Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 36 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 319 2022-06-02

Name

Mohammed Said Issa

Sex

Male

Party

ACT

Constituent

Konde

Primary Question

MHE. MOHAMED SAID ISSA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza kuhamasisha kilimo cha zao la Mwani?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Said Issa, Mbunge wa Jimbo la Konde, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilishaanza kuhamasisha na kutoa elimu kuhusu zao la mwani na tayari jumla ya wakulima 4,569 wamepatiwa mafunzo ya uzalishaji, uhifadhi na kuongeza thamani katika zao la mwani. Ahsante sana.