Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 34 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 303 2022-05-31

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaviunganishia umeme vijiji vya Jimbo la Ndanda vilivyopitiwa na nguzo za umeme wa msongo wa 33KV kuelekea Masasi?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge wa Ndanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Jimbo la Ndanda lina jumla ya kata 16 na vijiji 69, vijiji 33 vina umeme na 36 bado havijapata umeme vikiwemo vijiji vya Mkungu, Chipite, Mkangā€™u, Mumburu B, Muongozo, Mdenga na Mbemba vinavyopitiwa na njia ya umeme ya msongo wa kilovoti 33 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Mahumbika kuelekea Masasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, vijiji vyote 36 ambavyo havina umeme katika Jimbo la Ndanda vinapatiwa umeme kupitia mradi wa REA III mzunguko wa pili unaotekelezwa na Mkandarasi M/s Namis Corporate Engineers and Contractors. Mradi huu unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2022.