo, hatutafika popote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mkakati mkubwa ambao nashauri utumike kuweza kufufua uchumi wetu kwa haraka ni ule wa kushirikisha sekta binafsi. Inavyooneka sekta binafsi yetu haichangamkii fursa. Haioni fursa. Tunatengeneza miundombinu mizuri, kila kitu kinafanyika sawa sawa kwenye upande wa Serikali na utaona kwamba sekta zilizokuwa kwa kasi zaidi ya 8% ni zile ambazo zinapata uwekezaji wa Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sekta ya maji imekua kwa asilimia 11.9, huduma za jamii, ni asilimia 8.5, habari 8%, fedha na bima asilimia 10, madini na kadhalika. Ukienda hizi sekta nyingine ambazo tunashirikisha sekta binafsi, uchukuzi na uhifadhi imekua kwa asilimia 1.7 tu na ndiyo huko wenzetu tuko tunakimbizana. Ukienda kwenye kilimo 4%, pesa yote inaenda huko kwenye bajeti ya kilimo lakini ina-grow kwa 4% licha ya kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Bashe. Viwanda imekua kwa asilimia 6.3, biashara asilimia 4.4, ujenzi asilimia 5.3, upangishaji na majengo asilimia nne na nukta. Sasa hizo ndiyo sekta hasa za wajasiriamali, lakini hazikui. Hawajaweza kuchangamkia fursa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri njia ya kuweza kulazimisha watu wajiingize kwenye uchumi huu pengine, badala ya kutupa fedha za kupeleka kwenye barabara za TARURA kwa sababu tumeshapeleka kiasi kidogo na barabara zimeanza kuwa nzuri, tupe hiyo Shilingi milioni 500 kila Mbunge achangamkie mradi wake kwenye jimbo lake, aajiri watu, ahakikishe wajasiriamali 500 mpaka 1,000 wanaingia kwenye mradi huo, waanze kuzalisha, na hiyo iwe ni mbegu itakayozalishwa mwaka hadi mwaka. Pia tutakuwa tunashirikisha wajasiriamali wetu kwa nguvu zaidi kuliko kusubiri ile mikopo ya 4,4,2.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini tukiweza kufanya vile itatusaidia. Lazima ile miradi inayoletwa ionekane kwamba itatekelezeka na Wabunge wasimamie na wajitolee katika kusimamia kweli.
Mhshimiwa Mwenyekiti, inavyoonekana, sekta hii haiwezi kupata fedha kutoka kwenye vyombo vya fedha. Kwa nini? Kama alivyosema Mheshimiwa Profesa Muhongo, riba ziko asilimia 16. Bbado asilimia 16, haijapungua! Toka mimi niingie huku Bungeni miaka ya nyuma riba ni asilimia 16. Sasa hii issue ni kwamba mtu mwingine anaogopa kuchukua mkopo wa riba asilimia 16. Watu wengi wanaogopa kwa sababu hakuna faida ya haraka namna hiyo, lakini tukitumia huu mpango wa sasa hivi wa fiscal stimulus, tuache hii monthly stimulus ambayo imeshindwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, monthly stimulus imeshindwa kwa sababu ukweli ni kwamba inflation iliyopo na kadhalika, siyo a man management type ni supply oriented. Kwa hiyo, ni lazima tutumie mbinu nyingine ya kufanya fiscal stimulus; tutapeleka fedha namna gani kwenye uchumi wetu vijana waweze kuchakarika tuanze kuona mabadiliko yanatokea kwenye zile sekta ambazo naamini Mheshimiwa Prof. Muhongo amezitaja vizuri. Kama hilo likifanyika naamini tutakuwa na kitu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, imezungumzwa issue ya inflation, mimi naamini bado tuko vizuri. Asilimia 4.6 ni nzuri, lakini naamini pia kuna suppressed inflation hapa. Watu wanaona bei zinakua sana, lakini tukienda kwenye karatasi tunaambiwa ni asilimia 4.6. Haiwezekani iwe 4.6 wakati Ulaya ambako inflation yao kwa kawaida ni 2% mpaka 3% iko asilimia 10. Ukienda UK ni asilimia 10, EU huko kwa wastani ni asilimia 10, na ni plus!
Mheshimiwa Mwenyekiti, East Africa, nchi za wenzetu hawa, wao inflation ni 9%. Wastani wa block yetu ni asilimia 9.5. Ukisema sisi ni asilimia 4.6, nasema na sisi tuko kwenye kisiwa fulani ambacho Mungu ametubariki. Kwa hiyo, naamini pengine siyo rahisi sana kufikia lengo hilo ambalo tumejiwekea sasa hivi ni 3% mpaka 5%, tutajiminya sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ina maana lazima tuache ile monthly accommodation kwamba mikopo itolewe kwa sababu kinacho-drive inflation ni mikopo ambayo inaongeza ujazo wa fedha, kufukuzana na supply ndogo. Kwa hiyo, lazima mikopo itolewe ili tufungue mwanya huo ili tuweze kusaidia sekta zile ambazo zinahitaji mikopo ili ziweze kuongeza uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatuwezi kubana kiasi hicho, lazima tufuate monthly accommodation kukubali kwamba tuongeze kidogo inflation lakini kwa sababu ni muda mfupi, pengine ugavi (supply) itajifungua, halafu inflation itaanza kushuka tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye upande wa kilimo naona matatizo. Ukweli ni kwamba tumejitahidi, lakini gharama za kilimo zimeongezeka sana. Kwenye korosho kwa mfano, wametumia gharama kubwa, wanasema kwamba bei za chakula duniani zinapanda kila mahali, lakini yule mtu aliyetumia gharama kubwa sana za kuvuna korosho yake this time anaambiwa bei zimeshuka. Hii dunia inatuonea namna gani? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani jitihada tunazoona Mheshimiwa Rais wetu anafanya kutafuta masoko, specific masoko kwa Marekani, ndiyo jitihada tunazohitaji kwa mazao mengine ili tuwe na a captive market ambayo tunajua kabisa kwamba kwa bei za kule tutapata kiasi hiki, lakini sasa hatuwezi kumwambia mtu aliyetumia gharama sijui mara ngapi, halafu unamwambia eti bei ya kuuzia korosho sasa imeshuka. Wanalia! Mimi nimesikia wanalia, lakini siyo kwa korosho tu, ni kila zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo ilivyo kwenye kilimo, wale wenzetu wanatusubiri, wanatupiga. Wewe unatumia gharama kubwa, unaenda step mbili forward unarudi nne nyuma kwa sababu bei inashuka unakuta income yako ni ile ile, gharama hujai-recover. Ni ngumu sana. Kwa hiyo, naona tuangalie hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kuna tatizo lingine kwa upande wa mabwawa, ni mojawapo ya kufanya decision. Ni kwamba pale unapoona kwamba kuna mwanya wa mfanya maamuzi ili kupendelea, the only way ni kumfanya afanye kitu kwa haki. Kila mtu apate kwa usawa, basi unaamua kuweka rules au vigezo ambazo zita-guide ile decision. Ukiwa na rule, ni lazima kama yule mtu anagawa kwa mfano cake ya Taifa wanagawa hapa, ile bajeti ya kilimo inagawanywa, kungekuwa na rooms zinazosema kwamba ili upeleke bwawa mahali fulani, ni lazima kigezo hiki na hiki kifikiwe. Siyo unaenda kufikiria tu mwenyewe, unaamua peke yako, unaweka bwawa kubwa hakuna hata mtu, yaani mwaka mzima upepo ni mkubwa hata kitu hakioti, wewe unaenda kuweka mabwawa kule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuweke vigezo ili kuhakikisha kwamba decisions zinafanyika kwa uhakika na kwa njia ambayo ni objective na sahihi. Kwa sababu fedha hizi za kwetu kwenye bajeti na kwenye mpango zinapotea wapi? Kwenye matumizi. Wewe utatafuta hela nyingi utapata, lakini kwenye matumizi ukitumia ovyo ovyo tu, ukatupatupa hutapata tija. It is not efficiently invested and you don’t get anything.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yaani naomba, hata tusipoongeza ile bajeti, lakini tukatumia kwa namna ambayo itatumika na itasimamiwa vizuri na miongozo ikatolewa sahihi na watu tuione; tutaiona hapa Bungeni, lakini miongozo itolewe, watu watumie kwa haki na wawe waadilifu na hatua zichukuliwe. Niliona Wabunge walikuwa wakali sana kwenye CAG report. Kwa hiyo itumike, naamini tutafika mahali penyewe na hakuna haja ya kuongeza kodi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho, tunasema uchumi ukue lakini kwenye mazingira tulivu, natural economic stability. Sasa issue inajitokeza ni hivi, niliangalia bajeti kwa mfano ya wenzetu, majirani zetu, mwaka jana wao hawakutangaza new measures za revenue, walisema revenue measures za mwaka jana zitaendelea ku-hold, unaona lakini tutaongeza ufanisi kwenye ukusanyaji na kuziba mapengo kwenye ukusanyaji wa kodi. Kwa hiyo sasa maana yake nini? Ile kalenda ya kodi ikawa izingatiwe kwa hiyo tunamuomba pia Waziri, anapoenda kufikiria hili aione kama…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nashukuru sana na nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais na Baraza lake la Mawaziri kwa namna ambavyo wameweza kutuletea mafanikio kwenye mazingira ambayo ni magumu sana, mazingira ambayo hata nchi zile ambazo zina chumi komavu hazijaweza kuyakabili inavyostahili na kwa hiyo mfumuko wa bei kwenye nchi hizo kubwa, nchi zilizoendelea, mfumuko wa bei uko juu ya tarakimu mbili na hapa kwetu unaona bado mfumuko wa bei ni takribani asilimia Tano au ni asilimia 4.8 na pia tunaendelea kukua kwa asilimia ambayo ni kubwa kuliko maeneo mengine na tumeweza kui-stabilize vizuri kwa namna moja au nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti kitu ambacho ni lazima tujivunie sana kwamba Serikali imefanya mambo ambayo lazima tufurahi kwamba inajizatiti na imeweka mifumo ambayo pengine kama itakuwa endelevu, kwa sababu tunaweza tukasema kwamba tumefanikisha lakini bado kuna viashiria kuna risk ambazo bado ziko kwenye uchumi ambavyo vinaweza vikapelekea hali ikabadilika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, inafurahisha pia kwamba malengo ya bajeti kwa mantiki ya matumizi na mapato yake yamefikia kwenye asilimia kwa wastani wa 95, ni nzuri yaani hatuja-miss sana malengo yetu. Kwa hiyo, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Fedha na viongozi wengine wa Wizara niliseme hiyo ni jambo la kufurahisha. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema kweli suala la visababishi vya mtikisiko kwenye chumi nyingi siyo suala ambalo linakuwa ni la muda mfupi, siyo la mpito kwa sababu hivi vita vya Ukraine vinaonekana vinaendelea na vitaendelea, hatuoni upeo wake vitaisha lini. Kwa hiyo, siyo jambo tu la kusema kwamba tutapigana kwa mambo ya dharura kwa kufanya mambo ya dharura kwa kutoa ruzuku na kadhalika ni jambo ambalo lazima tuliangalie kwa mapana yake kwamba tuchukue hatua madhubuti ili kusema kweli tusipoteze muda.
Mheshimiwa Mwenyekiti, turuhusu kwamba vitu vifanyike kwa namna ambayo inastahili na katika kufanya maamuzi yoyote ambayo tunajua kanuni moja ya kufanya maamuzi ni kutathmini kama lile jambo ni la mpito au kama litakaa, kama litakaa basi maamuzi unatakiwa kufanya ni maamuzi ya ku- accommodate ile na kuruhusu uchumi uanze kwenda kwa namna nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuje kwa mfano kwa upande wa suala zima la mfumuko wa bei. Mimi najiuliza tunatumia vigezo gani kulalamika sana? Kwa sababu asilimia Tano sisi tulioishi miaka ya kale hiyo, tulikuwa na mfumuko wa bei asilimia 30 tukaishi nao, yaani ukiwa na hela inaishia huko huko kabla hata hujaamka. Kwa hiyo, sasa kama kweli mfumuko wa bei tarakimu tunazopewa ni za uhalisia, mimi naamini kwamba pengine watu hawangelalamika kiasi hicho! Naamini kuna tatizo aidha katika hiyo takwimu tunayopewa, haijawa ya uhalisia kwa sababu kama mfumuko wa bei ya mahindi ingepanda zaidi mara mbili, asilimia Moja na Tano katika kipindi cha Septemba 2022, unachelea kusema pengine kuna kitu, mfumuko wa bei ungekuwa kidogo uko juu zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia niseme kuna jambo ambalo tulijue kwamba kuna ile base, ile index yenyewe ambayo inatakiwa iwe na episode za kupanda juu lakini baadae unaanza kui-stabilize kwenye level tofauti. Kiwango kile kinakuwa kimepanda halafu unai-stabilize kwenye level ile na inflation sasa inakuwa kwenye level nyingine kwa sababu ile index imepanda, lakini sisi hatuangalii hivyo vitu. Kuna two things, kuna kupanda ile index na yale mabadiliko ya ile index from time to time.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naamini kwamba hiyo ya kupanda, hiyo spike inatakiwa kwenye index ni nzuri mara nyingine. Kwa mfano, bei, nashukuru sana Mheshimiwa Mwigulu alisema siku moja, alisema mahali pengine sijui ni hapa, lakini ukweli ni kwamba bei za mazao ya wakulima zilikuwa chini sana kwa miaka mingi, miaka kama 10 hivi. Bei za mazao ya mahindi, mazao yote ambayo tunasema ni ya vyakula, zimekaa kama maji yaliyotulia. Sasa kwenye hali ya uchumi ya namna ile watu hawapati hamasa kuongeza uzalishaji, it doesn’t work.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka mwaka huu nikizalisha, nipate faida kubwa, inanirudisha kule kwenye shamba niongeze kilimo. Sasa unapoongeza kilimo, bei itashuka kidogo halafu bado ikishuka kidogo maana yake ni kwamba watu watasema sasa kuna glut, yaani mazao yamekuwa mengi kwa hiyo watu wanayapunguza kidogo kuzalisha, wanakimbizana na vitu vingine halafu kipindi cha mwaka unaokuja wanaona tena kwamba aah! mbona bei zimeanza kupanda kwa sababu mazao yameshuka? Kwa hiyo, inakwenda namna hiyo na that is the only how you can make agriculture pay. Kilimo hakitalipa!
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa mazao ya export, utaona kwamba pia exchange rate imekuwa stable sana. Tumesahau kwamba exchange rate pia ni instrument ya kutuwezesha kuendesha huu uchumi. Ili kuongeza faida ya exporters, watu wanaouza nje na hao wanaozalisha mazao ya kahawa, katani na kadhalika ni lazima exchange rate iwe ina-move ili akiuza akipata dola moja kule kwenye bei ya dunia haibadiliki sana. Utakuja kupata dola moja, inabakia Shilingi 2,300 kwa miaka mitano, utakuwa wewe gharama zinapanda lakini wewe hupati chochote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ni lazima ifike mahali pia Serikali na Benki Kuu ione kwamba kuna umuhimu wa kuchochea exports kwa kuruhusu mabadiliko stahili kwenye exchange rate, siyo kuifanya tu ikae forever. Kwa sababu uzuri mmoja wa kufanya vile, ile haitakuathiri sana kwenye mambo ya ulipaji wa madeni kwa sababu export zipo kwenye dola ile ile na deni liko kwenye dola ile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme napongeza kukopa ndani zaidi kama tungekuwa kwa mfano, hiyo sekta binafsi haikopi, aidha sekta binafsi haikopi kwa zile riba ziko juu. Kwa sababu Serikali ikikopa actually deni linakuwa na uhimilivu zaidi kwa sababu deni la ndani halina tatizo la uhimilivu, lina tatizo la kukusanya tu mapato kwa sababu ni domestic revenue, lakini lile la nje lina tatizo kwa sababu lazima u- generate dollars, kama haujauza exports hutapata dola za kulipa zile dola na utapata matatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo issue ni kwamba lazima tukubali kwamba exports lazima ziongezeke kwa sababu lile deni tunalo na lazima tutalilipa na tutalilipa kwa madafu. Madafu ukiwa nayo lazima uyabadilishe yawe dola. Kwa hiyo, ni lazima tukazane na hiyo na ninaamini mfumo mzima wa kusema tukimbizane na kilimo ni sawa, lakini pia tukimbizane mimi nafikiri katika vipaumbele tunavyo vingi, vipaumbele ambavyo lazima tuvikazanie sana ni utalii ambao unaleta haraka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kilimo kina risk nyingi bado, hata ukijenga mabwawa, itajengwa kwa miaka mingapi uweze kuhamisha? Itachukua muda. Nadhani utalii, madini, mifugo utaona sasa hivi tuna-export nyama kwa wingi, mifugo na uvuvi pamoja pengine na madini, madini nimeshataja lakini naamini kwamba kuna ambavyo vipo najua kwamba ukifanya vitapiga. Ukisema utafanya hata ukiongeza itachukua muda na ile chances za ku-realize the potential ambayo wewe unalenga ni may be is fifty fifty. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme jambo la mwisho ukiniruhusu ni kwamba kuna hii mikopo ambayo imetengwa kwenye dirisha lile la Shilingi Trilioni Moja ambayo imetolewa wanasema Benki Kuu iko tayari kutoa, kusema kweli hiyo siyo realistic. Ukweli ni kwamba Benki Kuu Kifungu cha 40 cha Sheria ya Benki Kuu hakiruhusu Benki Kuu ikopeshe mabenki zaidi kwa kipindi zaidi ya miezi mitatu, sasa kilimo gani kinalimwa kwa miezi mitatu, hakuna! Mkimkopesha mtu utaenda kuvuna mazao yale ili akulipe?
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna tatizo hapo ni kwamba ni dirisha ambalo ni zuri lakini mimi naamini kwamba, hata hivyo wamewekea masharti kwamba lazima Benki ipeleke dhamana za Serikali, lakini ambacho wangefanya ni kwamba wangesema benki ilete mikopo ambayo imetoa kwa sekta binafsi kwa riba chini ya asilimia 10, walete hiyo portfolio halafu wa i–refinance wakifanya hivyo, benki ambazo hazina hata hii dhamana zitakopesha zitapeleka ile mikopo ita-refinance watapewa fedha wataendelea kukopesha sehemu nyingine watapewa kwa hiyo asilimia Tatu. Kwa hiyo, that is the only realistic way, otherwise mimi nafikiri kwamba ni ngumu sana kupata mabenki ambayo yatakopa na kukopesha kama inavyohitajika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, najua kwamba muda umekwisha, naunga mkono hoja, mimi pia ni Mjumbe wa Kamati ya Bajeti, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa fursa hii. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara na Katibu Mkuu, kwa kazi nzuri wanayoifanya, kweli inaonekana. Niwapongeze sana uongozi mzima wa Wizara pamoja na Mheshimiwa Rais ambaye anawasimamia.
Mheshimiwa Spika, naomba niseme machache tu, mambo kama manne. La kwanza, kuna eneo zuri sana na la kimkakati la kuweza kuweka kongani au kuweka export processing zone kwenye Jimbo la Vunjo, eneo lile la mpakani na Nchi ya Kenya ambalo linaitwa Lokolova. Ni eneo ambalo limekuwa na migogoro kidogo kwa sababu ya wafugaji na wakulima wanapigana kidogo pale, lakini kuna eneo la zaidi ya eka 2,500 na Serikali tayari ina eka 140 ambazo zinaweza zikachukuliwa na zikaanza kutumiwa kwa kujenga kongani hilo.
Mheshimiwa Spika, naamini hilo litakuwa jambo la msingi kwa sababu litakuwa limefungua nchi yetu na mpaka wa Kenya pamoja na South Sudan, Djibouti na kadhalika ambapo naamini sehemu ile ilikuwa tayari pale Himo palikuwa pameibuka Soko la Kimataifa la Grain, ikawa ni reference point ya bei za mahindi na nafaka nyingine kwa nchi zote za kaskazini pale. Kwa hiyo naamini kwa vile zimepakana kuna eneo la kutosha, naamini kwamba Wizara itafikiria kuona mkakati wa kujenga kongani au export processing zone kama itawafurahisha.
Mheshimiwa Spika, kuna suala tulikuwa tunaizungumza sana la ETS. ETS naizungumza kwa sababu baadaye nitazungumza kidogo kuhusiana na uwekezaji pamoja na Business Competitiveness Index ya Tanzania. ETS sijui imekuja kuishia wapi, hatujui, sisi kama Wabunge hatujapata ripoti ambayo inaweza ikaturidhisha kwamba suala hili limekamilika na kwamba wanaviwanda wale ambao wanalipa hela nyingi sana kwa kutumia electronic tax stamps ambapo kweli ni kitu kimoja ambacho naamini hao watu watakuja kufidia gharama kwa walaji kwa kutumia hizo.
Mheshimiwa Spika, kuna suala ambalo mwenzangu, Mheshimiwa Mnzava, amelizungumzia kidogo, kuhusiana na idadi ya viwanda. Nilipoingia hapa Bungeni mwaka 2021 tulikuwa tunaambiwa kwamba viwanda vilivyotengenezwa katika mwaka ule vilikuwa ni 8,000 sijui, sasa hatujapata tena hiyo idadi. Sijui vimefika vingapi sasa hivi, lakini inaonekana kwamba pengine ile dhana ya kutaka kwamba kila mkoa au wilaya iwe na specialization fulani ya kiwanda chake ambacho Serikali itasaidia kuhimiza wawekezaji waweze kwenda kule kufanya na kupewa incentives ili waweze kuendeleza viwanda vile, sijui ile sera imeishia wapi.
Mheshimiwa Spika, niseme pia suala nyingine kwa harakaharaka kwa sababu yale ya jumla nitayasema mwishoni hapa, suala la SIDO, TEMDO na kadhalika wamekuwa wanajaribu kubuni mashine na vitendea kazi mbalimbali ambavyo vitasaidia kwenye ujasiriamali wetu; kwenye kilimo na kwenye viwanda na kadhalika, lakini nafikiri kwamba kazi ya ubunifu imekuwa ni ndefu sana, kama vile unataka ku-invent a wheel, unataka kuvumbua gari ambayo tunaona linatembea ambayo hata hayatushangazi sana sasa hivi.
Mheshimiwa Spika, sasa wewe unataka kuvumbua kwa kujenga, kutengeneza mwenyewe. Nafikiri kwamba wangekita nguvu zao sana kwenye kwenda kwenye maonyesho ya bidhaa za viwanda kwenye nchi hizi ambazo wana maonyesho ya muda mrefu kama China au India wanakuwa nayo, waone vitu gani halafu tu-expose vijana wetu kwa teknolojia ambazo zipo rahisi, very simple ambazo pia zinazaa matunda kwa haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, pale kwenye jimbo langu kwa mfano nikiwaambia kwamba kuna mashine ya shilingi 200,000 ya kuchakata ndizi na kuweza kuzigeuza zikawa ni chipsi wanashangaa kwa sababu ni cheap, lakini pia unaweza ukatumia kwenye scales mbalimbali, scale kubwa na ndogo, lakini ukweli ni kwamba ukisema unabuni, innovation lazima tujaribu ku-leverage na ku-leapfrog kwenye vile vitu ambavyo viko sehemu nyingine.
Mheshimiwa Spika, kuna suala hili la TIC; ukienda kwenye website yao unashangaa. Mtu anasema je, kuna fursa gani ya uwekezaji Tanzania wanasema iko fursa kwenye sekta ya mining, kwenye kilimo. Lakini huwezi kujitangaza namna hiyo, kwa kusema njoo kwenye industry au kwenye mining au kilimo.
Mheshimiwa Spika, nilitarajia kwamba kwenye website ya TIC ukiingia utakuta a package of areas and projects ambazo tayari zimefanyiwa tathmini na upembuzi yakinifu, lakini hawatoi information yote wanatoa little/scant information kwamba tumefanyia uchambuzi na huu uchambuzi umefanyika na wabobezi, ma-investment bankers au wachambuzi wazuri ambao wana business analytics zao.
Mheshimiwa Spika, twende tu hata hii ya Liganga na Mchuchuma, kuna Mradi wa kimkakati wa Liganga na Mchuchuma na parameters zake ziko hivi na hivi, payback period yake itakuwa hivi, investment itakuwa hivi na faida itakuwa hivi. Kwa hiyo unakuwa ume-package hii miradi ya kimkakati kwa kuweka information ambayo wewe umeshaifanyia tathmini na upembuzi.
Mheshimiwa Spika, tatizo ni hili; hakuna mtu yuko nje ya Tanzania anayeweza akaufanya tathmini mradi mkubwa bila kutumia hela nyingi sana. Kwa hiyo inawa-put off, lakini akikuta kwamba imeshafanyika kuna basic information ambayo inaweza ikam-lead yeye kupeleka pesa inakuwa rahisi kwake kusema, okay, najua hiki, hebu ngoja nipate hiyo package, nitanunua.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo atakulipa wewe TIC, wewe Wizara uliyetengeneza hiyo feasibility study halafu atakulipa ili achukue ile package yeye mwenyewe akaiangalie, akafanye stressing testing zake halafu aseme anapeleka hela yake Tanzania kwenye Mradi wa Liganga na Mchuchuma. Hiki siyo kitu ambacho ni siri. Kama unajiuza useme unafanya siri, watu wanasema huu mchakato wa kupata wawekezaji wa Liganga na Mchuchuma inakuwa siri kabisa, huambiwi kuna nini on the table, what is on the table.
Mheshimiwa Spika, kwenye kila sekta kuna mradi wa kimkakati ambao ukifanyiwa uchambuzi halafu ukawekwa kwenye package yetu ya kujitangaza, siyo kusema hapana njoo tu kuna tourism. Tourism is not enough, sema ukija kule kuna eneo limekuwa identified unaweza uka-invest kwa kiasi hiki cha pesa na return yako itakuwa hivi. Kwa hiyo hiyo itakuwa ni rahisi sana kupata wawekezaji.
Mheshimiwa Spika, ninachosema ni kwamba huwezi kuwa tu na Mheshimiwa Rais anayekimbizana, anapata pledges za miradi, watu wanasema watakuja lakini unaona kwamba hawaji, kwa nini; kwa sababu mpaka wanze sasa kutafuta information. From where?
Mheshimiwa Spika, nilifikiri kwamba kila mahali anapokwenda Mheshimiwa Rais au viongozi wetu wa juu wa Serikali wakasema kama kuna investors wanataka kuja Tanzania basi iundwe timu ya investment bankers au relationship managers ambao watakuwa moja kwa moja wanafanya direct communication na wale walioonesha nia ili wale watu waone kwamba wana contact person ambaye akitaka kumwona Rais yule jamaa yupo, atanipeleka. Kwa hiyo itakuwa ni rahisi sana kupata hawa watu, lakini tukikaa tu kimya hivi, haitakuja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, hili suala la blueprint. Blueprint ni nzuri, tumeitengeneza yetu wenyewe, tunasema tufanye hivi tutapanda, lakini mpaka tutengeneze blueprint actually tumeshuka kwenye Business Competitiveness Index. Ya mwisho ilikuwa 2019 kwa sababu baada ya UVIKO hawakufanya, lakini ukweli ni kwamba hii Business Competitiveness Index ya World Bank ina vigezo 98 lakini vinajikita kwenye maeneo 12.
Mheshimiwa Spika, tungejaribu kupitia hivyo vigezo vinavyotumika internationally ambavyo vimewekwa kama standard, tujaribu kupitia na tulinganishe na vile vyetu vya blueprint ili tuweze kukamilisha, kila mtu amepewa kazi yake, wewe fanya hivi, mwingine afanye hivi, tunamaliza tunaweza kuona kwamba nchi yetu ina-move kutoka 118 kwenye index ile, ije hata kwenye 70. Turudi kule, siyo tuendelee tu tunatengeneza blueprint, lakini tunaona kwamba bado hatujaweza ku-improve mazingira yetu ya biashara kwa maoni au kwa macho ya wawekezaji kutoka nje. Kwa hiyo naamini tukiweza kufanya hivyo tutaharakisha mambo.
Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba niseme hivi; kuna suala hili la masoko, sasa inakuwa ni vigumu kujua hata masoko yako wapi. Kwa mfano lile soko lililoanzishwa pale Stock Exchange linaitwa Tanzania Mercantile Exchange, linatoa fursa nzuri kwa wakulima wetu kujua bei gani wauze mazao yao kwa sababu vigezo viko pale, siyo hii ya kwenda mmoja mmoja kutafuta. Tujaribu kuingiza mengi kwenye stock exchange, lakini ninachosema ni hivi; mpaka sasa hivi hatujaelewa kama masoko yako kwenye Wizara hii ya Viwanda au yako kwenye Kilimo…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa Kimei, sekunde 30.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa fursa hii ya kuchangia kwenye mjadala huu wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nisichelewe kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais wetu kwa kuweza kuchukua hatua za kimapinduzi katika sekta hii ya elimu ambayo tumekuwa nayo muda mrefu lakini kila wakati tumekuwa tunashangaa kwa nini hatuoni wajasiriamali wakijitokeza, hatuoni watu wakifanya mambo ambayo yametokea maeneo mengine duniani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Naibu wake pamoja na Katibu Mkuu na uongozi mzima wa Wizara hii. Kabla sijasema lolote niseme kwamba niliposoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri nilikuwa nasisimka sana kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo kusema kweli ni ubunifu na ni vitu ambavyo vitahitaji nguvu ya kifedha kutekeleza katika kipindi cha miaka hii inayokuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini nilipoangalia upande wa maduhuli, maduhuli yaliyokusanywa mpaka mwezi Machi, 2023, yalikuwa ni shilingi bilioni 338.2 ambayo ni asilimia 54 ya kilichokuwa kimekadiriwa ambacho ni shilingi bilioni 624.7. Kwa hiyo nikajiuliza kwa nini wakaendelea kuweka maduhuli makubwa hivyo kwa mwaka unaokuja, wameweka shilingi bilioni 667.3, ongezeko kubwa tu, lakini kwa jinsi ambavyo naona maduhuli yamekusanywa mwaka huu naamini hawataweza kufikia level hiyo na pengine wangepunguza hayo maoteo ya maduhuli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye hoja zangu; kwanza ni kweli kwamba tunaona kwamba kuna upungufu wa watumishi katika sekta ya elimu na sekta ya afya pia tunajua tuna upungufu mkubwa sana wa elimu. Lakini kwanza tujue kwamba tatizo siyo kwamba hakuna walimu Tanzania, walimu wapo, tatizo ni bajeti. Bajeti ina ukomo, ina constraints, huwezi kuweka pesa zote mahali pamoja na wakati kuna mahitaji mengi kwenye sekta nyingine za kilimo, maji na kadhalika na kote kunahitaji fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo bajeti ina ukomo na kwa sababu Serikali haiwezi kusema tunaajiri leo kila mtu anayetaka walimu 200 au 300 wapate. Kwa hiyo mimi na- sympathize sana na uongozi wa Serikali, kwamba tumeji- overstretch sana, tumejiongeza sana kwa kuingiza concept ya universal primary education na universal health care, siyo kitu ambacho hakina gharama, gharama zake ni kubwa. Nchi nyingi zilizoendelea hazijaweza kufanya mambo haya makubwa ambayo Serikali yetu inafanya, ndiyo sababu kweli tunatakiwa tuipongeze tumeji-overstrain lakini bado tunaendelea na ndiyo tunajikongoja hivyohivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuangalie kwa mfano katika upungufu wa walimu, mimi nafikiri kwamba tujiongeze zaidi. Kwanza kuna tatizo moja la kwamba walimu wale walio mtaani bado hawajapata uzoefu. Sasa kwa sababu hiyo mimi nina-suggest kwamba wale ambao wanatakiwa wastaafu kwa miaka 60 tuongeze kidogo ule muda wao wa kustaafu hata wakifika 65, lakini wale wana uzoefu na tukiwa- refresh kidogo wanaweza wakaendelea kufundisha, hasa yale masomo ambayo ni magumu kidogo kufundisha kama masomo ya sayansi, hesabu na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hiyo, hatukujifunza wakati wa Covid watu walijifunza namna gani? walitumia artificial intelligence. Mahakama imeweza kutengeneza mfumo ambao unatafsiri Kiswahili kwenda Kiingereza hapo kwa papo. Kwa hiyo, wakitoa ile hukumu ya Kiingereza na ya Kiswahili inatoka hapohapo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo kuna mambo mengi yametokea duniani jamani, huku tunakoenda kweli ni kutumia teknolojia kufundisha, siyo lazima kuwe na mtu asimame pale. Kutakuwa na robot anafanya hesabu zake, kutakuwa na mtu mmoja anaangalia tu vizuri watu wamekaa wanasikiliza na baadaye kusaidia ku-interact. Otherwise mimi naamini katika miaka mitano inayokuja mtashangaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, artificial intelligence inakwenda mbali sana na internet inakwenda mbali sana. Kwa hiyo, hakuna sababu ya kujibana sana, tujue kwamba kuna uwezekano wa kupunguza gharama za uendeshaji, siyo tu kwenye elimu lakini pia kwenye afya kwa kutumia mifumo hii ambayo inajitokeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwamba Serikali pia imeona umuhimu wa kutia mkazo kwenye shule za awali, shule za awali mnajua hazikuwepo, zilikuwepo za kudanganya danganya hizi za private na nini, lakini shule za awali proper hazikuwepo na ninashukuru sana Wizara imeweza kutupa shule moja ya mfano pale kwenye Kata ya Kahe Magharibi kule Vunjo, lakini ukiangalia ile shule ilivyowekwa ni shule ambayo kweli watoto wengine wakienda wanaona wivu kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, je, kuna mkakati gani sasa wa Serikali kuhakikisha kwamba kwenye kila shule ambayo ni ya msingi kuna shule ya awali ya kuanzia wale wadogo ili kuweza kutekeleza sasa huo mkakati ambao pia watu wengi wanasisitiza kwamba uelewa wa mtoto unakuzwa kuanzia akiwa na miaka miwili au mitatu, siyo miaka mitano halafu hatajua kitu kabisa. Naomba hilo liangalie kwa sababu ni jambo ambalo ni la msingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na hiyo, kutekeleza hii mitaala mipya siyo kitu cha kufanya kwa siku moja, ni kitu ambacho kitahitaji muda wa mpito. Hatuwezi kusema mwaka huu tunaanza, hapana, hakitakwenda. Kwa sababu tunahitaji kuwaandaa hawa walimu na kuwa reskill na kuwa retune hawa walimu ambao tunao. Kwa sababu lazima tuwape nyenzo mpya za kufanyia kazi. Lazima tuwape elimu mpya namna gani kwa mfano mtoto mdogo unaanza naye, waangalie kipindi cha Ubongo Kids, mimi naangalia kipindi mpaka nashangaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, yule mtu anayetengeneza Kipindi cha Ubongo Kids ambacho kipo kwenye runinga nyingi za hapa kwetu, utaona kitu gani wanafanya, unaona wanafundisha watoto mpaka unashangaa unasema hata mtoto wangu akipita hapa akiangalia ataelewa maana ya utu ni nini na wanauliza maswali, na hiyo issue ya continuous assessment unaona kabisa pale inafanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninashukuru sana kwamba pamoja na hiyo nafikiri Serikali iangalie namna gani itaingiza kipindi hiki cha mpito kabla haijaanza kutekeleza.
Maandalizi gani, tunahitaji bajeti kubwa, hii bajeti waliyonayo Wizara hii ni ndogo kwa kipindi hiki ambacho tunakwenda. Kwa hiyo naamini kwamba watapata nyongeza zaidi ili waweze kujiandaa na waandae walimu na kadhalika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la VETA. Wanasema wanajenga vituo vya VETA kwenye Wilaya. Wilaya yetu ina Jimbo moja Moshi Municipal halafu ina Halmashauri ya Moshi Vijijini ambayo ina Majimbo mawili. Sasa unaposema unatoa VETA moja inaenda pale Mjini Moshi basi. Kwa hiyo yale Majimbo mengine hayana kituo cha VETA ni makubwa watu chungu nzima. Unajua mtu anakwenda kusoma VETA ukamwambia achukue transport kila siku aende Mjini kusoma inakuwa vigumu sana, gharama zinakuwa kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi naomba tuangalie upya, kwamba pale ambako una Majimbo matatu au mawili kwenye Wilaya basi tuangalie namna gani tuta- allocate hivyo vituo vya VETA ili viweze kunufaisha watu. Hakuna sababu ya kuwa na kituo cha VETA ambacho kukifikia yule mwanafunzi lazima atumie shilingi 5,000, itakuwa ni kazi ngumu, kama kule kwangu ni vigumu sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo namuomba Mheshimiwa Waziri aangalie hilo suala ili aweze kuona kwamba kweli wasituwekee kila kitu pale Mjini, Mimi sichukii kuwekwa Mjini lakini ukweli ni kwamba nataka tujue kwamba distribution spatially itakuwaje, in terms of spatial benefits.
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu nashangaa tunavyozungumza ufundi stadi. Hivi hakuna vyuo vya kilimo? Kwa nini hatuna vyuo vya kilimo vile ambavyo tunachukua kwenye hii kada ya kati? Kama vipo, ni vichache. Watu watajifunza saa ngapi? Au kilimo hatujifunzi? Au tutajifunzia huko huko tulikozaliwa? Sasa hivi kimekuja kilimo cha umwagiliaji, kilimo ambacho ni chenye tija, kinaendeshwa na watu wanaofundishwa na wakajua faida zake nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini kwamba tunapozungumzia Vyuo vya VETA, tujaribu kuweka vyuo vya kufundisha kilimo kwenye ngazi ya chini kabisa kuanzia hata darasa la saba au hata kuanzia darasa la tano kwenda juu huko, na wale wanaobobea zaidi wanakuwa ndio wataalam, mabwana shamba na kadhalika, tunawapeleka, lakini usitaje tu vituo hivyo. Tena vinahitaji hela sana hivyo vya VETA. Hivi vya kilimo hata havihitaji nyenzo nyingi sana, ni vitu vichache. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme tu kingine kwamba pengine kwenye suala zima la bajeti hii niliangalia kwamba, pengine ili kuleta tija kwenye elimu, walimu kuendelea kuripoti kwa TAMISEMI au kusimamiwa na TAMISEMI, naona hiyo, kwanza unapoteza kabisa mwelekeo wa walimu hapa. Ila kama wenzangu walivyosema, walimu kusema kweli ingefaa waangaliwe na wawe graded na Wizara ya Elimu, wasibakie tu kwenye sera lakini walimu wawe pale kwa sababu tutajua jinsi ya kuwafundisha na kadharika nakadharika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa fursa hii ya kuchangia kwenye mjadala huu ambao ni muhimu sana kwasababu ya jukumu la Wizara hii katika kuendeleza nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Profesa Ndalichako, na Naibu wake pamoja na uongozi mzima wa Wizara kwa kazi nzuri kwenye mazingira ambayo ni magumu na kwenye changamoto nyingi.
Mheshimiwa Spika, kwasababu uchumi wowote unapobadilika haraka sana sekta ya elimu inatakiwa na yenyewe iweze kujibadilisha na kuwa bunifu ili iweze kutengeneza wahitimu ambao wanakidhi mahitaji ya wakati huo. Sasa tukiangalia na tukijaribu kufikiria kwamba tuko wapi na tunakwenda wapi katika dunia hii, utajikuta kwamba sekta hii inatakiwa ibadilike sana kwa namna ambavyo tunakwenda mbele.
Mheshimiwa Spika, sekta ya viwanda ilivyobadilika, industrial revolution ilivyoingia, tija kwenye kilimo iliongezeka sana na hivyo bei za vyakula zikashuka kwa hiyo faida kwenye kilimo ikashuka pia. Kwa hiyo, watu wakaamua kukimbilia mijini wakapata kazi kwasababu viwanda vile vilikuwa vinazalisha ajira.
Mheshimiwa Spika, lakini sasa hivi viwanda havizalishi ajira. Bahati mbaya ukienda kiwanda chochote kikubwa utakuta kwamba robots wame-automate na artificial intelligence utakuta kwamba pengine ma-robot yanafanya kazi. Hata kule kwenye mabenki yetu sasa hivi unakuta kwamba watu hawaajiri, walikuwa wanaajiri watu 400 sasa hivi hawaajiri kwasababu tunatumia sim banking na vitu kama hivyo ambavyo vina-replace employment ya watu.
Mheshimiwa Spika, sasa tunapokwenda hii karne siyo ya viwanda ambavyo ni labor intensive, ni kadri sasa ya TEHAMA na hii TEHAMA inatupeleka mbali sana tukijifikiria vizuri. Tukijifikiria vizuri tutafanya mambo mengine na ni kweli kwamba vyuo hivi ambavyo tumekuwa tunazungumza toka asubuhi kwamba tuviboreshe, tufanye hiki na kile, tukichunguza vyuo hivi vya ufundi vya kuwasaidia vijana wetu wapate maarifa na ujuzi waweze kutenda kazi na waweze kujiajiri.
Mheshimiwa Spika, pengine kwanza havifai kwenye karne hii, havina karakana na vifaa vya kufundishia vitu ambavyo vinahitajika kwenye uchumi wa kisasa, kwenye uchumi huu ambao sasa hivi ndiyo tunakwenda. Na mtu akisema kwamba hatujui tunakokwenda ni mtu ambaye haoni kwasababu ukweli ni kwamba tunakokwenda ni tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sekta zinazozalisha ajira ni sekta za huduma; mawasiliano, kwa sekta kama za usafiri, uchukuzi, afya itazalisha utalii, itazalisha utawala, sales and marketing, lakini ukiangalia upande huu wa viwanda hawatazalisha kwasababu automation imefika mbali sana na tija imekwenda mbali sana.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwamba tunapoangalia hivi vyuo kuvipa uwezo lazima na walimu wale wapite kwenye mafunzo tofauti na waweze ku-identify ni kitu gani ambacho watafundisha ili tuweze kuwasaidia watu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kitu ambacho nakiona ni kwamba vyuo vilivyo kila kata kuna vyuo. Sasa vyuo hivi usipofanya vikawa-specialized hutaweza kuvi-equip na vile vitu ambavyo vinahitajika; hutaweza. Kwa hiyo, lazima viwe specialized na vitangazwe kwa wananchi wajue kwamba nikienda Bukoba ntapata chuo ambacho kinatengeneza watu wanaojifunza kutengeneza simu, au nikienda Lindi kule ntapata watu ambao wanaweza wakatengeneza au kuhudumia mashine za oil and gas, and so forth. Kwa hiyo, ni lazima tuvifanye viwe specialized kidogo angalau kuwe na specialization kidogo ili tujue ni vipi na viko wapi.
