Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 33 Industries and Trade Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara 288 2022-05-30

Name

Dr. Charles Stephen Kimei

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vunjo

Primary Question

MHE. CHARLES S. KIMEI aliuliza;

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa soko la Kimataifa katika eneo la Lokolova mpakani mwa Tanzania na Kenya?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA, alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru na kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Charles Stephen Kimei, Mbunge wa Vunjo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 140 katika eneo la Lokolova kwa ajili ya ujenzi wa soko la mpakani. Hatua inayofuata ni kupata hati miliki ya eneo hilo na hatimaye kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya soko hilo, nakushukuru.