Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Answers to Primary Questions by Hon. Maryprisca Winfred Mahundi (210 total)

MHE. DKT. DAVID M. DAVID Aliuliza: -

Upatikanaji wa maji katika Mji mdogo wa Same ni asilimia 34; na mradi mkubwa wa maji Same – Mwanga – Korogwe umechelewa kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa: -

(a) Je, ni kitu gani kilichochelewesha mradi huo na ni hatua gani zimechukuliwa kwa watu waliohusika na ucheleweshaji huo?

(b) Je, ni lini sasa mradi utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema yote ambayo amenijalia hata siku ya leo nami nimekuwa mmoja wa Wabunge katika Bunge hili Tukufu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile napenda kumshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyoonyesha juu yangu kwa sababu Bunge la Kumi na Mbili ni Bunge ambalo hakika Wabunge wote wako imara. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda pia kuwashukuru sana wanawake wa Mkoa wa Mbeya kwa kunipa imani kubwa na kuona naweza kuja kuwawakilisha na kulisukuma gurudumu la maendeleo. Nakushukuru wewe binafsi Naibu Spika kwa sababu nawe ni mpiga kura wangu halali na mwaminifu sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba niendelee kushukuru familia yangu, hasa mume na baba yangu mzazi pamoja na watoto wangu waliofanikisha kuwa hivi nilivyo. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mhe. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza Mradi Mkubwa wa Maji wa Same-Mwanga-Korogwe kwa gharama ya shilingi bilioni 262. Mradi huu unahusisha ujenzi wa miundombinu ya chanzo cha maji, ulazaji wa bomba kilomita 71, vituo vya kusukuma maji 3 na matanki 7 yenye ujazo kuanzia lita laki tatu hadi milioni tisa na ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji kilomita 204. Katika utekelezaji mradi huu mkataba wa mwisho ulitarajiwa kukamilika Machi, 2021. Hata hivyo, kumekuwepo na kasi ya utekelezaji usiyoridhisha hadi Serikali imefikia hatua ya kusitisha mikataba na wakandarasi mwezi Desemba, 2020.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inafanya juhudi kuhakikisha taratibu za kupata wakandarasi wapya wa kumalizia kazi za mifumo ya umeme na ulazaji wa bomba kuu kilomita 34.

Aidha, kazi za ulazaji wa mabomba ya kusambaza maji zinatekelezwa na wataalam wa ndani wa Wizara wakishirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa kumtumia mkandarasi wetu Seprian Lwemeja.

Mheshimiwa Naibu Spika, tunatarajia mradi huu ukamilike Desemba 2021 na utanufaisha wananchi wapatao 438,820 kwa Mji wa Same-Mwanga pamoja na vijiji 38 vya Wilaya ya Same, Mwanga na Korogwe. Awamu ya kwanza itahudumia wananchi 168,820 katika miji ya Same na Mwanga. Awamu ya pili ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka wa fedha 2021/2022 utanufaisha wananchi 270,000 katika vijiji vilivyo eneo la mradi ambapo Wilaya ya Same ni Hedaru, Mabilioni, Gavao, Makanya, Mgwasi, Bangalala, Chanjo, Mwembe, Njoro, Majengo, Bendera, Mkonga, Ijinyu na Mgandu; Wilaya ya Mwanga ni Kifaru, Kiruru Ibwejewa, Kisangara, Lembeni, Kivegere, Mbambua, Kileo, Kivulini, Kituri na Mgagao; na Wilaya ya Korogwe ni Bwiko, Mkomazi, Nanyogie, Manga-Mtindilio na Manga-Mikocheni.
MHE. LEAH J. KOMANYA Aliuliza: -

Mji wa Mwanhuzi unakabiliwa na tatizo kubwa sana la maji safi na salama kutokana na chanzo chake cha maji cha bwawa la Mwanyahina kujaa tope: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wananchi wa Mji wa Mwanhuzi na vitongoji vyake wanapata maji safi na salama ya kutosha kwa mwaka mzima?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Mwanhuzi, Wilayani Meatu unategemea chanzo kimoja cha Maji ambacho ni Bwawa la Maji la Mwanyahina. Bwawa hilo lilijengwa mwaka 1999 lenye uwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo millioni 1.6. Bwawa hili kwa sasa limejaa tope jingi na kusababisha kupungua kina cha kuhifadhi maji kutoka kina cha mita 9 hadi mita 5 zinazohifadhi maji kwa matumizi ya wakazi wa Mji wa Mwanhuzi na vijiji jirani.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuboresha huduma ya maji katika mji wa Mwanhuzi na vitongoji vyake, Serikali imekamilisha utafiti, usanifu na kuanza kutekeleza ujenzi wa chanzo mbadala cha ukusanyaji na usafirishaji wa maji kutoka bonde la Mto Semu hadi kwenye matanki yanayotumika kusambaza maji katika Mji wa Mwanhuzi. Gharama za mradi huo shilingi milioni 742. Tayari Serikali imetuma kiasi cha shilingi milioni 276.6 kwa ajili ya kazi hizo za ujenzi wa mradi mbadala wa kutoa maji katika bonde la Mto Semu na kuyapeleka mjini Mwanhuzi. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa lengo la kutatua tatizo la muda mrefu katika mji wa Mwanhuzi na vitongoji vyake, Serikali ipo katika hatua za awali za kutekeleza mradi mkubwa wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria unaolenga kumaliza changamoto za huduma za maji katika mkoa wa Simiyu zikiwemo Wilaya za Busega, Bariadi, Maswa, Itilima na Meatu.
MHE. MASACHE N. KASAKA K.n.y. MHE. ALLY A. MLAGHILA aliuliza: -

Suluhisho la tatizo la maji katika Wilaya ya Kyela ni kutumia chanzo cha Ziwa Nyasa kama ilivyoelezwa kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020.

Je, ni lini sasa mradi huo utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyigulile Mlaghila, Mbunge wa Kyela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua tatizo la huduma ya maji linaloikabili Wilaya ya Kyela. Katika kuhakikisha wananchi wa Wilaya hiyo wanapata huduma ya majisafi, salama na ya kutosha, Serikali ina mpango wa muda mfupi na wa muda mrefu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mpango wa muda mfupi Serikali imeendelea na ukarabati wa miradi ambapo baadhi ya miradi iliyokarabatiwa tayari inatoa huduma ya maji ukiwemo mradi wa maji wa Makwale Group ambao unahudumia vijiji viwili vya Ibale na Makwale, Mradi wa maji wa Matema unaohudumia kijiji cha Matema (kitongoji cha Ibungu) na Kijiji cha Ikombe (Kitongoji cha Lyulilo) na mradi wa maji wa Lubaga ulioharibika muda mrefu umekarabatiwa na wananchi wanapata maji kwenye vituo 15 vya kuchotea maji. Aidha, kupitia bajeti ya mwaka 2020/ 2021 Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Mababu, Kisyosyo, Katumbasongwe, mradi wa Kapapa kwenda kijiji cha Mwaigoga na mradi wa Sinyanga Group.

Mheshimiwa Spika, katika juhudi za muda mrefu, Serikali imepanga kutumia Ziwa Nyasa kama chanzo cha kudumu cha kusambaza maji kwa wananchi waliopo Wilayani Kyela pamoja na maeneo ya jirani. Hadi sasa timu ya kitaifa ya wataalam imefanya upembuzi wa awali kwa kufika Kyela na kubaini eneo la kijiji cha Ikombe kilichopo katika mwambao wa Ziwa Nyasa kuwa linafaa kujengwa chanzo cha maji. Mradi huu unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2021/2022.
MHE. FLORENT L. KYOMBO Aliuliza: -

Kata za Gera, Ishozi, Ishunju, Kanyigo, Kashenye, Bwanjai, Bugandika, Kitobo, Buyango na Ruzinga katika Jimbo la Nkenge zina shida kubwa ya maji licha ya kwamba zipo kwenye mwambao wa Ziwa Victoria.

Je, ni lini Serikali itawafikishia wananchi wa kata hizo maji kutoka Ziwa Victoria kama inavyofanya kwa mikoa mingine inayopata maji kutoka katika ziwa hilo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Florent Laurent Kyombo, Mbunge wa Nkenge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali inaendelea kutekeleza miradi ya maji katika vijiji 32 ambapo imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.084 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Wilaya ya Misenyi.

Aidha, Wilaya ya Misenyi inatarajiwa kunufaika na Mradi wa Maji wa Maziwa Makuu kupitia Ziwa Victoria ambapo Mtaalam Mshauri anaendelea na usanifu wa kina unaotarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2021 na ujenzi wa mradi kuanza mwaka wa fedha 2021/2022. Vijiji 11 vitanufaika ambavyo ni Ishunju, Luhano, Katolerwa, Kyelima, Kashenye, Bushango, Kigarama, Bweyunge, Bukwali, Kikukwe na Bugombe.
MHE. FREDRICK E. LOWASSA Aliuliza:-

Mradi wa maji wa BN 520 una ziada ya lita milioni 100 kwa mujibu wa wataalam na Mheshimiwa Rais alikubali ombi la ziada hiyo kujumuishwa kwenye mradi:-

Je, ni lini utekelezaji wa ahadi hiyo utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fredrick Lowassa, Mbunge wa Monduli, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji wa BN 520 katika Jiji la Arusha, ujenzi wa tanki la maji eneo la Mlima wa Ngorbob Kisongo umeshakamilika. Tanki hili litahudumia Kata ya Mateves, Olmoti na Monduli (Meserani, Kambi ya Sokoine, TMA na Monduli Mjini).

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali tayari imefanya upembuzi yakinifu wa mradi wa kupeleka maji katika Kata ya Mateves na Monduli (Meserani, Kambi ya Sokoine, TMA na Monduli Mjini). Mradi huo umepangwa kutekelezwa katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Mheshimiwa Naibu Spika, wakati Serikali inajipanga kutekeleza mradi huo, Wizara kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Arusha inatekeleza miradi miwili ya Lolomsikio na Komolonike ili kuboresha huduma ya maji Mjini Monduli. Miradi hiyo inatarajia kuongeza upatikanaji wa maji Mjini Monduli kutoka mita za ujazo 1,430 ya sasa mpaka 2121 na inatarajiwa kukamilika mwezi Februari, 2021.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA Aliuliza:-

Je, ni lini mradi wa kusambaza maji Mji wa Njombe kutoka Mto Hagafilo utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika, Mbunge wa Njombe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya Dola za Marekani millioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 Tanzania Bara na Zanzibar. Moja ya miji itakayonufaika na mkopo huo ni Mji wa Njombe, kwa sasa mradi upo katika hatua za manunuzi na tunatarajia Wakandarasi watakuwepo eneo la mradi kwa ajili ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi ifikapo mwezi Aprili, 2021 na ujenzi wa mradi utachukua miezi 24.
MHE. MASACHE N. KASAKA Aliuliza:-

Je, ni lini ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Chunya Mjini na kata za jirani utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Masache Kasaka, Mbunge wa Jimbo la Chunya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto inayoukabili Mji wa Chunya. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, hatua mbalimbali za muda mfupi na mrefu zimeendelea kuchukuliwa. Kwa upande wa muda mfupi, Serikali imejenga mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika Mji Mdogo wa Chunya uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 946.8. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tanki la ukubwa wa mita za ujazo 500, ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilometa 10.49. Mradi umekamilika kwa asilimia mia moja mwaka 2019 na umesaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 36 hadi 51.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa hatua za muda mrefu, Serikali kupitia Wizara ya Maji ina mpango wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji kwa ajili ya wananchi wa Mji wa Chunya. Mradi huo utatekelezwa kupitia fedha za mkopo kiasi cha dola za Marekani milioni 500 kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim kwa ajili ya miji 28 Tanzania Bara na Zanzibar. Kwa sasa mradi upo katika hatua ya manunuzi ya Wakandarasi wanaotarajiwa kuwepo eneo la mradi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi ifikapo Aprili, 2021 na ujenzi wa miradi unatarajiwa kuchukua miezi 24. (Makofi)
MHE. NOAH L. S. MOLLEL Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa maji kwenye Vijiji vya Engutukoiti, Losineni, Juu, Losineni kati, Oldonyawasi, Lemanda, Lemengrass, Oldonyosambu, Likurat, Olkeejulbendet, Lenigjape, Olkokula, Lemanyati, Lenjani, Seuri, Ekenywa na Ngaramtoni na Kata za Kimyak, Sambasha Tarakwa, Oloirien, Kiranyi, Likidingla, Sokon II, Olturito, Bangata, Mlanganini, Nduruma, Bwawani, Oljoro na Lahni Musa, Kisango, Mwandet Wilayani Arumeru?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lemburis Saputi Mollel, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli vijiji hivi vilikuwa na changamoto ya huduma ya maji, lakini kuanzia mwezi Disemba, 2020, Vijiji vya Lengijave, Olkokola, Seuri, Ekenywa na Ngaramtoni vimeanza kupata huduma ya maji kutoka kwenye mradi uliofadhiliwa na Shirika la Uingereza la DFID kupitia Shirika la Water Aid Tanzania. Aidha, Vijiji vingine vya Oldonyosambu, Oldonyowasi, Lemanda, Losinani Kati na Juu na Ilkuroti vinatarajiwa kupata huduma ya maji kutoka kwenye mradi huu kupitia upanuzi unaofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Jiji la Arusha kutoka kwenye tanki la maji lililopo kijiji cha Lengijave, lenye ukubwa wa mita za ujazo 450. Kijiji cha Lemanyata kina huduma ya maji kupitia Mradi wa Olkokola – Mwandeti.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2020/ 2021, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.13 kwa Wilaya ya Arumeru kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji mbalimbali. Miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa Mradi wa Maji wa zamani wa Nduruma – Mlangarini na kukarabati Mtandao wa Bomba unaopeleka maji Vijiji vya Themi ya Simba, Kigongoni na Samaria na ukarabati wa Mradi wa Manyire – Maurani – Majimoto utakaonufaisha Vijiji vya Maurani, Manyire na Maji moto kuwa na maji ya uhakika na Miradi ya Likamba na Oloitushura & Nengungu.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE Aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Maji wa Nyashimo, Kata ya Nyashimo ambao ulitegemewa kukamilika mwezi Oktoba, 2020 utakamilika ili wananchi waweze kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Jimbo la Busega, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Nyashimo ulianza kutekelezwa mwezi Julai, 2019 na ulitegemewa kukamilika tarehe Oktoba, 2020 kwa gharama ya shilingi bilioni 1.58. Wakati utekelezaji wa mradi, Mkandarasi alipata changamoto zilizosababisha kuomba kuongezewa muda na hivyo mradi huu unatekelezwa kufikia mwaka huu 4 Aprili, 2021 ambapo ombi lake lillikubaliwa.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua ya majaribio ya kusukuma maji kupeleka kwenye tanki baada ya kufanikiwa kufunga umeme tarehe 9 Januari, 2021. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2021 na kuhudumia wakazi wapatao 12,000. (Makofi)
MHE. ESTHER NI. MATIKO Aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tarime utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Mji Mdogo wa Tarime wanapata huduma ya maji safi na salama kupitia Mradi wa Maji wa Mserereko Nyandulumo; visima vitatu Rebu, Jeshi la wokovu na Viambwi, na bwawa la maji Tangota. Vyanzo hivi vyote vinazalisha wastani wa lita 1,200 kwa siku wakati jumla ya mahitaji ni lita 6,000 za maji kwa siku. Utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria utaweza kuhudumia maeneo yote ya mji wa Tarime kwa kuzalisha wastani wa lita 6,500 kwa siku ambazo ni zaidi ya mahitaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Tarime, Serikali imepata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim jumla ya Dola za Marekani millioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar. Moja ya miji itakayonufaika na mkopo huo ni Mji wa Tarime ambao utatumia chanzo cha Ziwa Victoria. Kwa sasa mradi upo katika hatua za manunuzi ya wakandarasi wanaotarajiwa kuwepo eneo la mradi ifikapo mwezi Aprili, 2021 na ujenzi wa mradi unatarajiwa kuchukua miezi 24.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE Aliuliza:-

Je, lini utekelezaji wa mradi wa maji kwa vijiji 57 vya Wilaya ya Kyerwa utaanza kwa kuwa usanifu wa kina wa mradi huo umeshakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sebba Innonent Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Kyerwa, Serikali katika mwaka wa fedha 2019/2020 kupitia Programu ya PforR na Programu ya Malipo kwa Matokeo (PBR) imetekeleza miradi ya maji katika vijiji vya Nkwenda, Rugasha, Kitwechenkura, Kaikoti, Rwensinga, Kagenyi pamoja na sehemu ya Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya Kyerwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kwa mwaka huo, ukarabati wa visima virefu na vifupi umefanyika katika vijiji vya Kibale, Nyamiaga, Magoma, Rutunguru, Kihinda, Rwenkende, Kyerwa, Mirambi na Nyakakonyi ambapo wananchi wapatao 51,025 wananufaika na huduma ya maji safi. Utekelezaji wa miradi katika vijiji tajwa hapo juu ni sehemu ya utekelezaji wa miradi katika vijiji 57.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha vijiji vilivyobaki kati ya 57 vya Wilaya ya Kyerwa vinapata huduma ya maji, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.56 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji 12 vya Runyinya, Nkwenda, Nyamweza, Rwabwere, Karongo, Iteera, Muleba, Chanya, Muhurile, Kimuli, Rwanyango na Chakalisa. Pia vijiji hivi viko ndani ya mradi wa vijiji 57.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022, Serikali itaendelea kutekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji 35 vilivyobaki ili kukamilisha utekelezaji wa mradi wa vijiji 57. (Makofi)
MHE. YAHYA A. MHATA Aliuliza:-

Je, ni lini utekelezaji wa mradi wa kutoa maji Mto Ruvuma kwenda Mji wa Manyaka utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ali Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim jumla ya Dola za Marekani Milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 Tanzania Bara na Zanzibar. Moja ya mji unaonufaika na mkopo huu ni Mji wa Mangaka. Kwa sasa mradi upo katika hatua za manunuzi na wakandarasi wanatarajiwa kuwepo eneo la mradi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi ifikapo Mei, 2021 na utekelezaji ni muda wa miezi 24.
MHE. ANTON A. MWANTONA Aliuliza:-

Serikali ilifanya upembuzi yakinifu na kubaini kuwa jumla ya shilingi Bilioni 21 zinahitajika ili kukarabati miundombinu ya maji Mji wa Tukuyu:-

Je, ni lini Serikali itatenga fedha na kuanza ukarabati wa miundombinu hiyo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Albert Anton Mwantona, Mbunge wa Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha wananchi wa Mji wa Tukuyu wanapata huduma ya maji safi na salama ya kutosha, Serikali imeendelea na mikakati ya muda mfupi na mrefu. Mkakati wa muda mfupi ulihusisha uboreshaji wa chanzo cha maji cha Masalala, ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 200,000 pamoja na ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa mita 750. Kazi hizo zimesaidia kuimarisha huduma ya maji kwa wakazi wa Mji wa Katumba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa mkakati wa muda mrefu wa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi katika Mji wa Tukuyu, Serikali kwa kutumia wataalam wa ndani wa Mamlaka za Maji na Usafi wa Mazingira za Mbeya na Tukuyu inafanya mapitio ya usanifu wa mahitaji kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji katika Mji wa Tukuyu kwa kutumia chanzo cha Mto Mbaka. Kulingana na usanifu kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mradi huu ni pamoja na ujenzi wa bomba kuu la kilometa 15.5, ujenzi wa bomba la usambazaji maji kilometa 20, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 2,000,000. Mradi huu utatengewa fedha katika mwaka wa fedha 2021/2022 na utekelezaji wake unatarajia kuanza mwezi Julai, 2021.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa kutoa maji toka Ziwa Victoria kuyapeleka Biharamulo kama Mheshimiwa Rais alivyoahidi hapo tarehe 16/09/2020 alipokuwa Biharamulo katika Kampeni za Uchaguzi Mkuu, 2020?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Eng. Ezra John Chiwelesa, Mbunge wa Biharamulo Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto za upatikanaji huduma ya maji katika Wilaya ya Biharamulo. Hivyo, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali inatekeleza mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji wenye urefu wa km 10.9 katika maeneo ya Ng’ambo, Kalebezo, Nyakatuntu, Rubondo Chuoni na Rukaragata na kuchimba kisima katika eneo la Rukagarata. Thamani ya mradi huu ni shilingi milioni 178.9 na utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 70.

Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na changamoto ya uhaba wa maji katika Mji wa Biharamulo, Serikali iliamua chanzo cha uhakika cha maji kiwe Ziwa Victoria badala ya bwawa na chemichemi vinavyotumika kwa sasa. Hivyo mradi wa usambazaji maji katika Mji wa Biharamulo ambao utatoa maji katika Ziwa Victoria umefikia katika hatua ya kuandaa makabrasha ya zabuni (tender documents). Utekelezaji utaanza katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Aidha, kupitia Mradi wa Maziwa Makuu, Wilaya ya Biharamulo itanufaika kupitia chanzo cha Ziwa Victoria ambapo jumla ya vijiji 12 vya Rwekubo, Rusese, Kabindi, Runazi, Rukora, Kikomakoma, Kagoma, Songambele, Kasozibakaya, Nyamigogo, Chebitoke na Nyabusozi vitapata huduma ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya maji kulingana na upatikanaji wa fedha.
MHE. MARGARET S. SITTA Aliuliza:-

Serikali iliahidi kufikisha Urambo maji ya Ziwa Victoria na kwa sasa yameshafika Tabora:-

(a) Je, ni hatua zipi zimechukuliwa katika kutekeleza azma hiyo?

(b) Je, ni kiasi gani cha fedha kimetengwa katika mwaka huu wa fedha na ni lini maji yatafikishwa Urambo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Jimbo la Urambo lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imepata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim ya India ambapo jumla ya Dola za Marekani milioni 500 zitatumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 28 Tanzania Bara na Zanzibar. Kupitia mkopo huo, Mji wa Urambo ni kati ya maeneo yatakayonufaika na mkopo huo. Kwa sasa utekelezaji wa mradi huo upo katika hatua za manunuzi ya wakandarasi wanaotarajiwa kuwepo eneo la miradi ifikapo Mei, 2021 na utekelezaji wake ni muda wa miezi 24.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imetenga jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 1.89 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Urambo.
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA Aliuliza:-

Mradi wa maji wa Chipingo uliopo katika Jimbo la Lulindi ambao umegharimu Shilingi Bilioni 3.9 ni wa muda mrefu tangu mwaka 2013, lakini umekuwa hauna tija kwa kuwa hautoi maji; mabomba kupasuka mara kwa mara na mpaka sasa bado haujakabidhiwa kwa Serikali:-

Je, Serikali inatoa kauli gani juu ya mradi huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Jimbo la Lulindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji wa Chipingo upo katika Jimbo la Lulindi, Wilaya ya Masasi. Mradi huu ulianza kujengwa Aprili, 2013 na ni miongoni mwa miradi ambayo haikukamilika kwa wakati kulingana na mkataba. Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi, Serikali ya Awamu ya Tano imefanya jitihada za kukamilisha mradi huu na hivi sasa mradi huo unatoa maji na upo katika hatua za majaribio ambapo vijiji 6 kati ya 8 ambavyo ni Manyuli, Chipingo, Mnavira, Chikolopora, Namnyonyo na Mkaliwala vinanufaika.

Mheshimiwa Spika, Vijiji viwili vya Rahaleo na Mapiri vya mradi huo bado havijaanza kupata huduma ya maji ambapo ujenzi wa mtandao wa maji kwa ajili ya vijiji hivyo unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Machi, 2021.

Aidha, kuhusu suala la upasukaji wa mabomba katika kipande cha bomba kuu chenye urefu wa kilomita 1.2, Serikali inaendelea kusimamia maboresho yanayofanywa na mkandarasi kipindi hiki cha majaribio ya mradi ili wananchi waweze kupata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa. Utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 90.
MHE. TUMAINI B. MAGESSA Aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Maji wa Chankorongo utawekewa vituo vya kuongeza kasi ya maji ili upate uwezo wa kutoa huduma katika maeneo mengi zaidi Jimboni Busanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tumaini Bryceson Magessa, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji wa Chankorongo unatumia maji ya Ziwa Victoria ukiwa na pampu yenye uwezo wa kuzalisha lita 155,000 kwa saa ambapo kwa sasa unatoa huduma kwa wakazi wapatao 23,756 wa vijiji vitano vya Chankorongo, Chikobe, Nyakafulo, Chigunga na Kabugozo katika Jimbo la Busanda.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha mradi huu unanufaisha wakazi wengi wa Jimbo la Busanda, Serikali imeanza upanuzi wa mradi huo wa maji kwa kuanza utekelezaji wa Mradi wa Maji Katoro-Buseresere wenye thamani ya shilingi bilioni 4.2. Kupitia mradi huo wakazi wa vijiji vya Luhuha, Nyakagomba, Inyala na Mji Mdogo wa Katoro watanufaika na huduma ya maji. Kwa sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 20 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili, 2021.

Aidha, katika kuhakikisha wananchi wengi wananufaika na huduma ya maji, Serikali kupitia programu ya Mpango wa Malipo kwa Matokeo inaendelea na ujenzi wa miradi ya maji ya bomba katika vijiji vya Nyakagwe na Rwamgasa ambapo wakazi wapatao 14,315 wa vijiji hivyo watanufaika na huduma ya maji safi.
MHE. GEORGE N. MALIMA Aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji kwa wananchi wa Mji wa Mpwapwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua tatizo la muda mrefu la uhaba wa maji katika mji wa Mpwapwa. Katika kutatua tatizo hilo, mikakati ya muda mfupi na muda mrefu imekuwa ikitekelezwa. Kwa upande wa mikakati ya muda mfupi, mwaka 2020/2021 Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuchimba visima virefu viwili katika eneo la Kikombo. Ujenzi wa bomba kuu kutoka katika visima hivyo viwili mpaka katika tanki la Vingh’awe, kuongeza mtandao wa maji katika maeneo ya pembezoni ambayo ni Vijiji vya Vingh’awe na Behero. Aidha, kazi nyingine itakayofanyika ni kufunga pampu mpya kwenye kisima cha Kikombo ambacho kitaongeza uzalishaji wa maji katika kisima hicho kutoka lita 40,000 kwa saa hadi lita 65,000 kwa saa. Kukamilika kwa kazi hizi kutaboresha upatikanaji wa huduma ya maji katika mji wa Mpwapwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mpango wa muda mrefu, Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mpwapwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji ya Dodoma (DUWASA) inaendelea kufanya usanifu unaotarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2021 na kubainisha maeneo ambayo yana upungufu mkubwa wa maji katika Mji wa Mpwapwa ambapo vitachimbwa visima virefu vinne na kuongeza mtandao wa mabomba katika Mji wa Mpwapwa na viunga vyake. Aidha, katika mwaka 2021/2022, Serikali itakarabati mradi wa maji wa mtiririko wa Mayawile na Kwamdyanga.
MHE. AGNESTA L. KAIZA Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka maji safi na salama Butiama ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Baba wa Taifa katika Taifa letu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Agnesta Lambart Kaiza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Wilaya ya Butiama ni 61.18%. Katika kuhakikisha wananchi wa Butiama wanapata huduma ya maji safi Serikali kupitia RUWASA imekamilisha miradi ya maji katika Vijiji vya Nyabanje, Magunga, Kongoto, Bukwaba, Kamgendi na Masurura, vinavyohudumia wananchi katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa lengo la kutatua tatizo la maji katika muda mrefu Butiama, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa Mugango – Kiabakari – Butiama mwezi Disemba, 2020 na unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022. Kazi zilizoanza kutekelezwa ni upimaji wa maeneo ya ujenzi wa matenki, mtambo wa kusafisha maji, njia kuu ya bomba na uletaji wa vifaa katika eneo la mradi. Mradi huu unatarajiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa asilimia 100 katika eneo la mradi pamoja na vijiji vilivyoko ndani ya kilometa 12 kutoka bomba kuu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huo utatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Kiarabu kwa Maendeleo ya Afrika (BADEA) na Mfuko wa Maendeleo wa Saudia (Saudi Fund for Development – SFD) kwa gharama ya dola za Marekani milioni 30.69 sawa na takribani shilingi bilioni 70.
MHE. DAVID M. KIHENZILE Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali italeta Mradi wa Kuhifadhi Mazingira Mufindi katika chanzo cha maji cha Mto Ruaha na shamba la miti la Sao Hill?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya kuboresha hali ya upatikanaji wa maji nchini. Chanzo cha maji cha mto Ruaha Mdogo ni miongoni mwa mito inayomwaga maji nchini katika kidakio cha Great Ruaha. Kutokana na umuhimu wa Mto Ruaha Mdogo na kwa lengo la kuhakikisha mto huo unatiririsha maji kwa muda wote, Wizara kupitia Bodi ya Maji ya Bonde la Mto Rufiji tayari imekamilisha kuweka mipaka ya vyanzo vya maji na taratibu za kuvitangaza katika Gazeti la Serikali zinaendelea. Hii ni pamoja na uanzishwaji wa Jumuiya ya Watumia Maji, utunzaji wa vyanzo vya maji, upandaji wa miti rafiki na maji pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi vyanzo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa shamba la miti la Sao Hill lililopo Wilaya ya Mufindi, shamba hili limehifadhiwa na Wakala wa Misitu (TFS) ambapo hakuna shughuli zozote za kibinadamu zinazoendelea.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA Aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka wakaguzi ili kuhakiki thamani ya fedha ya Shilingi bilioni 15 zilizotolewa na Serikali kwa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya mradi wa maji wa Masukulu ambao unaonekana kujengwa chini ya kiwango?
NAIBU WAZIRI MAJI: Mheshimiwa Spika; kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda Mbunge wa Rungwe Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika; ni kweli Serikali kupitia Wizara ya Maji ilitekeleza mradi wa Maji wa Masukulu katika Wilaya ya Rungwe ambao ulitenga kuhudumia vijiji viwili vya Ijigha na Masukulu kwa gharama ya Shilingi milioni 335.6 na si shilingi bilioni 15 kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa Mbunge. Mradi huo ulihusisha ujenzi wa chanzo, tanki lenye ujazo wa lita 90,000 na vituo 13 vya kuchotea maji vimekamilika na vinatoa huduma kwa wananchi wapatao 3,706.

