Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Contributions by Hon. Vincent Paul Mbogo (16 total)

Hotuba ya Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa Ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, Tarehe 13 Novemba, 2020
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha Wabunge wote, tumepata ushindi wa kishindo na Mwenyezi Mungu ametuwezesha kuwepo hapa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda kuunga mkono hoja Hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo imegusa nyanja zote; ametupa uelekeo wa nchi nzima na baada ya miaka mitano kama haya tutayasimamia kama Wabunge kwa nia njema ya maono na kumsaidia Mheshimiwa Rais, nadhani nchi ya Tanzania tutapiga hatua kubwa sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi natokea Mkoa wa Rukwa. Mkoa wa Rukwa ni tajiri kama maono ya Mheshimiwa Rais anaposema anataka mabilionea. Mkoa wa Rukwa ni matajiri kwa sababu hali ya hewa ni nzuri, ni wazalishaji wazuri, tatizo ni miundombinu. Naomba Wizara inayohusiana na miundombinu hasa upande wa barabara, baadhi ya barabara, mfano kwenye Jimbo langu la Nkasi Kusini, mimi sina mjini; ni vijijini, porini, ni wazalishaji tu, lakini hakuna barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukija Jimbo la Nkasi Kusini upande wa Ziwa Tanganyika, bado hatujalitumia. Ziwa Tanganyika bado linatumika ndivyo sivyo. Namshukuru Mheshimiwa Rais amesema ataweka meli ya mizigo, sasa meli ya mizigo ikija na miundombinu hamna, itakuwa bado ni shida.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara hizi ziangalie maeneo ambayo ni economic zone kila jimbo. Kuna barabara ambazo ni economic zone, ndiyo mhimili, ndiyo mgongo wa Jimbo. Mfano ni barabara ya Wampembe, Ninde, Kala na Mpasa. Zile ndiyo mwambao mwa Ziwa Tanganyika ambazo wale watu wamejikarantini kiuchumi. Tunaongea masuala ya kujikarantini, lakini kwenye Jimbo langu baadhi ya kata kama nne zimejikarantini, masika hakuendeki, labda utumie pikipiki; kwingine pikipiki haifiki inabidi utembee kwa mguu.

Mheshimiwa Spika, nadhani Mheshimiwa Jafo anapafahamu Wampembe. Naomba sana hizi barabara za Ninde, Kala na Wampembe ziingizwe TANROADS, hakuna namna, TARURA wamezidiwa, naungana na mama yangu Mheshimiwa Malecela. TARURA wamezidiwa, tuwapunguzie mzigo; baadhi ya barabara ziingie TANROADS na nyingine zibaki TARURA. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukiangalia katika mikoa inayozalisha ni pamoja na Rukwa; na katika Rukwa, Jimbo la Nkasi Kusini. Tukija upande wa pembejeo ni gharama mno kwa mkuma mdogo (peasant). Kwa nini isifike mahali kupata maeneo vijengwe hata viwanda vya mbolea? Wizara ikae, i-sort maeneo, kuwe na zone za kujenga viwanda hasa mikoa ile inayozalisha sana mazao ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Wizara ya Maji, katika Jimbo langu kuna watu bado wanaishi maisha ya ujima. Kipindi cha ujima tulisoma kwenye historia, lakini katika Jimbo langu watu wapo wana-depend on nature. Naomba Wizara hii; nilipita na watendaji wengi ambapo najua ni kilio cha nchi nzima; Wizara ya Maji inabidi ikae pembeni ifanye kama special operation, kwa sababu kilio cha wafanyakazi kule ni wachache, wataalam wa maji hakuna. Ingefanywa tathmini angalau hata robo kwenye baadhi ya miradi, Mheshimiwa Rais anahangaika anatuma fedha na fedha zipo nyingi sana lakini watendaji hakuna. Kuna mradi kama wa Wampembe, Mradi wa Kala, Mpasa na Mradi wa Chala, maeneo yote hayo fedha zipo ila wataalam wako wachache, wanazidiwa. Kwa hiyo, naomba Wizara ya Maji ikae chini iwe na special operation upande wa maji katika majimbo yetu, ni tatizo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, napenda sana kumshukuru Mungu, naunga mkono hoja ya Mheshimiwa Rais, sisi sote humu Mzee amesema alikuwa ana hofu sijui ni successor au nini, sisi ndiyo walinzi wa nchi hii. Maono ya Mheshimiwa Rais, ametukabidhi sisi Wabunge ambao ndiyo wanasiasa, ndiyo wa kusimamia kile kilichoanzishwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli. Ahsante sana. (Makofi)
Hoja kuhusu Halmashauri za Miji na Wilaya Kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kutatua Tatizo la Upungufu wa Magari ya Zimamoto pamoja na Vifaa Vinavyotumika Kuzima Moto na Uokoaji
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hoja ya Mheshimiwa Tarimo ya kuhusu Jeshi la Zimamoto na kwanza naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, watu fikra wanawaza zimamoto ni moto tu, hao ni mjini. Kutokana na maendeleo ambayo sasa hivi Mheshimiwa Rais anatupatia, anajenga ofisi za kisasa na miji inakua, kuna miradi mbalimbali ya kisasa. Zimamoto sasa hivi inatakiwa ianzishe Kitengo cha Zimamoto Jamii kwa sababu askari ni wachache, elimu vijijini hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, majanga siyo moto tu, vijijini huku kuna majanga mengi sana hasa wakati wa masika, watoto wanaangukia kwenye mafuriko, visima na mitaro, lakini wananchi hawana elimu na haya majanga hayatangazwi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu sasa hivi kuna mkakati wa Wizara ya TAMISEMI kusaidia Wizara ya Mambo ya Ndani kujenga vituo vya polisi, kila kwenye Kituo cha Polisi pawepo na Ofisi ya Zimamoto, ili wananchi waweze kupata elimu ya kuweza kujiokoa katika majanga mablimbali. Majanga mengi yanatokea vijijini, lakini hakuna elimu ya namna ya kuokoa. Kwa hiyo, kuna vifo vingi sana vinatokea vijiji ambavyo siyo moto. Kwa hiyo, hii elimu ya zimamoto ishuke katika kila Kituo cha Polisi cha Kata. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Kilumbe ameongelea kwenye Ziwa Tanganyika na maziwa mengine, huko kote hakuna mkakati maalumu wa kujenga ofisi za uokoaji. Boti nyingi zinazama, vituo vya polisi havina eneo la ujenzi wa ofisi za zimamoto. Kwa hiyo, naomba Wizara hii pamoja na TAMISEMI ijengwe ofisi za zimamoto kwa kila kata ili elimu itolewe. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, yapo majanga ya asili na ambayo siyo ya asili, hata kwenye lift maeneo mengi yanahitaji zimamoto. Kwa hiyo, Jeshi la Zimamoto ndio tumehuisha kwenye Kamati ndio sasa hivi inakuwa na uwezo wa kupatiwa fedha, mwanzo lilikuwa halipatiwi fedha. Kwa hiyo, kwa sasa hivi ndio limeanza kupatiwa fedha.

Kwa hiyo halmashauri kushirikiana na Jeshi la Zimamoto siyo lazima fedha na halmashauri ambazo hazina uwezo kushiriki tu ili kuliwezesha kuwa na mpango wa pamoja wa namna ya uokoaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, kwanza napenda niipongeze sana hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa sababu, imesheheni sehemu zote imegusa nyanja zote. Mimi nikiwa kama Mbunge wa Jimbo la Nkansi Kusini pia ni Mbunge wa Nkasi, Wilaya ya Nkasi, napenda kujikita katika upande wa kilimo kwa sababu sisi tunaotokea Rukwa, Nyanda za Juu Kusini, tusipoongelea kilimo ni shida. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wengi wameongelea suala la kilimo humu, napenda kuwaambia hivi wameongea wengi kuhusu utafiti, wako sahihi, lakini wanaenda kutafiti nini? Kilimo ambacho wanasema wakulima wanalima wanazalisha mazao ya aina ipi? Ni quantity au quality? Wengi wamesema South Africa imeteka zao la Kongo, Zambia, sawa; tunaweza kuwa tunalima lakini tunalima mazao je, yana ushindani kwenye soko? Mbegu hizi ambazo tunawaambia watafiti waende wakatafiti, je, watakuwa wanaotafiti wana nia njema na kutuletea mbegu zilizo bora ambazo zitaleta ushindani kwenye soko? Au ndio hao wanaokuja kusema kama bwawa la umeme halifai? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tutafute watu sahihi. Mbegu zinazofaa ni aina gani ya mahindi ambayo inauzwa kwenye soko, sio bora tu kuzalisha. Kwa hiyo, unakuta Tanzania inazalisha mazao mengi, lakini mahindi yanayolimwa ni bora? Ndio yanayohitajika kwenye soko huko kwenye soko la kimataifa? Nchi Jirani zinahitaji aina ya mahindi hiyo? (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tunaweza tukawa tunalima mahindi, lakini sio bora kwenye soko hayapo na watafiti wakatuletea tu bora kuzalisha mahindi. Lakini ningependa hizi Wizara tatu hizi ni Wizara pacha. Wizara ya mambo ya Nje, Wizara ya Kilimo, Viwanda na Biashara hizi zinatakiwa ziende pamoja, lakini sijui kama wanakaa pamoja ili waone namna ya kuinua kilimo kwa ajili ya kuinua Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi inatakiwa ikae itafute masoko kule ituletee jamani Sudan wanahitaji mahindi aina fulani, kwa hiyo kwenye utafiti tuleteeni mbegu wakulima wa Wilaya ya Nkasi kusini, Rukwa, Kigoma na Njombe walime aina fulani ya mbegu ndio tutakidhi kwenye soko la kitaifa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kilimo, tunakuja kwenye suala la pembejeo, pembejeo imekuwa ni shida ni aibu mwaka huu watu wamepata hasara wakulima ambao wamejitahidi wamekuja watu feki katikati hapa wanaleta mbolea ambazo sizo hazina tija, sasa sijui kama Wizara inayorudi itatuletea majibu wale walioleta mbegu feki zingine zinatoka nje zingine zinaenda wapi, wakulima wamepata hasara kubwa mno wanatakiwa hao watu wachukuliwe hatua, wewe - imagine mkulima anatoa fedha zake anatembea kilometa 60 - 70 kumbe anakwenda kubeba mbolea feki, mbegu feki na Wizara ipo sio sahihi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hii speed ambayo ni legacy ya mheshimiwa Rais Hayati John Pombe Joseph Magufuli, Rais hakuweza kuyafanya haya peke yake Rais ni taasisi ambayo ipo ndani Mheshimiwa Mama Samia yupo Mheshimiwa Hayati Magufuli yupo Mheshimiwa Naibu Spika upo Wabunge wote ni legacy ya Chama Cha Mapinduzi, mendeleo yote haya yanaletwa na Chama Cha Mapinduzi pamoja na legacy ya Waheshimiwa hawa wote kwasababu ni tasisi walikuwa wanaungana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli asingeweza vyote hivi bila kuungana na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mama Samia kwahiyo mtu anayekuja kutaka kubeza nawaomba Waheshimiwa Wabunge kwa umoja wetu tunaamini hawa ni asilimia ndogo sana hawawezi kutushinda sisi kama tulivyo kuweza kufuta legacy ya Mheshimiwa Rais ili waweze kufuta legacy ya Mheshimiwa Mama Samia Suluhu ni jembe ni mtekelezaji yeye ndiye alikuwa ni mtendaji yeye ndiye alikuwa front line pamoja na Waziri Mkuu. Hivyo hasi kama wanajaribu kubeza… (Makofi)

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Spika, naomba kumpa taarifa.