Mheshimiwa Spika, lakini nikihesabu kule kwangu kuna Vyuo viwili; Mshiri na kingine kiko kule Mwika, hakina hata walimu, hata hao ambao tunasema kwamba ni wa kale ambao sidhani kama wanaweza waka-cope na skills zinazohitajika, bado hawapo hata hao walimu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nataka niombe kwamba pengine, kwanza hiyo kanzidata ya walimu wa vyuo hivi vya ufundi na stadi mbalimbali ijulikane ili waweze kuwa allocated properly. Hayo majengo ambayo yamekaa idle hayaendeshi kozi zozote kwasababu ya kukosa walimu yaweze kutumika lakini cha msingi ni kwamba wapate training, wapelekwe hata nje.
Mheshimiwa Spika, hata tukikaribisha Wachina na Wahindi wakaja wakatuonesha wao wanafanyaje na wanakwendaje kwasababu nchi nyingi sasa zinajikita kwenye upande wa training ya mambo haya ya hudua na kutengeneza vitu vya kisasa, siyo kutengeneza magari ya, hata magari manual siku hizi hakuna kabisa.
Mheshimiwa Spika, sasa niseme hivi; kwasababu watu wa ku-train ni wengi sana hebu tufikirie wazo moja. Kwa mfano tunasema mambo ya soft skills hizi za watu kuwa na tabia ya kuweza kujituma, kuweza kuheshimu kazi na kadhalika, zinapatikana zaidi kule JKT.
Mheshimiwa Spika, ukienda JKU sasa hivi ukaweza kupiga mark time pale vizuri halafu jioni ukafundishwa skills zozote hizi ambazo tutakuwa tumesema Ruvu wafundishe hiki na hiki, ukifundishwa hivyo ukimaliza pale baada ya miezi mitatu au sita unakwenda unaajiriwa na utakuwa na heshima na utakuwa mwaminifu na utafanya kazi vizuri kwasababu umejifunza discipline na skills kwa namna ambayo itasaidia sana watu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi nafikiri hiyo ndiyo njia ambayo inaweza ikafanya kwa haraka sana watu ambao wanamaliza form six, hata wanaomaliza university wanaambiwa piteni kule mtapata skills kwa ujumla kwa haraka zaidi na kule kuna vifaa vya kufanyia majaribio na kadhalika. Kwa hiyo, hicho ni kitu ambacho mimi nafikiri kingekuwa cha msingi.
Mheshimiwa Spika, lakini pia niseme kwamba tukizingatia kwamba kuna haja ya kuwa wabunifu kwenye hii nyanja ya TEHAMA, kuna haja ya vyuo vyetu hivi vikuu sasa hivi viwe na vitengo. Kila chuo at least kiwe na kitengo cha incubation ambapo mtu akiwa na wazo lake anakwenda kwenye kitivo au kitengo kile cha chuo kikuu, wanamsaidia kuboresha na kumuonesha namna gani anaweza aka-implement.
Mheshimiwa Spika, wanaweza wakamuonesha pia kwamba pengine mashine za namna hii zinapatikana TEMDO, zinapatikana wapi, hebu tukusaidie, wanamsaidia kina-take off wanamuachia anaendelea na watu wataajiriwa wengi.
Mheshimiwa Spika, lakini kwa namna hii ambayo tunaona naona kuna shida sana; ijasiriamali haufundishwi darasani, unafundishwa kwenye field. Mtu kama umemaliza kama usipopata on job training hutaweza. Sasa hivi vyuo vina watu, walimu wako wengi ambao wana-retire, maprofesa wana-retire, wajasiriamali wengi nao wana-retire.
Mheshimiwa Spika, kwa nini tusiwapeleke tukawaombe waanzishe hivi vitengo ili watu waweze kupata skills zao wakajifunza. Kuna mmoja alisema kwa nini akina Dewji hawaandiki vitabu. Watu wamejifunza kutoka kwa akina Dewji waka-implement mambo ambayo yataleta tija katika nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, nafikiri kwamba kule kwenye jimbo letu, na nitafurahi sana kama kweli tutaweza kupata specialization ya mambo ya…
SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kimei, muda hauko upande wako.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
SPIKA: Nakushukuru sana, ahsante sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, naunga mkono hoja kwa asilimia 100; ahsante. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, napongeza dhana ya Serikali ya kuhamasisha utafiti. Hata hivyo kuna taasisi za utafiti ambazo hazipati fedha yoyote kutoka Serikalini na kuishia kuwa tegemezi kwa wahisani. Mojawapo ya taasisi hizo ni REPOA ambayo ni kati ya top ten research instructions Barani Afrika.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona. Nami nianze kwa kumpongeza Waziri mpendwa, Mheshimiwa Dkt. Ndugulile kwa kuweza kuwasilisha hotuba yake vizuri, hotuba nzuri iliyosheheni ubunifu mkubwa na ninaamini kwamba atakwenda kutekeleza kama walivyoainisha kwenye bajeti hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba tunamshukuru Waziri kwa sababu ni mtu mnyenyekevu sana. Mimi toka nije hapa Bungeni sijaona Waziri amenifuata akaniambia pale kwako vipi mambo? Kwenye mambo ya mawasiliano yako sawa? Sijaona. Sijaona mwingine aliyenifuata akaniambia vipi maji? Sijaona; lakini yeye ameweza kuja kwetu na kutuuliza kwamba vipi tunaonaje mambo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru kwa kuamini kwamba zile Kata zetu za Kirua Vunjo, Marangu, Mwika na Makuyuni ambapo pia tuko mpakani, lakini zaidi ni kwamba vijiji vingi vimepakana na Mlima Kilimanjaro na msitu. Kwa hiyo, kule mawasiliano yanakuwa ni vigumu sana. Naamini tutatafuta mbinu ya kupeleka minara au kupeleka njia nyingine za mawasiliano kwa hawa watu walio kule kwenye mpaka na kwenye vijiji ambavyo kusema kweli hawapati mawasiliano sasa hivi na kidogo wanayopata ni ya Kenya, hata kama ni redio pia zinapatikana za Kenya na siyo sehemu nyingine. Kwa hiyo, nataka niwaombe watekeleze hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimeamua kukazia mambo machache. Natumai yanaweza yakawa yamezungumzwa, issue ni kwamba ni lini tutaweza kufungamanisha mifumo yetu ya utambulisho wa wananchi? Utambulisho wa wananchi umekuwa ni tatizo kubwa. Ukitaka kwenda kwenye Passport unaambiwa jaza fomu zile zile ambazo unajaza unapokwenda NIDA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mahali utakapokwenda utajaza; hospitali utajaza, utarudia na bado una kitambulisho chako cha NIDA, lakini bado ukienda hospitali hawawezi kutumia kile kitambulisho waka-access zile data kwa sababu ile database inaonekana kwamba bado haijafungamanishwa ili iweze kuwa accessed na wadau wote wanaotaka kupata taarifa za mwananchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kufungamanisha huko pia kunawezesha kabisa hata kuongeza usalama kwa sababu ukweli ni kwamba mtu anapofanya makosa; na kama anajua kwamba namba ya NIDA aliyonayo, yale makosa yataandikishwa kule, basi anakuwa na uwoga zaidi kwa sababu inakuwa ni rahisi kumfuatilia mtu makosa aliyofanya na mazuri aliyofanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na inakuwa ni rahisi sana hata kwa mabenki kuweza kumfahamu huyu mtu ni wa namna gani wanaku-access katika database ile ambayo itakuwa imefungamanishwa kwa watu wote, iwe ni simu na kila kitu kitakuwa kule. Naamini kwamba kwa zile reference bureau nazo zitaingiza database yao huko. Kwa hiyo, tutakuwa tunaweza kufanya mambo kama hayo. Nchi zote zilizoendelea zinafanya hivyo, mtu anakuwa na namba moja, hawi na namba mbili, na ninaamini kwamba kitambulisho kinakuwa ni kimoja siyo viwili ili mtu yule aweze kutambulika kila mahali anapokwenda na saa yoyote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kwamba sekta ya TEHAMA ndiyo inayokuwa kwa kasi zaidi sasa. Sasa tumeunda Wizara ya Teknolojia na TEHAMA kwa ujumla. Nataka niseme hivi, fursa zilizopo ni nyingi sana, nchi nyingine zimeamua kufanya kwamba TEHAMA ndiyo sekta ya muhimu kuliko zote; nchi kama Rwanda mnafahamu. Nia yake ni nini? Ni kwa sababu wako vijana wengi wanapokwenda shule na kwenye vyuo wanajiunga kwenye hii fani, lakini kuwatumia inakuwa vigumu. Kwa sababu hakuna mitandao inayofanya kazi vizuri kwenye maeneo yale ambayo vijana hao wanamalizia shule zao. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tuna mkonga, kwa nini hatuwezi kuwezesha Wifi ikapatikana kwenye maeneo mengi tu hata kwa bure? Nami nakubaliana na mwenzangu aliyesema kwamba TTCL ikiwezeshwa ikatumia mkonga huu ikawekeza vizuri kwenye maeneo mengi ya vijijini, siyo mijini tu, vijijini zaidi kwa sababu kuna fursa. Sasa hebu niulize kwa mfano, masoko sasa hivi hayatafutwi kwa mtu kusafiri kwenda kuangalia soko, mtu anatumia simu, hii simu imekuwa ni ofisi, huhitaji ofisi yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilikuwa nawaambia wapigakura wangu kwamba hii simu ni ofisi yenu, huna haja ya kwenda kutafuta mnunuzi wa ndizi Dar es Salaam wakati unaweza ukapiga ndizi yako picha ukaituma kwa rafiki yako Dar es Salaam akakwambia nitumie kwa shilingi fulani, umeshafanya biashara. Kwa hiyo, biashara unaweza ukaifanya kwa kutumia tu kiganja chako na uwe na simu, lakini iwe janja kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka niombe hiyo kwamba kweli tufanye hivyo. Pia Wizara ione namna ya kutoa mafunzo kwenye vyombo vya Habari; kwenye TV na kwenye redio, kueleza watu ni fursa zipi zinafunguliwa kwa kuwa na uwezo wa kuwasiliana nchi nzima na nchi za jirani, hata dunia nzima inawasiliana na hii simu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, vile vile lazima gharama zipunguzwe. Sasa tutapunguzaje gharama? Nafikiri kwamba tunavyozidi kuongeza mtandao, hasa huu wa TTCL; na tunaamini kwamba wataweza kuleta ushindani ambao utalazimisha wale wengine ambao wanafanya tu biashara waweze kushusha bei zao, lakini ni lazima TTCL ifanye kazi kwa nguvu zaidi. Kwa hiyo, naomba kwamba kuwepo na hivyo vipindi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Mheshimiwa alizungumzia kuhusu technology hub. Tuna COSTECH, imeweza kuanzisha incubation centers na hizo incubation centers ndiyo zinachukua na zinashindanisha; unaweza ukatangaza kwamba watu wenye uwezo hasa wale waliosoma IT, ambao wana ubunifu wowote wa teknolojia, waweze kufikisha pale. Hiyo ndiyo njia ambayo itaweza kuwaajiri hawa vijana na pia ku…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante Mheshimiwa Dkt. Kimei kwa mchango mzuri.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa fursa hii na mimi nianze kwa kutoa pongezi na shukrani nyingi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wetu. Kipekee nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha pamoja na viongozi wake kwenye Wizara hii tusimsahau Gavana wa Benki Kuu kwa kazi nzuri ambayo wamefanya na kutuonesha kwamba inawezekana mahali popote kufikia au kuendeleza uchumi wa jumla ambao ni tulivu ukiwa na inflation iliyo ndogo.
Mheshimiwa Spika, kabla sijasema machache kuhusu hii bajeti ambayo nasema ni bajeti nzuri kulinganisha na bajeti nyingine ambazo nimesoma, niseme kidogo kuhusu mambo ya jimboni kwa sababu wananchi wa Vunjo wamesema hawajanisikia.
Mheshimiwa Spika, kwa kuanza niseme kwamba nashukuru kwamba Serikali imeweza kuendelea kuipa TARURA fedha ya kutosha kiasi na kwa hivyo TARURA inakuwa imeendeleza kujenga na kukarabati barabara kule vijijini kwetu.
Mheshimiwa Spika, pia nawashukuru kipekee kwamba TARURA wamesikia agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwamba waweze kujenga barabara ya Himo sokoni kwenda Makuyuni na Rotima kwa kiwango cha lami, na wameanza kuijenga lakini nawakumbusha kwamba Mheshimiwa aliagiza ipate kilometa 7.4 wasije wakaishia mita 800 ambazo naona wanakazana nazo sasa hivi, naamini watafikisha kama ilivyokuwa.
Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine tumeweza kuwasilisha kupitia Bodi ya Barabara ya Kilimanjaro, Mwenyekiti wetu amewasilisha maombi kwa Wizara ya Ujenzi waweze kupandisha hadhi barabara tatu; barabara ya kwanza ni ile ya Pofo - Kilema - Mandaka ambayo tayari wanaanza kuiweka lami, lakini kuna Uchira – Kisomachi – Kolarie; na Chekereni - Kahe hadi TPC hizo ni barabara ambazo tumeziombea sasa zipandishwe hadhi ziwe ni barabara za kimkoa, kwa hiyo, ziweze kuhudumiwa na TANROADS. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naamini kwamba sasa kwa sababu kwenye ile bajeti ya Wizara hii zaidi ya shilingi trilioni 3.7 wanaweza pia na sisi tukapata kidogo wakapokea barabara mojawapo na sisi tukapata kidogo. Hatukupata fedha yoyote au mradi wowote kwenye Wizara hii katika bajeti inayokuja.
Kwa upande wa vituo vya afya, tulishukuru pia kwamba Serikali imeweza kutupa Kituo cha Marangu Head Quarter ambacho tulipewa shilingi milioni 500 na kama kinakamilika isipokuwa kuna jengo la maternity na theater ambalo halitaweza kukamilika kwa fedha hizi. Tunaomba TAMISEMI waweze kuona namna gani wataongeza fedha hiyo, siyo nyingi sana itahitajika shilingi milioni 50 tu kuweza kukamilisha hilo.
Mheshimiwa Spika, tunaomba pia kwamba Serikali iweze kutuletea vifaa tiba ili waweze kuanza kazi kwenye kituo hiki ambacho kiko karibu sana na wananchi wengi. Pia tunaomba kituo kile cha Koresa ambacho tumeahidiwa na Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI aliyekuwepo basi nacho kianze kujengwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa maji nilizungumza hapa kwamba Mheshimiwa Waziri atakuja, Naibu Waziri atakuja kule ili tuweze kuhakikisha kwamba ile miradi ambayo ipo kwenye Kata zile za Mwika Kusini na Kaskazini, Mamba Kusini na Kaskazini, Marangu Mashariki na Magharibi na Kilema kwamba kazi yenyewe ziwe zinakamilisha kwa sababu ilikuwa iwe mwaka mmoja, lakini sasa imechukua miaka mitatu bado hatujamaliza.
Mheshimiwa Spika, kwenye upande wa elimu; tuna shule tatu tu ambazo zimepewa kidato cha tano na sita. Sasa hiyo ni changamoto kwa sababu tuna shule za sekondari ya kawaida ni 32 na ushee, kwa hiyo, tunaomba kwamba sasa na hasa tukizingatia hii mitaala mpya inayoingia na mfumo mpya wa elimu tunaokuja ku–adopt basi waanze kupandisha hadhi baadhi ya shule hizi za kawaida hususani shule kwa mfano ile shule ya Mboni, kuna shule ya Kokirie, kuna shule kule Marangu na kadhalika. Tunaomba kwamba sasa tuanze mchakato wa kuainisha ili zianze kupandishwa hadhi kupata kidato cha tano na cha sita.
Mheshimiwa Spika, mwisho niseme kwamba nije sasa kwenye upande wa bajeti hii ambayo nimesema ni bajeti ambayo kwa ujumla inavutia kwa sababu gani? Kuna wakati nilisimama hapa mwaka 2022 ile bajeti tulivyokuwa tunapitisha, kwa hivyo, ile bajeti ilikuwa contractionary kwamba isiwe bajeti ya kuchochea uchumi, kwa sababu wakati ule kusema ukweli kuwa na nakisi ya bajeti ambayo ina asilimia tatu ya pato la Taifa, ilikuwa hairuhusu ina maana Serikali haikuona kwamba kuna uwezekano wa kukopa zaidi na kwenye soko la ndani wakati ule ambapo hata sekta binafsi ilikuwa haikopi, haihitaji kukopa kwa sababu mazingira yalikuwa hayaruhusu sana kufanya biashara yenye tija.
Kwa hiyo, wakati ule ilikuwa ni wakati ambao ilikuwa inatarajia kwamba Serikali itakuwa na nakisi kubwa zaidi iweze kukopa zaidi na iweze kuchochea uchumi wakati ule private sector ikiwa inaogopa risks zilizokuwepo.
Mheshimiwa Spika, lakini na pia kwa wakati ule naona huko kulikuwa hali hata riba zilikuwa ziko juu, lakini siyo Serikali hazikuweza kufanya chochote kwa upande ule. Lakini nilisema kwamba ni contraction lakini mwaka huu tunaona pia kwamba ni contraction kwa sababu nakisi kwa uwezo wa pato la Taifa iko 2.7 lakini wakati ule ni wakati wake kabisa na mimi napongeza hayo maamuzi kwamba tujaribu kupunguza matumizi na ukopaji kwa sababu hatuna uwezo sasa hivi kuna cons trait mbili, cons trait ya kwanza sasa hivi ndiyo kubwa zaidi ni hii nakisi kwenye malipo ya nje pamoja na upungufu wa dola. Sasa hiyo ndiyo inatubana kwa sababu unaweza ukawa na miradi mikubwa, lakini mwisho wa ukomo wako utaishia kwenye kuomba fedha za kigeni unazo, na kama huna utalazimika kuishia hapo.
Mheshimiwa Spika, nashukuru kwamba hapa wamesema pia wanakopa, wamepunguza maoteo ya kukopa nje kwa masharti ya biashara. Lakini utaona kwamba mimi naamini kwamba tunapoendelea kutekeleza hii bajeti utakuta kwamba tutalazimika kukopa zaidi kwa sababu tukiongeza miradi hii ambayo tunayo hatutaweza kutokulazimika kukopa zaidi nje ili tuweze kupata dola ambazo zitatusaidia kuendeleza hii miradi ambayo yenye uwezo ambayo tunaenda nayo.
Mheshimiwa Spika, mimi napongeza pia kwamba Serikali pamoja na Benki Kuu wameweza kushikilia kweli sera zao za kifedha na kibajeti na kuhakikisha kwamba uchumi wetu umebakia tulivu, inflations ni 4.3 katika mazingira ambayo ni magumu sana. Japokuwa bado naamini kwamba bado riba haziendani na hii inflation ndogo ya kiasi hiki ambayo imekaa kwa muda mrefu. Mimi naamini bado riba tuna kazi ya kufanya pale. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napongeza pia hii ukamilishaji wa tathimini na ukopeshakaji wa nchi yetu; fitch ratings wakatupa B2 plus na ile watakupa B+ ambayo ni nzuri (rate nzuri sana) kwa nchi ambayo inaendelea kama ya kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, napongeza pia kwamba hiyo nisiseme, lakini nisemi hivi kuna jambo moja ambalo ninataka nishauri ili kuongeza mapato yetu na kupunguza ruzuku tunazotoa kutokana na mapato madogo, mimi nafikiri kwamba kwamba kwa upande kwa mfano wa mafuta, mafuta yanashuka bei petrol na diesel zinashuka bei, mimi nafikiri kwamba tungekuwa na threshold tukisema ikizidi 3,000 tutatoa ruzuku, tunaingiza kwenye mfuko wa ku–standardize bei za mafuta siyo Serikali iingie tena kwenye bajeti yake kutoa ruzuku tutengeneze huo mfuko kutokana na hii fluctuation’s ikishuka, ikizidi 3,000 tuwape ruzuku, ikishuka tuendelee kuchukua kwa muda kiasi halafu tuone inaendelea kushuka basi tunaji–adjust na sisi chini hivyo hivyo, hiyo ndiyo njia pekee ya kuweza kuwa na ruzuku ya mafuta ambayo itasaidia uchumi wetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia kwamba kuna tatizo la takwimu hizi za ukuaji wa uchumi ni ukuaji wetu wa uchumi. Ukiangalia figure tulizonazo kwenye bajeti, kitabu cha bajeti uchumi wetu GDP ilikuwa kutoka trilioni 169.8 mwaka 2021/2022 ikafika trilioni 188.6 mwaka 2022/2023. Kwa hiyo, ina maana kuna ukweli wa asilimia 11 kwa bei ya miaka husika. Sasa kama ni bei ya miaka husika kama inflation ni four percent ina maana tofauti ya bei za soko ya mwaka husika na constant price inakuwa sana sana ni hiyo ya inflation ile unatoa.
Kwa hiyo, inatakiwa iwe kwamba kama ni 11.1 percent ukitoa hapo 4.3 percent unabakiwa na almost 7 percent ya real growth hasa inawezekana kwamba kuna mahali ambapo tuna-miss kidogo huo ukuaji na ukiangalia kwa dola, dola ni fedha ambayo haina inflation, inflation yake ndogo sana ile sasa hivi ni kubwa, lakini imekuwa pia kuchukua kwa dola tulizonazo, dola zilikuwa ni bilioni 77.6 iliyo pato letu hasa ikapanda mpaka bilioni 85.3 ambayo ni ukuaji wa eleven; ten percent kwa maana ya miaka hiyo miwili.
Mheshimiwa Spika, kwa nini iwe kwamba tunapokuja kwenye shilingi ni 4.3 percent au and around five percent? Sasa five percent utakuta ni chini sana kutokana na kwamba nchi nyingine average ya East Africa ni 6.3 percent.
Kwa hiyo, mimi nataka kusema kwamba tuangalie hizi takwimu zetu na kuna mahali kumejificha kitu hakijulikani na kwa nini nakubali kwamba inawezekana hivyo? Hakuna ambacho tulikuwa tunafanya miaka ile ya nyuma kabla ya mwaka 2019 na ambacho hatufanyi sasa hivi tunafanya tena zaidi, kwa nini sasa uchumi utasema bado unakuwa kwa asilimia tano? Mimi nafikiri tuangalie kuna kitu ambacho hakiendi sawa sawa na ningemuomba hapa Waziri wa Fedha kupitia Ofisi ya Takwimu aweze kuangalia na kuona atafanya namna gani.
Mheshimiwa Spika, lakini pamoja na hiyo nilijaribu kwenye swali moja nilitaka kuuliza asubuhi wakati…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa sekunde 30, kengele ya pili imeshagonga.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Nishati
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuniona na kunipa fursa hii, nitazungumza machache na nitaomba nisitoe pongezi kwanza nimalize kwanza kwa sababu muda wangu ni mfupi na mimi nina mambo mengi ya kusema, lakini nitakuwa nakosa fadhila nisipoanza kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu ambaye wote tunasema tunampenda sana, lakini sisi Wanavunjo tunampenda zaidi kwasababu tumeona miradi mingi imekuja pamoja na kwamba mradi wa ujazilizi (densification) ya umeme ulikuja kuzinduliwa pale kwetu kwenye Kijiji cha Nganjoni na ninashukuru sana ni jambo la kumshukuru Mungu sana kwa sababu kwa muda mrefu kule Vunjo tulikuwa hatujaona miradi kama hii chini ya Awamu ya Sita namshukuru sana pia Waziri anayehusika Mheshimiwa Makamba na uongozi mzima wa Wizara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pamoja na kwamba tulifaidika na tulikuwa na bahati ya kuzinduliwa mradi wa densification, lakini ule mradi haukuendelezwa, naona umeanzia pale kwenye Kijiji cha Nganjoni kwenye Jimbo letu, lakini naona haujaendelezwa sana, lakini pia kuna tatizo kubwa sana na ambalo tumeambiwa na tunamshukuru Waziri ametuletea watendaji wetu kwenye mabanda tukazungumza nao wakasema kwamba sasa fedha zimepatikana za kuweza kuwaunganisha wananchi wetu ambao tayari wameshalipia kufungiwa umeme kwa miaka zaidi ya mitatu, lakini hawajafungiwa wananchi zaidi ya 2,500 kwa Wilaya yetu ya Moshi Vijijini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini tumeambiwa kwamba fedha inapatikana na mpango upo sasa na vifaa vipo, kwa hiyo, wataanza kufanya hiyo kazi na ninaamini kwamba wakati huo hawadanganyi na ninaamini kwamba Waziri tuliye naye ni makini, ataweza sasa kutuhakikishia kwamba hii kazi itafanyika kwa sababu kusema kweli ni kazi ambayo inaendana na kipaumbele chake cha kwanza japokuwa ninaamini kwamba vipaumbele hivi viliorodheshwa vya kwanza mpaka kumi na viwili sio kwa umuhimu wake kwamba vyote vitatekelezwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nilipoanza kusoma hotuba ya Mheshimiwa Waziri na naomba nieleze pale alipoishia Mheshimiwa Vita Kawawa jana, nilijiuliza maswali machache; swali la kwanza kwamba je, Wizara inaweza ikatuambia mahitaji au makisio ya mahitaji ya umeme hapa nchini katika kipindi cha miaka mitano kwa uhakika yakoje? Kwa sababu ukiangalie kwa miaka 60 tumekuwa na uzalishaji ambao haujazidi megawati 2,000; uzalishaji ulipo kutokana na kielelezo cha kwanza kwenye hotuba ya Mheshimiwa Waziri ni megawati 1,694 na nimekuja kuangalia matumizi ya kiwango cha juu wanasema kiwango cha juu cha matumizi ni megawati 1,335 na miaka 60 ya uhuru. (Makofi)
Sasa ninapoangalia tukienda na uzalishaji huu ambao tunaambiwa nao unaongezeka kwa kasi tukiweka Kinyerezi Extension megawati 185 tunaweka Rusumo megawati nane, tunaweka Nyerere megawati 2115 tunakuwa tumeshaongeza megawati 2,700; ni karibu mara mbili ya matumizi yetu ya sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini bado kuna mingine, kuna hii ya Ruhudji, Kakono, Rumakali, Malagarasi na kuna Kikonge ukiongeza yote hiyo tunakuja kuwa tunaongeza katika haya matumizi yetu tumeshaongeza megawati 4,205 na ukiweka kwenye hii ambayo tunayo tunafikia megawati 5,899. Je, mahitaji haya tunajua tutayatumia kweli kwa kasi hiyo? Kwa sababu kama tunatumia megawati 1,300 sasa tunakuwa na megawati 5,800 makisio ya matumizi yako hapa huwezi kuongeza kukimbizana na ongezeko la uzalishaji au kupanua uzalishaji bila kuwa na uhakika kwamba utapata wanunuzi wa matumizi kwa sababu ni fedha tunaweka na hii fedha tunayoweka kwenye umeme kwa kasi sana tunataka umeme uwepo wa ziada, lakini sio kwa ziada sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu tunatumia fedha za kukopa kwa kutengeneza miundombinu hii, kwa hiyo lazima twende na kasi ambayo inakubalika, kasi ambayo nayo pia itapunguza ukopaji, kasi ambayo itahimilika. Tukiweka tu for the sake tutakuwa tunajiingiza mahali pabaya, lakini tungeweza kuhakikisha kwamba tunajua vianzio na vianzio vile tunajua deploy quickly na vingine vinachukua muda sana hiyo ni moja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili suala hili la subsidy na suala hili la kuhifadhi/kuweka strategic reserve ya mafuta. Mimi nafikiri hivi tuangalie options za hii kwa sababu unaweza ukaweka akiba kwenye fedha au ukaweka akiba kwenye bidhaa; ukiweka akiba kwenye bidhaa ya mafuta, bidhaa ya mafuta inabadilika badilika bei, kwa hiyo unaweza ukanunua mafuta leo ni dola 100 kwa bulk, lakini baada ya siku chache hizi zinazokuja miezi mitatu ikaja mafuta yakashuka bei yakawa dola 73 kwa bulk, utakuwa umeshapata hasara ya dola 25 kwa bulk.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ungeweza ukanunua option futures option, future options ni kwamba unailipia premium kidogo lakini yule m-supplier atakwambia endapo unahitaji mafuta kwa mwezi unaokuja wa Juni, mwezi unaokuja wa Julai, Septemba, utampa stagged delivers.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kila staggered delivery inategemea ni muda gani unailipia premium yake na ile premium unayolipa ni option kwamba naweza nikanunua au nisinunue. Kama itakuwa bei imeshuka sitanunua kwa ile bei ambayo nimei-hedge kama ikipanda basi nitanunua kwa sababu najua kwamba nimekua nimei-hedge ile bei kwa bei ambayo ni ya leo na bei ya leo ndiyo hii sasa nimeshalipa subsidy na ile subsidy badala ya kuitumia kugawa ingetumika kununua futures options za kuletewa mafuta kwa bei ambayo tunaijua ya leo, hapo utakuwa ume-stabilize. Pia itapanda huna pressure ya kwamba bei itapanda halafu nitanunua kwa sababu umei-hedge na ile gharama ya ku-hedge ni very little ya ile volume ambayo tunaweka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini kwamba tukae chini wale watu ambao wanajua financing na hizi hedging na features tufanye kitu ambacho kinakubalika kitakaa forever na kila wakati TPDC ipate hiyo option ya formular inanua mafuta kwa bei ambazo zinajulikana leo lakini kwa ku-deliver in the feature kama ni six months. Kwa sababu kama wewe utanunua tu yaani hivi vitu haviendi tu kiholeholea utapata hasara, tutakuja kupata hasara tuhangaike bure. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili ni kwamba tunapozungumza suala zima la kuzalisha na mimi nakushukuru sana, kipaumbele alichokiweka pale cha uzalishaji na usambazaji. Wanasema hivi, asilimia 78.4 ya Watanzania wamefikiwa na gridi, lakini watu waliounganishwa kwenye gridi ni asilimia 37.7 tu! Wengine hawajaunganishwa na wengine wanaotumia tunasema umeme upo lakini watu wanaotumia solar na tunashukuru Serikali hii tukufu ambayo iliweza kushusha VAT kwenye solar panels, sasa watu asilimia 30 ya Watanzania wanatumia solar! Kwa hiyo, inakuwa about 66 percent ya Watanzania wanapata umeme lakini wengi nusu yao wanapata kwa solar lakini umeme wa solar hauwezi kufanya mambo fulani fulani ya viwanda na nini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba pamoja na hela tulizonazo nyingi hizi tujaribu kuona ni wapi tukimbizane napo ambako ni kusambaza umeme wa gridi ku-stabilize ili kile kiwango tulichonacho kiweze kutumika vizuri kisipotee na kila mtu aweze kupata umeme ule usambazwe ufike kwenye nyumba zetu na kwenye viwanda vidogo vidogo na kwenye maeneo yetu, shuleni na kwenye hospitali. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ikifanyika hivyo sasa tunaanza kuona tija ya hiki tunachozalisha na hicho ambacho kinapangwa kuzalishwa kwa kuongeza tusikimbizane tu tunafuta lakini tunataka ufafanuzi je, mnasema mta-export kama mta-export; je, mna bei za ku-export kweli ambazo mmeshazifungamanisha vizuri mkajua kwamba mtapata faida? Tusije tuka-subsidize kwa wenzetu umeme na sisi tumejenga kwa fedha ya kukopa hiyo ni moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba pengine kitu ambacho kingetakiwa pia tukiangalie ni suala zima la kujua mikakati gani hili suala la stabilization project kwamba je, itatekelezeka kwa muda gani? Kwa sababu fedha ambayo inahitajika sidhani kama imetengwa yote, walisema Bilioni 500 au Milioni 500, naona hata muda wa kuzungumza unaisha lakini ninaunga mkono hoja, naamini kwamba kweli kuna mambo mazuri yanafanyika kwenye Wizara na mimi nampongeza sana Mheshimiwa January kwa yote hayo anayofanya, waendelee kufanya na waendelee kutuletea vitu vizuri, summaries ambazo zimekaa hivi zinasaidia. Ahsante sana. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa na Serikali Kuu, Mashirika ya Umma na Kaguzi za Ufanisi kwa Mwaka wa Fedha uliuoishia tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa kuhusu Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Seriakli za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioishi tarehe 30 Juni, 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezajiwa wa Mitaji ya Umma kuhusu uwekezaji wa mitaji ya umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa fursa hii. Mimi naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi wetu Mkuu kwa mambo mengi anayofanya. Pamoja na kumwaga fedha nyingi kwenye Jimbo langu la Vunjo; papo tu na mimi inabidi nimpe maua ya Vunjo. Lakini zaidi kwa namna ambavyo alichukua hoja zilizoletwa kwake na CAG na akaweza kuzifanyia kazi. Kwa wale wanaofuatilia watajua kwamba Mheshimiwa Rais ameshafanyia kazi hoja nyingi, ikiwemo kubadilisha watendaji kwenye taasisi fulani fulani ambazo zilionekana kwamba zina udhaifu. Pamoja na miongozo mingine ya kutekeleza zile hoja, nampongeza sana kusema kweli.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nampongeza CAG mwenyewe kwa namna ambavyo ameweza kutuletea hoja nzuri na amechambua vizuri hesabu hizi na akatoa ushauri ambao kweli umeweza kuongoza mjadala kwenye Bunge hili kuhusiana na utendaji wa Serikali katika kusimamia fedha za umma.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nawapongeza wanakamati wa PAC, PIC na LAAC kwa kazi nzuri na maazimo mazuri ambayo wameyaleta, na ninasema kwamba mimi nayaunga mkono kwa asilimia 100. Kuna moja tu ambalo sitaliunga mkono sana, kwa sababu lile la taasisi za umma au mashirika ya umma kupeleka asilimia 15 ya mapato yao ghafi Serikalini kabla ya kufanya hesabu kwamba wanapata hasara au faida, hilo mimi nafikiri kwamba linapunguza sana uwezo wa mashirika ya umma yaweze kuendelea kufanya kazi kibiashara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba niwasilishe hoja moja, na nitajikita zaidi kwenye mashirika ya umma. Endapo mashirika ya umma yataendelea kufanya kazi kwa namna tulivyoona kwenye hoja zilizoibuliwa na Mheshimiwa CAG ninaamini kwamba hatutaweza kuwa na uhakika wa prudence of fiscal stability; yaani utulivu wa fedha za kibajeti kwa miaka inayokuja. Kwa sababu issue ni hii; kwenye sheria ya bajeti tunaambiwa kwamba msingi ni mmoja; ni kwamba Serikali ijiendeshe na ijiendeshe kwa fiscal policy yake kwa kuhakikisha kwamba kuna utulivu endelevu kwa vizazi vijavyo; kusije kukawa na madeni yameji-accumulate kila mahali halafu wewe huyajui, huyatambui, halafu yakiibuka hapa unaambiwa ulipe. Kwa sababu hii unakuwa unaingiza bajeti kwenye stress kubwa na hii inakuwa ni fiscal risk kubwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema kwamba, kwanza cha msingi ni lazima tuchukue hatua za kuhakikisha kwamba mashirika ya umma yanabadilika kwa namna yanavyojiendesha. Tumeambiwa kwamba mashirika ya umma yanajiendesha kwa hasara. Hasara iliyofanywa na mashirika 14 yaliyo kwenye ripoti ya CAG kwa mwaka 2020/2021 na 2021/2022 ni shilingi bilioni 217. Hasara ya mashirika 14 tu. Hatujayaweka mashirika mengine yote kwa sababu na yeye ametupa sample tu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kitu cha ajabu. Utaona kwamba kwa mfano, Shirika la ATCL, limefanya hasara ya shilingi bilioni 105, ukijumuisha fedha ya ruzuku ambayo walipewa. Kama wasingalipewa ruzuku ya shilingi bilioni 30.6 wangefanya hasara ya jumla ya bilioni 105 kwa hiyo miaka hiyo miwili, ni fedha nyingi. Ukiangalia Shirika la TRC limefanya hasara ya shilingi bilioni 54, NDC imefanya hasara bilioni 38, ukiangalia Mkulazi Holding imefanya hasara ya bilioni 20, Kilimanjaro Lather bilioni saba. Vyote hivi vinakula ndani either ni ruzuku au wamechukua mkopo au sijui wame-finance namna gani hiyo hasara, lakini ni kwamba inaingiza bajeti yetu kwenye kutokuwa na sustainability ya uhimilivu wake kwa miaka ile inayokuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kinachosikitisha ni kwamba mashirika haya yanayofanya hasara hamna mkakati ambao wamejijengea ya kuweza kujinasua kwenye kufanya hasara hizi, na hawalazimishwi kutengeneza hizo business plan za kuhakikisha kwamba baada ya miaka miwili au mitatu wanajiondoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nafurahi kwamba TTCL walikuja kwetu kwenye Kamati ya Bajeti; wakaonyesha kwamba wamefanya hasara kubwa lakini ndani ya mwaka huu na mwaka ujao watakuwa wamekuwa sustainable. Kule tunaona kwamba Mkurugenzi Mtendaji naye alibadilishwa na Mheshimiwa Rais. Lakini kwa kweli ni tatizo kubwa kwa sababu hatuwezi kujua mbeleni ni wapi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Shirika la ATCL, Mkaguzi Mkuu anasema kwamba ilipata hasara kwa sababu ndege zilikuwa grounded. Mimi Nakasema niseme kwamba kama ndege zisingekuwa grounded basi hasara ya ATCL ingekuwa kubwa zaidi; kwa sababu mashirika mengi ya ndege duniani yamepata hasara kubwa tu. Kwa hiyo, ni kwamba pengine lingepata hasara kubwa zaidi kwa sababu haya mashirika hayako proactive katika ku-adjust to market changes.
Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi niseme hiki, hata nasikitika kwamba kuna kiongozi mmoja alisema kwamba anasikitika kwamba alibinafsishwa. Lakini kama asingebinafsisha tungekuwa wapi kama mashirika ndiyo yanajiendesha hivi? TANOIL tumesikia imefanya hasara ya bilioni saba. Kwa hiyo, takribani kila shirika ambalo linajiendesha kwa kusimamiwa na Serikali linamatatizo. Kwa nini Serikali isiingie ubia ikawezesha private sector kwa management contract kuendesha mashirika haya na wakaachana na haya mambo ya kufanya hasara. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili ambalo linasumbua kwenye mashirika ya umma ni madeni. Mashirika ya umma yana madeni ya ajabu. Nilishangaa mimi, kwanza nilisoma nikasema ni bilioni au trilioni. Mashirika 11 ya umma ukichanganya yana madeni yanafikia jumla ya trilioni 27.5. Ni trilioni 27 siyo bilioni. Na haya ni yale mashirika yanayosemekana ni ya kibiashara. Sasa ukiongeza taasisi za Serikali ambazo hazitakiwi kufanya biashara na kupata faida, jumla ya madeni ni trilioni 5.2. Ukijumuisha inakuwa ni trilioni 32 kwenye mashirika ya umma, imekaa kwenye vitabu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tatizo tunalojiuliza ni hivi, ukichanganya hilo kwa sababu hata extended public sector debt unajumuisha ile ya Serikali ya about 8 trillion inakuwa ni 112 trillion. Sasa hilo ni deni kubwa sana kwa sababu huwezi kusema kwamba madeni ya mashirika ya umma hayatalipwa unless kuna namna nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninachoshauri na ninaomba Bunge likubaliane ni kwamba, haya madeni ya mashirika ya umma yafanyiwe uchambuzi, tujue yametoka wapi na nani Aliya-finance. Je, kuna transactions au miamala ambayo imefanyika na Serikali Kuu? Kama ipo, je, kuna uwezekano gani wa kugeuza madeni haya kuwa ni mtaji wa hisa? Halafu vile vitabu vya mashirika haya vikawa angalau a little bit clean, na vikiwa vimesafishwa, hiyo balance sheet ikiwa imesafishwa ina maana kwamba mashirika haya kama yatakuwa yamegeuka kuwa mashirika ambayo siyo mabaya, basi pengine hata yanaweza kukopa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu kimoja ambacho naomba tu-encourage mashirika ya umma yaweze kuchukua mikopo ya biashara, overdraft ili kuendesha biashara zao kwa gharama nafuu.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo mimi naomba hiyo ifanyiwe kazi, na kama isipofanyiwa kazi tujue kwamba tunaweka mrundiko wa matatizo kwenye bajeti ya Serikali kwenye miaka hiyo inayokuja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, hili la Mkulazi ni tatizo sana. Mkulazi imefanya accumulative growth kati ya 2020/2021 na 2021/2022 ya bilioni 20. Astaghafiru-llah, sasa inakuwaje? wenzake wamekuja nyuma, Bagamoyo Sugar imekuja wanaanza kufanya faida, hawa wanaendelea kupata hasara, hawajaanza hata biashara wanafanya mahasara. Mimi ninaomba Serikali iangalie namna gani ifanyike. Kama ambavyo nimeshauri, kwamba tuendelee sasa kuona namna. Kwa mfano, kampuni kama hiyo immideately ipewe private sector aiendeshe ili tuweze kuepukana na matatizo. (Makofi/Vicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti,…
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa kengele imelia ya pili. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, haya kumbe imelia ya pili. Naomba tu nitoe kahoja kamoja, yaani one minute.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni mambo ya mifuko ya pension. Mifuko ya pension return investment yake iliyofanya ya 604 billion kwa miaka hii miwili inayozungumzwa, imekuwa ni 0.4 percent. Sasa 0.4 percent ni kidogo sana ukilinganisha na average return kwa mifuko hiyo ambayo inatakiwa iwe 5 percent. Kwa hiyo iko 4 percent ten times. Sasa kama wangefanya biashara yao ya uwekezaji sawa sawa hata wasingelia kwamba sasa ukwasi umepungua kwa sababu Serikali haitoi michango yake na kadharika; wangepata fedha za kutosha kwenye uwekezaji. Kwa hiyo, mimi nasema kweli, nawaomba wale wanaosimamia mifuko hii wajiangalie upya kwa sababu 0.5 percent kwenye return on asset ni haiwezekani (Makofi/Vicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, basi naunga mkono tena na Mungu atujalie wote tuishi na mashirika haya. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona.