Mheshimiwa Spika; katika kuhakikisha vijiji vya Ijigha na Masukulu vinapata huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza; RUWASA Wilaya ya Rungwe inatumia chanzo cha maji cha Mto Mbaka ambacho kina cha maji kinatoa maji ya uhakika na tayari mradi huo umewekwa kwenye mpango wa bajeti ya RUWASA ya mwaka 2021/2022.
MHE. ALEXANDER P. MNYETI Aliuliza: -

Chanzo cha Maji cha Ihelele kilichopo Kijiji cha Nyanhomango kinasambaza maji katika Mikoa ya Shinyanga na Tabora: -

Je, ni lini Serikali itapeleka miundombinu ya maji kwenye Kijiji hicho pamoja na vijiji vingine vinavyozunguka chanzo hicho?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Nyanhomango kilichopo katika Kata ya Ilujamate, kinapata huduma ya maji katika Skimu yenye chanzo kilichopo katika Ziwa Victoria kwenye bomba la kutoka Mabale kwenda Mbarika. Skimu hiyo inazalisha lita 1,555,200 kwa siku ambapo maji yanayozalishwa yanatosheleza mahitaji ya eneo lote ikiwemo Kijiji cha Nyanhomango. Huduma ya maji inapatikana kwenye vituo 9 vya kuchotea maji na tanki moja lenye ujazo wa lita 135,000.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Isesa katika Kata ya Ilujamate kinapata huduma ya maji kupitia skimu yenye chanzo cha kisima kirefu inayozalisha lita 116,000 kwa siku ukilinganisha na mahitaji ya kijiji hicho ambayo ni lita 91,100 kwa siku. Skimu hiyo ina vituo 12 vya kuchotea maji na tanki moja lenye ujazo wa lita 135,000.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2021/2022, Serikali kupitia RUWASA inatekeleza Mradi mkubwa wa Maji Ilujamate – Buhingo utakaonufaisha vijiji 16 vilivyopo karibu na chanzo cha Ihelele. Vijiji hivyo ni Gukwa, Mbalama, Buhunda, Mwagimagi, Kifune, Gulumungu, Lukanga, Nyambiti, Busongo, Ng’hamve, Nyamayinza, Songiwe, Seeke, Buhingo, Kabale na Mwasagela.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2021. Kazi zitakazofanyika ni ujenzi wa matenki matatu yenye jumla ya ujazo wa lita 850,000, ulazaji wa bomba kuu kilometa 34.4, mabomba ya usambazaji maji kilometa 35 na vituo vya kuchotea maji 25. Kukamilika kwa mradi huo kutaboresha huduma ya maji kutoka asilimia 73 za sasa hadi asilimia 88 mwaka 2023.
MHE. JACKSON G. KISWAGA Aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka fedha kiasi cha shilingi milioni 200 zilizoahidiwa na Waziri wa Maji Mwaka 2017 alipotembelea mradi wa Jumuiya ya Watumiaji Maji wa Magubike Kata ya Nzihi uliokarabatiwa na WARID kwa kiasi cha shilingi bilioni 1.3?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji Kijiji cha Magubike upo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Mradi huo unahudumia vijiji sita vya Kata ya Nzihi ambavyo ni Nzihi, Kipera, Kidamali, Nyamihuu, Magubike na Ilalasimba. Kwa lengo la kuboresha huduma ya maji katika vijiji hivyo na kufikisha huduma ya maji katika vitongoji vingine ambavyo havina huduma ya maji, mwaka 2017 Waziri wa Maji aliahidi kutuma shilingi milioni 200 kwa ajili ya upanuzi wa mradi wa Magubike.

Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza ahadi hiyo, Serikali mwezi Juni na Agosti, 2021 imetuma jumla ya shilingi milioni 180 ambapo kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita tisini elfu katika kijiji cha Nzihi, ulazaji wa bomba umbali wa kilomita 11.25 kwa ajili ya jamii kuingiza maji majumbani. Ujenzi huo unatarajiwa kuanza mwezi Oktoba, 2021 na kukamilika ifikapo mwezi Januari 2022. Kukamilika kwa kazi hizo kutaboresha huduma ya maji katika vijiji husika pamoja na vitongoji vya Mji mwema B, Mbega na Kayungwa ambavyo havina huduma ya uhakika ya maji.
MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-

Je, ni lini ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ya ujenzi wa bwawa la maji katika Kata ya Mikangaula Wilayani Nanyumbu itatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Serikali iliahidi kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Nanyumbu kwa kujenga mabwawa katika Vijiji vya Mikangaula, Mchiga, Maratani, Chilunda na Nangova.

Katika kutekeleza ahadi hiyo, Serikali imeanza ujenzi wa bwawa katika Kijiji cha Maratani ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 95 na utakamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa tuta, spill-way, chemba za kutolea maji na kupokea maji, birika la kunyweshea mifugo na kituo kimoja cha kuchotea maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022, RUWASA Wilaya ya Nanyumbu imepanga kuanza kazi za ujenzi wa mabwawa ya Mikangaula na Chilunda.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza kutumia maji ya Mto Ruvuma kwa ajili ya kujenga miradi mikubwa ya maji ambayo itatatua changamoto za maji katika Jimbo la Nanyamba na maeneo jirani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji kutoka Mto Ruvuma ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati ambapo Serikali inatarajia kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha 2021/2022 kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Spika, aidha, kupitia RUWASA ukarabati na upanuzi wa Mradi wa Maji kwenye Vijiji vya Makongo na Migombani umekamilika na unatoa huduma kwa wananchi. Vilevile, visima viwili vimechimbwa, nyumba ya mtambo wa kusukuma maji, ulazaji wa bomba kuu kilomita 3.5, ujenzi wa tenki moja la ujazo wa lita 100,000 na ujenzi wa matanki mengine manne unaendelea kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji Nanyamba Mjini. Pia utekelezaji wa miradi katika Vijiji vya Ngonja – Chawi, Mayembejuu, Nyundo A na B, Nitekela na Misufini upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
MHE. DEO K. SANGA aliuliza: -

Je, ni lini Mradi wa Kusambaza Maji Mji wa Makambako utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Kasenyenda Sanga, Mbunge wa Makambako, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28. Utekelezaji unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuchukua miezi 24.
MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupima na kuchimba visima virefu Mkoani Arusha hasa Wilaya ya Longido katika Vijiji vya Noondoto, Matale, Wosiwosi na Ngereani ambapo kuna uhaba wa vyanzo vya maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kutokana na Wilaya ya Longido kuwa na uhaba wa vyanzo vya maji hasa chemichemi, Serikali imeendelea na jitihada mbalimbali ikiwemo kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi na kuchimba visima virefu, ambapo katika Kijiji cha Matale B, uchimbaji wa kisima unaendelea kupitia Bajeti ya mwaka 2020/2021 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Juni, 2021.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Noondoto, kinapata huduma ya maji kupitia mradi wa maji wa Kijiji cha Elang’atadabash unaohudumia vijiji vitano vya Elang’atadabash, Sokoni, Olchonyorokie, Noondoto, Losirwa na Naadare. Katika Kijiji cha Wosiwosi kisima kilichochimbwa, maji yake yalibainika kutofaa kwa matumizi ya binadamu kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha madini chumvi ukilinganisha na kiwango kinachokubalika.

Mheshimiwa Spika, hivyo, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali itatumia vyanzo vya Mto Engaresero kutekeleza mradi wa kufikisha maji Kijiji cha Matale na Wosiwosi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 kwa ajili ya kijiji cha Wosiwosi, tumeweka bajeti ya kujenga bwawa litakalosaidia mifugo na wananchi.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Ngereani kinapata huduma ya maji kupitia Mradi wa Maji Tingatinga Ngereani. Serikali itaendelea na jitihada mbalimbali za kuhakikisha wananchi wa Wilaya ya Longido wanapata huduma ya maji safi na salama kwa kutumia vyanzo mbalimbali vitakavyoonekana vinafaa ikiwemo mito, visima na mabwawa.
MHE. NICODEMUS H. MAGANGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Wilayani Mbogwe maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya matumizi ya Wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicodemus Henry Maganga, Mbunge wa Mbogwe, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Mbogwe ni wastani wa asilimia 55. Huduma hiyo ya maji inapatikana kupitia miradi minne ya skimu, visima virefu 26, visima vifupi 460 na matanki 55 ya kuvuna maji ya mvua, vituo vya kuchotea maji 61 na maunganisho ya nyumbani 192.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuboresha huduma za maji, Serikali katika mwaka wa fedha 2020/2021, ilitenga jumla ya shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya upanuzi wa miradi ya maji Lulembela na Nyakafuru, ujenzi wa miradi mipya ya maji Mbogwe, Nanda na Kabanga-Nhomolwa. Hadi sasa jumla ya shilingi bilioni 1.8 zimetolewa, ambapo kazi zilizofanyika ni ujenzi wa nyumba ya pampu ya kusukuma maji, matenki matano, vituo vya kuchotea maji 48 na ulazaji wa bomba lenye urefu wa kilometa 31. Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021 na kuongeza upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kufika asilimia 61 ifikapo mwezi Disemba, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali kupitia Mpango wa Mradi wa Maziwa Makuu kupitia Ziwa Victoria, katika Wilaya ya Mbogwe itatekeleza miradi katika Vijiji vya Kagera, Ilolangulu, Buningozi, Ngemo, Isungabula na Iponya.
MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza kutekeleza mradi wa maji kutoka Mto Mavuji kwa ajili ya wakazi wa Miji Midogo ya Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika Miji 28. Mji Mdogo wa Kilwa Kivinje na Kilwa Masoko ni miongoni mwa Miji itakayonufaika. Utekelezaji unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021 na unatarajiwa kuchukua miezi 24 kukamilika.
MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. ZAINAB A. KATIMBA aliuliza:-

Kijiographia Tanzania ipo kwenye ukanda wenye mvua za kutosha:-

Je, Serikali imejizatiti vipi kuhamasisha zoezi la uvunaji wa maji ya mvua kwa matumizi ya wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zainabu Athman Katimba, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli Nchi yetu ipo kwenye ukanda wa mvua za kutosha, hivyo ujenzi wa miundombinu ya kuvuna maji ya mvua ni muhimu kwa kuwa itawezesha kuwa na maji ya uhakika kwa kipindi chote cha mwaka bila kujali hali ya hewa. Vilevile, miundombinu hiyo ni muhimu kwa kuwa itawezesha kudhibiti mafuriko na pia kuokoa miundombinu, ikiwemo ya kuhudumia maji pamoja na mali na maisha ya wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutimiza azma hiyo mkakati mwingine ni Wizara ya Maji kukutana na TAMISEMI kwa lengo la kuhusisha mashule, kujenga gats za maji na matenki, pia kuhamasisha wananchi wanapojenga nyumba zao waweke miundombinu rafiki ya kukusanya maji, lengo zoezi liwe shirikishi. Aidha, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa ukarabati wa mabwawa kwa kila wilaya, hususan katika wilaya kame.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa Mwaka wa Fedha 2020/21 Wizara imekamilisha ukarabati wa mabwawa ya Mwadila lililoko Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu, usanifu kwa ajili ya kukarabati mabwawa matatu ya Itobo lililoko Wilaya ya Nzega, Ingekument lililoko Wilaya ya Monduli na Horohoro lililoko Wilaya ya Mkinga na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa mawili ya Muko na Chiwanda yaliyoko Wilaya ya Momba.

Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile, usanifu wa Malambo ya kunyweshea mifugo sita, umekamilika katika mwambao wa barabara kuu ya Dodoma Babati, ikihusisha Wilaya ya Bahi malambo mawili na Chemba malambo manne. Vile vile, Serikali inaendelea na mpango wa kujenga mabwawa ya kimkakati ya Kidunda Mto Ruvu, Falkwa katika Mto Bubu na Ndembela Lugoda katika Mto Ndembela.
MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya maji katika Mkoa wa Katavi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Mariki, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Mkoa wa Katavi ni asilimia 70. Serikali kupitia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mpanda inatekeleza miradi miwili ya maji ambayo ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji na imeshaanza kutoa huduma ya maji. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa banio, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 24 kutoka katika chanzo cha maji Ikolongo II na ujenzi wa tenki la lita milioni moja kwa ujumla wa mradi, unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa Manispaa ya Mpanda ambapo mji huo ni miongoni mwa miji 28 itakayonufanika na utekelezaji wa mradi wa maji kupitia fedha za mkopo kutoka Serikali ya India. Kazi hii inatarajiwa kuanza hivi karibuni na itachukua miezi 24. Aidha kupitia RUWASA utekelezaji wa miradi 30 unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2021. Miradi hii, ikikamilika jumla ya vijiji 138 vya Mkoa wa Katavi vitakuwa na huduma ya maji ya uhakika, hivyo kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kazi za maendeleo.
MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. ZAKARIA P. ISSAAY aliuliza:-

Je, ni lini Wakala wa Maji Vijijini atachimba visima sita katika Vijiji vya Aicho, Gidamba, 7 Gunyoda, Silaloda, Boboa na Titiwi katika Jimbo la Mbulu Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zakaria Paulo Issaay, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kazi ya kuchimba visima kwa ajili ya kutumika kama vyanzo vya maji inafanyika maeneo mengi hapa nchini hivyo ili kuepuka ucheleweshaji inabidi kushirikisha makampuni binafsi kuchimba visima baada ya Wataalam wa Mabonde kufanya utafiti na kuainisha maeneo yenye maji chini ya ardhi. Hivyo, kazi hii zabuni imetangazwa kupitia Bodi ya Zabuni ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mkoa - Babati (BAWASA) ambapo Visima virefu vitatu katika vijiji vya Aicho, Boboa na Titiwi vitachimbwa kuanzia mwezi Mei, 2021 na kukamilika mwezi Juni, 2021.

Mheshimiwa Spika, visima vilivyobaki katika vijiji vya Gidamba, Silaloda na Gunyoda vitachimbwa katika mwaka wa fedha 2021/22.
MHE. SHAMSIA A. MTAMBA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Mto Ruvuma kwa Wananchi wa Mtwara ili kuondoa shida ya maji iliyodumu kwa muda mrefu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shamsia Azizi Mtamba, Mbunge wa Mtwara Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maji kutoka Mto Ruvuma ni miongoni mwa miradi mikubwa ya kimkakati ambapo Serikali inatarajia kuanza utekelezaji wake katika mwaka wa fedha 2021/2022 kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika kuhakikisha wananchi wa Mtwara wanaendelea kupata huduma ya majisafi na salama, wakati ukisubiriwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kutoa maji Mto Ruvuma, Serikali imeendelea kutekeleza kazi mbalimbali za kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa Mtwara Mjini ikiwemo uchimbaji wa visima vinne, ufungaji wa pampu tatu, ujenzi wa matanki matatu, ulazaji wa bomba kuu kilomita saba na bomba la usambazaji maji kilometa 27.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa vijijini, Serikali kupitia RUWASA inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji 81. Miradi hii itakapokamilika itahudumia vijiji 285 ambapo jumla ya vituo vya kuchotea maji 1,562 vitajengwa/ kuboreshwa na inakadiriwa kunufaisha wananchi zaidi ya 454,375, hivyo, kuboresha utoaji wa huduma ya maji na kufikia wastani wa asilimia 79.91 kutoka asilimia 64 za sasa.
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapeleka maji katika Kijiji cha Matandarani Kata ya Sitalike?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Jimbo la Nsimbo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza mradi wa maji wa Magula ambao unahusisha ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa kilomita 14.9, ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 200,000 na nyumba ya mtambo wa kusukuma maji. Ujenzi wa mradi umeanza mwezi Machi, 2021 na unatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2021 kwa gharama ya shilingi milioni 545.62. Mradi huo utanufaisha jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Mtisi (Magula), Matandarani na Ibindi.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha Mradi wa Maji wa Kintinku – Lisilile ili wananchi wa vijiji 11 vya Kata za Chikuyu, Makutupora, Maweni na Kintinku waanze kupata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Kintinku- Lusilile ni mradi mkubwa ambao unatekelezwa kwa awamu nne na hadi mwezi Machi, 2021 utekelezaji wa awamu ya kwanza umefikia asilimia 90 kwa gharama ya shilingi bilioni 2.085. Kazi zilizofanyika ni pamoja na ufungaji wa mitambo ya kusukuma maji, ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji, tanki la kukusanya maji la lita 300,000 na ujenzi wa tanki la kuhifadhi na kusambaza maji la lita milioni mbili na ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilometa 1.2. Aidha, vijiji vitatu vya Chikuyu, Mwiboo na Mbwasa vinatarajiwa kuanza kupata huduma ya maji mwezi Juni, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia RUWASA imepanga kukamilisha usambazaji wa maji katika vijiji vyote 11 katika mwaka wa fedha 2021/22 na utahudumia wakazi zaidi ya 55,000.
MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza:-

Jimbo la Namtumbo lina tatizo la maji karibu maeneo yote ya Vijijini pamoja na Makao Makuu ya Wilaya: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua tatizo hili katika bajeti ya mwaka 2020/2021?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa Mbunge wa Namtumbo kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji vijijini Wilayani Namtumbo ni asilimia 69. Katika kutatua tatizo la maji Jimbo la Namtumbo, Serikali Katika mwaka wa fedha 2020/2021 kupitia RUWASA imekamilisha miradi miwili, ambayo ni mradi wa maji Mkongogulioni - Nahimba na mradi wa maji Mtakuja. Miradi hiyo itahudumia jumla ya wananchi 9,683 katika vijiji vya Mkongogulioni, Nahimba na Mtakuja. Utekelezaji wa miradi ya maji ya Likuyusekamaganga, Njoomlole, Ligunga, Lusewa na Kanjele unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2021 na miradi ya Litola – Kumbura, Luhimbalilo – Naikesi, inatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Mji wa Namtumbo Serikali inaendelea na mipango ya muda mfupi na muda mrefu. Kwa muda mfupi utekelezaji wa mradi wa uboreshaji, ambapo bomba kuu na mabomba kwa ajili ya usambazaji yamelazwa umbali wa kilometa 31.92 na umegharimu Shilingi milioni 653.2. Pia, kazi ya kuunga wateja 1500 katika urefu wa bomba kilometa 24 inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, kupitia mpango wa muda mrefu, Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa kwa ajili ya maji kutoka vyanzo vya maji vya Likiwigi na Libula vyenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya Lita Milioni Nne kwa siku. Usanifu wa mradi umekamilika na ujenzi unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2021/2022.
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Maji wa Ziwa Victoria utapelekwa katika Mkoa wa Simiyu hususani katika Wilaya ya Meatu kama inavyoelekezwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la KfW la Serikali ya Ujerumani imekamilisha taratibu za kupatikana kwa wataalam washauri ambao watasimamia utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoa wa Simiyu. Mradi huu unahusisha ujenzi wa bomba kuu kilometa 195, matenki nane yenye ujazo wa lita milioni 11.9 na mabomba ya usambazaji kilometa 49.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa mradi unatarajia kuanza mwezi Agosti, 2021 na miji mikuu ya Wilaya itakayonufaika ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa, Meatu na vijiji vya vilivyoko pembezoni mwa bomba kuu umbali wa kilometa 12 kila upande. Mradi umepangwa kutekelezwa kwa miaka minne. (Makofi)
MHE. ALEXANDER P. MNYETI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji kwenye Mji wa Usagara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani Misungwi ni asilimia 73. Katika juhudi za kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa maeneo hayo, katika mwaka 2021/2022, Serikali kupitia Programu ya Lake Victoria Water and Sanitation imepanga kutekeleza mradi wa maji katika maeneo ya Usagara, Buswelu, Kisesa na Buhongwa. Mradi huu utahusisha ujenzi wa vituo vya kusukuma maji viwili, mifumo ya usafirishaji na usambazaji maji yatakayozalishwa na Chanzo kipya cha Maji Butimba, ulazaji wa mabomba makubwa yenye ukubwa wa kuanzia milimita 50 hadi 600 kwa umbali wa kilomita 50, ujenzi wa matanki manne ya ukubwa mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huo utanufaisha maeneo yote ya Mji wa Usagara ikiwemo Usagara, Fela, Nyang’homango, Idetemya, Ukiliguru, Ntende, Sanjo, Isamilo, Mayolwa, Bukumbi na Kigongo.
MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza.

Je, ni lini mradi wa maji wa kutoka Nyamtukuza, Kakora, Kharumwa, Izunya, Kayenze hadi Bukwimba utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu.

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nassor Amar Hussein, Mbunge wa Nyangh’wale, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi wa Maji wa Nyamtukuza uliopo Wilaya ya Nyang’hwale unalenga kuhudumia Vijiji 12 vya Nyamtukuza, Kakora, Bugombela, Nyarubele, Kitongo, Ikatangala, Kharumwa, Busengwa, Izunya, Kayenze, Bukwimba na Igeka. Hadi mwezi Machi, 2021, vijiji vinane (8) vimepata maji. Vijiji vilivyopata maji ni Nyamtukuza, Kakora, Kitongo, Ikatangala, Kharumwa, Busengwa, Nyarubele na Bugombela vimeanza kupata huduma ya maji.

Mheshimiwa Spika, mradi umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2021 na vijiji vyote 12 vitapata huduma ya maji ambapo wananchi wapatao 51,500 watanufaika. (Makofi)
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya ujenzi wa mradi mkubwa wa maji Handeni Trunk Main (HTM)?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Kwagilwa kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali ilipata mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim, jumla ya Dola za Marekani milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 nchini ukiwemo Mradi wa Maji wa Kitaifa Handeni (Handeni Trunk Main) utakaohudumia vijiji 84 katika Wilaya ya Handeni pamoja na Miji Midogo ya Mkata, Komkonga, Kabuku, Michungwani,Segera pamoja na Mji wa Handeni.

Mheshimiwa Spika, taratibu za kupatikana kwa wakandarasi watakaotekeleza mradi huu zimekamilika na unatarajiwa kuanza wakati wowote katika mwaka wa fedha 2020/2021 na ujenzi wa mradi umepangwa kutekelezwa miezi 24.
MHE. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Katerela kwa ajili ya Kata za Kasharunga na Rulanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Ahsante. kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini Kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jitihada za kuhakikisha wananchi Wilayani Muleba wanapata huduma ya maji, katika mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imekamilisha miradi ya maji ya Bulembo, Kasharunga, Ruteme, Ilogero na Kyota. Pia, utekelezaji wa miradi ya Nshamba, Kishamba na Kashansha unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia RUWASA katika mwaka wa fedha 2021/2022 imepanga kuanza ujenzi wa mradi wa maji kutoka chanzo cha maji Katerela utakaowanufaisha wakazi wapatao 19,619 katika Kata za Kasharunga na Rulanda. Mradi huu unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi million 700 ambapo utahusisha ujenzi wa chanzo cha maji, ujenzi wa matanki mawili ya maji ukubwa wa lita 200,000 na lita 300,000, ujenzi wa nyumba ya mtambo, vituo vya kuchotea maji 25 na ujenzi wa mtambo wa bomba za maji umbali wa mita 40,130.
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuwasaidia Wananchi wa Mji wa Itigi kuweza kuvuna maji katika Mbuga inayozunguka Mji huo?
NAIBU WAZIRI MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Itigi ni miongoni mwa miji miwili iliyopo katika Wilaya ya Manyoni. Mji huu unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 32,000. Serikali imeendelea kutekeleza ahadi iliyoitoa kwa kuwasaidia wananchi wa maeneo yanayozunguka Mji wa Itigi kuweza kuvuna maji ambapo imekamilisha utambuzi wa awali wa maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa katika Mji wa Itigi na katika Kijiji cha Kayui, Kata ya Magandu, Kijiji cha Muhanga, Kata ya Ipande pamoja na Kjiji cha Kaskazi, Kata Kitaraka ambayo yameonekana yanafaa kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa. Katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Serikali itakamilisha usanifu wa kina na kuainisha ukubwa wa mabwawa yatakayojengwa kuanzia mwezi Januari, 2022.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mwaka wa 2020/2021 katika kuimarisha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji wa Itigi Serikali imekamilisha ujenzi wa mradi wa maji mkubwa unaohudumia vijiji sita vya Songambele, Mlowa, Majengo, Tambukareli, Zinginali na Itigi. Mradi huu umekamilika mwezi Disemba, 2020 na kugharimu shilingi bilioni
2.64. Mradi umewezesha upatikanaji wa maji katika Mji wa Itigi kufikia asilimia 80.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kiburubutu katika Jimbo la Kilombero?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Kilombero, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilipata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya dola za Marekani millioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 nchini ukiwemo Mji wa Ifakara ambao utapata maji kupitia chanzo cha Lumemo. Mradi utahudumia jumla ya Kata tisa na vijiji tisa.

Mheshimiwa Naibu Spika, taratibu za kupatikana kwa wakandarasi watakaotekeleza mradi huu zimeshakamilika na unatarajiwa kuanza wakati wowote katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 na ujenzi wa mradi umepangwa kutekelezwa kwa miezi 24.
MHE. AIDA J. KHENANI atauliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza changamoto ya maji katika Wilaya ya Nkasi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenan, Mbunge wa Nkasi Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika; hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Nkasi ni wastani wa asilimia 48. Katika kutatua changamoto ya huduma ya maji, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Wilaya ya Nkasi imeendelea na ujenzi wa jumla ya miradi 12 ambayo ni Kirando, Kabwe, Kisula, Isale, Mpasa, Matala, Kantawa, Sintali, Chonga, Kate, Mtambila na Katongolo ambapo itakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, mradi wa uchimbaji wa visima virefu sita umekamilika katika vijiji vya Ntumbila, Kachehe, Itindi, Lyazumbi, Nkomo II na Milundikwa. Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji utafanyika katika mwaka wa fedha 2021/2022 ambapo utahusisha matanki matatu ya maji yenye ukubwa wa lita 90,000 na lita 45,000 na vituo vya kuchotea maji 23.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa upande wa Mji wa Namanyere, Serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma ya maji kwa kutumia chanzo cha maji cha bwawa la Mfili ambapo kazi mbalimbali zitafanyika ikiwemo ufungaji wa pampu mbili katika bwawa la Mfili, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 3.9, ulazaji wa mabomba na ujenzi wa tanki la lita 500,000 la kuhifadhi maji. Kazi hizo mradi zinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Julai, 2021.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza:-

(a) Je, ni lini Serikali itaimarisha na kuboresha miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Maji Makonde ili Wananchi waweze kupata maji ya uhakika?

(b) Je, Serikali inachukua hatua gani za dharura kuboresha upatikanaji wa maji Newala Vijijini ambapo kwa sasa uzalishaji ni ujazo wa lita 6,700 tu kwa siku badala ya lita 23,741?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya maji ya Mamlaka ya Maji Makonde inayohudumiwa Wilaya za Newala, Tandahimba na Nanyamba.

Katika kutatua changamoto hiyo, Serikali imeendelea na ukarabati wa miundombinu ambapo katika mwaka huu wa fedha 2020/2021 kazi zinazofanyika ni kukarabati mitambo na mfumo wa umeme katika vituo vya kuzalishia na kusukuma maji. Utekelezaji wa kazi hizi unalenga kuongeza uzalishaji wa maji kutoka meta za ujazo 6,700 kwa siku hadi meta za ujazo 11,116 kwa siku, kazi inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kupata suluhisho la kudumu la tatizo la maji katika maeneo hayo, Serikali kuanzia mwaka 2021/2022 imepanga kutekeleza kazi mbalimbali ikiwemo kuongeza idadi ya visima vya kuzalisha maji kutoka 6 hadi 12 kwenye Bonde la Mitema pamoja na kupanua miundombinu ya kusafirisha maji uchimbaji wa visima utaongeza uzalishaji wa maji kutoka meta za ujazo 11,116 hadi Meta za ujazo 23,741 kwa siku. Kukamilika kwa kazi hizo kutaboresha upatikanaji wa huduma ya maji kutoka asilimia 58 za sasa hadi asilimia 95.

Vilevile Wizara ya maji kupitia RUWASA katika mwaka wa fedha 2020/2021, imeendelea na utekelezaji wa miradi ya maji Mchemo na Chiule iliyotarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2021 na miradi ya maji Mtongwele, Miyuyu na Mnima inayotarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2021. Katika mwaka 2021/2022, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni
1.95 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika Wilaya Newala Vijijini.