NAIBU SPIKA: Ngoja Mheshimiwa Sophia nitakupa fursa, subiri.

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, haya Ahsante.

NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kanuni zetu zinataka mtu akiwa anazungumza ndio anapewa taarifa lakini mzungumzaji haachi kuzungumza mpaka niwe nimemwita wa taarifa unatakiwa uendelee kuchangia mpaka nimpe fursa huyo anayesema taarifa.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, hongera sana.

NAIBU SPIKA: Sasa nikupe nafasi Mheshimiwa Mwakagenda japo kuwa mwanzoni ulisema mwongozo, mwongozo pia hauruhusiwi kuombwa wakati kuna mtu anazungumza, mtu akiwa anazungumza unaweza kuomba vitu viwili moja ni taarifa cha pili utaratibu kama kuna kanuni inavunjwa, Mheshimiwa Sophia Mwakagenda.

T A A R I F A

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante tunaendelea kujifunza bado nashukuru kwa kunielewesha, naomba nimpe taarifa mzungumzaji anayeongea kwamba sasa hivi tunazungumzia Wizara ya Waziri Mkuu tunaichangia hiyo na kutoa maoni yetu, na hakuna mtu yeyote hapa ndani ya Bunge ambaye hataki maendeleo ya Taifa hili. Kwa hiyo, nataka ajielekeze zaidi kwenye hotuba na kuweza kuijadili hiyo sote tunataka Tanzania iliyo bora, ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo unaipokea taarifa hiyo.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei yeye jana ameisifia Standard gauge amemsifia Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa hiyo legacy bado inaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana napenda nijikite tena kwenye upande wa Kilimo, kilimo upande wetu kimekuwa kwenye hali ngumu kutokana na hizi Wizara tatu…

MBUNGE FULANI: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

MHE. VINCENT P. MBOGO: …hizi Wizara tatu zingeweza kujikita kwa pamoja, moja isiteleze… …(Makofi)

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbogo kuna taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Ngassa.

T A A R I F A

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante napenda kumpa taarifa mzungumzaji Mheshimiwa Mbogo hiyo Stigler’s Gorge anayoiongelea ndio ile Waziri wa Nishati amesema itawekewa maji tarehe 15 Mwezi 11 ahsante. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo unaipokea taarifa hiyo.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naipokea kwa mikono miwili ahsante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Sekunde tano malizia mchango wako.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana napenda kwenda kujikita kwenye upande wa uvuvi ziwa Tanganyika, ziwa lile bado halijatumika ipasavyo ukanda ule mapato yanapotea wavuvi wanakwenda kuvua nchi za jirani hawaji kuvua huku kwasababu ya mazingira sio rafiki na tozo, tozo ni nyingi mno mazingira sio rafiki na wavuvi, mabwawa yote, maziwa yote hata nchi za jirani kwa Tanzania nzima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Bahari ya Hindi wanaziwa wanavulia Mombasa, ziwa Tanganyika wanakwenda Kongo, Burundi kwahiyo tunapoteza mapato, naomba Wizara ikija hapa ijikite namna ya kutengeneza mazingira rafiki itakavyoweza kuwarudisha wavuvi tuweze kupata mapato Tanzania. Pamoja Wizara ya uvuvi itenge maeneo ya uwekezaji ijenge uvuvi, ahsante sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nitampongeza kidogo sana Mheshimiwa Aweso kwa sababu, katika hotuba yake jimbo langu halijaguswa, limeguswa kidogo kuna ukakasi. Ma-engineer ndani ya Wilaya ya Nkansi wako wawili, tena ni technicians, engineer hakuna. Kwa hiyo, Wilaya ya Nkansi nzima suala la maji ni sifuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ahadi alizotoa Mheshimiwa Hayati pamoja na Mheshimiwa Samia Suluhu. Katika mji mdogo ambao katika jimbo langu ndio mji ambao najisifia ulitakiwa kuwe na mradi wa mabwawa ambayo yanaweza kuhudumia vijiji vitatu hadi vinne, lakini kwenye hotuba yake hayapo. Na hii nadhani kutokana na kwasababu, kule wilayani engineer wa maji hamna kwa hiyo, hapati taarifa sahihi. Kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Aweso njoo uokoe Jimbo la Nkansi Kusini maji ni hoi, hakuna maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Nkansi Kusini nina kata tatu hawajawahi kuona maji ya bomba kila siku ni vifo vya mamba na magonjwa ya tumbo basi. Kwa hiyo, Mbunge nimebaki gari langu ndio ambulance kubebea watu kupeleka hospitali magonjwa ya tumbo na vifo vya mamba, wanaliwa na mamba. Mheshimiwa Aweso baada ya kumaliza Bunge nakuomba hairisha ziara nyingine zote za majimbo, Nkansi Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, nimeona Wabunge wengi wamechangia humu, kwanza nawashangaa, wengine matenki mabovu, wengine miundombinu chakavu, mimi hakuna miundombinu, hakuna matenki. Kwa hiyo, nakuomba baada ya Bunge mara ya kwanza Nkansi Kusini, ingia Ninde, ingia Kate, ingia Wampembe, utakuja na taarifa kamili. Kule wananchi wanajihesabu kama wako Kongo. [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya wananchi ya maji hawajaifurahia nchi yao wananipigia simu wanalalamika wamesahaulika. Mheshimiwa Aweso, Wizara ya Maji, Nkansi Kusini anza nako kule ndio iwe kama sample nakuomba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vipo vijiji ambavyo viko mwambao kule mwa Ziwa Tanganyika hakuna miundombinu. Watu wanasema hapa wanakunywa maji na mifugo kule wanakunywa maji na nguruwe pori. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanasema wana maji mekundu kule wana tope, wanatumia maji machafu, yaani ni shida Wilaya ya Nkansi Kusini. Mheshimiwa Aweso njoo ukomboe Nkansi Kusini upande wa maji, anza na mabwawa ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, njoo uanze na visima. Nakushukuru umeweka visima kidogo, lakini bado asilimia ni ndogo mno. Ipo miradi iliyotelekezwa wameweka tu mabomba ya maji pale mipira hamna miaka, ukiuliza ina miaka nane, mengine mabomba yana miaka saba, yana miaka tisa, ni shida. Maliza bajeti yako Nkansi Kusini moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, yapo majimbo au vijiji ambavyo kama Mbunge wa Wilaya, naongea Wilaya ya Nkansi kwa ujumla kwasababu, ndio Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi na ndio chama tawala ambacho naamini ndio kinacholeta maji, ndio kinacholeta huduma ya mabomba kila maeneo kwa Wilaya ya Nkansi jumla. Kwa hiyo, Mheshimiwa Aweso…

MHE. AIDA J. KHENANI: Taarifa. Mheshimiwa Naibu Spika,

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Aida Khenani.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ndio naipokea Mbunge wangu pacha. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Ukae kwanza yeye azungumze. Ahsante. Mheshimiwa Aida Khenani.

MHE. AIDA J. KHENANI: Taarifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa Taarifa kaka yangu, pacha wangu anayetoka Nkansi Kusini kwamba, Wilaya ya Nkansi ina Majimbo mawili Nkansi Kusini anakochangia yeye ambako ndio anatoka, lakini Nkansi Kaskazini Mbunge wake aliyechaguliwa na wananchi anatoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo unaipokea Taarifa hiyo.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei kwasababu, hawana Serikali. Na hata huduma ninazoongea hizi kinacholeta ni Chama Cha Mapinduzi kwa hiyo… (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eeh, kengele imegonga?

MBUNGE FULANI: Bado.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, aah, naunga mkono hoja. Ahsante sana na Mbunge wangu pacha, asante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Asante sana. Taarifa iliwekwa kwa namna ya kuweka mambo sawasawa, lakini wakati ukizungumza Mheshimiwa Vincent Mbogo ulieleza zile kata tatu ambazo hazina miradi ya maji yoyote na ukasema kama wako Kongo. Sasa kwa sababu, ulikuwa unaeleza jambo ambalo wananchi wana hali mbaya nalo na haturuhusiwi kutumia michango ya nchi nyingine, unaweza kuitumia humu ndani ile ambayo inafanya vizuri unataka nchi yetu iige huko. Lakini ile ya kuonesha kwamba, pengine kuna hali fulani hivi ambayo haiku sawasawa hairuhusiwi. Kwa hiyo, ifute hiyo kama wako Kongo halafu tuendelee na mchangiaji mwingine.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naifuta hiyo kauli, wako Tanzania. (Makofi/Kicheko)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Maji
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwanza nitampongeza kidogo sana Mheshimiwa Aweso kwa sababu, katika hotuba yake jimbo langu halijaguswa, limeguswa kidogo kuna ukakasi. Ma-engineer ndani ya Wilaya ya Nkansi wako wawili, tena ni technicians, engineer hakuna. Kwa hiyo, Wilaya ya Nkansi nzima suala la maji ni sifuri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna ahadi alizotoa Mheshimiwa Hayati pamoja na Mheshimiwa Samia Suluhu. Katika mji mdogo ambao katika jimbo langu ndio mji ambao najisifia ulitakiwa kuwe na mradi wa mabwawa ambayo yanaweza kuhudumia vijiji vitatu hadi vinne, lakini kwenye hotuba yake hayapo. Na hii nadhani kutokana na kwasababu, kule wilayani engineer wa maji hamna kwa hiyo, hapati taarifa sahihi. Kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Aweso njoo uokoe Jimbo la Nkansi Kusini maji ni hoi, hakuna maji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Nkansi Kusini nina kata tatu hawajawahi kuona maji ya bomba kila siku ni vifo vya mamba na magonjwa ya tumbo basi. Kwa hiyo, Mbunge nimebaki gari langu ndio ambulance kubebea watu kupeleka hospitali magonjwa ya tumbo na vifo vya mamba, wanaliwa na mamba. Mheshimiwa Aweso baada ya kumaliza Bunge nakuomba hairisha ziara nyingine zote za majimbo, Nkansi Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu, nimeona Wabunge wengi wamechangia humu, kwanza nawashangaa, wengine matenki mabovu, wengine miundombinu chakavu, mimi hakuna miundombinu, hakuna matenki. Kwa hiyo, nakuomba baada ya Bunge mara ya kwanza Nkansi Kusini, ingia Ninde, ingia Kate, ingia Wampembe, utakuja na taarifa kamili. Kule wananchi wanajihesabu kama wako Kongo. [Maneno Haya Siyo Sehemu ya Taarifa Rasmi za Bunge]

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma ya wananchi ya maji hawajaifurahia nchi yao wananipigia simu wanalalamika wamesahaulika. Mheshimiwa Aweso, Wizara ya Maji, Nkansi Kusini anza nako kule ndio iwe kama sample nakuomba. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, vipo vijiji ambavyo viko mwambao kule mwa Ziwa Tanganyika hakuna miundombinu. Watu wanasema hapa wanakunywa maji na mifugo kule wanakunywa maji na nguruwe pori. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wanasema wana maji mekundu kule wana tope, wanatumia maji machafu, yaani ni shida Wilaya ya Nkansi Kusini. Mheshimiwa Aweso njoo ukomboe Nkansi Kusini upande wa maji, anza na mabwawa ambayo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais, njoo uanze na visima. Nakushukuru umeweka visima kidogo, lakini bado asilimia ni ndogo mno. Ipo miradi iliyotelekezwa wameweka tu mabomba ya maji pale mipira hamna miaka, ukiuliza ina miaka nane, mengine mabomba yana miaka saba, yana miaka tisa, ni shida. Maliza bajeti yako Nkansi Kusini moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, yapo majimbo au vijiji ambavyo kama Mbunge wa Wilaya, naongea Wilaya ya Nkansi kwa ujumla kwasababu, ndio Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi na ndio chama tawala ambacho naamini ndio kinacholeta maji, ndio kinacholeta huduma ya mabomba kila maeneo kwa Wilaya ya Nkansi jumla. Kwa hiyo, Mheshimiwa Aweso…

MHE. AIDA J. KHENANI: Taarifa. Mheshimiwa Naibu Spika,

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo kuna Taarifa kutoka kwa Mheshimiwa Aida Khenani.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ndio naipokea Mbunge wangu pacha. (Kicheko)

NAIBU SPIKA: Ukae kwanza yeye azungumze. Ahsante. Mheshimiwa Aida Khenani.