Mheshimiwa Spika, kwanza nishukuru sana kwa hotuba nzuri iliyosheheni mikakati mizuri ya kuboresha na kuinua sekta ya kilimo. Naamini wakipata fedha hizi ambazo zinaombwa basi wataweza kutubadilishia sura ya kilimo na pengine tutaona tija ikiongezeka kwa kasi katika sekta hiyo.
Mheshimiwa Spika, nianze kwanza kwa mtizamo wa kinadharia kwamba, duniani kote tija kwenye kilimo inaongezwa kwenye nchi zote tija inaongezeka kuliko idadi ya watu, watu wanaongezeka kwa asilimia mbili au chini ya asilimia mbili wakati tija kwenye kilimo, kwenye mataifa takribani yote inaongezeka kwa asilimia siyo chini ya saba.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naamini kwamba kutokana na hilo ni kwamba tunachangamoto kubwa ya kuhakikisha kwamba bei za wakulima zitapanda, haziwezi kupanda ikiwa kwamba supply inaongezeka kuliko demand. Na pili hili linajitokeza hapa kwetu pia kwamba mwaka ambapo tumepata neema ya mvua zao likawa kubwa, mahindi walikuwa wanasema bei za mahindi zinashuka kwa zaidi ya nusu inashuka by more than fifty percent na nyingine hata thirty percent ya mwaka ule ambapo kumekuwa na changamoto za uzalishaji inashuka zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, na kwamba mkulima anajaribu sana anatumia gharama nyingi lakini inapokuja kuuza kwa sababu ni cobweb theory iko hapo inaitwa cobweb theory inakuwa kama mkulima hawezi kuwa tajiri. Kwa hiyo, njia pekee ya kuweza kuwa wakulima wenye kupata utajiri ni lazima tujitofautishe na wengine duniani tujue kwamba ni zao lipi ambalo likizalishwa lina soko. Kwa mfano, tukiweza kuwahamasisha watu kutumia organic crops tukaweza kuotesha bila kutumia nanii sana unakuta kwamba bahati nzuri ndiyo unapata bei nzuri.
Mheshimiwa Spika, unatofautisha zao lako na la wengine duniani iwe Kahawa iwe chochote kile lakini organic ndiyo kinatafutwa, lakini pia kuna mazao kama maparachichi/avocado hizi ambazo pia na zenyewe zinaweza kupata demand kubwa ni vitu vya kuhamasisha tusing’ang’anie vilevile vya zamani, tusing’ang’anie tu mahindi tung’ang’anie vitu ambavyo tunaweza tukauza. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nashangaa katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri hajazungumzia masuala mazima ya horticulture, mboga mboga, matunda na vituo kama hivyo ambayo kweli unaweza ukaotesha mara tatu, mara nne hasa ukiwa na umwagiliaji ukaotesha throughout the year na ukawa tajiri. Lakini nataka kusema kwamba hilo ni jambo ambalo lazima walivalie njuga kwa sababu linahitaji mkakati ambao ni endelevu ili tuweze kulitekeleza hili.
Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine watu wameonyesha changamoto sana kwenye ushirika lakini nataka niseme kwamba, nadharia ya ushirika inabakia palepale ni nadharia nzuri hatuwezi kuwasaidia wakulima bila kuwa na ushirika. Tatizo la ushirika ni nini? utawala bora na hiyo lazima sheria hii ya ushirika ibadilishwe ili kuwe na udhibiti zaidi kwa wale wanaochaguliwa kuongoza taasisi hizi, waweze kutoa mrejesho kwa kuwa na financial statements zinazotoka na zinaenda kwa wanachama wake na wanazijadili na wale viongozi wanaoshindwa wanatolewa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nafikiri hilo ni jambo la msingi na matatizo yote bila Serikali kujikita na Mrajisi ile Ofisi ya Mrajisi kuwa na uwezo hatutaweza kuleta nidhamu kwenye ushirika na kila wakati tutasema kwamba ushirika ni wezi na nini lakini wataendelea kuiba kama hawana udhibiti wa kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna issue ya skimu za umwagiliaji, kule kwetu kuna skimu ya Kahe hasa ile ya Mawala kule kunachangamoto sana na naomba kwamba kusema kweli tumeorodheshewa nyingi kwenye kwenye kiambatisho tuliyopewa na Mheshimiwa Waziri, lakini naamini kwamba kuna ambazo ni kubwa na zinahitaji marekebisho makubwa haraka sana na hasa hii ya kwetu za Kahe kule ndiyo tunazalisha, Kilimanjaro hatuna Mpunga isipokuwa sehemu hizi za Kahe.
Mheshimiwa Spika, naomba pia tuangalie mambo mengine kwa mfano kuwezesha wakulima kupitia constituency au ward mechanization centers tusiseme kwamba tunawasaidia wakulima kwa kuwapa mmoja mmoja lazima tuwe na center moja ambayo itachukua na vifaa vile mtu anaweza akakodisha kwa bei nafuu au akakodishiwa bila kuchajiwa mpaka akaja akakatwa wakati anapouza mazao yake.
Mheshimiwa Spika, lakini ni vigumu mkulima kununua trekta na mwisho waziri amezungumzia hili la kuongeza mitaji kwa wakulima. Lakini nafikiri badala ya kuwapa fedha tuwape lease arrangement ambapo yaani wanapewa mashine halafu wanalipa polepole wanapoendelea kuuza vifaa vyao. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kufirikia hilo la kwamba financing ni kitu cha msingi na naona amesema anaunda kamati ambayo itamsaidia kufirikia zaidi namna gani wakulima wapate mikopo ya riba nafuu.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Nianze kwa kuwapongeza Mawaziri wote wawili kwa mawasilisho mazuri na Mapendekezo mazuri ya Mpango pamoja na Mwongozo wa Bajeti kwa mwaka unaokuja. Najua kwamba hii siyo Mpango, ni mapendekezo. Kwa hiyo nitajikita zaidi kwenye yale yanayoyendana na yale yaliyowasilishwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kuweza hatimaye kurejesha Tume ya Mipango na Wizara ya Mipango na Uwekezaji. Naamini hivi ni vyombo viwili ambavyo vilikosekana na pengine ndiyo sababu tumeshindwa kwa muda mrefu kuweza kufuatilia utekelezaji wa dira yetu, kuweza kufuatilia na kutathimini mipango ambayo tumejiwekea. Hatimaye sasa tumeipata na ninaamini huko tunakoenda tutaweza kusimamia vizuri zaidi kutathmini na kujua ni kitu gani ambacho kimekosekana kwenye mikakati yetu ili kuendelea kuboresha kila wakati yale ambayo tutakuwa tunayatekeleza kwenye mipango yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kwamba institution building ni kitu kizito sana kwenye nadharia ya uchumi. Ni kitu ambacho kinawezesha. Ukiwa na taasisi zinazostahiki, taasisi za kijamii, taasisi za kiserikali, taasisi za sekta binafsi zikiwa zimejipanga vizuri katika kusimamia maendeleo na kushauri maendeleo, basi hapo tutaona tunapata maendeleo yale ambayo tunayategemea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba Wakoloni waliamua kuvunja zile taasisi zetu za kiasilia ili tusipate mahali pa kujishika. Ndiyo sababu tunapata shida sana kurejesha hizi taasisi ambazo tunaamini kwamba zingekusaidia kutekeleza. Kwa mfano, kwenye kilimo bila ushirika, actually huwezi kufanya mambo mengi kwenye uchumi ambao umetawaliwa na wakulima wadogo wadogo. Kwa hiyo, ni mambo ya kujenga. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nikimbilie kwenye moja niliyonayo kwenye mwongozo wa bajeti; katika mpango huu wa miaka mitano, tulikuwa tumejiwekea lengo kwamba matumizi ya maendeleo yawe kati ya asilimia thelathini na arobaini ya bajeti yetu, na kusema kweli Bunge hili kazi yake kubwa ni kuhakikisha kwamba bajeti ya maendeleo inaongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa bajeti ya maendeleo imebakia pale pale trilioni 15 na kiuwiano inazidi kupungua kwa sababu ilikuwa asilimia 34 ikaenda ikafika sasa ni asilimia 32. Hili jambo bado naamini kwamba tusilikubali sana, tujaribu kumbana Waziri wa Fedha ili atekeleze vile anavyosema kwamba atajaribu kubana matumizi yasiyo ya lazima na fedha hiyo inayokuwa served iende kwenye maendeleo badala ya kupunguza maendeleo. Kwa hiyo, mimi naomba kwamba wakati tunapopeleka hii tuhakikishe kwamba tunaweka ukomo, kwa mfano bajeti ya kawaida isiwe zaidi ya inflation rate, something like that, tungeweka ukomo wa namna ile ili isikue sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini ukimpa mtu fedha atatumia tu, utakuta kwamba unakaribisha Waziri aje kwenye Kamati anakuja na watu hamsini. Watu hamsini wanahitajika? Wakija watatu tu au wawili wanatosha, ukweli ni kwamba tunawapa fedha nyingi mno za matumizi ya kawaida, ndio sababu wanaweza, kama ni kuhamishia task force zikaenda Arusha na nini lakini wanatumia hii fedha ya kawaida bila kujali sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu cha pili, kwenye hilo ni kwamba hatujafanya public expenditure review kwa miaka mingi kidogo, naamini turejeshe kufanya public expenditure review ili tuweze kufanya strategic resources allocation na tuone kwamba fedha zinaenda mahali pake nani wapi ambapo tunaweza tuka-serve ili kuweza kuchangia zaidi kwenye maendeleo ya majimbo yetu na wananchi wetu wakafurahi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mimi nafikiri hilo ni la msingi na nafikiri kwamba Mheshimiwa Waziri anapokuja na mpango kamili atakuwa na fedha nyingi zaidi ya hiyo fedha ili angalau twende asilimia 34 kama tulivyokuwa hapo awali ili ibaki kwenye maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mapendekezo ya mpango hayajabadilika sana na yale ya miaka hii mitatu ya nyuma na ninajua ni kwa sababu gani? Kwa sababu pengine ni mpango ule ule wa miaka mitano ndio tunautekeleza, kwa hiyo, kuna miradi inaingiliana na kadhalika lakini pia Tume ya Mipango ilikuwa ni mpya bado haijajikita sana kufanya tafiti zinazohitajika ili waweze kuleta mpango ambao una ubunifu wa kwao wenyewe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho kinasikitisha ni kwamba bado hatujaona mwanga unaotupeleka kukuza kasi yetu ya ukuaji wa pato letu kufikia asilimia nane. Asilimia nane ndio ilikuwa kwenye dira na karibu tungeifikia lakini ndio tukaja tukayumbushwa na Uviko lakini bado kinachosikitisha ni kwamba mipango inayokuja haijaweza kusema ni lini tutaanza kuona uchumi unarejea asilimia saba mpaka nane. Naamini bado kuna mikakati kama hii ya sekta ya kilimo na sekta nyingine inaweza ikasaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi niseme kwamba, tunafahamu kwamba Waziri wa Mipango amesema vizuri sana kwamba, kupanga ni kuchagua na amesema kwamba tutakamilisha kwanza ile miradi ambayo inaendelea kabla hatujaingiza miradi mipya mingine kwenye bajeti yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hiyo ni sawa kabisa na kwa sababu inaendana na ukweli kwamba resources zetu ziko limited na ukweli kwamba, hususan kwenye sekta hii ya nje hatujawa na mikakati ambayo inaweza ikawa na uhakika wa kuongeza fedha za kigeni. Fedha za kigeni zimekuwa ni utata na sasa hivi kitakachokuwa consumed katika kutekeleza malengo yetu ni fedha ya kigeni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa issue inayojitokeza ni kwamba tunasema kilimo na sekta nyingine lakini na Kamati ilisema, imeona kwamba maeneo rahisi zaidi ni kwenye eneo hili la utalii na eneo la logistics, usafirishaji hasa kutoka kwenye Bandari ya Dar es Salaam. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa Bandari ya Dar es Salaam tuna bahati, Mungu ametupa bahati tumepata DP World imekuja wakati wake, kwa hiyo, naamini kwamba inaweza ikafungua ile logistics ya hub yenyewe tukaanza kuona kwamba hii infrastructure iliyojengwa, barabara na SGR inatumika kwa uhalisia kupeleka mizigo kwa nchi jirani na kuanza kuongeza sana pesa zetu za kigeni, kutumia DP World. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kwamba hili ni jambo ambalo tutaiomba Serikali ilifanyie kazi na ijaribu kumuomba Mheshimiwa Rais wetu na tumuombee ili aweze kuhamasisha hawa jamaa zetu ili waweze kuingiza ule uwekezaji ambao walikuwa wameahidi, wauingize haraka kwenye hii bandari yetu na tuweze kuona tunabadilisha kabisa suala zima la foreign exchange hapa kwetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo nimeliona ni kwamba, matumizi ya takwimu za sensa hayajakaa sawa kwenye mipango na kwenye miongozo. Nilifikiri kwamba Serikali na Wizara hizi zingeangalia zile statistics za sensa ili waone kwamba ni kitu gani wanaweza kutumia kupata mapato zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano kuna idadi za nyumba na tunajua nyumba zimeandikishwa, makazi yanajulikana, kwa hiyo kuna uwezekano wa kukusanya zaidi kwenye kodi ya majengo. Tungeweza kuona kwamba ni vitu gani tunatarajia kule, hata huku kwenye DP World hajaweza kuona kwamba mapato tutakayopata yataongezeka au yatakuaje kwa sababu kusema ukweli projected revenue ni kubwa sana ukilinganisha na uhalisia wa 2022/2023 ni thirty-nine trillion halafu mwaka huu 2023/2024 tumeweka forty-four utaona kwamba niongezeko kubwa sana kwa hapo kama ukitumia uhalisia wa mapato tuliyopata.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ukienda forty-seven trillion ukitumia uhalisia huu tunaona utakuta kwamba hatutafikia. Forty-seven trillion ni fedha nyingi sana pengine unless mnasema DP World wataanza kutuingizia fedha kwenye akaunti yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba kwa vile usanifu wa miradi umekuwa ni hafifu na Wizara ime-recognize kwamba ubora ule wa usanifu wa miradi hatuna, yaani ubora ule wa usanifu na usiposanifu vizuri huwezi kupata hata financing cost ya miradi ile. Kwa hiyo, ndio sababu miradi inachelewa kwa sababu haikusanifiwa kwa ubora, na unaenda sokoni ukiwa na mradi ambao umesanifiwa nusunusu, haijatathminiwa na watu wawili au watatu, halafu unaenda unapata bei kubwa unashindwa kutekeleza mkakati na unaanza kupata matatizo njiani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri hilo ni jambo la kuangalia na ningeomba sana wizara isiingize kwenye mpango miradi ambayo haijasanifiwa. Ifanyiwe upembuzi yakinifu mapema na isanifiwe mapema ili wakati tunaingiza kwenye mpango wetu wa mwakani basi iwe inajulikana kwamba inapoenda kutekelezwa maandiko yake yamekaa vizuri na tunaweza kuyauza kwa PPP.
Mheshimiwa Mwenyekiti, halafu niseme, nafurahi kwamba kwenye mpango huu, mkazo unawekwa kwenye sekta binafsi kushirikishwa na hii inaenda sambamba kabisa na ile sheria ya PPP tuliyoipitisha ambayo sasa hivi iko vizuri na ninaamini sasa hivi tutapata wawekezaji wengi ambao wataweza kuja kuwekeza kwa mpango huu wa PPP.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tena nirejee kuwashukuru Mawaziri, pia nimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi hii anayoifanya.
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu shughuli za Kamati kwa Mwaka 2023
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa fursa ya kusimama siku hii ya leo kuzungumza machache yanayotokana na majadiliano kwenye Kamati yetu ya Bajeti ambapo mimi ni Mjumbe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kutoa pongezi nyingi sana kwa Mheshimiwa Rais kwa namna ambavyo anaongoza Serikali yake na namna ambavyo amewezesha Serikali hii kufikia yale malengo makubwa ya kiuchumi ambayo tulijiwekea kwenye mwaka huo 2022/2023 na kwenye nusu ya mwaka huu wa 2023/2024. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kusema kweli malengo mengi yamefikiwa. Ukienda kwenye upande wa mapato tumefikia lengo kwa asilimia takribani 94, upande wa matumizi of course inatumika ikipatikana fedha. Niseme uzuri mwingine kwamba ukiangalia overall nakisi ile ya bajeti ambayo tulitarajia iwe around 3% bado iko kwenye 3.6%, siyo mbaya kwa sababu ni ndogo sana ukilinganisha na za wenzetu hapa jirani wanazungumzia 7%. Ni kweli kwamba ukitaka kuwa na uchumi tulivu sana basi unataka kuwa na nakisi ya bajeti ndogo maana yake hufanye deficit financing kubwa na hiyo ni njia moja ya kudhibiti mfumuko wa bei. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kitu ambacho nikizungumzie zaidi ni suala zima la ukuaji wa pato letu la Taifa ambalo kwa bahati mbaya bado tuko around asilimia 5. Tunatarajia sasa mwaka huu wa 2023 tufikie asilimia 5.3 lakini ni chini ya lengo lililokuwa kwenye dira ya 2020 ambayo ilisema iwe ni zaidi ya asilimia 8 na tuliweza kufikia fikia kule hapo nyuma tukafikia around 6%, 7%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba tulivyofika kwenye growth ile nilishangaa kwamba kuna taasisi za kimataifa hazikutupongeza lakini sasa hivi tuko 5% wanatupongeza basi kuna mahali kitu kimejificha. Niseme hivi, tatizo la ukuaji wa pato la Taifa hapa nchini hatujapata ufumbuzi wake na hatujajua chanzo chake ni nini hatujabaini sawa sawa. Ngoja mkinipa fursa nielezee kwa nini nasema hivi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tulikuwa tunasema mambo ya blueprint tukifanya blueprint ile tukatekeleza basi Sekta Binafsi itaibuka. Tukasema kwamba tukifanya kuboresha miundombinu Sekta Binafsi itachangamka lakini hili jambo halijatokea, kwa nini? Niseme hivi ili Pato la Taifa likue, kichocheo kikubwa licha ya kuwa na rasilimali ya watu na rasilimali ya resource ya land ambayo ni very rich, tunahitaji financial resources. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, financial resources zipo; watu tuliowapa jukumu la kukusanya akiba zote za watu binafsi hapa nchini ni benki. Sasa tuseme kwamba tumeona kwamba kweli benki zimeweza kuongeza mikopo kwa Sekta Binafsi kwa 16% na mwaka juzi ilikuwa 20% na ushee. Sasa lakini tunasema kwa nini hili ongezeko halichochei ukuaji wa pato la Taifa? Kwa nini halichochei?
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka niwasilishe kwamba ukweli ni kwamba haliwezi kuchochea kwa sababu benki zimeondoka kwenye commercial banking proper (kwenye kukopesha kwa business sector) wanaenda kukopesha kwa sekta ya consumption (sekta ya watu binafsi). Ndiyo sasa unaona benki zinakimbizana na watu walioajiriwa kukopesha watu wenye mishahara ili wasifanye risk yoyote. Maana yake ni kwamba kwa mfano sisi hapa Bungeni kwenye Kamati yetu tulisema wapunguze riba wanayotoza kwa fedha hii ambayo wanakusanya kwa urahisi bila kuingia kwenye risk. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa issue iliyojitokeza hapa ninasema kwa nini benki zifanye hivyo? Kwa sababu tulipokuwa sisi tunaanza benki pale, nilivyokuwa pale tunaanzisha ile benki tulikimbizana na wateja kwenye corporate sector lakini kilichokuwa kimetukuza tukaanza kukua haraka ni kwamba corporate banking (mikopo kwa wateja wakubwa kwenye biashara na kwenye uzalishaji) tulikuwa tunakimbizana nao na tulikuwa tunawafanya wao wanakuwa ni marafiki zetu, siyo tupate hongo ila tuweze kuwakuza wawe wateja ambao ni endelevu kwa benki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi badala ya kukimbizana na hiyo corporate sector ambayo ndiyo inazalisha, ndiyo inafanya biashara, kwenye utalii ndiyo ipo, unakuta benki zinakimbizana kufanya michapalo huku na kule ili sisi tukachukue mikopo kwao kwa bei ambayo ni ile ile ya corporate sector, kwa hiyo ukweli ni kwamba hatuwezi kukua. Sasa kilichopo ni hivi, kilichofanya benki wafanye hivyo siyo kwamba ni wao wenyewe. Benki Kuu imeweka hii limit ya kwamba mikopo chechefu isizidi 5%, ok ni nani atadanganya kwamba atafanya biashara kuanzia mwaka wa kwanza aweze ku-limit ile risk yake ya kutokuweza kulipa au default risk yake kwa 5%? Mtu aliyefanya biashara yoyote atasema it is impossible kabisa tena wengine watasema the dream was impossible. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tulikuwa tunachukua mikopo tukijua kwamba tutafanya restructuring, tutafanya nini lakini unajua kwamba unachukua risk above 5%, nachukua 10%, 15% benki inachukua. Inaweza ikachukua mwaka wa kwanza lakini baada ya miaka miwili yule mtu ana turn around anakuwa mteja mzuri. Kwa hiyo, hapo tunakopesha wale watu. Sasa hivi kwa sababu huwezi kufikia hiyo limit ya 5% ya mikopo chechefu, the only thing you can do ni kutafuta wakopaji ambao wana-cashflow ambayo ni guaranteed ambao ni wafanyakazi kwenye Serikali, Bunge na kwenye mashirika makubwa lakini siyo kukopesha business kabisa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tatizo ni hilo na mimi nasema kwamba ukiangalia kwamba benki zimekuwa overcapitalized sasa hivi kwa sababu risk ile ya kwao risk premium zao zimeshuka sana. Kwa hiyo, wanafanya faida bila kutumia earn ya ile capital, wako overcapitalized unakuta badala ya kuwa na capital minimum ya about 14.5% ambayo ndiyo required wako kwenye 20% wame-accumulate capital kwa sababu they are not taking risk but they are getting a lot of profit sasa tatizo ndiyo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninasema hivi kwamba kama hatuta address hiyo issue kwamba sekta hii ya benki ambayo imekusanya akiba zetu ikopeshe private investors kwenye business, hata kwenye biashara ndiyo sawa lakini mnyororo mzima wa biashara basi tusipofanya vile hatutaweza kuona tumeepukana na hili tatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme cha pili ni hivi; utaona pia kwamba tumeweza ku-maintain very low inflation. Tujiulize; je, kwa nini basi tusiweke target ya inflation ya sifuri kama tungetaka low inflation basi iwe sifuri lakini tunaweka lengo kwamba target iwe tatu na kwa nini iwe tatu? Ukikaa kwenye TV unaangalia … utakuta kwamba watu kila wakati wanasubiri takwimu inapokuwa released ya inflation rate Marekani kwenye Nchi zote mtu anasema inflation imeongezeka ngapi? Je, kwa hiyo Federal Reserve itaongeza riba au itafanya nini kwa sababu inflation ikipanda riba inatakiwa ishuke, ipande na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tumekuwa na 3% constant, figure ambayo ni constant sasa hivi kwa miaka mingi ni lengo letu. Sasa nauliza what do you do when you have a low inflation ambayo iko very low? Faida yake ni nini? Utakuta kwamba faida ni ndogo sana. Maana yake ni kwamba tumezuia kuingiza fedha kwenye mzunguko kwa mikopo kwa sababu fedha kwenye mzunguko inaingia kwa mikopo. Hutaweza kukuta mtu anaenda kuchukua pale Benki ataipataje hiyo fedha ya Benki Kuu bila kuchukua mkopo benki? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, benki ndiyo zina-create money, inavyo-create money ndiyo inachochea uchumi. Sasa maana ya kusema kwamba umekandamiza kwenye 3% maana yake ni kwamba unasema kwamba mikopo isitoke na fedha isizunguke. Issue ni kwamba hakuna mtu yeyote ambaye aliwahi kuja hapa mchumi akasema optimal inflation ni nini? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa optimal inflation kwa Marekani inaweza ikawa ni 3% kwa sababu wako almost full employment, unemployment yao ni around 5% - 6%. Unemployment yetu kwa kipimo ambacho yaani sijui ni kipimo cha ngapi inasema ni 14% lakini ukihesabu partially employed people (mtu anayefanya kazi masaa mawili) halafu anaenda kunywa chai na kahawa huko kijiweni pengine unemployment yetu iko 20% - 30%. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuonyesha kwamba unemployment ni kubwa ni kwamba kuna watu wako tayari kufanya kazi bure. Mimi watu wamenifuata wananiambia tutafutie tu tukajishikize pale hata temporary halafu tutakaa tu pale usinipe chochote. Sasa mtu unaogopa inflation kwamba itakuwa driven kama resources ziko full employed lakini sisi tuna resource ambazo haziko employed; watu, ardhi sijui na kitu gani kingine hicho na hizo financial zote ambazo haziendi the right place.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo lazima tumuombe Gavana kwamba kwanza aangalie hiyo issue kwamba you don’t just want to bank, they don’t lend; actually, watu wanasema hizi benki zetu hapa ni saving banks, they are not commercial banks at all, katika nadharia ya finance hizi benki zetu ni saving banks basi. Kwa hiyo, hazisaidii na hazitakaa zisaidie kwa sababu wanachukua hela wanaweka, wanawapa watu zinaenda hovyo hovyo halafu hazisaidii kwenye kutengeneza ajira, kufanya nini na nini. Ni lazima tuangalie hili. (Makofi)
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba kusema kweli…
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Taarifa.
MWENYEKITI: Mheshimiwa Musukuma muda wake umeisha nimemuongezea lakini nakupa ruhusa utoe taarifa.
TAARIFA
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. nilikuwa napenda kumpa taarifa mzungumzaji anatoa somo zuri sana kwa leo mpaka na mimi Daktari nime-appreciate. Sasa nilikuwa nakuomba umuongeze walau dakika tano tu ili somo lituingie vizuri. (Makofi)
MWENYEKITI: Mheshimiwa Dkt. Charles naomba uendelee kidogo.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. Musukuma nakushukuru sana kwa taarifa yako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio nasema hivi kwamba katika hilo ni kwamba kuna mikopo ile tunaizungumza itakayoenda kwenye private sector yes, lakini wakati private sector inakuwa kwamba inasuasua haichukui ile mikopo na kuiingiza kwenye miradi Serikali pia ina-widen ile nakisi ya bajeti wanafanya deficit financing. Wanaweza wakachukua mikopo pia kwenye benki zetu wakaipeleka hata kwenye ile mifuko ya uwezeshaji kama ikiwa imeundwa sawa sawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikopo ya uwezeshaji ni ile ya 10 ambayo ina 4:2:2 na ukatumia njia nyingine ukaiweka hizo zote mahali pamoja ukaunda hata guarantee fund ambayo itakuwa inawa-guarantee watu wote na pesa itakuwa ni nyingi halafu Serikali sasa ikaweza kutumia hiyo hela ikaingiza kule watu wanakopeshwa hata kama kwa masharti nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii TIB tunayoambiwa hapa kwamba ina matatizo, TIB waambiwe wa-focus kwenye kitu kimoja tu. Wawachukue vijana wajasiriamali wawaweke kwenye incubation (viatamishi). Wakishawaweka kwenye incubation wanawapa mitaji wanaenda kuwasimamia huko mtaani wanafanya kazi kwa kutumia agency, ni hawa watu ndiyo wataanza kuibua uchumi tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, wewe unawaambia TIB sijui ikagawe mafuta sijui wapi, ikagawe majiko ya gesi; what are you doing? Kwa nini tusiwape kazi hiyo kwamba nyinyi haya makubwa mmeshindwa, hizo corporate landing wameshindwa, sasa kama wameshindwa corporate landing nenda kule kwa wale ambao tunahitaji, startups hapa nchini hamna mkopeshaji, siyo commercial bank siyo nini. Kwa hiyo, lazima hizi benki zetu ambazo tumeziunda kwa mitaji ya Serikali basi ndiyo zifanye hiyo kazi ya kuatamisha startups na hiyo itasaidia sasa kuibua vitu tofauti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba ukienda kwenye benki kitu wanachoumiza sana, corporate banking departments zilizokuwa tumezikuza yaani ndiyo zinazunguka, wateja wengi wako hapa wanajua wanawakumbuka wale vijana wangu wakina Mlabwa, akina Alfred Philipo Alfred na wengine wanakimbizana nao wanaenda kuwasadia halafu hii miradi mikubwa tunayoiona sasa hivi mingi imetokana na corporate landing basi. Wakati ule niliona tukimbizane na consumer landing, consumer landing ni hii personal landing ambazo sasa hivi zina-occupy more than 35% ya mikopo yetu hapa nchini na mingine itakuwa iko kwenye Serikali. Nataka kuomba kwamba kweli tujaribu kuangalia upya na tubuni upya. Namba ya blue print naona haisaidii sana hivyo lakini yale ni madogo sana lazima tuibue mambo mapya haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho kabisa niseme, kwa sababu naona nisije nika nani hii. Natumai kazi kubwa tuliyonayo hapa Bungeni ndiyo hii ya kuwezesha Pato letu la Taifa lianze kukua kwa haraka zaidi. Linakua lakini likue kwa haraka sana kwa sababu we have the windows za kufanya hilo Pato la Taifa likue haraka. Kwa hiyo, kama tunazo tufanye hivyo, hiyo ndiyo njia pekee ya kuboresha maisha ya Mtanzania. Ndiyo njia pekee ya kufikia lengo na dira yetu, ya kwamba tunataka tuboreshe maisha ya Mtanzania. Lazima tufanye hayo na mengine ambayo sasa kwa sababu ya muda naomba niishie hapa, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nami nianze kwa kurudia pongezi zilizotolewa na wengi. Shukurani kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunda Tume ya Mipango na kuunda hii Wizara ya Mipango na Uwekezaji ambavyo vyote ni taasisi, ameviweka chini ya ofisi yake. Tunaamini kwamba taasisi hizi zimeweza kuanza kutekeleza majukumu yake kwa kasi ya juu sana kutokana na usimamizi shupavu wa Mheshimiwa Rais mwenyewe.
Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Profesa Kitila Mkumbo pamoja na timu yake, Dkt. Kida, Lawrance Mafuru pamoja na Mchechu na wafanyakazi wote wa pale kwenye Wizara hii mpya.
Mheshimiwa Spika, kama ungeniambia niseme majumuku ya hii Tume ya Mipango ni nini? Yameorodheshwa 20, lakini naweza kusema ni coordination ya Mipango ya Serikali; ni coordination ya Sera za Serikali kwenye sekta mbalimbali. Kila sekta inakuwa na interest zake. Kwa hiyo, kila sekta inataka ipate zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mtu ambaye ni neutral, au taasisi ambayo ni neutral ambayo Wabunge walisisitiza iundwe, ni Tume ile, kwa sababu haina sekta. Kazi yake ni kuhakikisha kwamba resources zinakuwa allocated in a balance manner ili uchumi ukue in a balance way. Kuwe na both, social and economy balance. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sekta za jamii zisipokee too much zikasahau kwamba ili sekta za jamii ziweze kuzalisha huduma zile ambazo zinahitajika za afya, elimu na kadhalika, ni lazima zipate fedha kutokana na sekta za uzalishaji, sekta za kilimo, viwanda na huduma mbalimbali kwa jamii, pamoja na sekta nyingine. Kwa hiyo, naamini kwamba sasa tumepata chombo ambacho kitatuwezesha kututengenezea mipango ambayo ina tija kwenye maeneo yote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mchangiaji wa mwanzo alisema tusianze tena kuongeza walimu na kadhalika, lakini kazi ya mipango ndiyo hiyo, kuona kwamba ni wapi ambapo sasa tulenge rasilimali yetu ili iweze kuchaji maeneo yale ambayo yamekwama. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna dhana moja kwamba ili uweze kwenda sawasawa, ni lazima uweze kusema nalenga kitu gani? Inavyoonekana, mwelekeo wa Tume so far, au wa Wizara, zaidi unalenga wawekezaji wakubwa kutoka nje, na wawekezaji wa ndani wakubwa.
Mheshimiwa Spika, mimi naamini kwamba nchi hii haiwezi kutoboa bila kulenga SMEs na wawekezaji wadogo wadogo, ambao ndiyo kule chini tuliko, ndiyo kule kwenye halmashauri zetu tuliko, wawekezaji wadogo; kuona ile mikopo ya wanawake, vijana na walemavu isimamiwe namna gani ili iweze kuleta tija? Iendelee kutolewa kwa mbinu zipi? Ni kitu gani cha ziada kifanyike ili mikopo inayotolewa kwa kupitia empowerment funds zote na kwa namna nyingine ambayo mabenki yanatoa ili iweze kuleta tija kwenye uchumi wetu na fedha yetu iwe na thamani na kadhalika?
Mheshimiwa Spika, naomba katika vitengo vyote, na sijaona kama kuna kitengo kwenye hii Wizara ya Mipango kinachoshughulika na wawekezaji wadogo wadogo na SME. Ukishakuwa nacho na kikatumia sasa wale Maafisa Mipango na Maafisa Uwekezaji kwenye halmashauri, tutaweza kuhamasisha uwekezaji mdogo mdogo na kufanya incubations ili watu waweze kutekeleza miradi midogo midogo ambayo itakuwa ina-hide kwenye mnyororo kwa thamani (value chain) wa hawa wakubwa wakubwa ambao Mheshimiwa Rais amefanikiwa kupata.
Mheshimiwa Spika, ninaamini pia kwamba hawa wawekezaji wanaosajiliwa kwenye TIC, pia hiyo orodha ingekuwa inachapishwa ili tujue ni wapi wanaenda kuwekeza, ili nasi tuanze kujipanga, wanapokuja kuwekeza tuweze ku-supply vile vitu ambavyo wanahitaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nafikiri hilo ni la msingi sana na ninaamini pia kwamba suala zima la PPP liwekewe mkazo kwenye Wizara hii ambayo ndiyo inaenda kusaidia kuona kwamba wakubwa na wadogo wanapata msaada. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo, pia niseme kwamba kuna ile investments forums ambazo zilikuwa zinafanyika, zilikuwa zimeanza kwenye mikoa na kwenye wilaya mbalimbali na naona zimefanyiwa tathmini na Tume. Naamini kwamba hizo nazo sasa zianze kuhimizwa ili ziweze kusaidia. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Tume ya Mipango ni think tank, kwa sababu ina-coordinate vitu vingi na inatakiwa iwe na utaalamu, iwe na watu ambao inawasaidia katika kufanya utafiti. Wasifanye utafiti wenyewe, wawe na Taasisi za Utafiti. Sasa kuna Taasisi za Utafiti kama REPOA. Na-declare conflict of interests, mimi ni Board Member wa REPOA.
Mheshimiwa Spika, ESRF, REPOA na Taasisi nyingine hata Vyuo Vikuu kama Sokoine wana taasisi na Idara za Tafiti. Sasa watenge fedha kwa ajili ya utafiti. Kwa mfano taasisi hizi ninazotaja, hiyo sarafu, wanapata kidogo, lakini wanapata fedha za nje, ni wafadhili ndiyo wanafadhili utafiti ambao unaenda kusaidia Serikali hii kutengeneza sera za kiuchumi na kutengeneza mipango ya kiuchumi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, haiwezekani, kwa nini hawajatenga fedha kwa ajili ya taasisi za utafiti? Naomba sana, sijawahi kushika shilingi ya Waziri, lakini nitashika shilingi kama hatasema kwamba ametenga kiasi gani cha fedha ambazo zitaenda kugawa kwa hizi taasisi za utafiti ili zimsaidie yeye na zitusaidie sisi Wabunge pia.
Mheshimiwa Spika, watu wanakuja kutusaidia kutupa percentage kwenye Kamati ambazo hata wazungu hawawezi kutengeneza. Wale wanakujanazo wanatuelewesha namna gani mapato yanaweza kukua, kwa nini hatuwapi fedha? Naomba sana jamani, naomba sana Mheshimiwa Waziri na Profesa Kitila uende ukaangalie hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nilishangaa kidogo, huwezi kuwa na mpango ambao hauna bajeti, yaani bajeti na mpango zinaenda sambamba, zile process zinaenda sawia. Ukiniambia kwamba msimamizi wa Tume ya Wizara hii ya Uwekezaji na Mipango na Tume yuko kwenye; sijui namna gani unapita kwenye Kamati ya Bajeti. Kwa sababu mimi niko kwenye Kamati ya Bajeti na sijaona chochote na nilikuwa nasita hata kuchangia, lakini nimeona nichangie tu kwa sababu ni vizuri kuchangia.
Mheshimiwa Spika, nilikuwa nafikiri kutafutwe namna yaku-link hapo ili Kamati ya Bajeti iweze pia kupata nafasi ya kuona mipango hii na ndiyo watu wanaweza pia wakajua bajeti inaweza kuwa ya namna gani? Siyo tu ya Wizara, lakini bajeti kwa ujumla na mipango ya kutekeleza mipango hii. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nimefurahi sana kuona kwamba blue print inatekelezwa kwa ujumla na inatekelezwa vizuri, na inawasilishwa kwenye wasilisho. Hata hivyo, nafikiri ni wakati sasa wa kusema kwamba hii blue print tui-review tena, tuone kwamba ni kitu gani bado kimebaki? Ni kitu gani kimefanyika, lakini kimefanyika kinyume ya namna tulivyotarajia? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kupunguza tozo siyo kusaidia uwekezaji. Unaweza ukatoa tozo zote na usipate hata mwekezaji. Kuna vitu vingine ambavyo vinahitajika ili uwekezaji uweze kuonekana katika nchi hii.
Mheshimiwa Spika, naomba Waziri anayehusika aone namna gani pia ya kurahisisha na kuelimisha umma ni kitu gani kimefanikisha kwenye hili la kurahisisha uwekezaji na kuhamasisha au kupunguza gharama za uwekezaji katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nafurahi pia kuona kwamba Tume chini ya Mheshimiwa Mafuru imeanza sasa kufikiria upya namna ya ufuatiliaji, kwa sababu ufuatiliaji na tathmini ndiyo jambo kubwa pia katika kuhakikisha kwamba fedha inapata thamani. Sasa kama kweli Tume inafikiria namna hii, maono yake ni kwamba tutengeneze mifumo ya ufuatiliaji. Mradi ukiingia tu kutekelezwa kunakuwa na dashboard ambayo hata Mheshimiwa Rais mwenyewe anaweza akaona dashboard kwamba mradi huu sasa umefikia hapa na hapa na hapa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tuliona juzi Mheshimiwa Waziri wa Nishati na Mheshimiwa Naibu Waziri Mkuu alituonesha pale. Unaenda pale unaangalia Bwawa la Nyerere, huna haja ya kwenda kule, unaliona linavyotiririsha maji na linavyozalisha umeme. Ni mambo ya namna hiyo tunataka kuona. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, unaweza ukafungamanisha ule mfumo wake wa mradi na mifumo mingine, ukafungamanisha, na kila mtu anaweza akajiaonea, hata Spika akikaa ofisini kwake akaweza kuona akiingia kwenye websites. Siyo lazima atengenezewe mfumo wa ajabu, ni web base system ambao mtu ukiingia ukitaka kuona huo Mradi wa SGR umefika wapi? Unaingia, unaona. Mradi huu umezalisha kiasi gani au umekufa au ni kitu gani? Unaona. Naomba tuendelee kwa mawaidha hayo ili tuweze kurahisisha shughuli nzima ya uwekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naamini kwamba mawanda ya ufuatiliaji ya Tume yako limited kwa sababu ya resource ya watu pia. Sasa kuna miradi hii ya Pension Funds, miradi ya Pension Funds inafadhiliwa na nani? Kwa sababu ile miradi katika zile sijui shilingi trilioni 76 au 78 alizosema Mheshimiwa mwenzangu ni kwamba, nyingi pengine ni miradi ya pension.
Mheshimiwa Spika, sasa tunachouliza, inafadhiliwa na nani? Return kwenye Assets ya miradi ya Pensions ni zero point something percent. Mimi nashukuru kwamba sasa hivi Registrar Mheshimiwa Mchechu ameanza ku-recruit wasimamizi na Bodi kwa njia ya ushindanishi na ameanza kuwapa mafunzo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa huyu kwa sababu anajua mambo, naomba katika mafunzo anayotoa, achukue top business schools, Harvard Business School kuna wahadhiri wazuri, waletwe wawafundishe hawa watu namna ya kusimamia, wanatoa case studies ambazo ni nzuri. Mkienda kule tutatoboa, seventy six trillion is a lot of money. Kwa hiyo, mimi naamini kwamba…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Mheshimiwa kengele ya pili imeshagonga…
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nilifikiri nitazungumza kidogo sana, lakini naona muda umeenda.