Mheshimiwa Naibu Spika, Katika mpango wa muda mrefu, Serikali ilipata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya dola za Marekani Milioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa Miji 28 ukiwemo mradi wa Makonde; ambapo maeneo yatakayonufaika ni vijiji 155 vya Wilaya ya Newala. Ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote katika mwaka wa fedha 2020/2021.
MHE. KUNTI Y. MAJALA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua changamoto kubwa ya maji inayowakabili wananchi wa Mji wa Chemba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kunti Yussuf Majala, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya huduma ya maji inayowakabili wananchi wa Mji wa Chemba ambapo kwa sasa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ni chini ya asilimia 50. Katika kutatua changamoto ya huduma ya maji katika mji huo, Serikali ina mpango wa muda mfupi na mpango wa muda mrefu.

Mheshimiwa Naibu Spika katika mpango wa muda mfupi, kazi zilizopangwa kwa ajili ya kuboresha huduma ya maji katika mji huo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ni pamoja na ujenzi wa matanki mawili ya kukusanya maji ya ukubwa wa lita 50,000, nyumba ya mitambo ya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu nne (4), ununuzi na ulazaji wa mabomba ya umbali wa kilometa 11.6. Kukamilika kwa kazi hizo kutaongeza uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita 50,000 kwa siku hadi lita 320,000 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, kwa mpango wa muda mrefu, Serikali ilipata mkopo kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim India jumla ya Dola za Marekani millioni 500 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika miji 28 nchini ukiwemo Mji wa Chemba. Maeneo yatakayonufaika katika utekelezaji wa Mradi huo ni pamoja na Paranga, Makamala, Kambi ya Nyasa, Gwandi, Chambalo na Chemba yenyewe. Ujenzi unatarajiwa kuanza wakati wowote katika mwaka huu wa fedha 2020/2021 na umepangwa kutekelezwa kwa miezi 24.
MHE. KENETH E. NOLLO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga mabwawa makubwa ambayo yatahifadhi maji ya mvua ili yaweze kutumika kwa shughuli za kibinadamu, kilimo na mifugo katika Mkoa wa Dodoma ambao umekuwa haupati mvua za kutosha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Keneth Ernest Nollo, Mbunge wa Jimbo la Bahi, kama ifuatavyo:-

Mheshmiwa Naibu Spika, katika jitihada za kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa Dodoma, katika mwaka 2020/2021, Serikali imekamilisha usanifu kwa ajili ya kukarabati Bwawa la Chikopelo lililopo umbali wa kilomita 70 kutoka Bahi Mjini ili kuongeza upatikanaji wa maji katika vijiji sita ikiwemo Mji wa Bahi na usanifu kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Kidoka litakalohudumia vijiji saba ikiwemo Mji wa Chemba.

Mheshimiwa Naibu Spika, ukarabati na ujenzi wa mabwawa hayo unatarajiwa kufanyika katika mwaka 2021/ 2022, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa malambo sita katika Vijiji vya Mpamwata, Uwekela, Kambia, Nyasa, Kolema Kuu, Kidoka na Palanga katika Wilaya za Bahi na Chemba.

Mheshmiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali ina mpango wa kujenga bwawa la kimkakati katika Kata ya Farkwa ambapo mpaka sasa usanifu umekamilika na ulipaji wa fidia kwa wananchi wanaotakiwa kupisha eneo la mradi wa ujenzi wa bwawa hilo umefanyika kwa asilimia 99. Bwawa hilo lenye mita za ujazo milioni 470 linatarajiwa kujengwa kwa awamu kutegemea na upatikanaji wa fedha.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Dodoma, Serikali imechimba visima visima nane na kukarabati visima vitatu vya zamani. Kazi ya ufungaji wa miundombinu inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2021.
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:-

Mheshimiwa Naibu Spika, je, ni lini Serikali itaanza mkakati wa kusambaza maji kutoka Mto Dibuluma kata ya Kibati Wilaya ya Mvomero na kuyasambaza katika kata ya Tunguli, Kwekivu, Masagalu na Songe Wilayani Kilindi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa niaba wa Waziri wa Maji naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ina mpango wa muda mrefu wa kutekeleza mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha mto Diburuma kwa lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi. Hatua iliyofikiwa ni kufanyika kwa utafiti wa ubora na uwingi wa maji katika chanzo hicho ili kujiridhisha na kiwango cha maji kwa ajili ya kunufaisha vijiji vilivyopo kwenye kata nne (4) za Tunguli, Kwekivu, Masagalu na Songe. Utafiti huo utakamilika kabla ya mwezi Juni, 2021 na takwimu zitakazopatikana zitatumika kufanya usanifu wa kina kwa mradi huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa kata za Tunguli, Kwekivu, Masagalu na Songe zinapata huduma ya maji safi na salama kupitia visima virefu vitano (5) na visima vifupi kumi na tano kwa lengo la kuendelea kuboresha huduma ya maji katika kata hizo na Halmashauri ya Kilindi kwa ujumla, na mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 2.14 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji.
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kusambaza Maji kutoka katika mradi wa Maji Kata za
Miangalua na Mnokola katika Jimbo la Kwela?

(b) Je, ni lini Serikali itapeleka Pesa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi katika maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa maji katika Kata za Miangalua na Mnokola ni asilimia 51.2. Kata hizi ya Miangalua inapata huduma ya majisafi kupitia mradi wa Maji wa Skimu ya Miangalua ya visima virefu vinavyohudumia vijiji vya Miangalua, Tunko, Movu, Kavifuti na Nampako vya Kata hiyo na kijiji cha Mnokola kilichopo katika Kata ya Mnokola.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha hali ya upatikanaji wa maji Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga inazidi kuimarika, Serikali imeendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji ambapo kwa mwaka wa fedha 2020/ 2021 jumla ya miradi mitano ya maji imetekelezwa na kukamilika katika Vijiji vya Nankanga na Sakalilo (Kata ya Ilemba), Milepa na Kisa (Kata ya Milepa), Kizungu (Kata ya Muze) na miradi minne ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji katika Kata za Mtowisa, Ikozi, Msandamuungano na Mufinga.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/ 2022, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.76 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 18 ya maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga. Aidha, Serikali itatoa fedha kwa kuzingatia miongozo ya kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi itakayopangwa katika bajeti husika.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza:-

Je, ni lini Mradi mkubwa wa Maji wa Kabwe katika Wilaya ya Nkasi utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakangata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Kabwe una miundombinu yote kwa ajili ya kutoa huduma ya maji. Miundombinu hiyo ni matanki matatu yenye ujazo wa lita 50,000, lita 10,000 na lita 135,000, vituo vya kuchotea maji 29, nyumba ya pampu ya kusukuma maji na mabomba ya kilometa 10.9. Changamoto iliyojitokeza kwenye mradi huu ni uwezo wa nishati ya umemejua kushindwa kusukuma maji ipasavyo kwenda kwenye matanki hayo, hivyo, kusababisha huduma ya maji kusimama kwa wananchi hususan kipindi cha usiku.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha huduma ya maji kwa wananchi wa Kabwe inapatikana muda wote, Serikali imeamua kubadili mfumo wa umemejua kwa kufunga umeme toka kwenye gridi kupitia REA na kazi hiyo inatarajiwa kukamilika kabla ya mwishoni mwa mwezi Juni, 2021.
MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza upatikanaji wa maji katika Mji wa Ruanda Wilayani Mbinga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Liuka Kapinga Benaya, Mbunge wa Mbinga Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Ruanda unakua kwa kasi hivyo kuongezeka kwa mahitaji ya maji kufikia wastani wa ujazo wa lita 210,100 kwa siku ikilinganishwa na uzalishaji wa sasa wa ujazo wa lita 162,000 kwa siku. Serikali katika mwaka 2021/2022 imepanga kukarabati Mradi wa Maji Ruanda ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na kujenga vituo 15 vya kuchotea maji, kujenga chemba moja ya kugawa kwenda kwenye njia kuu, kufanya ukarabati wa chanzo, kulaza bomba njia kuu na njia ya usambazaji umbali wa kilometa 22.9 pamoja na ukarabati wa matanki mawili ya kuhifadhia maji ya ujazo wa lita 50,000 na 75,000.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 1.39 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji Wilayani Mbinga ukiwemo ukarabati wa Mradi wa Ruanda kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa maji katika Mji wa Ruanda.
MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:-

Je, ni lini Mradi mkubwa wa Maji wa Ziwa Victoria kutoka Busega mpaka Itilima kupitia Bariadi utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Simon Songwe Lusengekile, Mbunge wa Busega, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la KFW la Serikali ya Ujerumani imekamilisha taratibu za kupatikana kwa wataalam washauri ambao watasimamia utekelezaji wa mradi huu mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoa wa Simiyu. Mradi huu unahusisha ujenzi wa bomba kuu kilomita 195, matenki 8 yenye ujazo wa lita milioni 11.9 na mabomba ya usambazaji kilomita 49.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa mradi unatarajia kuanza mwezi Agosti 2021 na miji mikuu ya Wilaya itakayonufaika ni Busega, Bariadi, Itilima, Maswa, Meatu na vijiji vilivyoko pembezoni mwa bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande. Mradi umepangwa kutekelezwa kwa miaka minne.
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo la Sumve?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Sumve kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, huduma ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kwimba kwa kutegemea visima virefu ni asilimia 72 ambapo Vijiji vya Mwabaratulu, Nyashana na Sumve Mantare, Ishingisha, Mwabilanda, Nyambiti, Isunga, Kadashi na Malya vinapata huduma ya maji kutoka kwenye vituo 122 vya kuchotea maji na wateja wa majumbani ni 1,208.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali itakamilisha usanifu wa kina wa mradi wa maji kwa ajili ya kuhudumia Miji Midogo ya Malampaka, Malya na Sumve na vijiji katika maeneo hayo ambavyo huduma ya maji haitoshelezi. Usanifu huu unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba, 2021 na utekelezaji wa mradi utaanza kutegemeana na upatikanaji wa fedha.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-

(a) Je, ni kwa nini miradi ya maji katika Mji wa Kakonko kwa muda mrefu haijakamilika?

(b) Je, ni lini Mji wa Kakonko na vitongoji vyake vitapata maji safi na salama ya kutosha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Buyungu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hadi Desemba, 2020 miradi 15 ilikuwa inatekelezwa katika Wilaya ya Kakonko ambapo miradi 14 imekamilika na inatoa huduma ya maji kwa wananchi, mradi mmoja uliobaki ni mradi wa Kakonko ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 65 na unatarajiwa kuhudumia Mji wa Kakonko pamoja na kijiji cha Kasuga.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji wa Kakonko unatekelezwa na RUWASA kwa kutumia Wataalam wake wa ndani kwa ajili ya kuukamilisha. Utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ambayo inahusisha ulazaji wa bomba kilometa 35 na ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 500 kila moja utakamilika mwezi Desemba mwaka 2021 na kunufaisha Mji wa Kakonko pamoja na vijiji jirani vya Kasuga, Mbizi, Kanyonza pamoja na Kata ya Kiziguzigu yenye Vijiji vya Kiziguzigu, Kibingo, Kiyobera na Ruyenzi.

Mheshimiwa Spika, awamu ya pili itahusu kufanya upanuzi kwa kulaza mabomba urefu wa kilometa 78 kuelekea vijiji vya Njoomlole, Muganza, Kihomoka na Nyakayenzi ambapo itakamilika mwezi Juni, mwaka 2022.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali pia imepanga kujenga miradi mipya katika Vijiji vya Chilambo na Kinonko, ukarabati na utanuzi wa mradi wa Muhange kwenda Muhange Juu na Shule ya Sekondari Ndalichako pamoja na kuchimba visima virefu viwili katika Vijiji vya Chilambo na Nyakiyobe.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:-

(i) Je, ni lini ujenzi wa mradi wa katika Kata za Izimbya, Kyaitoke, Ruhunga, Mugajwale, Katoro na Kaibanja utaanza na kukamilika?

(ii) Je, ni lini mradi wa maji wa Kata za Kemondo, Katerero na Bujugo utaanza na kukamilika?

(iii) Je, ni lini mradi wa maji wa Kata za Karabagaine, Maruku na Kanyangereko utaanza na kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kuanza utekelezaji wa miradi ya maji ambayo itahudumia Kata za Izimbya, Kyaitoke, Ruhunga, Mugajwale, Katoro na Kaibanja katika mwaka wa fedha 2021/2022 na muda wa utekelezaji ni miezi 12 na mradi utakamilika mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Kemondo – Maruku umeanza kutekelezwa ambapo kwa sasa upo katika awamu ya kwanza iliyoanza mwezi Januari, 2021. Utekelezaji wa mradi huu utatumia miezi 18 hivyo utakamilika mwezi Julai, 2022. Kupitia mradi wa Maji Kemondo – Maruku; Kata za Kemondo, Katerero, Bujugo, Maruku, Kanyangereko na Karabagaine zitanufaika.
MHE. KASALALI E. MAGENI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Jimbo la Sumve?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kasalali Emmanuel Mageni, Mbunge wa Sumve kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, huduma ya upatikanaji wa maji katika Wilaya ya Kwimba kwa kutegemea visima virefu ni asilimia 72 ambapo Vijiji vya Mwabaratulu, Nyashana na Sumve Mantare, Ishingisha, Mwabilanda, Nyambiti, Isunga, Kadashi na Malya vinapata huduma ya maji kutoka kwenye vituo 122 vya kuchotea maji na wateja wa majumbani ni 1,208.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali itakamilisha usanifu wa kina wa mradi wa maji kwa ajili ya kuhudumia Miji Midogo ya Malampaka, Malya na Sumve na vijiji katika maeneo hayo ambavyo huduma ya maji haitoshelezi. Usanifu huu unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Desemba, 2021 na utekelezaji wa mradi utaanza kutegemeana na upatikanaji wa fedha.
MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-

(a) Je, ni kwa nini miradi ya maji katika Mji wa Kakonko kwa muda mrefu haijakamilika?

(b) Je, ni lini Mji wa Kakonko na vitongoji vyake vitapata maji safi na salama ya kutosha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Buyungu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, hadi Desemba, 2020 miradi 15 ilikuwa inatekelezwa katika Wilaya ya Kakonko ambapo miradi 14 imekamilika na inatoa huduma ya maji kwa wananchi, mradi mmoja uliobaki ni mradi wa Kakonko ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 65 na unatarajiwa kuhudumia Mji wa Kakonko pamoja na kijiji cha Kasuga.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji wa Kakonko unatekelezwa na RUWASA kwa kutumia Wataalam wake wa ndani kwa ajili ya kuukamilisha. Utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ambayo inahusisha ulazaji wa bomba kilometa 35 na ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 500 kila moja utakamilika mwezi Desemba mwaka 2021 na kunufaisha Mji wa Kakonko pamoja na vijiji jirani vya Kasuga, Mbizi, Kanyonza pamoja na Kata ya Kiziguzigu yenye Vijiji vya Kiziguzigu, Kibingo, Kiyobera na Ruyenzi.

Mheshimiwa Spika, awamu ya pili itahusu kufanya upanuzi kwa kulaza mabomba urefu wa kilometa 78 kuelekea vijiji vya Njoomlole, Muganza, Kihomoka na Nyakayenzi ambapo itakamilika mwezi Juni, mwaka 2022.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali pia imepanga kujenga miradi mipya katika Vijiji vya Chilambo na Kinonko, ukarabati na utanuzi wa mradi wa Muhange kwenda Muhange Juu na Shule ya Sekondari Ndalichako pamoja na kuchimba visima virefu viwili katika Vijiji vya Chilambo na Nyakiyobe.
MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:-

Jimbo la Kibaha Mjini bado lina changamoto kubwa ya maji katika maeneo ya Kata za Mbwawa na Pangani; na Mradi wa Ujenzi wa matanki ya maji unakwenda kwa kusuasua. Je, ni lini Mradi huo utakamilika ili Wananchi wa Kibaha Mjini waondokane na adha ya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/21, Serikali imekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji ambao ulihusisha ulazaji wa bomba kuu pamoja na mabomba kwa ajili ya kutawanya maji kwa wananchi yenye urefu wa kilomita 27. Wananchi wapatao 6,500 wa Kata ya Mbwawa wananufaika na huduma ya maji tangu mwezi Aprili, 2021. Kwa upande wa Kata ya Pangani usanifu kwa ajili ya ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lita millioni 6 umekamilika.

Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2021/2022, jitihada za kuboresha huduma ya maji katika maeneo ya Kibaha Mjini zinaendelea na kazi ya ujenzi wa tenki kubwa utaanza na ulazaji wa bomba kuu urefu wa kilomita tano utaanza katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/ 2022. Mradi huu utanufaisha wananchi wa Kata ya Pangani, pamoja na eneo la Viwanda la Kibaha Mjini (TAMCO).
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itavipatia huduma ya maji safi na salama Vijiji vya Kinyamwenda, Igauri, Matumbo, Itamka na Msimihi katika Jimbo la Singida Kaskazini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abeid Ighondo Ramadhan, Mbunge wa Singida Kaskazini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/21 imekamilisha miradi ya maji katika vijiji 7 ambavyo ni Mughamo, Mgori, Ngimu, Sefunga, Ghalunyangu, Kijota na Malolo hivyo, huduma ya upatikanaji wa maji kufikia asilimia 66.4 katika Wilaya ya Singida Vijijini.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 utafanyika utafiti wa kina kwa ajili ya kuainisha maeneo yenye maji ya kutosha chini ya ardhi. Hivyo vijiji vya Kinyamwenda, Igauri, Itamka na Msimihi vitapata maji baada ya kukamilisha uchimbaji wa visima na ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji.

Aidha, kijiji cha Matumbo kitapata huduma ya maji ya uhakika baada ya ukarabati wa mradi wa maji kukamilika mwezi Julai, 2021.
MHE. JOSEPH K. MUSUKUMA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Mradi wa Maji ambao ulishafanyiwa upembuzi yakinifu kwa Wananchi wa Vijiji vya Nkome, Mchangani, Katome, Nyamboge, Nzera na Rwezera?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Kasheku Musukuma, Mbunge wa Geita Vijiji, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wa maji ambao utahudumia Vijiji vya Nkome, Mchangani, Katome, Nyamboge, Nzera na Rwezera utaanza katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022. Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 mradi huo umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuanza kazi ambazo itahusisha ujenzi wa chanzo cha maji na kituo cha kusukuma maji kwa maana ya booster; ulazaji wa bomba zaidi ya kilometa 70, ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji pamoja na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji. Aidha, mradi huo umepangwa kunufaisha Vijiji vingine vya Mnyala, Ihumilo, Nyambaya, Nyakazeze, Itale, Njingami, Lukaya, Chelameno, Bugando, Igate, Bweya, Idosero na Nyarubanga.
MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza mradi wa kuyatoa maji toka Ziwa Tanganyika na kuyapeleka katika Manispaa ya Mpanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sebastian Simon Kapufi, Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Mpanda ni miongoni mwa miji itakayonufaika na mradi wa miji 28 kupitia mkopo wa Dola za Kimarekani milioni 500 kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim ambapo utekelezaji wa mradi huu kwa Mji wa Mpanda utahusisha matumizi ya chanzo cha maji cha bwawa la Milala lililopo katika Manispaa ya Mpanda kwa kujenga chujio na miundombinu mingine. Mradi huu unatarajiwa kuanza mwaka huu.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mpango wa muda mrefu, Serikali ina mpango wa kutumia Ziwa Tanganyika ili kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Mpanda na maeneo mengine ambayo itakuwa rahisi kutumia ziwa hilo.
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:-

Je, Serikali imefikia hatua gani katika mradi wa kutoa maji kutoka Nzega Mjini, tenki la Ushirika hadi Bukene ambapo vijiji 20 na vitongoji zaidi ya 100 vitanufaika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2020/2021 Serikali imekamilisha kazi ya usanifu wa mradi wa kutoa maji katika tenki la Ushirika Mjini Nzega kwa ajili ya kuhudumia watu zaidi ya 79,485 katika vijiji 20 na vitongoji vyake. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha fedha shilingi bilioni mbili kimetengwa na utekelezaji wa mradi huu utaanza, ambapo utahusisha kulaza mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilometa 176, kujenga matenki matano ya kuhifadhi maji ya ujazo wa lita 100,000, lita 150,000, lita 250,000 na lita 300,000 na kujenga vituo vya kuchotea maji 83.
MHE. ALEXANDER P. MNYETI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itamaliza changamoto ya Maji katika Kituo cha Utafiti na Chuo cha Kilimo Ukirigulu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti, Mbunge wa Misungwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Utafiti na Chuo cha Kilimo Ukirigulu kilikuwa na Skimu ya Maji iliyojengwa mwaka 1965. Chanzo cha maji cha skimu hiyo ni Ziwa Victoria na ina matenki mawili ya maji. Moja lipo Kijiji cha Mwalogwabagole na lingine liko eneo la chuo hicho. Skimu hiyo ina vituo vya kuchotea maji 15.

Mheshimiwa Naibu Spika, usanifu wa mradi kwa ajili ya ukarabati wa skimu hiyo umekamilika na katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imetenga shilingi 630,733,364 ili kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji na kutahusisha ulazaji wa mabomba mapya kilometa 40.4 na ukarabati wa matenki mawili katika Kituo cha Ukirigulu na Kijiji cha Mwalogwabagole yenye lita za ujazo 225,000. Chuo cha Ukirigulu pamoja na Vijiji vya Mwalogwabagole, Buganda, Nyagholongo, Ngudama, Nyamule, Mwagala, Nyamikoma vitanufaika baada ya kukamilika kwa mradi na ukarabati wa skimu hiyo na jumla ya wananchi 19,658 watanufaika.
MHE. JUMANNE A. SAGINI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha Kata za Bwiregi, Nyamimange, Buswahili na Sirorisimba zinapata maji ya Ziwa Victoria kwa kuwa Mradi wa Maji wa Mgango – Kyabakari – Butiama hautazifikia?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jumanne Abdallah Sagini, Mbunge wa Butiama, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Kata za Bwiregi, Nyamimange, Buswahili na Sirorisimba zinapata huduma ya majisafi na salama, Serikali katika mwaka wa fedha 2020/ 2021 imekarabati miradi ya maji katika Vijiji vya Kamgendi, Masurura, Kongoto, Kitaramanka na Rwasereta.

Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanyika ni ukarabati wa vituo 42 vya kuchotea maji, kukarabati bomba kuu na bomba la kusambaza maji kilometa 18.5. Ukarabati wa nyumba ya mitambo ya kusukuma maji, ununuzi na ufungaji wa pampu, ufungaji wa umeme wa TANESCO katika Kijiji cha Masurura. Ukarabati wa miradi hii umekamilika ambapo wananchi wapatao 12,220 wananufaika na huduma ya maji kuanzia mwezi Machi, 2021.

Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuboresha huduma ya maji katika Kata za Nyamimange, Buswahili, Bwiregi na Sirorisimba, Serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji yenye lita za ujazo 150,000, 90,000. Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 30, ulazaji wa bomba kuu na bomba la kusambaza maji jumla ya urefu wa kilometa 26. Ujenzi wa nyumba za mashine, ujenzi wa nyumba za jumuiya za watumia maji na ufungaji wa mfumo wa umeme.

Mheshimiwa Spika, miradi hii ikikamilika itanufaisha wakazi wapatao 7,024 wa kata hizo. Katika mpango wa muda mrefu, huduma ya maji itaboreshwa katika Kata ya Bwiregi, Nyamimange, Buswahili na Sirorisimba na maeneo mengine kupitia upanuzi wa mradi wa maji Mugango, Kabari na Butiama.
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha Mradi wa Maji Kintiku -Lusilile?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aysharose Mattembe, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Kintinku -Lusilile ni mradi mkubwa ambao unatekelezwa kwa awamu nne na hadi mwezi Mei, 2021 utekelezaji wa awamu ya kwanza imekamilika ambayo ilihusisha ujenzi wa tenki la kukusanya maji la lita 300,000, ujenzi wa nyumba ya mtambo wa kusukuma maji na kufunga mitambo ya kusukuma maji, ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji lita milioni mbili na ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilometa 1.2. Aidha, utekelezaji wa awamu ya pili unaohusisha ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa kilometa 1.3 unaendelea na unatarajiwa vijiji vitatu vya Chikuyu, Mwiboo na Mbwasa ambavyo vina jumla ya wakazi wapatao 6,020 vitaanza kunufaika na huduma ya maji kabla ya mwezi Julai, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa mradi huu unatarajia kukamilika katika mwaka wa fedha 2021/2022 na utahudumia wakazi zaidi ya 55,000 wa vijiji 11.
MHE. SEIF K. GULAMALI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya Makamu wa Rais ya kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Tarafa ya Simbo na Manonga katika Jimbo la Manonga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manonga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa kupeleka maji kutoka Ziwa Victoria, ambapo hadi sasa Vijiji vya Ziba, Igumila, Ibologero, Itibula, Mwalamo, Ngulu, Mwabubele, Nyandekwa, Itale na Usongo vilivyoko katika Tarafa ya Manonga, vimefikiwa na huduma ya maji kupitia mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuanzia mwezi Aprili, 2020.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022, utekelezaji wa miradi ya maji utaendelea endapo mradi wa Maji toka Ziwa Victoria utatekelezwa na utanufaisha vijiji vya Ulaya, Nkinga na Barazani vilivyopo katika Tarafa ya Simbo na vijiji vya Imalilo, Ngulu, Igumila, Ndembezi, Itulashilanga, Njia Panda, Mwanzelwa vilivyopo Tarafa ya Manonga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zitakazofanyika ni ulazaji wa bomba takribani kilometa 50, kujenga Matenki matano ya kuhifadhia maji katika vijiji vya Igulu (lita 50,000), Ndembezi (lita 100,000), Ulaya (lita 50,000), Kitangili (lita 60,000) na Nkinga (lita 300,000) na kujenga vituo 60 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa mradi huu utaboresha hali ya upatikanaji wa maji katika Tarafa ya Simbo na Manonga kufika asilimia 85.
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafikisha huduma ya Maji kwa Wananchi wa Kata za Kipatimu, Kibata, Chumo, Kandawale, Namayuni, Miguruwe, Njinjo, Mitole na Kinjimbi katika Jimbo la Kilwa Kaskazini ili kuwaondolea adha ya maji inayowakabili?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis K. Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 Serikali imeendelea kuboresha huduma ya maji kwa kutekeleza miradi Wilayani Kilwa ambayo imehusisha uchimbaji wa visima virefu nane, ukarabati wa tanki la maji la lita 45,000 katika Kijiji cha Kipatimu, ukarabati wa mradi wa maji Mtubei Mpopera katika Kata ya Kandawale na ujenzi wa vituo 11 vya kuchotea maji. Kukamilika kwa kazi hizo kumeboresha upatikanaji wa huduma ya maji kufikia asilimia 68.5.