MHE. AIDA J. KHENANI: Taarifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumpa Taarifa kaka yangu, pacha wangu anayetoka Nkansi Kusini kwamba, Wilaya ya Nkansi ina Majimbo mawili Nkansi Kusini anakochangia yeye ambako ndio anatoka, lakini Nkansi Kaskazini Mbunge wake aliyechaguliwa na wananchi anatoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Vincent Mbogo unaipokea Taarifa hiyo.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, siipokei kwasababu, hawana Serikali. Na hata huduma ninazoongea hizi kinacholeta ni Chama Cha Mapinduzi kwa hiyo… (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, eeh, kengele imegonga?

MBUNGE FULANI: Bado.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, aah, naunga mkono hoja. Ahsante sana na Mbunge wangu pacha, asante sana. (Makofi)

NAIBU SPIKA: Asante sana. Taarifa iliwekwa kwa namna ya kuweka mambo sawasawa, lakini wakati ukizungumza Mheshimiwa Vincent Mbogo ulieleza zile kata tatu ambazo hazina miradi ya maji yoyote na ukasema kama wako Kongo. Sasa kwa sababu, ulikuwa unaeleza jambo ambalo wananchi wana hali mbaya nalo na haturuhusiwi kutumia michango ya nchi nyingine, unaweza kuitumia humu ndani ile ambayo inafanya vizuri unataka nchi yetu iige huko. Lakini ile ya kuonesha kwamba, pengine kuna hali fulani hivi ambayo haiku sawasawa hairuhusiwi. Kwa hiyo, ifute hiyo kama wako Kongo halafu tuendelee na mchangiaji mwingine.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, naifuta hiyo kauli, wako Tanzania. (Makofi/Kicheko)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 – Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Napenda kuwapa pongezi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika nchi hii yapo majimbo yaliyokatwa kutoka Majimbo mengine kutokana na ukubwa wa eneo pamoja na Mikoa. Hii Mikoa ambayo ni michanga inatakiwa hii Wizara ya Uchukuzi iwaone kwa jicho la kipekee kwa sababu miundombinu bado. Ile mikoa ambayo ni mama ikagawiwa ikatoa Majimbo mapya ambayo bado machanga, inatakiwa hii Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ifanye tathmini, iende ikaangalie barabara ambazo ni main road za Majimbo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hii TARURA au TANROADS imebaki kwenye yale Majimbo mama. Ukichukua sisi watu wa Rukwa, Songwe, Kigoma Nyanda za Juu Kusini, Mtwara, Lindi, Wizara ya Uchukuzi inatakiwa ikae chini iangalie hii Mikoa ambayo kidogo ilikuwa imesahaulika. Nirudi kwenye Jimbo langu; Jimbo langu limekatwa kutoka Jimbo la Nkasi Kaskazini. Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini. Ukiangalia Jimbo la Nkasi Kusini halina barabara ya TANROADS ina kilometa sita tu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna Kata nne ambazo toka mwezi wa 11 mvua imeanza, sasa hivi ni miezi sita au saba, wala magari hakuna, hakupitiki barabara zina miaka karibu 10, 20, sasa unakuta barabara huku wametenga maintenance; tena barabara ile ya TANROADS kupitia hiyo maintenance wanatengeneza barabara ambayo tayari inapitika. Sisi kule ni lami, hiyo hiyo moram ni lami wakati kuna barabara huko kata nyingine hazipitiki, magari hayaendi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hawa ni wananchi, TANROADS na TARURA wote wanahudumia wananchi. Kwa hiyo, wanatupa wakati mgumu sisi majimbo ambayo yapo pembezoni. Mfano Jimbo la Nkasi Kusini, kuna bandari mbili Wilaya ya Nkasi ambazo zimejengwa kwa fedha nyingi sana za Serikali, lakini miundombinu ya barabara ambazo zinakwenda kwenye bandari hiyo hakuna. Barabara ya kutoka Paramawe kwenda kwenye bandari ya Kipili na barabara ya Kabwe ziwekwe lami ili kuweza kuinua uchumi wa mwambazo mwa Ziwa Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo barabara ya Ninde – Wampembe; Wampembe ni main feeder road. Wanasema feeder roads hazikidhi vigezo, lakini kila Jimbo lina barabara zake. Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi inatakiwa iwasiliane na sisi Wabunge tunaowakilisha Majimbo tuwaambie barabara zipi ziingizwe TANROADS? Kwa sababu mwanzo ilikuwa ni mfumo, kuunganisha Mkoa na Mkoa, tayari Mikoa mingine imeshaunganishwa. Sasa tuje kwenye barabara za vijijini. TANROADS hata ikiweka barabara za lami, hizi barabara za vijijini ambako ndiko mazao yanazalishwa, hivi barabara za TANROADS itabeba nini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara za vijijini ndiyo viwanda ambako mazao yanazalishwa. Huko barabara ziboreshwe, zikishaboreshwa, hizi main roads ndiyo zitakuwa zina umuhimu zaidi. Kwa sababu tunatengeneza barabara ya lami, lakini mazao hayafiki, ni kazi bure. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, katika mji wangu mdogo wa Kijiji cha Chala TANROADS barabara imepita wamebomolewa nyumba miaka 10 sasa wale wazee hawajapata fidia. Piga mahesabu, mtu wa kijijini amebomolewa nyumba yake ambayo alikuwa anategemea kupata fidia, hajapata fidia na wale wengi ni wazee.

Naomba Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, njooni katika Wilaya ya Nkasi katika Kijiji cha Chala mje mtoe tamko la kuwapa fidia wale watu waliobomolewa nyumba zao. Wengi wanalalamika, wengine wamesha-paralyze, maisha ni magumu. Yote haya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi nawaomba njooni muwape fidia wale watu, muwalipe haki zao, wanalalamika. Sisi Wabunge tunapata shida, tunawajibia nyie majibu ya Wizara ya Ujenzi wakati haupo Wizara ya Ujenzi, inabidi ujibu tu kwa niaba ya Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, hizi kata tatu ambazo toka mwezi wa 11 magari hayaendi, naomba kwa namna ya pekee Wizara ije ijenge zile barabara. Sasa hivi namkabidhi hizi barabara ziingizwe TANROADS.

Mheshimiwa Naibu Spika, samahani, mhudumu aje amkabidhi barabara Waziri wa Ujenzi.

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbogo.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Naunga mkono hoja. (Makofi)

Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Ofisi ya Waziri Mkuu
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili na mimi niweze kuchangia hotuba ya Waziri Mkuu kwenye bajeti yake ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, hotuba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ni nzuri sana imegusa maeneo mengi ya nchi hii. Kwanza kabisa napenda nimshukuru sana Mheshimiwa Rais ameupiga mwingi sana. Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana ya maendeleo ndani ya nchi yetu na nje ya nchi. Ukiangalia katika Jimbo langu la Nkasi Kusini lilikuwa na Kata 11 kituo cha afya kilikuwa kimoja tu, ndani ya uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan nimejengewa vituo vya afya vine! Mama Samia safi. Madarasa yamejengwa, Vituo vya Afya vimejengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu maji. Kwenye changamoto ya maji kuna miradi mingi kichefuchefu ndani ya Wilaya ya Nkasi pamoja na Mkoa wa Rukwa mzima. Naomba ile miradi kichefuchefu ipewe Jeshi la Ulinzi. Jeshi la Kujenga Taifa tumeona linafanya kazi vizuri sana kwenye miradi mbalimbali, ile miradi kichefuchefu basi wakabidhiwe Jeshi ili iweze kwenda kwa haraka na kumalizika kwa muda mfupi.

Mheshimiwa Naibu Spika, upo mradi wa maji Mlale, upo mradi wa maji Kizumbi una miaka nane sasa hivi bado umetekelezwa ninaomba Wizara ya Maji ikae chini miradi hii ikabidhiwe Jeshi la Wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Nkasi Makao Makuu ni aibu, ina changamoto kubwa sana. Nadhani Tanzania nzima Wilaya ya Nkasi haina maji, ninaomba kuna mradi wa Ziwa Tanganyika lakini tuwe na mradi wa dharura kwa sababu huu mradi wa Ziwa Tanganyika utachukua muda, tuwe na mradi wa dharura wa kuokoa maisha ya watu wa Wilaya ya Nkasi. Ipo mito, mto Mfwizi na Mto Zimba, mito hii ni vyanzo sahihi havikauki maji kiangazi na masika, ninaomba Wizara ya Maji ije itengeneze mradi wa maji kwenye hii mito miwili Zimba na Mfwizi maji ya mserereko yaweze kwenda Wilaya ya Nkasi kama mradi dharura ambao utaweza kunusuru maisha ya watu wa Wilaya ya Nkasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, nije Ziwa Tanganyika. Ziwa Tanganyika toka tunasoma tunaulizwa Ziwa lenye kina kirefu majibu ni Ziwa Tanganyika, Ziwa hili hakuna meli hata moja, hakuna usafiri wowote ndani ya Ziwa Tanganyika. Kwa hiyo, uchumi wa Mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi ume- paralyze japo bajeti ipo ya kutengeneza meli Liemba na Meli MV Mwongozo, naomba hili la meli Ziwa Tanganyika liwe dharura ni janga kama UVIKO! haya ndiyo maeneo ya kiuchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunamwona Mheshimiwa Rais anahangaika kufungua milango ya kiuchumi, Congo imeingia Afrika Mashariki, amejenga Ubalozi lakini miundombinu inayoelekea kwenye lango la uchumi bado ni shida, niiombe TARURA iongezewe bajeti.