SPIKA: Mheshimiwa, nakupa dakika moja, malizia.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Naomba basi tuangalie namna ya kutumia wahadhini kutoka kwenye top business school, kwa sababu ni njia pekee ya kuweza ku-sharpen skills za management katika nchi yetu na katika Mashirika ya Umma. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ahsante, naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Niende moja kwa moja kwenye hoja kwa sababu nikishasimama mimi hiyo saa inakosa speed governor. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nianze kwa kusema hivi, kuna changamoto moja ambayo lazima tuifahamu kwamba, bajeti yetu siyo kubwa ni ndogo sana, bajeti ya nchi jirani na kwetu Kenya ui-convert kwa Tanzanian Shillings ni trilioni 77. Bajeti ya Uganda nchi ambayo ni ndogo na kulinganisha na sisi ni trilioni 50 nukta something za Tanzania, bajeti yetu ni trilioni 49, kwa hiyo tuko nyuma licha ya kwamba, nchi yetu ni kubwa sana na licha ya kwamba watu wetu ni wengi sana, idadi ya watu ni kubwa, lakini bajeti yetu ni ndogo. Ni ndogo kwa sababu, bajeti inatokana na mapato. Sasa kama mapato hatujakusanya ya kutosha ina maana basi ni lazima tujifunze tujue namna gani tutatumia vizuri, tubane matumizi, ili iweze kutosheleza kwa namna yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, ukichukua uwiano wa bajeti ya wenzetu Wakenya kwa Tanzanian shillings kwa uwiano wa mwananchi mmoja mmoja, wastani ni shilingi 1,400,0000. Ukiangalia hii ya Uganda ni shilingi 1,100,000 ya Tanzania ni shilingi 750,000 tu basi, kwa kila mtu wastani wake. Kwa hiyo, shilingi 750,000 ni kidogo sana ukichanganya kila kitu; uendeshaji wa Serikali, huduma za jamii, ukiweka kulipa madeni, yote iko kwenye shilingi laki saba, wastani wa kila mtu.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ni fedha ndogo na ni lazima tusibweteke kwamba, imeongezeka kwa asilimia 11, asilimia 12, bado inatakiwa iongezeka zaidi, ili iweze ku-catch up na ukilinganisha kwa square kilometre tulizonazo sisi tunaonekana ni duni sana. Kwa hiyo, ninataka niseme kwamba, hilo ni jambo la ku-address na ndiyo sababu ninaamini kwamba, nadharia wanayokujanayo ya kwamba, tutumie vizuri bajeti na hiyo bajeti tuitumie kwa kuweka, ile ambayo mwenzangu amesema ni, monitoring and evaluation ifanyike vizuri na kwa KPIs hizi zinawekwa, kama kweli zinawekwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaamini KPIs haziwezi kufanya kazi kama hatuna mipango ambayo ni SMART. SMART maana yake ni Specific, Measurable, Attainable, Realistic and Time Bound na ina Time Bound. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano ukiangalia hii wanasema Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kiteto – Mtoro mpaka Singida ni Barabara ya kilometa 433. Sasa kama hujaiwekea specific target kwamba, Mwaka huu 2024/2025 kwenye hii pengine tutajenga kilometa 50 na mtu aone kwamba, anaweza akazifikia na ukazitengea fedha, hatutafika mbali. Utamwekea mtu KPI ya namna gani? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, KPI haiwezi kufanyika bila kuwa na mipango ambayo ni smart na smart ni framework ambayo inatumika kila mahali. Ninaamini kwamba, watu wetu wa Tume ya Mipango wataendelea kuangalia hilo suala na kuhakikisha kwamba, kila barabara ikiainishwa basi tunajua mwaka huu itajengwa kiasi gani na siyo kuainisha tu, toka mimi niingie hapa Bungeni ziko kwenye mpango. Hazijaisha na hatuambiwi zimejengwa kiasi gani, lakini zinajirudia tu, hazitakaa ziishe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namalizia kwenye suala la mpango. Mimi nasema ukweli ni kwamba, kwa hali ilivyo tete kwenye Soko la Kifedha na Mitaji ya Kimataifa sasa hivi, kukopa ni kama ku-commit suicide kwa sababu, riba ni kubwa sana zinafika mpaka asilimia 12, asilimia 13 kwa dola, siyo kwa shilingi. Hiyo ni riba kubwa sana, siyo wakati mzuri wa kukopa kwa hiyo, lazima sasa tujue kwamba, pengine tunge-focus kumalizia hii miradi ambayo imeshaanza na ambayo inatakiwa sasa itupeleke kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 tukiwa tunasema kwamba, angalu tumefanya kidogo kwenye ile miradi ambayo tulipewa na tukaenda kuitangaza huko kwenye majimbo yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala lingine ambalo ninataka nizungumzie ni hili ambalo wenzetu wamezungumza, la uhaba wa dola. Mimi ni mtaalamu wa mambo ya fedha kwa hiyo, nisipolizungumzia nitakuwa sijatenda haki. Ukweli ni kwamba, kuna njia mbili, njia tatu za kukabiliana na uhaba wa bidhaa yoyote na dola ni bidhaa tu, wala siyo kitu cha ajabu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, moja ni kwamba, una-control, unafanya exchange control. Ukifanya Exchange Control maana yake una-allocate administratively, tena una-allocate ile dola iliyopatikana kwa ile mitaji ambayo unaona ni priority, ile mingine basi haipati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hiyo ni distortive kwa sababu ni kwamba, kuna wengine ambao wangetumia ile dola kwa tija zaidi kwa sababu, wana miradi mizuri zaidi kuliko hii ambayo wewe unafikiria ni mizuri. Kwa hiyo, Administrative Allocation au hizo Exchange Controls ambazo zilikuwepo tukaondokana nazo miaka hii ya 1990, siyo njia sahihi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, njia nyingine ni hiyo ambayo wenzetu wote hapa tunasema tuongeze uzalishaji wa huduma na bidhaa za kuuza nje, lakini hiyo ni structural measure. Yaani unachukua the structural policies, hasa za kibajeti, ili kuibua au rather ku-debottleneck production problems kwenye sekta zetu, kama ni ruzuku kwenye mbolea na kadhalika, lakini hiyo inachukua muda. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hiyo ni lazima isaidiwe na incentive ya kibei na bei maana yake ni kwamba, dola inauzwa kwa shilingi chache sana. Bei ya dola ni ndogo mno hapa kwetu ndiyo sababu inakuwa adimu, kila mtu anataka dola. Mtu ana-import, ananunua dola kwa bei chee, halafu ikifika hapa ina maana kwamba, hata hizi products zetu hapa ndani haziwezi ku-compete na imported goods kwa sababu ya dola iko mispriced. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi ninafikiria hiyo question ya debottlenecked supply is okay, lakini it will take some time. Meanwhile ni lazima tukubali tutumie demand management tool, ambayo ndiyo hiyo exchange rate, kuiruhusu na ninashukuru kwamba, Benki Kuu imefanya, imeruhusu na imepunguza kidogo makali, msererko huo wa around 11 percent. Tunashukuru Wizara imeweza kufanya hilo, lakini unaona kwamba, bado iko kwenye equilibrium. Hatujawa kwenye equilibrium exchange rate so far na ndiyo sababu, unaona kabisa dola zile hazipatikani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitoa mfano huu juzi, Jumamosi, nikasema kwamba, pale kwa wenzetu majirani, wao waliruhusu exchange rate ika-overshoot ikafika 160 kutoka around 90. Sasa, baada ya muda kwa vile waliiruhusu ikafanya adjustment yenyewe, imerudi sasa imeanza ku-appreciate inarudi kule ilikokuwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata hii ya kwetu ingeruhusiwa, ingekwenda kule halafu exporters wakaona faida zaidi kwa hiyo, wangeamua kuzalisha na kuuza nje zaidi kwa ushindani mzuri. Kwa hiyo, gradually ile supply ina-pick up na inapo-pick up basi ina-equilibrate na exchange rate inashuka ina-appreciate tena, inarudi pengine inaweza kuwa shilingi 2,300 siwezi kusema.
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini nasema kwamba, bila kutumia hiyo ushindani wa uchumi wetu haupo. Kwa sababu, tunashindanisha uchumi na uchumi na kitu kimoja kinachoshindanisha ni productivity na efficiency na kingine ni exchange rate. Ndiyo kitu kinacholeta uwiano kwenye uchumi na ndiyo uchumi shindani. Kama uchumi ni shindani na wewe unaubana hautafika mbali. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, narudi kwenye suala zima la ukusanyanji wa mapato ya TANAPA, Ngorongoro na TAWA. Sasa sisi tunaona kwamba, pengine ni vizuri kwa sababu, hawa wanafanya biashara kusema kweli, wanafanya biashara siyo TANAPA wanacheza. Wanafanya biashara na siyo watu wa kusubiri kwamba, wapate migao kama hii inayotoka Hazina kwenda kwenye Wizara nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi ninafikiri kwamba, ili waweze kuwajibika internationally, waweze kuwajibika kwa kufuata accounting standards za Kimataifa, tuweze kuwapima na waweze kupewa malengo. Msajili wa Hazina anasema anajua, anawawekea malengo na ufuatiliaji na bado haohao wana bodi zao.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi ninafikiri kwamba, tumuombe Mheshimiwa Waziri wa Fedha ajaribu kuliangalia hili jambo, arudishe ukusanyaji wa mapato ya haya mashirika ya kibiashara yarudi kwenye mahali pake. Ni pale ambapo wanakusanya na usually mapato yanaendana na expenditures na baadaye kunakuwa na surplus, then surplus can go away out there. Kama inakuwa ni ngumu sana kufanya yote kwa mpigo, amefanya kwa TPA kwa hiyo, tunaomba tena afanye na...
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Dkt. Kimei.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: …mojawapo halafu baadaye aende gradually, lakini siyo lazima afanye yote kwa mpigo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho niseme kwamba...
NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kimei, ahsante.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa nafasi hii. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kusimamia mchakato wa kutengeneza mapendekezo na mwongozo huu ambao tunaujadili siku ya leo, maono yake na maelekezo yake ambayo ninaamini yamesheheni kwenye maandiko ambayo tumepokea ya mapendekezo ya Mpango na Mwongozo wa Bajeti. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hivyo, nawapongeza pia Mawaziri wanaohusika kwa sababu ninaamini kusema kweli wamechakata vizuri yale maelekezo waliyopewa na Mheshimiwa Rais. Vilevile, nazipongeza na timu zao kwenye Wizara hizi mbili zinazohusika na Tume ya Mipango. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma maandiko yanayohusiana na hali ya uchumi ambayo wameeleza vizuri sana kwenye Mpango na Mwongozo utahitimisha kwamba, uchumi wa dunia, uchumi wa kanda na uchumi wa Tanzania sasa unaelekeza kwenye hali iliyokuwepo kabla ya UVIKO-19, utaona kwamba, hali ya uchumi kwenye nchi zote duniani kwa mfano, ongezeko la pato limefikia kwenye 3.3% na kwenye nchi hizi ambazo zimeendelea utaona ongezeko la pato lao linakwenda kwenye 1.7% mpaka asilimia mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo hivyo ilivyo kwa nchi zilizoendelea, haziwezi kuendelea kukuza uchumi wao kwa kiasi kikubwa kwa sababu resources zinakuwa almost fully employed na hawana uwezo wa kukuza sana mapato yao kama sisi tunavyostahili kukuza kwenye asilimia tano mpaka 10%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, utaona kwamba mfumko wa bei duniani umepungua kutoka 8.1% umefikia kwenye 5.9% katika kipindi cha mwaka huu tulionao. Kwa hiyo, naona kwamba maendeleo haya tunaona mwelekeo unatupatia fursa nyingi. Kwa mfano, ikiwa mfumko wa bei umeshuka; na ninyi mtakumbuka kwamba nchi zinazoendelea ikiwemo Marekani zilianza kutekeleza Sera ya Kubana Money Supply (Ujazi wa fedha) kwa kuongeza riba mara tu, inflation ilivyokuwa juu sana. Sasa, inflation imeshuka kwenye two digit, sasa hivi ipo kwenye 5.9% kwa wastani na kwenye nchi nyingine inashuka. Kwa mfano, wanaita secure overnight financing rates (SOFR) ambayo imekaa badala ya LIBOR. Sasa hivi ipo kwenye 3.5%. Hii inasema nini?
Mheshimiwa Mwenyekiti, inasema kwamba, nchi ya Marekani inaelekea sasa kulegeza ile Sera ya Fedha ya Kubana na kwa hiyo, riba zitashuka na itatupatia fursa sasa ya kuweza kukopa kwa gharama nafuu sana ukilinganisha na zile ambazo tumekopea mwaka 2023.
Mheshimiwa Mwenyekiti, issue ni kwamba hii SOFR ni inasema ndiyo benchmark ambayo unaongeza kwenye ile grace premium ambayo mmekubaliana. Kila wakati ikipanda ina maana na gharama zako zinapanda hata kwa mikopo ya nyuma. Kwa hiyo, ninaamini kwamba gharama za ku-service mikopo zitapungua na kuchukua mikopo mingine zitapungua na ninaamini Serikali itakwenda vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo mazuri sana yametokea kwenye nchi zilizo kwenye Kanda yetu ya East Africa na SADC, inflation imepanda sana. Kuna nchi kwa mfano Burundi, inflation yao ni takribani 20%; ukienda South Sudan, inflation ni 40.2% na ukija hata kwenye nchi nyingine za East Africa zinakuwa zina inflation kubwa kuliko ya kwetu ambayo ni asilimia tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sababu ya hizi inflation kwenda juu ni upungufu wa vyakula, lakini sisi tuna vyakula na tuna-reserve kwenye NFRA. Kwa hiyo, naamini kwamba sasa tunaweza tukafaidi na tukaruhusu wananchi wetu wakanufaika kwa kuwawezesha kuuza chakula kile karibia na msimu mwingine unaingia kwa bei nzuri, lakini siyo tu chakula, na bidhaa nyingine ambazo zinazalishwa kwenye viwanda vyetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia sasa bajeti yenyewe utaona kwamba bajeti ya mwaka huu imepanga kutumia shilingi trilioni 55.1. Sasa hilo ni ongezeko la 16.2%, ni ongezeko kubwa sana. Ongezeko la mapato ni 12.6% kutoka trilioni 34.6 hadi 38.46. Kwa hiyo, utaona kwamba matumizi yanakua kwa kasi kubwa sana ukilinganisha na mapato. Kwa hiyo, hilo ni jambo la kuangalia vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwamba bahati mbaya kwenye matumizi, bajeti ya maendeleo sasa inapungua kwa uwiano wa bajeti yote. Inapungua, inakwenda kwenye 29.9%. Kwa miaka ya nyuma hii mitatu iliyoisha, bajeti ya maendeleo ilikuwa inachukua 33.7% ya bajeti yote. Mimi ninaamini kwamba tulikuwa tumejiwekea some sort of indicative parameter kwamba, bajeti ya maendeleo isipungue chini ya 30%, lakini naona kwa mwaka huu inakuwa ngumu kidogo kwa sababu pengine kuna uchaguzi, gharama zinakuwepo za ziada na tunafungua vitu vingi vipya kwenye miradi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni lazima tuongeze matumizi ya kawaida, lakini tuangalie vizuri tusiondoke kwenye benchmark ya 30%. Tujaribu kwenda kwenye hilo. Niseme kwamba bajeti hiyo kwa namba imeongezeka kwa 7.4%, lakini bado uwiano wake kwa bajeti nzima siyo mzuri. Ubaya mmoja wa ongezeko kubwa la namna hii, halafu tunaweka kwenye ukomo, tunaunda pipeline kubwa ya miradi ambayo haitekelezeki ikamalizika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, kinachotokea ni kwamba ile bajeti ya kawaida inakuwa disbursed, lakini bajeti ya maendeleo inabakia kuwa Mawaziri wameshapewa ukomo, kwa hiyo, Julai wana-contract ile miradi yote bila kujali kwamba, je, fedha itapatikana? Tunazungumzia cash budget, lakini inakuwa siyo cash budget.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi imeshakuwa contracted, wameshapewa advance payment, kwa hiyo, unakuta ile miradi inaanza kukaa kwenye pipeline, fedha haiwi disbursed kwenye ile miradi. Hii ndiyo chanzo cha tatizo hilo unaloona la kusema kwamba, jamani sasa mbona hawalipi? Mbona wameondoka kwenye miradi! Wakandarasi hawafanyi kazi, wanaondoka, wanakimbia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukweli ni kwamba kwa sababu pipeline ipo na inakuwa carried forward from a year to a year. Ukiangalia deficit tunayopata kwenye makusanyo ni five percent, yaani kwa miaka mitano ukichukua tumefanya hesabu hizo ni five percent tuna-miss kila mwaka. Sasa, kila mwaka uki-miss five percent kwenye 40 trillion ina maana kwa five years unakuwa umeshaunda pipeline ya vitu ambavyo havijalipika kwa sababu ya makusanyo, 10 trillion. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sijui kama hiyo ni ya kweli, lakini ukweli ninaamini kwamba kwenye pipeline Wizara ya Fedha ikiangalia vizuri itakuta kuna vitu vya kulipa. Wakandarasi wa kuwalipa na hawa wa chakula shuleni kama 10 trillion it is a lot of money.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashauri hivi, Serikali sasa iwaagize Maafisa Masuuli waweke line item kabisa ya kulipa madeni haya na ninashukuru kwamba Mheshimiwa Dkt. Mwigulu alivyo-present alisema kwamba mwaka huu hawataingia kwenye miradi mipya. Nafikiri that is nice and it is a very good stance. Wafanye ili waweze kuweka ile line walipe madeni ya zamani, halafu ndiyo tuanze sasa kuwekeza, lakini ile ya vituo vya afya vya kimkakati msituache solemba na msitutoe, acha ikae tu tutekeleze. Bwana asifiwe! (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, niseme hilo ni tatizo ambalo tumeliunda wenyewe na ni tatizo ambalo lazima tu-deal nalo. Ukiangalia vizuri sasa kwenye mambo mengine ya kimkakati utaona kwamba, kitu kitakachotutoa kwenye hali hii ya makusanyo na Serikali yenyewe inasema ni private sector kuweza kuwekeza. Miradi hii ya kimkakati imeingia kwenye stream sasa inazalisha, lakini private sector bado hawajahamasika kuanza kuwekeza na kuzalisha, wale wa nje na hapa ndani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa, naomba hivi, ili tujiridhishe kwamba kweli hakuna tatizo ambalo linasumbua watu kuwekeza, tutengeneze international competitiveness index yetu wenyewe. Tujiulize, watu wa nje wanatu-rank hivi, lakini tuchukue vile vigezo vichache tutengeneze kwamba, sisi bei yetu ipo hivi na tuweze kuiuza kwa wawekezaji kwamba kweli hii nchi yetu wanavyosema siyo hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna bwawa, umeme una-stabilize, reli na yenyewe itakuja i-stream na vitu vyote hivyo, ili kuanza kuuza hii nchi yetu vizuri zaidi na sisi tujiridhishe kweli tunakidhi mahitaji kwa sababu competitiveness yetu kulingana na nchi nyingine hapa Afrika ipo juu. Naamini tukitengeneza na tukifuatilia walikuwa wameanza hapo nyuma kidogo, walikuwa wanakaa Makatibu Wakuu wanaorodhesha mambo ambayo ni ya msingi ili kuweza ku-boost business indicator yetu, lakini Mheshimiwa Waziri ninaona siku hizi hiyo haipo tena.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niseme cha mwisho kwamba, nafikiri tumefanya makubwa, na Bwawa la Nyerere limeleta mambo mazito. Baada ya kuleta mambo mazito sasa ni kwamba, yaani hakuna kitu muhimu kama umeme wa uhakika kwenye nchi. Nchi zote hizi hapa kwetu, nyuma huku, ukienda huko SADC, umeme ni matatizo. Sasa, hapa kwetu tunaanza kupata umeme wa uhakika, ni Mungu ametuletea hiki kitu, ni bingwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutumie hilo na pia, tusibweteke, ila tuwaombe TANESCO wawe flexible katika kuingiza watu binafsi kuzalisha umeme. Tatizo la watu binafsi kuingia kuzalisha umeme, kwa mfano kule Ruhuji na Rumatali watu binafsi wangewekeza fedha, hata wa nje wangewekeza kwa sababu, umeme unauzika anywhere. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, issue ni kwamba, tatizo ni pricing model ya TANESCO. Pricing model, sisi umeme wetu bei yake ni ya chini, kwa hiyo, mtu ukiwekeza kwa bei hii ya chini ambayo umeme unapatikana hapa kwetu, mwekezaji binafsi hawezi kupata faida. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, lazima tuwe flexible, tujue kwamba, tutafanyaje ili watu binafsi wawekeze, hata kama watapata subside kidogo kupunguza yale makali. Wawekeze halafu tuone namna gani tuta-price ule umeme wetu. Tusiongeze bei, lakini kwa sababu unakuwa mwingi, basi inaweza ikawa rahisi ku-manage, lakini tusizinyime private sector kuingia kuzalisha, siyo tu umeme wa maji, ila hata geothermal sasa ndiyo umekuwa umeme ambao una tija sana. Wenzetu hapa majirani wameingiza umeme mwingi wa geothermal ambao ni umeme unaozalishwa kwa namna ambayo inatunza mazingira. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja. Nawaomba wenzangu wote wakubaliane na mapendekezo haya ili tuweze kuendelea mbele. Ahsanteni sana. (Makofi)
The Water Resources Management (Amendment) Act, 2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa fursa hii. Nichukue pia fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Rais wetu anayeongoza Serikali na Wizara hii husika ambayo ameona umuhimu wa kuleta marekebisho haya ya kuboresha usimamizi wa rasilimali ya maji katika nchi yetu. Ninaamini ni jambo muhimu na ninamshukuru sana na kumpongeza Waziri wetu, Kijana wetu Mheshimiwa Jumaa Aweso, Mheshimiwa Maryprisca ambaye ni Naibu wake pamoja na Viongozi wa Wizara hii kwa umakini wao.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninawashukuru pia kwamba wameshirikisha, wamepokea maoni ya wadau kuhusiana na masuala haya ambayo yanakwenda kurekebishwa na ninaamini kwamba ukiangalia utaona kwamba siyo masuala ambayo kama wangekuwa sio watu makini sana wangeweza kuyaibua lakini wameweza kuyaibua kwa sababu kweli wanataka ufanisi katika suala hili zima, ambalo mimi nimejiona kama ni sheria ambayo inapaswa kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali ya maji kwa kukabiliana na vitendo vinavyosababisha uharibifu na uchafuzi wa vyanzo vya maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hii ni shughuli ambayo inaenda kudhibiti au kuhakikisha kwamba wanadamu ambao sisi tunahitaji maendeleo tunatumia vyanzo vya maji kwa namna ambayo itakuwa endelevu na ndiyo sababu kwenye hifadhi nyingine, mimi ninafikiri kwamba kwenye mabonde ni kama hifadhi tu hakuna tofauti na hifadhi nyingine wameenda mkondo ule wa kuunda hata majeshi kabisa kule ambako ni hifadhi watu wasitumie ile ardhi kwa namna ambayo itaharibu au kupoteza kabisa utajiri huu ambao Mungu ametupa.(Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwamba hawa hawajaenda kwa kufuata nadharia ya kuunda majeshi kuhifadhi maji, lakini wanataka kutumia naona nadharia inayotumika na msingi wake ni ushirikishwaji wa wananchi katika kusimamia vyanzo na matumizi ya maji haya tuliyopewa. Tofauti kidogo pia ambayo ninaiona na ninashukuru kwamba Profesa Manya amezungumza mambo mazuri sana sitaki kuyarudia, nayaona kwamba kuna umuhimu wa kufungamanisha usimamizi wa maji kwenye mabonde lakini pia tuangalie pia zile mamlaka ambazo zinasambaza maji, zile mamlaka ambazo zinasimamiwa na Mamlaka za Usambazaji Maji Mijini na Vijijini kwasababu zenyewe ndiyo zinaenda sasa kuona kwamba watu wale wanaoshirikishwa kwenye usimamizi wana motisha na wanajua namna gani na umuhimu gani wanaweza wakapata katika suala hili zima la kusimamia maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni vizuri pia ieleweke kwamba maji yanapita kwenye mikondo, maji yanatokea kwenye chemchem mbalimbali na yanapita kwenye mashamba ya watu walikuwa wanazitumia zile chemchem kunywesha mashamba, kule kwetu ni kawaida kabisa chemchem zipo karibu hata kwenye shamba langu kuna chemchem ambayo ninaweza nikatumia, lakini ukweli ni kwamba lazima tuweze kulinda sasa haya maji yanatiririka namna gani yapelekwe kwenye maeneo ambayo yanahitajika na yatatumika kwa ufanisi zaidi katika shughuli za kibinadamu pamoja na ikiwa ni maji safi wa kunywa na pia maji ya kuendeshea shughuli mbalimbali kwenye sekta za uzalishaji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo ninaamini kuna umuhimu huo na ndiyo sababu ninaamini kuwa hii nadharia ya kushirikiana wale watu ambao wanaweza kwa urahisi sana kufikia hivi vyanzo na kuviharibu inakuwa ni jambo la msingi na ndiyo maana kwamba wenzangu waliozungumza suala zima la elimu, kutoa elimu sana kwa wananchi siyo tu wanaoishi kwenye maeneo ya vyanzo vya maji lakini pia wale ambao wanaweza wakachimba visima na wale wanoatumia. Watu wajue kwamba maji yana umuhimu, kuna maji ya kutumia kuoshea magari na kuna maji ambayo yanaweza yakatumika kunywesha mashamba, lakini siyo yale yale maji yanastahili kutumika kwa kunywa. Kwa hiyo watu wajue kwamba maji yale ambayo wanatumia kufanya shughuli zao siyo maji ambayo yangeweza kutumika kwa shughuli za watu kunywa ambayo ni msingi sana ni maji safi hayapo kila mahali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kabisa kwamba kama nilivyosema hatuwezi kuzungumzia suala zima la usimamizi wa rasilimali maji bila kuzungumzia wale wanosambaza na maana yake ni kwamba lazima Kanuni zinazotungwa chini ya vifungu husika au huko baadae tutakapoangalia hii sera ya maji tuone kwamba namna gani wale wanaosambaza maji wanabanwa ili waweze kusambaza maji kwa namna ambayo ni endelevu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia hatuwezi kuondokana na ukweli kwamba, hatuwezi kutokuzungumzia gharama za kuwafikishia wananchi wetu maji kwenye nyumba zao na katika maeneo yao ya kufanyia shughuli mbalimbali, hizi gharama zimekuwa ni kero na jambo ambalo mimi ninaamini kwamba watu wanaanza sasa kukiuka kutumia yale maji kupitia mikondo husika ambayo tunafikiri kwamba inahifadhi na badala yake wanaanza sasa kutoboa toba ili wapate maji kwa gharama ambayo ni nafuu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia naamini kwamba suala la motisha la kuhifadhi kama nilivyosema haliji endapo utasema kwamba mtu ambaye anaweza akafikia maji kwa urahisi pale alipo unaenda kumtoza Shilingi 800 kwa unit ambayo ni fedha kubwa kwao, wanaona kwamba pengine afadhali wapindishe yale maji yaende kwenye nyumba zao bila kulipa chochote. Kwa hiyo masuala ya gharama lazima yaangaliwe, ninaamini kwamba Naibu Waziri husika atachukua hili suala zima la kusema kwamba atafanyaje, atatumia Kanuni gani ili wale wanaosambaza wasambaze maji kwa gharama ambazo ni muafaka. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nitoe maoni yafuatayo ya kuzingatia pia, kwamba mabonde haya tumeona hayana vyanzo ambavyo vinatosheleza kwa fedha, kwa hiyo naomba kwamba ili haya mabonde yaweze kutoa elimu kama tunavyosema basi ni lazima yawezeshwe kupata rasilimali ya kutosha ya kuweza kuelimisha kutoa elimu kwenye ngazi zote kuanzia kwenye Vijiji hata kwenye Kata na kwenye Wilaya. Mabonde haya pia yapewe uwezo wa kufanya doria pengine kwa kushirikiana na Kamati za Usalama na Ulinzi kwenye maeneo yetu ili waweze kukagua vyanzo hivi vya maji na kuhakikisha kwamba hivi vyanzo vipo vinatunzwa na vinatumika kwa namna ambayo ni sahihi na maji hayachafuliwi na watu wengine wakawa wakakunywa maji chini ya bonde, maji ambayo yamechafuka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jumuiya za Watumia Maji pia nafikiri kwamba watumiaji maji hususani wale wanaomwagilia wasaidiwe kuboresha miundombinu yao ya mifereji ili kuepuka matope kujaa kwenye vyanzo vile na kuhakikisha maji yale hayaendi kwenye mkondo na kwenda kwenye maeneo mengine ambayo yanahitajika maji kufika kwenye bonde hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninajua kwamba Bonde la Mto Pangani kwa mfano, lina matatizo na wanahitaji kweli kuweza kuwawezesha wale wanotumia waweze kuboresha mifereji yao ili maji yaendelee kwenye mikondo inayostahili hata kufika kwenye Bahari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Wizara ifanye maboresho kwenye bei za maji kama nilivyosema kwenye maeneo mbalimbali ili maji yawafikie watu kwa njia ambayo ni sahihi na gharama ambayo inakubalika lakini natumaini kwamba pia kwa sababu suala hili lote ni mtambuka Wizara ya Mifugo ninaamini kwamba na wao wamepitia Muswada huu. Wizara ya Mifugo wasaidie kujenga mabwawa na mabirika ya mifugo kuweza kupata maji katika nyakati zote za mwaka ili mifugo sasa isiwe inafunguliwa kwenda kuharibu vyanzo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mtu anayefuga akiona ng’ombe wake anakufa kwasababu ya maji anapeleka yule ng’ombe mahali popote, kwa hiyo naomba Wizara ya Maji sasa ijikite na iwezeshwe kutengeneza mabirika ya mabwawa ambayo yanaweza kusaidia sasa ng’ombe na mifugo mingine kupata maji. Pia naamini kwamba Kamati zile ambazo mnasema zitaundwa kwenye vidaka maji, zile kamati ninaomba Wizara ifikirie kuweka vigezo vya wanakamati, kwa sababu tumeona kwenye jumuiya wameweka watu kwenye jumuiya za maji za RUWASA ambao hawana uwezo, hawaelewi hata ni kitu gani kinafanyika, hawafanyi hesabu na hamna vitabu vinavyojitosheleza kutoa hesabu yam aji, bili zile wanazokusanya zimekuwa Shilingi ngapi, mapato na matumizi kiasi gani hela zimepelekwa kwenye Serikali Kuu kusaidia uendelevu wa miradi ya maji ambayo inatekelezwa hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaunga mkono hoja na ninaendelea kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuleta Muswada huu. Ahsante sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naomba Wizara ifikirie pia kuweka vigezo vya wanakamati, kwa sababu tumeona wameweka watu kwenye jumuiya za maji za RUWASA watu ambao hawana uwezo, hawaelewi hata ni kitu gani kinafanyika. Hawafanyi hesabu na hamna vitabu vinavyojitolesheleza kutoa hesabu ya kwamba maji, bill zile walizokusanya zimekuwa shilingi ngapi mapato na matumizi na kiasi gani hela zimepelekwa kwenye Serikali kuu kusaidia uendelevu wa miradi ya maji ambayo inatekelezwa hapa kwenye nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja na ninaendelea kumshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa kuleta Muswada huu. Ahsanteni sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Ununuzi wa Umma wa Mwaka 2023.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Nashukuru kupata nafasi ya kwanza kuchangia kwenye mjadala huu unaohusu Muswada wa Ununuzi wa Umma, Ugavi na Uondoshaji Mali za Umma wa Mwaka 2023, ambao naamini utaenda kupita na kufuta ile sheria ambayo tunatumia sasa hivi ya Public Procurement Act No. 7 ya mwaka 2011.
Mheshimiwa Spika, kwanza nianze kwa kuipongeza Serikali kwa dhati; Serikali hii inayoongozwa na Mama yetu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo imekuwa sikivu na kuona kwamba kulikuwa na malalamiko mengi na mapungufu mengi yaliyojitokeza katika utekelezaji wa sheria hii ambayo sasa wamependekeza kufuta. Wote tunafahamu na tunajua mijadala iliyoendelea hapa Bungeni; Bunge limekuwa likijadili upotevu wa fedha kwa namna nyingi, na tuliishia kusema kwamba, pengine hatupati thamani ya fedha kabisa kwa kutumia mchakato uliokuwepo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tumekuwa tunaona malalamiko mengi na kero nyingi ambazo analeta Mheshimiwa CAG. Dhana nyingi zinatokana na mchakato wa sheria ya ununuzi. Kwa hiyo, naamini kwamba baada ya sheria hii kupita, ambapo tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kukubali ije kwa haraka, na naamini kwamba imekuja kwa wakati muafaka. Sasa tutaenda kupata thamani ya fedha ambapo ni asilimia 70 ya bajeti tunayopitisha au takribani asilimi 14 ya pato la Taifa inapitia kwenye ununuzi. Kwa hiyo naamini tukipata thamani hiyo ya fedha, basi tutaona miradi inatekelezwa kwa tija na manunuzi yanafanyika kwa tija na hivyo, kuwaletea wananchi manufaa yale ambayo yanatarajiwa na bajeti na mapitio ya Bunge hapa.
Mheshimiwa Spika, niseme kwamba, cha kwanza kabisa ambacho kimetushangaza ni kwamba utekelezaji wa sheria unafanyika lakini hakuna sera. Mimi nafikiri kwamba Serikali izingatie kwamba, kabla haijatengeneza Muswada au sheria tupitie kwanza kwenye mchakato wa sera ili tujue kitu gani tunaenda kukihalalisha kiwe ni sheria. Kwa hilo mimi naamini kwamba tutafuatana na Kamati kama alivyoeleza Mheshimiwa Mwenyekiti wetu. Tunaiomba Serikali sasa iende kutengeneza sera ambayo itajulikana wazi na iwe na mkakati wake wa kuitekeleza hiyo sera. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kama alivyosema Mwenyekiti wetu, Kamati ilipitia na kuchambua kwa kina sana huu Muswada. Tulipata muda wa kutosha kabisa kuchambua lakini pia kukutana na wadau na wametupatia maoni yao. Baada ya kupata maoni yale tukaweza kutoa mapendekezo kwa Serikali; na nashukuru sana Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba na timu yake kwa kukubali kuingiza mengi ya yale mapendekezo ambayo tulipendekeza. Ndiyo sababu sisi wanakamati tunaunga mkono hii hoja kwa nguvu zote, kwa asilimia 100, na tunawaomba Wabunge wenzetu wakubali hii ipite. Hakuna kitu ambacho kinapita ambacho ni full, kwamba hakina mapungufu lakini naamini kwamba hii sheria ni kati ya sheria ambazo zimefanyiwa kazi kwa kina sana. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kabla sijasema mawili au matatu ambayo mimi ninafikiri kila mmoja anapaswa aelewe sheria hii inaleta kitu gani nizungumzie suala la upendeleo kwa wazawa au upendeleo kwa kampuni zinazosajiliwa hapa nchini na upendeleo kwa manunuzi yanayozalishwa hapa nchini, pamoja na wakandarasi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naamini kwamba njia pekee ya kupeleka fedha kwa wananchi, tunasema kwamba Serikali inasaidia wananchi wapate fedha, njia pekee ni hiyo ya kutoa upendeleo, kwa sababu sisi ndiyo tunalipa kodi, sisi wananchi ndiyo tunalipa kodi na tozo ambazo ndiyo zinaingia kwenye Mfuko wa Serikali, ndiyo zinatakiwa zitumike hapa ndani na zizunguke hapa ndani. Sasa mzunguko huo hautakamilika endapo sehemu kubwa ya miradi inayotekelezwa, sehemu kubwa ya manunuzi tunayofanya tunatoa nje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hiyo hela ambayo tunaitoa mifukoni kwa watu tunaenda kuirudisha na watu wa nje wanafaidika kwenye viwanda vyao, sisi tunabaki hapa tunazubaa tu. Kwa hiyo, naomba kabisa kwamba kama kweli uadilifu utakuwepo na hii sheria nia yake ni kuingiza uadilifu, kulazimisha watu wawajibike kwenye mchakato huu, ina maana kwamba pengine tutakwenda kushuhudia kwamba sehemu kubwa ya manunuzi yatakayokuwa yanapita kwenye zabuni, basi yatakwenda kwa wananchi ambao watanufaika.
Mheshimiwa Spika, nasema hivi siyo kwamba ni kitaifa tu, lakini hata kwenye vitongoji tunavyotoka. Tunapotekeleza miradi ya maendeleo au manunuzi tukafanya kwenye maeneo yale ya vijiji vyetu, kwenye majimbo yetu yakafanyika mlemle kama local hata force account lakini kwa namna hiyo kwamba manunuzi yafanyike pale ili wale watu washiriki kwenye utekelezaji wa ule mradi, ndipo watakuwa na ownership na umiliki wa ule mradi na kuutunza na kuhakikisha kwamba ule mradi unaendelea kuwepo, kwa sababu wameshiriki kwenye utekelezaji, wamefaidi kwa kupata kipato kutokana na mradi ule. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa kufanya hivyo, wataupenda na mara nyingi inakuwa ni kitu kizuri sana na niseme hata kwa watu binafsi tu. Tunashangaa kwa mfano Tour Operators, Tour Operator anapandisha watu katika Mlima Kilimanjaro wageni, watalii, anatoka na nguvu kazi kutoka mjini, anatoka nao wengi kutoka Mjini Arusha, kutoka Moshi wanakuja kupanda mlima, wanafika pale wanakuta vijana wamekaa usiku kucha, hawajapata kazi, kipato chochote na wengine wanazungumza tusaidiane basi tuwe wapagazi tuweze kupandisha hawa watu mlimani.
Mheshimiwa Spika, huwa anakuja na watu wake kiasi kwamba anavunja moyo sana wale watu ambao wapo kwenye lile eneo na wale watu waliopo kwenye lile eneo hamna kipato kingine, hakuna source nyingine ya income. Wanabakia sasa kusema ili tupate kazi hizi, basi na sisi tukimbilie mijini, tukiwa kule mijini tunajulikana, tutaanza kujikuta na vikundi vya mjini, basi na sisi tutapata hizo kazi za Tour Operator na kadhalika.
Mheshimiwa Spika, naomba sana hata sekta binafsi tuhakikishe kwamba kule tunapoenda kujenga, hata kama umepata ukandarasi, umeupata mjini kwa sababu ya vifaa ulivyonavyo, lakini uhakikishe unaenda kwenye lile eneo, kwenye kile kijiji, unachukua nguvu kazi pale. Unaweza ukawa na wataalam wa kusaidia kutoka mjini lakini sehemu kubwa ya nguvu kazi itoke kwenye maeneo hayo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, niseme machache kwamba kusema kweli kama tulivyosema, nitasema vitu vitatu ambavyo vinanifurahisha sana kwenye Muswada huu. Kwanza ni kuomba kuongeza uwazi na usawa kwenye zabuni kwa kulazimisha kwamba ni lazima sasa ununuzi wote wa Taasisi Nunuzi, ufanyike kupitia mchakato huu wa mifumo ya eletroniki. Ninachojua kwamba kitu kinachosababisha watu kuanza kuombana hongo, rushwa ni kwa sababu wanakutana uso kwa uso.
Mheshimiwa Spika, kama hawakutani uso kwa uso kama mabenki tunasema hawakutani, wanachakata hata mikopo bila ya kukutana na wateja wale. Kwa sababu ukishaweza kuzuia kile kinapunguza sehemu kubwa ya ushawishi wa kutoa rushwa. Sasa kama unapitisha kwenye mfumo moja kwa moja na jawabu linatoka kwenye mfumo basi itakuwa kwamba siyo rahisi kuwe na intervention ambayo binadamu atanufaika nayo. Kwa hiyo nafikiri hilo ni moja.
Mheshimiwa Spika, pia naamini kwamba imekataliwa kabisa usinunue bila kupitia hiyo mifumo, lakini naamini kwamba pia kwa sababu ununuzi unachukua muda mrefu sana. Kwa mfano, kuna barabara zinatangazwa, baada ya muda mrefu, unasikia kwamba bado, mpaka mwisho wa mwaka ndiyo unakuta mkandarasi amepatikana, lakini bajeti tulikuwa tumetenga toka Julai. Kwa hiyo, naamini kwamba issue hiyo ni kitu cha msingi sana, naamini Muswada huu umepunguza siku kama alivyoeleza Mheshimiwa Mwenyekiti wetu na naamini hilo linaweza kufanyika.
Mheshimiwa Spika, kitu kingine ambacho kinasaidia ni kwamba ununuzi wa dharura utakuwepo tu kwa namna moja au nyingine, lakini huu Muswada unalazimisha kwamba iwe ni cha kidharura kwelikweli. Baada ya kufanya huo ununuzi wa dharura, lazima uripoti kwa Mdhibiti, kwa Mkurugenzi wa Mamlaka ambaye naye atakuja kutathmini kama ulifuata kanuni zitakazokuwepo kwenye Muswada huu.
Mheshimiwa Spika, naamini kwamba ununuzi wa holela hatuwezi kuukwepa kwa sababu kuna mambo ya majanga na kadhalika nayo lazima yawe accommodated, lakini uzuri wa Muswada wake, umekwenda zaidi kwa kusema kabisa kwamba ni mazingira yapi yanaweza kusababisha ununuzi wa dharura.
Mheshimiwa Spika, pia kwenye Muswada huu kuna jambo moja ambalo litasaidia sana hasa kwenye manunuzi wa vifaa vya tiba pamoja na madawa. Ununuzi moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji au mawakala wao. Hii tunaondoa yule mtu kati (middle man) ambayo maana yake kwamba, tunapunguza gharama, tozo za middle man zinaondoka. Kwa hiyo, pia hicho ni kitu ambacho nashukuru kwamba thamani ya fedha inakwenda kupatikana. Kingine ambacho pia wote tufahamu, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hii ya ununuzi na Ugavi atakuwa anafanya continuous follow up ya mienendo ya ununuzi kwenye Taasisi za Umma na mwishoni anatakiwa atengeneze ripoti yake ambayo itafika mpaka kwa Mheshimiwa Rais. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwanzoni sisi kwenye Kamati tulikuwa na wazo kwamba pengine hiyo ripoti pia ije hapa Bungeni, lakini kwa ushawishi wa Mheshimiwa Dkt. Nchemba, tumeamua kukubaliana naye kwamba, basi pengine Mheshimiwa Rais, atakapopokea hii ripoti, basi impendeze kuirudisha kwa Waziri anayehusika ili aweze kwenda kuifanyia kazi, lakini pia tunajua kwamba masuala mengi pia yatakuwa yametufikia kupitia kwenye ripoti ya CAG ambayo na yenyewe inakuja Bungeni. Kwa hiyo, tukasema tusi-duplicate. Hili wazo nafikiri siyo baya sana, lakini liwe kama tulivyokubaliana na Serikali.