Mheshimiwa Naibu Spika katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali itaendelea kuboresha huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza katika Wilaya ya Kilwa kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maji ikiwemo uchimbaji wa visima virefu sita katika Vijiji vya Mitole Kata ya Mitole, Zinga kibaoni Kata ya Miguruwe, Namayuni Kata ya Namayuni, Kisima-Mkika Kata ya Njinjo, Kibata Kata ya Kibata na Ruhatwe Kata ya Kikore. Pia, ujenzi wa miradi mitano ya mitandao ya mabomba ya matanki ya kuhifadhia maji katika Vijiji vya Kinjimbi Kata ya Kinjimbi, Chapita Kata ya Migumbi, Chumo Kata Chumo, Marendego Kata ya Somanga na Kipindimbi Kata ya Njinjo. Aidha, katika vijiji hivyo kutajengwa vituo 50 vya kuchotea maji.
MHE. DKT. STEVEN L. KIRUSWA aliuliza: -

Je, ni lini Tarafa ya Enduimet pamoja na Vijiji vya ELerai, Tingatinga na Sinya vitaunganishwa na mradi wa maji kutoka Mto Simba hadi Longido ambao umepita katika maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Steven Kiruswa, Mbunge wa Jimbo la Longido kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi wa Maji Longido kutoka chanzo cha Maji Mto Simba kulingana na miundombinu iliyopo unazalisha lita 2,160,000. Mradi huo kwa sasa unahudumia Mji wa Longido na Vijiji vya jirani vya Ranchi, Orbomba, Tingatinga pamoja na Mji mdogo wa Namanga na vijiji vya Kimokouwa na Eworendeke.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mahitaji ya maji kwa vijiji vya Tingatinga, na Sinya ni zaidi ya lita 500,000 kwa siku, na vinapata huduma ya maji kupitia miradi ya Magadini, Makiwaro na visima virefu vitatu 3 vilivyopo maeneo ya Donyomali, ldonyo na Sinya. Vijiji vingine vya Tarafa ya Enduimet vinapata huduma ya maji kupitia skimu za maji ya Mtiririko ya Tingatinga Ngereyani, Larang’wa na Kamwanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2021/2022, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kuboresha huduma ya maji katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Aidha, lengo la muda mrefu ni kutumia vyanzo vya uhakika vya maji ikiwemo kufanya upanuzi wa mradi wa kutoa maji Mto Simba hadi Longido.
MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: -

Je, ni nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kuwa Wananchi wa Jimbo la Kiteto wananufaika na Miradi ya Maji safi na salama ili waweze kufikia azma ya asilimia 85 na asilimia 95 Vijijini na Mijini ifikapo Mwaka 2025?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edward Kisau Olelekaita Mbunge wa Kiteto kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa maeneo kame nchini ambayo chanzo kikuu cha maji ni maji chini ya ardhi. Huduma ya maji ya uhakika katika Wilaya Kiteto kwa upande wa vijijini inapatikana vijiji 35 kati ya 63, sawa na asilimia 53 kwa mjini ni asilimia 44.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa vijijini, Serikali imepanga kutekeleza miradi mitano au zaidi kila mwaka ili huduma ya maji ifike katika vijiji vyote 63 na kufikia lengo la asilimia 85 au zaidi. Kwa upande wa Mji wa Kibaya kwa mwaka 2021/2022, Serikali imepanga kutekeleza mradi ambao utahusisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji ambapo huduma ya maji itakayopatikana itakidhi mahitaji ya wananchi wa Kibaya kwa asilimia 95 au zaidi ifikapo mwaka 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha huduma ya maji katika maeneo kame, Serikali itatekeleza mpango wa ujenzi wa mabwawa madogo na makubwa na ukubwa wa kati kwa ajili ya kuvuna maji ya mvua na kuongeza uhakika wa upatikanaji wa maji wakati wote.
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka Mradi mkubwa wa maji katika Mji wa Tunduma ili kutatua changamoto wanayoipata wakazi wa mji huo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mji wa Tunduma unapata maji kutoka kwenye visima virefu tisa vilivyoko maeneo ya Ikulu, Sogea, Mamboleo, Tazara, Maporomoko, Mahakamani, Majengo, Msongwa na Makambini. Visima hivyo vinazalisha maji lita 2,072,000 kwa siku wakati mahitaji ya maji kwa Mji huo ni lita 4,413,000 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuboresha huduma ya maji safi na salama katika Mji wa Tunduma, Serikali inatekeleza mipango ya muda mfupi na muda mrefu, ambapo katika mpango wa muda mfupi mwaka 2020/21, Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), imechimba visima virefu sita vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita 600,000 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji ya visima hivyo utafanyika kuanzia mwezi Julai, 2021, na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Septemba, 2021. Vilevile, Serikali itafanya upanuzi wa mtandao wa maji katika maeneo mengine ya Mji wa Tunduma ikiwemo maeneo ya pembezoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa muda mrefu wa kuboresha huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza katika Mji wa Tunduma, Serikali imepanga kujenga mradi kupitia chanzo cha maji cha Mto Bupigu uliopo Wilaya ya Ileje wenye uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita milioni 73 kwa siku.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa kina (detailed design) wa mradi huo anatarajiwa kupatikana katika robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/2022. Aidha, Serikali itaendelea kufanya utafiti wa vyanzo vya maji juu na chini ya ardhi ili kupata maji yenye kutosheleza katika Mji wa Tunduma na miji mengine hapa nchini.
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa Kata za Mwamala, Samuye, Busanda, Usule, Bukene na Imesela?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika Kata ya Mwamala, Samuye, Busanda, Usule, Bukene na Imesela kupitia mpango wa muda wa kati na muda mrefu. Kwa mwaka wa 2020/2021, kazi zilizofanyika ni pamoja na kufanya usanifu wa matanki mawili yenye lita 100,000 na lita 200,000, mtandao wa kusambaza maji wa urefu wa kilometa 44.8 na vituo vya kuchotea maji 39.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022, ujenzi wa miundombinu ambayo itatumia maji kutoka mradi wa maji wa Masangwa, Ilobashi, Bubale utafanyika ili kuongeza upatikanaji wa maji katika Kata za Mwamala na Samuye.

Aidha, kwa mpango wa muda mrefu ni kutumia maji ya bomba kuu la kutoka Ziwa Victoria kupeleka maji Tinde, Shelui, ambapo kata zote sita zitapata huduma ya maji kwa zaidi ya asilimia 85 ifikapo mwezi Desemba, 2022.
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, ni lini wananchi wa Kata Saba za Tarafa ya Chamriho watapatiwa maji kutoka mradi wa maji ya Ziwa Victoria?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ni endelevu. Kwa kata saba zilizopo Tarafa ya Chamriho, upatikanaji wa huduma ya maji ni asilimia 61, ambapo vijiji vyote katika Kata tatu za Hunyari, Salama na Nyamuswa vinapata maji kutoka kwenye visima na chemchem.

Mheshimiwa Naibu Spika, na Kata nne, vijiji ambavyo huduma ya maji siyo ya uhakika ni Mahanga na Mamicheru katika Kata ya Mihingo, Kiroeli, Kambumbu na Nyambuzume Kata ya Nyamanguta, Marambeka na Nyamburumbu Kata ya Ketere na kijiji cha Sanzate Kata ya Mgeta.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 mpango wa muda mfupi ni kuboresha huduma ya maji katika vijiji hivyo sita, kupitia utekelezaji wa miradi wa visima virefu ambao utaanza mwezi Oktoba, 2021.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mkakati wa Serikali ni kutumia vyanzo vya maji vya uhakika hasa Maziwa makuu. Hivyo, mpango wa muda mrefu ni kufanya upanuzi kutoka miradi mikubwa ya maji inayotumia maji ya Ziwa Victoria.
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itachimba visima vya maji katika Kata ya Mwamanyili Kijiji cha Milambi Wilayani Busega ili kuwapunguzia adha ya maji akina mama wa Kijiji hicho?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama. Serikali itafanya upanuzi wa mradi wa maji wa Mwamanyili ambao chanzo chake ni Ziwa Victoria kwenda katika Vijiji vya Mwamanyili, Mwanangi, Milambi na maeneo ya Nassa Ginery. Upanuzi huo utahusisha ukarabati wa chanzo cha maji, ulazaji wa bomba la urefu wa kilometa 13.6 na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 15. Kukamilika kwa utekelezaji wa mpango huo kutaboresha huduma ya maji hadi kufikia asilimia 54. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mpango wa muda mrefu, Serikali imepanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Miji ya Busega, Bariadi na Itilima Mkoani Simiyu. Mradi huo utanufaisha zaidi ya vijiji 200 vya Miji hiyo.
MHE. JOHN M. SALLU K.n.y. MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuvipatia maji kutoka mradi wa Mapatano Vijiji vya Kwangena, Bantu na Machimboni Wilayani Mkinga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula Mbunge wa Jimbo la Mkinga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha maeneo yote ya vijijini huduma ya upatikanaji wa maji inaboreshwa. Ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 kazi ya upanuzi wa skimu ya maji ya Mapatano inafanyika. Ili kufikisha maji katika vijiji vya Kwangena, Bantu na Machimboni ambavyo mahitaji ya maji ni lita 251,000 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, katika upanuzi huo kazi zitakazofanyika ni kulaza mabomba Kilomita 29 na kujenga matenki mawili (2) ya kuhifadhi maji lita 45,000 na lita 135,000. Kazi hii inatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2022 na utanufaisha wananchi takriban 11,000.
MHE. DEO K. SANGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha Mradi wa Maji katika Vijiji vya Ikelu, Ibatu, Mtulingala, Nyamande, Usetule Mahongole Wilayani Makambako?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Kasenyenda, Mbunge wa Jimbo la Makambako, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vya Ikelu, Ibatu, Mtulingala, Nyamande, Usetule na Mahongole. Utekelezaji wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ikelu umefikia asilimia 98 na umeanza kutoa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji husika. Kazi zilizobaki ni ulazaji wa bomba umbali wa kilometa 29.8, ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 25,000 na ufungaji wa pampu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba, 2021.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wa maji katika Kijiji cha Ibatu umefikia asilimia 56 ambapo kazi zilizobaki ni ukamilishaji wa ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 100,000, ufungaji wa pampu ya kusukuma maji pamoja na uunganishaji wa umeme. Mradi huo umepangwa kukamilika mwezi Machi, 2022. Aidha, utekelezaji wa miradi katika Vijiji vya Mtulingala - Nyamande - Mbugani na Usetule – Mahongole kwa pamoja umefikia asilimia 67 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi, 2022.

Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa utekelezaji wa miradi hiyo kutaboresha huduma ya upatikanaji wa maji na kunufaisha wananchi wapatao 18,000 wa vijiji hivyo.
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itamaliza changamoto ya maji katika Jimbo la Nkasi Kaskazini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika Wilaya ya Nkasi ni wastani wa asilimia 52.2. Katika kutatua changamoto ya huduma ya majisafi na salama katika Jimbo la Nkasi Kaskazini, Serikali imeendelea na utekelezaji wa miradi minne ambayo ni Kirando, Namanyere, Matala na Katongolo. Miradi hii imepangiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba, 2021.

Mheshimiwa Spika, aidha, kuanzia mwezi Januari, 2022 Serikali itaanza utekelezaji wa miradi ya maji katika Vijiji vya Korongwe, Lyazumbi, Masolo, Mpata, Isale na Kakoma na utekelezaji wa miradi hiyo umepangwa kukamilika mwezi Oktoba, 2022. Kukamilika kwa miradi hiyo, kutawanufaisha wananchi wapatao takribani 97,000.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mji wa Namanyere, Serikali inaendelea na uboreshaji wa huduma ya majisafi na salama kwa kutumia chanzo cha maji cha Bwawa la Mfili. Ujenzi wa mradi huo unahusisha kazi za ujenzi wa chanzo, ufungaji wa pampu mbili zenye uwezo wa kusukuma lita 80,000 za maji kwa saa, ulazaji wa bomba kuu kilometa 3.9, ulazaji wa bomba la kusambaza maji kilometa 6.4, ujenzi wa tanki la lita 500,000. Ujenzi wa mradi huo umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba, 2021.

Mheshimiwa Spika, aidha, kupitia mradi wa Maziwa Makuu wa kutumia Ziwa Tanganyika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina na uandaaji wa makabrasha ya zabuni ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Ziwa Tanganyika. Kupitia mradi huo, vijiji 32 vya Halmashauri ya Nkasi vinatarajiwa kunufaika.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, ni lini tatizo la maji litakwisha katika Mji Mdogo wa Mikumi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifauatavyo: -

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa Mji wa Mikumi ni wastani wa asilimia 62.3. Mahitaji ya maji kwa sasa kwa Mji wa Mikumi ni takriban lita milioni 3.4 kwa siku ukilinganisha na uzalishaji wa maji wa lita 900,000 kwa siku. Katika jitihada za kumaliza tatizo la maji, Serikali ina mpango wa muda mfupi na muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, katika mpango wa muda mfupi, katika mwaka huu wa fedha 2021/2022, Serikali imepanga kuboresha Mradi wa Maji wa Msimba kwa kufunga pampu mpya, ujenzi wa tangi la ujazo wa lita 90,000 na kuongeza mtandao wenye urefu wa Kilometa 6.5. Maeneo yatakayohudumiwa na mradi huu ni pamoja na Mitaa ya Msufini, Ng’apa, Msimbakati na Miomboni. Vilevile, mpango huu wa muda mfupi unahusisha ujenzi wa Mradi wa Maji Rutwina ambao unahusisha uchimbaji wa kisima kipya, ufungaji wa pampu na ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 1.5 kutoka kwenye kisima hadi kwenye tanki la kuhifadhi maji eneo la Kidoma Mlimani. Maeneo yatakayohudumiwa ni pamoja na Kikwalaza, Tambukareli, Kidoma na Chekereni. Utekelezaji wa miradi hii unatarajiwa kuanza mwezi Disemba, 2021 na kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, katika mpango wa muda mrefu, Serikali imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi wa kutumia chanzo cha Mto Madibila. Mradi huo utahudumia maeneo ya Chekereni, Kikwalaza, Kidoma, Tambukareli, Magoma, Mjimpya, Mowlem na Green. Zabuni ya kumpata Mkandarasi wa kujenga mradi huo, imetangazwa tarehe 21 Oktoba, 2021. Ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2022 na kukamilika mwishoni mwa mwezi Disemba, 2022.

Mheshimiwa Spika, miradi hiyo yote ikikamilika itamaliza changamoto ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Mikumi na kufikia lengo la asilimia 95.
MHE. ALLY A. J. MLAGHILA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itahuisha Sera ya Maji ili iendane na wakati kwa kukidhi mahitaji halisi kwani kwa sasa haiendani na viwango vya kimataifa na imepitwa na wakati?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyigulile Jumbe Mlaghila, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Maji ndiyo mwongozo unaotumika katika kutekeleza jukumu la Serikali la kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama. Lengo la Sera ya Maji ya mwaka 2002, ilikuwa ni kuweka mfumo madhubuti na endelevu wa kuendeleza na kusimamia kikamilifu rasilimali za maji. Kupitia Sera hii, umekuwepo ushirikishwaji wa walengwa wa huduma ya maji katika hatua zote za utekelezaji, uendeshaji na matengenezo ya miradi ya maji.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2020/ 2021, Serikali ilianza utaratibu wa kuhuisha Sera ya Maji hiyo ambayo imetekelezwa kwa takribani miaka 19 ili iweze kukidhi mahitaji ya Mipango iliyopo ambayo ni; Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Awamu ya Tatu 2021 – 2026; Malengo ya Maendeleo Endelevu 2015 – 2030; na Mageuzi ya Viwanda Awamu Nne (Fourth Industrial Revolution).

Mheshimiwa Spika, matarajio ni kukamilisha hatua zote ifikapo mwezi Juni, 2022 na Sera mpya ya Maji ianze kutumika ikianzia mahitaji halisi na kufikia malengo ya Uchumi wa Kati na Maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla.
MHE. VITA R. KAWAWA K.n.y. MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupelekea maji katika Vijiji vya Lingusenguse, Lusewa, Namwinyu, Mchomoro na Luchiri Wilayani Namtumbo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani Msongozi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali ni kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji inaboreshwa katika Wilaya ya Namtumbo, ambapo kwa sasa hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani humo ni asilimia 69. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inaendelea kuboresha huduma ya maji katika Halmashauri hiyo ambapo katika Vijiji vya Lingusenguse, Lusewa na Mchomoro kazi zinazoendelea ni pamoja na ukarabati wa pampu ya mkono, ujenzi wa chanzo, ukarabati wa tanki la ujazo wa lita 50,000, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji (16) na ulazaji wa bomba la kusambaza maji urefu wa kilomita tisa. Kazi zote zinatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2022.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Kijiji cha Namwinyu ujenzi wa mradi utaanza robo ya tatu ya mwaka 2021/2022 na utahusisha uchimbaji wa kisima kirefu, vituo vinne (4) vya kuchotea maji, ulazaji wa bomba kilomita tatu (3) na ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji la lita 90,000.

Mheshimiwa Spika, katika Kata ya Luchili wananchi wa Vijiji vya Namanguli, Misufini, Chengena na Kilangalanga wanapata huduma ya maji kupitia visima 24 vinavyotumia pampu za mkono. Katika mwaka 2021/2022, Serikali kupitia RUWASA itachimba visima virefu viwili (2) na kujenga miundombinu ya kusambaza maji. Kazi hizo zinatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa utekelezaji wa miradi hiyo kutaondoa tatizo la maji katika vijiji vilivyotajwa. (Makofi)
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatenga fedha za kuendeleza Mradi wa Maji wa Lukululu ili kumaliza tatizo la maji katika vijiji 14 vya Jimbo la Vwawa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji wa Lukululu unatekelezwa kwa awamu ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetenga shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kujenga miradi ya maji katika vijiji vitano kati ya 15 vya Mradi wa Maji Lukululu ambavyo ni Myovizi, Mbewe, Mahenje, Mlangali na Ndolezi. Kazi zitakazofanyika ni ujenzi wa matanki manne ambapo kwa pamoja yatahifadhi maji lita 450,000 na mtandao wa mabomba wa urefu wa kilomita 58.3. Kazi hii itaanza kutekelezwa mwezi Desemba, 2021.

Mheshimiwa Spika, awamu ya pili itahusisha Vijiji 10 ambavyo ni Mbulu, Ivugula, Igunda, Ichesa, Shaji, Shomola, Shidunda, Ilea, Mbwewe na Lukululu. Kazi ya usanifu imepangwa kukamilika robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2021/2022 na matarajio ni kupatikana Mkandarasi na utekelezaji utaanza Julai, 2022.

Mheshimiwa Spika, jitihada hizi za Serikali zinalenga kuboresha huduma ya upatikanaji majisafi na salama Wilayani Mbozi.
MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la maji safi katika maeneo ya Ngara Mjini pamoja na maeneo ya jirani ya Murukulazo, Nyamiaga, Muruguanza na Buhororo yanayohudumiwa na Mamlaka ya Maji Safi Ngara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Mji wa Ngara ni wastani wa asimilia 63. Uzalishaji wa maji ni mita za ujazo 1,500 kwa siku ambapo mahitaji ni mita za ujazo 2,500.

Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Ngara, kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, Serikali itachimba kisima kirefu chenye uwezo wa kuzalisha maji lita 80,000 kwa saa, kukarabati mtandao wa bomba umbali wa kilomita 1.73 na kuongeza mtandao wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilomita 1.5. Kazi hizo zitaanza kutekelezwa mwezi Desemba, 2021 na kukamilika mwezi Aprili, 2022. Kukamilika kwa kazi hizo kutaboresha huduma ya maji katika Mji wa Ngara kufikia asilimia 78.9.

Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mrefu ni kujenga mradi mkubwa wa maji utakaotumia chanzo cha Mto Ruvuvu. Mradi huo utanufaisha Mji wa Ngara na maeneo/Vijiji vya jirani vya Nterungwe, Nyakiziba, Kumutana, Mayenzi, Mukirehe, Murukulazo, Nyamiaga, Muruguanza na Buhororo. Kazi ya usanifu imepangwa kukamilika katika robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 2021/2022. Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa mradi anatarajiwa kupatikana kabla ya mwezi Julai, 2022.
MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya maji katika Jimbo la Momba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Jimbo la Momba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma ya maji safi, salama na ya kutosha. Upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani Momba ni wastani wa asilimia 59.07 kupitia visima vifupi (16), visima virefu (43), skimu za usambazaji maji (17) na matanki ya kuvunia maji ya mvua (3). Katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani Momba, Serikali inatekeleza miradi ya maji katika Vijiji 13 vya Nkangamo, Itelefya, Mbao, Mkonga, Papa, Masanyinta, Kasamu, Samang’ombe, Lwatwe, Ivuma, Kapele, Mkutano na Kalungu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zinazofanyika ni pamoja na ujenzi wa matanki saba (7) yenye ujumla ya ujazo wa lita 600,000, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilomita 32, vituo vya kuchotea maji 66 na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilomita 72. Utekelezaji wa miradi hiyo umefikia wastani wa asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022. Kukamilika kwa miradi hiyo kutaboresha upatikanaji wa huduma ya maji. Serikali itaendelea kutenga fedha za utekelezaji wa miradi mwaka hadi mwaka ili kumaliza tatizo la maji katika Jimbo la Momba na kufikia lengo la asilimia 85 ifikapo mwaka, 2025.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itawapatia maji wananchi wa Wilaya ya Kyerwa kwa kutengeneza miundombinu ya kupeleka maji kwa Wakazi waishio sehemu za miinuko?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama Wilayani Kyerwa ni wastani wa asilimia 56.8. Katika kuboresha huduma ya maji kwa wananchi wa Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na wale wanaoishi kwenye maeneo yenye miinuko, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mipya ya Kagenyi - Omukalinzi na Mabila. Ujenzi wa miradi hiyo unahusisha ulazaji wa bomba umbali wa Kilometa 7.2, matenki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 105,000 na vituo sita vya kuchotea maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa miradi hii umefikia asilimia 70 na umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2022. Sambamba na miradi hiyo, Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuajiri Wakandarasi kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya Runyinya - Chanya, Kimuli - Rwanyango na Nyamiaga - Nyakatera.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi hiyo, itahusisha ujenzi wa matenki matano yenye jumla ya ujazo wa lita 1,700,000, ulazaji wa mabomba umbali wa Kilometa 86.1 na ujenzi wa vituo 146 vya kuchotea maji. Kukamilika kwa miradi hiyo kutanufaisha Vijiji vya Nkwenda, Runyinya, Rwabwere, Muhurire, Karongo, Iteera, Muleba, Chanya, Chakalisa, Kagu na Nyakatera. Vijiji vingine ni Chakalisa, Kishanda, Nyakahita, Kyerwa, Nyaruzumbura, Milambi na Katera. Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi, 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali pia imesaini mkataba mwezi Januari, 2022 na Mkandarasi kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji Kijiji cha Murongo kwa kutumia fedha za UVIKO-19. Mradi huo unahusisha ujenzi wa tenki moja la lita 150,000, ulazaji wa mabomba umbali wa Kilometa 16.6, ujenzi wa vituo 25 vya kuchotea maji. Mradi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Juni, 2022. Kukamilika kwa miradi yote hiyo kutaboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa Wilaya ya Kyerwa. Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingine ili kuhakikisha kuwa huduma ya maji safi na salama ndani ya Wilaya ya Kyerwa inafikia kiwango kisichopungua asilimia 85 mwaka 2025.
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Tanganyika kwenda Mpanda Mjini ili kutatua tatizo la maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa huduma ya maji katika mji wa Mpanda ni wastani wa asilimia 60. Katika kuboresha huduma ya maji katika mji huo, Serikali mwishoni mwa mwezi Februari, 2022 itaanza utekelezaji wa miradi ya Kanoge II na Shangala. Kazi zitakazotekelezwa ni ujenzi vidakio vya maji vitatu, kufunga pampu, kujenga nyumba ya mitambo (pump house), ujenzi wa tenki lenye ukubwa wa mita za ujazo 200 na mtandao wa kusafirisha maji umbali wa kilometa 28. Miradi hiyo ipo kwenye hatua za manunuzi na inatarajiwa kutekelezwa kwa muda miezi sita na kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 6,000 hadi kufikia 8,000 kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa muda mrefu, Serikali imefanya tathmini ya awali ya kutumia Ziwa Tanganyika kuwa chanzo kuu cha maji kwa Mji wa Mpanda na maeneo ya kandokando mwa ziwa hilo. Katika mwaka 2021/2022 Wizara itakamilisha usanifu wa miundombinu inayohitajika kwa ajili ya utekelezaji mwaka wa fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Mji wa Mpanda ni miongoni mwa miji itakayonufaika na mradi wa miji 28 na wakandarasi wataanza kazi katika mwaka wa fedha 2021/2022. Miradi hiyo itasaidia kufikia malengo ya kisekta yaliyopo ya zaidi ya asilimia 85 vijijini na zaidi ya asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025.
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: -

(a) Je, ni lini Mradi wa Maji ya Ziwa Victoria Wilaya ya Urambo utaanza ili kutatua tatizo la maji katika Wilaya hiyo?

(b) Je, ni lini Serikali itachimba mabwawa katika Kata za Uyumbu na Kalemela hasa ikizingatiwa kuwa maombi yalishawasilishwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Jimbo la Urambo kwa pamoja kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Urambo ni wastani wa asilimia 40. Katika kuboresha huduma hiyo, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 inatekeleza miradi ya Itibulanda na upanuzi wa mradi kutoka Itibulanda kwenda Nsenga. Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa matanki mawili yenye ujazo wa lita 50,000, vituo 13 vya kuchotea maji na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 17.6. Miradi hiyo itaongeza uzalishaji maji wa lita 32,000 kwa siku.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha huduma ya maji katika Kata za Uyumbu na Muungano, Serikali imepanga kujenga mabwawa mawili ya Kilemela kata ya Muungano na Izimbili kata ya Uyumbu. Mabwawa hayo yatahudumia jumla ya vijiji vya 22 na mkandarasi wa ujenzi wa bwawa la Kilemela atapatikana mwezi Aprili, 2022 Kwa upande wa bwawa la Izimbili kazi ya usanifu inaendelea na itakamilika mwezi Juni, 2022. Ujenzi wa mabwawa hayo utafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Aidha, Mji wa Wilaya ya Urambo unatarajiwa kupata huduma ya maji kupitia Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Miji 28 ambapo chanzo cha maji kitakachotumika ni Ziwa Victoria. Taratibu za upatikanaji wa wakandarasi zimekamilika mwezi Desemba, 2021 hivyo utekelezaji utaanza ndani ya mwaka wa fedha 2021/2022.
MHE. JAFARI W. CHEGE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO Aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itasambaza maji katika mitaa ya pembezoni kwa Kata za Kabasa, Guta, Kuzungu, Sazira, Nyatwali, Mcharo na Wariku katika Mji wa Bunda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Robert Chacha Maboto, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama na endelevu. Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Bunda ni wastani wa asilimia 69.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Guta inapata huduma ya majisafi na salama kupitia mtandao wa maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda. Aidha, kwa Kata za Kabasa, Sazira, Mcharo, Kunzugu, Wariku na Nyatwali zinapata huduma ya maji kupitia visima thelathini (30) vilivyofungwa pampu za mikono.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwenye kata hizo, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022, inatekeleza ujenzi wa miradi ya maji katika Kata za Nyatwali, Mcharo na Guta na ujenzi wa miradi hiyo utakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Mei, 2022. Serikali itaendelea kutenga bajeti katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye Kata za Kabasa, Sazira, Kunzugu na Wariku.
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafikisha maji safi na salama katika Kata za Kikolo, Utiri, Mbangamao, Kilimani na Mateka?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Mbinga Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa huduma ya Majisafi na salama katika Wilaya ya Mbinga ni wastani wa asilimia 59.2. Katika kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Mbinga, Serikali imeendelea kutekeleza Miradi ya Maji ya Mpepai, Mabuni, Amanimakolo, Luhagara, Myangayanga, Luwaita, Lifakara/Uzena na Ruanda. Miradi hiyo inahusisha ujenzi wa Matangi kumi na moja (11) yenye jumla ya ujazo wa lita 775,000, ulazaji wa mtandao wa mabomba umbali wa kilometa 105.1 na ujenzi wa Vituo 116 vya kuchotea maji. Miradi hiyo ikikamilika itanufaisha wananchi wapatao 45,478.

Mheshimiwa Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Mbinga yanapata huduma ya majisafi na salama na yenye kutosheleza. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imekamilisha kazi ya usanifu wa Miradi ya Maji katika Kata za Mateka, Kikolo na Utiri na ujenzi wa miradi katika Kata za Mateka na Utiri utaanza mwezi Aprili, 2022 na Mradi wa Maji wa Kikolo unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2022/2023. Vilevile, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji katika Kijiji cha Uzena (Kata ya Kikolo) kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO – 19 na unatarajia kukamilika ifikapo Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Kilimani inapata huduma ya maji kupitia mtandao wa maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbinga. Katika kuboresha huduma ya maji katika kata hiyo, Serikali imepanga kutekeleza upanuzi wa Mradi wa Maji wa Lifakara kupeleka Kata ya Kilimani katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: -

Je, ni lini ahadi iliyotolewa wakati wa kampeni za Urais ya ujenzi wa mabwawa mawili ya maji katika Wilaya ya Kiteto itatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Edward Kisau Olelekaita, Mbunge wa Jimbo la Kiteto, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika Wilaya ya Kiteto kwa sasa ni asilimia
52.58. Katika kuboresha huduma ya majisafi na salama katika Wilaya ya Kiteto, Serikali katika mwaka fedha 2021/2022, inatekeleza miradi katika Vijiji 21 vya Nchinila, Engusero, Ngipa, Nasetani, Ngarenaro, Mafichoni, Kibaya Kati, Kanisani Bomani, Magubike na Msakasaka. Vijiji vingine ni Jangwani, Magungu, Kaloleni, Majengo Mapya, Msikitini, Vumilia, Esuguta na Kiperesa.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi hiyo unahusisha ujenzi wa matangi 11 yenye jumla ya ujazo wa lita 1,325,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 99.49 na ujenzi wa vituo 69 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa miradi hiyo umefikia wastani wa asilimia 10 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Spika, Mpango wa muda mrefu, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022, imefanya mapitio ya usanifu wa Bwawa la Maji la Dongo na usanifu wa ukarabati wa Mabwawa ya Dosidosi na Kijungu na taratibu za kupata wakandarasi zitakamilika kabla ya mwezi Juni, 2022. Ujenzi wa Bwawa la Dongo pamoja na ukarabati wa Mabwawa ya Dosidosi na Kijungu unatarajiwa kuanza katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. HASSAN Z. KUNGU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kuwapatia maji wananchi wa Kijiji cha Fundimbanga, Kata ya Matemanga katika Jimbo la Tunduru Kaskazini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hassan Zidadu Kungu, Mbunge wa Tunduru Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Wilaya ya Tunduru ni wastani wa asilimia 69. Katika kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Tunduru, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 inaendelea kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Mradi wa Maji Muhuwesi, Semeni, Ndaje- Mbesa kwa awamu ya pili na ukarabati wa Mradi wa Maji Njenga na Misyaje, ukarabati wa Mradi wa Maji Nalasi na Namwinyu, ujenzi wa Mradi wa Maji Masuguru, upanuzi wa Mradi wa Maji Majimaji, Chalinze, Ligoma, Makoteni na Imani, Kazamoyo na Daraja Mbili.