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais alitupa Bilioni Moja na Milioni Mia Tano kwa ajili ya Miundombinu katika Majimbo yetu, Mheshimiwa Rais Ahsante sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hili la TARURA iongezewe kuna barabara ya Ninde, Kizumbi, Wampembe, kuna vilima hizi barabara hazipitiki. Ndani ya Jimbo langu Kata Nne magari hayaendi, ikifika masika ndiyo kabisa. Kwa hiyo, meli usafiri wa ndani ya Ziwa Tanganyika meli hakuna na hizi Kata zipo ndani ya Mwambao wa Ziwa Tanganyika, usafiri ndani ya Ziwa hakuna, barabara hakuna kwa hiyo, wale watu unaweza ukapata picha wanaishi maisha ya namna gani, hata mzunguko wa pesa hakuna! Kwa hiyo wanamaisha magumu sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo naomba Wizara ya Miundombinu suala meli Ziwa Tanganyika ni janga ifanye kama dharura imeingiza kwenye bajeti lakini bajeti inaweza ikatumia miaka miwili mitatu wananchi wanateseka hakuna mawasiliano na nchi za jirani za Congo, Zambia na Burundi ambao ndiyo chanzo cha uchumi.

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa ajira nashukuru sana Ndugu yangu Mama yangu Jenista Mhagama amesema Rais atatangaza ajira, nipende kumshukuru sana. Ajira hizi wafanye utafiti zielekee vijijini kwa sababu kuna shule zina Walimu wawili, vituo vya afya vina Muuguzi Mmoja, mfano Nzinga kuna Muuguzi Mmoja, Mwinza kuna Muuguzi Mmoja, Kizumbi kuna Wauguzi Wawili, kwa hiyo wanapotoa ajira hizi waelekeze maeneo ambayo kuna upungufu wa Wauguzi au watumishi wa afya. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tunakuja kwenye Mahakama, hotuba ya Waziri Mkuu hapa ilionyesha mahakama nyingi nchi nzima zinajengwa lakini nchi hii tuwe na vipaumbele kuna maeneo ambayo ni nyeti kila Mbunge humu akikaa akaorodhesha maeneo nyeti kwa sababu mahitaji ni mengi, vipaumbele vipo vingi, lakini tufike sehemu fulani tuwe na maeneo ambayo yanaweza kuchangia pato ndani ya nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano ndani ya Jimbo langu ipo Kata ambayo Hakimu anatumia stoo ya mazao ndiyo anahukumia kesi mule ndani! Mheshimiwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Pinda alifika tumemkuta hakimu yupo ndani ya godown. Kwa hiyo, tungeanza kuwatoa kwanza Mahakimu ambao wanatumia ma-godown ndiyo tuanze kukarabati hizo nyingine na tujenge hizo nyingine. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa mawasiliano. Nina Kata tano kwangu Jimboni hakuna mawasiliano kabisa. Simu hamna na zipo mwambao kwao hata uhalifu na hata usalama wa nchi hii unakuwa hatarishi. Mfano Kata ya Kala, Kata ya Wampembe, Kata ya Ninde, Kata ya Kizumbi, hizi Kata ndiyo uvuvi unafanyika mkubwa sana hakuna mialo, miundombinu mizuri, hakuna masoko hakuna vituo vya Polisi, kwa hiyo mtu akivua leo hii akiuza jioni anavamiwa anachukuliwa nyavu ananyang’anywa fedha. Ninaomba Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya bajeti hii anapohitimisha aje aseme Kala Kituo cha Polisi kinaanza kujengwa lini? Kwa sababu mimi kama Mbunge wao tumeshachanga fedha cement tumejenga imefikia kwenye renter ni wao Wizara ya Mambo ya Ndani kuja kumalizia pale.

Mheshimiwa Naibu Spika, ndani ya mwaka mmoja wamevamiwa mara nne wananyang’anywa dhana zao za uvuvi, wananyang’anywa fedha, wanapigwa baadae wanahamia ng’ambo wakisha wadhulumu wakishawaibia, wakishawavamia kwa sababu hakuna Kituo cha Polisi. Kwa hiyo watu biashara zao hawafanyi kwa sababu hakuna amani, hakuna mialo kama miundombinu.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika bajeti hii sijaona ujenzi wa masoko ukanda wa Ziwa Tanganyika ambako ndiko mazao ya samaki inatakiwa kuwe na kituo cha Kitaifa cha masoko ili mtu anapokwenda kufanya biashara yake ya mahindi kupeleka Congo kuwe na kituo.

Mheshimiwa Naibu Spika, njooni mjenge soko Wampembe, Mheshimiwa Jafo amefika Wampembe anakufahamu, njooni mjenge Wampembe soko la biashara la mazao ya Samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu lina changamoto kubwa sana, upande wa vituo vya afya. Nimesema toka nimeingia kituo cha afya kilikuwa kimoja nacho kilijengwa kwa kuchukua fedha za zahanati. Ina maana mpaka tunavyoongea hivi ni ndani ya Mama Samia ndiyo vituo vya afya vinajengwa Vinne. Hakuna vituo vingine. Kwa hiyo, ni shida sana jiografia ya Jimbo langu la Nkasi Kusini kidogo lilikuwa limesahaulika upande wa miundombinu.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba TARURA waongezewe fedha ili tuweze kumaliza changamoto ya barabara mwambao mwa Ziwa Tanganyika pamoja na Jimbo la Nkasi Kusini.

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Naunga mkono hoja. (Makofi)
Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022 na Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2022
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia hoja iliyoko mbele yetu, ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi anayoifanya, amekuwa kinara kwa matendo kukuza diplomasia ya uchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, elimu kuhusu diplomasia ya uchumi kwa wananchi bado iko chini, hakuna uelewa, kuanzia wizarani, mikoani, wilayani mpaka vijijini, hasa maeneo ya mipaka ambako wafanyabiashara wengi hawajapewa elimu kuhusu diplomasi ya uchumi, kwahiyo bado wanafanya shughuli zao za kiuchumi kienyeji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kukuza diplomasia ya uchumi, Wizara ya Kilimo, Viwanda na Biashara, Wizara ya Ulinzi pamoja na Maliasili lazima viwe coordinated pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mfano Wizara ya Kilimo ina mpango wa kuanza hizi block farming ambazo zinaenda kuanzishwa nchi nzima, ndio mwanzo pekee ambao tunahangaika vijana hawana ajira. Wale vijana wanaotoka JKT kwa sababu watakuwa tayari wameshajifunza kilimo, kufanya kazi kwa bidii, wakishatoka JKT wapelekwe kwenye hizi block farming ambazo zinaanzishwa na Wizara ya Kilimo. Na hii Wizara ifanye tathmini kwa yale mazao ambayo yana soko. kwa mfano kwa upande wa Nyanda za Juu Kusini waje waanzishe block za kulima mahindi kwa sababu tayari wananchi wana uelewa wa uzalishaji wa mahindi. Waje na block za kuanzisha ngano, soya, alizeti pamoja na Ukanda wa Ziwa Rukwa na Ziwa Tanganyika wafanye utafiti kuanza hizi block hata kilimo cha miwa. Na kwenye hizo block waanzishe kutengeneza viwanda vidogo vodogo ambazo block wakishatoa mazao yao tusiuze mazao ghafi, tuweke mashine, viwanda ili ziweze ku-process tuuze nje mazao yanye thamani kamili, tusiuze mazao ambayo yamelimwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye hizo block farming ifike mahali tupangiwe taratibu na kanuni, hizi block farming ziwe connected na Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya watu wakitoka JKT.

Mheshimiwa Mwenyekiti, fedha nyingi Mheshimiwa Rais atazipeleka kwenye block farming, ukishazipeleka kule watapelekewa raia ambao hawana utaalamu na hivyo hizi block farming zitageuka kama ndiyo sehemu ya kujifunzia. Kwa hiyo JKT waunganishwe na hizi block farming ili waende kuwa wasimamizi wa hizi block farming, kwa sababu fedha nyingi zitaenda, wataenda kuanza kujifunza kulima. Lakini zikiunganishwa na Jeshi la Ulinzi tutapata mazao, mashine zitapelekwa viwanda vidogo vidogo wananchi wa kule wakiungana na wanajeshi kazi itafanyika vizuri kwa bidii. Wizara ya Viwanda na Biashara itafute masoko. Kwa hiyo hizi block farming zitengenezwe kulingana na aina ya masoko ya mazao yanayohitajika na nchi jirani ili kukuza diplomasia ya uchumi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa imeongelea kuhusu mipaka. Ukitaka kutazama kwa undani kabisa Wabunge wengi wamelalamika uzalendo unapungua na tukiona nchi jirani kuna changamoto ya uhalifu hasa maeneo ya buffer zone. Maeneo ya mipakani kuna uhalifu unaojirudiarudia. Wizara ya Ujenzi na Wizara ya Ardhi watengewe bajeti ili waweze kwenda kuimarisha miundombinu ya kuweka bicon kwenye mipaka na barabara zile za kiuchumi pamoja na za kiulinzi ili vyombo vyetu vya ulinzi vinapofanya kazi ya ulinzi mawasiliano yaweze kufika kwa urahisi, kwa sababu wahalifu wengi wanakaa maeneo ya buffer zone maeneo ambayo ndiyo vichaka vya uhalifu unaoendelea, hasa katika maeneo yale ambayo shughuli za kiuchumi zinafanyika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili wafanyabiashara wafanye vizuri maeneo ya mipaka Wizara ya Ardhi pamoja na Miundombinu watenge na waainishe barabara za kiuchumi, beacon ziwekwe ili mambo yaende vizuri. Kwa sababu hizi wizara; kwanza nizipongeze kwanza, zinafanya kazi kubwa mno; Wizara ya Ulinzi, vyombo vya ulinzi vyote kwa pamoja amani na utulivu tulionao Tanzania ni kwa sababu haya majeshi yetu, Jeshi la Polisi, vyombo vya ulinzi vinafanya kazi usiku kucha; na hata sisi wenyewe Bungeni tunakaa kwa usalama kwa sababu ya vyombo vya ulinzi vinafanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, ndio maana naendelea kumpongeza Mheshimiwa Rais kwa sababu anaendelea kutoa ajira kwenye hivi vyombo ili viendelee kufanya kazi kwa ufanisi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukisoma kwenye Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Mambo ya Nje na Usalama hizi wizara bado zina bajeti finyu sana. Nashauri Wizara ya Fedha itenge bajeti ili iweze kuipatia hivi vyombo vya ulinzi pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Sehemu kubwa ina changamoto kubwa sana. Mheshimiwa Rais anahangaika huko nje kutafuta masoko lakini ukiangalia hata makazi ya balozi pamoja na ofisi zetu huko nje, pamoja na viwanja vingi havijaboreshwa. Muonekano wa kuvutia diplomasia ya uchumi pamoja na watalii ianze kuonekana nje. Kwa hiyo wizara hii ipewe fedha ili iweze kujenga miundombinu mizuri na kuweza kutangaza Tanzania nje kwa muonekano wa viwanja vyetu pamoja na ofisi.

MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Ali taarifa.