Mheshimiwa Spika, nataka kusema kwamba issue ya Bei Kikomo ambayo ningependa sana iwe inaitwa Bei Elekezi kwa sababu huwezi kuwa exactly. Kutakuwa na upungufu wa asilimia 10 au plus minus ten percent, ni kitu ambacho kisitusumbue sana. Naamini kwamba bei za ukomo hizi zitajitokeza baada ya muda na kutokana na hiyo kanzidata ambayo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka atatengeneza, basi ataanza kuona evolution ikoje, Kilimanjaro au Mwanza au wapi, bei za kujenga darasa zitakuwa shilingi ngapi? Anatoa sasa hiyo bei, lakini isiwe bei ambayo ni cut stone ambayo huwezi kushuka plus minus, yaani ningependa sana sana labda pengine hilo la bei elekezi lifahamike vizuri…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa, kengele ya pili imegonga.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, jambo lingine zuri…
SPIKA: Mheshimiwa kengele ya pili ilishagonga.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, kumbe muda ulishakwisha, nilifikiri napata, basi…
Mheshimiwa Spika, naomba niunge mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, nashukuru sana kupata fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii ambayo inamajukumu makubwa sana hususani katika kipindi hiki.
Nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kuwapata watu makini wanadiplomasia makini kuongoza Wizara hii. Namfahamu sana Mheshimiwa Mama yetu mpendwa Balozi Mulamula, kazi aliyofanya kujenga diaspora pale Washington na Marekani kwa ujumla na ninaamini sasa tutaona tofauti kubwa kwenye suala hili la diaspora kwa sababu ni mtu anayelifahamu, anafahamu uwezo wa diaspora kuchangia kwenye maendeleo ya nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, na ninaamini kwamba suala linalozungumzwa la dual passport (passport pacha) litashughulikiwa, lakini pia tukijua kwamba hawa watu hawawezi kuja kuwekeza kwenye nchi ambayo siyo raia, hata kuweka akiba tu wakitaka kufungua account kwenye mabenki yetu inakuwa shida. Kwa sababu wanaambiwa onesheni passport ya Tanzania, kwa hiyo, inakuwa kwamba akiba nyingi ambazo tunaweza tukazileta remittances kutoka nje huko, kutoka kwa diaspora, ambako kwa nchi nyingine zinachangia sehemu kubwa ya pato la Taifa, mpaka asilimia tano kwa watu wa Ethiopia inachangiwa na watu wa diaspora. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hapa kwetu hata ukisema unahesabu haifikii hata 0.1 percent of GDP. Kwa hiyo, ina maana tunapoteza uwezo, lakini pia tunapoteza nguvu kazi ambayo ina uzoefu tofauti na wana-skill tofauti, ambayo wakija hapa wakiwa na uhuru wa kuja na kuondoka wataiacha hapa nchini. Kwa hiyo, nataka kusema kwamba mimi ninamuamini sana kwamba sasa kwenye Wizara hii tumepata watu Mheshimiwa Mbarouk na Mama Mulamula naamini hawa watatufanyia kazi nzuri sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwenye suala zima la diplomasia ya kiuchumi ambalo limezungumzwa na wengi. Mimi ningesema hivi, hauwezi kuwa na Balozi ambazo hazina wafanyakazi wa kutosha, tunataka Balozi ziwe na wanamasoko, zamani ilikuwa ni trade attachees, wanakaa kwenye Balozi kazi yao ni kuzunguka na kuangalia ni nani anawekeza, nani mwenye interest, nani anauza nini kwenye masoko yale na kuunganisha watu wetu na wale watu kule pamoja na wawekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi nataka niombe kwamba tusiseme tu kwamba tunapeleka mabalozi wazuri tupeleke pia wafanyakazi wa kutosha kwenye Balozi hizi na tusifungue tu Balozi nchi kama China jamani unakuwa na Balozi moja kwa nini usifungue consul nyingi miji mingi kule Thailand, miji hata mitano tukawa na consulars. Tukiwa na hizo ofisi ndogo ndogo za Balozi, zitakuwa na watu ambao sasa sio tu wanadiplomasia, sasa hivi tutawapeleka watu ambao watasaidia kwenye mambo ya masoko, kwa sababu masoko yako Guangzhou yako na sehemu nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwamba nimeona mmefungua Ofisi ndogo kule Mumbai, tufanye zaidi China jamani ni Taifa la kimkakati, lakini yako mataifa mengine kama Marekani, Uingereza pengine Ujerumani na wapi pia ni ya kimkakati basi tufanye mbinu ya kuongeza presence yetu kwenye hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kingine ambacho ningeomba kuzungumzia ni issue ya ushirikishwaji wa wafanyabiashara kwenye safari za viongozi wetu. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwamba alivyoenda Kenya juzi hapo alianza kutuonesha mfano mzuri kwamba anachukua watu waliochujwa, wafanyabiashara waliochunjwa kutoka TPSF pamoja na may be CTI pamoja na Mawaziri. Lakini ukweli ni kwamba, wakienda wenyewe hawa wafanyabiashara wanakuwa wanajua na watakuwa wamelenga na wanaunganishwa na watu ambao wataleta uwekezaji haraka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu kila mtu atataka mbia, wewe ukiwa hapa ndani ukitaka kuanzisha biashara kubwa ni lazima uwe na wabia kutoka sehemu hizo na mimi ninaamini hili linakuwa na tija na ninaomba kwamba liendelezwe sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine ni kwamba tumeona pia kwamba mmejaribu na ninawapongeza sana Wizara, kusema ukweli nawapongeza Wizara kwa sababu wamejaribu kuunganisha wajasiriamali kwenye maonesho ya viwanda nimeona kuhusu China na NMB wameweza ku-sponsor, wameweza kutoa ufadhili kwenye jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nafikiri hili ni jambo la kuomba sana kwamba liendelezwe, lakini na mabenki mengine au na wafadhili wengine hata wabia wenyewe watu wa maendeleo tuwaombe waweze kuchukua vijana wetu kwenda kuona, kwa sababu kuona ndiyo kuelewa na ndiyo kuamini. Kule China viwanda vidogo vidogo vimejaa na bei zake ni bei chee kabisa, unaweza kununua kiwanda kidogo cha shilingi hata laki tano ukaja nacho hapa ukachakata vitu, ukatengeneza fedha, ukawa tajiri, tena tuna umeme. Kwa hiyo naamini kwamba, tukiwapeleka wale vijana kule wakiona hata wale wanaofanya kama mashamba wataunda vitu ambavyo ni demonstration tukiwapeleka wale wachache, lakini watakuja kuwaonesha wenzao kwamba ni possible kufanya vitu vikubwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, lakini kingine ni ujenzi wa maofisi ya Balozi ambapo ni vizuri tujenge, nimeona kwamba wanamkakati wa kujenga hizo ofisi, nilikuwa nasema kwanini tusitumie mortgage financing kule? Bei ya mkopo kule Marekani au Uingireza nchi nyingi bei ya mkopo riba ni asilimia mbili na hususan ya mortgage. Tunaweza tukachukua mortgage zile na kwa sababu hatuna mtaji wa kutosha wakati huu kwa sababu tunawekeza kwenye miradi ya kimkakati basi tunaomba mkopo kwenye benki ya kule, tunachukua mortgage ile fedha tunaipeleka Balozi kwa pango ikatumika kama ni fedha ya kulipa mortgage na baada ya miaka siyo zaidi ya 10, 20 mnakuwa mmeshalipa mortgage, nyumba ni yenu na hamjatoa fedha yoyote. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna wakati mimi nafurahi kwamba NSSF walitaka kufanya vile, lakini ilikuwa pia siyo nadharia nzuri, kule mortgage ni kitu straight forward. Kwa hiyo, tunaweza tukafanya, tukakopa kwenye benki kule balozi ikajengwa wakakaa lakini wanajipa ile mortgage kwa fedha ya pango. Hata wafanyakizi wa balozi wanaweza wakafanya vile. Naomba sana hilo lizingitiwe kwa sababu naamini litaweza kuleta tija. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, la mwisho, ninataka niseme kwamba, nimefurahishwa sana na nilivyosoma kwamba kwenye taarifa ya utekelezaji ya mwaka uliopita, wameweza kufanya vitu vingi, miradi mingi ambayo wemeweza kuhamasisha kutoka kule na nikasema kwamba kweli Wizara hii imechangia vizuri na ninawapongeza kwa sababu huu ulikuwa ni mwaka mgumu sana ni mwaka wa ku-survive, lakini bado tunaweza kupata miradi, tunaweza kupata ufadhili wa kutosha kutoka kwenye nchi mbalimbali na tunaweza kupata wawekezaji.
Mimi nawapongezeni na ninaamini kwamba kweli tukitia nguvu kwenye Wizara hii basi uchumi wa kati wa kipato cha juu unaweza ukafikika kwa kipindi ambacho tunataraji. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2023
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa ya kuchangia kwenye hoja hii ambayo inahusu Muswada wa Sheria ya Fedha. Mimi pia ni Mjumbe wa Kamati ile ya Bajeti, na kwa hiyo kilichosomwa na Mwenyekiti wetu, Mheshimiwa Daniel Sillo, ni jambo ambalo naafiki na ni zuri sana, na tulichambua kwa kina sana na ninaamini kwamba watu hawatakuwa na mengi sana ya kusema kwa sababu huu ni Muswada ambao ni mzuri.
Mheshimiwa Spika, na niseme hivi; kabla sijaenda kwenye Muswada huu kabisa niseme kwamba lazima tuipongeze Wizara ya Fedha na tumpongeze Mheshimiwa Rais wetu kwa kutuletea bajeti miaka hii ya kwake ambazo zimeboreka kwa kuongeza usahihi wake na uhakika wake.
Mheshimiwa Spika, Benki ya Dunia imetoa vigezo vya kuweza kupima budget reliability ambao ni uhakika na usahihi wa bajeti. Na uhakika huu unapimwa kwa kuangalia nakisi inajitokeza katika makusanyo ya mapato ukilinganisha na ile ambayo tulikuwa tumepitisha kwenye bajeti.
Mheshimiwa Spika, utaoa kwamba katika mwaka 2017/2018 nakisi ilikuwa asilimia 16 ya mapato tuliokisia kwenye bajeti hayakupatikana. Mwaka uliofuata 2018/2019, nakisi ilikuwa asilimia 11, pungufu ya mapato tuliokusanya ukilinganisha na bajeti ambayo tulitegemea.
Mheshimiwa Spika, utaangalia kwamba baada ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingia kwenye madaraka, nakisi hiyo ilipungua kutoka asilimia hizo nilizosoma na kufikia asilimia sita tu. Niseme hivi; katika mwaka 2021/2022, sasa ukiwa mwaka ule ambao alishika hatamu kwenye kutengeneza bajeti hii hapakuwa na nakisi, tulikusanya mapato asilimia mbili zaidi ya tulizokadiria kwenye bajeti; hili jambo huwa halitokei sana, kwamba unakusanya zaidi kuliko ulivyokisia. Ninataka tuipongeze sana Wizara kwa sababu ina maana kwamba makisio yao yamekuwa ya uhakika na usahihi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naamini pia kwamba muswada huu tunaokwenda kupitisha kuwa Sheria ya Fedha ya mwaka 2023/2024 utakuwa hivyohivyo, kwamba tutaona makisio haya yatapitwa katika ukusanyaji na ina maana kwamba kweli tumeweka mikakati ya kukusanya na viwango vya kodi ambavyo tumeweka viko realistic kidogo. Na ninaamini kwamba hiyo itakwenda kutokea na ndiyo sababu tunaunga mkono mapendekezo yaliyoletwa na Wizara baada ya kutoa maoni yetu na wakakubali maoni yale na wakaenda kuyatekeleza kwenye marekebisho waliyoleta.
Mheshimiwa Spika, niseme kwamba tulikuwa tunaimba sana issue ya budget calendar. Kalenda ya budget tulikuwa tunasema ni njia pekee nzuri ya kuweza kumhakikishia mwekezaji kwamba makisio yake ya kweli atakayolipa ndani ya kipindi fulani hayatabadilika badilika. Na naamini kwamba sasa Wizara na Serikali ya Samia Suluhu Hassan imekubali kwamba sasa tuingie kwenye mchakato huo na wameanza sasa kwa vitendo kutengeneza mikakati ya kukusanya kodi ambayo inatupa predictability na naamini kwamba hiyo itaweza kuongeza pia wawekezaji ambao wataona ukweli kwamba sisi tunaweza tukakaa miaka mitatu bila kubadilisha badilisha hizi kodi mbalimbali.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, hilo ni jambo la busara limefanyika, na tunalishangilia sana kwa sababu ni jambo ambalo Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania pia walikuwa wanalifuatilia sana kwenye Kamati yetu.
Mheshimiwa Spika, kuna vitu kwa mfano ambavyo wamerahisisha, na kodi zilizo rahisi ni zile ambazo zinaeleweka za wale walipa kodi na pia yule mkusanyaji wa ile kodi anaelewa vigezo ambavyo viko straightforward. Na hilo ni jambo ambalo limeanyika.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano hili la wachimbaji wadogo wadogo ambao ni vigumu sana wao kutengeneza accounts zao, kubadili statements zao, na kuweka risiti zao na kuweza kuwasilisha kwenye mamlaka zinazohusika. Wamerahisisha kwa kusema kwamba sasa watalipa tu asilimia mbili wakishalipa hiyo ni mwisho, hawatalipa kitu kingine na Serikali haitawafutailia, na ninaamini kwamba compliance itakuwa kubwa na tutaona ongezeko la mapato yetu kutoka kwenye maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, pia tunaona kwamba kuna bidhaa, na ugumu wa kuanza mchakato wa kutengeneza bajeti kwa kuzingatia predictability, ni suala zima la kwamba unapoanza huu mchakato unakuta kwamba miaka mitatu hutaongeza. Kwa hiyo, inakuwa kwamba sasa ili uweze kulinda thamani ya fedha, kulinda thamani ya makusanyo yako, lazima u-predict na uweze ku-fight a lot sehemu ya hiyo sheria za zamani ya ile … itakayofuata katika miaka hiyo. Kwa hiyo, ndiyo sababu utaona kwamba kuna viwango vimeongezeka vikawa juu kidogo.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano kuna bidhaa ambazo sasa zimeongezeka kwa excise duty ambayo itakuwa ni asilimia 20 kwa sababu zilikuwa tu hazijafanyiwa marekebisho kwa miaka mitatu iliyopita. Kwa mfano bia, watu wanazinywa lakini ukweli ni kwamba tulihoji sana lakini baadaye tukaona kwamba kwa sababu miaka hii mitatu inayokuja hawatakuwa na fursa ya kubadilisha hivyo viwango, basi kwa kuanzia kulinda thamani hiyo basi tukubali kwamba rate, hicho kiwango kiongezeke kwa staili hiyo ya asilimia 20.
Mheshimiwa Spika, kuna bia na vinywaji vingine lakini naamini kwamba ni kitu ambacho ni busara na kwamba tuelewe Wabunge wote tunaposimama hapa tunatafuta miradi ya maendeleo na tunapata. Sasa tuelewe pia hiyo inaashiria kwamba ni lazima tukubali pia kodi zikusanywe, kama Mheshimiwa Waziri alivyokuwa anahimiza, na ziongezwe kodi mpya ili ziweze pia kuchangia katika miradi hiyo ambayo inakwenda kuboresha mazingira ya biashara na mazingira ya uzalishaji katika maeneo yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naamini hilo ni jambo ambalo pia wananchi watalipokea kwa kuelewa kwamba hatutabadilisha kwa miaka mitatu ijayo lakini pia ni sehemu yetu sisi wananchi kuchangia na maendeleo tunaona nchini mwetu.
Mheshimiwa Spika, kulikuwa na utata kidogo kwenye suala zima la bidhaa ya cement. Imeongezeka, tumeweka shilingi 1,000 kwa mfuko wa kilo 50. Lakini tumegundua kwamba kusema ukweli sisi bei zetu ziko chini sana ukilinganisha na bei zilizo kwenye masoko ya nchi jirani. Kwa hiyo, pia hiyo tukaona kwamba itakuwa ni vyema kwa sababu kiasi cha fedha ambazo tunatarajia kupata kwenye hicho chanzo ni takribani shilingi bilioni 200, kwa hiyo, ikawa ni vigumu sana kuigusa. Naamini pia kwamba hiyo ni njia moja wapo pia ya kusaidia hii cement ichangie, viwanda vichangie kwenye hiyo, na mengineyo.
Mheshimiwa Spika, kuna suala zima la tozo za miamala, hii sasa siyo tozo ya miamala lakini tulikuwa tumenuwiya kwenye Muswada wa mwaka jana tuliweka tozo kwenye airtime usage, matumizi ya muda wa maongezi kwenye simu. Sasa hiyo imetufurahisha kwamba sababu Mheshimiwa Waziri amefuta hiyo tozo, haitakuwepo. Ilikuwa kwenye sheria, haikuwa implemented lakini imefutwa na ninaamini kwamba wananchi watafurahia sasa kwamba tunajua kilichopo kwenye tozo hazitabadilika tena na mambo yatakwenda vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho sijui kwa nini najiskia kukuita Mwenyekiti, kumbe wewe ni Spika mkubwa sana na tunakuombea Mungu akubariki sana kwa sababu hata kule tunakoelekea utakuwa mtu wa kimataifa sana kwa hiyo, unastahili zaidi ya cheo hicho. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mwisho niseme kwamba sheria imejaribu kulinda wasanii wetu ambao wamekuwa wanaibiwa ubunifu wao na watu ambao ni wajanja ambao wanakuja wanachota nyimbo, wanachota maigizo halafu wanapeleka bila kulipa chochote. Kwa hiyo, nashukuru kwamba ili waweze kubana kila mtu anayeweza kufanya kitu hicho asiweze, wameongeza aina ya vifaa ambavyo vitalipiwa ule ushuru wa asilimia 1.5 na hivyo vifaa ni kama vile compact discs kama DVDs na CDs n.k., vimeongezwa pia. Kwa hiyo, sasa tunaweza kubana zaidi watu kuongeza huo mfuko wa kusaidia wasanii wetu ambao wanatupa burudani za kutosha na pia wanatangaza kimataifa.
Mheshimiwa Spika, upande mwingine nimefurahia pia kwamba unajua excise duty inalenga zaidi kuzuia au kupunguza uhitaji wa bidhaa fulani, kwa hiyo, hata kwenye sigara ambazo zinaletea watu madhara wameongeza pia sigara aina nyingine, kumbe kuna na electronic cigars, kuna shisha, wanaruhusu utumie lakini utalipia.
SPIKA: Kengele ya pili imeshagonga Mheshimiwa Dkt. Kimei.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
The Finance Bill, 2022
MHE. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii uliyonipa. Nianze kwa kusema kwamba mimi pia ni mjumbe wa Kamati ya Bajeti, kwa hiyo sitakuwa na mengi sana isipokuwa nitakazia mawili au matatu.
Mheshimiwa Spika, nianze kwa kukushukuru wewe kwa namna ambavyo umeendesha Bunge hili kwa kipindi hiki cha bajeti na kwa namna ambavyo umetuelekeza vizuri na kutulea hasa sisi ambao ni wapya kwenye Bunge hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kwamba nampongeza pia Mheshimiwa Rais kwa sababu naamini wote tumesikia hotuba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti namna ambavyo Waziri wetu Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba Madelu, kwa namna ambavyo alikuwa flexible na kukubali na kuwa tayari kurekebisha kama vile alivyoshauriwa na watalaam wake lakini pamoja na kamati yetu. Tunamshukuru sana kwamba kweli ameonyesha uelewa na naamini kwamba uelewa huu na utayari huo umetokana pia na Rais mwenyewe kukubali marekebisho haya yafanyike kwa sababu tunaelewa kwamba bajeti hii Rais ameweka mkono wake kwa nguvu zote. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, niseme kwamba pia nilipokuwa nachangia kwenye hotuba ya bajeti nilianza kusema kwamba Wizara ya Fedha imekuja na nadharia ambayo kweli ni bunifu kuelewa kwamba kuongeza kodi siyo njia pekee ya kuongeza mapato ya Serikali. Nadharia nzima ya Tax Calendar, calendar ya kodi inaendana na ukweli huo kwamba ukishaweka tozo kwenye kiwango fulani kikakaa kwa muda fulani kwa sababu kile kianzio kinakuwa kwa matumizi ya kile kianzio kuongezeka mwaka hadi mwaka namna ambavyo pato la Taifa linatarajiwa liongezeke in nominal term kwa bei za sokoni, basi utakuta kwamba na wewe hivyohivyo utakuwa unaongeza mapato yako bila kugusa kile chanzo.
Mheshimiwa Spika, kile chanzo kinakua kwa sababu ya confidence ya watu kuamini kwamba wanaweza wakaweka hesabu zao sawa sawa kwa sababu hakutakuwa na mabadiliko makubwa na pia wawekezaji kuongezeka kwenye eneo husika. Kwa mantiki hiyo, naamini kwamba tataanza kuona sasa kwa sababu bajeti hii haikuwa ya kuongeza kodi zaidi, ni bajeti ya kuboresha na kuweka mazingira ya wawekezaji kuona kwamba uchumi wetu unatabirika kisera, hasa Sera ya Bajeti ndiyo muhimu sana kwa upande huu, basi naamini kwamba uzalishaji utaongezeka na hivyo tutaweza kupata kodi kwa wingi zaidi, mapato ya Serikali yataongezeka kwa wingi zaidi sokoni na hivyo tutaweza kufikia malengo ya matumizi ambayo Serikali imejiwekea.
Mheshimiwa Spika, cha msingi kingine ambacho kimejitokeza hapa ni rekebisho lililopendekezwa kwenye Sheria ya Benki Kuu. Pendekezo hili limeongeza uwezo wa Serikali kukopa hapa ndani. Unafahamu kwamba mikopo ya Serikali inapoongezeka hapa ndani, kwanza uhimilivu wa deni la ndani siyo changamoto kama uhimilivu wa deni la nje. Uhimilivu wa deni la nje una changamoto ya kubadilika badilika kwa thamani ya fedha yetu. Unakuta kwamba nchi zote ambazo zinakopa ndani; na hata tunapokokotoa, kama tungekuwa tumekopa ndani kwa asilimia 100 hatungekuwa na tatizo lolote la uhimilivu kwa sababu tunajua kwamba hilo linalipika. Unaweza ukaamua hata kuchapisha hela ukalipa. Ndiyo maana nasema hilo la nje ndiyo changamoto.
Mheshimiwa Spika, ndiyo sababu nasema kwamba kusema kweli hii nadharia na pendekezo lililotoka kwenye Wizara yetu kwamba tubadilishe, tuongeze uwezo ule. Wakati ambapo pia utulivu wa uchumi mkubwa kwa upande wa mfumuko wa bei kwa muda mrefu umekuwa vizuri; inflation iko chini sana. Naamini kwamba hii itaenda kuchochea ongezeko la ukwasi kwenye uchumi na pia uwekezaji na pia inaweza ikapunguza kwa kiwango kikubwa ule ucheleweshwaji wa utekelezaji wa miradi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa sababu kama tunavyojua mtiririko wa mapato ya Serikali na matumizi ni tofauti. Sasa unapoipa Serikali mwanya kidogo wa kukopa fedha hata zile za muda mfupi ili itumie huku ikikusanya na kurejesha, basi hiyo inasaidia pia miradi ile ambayo tunapelekewa kwenye maeneo yetu iweze kutekelezwa ndani ya wakati badala ya kusubiri kwamba mwishoni mwa mwaka ndiyo tunaanza kuona fedha nyingi inapelekwa kule. Kwa hiyo, naamini na ninampongeza sana Mheshimiwa Waziri wetu wa Fedha kwa kulileta hilo.
Mheshimiwa Spika, ili uone kwa namna gani Serikali imejipanga kwa wale wengine ambao sisi tulichambua sana tumekutana na wadau wengi sana na tumechambua sana kwenye Kamati, na ninaweza nikawahakikishia Watanzania wenzangu kwamba bejeti ya wakati huu ni tofauti na itakuja kutekelezwa vizuri.
Mheshimiwa Spika, niseme tu kwamba kero zote au maoni yote yaliyowasilishwa na wadau yamezingatiwa na niseme kwamba, naamini sasa hivi kuna watu wengi wanafurahia na wanachekelea hususan suala zima la TASAC limepata ufumbuzi. Pale kwenye bandari yetu kwa mfano, Bandari ya Dar es Salaam siku zote imebaki ikilalamikiwa kwa kukosa ufanisi kwa sababu ya uwepo wa siyo tu tozo za TASAC, lakini pia ukiritimba ambao uliingizwa kwenye uondoaji wa mizigo kwenye bandari yetu kutokana na uwepo wa shirika hilo.
Mheshimiwa Spika, ni shirika zuri, lakini kwa vile yeye ni msimamizi, na tunaamini wazi kwamba ni vizuri ile biashara nyingine ambayo siyo nyeti, maana ile nyeti wamebakiziwa, lakini ile biashara ya mizigo ya kawaida iwe handled na Clearing and Forwarding Agency wengine.
Mheshimiwa Spika, nataka pia nipongeze kwamba katika suala zima la Charter Flights, tunamshukuru Waziri alikaanalo sana, lakini baadaye alikubali kwamba lisitishwe kidogo, lisogezwe applicability yake iwe ni miezi sita ijayo. Pia bado naamini kwamba kusema kweli kwa namna ambavyo tunakimbizana na Royal Tour na utalii kuwa ni sekta muhimu sana, naamini kwamba ili tuweze kushindana na wenzetu majirani ambao wao wamekwenda mbali na walikuwa wameshika nafasi kubwa katika soko hili la utalii, inaweza pengine baadaye Waziri akaja akaridhia kwamba tuendeleze hata kwa mwaka mzima tusiweke VAT kwenye Charter Flights Services ili wale watalii wanaokuja na kukaa kwa muda mrefu zaidi nchini kufanya hunting (kuwinda) nasikia wanakaa mpaka siku 21, wale wengine wanaokuja, wale wadogo wadogo wenzangu, wanakaa siku nne sana sana on average.
Mheshimiwa Spika, sasa hawa wanaokuja wanakaa muda mrefu wakachukua Charter Flights zetu kwa bei ambayo haina VAT, tutaona kwamba matunda ya Royal Tour tunayozungumza yataonekana kwa uharaka na kwa ukubwa zaidi. Kwa hiyo, naendelea kusihi Serikali iangalie hili kwa sababu sekta imeanza kufunguka na sisi tumeanza kuona matunda ya Royal Tour na tumeweza kuona kila mtu anafaidi kwenye mnyororo mzima wa sekta hii ya utalii.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba kwamba Waziri aendelee kuliangalia. Namshukuru sana kwamba amekubali lisogezwe lakini naamini kwamba baadaye atakavyozidi kuona mapato yanaongezeka kutoka vyanzo vingine vya sekta hii, basi atalisitisha kabisa mpaka pengine baada ya mwaka mmoja au miwili. Aliwekee kalenda ndefu zaidi, kalenda ya miezi sita haitoshelezi.
Mheshimiwa Spika, naomba niunge…
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Spika, taarifa.
SPIKA: Mheshimiwa Kimei, kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Kwagilwa.
T A A R I F A
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa fursa hii nimpe taarifa mzungumzaji kwamba baada ya ile shughuli ya Mheshimiwa Rais ya Royal Tour takwimu zimebadilika sana. Mwaka 2021 mwezi kama huu tulikuwa na watalii 43,966. Hivi tunavyozungumza tuna watalii 79,405. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, tafsiri yake ni kwamba watalii hawa 79,000 wakiwemo wawindaji, wengi wao wanatumia ndege zetu hizi. Tukichaji VAT tutawa-discourage kuja. Tujitahidi sana tui-wave out hii VAT kwenye ndege ili waweze kuja kwa wingi. Kwa sababu tusipofanya hivyo watatumia ndege nyingine kwa mataifa mengine kwenda sehemu nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei, unaipokea taarifa hiyo?
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naipokea kwa mikono miwili taarifa ya Mheshimiwa Reuben Kwagilwa, ni taarifa nzuri na hizo takwimu ni sahihi na ninaamini kwamba zitazidi kuongezeka kwa sababu kasi ni kubwa sana. Kwa sisi ambao tumepita kwenye hoteli tukafanya survey kidogo, tunaambiwa kwamba hoteli zimekuwa booked kwa miezi mitatu yote ijayo zimejaa.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naamini Mheshimiwa Waziri atapata fedha nyingi zaidi na pia atapunguza uwekezano au umuhimu wa kutoa ruzuku yoyote kwa taasisi hizi ambazo zinashughulika na sekta hiyo kama tulivyotoa miaka iliyopita. Fedha hiyo itaingia kwenye bajeti kwa sababu zile sekta, hoteli na Ngorongoro Observation Unit na TANAPA na wenyewe sasa watakuwa wanajitegemea na pia kutoa gawio lao la kutosha kwa Serikali.
Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa kushukuru tena, naunga mkono hoja.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
The Prevention and Combating of Corruption (Amendment) Act, 2024
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa fursa. Naomba nianze kwa kumpongeza Rais wetu kwa kuleta sheria hii ambayo ni Sheria ya Kimataifa. Kusema ukweli ni mambo ya kupambana na ugaidi au kupambana na rushwa, ni mambo ya Kimataifa na yanatakiwa yazingatie viwango vya Kimataifa ambavyo vimekubalika kwenye mashirika yetu ya Kimataifa, United Nations na mahali pengine. Kwa hiyo, tunamshukuru sana kwa kuleta hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Waziri wa Utawala Bora na Utumishi kwa kuleta na kuiwasilisha vizuri Sheria hii ya Kupambana na Kuzuia Rushwa. Kabla sijaendelea zaidi, pengine ingekuwa ni sahihi kuwapongeza Mawaziri wote wapya waliochaguliwa na Mheshimiwa Rais, ni Mawaziri Wazuri, tunawaombea Mungu na wale waliobadilishwa Wizara zao, nao pia tunajua kwamba Mheshimiwa Rais ameona kwamba wanaweza wakatumika vizuri zaidi kwenye maeneo ambayo amewapeleka. Kwa hiyo, nawapongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza pia Mwanasheria Mkuu kwa kuwasilisha vizuri hili wasilisho la Marekebisho kwenye sheria nyingine ndogo ndogo. Nakushukuru na wewe kwa jinsi ambavyo unatuendesha, unatuongozea Bunge letu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kusema hivi kwamba, dhana ya Sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa nchini ni kuwafanya wananchi waogope, wajue kwamba wakijiingiza kwenye masuala yoyote ya rushwa, kwenye mnyororo wowote unaowapelekea rushwa, watachukuliwa hatua nzito ambazo zitawafanya wajute, pia zinawaingiza kwenye uwoga kwamba nisifanye. Ndiyo maana inasema ni kupambana na kuzuia.
Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi sheria hii siyo kwamba ni kuadhibu, ni kuhakikisha kwamba hivyo vitu havitokei. Kwa sababu, by the time vinakuja kutokea, nchi inakuwa imejiingiza kwenye hasara kubwa, kupoteza thamani ya fedha inayoenda kwenye miradi na mambo mengine.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nasikitika kwamba kusema kweli ili watu waogope lazima waone kwamba sheria ile na vile vigezo vilivyoko kisheria vinatumika kuwaadhibu na kwamba kuna ukweli watu wanashikwa na wanafungwa, wanatozwa na hata kama ikilazimika sheria iwe imeweka viwango vikubwa vya adhabu, kwa sababu kigezo cha kuogopa sheria pia ni kiwango cha adhabu.
Mheshimiwa Naibu Spika, ukisema hapa unaenda kumfunga mtu miaka miwili, siyo adhabu ambayo inatisha sana. Miaka mitatu haitishi, miaka mitano haitishi, miaka inayotisha ni miaka 30 lakini inayotisha zaidi ni kifo. Tukisema kwamba mtu ukishikwa umejiingiza kwenye rushwa unaenda kuuawa, kuna nchi zimefanya hivyo, nafikiri kama China, ukishikwa mtuhumiwa ni kifo. Kwa hiyo, watu waliogopa kabisa, sasa hii kupambana kwetu unaona kunaishia chini huku.
Mheshimiwa Naibu Spika, nasikitika kwamba ile taasisi yetu TAKUKURU katika miaka yote hii kuna mambo mengi yametokea, lakini sijasikia mtu amepelekwa Mahakamani au sijasikia mtu amechunguzwa kwa sababu ameonekana anajilimbikizia mali kwa wingi na haijulikani kwamba anapata wapi hizo fedha kwa sababu tunajua kiwango chake cha mshahara na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, vitu vinatokea, lakini hatuoni kinachotokea. Kwa hiyo, mwananchi ataogopa nini? Hata ukibadilisha hii sheria leo, kama hakuna kitakachotokea, mtu atajua aah, hata nikifanya, pengine ile ile hela ambayo nimepata rushwa ndiyo nitaitumia hiyo hiyo hela kuniokoa. Kwa hiyo, inakuwa haitishi.
Mhehsimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nataka niseme kwamba, kitu cha kwanza ambacho sheria inatakiwa ije i-address na iangalie ni viwango na watu kuona kwamba kweli ile taasisi inayoshughulika inafanya kazi yake na adhabu zinatolewa na hizo adhabu zinatisha. Kwa hiyo, naomba wenzetu wa TAKUKURU waanze sasa kuwa wakali, waanze kushughulika wakijua kwamba wanalinda maslahi ya nchi hii na ndiyo njia pekee.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba, kwa mfano miaka yote hii ambayo hatujasikia toka waanzishe ile Mahakama inayoitwa ya Mafisadi, ile Mahakama sijui imeishia wapi sasa. Hakuna! (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, issue inayotokea ni kwamba, kama watu hawajasikia wanasema, hakuna kitu bwana. Wanaendelea tu kama business as usual. Aidha, watuambie kwamba hakuna rushwa, rushwa imepungua sana, lakini mimi nitasita kukubali kwani rushwa ipo, inaendelea na tunawajua watu wetu. CAG anaonyesha mifano mingi au matukio mengi ambayo unaweza ukayahusisha na rushwa, lakini pia wale wa nje wanaotutathmini sisi watasema hii nchi iko juu sana kwa kiwango cha rushwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba tuchukue hilo na tujaribu kulifanyia kazi na kwamba hata kwenye huu Muswada ambao marekebisho yanakuja, tunaona adhabu ime-range kati ya shilingi milioni tatu mpaka 20 maximum, ndiyo ninaona huko, hamna mtu anayetozwa shilingi milioni 100, hamna. Halafu isipokuwa ile advantage wanasema ni value advantage lakini ukweli ni kwamba, vifungo navyo ndiyo hivyo miaka miwili mpaka miaka 10 sana sana. Kwa hiyo, hiyo bado haijawa na makali ambayo yanastahili.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni vizuri watu waelewe kwamba, mtu anapokuja kushikwa kwamba amepokea rushwa au ametenda vitendo vya rushwa ya ngono, ni kwamba anakuwa ameshatenda mara nyingi, yaani unamshika mara moja lakini akiwa mtu ana hiyo tabia, kwa sababu rushwa ni tabia, kwa hiyo, mtu ameianza siku nyingi, halafu siku anayoshikwa ni siku ya 40 ndiyo anakamatwa. Kwa hiyo, basi ahesabiwe kwamba huyu mtu tumemshika, lakini amechukua nyingi kiasi gani katika kipindi hiki cha miaka hiyo 40, au miezi 40 au siku 40 au miamala 40. Kwa hiyo, atozwe na aadhibiwe kwa kusema okay, tumekushika kwa hili, lakini wewe tabia yako ilikuwa ni hii na kama kweli ni mtu ambaye amechukua rushwa ya ngono, basi atakuwa ametembea na wanawake 40 akawapa vyeo. Kwa hiyo, naomba sana turudie kwenye hiyo ili tuweze kufanya kitu ambacho kitatusaidia kuogopesha watu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana sana na wale wanamtandao wanaopinga rushwa ya ngono. Wamesema huwezi kulinganisha yule mwanamke ambaye ameshawishiwa kutoa rushwa ya ngono ukasema naye ana dhambi. Kwa hiyo, naye lazima aingizwe kwenye ule mtego.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nasema hivi, unajua ni kama binadamu. Sisi binadamu ni subjects wa shetani. Shetani anakuja anatushawishi kila siku, anataka tufanye dhambi. Sasa sisi tuna maamuzi ya kusema tunataka tufanye ile dhambi au tusifanye. Kama tukienda na ushawishi wa shetani, mtu anayepata dhambi siyo shetani, ni wewe. Sasa, wewe ndio mwenye mamlaka, umemshawishi au haujamshawishi mwanamke au mwanaume the other way round ukafaya mambo hayo, ina maana kweli kwamba hatuwezi kumhusisha yule ambaye ameshawishiwa? Yule aliyeshawishi hatuwezi kumwingiza kwenye mtego. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, shetani anabaki hana dhambi, wewe unabaki una dhambi na kwa hiyo, subject ni mwenye mamlaka na mtu anayetakiwa ashtakiwe ni yule mwenye mamlaka, siyo yule ambaye amelazimishwa au amefanya kwa namna ile, anajikuta kwamba amejiingiza kwenye haya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninashauri hivi, ili kuweza kuonyesha ni kitu gani kinafanyika kwenye suala zima la rushwa, tujaribu kuomba mamlaka. Ile Ripoti ya TAKUKURU inayokwenda kwake ya mwaka kama ile ya CAG, basi ije kwenye Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ili waijadili na waonyeshe watu kwamba tunapokea na katika mwaka huu kuna kesi za namna hii za rushwa zimepatikana na watu wamepata adhabu hizi na Bunge tumesikia na watu wakaanikwa, kwa sababu ukifichaficha haisaidii kwenye mambo haya ya rushwa. Njia tu ya kupunguza ni hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukirudi kwenye Muswada, mimi ninafikiri kuna neno moja linaitwa instrumentalities Section number seven na number eight zipo na maeneo mengine kwenye Muswada huu imetumika, lakini kusema ukweli ni watu wachache wanaelewa instrumentalities hizo ni nini? Ni kitu gani? Kwa hiyo, tunaomba hiyo iwe defined.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia kwenye maeneo mengine mengi tunaona kuna issue hii ya advantage; thamani ya advantage ambayo mtu amepata kwamba, kama kwa mfano mtu umepandishwa cheo bila kustahili kwa sababu umetoa ngono, ina maana kwamba kuna advantage.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hapo utai-measure namna gani na advantage ya mtu ambaye amepata cheo kwa kutumia rushwa ya ngono au kitu kama hicho? How do you measure it? Yaani inaacha mwanya mkubwa sana na discretion kubwa sana kwa yule Hakimu atakayeamua, yaani inampa discretion ambayo haina mwisho.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nafikiri pengine tujaribu zaidi ku-define hiyo advantage itakuwaje? Itakuwa kwa sababu kitu kama kile ambacho kusema kweli advantage uliyopata unaweza ukai-measure kwa mwaka mmoja, kwa mshahara wa mwaka mmoja ulioongezeka, unaweza uka-measure kwa miaka 10 ijayo ukafanya net present value ukasema wewe hii kazi uliongezewa cheo kwa sababu ulitumia ngono, basi unapiga Net Present Value ya lile ongezeko ambalo amepata.
Mheshimiwa Naibu Spika, lazima uji-define better ili mtu ajue ni kitu gani unazungumza unaposema kwamba, ni thamani “advantage.” Kwenye upande wa election, narukaruka kwa sababu, naona muda unakwenda. Upande wa election, wanasema ni rushwa kwenye election, kwenye chaguzi na wanasema election ni process. Hebu niambie process ya uchaguzi inaanza lini?
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi kule majimboni kwetu wanapita watu wanashawishi watu kwamba wawe kwenye timu zao, wanahonga. Sasa election process haijaanza kwa sababu, tume haijatangaza. Sasa mtu huyo utamkamata kwa sheria hii, ni jambo gumu sana. Lazima u-define process ya uchaguzi inaanza lini na inaisha lini?
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tungeomba ninyi wanasheria mwangalie, mweze ku-define kwa sababu, kweli uchaguzi kabla mchakato haujatangazwa na tume kwamba unaanza unakuwa haujaanza, lakini watu wameanza, watu wanaanza mapema, wanatoa vishawishi vingi.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lingine ambalo nimeliona hapa kwenye hii sheria ni kwamba ime-define vitu vingi, ila haijasema ile takrima. Zamani kulikuwa na mjadala ulipita Bungeni hapa, unatofautisha rushwa na takrima. Sasa kwenye hii takrima inaanzia wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi niliitisha mkutano pale kwenye Jimbo langu la Vunjo, watu hawaji kama hawajui kwamba nitatoa mbege kidogo, wanaita kitochi. Kama hamna kile, utapata leo watu 200, kesho utapata watu 20. Kwa hiyo, lazima kuwe na hiyo takrima. Sasa watu wengine wanaogopa kabisa.