Mheshimiwa Spika, Kata ya Matemanga ina jumla ya vijiji vinne, ambavyo ni Milonde, Changarawe, Fundimbanga na Matemanga. Katika vijiji vitatu vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia mradi mkubwa wa maji wa Matemanga. Vilevile Kijiji cha Fundimbanga kinapata huduma ya maji kupitia visima virefu viwili vya pampu za mkono, ambavyo havitoshelezi mahitaji kwa wananchi wa kijiji hicho.

Katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwenye Kijiji cha Fundimbanga, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 imekamilisha utafiti wa maji chini ya ardhi na uchimbaji wa kisima utafanyika mwezi Aprili, 2022. Ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji utafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. MOHAMED MAULID ALI aliuliza: -

Je, Serikali haioni haja ya kujikita zaidi kwenye uchimbaji wa Malambo ya kuhifadhia maji ya mvua na kujenga mabomba ya kuchukua maji toka kwenye maziwa na mito yote kuliko kuendelea kutumia gharama kubwa za kuchimba visima bila mafanikio?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Maulid Ali, Mbunge wa Kiembe Samaki, kama Ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha kuwa uvunaji wa maji ya mvua kupitia mabwawa unatekelezwa kwenye maeneo mengi nchini ili kuongeza upatikanaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, kazi ya ukarabati na ujenzi wa mabwawa na malambo inaendelea katika vijiji 20 vya Mlele, Kisarawe, Bunda, Kalambo, Mkinga, Handeni, Chalinze, Songwe, Chamwino, Chemba, Bahi, Kaliua, Kilindi, Itilima, Kishapu, Monduli, Kibaha na Kondoa. Aidha, kazi ya kuainisha maeneo 58 yanayofaa kujenga mabwawa madogo na malambo imefanyika na ujenzi utafanyika mwaka wa fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, Mpango wa Serikali ni kuhakikisha miradi ya maji inajengwa kwa kutumia vyanzo vya uhakika ambavyo ni maziwa makuu na mito mikubwa. Mradi huo ni wa kutoa maji Ziwa Victoria kuyapeleka Shinyanga, Kahama, Tabora, Igunga na Nzega Bukoba, Musoma, Misungwi na Magu. Vilevile, Utekelezaji wa miradi ya Mugango, Kiabakari, Butiama, Tinde, Shelui, na mradi wa maji katika miji ya Busega, Bariadi na Lagangabilili unaendelea kupitia Ziwa Victoria na mradi wa maji wa kutoa maji Ziwa Tanganyika kupeleka Kigoma Mjini, Kirando na Kabwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hilo, Serikali imeanza mpango wa kutekeleza miradi kupitia maziwa makuu ili kunufaisha maeneo ya pembezoni mwa maziwa hayo; kwa upande wa mito; mradi wa maji wa Kyaka - Bunazi ambao unatumia maji ya mto Kagera.

Mheshmiwa Naibu Spika, huduma ya maji yanayotokana na maji ya chini ya ardhi ni katika maeneo kame ambayo hayana vyanzo vya uhakika vya maji juu ya ardhi. Haya maeneo ni kama vile Dodoma, Singida, Lindi, Simiyu, Kigoma na Katavi.
MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: -

Je, Serikali inachukua hatua gani ili kuhakikisha kwamba maji yote yaliyopo ardhini yanabaki salama kwa kuwa tone moja la oil (vilainishi) huharibu lita 600 za maji yaliyoko ardhini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Anyigulile Jumbe Mlaghali, Mbunge wa Kyela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na. 11 ya mMwaka 2009 na Sheria ya Mazingira Na. 20 ya Mwaka 2004 kwa pamoja zinasisitiza uhifadhi, utunzaji na usimamizi wa vyanzo vya maji. Maji chini ya ardhi ni rasilimali ambayo inalindwa dhidi ya uchafuzi wa aina zote hii ni pamoja na oil. Hii ni kutokana na kuwa maji chini ya ardhi yakishaharibiwa ubora wake ni vigumu na ni gharama kubwa kuyasafisha ili yaweze kutumika kwa shughuli za maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Bodi za Maji za Mabonde inaendelea na jukumu la kutambua vyanzo vya maji juu ya ardhi na chini ya ardhi, kuweka mipaka na kutangaza katika Gazeti la Serikali ili yalindwe kisheria. Hivyo, maeneo tengefu ambayo yametangazwa ni Saba (7) ambapo Sita (6) ambayo yalitangazwa mwaka 2016 yapo Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Rukwa maeneo ya Chokaa, Kidole, Kiswaga, Matundasi A, Matundasi B na Mkola katika Wilaya ya Chunya Mkoa wa Mbeya na eneo moja Makutupora Mkoani Dodoma katika Bonde la Wami-Ruvu lilitangazwa mwaka 2012.

Mheshimiwa Spika, vilevile, maeneo Hamsini na Nne (54) katika Bodi ya Maji Bonde la Rufiji (16), Ziwa Tanganyika (3), Pangani (7), Wami/Ruvu (5) Ruvuma na Pwani ya Kusini (13), Ziwa Nyasa (8) na Ziwa Victoria (1), Bonde la Kati (1) yamewekewa mipaka ili yatangazwe mwaka huu 2022.

Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha utekelezaji wa Mipango ya Uhifadhi wa Vyanzo vya maji, Wizara ya Maji inatekeleza kazi ya kuainisha miamba yenye maji (Aquifer Mapping) katika Mabonde manne ambayo ni Bonde la Kati, Pangani, Wami/Ruvu na Rufiji.

Mheshimiwa Spika, kazi ya kutathmini maeneo yenye maji chini ya ardhi imekamilika na hatua inayofuata ni kuchimba visima ili kupata takwimu za wingi na ubora wa maji katika maeneo hayo. Baada ya hatua hii, itaandaliwa ramani ili kutangaza maeneo hayo katika Gazeti la Serikali ili yalindwe kisheria na yaweze kutumika kulingana na mahitaji ya shughuli za maendeleo.
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itasambaza maji katika Vijiji vya Mwanjoro, Jinamo, Mbushi na Witamihya Wilayani Meatu baada ya ujenzi wa Bwawa la Mwanjoro kukamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, vijiji vya Mwanjoro, Jinamo, Mbushi na Witamihya kwa sasa vinapata huduma ya maji kwa wastani wa asilimia 24 kupitia visima vifupi 13.

Mheshimiwa Spika, bwawa la Mwanjolo lilikamilika mwishoni mwa mwaka 2018 likiwa na lengo la kuhudumia vijiji vya Jinamo, Mbushi na Mwanjoro, lakini katika utafiti uliofanyika hivi karibuni bwawa hilo limeonekana kupungua kina kutokana na kujaa kwa mchanga unaosababishwa na kunyweshea mifugo na changamoto ya uharibifu wa mazingira iliyopelekea pia kuathiri ubora wa maji hayo.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa Bwawa la Mwanjolo linatumika kusambaza maji vijiji vya Mwanjoro, Jinamo, Mbushi. Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 itatenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa Bwawa la Mwanjolo ambapo ukarabati huu utahusisha kuongeza kwa kina cha bwawa, kujenga kingo za bwawa ambazo kwa sasa zimechakaa. Kujenga miundombinu ya kuzuia mchanga kuingia katika Bwawa (sand trap) pamoja na upandaji wa miti na nyasi ili kuzuia mmomonyoko wa ukuta. Pia katika bajeti hiyo Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kunyweshea maji mifugo ili wafugaji wasiweze kuingiza mifugo yao kwenye bwawa na mwisho wananchi wa maeneo haya watapewa elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mrefu vijiji hivi pia vitaweza kunufaika na mradi mkubwa unaotarajia kujengwa katika Mkoa wa Simiyu kupitia program ya mabadiliko ya tabia ya nchi maana vijiji hivi vya Mwanjoro vipo umbali wa kilomita 12 toka kwenye eneo la ujenzi wa bomba kuu.
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kuvuna maji katika Mji wa Itigi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali inaendelea na ukarabati wa mabwawa mawili ya Rungwa na Muhanga yenye thamani ya zaidi ya milioni 460 yenye ukubwa wa kati katika Wilaya ya Manyoni ili kuongeza uvunaji wa maji ya mvua yatakayonufaisha wananchi katika Wilaya hiyo.
MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -

Je, ni lini Mradi wa Maji wa Halmashauri 28 ambapo Njombe ni mojawapo utaanza kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifauatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imeanza kutekeleza mradi wa maji wa Miji 28 ambapo Wakandarasi wote walisharipoti site mwezi Julai, 2022. Kwa sasa, Wakandarasi wanaendelea na usanifu wa kina na ujenzi wa miradi kwa Miji 28 ikiwemo Njombe utaanza mwezi Novemba, 2022.
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: -

Je, ni nini tamko la Serikali kuhusu uchimbaji unaoendelea katika Mto Nyandurumo ambao ni chanzo cha maji kwa wakazi wa Tarime?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ghati Zephania Chomete, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo cha maji cha Nyandurumo ni chanzo ambacho kinatoa huduma ya maji kwa Mji wa Tarime ambapo kina uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000,000 kwa siku kwa kipindi cha masika na lita 1,500,000 kwa kipindi cha kiangazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na uharibifu unaojitokeza kwenye chanzo hicho, Serikali kupitia Watalaam wa Mazingira wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Bonde la Ziwa Victoria na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Mara wamewaondoa wachimbaji waliokuwa wanafanya shughuli za kusafisha madini karibu na chanzo hicho cha maji na kupanda miti 205 ambayo ni rafiki kwa mazingira ikiwa na lengo la kulinda na kuhifadhi chanzo hicho. Umbali wa kutoka maeneo ya uchimbaji hadi kwenye chanzo cha maji ni takribani kilometa tatu.
MHE. JUDITH S. KAPINGA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuweka mita janja za maji ili watumiaji wachague kutumia kulingana na matumizi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Judith Salvio Kapinga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuboresha utoaji wa huduma ya maji na watumiaji kulipa gharama kulingana na matumizi, Serikali imeshaanza kutumia mita za malipo kabla ya matumizi (water prepaid meter) katika maeneo tofauti tofauti ikiwemo katika Mamlaka ya Maji Iringa, Arusha, Tanga, Singida, Mwanza, Mbeya, Kahama na Mtwara. Aidha, mita hizo pia zimefungwa kwenye maeneo ya taasisi kama vile shule, hospitali na Majeshini wakati Serikali ikiendelea kujiridhisha na ufanisi wake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa kufunga mita za malipo kabla ya matumizi (water prepaid meter) utafanyika kwa awamu ili kuweza kufikia maeneo mbalimbali katika mikoa yote nchini. Aidha, jitihada hizi zinaenda pamoja na kuhakikisha mamlaka za maji zinatumia mfumo wa malipo kutoa ankra za maji kulingana na matumizi ya wateja (unified billing system).
MHE. MWANTUM M. ZODO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha mradi wa maji wa Vuga - Mlembule katika Mji Mdogo wa Mombo Wilayani Korogwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwantum Mzamilu Zodo, Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Tanga kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa Vuga - Mlembule ulioanza kutekelezwa mwezi Julai, 2020 ambapo utekelezaji hadi sasa umefikia asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2022. Kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa dakio (intake), ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi maji mita za ujazo 500, ujenzi wa matanki punguza mawili (2) na ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa Kilometa 10.2.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zinazoendelea ni ujenzi wa matanki punguza manne (4) na ulazaji wa mabomba ya usambazaji Kilometa 4.3. Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha wananchi wapatao 21,284 wa Vijiji vya Mlembule, Mwisho wa Shamba, Mombo na Jitengeni.
MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: -

Je, ni lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Mji wa Tarime, Sirari, Nyamwaga na Nyamongo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza. Katika mipango ya muda mfupi ya kupunguza kero ya uhaba wa maji katika Wilaya ya Tarime, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imekamilisha Miradi ya Maji ya Sirari na Nyamwaga na inaendelea kutekeleza Miradi ya Nyangoto (Nyamongo), Sabasaba na Gimenya (Mjini Tarime). Miradi hiyo inatarajia kukamilika mwezi Juni, 2022 ambapo hali ya huduma ya maji katika Mji wa Tarime itaimarika kutoka asilimia 45 hadi asilimia 56 na maeneo mengine ya Wilaya ya Tarime kutoka asilimia 70 hadi asilimia 75.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa muda mrefu, Wilaya ya Tarime itanufaika na Mradi wa Kuboresha Huduma ya Maji katika Miji 28 ambapo chanzo cha maji cha Ziwa Victoria kitatumika. Kupitia Mradi huo Miji ya Tarime, Sirari, Nyamwaga na Nyamongo na maeneo mengine ya Wilaya ya Tarime yatanufaika na lengo la asilimia 85 vijijini na 95 mijini litafanikiwa ifikapo mwaka 2025.
MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha Mradi wa Maji Igando - Kijombe ili kupunguza changamoto ya maji Jimbo la Wanging’ombe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging’ombe ni wastani wa asilimia 76. Katika kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Wanging’ombe, Serikali inatekeleza Mradi wa Maji ya Mtiririko wa Igando – Kijombe ambao utahudumia wakazi wapatao 14,377 katika vijiji 10 vya Malangali, Igando, Mpanga, Luduga, Mayale, Kijombe, Wangamiko, Hanjawanu, Iyayi na Lyadebwe.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji, chujio, ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa kilometa 28.9 na mabomba ya usambazaji yenye urefu wa kilometa 18.2; ujenzi wa matenki mawili ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 150,000 na lita 100,000, vituo vya kuchotea maji 22 na mabirika mawili ya kunyweshea mifugo (cattle trough). Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022 na kuboresha huduma ya maji kutoka asilimia 76 ya sasa na kufikia asilimia 80.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi iliyoainishwa katika mpango wa kuhakikisha lengo la kufikisha huduma ya maji vijijini ni asilimia 85 na asilimia 95 mijini ifikapo mwaka 2025.
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -

Je, ni lini ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya ujenzi wa Bwawa katika Mji wa Itolwa, Kata ya Jangalo itatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilikamilisha utafiti wa ujenzi wa bwawa la mita za ujazo 106,100 katika Kijiji cha Itolwa Wilayani Chemba. Gharama za ujenzi wa bwawa hilo ni shilingi bilioni 1.7 na katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bwawa hilo. Maji yatakayohifadhiwa katika Bwawa la Itolwa yatatosheleza mahitaji ya wakazi wa Kijiji cha Itolwa.
MHE. LUCY J. SABU aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza magari RUWASA – Simiyu ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lucy Sabu, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuijengea uwezo RUWASA, Mkoa wa Simiyu ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, jumla ya magari 37 yalinunuliwa ambapo gari moja lilikabidhiwa RUWASA, Mkoa wa Simiyu na gari nyingine ilipelekwa Wilaya ya Itilima.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika jitihada za kuendelea kuboresha mazingira ya kazi ya RUWASA nchini, Serikali itanunua jumla ya magari ya 86 kwa ajili ya RUWASA na magari hayo yatapelekwa kwenye wilaya mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Simiyu.
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatoa fedha kwa ajili ya Mradi wa Maji wa Kiwira ili uanze kutekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha mapitio ya usanifu kwa ajili ya mradi utakaotumia chanzo cha Mto Kiwira kupeleka maji katika Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi. Hatua inayoendelea sasa ni manunuzi ya Mkandarasi na katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga shilingi 4,000,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa chanzo na utekelezaji wa mradi utafanyika kwa awamu.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji katika Manispaa ya Morogoro?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jukumu mojawapo la kusimamia rasilimali za maji ni kudhibiti uharibifu kuhakikisha vyanzo vya maji vinahifadhiwa kwa ajili ya uendelezaji na uharibifu unadhibitiwa wakati wote. Katika Manispaa ya Morogoro, Serikali inaendelea na utambuzi wa maeneo ya vyanzo vya maji, kuweka mipaka na kuyatangaza kuwa maeneo tengefu. Hadi Desemba 2021, vyanzo vya maji kumi vimewekwa mipaka, hii ni pamoja Bwawa la Mindu ambacho kimetangazwa kuwa eneo tengefu.

Mheshimiwa Spika, vilevile, jumuiya za watumia maji Saba zinashiriki katika uhifadhi wa vyanzo vya maji katika maeneo yao. Pia, vilabu 10 vya michezo vya watoto vimeundwa katika Shule za Msingi ili elimu ya utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji na mazingira inatolewa kwa jamii. Aidha, hadi Machi 2022 jumla ya miche ya miti 96,500 imepandwa katika maeneo mbalimbali ya vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, mkakati wa muda mrefu wa kudhibiti uharibifu wa vyanzo vya maji ni kuimarisha Bodi za Maji za Mabonde ili ziweze kutekeleza Mipango ya Uhifadhi wa Vidakio vya Maji nchini kwa Mabonde yote likiwemo Bonde la Wami-Ruvu. Mipango hiyo imeainisha maeneo ya vipaumbele kwa ajili ya shughuli za uhifadhi wa vyanzo vya maji ikiwemo kupanda miti rafiki kwa maji kwenye maeneo ya vyanzo vya maji, kilimo cha makinga maji, urejeshaji wa uoto wa asili kwenye kingo za mito na udhibiti wa utiririshaji wa majitaka kwenye mazingira.
MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka maji katika Kata za Namajani, Mpanyani, Mlingula, Msikisi na Chingulungulu (Kata ni Namalutwe) zilizopo katika Jimbo la Ndanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kata ya Mlingula ina Vijiji vitano vyenye huduma ya maji ambavyo ni Mlingula, Chikoweti na Nambaya. Aidha, katika kuboresha huduma ya maji kwenye Kata hiyo vijiji vya Namichi na Masikunyingi vinapata huduma ya maji kupitia bomba kuu linalopeleka maji kwenye maeneo yanayohudumiwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (NAWASA). Kazi ya usanifu wa miundombinu ya maji itakamilika mwezi Juni, 2022 na ujenzi utafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.

Mheshimiwa Spika, Kata za Namajani zina vijiji vitano ambavyo vinapata huduma ya maji ni Namahinga, Ngalole, Namajani. Kata ya Mpanyani ina vijiji vitano ambapo Vijiji vya Muungano Nambawala A na Nambawala B vinapata huduma ya maji. Kata ya Nsikisi ina vijiji vitatu ambapo Kijiji cha Namalembo kinapata huduma ya maji. Vile vile katika Kata ya Namalutwe pale pameandikwa Chingulugulu, naomba isomeke Namalutwe kwa sababu Chingulugulu ni kijiji na Kijiji cha Chingulugulu kina huduma ya maji. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 kazi ya utafiti wa maji chini ya ardhi imekamilika katika vijiji nane katika Kata hizo nne na uchimbaji wa visima unaendelea na miundombinu ya maji itafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. ALEXANDER P. MNYETI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka maji katika Mji wa Misasi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waaziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alexander Pastory Mnyeti Mbunge wa Misungwi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Misasi ina vijiji Vinne (4) vya Inonelwa, Misasi, Mwasagela na Manawa na vinapata huduma ya maji kupitia visima virefu viwili pamoja na skimu za maji za mtandao wa bomba. Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Kata hiyo ni asilimia 40. Katika kuboresha huduma ya maji katika Kata ya Misasi, Serikali inaendelea na ujenzi wa mradi unaotoa maji kwenye bomba kuu la Mabale-Mbarika kwenda kwenye vijiji vya Kata hiyo ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 90 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2022.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kukamilika kwa mradi huo kutaboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Kata ya Misasi kufikia asilimia 80. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali itaendelea na upanuzi wa mradi huo ili kuhakikisha wananchi wote wa Kata ya hiyo wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza.
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza Mradi wa Maji wa Darakuta hadi Minjingu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Darakuta - Magugu ndio unaoendelezwa mpaka Minjingu ambapo utagharimu shilingi bilioni 5.672 na kazi zinazoendelea kufanyika ni pamoja na ulazaji wa bomba kuu kwenye umbali wa kilometa 46, ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilometa 66, ujenzi wa tanki la lita 250,000 na ufungaji wa pampu. Utekelezaji wa mradi huu umeanza mwezi Septemba, 2022 na unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo wananchi wapatao 23,000 wa Kata za Mwada na Nkati watanufaika.
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, hadi sasa mpango wa kutatua kero ya maji katika Mji wa Tunduma umefikia hatua gani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma ya upatikanaji ya maji safi na salama inaboreshwa katika Mji wa Tunduma na maeneo yote hapa nchini. Katika Mji wa Tunduma, Serikali inaendelea na upanuzi wa mtandao wa usambazaji maji kilometa10.5 ambapo Kata ya Uwanjani, Tunduma na Makambini zitaanza kupata huduma mwezi Machi, 2023.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali imedhamiria kutekeleza mradi wa kutumia Chanzo cha Mto Bupigi kilichopo katika Wilaya ya Ileje na taratibu za kumpata Mkandarasi zinaendelea na ujenzi wa mradi utaanza kabla ya mwezi Julai, 2023. Mradi huu umepangwa kuhudumia Miji ya Tunduma, Vwawa Mlowo, vijiji 14 vya Ileje na maeneo ambayo bomba kuu litapita. (Makofi)
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: -

Je, lini maji yatasambazwa Toangoma, Chamazi, Mianzini, Kilungule, Kiburugwa, Kijichi, Mbagala, Charambe, Kibondemaji na Mbagala Kuu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Mbagala, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kata za Toangoma, Chamazi Mianzini, Kilungule, Kiburugwa, Kijichi, Mbagala, Charambe, Kibondemaji na Mbagala Kuu zinapata huduma ya majisafi na salama kupitia vyanzo vya maji ya visima virefu na vifupi. Changamoto iliyopo katika kata hizo ni kuwa baadhi ya maeneo hayajafikiwa na mtandao wa maji.

Mheshimiwa Spika, Serikali imepanga kutumia vyanzo vya visima vya Kimbiji kwa ajili ya kumaliza tatizo la maji katika kata hizo. Kwa sasa, taratibu za kumpata mkandarasi zinaendelea na ujenzi unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2023/2024.
ASYA SHARIF OMAR K.n.y. MHE. TAUHIDA CASSIAN GALLOS aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kulinda miundombinu ya maji nchini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tauhida Gallos Nyimbo Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha miundombinu ya maji inayojengwa inatunzwa na kulindwa ili kutoa huduma endelevu. Katika kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi, Serikali ilitunga Sheria Na.5 ya Mwaka 2019 ambayo inakataza kuharibu, kuvamia au kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo yenye miundombinu ya maji. Kupitia sheria hiyo ni kosa la jinai kuharibu miundombinu ya maji. Aidha, Serikali inaendelea kujenga uzio kwenye miundombinu ya maji ikiwemo matanki ya kuhifadhia maji na mitambo ya kutibu maji. Vilevile, elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kulinda miundombinu ya maji nchini inaendelea kutolewa.
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, ni lini visima viwili vilivyochimbwa katika Mji wa Mpwapwa Mwaka 2021 vitaanza kufanya kazi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka fedha 2022/2023, Serikali imepanga kutekeleza ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji kutoka kwenye visima viwili vilivyochimbwa katika Mji wa Mpwapwa mwaka 2021. Kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilometa 48.8, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 200,000 na ujenzi wa vituo 18 vya kuchotea maji. Taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa Ujenzi zinaendelea na ujenzi wa mradi unatarajiwa kuanza mwezi Aprili, 2023 na kukamilika mwezi Aprili mwaka 2024. Kukamilika kwa mradi huu kutanufaisha wananchi wapatao 21,360 waishio kwenye Kata za Vihangwe na Mpwapwa Mjini.
MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kusafisha maji kabla ya kusambazwa ili kuondoa Floride ambayo huleta ulemavu kwa Wakazi wa Arumeru?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati ya kuondoa madini ya fluoride kwenye maji ya kunywa na kupikia katika maeneo mbalimbali yaliyoathirika na madini hayo. Mikakati hiyo ni pamoja na kujenga Miradi ya Kusambaza Maji Safi na Salama kutoka kwenye vyanzo vya maji vya uhakika ambavyo havijaathirika na madini ya fluoride; kusambaza teknolojia ya kuondoa madini ya fluoride kwa kutumia chengachenga za mkaa wa mifupa ya ng’ombe; na kuweka mitambo ya reverse osmosis kwa ajili ya kusafisha maji ikiwa ni pamoja na kuondoa madini ya fluoride kwenye maji ya kunywa na kupikia katika Kata za Oldonyosambu, Ngaramtoni, Embasenyi katika Wilaya za Arumeru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Wizara kupitia Kituo cha Utafiti cha Kuondoa Madini ya Fluoride cha Ngurdoto imeendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya kiwango kikubwa cha madini ya fluoride katika maji ya kunywa na matumizi sahihi ya teknolojia ya kuondoa madini hayo kupitia vyombo vya habari, mikutano na makongamano mbalimbali.
MHE. TUNZA I. MALAPO aliuliza: -

Je, ni lini chujio la maji linalojengwa katika Manispaa ya Mtwara Mikindani litakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilika ujenzi wa chujio la kuchujia maji mwezi Aprili, 2022. Kukamilika kwa ujenzi wa chujio hilo kumeweza kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kudhibiti kuhama kwa Mto Ruvu-Kibaha ili kuzuia uharibifu wa mashamba na miundombinu ya Reli ya SGR?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Costantino Mwakamo Mbunge wa Kibaha Vijijini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mto Ruvu eneo la Kibaha hadi Bagamoyo umekuwa na kawaida ya kuhamahama kwa vipindi tofauti tofauti kutokana na kuwa katika uwanda wa chini karibu na Bahari ya Hindi. Hali hii hupunguza kasi na kufanya udongo kutuwama ndani ya mto na kusababisha mto kuhama.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea na kazi ya kunyoosha mto pamoja na kuimarisha kingo zilizoathiriwa kwa kuweka gabions na njia mbalimbali, ikiwemo upandaji wa miti pembezoni mwa mto na kwenye vyanzo vya maji, kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji, kuiwezesha jamii kutekeleza shughuli mbalimbali za kujipatia kipato ili kuondoka ndani ya vyanzo vya maji. Kuweka alama na mipaka na mabango ya makatazo ya kuzuia kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya vyanzo vya maji ili kurudisha uoto wa asili na kupunguza athari za mmomonyoko. Jitihada hizi zitaepusha mashamba katika eneo hilo kuathiriwa na maji ya mto Ruvu.
MHE. ANNE K. MALECELA aliuliza: -

Je, Serikali haioni umuhimu wa kujenga mradi mpya wa maji safi na salama kuliko kuendelea na ukarabati wa Mradi wa Kata ya Kihurio ambao ulijengwa mwaka 1967?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anne Kilango, Mbunge wa Same Mashariki kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali ni kujenga mradi mkubwa utakaoondoa kabisa tatizo la maji katika Kata ya Kihurio ambapo kwa sasa usanifu unaendelea na ujenzi utafanyika katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Aidha, katika kupunguza kero ya uhaba wa maji, Serikali kushirikiana na Jumuiya ya Watumiaji Maji inaendelea kufanya ukarabati mdogo wa miundombinu ya maji kwenye Kata ya Kihurio. (Makofi)
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itamaliza tatizo la maji kwenye Mji Mdogo wa Laela na Mpui katika Jimbo la Kwela?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji Mdogo wa Laela ni 51%. Ili kuboresha huduma ya maji Laela kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imeendelea na upanuzi wa Mradi wa Maji wa Laela na kazi zinazofanyika ni pamoja na ulazaji wa mabomba yenye urefu wa kilometa 2.6 na ukarabati wa tenki lenye ujazo wa lita 225,000.

Aidha, kwa upande wa Kata ya Mpui yenye vijiji vya Mpui A na Mpui B wananchi wanapata maji kupitia chanzo cha mserereko na kisima na hali ya huduma ya maji ni 36%. Ili kupunguza kero ya maji Kata ya Mpui katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itachimba kisima kirefu kimoja.

Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mrefu wa kumaliza tatizo la maji katika Mji Mdogo wa Laela na Kata ya Mpui, kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itajenga mradi mkumbwa utakaotumia chanzo cha Ziwa Tanganyika au Mto Momba. Kwa sasa usanifu wa mradi huo unaendelea.
MHE. BENAYA L. KAPINGA K.n.y. MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kukarabati miundombinu ya maji katika Kata za Jimbo la Arumeru Mashariki?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Arumeru hali ya huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ni asilimia 71.5 huduma hii inapatikana kutoka kwenye skimu 39 zilizojengwa kabla ya mwaka 2000. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imeendelea na ukarabati wa miundombinu ya miradi ya maji kwenye skimu za Kikwe-Msitu wa Mbogo, Kata ya Kikwe na Mbuguni Olkungabo - Ngabobo (Kata ya Ngarenanyuki na Ngabobo na Ngurdoto-Sakila - Ngyeku Kata za Imbaseni, Maji ya Chai na Kikatiti. Kazi hii itakamilika Mwezi Juni, 2022. Aidha, katika kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji, miradi mipya itajengwa kwa ajili ya kutoa huduma kwenye Kata za Nkoarisambu na Akheri ambapo kazi hii itakamilika Septemba, 2022.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2022/ 2023, ukarabati wa miundombinu ya maji utaendelea ili kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji katika Kata zote inakuwa endelevu.
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka maji ya Ziwa Victoria kwenye Kata 24 zilizopo katika Tarafa tatu Wilayani Kishapu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Nyangindu Butondo, Mbunge wa Jimbo la Kishapu kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha wananchi katika maeneo ya Mijini na Vijijini wanapata huduma ya uhakika ya maji safi na salama.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/ 2023, kazi itaendelea kuhakikisha Kata 24 za Wilaya ya Kishapu zinapata huduma ya maji safi na salama na kufikia lengo la asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, mpango wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria kutoka Bunda Mjini kwenda Vijiji 33 vya Tarafa ya Chamriho umefikia hatua gani?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniface Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuboresha huduma ya maji katika Tarafa ya Chamriho ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022 inatekeleza ujenzi wa miradi mipya mitatu ya KirolerI - Kambubu, Mariwanda na Sanzate pamoja na ukarabati wa mradi wa maji wa Nyang’aranga ambayo itatoa huduma ya maji kwa wananchi wapatao 12,648.

Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali ni kuhakikisha Wananchi wa tarafa ya Chamriho wanapata huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza. Katika kutimiza lengo hilo, taratibu za kumwajiri Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa mradi wa maji wa kutoka Ziwa Victoria zinaendelea. Matarajio ni kuanza ujenzi wa mradi katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. FLATEI G. MASSAY aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya kujenga mabwawa katika Jimbo la Mbulu Vijijini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Gregory Massay, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutekeleza miradi ya maji katika Wilaya ya Mbulu Vijijini kwa lengo la kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji. Katika Mwaka wa Fedha 2021/2022, ujenzi wa miradi ya maji ya visima virefu kwenye vijiji vya Ng’orati, Maretadu Juu, Labay, Genda, Masqaroda, Mewadani, miradi ya maji ya Singu na ukarabati wa visima katika vijiji vya Domanga, Eshkesh unaendelea. Miradi hiyo itakamilika Septemba, 2022 na itaboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Mbulu Vijijini kutoka asilimia 61 hadi kufikia asilimia 76 ifikapo Desemba, 2022.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa mabwawa hasa katika maeneo kame unalenga kukusanya maji yaweze kutumika wakati wa kiangazi ili kuhakikisha shughuli za kilimo na ufugaji zinaimarika.

Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali itaendelea kuainisha maeneo ya ujenzi wa malambo na mabwawa madogo katika Wilaya ya Mbulu Vijijini ili kukusanya maji kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza: -

Je, ni lini mradi wa maji wa Tukuyu utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anton Albert Mwantona Mbunge wa Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imeendelea kutekeleza mradi wa maji wa Tukuyu Mjini ambapo kazi zilizopangwa ni pamoja na uhifadhi wa chanzo, ulazaji wa bomba kuu Kilometa 9.5, ulazaji wa mabomba ya usambazaji Kilometa 20 na ujenzi wa tenki la ukumbwa wa lita 1,500,000.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa kazi zilizofanyika ni pamoja na uboreshaji wa chanzo cha maji na ulazaji wa bomba kuu lenye urefu wa Kilometa tatu.

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi huo ulianza mwezi Septemba, 2021 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Machi, 2023. Mradi huo utasaidia kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Tukuyu kutoka asilimia 67 na kufika asilimia 90.
MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Mradi wa Maji wa Kintinku- Lusilile katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Maji Kintinku-Lusilile ni mradi uliopangwa kuhudumia Vijiji 11 vya Chikuyu, Mwiboo, Mbwasa, Makutupora, Mtiwe, Chilejeho, Maweni, Mvumi, Ngaiti, Kintinku na Lusilile. Mradi huo unatekelezwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ilikamilika mwezi Oktoba, 2021 na Vijiji vitatu vya Chikuyu, Mwiboo na Mbwasa vinapata huduma ya maji. Katika mwaka wa fedha 2022/ 2023, utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi unaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba, 2022 na kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji katika vijiji vyote 11.
MHE. GHATI Z. CHOMETE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kumaliza tatizo la ukosefu wa maji katika Wilaya za Mkoa wa Mara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ghati Zephania Chomete Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Mara kwa sasa ni wastani wa asilimia 66 vijijini na asilimia 71 mijini. Katika kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Mara, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi mikubwa miwili ya Mugango, Kyabakari hadi Butiama na mradi wa maji Bunda ambayo itanufaisha Wilaya za Butiama, Musoma na Bunda za Mkoa wa Mara. Aidha, utekelezaji wa mradi wa Miji 28 unatarajiwa kuanza katika mwaka huu wa fedha ambapo Wilaya za Serengeti, Tarime na Rorya zitanufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza miradi mingine 72 katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara. Kukamilika kwa miradi yote kutaboresha huduma ya maji kufikia lengo la asilimia 85 vijijini na asilimia 95 mijini ifikapo 2025.
MHE. NEEMA K. LUGANGIRA aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha shule zote nchini zinapata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Neema Kichiki Lugangira, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuhakikisha huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza inapatikana kwenye shule na vituo vya afya kote nchini. Katika kutimiza azma hiyo, Wizara inaendelea na zoezi la kubainisha shule na vituo vya afya vyenye changamoto ya huduma ya maji, kazi itakayokamilika mwezi Juni, 2022. Baada ya kukamilika kwa zoezi hilo, kuanzia mwaka 2022/ 2023, Serikali itatekeleza mpango maalum wa miaka mitatu wa kupeleka huduma ya maji kwenye taasisi hizo.
MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itakomesha shughuli za ukataji miti, kilimo na ujenzi karribu na vyanzo vya maji ili kulinda vyanzo vya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji Na.11 ya mwaka 2009. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imekamilisha uandaaji wa Mipango ya Muda Mrefu ya Kuhifadhi Vidakio vya Maji (Catchment Conservation Plans) katika mabonde yote tisa nchini. Mipango hiyo imeweka dira, vipaumbele na utaratibu mzuri wa utunzaji wa vyanzo vya maji katika maeneo ya vidakio vya maji na mipango hiyo itatekelezwa hadi mwaka 2035.

Mheshimiwa Spika, Serikali katika kuhakikisha inakomesha shughuli za ukataji miti kilimo na ujenzi karibu na vyanzo vya maji, hadi sasa jumla ya vyanzo vya maji 191 vimewekewa mipaka ikiwa ni hatua za kuzuia shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo na vyanzo 44 vipo katika hatua ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili vilindwe kisheria. Vilevile, jumla ya Jumuiya za Watumia Maji 162 zimeanzishwa katika maeneo ya vyanzo vya maji ili kuwashirikisha wananchi katika shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, elimu ya utunzaji wa vyanzo vya maji itaendelea kutolewa kwa wananchi ili wafanye shughuli za kiuchumi katika maeneo ambayo hayana athari kwa vyanzo vya maji na mazingira kwa ujumla.
MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka mradi wa maji safi na salama katika Kata ya Rabour?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege Mbunge wa Rorya kama ifuatavyo: -

Mheshimwa Spika, Kata ya Rabour ina jumla ya Vijiji vitatu vya Oliyo, Rabour na Makongoro. Vijiji vya Oliyo na Rabour vinapata huduma ya maji kupitia visima virefu. Katika kuboresha huduma ya maji katika Kata ya Rabour (Kijiji cha Rabour), Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 inatekeleza mradi wa maji katika kijiji hicho. Kazi zilizopangwa kutekelezwa ni ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 225,000 na ujenzi wa mtandao wa usambazaji maji wenye urefu wa kilometa 12.8. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2022 na utanufaisha wananchi wapatao 4,792.

Mheshimwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika Vijiji viwili vya Oliyo na Makongoro. Kukamilika kwa miradi hiyo kutaboresha huduma ya maji safi na salama katika Kata yote ya Rabour.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -

Je, ni lini mradi wa visima vitatu katika Kijiji cha Turuki utakamilika kwa ajili ya kupeleka maji Liwale Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mohamedi Kuchauka, Mbunge wa Liwale kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma ya maji katika Mji wa Liwale katika mwaka wa fedha wa 2022/2023 Serikali imechimba visima vitatu katika Kijiji cha Turuki. Visima hivyo kwa pamoja vina uwezo wa kuzalisha lita 1,008,000 kwa siku na vitaongeza uzalishaji wa maji kutoka lita 1,200,000 kwa siku hadi kufikia lita 2,208,000 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, usanifu kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya usambazaji maji hayo ulikamilika mwezi Machi, 2023 na ujenzi umepangwa kutekelezwa na kukamilika katika mwaka wa fedha 2023/2024. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na ulazaji wa mtandao wa bomba umbali wa kilomita 78 na ujenzi wa matanki mawili (2) yenye ujanzo wa lita 1,300,000.
MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya kukamilisha Ujenzi wa Mradi wa maji Tukuyu Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Suma Ikenda Fyandomo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Maji Tukuyu Mjini ni wa miaka miwili na ulianza mwezi Agosti, 2021 na unatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2023. Hadi sasa utekelezaji unaendelea na umefikia asilimia 82. Kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa banio katika chanzo, ulazaji wa bomba kuu lenye urefu Kilomita 9.5, ujenzi tanki moja lenye ujanzo wa lita milioni 1.5 na ulazaji wa mtandao wa bomba wa umbali kilomita 20.
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Bwawa la Mandela Kwenjugo na Kamkole Mabanda?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Reuben Nhamanilo Kwagilwa Mbunge wa Handeni Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma ya maji Wilayani Handeni, Serikali ipo kwenye hatua za mwisho za usanifu wa Mabwawa ya Mandela – Kwenjugo na Kamkole – Mabanda na usanifu huo utakamilika mwezi Juni, 2023. Ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2023/2024. Kukamilika kwa ujenzi wa mabwawa hayo kutanufaisha wananchi wapatao 11,004 wa mitaa ya Mabanda, Komoza, Kwenjugo, Ngugwini, Bwila, Kwedisewa na Kwedigongo.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali isiingize gharama za mita za maji kwenye vitabu vyao vya fedha badala ya kuweka pale inapounganishwa maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Jimbo la Vunjo kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, jukumu la Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na dira za maji na kuwafungia wateja wanaoomba huduma za maji. Kwa kutambua changamoto za uunganishaji wa maji kwa wateja hususani kwenye suala la dira, Serikali imeandaa mwongozo wa ugharamiaji wa maunganisho ya maji vijijini ambao pia utajumuisha suala la dira za maji kuwa ni sehemu ya gharama za Serikali. Mwongozo huo utaanza kutumika mwezi Julai, 2023.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa maji wa Kyerwa, Nyaruzumbura, Nyakatuntu hadi Kamuli Wilayani Kyerwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Sebba Bilakwate Mbunge wa Jimbo la Kyerwa kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itakamilisha usanifu wa miradi ya maji Wilayani Kyerwa mwezi Mei, 2023 na baadae kufuata taratibu za manunuzi ya Wakandarasi. Ujenzi wa miradi utaanza mwezi Septemba, 2023 na utanufaisha jumla ya vijiji 20 vikiwemo Vijiji vya Kyerwa, Nyaruzumbura, Nyakatuntu na Kamuli.
MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza kujenga Mradi wa Maji katika Vijiji vya Sawala, Mtwango, Rufuna na Kibao vilivyopo Mufindi Kusini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Grace Tendega, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika Kata ya Mtwango, na miradi imekamilika kwenye Vijiji vya Sawala na Mtwango. Kwa sasa miradi inaendelea katika Vijiji vya Rufuna na Kibao ambapo utekelezaji umefikia asilimia 52. Kazi zinazoendelea ni pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa Kilometa 21, ujenzi wa matenki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 450,000 na vituo 21 vya kuchotea maji. Utekelezaji wa kazi hizo utakamilika mwezi Julai, 2023 na wananchi kupata huduma ya maji safi na salama.
MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatatua tatizo la ukosefu wa maji katika Jimbo la Mbogwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicodemus Henry Maganga Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani Mbongwe ni wastani wa asilimia 55. Katika kupunguza kero ya maji kwa wananchi wa Wilaya hiyo, Serikali ina mipango ya muda mfupi na muda mrefu, ambapo Katika mpango wa muda mfupi Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji ya Iponya, Kagera, Kanegere na Lugunga-Luhala. Miradi hiyo imeanza kutoa huduma kwa wananchi. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itachimba visima virefu 28 sambamba na kufanya upanuzi wa miradi ya maji ya Lulembela, Kagera, Kanegere na ujenzi wa miradi mipya ya maji katika vijiji vya Kisumo, Nyang’holongo, Ikobe, Ngemo, Bwendamwizo, Isebya, Ushirika, Mlale, Kadoke, na Mpakali. Kukamilika kwa Miradi hiyo kutaongeza huduma ya maji kufikia wastani wa asilimi 75.

Mheshimiwa Spika, mpango wa muda mrefu ni kutekeleza mradi mkubwa wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda Wilaya ya Mbogwe ambapo usanifu wa mradi huo unaendelea na utakamilikaji katika mwaka wa fedha 2023/2024 na ujenzi kuanza.
MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka Mradi wa Maji katika Kijiji cha Nkundi – Nkasi Kusini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Kijiji cha Nkundi kinapata huduma ya maji kupitia Mradi wa Maji wa Bwawa la Kawa uliojengwa mwaka 2016. Hata hivyo, huduma ya maji kwenye kijiji hicho ilisimama kutokana na changamoto za kiuendeshaji zilizosababishwa na gharama za kusukuma maji kulingana na uwezo wa wananchi. Katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali imechukua hatua ya kuunganisha Chombo cha Watumiaji Maji Ngazi ya Jamii (CBWSO) cha kijiji hicho na vijiji vingine viwili vya Kipande na Kantawa ili kumudu gharama za uendeshaji. Tayari maji yameanza kusukumwa na kazi inayoendelea sasa ni kukarabati mabomba kwenye maeneo yaliyopasuka. Baada ya kazi hiyo, wananchi 4,540 wa Kijiji cha Nkundi wataendelea kupata huduma ya maji.
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, lini ahadi ya kupeleka mradi mkubwa wa maji Tunduma utatekelezwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua tatizo la maji linaloukabili Mji wa Tunduma na hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali inakarabati miradi ya Uhuru, Nyerere, Ipito, Tunduma na miundombinu ya maji safi Mjini Tunduma. Ukarabati huo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2023 na kunufaisha wakazi 37,853 katika Mji wa Tunduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Serikali itaanza kutekeleza mradi mkubwa wa maji kupitia chanzo cha Mto Momba na kwa sasa taratibu za kuajiri Mkandarasi zinaendelea. Kukamilika kwa mradi huo kutaondoa tatizo la upatikanaji wa huduma ya maji katika Mji huo.
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga miradi ya maji katika Vijiji vya Mateka, Tukuzi, Kitelea na Sepukila Wilayani Mbinga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Wilayani Mbinga ambapo kwa Vijiji vya Kitelea na Sepukila utekelezaji wa miradi ya maji unaendelea na utakamilika mwezi Juni, 2023. Aidha, kwa Kijiji cha Tukuzi usanifu umekamilika na kwa Kijiji cha Mateka usanifu utafanyika katika mwaka wa fedha 2023/2024 na ujenzi wa miradi ya maji kwenye vijiji hivyo utafanyika katika mwaka wa fedha 2023/2024.
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA aliuliza: -

Je, ni lini wananchi wa Mji Mdogo Gairo watapata maji ya kutosha?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Christine Gabriel Ishengoma, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua tatizo la maji linaloukabili Mji wa Gairo na jitihada zinaendelea kuchukuliwa ili kupunguza adha ya maji kwa wakazi wa Mji huo. Jitihada zinazofanyika ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu viwili na sasa mkandarasi yupo eneo la mradi anaendelea na kazi. Vilevile, Serikali itafanya ukarabati wa mradi wa maji ya mserereko Gairo, Mkandarasi ameajiriwa na kazi inayoendelea ni mapitio ya mradi na ujenzi utaanza mwezi Juni, 2023.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango wa muda mrefu ni kutumia chanzo cha Mto Chagongwe utakaohudumia wananchi wa Mji wa Gairo na kwa sasa Wizara inaendelea kufanya usanifu na ujenzi utafanyika katika Mwaka wa Fedha 2023/2024.
MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka maji katika Vijiji 62 Jimbo la Newala Vijijini ambavyo havina huduma ya maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Maimuna Salum Mtanda, Mbunge wa Jimbo la Newala Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Newala ina jumla ya vijiji 155 na kati yake vijiji 77 vinapata huduma ya maji. Serikali inaendelea na jitihada za kupeleka huduma ya maji kwenye vijiji visivyo na huduma na katika mwaka wa fedha 2022/2023 miradi 12 inaendelea kutekelezwa ukiwemo mradi mkubwa wa Makonde. Kukamilika kwa miradi hiyo kutanufaisha vijiji 61. Aidha, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itafanya usanifu wa miradi ya maji katika vijiji 17 vilivyobaki ikifuatiwa na utekelezaji.
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -

Je, lini fedha itatengwa kufanya usanifu na upembuzi yakinifu wa Mradi wa kutoa maji Ziwa Nyasa kupeleka Tarafa ya Masasi – Ludewa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Zacharius Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Masasi Wilaya Ludewa ina jumla ya vijiji 15, ambapo vijiji 12 vinapata huduma ya maji na vijiji viwili vya Igalu na Kiyogo utekelezaji wa miradi unaendelea na unatarajia kukamilika mwezi Juni, 2023.

Mheshimiwa Spika, mojawapo ya vipaumbele vya Wizara kwa mwaka 2023/2024 ni kusanifu na kutekeleza miradi ya maji kwa kutumia vyanzo vya uhakika ikiwemo maziwa makuu, kupeleka maji kwenye maeneo yenye uhaba pamoja na vijiji vilivyomo pembezoni mwa maziwa hayo. Kwa upande wa Ziwa Nyasa, fedha za awali zimeshatengwa kwa ajili ya usanifu na tathmini ya athari za kimazingira na kijamii ambapo vijiji vya Tarafa ya Masasi Wilayani Ludewa vitanufaika na miradi ya maji kupitia chanzo hicho.
MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza: -

Je, maeneo mangapi yameshabainishwa kuwa ni vyanzo vya maji salama ardhini na hatua gani zinachukuliwa kulinda maeneo hayo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shally Josepha Raymond, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara kupitia Bodi za Maji za Mabonde nchini na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ina jukumu la kutambua, kutunza, kuhifadhi na kuendeleza vyanzo vya maji vya juu ya ardhi na chini ya ardhi pamoja na kutambua uwezo wa chanzo na ubora wa maji yake. Hadi sasa vyanzo vya maji chini ya ardhi vilivyotambuliwa ni 152 na kati yake, vyanzo 30 vimewekewa mipaka na vyanzo 10 vimetangazwa kwenye gazeti la Serikali na hivyo kulindwa kisheria. Vilevile, Wizara inaendelea kufanya utafiti katika maeneo mengine 172 yenye maji chini ya ardhi ili kubaini uwezo wa chanzo na ubora wa maji yake.

Aidha, Serikali kupitia maabara za maji nchini hufanya ufuatiliaji wa mwenendo wa ubora wa maji chini ya ardhi kupitia visima vya uchunguzi vilivyochimbwa kwenye maeneo mbalimbali nchini. Sampuli za maji huchukuliwa kutoka visima hivyo na kufanyiwa uchunguzi na pale inapothibitika kuwepo kwa mabadiliko ya mwenendo wa ubora hatua stahiki huchukuliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali kulinda maeneo yaliyotambuliwa kuwa vyanzo vya maji chini ya ardhi ikiwemo kuyawekea mipaka na kuyatangaza kwenye gazeti la Serikali kuwa maeneo tengefu, pamoja na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzani na uhifadhi wa maeneo husika.
MHE. DKT. DAVID M. DAVID aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kutatua tatizo la uhaba wa maji tambarare ya Same wakati ukisubiriwa Mradi wa Maji wa Mwanga – Same hadi Korogwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. David Mathayo David, Mbunge wa Same Magharibi kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, wakati utekelezaji wa mradi mkubwa wa Same – Mwanga – Korogwe unaendelea na unaotarajia kukamilika mwezi Juni, 2024 na kunufaisha baadhi ya maeneo ya Wilaya za Same, Mwanga na Korogwe, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua changamoto ya maji kwa wananchi wa Wilaya ya Same. Mathalani katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imekamilisha miradi ya maji katika Vijiji vya Kirinjiko, Mabilioni Kijomo na Gunge na tayari inatoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi. Aidha, visima vitatu vimechimbwa katika eneo la Mahuu kwa ajili ya kuhudumia eneo la Same Mjini ambapo kwa jumla vina uwezo wa kuzalisha jumla ya lita 720,000 kwa siku.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2023/2024, Serikali itafanya utafiti wa maji chini ya ardhi pamoja na kuchimba visima virefu viwili katika maeneo ya Same Mjini na Kijiji cha Marondwe, Njoro ili kuongeza vyanzo zaidi vya maji. Utekelezaji wa visima hivyo unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2024 mara baada ya uchimbaji kukamilika na maji kupatikana.
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y. MHE. AMANDUS J. CHINGUILE aliuliza:-

Je lini maji safi na salama yatapelekwa katika Kata za Kiegei, Kilimarondo, Matekwe na Namapwia – Nachingwea?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Amandus Julius Chinguile, Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu spika, katika kuhakikisha Kata za Kiegei, Kilimarondo, Matekwe na Namapwia zinapata huduma ya majisafi na salama na yenye kutosheleza, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 itafanya utafiti wa maji chini ya ardhi (Hydrogeological Survey) pamoja na kuchimba visima virefu vinne katika kata hizo. Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika na kukamilika mwezi Disemba, 2023. Uendelezaji wa visima hivyo utafanyika mara baada ya uchimbaji kukamilika na maji kupatikana.
MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka huduma ya maji ya DAWASA katika Kata za Buza, Vituka, Makangarawe na Sandali - Temeke?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dorothy George Kilave, Mbunge wa Jimbo la Temeke, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha wananchi wa Kata za Buza, Vituka, Makangarawe na Sandali katika Manispaa ya Temeke wanapata huduma ya maji, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Usambazaji Maji wa JET-Buza ambao hadi kufikia mwezi Agosti, 2023, utekelezaji umeweza kufikia asilimia 30 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Mradi huo utanufaisha wananchi zaidi ya 173,810 wa Kata hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika kuboresha huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 itaanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji utakaonufaisha Jimbo la uchaguzi la Temeke, Kata za Buza, Vituka, Makangarawe na Sandali pamoja na Majimbo mengine matano ya uchaguzi ya Kibamba, Ubungo, Kinyerezi, Ukonga na Ilala. Kazi zilizopangwa kufanyika ni pamoja na ujenzi wa tenki la lita milioni tisa eneo la Bangulo na ulazi wa mtandao wa mabomba wa umbali wa kilometa 124. Mradi huo unatarijiwa kukamilika ifikapo Desemba, 2024.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kutekeleza mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwenda vijiji na vitongoji vya Kata za Nguvumoja, Lugubu na Itumba – Igunga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Igunga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu spika, katika jitihada za kuboresha huduma ya maji safi na salama kwenye Kata za Nguvumoja, Lugubu na Itumba zilizopo Wilaya ya Igunga, Serikali inatekeleza mipango ya muda mfupi na muda mrefu, ambapo katika mpango wa muda mfupi kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itafunga pampu za kutumia Nishati ya umeme jua katika visima virefu vya Vijiji vya Nguvumoja, Mwanshoma, Lugubu na Itumba ili kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji na kupunguza gharama za uendeshaji wa miradi hiyo.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, Serikali imepanga kufanya utafiti wa maji ardhini na kuchimba kisima kirefu katika Kijiji cha Chagana kilichopo Kata ya Lubugu katika kipindi cha Mwezi Desemba, 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa muda mrefu, Serikali itaboresha huduma ya maji safi na salama na yenye kutosheleza katika Kata za Nguvumoja, Lugubu na Itumba – Igunga kwa kutumia mradi wa maji wa Ziwa Victoria ambapo upembuzi yakinifu na usanifu wake wa kina umekamilika na utaanza utekelezaji mara fedha zitakapopatikana.
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka maji safi na salama katika Kata ya Kwekanga?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shabani Omari Shekilindi, Mbunge wa Jimbo la Lushoto, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua adha ya maji wanayoipata wakazi wa Kata ya Kwekanga yenye Vijiji vitano vya Kwekanga, Mziragembei, Bombo-Kamghoboro, Mategho na Mshangai. Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali katika Mwaka wa fedha 2023/2024, itafanya utafiti wa maji chini ya ardhi (Hydrogeological survey) pamoja na kuchimba visima virefu katika Kata za Kwekanga, Kwai, Kilole, Malindi, Makanya na Lushoto Mjini. Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika na kukamilika mwezi Disemba, 2023. Uendelezaji wa visima hivyo utafanyika mara baada ya uchimbaji kukamilika na maji kupatikana.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA K.n.y. MHE. HALIMA J. MDEE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha usambazaji wa maji Mitaa yote ya Kata za Mbezi Juu, Wazo na Mabwepande katika Jimbo la Kawe?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima James Mdee, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuboresha huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa maeneo ya Kawe, Kata za Mbezi Juu, Wazo na Mabwepande. Hadi kufikia mwezi Desemba, 2022, kazi ya ulazaji wa mtandao wa mabomba ya kusambaza maji umbali wa kilometa 391.306 ilikamilika kupitia mradi mkubwa chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi inayoendelea sasa ni ulazaji wa mabomba ya maji umbali wa kilometa 64.3 kuanzia ulipoishia mradi mkubwa kwenda maeneo ya Mpiji Magohe, Mbopo, Mbopo Chekanao na Kinondo na itakamilika mwezi Desemba, 2023.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilika kwa kazi hiyo, maeneo yote katika Kata za Mbezi Juu, Wazo na Mabwepande yatakuwa yamepata huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza.