T A A R I F A

MHE. ALI JUMA MOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nimpe taarifa mchangiaji kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita Wizara hii ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilitengewa takribani bilioni 48.5; lakini mpaka tunafikia sasa katika kipindii chote cha miaka 5 wizara hii ilikabidhiwa bilioni tisa tu.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Mbogo unaipokea taarifa.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, naipokea kwa mikono miwili. Hii Wizara ya Mambo ya Nje haijapata fedha kwa muda mrefu, imesahaulika. Kamati ilienda Ethiopia tukakuta kuna viwanja ambavyo bado havijajengwa, Kamati ikaomba miadi na Mheshimiwa Rais wa Ethiopia, Mheshimiwa Rais kwa kuheshimu diplomasia na nchi yetu akaahirisha safari zake akakutana na Kamati. Akaturuhusu na akatuhakikishia viwanja hivyo ambavyo vingeweza kuchukuliwa virejeshwe na akashauri pajengwe ubalozi mzuri ambao utarudisha mahusiano kati ya Tanzania na Ethiopia. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana.
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi nami niweze kuchangia Wizara ya TAMISEMI. Kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kutuletea fedha nyingi sana pamoja na miradi hasa katika Majimbo ambayo yalikuwa yamesahaulika nchi hii. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, tukubali ukweli Wabunge tunatoka kwenye Majimbo ambayo yana historia tofauti. Jimbo la Nkasi Kusini lilikuwa halina miundombinu, miundombinu imeanza kujengwa ndani ya kipindi cha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu la Nkasi Kusini lilikuwa na Kituo cha Afya kimoja tu, nacho kilikuwa hakijakamilika kwa hiyo ina maana mimi nimeingia ndani ya Jimbo la Nkasi Kusini halina Kituo cha Afya na lina Kata 11 na umbali wa kutoka Kata moja kwenda Kata nyingine kuna umbali wa kilomoita 40 mpaka 50, kwa hiyo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI naomba mgao wa Kata ili huduma za kijamii wananchi waweze kupata kwa uraisi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo langu linapakana na Nchi za Jirani Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Kule kuna makambi ya wavuvi ni maeneo mazuri sana kwa uchumi lakini wananchi wamekuwa wanaishi katika mazingira ambayo kuna uhalifu wa mara kwa mara, ndani ya miaka mitatu wamevamiwa mara sita. Vipo Vijiji karibia ishirini ambavyo viko mwambao wa Ziwa Tanganyika ambapo hali ya hewa ikichafuka, Ziwa likichafuka usafiri wao ni ndani ya Ziwa Tanganyika. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, hawana mbadala kwa hiyo wakinamama wajawazito wanapoteza maisha, wakinamama hawapati huduma ya afya na hata huduma za jamiii ambazo Mheshimiwa Rais anatoa kwa ajili ya maendeleo kufika kwake tu kule hakuna barabara, hakuna miundombinu. Mheshimiwa Rais ametoa magari ya kuchimba visima, tulikuwa tunajadili na Wakurugenzi wa Maji, namna ya vifaa vile kufika kule kuchimba visima hakuna kwa sababu hakuna barabara. Nikuombe Mheshimiwa Waziri tena nikushukuru sana hiyo timu mnaenda kwa kasi mmevaa kiatu cha Mheshimiwa Rais, nawapongezeni sana. Kwanza ni wasikivu, mlituita tukakaa tukawapa vipaumbele vyetu vya Majimbo na tumeishawapa tunaomba mtekeleze. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini lina Vijiji ambavyo havina maboma, vingine vina maboma wananchi wamejitolea kwa nguvu zao, maboma ya zahanati na maboma ya shule pia baadhi ya shule hazina madawati nilikuwa naomba Mheshimiwa Waziri, mje na mkakati maalumu kwa sababu ya kuleta madawati pamoja na viti shule za msingi kuna hali mbaya sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo shule ambazo watoto mpaka sasa hivi wanasoma chini ya mwembe (chini ya mti) na huo ni mfano wa Kijiji cha Tundu, Mkomachindo, Kapumpuli, Kilambo cha Mkolechi, Tuondokazi, Msamba, Lyela, Mwinza, Izinga, Katani, Kata, Yapinda, Isambara, King’ombe kuna Vijiji ishirini wanafunzi wanasoma chini ya mti Pamoja, kijiji kimoja wanafunzi wanasoma chini ya mwembe, vijiji vingine wanakalia mawe! Karne ya Ishirini na moja wanafunzi wanakalia mawe hata elimu wanayoipata wanaipata katika mazira magumu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, namshukuru Mheshimiwa Rais ametangaza hizi ajira ninakuomba Mheshimiwa Waziri kwa sababu kuna mazingira ambayo ni magumu, tuleteeni fomu sisi Wabunge, tumepita huko kero na mazingira tunayajua tujaze fomu mazingira yale ambayo watumishi waende moja kwa moja. Kwa sababu mkiwapeleka kule wataishia Mjini wata robu kwa hiyo wanafunzi wa nchi hii hawatapata haki ya walimu wanao husika kwa sababu kuna shule nyingine kuna mwalimu mmoja nyingine hakuna wana azima kutoka shule jirani kwa hiyo ajira hizi tuleteeni fomu tuwape vipaumbele vya maeneo yetu yenye changamoto ili mnapo ajiri waende moja kwa moja. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo ahadi za viongozi, ahadi za viongozi hizi wanapofika kwenye Kata zetu wananchi wana amini sana Viongozi Wakuu wa Nchi yetu. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye kampeni alihaidi Ujenzi wa Kituo cha Afya Tarafa ya Chala ni Makao Makuu ya Tarafa ambapo Kata hii Kituo chake hiki kina hudumia Kata Tatu. Kina hudumia Kata ya Ntuchi, Kata ya Katumbila na Kata ya Chala, ambazo mpaka sasa hivi kuwa ahadi ya Mheshimiwa Rais lakini bado hakuna kinachoendelea, akaja Mheshimiwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Chama Mheshimiwa Daniel Chongolo nae kahaidi Ujenzi wa Kituo cha Afya Chala nacho bado, akaja Mheshimiwa Waziri Mkuu kapita napo katoa maagizo kijengwe Kituo cha Afya Chala pia Hayati Mheshimiwa John Pombe Magufuli nae alitoa ahadi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Chala bado mpaka sasa. Ahadi ya Viongozi Wakuu wa Nchi karibu watatu bado maandalizi Mheshimiwa Waziri, naomba Kituo cha Afya Chala kianze kujengwa. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia zipo Kata ya Sintali, Miula wananchi wanapata huduma ya mbali sana wanatoka maeneo wanatembea karibu kilomita 20 mpaka 40. Naomba Kata ya Sintali, Kata ya Miula pamoja na Kata ya Chala ijengewe Vituo vya Afya. Ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 – Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani. Kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa kazi anayoifanya ya kuendelea kutoa ajira mpya ili kuliboresha Jeshi letu na Majeshi yetu nchini. Niwapongeze Mheshimiwa Waziri Naibu pamoja na timu nzima ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa kazi kubwa mnayoifanya, ni kazi ya kiuzalendo; pia askari kazi wanayofanya ya kulinda mali na kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi naenda kujikita kwa maeneo machache sana, hasa Jeshi la Zimamoto. Wabunge wengi wameongelea masuala ya makazi lakini Jeshi la Zimamoto lisipoanza na kuwa na mfumo wa zimamoto jamii; zimamoto jamii katika maeneo mengi miji inakua hata taarifa za majanga zinapotokea Jeshi la Zimamoto mpaka lifike kuna malalamiko kwamba either maji hamna ama wamechelewa kufika. Kwa hiyo wasipoanzisha zimamoto jamii katika maeneo ambayo ni hatarishi ili wanapopata taarifa ya majanga tayari wanakuwa na taarifa kutoka kwa wale zimamoto jamii kwamba ni vifaa gani vinatakiwa viende katika tukio linalotokea. Kwa sababu sasa hivi wanaweza wakaenda na vifaa ambavyo havifai kwenye tukio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakianzisha sera ya kuwa na zimamoto jamii wataweka coverage kubwa sana ambayo itawapunguzia kazi askari wa zimamoto. Hata ile ajali ya ndege ya Ziwa Victoria tungekuwa na zimamoto jamii maeneo yale wangeweza kuchukua hatua mapema zaidi; kabla ya Jeshi halijafika tayari. Hakungekuwa na hata mgongano wa wananchi kulalamika kuwa hawajafika; wanakwenda kuongezea nguvu tu kwenye zimamoto jamii. Vilevile wanakuwa tayari na taarifa. Kwa hiyo kazi itafanyika vizuri kwa sababu tayari wana taarifa kamili na nini hatua ya kuchukua.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nije kwenye upande wa NIDA, Wabunge wengi wamechangia, lakini nitoe ushauri kwa upande wa taarifa kwa wananchi wanaoishi vijijini. Wizara waje na mkakati maalum namna ya kuwapelekea taarifa wananchi ambao wanaishi vijijini kwa sababu wanatembea umbali mrefu, wanatumia gharama, hawana taarifa, akifika wanamwambia kitambulisho chako, bado, rudi. Mwananchi anatumia hata nauli elfu 30 mpaka 40, mwisho anakata tamaa anaacha, kwa hiyo watumie local radio, tv, Viongozi wa Serikali, Madiwani na hasa Madiwani wa Chama cha Mapinduzi ndio watapata taarifa kamili. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kamati ilitembelea kwenye vyuo vyetu, bado vina hali ngumu ukizingatia Jeshi la Uhamiaji pamoja na Jeshi la Zimamoto tumeuhisha sasa hivi ndio wanaanza kujitegemea kama majeshi, hawana vyuo ndio wanaanza kujenga. Kwa hiyo Wizara itenge fedha, wapewe bajeti ili waweze kumaliza vyuo vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kuna Sheria ya Parole; Sheria hii ndio itapelekea kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na hili Mheshimiwa Rais ameliona na ndio maana amemchagua Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Mheshimiwa Kagasheki kuwa wakatazame walete sheria ya mabadiliko itakayowezesha wafungwa kupata unafuu na kupata msamaha ili waweze kupunguziwa kesi pamoja na kupunguza msongamano magerezani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, zipo kata za kimkakati ambayo jiografia imekuwa ni ngumu, uhalifu unapotokea mpaka askari polisi wafike inakuwa ni tatizo hasa katika Jimbo langu la Nkasi Kusini, Kata ya Sintali, Kata ya Kizumbi, Kata ya Myula, pamoja na Kata ya Nyinde. Hizi kata zote ziboreshwe, vituo vya polisi vimechoka, vina hali ngumu pamoja na makazi. Wabunge wengi wamechangia kuhusu makazi ya askari wetu, kwa kweli ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Waziri anapokuja kumalizia, kwa kuwa yeye ni msikivu mzuri, safi kabisa, anatenda kazi vizuri, aje na mkakati wa namna ya kuboresha makazi ya askari wetu, yako katika hali ngumu sana pamoja na Ofisi zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia bajeti ya Wizara ya Ardhi. Kipekee kabisa nimpongezee Mheshimiwa Waziri pamoja na Naibu wake Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete na kipekee zaidi Mheshimiwa Rais kwa kupata tuzo kwa sababu nchi za nje zimetambua mchango mkubwa wa maendeleo anayowaletea Watanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara hizi tatu, TAMISEMI, Maliasili na Ardhi ndiyo chanzo cha migogoro kwa wananchi, kwa sababu hizi Wizara hazikai pamoja zikaja na muelekeo mmoja wa namna ya kutatua migogoro kwa wananchi. Kila Wizara inafanya kazi kivyake, kuanzia sasa hivi wanatakiwa wakae pamoja, waje na jibu moja namna ya kutatua migogoro kwa wananchi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo langu lina kata 11, kata sita zote sehemu ambayo ni salama haina migogoro ni Makao Makuu ya Kata; Vijiji vyote vinavyozunguka kwenye hizi kata sita vyote vina migogoro ya ardhi. Ukigeuka huku kuna ranchi, ukigeuka huku Hifadhi ya Lwafi, hii Hifadhi ya Lwafi wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini pamoja na Rukwa ni wakulima. Lakini hizi hifadhi wananchi wameongezeka, lakini sehemu ya kulima wanapata tatizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nakuomba Mheshimiwa Ridhiwan - Naibu Waziri, baada ya kikao cha Bunge break ya kwanza njoo Rukwa kuna migogoro mikubwa sana ya ardhi, umasikini wa Mkoa wa Rukwa unachangiwa na migogoro ya ardhi. Njoo utataue migogoro ya ardhi Mkoa wa Rukwa ili wananchi waweze kufanya kazi, waweze kulima kwa amani kwa sababu ni wachapakazi ili wanakwamishwa na migogoro ya ardhi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mfano Jimbo langu la Nkasi Kusini, vijiji vya Mkukwe, Kwamachindo, Mkata, China, King’ombe, Nundwe, Yasimba, Tundu, Tolesha, Izinga, Mwinza, Yela, Kwemanchindo hawa wote wako ndani ya hifadhi, akigeuka huku ni Ranchi ya Mkalambo, akigeuka huku Ranchi ya Nkundi; kwa mfano Ranchi ya Nkundi ni shamba la mwekezaji. Kijiji cha Nkundi hakuna hata eneo la kuweza kujenga shule, ofisi, mambo ya kijamii eneo hakuna.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimuombe Mheshimiwa Waziri njoo utupatie Kijiji cha Nkundi eneo la kujenga shule kwa sababu hili shamba la Nkundi linapakana na kijiji. Wanakijiji wanahitaji maeneo ya shule, ofisi na mambo mengine ya kijamii pamoja na zahanati. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vinavyozunguka mfano Kalambo, Kalambo Ranch; Kijiji cha Sintali Komanchindo hawana eneo la kulima linapakana na hifadhi ya Lwasi, mwiba mkubwa zaidi Mkoa wa Rukwa ni shamba la Efatha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Deus Sangu ameongea jana, hii ni ajenda ya Wabunge wote wa Mkoa wa Rukwa huyu mwekezaji amekuja sio kuwekeza, ni udalali, mashamba yanakodishwa, wananchi hawana maeneo la kulima, wakilima anaenda kupitisha trekta heka 100, heka 50 anavuruga mashamba ya wananchi, wananchi wanakamatwa akina mama wakipelekwa mahabusu kesi inaisha mahakamani hawa na lolote wanarudishwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Rukwa hasa shamba la Efatha ni mwiba, Kijiji cha Sikaulu wananchi wamekuja kufika hapa sisi Wabunge tumeanza kuhangaika kutatua migogoro ya shamba la Efatha. Mheshimiwa Waziri wewe ni mcha Mungu, Mheshimiwa Ridhiwani tukimaliza hapa njoo anza na Efatha. Unapokuja kuhitimisha uje useme mgogoro wa Efatha unaisha lini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkoa wa Rukwa ni wakulima, wanafanya kazi nzuri zaidi, wanahamia shambani kwenda kuweka makambi ili apate muda wa kulima, Wizara inaenda Maliasili wanachomea watu, wanafukuzwa wanaharibiwa mashamba yao hii sio haki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naiomba Wizara break ya kwanza njoo Rukwa uje utatue migogoro ya ardhi Rukwa inachangiwa umaskini kwa sababu Wizara hii haijaitendea haki Mkoa wa Rukwa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana naunga mkono hoja. (Makofi)
Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2021 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia bajeti kuu ya Serikali. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu, pamoja na timu nzima ya Wizara ya Fedha kwa kutuletea hii bajeti. Bajeti ni nzuri imegusa maeneo makubwa ya mwananchi kwa ajili ya maendeleo. Kipekee nimpongeze Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa sana anayoifanya ya kuliletea Taifa maendeleo, hasa wananchi wa Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kuchangia kwa kutoa ushauri upande wa vifaa vya ujenzi ambao bei imekuwa kubwa sana, ambapo kwa mwananchi wa kawaida kugharamia ujenzi wa nyumba kuweza kupata bati inakuwa ni tatizo kwa sababu wananchi wa Tanzania wengi wao vipato vyao ni duni. Kwa hiyo nikuombe Mheshimiwa Waziri naomba unisikilize, kidogo, ukienda Uganda asilimia karibia 80 ule mji wa Kampala umeezekwa kwa vigae na vile vigae vinatengenezwa na wananchi wa kawaida kutumia tu udongo wanachanganya na simenti na baadhi ya mechanical.

