Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 33 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 283 2022-05-30

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Primary Question

MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami inayounganisha Mji Mdogo wa Mtowisa na Sumbawanga Mjini kupitia Mlima Ng’ongo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, awali barabara hii ilisanifiwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe kabla ya ahadi ya Mheshimiwa Rais kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami ambapo katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali imetenga shilingi milioni 875 kwa ajili ya kujenga urefu wa kilometa 25 kwa kiwango cha changarawe.