Mheshimiwa Naibu Spika, yaani, nilivyokuwa nafanya kwenye mikutano yangu, nilikuwa naogopa kabisa kuwapa watu mbege kidogo au maji. Kuna wengine hawanywi. Kama wale waislamu kule kwenye upande wangu wa tambarare wao hawanywi, wanakunywa maji. Sasa ukiwapa maji, ukawapa mbege inakuwa mambo mazuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa nini hamja-define vizuri huku ikaeleweka kwenye mambo yale…
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
NAIBU SPIKA: Ahsante Mheshimiwa Dkt. Kimei. Muda wako umekwisha.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maliasili na Utalii
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa fursa ya kuchangia kwenye Wizara hii muhimu sana kwa Jimbo letu na kwa Mkoa wetu wa Kilimanjaro. Nawashukuru na nawapongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na Katibu Mkuu wake kwa kuwa wenye mwamko chanya katika kushughulika na matatizo yetu kwenye mikoa yetu hasa sisi ambao tunapakana na hifadhi na tunasimamiwa na TFS ambayo imekuwa inanyanyasa sana watu.
Mheshimiwa Naibu Spika, nitaanza kuzungumza jambo moja hili la nusu mile na natumaini limezungumziwa vizuri sana, nusu mile ni kitu ambacho kwetu kinatuuma kwa sababu kama mnajua kwamba ardhi yetu kule Kilimanjaro ni ndogo, lakini pia ukiwa unapakana na msitu huu unaozunguka Mlima Kilimanjaro unakuta kwamba fursa iliyopo ni kuokota kuni, kukata majani, kuweka mizinga ya nyuki na kadhalika. Mwanzoni tuliruhusiwa kuingia hadi nusu mile hiyo, lakini baadae TFS wakang’ang’ania kuchukua hata eneo hilo, walikuwa wanaturuhusu hata angalau wanawake waingie kukata kuni na kuchukua majini, lakini sasa hawaruhusiwi. Naomba hilo jambo lifikiriwe na nimeshazungumza pamoja na Mheshimiwa Waziri na Katibu Mkuu, naamini kwamba litakwenda vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nazungumzia kuhusu stimulus package kwa sekta hii muhimu ya utalii. Naamini kwamba wengi wanaelewa jinsi ambavyo watu wameathirika; mahoteli yameathirika, hayajatengeneza fedha, yametengeneza hasara kwa muda mrefu na hawa tour operators pia wametengeneza hasara. Hivyo nafikiria itafaa kujua ni namna gani ya kuweza kuwanusuru kwa kuwapa muda kama wana mikopo, kama wana tozo wanadaiwa kwenye vitalu au kwenye maeneo yao wanayoshughulika nayo, Serikali iweze kuona ni namna gani ya kuwanusuru kwa kuwapa muda mrefu wa kulipa au kuwasamehe kwa maeneo mengine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme pia kwamba kuna tatizo baada ya hilo na kama ikiwezekana naamini linawezekana kama tukilifikiria vyema, tukijua hii ni sekta muhimu.
Mheshimiwa Naibu Spika, tatu ni issue ya tour operators; niliwahi kuzungumza kuhusu tour operators hapa. Tour operators wameunda jumuiya yao kule kwetu Kilimanjaro kupandisha watalii mlimani. Wameunda hii jumuiya ili kui-serve na kui-regulate; waweze kujiwekea discipline na namna gani wanapandisha watu na nidhamu katika kushughulikia watalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hawa walikuwa wanafikiri kwamba ni vizuri ili waweze kujadiliana vizuri malipo yao na tour operators waweze kupata au waweze kupewa fursa ya kujadiliana na wawekezaji wa tour operators na pia kujichagua wenyewe nani anapandisha huyu kwa vile anajua Kiswahili, Kifaransa na kadhalika. Kwa hiyo tunaomba kwamba tour operators wapewe mwongozo huo wa kutumia jumuiya hiyo ili waweze kupandisha watu/watalii mlimani wakiwa wamekaa vizuri na mtalii.
Mheshimiwa Naibu Spika, watalii hawarudi kwa sababu hawawi-treated properly, lakini wakitumia jumuiya hiyo ambayo ni wataalam watawaweza wakawa-treat na wale ambao wanafanya mambo ambayo siyo ya kinidhamu, wakashughulikiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, mwisho, ni suala zima la utalii wa vivutio vya kiasilia. Watu wanasema kwamba kivutio cha kiasilia hapa Tanzania ni Mmasai tu, kumbe kuna vivutio vingi, kuna mahandaki, kule kwetu Mamba, Komakundi kuna mahandaki ambayo ukiingia utashangaa, utafikiri upo mahali tofauti kabisa, kule Tanga - Amboni; sio Amboni, watu wamechimba kujificha wakati wa vita, kuna mengi ya namna hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi pia kuna vivutio kwa mfano, namna watu walivyokuwa wanafua vyuma asilia, uhunzi kule kwetu watu wanafua, wanatumia namna ambayo ni teknolojia ambayo ni ya kizamani lakini watalii wakiona wanashangaa ni kitu gani kinafanyika. Kwa hiyo, nashauri, tusing’ang’anie tu hifadhi ya misitu, hifadhi za wanyama na kadhalika, tuanze sasa kuunda kitengo maalum ambacho kitashughulika na vivutio asilia, vitangazwe na viorodheshwe, ni wapi utaona nini na wapi utafanya nini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.
Mheshimiwa Spika, nimewasikiliza wenzangu vizuri sana lakini kabla sijasema hapo, nitumie fursa hii pia kumpongeza Waziri, Naibu wake, Katibu Mkuu na uongozi mzima wa Wizara.
Mheshimiwa Spika, lakini pia tumpongeze yule aliyekuwa anashikilia Wizara hii, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, ambaye aliweza kusimamia Ilani ya CCM tukaweza kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati na tukapata ushindi sisi tunaoingia sasa kama Wabunge. Naona ni vigumu sana kujua walifanyaje wakaweza kutekeleza miradi hiyo na hali kwamba deni letu likabakia bado himilivu.
Mheshimiwa Spika, mimi nilikuwa najua kwamba bajeti ni sheria, lakini naamini hii ya kwetu siyo sheria, kama inatungwa bajeti tumekaa hapa miezi mitatu tunatunga bajeti hapa halafu tunaambiwa imetekelezwa kwa asilimia 50; nani anashikwa, nani anapelekwa kortini? Nani anawajibika kwa hilo? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nafikiri lazima sisi wenyewe tujue kwamba sisi ndio tunatakiwa tuwajibike pengine kwa sababu hatukuweza kuisimamia Serikali ikaja na bajeti ambayo inatekelezeka kwa asilimia mia moja, ahadi zinazotolewa hapa zikatekelezwa kweli. Wewe utaahidiwa mradi lakini mradi hautatekelezeka kwa sababu kama mapato hayatapatikana hatutapata hiyo miradi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nina shaka sana kwa sababu tunajua kwamba kazi kubwa ya Wizara ya Fedha ni kutafuta mapato, matumizi tumeshajua, kwa hiyo ni kutafuta mapato yatakayokidhi utekelezaji wa bajeti ile. Sasa mapato yanatokana na kodi au kukopa.
Mheshimiwa Spika, sasa nafikiri sana Waziri achakarike aanze kutafuta mikopo, siyo ya ndani. Naona wenzetu alipokuwa Mheshimiwa Msuya alikuwa kila saa yuko nje anatafuta fedha za kuweza kutekeleza bajeti, siyo lazima upate yote ndani, na ukipata yote ndani ndiyo inasababisha haya mambo tunayoona sasa kwamba mwenzangu anasema kwamba riba ziko juu sana.
Mheshimiwa Spika, bahati mbaya amesema kwamba Benki Kuu ndiyo inapangia benki viwango vya riba, lakini Benki Kuu kusema kweli haipangii mabenki viwango vya riba isipokuwa wanakuwa ni waelelezaji kwa zile riba ambazo wanatoa kwa dhamana za Serikali.
Mheshimiwa Spika, nimeona kwenye bajeti ya Mheshimiwa Waziri hakuna ongezeko la mshahara, badala yake mishahara inapungua… lakini nataka niseme kwamba pengine ni muda sasa wa kufikiria ongezeko la mshahara kwa wafanyakazi wa Serikali. Kwa sababu ni miaka mitano na … tulisikia Mheshimiwa Rais akisema kwamba ataona namna, lakini kama hatujaingiza kwenye bajeti inakuwa kwamba ni matatizo. Hakuna Wizara hata moja iliyoonesha kwamba kutakuwa na ongezeko la mshahara, na mimi nataka Waziri wa Fedha aliangalie kwa upya aone litafanyikaje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, katika kupunguza makali ya utekelezaji wa miradi yetu, naamini kwamba Serikali inatakiwa kuangalia upya msimamo wake wa kurejesha kwa Msajili wa Hazina yale mashirika yaliyokuwa yamebinafsishwa sekta binafsi ikashindwa kuyaendesha halafu Serikali inarudisha. Kitu ambacho kimeshindikana kwa sekta binafsi kwa biashara, Serikali haitaweza.
Mheshimiwa Spika, unless unasema kwamba hiyo ni mkakati kama Air Tanzania. Kama ni Air Tanzania twende kwa sababu tunajua ni mkakati, basi. Lakini lazima tuangalie ni mashirika yapi; ni viwanda au ni taasisi zipi ambazo zilikuwa zimebinafsishwa halafu zikarejeshwa, tuone mkakati wake uko wapi. Kama upo then tuendelee lakini siyo hivyo, tunaona kwamba Msajili wa Hazina ametoa ruzuku na nyongeza kwa mitaji ya mashirika takribani shilingi bilioni 27. bilioni 27 ni hii 500 tumepewa kwenye majimbo yetu mara tatu? Kwa hiyo, naomba hiyo iangaliwe vizuri.
Mheshimiwa Spika, sasa niseme hivi; mimi nafikiri katika mambo yote ya kukusanya kodi ambayo ni kazi kubwa ya Wizara, mahali penye leakage kubwa ni kule kwenye Serikali za Mitaa. Serikali za Mitaa hawakusanyi, na wakikusanya zinaingia mifukoni mwa watu. Kwa nini tunawaambia kwamba waingie kwenye GEPE, muda mwingi kule kwenye vijiji vyetu kwenye halmashauri hakuna mawasiliano, hawana Point of Sale za kukusanya hayo mapato. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo unakuta kwamba ukimpa mfanyakazi Point of Sale akatembea nayo barabarani huko, haina hata risiti ile roll imekwisha, unakuwa ni mtaji kwake na ukimnyang’anya analia machozi ya damu, anakwambia umrudishie hiyo Point of Sale kwa sababu anajua kwamba ni njia rahisi sana ya kupata mtaji wa bure. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na naomba kwamba ili mradi hatuwezi kusambaza Point of Sale za kutosha kwenye halmashauri zetu, kwenye vijiji kwa sababu na kule wanakusanya kodi, tusiseme kwamba tutakaa tu tuangalie halafu tutakusanya kodi au tutaongeza wigo wa kodi. Naamini kwamba kwa wale walio kwenye wigo wanalipa na wanafuatiliwa lakini kwenye sehemu nyingi watu hawafuatiliwi.
Mheshimiwa Spika, na kitu kitakachotupa mapato kwenye mwaka huu ni usimamizi mzuri. Kwa sababu kwa muda mfupi hatuwezi kuongeza wigo wa walipa kodi, hatuwezi kuongeza kwa siku tatu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa niseme pia kwamba kwenye suala hili la riba za Serikali, kwa sababu unajua kitu kinacho- drive deni la Serikali zaidi ni riba kubwa. Na ninasema kwamba uhimilivu wa hili deni hautakuwepo kama riba zitakuwa kubwa. Na riba zimekuwa ni asilimia 15.9, alisema mwenzangu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, wanapokea hiyo, mkopo, kama ni mkopo umelimbikiza mwaka mmoja unaongezeka kwa asilimia 15 na zaidi. Kwa hiyo, inakuwa kwamba hutaweza kabisa kulipa. Tunalipa asilimia 25 ya mapato yetu kwenye ku-service deni hili. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nafikiri hivi; njia pekee ni kwamba sasa tukubali kwamba inflation au mfumuko wa bei ni asilimia tatu. Na kwa kawaida huwezi kuwa na zaidi ya asilimia nane hapo kwa sababu unaongeza hapo asilimia tano, asilimia tano ndiyo inakuwa ni riba ambayo inakubalika. Inakuwa inflation plus five percent ni eight percent, kwa hiyo, ukiwa juu ya pale ni matatizo, ni majanga kwa sekta binafsi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninachowashauri Benki Kuu na Waziri wa Fedha ni kwamba ile coupon rate ya dhamana za Serikali wanayotoa Benki Kuu, kwa sababu wanasema tuna option na riba itakuwa ni asilimia 15.6. Kwa hiyo, kila mtu anakwenda ku-bid, ananunua. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ile coupon rate inayotangazwa asitangaze tena sasa ya asilimia 15, atangaze asilimia kumi; mabenki na wawekezaji wengine hawana mahali pa kuwekeza fedha zao salama zaidi ya kuweka kwenye dhamana. Kwa hiyo, ina maana kwamba watakwenda watu watanunua tu, hakuna njia nyingine kwa hiyo watanunua. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na ni kweli kwamba hiyo faida watakayopata bado ni kubwa kwa sababu ni risk free, hawana gharama yoyote, wanakusanya tu bure. Kwa hiyo, naamini kwamba kama tukisema kwamba, okay, kuanzia minada inayokuja, coupon rate yetu itakuwa ni asilimia kumi, anayetaka aje, asiyetaka asije. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, baada ya muda watakuwa na maukwasi yamerundikana wataamua kuja kununua kwa asilimia 10. Na hiyo itasaidia pia kushusha riba za mabenki binafsi kwa sababu riba zimelegezwa kwenye riba hizi za dhamana za Serikali. Kwa hiyo, hakuna njia nyingine ya kushusha riba kwenye mabenki kama siyo kufanya hicho, kwamba hatutauza dhamana kwa juu ya asilimia kumi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa hivi wanauza treasury bills chini ya asilimia tano, za mwaka mmoja. Sasa kwanini na zilikuwa asilimia 14? Sasa ameshusha, inakuaje kwamba wameshusha hizo za na nanii, na tunajua kwamba upeo wetu wa inflation ndiyo hiyo asilimia tatu. Hakuna sababu ya kushindwa hicho kitu. (Makofi)
Niombe kwamba ikiwezekana, hasa kwenye mambo ya ugawaji wa fedha, wenzangu wamesema, lakini ukweli kama hatutagawa fedha kwa vipaumbele au kwa kuzingatia kasma, hatutakwenda mbali…
SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Dkt. Charles Kimei.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: …kwa hiyo Wizara ipeleke kufuatana na jinsi ambavyo imepitishwa.
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu Shughuli za Kamati kwa Mwaka 2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa fursa hii uliyonipa, naomba nichangie machache kwenye mawasilisho ya Kamati hizi mbili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kusema kwamba ninaunga mkono hoja zote za Kamati hizi na mapendekezo waliyotoa, kwa hiyo, nawapongeza Wabunge wenzetu wanaotuwakilisha kwenye Kamati hizi na hususan Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati hizi pamoja na Mawaziri na Naibu Mawaziri ambao wanaendesha Wizara hizi ambazo zimewakilishwa na Kamati hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri kwamba tunafahamu wote kwamba nia na lengo la Serikali kuwekeza sana kwenye miundombinu ni kuhamasisha uwekezaji. Lakini ukiangalia utaona kwamba hatujaona miradi yoyote inayoibuka kwa kasi kwenye maeneo yale ambayo miundombinu hususan ya reli na barabara inapowekwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa tatizo tunasema ni nini? Na nafikiri kwamba hatujaweza kubainisha sawasawa tatizo la uwekezaji nchini linatokana na nini? Ni changamoto zipi? Zinafanya wawekezaji kutoka nje na hapa ndani wasiweze kuchangamkia fursa zinazotolewa na miundombinu mizuri na yenye uhakika na ambayo kusema kweli ni mingi inakamilika na inaonesha kwamba itaongeza tija sana kwa wawekezaji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nafikiri tatizo moja ni kwamba kumekuwa na hisia kwamba tatizo kubwa ni mikopo, lakini niwaambie katika soko letu la mitaji, katika financial market yetu, tatizo kubwa ni mitaji ya usawa au mitaji ya ubia (venture capital), hakuna hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hapa nchini Watanzania wachache sana wanaweza wakaanzisha miradi mikubwa. Na ukweli ni kwamba wale tunaowaona wanajiwezaweza kidogo wameanza kidogokidogo wakajidunduliza wakachukua mikopo na ikafika mahali kwamba hata mikopo hawawezi kuongeza kwa sababu lazima mabenki au taasisi za maendeleo zinaangalia uwiano kati ya mtaji na deni, huwezi kupata mkopo zaidi ya mara mbili ya mtaji wako, kwa hiyo inakuwa ni ngumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme kwamba Serikali kupitia Wizara hii ya Uwekezaji natumaini ingechukua lessons kutoka katika nchi nyingine. Na hata hapa nchini iliwahi kufanyika; chombo pekee cha kuweza ku-intervene katika kuongeza mitaji nchini ni hizi benki za maendeleo. Benki za maendeleo zisijikite kwenye mikopo, zijikite kwenye kusaidia ku-leverage mitaji ya wawekezaji wa ndani, hata wa nje wanaweza wakasaidiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, na hakuna nchi ambayo imekuza private sector bila Serikali kujiingiza yenyewe kwa kuingia ubia na sekta hizi binafsi. Kwa sababu kwanza Serikali ikiingiza hata hela kidogo tu ikaingiza kama hisa ikachukua hata asilimia 20 au 10, hata chini ya hiyo, baadaye baada ya mtaji ku-take off wanaweza wakauza zile hisa kwenye soko la hisa au wakauza kwa wale wanaotaka kujiingiza kwenye biashara husika halafu wakachukua zile fedha zikarudi kwenye taasisi zikaenda kuwekezwa kwenye mradi mwingine. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ndiyo hivyo benki nyingi zinafanya, benki za maendeleo hizi zilitakiwa zifanye kazi hiyo ya kukuza mitaji na kuhamasisha watu waje kuwekeza kwa sababu kuna mtaji ule ambao ni seed utalinda ule mtaji wa yule mwekezaji binafsi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba kwamba ifanyike jitihada ili sekta binafsi iweze kusiadiwa na Serikali katika kuwaongezea mitaji lakini Serikali ikae kidogo na ijiondoe ili ile fedha iweze kuzunguka kwenye miradi mingine ya harakaharaka naamini hilo ni jambo la msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo lingine ambalo naamini ni la msingi ni kwamba sera ndiyo ni muhimu kwenye uwekezaji na mazingira hayo ya uwekezaji yakijulikana vizuri inasaidia, pamoja na some incentives. Lakini incentive siyo cha muhimu kama hayo mengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme hivi; tumefanyia sheria yetu ya uwekezaji marekebisho siku za karibuni na imepita. Sasa kama imepita nafikiri taasisi husika zingekuwa mbele kutangaza yale marekebisho yaliyofanywa na faida yake ili watu waweze kujua. Watu hawajui, siyo wengi wanasoma sheria hizi na ninaamini hilo ni la msingi la kufanya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa ardhi, kusema kweli mimi nianze kusema kwamba watu wanaosababisha migogoro ya ardhi ni kile kitendo cha Wizara kuwaacha maafisa wake kukaa kwenye mikoa kwa miaka 20 bila kubadilishwa. Wao wanapima ardhi wanaigawa kiajabuajabu, wanaweza ku-double allocate n.k. kwa sababu tu wamekaa miaka mingi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naliomba Bunge hili lije litoe fedha kwa Wizara husika ili waweze kubadilisha watu, watolewe kwenye mkoa mmoja wapelekwe kwenye mwingine, wale wengine wakija wataibua na watajua chanzo cha migogoro ambayo ipo na wanaweza pengine kuisuluhisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba niseme kidogo kwenye suala zima la Wizara ya Utalii na Maliasili. Kule kwetu Vunjo, Kata za Mwika Kaskazini, Mamba, Marangu tumeotesha miti mingi lakini tatizo moja tumekaribisha tumbili na gedere wamejaa kule, ndiyo wanawahi kuvuna mahindi yetu kabla hatujavuna, njaa itakayokuja kule kwetu itatokana na tumbili na gedere! Wale wenzetu wanasema wanyama wakali ni pamoja na tembo, lakini sisi ni gedere na tumbili, wanazaliana hawana mpango wa uzazi, wanazaliana hovyo hovyo, wamekuwa wengi sana! Yaani unakuta unapika wanakuja kuingia ndani wanakula chakula. Kwa hiyo, naomba Serikali ijipange kutekeleza mpango wa kuvuna hawa, sijui watawavuna, sijui watawaua! Wakiwa hawawezi watuambie basi sisi tushughulike nao kwa njia zetu. Lakini ukweli ni kwamba hatuwezi kukubali kwamba tufe njaa huku tunalima usiku na mchana na tunatumia mbolea ya ruzuku! Hapana siyo vizuri, tutafute namna ya kuwaondoa. Pia katika Kata ya Makuyuni ni wengi sana hawa Wanyama ambao ni waharibifu tu. (Makofi/Kicheko)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimalizie hapo, mwisho kabisa kwenye hili la ardhi, nilisahau kusema kwamba Rais wetu wa Awamu ya Tano, alitoa maagizo kwamba ardhi itolewe kwa miaka 99, lakini nashangaa watu kwenye Mikoa yetu wanatuambia kwamba ardhi ni miaka 33 na wanaendelea kutoa Hati za miaka 33. Nilijua kwamba agizo la Rais ni Sheria pia, kwa hiyo, naomba tuambiwe kuwa kwa nini hii ya Hati Miliki za miaka 33 bado zinatolewa wakati imeshatangazwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja mara nyingine. Ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nami nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa kuzindua Royal Tour ile juzi tarehe 18. Niseme kweli amekuwa President celebrity, wale walioangalia waliona ilivyopendeza na jinsi ambavyo alituuza vizuri kwenye interview aliyofanya kule New York. Kwa hiyo tunampongeza sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nimpongeze kwa kuwa na timu nzuri ya Mawaziri, Naibu Mawaziri na viongozi wengine Serikalini ambao wanatuwezesha sisi Wabunge kutembea kifua mbele na kusema kwamba kweli kazi inaendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kusema hivyo, nimpongeze kipekee Waziri wa TAMISEMI na Manaibu wake kwa kazi nzuri wanayofanya, nimpongeze Katibu Mkuu kama wenzangu walivyosema, kwa sababu anafanya kazi iliyotukuka sana na hatuna cha kusema isipokuwa kuwaombea Mungu waweze kuendelea wakiwa na afya, wakifanya kazi hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuende kwenye Jimbo langu. Kwanza niseme kwamba kuna dharura, TARURA wana dharura kule kwetu. Mheshimiwa Spika alitoa tamko hapa akasema TARURA wafanye tathmini katika Sitting iliyopita, wakafanya tathmini. Lakini nakwambia ukienda Vunjo ambako mvua zimeendelea kunyesha toka wakati ule na hazijaisha mpaka sasa, barabara zote za vijijini kwenye Kata zote za Mwika, Mamba, Marangu, Makuyuni, Kahe, Kirua Vunjo, Kilema, kule barabara zote za vijijini hazipitiki. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, juzi nimepita mimi mwenyewe nikashindwa kupita nikaamua kuja kujificha hapa Dodoma, lakini ukweli hali ni ngumu, naomba tukafanye tathmini tena tuone kwenye maeneo haya ya vijijini kule ambako mvua zimeendelea kunyesha kwa fujo ni kitu gani tutafanya ili watu waweze kupita. Imekuwa matope wakati TARURA ilikuwa imetengeneza vizuri sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru sana yule mratibu wetu anaitwa Olota, kwamba walifanya kazi nzuri sana mwezi Novemba na Desemba sasa ukienda kupita ni pa kurudia, ninaamini lazima tutafute mbinu mpya ya kutengeneza barabara za vijijini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tujaribu kutumia mawe zaidi, tutumie Local Based Contactors ili watumie vijana wale wa kwetu, wapasue mawe tuweke mawe kwenye yale maeneo ambayo ni korofi sana ili barabara ziweze kukaa angalau kwa miezi michache. Tukijenga kwa mawe badala ya kutumia hizi traditional methods tunaweza tukajenga kwa bei nafuu lakini pia kwa kitu ambacho ni sustainable. Hivi tunavyofanya tunacheza, naomba tufanye kitu kama hicho na tutumie hizi force accounts, tuache kusema kwamba TARURA hawawezi kutumia force account. Force account inakuwa ni cheaper na tulifanya tathmini sisi tukapata mambo mazuri. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme pia tunatoa pongezi na shukrani kwa Mheshimiwa Rais na Wizara hii ilivyotutumia fedha, tumeweza kukarabati Kituo cha Kirua Vunjo, kimekuwa na majengo sasa ya upasuaji. Tumepata fedha Shilingi Milioni 250 kwenye kituo cha Marangu ambacho hakitaisha ni nusu tu. Naomba hizo hela zilizobaki tupate ili tukamilishe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo kingine OPD ambapo tumeahidiwa kwamba kimepandishwa hadhi kikawa kituo cha afya, kilikuwa ni zahanati, basi kipate Shilingi Milioni 500 tuweze kukamilisha na penyewe tuwe na kituo cha pili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo cha Mwika ambacho pia ni kituo kongwe sana, kituo cha miaka hiyo ya Hamsini mpaka leo hakijapata ukarabati, hakijapata majengo yale ambayo ni stahiki kuitwa kituo cha afya. Naomba sana Wizara hii sasa ikaangalie hilo katika mwaka huu unaokuja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kule kwetu Kilimanjaro kwa ujumla na Vunjo in particular utakuta kwamba shule zote za msingi na sekondari ni kongwe kabisa. Sasa wale vijana wanaosoma kwenye shule kongwe wakaona tumejenga madarasa 32 juzi, tumepewa chini ya UVIKO wanakwenda kutazama na kusema Mungu wangu, hivi hawa wenzetu wanaishi kwenye dunia ya Marekani na sisi tunaishi jehanamu au namna gani? Kwa sababu zile shule zao hazina vyoo, hazina miundombinu, ni za kukarabati kabisa, na ninaomba Serikali iende kwa awamu. Tuende kwa kuangalia ni zipi kongwe Zaidi, zilizojengwa miaka ya sitini, miaka ya sabini, lakini twende hivyo kwa tabaka ili tuweze kwenda kukarabati kufuatia age za shule zikoje.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kwamba kama tusipoinua hadhi ya shule hizi za zamani wakati tumewaonesha kwamba kuna uwezekano wa kujenga shule nzuri, madarasa mazuri, wale vijana wanaosoma kwenye shule ambazo zimeoza kabisa wanasononeka sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mwisho ni hili suala zima la mikopo. Mimi niseme hivi, kigezo kikubwa cha mafanikio ya mchakato au mkakati wowote wa Serikali kutoa mikopo kuwezesha wananchi ni ili mikopo inayotolewa kuzunguka, maana yake kurejeshwa, ili iweze kuzunguka kwa watu zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini inavyoonekana huu mchakato wa kulenga vikundi duniani kote haufanyi kazi, hata kule benki tulifanya, hai-work. It doesn’t work. Tutumie mbinu mpya sasa kwa sababu kuna njia za kidigitali za kuweza kujua ni nani mhitaji na mwenye mradi mzuri wa kuweza ku-sustain, tuweze kutumia methods ambazo zinatumia big data logistics tuweze kutoa mikopo hiyo kwa wale watu, hata mmoja mmoja utaona kwamba zinarejeshwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini kutoa kwa groups, groups ni vigumu sana kuwajibika, uwajibikaji ndani ya group inakuwa vigumu sana kusimamia, kwa sababu mmoja aki- default na mwingine ana-default, na mwingine na mwingine. Kwa hiyo naomba sana tuangalie, tutathmini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nina mawazo ya namna gani ya kufanya pengine tuangalie upya kabisa, hata tuwe na mjadala mzima ili uweze kusema twende wapi kwenye hili suala zima ambalo ni zuri la kuwezesha wanawake, vijana, walemavu, pengine baadaye tuweke na wazee.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nami pia kwa niaba ya wananchi wangu wa Vunjo nianze kwa kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa madarasa aliyotupa pamoja na shule ya sekondari ambayo ametuwezesha kujenga pale Himo eneo la Njia Panda.
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru na kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa Elimu pamoja na timu yake; Naibu Waziri, Katibu Mkuu pamoja na viongozi wote wa Wizara kwa kazi nzuri wanayoifanya, na zaidi kwa kuisoma vizuri dira ya Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuhusiana na mwelekeo wa elimu unaohitajika katika kipindi kijacho; na kuanzia sasa kwamba elimu ilenge zaidi kuwapa wanafunzi maarifa ya kiufundi, ujuzi wa kutenda na stadi mbalimbali. Ninaamini kwamba wameisoma vizuri dira hiyo na ndiyo sababu wamekuja na hili ambalo sasa tunalizungumza la kubadilisha mitaala ya elimu yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme hivi, tatizo kubwa litakaolojitokeza ni walimu wa ufundi na walimu wa stadi mbalimbali. Stadi zimebadilika sana. Stadi zinazohitajika sasa hivi siyo zile za zamani zinazoendeshwa na VETA za magari ya zamani. Sasa magari yaliyoingia ni ya kidijitali, yako computerized. Ndiyo sababu unaona magari mengi yanatengenezwa kwenye garage za Wachina na wanatengeneza kwa fedha nyingi. Huwezi kuona vijana wetu wakipata stadi hizo za kuanzisha garage za kisasa ambazo ni za stadi ambazo zinahitajika sasa hivi kwa sababu magari ya sasa hivi ni tofauti.
Mheshimiwa Naibu Spika, mara nyingi tunafikiria kwamba ufundi na maarifa ni kwenye mambo ya kujenga, kushona, useremala na kadhalika, lakini mimi nataka niseme kwamba sasa hivi tulenge zaidi sekta ya huduma; kutoa mafunzo ya maarifa kwenye sekta ya huduma kwa sababu ndiko dunia inapokwenda na ndiko kwenye tija na ndiko ajira inazidi kuongezeka. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kama sijaonyesha kwa nini nimesema hivyo, nataka niseme hivi, katika kipindi cha nyuma wakati tukisoma, tofauti iliyokuwepo ni kwamba unapofika Darasa la Kumi na Mbili (Form Four) kunakuwa na Careers Masters na Walimu wanakaa wanamwangalia kila mwanafunzi, wanamshauri kwamba wewe sasa tunaona uko vizuri sana kwenye hesabu, au uko vizuri kwenye biology, au uko katikati au uko chini sana. Kwa hiyo, inapofika wakati wa mwisho, unaletewa fomu ya kuchagua na mwalimu anakuwa ameshakushauri kwamba wewe unaweza kwenda mbele au huendi. Ukienda mbele hutafika mbali kwa sababu anajua wewe ni mtu una talent ya namna hii na hii. Kwa hiyo, unapoletewa unaambiwa chagua, kuna vyuo vilivyokuwepo Technical School, kulikuwa na vyuo vya maarifa kulikuwa na vyuo mbalimbali ambavyo vinaorodheshwa, pia pamoja na University.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mtu anapewa fomu ambayo anachagua kwamba baada ya kupata ushauri na mwalimu wake, kwamba wewe lini unataka kwenda kusoma mambo ya magari? Unataka kusoma mambo ya Fitter and Turner nataka kusoma hiki na kile. Kwa hiyo, kunakuwa na michepuo kuanzia hapo hapo kwenye kidato hicho ambacho kwetu sisi ni Form Four itakuwa hata na Form Six, pia mnapewa uchaguzi ule. Hiyo michepuo ndiyo inakuwa mikondo mbalimbali ya kutunza talent. Kuna watu wengine wanapenda kwenda kusoma music, kungekuwa na Chuo cha Music, kungekuwa na hiki na kile.
Mheshimiwa Naibu Spika, bahati mbaya baada ya kuvunja hiyo taratibu tukasema tunaingiza sijui kitu gani au mfumo gani? Hatukuendeleza hivi vyuo vya ufundi na maarifa, tukabakia tu tunakimbizana na university na colleges zikabadilishwa zikawa ni vyuo. Kwa hiyo, ikawa sasa mtu hapewi namna ya kuchagua kwamba sasa nimefikia mahali ambapo ni lazima nichague niende huku na michepuo ile inakupeleka kwenye kujifunza stadi, kujifunza ufundi na ujuzi mbalimbali ambao baadaye unakuja kusaidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa kwa hii mitaala tunayounda, nami nakubalina na mwenzangu mmoja natumaini ni Mheshimiwa Kingu, alisema jana kwamba Waziri awe na Baraza la Ushauri liwe linamwezesha kujua kwamba atabadilisha namna gani hiyo mitaala badala ya kuleta mambo ya siasa kwenye mitaala. Mitaala siyo siasa. Hii ipo, inajulikana duniani, kuna system ya UK, kuna British System, kuna American System na kadhalika, lakini mitaala hiyo siyo kitu cha kuweza kuibua, ni kwamba ni kuchagua twende na kipi na tukizingatie, lakini kuwe na watalamu ambao ni baraza. Hilo alikuwa analisema Mheshimiwa Kingu jana kwamba liwe linamshauri Waziri na Waziri analeta hapa kitu ambacho kimekaa sawasawa.
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi hiyo ninaiunga mkono, lakini niseme hivi tuangalie tunaenda wapi, tunapoenda ni tofauti kabisa. Hebu tuone kwa mfano uchumi wa France na US mwaka 1,800 kilimo ilikuwa inaajiri watu asilimia 64, 1,900 kilimo kiliajiri watu asilimia 43 tu, 1,950 kilimo kiliajiri watu asilimia 32 na mwaka huu inaajiri asilimia tatu ya watu walioajiriwa. Ukienda kwenye manufacturing France ilikuwa 1,800 manufacturing iliajiri watu asilimia 22, 1900, 29 imeongezeka, 1950 manufacturing ilikuwa asilimia 33, lakini sasa hivi asilimia 20 tu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Huduma (Services) 1,800 ilikuwa imeajiri asilimia 14, 1,900 asilimia 28, 1,950 asilimia 35 sasa hivi 76. Asilimia ya watu walioajiriwa kwenye nchii hizi ni kwenye Services. Ukiangalia kwenye matangazo ni hivyo hivyo ilishuka, services ilikuwa 13 percent 1800, sasa hivi ni asilimia 80; watu wote wapo kwenye services. Na services utakuta kwamba kwenye health and education 20 percent, kwenye hotels and restaurants na leisure na culture na haya mambo ya muziki 20 percent. Consulting, Accounting, Design, na kadhalika pamoja na financial services inachukua another 20 percent na kwenye Government Administration na Security pamoja na Armed Forces ni 20 percent.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo ina-add 80 percent, na utakuta kwamba mapato ya Serikali asilimia 75 yanaenda kwenye maeneo haya ya huduma hasa hizi za afya na elimu na administration.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo utakuta kwamba mahali sasa pa kulenga elimu yetu, namna gani kuwawezesha watu kuingia kwenye kutoa huduma mbalimbali, isiwe kwenye hoteli tu; kupika vizuri, design and so forth; music na kadhalika. Huko ndiko tunakotaka tulenge.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo tujenge vyuo ambavyo vitatoa maarifa hayo kwa vijana wetu; watapata ajira kwa sababu ajira ndiyo inakuwa huko, huku kwingine kote productivity inaongezeka haraka sana. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Kilimo Mheshimiwa Bashe mambo anayoyafanya pale kwenye kilimo productivity itaongezeka siku za karibuni, na tutaona kwamba ajira zinafunguka sana kutoka kule au watu wataweza kutafuta kazi mahali pengine. Na huko kwenye viwanda pia productivity itaongeza sana kwa sababu wana-digitizer wanafanya automation, kwa hiyo lazima wata-realize watu. Watu hao watakwenda wapi… (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, na mimi nianze kwa kwa kukushukuru wewe kwa kunipa fursa hii. Pia ninamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kazi nzuri anayofanya katika nchi yetu ikiwa ni pamoja na kutuletea bajeti hii ya kilimo ambayo ni ya kimapinduzi, nashukuru kwamba Mheshimiwa Waziri ametupitisha kwenye awamu tulizopitia za dira mbalimbali za kuendeleza kilimo, naamini mpango huu unaleta mapinduzi kwa sababu unazingatia mambo muhimu sana ya kimkakati na dira na naamini kwamba Awamu hii ya Sita itakwenda kubadilisha sasa kilimo hiki ambacho kitakuwa kimewaondolea asilimia zaidi ya 65 wananchi wetu wengi umaskini. Namshukuru pia Waziri na nampongeza sana Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri wake pamoja na uongozi wa Wizara yote kwa kazi nzuri na kwa wasilisho zuri la bajeti hii. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze na machache ambayo ni ya haraka haraka kwa sababu muda mfupi. Kwanza niseme kwamba ni vizuri katika kutekeleza tujue kwamba tunataka kupata tija ya haraka, kupata tija ya haraka ni lazima tuangalie Serikali ifanye tathmini ya mazao ya kimkakati kwa kila Mkoa. Siyo kila mkoa una comparative advantage zinazofanana. Unaweza ukazalisha mahindi kule Rukwa kwa bei nafuu sana ukayauza kwa tija sana kwa hiyo ikawa ni nzuri, lakini ukaanza kuweka tu kila zao liende kila mahali ukapeleke korosho kule Kilimanjaro itakuwa haifai. Kwa hiyo, lazima tuainishe kwamba Mikoa hii wale wenzetu walifanya hivyo, Mikoa hii kwa ardhi yake itafaa kwa mazao one, two, three au moja la kimkakati na lingine linaendelea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano, Kilimanjaro sisi zao letu la kimkakati kiasilia lilikuwa ni kahawa, lakini kwa sababu ya uzembe tuliofanya hapo katikati huduma za kiugani zikapotea ile kahawa kule sasa imekuwa haioti tena, hasa kule Vunjo. Kwa hiyo, sasa tumeanza kuingia kwenye mazao mengine hasa horticulture mazao ya mbogamboga, matunda na maua na kadhalika. Kwa hiyo, sasa naomba hivi katika mpango mkakati huu uliokuja wa kujenga maghala madogo madogo ningeishauri Serikali iende iangalie yale maghala yaliyokuwa yanamilikiwa na Vyama vya Ushirika madogo madogo kwa kila Kijiji halafu ijaribu kuyaboresha yale maghala na kuyaboresha hasa siyo kuyaweka tena kuhifadhi kahawa ni kuhifadhi mbogamboga, ndizi ndiyo zinauzika ndiyo zenye tija, ina maana muweke majokofu kwenye yale maghala ambayo siyo makubwa lakini yanaweza kutosheleza kuhifadhi mazao haya ambayo sasa hivi ndiyo yamechukua nafasi ya kahawa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakuomba kwa vile sasa tulizembea kahawa ikafa kule kwetu, basi wale ambao wanaotaka kuendelea kuzalisha kahawa basi tuwape mbegu za kahawa, miche ya kahawa bure. Waziri alituahidi naamini itatokea hivyo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuseme kwamba tatizo kubwa katika kilimo ni kwamba tunazalisha kabla hatujajua bei. Kwa hiyo mbolea ikipanda bei wewe unatumia gharama kubwa kununua mbolea ile lakini hujui kwamba utaenda kuuza namna gani, bei utakayopata ukiuza ile kahawa yako au mahindi ni shilingi ngapi. Mimi nafikiri kama mwenzetu alivyosema pale kwamba ni vizuri Serikali itafuta masomo halafu iwe inatoa zile bei, inatangaza zile bei ambazo imepata kule nje. Inatangaza bei elekezi kwa kusema kwamba ukilima mahindi au ukilima mbogamboga hizi au ukilima kahawa au pamba kwa msimu huu tuna kuhakikishia kwamba tumeshapata wanunuzi contract buyers ambao watakubali kukulipa shilingi fulani, kwa hiyo margin utakayoipata kwa cost management ambayo tumefanya utapata margin hii, na ukimwambia mkulima atanunua mbolea bila hata ruzuku kwa sababu anajua kwamba tayari ukifuata ile bei ya mbolea na input nyingine kwenye ile bei ambayo utapata ni faida. Sasa sisi tunazalisha halafu tunakwenda kupata hasara hata ukiweka ruzuku halafu ukienda kuuza kwa hasara it doesn’t help na tumeshapoteza ruzuku yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nijikite kwa mfano sasa hivi suala zima la mahindi. NFRA ina mahindi mengi lakini bei za mahindi zimepanda zimefika mpaka shilingi 800 kule Arusha. Mimi nafikiri kwamba huu ndiyo wakati ambapo sasa NFRA isiuze kwa middlemen yale mahidi, mahindi yauzwe ili yamfikie mlaji moja kwa moja. Kwa sababu ukiuza kwa middlemen ina maana ile faida ya yale mahindi ambayo tumewezesha NFRA ikanunua itakwenda kwa wale wafanyabiashara wa kati. Kwa hiyo, naomba hilo lifanyiwe kazi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna haja ya kuangalia ununuzi, uuzaji wa mazao yetu kama pamba. Tunajikuta kwamba kwa sababu riba zilikuwa kubwa, zinaanza kushuka hapa lakini ni kwamba riba kwetu bado zipo juu sana na watu wanaouziwa mazao yetu ni wale ambao wana-process hapa kama pamba kutengeneza nguo. Kwa hiyo, tunaomba hivi ile Benki ya TADB iwe inawawezesha wale wanunuzi wenye viwanda vya ku-process mazao yetu hapa kupata mikopo kwenye riba kati ya Mbili mpaka Nne hivi ili waweze kununua kwa wingi na wakienda kuuza nje wao zile bidhaa walizo- process hapa waweze kuziuza kwa faida in a way ambayo ina ushindani, ndiyo tunasema sasa dira yetu sasa ni uchumi shindani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaamini kwamba hiyo haitawezekana kama watu watakopa wahifadhi hii pamba ya kuchakata mwaka mzima halafu riba inaongeza zile bei kwa hiyo baadaye itakuwa hawawezi kushindana wanapoenda kwenye soko la dunia. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana kwa nafasi uliyonipa naamni kwamba kweli bajeti hii ni bajeti ambayo ni tofauti, ni bajeti kabambe, ni bajeti itakayotekeleza dira ambayo inayosadikika. Isipokuwa naomba Mungu aniweke hai mpaka mwaka 2030 ili nione mafanikio haya. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii. Pia nimpongeze Spika wetu pamoja na Naibu Spika na Wenyeviti wote ambao wamechaguliwa kwa namna ambavyo mnaendesha shughuli za Bunge hili kwa uwazi na kwa namna ambayo tunapata tija. Pia nichukue fursa hii kutoa shukrani za pekee na pongezi ambazo zinatoka kwa wananchi wangu wa Vunjo kwa Mheshimiwa Rais wetu na Amiri Jeshi wetu Mkuu Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu wake na Waziri Mkuu pia kwa namna ambavyo wanaendesha nchi yetu tukabaki tukiwa na nchi iliyotulia kisiasa na kiuchumi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kasi ya ukuaji wa Pato letu la Taifa bado linaridhisha ukilinganisha na sehemu nyingine ambapo tunaanza kuona recession ikitokea, mporomoko ukitokea lakini hapa kwetu tunaona kwamba pato linakua kwa takribani asilimia tano. Vilevile mfumuko wa bei uko chini kuliko kwa majirani zetu, pia na riba zimeanza kushuka, ingawa si sana lakini zimeanza kushuka; jambo ambalo linatuonesha kwamba pengine hapa tunapokwenda ni pazuri zaidi kama hali ya dunia nayo itarudi kwenye hali ambayo ni tulivu kutoka hii ya sasa ambayo mambo yanakuwa magumu. Naamini kwamba kwa wanavyotabiri wenzetu ni kwamba ndani ya mwaka huu wataona mafanikio sana kwa sababu vita vinaendelea na kuna mkanganyiko kwenye soko la kimataifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti,sasa niseme hivi, kusema kweli wana-Vunjo wamemshukuru Mheshimiwa Rais pamoja na Serikali yake kwa ujumla kwa miradi mingi kama wengine wanavyosema. Tumepata miradi mingi kama vile mradi wa maji kule Njia Panda ambao umeshakamilika, shilingi bilioni 2.3 zimekwenda huko. Vilevile kuna miradi ya maji kwenye Kata za Mwika Kaskazini, Mwika Kusini, Mamba Kaskazini, Mamba Kusini, Marangu Mashariki na Magharibi, Kilema Kati na Kilema Kusini na yote inaendelea. Miradi yote ina takribani shilingi bilioni tatu, haijakamilika. Hata hivyo Mheshimiwa Waziri nilikutana naye na ameniahidi kwamba fedha zitakwenda kukamilisha miradi hii kabla ya mwisho wa bajeti inayoendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tumepata vituo viwili vya afya, kituo kimoja tumepata kule Kirua Vunjo ambacho kilikuwepo lakini kikainuliwa hadhi ya kuwa kituo cha afya na kimepata vifaa vyote ambavyo vinastahili. Pia tumepata Kituo cha Afya Malangu Mashariki. Vyote hivi tunazungumza zaidi ya bilioni moja ambazo zimetumika na Serikali.