Mheshimiwa Naibu Spika, nchi kama ikiweza kutoa elimu, utaalam kama wa Uganda wanavyofanya hata mwananchi wa kawaida ataweza kuezeka nyumba yake kwa kupitia vigae. Vigae ni mbadala wa bei ilivyo juu ya mabati na vifaa vya ujenzi, hasa kupitia VETA, majeshi yetu pamoja na magereza, hivi vyuo vya VETA tukiviwezesha tujenge na viwanda vya vigae, wanafunzi wanapopata utaalam wa utengenezaji wa vigae itamrahisishia mwananchi wa kawaida kwenda kupata huduma ya vigae na kuweza kuezeka nyumba yake kwa urahisi zaidi. Kwa sababu sasa hivi hata mabadiliko ya tabia nchi vijijini hata nyasi zenyewe za kuezekea nyumba hazipo kwa hiyo vigae ndio suluhu pekee hata nyumba za tembe wenzengu Wagogo wataezekea vigae Mheshimiwa Waziri. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nije upande wa ranchi, hii ya Kongwa; kwenye bajeti yako ulielezea kuhusu Kongwa. Mheshimiwa Waziri ile ranchi ya Kongwa naomba uachane nayo kwa sababu mji wa Dodoma ni jiji; hadi sasa hivi kuna mahitaji makubwa sana ya nyama, hasa ukizingatia Kombe la Dunia. Ukiingia huko bei ya nyama sasa hivi ni tatizo. Sasa ranchi hii tukianza kuivuruga na kuibadilisha kuwa ya kilimo ilhali Jiji la Dodoma linakua, na mahitaji ya nyama pia; hata mnadani tunaenda kula nyama kule, tutakosa kula nyama za mnadani siku ya Jumamosi. Kwa sababu ile ranchi inasaidia, hata wafugaji wa kawaida wanaweza wakatumia kulisha wanyama kama ng’ombe katika hifadhi ya Kongwa. Tukiivuruga tutasababisha mahitaji ya nyama Jijini Dodoma kuwa ni ya shida.

Mheshimiwa Naibu Spika, yapo maeneo mengi zipo skimu nyingi sana Mkoa wa Rukwa zimetelekezwa, miundombinu ipo, lipo ziwa Tanganyika hakuna gharama ya miundombinu; kuliko kuanza sasa kuivuruga Ranchi ya Kongwa. Naungana na wabunge wote, hii Ranchi ya Kongwa isiguswe. Ikiwezekana iboreshwe, mitambo ya ngombe pamoja na madume; hapa tunalalamika wananchi wetu wanafuga mifugo ya kienyeji ambayo haina tija. Sasa ranchi ile inatakiwa irekebishwe, iboreshwe hawa wananchi wafugaji wapewe mbegu bora kutoka Ranchi ya Kongwa na rachi nyingine zote zinazomilikiwa na Serikali. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, tuje kwenye gridi ya Taifa. Mkoa wa Rukwa tunatumia gridi ya taifa kutoka nchi Jirani, siwezi kuitaja jina. Kwa sasa hivi ninamshukuru Mungu kwenye bajeti yako umesema unatuunganisha Gridi ya Taifa kutokea Iringa. Hili jambo linatakiwa lipewe kipaumbele kwa sababu tupo kwenye ushindani wa kiuchumi. Tupo kwenye ushindani wa kiuchumi lakini umeme tunategemea nchi Jirani. Kwa hiyo hujuma (sabotage) ya aina yoyote ile ya kuweza kudhoofisha maendeleo ya Mkoa wa Rukwa ni rahisi.

Kwa hiyo, hii gridi ya Taifa mmesema mnaunganisha na Iringa fanyeni hili jambo liwe la kipaumbele, hii kazi ikamilike mapema kwa sababu tupo kwenye shindano la kiuchumi, kwa hiyo sabotage, umeme unaweza ukakata, watu viwanda vyao vikaharibika. Mambo ya kiuchumi na ushindani kuna sabotage nyingi, ni ushindani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja kwenye uchumi wa bluu, uchumi wa bluu hasa mikoa mitatu; Rukwa, Katavi na Kigoma, tunashukuru mmetupatia meli kwenye bajeti, imeingia baada ya Wabunge wa mikoa mitatu kupiga kelele, tumepata meli Ziwa Tanganyika. Kwa hilo jambo, tunasema ahsante. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja upande wa miundombinu. Miundombonu bado. Kuna baadhi ya mikoa jamani, tuongee ukweli, ilisahaulika katika nchi hii. Hii mikoa ya pembezoni ilisahaulika na ndiyo maeneo yenye uchumi. Miundombinu mpaka sasa hivi kwa mfano kwenye Jimbo langu la Nkasi Kusini kata nne ambazo barabara hizi za uchumi, siyo za uchumi tu, ni pamoja na ulinzi kwa ajili ya wananchi, kwa sababu wananchi kule hata wakipata tatizo la uharamia, askari hawezi kufika kule kwa sababu miundombinu haipo. Kwa hiyo, ndiyo fursa ya maharamia na majambazi na wahalifu kwa ajili ya ukosefu wa miundombinu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nikuombe, Mheshimiwa Mwigulu unapokuja wind-up, utuambie hizi barabara za kimkakati katika majimbo yale yaliyosahaulika nchi hii hasa Kigoma, Nkasi Kusini toka uhuru barabara, hakuna. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja kwenye soko la mahindi, tena mwaka huu ndiyo kuna changamoto kubwa sana. Soko la mahindi mkulima anahangaika huko pembejeo gharama; tunashukuru mmeweka ruzuku katika pembejeo, lakini mnapokuja kununua pamoja na kuweka ruzuku, kama ni NFRA, mje mkae na wakulima mjue gharama ya gunia moja huyu mkulima wa kawaida ameligharamia kwa Shilingi ngapi, ili muweke bei inayolingana na thamani ya gunia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, NFRA wanaweza wakaja wakasema hili gunia tunanunua kwa shilingi 55,000 kwa mkulima, kumbe gharama hizo za gunia ni shilingi 120,000 mpaka shilingi 100,000. Kwa hiyo, unakuta huyu mkulima hamumsaidii, mnamdidimiza. Kwa hiyo, wakati wakununua bei za mahindi NFRA mfanye utafiti kujua gunia moja huyu mkulima wa kawaida ametumia gharama ya shilingi ngapi mnunue kulingana na thamani ya gunia. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, nakuja vyuo vya kati. Namshukuru sana Mheshimiwa Rais amefuta ada Kidato cha Tano na cha Sita. Kwa hiyo, nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa kazi anayoifanya. Vyuo vya kati ndiyo vinavyotengeneza utaalam na ajira. Hivi vyuo mafundi gereji wengi mtaani huko ni darasa la saba. Pia ni mafundi wazuri mno, ambao hawa wanapomaliza Darasa la saba wakiingia kwenye VETA hapa, naomba Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Nchemba ahakikishe kama Serikali aone namna ya kuweza kufuta ada kwenye vyuo vya kati, atasaidia kundi kubwa sana ambalo linachangamoto ya ajira. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye bajeti yake ameisoma, upo ubadhirifu wa fedha za UVIKO. Mheshimiwa Rais anatafuta fedha, anahangaika huku na kule na ametuletea maendeleo makubwa…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbogo kengele ya pili.