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatoa bei moja elekezi kwa kila unit moja ya maji Wilayani ya Karatu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Awack Tlemai, Mbunge wa Jimbo la Karatu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, huduma ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Karatu inatolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (Karatu Urban Water Supply and Sanitation Authority - KARUWASA). Awali kulikuwa na changamoto ya kuwepo kwa Taasisi mbili zinazotoa huduma ya maji ambazo ni Karatu Village Water Supply (KAVIWASU) na KARUWASA na kila moja ilikuwa na bei yake. Mwezi Agosti 2022, Serikali iliziunganisha taasisi hizo na kuwa na taasisi moja inayoitwa KARUWASA na kutoa bei elekezi ya maji ya shilingi 1,300 kwa unit moja.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa eneo la Karatu Vijijini linalohudumiwa na RUWASA, Serikali ilitoa bei elekezi kulingana na teknolojia inayotumika kuwafikishia wananchi maji na bei hizo zinafuatwa.
MHE. ESTHER L. MIDIMU aliuliza:-

Je, lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya mradi wa maji Sumve, Malya na Malampaka baada ya kukamilika kwa upembuzi yakinifu?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Lukago Midimu, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa miradi ya maji Sumve, Malya na Malampaka kupitia chanzo cha maji cha Ziwa Victoria. Mji wa Sumve utapata maji kupitia mradi wa maji Ukirugulu – Usagala – Kolomije hadi Sumve. Mkandarasi yupo eneo la mradi anaendelea na kazi. Aidha, Miji ya Malya na Malampaka itapata maji kupitia mradi wa maji wa Hungumalwa na Mkandarasi ameajiriwa mwezi Mei, 2023.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 2.5 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo, na Serikali itaendelea kutenga fedha kila mwaka hadi kukamilika kwa miradi hiyo.
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka fedha za utekelezaji wa Miradi ya Maji katika maeneo ya Mkunda Kaengesa, Kaoze Group na Ilemba Kwela?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza utekelezaji wa miradi ya maji ya Mkunda Group, Kaoze Group na Ilemba. Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kunufaisha wananchi wa vijiji vya Mkunda, Kaengesa A, Kaengesa B, Kianda, Ilemba A, Ilemba B, Kaswepa na Kaoze.
MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza:-

Je, lini Serikali italeta mradi wa kuhifadhi Mazingira katika chanzo cha maji cha Mto Ruaha na shamba la miti la Sao Hill?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inatambua umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo chanzo cha Mto Little Ruaha kilichopo kwenye Shamba la Miti la Sao Hill. Mto huo ni chanzo cha maji kwa wananchi wa Mji wa Iringa na viunga vyake na unatumika kwa shughuli za uzalishaji umeme, ufugaji na kilimo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jitihada mbalimbali za kutunza vyanzo hivyo zinaendelea ikiwemo kuanzisha Jumuiya nne za Watumia Maji Wilaya za Mufindi, Kilolo na Iringa; kutoa elimu ya uhifadhi wa vyanzo; na kutekeleza program ya kupanda miti rafiki na maji ambapo miti 3,000 imepandwa katika halmashauri hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara inaandaa Mpango wa Uhifadhi wa Vidakio wa mwaka 2021 hadi 2035. Kwa kupitia mpango huo, katika Mwaka wa Fedha 2023/2024, Serikali imepanga kuweka alama ya mipaka ya kudumu katika chanzo cha Mto Little Ruaha ndani ya Shamba la Miti la Sao Hill; kuweka mabango yenye jumbe za katazo za shughuli za binadamu katika chanzo cha uhifadhi wa chanzo; kupanda miti rafiki na maji; kutoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi endelevu wa vyanzo vya maji na mazingira; na kuajiri walinzi wa kulinda vyanzo vya maji kwenye shamba hilo hususani kwenye maeneo yenye uharibifu.
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Mabwawa katika Mito Ghona, Rau na Deu ili kupunguza athari za mafuriko?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mito ya Ghona, Rau na Deu inapitisha maji kiasi cha lita 103,310 kwa sekunde (sawa na mita za ujazo 267,940.21 kwa siku) ambapo Mto Rau ni lita 98,000 kwa sekunde, Mto Dehu Lita 3,100 sekunde na Mto Ghona ni lita 2,210 kwa sekunde. Mito hiyo hupeleka maji yake katika Mto Ruvu na hatimaye kufika katika Bwawa la Nyumba ya Mungu. Serikali kupitia Bodi ya Maji Bonde la Pangani imeshafanya upembuzi wa awali na kubaini kuwa sehemu ya maji ya mito hiyo haifiki kwa wakati kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu na badala yake husambaa na kuacha mkondo wake na kuathiri wananchi kandokando ya mito hiyo ikiwemo Vijiji vya Chekereni na Kileo kupitia Mto Ghona; maeneo ya Majengo, Msaranga, Mabogini, Oria, Ngasini, Mandakamnono yanayoathiriwa na Mto Rau; na Vijiji vya Mongalia, Soko, Ngaseni na Kiterini huathiriwa pia kupitia Mto Deu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sababu kubwa ya maji ya mito hiyo kusambaa ni kutokana na kuharibika kwa kingo za mito husika katika maeneo ya tambarare kunakosabisha maji kutoka katika mikondo yake na kusambaa katika maeneo wanayoishi wananchi. Serikali imeanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na ufukuaji wa mikondo ya mito katika baadhi ya maeneo korofi ya mito hiyo na kazi ya ufukuaji itaendelea katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 mpaka itakapokamilika. Aidha Bonde la Pangani litafanya tathimini kwenye maeneo yanapitiwa na mito hiyo ili kubaini kama kuna uwezekano wa kujenga mabwawa bila kuathiri upatikanaji wa maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo linatumika katika shughuli nyingi za kijamii na kiuchumi.
MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:-

Je, ni lini Wananchi wa Mpiji – Magohe, Kibesa, Msumi, Makabe, Msingwa, Ukombozi na Goba watapata majisafi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Jumanne Mtemvu, Mbunge wa Kibamba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ukamilishaji wa Miradi ya Maji ya Changanyikeni - Bagamoyo, ujenzi wa matenki ya maji katika maeneo ya Mshikamano, Tegeta A, Malolo na mradi wa usambazaji maji kusini mwa Dar es Salaam ambapo kukamilika kwa miradi hii kutawezesha wakazi wa maeneo ya Mpiji-Magohe, Kibesa, Msumi, Mbezi, Makabe, Msakuzi, Msingwa, Ukombozi, King'azi, Malamba Mawili, Msingwa, Kipesa Mapwepande, Mpakani na Goba kupata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza.
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-

Je, upi mpango wa Serikali kumaliza kero ya upatikanaji wa maji safi na salama Wilayani Ukerewe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Jimbo la Ukerewe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ukerewe ina jumla ya vijiji 76, kati ya vijiji hivyo 37 vinapata huduma ya maji safi na salama. Aidha, katika mwaka 2022/2023, Serikali inatekeleza miradi katika vijiji vingine 26 na inatarajia kukamilisha miradi hii mwezi Julai, 2023.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itajenga miradi ya maji kwenye vijiji 13 vilivyobaki ambapo ni Bugula, Kameya, Halwego, Chamuhunda, Mukunu, Bugorola, Kamasi, Busumba, Kaseni, Bukonyo, Busagami, Msozi na Kweru. Kukamilika kwa miradi hiyo kutaondoa kero ya maji Wilaya ya Ukerewe na wananchi wote watapata huduma ya maji safi, salama na yenye kutosheleza. (Makofi)
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza: -

Je, Serikali ina mipango gani ya kuliendeleza Bonde la Mto Ruvu kwa kushirikiana na wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Michael Costantino Mwakamo, Mbunge wa Kibaha Vijiji kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza Mpango wa Uhifadhi vidakio vya Maji wa mwaka 2021-2035 ambao unahusisha ushirikishwaji wa wadau mbalimbali ikiwemo wananchi. Kupitia mpango huo, jamii inaelimishwa kuhusu umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji ambapo zimeundwa Jumuiya za Watumia Maji 11 na kupitia Jumuiya hizo, wananchi wanashiriki moja kwa moja kulinda na kutunza rasilimali za maji kwenye maeneo yao. Vilevile, kupitia mpango huo, Bodi ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu inaendelea kujenga miundombinu ya kunyweshea mifugo ili isiendelee kunywa maji kwenye vyanzo vya maji hasa mitoni.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile kutafanyika uainishaji wa maeneo ya malisho na vivuko kwa ajili ya mifugo, na kuweka mipango ya pamoja ya matumizi bora ya ardhi hususani kwenye maeneo yanayohusisha vyanzo vya maji. Aidha, katika kuliendeleza Bonde la Wami Ruvu, kazi nyingine zinazotekelezwa kupitia mpango huo ni pamoja na kutambua maeneo ya uhifadhi wa vyanzo, kuyawekea mipaka na kuyatangaza kwenye Gazeti la Serikali kuwa maeneo tengefu ambapo hadi sasa maeneo 230 yametambuliwa, 13 yamewekewa mipaka na mawili yametangazwa kwenye Gazeti la Serikali.
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -

Je, ni lini Mkandarasi wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria kwenye Vijiji 33 vya Jimbo la Bunda ataanza kazi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Boniface Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeajiri Mtaalam Mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kwenda vijiji 33 vya Wilaya ya Bunda utakaokamilika mwezi Julai, 2023. Vilevile, Mtaalam Mshauri huyo ataandaa pia makabrasha ya zabuni kwa ajili ya kuajiri mkandarasi wa ujenzi atakayeanza kazi katika mwaka wa fedha 2023/2024. Aidha, katika kupunguza adha ya maji kwa wananchi wa Wilaya ya Bunda wakati wakisubiri mradi mkubwa, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali inaendelea kuboresha huduma ya maji Wilayani Bunda kwa kujenga miradi ya maji ya Kiroleri-Kambubu, Mariwanda na Hunyari. Miradi hiyo inatarajia kukamilika mwezi Julai, 2023.
MHE. ATHUMAN A. MAIGE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itachimba visima katika Shule ya Sekondari Ndono Uyui?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Athuman Almas Maige, Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, nia ya Serikali ni kuona maji yanapatikana kwa ajili ya matumizi ya jamii, maendeleo ya kiuchumi na mazingira. Shule ya Sekondari Ndono ilikuwa na changamoto ya maji, na katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepeleka maji shuleni hapo kupitia kisima kilichopo katika Zahanati ya Kijiji cha Ndono na sasa wanafunzi wanapata maji safi na salama. Aidha, Serikali imeanza maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa bomba la maji kutoka mradi wa Ziwa Victoria kwenda Wilaya za Urambo na Kaliua ambapo wananchi wa Kijiji cha Ndono ikiwemo wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ndono wataongezewa upatijanaji wa huduma ya maji.
MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, ni lini changamoto ya upatikanaji maji Mji wa Mlowo itatatuliwa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua adha ya maji wanayoipata wakazi wa Mji wa Mlowo ambapo hali ya upatikanaji wa huduma hiyo ni asilimia 49. Katika kukabiliana na hali hiyo, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali inatekeleza miradi mitatu ambayo ni Mradi wa Uboreshaji Huduma ya Maji Mlowo ambao umekamilika mwezi April 2023, na inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Upanuzi wa Mtandao wa maji Vwawa-Mlowo na Mradi wa Ukarabati wa Chanzo cha Maji Mwansyana na Mlowo. Miradi hii inatarajia kukamilika mwezi Septemba, 2023 na kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji Mlowo kufikia asilimia 65.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali imepanga kujenga miradi mingine miwili ambayo ni Mradi wa Maji kupitia chanzo cha Mto Mafumbo, na Mradi wa Maji wa Vwawa-Mlowo na Tunduma kupitia chanzo cha Mto Momba. Miradi hiyo ipo kwenye hatua ya manunuzi ya Wakandarasi na ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kutekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili. Kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha wakazi wa Mji Mlowo kupata huduma ya majisafi, salama na yenye kutosheleza.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA atauliza: -

Je, ni lini mradi wa maji Kata za Kaengeza na Kanda Sumbawanga Vijijini itakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kata ya Kaengesa ina vijiji vinne ambapo katika mwaka 2022/2023, Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa maji Mkunda Group utakaohudumia vijiji vya Mkunda, Kaengesa A na Kaengesa B. Mradi huo unatarajia kukamilika mwezi Septemba, 2023 na wananchi Kijiji cha Mkunda wameanza kupata huduma ya maji. Kwa Kijiji cha Itela, Serikali itafanya usanifu na kujenga mradi wa maji katika mwaka wa fedha 2023/2024.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Kata ya Kanda yenye vijiji vinne, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa maji utakaohudumia vijiji vya Lula na Chitete. Vijiji vinavyobaki vya Lyapona A na Lyapona B usanifu utafanyika katika mwaka wa fedha 2023/2024 na miradi kujengwa.
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA K.n.y. MHE. VENANT D. PROTAS aliuliza: -

Je, nini mpango wa kuweka miundombinu ya kuhifadhi maji ya mvua badala ya kusababisha mafuriko Kata za Loya na Miswaki?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Venant Daud Protas, Mbunge wa Jimbo la Igalula, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilifanya upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bwawa katika Kata ya Miswaki, lakini taarifa za kitaalam zilionesha eneo hilo kutokukidhi. Usanifu wa bwawa uliofanyika katika eneo la Kata ya Kizengi ulileta matokeo mazuri na Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa bwawa katika mwaka wa fedha 2023/2024. Kukamilika kwa bwawa hilo kutaboresha huduma ya maji kwenye vijiji kumi vya Kata za Loya, Miswaki na Kizengi. Aidha, wananchi wanaofanya shughuli za kilimo maeneo ya mabondeni wanashauriwa kuhama kipindi cha mvua kubwa.
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: -

Je, ni wananchi kiasi gani wa Wilaya ya Kyerwa wamefikiwa na huduma ya maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 Wilaya ya Kyerwa ina jumla ya wananchi 368,360 ambapo kati yao wananchi 209,965 sawa na asilimia 57 wananufaika na huduma ya maji kupitia skimu 26 za maji zilizopo. Aidha, katika mwaka fedha 2022/2023 Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji ya Runyinya - Chanya, Nyamiaga – Nyakatera - Kagu, Kimuli - Rwanyango na Chakalisa. Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2023 na kuongeza idadi ya wanufaika kufikia 265,219 sawa na asilimia 72 ya wananchi wa Wilaya ya Kyerwa.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali itaendelea kuboresha huduma ya maji Wilayani Kyerwa kwa kujenga miradi ya maji mipya ya Kikukuru - Mkunyu, Lubilizi, Businde - Nyakashenye, Bugara pamoja na kukarabati Mradi wa Maji Songembele. Kukamilika kwa miradi hiyo kutawezesha wananchi wote Wilayani Kyerwa kupata huduma ya maji safi, salama na ya kutosheleza. (Makofi)
MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Mradi wa Maji wa Tarafa ya Suba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Suba ina vijiji 17 ambapo kati yake vijiji 16 vinapata huduma ya maji kupitia Vyanzo vya Ziwa Victoria, visima virefu na visima vifupi. Hata hivyo, kulingana na jiografia sio vitongoji vyote kwenye vijiji hivyo vinafikiwa na huduma ya maji.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha wananchi wa vijiji hivyo 16 wanapata huduma ya maji salama na ya kutosheleza ikiwemo Wananchi wa Kijiji cha Kibui ambacho wananchi wake hawana maji, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2023/2024 itafanya usanifu wa mradi wa kutoa maji kwenye bomba kuu litakalopeleka maji Miji ya Tarime na Rorya ili kupeleka maji Vijiji vya Tarafa ya Suba. Baada ya kujengwa kwa mradi huo wananchi wote katika Tarafa ya Suba watapata huduma ya majisafi, salama na ya kutosheleza.
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya ukarabati wa miundombinu ya maji iliyochakaa na kusababisha upungufu wa maji – Chemba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Jimbo la Chemba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inafahamu changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya maji katika Wilaya ya Chemba na imeanza kuchukuwa hatua kwa Vijiji vya Humekwa na Mlongia ambapo manunuzi ya vifaa kwa ajili ya ukarabati yanaendelea. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itafanya usanifu na kufanya ukarabati wa miradi ya maji kwa Vijiji vya Njoeni Muone, Mtakuja, Bugenika, Msera, Mengu, Pangalua, Wahilo, Wisuzaje, Msaada na Mwailanje. (Makofi)
MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: -

Je, mchakato wa mradi wa kutoa maji Ziwa Tanganyika umefikia wapi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kutumia chanzo cha Ziwa Tanganyika kuwapatia wananchi wa Mkoa wa Rukwa huduma ya majisafi na salama. Usanifu kwa ajili ya kuwapatia wananchi maji katika vijiji 40 vya pembezoni mwa ziwa umekamilika na tayari wananchi kwenye vijiji tisa wanapata maji na miradi inaendelea kutekelezwa kwenye Vijiji vilivyobaki hatua kwa hatua. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali itaajiri mtaalam mshauri kwa ajili ya kufanya usanifu wa miradi ya maji kupitia chanzo cha Ziwa Tanganyika ili kunufaisha maeneo mengi zaidi Mkoani Rukwa.
MHE. HAMIS M. MWINJUMA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha matengenezo ya miundombinu ya usambazaji maji katika kata sita za Muheza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hamis Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Jimbo la Muheza, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka 2021/2022 inaendelea na ukarabati wa miundombinu ya maji katika kata sita za Muheza ambazo ni Mbaramo, Genge, Masuguru, Tanganyika, Majengo na Kwemkabala. Ukarabati huo unahusisha kazi ya kubadilisha bomba kuu lenye urefu wa kilomita Mbili na ukarabati wa bomba la usambazaji maji lenye urefu wa kilomita 14.5. Kazi hii itakamilika mwezi Oktoba, 2022.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Serikali imepanga kuendelea na ukarabati wa miundombinu katika Kata Sita za Mji wa Muheza ikiwa ni pamoja na kusambaza maji katika maeneo ambapo mtandao wa usambazaji maji haujafika kwenye Kata hizo.
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA aliuliza:-

Je, ni lini Mradi wa Maji kutoka Ziwa Basotu kwa ajili ya Vijiji zaidi ya tisa (9) utaanza kutekelezwa Wilayani Hanang’?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Samwel Xaday Hhayuma, Mbunge wa Jimbo la Hanang’, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa kutuma Ziwa Basotu kwa ajili kupeleka maji katika vijiji kumi vya Diling’ang, Wandela, Gawindu, Bassotu, Muungano, Milingori na Ming’enyi vilivyopo Wilaya ya Hanang. Utekelezaji wa awamu ya kwanza utanufaisha Kijiji cha Bassotu ambapo kazi zinazofanyika ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji, vituo 13 vya kuchotea maji, na ulazaji wa bomba lenye urefu wa kilometa 14. Mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai, 2022 na utanufaisha wananchi wapatao 16,553.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2022/2023 utekelezaji wa mradi huu wa maji utaendelea katika vijiji tisa vilivyobaki ili kuimarisha huduma ya upatikanaji wa maji kwa vijiji vyote.
MHE. MOSHI S. KAKOSO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji katika Kata ya Katuma ambayo ndiyo inatunza chanzo cha maji cha Mto Katuma?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Moshi Selemani Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inatekeleza mradi wa maji kwa kutumia visima virefu vinne na kazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa matanki matano yenye ujazo wa lita 400,000, ujenzi wa vituo 25 vya kuchotea maji na mtandao wa bomba wenye urefu wa kilometa 30.4. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba, 2022.

Mheshimiwa Mwenyekiti, chanzo cha Mto Katuma kinanufaisha wananchi wa Kata ya Katuma kwa shughuli za kilimo ambapo Serikali imetoa vibali vitano vya kutumia maji kwa skimu za umwagiliaji wa kilimo cha mpunga. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali itaajiri Mtaalam Mshauri wa kufanya usanifu wa mradi wa maji kwa kutumia chanzo cha maji cha Ziwa Tanganyika kupeleka Mkoa wa Katavi ambapo Wilaya ya Tanganyika itanufaika.
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza:-

Je, ni lini mradi wa maji mserereko wa Kiburubutu Ifakara utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abubakari Damian Asenga, Mbunge wa Jimbo la Kilombero, kama ifutavyo:-

Mheshimiwa Spika, mradi wa maji wa Mserereko wa Kiburubutu ni miongoni mwa miradi itakayotekelezwa kupitia mradi wa Miji 28 ikiwemo mji wa Ifakara. Ujenzi wa mradi huo utaanza kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022.
MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali italishughulikia tatizo la maji kwa vijiji zaidi ya 14 vya Tarafa ya Mtae?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Rashid Shangazi, Mbunge wa Mlalo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Tarafa ya Mtae ina jumla ya vijiji 20 ambapo vijiji 16 vinapata huduma ya maji kupitia visima vifupi na mito. Katika kuboresha huduma hiyo, kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imekamilisha ujenzi na ukarabati wa miradi ya maji ya Bokoboko, Shaghayu na Rangwi inayonufaisha vijiji sita vya Masereka, Mamboleo, Kwemtindi, Tema, Mpondekaya na Kweshindo.
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itakamilisha ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga mradi wa maji wa vijiji tisa vya Kata za Oldonyosambu na Oldonyowas?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Noah Lemburis Saputu, Mbunge wa Arumeru Magharibi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatekeleza mradi wa maji wa Oldonyosambu kwa ajili ya kuhudumia vijiji tisa vya kata za Oldonyosambu na Oldonyowas. Utekelezaji wa mradi huo unahusisha ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 47.8, ujenzi wa matanki matatu yenye ujazo wa lita 575,000, ujenzi wa vituo vitatu vya kuchotea maji na booster stations mbili. Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2022 na kuimarisha upatikanaji wa huduma ya maji katika kata hizo.
MH. TASKA R. MBOGO aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Katavi wanapata maji safi na salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Taska Restituta Mbogo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hali ya upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Katavi ni wastani wa asilimia 71 kwa vijijini na asilimia 60 kwa mijini. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji 42 katika Wilaya zote za Mkoa wa Katavi lengo likiwa ni kuhakikisha Wananchi wanapata maji safi na salama. Miradi hii ni pamoja na mradi wa maji Karema kwa kutumia Ziwa Tanganyika katika Wilaya ya Tanganyika unaotarajiwa kukamilika mwezi Septemba, 2022. Vilevile Mji wa Mpanda utanufaika na utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28.

Aidha, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itaajiri Mtaalamu Mshauri wa kufanya usanifu kwa kutumia vyanzo vya Ziwa Tanganyika ili kuwapatia maji wananchi wa Wilaya za Tanganyika, Mlele, Mpanda na maeneo ya karibu na kufikia lengo la asilimia 95 mijini na asilimia 85 vijijini ifikapo mwaka 2025.
MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuwatua ndoo kichwani wanawake wa Mji wa Mlowo?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Serikali ni kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji inaboreshwa nchi nzima. Hali ya upatikanaji wa maji katika Mji wa Mlowo ni wastani wa asilimia 44.5. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imekamilisha mradi wa maji wa Selewa - Mlowo ambapo mradi wa maji wa Mahenje - Mlowo utakamilika mwezi Juni, 2022. Miradi hii itaboresha upatikanaji wa huduma ya maji kwa asilimia 53.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itatekeleza mradi kwa kutumia chanzo cha maji cha Mto Bupigu ulioko Wilayani Ileje. Aidha, mpango wa muda mrefu ni kujenga miundombinu ya kuchukua maji kutoka mradi mkubwa wa Mto Kiwira ambao utahudumia Jiji la Mbeya na maeneo jirani ikiwemo Mji wa Mlowo na maeneo ya pembezoni.
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza:-

Je, ni lini Wananchi wa Kata ya Bosha na Mhinduro watapata maji salama?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula, Mbunge wa Jimbo la Mkinga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa Mradi wa Maji wa Mhinduro utakaohudumia Kata za Bosha na Mhinduro na ujenzi utaanza mwezi Juni, 2022 na kukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023.

MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaipatia ruzuku Bodi ya Maji ya KAVIWASU kwa kuwa imekuwa ikiendeshwa kwa gharama za wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante; kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Maji Namba 5 ya mwaka 2019 ya Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira kupitia kifungu cha 13(1)(b) vyombo vya watumia maji vinaruhusiwa kutoa huduma za maji kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo chombo cha watumia maji cha KAVIWASU kinatoa huduma kwenye baadhi ya maeneo ya mji wa Karatu. Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha hakuna changamoto katika utoaji wa huduma ya maji kwa wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, hivi sasa mji wa Karatu unapata huduma ya maji inayotolewa na kusimamiwa na taasisi mbili za KARUWASU na KAVIWASU. Hivyo, Serikali inao mpango wa kuanzisha taasisi moja na imara itakayotoa huduma ya maji kwa ufanisi kwa eneo lote la mji wa Karatu. Taasisi hiyo itapata ruzuku kwa kuzingatia miongozo iliyopo.
MHE. FESTO R. SANGA aliuliza: -

Mheshimiwa Spika, je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi wa maji Kata ya Iwawa Makete Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji wa kuhudumia Kata ya Iwawa kwa kutumia chanzo cha Mto Isapulano. Mradi huu unahusisha ujenzi wa chanzo, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilometa 12.5, ulazaji wa mabomba na usambazaji umbali wa kilometa 39 na ujenzi wa matanki matatu yenye ujazo wa lita 450,000. Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -

Mheshimiwa Spika, je, ni lini mradi mkubwa wa maji toka Mto Rufiji utaanza kutekelezwa ili kuwaondolea wananchi wa Kata 23 za Wilaya ya Kilwa tatizo la ukosefu wa maji safi na salama ambalo limekuwa likiwakabili kwa muda mrefu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Francis Kumba Ndulane, Mbunge wa Kilwa Kaskazini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, hali ya upatikanaji huduma ya maji katika Wilaya ya Kilwa ni wastani wa asilimia 64. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi tisa ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi wa Julai, 2022 na kuboresha huduma ya maji kufikia asilimia 86.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali itaajiri Mtaalam Mshauri na kufanya usanifu wa mradi wa kimkakati na kwa kutumia chanzo cha maji cha Mto Rufiji ikiwa ni mpango wa muda mrefu wa kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Kilwa na maeneo mengine ya Mkoa wa Lindi.
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -

Je, ni lini Mradi wa Maji wa Ikozi uliopo Sumbawanga Vijijini utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imeendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bwawa la Ikozi unaohudumia Viijiji vya Ikozi, Kazwila, Chituo na Tentula vya Kata ya Ikozi, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini. Mradi huo unahusisha ujenzi wa bwawa, ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilometa 1.2, nyumba ya mtambo, ununuzi na ufungaji wa pump za kusukuma maji na ujenzi wa mfumo wa kusafisha na kutibu maji. Utekelezaji wa mradi utakamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza:-

Je, kwa nini Serikali ilivunja Mradi wa Maji wa KAVIWASU katika Mji wa Karatu bila kuwashirikisha wananchi?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria ya Maji Namba 5 ya mwaka 2019 ya Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira kupitia kifungu Na. 13(1)(b) vyombo vya watumia maji vinaruhusiwa kutoa huduma za maji kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini ambapo chombo cha watumia maji cha KAVIWASU kilikuwa kinatoa huduma kwenye baadhi ya maeneo ya Mji wa Karatu.

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha huduma ya maji kwenye Mji wa Karatu, Serikali iliunganisha vyombo viwili vya kutoa huduma ya maji vya KARUWASU na KAVIWASU kuwa chombo kimoja ambacho mpaka sasa kimeendelea kutoa huduma ya maji kwa ufanisi katika eneo lote la Mji wa Karatu. Uundaji wa chombo hicho ulishirikisha wananchi ambapo Wizara ilifanya majadiliano ya kina na Mamlaka za Serikali, Wawakilishi wa Wananchi wa Karatu na wadau wa maji na kufikia maamuzi ya kuviunganisha vyombo hivyo viwili ili kiwepo chombo kimoja madhubuti kitakachosimamia utoaji wa huduma endelevu na kuondoa mkanganyiko wa bei za huduma.
MHE. SALMA R. KIKWETE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itapeleka maji katika Jimbo la Mchinga kutoka kwenye chanzo cha maji cha Ng’apa?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salma Rashid Kikwete, Mbunge wa Jimbo la Mchinga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imeendelea kuboresha huduma ya maji katika Manispaa ya Lindi kwa kujenga miradi ya maji inayotumia chanzo cha visima vya Ng’apa. Maji yamefika eneo la Mitwero na kazi inayoendelea ni kuyafikisha maji Mchinga ambapo Kata za Mchinga, Mvuleni, Kilolambwani na Kilangala zenye jumla ya vijiji 18 zitanufaika.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, wananchi katika vijiji nane katika Kata ya Mbanja inayopitiwa na bomba kuu kwenda Mchinga watanufaika. Kwa sasa, Mkandarasi anaendelea na kazi. Kazi zinazoendelea ni ulazaji wa bomba kuu umbali wa kilometa 42, ulazaji wa mabomba ya usambazaji kilometa 12.9 na ujenzi wa matanki manne yenye ujazo wa lita 100,000, mawili yenye ujanzo wa lita 200,000 na moja la lita 680,000. Kazi hiyo inatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaharakisha na kumaliza upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa maji katika vijiji 46 Wilaya ya Rungwe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge Viti Maalum, Mkoa wa Mbeya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022 utekelezaji wa miradi ya maji unaendelea katika vijiji 15 na kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwa wastani wa asilimia 70. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 kazi za usanifu kwa vijiji 31 itakamilika na kuanza ujenzi wa miradi, matarajio ni kuhakikisha wananchi wa vijiji 155 Wilaya ya Rungwe wanapata maji kwa lengo la kufikia asilimia 85 ifikapo mwaka 2025.
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kuunganisha mita za maji za kulipia kabla ya matumizi kama za TANESCO Arusha Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AWSA) imeshaanza kufunga dira za malipo ya kabla kwa taasisi za Serikali na baadhi ya wateja wa kawaida. Mpaka sasa jumla dira 345 zimeshafungwa na zoezi la ufungaji wa dira hizo linaendelea. Baadhi ya Taasisi za Serikali zilizofungwa dira hizo ni pamoja na Jeshi la Polisi, ofisi pamoja na nyumba za watumishi, ofisi za Serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya NIDA, Ofisi za Kata, Ofisi za Magereza na Makumbusho, baadhi ya vituo vya afya na zahanati pamoja na Shule za Msingi na Sekondari zimeshafungiwa dira hizo.
MHE. JOSEPH A. TADAYO K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-

Je, lini mradi wa maji wa Tukuyu utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anton Albert Mwantona, Mbunge wa Jimbo la Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ukamilishaji wa Mradi wa Maji Tukuyu Mjini unaolenga kuhudumia wakazi wapatao 63,647 waishio kwenye Mitaa ya Mabonde, Kasyeto, Ndyonga, Batini, Bulyaga na Makandana. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 85 ambapo kazi zilizotekelezwa hadi sasa ni pamoja na ujenzi wa banio katika chanzo cha Mto Mbaka, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye tenki umbali wa Kilometa 9.5, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji, umbali wa kilometa 20 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira mpya za maji 125.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zilizosalia ni ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa lita 1,500,000 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira nyingine mpya 5,875 ambapo kazi zote hizi zinatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2024.
MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka mradi wa maji katika Kata za Kizumbi na Wampembe – Nkasi Kusini ?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri ya Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023, imekamilisha usanifu wa Mradi wa Maji Wampembe utakaohudumia Kata mbili za Kizumbi na Wampembe. Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Januari, 2024 na kukamilika mwezi Desemba, 2024 ambapo utanufaisha wananchi wapatao 15,089 waishio kwenye vijiji sita vya Wampembe, Mwinzana, Kizumbi, Lyapinda, Ng’anga na Katenge.

Mheshimwa Mwenyekiti, mradi huo unatarajiwa kutekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la USAID kupitia Mradi wa Programu ya Maji na Usafi wa Mazingira (MUM), ambapo baadhi ya miundombinu inayotarajiwa kujengwa ni pamoja na matenki Manne (4) ya kuhifadhia maji yenye jumla ya lita 405,000, ujenzi wa vituo 39 vya kutolea huduma kwa wananchi sambamba na mtandao wa bomba kuu na mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 41.
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza: -

Je, lini wananchi wa Kata za Nalasi Tunduru watapata maji ya uhakika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu,

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kata mbili za Nalasi Mashariki na Nalasi Magharibi zenye jumla ya ya wakazi 21,989; na vijiji saba vya Nalasi, Wenje, Lipepo, Mkapunda, Lukumbo, Nasomba na Chilundundu zinapata huduma ya maji kupitia Skimu ya Maji ya Nalasi na Nasomba zilizojengwa mwaka 2012. Katika kuboresha huduma ya maji kwenye kata hizo, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 itafanya ukarabati wa miradi hiyo ili kuongeza ufanisi wa utoaji huduma ambapo utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Novemba, 2023 na kukamilika Februari, 2024.

