Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 35 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 311 2022-06-01

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Primary Question

MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga miundombinu ya mawasiliano katika Kata za Idete, Kiyowela, Maduma, Idunda, Makungu na Ihowanza?

Name

Nape Moses Nnauye

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtama

Answer

WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile Mbunge wa Mufindi Kusini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) inatekeleza miradi ya kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata za Idunda na Ihowanza, Wilayani Mufindi ambapo ujenzi wa minara unaendelea na utakamilika ifikapo Julai, 2022. Mwaka wa fedha wa 2022/2023, Serikali itafikisha huduma za mawasiliano ya simu katika Kata za Idete na Maduma. Aidha, Kata za Kiyowela na Makungu zitafanyiwa tathmini ya kiufundi kubaini changamoto halisi iliyopo ili kutatuliwa.