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Kwanza naunga mkono hoja. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kipekee nampongeza Mheshimiwa Rais, kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbalimbali za afya, elimu, miundombinu pamoja na mawasiliano. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo Nkasi Kusini lina barabara za kiuchumi ambazo ni barabara ya Wampembe - Kala - Mpasa - Kizumbi. Hizi barabara zimeathirika sana. Kwa hiyo, naiomba Serikali itenge fedha za dharura ili ziweze kwenda kufanya matengenezo ili wananchi waendelee kupata usafiri na huduma za kiuchumi na biashara zao ziendelee, kwa sababu zinaelekea ukanda wa Ziwa Tanganyika. Kwa hiyo, zilipokatika, wananchi wamebaki kwenye kisiwa. Ziwa likichafuka, hawana pa kwenda. Kwa hiyo, wagonjwa wengine wanakufa kwa sababu miundombinu imeharibiwa. Nilikuwa naishauri Serikali itenge fedha kwa haraka iende ikatengeneze hizo barabara za Wampembe - Kizumbi - Kala - Mpasa. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni umeme. Yapo maeneo ya uzalishaji ya vijiji, ambayo nilikuwa naomba kabla hii miradi ya umeme kwenda, ukafanyike utafiti kwenye yale maeneo ambayo vijana wamejiajiri katika maeneo ya uzalishaji, ndiyo waanzie huko kupeleka umeme. Mfano, Vijiji vya Masamba, Kyela, Mwinza, Izinga Kapumbuli na Kilambo cha Mkolechi. Haya maeneo ni ya uzalishaji ukanda wa Ziwa Tanganyika na yanahitaji umeme. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Naibu Spika, lingine ni suala la fidia. Kuna barabara hizi za TANROADS zilijengwa. Nyumba nyingi zilibomolewa hasa Kijiji cha Chala. Watu hawaelewi kuwa wananchi wanacheleweshewa maendeleo. Naomba wananchi wangu wapatiwe jibu, wanalipwa ama hawalipwi, ili waendelee kufanya shughuli zao za maendeleo na kujenga nyumba bora. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Nkasi Kusini, Kata ya Kizumbi na Ninde yapo maeneo mazuri ya kuanzisha uboreshaji wa skimu ya umwagiliaji, lakini katika jimbo zima hakuna skimu hata moja na haya maeneo Kata zilishaandaa. Kwa hiyo, naiomba Wizara ya Kilimo iende kuanzisha skimu za umwagiliaji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Nkasi Kusini pamoja na Mkoa wa Rukwa, kuna Ziwa Rukwa na Ziwa Tanganyika, lakini hatuna Chuo cha Uvuvi. Hawa wananchi hawapati elimu ya uvuvi. Pamoja na kupumzisha ziwa na mikakati mingi, lakini kama wananchi hawana centre, hawana chuo cha kupata elimu ya uvuvi itakuwa ni kazi bure. Hata tukipumzisha ziwa, samaki wakazaliana, uvuvi haramu utaendelea, kwa sababu wanavua kienyeji. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Naibu wa Waziri Mheshimiwa Mnyeti, alifika Rukwa na nilimwomba akatuahidi ujenzi wa Chuo cha Uvuvi Kata ya Wampembe kati ya Kata tatu ili wananchi wafike pale wapate elimu. Wananchi wa Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa wapate elimu waanze uvuvi wa kisasa. Naomba kwenye bajeti uwekwe huo ujenzi wa Chuo cha Uvuvi Kata ya Wampembe, Jimbo la Nkasi Kusini. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, lipo suala ambalo linachanganya sana. Kwanza niwape pole wananchi wa Wilaya ya Nkasi, Ukanda wa Ziwa Tanganyika. Nimefanya takwimu, ndani ya miaka mitatu, siyo chini ya wananchi 30 wameliwa na mamba ikiwa ni pamoja na wanafunzi, kwa sababu wengi wanafuata huduma ya maji katika Ziwa Tanganyika. Wakienda kule wanakutana na mamba, wengi wameliwa na mamba hasa wanafunzi na watu wazima. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba Wizara hizi tatu; Wizara ya Uvuvi, Mheshimiwa Mnyeti, Naibu Waziri wa Uvuvi, naomba unisikilize Bwana! Hili suala lipo serious, na picha nilimtumia Waziri wa Maliasili watu wanavyoliwa na mamba. Wapo wavuvi ambao unawapumzishia ziwa, wanaliwa na mamba. Kwa hiyo, Wizara ya Uvuvi, Wizara ya Maliasili na Wizara ya Maji wakae pamoja watenge bajeti waende wakaainishe maeneo yaliyo salama kwa kila kijiji ili wananchi wajue kuwa wanapoenda kutafuta huduma ya maji, ni sehemu salama. Kwenye maeneo hatarishi wawekewe mabango, wajue, kwa sababu wanaoliwa ni wanafunzi na wananchi wanaofanya biashara za samaki. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru Mheshimiwa Rais, alihamasika sana kutoa ruzuku za mbolea na wananchi wamelazimika kulima, na mwaka huu kuna mavuno mengi sana ya mahindi. Naomba Wizara itenge na iongeze vituo vya ununuaji wa mazao, mwananchi asije akapata gharama ya kusafirisha mazao mbali kutoka eneo analolima. Mfano, Kata ya Kala na Kate kutengwe vituo vitakavyomwezesha mwananchi kutokupata gharama ya kusafirisha kutoka eneo la kununulia mazao.