Mheshimiwa Spika, vilevile tumepata madarasa; kila mtu anayafahamu madarasa ya UVICO pamoja na madarasa mengine. Tumepata madarasa shule nzima ambayo ni ya wasichana pale Njia Panda. Kwa hiyo nataka niseme kwamba Serikali imewekeza vizuri na Mungu awajalie wote ambao wamewezesha miradi hii kuendelea.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tuseme pia kwamba TARURA wamepata pesa, tumepata barabara, zimechimbwa vizuri. Hata hivyo ninachosema ni kwamba barabara nyingi sasa hivi zimeharibika tena. Hii ni kwa sababu barabara zinazopitishwa grader mvua zikinyesha, na kwa sababu kule kwetu ni mwinuko basi zitakuwa zimepoteza hadhi. Lazima sasa tuombe TARURA wapate fedha ya ziada kwenda kukarabati hizi barabara ambazo zimeharibika sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naweza nikatumia muda mwingi sana kuzungumzia mambo ya jimbo, lakini nasema kwamba wote tunashukuru; tunajua kwamba fedha imetafutwa na Mheshimiwa Rais. Mimi sitazungumzia juu ya CAG kwa sababu nitatoa machozi hapa nikianza kuizungumzia CAG. Mngeacha nimalize haya kwanza na baadaye tutaanza kuzungumza, kama mwenzetu alivyosema, pengine tutakuja kwa wakati mwafaka.
Mheshimiwa Spika, lakini nitumie fursa hii kuzungumzia mambo mengine ya kitaifa ambayo si lazima yawe ya kijimbo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza unajua kwamba Sensa imetoka, takwimu zimeanza kutoka na takwimu muhimu zimeshaanza kutoka lakini nashangaa sana hatujaona hii mipango inayokuja ikigusia na kuonesha kwamba kuna namna gani tunaenda kujipanga upya ili tutoe miradi na huduma zetu hasa za jamii kwa kuzingatia idadi ya watu kwenye majimbo.
Mheshimiwa Spika, kwa mfano kwenye Serikali kuna baadhi ya halmashauri yenye majimbo zaidi ya moja, zinayo majimbo matatu. Sasa inapofika kwamba wakati Serikali inapoanza kugawa keki hii wanasema tunapeleka kwenye halmashauri, halmashauri inakuwa na majimbo mawili tunaanza kugombana na majimbo yote ni makubwa. Kwa mfano Jimbo la Vunjo lina idadi zaidi ya watu 255,000, Jimbo la Mheshimiwa Ndakidemi, Moshi Vijijini lina watu 284,000 halafu unatoa ambulance moja. Tunaanza kugombana na mwenzangu hapa, kwamba sasa zitaenda wapi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, mimi naamini ni vyema kwamba mzingatie kuwa kuna halmashauri zina majimbo zaidi ya mawili, na aidha muangalie ukubwa wa hayo majimbo. Kuna halmashauri ambazo idadi ya watu ni nusu ya hao tulio nao sisi lakini wao wanakuwa treated kama halmashauri wanapata kama sisi tunavyopata mpaka tunabakia kupigana huko bila sababu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kingine, nataka nizungumzie suala zima la kutengeneza bajeti hii ya mwaka huu. Bajeti tunayotengeneza sasa hivi haikuzingatia uhalisia wa hali ya uchumi wa dunia, na ndiyo maana tunaona kwamba fedha zilizopokelewa katika Wizara nyingi kwenye upande wa miradi ya maendeleo zimekuwa zinaenda kwa kusuasua sana. Sehemu nyingi zimepata chini ya asilimia 50 ya bajeti ya maendeleo; na sababu ni nini; tulitegemea kwamba tutapata fedha nyingi kutoka nje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, lakini nawaambia kwamba kwa hali ilivyo sasa hivi kwenye uchumi wa wenzetu ambaoo unapata matatizo ya recession inakuwa vigumu sana wahisani kuja kwa kasi hiyo waliyokuwa wanatumia mwaka uliopita. Kwa hiyo ni lazima tujaribu kwa kuona tutafanyaje na ili mwaka huu tuweze kuzingatia. Kusema kweli riba zimepanda juu kwenye soko la kimataifa; na kwa vile zinapanda juu inakuwa vigumu sana kupata mikopo. Wale wawekezaji wetu wanapeleka fedha Marekani kwa sababu riba za Marekani zimepanda hadi kufikia asilimia tano. Kwa hiyo wanapeleka fedha badala ya kutukopesha sisi; na wakitukopesha riba itakuwa juu sana kwahiyo itakuwa si himilivu na hivyo Deni la Taifa linaweza likaanza kuwa si himilivu. Kwa hiyo nataka niseme kwamba hilo ni jambo ambalo tunahitaji kuliangalia sana tuvyoelekea mbele, na ninaamini tutaona kwamba hali itakwenda vizuri.
Mheshimiwa Mwenyekiti,naomba niishie hapo, lakini naendelea kutoa shukrani kwa nafasi niliyopewa. Ninaamini kwamba Serikali itazingatia ushauri tunaoutoa kwa sababu ninamini una uhalisia na itatuwezesha kuwa na mpango ambao unatekelezeka bila kulaumiana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Kilimo
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa fursa hii ya kuchangia kwenye bajeti hii ya Wizara ambayo ni muhimu sana kwetu. Nianze kwa kusema kwamba tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu na kipekee kwa hapa, Waziri wa Kilimo, wametutendea haki kwa kuongeza fedha ambazo zinaenda kusaidia Watanzania wengi sana kama zitatumika ilivyokusudiwa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, nianze kusema kwamba mkakati unaotekelezwa sasa hivi na Wizara hii ya Kilimo ni mkakati ambao ni tofauti sana na miaka yote ambayo tuliwahi kuutekeleza. Ni tofauti sana na ninaona kwamba lawama nyingi zinazojitokeza kwa wakulima na hata kwetu sisi Wabunge zinatokana na ukweli kwamba hatukuwa tumeidhinishwa vizuri, hatukuwa tumepata miongozo ya kutosha ili kuweza ku-communicate na wale watu wetu kule vijijini wakaelewa ni kitu gani kinakuja. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo najua kwamba tunajifunza kwa kufanya na tunapojifunza kwa kufanya tunafanya makosa, kunatokea makosa na ninaamini kwamba kiongozi mwerevu ni yule ambaye sasa anachukua yale makosa na kuya-address ili huko mbeleni yale makosa yapungue tuweze kuona mkakati huu ukifanikishwa.
Mheshimiwa Spika, kusema kweli huu mkakati ni mkakati ambao ulihitaji uhamasishaji mkubwa na maandalizi mapema, ninaomba sasa kwamba Serikali iendelee kuwaandaa mawakala. Kule kwetu Vunjo tulikuwa na mawakala watatu tu kwenye Kata 16 zenye watu 255,000 ni wachache sana, kwa hiyo watu walikuwa wanatembea mbali kutafuta na mara nyingine wanakuta kwamba wale mawakala wameishiwa na mbolea au wana mbolea aina moja kwa hiyo unaenda unarudi. Kwa hiyo, kusema kweli ni mkakati ambao tunauunga mkono lakini sasa Serikali ijiandae vizuri kwa kutengeneza huo mfumo wa kugawa hii mbolea ya ruzuku, ninaamini kwamba itaendelea kwa sababu bei za mbolea duniani bado ziko juu kiasi, lazima tujue kama alivyosema mmoja wetu, kwamba tuna-subsidize au tunatoa ruzuku kwa bei tunayojua, tusitoe ruzuku kabla hatujajua kwamba bei ya kufikisha zile mbolea hapa Tanzania zitakuaje. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kule kwetu Vunjo na Kilimanjaro kwa ujumla, natumaini tumenufaika kidogo sana kwa miradi ambayo imetekelezwa. Kitu cha kwanza ambacho ninataka niulize ni kwamba, vigezo vilivyotumika kugawa miradi mbalimbali ya umwagiliaji, miradi ya mabwawa, miradi ya maghala na miradi ya uhifadhi wa mazao imefanyika namna gani na vigezo gani vimetumika? Kwa sababu la sivyo, tutabaki kusononeka wenyewe, tunasema hapa kuna upendeleo. Kwa sababu ili kuondoa masuala ya upendeleo au siyo upendeleo, lazima kuwe na criteria na rules ambazo zinam-guide yule anayesema sasa napeleka ghala Songea au sehemu nyingine (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa nashangaa kwa sababu kwa mfano kule kwetu tuna magulio au masoko ambayo toka kabla ya uhuru yapo, yamezeeka. Mama anakwenda ananyeshewa mvua wakati wa mvua, jua linampiga, hakuna hata paa, hakuna allocation yoyote iliyofanyika kusema kwamba hebu tusaidie wale watu wa kule Vunjo kwa mfano kwenye Masoko ya Himo, Mwika, Mombi, Kisambo, Marangu Mtoni na kadhalika, wakapata angalau mahali pa kujiepusha.
Mheshimiwa Spika, inavyotokea ni kwamba mkulima anapokwenda na mazao yake, mahindi au mbogamboga, akishindwa kuuza siku ile basi lazima ama aviache, avitupe au arudishe nyumbani ambapo hakuna walaji. Kwa hiyo, inakuwa kwamba kungekuwa na miundombinu hii ya maghala ambayo naamini kwamba haya ambayo yanatengenezwa sasa hivi na Mheshimiwa Bashe yana viwango vya kuweza kuhifadhi mbogamboga hizo, ndizi hizo baadaye zikauzwa kwa wale wachuuzi wanaojitokeza inakuwa ni vigumu sana kusema kwamba tumesaidika vya kutosha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naomba sana ikiwezekana hiyo iangaliwe na ninaamini kwamba soko linakuwepo lakini wale madalali wanaokuja kununua kutoka Dar es Salaam lazima waweze kuhifadhi mahali yale mazao. Nashukuru pia Mheshimiwa Bashe ameona umuhimu wa ku-emphasize kwenye huu mkakati wake kwamba analenga kuongeza zaidi uzalishaji wa mazao ya chakula, maana yake nafaka, mbogamboga na matunda ambayo yana tija lakini ni very delicate haya mazao, ni perishable, ukiweka baada ya siku mbili, tatu, yanaharibika kama hayakuhifadhiwa sawasawa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naambiwa kwamba tani milioni 2.75 zinazozalishwa za mazao haya ya matunda na mbogamboga ni asilimia Nne tu inachakatwa. Kwa hiyo ina maana nyingine inaharibika na wale wanaobahatisha zinanunuliwa na wenzetu wa mpakani ambao wana chain nzuri ya kuweza kuhifadhi na kusafirisha haya mazao kupeleka sokoni, sisi tunabakia hapa kusema kwamba watu wanao-export maparachichi yetu ni majirani zetu! Ukweli ni kwamba kama hatujajenga miundombinu ya kufikisha mazao yetu sokoni yataishia kwa majirani, kwa sababu wale wana miundombinu, wanazo quality cold rooms za kusafirisha haya mazao ambayo ni perishable ambayo yanaharibika kwa haraka. Kwa hiyo, naomba katika mchakato huu Mheshimiwa Waziri aone namna gani atatusaidia kwenye kulinda hiki tunachozalisha kwa wingi kidogo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, naona wenzangu wamekuwa wanasema huwezi kutekeleza mkakati mmoja unaofanana kwenye nchi kubwa namna hii kwenye Kanda zote na Mikoa yote, it’s impossible. Huwezi kusema kwamba labda uanze kulima korosho kila mahali au kahawa kila mahali, haitawezekana! (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninaamini kwamba kwa mfano mwenzangu mmoja alitoa mfano wa Malaysia, lakini nataka kusema kwamba kweli kule kwetu Kilimanjaro ambako hatuna ardhi, mkakati wetu unataka intensive farming, kumuwezesha mkulima azalishe kingi kwenye kaeneo kadogo na azalishe kwa mwaka mzima, which means umwagialiji ni kitu cha msingi sana, azalishe kwa mwaka mmoja lakini atumie eneo dogo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kuna maeneo mengine kusema kweli huhitaji hata mbolea. Kwanza maeneo mengi hayajatumika na mmomonyoko wa udongo haujaharibu sana kwa hiyo ukifanya extensive farming, ukawapelekea hizi tractors na mashine zikasaidia mechanization, utaongeza tija yao extensively, maana yake kwa kutumia maeneo makubwa. Kwa hiyo ninataka kusema kwamba kusema kweli tuangalie, bila kufanya vile tutapata matatizo. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kingine ninacholalamika ni kwamba kule kwetu nimetafuta kila mahali kwenye hii document ya Mheshimiwa Waziri nione BBT kule Vunjo imefikaje. BBT iko wapi Vunjo? Huwezi kugawa vitalu kwa miaka 66 kwa mtu yuleyule! miaka 66 si atauza na yeye kwa sababu lazima i- rejuvenate. Kusema kwamba hii ingekuwa ni seed mtu anapewa kwa mwaka mmoja wa pili anakuwa amechota faida ya kutosha anapeleka ku-invest mahali pengine, anamwachia mwingine, wanapeana vijiti, nae anazalisha, akishakaa miaka miwili anaenda inakuwa ni rotation. Hata kama unasema unampa mtu mmoja, mimi sijui nani atapewa, lakini naamini kwamba hiyo kitu ambayo hata criteria ya kusema unachagua eti watu waombe, mtu aombe wakati hajawahi kuona shamba unamwambia omba! Kwa sababu ana uwezo wa kuingia kwenye kishkwambi anaomba, pengine hata siyo yeye atakwenda kufanya kazi. Halafu ukweli ni kwamba kwenye hivi vitalu hata ikiwa ni eka tano, watahitaji wafanyakazi pia. (Makofi)
SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Kimei, muda wako umekwisha.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Fedha na Mipango
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa fursa hii ya mimi nihutubie pia Taifa kidogo. Kusema kweli wanahitaji pongezi nyingi uongozi wa Wizara lakini zaidi Mheshimiwa Rais ambaye amewezesha fedha kupatikana na Wizara zote zikapata fedha kwa uwiano uliokuwepo mzuri zaidi ya kama alivyosema mwenzangu Mheshimiwa Komanya zaidi ya asilimia 80 Wizara zimepata mpata mpaka hadi Aprili ambaye ni ndugu yangu mzuri na nampongeza sana Mheshimiwa Waziri kwa hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Nampongeza pia Mheshimiwa Rais kwa kuweza kupangua wakurugenzi wa halmashauri zetu hiyo ni njia moja ya kupunguza maficho ya ufisadi. Kwa hiyo, nashukuru kwamba amefanya hilo naamini litasaidia na naamini kwamba Wizara nyingine hasa ile Wizara ya Ardhi itaanza na yenyewe kutafuta namna ya kupangua maafisa ardhi kwenye mikoa na kwenye wilaya zetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya kusema hayo niseme kidogo kwamba nashangaa Mheshimiwa Kishimba anapata wapi hizo hoja zake anaziibua kutoka wapi lakini nimefurahi hoja zake zimenifurahisha. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kwa vile Wizara imeweza kulipa madeni vizuri sana, karibu madeni yote yamelipwa kwa wakati ningeomba niseme kwamba kuna suala la madeni ya fidia, madeni ya fidia hayaonekani kwenye vitabu ni contingency liabilities lakini yapo hayo madeni.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuna madeni kwa mfano kule kwangu Vunjo wakazi wa Eneo la Chekereni, Njia Panda ambako wanajenga kituo cha one stop center ya customs pamoja na kule Uchira toka mwaka 2013 wanadai zaidi ya bilioni 10 na hawajalipwa. kwa hiyo, naona niwa-dominate Waziri alichukue na hilo najua kwamba siku ya karibuni walifanya tathmini upya na naamini zile dhamana zilizokuwa zimepatikana miaka ile wataongezewa fidia yao inavyostahili kisheria. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, langu la pili linahusu vyuo vilivyo chini ya Wizara ya Fedha na vingine vipo chini ya Wizara ya Biashara, vyuo ambavyo viliundwa kwa mantiki ya kutengeneza au kutoa skills kwa waliomaliza shule ili waweze kuingia kwenye kazi moja kwa moja. Kwa mfano IFM tulijua kwamba ilikuwa diploma, advanced diploma na post graduate diploma na zingine zilikuwa hivyo hata Mzumbe lakini baadaye hata CBE nayo ilianza sasa kuwa kama university lakini mantiki yake ilikuwa ni vyuo vya kati ambavyo vitataengeneza watu wenye study kwenye fani husika. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa wamebadilisha kabisa hiyo dira iliyokuwepo toka mwanzo na wameingia sasa kuwa ni vyuo vikuu na kwa bahati mbaya na kwa sababu hiyo utaona kwamba pia hivi vyuo havi-publish nyaraka ambazo za kitafiti ambazo zinaongeza nanii duniani. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo mimi nafikiri hivi vyuo haviko mahali pake. Kwa sababu sasa tumeshabadilisha ile dira tunafikiri vyuo hivi virudi kwenye Wizara ya Elimu ivisimamie kama inavyosimamia vyuo vile vingine vyote, lakini kukaa kwenye Wizara hizi havipati usimamizi unaostahili na ninaamini ndiyo sababu tunaona hata kwenye vyuo elimu inaporomoka.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa nizungumze suala la Kitengo cha Mkaguzi Mkuu lakini naona limeshazungumziwa vya kutosha. Lakini kuna hoja pia zingine nitazungumza; hoja ya kwamba tutenge fungu la contingency la dharura kwenye bajeti (Mfuko wa Dharura kwenye Bajeti). Ni jambo ambalo liko kwenye constitution kwenye katiba na pia ni hitaji la Sheria ya Bajeti. Hatujaweza kufanya vile na mimi nasema kwamba silaumu na mimi nina hoja yangu binafsi, nasema ukianza kutenga fedha kwenye Mfuko wa Dharura unaweka akiba kwa tatizo litakalokuja na unaweza kufanya vile kama una bajeti ambayo haina nakisi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti zote tangu tupate uhuru zimekuwa ni bajeti ambazo zina nakisi kubwa ndiyo sababu tunakwenda kukopa na kuomba wahisani na kadhalika. Endapo tutasema tunatengeneza mfuko wa dharura ukienda kwa mhisani atakwambia kwamba kula kwanza uliyoweka akiba ndipo nikupe mimi; kwa hiyo hatakupa na misaada itapungua na kadhalika.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naamini hapo tutakapofikia uwezo wa kuwa na bajeti ambayo ni surplus budget basi tunaweza kuzungumzia suala zima la kuweza kuweka fedha kwenye mfuko wa dharura ambao unahitajika bahati nzuri sasa hivi tunajua kwamba unatenga shilingi bilioni 100 ambazo zinaweza zikatumika wakati wowote, lakini sheria inataka mfuko kamili ambao utakuwa unakuzwa na wenyewe uwe na kanuni zake.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapongeza sana kwamba tumeanza kutengeneza dira ya 2050. Ninaamini ni jambo jema lakini mimi nilikuwa nafikiri huwezi kutengeneza dira kabla hujafanya tathmini ya ulikotoka, ulipo ndipo uweze kusema ninaenda wapi. Naona kwamba hatujaweza kufanya hiyo tathmini. Tunaambiwa tathmini imeanza kufanyiwa kazi lakini nilishangaa kwamba tumeweza kufungua. Of course, tulizindua mchakato huu wa kutengeneza hii dira lakini bahati mbaya naona kama itakuwa siyo vizuri kama hatujapata tathmini nzuri au hata wale waliopewa kuifanya hiyo kazi watafutiwe kwa upesi sana tathmini hiyo ikamilike ili waweze kutumia na kuelewa ni wapi tumetoka na tumejifunza nini kutokana na utekelezaji wa dira ya 2025. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka pia niseme kwamba mimi naunga hoja mkono, ahsante sana. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunivumilia. Nimeomba sana nichangie mapema, na umenivumilia ukanipa fursa hii. Nakushukuru sana.
NAIBU SPIKA: Sasa vipi, umekasirika uondoke au?
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, niko vizuri.
NAIBU SPIKA: Aah, okay. Ahsante.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Rais wetu kwa kutuletea bajeti ambayo ni nzuri sana kusema kweli. Pia nampongeza Mheshimiwa Waziri wetu mchumi msomi Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Mchemba, Naibu wake, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na timu nzima ya Wizara kwa kazi nzuri. Niseme kwamba wamefikiria sana nje ya box wakati huu, ndiyo sababu unaona kwamba sera wanazotuletea ya matumizi na mapato ni sera ambayo ina vitu vipya, vitu ambavyo hatukuviona huko nyuma. Nasema kwamba, kweli ninyi mmechapa kazi vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, nataka niseme kwamba, nitaendelea kuwapongeza endapo watakumbuka kwamba tuna wananchi kule Kahe Mashariki ambao wanadai shilingi bilioni 5.2 kwa thamani ya mwaka 2013 ambao wametoa maeneo ya kujenga One Stop Inspection Center pale Njiapanda Himo.
Mheshimiwa Naibu Spika, nije kwenye bajeti yenyewe. Niseme kwamba, hii bajeti ni bajeti ambayo kweli imetengenezwa kwenye mazingira ambayo mimi nasema ni magumu kwa sababu kuna vihatarishi vingi ambavyo havitabiriki kutokana na uchumi wa dunia na uchumi hata huu uchumi wetu. Kwa hiyo, naamini kwamba tutapitisha hii bajeti, lakini mimi naamini ni vizuri utekelezaji wake ukawa unafanywa continuous risk assessment ili kujua kwamba, je, ni kweli kwamba, zile assumptions zitakuwa fulfilled?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ni kwamba bajeti imebana, inaonesha kuwa na fiscal measures ambazo ni nzuri na ndiyo sababu unaona kwamba financing ukiondoa ile rollover, financing inayokuwa required na angalau 3% ya GDP ambapo kusema kweli kwa hivyo naona kwamba tumeji-tighten.
Mheshimiwa Naibu Spika, niseme kwamba, kwa viashiria hivi tunavyoona kule Ulaya sasa hivi, UK wanatangaza inflation ya 11%, Marekani inflation iko juu 7% na viashiria hivi vya interest rate kupanda kuendana na inflation; na kule Marekani sasa hivi riba kwenye hizo third reserve rate ni 3.5%. Kwa hiyo, inaonekana kwenye masoko ya kukopa, masoko ya International Re-capital Market riba zitapanda sana. Zitapanda sana kwa maana kwamba sio wakati wa kukopa nje kwenye masharti ya biashara kwa sababu ni lazima tujiangalie.
Mheshimiwa Naibu Spika, ndiyo sababu nikasema kwamba, cha kwanza ni kuona kwamba kweli kuna mambo ambayo tumeweka. Kwa mfano, ukopaji wa about three trillion kutoka kwenye masoko ya nje, inawezekana baadaye tukaona kwamba pengine tusitishe au tupunguze miradi ile ya maendeleo, hususan ununuzi wa ndege nyingi sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, nafikiri ndege tunazozitaka sasa hivi ni lazima tumwombe Mheshimiwa Rais atuletee ndege ya mizigo kwa sababu inahitajika, ndio big constraint ya ku-export bidhaa za bustani (hot culture products). Ni hazina, ni kwamba hatupati kutoka nje flights za kutosha kwa sababu pia uzalishaji wetu hautoshelezi kwa ndege za nje ziweze kuja na zitue mahali pamoja, lakini tukiwa na ya kwetu itatua Mbeya, ije Dar es Salaam, iende Arusha, itajaa itapeleka nje. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, katika ubunifu nilioona hapa ni kwamba Serikali na timu ya finance wamegundua kwamba, sasa hivi nadharia ya kuongeza tu kodi siyo njia pekee ya kuongeza mapato ya Taifa. Pia unaweza ukahamasisha matumizi kwa mfano, kama ni wanywa bia wanywe kwa wingi zaidi, kama ni watumia simu, watumie kwa wingi. Kwa hiyo, this time tunaona wamejaribu kuangalia ni namna gani waongeze volume. I think tutapata mapato makubwa zaidi kwa kupunguza au kwa kutokuongeza kodi za vinywaji; bia na vinywaji vingine pamoja na vinywaji vya baridi, hawakuongeza. Nawapongeza kwa sababu watu watatumia na volumes zitaongezeka, kwa hiyo, naamini mapato yatakayotokana na ile volume itakuwa ni vizuri.
Mheshimiwa Naibu Spika, naona ile ya tozo tuliyozungumza mwaka 2021, wamepunguza, lakini pamoja na kupunguza kidogo baada ya mkutano wa mwaka 2021, na mwaka huu 2022 wamepunguza ile tozo ya miamala. Ninaamini kwamba, hiyo imetokana na ukweli kwamba, matarajio ya makusanyo kutoka kwenye tozo hayakufikiwa by more than 70% I think kutokana na takwimu. Kwa hiyo, hiyo kupunguza huko kutasababisha watu waendelee kutumia hiyo financial improvement iendelee kupatikana kupitia hiyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia hatua nyingi zilizochukuliwa kwenye bajeti hii zinalenga zaidi kuwapunguzia wananchi makali ya mfumuko wa bei ambao tunaona unatoka nje. Nataka niseme hivi, nitoe angalizo kwamba tusipeleke matarajio ambayo hatutaweza kuyafikia. Matarajio kwamba tunaweza tukadhibiti mfumuko wa bei kwa sasa hivi, naomba tujaribu kuwaelimisha watu kwamba kwa nini huu mfumuko ni mgumu?
Mheshimiwa Naibu Spika, huu mfumuko siyo ule wa kawaida ambao Benki Kuu wanaweza wakaenda tu wakasema tunapunguza ujazo wa fedha kwenye mzunguko wa uchumi wetu. Hawawezi, kwa sababu wakifanya vile siyo source yake. Source ya huu mfumuko ni ugavi; ni upungufu au uhaba wa bidhaa duniani, na uhaba wa bidhaa unachukua muda. Kwanza kuongeza uzalishaji kunachukua muda, kwa hiyo, hata ufanyaje ni kitu kinachukua muda.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ili kuongeza uzalishaji ni lazima tuweze kutoa mikopo. Hiyo mikopo ni ya kuwasaidia wale watu waweze kuanzisha miradi ile na kama kilimo wafanye. Ila ukweli ni kwamba, ukiongeza hiyo mikopo maana yake unaongeza fedha kwenye mzunguko, na unachochea demand. Kwa hiyo, hiyo inasababisha mfumuko wa bei uwe mgumu sana kuudhibiti kwa sababu, ukiingiza hela ili watu wazalishe, lazima itasababisha mfumuko. Ila ukweli hatuwezi kuepuka hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, ina maana kwamba, tukubali, hata kama mfumuko utaongezeka kidogo, lakini itakuwa ni temporary transitory, baada ya muda kidogo uzalishaji utakuja, tutapata mawese, na kadhalika halafu tutaanza sasa kushusha tena ule mfumuko. Kwa sasa hivi tusing’ang’anie sana hiyo.
Mheshimiwa Naibu Spika, lingine, kuna suala zima la stabilization fund ya bei za commodities. Nafikiri badala ya kufanya vile, mimi niende haraka niseme kwamba, nashauri Wizara iangalie mfumo wa commodity pricing insurance. Sisi tulifanya kwa kushirikiana na IFC pamoja na Rabobank pale wateja wetu wakafaidi sana. Tutumie huo mfumo badala ya kuanza funds na kadhalika. Hilo linawezekana sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, kingine kuna issue hii ya kutengeneza Dar es Salaam kama hub, na jana au juzi uliizungumza, naamini kitu cha msingi, hizi measure zilizochukuliwa sasa hivi ni za kupunguza ushuru ili watu waweze ku-trade kutoka Dar es Salaam zaidi badala ya kwenda jirani halafu mizigo inarudi kwetu, naamini kwamba hiyo itasaidia. Ila kwenye issue ya changamoto…
(Hapa, kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, aah, time keeper naona, huyu time keeper huyu!
NAIBU SPIKA: Ahsante kwa mchango mzuri. (Makofi)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, tum-audit huyu time keeper. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naunga mkono hoja na ahsanteni sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana, nikupongeze kwa namna unavyoendesha kikao chetu, nikupongeze kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze Mheshimiwa Rais wetu kwa kuendelea kusimamia na kuimarisha mhimili huu ambao unasimamia utoaji wa haki kwa wananchi wa Tanzania na ambao kama mwenzangu alivyosema ndiyo chanzo cha amani na utulivu tulionao katika nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia nitoe pongezi sana kwa Mheshimiwa Waziri wa Wizara hii, nitoe pongezi kwa Naibu wake pamoja na Katibu Mkuu, bila kumsahau Jaji Mkuu, pamoja na AG. Nimkumbuke rafiki yangu na mtendaji mzuri sana, Ndugu Elisante OIe Gabriel, Mtendaji wa Mahakama hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitatoa pongezi kidogo za kijumla halafu nitazungumza mambo ambayo nafikiri wengine wanastahili kuiga kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Wizara hii, ambayo tumezungumza sisi tukiwa kwenye Kamati ya Bajeti. Pia nitazungumza kidogo kuhusu Jimbo langu, Mahakama za Mwanzo zilivyokaa, zilivyo duni na zinastahili ukarabati. Mwishoni nitajielekeza kwenye kushauri kwamba ni vizuri supporting institutions, mamlaka zingine zinazo-support Mahakama kama vile DPP, TAKUKURU, Magereza, Polisi, wakachukua hatua za haraka na mikakati ya haraka ili kwenda sambamba na mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye Mhimili wa Mahakama, otherwise itakuwa haisaidii sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, pongezi za mwanzo na jumla ni kwamba na Watanzania wafahamu kwamba, Mahakama yetu ina jengo la state of art lililojengwa hapa Dodoma. Limejengwa kwa fedha siyo nyingi lakini ni jengo wanasema kwamba kimataifa pengine ni jengo la sita duniani la mahakama ambalo ni zuri zaidi. Jengo la sita is the state of art building watu wanaweza wakaja wakaliona, sisi tuliliona kwa kweli ni jengo lenye hadhi ya mahakama na ni jengo ambalo linatisha pia kwenda, utasema nisiende kule, nita-avoid kwenda kule kwa sababu unaweza ukapotea. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitoe pia pongezi kwa Mahakama hii especially kwa ubunifu wa Mtendaji wetu kuhusiana na mobile courts (mahakama zinazotembea). Naamini zimeshaanza, zimeanza mijini ila naamini zitasaidia sana kama wataweza kuziteremsha kwenye ngazi ya majimbo yale ambayo yako vijijini, kwa sababu kule juu kunahitajika sana na ndio kwenye ukandamizaji mkubwa na watu hawana fedha za kutafuta haki. Kwa hiyo, naamini kwamba hizi mobile courts zitafanya kazi yake na zitashushwa kwenye ngazi za chini kwa sababu zinatoa haki kwa namna ambayo ni gharama nafuu zaidi kwa wale watu ambao wanastahili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna hawa ambao wamezungumza kuhusu TTS, huu mfumo ambao sasa ni wa kwanza naamini kwa macho yangu mimi nimekuwa wa kwanza kuona kumbe artificial intelligence inaweza ikatumika very effectively na naamini kwamba ni ubunifu mzuri, waliweza kufanya jambo hili ambalo limerahisisha sana utoaji na uandikaji wa hukumu na tafsiri za hukumu ambazo zinatolewa baada ya kesi kusikilizwa. Pia inaweka kumbukumbu nzuri zaidi kuliko ambapo kama imefanyika na binadamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niende kwenye eneo la pili ambalo nataka kuchangia ni kwamba, kitu ambacho kimetufurahisha sana kwenye Kamati yetu ya Bajeti, ni namna ambavyo watendaji kwenye hiki kitengo utendaji wa Mahakama unafanya katika kutekeleza miradi. Wanaingia kwenye miradi na wakandarasi ambao wanapatikana kwa njia ya kawaida ambayo tunatumia NeST. Wakishafanya wanaandika mikataba ambayo inawaruhusu endapo baada ya mradi kutekelezwa wanaenda kufanya tathmini kuona kwamba, kweli ule mradi umetekelezwa kwa gharama zile walizokubaliana nazo au siyo na mara nyingi unakuta kwamba mradi umetekelezwa kwa gharama ambayo ni much less, kwa sababu wametumia vifaa pengine siyo vile. Nashukuru kwamba wanaweza kupata bakaa, wamekuwa wanapata bakaa kubwa kwenye utekelezaji wa miradi yao, bakaa ambayo wanaipeleka kwenye maeneo mengine, kwenye miradi mingine ambayo ilikuwa hata kwenye bajeti pengine haijapata nafasi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nashangaa na niliwauliza nikasema pengine ninyi kwa sababu ni Mahakama bado hawa jamaa wakandarasi wanaogopa kuwatapeli, kwa sababu sehemu nyingine wakandarasi hawa wanatapeli. Wewe unamwambia ajenge kitu cha gharama hii, value for money inashuka, wanatumia tu vitu wanavyotaka kutoka anywhere. Nashukuru na nasema kwamba, pengine tujifunze kwao mikataba ya utekelezaji miradi ya maendeleo nayo ifuate mkondo huo ili tuone kweli tunapata thamani ya fedha kwenye miradi yetu. Hilo ni jambo linalofurahisha sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ufanisi uliotekelezwa au miradi hii ya maboresho iliyotekelezwa kwenye Mahakama imewezesha kumkabidhisha miradi mingi na kesi nyingi zilizokuwa za muda mrefu, alisema 196,895 kesi za zamani. Wakaweza kuondoa 68% wakatekeleza, wakaondoa zile kesi ndani ya kipindi cha Julai kuja Februari, 2024. Ni jambo la kufurahisha sana na nawapongeza watendaji, ni jambo ambalo tunaona kwamba, kweli mwishoni tutaondokana na kesi za muda mrefu. Katika kesi hizi za muda mrefu, miezi sita tu wanasema ni ya muda mrefu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya kutoa haki kwenye majimbo yetu imeharibika, wamesema wenzangu, inahitajika zaidi ya Mahakama za Mwanzo 3,000, lakini ziko kama 900, tofauti ni kubwa sana. Naangalia kule jimboni kwetu kwamba, kweli nashukuru kwamba nilipata ukarabati wa mahakama moja ya pale Kilema, lakini mahakama nilizonazo kwanza ni kama nne tu kwenye kata zaidi ya 16, lakini ukweli ni kwamba zimechakaa, ni za miaka, tena huwezi hata kukaa, ni mahali pachafu kabisa, hapafai. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sana Mheshimiwa Mtendaji wa Mahakama, akatupatie Mahakama za Mwanzo kwenye Kata ile ya Kirua Vunjo Magharibi hatuna, Kata ya Kirua Vunjo Mashariki, Kata ya Marangu Mashariki na Magharibi hatuna, Kilema Kusini na Kati hatuna, pamoja na kule Kahe hakuna hata Mahakama moja. Nitaomba Mungu akituwezesha bajeti ile naona amepata 100,005 bilioni ya maendeleo atuangalie huko, atusaidie. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naona changamoto kubwa ambayo imebaki kwa Watanzania sasa kupata full enjoyment ya maboresho yanayofanyika kwenye Mahakama zetu na utoaji wa haki. Suala hili la kwamba sasa Mifumo ya Jeshi la Polisi, Mifumo ya DPP iko vizuri lakini anatakiwa na yeye achukue hatua. Mifumo ya kule TAKUKURU na Magereza ambayo ndiyo inapeleka kesi kwa Mahakama, basi iboreshwe ipate bajeti za kutosha ili iweze kuendana na speed ya Mahakama inavyokwenda. Mandhari ya kutolea haki kwenye maeneo haya ya mahakama kwenye ngazi zote kuanzia Mahakama ya Mwanzo basi iweze kuboreka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kuona kwamba hivi vituo jumuishi vinakuwa mpaka na sehemu za watoto kucheza. Kuna vitu ambavyo unaanza kuona kweli nchi yetu ni nchi ya kipato cha kati, japokuwa kwenye kiwango cha chini kidogo, lakini kweli tumepiga hatua sana kwenye mambo ya haki. Namshukuru Mungu na atuwezeshe sana. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naunga mkono hoja, nawatakieni Wenyeviti wa Kamati zote na Wajumbe wa Kamati zote zinazohusika na masuala haya, Kamati ya Bajeti na Kamati ya Utawala na wewe mwenyewe nawatakieni kila la kheri. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa fursa. Nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na uongozi mzima wa Wizara kwa yote yale ambayo wametekeleza katika mwaka huu. Ninaamini kwamba wataendelea kufanya kazi vizuri. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninampongeza sana kwa kusema kwamba anakutana na wafanyabiashara binafsi na kujaribu kutatua kero zao. Mimi ningeomba kwamba akutane na wazalishaji binafsi wazawa waliozaliwa hapa Tanzania, weupe au weusi. Azungumze nao ajue kero zao ili aweze kujenga mazingira wezeshi kwa uwekezaji katika nchi hii. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nimekutana na wachache. Juzi nilipokuwa Arusha nimekutana na wachache na wanasema, kusema kweli Mtanzania mzawa kuanza biashara au uzalishaji wowote hapa inakuwa shida sana. Akiingia kwenye ofisi yoyote ya mamlaka au taasisi ya Serikali, wanamwangalia kama vile huyu mtu amekuja kuomba pesa. Kumbe amekuja kujaribu kupata leseni au kufanya malipo ili aweze kuendeleza biashara yake. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, wanalalamika wanasema kwamba kwa mfano, Mheshimiwa Rais aliweka ukomo wa TRA kwa mfano kukagua au kutathmini hesabu za kampuni ili kuona kama vile walilipa kodi yao sawasawa lakini inakuwa ule ukomo waliouweka wa miaka mitatu, watu wanaingiza mbinu ya tathmini (Investigative Audit) ya tax. Kwa hiyo, unaweza ukakuta hata miaka 20 ule ukomo haufanyi kazi, halafu ule ukomo wenyewe haujawekwa kwenye Waraka ambao unakuwa unatekelezeka kwa watu wa TRA. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa tungeomba kwamba Waziri wa Viwanda na Biashara ambaye kazi yake na jukumu lake kubwa ni kuweka mazingira wezeshi, aone basi kwamba kila agizo lililotolewa na mamlaka au kila kilicho kwenye sheria kinatekelezeka kwa maslahi ya wawekezaji ili watu waweze kuwekeza kwa amani na wakijua kwamba hawatafuatiliwa ovyo ovyo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, pia, kuna tatizo hilo hilo linaweza likaendeleza mambo ya TRA kukagua akaunti za watu kwenye benki. Wanatuma Agency Notices kwamba huyu mtu hajalipa kodi kwa hiyo kama atapata malipo yoyote kwenye akaunti yake hayo malipo yaende moja kwa moja TRA. Haya mambo ni yale ambayo yalikuwa yameisha na mnaamini katika agizo la Mheshimiwa Rais kwamba wasibugudhi wafanyabiashara na wazalishaji hapa nchini. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, mojawapo ni hilo kwamba, siyo kutoa Agency Notices ambazo zinawapa watu shida sana katika kufuatilia na pia kutokuwa na amani katika uzalishaji wao. Ninaamini kwenye hilo Mheshimiwa Waziri atazungumza na Mheshimiwa Waziri wa Fedha ili waweze kutatua. Kuna tatizo ulisema kwamba kuna kero 300 zimetolewa, wanatangaza hapa Bungeni, lakini hata mimi ukiniambia hizo kero zilizoondolewa ni shida sana kuziona zimekuwa published kwenye gazeti ili wale ambao wanafaidika na kero zile waweze kutumia.