Mheshimiwa Spika, Serikali pia katika mwaka huu wa sedha 2023/2024, itafanya utafiti wa maji chini ya ardhi pamoja na kuchimba visima virefu vya maji katika Vijiji vya Nalasi, Wenje na Mkapunda ili kupata vyanzo vya uhakika vitakavyosaidia kujenga mradi mkubwa wa usambazaji maji utakaoweza kuhudumia vijiji vyote vya Kata zote mbili za Nalasi Mashariki na Nalasi Magharibi. Kazi ya utafiti wa uchimbaji visima hivyo, inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Novemba, 2023 na kukamilika Februari, 2024.
MHE. NDAISABA G. RUHORO aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa mradi mkubwa wa bilioni 41 wa kupeleka maji safi Ngara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu,

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge Jimbo la Ngara Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Maji inatarajia kutekeleza wa mradi mkubwa wa maji Ngara Mjini kwa gharama ya Shilingi bilioni 41. Usanifu wa mradi huu umekamilika na na unatarajiwa kuhudumia wananchi wapato 170,678 waishio katika Kata ya Ngara Mjini, Kanazi, Kibimba, Nyamiaga na Murukulazo. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili utekelezaji wa mradi huo uanze.

Mheshimiwa Spika, kwa mpango wa muda mfupi wa kupunguza kero ya maji katika Mji wa Ngara na viunga vyake, Serikali katika mwaka huu wa fedha 2023/2024 imetenga kiasi cha fedha shilingi milioni 600. Kazi zitakazofanyika ni pamoja na uchimbaji wa visima viwili ambapo kisima kimoja kimekamilika, ujenzi wa tanki la ujazo wa lita 250,000 na ulazaji wa mtandao umbali wa kilometa 12 na ufungaji wa pampu mbili za kusukuma maji.
MHE. ERIC J. SHIGONGO aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha uchimbaji wa visima vya maji vilivyoanza kuchimbwa katika Jimbo la Buchosa?

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Eric James Shigongo, Mbunge wa Jimbo la Buchosa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa 2023/2024 Serikali inaendelea na zoezi la utafiti wa maji chini ya ardhi pamoja na uchimbaji wa visima 13 katika Jimbo la Buchosa Wilayani Sengerema. Hadi sasa jumla ya visima sita vimechimbwa, ambapo kati ya visima hivyo tulivyopata maji ni visima vinne vilivyochimbwa katika vijiji vya Bulolo, Nyonga, Bulyahilu na Izindabo. Aidha, kazi ya utafiti wa maji ardhini na uchimbaji wa visima inaendelea katika Vijiji vya Kisaba, Busikimbi, Kasalaji, Nyamiswi, Luharanyonga, Irenza na Bugoro ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024.
MHE. MIRAJI J. MTATURU aliuliza:-

Je, lini Serikali itachimba Mabwawa ya maji Kata za Kikio, Misughaa, Lighwa, Mungaa, Siuyu, Issuna na Mkiwa – Singida?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Ikungi ina jumla ya kata 28 zikiwemo Kata za Kikio, Misughaa, Lighwa, Mungaa, Siuyu, Issuna na Mkiwa. Vyanzo vikuu vya maji katika kata hizo ni maji chini ya ardhi kupitia visima vilivyochimbwa na kuwekewa miundombinu ya kutolea maji. Vijiji vyote vya Kata za Mungaa, Siuyu, Issuna na Mkiwa vinapata huduma ya maji kwa kutumia visima vilivyochimbwa kwenye vijiji hivyo. Aidha, baadhi ya vijiji katika Kata za Kikio, Misughaa na Lighwa bado havijapatiwa huduma ya maji ya kutosheleza.

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira zinatosheleza katika Wilaya ya Ikungi Ikiwemo Kata za Kikio, Misughaa, Lighwa, Mungaa, Siuyu, Issuna na Mkiwa, Serikali imeandaa Mpango Mkakati wa Miaka Mitano kuanzia 2022/2023 – 2025/2026 wa kujenga mabwawa ya kuvuna maji ya mvua ili yatumike wakati wa kiangazi sambamba na kudhibiti mafuriko. Mwaka 2024/2025 itafanya usanifu wa kina na kubaini maeneo yanayofaa kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa katika kata hizo.
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza kuunganisha mita za maji za kulipia kabla ya matumizi kama za TANESCO Arusha Mjini?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Arusha (AWSA) imeshaanza kufunga dira za malipo ya kabla kwa taasisi za Serikali na baadhi ya wateja wa kawaida. Mpaka sasa jumla dira 345 zimeshafungwa na zoezi la ufungaji wa dira hizo linaendelea. Baadhi ya Taasisi za Serikali zilizofungwa dira hizo ni pamoja na Jeshi la Polisi, ofisi pamoja na nyumba za watumishi, ofisi za Serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Ofisi ya NIDA, Ofisi za Kata, Ofisi za Magereza na Makumbusho, baadhi ya vituo vya afya na zahanati pamoja na Shule za Msingi na Sekondari zimeshafungiwa dira hizo.
MHE. JOSEPH A. TADAYO K.n.y. MHE. ANTON A. MWANTONA aliuliza:-

Je, lini mradi wa maji wa Tukuyu utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anton Albert Mwantona, Mbunge wa Jimbo la Rungwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ukamilishaji wa Mradi wa Maji Tukuyu Mjini unaolenga kuhudumia wakazi wapatao 63,647 waishio kwenye Mitaa ya Mabonde, Kasyeto, Ndyonga, Batini, Bulyaga na Makandana. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 85 ambapo kazi zilizotekelezwa hadi sasa ni pamoja na ujenzi wa banio katika chanzo cha Mto Mbaka, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo kwenda kwenye tenki umbali wa Kilometa 9.5, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji, umbali wa kilometa 20 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira mpya za maji 125.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi zilizosalia ni ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa lita 1,500,000 pamoja na ununuzi na ufungaji wa dira nyingine mpya 5,875 ambapo kazi zote hizi zinatarajiwa kukamilika mwezi Aprili, 2024.
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Je, lini Halmashauri ya Mji wa Kasulu itaondokana na matumizi ya maji machafu kutokana na ukosefu wa chujio?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Gezabuke, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuna ukosefu wa miundombinu ya kusafisha na kutibu maji katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu. Ili kutatua changamoto Serikali imekamilisha ukarabati wa chujio la maji la Kabanga ambalo limeanza kufanya kazi. Chujio hilo lina uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 1,000,000 kwa siku. Aidha, ujenzi wa machujio ya maji kutoka vyanzo vya Mto Chai na Miseno umeanza na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili, 2024. Machujio haya yatakuwa na uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 3,000,000 kwa siku. Kwa sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 15.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia mradi wa maji wa miji 28 imeanza ujenzi wa chujio la maji kutoka chanzo cha maji cha Mto Ruchunji. Kwa sasa mradi huo utekelezaji wake umefikia asilimia 5 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Aprili, 2025 ambapo chujio hilo litakuwa na uwezo wa kuchuja maji jumla ya lita 15,000,000 kwa siku.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:-

Je, ni lini ujenzi wa Mradi wa Maji Kemondo - Maruku katika Jimbo la Bukoba Vijijini utakamilika.
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali inaendelea na utekelezaji wa awamu ya kwanza inayohusisha ujenzi wa chanzo cha maji na ulazaji wa bomba kuu kilometa nne na tenki la ujazo wa lita 3,000,000. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 utekelezaji wa mradi utaendelea na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023.

Mheshimiwa Spika, mradi huo utanufaisha Kata Tano za Bukoba Vijijini ambazo ni Kemondo, Bujogo, Katerero, Maruku na Kanyangereko.
MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji ya Ziwa Victoria katika Halmashauri ya Ushetu?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani, Mbunge wa Ushetu kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imekamilisha ujenzi wa Miradi ya Maji katika Vijiji vya Kisuke, Igunda na Nyankende. Vilevile utekelezaji wa Miradi ya Maji katika Vijiji vya Mpunze, Sabasabini, Iponyanholo, Itumbili, Mitonga na Ididi inaendelea na inatarajiwa kukamilika mwezi Julai, 2022. Kukamilika kwa miradi hii kutaboresha huduma ya upatikanaji wa maji toka asilimia 58 hadi asilimia 62. Aidha, mpango wa muda mrefu ni kutekeleza mradi utakaotumia chanzo cha maji cha Ziwa Victoria ambapo usanifu utafanyika katika mwaka wa fedha 2022/2023.
MHE. DANIEL B. SILLO aliuliza:-

Je, lini Serikali itatekeleza mradi wa maji wa Darakuta – Magugu - Mwada hadi Minjingu – Babati?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Daniel Baran Sillo, Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi wa maji Darakuta-Magugu ndiyo unaoendelezwa kwa awamu ya pili mpaka Minjingu ambapo utagharimu shilingi bilioni 5.672 na kazi zinazotarajiwa kufanyika ni pamoja na ulazaji wa bomba kuu umbali wa Kilometa 46, ujenzi wa tenki la lita 250,000 na ufungaji wa pampu za kusukuma maji. Utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Juni, 2022 chini ya Mzabuni Plasco Limited na kazi hiyo ilitarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 3 Julai, 2023, Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Babati (BAWASA) ilivunja Mkataba na Plasco Limited baada ya kushindwa kukamilisha kazi kwa wakati. Kwa sasa, Serikali imeanza ununuzi wa mabomba kupita mfumo mpya wa Ununuzi wa NEST, na ifikapo mwezi Desemba 2023, Mzabuni wa mabomba atakuwa ameshapatikana.

Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi sita na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Juni, 2024 na utanufaisha wananchi zaidi ya 23,000 wa Kata za Mwada na Nkaiti.
MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -

Je, lini mradi wa kupeleka maji katika Kata Sita za Izimbya, Kyaitoke, Mugajwale, Ruhunga, Katoro na Kaibanja kutoka Ziwa Ikimba utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa mradi wa maji wa Ziwa Ikimba uliopangwa kunufaisha Kata Sita za Izimbya, Kyaitoke, Mugajwale, Ruhunga, Katoro na Kaibanja zenye jumla ya Vijiji 17. Utekelezaji wa mradi huo unatarajiwa kuanza mwezi Machi, 2024. Aidha, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 inaendelea na uchimbaji wa visima katika Wilaya ya Bukoba Vijijini ambapo uchimbaji wa visima virefu Sita utafanyika katika Kata za Ruhunga, Kaibanja, Mgajwale, Izimbya, Katoro na Kyaitoke. Kwa ujumla uchimbaji huo umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Novemba, 2023.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, Serikali inatarajia kutekeleza mradi wa maji mwingine katika Kata ya Katoro utakaohusisha, ukarabati wa tanki la lita 150,000, Ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 35, ulazaji wa miundombinu ya kusambaza maji kilometa 37, kujenga nyumba ya pampu, kufunga umeme na Kununua na kufunga pampu ya kusukuma maji. Mkandarasi wa ujenzi wa mradi huo anatarajiwa kupatikana mwezi Januari, 2024.
MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa muda mfupi na mrefu wa kukarabati Mradi wa Maji wa Makonde Mkoani Mtwara?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, Mbunge wa Jimbo la Nanyamba, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua Mradi wa Maji wa Makonde ni chakavu na unahitaji ukarabati. Katika mpango wa muda mfupi kwa mwaka 2023/2024, Serikali imetenga shilingi bilioni 1.5 ambapo tayari zaidi ya shilingi milioni 200 zimetolewa kwa ajili ya kufanya ukarabati wa mabomba ambapo, kazi ya ulazaji mabomba inaendelea na tayari umbali wa kilometa tano umekamilika kati ya 31 zilizopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mpango wa muda mrefu, Serikali inaendelea na ukarabati mkubwa wa mradi wa Makonde kupitia mradi wa Maji wa Miji 28 utakaogharimu shilingi bilioni 84.7. Utekelezaji wa mradi huu umeanza mwezi Juni, 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2024. Hadi sasa utekelezaji 40% umekamilika. Kwa mradi huu kutaondoa tatizo la maji katika Halmashauri ya Mji wa Newala, Wilaya ya Tandahimba na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba. (Makofi)
MHE. CONDESTER M. SICHALWE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutatua changamoto ya maji katika vijiji 42 vya Jimbo la Momba?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Condester Michael Sichalwe, Mbunge wa Momba, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Momba lina jumla ya Vijiji 72 ambapo mpaka sasa vijiji 30 vinapata huduma ya Majisafi na Salama kupitia miradi ya maji ya bomba. Katika kuhakikisha vijiji vyote vinapata huduma ya maji, katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali imeendelea na utekelezaji wa miradi ya Maji katika vijiji 12 vya Muungano, Ipata, Ntinga, Chindi, Makamba, Naming’ongo, Yala, Isanga, Kalungu, Lwatwe, Samag’ombe na Kakozi kwa gharama ya shilingi bilioni 9.45. Utekelezaji wa miradi hiyo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024.

Mheshimiwa Spika, vilevile Serikali imeanza kazi ya utafiti wa maji chini ardhini na uchimbaji wa visima virefu katika vijiji 16 vya Mkutano, Nzoka, Chilangwi, Itumba, Miunga, Mfuto, Machimbo, Mpwinje, Njeleke, Isunda, Chafuna, Msungwe, Sante, Siliwiti, Chole na Mtungwa ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2024 kwa shilingi milioni mia sita. Kukamilika kwa uchimbaji wa visima hivyo kutawezesha usanifu wa miundombinu ya usambazaji, kufanyika katika mwaka wa fedha 2024/2025 na utekelezaji wake kuanza. (Makofi)
MHE. NEEMA W. MGAYA aliuliza:-

Je, lini Mradi wa Maji wa Igongwi utakamilika katika Tarafa ya Igominyi Wilayani Njombe?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji nijibu swali la Mheshimiwa Neema William Mgaya, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na Utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Igongwi katika Halmashauri ya Mji wa Njombe unaolenga kutatua tatizo la maji kwa wakazi 9,717 waishio katika Vijiji vya Kitulila, Madobole, Luponde na Njoomlole. Hadi sasa utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 78.

Mheshimiwa Spika, Serikali katika mradi huo imekamilisha ujenzi wa vyanzo vinne vya maji, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu kilometa 49.7, ulazaji wa mabomba ya usambazaji maji umbali wa kilometa 26 kati ya 35, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 32 kati ya 55, ujenzi wa matenki mawili yenye jumla ya ujazo wa lita 100,000 kati ya matenki manne pamoja na ujenzi wa miundombinu sita ya mfano ya kuvuna maji ya mvua iliyojengwa katika Shule za Msingi Madobole na Kitulila, Ofisi ya Serikali ya Kijiji Madobole na Zahanati ya Kijiji cha Kitulila. Kazi zote zilizosalia zinatarajiwa kukamilika kabla au ifikapo mwezi Juni, 2024.
MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -

Je, lini mradi wa maji wa vijiji 57 ambao utaanzia Kyerwa, Nyakatuntu mpaka Kimuli Wilayani Kyerwa utaanza?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante; kwa niaba ya Waziri wa Maji naomba kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Seba Bilakwate (Mb) kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa maji katika vijiji 57 Wilayani Kyerwa. Hadi sasa, utekelezaji wa mradi huo unaendelea katika vijiji 27 ambavyo ni Nkwenda, Rwabwere, Karongo, Nyamiaga, Nyakatera, Kagu, Masheshe, Nyamweza, Kaikoti, Iteera, Muleba, Chanya, Kimuli, Rwanyango, Chakalisa, Kikukuru, Karambi, Rwele, Mukunyu, Rukuraijo, Makazi, Kibimba na Mabira.

Mheshimiwa Spika, kazi zilizotekelezwa katika miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa matenki matano (5) yenye jumla ya ujazo wa lita 1,450,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 110, ujenzi wa vituo 102 na vioski 18. Utekelezaji wa miradi hiyo umefikia wastani wa asilimia 80 na unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2024. Mradi utakapokamilikautawanufaisha wananchi wapatao 83,000. Miradi hiyo katika vijiji 30 vilivyobaki itatekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/2025.
MHE. TECLA M. UNGELE aliuliza: -

Je, ni lini Wananchi wa Kata za Nachingwea, Kiegei, Matekwe na Namapwia – Nachingwea, Lihimalya na Kandawale - Kilwa watapatiwa maji?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tecla Mohamed Ungele, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Katika kuboresha huduma ya maji kwenye Kata za Matekwe, Kiegei na Namapwia, Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 inaendelea na zoezi la uchimbaji wa visima vinne ambapo kisima kimoja tayari kimechimbwa katika Kijiji cha Kilimarondo na uchimbaji wa visima vitatu unaendelea na unatarajiwa kukamilika Mwezi Juni, 2024.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye Kata ya Nachingwea, Serikali inaendelea na kazi ya usanifu wa mradi pacha toka vyanzo vya Mbwinji na unatarajia kukamilika mwezi Juni, 2024, ambapo utekelezaji wa mradi utaanza katika Mwaka wa Fedha 2024/2025. Aidha, Kwa upande wa Kata ya Kandawale yenye jumla ya Vijiji Vinne, Vijiji viwili vya Kandawale na Mtumbei vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia miradi iliyojengwa yenye jumla ya vituo 13. Pia, Vijiji vya Ngarambi na Matewa vinatarajiwa kuchimbiwa visima katika Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Kata ya Lihimalya, Serikali katika Mwaka wa Fedha 2024/2025 itafanya upanuzi wa Mradi wa Maji wa Pande kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye vijiji vya kata hiyo.
MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kumalizia Mradi wa Maji wa Mageri utakaohudumia vijiji nane Wilayani Ngorongoro?
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai, Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikitenga fedha za utekelezaji wa Mradi wa Maji Mageri utakaohudumia vijiji nane vya Tinaga, Oloirien, Ng’arwa, Yasi, Mdito, Mageri, Mugongo na Magaiduru, ambapo hadi sasa jumla ya shilingi 2,264,520,000 zimetolewa. Fedha hizo zimesaidia kukamilisha utekelezaji wa Banio la Chanzo cha Maji Orkanjor, ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo hadi kwenye tenki umbali wa kilometa tatu na ununuzi wa pampu mbili zenye uwezo wa kusukuma maji lita milioni 2.05 kwa Siku. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa matenki tisa yenye jumla ya ujazo wa lita 2,000,000 na uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa kilometa 80. Aidha, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2024. (Makofi)
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itaijumuisha kata ya Bukiko katika mradi wa kuboresha huduma za mawasiliano kwa kuongeza teknolojia za 3G na 4G na pia mradi huu utaimarisha miundombinu ya nishati ikiwemo ya kuweka generator. Utekelezaji wa mradi huu utaanza katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-

Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa Kata za Ngimu, Kijiji cha Lamba, Kata ya Msisi Vijiji vya Mnung’una na Mkwae, Kata ya Msange, Vijiji vya Muriga na Endeshi UCSAF imeingia makubaliano na TTCL kupeleka huduma za mawasiliano katika kata tajwa. Aidha, UCSAF pia imeingia makubaliano na Vodacom kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata ya Ughandi, Kijiji cha Misinko na kwa upande wa Kata ya Mudida, Kijiji cha Migugu UCSAF imeingia makubaliano na Kampuni ya Simu ya Halotel.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa miradi hii, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika kata hizo na kuchukua hatua stahiki kulingana na upatikanaji wa fedha.
MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga minara ya Mawasiliano katika Kata ya Litapunga – Nsimbo?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kuendelea kuniruhusu kutimiza majukumu yangu. Pia nimshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini na kunipa kazi na namuahidi kuendelea kujituma zaidi. Namshukuru zaidi pia Dkt. Tulia Ackson, Spika na Rais wa IPU pamoja na wewe Mheshimiwa Naibu Spika kwa kuendelea kutuongoza vizuri hata tunaweza kutimiza majukumu yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumshukuru Mheshimiwa Juma Hamid Awesso, kwa kunipa ushirikiano zaidi ya miaka mitatu na kunifanya niweze kutimiza majukumu yangu. Mwisho si kwa umuhimu, naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri Nape Nnauye kwa kunipokea vizuri ndani ya Wizara pamoja na Katibu Mkuu na Menejimenti, nawaahidi kutoa ushirikiano wangu wa dhati ili kuweza kutimiza majukumu ya Wizara yetu.

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Anna Richard Lupembe, Mbunge wa Nsimbo kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeingia makubaliano na Shirika la Mawasiliano (TTCL) kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano katika Kata ya Litapunga ambapo TTCL anajenga mnara katika Kijiji cha Kambuzi ‘A’ ambao utahudumia Vijiji vya Kambuzi ‘A’ na Kambuzi ‘B’. Utekelezaji wa mradi huu ni miezi 24 kuanzia tarehe 13 Mei, 2023 Mkataba uliposainiwa.
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JUMA USONGE HAMAD aliuliza: -

Je, lini Serikali itatuma wataalamu kwenda Kijiji cha Kandwe kilichopo Wilaya ya Kaskazini Unguja ili kutatua changamoto ya mawasiliano?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano katika pande zote mbili za Muungano kwa kushirikiana na watoa huduma. Kwenye mradi wa kufikisha mawasiliano katika Shehia (Kata) 38 Visiwani Zanzibar uliokamilika mwaka 2022, Kijiji cha Kandwi kilijumuishwa katika mradi huu na Kampuni ya Tigo – Zantel ilipewa jukumu la kufikisha mawasiliano katika Kijiji hicho.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara imeiagiza UCSAF kufika katika Kijiji cha Kandwi kufika wiki ya kwanza ya mwezi huu Septemba kwa lengo la kufanya tathmini ya kina ili kubaini kama kuna eneo lolote lenye changamoto ya mawasiliano liweze kutatuliwa.
MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuimarisha upatikanaji wa mtandao wa simu katika kata 29 za Tabora Mjini?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imejenga minara ya mawasiliano ya simu saba katika Jimbo la Tabora Mjini. Minara hiyo ilijengwa na Vodacom na Halotel katika Kata za Itetemia, Kabila, Kalunde, Ndevelwa, Tumbi na Uyui kupitia awamu mbalimbali za miradi iliyotekelezwa kati ya Agosti, 2017 na Januari, 2020.

Mheshimiwa Spika, kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidigitali Kata za Ifucha na Kiloleni zitajengewa minara na kampuni ya Honora (Tigo). Kwa upande wa Kata ya Kakola UCSAF imeingia mkataba na TTCL kwa ajili ya kujenga mnara katika kata hiyo. Utekelezaji wa mradi huu ni miezi 24 kuanzia tarehe 13 Mei, 2023.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa utekelezaji wa miradi inayoendelea, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika Jimbo la Tabora Mjini ili kubaini maeneo yenye uhitaji wa kufikishiwa mawasiliano.
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, ili kurahisisha mawasiliano?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Serikali kupitia UCSAF inatarajia kufikisha huduma za mawasiliano kwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) ambapo jimbo la Mbinga Mjini limenufaika kwa kupata minara mitatu. Minara miwili inajengwa na AIRTEL katika Kata ya Kitanda ambapo mnara mmoja umejengwa katika kijiji cha Utiri na ujenzi wa mnara wa pili uko katika hatua za mwisho. Vilevile Kampuni ya Simu ya VODACOM inatarajia kujenga mnara katika Kijiji cha Ruvuma Chini kilichopo katika Kata ya Mpepai. Baada ya kukamilika kwa minara hii Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga na kuchukua hatua stahiki kwa maeneo yatakayokuwa hayana mawasiliano.
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kusimamia ipasavyo biashara za mitandaoni nchini?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa biashara za mtandaoni zinasimamiwa ipasavyo, Serikali imetunga sheria za usalama wa mtandao ambazo ni Sheria ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015, Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya Mwaka 2015 na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022, ili kuwa na anga salama ya mtandao na mazingira mazuri ya kuwalinda watumiaji wa mitandao. Aidha, tumefanya marekebisho ya Sheria ya Miamala ya Kielektroniki ya mwaka 2015 pamoja na kuandaa za kanuni za watoa huduma za uidhinishaji ili kuwezesha matumizi ya saini za kielektroniki kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa watumiaji wa mtandao ambayo itawezesha usimamizi mahiri wa biashara mtandaoni.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na wadau tumeandaa Mkakati wa Uchumi wa Kidijitali (2024 – 2034) ambao pamoja na mambo mengine unaweka mazingira mazuri ya biashara mtandaoni ambayo yatazingatia ulinzi, usalama na faragha za watumiaji wote wa bidhaa na huduma ya TEHAMA nchini.

Aidha, tuko katika hatua za kufanya mapitio ya Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016 ili kuimarisha mazingira ya matumizi ya teknolojia zinazoibukia katika utoaji wa huduma mbalimbali kidijitali ikiwemo biashara mtandaoni. Vilevile, Wizara inashirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara katika ukamilishwaji wa Mkakati wa Taifa wa Biashara Mtandao ambao pia utaimarisha biashara ya mtandaoni nchini. (Makofi)
MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-

Je, lini minara itajengwa vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Oloitushula, Olchorovus, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imekamilisha utekelezaji wa ujenzi wa minara mitano ya kufikisha mawasiliano ya simu katika Kata za Oljoro, Olmotonyi na Oldonyosambu zilizopo Wilayani Arumeru.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini katika Vijiji vya Kata ya Bwawani na Vijiji vya Nengung’u, Engutukoit, Losinoni Juu na Losinoni Kati ili kubaini mahitaji halisi ya huduma za mawasiliano katika kata hizo na kuweka mkakati wa namna bora ya kufikisha huduma za mawasiliano hitajika.
MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaona umuhimu wa kuwezesha mawasiliano ya redio kwa Tarafa ya Kiwele, Kata za Kitunda, Uloli, Kilumbi na Kipili – Sikonge?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Shirika la Utangazaji Tanzania limejenga mitambo ya kurushia matangazo ya redio masafa ya FM katika eneo la Usungilunde Kata ya Sikonge, Wilayani Sikonge ambapo TBC Taifa inapatikana katika masafa ya 87.9 MHz na Bongo FM masafa ya 89.9 MHz. Mitambo hii inafikisha matangazo umbali wa kilometa 60 za hewani (Air distance) kutoka Usungilunde. Kata ya Kitunda ipo umbali wa zaidi ya kilometa 130 za hewani, Uloli, Kilumbi na Kipili zipo umbali wa zaidi ya kilometa 140 za hewani, hivyo kutokufikiwa na matangazo ya TBC kutokea mnara uliopo Eneo la Usungilunde Kata ya Sikonge. Serikali kupitia TBC imeweka maeneo haya katika utekelezaji wa Mwaka wa Fedha 2025/2026.
MHE. DEODATUS P. MWANYIKA aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa mnara wa mawasiliano katika Kijiji cha Uliwa - Njombe utakamilika?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante! Kijiji cha Uliwa kipo katika Kata ya Iwungilo inayoundwa na vijiji vya Ngalanga, Iwungilo, Igoma na Uliwa, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliijumuisha Kata ya Iwungilo katika mradi wa mawasiliano wa awamu ya pili ‘A’ (2A) ambapo mtoa huduma HONORA (TIGO) alijenga minara katika vijiji vya Iwungilo na Ngalanga inaohudumia vijiji vya Ngalanga, Iwungilo, Igoma na Uliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia UCSAF ilifanya tathmini katika Kijiji cha Uliwa na kubaini kuwa kulingana na jiografia ya kijiji cha Uliwa ambacho kipo bondeni, minara iliyojengwa awali haifikishi mawasiliano katika kijiji hiki. Hivyo, UCSAF tayari imekijumuisha kijiji hiki katika orodha ya vijiji vitakavyonufaika kupitia mradi wa mawasiliano vijijini utakaotekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/2025.
MHE. ASIA A. HALAMGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka huduma ya Mawasiliano Kata ya Simbay - Hanang’?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asia Halamga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeainisha changamoto ya mawasiliano katika Kata ya Simbay (Kijiji cha Simbay) na utekelezaji wa mradi huu utafanyika kwa kadri ya fedha zitakapopatikana. Ahsante.
MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA K.n.y. MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya kuhamishia Mfumo wa Cyber kuwa chini ya udhibiti wa Jeshi la Polisi?
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, mkakati wa Taifa wa Usalama umeweka malengo na mpango wa kimkakati wa nchi kuhakikisha ulinzi na usalama wa anga yetu ya mtandao (cyber space). Ndani ya Mkakati huo, taasisi zote zinazohusika na ushughulikiwaji wa makosa ya mtandao zimetambuliwa na majukumu yao kuwekwa bayana ili kuwepo utaratibu mzuri wa kushirikiana.

Mheshimiwa Spika, Tanzania Computer Emergency Response Team, Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Mamlaka ya Serikali Mtandao na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kwa pamoja zinashirikiana kusimamia masuala ya ushughulikiwaji wa makosa ya mtandao.

Mheshimiwa Spika, suala la ushughulikiwaji wa anga ya mtandao kwa maana ya (cyber) ni mtambuka na haliwezi kutekelezwa kwa ufanisi na taasisi moja hivyo ni muhimu taasisi hizo ziendelee kutekeleza usimamizi huo kwa kushirikiana na kwa utaratibu jumuishi ili kuongeza tija katika jukumu hilo. Hata hivyo, Serikali ipo tayari kupokea ushauri utakaowezesha kuboresha usalama wa matumizi ya mtandao hapa nchini. (Makofi)