Mheshimiwa Naibu Spika, zipo shule chakavu sana hasa sekondari zile kongwe. Mfano, Sekondari ya Chala ni kongwe, iliyojengwa na wazazi, haikujengwa na lenta, imeharibika. Itengwe bajeti ikaboreshwe pamoja na kupatiwa madawati. Kuna shule za msingi zimechoka, mfano, Shule ya Msingi Yondokazi, Liyapinda, Sintali na Ninde. Hizi shule zimechoka, pamoja na Mahakama za Mwanzo. Mfano, Kata ya Kate, mahakama wanayotumia ni godauni, huku wameweka magunia, huku hakimu anaendelea kuendesha kesi; na nyingine ni Mahakama ya Mwanzo Kata ya Chala. Mahakama hizo zimechoka, naomba zitengwe fedha ili ziweze kuboreshwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia bajeti ya Wizara ya Ulinzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza naunga mkono hoja, lakini pia nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu, Mkuu wa Majeshi na timu yote ya Wizara ya Ulinzi kwa bajeti nzuri waliyoileta ndani ya Bunge na naomba Wabunge wote tuipitishe ili jeshi liweze kufanya kazi kwa bidii. Kipekee nimpongeze sana Mheshimiwa Rais kwa sababu tunaona anaendelea kuviboresha vyombo vya ulinzi na usalama hasa jeshi letu. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, upande wa mipakani na hasa katika maziwa, mfano Ziwa Tanganyika, upande wa Ziwa Tanganyika ndiyo kuna lango kuu kubwa sana la uhalifu kwa sababu lipo mipakani na nchi jirani. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Mkoa wa Rukwa hasa wavuvi mikoa hii mitatu Kigoma, Katavi na Rukwa wana changamoto kubwa sana ya wahalifu wanaotoka nchi jirani, wanapoenda kufanya shughuli zao za uvuvi, wanavamiwa wananyang’anywa nyavu zao na zana za uvuvi na pengine kuvuka kabisa kuja upande wetu na kunyang’anywa mali zao na fedha. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, niishukuru sana Wizara ya Ulinzi pamoja na Mheshimiwa Waziri na timu yote. Mimi kama Mbunge na mwakilishi wao natokea ukanda wa Ziwa Tanganyika niliandika barua ya maombi kuwaomba ili waweze kuja kujenga Kambi ya Jeshi ukanda wa Ziwa Tanganyika. Hatua hii imechukuliwa kwa haraka, wameshatuma timu ya wataalamu, wamekuja kuainisha eneo la Tarafa ya Wampembe, Kata ya Kizumbi, tayari eneo limeshapatikana. Kwa hiyo, niombe Wizara ipewe fedha ili kambi hii ikishajengwa wavuvi na wananchi wa ukanda wa Ziwa Tanganyika wamepokea kwa raha sana na wanampongeza Mheshimiwa Rais, kwa sababu hawana hofu tena ya uvamizi (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kambi hii ikijengwa wavuvi wanaofanya shughuli za kiuchumi watafanya kazi bila hofu na maendeleo yatakuwepo, kwa sababu kutakuwa ulinzi ndani ya Ziwa Tanganyika. Kambi ikijengwa itakuwa inafanya kazi ya intelligence gathering ndani ya ziwa na kutoa elimu katika ukanda wa Ziwa Tanganyika hasa kwa wavuvi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Kambi za JKT; sasa hivi tunaona kuna mwamko na mwitikio mkubwa sana wa vijana wetu kujiunga na Kambi za JKT. Kambi za JKT zilizopo ni chache. Tunaomba Wizara ipewe fedha ili vijana wetu waende wakapewe elimu ya uzalendo ili wawe na mapenzi na nchi yao. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge wengi wamechangia kuhusu bomu la kufukuza tembo, niiombe Wizara ya Maliasili na Utalii, sasa iweke ushirikiano na Jeshi letu lililovumbua bomu la tembo, ili pale mara inapotokea changamoto ya tembo kuvamia makazi ya watu, Jeshi la Ulinzi pamoja na Wizara ya Maliasili kwa pamoja waende kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto hiyo kwa haraka ili wananchi waendelee kufanya kazi zao kwa amani na usalama. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuna maeneo ya jeshi wamesema tunaona kuna changamoto; niiombe Wizara ipewe fedha maeneo yote ili yapate hati kamili ili maeneo ya jeshi yasivamiwe, yawe na hati kamili ili kuondoa migogoro kati ya wananchi na wanajeshi. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha, ahsante sana na ninaunga mkono hoja. (Makofi)
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi na mimi niweze kuchangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji. Kwanza, niunge mkono hoja, pia namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Aweso na timu yote ya Wizara Naibu, Katibu Mkuu pamoja na Meneja wa Maji Mkoa wa Rukwa Ndg. Boaz pamoja na Wilaya ya Nkasi kwa sababu wanatupa ushirikiano mkubwa sana; nasema hongereni sana. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipekee nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kazi kubwa ya uboreshaji wa miundombinu ya maji nchini ikiwa ni pamoja na Jimbo la Nkasi kusini. Kwanza, nitumie nafasi hii kuwapa pole wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini kwa kupatwa na mafuriko Kata nne; Kata ya Wampembe, Kata ya Ninde, Kata ya Kizumbi na Kata ya Kala, timu ya wataalam ukijumlisha Mkuu wa Wilaya na viongozi wote wa wilaya wanaenda kutathmini tuone namna ya kuwasaidia walioathirika na mafuriko. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nitoe nafasi hii kuwatoa hofu wavuvi wa Jimbo la Nkasi Kusini na Mkoa wa Rukwa hasa suala la kupumzisha ziwa, wenyewe wanajua mtu yeyote haruhusiwi kuingia. Hata mvuvi yule wa ndoano wanaona kama hata kitoweo cha familia watakikosa lakini uvuvi wa ndoano kitoweo cha kwenda kula na familia unaruhusiwa, hii ni Serikali Sikivu ya Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Nkasi Kusini lina changamoto kubwa sana ya maji hasa baadhi ya miradi iliyokuwepo imesuasua kwa muda mrefu. Ukianza na mradi wa Isale ambao una miaka 11 toka uanze lakini mpaka sasa hivi haujaisha. Mheshimiwa Waziri nikuombe utakapokuja kuhitimisha Hotuba yako ya Bajeti ya Wizara ya Maji uwahakikishie wananchi wa Jimbo la Nkasi Kusini huu mradi wa Isale ambao utanufaisha Kijiji cha Mkata, Nkukwe, Temba, China, Kitosi, Ifundwa, Ntuchi na Chenje unakwisha lini? Huu mradi wameusubiri kwa muda mrefu. Vijiji vimeteseka sana kwa kukosa maji. Mabomba yamewekwa pale lakini matumaini ya maji hawayaoni kwa sababu kulikuwa na changamoto ya mkandarasi nadhani kesi imeshaisha., tumeshapata taarifa na tumekufata ofisini na mimi mwenyewe nimekufata ofisini umenihakikishia mradi huu wa maji unaenda kwisha. Kutokana na umahiri wako na usikivu wako kama ulivyofanya katika Kijiji cha Kasu ulikuja nikakuomba shilingi milioni 400, wananchi wa Kijiji wameshapata maji na wanakushukuru sana, tupelekee salamu kwa Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia Katibu Mkuu Dkt. Nchimbi alikpokuwa niliwasilisha changamoto ya maji Wilaya ya Nkasi. Ulipigiwa simu palepale ukatupatia shilingi milioni 400, zimeshafika na ukarabati wa mabwawa Wilaya ya Nkasi kutatua changamoto ya maji kama dharura umeshaanza; tunakushukuru sana wananchi wa Wilaya ya Nkasi. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, nje ya hapo Wilaya ya Nkasi ina changamoto kubwa, suluhu ya kutatua hii changamoto ya maji ni kutoa maji Ziwa Tanganyika, tumemfata Mheshimiwa Waziri ofisini ametuhakikishia upembuzi yakinifu umeshaanza. Nikushukuru sana Naibu Waziri ameshafika Wampembe kwa sababu mradi huu wa maji kutoa Ziwa Tanganyika unaanzia Jimbo la Nkasi Kusini Kata ya Kizumbi Tarafa ya Wampembe, tenki kubwa linajengwa Kijiji cha Kantawa, baada ya Kantawa maji yanaenda wilayani; tunasema ahsanteni sana, mradi huu ukamilika mapema ili wananchi waweze kupata maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia vijiji vinavyopita katika mradi huu viweze kupata maji na wananchi pamoja na vijana wengi wa Jimbo la Nkasi Kusini wapate ajira kupitia mradi huu mkubwa wa maji. Pia, upo mradi wa Kizumbi kwenda Wampembe, tarafa nzima hii haina mradi wa maji. Nikuombe mradi huu ni wa muda mrefu, Kata ya Kizumbi kwenda Wampembe kuna changamoto tarafa nzima haina mradi wa maji. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshmiwa Waziri, utakapokuja kuhitimisha hotuba yako uje na majibu ya namna ya kutatua changamoto ya mafundi wa pampu kwa sababu pampu ikiharibika wanasema inakaa muda mrefu, wananchi wanasubiria. Tuandae mafundi mahalia kama ni wilayani na kama ni kijijini tuwa-train ili pampu ya maji inapoharibika awepo fundi mara moja anaenda anatengeneza na wananchi wanaendelea kupata maji. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, bili za maji zimeongelewa humu, hizi bili za maji ziendane na vipato vya wananchi. Kuna wananchi wa TASSAF wengine hali duni vipato viko chini. Kwa hiyo, bili walau tukae chini muone namna ya wananchi watavyolipa kulingana na vipato vyao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha naunga mkono hoja. Ahsante sana.
Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2023 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.
MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi kuchangia bajeti ya Serikali. Kwanza kabisa napenda nimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai tupo hapa tunachangia bajeti ya Serikali.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza napenda nianze na shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri ambayo ameifanya kwa watanzania hususan kwenye mambo mbalimbali ya elimu, afya, miundombinu pia mpaka juzi amedhihirisha upendo wake kwa watanzania kwa kuunda Tume ya Haki Jinai ambayo inamwezesha kila mtanzania kupata haki yake. Mheshimiwa Rais anahitaji pongezi kwa sababu ni kwa mara ya kwanza nchini kwetu Tanzania inaundwa Tume ya Haki Jinai. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizo ningependa kujielekeza kwenye suala la miundombinu nchini Tanzania. Sisi wananchi wa Mkoa wa Katavi tunaishukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa barabara kutoka Tabora kuja Mpanda kwa kiwango cha lami. Pamoja na hizo shukrani tunamshukuru pia kwa ujenzi wa Bandari ya Karema kule kwenye Ziwa Tanganyika ambayo itawezesha meli kutoka Congo kuja kutua kwenye Bandari ya Karema na pia itaweza kubeba mzigo kutoka Karema - Mpanda hadi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na pongezi hizo ninayo maombi kwa Serikali ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Maombi yetu ni suala la kufungua Mkoa wa Katavi, pamoja na hizo barabara ya Tabora - Mpanda, bado Mkoa wetu wa Katavi haujafunguka kwenda kwenye Mikoa mingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunaomba tupewe barabara ya kutoka Kibaoni kuja Stalike ambayo ina kilometa 71, lakini kwa sasa hivi ujenzi wa barabara hiyo umesimama kwa sababu ya ukosefu wa pesa, hata Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi alikwenda pale akawatoa wafanyakazi ambao ni wabovu lakini bado barabara hiyo imesimama. Ombi langu kwa Serikali itupe pesa barabara yenye kilometa 71 Kibaoni - Stalike iweze kukamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la pili, tunaomba tupewe barabara kutoka Kibaoni – Usevya - Majimoto mpaka Inyonga, Inyonga pale wanakuja kuungana na barabara ya lami ambayo inatoka Tabora-Mpanda. Barabara hii ni muhimu kwa sababu inabeba mazao yanayotoka kwenye Bonde la Mwamapuri, bonde hilo lina kilometa takribani hekta 18,000 ambazo zinatoa mpunga unaolisha nchi jirani za Congo, Rwanda, Burundi lakini na nchini kwetu Tanzania. Hivyo basi, upo umuhimu wa kuijenga barabara hii ya kutoka Kibaoni – Usevya - Majimoto mpaka Inyonga kwa kiwango cha lami, barabara yenye urefu wa kilometa 165 ili tuweze kufanya biashara vizuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunalo ombi la barabara nyingine ya kutoka pale Mpanda Mjini kwenda mpaka maeneo ya Karema ambako tumejenga Bandari ambayo iligharimu takribani bilioni 47, fedha za kitanzania.

Mheshimiwa Naibu Spika, barabara kutoka Bandarini kuja Mpanda Mjini haina lami, ni barabara ya vumbi. Hivyo basi, azma ya kujenga Bandari inaweza isifanikiwe vizuri kama hatutaweza kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Ombi langu; ninaiomba Serikali ijenge barabara hii ambayo ina takribani kilometa 125.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi lingine ni la ujenzi wa barabara ya kutoka pale Vikonge – Luhafwe mpaka Uvinza ili Mkoa wetu wa Katavi uweze kuungana na Mkoa wa Kigoma.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi la tatu ni la barabara ya kutoka pale Mpanda Mjini kupitia Ugala ambako kuna daraja linajengwa. Hivyo tunaomba fedha za daraja hilo ili liweze kukamilika na barabara hiyo iweze kutoka Mpanda – Ugala – Kaliua – Kahama mpaka Nyakanazi ili tuweze kupata wafanyabiashara kutoka Rwanda na Burundi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na maombi ya barabara hizo sisi tunapenda kusema ahsante kwa Serikali ya Awamu ya Sita kwa fedha ambazo zimekuja kwenye Mkoa wetu huu wa Katavi kwa kipindi cha miaka mitatu. Ombi letu ni kukamilishiwa huu usafiri ili Mkoa wetu wa Katavi uweze kufunguka.

Mheshimiwa Naibu Spika, ombi lingine ambalo ningeweza kuliomba kwa Serikali ya Awamu ya Sita, tungeomba pia tukamilishiwe baadhi ya miradi. Kwa mfano tunao mradi wa kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika kuja pale Mpanda Mjini. Mradi huo wa kuvuta maji kutoka Ziwa Tanganyika kuja Mpanda Mjini utaweza kunufaisha mikoa ya jirani kama Mkoa wa Rukwa pamoja na vitongoji ambavyo vinapita pembeni mwa mradi huo. Mradi huo ni mkubwa, bado haujaanza, lakini uko kwenye kufanyiwa tathmini. Tungeomba, ili kutatua tatizo la maji kwenye Mji wa Mpanda Mjini tunahitaji maji yavutwe kutoka Ziwa Tanganyika. Sasa hivi maji yaliyopo hayatoshelezi kwa sababu wananchi wameongezeka. Kama sensa ilivyopita mwaka jana, Mji wa Mpanda umekua na wananchi wameongezeka, hivyo mahitaji ya maji ni makubwa, yaliyopo hayatoshelezi na yanatoka kwa mgao kwa siku moja moja.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia ombi lingine ambalo ningeiomba Serikali ya Awamu ya Sita tunaomba ule Mradi wa Umwagiliaji wa Mwamapuli ambao uko kwenye Halmashauri ya Mpimbwe utekelezwe. Mradi huu ni ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ambaye aliwaahidi wananchi wa Mwamapuli…

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa Mzungumzaji)

NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mbogo….

MHE. TASKA R. MBOGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante naunga mkono hoja.