Mheshimiwa Naibu Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri ahakikishe kwamba kero zilizotolewa na amesema nyingine zimetolewa pia kwa wafanyabiashara wa Kariakoo, basi hizo nazo wajaribu kuziweka bayana ili watu waweze kuzitumia kero hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nichangie zaidi kwenye suala zima la mkakati wa viwanda. Mimi sasa hivi nasema kwamba mkakati huu tunaofuata wa viwanda vikubwa kwenda kuomba viwanda vikubwa wanakuja kuweka assembly plans hapa hatutatusaidia sana. Mkakati utakaotusaidia ni kuhakikisha kwamba tunaenda kwa viwanda vidogo vidogo hata kwenye majumba yetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, sasa hivi pale Mikocheni ukienda kwenye nyumba nyingi walizopangisha wageni fulani fulani hapa, wageni wa Taifa fulani fulani, wamekuja kuweka viwanda vidogo vidogo huko ndani wanatengeneza yebo yebo, wanatengeneza kila kitu. Halafu wanapeleka sokoni hawalipi kodi kwa sababu hivyo viwanda havijasajiliwa. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naona kwamba wanaharibu biashara za wengine kwa sababu wameweza kuweka viwanda vidogo vidogo. Vimashine vidogo vidogo wanatengeneza chipsi za ndizi, kila kitu wanatengeneza. Halafu tunasema tunakimbizana na viwanda vikubwa wakati tuna kilimo chetu. Kila kaya au kila kata inaweza ikachakata mazao yake kwa kuwa na viwanda vidogo tu na bei rahisi ambazo tunaweza tukaagiza kutoka nje.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili suala zima la kusema kwamba SIDO kama TXP wanatengeneza mashine, uongo huo. Ni kiwanda kipi kinatengeneza mashine (injini) hapa Tanzania? Mashine ni injini, siyo kudanganyadanganya hapa. Unapoteza hela nyingi kuvumbua kitu ambacho tayari kipo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ukienda utanunua mashine kwa bei nafuu, zile mashine utazi-deploy kwa kila mtu kwa bei nafuu kabisa. Kwa hiyo, hiyo hela ambayo tutatoa ruzuku kwa mashirika haya tunaweza tukawapa kata, kama ni ndizi wakafanya, kama ni viazi au nini, wakachakata. Ina maana wanaongeza thamani halafu pia wanaweka uwezo wa kuhifadhi yale mazao. Kwa hiyo, tukienda hivi tutakwenda haraka. Hatuwezi kufanya tu, yaani leapfrogging maana yake ni ku-imitate. Una leapfrogging kwa ku-imitate na kuorodhesha ile imitation uliyofanya ili uweze kupata tija zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, mimi naomba SIDO wajiangalie na wajitathmini, liwe ni shirika la kubuni, la kuwezesha kuchukua technology nje kui-customize ili iweze ku-fit scale ya production kwenye maeneo yetu na tuanze mara moja kusambaza na kuuza, tunauza cheap. Unawapa kwa mkopo wataongeza thamani watapata fedha nzuri zaidi watalipa mkopo ule. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, hii TIB nilikuwa ninasema igeuzwe kuwa ni benki ya starter ili watu waweze kupata mikopo kwa urahisi. Kwa hiyo, mimi naona hiyo itakuwa ni njia mojawapo ya kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda katika nchi yetu. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kila mwaka tulikuwa tunapewa idadi ya viwanda ambavyo vimeanzishwa ile idadi siku hizi hatupewi tena. Sijui ni kwamba imeisha, siku hizi viwanda havifunguliwi na siku zote tunasema kwamba kila wilaya iwe na specialization. Huo ni mkakati, huu mkakati umefia wapi?
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba huo mkakati ufuatiliwe tena ili kwa mantiki hiyo kwamba kila mahali kwenye zao, tuwape watu nyenzo hizo za kuanza viwanda na kuchakata na kuongeza thamani ya hayo mazao yao. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, naamini kwamba huko tunapoenda n` i kuzuri na ukiangalia vipaumbele vya mwaka unaokuja vilivyowekwa na Wizara, vipo vizuri vimekaa bayana lakini naomba basi hiyo kasi ya kutekeleza kwa kushirikiana na kuhakikisha kwamba local content inakuwepo.
Mheshimiwa Naibu Spika, tukiangalia hesabu zote tulizoambiwa hapa za exports za mazao na bidhaa za viwanda hatungeweza kuona uhaba wa dola hapa nchini, lakini ubaya hamwoni kwamba siyo sisi, wanatoa bidhaa kwenye export processing zone wanapeleka nje, pesa inaenda kwenye nchi, kwenye mataifa yale ambayo wale wawekezaji wapo, haiji Tanzania. Kwa hiyo, siyo hela yetu ile, hatutozi kodi, hatufanyi nini licha ya wafanyakazi wetu kufanyishwa kazi na kwenye mazingira magumu sana, lakini ukweli ni kwamba inapokuja ni export tunashangilia, tume-export, lakini hela hiyo ya kigeni iko wapi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, tukifanya sisi hii kuongeza thamani ya bidhaa zetu za kilimo, tukianzia kile tulichonacho halafu tukapeleka nje, nakwambia thamani ya export zetu itakuwa kubwa na zitakuwa earned na watu wetu hapa na ni lazima kweli kubali kwamba lazima tulinde na tujali masilahi ya wazawa. Wazawa, mimi sisemi wazawa ni weusi na weupe ambao wamekaa wanazaliwa hapa tuwatetee. (Makofi)
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunifanya niwe wa mwisho kwenye kipindi hiki cha asubuhi. Mimi nianze kwa kumsifu na kumshukuru mtukufu Mheshimiwa Rais wetu kwa kuwa mdau wa kwanza wa Sekta hii ya Utalii na kujua kwamba, Sekta hii ya Utalii ilitakiwa iwe ni Sekta ya kipaumbele baada ya Sekta ya Kilimo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sekta ya Utalii pekee ndiyo inaweza ikatuletea ukuaji mkubwa wa Pato la Taifa kwa wakati bila kuwekeza sana. Halafu pia, inaweza ikatusaidia sana kuongeza fedha za kigeni. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema kwamba, unapozungumza kwa mfano Sekta ya Madini ambayo tumeichangamkia. Sekta ya Madini fedha yote ya mapato yake inayopatikana, mapato yake yote makubwa yanaishia nje na fedha za kigeni zinazokuja pengine unaambulia asilimia sita ile ya mrahaba tu. Kwa hiyo, mimi nasema hii ni Sekta muhimu na bila kupoteza muda ninataka nimpongeze pia Mheshimiwa Waziri wa Utalii, Mheshimiwa Kairuki pamoja na Naibu wake na viongozi wote wa Wizara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi nasema hiyo kwa mambo tuliyosikia toka asubuhi yakisomwa kutoka Buchosa, halafu baadaye tukasikia kutoka kwa Kamati na kwenye hotuba yenyewe ya Mheshimiwa Waziri inahitajika pengine tufanye upya tathimini ya sera, sheria na kanuni za hifadhi za wanyamapori na hifadhi za misitu kwa sababu kuna changamoto nyingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naona kwamba tunaendelea kutenga hifadhi bila kujali kwamba wanadamu nao wanahitaji sehemu za kukaa na halafu hizi hifadhi zinakuwa ni heritage ya dunia nzima. Sasa inavyokuwa vile, ni lazima Dunia nzima iwe inachangia kwenye kufidia wale watu au wananchi wanaohamishwa au wale wanaopata athari mbalimbali. Kwa hiyo, somehow tutafute njia ya kuwalazimisha wenzetu kwenye hizo nchi tajiri waweze kuwa wanachangia kwenye athari zinazotokana na uhifadhi huu wa hifadhi za wanyama pamoja na misitu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi, kwa mfano pale kwangu, kwenye Jimbo langu la Vunjo, Kijiji cha Komela, Kitongoji cha Komela, tarehe 09 Mwezi Mei, mwaka huu, askari wa hifadhi walimpiga risasi mbili kijana wangu na mpigakura wangu mwenye miaka 39, Octavian Temba. Baada ya kumpiga kijana huyo alikufa pale pale. Kijana huyo aliacha familia ya watu watano, mmoja akiwa bado hajazaliwa lakini wanne wakiwa ni wadogo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa mimi nikasema, kweli nilitakiwa nilete hoja binafsi Bungeni hapa lakini nikajizuia sana. Nikatumia nguvu zangu sana kujizuia nisilete ile hoja wakati ule kwa sababu walisema ngoja uchunguzi ukamilike; lakini zaidi nilisaidiwa na Mheshimiwa Waziri msikivu. Mheshimiwa Waziri alinipigia simu akaniambia subiri tuone sheria itachukua mkondo wake na kweli wale askari walikamatwa na kuwekwa rumande. Sijui wamefikia wapi lakini tunafuatilia jambo hilo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachosema ni kwamba, pamoja na kwamba KINAPA walishiriki katika mazishi ya yule kijana baada ya wananchi kuwa wakali sana na kuvuruga miundombinu lakini nafikiri lazima Serikali itoe tamko lingine, kwamba hata rambirambi hawajatoa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Serikali itoe rambirambi kwa familia iliyobakia. Ni watu masikini na ni watoto. Watoe rambirambi na ninaomba kwamba Serikali iweze kutoa neno au kauli kwa suala hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwamba Kamati na pia hotuba ya Mheshimiwa Waziri imeelezea kwamba, inataka kuongeza fidia kwenye maeneo hayo yanayotokana na hifadhi hizo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, huyu kijana alikuwa anakata majani tu ya ng’ombe. Kwa hiyo, alikuwa hakati mti au hafanyi chochote. Naomba hicho kifanyike na hiyo Sheria sasa ikiwa reviewed, tuweze kuona ni namna gani tutaingiza masuala mazima ya kuvuna wanyama, masuala mazima ya carbon trade. Hii carbon trade inatakiwa kuleta fedha za kufidia wale watu wanaokaa jirani ambao walikuwa wananufaika kukata majani na kadhalika. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hile concept ya carbon trade mimi niliizungumza hapa baada ya hili suala la nusu maili kushindikana, nikasema basi tufanye carbon trade hela ikipatikana, sehemu ya ile hela iende kwa wale wananchi wa vijiji vinavyozunguka ile milima.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa utalii, natoa pongezi sana kwa TATO na TAHOA, ambao wameingia wenyewe wanaanza ku-market. Wanaenda kwenye Soko la Dunia na kwenye mikutano ile mikubwa wanaenda kuuza utalii wetu wakati hapo zamani ni Serikali ndiyo ilikuwa inafanya yenyewe. Sasa hivi binafsi wanaenda na ndiyo sababu wanaleta tija na ongezeko kubwa linatokana na jitihada za kutangaza za watu binafsi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka niseme hivi, lazima tuwasaidie. Nashukuru Mheshimiwa Waziri ametangaza kwamba, tozo zinatolewa na leseni zinafanywa upya kwa mfumo mpya. Nasema kwamba, tatizo la watu wanao-operate biashara hapa nchini, wote tunaowasikia wanasema tatizo pamoja na hizo tozo kuwa utitiri lakini zikusanywe na mamlaka moja. Hiyo mamlaka moja izisambaze kwenye zile mamlaka nyingine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa issue ya kwamba mtu mmoja anaenda kulipia leseni au kulipia levy mahali kwa watano na hajui ni wangapi kwa sababu wanaongezeka siku hadi siku inakuwa inaongeza sana gharama ya kufanya biashara hapa nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naomba sasa pamoja na haya yanayofanyika basi kwa kusaidia wafanyabiashara wote basi Mheshimiwa Waziri azungumze na Mheshimiwa Waziri mwenzake ili tuhakikishe kwamba hizi tozo zinakusanywa mahali pamoja. Pia, tozo hizo kuna zingine hata hazi-apply. Kuna hizi mamlaka zote za NEMC, CAMARTEC, LATRA, TBS, TARA kwa upande wa hawa, Local Government Authority na wenyewe wanakusanya service levy, inakuwa very difficult. Kwa hiyo, naomba hilo suala lichukuliwe na litiliwe maanani na mambo haya yakamilike kama inavyostahili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sababu ya muda naomba niishie hapo. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa fursa hii ili nichangie kwenye hili jambo ambalo ni la msingi. Ni sekta ambayo inagusa kila mtu katika nchi hii na hata nje ya nchi hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, watu wanaothubutu kutekeleza mambo magumu ni wachache sana hapa duniani na naomba niseme kwamba Mheshimiwa Rais wetu kweli ana uthubutu…
MWENYEKITI: Waheshimiwa naomba tutulie, tumtazame na tumsikilize Mheshimiwa.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tumpongeze sana kwa kukubali kutengeneza sera mpya na mitaala mipya ambayo itaenda kubadilisha kabisa mfumo wa elimu nchini. Mfumo siyo kitu rahisi sana kubadilisha ni kitu kigumu na ni kitu ambacho ni nyeti, ni kitu ambacho lazima kweli twende kwa usahihi wake. Profesa Muhongo alituelimisha hapa lakini nataka niseme kwamba ni kitu cha msingi sana, kwa hiyo tukichezea tutakuwa tumeharibu sana shughuli zote hizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nimpongeze sana Profesa Mkenda na Naibu wake Mheshimiwa Omari na Timu yake yote kwa kazi ambayo wanafanya, tunaiona. Najua ni ngumu lakini kama anapata usingizi, basi naye ni mtu anayethubutu sana, lakini ukweli ni kazi ngumu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza sitaki kuingia kwenye viatu vya wale maprofesa walioanza kuzungumza. Nianze kwenye jimbo langu, kule kwenye jimbo langu nina wakazi 255,000 na hatuna Chuo cha Ufundi cha VETA, ina maana kwamba mwanafunzi aliyemaliza shule ya msingi au sekondari akitaka kupata mafunzo ya ufundi lazima atumie shilingi elfu nne mpaka elfu kumi kwenda Moshi Manispaa ambako ndiko karibu vyuo vyote vya VETA vimewekwa. Sasa naomba sana kwamba kusema kweli hili halitatufikisha mbali, naomba sana Serikali ione namna gani ya kutupa fedha tuweze kujenga angalau chuo kimoja cha VETA kwenye Jimbo langu la Vunjo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia tuna shule moja pale kwenye kata ya Mwika Kaskazini inaitwa Shule ya Lole ilikuwa shule ya awali, msingi na ufundi wa VETA lakini kuanzia mwaka 2000 shule hii haijatoa tena masomo ya ufundi kwa sababu imekosa walimu na karakana zake zimekuwa ni chakavu sana. Pia, majengo yale hayafai yanastahili kupata ukarabati ili tukipata na walimu basi tunaweza pia kuanza shughuli ya kuanza kufundisha vijana pale. Hayo ni ya Vunjo, ya Vunjo yako mengi lakini ngoja niseme hayo mawili ili niweze kuzungumza na mengine ambayo nafikiri ni ya muhimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama alivyozungumza Mheshimiwa Profesa Muhongo, lakini kitu ambacho hakukisema nafikiri ni ile nadharia ya education for Self-reliance ilikuwa inalenga sera hii hii ambayo tunataka kutengeneza sasa hivi, isipokuwa kwa namna moja au nyingine tulitekeleza bila kuwa consistent na bila maandalizi ya kutosha. Kwa hiyo ikaonekana baadaye tuka-abandoned ule mfumo wa education for self-reliance ambapo watu walijifunza nadharia, lakini na vitendo pia vilikuwepo. Nakumbuka tulikuwa tunalima sana, lakini hatukuibuka kuwa wakulima wazuri kama tulivyotarajiwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo nasema kwamba tumejaribu lakini tukashindwa, tukaacha tukarudi kule kule, kwa sababu mfumo ni vigumu sana kutekeleza na unahitaji rasilimali nyingi ya fedha na watu. Kwa hiyo, nasema kwamba, sidhani kama bajeti ambayo imetengwa na hata hii nimekuwa naiangalia, haitatosheleza. Kama kweli tunataka kwenda na kasi ambayo Mheshimiwa Rais anaonesha, anataka kwenda nayo na Wizara inataka kuonesha kwamba inaweza kwenda nayo, basi ni lazima tutenge fedha za kutosha kutengeneza miundombinu ambayo inastahili hususan kwenye mkondo wa amali ili watu waweze kujiandaa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, miundombinu ya sasa siyo ile ya zamani, naona wanazungumzia masuala ya seremala na masuala ya ufundi uwashi, sasa hivi kwenye mkondo wa amali tunahitaji kwenda na teknolojia ili tujue kwamba kama ni ufundi wa magari siyo yale magari ambayo unachochea, ni magari ambayo yanatumia umeme na mfumo wa kidijitali ambao ni wa kisasa, hivyo hawa vijana lazima waandaliwe na vifaa kwenye zile karakana ni lazima viendane na mahitaji hayo ya sasa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kama tutaenda kujenga ili mradi tunajenga madarasa na kuweka vifaa vya zamani ambavyo ni vizito sana, hatutafika mbali, by the time tunafika kule utakuta wale vijana hawatapata kazi na hataweza kujiajiri kwa sababu hakutakuwa na mahitaji hayo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, bajeti inaonekana haitoshi, kwa sababu gani? Ukiangalia data zilizo kwenye randama, kwa mfano, nalenga tu kwenye upande huu wa mkondo wa amali. Katika mwaka uliopita wameongeza uandikishaji wa wanavyuo lakini kwa upande wa technical education training utakuta kwamba shule ziliongezeka na ndizo zilizoongeza wanachuo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jumla ya shule za TET (Technical Education Training) zilikuwa 465 Mwaka wa Fedha 2022/2023, zikaongezeka zikafika jumla ya vyuo 474, vimeongezeka vyuo tisa kwenye huo mwaka ambao tunatekeleza bajeti yake, kati ya hivyo Serikali haikuongeza chuo hata kimoja, vyuo vyote tisa vimetokana na private sector. Sasa, kama kweli tunajenga huo mkondo tutaujenga bila kuongeza vyuo na tutategemea private sector?
Mheshimiwa Mwenyekiti, vivyo hivyo katika VETA. Vyuo vya VETA jumla vilikuwa 687 ilipofika Juni, 2023. Katika miezi hii tisa vimeongezeka 145 na kufikia 830. Kati ya hivyo nyongeza ya 145 Serikali imeongeza chuo kimoja tu na vyuo vingine 144 ni vya sekta binafsi. Sasa najiuliza kwamba, je ni kweli kuna nia ya kwenda na kasi hiyo ambayo inastahili? Tunataka 2027 tuanze kutekeleza full-blown? nafikiri tunahitaji bajeti sana kwenye suala hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba strategy bila kuwa na execution inakuwa ni ngumu sana kufika mbali. Kwa hiyo, nafikiri lazima watu wajipange zaidi na pengine tujaribu kuiga ili kuona hawa wenzetu wamefanyaje katika nchi zile. Seychelles ambayo ameitaja Mheshimiwa Muhongo iko juu sana, kwa Afrika ni namba moja kwa mfumo bora wa elimu. Kwa hiyo, tujaribu kujifunza ni kitu gani na wametekelezaje ili tusije tukarudia makosa na nafikiri kule tulikotoka tungeweza kwenda incrementally tukaboresha ile Sera ya Education for Self-Reliance, halafu tukaiongezea vitu vingine ambavyo havikuwepo hususani kuboresha namna karakana ambazo zilikuwa zinatumika, zile workshops kwenye shule zetu zilizokuwepo middle schools, tungeenda vile pengine tungekuwa tuko mbali zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuunga mkono hoja. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (Toleo la Kiingereza)
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru sana, nianze kwa kumshukuru na kumsifu na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa msikivu na kuelekeza baraza lake la mawaziri vizuri.
Nimpongeze pia Makamo wa Rais nimpongeze Waziri Mkuu, nipongeze baraza zima la Mawaziri, pia nimpongeze sana kipekee kabisa Mheshimiwa Dkt. Nchemba kwa hotuba nzuri aliyotoa jana, na kwa kuwa ni msikivu sana, la tatu nisema kwamba ametendea Ph.D yake haki jana, allitoa mada yake alitoa hoja yake vizuri na ninaamini ndio sababu wengi wanapenda kuchangia kwenye jambo hili. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba ukiangalia mswada ambao umeletwa Mbele yetu, ni mswada ambao unakidhi matakwa ya kufikia malengo ambayo ni makubwa kwa bajeti yetu ya 2021/2022 pamoja na mpango wetu wa maendeleo ambao nitasema kwamba ni ile miradi ya kielelezo ambayo tunajua itapata fedha, kuendeleza miundombinu ya kiuchumi na huduma za kijamii, kujenga mazingira Rafiki kwa wawekezaji, blue prints na hasa jana tukasikia Mheshimiwa Waziri anasema nini, kwamba hata areas au yale madeni ambayo privet sector wa contactors hawajalipwa yanaweza yakalipwa pia kutokana na fedha hii ambayo itapatikana ya ziada, kutokana na ubunifu ambao imejitokeza kwenye kuangalia na kubuni vyanzo vya mapato ya Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba ukijumlisha zile fedha ambazo Mheshimiwa Waziri wa Fedha jana alizielezea kwamba ni za ziada na zitapelekwa kwenye maeneo mbali mbali, unaona kwamba sasa tunaweza tukakusanya kitu kama tilion 26, ndio mapato ambayo yanayijitokeza kwa hesabu za haraka haraka, hii inamaana kwamba tunakusanya mapato ambayo ni asilimia 17.5 ya pato la Taifa. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutakuwa tumefanya tax effort kubwa sana, kwa hiyo tatizo kubwa letu kwenye hii bajeti na kuhakikisha kwamba tunatekeleza tukae mpango wa kukusanya vizuri, inamaana gani? Inamaana kila mtu Serikalini hata sisi wabunge tuhakikishe kwamba ile elimu kwa walipa kodi inakwenda na kwamba tunafanya kila kinachowezekana ili Serikali ipate pato lake na ili hii miradi iweze kutekelezeka na sera yetu na bajeti yetu iwe na muoleleo huo ambayo sasa unaona kwamba itaendelea kupunguza in-quality katika mapato ya watu. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inapotumia fedha nyingi kwenye huduma za kijamii, na kutumia fedha nyingi kwenye miundombinu ya kiuchumi inamaana kwamba inapunguzia mtanzania, inampunguzia mwananchi wa kawaida mzigo wa kulipa kwa sababu anakuwa amepata bure kama kapata bima ya bure inaama unakwenda kutibiwa bure, inamaana fedha haikuingia mfukoni mwako lakini imekusaidia wewe sasa kuongeza kipato kwa njia ambayo ni in direct. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi kwamba nafikiri katika yote yanayo zungumzwa, jambo muhimu ni kutengeneza ile guideline au mwongozo wa kutekeleza hizi kodi mpya zilizokuja. Kodi ya luku, kodi ya majengo kupitia luku, kama ile program ambayo alikuwa ametueleza Waziri hapa jana, program ambayo inatengenezwa kuweza kukusanya kupitia luku. Kama haijakamilika upesi tutacheleweshwa, na inatarajiwa kwamba wakati huu kodi hii ya mapato imebuniwa kutoa au imekadiriwa kutoa fedha nyingi sana kwa Serikali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo hivyo kodi inayotozwa kwenye fedha za mobile money na airtime. Sasa niseme kuna wakati ule tulivyoingiza extra duty on financial transition, TRA iliwachukua muda mwingi sana kuja na guideline ya kwamba itatozwa namna gani. Nawaomba watu wa TRA wapo hapa wafanye haraka ili kuwa muongozo uende kwa wale wanaohusika wale wadau wetu ambao ni makampuni ya simu na mabenki waweze kujua kwamba wana-adjust mifumo yao pia kuweza kukusanya hiyo fedha electronical, hiyo ni moja. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha pili ni issue hii ya uwezo wa Tanzania Revenue Authority mamlaka ya mapato, kusema kweli unaambiwa kwamba kwenye majimbo au halmashauri waajiriwa wa TRA ni wachache sana. Sasa kama TRA haitajipanga haitaongezewa rasilimali watu na rasilimali fedha naamini kwamba hatutafika. Kitu kikubwa katika utengezaji wa sheria hii ambayo itakuja kutufinya sisi wenyewe kwa vile tutakuja shindwa kitekeleza na tutashindwa kusimamia Serikali, kikuwa ni kwamba uwezo wa kukusanya hayo mapato. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, mapato ni mengi na inaonekana kwamba vianzio ni bunifu sana, naamini kwamba tukikusanya tutafika pazuri na tunaweza kutekeleza malengo yetu ya bajeti na malengo wa mpango wa maendeleo. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa niseme hivi kuna mambo ambayo tunaona kwamba yangeweza yakaongeza revenue base yetu au taxi base yetu, moja ni kufanya Dar es Salaam iwe a logistic hub kweli kweli. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Sasa hivyo unfortunately Inakuwa na vikwazo vingi lakini moja wapo ni East African Customs Management Act, inakuwaje hivi, kwa sababu huku kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki axle load inayokubalika ni maximum thirty tonnes huku ambako ziko mizigo mingi inakwenda mizigo inapita sasa hivi Dar es Salaam sasa hivi mingi inaenda SADC, sisi pia ni watu wa SADC ni jumuia ya SADC. Sasa hatuwezi kubeba mzigo iende Kongo inazidi au iende Zambia au iende huko kusini kwetu Mbeya inazidi tani 30.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa utakuta kwamba watu wengi na tunaambiwa na watu wa TPA kwamba meli nyingi hasa zinaenda Beira kwa sababu kule wanaruhusu axle load ya 50 tonnes. Sasa mimi nataka niseme hivi tujaribu nataka pale wenzetu kwenye jumuia ya wenzetu partners wajue kwamba sisi iyo inatuzuia maendeleo, hiyo ya kuzuia mzigo mkubwa wa tonne 50 kupita kwenye barabara zetu ni jambo ambalo haliwezi ku-facilitate industrialization kwetu kwenye zone ya kusini au hata kuwasaidia wenzetu kupitisha mzigo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nafikiri hiyo ikitokea inaweza kuwa njia pekee au njia kubwa ya kutupa mapato siku za Mbele. Sasa niseme pia kwamba hili la ushuru wa bidhaa ya pombe tamtam hizi kali, nafikiri hivi ukweli ni kwamba miaka mitatu au zaidi huku nyuma bei hazikuwa zinaongezwa kwa kasi ya mfumuko wa bei, sasa ukichukua compound rate ya three point of inflation kwa miaka mitatu tu inakuja 3x3x3 ni 27, kwa hiyo wazee wa fedha inakuja na 30 it was within. Sisi tukasema hapana kuja kwenye Kamati ya Bajeti ikasema hapana punguza kidogo ikashushwa ikawa 20.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, naamini kwamba hawakuwa nje ya sheria, wako ndani ya Sheria hasa baada ya kushuka kwenda 20. Kwa hiyo, napenda kinywaji changu lakini hiyo hainitishi sana laizima tulipie mfuko wa Serikali ili Serikali ipate mapato. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa nataka niseme kuna suala la hizi fedha ambazo zimeongezewa kwenye maeneo mbali mbali. Sasa kuna pendekezo la bajeti escalating inasema kwamba ile wakati bei za mafuta zina fluctuate, zikishuka ile asilimia 50…
MWENYEKITI: Ahsante, Dkt Kimei mda wako umekwisha.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: …kutokana na hiyo inakwenda kwenye kilimo, kwa hayo naomba niunge mkono hoja, ahsante. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Utakatishaji wa Fedha Haramu wa Mwaka 2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa fursa hii. Nianze kwa kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu kwa kukubali kwamba muswada huu uje kwa hati ya dharura. Nimpongeze Mheshimiwa Waziri wa Fedha, Naibu wake na timu yake kwenye ile Wizara pamoja na Mwanasheria Mkuu na CPD kwa kuweza kuwa wasikivu sana katika kusikiliza hoja ambazo zimetolewa na ndiyo sababu tukaona kwamba ile draft iliyokuja imebadilishwa kwa namna ambayo inaridhisha sana.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba nimekuwa reporting agent kwa miaka mingi sana, miaka kama 13, kwa hiyo najua namna gani nchi itafaidi kutokana na suala hili la kuweka sheria na sera ambayo najua itakuja baadaye itakayoweza kudhibiti utakatishaji wa fedha haramu pamoja na ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa proliferation ya weapons of mass destruction (silaha za maangamizi).
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme kwamba mimi ninavyouona na nafikiri kwamba wananchi wataelewa vizuri, kwamba sasa nchi yetu inajiingiza kwenye mfumo wa kimataifa wa malipo (international payment system), tunaingia sasa tukiwa na hadhi tofauti na ile ambayo tulikuwa tunaonekana. Kwa sababu hiyo naamini kwamba itaipa heshima hata passport yetu, ukiwa unasafiri sasa unakwenda mahali popote kwenye nchi nyingine mtu akikuona hakushuku kwamba huyu mtu anaweza akawa amebeba fedha ambazo ni haramu, hutaweza kupekuliwa sana pengine.
Mheshimiwa Mwenyekiti, zaidi ya hiyo, ni kwamba inainua hadhi ya mabenki yetu. Mabenki yetu mengi yale madogo na ya kati yamepata shida sana katika kufungua akaunti na mabenki mengine ya nje ili waweze kufanya miamala na akaunti zile za mabenki mengine kwa sababu mabenki mengine huku nje yanahisi kwamba mabenki haya hayajajiweka sawa katika kudhibiti fedha haramu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo imekuwa vigumu sana kupata correspondent banking relationships ambapo hakuna benki inayoweza kufanya biashara vizuri bila kuwa na mahusiano na mabenki ya nje. Naamini sasa watakwenda kufungua milango ile na mabenki yale ambayo yalikuwa bado hayajaweza kufungua badala ya kupitia milango ya nyuma au migongo ya mabenki makubwa, nazo ziweze kuingiza biashara yake kwenye mifumo ya kimataifa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka kusema kwamba of course kuna faida za kiusalama kubwa na naamini kwamba hilo limefanyiwa kazi vizuri na haitakuwa tatizo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niseme hivi; kwa wale ambao hawajui kitu gani kinafanyika, kushuku miamala ni nini? Unashuku kitu ambacho ni abnormal kwenye mtiririko wa mapato ya mtu au kwenye akaunti ya mtu. Naamini kwamba huu muswada umekwenda mbali sana, kwa nchi nyingine nyingi kwa kiwango cha kimataifa watu wanaofanya ripoti hizi, wanaotoa taarifa hizi ni financial institutions, mabenki na taasisi za kifedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa sisi tumeweka na wengine wengi, kwa hiyo naamini sasa tutaonekana kama vile tuko juu ya kiwango cha kimataifa, kwa sababu tunasema hata customs wataripoti. Of course, customs watakuwa wanaripoti kwa sababu ya fedha zinazopita mipakani lakini naweza kusema kwamba kwa wale wengine, kwa mfano car dealers et cetera pengine hawataripoti kwa sababu hawataona kitu chochote cha kuripoti, hakuna mtu ambaye hataki kuuza halafu uende kwake kuuliza maswali 20 anapotaka kukuuzia gari, lakini itaonekana kwenye akaunti za mabenki.
Mheshimiwa Mwenyekiti, naamini kwamba ultimately the major reporting person itakuwa ni taasisi za kifedha na watu wasiogope kwamba eti kila mtu atakuwa reporting agent, haitakuwa hivyo. In fact, itakuja kugeuga kuwa hivyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna tatizo moja ambalo naliona, hii issue ya elimu; wananchi wanaogopa kwamba ukiweka fedha benki unakuwa reported kila wakati, kumbe hapana. Ile hela yako iliyo kule benki kama ni deposit yako haiwi reported kinachokuwa reported ni ile miamala ambayo inapita kule ambayo inaonekana kwamba haihusiani na kitu unachofanya. Kama wewe ni Mbunge halafu suddenly ukaingiziwa shilingi milioni 50 na hujui zimetoka wapi, lazima benki itaripoti na utatafutwa, lakini siyo ile balance, haina tatizo sana, siyo muamala.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninachotaka kushauri hapa ni kwamba elimu ifanyike kama walivyosema wenzangu, kuwe na elimu kwa wananchi waelewe kwamba ni namna gani haya mambo ya kushuku yanafanyika, inatokea wapi na implementation ya sheria hii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, cha mwisho niseme kwamba, ibara ya 12 kifungu cha 15 kwenye ile iliyorekebishwa kinaweka sharti la kufanya tathmini ya viashiria hatarishi vya utakatishaji wa fedha. Sasa haijaweka itafanyika kwa muda gani; itafanyika kila baada ya miaka mitano au baada ya miaka kumi au kila mwaka? Sasa zoezi la kufanya tathmini lina gharama sana na ndiyo sababu halifanyiki hovyohovyo, gharama zake ni za juu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo tunaomba kama pengine kwenye kanuni zitakazozungumzwa na Mheshimiwa Waziri, ziweze kuainisha hilo kwamba hii tathmini haitafanyika hila mwaka itafanyika baada ya miaka mitatu au baada ya miaka mitano au kitu kama hicho.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, hilo ni la msingi na naamini kwamba kweli tukipitisha sheria hii ambayo naiunga mkono kwa asilimia 100, basi tutakuwa tumeiweka nchi yetu kwenye hadhi iliyo juu sana katika masuala haya ya fedha haramu pamoja na utakatishaji fedha.
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
MWENYEKITI: Ahsante sana.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. (Makofi)
Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa Mwaka 2022
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa fursa hii na nianze pia kwa kujiunga na wenzangu kumshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa Rais wetu anayeongoza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuanza kuchukua hatua madhubuti na za kimkakati za kuongeza uwekezaji na kasi ya uwekezaji katika uchumi wetu, kwa vile mimi naona kwamba Muswada huu una maudhui ya kimkakati kabisa na siyo tu kwamba, tunaona kwamba kuna kupunguza hapa na pale lakini utaona kwamba ni Muswada au ni marekebisho ambayo yanaenda kumpa Mheshimiwa Waziri wa Fedha uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka ili kuweza kuruhusu miradi ile mahiri na ya kimkakati kuanza hapa nchini upesi bila kusubiri bureaucracy ya kupeleka kwenye Bunge kwa sababu sheria za kikodi mara nyingi zinahitaji zirudi huku Bungeni, na naamini kwamba Mheshimiwa Rais ameruhusu Muswada huu uje ili uweze kufupisha ule mchakato wa Mwekezaji kuweza kufika na kuanza mradi wake. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa sisi tunaofahamu ni kwamba, Wawekezaji wote na miradi mingi inakuwa na mahitaji tofauti tofauti ili iweze kuonesha kwamba itakuwa na faida katika kipindi ambacho yule Mwekezaji amejiwekea. Bila yale masharti au zile athari ambazo yeye anaziona kwenye mradi ule, hazijawa addressed kwa namna ambapo yeye na Bodi zake, kama ziko nje ya nchi au ziko hapa hapa nchini, basi inakuwa vigumu sana kuchukua hatua ile ya kuanza kutekeleza mradi.
Mheshimiwa Spika, mara nyingi watapita kwenye maeneo mbalimbali, wataanza TIC ambapo baadaye wataishia hata kwenye National Investment Steering Council - Kamati ya Uwekezaji ya Taifa, lakini kama hawana uhakika kwamba yale wanayojadili, yale yanayojadiliwa na taasisi hizi hayatatekelezwa haraka, ni lazima pengine yaje Bungeni yaulizwe maswali mengi, pengine yasipite, basi inakuwa ni vigumu sana miradi ile kuanza.
Mheshimiwa Spika, nami naamini kwamba hili mkakati wake unatokana hilo; kwamba sasa Waziri wa Fedha, na niseme kwamba sio tu Waziri wa Fedha; na tumeridhika sana kule kwenye Kamati yetu kuona kwamba Waziri wa Fedha atatekeleza haya baada pia ya kupitia kwenye cabinet kwenye maeneo fulani fulani; lakini ni miradi ile ambayo imepita kwenye Kamati ya Taifa ya Uwekezaji ambayo inasimamiwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu. Siyo tu Waziri Mkuu, pia ndani yake kuna kuna watu ambao ni mahiri, ni watu ambao ni wazalendo ambao tunajua kwamba wanaongoza taasisi ambao zinaelewa masuala ya uwekezaji kwa mapana kama vile Benki Kuu na wengine. Kwa hiyo ninaamini tutakwenda mbali.
Mheshimiwa Spika, lakini pia tunajua kabisa kwamba, tena tumeambiwa, kuna congress man mmoja kule Marekani ambaye ame-trend sana; natumaini wengi wameona; anatoa changamoto. Kwamba ukweli tatizo kubwa la uwekezaji huku nchini linatokana na kodi nyingi na kubwa. Ile corporate tax, ukienda kwenye VAT ziko juu. Na nini, mimi ninakubaliana naye kwa namna fulani. Ni kweli kwamba tusipoangalia vizuri na tusipoweza ku-treat kila mwekezaji kwa namna fulani ambayo inampa au kinampa uhakika; kwamba zile gharama zisipoweza kupunguzwa, zikafanywa hivi kwa kupunguza VAT kwa muda fulani tutakaa muda mrefu bila kuona uwekezaji ukiongezeka. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, na huu uwekezaji unashindaniwa. Kila nchi inashindania uwekezaji kwasababu inajulikana kwamba capital discuss duniani ni taji, haipo tu hovyo hovyo, ni taji inashindaniwa na nchi mbalimbali na shughuli mbalimbali, na kila nchi inajaribu kutoa kwa namna fulani vivutio ambavyo vinaweza kuwezesha wawekezaji wakaingia. Kuna nchi nyingine sasa hivi zimeanza, na natumaini ni nadharia mpya ambayo inakuja; kwamba the only way ya kuongeza tax base ili kuongeza government revenue bila kuongeza viwango vya kodi ni kuongeza uzalishaji. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa, kama hatuwezi kuongeza uzalishaji kwa namna hii ya kuvutia wawekezaji, kitu ambacho hatuna uzalishaji ambao haupo lakini tukiwavutia watakuja tukawapa dispensations fulani, tukawapa misamaha fulani kwa kipindi ambacho kinakubalika hawa wawekezaji wakaja wakaongeza uzalishaji tukaanza kuvuna Pay as You Earn, tukaanza kuvuna vyote vile vingine vinavyotokana na uzalishaji kuongezeka katika nchi hii hakutafika mbali. Kwa hiyo nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Fedha kwasababu naona kwamba hii nadharia ameweza kuiona. Kwamba njia pekee sasa ya kuweza kuongeza taxbase yake si tu kuchukua from kilichopo lakini tuongeze uzalishaji.
Mheshimiwa Spika, na hata tusipowakaribisha kwa kuwapa hizi dispensations wanazoomba hatutakuwa nao, uzalishaji hautakuwepo; lakini tukifanya vile kwa muda mfupi watakuwepo, tutaona uzalishaji utaongezeka na taxbase yetu itakuwa ina-grow na itakuwa inakwenda vizuri.
Mheshimiwa Spika, ninaamini kabisa kwamba Muswada huu umebuniwa vizuri. Kwa mfano tumeona kuna vingi vinalenga mwenye kiwanda hiki cha kuzalisha mbolea, utaona kila mtaji ukija utakuwa hivyo hivyo, utakuwa na vitu vingine vinahitajika, si kupunguza tu bei ya phosphate au kutoa mrahaba kwenye phosphate, mwingine atakuja na ombi lingine kutokana na jinsi ambavyo anawekeza. Kwa hiyo ni vizuri tukampa Waziri wa fedha na pia tukahakikishiwa kwamba kwa vile hivi vitu sio yeye anafanya mwenyewe, vitaenda hadi kwenye Cabinet ambayo Mheshimiwa Rais mwenyewe atakuwepo; hivyo haiwezi kuwa abuse. Mimi ninaamini kwamba tutakwenda vizuri, na hiyo ndiyo inaonesha wazi kwamba miradi mingine ili iweze kwenda fast na iweze kutekelezwa kwa kipindi kifupi ni lazima tutoe uwezo kwa Serikali kuweza kufanya hayo mambo bila kupoteza muda mrefu sana.
Mheshimiwa Spika, lakini pia ninachelea kusema kwamba naungana na Kamati na nilikuwepo, na ninashukuru kwamba Kamati imeshauri pia kwamba kwa baadhi ya misamaha inayotolewa iwe inachapishwa na Serikali kwenye gazeti ili watu wajue, kwamba katika kipindi hiki Serikali imetoa misamaha hii na watu wataona mahudhui kwasababu gani misamaha hiyo imetolewa na hakuna mtu atalalamika kwamba kuna misamaha ambayo imetoka kienyeji enyeji. Kwa hiyo ninaamini ikichapishwa itakuwa imesaidia, lakini pia ni transparence na ndio dhana zima ya uendeshaji wa Serikali (good governance) sasa hivi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, halafu pia ninaamini kwamba huo ushauri ambao umetolewa, kwamba Serikali iwe inafanya tafiti za mara kwa mara, kufanya tathmini ya ile misamaha iliyotolewa au zile punguzo zilizotolewa kwenye maeneo fulani fulani ya kodi kama ni VAT whatever kwamba imeleta matokeo chanya yanayoendana na mahudhui ya marekebisho yaliyofanywa na Mheshimiwa Waziri.
Mheshimiwa Spika, Kamati imeshauri pia kwamba kuwe na timeframe ya hiyo …
(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)
SPIKA: Dakika moja Mheshimiwa malizia.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Spika, … time flame iwepo. Kwamba wakati unapotoa ile misamaha ijulikane inaisha ndani ya utekelezaji wa mradi na pia ndani ya muda mfupi baada ya mradi kutekelezwa.
Mheshimiwa Spika, ninashukuru sana kwa fursa hiyo, nataka niseme kwamba naunga mkono hoja iliyoletwa na Mheshimiwa Waziri ya kurekebisha hizi sheria lakini pia naomba Wabunge wenzangu waweze kona maudhui haya kwa u-chanya wake ili waweze kupitisha hoja hii ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha. Ahsante sana. (Makofi)